Simulizi : Facebook Imeharibu Maisha Yangu
Sehemu Ya Tano
(5)
Lwebe na kundi lake baada
ya kumpiga risasi mbili Adam waliamini katu asingeweza kunyanyuka kutoka katika
eneo lile,na hata angeweza kuinuka hakuwa na pa kwenda hakuujua mkoa huo hata
kidogo. Waliingia ndani na kupiga simu kwa Bi.Gaudensia kwamba mtu wake tayari
ana risasi mbili mwilini
?msimuue jamani,tafadhali sana kesho
naileta pesa yenu mapema kabisa?
?nimechoshwa na ahadi zako
mheshimiwa jiandae kuchukua maiti yako siku yoyote utakayotaka utaikuta
nimeihifadhi na kama na kuizika nitakusaidia? alijibu kwa ghadhabu kasha akakata
simu
Bi Gaudencia akapiga
tena
?nakusikiliza?
?basi nielewe kwa leo na
hili ni ombi la mwisho tafadhali usimuue kesho asubuhi sana nakuja
huko,ninaondoka huku saa nane usiku tafadhali? alibembeleza
?na
iwe hivyo atalala nje leo na hata kula hadi utakapokuja
?sawa
mkurugenzi? alijibu kwa unyenyekevu Gaudensia
Akini ya
Bi.Gaudensia ilifanya kazi haraka haraka akapekua kila kona katika chumba
anacholala na mumewe na kwa bahati nzuri kwa akakutana na kadi ya benki ya mume
wake ambayo alikuwa akifahamu vizuri kabisa namba zake za
siri.
Bila kupoteza muda akampigia dereva wake wa siri ambaye
huwa anampeleka Iringa naye haraka haraka bila kuhoji akatii amri aliyopewa.bila
Reshmail kujua Bi.Gaudensia akaondoka majira saa saba usiku,nafsi ilikuwa
ikimuhukumu juu ya baya lolote litakalomkuta Adam
?damu ya Adam
ipo juu yangu?
?naenda kwa rafiki yangu ameugua ghafla ? mama
Reshmail alimuaga mlinzi wa getini
?sawa bosi? alijibu mzee
yule wa makamo huku akifunga geti baada ya mama kuwa ametoka nje
Kwa
kasi ya ajabu gari iliondoka jijini Dar-es-salaam kwa kuwa ilikuwa usiku sana
vizingiti vya watu wa usalama pamoja na foleni havikuwepo sana hivyo dereva
alikimbiza gari kwa kadri ya uwezo wake.
Breki ya kwanza
ilikuwa ni katika benki ya C.R.D.B maeneo ya Ubungo ambapo mama Reshmail
alishuka na kuvuta pesa kutoka katika akaunti ya akiba ya mzee
Manyama
Badala ya masaa matano kwa gari binafsi kufika Iringa walitumia
masaa matatu pekee
?mh!! Huku napo kijijini kweli huyo nae
sijui ni mgonjwa sasa usiku huu atapata wapi lifti ya
gari?
Mama Reshmail alimwambia dereva wake alipoona watu wawili
wakisimamisha gari
?ah!! Ndo maisha ya Tanzania yalivyo?
alijibu dereva huku akiongeza zaidi mwendo wa gari hadi wakaifikia ngome ya
vigogo waliyokuwa wakiifuata
**** ****
*****
Magari makubwa ya mizigo yatokayo Morogoro kwenda Zambia
na Malawi ndiyo yaliyotoa msaada kwa Bite na Adam ambapo Bite alijitambulisha
kama mke wa Adam na kwamba wamevamiwa na majambazi na mumewe (Adam) amepigwa
risasi.
Laiti kama madereva wangekuwa watanzania kwa jinsi
walivyo waoga katu wasingewapandisha wawili hawa lakini wakongomani wale ambao
vita kwao ni jambo la kawaida waliwachukua Adam na Bite hadi Iringa mjini
walipowaacha jirani kabisa na hospitali ya rufaa.
?bila RB
hatupokei mgonjwa wa aina hii? alisema muuguzi wa kike wa hospitali ile wakati
Bite anajieleza.
Ni kweli yule muuguzi(nesi) alikuwa na haki
zote za kupingana na ujio ule kwani hali aliyokuwa nayo Adam ilihitaji taarifa
za polisi kwanza
?haa!!! Mama Christian, ni wewe hata siamini
au nakufananisha??
wakati Bite akijiegemeza kwenye ukuta huku
akiwa amekata tama alishangaa kutambulika kwake na nesi
yule
?Mungu wangu mama wawili jamani!!!?
