Simulizi : Mkuki Kwa Nguruwe
Sehemu Ya Tatu (3)
‘Yaani tena kwa karaha, maana
walijua nipo hapo nje, na mvua inanyesha..lakini kila kilichokuwa kikifanyika
huko ndani, nilikuwa nakisikia, kwa dharau..ili kunionyesha kuwa mimi sina
maana..’nililowana, maana kibaraza kilikuwa hakina sehemu nzuri ya kujificha, na
walipomaliza starehe zako, wakatoka wakaenda bafuni kuoga, wakavalia,
wakaondoka, sijui walipokwenda, nikabakia hapo hapo..nje,sijui niende
wapi…nalia…nifanyeje sasa, na kuja mjini nilipanga nije kupambana na hao
wanawake wanaoniibia.
‘Bahati nzuri jirani yao, akanikaribisha
ndani, akanipa nguo nikabadili, akanipikia tukala, japokuwa chakula hakikushuka
vyema, na huyo huyo jirani yake ndiye aliyenisaidia nauli, kesho yake asubuhi
nikaondoka nikarudi nilikotoka,...hebu ona huo unyama, hata nauli
hakunipa...nimesaidiwa na majirani ambao waliniambia mume wangu kila siku
anakuja ni mke mwingine...na sijui kwa vipi hakupata ukimwi...’akasema huku
akikunja uso.
‘Niliporudi kijijini, nikamsimulia mama yangu
hayo nailiyoyaona, akasema, hayo ndio yo niliyoyataka, waliniambia sikusikia, ni
kweli , walinisema sana, kipindi hicho, nilipoanza mahusiano na marehemu, wazazi
wangu walichapa sana, lakini sikuwasikia, na hayo yaliyokuja kutokea nilikiri
kuwa ilikuwa ni dhambi zangu ndizo ziliandama ngoja nipatilizwe, ...nilitubu
sana, nililia sana, lakini itasaidia nini…’akasema.
‘Niliishi
kijijini kwa shida, hadi nilipokutana na huyo mume
wako....’akasema
‘Na mume wangu..!! ?’ nikauliza nikianza kuwa
na hamasa zaidi kwani huko ndipo nilipataka kufahamu ukweli zaidi wa mume
wangu.
‘Ndio na …mume
wako,…’akasema
‘Mkawa….eeh..’nikasema
hivyo
‘Hahaha…mume wako kwangu namuona kama mdogo wangu, lakini
alinionea huruma sana, kwani alikuwa akiniona ninavyoteseka, yeye alikuwa
akihangaika na shughuli zake anapita kwetu ananiachia chochote,, huwa alikuwa
akiniita shemeji....basi ndivyo tulivyozoeana. Hakuwahi kupita hapo bila
kuniacha kitu.
‘Kuna kipindi niliumwa sana...karibu ya kufa,
hatukuwa na hata senti nyumbani, sina pesa ya kununua dawa, kwani nikwenda
hospitalini na kuandikiwa dawa za kununua, ...hatuna pesa, na tatizo hilo
lilikuwa kubwa, hadi nikaambiwa nikafanyiwe upasuaji,
..nipelekwe mjini, sina pesa, wazazi hawana pesa , na mume wangu alipoambiwa hakujali..alitaka nife tu...’akatulia.‘Namshukuru sana mume wako, nafahamu kipindi hicho, alikuwa hajaku-oa...kama sikosei, akauza mbuzi wake, akapata pesa, na kuzileta nyumbani, hatukuamini, akasema amekuja kunisaidia ili nikatibiwe...na kweli nikapelekwa mjini nikafanyiwa upasuaji, nikatibiwa nikapona..sitamsahau mume wako...’akasema.‘Je alifanya hivyo kwa sababu gani hasa?’ nikamuuliza‘Yeye, alisema alifanya hivyo, kwa vile mume wangu ni rafiki yake ,mume wangu alikuwa akimfundisha fundisha ufundi wa magari, ..udereva,..unafahamu mambo ya kijijini, basi wakaivana, sijui zaidi ya hapo ilitokeaje wakaivana kiasi hicho, kwahiyo yeye alinitambua kama shemeji , mke wa rafiki yake, akanijali kihivyo.....na ujirani mwema tu...’akasema.‘Kwahiyo kwetu sisi , kama familia, tunamthamini sana mume wako, ni mtu mwema sana, mume wako ana roho nzuri , uliza huko kijijini, alipenda kuwasaidia sana watu,..sio mimi tu, ..yeye alikuwa na tabia yake ya kupenda kusaidia watu, .. japokuwa familia yao ina tabia ambayo wengi wanaiona sio nzuri, baba yale ni mlevi kupindukia, na mama yake akawa hivyo hivyo....basi ni familia ya shida, lakini yeye akawa anajibidisha na maisha yake, kuhangaika kivyake..hadi hapo mlipokutana naye...’akasema.‘Mhh, kweli umenifungua masikio, hayo yaliyokukuta ni makubwa, mimi niliona nipo kwenye mitihani, lakini kumbe wapo wengine wanakutana na mitihani zaidi ya unavyowazia, wewe ya kwako ilikuwa zaidi, sasa ikawaje, maana muda umekwenda, kuna mambo ulitaka kuongea na mimi na mimi nataka kujua…eeh..?’ nikamuuliza. Na sote tukageuka kuangalia kule mlango mwa nyumba yangu, kulikuwa na jambo…‘Sasa ikawaje…oh, namuona mume wako anatoka, nilionana naye hapo nje wakati anaingia, tukaongea kidogo…ana haraka zake…?’ akasema,na ni wakati huo mume wangu alikuwa akitoka na wakili wake, na aligeuka akatuona ni kama vile ndio anatuona kwa mara ya kwanza, ikabidi sasa aje pale tulipokaa…......NB: Nimejitolea leo kuleta sehemu hii…Ni kisa mkasa, lakini kwa huyu mama kuna mengi ya kujifunza, tutakuja kuona ilikuwaje kati ya mama huyu na mume wake, na kwanini alifika huku mjini, je inaweza ikawa njia ya kumfanya mdada abadili nia yake na kumsamehe mume wake..tuzidi kuwemo..?WAZO LA LEO: Maisha yana mitihani yake, ukiona kwako ni kugumu, ujue kuwa kuna wenzako kwao ni kugumu mara mbili zaidi yako, ukipatwa na mitihani, ujue kuna wengine mitihani hiyo ni mazoezi tu ya nyumbani(homework), kwahiyo ili uone uhalisia waangalie hawa waliopo chini yako, ambao wanataabika zaidi yako.Na ili uvuke huo mtihani waangalia walipo juu yako, jifunze kutoka kwao,uwe na wivu wa maendeleo...usikate tamaa, pambana, lakini kwenye njia iliyo sahihi, ukijua kuwa wewe sio wa kwanza kupata mitihani kama hiyo, wapo waliopata mitihani hiyo na wakaishinda, kwanini wewe usiweze...kumbuka jambo moja, kila kitu kila jambo lina ugumu wake, lakini baada ya dhiki, mara nyingi huwa ni faraja, hasa kwa wale wenye kuvumilia na kujibidisha kwenye shughuli zao.., huku wakimtegemea mola wao.Mhh, kweli umenifungua masikio, hayo yaliyokukuta ni makubwa, mimi niliona nipo kwenye mitihani, lakini wewe ilikuwa zaidi, sasa ikawaje?’ nikamuuliza.nikitaka kufahamu mengi kuhusu maisha ya huyo mama, ambaye nilimuita dada...Aliendelea kunisimulia maisha yake na mume wake ambaye sasa ni marehemu...*******`Mimi sikukata tamaa na mume wangu, niliendelea kumsubiria, nilimuomba mungu, kuwa ipo siku,atajirudi, na kunikumbuka , lakini haikiutokea, mimi nikaendele kuishi kijijini, nikijitegemea, na hata ikafikia wazee wao wenyewe wakaamua kuliingilia kati. Ikabidi mume wangu aitwe kwenye kikao cha wazee, na yeye mbele yako akaja kukubalia kuwa kakosea, na akakubali kuwa mimi ni mke wake wa halali, na yeye anawajibika kwa hilo.‘Sasa kwanini unamfanyia hivyo mwenzako?’ akaulizwa‘Nilipitiwa tu na mihangaiko ya kutafuta riziki’akasema.‘Hizo riziki unamtafutia nani sasa?’ akaulizwa‘Mimi na familia yangu..’akasema‘Mbona hukimbuki familia yako, au familia yako ni akina nani?’akaulizwa‘Ni mke na watoto wangu, lakini pesa haitoshi...mambo ni mengi sana huko mjini, kuna kodi za nyumba kuna gharaam nyingi tu, lakini najitahidi au sio ...’akajitetea‘Sasa unasemaje, ?’ wakamuuliza‘Wazee wangu, mimi najitahidi na kiukweli nimeanza kujiweka sawa, kwani nina ndoto ya kusoma sana, na kuwa wakili…kwahiyo mambo yatakuwa sawa na nina uhakika familia yangu nitaihudumia vyema…’akasemaKiukweli hata mimi kwenye kikao hicho niliona kama mume wangu kabadilika, sikusikia kauli zake zile..sijui kwa vile ni wazee, au ..lakini moyoni nikaamini kuwa huenda kweli mume wangu kabadilikaIkafikia muda akaniomba msamaha mbele ya wazazi kuwa kakosa na hatarudia tena, uone wanaume walivyo…, lakini aliporudi mjini hali ikawa ile ile...hata wazee hawakuamini kuwa ndio Yule mtu aliyekiri na kuomba msamaha..basi ikabidi tukachoka, tukaamua kumuacha aendelee na maisha yake, na mimi nikajibadili sasa ..maana mitihani ni shule…ndio mwanzo wa kuanza kujiajiri...Bahati nzuri, walikuja wawekezaji wanasaidi wanawake waliokatiza masomo kwa uja uzito na mimi nikajiandikisha, ufadhili ukanisaidia nikaanza kusoma, masomo ya watu wazima sasa, japokuwa mimi bado nilikuwa sio mkubwa kihivyo,.. nikafanya mtihani wa darasa la saba nikafaulu kwendaNikaanza elimu ya sekondari ya miaka miwili…nilikuwa na akili darasani kwahiyo niliweza kufaulu vyema…hadi nikafika elimu ya juu,...hutaamini, nilifaulu kwa njia hiyo nikasomea…diploma, nikaishia hapo...nikaanza mapambano ya kujiajiri…nilikuwa nasoma huku nafanya vibiashara…nalea..hivyo hivyo..‘Ukiniona hivi huwezi amini, lakini nia na lengo langu ilikuwa kufika chuo kikuu, watu hawajui, hata huyo mume wangu alikuwa hajui..hamna aliyemwambia,maana haulizi hana habari na mimi, ..ni kama hana mke, ..mimi niliamua na nikafanikiwa, lakini sikuwahi kumkataa kuwa yeye sio mume wangu.‘Alishangaa siku moja nipo Dar, nahutubia akina mama mpango wa kuwezeshana akina mama, waliokatisha masomo kwa ajili ya uja uzito, sijui ilitokeaje na yeye siku hiyo alikuwepo kwenye huo mkutano, nilipomaliza kuhutubia akanifuata na kuniuliza‘Wewe mwanamke, umewezaje kufikia hatua hiyo, na kwanini unasimulia maisha yangu mimi na wewe…, ina maana mimi nilikutesa kiasi hicho…kwani nilikulazimisha, unakumbuka, nilikuambia sikutaka kukuoa, ni wazazi wako walinilazimisha, unakumbuka, sasa unakuja kunilaumu mbele ya vikao kama hivi, ujinga mtupu…akanilaumu sana…?’ akaniuliza na mimi nikamjibu‘Ni kutokana na hayo uliyonitendea, hata hivyo mimi nashukuru sana...’nikamwambia, na ghafla huyo …akaniomba msamaha, mimi nikamwambia mimi sina kinyongo na yeye na bado mimi ni mke wake, lakini siwezi kwenda kwake, maana bado nipo kwenye hiyo adhabu aliyonipa...Kuna kipindi aliniambia amenipa adhabu, ya yeye kulazimisha kunio mimi wakati alikuwa hanipendi, ...na ndio maana nikamwambia hivyo, kuwa mimi bado nipo kwenye adhabu yake...nikaondoka kesho yake, kiukweli mimi sikufika nyumbani kwake, japokuwa aliniomba nifanye hivyo,.. nilimwambia naogopa yasije yakanikuta yale yaliyonikuta kipindi cha nyuma.Basi kuanzia siku hiyo, sasa ikawa yeye anakuja huko nyumbani kijijini, na akafika kwa wazee wangu, akawaomba msamaha,…na mimi pia, na mimi niliendelea kumwambia kuwa mimi ni mke wake, asiwe na wasiwasi, sina kinyongo na yeye, lakini bado nipo kwenye adhabu yake...‘Ina maana alipokuwa akifika, alikuwa anakuja kwako, au kwao…kwani wewe ulikuwa unaishi wapi hadi muda huo , ?’ nikamuuliza‘Alikuwa anakuja kwao, mimi nilikuwa naishi na babu na bibi, ...kwa wazazi wake, au nyumbani kwao, sikuweza kuishi nao, kulikuwa na manyanyaso, ikabidi niwe naishi na wazee wangu hao, na walikuwa wakinihitajia sana…ilikubalika iwe hivyuo, sio kwa kulazimisha…’akasema‘Sasa alipokuwa kija kama hivyo, mimi sikumkubalia kuja kulala kwangu, nikimwanbia bado nipo kwenye adhabu aliyonipa...hali hiyo ilimtesa sana,...akahangaika, sijui kwanini aliamua kufanya hivyo...kiukweli mimi sikugeuka nyuma,...’akasema.‘Vipi mtoto…alikuwa akiishi wapi..?’ nikamuuliza‘Mtoto naye akawa anakuwa akawa an juhudi sana darasani…akafaulu hadi sekondari, na hatukutaka msaada wa baba yake sio kwamba tulimkataza hivyo, hapana ni yeye mwenyewe tu....ila aliendelea kumtambua kama baba yake, nilimwambia huyo ni baba yako,asije hata siku moja kumkana, au kumsema lolote baya, na alinitii, ila hatukutaka msaada wake, akiwa na shida ni mimi nawajibika.Sasa baada ya kuniona huko Dar, akawa sasa anatuma pesa za matumizi, tulipokea na kiukweli sikupendelea kuzitumia, hata hivyo, kwa vile ni wajibu wake, ikabidi tuwe tunazitumia tu, ila sikuwa na ile hali ya kumtegemea yeye kabisa.....’‘Ikatokea wazazi wakaingilia kati, hadi tukasuluhishwa...nikaona haina haja, na kwa vile mimi nampenda mume wangu, nikakubali yaishe, tukaanza maisha mapya,..lakini kwa masharti kuwa mimi nitaendelea kuishi huko huko kijijini, yeye aendelee kuishi mjini na wanawake zake, siku akijiskia anakuja huko kijijini namkaribisha kama mume wangu, anakaa siku mbili anaondoka zake, nimezoea, sina shida naye, mpaka umauti ulipomkuta.‘Oh…kweli wewe.., una moyo kweli…’nikasema‘Nilikuja kuajiriwa na kampuni isiyo ya kiserikali kwa ajili ya kusaidia akina mama waliokatiza masomo kwa ajili ya uja uzito, kwahiyo sikuwa na shida, ya kumtegemea mume tena,...sikuwa namfuatilia maisha yake, na mengi nilikuwa naambiwa na watu tu...mtoto wangu ndiye aliyejitahidi kumfuatilia na kujaribu kumkanya, lakini hakumsikiliza mtu, alidai kuwa hayo ndio maisha yake, mtu asimuingilie.‘Sasa kwanini nije kuchukua urithi wake, .kwanini nije, kuchukua mambo yake, ambayo hatujui yametoka wapi...sisi tuliamua kila kitu chake tukiuze, tulipe watu, na kama hakuna watu tutatoa sadaka…’akasema‘Mhh…lakini..’nikataka kusema neno lakini hakunipa nafasi akaendelea kuongea.‘Na katika huu msiba ndio tukaja kugundua kuwa kumbe ana watoto wengi wa nje, ana madeni mengi ya watu,...na hawo waliofanyiwa ubaya, ni wengi, japokuwa awali hawakutaka kujitokeza…ndio tukajaribu kuwalipa lipa na kuwaomba msamaha, na hili zoezi ndilo tunaendelea nalo mpaka sasa nia ni kumsaidia marehemu,....’akasema.‘Kwahiyo ndio maana mlikuwa mnanitafuta mimi, lakini mimi simdai, ila nasikia anamdai mume wangu, mimi sijui..?’ nikamuuliza‘Ni pamoja na hayo, ila cha muhimu kwa hivi sasa ni huo mkataba, madeni hayana nguvu sana…sasa sisi tunachotaka kwako ni kujua ukweli, na kama tulivyohisi, tumegundua kuwa ni yale yale ...kwahiyo, tunaomba, mtuambie tufanye nini, kwani sisi hatutaki kitu chochote kutoka kwake, ila tunachotaka ni kuyaweka mambo yawe sawa, kusiwe na kudaiana , na tunafanya haya kwa vile mtoto wangu ndiye kapewa hilo jukumu....’akasema‘Je unafahamu lolote kuwa mkataba huo mlio nao…umetokana na kugushi mkataba mwingine uliokuwa halali?’ nikamuuliza‘Nimesikia hilo kwa wakili wetu, na yeye alisikia kutoka kwa wakili wako,sasa ukweli upo wapi, ndio tukaona kuna umuhimu wa kuonana na wewe ...’akasema.‘Je mna amini hilo, kuwa mume wenu alikuwa na hisa kwetu?’ nikamuuliza‘Sisi hatuna haja ya kupekenyua ukweli, ukweli mnaufahamu nyie..sisi hatuna haja na hizo hisa, hata kama kulikuwa na ukweli, hatuna haja nao....tulishaanza maisha yetu, hatukuwa tunamtegemea yeye, kwanini sasa kafariki tuanze kugombea mali yake, kama walivyokuja watoto wake wa nje kuja kugombea mali yake....sisi tuliwaambia kuwa kama wanahitaji mali ya marehemu, basi wakubali na madeni yake, na alipopigwa mahesabu ikaonekana madeni na mengi, kuliko, wenyewe wakakimbia.‘Hayo ni ya mume wako, sasa tuongee kuhusu mume wangu,...kwanini mnamtetea yeye mnajuaje kuwa yeye sio mkosaji kama alivyokuwa mume wako ?’ nikamuuliza‘Sisi hatumtetei, ila tunatimiza wajibu wetu, yeye kama wengine, ni miongoni mwa watu walioathirika kutokana na tabia ya mume wangu....anahitajia kupata haki yake,...alihadaiwa, na akajikuta anatoa hisa kwa mume wangu, tunahisi hivyo, …japokuwa bado hatujaupata ukweli, ukipataikana ukweli tutafanya inavyostahiki...’akasema‘Kwa vipi mtaweza kuupata huo ukweli?’ nikamuuliza‘Kutokana na mikataba,.wakili wetu katushauri hivyo..hatuna jinsi nyingine, sisi , na mtoto wangu,..tunajitoa kwenye huo mkataba, na nio bora uvunjwe kabisa, lakini kama miktaba hilo ilitengezwa kisheria, basi sheria ifanye kazi yake kuivunja, au sio, ndio utaratibu muafaka, tusaidiane kwa hilo…’akasema‘Ndio lakini huo mkataba mliona nao, sio sahihi, ni wa kugushi…’nikasema‘Ndio maana mwanasheria wetu anaufanyia kazi, ila tunahitajia msaada wenu, ..mume wako kasema wewe unaweza ukawa ni kikwazo, ndio maana tokea awali tumekuwa tuklitaka kuonana na wewe..hukushangaa nilivyokuuliza awali, je mna matatizo gani wewe na mume wako…nashukuru kuwa tumekuona na iliyobakia ni wewe kushirikiana na sisi, tulimalize hili jambo..’akasema.‘Nakushukuru sana kwa kuwa mkweli kwangu na kunielezea sehemu ya maisha yako, na mimi sina kinyongo na nyie tena, ...ama kuhusu maswala ya mume wangu, hayo hayawahusu, nawaombeni msijaribu kuyaingilia,...kama mnataka kumsaidia kwa hilo, nyie mshaurini yeye aulete ule mkataba wetu wa awali, ambao tuliandikishana mimi na yeye,kuhusu mambo yote,yeye akaghilibiwa na mume wako akakubali ubadilishwe, ...hilo tu, ...’nikasema.‘Sisi hatuujui kama kuna mkataba mwingine tumaliskia hili hivi karibuni kutoka kwa hao mawakili, .sasa..hata sijui huo mktaba mwingine upo wapi..na je uhalali wa hiyo mikataba itakuwaje…’akasema huyo mama‘Hata mimi siujui huo mkataba wenu mnao-uongelea, na wala siutambui, maana ulitengenezwa kimbinu kutokana na kuvunja mkataba watu wa awali bila mimi kujua, umegishiwa na sahihi na kila kitu, sijui walifanyaje...kwahiyo huo mkataba mlio nao ni batili,..’nikasema.‘Kwahiyo nyie au wewe unataka sisi tufanye nini?’ akaniuliza.‘Kwa hivi sasa niseme tu, kuwa nyie mumeshatimiza wajibu wenu, ..nawashukuru sana kwa hilo, sisi au mimi sina kinyongo na nyie na kwa vile mume wako, ...hayupo tena hapa duniani, huwezi kumuhukumu maiti au sio…, anayehukumiwa kwa hivi sasa ni swahiba wake..naye ni ni mume wangu...nafikiri umenielewa hapo….’nikasema.‘Mdogo wangu, mimi nataka kukupa ushauri tu, ni ushauri wa bure, kama utauona una maana haya, kama ndio wa kupitwa na wakati haya, ukitaka kuufuata ufuate kama hutaki basi, ni hivi, hakuna mkataba wa ndoa zaidi ya ndoa yenyewe, mkataba wa ndoa ni kiapo chenu cha ndoa, pale mliposimama wewe na mume wako, ukakubali kuolewa na yeye na yeye kukubali kukuoa,..au sio’akatulia kidogo huku akionyeshea kwa mikono.‘Hilo ni sawa, lakini matendo ya wanandoa yanaweza kuuvunja huo mkataba…amini hilo, …kuna matendo yanaharibu kabisa ndoa…lakini watu hatufuatilii..je ni nani wa kulaumiwa hapo…’nikasema‘Ni sawa, lakini kusameheana kupo, au sio…nakubali hilo..lakini ninachotaka kusema kuhusu ndoa,…msije kuvunja ndoa kwa sababu ya vitu vingine kama mali..na watoto..’akasema‘Watoto kwa vipi…?’ nikamuuliza‘Ndugu yangu tusiongee sana, huo ndio ushauri wangu, unajua kwenye hii kazi nimejifunza mengi, nakubali ukweli, kuwa wanandoa, tupo kwenye mitihani mikubwa sana, hasa mmoja wapo anapokuwa sio mkweli,.....’akasema‘Sasa hapo utafanya nini..hebu niambie kama mmoja wapo anavunja mkataba, na hakuna kitu mlichoandikiana naye….’nikasema‘Nikuambie ukweli, sisi wanadamu , nikiwa na maana sisi wanandoa, hata kama tutajaribu kuwekeana mikataba mingine, tunayoona sisi ni kisheria zaidi, tukajenga ukuta wa kulindana, tukaweka na walinzi wa kutulinda, ndani na nje, ...tukafanya kila iwezekanavyo, ili mmoja asivunje miiko ya ndoa, …hatatuweza..’akasema‘Kwanini..?’ nikamuuliza‘Mikataba halisi ya ndoa ipo kwetu sisi wenyewe…kama mioyo yetu, kama sisi wenyewe hatukujibidisha hivyo, tukakubali mioyoni mwetu kuwa ndoa ni kati ya muma na mke, kuwa ina masharti yake, ambayo kila mmoja anatakiwa kuyatimiza kidhahiri na kificho,...kama hatutajua hayo sisi wenyewe, tukayakubali sisi wenyewe ndani ya nafsi zetu, haiwezi kusadia kitu,...kamwe, hatutaweza kufanikiwa....’akasema.‘Kwahiyo unataka mimi nifanye nini…?’ nikamuuliza‘Mimi nakushauri kama mkubwa kwako, maana kiukweli wewe ni mdogo wangu mbali tu, nimkuzidi kiumri, na huenda hata kiuzoefu, mimi nimepitia kwenye mitihani mingi migumu, niliyokusimulia hapa ni cha mtoto, nikushauri jambo, hakuna haja ya kuhangaika sana kwa hili…, cha muhimu kwa sasa ni kumsameheana tu…’akasema‘Kusamehe sio tatizo tatizo unasamehe nini sasa…’nikasema‘Sio lazima kila la kusamehe liwe wazi kwako mengine ni bira uyasamehe bila kuyafahamu maana ukiyafahamu huenda ukashindwa kuyasamehe, yaache yabakia na muhusika mwenyewe atajuana na mola wake, nina uhakika mumeo kakukosea, hata kama hajakutamkia, maana madume, wanaweza kujifanya hawajakosea, lakini kiukweli kwenye nafsi zao, wanajua kabisa wamekosea...na wengi hujijutia..’akatulia kidogo.‘Ni rahisi kumsema mwenzako au sio…’nikasema‘Unajua nikuambie jambo sisi wanawake, kwa waume zetu ni kama mama zao, tunabeba yote kama mzazi anavyobeba makosa ya mtoto wake, ..mtoto, anaweza kukosea sana, lakini mwisho wake kama mzazi, unamsamehe, unaona mtoto ni mtoto tu…’akasema‘Lakini mume sio mtoto, ana akili zake na pia kapewa wadhiaf wa kiongozi wa familia, au sio…’nikasema‘Ndio…lakini kuna mambo sisi tumetukuzwa nayo,…uvumilivu, malezi, kunyenyekea,…mapenzi haya ni tunu kwetu, tusiyabeze, wapo waliojaliwa ni heri kwao, lakini..nasema tena lakini wapo,...wengine wanaweza kuleweshwa na tama ndogo tu, ya kiwiliwili cha mwanamke, akaghilibika, na akajikuta kafanya lisifanyika, kama walivyo watoto...ukimuuliza anajifanya hajui, au hata kukataa, anakataa…, sasa sisi tujitahidi tu kuwasamehe....’akasema na mimi nikawa natikisa kichwa kutokukubaliana na maneno yake.‘Nikuambie tena,....wengine wanaweza hata kukubali makosa yao, lakini anakubali mdomoni tu, mwingine anaweza asikubali, lakini moyoni kakubali makosa, ila anaogopa kuonekana kakosea,sasa mimi namfahamu sana mume wako,... kama kakubali kujirudi, kama yupo tayari kuishi na wewe, na kuwa hatafanya tena hayo makosa yaliyotokea,...basi msamehe tu,….mengine muachie mola wako…’akasema‘Hapana, mimi nataka mkaaba ufanye kazi yake ili watu wajifunze…tusiendekeze mambo…’nikasema‘Mkataba,..mkataba…mama nanihii…kwani huo mkataba ndio ndoa,..huo mkataba hauna maana yoyote kama hutaweza kuishinda nafsi yako.. ..unaweza ukawepo na bado kwa siri watu wakawa wanauvunja tu, utajuaje…, sasa inasaidia nini hapo..mkataba mnzuri upo ndani ya mioyo yenu....’akasema.‘Mhh..mimi naona nyie mnamtetea sana jamaa yenu, kwa vile lakini kama mngelitendewa kama mimi najua mngelichukua hatua……’nikasema‘Sio kumtetea, nakushauri tu, …mangapi yametokea kwangu, nimekuhadithia ili ujifunze kidogo kutoka kwangu, nakushauri tena, achana na kuhangaika na huo mkataba, ...wao wanajua wenyewe kwanini waliubadilisha, wewe shikilia mkataba wao ambao mungu anautambua, kiapo cha ndoa, na timiza wajibu wako kwenye hilo, sasa kwa ushauri wangu, kaeni tena pamoja, jadilianeni, muone chanzo cha kosa ni nini, huenda chanzo ni wewe mwenyewe lakini hujatambua hilo,…’akasema‘Kama chanzo ni mimi, kwanini hajaniambia, nikajijua na kujirekebisha, yeye si mume wa familia, ilitakiwa yeye aniambie, ..kama alikaa kimia, mimi nilijionea ni sawa tu,…sasa mimi natimiza wajibu wangu siwezi kukaa kimia, …tuje kuangalia sote…’nikasema‘Jingine si nyie mna watoto, sasa mnataka watoto wenu waje kujifunza nini kutoka kwenu,...wakiona baba na mama wapo kitu kimoja, wanakaa wanashauriana kila mara wanafikia muafaka, na wao wanajiwekea nadhiri mioyoni mwao kuwa nikiwa mkubwa, nikaoa, nitaishi kama walivyokuwa wakiishi baba na mama...’akasema na mimi hapo nikakaa kimia.‘Sasa kama nyie wawili, kila mara mazozano, au mumanuniana,..au kila mtu na hamsini zake…na baadae mnaishia kutengana,..kuachana,..wao watamfuata nani, au wao watajifunza nini, wataona kumbe kuishi kila mtu maisha yake, inawezekana, ndio mtindo wa maisha, lifikirieni hilo kwa ajili ya kizazi chenu, na huo ndio mzigo tunaoubeba sisi wanawake...’akasema.‘Nakushukuru sana kwa ushauri wako dada yangu, lakini nilikuwa na swali moja nataka nikuulize, ili nione kama kweli wewe unatetea pande zote mbili, ili kuona suluhu ya kweli, .. je mume wangu aliwahi kukuambia kuwa ana mtoto nje ya ndoa?’ nikamuuliza. Alikunja uso kidogo, halafu akatabasamu, na kusema…‘Mhh, kwa jibu la moja kwa moja, kiukweli kwangu hajawahi kunitamkia hivyo, huwa naongea naye, kama mtu na dada yake, kama shemeji yake, tunataniana hapa na pale, lakini kwa hilo hajawahi kuniambia, siwezi kukuficha…’akasema na akawa kama anawaza jambo, halau akasema‘Unajua watoto wa nje..kwangu wapo..na siwezi kuona ajabu kwako pia…lakini hayo sio kosa lako, au sio..na sio kosa la hao watoto au sio….na wao wana haki yao,..sio kwamba natetea hilo, hapana, lakini kama limetokea ..ufanyeje sasa…ndio iwe kigezo cha kuvunja ndoa…’akasema‘Sio kigezo kwa mimi, ni kigezo cha yeye, kuwa kavunja ndoa,…je hilo ni sahihi kwenye ndoa..kwenye ndoa, ilisemwa kuwa anaweza kuzaa nje bila ndoa..niambie ukweli hapo…je kuzini sio dhambi, ni nini adhabu ya mzinifu ndani ya ndoa..tusije kutetea dhambi tukaja kupata dhambi…’nikasema‘Hahahaha…ukisema hivyo, nahisi wengi watavunaj ndoa zao, na wengi watapigwa mawe mpaka kufa…sasa sijui…lakini msamaha ni bora zaidi au sio..ukimsamehe abada ya kukiri kosa basi,…tufanyeje sasa…’akasema‘Unaona..udhaifu wetu huo..wewe awali umesema sisi wanawake ni wazazi ni walezi, na kila mmoja ni mchungi kwa mwenzake, je tutachungana hivyo kwa kuyakubali makosa, yafanyike tu..tusamehe tu..wengine wataona ni mchezo, acha adhabu ifanye kazi yake uone watu kama hawataogopa….’nikasema‘Ni sawa, lakini wewe hujafanya makosa yanayofanana na hilo…usiangalie upande mmoja tu…unaweza ukawa umezini kwa namna nyingine..samahani usiona natetea hayo, maana hata mimi yananiuma sana..lakini tuangalia jinsi gani ya kuokoa, kuliko kubomoa…nakubali kama kafanya hivyo kakosea, lakini tufanyeje..naangalia upande wa watoto…’akasema‘Watoto, watakua watajifunza, ukweli utakuwa bayana, …mimi bado nipo pale pale…ukweli, na ukweli wetu ulisimamiwa na mkataba, ni kwanini wakaja kuuharibu mkataba , kama kweli alitaka haki, …kama kweli alikosea, basi angelikuja akaniambia, ndio ningeumia..lakini ningelijua kuwa kweli mwenzangu kateleza, lakini kwa hatua waliyofikia, hapana..’nikasema‘Unajau kiukweli mimi sina uhakika na hilo, ila…, ninachokumbuka, ni kuwa, kuna siku nimemuuliza, hivi yeye kwa sasa ana watoto wangapi, aliniambia kuwa tu ana watoto wengi, lakini.., hakusema idadi,....’akasema.‘Hakukuambia kuwa ana watoto wangapi..na hujui kuwa mimi nina watoto wangapi?’ nikamuuliza…’ nikasema.‘Hakusema idadi kiukweli, ila nakumbuka kauli yake aliyotoa ni kuwa, yeye atahakikisha watoto wake, wote, bila kujali ni mke au ni mume, atawaandikishia haki zao, na ni vyema kufanya hivyo kimaandishi....’akasema‘Ehee…kama ni wakike au wa kiume…unakumbuka ni lini..?’ nikauliza‘Sio muda mrefu,…na alisema, kitu kama hicho kuwa hataki watoto wake waje kubaguana, awe wa kiume au wa kike….nakumbuka kitu kama hicho, na kwa kauli hiyo, nilifahamu kuwa nyie mna watoto wa kike na wa kiume’ akasema.‘Hapo kuna kitu, …lakini kwa kauli yako tu, sasa naanza kuhisi kuna yawezekana kweli kuwa akawa na mtoto nje, huyo mtoto wa kiume katoka wapi...?.’nikamuuliza huku nikionyesha kushangaa, na yeye akaonyesha kushangaa jinsi nilivyomuuliza, akaniuliza swali;‘Kwani nyie mna watoto wangapi?’ akauliza huku akiangali huku na kule, kama anawatafuta watoto.‘Mhh, usijali dada yangu, naona tuishia hapo, au kuna jingine ulitaka kuniuliza maana nyie mumesema mlikuwa mkinitafuta sana…maana haya mambo mengine ni mambo yangu na mume wangu, tutaelewana tu...’nikasema.‘Aaah, uliniuliza swali, nikakujibu, na wewe naomba unijibu swali langu...ili kama nina cha kukushauri, nitakushauri, sina nia ya umbea,au nimekosea jamani...’akasema.‘Kiukweli, sisi tuna watoto wawili tu, tena wakike wote...’nikasema.‘Basi labda mimi nilisikia vibaya, lakini nina uhakika, kutokana na kauli yake, ni kama vile mna watoto wa kike an wa kiume...hata kwenye huo mkataba niliouona, mimi sikuusoma sana,..maana sikuona umuhimu wake, kuna kitu kama hicho,...sikumbuki vizuri, na kwahiyo hapo siwezi kusema kitu,...nisije nikawa mbeya,, ila lisemwalo lipo, kama halipo laja....’akaniangalia kwa macho ya udadisi.‘Nitaligundua tu, nina uhakika kabla ya wiki nitakuwa nimeshagundua ukweli...na hapo ..sijui, maana huo ni ushahidi wangu wa kutosha, na kuanzia hapo nitajua nichukua maamuzi gani..na ka hatua hii,.....’nikasema.‘Kwahiyo huenda hilo ndilo linafanya msielewane nyie wawili au sio, ....na hilo huenda ni moja ya jambo ambalo wewe unaliona linalovunja mkataba wenu au sio..ni sawa kwa hilo hata mimi silipingi, unapotoka nje ya ndoa umeshavunja mkataba wa ndoa..lakini kusameheana ni bora zaidi, au sio…’akasema‘Sio rahisi kihivyo….mimi ni mvumilivu sana, na wengi mpaka huniona ni mjinga, sielewi, sikubali ukweli…lakini nina subira ya namna hiyo, ila sasa ikizidi kama hivi, basi moyo wangu ukikengeuka, siwezi tena…’nikasema‘Yeye si kakubali kuwa kakosa au sio, na wewe ukubali kumsamehe....kama kuna mtoto nje, ambaye humjui, basi jadilianeni muone jinsi gani mtamtambua huyo mtoto...wewe waonaje kwa hilo…?’ akasema na kuuliza.‘Mkataba wetu ulikataa hilo, na hadi hii leo yeye hajakubali hilo, sasa wewe unanishaurije hivyo,kwanza kazini, kuzini si kuvunja mkataba, halafu kama ana mtoto, sio ndio ushahidi wenyewe…tatu anavinja mkataba, anaugushi..kwanini afanye hivyo,…anamdanganya nani hapo.., aah, mimi hilo sitavumilia kabisa…’nikasema‘Kama nilivyokushauri, labda mimi ni tofauti na wengine, unielewe vizuri hapo, maana kiukweli mimi sijui...kama limeshafanyika, na mtoto yupo, na yeye anawajibika kwake, na sijui labda huenda anawajibika na kwa mama wa mtoto pia, na kama bado mtoto ni mchanga,kiukweli ni lazima awajibike, hana ujanja hapo, na ni vyema, akuambie ukweli....muulize, kwa wakati muafaka, atakuambia...’akatulia.‘Nimeshamuuliza sana, lakini hataki kuwa mkweli…’nikasema‘Kwahiyo kumbe mna mabinti wawili, hamjajaliwa kupata mvulana....ndio maana niliwahi kusikia zamani kidogo, kuwa akizaa mtoto wakiume atakuwa katimiza ndoto yake...lakini ni zamani kidogo,...’akasema‘Zamani ya vipi…?’ nikauliza‘Aaah, zamani, sikumbuki, ila muhimu kaeni mliongelee kama wanandoa,....ili mambo yaishe, mgange yajayo..msisubiri mpaka kutokea msiba, mmoja wenu hayupo duniani ndio hawo watoto wa nje, wanaanza kujitokeza, na kuleta mfarakano, kama ilivyotokea kwetu, japokuwa tumeshayamaliza kiaina, ..’akasema.‘Nimekuelewa dada yangu, nakushukuru kwa ushauri wako,...lakini hayo ya mume wangu, yaacheni kama yalivyo, ninafahamu jinsi gani ya kufanya, nilitaka kuwa na uhakika tu,…’nikasema.‘Sasa nikuulize kitu, je akija kwa hivi sasa akakuambia ukweli, utamsamehe?’ akaniuliza. Na kabla sijamjibu macho yetu yakaona jambo….Kule mlangoni nikawaona mume wangu na Yule wakili wake wakitoka, wakawa wanashikana mikono kama kuagana, na mume wangu akageuka na kutuona ..akamshika bega wakili akaongea naye jambo, na wote wawili wakawa wanakuja kuelekea pale tulipo…NB: Ni nini kitaajiri hapoWAZO LA LEO: ushauri mnzuri ni ule unaoangalia usawa, kuwa ninachomshauri mwenzangu hata mimi ningalifurahia kufanyiwa hivyo. Mshauri mwenzako kwa wema, mshauri kwenye mambo ambayo yatamjenga,..na hata yeye akifanya au wewe ukifanyiwa hatupata madhara yoyote.‘Nimekuelewa sana dada yangu, nakushukuru kwa ushauri wako,...lakini. eeh…’nikasita maana niliona kama gari linaingia getini, halafu nikasema‘Hayo ya mume wangu,..najua mnampenda na kumthamini sana, lakini nawaombeni hayo mniachie mimi mwenyewe…’nikasema na sasa geti likawa linafunguliwa, lilikuwa gari la mume wangu.‘Oh wamerudi na kunikuta tena hapa, mimi naondoka…’akasema‘Kwanini haraka hivyo…hatujamalizana …’nikasemaNa kabla hajajibu mume wangu akateremka kwenye gari, na wakili wake,…na walipoteremka, badala ya kuelekea ndani, wakawa wanakuja pale tulipokuwa tumekaa, na ikabidi tukatizie mazungumzo yetu.Tuendelee na kisa chetu.....‘Aheri bado mpo..nahisi hili litatufurahisha sote,…maana shemeji yangu upo, na…na mke wangu ..unajua leo kutwa nzima tumekuwa tukilihangaikia hili,…kutafuta haki, ..na haki haiji hivi hivi wakati mwingine au sio..’akasema mume wangu na kumuangalia wakili wake ambaye alitikisa kichwa kukubaliana na yeye.‘Sasa hivi tumetokea polisi, kumuona Yule mpelelezi anyeshughulikia hii kesi yako ..mke wangu mambo sasa yanakwenda vizuri tu..imebakia maswala machache,..si unajua tena nchi yeu ilivyo…’akasema na kumuangalia wakili wake.‘Kwanini…maana haya yapo mikononi mwao, na tulikubaliana kuwa hakuna haja ya kuwafuatilia, tuwaachie wao wafanye kazi yao…’nikasema‘Ndio hivyo mke wangu, lakini ni wajibu wangu, eeh, na wakili hapa kulifuatilia hilo, kuhakikisha kuwa, mke wangu upo na amani, haiwezekani watu wakushuku tu, haiwezekani mtu auwawe tu, na sisi tubakie kimia, ni kwanini …eeh, Yule alikuwa ni rafiki yangu mkubwa..hapana mimi sitakubali kukaa kimia mpaka haki ipatikane…’akasema‘Ok, kwahiyo…?’ nikauliza, na sasa wakili ndiye akaanza kuongea.‘Kifupi ni kuwa polisi wanasema bado wanalifanyia kazi, lakini kwa kuhusu wewe kama mshukiwa muhimu, halipo tena,…’akasema‘Kabisa…kazi nzuri ya wakili wetu…’akasema mume wangu.‘Lakini hata hivyo kabrasha la kesi halijafungwa, si unajua tena mambo ya kisheria, kuna taratibu zinatakiwa kufutwa, ..na hilo ndilo tulikuwa tunalifuatilia, ili kuhakikisha kuwa gabrasha hilo limefungwa..na wewe utakuwa huru kabisa…’akasema‘Lakini mimi nina wakili wangu analifanyia kazi hilo…’nikasema‘Haina shida, yeye afanye kivyake na sisi kivyetu,..lengo letu ni moja, na mwisho wa siku tutakaa pamoja…na kuona kila mmoja kafikia wapi, muhimu ni kuhakikisha kuwa kesi hii haipo tena, ..lakini wkati huo huo, haki imetendeka, na muuaji kapatikana…maana aliyefariki ni jamaa yetu..’akasema wakili.‘Sawa nashukuru …’nikasema‘Sasa tatizo mke wangu, kila kitu ni gharama au sio..na unajua hali niliyo nayo, nakwama kabisa, nilikuwa naomba…tukaongee ndani, unipitishie hundi yangu..’akasema‘Hundi ya malipo gani…?’ nikauliza‘Ya wakili, na kufuatilia..na mambo mengine ya kikazi..ni pesa nyingi kidogo, na sitaweza kupitisha hundi hiyo kwa sahihi yangu tu..’akasema‘Naomba hilo tutaliongea baadae..’nikasema‘Ni muhimu na haraka kuna mambo mengine nayafuatilia,…’akasema‘Mume wangu tulishaliongea hilo, mimi siwezi kuweka sahihi yangu …kwa kazi yoyote ya ushirika, hasa za makampuni, mpaja swala langu litatuliwe, hilo lipo wazi, kwahiyo kama ni hundi ya namna hayo, samahani sana…’nikasema‘Mke wangu hili ni la muhimu sana, tunataka tumalizane na kesi yako,..na haki ya marehemu ipatikane,..ina maana wewe huna uchungu na hilo..na hata kama huna uchungu na hilo,na je wewe hutaki uwe huru…?’ akauliza‘Nitaongea na wakili wangu…’nikasema sasa nikisimama kutaka kupiga simu kwa wakili wangu.‘Wakili wao wa nini sasa haya ni yetu, hayamuhusu…’akasema‘Wakili wangu ndiye anasimamia kesi ya mkataba..kila jambo kama ni muhimu yeye ndiye anatakiwa atoe maamuzi ya kisheria, siwezi kulikwepa hilo…’nikasema na wakili wangu akawa hewani.‘Vipi umefanya kama nilivyokuambia…?’ akatangulia kuniuliza‘Kabisa…lakini kuna tatizo hapa, mume wangu kaleta hundi ya ushirika anasema anataka niweke sahihi yangu..nishauri…’nikasema na kumsikiliza kwa makini halafu nilipomaliza kuongea naye, nikasema;‘Kama nilivyosema kila kitu kinachohusu mkataba wangu wa zamani kitapitia kwa wakili wangu,kwahiyo kama ni ya haraka usubiria anakuja…’nikasema na hapo mume wangu akamgeuikia mwenzake na kusema‘Twende zetu…’akamshika mkono na wakaanza kuondoka.‘Vipi tena…?’ nikauliza lakini hawakunijibu kitu haoo, wakaingia kwenye gari na kuondoka zao.********* Yule mama akawa kimia, nahisi alijifunza jambo hapo, akasimama sasa akitaka kuondoka.‘Mimi naondoka maana kijana wangu ana mambo mengi ya kufuatilia…’akasema‘Umeona mwenyewe mambo yalivyo..’nikasema‘Lakini yatakwisha tu, ila nahisi mume wako ana jambo…ila anaogopa kukuambia, hebu nikuulize ni nini kikubwa kwenye huo mkataba wenu ..ambacho unahisi kakivunja,…?’ akaniuliza‘Siwezi kusema lolote kwa hivi sasa, ..’nikasema na hapo akakaa tena kwenye kiti na kwa sauti ya chini akaniliza‘Nilikuuliza kitu, je mume wako akiamua kukuambia ukweli, utamsamehe?’ akauliza sasa akiangalia saa yake ya mkononi.‘Hapo mimi sijui, ..kiukweli kachelewa sana kuwa mkweli na zaidi anazidi kuharibu, na kwahiyo kama ataamua kufany ahivyo, najua kabisa itakuwa ni kutokana na kushawishiwa, au kwa vile kaona kakwama…’nikasema ‘Nimekuelewa sana dada, ila nauliza hivyo maana ndoa ni mashikamano ya mume na mke, na kila mmoja anawajibika kuitii ndoa yake, lakini ni lazima mfike sehemu myamalize au sio…’akasema.‘Ni kweli yataisha tu, lakini kuisha kwake ni baada y akuupata huo mkataba wa zamani, tukae tuona unaemaje, na yeye akiri makosa yake, ..mengine yatafuta baada ya hapo…‘Nakuelewa sana mdogo wangu,...unajua kuna makosa madogo madogo tunayoyafanya sisi wanandoa hasa wa kike, tunaona ni sahihi au ni madogo tu, kwa namna yetu, kumbe kwa wenzetu ni tatizo kwao, na wao kwa uwezo wao wanaweza kufanya jambo, na matokea yake kuna leta matatizo, na ushukuru wewe una uwezo wako…’akasimama sasa akitaka kuondoka‘Nafahamu hilo,najua hata mimi nina makosa yangu, lakini sio ya kuvunja mkataba ..maana ni mambo ya kuelezana, kama nilikosea, angeniambia,..usitetee hilo…sawa tulikuwa tunahangaika na majukumu ya kazi, na mambo mengine yakawa kama hayana msingi, lakini je hayo ndio yafanye mtu aka…hapana…’nikasema. ‘Ndio awali nikakuambia kuwa sisi wanawake tuna dhima ya kuwalea wanaume wakati mwingine kama watoto wetu,…sina nia mbaya hapa…’akatulia kama anawaza jambo.‘Mfano nikuulize hivi ukiwa unamlisha mtoto wako vyema, akanisha vyema anaweza kwenda kuomba chakula kwa jirani…?’ akaniuliza‘Una maana gani…?’ nikamuuliza‘Nijibu tu…’akasema‘Hawezi…’nikasema‘Basi ndio hivyo, wakati mwingine tunaweza kuwanyima watoto wetu, eeh, unanielewa hapo, chakula,..haki yake, ikafikia akazidiwa, sasa akienda kuom,ba chakula kwa jirani, utamlaumu nani…hahaha…’akasema na kucheka.‘Sijawahi kufanya hivyo…labda …hapana, unajua hayo ni maswala ya kuambiana, kwani mimi si mke wake, kwanini aogope kuniambia…ana njaa…’nikasema‘Haahaha..tuyaache hayo..ila yakitokea haya ndio tunapata fundisho, mimi nitashukuru sana mkilimaliza hili kwa amani, na sitafurahi kama mtaishia kubaya, haya juhudi yetu itakuwa haina maana…’akasema'Msimamo wangu upo wazi, …sifanyi kwa nia mbaya, lakini ikifikia huko, nitafanyaje, je kama ndio imeanza hivyo, huko mbele itakuwaje, sasa hivi kaanza kuandikisha watoto wa nje, je mama wa hao watoto ana dhamira gani,…ni lazima niwe makini hapo…’nikasema‘Ninachoweza kusema kwa msameheane, wewe ulivyo,....hutapoteza kitu hapo au sio, bado una nafasi ya kuendelea na ..na kampuni yako,…nasema hivyo sio kwavile na mtetea shemeji yangu, hapana…’akasema‘Mhh…unajishuku dada…’nikasema‘Pamoja na hayo, mimi namfahamu sehemu nyingina ya tabia yake…kila mtu ana hulka lakini kuna hulka hujificha,..yeye ni mwanaume mwema sana, akimpta mtu wa kumjua alivyo, ana huruma sana kwa watu, japokuwa katokea kizazi cha tabia hizo zisizopendeza watu, na mengine ni shida tu..watu hawajapenda wawe hivyo.....’akasema.‘Nimekuelewa….ngoja tuone ..’nikasema‘Sasa mimi naondoka tuonane lini sasa…nafahamu kuna maswala hayo ya mawakili, wanafanya kazi zao, naona wanakipizana huku na kule,.. hata hivyo ni lazima maisha yaendelee, naopmba tuje tukae tuongee tuone maisha yanakwendaje, …haya yanayotokea sasa yasitufanye kusimamisha mambo mengine, naomba nije tusaidiane mawazo ya maendeleo…’akasema‘Sawa kwa hilo tu, hamna shida kabisa, tupo pamoja…’nikasema‘Na kwa hili je…?’ akauliza sasa akinyosha mkono wa kuagana.‘Hahaha, dada hujanielewa mpaka hapo…niakuambie kitu, baada ya wiki mimi nitawapatia jibu langu,…kuhusu hili…kwa hivi sasa niacheni nipambane na mume wangu.....’nikasema na kikunja uso wangu kuashiria dhamira ya kweli.‘Mhh, baada ya wiki sio sawa, basi ngoja waupitie huko mkataba waone wafanyeje, hayo ni mambo ya kisheria, au sio…?’ akauliza‘Huo mkataba wa kugushi, ..au?’ nikasema kama nauliza‘Mhh..mimi sijui sasa…naona kwa hili litaleta utata…na hapo ndio tunazidi kuchelewa,…namuonea huruma sana kijana wangu…kwani na yeye anachelewa kuondoka, lakini hawezi kuondoka kabla hili tatizo halijaisha, ya mungu mengi...’akasema.‘Ninachoweza kukuambia dada, huo mkataba kwangu ni batili, na kama mtaendelea kuutumia basi msije kunilaumu, itabidi mimi niende mbele ya sheria, ili haki itendeke…sasa kwa ushauri wangu wa haraka, msubirie baada ya wiki, au hata kabla ya hapo, kama mume wangu atakuwa tayari kutimiza masharti yangu, nitawaambia, ni nini cha kufanya..’nikasema‘Sawa nimekuelewa, nashukuru sana,..’sasa akataka kuondoka na ghafla akasimama.‘Mungu wangu sijui kama mliongea na kijana wangu..kuna jambo limezuka…’akasema sasa akarudi kukaa..‘Samahani kidogo, ni muhimu kwa kweli…’akasema‘Jambo gani tena…?’ nikauliza‘Unajua huku kuzaa ovyo ovyo nje ..mitihani yake ndio hiyo,,..juzi,..kuna msaidizi wa kijana wangu. Msaidizi katika mambo hayo ya mirathi,… Unajua marehemu kila kitu alikiacha kwenye maandishi, utafikiri alijua atakufa…ndio hivyo, usomi nao unasaidia, au sio…si ndio hivyo hata nyie mnakuwa na mikataba ya ndoa nk..kusoma huko…’akasema‘Mhh..kuna tatizi gani ..?’ nikauliza‘Huyo msaidizi wake sasa..ni mtoto wa marehemu mwingine, alizaa na mwanamke mwingine..na katika maelezo yake kwenye hayo maandishi aliyoacha,..alitaka huyo kijana atambulikane na awe msaidizi wa kijana wangu, kila kitu kwenye maandishi tena ya kisheria..unaona hapo..’akasema.‘Sasa huyu msaidizi wake,…ni tatizo, yeye ni mtoto kama baba, unanielewa hapo…’akaniangalia‘Bado sijakuelewa…’nikasema‘Ni hivi huyo kijana kamlanda baba yake sio kimatendo tu, bali pia na yeye aliamua kusomea sheria..na ni wakili pia…’akasema‘Mhh..kwahiyo…’nikasema‘Na hata tabia za kazi ni kama alivyo baba yake, utafikiri alimfunza hiyo tabia, si unamuelewa marehemu alivyokuwa, basi mtoto ndio zaidi, na kiumri hajapitana sana na kijana wangu…’akasema‘Sawa kwani kuna tatizo gani hapo, sioni tatizo maana sina jambo na yeye, hayo ni yenu ya kifamilia au sio, au unataka kusema nini hapo…’nikasema‘Mengi yaliyopitishwa kwenye kikao cha kifamilia yeye alikuwa mpingaji sana, yeye alitaka kila kitu alichosema marehemu kitekelezwe hasa kikiwa kwenye maandishi, mkataba…, unajua nilimuambia kijana wangu mapema awe tayari kwa hili, kwahiyo mambo mengine asiyaweke wazi…’akasema‘Kwanini sasa na ni haki ya kila mtu au sio, haikuwa na haja y akuficha jambo…’nikasema‘Wewe ni mungu tu alituongoza, maana huo mkataba wa kuelezea kuwa kuna ..hizo kwenye makampuni yenu, haukuwahi kwenye hicho kikao, kijana wangu alikuja kupewa baadae na kwahiyo hilo halikuzungumzwa siku hiyo..siku hiyo ilikuwa ni madeni, na watoto hao wa nje waliposikia madeni ni mengi kuliko mali za kurithi, wakaondoka mmoja mmoja, maana kijana wangu aliwaambia kila mtu akubali kushika sehemu yake ya deni,…nani akubali hapo, hata huyo msaidizi wake akaondoka akidai ana kesi anafuatilia...’akasema‘Kwahiyo…unataka kusema kuwa huo mkataba wa kugushi bado haujafika kwa warithi, kama huyo ..na wengineo ..ni vizuri, lakini mimi siutambui…’nikasema‘Sasa huo mkataba halali upo wapi mdogo wangu…’akawa kama anauliza‘Utapatikana tu dada….mume wangu atakuwa anafahamu upo wapi…’nikasema‘Tatizo ni muda..mana sijui kajuaje …huyo mtoto, katupigia simu akidao kuwa tumemficha ukweli…sasa ni hivi kutokana na muda, kama kijana wangu akiondoka, kurudi ulaya kabla hatujamalizana na hilo, mtakuja kupambana na huyo mtoto, ni mkorofi kweli kweli, nina uhakika …hamtaelewana naye, ndio maana tunataka mambo haya yaishe haraka, iwezekanavyo, wewe kaa na mume wako myamalize haya mambo kwa haraka jamani, …’akasema‘Kuisha haraka ni mume wangu…nimeshakuambia hilo, yeye ndiye anachelewesha haya mambo, kama nyie mnaweza kumshauri fanyeni hivyo, alete mkataba wa zamani, umenielewa hapo dada…’nikasema‘Nilivyosikia, huu mkataba uliopo sasa nakala zipo kila mahali panahusika, sasa sio rahisi mtu kukubaliana na kauli yako, sijui unanielewa hapo…’akasema‘Usijali, hilo litafanyiwa kazi..hamna shida …’nikasema‘Mimi sitaki kubishana kwa hilo, ila ninachotaka kukisema hapa ni hivi…unajua huyo kijana ni mtata kwa sheria,…anapenda sana kesi, nina uhakika atawasumbua sana kwa hilo, na kama siku ile huo mkataba ungelifika mikono mwake, sijui uingekuwaje...’akatulia‘Dada…’nikataka kusema na yeye akanikatisha, akisema;‘Sisi kuwa kusaidia hilo, tumesema hatujui, hatuna uhakika, tutalifuatilia tukiupata basi tutamjulisha, lakini hakukubali, kasema huo mkataba tunaufahamu tumemficha…...ndio maana tunataka tulimalize hili haraka…’akasema‘Kwahiyo mlitaka mimi nifanye nini..?’ nikauliza‘Sisi lengo letu ni kuhakikisha kuwa huo mkataba unafanyiwa kazi, na kuondolewa kabisa,..mimi kwa ushauri wangu, kubali tu huo mkataba uliopo halafu tunaongea na wakili sisi kama familia tunajitoa, nyie sasa mtajua mnafanyaje na mume wako,..ni ushauri wangu huo…’akasema.