Search This Blog

Friday, November 18, 2022

SITOWEZA KUKUSAHAU - 5

 





    Simulizi : Sitoweza Kukusahau
    Sehemu Ya Tano (5)




    ***

    Hali ya Zulfa ikawa imeimalika,siku hiyo wakapata ruhusa ya kurudi nyumbani.Wakati wanatoka nje kwenye kordo,Ramso akasimama na kumtazama mwanamke ambaye aligongana nae kikumbo siku chache zilizopita akiwa amefuatana na Bi mkubwa wake.

    "Zulfa hebu nisubiri hapo hapo nakuja" Ramso akasema na kuanza kupiga hatua kuelekea alipo mwanamke huyo.Alipofika akawasalimia wawili hao.

    "Vipi mgonjwa wenu hajapona?" Ramso akaukiza.

    "Ndio,amepatwa tena na malaria amelazwa tena"

    "Eeh poleni sana,ni mtoto wako eeh?"Swali la Ramso likamfanya mwanamke huyo amtazame bi mkubwa aliye pembeni yako.

    "Wee mtoto huyu sio wetu,alikuja kutuomba tu msaada maana hakuna na pa kulala" Bi mkubwa huyo akasema huku akimtazama Ramso,akamuelezea kila kitu kilichokatokea mpaka hali ya sasa ya Gadna.

    "Unasema anaitwa nani?" Ramso akauliza tena kwa sauti ya juu baada ya kusikia jina la mtoto wake Gadna linatamkwa kwenye kimywa cha binti huyo.

    "Gadna"

    Mapigo ya moyo yakaanza kumuenda mbio Ranso.Hakuamini kabisa anachokisikia masikioni mwake.Akajikuta anajipikicha masikio ili hali asikie vizuri lakini bado jibu lilikuwa lile lile.Akajikuta anaunganisha maneno ya Inspekta Makurumla kuwa mtoto wake alitoroka siku nyingi tu zilizopita na hapa anakutana na watu ambao walimsaidia Gadna baada ya kukosa sehemu ya kujihifadhi.

    "My son Gadna,amelazwa!" Ramso akatoa sauti kubwa kiasi kwamba watu walio karibu na mahali hapo wakageuza vyuso zao na kuwatazama Ramso na wenzake.Hata zulfa naye akashindwa kuelewa ni kitu gani kinaendelea kati ya Ramso na wawili wao.

    "Mwanao?" Mwanamke huyo akaukiza kwa mshangao.

    "Ndio nionesheni chunba alicholazwa" Ramso akaomba na bila kusita akapelekwa mpaka kwenye wodi maalumu wa watoto.Ila cha kushangaza hawa Bi mkubwa na mwanae hawakuweza kumuona Gadna zaidi ya kiyanda tupu.

    "Eeh si alilazwa hapa?" Bi mkubwa akauliza

    "Ndio hapa hapa"

    "Itakuwa kaenda wapi? au katoroka?" Wakajiuliza maswali mengi pasikubata jawabu la maswali yao.Ramso akaanza kupoteza tena matumaini ya kumpata mtoto wake,akajiinamia na kuanza kutokwa na machozi huku akiwa na uchungu mkubwa wa kumkosa mwanae.

    "Hebu tukamuulize daktari" wakaongozana mpaka aliposimama nesi mmoja na kuuliza kama kuna mgonjwa wowote ambaye ameruhusiwa.Jibu la nesi huyo likawavunja maini na sasa wakabaki wamekoa macho kwa hofu.

    "Sisi hawa mtoto wote wana walezi wao ma hatuwezi kumruhusu mtoto wowote kutoka bila idhini ya mlezi"nesi akafafanua kiundani zaidi.

    "Sasa mtoto wa kitanda kile yupo wapi?"Ramso akauliza kwa hasira huku macho yake yamebadilika na kuwa mekundu.Alipofanya hivyo nesi huyo akaanza kuogopa kwani mtu anayezungumza nae amebadilika ghafla bila kutegemea.

    "Basi subirini nikamuulize dokta maana mi nimeingia leo na ndio zamu yangu" Nesi akasema na kutoka kwenye wodi hiyo huku akitazama nyuma kwa hofu kubwa.



    Wakati taharuki imetanda mahali hapo,mara Gadna akatokea kutoka mlango wa chooni.Ni kama haamini kabisa Ramso pale macho yake yalipogongana uso kwa uso na Mtoto wake Gadna.



    "Gadna!" Ramso akaita kwa sauti.

    "Dady" Gadna akakimbia na kumrukia baba yake kwa furaha mno.Wote machozi yakaanza kuwamwagika.



    "Are you okay"

    "Yes Dady"



    Wakakumbatiana kwa furaha sana.Baada ya hapo wakaanza kufanya utaratibu wa kumtoa hosptalini hapo.



    ****



    Ndugu wabunge wakaendelea kukusanyika katika Bunge tukufu la Tanzania kufuatia kwa ujio wa rais kuliutubia bunge.Kila waziri wa nchi hiyo walikusanyika akiwemo waziri mkuu mh. Mokwa ambaye anashilikiana na Mzee Kibangara katika kuhakikisha serikali hiyo inapinduliwa na Mzee Kibangara kuchukua dola.



    Vipasa sauti vimewekwa tayari kwenye meza rasmi ya kuhutubia Mh raisi,kilichofuata ni wimbo wa taifa.Wakamaliza na wabunge wote wakakaa chini.



    "Hebu subiri mkuu nikague" mlinzi wa rais akamwambia rais na kuelekea kwenye meza ile ambayo imeandaliwa kwa ajili ya hotuba.

    Akafika na kuvitazama vipaza hivyo,akavipuliza,ghalfa akaanza kukohoa mfululizo.Sumu aliyowekwa kwenye vipaza hivyo.



    Haraka askari wa usalama wakamchukua mlinzi huyo na kumuingiza kwenye kisha wakamkimbiza hospitalini.Hotuba ya mheshimiwa raisi ikaishia hapo.Kitendo kile kikamuudhi mno.Jaribio la kwanza la kumuua raisi likawa limeshindikana.



    ****

    Safari ya Liberia ikawadia,Ramso,zulfa pamoja na Gadna wakajiweka sawa.Kila mmoja akawa na hamu kubwa ya kuondoka kwenye jiji hilo ili wapoteze matatizo waliokuwa nayo.



    "Jamila mpenzi nakuamchia hii nyumba,mimi mwaka wowote nitarudi,nimeamua kuondoka ili nisitafutwe"Zulfa akaongea huku machozi yanamwagika,kumuacha rafiki yake kipenzi ni jambo ambalo linamuumiza kichwa lakini hakuwa na jinsi zaidi ya kumuachia Mungu kwa kila kitu.



    "Sawa mwaya ila nitakumisi sana"Jamila akajibu huku machozi kwa mbali yanamlengalenga.Walipomaliza wakaingia ndani ya gari na sasa safari ya kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere ikaanza.Kutoka Mbezi mpaka airport wakafanikiwa kufika mapema sana majira ya saa tatu usiku.Ndege ambayo iliwapaswa kuwachukua ilitakiwa kusafiri saa nne na nusu usiku.



    Kama walivyopanga,wakapita kwenye sehemu ya ukaguzi salama kabisa na baada ya dakika kama kumi,ndege hiyo ikaanza kunguruma na abiria wote wakaingia ndani.



    "Ndugu abiria,tafadhali funga mkanda wako na kaa kwenye kiti chako" ni sauti nyororo ya mhudumu wa ndege iliyopenya kwenye ngoma za masikio ya abiria wote.



    ****



    NCHINI LIBERIA

    "Ndugu yangu mbona umekonda namna hii?" rafiki wa Ramso akauliza kwa mshangao.



    "Daah kwa kweli ni shida tu kaka" Ramso akajibu huku anatabasamu.



    " Na huyu ni shemu wetu wa pili nini?"

    "Hamna kaka huyu ni dada yangu tu,shem wako kanifanya vibaya sana mpaka nikaikimbia South"Ramso akasema hivyo.Rafiki yake Jerry akamnyanyua Gadna.Wakaingia ndani ya gari lao na kuondoka kwenye uwanja wa ndege huo wa Liberia.Nyumbani alikopanga Jerry hakukuwa mbali sana kwani walitumia dakika arobani mpaka kufika kwenye nyumba ya Jerry.

    "Karibu kaka hapa ndio maskani napojificha,nimepewa na bosi wangu nayemfanyia kazi"

    "Asante kaka"

    Jerry akafungua buti la gari na kutoa mizigo yote.Wakasaidia na Ramso wakaingiza ndani.Nyumba hiyo yenye vyumba vinne na sebule imenakishwa kwa samani za ghalama kubwa.Kila kitu kilichohitajika katika nyumba,katika nyumba ya Jerry vilikuwamo.



    "Kaka Jerry umepiga hatau kwa kweli"

    "Haha hamna kawaida tu na wewe si ulipata mchongo na yule mzew wa kishua kule Tanzania,mchongo ule umeishia wapi?" Jerry akauliza,swali hilo likamfanya Ramso ainame na kumtazama Zulfa.

    "Daah lile dili ndio linalonisumbua mpaka sasa huwezi amini kabisa,pesa zote sina na familia yangu mzima ipo mashakani kama hivi,yule mzee hapa navyokuambia ananiwinda kama ndege"Ramso akaongea mengi sana huku muda mwingine akifuta machozi.Safari yake ya maisha ni kama ndoto inayoendeshwa na usingizi mkali katika kitanda kikubwa,maisha ambayo hakuwahi kuyaona hata kuyawaza kama kweli yatakuja tokea maishani mwake.



    " Daah pole sana mshikaji wangu,mimi nimeondoka kule south nimezinguana na tajiri mmoja hivi.Aah si nikamzingua kaka" Jerry akazungumza.

    "Yaani ukamuua au?" Ramso akauliza.

    "Yaah nikamtia pistal ya kuchwa pale nikaamsha zangu,mzee siku mbili mbele si jamaa zake wakaanza kunimendea,aaah nikaamsha nikaenda Marekani,baada ya mwaka mmoja si nikapata dili lingine la kuja kufanya kazi hapa...."Jerry akaendelea kuadithia maisha yake ya umafia kiundani zaidi huku swaiba wake Ramso akimsikiliza kwa umakini mno.

    "Kaka umetisha sana aisee,kwa hiyo hapa umekuja kufanya kazi gani?"



    "Huku kaka kuna mzungu mmoja wa kike nimetumwa nimchunguze,sasa mzungu mwenyewe ana walinzi wakali balaa,ila kwa kuwa umekuja tutasaidia hii kazi,ina pesa ndefu unajua!" Jerry akasema kwa msisitizo na kuachia tabasamu.Ramso akafikiria kazi hizi zitakwisha lini,ni kazi za hatari sana na uhai wake upo mkononi muda wote.Akakohoa na kusema.

    "Tutaangalia kaka" Ramso akasema na Jerry akatoka na kuingia chumbani.Akarudi akiwa ameshika akiwa amebadilisha nguo.



    Baada ya muda akawaonesha vyumba vyao vya kupumzikia.Ndani ya dakika kumi akaingia msichana akiyevalia jinzi iliyombana vizuri.



    "Waooh kuna wageni leo" msichana huyo akadakia baada ya kuwaona akina Ramso.



    "Yaah kafanye mambo ya msosi,wapate kidogo"Jerry akaongea na kuwatambulisha wageni hao kwake.

    "Mshkaji wangu Ramso huyu ni demu wangu anaitwa Flora,ni toto la kirwanda hili" Jerry akasema na wote wakatabasamu.Flora akaingia chumbani na kubadilisha nguo kisha akaenda jikoni kwa mapishi.





    Asubuhi na mapema Jerry pamoja na Ramso wakaingia kwenye gari na kuelekea mjini.Huko wakapanga jinsi kazi itakavyokwenda.Wakaingia kwenye duka moja la nguo na kuanza kuchagua nguo za kazi.Ramso akachukua koti jeusi na glovusi za kuvaa mikononi.Akachukua jinzi nzito nayo nyeusi,Jerry naye akafanya kama alivyofanya Ramso.



    Wakatoka kwenye duka hilo na kuondoka zao.Safari hii wakaingia katika jengo moja ambalo kwa haraka Ramso hakugundua linajishughulisha na kazi gani.



    "Humu Ramso kuna rafiki yangu tumezoea sana,muuzaji wa silaha za moja"



    "Ahaa nikawa najiuliza jengo hili la nini?"

    "Ndio hivyo kaka"

    Wakaingia ndani ya jengo hilo.Kitu kilichomshangaza Ramso ni lifti aliyoipanda inaanza kushuka chini kwa kasi sana.Wakajikuta wamesimama na kutoka kwenye lifti.Wakaendelea kutembea huku wakipishana na baadhi ya wafanyakazi wa jengo hilo.Baada ya mwendo wa dakika tano Jerry na Ramso wakasimama nje ya ukuta,jambo ambali likamsajabisha Ramso.

    "Sasa mbona tunautazama ukuta?"



    "Haahaha kaka hapa kuna mlango bhana" Jerry akasema na kucheka.Marafiki hawa wawili wamezoeana tangia walipokutana Afrika Kusini zamani sana,utani kwao ulikuwa kawaida na kila mmoja alimtania mwenzake kadri anavyotaka.



    "Daah kuna kazi kweli kweli"

    "Haha poa tuingie"Jerry aliposema hivyo mlango huo ukafunguka na wote wakaingia ndani.Kabla hawajafika kwa mhusika mwenye,mlangoni wakakutana na kioo kidogo ambacho kina ruhusu mtu kuingia ndani kama kikimruhusu.Kioo hicho kinauwezo wa kusense miguzo ya watu.Baada ya sekunde chache mlango ukafunguka na kuingia ndani.



    "Oooh brother leo umekuja na mgeni naona" jamaa mmoja mwembamba akauliza huku akimtazama vizuri Ramso.



    "Ndio kaka ninafanya nae kazi moja" Jerry akajibu.

    "Ahaaa poa karibu,leo kuna mzigo mpya aisee"Jamaa akasema.Akafungua kabati la vioo na kutoa bunduka tano za aina tofauti,akafungua kabati lingine na kutoa bastola nne nazo ni za aina tofauti.Akaanza kuzichomoa magazini zake na kuziweka pembeni.



    "Hii inadungua umbali wa mita mia mpaka mia mbili hamsini,na hii inauwezo wa kudungua mita mia tano na zaidi,ni mashine mpya kabisa kwa waka wewe ndugu yangu Sniper unafurahi sana" Jamaa akasema huku akiveshea mikanda ya risasi ya bunduki aina ya AK 47.Alipomaliza wakatoka na kwenda shemu nyingine.Jamaa huyo akabonyeza namba za siri na kufungua kabati ndogo kiasi,kabati hilo lililojaa mabomu ya aina mbalimbali yakiwemo ya kurushwa kwa mkono na mengine ya kutumia mashine.



    Wakaamua kuchukua bastola moja moja na silaha kali ya kudungulia.Wakalipia pesa kisha wakaondoka zao.Wakaenda moja kwa moja mpaka nyumbani kwao ili waanze kuisoma ramani ya jumba la Mlengwa wao.Baada ya kuweka sawa ramani yao,Jerry akachukua kompyuta mpakato (Lap top),akafungua faili moja na picha za Mwanamke huyo wa kizungu zikaonekana.



    "Huyu ndiye mzungu mwenyewe au?" Ramso akauliza.

    "Ndio ni barozi wa Marekani nchini humu" Jerry akajibu huku akipekua faili hilo kiundani zaidi.

    "Ahaa sasa kitu gani kafanya huyu mama?"

    "Hata najua ndugu,mi ni kazi tu nacheki pesa mfukoni" Jerry akasema huku anaendelea kuchambua faili ya barozi huyo.



    "Poa"

    Ramso akatoka na kwenda sebleni ambako kuna Zulfa,Flora pamoja na Gadna.Akaungana nao katika kutazama matangazo yanayorushwa kwenye kituo kikubwa cha BBC news.Kikubwa kabisa kilichoingia punde ni taarifa za Barozi huyo wa Marekani nchini Liberia kuhutubia wananchi kuhusiana na ugonjwa wa Ebora ambao umeshambulia sana na kuua watu wengi sana.



    "Jerry!" Ramso akamuita Jerry.Akafika na moja kwa moja macho yake yakaganda kwenye kioo cha televisheni.



    "Hapo mpango mzima" Jerry akatabasamu.



    Jerry na Ramso wakatoka na kuingia kwenye sehemu ya mawasiliano.



    ****



    Mgodi wa Hamizona uliopo nchini Somalia,likaendelea kuwaajiri watu hususani wakina mama na watoto walio na wasio chini ya miaka kumi na nane.Mgodi huo ndio mradi mkubwa wa Mzee Kibangara ambaye anamiliki kikundi cha ugaidi katika nchi kadhaa za Afrika.



    Wafuasi wake ambao wanasimamia shughuli mzima za uchimbaji,walisifikana kuwa na ukatili wa hali ya juu.Hawakuona huruma kumtia mtu risasi au kisu ya tumbo mfanyakazi yeyote ambaye ataenda kinyume na sheria zao.Hawakujari hata kuthamini nini maana ya utu,kwao kazi ya kutoa roho za watu,ni kazi ndogo sana.Sio hao tu bali kuna wafuasi wengine ambayo hutembea sehemu mbalimbali za Afrika na kuwateka wanawake pamoja na watoto wao na kwenda kuwatumikisha katika mgodi huo ulio chini ya ardhi bila malipo yoyote.



    Nguvu aliyonayo Mzee Kibangara,ni nguvu ambayo inapelekea baadhi ya mataifa kumuogopa pale panapofika katika kutumia silaha na majeshi yao.Vikao zaidi ya kumi vya mataifa kadhaa ya Afrika yalikaa na kumjadili Mzee huyu lakini wakaishia patupu baada ya kupewa vitisho vya nguvu.



    Katika mgodi kuna mwanamke mmoja ambaye ameenda kiumri mno.Yupo katika mgodi huo takribani miaka kumi.Mwili wake umedhoofu na kukosa kabisa muonekano ulio wa kawaida kwa binadamu.Mwili mzima amejawa na vipole na ngozi yake kuwa kavu na tena iliyo ya makwinyasi.



    Mwanamke huyo akainuka,baada ya kusikia filimbi ambayo inawaruhusu watu wote kukusanyika sehemu ya kupewa chakula.Akajivuta na kuchukua bakuri lake na kupanga foleni.



    "Mama Ramadhani pole mwaya, njoo ukae huku mbele" sauti ya mmoja wa wanawake ikasikika na kumfanya Mama huyo anayejulikana kwa jina la Mama Ramadhani akasogea mbele kwa unyonge.



    "Asante sana rafiki yangi" Mama Ramadhani akamshukuru sana mama huyo.



    Wakajipanga na kupokea ugali ulio ngumu na mboga ndogo sana,waketi pembeni na kuanza kula.



    "Noo haiwezekani,ugali mkubwa huu wote kijimboga hiki,kama vipi bora msitupatie na namwaga" sauti ya mfanyakazi mmoja ikasikika kutoka kwenye meza ya kugawa chakula.Analalamika juu ya ugawaji mdogo wa mboja tofauti na ugali.Alipomwaga tu ule ugali na mboga,hapohapo akaonekana na mfuasi mmoja ambaye alikuwa anasimamia shughuli ya ugawaji chakula.Akachomoa bastola yake na kumfyatulia mguu,hakukaa vizuri akafyatua nyingine iliyompata vyema kwenye paja lake.Sauti ya maumivu ikatoka kutoka kwa kijana huyo ambaye anavuja damu kwa wingi.





    "Hiki chakula amenunua babako,unajua bei yake?,sasa leo subiri nikuoneshe" Jamaa huyo akamchukua mfanyakazi aliyemwaga chakula na kuanza kumvuta.Akaingia nae kwenye kijichumba kidogo na kuanza kumpa adhabu.



    Helkopta ndogo ikatua nje kabisa ya mgodi huo.Mtu aliyevalia suti na kofia ya Pama akashuka baada ya watu wake kufungua mkango huo.Hakuwa mwingine zaidi ya Mzee Kibangara,akaanza kutembea kuelekea kwenye chumba kimoja ambacho kinatumiwa na wafanyakazi wake.



    "Karibu bosi" mfuasi aliyevalia shati jeupe na tai akamkaribisha mzee Kibangara kwa lugha ya kiingereza.

    "Asante,nipe kitabu cha orodha ya wafanyakazi wapya" Mzee Kibangara aliposema hivyo,jamaa huyo akatoa haraka kitabu cheusi na kumkabidhi.Baada ya kutazama,akaomba kuingia ndani mgodini ambamo shughuli mzima ya uchimbaji inaendelea.kweli wakaingia ndani na Mzee huyo akaanza kutazama wafanyakazi jinsi wanavyomaliza nguvu zao bila ujila.Kila aliyemtazama usoni amekunga uso kwa hasira na chuki za wazi kabisa.Wahakumpenda hata siku moja.Hali ikawa tofauti baada ya kumfikia mama Ramadhani,Mama Ramadhani alipomuona tu Mzee kibangara akasonya kwa nguvu na kuanza kumtupia matusi mazito.



    "Mwanaume una roho mbaya sana wewe,ni ninakulaani,Mungu atalipa haya yote unayotufanyia na lazima kisasi kitakuja,Mwanaizaya wee,mwanaalamu mtoka pabaya"Mama Ramadhani akazungumza kwa hisia zilizonyanyika na hasira mbele ya mzee huyo mwenye ukatili wa kiwango cha juu.



    "Haha hapo mama dua la kuku halimpati mwenye hata siku moja" Mzee Kibangara akasema maneno hayo na kuondoka kwenye eneo hilo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Wasaa wa kumpumzika kwa dakika chache ukawaendea watumwa hao ambayo hata siku moja hawajawahi kuliona jua,hii ni kutokana na kuishi chini kwa miaka mingi,hawakupata kujua mwanga wa jua unafananaje zaidi ya mwanga wa taa kubwa zilizomulika mgodini kote na kulifanya giza kutoweka kabisa ndani humo.



    Dakika chache hizi ambazo zilitunukiwa kwa wafanyakazi,Mama Ramadhani akatoa khanga yake ya juu na kutandika ili hali apate kumkumbuka Mungu japo hata kwa dakika tano hizo.Mama Ramadhani akaanza kuswali kwa upesi kabla ya watu hawa wanaharamu hawajaja kumharibia swala yake.Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu Mama Ramadhani akamaliza swala yake salama na kukunja kanga yake kisha kengere ya kuendelea na kazi ikaendelea.



    "Maskini mwanangu tangia nimuone akiwa na miaka tisa,sijui atakuwa katika hali gani maskini" Mama Ranadhani akaongea kwa uchungu huku akimkabili mwenzake aliye pembeni yake akichangua baadhi ya mawe yanayochimbwa.



    "Usihofu ipo siku moja Mungu atatufanyia wepesi inshallah tutaiona tena dunia" mama huyo akajaribu kumliwaza Mama Ramadhani japokuwa ilikuwa ngumu kuamini kama kweli watakuja kutoka katika shimo hilo.



    ******



    "Wewe utakaa hapa halafu mimi nitakuwa upande wa pili,hakikisha unamuweka kwenye target nzuri,nakuaminia sana Ram boy" Jerry akasema kwa msisitizo huku akimuacha Ramso kwenye ghorofa ndefu ambayo inamuwezesha kuweza kumdungua mhusika wao.Mwili wa Ramso ukapatwa na joto huku akitazama umati wa watu ulioendelea kumiminika katika uwanja huo,ambayo utatumiwa na Barozi wa Marekani nchini Liberia.



    Ramso akatoa kifaa kidogo cha mawasiliano na kujiweka sikioni,akakiwasha na mawasiliano baina yake na Jerry yakaanza kupamba moto huku wakijuzana kila kitu kinavyoendelea.



    Katika uzoefu wa miaka takribani mitano katika kazi hiyo ya kifo mkononi,hakuwahi kuona uzito wa kazi kama ile akiyopewa na Jerry.Kitendo cha kumuua Barozi huyo wa marekani basi wazi kuwa lazima utakuwa mwisho wake wa kuishi katika dunia hii.Anajua fika kwamba wamarekani ni wazoefu na wataalamu sana kutumia Majasusi ambao hutafiti jambo kwa kina na kuweza kubaini wapi anapatikana na kumnasa mapema mno.



    Raia bado wanaendelea kumiminika katika uwanja huo huku gari kadhaa za wanajeshi na askari wa usalama ambao wameweka ulinzi wa kutosha na kuhakikisha kuwa hakuna uchafunzi wowote ambao utajitokeza uwanjani hapo.Mbwa wengi wenye uwezo wa kunusa na kubaini wapi mahali yalipotengwa mabomu,wakaendelea kunusa kila sehemu ya uwanja huo.



    "Ramso Ramso" Jerry akaita kupitia kipasa sauti cha Ramso na kumfanya Ramso aitike.



    "Nakupata kaka"



    "Umeona hizo gari zinazoingia?"