Baada
ya kumkazia macho naye Bite akamtambua yule nesi kuwa waliwahi kufanya nae
biashara katika soko la Uyole Mbeya na pia alikuwa jirani yake pale alipokuwa
anaishi,ulikuwa mshangao mkubwa sana
?ehe!! Kulikoni tena ndugu
yangu yamekukuta yapi tena mwenzangu?? alihoji nesi huku akiwa amechangamka sana
safari hii
?ni makubwa sana,lakini ningeupata msaada wako
kwanza kwa mume wangu ndio tungeongea vizuri shoga? alijibu Bite akiwa na
matumaini tele
?ondoa shaka shoga huduma mnaipata sasa hivi
tena huduma bora,daktari tunaheshimiana naye sana na pia ni shemeji yangu? nesi
aliongea hayo huku wakisaidiana kumwingiza Adam ndani ya chumba cha
wagonjwa,hapakuwa na maswali mengi,undugu ulitawala pale.
Adam
akafanyiwa upasuaji mdogo wa kuondoa risasi katika ambao haukuchukua hata hata
nusu saa damu na maji pia vikaongezwa katika mwili wake uliokuwa dhaifu
sana.kufikia majira ya saa kumi na moja alfajiri Adam alikuwa amepata nafuu
kubwa na aliweza kutembea japo kwa kuchechemea
?shoga nikueleze
wazi tu kwamba sisi pa kufikia hapa Iringa mimi na mume wangu hatuna! Tangu
niondoke ghafla niliacha sijalipa kodi nina uhakika chumba sio changu tena kwa
hiyo pa kwenda hatujui? Bite alimweleza hayo mama wawili baada ya kuwa
amemsogeza pembeni ili mtu mwingine asiweze kusikia
?Ondoa
shaka Bite mimi kwangu pana nyumba kubwa tu!! Nimejengewa na mnyakyusa
mmoja,nimemweka kwenye kiganja kwangu mimi hasikii,haoni wala hasemi,ni kaka
yake na huyu daktari we mwenyewe si umeona alivyowashughulikia haraka? kwa sauti
ya chini kabisa nesi alijibu
Wote watatu katika teksi
wakaongozana hadi nyumbani kwa nesi ni kweli nesi hakuwa na chembe ya utani hata
kidogo nyumba ile ilikuwa kubwa sana na haikuwa haki kukaliwa na watu wawili
pekee vilikuwa ni vyumba sita pamoja na sebule
?karibuni!
Karibuni sana! Nesi aliwakaribisha walipofika nyumbani
kwake.
?asante sana ndugu yangu ama kweli ishi na watu uvae
viatu? alisema Bite kwa upole sana
?usijali Bite tumeishi
vizuri,hatukuwahi kugombana hata siku moja,tumetwishana matenga ya nyanya kwa
nini sasa nishindwe kukutendea wema!!!? nesi alimtoa hofu
Bite
Chumba walichopewa kilikuwa kikubwa cha kuwatosha
kabisa,kitanda cha tano kwa sita kilikuwa saizi yao
kabisa.
Adam alishangazwa sana na wema huo wa nesi lakini
mshango wake uliongezeka maradufu baada ya kukutana na mume wa nesi siku ambayo
walikuwa wakitambulishwa kwake kama shemeji zake yaani ndugu zake Bite.mzee huyu
wa kinyakyusa aliyeitwa Gwakisa ni kama heshima ilipitiliza na kuwa kama
anawanyenyekea wawili hawa.
Adam alihudumiwa na yule daktari
kana kwamba alikuwa ni mgonjwa wa kisukari au alikuwa ni mtoto wa mfalme,Adam
alipata farijiko kubwa sana kuishi pale
Bite kama kawaida
alikuwa mwanamke wa kujituma sana,ndani ya wiki moja tayari alikuwa amepata kazi
ya ndani katika nyumba nzuri waliyoishi wanafamilia watatu, mwanaume na mke
pamoja na mtoto wa kama miaka mitatu wa kike aliyekuwa anasoma shule ya
awali
***** ****** ******
******
?bite mama!!?
?bee
mama?
?mpeleke mtoto shule halafu baadaye mpeleke pale zahanati
akapimwe jana usiku amekohoa sana?
ilikuwa sauti ya Eveline
akimpa maelekezo Bite ambaye alikuwa mfanyakazi wake mpya na wa kwanza wa ndani
ya nyumba yake na mchumba wake.
Ratiba ya Bite ilikuwa ni kazi
kuanzia asubuhi ya saa mbili ambapo alikuwa akimpeleka Loyce {mtoto wa kaka yake
Benny} shuleni na kisha akirejea anaandaa chakula cha mchana kwa siku ambayo
Benny hurudi nyumbani mchana na baada ya hapo humfuata Loyce shuleni,kisha
maandalizi ya chakula cha jioni na majira ya saa kumi na mbili huaga na
kuondoka,ilikuwa kazi ambayo haikumtoa jasho Bite na malipo ya shilingi laki
moja kila mwezi yalimtosheleza kabisa kupanga chumba kidogo walicholipia
shilingi 15000 kwa mwezi
?tunashukuru sana kwa ukarimu wenu
bwana na bibi Gwakisa Mungu awazidishie baraka katika kazi zenu? alitoa shukrani
za dhati Adam kwa niaba ya mke wake wa bandia
(Bite).