‘Msiwe na shaka na mimi, mimi simuogopi yoyote, ilimradi nipo kwenye haki yangu, wanachotaka kupata sio haki yao, au sio.....kama kweli huyo wakili na anaifahamu sheria, tutaangalia ukweli upo wapi na haki itatendeka, lakini kama ndio hawo wenye tamaa..basi tutapambana hadi mahakamani, hilo usijali kabisa…’nikasema.‘Lakini muda sasa, na gharama…kijana wangu anaondoka hivyo, lifikirie hilo kwa makini..’akasema.‘Sawa nimekuelewa...’nikasema na mara simu yangu ikalia, nilipoangalia nikaona ni namba ngeni kwenye simu yangu,, ...sikutaka kuongea na mtu nisiyemfahamu kwa muda huo...tukaagana na mgeni wangu huo, huku simu inaendelea kulia, baada ikakatika, ..baadae kidogo ikaita tena…, nikapokea na kuuliza‘Nani mwenzangu...?’ nikauliza‘Mimi ni mtoto wa marehemu Makabrasha....’akasema‘Yupo huyo..na unasemaje?’ nikuliza‘Nimesikia tetesi kuwa kuna mkataba unaoonyesha kuwa marehem alikuwa na hisa kwenye kampuni zako, ni kweli si kweli…?’ akauliza‘Mimi sijui hilo, ni nani kakuambia..?’ nikauliza‘Wewe si mmoja wa wakurugenzi, kwanini hujui, na ni haki yetu kaam warithi kulifahamu, je ni kweli au si kweli…?’ akauliza‘Nimeshakuambia mimi sijui…je ndio taratibu za mirathi zipo hivyo, wewe kuuliza hivyo tu kwenye simu,..unajua sheria wewe..?’ nikauliza‘Naifahamu sana, mimi ni wakili, nimekuuliza hivyo, kwasababu kuna hali inayoendelea kwa kiongozi wetu wa familia, analifahamu hilo na alilificha, sasa natafuta ukweli, ili sheria ichukue mkondo wake…’akasema‘Kwa kifupi, fuata sheria, ongea na kiongozi wenu, na ikibidi ongeeni na wakili wetu, unanielewa,…’nikasema‘Nasema hivi kama marehemu alikuwa na hisa kwenye kampuni zako, inatakiwa utuambie, utupe memorandum, na vielelezo vyote vinavyostahiki, ili tuweze kuorodhesha kwenye madai yetu, ndio maana nikakuuliza ili kuupata huo ukweli..’akasema‘Na mimi ndio nimekupatia hilo jibu…’nikasema‘Sawa mimi nitafuatilia kuupata huo ukweli, na kama kuna njama zozote za kuuficha ukweli, basi, sitasita kwenda mbele ya sheria…’akasema‘Na samahani nikuulize tu, ni nani kakuambia mambo hayo?’ nikamuuliza‘Nimesikia tetesi, hata kwenye kikao walisema kuna mikataba mingine haijapatikana, wanaifuatilia…., niliwaambia mimi ni wakili wanipe mimi nifanye ufuatiliaji wakachelea kunipatia, sema siku ile nilikuwa na kesi nyingine ya haraka siweza kusubiria.., lakini sasa nipo na nafasi, nataka kuuona huo mkataba...’akasema‘Unasema ulisikia tetesi,..na unadai wewe ni wakili, unajua mambo hayo ya kisheria yanafuatiliwaje au sio..au wewe tetesi tu kwako ni sababu, je ukisikia tetesi kuwa wewe sio mtoto halali wa marehemu utasemaje…?’ nikamuuliza.‘Unasema nini?’ akauliza kwa hamaki‘Kuna tetesi kuwa wewe sio mtoto halali wa marehemu, wewe ni mtoto wa kusingiziwa, je unazikubali hizo tetesi?’ nikamuuliza.‘Sikiliza mimi nakuuliza mambo ya muhimu wewe unaleta mzaha, sikiliza mimi nafahamu sana sheria, kama ni kweli, huo mkataba una haki zetu, nakuhakikishia mimi nitafika hadi mahakamani…sasa kwa vile umejibu ki-huni, nakupatia wiki moja tu, hilo liwe wazi, na ...hizo tetesi zako, hawo waliokuambia waambie, hawana akili kwanini hawakusema hivyo wakati marehemu yupo hai...’akasema.‘Nilikuwa nataka kukuonyesha kuwa tetesi sio ukweli wa mambo, kama ulisikia tetesi kuwa kuna mkataba kama huo wa halali wa hivyo unavyosema, ilibidi ufuatilie kwanza sehemu husika..na ni vyema ukamuona wakili wenu, kwani si mna wakili anayefuatilia mambo yenu ya kifamilia..’nikamwambia.‘Mimi mwenyewe ni wakili, ndiye nimeteuliwa katima mambo ya kisheria, lakini siku ile walinificha hilo jambo, sasa nimeanza kulifuatilia mpaka nione mwisho wake...’akasema‘Sawa, kama unaona ni haki yako fuatilia, ...ila ni vyema ukawa na uhakika na hicho unachokidai,..sawa muheshimiwa..’nikamwambia.‘Sawa …ila nitegemee kukuona, siku yoyote naweza kuja kuongea na wewe kaika kulifuatilia hilo, nataka nionane na wewe uso kwa uso,….jiandae kwa hilo….’akasema na kukata simu.NB: Tuhitimishe? sehemu hii ilihitajia marekebisho mengi..lkn hatukupata muda,....WAZO LEO:Kunapotokea mzazi mmoja kufariki hasa wa kiume, kuna watu wanajitokeza kudai, mali wakisema na wao wana haki ya urithi, watu hawa wakati wa uhai wa merehemu, walikuwa hawaonekani, na zaidi inawezekana kabisa marehemu alikuwa akiumwa kwa muda mrefu, lakini hawakuwahi kufika, angalau hata kusaidia kidogo, hata angalau kutoa pole, mpaka mzazi huyo nafariki.Watu kama hao huja kujitokeza baadae wakati wa mirathi. Je huo urithi, umetokea wapi, ukumbuke hiyo mali ilitafutwa na watu, na ni hawo hao waliohangaika na marehemu, wenye uchungu naye…, wewe unakuja baadaye unadai, mali, hiyo mali kwako itakuwa sio halali ...ni vyema tukajua kuwa, kila penya faida kuna gharama zake pia.Ilikuwa siku maalumu ya kupokea taarifa kutoka kwa watu wangu, kuna vijana huwa nawapa kazi zangu, kwa kuwaamini, hasa zinazohusu mambo yangu binafsi, hata ya kikazi pia…nilifika ofisini na kumwamboa katibu muhutasi kuwa hao vijana wangu waitwe mmoja mmoja…na wakati nipo tayari, mara mlango ukagongwa...‘Unaweza kuingia..’nikasemaAkaingia jamaa mmoja…yeye ni mtu wa masoko, lakini pamoja na kazi hiyoo yeye nimatumia kwa mambo ya uchunguzi ikibidi..ana utaalamu huo, na nilishampeleka shule kusomea upelelezi kidogo, inasaidia kwa kazi zangu…Nilimwambia kuwa nataka asomee upelelezi kidogo, kwa nia ya mashindano ya kibiashara, lakini pia nataka anisaidie kwenye kazi zangu.Tunaelewana sana.‘Kutokana na uchunguzi wangu, mtu aliyechukua huo mkataba atakuwa ni mtu wa humo humo ndani, alitumiwa,…maana hakuna mtu wa nje aliyweza uingia kwenye ofisi yako, akaonekana…’akasema‘Huyo mtu wa nje ni nani, uliweza kumtambua …?’ nikauliza‘Imekuwa ngumu kidogo…’akasema‘Je ni nani aliwahi kuifika kati ya watu niliokuambia uwachunguze, ?’ nikamuuliza‘Mtu ambaye aliweza kufika mara kwa mara ni docta Yule unayemuita Rafiki wa mume wako,…’akasema‘Ehe…je uliweza kufahamu, kama aliweza kuingia ofisini kwangu au kuongea labda na mfanyakazi wangu wa usafi…?’ nikamuuliza.?’ nikamuuliza‘Yeye hata wakati ukiwepo alikuwa akifika kama alivyofika kipindi hiki…yeye hufika kwa minajili ya kikazi, akifuatilia malipo yake ya matibabu ya wagonjwa, ya wafanyakazi wako, na mara zote alizofika alikuwa akiishia mapokezi....’akasema.‘Una uhakika na hilo…?’ nikamuuliza‘Kwa uchunguzi wangu naweza kusema hivyo, sizani kama aliweza kuingia ofisini mwako,…’akasema‘Mwingine ni nani…?’ nikamuuliza akilini mwangu nikianza kujiuliza kama docta anaweza kufanya kitu kama hicho, haiwezekani, kwasababu hana faida yoyote na huo mkataba…labda kumsaidia rafiki yake…hapana haiwezekani.‘Na mwingine aliyeonekana, ni bosi, nina maana ....rafiki yako, kuna kupindi alifika kabla hajaondoka kusoma na pia aliporejea,..’akasema‘Aliporejea..!?...alifuata nini…?’ nikamuuliza‘Alikuja akikuulizia, lakini hakuweza kuingia ndani ya ofisi yako, naye aliishia mapokezi, na hakukaa sana, kwani aliambiwa haupo....’akasema‘Na kabla…?’ nikauliza‘Kabla ni kipindi ukiwepo, au…kama haupo, anaishia mapokezi tu…..’akasema‘Kwahiyo hakuna mtu yoyoye mwingine ambaye tunayemshuku, aliyeonakana akiongoea na mfanyakazi wangu wa usafi, ambaye ndiye anayetunza ufunguo za ofisi yangu?’ nikamuuliza‘Tatizo ni kuwa huyo mfanyakazi wako wa usafi, anaongea na watu wengi sana, sasa sio rahisi kuhisi yupi ni yupi, hata nilipotumia mbinu za ziadi kupata taarifa kwake, ilionekana kama tunamshutumu mtu ambaye hajafanya jambo kama hilo, nina uhakika kama ni mtu aliingia, yeye atakuwa hajui kabisa..’akasema.‘Sasa alipaje ufunguo….?’ Nikauliza‘Hapo hatukuweza kupata ukweli,….’akasema‘Ina maana kwa uchunguzi wako,…maana nimekupa kazi hiyo ili nimpate huyo mtu, wewe umegundua nini, angalau kidogo cha kusaidia…au umeshindwa kumpata…?’ nikamuuliza‘Mwanzoni nilimuhisi katibu wako muhutasi, kwasababu yeye ana haki ya kuingia na kutoka ofisi kwako, lakini nilipofuatilia nyendo zake, niliona hahusiki, maana alikuwa likizo kipindi chote hicho ambapo wewe hukuwepo ofisini.’akasema‘Kwa kifupi bado hujamgundua ni nani alifanya hivyo..?’ nikauliza‘Kiukweli bado bosi, tatizo wewe hutaki tufanye tuonavyo sisi, wewe umeteka tufanye utakavyo wewe sasa inakuwa ni ngumu kidogo, ukitaka tumgundue kwa njia zetu, tupe hiyo nafasi, tutampata tu,…’akasema‘Hapana msifanye hivyo, nilitaka kufahamu mambo machache kutoka kwenu sitaki kuleta utata kwa hili, unanielewa, basi tusipoteze muda, wewe endelea na kazi zako…’nikasema‘Sawa bosi….’akasema hivyo na kuondoka.Wa pili alikuwa mtu ambaye nilimpa kazi ya kuchunguza nyendo za mume wangu kipindi hicho, kabla hajapata ajali..akasema;‘Siku mume wako alipopata ajali, alionekana akiwa katokea maeneo ya rafiki yako,kwahiyo huenda alipita hapo,au alitokea hapo kwa rafiki yako ...’akasema‘Huna uhakika kuwa alitokea kwa rafiki yangu…?’ nikauliza‘Uhakika wa moja kwa moja haupo…kwasababu hakuonekana akiingia au kutokea kwenye nyumba ya rafiki yako,…’akasema‘Kwahiyo ni kweli kuwa alipita tu…?’ nikauliza‘Mara nyingi yeye anasafisha gari lake kwa muosha magari karibu na anapoishi rafiki yako,…cha ajabu muosha magari, japokuwa hayupo, lakini nilimfuatilia mpaka huko kijijini kwao, nikaweza kuongea naye, hakuataka kabisa kuongea na mimi, ila baada ya kumpatia chochote, ndio akaongea‘Anasemaje..na kwanini kaondoka hapa Dar..?’ nikamuuliza‘Anasema maisha yamemshinda tu, kaona akafanyie shughuli zake kijijini…’akasema‘Ehe,siku hiyo ilikuwaje…akiwa kazini kwake,..hakuwahi kuosha gari la mume wangu..?’ nikamuuliza‘Anadai hakuwahi kuosha gari la mume wako, hakumbuki kabisa..anasema yeye anaosha magari ya watu wengi, na sio kazi yake kukariri..lakini ana uhakika hakuwahi kuosha gari la mume wako, …’akasema‘Ni kweli au anaogopa tu kusema ukweli..?’ nikauliza‘Nimetumia kila mbinu hajakubali hilo, nahisi hakuwahi kuosha, au hakumbuki kweli, sizani kama angetuficha...’akasema‘Kwahiyo ni kweli kuwa mume wangu alipita tu maeneo hayo na hakuwahi kufika kwa rafiki yangu..?’ nikauliza‘Itakuwa hivyo, ila waliomuona akiendesha gari, wanasema alikuwa katokea maeneo ya huko, na alikuwa akiendesha kwa mwendo kazi sana, nikama vile alikuwa akiwahi jambo, na.....hakuwa amelewa kabisa, kwani ofisini kulikuwa na kikao, na alipotoka kwenye kikao hakupitia kwenye ulevi..’akasema‘Hakupita kwenye ulevi, aliyekuambia hivyo, amejuaje, …ina maana alifahamu anapoelekea …alipokwenda mume wangu..?’ nikauliza‘Wanafahamu wapi anapokunywa mara kwa mara..na hao walimuona akitoka ofisini, na kuendesha gari…kuelekea upande mwingine, hawakufuatilia,…na tulijaribu kutafuta mtu mwingine …hakuna aliyemuona akielekea kwa rafiki yako…’akasema‘Hilo naweza kuamini kuwa hakuwa huko kwa rafiki yangu maana mimi mwenyewe nilikuwa huko, kama angelifika mimi ningelimuona.’nikasema‘Sasa ajali yake ilitokea kwa vile alikuwa kwenye mwendo kazi, na alipokuwa akata kona..ndio akakumbana na hilo gari jingine..akafunga breki lakini zilikataa, ndio ikapatikana na hiyo ajali...., alikuwa mwepesi kuruka nje..,na wakati anatoka alionekana, akiwa na mkoba, .....’akasema‘Aliruka kabla…mmh, hapo, unataka kusema nini, na huo mkoba wa…komputa au…?’ akauliza‘Ni mikoba hii ya kawaida, na kwa vile aliumia sana, aliyekuja kumsaidia, anasema mume wako hakutaka kabisa kuachana na huo mkoba, na kuna mmoja alitaka kumsaidia, lakini akakataa,...’akasema.‘Na alipofika mlangoni mwa nyumba yenu, alionekana kupiga simu,..ndio akaja jirani yenu mmoja…ndiye aliyemsadia hadi kwa nyumbani kwa docta..na huyo docta ndiye aliyemsaidia kwa huduma ya kwanza...’akasema.‘Mlipochunguza nyendo zake za huku nyuma , mligundua nini?’ nikamuuliza.‘Mara nyingi alikuwa akienda kunywa na rafiki yake, yule docta, na wakati mwingine akiwa peke yake, alionekana mpweke, na hakupenda kukaa na watu asiowafahamu…’akasema‘Na zaidi ya huyo docta ni nani wengine alipenda kunywa nao…nikimaanisha wanawake labda?’ nikauliza‘Kiukweli hao hawakosekani, wakiwa kwenye makundi, …lakini haikuonyesha wazi kuwa ana rafiki wa kike wa kupitisha naye muda…’akasema‘Hakuna mwanamke ambaye alikuwa naye karibu sana..hakuna hata mmoja..?’ nikauliza‘Mwanamke ambaye mara nyingi anakuwa naye karibu ni rafiki yako, huyo anayesoma huko nje, yeye mara kwa mara walikuwa wakionekana naye, najua hata wewe mwenyewe unalifahamu hilo, ni hata mkiwa wote yeye anakuwepo, au sio, huwezi kumshuku vibaya..na wengine ni wafanyakazi wake, au wa ofisi anayoifanyia kazi...’akasema.‘Je mume wangu hakuwahi kumsindikiza rafiki yangu huyo hadi kwake,, na hata kuingia kwake, na hata kukaa kwa muda mrefu wa kutilia mashaka, au japokuwa kwa muda mfupi?’ akaulizwa.‘Ndio, mara nyingi tu, huwa wanamfikisha kwake, na kuondoka, kuna muda wanafika na kukaa humo kwa kipindi kirefu tu, kwa vile ni rafiki yako, hatujaona kama kuna lolote baya, sizani kama wanaweza kuvuka mipaka, ulisema wewe unamuamini kwahiyo hata sisi tumechukulia hivyo....’akasema‘Kwa uchunguzi wako, hakuna dalili zozote za mahusiano ya kimapenzi kati ya rafiki yangu, na mume wangu,..?’ nikauliza‘Hatukiliona hilo…hawajawahi kulionyesha hilo hadharani…, maana hata wakiwa kwenye starehe, walionekana wakijali, kuheshimiana, na mume wako sio mtu wa kufanya mambo ya aibu anajichunga sana, kama alivyo rafiki yako, hatukuweza kulibaini hilo…’akasema.‘Na huyo rafiki yangu hakuwa na mahusiano na mdogo wa mume wangu..?’ nikauliza‘Kwa uchunguzi wetu, yaonekana rafiki yako hayupo karibu sana na huyo shemeji yako, na yaonekana kama hawaelewani kina namna fulani, kwahiyo haiwezekani wakawa wapenzi....’akasema‘Haiwezekani, ina maana mume wangu hakuwa na rafiki mwingine wa kike.....sasa huyo mtoto ninayesikia anaye ni kutoka kwa mwanamke gani?’ nikauliza‘Mtoto…mmh, hapana, ..kwa uchunguzi wetu, ....hilo halikuweza kuonekana, kwani kama ulivyotaka, ni kuwa tuchunguze bila kuweka tetesi, tuwe na uhakika na hicho tulichokifanya, na sisi hatukuona au kugundua mwanamke mwenye mahusiano na mume wako…’akasema‘Na ni kweli mumegundua kuwa hana mtoto nje…?’ nikauliza‘Hilo hatujaligundua, hatuwezi kusema kitu ambacho hatuna uhakika nacho kama ulivyotaka..kama unataka tulifanyie kazi hilo, kuwa kama ana mtoto nje, tunaweza kulifanyia uchunguzi, lakini kwa mipaka uliyotuwekea sisi hatujagundua chochote kuhusu mtoto wa nje…’akasema‘Sawa, ndivyo nilitaka,…sikutaka hayo myafanyie kazi, kama kesi, hakuna kesi hapa ni kutaka kujirizisha tu,..ila kuna kitu nataka unifanyie, nenda huko alipojifungulia huyo rafiki yangu uone kama utagundua baba wa huyo mtoto wake, je alizaa na nani, unaweza kulifanyia kazi hilo…?’ nikamuuliza‘Naweza bosi…’akasema‘Unajua …awali sikutaka ulifanye hilo, sasa kalifanyie kazi, na pili, utafute kama kweli mume wangu ana mtoto nje, mmh, yah, lakini usifanye kuonyesha mimi nataka kulifahamu hilo, chukua muda, unanielewa…’nikasema‘Sawa nakuelewa bosi, ila kuna kitu, nilitaka kukuambia,....ila wewe ulisema tusihangaike sana na rafiki yako na ..na…’akasita kidogo‘Niambie ni kitu gani…?’ nikauliza‘Ulisema haina haja ya kumchunguza rafiki yako, na ulisema kuna mwanaume aliwahi kufika hospitalini,..wa kwanza, kuna kitu kama hicho, ila ulisema haina haja ya kulichunguza hilo, lakini kwa uchunguizi wetu mwanaume wa kwanza kumtembea pale hospilaini alikuwa ni mume wako, hakuna mwingine …..’akasema.‘Unasema kweli,…haiwezekani, mbona rafiki yangu alinificha hilo.., na hata mume wangu, mmh..hapa kuna kitu,..una uhakika na hilo..!?’ nikauliza kwa mshangao‘Ndio…nina uhakika na hilo…’akasema na alitaka kuongea jambo, lakini mimi nikamtiza kwa swali jingine‘Je vyanzo vyenu viliwahi kumuona mtoto wa rafiki yangu, kisura,..anafananaje?’ akaulizwa‘Ni kitu ambacho wengi wetu waliona ni ajabu, kwani mtoto huyo amekuwa akifichwa sana, hajawahi kuonekana sura yake na mtu yoyote....’akasema‘Haiwezekani, ina maana na ujanja wenu wote hamkuweza kuiona sura ya huyo mtoto wake, hajawahi kupiga picha, ?’ nikawauliza‘Unamfahamu sana rafiki yako huyo, kazi za uchunguzi, ulinzi na usalama anazifahamu sana, na akiamua kufanya jambo, analifanya kwa makini sana, nahisi hakupenda kabisa mtu kuiona sura ya mtoto wake…’akasema‘Mhh..haiwezekani, kwahiyo nyie hamjafahamu yupo je…?’ nikamuuliza‘Wengine wanasema ana sura ya kihindi, wengine ana sura ya kizungu,…sasa hatujui kwakweli, nahisi basi atakuwa akimvalisha vitu ambavyo huwezi kabisa kugundua sura ya mtoto ya asili, nahisi alikuwa akimvalisha nywela za bandia hata sura za bandia....’akasema.‘Sura ya kihindi, hahaha..hapana mimi nimemuona ni mwafrika kabisa…’nikasema‘Ndivyo watu waliobahatika kumuona wanadai hivyo…’akasema‘Unahisi ni kwanini amefanya hivyo....?.’nikawauliza‘Huenda hataki baba wa mtoto huyo ajulikane, au huyo baba amfahamu huyo mtoto kuwa ni wake...’akasema‘Kwanini?’ nikamuuliza‘Huenda ni kuogopa kashifa... Au yeye mwenyewe rafiki yako hataki baba wa mtoto huyo afahamu kuwa ni mtoto wake....’akasema.`Nashukuru, huenda nikakuhitajia tena, endelea na uchunguzi....’*******Baadaye alikuja mtu ambaye nilimpa kazi ya kuchunguza kifo cha Makabrasha, yeye aliwahi kufanyia kazi za upelelezi, lakini kwasababu za kiafya akaacha kazi, ..na hata alipopona hakutaka tena kuirudia hiyo kazi, akawa anafanya kazi hiyo binafsi, na yeye akatoa taarifa yake.‘Kifo cha Makabrasha, kimefunikwa kiaina, nahisi hata polisi walishachoka na tabia ya huyo mtu, na waliona kufa kwake ni bora tu, japokuwa walifanya juhudi ya kumtafuta muuaji, lakini hawakufika popote, wakahitimisha walivyoona wao....’akasema‘Kwanini unasema hivyo?’‘Kwasababu ya matendo ya marehemu, kwani alifikia hatua ya kuwawekea hata hao polisi mitego, akiwanasa kwenye mambo yanayoenda kinyume na maadili ya kazi zao, anawarekodi, na huja kutumia kumbukumbu hizo kuwatishia, kuwa wakifanya lolote na yeye atawalipua, kwahiyo hata wao, wakawa hawana jinsi, ila kufuata anavyotaka yeye....unaona eeh..’akasema‘Kwahiyo unataka kusema nini?’ nikamuuliza‘Ninachotaka kukuambia ni kuwa ukweli wa kifo cha Makabrasha hautaweza kugundulikana kiraisi unaweza ukaweka shaka shaka kuwa huenda hata hao watu wa usalama wanajua kitu fulani,lakini hawataki..kiukweli, haipo wazi, na hata wao hawajachukulia kifo chake kwenye uzito wake...’akasema‘Haiwezekani, ina maana watu wa usalama wanaweza kuhusika..hiyo dhana unaiwekaje hapo…?’ nikauliza‘Sijasema wanaweza kuhusika, ila wanaweza kujua jambo..unielewe hapo..’akasema‘Sasa ni nani anaweza kuhusika kwa uchunguzi wako, sizani kama muuaji anaweza kupotea hivi hivi..?’ nikauliza‘Huyo muuaji aliyefanya hayo mauaji, ni mtu ambaye alijua ni nini anakifanya, na inaokena sio mauaji ya kukurupuka, ni mtu alijiandaa kwa muda mrefu, huenda alikuwa kwenye hilo jengo, siku mbili kabla akimvizia..’akasema‘Kwa vipi…?’ nikauliza‘Ni lazima huyo mtu awe anafahamu taratibu zote za marehemu, ratiba yake, na..anafahamu mfumo mnzima wa mawasiliani, na mfumo wa jengo na ofisi ya Makabrasha...’akasema.‘Mapka kufahamu mfumo, ina maana basi anaweza kuwa alihusika na ujenzi wa hilop jengo au..?’ nikamuuliza‘Anaweza asiwe ni mjenzi, badi ni mtu aliyelisoma hilo jengo…maana ukisema ni mjenzi wa hlo jengo, huyo jamaa tunamfahamu, na kwa muda sasa wapo mikoni kuna ujenzi wanafanya huko, lakini wanaweza kuuza siri za mjengo huo,..huyo mtu aliyefanya hayo mauaji sio wa kawaida, ni mtaalamu kweli kweli.....kwani kwa jinsi alivyoingia, na kwajinsi alivyoweza kusoma mfumo wa mawasiliano, na mtandao uliokuwa umewekwa humo ndani,, ...sio mtu wa kawaida....’akasema‘Haya niambie kutokana na uchunguzi wenu Makabrasha aliuwawa kivipi, na kwanini?’ nikamuuliza‘Huyo mtu inawezekana alikuwepo humo ndani kwa siku mbili kabla, kama nilivyosema, na silaha aliyoitumia, itakuwa ililetwa usiku wake, na ikaingizwa kwa kupitia nyuma ya ukuta....’akasema‘Kwanini unasema hivyo..?’ nikauliza‘Kwasababu kama ingelipitia kwenye njia ya kawaida, kupitia mlangoni, ...kungelitokea milio ya kuashiria hivyo.....kuna mfumo mle ndani, wa kugundua kuwa mtu kabeba kitu cha hatari, kuna mfumo wa kuchukua kumbukumbu za matukio, ina maana kila anayeingia ataonekana,..lakini cha ajabu siku hiyo ya tukio, hayo yote hayakuonekana kwenye mtandao uliowekwa humo ndani...’akasema.‘Ili uingie kwenye jengo hilo kuna njia moja tu, na ukishaingia kwenye jengo, ili upande juu, kuna njia moja tu, na huko kote waliweka vinasa matukio na sauti,..hebu fikiri, kote huko hakukuonekana hilo tukio, kumefutwa kabisa..ina maana huyo mtu hakutaka kabisa kuonekana chochote siku hiyo..‘Na ina maana basi hata kama huyo mtu aliingia na silaha, ...labda akamuhonga mlinzi, lakini angelipita wapi na hiyo silaha, kwasababu mawasiliano ya kudhibiti hiyo hali ipo sehemu ya siri, huko juu, ...inawezekana basi walinzi wawe wamekula njama,...’akasema‘Si ndio hapo hata mimi nashindwa kuelewa na kwanini polis wasimkamate hata Yule mlinzi, wangembana nahisi angeweza kuwafahamisha jambo..’nikasema‘Alikamatwa, lakini hawakuweza kupata chochote kutoka kwake…’akasema‘Pale mlangoni huwezi kuingia na silaha, pamoja na kukaguliwa na mlindi lakini pia kuna mtambo,...mtu akipita silaha, kuna kelele za kuashiria hatari, na hizo kelele, zingelijulikana kwa watu wote, pale huwezi kuingia na silaha mle ndani kabisa,....’akasema.‘Sasa hiyo silaha iliingiaje humo ndani…?’ nikauliza‘Hiyo silaha itakuwa ilipitishwa nyuma ya jengo, na walichofanya ni kutengeneza kamba ndefu, iliyoshuka hadi chini, na mtu aliyekuwa chini, akaifunga ile silaha kwenye hiyo kamba, na huyo aliyekuwa juu, akavuta hadi juu, na kuhakikisha, haipiti sehemu zenye kuhisi au kugundua kitu cha hatari..na huenda kwa muda huo, huyo mtu alikuwa keshazima viwambo vya hatari vya ndani....’akasema.‘Mtu huyo asingeliweza kuzima viwambo hivyo kwa jengo zima, walinzi wa chini wangeliona hilo, na wangeliweka kwenye taarifa zao, hakuna taarifa kama hiyo, na hata tulipojaribu kufanya uchunguzi kwa watu hao, haukukuwa na dalili zozote kama hizo siku hiyo...’akasema‘Kwahiyo muuaji, atakuwa alikuwa ndani, na muda ulipofika, akafanya kazi yake kirahisi, akaondoka..na cha ajabu basi hata tukio lenyewe,hilo la mauaji halipo...polisi wanadai kuwa walioona baadhi ya sehemu ya tukio hilo, lakini sio kweli..hakuna kitu kama hicho,...kuna mtu aliyekuja kuondoa kila kitu...cha siku hiyo, na huyo mtu alifahamu ni nini anakifanya , ...’akasema.‘Kwahiyo hamkuweza kugundua lolote, kwa njia zenu, kuwa huenda mtu fulani anaweza kuhusika?’ nikamuuliza.‘Huyo aliyefanya hivyo ni mtaalamu, kweli..hatukuweza, na kwa vile polisi wenyewe wamesalimu amri na kuona kuwa ni kifo cha kulipiza kisasi, mimi naona haina haja ya kuhangaika sana..ila kuna kitu ninachoshangaaa,...’akasema‘Kitu gani....?’ nikauliza‘Siku ile ya tukio, kuna watu wanasema kuna mtu, japokuwa alijibadili, lakini anafanana na mume wako kimaumbile’akasema‘Unataka kusema nini hapo?’ nikamuuliza‘Mume wako alikuwepo kwenye hilo jengo, wakati tukio hilo linafanyika, na polisi hawakuligundua hilo, ..kama wangeligundua hilo, nina imani kuwa mume wako angelikuwa hatarini, wangemshika....mimi nilijaribu kufanya uchunguzi wangu, na hata kuongea na mume wako, lakini hakutaka kutoa ushirikiano...je kuna njia yoyote naweza kuongea naye,...?’ akaniuliza.‘Hapana, haina haja, inatosha....’nikasema.‘Lakini nina uhakika sio yeye aliyefanya hayo mauaji, ila nahisi atakuwa anamfahamu huyo muuaji....’akasema‘Kwanini unasema hivyo?’ nikamuuliza‘Mume wako sio mtaalamu sana wa kutumia silaha, huyo muuaji, anafahamu kutumia silaha, na alifahamu wapi pa kulenga, ...ni mtaalamu kweli kweli, na alijua akilenga wapi mtu haponi....na kwahiyo huyo mtu atakuwa kapitia jeshi au kitu kama hicho, sio raia wa kaiwada tu..ni mtu anayefahamu ni nini anakifanya.’akasema‘Nashukuru kwa taarifa yako....’ nilisema hivyo, na sikutaka kujua zaidi,…na hasa niliposikia kuwa mume wangu keshagundulikana kuwa alikuwepo humo kwenye jengo, na ina maana hata polisi watakuwa wameshagundua, sasa ni kwanini hajamkamata…Nilihitajia muda wa kuliwazia hilo, na huyo jamaa akawa anataka kuondoka, halafu akasema;‘Yule mdada, rafiki yako…unamuamini sana…?’ akauliza‘Kwanini…?’ nikauliza‘Nakuuliz tu…kuna kitu nimekigundua, nitakuja kukuambia, lakini kwa hivi sasa bado sijamuelewa, ndio ni mtu wako wa karibu, lakini…kuna kitu simuelewi..mbona walikuwa karibu sana na marehemu…’akasema‘Kwa vipi…?’ nikamuuliza‘Kuna matukio mbali mbali wameonakana wakiwa pamoja, wanaongea, na mara nyingi, rafiki yako anakuwa hayupo wazi kuonekana, ina maana wanaongea kwa siri, na hataki watu wafahamu kuwa anawasiliana na huyo marehemu…’akasema‘Kwani siku hiyo ya tukio walionekana na marehemu…?’ nikauliza‘Ndio..lakini kwa njia hiyo hiyo…’akasema‘Unahisi yeye anaweza kuwa muuaji…?’ nikauliza‘Sijasema hivyo, na wala haijagundulikana hivyo,…na hawezi kufanya kosa hilo.. lakini ngoja nilifanyie kazi, nipe muda,…’akasema‘Nauliza hivi, kwa hisia zako mpaka hapo anaweza akawa ndiye muuaji..?’ nikauliza na huyo jamaa akaanza kuondoka, baada ya kutikisa kichwa tu,.. hakusema neno.WAZO LA LEO: Dhana mbaya, au tetesi zisizo kuwa na uhakika, zaweza kukushinikiza kufanya jambo lisilo faa, tuweni makini sana na dhana, au mambo ya kusikia, hasa atika dunia hii ya utandawazi, ukisikia jambo, au kusoma jambo, lihakiki kwanza ukweli wake, kabla hujasema neno, au kabla hujaamini ukweli wake, fanya uchunguzi kwanza, ili kujiaminisha, usikimbilie kushutumu au kutoa kauli zenye kuumiza, kulaani au kuhukumu watu wengine.Tukumbukeni ulimi na kalamu(mitandao) inaweza kuwa ni chanzo cha fitina mbaya kwa jamii, tuweni makini sana kwa hili, siku ya hukumu kila kitu tutaulizwa, na kwanini tuwe sababu ya kuumiza wengine,..maandishi tu yaweza kuua, yanaweza kutesa nafasi ya mtu na huwezi kujua ni namna gani mtu huyo ataumia, mauimvu thamani yake ni kubwa sana, utawezaje kuilipa hiyo. Tumuombe mola wetu atusamehe na atupe hekima ya kuandika membo yenye maana kwa jamii..!Baada ya kuongea na watu wangu, nakuona hakuna kingine cha maana, nia ilikuwa kama nitapata kitu kingine cha ziada, lakini sikufanikiwa, zaidi ya yale ninayoyafahamu mwenyewe,…baadae, nikaona nitoke ofisini, nia ilikuwa kurudi nyumbani, nikapitia kwa fundi wa gari langu, nikamuachia ili lifanyiewe service, nikachukua bajaji, hadi kukaribia nyumbani kwangu.‘Kabla sijapita kwangu nikachungulia ndani kwa docta, nikaona gari lake lipo, sijui kwanini leo yupo nyumbani, nikaona kama jirani mwema ngoja nimsalimie tu.‘Bajaji nisimamishe hapa..chukua pesa yako, inatosha..’nikampa pesa yake na kwaharaka nikatoka kwenye bajaji na kuingia kwa docta, geti lilikuwa wazi, sikuona mtu nje, nahisi hata mfanyakazi wao hayupo…na wakati huo nikakumbuka maneno ya mtu wangu alipokuwa akitoa taaarifa….Yeye hata wakati ukiwepo alikuwa akifika kama alivyofika kipindi hiki…yeye hufika kwa minajili ya kikazi, akifuatilia malipo yake ya matibabu ya wagonjwa, ya wafanyakazi wako, na mara zote alizofika alikuwa akiishia mapokezi…’‘Ngoja niongee naye tu, lakini nina imani hana zaidi cha kunisaidia…’nikasema wakati huo nimeshafika kwenye mlango, nikagonga..‘Fungua mlango upo wazi…’ilikuwa sauti ya docta Ninajua kuwa mke wake hayupo, kwahiyo sikuwa na mashaka ya kuwasumbua, maana muda kaam huo wanakimama wengi wapo na pilika pilika za kuwajibina na familia zao kwa maandalizi ya usiku, ..Nikaingia ndani, …alikuwa kalala kwenye sofa, akionyesha katingwa na mawazo, na nahisi alikuwa kachoka kutokana na kazi zake za kuwatibu wagonjwa,..alikuwa akiangalia…aliponiona kuwa ni mimi, akashikwa na mshangao, akasimama, tabasamu kwa mbali mdomoni..‘Niambie hamna tatizo..maana nimechoka kweli..kuna tatizo..?’ akaniuliza akionyesha mashaka na kweli hata kusimama ilikuwa yaonyesha kachoka.‘Nimekuja kwako mara moja, kuna maswali machache tu nataka unisaidie kunijibia, kama hutojali...’nikasema‘Ok, afadhali…uliza tu zilipendwa wangu…, lakini ukumbuke tulishakubaliana, kuwa mimi sihitajiki tena kwenye mambo yenu wewe na mume wako au sio, hata mume wako alinijia juu sana, akanisema kuwa mimi nachangia kuivunja ndoa yenu, kwahiyo nimeona bora niwe mbali nanyi kidogo…’akasema akijihami‘Ninachotaka kusikia kwako ni ukweli, ukiniambia ukweli, aah, mimi sina shida na wewe,...tatizo wewe huwa unanificha mambo ukijidai kuwa unanijali, kunijali gani huko, wakati unaona naharibikiwa katika maisha yangu…’nikasema‘Ukweli gani unautaka kutoka kwangu shemeji, kuwa mkweli na wewe kwangu, nimejaribu kila niwezevyo, mlitaka mimi nifanye nini, eeh, niambieni..?’ akaniuliza.‘Nataka kufahamu kuwa je ni kweli kuwa mume wangu ana mtoto mwingine nje..nina uhakika unalo jibu lake…niambie ukweli, ili nikuache upumzike,...?’ nikamuuliza‘Unarudi kule kule...nakuomba utoke tu, kiukweli hapa nimechoka, kulikuwana kazi kubwa sana,..na akili yangu yahitajia, kitu cha kuniliwaza sio kunitesa…’akasema‘mpigie simu mkeo aje…kwanini unamuacha anakaa kipindi kirefu huko, utaibiwa…’nikasema‘Hahaha…nitaibiwa, akitaka siwezi kumzuia,..ndoa ni mwanandoa mwenyewe, hakuna mtu wa kumchunga mwanandoa zaidi ya yeye mwenyewe…’akasema‘Ni kweli ndio maana nimekuja kwako, kwani unaweza ukawa na nadharia hiyo kichwani lakini mwenzako akakuchezea shere…je ni kweli mume wangu ana mtoto mwingine nje…ya ndoa..?’ nikauliza‘Shemeji, haya ni matokea ya maisha yenu,…na sina jibu la swali lako, ila nina maelezo ya kukumbusha tu, kuwa hayo unayowaza, hiyo hali inayokusumbua ni matokea ya maisha yenu wenyewe…’akasema‘Unajichelewesha mwenyewe, hutaki kupumzika…’nikasema‘Ni lazima nikuambie hili, kuwa..nilishakuambia kuwa mume wako, alifikia kubadilika kutokana na jinsi mlivyokuwa mkiishi..sasa mimi sijui, huenda labda alikuwa na mahusiano na mwanamke mwingine, ila mimi simfahamu…’akasema akinyosha mikono ya kujitoa hivi.‘Nasubiria jibu…’nikasema‘Unajua ni hivi, mwanzoni nilihisi huenda mume wako kabadilika na kuanza kujiingiza kwenye mahusiano ya nje,lakini baadaye, nilipochunguza sana, nikaona kama hakuna ukweli ndani yake, huenda, kama waliwahi kufanya hivyo, basi ilikuwa ni bahati mbaya tu...’akasema‘Ilikuwa bahati mbaya, kwa nani, hiyo kauli inaonyesha kuwa unamfahamu mtu aliyekuwa karibu na mume wangu,…kwahiyo nastahiki kuupata ukweli kutoka kwako, je ni kweli kuwa mume wangu ana mtoto nje ya ndoa, ni nani huyo, ?’ nikamuuliza‘Nimekuambia kama iliwahi kutokea hivyo, mimi sikuwahi kuona, na kama ilitokea, basi ni siku mimi sikuwepo, kwasababu mimi nisingelikubali hilo litokee, unajua jinsi gani ninavyokujali…’akasema‘Kwahiyo zile tetesi zako za awali, sio za kweli,…?’ nikamuuliza‘Tetezi zipi hizo…?’ akauliza‘Kuwa huenda mume wangu ana mahusiano nje…’akasema‘Niliwahi kukuambia hivyo!! ? …hapana ulinichukulia vibaya, mimi nakumbuka kuwa nilikuonya tu , kuwa kwa mienendo yenu, kwa tabia zenu, za kuwa hata mkirudi nyumbani mnajifanya mpo bize, hamjali hata ndoa zenu ipo siku mume wako atakwenda kutembea nje ya ndoa, wewe si hujali, unajifanya huna hisia, sasa wanaume wengu kuvumilia ni shida, nilikuambia hivyo, au….’akasema‘Na kwanini kila ukiwepo,…hasa kule hospitalini, kila nikitaka kumuuliza mume wangu aniambie ukweli, ulikuwa unamzuia, ni kama unafahamu jambo, lakini hukutaka mume wangu aniambie ukweli, ni kitu gani hicho, niambie ukweli, kwani baada ya hapa, naweza tusiwe na urafiki tena mimi na wewe…?’ nikamuuliza‘Kwa kipindi kama kile, mimi kama dakitari, pia mimi kama rafiki yenu mkubwa, nilijitahidi kuzuia madhara, kwa mumeo na kwako, nakufahmu kama nilivyomfahamu mume wako, haikuwa na haja ya kuongea mambo yanayoweza kuamusha hisia na matokea yake yangelikuwa mabaya, ..’akasema‘Hahaha..hata sikuamini, …kwanini lakini…’nikasema‘Na ningekuzuiaje usiongee na mume wako wakati mpo naye siku zote…’akasema‘Na kwanini ulimshuku rafiki yangu kuna anaweza akawa na mahusiano na mume wangu..bado nahisi wewe una ukweli hutaki kuaniambia,…niambie kama kweli wewe unanijali..?’ nikamuuliza‘Awali nilikuwa na shaka hiyo...lakini nimekuja kufanya uchunguzi nikaona hilo halipo, na kama lipo,…mimi sijui, labda lilifanyika kwa siri kubwa sana, nimeongea na rafiki yangu, nikamuomba aniambia ukweli...hajataka kuniambia ukwelina tukaishia kukwaruzana, mpaka ananipiga marufuku ya kufika kwako, uelewe hali ilipofikia hapo…’akasema‘Kwa kukukataa kwa mume wangu kukuambia ukweli ndio umerizika kuwa ni kweli hakuwa na mashusiano ya yeye, au unaogopa kusema kwa vile mumekwaruzana na mume wangu…?’ nikamuuliza‘Pamoja na hilo, lakini kwa juhudi zangu nyingine nimeona hakuna kitu kama hicho, na mtoto wa rafiki yako, wengine wanasema ana sura ya kizungu, wengine mwarabu, sasa mume wako ni mwarabu, …kwakweli, baada ya yote hayo, nimeona niachane na nyie, mpaka hapo mtakaponihitajia…’akasema‘Swali langu ni hili, Je ni kweli mume wangu ana mtoto nje..nijibu tu kwa kifupi, ili niondoke zangu?’ nikamuuliza‘Mimi sijui, kwasababu hajawahi kuniambia hivyo...’akasema‘Una uhakika na hilo…?’ nikamuuliza‘Siwezi nikasema nina uhakika na hilo, je kama anaye, na mimi sijui, ukaja kugundua uaminifu kwangu kwako utakuwaje, nakushauri tu, hujachelewa, kwanini usimuulize kwa staha akuambie ukweli yeye mwenyewe…’akasema.‘Mara nyingi unamkinga rafiki yako,…sasa unasikia, kama nikija kugundua kuwa ana mtoto nje utasemaje, ..maana kama anaye nina uhakika wewe unalifahamu hilo, ina unamficha siri rafiki yako, lakini kwanini hujiulizi na mimi je..itaniathiri vipi, je inaathiri vipi familia yangu, umejiuliza hilo…’nikasema‘Kwa hali ile mliyokuwa mkienda nayo, na kwa tabia yake ile ya kulewa, kupitiliza, hilo siwezi kuona ni ajabu....kama nilivyokuambia awali, kwahiyo kama nikujilaumu jilaumu wewe mwenyewe,…....’akasema‘Kwahiyo wewe huwezi kuona ajabu kuwa yeye ana mtoto nje, ndivyo mlivyo wanaume, je ni sahihi kufanya hivyo, je mimi ningelikuwa hivyo, mgelikubaliana na hilo…?’ nikauliza‘Kwanini unaniuliza maswali hayo, kuna nini kimetokea shemeji hebu niambie ukweli…?’ akaniuliza‘Mimi ninachotaka ni ukweli tu…’nikasema‘Ukweli mimi sina..na zote hizo ni shaka shaka tu, na shaka shaka, zimekujaje kwako, wakati hupendelei tabia hiyo, usiige tabia hiyo utajitwika mzigo kabla haujatua kichwani mwako, utajiumiza mapema, kaeni wawili muongelee matatizo yenu yaishe…’akasema‘Yataishaje wakati kuna matatizo mengi ambayo, nahitajia maelezo yake, yatakiwshaje wakati kama huu ambapo kuna mambo ya kuharibu kila kitu,.., kuna njama za kuhakikisha kuwa mali za familia zinachukuliwa na watu wengine, mimi sijui, na ni nani kaidhinisha hilo…’nikasema‘Mhh..kwahiyo tatizo ni wasiwasi wa mali, au sio…?’ akauliza‘Kutokana na mkataba wa kugushiwa, mali itagawiwa kwa watoto wa nje, kwa wtoto wa marehemu pia, na huyo mtoto wa nje ana haki sawa na watoto wetu…hayo kayaidhinisha nani,…mkataba wa kugishiwa unasema hivyo,…haya sawa, je ni kweli yupo huyo mtoto wa nje, mbona siambiwi ukweli, je kweli sina haki ya kulifahamu hilo….sio kwamba natetea mali, nataka kulifahamu je hiyo sio haki yangu….’nikasema‘Hapo mimi siwezi kukusaidia kabisa, mkataba mliweka wewe na mume wako na wakili wako, au sio…hao ndio wa kupambana nao, na wala usiwarushie watazamaji mpira ukategemea kuwa watakusaiaid kufunga magali,..huo ni mchezo wako, cheza na mumeo au nimekosea hapo…?’ akauliza‘Najua sasa utajiweka pembeni, ufurahia ndoa ikisambaratika, si ndio ulichokuwa wewe unakitaka, sawa, nitaucheza huo mpira mwenyewe, ..tatizo ni mkataba wangu upo wapi…’nikasema‘Kwani ulikuwa haukusajiliwa..?’ akaniuliza‘Ulisajiliwa na kwa taratibu zote kabisa..lakini sijui kilichotokea, ukaja kubadilisha, kila sehemu husika,..hata nakala yangu ya halali, ikapotea na kuwekewa nakala ya bandia,..’nikasema‘Hata huko kwa mdhamina …haiwezekani…’akasema‘Ndio hivyo…’nikasema‘Kiukweli kutokana na majukumu yangu kuwa mengi, niliacha kabisa kufuatilia mambo yako, na hata wazazi wako wamesema tuachane na familia yako,kwa vile nawe umezidi kiburi, wanakuangalia tu, wameshasema utaweza mwenyewe na uskishindwa utawatafuta…’akasema‘Sijashindwa bado…ila kuna hayo yaliyozuka kuwa mume wangu ana mtoto nje…hilo linanifanya niwe na wakati mgumu, na hataki kuniambia ukweli,..na kila hatua anazidisha matatizo, je nitaishi na matatizo haya mpaka lini, je nitaweza kuyavumilia…’nikasema‘Nikuulize tu swali, Je kama ni kweli..unielewe hapo, mimi sijui, ila nauliza tu je kama huyo mtoto yupo utafanyaje…?’ akaniuliza‘Kwanza nikufahamu ukweli,..hiyo ni haki yangu ya msingi,..kwasababu kama ni kurithi mali, hiyo mali, tumechuma wote..na mali hiyo imetokana na wazazi wangu, je ni haki kuitoa kwa watu baki, bila maelezo…sasa mimi nitafanyaje, hilo tulishawahi kuongea mimi na mume wangu,kutokana na hali ilivyo, ndio tukakubaliana kuwe na mikataba..kwahiyo kwangu haina shida, sheria itafuta mkondo wake…’nikasema‘Na huo mkataba mpya unasemaje kuhusu hilo…?’ akaniuliza‘Siutambui,..najua wameweka vipengele vya kujilinda, haina haja ya mimi kuupekenyua sana, haunihusu …’nikasema‘Lakini mimi bado nina mashaka, maana hilo la mtoto wa nje, mara nyingi halina siri, watu hawawezi kulivumilia hilo, kama kweli angelikuwepo, hiyo taarifa iingeshavuma, ni kwanini iwe siri kihivyo...’akasema.‘Ndio maana nilitaka kuufahamu ukweli kutoka kwako, maana mpaka inatokea hisia hizo, ina maana kuwa mume wangu alikuwa na mahusiano na mwanamke fulani, sasa kazaa naye au sio yeye, bado haijasaidia kuuficha ukweli kuwa mume wangu alikuwa akitembea nje ya ndoa, au sio...?’ nikamuuliza.‘Kutokana na ulevi wake, yote yawezekana, ila nasema ukweli kutoka moyoni, kama ilitokea hivyo, basi siku hiyo mimi sikuwepo, kwa ushauri wangu shemeji, kuliko kujiumiza kihivyo, naona hilo achana nalo, litakupotezea muda, na mawazo mengi bure, kama yupo yupo tu....’akasema‘Sasa hapo unataka kusema nini, kama yupo yupo tu, ina maana mimi nikubali tu hivyo kirahisi..na nikikubali unafahamu madhara yake, leo hii watu baki wameshaanza kugombea mali..wanayodhania ni ya baba yao..unahisi sababu ni nini, ni kwa vile watu mnakumbatia haramu…sasa ngoja niupate huo mataba wangu uone nitakachokifanya...’nikasema.‘Mimi sijakumbatia haramu , mimi sijaunga mkono hayo, najua ni makosa, lakini ni nini chanzo cha hayo makosa, usije ukawa wewe ndio chanzo…’akasema akiangalia saa yake‘Nikuulize swali hili, halafu niondoke zangu, awali ulisema kuwa utafany auchunguzi kugundua baba wa mtoto wa rafiki yangu, je uliwahi kuufanya…umegundua baba wa huyo mtoto ni nani..?’ nikamuuliza.‘Hiyo imekuwa ni siri ya hali ya juu, na hata nilipokwenda kumuuliza dakitari aliyehusika naye siku ile sikuweza kupata lolote, hilo limekuwa siri kubwa sana,..na ni ajabu kutokea hivyo…lakini sikutaka kulifuatilia sana, kutokana na kauli yako wewe mwenyewe, nikajua huenda umeridhika na hilo, huenda wewe unahusika, nikuulize swali wewe si uliwahi kumuona huyo mtoto, je sura yake ipoje,....?’ akaniuliza.‘Sura yake ipoje,!!!..haiwezi kunipatia uhakika wa swali langu maana sura yake inaweza kufanana nay a watoto wangu, ya watoto wa shemeji, ya….kwahiyo hilo bado halileti jibu sahihi…’nikasema‘Kama ni hivyo, kwanini uumize kichwa chako, kumbe jibu unalo tayari, muhimu kwa sasa ni kumbana mumeo, au sio….tafuta njia ya kumfanya mumeo aongee, nina imani huwezi kushindwa hilo, au ..unahitajia msaada wangu…?’akasema na kuuliza‘Kirahisi hivyo, unajua kilichotayarishwa na mume wangu,…tatizo sio hilo tu, ni baada ya kukubali hilo,…na hayo makubaliano ya kuwa haki ziende huko, kwanini mume wangu hakunishirikisha,…huo mkataba mpya ni wa nini…na kwanini hadi familia za marehemu zihusike, huoni kuwa kukubali kwangu kutaharibu mengi…’nikasema‘Mhh…hapo kuna kazi..lakini..kama ni kweli, utafanyaje sasa, utavunja ndoa yako…?’ akauliza‘Hayo sio muhimu kwangu kwa hivi sasa… , muhimu kwangu ni kuufahamu ukweli kwanza…na pili muhimu kwangu ni kuwa na huo mkataba wetu wa asili, basi, baada ya hapo kila kitu kitajimaliza chenyewe, na matatizo yataisha..swali ni kwanini ukweli unafichwa, kuna nini kimetayarishwa, mume wangu anaogopa nini…’nikasema‘Jibu ni tahisi tu…anaogopa huo mkataba wenu wa awali…’akasema‘Ok…nimekuelewa…’nikasema‘Mimi nakushauri hivi, kwa vile mume wako kajirudi, ..achana na mambo hayo, ya kumchunguza chunguza sana…kwasababu hilo limeshamuweka kubaya, sasa hivi anatapa tapa..na huwezi kujua zaidi ya hapo ana malengo gani…’akasema‘Kwahiyo..?’ nikauliza‘Yavutie subira, kubali kwanza kwa nia ya kuupata ukweli, baada ya hapo, utajua mwenyewe la kufanya…’akasema‘Huo ni mtego…mimi siwezi kujiingiza kwenye mtego wa tembo..sina uwezo huo…muhimu nitasimamia kwenye ukweli na haki…’nikasema‘Ni sawa, lakini nilikuambia, je kama hayo yote ni matokea ya wewe mwenyewe utasemaje…?’ akanuliza‘Hivi, ..mume wangu ni mtoto mdogo, au hao alioshirikiana nao ni watoto wadogo, hawafahamu njia sahihi…unataka kusema mtu akikuambia ule mavi utakula, kwa vile umeshauriwa na rafiki yako mpenzi…hilo sio swali la kuniambia hivyo, kuwa huenda inatokana na mimi..’nikasema‘Una maana gani..ina maana kuwa kuna mambo yamtokea hapo kutokana na ushauri wako, au…niambie ukweli…’akasema‘Unanipotezea muda wangu swali jingine kabla sijaondoka je wewe uliwahi kuongea na wazazi wangu hivi karibuni?’ nikamuulzia‘Jana tu, nilikuwa na wazazi wako…tulikuwa na kikao kirefu tu mimi na wao…’akasema‘Wanasema nini juu ya hili tukio...?’ nikamuuliza‘Wao wameamua kukuachia mambo yako, ila wanachoogopa ni kuwa mume wako anaweza kukuingiza kwenye kashifa kubwa, wanahisi hiyo iliyotokea ni ndogo tu…wanaweza kuihimili…, lakini baadaye kunaweza kukazuka mambo ambayo hata wao hawatataka kuyasikia..si unamfahamu baba yako alivyo....’akasema‘Kwahiyo wao wanashauri nini?’ nikamuuliza‘Unafahamu msimamo wa wazazi wako toka awali, msimamo wao ni ule ule, hawana imani na mume wako, hilo, sio wao tu, hata wale waliopo karibu na baba yako wanamuonya dhidi ya mume wako,..sasa sijui, ..’akasema na kutikisa kichwa.‘Mhh..najua tu, hayo ni mambo ya kisiasa, na likitokea wanavyotaka wao, bado italetwa ajenda nyingine, …’nikasema‘Unajua kuwa wazazi wako wamegundua kuwa mume wako sio mkweli, na ana tamaa, na anaweza akaharibu maisha yako ya baadaye, kuna kipindi waliniomba niingilie kati, ikibidi, ....ooh, sipendi huo ushauri wao’akasema‘Ikibidi nini..?’ nikauliza‘Wao, wanazidi kusema kuwa ndoa yako na mume wako haifai,…itakuja kukuumiza sana, na huenda, usiwezi kufaidi matunda ya jasho lenu,..mumeo, ana watu wanaomzunguka, na kumtumia yeye kama daraja, …yeye bila kulifahamu hilo anakubali tu,..mwisho wa siku watamtekeleza, kifupi wao, wanaona ni bora, ndop hiyo ivunjwe, kwa masilahi ya kizazi cha baadae,...’akasema.‘Hivi nyie mnaona kuwa hilo jambo rahisi sana...?’ nikauliza‘Ni ushauri wao,..ni ushauri wa marafiki za wazazi wako, ni ushauri wa ….kila mtu mwenye nia njema na nyie… ila hawajataka kukushinikiza kwa vile baba yako yupo kwenye ushindani wa kisiasa…hataki kujiingiza sana kwenye ndoa yako,…’akasema‘Mimi siwezi kulisikiliza hilo kwa vile yule ni baba wa watoto wangu, ...hamuoni kuwa nikifanya hivyo, nitawaumiza watoto wangu, kwanini hamliangalii hilo pia, sio kwangu tu, je kwa watoto wangu, watoto wangu wanampenda sana baba yao..’nikasma sasa nikitamani hata kulia.‘Usijiweke mnyonge kihivyo, sitaki ulie kwa hilo, wewe ni shupavu, pambana, mimi nina imani kuwa utashinda…’akasema‘Hapana inaniumiza sana..nikiona mtu, ambaye niligangaika naye, ili tu atokane na ile hali, nilimpenda nikijua atabadilika, leo hii..hapana..hata hivyo, mimi sitaki watoto wangu waje kuumia, ni kweli hata mimi imefikia hatua natamani nifanye hivyo..lakini kila nikiwaangalia watoto wangu, nakosa amani...nashindwa kuchukua huo uamuzi...’akasema‘Hata mimi, nimeliona hilo,..ndio maana nimekuwa nikipingana na ushauri wa wazazi wako, kama ningelikuwa sijaoa, ningelifanya juhudi ya ziada , na ningafanya hivyo,...hata hivyo, mwisho wa yote ni wewe mwenyewe, kama kosa limetokea, na una uhakika halitajirudia tena basi msamehe mume wako, sio lazima mtu awe kama watu wanavyohisi, yeye kama binadamu anaweza kujirudi na akabadilika....’akasema.‘Tatizo mume wangu hajakubali kuwa mkweli, na ili kuficha uwongo wake, yeye anazidi kuzua mambo mengine makubwa, na makubwa zaidi, ambayo sitaweza kuyavumilia, na nahisi kutokana na hayo mambo makubwa, yatazuka mengine makubwa, na amani kwenye familia itakuwa haipo tena, je nikae tu nivumilie, nivumilia mpaka lini..’nikasema.‘Hayo mambo mengine makubwa ni nini,…ni huo mkataba mpya au…?’ akauliza‘Kuhusu huo mkataba, kuhusu watoto wa marehemu, kuhusu huyo mtoto wake wa nje…asiyejulikana…hayo yanazidi kuongezeka, bado sijamfahamu mama wa huyo mtoto, je atakuja na ajenda gani..bado watoto wa marehemu hawanipi amani…kwanini hivyo….’nikasema.‘Hata wazazi wako wanahisi hivyo hivyo’akasema‘Ina maana wazazi wangu wanafahamu kuwa mume wangu ana mtoto nje?’ nikamuuliza.‘Huwezi kuwaficha wazazi wako kitu, wazazi wako wana macho ya kuona mbali, wana masikio yakusikia kila kinachotokea kwenye ardhi, kukuhusu wewe, japokuwa hawataki kuthibitisha hilo, lakini nahisi wameshaliona hilo, na hilo ndilo linalowafanya wasimwamini mume wako, ...’akasema‘Waliwahi kukuambia au kukuulizia hilo…?’ nikauliza‘Hapana,…hawajasema moja kwa moja, na wao wanakwepa kuliongelea hivyo, najua wana maana yao…ila hilo la watoto wa marehemu kuja kudai hisa,…wamasema wanalisubiria kwa hamu....’akasema.‘Je wao wanataka mimi nifanye nini?’ nikauliza‘Wanasema waliwahi kugundua kuwa wewe una mkataba ambao ukiutumia utaweza kumaliza kila kitu, lakini cha ajabu mkataba waliokuja kuuona wao, hauna manufaa kwako, na ndio baadae wakasikia kuwa mkataba huo sio halali, ulikuwepo mwingine. Na ndio maana hawajui ukweli upo wapi…’akasema‘Ni nani aliwaambia kuhusu kugushiwa kwa huo mkataba je ni wakili wangu nini?’ nikauliza‘Hapana, ni wakili wao....’akasema‘Kwahiyo wakili wao anafahamu mengi kuhusu hiyo mikataba?’ nikauliza‘Sina uhakika na hilo, kwani yule ni mtu wa wazazi wako hawezi kuongea zaidi, yeye anaongea yale wazazi wako wanayotaka aongee, hasa inapofikia maswala ya kifamilia...’akasema.‘Je nitawezaje kuupata mkataba huo wa awali....?’ nikawa kama namuuliza yeye‘Je ukiupata huo mkataba wa awali, unaweza kufanya nini?’ akaniuliza akiniangalia kwa macho ya kunijaribu‘Mkataba wenyewe utaongea, na kiukweli, sijui…sizani,…nasema hivi, safari hii sirudi nyuma, mkataba wenyewe utasema ni nini cha kufanya, kwakeli nimechoka, ....naona sasa basi....na kama ni kweli kuna mtoto nje, ..nitahakikisha nafanya lile lilipo kwenye huo mkataba, sitavunja ahadi yangu kamwe...’nikasema‘Uwe makini lakini.., usije ukafanya jambo ukaja kujilaumu baadae...’akasema.‘Huwezi kubeba mtu asiyebebeka, ...wema wangu usiniponze, ...siwezi kutengeneza maadui kutoka ndani kwa marafiki zangu wenyewe, ni lazima,nijue ukweli, na kama ukweli ndio huo, basi, ni bora nibakie bila marafiki kuliko kuwa na marafiki wanafiki, ambao wananichekea tukiangaliana wakigeuka, wananing’ong’a....’nikasema na kusimama kutaka kuondoka.‘Una uhakika na hilo…?’ akauliza‘Lipi sasa..?’ nikauliza‘Kuwa ukipata mkataba wako wa zamani, hutarudi nyuma, utaacha sheria ichukue mkondo wake..?’ akaniuliza‘Umenisikia au sio, kama ungelikuwa wewe ungelifanya nini hapo…, baada ya haya yote, jiulize tu…nimevumilia mangapi, wangapi wamenicheka kuwa naona lakini najifanya sioni..sasa imetosha,…lakini muhimu ni ukweli, na ushahidi…sitaki mambo ya kuhisi tu..’nikasema nikianza kuondoka, huku machozi yakinitoka natamani kulia...‘Sawa ngoja tuone…ili jikaze usiwe dhaifi kihihivyo, hiyo sio damu ya baba yako..thibitisha hilo kwa vitendo…’akasema na mimi nikawa nipo nje, naondoka zangu, sikusubiria anisindikize kama kawaida yake.********Nilipofika nyumbani, niliona gari la mume wangu, siku hizi anatumia gari jingine, la kampuni yake, nikajua yupo ndani, nikatembea kwa haraka kwenda ndani, akilini nikitaka kuongea naye niufahamu ukweli wote, hilo la mtoto wan je liliniumiza sana kichwa.‘Leo ataniambia ukweli wote…’nikasema nikiingia ndaniNilitaka leo tukae naye kikao, ..sikutaka tena kuzungushana, kama hataki itabidi nichukuea hatua kubwa zaidi, ikibidi niende mahakamani kwa kugushi mkataba, kwa kuvunja kiapo cha ndoa, kwani kwasasa nina ushahidi wa kutosha, na nina mashahidi..Nikaingia ndani, hadi chumbani, sikumuona nikajua yupo maktaba, nikafungua mlango wa makitaba, hakufunga kwa ndani kwani mara nyingi, kama hutaki kusumbuliwa, huwa unajifungia kwa ndani, nikafungua mlango taratibu na kuingia ndani.Mume wangu alikuwa kachuchumaa kwenye kabati langu, ...!Hilo ni kabato langu, na mara nyingi nalitumia mwenyewe, na akitaka kitu huwa nakwenda kukichukua mimi mwenyewe, kwani hana ufunguo wake… na hapo ndipo niliweka ule mkatabaNa nilipotupa macho kwenye kabati ninapoweka bastola, niliona kabati lipo kama limefunguliwa, moyo ukanilipuka, huyu mtu kapatia wapi ufungua, alikuwa hajanigundua kuwa nimeingia, alikuwa kainama akiwa anapekuapekua , ..katoa vitu vingi nje, kuna kitu anatafuta, ...nikavuta subira.‘Mbo-mbo-na haipo ooh….’akasema akijiuliza na sasa akataka kugeuka, kabla hajageuka nikamuuliza‘Unatafuta nini kwenye kabati langu, na ufunguo umaupatia wapi...’nikamshitua, oh...alivyoshituka, nikajua nimeua, nimefanya kisichotakiwa kutokana na afya yake!NB: Mambo yanaanza kujitokeza, wewe unahisi nini hapo…hii ndio ya wikiendi, tujadilikidogo kuhusu hili..je mtoto wa nje ana haki sawa na watoto wa ndani..kama baba akiamua hivyo, je mama hastahiki kufahamu kila kitu, na je akifahamu hatua gani achukue…TUJADILI?WAZO LA HEKIMA: Mnapo-oana,na mkafikia kwenye msigishano ambao unaweza kuleta madhara ya ndoa, mjaribu kuangalia hatima ya watoto wenu, je tatizo hilo ni kubwa sana la hata kuvunjika kwa ndoa yenu, inawezekana ikafikia hapo,na hakuna njia nyingine, kama ni hivyo basi ni bora mkapata ushauri wa kitaalamu ni jinsi gani mnawezaje kuwasaidia watoto wenu, ili wasije kuathirika kisaikolojia....msiwajengee watoto wenu chuki, kwa mama au baba kwa kuwapandikiza uhasama watoto ili tu eti wamchukie baba au mama, hilo ni kosa kubwa sana kwani wao hawahusiki kwenye matatizo yenu na kuwapandikizia chuki hizo mnawajengea tabia mbaye kwenye maisha yao ya baadae Labda nielezee vizuri,... jinsi chumba chetu maalumu, tulichokiita ,maktaba kilivyokuwa,…Kwa vile kila mmoja alikuwa na kampuni yake, na mara nyingi kulikuwa na kazi nyingine ilibidi tuzifanyie nyumbani,kila mtu kwa wakati wake, au siku nyingine tunakutana na kuwemo humo, …Kutokana na hali hiyo, tukapanga kuwa maktaba hiyo ibororeshwe zaidi iwe kama ofisi ndogo ya nyumbani..na kwa vile kila mmoja ana ofisi yake, tukakubaliana kugawanywe sehemu mbili, lakini sio kuwa kuweka uzio kabisa, ni kwa mtindo wa makabati na meza, kutenga huku na kule,..kiukweli tulipatengeneza vizuri sana.Hakuna aliyekuwa akihangaika na sehemu ya mwenzake, labda uamue tu kumtuma mwenzako, kuwa nisaidie kunichukulia kitu fulani kwenye sehemu ya vitu vyangu..sasa kila mmoja akawa anapaboresha sehemu yake kwa jinsi aonavyo yeye.Kwangu nikaongeza kabati moja imara, ukiliona utasema ni meza au kabato la vipodozi na vitu vya kike lakini kwa ndani, nikaongeza sehemu maalumu ya kuweka vitu vyangu vya siri,..ambavyo sitaki mtu aviguse..hata mume wangu sehemu hiyo alikuwa haijui..Anaweza akawa anaifahamu, maana sikuwa namficha sana, lakini hakuwa na habari kabisa na vitu vya kabati hilo.‘Hilo kabati lako la kike kike, sitaki hata kulisogelea,…’kuna siku aliwahi kuniambia hivyoSasa humo ndio niliweka nakala ya mkataba wangu, kwangu mkataba huo ulikua ni moja ya vitu muhimu sana ..nikimaliza kusoma kama kuna kitu nataka kukifuatilia, naurudisha hapo…Kulikuwa na kabati la vitu vya kuchangiana, lakini pia ni maalumu kwa kumbukumbu zetu za nyumbani, hapo kila mtu angeliweza kuweka au kuchukua vitu,lakini mara nyingi,nimekuwa nikilitumia mimi mwenyewe tu na mume wngu hana habari nalo.Lenyewe lina sehemu ya nje na ya ndani, unaweza ukachukua vitu vya nje, bila kujua kuwa kuna sehemu nyingine ya ndani,..sasa sehemu hiyo ya ndani, ndio kuna vikabati maalumu,..humo kuna nyaraka za nyumbani za kuchangia…na kuna sehemu maalumu, ndio kuna sehemu tunaifadhia silaha….Kupotea kwa mkataba wangu, kwenye kabati langu, na mimi mwenyewe ndiye mwenye ufungua, kuliniweka kwenye njia panda, sikutaka hata siku moja kumshuku mume wangu kwa baya lolote lile, yeye ni mimi, na mimi ni yeye, nilimuamini sana kutoka moyoni mwangu, ....sasa mkataba wangu umepotea, na mtu ambaye anayeweza kuuchukua ni mume wangu, swali lilikuja kwa kutumia ufungua gani, na mimi ufungua za kabati langu ninao mimi mwenyewe, na hakuna nakala ya akiba ambayo niliwahi kuiweka sehemu, na ufunguo zangu mara nyingi natembea nazo.Leo hii ninafika nyumbani ninamkuta mume wangu akiwa kwenye kabati langu,..na kabati limefunguliwa, na ufungua zipo zimening’inia kwenye sehemu yake..na kulihakikisha hilo nilisogea taratibu hadi pale alipochuchumaaKwa muda huo hakuwa na habari kabisa kuwa nimeingia, na alionekana kuna kitu muhimu anakitafuta hasa pale aliposema‘Mbo-mbo-na haipo ooh….’Na kilichoniuzi zaidi ni kuona nyaraka muhimu za ofisi nyaraka ambazo kwangu ni muhimu sana, alikuwa kazisambaza chini, bila mpangilio maalumu, mimi napenda vitu vyangu viwe kwenye mpangilio maalmu,..hapo subira, ilinishinda ndio nikasema...‘Unafanya nini kwenye kabati langu...’nikamshitua...Tuendelee na kisa chetu..............Mume wangu aliposikia sauti yangu, alishituka, hadi ile karatasi aliyokuwa kaishikilia mkononi kwa muda huo, ili ilimdondoka,… kwanza alitulia, kama anatafakari jambo, na baadaye akajifanya kama hajali..na kwa haraka, akaikota ile karatasi, halafu . akageuza kichwa kidogo na kuniangalia usoni, halafu akasema;‘Afadhali mke wangu umekuja, maana hapa akili yote imevurugika,..kauli zako za hivi karibuni zimenifanya nichanganyikiwe kabisa…’akasema na sasa akawa anaendeela kama kutafuta kitu.‘Unajua, ..sijui ndio huku kuumwa,..hii ajali imenifanya niwe mtu wa ajabu kabisa,..uliposema kuhusu mkataba mwingine wa zamani,…nimekuwa nikihangaika kujiuliza ni upi huo…lakini kuna kitu,,…unasikia..’ sasa akaacha kutafuta na kukaa vyema sakafuni.‘Nakumbuka hata wewe ulikuwa nayo, nakala yako au sio..na mimi ya kwangu, hii niliyo nayo mimi, ni ambayo niliitoa nakala , kutoka kwenye ila nakala ya mwanzo, nahisi ndio hiyo unayoiita nakala ya mkataba wa zamani, kweli si kweli..’akatulia‘Sasa akili ikanijia,…kama wewe ulikuwa na nakala yako, kwanini usema kuwa imebadilishwa,…sasa nikawa natafuta ukweli..tatizo ni hili nakala yangu, ya zamani…eeh, siioni, nia nione kama kweli ipo tofauti na hii ambayo nilikwenda kuitoa nakala..unielewe hapo, nakala ni ile ile,, ila nilikwenda kuitoa nakala nyingine kwa ajili ya wakili..ni ile ile..‘Cha ajabu, kwenye kabati langu haipo…ni ile ya zamani, unanielewa hapo, ambayo niliichukua na kuitoa nakala,…hapo kabisa..ipo hii ambayo ni nakala kutoka kwenye nakala hiyo…hii ya sasa unaiona imefifia kidogo,…kama imefutika futika vile lakin ikila kitu ni kile kile...sasa nikawa nahangaika weeeh, mwishowe nikasema, aah..’akasema na mimi nikamkatisha kwa kuuliza‘Kwahiyo unatafuta nini hapa kwenye kabati langu, ndio mkataba au..?’ nikauliza‘Kiukweli, nikuombe samahani kwa hilo..lakini sio kosa,..si ndio…niambie mke wangu hapo nimekosea nini…sawa, kiutu , ilitakiwa nifanye hivyo,..lakini nikuulize kwani..kuna kosa mtu akitafuta kitu kwenye sehemu za mke wake..mhh, kosa labda ni kwa vile sikukufahamisha mapema kwa vile…kuna vitu vyako vya kiofisi, lakini ofisi zi zetu wote au…ama kwa hilo, basi nikuombe samaha mke wangu…’akasema.Aliinua macho na kunitizama..nilishikwa na kitu kama mshangao…hayo macho…sio yale ya mume wang ninayemfahamu…lakini sikujali hilo‘Mume wangu, toka lini tukawa tunachangiana makabati, kila mmoja ana kabati lake na kila mmoja ana vitu vyake na humu naweka vitu vyagu vya kikazi, angalia jinsi gani ulivyoviweka ovyo vitu vyangu sakafuni, …kwanini jamani…’nikawa naviangalia vile vitu, sakafuni.Hapo akatikisa kichwa, ni kama vile haamini, na akaehema kwa nguvu, halafu akaendelea na shughuli yake kama hajali, na mimi nikasema kwa hasira.‘Mume wangu unafanya nini…unajua utaratibu wangu wa kikazi ulivyo,..kwa jinsi ulivyovuruga hivi…hata ule utaratibu wangu wa kumbukumbu za kwenye kabrsaha umeuharibu, itachukua muda tena kuutengeza vizuri,...huoni kuwa unataka kuniweka mimi mahala pabaya..vikiharibika hivi au vikipotea..unaniweka mimi kubaya....’nikasema.‘Usijali kabisa mke wangu hakitaharibika kitu hapa, niamini mimi, mimi ni mume wako, nitahakikisha hakiharbiki kitu hapa, hata hivyo…kama nilivyokuambia, siku hizi akili yangu imekuwa ya ajabu kabisa, inanasa kila kitu ninachokifanya, yaani siku hizi mke wangu naona nipo mtu wa ajabu sana, nina akili mbili tofauti, hii ya ajabu, inakuja na kuondoka, ..wewe mwenyewe utaona, nitakirudisha kila kitu kwa mahali pake, bila hata kukosea wewe mwenyewe utaona...’akasema.‘Kwahiyo umesema ulikuwa unatafuta nini humu,… mkataba wako kwenye kabati langu, kwanza ni mkataba upi huo, unajifanya nini hapa..?’ nikamuuliza kwa hasira.‘Nakala ya zamani, ya mkataba...mwenyewe ulisema unahitaji ile nakala yangu ya zamani, si ndio hivyo…umesema bila hiyo huwezi kukaa kiti kimoja na mimi na wakili au sio..’akasema‘Kwahiyo ipo kwenye kabati langu, uliiweka wewe..?’ nikamuuliza‘Ni hivi… pale nilipokuwa nimeiweka nakala yangu, kule kwenye kabati langu, siioni, siku hizi akili yangu inanituma mambo mengi, na nikiweka kitu sisahau pale nilipokiweka, sasa ni ajabu kabisa kuwa siuoni, imekuwaje tena, hapana lazima kuna tatizo...’akatulia sasa akianza kupanga karatasi zangu zilizokuwa sakafuni.‘Mume wangu…tafadhali…’nikasema kabla sijamaliza akasema‘’Najua utanifikiria vibaya, lakini sivyo hivyo…mimi nilijua labda wewe umeamua kuichukua il nakala yangu ya zamani,…na kwa bahati mbaya ukaja kuiweka hapa kwako, kiusalama zaidi, hapa kwako kuna usalama sana au sio…’ akasema, huku akiendelea kupekua kwenye mafaili yangu.‘Sikiliza mume wangu, ..sijapendezewa kabisa na hiki kitendo ulichokifanya, ..na sio tabia yako, imekuwaje siku hizi, mume wangu, ...kuna nini unanitafuta wewe mume, kuna tatizo gani limekutokea ili niweze kukusaidia..kwanini unahangaika hivi mpaka unaniletea matatizo makubwa kwenye maisha yangu..?’ nikamuuliza huku nikiendelea kumwangalia.‘Hujapendezewa na mimi, kwanini…..hapana mke wangu usinifikirie vibaya kabisa,…na mke wangu, nikuulize, wewe si mke wangu, nimekuoa kwa taratibu zote za ndoa, au sio…je nikifanya hivi kuna kosa gani…?’ akauliza‘Kuja kupekua kwenye kabati langu, tena kuna mambo ya kofisi, je mimi nikifike kwenye kabati lako nikafany ahivyo utafurahia,…kila siku unazidi kunichefua, kuna kitu gani kinakusumbua hivyo…’nikasema na kumuuliza‘Hakuna kitu kinanisumbua, ila kwanza nijibu swali langu halafu nitakuambia tatizo ni nini….swali langu ni hivi…, wewe si mke wangu..?’ akauliza na mimi nilikaa kimia, akauliza tena‘Mke wangu nauliza tena, samahani nijibu tu, wewe si mke wangu…?’ akauliza na mimi nikaona isiwe shida nikajibu‘Ndio..’nikasema hivyo tu.‘Sasa kama ni hivyo, nina makosa gani kumkagua mke wangu…’akasema‘Mume wangu acha maneno yako ya mitaani, kunikagua kwa vipi..?’ nikauliza‘Kama mimi ni mume wako, kila chako ni change au sio…na pia changu ni chako au sio..tuseme kiukweli kutoka haki za kindoa, achilia mbali mambo ya mikataba, achilia mbali sheria za kidunia,...na hata ukirudi kwenye mkataba kama umeusome vyema inasema hivyo hivyo,… na wewe mwenyewe ni mmoja wa waanzilishi wa huo mkataba wetu na sahihi yako ipo, usikate ukweli mke wangu, ach ubinafsi…’akasema‘Mimi siutambui huo mkataba wenu wa kugushi..’nikasema kwa hasira,…mume wangu kwanza akatabsamu, halafu taratibu akanigeukia, na kuniangalia…Kama kuna mtu kampanga mume wangu, basi huyu kafanya kazi kubwa sana, anavyofanya sio kuigiza, utafikiri ni kweli kabisa, yaani utafirikia naongea na mto tofuati sio kama yule mume ninayemfahamu ukimuambia kitu hewala, hewala..tu.‘Hapana…sio wa kugushi mke wangu, kwanini unasema hivyo,…ni ule ule tulioutengeza pamoja…,tuwe wakweli hata mkataba wa halali wa ndoa, unasemaje, mimi ni mume wako, na wewe ni mke wangu, kwanini sasa isiwe halali kwangu kufanya ya halali…hili ni halali kwangu au sio…nakagua vitu vya mke wangu, ambaye ni mke wangu, au sio,…?’ akauliza.‘Usipoteze lengo…tafadhali…’nikasema***************‘Mke wangu nikuulize tu, kwanini huniamini,..eeh, na …na ..kimkataba…, mimi kama mume wako nina haki ya kuangalia chochote kwenye mali zetu, ...au nimekosea..kasome mkataba vyema…?’ akaniuliza na safari hii alianza kurudisha vitu kwenye kabati, nikawa namwangalia tu.Hutaamini baada ya dakika moja, alikuwa karudisha kila kitu kama kilivyokuwa awali, halafu akaniangalia, kama vile anataka mimi nikague kama kila kitu kipo sawa, baadae akainama na kufunga, ufunguo ulikuwa umening’inia pale pale…alipogakikisha kafunga, akauchomoa ufungu…, nikagundua kuwa ufunguo ule ni kuchongesha, aaaah, kumbe, ...‘Huo ufungua uliupatia wapi?’ nikamuuliza, sasa nikijaribu kuukagua huo ufungua, na yeye kwa haraka akauweka mfukoni mwake.‘Mbona ninao siku nyingi mke wangu...niliamua kuwa na nakala ya ufungua zote, maana sisi sote ni binadamu tu, tunaweza kupoteza ufunguo, kwahiyo kuna haja ya kila mmoja awe na nakala za mwenzake, ni vibaya kufanya hivyo, au…’akasema kama ananiuliza‘Hilo ulilifanya lini bila ya mimi kufahamu..?’ nikamuuliza‘Hilo la kuchongesha ufunguo…?!! Mmh, mke wangu umesahau jambo kuwa mimi ni mume wako, natakiwa kuwa mbele kwa ajili ya familia yetu,..ni lazima niwe makini kwa kila kitu, na usalama wetu, na mali zetu pia, kwahiyo hilo sio la kuniuliza, nilifanya muda tu,..na hivi sasa nina uhakika kila kitu kipo salama au kufanya hivyo,..ni-ni..nimekosea mke wangu…’akasema Alisema hivyo sasa akiwa kamaliza kupanga kila kitu, akawa kama akumbuka kitu, kwa haraka sana akageuza kichwa kule kwenye kabati la pamoja, lipo wazi…kwa haraka ya ajabu, akaliendea, akahakiki kama kila kitu kipo sawa, huyoo, akalifunga.‘Umeona eeh…kila kitu kipo sawa..kama kilivyokuwa..umeonaeeh,…’akapitisha macho huku na kule, baada y akurizika akaniangalia mimi.‘Twende…’akasema‘Mume wangu usijifanye mjanja sana, unajua mimi nafahamu kila kitu, hizo zote ni mbinu zenu, kwanza mumefanya njama za kubadili mkataba, ili kutengeneza mkataba utakaokidhi matakwa yako, na mkafanya mbinu ya kuhakikisha nakala zote za mkataba huo wa kugushi zipo kile idara, lakini mumesahau kitu kimoja…’nikasema‘Kitu gani mke wangu…’hapo akasema kama kashtuka, halafu akajifanya yupo sawa.‘Nina uhakika, mliamua kuchongesha hizo ufunguo, ili wewe uje kuiba mkataba wangu, ili mkabadili na kuhakikisha nakala za awali, mumeziharibu, na pia ukaja ukachukua bastola yangu, nakumbuka wewe ulikuwa hutaki hata kuishika hiyo bastola,....imekuwaje sasa…?’ nikamuuliza‘Bastola!!!…mke wangu, toka lini nikagusa silaha yako, mimi naogopa sana siliha hiyo, aah, hapo umezidi, bastola, mimi na bastola wapi na wapi…’akasema‘Na kwa taarifa yako, silaha iliyotumika kwenye hayo mauaji ya wakili wako,..ni hiyo bastola, na wewe ndiye mwingine mwenye nakala ya kabati hilo, mimi wamegundua kuwa sihusiki, sasa wao wanamtafuta huyo mtu mwingine mwenye nakala ya hilo kabati, kumbe ni wewe, ole wako polisi wakifahamu hilo...’nikasema‘Unasema nini mke wangu, sijakuelewa hapo bado, kwanini mimi nilichongesha ili nije kuiba, hahaha, hapo mke wangu unakosea sana,.... kwa nini niibe, kuna mtu anaiba kitu chake, mbona mke wangu unaniangusha,...usisahau kuwa mimi ni mume wako, sio mtu mwingine yoyote,...’akasema,Moyoni, akilini, nilikwua nimejawa na hasira, lakini nilikumbuka jinsi alivyokuwa akinishauri docta, kuwa nisije kulogwa na kusema mume wangu kapona, kwani hapo alipo ikitokea tena,… mshtuko,… akapatwa na kiharusi (stroke) basi, sitaweza kumponya tena!Hapo mimi.., nikabakia kukunja uso, na aliponiangalia usoni jinsi nilivyobadilika, aligeuka kwa haraka akatoka nje ya hiyo makitaba…alikuwa anatembea kwa mwendo wa haraka …kama haumwi, kikawaida yeye anatembea kwa shida, kwa kuchechemea..!**********Nilichukua mkoba wangu na kuutafuta ufunguo wangu, ulikuwepo kwenye moja ya fungua zangu ninazotembea nazo, nikafungua lile kabati na kila kitu kilikuwa kwenye nafasi yake, na ule mkataba wa kugushi upo hapo hapo..Sikutaka hata kuukagua kama ni ule ule wa kugushi au ni ule wa awali nikafunga lile kabati vyema, na akilini mwangu nikapanga nikitoka hapo nabadili ufunguo zote na naweka taratibu mpya za kufungua hilo kabati kwa namba za siri.Nilitoka mle makitaba na kuingia kwenye chumba chetu cha kulala, kuna mlango wa kuingilia huko,..nilitarajia nitamkuta mume wangu kalala huko,..lakini hakuwepo, mimi kwa haraka, nikabadili nguo, na kuelekea sebuleni, chumba cha maongezi.Chumba cha maongezi, nilimkuta mume wangu akiwa kakaa huku kashikilia mkataba, ..mwanzoni nilifikiria ni ule mkataba wa zamani, lakini ulikuwa ule ule waliougushi wao, niliugundua kwa jinsi ulivyo juu, ..jalada lake limefifia kidogo.Nilimsogelea na kumwangalia, alikuwa katulia, hana wasiwasi, na alionekana alikuwa akisoma sehemu fulani kwenye huo mkataba, kwa makini, na alipohisi nimesimama karibu yake, akauweka pembeni huo mkataba, na kuinua uso kuniangalia, akatabasamu na kabla hajasema neno, nikasema;‘Haya hebu niambie ukweli, ni kitu gani kinachoendelea hapa kwenye nyumba yetu?’ nikamuuliza..yeye akasogea kidogo, kama kunipa nafasi nikae karibu yake, sikufanya hivyo.‘Mke wangu hebu kwanza kaa, njoo ukae karibu yangu,…mimi ni mume wako wala usiniogope, kuwa labda kwa vile naumwa, ninaweza kukudhuru, hapana, hilo halitaweza kutokea abadani, ninakupenda sana mke wangu…’akasemaNa mimi nikakaa, lakini sio karibu yake kihivyo, akasema‘Mhh, mke wangu, kwani kuna nini kibaya umeiona kimetokea ambacho kinakufanya useme hivyo,…, mimi sioni kama kuna kitu kibaya kimetokea, hiyo ajali isiwe ni sababu ya kuharibu maisha yetu, ajali ni ajali tu, na ajali haina kinga, na mengine yanatokea ni…maisha tu…’akasema na mimi hapo nikabakia kimia kwanza.‘Mke wangu haya yanaweza kumtokea yoyote, hasa sisi tunaotumia vifaa vya moto..kilichotokea kwangu sio uzembe, sio…au kama watu wanavyosema,..ilitokea tu..na hali ninayokwenda nayo itakwisha tu, nisaidie nipone kabisa…’akasemaHapo nilitaka kumuambia kumbe kweli hajapona, maana wakati mwingine ukimuuliza anasema kapona lakini hapo anajifanya hajapona kabisa.‘Ni haki yako kunisaidia..nikikosea,…nikifanya kinyuma na kawaida, ujue ni madhara hayo ya ajali..na hapa nilipo, sio kwamba nakumbuka kila kitu kihivyo, inatokea …nika-ka-sahau,..yawezekana, wakati mwingine nahis kama nipo kwenye njozi, lakini kiukweli nimepona, au sio…’akasema, na mimi sikumjibu kitu.‘Au mke wangu niambie …, labda mimi sijui, maana muda mrefu nimekuwa hopsitalini, je kuna tatizo lolote…nipo tofauti, nimechanganyikiwa labda..niambie ukweli au…? ‘akauliza‘Mume wangu, leo ni siku ya mwisho, sitakaa tuongee hivi tena, labda kuwe na kuelawana, na kuelewana kwetu, nimeshakuambia,kutakuja pale tu, wewe utakapokubali kuniambia ukweli, wote na pili ule mkataba wa asili uweppo mezani…’nikasema‘Eheee,…wewe unautaka ukweli, lakini,…ukweli upi.. hamna shida, mimi nitakuambia kila kitu, ila sasa nikuulize unataka mimi nikuambia ukweli gani labda, nisaidie hapo mke wangu…’akasema‘Leo ni siku ambayo…kama hutaniambia ukweli, sijui…maana tukimaliza hapa ni utekelezaji,…hata kama utauficha huo mkataba,…na vinginevyo,..tutafikishana mahakamani, au….’hapo nikatulia, alipogeuka kuniangalia‘Mahakamani, kuna nini cha kwenda huko, hapana mahakamani hapafai, yetu tutayamaliza hapa hapa nyumbani au sio....?’ akauliza‘Vitendo vyako vimenichosha, kwanza umekiuka makubaliano yetu, umevunja mkataba wa ndoa, na hata sikuelewi,…. na hutaki kuniambia ukweli, ...ni kwanini lakini, kwanini unanitesa hivyo, una lengo gani na mimi…?’ nikamuuliza na yeye akanitupia jicho, halafu akafungua ule mkataba wake, akawa kama anasoma jambo, mimi sikutaka hata kumsogelea na kuangalia anasoma kitu gani.‘Kwanini unasema ….eeeh,maana tukimaliza hapa na utekelezaji, ama twende mahakamani,…hapana usiseme hivyo, tupo wote, na kila siku tutaongea tu huo ndio utaratibu wa mke na mume au sio..hata bila mikataba, hilo la kuongea ni jambo la kawaida kwa mke na mume, sasa niambie nimekufanya nini kibaya, mpaka useme hivyo…?’ akasema na kuuliza, na aliponiona nipo kimiya akasema;‘Kwani mke wangu situlishaelewana, na ndio maana nilikuwa nataka niutafute ile nakala yangu ya zamani,…ili tukae tulianganishe kama kuna maneno yameongezeka au kupungua,…sijaiona kabisa..na ya kwako ipo pale pale au sio…kwanini tuandikie mate,..nenda kaulete, ..tulinganishe tuone kama kuna utofauti wowote, utakuta kitu ni kile kile neno kwa neno....’akasema.‘Mume wangu…’nikataka kusema, yeye akanisogelea akiwa kafungua mkataba wake na kusema…‘Hebu angalia, mwenyewe, ....maneno ni yale yale..hebu soma uone…’akasema huku akinipa ule mkataba, na mimi sikuugusa na wala sikuinua mkono wangu, nikawa namwangalai usoni nikasema.‘Mume wangu kwanini upo hivyo, upo sawa kweli wewe, ni kwanini hutaki ku-usema ukweli, ni kwanini mlichukua hatua ya kuubadili huo mkataba bila makaubaliano na mimi…niambie tu ukweli, ili twende sawa….?’ nikamuuliza‘Mke wangu, mimi nakumbuka , hilo swali nilishakujibu, hakuna aliyebadili huo mkataba,mbona huniamini mke wangu, mimi nipo sawa kabisa, kifahamu, au..?, tuache kuhusu mimi, eeh,...hebu niambie ni wapi huo mkataba umebadilishwa, na kama ulibadilishwa kwanini sahihi yako iendelee kuwepo hapo, huoni unakosea kabisa kisheria….eeh, niambie sahihi zote za wahusika sizipo, angalia hapa, hii sio sahihi yako…hata ukienda mahakamani watahakiki hilo…’akasema.‘Kwahiyo kumbe bado upo na msimamo wako ule ule,....hutaki kusema ukweli, hutaki kuniambia ni nini kinachoendelea, na ni ni kusudio lako,au kusudio lenu, na washirika wako....eeh, na sasa watoto wanadai wanachohisi ni haki yao , si ndio unataka hivyo…’nikasema huku nimemkazia macho, yeye akaniangalia mara moja halafu akatabsamu, na kusema;‘Haki ni haki tu…tusiibeze haki, au sio, na…hayo niachie mimi, na nikuulize tena mke wangu, labda kuna kitu wewe unakihis hakipo sawa, ni kitu gani, niambie ukweli, kama ni mkataba upo vile vile..na kwanini mtu afanye ufoji huo, agushi, kwanini,...hebu niambie wewe…?’ akaniulizaMimi hapo nikakaa kimia.‘Mke wangu , tusaidiane, huenda mimi nipo dunia nyingine, huenda kuna kitu umekigundua kwangu na unaogopa kuniambia, au nimebadilika, baada ya kuumwa, nimekuwa tofauti, ...’akasemaHapo nikasimama,..nilitaka kuondoka kabisa kwa hasira…, lakini nikajiuliza nitakuwa nimefanya nini sasa, leo ni lazima nimbane mpaka asema ukweli wote hawezi kujifanya mjanja hivyo hapo ndio..nikageuka kumuangalia,Yeye akawa anausoma ule mkataba, hajali kabisa, hana wasiwasi….Nilimuangalia mume wangu, kiukweli nilimuona kama sio Yule mume ninayemfahamu kabisa,…maana mume niliyemzoea alikuwa nikimuuliza jambo, tunakubaliana, tunaongea yanakwisha, lakini huyu wa sasa, wala hanijali, na pili amekuwa kama yupo mbali, kama alivyosema, ni kama yupo dunia nyingine tofauti ya ukweli….‘Mume wangu , pengine, hujanifahamu , pengine unafikiria kuwa nakutania, pengine, nahitajika kuchukua hatua nyingine ndio utanielewa,....’nikasema na kutulia kidogo.‘Nakusikiliza endelea…’akasema hivyo akiendelea kuusoma huo mkataba.‘Hivi unajidanganya nini, hivi wewe hufahamu kuwa hilo unalolifanya linaweza likakufunga, na hata kukuvunjia ndoa yako, unayoringia nayo wakati wewe mwenyewe umeshaivunja…ukweli ndio huo, umeshaivunja ndoa yako,..hebu niambie imebakia nini…sasa...’nikamwambia na yeye hapo akashituka, na kuinua uso kuniangalia...‘Unasema nini..kuvunja ndoa yetu, hapana mke wangu, hilo halipo, na hali-hali-tatokea abadani, labda mimi niwe nimekufa....kwanza kwanini unasema hivyo?’ akaniuliza na safari hii akawa ananiangalia moja kwa moja usoni,akionyesha wasiwasi. Kikweli kuna kitu kwenye macho yake nakiona sio cha kawaida….lhata hivyo, hali ya kujali haikuwepo tena.'Kutokana na makubaliano yetu ya awali, hata kama mumeugushi huo mkataba halali, na kupandikiza huo wa kwenu, na kuweka mambo yenu ya kujihami…lakini ukumbuke, kugushi ni dhambi, kugushi nyaraka za kiheria ni kosa kubwa sana…sasa jiulize unataka kufanya hivyo kwa ajili ya nani…’nikasema‘Hapo jiulize wewe mwenyewe…’akasema kwa kujiamini kabisa‘Sawa nikuambie kitu.., hata kama unajifanya mjanja sana,lakini ukumbuke kuwa makubaliano yetu ya awali yapo pale pale, na moja ya makubaliano yetu ni kuwa mmoja akivunja miiko ya ndoa..unaifahamu hiyo miiko, ile mikubwa…’nikasema‘Kama upi huo…?’ akauliza‘Kuzini…kutembea nje ya ndoa…’nikasema‘Nini, …wewe mke wangu ni nani anaweza kufanya dhambi hiyo, hapana…mimi nakubali hilo ni kosa, ..na kwenye mkataba wetu inasemaje..hebu kidogo…’akasma na sasa akifungua mkataba wake, na akawa kama ansoma‘Yah, hapa kupo wazi…ni kosa, ila sasa unajua kiubinadamu, eeh..si semi hivyo kwa vile, labda..hapana mimi sijafanya, ikitokea wewe ukafanya hivyo, kwanza kuwepo na ushahidi…wa bayana, lakini pia…sisi ni wanandoa, tumzee, tuna watoto…mmoja akaghafilika, kutokana na sababu…maana huwezi kufanya dhambi kama hiyo bila sababu…’akasema‘Sababu gani,…hakuna sababu hapo, kuzini ni kuzini tu…’nikasema kwa hasira.‘Je kama imetokana na wewe..’akasema‘Kwa vipi..?’ nikauliza‘Tuache hayo, ila hapa kwenye mkataba inasema hivi, kama …itatokea hivyo, kwasababu za kujitetea, kuna sababu japo kidogo, ya kujitetea, inayoingia akilini, japokuwa..ushahidi upo, na mmoja akaomba msamaha, ukakubalika, basi,..ni kusameheana ya kale yaishe watu wagenge yajayo,…hiki ni kipengere cha nyongeza..’akasema‘Hivi wewe mume wangu kweli hilo lilikuwepo…?’ nikamuuliza.‘Si ndio nimesoma hapa…hebu soma wewe mwenyewe…lakini pia kuna vipengele vingine hakuna haja ya kivisoma,…kama vile mume wakiona kuna haja, ya kufanya jambo lenye tija kwa familia,..yeye kama kiongozi wa familia anaweza…ni vipengele vye kujitetea,..vinasaidia kisheria,..lakini muhimu ni kusameheana …’akasema‘Kwahiyo uliongeza hivyo, ulipobaini kuwa umezini….?’ Nikamuuliza‘Nani kazini,…mimi,…mke wangu unanifahamu nilivyo, mimi….hapana sijaweza kufanya hivyo, kwanza ni nini kuzini….mmh…hivi kuna kipengele hapa…’akawa anafunua kutafuta.‘Hapana achana na huo mkataba wa kugushi, nijibu swali langu,…’nikasema kwa ukali,‘Kabla sijakujibu swali, twende pole pole, kwani huo mkataba unaojua wewe ulisemaje…?’ akauliza‘Unajifanya hujui..ni hivyo…kama umezini, ina maana umetembea nje ya ndoa,… kukawa na ushahidi wa kutosha, basi ndoa haipo..na huna haki tena kwenye mali zilizochumwa kwenye ndoa…’nikasema‘Wauuuh…hiyo mpya kwangu…’akasema‘Na kwenye kile kikao, wewe mwenyewe ulilisitiza sana hilo kwa kujiamini,..na ukasema ushahidi ni lazima uwepo, nikakuuliza ushahidi gani na watu wanafanya kwa siri, ulisema wewe mwenyewe, mtu kama huyo ataumbuka, anaweza akapata mtoto , huo ni ushaidi tosha,..ikipimwa ikahakikiwa kwa DNA, basi huo ni ushahidi wa kisheria, unabisha…’nikasema‘Kikao gani hicho..?’ akauliza akionyesha mshangao‘Utabisha lakini mbele ya sheria, utanaswa tu…na kwa vile hutaki kukiri kosa, ukasema ukweli, basi mimi kuanzia leo, najiandaa kwenda mahakamani…’nikasema‘Mke wangu unakwenda mahakamani kwa kosa gani, mimi nimefanya kosa gani…?’ akaniuliza‘La kuvunja mkataba wa ndoa, na kugushi mkataba halali wa ndoa…’nikasema‘Nimevunja mkataba wa ndoa…!! ?’ akauliza kwa mshangao‘Ndio umezini…’nikasema‘Kuzini….’akasema hivyo, sasa akawa anatoa macho kama kuogopa‘Mimi,…hapana, sijawahi kufanya hivyo, hata kama ulitoa kibali hicho, lakini mimi sijafanya…’akasema hivyo akiongea kwa haraka haraka kiasi kwamba sikumsikia vyema.Akatulia kama anasubiria mimi niongee, kiukweli, ukimuangalia mume alivyo, ni kama mtu aliyechanganyikiwa, hajui kabisa anachokisema, lakini hakuweza kunishawishi kwa hali hiyo, kangu mimi , nilimuona kama anaigiza tu.‘Ndio wewe umezini, usijitete hapa, kubali tuyamalize, hapa hapa…maana tukifika huko mbele mimi ninao ushahidi…’nikasema na nilitaka aulize ushahidi gani lakini hakuuliza hivyo, yeye akasema‘Mke wangu unasema nini,....sijawahi kufanya hivyo,.....ni nani kakuambia nimezini, ....na na...mbona sikuelewi..nimezini na nani , umedanganywa mke wangu, temea mate chini, sijawahi, ..kamwe…’akawa sasa kama anahangaika hivi.‘Usijifanye mjanja,..leo imefika mwisho wako, ..leteni mkataba ule wa zamani tuyamalize kwa amani, mimi nitakusamehe, lakini kama haupo huo mkataba wa zamani, basi kitakachofuatia hapo ni mimi kwenda mahakamani..’nikasema‘Mke wangu…’akasema hivyo na mimi nikaa kimia, na akarudia tena... , ‘mke wangu kwanini unalirudia hilo, mimi nakupenda sana mke wangu, kweli kabisa....hilo la mkataba wa zamani, silijui mimi, sikumbuki kama kuna mkataba mwingine zaidi wa huu, kama ungelikuwepo,ningeuleta, tuyamalize mimi na wewe mbona tumekuwa wa kuridhiana mambo,ulishawahi kuniambia jambo nikakataa..eeh…sasa huo mkataba ..upo wapi huo…’akasema ‘Sikiliza,… usijifanye kuigiza mambo hapa,..najua yote hayo, mumepanga uigize hivyo..ujifanye umechanganyikiwa, ujifanye hukumbuki kitu….na ujanja wako umeshafika mwisho,..sasa ni muda wa wewe kuniambia ukweli ili tuyamalize kwa amani,..kwani unataka nini, niambie…sasa nakuulize tena kwa amani, ..je sio kweli kuwa wewe una mtoto nje ya ndoa?’ nikamuulizaKwanza ilikuwa kama kapatwa na kitu kimemfinya hivi, akashtuka, na alitulia kidogo, halafu akainua uso, na kuniangalia…kiukweli hayo macho yake sijayaona kabla…akaniangalia, ..mpaka mimi sasa niangalia pembeni..‘Mtoto nje wa ndoa…!!!’akasema hivyo halafu akatulia, …hakusema neno, mpaka nilipouliza tena..‘Nimekuuliza hivi, sio kweli kuwa wewe una mtoto nje wa ndoa, ambaye hata kwenye mkataba wenu mwingine wewe umemuandikishia urithi, na kwenye huu mkataba wangu mimi na wewe wa kugushi, kuna maneno mumeyaongezea kuwepo kwake, ili na yeye atambulikane na apewe haki sawa na wengine, sio kweli ..na hapo hapo nakuuliza ni kwanini kipengele hicho mkakiongezea maneno kama hayo, kama sio kweli….?’ Nikamuuliza‘Mkataba unasema hivyo au sio..huu mkataba, niliona sio, mkataba wetu mimi na wewe au sio…sasa ngoja nikuonyeshe hapo…unaona hapa, na huu ndio mkataba wetu au sio…, umeukubali mwenyewe..kwahiyo hiyo sehemu inasemaje, nikumbushe kidogo mke wangu, mimi nashahau sahau wakati mwingine…’akasema‘Hapo hukumbuki vyema, lakini kwenye kurudisha vitu kwenye kabati, hukusahau kitu..hapa kwa hivi sasa huna akili za ajabu,..huoni kuwa unajifunga wewe mwenyewe…’nikasema‘Hahaha, hapana mke wangu, sijifungi bwana…ila wewe wanipambikia mambo, huyo mtoto eeh,....mke wangu kiukweli mimi sikumbuki hilo, ila kuna kitu nataka nikuambie ukweli, ..hebu kaa kwanza, nitakuambia kila kitu…’akasema na mimi sikukaa, akainaimisha kichwa chini kwanza kama anawaza jambo…‘Mke wangu nimekuwa nikiota ndoto ya ajabu sana, kuwa kweli mimi nina mtoto, tena mtoto huyo ni wa kiume….’akasema‘Hahaha, umeshaanza kukubali, …haya sema ukweli wote mimi sasa nitakusikiliza…’nikasema sasa nikikaa.‘Sasa tulia basi nikuambie..hiyo ni ndoto jamani…’akasema‘Haya wewe singizia vyovyote vile, ..una mtoto wa kiume au sio, na huyo ndiye kakufanya ubadili hadi huo mkataba…’nikasema‘Sikiliza kwanza, nikuhadithis hiyo ndoto, sio kweli, ni ndoto,..ndoto,..kuota usiku, na kwa bahati mbaya,…nimekuwa nikiota hiyo ndoto sana baada ya ajali,…wakati nilipoanza kupata kumbukumbu zangu…kuwa nina mtoto wa kiume,’ akasema‘Una mtoto wa kiume au sio, sasa swali ulizaa na nani huyo mtoto…?’ nikauliza ‘Kwanza nikuulize wewe huyo mtoto yupo au hayupo…?’ akaniuliza mimi sasa.‘Unaniuliza mimi tena…’nikasema‘Mke wangu nisaidie kujibu hilo swali, maana nateseka sana, kumuwaza, kama yupo, ni heri sana kwangu na kwetu kama familia…’akasema‘Mume wangu…nimechoka, na maneno yako,…nakuuliza tena hili swali, kama ni ndoto au ni kweli, je una mtoto nje ya ndoa, kauli yako ndiyo itathibitisha hili, kama hayupo, basi hatakuwepo,…ilo uweke akilini, kimkataba na kila hali, sasa kama yupo, ni vyema hilo uliweke wazi,…’nikasema‘Kama hayupo..hatakuwepo, au sio…’akasema sasa akitabasamu.‘Ndio hivyo, ukitoa kauli yako sasa hivi, kuwa hakuna mtoto wa nje..ndio hatakuwepo hivyo…, akitokea…huyo shetani, au sio….’nikasema, nikijua kama yupo hawezi kumkana.‘Usiseme hivyo, damu ni nzito kuliko maji…’akasema‘Hahaha, umeona eeh, hebu rudia tena…?’ nikauliza kama sikusikia‘Nasema hivi, usiite watoto wa nje mashetani, kwani wao wana kosa gani,…’ akauliza‘Kwahiyo wewe unaye, ili tusimuite ni shetani, sema ukweli wako usimkane mtoto wako…?’ nikamuuliza‘Mimi sijui….’hapo akasema hivyo‘Haya niambie uliota nini…?’ nikamuuliza‘Ehee hapo sasa tuendelee na ndoto yangu, na tusaidiane kwa hili, ninaota mara nyingi tu, kuwa tuna mtoto wakiume, tatizo sasa ni huyo mama yake,..hataki ..’akasema‘Hataki nini..?’ nikauliza‘Hataki huyo mtoto atambulikane kwa jamii…’akasema‘Kwanini, ni kashfa au..?’ nikamuuliza‘Sijui,…ni ndoto, inanitesa sana, sasa nataka wewe unisaidie kwa hilo, akili yangu inawaza sana hilo, na zaidi ni kauli ya madocta,..hawajaniambia wazi wazi, lakini nayo ilikuwa kama ndoto…’akasema‘Wamesemaje…hao madocta..?’ nikamuuliza‘Mimi sitaweza kuzaa tena…’akasema kwa sauti ya unyonge..‘Hayo ni ya kwako, nikuulize tena, ni nani mama wa huyo mtoto..?’ nikamuuliza‘Huyo mwanamke…cha ajabu kabisa, alikimbia na huyo mtoto na ghafla, sasa wakati nahangaika, eeh…puuh, ajali..na ghafla, nikashtuka kutoka usingizi…’akasema‘Mume wangu acha ujanja…’nikasema‘Sasa nikuambie kingine mke wangu, huyo mtoto wetu anafanana kabisa na watoto wetu utafikiri mapacha..sasa najiuliza ni kwanini huyo mwanamke akimbie na mtoto wetu,…’akawa kama anataka kulia.‘Nakuuliza hivi,…huyo mama aliyekimbia na huyo mtoto si unamfahamu…?’ nikamuuliza‘Ndio namfahamu, kwanini nisimfahamu…’akasema‘Ni nani sasa…?’ nikamuuliza na hapo akainua uso, akanitizama na sasa niliona dalili za machoni machoni kwake…anataka kama kulia, moyoni sikuwa na huruma naye tena, kila kitu cha huruma kilikuwa kimefungwa, nikamkazia macho yaliyojaa hasira nikisubiria jibu lake.NB: MBONA NDEFU HIVIWAZO LA LEO: Huwezi ukahalalisha dhambi kwa kutengeneza dhambi nyingine juu yake…, usifanye dhambi ili kuficha dhambi uliyowahi kuifanya, dawa ya dhambi ni kutubu, na kutubu kupo kwa namna nyingi, …moja wapo ni kukiri kosa, kwa Yule uliyemtendea ukamuomba msamaha, akikubali kutoka moyoni kuwa kakusamehe, basi hapo huna shaka…lakini kutumia ujanja wa kuhadaa ili kosa lisionekane kosa na ili Yule uliyemkosea aseme tu kakusamehe,…bila ya ridhaa yake kutoka moyoni, bado utakuwa kwenye deni ya dhambi.‘Sikuwahii kumuona kwa sura,…maana kila nikimuota, anakuwa kambeba mtoto, halafu anageuka kunipa mgongo, usoni…simuoni, najaribu kumuangalia,..hapo hapo nashtuka kutoka usingizini… lakini kwa maumbile na wajihi namfahamu…’akasema‘Kwanini unaficha ukweli mume wangu kwanini uanigiza uwongo…?’ nikamuuliza‘Ukweli ndio huo ninaokuambia mke wangu, na ilikuwa ni njozi, na njozi kama hizo ni nyingi za ajabu, na…wakati mwingine nahisi kama ni kweli…’akasema‘Kwanini unahisi hivyo..?’ nikamuuliza‘Watu wanaongea….wanayosema ni kama kweli nilifanya…lakini nikija kwenye akili ya kawaida,…sikumbuki kitu, …nachanganyikiwa mke wangu, niamini, wewe hujui ni hali gani ninayopitia, najua utafikiria na..na…naigiza, lakini mungu mwenyewe anajua…’akasema hivyo‘Sasa hiyo ndoto…iliishaje, na huyo mtoto ulimpataje..?’ akauliza‘Ndoto!!? Eeh, ..ndoto, inakuwa hivi, ni…sehemu sehemu tu…ila hiyo ya mtoto kila ikija, haiishi, au ..hata sijui…wakati mwingine nahisi labda ni kwa vile…labda, nasema labda ni kwa vile.. nilitamani sana kuwa na mtoto wa kiume…si ndio hivyo…’akasema, hapo ndio akazidi kunipandisha munkari wa hasira.‘Nasikia kwenye mkataba wenu, mumeandika kuwa mtoto wa kiume atapewa mamlaka ya kusimamia mali , kama wazazi watakuwa hawapo…na huyo mtoto umempata nje ya ndoa, ina maana anakuwa na haki zaidi ya watoto wa ndoa ni haki hiyo…?’ nikamuuliza‘Mke wangu, hebu kwanza nipe nafasi ya kufikiri…nahisi ..sipo sawa,..na hayo ya mkataba,..kuna mkataba mwingine upo tena,…ooh , hata sikumbuki, …basi hilo la mkataba mwingine nitakuja kukuambia ni kwanini, kwanza tugange hili hapa…’akainua ule mkataba juu.‘Nilishakuambia huo mkataba wako siutambui, na sitautambua,..na kwa vile umedhamiria kuung’ang’ania, sawa…mimi nitachukua hatia za kisheria, na ngoja sheria ichukue mkondo wake…’nikasema‘Mke wangu mkataba huu ni nani aliubuni, nijibu swali hilo kwanza, halafu twende sawa…?’ akauliza‘Huo uliubuni wewe na marehemu..’nikasema‘Huo unaosema ulikuwepo, sijui ni gani,….aliubuniwa na nani…?’ akaniuliza‘Huo, ambao ni wahalali, ambao tulikaa mimi na wewe na wakili wetu, sio huyo marehemu, ilikuwa ni wazo langu…nielewe hapo, usilete ujanja ujanja wako, mimi nazungumzia mkataba huo…ambao mumeuharibu nyie wawili…’nikasema hapo akanywea.‘Sasa mke wangu ni hivi, kama unaona huu mkataba una kasoro,..kiukweli mimi sifahau,… tufanye jambo moja, ..tukae kikao, tujadili, tupitia vipengele kimoja baada ya kingine, kama kuna makosa, wakili si wapo, yupo wakwako na wa kwangu au sio, basi tutarekebisha hayo makosa, unaonaje hilo wazo langu…’akasema‘Tatizo lako mume wangu, marehemu alikughilibu, unafikiri mimi ni mtoto wa jana,, huo ni ujanja wako, nia ni kukwepa sheria, unauogopa ule mkataba wa awali, kwa makosa uliyoyafanya,… kwahiyo unachotaka hapa ni kuvuta muda, ili uanzishwe mkataba mpya, na utaanza kufanya kazi lini…huo ujanja kawadanganye watoto sio mimi…’nikasema‘Mke wangu nisaidie, unajua hali niliyo nayo inanitesa, si nimekuambia, kuwanahisikama bado kuna tatizo, na tatizo hilo kama walivyosema madocta, haliwezi kupona,..na toka siku ile waniambie hivyo, mimi nikawa sitaki hata kuhudhuria kiliniki zao…’akasema.‘Tatizo gani…?’ nikamuuliza‘Mimi sitaweza kuzaa tena…’akasema‘Kwanini…?’ nikauliza‘Kutokana na athari za ajali, uti wa mgongo umeathirika…’akasema‘Mbona mimi hilo sijui, sijaambiwa na docta…?’ nikauliza‘Hilo sikutaka wakuambie wewe …’akasema‘Kwanini sasa umeamua kuniambia mimi..?’ nikauliza‘Ni ili uone umuhimu wa watoto…mtoto wa kiume…’akasema‘Hahaha, mtoto wa kiume ndiye kakufanya ukafanya haya yote, sasa unaona madhara yake,..umezini, umevunja mkataba wetu, na matokea yake ni nini, unaona madhara ya zinaa yalivyo, unatusumbua hata sisi tusiohusika, ndio huyo mtoto wa kiume unayemtaka, au sio…?’ nikauliza‘Hapana mke wangu,…nielewe hapo, mimi nimekuwa nikiwaza sana, hadi naota, eeh, kwahiyo hali hiyo ndiyo inaniandama hadi kuja kufanya mambo ambayo siyakumbuki, mawazo…na docta kaniambia hiyo hali isipodhibitiwa naweza nika…potea, hata sijui…au kufanya mambo maovu…’akasema‘Kama yapi…?’ nikauliza‘Kama kuna kitu …kimeniudhi, au kukasirika, au ..si unajua tena wanadamu tulivyo, unaweza ukatamani hata kuua, ..mtu ambaye unaona ni kikwazo kwako…unielewe mke wangu naongea kama alivyosema docta…’akatulia alipoona namuangalia kwa mashaka na uso umejaa hasira.‘Siwezi kuamini maneno yako …siku hizi sitakuamini tena, na haya yote unaongea tu, kujihami, au umeambiwa useme hivyo, uigize hivyo, ili nikubaliane na matakwa yako, na kwa hilo, usijisumbue kitu…’nikasema‘Mimi nakuambia ukweli, kama utaamini sawa, kama hutaamini, shauri lako, ili yasije kutokea ukaja kujutia baadae,…’sasa akasema kwa sauti ya kawaida sio kama ile ya kudeka.‘Kwahiyo hayo maovu umeshayafanya au..?’ akaniuliza‘Maovu gani..?’ akaniuliza kwa mshangao tena‘Si umesema kuna hali inaweza kukutokea kwasababu ya msongo wa mawazo, na hali hiyo inaweza kukutuma kufanya maovu…je umeshayafanya hayo maovu, usisingizie kuzini, maana hilo tendo, ulilifanya kabla ya ajali…’nikasema‘Kuzini…?’ akauliza sasa akiwa kama anashangaa,‘Acha ujanja wako bwana…nimeshakuelewa, na tusipoteze muda hapa, kuna maswali nataka kukuuliza, na ukumbuke kwenye mkataba wetu wa awali, ulisema tusije kudharauliana, kila mtu aheshimiwe kauli yake,…’nikasema‘Lakini mimi sijazini…’akasema‘Huyo mtoto ulimpataje..?’ nikamuuliza‘Mtoto…!! Wa kiume eeh, nikuulize wewe,…’akasema hapo nikamuangalia machoni, nikamuona kweli anahangaika, kama kukumbuka jambo, lakini akilini nikajua anaigiza tu,‘Mtoto, umesema mtoto,…yawezekana,..ni kweli labda sio ndoto,..mtoto wa kiume eeh, basi,…mke nisaidia jambo, tumtafute mtoto wetu, ..unaelewa,…’hapo akatulia aliponiona namuangalia kwa uso uliojaa hasira.‘Wewe umezini, una mtoto nje ya ndoa, ndio maana mlikaa wewe na marehemu mkaandika maelezo kuhus huyo mtoto wa nje, awe na haki sawa, haya uliyafanya ukiwa na akili zako timamu, kabla ya ajali…na siku ile ya ajali, ilitokea kwa vile ulikuwa una haraka ya kubadili mkataba wa awali, na huo wa kugushi…’nikasema‘Unasema nini…?’ akaniuliza kwa mshangao‘Ndio maana nakueleza kuwa kila jambo mimi nalifahamu…’nikasema‘Mke wangu ...kwanza tuanze moja, hilo la mkataba, au sio, tumeshamalizana nalo kuwa mkataba uliopo ni huu, kama upo mwingine basi tutautafuta, tukubaliane hivyo, ili tuyamalize haya…’akasema‘Na nikikubali, ili iweje…?’ nikauliza‘Ili maisha yaendelee, tuendee na shughuli zetu za uzalishaji kama kawaida, kampuni hazifanyi kazi, …madeni yanaongezeka, watu wa kodi wamenijia juu, wataka kufunga kampuni,..na hali hiyo inaniweka kubaya,..naombe mke wangu uyamalize ili na mimi nipate nafuu, niondokane na dimbwi hili la mawazo na mashaka…’akasema‘Hilo sitachoka kulirudia, hata mbele ya Mahakam, kuwa Mkataba ninaoufahamu mimi ni ule ule wa mwanzo, ambao haukuwahi kufanyiwa mabadiliko, hata kama utaumwa,..au… utachanganyikiwa hiyo umejitakia wewe mwenyewe…vinginevyo…’hapo nikatulia‘Nakusikiliza mke wangu, vinginevyo,..nini…?’ akaniuliza‘Uniambie ukweli wote…’nikasema‘Ukweli gani sasa mke wangu mbona tunarudia kule kule, sasa sikiliza mke wangu tusipoteze muda, niambie kile unachokitaka…huo ukweli ni upi, eeh…na mimi nitakujibu, naona tunapoteza muda bure, na mimi sijisikii vyema…’akasema, nikamtupia jicho, kiukweli hali aliyokuwa nayo, yaonekana kama kweli hayupo vyema, lakini sikujali tena moyo nafsi ilishakataa…hapohapo nikasema‘Kwanza nataka unipe majibu kwa haya maswali nitakayokuuliza..’nikasema‘Haya uliza…’akasema sasa akiwa kama anakata tamaa.‘Na..kama usiponijibu tukitoka hapa wewe nenda kwa wakili wako na mimi kwa wakili wangu tunakwenda kukutana mahakamani, na ndoa hapo haipo tena, umeshaivunja wewe mwenyewe..na ukumbuke kwenye mkataba wetu wa awali kuna kipengele hicho, cha kupuuzana, .....’nikatulia kidogo‘Nakusikiliza mke wangu uliza tu hayo maswali..kabla sijazidiwa kabisa, mwili hauna nguvu,…ki-ki-ukweli…! Sa-sawa..mimi sitakupuuza kabisa, hicho kipengere hata mimi nimekiona, .. lakini hilo la kuvunja ndoa sikubaliani nalo na halipo, na halitakuwepo.....’akasema.Alipiga miayo, akajinyosha, halafu akaniangalia, na kusema‘Sasa nipo tayari…’akasema‘Kwanza kwanini mliamua kubadili huo mkataba bila ya kunishirikisha?’ nikamuuliza‘Jibu nimeshakupa ama kwa kumbukumbu jibu ni hivi...mimi sijui kama kuna mabadiliko yoyote yaliyofanywa kwenye huu mkataba, naapa…, na ndio maana naona leo tukae kama yapo basi tukayafanye, mimi sina shida,, mimi nafahamu kuwa huu ndio mkataba wetu, kama kuna mkataba mwingine zaidi ya huu nionyeshwe basi, kwanini tupoteze muda...’akasema akionyesha kujiamini.‘Swali la pili...’nikasema‘Aaah, umerizika na jibu langu kwanza, sijakupuuza mimi, kwanza turiziane?’ akaniuliza‘Hujanijibu swali langu, sijarizika na jibu lako, lakini tusipoteze muda, hapo kwangu naona kama umenipuuza tuendelee na swali jingine’nikasema‘Unataka niseme nini mke wangu sasa, mbona unaniweka kwenye wakati mgumu, au wewe una majibu unayataka, basi niambie hayo majibu,...’akasema‘Swali la pili, je una mtoto nje, uliyezaa huko nje ya ndoa....?’ nikamuuliza‘Jibu la swali hilo,…eeh,… sina uhakika na hilo, nakumbuka ndoto inasema hivyo, ila kiuhalisia mimi sina uhakika, kama huyo mtoto yupo basi niletewe, itakuwa heri na kwangu pia, ili nispate shida ya mawazo na mashaka, kiukweli hilo linanipa shida sana mke wangu,....’akashika kichwa chake kwa mikono yote miwili.‘Usijifanye mjanja wa kujizulia ugonjwa wa kuchanganyikiwa, usinifanye mimi mtoto mdogo, wewe ulishapona, huo ni ujanja ujanja wako tu, wa kutaka kunighilibu, nijibu swali langu, je wewe una mtoto nje, na ulizaa nani?’ nikamuuliza.‘Kama wewe unadai nina mtoto,…mimi sijui..na ndoto huwezi kuiamini, au sio…sasa kama yupo na umeshamuona niletee ili iwe ushahidi..na utakuwa umenisaidia na mimi, hilo ndilo jibu langu…’akasema‘Kwahiyo wewe unataka ushahidi…si ndio…basi utaupata, na je ukiupata nichukue hatua gani..?’ nikauliza‘Mkataba huu utahukumu..ndio ulioupendekeza wewe au sio, tutaangalia sheria inasemaje, au sio…vinginevyo…’akasema na kutulia kama anawaza jambo‘Vinginevyo nini…?’ nikamuuliza nilimuona akihangaika kama anasumbuliwa na kitu kichwani, ..lakini kama nilivyosema awali, huruma ilishaondoka, sikujali tena‘Mke wangu naomba unipe muda, nikafanyie uchunguzi,…’akasema‘Uchunguzi wa nini tena…?’ nikauliza‘Kuhusu hilo la mtoto… sikumbuki hilo kabisa, sina uhakika siwezi kukudanganya,..ndoto nyingi niliota zinakuwa kama za ukweli…kuna …unasikia mke wangu, lakini ni siri yetu, hata…siku marehemu anauwawa, ok, tuache tu…’akasema sasa akinitolea macho.‘Hayo utayasema mbele ya mahakama,…na mimi nitakuwa shahidi, na ukumbuke hapo sitasimama upande wako,…kuna mengi nayafahamu dhidi yako, siku hiyo ndio utayasikia…’nikasema‘Mke wangu nisaidie, mimi ni mume wako…nahisi kama nimetenda kosa…isije ikawa ni kweli…labda nimeua kweli…’akasema sasa akinitolea macho‘Umeua…?’ nikamuuuliza‘Sijui…mke wangu sijui…ndoto zinaniandama, siwezi kulala….nisaidie mke wangu….’akasema akiwa kama ananiomba kwa mikono‘Umemuua nani…?’ niikamuuliza‘Usirudie hiyo kauli tena, mimi sijaua, au sio, ni ndoto tu mke wangu,…naogopa mke wangu, usije kusema hivyo tena, unasikia, …’akasema kweli sasa akionyesha kuhaha‘Swali la tatu, ni nani mwanamke mliyezaa naye?’ nikamuuliza, sikujali huko kuhaha kwake, japokuwa kiukweli nilimuona akipata shida.‘Mwanamke niliyezaa naye!?..mungu wangu, ni nini tena hiki…!’akashika kichwa‘Jibu swali acha ujanja…’nikasema‘Mke gani jamani, mke wangu ni wewe, nimezaa na wewe, nimekumbuka mwanamke niliyemuona kwenye ndoto ni wewe…wewe ndiye aliyemchukua mtoto, ukakimbia naye, unasema sio wangu, sio wa halali…ukataka kwenda kumtupa, ni wewe, niambie mtoto wangu yupo wapi, niambie ....’akasema sasa anasimama kwa hasira akinielekea mimi.‘Wewe mwanaume…hebu acha huo mchezo wa kuigiza…’nikasema sasa akawa ananisogelea katoa macho, anatetemeka, mimi nikasogea, na nilipoona hali inazidi, nigeuka na kukimbilia mbali na yeye, mara akadondoka sakafuni, na nikasikia kama akakoroma nikajua nimeua…*********** Nikarudi pale alipolala sakafuni…niliona sasa katulia, nikashika mapigo ya moyo, nikaona yanapiga kwa mbali, lakini inatia mashaka, haraka nikachukua simu, nikitaka kumpigia docta, mara mtu huyo katikisikaNikaacha simu, na kumuangalia….akaanza kujiinua, halafu akakaa…akawa sasa anaangalia huku na kule, mara akasimama,..huku anayumba yumba‘Kumetokea nini…?’ akauliza‘Hebu kaa pale maswali yanaendelea…’nikasema‘Maswali!!, maswali gani…?’ akauliza`Swali la nne, je ni wewe uliyechukua mikataba kwenye kabati langu, la hapa na kule ofisini ?’ nikauliza‘Mimi.!!!...ofisini kwako, lini,..?’ akawa anashangaa , akageuka akauona ule mkataba, kwa haraka akauchukua na kuishikilia mkononi, halafu akageuka kuniangalia..halafu, akageuka kuangalia mlango unaolekea maktaba, akaangalia saa;‘Mbona umewahi leo kutoka kazini, …?’ akaniuliza‘Swali jingine…umeniupuuza kunijibu swali la awali, hiyo inanakiliwa kwenye kumbukumbu, wakili sikia hiyo…’nikasema, akageuka huku na kule kama anatafuta mtu, nahisi ni hapo niliposema wakili sikia hiyo, hakuelewa mimi nina maana gani.Swali la tano…, Je siku makabrasha alipouliwa ulikwenda kwake kufanya nini?’ swali hili likamfanya ashituke na kugeuka akaniangalia kwa mashaka, akageuka na kuangalia mlango wa kutoka nje, kama anaogopa vile, baadae …, akasema;‘Ma-mamamaah...ina maana ni kweli.....haiwezekani, mke wangu kumetokea nini, ulirudi ulinikuta nipo wapi, niambie mara moja, maana hii ni dalili mbaya, mke wangu tafadhali...halafu alishazikwa, ….au..sikumbuki mimi, hivi kweli eeh…’akasimama sasa..na kuanza kutoka nje‘Unakwenda wapi, haujamalizana, nimeshakuambia nikitoka hapa mimi naelekea kwa wakili wetu, nafuata hatua nyingine, tutakutana mahakamani...’nikasema lakini mwenzangu alikuwa anaondoka, haangalii nyuma akasema;‘Nawahi mazishi....’akatoka, mimi nilicheka kidogo na kusema‘Janja yako...nafikiri wewe hunifahamu eehe...’na mimi nikamfuatilia huko huko nje, nilitaka hili tatizo nilimalize leo, nimuachie hiyo kazi wakili, sasa asonge mbele, tulifikishe hili tatizo kwenye vyombo vya sheria,…Kwa haraka na mimi nikatoka nje, nikamuona akiingia kwenye gari lake, na mara simu yangu ikaita, nikaipokea kabla sijaangalia mpigaji ni nani. Huyo mtu akasema;‘Mimi ni docta .....’akasema kumbe alikuwa yule docta aliyemtibia mume wangu, nikashukuru maana nilikuwa na mpango wa kumpigia, kuhakiki haya anayoyafanya mume wangu kuwa ni ya ukweli au anaigiza tu.‘Hali yako docta tena nilikuwa nataka kuongea na wewe..’nikasema‘Ndio ...ndio maana hata mimi nilitaka kujua hali ya mume wako, anaendeleaje kwani kipindi kile cha matibabu, kulikuwa na docta mwenzangu, ambaye alikuwa akimwangalia kwa upande wa kumbukumbu, na alitaka kujua kama kuna hali yoyote inayojitokea kwake..yupo hapa nyumbani ?’ akaniuliza‘Ndi-ndio…lakini anatoka..’nikasema‘Sasa Yule docta wake kaja leo ndio karudi toka safari’akasema‘Kwahiyo anasemaje…?’ nikauliza nikionyesha kushangaa.‘Sijui kama mliwahi kuongea naye kipindi kile, kuna kitu kwa mume wako ambacho alikigundua, na kwa muda ule hilo hatukuwa tumelitila maanani sana..lakini kuna matukio yalitokea…kipindi hicho docta ameshaondoka…’akasema‘Matukio gani…?’ nikauliza‘Kusahau..au kujiwa na kitu kama njozi…anaweza akalala, na kuota, akafanya vitu kwa vitendo, au mchana, akawa kama kalala, akafanya mambo tofauti na utashi wake, inakuwa kama njozi…’akasema‘Unasema nini…?’ nikauliza kwa mshangao.‘Kuna matukio yalitokea akatoweka hapa hosp, na baadae akarudi, akiulizwa kafanya nini, anakuwa hakumbuki,…au akakumbuka jambo, akafanya kwa umakini zaidi, au anakuwa na akili ya ajabu unaweza kumuuliza jambo, akakujibu kwa umakini sana,..na hali hiyo ikiisha, hawezi kufanya hivyo…’akasema‘Docta …’nikasema sasa nikianza kuingiwa na mashaka.‘Sasa docta wake kaja, na kaniambia hayo yanaweza kumtokea mgonjwa wa namna hiyo, inatakiwa kuwa makini naye sana, kwani anaweza kufanya jambo la hatari....’akasema‘Unasema nini docta mbona hamkuwahi kuniambia kitu kama hichoo’nikasema kwa hasira.‘Baada ya uchunguzi, ...kipindi kile tulipokuwa naye, alionyesha dalili, kuwa kapona, na mwenzangu akawa keshaondoka, ...tulimwambia yule docta mnayeishi naye, maana wakati huo wewe ulikuwa na matatizo… ulikuwa jela,..sasa kwa vile mwenzangu karudi leo na tukawa tunafuatilia jarida la mume wako..’akasema‘Docta …’nikataka kusema lakini yeye akaendelea kuongea‘Sasa… kwanini, mume wako hafiki kwenye kliniki yake maana hiyo ingelisaidia kujua hatua za maendeleo yake, yeye aliandikiwa afike kila mara hapa hospitali kwa kliniki yake,hajafika kama tulivyomuagiza, ndio maana tukaamua tukupigie’akasema.‘Docta mimi ninaweza kuwashitaki, ..hilo ni kosa kubwa sana, maana sasa hivi nimemuona mume wangu kama kachanganyikiwa, na mimi nilifikiria kuwa anajifanya..kwasababu nimekuwa nikimuuliza maswali., anajibu kama anaigiza, kuwa hajui, mara anasema kasahau, mara aliota,..katoka sasa hivi na gari, yupo kama ...’nikasema.‘Mfuatilieni haraka,...na mleteni hapa hospitalini hiyo dalili inaweza kuleta matatizo mengine docta wake yupo, na akiondoka itachukua muda kurudi. ....’akasema docta, na mimi nikakata simu yake na kuingia kwenye gari langu, nikijaribu kumfuatilia, sikujua kabisa kaelekea wapi.....oh, ina maana mume wangu akchanganyikiwa kweli....NB: Kwa leo ndio hivyo,WAZO LA LEO: Kwa wandoa mmoja anapoumwa, ni vyema mkajaliana kwanza, hata kama kulikuwa na sintofahamu, migongano ya kindoa, ya kifamilia, na mitihani mingine ya kimaisha, hayo yote ya kibinafsi, na masilahi yawekwe kando kwanzao, muangalie swala la afya, swala la ugonjwa, kwani afya ni bora kuliko mali, kuliko hayo mnayokosana nayo..na huenda huo ukawa na mtihani katika kutatua matatizo yenu.‘Kuna matukio yalitokea akiwa hospitalini, kipindi hicho nahisi ulikuwa jela.., akatoweka hapa hosp, na baadae akarudi, akiulizwa kwanini katoroka na alikwenda wapi, kafanya nini, anakuwa hakumbuki,…’ilikuwa kauli ya docta.‘Na anaweza akafikiria jambo kwa muda, likamkwaza, basi hali hiyo ikitokea analifuatilia hilo jambo kwa vitendo…hapo sio kwa akili yake ya kawaida…au anaweza akafanya jambo kama kubomoa kitu, kuvuruga vitu halafu akaja kuvipanga kaam vilikuwa awali hata bila kukosea…hayo yote yalitokea tukayaona…’akasema docta…‘Na hali hiyo ikiisha, hawezi kufanya hivyo, anaweza akaukumbuka au asikumbuke..’Hapo sikutaka hata kumsikiliza zaidi.Endelea na kisa chetu....***********Ina maana mume wangu kachanganyikiwa, na kuchanganyikiwa huko ni kwa muda gani, je huko kuchanganyikiwa hakutakuwa na madhara yoyote kwake, na pengine kwangu, maana anaweza kufanya jambo la kuhatarisha hata maisha yangu au yake, au ya watoto wake mwenyewe..’nikamuuliza docta, muda huo nipo kwenye gari namfuatilia mume wangu, na sijui atakuwa kaelekea wapi.Nikiwa naendesha wazo likanijia kuwa nielekee njia ambayo mara nyingi hupita akielekea kazini kwake, sikuwa na uhakika, nilijiwa na wazo hilo tu, na hisia zangu zilinituma nifanye hivyo…nikaendesha kwa muda hadi kukaribia kazini kwake, sikuona dalili ya gari lake.Nikatoka hapo, nikaelekea barabara nyingine ambayo huwa anapitia wateja wake..nikapita nikiulizia kama kuna mtu kaona gari lake,‘Hatujaliona…’ilikuwa kauli ya kila niliyemuuliza.Nigeuza gari, sasa nikawa naelekea njia ya alipokuwa akiishi rafiki yangu…niliendesha hadi pale kwa fundi, ambapo alipendelea kuosha magari, nilipouliza hapo nikaambiwa.‘Alipita hapa, na kaingia kwenye hiyo nyumba hapo…’akasema fundi mmoja, hapo nikapumua.Ilikuwa ni nyumba hiyo aliyokuwa akiishi rafiki yangu, nikajiuliza hapo kafuata nini, maana rafiki yangu hayupo hapo tena…nikaelekea kwenye nyumba hiyo na kweli nililiona gari la mume wangu limesimama kando kando ya hiyo nyumba.Nilisogeza gari langu hadi kwenye hilo gari lake, na kutoka nje ya gari langu, nilisogea hadi kwenye lake kwa tahadhari, sasa naanza kumuogopa mume wangu mwenyewe.Mimi nilijua labda yupo humo ndani ya gari lake, lakini hakuwemo humo, nikageuka, kuangalia kwenye ile nyumba, nilimuona mume wangu akiwa kasimama pale mlangoni, akiwa anaongea na mtu, na huyo mtu anayeongea naye yupo kwa ndani, ina maana yeye kasimama mlangoni lakini huyo mtu anayeongea naye hakutaka kutoka nje…baadae mlango ukafungwa na mume wangu akabakia hapo mlangoni, baadae nikaona anagonga tena, na mlango ukafunguliwa.Kuna mtu alijitokeza sehemu ya juu, yaani kichwa na sehemu ya ndogo ya kiwiliwili, wakawa wanaongea na mume wangu, na yule mtu alionekana kama kushangaa, halafu akaongea jambo, kwa umbali ule sikuweza kufahamu wanaongea nini, lakini baadaye nilimuona mume wangu akigeuka, na kuanza kuja muelekeo wa gari lake. Kwa muda ule nilikuwa bado nimesimama pembeni ya gari lake, ina maana jinsi anavyokuja angeliniona lakini cha ajabu hakuniangalia wala hakuonyesha dalili ya kuniona au kushituka, na inavyoonekana ni kama hakunitambua kabisa, akafika kwenye gari lake akaingia na kuliwasha, akasogeza nyumba kidogo, akageuza gari na kuelekea barabara kuu.Mimi kwa haraka nikakimbilia gari langu na kuliwasha, na hapo nikaanza kumfuatilia kwa nyuma, na wazo likanijia, kuwa nijaribu kumpigia rafiki yake niongee naye, huenda akanipa ushauri ;‘Unasema mume wako anaonekana kuchanagnyikiwa kwa vipi?’ akaniuliza, nikamuelezea ilivyokuwa kwa kifupi , na yeye akasema;‘Ndio ni kweli madakitari wake, kipindi kile waliniambia niwe nikifuatilia nyendo na afya yake, kama kuna mabadiliko kama hayo, mwanzoni nilijaribu kumfuatilia na kumpima kwa kila nijuavyo mimi, na hata kuwa karibu naye, na sikuweza kuona dalili kama hizo, kwangu mimi nikaona huenda hali kama hiyo haitaweza kutokea, na kwa vile alishaonyesha dalili za kupona....sikuona hata umuhimu wa kukuambia hilo,...’akasema‘Kwahiyo nifanyeje sasa?’ nikamuuliza, sikutaka kumlaumu‘Cha muhimu ni kumfuatilia, kuna mambo kayapanga kichwani mwake labda hivyo, anataka kuyafanya, akiyamaliza atarudi nyumbani, wasiwasi wangu ni kuwa, asije akawa kapanga kufanya jambo baya, au akakasirika kutokana na watu kutokumuelewa akafanya fujo,…‘Mungu wangu…’nikasema hivyo‘Usiogope,…wewe fanya hivi,kwa vile hana habari na wewe, akili yake hapo haipo na wewe,..wewe mfuatilie kwa karibu karibu tu, na wala usimshtue, ukimshutua unaweza kumuharibu, hatujui anaweza kupata mshtuko wa moyo....’akasema‘Una maana gani kusema hivyo?’ nikamuuliza‘Hapo alipo yupo kama vile mtu aliyelala, na anakuwa kama anaota, ...sasa anaweza akapanga kufanya jambo kutokana na fikira zake zilizopita,anaweza akawa kajenga kisasi moyoni, na akataka kufanya jambo lolote kwa mtu anayemuhisi ni mbaya wake, hiyo inaweza ikatokea, lakini sio lazima itokee hivyo, hayo ni maelezo tu kwa ujumla wake.....’akasema‘Mbona unanitisha hivyo..’nikasema‘Nakuambia hayo ili uwe makini naye, na wala usione ajabu ya hayo matendo yake,..unachotakiwa ni kuwa muangalifu kwa sasa,…hiyo hali inaweza ikakusumbua sana,..ni vyema uache mipango yako mingine yote dhidi yake, huenda hiyo miapango na unavyomuuliza ndio sababu ya hali hiyo kujitokeza…na kwa hali hiyo, yeye anaweza akafanya matendo hata akiwa usingizini..’akasema‘Kwa vipi , mbona sikulewi’nikasema‘Hujawahi kusikia watu wanafanya matendo wakiwa usingizini , inaitwa `disambiguation’, au ‘somnambulism’ kwa maneno ya kitaalamu… mtu mwenye matatizo kama hayo anaweza akaamuka kabisa kitandani, akatoka hata nje, akaenda kufanya kazi, lakini kwake inakuwa ni kama njozi, anaota, lakini kwa vitendo vya kweli, ..’akasema‘Mungu wangu...!’ nikasema‘Wasi wasi wangu kwa jinsi mnavyoishi naye kwa kwasasa, mnaweza mkawa mumekwaruzana, na ikawa imemkwaza, na akili za kwenye ndoto zikamtuma kufanya jambo baya dhidi yako, anaweza akafanya hivyo, kwahiyo, hakikisha mkilala, vitu kama visu, mapanga,...na...oh, na ile bastola yako umesharudishiwa?’ akauliza‘Ndio ninayo, polisi walishamaliza kazi nayo...’nikasema‘Oh, sasa inabidi uiondoe hapo unapoweka, uiweke sehemu ambayo hataweza kuiona, vinginevyo kwa hali kama hiyo anaweza kufanya lolote baya, sio kwako tu, hata kwa mtu mwingine kwa jinsi akili yake itakavyomtuma....’akasema‘Ina maana basi yawezekana yeye ndiye …ka-ka…hapana, ingelionekana kwenye video ya matukio au sio…sio yeye…’nikasema‘Hiyo hatuna uhakika, …yawezekana pia,..lakini hakuna ushahidi huo, au sio…’akasema‘Kwa namna ina maana mume wangu ndio keshaharibikiwa na akili kabisa?’ nikauliza‘Hapana..sio kihivyo kuwa kaharibikiwa, kwa muda unaweza kusema hivyo, lakini ni swala la muda, hiyo inaonyesha kuwa alikuwa hajapona, na msongo wa mawazo, unamtonyesha,..’akasema‘Oh, kwahiyo ni kosa langu…’nikaanza kujilaumu‘Huwezi kujilaumu, wakati mwingine wa kulaumiwa ni yeye kwa mambo yake, ni kwanini hataki kujiweka wazi, ..ili kuondokana na shida hiyo alitakiwa awe muwazi kwako, aseme ukweli wote yaishe ..vyovyote itakavyokuwa lakini nafsi yake inakuwa huru…’akasema‘Hataki kufanya hivyo, na kwa jinsi nilivyomuhoji, sio mtu wa kukubali ukweli tena,nakeshajiamini kuwa alichofanya ni sahihi, ..namlaumu sana marehemu…’nikasema‘Lakini hiyo hali itakuja kuisha, au ikawa inarejea kidogo kidogo kwa kipindi fulanifulani, na walichoshauri wataalamu ni kuwa kama hali kama hiyo itatokea, ni vyema, akarudishwa na kuwa kwenye mikono yao....wamachunguze tena...nikuulize tu, kwani mumekorofishana nini tena?’akasema na kuuliza‘Hatujakwaruzana kihivyoo…, ilikuwa mazungumzo ya kawaida ya kumuhoji kutaka kujua ukweli, kwa haya yanayojitokeza sasa, maana ni muhimu nijue ukweli wake, watu wanakuja wanadai hisa, kwanini..kwahiyo mimi ni wajibu wangu kuhoji, ni hivyo tu..na kiukweli, ni lazima ifike mahali tuyamalize haya matatizo, na ndivyo nilivyotaka, iwe, sikujua kuwa kuna tatizo kama hilo...’nikasema.‘Pole sana, ....najua haliunayokabiliana nayo, na ubishi wako utakusumbua sana, lakini komaa hivyo hivyo..ni mume wako au sio..’akasema na kutulia.‘Kwahiyo sasa nifanye nini, mfano akirudi nyumbani akatulia, nimwambieje kuwa anatakiwa hospitalini?’ nikauliza‘Kwasasa mfuatilie kwanza , uone anataka kufanya nini, na huenda huko anapokwenda kukaweza kukupa majibu ya mambo mengine, japokuwa nakushauri usichukulie kuwa ndio ukweli wenyewe halisi…wakati mwingine na yeye ni hisia zake zinamtuma tu..hana uhakika..’akasema..’akasema‘Kwanini nisiwaambie polisi, wakaifanya hii kazi, ili tuwe salama, na kama kuna lolote baya wao wanaweza kumdhibiti, na kumshika na kumfikisha haspitalini, je akiua, mimi nitasemaje,...?’ nikasema‘Hapana, usije ukawaambia polisi kwanza, hatujui mume wako alikumbwa na nini huko nyuma, ngoja kwanza tumfuatilie wenyewe, muhimu kwasasa ni namna ya kumfikisha hospitalini…’akasema‘Una maana gani,..yawezekana ..’sikumalizia‘Ndio, yawezekana, huenda aliwahi kufanya jambo baya hatuwezi kulifahamu hilo, ni kwa tahadhari tu, na ujue matatizo yaliyotokea hayajakwisha kwa polisi bado wanafuatilia, kwahiyo wakimuhisi tu, wanaweza kumkamata…na hapo hawatajali kuwa huyo mtu ana matatizo gani, kwasababu alishaonekana kapona, wanaweza kusema anasingizia,…na huwezi kuja kuwalamu, maana watakuwa wanatimiza wajibu wao…’akasema‘Mhh…hapo sasa unanipa mtihani, ..’nikasema‘Kwa hivi sasa fanya nilivyokuagiza,…muhimu asije kuingia kwenye mikono ya polisi, labda akafanya jambo baya akakamatwa, kwani akiwekwa ndani, kwa hali kama..tutazidi kumweka mahali pabaya...’akasema.‘Ok, nimekuelewa, ....’nikasema na kabla sijakata simu, akasema‘Je unaweza kuyafanya hayo peke yako, au nije kukusaidia?’ akauliza‘Ninaweza, usijali....’nikasema hivyo japokuwa kiukweli nafsini nilishaanza kuingiwa na uwoga,…maana mtu ndio yupo hivyo, je akinigeuka,..je lolote likitokea…na wakati nawaza hivyo, mara nikamuona mume wangu akielekea barabara ya kuelekea uwanja wa ndege.‘Huyu mtu sasa anakwenda wapi …?’ nikajiuliza na wakati huo sijakata simu, nikasikia docta akisema‘Mfuatilie usimuache..unasikia..’hapo mimi nikakata simu.Nikawa namfuatilia kwa nyuma na gari langu, kwa muelekeo huo wa uwanja wa ndege, nikahisi labda…, huenda atakuwa anaelekea kule kulipokuwa ofisi za marehemu, maana hata alipotoka hapo nyumbani alisema kuwa anakwenda kwenye mazishi,..sasa sijui mazishi ya nani,..Nikawa naendelea kuwaza akilini, …‘Huyu kachanganyikiwa na akili yake hapo nahisi ipo kwa marehemu, je kuna kitu gani anakifuatilia…mmh, ngoja nione…’nikawaza hivyo kwa kuongea akilini.‘Lakini alisema anakwenda kwenye mazishi, sasa kwanini tena anakwenda kwenye ofisi zake, kufuata nini huko..?’ nikajiuliza, kiukweli Makabrasha alishazikwa muda sasa.Nilimfuatilia kwa karibu, nikiogopa asije akafanya jambo la hatari, alikuwa akiendesha kwa mwendo wa kawaida tu, na hakukuonekana kuyumbayumba hivi , au kwenda kinyume na utaratibu wa barabarani, na hapo sikuwaelewa , huko kusema anafanya hayo akiwa usingizini..haya ndio mtihani huu nitafanyaje.Tukafika maeneo karibu na uwanja wa ndege, na kama nilivyohisi, nilimuona akigeuza gari kulia kwake, na kuingia eneo lililopo lile jengo, alipokuwa akifanyia kazi Makabrasha, alifika kwenye eneo la kuegesha magari, akasimamisha,Na mimi nikafika na kugesha gari langu pembeni ya gari lake, nikatoka, na kumfuatilia, nilimuona akiongea na mhudumu mmoja, na baadaye akasogea pale alipokaa mlinzi wakawa wanaongea, ilionekana kama hawaelewani, na yule mlinzi akawa kama anafoka, na kumzuia mume wangu, kuna kitu mume wangu alikuwa anataka kukifanya. Lakini mlinzi anamkatalia…Mimi sikutaka kuingilia kati kwanza, …niliona jinsi gani wanavyobishana na huyo mlinzi, na sasa mlinzi anamzuia, na baadaye nikaona walinzi wengine wakija kumsaidia mwenzao, na mlinzi mmoja akamshika mkono mume wangu na kumvuta pembeni, wakawa wanaongea naye halafu mume wangu akaonekana kutikisa kichwa kukubaliana naye.. Nahisi walikubaliana jambo, maana nilimuona mume wangu akigeuka na akawa anarudi kwenye gari lake, alifika kwenye gari lake, hakuingia ndani, badala yake akasogea kwenye kiambaza cha hilo jengo, na kusimama akawa kama kajiegemeza na kuinamisha kichwa chini, alikaa vile kwa muda, na mimi kwa haraka nikaenda kuongea na wale walinzi.‘Yule ni mume wangu kuna nini kinaendelea?’ nikawauliza‘Yule jamaa sijui kachanganyikiwa…eti anakuja hapa anamuulizia Marehemu Makabrasha, sisi tumemwambia huyo mtu hayupo tena duniani, keshafariki, lakini hatuelewi, yeye anadai wameahidiana kukutana na marehemu ofisini kwake, na anasema yeye ana uhakika huyo mtu yupo ndani,....’akasema‘Oh, ...’nikasema hivyo tu, na huyo jamaa akageuka kumuangalia mume wangu halafu akaendelea kuongea kwa kusema;‘Tukamwambia huyo mtu hayupo duniani tena, lakini cha ajabu, huyo jamaa unasema ni mume wako…?’ akauliza sasa akiniangalia mimi kwa uso wa kunichunguza‘Ndio…’nikasema‘Mhh…unajua kasema hivi, yeye ana uhakika Makabrasha yupo ofisini kwake, kwani waliongea naye kwenye simu wakakubalina kuwa aje wakutane naye hapo ofisini kwake kwani kuna jambo muhimu wanataka kulimalizia....’akasema‘Alikuambia ni jambo gani…?’ nikamuuliza‘Ndio,..unajua anaongea sana,…kasema sijui kuna mikataba yao muhimu anatakiwa wakamalizane naye,..na huyo marehemu ni wakili wake, kwahiyo kwake ni muhimu sana wakutane naye…kwa haraka, kabla hajachelewa, na hapo alipo katoroka hospitalini…’akasema‘Hamna shida, ....muachenia atulie, nahisi akili zake zinakwenda mbele na kurudi nyuma,… mara anakwenda mazishi, sasa anawaza tena siku za nyuma, akiwa na huyo rafiki yake,..najua kwa hivi sasa hajaamini kuwa rafiki yake hayupo duniani.., alikuwa rafiki yake mkubwa sana...’nikasema‘Oooh,…kumbe, basi ndio hivyo, sisi tulitaka tumkamate tuwaite polisi, lakini bosi kasema tumuache tu…’akasema‘Hamna shida nitaondoka naye…’nikasema‘Sasa kwanini hamu-mpeleki hospitalini, na kama kachanganyikiwa kwanini anaendesha gari….si hatari namna hiyo,..halafu nakumbuka kama niliwahi kumuona mahali, lakini muda kidogo, …’akasema mlinzi mwingine yeye muda mrefu alikuwa akimuangalia mume wangu kama anamchunguza kwa macho‘Wapi…?’ nikauliza, sasa nikimuangalia huyo mlinzi, na wakati huo bado anamchunguza mume wangu kwa macho.‘Aliwahi kufika hapa…nimemkumbuka atakuwa ndio yeye..’akasema‘Kwani kufika hapa si kila mtu anafika, hebu acha uchumvi wako, njaa zitakuua…’akasema mlinzi mwingine na kuondoka, nikabakia na huyo askari anayemchunguza mume wangu kwa macho.‘Unasikia dada, eeh, sijui nikuite madam,..huyu mtu nimemkumbuka vyema…alifika siku hiyo na bajaji, kwa haraka akaingia chooni,…kule chooni hakukuwa na mtu mwingine mara naona anatoka mtu mwingine, sio Yule aliyeingia, kwa…sura..lakini kwa maumbile ni Yule Yule…unasikia..’akasema‘Wewe ulikuwa wapi…?’ nikamuuliza‘Nilikuwa pale karibu na sehemu ya kuingilia chooni, nilikuwa nimetokea huko huko chooni,…sasa, ..atakuwa ndio yeye, tatizo siku ile kwa mihamaniko yangu ya maisha, wanaite stress, nikaamua kugida siki ya kazi, lakini sio sana, maana kumbukumbu bado zilikuwepo, uzuri mimi nina kichwa cha kukariri sana sura za watu,…’akasema‘Na nimekumbuka hivyo kwasababu ilikuwa siku ile ya tukio baya hapa kwenye hili jengo,..ni siku ile alipouwawa marehemu…’akasema hivyo na hapo nikahis mwili ukinywea, nikajua sasa kunakuja tatizo jingine.‘Unajua polisi walinihoji sana siku ile, lakini sikuwa na kumbukumu ya huyu mtu…kabisa, ilinitoka, sasa nilipomuona ndio nimekumbuka, kwa ushauri wangu huyu mtu anaweza kuwa matatani, ama anajiigiza, au kweli kachanganyikiwa, lakini nahis yawezekana pia ni kutokana na marehemu,..unajua damu ni mbaya sana…’akasema‘Una maana gani kusema hivyo..?’ nikamuuliza‘Jinsi siku ile alivyofanya, mimi namtilia mashaka…’akasema‘Mashaka gani, usitake kuzua mambo…?’ nikauliza na kusema‘Kwanini alipofika hapa akakimbilia chooni na kuvaa sura ya bandia…’akasema‘Sura ya bandia kwa vipi,..huyu mtu alikuwa mgonjwa…anaumwa, kwahiyo hayo unayowaza hayamuhusu umefananisha…’nikasema‘Nina uhakika ni yeye, sikosei, kwahiyo kachanganyikiwa, na nahisi ni baada ya kifo cha marehemu, kinamchanganya au sio, na kama anahusika, ndio maana….’akasema ‘Wewe, umesikia nilivyokuambia, huyu alikuwa kalazwa hospitalini, siku hiyo ya tukio, kwahiyo hayo unayowaza hayamuhusu kabisa…’nikasem‘Polis na hakimu watahakiki wenyewe…’akasema‘Kwanini unasema hivyo….?’ Nikamuuliza‘Nikiwaambia nilichokiona, …na hata polisi wananifahamu kwa kumbukumbu zangu, sura hazinipotei, hata tukio likitokea kwenye kundi kubwa, nikapitisha macho yangu kuwaangalia waliopo, siwasahau,…’akasema‘Hongera, lakini kwa hili umekosea…’nikasema‘Tutaona, kama kweli nimekosea…’akasema‘Mhh….hamna shida, sio tatizo kubwa sana ni kuchanganyikiwa tu kwasababu ya huo msiba…na wakati mwingine akichanganyikiwa anafanya hivyo, kujivalisha sura za bandia…’ Mimi nikasema hivyo kwa nia ya kumlinda mke wangu.‘Kama ningelikumbuka siku ile polisi waliponihoji, ningewaambia kila kitu, sijui ingelikuwaje…na hata wewe nimekukumbuka, ulifika siku ile, baadae, kweli si kweli, na..nimekumbuka wewe walikukamata, kukushuku, ..na hivi kesi yako iliishaje, nina uhakika sio wewe uliyeua…’akasema‘Una uhakika gani…?’ nikauliza‘Muuaji anaweza kuwa kama huyo jamaa…muda aliofika, na vitendo alivyovifanya, yeye anaweza kuwa ndiye muuaji, wewe, kutokana na walivyosema wachunguzi wa kitaalamu kama hawakukosea, wewe ulifika wakati marehemu keshauwawa..au sio..’akasema‘Hayo ni mambo ya polisi..’nikasema‘Sisi sote ni polisi ndio maana leo hii nalinda hapa,…niliacha kazi ya polis kwasababu za kifamilia, lakini ni kazi niliyokuwa nimeipenda sana, na nilitunukiwa zawadi ya kuwa na kumbukumbu, kukumbuka matukio, sura….lakini, kukatokea tatizo, nikafukuzwa kazi…’akasema‘Kwasababu ya umbea wako…’nikajikuta nimesema hivyo.‘Hahaha…sio hivyo madamu, maisha tu…na ujanja ukiwa mwingi, na..tamaa, kipindi kile nilikuwa kijana natamani mengi, hata hivyo ufanyeje, kama hali inakutuma hivyo, maisha magumu…’akasema‘Ni kweli mimi nilifika, ni kweli, nilikamatwa lakini hayo yamekwisha…’nikasema‘Pole sana,..ila kwa hili la mumeo, nahisi polis watafurahi wakimpata,..si muuaji hajapatikana,..si ndio hivyo, sasa wakimpata huyu mtu, atakuwa …ndio yeye, sijakosea…’akasema akiendelea kumuangalia mume wangu.‘Mume wangu hahusiki kwa lolote lile..’nikasema sasa nikitaka niondoke mbali na huyu mtu, lakini akawa ananifuata , akasema‘Sasa madamu, mimi nitakupigia simu…’ huyo jamaa akasema hivyo, nikawa najiuliza namba yangu ataipataje, sikutaka kumuuliza, ila nikasema‘Kwanini unipigie simu..?’ nikamuuliza‘Taarifa kama hizo wakizipata polisi, nahisi watanishukuru sana, sasa mimi sitaki polisi wazipate, …au unasemaje mama… mimi nitakupigia tuongee, mimi, eeh…siwezi kusema kwa polisi kabisa, unajua nilikuwa nawaza sana…sasa nimekumbuka, ni yeye,..na hata wewe ulikuja, …nimekumbika kila kitu,..je niwaambie polisi, ili niwe raia mwema, au tuongee..’ akasema kama ananiuliza‘Sikiliza, usijiingize kwenye matatizo,…haya mambo yameshakwisha, lakini kama unaona ni sawa, wapigie tu polisi, hamna shida ..’nikasema kama kumpima tu, lakini moyoni nikawa na wasiwasi sana.‘Jana tu polisi walifika hapa…wanauliza uliza tena kujua kama kuna lolote hatujawaambia, bahati nzuri, mimi nilikuwa pembeni, hawakuniona, ila nasikia walitaka na mimi wanihoji, maana nilikuwepo siku ile ya tukio …sasa ni wewe mama, kama hamna shida, ngoja nimpigie Yule mpelelezi …’akashika simu yake‘Unataka kufanya nini…?’ nikauliza‘Nataka niongee na polisi maana nitakuwa nafanya makosa, huyo mume wako alifika akaingia chooni, alipotoka akawa kava..kitu, …sura tofauti..nina uhakika ni yeye… nimemkumbuka, lazima haki ya bosi wetu itimilizwe…’akasema‘Unapoteza muda wako bure huyu mtu alikuwa mgonjwa kalazwa, wewe unataka kujiingiza kwenye matatizo y abure, haya ukiwaambia utapata faida gani…na una ushahidi gani kuwa ni yeye,..?’ nikamuuliza‘Umbile…na viatu alivyokuwa amevaa siku ile…alipoingia chooni na alipotoka, nakumbuka, na kitu kilichonifanya nijue kuwa ndiye huyo huyo, kwanza mimi nilitokea chooni, kulikuwa hakuna mtu mwingine aliyeingia, pili alipotoka ..viatu alisahau kubadilisha,..japokuwa eeh,..siku ile nililewa nikawa mvivu kufuatilia, ningelimkamata, nilichoka na kazi za hapa zina karaha …’ mara akaitwa, akaniashiria kwa mkono kuwa atanipigia simu.Mimi pale mwili mnzima ukawa hauna nguvu, linatoka hili linaingia jingine na najua huyu nia yake ni ili apewe chochote na akija kugundua kuwa mimi ni nani ni lazima atadai pesa nyingi, lakini dawa ya hawa watu naifahamu. Nikaona kwanza nimalizane na mume wangu, na kwa haraka nikageuka kumwangalia mume wangu, ambaye kwa muda huo alikuwa bado kasimama pale alipokuwa, sijui anasubiria nini muda wote huo,…Baadae akatembea kama anataka kuja kuongea na walinzi, na Yule mlinzi niliyekuwa naongea naye alikuwa kasimama akiongea na mlinzi aliyemuita, nahisi ni mkubwa wake wa kazi, na alipoona mume wangu anakwenda kuongea na wale walinzi wengine.Wakati mume wangu anawasogelea walinzi waliokuwepo karibu yake, nikamuona huyu mlinzi aliyekuwa akiongea nami, akitoa simu yake akampiga picha mume wangu kwa siri, mimi nilimuona.‘Huyu mtu anataka kufanya nini…?’ nikajiuliza nikisema kwa sauti na kwa haraka nikamfuata, na kumsogelea nikamuuliza;‘Kwanini unampiga picha mume wangu bila ridhaa yake..?’ nikamuuliza‘Mama nimeshakuambia nitakupigia simu, tutaongea, mimi hapa nipo kazini, na ni lazima niwe na ushahidi, nimeshampata huyu mtu, picha ya gari lake na namba ya gari …mimi natimiza wajibu wangu eeh..’akasema sasa akiendelea kupiga picha‘Unajua, wakati mwingine tunasaidiana au sio, sasa ni wewe tu…ikibidi nitawapatia au kutowapatia polisi, na nitakuwa nimetimiza wajibu wangu, au sio, nashukuru sasa nina ushahidi wa kutosha…’akasema na wakati huo gari la mume wangu linaanza kuondoka. Jamaa akawa anaendelea kupiga picha kwa siriMimi nikaona nimuwahi mume wangu, nikaingia kwenye gari na kuanza kuondoka, na kwenye kiyoo cha kuangalia nyuma nikamuona jamaa akiendelea kupiga picha, akipiga picha gari langu,… sikumjali tena, nikaanza kazi ya kumfuatilia mume wangu kwa nyuma, sijui akitoka hapo anaelekea wapi tena.Matatizo yanazidi kuongezeka…NB: Je itaishia wapi hii hali, hapo imeanza tuWAZO LA LEO: Kuna watu wanadai kuwa ili uwe tajiri ni lazima uwe na roho mbaya, sijui uhakiki huu waliupatia wapi, kuwa matajiri wote walikuwa hivyo, au wapo hivyo, (na roho mbaya). Roho nzuri, ukarimu utu wema, peke yake ni utajiri, na ukiwa kinyume chake wewe ni masikini hata kama una mali. Kuna watu wana mali lakini hawana amani, kila siku wanahisi wataibiwa, mioyo yao ina wasiwasi , wivu, dharau, choyo na ubakhili, hali kama hii inamfanya mtu asiwe na amani, je huu ni utajiri gani. Ni bora kuwa na riziki za halali, ukawa mwema kwa kila mtu, ukarimu na kusaidia, ukifanya hivyo utakuwa tajiri hata kama kwa walimwengu haupo kwenye orodha ya hao matajiri wanaotambulikana duniani. Usiku huo kwangu ulikuwa wa historia,Niliendelea kufuatana naye, nikawa sasa nachoka, lakini nitafanyaje, na ikafika sehemu sasa nikahisi anarudi nyumbani, nilipoona hivyo, nikajiuliza, haya akirudi nyumbani itakuwaje, mume sasa naanza kumuogopa!.‘Haya tisa, usiku nitalalaje naye, akiamua kuniua, au kuleta fujo….?’ Nikajiuliza na muda huo bado nipo nyuma yake kila anapokwenda nipo naye. Kwa haraka wazo likanijia, ..nikampigia simu mdogo, huyu ndiye wanawezana.‘Shemeji kuna tatizo gani?’ akaniuliza, alipopokea simu yangu‘Nakuomba uje nyumbani, ni muhimu sana ...’nikasema‘Kuna nini tena shemeji…unajua mimi bado nipo kazini, ?’ akauliza kwa mashaka, yeye kazi zake wakati mwingine anafanya hadi usiku‘Kuna kitu nataka unisaidie kuhusu kaka yako,....’nikasema, sikutaka kumwambia ni nini kinaendelea kwa wakati ule, lakini nilifahamu nikimwambia kuwa ni mambo ya kaka yake, atakuja haraka.‘Sawa nakuja shemji, lakini haumwi sana?’ akauliza‘Haumwi sana.., ni jambo dogo tu nitakuambia ukifika nyumani kwangu, lakini kwa hivi sasa sipo nyumbani, nitakuarifu nikifika…’nikasema na kukata simu, sikutaka kumpa maelezo mengi Nikaendelea kumfuatilia mume wangu, badala ya kueleka nyumbani sasa anaelekea njia ya kwenda ofisini kwangu,…alipofika getini kuingia kwenye jengo la ofisini yangu akasimamisha gari, akapiga honi, na mlinzi akatoka, na nikasikia akimuuliza;‘Mke wangu yupo ofisini kwake?’ akauliza‘Hapana, sio muda wa kazi sa hizi…’akasema mlinziWakati huo nilikuwa nimeshasimamisha gari langu, na hatua chache nyuma ya gari lake, na kwa vile mlinzi anaongea akiwa ndani kwa kupitia kidorisha, hakuweza kuona pale nilipokuwa nimesimamisha gari langu. Pale nikaona nikatoke ndani ya gari langi, ili niweze kusikia ni nini wanachokiongea,Kwa haraka nikatoka kwenye gari langu na kusogea karibu kidogo na wao,sehemu ambayo hawo wawili hawawezi kuniona, nikawa nawasikiliza, nilisikia na maswali hayo ya kutaka kujua kuwa mimi nipo ofisi, akauliza ni kwanini sipo ofisini na yeye anajua kuwa mimi nipo ofisiniMlinzi alimjibu vyema tu, japokuwa ilikuwa na maswali ya kushangaza, hapo nikaona nitumie mbinu, nikachukua simu yangu na kutuma ujumbe kwa yule mlinzi.‘Mwambie mimi nipo nyumbani namsubiria, je yupo wapi...’nikatuma ujumbe huo wa maneno kwa yule mlinzi, ambaye kwa vile gari la mume wangu limemzuia, hakuweza kuliona gari langu, akasikia sauti ya ujumbe kwenye simu yake, akawa anausoma, halafu akamwambia mume wangu.‘Mbona mke wako anasema yupo nyumbani anasema anakusubiri, anauliza wewe upo wapi...’akamwambia‘Hapana mimi nina uhakika yupo ofisini kwake, nina uhakika huo, ..nataka kwenda kuonana naye fungua geti, unanifahamu mimi ni nani au sio...’akasema‘Hapa ofisini kwasasa hayupo bosi, na haturuhusiwi kumfungulia mtu yoyote zaidi yake, saa kazi zimepita na mke wako aliondoka mapema tu, hakuna mtu ndani, zaidi ya sisi walinzi huku nje...’yule mlinzi akasema‘Mh, oh, ina maana muda wa kazi umekwisha, sio hamnijali mimi, ok, sawa,..oh, samahani, kwa usumbufu ....’akasema na kulirudisha gari lake nyuma na kuligeuza, nikajua kwasasa atakuwa akielekea nyumbani.*******Nilimfuatilia hadi tukafika nyumbaniTulipofika nyumbani, nikaliona gari la mdogo wake limeshafika, mjamaa, kwa akateremka kwenye gari, hakuangalia pembeni, kwa haraka haraka akakimbilia ndani, wala hakuangalia pembeni,Mimi nikateremka na kukagua gari lake kama kila kitu kipo sawa, mlango kafunga, na nilipohakikisha kama kila kitu kipo sawa, nikaingia kwenye hilo gari, na kulisogeza sehemu salama, na mimi nikaingia kwenye gari langu na kuliingiza sehemu maalumu ya magari, halafu, kwa haraka nikakimbilia ndani.Nilipofika ndani nilimuona mdogo wake, akiwa kakaa kwenye sofa, lakini mume wangu hakuwepo, nikamuuliza‘Umemuona kaka yako akiingia?’ nikamuuliza‘Ndio kaingia, lakini hakunisemesha, alionekana kama hanioni, kanipita kwa haraka akakimbilia chumbani kwenu, kwani kuna nini shemeji, maana hata machoni, sio w wa kawaida?’ akaniuliza‘Nitakuambia, ila muhimu nataka ulale hapa leo, kesho inabidi tumpeleke kaka yako hospitalini, kaka yako anaonekana kuchanganyikiwa kidogo....’nikasema.‘Ina maana hiyo hali imejitokeza?’ akauliza, na mimi nikamuangalia kwa mshangao na kumuuliza;‘Ina maana ulikuwa unafahamu kuwa kaka yako ana hali kama hiyo ya kuchanganyikiwa, kwanini unasema hiyo hali imejitokeza?’ nikamuuliza‘Ndio nafahamu… kipindi kile akiwa kule hospitali kwenye uchunguzi walisema hivyo, lakini jinsi alivyokuwa na maendeleo mazuri wakati anaruhusiwa, tuliona kuwa haitaweza kutokea tatizo kama hilo, hata docta, rafiki yake, alisema huenda hiyo hali haitajitokeza tena, baada ya yeye kumfuatilia kwa muda.....’akasema‘Sasa ndio hivyo imejitokeza, na kwa hali kama hiyo, kunahitajika mtu wa kuwa naye karibu wakati wote, naogopa usiku nisije nikashindwa, nikapitiwa na usingizi, ndio maana nikakuita. Sasa hivi cha kumsaidia hapa ni dawa, nahisi ndio maana walikuwa kuna madawa yale ya usingizi,..’nikasema‘Ndio, sib ado zipo..?’ akauliza‘Zipo tele tu, hazitumii siku hizi..’nikasema‘Tunaweza kumpa au sio…’akasema‘Sawa tutampa,ila wewe inabidi ulale hapa, sasa kama kuna lolote la kufuatilia huko kazini kwako nenda kalimalize urudi haraka , au wapigie simu, ...kuwa kuna dharura, hutarudi tena huko...’nikasema‘Hakuna shinda shemeji mimi nimesha waaga kabisa,...’akasema na mara mume wangu akatoka na kuniangalia alionekana kama kunishangaa, halafu akasema;‘Mke wangu, sijui kuna nini kinaendelea kwenye kichwa changu...hivi nipo sawa kweli…’akasema akishika kichwa chake.‘Kwani unajisikiaje?’ nikamuuliza‘Hivi nikuulize ni lini tulikuwa tunaongea kuhusu mtoto, ukaniuliza kuwa labda mimi nina mtoto nje, tena mtoto mwenyewe wa kiume?’ akaniuliza akiniangalia kwa macho ya kujiuliza. Kidogo, macho yanaanza kurejea kwenye uhai, lakini…‘Mchana, au…jioni hivi,…tuliongea ndio, kwani vipi?’ nikamuuliza‘Nimekwenda kumfuatilia huyo mtoto, hayupo,... hayupo kabisa …nahisi kuna tatizo, unajua hata huyo mama anayekaa na huyo mtoto hayupo.....nahisi watakuwa wameamua kutukimbia na mtoto wetu, huenda wameamua kunisaliti, una uhakika, kuwa nina mtoto ....tuna mtoto wa kiume, una uhakika?’ akawa ananiuliza‘Hamna kitu kama hicho mume wangu, nilikuwa nakutania tu, nilikuwa nakuuliza kama kukupima akili yako, kwani vipi tena ...’nikasema‘Huo sio utani mke wangu, nikweli nina..tuna mtoto...ni lazima tumchukue mtoto wetu, Yule mama eeh, hawezi kumlea kabisa…eti siku moja anadai kuwa mtoto ni wake na mimi hanitambui…wewe, hahaha, eti yeye ni mama yake na mimi sina haki naye,..’akasema‘Mama yake!! Kwani mama yake ni nani…?’ nikamuuliza bila kujali kuwa namuongezea mawazo‘Mama yake, eeh!!!,…mama yake si wewe, tatizo wewe umechanganyikiwa, sijui kwanini, hivi kwanini ulitaka kumtupa mtoto wetu…niambie ni kwanini, sasa mimi namtaka mtoto wangu , leo hii hii…hili sio jambo la mdhaha, mimi namtaka mtoto wangu haraka…’akasema kwa hasira sasa.‘Sikiliza mume wangu tutamtafuta huyo mtoto kesho, unasikia, kesho tutakwenda mimi na wewe hadi kwa huyo mama yake unasikia, usiwe na wasiwasi…’nikasemaKidogo akatulia, na akatizama saa yake mkononi, halafu akasema;‘Tatizo ni huyo Makabrasha nilimpa kazi sasa sijui imekuwaje, unajua nimefika hadi ofisin kwake, ili aweze kulifuatilia hili jambo kisheria, yaani hiyo ndio njia sahihi, kwenye sheria, na mikataba ikiwepo, mtu hawezi kuvuka kihunzi, sheria itambana,…kiukweli mimi siwezi kuacha damu yangu ipotee hivi hivi, halafu mtoto mwenyewe ni wa kiume,…’akasema na mimi hapo nikawa kimia‘Mke wangu, si wewe ulikuwa unataka mtoto wa kiume, ni wewe au ni mimi, …haah, ndio, sote tulikuwa tunataka mtoto wa kiume si ndio hivyo…?’ akauliza‘Ndi-ndio hivyo…, mungu lakini hatuja-jalia kumpata mtoto wa kiume.., tutampata tu, mungu akipenda…’nikasema‘Keshatujalia bwana, wewe vipi, si ndio huyo, huyo mwanamke ni mwizi tu…kamchukua, nikuulize kwanini ulikuwa unataka kumtupa, mtoto wetu…eeh..?’ akanigeukia tena kwa hasira.‘Si nimekuambia mume wangu kesho tutamfuata sijamtupa..’nikasema‘Yah…kesho,..maana yule ni mwizi tu, unasiki,a huyo ni mtoto wetu, …sasa tuyaache hayo, wakili atalishughulikia hilo, Yule wakili hana mchezo, yaani vyovyote utakavyo, anakufanyia, ni mjanja kweli kweli, sasa mke wangu, ni kuhusu ule mkataba wetu, eeh, si unaujua eeh…’akasema‘Ndio ule wa zamani…’nikasema‘Kwani kuna wa zamani na wa sasa…mke wngu umechanganyikiwa nini…ngoja nityampigia wakili aje, tumalizane, nataka tulimalize leo hii , hii, sitaki cha zamani na sasa, mkataba ni mmoja, au sio mke wangu..?’ akaniuliza na mimi hapo nikamuuliza‘Huyo wakili ni nani ..?’ nikamuuliza‘Si Makabrasha, na wewe bwana umeshamsahau tena, ndio huyo huyo, sasa hivi nimetoka ofisini kwake, yeye hayupo, walinzi wake wababaishaji, eti wanadai, kafariki, hawa watu bwana, kama hawampendi mtu watamzushia uwongo tu , hivi kuna mtu anaweza kumzulia mwingine kifo, ngoja nitamuambia, na Yule atafukuzwa kazi, wewe subiria tu…’akasema‘Basi usijali mume wangu…hilo tutalifuatilia hiyo kesho usiwe na wasiwasi kabisa…’nikasema‘Sawa kabisa mke wangu, mtoto yule ni wa kwetu, kwahiyo tuna watoto hawa....’akasema akionyesha vidole vitatu.‘Hapana mume wangu sisi tuna watoto wawili,....’nikajikuta nimesema hivyo‘Usinibishie mimi, ...., mimi ndio najua, mimi ndio mume wako,...tuna watoto hawa…w-nne, ...na ...’akasema‘Wanne tena…’nikasema, na kabla hajanijibu, ndugu yake akakohoa, sijui ni makusudi au ilitokea tu, na hapo hapo akageuka ndio akamuona mdogo wake, kwanza alimuangalia kama anamshangaa, baadae, akatabasamu na kwa haraka akamsogelea, kama vile anataka kumkumbatia, lakini mdogo wake akanyosha mkono wakashikana kusalimiana.‘Jembe,…hahaha! Jembe langu umekuja, sasa mambo safi, utanisaidia kazi moja..kuna kazi moja usiku huu huu…unazijua zile zetu, kwanza sina pesa, lazima tufanye dili la nguvu, pili, kuna yale mambo yetu,..mmh,…, hiyo ni siri yetu,..unasikia, sitaki mke wangu afahamu,...unasikia jembe....’akasema na hayo maneno kuwa hataki mimi nifahamu akawa kama anamnong’oneza, .Mdogo wake akawa anamwangalia kaka yake kwa mashaka.Nilimuonyeshea ishara akubali tu, na mdogo wake, akamsogelea kaka yake na wakawa kama wanakumbatiana, nilimuona mdogo wake akijizuia kutoa machozi. Nahisi kuna hisia za kulia zilitaka kumjia, anampenda kaka yake pamoja na wakati mwingine hawaelewani.Niligeuka na kuangalia pembeni, maana kwa hali kama ile hata mimi mwenyewe hiyo hali ilinijia, nikiwazia mbali, kuwa huenda mume wangu ndio hivyo kaharibikiwa hatapona tena, karibu hata mimi nilitaka kutoa machozi,..kiukweli mimi nilishajua kuwa mume wangu keshapona, na tunatakiwa kuganga yajayo.‘Sasa hili tatizo litaisha lini..?’ nikajikuta nimejiuliza hivi tena kwa sauti, na sijui kama walinisikia, kumbe kweli walinisikia kwani mume wangu akasema;‘Kesho…unasikia mke wangu, kesho, litaisha,..’akasema mume wangu hivyo, sijui alikuwa na maana gani, na muda huo alikuwa bado kamuangalia ndugu yake, wanaongeaNa ndugu yake akaingilia kati na kumuongelesha kitu kingine muda huo huo, kwahiyo wakawa wanaongea sasa wao wawili , na mimi nikaa kimia…kama vile mimi sipo, na kuna wakati anamuambia mdogo wake kuwa hayo ni ya siri hata mke wangu hatakiwi kujua, keshasahau kuwa na mimi nipo hapo karibu.‘Sasa hili ni tatizo…’nikajisema kimoyo moyo sasa.Kwa muda huo nikamkumbuka docta rafiki wa mume wangu, nilitamani nimpigie mambo kama hayo angenishauri vizuri tu, lakini kwa hapo nisingeliweza kufanya loloteAliendelea kuongea na mdogo wake mambo mengi tu, na kama kweli hayo anayoyaelezea kayafanya basi mume wangu yupo kwenye mambo ya hatari ambayo yatamweka pabaya.‘Mdogo wangu, tuna mtoto wa kiume, nilikuambia, ukanibishia ni kweli sio ndoto, sasa nimeamini…’akasema na mdogo wake akawa anaitikia tu‘Tatizo ni hawa wanawake hawaeleweki kabisa, mambo mengine ya siri wanaharibu, sasa kaharibu…na mke wangu akijua mmh..lakini usijali nitayamaliza tu…si unanifahamu, ..we acha tu..’akasema na mdogo wake akawa ananiangalia mimi, hapo akaharibu, kwani mume wangu akageuka kuangalia nyuma, ndio akaniona...Aliponiona akawa kama kashtuka, halafu akasema‘Oh kumbe upo, umekuja saa ngapi…oh, nilikuwa nongea na bwana mdogoo, siunajua tena, huyu ndiye mtu wangu kabisa..lakini mke wangu kama tulivyoongea, eeh, usiniangushe, Yule ni mtoto wetu kabisa, ukimuona utaniambia…wanafanana na watoto wetu kabisa,…’akasema.‘Sawa, sawa nimekuelewa, sasa unywe dawa ukalale…’nikasema‘Mimi nilale saa hizi, ...hapana bado naongea na bwana mdogo…’akasema‘Unatakiwa kunywa dawa zako kwanza huu ndio muda wake..’nikasema nikijua akizinywa hizo dawa, atazidiwa, ataishia kulala tu‘Dawa kwani mimi naumwa bwana, usiharibu mada,…’akasema na kumgeukia mdogo wake‘Unaona ndio mambo siyataki haya, hawa akina mama…mmh, unajua bwana mdogo nikuambie kitu, hapa nikutoka tu, sisi tutoke hapa twende sehemu, tukafanye mambo yetu, halafu kitaeleweka, au sio..mimi hapa sina pesa, tutapata wapi pesa..dili kwanza..au sio?’ akasema sasa akiwa kanisahau kidogo, akasimama na kumshika mdogo wake mkono ili waondoke. ‘Sasa mke wangu nataka kutoka na mdogo wangu, tutaonana baadaye...’akasema na mdogo wake akawa anasita kuondoka, na wakati huo kashikwa mkono ili watoke naye‘Kaka hebu kunywa dawa kwanza ni muhimu, si unajua afya ni bora kuliko mambo mengine, mimi nipo, tutatoka tu..’akasema mdogo wake‘Usimsikilize shemeji yako,..twende bwana, amri, kaka akiongea jambo ni amri,..twende, halafu.., tutarudi, kwani dawa zitaharibika…’sasa akawa anamvuta mdogo wake waondoke.‘Mke wangu usijali, mimi nitarudi, sifanyi fujo, mwenyewe utaona, hapa,..nikiwa na hili jembe, sina wasiwasi, huyu ndiye mimi, ukimuona huyu umeniona mimi, hata nikifa leo, usije ukamtupa mdogo wangu huyu, unasikia…’akawa anaongea sasa kama kalewa.‘Mume wangu…mbona haupo sawa…’nikasema‘Nani kasema sipo sawa, halafu wewe mjanja kweli kweli,…hahaha, umejuaje,…nilipoingia ndani, kuondoa mawazo, nilikunywa kidogo tu…kidogo…, hahaha, hamuwezi kininyima starehe yangu, hahaha’ akacheka sana tu‘Sasa sikiliza, huyu ni jembe langu,,....usije ukamnyanyasa mdogo wangu, hata kama nimekufa, mimi nitafufuka na kuja kumtetea, nampenda sana mdogo wangu huyu, achana na Yule mwingine, Yule … Yule anajifanya mtakatifu saana,.....hili ndilo jembe langu...’akasema na kumshika mdogo wake mkono, wakatoka naye nje…Nilibakia mle ndani nikiwa sijui nifanye nini, …lakini kwa vile sasa yupo na mdogo wake, nilihisi amani kidogo,…‘Ngoja sasa nione kitakachofuata,..hili ni langu tena..’nikasema Na hata kabla sijasimama, ili nielekee chumbani, mara simu yangu ikaita, moyo phaaa! Mlio wa simu sasa unanipa kero, naogopa na kuogopa…Nikaangalia mpigaji,.. ilikuwa ni namba ya nje, kidogo nikatulia, nikijua huyo atakuwa ni yule rafiki yangu anayesoma nje….**********‘Habari za huko?’ nikauliza‘Nzuri tu, bosi, tumemaliza mitihani mmoja kesho tunafanya mwingine, na huenda nikaja huko siku za karibuni...’akasema‘Itakuwa vizuri sana, maana kuna mambo nataka tuyamalize...’nikasema‘Yale yale..au?’ akauliza‘Ndio,..yale yale, na hapa tunapozungumza mume wangu anaonekana hayupo sawa..kachanganyikiwa…’nikasema‘Mhh, hiyo hali imeshajitokeza tena ehe..?’ akawa kama anauliza‘Ina maana unafahamu?’ nikamuuliza‘Ndio, nilipofika kwa docta wake, moja ya jambo alilonielezea ni hilo, nilijua na wewe unafahamu..’akasema‘Hapana…’nikasema‘Basi ni hivyo uwe makini naye sana…na bora umueleze docta yake achukue hatua anaweza kufanya jambo baya...’akasema‘Kwanini docta alikuambia wewe na hayo ni mambo ya siri ya mgonjwa au mke wake ?’ nikauliza‘Umesahau kuwa mimi ni ndugu yako wa karibu na hakuniambia kwa nia mbaya, ...’akasema‘Ni ndugu yangu wa karibu,ehe, ...kweli wewe ni ndugu yangu wa karibu, kama ungelikuwa ni ndugu yangu wa karibu ungelinifanyia hayo uliyonifanyia…’nikasema kwa hasira‘Yapi tena bosi, mbona kila siku unakuja na hoja mpya, ...?’ akauliza.‘Unayafahamu sana.....’nikasema.‘Bosi nakuomba bosi, usichukulie hayo mambo kwa hasira, nikirudi tutaongea, nina imani hakitaharibika kitu..’akasema‘Kama ni kweli, ninavyosikia, kama ni kweli, wewe umezaa na mume wangu...sizani kama tutakaa kwenye meza moja tuongee, hilo sahau, na nilishakuambia, kama kuna mtu anataka ubaya na mimi ...basi atembee na mume wangu, sitajali kama ni nani, hata kama ni ndugu yangu wa tumbo moja, nitafanya yale yale niliyowahi kukuambia...’nikasema.‘Lakini...’akaanza kujitetea.‘Sasa hivi mume wangu anaumwa, na hali aliyo nayo siwezi kufanya lolote, lakini akipona tu,...kama ni kweli, basi, ...mkataba utafanya kazi yake, na mengine yatafuta baadaye....’nikasema.‘Mkataba upi bosi ...maana kama nilivyoona, na kuambiwa, kwenye mkataba hakuna tatizo, ...mume wako ana uhuru wa kufanya lolote, huoni kwamba ukitumia huo mkataba utakuwa umejimaliza wewe mwenyewe..’akasema‘Kumbe hata hayo ya mkataba unayafahamu au sio…naanza kupata picha, sasa kama ndivyo mlivyopanga hivyo, tutapambana mahakamani…si ndio ujanja wenu huo, kuwa mumegushi mkataba ili mtoto wake aje kurithi mali yangu, au sio?’ nikauliza‘Mimi sijapanga lolote, mimi niliitwa kuja huko kwa dharura, na nilipofika hapo, nikajikuta naingizwa kwenye mambo ambayo hata siyafahamu, na kuhusu mtoto, mtoto ni wangu, hana baba,..hayo ni yao, na ndoto zao, wala usiwe na wasiwasi na mtoto wangu…’akasema‘Kwahiyo wewe kilichokurudisha huku, ilikuwa nini hasa…?’ nikauliza‘Mimi sikurudi kwasababu hiyo, nilirudi kwasababu niliambiwa kibali change kina matatizo, kwahiyo nahitajika kurudi kukirekebisha, kwanza nilijua ni wewe umefanya hivyo, ili kuondoa udhamini wako, nikaona isiwe shida, na bahati nziri akapatikana mdhamini mwingine,…sasa sijui kama ni wewe ulifanya hivyo, au kuna jingine ndani yake, mimi sikutaka kulichunguza muhimu nimalize haya masomo mengine nitakuja kuyafahamu baadae…’akasema‘Usinidanganye kila kitu nimeshakifahamu, na kwanini hukuniuliza, kuhakikisha hilo, na kwanini nifanye hivyo, maana mpaka unakuja mimi sijui lolote kuhusu ujio wako, nimesikia siku ulipofika, ndugu yangu, dunia hii ni mapito, acheni hayo jamani…’nikasema‘Kiukweli, utaamini utakavyo, sikulaumu kwa hilo,… lakini ukweli ninaokuambia mimi ni huo, kuwa hiyo mipango yao sikuwa na ufahamu nayo kabisa,....walipanga wao wenyewe, ..kama ningelifahamu hivyo nisingelikuja huko kabisa, ningetumia njia nyingine ya kulimaliza, bila hata ya wao kuhusika,…mimi kilichonirejesha hapo ni taratibu za kibali changu…’akasema‘Tutakutana tu…dhuluma hata siku moja haidumu,..kiukweli kama ni kweli, umefanya kosa kubwa sana ambalo …sizani kama naweza kukusamehe,..mpaka sasa sijaamini hilo, siwezi kuamini kuwa wewe unaweza kunifanyia hivyo, …’nikasema‘Bosi, niamini haya ninayokuambia, sikuwa nafahamu lolote…mimi nilipofika tu, yakatokea hayo yaliyotokea, kama nilivyokuambia awali, na ndio nikauona huo mkataba, sijui lolote jingine, na hata kama nimeweka sahihi yangu hapo, sihusiki, na hawatafanikiwa mipango yao ....’akasema‘Sawa, endelea kunidanganya, najua nalipa fadhila zangu kwenu, lakini ahadi yangu na dhamira yangu ipo pale pale, mwenyewe utaona ukirudi , labda upotelee huko huko, hilo nakuahidi, nyie si ni wajanja sana, ngoja urudi ....’nikasema kwa sauti ya dhamira‘Jamani dada, ...bosi, usinifikirie hivyo kabisa, sipo kabisa kwenye hayo mambo yao, ndio maana wakatumia mbinu hizo walizotumia, ...hebu niambie mimi ningelifanya nini kwa hali kama hiyo,...Bosi, nakuhakikishia mimi nikirudi tutayamaliza hayo, wala sipotei, nitarudi...’akasema‘Najua utarudi labda na ndoto ya kuwa mke mwenza, au mshirika mwenza, au nani utakavyojua mwenyewe na hawara wako ?’ nikamuuliza‘Mimi sielewi una maana gani kusema hivyo bosi..hayo yametoka wapi tena, mimi ni mdogo wako jamani…’akasema‘Unaelewa sana nina maana gani, sasa hivi sipo kule kwenye kuamini kinyume chake, wengi waliniona mjinga kuwa ukweli upo, lakini akili imefungwa, sasa akilio imefunguka, na sitaamini uwongo wenu tena, na sitaki utetezi wako wowote....’nikasema.‘Basi wewe subiri nirudi, naona hapa kwenye simu hatutaelewana, ila nakuhakikishia kuwa sijui lolote kwenye mambo yao, na mimi siwezi kufanya jambo baya dhidi yako, na ukiona nimefanya jambo, ujue ni kutokana na ushauri wako, sijawahi kukusaliti mimi, niamini hivyo....’akasema‘Niliwahi kukushauri uje ufanye ufusuka na mume wangu?’ nikamuuliza‘Bosi, ufuska gani jamani, mmh mimi naona hapa hatutalewana tena,...kwahivi sasa, naomba uniache ili nimalize masomo yangu kwanza, hayo na mengine mengi tutayamaliza tu.., hakuna tatizo kabisa....mimi sijawahi kufanya jambo kinyume na matakwa yako, kweli si kweli ? sema ukweli wako, na kwahiyo hata hili, litakwisha tu kwa amani, hilo nakuthibitishia, ...’akasema‘Sina amani na msaliti mimi,..rafiki anyekuwa nyoka, sina amani nay eye tena,….wewe hujui nitavyoteseka huku, hujui kabisa, wewe na mwenzako ni nyoka wanafiki wakubwa....’nikasema‘ Oh imekuwa hayo..lakini sawa, samahani kwa hilo, nina imani yatakwisha tu bosi, pole sana,…’akasema na nikahisi analia‘Unalia nini sasa…’nikasema‘Inaniuma sana…hujui hata mimi ninavyoumia, sikutarajia haya kabisa, ila mimi nakuthibitishia kuwa hilo litakwisha kwa amani tu, kama utanielewa, maana unavyofikiria wewe sivyo kabisa, samahani sana kwa kukufikisha hapo, na matatizo yote yanayokukumba,… nakuomba niwahi darasani tafadhali, kwaheri,… nisalimie shemeji na watoto, ..’akasema na kukata simu.NB: Kisa kinarudi kuleee..hii ni kuashiria kuwa mambo sasa yanaanza kuwekwa hadharani.WAZO LA LEO: Tuwe makini na kauli zetu , ulimi unaweza ukasababisha mema na mabaya,ukiutumia vyema ulimi wako unaweza ukaleta faida kubwa kwenye jamii, lakini ulimi huo huo, ukiutumia vibaya, unaweza ukaleta majanga makubwa kwenye jamii za watu, tena wenye elimu zao. Ulimi unaweza kugeuza marafiki wakawa maadui. Tumuombe mola wetu atujalie tuweze kudhibiti ndimi zetu, ili jamii ziishi kwa amani na upendo.Ilikuwa ni muda wa usiku, nahisi ilikuwa ni saa sita na nusu hivi, kwani niliangalia saa ya ukutani, tatizo, siwezi hata kugeuza kichwa, lakini niliona ni saa sita, mshale unaonyesha hivyo.Cha ajabu mwili hauna nguvu, na pumzi ilikuwa ndogo sana, nipo wapi hapa, ni jela au ni chumba gani hiki hakina hewa…nikajiuliza, nikijaribu kugeuza kichwa siwezi, lakini naona, kwa hisiaMara ghafla mishughuliko, kama kuna kugombea jambo..sijatahamaki mara mkono ukanishika shingoni, unanikaba, na mwingine , na mwingine..ikawa inakuja mikono mingi kunikaba, lakini simuoni mtu ila nahisi ni mikono ya watu inanikaba kila nilipojaribu kugeuza kichwa au kujitetea, sikuweza, mwili ulikuwa haukubali ilikuwa kama mtu aliyenyweshwa madawa ya kulevya au nusu kaputi.Akili ilikuwa inaona, au nahisi hivyo, kuwa kuna mikono mingi inanikaba, tena ya kiume..na pia ya kike, ni nani hao, wanataka kuniua,..wote walikuwa wamenishikilia na kila mmoja akiapiza kivyake, kuwa ananiua kwa vile..hiki na kile, na sauti hazisikiki vyema, ila sasa mmoja ndio akasema‘Nataka ufe kwa vile unakuwa kikwazo kwetu…ila tunakupenda, na kukupenda huko, ili usihangaike ni bora ufe tu…’ilikuwa suti ya kike, iliyochanganyikana na sauti ya kiume kama wanaongea kwa pamoja.Mikono hiyo mingi iliendelea kunikaba, na mara kwa mbali, nikamuona mtu…anakuja taratibu, akatabasamu, na kusema;‘Nilikuambia mimi ndiye rafiki yako wa ukweli, sasa nikuokoe au nikucha wakuue..?’ akauliza hivyo, na mimi nikawa najitahidi kujiokoa, sitaki huyo mdada aniokoe namuona kama mnafiki kwangu ,ananihadaa tu, ananivunga, nikawa nataka nijiokoe kivyangu,..hapo sasa pumzi ndio kama inishia, sasa nataka kukata roho.Yule mtu, ni mdada, lakini mrefu..akaniuliza tena..tena, 'Hutaki, nikuokoe unajua wewe ni rafiki yangu, nakupenda sana,na kila kitu nafanya kwa ushauri wako,wewe ndiye ulinijenga, akili yangu ikawa inakuwaza wewe, usemacho kwangu ni kama askari anayepewa amri,..ua, naua, kamata , nakamata , sasa iweje…sasa niambie nikuokoe au niache ufe..'‘Mna-na-fiki wewe…’nikajaribu kusema hivyo, kinafsi niliweza, lakin mdomoni siwezi hata kufunua mdomo mkavu,..kwa sababu ya kukabwa, ulimi umetoke nje...na Yule mdada, akainua mikono, kama vile na yeye anataka kunikab au kunikoa, mimi nakataa, sitaki afanye anachotaka kukifanya,…, Ni wakati huo nimeshakata tamaa, namuomba mungu anisamehe makosa yangu ili nife kwa amani,…sasa sina uwezo tena hata wa kuongea, kauli imeshakata,..mara kikaja kitu kama mwanga, kikanipiga usoni, nikashituka,...nipo wapi, .. ooh, kumbe ilikuwa ni ndoto.‘Ndoto mbaya hii…ooh..’nikasema sasa nikijaribu kuweka fikira zangu vizuri, mwanga ulikuwa ukitokea dirishani,ni mwanga wa taa za nje...!Jasho lilikuwa linanitoka, haraka nikainua mikono yangu na kushika shingo, sikuona dalili yoyote ya maumivu, ya kukabwa,..na nikageuka huku na huku kunyosha shingo, sikuhisi kuumia, na wakati huo macho bado mazito kufunguka, naogopa nitayaona haya majitu.Baadae nikafungua macho…nipo chumbani kwangu , kitandani,…hapo nikajitahidi na kujiinua kidogo, nikajikuta nipo sawa, nikajinyosha, halafu nikageukia ubavu wa pili, upande ule aliolala mume wangu,Hakuna mtu!!Mume wangu hayupo kitandani, na nina uhakika alikuja usiku ule tukalala naye, japokuwa alikuwa kalewa, sikuweza kumkatalia, kwa ile hali, lakini awali sikuweza kupata usingizi hadi niliposikia anakoroma kuashiria kuwa kalala, na ndipo usingizi ukanishika,, sasa mume wangu hayupo kitandani‘Labda katoka kidogo,..’nikajipa matumainiUsiku ule walipofika na mdogo wake, niliongea naye kumuuliza hali ya mgonjwa, maana ni mgonjwa sasa, ..‘Shemeji yupo safi tu, ila anaongea sana…’akaniambia‘Sawa sasa ni usiku sana, ila kesho kama nilivyokuambia,huyu ni wa hospitalini…’nikasema‘Amekataa, anasema yeye haumwi, sijui tutafanyaje…’akasema‘Basi nitamuita rafiki yake docta, aone atatusaidiaje, ila kwasasa ukalale naye..’nikasema‘Hapana, shemeji,..kasema anataka kulala na wewe kwa vile wewe ni mke wake, nilimuambia hilo wakati tunakuja, kakataa katakata…kasema ukimkitaa, atakufanya kitu ambacho hutamsahau…’akasema‘Atanifanya nini..?’ nikauliza‘Kasema hivyo tu…’akasema‘Oh,…sasa akileta vurugu usiki itakuwaje..?’ nikauliza‘Wewe shemeji usijali, hakikisha simu yako ipo karibu, akifanya fujo, au hali ikiwa mbaya, wewe nibeepu tu, weka namba yangu tayari, na mlango usifunge kwa kubana,…’akasema Kwahiyo tukaishia hapo, na kweli nilifika na kumkuta mume wangu ameshatangulia kitandani, na sasa kalala… ‘Sasa kaenda wapi huyu mtu..?’ nikajiuliza hali ya ndani kulikuwa kimia kabisa, husikii kitu …nikakaa kimiya kidogo, nikisubiria huenda kweli katoka kujisaidia, lakini hakutokea kabisa, moyoni nikahisi ni yale yale, nilikuwa nikiogopa, na nikikumbuka hiyo ndoto ndio nikawa na mashaka kabisaUzuri watoto walikuwa hawapo, wapo shule za bweni, kwahiyo upande huo nilikuwa na amani nako, sasa ni mimi na mume…na shemeji yupo chumba kingine.‘Uwe makin na huyo mtu, hata ukilala usilale kupitiliza…’nikakumbuka ushauri wa docta rafiki wa mume wangu.Nilipokumbuka hilo kwa haraka, akili ikanijia, nikaona nifanye jambo , jambo ambalo niliwahi kuliona kwenye sinema, lilinijia hilo wazo tu. Taa ya ndani ilikuwa inawaka, lakini sio ile ya mwanga mkali, huwa sipendi kulala na giza,Kwa haraka nikaamua nifanye hivyo, sijui kwanini niliamua kufany ahivyo, ila nilifanya hivyo tu, sijui…Kwa haraka nikachukua mto wangu wa kulalia,na mashuka ya akiba nikayaweka pale nilipokuwa nimelala, nikayafunika kama mimi niliyelala, na mimi mwenyewe nikatafuta sehemu ya kujibanza, nikajaribisha na kuona ninaweza kujibanza hapo bila ya yoyote kuniona.‘Najihami tu…’nikasema hivyo.Nilikaa pale kwa muda bila kuona mtu akitokea, nikawa najiuliza je ni kweli ninavyowaza au ni wasiwasi tu.‘Ngoja kwanza nikahikishe labda jamaa kaenda kulala chumba cha maongezi,..’nikajisema moyoni, kwahiyo taratibu nikafungua mlango na kuchungulia huko…hakuna mtu…nikasikia kitu kama kimegonga, kwa haraka nikarudi kwenye maficho yangu na kutulia, kukapita muda, hakuna mtu aliyetokeaNikakumbuka jambo,…kila kitu kinahitajia ushahidi au sio, ngoja niweke ushahidi kama kuna lolote laweza kutokea.Kuna video, niliyokuwa nimeweka chumbani, ni katika kutafuta ushahidi tu, lakini baade niliizima, ni videi inayochukua matukio…nikasogea kwenye lattop yangu nikaisha na kuiweka hai, ili ichukue matukio yote humo ndani.Mara nilisikia kitu kimegonga upande ule wa makitaba, ...oh, kumbe mume wangu yupo huko, huenda aliamua kwenda kupoteza muda, nikataka kwenda huko, lakini nikaona ngoja nitulie kama dakika tano hivi, huenda kuna kitu anakitafuta, nikasikiliza lakini sikusikia tena…nikatoka mafichoni, na sasa nataka kwenda huko maktabaMara ....nikasikia kama mchakato, wa mtu kutembea, na niliposikia hivyo, nikakimbilia ile sehemu yangu ya maficho. Huwezi jua, huenda ana lake jambo ngoja nione anataka kufanya nini.Nikawa najiuliza kama mume wangu alikwenda tu kupoteza muda, ...akaja akaikuta ile hali, anaweza kuniona simwamini...hapana nitamtania tu kuwa nilikuwa namfanyia mzaha. Nikatulia, huku nikiwazia mataayrisho ya kesho kuwa kesho ni lazima nimtafute fundi, abadili vitasa vyote vya makabati, na hata ikibidi nyumba nzima, maana hakuaminiki tena...‘Bastola...’ oh nilipokumbuka hivyo mwili mnzima ukazizima, woga!!‘Mungu wangu , kwanini sikuiondoa pale…’nikajilaumu Hapo moyo wangu ukawa unanienda mbio, sijui kwanini nilisahau, kwani nilipanga, kuja kuiondoa ile bastola kwenye kabati na kuificha sehemu nyingine, lakini kutokana na mishughuliko, na hayo mambo ya kufuatilia, nikawa nimesahau kabisa,Nakumbuka mume wangu walipoondoka na mdogo wake hawakuchukua muda, walirudi, wakiwa wanaongea kwa furaha, na nilipopata muda wa kuongea na shemeji yangu, yeye alisema kaka yake muda wote walikuwa akiongea kwa furaha, hakukuonekana tatizo lolote...**********‘Inabidi kujihami tu...’nikasema kujipa moyo nikiwa bado mafichoni Kila hatua nilihis nipo hatarini, na kila nikitaka kumbipu shemeji, nahis kama nitaonekana muoga, simuamini mume wangu, basi nikaona niache tu, nione kwanza mwisho wake ni niniMuda ukawa umepita sikuona dalili za mume wangu kutokea.‘Au kaenda kulala na shemeji au kule kwenye chumba chake kingine…anapolala akiwa kalewa…’nikasema hivyo kimoyo moyoNilipoona muda unakwenda nikataka kutoka na kumfuata mume wangu huko huko kama ni chumbani kwake au kwenye maktaba yetu, na mara mlango wa maktaba ukafungulia!Mume wangu akajitokeza…akiwa na pajama la kulalia, mkononi kashika kitu,Kwanza sikuweza kukiona hicho kitu alichokishikilia, kwa jinsi alivyokishikilia usingeliweza kuona na pale nilipo ikawa siwezi kujisogeza, na kwa vile nilikuwa nimesimama kwa muda, mwigi kwenye shemu ndogo, miguu ilishaanza kuuma, lakini hata hivyo niliogopa kijitikisa sikutaka mume wangu ajue kuwa nipo pale.Mume wangu akawa anakuja ule muelekeo wa kitanda, alikuwa akitembea mwendo ule wa kunyata,yaani utafikiri ule mwendo wa kwenye picha wa kunyata, taratibu, na kila hatua ilikuwa kama mtembeaji anahakikisha kuwa mguu umefika pale alipopataka,..akasogea hadi karibu na kitanda, na hapo nikaona kashikilia nini,...moyo ulinilipuka, nikawa nahisi kuishiwa nguvu..Yale yale niliyokuwa nikiwaza, na hapo nikazidi kujilaumu, kwanini sikufanya kama nilivyoambiwa, haya mambo ya kuzarau, sasa naona matokeao yake ...huwa kila anachoniambia rafiki wa mume wangu nimekuwa na tabia ya kukizarau, na nimejikuta nikipatwa na matatizo na baadaye ndio najiona nimefanya makosa, ni aheri ningelimsikiliza ushauri wake. Tatizo huyu rafiki wa mume wangu, ni mtu anayejitahidi sana kunisaidia, japokuwa ni mume wa mtu, lakini bado anaonyesha ile hali ya kunipenda, hata wakati mwingine najisikia vibaya kutokana na matendo yake. Na kuna wakati anajisahau kabisa kuwa yeye ni mume wa mtu na anataka kufanya yale tuliyokuwa tukifanya tukiwa wapenzi, kwakweli kwa hilo sikutaka upuuzi huo. Sasa kupuuzia yale anayonishauri matokea yake ndio haya...Wakati huo mume wangu alikuwa ameshafika eneo la kitandani na hapo akainua kile alichokishikilia na sasa kikawa kinaonekana dhahiri,Bastola…!!Sasa akawa kaishikilia bara bara, japokuwa mikono yake inakuwa kama inatetemeka,..sasa anailenga ile bastola pale nilipokuwa nimelala, niliona mikono yake ikitetemeka, sijui kwaniniKwa haraka nikamchunguza kwenye macho yake, awali alipokuwa kasimama nisingeliweza kuyaona vyema, kwani mwanga wa taa ya ndani ulikuwa ni hafifu, ila aliposogea karibu na kitanda pale aliposomama sasa ndio nikamuona na ni kutokana na mwanga wa taa nje.Taa ya nje ilinipatia nafasi ya kumchunguza vyema machoni alikuwa kafungua macho, ila ukiangalia kwa makini macho yake yalikuwa meupe,...sio ya kawaida, nikakumbuka zile hadithi za watu wanaofanya kazi wakiwa usingizini,..Kweli mume wangu hapo hayupo sawa, na ilivyo, hutakiwi kumshitua, ..unaweza ukamsababishia mshituko wa moyo, na hata kusababisha kifo, kwahiyo nikatulia kimiya, nione ni jambo gani anataka kulifanya,..************** Mume wangu hajui kutumia vyema bastola, niliwahi kumfundisha lakini hakupenda kabisa kuitumia, nahisi ndio maana mikono yake ilikuwa ikitetemeka,..ila nilimfundisha jinsi gani ya kuweka risasi na kutoa, kwahiyo yawezekana atakuwa keshaweka risasi kabisa kwenye hiyo‘Hii imepangwa itokee, ili iwe fundisho kwangu...’nikasema kimoyo moyo.‘Jembe njoo huku...’sauti ikatoka mdomono kwa mume wangu, ilikuwa kama ya kuwewesa..na anaongea kama mtu aliyelewa hivi.Huyo jembe ni nani..?’ nikajiuliza, nikakumbuka ..jembe ni mdogo wake, lakini hapo hayupo, mbona anamuita kama vile yupo naye karibu.‘Jembe, ..nakutegemea wewe....lakini hili ngoja nilifanye mimi mwenyewe, sitaki wewe uje kuingia matatani, na kama unaogopa ondoka....’ikatoka ile sauti, ni kama ya wale wanywa madawa ya kulevya. Niliweza kuisikia kwa shida, hapa nikuelezea kwa vile nilivyoelewa, lakini alivyokuwa akiongea ni maneno ya kutafuta.‘Na-na-taka ku-ku-limaliza hi-li ka-ka-bisa, tuwe huru...’akasema huku akisogeza ile bastola palen nilipoweka mto, na kama angegusa kwa mkono angeligundua kuwa hakuna mtu, lakini nikamuona akisogea nyuma, akapiga magoti.‘Oh, Jembe nisaidie jamani.. , nashindwa kufanya hili....nashindwa kumaliza hii kazi, namuonea huruma, lakini jembe , nisipofanya hivi tutakosa kial kitu,...kazi yangu yote na juhudi zangu zote zitapotea bure, mtaishije, nitaishije,..nirudi kuwa masikini hapana, sikubali, ni bora nimfuate Makabrasha, ....’akatulia.‘Unasikia eti, wana-se-sema Makabrasha ka-fa…yu-le, afe…hapana, kama ni hivyo, basi hata mimi nataka kumfuata huko huko…najua hata mimi ndio njia yangu…nitakufa, lakini abla ya kifo changu, nataka niachie familia yangu jambo la kunikumbuka.‘Sitaki ubaguzi..ooh, mtoto wan je..nani kasema hayo..sasa ili huyo mtoto wa nje naye atahaminiwe, basi nataka huyu kizuizi aondoke,… Jembeeh, unanisikia,..sasa nisaidie tumalize hii kazi, mbona husogei, sogea huku...mkono hauna nguvu kuvuta hiki kiwashio…traigaaaaa..’akasema.‘Oh, wewe sasa unaogopa eeh,,..ngoja mimi nimalize hii kazi mwenyewe, maana wiki imeshapita, kinachofuata hapo ni nini....ni mkataba wa zamani, ukipatikana huo, mimi sina changu, hivi huo mkataba wa zamni ni upi,...ananishangaza kweli, kweli mke wangu kachanganyikiwa, mimi siujui huo..sija—labda makarasha atanisaidia, mimi sijui....’akatulia‘Sikiliza jembe, tusipolimaliza hili, tutakosa kila kitu, tukilimazlia hili, tutakuwa huru, na mimi nitamfuata Makabrasha, nimekutana naye, kasema huko alipo kuna amani…yupo wapi huyu mtu…’akatulia‘Ananiita, unasikia, suti yake hiyo, ananiita…hahahah..ngoja nimalize hii kazi, anasma nimalize hii kazi halafu nimfuate huko alipo…’akatulia kama anasiliza‘Mke nakupenda lakini …wewe ni kikwazo..bora nije kuishi na huyo mwingine, hana shida,..kwanza …anadai yeye ndiye kanizalia dume, hivi ni kweli eeh, yawezekana ni yeye,..hahaha, kanizalia dume, kama ni kweli, basi kweli ananipenda, tofauti na wewe mke wangu ambaye anaogoma kunizalia dume..Tatizo wewe mke wangu,..unathamini tu mali, wazazi wako, familia yako..na kunifanya mimi bweeege.’akasemaPale nilipokuwa nimejificha, nilihisi hasira, nikahisi nijitokeze nikafanye lolote , lakini mwili ulikuwa kama umekufa ganzi, nikabakia kuumia ndani kwa ndani, kumbe....kumbe, ni kweli mume wangu ana mwanamke mwingine nje na huyo mwanamke anampenda kuliko mimi, sasa ni nani,…ni..ni…hapana mbona hamtaji!‘Ni mwanamke gani huyo…?’ nikajiuliza‘Tatizo mwanamke wewe unayenipenda sikuoni…upo wapi…ni nani wewe..mbona inakuwa kama jinamizi, nashindwa ku-kumbuka, ni nani wewe..nakuwa kama mtu anayempenda shetani, ..jini mahaba, asiyeonekana, umekwenda wapi wewe…je ni kweli ni wewe ulinizalia jembe…’akatulia‘Ni kweli maana ni kwanini mke wangu alitaka kumtupa mtoto ..kwa vile hana uchungu naye..yaah, nimegundua, mke angu hanipendi, kama hampendi mtoto wangu hata mimi hanipendi, sasa nakuua…ufe,..ufeee...na hii silaha yako…na mimi,…hahaha’‘Sasa jembe mimi namaliza kazi, nikimaliza kazi, kinachofuata tukamtafute mtoto wetu, ...tutakuwa na jembe jingine, dume la kazi....ukiwa na jembe ndani ya familia raha, watoto wote nawapenda, lakini wa kike watapendwa na wengine zaidi, watachukuliwa, nitabakia na nani sasa....mungu kanisaidia nimepata mtoto wa kiume, eti nimuachie hivi hivi..hapana, ni lazima ..ni lazima, tukamchukue, sasa jembe mimi namaliza kazi ..‘Wewe sihutaki kunisaidia eeh ...mimi naifanya hii kazi peke yangu, wewe ....unisaidie jambo moja, nikikamatwa, unilelee watoto, nikifa, halikadhalika, nakuachia kila kitu kikiwa sawa,...hata nikifungwa, wewe chukua jahazi, najua kwa sasa kila kitu kipo makini, ahsante Makabrasha, nakuja nisubirie, nakujaa.....’akasemaAkasogea karibu kabisa sasa na pale nilipoweka kanyaboya akaelekeza ile bastola kwenye mto, akaisogeza karibu sana, na kusema;‘Samahani sana mke wangu ...nalifanya hili kwa vile sina namna nyingine, na nikimaliza hili na mimi nikiona vipi nitajimaliza mwenyewe, kwa manufaa ya familia…’akawa sasa anakaza kidole cha kuvuta kiwambo cha bastola‘Najua..nitapatilizwa na kusakamwa sana..lakini kama wanavyodai wamemfanya hivyo Makabrasha, kwanini hililisifanyike , na kuna shida gani maana kila kitu sasa kipo makini, kila kitu kipo makini au sio best Makabrasha, nakushukuru sana...’akasema na kuisogeza bastola karibu kabisa na mto....‘Kila kitu kipo makini....’akawa anayarudi hayo maneno mara kwa mara sasa, nikawa najiuliza hayo maneno yana maana gani, kwanini ameyependa kuyarudia, amejihakikishia vipi kuwa kila kitu kipo makini, nikawa najiuliza huku nikimwangalia mume wangu, nikiwa pale nimejibanza,‘Makabrasha kafa…nani kasema kafa, wehuu nyie…, basi kama kafa nimemuua mimi, mwenyewe, hivi hivi….hahahha. Kama nimemuua rafiki yangu aliyenithamini, kwanini nishindwe kukua, wewe…hahahaha, kwaheri…Mara mlio ukasikika, ...mlio ulitetemesha ndani,....na mlio ule ulimshitua hata huyo aliyeusababisha, na yeye akadondoka chini, na mimi pale nilipokuwa ilikuwa kama mtu kaniziba masikio ghafla,.Hata hivyo nikajitahidi, maana ni lazima nifanya jambo, kwani huenda mlio huu umesikika hadi huko nje, itakuwa ni kashifa,...nikatoka pale nilipokuwa nimejificha, na kwa haraka nikaenda pale alipodondokea mume wangu, alikuwa amedondoka sakafuni, sasa kalala, ..ametulia....anahema kwa mbali, na sauti kama ya kukoroma, ya kuashiria kuwa mtu yupo kwenye usingizi,...Nikaiangalai ile bastola ipo wapi ilikuwa imemtoka mkononi na kudondokea kitandani, na hapo nilitaka kuichukua lakini nikatulia, kwani nilisikia mlangoni ukigongwa.‘Shemeji kuna nini huko....’alikuwa mdogo wa mume wangu, na mara simu ikaanza kuita….NB: Kwa leo naishia hapa, naogopa na kuogopa,WAZO LA LEO: Tuwe ni wenye kuhurumiana, na kusaidia, hasa pale tunaposikia kuwa mwenzako yupo kwenye mitihani ya maisha huo ndio upendo wa kweli. Mitihani ya maisha ipo mingi, lakini mtihani wa maradhi ni mgumu sana, kwa mgonjwa mwenyewe na muugazaji, Ni wangapi wanakuwa wepesi kusaidia mtu akiumwa, ni vigumu sana kuwaona,..lakini mtu huyo huyo akisikia mwingine kafa, hata kama ni nauli atakopa,..najiuliza tu, je twawapenda watu wakiwa maiti zaidi ya wakiwa wagonjwa! Najiuliza sana sana hili. Tupo pamoja.. Ilipofika asubuhi, nikiwa nimechoka, macho yana usingizi, maana ilikuwa hakuna kulala…mjamaa yeye alikuwa anakoroma tu, usingizi kwa kwenda mbele. Hata asubuhi ilikuw kazi sana kumuamusha.‘Leo sijisikii vizuri mwili umechoka sana…’akasema‘Ndio maana tunataka twende hospitalini…’nikasema‘Hapana wewe nipe zile dawa zangu, leo hata kazini nitachelewa kwenda ..’akasema‘Sikiliza…’nikasema na kabla sijaendelea kuongea yeye akasema;‘Kuna ndoto mbaya niliota usiku.., lakini sikumbuki ni ndoto gani,...sikumbuki kabisa, lakini ilikuwa ya kutisha inavyoonekana, sitaki…hata kuikumbuka maana sio nzuri, muhimu nimegundua ni ndoto tu....’akasema huku akijaribu kukumbuka‘Uliotaje..?’ nikamuuliza‘Yaani najaribu kukumbuka lakini haiji akilini….na bora nisiikumbuke tu..’akasema‘Kwanini…?’ nikauliza‘Ni mbaya…’akasema akiniangalia mimi kwa macho yaliyojaa wasiwasi, ni kama haamini, au…‘Nikuulize hukumbuki kabisa kilichotokea jana..?’ nikamuuliza‘Jana..hapana..sikumbuki zaidi ya ndoto mbaya, hata hiyo ndoto haiji akilini, …’akasema‘Jana wewe hukuwahi kuingia maktaba usiku ukachukua kitu?’ nikamuuliza‘Kitu…! Kitu gani…hapana, mimi sijaingia huko kabisa, hilo usinidanganye, nakumbuka nilipotoka matembezi na mdogo wangu, ila kuna sehemu, nakumbuka kuwa nilitoka na mdogo wangu, mdogo wangu yupo..?’ akauliza‘Ndio..hilo unakumbuka sio..?’ nikauliza‘Sasa hapo sijui..ni ndoto ama ni kweli, kama mdogo wangu yupo basi, inawezekana ikawa ni kweli, lakini mengine sitaki kukumbuka…’akasema‘Na ulipolala hukuwahi kuamuka hata kwenda kujisaidia hata mara moja?’ nikamuuliza‘Nilala kama gogo, nahisi nilikuwa nimelewa,ni kama nililewa, hivi nilikunywa, kwanini hukunikataza....’akasema.‘Basi kuna tatizo, kama hukumbuki uliyoyafanya jana basi ujue unahitajika kwenda kumuona docta hakuja jinsi hapo...’nikasema‘Kwani kuna nini kimetokea mke wangu..?’ akaniuliza akionyesha mashaka sasa‘Nakumbuka kama ulitoka nje, ukaenda maktaba...ukachukua kitu’nikasema‘Mke wangu hapana…nakumbuka niliporudi kazini nililala ..hata hiyo kunywa pombe mimi sikumbuki kabisa..ila kuna kitu nahisi kuwa mimi nilikuwa na mdogo wangu, hapo sina uhakika…’akasema‘Hakuna shida, wewe jitahidi sana kutuliza kichwa, ili uweze kukumbuka vyema, na ili akili yako iwe sawa, inabidi twende hospitalini wakafanye uchunguzi wa kina maana hali kama hiyo sio nzuri…’nikasema.‘Mimi siumwi mke wangu hali kama hiyo walisema inaweza kutokea , na itapita, usiwe na wasiwasi, ilimradi tu, nikumbuke, maana hata ukinirudisha hospitalini, itasaidia nini, itaisha yenyewe tu...’akajitetea.‘Ulitakiwa mara kwa mara uwe unakwenda kiliniki, hujaenda, na ukumbuke kuwa uliambia kukitokea jambo lisilo la kawaida pia uende haraka ukamuona dakitari, na unaona hali uliyo nayo, unapoteza kumbukumbu, unafanya mambo usiku na hukumbuki kuwa ulifanya, ....ni muhimu tukamuone dakitari, hilo halina mjadala...’nikasema.‘Oh…kwanini lakini, haya bwana, kama unaona hivyo ni vyema, tutakwenda tu mke wngu,.....’akasema.‘Na utakwenda huko ukafanyiwe uchunguzi wa kina, ili tuone tatizo ni nini, kwahiyo unajiandaa kwenda kukaa huko kwa muda...’nikamwambi na hapo akashituka na kusema;‘Hapana, kwenda tutakwenda kw vipimo, halafu tunarudi nyumbani, ...siwezi kupoteza muda wangu huko, kuna mambo mengi ya kushughulikia, bila kuyamaliza hayo mambo, sitakuwa na amani...’akasema.‘Wewe unasema hivyo, lakini mimi niliyeshuhudia mambo ya usiku, siwezi kukubali, ukalala hapa nyumbani tena.. ni lazima ukafanyiwe uchunguzi wa kina, kwa hiari , au...’nikataka kusema neno lakini yeye akakatiza na kusema‘Sawa mke wangu nimekuelewa, nitakwenda,...nitafanya yote wanayotaka wao, sitaki mke wangu uishe kwa mashaka,..na kukosa amani kwa ajili yangu, mengine nitayafanyia huko huko hospitalini, . nakupenda sana mke wangu ...’akasema huku akionyesha kutokufurahishwa na uamuzi huo....‘Ujitahidi sana, kufuata msharti ya dakitari...’nikamwambia‘Sawa mke wangu, usijali, nitajitahidi sana,....maana nataka kuondokana na hii hali,...unajua mke wangu niliacha kwenda kiliniki nikijua kuwa sina tatizo tena,...najua docta atanilaumu sana, lakini ...aah, hata hivyo najiona nimepona. Mke wangu nataka nipone kabisa tuchape kazi kama zamani. Tukae tufanya kazi, sitaki nije kuonekana sijui kulea familia yangu...’akasema.‘Hamna shida, siku ukikumbuka yote yaliyopita ukaniambia ukweli moja baada ya jingine, ndio nitafahamu kuwa kweli umepona, na hutarudi hapa nyumbani mpaka nihakikishe hilo...’nikasema.‘Kwani sijakuambia kila kitu mke wangu, sizani kama kuna jambo sijakuambia, eti mke wangu kuna kitu sijakuambia kweli, kuhusu nini hasa, ...?’akauliza akiniangalia kwa mshangao‘Kwa swali lako hilo inaonyesha bado haupo sawa,… hujapona, ukipona utakumbuka kuwa hujaniambia ukweli wote, na ni muhimu sana kwangu, ni muhimu sana kwa ajili ya familia hii, umesikia, ukweli wote ndio kibali cha kuwa wewe umepona vinginevyo, utadumu sana huko hospitalini...’nikasema.‘Mhh, kweli , hakuna shida...’akasema na tukaondoka kuelekea hospitalini.**************Baada ya mume wangu kufikishwa hospitalini nikarejea nyumbani na kwanza kabisa nilihakikisha kuwa kila kitu kipo kama kawaida, na ule mto na shuka lililotobolewa na risasi nilivikunja vizuri, na kuvihifadhi mahala salama, kama vitahitajika kama ushahidi. Hata ile bastola, mimi nilihakikisha siugusi bila soksi ya mkononi, vyote hivyo nikavihifadhi sehemu salama.Nilijua kabisa sauti ya mlio huo wa bastola itakiwa imesikika kwa majirani, na nilishapanga jinsi gani ya kuwajibu, niliwaambia hakuna tatizo,....sikutaka kuwaambia lolote, kwani kila kauli utakayotoa, inaweza kuwa ushahidi baadaye, japokuwa wengi walipoona mume wangu akitoka na kufuatili na kuona tunaelekea hospitali walijua ni hayo matatizo ya mume wangu ...Docta jirani yetu ambaye alinipigia simu , nilimuambia kuwa ni yale yale matatizo ya mume wangu..‘Lakini nimesikia sauti ya mlio wa bunduki, ..kulitokea nini..?’ akauliza‘Ni utundu wake tu, ina maana hukuiondoa hapo ilipokuwa...’nikasema‘Nilikuwa mbioni kufanya hivyo, lakini si unajua mambo yalivyofungamana…’nikasema‘Utakuja kukumbuka ushauri wangu, sasa umeamuaje…?’ akasema na kuuliza‘Kama nilivyokuambia, hali yake bado, kwahiyo asubuhi tunampeleka hospitalini…’nikasema‘Akibisha, wewe niambie nitajua la kufanya..’akasema‘Sawa nitafanya hivyo…’nikasemaDunia haina dogo, hata mwandishi mmoja wa habari jirani, alifika kutaka kujua zaidi nikamwambia hakuna cha zaidi, hakuna tatizo, na ole wake akiandika mambo ya kizushi...na wananifahamu hakuna lolote lililoandikwa kwenye magazeti.Tuendelee na kisa chetu....*****************Kutokana na afya ya mume wangu kubadilika hivyo…, mimi ilinibidi nianze kufikiria mipangilio mingine. Kuna muda nilitaka niachane na haya mambo kabisa, lakini kwa vipi…maana kuna mambo ya kisheria ndani yake, na hata nikisema niache yabaki kama yalivyo, nigange yajayo…lakini, hali halisi ikawa inanisukuma nifanye hata yale nisiyoyataka kuyafanya.... Ndio nikakaa kwenye kiti na kuanza kuandika…‘Afya kwanza…’ mkataba wa asili ulitaka hilo, lazima nitimize hilo kwa ajili ya mume wangu, na hata wakili wangu alinisisitizia hilo, hata hivyo, hata bila mkataba kiubinadamu, nilitakiwa kuwajibika kwa mume wangu japokuwa mengi yalishajitokeza yaliyonifanya nianze kubadilika kinafsi,..chuki ilishaanza kugusa nafasi yangu.‘Lakini lazima hili tatizo liishe, ..’ hiyo ilikuwa fikra ya pili, kuwa pamoja na hayo, lazima nifikirie namna gani ya kulimaliza hili tatizo kabisa ili maisha yaendelee sasa kwa vipi‘Kwa vipi…’nikatulia kuwaza‘Ehee..hapa kuna mambo mawili…’nikasema‘Jambo la kwanza…labda mimi nikubali yaishe.. na je nikikubali hilo, je kutakuwa na madhara gani…?’ nikaandika kwenye laptop yangu… Je nikikubali …mkataba wao unasemaje....?’ nikajaribu kukumbuka mkataba wao unavyosema, japokuwa sikutaka kabisa kuugusa huo mkataba, nikakumbuka kama nilivyowahi kusoma‘,…kwenye mkataba wao, kama nitakubali yaishe inabidi nikubali maamuzi ya mume wangu,..kwanza kuwa kakosa na mimi nimeshamsamehe, na kwa maana hiyo moja kwa moja ninakubaliana na yale waliyoyapitisha kwenye mikataba yao mingine eti kwa masilahi ya familia, na yaliyomo humo…-Mume kama mume anashika hatamu…’sio mbaya mimi sikatai,yeye ashike hatamu tu, lakini kwa msingi gani, sasa…wa haki , au wakutumiwa yeye kwa masilahi yaw engine, maana hapo anatumiwa tu, halijui hilo…-Haki za watoto, ikiwemo huyo mtoto wa nje, na kwa vile ni wa kiume yeye atakuwa kiongozi wa familia…: Mhh, haiwezekani..hili haliwezekani hata kidini, …siwezi kulikubali, lakini lipo kwenye mkataba, na nikikubaliana na mume wangu hili linapita bila kupingwa…-Nikikubali pia, ina maana nimekubaliana na mkataba wao mwingine ambao mume wangu ndiye anausimamia kama kiongozi wa familia, kwenye huo mkataba mwingine ambao moja kwa moja unafungamana na mkataba wa asili wa familia, umewapa watoto wa marehemu hisa, kutoka kwenye urithi wao…Hawa watu wana kichaa…sitakubaliana na hili.‘Njia ya pili ni ya kwenda mahakamani, na ikifikia hapo, ndoa, hakuna…uadui mimi na mume wangu….’Simu ikaingia ujumbe wa sauti….Tuendelee na kisa chetu…*******‘Mimi ni Yule jamaa mliyekutana naye kule uwanja wa ndege,..nilikuambia tutakuja kuongea, na sababu kubwa ni kuwa polisi wamenitaka kunihoji, na pia nasikia wanahitajia mimi niwe shahid kwenye kesi…’akasema‘Kesi ipi…?’ nikamuuliza‘Najua madam wewe ni mkurugunzi, unamiliki hisa kubwa kwenye familia yako, lakini humo pia kuna hisa za watoto wa marehemu, hilo halipo wazi, na..kutokana na ushahidi nilio nao, hilo litakuja kuwa wazi..achana na hilo, lakini pia, watoto wa marehemu wanastahiki kumiliki kampuni ya mume wako..kwa wingi wa hisa walizo nao, na mume wako, hana pesa ana madeni, kwahiyo uwezo wa kufany alolote hana‘Na zaidi anakabiliwa na kesi ya mauaji, mimi ninao ushahidi wa kutosha wa kumweka ndani,…ni swala la mimi tu kukutana na huyo mpelelezi wao, lakini huyo mpelelezi wao, sipatani naye…ndio maana nikaona nioane na wewe, tuone tutasaidianaje..’akasema .‘Mimi kwa ushauri wangu wewe kama raia mwema unawajibika kushirikiana na polis, na haki itajulikana au sio..kwahiyo kwani kuna ubaya gani ukiutoa huo ushahidi polisi…?’ nikasema‘Ina maana upo tayari kuacha mume wako afungwe, maana ushahidi wangu ni kumfunga mume wako, lakini pia upo tayari kuachia hisa zako ziende mikononi mwa watoto wa marehemu…mimi nina ushahid kuwa wao, hizo hisa wamezipata kimagendo, je hutaki nikusaidie kwa hilo,…’akasema‘Ushahidi gani ulio nao, wa kusaidikisha hayo…?’nikauliza‘Nina ushahid hapa nikiutoa mume wako anafungwa,..na wewe pia utaonekana kama mlishirkiana hilo ni lakwanza lakini pia nina ushahidi wa kuwa hisa zao, japokuwa zipo kwenye mkataba, lakini unaweza kuutumia kuhalalisha kuwa hazikupatikana kwa haki,..je hutaki nikusaidie kwa hilo, na pia nimsaidie mume wako..huyo wakili mtoto wa marehemu ananitafuta sana, lakini hatujaweza kukutana mimi na yeye, sasa kabla ya kukutana na yeye, ..nimeona nikupigia simu…’akasema‘Nimekuuliza huo ushahidi upoje…?’ nikauliza‘Tukikutana utaweza kuuona, haina shida kabisa, mimi nawajali, sitaki mume wako ambaye ni mgonjwa asumbuane na polisi, na bila huo ushahidi ambao polisi wanautafuta kwa hivi sasa, bado hawataweza kumkamata mume wako, lakini cha muhimi ni wewe kuliweka hili liwe siri, ukilivujisha basi mimi sina budi, itabidi niwasiliane na polis, unaona ilivyo, kwahiyo iwe siri…’akasema‘Kwani mume wangu ni muuaji, hajaua bado, alikuwa mgonjwa, nilikuambia hilo, …’nikasema‘Huo ushahid utasema…hakuna shaka na hilo….’akasema‘Kwahiyo unataka nini…?’ nikamuuliza‘Nitakupigia…’akasema na kukata simu.Alipokata simu, kwanza nikatuliza kichwa, kitu kilichonishtua ni kuhusu huyo wakili, kijana wa marehemu…kama huyu mtu atakutana na huyu mlinzi wanaweza kujenga ubia ambao unaweza ukawa mbaya sana wa kunisumbua mimi, sasa nifanye niniHapo hapo nikashika simu na kuwasiliana na wakili wangu:‘Kuna swala hili la familia ya marehemu, siku zinakaribia, natakiwa kukutana nao ili kumalizana kuhusu huo mkataba wao, unaodai kuwa wao wana hisa kwenye kampuni ya mume wangu, ..na seehmu kwenye kampuni yangu..’nikasema‘Hilo niachie mimi….’akasema‘Lakini ni muhimu nikutane nao, maana waliniona kirafiki..kuacha huyo ndugu yao mwingine…’nikasema‘Nitaongea na wakili wao kuhusu, hilo, ili niende mahakamani kuweka pingamizi, ili twende kisheria…’akasema‘Lakini..hapo huoni nitakuwa sikuwasikiliza, maana wao walikuja kwangu wakasema wapo tayari kuridhia makubaliani, bila ya kwenda mahakamani…’nikasema‘Wao wamesema hivyo, kama ukikubaliana na mkataba huo, au sio, huoni kuwa wamekutega, kwa namna moja kwa njia ya kumsaidia mume wako,..hulioni hilo..hata hivyo, huo mkataba upo kisheria, ni lazima sheria ndio iutengue, na huwezi kuutengua bila kupitia kwenye haki za kisheria, na hapo inabidi mimi nikutane nao…na ili uoekane huo ni batili, ni lazima twende mahakamani…’akasema‘Kwahiyo tufanyeje…?’ nikauliza‘Kwa hivi sasa wewe subiria kwanza, wao waanze, maana wao ndio wanadai mirathi, ni wajibu wako kwenda mahakamani kudai wanachostahiki kukidai..’akasema‘Sawa….lakini kuna kitu kingine ambacho kinanifanya nitaharuki…’nikasema bado nikiwa sina uhakika kama kweli hilo ninaweza kumuambia wakili wangu au la..lakini wakili wangu ndiye kila kitu kwa mambo hayo‘Kitu gani…?’ akauliza Huyu mlinzi sasa ananiweka roho juu, sio tu kwa ajili ya mume wangu lakini kwa namna moja anataka kugusa haya ya mikataba, na hayo wanayodai wanafamilia hawa, kuwa wana hisa ndani ya kampuni zetu, inatakiwa kumdhibiti huyu mtu mapema, kwani akiungana na wakili mtoto wa marehemu itakuwa ni vita nyingine, ..nikasema‘Kuna mtu mmoja ananitishia kuhusu mume wangu, muda hivi kanipigia simu anataka kuonana na mimi, nataka na wewe uwepo, japokuwa kasema kuwa hataki mtu mwingine awepo, ila nataka uwepo wako usiwe wazi, …’nikasema‘Anadai nini kwani…?’ akaniuliza‘Anataka eti nimfunge mdomo, ili asiwe shahidi kuwa mume wangu, kwani ana ushahidi wa kubainisha kuwa mume wangu alikuwepo siku ya tukio…na huenda akawa anahusika kwa hayo mauaji ya Makabrasha…’nikasema‘Kwani mume wako kashitakiwa tayari , au kuna dalili hizo za kushitakiwa kuwa anahusika…?’ akauliza‘Hapana , lakini kuna tetesi kuwa itafanyika hivyo,…’nikasema‘Ili mimi niingilie kati, ni lazima kuwe na mashitaka, mimi nakushauri hivi, kama anataka kuongea na wewe usimkatalie kama una nafasi, kama huna nafasi, haina haja kabisa kusumbuka naye..’akasema‘Wasiwasi wangu ni kuwa anaweza kumtumia mume wangu kama kitega uchumi, na hali aliyo nayo mume wangu akitaka pesa, nitafanyeje…na docta kasema hali aliyo nayo sitakiwi kumkwaza..sasa je akimuendea mume wangu kwa kumrubuni itakuwaje..na..?’ nikauliza na kabla sijaendelea wakili akasema‘Kwani ni nani huyo…?’ akauliza na nikamtajia, kuwa ni mlinzi kwenye jengo alilofarikia makabrasha, na nikamtaja jina lake‘Huyo mtu ni hatari…yeye ndiye anashukiwa kama mtumiwaji wa Makabrasha, aliwahi kuwa mtu wa usalama akafukuzwa, akaenda kuajiriwa nchi ya jirani na huko nako akafukuzwa, na hata kufukuzwa kwake hakupo wazi sana kuhusu kosa lake, ila walisema kwa usalama wa kikazi…inatilia mashaka, ni mjanja sana…’akasema‘Sasa nifanyeje…?’ nikauliza‘Natamani sana kukutana na huyo mtu kwenye uwanja huo wa sheria, nione huo ujanja wake …’akasema wakili‘Kwanini…?’ nikauliza‘Watu wakorofi kama hao wananipa changamoto kwenye kazi yangu, sasa wewe subiria, akikupigia simu tena, fanya kama nilivyokuelekeza nitakuwa hewani, nikiona alama ya kuwa mpo naye, sawa..mengine yatafuata kuanzia hapo…’akasema************ Basi siku hiyo ikawa inakwenda salama, na kabla sijajipanga kwenda kumtembelea mume wangu hospitalini, mara simu yangu ikaita,…nilipoangalia nikaona hakuna jina au namba (anonymous) ..ina maana muitaji ni mtu asioyefahamika.Kwa haraka nikaweka simu yangu kwenye kurekodi, mazungumzo, na kuiweka hewani‘Nipitie Maringo hoteli, ukienda kumuona mgonjwa, nitakusubiria nje ya hoteli….’akakata simu.‘Kajuaje kuwa nakwenda hospitalini…?’ nikajiuliza Kwa kukisia tu anaweza akawa ndio huyo jamaa, lakini sikuwa na uhakika, na nisingeliweza kumpigia simu maana namba ya simu haisomi..nikawaza kiusalama nifanye nini.‘Docta, nakwenda kmuona mgonjwa, je tunaweza kuongozana..?’ nikampigia docta jirani yangu‘Mimi nipo hospitalini kwangu, kama ni muhimu kuja huko nitakuja…’akasema‘Basi hamna shida..’nikasema,‘Huyo mtu ni hatari…yeye ndiye anashukiwa kama mtumiwaji wa Makabrasha, aliwahi kuwa mtu wa usalama akafukuzwa…, ni mjanja sana…’nikakumbuka maneno ya wakili akimuelezea huyo mtu‘Hata kama ni mjanja mimi ni mjanja zaidi yake…’ nikasema kimoyo moyo, kwanza nikaegesha laptop yangu ambayo ipo nyumbani, ambayo inatumia waya za hewani, iwe na mawasiliano na simu zangu za mikononi, na chombo kingine nitakachokuwa nacho,..kwahiyo nikiwa naongea na huyo jamaa, tukio hilo litachukuliwa moja kwa moja kwenye laptop yangu, japokuwa ipo nyumani…,Nikaseti nywele zangu na kuchukua kibanio maalumu, na kuzibana nywele zangu, hicho kibanio, sio cha kawaida….Pia nikachukua simu zangu mbili zote zinauwezo wa kuchukua matukio ya sauti zikiwa na chaji ya kutosha, na kwenye begi langu nikaweka kitufe kingine chenye kazi hizo-hizo…hicho huwezi kukibaini kwani kinalengeshwa kwenye mkanda wa hilo begi..…Nikatoka nyumbani na kuingie kwenye gari langu…kuelekea hospitalini, lakini nikikumbuka kuwa natakiwa kupitia Maringo hoteli, ili kukutana na jamaa huyo mwenye ushahidi na wakati nipo kati kati ya bara bara, nikapigiwa simu‘Nani mwenzangu…?’ nikauliza‘Mimi ni wakili wa familia ya Makabrasha..’ akasema‘Unataka nini..?’ nikauliza‘Kijana wa marehemu kanipigia simu, kuwa anataka kuonana na wewe na mimi nikiwepo, ana mambo muhimu ya kifamilia, …na kwa vile mume wako anaumwa, anataka wewe uwajibike nayo, kwani muda wa kuwakilisha mirathi unakaribia…’akasema‘Siwezi kuliongelea hilo, kwa vile mambo yote alikuwa akiyashughulikia mume wangu, na yeye kutokana na hali yake hawezi kuongea kisheria ikakubalika..’nikasema‘Katoka kuongea na mgonjwa muda mfupi uliopita, na mgonjwa kasema kutoa na hali yake kuwa mbaya, anashindwa kufanya lolote, lakini kwa vile wewe upo, basi unaweza kuongea naye…’akasema‘Kaongea na mgonjwa, ni nani kamruhusu kuongea na mgonjwa,…?’ nikauliza‘Mgonjwa mwenye ndiye alishinikiza kuwa anataka kuongea na huyo jamaa, sijui ilitokeaje mpaka ikafikia hapo…’akasema‘Madocta wana akili kweli..’nikasema kwa hasira‘Ilibidi, huwezi kuwalaumu madocta, unajua mume wako akitaka kitu hataki kukataliwa, na kwa hali aliyokuwa nayo haikuwa na jinsi…lakini waliongea kwa amani tu.., hata madocta wanasema baada ya huyo jamaa kuongea na mgonjwa, imesaidia sana, kwani hata shinikizo la damu limetulia…’akasema‘Sawa nimekusikia..’nikasema hivyo tu nikijua hapo kuna jambo linatengenezwa‘Tatizo jingine polisi wanataka kuongea naye…na mimi nimewazuia..’akasema‘Kuongea na nani..?’ nikauliza‘Na mgonjwa…’akasema‘Kuhusu nini tena…?’ nikauliza sasa nikianza kuhisi kichwa kikiniuma‘Kuhusu mauaji ya Makabrsha…’akasema‘Kwani mume wangu anahusika nini na hayo mauji..?’ nikauliza‘Wanadai wana ushahidi mkubwa wa kuonyesha hilo, kuwa mume wako anahusika…’akasema‘Wameupatia wapi huo ushahidi..?’ nikauliza‘Mimi sijui..ila wanasema wanao huo ushahid na sasa wanahangaika kutafuta mashahidi wa kutosha, na wana uhakika safari hii ni lazima huyo muuaji atahukumiwa kwa kosa la kuua, kuna shahidi mmoja tu bado hawajampata nasika yeye, alimuona muuji kabisa..’akasema‘Ni nani huyo, shahidi…?’ nikauliza kwa hamasa‘Sijui..nasikia hata mtoto wa marehem kaniambia anamtafuta huyo shahidi ili haki itendeke, kasema atashirikiana na polisi kuhakikisha huyo mtu kapatikana..’akasema‘Hujanitajia huyo mtu…’nikasema‘Watu wanahisi labda ni mmojawapoo wa walinzi, kuna mlinzi mmoja kachukua likizo, hapatikani, hayupo yumbani kwake, wanahisi labda kasifiri kijijini kwako, polisi wanamtafuta…’akasema Hapo nikakata simu...kwani kuna simu nyingine ilikuwa inataka kuingia…ilikuwa ya mpelelezi anayeshughulikia kesi ya mauaji ya Makabrasha…WAZO LA LEO: Anayepitia uchungu ndiye anayeweza kuhadithia uchungu huo ulivyo;‘Haloo, afande unasemaje…’nikauliza baada ya kuiweka simu hewani‘Nilikuwa nyumbani kwako nimeambiwa umeelekea hospitalini, basi kama utakuwa na nafasi nataka kuongea na wewe, sijui…kesho labda…’akasema‘Kuhusu nini..?’ nikauliza‘Kuna muendelezo mpya wa upelelezi kuhus kifo cha Makabrasha, kuna maswali mawili matatu nilitaka kukuuliza…’akasema‘Bado mnanishuku mimi…?’ nikamuuliza‘Hapana,..ni kuhus mumeo…’akasema‘Kafanya nini..?’ nikauliza‘Nitakuambia tukikutana mimi na wewe,..kama hutojali…’akasema‘Kama ni kuhusu mume wangu msubiria apone, labda kama linanihusu mimi, na kama linanihusu mimi pitia kwa wakili wangu, ingelikuwa ni bora zaidi…’nikasema‘Hamna shida..’akasema na kukata simu********* Nilipofika hapo hotelini, sikuweza kumkuta huyo mtu, nikasubiria kidogo, nikawa najiuliza nifanye nini sasa maana sina namba yake…nikasubiria robo sasa ikapita, nusu saa ikapita….nikaona sasa napoteza muda wangu na muda huo natakiwa niwe hospitalin, nimeshaanza kuchelewa,..Ni wakati naingia kwenye gari langu, sasa nimeshaamua kuondoka, ndio ukaja ujumbe wa maneno, kuwa yeye ameondoka hapo kwasababu za kiusalama, atanijuliasha baadae ni kwanini;‘Mjinga sana wewe…’nikasema hivyo tu Nikaondoka hapo nikiwa nimeanza kuchelewa kufika huko hospitalini, huku akili yangu ikiwa na hasira kuwa maandalizi yangu yote ya kumnasa huyo mtu yamekwenda bure;Nikafika hospitalini…‘Mgonjwa yupo na docta wa magonjwa ya akili, kasema ukija uwafuate huko chumba cha uchunguzi…’nikaambiwa na kwa haraka nikaelekea huko kwenye chumba maalumu‘Tumekusubiria sana …’akasema docta‘Foleni za dar, lakini hata hivyo nimejitahidi sana…’nikasema‘Hukuonana na huyo jamaa?’ mume akaniuliza, swali lake likanipa mashaka, nikabakai kumuuliza‘Jamaa gani…?’ nikamuuliza kwa mshangao, na yeye akaniangalia kwa mshangao, na baadae akasema;‘Ok,.. basi samahani, hata sijui, …, tuendelee…’akasema hivyo, na docta akaingilia kati na kusema‘Tuendelee mgonjwa au umechoka…’akasema‘Hapana sijachoka wewe uliza maswali yako tu…’akasema mume wanguHuyo docta akawa anamuuliza mume wangu maswali mengi nikiwepo hapo hapo, yeye mwenyewe anajua ni kwanini anamuuliza hivyo, na mengi ya hayo maswali yalijibiwa kuwa ‘hakumbuki’ ‘hana uhakika’…au ‘hajui’‘Hata kilichotokea usiku…hukumbuki…?’ akaulizwa‘Kiukweli sikumbuki, na nawaza sana kuhusu hilo,..lakini sipati jibu…’akasema Baadae akaulizwa maswali mengine mengi ya nyuma, hadi ikafikia kuulizwa maswala ya historia yake, kuhusu maisha yake, na baadae akaulizwa kama ana kitu anakitafuta kinampa mawazo je anahisi labda ana mtoto wan je au aliwahi kufanya jambo gani baya, docta akawa na maswali mengi akitafuta jamboHata hivyo majibu mengi ya hayo maswali yakawa yale yale ‘hakumbuki’ au ‘hajui’ au ‘hana uhakika..’Basi hatua ya pili ikatakiwa mume wangu akapimwe kipimo cha ubongo, na uti wa mgongo,…docta alitaja vipimo hivyo, kama CT scan, na PET scan, …akachukuliwa kuelekea huko‘Baada ya hivyo vipimo ndio nitaweza kutoa taarifa yangu kwa ukamilifu…’akasema huyo docta..Baadae nilikaa mimi na huyo docta, wakati huo mume wangu yupo huko kwenye vipimo, na docta akaanza kunihoji na mimi.‘Hebu niambie kuna kitu gani kigeni kimetokea kwa mume wako?’ akaniuliza‘Kwanza namuona kabadilika kabisa sio yule mume wangu ninayemfahamu, sasa sijui ni kwasababu ya hayo matatizo au anaiigiza, maana simuelewi,..., kitabia, na hata kimatendo ni tofauti na zamani, na zaidi anakuwa msahaulivu,...’nikasema‘Hiyo ni kawaida...nionavyo mimi ni kwasababu ya hilo tatizo,...na ushukuru kuwa yeye haikumuathiri sana, ....na hali yake sio mbaya,....yanayotokea ni matatizo ya kawaida tu. Nina uhakika kuwa akitoka hapa safari hii hali itakuwa njema kabisa,...Je kuna jingine lolote uliloligudua ambalo hakuwa nalo kabla?’ akaniuliza na mimi nikatulia kidogo akili ikiogopa kusema tukio la jana, sikutaka lijulikane na watu wengi, nikasema;‘Eti docta kuna mtu anaweza kuamuka usiku akafanya kitu na akiamuka asubuhi hakumbuki kabisa?’ nikamuuliza‘Kwa vipi,..je mtu huyo anaamuka akiwa na fahamu zake, au anakuwa amelala..?’ docta akaniuliza‘Hata sijui nisemeje..’nikasema hivyo‘Nakuelewa, ila nataka uhakika kidogo, ....maana kuna ugonjwa wa namna hiyo, lakini mtu wa namna hiyo anakuwa amelala, anaamuka akiwa usingizinini, na kutenda matendo akiwa usingizini,..hajijui hapo, yeye hapo anaota, japokuwa ndoto za namna hiyo muotaji hazikumbuki ....’akasema.‘Mhh, ndio hivyo..’nikasema hivyo nikiwa sina uhakika kabisa na hilo.‘Ni hivi mtu wa namna hiyo, anakuwa kwenye ndoto, lakini tofauti ya ndoto yake na ndoto za kawaida ni kuwa, yeye anatenda yale matendo kivitendo, ....’akasema.‘Sasa mimi siwezi kujua kama alikuwa usingizini au alikuwa anaigiza…’nikasema‘Ili umfahamu huyo mtu vyema, mchunguze machoni, na jinsi anavyotembea,..macho yake yanakuwa na weupe kile cheusi hukioni,…pili kutembea kwake ni kama kwa kunyata,...hivi…’akasema‘Oh, mume wangu alikuwa hivyo hivyo, ulivyosema…’nikasema‘Basi ndio tatizo hilo la kuota huku unatenda kwa vitendo…na hebu nikuulize je tatizo hili lilianza lini…?’ akaniuliza‘Mimi naona ni baada ya hii ajali, maana mimi sijawahi kumuona hivyo kabla ya hapo…’nikasema ‘Inaweza ikawa hiyo ajali imesababisha hayo, maana ubongo ni kitu nyeti (delicate )sana, kikipata mtikisiko wa namna kama hiyo ya ajali, unaweza ukaharibu mfumo mzima wa mawasiliano mwilini, akili, ikawa sio yako tena, ndio maana unakuta watu wanapooza viungo, wanapoteza kumbukumbu na wengine wanaharibikiwa kabisa...’akasema.‘Oh…’nikaguna hivyo‘Lakini pia tatizo kama hilo linaweza kuwa ni la kurithi, huenda familia hiyo kuna mtu mwenye tatizo kama hilo, baba,mama, au wazee wao, lakini hili la mume wako, litakwisha tu maana kwa silimia kubwa tunaona ni kutokana na hiyo ajali iliyomkuta, na kama ni la kizalia ndio limejitokeza sasa, tutajua jinsi gani ya kulidhibiti..’akasema‘Kwahiyo anaweza hata kufanya mambo mabaya bila kukusudia?’ nikamuuliza‘Ndio... wengine wanafiki hata kuua, ukisoma visa vingi, huko Ulaya imetokea hivyo, hata hapa kwetu mhh.., tatizo huku kwetu hatuna kumbukumbu za kulithibitisha hilo, lakini wenzetu wanakuwa na kumbukumbu za kudumu za kitaalamu ...’akasema‘Oh, sasa utawezaje kuishi na mtu kama huyo..je akija kunigeuka na kunidhuru mimi mwenyewe au watoto…?’ nikauliza‘Cha muhimu ni kufahamu chanzo cha matatizo hayo, je tatizo la kuzaliwa. Labda karithi kutoka kwenye ukoo wao, au ni kutokana na majanga kama haya ya ajali,...baada ya hapo kuna utaratibu wa matibabu,...cha uhakika kujua historia yake ni kujua kutoka kwa watu wanaomfahamu toka utotoni, au hata mke, kama ilishatokea ukiwa naye, lakini pia kutoka kwa wazazi wake, je wao, wana tatizo hilo au kwenye jamaa zao….je mume wako amekuwa na tabia kama hizo kabla, ni muhimu sana hilo..’akasema‘Kabla hapana, tangu tuoane sijawahi kuliona hilo kabla…’nikasema‘Hiyo jana ilikuwaje…?’ akauliza‘Hiyo jana kama nilivyosema, alitoka kitandani akaenda sehemu nyingine, akafanya matendo , na akarudi na bahati mimi nilikuwa sijui , nikamshitua, akadondoka akapoteza fahamu...sio kupoteza fahamu …sio hivyo.., ila alionekana kama kalala tena,...pale alipodondoka...’nikamwambia.‘Mtu wa namna hiyo haitakiwi kushutuliwa kabisa..,ukimuona mtu wa namna hiyo wewe unachotakiwa kukifanya ni kumfuatilia taratibu kimiya kimiya, ili kuhakikisha usalama wake, kwani atafanya kile kitu anachotaka kukifanya na baadaye anarudi kulala kama kawaida, ukimshitua, unaweza ukamsababishai madhara mengine...’akasema.‘Oh, ...sasa kama ni hivyo, mbona inanitisha docta....’nikasema‘Usiwe na wasiwasi, mimi matatizo hayo nayafahamu sana, ndio ujuzi wangu, hilo tutaliangalia kwa makini, kuna jinsi ya kumpima, na tutagundua ukweli zaidi, usiwe na hofu, ..kama ni kutokana na ajali litakwisha lakini kama ni kutokana na kizalia, tutaweza kuliangalai kwa namna nyingine zaidi...’akasema‘Oh, haya docta huyo ni mgonjwa wako sasa…’nikasema‘Unajua mara nyingi tatizo hilo linahitajia muda sana kulitatua, hasa kama ni la kizalia, na wewe mke utakuwa na kazi ya kutusaidia, ili tujue hatua kwa hatua maendeleo yake, kwa hivi sasa tunahitajia tukae naye, tumchunguze, tuone tatizo lipo wapi zaidi...na tuta-mu-hypnotize…ndio matibabu yake makubwa’akasema‘Mhh, sijui kama ni kizalia,....maana haijawahi kutokea hivyo kabla, labda kwa vile sikuwa makini na hali kama hiyo, umesema kitu gani..?’ nikauliza maana alitaja neno sikulielewa, na hata baada ya kumuuliza hakulifafanua kuwa maana yake ni nini...‘Basi hiyo kazi tuachie sisi, tunafahamu jinsi gani ya kuligundua,lakini hata hivyo ningelihitajia niongee na watu wake wa asili, kuna ndugu yake yoyote wa kuzaliwa naye, baba au mama ninaweza kuongea nao kidogo, kwani hilo linaweza kutupunguzia muda, kama hakuna tutajua jinsi gani ya kuligundua kitaalamu zaidi?’ akaniuliza‘Yupo mdogo wake lakini sizani kama anafahamu lolote kuhusu historia zao, mimi nahisi kuwa tatizo hilo limetokana na ajali....’nikasema.‘Kama limetokana na ajali lingejitokeza mapema,tungeliligundua siku za mwanzoni kwenye uchunguzi wetu...hata hivyo, kwa vile yupo kwenye mikono yetu, tutaliangalia kwa mapana yake, usijali....’akasema‘Sawa docta nitafurahi kama nitapata taarifa zake, na ni kitu gani mumekigundua, kama ikiwezekana mapema zaidi, kama itawezekana, vinginevyo, mimi nawategemea nyie ...’nikasema.‘Hamna shida tutawasiliana...karibu sana..’akasema na mimi nikaondoka kurudi kule alipolazwa mume wangu,…alikuwa kaka kitandani,‘Unajisikiaje..mume wangu?’ nikamuuliza naa alionekana kama anataka kulala, labd ni dawa au kuchoka‘Mhh..mimi sijambo, ni usumbufu wao tu, maswali mengi, vipimo vingi, lakini mimi sioni kama ninaumwa mahali..ila hapa nahisi kutaka kulala..’akasema.‘Lakini ni vyema ukafuata ushauri wao ili kuondokana na tatizo hilo kabisa….’nikasema‘Sawa…hamna shida nitafanya hivyo..’akasema‘Kuna lolote zaidi maana nataka kuondoka muda wa kuona wagonjwa umeshapita, wamenisaidia tu kwa dharura…’nikasema‘Mke wangu unaweza kwenda tu, usiwe na wasiwasi na mimi kabisa, mimi hapa sina tatizo, sihisi tatizo kwa sasa, na ningependekeza kuwa wewe haina haja ya kuja hapa mara kwa mara kuniangalia, mdogo wangu anatosha, yeye nitakuwa nikimtumia kama nitahitaji kitu, wewe hangaika na shughuli za kikazi, hasa kwenye kampuni unayoihudumia wewe, au sio...’akasema‘Hamna shida...wewe angalia afya yako, hakikisha unafuata masharti ya dakitari, tafadhali, usije ukatoroka, hayo maswala ya kazi usiyafikirie kabisa, afya ndio muhimu, ukiwa huna afya hata kazi haina maana tena au sio…mimi nitajitahidi kufika kazini kwako nione kama naweza kufanya lolote..’nikasema‘Kwanini nitoroke,...’ akasema hivyo akiniangalia, na mimi sikusema kitu hapo‘Mke wangu mimi sijawahi kutoroka hospitalini, mimi sio kichaa, au mfungwa,...nimekuja hapa kwa hiari yangu mwenyewe, na nitafuata kila kitu, usiwe na wasiwasi na mimi kabisa..’akasema‘Sawa hamna shida, ..muhimu ni kujali afya yako, na nikutakie afya njema, kila-laheri...’nikasema na kuagana naye, kabla sijaondoka akasema‘Na kazini kwangu pasikusumbue sana, kuna mtu nikiwa hivi yeye anafanya shughuli zote,…’akasema‘Sawa hamna shida…’nikasemaWakati natoka mlangoni, niligeuka nyuma, nikamuona akipiga simu, aliponiona nimegeuka kumuangalia akairejesha simu kwa haraka kama kuficha ili nisijue kuwa alikuwa akipiga simu, sikuelewa kwanini anafanya hivyo…********Nikarudi nyumbani, na kumuita fundi ambaye nilimuagiza abadili vitasa vyote vya makabati, ....nikasimamia hilo zoezi mpaka likamalizika, halafu nikahakikisha kuwa kila kitu kipo sawa, sikutaka kuangalia ndani ya makabati, japokuwa nilikuwa nataka kupitia pitia kabati la mume wangu, lakini nikaona huo sio wakati muafaka, kwani nilijua hakuna kitu cha zaidi ndani ya kabati hilo.Wakati nataka kuelekea bustanini , kwani napenda sana kupumzika kwenye bustani yangu, mara nikasikia gari linaingia getini, alikuwa mdogo wa mume wangu, alionekana kuwa na haraka, alisema kaja kuchukua baadhi ya vitu vyake alivyokuwa akivifanyia kazi usiku, nikamwambia hakuna shida mimi nipo bustanini, akitaka kuondoka aniambie.‘Sawa, na kuna vitu kaka kaniagiza,nije kuvichukua, kanielekeza wapi pa kuvipata ....’akasema‘Sawa wewe mchukulie…kama kuna kingine hutakiona au unakihitajia kwa ajili yake wewe niambie tu….halafu ukishakuwa tayari kuondoka, nataka tuongee kidogo....’nikasema.‘Sawa lakini nina haraka kwani kaka anahitaji hivyo vitu vyake kwa haraka, kaniambia nisichelewe...’akasema‘Sawa sitakuchelewesha sana…’nikasemaBaadaye alikuja bustanini, na kuniambia anataka kuondoka, na alionekana kama ana wasi wasi fulani, nikamuuliza keshachukua hivyo vitu alivyomuagiza kaka yake;‘Ndio, lakini kuna kitu kaniagiza kaka, ...sasa hilo kabati alilonielekeza halifunguki..’akasema.‘Kabati gani hilo na ni vitu gani?’ nikamuuliza‘Basi hakuna shida, ....labda ufunguo sio wa kwake, lakini...’akasema akiangalia ufunguo aliokuwa nao mkononi.‘Hivyo vitu ni vitu gani na ni kabati lipi hilo?’ nikamuuliza‘Kwenye lile kabati kubwa kule maktaba kwenu...’akasema huku akiwa na wasiwasi‘Ina maana umeingia chumbani kwangu bila kuniambia kwanini usingelianiambia nikaenda kukuchukulia, ni kitu gani unakihitajia ?’ nikamuuliza‘Mhh, niliona nisikusumbue, niliingia mara moja, kwenye kabati la kaka, kanipa ufunguo wake, kanielekeza kuwa kuna kitu kwenye hilo kabato kubwa, ni makaratasi yake ya kazini, na makabrasha tu.... ’akasema‘Makaratasi gani ya kazini, wakati dakitari kasema hahitajiki kujishughulisha na jambo lolote la kumfikisrisha, hebu niambie kwa uhakika ni kitu gani alichokutuma,...na kwanini hakuniambia mimi, wewe unamua kuingia kweye chumba changu hadi maktaba bila ya mimi kujua?’ nikasema kwa ukali nikamuon aakinywea.‘Samahani shemeji, niliona nisikusumbue tu…’akasema‘Nilishakufundisha tabia njema, kuomba kitu, kuomba msamaha, salamu nk, hivyo ni vitu vidogo tu lakini vina thamani kubwa sana kwa mpokeaji,..au ni kaka yako alikuambia uchukue bila ya mimi kufahamu au sio…?’ nikamuuliza nikaona anasita sita, halafu akasema.‘Kaka kaniagiza nikamchukulie, na alisema nitaviona, kwahiyo sikuona haja ya kukusumbua shemeji, hebu nielewe hapo, kusudio langu halikuwa baya...’akasema‘Akakuambia kuwa uingie bila kuniambia mimi, ?’ nikamuuliza‘Hajasema hivyo...’akasema, na mimi nikaona nisiendelee na hayo malumbano, nikaona nimuingie kwa njia nyingine.‘Hebu niambie jana mlipoondoka na kaka yako mliongea nini?’ nikamuuliza na hapa akaangalia saa kuashiria kuwa namchelewesha.‘Mambo ya kawaida tu ya kimaisha…unajua kaka akielewa anaongea sana mambo mengi…na kwa vile alishachanganyikiwa mengine niliona hayana umuhimu…’akasema huku akionyesha kutaka kuondoka, na mimi sikujali nikaendelea kumuuliza‘Mimi nataka kujua, nina maana yangu, nimetoka kuongea na dakitari, na maelezo yako yanaweza kusaidia sana..sasa niambie aliongea nini, usijali umuhimu wake..’nikasema;‘Ni yale yale ya kuchanganyikiwa, kuwa anahisi ana mtoto wa kiume, na tunahitajika kumtafuta, na kulinda haki zake..pia anataka mimi nijibidishe kwenye kazi..ni mambo hayo ya kama ananihusia vile..ni hivyo tu shemeji…’akasema‘Ulisikia jana mlio wa risasi..?’ nikamuuliza na hapo akashtuka na kusema;‘Ndio hivi ilikuwa ni nini, maana nilisikia kama mlio wa bunduki, au bastola, kuna muda nimemuliza kaka, yeye anasema hajui kama kuna kitu kama hicho kilitokea…mimi mwenyewe nilishapitiwa na usingizi lakini nikashtuka, na nilipokuja ukasema hakuna tatizo basi sikulichukulia maanani…’akasema‘Yote hayo aliyafanya kaka yako, ..ndio maana nataka kufahamu jana mlipoondoka wewe na yeye mliongea nini…kuna umuhimu mkubwa kulifahamu hilo, usione kama nakupotezea muda, sio jambo rahisi kama unavyofikiria wewe…’nikasema na yeye akaniangalia kwa mashaka, na kusema;‘Tulichongea ni hayo niliyokuambia shemeji, mengi ni mikakati yake ya maisha kuhakikisha kampuni yake imekuwa kubwa, ana ndoto za kuwa tajiri, na vitu kama hivyo, amesema kuwa sasa hivi kaamua kutimiza wajibu wake, kwani sasa ana kampuni zaidi ya moja, na yeye ndiye msimamizi...’akasema‘Kakuambia kampuni zake, kwani yeye ana kampuni gapi nyingine unayoifahamu wewe..?’ nikamuuliza‘Mimi hapo sijui…ndio maana nikasema mengine alikuwa akiongea tu, kwa kuchanganyikiwa kwake..’akasema‘Ndio akasema sasa hivi anataka kutimiza wajibu wake kwa vipi, kwani huko nyuma ilikuwaje? Nikamuuliza na akaangalia saa tena.‘Anasema huko nyuma, alikuwa hajajitambua kuwa ana majukumu makubwa, kiasi hicho, sasa hivi kashajitambua kuwa ana majukumu makubwa kama baba wa familia, kama mtendaji mkubwa wa makampuni yake, kwahiyo inabidi abadilike, hataki kuja kulaumiwa...’akasema‘Je mliongea lolote kuhusu mkataba?’ nikauliza na hapo akashituka na kugeuka kuangalia sehemu nyingine, nikahisi hapo kuna jambo, kwanini nilipotaja mkataba ameonekana kama kutahayari….akakaa kimia akiangalia saa‘Unajua shemeji muda umekwenda..mengine utamuuliza mwenyewe, tafadhali shemeji..’akasema‘Umenisikia swali langu, nililokuuliza...?’ nikasema.‘Sijui unazungumzia mkataba gani, maana sielewi mambo yenu na kaka’akasema‘Una uhakika na hilo, ...kuwa huelewi lolote kuhusu mkataba, wakati jana niliongea na kaka yako akaniambia yote, kuwa wewe unafahamu kila kitu, wewe ndio yeye, au nimekosea...’nikasema‘Kaka alisema hivyo?..haah shemeji unajua Yule mtu kachanganyikiwa anaongea tu..’ akauliza kwa mshangao‘Ndio kaongea hivyo, ...sasa niambie ukweli, jana mlipokwenda na kaka yako hamkuongea lolote kuhusiana na mkataba, maana kama kakuambia kuhusu makampuni yake, huenda kafungua kampuni nyingine mimi siijui, huenda hayo yapo kwenye mkataba uliotengenezwa na yeye na marehemu, hilo unalifahamu sana, kweli si kweli,?’ nikamuuliza‘Lakini shemeji umesema, kuwa mliongea na kaka kama mliongea naye kwanini unaniuliza mimi tena, na shemeji ni vyema hayo mambo yenu mkayamaliza nyie wenyewe, hayo ni mambo yenu ya ndani, na mimi sifurahii kuwekwa mtu kati…’akasema kwa hali ya kama kukasirika hivi lakini hakuionyesha hiyo hali, maana kiukweli jamaa huyu ananiheshimu sana na mara nyingi anakuwa kama ananiogopa japokuwa sasa ni mtu mwenye mke wake,....’akajitetea‘Kama ni mambo yetu ya ndani kwanini kaka yako anakutuma wewe mambo ambayo unajua ni mambo yetu ya ndani ya mimi na mume wangu, wewe unayafanya tena kwa siri bila ya mimi kufahamu..?’ nikauliza na yeye akakaa kimia‘Na ni kwanini wewe uwepo kwenye huo mkataba usifahamu kuhusu huo mkataba,halafu kwanini kaka yako akakuambia mkaongee naye huko mlipokwenda jana , na kwanini anakuita wewe ‘Jembe lake’ hayo yote nayafahamu mimi sasa niambie ukweli?’ nikamuuliza na y eye hapo akawa kama hataki kusema lolote,akaniangalia mara moja na kusema;‘Shemeji naomba unielewe, nafanya hayo kwa vile kaka ananituma, na mimi kama mdogo wake, ninawajibika kumtii, lakini ...sina haja ya kuingilia mambo yenu ya ndani, sitaki kabisa kufanya jambo ambalo wewe litakuumiza…’akatulia na kuangalia sasa‘Usiangalie saa hili tunaloongea hapa ni muhimu sana…’nikasema‘Shemeji ..kaka kaniambia nisichelewe …’akasema‘Utamwambia nilikuchelewesha mimi…unasikia…’nikasema‘Nikimwambia hivyo itamkwaza sana, sitamuambia lolote kama tulikaa tukaongea, mimi na wewe kumhusu yeye, najua itampa shida sana kuwaza, natumai unanielewa na kuniamini kwa hilo..na pia kwa vile…’akakatiza hapo kuongea na kujifany akuangalia saa.‘Kwa vile alikutuma na kukuambia usiniambie kuwa kakukutuma kitu, ujifanye unakuja kuchukua vitu vyako au sio…?’ nikauliza‘Shemeji mimi namtii kaka yangu, kama ninavyokutiii wewe, kwangu mimi nyie watu wawili ni muhimu sana kwangu, na-na-waheshimu sana..sitaki kumkwaza kaka , na halikadhalika wewe, wakati mwingine nafanya mengine ili tu kaka asije kukasirika akahamanika na hilo docta kasema tulichunge sana....’akasema‘Hebu niambie ni jambo gani ulilowahi kulifanya kwa vile kaka kakuambia tu, lakini wewe hukulitaka kulifanya umelifanya ili kaka yako asije akaathirika?’ nikamuuliza na hapo akatulia kimiya, nikaona nisimpotezee muda .‘Kuna kitu nataka nikuonyeshe na kama usiponiambia kile ninachokuuliza inabidi niwaite polisi, maana naona yeye sasa anashirikiana na watu wa nje , ukiwemo wewe, ili kuja kunifisdi, na tukio la jana limenithibitishia hilo, nyie mnataka kuniua, na sijui lengo lenu ni nini baada ya mimi kufa...’nikasema.‘Shemeji, hayo yametoka wapi…?’ akaniuliza akionyesha uso wa mshangao.‘Ushahidi upo,..sio kwamba naongea tu kutoka hewani, sasa kama kweli ulivyosema wewe ni kweli kuwa unanijali, na mengine unayafanya kumrizisha tu kaka yako japokuwa wewe hutaki kuyafanya hayo….sasa nataka kulihakikisha hilo..na huu ushahidi umenifungua macho, kuwa nyie wawili mna njama na mimi…’nikasema‘Shemeji ushahidi gani huo, na kuna nini…kinachoendelea shemeji, mimi sitaki kabisa kushiriki kwenye mambo yenu, hata hilo la mkataba, nililikataa kata kata.., lakini kama nilivyokuambia, mengine nayakubali ili tu kumrizisha kaka…’akasema‘Kwahiyo uliitwa kuweka sahihi tu au ulikuwepo kwenye hicho kikao chao…?’ nikauliza‘Niliitwa kuweka sahihi tu,..na nilipojaribu kukataa, nikaonywa, …sasa shemeji usinilazimishe mimi niongee mengi, hebu jiweke wewe kwenye nafasi yangu, ungelifanyaje…’akasema‘Na kwasababu hiyo, kama umekubali kushirikiana na matepeli, wezi, walaghai na wewe utakuwaje? Ee niambie..! Sasa mimi nataka nilione hilo, kama kweli hutaki kushirikiana nao…nataka unionyesha, na mimi nitakulinda, nakuhakikishia hilo, lakini kama hutajitoa kimatendo, basi nitachukulia kuwa na wewe ni miongoni mwao, na sitasita kuchukua hatua,..na sio kusita hatua zimeshaanza kuchukuliwa…’nikasema‘Shemeji kwni kuna nini..mbona mnaniweka kwenye wakati mgumu…’akalalamika‘Je jana hamkupanga kuja kunimaliza, na labda hukupenda lakini ulifanya kwa vile kaka yako alitaka kulifanya hilo, niambie ukweli..?’ nikamuuliza‘Shemeji, mimi hiyo kauli siitaki, nakuheshimu sana shemeji yangu, wewe ni sawa na dada yngu mkubwa, nimeishi nawe hapa ukanisaidia sana, lakini hilo unalolizungumza sasa hivi limevuka mpaka, kwanini mimi nifanye hivyo, kwanini…’akasema sasa akionyesha kukerwa.‘Sikiliza …’nikasema‘Hapana shemeji mimi naona niondoke, maana haya mazungumzo yatanikosesha adabu, na mimi silitaki hilo litokee nitajilaumu sana, hapana shemeji ngoja niondoke tu…’akasema, lakini sikumpa muda huo, nilijua leo ni leo tu.‘Nimekuambia nina ushahidi na hicho ninachokisema, sisemi kwa kukisia tu, na hapa najipanga jinsi gani ya kuongea na askari, atafika hapa muda wowote, sasa nilitaka kujua ukweli kutoka kwako, kama hutaki kusema ukweli, basi wewe utausema yote mbele yao, watajua jinsi ganu ya kukufanya uongee..’nikasema na hapo akatulia, na akaonekana kuwa na mashaka‘Kwani kulitokea nini shemeji…?’ akauliza sasa akionekana limemgusaNikachukua ile mashine ya kuchukua kanda ya video zamatukio nikaweka sehemu ambayo anaweza kuona, nilitaka kumuonyesha sehemu ndogo tu, ili niweze kumchota mawazo, na najua kuna ukweli mkubwa anaufahamu lakin anaogopa kumchongea kaka yake....‘Haya angalia ushahidi huo…’nikasema nikimuacha aangalie‘Oh shemeji....mbona, ...oh, inaonyesha anampiga mtu, sio wewe ulikuwa umelala hapo...mbo-mbona ....’akawa hamalizii‘Sasa niambie ukweli jana mlipotoka wewe na kaka yako, mliongea nini au mlipanga nini maana ushahidi umeuona,..polisi wanakuja, na wewe ni mzima, kaka yako ni mgonjwa, kwahiyo wewe utahusika kwa hili moja kwa moja‘Shemeji..mimi sijui-ki-kitu…’akasema sasa akiangalia kule getini, aliposikia gari linapita akajua ni polisi hao wanakuja‘Unakumbuka asubuhi nilikuambia nini,…’mbona unashtuka kuniona, unakumbuka..?’ nikamuuliza‘Mhh..akaguna hivyo‘Sio kweli kuwa uliponiona ulionekana kama unashtuka,..sasa hivi wajifanya hujui,..ulishtuka nini, ni baada ya kuniona mimi nipo hai, au sio… au unajifanya hujui mlichokipanga wewe na kaka yako, au niambie kaka yako alisema anataka kunifanyia nini mimi…?’ nikamuuliza hapo kwa ukali…NB: Tutaendelea na sehemu hii uone mdada alivyoliweka hilo jambo, na hatimaye ikawa ni sehemu ya kupiga hatua kuishinda hiy mitihani inayomkabiliWAZO LA LEO: Asili ya nafsi ya binadamu ni ubinafsi, na usipoweza kuidhibiti nafsi yako, tamaa huchukua nafasi, na shetani anakuwa ndiye rafiki yako mkubwa, na hapo ndio unajikuta hujali kufanya maasi, dhuluma inakuwa ndio jadi yako, na ukifika hapo hutawajali wanadamu wengine, hutakuwa na huruma...imani ya ucha mungu kwako inakuwa ni hadithi. ‘…Jana asubuhi uliponiona ulionekana kama unashtuka,..kweli si kweli kwanini ulikuwa unashutuka, si ina maana hukutegemea kuniona nikiwa hai, au sio… au unajifanya hujui mlichokipanga wewe na kaka yako, vinginevyo uniambie ukweli…mlipanga nini wewe na kaka yako,…?’ nikamuuliza hapo kwa ukali…‘Shemeji hapana, hatujapanga kitu kama hicho, na wala sielewi kwanini kaka alifanya hivyo....kwanini tupange kuku-ua shemeji, mimi nakujali sana, kuwepo kwako ni muhimu sana kwangu…, ’akalalamika huku akishika kichwa akionyesha masikitiko.‘Sasa mimi nimeamua, nichukue hatua, nakuambia wewe kwa vile kaka yako ni mgonjwa, na kwa vile wewe ni mzima, na inaonekana mpo shirika, basi wewe utaisaidia polisi ili ukweli uweze kupatikana,…kwasababu mimi nimeyavumilia haya mambo mpaka watu wananiona mimi ni mjinga…’nikasema na mara simu yangu ikaitaShemeji akawa ananiangalia kwa mashaka, akihisi labda ni polisi wananipigia na nilipoitizama hiyo namba nikaona ni ya yule mpigaji asiyejulikana, nikaiweka hewani na kusema;‘Niambie…?’ nikasema‘Polisi wananitafuta sana ili niongee nao, na naogopa nitaongea nao kabla sijakutana mimi na wewe, nahisi ni wewe umewaambia, sasa litakalo tokea mimi sina lawama …’akasema‘Sasa kwanini huongei nao, mimi siwezi kukulaumu, kama una ushahidi huo kawape polisi, si una uhakika nao, kwanini unaogopa kuwaopatia polis, lakini kama nia yako ni kupata masilahi, kwangu hupati kitu…’nikasema‘Tatizo wewe hujui kitu gani nilicho nacho,..sawa…kama unasema hivyo, sawa, lakini namuonea sana mume wako huruma, na zaidi nashangaa kwanini mke wake hana huruma naye, huyo akienda jela atafia huko, ndio unalolitaka au sio…’akasema‘Hayo ni maneno yako na hisia zako, hayawezi kubadili sheria za nchi…’nikasema‘Unajua madamu, mimi nilitarajia leo ningewakabidhi kila kitu, ili mjua wenyewe jinsi gani ya kufanya, lakini mpaka sasa naona muda unakwisha tu..sipati marejesho…’akasema‘Marejesho gani, kutoka kwngu, mimi na wewe tulikubaliana kitu gani, wewe ulisema tukutane unionyeshe huo ushahidi, mara eeh, unatafutwa na polis, kumbe na wewe ni mhalifu unatafutwa na polis, eeh, sasa kajisalimishe huko na huo ushahidi wako…’nikasema‘Mimi nimeongea na mume wako nikamuelezea yote , na pamoja anadai kuwa hakumbuki, lakini ushahidi kidogo niliomuonyesha kakiri kuwa yupo matatani, hata kama anaumwa,…na kasema nimuachie huo ushahidi, akasema kuna mtu atamtuma,…ili nimkabidhi…’akasema‘Sawa kama mumeongea na mume wangu basi mtamalizana naye, mimi sihitaji sana kuongea na wewe, kwani msimamo wangu ni ule ule, na huyo mtu ni nani..?’ nikamuuliza sasa nikimtupia macho shemeji yangu akawa ananiangalia kwa mashaka.‘Anamfahamu yeye mwenyewe huyo mume wako…’akasema‘Alishawahi kutumwa kwako kabla, au umesahau kuwa wewe ulikuwa tarishi wa marehemu, ….au sio..’nikasema‘Sawa tuyaache hayo, ila nilifanya hivyo kwa manufaa yenu, kama umefikia kunidharau hivyo, basi mimi nitawakabidhi polisi, itakwua usumbufu kwako mkurugenzi mnzima ukishitakiwa wewe na mume wako, maana huo ushahidi unaonyesha kama nyie wawili mlishirikiana …’akasema‘Kwa vipi…?’ nikauliza‘Yeye alifika akamaliza kazi, na wewe ukaja kuhakikisha,..bahati mbaya wewe ukakamatwa, lakini mume wako bado yupo mafichoni, kwa maana ya kuwa polis bado hawajamtambua, …wameshatambua hilo, ila wanahitajia ushahdi zaidi na shahidi muhimu ambaye ni mimi…’akasema‘Sawa nimekuelewa sasa unataka nini..?’ nikauliza na mara yeye akakata simu.************Niligeuka kumuangalia shemeji yangu aliyekuwa akisikiliza kwa makini, akasema‘Nahisi ni….nilijua ni polisi..’akasema‘Ni mtu wenu huyo…nahisi kaka yako alitarajia kukutuma kwake kumpelekea pesa ili asitoe ushahidi kuwa kaka yako anahusika kwenye mauaji ya Makabrasha, na inaonekana kazi yako ndio hiyo ya kutumwa na kaka yako, au sio….’nikasema‘Sasa shemeji ngoja mimi niondoke…’akasema‘Nimekuambiaje..maana hata ukiondoka sasa hivi utakutana na polis njiani, ..’nikasema‘Kwani mimi nina kosa gani…?’ akauliza na kabla sijamjibu simu ikapigwa tena‘Hebu subiri kuna huyu tena anapiga simu…’nikasema na kuipokea hiyo simu, ilikuwa namba ambayo sijaiweka kwenye kumbukukumbu zangu.‘Halloh nani mwenzangu..?’ nikauliza‘Ni mimi yule mtoto wa marehemu…nilikuwa nauliza kama upo tayari ya kikao chetu, ni kesho au sio…?’ akauliza na kabla sijamjibu akaendelea kuongea‘Japokuwa baba mdogo, nikiwa na maana mumeo kalazwa, lakini sizani kama hilo litasumbua kitu au sio maana tulishaongea iliyokuwa imebakia ni sisi kurejesha maelezo kutoka kwa mawakili wetu..je kesho upo tayari..?’ alikuwa Yule mtoto wa Marehemu ambaye ni kiongozi wa familia.‘Mimi sina shida ya hicho kikao , ila msimamo wangu ni ule ule, je mumeupata ule mkataba wa zamani…?’ nikauliza‘Hilo ni tatizo madam , hatujaweza kuupata huo mkataba unaosema ni wa zamani.., ni kama vile haupo..’akasema‘Sasa tutajadili nini, iliyobakia ni mimi nifuate sheria, ili ijulikane kabisa kuwa mkataba huo mlio nao ni wa kugushi..’nikasema‘Mimi nataka kuondoka, na ..natarajia kukaa na familia yangu, ili majukumu yote niyaache kwa huyo msaidizi wangu siwezi kuendelea kusubiria…’akasema‘Mimi sina shaka, yoyote Yule nipo tayari kukabiliana naye, ilimradi tu, huo mkataba wa awali uwepo..’nikasema‘Kiukweli madamu, kwa hilo, itakuwa ni vigumu sana, maana wakili wetu amefanya jitihada zote ameshindwa kuupata huo mkataba unaosema ni wa zamani, sasa tufanyeje..?’ akaniuliza‘Hilo ni swali ambali unatakiwa umuulize wakili wenu au sio..’nikasema‘Yeye kashauri hivi, wewe ukubaliane na huu mkataba tulio nao sasa, maana swala sio kuufuata, swala ni kuhakikisha kuwa haupo tena, na kuufuta ni lazima taratibu za kisheria zifuatwe…umeliona hilo…’akasema‘Kwangu mimi siwezi kufanya hivyo, huo mkataba siutambui, na najua dhumuni la hayo yote, kwahiyo msimamo wangu bado ni huo huo…’nikasema‘Basi hilo nitawaachia nyie mpambane na huyo msaidizi wangu… , kiukweli siwezi kuendelea kusubiria tena, hata mama naye anataka kurudi huko kijijini, akahangaike na shughuli zake,…, ngoja nikae na wanafamilia, ili hili jambo sasa liwe bayana kwa wanafamilia wote, kitu ambacho sikukipendelea, unajua kila mmoja anamtizamo wake…’akasema‘Hilo ni juu yenu nyie kama wanafamilia..ila ninacho kushauri, hata mkikaa na wanafamilia usije kuwaficha kuwa huo mkataba ni batili, unasikia..vinginevyo, hata kama utakwenda huko unapokwenda, ujue unaweza kuitwa kama shahidi kwenye kesi nitakayoiwakilisha mahakamani…’nikasema‘Sawa..ngoja tuone, nitakujulisha baada ya kikao cha wanafamilia..’akasema na kabla hajakata simu nikasema ;‘Nikuulize kitu, ulisema wewe kwenye ile video ya matukio kwenye ofisi ya Makabrasha uliona Yule aliyemuua baba yako, au sio..?’ nikamuuliza‘Sikumuona, nilikuambia sura haikuonekana,..alitokeza kichwa tu, na kichwani alivaa kitu kama soksi, ya kuziba uso na kichwa kizima akaacha macho na pua..’akasema‘Na wakati anamlenga marehemu risasi, mume wangu alikuwa amekaa mbele ya huyo marehemu au sio, sambamba, au sio ,..?’ nikauliza‘Ndio walikuwa wamekaa wawili mmoja huku na mwingine kule, meza imewatenganisha, kama ilivyo kwenye ofisi…sio sambamba ya kukinga..lakini walikuwa wanaangaliana na huyo mpigaji alipiga risasi akiwa mlangoni, akimlenga marehemu, naelewa unachotaka kukisema hapo, kuwa labda isingeliwezekana mtu akiwa mlango kumlenga marehemu…angalia mlango ulipo, na meza ilipo, na muuaji ana shabaha..’akasema‘Kwahiyo kwa vyovyote vile, kutokana na huo ushahidi mume wangu hawezi kuhusika na hayo mauaji au sio…?’ nikamuuliza‘Hawezi kuhusika,..hao ni polisi wanatapa tapa tu, nimelisikia hilo, kuwa wao wana ushahidi wa kutosha kuwa mume wako kahusika, ni waongo..au kama wana ushahidi mwingine mimi siujui..ila nilio nao ndio huo, na kama mume wako angelihusika mimi mwenyewe ningehakikisha anakwenda kuhukumiwa…’akasema‘Kwanini sasa hutaki kuwaonyesha polisi huo ushahidi ulio nao wewe…?’ nikauliza‘Kwasababu utamtia hatiani mume wako kwa jinsi unavyoonekana , kwa namna moja au nyingine, ataonekana anahusika, ama kwa kushirikiana na hao watu, au kujua ukweli halafu akauficha, halafu nimeshachelewa kufanya hivyo, nikifanya sasa unajua ni nini kitatokea, its too late! …’akasema‘Lakini kwenye maelezo yako ya mwanzo hukusema hivyo…’nikasema‘Nilisemaje..?’ nikauliza‘Ulisema hutaki kuonyesha huo ushahidi kwa polisi kwa vile unaogopa kuwa polisi watajua kuwa mume wangu alikuwepo kwenye hicho chumba kwahiyo atashukiwa,..ni kitu kama hicho..’nikasema‘Ndio,… hiyo pia ni sababu moja wapo, na hilo la kuwa mume wako alionekana hapo ofisini, bado halina nguvu, hakuna mtu wa kulithibitsha hilo, …’akasema‘Una uhakika na hilo kuwa hakuna mtu anayefahamu kuwa mume wangu alikuwepo huko…?’ nikauliza‘Aaah, uhakika gani, mimi nilijaribu kuulizia, hata mpelelezi wangu alijaribu kufanya uchunguzi , hakuna mtu aliyewahi kumuona mume wako hapo kwenye hilo jengo, pili hospitali wanatambua kuwa mume wako alikuwa mgonjwa, alilazwa, na hali yake isingeliwezesha yeye kufika huko..’akasema‘Sawa nashukuru..’nikasema na kukata simu. Nikageuka kumuanga shemeji yangu , na alionekana akitabasamu kidogo‘Umefurahi nini..?’ nikamuuliza‘Nimesikia kama umesema kaka hahusiki, ni kweli itakuwaje, mtu alilazwa hospitalini angeliwezaje kufika huko…’akasema‘Wewe ungeliweza kumsaidia, wewe si jembe lake..wewe si anakutuma mara kwa mara kumfanyia kazi zake…’nikasema‘Nini ..!!’ akasema akionyesha mshtuko‘Wewe sio jembe lake, wewe si ndio anakutuma mara kwa mara, na akitaka kufanya jambo anakuita wewe, je siku hiyo sio wewe aliyekuita ukampeleka huko, ..?’ nikauliza‘Wapimwishowe nimeona ni muhimu kuwafahamisha watu wa usalama, ili baadae nisije kualaumiwa,unaona, ..wao wanakuja, ..sijui kwanini hawajafika mpaka muda huu, na wewe watakiwa kuonana na kaka yako…’nikasema‘Shemeji, kwanza nimeshachelewa, kaka atakuwa ananiulizia huko…’akasema‘Huwezi kuondoka, mpaka uonane na polisi,…acha akupigie simu, na polis watajua jinsi gani ya kumjibu, wanajua kuwa kaka yako yupoje...kwani wakati anakutuma, ilikuwaje, alikupigia simu au..?’nikauliza‘Mimi sijui lakini yeye alinipigia simu niende hospitalini, kuna kitu anataka kunigaiza, ndio nilipofika akaniagiza nije kuvichukua hivyo vitu…’akasema‘Ni kimojawapo ni mkataba, au sio mkataba ambao bado anahangaika nao, mkataba wa kugushi, mkataba ambao utampa mamlaka ya kumiliki mali ili na wewe ufaidike au sio?…yeye anafikiria kuwa huo mkataba utamsaidia..na kingine ni nini alichokuagizia…?’ nikauliza‘Ni hizi nyaraka tu za ofisini kwake…’akasema na kunionyesha, sasa alionekana kuwa huru kufanya ninavyotaka, na ndicho nilikitaka,…nikachukua zile nyaraka na kuanza kuzikagua, nikakuta kuna mkataba wa kuuza gari…‘Kwanini anataka kuuza gari…?’ nikauliza‘Mimi sijui, yeye wakati ananituma alisema, kuna mkataba wa mauzo, anatakiwa aufanyie kazi haraka maana kuna watu wanahitajia pesa kwa ajili ya kuimaliza kesi ya mauaji, hataki wewe usumbuliwe tena…na asipowalipa hizo pesa wanazomdai, unaweza kufungwa..’akasema‘Mimi au yeye…?’ nikauliza‘Yeye alisema ni wewe…’akasema‘Kwanini mimi nifungwe wakati sihusiki na hayo mauaji..?’ nikauliza‘Mimi sijui…’akasema‘Kuna jingine alikuagiza..?’ nikauliza‘Hapana…’akasema kwa kusita‘Una uhakika, hakuna kitu kakuambia uweke…au uchukuze zaidi ya hivyo…kama anavyokuagiza kila mara , hujawahi kuagizwa kule ofisini kwangu kuchukua kitu..?’ nikamuuliza‘Hakuna shemeji…zaidi ni karatasi za madeni,hakuna,..hapana shemeji, ofisini kwako, hapana, mimi kama niliwahi kufika huko, ni wakati upo ofisini, sijawahi kufika wewe ukiwa haupo …’akasema‘Wewe unahisi hizo pesa anataka kumlipa nani..?’ nikauliza na hapo akaniangalia kwa mashaka, halafu akasema;‘Hapo sijui…lakini jana nilisikia wakati anaongea ovyo, kuwa una mtu kasema asipomlipa pesa anaweza kutoa siri, siri ambazo zinaweza kukufunga na hata yeye anaweza kuwa hatiani…, nikamuuliza siri gani, akasema ni vyema mimi nisijue itakuwa bora kwangu….’akasema‘Unahisi kweli kaka yako hajaua..huoni kama vile kafanya yeye hayo mauaji ndio maana anajaribu kuuficha ukweli…na kama hajaua kwanini ahonge, unaona eeh, na wewe unaingizwa kwenye janga hilo…’nikasema‘Lakini atauwaje na wakati alikuwa mgonjwa, mimi nahisi anaongea kwa kuchanganyikiwa…’akasema‘Kuchanganyikiwa mpaka leo, si sasa hivi ni mzima, ana akili zake sawa sawa, mbona analikumbuka hilo, …kwanini kakuagiza huu mkataba, kwanini analikumbuka hilo la huyo mtu, anayedai pesa, kuwa ana ushahidi..? ..na docta kasema mara nyingi mtu akiwa kwenye hiyo hali anaweza asikumbuke alichokifanya akiwa kachanganyikiwa, hebu acheni hayo maigizo..?’ nikamuuliza‘Lakini shemu yawezekana ni kweli…maana alivyoongea leo sio sawa na alivyoongea jana usiku…’akasema‘Leo kaongea vipi…?’ nikamuuliza‘Nilipofika, nilimkuta kama yupo kwenye dimbwi la mawazo, halafu akaniuliza, jana nilifanya nini..mimi sikutaka kumuambia, ukweli wote, halafu akasema hivi,..leo kuna mtu kampigia simu, kuwa ana ushahidi ambao akiwaonyesha polisi yeye na wewe mnaweza kuwa hatiani, lakini hakumbuki huyo mtu ni nani, akasema kwa kuepusha shari ni bora ampe huyo mtu akitakacho na ili huo ushahidi upatikane uharibiwe,..…’akasema‘Mbona hukuniambia awali hivyo, mpaka nimekubana kwa njia hiyo, wewe kuna kitu unaficha,..unamficha nani,…sikiliza mimi sitaweza kukubeba kwa hili, unasikia…kama hutaniambia ukweli wote, basi, …’nikasema‘Ukweli upi tena huo shemeji…’akasema kama kukereka‘Hapa unaona nakukera, lakini polis ni mara ya ya hapa, watakuuliza kitu kile kile, hadi wakuchanganye kichwa, na mwisho wa siku wataubaini ukweli wanaoutaka, sasa niambie, jana aliongea nini…?’ nikamuuliza‘Shemeji nimeshakuambia jana alikuwa anaongea mambo mengi tu, ovyo ovyo, wakati mwingine anachanganya mada, …’akasema‘Kwahiyo unavyohisi wewe ni kweli hajui alichokifanya jana…nataka useme ukweli ili tuweze kumsaidia kaka yako, na pili ili tuweze kumshika huyo tapeli anayetaka kupata pesa kwa njia isivyo hali, wewe huoni kuwa kaka yako anatumiwa tu…’nikasema‘Mimi namfahamu kaka vizuri sana, …anavyoongea leo, sio kama ilivyotokea jana, mengi nikimuuliza hakumbuki kabisa…anahisi kama likuwa anaota tu shemeji….’akasema‘Ngoja polisi waje natumai wakija wewe utakuwa na habari nzuri ya kuwaeleza, wao ndio watayapima hayo maelezo yako, lakini kwa kukutahadharisha tu, hayo maelezo yako yanaweza kukufunga, unageuza geuza maneno, hata mimi naanza kukushuku kuwa wewe una mpango mmoja wewe na kaka yako…’nikasema‘Mpango gani shemeji, ..mimi siwezi kufanya hivyo,….ninachofanya sasa ni kujaribu kumsaidia kaka ili aondokane na haya mambo, kiushauri pia..ili muishi wawili kwa amani…’akasema‘Wewe na kaka yako, mlipanga jana kuniua,..hilo huwezi kulikwepa..hata kama …lakini kaka yako alikuwa na nia hiyo…’nikasema‘Sio kweli shemeji, hilo …nakuapia, mimi siwezi kufikiria hilo,na kama ningelifahamu kuwa kaka anataka kufanya hivyo, ningekuarifu…’akasema‘Na hayo mauaji mengine..?’ nikauliza‘Mauaji gani, ..shemeji, hivi kweli mimi naweza kumuua mtu…’akasema‘Umeshirikiana wewe na kaka yako kulikamilisha hilo..hata kama wewe hujafanya, ila unafahamu hizo njama kwahiyo mumeshirikiana naye…’nikasema‘Hapana…mimi sijui lolote ..’akasema‘Haya, nakupa muda wa kuliwazia hilo, hapa hapa, kabla polisi hawajafika, maana wao wakifika utawaelezea vyema, kwanini kaka yako alitaka kuniua hilo lazima watakubaba mpaka useme, …’nikazidi kumshinikiza kwa hilo, nia ni kumjenga hofu ili aweze kuja kuniambia kila kitu ninachokitaka‘Pili, kaka yako nashukiwa kuwa kashiriki au ndio yeye kamuua Makabrasha, aliwezaje kwenda huko wakati anaumwa, ni lazim akuna mtu alimsaidia, ni nani, kama sio wewe jembe lake, kwahiyo alikuita ukampeleka au sio…?’ nikamuuliza na hapo akashtuka na kuangalia kule getini.‘Sema ukweli shemeji, …ukweli ndio utakusaidia..’nikasema‘Kaka alikuwa mgonjwa, huenda ugonjwa wake ndio uliomfanya akafanya hivyo, mimi sijui lolote utanionea bure tu shemeji…’akasema‘Haya…, kama ni ugonjwa, angwezaje kufika huko….ni lazima kuna mtu alimsaidia,…hapo huwezi kukwepa…’akasema‘Shemu mimi naomba tafadhali..usiwaambie polie lolote kwa hivi sasa, subiria kaka apone kwanza…’akasema‘Haya ni lazima yawekwe kwenye kumbukumbu za polisi, kuna leo na kesho, je ikitokea akafanikisha dhamira yake,..kutapatikana wapi ushahidi wa rejea…hapa ni kauli yangu na yako, ni lazima watu wa usalama wawe na habari hizi..’nikasema‘Hapana, sio vyema shemeji, na kwanini mimi nihusike hata hivyo..?’ akauliza‘Kwasababu hata wakati anataka kuniua, alikutaja wewe, na kakiri kuwa wewe ndiye jembe lake…, kwanini akutaje wewe kuwa umsaidie hebu jiulize hapo…’nikasema‘Mimi sijui labda ni kuongea tu, …’akasema‘Docta anasema mengine anayafanya kutoka na kumbukumbu alizokuwa nazo kichwani, na moja ya kumbukumbu zake ni wewe. Mlivyoongea , mlivyopanga…ndio maana nakutilia mashaka, hata polis wanakutilia mashaka, ndio maana wanataka kukutana na wewe, mimi nimetaka kukusaidia, lakini hutaki kuniambia ukweli, basi nanawa mikono...’nikasema‘Shemeji mimi jana nilipokuja nilienda chumbani kwangu, kweli si kweli, na kiukweli mimi nilichelewa kulala , kwahiyo hata usingizi uliponishika nilala fofofo, ndio nikaja kuamushwa na huo mlio wa bunduki, sikujua kabisa ni nini kimetokea, na nilipoamuka ndio nikakimbilia kuja kuwaona, nilijua kua mtu kaumizwa, nilipokuona upo sawa, ndio nikashikwa na butwa, nikijiuliza huo mlio wa bastola ulikuwa wa nini,.....’akasema‘Kwahiyo kwa kauli yako hapo, ulijua kaka yako kaniumiza..au kaniua…?’ nikamuuliza‘Kaka nimemuona yupo vile, hajaumizwa, hana jeraha, kwahiyo iliyokuwa imebakia ni wewe..ndio nilipokuona nikawa na hiyo hali, unayosema ni ya kushangaa…’akasema‘Haya sawa, kuna jambo nataka uniambia maana ukitoka hapa, hutakuwa na mimi tena, utakuwa mtu wa polisi, huyo mwanamke aliyezaa na kaka yako ni nani, umesikia akisema kuna mwanamke wake, huyo mwanamke anampenda sana kwa vile kamzalia mtoto wa kiume, jembe jingine…, ni nani huyo mwanamke?’nikamuuliza.‘Mimi simjui huyo mwanamke, ...naona alikuwa anaongea tu kama mtu aliyechanganyikiwa...huoni hata sauti yake inasikika kama mtu aliyelewa, kama teja, kama mtu yupo usingizini, na shemeji kwanini unasema hutakuwa na mimi, nitakuwa na polisi kwa kosa gani...?’akasema sasa akijua simtanii…‘Kila kitu nikikuuliza mimi unasema hujui, …nitakusaidiaje eeh, hebu niambie,na wao wanataka kukutana na wewe, kukuhoji..kuujua ukweli,..na kwa maelezo yak ohayo, ni nani atakuamini, unaichanganya…wewe...utakwenda kulala jela...’nikasema sasa nikichukua simu yangu, hapo akawa ananiangalia huku akionyesha kuogopa‘Shemeji mimi nina uhakika , kaka anakupenda sana asingeliweza kufanya kitu kama hicho akiwa sawasawa, mimi nahisi kafanya hivyo, kutokana na kuchanganyikiwa...na unataka nikuambie kitu gani ili uniamini, ..mimi sijui zaidi ya hayo, msubirie tu kaka akipona utamuuliza’akasema‘Ngoja polisi waje…, naona wamechelewa sijui kwanini..natumai ukiwaona ndio utajua kuwa wewe upo matatani. Kwa maelezo yako tu, mimi nimethibitisha kuwa kuna kitu mpo ushirika na kaka yako, na haya yaliyotokea na wewe unahusika, sasa..wewe utaweleza yote jinsi gani unavyofahamu wewe, ili ibakie kwenye kumbukumbu zao, unasikia....’nikasema.‘Shemeji, acha usiwapigie simu polisi…,’akasema‘Nikiwapigia, nisiwapigia ni hali moja, wewe utahojiwa na wao, na wao walisema watakuja hapa,..na nimeoa ni bora wakuhojie hapa, kuliko kukupeleka kituoni, ili nisikie wanachokuhoji…’nikasema‘Shemeji, nisaidie, na msaidie kaka..huyo ni mume wako, kwa hili utamtia hatiani, ..kama kuna kitu kingine niulize tu, nitakuambia kila kitu utakavyo, lakini waweke mbali polis na kaka,, utamchanganya kichwa kabisa ..’ akasema na mimi nikawa tayari nimeshampigia simu ofisa mmoja wa upelelezi ninayemfahamu..NB: Sehemu hii nimeandika kwa haraka haraka, naweza nikawa nimerudia rudia, naomba ipite hivyo, ili tusonge mbele.WAZO LA LEO: Moja ya rehema za mwenyezimungu, ni mapenzi kati ya mume na mke, kuhurumiana na kujaliana. Wawili hawa wanakuja kujenga familia , na huenda walikutana tu bila hata kujuana, ni nani alijua wewe utamuoa huyo uliye naye au kuolewa naye, ni kwa rehema za mola wetu….sasa kwanini tunakuja kuliharibu hilo, watu wanakuwa hawaelewani tena, ndoa zinakuwa ndoana. Tumuombe mola wetu azijalie ndoa zetu, ziwe za upendo, na furaha, na wale ambao hawajajaliwa kuwa na ndoa, mola awajalie walifanikishe hilo, kwa rehema zake. Aamin. Nilishaanza kumshuku shemeji yangu kuwa anafahamu mengi, na siku ya leo niliona ndio siku pekee ninayoweza kumbana , na kusema ukweli wote, lakini sikutaka niongee naye peke yangu, nilishaongea na watu wa usalama, ambao nafahamiana nao,na niishawaeleza ni nini lengo langu, na nikaona niwaite watu hao waje kunisaidia ...Endelea na kisa chetu*********Shemeji yangu huyo alipooa nafanya kweli akageuka huku na kule akitaka kukimbia, na kabla hajafanya hivyo nikamuonyeshea ishara ya kumuonya..., akatulia nikamaliza kuongea na huyo ofisa upelelezi, ambaye nilishamgusia kuhusu hayo mambo yanayoendelea katika nyumba yangu na yeye akaahidi kuwa atalifuatilia hilo tatizo kwa karibu.‘Shemeji ...ina maana unataka sisi tufungwe?’ akauliza shemeji yangu huyo sasa akionyesha ile sura adimu ya chuki, sura kama hizo kwa wengine ni nadra kuonekana.‘Ukweli wako ndio utakaokusaidia wewe na kaka yako, nilishawapa muda wa kutosha, sasa wakati umefika, kama kweli unataka kumuokoa kaka yako na wewe mwenyewe sema ukweli, niambie kila kitu nitakachokuuliza kabla huyo jamaa hajafika..’nikamwambia.‘Lakini shemeji mimi nitakuambia nini, nimeshakuambia kila kitu ninachokifahamu mimi, mengine sina uafahamu nao, sio kila kitu kaka alikuwa akiniambia, ananiita ananituma na kama hilo tukio, ..mimi nilikuwa sijui kitu..shemeji kiukweli hivyo sio sahihi kabisa..’akasema.‘Sawa ...basi kama umeshaniambia kila kitu ngoja hawo polisi wafike, wao wana utaalmu zaidi yangu mimi, baada ya hapo, najua sitakusumbua tena, unasikia,.tatizo wewe unafikiri mimi ninatania ..’nikasema na mara mlinzi akaja, na kutuambia kuwa kuna jamaa wamefika wanataka kuonana na mimi.‘Ni watu gani?’ nikauliza.‘Wanasema wao ni watu wausalama, wamenionyesha vitambulisho vyao...ni kweli ni watu wa usalama…’akasema huyo mlinzi, na hapo shemeji yangu ambaye alifikiria nafanya utani, akasimama na kushika kichwa, na mimi nikamwambia huyo mlinzi.‘Waambia waje huku bustanini’nikasema huku nikiweka ile mashine yangu vizuri, sikutaka mazungumzo hayo yaishie hewani.‘Shemeji umafanya makosa makubwa sana, kaka akilisikia hili, na hayo matatizo yake sijui kama mtaweza kuishi nyumba moja,...ina maana kweli ni wewe shemeji, sasa unataka kaka afungwe,...aheri hata mimi mnzima nikifungwa haijalishi kitu , lakini mume wako ni mgonjwa..huo ndio ukweli wenyewe, kama ana matatizo…’akawa anasema kama anataka kulia.‘Muda wa utani umekwisha ndugu zanguni, , maana mimi wakati nawaonea huruma nyie mnafanya kweli..hamnionei huruma na mimi, hamfahamu kuwa hata mimi ni binadamu,.., sasa ngoja na mimi nifanye kweli tuone mwisho wake utafikia wapi, nina ushahidi wa kutosha wa kukuweka wewe na kaka yako ndani ..’nikasema.‘Ina maana hata kaka, mumeo humpendi tena,...unataka umweke ndani hujali kuwa anaumwa, siamini hilo shemeji?’ akauliza.‘Wewe ndio utakwenda ndani kuisaidia polisi, ....kaka yako atasubiri hadi hapo atakapopona, mjue mna makosa mengi ,kwanza kwa kuniibia, pili kwa kugushhi mikataba halali, tatu kwa mauaji ya Makabrsha , nne kwa wizi, na jingine hilo la jana la kutaka kuniua,..na mengine mengi...’nikasema na mara hawo jamaa wakafika mmoja akiwa na pingu tayari mkononi kuonyesha yupo kazini.************‘Mungu wangu kumbe ni kweli…’akasema hivyo sasa akionyesha ule uwoga wa dhahiri, sikufahamu kuwa shemeji yangu ni muoga hivyo mpaka nikamuonea huruma, lakini hiyo ndio njia pekee ya kuupata ukweli.‘Wakaribishe huku…’niliona wale wageni wakiaka kuingia ndani, ikabidi niwaite kwa sauti, watuone kuwa tupo huku bustanini..‘Shemeji, mimi sitaki kwenda jela, kwasababu sihusiki kabisa, yote niliyafanya kwasababu ya kaka..kwasababu ya kumsaidia kaka, angalia ali yake ilivyo, ...muhurumie kaka, shemeji...’akasema sasa akininong’oneza, na mimi sikumjali.`Ukitaka usalama wako ongea ukweli, maana mengi yanafahamika, wao watakachofanya ni kupima ukweli wako,...sema yote unayoyafahamu, ukipindisha na kusema uwongo, jela inanukia, jela sio mchezo, isikie hivyo hivyo, mimi nimeionja na niliwekwa sehemu wanayosema ni nzuri, lakini taabu niliyipata siwezi hata kusimulia....’nikasema na wale jamaa wakafikaKwanza walijitambulisha na wakaonyesha vitambulisho vyao. Mimi nikajifanya navikagua, halafu nikasema‘Karibuni sana, niambieni shida yenu, maana mnatutisha, silaha,..pingu, ni mimi mhalfu tena..’nikasema nikijifanya kunyosha mikono kujisalimisha, na wao wakacheka kiogo, na kusema;‘Haaah, hapana sisi tupo kazini, ni kweli..kazi yetu ni hiyo kuwatafuta wahalifu, sasa tutashukuru na sisi tukisikia utambulisho wenu…’akasema mmojawapo, na mimi nikajitambulisha na kumtambulisha shemeji yangu.‘Sawa karibuni..’nikasema‘Kwanza tunachohitajia hapa ni ushirikiano wenu, tupate ukweli kwa hayo tutakayoyauliza, …’akasema‘Sawa ..’nikasema‘Mama mwenye nyumba,..wakati, umeshikiliwa kituo cha polisi, na hata kupelekwa Segerea, ulisema kuwa nyumbani kwako kulitokea upotevu wa vitu, kweli si kweli..?’ akauliza‘Ni kweli…’nikasema‘Je hebu kwa kutukumbusha tu, kulipotea vitu gani…’akasema mwingine.‘Ni kweli, kuna vitu vilipotea, na ni vitu muhimu sana, mojawapo ni mikataba wangu halali, na zaidi hata silaha yangu...’nikaanza kuongea , japokuwa nilishaongea naye, lakini sikutaka shemeji yangu afahamu kuwa nawafahamu hawo watu.‘Una maana ile silaha iliyotambulikana kuwa ndiyo iliyomuua Makabrasha?’ akauliza huyo ofisa usalama.‘Ndio ..’nikasema.‘Kwahiyo kumbe kwa kupitia hivyo vitu tunaweza sasa kumpata muuaji halisi wa Makabrasha, ..’akasema huyo mwingine‘Na huyu umesema ni shemeji yako..?’ akauliza‘Ndio…’nikasema na shemeji yangu alikuwa kanywea kweli kweli haamini kinachotokea.‘Huyu hapa ni shemeji yangu, kiukweli ni mtu niliyeishi naye hapa namtambua vyema, ni mtu mwaminifu sana..’nikasema.‘Hebu tuambie ndugu, ujue tunachokiuliza hapa tumekifanyia kazi, na hatutaki kupoteza muda mwingi hapa…wewe na kaka yako mnaelewanaje..?’ akaulizwa swali.‘Ni..ni..kak yangu, tunaelewana tu…’akasema‘Kwahiyo shughuli zake nyingi unazifahamu…?’ akaulizwa‘Zile anazoniambia, nazifahamu…’akasema‘Sasa kutokana na uchunguzi wetu, wewe ni mtu wa karibu sana na kaka yako, kuna mambo mengi sana mumekuwa mkishirikiana naye…huwezi kutuficha, lakini tunahitajia kauli yako kukupima je unahusika au huhusiki…’akasema mmojawapo‘Kuhusika kwa lipi..?’ akauliza shemeji, naona kaamua kujikakamua.‘Wewe ndiye uliyekuwa ukitumwa na kaka yako, kuchukua vitu mbali mbali, na katika upotevu wa vitu, kama alivyosema shemeji yako, makabati, au nyumba haikuvunjwa, ina maana kuwa mtu aliyefanya hayo yote ni mtu wa nyumbani,…kama kaka yako alikuwa hospitalini mtu mwingine anayeweza kuifanya hiyo kazi ni wewe…’wakasema‘Kazi ipi…?’ akauliza‘Sikiliza sisi hatuja kupoteza muda, tunakuuliza kitu amacho hata wewe unakifahamu, unasikia, tuna namna nyingi za kukufanya useme ukweli wote, lakini kwanza tunahitaji ushirikiano wako,… hapa tunamstahi shemeji yako tu, lakini tukifika huko utaimba yote kama wimbo unaoufahamu sana..’akaambiwa.‘Sasa mnataka niseme nini?’ akauliza huku akijaribu kujitutumua, naona alishaniona sio mtu wake tena, alishaniona mimi ni msaliti wake.‘Kwanza kuna mkataba wa shemeji yako uliibiwa, je upo wapi?’ akaulizwa‘Mimi sijaiba huo mkataba,...muulizeni kaka....’akasema.‘Kwahiyo kaka yako ndiye anafahamu wapi huo mkataba upo, au sio..?’ akauliza‘’Mimi sijui…’akasema‘Ok, shemeji tunaomba tuondoke na huyu mtu, sisi tunakuhakikishia tukifika naye huko atataja kila kitu, sisi tulishamchunguza nyendo zake kwa kirefu, tuna ushahidi wote kuwa anahusika kwa kiasi kikubwa sana,kuna mambo mengi anayafahamu,na ameyafanya sasa hatuna muda wa kupoteza tena ...’akasemaNa mimi nikamuangalia shemeji yangu huyo ambaye alikuwa kama kamwangiwa maji. Alikuwa hataki hata kuniangalia, nahisi chuki dhidi yangu zilikuwa kubwa, lakini sikuwa na njia nyingine.‘Shemeji hiyo ndio nafasi yako ya mwisho, kama unamjali kaka yako sema ukweli, kama unaona kukaa kimiya ndio kutamsaidia kaka yako haya, mimi nitawaruhusu muondoke nao, na unafahamu ni kitu gani kitakukuta huko mbele, unamkumbuka yule rafiki yako aliyejifanya anaweza kuvumilia mateso ya huko, alikuambia nini kilichompata,....kama wewe unajiamini zaidi yake niwaruhusu muondoke ....’nikasema na yeye kwanza akaniangalia kwa jicho lenye chuki, halafu akasema.‘Haya mimi nitawaambia ukweli lakini naombeni mumuache kaka yangu , kaka yangu anaumwa, na mengi aliyafanya bila kujitambua..’akasema‘Hiyo sio kazi yako, sisi tunalifahamu hilo ndio maana tunakuuliza wewe, hatujakwenda kumuliza kaka yako kwasababu anaumwa,...kama tungelikuwa hatulitambui hilo, kaka yako sasa hivi angelikuwa jela. Sasa kwa vile wewe ni mzima huna matatizo unahitajika utuambie ukweli, kwani wote lenu ni moja....’akaambiwa, na akatulia kimiya kwa muda kama anawaza, halafu akasema;‘Haya ulizenu maswali yenu nitawajibu, kwa kile ninachokifahamu...’akasema‘Swali la kwanza, tuambie mkataba wa wanandoa hawa wawili ulioibiwa upo wapi?’ akaulizwa.‘Mimi sijui huo mkataba ulioibiwa ni upi, ...’akasema‘Wewe unafahamu mikataba mingapi?’ akaulizwa‘Mimi nilishaiona mikataba zaidi ya mmoja, sasa sijui upi ni upi?’ akasema.‘Kwa hivi sasa wewe una mikataba mingapi?’ akaulizwa‘Nina huu mmoja alisema nimpelekee huko hospitalini....’akasema‘Ulishawahi kutumwa kuchukua mikataba kama hiyo kabla?’ akaulizwa‘Ndio…’akasema‘Ulipotumwa hukuambiwa ni kitu gani, …?’ akaulizwa‘Niliambiwa nikachukue nyaraka, imeandikwa mkataba…wa hivyo na hivyo, na upo mahali fulani, na ufunguo huu hapa, mimi namtiii kaka yangu, nafanya hivyo…’akasema‘Kwahiyo ulipochukua hiyo mikataba ulimpelekea nani..?’ akaulizwa‘Kaka…’akasema‘Kulikuwa na mkataba uliokuwa nao wewe , ambao haujaonekana mpaka sasa, mkataba huo ndio shemeji yako anaoutafuta, kwa uchunguzi wetu, unao wewe, tunahitajia huo mkataba ambao ni ule wa mwanzao uliotumwa kuuchukua, sisi tunao ushahidi kuwa unao wewe...’akasema huyo ofisa.‘Nimesema nilishamrudishia kaka....’akasema na kukatisha‘Sema ukweli, ilivyoupata huo mkataba, uliingiaje kwenye nyumba ya mtu , na ukifahamu mwenyewe yupo, ....ina maana uliuiba au sio?’ akaulizwa.‘Kaka ndiye alinituma niuchukue...mimi sijaiba, kaka ni mwenye nyumba pia...’akasema.‘Ehe, uliwezaje kufungua makabati, ya shemeji yako?’ akaulizwa.‘Nilipewa ufunguo na kaka, ....’akasema‘Hebu tuonyeshe hizo ufungua’akaambiwa, na akatoa zile ufunguo alizo nao akazionyesha kwa hawo watu, waliziangalia tu, kwa mbali bila kuzigusa, halafu wakauliza‘Kwahiyo hizo ufunguo zote ulizo nazo, alikupa kaka yako, na zinaonekana ni za kuchonga?’ akauliza‘Ndio alinipa kaka, lakini mimi sijui kama ni za kuchonga,...’akasema.‘Alikutuma pia ukachukue na ule mkataba uliokuwa huko ofisini kwa shemeji yako?‘Ukazipeleka wapi hizo mikataba, ulizotumwa‘Nilimpelekea kaka..’akasema‘Kuna mkataba mmoja unakosekana, wewe bado unao,..tunauhitajia huo..usitupoteze muda…’akaambiwa na hapo akasita kidogo‘Kaka yako ndiye alikutuma hiyo mikataba sio..wa nyumbani, na wa ofisini, au sio../’ akaulizwa‘Ndio…’akasema‘Kwa ujumla nakala za mikataba yote uliichukua wewe, baada ya kutumwa na kaka yako…kweli si kweli…?’ akaulizwa‘Ndio alinituma yeye, kwanza huo wa nyumbani alikuwa nao yeye mwenyewe, alikuwa na nakala mbili, sikujua kuwa mmoja ni wa shemeji, baadaye, akaniambia nizipeleke kwa Makabrasha...’akatulia.‘Nilipofika kwa Makabrasha akaniambia nihakikishe kuwa hakuna nakala inayobakia, mimi nilikuwa nimeshaficha nakala moja,...bila kaka kujua,..’akasema‘Kwanini ulifanya hivyo?’ akaulizwa.‘Nilitaka nitoe nakala nyingine, kwani nilihisi baadaye inaweza ikahitajika, kaka huwa anachanganyikiwa, baadae anaweza kuhitaji nakala au kumbukumbu, huwa naan ahivyo kwa akiba…ila kiukweli mimi sikuwa nafahamu malengo yao ni nini....’akasemaUlijua lini malengo yao....?’ akaulizwa‘Kuna siku waliniita kwenye kikao wakaniambia kwanini wameamua kuziharibu hizo nakala zote...’akasema‘Walikuambiaje , lengo lao ninini?’ akaulizwa na hapo akaa kaa kimia, na hapo yule ofisa akauliza swali jingine.‘Na kule ofisini uliwezaje kuingia , wakati muda wote kuna walinzi?’ akaulizwa‘Niliingia muda wa kawaida tu, yule mhudumu alikuwa hayupo, na mimi niliwaonyesha kibali kuwa nimetumwa na shemeji, nikaweza kuingia kwasababu nilikuwa na ufungua, alionipa kaka....’akasema.‘Kibali gani hicho, ina maana ulikwenda kwa shemeji yako ukamuomba hicho kibali?’ akulizwa‘Aliwahi kunipa kibalia kabla,,...nikawa naendelea kukitumia..kuna siku nafika kwa ajili ya matengenezo ya ofisi yao’akasema.Hicho kibali hakina tarehe?’ akaulizwa, na kukaa kimiya, na yule ofisa akauliza swali jingine.‘Ina maana uligushi tarehe....?’akasema huyo mpelelezi‘Kilikuwa hakijaandikwa tarehe....’akasema‘Kwahiyo kumbe kaka yako alikuwa ana ufunguo zote za ofisini na za makabati ya mke wake?’‘Mimi sijui, hilo swali ingelifaa mumuulizeni yeye mwenye kaka, yeye alinipa ufunguo akanituma niende ofisini akanielekeza wapi pa kuipata hiyo nakala ya mkataba, mimi nikafanya kama alivyoniagiza....’akasema.‘Wewe kwanini hukumwambia shemeji yako ?’ akauliza‘Kwanini nimuambie, kama kaka angetaka nifanye hivyo angeniambia nimwambie, kaka kafanya hivyo kama mume wake, na mume wake ana haki kwenye kampuni za mkewe, kuna ubaya gani hapo eeh , ‘akasema na kuniangalia mimi , na mimi nikawa nimemkazia macho, akaangalia pembeni.‘Ohooo, kwa vile yeye ni mwanaume, sio…safi kabisa, mlishalipana hilo, ..’akasema mmojawapo.‘Kaka aliniambi ahivyo…’akasema‘Kuwa yeye ana mamlaka popote, hata kama kampuni sio yake,wewe hujui kuwa kampuni hiyo uliyokwenda kuchukua huo mkataba ni ya shemeji yako sio ya kaka yako ...huoni kuwa ni makosa?’akaulizwa‘Hayo muulizeni kaka yeye mwenyewe , mimi nimejitolea kuwaambia yale ambayo hata kaka hakutaka niwaambie, ...najua nimefanya makosa sana kuwaambia, kaka hatanisamehe kwa haya, lakini sina jinsi...’akasema kwa uchungu.‘Swali jingine, je kaka yako ndiye aliyekutuma kuchukua bastola kwenye kabati la shemeji yako?’ akaulizwa na hapo akatulia kidogo, halafu akasema.‘Lakini kaka sio yeye aliyemuua Makabrasha, ...’akasema‘Una uhakika gani na hilo?’ akaulizwa na kukaa kimiya, na huyo ofisa hakutaka kumshinikiza kwa hilo, kwa vile wao wanafaahmu zaidi, wakauliza swali jingine‘Kama sio kaka yako basi ni wewe uliyemuua Makabrasha?’ akaulizwa‘Sio mimi wala sio kaka..’akasema‘Unaposema sio kaka yako au wewe, ina maana unamfahamu muuaji, ni nani aliyefanya hivyo?’ akaulizwa‘Kwakweli mimi sijui,....’akajibu na kutulia na yule ofisa akatabasamu na kutikisa kichwa, halafu akauliza swali jingine‘Tuambie ilikuwaje siku hiyo ambayo Makabrasha aliuwawa,, maana usipotuambia ukweli , ujue hapo wewe utakamatwa kama muuaji, wewe na kaka yako’akaambiwa.‘Mimi sio muuaji, ..sijamuua Makabrasha, japokuwa ni kweli mimi ndiye niliyekwenda kuichukua hiyo bastola kwenye kabati la shemeji, ...nilifanya hivyo nikiogopa kuwa shemeji kwa jinsi alivyokuwa na hasira , angeliweza kuitumia kumuua kaka, nikaona bora niichukue hiyo silaha nikaifiche mbali kabisa na wao’akasema‘Kwahiyo hukutumwa na kaka yako kuichukua hiyo bastola?’ akaulizwa‘Hapana kaka hajanituma kuchukua hiyo bastola, niliichukua mwenyewe baada ya kuiona hapo, siku aliponituma kurudisha hiyo mikataba mipya...wakati nafungua kabati la shemeji nikaiona hiyo silaha, na najuta kwanini niilichukua hiyo silaha’akasema‘Ulipoichukua hiyo silaha uliipeleka wapi?’ akaulizwa‘Niliificha ofisini kwetu, na siku moja, nikaichukua kwenda nayo porini kuitupa...’akasema na huyo ofisa akatabasamu, na kumwangalia mwenzake, ambaye alitikisa kichwa kama kukubali kitu.‘Kwanini ufanye hivyo?’ akaulizwa‘Kwa wazo hilo hilo kuwa ikiwemo mle ndani inaweza kuleta majanga, na bora niitupe mbalii kabisa,..’akasema‘Ikawaje sasa, ...?’ akaulizwa‘Nikiwa ndani ya gari, nikiwa naelekea huko porini , nilifika mahali gari likawa halina mafuta, ....kituo cha mafuta kilikuwa karibu tu, lakini gari lilikuwa haliwezi kufika hapo, kwahiyo nikaona nichukue galoni niende kununua...’akasema .‘Unaweza kutuambia ni kituo gani hicho, na una risiti na mafuta uliyonunua siku hiyo, kama ushahidi?’ akaulizwa‘Mh,hata sikumbuki, na hata jina la kituo, sikumbuki, na nakumbuka sikuchukua risiti...’akasema‘Ehe, ikawaje?’ akaulizwa‘Niliporudi kwenye gari langu sikuuona ule mkoba wangu uliokuwa na silaha, ulikuwa haupo,....inaonyesha kuwa kuna watu walikuja kwa haraka wakafungua kiyoo, wakauchukua, sikuwa makini kufunga viyoo vya gari, ningelijua ningelifunga hivyo akasema‘Endelea…’akaambiwa‘Nahisi kuna mtu alikwua akanifuatilia, kwasababu ni nani angelijua kuwa ni na vitu kama hivyo,...nilijaribu kuangalia huku na kule lakini sikuona dalili ya mtu, nikajua nimeibiwa, na silaha ya watu imeshachukuliwa, sikujua nifanye nini, nikaamua kukaa kimiya, ..hadi hapo niliposikia kuwa hiyo silaha ndiyo iliyofanyia hayo mauaji,..huo ndio ukweli wenyewe, ..’akasema‘Hiyo hadithi yako hukuipanga vyema, inabidi ukaipange vyema, hiyo hadithi yako haina vina wala mizani, itakutia matatani, usiposema ukweli,..’akaambiwa.‘Ndio ukweli wenyewe huo....’akasema‘Sema ukwei ni nani uliyempa hiyo silaha, ujue ulichukua silaha ya watu inayomilikiwa kisheria, na silaha hiyo ikatumiwa kufanyia mauaji, na muuaji mpaka sasa hajapatikana, kwanini wewe usikamatwe kwa kosa hilo, tuambie ukweli ulivyo..’akaambiwa.‘Ukweli ndio huo, sina ukweli mwingine, ...’akasema‘Inavyoonekana ni kuwa kaka yako alikutuma hiyo silaha, ili ukampe mtu fulani, ambaye ndiye aliyemuua, Makabrasha, sisi tunafahmu kuwa ni wewe uliifanya hiyo kazi, ulitakiwa uifanye wakati kaka yako anaongea na marehemu....’akasema‘Hapana,kaka hajawahi kunituma hiyo silaha, kaka kipindi hicho anaumwa, hajui kabisa kuhusu hiyo silaha, ....na mimi sijaua mtu, na siwezi kufanya hivyo..kwanini tumuue mtu kama yule ambaye anatusaidia sisi, hilo hamlioni jamani, Makabrasha alikuwa ni mtu wetu wa karibu,....’akasema akiwa na wasiwasi.‘Anaweza akawa mtu wenu wa karibu lakini mkaona hawafai tena, akifa yeye, hisa zake mtazichukua nyie, kwasababu akiendelea kuwepo, hisa zote mtazipoteza kwa vile alikuwa anawadai pesa nyingi sana, na madeni yake alipanga yalipwe kwa hizo hisa,..hiyo ndio mipango yenu,...’akasema huyo mtu wa usalama.‘Hapana hatujamuua Makabrasha, sijui ni nani aliyefanya hivyo...tunasikitika sana kwa kifo chake...’akasema‘Ni nani aliyemchukua kaka yako kutoka hospitalini hadi kwa Makabrasha?’ akaulizwa‘Ni mimi, alinipigia simu kuwa niende kumchukua,...kwani ana mazungumzo muhimu na marehemu’akasema‘Kwahiyo alikutuma pia ukachukue hiyo silaha, umpe mtu mwingine kama unakataa kuwa sio wewe na huyo mtu mwingine ni nani,..usipomtaka huyo mtu ni wewe, nakuuliza haya ukijua sisi tunafahamu kila kitu, lengo ni kukupima yawezekana haya uliyafanya kwa kumsaidia kaka yako ...’akasema kabla hajamaliza shemeji akamkatisha na kusema;‘Mbona mnanitungia uwongo, sijafanya hivyo, hata silaha yenyewe sijawahi kuitumia,...’akasema.‘Unaweza usiweze kuitumia ukabahatisha,kwani ina ugumu gani , yoyote anaweza kutumia, kama anafahamu jinsi ya kufyatua risasi, hata hivyo hatujasema wewe ndiye uliyemuua, kuna mtu uliye mpa hiyo silaha, ndiye aliyefanya hayo mauaji, na unamficha, na kwahiyo wewe utashitakiwa kama ndiye uliyefanya hayo mauaji ...’ akaambiwa.‘Mimi nimeshawaambia huko ukweli, na kwanini tumuue Makabrasha wakati ni mtu anayetusaidia?’ akauliza.‘Hilo swali unatakiwa ujibu wewe,...’akaambiwa.‘Mimi nimeshawaambia ukweli,....’akasema.‘Hilo litajulikana baadaye, kama unasema ukweli, sisi tumeshaujua ukweli, nia yetu hapa ni kukupima, na ukweli ndio utakao-kuokoa wewe...’akasema.‘Nimeshawaambia ilivyokuwa,...mnataka niseme ukweli gani zaidi ya huo’akasema.‘Hujatuambia ni nani uliyempa hiyo silaha, ...hilo unatuficha, ili hali sisi tumeshamfahamu, ’akaambiwa.‘Mimi nimeshawaambia hiyo silaha sijampa mtu...’akasema.‘Ehe, ulipomchukua kaka yako wewe ulikwenda wapi..hebu elezea hapo…maana ni lazima umfikishe pale, wewe ulipomfikisha ulikuwa wapi ukimsubiria kaka yako....?’ akaulizwa.‘Mimi nilimsubiria nje, barabarani..’akasema.‘Ni nani aliyekuona ukimsubiria,maana hapo usipokuwa na ushahidi wa kutosha, utaingia matatani...’nikamwambia.‘Yule mlinzi wa nje wa hiyo hoteli iliyopo karibu na lile jengo, nilicheza naye drafti, hadi kaka alipokuja, na tukaondoka naye...’akasema. Na huyo jamaa akaandika jambo kwenye karatasi yake, na kusema.‘Hilo nilishalifuatilia, ni kweli...ulionekana ukicheza drafti na huyo mtu, lakini kabla ya hapo...mhh, sawa hilo tuliache hivyo kwanza au sio mwenzangu..?’ akasema akiangaliana na mwenzake..‘Yap, weka akiba..’akasema mwenzake.‘Lakini bado hatujamalizana na kipengele hicho, kuna ukweli mwingi unatuficha hapo, na hatujui kwanini unafanya hivyo, tutakuja kuuliza sana sehemu hiyo muda ukifika....’akasema na kukatisha.`Swali la tatu, hiyo nakala ya mkataba wa zamani uliokuwa nao wewe upo wapi?’akaulizwa‘Niliurudisha kwenye kabati la kaka.....’akasema‘Lini?’ akaulizwa.‘Leo asubuhi...wakati shemeji walipompeleka kaka, mimi nilibakai nyuma, nikaurudisha ..kimia kimia, niliuweka pale ulipokuwa,...’akasema.‘Kwanini ulifanya hivyo?’ akaulizwa‘Niliogopa kuwa kaka akifahamu nina nakala nyingine ya huo mkataba atagomba, kwani wao walitaka nakala zote ziharibiwe, ..lakini pia nilisikia kaka akihangaika kuutafuta huo mkataba wa zamani,na pia nimesikia shemeji akiuulizia huo mkataba, nikaona jambo jema kuondoa hili tatizo nikuuweka huo mkataba wa zamani, ili kaka akija akiuona, aurudishe kwa shemeji mambo yaishe...’akasema‘Hapo pia kuna kitu unakificha, kama wewe uliona kuwa mkataba huo ni tishio kwenu, hasa kwa kaka yako, na mkakubaliana kuwa mikataba yote iharibiwe, ibakie hiyo mipya, ni kwanini ukaamua kuurudisha hapo tena,....kuna nini kilikusukuma kufanya hivyo, au ulitaka kuuficha hapo kwa muda ili baadaye uje uuchukue, maana ulishajua kuwa kule kwako hakuna usalama tena,..’kaulizwa‘Mimi niliamua kuurudisha kwa nia njema kabisa…,kama nilivyowaambia...’akasema‘Kwahiyo huo mkataba kwa sasa upo wapi?’ akaulizwa‘Nimefika leo kuuangalia, nimekuta kabati halifunguki, kwahiyo sijui kama upo hapo hapo, ila nina uhakika niliuweka hapo hapo....’akasema‘Swali kubwa hapo ni kwanini uliurudisha?’ akaulizwa‘Nilitaka kaka aje auchukue mwenyewe,...., sikutaka tena kuendelea kujihusisha na mambo ya familia, na niliona nafanya makosa, na nilitaka kaka na shemeji waje waelewane....’akasema.‘Waelewane, kwani walikuwa hawaelewani…kwasabababu ya mkataba au kwasababu ya matendo ya kaka yako…?’ akaulizwa na kukaa kimia.‘Ina maana huo mkataba hadi hivi sasa upo kwenye hilo kabati...?’ mimi nikamuliza na akaniangalia akionyesha uso wa kunikasirikia , akasema;‘Ndio upo humo kwenye kabati..., lakini kabati halifunguki kabisa, kama vile kitasa kimebadilishwa, kama likifunguka mtauona, upo .... maana mimi ndiye niliyeuweka leo asubuhi,...na kuna kitu changu kingine, sijui kama kipo humo au vipi....’akasema na mimi kwa haraka nikainuka na kuomba niende kwenda kuuangalia kama kweli ndio huo mkataba wetu wa zamani.‘Nenda kahakikishe, halafu uje, tuendelee, maana huyu mtu asipotuambai ukweli, leo tunakwenda naye..’aaksema huyo ofisa.‘Mimi nimeshawaambia ukweli, naomba niende nikamuone kaka, yeye ndiye aliyenituma… na jinsi ninavyochelewa nampa mashaka, na wasiwasi, na hivyo vitu havitakiwi kwa afya yake...’akasema‘Yeye ndiye aliyekutuma nini, huo mkataba, au sio…kuna mengine kakutuma hujatuambia…au sio?’ akaulizwa‘Ndio alinituma huo mkataba na vitu vingine,....’akasema‘Shemeji wewe nenda kahakikishe hilo,..huyu haendi mahali, hadi hapo kitakapoeleweka, kuwa tunakwenda naye kituoni, au anafunguka ukweli wake wote, na ukweli wake ndio utakaomfanya sisi tumwamini, na akifanya hivyo basi sisi tutakuwa upande wake, kumlinda..’akasema huyo ofisa.Mimi nikawa nimeshaanza kutembea kuelekea ndani , moyoni nikiwa na hamasa kuupata huo mkataba wa zamani, …mkataba utakaoleta haki ndani ya familia yangu,…na huku nyuma nikasikia shemeji akiniambia;‘Shemeji ...ukiona kitu changu ndani ya huo mkatana nakuomba tafadhali, unipatie, nahisi nimekiacha ndani ya huo mkataba...’akasema na mimi sikumjali nikaharakisha kwenda kufungua hilo kabati na wale watu wa usalama wakiendelea kumuhoji, hawakujua kuwa nimeacha mshine ya kurekodia matukio, ikiwa inafanya kazi....NB Ni hayo kwa leo, natumai leo mumefurahia sehemu hii kama mumefurahia,naomba comments nyingi sana..WAZO LA LEO: Katika maisha yako jifunze kuwa mkweli, kusema ukweli na kutenda yaliyo haki, hiyo ndio njia ya kuiweka nafsi yako huru, kujiamini na na kutokuwa na wasiwasi…na matokea yake huwa ni chanya,…na hutajuta katika maisha yako yote, kinyume chake ni mashaka, na mwisho wake ni kuzalilika tu. Nilifika chumbani kwangu na kwa haraka nikaingia maktaba nikiwa na shauku ya kuuona huo mkataba, shauku niliyokuwa nayo ilikuwa haimithiliki, utafikiri nilikuwa nakwenda kugundua alimasi iliyofichwa, kwangu mimi huo mkataba ulikuwa na thamani kubwa, sio kwa ajili ya kulinda masilahi yangu tu, lakini pia kulinda utu wangu, kilichokuwemo humo, kilikuwa ni kwa ajli ya utu wangu, na kama utapotea basi mimi nitaonekana sina maana,, nitadhalilika,....Nikawa natembea kwa haraka haraka,nikijua kuwa sasa ukweli utadhiri, na wale wote waliotaka kunidhulumu, na kuishia maisha ya hadaa nyuma ya mgongo wangu wataumbuka, ...na hilo nilishaliahidi kwa wazazi wangu kuwa nitahakikisha, nalifanyia kazi bila ya msaada wao, na wao waliniona kama mfa maji,....lakini sasa ukweli watauona, na kile nilichokuwa nimekiahidi mbele yao watakiona kwa macho yao. Sikutaka kubweteka, sikutaka kudeka,kwao kuwa kwa vile mimi ni mtoto wa kike, sitaweza kuishi bila ya msaada wao.Nilitaka kuionyesha jamii, kuwa hata sisi wanawake tunaweza, tunaweza kutunza siri, tunaweza kutunaza dhamana, ...kwangu mimi kipao cha ndoa, nilikiona ni muhimu sana, ndio maana sikutaka kughilibiwa, kama nilijitahidi kufanya hivyo, japokuwa kulikuwa na mapungufu, kwanini mwenzangu afikie hatua hiyo kubwa ya kunisaliti, hapana, kama kafanya hivyo, ni lazima sheria ichukue mkondo wake, lakini sheria ipi, maana huo mkataba ndio ulikuwa ni sheria yangu..sasa umepotea‘Kama nitaupata huo mkataba, nitawaonyesha watu kuwa hili linawezekana, kama kutakuwa na mkataba wa ndoa na mkaufuatilia, mwenye makosa akahukumiwa kutokana na amkubaliano yenu, basi kila mwanandoa ataogopa kufanya maasi, ....’nikasema huku niendelea mbele kuelekea sehemu iliyopo sheria yangu, mkataba wangu, utakaonilinda kwa hilo...‘Na wale wote walionisaliti, itabidi wawajibike, sitajali kama ni rafiki yangu, au ndugu yangu...’nikasema huku nikifungua mlango wa maktaba, ambao sasa nilikuwa na ufungua mwingine mpya,japokuwa nilipotoka sikuwa nimefunga na ufunguo, ila nikitoka nje , nitakuwa nafunga sehemu zote nyeti...‘Nikimalizana na huyu shemeji yangu, nitaanza kupambana na rafiki yangu, sitajali urafiki tena, mapaka kieleweke, na mwishi namalizia na mume wangu,...nina uhakika kuwa mume wangu kasaliti ndoa yangu, na ninachotakiwa kupata ni ushahidi, na ....na mkataab wetu utahukumu....’nikasema.Nikalifungua kabati la mume wangu, kwa ufungua ambao unafungua kwa namba maalumu, ...hata uchonge ufungua, usingeliweza kufungua, nilifanya hivyo, ili kila mmoja awe na namba zake za siri, kwahiyo mume wangu akija nitampa ufunguo wake, na namba zake za siri.Nikafungia hilo kabati lake, kwa ndani kuna sehemu tatu, nikavuta kidroo cha sehemu ya kwanza, niliona makaratasi ya malipo, stakabadhi za malipo na vyeti vya biashara, hakuna huo mkataba...Nikafungua sehemu ya pili, hakuna kitu, hapo hasira zikaanza kunipanda ina maana huyu kijana kanidanganya, nikasema na kufungua sehemu ya tatu, hakuna kitu...nguvu zote zikaisha, na sikujau nifanye nini tena, na wakati nimekata tamaa, kwa pembeni nikaona bahasha kubwa,iliwekwa kwa kusimama, isngelikuwa rahisi kuiona, nikaitoa ile bahasha, ilikuwa nzito, nikaitoa, na kuigeza juu chini kukitoa kilichopo, kikatoka kitabu....Kumbe ilikuwa sio kitabu , ulikuwa mkataba, na mwanzoni nilifikiria ni ule mkataba wa kawaida, lakini pale nilipoona alama yangu nikagundua, ni ule ule mkataba niliokuwa nautafuta, nikauchukua na kuanza kuufungua, kuhakikisha kuwa ndio wenyewe, na nilipojirizisha nikafunga yale makabati na kuanza kutoka. Wakati nainua mguu, nikakanyaga kitu, nikainama kukiangalia, kilikuwa kidude kidogo,cha kuhifadhia kumbukumbu, unaweza kukiweka kwenye simu au kwenye komputa, nikakiokota, nahisi kilidondoka kutoka kwenye hiyo bahasha, waakti nilipoiinamisha juu chini kuutoa huo mkataba,na hapo nikakumbuka kauli ya shemeji yangu;‘Shemeji kama kuna kitu changu naomba uniletee, ...’`Huenda hiki kitu ndicho anachokitafuta....’nikasema huku nikikiangalia kwa makini, moyoni nikaingiwa na shauku ya kujua kuna nini humo ndani, lakini kwa namna nyingine niliona nafanya makosa, nitakuwa nachunguza vitu vya watu, na mimi sitaki tabia hiyio, hata hivyo kwa hali ilivyo kwasasa hamasa za kufahamu ni kitu gani kimo humo ndani ikanijia, nikatoka hadi chumbani hadi kwenye laptop yangu, nikakichomeka, na maandishi yakatokea;‘Diary yangu, kumbukumbu za kila siku.....’‘Oh, kumbe ni kumbukumbu zake, hakuna shida..na wakati nataak kukichomoa, nikaona maelezo yaliyonivutia, nikayasoma kwa haraka..‘Kumbe...’nikasema‘Sasa nimekupata, kama atakuwa anaweka kila kumbukumbu za kila siku, kumbe nitaweza mambo muhimu ninayoyatafuta, amekwisha, hana ujanaj tena, ...’nikasema na kwa haraka nikaweka sehemu ya kunakili hizo kumbukumbu kwenye komputa yangu, ilichukua muda kidogo, na kumbukumbu zote zikanakiliwa kwenye komputa yangu, halafu nikakitoa kile kitufe, na kukiweka kwenye ile bahasha nikatoka nacho hadi kule bustanini.‘Shemeji kwenye hiyo bahasha uliona kitu changu?’ akaniuliza‘Kitu gani?’ nikamuuliza kama vile sijui,‘Naiomba hiyo bahasha, umeshautoa huo mkataba unaoutaka, natumai sasa tumemalizana, uliouona eeh....?’ akauliza huku akichungulia ile bahasha kwa ndani, na mara akakitoa kile kitufe na kwa haraka akakiweka mfukoni‘Ni kitu gani hicho?’ akaulizwa na wale maofisa wa upelelezi‘Ni kifaa cha kazi zangu za ofisini, ni muhimu sana, ningelipoteza kazi za watu...’akasemaMimi nilikaa kimiya sikusema kitu na hapo yule ofisa akaniuliza kama nimeuona huo mkataba na kama ndio wenyewe niliokuwa nautafuta, nikamwambia ndio nimeuona ndio wenyewe.‘Shemeji kwa hali ilivyo huyu mtu inabidi tuondoke naye...’akasema huyo jamaa wa usalama‘Hapana, mimi nimewaambia kila kitu, kwanini sasa mnanigeuka, ...tulikubaliana nini?’ akalalamika huyo shemeji yangu na mimi hapo nikamuonea huruma na kusema;‘Kwa vile kakubali kushirikiana na sisi mimi sioni kwanini muondoke naye, ...mimi nitamdhamini, siku mukimuhitaji atakuja, mnaonaje ombi langu hilo?’ nikawauliza‘Kuna mambo mengi bado anayaficha, hajakuwa mkweli, ndio maana tunataka tuondoke naye..tunauhakika akifika huko atasema kila kitu.’akasema‘Nimewajibu kila kitu, sijaficha jambo lolote kwenu…kuweni wakweli basi, mlisema nikiwaambi akila kitu nitakuwa salama..na hebu niambieni ni jambo gani nimelificha?’ akauliza shemeji yangu akiwa kakasirika.‘Tunashindwa kurudia swali mara nyingi,...wewe usituone kuwa sisi ni watoto wadogo, hapa tulikuwa tunakuuliza maswali ya kukupima tu, mengi tunayafahamu,..’akasema mtu wa usalama na mwingine akaongezea‘Hebu kwa mfano tu, hilo la kusema ulikwenda kutupa hiyo silaha porini halafu ikaibiwa hiyo sio kweli,ukweli ni kwamba kuna mtu ulimpa hiyo silaha, hilo umetuficha,hukusema ukweli, kuna mengi tunayahitajia kutoka kwako,na usiposema huo ukweli, utaozea jela...’akasema huyo mtu wa usalama, na kumfanya shemeji yangu atulie kimia.‘Mimi naomba nimdhamini, kwa vile bado mnafuatilia mambo mengine, huyu niachieni mimi, nawashukuru sana, kwa msaada wenu, mimi bado nina maongezi na shemeji yangu, mkiwa tayari kumuhoji, mtaniambia, ila kwa leo naombeni tuishie hapa , kwani kile kitu muhimu nilichokuwa nikikihitajia nimekipata...kama kuna zaidi tutafahamishana...’nikasema‘Huyu ni mhalifu, ..huo alio-ufanya ni wizi, japokuwa anamtupia lawama kaka yake , kamaa anaamini kuwa kaka yake ni mgonjwa , kachanganyikiwa basi singelifany hayo, …unaona eeh, angekuja kwako akuambie ili muone jinsi gani ya kumsaidia jamaa yenu…lakini ulifanya hivyo..?’ akaulizwa‘Ha-a-pana, lakini sasa…’akasita kuongea‘Lakini sasa nini…eeh tuambie awali tulikuuliza ukawa unsita kusema ukweli pia, hii inamaanisha ulidhamiria kuyafanya hayo uliyoyafanya, hii sio mara ya kwanza kuhojiwa kweli si kweli, ukaficha huo ukweli, hata kama waliokuhoji ni watu wengine, lakini ni watu wa usalama, umeacha mpaka sisi tukahangaika kuupata ukweli,…huyu ni mhalifu …’akasema.‘Yeye hajui kuwa kila siku anafuatailiwa, hajui kuwa bado uchunguzi unaendelea,na hatua iliyofikia, ni ya kumalizia, tu, ...wote hawa watafikishwa mahakamni kujibu makosa waliyoyafanya, ikiwemo hilo la kumuua Makabrasha....hata kama sio yeye aliyefanya hivyo, lakini alishiriki kwa namna moja au nyingine...’akasema huyo mtu wa usalama.‘Lakini mimi sijau..hata kaka hajafanya hilo…’akajitetea, na mimi nikaona niingilie kati ili kuokoa muda.‘Sawa kama mumefikia huko, siwezi kuwapinga, ila kwa vile bado hamjakamilisha uchunguzi wenu, basi mimi naomba huyu mtu msimchukue kwanza, mimi namdhamini kwa kauli tu, namfahamu sana shemeji yangu huyu, siku mukimuhitaji, nitahakikisha anafika huko kituoni,...’nikasema na wale watu wa usalama wakakubaliana na mimi wakaondoka, na mimi nikabakia na shemeji yangu.********‘Shemeji sasa umefanya nini?’ akaanza yeye kunilaumu.‘Ndivyo ulivyotaka wewe iwe hivyo au sio…’nikasema‘Hapana shemeji umefanya kosa kubwa sana…’akasema‘Hapo ni mwanzo tu shemeji, kuna mambo mengi bado nayahitaji kutoka kwako, ndio maana nikawazuia wasikuchukue, na usiponijibu leo, mimi nitawaambia hao watu waje wakuchukue,…sasa sikiliza haya mambo nataka tuyaongee mimi na wewe kwanza, ukiniambia ukweli, mimi nitajua jinsi gani ya kukusaidia ,...’nikasema‘Mambo gani tena hayo shemeji hapa nilipo nimechanganyikiwa nafahamu kaka atakuwa ananisubiri na nimechelewa kwenda kumuona, na akisikia kuwa nime..yaongea haya sizani kama atanisamehe…unataka nini tena shemeji?’ akauliza kwa wasiwasi. Na mara simu yake ikaitaAliangalia mpigaji halafu akasema;‘Kaka huyu …’akasema akisita kupokea simu‘Pokea, mwambie upo na mimi, unaogopa nini…’nikasemaAkaipokea , halafu akageuka kunipa mgongo, na kusogea mbali na mimi, akawa anaongea na kaka yake.‘Nimezipata…nini, hapana, kabato halifunguki,…ndio, hapana sijui…ndio, kuna tatizo kidogo, nitaku-kuambia, …nakuja kaka, kwanini unasema hivyo, kwa ni nani…?’ akauliza na akawa anasikiliza kwa muda‘Kama mimi nakuomba kama kuna jambo umelipanga, bora uachane nalo tu,..angalia afya yako kwanza, ..hawezi kufanya lolote kwa sasa, huyo ni muongo, na huenda kwa hivi sasa yupo mikononi mwa polisi, ndio maana na kuambia..sikiliza kwanza kaka…’akasema na kutulia akawa anasikiliza‘Kaka, sikiliza nikuambie,…acha ubishi kaka…’akawa anaongea na kukatizwa katizwa na kaka yake mwishowe wakamalizana naye, halafu akanigeukia.‘Kaka kachanganyikiwa kweli, anasema huyo mtu anayemdai….yupo mbioni kuonana na polis,..kwahiyo ..hata sijui, ana kitu gani…’akasema‘Mwongo huyo, huyo ni tapeli, hata kama ana ushahidi, kwanini asiende kuwaona polisi…anajua na yeye ana makosa, hapo anatafuta pesa za kupata wakili, hakuna lolote anatafuta hapo..’nikasema‘Sasa shemeji niruhusu niondoke…’akasema‘Kwanza tumalizane, …nashukuru nimeupata huo mkataba, lakini kuna jambo nataka kulifahamu ili mwisho wa siku nimalizane na nyie,…je ni nani huyo mwanamke aliyezaa na kaka yako..?’ nikamuuliza‘Shemeji mbona huyo mtu mimi simjui, na kaka hajazaa na mwanamke yoyote, mimi nina imani hizo ni ndoto zake tu,...’akasema‘Hajazaa na mtu, wakati hadi kwenye mikataba huo wa kugushi, kuna kipengele cha kumpa haki huyo mtoto, na huo mkataba uliandikwa hata kabla kaka yako hajapatwa na ajali…kwahiyo hapo hakuna kuchanganyikwa…’nikasema‘Kiukweli mimi simjui..ila hilo la kuombea kupata mtoto wa kiume, nimemsikia sana akiliongelea, kwahiyo kwa matarajio hayo, sioni kwanini asiweke kipengele kama hicho…’akasema‘Una uhakika na hilo jibu lako, maana nikigundua kuwa unanificha, basi sitakuamini tena, unanifahamu nilivyo, ninapokuahidi kitu, siachi kutekeleza, na ukinidanganya, siwezi kukuamini tena, na lile nililoahidi dhidi yako huwa sirudi nyuma.....’nikasema na yeye akaa kimiya, nikasema‘Sawa kama hutaki kuniambai huo ukweli, mimi bado nalifuatilia hilo, kama nitagundua kuwa unafahamu au unahusika kwa hilo, kwa namna yoyote ile, basi, mimi na wewe hatutakuwa marafiki tena…’nikasema‘Shemeji lakini nimekuambia kila kitu…’akalalamika‘Wewe umekuwa kwangu, nimekusaidia kwa nguvu zangu zote kama mdogo wangu, kwanini hufanyi jambo angalau na mimi nikakuamini...’nikasema‘Shemeji kwanini unataka kuniweka mimi kama rehani, mume wako yupo, ndiye muhusika mkuu, kwanini usimsubiri apone uje umuulize yeye hayo maswali, ukiniuliza mimi hayo maswali inakuwa kama mtego kwangu, nichagua ama wewe au kaka…kama nilivyowaambia watu wa usalama hapa..mimi nafanya mengi kwa shinikizo, najikuta sina jinsi,...’akasema na mimi nikawa nimemuangalia tu, halafu akasema;‘Hivi shemeji, hebu niambie haya niliyoyaongea leo hapa kwa hawa watu wa usalama, je akija kuyagundua haya niliyoyasema hapa itakuwaje, ...mimi najuta sana, nimeshindwa ...oh, nimemsaliti kaka yangu, kaka ambaye ananipenda sana, na ambaye kajitolea kwa hali na mali kwa ajili yangu...’akasema‘Ina maana kaka yako ndiye aliyejitolea kwa hali na mali juu yako, unakumbuka mwanzoni kaka yako alikuwa akisemaje juu yako, alikuwa hakuamini, alishakuweka kwenye kundi la wavuta unga,mimi nikajitolea na kumhakikishia kuwa nitakusaidia hadi utabadilika, je ni nani aliyejitolea kwa hali na mali kati ya kaka yako na mimi..umesahau hayo eeh, kwasababu ya tamaa, kuwa mtamiliki kila kitu eeh?’ nikamuuliza‘Shemeji nakushukuru sana..kiukweli hata kaka ninamuambia hilo, kuwa asije akafanya makosa mkaachana…wewe ni mtu muhimu sana kwangu, wewe na kaka mumejitolea kila mtu kwa nafasi yake, hilo nashukuru sana, ndio maana kuna mambo ambayo nimekuwa siyafurahiswi kuyafanya…’akatulia‘Kama yapi…?’ nikamuuliza‘Kama haya niliyowaeleza watu wa usalama…’akasema‘Na haya ninayokuuliza je, je ulikuwa unafurahia mimi nikisalitiwa, kaka yako akifanya mambo kinyume na matakwa ya ndoa, na watu ambao wanataka kumrubuni tu …je huko ndio kunishukuru…’nikasema‘Shemeji hayo mimi sijayaona kwa macho yangu…na nisingelikbali hayo yafanyike nikiwa naona,..na ndio maana nikajitolea na mimi kule kunapowezekana, ..wewe hujui tu ....lakini siwezi kusema zaidi, ninachoweza kusema kwa sasa ni ahsante kwa wema wako huo..’akasema karibu kunipigia magoti.‘Nitakuamini pale tu utakaponiambia ukweli…’nikasema‘Shemeji, nimakuambia kila kitu, na yale ambayo kaka hakutaka nikuambie, hebu jaribu kukaa upande wangu unionee huruma na mimi…hata kama unaona kwasasa namukuwa sio mtiifu kwako, lakini sio kwa nia mbaya, ni pale inapofikia hatua ya kuchagua kaka au wewe,hapo mimi mnaniweka kwenye njia panda....’akasema‘Sasa sikiliza,shemeji yangu, wewe ni mtoto wa juzi, ulipolala ndipo nilipokuwa nimelala siku nyingi, nikaamuka na kufanya kazi, maendeleo yote hayo unayoyaona ni juhudu na kusimamia kila kitu kiende sawa, hebu angalia kampuni ya kaka yako inavyokufa, ni kwanini…?’ nikamuuliza‘Madeni…’akasema‘Kwanini kuwe na madeni mengi kiasi hicho, kwanini hamuahangaiki kutafuta wateja, kwanini hamnisikiliza kila siku nawaambia jinsi gani ya kuendesha kampuni, kampuni ni masoko, nyie mnafikiria njia za mikato, mnaona matokea yake,..rushwa, utapeli ndio umewafikisha hapo mlipo…’nikasema‘Ni kweli, nimekuwa nikimuambia kaka sana kuhusu hilo, lakini hanisikiliza zaidi alikuwa karibu na marehemu..kila kitu marehemu atasaidia,…sasa sijui atasaidiwa na nani tena…’akasema‘Haya, na mimi hamuniamini sio….’nikasema‘Shemeji tunakuamini sana, na mara nyingi nilikuwa namshauri akuhusishe kwenye matatizo yake, lakini alikuwa mbishi, anasema yeye hawezi kumtegemea..mwa-mwanamke, ni kasumba tu…’akasema‘Kwahiyo sasa ni juu yako, nimewabeba kiasi cha kutosha, nimewambembeleza kiasi cha kutosha, naona sasa ni muda wenu wa kuwajibika, na bila kukuficha wewe na kaka yako, mpo kubaya..kuhusu muuaji ya Makabrasha, ...unalifahamu hilo’nikasema‘Lakini shemeji kiukweli sisi hatujalifanya hilo kabisa…na mimi sijui kaka alipokwenda kuongea na marehemu ilikuwaje,…hata hivyo nina imani hajaua, ..japokuwa wakati mwingine anaropoka tu..na hiyo bastola angeipata wapi, maana kama nilivyowaambia watu wa usalama mimi niliitupa…’akasema‘Yawezekana kuna mbinu zenu nyingine au ulimpa Makabrasha kwa nia fulani, na wakati wanabishana huko ndani, ndio kaka yako akamuua, mwenzake au wewe ndiye uliyefika na kufanya hayo mauaji..kwa namna moja au nyingine nyie wawili mnahusika kwa maujai hayo…’nikasema‘Shemeji nikuambiaje mnielewe, Makabrasha, yule ni ndugu yetu, hivi kuna mtu anaweza kumuua ndugu yake, na uone kaka alikwenda kuonana naye kwa ajili ya mambo ya kisheria, yeye alijitolea kumsaidia kaka, sasa tuje kumgeuka na kumuua, mbona haliji akilini...huo ni uzushi tu’akasema na kutulia‘Elewa kuwa,..hiyo bastola ndiyo iliyotumika kwenye mauaji, na hiyo bastola ndio wewe uliiba kutoka sehemu niliyoiweka,..utawashawishi vipi polis kuwa wewe au kaka yako hahusiki na hayo mauaji, hapo hauwezi kukwepa mkono wa sheria, baba maelezo yako uliyoyatoa hapa yanaonyesha hivyo,hayo tu yameshakufunga...’nikasema huku nikigeuka kwenye meza ndogo iliyokuwa pembeni yetu.‘Unaona kile kifaa pale, kinachukua kila kitu tulichoongea hapa, kwahiyo, kwangu mimi huna ujanja, pili nina ushahidi mwingine utakaokutia jela, ushahidi ambao, utaongea badala yako,nina imani ushahidi huo utaniambia kila kitu...’nikasema‘Ushahidi gani huo shemeji...’akasema huku akiniangalia kwa mashaka.‘Nikuulize kitu , hicho kitufe chako unahifadhia kazi za ofisini tu kama ulivyodai, au kuna mambo mengine ya binafsi?’ nikamuuliza‘Nini..hii flash disk(kinyonyi)..aah ni mambo ya ofisini na mamba yangu binafsi, yanakuwepo, kwanini umeniuliza hivyo..?’ akaniuliza kwa mashaka.‘Hapana nataka kujua tu, ..najiuliza kwanini ukaificha kwenye mkataba.’nikasema‘Nilisahau, ..nahis ni wakati naifanyia kazi jana, huwa na andika kumbukumbu zangu humo,…’akasema‘Kwahiyo jana ulikuwa unaandika yaliyotokea,…ni diary yako pia…?’ nikamuuliza na hapo akaniangalia kwa mashaka…na akatoa macho ya uwoga, akainamana na kusema;‘Ina maana shemeji umefikia hapo siku hizi, mbona sio tabia yako, kuchukua vitu vyangu bila idhini yangu, una maana umeangalia kilichokuwepo...!?’akasema na kuuliza‘Nimekuuliza tu…’nikasema lakini hakuamini‘Shemeji shemeji..hapana ni lazima umeangalia kilichokuwemo humo, ni kwanini nilisahau…mungu wangu..’akasema sasa akionyesha kuchanganyikiwa.‘Kwani kuna nini kikubwa, mbona unakuwa hivyo, unasikia, za mwizi ni arubain, hata ufanye nini ipo siku utanaswa tu..’nikasema‘Kwanini lakini shemeji, humo kuna vitu vyangu sitaki mtu mwingine avione..nilikuwa nataka kuvihamisha kutoka kwenye…oops, makosa makubwa haya,..kwanini shemeji hujali siri za watu, nilikuambia hicho ni kitufe changu, wewe umefanya nini sijui…’akasema akinitolea macho.‘Ni nani aliyeanza kuchukua vitu vya mwenzake bila idhini ya mwingine, mimi sikuwa na tabia hiyo, nilikuwa nakuamini kupita kiasi, lakini wewe na kaka yako mukanigeuka, na nimeona hakuna njia nyingine ila ni kufanya hivyo, na nitafanya vikubwa zaidi ya hivyo, .....sikutaka kabisa kufanya hivyo..’nikasema‘Kwahiyo shemeji unataka mimi nifanye, nini,..hebu jaribu kuniangalia na mimi,...huku kaka huku wewe, kama ingelikuwa kwako, huku yupo ndugu yako, huku yupo shemeji yako, ungelimsaliti ndugu yako, kwa ..kwa.. mbona mnanionea bure, ...’akawa analalamika.‘Hayo ni juu yako, maana ukweli hauangalii kuwa huyu ni ndugu yangu au sio ndugu yangu, ukweli na haki ni msumeno hukata mbele na nyuma…ulitakiwa kuliangalia hilo, dhuluma ni dhuluma tu..’nikasema‘Shemeji mimi nakuomba tafadhali, nipo chini yamiguu yako, kama umekiangalia hiki kitufe, naomba iwe siri yako, kuna mambo yangu mengi sana ya siri, nimefany makosa kukiacha hapo..nakuomba tafadhali,.....’akasema na kutaka kunipigia magoti , na mimi nikageuka kuondoka, nikisema;‘Nimeshakupa muda wa kutosha, ...na bado hutaki kuwa upande wangu, na nafanya haya kwa manufaa yenu, hebu fikiria jinsi kaka yako alivyofanya, nini ingekuwa mwisho wake, unafikiri nyie mngelifaidi nini, jasho letu lote lingeishia wapi, si kwa hao watu wa njee, nab ado hata sijui tutafanya nini..’nikasema‘Nafahamu hilo shemeji, lakini..nisaidie na mimi…’akasema‘Unafahamu eeh, sasa fikiria jinsi gani y akuliweka hili sawa, fikiria jinsi ya kumuokoa kaka yako, na wewe mwenyewe, maana mimi sasa nimenawa mikono yangu..’nikasema.‘Oh shemeji,...mimi hayo nilimuonya kaka, hakunisikiliza, kaka akiamua jambo lake, haambiliki, mpaka aone mwisho wake,...oh shemeji kama una.. umeangalia mambo yangu, umeniweka kubaya, nakuomba iwe siri yako, yaishie hapa hapa...’akasema huku akiangali huku na kule‘Umejiweka mwenyewe kubaya, ..wewe na kaka yako mpo ukingoni mwa mto uliojaa mamba, mumejichimbia wenyewe kaburi, sitaki kuwatisha, ila nawaonya na kuwapa muda kidogo wa kusema kila kitu,bado muda mnao, jitokezeni mseme ukweli kabla mambo hayajaharibika..’nikasema‘Kila kitu nimeshakuambia shemeji, unataka nini zaidi…’akasema‘Bado sana…pamoja na yote ni nyie kutubu dhambi zenu, kusema makosa yenu yote, ili sheria iangalia mlichokikosea, na hilo lianzie kwangu,..kama mimi mliyemkosea hamtaki kutubu kwangu, je sheria ya mahakamani itafanyaje….. suluhu juu ya hili, inawategemea nyie wawili, sasa nenda kaongee na kaka yako, mjipange vyema...’nikasema na kuondoka.‘Nitaongeaje na kaka wakati anaumwa?’ akaniuliza na mimi sikumjibu kitu, nikaondoka na kumuacha akiwa kasimama, kachanganyikiwa, na haukujua afanye nini....mimi sikumjali, nikaondoka kuelekea ndani.Nikasubiri kama nusu saa, sikumuona akitokea, …baadae nikasikia gari likiondoka huko nje, nikajua keshaondoka, na mimi nikaichukua laptop yangu na kuanza kuangalia ni kitu gani kilikuwa kwenye kile kitufe (flash disk), alichokuwa nacho shemeji yangu...NB: Kisa sasa kinafikia mteremko Lakini hadi sasa lipo swali kubwa;‘Je ni nani aliyemuua Makabrasha, na je mdada atagundua ukweli wa msaliti wake wa ndoa, je atatimiza ahadi yake...tusubiri tuone.WAZO LA LEO: Kuna watu inapofikia hatua ya kupata mali, wanapohisi kuwa kuna masilahi, wanapokuwa na uhakika wa kupata pesa, vyeo, ....hawaangalii tena utu na ubinadamu, wanasahau wema wote waliowahi kutendewa kinachobakia moyoni ni ubinafsi,....watu kama hao wapo tayari hata kuwadhulumu wazazi wao, au ndugu zao au jamaa zao…achilia mbali ya bosi kwa mfanyakazi wake. Mali , pesa , vyeo ni mtihani mkubwa kwetu, tuweni makini kwa hilo, tuangalie na kuchunga haki ya mtu, tuangalie na kuchunga dhamana za watu, hayo ni madeni makubwa, kama tutahini. Sasa nikiwa nyumbani,… akili ikiwa haikubali kupokea hayo niliyoyaona , na kusikia,…bado nahisi sio ushahidi wa kutosha, bado...maana nimeshawahi kusimama mahamani nafahamu ...jinsi gani ya kumshawishi hakimu...'Hata hivyo, ..hii ni hatua kubwa sana...'nikajipongeza, na hapo ndio nikaamua nijitulize kidogo kitandani ili kupumzisha akili yangu, lakini hata kabla sijafumba macho, mara nikasikia nina ugeni.‘Nimekuambia napumzika, sitaki usumbufu, mbona hunielewi mdogo wangu....’nikamwambia msaidizi wangu wa nyumbani kwa hasira.‘Lakini huyo aliyefika ni baba yako dada…’akasema‘Oh, baba yangu!!.., kuna nini tena jamani…' nilijikuta nasema hivyo, maana bba sio mtu wa kufika kwangu mara kwa mara na akitaka kuja ataniarifu, ili sipoteze muda wake akute sipo...'Samahani kwa kauli yangu, haya ..mkaribishe ndani, keshaingia ndani, ok, ok…haya nakuja…’hapo uchomvu ukaniishia, baba akifika kwangu ni kama bosi wa kampuni yako uneyemuogopa, na kumuheshimu sana kafika nyumbani kwako.Kwa haraka nikajiweka vizuri na kuelekea chumba cha maongezi, nikamkuta baba akipata kinywaji, huku kasimama, kuonyesha kuwa hana hata muda wa kukaa, ...yeye nyumbani kwangu ni kama nyumbani kwake, akifika hasubiri kuhudumiwa, anakwenda kwenye jokofu anajisaidia mwenyewe… japokuwa anapaheshimu kama sehemu ya mkwe wake.Alikuwa kasimama akingalia nje kwa kupitia dirishani na aliposikia nyayo za mtu akageuka na kunikagua kwa macho hata sijamsalimia akasema;'Bint yangu upo sawa kweli…?’ akaniuliza aliponitupia jicho, unajua tena huyo ni mzazi wangu akikuangalia tu anafahamu kuwa upo sawa au una matatizo.‘Nipo sawa baba, ni majukumu tu ya kila siku… na kuchoka choka kidogo..hamjambo wewe na mama, kupo salama huko..?' nikamuuliza hivyo‘Upo sawa wakati upo nyumbani, unajua nilipitia kazini kwako nikaambiwa hujafika leo, unaumwa…?’ akaniuliza‘Hapana baba mimi siumwi, zaidi ni mume wangu, nilikuwa na kazi, nikapanga kuwa nizifanyie huku nyumbani, lakini kila ukimaliza moja inakuja nyingine,, mpaka nikaona leo sitaweza kufika kazini kabisa,..kiukweli kazi nilizozifanya hapa nyumbani leo, hata ningekuwa ofisini nisingezifanya hivyo..’nikajitetea‘Lakini nyingi ni za kifamilia au sio..?’ akaniuliza kwa sauti ya kawaida tu‘Ndio baba..’nikasema‘Na hizo kazi za kifamilia , ndizo zinakufanya hata ushindwe kutuliza kichwa chako kwa ajili ya kazi za ofisini ambazo pia ni muhimu kwako, au sio..?’ akaniuliza nikajua baba ananitega kuna kitu kaja nacho anatafuta njia ya kuniingia.‘Baba lakini mimi ni mzazi, ni mwanamke wa nyumbani pia, na zaidi unafahamu kuwa mume wangu ni mgonjwa, kwahiyo inanibidi niwajibike kote kote…’nikasema‘Sawa sijalipinga hilo, ..nafahamu sana, lakini ukweli ni ukweli tu, kuwa majukumu ya nyumbani yamekuwa makubwa zaidi ya uwezo wako, …au sio, au niseme mitihani ya nyumbani umakuzidi, na bado hutaki kusaidiwa, sio mbaya..lakini nina uhakika hayo unaykabiliana nayo kwa sasa yanakuchanganya kichwa, kweli si kweli…’akasema‘Ni kawaida tu baba…’nikasema‘Ni kawaida tu eeh, hahaha…niambie ukweli ni nini kinachoendelea kwa hivi sasa ndani ya nyumba yenu..?’ kwanza alicheka lakini alipoongea hiyo 'niambie' akapandisha sauti.‘Baba nimekuambia ya kawaida tu, ni yale yale...'nikasema'Akatikisa kichwa kama kukubali, halafu akaniangalia kwa makini akasema'Haya niambie, huo ukawaida wake...'akasema'Baba kwani kuna nini, mambo ni yale yale bado napambana nayo hatua kwa hatua naanza kuyakabili, najua mwanzo ni mgumu,…lakini hadi sasa nimeanza kuthibitishia baadhi ya mambo, ambayo yalikuwa yakiniumiza kichwa, na leo tu, nilikuwa nahitimisha baadhi ya hayo mambo, …’nikasema,‘Binti unanifahamu sana, nikija hapa kwako ujue ni jambo nzito, ..najua kuna wagonjwa, lakini mgonjwa huyo, yupo huko hospitalini na huko anafanya mambo yake..ofisi kaihamishia huko..au sio.. hata hivyo, ni wajibu wangu kukutembea, lakini siwezi nikaja kwa kukushtukizia kama hivi, bila sababu maalumu, naheshimu mila na desturi zetu kuwa hapa ni nyumbani kwa mkwe wangu hata kama hayupo…’akasema‘Baba lakini hapa ni nyumbani kwa watoto wako unaweza kufika muda wowote utakavyo…’nikasema'Binti…huyo jamaa anayetaka pesa kwa ajili ya kuuza ushahidi dhidi ya mume wako ni nani…?’ akaniuliza na moyo ukalipuka paaah, nikajua rungu jingine linaniangukia kichwani, kama baba kalifahamu hilo, je polisi..na je kuna nini kwenye huo ushahidi, na kwanini baba akalifahamu hilo…nikakaa kimia kwanza kutafakari huo mtego wa baba.‘Ina maana gani, yaani kila mara ninapofanya jitahada ya kulisafisha jina langu, kwa sababu ya madhambi yenu, mnanipachika mzigo mwingine… ni kwanini mnafanya hivyo, mnataka wazazi wenu tufe kwa shinikizo la damu...au, halafu mje kulia..wakati chanzo ni nyie…’akawa kama anauliza'Baba kwani...'nikataka kusema lakini yeye akaendelea kuongea,....‘Ilikuwa ni wewe, kwa kashfa ya mauaji,..unajua jitihada gani nilizozifanya kuisafisha hiyo kashfa,…unakumbuka ilibidi hadi nikutane na waandishi wa habari kuliweka hilo bayana kuwa hauhisiki na hayo mauaji, baada ya ushahidi… haya, hayo yakaisha, …sasa hili tena, kuna nini hapa kwenye nyumba yenu..’akasema kwa ukali‘Baba, hata mimi ndio…nimesikia na…bado..hakuna uhakika kuwa ni kweli…ushahidi hakuna..’nikajitetea hivyo.'Sikilizeni, hili naliongea mbele yako, hata kama utanielewa vibaya, sitojali, maana kila dalili zipo....mume wako huko kuumwa kwake kwasasa kuna walakini, yaonekana kama anaiigiza tu...alishapona, ila anafanya hivyo kwasababu maalumu, hilo nakuambia wewe ulisikie hivyo…' hapo nikabaki kimia.‘Na hata kama angelikuwepo yeye hapa ningelimwambia hivyo hivyo, …’akasema akinikodolea macho ya kutisha, baba hana mchezo akikuangalia unatamani ujifiche.'Baba..." nikata kuongea akainiashiria kwa mkono kuwa hajamaliza kuongea.'Najua utamtetea mume wako, najua kutokana na kauli za madocta utasema ni kweli anaumwa,..sawa anaumwa,..nisije nikakufuru, lakini hayo matendo anayoyafanya mbona yanapingana na ugonjwa wake…usifikiri mimi sijui matatizo kama hayo yapoje,….mimi sijazaliwa kesho, watu kama hao nimeshakutana nao sana..lakini hilo la kwake limezidi kipimo…’akatulia'Baba lakini huyo aliyesema hivyo ni docta bingwa wa hayo matatizo...'nikasema'Ni kweli, ..ni nani huyo docta bingwa'Ni yule yule wa awali, nakumbuka uliwahi hata kuongea naye..'nikasema'Ok...siku kadhaa alikuwa karibu sana na huyo mpinzani wangu wa kisiasa...unajua kwenye haya mambo kila kitu kimachunguzwa...kuonekana na huyo mpinzani wangu sio tija, maana yeye ni dakitari wa wote..lakini kwangu mimi inanipa maulizo mengi...lakini..'hapo akatulia'Ina maana baba humuamini huyo docta...?' nikauliza'Sio kwamba simuamini..lakini yeye kama docta anafuata vielelezo vyake, na huo ugonjwa, pamoja na mengine kinachoangalia zaidi nai matendo ya mtu, je mtu ukiijua huo ugonjwa ulivyo, ukaigiza sawa na hayo matendo, docta atagundua ...?' akasema'Baba haiwezekani sio kwa madocta bingwa...'nikasema'Mimi nikiwa shuleni, niliteguka nyonga, nikaenda kwa docta..na nikatibiwa, wakati natoka kwa huyo docta, nikajikakamua tu, ili kutokujilegeza, wakati kweli hapo naumia, huyo docta bingwa, akanijia na kusema siumwi...akachanga karatasi ya mapumziko,..lakini kweli naumwa...'akasema, na mimi nika kaa kimia'Ninachotaka kukuambia ni hivyo, kuna magonjwa, docta anakuamini wewe, ukiigiza, hewala yeye atafanya nini, atahitimisha jinsi anavyoona kwa macho yake, hana makosa, ..unielewe hapo, mwenye makosa ni wewe unayeigiza, ..na hatari ya ugonjwa ulivyo ukiigiza ipo siku utakupata kiukweli...'akasema'Baba mimi nawaamini sana madocta..'nikasema'Hata mimi..sijasema siwaamini, ila kwenye tatizo, walakini hauchezi mbali hasa ukiwa unagusa kinyume na matarajio yako...tuombe mungu kuwa ni kweli, kuwa anaumwa kihivyo, lakini kama anaigiza, ...nakuambia hili, mume wako ataumbuka sana...'akasema'Baba huyo mtu anaumwa, sema yeye anaweza akautumia huo ugonjwa...lakini mimi sina mawazo hayo mabaya, ninaamini kuwa anaumwa, mengine ..ni juu yake...'nikasema‘Sasa sikiliza najua utarejea kauli yako kuwa labda nayasema haya kwa kutokuwajali watu wengine, au kwa vile sikupenda wewe uolewe na mtu kama huyo, au kama wengine wanavyosema kuwa labda nabagua,...lakini eeh, mimi kama mzazi sina makosa, kwa hilo, yoyote atafanya jitihada kuhakikisha bint yake anaolewa sehemu salama, na kwa hili wewe mwenyewe umeshajionea…na sitakosea nikisema bado…bado binti yangu upo kwenye mtihani mkubwa... ‘akahema na kuangalia pembeni.‘Baba lakini kwani kuna nini…?’ nikamuuliza"Kuna nini!!, mhhh....wajifanya hujui sio, …eti kuna nini,...'akatikisa kichwa halafu akaendelea kuongea'Binti...umejifanya kunificha mengi lakini mengine hayafichiki,..je wewe husomi magazeti, hata kama ni ya udaku, lakini ndiyo watu wengi wanayasoma, na hao watu wengi eeh, ndio hao wapiga kura wangu…unafikiriaje…wakisoma kashfa kama hizo, unafikiri kwa mtizamo wako wao watasemaje, sio kwamba nawadharau, lakini akili zao zitawatuma hivyo, kuwa ni kweli,...upeo wa kufikiria kwa kila mtu unatofautiana, au sio…’akasema‘Sisomagi hayo magazeti baba…’nikasema‘Ndio najua...mkurugenzi mkuu usome magazeti kama hayo,...hahaha, ni sawa wewe..huwezi kuyasoma hayo maana hayagusi masilahi yako,..lakini kwangu mimi ni muhimu sana kuyasoma, kila gazeti mimi nasoma hata yale yanayoandika uchafu....ili kujua kila kitu kwa watu wangu..., kila kitu kinachohusu wapiga kura wangu, ni muhimu kwangu,....na wengi wa hao ndio hao, wanaoyaamini hayo magazeti, na mpinzani wangu ndiye anayatuumia sana hayo magazeti unajua ni kwanini…’akasema‘Kwani, wamesema nini baba…?’ ikabidi nimuulize ‘MKWE WA MWANASIASA MKONGWE ANASHUKIWA KWA KUMUUA WAKILI WAKE, kichwa cha habari kikubwa, na kidogo....'WAKILI MTETEZI WA WANYONGE…’ hicho kichwa cha habari hapo, …unafahamu athari za maelezo hayo tu,..kwenye uwanja wangu wa kisiasa…na hapo hujasoma huko ndani…huko, nasikia, nasikia zipo nyingi tu, zikianisha kashfa na uchafu dhidi ya mumeo…’akasema‘Mauchafu gani…?’ nikauliza nikijifanya sijui lolote‘Mumeo kamwe hawamtaji kwa jina lake…kwangu mimi wananitaja kwa jina alngu mkongwe wa siasa so and so…, ni kwanini…na ni kwanini yeye wanamtaja kama mkwe wangu...kwanini…uone kwanini nawaonya sana kuhusu kashfa..’akasimama'Baba mimi sijui maana sijalisoma hilo gazeti...'nikasema‘Ukiangalia hata maoni ya watu kunihusu mimi, kiwango cha uaminifu kwangu kinashuka na wambeya wameshapata la kuongea, na ikitoka hapo, nisipofanya jambo hata magezeti haya ya kawaida wataanza kundika…unataka mimi nifanye nini hapo, niendelee kukaa kimia au sio..., nikae kimia tu kwa vile wewe binti yangu kipenzi,...hutaki mimi niingilie mambo yenu au sio, ..eeh, hebu hapo niashauri mimi…’akasema'Lakini baba…’nikataka kujitetea, na yeye akanikatisha kwa kusema;'Lakini baba..lakini baba…najua unataka kusema nini, kuwa familia yako haihusiani na maisha yangu ya kisiasa, kuwa hizi ni familia mbili tofauti , kila mtu na maisha yake,..au sio...hilo wewe wasema, lakini sio wapinzani wangu....'akasema'Mhh...'nikaguna hivyo.‘Umenielewa hapo, kama ingelikuwa ni hivyo, utakavyo wewe, ni kwanini hao waandishi hawaandiki wakirejea familia yako tu , wewe na mume wako, wanaandika kwa majina makubwa, ‘mkwe wa…’ …kwanini, kwanini..…ndio maana ni lazima niwajibike…’akasema‘Baba, niachie hiyo kazi, naomba nilifahamu hilo gazeti , mimi nitakwenda ofisini kwao, ikibidi tuwafungulia mashitaka..’nikasema‘Utakwenda kufanya nini wakati jeraha limeshavuja damu..unajifanya wewe unafahamu kuliko mimi, eeh..haya nenda kaonane nao, ...utawaambia wasiandike kuhusu mimi,…unajua ni nini wataandika kesho yake…unalifahamu hilo…BINTI WA KIGOGO WA SIASA KAVAMIA OFISI YA MAGAZETI, kitakachofuata ni nini, waandishi watafika nyumbani kwangu, hata wale waliokuwa wamekaa kimia, …’ akatulia akiangalia saa yake.‘Kwahiyo baba wataka mimi nifanye nini…?’ niamuuliza‘Wapinzani wangu wa kisiasa wameshaona uchochoro wakuniharibia mimi ni kupitia nyie wawili..hawachezi mbali na nyie sasa mumekuwa 'super stars,..' lakini wa nini basi,...…wameshawasoma na kufahamu madhaifu yenu, na mume wako kafanywa ndondocha, na sio ndondocha wa ucahwi,...ila wanamtumia,...bila hata ya yeye kufahamu,..sasa hivi wanatafuta kila mbinu za kuhakikisha mgogoro wenu hauishi, bali unafichua kashfa zaidi na zaidi....’akatikisa kichwa kama anasikitika.'Sasa baba....'nikataka kusema wazo langu lakin hakutaka kunipa muda.‘Mimi siogopi kupambana na hao watu…lakini nawahofia nyie…mtaumia,..na kwenye vita macho hayaoni,..aliyepo mbele yako ni adui yako, sasa kama nyie mumewekwa kama kinga yao, nitafanya nini…mwishowe nitaishia kusema bahati mbaya, na nani ataumia kama sio mama yako....’akasema‘Kwahiyo baba unataka kusema nini hapo..?’ nikauliza‘Nitasema nini ..eeh, niambie nitasema nini, wakati binti yangu, mkurugenzi mkuu wa kampuni A nd Z, yupo, eeh,..mke jasiri, eeh…hata siku moja hawakutaji kwa MRS mumeo,wanataja binti ya, na kwa mumeo, 'mkwe wa…' sijui unanielewa lakini…hata siku moja hawawezei kutaja mazuri yako kwa kurejea jina langu, ila mabaya wanafanya hivyo,….ujue ni kwanini nawaandama …mimi sitaki kupoteza muda wangu kwa maisha yenu..maana nyie sasa ni familia tegemezi, lakini kwa haya mimi nitafana nini...’ akatulia.Hapo nikaanza kuvutia hisia kujua ni kwanini baba kafika kwangu kwa hasira*************'Huyo mtu anayenitishia mimi, kuwa nisipojitoa kwenye uchaguzi ujao, atauweka uchafu wa familia yangu ni nani..najua keshawasiliana na wewe…sasa sikiliza , sitaki ufanye anavyotaka yeye, kufanya hivyo ni udhaifu..unasikia hata kama mume wako atakwenda jela…pambana kwenye haki na ukweli, unasikia...’akasema‘Lakini hakuna ukweli wa hilo au sio baba…?’ nikasema‘Ninachotaka ni wewe kutokukubaliana na yeye, kwa hivi sasa hawezi kukutana na wewe uso kwa uso,... anatumia mbinu za simu tu, kukusumbua...anafahamu mkikutana na yeye atakamatwa, na sio kwamba polisi wameshindwa kumkamata, lakini kuna kitu kinaendelea hapo, wewe huwezi kukufahamu, ila sisi tuliopo kwenye huo ulingi wa siasa tunakifahamu ni nini...unasikia bila kukuficha kinachoendelea kwa sasa ni mambo yetu ya kisiasa…’akasema'Kwahiyo baba, mimi nifanye nini..ndio swali la msingi hapo....?' nikauliza'Kwanza jichungeni..niliwaambia jamani, kuweni mbali na kashfa, ukasema nini...hilo nikuachie kwa vile ni familia yako..haya nimewaacha matokea yake ndio haya...nilijua tu haya yatakuja kutokea, lakin nitafanya nini, na wewe ushapenda, haya kupenda sio kubaya, lakini mtu uliyempenda, habebeki...utaumia binti yangu...'akasema'Baba mimi nalifanyia kazi, wewe mwenyewe utaona,...kama ni kweli, baba, niamini ...ila sitaki kufanya jambo bila kuwa na uhakika,...na uhakika huo, wataubainisha wao wenyewe, baba, niamini mimi...'nikasema'Hahaha, siwezi kumuamini mtoto wangu, mtoto ni mtoto tu..kwa hivi sasa huwez kunidanganya,...'akasema'Haya baba...'nikasema‘Sasa narudia tena,…sitaki..umsikilize huyo tapeli, kama atawasiliana na wewe..nijulishe haraka…na kuanzia sasa nitaanza kuingilia mambo yenu yote, kuanzia kazini, hata ya nyumbani…siwezi kuvumilia tena…na hii sasa ni vita ya kisiasa, najua yenu ni ya kifamilia, lakini wameivumisha iwe hivyo, sasa kazi ni kwako, uwe na baba yako au uwe na maadui wa baba yako...’akasema'Unasema nini baba…! Huoni ndio utajiharibia kabisa, haya yangu usijiingize baba, nakuomba tafadhali, huyo mume wangu ninajua jinsi gani ya kumweka sawa, mpaka hatima yake, siwezi kumuacha, hilo baba nilishakuambia…’nikasema'Najua...nafahamu sana,..ila nakuambia hivi, kama ni mume wako, kama ni familia tegemezi, kwanini sasa nipo mbali na nyie, madongo yakirushwa kwenu yanailenga na mimi, je nitaweza kuvumilia hayo, nikae kimia tu…, au nifanye kama mnavyotaka wewe na mama yako, kuwa niachane na mambo ya kisiasa, hicho ni kifo cha kondoo,. mimi sikulelewa hivyo, nitapambana, unasikia, huyo ndiye baba yako…’akasema‘Baba hapana, mimi sijasema hilo, ila mimi sikupenda mambo yangu yahusishwe na nyie..mimi nina familia yangu, na nyie ni familia tegemezi..japokuwa kwa namna fulanii tunategemeana, …ndio maana nilitaka niende nikaongee na hao watu.., waandishi wa hilo gazeti….’nikasema‘Usije kufanya kosa hilo…’akasema sasa akitaka kuondoka, lakini hakuondoka, akanigeukia tena na kuuliza swali hili….‘Je ni kweli mume wako ndiye aliyemuua Makabrasha…’baba akaniuliza‘Hapana baba sio yeye…’nikasema‘Silaha iliyotumika si yako, na uliweka kwenye kabati maalumu, ni nani aliyefungua kabati lako na kuitoa hiyo silaha..?’ akaniuliza‘Baba kuna tetesi tu bado nazifanyia kazi, ila nimeshamfahamu , nitakuja kukuambia kwa wakati muafaka ..’nikasema‘Ni kweli kuwa mume wako alifika huko kwa Makabrasha siku ya tukio, ..alikwenda kufanya nini..?’ akaniuliza‘Nahisi ni kwa vile huyo marehemu alishakuwa ni wakili wake, kwahiyo alikwenda kuongea naye maswala yao..na ndio nimeanza kuupata ukweli huo leo, lakini bado naufanyia kazi, haujawa na uhakika wa kiushahidi…’nikasema‘Mume wako si alikuwa mgonjwa..aliwezaje kufika huko..?’ akaniuliza‘Kuna dalili, kuwa akiingiwa na hisia fulani anakuwa na nguvu za ajabu ugonjwa hutoweka, akafanya mambo, kihisia,..kwa vitendo..ni aina ya ugonjwa wa ajabu tu..’nikasema hapo atabasamu na kusema.'Ugonjwa huo unawezesha yeye kuongea, kufanya ya ukweli, hata marehemu aweze kuelewana naye,..marehemu hakuwa magonjwa, ..ya kuwa walikutana kwenye njozi, au...usinifanye mimi mjinga eeh, hivi..inakuja akilini hiyo,..ok, sawa, tuliacha hilo kama lilivyo...lakini mimi simini...'akasema'Kufanya hivyo alivyofanya si ile ya kindoto za usiku, ila hilo la mchana akauwa na hisia za kawaida, akili za kawaida, ila anapata nguvu ya ajabu, ni kama mashetani hivi, yanamuongoza, kama nilivyoelezwa hivyo, ila ni katika aina hiyo y akuchanganyikiwa,..ipo hivyo baba...'nikasema‘Ok..ok...'hapo akacheka, halafu akaendelea kuuliza,...'Pale kwenye jengo, kuna vyombo vya kuashiria hatari, pindi mtu akiingia na silaha, pia yupo askari mkaguzi, ana ujuzi wa hali ya juu,...silaha ilipitishwaje, ujue huyo muuaji alikuwa nje..si ndio..na huko kote kuna hiyo mitambo ya ishara ya hatari, akasogea hadi chumba alichokuwa marehemu, na humo kwenye chumba kuna mitambo yake ya ziada, haikupiga kelele...umegundua nini hapo..?’ akaniuliza‘Bado nalifanyia kazi…’nikasema
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment