Search This Blog

Friday, November 18, 2022

USILIE (DON'T CRY) - 2

 






Simulizi : Usilie (Don't Cry)

Sehemu Ya Pili (2)





Mama Suzi alichukua usafiri uliomfikisha mpaka hospital ya Mount Meru,mbio mbio hakukumbuka hata kumlipa yule mwenye usafiri.

"Daktari naomba unifanyie vipimo haraka"aliongea mama Suzi huku akihema kwa kasi.

"Vipimo gani hivyo mbona una kasi hivyo?Aliuliza yule Daktari.

"Nifanyie vipimo vya HIV"Aliongea mama Suzi huku akitoa mkono ili Daktari atoe damu.

"Sawa subiri"aliongea dakitari.Baada ya kutoa ile damu aliiweka kwenye vipimo,majibu yalitoka baada ya dakika tano kwamba mama Suzi ni mwathirika.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Pole sana mama,kuna mtu unaishi naye basi ndo huyo aliyekuua"aliongea Daktari.

"What!!(nini) inamaana nimeathirika?aliuliza mama Suzi huku akimkumbuka Daudi.

"Ndio mama,kula vizuri,fanya mazoezi,pumzisha mwili wako utaishi kwa amani kama wengine harafu punguza mawazo"alisema kwa kirefu yule dakitari.Mama Suzi hakutaka kuendelea kukaa pale alitoka kichwa kikiwa chini kwa mawazo.

"Pesa zimetuua,hii dhambi hata mungu hawezi kuisamehe,nimemuua mwanangu kwa tamaa za pesa"aliongea mama Suzi huku akipanda kwenye usafiri kurejea nyumbani kwake.huko nyumbani kwa mama suzi,suzi alikuwa tayari kile kitanzi ameshakiweka kwenye shingo yake taratibu alikivuta kuona kama kimekaa vyema.

"Mungu naomba upokee roho yangu"alisema Suzi huku akianza kuhesabu.

"Moja"

"Mbili"

"Tat..."hakuimalizia,alisukuma kiti kwa miguu kisha kitanzi kikamkaza shingoni kwake,hazikupita hata dakika tano Suzi aliaga dunia.

Wakati huo mama yake ndo alikuwa anafika nyumbani,aliita Suzi lakini hakumuona ndipo alipokufungua mlango na kukuta umefungwa kwa ndani,alisukuma kwa nguvu mpaka ukafunguka.

"Mungu wangu!!!!alitastuka mama Suzi alipomuona mwanaye akitoka mapovu mdomoni.

"Ashaaga dunia tayari"alijisemea mama Suzi huku akipanda kwenye kitu kusikiliza mapigo ya moyo ya Suzi alikuta yamesimama.

"Siwezi kupiga kelele,namimi namfuata mda si mrefu"alijisemea mama Suzi huku akitoka na kuchukua bodaboda.

"Kaka nipeleke stend"aliongea mama Suzi huku akitoa noti ya elfu kumi na kumpa yule dereva bodaboda.

"Dada sasa sina chenji labda ngoja nikaombe"alisema yule kijana.

"Hapana twende tu"alisema mama Suzi. Baada ya kuingia kwenye barabara kuu kuna wazo lilimjia mama Suzi.

"Hapa hapa panatosha"alijisemea mama Suzi baada ya kuona basi kubwa likija maenhttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/eo yale kwa sipidi Kali.

"Mungu pokea roho yangu najua utanikutanisha na mwanangu"kwisha kujisemea hayo mama Suzi aliruka na kujitupa katikati ya barabara,lile basi lilikuwa na mwendo mkali lilimkanyanga na kumsaga saga kabisa,kila mtu alistaajabu kitendo kile.Haraka lililetwa gari la mchanga na kufukia eneo hilo,hakuna kilichobaki zaidi ya damu.

"Kweli watu washachoka na maisha"alijisemea kijana mmoja aliyeona tukio lile.Hata Askari police walishindwa kuelewa sababu ya mama suzi kufanya vile,yule kijana mwenye bodaboda alikamatwa kwa mahojiano lakini badae aliachiwa huru.

Glory alizidi kufanya biashara yake ile ya kuuza genge,miezi ya kujifungua ilikaribia.

"Ngoja niende mjini nikanunue vyombo kwa ajili ya mwanangu"alijisemea Glory huku akichukua pesa yote na kwenda mjini.

Issa kila siku hakuchoka kumfikiria Glory,maneno ya mama yake hayakuacha kujirudia kichwani mwake.

"Wiki ijayo niende nikamwambie ukweli"alijisemea Issa.