    "Ndio bila shaka"



    "Sasa hao ndio viongozi wa nchi hii,baada ya dakika kumi mbele ndio ataingia Raisi na Barozi huyo wa kike,ni wa kizungu kama vilivyokuonesha pichani" Jerry akatoa maelekezo kwa kina kabla kazi yao haijaanza.



    "Sawà sawa nimekupata mkuu" Ramso akafunba jicho moja na kutazama lenzi ya kioo cha bunduki hiyo ya kudungulia,baada ya dakika chache zikaanza kuingia gari zenye askari wengine.Ndipo zikaanza kuingia gari aina ya BMW Zilizofanana kwa kila kitu isipokuwa namba zake za usajiri.



    Ikawawia ugumu kugundua gari ambalo lilitumiwa na Barozi huyo.Lakini kwa upande mwingine haikuwapa shida sana kwa sababu walijua atashuka tu katika gari zao na mhusika wako watambaini.



    Kama ilivyopagwa,gari hizo zikasimama na kiongizi mmoja mmoja akaanza kushuka na kupita kwenye zulia jekundu.Wakafanya hivyo mpaka pale alipokuja kushuka Raisi akiwa na mke wake pamoja na Barozi huyo wa kizungu.



    "Umemuona?" Akauliza Jerry

    "Ndio ndio"

    "Sawa take care,nitakuambia ikifika muda wa kumdungua"

    "Sawa"



    Ramso na Jerry wakaendele kuwasiliano kila baada ya dakika moja wakikihakisha kuwa lazima watimize kazi hiyo na kuvuta pesa ya ajabu kwa tajiri wa kimarekani.



    Hekaheka zikaanza huku kila kiongozi aliyeudhulia katika afra hiyo akapata wasaa wa kujitambulisha kabla ya raisi kuanza kuongea na kumaliziwa na Barozi.Wakati wote huo Ramso na Jerry wapo juu kabisa ya ghorofa ila maeneo tofauti wakitazama mkutano mzima jinsi unavyoenda.Lengo lao ni moja tu,ni kuichukua roho ya Barozi huyo ambaye ataingia kwenye kipaza sauti muda mchache baadae.



    Hakika siku ya kufa nyani,miti yote huteleza.Jasusi mmoja ambaye amevaa miwani ambayo inamuwezesha kuona kwa umbali mrefu,miwani yenye uwezo pia wa kukivuta kitu na kukiweka kwa ukaribu.Akagundua kabisa kuna mdunguaji mmoja ambaye hakukaa sehemu ambayo inatakiwa,kitu ambacho kiliwatia wasiwasi sana askari hayo.Haraka sana wakatuma askari wapatao sita wenye silaha mzito za moto na kuanza kupanda kuelekea kwenye chumba hicho alicho Ramso.

    "Kaka bado dakika tano tumalize kazi yetu" Jerry akasema.Ramso akatazama saa yake ya mkononi na kuanza kuhesabu sekunde huku akiufutilia vyema mshale huo wa saa........





    Zikasalia sekunde saba peke yake kabla ya Ramso kuachia risasi itakayompta barozi huyo.



    "Put your gun down(weka bunduka yako chini)" sauti ya mtu toka nyuma ya Ramso ikazungumza na kuikoti bastola.Moyo wa Ramso ukapwita kwa kasi huku akigeuka nyuma taratibu.Hisia za kujuta kuikubali kazi ile ikaanza kumjia kichwani na kuanza kumlaumu Jerry ambaye amempatia kazi ile.



    Akainuka na kuninua mikono juu akimaanisha kuwa yupo tayari kwa kukamatwa.Akawatazama askari hayo wapatao wawili ambao wamevalia. suti nyeusi.



    "Ayaaaaaaaaaaaa!" Sauti ya maumuvi ikamtoka askari mmoja ambaye alikuwa karibu sana na Ramso.Mkono aliorushwa na Ramso,ukambanika vizuri shingoni askari huyo,akaishika bastola ya askari kwa kasi ya ajabu na kumuwekea tundu la kutokea risasi upande wa sikio la kulia.



    "Shusha silaha zenu chini"Ramso akazungumza kwa lugha ya kiingereza.Askari hao wakashusha silaha zao chini na kunyoosha mikono yao juu.Ramso akaanza kumbuluza askaru huyo kuelekea mlangoni.



    "Nipisheni nitaua mtu" Ramso akazungumza kwa hasira na kuwafanya askari wengine walio nje kutengeneza njia ambapo ikampa Ramso mpenyo mzuri wa kupita.Akaendelea kumbuluza mpaka walivyofika kwenye mlango wa nje.Askari waliobakia hawakuwa na cha kufanya zaidi ya kumuacha akielekea kwenye magari yaliyojipanga katika safu ndefu.Ramso akarusha risasi moja na kuvunja kioo cha gari moja kisha akafungua mlango.Kitendo cha kuingia ndani ya gari tu,askari hao wakaanza kurusha risasi ambayo zilizompata vyema askari mwenye kwenye sehemu za tumbo.



    Akafunga mlango haraka na kukata waya ambao unapeleka mawasiliano kwenye swichi ya kuwashia gari.Akawasha kwa haraka na kuvuta moto mpaka gari ikagonga gari za mbele na kuzisogeza mbele huku zikiacha uwazi wa kutosha.Akakata kona na kuliweka gari sawa,wakati wote askari wote wanashambulia gari hiyo na kupasua vioo.Ramso akaisongesha gari mbele huku akikizana na risasi hizo.Akabahatika kutoka kwenye himaya hiyo,alipotazama pembeni bado maiti ya Askari ambae alipigwa risasi inavuja damu na kulowanisha siti za mbele za gari hiyo.



    Ramso akaongeza gia mara dufu na kufanikiwa kuzimaliza zote,akawa anacheza na spidi huku akiliacha jiji na kuelekea nje kabisa ya jiji hilo.Hakujua anakwenda wapi kwa yeye ni mgeni nchini hapo.Hisia za kukimbizwa na polisi ndio kitu pekee ambacho kinazunguka kwenye kichwa chake,kwani askari wa kimarekani hutumia njia yoyote ili kufanikisha kumnasa mharifu wao.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Ramso nimekwisha sasa"akazungumza peke yake huku ananyonga msukani na kukota kona ambayo imemkabili mbele yake,kwa kuwa alikuwa kwenye mwendo kasi akajikuta anaikosa kona na gari ikawa inaelekea porini.Kupoteza kwa muelekeo huo sasa akaanza kulidhibiti gari hilo na kuanza kugonga mawe makubwa kiasi ambayo yalikuwa mbele yake.Hakuliweka sawa vizuri akashtuka anakutana na korongo,moja kwa moja gari ikaingia ndani ya korongo hilo lililojaa mawe na miti.Gari ikawa inagonga miti na mawe kiasi kwamba ikawa inabonyea na kumkandamiza Ramso aliye ndani ya gari hilo.



    Baada ya kujigonga sana kwenye mawe na miti mingi,ikafanikiwa kutulia lakini matairi yote yakawa juu kabisa.Ramso damu ikaanza kumvuja huku akihisi kifua chake kinakosa hewa ya kutosha,msukani uliopinda ukamkandamiza ipasavyo kwenye kifua chake.Hakuwa na uwezo tena wa kujichomoa ndani ya gari hilo ambalo limekunjamana na kuwa kama limekanyagwa na kifaru.



    ******



    Jerry hakuamini kabisa kama rafiki yake kipenzi Ramso ametiwa mikononi mwa polisi,moyo ukawa unamuuma mno,atawezaje kuiambia familia yake,kuwa Ramso hana naye tena yupo kwenye mikono ya nguvu ya askari wa Liberia.



    Akiwa na mawazo mazito akafungwa breki nje ya bar kubwa,na kuanza kupiga hatua ndogondogo huku sura yake ikiwa chini kwa uchungu aliokuwa nao.Jambo hilo hakuweza kumshirikisha mtu yeyote,kwani kyfanya hivyo ni kufichua siri ya mpango wake.Akafika kauta na kuagiza pombe kali chumba mbili,akaishika chupa moja na kuifungua,akainywa nusu kwa mkupuo.



    "Kaka kunywa taratibu,pombe kali hizo" sauti ya kike ya mhudumu ikamfikia vizuri masikioni mwa Jerry.



    "Wewe kazi yako ni nini hapa?"swali hilo la Jerry likamstajaabisha mhudumu huyo na kufanya aulize.



    "Una maana gani?" Mhudumu akauliza

    "Nakuuliza unafanya kazi gani hapa" Jerry akauliza tena swali lake.



    "Ni muuzaji wa hivi vinywaji"mhudumu huyo akajibu na kufanya Jerry acheke kidogo.

    "Haha ahaa kumbe unajua kuwa kazi yako ni kuuza na sio kuwaimiza wateja wasinywe pombe kali" Jibu la Jerry kwa mhudumu huyo,likamfanya,atuluie tulii,akamuacha Jerry akajimiminia pombe hiyo bila kumpumzika.



    Alipohakikisha kuwa kichwa chake kimetulia kidogo akachukua pochi yake na kumlipa mhudumu huyo kisha akainuka na kuanza kuwlekea kwenye gari lake kwa mwendo wa kuyumba,Jerry akayumba huku na huko lakini hakuanguka,akaingia kwenyw gari lake na kuliwasha na safari ya kuelekea nyumbani kwake ikaanza.



    Alipofika nyumbani kwake,akafungua mlango kimya kimya na kuingia chumbani kwake,huko akamkuta Flora akiwa amejilaza nywele zake ndefu zikiwa zimelala vyema kwenye mgongo wake.Mtoto huyo wa kirwanda alimpagawisha kisawasawa Jerry.Jerry akaamua kuvua nguo zake za kazi na kuingia bafuni akajimwagia mji kisha akajitupa kitandani huku akiwa na mawazo tele kichwani,japokuwa alikunywa pombe kali lakini hakuweza kuyazuia mawazo yasimsetese.



    Msingizi mzito ukanfunika mara baada ya kuutafuta kwa mrefu sana.Akashtuka akiwa peke yake kitandani,mwanga wa jua uliopenya dilishani kwake ukamuonesha wazi kuwa asubuhi imekwishafika.Akainuka kivivu na kitu cha kwanza kukumbuka ni juu ya rafiki yake Ramso.



    "Dady Jerry,Dady yuko wapi?" Sauti ya Gadna ndio iliyomshtua Jerry akiwa anaelekea sebleni.



    "Oooh mwanagu,usijari baba yako anatafuta kitu fulani atarudi leo sawa eeeh" Jerry ikamkazimu afiche ukweli kuhusu Ramso,lakini alijua fika kuwa kuficha ukweli mwisho wake ni matatizo,lakini kwa upande mwingine hakutaka kueleza ukweli ili kulinda siri aliyonayo.



    ******

    NCHINI TANZANIA



    Waziri wa ulinzi na usalama wa nchini Tanzania,akazipata habari zote ambazo zinahusiana na mtu hatari ambaye anamiliki dola yake bila serikali kutambua.Akahutaji kukaa kikao na majeshi yote yanayohusika na ulinzi wa nchi.Mnamo saa nne za asubuhi,bila kusita,wakuu wa idara ya ulinzi wakakusanyika kwa pamoja ili kumjadili mtu huyo hatari.



    "Inakuwaje wanajeshi wanakufa kizembe namna hii,kwa nini msiweke mipango thabiti ili tuweze kumtia nguvuni huyu mtu" waziri huyo wa ulinzi na usalama akaongea na kunyamaza kimya,akasubiri maneno hayo yawaingie vizuri wakuu wa hao,kisha akaendelea.



    "Kifike kipindi,lazima kila mmoja wetu,asimamie kazi yake imara na kuiongoza kwa umahiri,la sivyo tunaweza kujikuta tunaingia katika matatizo makubwa,hii kutokana na sisi wenyewe kufuga majambazi" waziri akangurumana kwa hisia na uchungu na kusababisha jasho lake litoke mwilini na kulowanisha suti yake.Mipango mipya inayopangwa juu ya Mzee Kibangara ikaendelea na huku kila mkuu wa idara,zikiwemo jeshi la Magereza,jeshi la polisi,jeshi la wananchi (JWTZ),zikiwa makini zaidi kufiatilia maneno hayo yenye mashiko ndani yake.



    "Kumbukeni kuwa,serikali ni wananchi,sisi tumesimama kama madereva katika basi la serikali,tunahakikisha kwamba,tatizo lolote linalotokea tunalidhibiti mara moja" waziri huyu ambaye kwa kweli ana machungu juu ya taifa lake akazungumza kwa utulivu na hatimaye wakafikia muhafaka.Mikakati ya kuangamiza ubavu wa Mzee Kibangara ukaanza rasmi.Kila jeshi likatoa msaada wake ili hali wanateketeza hekalu ya mzee huyo.



    ******



    Ni baada ya kuteseka sana kwenye ule msukani ambao ulimbana ipasavyo,akafanikiwa kujitoa japokuwa damu zinaendelea kumvuja.Hakuchukua hata dakika mbili baada ya kutoka kwenye gari hilo,akaanguka chini na kupoteza fahamutena.

    Katika mizunguko ya wawindaji wa nchini humo,wakiendelea kuzunguka ili mradi wapate kijitoweo chochote kile,ambacho kitawawezesha kuendeshea maisha yao.



    Walikuwa wawindaji watatu.Mmoja akiwa ameshikilia upinde na mishale,huku mwingine akiwa ameshika mkuki ulio mweusi sana na wa tatu ameshika panga pamoja na rungu,walionekana ni wawindaji ambao wamebobea haswa katika fani hiyo.Kwa kuwa giza la usoni linaanza kuwanyemelea,wakachukua uamuzi wa kuanza kurudi nyumbani.



    "Mjomba kile nini?" Mmoja wa wawindaji hao akauliza huku akielekeza kidole chake sehemu ambayo aliitilia shaka.Wenzake wakarudi nyuma na kutazama sehemu hiyo elekezi.



    "Kama gari bovu hivi"

    "Ile sio gari,lile ni jiwe" mabishani baina ya wawindaji hao yakaanza.Hawakujua kitu kilichopo mbele yao.

    "Sasa mjomba mnabishana nini,si tuende tukatazame"

    Wote wakaafikia na wazo hilo,kwanini waandikie mate angali wimo ungalimo.Wakatembeza miguu yao isiyokuwa na hata kipende kiatu.



    "Shemeji nilikuwambia kabisa kuwa hili ni gari,nawe kwa ubishi wako" mwindaji huyo akasena huku alikizunguka gari hilo.



    "Aja jamani kuna mtu amekufa huku"



    "Mtu?"



    "Ndio"

    Wote wakakusanyika kwa pamoja na kuutazama mwili wa Ramso ambao umelala chini.Hajuwa anajitambua hata kidogo,kumbukumbu hazikumjia hata kidogo Damu nyingi zilimtoka mdomoni na zingine zikakauka kabisa.



    Mwindaji mmoja akainama na kuweka sikio lake upande wa kushoto wa kifua cha Ramso.



    "Ayaaaa mzima huyu,moyo wake unadunda kwa mbali sana,tumkimbize hosptali"



    "Shemeji umpeleke hospitali anamjua huyo?"



    "Acheni kubisha,shika hiyo miguu huko"



    Wawindaji hawa walioonesha kuwa na roho mzuri,wakambeba Ramso na kuanza kuondoka naye.



    Kitu cha kwanza walichokufanya wawindaji hao,wakamuwahisha zahanati ndogo ya kijiji chao.Mipango ya matibabu yakaanza.Nesi akishirikiana na mwenzake.



    "Huyu inaonesha alipata ajari,tazama kifua chake kimechanika kidogo"dokta mmoja akasema.Wakamshina nyuzi tatu za kifua huku wakimwekea damu kutokana na kupoteza sana damu yake ya mwilini.



    Wakati wanaendelea na michakato ya kumponya Ramso,mara kelele za watu toka nje zikawashtua madaktari walio kwenye chumba hicho alicholazwa Ramso.



    "Msogezeni huku na mumpe nafasi ili apate hewa"daktari huyo wa kiume mwenye nguo za kiraia akasema na mgonjwa ambaye alibebwa kwenye machela ya miti akashushwa chini.Damu zinamvuja toka puani na mdomoni huku mwili mzima umemkakamaa.Mgonjwa huyo inaonesha wazi kuwa anasumbuliwa na mgonjwa mkali sana.Wakamuingiza ndani haraka na kuanza kumshughulikia.kwa bahati mbaya hakuchukua hata dakika tano,mapigo yake ya moyo yakawa yanetulia tulii.Hakutazama tena hata kuhema,mauti ilikwishamfika hapo hapo.



    "Ni mgonjwa wa tatu sasa anakufa kimtindo huu huu,hivi ni nini chanzo?" Daktari akajiuliza bila kupata jibu lililo kamilika.Akaingia kwenye chumba alicholazwa Ramso,bado hali yake ni mbaya,hakuwa na dalili zozote za kuzinduka,usingizi wa nusu umauti ndio aliokuwa anapambana nao.



    ****



    "Sitaki sitaki ananibakaaaaaa!" Sauti ya kike iliyotoka kwenye kijichumba kidogo ndani ya mgodi huo.Mwanaume ambaye ameshika bunduki na mwili wake uliojazia,akiwa juu ya mwanamke huyo akimbaka.Matendo ya kunyama na ya kinyanyasaji kama hayo yalikuwa ni ya kawaida sana ndani humo.Wafuasi hao huwachukua wanawake na kufanya nao mapenzi bila hiari yao,tena bila huruma.



    "Kelele nitakuua wewe malaya" jamaa huyo akanguruma kwa sauti mzito ili amnyamazishe mwanamke huyo lakini haikuwa rahisi kabisa kwani kitendo anachofanyiwa hakikuwa cha kunyamazishwa kwa mtindo kama ule.



    Mama Ramadhani,hakuwa na la kufanya kabisa,akamuacha rafiki yake akibakwa na mfuasi huyo ni hali hakuwa na uwezo wa kumdhibiti kufanya jambo kama hilo.



    "Usilie mama,tumuombe Mungu tu atatusaidia" sauti ya mtoto wa kiume mwenye miaka ya kukadilia ipatayo kumi na tisa,akamliwaza rafiki wa Mama Ramadhani ,japokuwa hakuweza kabisa kuzinyamazisha kelele hizo lakini hakukata tamaa kumbembeleza huku akisaidiana na mama Rama.



    Mama Ramso mawazo yakampeleka mbali sana,hatimaye akaanza kutokwa na machozi,akainuka bila kuongea kitu usiku huyo na kujitosa kunako giza.Hakuogopa hata kidogo,kwani moyo wake amekwishauwekea lehani,jambo lolote baya au zuri limkute tu lakini sio kuishi maisha kama yale kwa takribani miaka kumi.Akafika sehemu ambayo imewekwa kamba toka juu,kamba hiyo husaidia katika kuvuka na kwenda juu ijapokuwa sio nje kabisa.Akaitazama mara kadhaa na kuishika kama ile,hisia za kuishi tena duniani zikamuishia na sasa moyo wake unatamani ukapumzishe mahali pema.......





    'Paaaaaaaaah!' Mlio wa risasi ukalia na kumshtua Mama Ramso ambaye alitaka kujitundika juu ya kamba.Zikapita sekunde chake bila hata kusikika kitu chochote.



    "Lala chini wote haraka" sauti ya msimamizi mmoja wa mgodi huo ikasikika.



    "Nataka mueleze wa wapi iliko mama Rama sasa hivi,takata mtu kichwa" Msimamizi huyo akazungumza kiswahili kibovu.Wote wakakaa kimya bila kusema chochote.



    ******



    "Kwa kweli nimechoka nataka kujua wapi aliko Ramso,ni siku ya tano sasa Ramso haonekani,sema kama umemuua nijue niondoke na huyu mtoto" Zulfa akazungumza kwa uchungu huku akimng'ang'ania Jerry shati lake.Hakika Jerry hakuwa na cha kujibu kabisa,ukweli uliopo unashindwa kumpa dhamana ya mzigo aliokuwa nao.



    "Dada Zuu tafadhali sana,naomba utulie kidogo nikueleze ukweli wa kupotea kwa Ramso"

    Jerry akazungumza kwa upole.Hapo Zulfa akatulia na kuanza kumsikiliza Jerry.Bila uficho wa aina yoyote ule,Jerry akaanza kuzungumza mambo yate aliyoyafanya akiwa na Ramso.



    "Sasa tunampaje?" Swali la Zulfa likamtuliza Jerry huku akitafakari jambo fulani.

    Wakati wanaendelea kuzungumza hayo akaingia Gadna toka chumbani,madai yake yaleyale,yu wapi baba yake.



    "Mummy where is my Dady?"

    Hawakuwa na kumjibu zaidi ya kumfariji na maneno matamu tu.



    "Usijari baba yako yupo kwa raisi,kuna kazi anamalizia,si unamjua raisi wewe?"

    Gadna akatikisa kichwa kuashiria kuwa anamfahanu.



    Jerry akaamua kuondoka,kuelekea kwenye jengo lile lile aliloingiliwa Ramso na askari.Akaingia na kukuta watu wengi wanaendelea na shughuli zao.Akaenda mpaka sehemu ya mapokezi na kuwakurmta wahudumu wa kike wawili.Akasogea na kiwasalimia.

    "Habari yenu"



    "Salama tu karibu"



    "Asante,nina shida!,mimi ni mpelelezi toka jeshi la ulinzi,nimeagizwa nije kutazama tukio la wiki iliyopitwa katika Kamera zenu" Jerry akazungumza huku yupo siriaz ya aina yake.Aliposema hivyo akawafanya wadada wale watazamane na kisha wakamjibu.



    "Samahani kaka,sisi hatuhusiki kabisa na kamera" akazungumza mmoja wa madada hao.



    "Labda tukakuitie mhusika mwenyewe" akadakia na mwingine,ndipo alivyokuja mhusika wa kamera hizo.Ni mwanaume aliyekuwa mwembamba kiasi.Jerry akaeleza tatizo lake lakini jamaa huyu akabaki kushangaa tu huku akijijukiza maswali kadha wa kadha.



    "Kamera gani wakati wamechukua askari?" Akasema jmaa huyo.



    "Ahaaa okay sawa" Jerry akageuka nyuma na kutokomea moja kwa moja,alikwishajua mahali pale sio salama tena.



    Siku tatu zikapita bila kujua mahali alipo Ramso.Hisia juu ya kufa kwake zikaanza kuingia ndani ya chumba cha mtima wake,lakini kwa upande mwingine hakutaka kabisa kuyamba nafasi mawazo hayo.Akapiga moyo konde na kuendelea na uchunguze wake wa chinichini.Jioni hiyo akapitia nyumbani kwa mpenzi wake Flora na kumchukua ili waende nyumbani kwake.



    Ukimya wa nyumba yao ukawashangaza sana ,kelele ambazo alizoea Jerry pindi wanapokuwapo akina Zulfa,hazikuwepo tena,hata alivyojaribu kuita hakukuwa na sauti yeyote ya mwitikio.



    "Itakuwa ameenda sokoni au?"Flora akauliza.



    "Hapana huwa sio mtokaji huyu,sijui itakuwa kaenda wapi" maswali mengi akajiuliza ambayo sio sawa na ufikiriaji wake.Akaamua kuingia chumbani kwao ili awatazame.Cha ajabu hakukuta mabegi.Hali hiyo ikaonesha wazi kuwa tayari Zulfa kaondoka zake na mtoto wa Ramso Gadna.



    "Eeh kaondoka na mtoto"Jerry akasema kwa sauti kubwa huku macho yamemtoka mno.



    "Ingia haraka kwenye gari tukamzame uwanja wa ndege" Jerry alivyosema hivyo tu,Flora akaingia ndani ya gari na kuitoa kwa kasi kuelekea airport.Wakati anaendesha,hakuwa na mawazo kabisa kama yupo barabarani,alichokiwaza yeye ni kufika airport na kumkuta Zulfa akiwa na mtoto wa swaiba wake Ramso.Akanyonga kona na kushika barabara iyendayo katika uwanja huo wa kitaifa wa nchini Liberia.



    "Piiiiiiiii! Pipiiiiiiii" gari ya wagonjwa ambalo lilikuwa mwendo kasi likiingia kwenye hiyo barabara kubwa,likapiga honi mfululizo,kuashiria kuwa inaomba uwazi mbele yake.Jerry kwa kuwa hakujari uharaka wa gari hiyo,ndipo alijikuta anagongwa ubavuni mwa gari yake.Mlio mkubwa ukasikika na gari hizo mbili zikaziba kabisa barabara hiyo iendayo airport.Gari ya Jerry imekwisha pinduka mara mbili mzima na kutulia huku tairi zake zikiwa juu kabisa.Kutokana na kugongwa kwa ubavu,tenk la mafuta likapasuka na mafuta yakaanza kumwagika kwa fujo.Taratibu moto ukaanza kudaka gari hiyo huku ukifuata mafuta yalikomwagika.Jerry akiwa na mpenzi wake Flora wapo ndani ya gari wamebanwa kisawasawa,hawana nguvu hata uwezo wa kutoka.Hakukuwa na kitu kingine kinachoendelea zaidi ya kelele za vilio kwa watu waliopata ajari hiyo.Jerry akatazama kwa shida sana na kumtazama mpenzi wake Flora jinsi anavyotokwa na damu nyingi sana huku akili sana.Akageuka tena na kutazama nje,huku akawaona watu mbalimbali wakijaribu kuwanusuru watu ambao wamepatwa na ajari ile.Wakati wanaendelea kunusuru watu hao ghalfa mlipuko mkali ukatokea na watu wengi walio karibu wakarushwa pembeni,papo hapo wakafariki dunia.Gari ya Jerry ambayo ilikwisha daka moto vizuri ikalipuka na kusababisha kifo chake na mpenzi wake Flora.



    Taarifa haraka zikawafikia kikosi cha zima moto,baada ya dakika zipatazo kumi na tano,gari tatu zikaingia na kuanza kuzima moto huo.

    Mpaka ulipokuja kuzimika,watu zaidi ya kumi wakaripotiwa kuwa wamefariki dunia kwa mlipuko huo.Miili yao ikachukuliwa na kupelekwa katika hospitali ya taifa ya Liberia.



    ****http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Homa ya ghafla iliyompata Ramso,ikawachanganya sana madaktari wa Zahanati hiyo ambayo alifika siku kadhaa zilizopita baada ya kuokolewa na wawindaji wasamalia wema.Siku moja wakiwa wanaendelea na matibabu ghafla hali ya Ramso ikabadilika mno,joto la mwili likapanda,maumivu ya kichwa yakamzidia zaidi,tumbo nalo halikumuacha hivihivi,nalo likawa linajinyonga na kumvuta mno.Kilichowashangaza mno madaktari ni zile damu ambazo alikuwa anavuja toka puani na mdomoni.



    "Huu ugonjwa,naukumbuka vizuri huu,ulishawahi kuwaondoka watu watatu siku za nyuma,ni hatari huu,hebu tupige simu hospitali ya wilaya waje na gari la wagonjwa" mmoja wa madakatari akasema na hapo ndipo utaratibu huo ukaanza.Manesi wakamchoma sindano ambayo itamsaidia kupunguza makali ya homa hiyo japokuwa kwa kweli hawakujua ni homa ya aina gani.



    Ndani ya dakika kumi gari ya wagonjwa,ikafunga breki nje ya zahanati hiyo na kitanda cha magurudumu kikashushwa toka ndani ya gari na kukiingiza ndani.Ramso akapakiwa ndani ya gari ila safari hii akiwa hana fahamu kabisa.Wakaingia nae garini na safari ya kwenda hosptali ya wilaya ikaanza mara moja.Dripu ya damu ikawa inayoyoma kwa kasi na kuingia kwenye mwili wa Ramso.



    "Huyu kwa kweli sijui kama atafika hospitali" nesi mmoja akazungumza huku sura ya kukata tamaa ya kupona kwa Ramso ikimkauka taratibu.Mpaka wanaingia jimboni na kaunza kuitafuta barabara iendayo airport .Dereva wa gari hiyo ya wagonjwa alikuwa mwendo kasi mno,alifanya hivyo ili aweze kunusuru roho ya Ramso kabla mauti haijamkuta.Wakati amechomeka gia zote,kwa mwali akaiona gari ndogo ikija kwa kasi sana.Licha ya kuwasha king'ora cha dharula lakini jamaa huyo mwenye gati ndogo hakujari hata kidogo.



    "My God" dereva akahamaki na kuanza kuangaika kutokana na gari hiyo ndogo kutojari uharaka wake.Alipokuja kushtuka akajikuta anamuingia jamaa mwenye gari hiyo na ajari kubwa ikayokea..





    Hakukuwa anayejua kuwa,yule aliyegongwa na gari ndogo ni rafiki mkubwa wa Mgonjwa aliye kuwa ndani.Kabla ya kutokea kwa mlipuko huo ambao ulisabaisha vifo vya watu wengi,gari nyingine ikaja eneo hilo mara baada ya kupata ajari na kimchukua Ramso ili wamuwaishe hosptali.Kitu kikubwa kinachopewa kipaumele sana ni afya kwa raia wake,hawakuwa tayari kupoteza maisha ya raia wake kirahisi sana,ndio maana wanapambana katika kulizuia tatizo hilo.



    Ramso akakimbizwa hosptalin ya Taifa na kuwekwa katika chumba maalumu cha wagonjwa mahututi.Kila daktari akawa na pilikapilika,hawakuwa na muda wa kupoteza katika kuokoa uhai wa raia huyo.



    "Leteni mashine ya kupumulia haraka sana" daktari mmoja ambaye hakuwa na nywele juu ya kichwa chake akasema na manesi wakaileta mashine ambayo humsaidia mwanadamu kpata hewa ya oksijeni.Wakamuwekea Ramso na kumdunga sindano zinaweza kumtuliza.



    *****

    Zulfa hakuona haja ya kuishi katika nyumba ya Jerry,kitendo cha Jerry kumpoteza Ramso na bila kutambua wanaweza kumpata vipi,kilimuuma sana.Siku hiyo akayaanda mabegi yake na kufunga kila kitu,si nguo za Ramso,zake na hata za Gadna,akazikusanya na kuziweka katika mabegi mawili.Alipohakikisha tayari mizigo yake imekaa sawa,akafungua pochi yake na kutazama Passport pamoja na tiketi yake ambayo aliikata siku mbili za nyuma baada ya upotevu wa Ramso.



    Ilipohitimu saa moja za usiku akamchukua Gadna na kuanza kutembea huku akiwa na mabegi mawili mkononi.Wakaingia ndani ya taksi,ambayo ikawapeleka hadi uwanja wa ndege.Kichwa cha Zulfa hakikuisha mawazo,labda amemkosea nini Mungu mpaka apatiwe lindo lote la mitihani,aliwaza sana lakini hakupata jibu,Majaribu ya Mungu kwa mja wake,kamwe hayawezi kukwepeka.



    'Zulfa mimi maskini maisha haya mpaka lini,nimekukosea nini Baba,mbona kila kitu mimi tu?' zulfa akawaza mno. Mpaka wanafika uwanjani bado mawazo hayakutoka ndani ya kichwa chake.



    "Dada unaacha begi zako" dereva huyo wa taksi akamshtua Zulfa baada ya kukuona anaondoka bila kutoa mabegi yake.Ni wazi kuwa alikuwa na mawazo yaliyopitiliza.Zulfa akachukua mabegi yake na kuingia mapokezi,baada ya utaratibu wa ukaguzi ya passport kumalika wakaingiza mabegi kwenye mashine ya ukaguzi.



    Mpaka ndani ya masaa mawili mbele,hatimaye ndege aina ya KG fly ikaacha ardhi ya Liberia na kuingia angani huku kila abiria akiwa kimya kabisa na kufuata maelekezo ya Wahudumu.



    ****



    KIBANGARA APATA PIGO



    Baada ya mikakati ya kutosha ya wanajeshi wa Tanzania (JWTZ),wakafanikiwa kuinasa ngome kongwe ya mzee Kubangara.Hawakutaka kukawia,mara moja wakatuma bomu moja la hydogen ambalo,lilitununuliwa kwa gharama kubwa kutoka nchini Marekani Ndani ya dakika moja hakukua na hata kitu chochote zaidi ya shimo kubwa sana.Wakazi ya Bunju baadhi yao wakaaanza kukimbia huku na huko kutokana na tetemeko ambalo kwa kawaida halijawahi wakumba hata siku moja.



    Wafuasi wa Mzee Kibangara waoatao hamsini na nne,waliokuwa wakiendelea na shughuli zao,wakafyekwa na bomu hilo lenye uwezo wa aina yake.



    Mzee Kibangara akiwa nchini Somalia,hakuamini kabisa kama kweli ngome yake imeteketea.

    "Ayayayaya! Sikubali aisee nimesema sikubali,dola milino hamsini nimeteketea hivihivi, i say no! No!" Mzee Kubangara akakemea vya kutosha juu ya hasara alizozupata katika ngome yake.Akazunguka huku na huko,bila ya kutulia,kwa haraka haraka mtu anayemtazama anaweza kusema mzee huyo ni mgonjwa wa akili au kaweuka.Hakika hakuweza kukaa hata kusimama,miguu yake kamwe haikuweza kutulia.Anazunguka jengo zima huku akiyukana kwa matusi makubwa ya kiswahili.



    *****



    MIKAKATI YA KIJESHI YA KUMNASA MZEE KIBANGARA.



    Baada ya kulipua ngome hiyo kimakusudi,sasa wakaandaliwa makomando wapatao sita ambayo wataingia nchini Somalia katika oparesheni ya kumuwinda mzee huyo.Ramani ya ngome nyingine ya Mzee huyo iliyopo Somalia,ikaanza kusomwa vyema na makomando hao ambao walikwisha kula kiapo tangia wanaingia kazi hiyo.



    "Tumeshindwa kufa nchini Cuba,halafu tufw somalia haha haiwezakani kabisa"komando mkuu wa oparesheni akazungumza kwa sauti mzito huku akiandelea kuwapa maelekezo juubya ramani hiyo.wakamaliza kuisoma ndipo walipoanza kuzighulikia silaha zao.Wakazipeki kwenye mabegi na kuvaa ngup maalumu kabisa kwa ajari ya kazi hiyo.



    Safari ilitakiwa ianze saa saba usiku ili wavamie ngome hiyo na kuwanasa wakiwa usingizini.Hawakujua kabisa kama wenzao huwa hawalali,mara nyingi watu hao hupeana zamu ya ulinzi na kushugulikia chumba cha mawasiliano.

    Ikahitimu saa sita na dakika arobaini na tano,komando hao wakaingia kwenye chopa za kisasa zinazoendeshwa na marubani mahili kabisa,safari ikaanza huku marubani hao wakizimiliki chopa zao kwa umakini wa hali ya juu.



    *****



    "Eeeh huyu mgonjwa mbona mapigo yake ya moyo hayafanyi kazi kabisa?"daktari ambaye alionekana mgeni kwa ugonjwa wa Ramso akahoji.



    "Aaah tumemuwekea mashine ya kupumlia,yaani unapomuana ana afadhali"

    Akajibu muuguzi.



    "Tumieni akili nyie,huyu amekufa kabisa,na huu ugonjwa naupata sana,unaitwa Ebola,ni mbaya sana" daktari huyo akazungumza huku akiuchambua ugonjwa huo hatari sana nchini Liberia.

    "Huu ugonjwa ni wa kuambukiza,unaweza kuua ndani ya dakika tano tu"

    Dokta akazungumza na kunfanya muuguzi huyo apeleke mkono kifuani kwa Ramso.Akaona haitoshi,akatoa mkono na kuweka sikio lake kifuani hapo.Hakika hakutaka kuamini kama kweli Ramso ameaga dunia ama laaah.



    "Mmmmh" ukamtoka mguno muuguzi huyo.Akaitoa mashine ya oksijeni na kuanza kumpuliza kinywani.La haula hapo hapo muuguzi huyo akaanza kutokwa na damu toka puani na mdomoni,akaanguka chini puuu! Kama zigo la mawe na ya taharuki ikaingia ndani ya chumba hiko...........





    Wakati tukio hilo linatokea,daktari yule akamlaza muuguzi na kukimbilia nje.Baada ya dakika zipatazo nne,wakaingia madaktari watatu wengine huku wakiwa wamevalia nguo zao ambazo zinasaidia katika kujikinga ili wasipate ugonkwa huo wa hatari.



    "Kwa kweli huu ugonjwa ni hatari sana" daktari huyo akazungumza kwa msisitizo wa aina yake.Wakamtoa muuguzi na kumuweka kwenye chumba cha peke yake.Lakini katika majaribio ya kutaka kuponya uhai wake,hawakuweza kufanikiwa kabisa,kwani walikwishachelewa kabisa kumtibia.



    "Amekufa" daktari akazungumza.



    Ramso akiwa amefumba macho,hakuwa anachokijua hata kimoja huku duniani.



    "Kwa kweli huyu amekufa,toeni mwili wake ukauhifadhi monchali" akazungumza daktari.

    Bila kuuliza kitu chochote,nesi akakizungusha kitanda na kuelekea chumba hicho cha kuhifadhia maiti.



    ****

    Makomando wapatao sita,wakashushwa ndani ya msitu ambao unasadikika kuwepo kwa ngome kuu ya Mzee Kibangara.Anayeenda misheni hiyo hakuwa kwingine bali ni kamanda mkuu aliyefuzu ukomando huko nchi Cuba anaitwa Komando Shaury.Komando huyu hakuwa kuharibu kabisa misheni yoyote ambayo alipewa na wakuu wake.



    Wakaanza kuchanganya kwato zao usiku na mchana kwani walishushwa mbali sana mpaka kuifikia ngome hiyo.



    "Bado kilometa moja na nusu kuikute ngomw hiyo" komando Shaury akasema.Wakafika sehemu ambayo ilikuwa tulivi sana,wakaamua kumpumzika hapo kwa kuwa giza lilianza kuinyemelea sehemu hiyo.



    "Aisee hapa panatisha sana"

    "Kushinda kule kwenye msitu wa Cuba?"

    "Aaah kule usiongew kabiaa kamanda,hakufai kabisa,mimi nikijuta kuzaliwa baada ya kutupwa kule" waongezi ya makomando hao yakapamba moto lakini hayakuweza kudumu baada ya mkuu wa Mr Shaury kuwapiga marufuku.



    "Mnaongea nini huu usiku nyie,kuweni na akili ya kujiongeza,kwa mfano mtu akitaka kutuvamia hapa mnadhani mtamsikia japo kwa uvunjifu wa vijiti?" Swali hilo la Mr Shaury likaawacha makomando wenzake wakiwa kimya kabisa.

    Wakaongeza kuni na kukoka moto ambao baada ya dakika kumi na tano moto huo ukazimwa na giza likatawala mahali hapo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Asubuhi na mapema kabisa wakaamka na safari ikaendelea,hakuna aliyethubutu kukataa tamaa katika safari hiyo,kwani kufanya hivyo ni kuvunja moja ya sheria ya kijeshi.

    Wakapiga mguu mpaka pale walipokuja kuona kuna kitu kama nyumba ipo kwenye mwinuko.



    "Bila shaka lile ndio ngome lenyewe"akasema Kamanda Shaury



    "Ndio maana hata picha yake inaonesha vilevile" akadakia kamanda mwingine huku akiitazama picha ambayo inafanana kabisa na jumba lile.



    "Haya tuanze kuswaga miguu,tuelekee kule kunako mjengo,ila umakini unahitajika"kamanda Shaury akasisitiza.Wakaanza kutembea kwa kasi huku wakitazama mlima huo.



    *****



    Ndege ya KG fly hatimaye ikaifikia anga ya Tanzania na kuanza kuitafuta airport ya Mwalimu J.K Nyerere.Haikuchukua dakika hata kumi tayari abiria wa ndege hiyo wakaanza kushuka na kuikanyaga ardhi ya Dar es salaam.Mmoja wa abiria hao alikuwepo Zulfa pamoja na Gadna,japokuwa sura zao hazikuwa na furaha kabisa kufuatia kwa kutorudi na Ramso.



    "Dada taksi hii hapa,ina kiyoyozi moja kwa moja" ni sauti za madereva wanaotafuta wateja kwa kuwavutia na maneno mazuri.Baada ya ukaguzi wa mizigo kumalizika,Zulfa akachukua mabegi yake na kumpatia dereva huyo aingize garini.



    "Unafika wapi dada yangu" dereva akahoji na Zulfa akataja sehemu anayohitaji kufika.Gari ikaondolewa na safari ya kwenda Mbezi mwisho ikaanza.



    "Dada inaonekana una mawazo sana kulikoni?" Dereva huyo akauliza

    "Hamna ni uchovu tu"

    "Ahaaa sawa"



    Wakati wanaendelea na maongezo ya hapa na pale,ghalfa gari ndogo aina ya RAV4 ikatokea kwa nyuma na kuigonga gari ya Dereva huyo.Katika mambo ambayo madereva wa taksi hawayataki,ni pamoja na kuharibiwa gari zao kwa maksudi kabisa.Kama ilivyo kwa dereva huyo,akashuka na kumuendea dereva wa gari hiyo.Akamchomoa haraka na kuanza kumrukia vinywa mfululizo.



    "Unaendeshaje gari boya wewe,halafu inaonesha umelewa,nyie ndio madereva majipu" dereva huyo akafoka kwa jazba huku akimshushia dereva huyo makonde mazito.



    "Unajua unampiga Inspekta hapa,nakuuliza tena, una....jua uunampiga nani?" Dereva huyo aliyejitambulisha kwa jina la Inspekta akazungumza kwa sauti ambayo inamuonesha wazi kuwa amelewa na anaropoka maneno yasiyoeleweka.



    "Inspekta wa wapi, nakuumiza leo mpumbavu wewe" dereva akajibu huku akiendelea kumpa ngumi zilizomfikia kisawasawa Inspekta Makurumla.Zulfa kupitia kioo cha upande wa dereva,akamuona dereva huyo akimpiga Inspekta Makurumla kwa macho yake.Akatambua kuwa kuna balaa kibwa linakuja mbele yake,kama sio kukamatwa na polisi kwa kesi ya ujambazi ambao aliufanya miezi mingi iliyopita.Akashuka haraka na kishusha mabegi yake bila kumuaga dereva,akapanda kwenye taksi nyingine kuendelea na safari yake huku nyuma akiuacha mzozo mzito baina ya Inspekta Makurumla na Dereva.



    "Samahani sikujua afande" dereva huyo sasa akawa anaomba msamaha mara baada ya kubaini kuwa aliyekuwa anampiga ni askari tena mwenye cheo kikubwa katika jeshi la polisi.



    "Nakufundisha adabu leo,pumbavu zako"Inspekta Makurumla akazungumza na kuwaachia vijana wake.Wakambeba dereva huyo na kuondoka nae mpaka kituoni,huku akiwa na kesi ya kuvunja sheria za barabarani pamoja na kumpiga askari.



    ****

    "Waooooh mpenziiii"Jamila akamrukia Zulfa na kufurahi zaidi,hakuamini kabisa aliye mbele yake ni Zulfa.Upole wa Zulfa ukamuogopesha kidogo Jamila rafiki yake na kupelekea kumuuliza maswali.



    "Vipi Zuu kuna nini?" Jamila akahoji.

    "Ramsoooo!"

    "Ramso kafanyaje?"



    "Kapotea Liberia" Zulfa akasema huku anaangusha chozi,Gadna nae akashindwa kuvumilia na yeye akaanza kumsaidia Zulfa katika kuangusha kilio.Jamila akachanyikiwa sana,aanze nani kumtuliza.





    ****



    Ubaridi mkali unaopenya kwenye makabati hayo ya kuhifadhia maiti,ukampa matesa mno Ramso ambaye hakuwa anaelewa yupo sehemu gani.Hata alivyofumbua macho yake ,akahisi giza ambalo hajawahi kuliona katika maisha yake.Kilichomuacha hoi ni kile chumba alichopo,kilibana sana kupita kiasi.



    "Nipo chumba cha aina gani?" akajiuliza bila kupata jibu.Akajaribu kujivuta kwa nyuma lakini akahisi kuna kani ya mvutano baina yake na sanduku hilo.Hakukata tamaa kwani katika ubongo wake,aliapiza lazima atoke ndani ya kabati lile.Ni nyakati za usiku kabisa,ndani ya chumba hicho cha kuhifadhia maiti,kilichojawa na giza.Jitihada za kutoka kwenye kabati hilo zikaendelea huku Ramso akijaribu kujisukuma kwa ngucu zake zote.Hatimaye msumari uliokuwa unashikilia kabati hilo ukaanguka na kabati likaanguka chini mithili ya gunia la viazi.



    "Eeeeeh" mlinzi wa chumba hicho akashtuka baada ya kusikia sauti hiyo.Akakimbilia ukutani na kuwasha taa,hapo ndipo alihisi kuwa mzimu wa babu yake aliyefariki miaka mia mbili iliyopita,akaanza kupiga yowe na kuanza kutafuta sehemu ya kukimbilia.Ramso kuona hivyo akajiokota haraka na kuelekea mlangoni.Hakuwa mlinzi peke yake ambaye alishuhudia Ramso akitoka kwenye kabati bali hata madaktari nao wakaanza kukimbizana huku wakipiga kelele.



    "Ina maana wananikimbia mimi?" Ramso akajiuliza bila ya kupata jawabu.Akafanikiwa kutoka nje ya hosptali hiyo na kuanza kutembea barabarani.Ramso hakuwa tofauti kabisa na chizi,nguo zake zimemchanika kupita kiasi,nywele nazo zimemtimuka na kuwa ndefu sana.Harufu aliyokuwa anatoa haikuwa safi hata kidogo.Akawa ni kituko ndani ya jiji hilo la Liberia.



    "Dada samahani naomba japo chakula kidogo nina njaa sana" Ramso akazungumza huku akiwa amesimama nje kabisa ya mgahawa mdogo,mbele yake amesimama binti ambaye anaosha vyombo.



    "Kaka samahani mimi mwenyewe nimeomba kazi tu hapa" anaposema hivyo,anaingia mama mwenye mgahawa,anamtazama Ramso kwa dharau na kumuuliza kwa ukali.



    "Wee unataka nini hapa?"

    "Naomba unisaidie japo chakula kidogo dada angu" Ramso akazungumza kwa huruma sana.



    "Nyoo kaombe kwa mama yako aliyekuzaa,mimi sigawi chakula hapa" Mama huyo asiye na huruma akampakulia Ramso kwa maneno ya kejeli.



    "Basi hata maji yankinywa dada yangu" Ramso akazungumza kwa msisitizo.Mama huyo akamtazama Ramso kwa hasira na kuinama,alipokuja kuinuka,Ramso akaolowana na maji yaliyochanganywa na ukoko wa wali.



    "Ma...maa" binti yule muosha vyombo akahamaki kwa kutendo alichokifanya mama huyo.

    "Weee funga bakuri lako" mama akaendelea kuwa mkali.

    "Na wewe sema umetosheka na maji?" Mama ntilie akauliza

    "Ndio mama asante" Ramso akajibu na kuondoka kwa hatua za kinyonge mno.



    "Ama kweli nimeamini kabisa wanaosema kuwa WANAWAKE WAUWAJI,masikini Ramso mimi nitapona kweli na njaa hii,halafu kifua sasa,kidume kifua kimenibana hatari hii" Ramso akazungumza peke yake huku mikono yake akiwa ameifunga kwa nyuma.Usiku wa saa tatu,bado Ramso hakujui anakoenda katika jiji hili la watu,njaa imemkaba mara dufu,hakuwa na senti hata tano ambayo ingemuwezesha anunue japo chakula kidogo apate usingizi.



    "La haula nimeamini kweli maisha ya kufara ni vituko,tazama leo hii Ramso mimi nateseka kwa njaa na ninaonekana kama chokoraa kabisa" Ramso akazidi kuongea peke yake,hakujua mustakabari wa maisha yake.

    "Haki za mnyonge nimeamini kweli lazima zipewe kipaumbele.Maradhi,njaa,mavazi duni, nani atawatetea?"



    Akavuka barabara na kuingia upande wa pili.Huku kidogo akakutana na watu wengi wakijichukulua mazagazaga ya kuwashibisha usiku huo.Akafika mpaka kwa jamaa mmoja muuza keki na kumuomba walau keki moja,lakini alichoambiwa hapo ni bora kule alikomwagiwa ukoko.Maneno machache lakini yakamuingia vizuri kichwani na kuuchoma moyo wake.Hakuwahi kuambia kabisa maneno kama hayo tangia azaliwe,ndio kwanza anayasikia kwa jamaa huyo.



    "Wewe boya huku sisi hatufagilii mashoga,kama unataka kuliwa mzigo amsha mbele huko" akazungumza maneno hayo na kumalizia kwa tusi kubwa la nguoni.Ramso ikamuwia awe mpole,akageuza kwato zake na kuondoka huku akiyanywea maneno ya jamaa huyo.



    Mpaka inafika saa sita usiku tayari amekwishalwgea kabisa,ameivumilia njaa,sasa imwmshinda,ghalfa akaanguka na kuzimia.



    ****



    Kamanda wa misheni Shaury,wakafanikiwa kulisogelea hekalu hilo na sasa wakawa wamejibanza kwenye moja ya kibanda ambacho kipo nje kabisa ya jengo hilo.



    "Sasa maafande,hapa ndio mjengoni,tukifanya mzaha tumekamuka sawa?" Kamanda Shaury akaeleza.



    "Kwanza kabisa lazima tumtangulize Mungu wakati tunaingia katika jengo hili Wazi!!"..

    "Waziiii!" Makamanda wenzake wakaitikia kwa pamoja.Wakazinduka toka kwenye kibanda kile na kuanza kusonga mbele huku wakitumia matumbo yao kutembelea.Kamanda Shaury akawagawa kila mmoja upande wake na yeye akaanza kutambaa kuuelekea geti ndogo kabisa.Jengo hilo halikupanda juu,kwa sababu lilikuwa na uwanja mpana chini ya ardhi.



    "Duuh hii musheni kama ile ya kumsaka Osama Bin Laden"Kamanda Shaury akajisemea.Akaswaga tumbo lake mpaka karibu na geti kabisa.Kwa kuwa ulikuwa usiku hawakupa wasiwasi kabisa katika kuingia kwenye kambi hiyo.Akainuka na kupiga magoti kisha akachunguliwa kwenye kijitobo kidogo.Hapo ndipo alibaini kuwa watu hao wapo bize na kunywa pombe katika ukumbe wao huo.Mziki ambao umefunguliwa kwa sauti ya chini,ukawakoleza kupita kiasi.Ni kosa moja kubwa ambalo wamelifanya jamaa hao.Kamanda Shaury akachukulia udhaifu ule na kutaka kuingia ndani kwa kuvunja waya ambao unashikilia geti hilo.Wakati anaandaa mpango huo akajikuta anashikwa na butwaa asijue wapi pa kuanzia.Mapigo ya moyo kaanza kumuenda kasi huku joto la tumbo lake linaongezeka kila baada ya sekunde.



    'Kwa kweli sijawahi kabisa kukamatwa kirahisi namna hii,leo mara ya kwanza kabisa kuingia mikononi mwa hawa wanaharamu,yaani bila papara kidume naenda kuchezea kichapo' kamanda Shaury akajisemea huku akiacha silaha yake chini na kunyoosha mikono juu.





    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Lete silaha yako haraka sana,kisha ongoza ndani" jamaa huyo ambaye amevalia kilemba huku mikononi mwake akiwa ameshika bunduki yenye uwezo wa aina yake,akamuamrisha Kamanda Shaury.Ni kosa ambalo alilifanya jamaa huyo,kitendo cha kumuambia kamanda Shaury ampatie silaha,ni moja kati ya nafasi ambayo aliihitaji kamanda shaury.Hakutaka kupoteza kabisa nafasi hiyo,ndipo aliporuka na kukaba shingoni.Kamanda akatuliza mikono yake kwa nguvu zake zote na baada ya dakika chache jamaa huyo akatulia kimya kabisa,alikwishakufa.



    Akaendelea kuukata waya huo na kufanikiwa kuingia ndani Alichokifanya ni kujibanza sehemu yenye giza na kutoa bomu la kutenga kwa dakika.Akalitega mahali hapo na kutoka haraka mno.Wakati wote hakukuwa na hata mfuasi mmoja wa Mzee Kibangara aliyetambua kuwa wameingilia.Ndio kwanza wakaongeza kunywa pombe mara dufu kama wafanyavyo siku za wikiendi.Kamanda Shaury akavaa kufaa cha mawasiliano na kumpata kamanda mwenzake ambaye anahusika zaidi katika suala zima la kutumia kompyuta.



    "Tazama upande wa ndani kabisa kuna nini kinaendelea" Kamanda Shaury akaeleza.Ndipo baada ya dakika mbili jibu likarudi.



    "Nao wapo bize wanakunywa kalinye"

    "Sawa sasa tunaingua ndani sawa?"

    "Sawa mkuu" baada ya kumaliza mawasiliano yao kamanda Shaury akakumbuka kuna mtu mkoja alikwisha muua lakini bado mwili wake upo hadhalani,kitu ambacho kinaweza kusababusha jamaa hao kugunduka kama wamevamia.Akarudi nje na kuuvuta pembeni kabisa.Akamvua nguo na kujivesha yeye huku zake akiziweka ndani ya begi.Akamakizia na kilemba,sasa akwa anafanana kabisa na jamaa hao.Akili ya kujichanganya na jamaa hao ikamjia na ndipo akaingia bila wasiwasi huku akidundika mno.Akafika eneo lile na bila kuuliza akachukua chupa moja ya bia,akaanza kunywa bila kusema kitu chochote huku mara chache akichunguza jinsi gani anaweza kupata mlango wa kuingilia ndani.Baada ya kuchunguza sana akafanikiwa kuuona mlango ambao hutumiwa na jamaa hao kutoka na kuingia kuja katika kumbi hiyo.Akaingia huku akipishana na wafuasi hao bila kufahamika.Njiani akawa anasalimia na jamaa hao kwa kukutanishana ngumi zao.Akazidi kushuka chini kabisa mpaka akakutana na kumbi moja kubwa ambayo imejaa wafuasi wakicheza mziki na kunywa pombe kali,akatazama huku na kule asijue nini cha kufanya.Mara akatokea msichana wa makamo na kumtaka kamanda Shaury acheze naye.Kweli akakubali na kujitosa uwanjani.



    'Loooh ananikumbusha mbali sana huyu binti,enzi hizo tunahitimu mafunzo ya kikomando nchini Cuba, wallah nikayarudi na kuyaruka majoka kama sina akili mzuri,leo tena nayaruka huku tena kwa wanaharamu' kamanda Shaury akajisemea huku akicheza taratibu.Akachukua nafasi hiyo kuaanza kumteka binti huyo na kuanza kumuuliza maswali ambao anayaona kuwa yanaweza kumsaidia katika hangaiko la kumpata Mzee Kibangara.



    "Mrembo...bosi yu wapi?" Kamanda Shaury akaukiza kwa lugha ya kiingereza.



    "Nimemuacha chumbani anajiandaa" akajibu.Kamanda Shaury akakumbuka kabisa katika mafunzo ya kikomando,kuna vitu unabidi uvielewe wazi pale unapomuhoji adui yako lazima uangalie na mazingira yalivyo,kitendo cha binti husema kuwa mzee Yupo ndani,akajua fika kuwa kuna kitu kinaendelea ndani hapo.Kama sio sherehe basi kuna kitu kinaendelea.



    "Okay sawa unaweza kunipeleka,nina ujumbe wake"Kamanda Shaury akasema.



    "Noo haruhusu mtu kwenda chumbani kwake anapojiandaa" binti huyo akasema huku akiendekea kucheza mziki.



    Baada ya dakika zipatazo kumi,mziki ukazimwa na MC wao akatangaza ujio wa Mzee Kibangara.Hapo ndipo kichwa cha Kamanda Shaury kikaanza kucheza kwa kasi.Labda aanze wapi na wenzake bado hawajaonekana mpaka muda huo.



    ******

    Jiji hilo la Liberia,likawa chungu na baya zaidi kwa upande wa Ramso,kifua pamoja njaa iliyokuwa inamtafuta sana ikawa ndio kawaida kwake.Hakupata kujua namna gani anaweza kupata msaada wowote.Katika kuwaza na kuwazua ndipo akajikuta anamkumbuka rafiki yake Jerry,lakini anajikuta anaishiwa nguvu baada ya kugundua kuwa hana kumbukumbu ya namba ya Jerry.Akajifikirisha tena na tena,ndipo wazo la kimtafuta Zulfa likamjia.Je anawezaje kupata simu ya kupiga?.Akawaza pasi kupata jibu.Safari yake ya kutafuta simu ikaanza,haikuchukua muda sana kukamilisha zoezi hilo,akafanikiwa kuipata na kupiga namba ya Zulfa.

    Bahati haikuwa yake kabisa,kwani namba ya Zulfa haikupatikana,hata alipojaribu zaidi ya mara tano ama kumi mzima,jawabu likabaki kuwa lile lile.Akajikuta anakata tamaa kabisa.



    Hakuwa na jinsi,kwani siku zote mficha uchi hazai,akachukua uamuzi wa kujiunga na ombaomba wakaao kando ya barabara.Ramso nguvu zimemuishia kabisa,hana kitu cha kuingiza mdomoni.



    'Nisipofanya hivi,Ramso mimi wanaweza wakanizika hawa' akawaza.Uzuri wa Liberia,watu wengi huwajari sana ombaomba hao,huwa haipiti dakika tano kabla ya mtu kudondosha bega lake na kutoa sadaka yake aliyokuwa nayo.Mpaka inafika saa kumi na mbili za jioni,Ramso akajipatia walau pesa kidogo ya kujipatia chakula.Siku hiyo akaenda kwa mama ntilie.Akaagiza chakula kilichomtosha na kuanza kukivamia kama mtu aliyeishi na njaa kwa muda wa siku tatu..



    "Asante mama"

    "Hunywi maji mwanangu?" Mama huyo akamuuliza Ramso kwa huruma sana.



    "Naomba tafadhali" Ramso akasema nankupewa jagi la maji.Katika kitu kisicho cha kawaida kwa mama huyo ni baada ya kumshuhudia Ramso anakata jagi la maji lenye uwezo wa kubeba glasi sita.Ramso akarudisha na kumshuruku mama huyo,akageuka kinyonge ma kuanza kuondoka kwenye mgahawa huo.



    "Sasa unakwenda wapi?" Mama ntilie akauliza.

    "Hata sijui napoenda mama yangu" Ramso akajibu huku tabasamu dhaifu likitoka kwenye sura yake.



    "Mmmh haya mwanangu" akazungumza mama ntilie huku akiwa na huruma mno kwa Ramso.



    Ramso akaondoka usiku ule na kuzama kusikojulikana kabisa.



    Katika oparesheni zinazoendeshwa na vijana wachache ambao wanashirikiana na baadhi ya askari wa nchini humo,bado ikaendelea huku vijana hao wakiwa na shughuli za kuwakamta vijana wenye nguvu na kuwasafirisha mpaka Somalia,huko hukutana na kazi nguvu za mgodini pamoja na mateso makali tena ya aina yake. Mradi huo wa kuwakamata vijana wenye nguvu ametua nchini Liberia ukiwa na muda mchache zana.Vijana hao hupendelea zaidi kufika nyakati za usiku katika mkusanyika wa vijana na njia nyingineno kisha husafirishwa kwa ndege ndogo ya binafsi.



    Tayari dau la dolla laki tatu likatolewa na Mzew Kibangara juu ya hitajiko la nguvu kazi ili hali shughuli zake zikue zaidi na zaidi.Dau hilo likatua mezani kwa kijana mmoja hatari sana anayeitwa Don Jungle,huyu ni kijana aliyebobea katika masuala ya utekaji na uuaji nchini humo.Hata baadhi ya vyombo vya dola vikamshindwa kabisa,kutokana na uwezo aliokuwa nao.



    Akiwa katika ofisi yake,mbele ya meza yake kukiwa na vijana walioshibiana wapatao sita,wakipata maneno kutoka kwa Don Jungle na baada ya dakika mbili mbele,mlango ukafunguliwa na mtu aliyevalia nguo kabisa za polisi,huku begani akiwa na nyota mbili,akaingia na kuketi kitini.Hakukuwa aliyezungumza kitu.Don Jungle akamtazama Jamaa huyo na kitikisa kichwa kuashiria kuna kitu kakielewa.Akafungua brifikesi ma kutoa dolla laki moja,akamkabidhi polisi huyo na sasa wakaanza kuzungumza.



    "Saa kumi na mbili juu alama nitawaandaa vijana wangu kwa hiyo kazi,hawa vijana wako wana silaha?" Akauliza polisi huyo.



    "Ndio afande,hilo ondoa shaka kabisa" Don akazungumza na kumfanya polisi ainuke na kuondoka zake .Tayari wamekwishakatiana pochi,hakukuwa na bughuza yoyote kwa polisi juu ya misheni yao.



    Kama kawaida yao,huwa ifikapo saa moja usiku,huchukua gari lao ndogo lenye uwazi nyuma na kuanza kutembea kuelekea katika makutano ya watu,hususani katika kumbi za starehe au vijiweni na.



    "Simamisha hapo hapo" mmoja wa watekaji hao akazungumza na gari ikasimamishwa.Wakachomoka watu wawili na kuanza kuwavia vijana hao.Haikuchukua muda wakawa wamewazinguka vijana saba na kuwaingiza ndani ya gari,mmoja wao akachukua kutambaa kilichochanganywa na madawa kisha akafuta usoni kila mmoja wao.Haikupita dakika tatu wote wakawa wamelala kabisa usingizi.Gari ikaendelea kujongea na kwenda mbele zaidi.Punde wakafika sehemu ambayo walalahoi hupendelea kuka na kuzungumza.Wakafika hapo na bila kuuliza wakawazunguka na kuwabana,hakukuwa na hata mmoja aliyepata kukimbia.Katika vijana wao,mmoja wapo ni Ramso ambaye alishikwa na kuingizwa ndani ya gari.Mpaka inafika saa sitabza usiku,jamaa hao wakafanikiwa kuwapata vibarua zaidi ya ishirini.Wakaingizwa ndani ya ndege huku wakiwa hawajitambui kabisa.



    *******

    Ukweli siku zote utabaki kuwa ukweli na damu ni mzito kushinda maji Ramso hakuamini kabisa kama siku moja atakuja kukutana na mama yake nzazi Ndio mara ya kwanza tangia aachane na mama yake na yeye kukimbilia Dar es Salaam,huko akakutana na vijana wenzake wenye ushawishi mkubwa wa maneno na kujikuta akizamia nchi ya watu Afrika Kusini.Ikawa ndio mwisho wa kumuona mama yake.Akabahatika kurudi tena nchini Tanzania akiwa kama mfanyakazi wa kukodiwa na Mzee Kibangara.Hapo ndipo kizaazaa kikamuanzia.



    Wakati huo anaingia nchini Tanzania baada ya miaka takribani kumi na miezi yake.Akakutana na wafanyakazi wapya,hapo akapata kuungana nao japokuwa hali ikaja kuharibika mara baada ya Ramso kugundua kuna matatizo makubwa katika kuifanya kazi hiyo.Akamkubuka Zulfa jinsi alivyoingizwa katika matatizo makubwa.Zulfa akiwa kama mfanyakazi ya supamaketi ambayo walitakiwa kuivunja,wakamtonya binti huyo na kuwasaidia katika kazi ya uporaji,hali ikaja kubadilika mara baada ya polisi kuingilia kati na kuanza kupambana nao.Baadhi ya wafuasi wakapata nafasi ya kukimbia na wengine walipigwa risasi na kufariki papo hapo.Ramso akiwa na mfuasi mmoja wakatumia njia ya kumteka Zulfa ili kuficha ushahidi,lakini kabla hawajafika mbali,ndipo mfuasi huyo anashtukizwa na risasi ya kichwa na kufariki.Sasa wakabaki Zulfa na Ramso ndani ya gari wakikanyaga gia na kuelekea ndani ya msitu mnene.Askari nao hawakuwa nyuma,wakaifukuza gari ile ambao inaendeshwa na Ramso kwa kasi sana.Inspekta Makurumla ndiye askari pekee aliyekuwa akiendesha msako hao.



    Ramso akamtazama mama yake na kuachia tabasamu.Naam! akaamini kuwa mama yake alikuwa amechoka tena sana kuishi maisha yale ya ugumu namna ile.Ndipo akainua kichwa chake kisha akamfuta matone ya machozi yaliokuwa yanamtiririka Mama huyo ambao moyo wake ulikwishakata tamaa kabisa ya kumuona mtoto wake.



    "Mama ikawaje mpaka ukaja huku mamaaa!?" Ramso akauliza na safari hii ikawa zamubyake kuangusha chozi,mama Ramadhani nae akafanya kama alivyofanya mtoto wake,akainua viganja vyake na kumfuta machozi.



    "Mwanangu ni hadithi ndefu sama" Mama Rama akazungumza na kumfanya Ramso amtazame.



    "Niambie japo kwa kifupi tu mama" Ramso akasisitiza.Ndipo mama yake akakohoa kidogo na kuanza kusema.



    "Lakini kabla yoyote lazima utambue kuwa huyu anayetutumika namna hii ni baba yako mzazi,tena nimezaa naye watoto wawili,yaani wewe una mwenzako"



    Maneno ya mama yakamuacha kinywa wazi Ramso huku akishindwa kuyazuia machozi yake na kuanza kuvuja bila kipingamizi cha aina yoyote.

    Kabla mama Ramso hajafunua kinywa tena na kutaka kuzungumza,mara kengere ya kasi ikapigwa na watu wakaanza kuchukua vifaa vyao.



    Siku ya kumi sasa tangia aingine ndani ya chimbo hilo lenye mateso makali na tena linamilikiwa na baba yake wa kumzaa Mzee Kibangara,kwa uzoefu wake wa kukaa ndani huko kwa siku hizi chache,akafanikiwa kuisoma ramani ya mgodi huo na njia mzuri ya kutorokea.Akatazama huku na kule na kubaini kuwa kuna mlinzi mmoja tu katika eneo alilopo,mlinzi huyo ambaye ameshika silaha yake kali,akavuta sigara yake na kutoa moshi mwingi puani na mwingine mdomoni.Mdomo wake wa juu ukiwa umenakshiwa kwa mustach,akatazama huku na kule ni hali anasimamia kazi inayomuhusu.



    'Mpige muue unasubiri kitu gani,kwani ana faida gani kukaa hapa duniani?'

    Maneno haya yakapita vyema kwenye moyo wa Ramso na huku taratibu akipata hamasa ya kuchukua uamuzi wa kushika sululu lakw na kumchimba nalo mlinzi huyo na lengo la maneno toka moyoni mwake liweze kutimia.Kweli kipensa roho hula nyama mbichi.Hakujari kabisa kama kuna kikundi kikubwa cha wafuasi wa mzee kibangara.Maamuzi ya Ramso hayakukawia,ndipo alipochomoka na kumrukia mlinzi huyo huku akimkaba kooni kwa nguvu zake zote,baada ya dakika kadhaa,mwili wa mlinzi huyo ukatulia tulii,ni wazi kuwa tayari ameagana na dunia hii pamoja na madhambi yake.Baadhi walioshuhudia tukio hilo,wakamtazama Ramso na kuachia tabasamu hafifu,hakuna aliyeamini kama kweli Ramso angeliweza kuua kirahisi tena bila kelele kutokana na wembamba wake.Haraka wakamsaidia Ramso kuuvuta mwili huo na kuusogeza kabisa sehemu iliyopo shimo kubwa na ndefu,wakautupa mwili huo na kuendelea na kazi.



    Muda huo huo wakaingia wengine wawili wakiwa na silaha zao,nao wakaanza kukagua mwenendo wa kazi.Moyo wa Ramso kilikwisha vaa umafia na ukatili,kichwa chake kikawa kinawaza kuua tu na sio kingine.Mwenzake aliyopo pembeni akapenua mboni za macho yake na kumkonyeza Ramso,mkenyezo ambao ulikuwa na dhamira ya kitu fulani kinachopaswa kitekelezwe ndani ya Muda mfupi.Ramso akamtazama mwenzake na wote wakijikuta wanafinyiana macho.Walipojitazama wote mikononi mwao wakabaini kuwa wana silaha zenye ncha kali,bila ajizi Ramso akarusha sululu hiyo na kumtandika nayo mlinzi aliye karibu yake,Sululu ikatua kichwani na hapo hapo mlinzi akaanguka chini.Katika hali ya kumshangaza Ramso,mara baada ya kumchimba sululu ya kichwa,alitegemea sana kuona mtu mmoja tu akianguka mahali pale,lakini akastaajabu baada ya kumuona mlinzi wa pili naye akianguka.Wakati anastaajabu hayo yule mwenzake akarusha sululu ya pili iliyomwingia vizuri tumboni.Maiti mbili zikatokea kwa muda mfupi tena kimyakimya.Nazo zikarushwa shimoni.



    *****



    Tahariki ikaingia ndani ya ukumbi huo wa mahakama,hakukuwa na hata mtu mmoja amvaye aliamini kesi ile inaweza kutetewa na kushinda Mzee Kibangara.Inspekta Makurumla ambaye yupo mbele kabisa ya mahakama hayo kama wakili kwa upande wa kushtaki,akatokwa na macho na kushangazwa mno.



    "Sikubali nimesema sikubali kabisa hapa kuna njama" inspekta Makurumla akazungumza kwa sauti kubwa na kuwashtua baadhi ya watu mahakamani hapo.Hisia za kukata rufaa zikamjia na ndipo kesi hiyo ilipoghailishwa na kuazimia kusikilizwa upya mwezi ujao huku Mzee Kibangara akiachiwa huru.Kitendo hiki kilimuima zaidi Inspekta Makurumla lakini hakuwa na jinsi,kwani sheria ndio inayopaswa kifuatwa katika nchi yoyote.



    Akatoka ukumbini hapo akiwa ana mawazo tele,akapanda gari yake na kuondoka katika eneo hilo la mahakama.



    MASAKI JIJINI DAR ES SALAAM



    Baada ya kughailishwa kwa kesi ambayo iliyokuwa inamuumiza kichwa sana Mzee Kibangara.Sasa wakarejea kwenye jumba kubwa la kifahari huku akiwa na watu wake.Wakaanzisha sherehe fupi ambayo ilirudhuliwa na matajiri wakubwa wa Afrika.

    Moja kati ya hao alikuwa Waziri,rafiki mkubwa wa Mzee Kibangara huku pembeni yake akisindikizwa na jaji ambaye alihusika kuipindika kesi ile.Si chini ya milioni hamsini zikateketea kuiandaa sherehe hiyo.

    Waziri huyo akaanza kuwatambuliza wageni waalikwa kwa Mzee Kibangara,na ndipo Kibangara akafanya hivyo kuutambulisha umma ule juu ya kumtambua Waziri.Bila shaka wote wakafurahia utambulisho

    Sherehe ikapamba moto na kuwaburudisha wengi ndani humo.Lakini furaha yao ikayayuka mara baada ya simu ya Mzee Kibangara kuita na kuisiliza.



    "Whaaaaaat!" Mzee Kibangara akahamaki na kuutazama umma ule ambao umekodoa macho ukisubiri nini kinachoendelea simuni.Kitu ambacho si cha kawaida kikamshtua sana Mzee huyo mara akajikuta analegea mwili na hapo wakamdaka kabla hajafika chini.



    "Sahamanini jamani tunaomba radhi,tusaidiane kumuingiza garini tumkimbuze hosptalini" mmoja wa wafuasi akazungumza na wote wakamnyakuwa Mzee Kibangara na kumuweka garini.Hakuwa anajitambua kabisa kutokana na mshtuko alioupata.Gari hiyo aina ya Hammer ikageuza kwa kasi ya ajabu na safari ya kwenda hosptali ya AGHAKAN iliyopo posta ikaanza mara moja.



    *****



    Matumaini ya kumpata Ramso yakaanza kupotea taratibu kichwani mwa Zulfa,akalazimisha mawazo hayo yafutike japokuwa amemuachia ukumbusho wa mtoto wake Gadna.Wakati wote wa Maisha ya Zulfa hakupenda hata siku moja ije siku akapata shida ya naoma ile,sio shinda ya pesa,sio shida ya chakula ,hapana ni shida kubwa ya kuachwa na mtu ambaye alipenda kumuona wakati wote na kushirikiana katika kila jambo.

    Akiwa hana la kufanya akachukua simu yake na kuenda kwenda namba iliyohifadhiwa kwa jina la Jerry.Amejaribu zaidi ya mara kumi na sasa lakini namba hiyo haikupatikana hata kidogo.Sasa akajaribu tena kwa mara ya kumi na sita lakini jibu likabaki kuwa lile lile la mteja anayempigia hapatikani.Aliamini Jerry ndip msaada pekee wa kumpata Ramso.Uamuzi wa kuondoka Liberia akaanza kuujutia na kuulaani uamuzi huo.

    Akajihisi anakosa amani kabisa ndani ya moyo wake.



    Mida ya saa mbili na nusu usiku,Zulfa,Jamila pamoja na Gadna wao,wakajiandaa kwenda kwenye tafrija ya siku siku ya kuzaliwa kwa rafiki mkubwa wa Zulfa anaitwa Jesca.Wakavaa nguo nzuri ambazo ziliwakaa vyema kwenye maungo yao,kisha wakaingia ndani ya gari yao.Safari yao ikaanzia hapo.Baada ya dakika kama arobaini wakafanikiwa kufika Mbezi beach ambako Jesca anaishi na wazazi wake.Wakafika na kukuta kuna gari nyingi sana za kifahani.Ni wazi kuwa Jesca alikuwa mtoto wa kitajiri.Wakaegesha gari lao nje ya jumba hilo na kuingia ndani.



    "Waoooh jamani Zulfa wangu" Msichana aliyevalia gauni jekundu lililopendeza sana akazungumza kwa nguvu na kumrukia Zulfa.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Poa mpenzi,umepotea mwaya,mzima lakini?" Zulfa akajibu na kumtupia swali.

    "Mzima karibuni huku"

    Wote wakamfuata Jesca kwa nyuma na kukaribushwa kwa wageni waalikwa.

    Katika hali ya kushangaza Gadna akaanza kumkodolea macho msichana mmoja ambaye amekaa kiti cha tatu kutoka pale walipo kaa akina Zulfa.Sura ya binti huyo anaufananisha sana kama kuna sehemu aliiiona.Akamshtua Zulfa na kumuoneshea kidole msichana huyo.



    "We una nini Gad?" Zulfa akauliza huku akitazama kule anaoneshewa kidole na Gadna.



    MWISHO



0 comments:

Post a Comment

Blog