uchangamfu wake na wingi wa vituko ulifanya nyumba ya
Gwakisa iwe iwe yenye shangwe na tabasamu kila siku,kitendo chake cha kuaga pale
kilimsononesha Gwakisa na mkewe lakini hawakuwa na jinsi, kutoka mfukoni mwake
aliwakabidhi shilingi laki mbili za kuanzia maisha yao huko
waendako
Tayari Adam alianza kumpenda kwa dhati Bite uchapakazi wake na
jinsi alivyomwokoa kutoka katika kifo ulichangia sana lakini kiunganishi cha
mtoto Christian ndio ilikuwa chachu kubwa ya mapenzi
yao.
walivyohama katika nyumba yao ya kupanga walianza rasmi
kuishi maisha ya mke na mume Adam hakuwa na amani hata kidogo na familia ya
Reshmail hasa baada ya kukuta katika nyumba hiyo ndogo waliyohamia magazeti
yaliyobandikwa kama mapambo likisema;
?imani za kishirikina
zamwondoa mheshimiwa Manyama bungeni? alitamani sana kuisoma habari hiyo
kiundani iliyotoka takribani miaka mitano iliyopita lakini ilikuwa imeandikwa
inaendelea ukurasa wa pili anbao haukuwepo pale ukutani
?Au
walikuwa wanataka kunitoa kafara? Mungu wangu!! Niliwakosea nini mimi?
alijiuliza Adam wakati wakiingiza yao ya Rambo ndani ya chumba hicho kimoja
kilichotenganishwa na pazia kufanya sebule na chumba
Hisi hizo
mbaya zikamfanya Adam aamue kuanzisha rasmi uhusiano na mwanamke ambaye amezaa
naye mtoto pia aliyeokoa maisha yake bila kutarajia mwanamke ambaye hajawahi
kumkwaza,mwanamke mpiganaji anayempa furaha tele kila
siku
?Bite nataka uwe mke wangu?
?Mh!! Niwe
mkeo mara ngapi mimi mkeo tayari jamani? alijibu Bite huku akichezea ndevu za
Adam ikiwa ni siku ya pili tu tangia wahamie katika makazi hayo
mapya
?una utani wewe mbona ulikuwa hujaniambia wala sijawahi
kusikia ukiniita mume wako?
?sio lazima nikwambie tayari nina
mtoto wako halafu humu ndani kuna kitanda kimoja tena kidogo tu,ulidhani chako
mwenyewe!!!? aliuliza Bite kisha wote wakacheka huku wakikumbatiana na kuangukia
kitandani
**** *******?
Maisha ya Reshmail
jijini Dar-es-salaam yalikuwa yamebadilika sana akiwa anasubiri wakati baba yake
akimtafutia kazi itakayompendeza alifurahia mara zote na Christian huku akiwa
amewabadili watu wote wanaomfahamu kwa ukaribu kutokea kumwita Reshmail na sasa
walimwita mama Christian na alikuwa amejivika pete ya ndoa katika kidole chake
cha shahada ikwa na jina Adam na nyingine ndogo akiwa amemvisha Christian ikiwa
imeandikwa Reshmail.
Hakuwa mtu wa kulialia tena wala msongo wa
mawazo haukumsumbua tena aliamini nafasi ya Adam ilikuwa imezibwa vyema na
Christian ambaye alikuwa Adam mpya kwake. Walilala wote, walicheza wote na
kusimuliana mambo mbalimbali.alipoenda kusalimia rafiki zake walienda wote
Christian mkono wa kulia.
Harakaharaka Christian alijikuta
akimpenda mno Reshmail kuliko hata ilivyokuwa kwa mama yake mzazi,maisha ya
kifahari ya kwao Reshmail yalimfanya Christian anawiri sana ungewakuta wakicheza
bustanini kama vile wanalingana umri walibembea pamoja na kupigana
kiuongouongo,kwa ufupi waliishi maisha ya kusisimua kwa kila
aliyewaona.
Akiugua Reshmail ni Christian atamuuguza kwa kukaa
pembeni yake bila kutoka nje hadi apone hivyo hivyo kwa Reshmail abaye
alimwogesha na kumlisha.
Wakati huo Reshmail ndio alikuwa
mwalimu wa Christian akimfundisha kusoma na kuandika jambo ambalo hata baba yake
alilipenda na Christian alikuwa mtu anayeelewa haraka akifundishwa ,reshmail
alifurahia sana.
Baada ya kukaa na Christian mwezi sita
reshmail kwa mara nyingine Iringa kwa rafiki yake jambo kubwa lililompeleka huko
ni harusi ya rafiki yahe huyo ambapo alitarajiwa kuwa matron wa kipenzi chake
hicho.
?shoga shughuli kesho kutwa hata haujaonekana jamani au
ndio mambo yetu yale haja ya kufanyiwa make up?.? Aliuliza
kiutani.
Eve katika simu alipokuwa anaongea na
Reshmail.
?Kesho asubuhi na mapema nakujua ,mume wangu alikuwa
na mafua ndio tatizo si unajua tena.?alijibu Reshmail.
Haya
mume huyo anavyoringiwa shauriro ?alijibu Eve .Christian alikuwa amependekezwa
kuwa bwana harusi mdogo pamoja na Loyce (mtoto wa kaka yake
Benny).
?He unatoka mume wangu asiuze sura,na jinsi
alivyoandaliwa huku Dar es salaam ,utachoka mwenyewe na simtoi mpaka siku ya
shughuli,atakayeruhusiwa kumuona ni bibi harusi mdogo(Loyce) peke yake wakati wa
kujifunza,sitaki mwingine amuone mpaka siku yenyewe?alijibu Reshmail kwa
furaha.
?Haya umeshindwa ambao hatuna waume tunalo,alijibu Eve
kisha wakaagana.
Asubuhi ya siku iliyofuata majira ya saa nne
asubuhi tayari Reshmail,Christian,mpambaji pamoja na dereva walikuwa ndani ya
gari la baba yake (Resh)taratibu safari ya Iringa
ikaanza.
?Usitupeleke kwa kasi sawa eeh,alitoa malekezo
Reshmail na kukubaliwa na dereva kwa sababu hawakuwa na haraka yeyote ila mbele
yao yalikuwa bado masaa mengi sana kabla ya harusi
kufanyika.
Kwa mwendo wa kinyonga kabisa gar lilifika mbele ya
nyumba ya Eve majira ya saa nne usiku na hakuna aliyekuwa ameschoka
sana.Shamrashamra zilikuwa kubwa sana maeneo ya pale kwa Eve kelele zilizidi
alipofika Reshmail, na kama alivyoaahidi kweli alishuka yeye peke yake kutoka
katika gari akifuatiwa na dereva,urembo wake utadhani alikuwa amepembwa tayari
kuingia ukumbini.
?Shoga tabia gain hiyo kupendeza kuliko bibi
harusi??aliuliza eve kiutani baada ya Reshmail kuingia katika chumba ambacho Eve
alikuwa amehifadhiwa akiwa na wapambaji wake.
?Hebu acha utani
wako,kila mara unadhani tuko shuleni?mwone,?alijibu Reshmail,Eve akajiziba mdomo
kwa aibu huku akiwatazama wapambaji wake waliokuwa wamejizuia kucheka lakini
uvumulivu ukawashinda wakacheka kwa nguvu.
Chumba kile
kikageuka kijiwa cha story kati ya Reshmail na Eve ,stori zingine zilikuwa juu
ya mume wa Reshmail (Christian),shoga hadi pete?
?Sina utani
mie mbona??alijibu Resh huku wapambaji wakiwa hawajui hata
kinachoongelewa.
?Mama kuna mtu anataka kukuona,ilikuwa ni
sauti ya kike ikimueleza Eve.
?Heh!!ushazaa na wewe??aliuliza kiutani
Reshmail.Mh!!niringe huyu ni msaidizi wangu tu wa kazi anaitwa Bite,nampenda
naye ananipenda pia.
?Sio kama mimi na Christian ?alidakia
Reshmail ambaye tangu aingie chumba kilitawaliwa na
vicheko.
?Bite humuwezi huyu anaitwa mam Christian ni rafiki
yangu tangu utotoni.
?Nafurahi kukufahamu mama Christian hata
mimi.
Alitaka kuondelea kuongea Bite akakatishwa na
Eve.
?Anayetaka kuniona nani huyo tena?,mwambie nina mgeni"
Bite akajiondokea bila kumalizia kauli yake.
Sherehe ilifana
kuanzi kanisani lakini mambo yote yalikuwa saa mbili usiku maharusi wadogo
walipokuwa wametangulia mbele wakifuatiwa na wana ndoa wenyewe(Eveline na
Benjamin)huku nyuma yao Reshmail na Fredrick wakifunika kila kitu kwa pale mbele
Christian aliteka macho ya watu huku kamera zimemulika
yeye.
Tabasamu lake pana la wakati wote lililoonyesha vishimo
katika mashavu yake yote lilisababisha watu wengine wahisi huenda sio kutoka
Tanzania , suti yake iliyoendana kabisa na mwili wake na viatu vyake pia jinsi
mkono wake ulivyokuwa umemshika kiustadi Loyce (bi harusi mdogo) ulimfanya MC
ashindwe kukaa kimya ?nani mwenyewe harusi,wa mbele,nyuma au kati? aliuliza kwa
mbwembwe
?mbeleeeeeeeee!!!.......nyumaaaaa!!!!? ndio majibu
yaliyosikika kutoka kwa wengi
?hayaa wageni waalikwa wanasema
maharusi wa katikati wamefunika sana? alidanganya MC aliyefahamu wazi Christian
na Reshmail wameteka macho ya watu wengi pengine kuliko maharusi
wenyewe.
Picha zilipigwa kwa wingi lakini Christian hakuonyesha
wasiwasi wowote ?mh!! Katoto kazuri halafu kajanja hako? wanawake walikuwa
wakinon?gonezana huku wakimtazama Christian anavyozidi kusonga
mbele
?wamekatoa nje,baba yake ni mreno? alidakia mama
aliyesifika kwa umbea pale mtaani aliyejulikana zaidi kwa jina la mama
mwingi.hata hawakuhangaika kujibishana nae kwani
walishamzoea
Taratibu kabisa kwa mwendo wa kunyata jozi hizi
tatu za kuvutia ziligawanyika huku jozi mbili za wakubwa zikienda katika meza
kubwa kabisa na watoto wakienda katika meza yao ndogo iliyokuwa akimeremeta soda
na vinywaji vingine baridi,
?kusema ukweli sherehe
imependeza,siongei kama MC bali kama ndugu Kidagaa Peter Kubalunga wengi
wananiita MC K.P? alichombeza Msema Chochote (MC) na kushangiliwa sana na umati
mkubwa uliohudhuria sherehe hiyo
**********
************ ********
?Dah!! Umependeza kweli sitaibiwa huko na
wajanja,hebu ona ona mgongo wako utadhani huna mamba ulivyopendeza,ona kifua
chako mpenzi wangu hapana nitaibiwa mke mie? Adam alikuwa akimtania Bite huku
akim funga zipu yake ya mgongoni
?Acha wivu mwanaume wewe,kaa
ndani usubirie ya kwako aniibe nani wataishia kutamani tu!!? alijibu Bite huku
akimun?gunya midomo yake ili lipstick aliyopakaa ikae vizuri zaidi na kioo
kikiwa mbele yake
?Nakupenda sana mke wangu,tambua hilo
niliamua toka moyoni mwangu na wala sijutii hata kidogo najionamwenye bahati
sana? Adam kwa sauti ya chini iliyomaanisha anachokisema alimwambia Bite ambaye
alitulia tuli akamtazama Adam kisha akamkumbatia na
kumbusu.
?nakupenda pia nakupenda sana? Bite akamwambia Adam
halafu akatoka nje na kupanda teksi iliyokuwa inamsubiri kwa nje na
kuondoka,Adam hakuthubutu kutoa hata pua yake nje kwani bado alikuwa na uoga wa
kurejea mikononi mwa watu wabaya
Majira ya saa tatu na nusu
Bite tayari alikuwa mlangoni akionyesha kadi yake ya mwaliko kwa watu wa ulinzi
kisha mwanadada kutoka kamati ya maandalizi akamwongoza Bite kuelekea katika
upande ambao ndugu zake na mwanamke walikuwa wamekaa,eneo la chini ya meza ya
bwana na bibi harusi mdogo.Bite alikuwa tayari kama ndugu wa damu kwa Eveline
walitokea kuheshimiana sana na hawakuwahi kuingia katika malumbano makubwa
sana.
Amani ilitoweka katika meza ya bwana na bibi harusi
wadogo,Christian alikuwa amekosa utulivu mara kwa mara alikuwa ananyanyua shingo
yake aweze kuona kitu Fulani ambacho hakuna aliyefahamu ni nini
kimemsibu
?Au kanaumwa tumbo?? alijiuliza matron huku akienda
kwenye ile meza kumsikiliza Chriss ana shida gani.
?Chriss ni
nini baba umekuwaje?? alimuuliza baada ya kumfikia
?nataka
kwenda kwa mama? alijibu kwa sauti iliyojaa manun?guniko
sana
?subiri kidogo mtoto mzuri nitakupeleka sawa? matron
alimdanganya Chriss huku akiamini shida yake ilikuwa kwenda kwa Reshmail,kidogo
Chriss alitulia japo bado hakuwa na katika hali ya uchangamfu kama
awali
Muda wa kutoa zawadi ulipofika maharusi wote katika jozi
tatu walitakiwa kuwa mbele ya umati kwa ajili ya kupokea zawadi zao.Christian na
Loyce waliwekewa viti wakakaa wakati Eve,Benny,Reshmail na Fredrick walisimama
wima kupokea heshima hizo
?heee! We mtoto vipi? Jamani huyu
mtoto kulikoni? yule mwanamke aliuliza baada ya kushikwa gauni lake na Christian
alipotaka kuondoka baaba ya kutoa zawadi.
Bahati mbaya muziki
ulikuwa umezimwa hivyo ukumbi mzima ulishuhudia tukio hili la
kushangaza
?mamaaaa!! Mamaaaa!!? Chriss alimpigia kelele
alipotaka kuondoka
?Chriss??.Christian??Christian wanguuuu!!!
Jamani ni mwanangu..ni mwanangu huyu? alipiga kelele mwanamke huyu, alikuwa ni
Bite na tayari akili yake imemgundu Christian,watu wote waliamini
amechanganyikiwa lakini alikuwa anasisitiza bado kwa maneno
hayohayo.
Hakika mbele yake alikuwepo mwanaye waliyepotezana
zaidi ya nusu mwaka sasa na dalili za kumpata zilikuwa zimeanza
kufifia.
Mayowe yake yalivyozidi yakapoteza usikivu pale
ukumbini na kila mtu kuanza kujiuliza kulikoni eneo lile
?mama
mama mama,huyu ni mwanangu?..Christian jamani? Bite kwa sauti ya juu sana
akaanza kumwambia Eveline ambaye alikuwa amekodoa macho kuangalia anachofanya
Bite pale mbele
?kuna nini jamani? Reshmail alishindwa
kujiuliza akamvagaa Eve na kumuuliza
?huyu ni Christian,mtoto
wangu jamani mtoto wangu kabisa? alisisitiza Bite.
Nguvu
zilimwisha Reshmail japokuwa hakuzimia lakini alianguka chini,alishuhudia kila
kitu lakini hakuweza kuzungumza,ulikuwa mshtuko wa hali ya juu sana haikuwa
sherehe tena bali kasheshe,huku Bite na mayowe yake huku Reshmail akiwa
chini.
Wapiga picha hawakuwa mbali walilichukua hili tukio
kikamilifu tayari kwa kuuza katika vyombo vya habari.
Mwanamama
mwenye nguo nyeusi alikuwa anapambana kupenya katika msitu mkubwa wa watu pale
ukumbini,mwanzoni hakuwemo kwenye sherehe
?vimama vya Kiswahili
navyo,hapo umbea tu ndo amefata humu,akipigwa hapo au akikanyagwa atamlalamikia
nani?
mwanaume mmoja aliyekuwa amevaa suti aliwaambia wenzake
huku wakimtazama mama huyo mwenye baibui iliyovaliwa kwa staili ya ninja hasa
hasa kwa waumini wa dini ya uislamu anavyopambana kwa juhudi ili apenye. Watu
kwa huruma wakampisha, moja kwa moja akiwa anakimbia kwa kasi alifika mbele ya
ukumbi akaanza kuzubaa na mara ghafla akakimbilia alipolala Reshmail na kuanza
kutikisa
?huyu maza vipi mwehu nini? Yaani mtu ameachiwa hewa
impige yeye anaenda kuweka usiku tena na manguo yake? kijana mmoja aliyekuwa
amevaa jinsi kwa staili ya mlegezo aliwaambia wenzake
?tulia
wewe huenda ni mamake huyo? alijibiwa na wenzake
?reshmail amka
amka mpenzi? alimwambia kwa sauti ya chini.
**** **
***
Wivu wa utani utani aliouonyesha mbele ya mke wake ulukuwa
unatoka moyoni mwake,Adam alihisi huko nje labda kuna mjanja anamchukulia mke
wake.
?ngoja nikamfumanie mtu leo? alijiwazia Adam huku
akipekua pekua nguo gani anaweza kuvaa iweze kumziba sura yake asiweze
kufahamika kwa urahisi mbele za watu,?baibui? ndio jibu alilopata, harakaharaka
akajitanda kwa ustadi,
Alifahamu vyema pesa ya mkewe ilipokuwa
inahifadhiwa akajichotea kiasi kilichotosheleza kwa nauli ?Mountain view?
alijikumbusha jina la hotel ambayo sherehe ilikua inafanyika,ni jina
alilolikariri kwenye kadi ya mwaliko.
Akiwa na baibui lake
alipanda teksi ikamfikisha moja kwa moja eneo la tukio,kukuru kakara aliyoikuta
pale ilimtia hofu kubwa sana aliamini lazima kuna kitu kimeharibika eneo lile
hakuwaza kitu kingine bali usalama wa mkewe (Bite) moja kwa moja naye
alijichanganya humo ndani.
Tofauti ya malengo yake ya kumjulia
hali mkewe,macho yake yanakutana na Reshmail akiwa sakafuni na vazi lake zuri la
harusi,sura yake bado ilikuwa haijasahaulika katika kumbukumbu za
Adam.
Nguvu zilizokuwa zimemwisha Resh pale chini zilirejea kwa kasi
kutokana na kusikia sauti ya kiume kutoka katika nguo za
kike
?mamaaaaaaaaaaa!!!!? alipiga kelele kwa sauti ya juu huku
tayari akiwa amesimama wima akijaribu kukimbia,kamera zikageukia eneo lao tena
nyingi zikimmulika mwanamke mwenye baibui (Adam).
Kabla
hajakimbia Reshmail alidakwa mkono wake.
?Adaam??Adaaaam!!!?
alipiga kelele kali zaidi wakati huuu Reshmail. Adam alikuwa amejivua baibui kwa
upande wa usoni, akiwa hajapewa jibu lolote reshmail palepale alifika
Bite,
?Adam! Umefikaje hapa mume wangu?si ulisema hauji?? Bite
aliuliza
?nini? Nani? Umemwitaje? Na huyu ni??.? Hakuweza
kumalizi kauli yake wakati huu,mawazo yakauzidi nguvu ubongo wake akazimia
palepale.
Wakati huo Chriss alikuwa analia tu hajui
kinachoendelea, Eve na Benny walikuwa wanahaha huku na huko bila kukumbuka
kwamba alikuwa na shera safi kabisa tena ya gharama za juu kabisa, Benny ndio
alikuwa kama tahira hajui hata pa kuanzia alikuwa ameshtuka
sana.
Ilikuwa kama vita vile lakini hakuna hata aliyejeruhiwa
wala aliyekuwa anapigana vilikuwa si vita vya risasi bali vita vya
mapenzi.
Wageni waalikwa waligeuza tukio hilo kuwa kama filamu
ya kusisimua lakini waliyokuwa wameianzia katikati bila kujua ilianzia wapi na
inaenda wapi.,nani nyota wa filamu na nani
adui.
***
Ni katika nyumba ya Eveline.
Reshmail akiwa mbele ya Beti amepiga magoti akilia kwa
uchungu
?Bite wewe ni mwanamke mwenzangu nionee huruma kwa haya
niliyopitia,nimeteseka sana, nimedhalilishwa kwa ajili ya Adam, ni kwa ajili
yake hadi leo mimi ni bikra, kwa ajili yake familia yake imetuchukia,kwa ajili
ya Adam baba yangu haeshimiki tena mtaani kwetu,Bite sitamani mwanaume yeyote
yule,ukininyan?ganya Adam na Christian mimi nitakufa Bite, ni furaha gani
utaipata kwa kifo changu kwa ajili ya upendo?, sitajali huyu mtoto uliyezaa nae
wala sitaumizwa na ujauzito wake uliombebea, ninakuomba Bite niache na mimi
nipate furaha japo kidogo tu katika siku zangu zilizobaki hapa ulimwenguni,
nisaidie niweze kurudisha upendo uliogeuka chuki kati ya familia yangu na Adam.
Bite uamuzi upo mikononi mwako,ukikataa utaniumiza sana na nina uhakika nitakufa
na pendo langu kwa Adam?
Kilio kilimzuia kuendelea
kuongea,lakini na yeye mgongoni mwake alilowanishwa kwa machozi ya Bite
yaliyokuwa yanatililika muda wote wakati Reshmail anaongea,kwa hali halisi
alimwonea huruma lakini pia kwa dhati kabisa aliwapenda Adam na Christian. Eve
na mumewe Benny walikuwa watazamaji,wenyewe hawakuwa na uwezo wa kutoa maamuzi
yoyote yale.
Christian alikuwa ametulia kwenye kochi, hali ya
utulivu aliyokuwa nayo ilipita siku zote.
?Adam tulipokutana
unapajua,yote tuliyofanya unayajua,upendo wangu kwako nadhani unautambua
pia??labda sikupangwa kuwa wako milele ndio maana aliyepangwa amejitokeza wakati
muafaka,asante kwa zawadi ya penzi lako,asante kwa mtoto na huu ujauzito hii ni
heshima kubwa kwako milele,neno gumu ninaloweza kulisema sasa ni kuwa kwa moyo
mmoja nakuruhusu uendelee na Reshmail,nayasema haya mbele ya mama yangu
Eveline?
Alizungumza Bite kisha akashindwa kujizuia kuangua
kilio kikuu kilichoamsha hisia za kila mtu pale ndani wote wakadondosha machozi
yao. Adam,Reshmail na Bite wote kwa pamoja wakakumbatiana huku machozi yao
yakitua juu ya Christian aliyekuwa katikati yao,ilikuwa ni picha ya kusisimua na
kuumiza sana.
******
*****
Kilikuwa kikao kikubwa cha familia yao
Reshmail,watu wote muhimu walikuwemo kasoro mama wa familia hiyo aliyesusia
kikao,mzee Manyama,Reshmail,Eve,Benny,Bite,na Paskalina walikamilisha kikao
hichi,Christian alikuwa bustanini akibembea.
Reshmail alikuwa
anatoa siri nzito nzito za kushangaza ambazo kwa namna kubwa kabisa zilitoa
taswira ya mambo yaliyokuwa yamefichika kwa muda mrefu,uhusiano wa kimapenzi
kati yake na mama yake mzazi ulimwacha kila mtu mdomo wazi,Reshmail aliomba
msamaha kwa hilo na alieleweka na kusamehewa. Ni katika usimuliaji wa upande wa
Bite kuhusu ngome ya vigogo iliyoleta fikra za mazingira ya kupotea kwa kadi
yake ya benki katika mazingira ya utata mkubwa,Benny hakuongea neno kwani yeye
alikuwa kama mgeni tu katika mkutano huo.
Mzee Manyama alikuwa
kimya akimtafakari mkewe kwa maovu aliyoifanyia familia yake,kwa mateso aliyompa
Adam na kwa uvunjifu wa amani aliouleta baina ya familia hizi mbili,kwa fedheha
aliyomletea na kumvunjia heshima yake bungeni na hata mtaani,akiwa mwingi wa
hasira alisimama bila kuaga na kuelekea chumbani,kwa hali aliyokuwa nayo
Reshmail aliamua kumfata kwa nyuma ili asije kufanya jambo baya huko
anapoenda,hasira yake ilipokelewa na na mwili wa mkewe ukiwa sakafuni,tayari
alikuwa maiti.
?ulistahili hukumu hii? bila kushtuka alisema
mzee Manyama huku akimpisha Reshmail aingie humo
ndani.
*** *******
*****
Mapema baada ya mazishi ya mama yake mzazi
Reshmail akiongozana na Adam katika gari ya baba yake,dereva akiwa Adam
walifunga safari ya kwenda Mwanza kwa wazazi wake
(Adam).
?utabaki ndani ya gari nitatangulia mimi najua watakuwa
wakali hao lakini wakikuona ndipo mzizi wa fitna utakapokuwa umekatwa? Reshmail
alimpa maelekezo Adam ambaye alikubali kwa ishara ya kutikisa
kichwa.
Gari ilipaki nje kidogo ya nyumba ya kina Adam,kama
walivyoelewana akashuka Reshmail akiwa amependeza sana,akaifunga gari kwa
kutumia rimoti aliyoshuka nayo na kwa mwendo wa kunyata akaanza kuusogelea
mlango akausukuma akaingia ndani,kupitia kwenye kioo Adm lishuhudi Reshmail
akitoweka machoni pake.
?umefata nini hapa we mchawi Adam
hajakutosha unamtaka na Rosemary ngoja sasa?.Rose!!!!?
Aliita
mama Adam,Reshmail akiwa anatabasamu kwani alijua ni muda mfupi wote watakuwa na
furaha kubwa.
Akiwa bado hajaanza kuongea alishuhudia mama Adam
akimfuata na kisu huku Rosemary akifika pale na mwiko mkubwa,wakati huu akili
yake ilifanya kazi haraka akaanza kukimbia lakini nguo yake ndefu ilimsaliti
baada ya kunasa kwenye geti la kutokea nje.
Kwa macho yake
mawili Adam alishuhudia Reshmail akiwa chini huku watu wawili wakimshambulia kwa
fujo,alijaribu kufungua mlango lakini ulikuwa umewekwa ?loki? sauti yake
haikuweza kusikika nje alipigapiga vioo vya gari lakini hakuna
aliyemsikia.
Alishuhudia damu nyingi sana ikiruka juu. Kwa
akili ya haraka haraka akakumbuka kushusha kioo akatokea
dirishani
?mamaaaaaaaaaaaaaaa!!!? Adam akaita kwa nguvu
palepale mama yake akageuka na kudondosha kisu alichokuwa
nacho,
?Adam mwanangu ni wewe!!!?
Alisema mama
Adam huku aimfuata Adam ambaye hakumjali bali alifika alipokuwa
Reshmail
?Reshmail,Reshmail?
? mama na dada
mmemuua mke wangu jamani mamaaaa!!? alilia Adam baada yakuona hajibiwi
kitu.
?A.d?.am!! ninaku?.fa mume wangu?.ninakufa kwa
furaha?..ni..meku..rudish?sha kwenu?naku?panda..sana?
Reshmail
aliongea kwa kujiumauma huku akivuja damu,raia wengine walikuwa katika harakati
za kutafuta msaada lakini msaada mkubwa uliopatikana ni wa polisi waliowatia
nguvuni mama Adam na mwanae Rosemary huku roho ya Reshmail ikimaliza muda wake
palepale Igoma jijini Mwanza.
kama usingekuwa ujasiri wa Adam
basi tukio lile lingegharimu maisha yake,tayari mama mkwe amepotea,na sasa
mpenzi wake Reshmail,mama na mdogo wake wakitupwa jela kwa kesi ya
mauaji.
**** **** ****
*****
?mapenzi yamenipotezea muda wangu nimekuwa
mfungwa miaka mitano, mapenzi yameivunja vunja familia yangu, mwanamke
niliyempenda ametoweka tayari tena mbele ya macho yangu,ni heri niisome hii
sheria vizuri zaidi ili ikiwezekana siku moja niwatetee ndugu zangu walioko
gerezani hao pekee ndio furaha yangu, kamwe siwezi kuhangaika tena na watoto wa
hapa chuoni hata siku moja sidhani kama wana maana sana kwangu nikithubutu tena
huenda yatakuwa makubwa zaidi ya awali.?
Alimaliza simulizi
yake
Adam.
?????MWISHO??????
0 comments:
Post a Comment