"Glory kodi ya nyumba imeisha,hivyo jitahidi ulipe ndani ya wiki hii"ilikuwa sauti ya mama mwenye nyumba akimwambia Glory.

"Haya mama usjali"alijibu Glory japo hakujua ile pesa ya haraka ataipata wapi,pesa alikuwa anaipata lakini alihakikisha ananua vifaa kwa ajili ya mwanaye.

Wiki moja iliisha,hapo mama mwenye nyumba alirudi tena.

"Glory usitake kunizungusha,leo ndo mwisho nataka hera yangu vinginevyo chukua mizigo yako uondoke"aliongea mama mwenye nyumba.Glory alichanganyikiwa hakujua pesa itatoka wapi.

"Lakini mama ngoja niunganishe ntakupa"aliongea Glory.

"Nimechoka ngonjera zako,ngoja nikuonyoshe"aliongea mwenye nyumba huku akiingia chumbani kwa Glory.Alianza kutoa nguo za Glory pamoja na vifaa vyote alivirusha nje.

"Chukua takataka zako uondoke humu"alifoka kwa hasira mama mwenye nyumba,Glory machozi yalianza kumtoka,alijitahidi kumuomba amvumilie lakini yule mama mwenye nyumba alikuwa mgumu.Ghafla tumbo la Glory likaanza kumuuma,alikaa chini huku akianza kuhisi uchungu wa kujifungua.

"Mamaaaa nisaiiiidiiee"aliongea Glory kwa shida.

"Acha mikwala mtoto wa kike nyanyuka hapa uondoke"bado mama mwenye nyumba alijua Glory anafanya masihara.

"Nakufaaaaa"alipiga kelele Glory hapo ndipo mama mwenye nyumba aligundua kuwa kweli Glory alitaka kijifungua baada ya kuona damu iliyokuwa inamtoka Glory.

"Siwezi kubeba mzigo usio wangu"alijisemea yule mama kisha akaondoka nyumbani kwake,hakutaka kumsaidia Glory aliyekuwa hawezi hata kutembea.Wapangaji wote waliishia kumtazama Glory aliyekuwa anapiga kelele.

"Leo ndo siku ya kumwambia ukweli,hivyo lazima niende na vizawadi vitakavyomfanya aniamini"alijisemea Issa huku akichagua nguo kwa ajili ya Glory. Alichukua usafiri uliomfikisha nyumbani pale,alishangaa kumuona Glory akiwa analia kwa sauti,alitupa ule mfuko uliokuwa na zawadi.

"Nini shida"aliuliza Issa huku akimuinua Glory.

"Tumbo linauma"alijibu Glory hakutaka kumwambia ukweli kwa kuogopa kuukosa msaada wa Issa.Issa aliita bajaji na kumchua Glory mpaka hospital ya Mount Meru.Glory alipokelewa na baadhi ya madaktari walionekana kuwa fasta sana.

"Habari yako kijana"alisalimia mwanaume mmoja aliyekuwa amevalia mavazi ya kidaktari.

"Salama kabisa"alijibu Issa.

"Hongera kijana umepata mtoto wa kiume,mtoto yuko vizuri labda mama yake ndo hajazinduka,ila tunaamini mda si mrefu atapataa nafuu"aliongea yule daktari.

"Waoooh,asanteni kwa msaada wenu"alijibu Issa kwa tabasamu la kutengeneza.Baada ya masaa matatu Glory alipata fahamu.

"Niitieni yule kijana niongee naye"alisema Glory.

"Kijana unaitwa"ilikuwa sauti ikimuita Issa aliyekuwa nje.Issa baada ya kuingia ndani ya wodi alimkuta Glory akiwa amelala.

"Asante sana kwa msaada wako bila wewe nilikuwa napoteza maisha"aliongea Glory.

"Usjali kawaida tu msaada mhimu,sijui unajisikia kula nini"aliongea Issa.

"Kwa sasa hapana,labda matunda"aliongea Glory.

"Basi ngoja nikakuletee"aliongea Issa huku akinyanyuka.

"Kwa dunia ya sasa hivi ni vijana wachache wenye moyo kama wa huyu mkaka,anaonekana ana upendo wa dhati"alijisemea Glory.Yaani yule mama mwenye nyumba sijui ana moyo gani ya kashindwa hata kunisaidia,msaada nimepewa na mtu mwingine ambaye nilikuwa simtegemei kabsa?sijui huyu mkaka nitamlipa nini"alijisemea Glory huku akimwangalia mwanaye.Issa alienda mpaka walipokuwa wanauza matunda alichagua mtunda mazuri,hakujali gharama yeye alijitoa kwa kila kitu.

