Simulizi : Muhanga Wa Mapenzi
Sehemu Ya Tatu (3)
“Nina kamba nimeshaiandaa na kuifanyia mazoezi.”
“Mmh, hayaa,” Joy hakuwa na la kusema.
Ilipotimu saa tano na nusu usiku Rachel alitoka kupitia dirishani kwa kutumia kamba. Kabla ya kuondoka Joy alimbembeleza asifanye hivyo kwani aliogopa atawajibu nini wazazi wake pindi wajapo na kutomkuta.
“Joy asikuambie mtu kupenda ugonjwa nimekuwa mtumwa wa penzi la Athuman, wiki sasa sijamwona machoni mpenzi wangu.”
***http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa Athuman alijikuta katika kipindi kigumu pale alipomkosa kumtia machoni Rachel. Kila alipojipitisha kwao hakufanikiwa kumuona alimanusra aende kuulizia lango kuu la nyumba ya Mzee Mulisa, lakini wazo hilo hakuliafiki. Siku zote usiku kwake ulikuwa mrefu kwa ajili ya kumuwaza Rachel mtoto wa tajiri.
Kila mawazo yalipozidi aliichukua picha ya Rachel aliyokuwa ameiweka chini ya mto na kuibusu kisha aliizima taa yenye mwanga mkali na kuwasha taa ya rangi ya kijani na kupunguza sauti ya muziki mololo kwa kutumia limoti uliutafuta usingizi kwa kubembelezwa na kibao laini my heart will go on kilichoimbwa Celine Dion.
Sauti ya kengele ya mlangoni ilimshitua Athuman toka katika usingizi ulioanza kumchukua. Alijiuliza atakuwa nani wote ule, saa ya ukutani ilimuonesha saa sita kasoro usiku.
Alinyanyuka kitandani na kwenda hadi mlango kabla ya kufungua mlango aliuliza.
“Nani?”
“Mimi,” sauti ile ilimshtua ilikuwa inafanana na ya mpenzi wake Rachel, akilini hakufikiria kama angeweza kuja usiku ule. Rachel alipaza sauti ya juu
yenye kuchanyanganyika na ukali ilikuwa kama inamzindua usingizini.
Athuman hakuamini masikio yake baada ya sauti ile kuwa kweli ya Rachel. Kabla hajajua nini kinaendelea, Rachel alisema kwa hasira:
“Athuman kufungua imekuwa mwaka, hunipendi au una mtu mwingine na mimi napoteza muda wangu kukupenda basi mimi naondoka.”
Alipofungua mlango mbele ya macho yake hakuamini kumkuta Rachel peke yake usiku ule. Alitaka kujua Rachel amefikaje pale, wasiwasi wake huenda ule ulikuwa mtego mwingine.
Lakini alipiga moyo konde na kumkaribisha ndani, baada ya kumuingiza ndani alitaka kujua amefikaje pale. Rachel alimpa picha kamili jinsi alivyo toroka kwao.
“Sasa wakija chumbani kwako na kukukosa itakuwaje?” Athuman alimuuliza Rachel.
“Hata siku moja hawawezi kqka chumbani kwangu usiku ndio maana wakanitafutia chumba cha self container.”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Athuman hakupoteza muda alimpokea Rachel , kwake ilikuwa kama majibu ya maumivu ya kumkosa mpenzi wake kwa wiki nzima.Twisheni! aliyoitoa kwa Rachel katika masuala ya mapenzi ilizidi kumchanganya mtoto wa watu, kutokakana na kuwa mgeni katika medani ile.
Lakini yalianza kutoa matunda naye Rachel aliweza kwenda naye sambamba katika medani ile huku akifurahia mapenzi. Baada ya kutwanga na kupepeta wote walikuwa hoi bin taabani.
Lakini Rachel ndiye alikuwa hoi zaidi, kutokana na muda kuwa umekwenda Athuman alimuomba Rachel arudi kwao kabla ya kupambazuka Lakini Rachel alikataa na kusema atalala mpaka asubuhi. Athuman alimbembeleza sana na kumkubalia kurudi kwao kwa shingo upande.
Alimsindikiza hadi kwao muda huo ulikuwa majira saa kumi alfajiri, baada ya kuhakikisha ameshaingii ndani ya uzio wa nyumba yao Athuman alirudi zake kuendelea na usingizi.
***
Rachel alipoingia chumbani kwake alijitupa kitandani bila kubadili nguo zake na kujilaza kutokana na mwili wote kuwa umenyong’onyea kwa mikiki mizito ya Athuman na kupitiwa usingizi mzito. Ilipotimu muda wa kwenda shule Rachel alikuwa bado amejawa na usingizi na mwili ulikuwa nyang’anyang’a hata nguvu za kunyanyuka kitandani hakuwa nazo.
Joy alipomuamsha waende shule, shoga yake alimwomba aende peke yake kwa vile alikuwa bado na usingizi mzito pia mwili haukuwa na nguvu. Joy alimbeleza waende shule, bado alishikilia msimamo wake wa kuendelea kulala. Mama Rachel alimuuliza Joy kuhusu Rachel ilibidi atengeneze uongo kuwa shoga alisoma sana mpaka alfajiri na kumfanya azidiwe na usingizi. Mama Rachel alikubaliana na uongo wa Joy na kumuacha Rachel aendelee kulala.
***
Siku ya pili kama kawaida ilipofika muda wake Richel alikwenda kwa Athuman na kumuacha Joy akijisomea na kurudi saa tisa usiku akiwa hoi na kushindwa tena kuamka asubuhi. Lakini Joy alimwambia kama hata kwenda shule basi siku ile angerudi kwao.
Rachel alijilazimisha kwenda ili kufanya rafiki yake aendelee kuwepo kwao ili kuzidi kuficha siri yake. Rachel alionekana amechoka na mama yake kuhoji hali ile.
“Vipi maendeleo yake kimasomo?” alimuuliza Joy
“Yanaridhisha.”
“Vipi na leo umekesha unasoma?”
“Ndiyo mama.”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Na kweli maana inaonesha leo hakulala kwa kijisomea, “ kauli ile Rachel alichekelea chini chini kama wazazi wake wangeujua ukweli wangeua mtu.
Rachel shuleni alishinda akisinzia, muda wote alifikiria mchezo uliomrusha akili kama sio kumpangawisha na kuona kusoma ni kupoteza muda bora aolewe na Athuman ambaye ndiye aliyemuingiza katika ulimwengu wa wapendanao.
Rachel alikuwa tayari kufanya lolote kuliko kumkosa Athuman mwanaume aliyeyateka mawazo yake na kumuwaza muda wote na kuyaona masomo hayana nafasi akilini mwake.
Siku ambayo hakwenda kwa Athuman muda wa kujisomea usiku aliutumia kumuwaza huku akikumbatia mto muda wote na kujisahau kuwa anatakiwa kusoma na aliposhtuka ilikuwa tayari kumepambazuka. Siku ya pili alipokwenda shuleni mtindo ulikuwa uleule wa kusinzia darasani. Mwalimu alimuona na kumfuata.
“Rachel vipi?”
“Maandalizi ya mtihani mwalimu.”
“Ooh! Pole sana kwa vile toka uingie unasinzia bora ukalale nyumbani upunguze usingizi.”
Rachel alipata nafasi ya kurudi nyumbani, hakwenda nyumbani alikwenda moja kwa moja kwa Athuman. Alimkuta mwenye mawazo mengi kitu ambacho hakupenda kukiona kikimtokea mpenzi wake.
“Vipi mpenzi mbona hivyo?” Rachel alimuuliza Athuman.
“Nina shida,” Athuman alijibu kiunyonge.
“Athuman, kwa shinda yako nipo radhi hata kumuua hata baba yangu ili kuhakikisha unapata furaha ya maisha yako.”
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hivi mpenzi maisha haya mpaka lini? Kaka akirudi nitakuwa wapi, pia hatutakuwa na nafasi ya kuinjoi mapenzi yetu.”
“Athuman ulikuwa anatakaje?” Rachel alimuuliza huku akichezea bustani la kifuani.
“Ungenipangia nyumba ili kaka akirudi tuendelee na raha zetu.”
“Athuman mbona hilo dogo ulikuwa anataka lini?”
“Kwa vile kaka amebakiza miezi miwili arudi ingekuwa vizuri mwezi mmoja kabla ya kurudi.”
“Basi hiyo kazi niachie unataka sehemu gani?”
”Yenye hadhi na sisi.”
“Hilo umepata omba jingine.”
Mara nyingi Rachel alikuwa akiiba ATM Card na kuchukua kiasi cha pesa kutumia lakini kupitia ombi la mpenziwe alipanga kuchota pesa nyingi hata milioni kumi kwenye card ya baba na mama yake.
*****
Mzee Mulisa na mkewe walikuwa wamesahau ya Athuman na kuelekeza nguvu zao kwa mtoto wao ili kuhakikisha anafanya vizuri katika mitihani wa kidato cha nne kwa kumpatia kila alichokitaka ili kuhakikisha anafanya vizuri. Kwao ilikuwa sawa na kutwanga maji katika kinu au kubeba maji kwenye gunia kutokana na mtoto wao kuhamishia mawazo kwa Athuman na si katika masomo.
“Mama Rachel siamini kama mtoto wetu angetulia kiasi hiki, alitaka kuchanganyikiwa bila kumbana na kumuahamishia kule sijui kama tungemuweza,” Mzee Muliza alimwambia mkewe.
“Lakini baba Rachel yote umeyataka wewe ulimdekeza hata mimi ulinizuia nisimkanye eti kipenzi chako, kwa vile mtoto wa tajiri atakiwi kukosa raha. Haya sasa kumdekeza kwako kidogo kututumbukie nyongo.”
Wakiwa katikati ya maongezi mara Rachel aliingia ndani.
“Vipi mama mbona hivyo unaumwa?”
“Hapana baba siku hizi nasoma sana usiku muda mwingi nikiwa shuleni nasinzia,” Rachel alitengeneza uongo.
“Punguza kusoma sana usiku,” Mzee Mulisa alisema.
“Lakini si ninyi mmenitia kizuizini ili nisome, tatizo nini?”
“Soma mama, lakini vipi maendeleo yako?” mama yake alimuuliza.
“Sio mabaya sana nina uhakika wa kufanya vizuri.”
“Nakuahidi ukifanya vizuri nitakutafutia zawadi mkubwa, kwanza nitakununulia gari la kifahari la kuendea shuleni,” baba yake alimtia moyo.
“Nitashukuru baba.”
Rachel aliagana na wazazi wake na kwenda zake kulala, ama kweli usilolijua sawa na usiku wa kiza. Kama wangejua usingizi ule mtoto wao unatokana na nini wangemmwaga mtu ubongo.
***
Rachel kila usiku masomo yake aliyasomea kwa Athuman kwa muda wote wa kujiandaa na mtihani. Familia mbili ya wazazi wa Rachel na Joyce ziliungana pamoja kuwafanyia watoto wao sherehe ndogo ili kuwapa moyo ili wajitayarishe vizuri na mtihani wa kidato cha nne.
Ilikuwa ni sherehe iliyoandaliwa katika Jumba la mzee Mulisa na wazazi wa Joyce, wazazi wote waliwahidi watoto wao zawadi nyingi pindi watakapofanya vizuri au kupata alama za kuridhisha katika matokeo yao.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sherehe ile pamoja na kuwa ya kupendeza kati ya familia mbili lakini ilikuwa kero kwa Rachel ambaye alikuwa kama bugudha kwake akili yake ilikuwa haiwazi mtihani zaidi ya penzi tamu kwa Athuman. Baada ya sherehe kwisha wazazi wake walimuweka chini ili kuongeza ahadi nzito.
“Mwanangu Rachel nakuahidi ukifanya vizuri katika masomo yako nitakununulia ndege kwa ajili ya kukupaleka shule,” Mzee Mulisa alimuahidi Rachel na mkewe kila mmoja aliahidi zawadi yake.
“Mwanangu ukipata division 1 kama alivyosema baba yako tunakununulia ndege na kuwa mwanafunzi wa kwanza Afrika kumiliki ndege na ukipata 2 mimi mama yako nitakununulia gari lolote la kifahari ulitakalo.”
“Sitawangusha wazazi wangu.”
Kama wazazi wa Rachel wangeingia moyoni kwa mtoto wao basi zawadi kubwa kuliko yote mtoto wao angetaka kuolewa na Athuman.
“Wangesema kama ni ningepata alama za kuridhisha ningeolewa na Athuman mbona ningesoma kama mwendawazimu. Lakini shule sina hata hamu nayo bora siku zifike nipunguze bugudha za wazazi, “ Rachel alijifikiria na kuona wazazi wake kama wanacheza makidamakida.
Alipokuwa shuleni alinielezea yote yaliyoahidiwa siku ya sherehe.
“Joy bora tumalize ili nipate muda wa kukutana na sweet heart wangu.”
“Lakini Ray jitahidi basi shoga katika mtihani usipate ziro,” Joy alimbembeleza rafiki yake ili afanye vizuri kwenye mtihani kuliko kuhamishia mawazo yake kwa Athuman.
“Ina maana kupata ziro itasababisha nimkose Athuman?” Rachel alimuuliza huku ameshikilia mkono kiunoni.
“Siyo hivyo Ray wazazi watajisikia vibaya.”
“Vibaya kama nilikaa nyumbani bila kuolewa.”
***
Siku ya kufanya mtihani ilipofika Rachel hakuisumbua akili yake zaidi ya kufanya yale anayoyaweza na kuyaacha asiyoyaweza wala hakutaka kuumiza ubongo wake. Cha ajabu siku ya mwisho ya mtihani alishangilia kitu kilichomshangaza kila mmoja wengi walikuwa na wasiwasi labda ana uhakika na alichokifanya katika mtihani au alikuwa na majibu hasa wakizingatia ni mtoto wa tajiri.
Wangejua anachoshangilia wala isingewasumbua akili yao , wazazi nao walimpongeza mtoto wao kwa kumaliza salama mtihani wake. Rachel alipofika nyumbani hakuwa na muda wa kupoteza zaidi ya kuomba ruhusa kwa wazazi wake anakwenda kwa Joyce.
“Wazazi wangu naomba nifike kwa Joy kuna vitu vyangu nilivisahau ni muhimu sana.”
“Nenda lakini uwahi kupumzika si unajua baada ya kazi nzito ya mtihani unatakiwa kupumzika” alisema mama yake.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Sawa mama sitachelewa.”
Wazazi wake walimuomba aende upesi ili awahi kurudi walipotaka kumpa gari ili awahi alikataa alisema atachukua Teksi.
“Chukua gari uwahi,” mama yake alisema.
“Hapana mama nitachukua teksi tu.”
“Haya basi nenda uwahi kupimzika.”
“Sawa mama.”
Alitoka nje na kuchukua teksi hadi kwa mpenzi wake huku wazazi wake wakiamini kabisa mtoto wao amekwenda kwa shoga yake Joy.
0 comments:
Post a Comment