"Ila nikimwambia ukweli ukakataa naamini nitaongeza swahabu kwa mungu,kama akikubali nataka niuvunje ule mwiko waliouweka vijana wa sasa kuwa hawaoi mwanamke aliyezaa kabla ya ndoa"alijisemea Issa.

"Aliyeleta hii mitandao ya kijamii ndo katuharibu kabisa yaani vijana wameshindwa hata kufanya kazi kutwa nzima kwenye hii mitandao na mada zao zile za kipuuzi"bado aliendelea kujisemea Issa wakati huo akiyasubiri yale matunda.

"Msaada wote huu ninao utoa lazima nifanye kitu"alijisemea Issa wakati anayapokea yale matunda.





Issa alirejea akiwa na matunda ya kutosha,bado Glory alijiuliza atamlipa nini huyu kijana aliyeonekana mkarimu mda wote.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Yataka moyo kulea mtoto ambaye si damu yangu"alijisemea Issa,lakini bado aliyakumbuka maneno ya mama yake.

"Ntahakikisha anapata malezi bora najua mungu ataniongezea baraka"alijisemea Issa.

"Sasa jioni mtaruhusiwa,hivyo kuna gharama kidogo hapa itabidi mzikamirishe"aliongea daktari mmoja akimwambia Issa aliyekuwa ameketi karibu Glory.

"Haina shida wewe tuambie ni shilingi ngapi inahitajika"alisema Issa.

"Sijui ntamlipa nini mkaka wawatu"alijisemea Glory baada ya kumuona Issa akilipa gharama zilizokuwa zinahitajika.

Baada ya kuruhusiwa walienda moja kwa moja mpaka alipokuwa anaishi Glory,Issa alilipa kodi iliyokuwa inahitajika pamoja na kuongezea miezi mingine sita.

Issa alihakikisha kila kitu kilichokuwa kinahitajika kinakuwepo.

"Mwenda pole hajikwai"alijisemea Issa kila alipokuwa anataka kumwambia Glory aliamini akienda haraka anaweza kuharibu.

Baada ya wiki moja Issa aliamua kuuvunja ukimya alienda kwanza mjini akanunua vyombo vya ndani vyote pamoja na nguo za mtoto.

"Mwanangu ntamuita jina la Bahati au unasemaje kaka"ilikuwa sauti ya Glory akimuuliza Issa.

"Sina neno juu ya hilo,jina zuri sana hilo"alisema Issa huku akiwaza jinsi ya kumwambia.

"Glory"aliita Issa.

"Abeee kaka"

"Kwanza kabisa nikuulize swali"

"Eee niulize"

"Sawa natambua wewe hapo ulipo tayari ushaitwa mama,je waweza kuniambia baba mwenye mtoto ninani?aliuliza Issa.

"Kwa ufupi ni hivi,Glory alifuta machozi kisha akaendelea.Mimi ni mtoto wa mzee mmoja anaitwa Gozbert,pia wazazi wangu wote hao walijitahidi kunilea kwenye maadili mema kabisa,hadi nahitimu shule ya msingi nilikuwa siwajui wanaume.Ndani ya kijiji chetu alikuja mwanaume mmoja aliyekuwa anaitwa Peter,Peter alikuwa mwanaume mpole sana.Siku moja naenda kisimani kuchota maji nilikutana naye,aliniangalia sana mpaka nikajihisi labda nina kasoro,siku hiyo ilipita.Ilikuwa siku ya jumapili siku hiyo nilikuwa nikitoka kanisani,nilikutana hapo aliita jina niligeuka kumwangalia kisha akaniita kwa mkono baada ya kumfikia akitoa noti ya elfu tano akanikabidhi mkononi,nilijaribu kuikataa lakini alilazimisha.

"Nenda katoe sadaka kanisani"aliniambia hivyo.

"Mimi natoka kanisani sasa hiyo sadaka nikaitoe kanisa gani?nilimuuliza.

"Hapana Glory hata jumapili ijayo utatoa pia"alinijibu,niliipokea ile pesa kisha tukaagana nikarudi nyumbani.Siku zilisogea,jumapili tena niliweza kuonana naye alifanya vile vile mpaka nikamzoea,siku moja aliniita na kuniambia yote yaliyokuwa moyoni mwake,nilitafakari huku nikimhaidi kumpa jibu wiki ijayo.Alikuwa mvumilivu sana.Hatimae nilimkabaria,nakumbuka siku nampa jibu alipiga magoti mbele yangu nakuhaidi kuwa hata nisaliti atakuwa nami kila sehemu,nilifurahi kuona upendo wake,mpaka ilifikia hatua akaramba damu yangu nakusema kuwa kila sehemu atakayokwenda nitakuwa kwenye damu yake,nilimuamini kupita kiasi,lakini siku alipogundua kuwa nina ujauzito uliokuwa wake asilimia mia alitoroka pale kijiji bila kuniaga,na sikujua alikoelekea.Namlaumu kwa kuniharibia maisha yangu.Wazazi wangu walipogendua kuwa nina ujauzito walinifukuza nyumbani na ndo maana mpaka sasa Niko hapa,hakika wanaume ni watu wabaya sana"alimaliza kusimulia Glory huku machozi yakimtoka.

"Pole sana Glory lakini usiseme kuwa wanaume wote ni waongo,wapo waaminifu pia japo ni ngumu kuwapata kwa hii dunia ya sasa"aliongea Issa.

"Ni kweli lakini toka siku ile wanaume nawachukia sana"aliongea Glory.

"Sasa mimi niko hapa nilikuwa naomba nikufute machozi hayo,pia sahau yaliyopita naomba tuanze maisha mapya"aliongea Issa,bila kusubiri jibu aliondoka eneo lile akimuacha Glory akiyatafakari yale maneno.Ilikuwa ni ngumu kwa Glory kuyakataa yale maneno,kila alipokuwa anakumbuka wema wote aliomfanyia Issa alishindwa kabisa kukataa.

"Ngoja akija lazima tupange maisha"alijisemea Glory ndani ya hizo siku alikuwa hajapata nguvu ya kwenda gengeni kwake.Yeye alikuwa anakaa ndani huduma zote alikuwa akizitoa Issa,Jioni ya siku ile Issa alikuja na zawadi mbali mbali kama ilivyokuwa kawaida yake,hata alipofika hakumuuliza tena Glory zile habari yeye alimpa zile zawadi kisha akaondoka.

"Mbona hana haraka kama vijana wa sasa,atakuwa na upendo wa dhati huyu"alijisemea Glory.

Baada ya wiki moja tayari Glory alikuwa anaishi na Issa,Glory furaha yake ilianza kurejea taratibu,maisha yao yalikuwa ya furaha kila siku waliishi kwa furaha,genge lao waliliendeleza huku kila mtu akiwa wa kutabasamu mda wote.Siku zilisogea huku Bahati mtoto wa akizidi kukua.Bado Issa hakufikiria sana kuhusu kulea mtoto ambaye si damu yake wengi walimsema lakini hakutaka kusikiliza la mtu.

"Yaani na unadhifu wako huo leo hii umeoa mwanamke aliyekimbiwa?hahaha.

"Sijawahi kufikiria kuoa mwanamke aliyezaa kabla ya ndoa"

"Binafsi siwezi hicho kitu,ila kaka jaribu kufuatiria sana mitandao ya kijamii huko kidogo utaweza kupata uelewa,mwanamke aliyekimbiwa sio wa kuoa kabisa"Yalikuwa maneno ya vijana wa kijiweni walipomuona Issa,kila kijana alisema lake.Issa aliishia kuwasikiliza tu hakutaka kuwajibu lolote.Hata alishindwa kutembea sehemu kutokana na kupata matusi kila sehemu aliyokuwa anapita,marafiki zake wote aliwatenga waliokuwa wanataka kumtenganisha na Glory.

"Maneno ya binadamu hayawezi kunifanya chochote,lazima nisimame mimi mwenyewe na Glory mpaka mwisho watu wanaosema hayo maneno ipo siku watanyamaza wenyewe"alijisemea Issa.

"Habari yako bwana Issa"alikuwa mwanaume mmoja akimsalimia Issa.

"Salama kwema huko"Issa alijibu.

Kabla hajajibu yule mwanaume alicheka kwanza.

"Huku kwema,nasikia unalea damu ya mtu mwingine,labda nikufungue akili,huyo mtoto unayemulea akija baba yake atamchukua na wewe utaishia kushika kichwa tu,na akija kumchukua huwezi kukataa wakati sio wako,bado najiuliza kijana mtanashati kama wewe umefikiria nini mpaka ukaoa mwanamke mwenye mimba?harafu mimba yenyewe sio yako hahahahaha kijana sijui umekwama wapi,ila bado nafasi unayo yakuweza kumuacha huyo mwanamke ukatafuta mabinti wengine mbona wanawake wengi sana hapa?,tafakari kijana"alisema yule mwanaume kisha akaondoka.Issa aliinamisha kichwa chini huku akitafakari yale maneno.

"Anayosema ni yakweli kabisa,lakini siwezi kumtenga Glory,wahenga walisema ukipenda boga penda na ua lake,mtasema mpaka mtachoka wenyewe"alijisemea Issa.

Fikiri rafiki yake Issa alizipata zile taarifa kuwa Issa tayari anaishi na Glory,toka mwanzo Fikiri alikuwa akimpenda Glory.alianza kumfuatiria Glory.

"Naam lazima nifanye mapinduzi"alijisemea Fikiri.





Upendo wa Glory na Issa ulizidi kukua,japo Issa aliambiwa maneno mengi na marafiki zake lakini hakuwa tayari kusikia la mtu,kila alichokuwa anaambiwa hakusita kumwambia Glory,naye Glory alizidi kumsihi Issa asisikie la mtu.Issa aliendelea kufanya kazi kwa bidii lengo amtunze Glory na mwanaye.

"Ngoja nipone ili nimpe penzi langu mwanaume huyu"alijisemea Glory,kila alipokuwa anamwangalia Issa alijikuta akiwaza mambo mengi sana.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Hapa ndo nimeamini baadhi ya maneno ya watu kuwa wanaume waaminifu wapo japo ni wachache"alijisemea Glory.Maisha yao yalisogea,ndani ya kipindi hicho hawakukutana kimwili,kila mtu alilala peke yake,Issa alikuwa analala chini,Glory alilala kitandani.

"Namsubiri apone ili nianze kurudisha gharama zangu"alijisemea Issa.Bado marafiki zake walizidi kumshauri aachane na Glory lakini yeye hakuwa tayari.

"Watazidi kusema lakini ndo hivyo nishampenda siwezi kumuacha"alijisemea Issa,kule mgodini kazi yake iliendelea.

"Yaani wewe mzee baba huna akili kabisa,hivi kweli umedhamilia kuishi na mwanamke aliyebebeshwa mimba?huoni aibu kijana mzuri kama wewe?yalikuwa maneno ya kijana mmoja akimwambia Issa.

"Nasema niacheni na maisha yangu,sitaki mtu yeyote anifatirie"alijibu Issa kwa hasira.

"Hapo umebugi mzee baba,ni sawa na kufuga nyoka atakung'ata mda wowote"bado yule kijana aliyekuwa anaitwa Yasin alizidi kumkebehi Issa.

"Yasin nasema tena niache,we fanya yako usisababisha tuharibiane siku"alisema Issa kwa upole.

"Hahahahaa,huna jipya wewe akili yako ndo itendelea kuwa chini"alisema kijana Yasin,maneno yale yalimkera Issa,ghafla lilitokea tafarani kati ya Issa na yule kijana Yasin,lakini fatarani hilo halikudumu baada ya wafanyakazi wengine kuingilia kati ugomvi ule.Issa alianza kujitenga na marafiki zake.Fikiri licha ya kuwa rafiki wa Issa lakini aliendelea kuwaza jinsi ya kumpata Glory.

"Siku hizi hakuna mwanamke mgumu,ngoja nisubiri mtoto wake akue"alijisemea Fikiri.Issa bado aliendelea kutoa huduma kama kawaida yake.Baada ya mwezi mmoja Glory alianza kutembea tembea,genge lake alilianza upya,bado Issa hakuchoka aliendelea kutoa matumizi.

"Sasa ni wakati wangu kwenda kumtembelea Glory,najua mda huu Issa yupo kazini"alijisemea Fikiri,alifunga safari mpaka nyumbani kwa Glory lakini hakumkuta,hakujua kuwa kwa wakati huo Glory alikuwa gengeni kwake.

"Ngoja nitarudi siku nyingine"alijisemea Fikiri,ila kabla hajatoka alifika Issa,Fikiri alionesha kustuka kwakuwa hawakuwa na uelewano mzuri kwa wakati ule.

"Karibu"alisema Issa.

"Ahaa asante,nilipita kukusalimia"alisema Fikiri.

"Sawa,karibu tena"alijibu Issa kisha akaingia ndani.Fikiri alisimama kwa dakika kadhaa akionekana kutafakari kitu.

"Naona Issa ameshaanza uadui na mimi,sasa namkaribisha kwenye uwanja wa vita"alijisemea Fikiri.Baada ya wiki moja Fikiri alirudi tena lakini bado alipakuta kimya,Glory aliendelea kumwomba mungu apone haraka lengo ampe nafasi Issa.Zikiwa zimesalia wiki tatu ili Glory afikishe miezi miwili,kwenye mgodi Issa aliokuwa anafanya kazi kulihitajika vijana kumi wa kusafiri kwenda nchini China,kulikuwa na wachina kwenye ule mgodi waliokuwa wanahitaji vijana kutoka nchini Tanzania ili kwenda kufanya kazi kwenye migodi iliyokuwa China,vijana waliokuwa wanahitajika Issa alikuwa miongoni,Issa hakutaka kupoteza ile nafasi.

"Ngoja nikatafute utajiri huko ili nije niishi vizuri na mpenzi wangu Glory"alijisemea Issa.Jioni ya siku ile alirudi nyumbani akiwa na furaha.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Mpenzi wangu leo nina habari njema kwako"aliongea Issa kwa furaha akimwambia Glory.

"Habari gani hiyo mme wangu"

"Tulia basi usiwe na papara,haya ni mambo mazuri hayataki haraka"

"Nambie basi"

"Nimepata nafasi ya kusafiri kwenda China"aliongea Issa,hapo Glory alishusha pumzi kidogo kisha akasema.

"Mme wangu huko China mnafuata nini?aliuliza Glory.kabla Issa hajajibu Glory alifikiria kitu.

"Nilijua tu kuwa watamshawishi mpaka akubali,ona sasa anatafuta sababu za kunikimbia"aliwaza Glory aliyeonekana kupoa ghafla.

"Glory acha mawazo mimi naenda China kikazi,usjali kuhusu hera ya kutumia nitakuwa nakutumia"alijibu Issa kwa sauti ya upole.

"Najua lakini kama unanikimbia bora uniambie nijue,najua watu wanakwambia mengi kuhusu mimi,kuliko unitafutie sababu bora uniweke wazi nijue"aliongea Glory.

"Glory hebu acha kufikiria mengine,mimi huko naenda kikazi,tambua naenda kutafuta pesa kwa ajili yetu ili tuishi maisha mazuri"aliongea Issa.moyo wa Glory bado ulikuwa mzito sana,hakukubali Issa aende mbali naye kutokana na kumzoea kwa mda waliokuwa wote.

"Sasa mimi hapa nitaishi vipi na huko China utakaa kwa mda gani?aliuliza Glory.

"Nadhani hawezi kupita miezi minne tutakuwa tumerudi,kikubwa mahitaji ya ndani yote yasikose,nitahakikisha kila baada ya wiki moja nakutumia pesa ya matumizi hivyo niruhusu nafanya haya kwa manufaa yetu"aliongea Issa kwa kirefu.

"Hapana mme wangu siko tayari uende mbali na mimi"aliongea Glory.

"Sawa nimekuelewa usijali tutakuwa wote"alijibu Issa,upendo aliokuwa nao Issa ulikuwa mkubwa hakutaka kumkwaza Glory hivyo alikubaliana naye,Glory alijawa na furaha,hapo ndipo alipodhibitisha kuwa kweli Issa ana upendo wa dhati.Usiku huo Glory hakupata usingizi kabisa aliwaza maisha yatakuwaje kama Issa akiondoka.

"Lakini kasema pesa atakuwa ananirushia kwanini nisimuruhusu?aliwaza Glory.

"Lakini ngoja nimtege kwa hizi siku mbili nione kama atabadirika"aliendelea kuwaza Glory.Siku mbili zilipita Issa hakugusia tena lile swala,aliendelea na kazi yake.Ilikuwa siku ya juma tano sikiwa zimebakia siku tatu kabla ya safari Glory alimuita Issa.

"Mme wangu najua unanipenda nami nakupenda,kwa moyo mmoja nimekuruhusu kabisa,pia na baraka zangu kama mke naziweka"aliongea Glory huku akitoa machozi.Issa alistuka hakutegemea Glory angeliweza kumruhusu.

"Kweli umekubari kabisa?aliuliza Issa akiwa haamini.

"Ndio ila najua huko utaenda kuwaona wenye ngozi nyeupe,hivyo kuwa makini sana mme wangu"aliongea Glory.

"Usjali kuhusu hilo nadhani upendo wangu utauona nitahakikisha naongea nawe kila siku"aliongea Issa huku akitoa simu kubwa aliyokuwa ameinunua na kuificha.

"Hii hapa simu tutakuwa tunawasiliana kwa njia ya kuonana"aliongea Issa huku akimkabidhi ile simu Glory aliyebaki kuduwaa.Taratibu alianza kumfundisha jinsi ya kuitumia,alipohakikisha kuwa Glory kaelewa kila kitu alimwambia kuwa.

"Mke wangu hii ni zawadi yako,hivyo hakikisha kila mda unakuwa hewani,weka bando la kutosha kwa ajili yangu"aliongea Issa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Kwa hilo usijali mme wangu nitahakikisha nafanya kama ulivyonambia"alisema Glory kwa sauti ya upole.

"Lakini mme wangu bado sijapona,sasa sijui itakuwaje"aliongea Glory.Alijua kuwa labda Issa atagusia swala la tendo la ndoa.

"Ondoa shaka,mimi najua kwahiyo nivumilie mpaka nirudi"aliongea Issa.

"Kweli huyu ananipenda"alijisemea Glory. Kwingineko Fikiri anapata taarifa kuwa Issa anasafiri kwenda China,moyoni alijawa na furaha.

"Hii ndo nafasi sasa"alijisemea Fikiri kwa furaha,alijua Issa akishaenda China hawezi kumkosa Glory.





Hatimae wiki waliyokuwa wamepewa wajiandae wale walikuwa wanasafiri kwenda China ilibaki siku moja,maandalizi yalipamba moto,Glory alihakikisha Issa andaa kila kitu.

"Jamani ntakumis mme wangu angalia usiniache mimi nakutegemea"yalikuwa maneno ya Glory akimwambia Issa kabla ya safari.Wale wachina walitoa pesa kwa watu waliokuwa na familia,Issa alipewa million moja,hiyo yote aliileta kisha akampa Glory aliyeruka kwa furaha na kumkumbatia Issa.

"Kweli unanipenda mme wangu"aliongea Glory kwa hisia.

"Usjali ntahakikisha unakuwa na furaha mda wote,hivyo basi jitahidi simu yako isiishiwe vocha,kila siku tutakuwa tunawasiliana,pia jitahidi mtoto apate huduma za kutosha,naamini kila kitu kitaenda saw a,kingine kuwa makini na wanaume nadhani unawajua walivyo waongo"bado Issa aliendelea kuongea yaliyokuwa moyoni mwake.

"Sawa nimekuelewa mme wangu kila kitu kitaenda vizuri"Glory aliongea mpaka mda huo hakuwa wamekutana kimwili,Glory alikuwa bado hajapona.

"Ngoja ntamtunzia penzi langu mpaka arudi"alijisemea Glory,kila alipomfikiria Issa alimuona mwanaume pekee kwenye hii dunia.

"Vijana wa sasa hakuna anayeweza kufanya hiki kitendo,huyu ndo mwanaume niliyeshushiwa kutoka kwa mungu,ona Peter kaniacha nikitaabika kanikimbia lakini Issa mpaka sasa yuko namimi"alijisemea Glory.

Siku ya Juma mosi kulipambazuka na hali ya hewa safi,vijana walikuwa tayari kwa safari,wale waliokuwa na wapenzi wao waliambatana nao mpaka kwenye uwanja wa ndege wa KIA(Kilimanjaro International Airport)uliokuwa Kilimanjaro bado Glory hakuamini kuwa ndo alikuwa akiagana Issa.

"Ngoja nimuage kisawa sawa najua huyu sio wa karudi leo wala kesho"alijisemea Glory huku akimkis Issa mdomoni.

"Mme wangu naomba utambue kuwa huku umemwacha mtu unayempenda,hivyo unikumbuke"aliongea Glory akiwa bado amemkumbatia Issa.Ndege aina ya Quarter airways ilitakiwa kutoka nchini Tanzania kwenda mpaka kwenye mji wa Guangzhou ulikuwa nchini China ilikuwa tayari,bado Issa alikuwa bado amekumbatiana na Glory.

"Mme wangu utarudi kweli?aliuliza Glory.

"Kwa uwezo wake mungu nitarudi,naomba zingatia yote niliyokwambia"aliongea Issa.

"Usjali mme wangu ntakuwa makini,safari njema basi mme wangu nakupenda"Glory alimalizia na busu shavuni kwa Issa.walipungiana mikono hadi Issa anaingia kwenye ndege alikuwa bado anamuangalia Glory.

"Safari sio kifo ntarudi"alijisemea Issa baada ya kumchungulia Glory kupitia kwenye madirisha ya ile ndege.Safari yao ilianza.

"Ngoja ninunue vocha kabisa ili Mme wangu asikute sipo hewani"alijisemea Glory huku akinunua vocha kutosha.Baada ya masaa kumi na mbili ndege ilitua kwenye mji wa China.

"Ngoja nione kama yuko hewani"alijisemea Issa huku akifungua mtandao wa WhatsApp.

"Yuko hewani mda wote huyu ngoja nimjulishe kuwa nimefika salama"alijisemea Issa huku akimpigia Glory,simu haikuita mda mrefu Glory alipokea.

"Nambie mme wangu"

"Asee vizuri ndo tumefika hapa"

"Oooh,pole na safari Mme wangu"

"Asante vipi Bahati hajambo"

"Huyu yupo tu naona kalala"

"Akiamuka mpe simu niongee naye"aliongea Issa kwa utani kidogo.

"Usjali natamani nije nikukande maana najua umechoka sana"aliongea Glory.

"Tena uwahi maana sio kwa kuchoka huku"

"Nakuja jamani Mme wangu"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Nikutakie usiku mwema naona tumeitwa hapa hivyo msalimie Bahati,ntakupigia kesho"

"Nawe pia ulale salama"baada ya maongezi yale Issa alikata simu.Fikiri baada ya kudhibitisha kuwa Issa kaenda nchini China alifurahi moyoni.

"Hapa haruki hawa wanawake wanarubunika kwa kitu kidogo tu"alijisemea Fikiri huku akiwaza jinsi ya kumwingia Glory.Kila siku Glory alijitahidi kufanya mawasiliano na Issa,ulikuwa upendo mkubwa sana japo kuwa Issa alikuwa mbali.

"Mme wangu,natamani angalau siku moja nami unipeleke huko nikaangaze macho"aliongea Glory kwa utani.

Siku zilisogea,genge alilokuwa analiuza Glory lilikuwa kwa kasi baada ya kuongeza vitu.Fikiri naye hakutaka papara.Ilikuwa siku ya jumamosi siku hiyo Glory akiwa gengeni kwake walikuja wasichana watatu,walikuja kununua ndizi,kila msichana alionekana bize huku macho yake yakiangalia simu ya mkononi.

"Jamani karibuni"aliwakaribisha Glory.

"Asante,ndizi shilingi ngapi?aliuliza msichana mmoja.

"Ndizi hizi miambili hamsini,hizi huku miambili"aliwajibu Glory.

"Ok tunaomba tatu za mia mbili mia mbili"Glory aliwafungia ndizi lakini bado walionekana kuwa bize ndipo Glory aliwauliza.

"Mbona mmeinama hivyo,kwani mnaangalia nini kwenye simu zenu?aliuliza Glory.

"Asee tupo tunasoma simulizi kwenye makundi ya facebook,asee huyu mkaka sijui anayeitwa MKAPA JR ana story nzuri sana za kugusia maisha harisi tunayoishi"aliongea msichana mmoja aliyekuwa anaitwa Lea.

"Huwa napenda sana kuzisikiliza kwenye radio,vipi namimi mnaweza kuniunganisha au mpaka mnalipia?aliuliza Glory aliyekuwa hajui lolote kuhusu simu.

"Hapana ni bure kabisa,kwenye kikundi wapo waandishi wengi na wote hao stori zao nzuri sana"alisema Lea huku akipokea simu ya Glory.

"Kumbe una simu nzuri kiasi hiki harafu bado huzipati stori kama hizi?asee pole sana"alisema Lea.

"Mimi najua lolote basi?labda najua kuwasiliana na Mme wangu tu"alijibu Glory. Baada ya kuunganishwa Facebook alipewa maelezo na namna ya kuitumia mpaka apate makundi ya stori,pia walimuunga na mitandao mingine ya kijamii,hakika Glory alijiona wa mwisho kwenye hii dunia.

"Kumbe duniani kuna vitu vizuri kama hivi?sijui nilikuwa wapi siku zote hizi"alijisemea Glory baada ya kuona vitu mbali mbali kwenye mitandao ya kijamii,siku hiyo alishinda akisoma stori,nyingi zilimgusa na ziligusa maisha yake na kuzidi kuipenda zaidi hiyo mitandao hasa Facebook.Ilifikia hatua mpaka alishindwa kumnyonyesha mtoto wake,mda mwingi alikuwa bize na simu.Fikiri aliamua kwenda alipokuwa anaishi Glory,lakini bado hakumkuta ndipo alipoulizia kwa majilani wa karibu.

"Yuko pale kwenye lile genge ndo kwake"ilikuwa sauti ya mtoto mdogo akimuelekeza kwa mkono Fikiri aliyekuwa makini kusikiliza,baada ya kuelekezwa alienda moja kwa moja kwa moja,lakini kabla hajafika mara ghafla simu yake ilipata kuita,aliitoa mfukoni na kuangalia jina la mpigaji,alipomaliza kuongea aliirudisha mfukoni kwa wakati huo alikuwa gengeni penyewe.

"Habari yako"alisalimia Fikiri.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Salama,karibu"aliitikia Glory huku macho yake yakiwa makini kutazama Simulizi aliyokuwa anaisoma.









ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog