Search This Blog

Thursday, November 24, 2022

MKUKI KWA NGURUWE - 1

 

     

     

     IMEANDIKWA NA : MSUYA M MSUYA (EMUTHREE)



    *********************************************************************************

    Simulizi : Mkuki Kwa Nguruwe

    Sehemu Ya Kwanza (1)

     

    Ni kisa na mkasa, chenye mafunzo ndani yake, kinachotokana na ushauri wa kirafiki kati ya marafiki wawili. Ushauri uliokuja kuzaa mtafaruku hadi marafiki hawa wawili wakaja kuwa maadui makubwa wakutaka hata kuuana.



    Ulikuwa ushauri wenye nia njema kwa mlengwa, lakini ….athari zake kwa wengine zinaumiza,…je hao wengine wakiwa ni wewe mshauri itakuwaje….



    Hutapenda kuona rafiki yako akiteseka, utafanya kila hali ili aondokane na shida hiyo, njia mbadala zilishindikana, ikabakia wazo hilo...lililokujia akilini na kumshauri mwenzako, afanye tu, bila kuangalia upande mwingine wa athari zake….



    Kisa hiki ni kumbukumbu za wale wanaoteseka, wenye shida mbali mbali, wenye mitihani ya maisha, wengine wakihitajia kuolewa lakini hawajapata wa kuoa au kuolewa, hawa wanahitajia ushauri, je tuwape ushauri gani…



    Wapo wengine wakihitajia watoto, lakini mola hajawajalia,..au wapo wengine walitendwa na wenza wao, wakaachika, au kuachwa kwa namna moja au nyingine. Wapo waliovumilia..wapo walioshindwa kuvumilia,…, na wapo waliojikuta kwenye njia panda…je tuwapatia ushauri gani…



    Kisa hiki hiki ni maalumu kwako wewe mtoa ushauri, na wewe mshauriwa…tuweni makini sana kwa dhamana hii ya ushauri! Ushauri sio kuongea tu kwa vile…sio wewe utayefanyiwa, sio wewe …hapana shauri ukijiweka kwenye hiyo nafasi , kama ingelikuwa ni wewe..ingelikuwaje…



    Japokuwa unaweza ukatoa wazo hilo kwa nia njema kabisa, ukitaka kumsaidia mwenzako, lakini jiulize huyo atakayetendewa hataumia,…au kama ungelitendewa wewe ungakubali kutendewa, ….maana isije ikawa MKUKI NI KWA NGURUWE TU.



    *************



    Ilikuwa vigelegele vya shangwe, pale nilipofunga harusi yangu, kiukweli ilikuwa harusi kubwa, kutokana na hali zetu, na aliyesaidia kuhakikisha kila kitu kimekwenda sawa, alikuwa rafiki yangu kipenzi…



    ‘Rafiki yangu, mume wako ni bonge la handsome…hapo sitii kasoro, na nikuambie kitu, wewe usisumbuke kwa lolote lile, mwili wako na wangu  kila kitu niachie mimi, muhimu ni gharama, nipatie fungu, na

     

    MKUKI NI KWA NGURUWE TU.*************Ilikuwa vigelegele vya shangwe, pale nilipofunga harusi yangu, kiukweli ilikuwa harusi kubwa, kutokana na hali zetu, na aliyesaidia kuhakikisha kila kitu kimekwenda sawa, alikuwa rafiki yangu kipenzi…‘Rafiki yangu, mume wako ni bonge la handsome…hapo sitii kasoro, na nikuambie kitu, wewe usisumbuke kwa lolote lile, mwili wako na wangu  kila kitu niachie mimi, muhimu ni gharama, nipatie fungu, na wewe kaa, tulia, kama ningelikuwa na pesa, nisingelipenda wewe utoe hata senti moja, lakini nitajitahidi…’akasema‘Ujitahidi kwa vipi, usije kutoa hata senti yako moja, pesa ya harusi hii ilishaandaliwa kwa kila kitu, wewe isimamie tu, na kila kitu nitakukabidhi wewe, nashukuru sana rafiki yangu, wewe ni mimi na mimi ni wewe, …wewe ni rafiki yangu tunajuana, kwa kila hali, nisingelipenda wewe kujiingiza kwenye madeni,… unasikia, ukifanya hivyo utaniudhi…’nikasemaBasi yeye akasimamia kila kitu, nikaja nikafunga ndoa na mume wangu..na maisha na rafiki yangu yakawa ni pale pale, ila alichojitahidi kwa hivi sasa yeye akawa hafiki mara kwa mara nyumbani kwangu, kama ilivyokuwa awali, yeye alifika akiwa na uhakika mimi nipo nyumbani…nilimuelewa, na sio kwamba nilimshuku vibaya hapana ni yeye tu, aliona isje ikajenga fitina…’akaendelea kusimulia. Masiku, miezi, miaka, ikaenda mimi nikajaliwa watoto, lakini rafiki yangu bado akawa hajaolewa , sio kwasababu kuwa hakupata wachumba, hapana, wachumba ni wengi waliotaka kumuoa, lakini yeye akawa hawakubali kutokana na sababu hii na ile, aliyoiona yeye. Na awali sikupenda kumuingilia sana kwa maamuzi yake hayo, maana ninamfahamu alivyo…ana msimamo wake.Lakini siku zilivyozidi kwenda mbele ikabidi mimi niingilie kati, nakuumuliza yeye anataka mume wa namna gani, ..japokuwa nafahamu kwa jinsi tulivyokuwa tukiongea awali kabla ya kuolewa, kuwa yeye angelipenda mume wa namna hii na ile, na mimi nikawa namuelezea hivyo, lakini mimi nilipoolewa nikaja kugundua kuwa ndoto za akilini za kuwa utampata mume mwenye kila kitu unachokitaka ni ndoto tu, aghalabu kuwa kweli…‘Nikuambie rafiki yangu ukweli, huyo  mwanaume unayemtaka wewe hajazaliwa, huwezi kumpata mume wa kila kitu unachokitaka wewe, vingine vitakuja huko mbele kwa mbele, na vingine hutaweza kuvipata hadi kufa kwako, ndivyo maisha yalivyo…’nikamshauri siku za mwanzoni,…‘Usijali rafiki yangu, ipo siku nitaolewa tu, na mume ninayemtaka mimi, hilo la kuwa hajazaliwa halipo,..wapo, ninajua wapo…nitasubiri, ipo siku nitampata , hata hivyo, kuolewa, ni kuolewa, …mimi mwenyewe bado nina malengo yangu..nisingelipnda kukimbilia kuolewa kwanza…’akasemaMaisha yakaenda hivyo, na umri ukakimbia, umri hausemi, …unashangaa sura inabadilika, na majina yababadilika, kijana inageuka mtu mnzima, dada, inageuka kuwa mdada, baadaye…, mama,…mama bila mtoto, baba bila mtoto, mawazo yanaanza kuingia akilini, mawazo..***************‘Rafiki yangu nilimpenda sana, tulianza urafiki tukiwa shuleni, na hata tulipoanza kazi, ninafahamu kuwa mimi nina uwezo kuliko yeye kihali, maisha ya familia yangu yalikuwa juu, mwenzangu alitokea familia ya chini, ninaweza kusema hivyo…’ akaendelea kusimulia‘Mimi nilijitolea kwa kila niwezavyo, rafiki yangu awe kama mimi, kila nilipoweza, akiniambia au hata kama hajaniambia, nilijikuta namsaidia mwenzangu, ilifikia muda kila ninachonunua namnunulia na mwenzangu, kwahiyo tulikuwa kama mapacha..‘Unajua ilikuwa sifanyi jambo mpaka nishauriane na yeye kabla sijafunga ndoa, na baada ya ndoa, ikaendelea hivyo, japokuwa mengine ya ndani ya ndoa ilibidi nisimuhusishe sana,….kama ujuavyo sheria za ndoa zilivyo.‘Lakini hata nilipoolewa, sikuacha hiyo tabia, ya kusaidiana na yeye..ila ikafika muda natakiwa kuwa na familia yangu na mume wangu zaidi, hii hali iliniuma pale rafiki yangu anapokuja ananikuta mimi nipo na mume wangu, yeye hana…iliniuma sana, nilitamani huyo mume awe wetu sote, lakini mmh…hapo pagumu. Baada ya ndoa mambo mengine yalijiweka yenyewe rafiki yangu, alianza kupanga muda wake, ni lini aje kwangu, au lini tukutane naye, hakupenda kuja nyumbani kwangu kama mimi sipo,…sio kwamba sikumiani kwa hilo…au hakupenda wakutane na mume wangu kupata chakula cha mchana bila ya mimi kuwepo, hadi mume wangu akaja kuniuliza ni kwanini;‘Huyo rafiki yako, ni mwaminifu sana, unajua kuna siku nakutana naye, namuomba nimpeleke lunch, hataki, eti kisa hapendi ije kulete fitina , mkaja kukosana wewe na rafiki yako…, sasa mimi ni shemeji yake nitamfanya nini , eti hivi kweli inaweza mimi nikakusaliti wewe mke wangu, kwa rafiki yako kipenzi…’akasema.‘Lakini nyie wanaume hamuaminiki,….mimi namuunga mkono kwa hilo,..hata hivyo mimi sina wasiwasi kamwe na rafiki yangu…’nikasema.‘Ina maana mke wangu kwa kusema hivyo huniamini…?’ mke akamuuliza mke wake.‘Sio swala la kuaminiana hapo, shetani ana mbinu nyingi, …na kwanini ujiweke kwenye rehani ya mitihani, kama unaweza kuikwepa ni bora kufanya hivyo, kuliko kujitwika mitihani hiyo,….’akasema mke‘Ok, nimekuelewa sana mke wangu, lakini nikuulize kitu ni kwanini rafiki yako hakubali kuolewa, yeye ni mnzuri ana umbo la mvuto, anataka nini na umri unakwenda…?’ akaniuliza mume wangu.‘Hata sijui, hajajaliwa bado, siku itafika, ataolewa, ni kweli umri umekwenda, na hata sijui nifanye nini ili ampate mume anayemtaka,…hata sijui…’nikasema.‘Japokuwa yeye ni mnzuri, lakini umri unakwenda mshauri sana rafiki yako, leo anapendeza hivyo, kila mwanaume anamtaka, lakini itafika sehemu hatavutia tena, hayo ndiyo maumbile yaliovyo, atakuja kujijutia muda umeshakwenda…’akasema.‘Najitahidi sana,…hata sijui nimfanyeje tena…’nikasema.Kiukweli rafiki yangu huyo sikuwa na shaka naye hata kama ningelimkuta yupo na mume wangu, ninamfahamu sana kwa msimamo wake…anaogopa sana waume za watu, ….huwa akiahidi kitu kaahidi, na kwangu nilimuona kama sehemu ya ndugu zangu, na hata watu walimfahamu hivyo kwa msimamo wake huo, wa kutokujihusisha na rafiki ambaye ni mume wa mtu. Wanaume wengi walimjaribu wakashindwa kwa msimamo wke huo.*************** Kuna kipindi alimpata mwanaume mmoja wakawa wanakutana mara kwa mara nikajua huyo atamuoa, lakini baadaye nilipomuulizia, akanipa jibu la kukatisha tamaa.‘Yule jamaa sitamkia tena,…hanifai, nilijua ni mtu mwenye msimamo, ..mtu wa matumizi, …lakini kumbe ni nguvu za soda, eti anakuja kunilalamikia kuwa anadaiwa hiki na kile, kwani nilimuambia akope….aah, nimeachana naye…’akasema‘Hilo tu…?’ nikamuuliza‘Wewe unaliona dogo hilo, achana naye, ..mengine sio lazima nikuambie,.hata kama wewe ni rafiki yangu, huyo nimeshambwaga…’akasema na sikutaka kumuingilia zaidi,..nafahamu msimamo wake ulivyo.Kiukweli urafiki wetu ulikuwa ni dhati, na kila mmoja alijua msimamo wa mwingine na hilo ndilo litufanya tuwe hatuyumbi,…lakini ikatokea la kutokea, urafiki ukageuka kuwa shubiri, ukagubikwa na uadui wa kutaka hata kuuana….’akasema‘Kwanini sasa, mimi nilijua marafiki kama nyie, mliojuana, hamtaweza kuachana…?’ nikauliza‘Hapana, yule simtaki tena, hata kumuona simtaki hata aje nyumbani kwangu…,’ akasema wka hasira….kwa kauli hiyo nikawa na hamasa ya kutaka kujua kilichoajiri kati yao wawili,Awali hakutaka kunisimulia undani wa maisha yao, hasa kilichosababisha hadi urafiki wako ukafa na kujenga chuki za kutaka kuuana, lakini baadae akaanza kunisimulia…kilichowafanya marafiki waliojulikana kuwa ni mrafiki wa kweli, marafiki ambao kila mtu alikuwa akitolea mfano kwao, lakini sasa ni maadui wakubwa….***********Miaka ikapita na mimi nikajaliwa kuwa na watoto wawili mapacha wa kike na rafiki yangu akawa akitoka kazini anakuja tunakuwa naye, ananisaidia kuwalea, kiasi kwamba watoto hawa walimuona kama mama yao. Na kwa ukaribu huo, watoto wangu walimpenda sana.‘Nawapenda sana watoto wako, natamani niwe na watoto kama hawa, kwa sura, …natamani mume wangu anizalie kama watoto hawa…’akasema‘Utawapata tu usijali…lakini muhimu uolewe, umri unakwenda, urembo wa msichana una kikono chake…’nikamwambia tukiwa tunaongea…Kuna kitu ambacho anacho rafiki yangu,  alipenda sana kuchagua wanaume…sio kwa wanaume tu, hata vitu vyake akitaka kununua, yeye anachukua muda mrefu sana kufikia maamuzi, atachagua wee, atatoa kasoro wee….mpaka aridhike, itachukukua muda sana..kilichoniumiza ni kuona rafiki yangu haolewi, na umri unakwenda, yeye hakulijali hilo mapema na siku zikazidi kusonga mbele.‘Rafiki yangu ukumbuke umri na urembo wa mwanamke, una kikomo, jinsi unavyozidi kukua, na urembo nao unapungua, ..na ujue mwenyezimungu anakupatia neema zake uzitumie, ukizipuuza, itafika muda atakunyang’anya, na hapo utaaanza kulalamika…’nikamwambia.‘Usijali…ipo sku nitakuambia kusudio langu ni nini…unajua rafiki yangu sipendi nije kuumia,…sipendi nije kujutia,..muda utafika na wewe hutaamini…’akasema‘Hapo sikuelewi, ina maana kuna kitu unanificha…?’ nikamuuliza‘Hapana…wewe niamini tu, siwezi kukuficha kitu , wewe ni mimi na mimi ni wewe,lakini siwezi kukuambia kitu ambacho hata mimi sina uhakika nacho , bado sijawa na uhakika wowote kwa hivi sasa, ni nani na nani wa kunioa, nimtakaye hajaonekana na kila ninayempenda, nakuta keshawahiwa, nashindwa kuelewa ni kwanini…’akasema**************Siku zikaenda watoto wangu wakawa wakubwa, na wanaanza shule, hebu fikiria, miaka mingapi, kama kumi hivi, bado rafiki yangu hajaolewa,…Siku moja mwenzangu huyu alikuja nyumbani kwangu, akanikuta mimi nipo na watoto wangu, huwa nikiwa nyumbani kama nimemaliza kazi zangu , huwa napenda kucheza na watoto wangu, najishusha nakuwa kama mtoto mdogo, tunacheza ile michezo niliyokuwa nikicheza nikiwa mdogo, basi ni faraja kwa watoto wangu. Rafiki yangu akaingia na akawa ananiangalia nikicheza na watoto, aliniangalia kwa makini sana,..nikahisi kama anataka kulia, siku zote huwa ana ujasiri fulani, akija kwa vile watoto wamemzoe kama mama yao, basi watamkimbilia, wataanza kucheza naye, na huku kucheza na watoto yeye ndio kanifundisha…Lakini siku hiyo, haikuwa hivyo, alikuwa akiwa kanywea, hana raha kabisa, ule uso uliojaa ujasiri haupo tena,, watoto kama kawaida yao walipomuona wakamkimbilia, na akasalimiana nao, kiukweli watoto wangu walimpenda sana rafiki yangu huyu, hata yeye, na hakuchoka kuwasifia kuwa ni watoto wazuri, anapenda kuwa na watoto kama hao.Siku hiyo hakuwa mchangamfu kabisa, nikajua kuna jambo, awali nilihisi labda anaumwa, lakini nilipomuuliza akasema haumwi,..nikaona kuna jambo jingine kubwa limemtokea, labda…, ikabidi niwatoe watoto ili nipate muda wa kuongea naye‘Ok.. rafiki yangu vipi leo,…sio kawaida yako, hutaki hata kujiunga tukacheze na watoto kama kawaida yako.., unajua watoto wangu wakikuona wanahisi furaha sana, wanakuona wewe ni mama yao wa ukweli, kuliko hata mimi, vipi leo kulikoni…?’ nikamuuliza‘Oh rafiki yangu jana sikulala, mawazo,….nahisi sio mimi tena,…sikuwa hivi kabla,….’ Nikaona machozi yakimlenga lenga.‘Mhh, usilie bwana, niambie kuna tatizo gani…?’ nikamuuliza.‘Unajua rafiki yangu mara nyingi huwa najipa matumaini, lakini kipindi hiki cha siku mbili tatu, nimekuwa nikiumia sana, nawaza kupitiliza, na hata kujiuliza, ni kwanini, unajua alipo…nitenda yule mwanaume, kunikasaliti wakati nilishapanga yeye ndiye wa kunioa, namkuta na mwanamke mwingine ndani, …imenivunja sana nguvu…’akasema‘Lakini wapo wengine au sio..keshaoa, achana naye….’nikasema‘Kwanini sasa inatokea hivyo, kile ninayempenda, tunakwenda vizuri, baadae hali inageuka, inatokea jambo tunakosana na huyo mwanaume ama awe msaliti, au awe na imani nyingine ya dini, na siwezi kuacha imani yangu ya dini, sasa nifanyeje jamani…yaani hata sielewi, inafikia muda siwaamini tena wanaume, kwanini nisimpate mwanaume kama huyo wako….’akasema‘Utampata tu rafiki yangu, wewe subiria muda utafika…’nikasema‘Yaani hata kwenye ndoto nimeota nakuona wewe upo na watoto wako na mume wako mnafurahi, mimi nipo peke yangu porini, mkiwa, ..oh, mara nikajiukuta nipo kati kati ya bahari nachukuliwa na maji, napiga ukelele, wa kuomba msaada, hakuna wakunisaidia, nikawa nawaita nyie, mje kuniokoa lakini mkawa hamnisikii, nikawa nazama, nikashtuka …’akatulia‘Hiyo si ndoto tu, au…?’ nikamuuliza‘Ni ndoto ndio..lakini nahisi imetokea kwa vile jana niliwaza sana,..mara nyingi najipa matumaini, nikirudi nafanya hiki na kile siwezi sana, lakini jana, sijui ilikuwaje, hawa watu wamenitibua kweli, ..ndio maana sitaki kuolewa…’akasema‘Akina nani tena…?’ nikamuuliza‘Si hawa wanaume..inafikia sasa wananiringia mimi, …kuna mmoja kanibwatukia mpaka hamu yake ikaisha, akafikia kusema, nitaishia kuzeeka bila mwanaume..sawa, labda ana ukweli wake, lakini haya ndio maisha yangu, kama anataka anioe, anioe basi, yeye anasema anataka kunipima kwanza, kunichezea, hapana hilo siwezi kabisa…’akasema‘Kwahiyo, umeshakata tamaa au sio…?’ nikamuuliza Hapo akakaa kimia akiwa kashika shavu ile ya kusononeka, kiukweli kama rafiki yake ilinuma sana, nikamsogelea na kumkumbatia, hapo akalia kweli, hadi alipotulia, nikamwambia akae , najua sasa ile hasira yake imekwisha‘Unajua rafiki yangu, ndio maana nilikushauri awali uolewe na yule mwanaume wa kwanza aliyekuwa rafiki yako, ukamkataa, na hawa wengine ilikuwa sio bahati yako, ni wao walikusaliti, sio kusidio lako, tumuachie mungu tu…’nikasema‘Mhh..ni kweli rafiki yangu sasa kweli naona nimechelewa, maana hata waume nao siwaoni kabisa wanaonifaa, wa umri ninaoutaka mimi hawapo tena, ninaokutana nao, ndio hao wanaotaka kuuchezea mwili wangu, kitu ambacho sikitaki,..natamani atokee mume wa kweli, alete posa, simuoni..wale niliowataka ndio hao wameshaoa…kiujumla kwa sasa sina raha tena…’akasema‘Sasa unatakaje, maana hata mimi sipati usingizi nikikuwazia wewe. Tumejadiliana na mume wangu tuone jinsi gani ya kukusaidia, lakini wanaume tulio-waona wanakufaa, ndio hao wameshaoa, kama ulivyosema, lakini bado wapo wengine, na wewe huwataki, kwasababu zako…na tulijua yule mliyekuwa naye angekufaa, sasa unasema hamuelewani tena,…sasa, tukusaidieje..?’ nikamuuliza.‘Kiukweli, nikikuona hivi, wewe upo na watoto wako, nawazia mbali kabisa, najua nilishakosea, na umri ndio huu umeshakwenda sana....naona jinsi gani ulivyo na raha na watoto wako,....nikiwaona watoto wako najisikia kukosa kitu muhimu sana katika maisha,…’akasema‘Utawapata tu…’nikampa matumaini hayo, lakini moyoni najiuliza kwa vipi.‘Nitawapataje sasa…?’ akauliza‘Kwanini unasema hivyo rafiki yangu, kuwapata utawapata tu, ukiolewa au sio, kwanza muhimu ndio hilo,kuolewa, mkubali mmojawapo akuoe, sasa sio muda wa kuchagua tena…’nikasema hivyo na siku hiyo ikaishia hivyo, na masiku yakazidi , miezi, miaka, rafiki yangu hajapata mume wa kumuoa.Na siku nyingine ambayo naikumbuka sana, akafika kwangu, akiwa hana raha, zaidi ya siku nyingine, nikajua ni yale yale…moyoni nikawa najiuliza nitamsaidiaje, nifanyeje, ningelikuwa na ndugu yangu wa kiume ningelimshinikiza amuoe, lakini sina,, ningekuwa sina wivu, ningemshauri aolewe na mume wangu, lakini nina wivu wa kufa mtu Hata mume wangu hataki kuoa wake wawili alishaniambia,…kwani siku moja nilimtania tu, akaniambia niache kabisa mawazo hayo, yeye hana uwezo wa kuoa mke zaidi ya mmoja, huyo mmoja kwake, anaona ni kazi…ni mwanaume wangu namfahamu hivyo, kweli hawezi, na hataki..sina shaka na hiloSasa nitamsaidiaje rafiki yangu….na katika maongezi ndio likanijia wazo….wazo ambalo lilikuwa ni kisu cha kunichoma mimi mwenyewe…Ni wazo gani hiloWAZO LA LEO: Urafiki mwema ni ule wa kujaliana kwa shida na raha, na mkikutana mnashauriana mambo ya heri, mambo yenye tija, na hakikisha kuwa pale unapotoa ushauri  kwa mwenzako  unampatia ushauri ambao hata wewe ungeliweza kuufanya au kufanyiwa. Usije ukamshauri mwenzako kwenye jambo ambalo kama utakuja kufanyiwa wewe hutakuja kupendezewa nalo. Ilipita muda rafiki yangu akawa haonekani, hafiki kwangu na sio kawaida yake na baya zaidi hata kwenye simu yake nikipiga simpati, kwa hali kama hiyo sikuweza kuvumilia, nikafunga safari hadi nyumbani kwake…Nilipofika nyumbani kwake, sikuweza kumpata, nikauliza majirani wake, wakasema, siku hizi  anatoka asubuhi sana kwenda kazini na anarudi usiku sana,…bado sikurizika na hilo jibu, nikaona nipitia kazini kwake, lakini wakati nataka kufanya hivyo, nikapigiwa simu ya muhimu kwenye shughuli zangu za kibiashara, ikabidi nikatize safari hiyo, moyoni nikijipa matumaini kuwa,.., huenda ana sababu zake za msingi za kufanya hivyo.Baadaye jioni, nikamuona huyu anakuja, alioneka kuwa mnyonge sana, kama mgonjwa, usoni hana raha, uso umesawajika, kachoka, mpaka nikaingiwa na mashaka, nikahisi kuna tatizo, ni lazima kuna tatizo…!Kwa muda huo, watoto walikuwa kwenye meza wanajisomea, kipindi hicho walikuwa darasa la tano,…wakubwa, na watoto wakike hukua haraka!Kama kawaida yao walipomuona mama yao kafika…, maana napenda kumuita hivyo, ‘mama yao’ kwa jinsi walivyomzoea, kwa haraka wakaacha kusoma na kusimama na kumsalimia kwa kumkumbatia, wamezoeana hivyo,  ..na yeye kama kawaida yake japokuwa alikuwa haonyeshi furaha akajitahidi kuongea nao, akawafundisha fundisha hapo mezani, baadae akawaachia kazi za kufanya, halafu…, tukaenda chumba cha maongezi.‘Haya niambie maana hata bila kukuuliza kila kitu kinaonekana dhahiri, kwanini tunafanyiana hivi, urafiki wetu umekwenda wapi…?’ nikaanza kulalamika.‘Rafiki yangu sio kwamba nimefanya makusudi, hata mimi nilikuwa na wakatu mgumu, lakini …kila nikitaka kukupigia, nashindwa, nahisi nitaishia kulia kwenye simu, ..nikitaka nije, ooh…lakini leo sijambo, naona naanza kuizoea hiyo hali, maji yameshamwagika hayazoleki..’akasema‘Mhh..bado, sijakuelewa…’nikasema‘Jana niliwaza sana…baada hayo kutokea, baada ya kujipa muda wa kutafakari kwa kina,…, unajua ni kweli,…nilifanya makosa, na kiukweli …hata sijui nifanyeje, na…na…umri wa mwanamke una ukomo wa kuzaa, na mimi nahisi naendea huko, baada ya kwuaza hilo, niliogopa sana kuwa sasa nimeshazeeka bila ya kuwa na …na…hata kumbukumbu…’akasema‘Mhh, wanasema kitaalamu ndio…lakini mbona watu wanazaa tena wazee tu, ni hivyo kiunjumla, lakini sio kwamba wote watakuwa kwenye hatari hiyo,…kuwa ukizee kw umru huo wa utu uzima ni hatari, hata hivyo…mb- mbona wewe bado tu mdogo, hujafikia kwenye hiyo hatari…, au sio…?’ nikamuuliza‘Mhh…hapo sasa, urafiki wetu ule wa zamani wa kuambizana ukweli naona umepita, kwa vile mimi sasa nimekiri hilo, kuwa…nimeshaze-zeeka, au sio,…naona hutaki kunishauri mambo ya ukweli, kwa ajili tu ya kunipa matumaini, au sio,….’akasema‘Mbona nilishakuambia sana hilo…, nikakushauri sana tu…, nikaona basi nijinyamazie tu, maana nakuelewa sana, wewe sio wa jana kwangu, ukiwa na maamuzi yako huingiliki, hata kama mimi ni rafiki yako, huwezi kubadilika mpaka mwenyewe upende…’nikasema‘Yaani rafiki yangu hilo ndilo limekuwa nikijiuliza akilini mwangu, baada ya kutafakari sana nikaona nije nikuone,...nimegundua kuwa sasa hivi natakiwa nichukue hatua nyingine kabla sijachelewa zaidi…na kiukweli baada ya kutoka hayo, nahisi kipaumbele changu kwa hivi sasa sio mwanaume, ..sio kuolewa, …huu sio muda wa kuwazia kuolewa tena…na baada ya yote hayo, naona ili kuepusha shari zaidi, bora niishi peke yangu, ..kwa kifupi mimi sitaki tena kujiingiza kwenye mawazo ya kuolewa…, nimeshajizoelea kuishi kihivi hivi, kivyangu-vyangu,  kuwa na uhuru wa kufanya nipendavyo…’akasema‘Sizani kama hilo ni sahihi, …hayo sio maisha ya kibina-adamu, lazima kuolewa, ili uweze kupata familia yako, au hutaki watoto,…?’ nikamuuliza‘Watoto…., watoto….mmh, ….yaani umeshanigusa, hilo….ooh, hata sijui nifanyeje…’akasema akiangalia mlangoni, nahis alitaka kuangali akitu ambacho hakioni.‘Ndio, sisi ni wanadamu umri wetu una …mipaka na hatujui lini mtu anaondoka duniani, na ubora wa mtu, uzae utoe mbegu na mbegu zije kuotesha mti mwingine, kizazi kinakua,…au sio, usipozaa hutakumbukwa tena hapa duniani…’nikasema‘Sawa kabisa, hilo ….ndilo lililoniumia jana,…lakini kwa vipi,…na mimi sipendi kuwa mtumwa wa kujipendekeza, eti nikajiangushe kwa mwanaume kuwa yamepita basi, nimekusamehe, hapana, na hata hivyo haiwezekani, siwezi kuingie kwenye mashindani ya kugombea mwanaume…’akasema‘Kuna kitu unanificha au..?’ nikamuliza‘Unajua rafiki yangu,  nikuambie ukweli, ninachotamani kwa sasa ni kupata mrithi,…kuhakikisha na mimi nabakia ni kizazi cha huko mbeleni, hata kama…hilo,…ndilo naliwazia….’akasema‘Ni kweli, ni lazima upate kizazi chako, ni lazima upate mtoto, na utapataje, bila kuingia kwenye ndoa,..hilo …labda ndilo la kuwazia,…’nikasema‘Hapana siwazii, ndoa…mimi nawazia kupata mtoto, ninajua  nikipata mtoto basi, maisha yangu yatakuwa na furaha sana…’akasema‘Hahaha, sasa leo umekuja na jipya, unataka mtoto bila ndoa,…leo umeshabadilika au,sijakusikia vyema,…kuwa unataka uzae nje ya ndoa, au mimi sijakuelewa, au hebu niambie vyema....utapataje mtoto bila ya mwanaume au unataka mtoto wa kurithi, sijakuelewa hapo..?’ nikamuuliza‘Ninataka mtoto wa kwangu wa kuzaa mimi mwenyewe, lakini nataka iwe halali, isiwe nafanya vibaya, …ndio maana nimekuja kwako tulijadili hilo, kama huko kuolewa hakupo, maana nimesubiri sana sijampata mume wa kunioa, wengi wanataka kuuchezea huu mwili wangu tu,…kwa vile hajatokea mume wa kunioa, basi, nipate angalau hata huyo mtoto, …’akasema.‘Unataka kusema nini sasa…?’ nikamuuliza na alikuwa kama kaichokoza fikra fulani niliyokuwa nayo akilini, lakini sikupenda kabisa kumshauri rafiki yangu nilijua ni makosa, lakini sasa naona anaelekea huko-huko, ila sikutaka kuianzisha mimi, nikasubiria.‘Natamani mtoto rafiki yangu, lakini kwa vipi, kama ulivyosema sijaolewa, na mtoto akizaliwa, najua hata kuwa na muonekano mnzuri kwa jamii, atapewa ‘majina mapya…’ akasema kama anaimba‘Na mbaya zaidi,..hilo mimi silitaki,..eti aje kuitwa mtoto aliyepatikana kwa njia za haramu, mimi nitaonekana muhuni…ooh, kwanini mimi..unajua najishia vibaya sana…kwanini lakini…, silipendi, ndio maana nimejitahidi kujizuia sana nisije kwanza hapa, maana ningelifika kwa muda huo ningeliishia kulia,..sitaki huo unyonge,..’akasema‘Sasa ina maana unatakaje sasa rafiki yangu..au kwani imekuwaje tena, maana sisi tulishajua sasa mambo yanaelekea kwema, au..?’ nikamuuliza‘Hapo sasa, ndio maana nimewaza sana hilo…mpaka kichwa kinauma, nimekuja kwako tushauriane, nilikuwa nimejitenga kidogo kuja huku nikiwazia hili jambo kwa makini sana, nimeshindwa namna, nifanyeje…mimi nataka mtoto, natamani nipate na mimi mtoto wangu…., nilitamani ndoa, ndoa haijatokea, sasa hata mtoto jamani…’akasema kwa sauti ya huzuni.‘Nikushauri rafiki yangu, ukianza mtindo huo, utazalishwa na waume tofauti tofauti, na kuwa na watoto wa kila mmoja na baba yake, huoni hiyo itakuja kukuletea mawazo mengine uzeeni kwako,…maana sawa, utakutana na mwanaume ilimradi mwanaume upate mtoto, utazaa wa kike, ..kesho utataka wa kiume, utaenda kutembea na bwana mwingine atakuzalisha,kumbe anakuja tena wa kike…kesho kutwa utataka mwingine…huoni itakuleta sifa mbaya…?’ nikamwambia‘Aaah, hayo ya huko mbele anayajua mungu peke yake, tugange haya  yaliyopo sasa,,, kwani wewe unajua kesho itakuwaje, nikifa hapa si ndio mtanisahau kabisa, sina hata kumbukumbu huku nyuma, au sio, hiyo ndio ajenda yetu, tuijadili …’akasema hivyo , na kwa vile namfahamu sana rafiki yangu sikutaka kumchukulia kwa haraka.‘Unajua rafiki yangu nilikushauri sana awali, ukanipuuzia, sasa umri ndio huo umekwenda, na tabia yako haibadiliki, wanaume wameshakusoma wameshakugundua ulivyo,…kuwa wewe ni mtu wa matumizi tu,..dharau, msomi sana,… mtoto wa bei mbaya, mtu wa matumizi makubwa, wanaume hawapendi hayo maisha,…wanmeshakuogopa, na maisha yenyewe yalivyo,..oh, angalia sana…’nikasema‘Sasa ndio imekuwa hivyo, mimi ndio nipo hivyo, sina mbadala, na hata nijitahidi vipi kwasasa ni nani ataniamini kuwa nimebadilika,..labda niende ulaya nikamtafute mnzungu mzee…hahaha, …nacheka utafikiri nina raha, naumia mwenzako,…ni nani atakayenipenda hivi sasa, hakuna…, lakini sitaki kuzalilika…, nataka maisha ya hapa hapa kwetu, nataka mtoto wa damu ya kiafrika, nataka mtoto kihalali, sasa kwa vipi….’akasema‘Vipi yule shemeji , kawaje kwani, mbona naona anakupenda sana imekuwaje, sisi tulitaka tuonane na nyie wawili tunishinikize ndoa…kwanini yeye asikuoe, ili upate huyo mtoto, mimi nakushauri hivyo…’nikamshauri.‘Mhh, ungelijua,..yule ..hahaha sitaki hata kumsikia tena, sitai simtaki, na hata hivyo ipo wazi, sio wangu tena…’akasema‘Kwanini…niambie..’nikasema‘Siku kadhaa , alisita kuja kwangu, sikujua ni kwanini, nikasubiria wee, niaona kwanini nisjiumize kwa mawazo, nikasema ngoja niende kwake…labda anaumwa, sikutaka kumpigia simu, maana tulishazoeana kihivyo…basi, nikaenda kwake,.., ile nafika eneo la nyumba yake,…nikahisi mwili unasisimuka ajabu…, nikahisi kuna tatizo…lakini nikajipa moyo, nikafika nikagonga geti…kumbe lipo wazi, nikafungua hadi kwenye mlango wa nyumba,…’ hapo akatulia kidogo.‘Unajua kabla sijagonga mlango, ukafunguliwa,…, mara anatokea mdada  half cast, si unajue waniga fulani,..kijamika jamaika fulani, alivyo sio….kavaa khanga moja, ile ya khanga moja hakuna kitu kingine ndani, mhh, kuashiria nini hapo, kuwa katokea wapi sio.. utajaza mwenyewe……’akatulia akikunja uso kwa hasira‘Mhh, kwahiyo ina maana gani hapo…?’ nikamuuliza‘Ndio hapo nakuambia, mimi nina gundu…nina mkosi gani sijui, na uelewe baada y aule ushauri wenu na shemeji, nilipanga niende nimwambie sasa tufunge ndoa, nimekukubali, na sitaki kupoteza muda tena, na hilo alikuwa akilisubiria, niliwahi kumwambia akasita, akawa haniamini, sasa nilitaka nimuhakikishie kuwa nipo tayari,… siku hiyo nilipanga iwe hivyo,..hebu jiweke kwenye nafasi yangu uone nilivyoumia,… sasa sijiu kwanini alinifanya hivyo, hata sijui muda wote huo, kwanini hakuaniambia ana mchumba wake anasoma huko marekani…leo hii, inatokea hivyo…’akasema‘Ulimuuliza baada ya hapo…?’ nikamuuliza‘Mimi tena, ..mimi, weeh, unanijua nilivyo, wee…mimi  nikamuuliza,hahaha, sikuwa na muda huo,… hapana,…nilipojua kuwa huyo ni mchumba wake, nikaondoka zangu na hata aliponipigia simu sikutaka kabisa kupokea, na hali hiyo ilinitesa sana, sikutaka hata kuja kuongea na nyie, na ningelikutana na yeye, angelinijua mimi ni paka mwenye makucha makali…’akatulia‘Sasa ulijuaje kuwa ni mchumba wake..sijakuelewa hapo?’ nikamuuliza‘Nilimuuliza, ilibidi amuite kwani alikuwa ndani, na mara huyu, ti-ti-ti…katoka na taulo na likitambi-tambi lake, unajua kajiachia sana, na likitambi lake,.. sipendi hali hiyo, lakini nilishafikia sehemu nikaanza kumpenda tu, alivyo, kubembeleza, hakati tamaa..kumbe alikuwa na lengo lake…’akatulia‘Nikamuuliza huyo kinyago ni nani…?’‘Kinyago, hahaha huyu ni mchumba wangu….’akasema na huyo binti, akasimama pemebni yake na kumwekea mikono hivi, kimahaba, kuninyaa…nikihisi ile hali natamani irejee niwe na gun, niwashoot…lakini yamepita…’akatulia‘Pole sana…’nikasema‘Kiukweli…niliumia sana, unajua kuumia, mtu nilishasema huyu sasa ndiye wangu, leo hii inatokea hivyo, ni mara ya ngapi yanatokea haya, hapana siwezi tena,siwezi kuyabeba haya tena…sitaki mwanaume tena,…’akageuka akizuia machozi.‘Pole sana sikujua,…na kwanini hukunipigia angalau simu…?’ nikamuuliza‘Hayo tuyaache, mimi nimekuja na wazo hilo unisaidie kwa ushauri nifanyeje sasa ili na mimi nimpate mtoto, maana …nimeshafika sehemu sitaki kupenda mwanaume tena…, nataka nimpate mtoto wa kuniliwaza tu..basi…’akasema‘Kwahiyo upo thabiti na msimao huo, are sure about it ….umedhamiria kufanya hivyo, au unatakaje, maana mtoto sio wa kupata hivi hivi tu kama kuku, au sio..kuwa upite hivi jogoo akupande, au sio…?’ Nikamuuliza‘Mimi kwa hivi sasa sitaki mwanaume, na kama yupo,  yupi tena, hao wakunitesa, hakuna tena mwanaume mwanifu, hawapo..wote ni waongo , wahuni, wana hadaa, wema wazuri, waaminifu wameshaoa, nina imani hiyo, hakuna…sasa nifanyeje nife bila hata ya  mtoto…’akasema‘Sijakuelewa hapo ina maana unataka mtoto kwa vipi hapo,…?’ nikamuuliza kwa mshangao kidogo.‘Vyovyote iwavyo,…kwani kama ingelikuwepo ndoa, angelikuwepo wa kunioa ningelihangaika hivi, kwanini nihangaike…ndoa siioni tena, siwaoni kabisa wa ndoa hapa, wengi wao nimeshawajua ni tamaa zao za mwili wangu tu,na hilo ndio sasa silitaki tena, nimechoka kuchezewa-chezewa, wakunioa simuoni tena, …’akasema‘Hapo sasa pagumu, ..maana wewe ni rafiki yangu, siwezi kukushauri jambo ambalo hata mimi silipendi,…’nikasema‘Rafiki yangu, wewe ndiye umenishinikiza na mawazo haya, sikuwa na mawazo kabisa ya kuolewa…unajua, nilijionea sawa tu…,sikuwa na mawazo ya maisha ya famalia, lakini wewe nikija hapa tukiongea unakuja na kauli zako hizo, olewa, olewa…mtoto , mtoto, na zidi nikikuona una watoto wako,  na mimi navutika, naingiwa na hamasa hiyo….’akasema‘Basi tafuta mume mwingine aku-oe, hata kama humpendi kihivyo, mtakuja kupendana mbele kwa mbele…’nikasema‘Hahaha..mume , ilimradi mume, mimi….haya tuseme hilo sawa, haya yupo wapi huyo mwanaume…’akasema‘Kwahiyo wewe kwa hivi sasa hufikirii kupata mwanaume wa kukupenda tena, mbona wewe ni mnzuri, wanume wanakutamani, mimi hilo siamini kuwa hakuna mwanaume anayekutaka tena..’nikasema‘Wewe unasema tu, kwa vile unaye,..sio rahisi kihivyo,..na siwezi, kujiuza, kujizalilisha,…ila wazo langu ni hilo, nishauri, kama huna ushauri niondoke zangu…’akasema‘Mhh kifupi nimekuelewa umefikia hapa kwa maamuzi hayo baada ya kutendwa,…chuki ikajitokeza dhidi ya wanaume au sio , achana na huyo piga moyo konde utapata mwingine au kwanini hadi ukate tamaaa kihivyo…?’ nikamuuliza.‘Ingewezekana akapatikana wa kunioa, ambaye pia namkubali, ..na asije kunitenda hivyo tena, ningekuwa na uhakika huo, sawa, lakini huyo mwanaume wa ngapi, watano wote wananifanyia hivyo hivyo…mimi, nina mkosi gani,…sitaki tena nimesha kata tamaa …licha ya tabia yangu ya kuchagua-chagua, lakini ilishafikia muda nikasema haya, si kuna kuolewa, haya nioeni,..anatokea huyu tukifikia mahali pa kufanikisha linatokea la kutokea..‘Ni bahati mbaya tu…’nikasema‘Huyu wa mwisho ndio akanimaliza kabisa…hapana,…nimechoka, kwanini mimi, ina maana adhabu za kuwakataa waume nikiwa binti ndio zinaendelea mpaka sasa, ina maana mimi nina madhambi makubwa kiaisi hicho…’akageuka kuangalia pembeni akificha machozi.‘Hapana sio sababu hizo, ila wanaume nao wana chaguzi zao, wana mitizamo yao, wengi wao akili zako ni moja, wao wanataka wenye tabia fulani, tabia nzuri, ..nk.. hata kama wao hawana tabia hizo,…hawajui kuwa na wewe ulikuwa na mtizamo wako…’nikwambia‘Tusipoteze muda …mimi sasa nataka mtoto tu inatosha, lakini mtoto….aweje, …kwa vipi, nitampataje, nataka ushauri wako, nisaidie rafiki yangu…‘Mhh, unaniweka pagumu,..unajua rafiki yangu, ukizaa mtoto bila ya mume, huyo- huyo mtoto atakuja kumuhitajia baba yake, utafanyeje huko mbele, …maana sawa, nitakushauri kapachikwe mimba sijui kama utakavyo, kwani kupata mimba ni ngumu, kama una kizazi…’nikasema‘Kwahiyo…?’ akauliza akikuna kuna kichwa.‘Au labda ukarithi, wapo watoto mayatima kwanini usiende kumchukua mmoja ukafuata taratibu za kurithi,…’nikamwambia hapo akaniangalia kwa jicho baya, halafu akasema kwa hasira.‘Nimekuambia mimi  nataka wa kumzaa mimi mwenyewe, aje kunyonya ziwa langu aje kupitia taratibu zote za mtoto wangu …na zaidi ya hapo awe mtoto atakayekidhi viwango vyangu, unajua, ...’akasema akiwaangalia watoto wangu, mbao walifika kuna kitu walihitajia, nikawasikilia halafu wakaondoka.‘Kama ni hivyo mbona ni kazi rahisi sana....’nikasema hapo akaniangalia kwa hamasa, sijui alitaka niseme hivyo, nilivyosema au kwanini aliniangalia machoni kwa hamasa kubwa.‘Ni kazi rahisi eeh, sasa niambie nifanyeje….maana wewe ni rafiki yangu, na kwenye dini wanasemaje, mpendelee rafiki yako, au sio..umpe kile unachokipenda, name natarajia utanifanyia hivyo..nishauri, nisiendelee kuteseka, maana baada ya hapo, unaweza ukasikia mengine, naweza hata kujiua,..sikutanii, nimeshafikia kubaya…’akasema‘Oh, imekuwa hayo…’nikasema‘Sitanii, niambie sasa, nifanyeje, …wewe ndiye rafiki yangu wa pekee nikishindwa hapa, basi, dunia, hainitaki tena, tumeshirikiana mengi tokea utotoni, hili nalo nahisi utanisaidia,...maana wewe ni mimi, japokuwa kwa hili  huwezi kujua ninavyoumia kichwani,…unajua … nilipowaona watoto wako wakiingia hapa, nikahisi ni wangu..nawapenda sana watoto wako….’akasema‘Basi kama umedhamiria hivyo,,…japokuwa sio sahihi, mimi nitakupa ushauri wangu ila..ninaona tena sana iwe siri, kati yako mimi na wewe….sawa….?...’mara mlango ukagongwa, mume wangu akafika….NB: Msiseme ninazunguka, ..hii ni tamithlya, inajiongeza, ngoja huo ushauri sehem ijayo.WAZO LA LEO: Udhaifi wetu kibinadamu unaweza kutufanya tufikie kufanya yale ambayo hata hatukukusudia, …uhimili wetu unafikia kikomo, hasa ukiwa huna imani thabiti ya kumjua mola muweza, kuwa yeye ndiye mpaji. Na imani hii haianzi ghafla tu, imani hii huanzia utotoni. Nawausia wenzangu na kujihusia mimi mwenyewe, tuwajenge watoto wetu mapema kwenye imani sahihi za dini. Ulimwengu hivi sasa unashuhudia mambo ya ajabu , yanayotokea hivi sasa, na zaidi ya yaliyoandikwa kwenye vitabu vya imani, yamepitiliza, …iliyobakia ni mungu mwenyewe anajua.Tumuombe mola wetu avilinde vizazi vyetu, kwenye mitihani hii , ambayo huko zama ilitokea gharika, ..watu wakaangamia, je hivi sasa itatokea nini…Ewe mola tunakuomba utusamehe, utuongoze kwenye njia sahihi tusije kuangamia kama hao, waliowahi kuangamia.Kama nilivyokwisha kusema awali, rafiki yangu tulishibana sana, na tulijaliana sana, na hakuna angelipenda kufanya jambo kwa mwenzake ila liwe la heri na lisiwe la kumkwanza mwingine, tulichunga sana hilo, tokea tulipokuwa na akili…kwa hali hiyo tulichunga mipaka yetu kuhakikisha hatukwazani.Na kwa upande wa mume wangu alikuwa mpole sana, hakupenda makuu, hakuwa na tabia mbaya , hakuwa mlevi, kuvuta sigara, au tabia za uhuni-uhuni, na alinijali sana na kuijali ndoa yake.  Sikuwa na wasiwasi kabisa na mume wangu, na usingeliweza kunidanganya kitu kuhusu mume wangu…na yeye hakupenda kufanya jambo linaloweza kunikera mimi au familia yake, alichunga sana hilo, ni mume wa pekee..ndio maana hata rafiki yangu alimuheshimu sana‘Mume wako namuheshimu kama mkwe,  nampenda sana kwa tabia yake, yaonyesha kabisa hana tamaa, au tabia mbaya, na wanaume wa namna hii ni wachache saa,..unajua nikimuona mahali natamani asinione, sipendi, hali ya kuwa naye faragha, japokuwa ananisalimia vyema tu…na kuna kipindi ananialika chakula cha mchana, namkatalia‘Kwanini unafanya hivyo, huoni atakufikiria vibaya, huyo ni shemeji yako, si zani kama mnaweza kufanya lolote baya…?’ nikamuliza rafiki yangu siku moja kipindi hicho nina uja uzito.‘Hapana sitaki watu waje kusema lolote dhidi yetu, najua watu wanaweza kujenga fitina na urafiki wetu ukaja kuleta madoa, nachunga sana hilo…sisi tumetoka mbali,..na kama tulivyowahi kuambizana,  muhimu ni kuchunga  yale yote yanayoweza kuvuruga urafiki wetu, sitakufanyia chochote kibaya, nikijua kitakuja kukuumiza, ni bora nikafanye kwa wengine na sio kwako…’akasema‘Usijali, mimi na wewe..sina shaka kwa hilo….mimi nafahamu hata kama itatokea mkalala chumba kimoja na mume wangu bado nina imani kuwa hutawezi kunisaliti, hahaha.’nikasema tukacheka.‘Ni kweli…hahaha eti tulale chumba kimoja ina maana vyumba vya wageni havipo, tusifikie huko ..pa kujaribiana…’akasemaMimi na rafiki yangu ilikuwa hivyo…Nayaweka haya  bayana kwanza, ili uone tulivyokuwa tumeshibana na huyo rafiki yangu, kwahiyo kwa kutoa kwangu ushauri kama ule.., sikuwa nina mashaka yoyote na yeye, maana wengine watasema kwanini, ukamshauri mwenzako hivyo, wakati una mume, kwanini sikumshuku vibaya…na najua itakuwa hivyo…. aah,  nilimshauri rafiki yangu nikijua atafanya kile ambacho hakiwezi kuniumiza na atafanikiwa na hatimaye na yeye atakuwa na furaha,…‘Sasa nilimshauri nini, hebu sikia ushauri wangu….Tuendelee na kisa chetu…*************‘Kama ni hivyo, mimi sioni kwamba kuna tatizo, kwanza wewe tayari ni mzoefu wa wanaume,…mimi sijawahi kuwa na mahusiano yoyote zaidi ya huyo mume wangu, kwahiyo kwako, sioni kama ni tatizo, au…?’ nikamuuliza, baada ya mume wangu kuondoka,…Mume wangu alipofika tulikatisha mazungumzo, hakukaa sana, alisema alikuja mara moja, kuna sehemu anakwenda mara moja…‘Ugumu unakujaje …nataka mtoto ambaye ana sura ninayoitamani mimi, ..yaani ninachowazia, sio ilimradi tu kupata mtoto, ukichagua nyama, chagua iliyonona, au sio, ….unajua sitaki kukufuru, ila kwa vile nimeamua hivyo, basi kiwe kile kitakachonisuuza moyo wangu….’akasema.‘Wewe cha muhimu si ni kupata mtoto, hujali tena cha ndoa, au sio..hapo uwe na uhakika,..usije kusema aaha rafiki yangu, kanichuuza…kama ni hivyo, …, basi zaa kwanza na mwanaume yoyote…ningependa kukushauri hivyo…’nikasema na kumkagua usoni.‘Hapana ….sio hivyo…’akasema.‘Sio hivyo kwa vipi tena, kwani unataka akuoe,….au wewe watakaje…mimi nilionea hivyo, wewe uzae kwanza na yoyote yule… , huku ukiendelea kusubiria kama utapata mwanaume chagua lako ambaye ataweza kukuoa, lakini huku ushapata mtoto wako ili kutokuingia kwenye umri hatari hujazaa..…unaona hapo, hata akiolewa umeshafikia huo umri,  huna haja ya kuzaa tena maana unaye mtoto tayari unaona hilo wazo langu lilivyokaa...’nikamwambia na yeye akaniangalia sasa kwa uso uliojaa hamasa.‘Hapo sasa nimekuelewa, hivi kweli hilo inawezekana kirahisi  hivyo…?’ akauliza‘Kwanini isiwezekane, hahaha, wewe ni mjanja bwana, usitake kunifanya kwua mimi sikufahamu, …’nikasema.‘Mhh, kunifahamu unanifahamu lakini sivyo kama nitakavyo mimi….’akasema‘Unatakaje…?’ nikamuuliza‘Kwanza niambie, kwa vipi hapo, maana nilitaka nizae ndani ya ndoa,..huo ndio ukweli wangu, sasa ndoa imegoma, hivi sasa tunashauriana kuwa  ni zae tu hata nje ya ndoa…si hivyo…?’ akaniuliza‘Hilo ni jibu lipigie mstari, au…?’ nikasema na kumuuliza‘Mmhh, hapo kwangu bado pagumu kweli kweli,…isingelikuwa hoja hiyo ya kuchelewa kwa umri, nsingelijali sana, isingelikuwa ….aah, hapana mimi nataka mtoto, kwa vyovyote vile…lakini sipendi maana   hapo nitakuwa nimekiuka kiapo changu,…nitakuwa msaliti wa ahadi yengu mwenyewe..unajua , niliapa mimi sitazaa nje ya ndoa, sasa nifanyeje mungu wangu,..?’ akaniuliza.‘Hili si unalifanya kwasababu, hii tuichukue kama dharura, maana …. umri umekwenda, au sio, unaogopa utafikia kikomo kabla hujapata mtoto, hiyo si dharura, au sio…. basi wewe cha kufanya ni kutembea na mwanaume yoyote, …mimi hapo nasema ‘yo-yo-te’  sijui kwako wewe….maana mtoto ni mtoto au sio, kwa mzazi kama mimi…’nikasema‘Ha-pa-na sio kwa yoyote, hilo hapo natofautiana na wewe kidogo, tuliweke sawa hilo, ..maana yoyote atanizalia mtoto yoyote, hapana, mimi nataka yule atakayenipatia nikitakacho, moyo unapenda, unaona hapo, tuliangalia kihivyo, mimi naona hapo turekebishe kidogo....’akasema.‘Mpaka hapo tunakwenda sawa, siwezi kukukatilia hivyo uakavyo, ila wasiwasi ni kuwa ukianza kumtafuta umtakaye inaweza ikachukua muda tena,…na hujui ya kesho au sio….’nikasema'Mhhh…hapo sasa, unaleta ugumu , mimi kama nimeamua kula haramu, basi acaha nile haramu haswaa…unielewe hapo, sitaki nile haramu halafu nisikie kichefu chefu, hapama, nataka mume anipatie mtoto ninayempenda….’akasema‘Wewe ndio unaleta ugumu, unarudi kule pa kuchagua chagua..mwishowe siku zinakwenda, …’nikasema‘Hapana si ndio tunawekana sawa, tukishakubaliana hilo, kuwa nataka mume atakaye nizalia mtoto ni nimpendaye,…hapo tutaingia kuangalia ni nani…unajua pamoja na yote mimi najali sana mtoto wangu aweje, naanza kuangalia sasa…nisije kujitia baadaye…mtoto awe na sura , tabia, maumbile…ninayoyatamani mimi, eeh, hapo hapo tufanyeje ..’akawa kama anaota au kujenga taswira fulani akilini‘Aaah, unajua kwangu mimi kama mzazi mtoto ni mtoto tu…hayo ya sura, sijui nini, hayo ni wewe ambaye hujabahatika kuzaa, …mmh, na wewe kwa kuchagua, unachagua mpaka maumbile ya mwenyezimungu, usikufuru kihivyo,….’nikasema‘We-we..unasema mtoto ni mtoto tu, ina maana mimi kuchukua dhima hiyo basi nijizalie tu,… hapana..ni lazima nifanye jambo nije kulifurahia mwenyewe, sitaki nije kujutia baadae,.. najua nimetenda dhambi, tena ya kudhamiria,…sasa nije kupata adhabu hivi hivi tu, mungu anisamehe tu, sipendi hili jamani,…sasa mimi nitakavyo nikipate nikitakacho,..nizae mtoto nikimuangalia  hivi eeh , moyo unasuuzika na wala nisije kujijutia…’akasema‘Oh, mungu wangu , hapo sio dharura tena,..ni dhamira mbaya,..hebu niambie kwahiyo wewe unatakaje…?’ nikamuuliza‘Ninataka huyu mwanaume akinipa mimba, nizae mtoto mwenye sura nzuri, umbo nzuri, maana na mtoto anarithi tabia, basi awe na tabia nzuri kutoka kwa baba yake,…na hata mimi nikimuona huyo mtoto ninafurahi  mwenyewe…’akasema akitabasamu sio kama alivyokuwa awali, sasa uso umeshaanza kunawiri na urembo wake ukawa bayana, kiukweli rafki yangu ni mrembo, sijui kwanini kapata bahati hiyo mbaya ya kutokuelewa.‘Mhh, ….haya, kama utakavyo ni hivyo, basi twende hivyo hivyo, nikubaliane na wewe, na lile wazo langu la mwanaume yoyoete tuliondoe, sawa, twende sasa,…kwahiyo inabidi hapo uchague mwanaume sasa kama ni hivyo mbona ulikosa wa kukuoa, maana usione ni rahisi kumpata atakayekidhi viwango vyote, ndoa inajengwa na wawili na ndiyo inazaa chema..’nikasema‘Ndio hapo unisaidie, wewe ushaingia kwenye ndoa, ..na najua vyovyote iwavyo, mtoto huwa anatokana na damu ya wazazi wake, hata tabia, uziri, umbile ndio basi tena…nisaidie kwa hapo…’akasema‘Unajua wewe unanitwika mzigo ambao mimi sina tabia nao…mimi sijui kuchagua chagua kihivyo, najua chema ukimuomba mungu atakupatia, sio mpaka nianza kuchagua tu..kama nguo,..hapa hatuzungumizii nguo, tunazungumzia mtu, na mtu huletwa na utashi, wa muumbaji, ..sio kweli kuwa unaweza kumpata mume akakupatia hichoukitakacho…’nikasema‘Rafiki yangu tuangalia uhalisia, hili ulilonishauri, la kuzaa eeh, hata nje ndoa, ni uhalisia, pia linaendana na maumbile, ..tusikwepe ukweli hapa…’akasema‘Ok, sawa nimekuelewa…..’nikasema‘Sasa tuseme tumeshakubaliana huyo mwanaume aweje, ..eeh,awe nitakavyo mimi, kazi inakuja , nitamuanzaje, kuwa nataka unipe mimba, au nataka…inakuwa kama nauza mwili wangu..huoni hapo najizalilisha…’akasema‘Hilo rafiki yangu utaanzaje, mimi siwezi kujua, najua wanaume wakiona ishara fulani wanajua huyo mwanamke anataka kitu..kapenda, tatizo ni huyo mwanaume uliyemchagua je…ana tabia hiyo,…’nikasema‘Unajua kuna kitu nikuambia ukweli rafiki yangu, pamoja na ya kuwa hawataki kunioa,..lakini nimegundua kitu,  wanaume wengi wananiangalia kwa matamanio,..wengine wananitongoza, tatizo ni hilo wengi wao, wanachotaka ni mwili wangu, na wengi wao sijawapenda…sasa hapo, nifanyeje….?' akasema.‘Unajua pamoja nakushauri hivyo, bado mimi silipendi hilo wazo,…lakini pia nakuona kweli umri umekwenda, na wanaume ndio hao, …mikosi, sijui tuite hivyo, au ndio huko kuchagua kwako kumefikia…’nikasema‘Tusirudi huko, tutashindwa kufikia muafaka,…najua mungu anakuadhibu, kwa kasumba yangu hiyo, sawa….’akasema‘Hapana usifikirie hivyo….mimi bado nilikuwa na imani kuwa muda bado upo,…lakini mtoto kweli ana umuhimu wake, cha kufanya mtafaute huyo unayempenda, mengine utajua mwenyewe cha kufanya, usitake mimi nikutanue kila kitu...’ nikasema na hapo akanikazia macho kwa kushangaa.‘Nimtafute yoyote ninaye mpenda, bila kujali,…aah ina maana unanishauri hivyo, yoyote ninayempenda, …mmh, hapo sasa ndio naanza kuogopa, maana,….sijui sijui..nifanyeje rafiki yangu…?’ akaniuliza' Wewe wazo lako si kuzaa tu na mwanaume yeyote unayeona atakuwezesha kupata mtoto mwenye sura unayoipenda wewe, si ndio hivyo naona hata `wadhungu’ wanafanya hivyo, wanaingia kwenye mitandao, wanaandika wakitakacho kuna mawakala wanakutafutia, sasa huku hakuna, ila wewe unaweza kutafuta mwenyewe,....na kwako wewe sizani kama itakuwa ni ngumu kihivyo, wewe mwenyewe unajifanya u mzungu, unaishi kizungu-zungu, matawi ya juu, kwanini kitu kidogo kama hicho kikushinde, haikuwa na haja ya kuja kuniuliza hayo yote.., au sio, mtafute unayempenda uzae naye...kwa siri…unielewe hapo…'hatimaye nikamshauri hivyo rafiki yangu.‘Sasa nikufuchulia ukweli,..sikuwa na wazo hilo kabisa, maana naogopa sana, ila uliponishauri hivyo wewe rafiki yangu kuwa naweza ..sas anikuambie ukweli, wengi ninaowapenda, kama mungu angenijalia, …wengi ninao ona wanaweza kunipatia mtoto nimtakaje ni waume za watu, ndio hapo naogopa sana.…’nikasema‘Oh waume za watu ina maana hakuna mwanaume mwingine ambaye hajaoa, hapo uanishangaza, waume wapo wengi, wana umbile, sura nzuri, kwanini ushindwe kuwapata, mimi hapo sioni kuwa ni tatizo …’nikasema‘Ni tatizo,..maana ni waume za watu, ndio sana nawapenda, ndio sana nikiangalia watoto wao nasema hata mimi nataka mtoto kama yule, nina ushahidi wa kizazi chao, hawa ambao hawajazaa, sina ushahidi nao, ndio maana naingiwa na mashaka nao, uone wazo langu lilivyo, hao, nawa-penda, sio kuwa….unielewe, sio kwamba nina nia mbaya nao, lakini ndio najua wataweza kunizalia kile nikitakacho na nina uhakika nacho..…’akasema‘Mhh, rafiki yangu utavuruga ndoa za watu, ….’nikasema‘Sasa mbona unaharibu, unanitisha, basi tuache….’akasema‘Sio nakutisha, nawazia mbali unajua…’nikasema‘Kiukweli  mimi sipendi kuvuruga ndoa za watu…yaani sijui kwanini, sijawahi kumuona wa kumpenda ninayevutika naye, ambaye nahisi nikizaa naye nitapata mtoto mwenye sura na umbile nilipendalo ambaye hajaoa,…huo ndio ukweli..nakuambia ukweli kwa vile wewe ni rafiki yangu,… sijawahi kumuona, nimezunguka nimeangaza huku na kule hakuna,....ninao waona na kuwapenda  wengi ni waume za watu...sijui kwanini inanitokea hivyo,…’akaniambia.‘Sawa mimi nimekuelewa sana, mimi sioni tatizo, kwa vile hutarajii kuishi na huyo mwanaume, ..nikuuliza hapo, kwani wewe najali nini sasa maana sasa unataka nikufundishe kila kitu, kwanza ninataka unihakikishie kuwa lengo lako sio kuvunja ndoa ya watu, ni kuzaa tu, na kuzaa huko kuwe ni siri yako…usije kuniingiza kwenye lawama ya kuvunja ndoa za watu, mimi sipo….’ nikasema‘Ndio hivyo….’akasema‘Na pili wewe unataka mwanaume salama asiye kuwa na tatizo, nahisi nimekuelewa hivyo…na unahisi kuwa wao watakuwa na tabia nzuri, sasa kama anakubali kutembea nje ya ndoa, mimi naingiwa na walakini na tabia hiyo, lakini wewe utakua jinsi gani ya kumshawishi , maana wanaume hata aweje, ukimfikisha mahali sizani kama anaweza kurudi nyuma….’ nikamwambia.‘Mhh, hapo kuna mawili, nimuambia lengo langu au nimfiche lengo langu, mimi sitaki iwe hivyo, unaona hapo, nataka iwe siri ili sije kuvuruga ndoa au sio, nionavyo mimi,…haaah…. unajua umenitia hamasa kwa wazo lako, nimelipenda, japokuwa sipendi kutembea na mume wa mtu,…kwani nitakuwa nimevunja ahadi yangu nyingine kubwa , tena kubwa sana…’akasema‘Ahadi gani…?’ nikamuuliza‘Ahadi ya kuwa sitatembea na mume wa mtu, vinginevyo aje kunioa…’akasema‘Nimeshakuambia uichukulie hiyo kama dharura tu, ikipita basi isahau kabisa, msahau huyo mwanaume na usahau kile kitu, usije kunogewa ikawa ndio basi tena…’nikasema‘Mhh, hapo nipagumu,  kutembea na waume za watu na huenda awe ni mume wa rafiki yangu,  hapana mimi nawaheshimu sana marafiki zangu....hilo mimi naliona tuliache tu,  sio wazo zuri, na kumpata ...ambaye atanipatia mtoto nimtakaye inakuwa ngumu, ninaowapenda zaidi ni waume za marafiki zangu, mmh, mimi naona mungu kapanga iwe hivyo, tuliache …..’akasema.‘Wewe usijali, ukimpata huyo mwanaume, hata kama ni mume wa mtu, tembea naye bila kumwambia kitu, hakikisha umelenga zile tarehe…., nia na lengo ni akupe uja uzito, mkishamalizana, unaachana naye kabisa…., na fanya hivyo ukiona kweli mimba imeingia,…maana yawezekana ukajaribu mara ya kwanza isiingie…’nikasema‘Hapo sasa si ndio nitaanza kujenga mazoea…’akasema‘Hapana, akili yako iswe kumchukua mume wa mtu,…mimi nina imani hiyo mara ya kwanza inaweza kuleta matunda,..ukishamalizana naye, achana naye,  usiwe na mawasiliano naye tena, achana naye kabisa mpige marufuku kukufuata fuata tena….mimi naona iwe hivyo.,…’nikamsahauri hivyo.‘Hiyo ni kazi kubwa, maana hapo natakiwa nitongoze mwanaume wa matu, wakati  siku zote natongozwa mimi, nitamuanzaje huyo mwanaume, tena mwanaume wa mtu tena labda awe ni mume wa marafiki zangu,…’akaangalia juu akiwanza.‘Mwanaume ukimuonyeshea ishara tu wao wanajua, na wewe bado mrembo unavutia, sizani kama hilo litakuwa tatizo kwako, mimi sioni kama ni tatizo, ndio inauma, na sijui, jitahidi umalizane na hilo usahau, mimi naona ufanye hivyo. Maana sasa unaniingiza kwenye kuchagua chagua……’nikasema‘ Sio hivyo, ..hapa tunapanga kitu chenye uhakika,….maana  hapo unazungumzia mume wa mtu ninayemfahamu ,maana ili niwe na uhakika inabidi awe ni mwanaume ninayemfahamu, si ndio hivyo,..ambaye natamani anizalie watoto kama ….unaona inakuwa ngumu, nitakuja kumuangaliaje huyo rafiki yangu, ndio maana nikasema hili wazo sio zuri, naona tuliache tu...’akatulia kidogo.‘Wewe unajali nini kwani unaondoka na huyo bwana..hahaha, naona unanifanya na mimi niwazie mambo niliyokuwa sinayo kichwani mwangu, wewe kama lengo lako ni mtoto na ni kweli umri ndio huo,… fanya hivyo, na iwe siri yetu wawili tu..,usije kumuambia mtu kuwa mimi nilikushauri hivyo….sitaki..’nikasema huku nikicheka.‘Mhh, unajua ni rahisi kusema, lakini kwenye kutenda ni kugumu,  maana ni kweli watoto  wa marafiki zangu nawapenda sana, na natamani niwapate kama hao hao....hapo ndipo naona ugumu, kuwasaliti marafiki zangu, wewe huoni hapo inaweza kuleta shida baadaye, wanaweza wakaja kugundua, urafiki utageuka kuwa ni uadui, sipendi kukosana na marafiki zangu....mmh, ngoja nifikirie huo ushauri wako…’akaniambia.‘Sio swala la kufikiria sasa rafiki yangu, …hapo ni swala la kulifanyia kazi, sizani kama itakuwa ni ngumu kwako,  wewe ni mrembo bwana, nashangaa kwanini hujaolewa, kila mtu anakushangaa mrembo kama wewe huna mume...’nikamwambia.‘Kila mtu ananishangaa, basi anipatie mume wake,, waache wafikiria watakavyo, mimi hilo sijali kabisa..maisha yangu hayawahusu....kwangu mimi hilo la watu kiukweli ninachohofia kwasasa, nisije nikafikia umri ambao hautakiwi kuzaa tena,  sijapata mtoto, yaani hilo ndilo tatizo kwangu si vinginevyo....’akaniambia.‘Kama ni hivyo , basi fuata ushauri wangu, na wala usipoteze muda, kama waume za watu ndio unaowatamani, ndio watakao kupatia mtoto unayemtamani, basi hao wapo wengi, ila chunga sana, ....’nikamwambia‘Nichunge nini tena, unanikatisha tamaa…?’ akauliza akiniangalia kwa mshangao.‘Kuna waume wana wake zao ni wakorofi, wakija kugundua wanaweza kukuharibu hiyo sura yako, tafuta waume ambao wake zao ni wastaarabu, ...na iwe siri yako, usimwambia yoyote...haya,usipoteze muda tena kalifanyie kazii hilo…’nikamshauri.‘Sawa rafiki yangu, maana umenipa wazo ambalo sikuwa nalo kichwani kabisa...kiukweli naogopa sana, waume za watu...bado naogopa....kutembea na mume wa mtu, na mbaya zaidi awe ni mume wa rafiki ninamyemuheshimu sana ..naogopa sana... hapana hiyo sio tabia yangu, itakuwa ni mara ya kwanza kutembea na mume wa mtu...’akasema. Rafiki yangu alitulia kwa muda, nadhani alikuwa akiwaza jinsi gani atakavyotembea na huyo mume wa mtu,  na wakishamaliza, jinsi gani atakavyojisikia vibaya, na kama kweli huyo mwanaume ni muungwana na yeye atabakia akiwa anajutia....nikamtoa kwenye mawazo hayo na kusema;‘Shauri lako kama na hilo nalo ni mpaka uchague chague kama nazi endelea kufanya hivyo, hilo halina kuchagua tena hapo, maana mwenyewe umeshasema kuwa waume za watu wapo wengi unaowapenda, na umeshaona watoto wao au sio, sasa watakaje, nikuchagulie mimi au..?’ nikamuuliza‘Hapana, umeshanipa njia inatosha…na kiukweli marafiki zangu wote nawafahamu watoto wao, nafahamu yupi ni yupi anafaa, nitachagua mmojawapo, au sio..?’ akaniuliza‘Ndio hivyo,  chagua yoyote atakayekukidhi matakwa yako, sizani kama hilo ni tatizo kwako, au…?’ nikamuuliza‘Sijui kama ni tatizo, maana sio kawaida yangu, lakini nitajaribu, maana wengi, nawaoana wakinitizama kwa jicho la kunitamani, kwahiyo..sawa, natumai sitaharibu kitu, ngoja nione itakavyokuwa, nashukuru sana rafiki yangu, kwa kunijali,..wewe ndiye rafiki wa kweli, hilo wazo limekaa vyema japokuwa ..mmh…’akasema‘Usijali,..sasa kazi ni kwako wewe ushawajua ni nani anakuvutia zaidi,  mweka kwenye anga zako, tembea naye,hakuna atakayejua...wewe mjanja bwana, hilo lifanyie kazi, haraka iwezekanavyo, kabla mambo hayajabanika..’nikamwambia na yeye akataka kuondoka‘Mbona huwaagi watoto , …naona wazo hilo limekuhamasisha sana…’nikasema‘Oh, yaani we acha tu,….’akasema na kuwafuata watoto kule wanapojisomea, na kuwa-aga…wakamsindikiza hadi mlangoni… , na alipofika mbele kidogo,  akageuka na kuwaangalia , akatabasamu na kuwapungia mkono na huyoo, akaondoka zake….‘Mlikuwa mnajadili nini….?’ Ilikuwa sauti ya mume wangu ilinishtua kwakweli… sikujua bado yupo, maana aliaga kuwa anaondoka!Nb, mkuki ukachongwa, tayari kwa kumchoma nguruwe......WAZO LA LEO: Wengi twachukulia rahisi tu kuongea, kutamka neno, vyovyote akili zetu zitakavyotutuma, tukumbuke kuwa kila neno lina thamani yake inaweza kuwa mbaya au nzuri... Neno dogo tu laweza kuzua sintofahamu, likajenga chuki, likaumiza, na hata kubomoa kile ulichoanza kujenga…rafiki wa leo anaweza kuwa adui mkubwa wa kesho, sababu tu ya kauli.. , kauli zaweza hata kuua. Wachamungu wa kweli wametuasa kuwa ni bora kufunga mdomo wako, ukauzuia ulimi wako, ili kujiepusha na mtihani wa ulimi.Najiusia mimi mwenyewe na kuwausia wenzangu, tuweni makini sana na kauli zetu, tuchunge sana ndimi zetu. Baada ya kuutoa ushauri kwa rafiki yangu, kukapita kipindi cha pilika pilika nyingi, mambo yakawa mengi ya kupambana na maisha, kiasi kwamba hatukuwa na muda wa kukutana na rafiki yangu , hata tukikutana ni ile ya haraka haraka kila mtu anakimbilia kwenye shughuli zake, na mara rafiki yangu akanipa taarifa kuwa anahamishiwa Zanzibar kikazi,‘Hamna shida kazi ni kasi, na popote uwapo tutazidi kuwasiliana…’nikamwambia aliponipigia simu na wakati ananipigia yupo tayari anaelekea kupanda express bot, kwani taarifa ilikuwa ya haraka, na alitakiwa haraka akawasili kwenye hicho kituo kipya, na huko atapata maelekezo zaidi…basi, tukawa tunawasiliana kwa simu tu, kuulizana hali na siku, na masiki yakapita. Ikawa akija Dar, hakai sana, na mimi nikawa na mishughuliko mingi ya shughuli zangu, wakati mwingine anakuja mimi nipo mikoani, kazi ni kazi, hakuna kulala, ilimradi afya zipo,…na kipindi chote hicho, tunapigiana simu au tunakutana kwa haraka, hutaamini sikuwa na hata na akili ya kumuulizia lile zoezi letu lilikwendaje…Miezi mingi ikapita, na siku moja akaja kunitembelea nyumbani kwangu, alifika mara moja kikazi, basi tukaanza kuongea hili na lile, alikuwa kavaa Madera yake mapana tu, mimi nilijuwa kwa vile kahamsihiwa huko Zanzibar, basi kajifunza asili za huko, za kujisitiri mwili mnzima,….ila nilihisi kuna mabadiliko, ukimuangalia usoni kazidi kuwa mweupe, na unene kidogo, sijui kwasababu ya hizo nguo alizovaa, japokuwa nilikuwa na haraka kama alivyo yeye, nikamuuliza.‘Vipi mwenzangu, toka lini ukavaa nguo hivyo, maana wewe ulikuwa ni mdhungu, haahaha, naona  sasa ushakumwa mnzaibari tena, na nahisi huko ushampata shemeji au sio, kwa hilo umbo na sura yako, sizani waname watakuacha upite hivi hivi tu, halafu hebu niambie, nahisi mmh,…na nakuona kama mambo tayari au, ..?’ nikaanza kumtania.‘Acha utani wako bwana, nimpate wapi mume mie, umri ushaenda, ..naona wengi wameamua kunikimbia, lakini sijali, ..na wala hilo haliniumizi kichwa,… kabisa, kabisa,….mimi  nimeamua kula, kuishi  kivyangu, yaani sitaki tena usuhuba na hao watu, huwezi amini, nimeamua hivyo na imewezekana....’akasema.Hapo ndio nikaumbuka kile nilichomshauri , ikabidi nimuulize‘Vipi lile swala letu uliweza kulifanyia kazi?’ nikamuuliza.‘Hahaha..unajua niliwazia sana hilo, nakumbuka tuliongea kuwa kama …unajua iwe siri, na..aah, …’akasita kuongea‘Aaah, mbona unasita kuongea, au ulizarau…?’ nikamuuliza‘Mhh, hapana sikuzarau, ..sio maana hiyo ya kuzarau,..unajua niliwaza sana huo ushauri,…, nikaona nisiende mbali…..lakini  wewe ni rafiki yangu, na hili tulilijadili pamoja, niliogopa ule usemi wako kuwa niwe makini maana wanawake wengine ni vichaa….’akatulia , sikuwa nimemuelewa hadi hapo ana maana gani.‘Kifupi ulifanya au hukufanikiwa…?’ nikamuuliza‘Ndio maana nimekuja kwako hivi leo, sina muda, hapa unaona meseji zimeshaanza kuingia natafutwa huko ...’akasema akitabasamu,…usoni ulionyesha furaha ya kweli, japokuwa kuna kiwingu cha kuonyesha ana mawazo fulani.‘Kwahiyo kifupi tuseme tayari…?’ nikamuuliza nikiwa na hamasa ya kutaka kujua'Mhh,…rafiki yangu, wewe na mimi ni marafiki, usingeliweza kunishauri kitu nikipinge bure bure…. ushauri wako nimeufuata na sasa hivi unavyoniona hapa nina uja uzito…hapa nilipo sitamani hata kula…kichefu chefu..yaani taabu kweli kweli..hivi mimba ndivyo zilivyo hivyo…, hapana nikizaa huyu mmoja, sizai tena, sitaki tena kuzaa.....’akaniambia.'Mambo si hayo, ....umefanya jambo la maana sana, ....ulikuwa unapoteza muda tu,.. na umri ndio huo, na kama ulivyosema waume wanakuona sasa umeshakuwa mtu mzima, huna ujana tena, ..na ukiachia mwili hivyo,…mmh,…’nikasema‘Sijaachia mwili, nachoka tu, halafu …sijisiki vyema,…’akasema‘Ni kawaida, hali kama hiyo ni kawaida, muhimu ni kufuata masharti ya dakitari, hakikisha huharibu ulichokitaka, sawa….usije kujipilikisha na kazi, mimba ikaja kuharibika…’nikasema.‘Hutaamini, nafuatilia masharti yote, naingia kwenye mitandao…nauliza madocta, sitaki kufanya makosa, na mungu anisaidie…’akasema‘Hongera sana…’nikasogea na kumkumbatia rafiki yangu huyo…lakini sijui kwanini kuna kitu nilihisi akilini mwangu,..hata siwezi kukielewa, hata hivyo furaha iliweza kukimeza hicho kitu, ni kama mashaka,…’‘Mhh,…hongera wakati hata sijafikia ….unipe nikishajifungua, au sio…na kiukweli, nashukuru sana rafiki yangu, umenishauri, na najua utaendelea kuwa name, hata siwezi kuelezea ninavyojisikia, japokuwa moyoni, kuna muda nawaza sana…’akasema‘Unawaza nini sasa, hayo yameshapita muhimu ganga hili lililope mbele yako, jinsi ya kupambana na ujauzito maana nao sio mchezo, mengine yasahau kabisa,…unanielewa, wala usifikirie kuwa umekosea, ..hayo muachie mungu atakusamehe..’nikasema‘Mhh…kweli wewe ni rafiki wa kweli..tatizo ndio hilo,… hapa nilipo, najisikia vibaya, sitaki kuongea saaana, mate yanajaa mdomoni…’akasema akitoa leso yake na kuweka mdomoni‘Pole ndio uuke huo…’nikasema‘Mungu anisamehe tu, na mnisamehe kwakweli….’akasema‘Hamna shida wewe tema mate yako tu…ilimradi uteme sakafuni…’nikasema‘Unajua  haya yote ni kutokana na ushauri wako, wakati mwingine najilaumu kwanini, niliamua kuvunja nadhiri yangu,  lakini sawa, kwa vile ni wewe sina shaka....’akasema.‘Usijali kabisa…..mimi nilikupatia ushauri huo nikiwa najua wewe ni rafiki yangu, nikupe ushauri wenye tija,…usiwe na shaka na hilo..na sioni tatizo lipo wapi, …muhimu kama ulifuata kama  nilivyokuambia, sizani kama itakuwa na tatizo,…kwani huyo mwanaume, uliwahi kumwambia baada ya kuhisi kuwa una ujauzito unaotokana na yeye?’ nikamuuliza.‘Mhh, …aah, …unajua wanaume walivyo, baada ya lile tendo,…nisikufiche, ili kuwa na uhakika zaidi,…nilikutana nae mara mbili, mara mbili tu….sasa ikawa ni taabu, unajua wanaume walivyo, na..na…nilipohamishiwa huko Zanzibar, nikashukuru sana, maana huko mpaka aje sio kazi rahisi…na, nilimkanya kabisa kuwa mimi, sitaki tena urafiki na yeye, ndio hivyo, na sitaki kuyaongelea hayo tena tuyaache tu, ila nilitaka ni…niwe muwazi kwako…’akasema‘Safi kabisa, lakini je baada ya kujihisi una mimba uliwahi kumuambia…?’ nikamuuliza‘Unajua.hapana sitaki tuliongelee zaidi…nataka kukuambia…hapana, naogopa…’akasema‘Unaogopa nini sasa, nimekuuliza hivi umemwambia…?’ nikamuuliza‘Kama nilivyokuambia, wanaume hawana dogo, na hata siku ile, ya kwanza nilimuambia nimfenya hivyo kwa vile nimeshindwa kuvumilia, ila naheshimu ndoa yake, kwahiyo iwe ni mwanzo na mwisho…’akasema‘Safi kabisa, inatosha ulivyomuambia…’nikasema‘Lakini bado akawa ananifuatilia, japokuwa nilijitahdii sana kumficha,...na nikajitahidi sana kuwa mbali naye, lakini sijui kwanini, imekuwa kama nimemuonjesha asali , ….yaani nipo kwenye wakati mgumu sana, ndio maana nakuambia nimekosea sana….sijui nifanye nini sasa…kwani hata nafsi inamtaka najizuia napata shida sana….’akasema.‘Lakini nilikuambia kuwa kama ni mume wa mtu, ukishahakikisha kuwa keshakupachika mimba, achana naye kabisa, nilikushauri kuwa usimwambie hata huyo mwanaume kuwa una mimba yake, utasumbuliwa sana…, unajua waume wengine walivyo, hawatakubali damu yao ipotee hivi hivi, na hujui hatima yake itakuwa…na kumbuka kama ni mume wa mtu , ….utakuja hatarisha ndoa ya watu, kuwa makini sana kwa hilo…’nikasema‘Hata sijiu nifanye nini, ndio maana nikaja kwako tena, nipata ushauri, au sijui niitoe maana najuta, na inanipa wakati mgumu, namtaka aje awe karibu nami, unaona ilivyo, hata sijui nifanye nini, ndio maana nafikia kujuta, najiona kama nimebeba dhambi mwilini mwangu…?’ akasema sasa akikwepa kabisa kuniangalia machoni‘Kwani , hebu niambie ukweli huyo shemeji ni nani, maana sasa unanivutia intake kumfahamu, inaonekana umempenda sana…., hebu niambie ni nani ili niweza kukupa njia nyingine ya kumfanya asikusumbue tena..?’ nikamuuliza,  nikiwa na shauku kubwa sana.'Na wewe bwana, ina maana hapana…. sasa, itakuwa wewe ni  wa kwanza kuvunja ushauri wako, mwenyewe ulianiambia nikishatembea na huyo mwanaume, nisimwambia yoyote hata wewe mwenyewe, sasa wewe unataka niseme, unajua hilo limekuwa likiniumiza kichwa, nawaza nikuambie tu, au ..hapana mimi naona nifanye kama ulivyonishauri, au sio…maana hakuna siri ya watu wawili..’akaniambia.‘Lakini mimi ndiye niliyekushauri,…sasa , anyway,….fanya ilivyo sahihi, ni kweli ni bora iwe siri yako, ..hata hivyo ukiona ni lazima kuniambia ni nani, usisite kuniambia, kwangu usiwe na shaka kabisa, maana hatufichanai au..’nikamwambia‘Lakini pia wewe ndiye uliyenishauri kuwa nikishahakikisha nina mimba nisije kusema au kumtaja huyo mtu,  kwa yoyote vile…, unakumbuka eeh, basi tufanye hivyo, najua utanisamehe…. tusubiri nizae kwanza, ....’akasema‘Usijali kabisa, kunificha ni sawa,….hiyo inanipa uhakika kuwa hutasema lolotekwa yoyote, kama umeshindwa kuniambia mimi, nina uhakika hutaweza kusema lolote kwa mwinginewe, au sio…’nikasema‘Ni kweli, basi,…haina haja kukuambia, ..na hapa nilipo najisikia vibaya,...ngoja niondoke, hapa nisije nikakutapikia bure, na na..nashindwa, natamani niku—ooh, najisikia vibaya sasa...’akasema na haraka akimbilia nje.‘Kama mambo yenyewe ni hivyo , hicho kinaweza kikawa ni kidume, na ukija safari nyingine  ni lazima uniambie huyo shemeji ni nani, ...au nitakuja nyumbani kwako, upo mpaka lini...’nikamwambia na yeye akawa ameshatoka nje, …nilipomfuata nilimkuta ameshaingia kwenye gari lake na kuondoka.                               ********* Miezi mingi ikapita, ... kwasababu ya kikazi na mambo ya hapa na pale, na kwa vile sasa yeye yupo huko Zanzibar, hatukuweza kuonana na rafiki yangu huyo, na siku moja nikapokea simu, namba ilikuwa ngeni kwenye simu yangu, nikapokea nikijua yawezekana ni wateja wangu.‘Habari nani mwenzangu..?’ nikaulizaSauti ya kinyongea kama mtu mgonjwa ikasikika,..kwanza sikujua ni nani..hata kufikiri,…mambo mengi kichwani,…‘Oh, …ni mimi, yaani …’akasema akitoa sauti ya kinyonge‘Ni, ni …wewe ni nani maana namba hii ni ngeni kabisa…?’ nikauliza nikjaribu kuwaza ni mteja gani huyo. Na kwanini anaonekana mgonjwa akilini nikahisi inawezekana akawa mmoja wa wateja ninaye mdai.‘Hii namba ni..simu ya rafiki yangu , ya kwangu imezima haina chaji,…’akasema‘Ok,….pole..nani mwenzangu, nikusaidie nini…’nikasema‘Nilikutumia ujumbe nilipofika juzi, lakini ukawa kimia,…..’akasema‘Ujumbe…ujumbe gani, kwani wewe ni nani…?’ nikauliza kikazi zaidi.‘Ni mimi…nilikutumia ujumbe nikitokea Zanzabar,….nikajua utakuwa wa kwanza kuja kuniona…nikaona kimia, nikakupigia , lakini kila nikipiga simu yako ipo inatumika, na bahati mbaya nilikuwa natumia namba nyingine, ambayo nilikuwa sijakupatia, ya Zantel…’akasema‘Oh, ina maana ni wewe..mbona sauti ipo hivyo…?’ nikamuuliza baada ya kugundua kuwa ni huyo rafiki yangu.‘Ni mimi …sipo vizuri ..aaah , maumivu…’akasema na kabla hajaongea zaidi  ni kasema;‘Ujumbe wako niliupata,nilipanga nije kwako nikiwa na uhakika kuwa umeshafika…, ulisema umechoka…punguza kazi, pata muda wa kupumzika, ikibidi chukua likiza usije kupata matatizo…’nikasema‘Unajua nilitaka niende kijijini kwa wazazi…, ili kukwepa yale uliyonishauri, lakini nikaogopa, unajua tena kijijini, nitaulizwa maswali mengi, nikaona bora nipambane kivyangu….’akasema‘Vizuri, usijali, mimi si nipo, kama utakuwa hapa Dar, usijali kabisa, ..hata ikibidi unaweza kuja kukaa hapa mpaka muda wa kujifungua…’nikasema,‘Kujifungua…hahaha…. nimekupigia kukufahamisha kuwa mimi nipo hospitali…’akasema na kukawa na ukimia, na nikasikia kama sauti ya kichanga kinalia.‘Umelazwa,….ina maana…?’ nikauliza‘Ndio nimeshajifungua mtoto wa kiume...’akasema na nikajikuta nashikwa na mshituko, kama vile nimeambiwa jambo baya, badala ya kufurahi, sijui kwanini…nikajikuta nimetulia kidogo.Mara simu ikawa inataka kuingia, …na  nakumbuka kulikuwa na mteja muhimu nilitakiwa niongee naye, na hapa rafiki yangu kanipatia jambo muhimu sana…sijui ilikuwaje nikajikuta nimekata simu ya rafiki yangu na simu nyingine ikaingia…alikuwa ni mume wangu.‘Oh, ni wewe…nilikuwa naongea na rafiki yangu, ….’nikasema na yeye akasema, alinipigia kuniarifu kuwa atachelewa, kuna sehemu atapitia…‘Wapi huko, maana hata mimi nataka kutoka, ….’nikasema‘Napitia hospitalini…..’akasema‘Unaumwa…?’ nikamuuliza‘Hapana kuna mtu nakwenda kumuona…’akasema‘Basi hata mimi nakwenda hospitalini, kuna mtu nataka kumuona…’nikasema‘Hospitali gani…..?’ akaniuliza…na hapo nikashindwa kumjibu maana nilikuwa sijamaliza kuongea na rafiki yangu, nikasema‘Subiri kidogo nitakujibu, wewe unakwenda hospitalini gani…?’ nikamuulizaNB: Haya mambo ndio hayo yameanza kujitokeza mkuki ulishafanya kazi yake, sasa tuone matokea yakeWAZO LA LEO:  Kwa watu wengi, ulimi huwa ni mgumu sana kuuzia, mnaweza kupanga kuwa hilo utakaloambiwa liwe siri, lakini kwa wepesi wa ulimi ulivyo, au kutokana na tabia zetu zilivyo, hatuwezi kuhimili, twatamani kuongea sana, ukaja kuliongea hata lile la siri, …siri ikavuja, na siri sio ya watu wawili. Tujifunze sana kutunza kile tulichoahidiana na wenzetu, kama uliambiwa iwe siri, basi na iwe siri kweli,..tukikumbuka kuwa ahadi ni dhamana. Ikabidi nimpigie simu tena rafiki yangu ili kuhakikisha kuwa hajatoka, maana hospitali nyingine ukijifungua kama huna tatizo, unaruhusiwa mapema tu, na mazungumzo yetu yakawa hivi;‘Samahani rafiki yangu, simu ilikatika, mzee aliingilia kati, unajua tena, mume ni mumw inabidi umpe kipaumbele au sio, nisamehe tu kwa hilo, …hebu niambie kwanza unaendeleaje?’ nikamuuliza‘Kiukweli, ni maumivu tu…hapa yananitesa kweli, wamenipa dawa za maumivu lakini bado,…oh, ….ila sikupata taabu kujifungua, sio ile kama ninavyohadithiwa, namshukuru sana mungu….ooooh, , nimejifungua salama, iliyobakia ni jinsi…lakini nitajitahidi kama ulivyonishauri …’akasema‘Yaani siamini ina maana miezi tisa tayari… hivi urafiki wetu umekuwaje, ndio ..lakini ndio maisha au sio…kweli, kweli siku zinakwenda na maisha yanabadilika, umesema ..upo hospitali gani vile maana mimi nimebahatisha tu?’ nikamuuliza.‘Hilo swali gani tena rafiki yangu…, mimi siendi kwenye hospitali tofauti na ile hospitali yangu niliyozoea kutibiwa na ndipo nilipojifungulia, wewe kama upo bize, haina haja…utanikuta nyumbani,..nilikuwa nakufahamisha tu...’akasema rafiki yangu huyo na mimi huwa naifahamu hiyo hospitali yake anayopenda kwenda mara kwa mara akiumwa.., sikutaka kumuuliza zaidi, nikasema;‘Eti kama nipo bize, hilo usithubutu kusema, mimi na wewe tena, ninakuja hivi sasa nipo njiani,…maana taarifa hiyo kwanza ilinishtua, na furaha ikawa kama mshtuko fulani, sijui kwanini…’nikasema‘Oh, unakuja….mbona unasumbuka hivyo, kuna mtu ….’akasema akiwa kama anauma uma maneno‘Ninakuja usiwe na shaka, kama ni kukuchukua nitakuchukua mimi,…oh, nimefurahi kweli, ....nakuja sasa hivi, nataka niwe wa kwanza baada ya manesi kumshika huyo mtoto na kumpa huduma stahiki, mimi ndiye wa kuendelea kutokea hapo, sijali kazi hilo ni muhimu kwangu kwa sasa...’nikasema na kukata simu.Kiukweli nilikuwa na mambo muhimu sana lakini niliamua kuyasitisha kwa kuona umuhimu wa jambo hilo, nilimthamini sana rafiki yangu na, haraka  nikaingia kwenye gari kuelekea huko hospitalini. Sikukumbuka kumpigia tena mume wangu kumuarifu mimi ninakwenda hospitali gani!Tuendelee na kisa chetu****************'Rafiki yangu nimejifungua, mtoto wa kiume...bado nipo hospitalini...' nilijikuta maneno hayo yakijirudia rudia kichwani, hasa nikikazia hilo la ‘mtoto wa kiume…’‘Mtoto wa kiume…mmh,….ana bahati kweli…’nikasema nikakumbuka mume wangu jana alivyokuwa akiongelea kuhusu watoto na alitamka neno kuwa hivi sasa anatamani kumpata mtoto wa kiume, akishampata huyo hasumbuki tena, nikamwambia‘Kupata mtoto wa kiume ni majaliwa ya mungu, ..’nilisema hivyo, tukaishia kuongea maneno mengine.Nikiwa kati kati ya bara bara ndio nikakumbuka kuwa mume wangu alitaka nimuambie naelekea hospitali gani, nikampigia simu , lakini kila nilipojaribu namba yake  inasema inatumika, sikujali sana, nikijua mwenzangu katingwa na majukumu, yake ya kikazi.Mimi nikaongeza mwendo, na kuelekea hospitalini hapo alipolazwa huyo rafiki yangu, na wakati naendesha nikaona nimpigie tena huyo rafiki yangu, nia ni kujua kinachoendelea kama nahitajika kumchukulia chochote cha kula. Lakini badala ya kuliongelea hilo kwanza tukajikuta tunaongea mambo mengine.'Oh, hongera sana mambo si hayo, ..wewe ulikuwa unapoteza muda bure, uzee ndio huo. Ulikuwa unasubiri mtoto aje akuite bibi,..’nikaanza kwa utani na akawa anacheka, na kusema.‘Usinitanie mbona sijazeeka kiasi hicho cha kuitwa bibi…ni kweli ukiangalia wenzangu wenye umri kama wangu, unaweza kuwasalamia lakini mimi bado naonekana kijana tu…sasa naogopa nisije kuelekea huko’akaniambia na mimi nikasema;‘Ni kwasababu ulikwepa majukumu ya kuolewa na kuogopa kuzaa mapema, ndio maana bado unaonekana bado kijana, ngoja upate mtoto wa pili, na upate shemeji anayejua mfumo dume, kama hutabadilika sasa hivi na kuitwa bibi...’nikaendelea kumtania.‘Nani azae tena, …mimi...subutu yake..na kwa vile sina mume, …hilo limepita.., hii kasheshe niliyoipata siwezi tena kubeba mimba, kwanza uone ilivyo, nimezaa nikiwa mzazi peke yangu, nawaza huko mbele, mtoto akikuwa, anaweza kuanza kudai baba yake ni nani….na ole wake akiniuliza , nitampa jibu hatakumbuka kuniuliza tena….’akasema.‘Oh, kwanini useme hivyo mpendwa, siumesema huyo shemeji anajua una mimba, na kwahiyo nahisi utakuwa umeshamwambia kuwa umeshajifungua, japokuwa kiukweli hayo uliyoyafanya hayanihusu , umekwenda kinyume na makubaliano yetu, ni hatari, nahofia ndoa za watu, ….’nikasema.‘Ukifika tutaongea bwana, ….pamoja na mengine niliwazia sana ushauri wako, kuwa nimtafute mwanaume ambaye sitakuja kupatishwa taabu na mkewe, na..laki ni stutakuja kuyaongea, nataka nije kuyaweka wazi mapema tu….’akasema‘Kwahiyo unataka kusema nini, kuwa utamuhusisha na huyo mzazi mwenzako je mke wake itakuwaje…?’ nikamuuliza‘Nitajitahidi sana …unajua, sizani kama ni tatizo, hata hivyo, ifike muda tuongee, tuone tutafanyaje, na huyo mwanaume …sihitajii sana kumueleza, japokuwa ananiganda sana, unajua awali kabla sijajifungua nilikuwa natamani sana awepo, kuna hali ilikuwa inanivuta awepo,..mpaka nakereka,…lakini sasa nimeshajifungua, sitaki hata kumuona, sijui kwanini ....’akasema‘Haya tutakuja kuongea tu, na kuhakikisha kila kitu tunakiweka sawa, mtoto wako ni wangu, hilo halina shida, usijali kabisa....’nikasema huku nikimuwazia huyo rafiki yangu na mtoto wake, nikikumbuka ushauri nilio mpa, na kujisifia moyoni kuwa nimefanya jambo moja kubwa kwa rafiki yangu, nikasema.‘Ninakuja na zawadi kibao kuonyesha jinsi gani nilivyofurahi, na shemeji nilimuambia kuwa ninakwenda hospitalini kumuona mzazi, unajua alichoniambia,….eti na yeye kuna hospitali anakwenda kumuona mzazi pia…’nikasema‘Oh, ndivyo kasema hivyo, …..’akasema hivyo.‘Nahisi ni mfanyakazi wao ….sijamuulizia sana, lakini anaweza akaja kukuona, ingelikuwa ni bora tungelifika sote,…wanaume hawajui zawadi gani kwa mtoto ningemshauri zawadi gani tuje nayo,…’nikasema‘Ok….sawa, nimekuelewa, …ukija tutaongea….’akasema na mimi nikaendelea kuongea;‘Unajua hizi kazi zetu tena,  mimi na yeye siku hizi tumekuwa kila mtu bize-bize, yeye na shunguli zake, na kazi zake za kuajiriwa, na bado anahitajika kusimamia, kwenye ofisi yake aliyoifungua, kwahiyo kazi zinamuendesha mbio mbio, kama ilivyo mimi,…mimi tu,  nina ofisi yangu mwenyewe bado nasumbuka hivyo, na wafanyakazi, je yeye mwenye majukumu mawili itakuwaje…kwenye ajira ya kuajiriwa na kwenye ofisi yake ya kujiajiri, sio mchezo. …’nikasema‘Hongera zenu mlioweza kujiajiri na sasa mnaajiri wafanyakazi, hata mimi natamani niwe hivyo, natamani sana maisha yenu, yaani sijui kwanini, nataka niwe kama nyie…’akasema‘Unajua …nilitaka nimwambieje shemeji yako, aje tukutane mahali ili tukakununulie kila kitu sitaki ugharimie chochote, cha mtoto hadi wewe mwenyewe…mimi ninataka kila kitu nitoe mimi, unasikia, wewe ni rafki yangu, hilo halina mjadala…’nikasema.‘Mhh, rafiki yangu, utanifanya nilemae bure…hapana… mimi nataka niwajibike kama mzazi, kuanzia mwanzo hadi mwisho, nataka nifaidi kile nilichokikosa miaka yote hiyo, nataka niwe mzazi,… sio mlezi,….’akasema‘Hili usiniambie, bado utaendelea kuwa mzazi,…najua tutanyaje….Hivi nikuulize maana tumeongea sana, vipi kuhusu chakula ….ngoja kwanza nikakununulie supu ya nguvu, napitia kwenye hoteli, .. nitakuja nayo hiyo supu sijapika mwenyewe, nitakuwa nakupikia …lakini kwa leo, kwa dharura, ngoja tununue hotelini…, sitaki mtu mwingine alete unasikia….najua ndio chakula chako kwa hivi sasa…’nikasema‘Haya usichelewe maana huenda wakaturuhusu leo hii…, kwa hivi sasa docta hajapita bado, …..na mimi sipendi kuendelea kukaa hapa ndani, madawa na harufu za kihospitali sizipendi ....we acha tu..hata hiyo supu sizani kama nitaweza kuinywa,…mimi naona ususumbuke kuinunua,..labda kama utainywa wewe…’akasema‘Ina bidi uanze kuzizoea hali za namna hiyo, maana kuna kiliniki ya mtoto, laaima ufike hospitalini, na huwezi jua, ...akiumwa unatakiwa kuja kumuona docta, tena docta wa watoto…’nikasema‘Najua najua..hayo baadae…’akasema‘Sio unajua sikiliza, hayo ni muhimu sana, mtoto mchanga akiumwa uhakikishe unampeleka kwa docta bingwa wa watoto,..sio unaitisha madocta mitaani, au nyumbani,..na usimpeleke  mtoto kwa docta wa kawaida, unaweza ukamkomaza mtoto kwa madawa yasiyomsaidia.....’nikamwambia.‘Haya bwana, wajifanya wewe ni mzoefu sana nakusikiliza, kwani upo wapi, maana nakusubiria, mshauri wangu, na…hebu kwanza,…ok, … nakata simu, maana naona kama docta anakuja....’akasema na mimi nikakata simu.************Nilifika kwenye hiyo hospitali mapema, maana kulikuwa hakuna foleni kama nilivyotarajia, nikampigia simu katibu muhutasi wangu abadilishe ratiba zangu za siku, ofisi yangu ya kujiajiri ni kubwa, ina kila kitu kinachohitajika kama kampuni inayojitegemea.Nilipofika hospitalini, nikapitia njia tofauti ya kuingilia, nilipitia njia wanayotumia wafanyakazi wa hapo maana wao wanasehemu yao, nikaenda kulisimamisha gari langu sehemu wanayosimamisha magari yao, kama mfanyakazi wa hapo, nikaongea na mlinzi alilalamika, lakini nikampa pesa ya soda, akanyamaza.Nikaenda moja kwa moja kwenye wodi ya wazazi, nikamuona rafiki yangu, akiwa amekaa kwenye kitanda, huku akiwa na mkoba wake pembeni, nikashangaa, na kumuuliza.‘Vipi tena, mbona umekaa mkao wakuondoka…?’ nikamuuliza nikimkagua akiwa kambeba kichanga chake na mimi nikasogea na kumpokea.‘Yaani ulipomaliza kuongea na mimi kwenye simu , akaja docta, na akaniambia sina haja ya kuendelea kukaa zaidi hospitalini, nilishukuru kitu, alisema kwa vile mimi sina tatizo lolote, ninaweza kuondoka tu…, basi, nikaona nifungashe-fungashe vitu vyangu, nimempigia simu ndugu yangu aje kunichukua, japokuwa....’akatulia kidogo akimwangalia mtoto.Wakati anaongea akili yangu ilishazama kwenye mtoto, nikawa namkagua,unajue tena sisi akina mama, macho yetu yameumbwa hivyo kudadisi, sura, umevaa nini upoje…kwahiyo kwa muda mfupi nilikuwa nimeshamkagua mtoto , usoni, ..na sikutaka kumuuliza kwanini kakatisha kuendelea kuongea, nikasema;'Mhh, mtoto mnzuri kweli, halafu,ana kila ngapi, mnzito…….umegundua kitu,  kwanini watoto wachanga wote huwa wanafanana, maana namuona mtoto wako anafanana sana na watoto wangu, walipokuwa wachanga...’nikasema na  yeye akaniangalia kwa haraka, halafu akageuka kumwangalia mtoto wake, huku akitabasamu, hakusema kitu akawa anamweka vizuri.‘Naona kweli ndoto yako imetimia, maana ule usemi wako wa kuwa unatamani mtoto wako afanane na watoto wangu, umekamilika…’nikasema‘Mhh, nashukuru kwa hilo,ahsante sana rafiki yangu, bila wema wako sijui ingelikuwaje, .….’akasema akitabasamu.‘Ni kweli, unajua rafiki yangu…ni kweli sasa kile tulichokitaka kimetimia, kweli mungu kasikia kilio chako…yaani nikimuangalia huyu mtoto wako, nakumbuka watoto wangu walivyokuwa wachanga,…’nikasema nikiendelea kumkagua mtoto.‘Kwanza  angalia vimdomo vyake, na…na, macho yake japokuwa kalala.....yaani kama ungelimuweka na watoto wangu enzi hizo wakiwa wachanga, ungelisema ni mapacha na watoto wangu….’nikasema huku nikiendelea kumchunguza yule kachanga.'Kweli,...japokuwa nilitaka wasichana kama wa kwako, na wawe mapacha kama wakwako, …unajua nilitakamani kuzaa mapacha kama wewe…lakini mungu kanipa mvulana, na kweli eeh,…kumbe … wanafanana na watoto wako, oh…’akasema‘Unajua watoto wangu wanafanana zaidi na baba yao kisura , na kirangi wanafanana na mimi, watu wengi wanasema hivyo, hata wewe uliwahi kuniambia hivyo…’nikasema‘Hivi eeeh, ni kweli, …anafanana shemeji…unajua nilikuwa sijaligundua hilo…akili yote ni kwenye furaha kuwa nimempata mtoto…'akasema na akawa kama anaonyesha uso wa haya, hata kuniangalia machoni inakuwa ni ngumu mimi sikuwa na mwazo yoyote zaidi ya kujua ni kufanana tu;‘Mhh, nina hamu sana ya kumuona huyo shemeji, maana sipati picha, kama umeamua kumuhusisha basi hata mimi nastahiki kumuona, au sio,..kwani nikuulize huyo  shemeji yangu ni nani, nahisi kama anafanana sana na watoto wangu, je ameshafika kukuona?’ nikamuuliza‘Bwanaeeh, hayo tuyaache kwanza, tutaongea vizuri tukifika nyumbani, najua una hamu kujua mambo mengi kwa wakati mmoja,…kila kitu nitakuambia,.. lakini kila kitu na wakati wake au sio, tukianza kuongea hapa, huoni watu watatusikia,a au….’akasema‘Mhh, leo twaanza kufichana, haya bwana, lakini kama umeamua kumuhusisha huyo shemeji,…kiukweli sikupendezewa na hilo, halikuwa kwenye makubaliano yetu,  mimi ni mwanamke…, nipo kwenye ndoa, nafahamu ndoa ilivyo…hili lilitakiwa liwe siri yako mimi na wewe, sasa umeshaanza kuharibu mapema, sijui una lengo gani, sijapendezewa na hilo, kwanini ukamwambia huyo mwanaume…’nikasema‘Lakini …sikupenda iwe hivyo,…nilijitahidi sana rafiki yangu… hata hivyo…sizani kama itakuwa na matatizo, sizani..’akasema‘Najua haitakuwa na matatizo,…nitajitahidi kukusaidia, na kukushauri inavyotakiwa, ila nakuonyesha hatari yake,…ndoa ni kitu kingine,…na kwa hili, mimi nataka nionane na huyo shemeji nimsomeshe mwenyewe, ili aelewe…, sitaki uje kupata matatizo, sitaki nikuone unakuja kuishi maisha ya kujihami, maana hujui wanawake wa ndoa walivyo…’nikasema Nikamuuliza huku akilini nikimuwazia huyo shemeji, ambaye nahisi atakuwa akifanana na mume wangu, kwani kiukweli watoto wangu wanafanana na baba yao, na kiukweli, ukimuangalia huyu kichanga,  anafanana sana na watoto wangu.‘Mwambie kuanzia sasa hatakiwi kabisa…na wala asije hapa kukuona…’nikasema‘Mbona keshafika, alikuwa  wa kwanza kufika hapa, na ,na hukumuona huko nje, au aliniambia anasubiria nikiruhusiwa mapema, kama ndugu yangu hajafika atanichukua yeye,… yupo huko nje, ila mimi nimemkatalia kama ulivyonishauri,nimemuambia aondoke, sasa kama bado yupo huko nje shauri lake…’akasema‘Ina maana alishafika…tatizo sikuingilia mlango wa kawaida, nimeingialia mlango wa mastafu…unajua rafiki yangu unafanya visivyo kabisa…’nikasema‘Sikutaka kabisa yeye aje nilimuelezea yote hayo, kuwa kuanzia sasa sitaki anifuate fuate, lakini akasema na yeye atachukua tahadhari, hata hivyo hawezi kuniacha, …ndio maana alikuja mapema ili anichukue , halafu arudi nyumbani kwake…hata yeye hapendi…lakini unajua tena…hata hivyo nilimuambia huu ni ushauri wako …’akasema‘Masikini…mmh, unajua naanza kuwazia mbali, huyo mke wa huyo mwanaume, unajua inauma sana....lakini tutaona la kufanya, ila nataka nionane naye huyo mwanaume kwanza ni muhimu nikutane naye nimsomeshe mimi mwenyewe.., kama ni lazima vitu vyote vipitie kwangu, na mimi nitajua jinsi gani ya kufanya…’nikasema‘Usijali rafiki yangu, …mimi nataka hili jambo niliweke wazi kwako, ndio maana nataka tukaliongelee huko nyumbani, wewe ni rafiki yangu, najua hutanilamu kwa lolote lile, nilifuata ushauri wako tu…’akasema‘Siwezi kukulaumu kabisa, kwanini nikulaumu..ushauri nimeutoa mimi mwenyewe, sasa itakuwa ni ajabu nianze kukulaumu, ila ni lazima tuchukua tahadhari, maana utu, ubinadamu,…kuna kuumia hapo, mwenye mume, akijua ni lazima ataumia, ndio hilo silitaki kabisa…’nikasema na rafiki yangu akawa kama ananywea fulani hivi.‘Umefanya makosa sana…’nikasema‘Usinilaumu rafiki yangu, maana nilifanya juhudi zote,….lakini ikashindikana…hata sijui alijuaje kuwa nimejifungua, sikutaka kabisa kumfahamisha hilo maana nilikuja kutoka Zanzibari kwa siri, na sikuwahi kumpigia simu, …’akasema‘Sasa alijuaje…?’ nikauliza‘Hata sijui, kaniambia … kumbe alikuwa akinifuatilia kila siku alipogundua kuwa nimefikia muda wa kujifungua, akawa anafuatulia nitakwenda hospitali gani, sijui kwanini …nashangaa nimejifungua, sina hili wala lile huyu hapa , akawa yeye ndiye  wa kwanza kuja kunipa hongera, na alipogundua kuwa nimejifungua mtoto wa kiume, amefurahi kweli kweli, nikampa onyo, kuwa huyo sio mtoto wake...’akasema‘Kwahiyo kumbe mlikuwa mnaelewana sana na huyo shemeji, mlikuwa karibu sana kihivyo usinidanganye rafiki yangu, umefanya makosa ambayo utakuja kujijutia, nakueleza ukweli ulivyo…, inatakiwa tuwe makini kuanzia hivi sasa, utakuja kupata lawama kubwa sana.‘Kuelewana kwa vipi, si tuliliongea hili kuwa nimetafute yule ambaye namuelewa sana,….na unajua,… nikuambie kitu, shemeji alinibana sana...mwanzoni nilimficha, lakini wanaume bwana, akawa akinidadisi mara kwa mara hasa alipoona mabadiliko, najuta kwanini nilishindwa kumdanganya, ...na tatizo kama nilivyokuambia awali , nilikuwa natamani sana awepo karibu yangu mara kwa mara..na…kila mara nataka angalau nisikie sauti yake, angalau, …mimba ina matatizo jamani….’akasema‘Nayafahamu sana, ukiwa na mimba unaweza ukampenda sana mume wako au ukamchukia sana, inatokea hivyo, lakini mimi naangalia kote kote, kwa vile mimi ni mzazi, mimi nipo kwenye ndoa, nayafahamu hayo zaidi, jinsi gani mtu unavyoumia ukiibiwa mume wako…’nikasema‘Usitake kunitia kwenye lawama tena, ushauri wako ndio umeifanya hii kazi, na najua wewe hutaweza kunilaumu kwa hili…’akasema kidogo akionyesha hasira.‘Sio kwamba nakualaumu, ..unasikia kwa vile ni mimi nimeutoa ushauri, nataka ushauri uende ilivyo, isje ukapata matatizo, tunahitajika kuchukua tahadhari zote, unielewe hapo…’nikasema‘Sawa basi tuondoke, maana dawa ndio hizo hap anazileta nesi, kila kitu sasa kipo sawa sawa….’akasema‘Kwahiyo mimi nashauri ni bora twende nyumbani kwangu ili niweze kukusaidia vizuri, sitaweza kujigawa, mimi nilikuja na wazo hilo japokuwa sijaongea na mume wangu, lakini hili sio lazima nimuambie anakufahamu wewe kama ndugu yangu…’nikasema.NB: Ngoja tuishie hapa kwa leoWAZO LA LEO: Urafiki wa kweli hujengwa na kuaminiana,..kama mtakuwa manafichana mambo yenu, ujue urafiki huo una walakini. Lakini pamoja na hayo, tusiwe tunafanya mambo kama kufurahishana tu, unamshauri rafiki yako, ili tu afurahi, bila kujali athari zake mbeleni.‘Kwahiyo mimi naona twende ukaishi kwangu…;’‘Hapana, hilo sio wazo zuri kabisa, mimi sikubaliani nalo, huwa nafuata ushauri wako, lakini sio huo…..nataka nikaishi kwangu, sitaweza kuishi nyumba moja na shemeji, hahaha, unajua mimi nataka nikakae kwangu ili niweze kumlea  mtoto wangu mwenyewe, nataka niipata ile shida ya mama…’akasema‘Mhh,..sijakuelewa kwahiyo kinachokukataza kuja kuishi kwangu ni kumuogopa shemeji yako, hayo yameanzia wapi, …ya kuanza kumuogopa, si unamfahamu alivyo, hana muda na mtu kabisa, ni simba mwenda pole, ila namuamini sana mume wangu hana tatizo na mtu, hajawahi kunificha ficha mambo yake, labda kama yapo mengine siyajui…’nikasema.‘Ni kweli simba mwendo pole, …hata hivyo, nimesema tu hivyo…’akasema‘Au wewe una lako jambo,nahisi mumeshapanga na mwenzako kuwa uendelee kukaa kwako, ili aweze kukutembelea…bila kuwa na kikwazo, si ndio hivyo….’nikamwambia‘Aaah, hapana..sio hivyo, sijaongea naye kuhusu hilo, ila sio vizuri,….na.., na kwanza hilo halimuhusu kabisa…ila mimi mwnyewe naona tu nikakae kwangu, tafadhali nielewe hivyo…, na hilo tusiishie kubishana nalo.., wewe kama huna muda, …na najua hutakuwa nao, kuna ndugu yangu kasema atakuja….’akasema‘Nikuulize swali moja, je huyo mzazi mwenzako unampenda….?’ Nikamuuliza‘Swali gani hilo jamani, nitampendaje mume wa mtu,…au umesahau tulichokijadili tokea awali, …yeye kazi yake imekwisha au sio….lakini nataka tukifika nyumbani tuongee vizuri, hili jambo tuliweke  wazi, nataka nikuambia kila kitu au unasemaje, ili isije kuleta matatizo baadae unaonaje…?’ akaniuliza‘Sawa, kwani kuna shida kwa hilo, mimi na wewe tena, au sio, hata mimi nina hamu ya kusikia ikiwezakana kila kitu, usinifiche mimi, sawa hilo litanipa faraja kuwa unaniamini …’nikasema'Unajua baada ya hili,..sizani kama nitarudia tena ….maana hata yeye, amekuwa kwenye wakati mgumu, japokuwa unajua tena wanaume,, sikutaka wazo la kuwa marafiki wa siri, hilo nimelipinga, japokuwa aliniomba hivyo…unajua hata kama imetokea hivi, bado msimamo wangu upo pale pale, sitaki mume wa mtu, hili nimetokea kama dharura basi..kuanzia leo..sitaki tena mwanaume, hasa mume wa mtu, iliyotokea imetokea, hiyo mara moja na sitarudia tena hili....’akasema.‘Hahaha, hata sisi tulisema hivyo, kuwa sitazaa tena, lakini kiukweli, watoto wanaraha zake, ukiona mwenzako ana watoto zaidi ya mmoja, wanakimbizana, utatamani sana na wewe uwe nao…, kama mimi sasa hivi natamani nipate mtoto, nipate mtoto wa kiume, kama anavyotamani shemeji yako, ...’nikasema.‘Mhhh….kweli eeh, labda…’akasema na kutulia kimia kama anawaza jambo.‘Unajua kama huyo mwanaume angelikuwa sio mume wa mtu, ningekushinikiza akuoe, maana naona umempenda kweli,…lakini sasa, kama ni mume wa mtu achana naye kabisa,…unasikia, ukitaka usalama, na ili hili lisivuje, achana na huyo mwanaume, ndio maana nilitaka nikutane naye, ili nimkanye, na mambo yaishie hapa hapa,kwani mlikubalianaje, kuwa atakuwa akikutembelea au,...?’ nikamuuliza.‘Nitakubaliana vipi bwana…., na mtu mwenyewe sio mtu wa kunioa...kwanza sipendi kumuongelea tena ...naona hilo tuliache kwanza….’akasema na niliona kweli hakutaka kumuongelea huyo shemeji, nilifahamu ni kwanini, lakini moyoni nilikuwa na hamu sana ya kufahamu huyo mwanaume wake.Kila mara nilipo-muangalia huyo kichanga, nakuwa kama nawatizama watoto wangu walipokuwa wadogo, na hamu ya kukutana na huyo jamaa ndio inazidi, kwani nahisi atakuwa anafanana sana na mume wangu. Wakati mwingine niliwazia huenda ni mmoja wandugu za mume wangu, lakini nani nisiyemfahamu.Basi taratibu za hospitalini zilipokwisha nikamshauri kuwa mimi nitampeleka nyumbani, haina haja ya kusubiria gari lake,..kwani aliagiza mtu aje kumfuata, hakutaka kupelekwa na mtu mwingine,‘Nimesema mimi ndio nitakufikisha nyumbani,…’nikasema, na hapo akawa hana ubishi kwa hilo, na muda huo, ….nikawa nataka kumpigia mume wangu simu, lakini nafasi ikawa hanipi kufanya hivyo, nilitaka nimuarifu kuwa tumeshaondoka hospitalini kama ananitafuta,..na huenda atakuwa na hamu ya kuja kumuona mzazi, lakini kama kawaida nilipojaribu kupiga simu  yake ikawa inatumika.‘Huyu shemeji yako bwana…’nikasema‘Shemeji yangu..nani, mume wako, kwani vipi, kasemaje…?’ akaniuliza akiniangalia kwa hamasa‘Kila mara simu yake ipo inatumika, yaani nikitaka niwasiliane naye labda nimtumie ujumbe wa maneno…, ndio baadae anakupigia, siwezi kumlaumu yupo na shughuli nyingi sana,..’nikasema‘Hamna shida, usimsumbue tafadhali….’akasema‘Sio kumsumbua, atakuja kunilaumu kuwa sijamfahamisha,…..’nikasema, na akaonekana hana raha, akawa kaangalia nje.‘Mhh, usiseme sasa tunataka kufichana nakuona kama una mawazo sana badala ya kuwa na furaha, hiki ni kipindi chako cha kufurahi au sio,  mimi ndiye rafiki yako, mshauri wako, na lako ni langu, kama kuna kitu unahisi kinakukwaza, niambie nijue ni jinsi gani ya kukusaidia, unanielewa hapo….au ni kuhusu huyo shemeji…?’nikamuuliza.‘Shemeji!….mmh,…’akasema na akawa kama anawaza jambo halafu akasema;‘ Ni kweli kama usingelikuwa wewe, nisingelikuwa na wazo hili, lakini  mhh, kuna kitu bado sijakielewa, na sijui kwanini naogopa,…labda kwa hivi sasa nibadili  mawazo….kwanini, nisifuate masharti yako kabisa, ili kuepusha shari,…’akasema‘Kuepusha shari…! Ahari gani kwani,…mimi nakushangaa, n kwanini ulikwenda kinyume na maagizo yetu, ungelifuata nilivyokuambia usingelikuwa kwenye wakati mgumu wa mawazo ..sasa nakuona huna raha, sijui kwanini….’nikasema‘Ni lazima iwe hivi, na hujui tu, nilijua ni rahisi kwa vile ni wewe, lakini mmh, unajua nilijitahidi sana, yaani mpaka nafikia hatua hiyo…niliwazia sana…kiukweli nimepitia wakati mgumu sana…sijui kwanini niliamua kwa haraka iwe hivyo, sikuwa na nia na yeye, lakini imeshatokea tena nitafanyaje, nakutegemea wewe tu…’akasema‘Ina maana huyo shemeji, ..hukuwa na …sijakuelewa hapo, hebu nifafanulie kidogo, ni kama ulilazimishwa, au ilikuwaje…?’nikasema na kuumuliza‘Unaonaje tukafunga huu mjadala wa huyo shemeji,..ili nifikirie zaidi, tukifika nyumbani nitakuwa na maamuzi kuwa tulijadili na mimi nikuambie kila kitu au la,  ….najua wewe ni mshauri wangu, lakini…kwa hivi sasa naomba tusimjadili shemeji, unaonaje,…tusubirie hadi nifikie muafaka fulani kichwani…’akasema‘Sawa ungeliwazia hilo tokea awali, lisingelileta mashaka, ingelikuwa ni siri yako tu, lakini sasa umeshaanza kuliweka wazi, na mimi huwezi kunificha tena, ni wewe umenihamasisha, na sio wewe tu hata mtoto ananifanya niwe na hamasa ya kumuona huyo baba yake, ni nani huyo shemeji yangu…’nikasema‘Sio baba yake jamani…, tafadhali, hiyo kauli siitaki kusikia,,…’akasema‘Naongea nikiwa mimi na wewe,…hata hivyo kwanini,…ndio nafahamu kwanini unasema hivyo,..lakini wewe mwenyewe umeshamshirikisha huyo mtu au sio, hata hivyo usijali, kwangu mimi najua kila kitu, ni siri yetu mimi na wewe au sio…’nikasema‘Ukisema ni baba yake wakati ni mume wa mtu naumia sana...mimi sina mpango wa kuolewa na yeye na wala sina mpango wa mahusiano na yeye tena,  ilikuwa ni kwa minajili ya hilo zoezi na sasa limekamilika basi….na kiukweli, sitaki hata kuyakumbukia hayo yaliyopita....’akasema na mimi nikaingiwa na hamu zaidi ya kujua ilikuwaje siku hizo walipokutana naye ilikuwaje , lakini sikutaka kushinikiza aniambie jinsi livyokuwa .‘Ok sawa, lakin kama rafiki yako nahitajia kufahamu mengi ili nisiumie kichwa changu kuwazia hilo,…usiniweke njia panda tena,… na kama umeshampa tahadhari huyo mwanaume,  ya kuwa iwe mwanzo na mwisho basi haina shida…’nikasema‘Nimemwambia shemeji, hili jambo limetokea lakini nataka iwe siri, kwani hata hivyo tangu awali sikutaka alifahamu hili kuwa ndio yeye aliyemipa huo uja uzito, ila kwa kunifuata fuata kwake mara kwa mara ndio nikajikuta nikimwambia hivyo…najua nimefanya kosa kubwa, kinachoniumiza zaidi ni kumuona jinsi alivyokuwa na furaha alipomuona huyo mtoto, sijui kwanini…’akasema.‘Eeeh,…alikuwa na furaha, ndivyo wanaume walivyo…na huenda na yeye alikuwa akihitajia mtoto, hana watoto nini…?’ nikamuuliza‘Mbona anao,…’akasema‘Basi huenda, alihitajia mtoto wa kiume, ..ndivyo ilivyo, ni kama mimi na mume wangu,  mfano si kama huyu mume wangu, anahitajia sana mtoto wa kiume, ila nimemuambia asije akakufuru, akaenda kutembea nje, sisi tumtegemee mungu tu, na ipo siku atawapata, …tena mapacha wa kiume kama walivyokuwa mapacha wa kike…hahaha…’nikasema na kucheka.‘Mapacha tena,!…Unanifanya nikumbuke kuwa hata mimi nilitaka nipate mapacha, ndio maana nilimuona shemeji ataweza kulifanya hilo,  kumbe …sio kwa kila mwanamke inaweza kutokea, ni mipango ya mungu au sio…’akasema‘Kwahiyo kumbe na yeye ana watoto mapacha, kama wangu ehe…wewe naye, kila kitu unataka sawa na mimi, hahaha…lakini ndio uafiki wetu ulivyo,..usingelikuwa wewe ni kama ndugu yangu, ningelisema…uolewe na mume wangu,…hahaha natania bwana, wewe, kuolewa uke wenza sio mchezo, ni heri yeye mwenyewe aamua,..hujui  mimi nina wivu sana, naweza kuua, hata hivyo, mume wangu hataki,..na mimi pia sitaweza,….’nikasema na kucheka.‘Hata mimi sitaki kuolewa uke wenza…..’akasema kwa sauti nzito‘Mbona umezaa na mume wa mtu…’nikasema kiutani huku nikicheka.‘Na wewe bwana unaanza kunigeuka, halafu....nimeshampa onyo, kuwa kazi yake imekwisha, sitaki tena mahusiano na yeye na nimemwambia hii iwe siri, kwani sijui kama litapokelewaje, maana kusema na kutenda ni vitu viwili tofauti…’akasema‘Kupokelewa na nani, na huyo mke wake au sio, ni ngumu, halitaweza kupokelewa vyema, hilo ndivyo ilivyo, najichukulia mwenyewe mimi, ..nisikie mume wangu kafanya hivyo, mbona kutachimbia, sio rahisi kihivyo, ndio maana nilitaka hili lifanyike kisiri na iwe siri yako, wewe…’nikasema‘Mimi nilijua kutokana na ushauri wako, wewe upo radhi..na nilijua hakutakuwa na matatizo, kwani ushauri wako ulikuwa wa kunitega mimi…’akasema‘Sio wa kukutega bwana, wewe ndio umeharibu, ..hukufuata kama nilivyokuagiza,..’nikasema‘Mhh, kwa kauli hiyo, mimi naanza kuhisi uwoga fulani hivi,..maana huwezi kujua msimamo wa mtu nafsini mwake,..na mimi ni jambo la mwisho nililotaka litokee maisha mwangu, mimi sikupenda na sitaki kabisa kuharibu ndoa za mtu. Nitaumia sana, itanifanya nihame huu mji…’akasema‘Nio maana nilikutahadharisha kuwa hata hilo tendo, eeh, usije kumfahamisha kuwa lengo lako ni nini..na mbegu ikiota usije kumwambia huyoo mkulima…umenielewa hapo…’nikasema‘Wewe ni rafiki yangu nakuamini sana, na siri hii unaifahamu wewe tu kwa vile wewe ndiye mshauri wangu,….na kama ulivyonishauri wewe kuwa iwe hivyo, ndivyo nilivyofanya, na kuanzia sasa itakwua hivyo, nimekosea huko nyuma, sitaki nikosee tena…,’akasema na kutulia kidogo.‘Sawa lakini niachosema hapa, eeh, ni wewe hukufanya nilivyotaka mimi…’nikasema‘Nasema hivyo wewe ulinishauri kuwa hata kama ni mume wa mtu, nisijali kwa vile ni jambo la dharura, na nichague kwa marafiki zangu ambao naona hawataniletea matatizo,..naomba unisikilize hapo kwa makini…’akasema‘Sawa basi tutaliongea huko mbele, au sio, au unataka tuliongelee humu kwenye gari nisimamishe kidogo,  au sio…?’ nikamuuliza na kusimamisha gari.‘Hapana nataka nikuweke wazi tu,…kuwa mimi hata kufikia kulifanya hilo haikuwa kazi rahisi kama unavyofikiria wewe..na nilijitahidi iwe hivyo,…kuwa ni dharura tu, lakini ikashindikana maana ilikuwa kama natishwa sasa, usipo..nitamuambia..vitu kama hivyo..unanielewa hapo…mimi sitaki nikuweke wazi kabisa,…maana nimeshaanza kuogopa,… ila naomba usinilaumu kwa hili kabisa, nilifanya juhudi zote ikashindikana…’akasema‘Ndio maana nasema, kuanzia sasa usifanye jambo bila kuniuliza na huyo mtu kama ingeliwezekana nilitaka awe anapitia kwangu, maana kwa hali yako kwa sasa huhitajiki kukutana naye tena, unanielewa hapo, kuna kitu kinaitwa kubemenda mtoto, uliwahi kusikia kitu kama hicho…, wengi wanakizarau, lakini kina maana yake kubwa sana…’nikasema‘Mimi wala sipo huko, huyo mtu ilitokea hivyo, na simtaki tena, hata kumuona, nikiwa na mimba ndio nilikuwa natamani …sasa hivi, sitaki kabisa, hata nikimuona naona aibu, nahisi dhambi,....na nitajitahidi kumfukuza akija…’akasema‘Lakini, sio nakualamu, haya yote umeyataka wewe, nilikushauri vizuri tu,...sasa ni hivi, kwa vile keshajua, na amekuwa na kimbelembele chake, kama atazidi  kukufuata fuata, eeh, nina wazo jingine…, usimwache hivi hivi, maana mtoto akikua anaweza kuanza kudai baba yake ni nani…’nikasema‘Unataka kusema nini…?’ akaniuliza akinitolea macho.‘Naongelea hili nikiwa na maana ya hali halisi, ..mtoto utamficha wewe kuwa baba yake ni nani, lakini jamii, itakuja kuligundua hilo, na mtoto atakuja kuambiwa, wakati huo wewe umeshaumia sana,..kulea nk…sasa kama anajilengesha kihivyo, basi, mbebeshe dhamana…. muwajibishe , sio kwamba hatuwezi kumtunza, hapana, lakini ili aone kuwa na yeye anathamani fulani, na ili asije kuharibu mpe bajeti yake..’nikasema. ‘Hapana, hapana,…hilo wazo siliafiki,  kwa hilo tutakosana, mimi bado nipo kwenye makubaliano yetu ya awali,…, naomba tuyalinde kabisa,..ndio nimeshaharibu kidogo…lakini tusiendelee kuharibu zaidi, na …mimi naona hata kile nilichotaka tukijadili kiishe tu, tuondoke tu….’akasema‘Usitake kuniudhi, si umeshamuambia yeye…sasa hapo kuna siri gani tena eeh, au mimi na yeye unayemthamini na kumuamini zaidi ni nani,…, mimi nataka tuwe sawa, inachotakiwa kwa vile umeshaharibu , basi na huyo muhusika naye awajibike kama baba, hutaweza kumtenganisha na huyo mtoto tena, huyo baba anaweza kujitahidi kuonana na huyo mtoto, unajua kitakuja kutokea nini,…unielewe hapo, …, hapo kwa hivi sasa hakuna  siri, kama tulivyopanaga awali….’nikasema‘Mhh, hapana,….mimi  sitaki kumuhusisha huyo mwanaume na mtoto wangu, sitaki anisaidie kwa lolote lile, mimi mwenyewe nilishajiandaa kwa hilo, nitajua jinsi gani ya kufanya,…na sitaki mtu yoyote yule kubeba majukumu ya kumlea mwanangu, sitaki lawama na mtu…usije kunielewe vibaya wewe ni rafiki yangu…’akasema‘Kwanini unasema hivyo…?’ nikamuuliza‘Huyu ni mtoto wangu, na lengo lake tulishaliweka bayana tokea awali,…au sio… hata jina la baba yake nitaandika ukoo wetu, basi, mengine tuyaache kama yalivyo,.....’akasema‘Ulitakiwa ulifahamu hilo kabla hujamuhusisha huyo mtu, wewe ndio umeharibu, nitarudia tena hilo mara nyingi ili uelewe,..na huenda hata sijui kwanini ulimchagua mtu kama huyo ambaye sasa anakuja kukusumbua, labda kumbe ungelinishirikisha na hilo, huenda hili lisingelitokea,…’nikasema‘Ndio nakiri kuwa nimefanya makosa, lakini sitaki kuendelea kuyafanya makosa zaidi,..na kumchagua huyo,  niliangalia mambo mengi tu..urafiki wetu nk…, na jingine kubwa ni usalama wangu na mtoto wangu,… lakini hata hivyo,  yeye ni mume wa mtu, na kwangu mume wa mtu ni sumu, hili kosa nililolifanya sasa naanza kulijutia,na kamwe sitarudia tena, namuomba mungu anisamehe, na anisaidie…’akainama kama anajijutia.‘Kwahiyo unataka kusemaje,…maana hapo ni kama unaniweka pembeni, kuwa nisijihusishe na mambo yako tena, au…?’ nikamuuliza‘Hapana sina maana hiyo, najua wewe ni muhusika mkuu wa hili, na kwako nahitajia msaada mkubwa kwako… bila ya wewe bado nitakuwa kwenye wakati mgumu, ..nashukuru kwa hilo, kuwa wewe ndiye umeliwezesha hili, kwa upande huo napata faraja sana, kwani nimepata kile nilichokuwa nikikitaka, kabla sijafikia miaka ya hatari ya kuzaa, ila mengine eeh, tuyaache kama yalivyo, ..’akatulia huku akimwangalia mtoto.‘Ok, japokuwa sijakuelewa….ngoja tufika nyumbani, na …najua hata shemeji yako akikuona atakuulizia baba yake ni nani…mimi siwezi kumuambia lolote hata kama ni mume wangu,..najua jinsi gani ya kumweka sawa…’nikasema‘Nampenda sana mtoto wangu..kinachonisikitisha ni tendo lenyewe, ..sikupenda kutembea na mume wa mtu, sikupenda kabisa....ni mawazo yako yaliniteka akili yangu, na sio kwamba nakulaumu kwa hilo,…lakini je yataisha salama,…ninaanza kuingiwa na mashaka,… je hizo lawama hazitaendelea,, hapo ndio naogopa zaidi…’akasema‘Mimi sioni kwamba kuna tatizo hapo, nakulaumu tu kwa vile hukutaka kufanya kama nilivyokuelekeza, na wasiwasi wangu ni kuwa huyo shemeji, huyo mwanaume anaweza kuwa ndiye tatizo, na lisije kufika hadi kwa mke wake, ndio hapo naogopa mimi…’nikasema‘Oh, sijui…lakini kwanini….’akashika kichwa huku akimuangalia mtoto wake…‘Kwanini vipi tena, yaishe tutatafuta njia ….tukishirikiana tutaliweka sawa,…na huenda ukampata mume ..ukimpata mume hili litajifunika kabisa…’nikasema‘Kumpata mume, wakati nimeshazaa tayari…mmmh, sijui,.. kuna wakati mwingine  nawazia mbali na kujiuliza, ni kwanini mimi, na ina maana mimi nilitakiwa iwe hivi, nizae tu bila kuolewa, na huenda nitaishia kuzalilika hivi…, na sasa naanza kuhisi uwoga ambao sikuwa nao…nilitarajia hili litakuja kuisha kwa salama tu, na kwa hili nimejifunza kitu, sitarudia tena makosa haya, huyu anatosha kabisa sitaki tena mwingine...’akasema.‘Pole sana rafiki yangu, hiyo ndio ujue kwanini watu wanasema ni nani kama mama,…sisi akina mama wakati mwingine tunabeba mzigo mnzito wa siri…usione wakina mama wana watoto wengine wanawabebesha waume wao watoto sio wao, lakini inabakia kuwa siri ya hadi kifo…ni maisha tu…’nikasema‘Ndio maana,  nataka nimlee mtoto wangu peke yangu….’akasema‘Hamna shida, lakini mimi nitakusaidia kadri ya uwezo wangu, nahili litapita tu.., na mambo yatakuwa sawa tu…, kama tutashirikiana na kuhakikisha huyo mwanaume hakusumbui na kujiweka kimbele mbele, kama ana mke wake, aendelee kuwa na mkewe, kosa limtendeka, basi liishie hapo hapo….’nikasema‘Na hapo ndio najikuta kujuta kuwa nimetenda kosa, kwanini sikuchagua mtu mwingine zaidi ya huyo, nilijua huyo ndiye chagua sahihi, lakini mmh, lakini `anyway’ cha muhimu ni kuwa kile nilichokitaka nimekipata, na nashukuru sana kwa ushauri wako huo, wewe ni rafiki yangu mwema sana, nakushukuru sana, mengine kwa sasa eeh, niachie mimi mwenyewe, usitake kujua zaidi..’akaniambia.Nikaangalia saa nikaona tumepoteza muda mwingi tukiongea, na muda huo tulikuwa tumesimamisha gari, nikasema;`Haya twende….kwahiyo sasa umeamua kuwa twende kwako, umeanza kunikimbia rafiki yako kidogo kidogo, naanza kulihisi hivyo,…mimi  nilipendelea huyu mtoto ikiwezekana akulie na kulelewa pale kwangu, ili uwe na nafasi ya kuhangaika na shughuli nyingine ujue wewe ni baba, na mama pia…’nikasema‘Hapana….nataka nikakae kwangu…’akasema‘Unajua niliposikia umejifungua, nikawaza huyo mtoto akiwa kwangu, na mabinti zangu waanavyopenda watoto, nikajua huyo atakuwa sehemu ya watoto wetu, sijawaambia na wakisikia, sijui itakuwaje, watafurahi sana, watataka wakae na  kaka yao… , mdogo wao, anayefanana na wao, kwanini unapinga wazo langu...’ nikamuuliza .‘Unajua hata huyo shemeji, alipofika hapa alisema hivyo hivyo…’akasema na akawa kama kasahau kitu akashika mdomo.‘Alisemaje…?’ nikamuuliza, na akasita kidogo, baadaye akasema‘Hamna shida …’akasema‘Mimi sitaki hiyo tabia, ya kuongea jambo, halafu unaghairi, hujui unaniweka kwenye wakati mgumu wa kuwawa waza, usingelikuwa wewe ni rafiki yangu, ningelikufikiria vibaya…’nikasema‘Alisema hivi, kaamua kuacha shughuli zake  kwa ajili yangu, kwa ajili ya mtoto, kwahiyo nisikatae yeye kunichukua hadi nyumbani…..sipendi kufuatana naye tena, nimemkatalia, na ungelifika mapema mngelikutana naye hapa, sijui ingekuwaje, na mimi sikulitaka hilo,....nimemuonya kuwa sitaki anifuate fuate tena, lakini namuona kama kapagawa,hasa  alipomuona mtoto utafikiri hana mke na watoto..’akaniambia..‘Mhh, kwani yeye ana watoto wangapi…?’ nikamuuliza‘Anaaaah, mh, ana watoto wawili wa kike…’akasema‘Kama mimi, wewe una hatari kweli, kwanini ukachagua mwanaume sawa na mume wangu, hahaha, nimekugundua, wewe unataka kila kitu tuwe sawa, lakini umezaa wa kiume na sio mapacha, yote ni heri tu au sio….’nikasema Akatabasamu….na kuangalia pembeni,  halafu akasema;‘Aaah mimi sijui, nilichotaka ni mtoto, sasa kama kuna mtu anapenda mtoto wa kike au mtoto wa kiume, mimi sina wazo hilo,…hilo kwangu halikuwa na sababu niliongea mengine wakati ule kuwa nataka awe hivi na vile lakini …ilikuwa ni kuonga tu, sasa hivi naona mtoto ni mtoto tu…hayo ya mtoto gani, wa kiume au wa kike, ni mawazo ya mtu binafsi, na sitaki hata kuyasikia, ...’akasemaNa tukaondoka kuelekea nyumbani kwake, maana alikataa kabisa niende naye kwangu, sikutaka kumlazimisha zaidi…  na mara simu yangu ikalia, alikuwa na mume wangu, nikapokea,‘Nimekuwa nikikupigia lakini ukawa hupatikani, simu yako muda wote inatumika, vipi ulikwenda kumuona mzazi uliyesema unakwenda kumuona..?’ nikamuulizaAkasema ndio, ameshamuona tayari, ila anaweza akaenda huko nyumbani kwake, kuna mambo anataka kuyaweka sawa….‘Kajifungua mtoto gani, mambo gani tena kwani ana udugu na  familia yenu….?’ Nikamuuliza, akasema mtoto wa kiume, hakusema zaidi‘Oh, nahisi umeona wivu sana kwa vile ni mtoto wa kiume na wewe unataka mtoto wa kiume nikuambie kitu hata huyu rafiki yangu kajifungua mtoto wa kiume…yaani we acha tu,..na sisi tukijaliwa tutampata tu, mtoto au watoto wa kiume hahaha, mume wangu, usiwe na wivu,.. …unasemaje…, sijakusikia vyema…’ nikasema kuna kitu aliongea lakini sikukisikia vyemaBaadae akaniuliza nikitoka huko nitakwenda wapi, au nitarudi nyumbani muda gani, nikasema;‘Sijajua, ila nikimfikisha huyu mzazi kwake, naweza kurudi nyumbani mara moja kuhakikisha shughuli zangu  zinakwenda vyema, baadae naweza nikurudi tena kuhakikisha kuwa mzazi yupo na mtu, au nikusubirie huko kwa mzazi, unasemaje, utakuja saa ngapi, ?’ nikamuuliza, na hakujibu mara moja nikazidi kumuambia‘Ni vizuri uwe wa awali awali, njooo bwana kwani upo wapi, kazini…’nikamuuliza, akasema yupo njiani, barabarani,…Mara  akageuza mazungumzo na kuanza kuniuliza mambo mengine ya kikazi, na baadae nikamuuliza tena‘Sasa utakuja huji, …mbona hujanijibu swali langu…’nikamuuliza na yeye cha ajabu akaniuliza kuja wapi....,‘Hivi upo sawa wewe, tunajadili kuhusu rafiki yangu, huyu ni mtu muhimu sana kwangu, kama upo na shughuli zako sawa, lakini nilitaka uje unikute hapa, kuna mambo nilitaka tuyajadili pamoja …’nikasema akauliza mambo gani‘Ukifika nitakuambia…kwahiyo unasemaje utakuja, ni muhimu sana kwangu…kuna kitu nimekigundua, na…ungelikuja …eeh, unasema, …mbona una mumunya maneno, sikuelewi, …nimefanya makosa gani, hebu uje….kwanini sasa…’nikasema na yeye akasema kwa hivi sasa hana nafsi, niwahi kurudi nyumbani kwani kuna jambo muhimu anahitajia tulijadili mimi na yeye, nikamuuliza jambo gani,  hakujibu hapo hapo, ….baadae akasema;‘Njoo haraka nyumbani nakusubiria…’‘Ok nakuja…’nikasemaNB: Haya mambo yanaanza kujipikaWAZO LA LEO: Tunaweza kupanga mambo yetu, lakini yawe ya heri, tukipanga mambo yenye ‘shari’ ndani yake, shari hiyo hiyo inaweza ikawa ni sababu ya kuharibu hayo mambo.  Hatutafanikia,na hata tukifanikiwa, shari bado itatusakama kwenye maisha yetu. Tusisahau kuwa tukiwa wawili, mwenyezimungu yupo nasi, ..kwahiyo hatuwezi kuficha mambo yetu. Ni bora tujitahidi sana kukwepa mambo mabaya, na kujadili mambo yenye heri, ambayo yatakuja kuleta baraka kwenye maisha yetu.Mume wangu aliponiambia yupo barabarani, nikakumbuka kitu, wakati tunatoka pale hospitalini, ..japokuwa sina uhakika sana, niliona kama gari la mume wangu likitoka,..unajua gari langu niliegesha sehemu ya nyuma ya jengo la hospitali…Hapo nikawaza jambo, huenda mume wangu alikwenda kumuona mzazi hapo hapo hospitalini, ..sikuweza kukumbuka kumuuliza huyo mzazi alilazwa hospitalini gani, kama ningelijua kumbe ingelikuwa ni rahisi tu, ningelimuita aje tumuone rafiki yangu.Lakini haikuwa na umuhimu kwa muda huo…Tuendelee na kisa chetu…**********‘Mhh, aisee, mtoto wako anafanana sana na watoto wangu, sasa nimemwangalia kwa makini, mwanzoni nilijua ni kwa vile watoto wachanga huwa wanafanana sana wanapozaliwa…, lakini kwa huyu, nimehakikisha, anafanana sana na watoto wangu, isingelikuwa wewe ni rafiki yangu,… ndugu yengu, ningelifikiria vibaya, lakini sizani kama wewe unaweza kufanya hivyo hahaha, sina mawazo hayo mabaya, samahani…’nikasema‘Kufanyaje…?’ akauliza akikwepa kuniangalia‘Hebu tuyaache hayo, haya niambie ilikuwaje, ni nani huyo shemeji , maana umekuwa ukisema tu shemeji, shemeji, unajia nikuambie kitu, kila hatua navutika kufahamu ukweli, niambie nisibakie hewani, maana kiukweli umeweza…, hujafanya makosa, na umekipata kile ulichokitaka, mimi nakuaminia, sikufanya makosa kukushauri…’nikasema‘Nikuambie nini tena rafiki yangu nimeshakuambia,… kosa la awali sitaki kulirudia tena, kuna kauli zako zimenitisha amani…, naona hata ushauri wako, haukuwa na usawa kivile…, ulinishauri tu, kwa kunifurahisha…’akasema akinikwepa kuniangalia machoni.‘Mhh, sijakuelewa, hapo una maana gani, ina maana mimi nilifanya makosa kukushauri hivyo au….rafiki yangu hapo sasa wanifanya nitake uniambie ukweli,…sasa niambie ukweli, tusije kuudhiana bure…unanifahamu nilivyo, subira yangu ni kubwa lakini ikifikia mahali …inakuwa siwezi tena,.., unanifanya nianze kuvuta hisia ambazo hazipo na mimi sio mtu wa namna hiyo , hasa kwako..’nikasemaRafiki yangu akabakia kimia, halafu akamuangalia mtoto wake, kwa muda huo nilikuwa naye mimi, ….akasogea na kumchukua, na mimi nikajiweka sawa, kusubiria maelezo,, namfahamu rafiki yangu huyo, akiamua jambo lake , kaamua, lakini pia ananifahamumimi nilivyo, nikisisitiza kitu ujue kweli ninakitaka, sio kawaida yangu kusisitiza kitu, kama hakina umuhimu,Alitulia kidogo huku akimuangalia mtoto wake,…ilikuwa kama yupo kwenye wakatimgumu sana, nilitaka kumuambia basi, asiumize kichwa, lakini mimi nitakuwa sina amani, sio amani ya kutokumuamini, mimi namuamini sana rafiki yangu huyo,..ila hali ile ilinifanya intake nimfahamu tu huyo mwanaume aliyempa mimba sijui kwanini,Baadae rafiki yangu akainua uso na kuniangalia,….uso ulikuwa kwenye hisia, ni kama mtu anayehisi maumivu, na kiukweli sikutaka mjadala huo uendelee, naona namtesa, lakini yeye baadae akasema;‘Kwanini unataka niendelee kuharibu, si wewe ulishaanza kunilaumu kuwa nimeharibu, sasa kwanini tuendelee kufany ahivyo tena…?’ akaniuliza‘Hapana…hata mimi sikulitaka hilo, ila hizo kauli zako, kauli zako zenyewe zinakusuta, zinavuta hisia nyingine kabisa,....nahisi kuna jambo unanificha, … isije ukawa kweli umetembea na mdogo wa mume wangu, hapana kama ulifnaya hivyo, sio vizuri, sijui lakini...!'nikasema na yeye hapo akacheka kidogo, na kilikuwa sio kicheko kile cha furaha ni kama kulazimisha hivi, yeye baadaye akasema;'Hapana sijatembea naye, na kwanini…hahaha, hapana…bwana, na wewe mawazo yako ….katika wote, …huyo sikuwa na mpango naye kabisa, unajua aliwahi kunitongoza kipindi fulani, unakumbuka nilikuambia…na tulivyokosana naye pale, ikawa basi tena tatizo lake…, hajui kubembeleza, analazimisha, alihisi mimi ni muhuni, tokea kipindi kile sijawahi kuwa na uhusiano naye wa karibu, nikusalimiana tu kama tukikutana,…kiukweli, siwezi kuficha, awali nilitamani sana awe rafiki yangu, sasa alipokuja kuoa ndio ikawa basi, nikamtoa kabisa akilini mwangu...’akasema sasa kwa kujiamini.‘Ulimtoa sasa ukamtafuta …hahaha, wewe bwana, nakufahamu ulivyo, ukitaka jambo lako hushindwi…au uniambie ukweli, ulimpata wapi mwanaume anayefanana na mume wangu,…na ni nani huyo, hapo ….sikuachii,… kama sio huyo basi ni nani mwingine,…niambie ukweli rafiki yangu..usiniache njia panda…’nikasema‘Unajua …hadi hapa nakuona kama huna amani na mimi, na ndio maana najiuliza ule ushauri wako ulikuwa wa nini hasa, kweli ulitoka moyoni,….sasa nafikia kuogopa,..ni kweli, wewe ni rafiki yangu mkubwa sana, na mara nyingi tumekuwa tukishauriana mambo mengi, na mara nyingi wazo lako huwa nalichukulia kwa uzito mkubwa sana, …sikutaka nikufiche kwa hili, kabisa, nilipanga nikuambie kila kitu, lakini naona bora tuyaache tu, kwa usawa wa urafiki wetu..’akaniambia na mimi hapo nikasimama.‘Hapana wewe niambie tu, ….usiponiambia moyo wangu utakuwa hauna amani….kiukweli ndio hivyo, sio kwamba nakudhania vibaya, katu wewe siwezi kukuweka huko huwezi na hutaweza, ila nataka kumfahamu huyo mtu tu..basi, ili niweze kukusaidia….’nikasema‘Unakumbuka, niliwahi kukuambia kuwa  nawapenda sana watoto wako, na ningelifurahia kupata watoto kama wako…hilo lilitoka ndani ya nafsi yangu, ni kweli nawapenda sana watoto wako, na mimi nilitamani nipate watoto wanaofanana na watoto wako…’akamuangalia mtoto wake.‘Na…, na uliponishauri hivyo, ..mimi nikaona nifanye juhudi za kumpata mtu atakayenizalia mtoto kama wako, na muda huo nilikuwa natamani nipate mapacha, kama wa kwako, ....’akasema na mimi nikamuitikia kwa kichwa na yeye akaendelea kuongea kwa kusema;‘Nililiwazia sana hilo,…sasa nifanyeje,…ndio nikaanza kuwachuja watu ninao watamani, maana sio kupenda…siwezi kusema nilimtafuta nimpendaye, …hivi utampandaje mume wa mtu,nikaona nisicheze mbali,…kiukweli,  sisi ni marafiki wa kweli na tunaweza kufichiana siri...au sio rafiki yangu…?’ akaniuliza na mimi nikatikisa kichwa, .‘Wewe na mimi ni kama pete na kidole….au sio…na umkuwa ukinipa kila ulicho nacho, na mimi halikadhalika, ilimradi tuchangiane kwa …urafiki wetu, hilo lipo wazi, wapo waliowahi kusema urafiki wa namna hiyo hawautaki…eti haufai, lakini mimi sioni kama kuna ubaya, au sio …?'akasema huku akisimama na kumlaza huyo mtoto kwenye kitanda chake chenye chandarua,Unajua kiukweli, wengi watashangaa kwa hili, lakini kwangu mimi akili ilifungwa kabisa kumdhania  vibaya rafiki yangu..kabisa kabisa, rafiki yangu nilimchukulia kama mdogo wangu, kwahiyo nisingeliweza kumfikiria chochote kile,…, hata alipotoa kauli hiyo sikuwa na mawazo yoyote mabaya, mimi akili yangu ilifikiria kwingine kabisa,…nikasema‘Sasa kwanini inanificha, unanificha hata mimi rafiki yako, nilijua tu..’nikasema hivyo, na yeye akanitupia jicho kidogo, na kusema;‘Unajua sikutaka kukuambia moja kwa moja, kutokana na kauli yako uliyoitoa awali, nikaona bora nisiseme ukweli, hata hivyo….’akasema hivyo na kukatisha, huko kukatisha katisha maneno kwake, ndio kulikuwa kunanipa hamasa ambayo haikuwepo kichwani kwangu kabisa. Hata hivyo sio hamsa ya kumdhania ubaya, hivi ndugi yako anaweza kutembea na mume wako,..kiuhalisia…hasa awe ni ndugu unayemuamini….huwezi kufikiria hilo kabisa.‘Lakini yule ni mdogo wa mume wangu huoni italeta picha mbaya…’nikasema , na yeye akanitupia jicho kwa sura ya kushangaa, akasema;‘Hahaha… rafiki yangu, mbona hivi…mimi siwezi kukuficha, na …hebu tuyaache hayo jamani,…’akasema akionyesha ile ishara ya mikono ya kuupia jambo.'Ni kweli kabisa sisi ni marafiki wa kweli...na hatuwezi kuangushana, lako ni langu na langu ni lako..nakubaliana na wewe, na wala usiwe na shaka na mimi, …mimi naona ajabu wewe kuogopa kuniambia ukweli, ….sasa nimeshaujua, hata kama, japokuwa bado nahitajia uhakiki wako,…mimi kama mimi  nakuahidi kabisa, hilo litaishia moyoni, na hakuna mwingine anayeweza kufalifahamu hilo zaidi yako na mimi,..na huyu uliyemuambia ukaharibu, hilo nakuthibitishia...'nikasema huku nikiweka kidole mdomo kama ishara ya kuahidi‘Hahaha kweli rafiki yangu, mmh, mbona nitashukuru, ila sio huyo jamani, unayemfikiria wewe, haaah, mimi hapo siwezi kuelewa, nilijua una..umeshafahamu, maana ..aah, sasa hata sijui nisemeji,…kwanini huelewi….’akasema‘Nimeshaelewa, nakushangaa leo ulimi wako unakuwa mnzito tu…imeshapita hiyo na maji yakimwagika hayazoleki labda yamwagike kwenye udogo wa mfinyazi uliokauka…hahaha…uliposema tu kuwa hukutaka kucheza mbali, basi hapo imejieleza kila kitu, usiwe shaka kabisa, mimi nimelipokea kwa moyo mmoja..., na wewe bwana kwa  kupenda stori ndefu, kwanini usiningeliniambia tu moja kwa moja kwa shemeji ndiye kayafanya hayo, basi, limekwisha, au….’nikasema‘Tafadhali mimi nakuomba, tuyaache….’akasema‘Tuyaache mbona unasema hivyo tena, au, …?’ nikauliza kwa kushangaa maana mpaka hapo nilishaamini kuwa ni mdogo wa mume wangu, ..yeye akabakia kimia, akiwa kainamisha kichwa chini.‘Ina maana sio yeye, au…unaogopa nini kuniambia…?’ nikamuuliza‘Tuyaache jamani…’akasema akitikisa kichwa.‘Mimi nauliza tu, kama sio mdogo wa mume wangu ni nani mwingine anayefanana na mume wangu…, maana sasa unaanza kuniweka roho juu, kama tumechangia kuna ubaya gani, limetokea limetokea, eeh,....kwanini unaogopa kusema huo ukweli kuwa tumechangia, siwezi kukulaumu zaidi, ..najua wewe ni rafiki yangu, kuchangia, tunachangia sana, au sio,…sasa itakuwa …, mimi mkubwa na wewe mdogo mtu au…?’ nikasema na kuuliza.‘Kama wewe ni rafiki wa kweli sizani kama hili jambo litakukwaza, ndivyo nilivyokuwa nimefikiria hivyo,…na…na…, na kama kweli ulikuwa na nia njema na wazo lako natumai hutaniona kuwa mimi  ni mtu mbaya, kwani yote niliyafanya kwa kufuata ushauri wako…. Zaidi ya hayo kuna kukosea, nimekubali nimekosea kuliweka hili bayana mapema…na kiukweli , hata mimi sikupenda iwe hivyo kwa hali hiyo, ila ningefanyaje basi, mmh,  …’akasema‘Sijasema, au kukulaumu kwa hili kuwa umekosea kumchagua huyo…sawa  lakini picha kwa jamii, ndio maana nilisisitiza sana usiri..jamii itatuelewaje au sio…, ninachojiuliza ni kwanini unifiche kitu kama hiki ambacho watu baadae watakuja kujiuliza na wengine watapa mwanya wa kusema la kusema…sasa ni vyema ningelijua mapema ili tuweze kuweka, kinga…’nikasema‘Mimi nilikuamini sana rafiki yangu kwa ushauri wako, nikaona ngoja nifanye kama ulivyonishauri...sizani kama nimekosea jambo, ni ushauri wako ndio umefanikisha hili, na...na nitafurahia sana na wewe ukilipokea hili kwa moyo mkunjufu...ndio maana sitaki nikufiche kitu...’akasema‘Kiukweli umefanya jambo la maana sana, kwani hivi ndivyo nilivyotaka,…. Uzae uapate mtoto na wewe…, maana mtoto ana raha zake, wewe mwenyewe utaona, utakuja kuniambia…sitawezi kukulaumu kwa vyovoye vile, maana ndivyo nilivyotaka mimi iwe hivyo, na kwanini nikwazike kwa hili ilihali wewe ni rafiki yangu kipenzi na pia hilo wazo nilikupa mimi. Nikuambie ukweli wazo hilo nililiwazia sana kabla sijakushauri,na lilitoka ndani ya moyo wangu, nipo tayari kukusaidia kwa vyovyote vile….’nikasema kwa kujiamini.‘Basi kwa vile umenihakikishia hilo na wewe ni rafiki yangu mpenzi, nitakuambia kila kitu bila kukificha, ila nakuomba uwe mkweli wa kauli yako hiyo,..kuwa utalipokea kwa moyo mkunjufua…na nanomba iendelee kuwa ni siri kati yangu mimi na wewe, ama kuhusu shemeji, basi, tutaona jinsi ya kufanya au sio …’akasema‘Hapo sasa umenena, na …unajua yule haivani sana na kaka yake, kwahiyo sina mazoea naye sana, usiwe na shaka na hilo, na tutajua jinsi gani ya kumbana kiasi kwamba hatafunua mdomo wake, anamuogopa sana mke wake yule, unasikia…’nikasema‘Tatizo, ….moyo unaniuma, na naingiwa na uwoga, sipendi kabisa urafiki wetu uje kuharibika kwa hili, nakuomba sana, maana sijui nitauweka wapi uso wangu kama wewe ukiamua kunisaliti, ukanitangaza vibaya kwa watu, nitavunjika moyo wangu sana tena san,… kama …oh, kama…wewe utafanya hivyo, lakini zaidi ya hayo nitaumia sana kama hili litakukwaza na kukuumiza…nakuomba sana, tena sana….for the sake of this baby…uwe mkweli kwa akuli yako hiyo’akasema akimwangalia mtoto wake.‘Kwanini unasema hivyo rafiki yangu kama vile huniamini au mimi siakuelewa hapo,..kwa hili nakuhakikishia kuwa tupo pamoja…hili nimekushauri mimi na nitakuwa mtu wa ajabu kama nitakulamu kwa lolote lile…wewe niambie tu,na nimeshajua ila ni uhakika wako…mimi nakuhakikishia kuwa tutakuwa pamoja kwa lolote lile, si ndio hivyo…mmh, sasa moyo umetulia...’nikatulia kidogoYeye akatulia na mara alipoinu akichwa na kuniangalia nikaona machozi yanamtoka,…hapo nikashikwa na mshangao kidogo, sio rahisi kwa rafiki yangu kutoa machozi, akitoa machozi ujue limemfika kweli, kama mwanamke inatokea…hapo mimi kwa huruma  nikamsogelea, na kumshika, tukawa kama tumekumbatiaana kiupande upande…alitulia kwa muda, halafu akasema;‘Rafiki yangu,.oooh, naumia, ….mimi ...nakuomba tuliache hili tu, nakuomba tena na tena, tuliache kama lilivyo, …sitaki,..na … nitaumia sana ikija kutokea kinyume na …..ulivyosema, ulivyoahidi, naogopa sana, kumbuka rafiki yangu ahadi ni deni, ulinishauri wewe, kumbuka hilo….’akasema‘Hili ninakuthibitishia kutoka moyoni mwangu…, sizani kama huyo mke wa shemeji atalijua hili..zipo namna nyingi ya kulificha…tutashauriana muda ukifika…huyo hatajua kabisa …maana akijua vumbi lake naye sio mchezo…’nikasema‘Hapo ndio waanza kuniogopesha…’akasema‘Hatajua bwana…usiogope kabisa..nani atamuambia…mimi nakuahidi kama rafiki yako , mimi nipo tayari kupitisha rupia,… ikibidi…japokuwa ni mkali, lakini namfahamu  madhaifu yake,…yule mwanamke anapenda sana pesa,...usiogope kabisa...mimi na wewe hakitaharibiki kitu,..na kwanini ulie, hebu nikuulize, niambie ukweli ni nani mwingine analijua hili….ni mimi na wewe tu au sio, usije kuwaambia hata wazazi wako unasikia, ukiharibu tena huko shauri lako..’nikasema.‘Oh, basi …mimi naona unipe muda,… niliwazie hili zaidi, nitakuambia kila kitu, usijali, sasa hivi akili yangu haipo sawa....nashukuru sana rafiki yangu…ningeomba nikapumzika, au…sio nakufukuza..jamani…ila kumbuka tu ahadi ni deni..’akasema‘Mimi nimeshakuambia hakuna kitu kitaharibika niamini mimi rafiki yako, kwanini nikuahidi kitu halafu nije kukusaliti, haitatokea kabisa, nakupenda sana..wewe ni sawa na mdogo wangu kabisa….hata mume wangu namuambiaga hivyo,  na kila nikitaja majina ya wadogo zangu na wewe nakutaja, uone ninavyokuthamini, najua wewe huwezi kufanya jambo la kuniumiza mimi au mimi kufanya jambo la kukuumiza wewe….’nikasema‘Mhh…hapo sasa….’akasema‘Ndio hivyo…kwahiyo mimi  siwezi kuja kukasirika eti kwa vile umefanya hivyo kwa shemeji…, hapana na kama wazo nilitoa mimi eeh,  kwanini nije kuumia,…hapana nikifanya hivyo, itakuwa  ni ujinga, …siwezi na sitaweza kukusaliti, unasikia, sawa…kama wahitajia kupumzika basi wewe pumzika, sijui nikufanyie nini kwa hivi sasa…’nikasemaNa mara simu yake ikaingia ujumbe, akaichukua na kuusoma, halafu akanitupia jicho, na mimi nikajifanya kama sikumuona, akawa anaandika kitu kwenye simu yake, nahisi alikuwa akijibu huo ujumbe wa simu, halafu akasema;‘Mimi naona wewe uende tu, usiwe na shaka na mimi, ndugu yangu anakuja, na nikikuhitajia nitakuambia, usiache shughuli zako, mimi nafahamu sana shughuli zako zilivyo, kazi kwanza au sio, hata mimi sizani kama nitajilaza tu kwa vile nimejifngua, mwili wangu ni kuhangaika sio wa kulala lala…’akasema‘Sawa mimi naondoka naona hata mume wangu ananisisitiza kwa ujumbe wa maneno kuwa niwahi nyumbani …na nikichelewa sitamkuta, sijui ana jambo gani muhimu kihivyo..ngoja niondoke ..haya ..ooh, baby kalala, hivi jina bado eeh, ..’nikasema‘Adamu….’akasema‘Safi kabisa, …ooh,babu Adam…bakia kwa amani eeh, …’nikasema nikipitisha mkono na kumshika kwa mbali kichwani, na taswira ile ile ya watoto wangu wakiwa wachanga ikanijia, ..sijui kwanini….na simu ya rafiki yangu ikawa inaita, ..aliangalia mpigaji, halafu akaniangalia,Mimi nikasema‘Haya mimi naondoka, wewe endelea, nitarudi…’nikasema na akawa kama anataka kunizuia, nisiondoke, nilijua anataka kuniaga huku anataka kuongea na simu, nikasema‘Wewe endelea usijali na wala usinisindikize…, nikatoka kwa haraka, nikiwahi kwenye gari langu, na..kuanza kutoka, na wakati natoka, gari kama la mume wangu likawa linakuja, …ikanifanya nisimame, nihakikishe kuwa ndio lenyewe, na linakwenda wapi…WAZO LA LEO: Ni rahisi sana kutamka neno, hasa la kuahidi, na hata kuapa kuwa nitaweza kutimiza malengo au kutimiza jambo fulani vyovyote iwavyo. Ni vyema, tukawa na uhakika na kauli zetu hizo, na kama hujalifahamu jambo sio vyema kuahidi kuwa ni lazima ufanya hivyo, `lazima’ sio kauli nzuri. Tukumbuke kuwa Ahadi ni deni, na ukiahidi jambo ujue unahitajika kulitekeleza, na ukikiuka ujue umehini ahadi yako, ni hiyo ni tabia ya mnafiki.Ikapita wiki, kutokana na shughuli za kazi nyingi, nikawa kama nimeshamsahau rafiki yangu huyo, na nikawa na migongano ya hapa na pale ya kifamilia, ni kawaida, lakini safari hi ilizidi, maana mume wangu ratiba zake zikawa hazieleweki sio kama ilivyokuwa awali, tukawa tunabishana, lakini kwangu nilichukulia ni mambo na kawaida tu.Basi  siku moja nikapokea simu kutoka kwa huyo rafiki yangu, akaniambia kuwa anajiandaa kuondoka kwenda Zanzibar, kuna mambo muhimu anatakiwa kuyafuatilia‘Mambo gani mbona mapema hivyo…?’ nikamuuliza‘Kuna jambo natakiwa kwenda kulifanya, natakiwa kukabidhi kabidhi ofisi, kwani  inawezekana nikasafiri kwenda kusoma nje ya nchi…niliwahi kukuambia kipindi fulani kuwa niliomba kwenda kusoma, sasa imetokea kipindi hiki na mimi siwezi kuachia hiyo nafasi,…’akasema nilitaka kumuuliza na mtoto vipi, nikasita yeye akasema‘Na uzuri..haitakuwa muda wote, nitaweza kulea na kusoma, mfadhili wangu kasema hilo halina shida..kwahiyo  sitakuwa na muda wa kukabidhi, nikimaliza likizo yangu ya maternity, yawezekana nikaondokea huku….’akasemaIlinisthua kidogo, ikizingatiwa kuwa mtoto bado mdogo, sikumuulizia sana kuhus mtoto,…. kwasababu hapa kati kati tulifikia sehemu hatuelewani na yeye kabisa, alichoka na maswali yangu na  hata kufikia kusema niache kumfuta fuata masiha yake na mtoto wake.., kauli hiyo ikaniudhi sana, ikabidi kweli nimuache na maisha yake. Hata hivyo kiukweli, sio kwasababu hiyo, ila sikuwa na muda wa kukutana naye mara kwa mara, majukumu yalizidi sana.Tuliongea kidogo kwenye simu …tukamaliza hivyo tu, na sikuweza kumpigia tena , na siku mbili baadae akapiga yeye, nahisi ni pale aliponiona nipo kimia, akasema;‘Rafiki yangu vipi, nilijua utakuja, kabla sijaondoka, si nilikupigia simu jamani, sawa najua labda, bado umenikasirikia,… lakini utakuja kuelewa tu, baadae, …ila nilikuwa na ombi moja kwako, kwa vile wewe nyumba yako ina nafasi naomba baadhi ya vitu vyangu nije kuviweka kwako maana hizi nyumba za kupanga nikiondoka, vitakuwa havina usalama kabisa....’akasemaKiukweli mimi sikuwa na hasira kihivyo, hasira zangu ni za hapo kwa hapo..na ukiniudhi naweza kufanya jambo kubwa hapo hapo…baada ya hapo, mambo yamekwisha, ila …kiukweli naweza kufany ajambo baya huwezi amini,..mimi kwa hilo nilishaliondoa nafsini kwangu sikuwa na kinyongo na yeye,..nikasema hakuna shida, nyumbani kwangu ni kwake, nikazidi kumsisitizia kwa kusema;‘Wewe ni rafiki yangu bwana, hakuna haja ya kuniomba, hapa ni nyumbani kwako pia, watoto wanakuulizia kila siku, wewe lete vitu vyako na wewe kama mkataba umekwisha kwenye hiyo nyumba haina haja ya kulipia tena, njoo ukae hapa, mapak siku ukiondoka, ...’nikamwambia.‘Hapana, sina maana hiyo, na sitaweza kufanya hivyo, urafiki wangu usiwe mzigo kwako, umeshanisaidia mengi sana, kiasi kwamba najihisi vibaya, na ..hata sijui nitawezaje kulipia hayo,…. ninachokuomba kwa sasa ni hilo tu....’akasema.‘Sawa hamna shida, wewe vilete wakati wowote utakapopata nafasi, au nikipta nafasi, hata kama wewe haupo ninaweza kuja au kutuma gari likaja kuvichukua haina haja ya kusumbuka sana, ila nitajitahidi nije kabla hujaondoka..’nikasema, nikiwa na mambo yangu mengi shughuli zangu, na sikutaka kuongea naye zaidi, hasa kuhusu maisha yake alishasema hataki nikikutana naye tuyaongelee maisha yake, hasa kuhusu mtoto na aliyezaa naye.Kesho yake nikapata nafsi nikaona nimpitie kidogom, nijua kinachoendelea, na kama vitu hivyo sio vingi, na kaviandaa, basi ninaweza kuondoka navyo, kwa kukodi gari, sikutaka kumpigia simu, mimi mwenyewe nikaenda nyumbani kwake…kwa mbali niliona gari kama ya mume wangu, lakini sikuwa na uhakika kama ilitokea kwake, au ilikuwa inapita tu, na mume wangu alikuwa kwenye mkutano.‘Hivi mkutano ulishamalizika,..au kuna mtu kamtuma na gari lake…?’ nikajiuliza, nikataka kupiga simu kwake, lakini ikaingia simu ya mteja wangu muhimu, nikajikuta naipokea kwanza, na nilipomaliza kuongea naye , nikiwa nimesimamisha gari nyumbani kwa rafiki yangu,..nikawa nimeshaua kumpigia simu mume wanguRafiki yangu alikuwa kasimama mlangoni kwake kunikaribisha, nikamsogelea tukasalimiana kama ada yetu, nikaingia ndani na swali la kwanza likawa hili.‘Mtoto kalala…?’ nikamuuliza‘Ndio….’ Akasema ile ya kulazimishwa, sio sauti kama ile niliyo-izoea, halafu akauliza‘Hujakutana na….’akasita,kwani simu yake iliita, akaisikiliza kwanza kwa muda, akasema‘Nimekuelewa hamna shida, lakini niache kwanza, sitaki, sikiliza, nilikuelezea, msimamo wangu basi…’akasema na kukata simu.Alionekana kama ana hasira na hataki kuongea, akawa kama anataka kuniambia jambo lakini anasita, nilihisi hivyo, ila na mimi nikasimamia kwenye msimamo wangu kuwa sitamuuliza tena kuhusu maisha yake na mtoto, …kwa jinsi alivyo  nilijua ana tatizo.Baadae mtoto akawa analia, kwahiyo akaenda kumchukua, na kumnyonyesha alipomaliza, akanipa nimpakate ili aniandalie kinywaji, ndivyo tulivyozoeana , nilitaka kujiandalia mimi mwenyewe, maana anajua mimi ni mpenzi wa sharubati ya baridi,… lakini akasema hapana‘Wewe mpakate mtoto ..hujamshika tokea siku ile….’akasema na mimi sikukataa nikamchukua mtoto.Unajua mtoto wa mwenzako hakawii, sasa anageuza macho, anangalia, na sura halisi inaanza kuonekana, sura haikujificha alikuwa akifanana kila kitu na watoto wangu, maana watoto wangu wanafanana, ni wale mapacha wanaofanana kwa kila kitu, mimi akilini nikaweza hitimisho kuwa rafiki yangu atakuwa atakuwa katembea na mdogo wa mume wangu. Hata hivyo sikuweza kuvumilia nikamwambia;‘Hapa sasa haijifichi kitu, lakini tuyaache hayo, lini unaleta hiyo mizigo, au nitafute mtu tupakie, kukurahisishia kazi…’nikasema‘Haijifichi nini, usianze yale mazungumzo tena, nimefikiria kwa makini nimeona, ni bora iwe hivyo, libakie kama tulivyokuliana basi… sasa ibakie utakavyofikiria wewe inatosha,..’akasema.‘Hamna shida, isiwe taabu, sasa unasemaje…?’ nikamuuliza‘Nilitamtafuta ,mtu, kuna mambo sijayaweka sawa, kuna mtu ananisumbua akili yangu, sipo sawa, ila nimeshukuru kuwa umafika….’akasema‘Ok, sawa mimi naondoka…’nikasema‘Kuna kitu nilitaka kukuambia, lakini bado sijawa na uhakika, nataka nipate ushahidi halafu tutaongea….’akasema‘Kuhusu nini….?’ Nikauliza‘Nataka uwe na amani na hili jambo tulimaliza kabisa….’akasema‘Jambo gani…?’ nikamuuliza‘Kuhusu huyo mtu niliyezaa naye….’akasema‘Sijakuelewa bado…na usiumize kichwa chako kabisa,..kama hutaki nijue haina shida, ..mimi nakujali sana, sitaki uumie, uwe na wakati mgumu kwa ajili yangu,…mimi nina amani kabisa, sina kinyongo na wewe, naahamu una sababu yako muhimu tu y akufany ahivyo….’nikasema‘Unajua mimi linanisumbua sana, nimejaribu kuliwazia tukio zima la siku ile sijaweza kulithibitisha,…sijawa na uhakika ilikuwaje…’akasema‘Tukio gani…?’ nikamuuliza‘La kuipata hiyo mimba….’akasema‘Mhh..sikuelewi, ...usinidanganye rafiki yangu..wewe sio mtu wa kubakwa, wewe sio mtu wa kufanyiwa tendo bila rizaa yako, nakufahamu sana, kwa hilo usinidanganya....’nikamwambia, ni kweli rafiki yangu ni mbabe, mjasiri na anajiamini, anaweza kupambana na midume, hata kama ni kwa kupigana ngumi.‘Kwakweli siku ile, nilizidiwa, na sijui kwa vile nilitaka iwe hivyo, ndio maana sikujali, hata hivyo nikuambie ukweli, sikuwa nimepanga itokee hivyo, sio siku ambayo nilisema leo nataka nikafanye hivyo, hapana, ...ilitokea tu , na huenda ilipangwa iwe hivyo, kwa kifupi siwezi kukumbuka siku ile nililewa...’akasema.‘Ulilewa, ulianza lini kunywa…?’ nikamuuliza‘Siku hiyo hiyo…na nilijuta …na mara pili, nikarudia tena, ..na kilichotokea ndio nikasema sitakunywa tena,…najuta…’akasema‘Wewe mtu…..ina maana ukinywa pombe…na wewe uliwahi kuapa kuwa katika vitu ambavyo hutaweza kuvitumia kimojawapo ni pombe…?’ nikamuuliza‘Nimevunja miiko mingi sana ya kwangu, na kila nilichokifanya kwa kuvunja miiko yangu nimekuja kupata matatizo makubwa..hadi sasa sina amani…’akasema‘Ilikuwaje maana wewe mwenyewe ndio umenichokoza, nilipanga nisikuulize tena, lakini umelianzisha wewe mwenyewe, utanieleza au niondoke, na nikiondoka sitaki tena kuniambia kuhusu maswala yak ohayo…’nikasema ‘Sawa kama umeamua hivyo, mimi nitakuambia ilivyokuwa siku ile, na wewe mwenyewe utajaza,…na naomba usije ukanilaumu,....maana wewe mwenyewe ndiye uliyenishauri...’akasema na mimi nikafurahi tukakaa na kuanza kuongea, na yeye alianza kusema hivi;Siku uliponipa ushauri wako, moyo wangu ulianza kuwa na shauku, …nikawa na hamu sana ya mtoto kuliko siku zote,….nikawa nawaza sana kupitiliza mpaka watu wakanifahamu kuwa nina mawazo…niliwazia nikiwa nimempakata mtoto wangu, na hasa wawe mapacha….nilipata shida sana....’akatulia kidogo.‘Unakumbuka ulivyoniashauri, nimtafute yoyote hata awe mume wa mtu nifanye naye tendo kwa minajili ya kupata mtoto, na nilijiuliza nitamuendeaje mwanaume bila..unajua mume ndiye anakutongoza, au sio..sasa nitakuwaje na uso usio na aibu….haraka nikasema kwanza labda nitafuta kitu cha kuniondoa aibu,…’akasema.‘Ndio ukaenda kulewa…kwenye mabar, au ilikuwaje…nashindwa hata kukuelewa, kwanini usingeliniomba ushauri nikakuelekeza jinsi gani ya kufanya…’nikasema‘Unajua rafiki yangu, kinachonishinda kwa hivi sasa ni kuhusu shemeji…’akasema‘Nani, huyo bwana mliyezaa naye…?’ nikamuuliza‘Ndio.....’akasema.‘Kasemaje…? Nikamuuliza.‘Ndio, kaniomba sana, tena sana hata kulia, hata kunipiga magoti, kuwa nisimwambie yoyote kwa sasa iwe siri kubwa kwani kuna mambo kayagundua yanaweza kumleta matatizo kwenye familia yake….’akasema‘Ni sawa,…hata mimi nilikushauri hivyo, je labda mkewe keshamuhisi vibaya au….?’ Nikamuuliza‘Anasema…kuna mambo yake ya kifamilia, ambayo hataki yaharibike, na ikigundulikana kuwa ana …mtoto nje, atayaharibu..ok, mimi nilion  ni jambo la maana, kama na yeye kakubali iwe hivyo itakuwa ni heri kwangu…ila kwa masharti kuwa anataka mtoto atambulikane kuwa ni kwake kwa siri..hapo ndio tukaanza kukorofishana,...’akasema.‘Unakubali nini na unakataa nini, kosa umelifanya wewe mwenyewe, kwanini toka mwanza usingelimdanganya kuwa mimba sio yake,..hii inaonyesha kuwa ulitaka afahamu, na huenda ulifanya hivyo kwa dhamira fulani ambayo unaogopa kuniambia...’nikasema na yeye akainama chini kuashiria kuwa kauli yangu umemgusa moyoni.‘Kwa hali kama hiyo nimeona nisimwambae yoyote ....shemeji kaniomba na mimi nikamuahidi iwe hivyo, kwa masharti kuwa na yeye asinifuate fuate tena..lakini naona yeye kaanza kuvunja ahadi, kila siku hodi, na mbaya zaidi ananunua vifaa vya mtoto..sipendi, na ndio maana ilipotokea nafasi hiyo ya kusoma mimi nikaikubali kwa haraka sana, na sijamwambia kuwa mimi nakwenda kusoma nje....’akasema.‘Kwahiyo eeh, unajua mimi unaniweka kubaya, …mimi naona nikuache na mambo yako, kwani kila hatua unanitamanisha intake kumfahamu huyo shemeji, na hutaki kuniambia ni nani…tuyaache kama ulivyosema au…?’ nikamuuliza nikiwa nimekunja uso kwa hasira.‘Mimi nitakuambia jinsi ilivyotokea siku ile...au niache maana wewe unakimbilia kumjua huyo shemeji lakini hutaki kujua ilitokea vipi, nataka ufahamu ilivyotokea, ili uone kuwa sikuwa nimekusudia siku ile,…japokuwa tulipanga iwe hivyo, lakini sio kwa huyo na …hata sijui, nisemeje ndio maana nataka nikuelezee ilivyo kuwa na sio alzima nikutajie kwua ni nani...’akasema‘Sawa hebu elezea, uonavyo wewe… maana na wewe sasa unajifanya mtunga tamithiliya, wengine hawapendi vitu virefu, sawa mimi sijali ila unipe kitu cha ukweli, sio hadithi za kubuni...’nikasema kutoka moyoni hadi hapo sikuwa na dhamira yoyote mbaya dhidi yake, sikua na wazo kuw ahuyu mtu anaweza kunifanya chochote kibaya, yaani sijui kwanini ilitokea hivyo, maana pamoja ya kuwa ni rafiki kwangu mimi nilishamweka kuwa ni ndugu yangu…moyo wangu umejengwa hivyo kuamini watu.‘Baada ya ule ushauri wako, nikajikuta nakutana na wanaume wale ambao wana watoto ninaowapenda, nilijipangia kama karatiba fulani, ..ni ngumu lakini…kwahiyo ikawa inatokea awali, kwa huyo na yule lakini ghafla ikaja kubakia kwa huyo mtu mmoja, bila hata kukusudia,…Cha ajabu sio kama awali wengi wakinialika kwenye chakuala cha jioni, inaishia kula na kunywa kidogo basi, tunaagana imekwisha, nahisi walishanisoma, na wengi hawakutaka kuniomba tufanye lolote zaidi ya hapo, ni ile raha ya kukaa na mimi kula kuongea, inaishia hapo tu,…na mimi  sikuweza kushinikiza ili lifanyike hilo tendo, siwezi, ningalianzaje..na hata  kwenye akili yangu bado nilikuwa na shaka...’akatulia.‘Kwahiyo baadae ndio akabakia huyo mmoja ambaye hutaki kumsema, japokuwa mimi nimeshamfahamu kuwa ni nani, au sio… shemeji yangu wa ukweli.. au sio..?’ nikamuuliza huku nikicheka.‘Ndio, sijui ilitokeaje, …ilikuwa kila nikienda kupoteza mawazo, shemeji yumo..ni kama ananifuatilia nyuma, utafikiri alikuwa ananilinda, au hata sijua ni kwanini alikwua akifanya hivyo, na ndiye niliyekuwa nikijaribu kumkwepa kuliko wengine, lakini haikuwa rahisi, kila nikitaka kutoka shemeji yupo nyuma, akiona sina mtu, anakuja kunipa pambaja,…nikaanza hata kuogopa, nikifahamu ukaribu wangu na mkewe, na familia kwa ujumla....’akasema.‘Ok,…tuendelee..’nikasema.‘Lakini mimi naona tuache tu kuyaongelea haya,…’akasema‘Umeshaanza, siwezi kuondoka mpaka uelezee, hapo utaniuzi, hatutaelewana…’nikasema‘Sawa, ngoja niendelee,  maana hata mimi sijawa na uhakika, ni  kwanini litokea hivyo na je ni yeye kweli,..nachanganyikwia ndio maana sina raha na kwanini ilitokea siku zote mbili, ilikuwa kama….haa, hata sijui nisemeje,....’akasema.‘Sawa endelea ilikuwaje, ...kwani naiona hiyo sasa ni tamithilya fulani , kuna kitu unanificha na nitakigundua tu,...’nikasema.‘Ofisini kwangu kupo karibu sana na ofisi za shemeji..’akasema. ‘Ok…ni sawa, ...ndio maana ilikuwa ni rahisi sana, kwako wewe ..mmh najaribu kujiuliza ni nani pale anafanana na mume wangu, mbona wengi wanaofanya kazi pale nawafahamu hata huyo mdogo wa mume wangu yupo karibu sana…ok..na upande huo wa pili yupo mume wangu,…, sasa naanza kuelewa, tuendelee..’nikasema na yeye akaniangalia huku akijaribu kutabasamu lakini uso ulikuwa umejaa huzuni.‘Ndio ni kweli ndio maana ilikuwa ni rahisi sana kwake.., kuniona nikitoka, na niliona kama kadhamiria kufanya hivyo, na mimi hata nilivyojaribu kumkwepa ikawa haisadii, nikaona isiwe shida, kwanza ni mtu ninayemwamini hawezi kunifanyia lolote baya na anafahamu kabisa kuwa mkewe ni mtu tunayefahamiana sana naye...’akasema.‘Mhh, ndio nafahamu si mlikuwa mashoga kipindi fulani na mkewe.., nikafikia kukukanya kuwa huyo mwanamke haaminiki, anajaribu tu kuficha ule ubaya wake , ili uone ni kawaida tu…maana kama angelikuwa rafiki wa ukweli, asingelikuibia mchumba wako, …mara nyingi marafiki wanaweza kuwa hivyo, unatakiwa rafiki awe kweli rafiki mnayeaminiana, ambaye huwezi hata kumdhania ubaya, au sio..?’ nikamuuliza na yeye akatikisa kichwa kukubali, hakusema neno‘Ni kama mimi na wewe, mtu hawezi kuniambia kitu kibaya kuhusu wewe, najua huwezi kamwe kunifanyia mabaya, kama mimi nisivyoweza kukufanyia mabaya, mtu kama humfanyii mwenzako ubaya, huwezi kufanyiwa ubaya, au sio..itakuwa ni ajabu sana wewe ukinifanyia ubaya, au sio…....’nikasema na yeye akatabsamu na kusema.‘Mhh, mabaya kama yepi tena rafiki yangu, wakati mengi tunafanyiana baada ya kushauriana…?’ akaniuliza‘Kama aliyokufanyia yule rafiki yako, mtu unamuamini, halafu anakuja kukuibia mchumba wako…kiukweli inauma, kuibiwa mume au mke, unajua inatokea kama nilivyokushauri,au sio, na huwezi kumfanyia rafiki yako, mpendwa,, ni lazima utafanya mbali kabisa,…maana kama ni rafiki yako, mtaumizana sana…’nikasema‘Mhh…hapo sasa…’akasema, akijikuna kichwa, halafu akajaribu kutabasamu na kusema;‘Nimewaza sana hili…..naona bora ….nikuambie tu, ilivyotokea…’akasema‘Ikawaje hebu endelea bwana, acha kusua sua, usinipe ugonjwa wa moyo….’nikasema‘Basi kutokana na hali hiyo, kuwa mke wake namfahamu, ni mtu tunaheshimiana, nikaona nisimzalilishe, maana kama unavyonifahamu,  huwa simkopeshi mtu, huwa siogopi mtu, kama sitaki sitaki...naweza nikamtolea nje mbele za watu akabakia kuzalilika na nisingeliweza kufanya hivyo kwa shemeji....’akasema.‘Ni kweli mimi nakuaminia,ndio maana hilo lililotokea siwezi kuamini kuwa lilitokea bila ya ridhaa yako, wewe utakuwa ulikubaliana nalo, vinginevyo kuna kitu unanificha, na sipendi unifiche kitu, maana nikigundua, haaa..weee, si unanijua nilivyo, mume wangu mwenyewe ananiheshimu kwa hilo, ananiogopa, ndio maana anajitahidi kuwa mkweli kwangu, kama nilivyo kwake...’nikasema.Hapo akatulia kidogo kama anawaza jambo, baadae akaendelea kunihadithia…‘Ikawa kila nikitoka kwenda kula jamaa huyu hapa, nikitoka kwenda kazini, jamaa huyu hapa, ikawa kila siku nakutana naye, nikajikuta sina raha, na hata yeye akaliona hilo,…lakini akaniambia niwe na amani, atajitahidi kuhakikisha hatuvunji heshima yetu, …kiukweli hata lile wazo likafutika, sikutaka tena,… lakini moyoni...nilikuwa unanijia ule ushauri wako,na nikawa natamani ufanye kazi, lakini sio kwa huyo mtu, mume wa mtu, siku zinasogea...’akatulia kidogo.‘Endelea…nina muda kidogo…ila najiuliza kwanini ulipoteze muda kwa huyo mtu, maana hapo ulikuwa unajichora kwa watu, walikuona, wanakuona au sio, kwahiyo hadi hapo wana ushahidi bayana  ….hapo eeh, uliharibu…’nikasema‘Kwa vile ni jamaa, ambaye…ni..ni .. shemeji yangu, sikuona tatizo, na ..unajua nisingeli…mkatalia hata chakula, japokuwa awali nilikuwa nafanya hivyo….’akasema‘Ok nimekuelewa, sasa nikuulize katika wanaume wote wewe uliona huyo ndiye anakufaa au kwa vile ulihisi atakuzaliwa watoto sawa na wakwangu au…?’nikauliza‘Kiukweli ndio hivyo, kama ungelianiambia nichague ni nani wa kunipa mimba, kama hakuna kikwazi, mimi kutoka moyoni, ningelimchagua yeye....lakini kutokana na ukaribu  ulivyo hapana,  sikupenda litokee kwake, lakini ndio hivyo, watu husema litokee ili liwe fundisho,...kwakweli hadi sasa siwezi kuamini, sikujua kabisa kuwa nitakuja kuzidiwa kiasi hicho…ni pombe, sitarudia tena…’akasema.‘Hebu kwanza nikuulize yule jamaa anakunywa, unajua mimi simpafahamu vyema maisha yake, na unijuavyo huwa sifuatilii maisha ya watu wengine hata mke wake hatupo karibu kihivyo, japokuwa ni mke wa shemeji yangu…?’ nikamuuliza‘Anakunywa lakini sio kihivyo….’akasema‘Mhh, hawa wanaume jameni…. unajua nilikuambia hata mume wangu anakunywa, lakini akiwa na wazee, watu wa heshima wa dini, anajifanya mtu wa dini sana, na kupinga ulevi,....mimi nafahamu siri yake, uzuri wake hata akinywa huwezi kufahamu, anajitahidi sana kujificha…, nimemkanya sana tabia hiyo ya kunywa pombe…, yeye anasema anakunywa kwa dharura, na kidogo sana…’nikasema‘Wanaume wengi wapo hivyo….sioni ajabu kwake,…’akasema.‘Ilikuwa sio sana kama ilivyotokea baada ya kunipa huo ushauri, mwanzoni nilikuwa nakutana naye, anaiomba tukale chakula pamoja, tunaongea,…ananishauri kuhusu maisha, ni nani angelipenda awe mume wangu,…nikawa nimezoeana naye sana, nikiwa sina raha, yeye anipa ushauri , lakini sikuwa na wazo jingine lolote dhidi yake, na yeye alilitambua hilo...’akasema.‘Mambo ya shemeji hayo , nafahamu sana ulichompendea, ni kw vile kwanza ni mtanashati,…. mrembo kama mume wangu, wanafanana sana, na mume wangu, kwahiyo nahisi ndio sababu ulimpendea hivyo au sio..?’ nikamuuliza..Kwanza akaniangalia kwa makini, halafu akawa kama anasita kunijibu baadae kwa shingo upande, akiwa kainamisha kichwa akasema…..Nb….naona inazidi kuwa ndefu na muda umekwisha, ngoja niishie hapa kwa leoWAZO LA LEO: Urafiki wa kweli ni ule wa kuangalia athari za kila jambo kuwa unalolifanya halitamkwanza mwenzako,... ni hilo litafanikiwa pale utakapojiuliza je, kama nitafanyiwa  mimi jambo kama hilo nitafurahia au nitachukia. Tukiwa na tabia hiyo ya kuchuja matendo yetu kwa wenzetu nina imani kuwa hatutachukiana, tukumbuke kuwa ubaya kwe wenzetu unauma kama vile tungelifanyiwa sisis, kwani mkuki sio nguruwe tu, na kwa binadamu mchungu.‘Kumpenda kwasababu hizo,…mhh…naomba uwe na stahimili…sitaki nikujibu swali lako kihivyo…hilo la kupenda lipo wazi,…maana mengine yanaweza kuja kuwa kuni,…lakini si wewe mwenyewe umetaka, na nataka nikisafiri niwe na amani, au sio…sasa mimi nakuomba unisikilie kwa makini…nikuelezee ilivyotokea, …tafadhali…’akasema‘Sawa uonavyo wewe uwanja ni wako, au sio…..lakini mimi nimeshajua kuwa ni nani unayemzungumzia, ni nani baba wa mtoto wako, hilo sina shaka,..na hata mume wangu japokuwa hataki kuliongelea hilo, eti anadai hayo ni mambo yetu hayamuhusu, lakini kwa namna fulani, anakubaliana na wazo langu….’nikasema.‘Ina maana mlinijadili, ..si ulisema hutaongea naye sana kuhusu siri zetu…?’ akaniuliza‘Tuliongea, yale ya kawaida, si lazima mtu aulize baba wa mtoto wako ni nani, na lazima wengi wataniuliza mimi, kwa vile mimi ni rafiki yako, na nimeshajipanga jinsi gani ya kuwajibu,..lakini kwa mume wangu nilitaka nichukue tahadhari, jinsi gani ya kumjibu, umenielewa hapo…’nikasema‘Ok, sawa…’akasema‘Kwani hajafika kukuona…alisema akipata muda atafika kwako, hajafika…?’ nikamuuliza‘Keshafika…’akasema‘Mhh, alikuuliza….kuhusu mtoto…?’ nikamuuliza‘Mhh…ndio…lakini …tuliongea, …’akasita‘Najua, …mume wangu sio muongeaji, sana, hawezi kukudadisii kivile, baba yake ni nani, una matarajio  gani, mengi anajua tumeshaonge, namfahamu sana..’nikasema‘Sawa….utakuja kuelewa huko mbele ya maelezo yangu, kama utavuta subira…’akasema‘Aaah, kama leo umeamua kunisimulia ukweli, nipo tayari kuvumilia mpaka umalize, nitafurahi sana…moyo wang utatulia,…’nikasema;Tuendelee na kisa chetu…***********‘Basi siku ile, ya tukio la kwanza ilikuwa kama bahati mbaya, au ndio niseme ilipangwa itokee hivyo, kwani siku ile kulikuwa na sherehe ya kampuni yetu, huwa tunafanya hivyo mara kwa mara kwa namna ya kujitangaza, na kuwapa pongezi wafanyakazi kwa kazi fulani iliyofanikiwa….’akasema‘Na sherehe kama hizo, familia inawajali sana familia na wafanyakazi, maana bila ya wao, wafanyakazi hawawezi kufanya kile walichofanya, tuna msemo hapo kazini kwetu kuwa juhudi ya mtu huanzia, nyumbani kwake…waingereza wanajua sana kuwale wafanyakazi wao…wajanja sana….’akasema‘Ni kweli hata mimi najitahidi kuwafanyia hivyo wafanyakazi wangu….’nikasema‘Basi kila mtu alipewa nafasi ya kuwaalika wanandoa wenza wao, na kama huna mwanandoa mwenzako, basi uje na mpenzi wako anayetambulikana, sio muhuni tu,…na wengi wanajulikana, hakuna siri hapo kazini kwetu,..au kama huna hata mpenzi, basi tulipewa nafasi ya kuja na hata ndugu yako..ilimradi kuwe na namna ya kupongezana kifamilia, na kijamii zaidi…’akasema.‘Na wewe ukamualika nani, …hahaha, najua ulimualika yeye,  au sio…?’ nikajikuta nimemuuliza hivyo…nitamani asema ndio, ni yeye, lakini haikuwa hivyo….ila akilini mwangu nilishajua kuwa ndio huyo ninayemfikiria mimi.‘Sasa cha ajabu siku hiyo sikuwa na mtu wa kumualika,..unajua tena wapenzi wangu walishaoa,..na nilikuwa kivyangu zaidi,…na siku hiyo,..sikuhitajia mtu, nilikuwa na yangu kichwani…’akasema‘Mhh..kweli hilo…’nikasema‘Kabisa kabisa sikutaka kuwa na mtu, nilikuwa nimetingwa na mawazo yangu maana siku zinakwenda, lile zoezi tulilolipanga halifanikiwi,…naona kama wanaume wannikwepa, na ninaokuwa karibu nao, siwezi kufanya nao…yaani ikawa shida, na  sikutegemea kuwa itakuwa vigumu hivyo.‘Yah..kiu ukikidhamiria inakuwa hivyo…’nikasema‘Ila kwa siku hiyo, kiukweli… nilitaka nisiwe na mtu karibu yangu anayeweza kunigusa…kunipa mawazo..nilitaka niwe peke yangu …, nilitaka hata kuwepo nisiwepo kwenye hiyo shughuli…, lakini ningeonekanaje na mimi ni mmoja wa mabosi wa vitengo, hapo nilipoajiriwa,,Kwahiyo siku hiyo nikaingia kwenye ukumbi kivyangu, sikuwa muongeaji siku hiyo niliwaambia wenzangu kuwa sitaongea kabisa, ..niliwaambia naumwa, …najisikia vibaya, na wenzangu walinielewa, wao wakaongea, walichoongea, na akili haikuwa hapo kabisa....’akasema.‘Wakati nimekaa naongea na wafanyakazi wenzangu, ..kikiwa ni kipindi cha kula na kunywa,…wenzangu wakawa  wananitambulisha familia zao, na wale waliokuja na watoto wao wakawa wananionyesha watoto wao,..basi hapo ndio nilikuwa sipataki…sio kwamba siwapendi watoto, wewe mwenyewe unanielewa, ila hisi fulani ndani kwa ndani…’akatulia‘Nakuelewa sana…’nikasema‘Mtu akiwa ana familia, ..anaweza hata kujingiza kwenye shirki, sio kwamba anataka,…maana inaumiza ndani kwa ndani, na huwezi kuelezea hilo labda liwe limeshakufika…Basi, wakawa wakinionyesha watoto wao, najitahidi kuwaonyesha ile hali yangu ya kupenda watoto lakini moyoni naumia,…na mpaka ikafika muda…, najiuliza ni kwanini, wote hapo tupo umri mmoja wana familia zao, na wengine nimewazidi, lakini wameshabahatika kuwa na familia zao, kwanini mimi....kwakweli niliumia sana, hadi nikajikuta machozi yananitoka,...na kabla sijaonekana nikainuka …‘Nilikimbilia washroom, kunawa nikiwa na maana nikitoka huko, sirudi tena kwenye sherehe, naondoka zangu kulala, na siku hiyo sikutaka kabisa kugusa kilevi, nilishadhamiria kuacha kilevi kabisa, niwe huru, niwe tofauti..…,Sijui nilikaa muda gani, ila nililia sana,…sijui,..nilimlilia mungu wangu..sana, na kama mtu angeliingia akanigusa,..sijui…nilikuwa sio mimi… na nilipohakikisha machozi yamekwisha, nikatoka mle ndani,…, nikarudi pale mezani kwangu kwa nia ya  kuchukua mkoba wangu, niondoke zangu…lakini haikuwezekana.‘Kwanini…?’ nikamuuliza*********‘Wakati nimetoka chumb cha kunawa, niliona mtu mgeni mezani kwangu…’akasema‘Mhh, hapo hapo,….’nikasema‘Tulia basi…’akasema‘Kwasababu alinipa mgongo sikuweza kumtambua kwa haraka, na akilini mwangu sikutaka …kuongea na mtu, kwahiyo sikutilia maanani, nikawa nakwenda mwendo wa haraka kwenda kuchukua mkoba wangu, na sikutaka kuaga…’akasema‘Ok…’nikasema‘Pale nilihisi machozi kama yanataka kunitoka tena,..nikajikaza ki-kike…na..niliposogea nikashikwa na butwaa, sikutarajia kabisa,…’akasema‘Una maana  ni …huyo bwana’ko...?’ nikajikuta nimemuuliza maana kwa muda ule nilikuwa nimetekwa na hisia za huruma, kama nilivykuambia awali rafiki akiumizwa na jambo ni kama mimi niliyeumizwa, kwahiyo hata mimi pale nilitamani kulia, lakini nikawa namuuliza maswali ilikupotezea….Kiukweli usichanani kwetu ilikuwa hivyo, ikitokea tatizo la kuumia, kulia, kuhis jambo kwa mwenzangu na mimi nakuw ahivyo hivyo..sijui ilikuwaje, kwa watu wasiotufahamu wakituona walihisi sisi ni mapacha…maana  kama ni tukioa la kulia, tutalia sote…mmoja akiwa na furaha, basi tunafurahi sote, …kwahiyo maneno yake hayo hapo yalinifanya nitoe machozi na mimi….sasa uone kiasi gani tulivyokuwa tumeshibana.Yeye hakujibu hilo swali mara moja…, muda huo alikuwa kimia kidogo, nahisi alikuwa akiwazia mbali,..basi ili kumpa unafuu, nikauliza swali la kumtoa hapo alipo‘Si huyo bwanako mliozaa naye, au…?’ nikauliza hivyo kumchochea, nafahamu hapendi kuambiwa hivyo, na kweli, akainua kichwa na kuniangalia huku akisema kwa jaziba;‘Huyo sio bwanangu bwana,…mume wa mtu atakuwaje bwana’ngu, …!’akasema kwa sauti ya kukereka…!‘Nauliza ni huyo aliyekupa huo ujauzito,  au huyo unayefikiria kuwa ndiye aliyekupa mimba…, maana awali umesema huna uhakika,…na mpaka sasa hujaelewa, nakushangaa, ina maana ulipewa madawa ya kulevya au ilikuwaje …..hahaha  mtu wewe, yaani wanificha hata mimi,  haya ngoja tuone unataka nini ….?’ Nikamuuliza, hapo akatikisa kichwa tu.‘Sio hivyo rafiki yangu, hujui nipo kwenye wakati gani sasa, unajua ..nilijua baada ya kumpata huyu mtoto, akili yangu itatulia,…nilijua kila kitu kitakwenda sawa,..lakini nashangaa sana,…nakuwa na wakati mgumu kuliko…lakini yote haya ni sababu ya ….anataka mambo ambayo …we acha tu…’akasema‘Una maana gani hapo…?’ nikamuuliza‘Nitakuja kukuambia tu…., wewe si unataka nikuambie…u-ukweli, subiria sasa, ila nakuomba tafadhali uwe na subira,…tafadhali sana, wewe ni rafiki yangu na hili tulilipanga pamoja, au sio..’akasema‘Kwanini unasema hivyo..?’ nikamuuliza nikimuangalia moja kwa moja usoni, yeye akanikwepa na kuangalia pembeni.‘Lakini si wewe umeamua tuvunje yale makubaliani yetu moja baada ya jingine…ulisema iwe siri, sasa unataka nikuambie ukweli, haya, au niache…?’ akaniuliza akiniangalia kwa macho ya kutia huruma‘Ndio, nataka uniambie kila kitu,…wewe ndiye ulianza kuharibu, sasa endelea, nautaka sana huo ukweli,…, wewe ni rafiki yangu nilijua utaniambia tu,…huwezi kunificha jambo hata siku moja, … au sio....ila kauli yako inanipa mashaka, nahsi kuna jambo baya lilikutokea unaogopa kuniambia kuwa labda na mimi nitaumia, usijali, wewe niambie tu..…haya endelea, mimi sina wasiwasi na wewe, wewe ni ndugu yangu, kama kuna jambo limekutokea, siwezi kukutupa kamwe, niambie tu ilikuwaje…’nikasema‘Mhh, wewe wasema tu, kwa vile hujausikia huo ukweli…lakini sina jinsi inabidi nikuambie tu…ila sitakuambia ni nani , ni wewe mwenyewe utamfahamu…kutokana na maelezo …sasa utakaloamua, sina jinsi…’ akasema na kugeuka pembeni.Niliwaza huyu mtu ana maana gani, nikajikuta nasema‘Wewe endelea bwana…acha kuniweka roho juu…’nikasema‘Kumbe mjamaa alishafika muda, kwani nilimkuta anakula, sikujua kuwa nilichelewa sana chomba cha kunawia mikono, ni kweli nilichelewa nikiwa nimezama kwenye mawazo, mawazo ya mitihani niliyo nayo…ok, ndio hivyo….’akasema‘Basi nikamkuta jamaa anakula...pembeni kilevi…nikajua ehee…kazi ipo leo,..sijui ni nani alimualika, maana mimi sijafanya hivyo, …japokuwa wengi pale ofisini walishaniona nikiwa naye, na wanajua ni nani kwangu, …na sijawahi kusikia mtu akiniongelea vibaya dhidi yake, maana wanamuheshimu sana…na, wanamfahamu kuwa ni mtu mstaraabu tu…’akasema‘Yule..hahaha, mstaarabu, au maana ya ustaraabu hamuijui nyie, acha bwana, hata wewe unamuita hivyo,…hahaha, ..labda , kwasabbu ulishapenda, utasemaje, ukipenda chongo utaita kengeza au sio, hahaha, hata hivyo sikulaumu,…’nikasema‘Ndio kupenda, nilipenda, kama nilivyowahi kukuambia awali lakini nilishaweka mpaka, kwa vile ni mume wa mtu..nielewe hapo….’akasema‘Nakuelewa sana, mimi ninachokataa ni kumuita eti mstaarabu,…hana hiyo sifa kabisa,…labda, maana mtizamo wa watu, unatofautiana,…nikuambia kitu, na nilishawahi kukuambia, unakumbuka nilikuwambia huyo jamaaa alifanya nini kwangu…ananitongoza mimi, shemeji yake mke wa kaka yake, nilichomuambia hajawahi kurudia tena…’nikasema.‘Mhh…sawa nakuelewa, ulishaniambia  bwana, hayo tuyaache, …ngoja niendelee au…?’ akaniuliza‘Sawa endelea, …lakini usimvike sifa hiyo ya ustaarabu, hamtoshi….’nikasema‘Utakuja kuelewa tu kwanini nasema hivyo…’akasema‘Sawa endelea….’nikasema‘Kwanza, nilitaka nigeuze , niondoke, ..kabla hajaniona, lakini macho ya watu, waliniona na yeye alipoona watu wanaangalia upande wangu, akageuka akaniona..ikawa haina jinsi, …nikasalimiana naye, naye akanikaribisha nikae utafikiri yeye ndio mwenyeji, mimi nikamwambia najisikia vibaya nataka kuondoka.‘Aaah,…mimi nipo nitakupa dawa…’akaanza utani wake, unajua kuna kitu kimoja nilimpendea, anajua kumfariji mtu…na hata kama ulikuwa huna raha, utatulia tu, mna bahati sana mlioolewa….’akasema‘Hata mume wangu ana tabia hiyo, ila kuna muda, akiwa na mambo yake, …hataki kusema, anaumia ndani kwa ndani, yeye akikuona upo huna raha, atakudadisi mpaka basi, lakini yeye, akiwa hana raha, ngumu kujua labda awe anataka kukuambia, anasema kuna mambo mengine ya kiume, sio lazima kumsumbua mkewe, basi, mimi najionea sawa tu, ila kiukweli hatufichani, …ndio hivyo tena, siku hizi, sijui uzee…’nikasema‘Eti uzee, unanitisha mimi, una uzee gani….’akasema‘Mkiishi sana na mwenzako, unajionea kawaida, hata ile …raha ya usichana inakuwa haipo, utaolewa utajionea wewe mwenyewe…’nikasema‘Basi mimi nikazidi kumsihi kuwa najisikia vibaya yeye aendelee tu, …mimi naondoka kurudi nyumbani,…unajua alisema nini….’akawa kama anauliza‘Yaani hiyo tabia gani,…mimi mgeni wako nimekuja, kwa ajili yako…, mwenyeji wangu unataka kuondoka, haiwezekani, kaa angalau kidogo, nimalize kinywaji, ..na hiki chakuka, ..au niaviache…?’ akauliza akiashiria kwa mkono pale mezani, uzuri pale mezani hakukuwa na mtu mwingine, watu walishajichanganya huku na kule,‘Hapana wewe endelea tu wapo wengine mtaendelea nao, usiwe na shaka jisikia upo nyumbani…’nikasema sasa nikidhamiria kweli kuondoka.‘Mimi wengine siwajui, nimekuja kwa ajili yako…nimekuja kukupongezeni, …na mimi ninayemfahamu hapa ni wewe…au nimekosea kuja, basi kama unaondoka, nikuombe kitu kimoja, wewe si unaumwa, subiri nimalizie hiki kinywaji nitakupeleka nyumbani kwako, vinginevyo ukae, au…?’ akaniulizaBasi nikaona sio vizuri..nikaa kidogo, na yeye akaendelea kunywa,    nilishangaa kumuona shemeji akinywa kwa pupa siku hiyo ,… sio kawaida yake, ni kama alikuwa na kitu kinamkera,…hata sielewi… mpaka nikaingiwa na wasiwasi , kwanini anakunywa hivi.…’akasema‘Lakini yule ni mlevi, anakunywa sana, hata kaka yake aliniambia, labda akiwa kwako ndio anajivunga, haya  ikawaje, …?’ nikamuuliza‘Nikamtahadharisha kuwa kunywa kwa namna ile mimi sikupendi, anaweza akazidiwa ikawa shida kwangu, nikamwambia mimi naondoka,….akanizuia, akisema hii moja basi, hii moja basi..basi moja baada ya nyingine…’akasema.‘Hapana shemeji…mbona leo hivi….?’ nikamuuliza‘Usijali, siku moja moja, nafanya hivi, ili akili yangu iwe sawa,…nataka nikirudi nyumbani sisumbui kichwa changu tena, nalala tu, sitaki shida,..na leo sijisikii kwenda nyumbani, sitaki, na..na mambo yangu ya kufanya mengi ofisini, ikibidi nitenda kulala ofisini…’akasema‘Shemeji mimi nakuhofia wewe, imetosha…’nikasema‘Mhh, wanaume jamaani…., mimi sioni ajabu hata mume wangu kuna kipindi ilikuwa hivyo, mpaka nikawa sielewani naye, hasemi tatizo ni nini, anarudi kalewa, na ilikuwa sio kawaida yake, sijui, wakati mwingine najilaumu maana hizi kazi zinanifanya nakuwa mbali na mume wangu, ndio hivyo…’nikasema‘Mhh, yawezekana, ndio maana ilitokea hivyo...’akaguna na kusema hivyo‘Endelea na kisa chetu, nilitaka tu kukuambia kuwa hayo ya ulevi ni kawaida ya wanaume, hasa waliopo kwenye ndoa ...usijali sana, na wala usimwazie sana mtu kama huyo, kama kakupa ulichokitaka mpotezee, haya niambie ikawaje baadae naona muda umekwenda sana, ..’ nikasema.‘Basi, aliendelea kunywa, na mimi sijui ikatokeaje, akanishawishi, nilianza na mimi kunywa kidogo, kidogo ooh… akawa ananiongelesha kunichkesha, utani, nakunywa, nakunywa,..weeeh, akili ikabadilika, nikawa nami nazipupia, …japokuwa kiukweli nilijitahidi kujizuia,…’akatulia‘Mhh, kumbe…naanza kuipata picha….’nikasema‘Basi bwana, ikafikia muda nikaanza kujisahau na mimi nikawa nakunywa kupitiliza, ila nikabakiwa na akili kidogo ya kukumbuka, hapo nikaingiwa na shaka..huyu mtu kalewa hivi atakwendaje nyumbani, sikujijali mimi, maana najua nitapara msaada kwa wenzangu, huwa wanafanya hivyo wakiona mmoja kazidiwa kwa kilevi,a pombe mbaya jamani...’akasema.‘Nikatoka kidogo, kwenda `wash-room’ …nikampigia ndugu yake mmoja, ili kama akizidiwa ahakikishe anamchukua na kumfikisha nyumbani kwake…’akasema‘Ok, namfahamu sana yule ndugu yake, wanasema eti ni mapacha,  sio mapacha ila wamepishana kidogo sana, kama miezi tisa hivi au pungufu ya hapo kidogo…, sijui ilitokeaje mama yao alishika mimba mapema, ..ndio hivyo tena, bahati mbaya, kwahiyo wanakaribiana sana, sio mapacha wale…’nikasema.‘Nikampigia simu…kumbe alikuwa naye karibu tu, …akasema anatuona nisiwe na wasiwasi...’akasema.‘Mhh, hata mume wangu akilewa mara nyingi anamuita mdogo wake aje amchukue...hilo ni kawaida kwa wanaume wengi, na wadogo zake kuna kipindi wanakosana na kaka yao kuna kipindi wanaelewana, damu ni nzito bwana asikuambie mtu ....’nikasema.‘Ndio..naelewa hayo sana…’akasema‘Ok, sasa ikawaje...?’ nikamuuliza.‘Yaani baada ya kurudi mezani, akili hayo iliganda, sijui nilikunywaje,..sijui ilitokeaje, mengi nimekuja kuhadithiwa,…maana ninachokumbuka ni wewe kuwa kichwani mwangu na wazo lako hilo, kila mara unanighasi, ukisemaa…sasa fanya lile jambo wakati ndio huu… usimwachie huyu ..mshawishi, ...ukishindwa hapo basi tena..’‘Mimi nipo kichwani mwako….?’ Nikamuuliza kwa kushangaa‘Nakuona mbele yangu, ….nakusikia kichwani mwangu, unanishurutisha, nifanye kile tulichopanga nikifanye,…..akili ilikuwa sio yangu,…pombe mbaya, jamani..sitaweza kulisahau hilo…na yaliyotokea hapo, hapana….’akashika kichwa‘Ikawaje sasa….?’ Nikauliza nikiangalia saa yangu‘Nilijikuta nipo kitandani kwangu, nilivyofika, sijui…na wakati nazindukana, mara mlango unagongwa,…nikasema nikiwa nimejichokea ‘nani wewe, fungua mlango…mlango upo wazi,’Mara mlango unafunguliwa taratibu, anayefungua anaonekana kama anaogopa,..halafu kama ana uhakika, akafungua mlango kabisa,Mtu niliyemuona pale mlangoni, alinifanya nipandwe na hasira, sijui kwanini, nikasimama kwa hasira nikitaka kumfukuza, ..oh, najikuta nipo kama nilivyozaliwa..‘Nani sasa…yeye, kwanini umkasirikie, na …ina maana hukukumbuka kilichotokea usiku….?’ Nikamuuliza‘Sasa subiri kwanza, unajua ni kwanini nilikasirika, na huyo aliyeingia unamfahamu ni nani…?’ akaniulizaNB: Naishia hapa kwa leo, kili imechoka kidogoWAZO LA LEO: Kiukweli pombe kwa wanyaji huwezi kuwaambia kitu, lakini pombe ni sababu kubwa ya maasi,…imekuwa ni kichocheo cha kuharibika maadili, kuharibu ndoa..na kuharibu afya za watu, …wengi wanasema kuna faida ndani yake, lakini ukilinganisha faida na hasara , hasara ni nyingi zaidi. Nawausia wenzangu na kujiusia mwenyewe tuachane na ulevi…ewe kijana ewe mwanandoa, kulewa sio suluhisho la matatizo, bali ni kuahirisha tu tatizo kwa muda, tusijidanganye kuwa pombe inaondoa mawazo.‘Huyo aliyeingia alikuwa ni nani, si huyo shemeji au…huyo aliyekufanya sasa una mtoto, si ndio huyo, hutaki kuniambia lakini mimi nimeshamfahamu...si ndio huyo, mdogo wa mume wangu au sio?’ nikamuuliza‘Hapana....'akasema'Ni nani sasa.mbona sikuelewi...?' nikamuuliza'Alikuwa mdogo wa huyo jamaa,…'akasema'Mdogo wake...!!!'nikasema kwa mshangao'Ndio, na tena kaingia huku kafunga taulo, kiuonini, …na tabasamu tele mdomoni, kama vile nilikuwa naye usiku kucha,....na sasa ana...yaani mimi  nilihisi kama kutapika, nikawa na hisia za ajabu,..nikawa nahisi huenda walinifanyia kitu kibaya hao watu…’akasema‘Mbona sielewi, na  huyo..unayemuita shemeji...alikwenda wapi, ina maana watakuwa walishirikiana hapana hawawezi kufanya hivyo, sio watu wabaya kiasi hicho au…?’ nikauliza‘Kwa muda huo akili ilikuwa hivyo, inadhania hivyo....sikuelewa kitu kwa muda ule, si unajua tena ukiamuka kutoka usingizini, , …hapo ilivyo, akili yangu ilinifanya nielewe hivyo kuwa walishirikiana,...'akasema'Lakini sio kweli...'nikasema'Mhh...ngoja niendelee...maana hadi sasa nahisi hasira,...kama ilivyokuwa siku ile, nilipomuona huyo mtu, akili yangu ikajawa na ..., hasira chuki, ..nahisi kuzalilika,..na hasa pale nilipogundua kuwa nipo kama nilivyozaliwa, nikarudi kitandani na kunywea, na huku akilini nikijiuliza kulitokea kitu gani..na kama kuna kitu kilifanyikabasi watu hao, watakuwa wametangaza vita na mimi,….mimi sio mtu wa kuchezewa hivyo…’akasema‘Kaka ameshaondoka, ,…alisema nije nikuangalie kama umeshaamuka..na kama unahitajia lolote uniambie niweze kukusaidia, ..’akasema na sikumjibu kitu, na jamaa akataka kusogea kuja pale kitandani, nikainua kumuangalia kwa chuki, akasimama, hakusogea tena.'Eeeh, imekuwa hayo...'nikajiukuta nimesema hivyo.'Nilimuambia kwa ukali, kwa ishara ya mkono,....'‘Naomba utoke humu ndani kwangu  kwa haraka…’nikasema, kwa msisitizo‘Oh,….imekuwaje sasa…ok.ok…hakuna shida,… ila nilitaka kuhakikisha tu kuwa upo salama, mimi nitaondoka tu,…sina nia mbaya, kwanza hata mimi nahitajika nyumbani haraka, si unajua tena…’akasema‘Na ole wenu,….kama mlinifanyia chochote kibaya, mtanitambua kuwa mim ni nani….’nikasema‘Kibaya, ....!!! Hapana,...shemeji.... yote yaliyofanyika kwa ridhaa yako, …na ok, mtaongea na kaka, mimi ngoja nikavae, niondoke , hamna shida, ….’akasema akirudi kinyume nyume karibu ajigonge mlangoni‘Kwa ridhaaa yangu….’nikajikuta nimesema hivyo, na wakati huo mjamaa alishatoka ndani kwangu,Nilijikagua,....kiukweli, sikuwa na hali mbaya....ila nilisi vibaya tu...na nikaona iliyo bora ni kwenda kuoga...basi nikaenda nikaoga, huku nikiwaza na kuwazua,,,, kilichotokea jana ni nini,...je sijafanya mambo ya aibu...Na maji yalipomwagika mwilini ndio nikaanza kumbukumbu, ...akili ikianiz  kwenye sherehe,....oh, nikahema, ...nikawa najidadisi, je sikufanya jambo la aibu mbele ya wafanyakazi wenzangu pale ukumbini...hapana....hilo nalikumbuka vyema, je  baada ya hapo….‘Oh mungu wangu…’nikajikuta nikisema hivyo na kurudi kitandani,...kujilaza, uzuri siku hiyo ilikuwa ya mapumziko...na nilipotulia vyema ndio taswira ya tukio nzima ikaanza kunijia akilini…********** Nilianza kukumbuka, kuwa nilikunywa kupitiliza, na hata  tulivyofika nyumbani ilikuwa ni kwa shida, kama isingelikuwa huyo mdogo wake shemeji sijui ingelikuwaje, japokuwa nay eye alikuwa kalewa pia, lakini sio sana, …Tulipofika nyumbani, gari likisimama , kwa muda ule sikujua tumefika, nikawa nafoka, kwanini kasimamisha gari, dereva ambaye ni mdogo wa shemeji akasema tumeshafika, …basi nikawa najitahidi kutoka kwenye gari, ni mshike mshike..hata nilipotoka nje,..mmh, sikua vyema nayumba.Hapo nikajua wataondoka wataniacha …nilianza kutembea kuelekea ndani huku nayumba, shemeji naye huyo, akawa keshateremka kwenye gari...akawa ananifuata naye hivyo hivyo, anayumbe, akanishika nikawa najaribu kumkatalia asinishike,..uhimili wa miguu yetu ukahindwa,... sote tukaserereka chini.'Hahahaha...kama nilikuwepo....'nikacheka‘Sasa wewe vipi…’nikasema, nikimuambia shemeji, hapo kanilalia, .. tukaishia kucheka, hapo tumelala chini, na mdogo wake shemeji ndio akaja kutusadia kusimama mmoja mmoja..., haya…mzobe mzobe hadi ndani kwangu...pombe mbaya jamani, narudia tena kauli hiyo...'akasema‘Haya ondokeni…’nikasema tulipoingia ndani…‘Haondoki mtu hapa….leo tunalala hapa hapa…’akasema na mdogo mtu akashangilia, ujue wote hao wana wake zao, wanafamilia zao...  Kwa muda huo hata sikutaka kubishana nao...macho manzito, yanatamani kulala tu..., mimi nikakimbilia chumbani kwangu…nashangaa mjamaa naye huyu hapa, kaniganda, na tukajikuta tupo kitandani kwangu…kilichotokea hapo,..aaah, hata siwezi kuongea, maana ilikuwa kama sinema fulani …’akasema.‘Hongera,…ikawaje sasa maana mlilewa, iliwezekana siku hiyo...sizani , maana mlikuwa bwiii..au ilikuwaje...?’ nikamuuliza‘Mhh, kwani hapo nakumbuka, siwezi kukuficha, sikumbuki sikumbuki ndio maana hadi sasa najiuliza.., …..ila kumbukumbu za baada ya hapo zipo,…'akasema'Unanificha...'nikasema'Kunaaaah, ....muda, ndio... nahisi ilikuwa usiku sana, nilishituka,…akili kidogo zilikuwa zimerudi, kichwa kinaniuma kweli..,..najikuta kuna mtu kalala pembeni yangu…hapo natamani,..sijui kutapika, kichwa, kichwa...’ akasema‘Hahaha…pole sana nyie mwafikiri pombe ina mema, ..ni shida, sijui kwanini mnaendekeza kunywa..haya ikawaje..?’ nikauliza'Kichwa, kichwa kinauma,...'nikalalamika, na jamaa akajizoa zoa, na kwenda kuniletea maji, akaniuliza nina ..dawa ya maumivu,...nikamwambia ipo ...akanichukulia nikanywa, nikatulia kwa muda, baadae kikapoa kidogo.‘Hapo...., akili zimesharudi, nikamwambia aamuke aondoke..lakini akasema hawezi kuondoka usiku huo,…nikatoka kujisaidia, vyoo ni ndani kwa ndani,  lakini , nikawa na wasiwasi, nikaelekea varandani, ..nashangaa kuna mtu kalala kwenye sofa.Nikaanza kukumbuka pale ilivyokuwa, hapo hapo nikamuamusha mdogo mtu, ili waondoke.., lakini shemeji hakukubali, akasema hawezi kuondoka usiku huo hata hivyo alishamuambia mkewe atalala kazini…nikaona isiwe shida, ..sijui ilikuwaje, nakumbuka nilisikia kiu, nikataka kunywa kitu…nikasikia shemeji akisema‘Bwanamdogo mpe kinywaji atulie…’akasemaKweli mdogo mtu akaniletea kinywaji,  nikanywa, …haikuchukua muda,...nahisi kama kilevi kilikuwa sio cha kawaida, maana nililegea ..hata sijui ilikuwaje,ila nahis kuna mambo yalifanyika tena hapo..sina uhakika, …ukumbuke hapo ilikuwa varandani, sasa naamuka asubuhi, najikuta nipo kitandani kwangu, nimelala, nipo kama nilivyozaliwa, je ilitokea nini..na hapo sikumbuki vyema imekuwa mtihani kwangu,…’akasema‘Ikawaje sasa, tuache hizo pazia unazoweka, hazina maana kwangu, ilikuwaje…?’ nikauliza‘Ikawaje, ikawaje, ikawaje... ..ndio hivyo, asubuhi, huyu mdogo mtu nikamuambia aondoke, nikabakia peke yangu….’akasema‘Mhh,… wanaume hawa bwana, …nakumbuka siku moja mume wangu alikuja na mdogo wake, naye akiwa amelewa bwii, sikutaka hata kuongea naye, nikamwambia alale huko huko sebuleni,….sikutaka shida, …kama huyo yupo hivyo, achana naye, ilimradi kakupatia mtoto basi inatosha, mwanaume mlevi ni tatizo, anaweza kukuleta magonjwa…’nikamwambia.‘Nikuulize kitu samahani lakini..kwani shemeji ana tatizo gani?’ akaniuliza. swali lake lilikuwa kama kitu cha kushitukiza ni kitu sikutarajia kuulizwa, nikawa kama nimeshtuka, nikajikuta nikisema;‘Nani shemeji, mume wangu kakuambia nini…?’ nikaamuuliza‘Ndio mume wako..., naona kama …ana matatizo, wewe ni rafiki yangu, na lako ni langu, niambie ukweli …kuna tatizo gani kati yenu wawili?’ akaniuliza‘Matatizo ni ya kawaida tu..leo hili kesho lile mimi nimeshajizoelea tu, kwani umemuonaje, sizani kama alipokuja hapa mliongea kitu, au kwanini unaniuliza hivyo…?’ nikamuuliza‘Hapana,....mmh, ... mimi si ninaona tu…alivyo, sio yule shemeji niliyemzoea, anaonekana hana raha kabisa…nahisi kuna tatizo kati yenu wawili , niambie ukweli....’akasema‘Ungemuuliza yeye kwanza,...maana mpaka unauliza hivyo si ina maana mlikaa mkaongea au...na ni  shemeji yako,..kwanini hukumuuliza...'nikasema'Aaah, ina maana hutaki mimi kukuuliza mambo yako...'akasema'Sijakuambia umefanya vibaya,.... mimi nimemuuliza anasema yupo sawa,..hebu jiuliza  kama wewe mtu baki umemuona hivyo, je mimi ninayeishi naye,…kiukweli mimi sitaki kujisumbua tena kichwa changu, maana nina mengi ya kufanya,..hayo nakuomba tuyaache tu nitayamaliza mimi mwenyewe, kwa muda wake,..., nashukuru kwa kuliona hilo…’nikasema‘Mhh, nahisi kuna tatizo kubwa sana linalomsumbua shemeji..., jaribu kuwa naye karibu, sio vizuri rafiki yangu, mimi nawajali pia...’akasema rafiki yangu huyo.‘Unafikiri,....mbona nalifanyia kazi...nimeshaliona hilo, na yeye,...nimeshajaribu kumdadisi,... hasemi,... sasa nifanyeje, na sitaki hata kumuuliza zaidi, …kwa hivi sasa nimeamua akili yangu yote kwenye mambo ya kimaendeleo , kwa ajili ya familia yangu basi, muda utafika nikiona mambo yamekaa vyema nitalijadili, na yeye aniambie kwanini hataki kusema ukweli, ana tatizo gani…’nikasema‘Kama ni hivyo huyo mtoto wa kiume mtampataje…?’ akaniuliza swali ambalo, pia lilitoka na kunifanya nishtuke, sio kwamba ni swali la ajabu, lakini nakumbuka kauli hiyo aliwahi kuitamka mume wangu, wakati tunazozana, ilinijia tu hivyi, lakini sio kwa kudhania ubaya...Nakumbuka katika kuzozana zozana na mume wangu, kuna kipindi alitoa kauli hiyo...‘Mke wangu, hivi kwa hali kama hii, ..tutapataje huyo mtoto wa kiume,…kila siku uko na kazi nyingi, umechoka,…unanifanya nifanye hata nisiyodhamiria kuyafanya,…’akasemaKiukweli kauli hiyo ilinifanya niwe kwenye wakati mgumu, kama binadamu, kama mwanamke, nilihisi kweli nimekosea, lakini hata hivyo kama mwanamke nilihitajika kubemebelezwa, sio kwa vile mimi ni mke wake basi iwe hivyo, ni mambo ya ndani sitaki kuyasema zaidi,, lakini kiukweli  …hayo niliwaza tu, sio kwamba niliongea na rafiki yangu.Pale mimi nikasema;‘Achana naye…kama yeye kaamua hivyo..., na kaona hiyo ndiyo starehe yake ya kulewa, na pombe  ndio kila kitu basi aendelee, sitaki tena kumuingilia, sana muda utafika lakini sio kwa sasa, kwa sasa kuna mambo yananiumiza kichwa...'nikasema'Hilo ni muhmu sana rafiki yangu....'akasema'Nikuambie kitu, mimi sio mtoto mdogo, ...kulikuwa na wakati wa hayo....sasa hivi sisi ni watu wazima, lazima tuwe ni kipaumbele cha kujali ni nini baadae,...sasa nikimueleza mwenzangu haelewi, sawa, ana mambo yake..lakini...hajayatilia maanani kihivyo....'nikasema'Lakini ulisema kuwa anajitahidi kwa kazi, ndio maana kafungua ofis yake...'akasema'Sasa hiyo ni baada ya kuongea sana..na akicheza atashindwa,...kama ataendekeza pombe, najua yeye ulevi wake ni pombe, sizani kama ana ulevi mwingine,...kwa hivyo, basi...naona ni sterehe yake, nimemuacha  aendelee nayo...'nikasema'Aakirudi inakuwaje...mnalala pamoja...?' akanuliza swali jingine lililonifanya sasa nicheke sana.'Hahaha, wewe sasa nona unataka kuvuruga ajenda yetu,....hahaha, kwanin unaniulza hivyo...nikuambie tu kwa vile wewe ni rafiki yangu...kwa muda sasa.., nimeamua kumsusa hata kulala naye tuna muda, hata tunaishi hivyo hiyo ni siri yangu nakuambia wewe tu kwa vile ni rafiki yangu,…na nilishamwambia akirudi kalewa, asilale na mimi chumba kimoja, sipendi harufu ya mipombe…na siku akiwa safi, aaha, hamna shida anakuja tunalala, lakini ndio hivyo, tupo tupo tu,….’nikamwambia.‘Rafiki yangu hilo ni tatizo, jaribu kumuuliza vyema, kwani tatizo ni nini,..nahisi mume wako ana tatizo, mimi kama rafiki yngu nakuomba ulifanyia hilo kazi kabla hujachelewa, sizani kama unataka uwe na mke mwenza….utakuja kujuta, ukiwa umechelewa, hali kama hiyo sio nzuri.., utampoteza mume kwa hali hiyo, huenda ana tatizo linamsumbua na mtu wa kumsaidia ni wewe mke wake...’akaniambia‘Hahahaha,unanichekesha, eti mke mwenza, hahaha..ajaribu..kama ni kuoa, aoe, mbona nilishamuambia hilo, ila asifanye siri...nikaja kugundua,...na leo, kweli umenichekesha, Hivi nikuulize, unajifanya unafahamu saana  maswala ya ndoa, wewe ngoja utakuja kuolewa, utakuja kuyaona haya wewe mwenyewe, ..ndoa nyingine ni ndoa,kuna matatizo chungu mbovu, ...., lakini sisi wanawake tunavumilia mengi,.we yaache tu..’nikasema‘Hata kama sijaolewa, lakini mengi ni ya kibinadamu , nayafahamu tu…’akasema‘Unafikiri mimi sijafanya juhudi, nikuambie kitu, ndoa..sio ..yeye akiwa na hamasa zake aje akuvamie tu, mimi ni mwanamke, nahitajia kubembelezwa, nahitajia, hali itakayonifanya nisahau mengine ya kikazi,..na hilo halianzii,..kitandani tu…’nikasema‘Mhh..hapo unanitisha ...ok, labda nikuulize hapo... unataka kusema nini, mbona shemeji mimi namuelewa sana, nakumbuka ulishawahi kuniambia, umempata mwanamume anayejali, anayejua kubembeleza, au ulikuwa ukinidanganya…’akasema‘Ilikuwa…ghafla, mambo yalipojiongeza, majukumu ya hapa na pale, unaelewa, hali nayo ikabadilika,…tukurudi nyumbani kila mtu na laptop yake, shughuli mtindo mmoja, ..mengine ni uhalisia, hata hivyo, ..siwezi kumlaumu au yeye kunilaumu, lakini pia, yeye anawajibika, kulibadili hilo…’nikasema‘Mhh..mnatakiwa muwajibike wote, ..rafiki yangu shemeji ni mtu mnzuri sana, …anajali, nahisi wewe ndio hutaki kulifahamu hilo, au kwa vile unacho, ukiwa nacho unaona ni kitu cha kawaida tu..’akasema‘Unajifanya unamuelewa sana kuliko mimi au..ni kweli, unalolisema, alikuwa hivyo, lakini sio hivi sasa..nahisi keshonja kwingine, na mimi sina muda wa kupoteza kumdadisi, ila nilimuambia, …kama atakuja kufanya jambo kinyume na ndoa yetu, ajue tumeshamalizana….’nikasema‘Una maana gani…?’ akaniuliza‘We tuyaache hayo, ….muhimu nataka nihakikishe jambo lako limekwisha, halafu nitayamaliza ya kwangu nionavyo ni sahihi…na najiuliza sana, kwanini umefikia kuniuliza haya yote..maana hayahusiani na tatizo lako au sio…?’ nikamuuliza‘Nimeuliza tu…kwa vile nimemuona alivyo, na sizani nimekosea kukuulizia hayo, kaam uanavyonijali mimi, ndivyo ninavyokujali wewe…’akasema‘Ni kweli,..ila yasikuumize kichwa, mimi mwenyewe ni mipangilio yangu, kuna haya mambo ya kikazi yakikaa sawa, nitatafuta mtu wa kuyafanya, na mimi nitakuwa kariu na familia yangu, hilo nimeshaliona, lakini kwa sasa, ngoja, nione ni kitu gani anakihitajia,..ila, siku nikigundua ana kimada nje,..ohooo..huyo na yeye nitakachowafanyia, watakuja  kunikumbuka….’nikasema‘Mhh, kama ni hivyo utanifanya mimi niogope kuolewa, na hilo litawafanya wanaume wengine wapate mwanya wa kutoka nje ya ndoa…mpaka hapo naogopa, na hata …sizani kama nahitajika kuongea zaidi…’ akaniambia.‘Usiogope, kuolewa kwa vile umesikia hayo kutoka kwa ndoa za watu , ndoa za watu hazina utaratibu maalumu kuwa yule akiwa hivi na wewe utakuwa hivi, kila mmoja ana utaratibu wake wa kuishi, na mwsho wa siku wote wawili mnakubaliana na hali halisi iliyopo, muhimu msifichane, msiwe na ajenda za siri, zinazovunja ndoa....’nikasema.‘Lakini mimi nina imani nikiolewa nitahakikisha kuwa mimi na yeye kwanza tunapeana masharti  ya jinsi gani ya kuishi, na kama nikihisi kuwa kuna tatizo nitamuuliza mpaka aniambie, kwani sitafurahi aje kutembea nje ya ndoa, na chanzo kiwe ni mimi....vinginevyo, nisijue …. ’akasema.‘Kwahiyo unataka kusema nini, kuwa mimi ninaweza kuwa chanzo, kuwa mimi ndiye nimemfanya mume wangu alewe , awe hivyo, au.. ..kama ana tatizo angeliniambia basi, moja kwa moja, mimi si mkewe, kwanini aone uzito kuniambia, eeh,.., ukiona anaficha kitu, ujue hataki kukuambia, mimi namfahamu sana,…vinginevyo mimi siwezi kumuingilia maisha yake aliyoamua kuwa nayo, muhimu mimi mwenyewe naweza kuishi maisha yangu...’nikasema.‘Mhh, haya bwana, kama ulivyosema ndoa kila mtu na utaratibu wake, na mimi nimejifunza kutoka kwa wenzangu sizani kama nitafanya hayo makosa,...maana mengine hayavumiliki, ...na wasiwasi wangu najiuliza kama likitokea tatizo hapo ni wa kulaumiwa, na je ni nani wa kuumia, kama sio sisi wanawake, hebu lifikiria hilo rafiki yangu....’akasema..‘Achana na mume wangu, hebu tuendelea na hili tatizo lako, likimalizika la kwako litanipa nafasi ya kuendelea na mambo mengine, …ilikuwaje baada ya hapo,...?’ nikamuuliza.‘Yaliyoendelea ni kama unavyoona, ....kwanza baada ya tukio hilo tulikaa kama wiki hivi hatuonani, na tulipoonana akawa ananionea aibu,..na mimi halikadhalika, na hatukuweza kubahatika kuliongelea hilo tukio hata siku moja, na ikawa kama vile tukio hilo limetushitua, sote wawili…’akasema‘Mhh, lakini ulisema ilitokea mara ya pili au…?’‘Ya pili, si ilikuwa siku ya pili yake, nikawa nahisi kuumwa, kumbe ni hiyo mipombe, akaja akaniambia dawa twende kunywa tena,..nikagoma, akanisihi mpaka nikakubali, ikaja kutokea kama vile…aliyetusaidia ni huyo huyo ndugu yake…’akasema‘Una hatari wewe…’nikasema‘Basi baada ya hapo,…nikaona atanizoea vibaya, nikaanza kumkwepa, akipiga simu sipokei, nikawa sasa siendi kula chakula cha mchana,nikingia ofisi nakuja a chakula changu, sitoki hadi jioni, na nikitoka najivunga kutoka na mmoja wa wafanyakazi ninaofanya nao....siku zikaenda...’akasema.‘Mara nikaanza kuhisi mabadiliko...nikashituka, mwezi wa kwanza wa pili sijaona siku zangu, nikaona oohoo,… ngoja nikapime, kupima, nikaambiwa hongera..una mimba.....’akatulia.‘Oh…ikawaje…?’ nikamuuliza‘Ikawa hivyo hivyo, namkwepa kuliko, awali, lakini ikafikia muda, hali inanivuta natamani kuonana naye, ..lakini sitaki nionekane na watu, nahisi aibu fulani hivi…basi siku moja akanitumia meseji kuwa hana raha,…bila kuniona hataweza kwenda nyumbani kuna kitu anataka kuniambia‘Kitu gani….?’ Nikamuuliza‘Mhhh…nilishindwa hata kumuelewa, kumbe alikuwa na ajenda ya siri, …na sijui kwanini ilitokea hivyo, ndio maana rafiki yangu nakukanya,..ndio mimi sijaolewa, ndio mimi sina uzoefu wa ndoa, lakini wanaume wengine wanafikia kufanya mabaya kutokana na jinsi tunavyoishi nao, tunawajenga,..tunawafanya wafanye hivyo,…tuweni makini sana…’akasema‘Hebu niambia alitaka kukuambia nini, maana mimi nataka kuondoka, naona unanifanya nijihisi siwajibiki, wakati wewe hujui mengi ya ndoa,..ipo siku nitakueleza, sio kweli kuwa mimi nimefikia kuyafanya hayo bila sababu, lakini mambo mengine ya ndoa, …hayazungumzwi….’nikasema‘Basi kwa vile hali hiyo ilinizidi, nikawa natamani nimuone tu, awe karibu yangu, awe akiongea, awe kinibembeleza…yaani nakuwa na raha, na kuwa na amani, na akuiondoka, nakuwa muogoa, naogopa, ni hali tu ilinitokea hivyo…basi, nikamkubalia siku hiyo aje, …na hiyo ikawa imekaribisha mimi na yeye kuwa karibu tena‘Sasa alipokuja siku nyingine ndio, akaniambia lake la moyoni….na hilo ndilo likafanya ajue kuwa mimi nina uja uzito….’akasema‘Alikuambia nini…?’ nikamuuliza na yeye, akasimama maana mtoto alikuwa akilia, na mimi simu yangu ikawa inaita…‘Alikuambiaje…?’ nikamuuliza nikiangalia ni nani anayenipigia, kumbe, … alikuwa ni mume wangu, nikamwambia rafiki yangu;‘Tafadhali kidogo…niongea na shemeji yako…’nikasemaNikawa sasa naongea na mume wangu , huku rafiki yangu akiniangalia kwa makini, ni kama ana shauku kufahamu naongea nini na mume wangu‘Njoo nyumbani haraka…’ilikuwa sauti ya mume wangu kwenye simu‘Kuna nini…?’ nikauliza, na mume wangu akakata simu…kutokana na sauti yake hiyo, nikajua kuna tatizo, kwahiyo sikutaka tena kuendelea na rafiki yangu, nikasema‘Rafiki yangu, tutaendelea baadae , nataka kufahamu, alikuambiaje, au ..alikuambiaje…ok..ngoja niondoke….tutaongea siku nyingine si bado upo,….?’ Nikamuuliza‘Kesho naondoka…’akasema‘Basi nitakuja, …nahisi nyumani kuna tatizo…’nikasema na kukimbilia nje, kuondoka..NB: Naishia hapa kwa leo,WAZO LA LEO: Ndoa ina siri zake nyingi sana, na iliyo wajibu,  ni wanandoa wenyewe kujaribu kuzikabili changamoto zao, na kufiachiana siri zao, kwa kadri wawezavyo, kwani siri nyingine ni mtihani mungu anawajaribu…ni changamoto za kuvuka daraja…Ni vyema kwa wanandoa, mkawa kitu kimoja kwa kuyajadili matatizo yenu, ni aibu kama wanandoa kama mtakuwa mkilalamika kwa watu wengine kuhusu mambo yenu ya ndani, ambayo mengine ni siri za ndoa, kwanini msiulizane, mkaangalia tatizo lipo wapi…kumbe yawezekana ni kitu kidogo tu… Tuweni makini kwa hili. Tumuombe mola azilinde ndoa zetu atuongoze tuwe kizazi chema.Basi niliondoka hadi nyumbani, namkuta mume wangu kazidiwa shinikizo la damu, ikabidi nifanye jitahada nyingine za kumuita docta, hakutaka nimpeleke hospitalini, akaja docta, akasema kweli shinikio la damu lipo juu, kwahiyo apate dripu…Baadae hali ikawa shwari, ikabidi nikae naye kumuhoji hili na lile, nilichelea kuongea naye maswali yanayoweza kumtatiza hata docta alinionya kwa hilo, lakini kuna swali lililokuwa kichwani mwangu;;‘Nikuulize kitu samahani lakini..kwani shemeji ana tatizo gani?‘Ndio mume wako, naona kama …ana matatizo, wewe ni rafiki yangu, na lako ni langu, niambie ukweli …?‘Hapana, mimi si ninaona tu…alivyo, sio yule shemeji niliyemzoea, anaonekana hana raha kabisa…’akasema‘Mhh, nahisi kuna tatizo kubwa sana linamsumbua, jaribu kuwa naye karibu, sio vizuri rafiki yangu, mimi nawajali pia..Kumbukumbu hizo ziliuteka ubongo wangu, na kiukweli sikuwa na amani kabisa..,Japokuwa mpaka hapo sikuwa na wazo baya dhidi ya rafiki yangu…ila nilianza  kuamini kweli mume wangu ana matatizo..na hilo ndilo nililipa kipaumbele, vipi nitaweza kumsaidia mume wangu, maana hiyo hali iliyojitokeza ikiendelea hivyo, kweli naweza kumpoteza mume, …niliwazia zaidi kwenye afya yakeBasi nilipoona mume wangu katulia, na anaongea vizuri, nikamuuliza‘Hivi mume wangu,  hebu niambie,…. kuna tatizo gani linalokusumbua…?’ nikamuulizaMke wangu matatizo ni ya kawaida tu, …tulishayaongea haya,…na mimi  sitaki ukwazike kwa hilo, na sijui kwanini leo hali yangu imekuwa hivi,..nijitahidi isitokee tena, lakini kuna mambo mengi yamenizonga, lakini yataisha tu, nitayamaliza kwa vyovyote iwavyo…’akasema‘Huo ni ugonjwa, halafu unasema utajitahidi isitokee tena, na tatizo hilo, ninavyoona sio bure, nahisi kuna kitu kinakusumbua,…sasa usipotaka kunishirikisha mimi, eeh, hebu niambie,…ni nani mwingine anaweza kukusaidia, zaidi ya mkeo …’ nikamwambia.‘Usijali mke wangu,…wewe endelea na kazi zako tu, najua una mipangilio yako mingi sana, …, na sitaki mimi niwe sababu ya kukukwamisha…’akasema‘Hujanisaidia kwa hilo, maana sasa sitaweza kufanya kazi zangu kwa amani, nitakuwa na mashaka muda wote, usiponiweka wazi…utanifanya na mimi nianze kuumwa.Basi nikaanza kuwa karibu na mume wangu na kumuomba samahani kama mimi ndiye chanzo cha hayo yote, na siku moja akaniambia;‘Mke wangu, uwe na amani, najua yametokea mengi, ambayo huenda hata mimi sikupenda yatokee, lakini isiwe sababu ya wewe kukatisha shughuli zako, muhimu ufahamu sijapenda yatokee, na kuumwa kwangu hata mimi ninaanza kuogopa, inabidi nibadilike..’akasema‘Ni kitu gani kinachokusumbua, hebu niambie kwanza…?’ nikamuuliza‘Kifupi hakuna…nimeshazoea, na…hakuna tatizo, …’akasema na sikuweza kuwa na amani tena…hasa nikikumbuka zile kauli za rafiki yangu, na sasa ninaona kweli mume wangu ana matatizo,…Kwasababu ya hayo matatizo, nikawa sina muda wa kumfuatilia rafiki yangu tena, kumbe alishaondoka kwenda Zanzibar.Na siku baadae nikamtembea rafiki yangu, katika kupoteza mawazo, na katika kuongea tukajikuta kwenye yale mazungumzo yetu, tukafikia pale pale…nikamuuliza‘Unajua siku ile tulipoongea ukanipa ushauri kuwa niwe makini naweza kumpoteza mume wangu, imenifanya nianze kujirudi, nimewaza sana, naona kweli nitakuja kuumiza mume wangu…’nikasema‘Nilikuambia lakini…sasa kwanini unaendelea kufanya hivyo, na je mume wako anaendeleaje…?’ akaniuliza‘Hajambo hajambo kabia…na  huwezi kujua ni yule siku ile nilimkuta kitandani akiwa kama kapoteza fahamu, ..shinikizo la damu ni baya… siku ile hata mimi niliogopa, maana alikuwa kama anataka kukata roho…’nikasema‘Oh,… lakini ni nini tatizo…?’ akaniuliza‘Mpaka leo sijafahamu…na hata sielewi, unajua kuna kauli alisema…lakini sio sababu nahisi kuna jingine..lakini hizo kauli zimenifanya niwaze tu, …japokuwa sizani kama zinaweza kuwa ndio sababu..’nikasema‘Kauli gani hizo mbona huzitaji…?’ akaniuliza‘Unajua kuna kitu, …mume wangu anatamani sana, kimojawapo ni hicho, ya kuwa anatamani kupata  mtoto wa kiume…na kingine ambacho hatusikilizani, yeye bado, anapenda ujana ujana,….hajui kuwa umri umekwenda…hilo sijui wanaume wengi kwanini haalioni…mzee mzima bado upo na mambo ya vijana.., mimi namemuambia sina muda huo…’nikasema‘Mhh kwanini unafanya hivyo, unafanya makosa, maana mume wako ni mwenza wako mwatakiwa mshirikiane, mfurahishane, sasa kama anataka hivyo akaende wapi, ndio maana wanakimbilie mitaani, ..hili hulioni wewe…?’ akaniuliza‘La kujiuliza ni hili mambo hayo, eeh yana faida gani kwetu, kwa umri huu…sawa kama ni watoto tutapata tu,….mungu akipenda, … ila nilitaka nimalizane na mipangilio yangu ili tukianza kuzaa, nisiwe na hangari hangari nyingine ndio mpangilio wangu, nimejifunza kwnye mimba hiyo ya kwanza, …na hilo nilishamuambia…’nikasema‘Ina maana hilo ndilo la kufanya usiwe karibu naye,…hilo ndilo linakufanya  usitimize haki za ndoa, ambazo ndio msingi wa ndoa au …’akasema‘Unasema nini.., nani kakuambia kuwa sitimizi haki za msingi za ndoa..?’ nikamuuliza kwa mshangao.‘Nakuuliza sio nasema mimi, nakuuliza wewe, na …’akasema na kabla hajamaliza nikasema;‘Umeyajuaje hayo,….!! Kwani aliwahi kukuambia hivyo, kuwa sijamtimizia hayo…aah, naona sasa unaingilia mambo yasiyokuhusu…’nikasema‘Lakini rafiki yangu rejea mazumgumzo yetu tuliyofanya siku  ile, kwani hukuwahi kunigusia hilo,…. au unafikiri mimi nakuzulia au urafiki wetu una mipaka sijakuelewa, …’akasema‘Ok,…ok… basi labda niliwahi kukudokezea hilo.., sawa, nimekumbuka nilikuambia …hata hivyo hilo mimi nimeshaliona, na nilikuwambia nitalifanyia kazi, kwahiyo lisikuumize kichwa, umenielewa…’nikasema‘Sawa, ….ni heri ulifanyie kazi, na kiushauri, kama kuna yaliyotokea yakakukwaza, au kama kuna kitu, jaribu kukiweka kapuni, kitupe… nakuomba uyasahau yote mabaya ya nyuma,…hali umeshaiona, hali hiyo inaashiria kuwa ,  sasa hivi uwe karibu naye, na…nahisi inaweza ikaleta heri ukifanya hivyo.., tusameheane tu, maana mengi yanafanyika ili tu, kutimiza adhima…’akasema‘Nimekuelewa,…’nikasema‘Unajua nilitaka nikisafiri niwe na amani, niwe nimeacha kiula kitu ni shwari..nisiwe na kitu moyoni mwangu kwako, na wewe kwangu…’akasema‘Hilo lisikutie shaka, hebu kwanza nikumbushe, siku ile tuliishia wapi…’nikasema‘Siku ipi tena….mmh, yale tuachane nayo bwana…ndio maana nataka tuhakikishe tumeridhiana, hakuna …jambo la kuumizana kichwa, na ukweli wote, nshakuambia au sio…’akasema‘Hapana hujambia,..ukweli wote.., maana nakumbuka siku ile ulisema…, alipokuja kwako,…kuna kitu alikuambia ndio kikafanya yeye agundue kuwa una mimba, ni kitu gani miliongea…?’ nikamuuliza‘Hahaha, na wewe bwana,….hahaha, unajua wakati mwingine nacheka, lakini wakati mwingine najiuliza hivi hili jambo litafikia mwisho tusahau , isije kuleta matatizo huko mbeleni,…na ikileta .. itakuwaje…maana nimejaribu kila njia unielewe, lakini sizani kama utanielewa, kwa hali kama hii…unakuwa mdadisi kwa kitu ambacho ulikanya wewe mwenyewe kuwa jambo hilo liwe siri….sasa labda mimi naona nikuambie kila kitu iwe iwavyo…’akasema‘Sawa lakini hapo …kuna kitu sijakuelewa…’nikasema‘Rafiki yangu, hebu nikuulize kwani unataka nini zaidi,..unataka matatizo, unatakaje ili iweje, …wakati mwingine naona ni bora tukae kimia, wakati mwingine naona ni bora niweke kila kitu kwenye meza, ..lakini sitaki  kuumizana , sipendi kabisa…’akasema‘Kwa hivi sasa bora uniambie kila kitu tu, maana ukiacha ndio utanipatia shinikizo la damu, maana nimekuwa nikijiuliza, na…nilitaka hata niende kuonana na mdogo wa shemeji ili niwe na uhakika fulani, kuna maswali yana nijia, na mimi nataka nimuulize, lakini siwezi kufanya hivyo mpaka nipate ridhaa yako,…wewe huelewi tu, …wewe ni kama mdogo wangu lazima niwe na uhakika na ulichokifanya, ili likitokea la kesho,  niweze kuwa na majibu, ukumbuke kuna leo na kesho…’nikasema‘Kwahiyo unataka nini hasa, na upo tayari kwa …mimi siwezi kuwa na uhakika na wewe, maana hili linaweza likawa sababu, na mimi sitaki, unielewe hapo, eeh, mmh…nasita kidogo hapo…’ akasema‘Swali lipo pale pale… ikawaje, usitake tuzunguke,…. huyo shemeji alifahamu vipi kuwa wewe una mimba, na ni kauli gani ilikyokufanya hata wewe ufikie kumwambia, au ilikuwaje…unajua, nimeanza kuandika kitabu changu, natunga true story ya maisha yetu mim na wewe vyema…hahaha, huwezi amini mengi yaliyotokea kati yangu na wewe nimeshayaandika…’nikasma‘Unasema kweli…?’ akauliza‘Ndio..ni pale ninapokuwa sina kazi,..akili imetulia huwa naandika, yale yaliyotokea kama hadithi fulani hivi,…sasa hivi nipo kwenye hilo tukio, naona lina maswali mengi yasiyokuwa na majibu, na sehemu hiyo nimeiita, ‘ukweli baada ya ushauri kwa rafiki yangu..’.‘Mhh, ushauri kwa rafiki yako, ambao umeleta matatizo au, itakuwaje sijui….’akasema‘Matatizo aah, nani kasema, hakuna kitu kama hicho, ni ushauri ulioleta matunda ya kuleta faraja…huoni sasa una mtoto, usiseme hivyo….’nikasema***********‘Kama nilivyokuambia, kuna muda nilikuwa natamani yeye awe anakuja, au nimpigie simu tuongee naye, nikifanya hivyo, nikasikia angalau sauti yake, kama hakuweza kufika, najihisi raha, nakuwa na amani fulani… lakini wakati huo sikutaka hayo yajulikane na watu.., sikutaka watu wanione nikiwa naye tena, naona aibu kuliko wakati wote, nilihisi kama watu watanigundua kuwa ndio yeye…’akaanza kusimulia‘OK…sawa endelea…’nikasema‘Siku hiyo alifika akiwa hana raha, nikamuuliza tatizo nini…akasema hakuna kitu ni mambo ya kawaida tu,..ni mambo ya kifamilia zaidi…’akasema‘Kama huniambii, sitakuwa na amani, siku hizi sijisikii vizuri, nataka wewe ukija uwe na furaha, na kama huna furaha ..ni bora usije ,..na usiponiambia tatizo lako, ni bora uondoke..’nikasema na moyoni nijiuliza hivi kweli akifanya hivyo si nitaumia sana, na mimi nataka awe karibu yangu.‘Ina maana muda huo mimba bado imejificha,..bado mapema au sio..?’ nikamuuliza‘Kitumbo bado ile yasana,… ila kimeshaanza kutuna, na mimi sijui kwanini, nilianza kuvaa nguo pana mapema, ..kama  Madera…kitu ambacho wengi walianza kunihoji nakawa nawapa majibu yao, na nikazoeleka hivyo kuwa nimebadilika, siku hizi sio yule mdhungu tena…ilinisaidia, hata dalili zozote zisionekane mapema, na siku baada ya siku …tumbo likaanza kukua…’akasema‘Safi kabisa, ulicheza hapo maana hata mimi sikuwahi kukushuku awali…’nikasema‘Nataka unizalie mtoto wa kiume…mjamaa alipofika alisema hivyo…’akasema‘Mungu wangu alikuambia hivyo…?’ nikauliza nikihema, muhemo, kama vile kauli hio inanihusu mimi.‘Ndio alisema hivyo na mimi kauli hiyo ilinishika kwa mshangao, lakini sikutaka kujionyesha, nikacheka kweli‘Kwanini unacheka, akaniuliza…?...’akasema‘Unanishangaza, ina maana kukuita hapa, umenifanya mimi kama hawara wako,..nilishakuambia yaliyotokea siku ile, mimi sikuyataka na yaninipa wakati mgumu sana, na..na..kwanza ole wenu nilitaka kuwashitaki, mlichonifanyia wewe na ndugu yako, sitaweza kuwasamehe..’nikasema‘Kitu gani, mbona sikuelewi…?’ akasema‘Tuyaache hayo…na umesema nini…?’ nikauliza kama vile sijasikia‘Natamani wewe unizalie mtoto, lakini awe wa kiume..’akasema‘Nikuambie kitu, hilo kamwambie mkeo, sio mimi…’nikajifanya kuwa mkali,‘Sikiliza,..najua hata wewe unataka mtoto, nimesikia hivyo..,..unatamani uwe  angalau na mtoto, hata mimi naliunga mkono, maana umri unakwenda au sio, sasa hebu tulia basi…’akasema na mimi muda huo nilikuwa nasimama nahisi kichefu chefu‘Ni nani kakuambia upuuzi huo…’nikasema nikigeukia upande wa pili leso mdomoni.‘Wakati mwingine wanawake mpo hivyo, kama hujaolewa kwa muda..umekaa na unahisi umri utakusuta..na sio siri kila mtu anatamanikuwa na mtoto, hata wewe itakuwa hivyo,…hilo lipo wazi, sasa nisaidie na mimi nikusaidie…’akasema‘Nikusaidie..wewe si mume wa mtu jamani, unataka nini…?’ nikamuuliza na mengi yakaendelea hapo ikawa tena hatuelewani…’akasema‘Mengi yapi..?’ nikauliza‘Tulibishana sana kuhusu hilo la mimi kumzalia mtoto, eti tena wa kiume,…hivi hilo si alitakiwa aongee na mkewe…anyaway, tulibishana hapo, na sijui ikatokeaje, nikaanza kujisikia vibaya, kutapika, nikakimbilia washroom, kumbe alinifuatilia kwa nyuma, sasa wakati natapika, ikafikia muda, nikasema;‘Kama mimba ni hivi, bora …nizae mapema tu..hiki kikombe kinipite…’nikasema na huku nyuma yangu nikasikia akisema;‘Kumbe una mimba…’akasema,..nilishtuka, karibu nizimie, na akaja haraka kunishika ili nisidondoke, na alipohakikisha nipo salama akasema;‘Oh, sasa niambie ukweli,…kumbe una mimba , kumbe ni kweli…mmh, nishathibistha inatosha, sasa niambie ukweli  ni yangu au kuna mwingine…’akasema‘Mimi sio Malaya bwana…’nikasema‘Ndio maana nauliza isije kuleta matatizo..najua mimi nimeshatembea nawe, sina uhakika na mwingine je ni ya kwangu au kuna mwingine…?’ akaniuliza‘Mimi sijui, maana mlichokifanya wewe na ndugu yako siku ile mimi sijui, mimi sijui na sitaki kujua, niache, ushaiharibu siku yangu  , ondoka…’nikasema‘Basi natosha, ninachoomba kwa mungu awe mtoto wa kiume…’akasema hivyo, na hakutaka kukaaa sana, akaondoka akiwa anaonekana ana furaha usoni , sio kama alivyokuwa amekuja.‘Kwahiyo hebu kwanza nikuulize kuna jambo nilitaka niwe na uhakika nalo..hivi ulipogundua kuwa una mimba, ulikwenda kupima wapi, maana nataka mambo haya yawe kwenye kumbukumbu zangu, hapo kasema, ‘kumbe ni kweli’…’nikasema.‘Kwanini unauliza hivyo…ina maana kweli kuna kitabu unatunga, au unataka jambo kama ushahidi fulani, ushahidi wa nini…?’ akaniuliza.‘Nimeshakuambia naandika tu  kujifurahisha, nilianza kama mzaha tu, lakini kadri siku zinavyokwenda naanza kufurahia,… na hasa hii kadhia, kuna muda.. inaniacha kwenye maswali mengi ya kutaka kujua zaidi,..unajua tena…na hata hivyo ni kawaida yangu kuwa na kumbukumbu, na  usinifikirie vibaya, kwanini nafanya hivyo, au hupendi, niwe naandika, kama hupendi nitaacha tu…’nikasema‘Ok.. nilikwenda kupima kwenye  ile hospitali iliyopo karibu na kazini,…na nilifanya hivyo kwa vile sikuwa na amani, nilikuwa sijisikia vibaya vibaya, hali ambayo sijawahi kuihisi kabla, huko kupoteza siku zangu , inatokea mara kwa mara kwahiyo haikuwa ni sababu…hata hivyo wakati naenda kupima, nilikuwa kama siamini, maana …kama tukio lilivyokuwa ilikuwa kama ni ndoto…na sikuweza kuwa na uhakika, niweke hivyo tu…’akasema‘Hukuwa na uhakika gani kuwa ni nani kati ya hao ndugu wawili au si..…au hukuwa na uhakika kwa vile..haiwezekani ulisema ..kitendo kilikuwepo au sio, … hapo usinidanganye kitu…mpaka hapo nahisi kuwa kuna kitu unanificha, halafu unajinasa mwenyewe  hiyo kauli ‘sikuwa na uhakika..’nikasema‘Nimekumbuka kitu…siku ile nilipokwenda kupima nilikutana na docta ambaye nafahamiana naye, naye kuna kipindi tulikuwa naye karibu baadae ndio akaoa, nikaachana naye,…sasa nikuchekeshe kitu,....’akasema.‘Nichekeshe…’nikasema‘Kumbe yule docta ni best sana wa shemeji….’akasema‘Shemeji,…una maana huyo bwana’ko…?’ nikauliza‘Na wewe bwana…sio bwanangu huyo..,..mwishowe utazoea hiyo kauli, mimi siipendi…’akasema‘Samahani, naongea hivyo kwa vile tupo wawili wala usiwe na shaka…’nikasema‘Sasa nahisi..au nilihisi huenda waliwahi kuongea kuhus mimi, kuwa nina mimba, nahisi hivyo kwa vile siku nilipokwenda kupima,..jana yake, au siku baada yake, nakumbuka,  mjamaa aliniuliza…. , japokuwa hakuwahi kuniambia kuwa kagundua kuwa nina mimba..na nijuavyo aligundua hilo baada ya siku hiyo wakati alipokuja, na kuanza kuongea hayo kuwa anataka nimzalie mtoto…’akasema‘Mhh, ...mambo ya huyo shemeji  hayo….yanafanana sana na mambo ya mume wangu, , unajua hata wakati naandika, nikawa najiuliza huyo mtu  ni nani,  sura ya mtoto inafanana na familia yangu, ina maana huyo baba yao, eeh, atakuwa anafanana na mume wangu, …na na…hili tena,….unajua mume wangu ni rafiki mkubwa wa huyo docta wa pale…walisoma wote…’nikasema.‘Ndio hivyo….mmh, sasa…mmh, unajua  yote haya ni kutokana na ushauri wako, nisingelifikia hatua hiyo, wakati mwingine nafikia kujilaumu ni kwanini nilikusikiliza, ….usinielewe vibaya hapo kuwa sikuupenda huo ushauri wako.., ila nasema haya kwa vile naona kila hatua kuna mtihani fulani na naona inaweza ikafikia sehemu…hata sijui itakuwaje……’ akasema‘Ni wasi wasi wako tu….unafikiri, unajua hayo yote nayafahamu na …kukushauri kwangu sikuwa na nia mbaya, nilijua haya yanaweza kutokea hivyo..na mimi nitayapokea kwa jinsi yalivyo, siwezi kukulaumu kwa lolote lile, unasikia,.., kwahiyo, wala usiwe na shaka kabisa…’nikasema‘Kwahiyo unataka kusema nini hapo.., kuwa unajua ni nani, na huna shaka lolote kwa hilo…yaani hutanifikiria vibaya , tukaja kukosana…?’ akaniuliza‘Hebu nikushauri kitu,  hebu kwanza nihakikishie kwa huyo shemeji ni nani , ili niweze kupanga jinsi gani ya kumweka sawa, mimi nataka nije kuonana naye, ili niliweke hili jambo sawa, sawa..’nikasema‘Mhh..kumbe bado…’akasema‘Ni hivi…ninachoogopa ni wewe unaweza ukavuruga huu mpango kabisa…, wewe unachukulia hili jambo kirahisi tu, hujui ni jinsi kwenye mwenye mume atakavyojisikia akiligundua hilo, unataka mim nije kujuta kwanini nilikushauri, sitaki itokee hivyo kamwe, unasikia,...sasa nataka uniambie ukweli huyo shemeji ni nani?’ nikamuuliza.‘Na wewe bwana , hapa nilijua unasema umeshamfahamu, na ulijua kitu kama hicho kinaweza kutokea,…ulikuwa na maana gani,..mimi naona haya tuyaache tu, yasije kukutia presha?’ akasema‘Mimi nishakuambia ..kwa hisia zangu ni huyo mdogo wake mume wangu, kwasababu nyingi tu, kuanzia kufanana watoto na tukio zima kama ulivyoliezea, na , naaeeh…sioni mtu mwingine anayefanana na hivyo,… labda uniambie wewe, ni nani huyo, na kwanini…eeh,  unaona ugumu kunihakikishia kuwa ni yeye, …mimi siwezi kufanya lolote, maana hanihusu kwa sana, japokuwa ni mume wa mtu,…hawa wanaume jaman…’nikasema.‘Lakini…mbona umesahau kuwa ulinishauri hivyo, ukisema hawa waume jamani, unanishutumu na mimi au…’akasema‘Ndio hivyo, ila …ukweli upo pale-pale, inauma sana, tena, sana, sijui ikitokea kwangu kama nitaweza kuvumilia, mimi aah, ..mimi siwezi,…ndio maana nilitaka nimfahmu huyo mtu ili madhara yasizidi kuendelea, umenielewa hapo…nataka niongee naye,nitajua jinsi gani ya kumweka sawa,…haya niambie ni nani huyo mtu….?’ nikamuuliza‘Ni shemeji jamani…nimeshakuambia ni shemeji’akasema, na kusimama, kama anataka kuondoka,…sijui kwenda wapi,  akageuka kuniangalia na mimi nikawa nimemuangalia, tukawa tunatizamana…Kiukweli  mpaka hapo bado mimi sikuwa na tashwishwi yoyote mbaya, maana kwa hilo neno ‘shemeji’ ndivyo alivyo kuwa akimuita huyo jamaa yake tangia awali, na nikajua anamuita hivyo kutokana na mimi, kuwa ni mdogo wa mume wangu…lakini bado naona kama anaogopa kunibainishia hilo, na kwa namna hiyo akazidi kunipa hamasa.‘Hahahah, nilijua tu, kwahiyo sasa umenihakikishia, kuwa ndio yeye, au sio….marafiki wawili wana waume kutoka familia moja, japokuwa…wewe unapita tu, hahaha…kiukweli, nimefurahi, japokuwa,…mmh, namuonea huruma sana mke wake….’nikasema na mara ujumbe wa simu ukaingia kwenye simu yake, akausoma, na mara kwa haraka akasimama, akiangalia kule mlangoni, sikusikia sauto ya gari…kwahiyo sikuwa na mashaka kuwa kuna mtu kaja…‘Unajua, …kuna mgeni anataka kuja, na sikutaka akukute hapa, wewe au mtu mwingine, na huyu mtu kawahi kabla ya muda,ujuo wako sikuwa na …..sasa sijui kwanini, mbona hivi…’akasema akijaribu kupigia simu, nahisi kwa huyo mtu,  lakini naona simu ilikuwa haipokelewi..‘Kwani una nini, mbona huna amani , ni nani huyo mtu…?’ nikamuuliza‘Hata sijui itakuwaje…na nilishamuambia asije hapa mpaka nimpe nafasi, au aniambie kabla, sasa anajileta tu, mbona huu mtihani.’akasema sasa akiangalia mlangoni‘Kwanini, mimi si rafiki yako…na huyo shemeji,…niambie ukweli..’nikasema‘Ndio yeye….’akasema‘Safi kabisa, …hilo sasa niachie mimi, wala usiwe na shaka,…na kwa vile mume wangu hajui kuwa nipo hapa, ..nitamtumia ujumbe kuwa nimepitia mahali, sitamwambia kuwa nipo hapa, nataka hili jambo tulimalize leo hii, au sio…’nikasema‘Ina maana mume wako, hajui kuwa upo hapa, umekuja huku bila kumuambia, kwanini lakini,  …?’ akaniuliza kama ana hamaki‘Nilikuwa na kikao na muwekezaji mmoja, na bahati kikao hakikufanyika kwahiyo yeye anafahamu nipo kazini..mimi kwa hasira…maana huyo muwekezaji kanipotezea muda wangu maandalizi, halafu analeta ujumbe mwishoni kuwa kaahirisha kuja..ameniboa kwa kweli,…’nikasema‘Mhh….’akasema akiangalia simu yake naona alitarajia kupata majibu fulani lakini hayaji.‘Sasa sijamfahamisha mume wangu kuwa nimetoka, ngoja…nimtumie ujumbe…’akasema akiandika ujumbe kwenye simu…akatuma na kusema‘Leo simu ya mume wangu haipo hewani, kulikoni…’nikasema‘Labda kwa vile…’akasema na kusita….kwani mlango uligongwa‘Huenda ni shemeji,...mungu wangu…’akasemaNikiwa natabasamu tele mdomoni macho yangu yakaelekea kule mlangoni, nimuone huyo shemeji, akilini kwangu najua ni huyo huyo, mdogo wa mume wangu….shemejiiiii…Nikamtupia jicho la pembeni rafiki yangu  nikamuona akiwa anahangaika hana amani kabisa, sikuelewa ni kwanini, labda ni kwa vile hakutaka nikutane na huyo shemeji, lakini kwa muda huo sikujali, nilijua nitalimaliza nikikutana na huyo mtu, sasa nilimuona kama anataka kwenda kule mlangoni,...huku mkono mmoja kashikilia mdomoni…!!!WAZO LA LEO: Tunapopeana ushauru, au tunapotoa ushauri tuhakikishe hicho tunachokifanya tuna uhakika nacho, kiimani ya kweli(kwenye dini zetu), au kiutarataibu uliokubalika na jamii zetu,  ili matokeo yake yasije kutuathiri sisi wenyewe au kuonekana watu wa ajabu katika jamii zetu. Lakini muhimu tuangalie je mola analiridhia hilo, je ningelifanyiwa mimi ningerizika nalo… Mlango wa geti la nje uligongwa ndio,…!Sio mlango wa nyumba yenyewe, maana hiyo nyumba imezungukwa na geti, , nina uhakika ni geti hili la nyumba anayoishi  rafiki yangu…nikamtupia jicho rafiki yangu huyo,….nikamuona, akitoa macho kuangalia kuelekea kule mlangoni…Ni kweli atakuwa huyo mgeni wa rafiki yangu, maana nilisikia sauti ya mlango wa geti ukilia,…geti linafunguliwa, sasa kuashiria kuwa huyo mtu kaamua kulifungua hilo geti yeye mwenyewe hapo ina maana gani, kuw huyo mtu kazoea kufika hapo, anapajua vyema.Hapo ikawa kama kamchokoza rafiki yangu huyo,  nahisi rafiki yangu hakutaka kabisa huyo shemeji tuonane naye mimi, kwa jinsi nilivyomuona akihangaika, na kwa jinsi alivyobadilika sura, usoni alionekana kutahayari…, mpaka nikamuonea huruma,…lakini nikawa sijali, kwanini …mimi sina nia mbaya, hanielewi tu…‘Kwanini unapata shida hivyo, mkaribishe mgeni…’nikasema lakini rafiki yangu alibakia akiwa kashika kichwa, akiniangalia kwa macho yenye huruma, au…kama anataka kulia…‘Hapana, sio leo jamani..sijajiandaa kwa hili, nahisi imekuwa ni haraka sana, …nahisi hatari…unasikia, rafiki yangu, wewe pitia mlango wa nyuma uondoke, sitaki matatizo hapa nyumbani kwangu, najua kabisa itakuwa hivyo….’akasema akishika kichwa.‘Kwanini…mbona sikuelewi…’nikasema nikimuangalia kwa macho ya kujiuliza na yeye akawa ananikwepa kabisa kuniangalia machoni.‘Tafadhali fanya hivyo….nitakuja kukuambia ni kwanini…lakini kwa hivi sasa ili kuepusha shari..ili , nisivunje uaminifu..unajua aliniomba tena sana nisije kumsema kwa watu, hadi muda muafaka ufike,…na nikifanya hivyo, ..na yeye…unanielewa hapo, haya nenda pitia mlango huo wa nyuma…’akasema‘Mimi siendi mahali, lao nataka hili jambo lifikie mahali na mimi, niwe na amani , nahisi kuna …sijui nisemeje, unanifanya nianza , kama nilivyokuambia nitunge kitabu, sasa ni kwanini, maana matendo yako, kauli, zako zinanihamasisha nifenye hivyo, kifupi nahisi kuna kitu unaficha, ambacho ni zaidi ya hilo tulilokubaliana, sasa ningeliomba umkaribishe huyo mgeni, najua tutayamaliza,….’nikasema‘Hapana, nielewe nina maana yangu kubwa sana, najua itafika muda hili itabidi liwe hivyo, lakini sio kwa leo, sio kwasasa…nakuomba mimi ni rafiki yako, niamini ninalokuambia…yanayotokea, na kauli zako…hapana, na iwe hivyo tu..ila nitakuja kukuelezea kila kitu..unajua, nitaumia sana ikifikia mahali pabaya….’akasema na mimi nikataka kusimama‘Unataka kufanya nini sasa ?’ akaniulizaMimi nikamtizama kwa macho ya kujiuliza, akilini nilishadhamiria kitu, lakini sina uhakika nacho, na alipoona kweli nataka kuchukua hatua akasema‘Rafiki yangu, ndugu yangu sivyo kama unavyofikiria wewe, tulia kwanza unataka kwenda wapi…nielewe maana hata mimi nilivyokuwa nikitegemea, imekuwa sivyo kabisa, nahisi nahitajia muda zaidi wa kulitafakari hili nisije kuleta hatari…..!’ akasema akiwa kasimama mbele yangu kama kutaka kunizuiaMimi pale nilishikwa na butwaa, sikumuelewa kabia, ni kwanini anafanya hivyo,..nikabakia kumuangalia, uso ukiwa na maulizo mengi, kujiuliza kwingi,  ..baadae nikasema‘Mhh..hatari…hatari gani….mbona  unanichanganya, au hatupo sawa tena,nieleze rafiki yangu kama kuna kitu kibaya kimetendeka nielewe mapema, hivi unanitesa kabisa, wewe hujui tu,…hapana mimi bado nakuamini, mimi bado nipo na wewe, usiwe na wasiwasi bwana…achana na mafikira potofu,…nikuambie ukweli, mimi nina hamu sana ya kumuona huyo shemeji yangu..’nikasema‘Utamuona…kwanza ushamuona sana..ila kwa sasa naomba nipo chini ya miguu yako tafadhali…’akasema akiashiria kutaka kupiga magoti.‘Unajua sijakuelewa, kwanini..…kila siku ni …shemeji, shemeji, nataka nimuone huyo shemeji, hata kama yupoje, labda unahisi hadhi yake haiendani na wewe labda, kama kweli sio huyo ninayefikiria mimi,… labda umekuja kutembea na mtu, asiyekustahili labda hivyo..mim hilo sijali kabisa , ilimradi kakupa kile ulichokitaka na mimi ndiye msiri wako…’nikasema‘Hapana, sio hivyo…ninasababu nyingine kabisa, ya nia njema, …nielewe hivyo tu…’akasema‘Mhh..mimi hapo sitakuelewa kabisa.., leo…eeh, hakuna jinsi, lazima nimuone huyo mtu, kama kaja yupo huko nje, mwambia aingie ndani, tuyamaliza hapa hapa…’nikasema na yeye akabakia kimia‘Sasa unaogopa nini, mtu yupo huko nje, anasubiria, unajua naanza kuingiwa na wasiwasi, kitu ambacho sikuwa nacho dhidi yako, na hizi eeh…kauli zako zinanipa mashaka, ..kwanza najiuliza kuna hatari gani, kuwa itakuwaje, kuwa nitatoa hii siri nikimfahamu au..hahaha, mimi nimeshamfahamu, muite tuyamalize leo hii, ili na mimi niwe na amani..’ nikasema‘Siwezi kufanya hivyo, for the sake of our friendship….kwa minajili kwa kuwa hata yeye mwenyewe hataki, na kama angelijua nipo na mtu asingelifika kabisa,…alishaniomba na akafikia kunitisha, kuwa ni..iwe siri yetu,…’akasema‘Kukutisha kwa vipi….?’ Nikamuuliza‘Bwana wewe liache kama lilivyo… na sijui kwanini unang’ang’ania hivyo, wakati hata wewe mwenyewe  ulitaka iwe hivyo…hapana, acha tu, iwe hivyo hivyo.., nakuhakikishia muda utafika kila kitu kitakuwa bayana, ikibidi….’akasema na mimi nikatikisa kichwa kukataa.Hapo akageuka kuangali mlangoni, …uzuri mlango ulifungwa..kuna namna ukifunga mtu wa nje hawezi kufungua, mpaka mtu wa ndani labda uwe na ufungua…sasa sikujua kama aliuegesha tu,…Nikawa naangalia kule mlangoni nikitamani huyo jamaa aingie, lakini nahisi alikuwa kasimama, anasubiria mwenye atoke, au kahisi kuna …na mara nikasikia sauti ya viatu vya mtu kukaribia mlangoni …ka-ka-ka-ka..huyo mtu kavaa viatu vinavyotoa sauti,Nakumbuka kuwa hata leo mume wangu wakati anaondoka kwenda kazini alikuwa kavaa viatu vinavyotoa sauti ukitembea, nikamwambia hivyo viatu vinavyotoa sauti sio vya kisasa, abadilishe, lakini hakutaka, siku ya leo alisema alivitamani kuvivaa viatu vyake maana vinamkumbusha mbali.‘Bebii…upoooh…’nikasikia sauti ikasema kutoka nje…..‘Bebii…..’nikajikuta nikisema hivyo, akili ikanipeleka mbali kabisa, hivyo ndivyo mume wangu alizoea kuniita, kipindi hicho, mambo hayajawa mambo, na sikumbuki tena kuniita hivyo,…na, mbona hata sauti ni kama …hapana…mmh,Unajua nilihis moyo ukinienda mbio nikishindana na nafsi yangu, sikupenda kamwe nafsi inishinde, ..lakini hata hivyo, hata huyo mdogo wa mume wangu ana sauti kama hiyo, isipokuwa ya kwake inakwaruza-kwaruza hivi, hiyo imetoka sawa sawa naya mume wangu. Na hata kufikiria hivyo, sio kwamba nilihisi kuwa ni mume wangu yupo huko nje, hapana siwezi kudanganya, akili yangu ilinizidi kunipa tashwishwi ya kumuona huyo mtu anayefanana mambo mengi na mume wangu.‘Mume wangu yupo ofisini sio…’nikajikuta nasema hivyo kwa sauti ndogo.Rafiki yangu akanitupia jicho aliposikia nikiweweseka hayo maneno, na ni kweli..nilikuwa na uhakika kuwa mume wangu yupo ofisini kwao, ana kikao muhimu sana, asingeliweza kuja huku,…ndio maana alizima hata simu yake kuchelea kusumbuliwa.Sasa kwanini moyo wangu ukashtuka hivyo, niliposikia sauti hiyo, inayofanana nay a mume wangu, na kwanini kauli hiyo neno hilo, liwe sawa sawa na neno alilopenda kulitumia mume wangu enzi mapenzi yamepamba moto....hapo nikagwaya...Lakini atakuwa ni shemeji tu huyo….**************‘Kumbuka ahadi yetu, kumbuka kuwa wewe ndio uliyenishauri hivyo, na naomba iwe hivyo ...nataka tukubaliane, ili lisije kuleta shida baadaye…’. Nikiwa nasubiria rafiki yangu amkaribishe mgeni wake, nikahisi maneno hayo yakijirudia rudia kichwani mwangu kama onyo…na mara mtoto akaanza kulia,…na muda huo rafiki yangu yupo mlangoni, anataka kufungua mlango,Mtoto alipolia akageuka kumuangalia, na akaniona mimi nasimama kwenda kumuhudumia, akawa na amani akashikilia kitasa kunyonga mlango ufunguke Mimi mtoto alipolia kwa haraka nikasimama na kuelekea pale alipolazwa huyo mtoto, alikuwa kwenye kitanda chake chandarua , nikamkagua na nikaona kakojoa, kwa haraka nikaanza kumbadilisha, na kuwa muda huo akili ikawa kwa mtoto sikuwa na muda tena wa kuangalia kule mlangoni, ila nilisikia sauti kwa mbali ikisema;‘Upo peke yako, …sijakuelewa, nauliza upo peke yako…mbona hunikaribishi ndani..?’ sauti hiyo niliisikia kwa kuunga unga, sikuweza kubahatisha vyema, maana kulikuwa na kelele za tv,na kulikuwa na kitu kama upepo nje, ulikuwa unapita, sikuweza kusema hiyo sauti inafanana nanni, sio ..kama ile ya awali alipotamka neno bebii, …na mara kukawa kimia.Mtoto akawa kalala , basi mimi nikasimama sasa, sasa namuangalia rafiki yangu, sisikii wanachoongea kama wanaongea itakuwa ni sauti ya chini sana,…hapo nikatamani nisikie wanachoongea, nikatembea taratibu kuelekea huko mlangoniNikasogea taratibu, hadi nikakaribia mlango, na nilipofika , kwanza nilikuwa na nia ya kuwaingilia, na kumkaribisha huyo mgeni, lakini nilipofika hapo nafsi ikataka kusikia wanachokiongea,..na kwa muda huo rafiki yangu alikuwa kazama kwenye mazungumzo na huyo mtu, na nilichoweza kusikia kwa muda ni haya maneno, yalikuwa ya kuwewesa zaidi kiasi kwamba huwezi kuyasikia vyema, alisema ;‘Kama upo peke yako unaogopa nini…’ni sautiya chini sana….kiasi kwamba sikusikia alichoongea zaidi‘Wewe nenda, siku ya leo sio nzuri, muhimu unielewe, …ondoka haraka sana,..mimi hapa nipo peke yangu, lakini muda wowote anaweza kufika mtu, nielewe hivyo, kwaheri…oh..’akasema rafiki yangu na kutaka kuufunga mlango, na sasa akageuka, na kunikuta nipo nyuma yake, alishtuka, ..na kunitolea macho yenye dalili ya uwoga fulani hivi‘Oh, ulikuwa unani…sikiliza…?’ akauliza kwa mashaka‘Vipi, mbona haingii…’nikasema, na akiniashiria nikae kimia, kwa vidole, akisema,Sshiii…huku akitikisa kichwa, na mkono mmoja bado umeshikilia mlango ina maana hataki huyo mtu huko nje ajue kuwa kuna mtu ndani…lakini mimi nikajifanya sijamsikia, nikasogea karibu sasa nikitaka kufungua huo mlango.‘Haya baadae nitakuja,…’sauti huko nje ikasema, hiyo sauti nikaisikia, sauti hiyo iliyonifanya nishtuke kidogo, lakini sio saana, maana haiwezi ikanihakikishia nilichokifikiria kwa muda, nikajikuta nikisema;‘Mhh..ni nani huyo anaongea sauti kama ya mume wangu..?’ nikauliza‘Ni shemeji…’akasema rafiki yangu akionekana kuwa na wasiwasi, na sasa akawa kasimama kati kati ya mlango kunizuia nisiweze kufungua mlango na kutoka nje.., huku akiniangalia machoni kwa yale macho ya mtu aliyetoka usingizini, au alikuwa analia, …au mashaka…hivyo! Mimi nilimuangalia kwa mashaka, ...na sasa kitu kama hasira zilianza kujijenga, ni kwanini rafiki yangu mwenyewe ana nifanyia hivyo, kwa vyovyote iwavyo rafiki yangu hataki nimuone huyo mtu, ni kwanini… na inawezekana ikawa sio huyo shemeji…, na kama sio shemeji atakuwa ni nani..au anaweza akawa ndio yeye, lakini hataki tuonane naye uso kwa uso..ni kwanini…, labda kutokana na jinsi walivyoelewana. Hata hivyo, ..Kwanza nilitaka nirudi, niyaache kama yalivyo, lakini nafsi ikasema, kwanini ..kwanini niyaache , hapana, ni lazima nihakikishe huyo ndiye kama ninavyofikiria, na kwanini nisimuone, ni  kwanini nisimuone tukaongea naye, haya mambo niyaweke sawa yaishe tu, nina imani nikionana naye nikaongea naye, yataisha tu..nataka nimuone huyo, she-she…shemeji….Hapo sikuwa na simile, nikasogea na kuubandua mkono wa rafiki yangu pale mlangoni, na kumpiga kikumbi cha kumsukumiza pembeni…, ili asogee, na hakulitazamii hilo, akapepesuka na kutaka kudonoka chini, mimi hilo sikujali, nikavuta mlango, ukafunguka…Nje…hakuna mtu…lakini hisia zinanifanya nihisi kuna mtu, ila simuoni..yupo wapi..!nikageuka huku na huku , sioni mtu…‘Mhh…haya..’nikasema hivyo tu**********‘Mbona hivi rafiki yangu, imekuwa ugomvi…’akasema sasa yeye akiwa kasimama mlangoni, akinitizama kwa mashaka,..Muda huo ndio naangaza huku na kule kumtafuta huyo mtu kwa macho lakini huyo mtu haonekani,…haiwezekani huyo mtu ayeyuke hivi hivi, haiwezekani kwa muda huo mfupi awe keshafika getini na kutoka nje,..hapo nikataka kuhakikisha, nikatembea hatua chache kuelekea getini, lakini sikuona mtu.‘Amekwenda wapi huyo mtu uliyekuwa ukiongea naye…?’ nikauliza‘Nani, …keshaondoka bwana…?’ akaniuliza  na kusema hivyo, sasa akionyesha uso wa kunishangaa mimi. Nikamtizamaa weeh, na kutikisa kichwa.‘Hahaha, haiwezekani, …huyo mtu anapaa au….yupo wapi huyo shemeji….nataka nionane  naye…kakimbije haraka hivyo na kutoka nje, haiwezekani, yupo wapi…’nikasema na nikaona kama uso wa rafiki yangu ukinawiri, ni kama vile alitarajia nitaongea kitu kingine kibaya, lakini akakuta nimeongea kitu ambacho hakikumkwaza, akasema;‘Utamuona tu ndugu yangu..subira huvuta heri, njoo ndani tuongee , tumalizane, maana leo sina amani, natamani niondoke leo hii hii nikakae huko Zanzibar, mpaka siku yangu ya kuondoka kusoma ifike.., lakini haiwezekani, mambo ya visa bado hayajakamlika…lakini sikufukuzi, njoo ndani tafadhali…’akasema‘Kweli ni bora niondoke zangu, huna maana wewe kabisa…yaani leo, sijui hasira zangu zimekwenda wapi..haya bwana fanya utakavyo, naona …aah, sijui kwanini,…mimi ninavyokujali na kukupenda malipo yake ndio haya, baya bwana…lakini…hiyo lakini iweke moyoni, ipo siku nitaimalizia,..’nikasema sasa nikitaka kuondokaNikakakumbuka kuwa nimeacha mkoba wangu ndani,…uone mambo ya mweneyzimunu yalivyo,..nikarudi ndani kwa haraka, muda huo nishakasirika nataka niondoke tu hapo.Mimi kwa haraka nikarudi kuelekea ndani, ila haraka, uso umeshakasirika, hata nampita rafiki yangu anaonekana kuogopa labda nitafanya kitu..yeye kasimama kwa tahadhari,, akionekana hana amani…mimi sikutaka hata kumuangalia machoni. Nilipofika ndani, mtoto alikuwa kaamuka, nikamuona anavyochezesha-chezesha vimkono vyake pale alipolazwa, nikavutika kumuangalia…unajua tena ukiwa na hulka ya kupenda watoto…, keshaamuka  macho yake yamefunguka, ananitizama, kama vile ananiona na hapo hapo taswira za watoto wangu wakiwa wadogo zikanijia akilini.Kila ninapomuangalia huyu mtoto , nawaza mengine ambayo siyataki, nahisi kama ni mtoto wangu, nahisi..kufanana…na… lakini hainijii akilini, na naishia kuhitimsha kuwa baba wa huyu mtoto atakuwa mdogo wa mume wangu…hivyo tu na kujiaminisha kwa msimamo wangu huo. Mungu mwenyewe ndiye anajua..Nilisimama pale kwa dakiki kadhaa nikimkagua huyo mtoto kwa macho, kabla sijageuka kuondoka, na mara huko nje nikasikia sauti ya viatu kama mtu anakimbia, tatatatata…sauti ya viatu…ni sauti ile ile…atakuwa ni huyo jamaa kumbe alikuwa hajaondoka, atakuwa alijificha sehemu kwanini sikuwa makini kukagua upande wa nyuma wa hiyo nyumba,Hapo, hapo…nikamuangalia rafiki yangu kwa macho yaliyojaa hasira, na kwa haraka nikawa nimeshauweka mkoba wangu mkononi, na sasa najiandaa kuelekea mlangoni, ili niweze kumuwahi huyo mtu, na rafiki yangu alikuwa hajaondoka pale mlangoni, malngo upo nusu wazi, lakini kaushikilia, na aliponiona akajua nataka kufany anini, akaufunga mlango na kuendelea kuushikilia…, kasimama kati kati ya mlango.Nikamsogelea nikiwa na haraka nataka kutoka lakini safari hii alikuwa kajizatiti, akawa hasogei, hata baada ya kumsukuma anipishe nipite..na huko nje nilisikia mlango wa geti ukifunguliwa na najua atakuwa keshaondoka, kiukweli kitendo hicho  kilinikwanza kweli……sasa ikawa kama shari, tunasukumana, na bado hataki mimi nitoke…baadae nikafanikiwa nikamtoa pale mlangoni, nikafungua mlango na kutoka nje,…nilishachelewa.‘Kwanini unanifanyia hivi lakini, kwanini, ..?’ nikamuuliza sasa akiwa kasimama pale mlango akiniangalia tu kwa mashaka..baadae akasema‘Ni bora nusu shari kuliko shari kamili, ni bora tu, iwe hivi, ili nisije kuharibu…najua utakuja kunielewa baadae, ..samahani sana rafiki yangu, nakuomba unielewe hivyo, sina nia mbaya kabisa, natimiza masharti yetu tuliyowekeana, na ahadi niliyoweka na huyo mtu, haitapendeza kabisa, nikifanya kinyume chake, nielewe hivyo tu, samahani sana rafiki yangu…’akasema‘Kwahiyo kumbe ni kweli…eeh,’nikasema huku nikitikisa kichwa changu‘Kweli kuhusu nini..nimeshakuambia huyo ni shemeji, hutaki kunielewa,sasa bora iwe hivyo hivyo tu…., na ukweli ndio huo, nimetimiza kile tulichokipanga, ni wewe sasa unayetaka kuharibu, sijui kwanini unataka kujisaliti mwenyewe…’akasema‘Shemeji ..shemeji,…, hata mimi ninao wengi tu… haya kaaga na huyo shemeji yako na sitaki tena kumuona, ila ole wako, litokee tatizo, unasikia, ole wako…si unanifahamu nilivyo, na usifikiri nimekata tamaa, …nitamfahamu tu, huwa sishindwi jambo  …haya kwaheri…’nikasema na kuanza kuondoka..Nikageuka nyuma, nikamkuta rafiki yangu kasimama mlangoni mwa nyumba anapoishi,..bado ananiangalia kwa mashaka, ..mimi nikatikisa kichwa kama mtu anayesikitika, sikusema kitu zaidi…nikaanza kutembea kuelekea kwenye geti na hapo simu yangu ikaita.Nilipoangalia mpigaji, nikagundua ni namba ya docta , huyu ni jirani yangu, sikutaka kuipokea kwa muda ule.., sijui kwanini. Docta ni mtu ninayejuana naye sana, na mara nyingi hunipigia simu tunaongea naye sana, huyo kwa viwango naweza kumweka kwenye nafasi ya marafiki zangu ninaoaminiana naye sana.Kwa muda ule sikutaka kuipokea simu yake maana mara nyingi akinipigia tunaishia kuongea mengi sana yaliyopita, kutaniana…kwahiyo nikadharau, kwa vile akili yangu haikuwa sawa, nikakata simuBaadae alipopiga tena, nikajua kuna jambo, nikapokea‘Upo wapi zilipendwa…’ akasema kiutani, najuana naye kiukweli‘Acha utani wako, nipo kwenye …jambo muhimu, tutaongea baadae, naelekea nyumbani…’nikasema, yeye akasema niende kwake.‘Nije kwako kuna nini…?’ nikauliza kwa mshangao.‘Pitia hapa ni muhimu tuonane…kama unaelekea nyumbani…’akasema‘Sawa…’nikasema , lakini sikuwa na shauku , na moyoni nilipanga nisipitie kabisa, namfahamu , tumezoeana kihivyo …nitakuelezea baadae ni kwanini nimezoeana naye hivyoNilielekea pale nilipoweka gari langu na kumlipa huyo kijana ambaye ninamuamini sana, nikaingia kwenye gari, na wakati nataka kuondoka, yule kijana akasema‘Shemeji naye alileta gari lake, nilisafishe … , lakini hakusubiria nimalizie kusafisha, anaonekana ana haraka sana, ameondoa gari kwa haraka sana, sio kawaida yake….’akasema‘Shemeji gani…?’ nikamuuliza na mara honi ikapigwa nyuma ya gari langu, kulikuwa na gari lilikuwa linataka kuingia, basi,…sikuweza kuongea na huyo kijana, ikabidi nisogeze gari langu mbele kwanza, na nilipomaliza, nikafungua kiyoo cha gari, kutizama nje, kumtafuta huyo kijana, nikamuoana anaongea nawateja wake, nikaona isiwe taabu…nikapandisha kiyoo changu kuanza kutoka nje ya eneo lile.Nikabakia kwenye kitendawili,..ni nani shemeji, ..ni kwanini rafiki yangu ananificha, kuna nini hapa….akili ilikuwa bado imefungwa kabisa….huwezi amini, ilikuwa hivyo…Wakati nakaribia nyumbani, nikaona nipitie supermarket, ninunue vitu fulani,…lakini nilihisi moyo wangu ukiwa hauna amani, sijui kwanini,..hata hivyo nikasema labda ni hayo mawazo, ya rafiki yangu…nikasimamisha gari…,lakini akili ikawa haitulii…‘Huyu kijana kasemaje, ‘shemeji naye alileta gari..’ naye shemeji, rafiki yangu shemeji..shemeji, shemeji….si alisema shemeji, au sikumsikia vyema, huyu shemeji atkuwa ni nani, ni mume wangu, hapana, mume wangu yupo kazini,…ana kikao muhimu sana, hawezi kutoka, aliniambia, hatatoka kazini mapema..Nikataka kumpigia simu mume wangu, ili nihakikishe,…lakini nikaona nitamsumbua tu, sasa hivi atakuwa kati kati ya mikutano yake…nikaachana na wazo hilo, nikaingie hapo, sokoni-duka, na kununua vitu nilivyovitaka.‘Oh, nimekumbuka , huyo atakuwa ni shemeji… mdogo wa mume wangu ..’nikasema kwa suti, niliwazia hivyo kwasababu huyo kijana kipindi fulani nilifika akawa analisafisha gari langu na mara mdogo wa mume wangu akafika, na aliponiona akasema‘Shemeji kumbe umeniwahi, basi ngoja amalize, na mimi nitafutia, vipi shemeji hatuonani…’akasema na tukawa tunaongea, na huyo kijana alipomaliz kusafisha, akafika na kusema‘Shemji zamu yako…’alipotamka hivyo sisi tukacheka,…basi akawa kila akionana na huyo shemeji yangu anamuita hivyo shemeji…sasa sijui kuwa alikuwa na maana ya huyo shemeji au la…mmh, shemeji, shemeji..hapa kuna kitu, kimejificha, nah ii itakuwa ufungua wa kuupata ukweli.Sikuwa na tabia ya kumdhania mtu vibaya,… hasa mume wangu, au huyo rafiki yangu, niliwaamini sana, kutokana na jinsi tulivyoishi,…mume wangu ni mwaminifu sana, na namuamini kwa hilo,sikuwa na shaka naye hata kidogo, licha ya tabia hiyo ya kulewa, ambayo ilianza baadae tu…hata sijui ni kwanini,  lakini binadamu bwana….Kiukweli hadi hapo sikutaka kuingia na dhana mbaya dhidi ya mume wangu, wala rafiki yangu…ndivyo nilivyokuwa, utaniona ni mtu ajabu lakini , sijui nisemeje, na ilinisaidia sana kuwa na tabia hiyo kipindi , hadi lilipotokea hili tukio.Mimi mwenyewe ili kulimaliza hilo akilini, ili nisije kuingiwa na shetani mbaya wa dhana chafu,  nikahitimisha kichwani kwangu kuwa, huyo aliyefika pale nyumbani kwa rafiki yangu atakuwa ni mdogo wa mume wangu, na kwa kujiridhisha tu, nitarudi kwa huyo kijana tena kumuulizia vyema au nitakwenda kwa shemeji, yaani mdogo wa mume wangu. Hilo nikalimaliza hivyo kichwani. Lakini bado nikasema;‘Huyu rafiki yangu kuna kitu ananificha..na hicho kitu ni zaidi ya tulivyokubaliana, na nafsi yangu haitatulia mpaka nikigundue, nitakigundua tu,..’ Wakati huo naendesha gari kulekea nyumbani….mara simu yangu ikaita, na kuangalia nikakuta ni mmoja wa wateja wangu , nikaipokea simu, muda huo ndio nataka kuingia kwenye gari,‘Unasemaje,…nini, ajali, …wewe una….hapana, sijasikia,…ndio naelekea huko, wapi lakini…’ nikahisi kitu kama kikigonga kichwani, kizungu zungu,…sikujitambua, baadae nafungua macho najikuta nipo nimelala chini, watu wamenizunguka.‘Ajali….!!!’ Nikajikuta nimesema hivyo, kwa haraka nikainuka kutaka kuingia kwenye gari langu.WAZO LA LEO: Ni kweli tunahitajia kitu, ni kweli tunataka kupata lakini je ni sahihi kupitia njia ambayo sio sahihi, kwa vile tu, muda umekwenda, kwa vile upo kwenye shida, kwa vile tu…je unauhakika utakipata na kuishi muda wa kukifaidi hicho kitu…..tuwe makini na mambo tunayotenda huku tukiangalia uwepo wetu hapa . Tumuombe mungu atupe hekima ya kutafakari mambo kabla ya kuyafanya Aamin.‘Ajali….’ Ilikuwa kauli yangu ya awali pale nilipozindukana, sijui kwanini hali hiyo ilinitokea,..kupoteza fahamu,…mmh.. nilijiuliza pale bila kujua sababu ni nini,.. labda ni kuchoka tu, mambo yamekuwa mengi kupitiliza…, niliinua uso na kuwaangalia watu , maana walishafika kuangalia kuna tatizo gani, …haikuchukua muda mrafu hiyo hali.Bahati nzuri, nahisi ni dakitari, alikuja kutokea hapo kwenye hilo jengo la soko-duka, alikuwa kavalia nguo za kidakitari, hilo jengo ni kubwa lina ofisi nyingi na mojawapo ni dispensary. Na kuwa huo  alikuwa kachuchumaa karibu yangu, na akawa ananiangalia tu, huenda alishanichunguza nikiwa nimepoteza fahamuMimi kwa haraka nikajaribu kusimama,…nikajikuta narudi chini,.. nilihisi kizungu zungu kidogo, huyo docta akanishika mkono, kunisaidia, nikaa vyema, nikawa najifunika vizuri, kushusha gauni vyema….‘Upo ok.., unajisikiaje sasa..?’ akaniuliza na mimi nikawa kimia, nikitafakari, kuvuta fikra.‘I hope so, nipo ok…’nikasema‘Mhh, unahitajika kutulia kwanza, naona hali yako bado haijawa sawa, unahitajika mapumziko kidogo, sijaona tatizo lolote kubwa kwako, lakini ni vyema, ukafika hospitali kwa uchunguzi zaidi, hapo ndani kuna zanahati, nahudumia hapo, kama hutojali unakaribishwa...’akasema huyo docta?’ akaniuliza‘Nipo ok…nahisi hivyo, natumai, hunidai kitu…’nikasema‘Hamna…sijafanya lolote, nilikukagua tu  Je utaweza kuendesha gari mwenyewe…, au tumpigie mume wako simu,au jamaa yako, simu yako hii hapa, tukusaidie kumpigia…?’ akauliza huku akiwa kashikilia simu yangu, nahisi waliichukua wakitafuta namba ya jamaa yangu yoyote.‘Hapana….niko ok..’ Ni alipotaja kuhusu mume wangu, ndio akili ikafunguka, nikakumbuka ile simu niliyopigiwa  na hapo hapo kwa haraka nikaingia kwenye gari…‘Ahsante sana kwa huduma yako,….’nikasema‘Hamna shida, uwe mwangalifu tu, na nazidi kukushauri fika hopsitali, usizarau hilo laweza kuwa chanzo cha tatizo , na huwezi kulijua mpaka ukapimwe…’akasema huyo docta na mimi nikawasha gari na kuanza kuondoka.Niliendesha gari langu kutoka eneo hilo, na muda huo sikuwa na wazo la kuangalia vitu vyangu kama vipo salama,..sikuwa na wazo la kuangalia simu yangu ambayo, alinikabidhi huyo docta niliweka pembeni ya kitu,..kumbe simu yangu …ilikuwa imezima..watu wananipigia wanipati.Nilipokaribia eneo la nyumbani kwangu ndio nikakumbuka kuwa dakitari alisema nipitie kwake,… lakini niliona haina umuhimu kwa muda huo,  kwanza nifike nyumbani kwangu, nijue kinachoendelea,…maana mpigaji simu, nakumbuka  alisema,..‘Kuna ajali, gari la mume wako limepata ajali, lakini hayupo….haonekani…. , tunahisi huenda kaimbilia nyumbani kwake… watu wanamtafuta haonekani sijui wapi alipo….’nilikumbuka hiyo sauti.‘Ajali halafu yupo nyumbani, haonekani wapi alipo…?’ nikajiuliza tu, hata sijui nifanyeje, lakini muhimu nikaona nifike nyumba kwangu kwanza, nianzie hapo.Ndio nikakumbuka simu yangu, nikaichukua na kuiwasha sijui kwanini ilizimika, maana chaji ipo ya kutosha, nia yangu nikujaribu kumpigia mume wangu… lakini ujumbe nyingi zikaanza kuingia, kuashiria kuwa watu wengi walikuwa wakinitafuta, nikapokea simu iliyokuwa inaita kwa muda huo.Alikuwa ni docta jirani yangu…. ‘Upo wapi…’ akaniuliza kwa haraka hivyo‘Nipo , ndio nafika kwangu…’nikasema,‘Ok sasa ni hivi, fika hapa kwangu mara moja ni muhimu sana, mume wako yupo hapa,…’akasema‘Yupo salama lakini…?’ nikauliza‘Ndio…anaendelea vizuri…mengine utayajua ukifika hapa….’akasema.‘Haya…nakuja…’nikasemaNikarudisha gari nyuma, maana sio mbali na kwangu, tunatenganishwa na bara bara na ukuta…‘Umeshafika…’akanipigia tena docta, nilishangaa kwanini kapiga tena kwa haraka, nikaanza kuhisi kuna tatizo kubwa.‘Nimeshafika eneo la getii ya nyumba yako....vipi kuna maendeleo gani…maana huyo mtu aliyenipigia simu, alisema kaona kama gari la mume wangu limepatwa na ajali, …lakini sizani kama ni yeye, kwani ninafahamu yupo kazini, yupoje mume wangu, ni yeye, kaumia, …’nikasema.‘Sawa ingia ndani, tutaongea ukifika, hajambo….’akasema.‘Nataka kujua ni kweli docta, niambie yupoje..?’ nikauliza.‘Mume wako ni kweli kapatwa na ajali..…, na yupo hapa nyumbani kwangu, ...’akasema‘Kwanini hajaenda hospitali, …?’ nikauliza‘Ukifika tutaongea, kama ni kwenda hospitali..au la…wewe ukifika unaweza kusaidia hilo, maana mwenyewe hajataka kwenda hospitalini ...’akasema‘Mhh..haya nakuja…’nikawa najiuliza imekuwaje, nijuavyo mume wangu alikuwa kazini, sasa hiyo ajali ilitokeaje, na wapi…nikawa najiuliza.Basi nikaingia nyumbani kwa docta************‘Oh, shemeji bora umewahi kufika, naona uliendesha kwa mwendo usio wa kawaida, msifanye hivyo....’akasema jirani yetu huyo mmoja, ambaye nahisi aliniona wakati naingia na gari kwa mwendo wa kasi.‘Mumeo ni kama unavyomuona kapatwa na ajali mbaya sana, kwa jinsi nilivyoambiwa na watu, …na ameponea kwenye tundu la sindano,hapa tumempatia huduma ya kwanza , hata hivyo alitakiwa awepo hospitalini kwa hali jinsi ilivyo...cha ajabu mumeo amekataa kata kata tusimpeleke hospitalini,…’akasema‘Kwanini jamani, hili sio swala la kuhitaji yeye kukubali au la, docta, rafiki yako huyo, unambembeleza kwa hilo…?’ nikauliza‘Yeye alisema afikishwe hapa nimpatie huduma ya kwanza, anahisi hana tatizo,..’akasema‘Kwahiyo..?’ nikauliza‘Muhimu afikishwe hospitalini haraka iwezekanavyo,  ...’akasema docta.Mimi sikuelewa, kwanini mtu apatwe na ajali ya gari, watu badala ya kumpeleka hospitali, wanamleta huku nyumbani kwa docta,...labda, au sijui alikuwa na maana gani kutibiwa nyumbani.‘Shemeji kwa hali ilivyo, tunahitajika tumuwahishe hospitalini, hatuwezi kumsikiliza tena yeye, na kwa vile wewe upo, utawezesha hili, tulishapigia simu gari la wagonjwa linakuja,,....’akasema docta.‘Haya, mimi sioni kwanini tusubiria hilo gari la wagonjwa, si tunaweza kumbeba hadi kwenye gari langu,au…?’ nikauliza‘Gari la wagonjwa linakuja na kitanda cha kumlaza, …isije kuleta matatizo mengina lakini kwa vile limechelewa, basi tumbebe tu, awahishwe hospitalini…’Nilimuangalia pale alipolala, shati ni vipande vipande…uso umevimba, na michubuko…‘Sasa hivi kapatwa na usingizi kwa dawa nilizompa…’akasema docta‘Basi abebwe hivyo hivyo, afikishwe hospitalini…’nikasema‘Ni kweli, lakini lazima atazindukana, na ataweza kuhisi maumivu kwa sasa , alikuwa kama kachanganyikiwa alivyoletwa hapa…’akasema‘Kwahiyo aliletwa kumbe…?’ nikauliza‘Kuna mtu alikuwa anamsaidia, alikuja naye, wakati mimi nataka kutoka nje..kiukweli alikuwa akitembea kwa shida sana, na muda huo hajaanza kusikia maumivu bado, nahisi sasa ataanza kuyasikia, nimempa dawa za kutuliza maumivu zitasaidia kidogo…’akasema‘Mhh, ...huyu mtu ana hatari kweli…angelifika hospitalini kwanza, kwa hali hii jamani anakuja kutibiwa nyumbani kama mhalifu…’nikasema,‘Hayo hayana maana kwa sasa, hakuna haja ya kusubiria hilo gari la wagonjwa,  tulionelea kama gari la wagonjwa lingelifika mapema, tungeliweza kumfikisha hospitalini bila kukwazika na foleni, na kuzidi kulete athari mwilini.’akasema docta. Docta akatoa kitanda chake ca kukunja, wakasaidiana kumweka mume wangu kwenye hicho kitanda, sasa alikuwa kilalamika maumivu., wakamtoa nje na kumlaza kwenye kiti cha nyuma cha gari langu, na tukaanza safari ya kuelekea hospitalini.Ndani ya gari pamoja na docta alikuwepo mtu mwingine na jirani mmoja, na hapo ndio nikaanza kusikia jinsi ilivyokuwa, lakini akili haikuwa sawa kusikiliza wanachoongea….‘Nimeambiwa hiyo ajali ni ya aina yake, ukiambiwa kuna mtu katoka hapo huwezi kuamini…’akasema‘Kwahiyo ilikuwaje, uliona ilivyotokea…?’ akaulizwa‘Hapana , mimi nililiona hilo gari, halina thamani tena…’akasemaSikutaka kusikia wanachoongea, kwani wanavyozidi kuongea hivyo, ndio nazidi kuogopa, nilitamani kuwaambia wanyamaze..sijui ilikuwa, wakanyamaza hadi tunafika hopsitalini.Kila nilipokuwa nikimtupia macho mume wangu, wakati sasa anatolewa kwenye gari kuweka kwenye vitanda maalumu vya wagonjwa, ndivyo nilivyoanza kuona kuwa kweli mume wangu yupo kwenye haali mbaya, hali yake ilishaanza kubadilika, alionekana kama anazidiwa, na hapo wasiwasi wangu ukazidi, na hadi anaingizwa  hospitalini,sikuwa na amani, nilimuona kama kapoteza fahamu.. Mwili uliniisha nguvu kabisa, lakini nikajitahidi kutembea hadi sehemu ya kusubiria…nilijiuliza tatizo ni nini hasa, ..maana  docta alisema mume wangu hajaumia sana. Hapo sikuwa na sababu za kuvumilia, nikamuendea docta, muda huo alikuwa akiongea na simu.‘Docta kuna nini tena kwa mume wangu....?’ nikamuuliza, na yeye akaniangalia machoni, na hakusema kitu hapo hapo, lakini baadaye akasema;‘Tutajua baada ya uchunguzi, hivi sasa siwezi kusema lolote, lakini kila kitu kitakuwa sawa....ngoja wakamchunguze na kumpiga x-ray. Na utra sound, tutakuja kufahamu hilo…’akasema, sasa hakusubiria akaelekea huko alipopelekwa mume wangu, chumba cha wagonjwa mahututi.‘Docta…’nikamuita, nilitaka kumuambia asichelewe kunipa taarifa, sijui kama alinielewa, yeye alinionyeshea ishara kuwa nitulie, nisijali kwa mkono,**********Dakitari huyu pamoja ya kuwa ni jirani yetu,pia ni rafiki mkubwa wa mume wangu na alikuwa mpenzi wangu wa awali kabisa ,kabla sijakutana na huyu mume wangu na wazazi wangu walitaka sana niolewe na yeye, lakini mimi nilipingana nao kwani hakuwa ndio chagua langu. Wazazi wangu waliona yeye ndio hadhi yangu, kiuchumi na kielimu.Kuna sababu za msingi, zilinifanya nisioelewe na yeye,  mojawapo ni kuwa mimi nilikuwa nimempenda huyu mume wangu bila kujali hali yake ya kiuchumi. Nilikuwa na sababu zingine tu ambazo hazina umuhimu wa kuzitaja hapa kwa sasa. Tulikuwa nje sasa tukisubiria,..mimi pale sina amani kabisa…na haraka nikataka nipate angalau mtu wa kuongea naye angalau niwe na amani, ndio nikampigia rafiki yangu simu, nikamwelezea kuhusu ajali iliyompata mume wangu..‘Unasema nini kapatwa na ajali saa ngapi…?’ akauliza, kama vile haamini, na mimi nikamuelezea jinsi nilivyosikia.‘Oh, labda…ilitokea muda ule, na kumbe ndio hiyo watu wanaiongelea, kuwa hajapona mtu kwenye hilo gari, ..nahisi sio hiyo maana wanasema hawezi mtu kupona kwa jinsi gari lilivyo…oh, kwanini aliendesha kwa mwendo kasi, kiasi hicho…’akasema‘Hata sijui, maana mimi najua alikuwa kazini, na muda ule ni wa kikao, kwasababu niliongea na mtu mmoja alikuwa kwenye hicho kikao chao, hata mpaka natoka pale kwako, najua yupo kwenye kikao, sasa  …alitoka saa ngapi..hapo sijui…’nikasema‘Oh ..na ile kona ni mbaya…’akasema‘Kona gani…?’ nikamuuliza‘Acha ile kona ya kutoka kwangu , unaipita hadi ile kona ya bara bara inayokwenda kuelelea kwenu…ndio nimesikia hiyo ajali imetokea hapo, lakini sizani kama ndio hiyo ya she- , …ya mume wako…’akasema, nilisikia mtoto analia, akawa anakat akata maneno.‘Oh, mungu wangu wakati napita hapo niliona watu wamekusanyika, sikutaka kuangalia, maana nilikuwa na haraka, ina maana…sasa huko alitokea wapi, …mbona kupo kinyume na barabara ya kutokea kazini kwao…?’ nikauliza‘Labda…alipotoka….hata sijui…hilo tuliache tu…’akasema‘Hapana,..tuliache kwa vipi, …yaani, muhimu ni kujiuliza huko alifuata nini, na….oh, mungu, ….mungu amjalie apone tu..,..maana hali ilibadilika ghafla tulipofika hapa hospitalini, naogopa kweli rafiki yangu…’nikasema‘Mhh…muhimu ni hali yake,…hiki kitoto kinasumbua, nakiogesha hapa,…basi, usijali rafiki yangu,  mengine hayana  tija, atapona tu kwa uwezo wa muumba, …’akasema‘Ni kweli,…mengine sijui yapi hayo…haya,  ndio hivyo rafiki yangu, ni siku  ambayo sitaisahau kabisa, maana njiani napo nilikutwa na mikasa, nikiwa soko-duka, nilipoteza fahamu ghafla..’nikasema‘Ulipoteza fahamu…!!!, ilikuwaje tena jamani… pole, na wewe umezidi kujiongezea mawazo, mengine yaache yatajipa yenyewe, ukitaka kufahamu kila kitu unaweza kuathiri ubongo wako…Haya utanipa taarifa kinachoendelea…’akasema‘Sawa nitakujulisha..’nikasema na kukata simu.*************Baadae docta mmoja akaja, akasema wameshaondoa ile hali mbaya, hakuna matatizo tena, hakuna athari za ndani, kwahiyo mume wangu atapelekwa chumba cha kulazwa wagonjwa wa kawaida, baadae kweli akatolewa huko ICU,‘Hii ina maana kuwa hana tatizo kubwa…’akasema docta jirani yangu, aliyekuja baadae‘Kwahiyo tunaweza kwenda kumuona….?’ Nikauliza‘Ndio..sizani kama kuna kikwazo…’akasemaTulipofika kwenye hicho chumba alicholazwa mume wangu, tulimkuta kama kalala, kafumba macho, kalala kaangalia juu, nilimkagua kichwani kafungwa fungwa, umebakia uso,..na shingoni kavaliwa dude kuashiria huenda kuna hitilafu shingoni….hiyo ni dalili kuwa kweli alikuwa kaumia, japokuwa alijikaza kuonekana kinyume chake..Baadae akafungua macho, nikamsogelea nilimuangalia mume wangu pale alipolala, nikahisi machozi yanataka kunitoka…kalala huku kaangalia juu, hakutaka hata kugeuza kichwa kuniangalia, labda hawezi kugeuza shingo,..nikamsogelea pale kitandani, na hapo akajitahidi kuniangalia, kwa kugeuza macho, nikaona machozi yanamtoka…akasema‘Pole sana mume wangu, mungu ni mwema utapona tu…’nikasema‘Nisamehe sana mke wangu, ni-sa-sa- mehe…’akasema huku machozi yakiendelea kumtoka, nikachukua leso yangu na kumfuta, sikuelewa, nahsi ni hiyo hali,…hata mimi pale machozi yakawa yananilenga lenga, nampenda sana mume wangu, na kumuona kwenye hiyo hali, niliumia sana, mawazo yalinipeleka mbali sana.‘Usijali utapona, tu…mume wangu…’nikajitahidi kusema hivyo. Sasa akafumba macho, akawa anahema taratibu, na hilo lilinipa moyo, kuwa kufumba macho huko sio kwa ubaya, nikasema‘Mume wangu utapona tu..tuzidi kumuomba mola…, umenielewa eeh, docta amesema hakuna tatizo kubwa…’nikasema, lakini akilini nikawa najiuliza ni kwanini kakimbilia kusema; nimsamehe…labda,…kawaida mtu akiumwa hujua hatapona ndio anaomba msamaha kwa watu, labda…‘Atapona tu…’nikasema hivyo‘Ndio atapona docta kasema ni athari ndogo za kuteguka …na ngoja tusubiria vipimo halisi havijatoka kwanza…’akasema docta huyo jirani yangu.Baadae mume wangu akapitiwa na usingizi, na tuliambiwa tumuache alale, sisi tutoke nja, tukafanya hivyo.Na wakati tupo nje, ndio nikajaribu kuwauliza watu walikuja nasi, yupo docta , na jirani mwingine na mfanyabiashara aliyenipigia simu, yeye alishafika, wengine yule mwingine tuliyekuja naye alishaondoka, huyu mfanyabiashara anasema yeye alishuhudia hiyo ajali,…‘Kwani ajali hiyo imetokeaje..?’ nikauliza‘Imetokea ile kona ya kutoka barabara kuu, kuingia barabara ya mitaa inayoelekea kwako, mume wako alitokea mitaa ya kutokea Uzunguni, mimi nilikuwa barabara kuu naelekea kwingine, nikasikia huko nyuma paaah, mlio wa kuogonga, unajua nilikuwa naendesha sikuona ilitokeaje, nikasimamisha gari, na kutoka nje…’akasema‘Ina maana ni huu mtaaa wanaouita ‘Uzunguni..’..huko alitokea wapi, …huko si ndipo anapoishi rafiki yangu, mbona mimi nilikuwa maeneo ya huko…, sijamuona ….?’ Nikasema na kuuliza‘Ndio hivyo..yawezekana alikuwa anaendesha kwa mwendo kasi, nahis alikuwa akiwahi jambo, au angelikuwa mhalifu tungelisema anawakimbia polisi…’akasema huyo mfanyabiashara‘Mhh, hata sielewi, na hana tabia ya kuendesha gari kwa mwendo kasi..sio kawaida yake…’nikasema‘Mimi nilijua mlikuwa naye labda…akawa anawahi kitu nyumbani, ..kama ulikuwa maeneo ya huko…’akasema jamaa mwingine.‘Oh, hata sijui…sikumuona kabisa maeneo ya kule…hakuna mtu aliyemuona,.., labda kwa vile nilikuwa  ndani naongea na rafiki yangu..labda kuna kitu alikuwa akikifuatilia, akapitia njia hiyo..akitokea wapi sasa…mmh, hata hivyo ni kwanini akimbize gari hivyo…’nikasema.‘Ni ajali tu…’akasema docta‘Kiukweli ana bahati sana, maana ukiliona hilo gari, utasena hakuna mtu aliyetoka humo ndani, halitamaniki, alikuwa kwenye mwendo kasi sana, ..na gari lenyewe baadae liliwaka moto, na hata watu walipouzima, lilikuwa limeshateketea kabisa…’ akasema jirani.‘Oh, ...niliona ajali hapo njiani wakati nakuja, lakini sikujua ndio hilo ya gari la mume wangu,....,’nikasema‘Sasa mimi nawashangaa huyo mtu aliyemleta hapo nyumbani kwako docta,  badala ya kumkimbiza hospitalini, alikuambia ni kwanini alifany ahivyo?’ akaulizwa docta.‘Nahisi alichanganyikiwa, na labda hakutaka ijulikane ajali hiyo imetokea wapi, labda maana tunajisema wenyewe tu kuhisia,..sabbu kubwa ni kuwa  alichanganyikiwa maana haina maana hapo…, gari si lipo, kama ni wazo hilo, la kuficha kuwa ajali ilitokea wapi…’akasema yule mfanyabiashara.‘Unajua watu walipofika kwenye hilo gari, walijua wanafika kutoa maiti tu..mimi mwenyewe nilishashika kichwa nilipogundua kuwa ni gari la mumeo…lakini watu walipofika hapo, wanashangaa kuona ndani ya gari hakuna mtu…ina maana huyo mtu alitoka kabla ya kugongana au alirushwa nje ya gari…’akaelezea‘Na walipoona hivyo hakuna mtu, wasamaria wema wakaanza kuhangaika kutafuta dereva yupo wapi, lakini hakuonekana kabisa…mimi mwenye nahangaika kukupigia, simu inatumika, mara hupatikani mara…baadae ikawa haipatikani kabisa….’akasema huyo mfanyabiashara.‘Mimi hata sijui….mume wangu jamani, apone tu,..sikujua kuwa ni gari lake wakati napita pale, nilikuwa na mawazo mengi, na kama ni ajali nilitegemea kwingine kabisa sio njia hiyo...’nikasema‘Gari halithaminiki, hakuna kumbukumbu yoyote ndani,..maana lilikuwa bado haliingiliki, baadae mimi kwa vile nalifahamu ni la nani, taratibu bila kuwaambia watu lolote, nikaanza kufuatilia, kukupigia simu ukawa hupokei, baadae mimi wazo likanijia...Nikaamua kwenda nyumbani kwanu, na nimefika pale haupo, na mumeo hayupo,,…nikaona hapa, isije ikawa mtu kaungulia ndani ya gari hatukuona vyema, nikataka kurudi tena kuhakikisha,…sasa wakati natoka pale kwenu,  ndio nikakutana na jamaa mmoja rafiki yangu, akaniambia, kuwa kakutana na mumeo, yupo kwenye hali mbaya, …kaingia nyumbani kwa docta.‘Mhh, hapo kwa haraka nikahisi aliruka alipohisi ajali, lakini mmh, yatakiwa uwe mzoefu kweli kama askari, sijui…yaani hapo ni kitendawili mpaka mwenyewe ajae kutuambia…’akasema‘Hata hatujui alifikaje kwa docta,…..rafiki yangu mmoja alikuwa anapita na gari lake, ndio akamuona yupo nje ya mlango wa docta akiwa kasimama, kashikilia mlango, ..yupo hoi,..kama aliyepatwa na ajali, ana damu, shati limechanika,..ikabidi asimamishe gari kuja kuangalia kuna tatizo gani, ndio akamuona yupo kwenye hali mbaya,… akamsaidia kuingia naye ndani,kwani aliadai aingizwe humo ndani kwa docta. ‘Nikamuuliza alimuachaje …hali yake vipi, maana siamini, mtu katokaje kwenye hilo gari…’akasema.‘Akasema kumbe docta huyu jirani yenu yupo likizo, walimkuta yupo hapo ndani, basi ikabidi aanze huduma ya kwanza, akaniambia kuwa kamuacha huko ndani akimuhudumia, lakini anaonekana hayupo vibaya, ila ni kama kachanganyikiwa…’akasema‘ Mhh… mungu mkubwa…’nikasema hivyo. Na mimi ndio nikaingia na kumkuta docta akimuhudumia na kwa muda huo hata docta hakujua kilichotokea, ndio nikamuelezea, nilichokiona huko nilipotoka, na ndio akajaribu kukupigia, naona simu yako ina matatizo,…simu yako haina matatizo kweli…?’ akauliza huyo mfanyabiashara.‘Haina matatizo, lakini kuna muda ilizima…’nikasema hivyo, sikutaka kuongea zaidi, pale nilikuwa na hamu nirudi ndani nikamuangalia tena mume wangu.Nikamsogelea docta kumuomba akaombe ili niweze kuingia ndani, nikamuone tena mume wangu.‘Sawa, hamna shida…’akasema na kuniambia tuongezane, basi tukaenda naye hadi pale alipolazwa mume wanguNilipomchungulia mwili wake, nilihisi mwili wangu ukisisimuka sikujuwa kwanini, kwanini kanyoka tu vile…, na muda ule alikuwa kafungua macho, sasa hataki hata kuniangalia machoni, mwili wangu hapo ukafa ganzi, nikawa nasubiria tu hiyo taarifa ya docta nisikie kama ana tatizo au hana...Pale docta akaongea nilipomuuliza ni kwanini alikuja kwake…‘Yeye ndiye aliyenipigia simu, na namba tofauti, nahisi alimuomba mpita njia mmoja, mtu wa bajaji…kwa bahati nzuri nipo likizo, kwahiyo nilikuwa hapo nyumbani, nikijua ni tatizo dogo, ndio hivyo  akaletwa, kiukweli nilimshauri aende hospitalini, lakini alisema ni muhimu atibiwe hapo nyumbani tu, na nilion akachanganyikiwa, anasema hataki ijulikane kuwa kapatwa na ajali, ..ni kuchanganyikiwa tu huko...‘Kwanini hataki, wakati keshapata ajali, mmh…?’ nikamuuliza‘Atakuja kukuambia mwenyewe, ndivyo alivyosema…’akasema docta‘Kiukweli nilipomfanyia uchunguzi wa haraka haraka na kufanya kile kinachowezekana, sikuona tatizo kubwa la nje, ila…ajali ni ajali, unaweza kwa nje usione kitu, tatizo likawa lipo kwa ndani, na unaona, kumbe kuna athari kwenye uti wa mgongo na shingoni, ngoja tusubiria taarifa za madocta,.. ’akasema huyo docta jirani yangu‘Uti wa mgongo…umeathirika..mungu wangu ina maana gani sasa ina maana hataweza kutembea tena,..’nikasema nikishika kichwa‘Usiwe na wasiwasi, …yupo kwa wataalamu..ngoja tusubirie uchunguzi wa mwisho….’akasema docta kunipa farajaNB: Ndivyo ilivyokuwa hivyo...., WAZO LA LEO: Mwili wa binadamu una uvumilivu wake, tunahitajika kuutunza sana, na unapouzidishie mambo juu ya uwezo wake, ukiulazimisha sana mwili, hasa kimawazo, tunaweza kujikuta tukipatwa na athari za kiafya. Mazoezi ni muhimu sana ili kuwezesha miili yetu, na akili zetu kubeba mambo kwa mpangilio. Lakini pia tusipende kuulazimisha kupita kiasi…hasa mawazo, mawazo yakizidi sana huja kuleta matatizo. Docta amekuwa mfariji wangu mkubwa, tokea enzi hizo, ananifanya nikumbuke mbali sana, maana mara kwa mara nikiwa sina furaha, basi naweza kumpigia simu,tukaongea akaniliwaza, na hata kunipa ushauri, na sijui kwa vile ni docta, lakini hata hivyo tumetoka naye mbali sana, na sehemu katika maisha yangu ndio maana sitaacha kumsimulia kwenye kisa cha maisha yangu….Kutokana na huyu docta ndio nilijenga na kuiendeleza tabia yangu ya kuamini watu, sio kwa kila mtu lakini wale unaoona wanaaminika, wale marafiki zako wa karibu, waamini, maana na wao watakuamini, yeye ndiye aliyenifundisha jambo moja, kuwa nisipende kuwadhania watu vibaya, maana ukifanya hivyo unajijengea hisia mbaya moyoni mwako, na kujitwika mzigo ambao haujatua kichwani mwako.Basi wakati nipo hapo hospitalini, docta huyu akawa karibu nami kunipa faraja ili nisahau maumivu ya kumuwaza mume wangu …na kiukweli nilikuwa kwenye hali ngumu sana…mawazo, na yote yaliyotokea siku nzima, yangeliweza kunifanya niathirike kisaikolojia, docta akanipa pambaja, nikahisi sasa nipo na watu wenye kutumania.Huyu docta  ndiye aliyewahi kuwa mchumba wangu, sasa kwanini ilitokea nikamuacha na kuolewa na huyu mume wangu,..ni kisa fulani chenye mazingatio kwa wenye hekima…Tuendee na kisa hiki***********Docta alikuwa pia ni rafiki ya mume wangu, wengi walitarajia angelikuwa nai adui yake mkubwa, baada ya kunyang’anywa tonge mdomoni, lakini haikuwa hivyo,…docta amekuwa seehmu ya kuijenga ndoa yangui kila inapolega lega..Naweza kusema pia docta ndiye aliyeniingiza kwenye dunia ya mapenzi, alinitoa kwenye ujana na kuniingiza kwenye usichana, nikafahamu ni nini maana ya mapenzi, enzi hizo, nikiwa kwa baba na mama yangu…hutaamini, kinyumbe na walivyotaka wazazi, sikuweza kuolewa naye….Huyu docta ni nilianza kujuana naye zaidi tukiwa chuoni, huku nyuma, miaka ya utoto, shuleni, … nilikuwa namuona tu, ..kwa vile walikuwa majirani zetu, na ni familia yao ni miongoni mwa familia zilizokuwa na uwezo wa mali, wasomi waliobobea, kwani hata mtoto wao huyu aliweza kusomeshwa nje, kabla hajarudi hapa nchini,Pamoja na mengine mengi sitaweza kumsahau kabisa katika maisha yanguIlivyotokea tunaweza kusema ni mipango ya mungu, maana kipindi nipo na huyu docta , ndio amerudi kutoka ulaya, wakati huo hajawa docta kamili, ndio alikuwa anachipukia, na kwa vile familia zetu zilishibana, aliporudi tu, akawa anakuja kwetu, na akija anakaribishwa vizuri, mtoto wa watu, basi tunakutana naye na kuongea mambo mbali mbali,  akanizoea mpaka tukafikia hatua ya kukubalina kuwa wapenzi.Basi ikawa ni jambo la furaha kwenye familia zetu, maana tupo kwenye daraja moja,…ni maisha yalivyo, kila mti na ndege wake. Familia zetu ikawa imeliidhinisha tamko la kuwa mimi ni mchumba wa docta, kwahiyo yeye aliweza kuja kwetu kunichukua, …unajua tena wao waliishi kizungu zaidi,..basi akija, ndio hivyo tena, ila hali ya wazazi kukuchunga kwake inapungua,  ananiombea ruhusa tunatoka kutembea sehemu mbali mbali,…kiukweli mimi sikupenda sana maisha hayo y akujichanganya kwenye majumba ya starehe nk..lakini utafanyajeNa kitu ambacho kilinifanya nisipende maisha hayo, ni ile hali ya kutizamana, nani kavaa nini, na zaidi pombe, tangia utoto nilitokea kukichukia kinywaji kinachoitwa pombe ya aina yoyote…namshukuru mungu kwa hilo.Na hata nikiandamana naye kama  mpenzi wangu, alifahamu kabisa mimi nipo mbali na ulevi, yeye kunywa kwake, ilikuwa kama kunywa soda, lakini hakuwa anakunywa kuelewa, alikuwa na kipimo chake, sijui kwa vile ni docta.Ikafikia muda akaanza kunishawishi ili nami niwe nakunywa kama yeye, hapo ndio hisia zetu zilianza kusigishana, na hilo ndilo lilofanya tukaja kukosana kabisa nay eye, lakini haikutokea hivyo tu kwa vile, hapana mimi naweza kukiri kuwa ni mipango ya mungu ilipangwa iwe hivyo.Kiukweli ilibidi afanye juhudi sana kunishawishi kwa kitu ambacho sikipendi, na sijui kwanini siku hiyo ilitokea nikakubali. Ilitokea siku hiyo, kulikuwa na shughuli za jirani, mmoja wa watu wenye uwezo, waliandaa tafrija kwenye hoteli moja kubwa tu, tukawa tumealikuwa…baada ya mambo mbalimbali, ikawa watu wanakula na kunywa, na hapo mpenzi wangu huyu akaanza kunishawishi, ninyweKwa vile niliona ni siku ya furaha, na sikutaka kumuuzi mpenzi wangu, siku hiyo nikasema ngoja nijaribu, nione ina ladha gani, ngoja nijaribu nione hiyo raha wanayoifaidi wenzangu,…ilikuwa ni aibu kwangu na ndio siku niliapa kuwa sitakunywa tena.Nilikuwa nimekunywa kidogo, kumrizisha mpenzi wangu ambaye kipindi hicho alikuwa ni huyu docta, nilikunywa gilasi moja tu tena kwa kujilazimisha, ilikuwa haipiti kooni, nahisi ni harufu mbaya, nilipomaliza hiyo gilasi moja tena haikumalizika,..,…Hapo hapo nikaanza kujisikia vibaya, tofauti na ninavyoona wenzangu wakichangamka, mimi nilihisi vibaya kupindukia, niliona kama dunia inageuzwa, inazungushwa, roho imechafuka, tumbo linapanda na kushuka, nataka kutapika lakini hakitoki kituYaani siku hiyo nilijuta ni kwanini nilikunywa,..nilimuona mpenzi wangu kama alitaka kuniua, na muda huo huo, nikamwambia mimi naondoka, siwezi kukaa hapo tena, akanisihi, na kunishawishi, kiukweli anajua kubembeleza, na unajua tena ni mpenzi wangu ikabidi nikae tu…kumrizisha.., na hata aliponishawishi ninywe tena sikukubali, nilimuambia kabisa ukiendelea kunishawishi kunywa hii sumu tutakosana kabisa. Kwa muda ile nikajitahidi, lakini hali haikuwa nzuri, bado nilikuwa najisikia vibaya,..ikafika muda, siwezi kuvumilia tena, kwani roho ilishachafuka kupitiliza, nikakimbilia chooni, (washing-room), nikamuacha docta na watu wengine wakiendelea kuongea na kunywa, wanajisikia raha zao.., ambazo kwangu mimi ilikuwa ni kero tu.Nilipokuwa kule hali ikatulia, kidogo cha ajabu sikutapika, kama nilivyodhania nitafanya hivyo,..nikaona labda, hali imetulia, ndio wakati nataka kutoka sasa,natoka chumba hicho cha usafi, nipo mlangoni, nikahisi kizungu zungu,na kama asingelikuwa huyo jamaa kunidaka ningelidondoka vibaya kwenye sakafu….‘Pole sana dada, ....’akanidaka huyo jamaa na kunisaidia kusimama vyema, lakini sikuweza, mwili ulikuwa hauna nguvu, tumbo linapanda na kushuka, na sikuweza kuvumilia zaidi nikaanza kutapika, na matapishi ya mwanzo yakaenda moja kwa moja kwenye nguo za huyo jamaa.‘Oooh...pole pole, inaonekana umelewa, wewe..oh, ..tulia kidogo,....’akasema bila kujali kuwa nimemchafua. Na kunisaidia ….Na hutaamini hakujali kuchafuka kwake, yeye alichojali kwangu  ni kunisaidia mimi akanishika vyema, akichelea nisichafuke na yale matapishi niliyomlowesha nayo mimi, ambayo yalikuwa kwenye nguo zake,....na akaweza kunisaidia hadi chooni, ilibidi aingie choo cha wanawake ili niweze kujisafisha,..alipohakikisha nipo sawa, yeye akakimbilia choo cha wanaume kujisafisha, nilijiskia vibaya sana siku hiyo.Hali ilipotulia nikatoka, kumbe huyu jamaa alikuwa hapo nje akinisubiria, alikuwa keshamaliza kujisafisha, na kukausha nguo zake usingeliweza kujua kuwa nilimchafua, na aliponiona nikitoka akanifuata pale mlangoni, na kuniuliza.‘Upo sawa sasa,…?’ akaniuliza‘Ndio nipo sawa, hamna shida, samahani sana, na nashukuru sana…’nikasema‘Usijali, inatokea tu…na samahani nikuulize ,upo na nani maana naona hiyo hali unahitajia msaada...?’akaniuliza huku akinisogelea, na sikutaka kuongea na mtu, nilichotaka ni kuondoka, na kwenda nyumbani kulala.‘Nipo na na...’nikasita kusema‘Na mume wako, au mpenzi wako, off course....’akamalizia na mimi nikakubali kwa kutikisa kichwa, ili nitimize ule usemi wa kubali yaishe, ili aondoke zake, na mimi niende kumuaga docta kuwa narejea nyumbani.Kiukweli kwa muda ule nilidhamiria kuondoka, sikujali tena kuendelea kukaa kumrizisha mpenzi wangu, wakati hajui kinachonisumbua, yeye aliona ni kwa vile ni mara ya kwanza, basi nitazoea,…hapana sikuzoea na sitaweza kuzoea maishani mwangu.Nikawa natembea kulekea kule walipo docta na marafiki zake, lakini nlikuwa nayumba, kizunguzungu, yaonekana kichwani bado nilikuwa sipo vyema,na kumbe jamaa yupo nyuma akiwa na mashaka kuwa naweza kudondoka tena,…na alipoona sipo sawa akanijia kwa nyuma na kusema;‘Basi ni bora nikusaidia hadi kwa huyo mume wako,maana unavyoonekana hujawa sawa, kwanini unakunywa pombe, wakati unaona hazikupendi,.....achana na pombe,pombe zinawenyewe bwana, mimi mwenyewe sinywagi kihivyo, ni kwa dharura tu....’akasema.‘Sinywi tena...hapana nitaweza mwenyewe…..’nikasema na nikamtupia jicho huyo mtu, na ilikuwa kama ndio namuona kwa mara ya kwanza, nikahisi hali fulani, kama mshituko , ni kama kuna kitu nilikihisi, lakini niliona ni sababu ya pombe, maana mtu mwenyewe simfahamu, lakini nikajiuliza ni kwanini nihisi kitu kama hicho, nikapotezea, na sikutaka kumwangalia tena machoni.‘Samahani nikuulize,… inakuwaje mume wako asijitokeze, kwani naona kama umekaa huku muda mrefu hajashtuka tu…kama ulikuwa na hali hiyo alitakiwa akujalia, au sio,,? Samahani lakini kama nawaingilia maisha yenu, au....?’akasema kama kuniuliza, hata mimi nililiona hilo , lakini sikujali, na sikutaka huyo docta afahamu kilichotokea.‘Wenyewe wameshalewa, sizani kama hata wanatambua kuwa nimechelewa huku....na nisingelipenda wanione kuwa nimetapika kwa ajili ya pombe, wala usije ukawaambia hata hivyo nipo safi, haina haja ya wewe kunisaidia nashukuru kwa wema wako huo..na sitakunywa tena hiyo mipombe yao, ....’nikasema.‘Pole sana....mimi kama ningelikuwa na mpenzi  kama wewe, ningeshtuka haraka sana, ulivyochelewa hivyo…sio kwamba namsema vibaya huyo mpenzi wako, lakini kwa hali hiyo alitakiwa awe karibu yako,…mimi hapa naogopa usije kudondoka tena.. sawa, basi tembea mimi nitakufuatilia kwa mbali kuhakikisha umefika salama kwa mume wako, ...’akasema, na kunifanya nifurahie sana wema wake.‘Hongera ...kama upo hivyo, na mpenzi wako atakuwa na bahati sana…hata hivyo, ni leo tu, mbina mpenzi wangu ananijali sana, sina shaka naye….’nikasema na nikatamani kumwangalia tena huyo jamaa usoni, na nilipomuangalia, akili yangu ikakumbuka kama niliwahi kuiona hiyo sura mahali, lakini sikuweza kukumbuka vyema ni wapi, na lini, sikutaka kuwaza zaidi , nikapotezea.‘Ina maana hunikumbuki mimi kabisa...?’ akaniuliza na kunifanya nisimame wakati huo nilishaanza kuondoka kuelekea kule walipokuwa docta.‘Kwani wewe ni nani…?’ nikamuuliza , na hapo ndio nikapa ujasiri wa kumchunguza vyema usoni baada ya kugeuka kumuangalia vyema…hata hivyo sikuweza kumkumbuka kuwa ni nani, akili ilikuwa haitaki kufikiria sana, na sikutaka kufanya hivyo nikasema;‘Samahani kwakweli sikukumbuki kabisa,..zaidi ya kukufahamu hapa kuwa wewe ni mtu mwema, ...tuliwahi kukutana wapi mimi na wewe, shuleni, au chuoni, au wapi?’ nikamuuliza ili tu kumuonyesha kuwa namjali kwa fadhila zake hizo, lakini sikuwa nataka kuongea...‘Kweli ukiwa mtu wa chini, ..watu hawakukumbuki kabisa, wewe sio wa kwanza kusema kuwa hunikumbuki, lakini nafahamu ni kwanini...’akasema hivyo.‘Hapana sio kwa vile wewe ni mtu wa chini, kwanini unasema hivyo, wewe ni mtu wa kawaida mbona, mimi sipendi watu kujishusha, hakuna mtu wa juu na chini, hizo ni hisia potofu, na kiukweli sipendi watu kujifanya hivyo…’nikasema, na nikamwangalia tena kwa makini,japokuwa akili iliona kuwa nilishawahi kukutana na mtu kama huyo, na sio kukutana tu, lakini moyoni nilikuwa kama nimeguswa na hamasa, lakini sikuweza kukumbuka kabisa kuwa huyu mtu ni nani.Muda ulikuwa umekwenda, sikumuona docta akija ..na sikupenda kumuacha huyu msamaria mwema hivi hivi, nilitaka niondoke akiwa amerizika, sio niondoke aone nimemdharau..hisia za wema wake ziliuteka ubongo wangu, ule ukaribu wake , kunijali, nilimuona kama mtu niliyemzoea….sijui kwanini, yaani kumbe kitu kidogo tu kinaweza kubadili hisia za mtu.‘Samahani sana, labda kwa vile nipo katika hii hali, ndio maana akili haifanyi kazi vyema, na nisingelipenda kufikiria zaidi, maana kichwa kinaniuma, labda unikumbushe tu, kama hutojali...’nikasema na huku nikikwepa kumwangalia tena moja kwa moja usoni na yeye akaniangalia na kusema;‘Mimi ni mtoto wa mzee Mchapakazi…’akasema‘Mchapakazi…?’ nikauliza, sikuweza kukumbuka ni nani anamuongelea kwa wakati huo..‘Humkumbuki yule mzee, aliyekuwa  mlinzi wa pale nyumbani kweny, na pia alikuwa akiwalimia mashamba yenu na mimi nilikuwa nafika kumletea baba chakula, na siku moja ukanisadia pesa za ada ya shule, kipindi mzee anaomba mkopo kwa baba yako, na baba yako akakataa kumpa hizo pesa..umeshanisahau ehe...’akasema‘Mungu wangu ndio wewe..mbo-mbona..hapana sio wewe…’nikasema huku  nikainua kichwa kumwangalia na mdomo wangu ukabakia wazi kuonyesha mshangao.‘Ndio mimi …huamini eeh…mlifikiri tumejifia au sio…’akasema‘Oh, …sio…ila kiukwe umebadilika sana..ooh, nimeshakukumbuka, ..oh jamani , mimi nilikuwa kasichana kadogo kipindi kile,…unajua baada y alile tukio, nilitokea kuwachukia sana wanaume, na nailijiskia vibaya sana kwa yale yaliyotokea, hata hivyo nilitamani nikuone tena, lakini hukuja, nilishaahidi kukusaidia ..kukulipa fadhila ulizonitendea...’nikasema.‘Kunilipia fadhila , si zilishalipwa na baba yako, au umesahau yaliyotokea..’akasema‘Usiseme hivyo, wazazi wangu na wao walipokea taarifa tu,..nakubali hawakutaka kuzichunguza,..’akasema‘Unaweza kuwatetea hivyo, sawa, ni wazazi wako ni lazima useme hivyo…ila kiukweli iliniuma sana kumuona baba yangu anazalilishwa, na sikutaka kurejea tena kwenu, na nikawa nafanya vibarua  tu pale waliponiachia jela, na sijui ilitokeaje kesi ikafutwa na kuachiliwa, nilihangaika sana...hadi nikapata pesa za kujisomesha, unakumbuka nilifaulu, na kwasababu ya kufungwa sikuweza kwenda sekondari,…’akasema‘Pole jamani…nilisikia, lakini aah, mimi sikuweza kufuatilia, maana sikuwepo tena yaliyotokea nyuma nilifanya kuhadithiwa, nilijua yameisha, kumbe..ndio hivyo tusamehe tu, na wazazi wangu…’nikasema‘Nilipata msamaha, sikufungwa muda mrefu,.. na nilipotoka nilimuomba baba tuhame hapo kijiji kabisa, tukaenda kuishi kijiji cha mbali, huko nikaweza kujisomesha kwa kufanya vibarua...Baba yangu aliumwa sana, naweza kusema ni  kutokana na hilo tukio, na kuumwa huko ndio ikawa sababu ya kufariki kwake...’akasema kwa uchungu. ‘Oh, pole sana, ina maana yule mzee alishafariki...?’nilimuuliza nikishikwa na huruma, na fadhaa, na nilitamani nimkaribie ni mkumbatie kumuonyesha jinsi gani nilivyojisikia….kiukweli niliona nina deni kubwa la kumlipa huyu mtu, maana hii ni mara nyingine ananiokoa na kunifanyia huruma…moyoni niliahidi kuja kumlipa kwa kadri nitakavyoweza.‘Alifariki......ndio mapenzi ya mungu, na mapenzi ya mungu ndivyo yalivyo, na moyoni hatukosi kuwa na sababu..ila kiukweli, baba alinipenda sana, na hali yake hiyo ya kuumwa, na ilianzia pale mama alipofariki , mama yeye alifariki mapema tu, tulipohamia huko,…na,… na hutaamini, baba alikuwa haishi kumkumbuka mama, na hicho ndicho kilichomfanya hali yake izidi kuwa mbayae....na hakupenda mimi niteseke, aliona ni bora yeye akafungwe, aliwaomba sana wahusika afungwe badili yangu...’akasema.‘Oh, jamani, poleni sana, sizani kama wazazi wangu walifahamu hilo, na ukweli wote wa hayo yaliyotokea…na kwa vile alikuwa mfanyakazi wao kwa muda mrefu wasingelifikia kumfanyia ubaya huo wote…na hata kufariki huko, sizani kama walikuwa na taarifa,..wangeliniambia, na hata wao kufika kwenye msiba, sizani kama wangeshindwa kufanya hivyo, sizani...’nikasema.‘Baba alikataa kabisa, mama alipofariki, hakutaka kutoa taarifa kwa watu wa mbali, na hata yeye alisema ikitokea akifariki..sisi tufanye hivyo hivyo..maana alishaona dunia haina wema..aliniusia kabisa,.., nisije kuja kuwaambia...na ndivyo ilivyotokea, alizikwa na watu wachache tu…, na wengi hawakufahamu zaidi ya ndugu na jamaa wa karibu tu .....ndio hivyo, lakini mimi sikukata tamaa ya maisha, nikasonge mbele, ....’akasema.‘Sasa hivi unafanya kazi wapi?’ nikamuuliza.‘Nipo hapa kwenye hii hoteli nabangaizabangaiza, nilipata tenda ndogo hapa, ndio naifukuzia, ikiisha nakwenda sehemu nyingine, maisha yanakwenda kidogo ninachokipata kinanisaidia, sitaki ile ya kuajiriwa maoja kwa moja, mpaka nikamilishe malengo yangu…’akasema‘Mungu wangu, imeniuma sana…sikutarajia hili , kweli milima haikutani, ila wanadamu..mmh…sijui nitakulipa nini, sijui nifanye nini ili hayo machungu yaliyokupata yaishe,..sijui, tusamehe tu, mimi na wazazi wangu..’nikasema‘Ndio maisha sisi watu wa chini kupata  kazi inakuwa shida, na sipendi kwenda kuwapigia watu magoti kuwa wanipe kazi, sitaki nizalilike kama alivyozalilika baba yangu, mimi nimeona njia iliyorahisi ni kujiajiri kwa njia hii...hapa leo, keshi kwingine maisha yanakwenda,…..’akasema na hapo nikamwangalia na kumbukumbu za nyuma zikanirejea...‘Maua unafanya nini huku….?’ Ilikuwa sauti ya docta, na nikageuka haraka na kuanza kutembea kumfuata, nilipomfikia, akaniuliza‘Ulikuwa na nani muda wote huo…?’ akaniuliza‘Nilikuwa najisikia vibaya, …sana…’nikasema‘Utazoea tu,…pombe kidogo tu ndio imekufanya hivyo, ajabu kabisa… tatizo lako hutaki kujifunza, starehe hiyo unaikosa bure, dunia hii kuna starehe gani kama oh, upo ok, lakini samahani, sikuja kukuangalia, kuliko na maongezi nyeti kidogo, nisamahe mpenzi…’akasema akinishika kiunoni kunifanya nisipepesuke.‘Nipo sawa, haina haja kunishika hivyo, mimi sipendi…’nikasema‘Ok, ok…samahani nimesahau…haya twende, na yule aliyekuwa karibu yako ni nani..?’ akaniuliza‘Ni mfanyakazi wa hii hoteli, kanisaidia, sana, maana nilizidiwa kidogo…’nikasema‘Mhh, ok, sijamshukuru, naona simuoni tena....haya, twende tukaendelee ..wenzangu ndio kumekucha..’akasema, na docta alikuwa hivyo hana hisia mbaya na watu, ndio nilimpendea hivyo, ukimuambia kitu atakuamini, na inaishia hapo.‘Hapana mimi naondoka…siwezi kurudi tena kule, nahisi harufu za pombe zitaniua,wewe nenda kaendelee tu na wenzako…’nikasema‘Oooh,..hapana usifanye hivyo,…utaharibu, nitawaambiaje rafiki zangu, kuna mambo muhimu tunaongea pale unajua kazi zangu ni watu, na watu ndio wananiongezea michongo ya maisha..unajua, ...na wale pale ni watu muhimu sana, ni madocta, wamenitangulia, nikiwa nao, najua nitafika sehemu ninayoitaka sana, elimu yangu nataka inifikishe mbali kabisa..’akasema‘Basi ..ndio maana nasema, wewe nenda kaendelee nao, wala sijali kuhusu mimi,   mimi nitarudi nyumbani peke yangu, maana hapa na nyumbani sio mbali, nitafika bila wasiwasi..’nikasema‘Siwezi kukuacha uende peke yako, na hii ni shughuli muhimu ya majirani zetu haitaonekana vyema tukiondoka, hata wazazi wako hawatafurahi, wakisikia hivyo, hebu lifikirie vyema hili, nikuombe kitu.., vuta vuta muda, tutaondoka pamoja ..’akasema, niliwaza sana baadae nikasema sawa, basi nikarudi pale mezani, lakini baadae nikamuomba mpenzi wangu kuwa nataka nikakae kwenye hewa, nipate upepo,..sijisikii vizuri.‘Wapi sasa, unaona mambo tunayoyaongea hapa ni muhimu sana, yanaweza kukusaidia hata wewe , kwenye maswala ya ajira, kujiajiri, kuwekeza, unaona, ni mambo muhimu kwenye maisha, leo wazazi, kesho ni sisi, tunahitajika kuchukua hatamu, au sio..umesikia mwenyewe, mimi  hatima ya haya ni kuwa ni hospitali yangu kubwa, ndio ndoto yangu…’akasema‘Usijali, mimi nitakuwa kule sehemu ya kutokea, ..palee , unaona, wamekaa akina mama , na wasichana wasiopenda kujichanga huku,…utakuwa unaniona au sio…’nikasema akakubali, kwa shingo upande, ..kiukweli kwa muda huo, sikutaka kukaa pale na akili yangu ilishaondoka, yaani kuna kitu kilinibadili ghafla, na ..hata sijui ni kwanini.Nikaenda ile sehemu na kukaa , kulikuwa na watu wengine wasiokunywa wamekaa hapo wanakunywa vinywaji vya kawaida, nikatafuta sehemu nikaa, na nikanyosha mkono kumuashiria docta, kuwa nipo sehemu hiyo, na akanipungia mkono kuwa kaniona..Sasa ni wakati nimetulia, mara akaja mtu pembeni na kukaa, …sikutaka kugeuka kwa haraka, kumuangalia ni nani, nilikuwa akili yangu imetekwa na tukio kwenye Tv, kuna tamithiliya nzuri inaonyeshwa, na mara sauti ikasema;‘Kumbe yule ndio mume wako, najua hata yeye keshanisahau, …yupo na akina kaka zetu wa enzi hizo,…mnaoana watu wenye hadhi zenu…’nikashtuka, kumbe alikuwa yule msamaria mwema, nikahisi moyo ukinienda mbio, maana sasa kakaa karibu yangu, nikageuka kuangalia kule alipokaa docta, nikawaona wanaongea na kucheka tu. Hana habari kabisa na mimi…‘Mhh…sio mume wangu…’nikasema‘Kwahiyo, kumbe hujaolewa bado…’akauliza‘Bado ndio tupo mbioni…’nikasema‘Oh, mungu wangu kwanini hivi lakini…’akasema‘Kwanini unasema hivyo…?’ nikamuuliza‘Unakumbuka ahadi yetu lakini…?’ akaniuliza‘Ahadi, mmmh…na..ndio na…nakumbuka,  lakini…hayo yalishapita au sio ni mud asana, na mambo yamebadilika,…na nishamuahidi docta kuwa ndiye mume wangu mtarajiwa, samahani sana..’nikasema‘Najua,hamna shida , nilitaka ukumbuke tu hilo, najua huwezi kuolewa na mtu kama mimi,….ila nakuuliza tu…je moyo wako bado upo kwangu, au uliniambia tu  kunifurahisha, utoto..lakini hatukuwa watoto kivile, au sio…samahani sana kukuuliza haya, najua umeshampata mtu wa hadhi yako…sizani kama nina maana tena kwako…’akasema‘Usiseme hivyo, wewe hujui tu….niliteseka sana,…sijui kwanini, na hadi naamua kumkubalia docta, ilikuwa ni baada ya kusikia kuwa wewe haupo hai, walisema ulifia jela au baada ya kutoka kitu kama hicho….’akasema‘Eti nini…nilikufa…hahaha.., hayo labda waliyatunga wazazi wako,..ili….lakini haina haja, najua, hutaweza kuolewa na mtu kama mimi, nafahamu hivyo,… lakini niliapa kuwa bila wewe sitaweza kuoa tena, ndio maana nikawa napambana ili niwze kufiki hadhi yenu, na nilitaka siku tukikutana unione tofauti, lakini ya mungu mengi tuakutana leo bila kutarajia…’akasema‘Jamani…..’nikasema hivyo nikigeuka kumuangalia kwa macho yaliyojaa hurumaNa wakati namuangalia, ndio kumbukumbu za nyuma zikaanza kunirejea, na ikawa ndio sababu ya kunibadili kabisa mawazo yangu, hasa kutokana na yaliyotokea siku za nyuma kweli kumbukumbu hubadili maisha…na kutokana na kumbukumbu hizo zikanifanya nimuache docta…haikuwa kazi rahisi, lakini…NB: Tutaendelea sehemu ijayo. Ilikuwaje, na ina umuhimu gani kwenye hiki kisa, tuzidi kuwepo…WAZO LA LEO: Tofauti za maisha, tofauti za kipato, tofauti na utawala na wasio kuwa watawala, isiwe ndio sababau ya kuzarauliana, maana huwezi kujua, ni yupi ni muhimu kwenye maisha yetu. Unaweza ukawa na kipato lakini ukawa na mapugufu fulani ambayo yanaweza kujaziliwa na yule unayemuona ni hadhi ya chini, au akaja kukusaidia yule ambaye hukutarajia kabisa. Mola ni mwingie wa hekima anajua ni kwanini maisha yapo hivyo,.. Kumbukumbu za nyuma ziliuteka ubongo wangu,…nikakumbuka yaliyotokea huko nyuma, yaliyompata huyu msamaria mwema, tena kwa ajili yangu, akafikia hadi kufungwa na wazazi wangu, …nikaapa kuwa siku nikikutana naye, nitajitahidi nifanye lolote kumlipa fadhila zake, sasa nitamlipa nini, …na nilishamsahau, nikujua hayupo tena duniani…na siku hiyo, ndio nikakutana naye, nikiwa na docta mtoto wa watu akiwa ni mpenzi wangu…je nilifanya nini, angalia mitihani hii ya maisha…*********** Nakurejesha nyuma kipindi nikiwa binti mdogo, wa miaka kumi na tano,…kipindi hicho ndio nilimuona kijana mmoja mara kwa mara akiwa anakuja kuonana na mzee mmoja aliyekuwa mlinzi wa nyumba yetu. Yeye kiumri alikuwa mkubwa kuliko mimi…nikaanza kuzoeana naye tu..Kuna kipindi baba yake alikuwa akitulimia shamba, basi na yeye anakwenda kumsaidia baba yake mimi, nikawa nafika shamabi kuchukua matunda, nawakuta wakiwa wawili, nawapatia chochote, mwanzoni  sikuwa naongea naye sana, kutokana na hali ilivyokuwa wakati huo. Wazazi walikuwa wakali hawakupenda kabisa nizoeane naye, au kuwa karibu naye,…Kila huyo mvulana akija, nilimgundua akiniangalia sana, na ikitokea tukikutanisha macho anayakwepesha kwa haraka na kujifanya kama alikuwa haniangalii, ikawa kama mchezo fulani wa utu-rika,.. na tukajikuta tunamezoeana kinamna hiyo, lakini sio ile ya ukaribu ya kukaa pamoja na kuongea. Ni ikaja muda hata mimi nikikaa nyumbani, namuwaza yeye, fikiria ni mtoto wa mkulima, mfanyakazi wetu tunaweza kusema wa ndani…lakini mimi sikulijali hilo, nilimuona sawa na wavulana wengine. Sio kwamba nilikuwa na tabia mbaya, ya kuwa na mazoea na wavulana, hapana..ila nilijali sana usawa na utu, hata nikiwa msichna mdogo.Basi kwa ile hali ya kunyanyapaliwa na wazee, kuwa wakifika wanakuwa na sehemu yao, hawaruhusiwi kuingia ndani, sikulipenda hilo kabisa, nikaona lazima nifanye jambo, la kuwasaidia hawa watu wawili…nilimjali sana huyo baba yake, alikwua na tabia nzuri tu,…huruma na upendo,.Basi…huyo kijana akifika, ninajua wapi nikae ili aweze kupita na kuniona, kwa haraka nikakuwa na zawadi yoyote ya kumpa, chakula au matunda,…maji ya baridi ili wakinda sahamba wapate kuyatumia yeye na baba yake..na nilijithidi sana wazee wangu wasiweze kuona hayo…Lakini ikatokea tukio, liloharibu kila kitu, na baada ya tukio hilo, tukaachana na familia hiyo sisi baadaye tukahama na kuja kuishi Dar, ambapo baba yangu alihamishia kampuni yake, na huko kijijini tukawa hatufiki mara moja moja tu. Na sikuweza kuwaona tena. Tukio hilo kwakweli liliniumiza sana kiasi kwamba niliwaona wazazi wangu kama ni watu wasio na utu-wema.*************‘Kwanini  hukunitafuta, ulipoachiwa kutoka jela...?’ nikamuuliza, nikikatiza mawazo yangu ya kumbukumbu za huko kijijini….‘Kwanini nikutafute..ulitaka niendelee kuumia, maana mimi ningelisemaje kwako, ..hebu nijishushe hapo, baada ya tukio lile, ningelionekana na wewe tena,  si ndio ningepeleka tena jela nikafie huko.., nakumbuka niliwahi kuandika barua kuja kwako, lakini sikuwahi kupata majibu...’akasema.‘Barua,…. hahaha..nani ana mipango ya barua siku hizi, ulindika hiyo barua kuja kwangu ukampa nani..mbona sijawahi kuona barua yako yoyote,...?’nikamuuliza,  niliona kama ananitania tu.‘Basi nahisi kuna mtu alikuwa akizipokea na kuzichana, mimi niliandika, nyie si mna box la barua, na kuna mtu alisema anakuja huko kwenu , nikampa barua, lakini nikajua umeshatekwa na familia yako, na huenda hata wewe hutaki hata kuniona tena, kwa jinsi watu walivonivumishia ubaya....’akasema akitikisa kichwa kusikitika .‘Kwanini usingelinipigia, angalau  hata simu...?’ nikamuuliza‘Nikupigie simu!!! Hahaha…, simu hiyo ningeliipata wapi, huko kijijini, hivi unayafahamu maisha yetu yalivyokuwa...anyway, hayo yameshapita na wewe una mume wako, ...naona nisikupotezee muda, ...’akasema na kutaka kuondoka, mimi nikamshika mkono asiondoke.‘Nimeshakuambia yule sio mume wangu, ni mchumba wangu, hatujaoana bado…Sikiliza, ..ahadi yangu ipo pale pale…’nikasema na hapo akaniangalia kwa macho yenye kushangaa.‘Kwahiyo unataka kusema nini…?’ akaniuliza‘Ahadi yangu ya kufanya lolote ilimradi niwe nimelipa fadhila zako, najua inaweza isikidh haja, lakini angalau na mimi niwe nimfanya jambo kwako la utu wema..sasa mimi nataka tuje tuongee tena nione nitakufanyia nini…’nikasema, na nikaona kama ananywea, hakuridhika na maneno yangu hayo.‘Hapana, mimi sihitajii msaada wako, sitaki kuwa mfanyakazi wenu, au ….kuwategemea nyie tena, hapana…hilo sitaki, …’akasema‘Najua ni kwanini unasema hivyo, ila mimi natamani zile siku zirejee tena, kiukweli mimi sijaolewa, na sisemi hivyo kwasababu kuwa nataka uwe ...mpenzi wangu, hapana mapenzi hayalazimishwi, na…mimi na mchumba wangu hatujafikia huko, bado kuna mipango mimi, yeye na mimi pia, lakini mimi ninaweza kufany ajambo la kukusaidia ukafika mahali, usilipuuzie hilo..’nikasema‘Hilo la kukutana kuongea tena, ni wewe, kama huogopi huyo mpenzi wako, sitaki kuja kuwaharibia mahusiano yenu, ikawa ndio sababu ya kufichua yale yaliyopita, sipendi hilo kabisa,…’akasema‘Kiukweli unanidai sana, mengi umenifanyia, lakini sijaweza kulipa chochote kwako, kwangu mimi naona ni deni, na nataka uwasamehe wazazi wangu, hata bila ya wao kufahamu, na hilo naweza kufanya nionavyo mimi, niamini tu,…usijali kabisa kuhusu hisia za wazazi wangu, nafahamu ni kwanini wanafanya hivyo,....’nikasema‘Hahaha, hapana , niliapa kuwa sitaajiriwa kwa watu kama mfanyakazi wa upendeleo, mimi nataka nihangaike kivyangu…sawa nashukuru kwa kuonana nawewe, mengine  tuyaache kama yalivyo, vipi maisha na mchumba wako, katulia siku hizi..?’ akaniuliza‘Mchumba wangu hana matatizo, ni mzungu kwakweli, muhimu nimuambie ukweli tu, hata akiniona tunaongea, yeye atadai nimuambie wewe ni nani, na ni hivyo, sina shaka naye, ila hayo hayana msingi, wewe sifikiria wako langu la kukuwezesha, unalionaje hilo…’nikasema‘Mhh…sivyo nitakavyo, najua hutanielewa, ndio maana nasema tuyaache tu, yabakie kama yalivyo, kwa maana mimi nilikufanyia nini kikubwa, ni kawaida tu, na yaliyotokea hadi wazazi wako kufanya hivyo, ni…naweza kusema hata mzazi mwingine huenda angelifanya hivyo…’akasema‘Hapana lile tukio lilikuwa kubwa, na kiukweli nakiri wazazi wangu walikosea, sana,..maana hawajui ulivyofanya, uliweza kuniokoa mikononi mwa wabakaji, mijitu mikubwa, na wewe ulikuwa sio umbile lako kabisa, ukapigana na wao kufa na kupona, hawakuliona hilo.Kiukweli mimi..sitalisahau hilo kamwe, nilikuona kama mtu maalumu sana kwenye maisha yangu ndio maa niliahidi siku nikikutana nawe, nitafanya lolote lililondani ya uwezo wangu, ili na wewe uone kuwa nakujali…...’ nikamwambia.‘Mhh…nilishaipata hiyo zawadi inatosha., wewe wasalimie wazazi wako na mchumba wako, mungu akipenda tutakuwa tunaonana, lakini nisingelipenda wafahamu kuwa tumekutana nafahamu watakavyojisikia, huenda ikaja dhahama kubwa zaidi ya ile…japokuwa sasa nimekuwa mkubwa siogopi, nafahamu haki zangu...’akasema‘Jamani ina maana hujatusamehe tu…’nikasema‘Usijali sana ndio ubinadamu ulivyo,..nilishawasamehe mbona…kwa hivi sasa nimeliona hilo, kuwa yale waliyoyafanya wazazi wako walikuwa na maana kwao, kwa ajili ya kulinda heshima ya familia yenu, na walitaka kutoa fundisho kwa jamii, na nasikia familia yenu imekuwa ikiogopewa sana,..ni sahihi, yamepita yapite.‘Tatizo wewe hufahamu jinsi gani niliumia...lakini ikafika mahali nikasema basi tena, mungu ndiye atakupeni yale yote mliyotutendea wewe na baba yako, na nikatubu sana kwa niaba ya wazazi wangu…kiukweli baba yako nilimuona kama baba yangu mkubwa...sikupenda kumuita babu, kama walivyozoea kumuita wengine, mimi ninajua kuzeeka kwake haraka ni kutokana na hali ya maisha, umri wake haupo mbali na umri wa baba yangu, …mimi nilipenda kumuita baba mkubwa.....’nikasema.‘Nashukuru kusikia hivyo, ni wewe tu ulikuwa tofauti na wengine, sijui kwanini wazazi wako, walikuja kutuchukia hivyo..niliona kabisa hawakupenda, hata nikukaribie..na nahisi  ilipotokea lile tukio, ndio wakaonyesha hisia zao dhidi yangu. Ni sawa, labda nisiwalaumu sana, maana huenda hata sisi tungelikuwa kwenye hiyo hali tungelifany ahivyo hivyo..hata hivyo nawashukuru wazazi wako, kwani pamoja na hilo tukio lakini walitusaidia sana kimaisha...’akasema.‘Mimi nilikutafuta sana, lakini sikutaka wazazi wangu walifahamu hilo, nilitaka kukulipa fadhila zako, niliahidi moyoni kuwa nikija kuonana na nawewe, nitafanya  lolote na nimekkuona naomba usilipinge ombi langu....’nikamwambia.‘Mimi sihitaji msaada wenu, ….’akasema‘Hapana ni lazima nifanye wema wowote, nakumbuka kama isngelikuwa ni wewe..sijui ingelikuwaje, na….’hapo tena ndio lile tukio likazama kwenye ubongo wangu nikawa naliona lilivyotokea….**********Ilionekana wazo hao vijana watukutu, walikuwa wakinivizia siku nyingi, na siku hiyo gari la baba lilichelewa kuja kunichukua shuleni, nikaamua kutembea na wenzangu, na kwa vile shule ilikuwa mbali, wenzangu wakawa wametawanyika kila mmoja na njia yake, ikafikia mahali nimebakia peke yangu, na ghafla ndio nikavamiwa na vijana wanne, na kunibeba juu kwa juu.Walinibeba juu kwa juu, hadi vichakani, na wakaanza kunivua nguo, na ukumbuke nilikuwa binti mdogo tu, nasoma sekondari..nilikuwa binti, nimeshavunja ungo, lakini sikuwa na mawazo hayo kabisa, na sikujua ni kitu gani kitakuja kunitokea,..japokuwa nilifahamu kuwa wanatka kunifanya kitu kibaya.Nilijitahidi kupigana lakini sikuweza kufurukuta kwa vijana hawa wenye nguvu zaidi yangu, na kabla hawajafanya lolote mara akatokea mtu, kijana..machozi yalishatanda usoni sikumuone vyema, akawa anapigana nao, akiwa na kigongo hivi kama rungu, alipambana nao kiume mpaka anakuja kuwazidi nguvu, ilikuwa ni kwa msaada wa mungu tu maana wote walikuwa wakibwa zaidi yake…ikafikia muda, ikabidi wakimbie, baada ya kusikia kelele za watu, wakikaribia eneo hilo..na yule kijana akapiga ukelele kuomba msaada. Wale vijana wakakimbia huku wakilaani kuwa watahakikisha wananifanyia hivyo, siku yake...Sikuweza kuongea nililia hadi nyumbani, nikiwa nimechafuka, nguo zimechanwa, nnipo kama nudu uchi…na huyo kijana alinsiindikiza hadi nyumbani, nikawahadithia wazazi wangu, na wao kwa haraka wakaifahamisha polisi na hawo vijana wakaanza kutafutwa lakini hawakupatikana kwa siku hiyo hata ya pili yake. Walihama kabisa, kijini hapo.Cha ajabu wazazi wakaongea na polisi wakaja kumshikilia huyo kijana kuwa atakuwa anawafahamu hawo watu, na alitakiwa kuwataja, na aliposhindwa kuwataja, wakamshitakia kuwa ni muhusika wa tukio hilo, ..wanasema walivyomuhoji, alivyojieleza inaonekana kama analifahamu hilo tukio na yeye alikuwa mwenza wao, japokuwa alikana kabisa.Baadae akafunguliwa mashitaka, na yote hayo wakati yanaendelea mimi nilikuwa sifahamu kinachoendelea kwani ilibidi niondoke hapo kijijini kwa usalama wangu, kwa vile walitishia kuwa ni lazima watanifanyia tena..ikabidi baadae wazazi wangu wanihamishe kabisa kwenda kusomea sehemu nyingine. Nilikuja kusikia kuwa kijana huyo kafungwa, na nilikuja kufahamu hilo baada ya muda, mtu alishahukumiwa kufungwa..kwani vijana wale waliofanya hivyo hawakuweza kupatika,ila mmoja wao alipatikana na alipofika mahakamani, akadai kuwa kijana huo alikuwa mmoja wa wenzao, walipanga wote, kulifanikisha hilo, nay eye ndiye alitoa maelekezo jinsi gani wanaweza kumpata huyo bint.Baba wa huyo kijana akawa anafika mara kwa mara kwa wazazi wangu kuomba kijana wake asamehewe, lakini haikusaidia kitu, na alichoambulia ni kufukuzwa kazi...hayo yote nilikuja kuyafahamu baadaye, na nilipolifahamu hilo nikawaambia wazazi wangu kama hawatamuachia huyo kijana aliyeniokoa basi mimi nitajiua...Hilo nilidhamiria kweli…Wazazi wangu awali walifikiri natania, wakaja kunifuma nataka kunywa sumu, na walipoona hivyo,  ndio baadaye wakaenda kuongea na polisi na baadae mahakama, kuwa kijana huyo aachiwe, wao wameshamsamehe..ili ifanyike maongezi, wanayojua wao wenyewe na ndio kijana huyo akaachiwa, hata alipoachiwa sikuweza kuonana naye tena wala baba yake, kumbe waliamua kuhama kabisa hapo kijijini, na baadae hata wazazi wangu wakahamia Dar, ndio ikawa mwisho wa kuonana na huyo jamaa hadi hii leo ndio nakutana naye…***********.‘Kwakweli sitaweza kusahau wema wako huo, uliniokoa kwenye janga, huenda ningelikufa, …’nilimuambia siku tulipokutana naye tena.‘Ile ni kawaida tu, mtu yoyote muadilifu angelifanya hivyo hivyo, na haina haja, kulipwa kwa kitendo kama kile, na sizani kama kuna kitu unaweza kunilipa kikazidi yale ya moyoni kwangu...’akasema na kuinama chini.‘Una maana gani,ya moyoni mwako, yapi hayo..… ?’ nikamuuliza.‘Mimi niliahidi siku ile ulipoleta chai na mkate, nilikuambia mimi nitakuja kukuoa, wewe uliona kama utani, nilimuambia hata baba, alinicheka sana,..nakumbuka hata wewe ukasema mungu akipenda,..ukimaanisha kuwa umekubali au sio…’akasema‘Lakini yale yalikuwa ya ujanani, na niliongea vile kama maongezi tu, ulitaka mimi niseme nini pale, na ni mambo ya ujanani, hayana maana au sio…’nikasema‘Hayana maana, ndio unasema hivyo, kwangu yalikuwa na maana sana, mimi nilikupenda na …samahani, nikisema hivyo, kuwa siku zote nimekuwa nikikupenda, na kutamani uwe mke wangu, usichukie, ila naelezea hisia zangu, najua ni ndoto za Alinacha, lakini ndio ukweli kutoka moyoni mwangu…’akasema‘Aaah, hapana,…sawa nashukuru kwa kusikia hivyo, na…hata sijui niseme nini, naogopa, nitakuja kuuumiza , naomba unipe muda..’nikasema‘Hapana nafahamu, huna haja ya kusema lolote, haiwezekani, mtu kama mimi kukuoa wewe, najua, ila sijui …’akasema‘Kwanini unasema hivyo…utampata msichana mwingine kwani mimi ni msichana peke yake hapa duniani..’nikasema‘Sijaona kama wewe, na wewe ndiye uliyeuteka moyo wangu, kama sio wewe basi, mimi naomba mungu nisioe tena, na nitaishi hivi hivi maisha yangu yote…sitaki shida…’akasema sasa akisimama kuondoka. Hapo nilibakia nikiwaza, sikujua kabisa mwenzangu kadhamiria hilo, na..kiukweli moyoni sikupenda kuja kumuudhi mtu kama huyu, ambaye naona kama ananidai … Moyo wa huruma uliniingia, nikikumbuka yeye ndiye aliniokoa, vinginevyo sijui ingelikuwaje, na zaidi ya hayo, ananijali sana, kiukweli docta nampenda, na kwa vile pia yupo kwenye hadhi inayoendana na …tusema hivyo..lakini huyo nimetokea kumjali, na labda kuna upendo lakini sio kwa vile…sasa nifanyeje..ilinipa wakati mgumu sana, nikijua kuna wazazi wangu, ambao hawatalisikiliza hilo kabisaBasi siku hiyo akaondoka, na hatukuweza kukutana kwani nikifika naambiwa katoka, nikimpigia simu hapokei.************ Baada kama ya mwezi hivi tukaja kukutana tena, tukaongea mengine , hakupenda kuliongelea hilo tena, nikajua keshakubali ukweli, kwahiyo hilo halipo tena, na huku kwa docta, naye kaanza kunisakama, anataka tuanze michakato ya ndoa..‘Niambia, lile wazo langu vipi…?’ siku moja akaniuliza sikutarajia hilo swali.‘Unajua, wewe unachukulia ndoa kama ni kitu rahisi hivyo, ujue mimi nina wazazi, na ndoa inakutanisha familia mbili, wakiwemo wazazi, sasa hebu jiulize, wazazi wangu wataliridhai hili,...je wewe umejiandaaje kuishi na mke, maana usije ukasema unanioa, kwa vile…’nikasema‘Mimi nimeshajiandaa kwa hilo, sio kwamba nakuambia kwa vile…ninachumba na varanda nimepanga, nina kiwanja kijijini, urithi wa baba, nitauza seehmu nitajenga nyumba,…tutaweza kuishi tu..lakini sikulazimishi, maana kiukweli hutaweza kuishi maisha y akitajiri kihivyo...’ akasema.Baada ya maongezi hayo, nikawaza sana, nikajiuliza sana, nifanye nini…maana sikuwa nimelichukulia kwa maana hiyo tokea awali,…nikaanza kujenga hisia za kumpenda tu…na huku kwa docta nikawa naharibu, ikawa siivani naye kwa kila anachokifanya.‘Vipi kwani kumetokea nini, nakuona umebadilika sana siku hizi, kama kuna tatizo lolote niambie mimi nitakuelewa tu mpenzi, sitaki kabisa, kukulazimisha kwa lolote lile, umenielewa, sitaki nikuoe ukiwa hunitaki, unasikia, unieleze mapema…?’ akaniambia‘Hakuna  tatizo lolote!....’nikawa namwambia hivyo maana bado nilikuwa sijaamua moja kwa moja, nikijua kuwa wazazi wangu hawataweza kunikubalia kumuoa huyoNikawa sasa najenga ukaribu sana na huyo jamaa hadi docta akaja kugundua mwenyewe, na aliponiuliza nikamwambia ni rafiki yangu nakutana naye tu na hawezi kunizuia‘Nimeshakuambia uwe muwazi kwangu, kama hupo na mimi , sawa, mapenzi hayalazimishwi, lakini nataka uwe muwazi, unanielewa, sitaki kupoteza muda wangu na mtu asiye na matarajia na mimi..’akasema‘Sawa si unataka jibu, sipo na wewe,… nataka kufikiria zaidi, kama una haraka kuoa katafute mwingine....’nikamwambia hivyo, kiukweli ilimuumiza sana, na akavumilia kwa kipindi fulani, baadae akalifikisha kwa wazazi kuona kama wataweza kusaidiaWazazi wangu waliposikia hivyo, hawakuamini…wakaamua kufanya uchunguzi ni nani kanighilibu, na baadae wakaja kugundua kuwa ni nani huyo ninayekutana naye mara kwa mara, na kipindi hicho nimeshamsaidia huyo jamaa hadi akapata kazi kwenye kampuni kubwa, na akaweza hata kujenga nyumba yake mwenyewe…nilitaka nifanye hivyo baadae…kama atampata mtu mwingine basi.Lakini kumbe mwenzangu anajua kuwa nayafanya hayo kwa ajili ya maisha yetu ya baadae, kukapita kipindi kirefu hapo,…sio jambo la miezi, hapana ilichukua karibu miaka miwili hadi docta akakata tamaa na mimi.....Siku moja wazazi wangu wakanikalisha kikao,  walikuwa wamekasirika kweli kweli..‘Hivi wewe una akili kweli,..hivi wewe hujaona mwanaume, hadi umchague huyo mtu,..kama kweli nia yako ni kupata mwanaume mwingine zaidi ya docta, huyo hakufai, yule ni mlalahoi, mtoto wa mlinzi wetu...bwana shamba, asiye fanana kabisa na hadhi yako, mbona unataka kutuaibisha....kwanini unamkataa docta, msomi , familia yao ni ya kiheshima, matajiri.....’akasema baba.‘Baba mimi sio mtoto mdogo, na sina lengo la kuwaabisha, mnakumbuka nilitaka kubakwa nikiwa kule kijijini, niliwaambia ni nani aliyeniokoa, ....mlifanya nini kwa huyo aliyeniokoa, ..badala yake mlikimbilia kumshika yeye ati alikuwa anawafahamu hawo watu waliotaka kunibaka, mkamfunga hata bila ya mimi kujua, kwa vile tu ni mtoto wa masikini..iliniuma sana na niliahidi kuwa ipo siku nikipata nafasi nitamsadia ili kulipa fadhila zangu kwake, na kutubu madhambi mliyoyafanya...’nikasema.‘Kwahiyo malipo yake ndio hayo, kutudhalilisha sisi au sio...sikiliza, kama sisi ni wazazi wako, tunasema achana na huyo mtu, sisi ni wazazi wako tulijua ni nini tulichokifanya, wewe hukuona kilichotokea, baada ya kumshika yeye na kumfunga, kijiji pale tuliogopewa sana…, hakuna hata mtu aliyewahi kuichezea familia yetu tena....sisi tulifahamu ni nini tulichokifanya, kutoa fundisho kwa wengine....’akasema baba‘Mtoe fundisho kwa mtu asiye na hatia,...kunikoa kwake ndio imekuwa taabu, kama asingelifanya hivyo nikabakwa, huenda ningelifikia kupoteza maisha au kuambukizwa magonjwa, mngelisemaje, ndio fadhila zeni hizo,  wema wao ndio malipo yake hayo,hapana mlifanyavibaya sana…’ nikasema‘Je na sisi tusingelifanya hilo, ikatokea tena, maana walidhamiria kweli kulifanya tena kukukomesha , na wale waliotoroka, walikamatwa wakiwa na mipango hiyo …walitaka hata kuja kuchoma nyumba na maeneo yetu..hujui kabisa yaliyokuwa yamepangwa …’akasema‘Wazazi wangu hamuwezi kujua ubaya huo unaweza ukawageukia nyie wenyewe siku moja, …au ubaya huo uje utendwe kwa watoto wenu, ili iwe fundisho, ...hamjui kibao kinaweza kuwageukia  nyie siku moja kwa tatizo jingine, hujafa hujaumbika...msijione kuwa nyie ni matajiri hamtaweza kupata shida, mung anaweza kuibadili hali bila kujua, kisa ni haya mnayoyaona ni madogo tu...’nikasema kwa sauti ya huzuni na mama akanionea huruma na kuniuliza‘Kwahiyo ewe ulikuwa unatakaje, tukae kimiya tu, wakati wahuni walishaanza kuiingilia familia yetu, tulifanya vile kwa ajili ya kuilinda famila yetu, na tulipofanya hivyo ilisaidia. Na baadaye tulimtoa, na tukampa pesa za pole,...japokuwa mzazi wake alizikataa lakini baadaye akazichukua hali ilipozidi kuwa mbaya....ile ni kawaida kwa mzazi yoyote anayetaka kulinda familia yake...’akasema mama.‘Mimi sitawaelewa kamwe, na mimi najua nafanya nini, itafikia mahali, nikiona kampata mtu wake, basi..lakini kwa hivi sasa sitaki kuolewa na docta…’nikasema,‘Sasa unataka nini, maana huyo kijana keshasema anataka kukuoa,..lakini sisi kamwe hatutakubaliana na ndoa hiyo,…’wakasema‘Baba mimi naona hatutafika popote kwa hili, ila nawaomba, ..kwa vile mimi ndiye niliyefanyiwa hilo, na namfahamu ni nani aliyenifanyia wema kwa kuniokoa, mniache tu, najua ni nini ninachokifanya, maana kwangu, alilonifanyia ni deni kubwa sana,..na.niliahidi kuwa nitamlipa fadhila zake, ....’nikasema.‘Kwahiyo unataka kumlipa fadhila gani...?’ akauliza mama.‘Hilo niachieni mwenyewe....sijaja kuwaomba chochote kwenu kwa ajili yake....’nikasema.‘Achana na huyo mtu, kama unataka kumuona akiendelea na maisha yake, achana naye, na kama unataka akaishie jela, endelea naye....hatuwezi kukuona ukituzalilisha ....atapotea kama alivyopotea baba yake....’akasema baba.‘Ina maana mnafahamu kuwa baba yake alifariki,,...?’ nikauliza kwa mshangao.‘Tumeshakuambia achana na hiyo familia, vinginevyo utajua kwanini hukutusikiliza....’akasema baba, na mimi moyoni nikasema‘Kama ni hivyo basi, nitakubali anioe, ili kuondoa kabisa hiyo dhana ya madaraja..najua wazazi wangu wamekosea, na hawataki kutubu, basi mimi nitatubu kwa niaba yao,na njia pekee ni kukubali kuolewa na huyu mtu basi…’nikapanga hivyo…NB: Kisa ndani ya kisa….ndivyo kisa hiki kilikuwa …kama nawachosha mniambie..WAZO LA LEO: Utofauti wetu wa hali za kiuchumi usiwe ni tija ya kutokujali utu wa mtu, utu wa mtu haununuliwi kwa pesa au mali, utajiri wako usiwe tiketi ya kudharau wengine, na kuwaoana hawana thamani, ukifanya hivyo,hutakuwa na amani katika maisha yako, kwani kilio cha hawo unaowatendea hivyo kitakuandama.‘Shemeji samahani nilikuwa nataka kukuuliza maswali kama hutojali...’ sauti hiyo ilinishitua kutoka kwenye dimbwi la mawazo ya maisha yangu yaliyopita.‘Unaonekana upo kwenye mawazo mazito, pole sana, najua unavyojisikia lakini usijali mumeo atapona tu….lakini baada ya hili, nawashauri kwa nia njema tu mkae muone tatizo lipo wapi ….’Alikuwa ni docta ambaye alizoea kuniita shemeji.Docta mara nyingi amekuwa mshauri wangu, hakujali yaliyopita kuwa tuliwahi kuwa wapenzi, hakujali, kuwa huyo mume wangu ndiye aliyefanya akanikosa mimi..ndio hapo unapoweza kumuona docta mtu alivyokuwa mtu wa peke yake.Nikamwangalia machoni kabla ya kumjibu, na yeye kwanza akatabasamu, pili akaonyesha uso wa kushangaa, na kabla hajasema lolote zaidi nikasema.‘Naomba usiniulize maswali ya kuzidi kuniumiza kichwa changu, maana leo imekuwa siku ya mikasa kwangu, hapa nilipo nina mawazo emngi sana....’nikasema.‘Lakini, …mmh, naweza kusema haya yote umejitakia mwenyewe, usimlaumu mtu yoyote, wazazi walikuambia kuchia mimi mwenyewe, ..anyway, ...sitaki kurudi nyuma, lakini wewe mwenyewe unalitambua hilo...’akasema .‘Ndio hayo siyataki kuyasiki, maana hayatanisaidia kitu,..nafahamu sana unamaanisha nini, lakini nikuambie ukweli, haya yanayotokea hayana msingi kabisa na mambo yetu ya nyuma, na unafahamu kabisa kwanini nilichukua uamuzi huo, na sitajutii kwa hilo...’nikasema.‘Kulipa fadhila...eeh, haya endelea kulipa fadhila, kiukweli, mimi nimekuvulia kofia, upo tayari kuyaweka maisha yako, rehani…kwa sababu ya kulipa fadhila, na nini unakipata sasa, eeh, mimi nitaendelea kukusaidia tu, hilo nakuahidi …’akasema‘Najua wewe na wazazi wangu mtasema hivyo sana, ..lakini hamjui ni nini kilicho moyoni mwangu, mume wangu nampenda na nilimpenda toka siku ile ya kwanza, nilipomuoana akiwa na hali yake hiyo hiyo ya umasikini..’nikasema‘Sio kweli…uwadanganye wengine, lakini sio mimi…’akasema‘Lakini kwanini unasema hivyo, mimi nimefanya kosa gani, kuwa eti kwa vile nimeolewa, mnayemuita wa daraja la chini au masikini,…hahaha,  hebu niambie sasa hivi ana umasikini gani, mbona mpo sambamba kimaisha, ni hali ya kusaidiana na kuinuana,....’nikasema kama namuuliza.‘Mimi sijakulaumu kwa uamuzi wako huo, lakini tabia za watu hazijifichi, zingine ni za kihistoria, hata ufanyaje ni kama vile wanavyosema, …mmh,  kuwa kunguru hafugiki,.. na ndivyo maisha yetu yalivyo, misingi ya kizalia ni vigumu sana kuigeuza...unajaribu lakini ipo siku itatokea na tabia itajionyesha na kukuathiri...’akasema.‘Tatizo lako wewe ni dakitari lakini ukifikia kwenye maswala haya unaacha udakitari wako pembeni, hutaki kuutumia hata katika mambo kama haya, kizalia kina nini na maswala ya mapenzi, ..kuacha kuolewa na wewe  imekua ni nongwa, kwani huyo mkeo uliyempata humpendani...mbona mimi sijaingilia maisha yenu..?’ nikamuuliza.‘Tuyaache hayo nataka kukuuliza mambo ya msingi, maana pamoja na yaliyotokea nyuma, bado nakuona wewe ni rafiki yangu, na mumeo ni rafiki yangu pia, ndio maana nilipogundua kuwa ndio yeye unayemtaka, sikutaka kupambana kwa vyovyote vile, niliona nikuachie tu, kwa vile ulinitamkia mwenyewe kuwa unampenda,..na ukaja kunitamkia kuwa mimi hunipendi tena…, nikaona kwanini ning’ang’anie mtu asiyekupenda,.....’akasema.‘Uliza maswali yako bwana, sijasema kamwe sikupendi, nilikuambia sababu za uamuzi wangu, na unazifahamu sana ...’nikasema na yeye akaniangalia kwa muda, halafu akasema;‘Nataka nikuulize maswali ya ndoa yenu,...’akasema‘Kama ni maswali kuhusu ndoa yangu, ningelifurahi kama ungeyaacha kama yalivyo, kwani akili yangu haijatulia, siku ya leo imekuwa ni ya mitihani, tangia asubuhi, ni matatizo, ofisi matatizo..nyumbani matatizo, huko kwa rafiki yangu matatizo..’nikasema‘Kwa rafiki yako kuna matatizo gani…?’ akaniuliza‘Haya hebu niulize, tuyaache hayo, unataka kuniuliza kuhusu nini?’ nikasema nikijua ni yale yale ambayo mara kwa mara ananilaumu eti kwanini nilimkataa yeye nikaamua kuolewa na huyo rafiki yake.‘Shemeji ...rafiki yangu…mpendwa…hahaha, wakati mwingine naogopa kuongeza maneni hapo..nikuambie kitu, iIli kuondokana na huko kuchanganyikiwa kwako ni bora ukajaribu kuyaongea hayo matatizo uliyo nayo kwa mtu anayeweza kukusaidia,..’akasema.‘Hapana, mimi nakufahamu bwana, ...wewe na wazazi wangu siku zote mnaombea ndoa yangu ivunjike, hebu nikuulize, kwa mfano ndoa yangu ikivunjika utapata faida gani, maana wewe sasa una mke, utamuacha mkeo ili uje unioe mimi, au ndio mnataka kunikomoa...?’ nikamuuliza.‘Hahaha..hivi wewe unafikiri mimi nachukia ndoa yenu, kuwa natamani ivunjike eti kwa vile ulinikataa, acha hiyo, mimi mumeo ni rafiki yangu,...unalifahamu hilo fika, na kama asingelikuwa ni rafiki yangu ningelipambana hadi nihakikishe nimekuoa, lakini niliona hakuna haja, kwanza umepata muda wa kumsaidi rafiki yangu ambaye katokea kwenye shida,....sitaki hata kumuongelea kuhusu maisha yake ya huko nyuma, na kwa kupitia kwako, nimeweza kulipa fadhila zangu pia...’akatulia.‘Najua hilo mtalirudia kila siku...na hamtafanikiwa, maana sasa mnaishia kumuonea wivu, ana kampuni, ana maisha mazuri,..nini tena cha kumsuta , hakuna, iliyobakia sasa ni majungu, nashukuru kwa ushauri wako wa mara kwa mara sikatai, ila nisingelipenda unilaumu kwa uamuzi wangu huo...’nikasema.‘Haya bwana, ngoja nikuulize hayo niliyotaka kukuuliza ili uone kuwa mimi najali sana ndoa yenu,...’akasema‘Uliza, na nitakujibu,....lakini kama ni mambo ndani ya familia yangu,sitaki...’nikasema‘Hebu niambie ukweli, mume wako alikuwa wapi, kwani watu walioona hiyo ajali wanasema mume wako alikuwa akiendesha gari kwa mwendo wa kasi sana...kama vile alikuwa akikimbizwa,au akikimbia jambo?’akaniuliza na mimi hapo nikashituka, nikikumbuka kuwa hata mimi nilifanya hivyo hivyo.‘Unataka kusema nini hapo, kuwa mume wangu…ni mhalifu au…?’ nikamuuliza.‘Nataka kujua kama unafahamu wapi mume wako alikuwepo leo hii, kabla ya hiyo ajali…kuna maswali mengi yanaulizwa, na yataulizwa na polisi pia, …?’ nikamuuliza‘Kwani hawo watu wanasema alikuwa akitokea wapi...!?’ nikamuuliza huku nikiashiria kushangaa na sijui kwanini niliuliza swali hilo badala ya kujibu swali.‘Shemeji mimi nakuuliza swali na wewe unaniuliza swali, kwani siku ya leo toka asubuhi, ...mliagana vipi,  na mchana kutwa, hamkuwahi kuwasilina, hamkuonana, au kuambizana mnakwenda wapi, mnafanya nini....nafahamu unafahamu wapi alipokuwa akitokea au hufahamu?’ akaniuliza.‘Sikiliza nikuambie, mimi na mume wangu tuna mishughuliko tofauti, kila mmoja akiamuka asubuhi anakwenda kwenye shughuli zake kivyake vyake, hakuna kufuatana..hayo ndio maisha yetu na sitaki uniulize kwanini maana hata mimi sijakuulizia kuhusu maisha yako wewe na mkeo, au sio…’nikasema.‘Sio hivyo, ninachotaka hapa ni kuwasaidia, na wala sio kubomoa, na hata kama wewe ungeliona kwenye nyumba yangu kuna matatizo na kwa vile tunafahamiana, ungeliniuliza, ili uone kama unaweza kunisaidia au sio...’akasema.‘Sijaomba msaada kwako, mimi na mume wangu tuna utaratibu wetu wa maisha na hatuna shida na hilo,, na haikuwa na umuhimu kuliulizia hilo, ni kama simuamini mume wangu..’nikasema.‘Lakini mwenyewe kwa kauli yako hapa, umesema siku ya leo imekuwa na mitihani mingi,ukasema matatizo nyumba, matatizo kwa rafiki yako....hii inaashiria nini, kama sio mna matatizo wewe na mume wako, kwanini hutaki kusema ukweli nikaweza kusaidia, hata kiushauri tu...?’ akaniuliza.‘Hatuna matatizo, na kama yapo ni ya kawaida tu , ya mume na mke..hayakuhusu, na kama yangelikuwa makubwa, ningekuuliza, mbona mara nyingi nakuuliza, au kuna jingine...’nikasema.‘Sawa, bado hujanijibu swali langu, ....’akasema.‘Swali lipi zilipendwa....?’ nikamuuliza na kucheka, yeye hakucheka, akasema;‘Hebu niambie utaratibu wenu wa leo ulikuwaje, ..?’ akaniuliza na mimi nikamwangalia kwa makini, nikaona nisibishane naye sana nikamwambia;‘Sisi utaratibu wetu ni kuwa, kwa vile kila mmoja ana kampuni yake, na ana mambo yake, tukiamuka kila mmoja ana hamsini zake, hatuaingiliani kabisa, wakati mwingine kama ni lazima ndio tunapeana taarifa, ...’nikasema.‘Hiyo ni kwa ujumla je kwa leo ilikuwaje, ...?’ akaniuliza, na sikumuelewa ana maana gani, kwani maswali yake niliyaona kama ya polisi nikasema.‘Ama kwa leo, nakumbuka aliniambia kuwa akitoka kazini anaweza kupitia kumona mke wa rafiki yake ambaye kajifungua, ...nakumbuka aliniambia kitu kama hicho, na sikuwa makini sana kumsikiliza maana nilikuwa na mambo mengine ya kikazi yalikuwa yamenitinga...’nikasema.‘Mke gani wa rafiki yake, aliyejifungua…?..., alikwenda kumuona mzazi, au mume wa huyo mzazi, maana mimi nijuavyo mara nyingi mke akijifungua wanaokuwa karibu na huyo mzazi ni wanawake, kwahiyo ilitakiwa wewe uende naye....au nimekosea?’ akauliza‘Kwahiyo unataka kusema nini hapo..?’ nikamuuliza‘Sitaki kusema kitu, ninachotaka ni ukweli ili niweze kusaidia,...kama ningelikuwa nataka kusema kitu, kwanini nikuzunguke, wakati wewe ni rafiki yangu, na mume ni rafiki yangu pia....’akasema.‘Nakuuliza hivi kwa maelezo yako una maanisha nini kuhusu rafiki yako?’ nikamuuliza‘Inawezekana  hakuwa katokea kazini,....maana mimi nilimpitia na nikaambiwa kuwa ametoka mapema tu, kikao chao kilivunjika mapema, kuna mambo yalikuwa hayajakamilika, kwahiyo alitoka mapema ofisini kwake,...’akasema docta.‘Mimi siwezi kujua  mipangilio yake, na siwezi kutabiri kuwa alikuwa wapi, ...kama hakuwepo kazini, basi alikuwa kwenye shughuli nyingine nje ya kazini kwake, hilo linawezekana na hilo la kusema mzazi ni lazima muandamane na mke wako, halina mantiki yoyote kwangu…, wewe unachotaka hapa ni kujenga sababu ya kumuona mume wangu ana tabia mbaya....’nikamwambia.`Shemeji lakini nakumbuka tulishaliongelea hili kabla, nilishawahi kuwakanya haya maisha yenu mnayokwenda nayo, ...sio mazuri kwa mke na mume, kiukweli kwa wanafamilia hilo sio jambo jema, hata kama mnaona kuwa huo ni usasa, au wengine wanasema ni uzungu...mimi siupendi. Mimi nawajali sana, kuliko unavyofikiria wewe....’akasema.‘Nashukuru kama unatujali, na ningelishukuru kama unalosema linatoka moyoni na lina ukweli, kwani hata wazazi wangu wanasema hivyo hivyo, wakati walishatamka kuwa,....nikiendelea na mume wangu watahakikisha maisha ya mume wangu yanakuwa ni mashaka, na huenda akaishia jela...nikakumbuka kauli ya wazazi wangu wakisema;‘Wazazi ni wajibu wao kumlinda mtoto wao, hata wewe ukifikia mahali pako, utasema hivyo hivyo kwa binti zako, hutapenda aende kuishi na mtu ambaye humuamini..’akasema.‘Haya unatushauri nini Docta...’nikasema kwa dharau.‘Mimi nasema hivi maisha hayo mnayoishi yana madhara yake hasa katika maisha yetu haya ya kiafrika,...miundo mbinu ni mibaya, hali za barabarani tunazijua wenyewe, usalama hauna uhakika, kwahiyo ni vyema kuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na kila mmoja kumjua mwenzake yupo wapi na anafanya nini, kwani simu zina kazi gani?’ akaniuliza.‘Unanichekesha kweli, ...yaani umefikia hatua ya kutudharau kiasi hicho...’nikasema‘Lakini mwenyewe umesema kuwa kila mmoja ana mambo yake, na leo hukujua kabisa kuwa mume wako alikuwa na taratibu gani, za nje ya kiofisi....sasa utajuaje mwenzako yupo wapi, kama likitokea tatizo....’akasema huyo docta na mimi sikuwa nimemuelewa sana, nikamsikiliza tu aendelee kuongea.‘Endelea doct-aah’ nikasema kwa dharau‘Mimi siwapingi kwa utaratibu wenu huo wa maisha, lakini ni vyema mkajenga tabia ya kuambizana wapi mmoja anakwenda, sio kila mtu akirudi nyumbani yupo kwenye laptop yake ...kila mtu yupo bize, na kazi zake, mnasahau majukumu yenu ya ndoa...’akasema kama mzazi anayemuelezea mtoto wake aliyekosana na mkewe.‘Umekuwa kungwi siku hizi au mwanandoa mzoefu, ...nyie mnajipa moyo kuwa ndoa yenu ipo safi eehe,  haina matatizo au sio, unaiona ndoa yangu ndiyo yenye matatizo au sio....?’ nikamuuliza.‘Mimi siwezi kujigamba kuwa ndoa yangu haina matatizo, yapo na kila ndoa ina matatizo yake, lakini yakizidi ni lazima tuambizane, ni mimi nawaasa, kama wewe ungeliniasha mimi ukiona utaratibu fulani sio mnzuri kwenye ndoa, hasa huo mnakwenda nao.’akasema na mimi nikahisi kukerwa na hayo maneno yake, niliona kama ananiingilia maisha yangu ya ndoa, japokuwa sikutaka kumkatiza, nikatulia tu.‘Mimi kiukweli sifurahishwi na tabia hiyo, halafu rafiki yangu huyu, siku hizi anaonekana kunywa sana pombe, bila mpangilio, naufahamu unywaji wake, huu wa sasa ni ulevi, sio unywaji...’akasema na mimi hapo nikaa kimia tu.‘Mimi nionavyo, ana tatizo,  ana msongo wa mawazo, ...mimi kwasababu ya safari zangu za hapa na pale, sijaweza kukaa naye tukaliongelea hili kwa kina, ila kila muda nilipopata nafasi kidogo ya kuwa naye, nimemuona sio yule rafiki yule ninayemfahamu..hana raha, anaonekana anakerwa na jambo fulani..nahisi kuna tatizo ndani ya ndoa yenu..’akasema.‘Wewe unahisi kuna tatizo kwenye ndoa yetu....kwani hiyo kuhisi imeanza leo?’ nikawa kama namuuliza‘Ndio maana nataka tusaidiane kwa hilo,...kama kuna tatizo lolote niambie shemeji, hiyo dalili aliyo nayo rafiki yangu inatokana na msongo wa mawazo, shemeji jaribuni kukaa na kuliongelea hili nahisi kuna tatizo..ongeeni ambizaneni, ili muwewe kuishi kama wana ndoa, na sio wabia...’akaniambia huyo dakitari nikacheka kwa dharau aliposema `wabia...’‘Eti eti unasema nini, ndio umefikia huko kuwa tunaishi kama wabia...dharau ya ajabu kabisa...’nikasema na kutuliaNilitulia kwa muda bila kusema neno..hayo maneno ya mwisho yalinichefua,, hasira zikanikaba, maana sikuona tatizo lipo wapi, na sikupenda mtu aniingilie maisha yangu, hasa huyu, ambye alikuwa ni mpinzani mkubwa, kwa vile alitaka anioe yeye. Mara akaja docta kutokea maabara, akapita na kuelekea kwa docta anayemuhudumia mume wangu, hakusema kitu.‘Rafiki zilipendwa mimi sijui kama kuna tatizo kubwa kihivyo, kama yapo ni mambo ya kawaida ya mume na mke. …’nikasema‘Una uhakika kweli na hilo unalolisema…?’ akaniuliza‘Nikuambie kitu, yule ni rafiki yako, kama umeona kuna tatizo nenda ukamuulize yeye mwenyewe, umesikia sana...’nikasema huku nikionyesha kukerwa.‘Shemeji ni sawa...sio kwamba nataka kuingilia maswala yenu ya ndani, hapana, ...na nafahamu kila tukiliongelea hili wewe unayaunganisha maswala haya na mambo yaliyopita, mimi nakuhakikishia kabisa sipo huko, nipo kwenye kuijali ndoa yenu,...’akasema.‘Sawa, nimekuelewa…’nikasema, na aliona sitaki kuliongelea hilo, tukaa kimia kidogo baadae akasema;‘Shemeji samahani nikuulize swali muhimu sana, nililokuwa nataka kukuulizia...usinielewe vibaya, na wala usilipeleke kwenye urafiki wetu wa zamani, ninachotaka kufanya hapa ni kujaribu kuangalia kama kuna tatizo maana nyie mnaweza msilione, lakini mimi kama docta ninaweza kuliona hata kama hujanielezea kwangu, nakuomba nikuulize maswali ya ndani ya ndoa yako, kama hutojali, ...’akasema.‘Wewe uliza tu, sioni ajabu na maswali yako,..nitakujibu kama ninavyojua, ..lakini mimi siwezi kumjibia rafiki yako, yeye huenda anaweza akawa matatizo yake binafsi, lakini kama hajaniambai siwezi kuyajua,..kweli mimi ni mke wake, lakini kama mmoja atakuwa sio mkweli kwa mwenzake, basi hilo ni tatizo lake, na huwezi kukimbilia kumlaumu mke au mume, bila kujua undani  wa maisha yao....’nikasema.‘Shemeji sasa mimi nataka nijue undani wa maisha yenu,..niamini mimi, nina nia njema kwenu, kama mlivyoniamini siku ya ndoa yenu, kama rafiki mkubwa wa mume wako, kama rafiki yako mpenzi wa zamani, nataka niingie ndani ya ndoa yenu, nijaribu kuangalia undani wa ndoa yenu, kama kuna tatizo....tusaidiane’akasema.‘Haya ....Unakaribishwa....ingia maana nimeshachoka kukuambia kuwa hakuna tatizo...sijui nikueleze vipi,..haya uliza hayo maswali ya ndani ya ndoa...’nikasema‘Shemeji, je katika mambo ya unyumba mnashirkiana kama kawaida?’ akaniuliza swali lililonifanya nishituke na kugeuka kumwangalia usoni…huku uso umeonyesha kutahayari…Na kabla sijamjibu, akaniuliza swali jingine,…‘Na huko kwa rafiki yako kuna tatizo gani, je tatizo la huko kwa rafiki yako haliwezi likawa linaingiliana na matatizo mlio nayo nyie wawili,…?’ akaniuliza na mimi hapo nikabakia kimia, nikiendelea kumuangalia kwa uso uliotahayari….‘Ukinijibu kwa uhakika…tunaweza kulitatua hili tatizo lenu, nina uhakika kuna tatizo, na...usipoangalia, utakuja kuniambia, je upo tayari kunijibu hayo maswali, tukasaidiana au..utaendelea kunificha,...?' akaniulizaNikainua uso na kumuangalia, ...na kabla sijamjibu, docta yule anayemuhudumia mume wangu akatokea....NB: haya, mambo ndio hayoWAZO LA LEO: Wakati mwingine unaweza ukawa na matatizo, lakini usijue kuwa una matatizo, wakati mwingine ndoa zinaweza zikawa na matatizo, lakini wanandoa wakajifanya hawana matatizo,…kila mtu akimtegea mwenzake, na kuona mwenzake ndiye anayestahiki kusema, au kulalamika…tukumbuke ndoa ni ya watu wawili, na wote wana dhima sawa ya kuona ndoa yao inasimama imara, tusijenge tabia ya kutegeana, kwani kukiharibika jambo, athari zitakuwa kwa wote, na familia yenu.‘Maswali gani hayo docta unayoniuliza, tulishawekeana mipaka kuhusu maswala ya ndoa yangu, na wewe ulishasema hutajaribu hata siku moja kuingilia ndoa yangu zaidi ya kusaidia kuijenga, au sio, sasa nikuulize…hayo maswala yako yanataka nini kwenye ndoa yangu, sipendi na sitaki, unanielewa…?’ nilikuta namuuliza kwa hamaki, lakini kabla docta hajasema lolote ndio akatokea huyo docta ambaye anamshughulikia mume wangu, na wote tukamsogelea.Mimi nilikuwa sijamuona mapema hadi alipotukaribia…‘Mpaka sasa hivi vipimo havionyeshi tatizo kubwa sana, matatizo yapo lakini sio ya kutisha,.tatizo ambalo limeonekana lipo kwenye uti wa mgongo, ambalo sio kubwa sana, ila inaweza ikachukua muda, kutegemeana na jinsi itakavyokuwa.., tutakuja kulijadili hili baadae,...'akasema docta'Ila kwa hivi sasa itakuwa vigumu kwake kutembea, kuna athari hizo, lakini ni kwa muda,…na kuna vipimo vingine bado, havijawa sawa, ila kwa kifupi ndio hivyo…’akasema docta, na kabla hajaondoka docta huyu rafiki wa mume wangu akamsogelea wakawa wananong’ona kidogo.Baadae yule docta akaondoka, na kutuacha tukitizamana, mimi nikamsogelea docta rafiki , nikamuuliza;‘Ina maana mume wangu atakuwa hatembei tena, kwa muda gani …?’ nikauliza‘Atatembea, ..ila kwa awali ni lazima atembelee kigari cha kukokota kwa mkono, hilo ni tatizo la muda, na kupona kwake kwa hivi sasa kwa haraka itategemeana na nyie wawili, hilo uwe makini nalo sana..’akasema‘Kwa vipi..?’ nikauliza‘Kwasababu pamoja na hayo, mawazo,…kutulizana kwa nafsi, kumliwaza na kumuondolea hofu, inategemeana na wewe ambaye mtakuwa naye karibu, ina maana hata kazi zako zingine inabidi uziache, ili asije akashikwa na msongo wa mawazo…’akasema‘Mhh, sawa ni mume wangu hilo nalifahamu hata kabla ya kuambiwa, hata kama ni kuakia nyumbani siku zote mpaka apone nitafanya hivyo,..ila wasiwasi wangu, kama kaathirika utu wa mgongo mhh!!1…hata sijui nilitaka kuuliza nini…’nikasema Pale nilizama kwenye mawazo, na wakati huo docta alikuwa akiongea na simu alipomaliza, akanisogelea na kuniangalia machoni kwa makini, halafu akasema;‘Najua unawaza nini….lakini ndio hali halisi, …muhimu ni kujua huyo ni mwenzako, na kwa hivi sasa anahitajia ukaribu wako sana, kuliko wakati wowote, na nakuomba sana, usije kumkwanza kwa maswali mengi ya kumtia mashaka…’akasema‘Maswali gani ya kumtia mashaka….mimi siwezi kuwa hivyo, mimi sio mtoto mdogo, najua wajibu wangu..?’ nikamuuliza na kusema;‘Ndio maana nilitangulia kukuuliza yale maswali yangu ya awali, nilitaka uwe tayari kwa matokeo hayo, na nijue jinsi gani ya kukushauri, ili sije ikaendeleza tatizo…’akasema‘Lakini kwanza nikuulize hayo matokea ya vipimo vyake yana athari gani zaidi, ok, mnasema atapona, je akipona, atapona kabisa au …?’ nikauliza nikiwazia mbali zaidi.‘Kabla sijakujibu swali lako nakuomba unijibu yale maswali yangu , maana yana mingi mkubwa wa maisha yenu,…najua, na nilijua utakuja kuniuliza maswali kama hayo, ndio maana nilitaka uniweke wazi, …unelewe hapo,…’akasema‘Mhh…’nikaguna hivyo‘Sikiliza, unaniamini sio…mimi ni rafiki yako, na tulikuwa wapenzi, nakufahamu kama ninavyomfahamu rafiki yangu, nataka kusaidia,.. na nisipoweza kulisaidia hili , nitakuwa sijaweza kuwatendea nyie marafiki zangu haki, kwa vile nahisi kuna dalili fulani isiyo ya kawaida ndani yenu…’akasemaMimi pale nikajikuta nimtulia na kuzama kwenye mawazo…kwanza nikijiuliza ni kwanini docta ameuliza maswali haya, ina maana labda mume wangu aliwahi kulalamika kwake kuhusu maisha yetu ya ndani..na hilo swali la pili,…hayo ni mambo yangu na rafiki yangu je huyu docta inawezekana anayafahamu, na kama anayafahamu kaambiwa na nani…maana mimi sijaongea na mume wangu kuhus hiyo siri yangu na rafiki yangu...‘Unawaza nini…?’ akaniuliza, na sikumjibu, nikawa nimetulia tu, nikiendelea kuwaza; Labda mume wangu aliwahi kuongea na rafiki yake kuhusu jinsi gani anavyotaka mtoto wa kiume, lakini hilo mbona halina msingi, sasa ni kwanini huyu mtu ananiuliza maswali haya… mahusiano ya kitandani yanamuhusu nini docta,..na sio kwamba anataka kuchokonoa ndoa yangu, ili iweje,… ni kweli nakiri kuwa  nimekuwa mvivu wa hilo, lakini sio ....hapana, nahisi docta ana lake jambo, sitamkubalia …‘Zilipendwa, hayo maswali yako yana jibu moja tu, kuwa hayo hayakuhusu kabisa,  sijui kwanini unataka kuingilia maswala ya ndani ya ndoa ya mtu, unahisi sisi hatujui umuhimu wa ndoa,..au?   au umetuona sisi ni watoto wadogo…au ….nashindwa kukuelewa….na nikuulize labda…huenda, mwenzangu alishawahi kuja kukulalamika lolote kwako,.....?’ nikamuuliza‘Sikiliza mimi nayafahamu hayo yote kabisa,…’akasema‘Kwahiyo kumbe alishawahi kukuambia, eeh, si ndio hivyo…?’ nikauliza nikipandisha sauti.‘Sikiliza…nazungumzia  kuhusu ndoa, na masharti yake ni kweli kuwa siri ya ndoa ni ya wana ndoa wenyewe…, ila mimi nimeuliza hayo maswali, sana sana sio kama docta, lakini pia kama rafiki yenu mpendwa, naweza kuhusika katika kuwasaidia, kwa nia njema kabisa, lakini kama utaona haina haja haya..sawa,lakini mimi sitachoka kuwasaidia…’akasema.‘Mimi nakuuliza hivi, je rafiki yako aliwahi kuja kukulalamikia kuwa mimi simtimizii haki zake za ndoa, na ..hayo yanahusikanaje na hiyo ajali yake…kuwa alikuwa na mawazo hayo, hahaha, docta mengine naona hayahitajii udocta kuyafikiria, niambie ukweli, …?’ nikamuuliza.‘Hajawahi kunilalamikia, hilo nikuambie ukweli, siwezi kukuficha , nikijua wewe ulikuwa mpenzi wangu, na sasa ni rafiki yangu, na tuliahidiana kuwa tutasaidiana kwa heri na shari, …mimi nataka kutimiza ahadi yetu hiyo sio zaidi ya hilo, suije kumfikiria mumeo vibaya, hajaniambia ....’akasema docta.‘Kwahiyo hizo ni hisia zako tu,ambazo nahisi umezijenga tu, kwa vile....’ nikakatiza.‘Hahaha,..eti kwa vile..malizia basi…! Sikiliza nikuambie..eeh, usiwe na dhana hiyo , narudia tena, nimekuuliza nikitaka kuwasaidia tu, kwasababu mimi siwezi kamwe kuingilia ndoa yenu,…kwanini nifanye hivyo, wakati nina mke tayari, ili iweje… na wakati wote nimekuwa nikiwasaidia,..leo kwanini iwe ni ajabu,… na maswali yangu hayo yamelenga katika kuwasaidia, kuna kitu nataka kukihakiki kwanza…’akasema‘Zilipendwa, rafiki , mpenzi wa zamani… kiukweli swali lako hilo,  linaingilia mambo yetu ya ndani ya familia siwezi kukujibu, kwani jibu lake lipo wazi...kama kungelikuwa na tatizo juu ya hilo, ningeshakuambia…eeh, na  kama mimi ningelikuwa nimekiuka hayo, na nikawa sitimizi wajibu wangu kwake, yeye kama rafiki yako, angelikuja kwako kulalamika, kuwa nimekuwa mkaidi, je aliwahi kufanya hivyo, mbona unakwepa kunijibu hilo?’ nikamuuliza.‘Hajawahi kufanya hivyo …hiyo dhana nimeiweka nikiwa na maana ya ujumuisho, kuwa mara nyingi, wanandoa wanaweza wakawa na matatizo kama hilo…, wakanyamaza, na wengine hasa wanaume wakalichukulia hilo kama kisingizio, kwa siri na kuanza kutoka nje ya ndoa, badala ya kulitafutia hilo tatizo ufumbuzi wake....’akasema.‘Unasema hivyo ukiwa na maana gani, umeona dalili zozote kama hizo kwa mume wangu, kuwa anatoka nje ya ndoa?’ nikaumuuliza.‘Nimesema kwa ujumla wake, nielewe hapo… sio kwa mume wako tu...nimesema kuna wanandoa wana matatizo kama hayo, na hawataki kuwa wawazi kwa wenza wao, na matokea yake, hasa wanaume, walio wengi, wanajikuta wakitafuta nyumba ndogo, na wengine wanakuwa walevi kupindukia…, na matokeo yake ni kuzaa nje ya ndoa.....’akasema.  ‘Kwa, …kwa..hiyo…unasema kusema  nini, ku-ku-kuwa mume hapana sio kweli na sitaki kusikia hilo…?’ nikauliza kwa hamaki‘Hiyo ndio hali halisi kwa wanaume,…sijasema kwa mume wako…na ni kweli wanaume wanakosea kufanya hivyo, swali tujiulize wenyewe wakikosea ni nani anaumia…usipoziba ufa unakuja kujenge nini…na wanawake mnalijua hilo, lakini mnaweza kukutana mkashauriana mambo ya kuumiza ndoa zenu wenyewe..’akasema‘Eti nini..ni nani kakuambia hilo…zilipendwa,  kama akili zetu zitajikita kwenye maswala hayo ya ndoa, ya mahusiano ndani ya familia,…aah,… mambo ya kindoa, mapenzi ya ndani..sijui…, hatutaweza kabisa kupiga hatua za kimaendeleo, maana hilo sio tatizo, na lini iliniona nikikaa na wenzangu kuongea mambo hayo, unanifahamu nilivyo…’nikasema‘Sawa nakuelewa sana huna tabia hiyo ya kukaa ndio,  …ila naelezea hali halisi ilivyo yanatotendeka katika jamii, na sisi na wanajamii, au sio, na sioni kwanini  ujishuku , maana mimi sijakushuku wewe bado, nakuulizia tu, kwa nia njema kabisa…’akasema‘Najua nyie wanaume, kitu muhimu kwenu ni, .. hilo tendo au sio…, jamani…hilo tendo kwenye ndoa ..ni.. ni kitu kidogo tu, kwanini mnakiona ni kitu cha msingi sana,..cha kusingizia,..kwanza mimi sitaki kabisa kulijadili hilo, kama nyie mnaona hilo ni la msingi kwenu, haya shauri lenu,…na, na nikuambie kitu...kama mtu ana tatizo kwa hilo, kwanini haniiambii...’nikasema.‘Hakumbii nani, una maana mume wako,…sasa sikiliza nikuambie  hilo sio jambo dogo…unaliona hivyo kwa hisia zako, labda kwa vile muda mwingi upo kwenye shughuli zako, na shughuli zako umezifanya ni muhimu sana, kuliko hiyo ndoa, ndio maana hulitiliii maanani, na matokea yake mnajisahau, na kulisahau hilo jukumu la msingi wa ndoa..na nakuambie kitu, usilipuuzie hilo kabisa, maana madhara yake yanakwenda kuleta matatizo mengine makubwa,....’akasema.‘Tuyaache hayo,..., hata kama wewe ni dakitari, hatujafika kwako kukuambia tuna matatizo kama hayo…na mimi silioni kama lina maana kuliongelea hapa, maana kila mwanandoa anafahamu umuhimu wake, na wajibu wa kila mmoja kuwa muwazi kwa mwenzake,  hilo eeh  ndilo la msingi…, kama mmoja akiwa kimya, akajitwika matatizo yake mwenyewe, utasema nini hapo?’ nikamwambia.‘Sawa, endelea naona unataka kunielewa…unataka kusema rafiki yangu hayupo muwazi kwako au sio…?’ nikamuuliza.‘Sijasema hivyo…ila nimekuuliza swali, je rafiki yako kakulalamikia, je alifika kwako akasema kuwa mimi simtimizii hayo mambo…kama kakulalamikia basi, una haki ya kuniuliza lakini kama hajafanya hivyo, na ni wewe unajenga hisia zako tu, unakosea…’nikasema‘Hajaniambia, ila nahisi hivyo, kwa vile nakufahamu na yeye namfahamu pia,…na unaweza kuona ni tatizo dogo kumbe kwa mwenzako ni tatizo kubwa…’akasema‘Hakuna kitu kama hicho, kulikuwa na matatizo madogo na hayo  tulishayaongea na mwenzangu, yanahitajia muda, sio lazima niyaseme kwako. Kama ni hayo, japokuwa zizani kama ni hayo, sizani maana ni kitu kidogo cha ndani ya familia…’nikasema hasira.‘Kwa jinsi ulivyotahayari... shemeji naona kuna tatizo zaidi ya hilo...na hali kama hiyo nijuavyo mimi kwa wanaume wengine wanaweza kuitumia kama mwanya, au kisingizio cha kwenda nje ya ndoa, naomba unielewe hapo...siwezi kusema rafiki yangu yupo hivyo, maana sijawahi kumuona akiwa na tabia hiyo,, ....’akasema huyo dakitari bila kujali jinsi  gani nilivyomjibu kwa hasira.Sikusema kitu hapo ,nikampa nafasi aendelee kuongea, kwakweli alijaribu kuongea kwa upole, kama ujuavyo madakitari wanaofahamu kazi yao vyema.‘Ila kiukweli naweza kuliweka wazi hili kuwa yule rafiki yangu, yule niliyemfahamu enzi hizo, sio huyu wa sasa, nahisi kuna tatizo, tena inaonekana sio tatizo dogo kama wewe unavyolichukulia hivyo…, na nahisi kuna chanzo, na wewe unakifahamu ila hutaki kuniambia...’akasema na kuniangalia machoni , mimi nikamkwepa na kuangalia pembeni.‘Hakuna tatizo bwana, usikuze mambo, …’nikasema‘Una uhakika na hilo, unasahau awali ulisema siku ya leo imakuamkia vibaya, matatizo nyumbani, kwa rafiki yako, umesahau au ?  …’akasema‘Si nimeshakuambia hakuna tatizo, ni ya kawaida tu, sio ya kuambizana kwa kila mtu, na hilo la mwenzangu la kutaka …kuzaa..mmh, kama kakuambia hivyo, kuwa anataka tuzae , tupate mtoto wa kiume, kwani mimi ndio napanga hilo, kuzaa tutazaa, na sio lazima awe wa kiume au,..si ndio hivyo ? alikuambia hivyo au…’nikajikuta nasema hivyo, na kumuuliza…‘Umeona eeh….hilo ulikuwa unanificha, kwahiyo kumbe, wewe umekuwa mbali na yeye labda kwa vile hujawa tayari kuzaa, na mwenzako , kwa kauli yako, anatamani kupata mtoto wa kiume kwa vile sasa hivi mna mabinti, au sio…?’ akaniuliza‘Mimi naona tuyaache hayo…unaonaje tukaongelea kuhusu hiyo ripoti ya docta, inasemaje je matatizo hayo ya mume wangu yanaweza kuleta athari gani baadae..?’ nikauliza kukwepesha huo mjadala.‘Siwezi kuyaacha hayo, maana yanaweza kuwa msingi mnzuri wa wewe na mwenzako hata hiyo ripoti ya dokitari ikija, itakuwa ni ahueni kwako, utajua kipi ufanya na kipi ukikwepe unanielewa hapo..?’ akasema‘Sijakuelewa, na huenda kama ni hivyo unavyofikiria wewe sitakuelewa au unataka nini hasa labda una lako jambo…?’ nikauliza kwa hamaki‘Majibu ya vipimo vya mgonjwa ni kitu kingine lakini ninachotaka mimi kwasasa eeh, ni wewe uwe tayari kwa vyovyote itakavyokuwa, kwa ajili ya kumsaidia mwenzako,…tunaweza kuongea haya kama akiba tu,  ili kupunguza mawazo yako ,na usisahau kuwa tumekuwa tukiambizana matatizo yetu na kusaidiana kiushauri, sasa iweje hili, unifiche …’akasema‘Mhh, hapo nahisi wewe waniuliza ukiwa umeguindua jambo,  na sasa unachotaka wewe ni kunichimba ili tu isionekane wewe unajenga fitina, na labda kunifanya mimi nisije kuumia baadae, au wewe kuna kitu unataka kukichimba ndani ya ndoa yangu yangu kutokana na tetesi za watu tu…, unataka kuhakiki kitu gani maana sio tabia yako ninayoifahamu mimi…’nikasema‘Kawaida yangu sitaki kubuni, na mimi sio mtu wa kusikiliza tetesi, unanielewa nilivyo, katika urafiki wetu, siku zote nimekuwa nikikuasa kuhus hilo, mimi nataka uhakika kutokana na vipimo, na ndio maana nimekuuliza  maswali muhimu yanayoweza kugusa hoja yangu..na nia ni kusaidia hili tatizo la mumeo..lakini msingi wa yote ni kwanini tatizo hili likatokea,..nahisi sio ajali tu,..nahisi kuna chanzo, nahisi kuna tatizo, kati yenu wawili,....’akasema‘Kama ni hivyo basii nimeshakujibu au, kuwa hakuna kitu kama hicho, tupo sawa, na maisha yetu ni ya kawaida tu, umeridhika sasa...’nikasema‘Hdi hapo sijaridikika,..sawa, labda nikuulize hili swali la pili, huko kwa rafiki yako kulikuwa na tatizo gani, maana ulisema wewe mwenyewe kuwa kuna matatizo kwenye familia na huko kwa rafiki yako pi… si ulisema hivyo…?’ akaniuliza‘Yaaah…lakini sio kwa ukubwa huo…’nikasema‘Hata kama sio kwa ukubwa huo, nakuuliza tu, je huko nako kulikuwa au kuna matatizo gani..?..., hebu niambie ukweli, maana huenda hayo matatizo yakawa na mahausiano fulani…yawezekana…ikawa hivyo.., wewe ukashindwa kutambua kwa vile yule ni rafiki yako…?’ akaniuliza na hapo nikashituka na kumwangalia machoni, na moyo ukaanza kunienda mbio,....ni kama kuna hisia inataka kujijenga na mimi siikubali.‘Ni ya kawaida tu…’hatimaye nikasema, baada ya kutulia kidogo‘Je mume wako wakati anapatwa na ajali alikuwa katokea wapi…?’ akaniuliza‘Sijui…’ nikasema hivyo, maana kiukweli sijui.‘Una uhakika hakutokea huko kwa rafiki yako…’akasema‘Kwa rafiki yangu,..hapana bwana…. hilo nina uhakika nalo, maana mimi mwenyewe nilikuwa huko kwa rafiki yangu..’nikasema sasa nikiwa makini na uhakika.‘Swali ambalo ninataka tusaidiane, najua nitakuja kumuuliza huyo rafiki yangu na nitafahamu kila kitu, ila kwa upande wako ni mhimu zaidi ukaliweka wazi, nakuuliza nikiwa na maana yangu na wala usinielewe vibaya….’akasema‘Umeshauliza na umeshapata majibu yake unataka nini tena…’nikasema‘Yule mtoto wa rafiki yako, …baba yake ni nani…?’ akaniuliza na mimi hapo nikageuka kumuangalia machoni, na yeye akanikazia macho, na ikawa mimi ndiye niliyekwepesha macho yangu, na baada ya muda nikasema;‘Sijajua bado, hajaniambia…na, kwanini umuulize rafiki yako, au una maana utamuliza rafiki yangu..sijakuelewa hapo,…’nikasema kwa upole.‘Basi, kama hajakuambia, …basi tuliachie hilo hapo, na kama kuna kitu unanificha ni bora uniambie mapema niweze kukusaidia kimawazo…’akasema‘Kwanini ukaniuliza mimi hilo swali, kwanini, usingelienda kumuuliza mzazi mwenyewe, maana ni kama vile unahisi mimi nahusika na mimba yake au , eeh,..…unataka kuweka fitina gani ndani ya ndoa yangu…’nikasema‘Fitina,!!!…hahaha, hapana, mimi au mwingine !!!?’ akauliza kwa mshangao‘Ndio, umeanza kusema mume wangu alitoka kwa rafiki yangu, kiukweli hajatokea huko, maana mimi nilikuwa huko,…hapo ukashindwa kukamilisha fitina yako,..au dhana yako potofu dhidi ya rafiki yako, na rafiki yangu, halafu ..unafikia kuniuliza mtoto wa rafiki yangu baba yake ni nani….huoni hapo unataka kujenga fitina…’nikasema‘Na ungelijua, usingelisema hivyo, kwasababu wewe ni rafiki yangu kama alivyo mume wako…na nimekuwa karibu sana na rafiki yangu , mambo yake mengi huwa ananiambia, lakini ikafika muda, ikawa nikimuuliza maswali hataki kunijibu…nikajua kuna tatizo..mimi naweza kuligundua hilo hata kabla hamjaniambia,…lakini nitatoa kauli ya uhakika nikipata uthibitsho, ndio maana nikakuuliza, ili kuondoa hisia mbaya…’akasema‘Kwahiyo umeshaupata ukweli au sio, sasa ondoa hizi hisia mbaya au kuna jingine…?’ nikamuuliza‘Bado..sijarizika na majibu yako…, maana hujanijibu kwa uhakika kile nilichokuuliza, unakwepa kujibu swali……’akasema‘Majibu gani unayo-yataka wewe sasa, mbona siku hizi unaanza udukuzi....sasa sikiliza nikuambie , mimi sitaki,…. na nakuomba tena na tena..huko unapokwenda ni kubaya, sana, mtakuja kukosana na rafiki yako kwa mambo yasiyo kuhusu, kwa ushauri wangu, hilo jambo usiliingilie kabisa, na liishie hapa hapa…’nikasema‘Hilo jambo lipi sasa…?’ akaniuliza‘Kuhusu sijui mimi naishije na mume wangu, au, mahusiano yangu na rafiki yangu, au mtoto baba yake ni nani, hayo mambo umeyaanza lini , mbona unabadilika sasa, hayo kiufupi ..hayakuhusu ..kabisa, hayo yaache, na sijawahi kufika kwako kuomba msaada…’nikasema‘Utakuja tu siku yake..ndio maana nataka kabla haijafikia huko,…nijue wapi pa kuanzia, ila nina uhakika ipo siku utakuja kwangu……si tupo…’akasema‘Kwanini unasema hivyo, nahisi kuina jambo unalijua hutaki kuniambia…’nikasema‘Kama mimi ninavyokuhisi wewe, kuwa kuna jambo unalijua, linakusumbua wewe na mume wako, lakini  hutaki kuniambia..sasa tukubaliane, uniambie ukweli, ili na mimi niweze kuhitimisha nadharia yangu, kwa nia njema kabisa,…ili tuweze kuweka akili zetu kwenye kumsaidia mwenzetu, hali aliyokuwa nayo inahitajia msaada wetu sote…sawa, utaanza kuniambia au tuache tu..?’akasema kama kuniulizaHapo nikawa sina jinsi, …NB: Choko choko za docta zitasaidia kuuvumbua ukweli, je docta anauliza hivyo akiwa na msingi gani, je huenda anajua ukweli fulani….mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu inakuwaje.....?WAZO LA LEO: Ndoa nyingi zimekuwa na sintofahamu kwasababu ya kuzarau mambo muhimu kwenye ndoa, na mengine yanaonekana ni madogo au tunayaona hayana maana kwetu… , na mengine ni msingi wa ndoa, lakini wengine wanayaona ni ya kawaida tu ..kama wana ndoa, ni vyema mkayaongelea, maana dogo kwako linaweza likawa kubwa kwa mwenzako, na kama hamtayaongelea wenyewe ni nani atawaongelea, kwanza ongeeni wenyewe, mkishindwa ndio mtafute msaada.Hatukuweza kuafikiana siku hiyo, hadi siku nyingine tukakutana tena hospitalini, na docta akafufua yale mazungumzo yetu…‘Unakumbuka nilikuuliza jambo, tukawa hatukuelewana…nahisi hukunielewa dhamira yangu,..nimeliwaza sana hilo nikaona ni lazima tuliongee na tufikie muafaka, sijui unanielewa….?’ akaniuliza na mimi nikawa nimeinama nikiwaza mengi kichwani. Nimekuwa mtu wa mawazo sana kiukweli. Sipati usingizi kabisa, na nahisi itanieletea matatizo, kwahiyo nikaona ni vyema nisikilizane na docta tu..‘Lakini, mimi sijaona kosa langu, sijaona kuwa nina matatizo kihivyo…, sioni kabisa, kichwa changu kimetaliwa na kazi zangu za kiofisi mambo mengine ni ya kifamilia zaidi, ni mambo ya kawaida tu na nina imani  yataisha tu…,sasa ukiniambia nikuambie kila tatizo la familia yangu unakosea….’nikasema‘Shemeji, umesema una matatizo ukayataja matatizo kuwa yapo matatozo ndani ya nyumba yako..ambayo uliyaita  ni ya kifamilia, ambayo naona umeshindwa kuyasema ni matatizo gani, kwangu nahisi huenda yakawa ndio chanzo cha yote hayo mengine..sijui lakini nahisi hivyo, maana hujanifafanulia...’akasema na mimi nikawa nimetulia tu.‘Lakini pia ulisema kuwa kuna matatizo ya huko kazini kwako, hayo ukasema  ni matatizo ya kawaida tu ya kikazi , au sio, siwezi kuingilia mambo ya utawala wako wa kikazi, sawa nimekubali kwa hilo, huko ni kwako na utaalamu wako…?’‘Yap…ya kawaida..napambana nayo, …’nikasema 'Hata hivyo nakushauri, hayo mambo ya kikazi, usiyaweke akilini sana, yakawa ndio kipaumbele chako,  kiasi kwamba yanameza maswala ya familia yako, kwani unafany akzi ili iweje, ni kwa masilahi ya familia yako, au sio…sasa ukiumiza kichw ahuko, kazi, ukaupa mgongo, ndo ayako utakuwa umefanya nini…unielewe hapo…’akasema‘Sawa nimekuelewa docta….’nikasema‘Lakini kuna hili,…ulisema kuwa kuna matatizo huko kwa rafiki yako,…kuna kitu nataka tuje kukijadili, sio kwa utesi,..sipendi tabia hiyo, bali nataka tujenge na kuondoa tatizo kama lipo…kwa kulianza hili je huko kwa rafiki yako  kuna tatizo gani hasa la kukusumbua kichwa, maana huyo ni rafiki yako, kama nilivyo mimi, au sio…,?’ akaniuliza‘Huko kwa rafiki yangu ni matatizo ya kawaida pia, wala yasikuumize kichwa, yule ni rafiki yangu namuona kama mdogo wangu , japokuwa tunalingana ki- umri. Kwahiyo mimi kama mzazi lipo ndani ya uwezo wangu....’nikasema na yeye akaendelea kusema;‘Hata kama ni ya kawaida...kama unavyodai, kitu ambacho sikiamini, kwa vile umeshataja kuwa ni matatizo, ina maana yapo akilini mwako, na yanakusmbua akilini, na yanaweza kukupa matatizo, ukadondoka kwa shinikizo la damu, huwa inatokea, sasa isje kufika huko,…’akasema na nilikuwa sijamueleza kuwa nilipoteza fahamu.‘Mhh, hata sikuelewi, …kwanini lakini, au kuna kitu unakijua mimi sikijui, kwanini usiniambie tu, kuliko tuzunguke zunguke…’nikasema‘Kuna kitu nahisi kuwa kipo kati yako wewe na mume wako hujaniambia…, na kuna tatizo kati yako wewe na rafiki yako, nataka kulijua hilo,  kuna kitu ambacho ungeniambia, ningeliweza kuhitimisha hilo ninalolifikiria mimi na tukaangalia njia sahihi ya kulitatua…, lakini kawaida yangu kama unijuavyo,…sipendeleo haya, nimekusihi uniambie wewe kwa vile ni rafiki yangu tu,  la sivyo nisingelihangaika kabisa…’akasema‘Ndio maana nakushangaa naona kama umebadilika siku hizi…, sio kawaida yako, kwanini uyatake haya ya watu, kuyafahamu,… na mwenyewe mara kwa mara umekuwa ukinikanya kuwa nisiwe na tabia ya kufuatilia mambo ya watu wengine.., na nisiwe mtu wa dhana mbaya kwa watu, au sio wewe…’nikasema‘Hili sio la dhana mbaya…, ila mimi nataka nikusaidie ili baadae usije kunilauamu, najua kabisa baadae unaweza kunilaumu, kuwa huenda, nahusika, huenda nilijua, nataka nijitoe kabisa, lakini ni muhimu kwangu kulitatua hili kadri inavyowezekana…sasa hebu niambie…huyo rafiki yako, ana kukwanza nini, ni kuhusu ndoa yako…?’ akaniuliza tena‘Ananikwanza,…!!! Sijasema hivyo… Nani kazungumzia kukwazana kwenye ndoa hapo!!!…nikuambie ukweli, huyo rafiki yangu hahusiani kabisa na lolote katika ndoa yangu,...nakuomba usije ukamuhusisha rafiki yangu na haya maswala yangu,..hahusiki na lolote lile..hilo nakuthibitishia...hayo matatizo niliyosema kuhusu  mimi na yeye, ni matatizo ya kawaida tu kati yangu mimi na yeye, hata mume wangu hajui...’nikasema.‘Nikuulize kitu, unakubaliana na mimi kuwa mume wako yupo karibu sana na huyo rafiki yako..?’ nikauliza‘Ndio hilo halina siri..ila kwa vipi sasa …kwa jinsi unavyofikiria wewe unakosea, sivyo hivyo, acha hilo…’nikasema‘Nisawa nitaliacha, ila…, nataka kuwa na uhakika tu kuwa hilo umeliridhia, kuwa mume wako yupo karibu na rafiki yako, wanakula pamoja, wanatoka wakati mwingine pamoja…na imekuwa sipo karibu sana na yeye kwa vile wanakuwa na huyo rafiki yako,.utasema labda nawaonea wivu, hapa…sasa ,.je hilo halina wivu kwako wewe,  na sio sababu ya matatizo yako na rafiki yako, …wivu labda..?’ akauliza.‘Karibu sana kwa vipi…ndio, kama umewaona wanaongea, au wanakula chakula pamoja, ni kawaida tu, tumezoea hivyo, wala usiwafikirie vibaya, siwezi kabisa kuona wivu kwa rafiki yangu, kuwa na mume wangu hivyo, na sizani kama inaweza kwenda zaidi ya hivyo, mengine ni dhana zako potofu, na ni wivu wako unakusumbua….’nikasema‘Kama ni hivyo, sawa, kama umeliridhia hilo, sawa…na sio kwamba nawachimba, au wivu kama unavyodai, hapana,  ndio maana nilitaka uhakika kutoka kwako, nilijua hayo matatizo na rafiki yako huenda ni maswala ya wivu, ok sasa…ili tusaidiane, na mimi nirizike, eeh, ..maana kuna kitu kinanitia mashaka…’akasema‘Kipi hicho kinachokutia mashaka, kuhusu rafiki yangu na mume wangu au…?’ nikauliza‘Rafiki yako naona kakimbilia kuzaa kwa kuchelea umri, au sio, ni sawa maana aliwahi kuongea na mimi, kuhusu hilo, na mimi kama dakitari nikamshauri kuwa ni bora aolewe mapema, maana umri umekwenda, akasema yupo mbioni kulitatua hilo, nikajua keshapata mume , sasa naona kazaa, simuoni huyo mume…’akasema‘Ndio hivyo hakuna shida, au ulitakaje wewe,…?’ nikamuuliza‘Nilimuambia awe lakini awe makini sana na mawazo hayo…maana yanaweza kumpelekea akataka kuzaa tu, kwasababu ya kukimbizana na umri…lakini hakutaka kuongea na mimi zaidi, ni kweli kuna muda alikuwa karibu sana na mimi, mpaka watu wakatushuku vibaya, hata mke wangu, nikaona aah, tukakosana...’akasema‘Ndio niliwaona mkiwa sambamba, lakini mimi nilijua mumarafiki tu kama alivyo karibu na mume wangu, japokuwa …alikuja kuniambia ulimtaka kweli si kweli…’nikasema‘Hahaha, hayo yaache, sasa ni hivi, maana wewe ndiye rafiki yake, kwanini akaamua kuzaa bila kufunga ndoa, ulimshauri wewe hivyo, na je baba wa mtoto wake ni  nani?’ akaniuliza huku akiniangalia kwa macho ya udadisi, na mimi kwanza nikaguna, halafu nikaangalia pembeni na kusema;‘Hilo hata mimi sijui..labda baba wa mtoto ni wewe,maana mlikuwa marafiki au sio, sasa sijui ,.. au ndio maana unataka kuchunguza kuhakiki kama mtoto ni wako au ni wa matu mwingine…’nikasema.‘Aaah, sio wangu bwana.. .kama angelikuwa ni wa kwangu angelifanana na mimi, sura yangu haijifichi..na wewe ungelishaniambia , na nafahamu wewe unafahamu mwenzako katembea na nani , kweli si kweli...?' akaniuliza lakini kabla sijamjibu akasema'Hivi wewe una uhakika kuwa mume wako hajawahi kutongoza wanawake wengine...hata kiutani tu, hayo yanatokea tu,...lakini baadaye unajirudi,... lakini hayo tuyaache maana ilikuwa zilipendwa, sasa niambie ukweli, unamfahamu aliyezaaa na rafiki yako, maana mimi naulizwa na wazazi wake...’akasema.‘Mimi simfahamu....’nikasema .‘Ok. Sio shida, nimewaambi ahivyo hivyo, lakini kuna mambo mengi wameniuliza, hasa kuhus urafiki wako na mwenzako…mmh, unajua mambo mengine unaweza ukayaficha, lakini wazee ni wepesi sana kuyagundua…’akasema.‘Walisemaje…?’ nikauliza.‘Hebu nikuulize  kwanza, una uhakika kuwa kweli mume wako hakuwa ametokea huko kwa huyo rafiki yako?’ akaniuliza  swali hilo na kunifanya nishtuke kidogo. Akilini nikajiwa na kumbukumbu, kuwa kuna muda niliona gari kama la mume wangu, pili, yule kijana wa kuosha magari, alisema ‘shemeji alikuwepo, huyu naye anasisitiza hilo hilo, na sijui anataka kuthibitisha nini… ‘Mimi nilikuwa huko kwa rafiki yangu...kama mume wangu angelikuwa huko si ningelimuona jamani…, labda alipita njia hiyo, sijui akitokea wapi, na sina uhakika na hilo, maana nijuavyo mimi alikuwa kwenye kikao…sasa alitokea wapi akapitia njia hiyo mimi sijui..’nikasema.‘Kwahiyo mkiwa huko hukumuona mtu, aliyefika kwa rafiki yako, au….?’ Akauliza‘Labda mdogo wake, nahisi hivyo tu…’nikasema‘Mdogo wake!!!’ akasema kwa mshangao‘Nahisi hivyo tu…sina uhakika…’nikasema‘Kwanini unahisi hivyo…?’ nikaulizwa‘Nimekuambia sina uhakika, tuliachie hapo tu, maana unanichimba sijui unatafuta nini…’nikasema hivyo maana nilijua hilo linaweza kuendelezwa mpaka nikasema yasiyotakiwa kusemwa.‘Mbona mdogo wake, nilikuwa naye, alikuja kwangu kuna mambo fulani ya mkewe aliyafuatilia kwangu, ya kiafya..tukawa naye hapa tukiangalia mpira kwenye runinga,na niliachana naye muda mfupi, kabla sijapigiwa hiyo simu ya ajali....sizani kwamba aliweza kuja huko kwa muda huo mfupi,...’akasema‘Mlikuwa naye nyumbani kwako…?’ nikauliza kwa mshangao‘Ndio…sasa sizani, kam ni yeye, hata hivyo, yeye aliniomba gari langu kuwa anafuatilia mzigo wake, ndio maana nilishindwa kumchukua mume wako kwa haraka, kwani sikuwa na gari...ndio maana pia tukaamua kuagiza gari la wagonjwa....’akasema.‘Ina maana gari lako mpaka sasa analo mdogo wa mume wangu?’ nikamuuliza.‘Ndio maana yake, aliniazima gari langu , kwa vile gari la mumeo alikuwa nalo kikazi, au sio, na anasema alipiga simu kwa mumeo akawa hapatikani, ..haiwezekani akawa ndio yeye, labda yule mdogo wake mwingine, na yule hayupo hapa dar, alisafiri jana kama si kosei kwenda mikoani....’akasema.‘Basi kama sio yeye, kuna mtu mwingine anafanana na ….huyo….’nikasema‘Kwanini unasema hivyo…?’ akauliza‘Hapana, tuyaache tu,  sioni kama kuna lolote baya, nitamgudnua tu kuwa ni nani yangu, ninachotaka kusema, ni kuwa mimi nilihisi kuwa yeye alifika huko kwa rafiki yangu wakati mimi nipo huko, kama sio yeye.basi kuna mtu mwingine anayefafana naye....ni hivyo tu basi...’nikasema nikiwa sina uhakika.‘Mhh..nisamehe tu..akilini mwangu nahisi kuna tatizo hapo,…’akasema‘Tatizo gani…?’ nikauliza‘Hebu niambie ukweli....unasema wakati upo huko, alifika mtu anayefanana na mdogo wa mume wako si ndio hivyo, nyie muda huo mlikuwa ndani, au nje…?’ akauliza‘Tulikuwa ndani…’nikasema‘Sasa ulimuonaje kuwa anafanana na shemeji yako…?’ akauliza‘Mhh..nilihisi tu hivyo, kwa vile mtoto anafanana na shemeji, na huyo aliyekuja alikuwa ….eeh, sasa unataka niongee yale ambayo sikutakiwa niyaongee…’nikasema‘Nimekuelewa kuwa hisia zako kuwa huyo aliyezaa na rafiki yako, anafanana na mtoto wake, na huyo mtoto anafanana na shemeji yako, … sawa, lakin huna uhakika maana hukutoka ukamuona sawa, na kwahiyo ..eeh, …inawezekana hakuwa huyo shemeji yako, kama unavyofikiria wewe, labda alikuwa ni mtu mwingine au sio, ?’akasema na kuniuliza‘Ni hivyo lakini rafiki yangu alisema ni shemeji ..akiwa na maana shemeji yangu ndivyo nilivyo muelewa…’nikasema na docta kacheka kiddogo‘Ah, shemeji..ok…kwa maana nyingine wewe ulifananisha huyo mtu na shemeji yako wewe…, kwa kuhisi tu, kwa kupitia kwa mtoto,….na hakutaka wewe umuone, au sio, kwahiyo yeye…shemeji,…alipogundua kuwa upo hapo,  ...akaondoka kwa haraka…au sio.., hamkuonana naye, uso kwa uso…au sio…?’ akauliza‘Ndio, kwahiyo unataka kujenga hoja gani hapo…?’ nikamuuliza‘Nijibu kwanza , …kuna kitu nataka kukipata hapo, ..kwa leo sitaki unielewe vibaya..’akasema‘Sawa, …ndio, lakini sikuonana na yeye maana alikimbia,..’nikasema‘Alikimbia!!!..alikimbia,.., kwanini akimbie hapo kuna ulizo, majibu ya haraka ni ili usimuone, labda, kwa vile alitaka iwe siri, lakini anajua kabisa wewe ni rafiki yake au sio..ila wewe ulitaka kuonana naye, ili muweze kuliweka sawa, au sio, kwa nia njema, lakini akakimbia..au sio?’ akaniuliza‘Mimi nilitaka niongee na yeye, lakini rafiki yangu hakutaka nikutane naye, na hata yeye alimuonya rafiki yake kuwa hataki yeye kujulikana,…nikaona ananiwekea uzito, ndio nikatoka nje , …sikumuona kwa wakati huo, kumbe alikuwa kajificha, sasa wakati nipo ndani ndio nikasikia akikimbia huko nje…’nikasema.‘Mpaka hapo inaashiria kuwa huyo mtu , ni mtu wako wa karibu hakutaka kabisa umuone, umeona hapo..na hadi kukimbia hivyo, ina maana kubwa, hakutarajia kukuta wewe hapo, ndio maana akakimbia, na huenda alipofika kwenye gari lake, akalichukua na kuendesha kwa kasi sana, sasa wewe huoni ni nani huyo mtu…?’ akauliza‘Sioni kuwa ni nani….hapana…sijaona kuwa ni nani zaidi ya shemeji yangu, ..lakini sina uhakika , maana sikuonana naye……’nikasema‘Nje kulikuwa hakuna gari, gari lake alikuwa kaliweka wapi..?’ akaniuliza‘Sikuliona gari lake hapo nje…na sijui alikuwa kaliacha wapi....’nikasema‘Je ana gari, rafiki yako hakukuambia hilo?’ akaniuliza‘Ndio analo, lakini hakuliacha hapo nyumbani,…na rafiki yangu hawezi kujua aliliacha wapi, maana alikuwa hajaingia wakaongea…’nikasema‘Kwahiyo huyo mtu alipotoka hapo, alipogundua kuwa ni wewe, akaogopa akihisi kuwa atamfuatiliwa, utakuja kumgundua kuwa ni yeye, akatoka akalifuata gari lake akaondoka kwa mwendo kasi, au sio….?’ Akasema‘Unataka kusema nini hapo mbona unarudia rudia hilo la ‘mwendo kasi’Najua dhana yako…, kuwa labda anaweza akawa ni mume wangu au si ndio hivyo...?’nikamuuliza.‘Mimi sijafikia kuhitimisha hivyo, ninachotaka ni kukuweka katika hali ya kuyakubali yote, kwasababu nijuavyo mimi, mume wako hawezi kukuficha kitu, au sio.. na kama kuna kitu kakifanya, atakuwa na wakati mgumu wa kutafuta ni namna gani atakuambia …hiyo ajali yake sio ya kawaida, kuna kitu hapo, ndio maana najaribu kutafuta hilo, ili umsaidie yeye, apone haraka…’akasema‘Sio mume wangu, kwani kama angelikuwa ni yeye, kwanini alifika kwa haraka, halafu anikimbie, si alikuja kwa nia njema kumsalimia shemeji yake...kuna tatizo gani la kunikimbia mimi…, ndio maana nasema sio yeye, hilo sikubaliani nalo...mume wangu hana tabia kama hiyo...’nikasema nikijaribu kumuwazia huyo mtu aliyefika na kukimbia anaweza kuwa ni nani.‘Kwani huyo mtu aliyefika, mkiwa huko ndani na rafiki yako alifikafikaje, kuna kitu gani cha tofauti unaweza kusema huyo mtu alikuwa nacho, cha kuweza kumkumbuka,,..?’ akaniuliza.‘Viatu vyake vilikuwa vikitoa sauti,….’nikasema.‘Mume wako alikuwa kavaa viatu vya kutoa sauti asubuhi ..?’ akaniuliza‘Mhh.. ndio alivaa viatu vya kutoa sauti, lakini huo sio ushahidi tosha, au sio…’nikasema‘Ok…hebu nirejee nyuma kidogo…, samahani lakini, rafiki yako alisema huyo aliyekuja wakati ukiwa kwake ndiye aliyezaa naye, sawa si sawa…?’ akaniuliza‘Ndio, na alimpigia simu nikiwa pale…’nikasema‘Una uhakika na hilo…’akasema akiniangalia kwa makini.‘Uhakika wa nini sasa…, si yeye kaniambia hivyo, nitakuwa na uhakika gani zaidi ya kauli yake, au…’nikasema‘Na ukiwa ndani, ukasikia akikimbia, lengo ni ili wewe usimuone, ulisikia viatu vyenye sauti…?’ akauliza‘Itakuwa hivyo, ndio…’akasema‘Kwahiyo hiyo kwa vyovyote huyo mtu aliyekimbia ni huyo huyo aliyefika awali,…sio kwamba huyo ni mwingine alikuwa kajificha, nataka uwe na uhakika hapo,…na kwa hiyo ndio huyo baba wa huyo mtoto, kutokana na kauli ya rafiki yako, na wewe ulikuwa na hamu sana ya kukutana na yeye au sio….?’ Akauliza‘Ndio, lakini mimi nilishahisi kuwa ni huyo mdogo wa mume wangu, sasa ukisema mlikuwa naye hapa,…hapo sijui atakuwa ni nani mwingine…’nikasema.‘Je tusaidiane kumtafuta huyo mtu…, kama ni muhimu sana kwako, na kama itasaidia kuondoka hiyo hali ya wewe na rafiki yako…ili usiwe na wakati mgumu,..?’ akauliza‘Haina haja, sihitaji msaada wako kwa hilo….’nikasema‘Sijui lakini…hata hivyo mimi nitaongea na rafiki yangu nitaujua ukweli wote, sio muhimu kwangu sana, lakini sitaki ije kuleta mtafaruku kwenye ndoa yenu,. Hata hivyo mimi…, sitaki sana kuingilia mahusiano yenu, …na usije ukaniona labda nayaongea haya kwa nia ya kukuharibia ndoa yako, ila mimi nataka nikuweke tayari, usije kusema mimi kama rafiki yako sikuwahi kukuambia hili, ukanioana mbaya baadae, nakufahamu sana wewe…’akasema docta‘Una maana gani kusema hivyo..?’ nikamuuliza‘Je ikitokea kuwa huyo aliyefika wakati upo hapo kwa rafiki yako ni mume wako utasemaje…’akasema‘Unasema nini, kwanini unafikiria hivyo, najua wewe unawaza nini, na hata wengine watawaza hivyo hivyo ,lakini wewe hujui mimi na rafiki yangu tulikubaliana nini, na mimi nipo tayari kwa lolote lile..kwasababu ni mimi nilimshauri, ila wewe unataka kuharibu kuwa yeye labda katembea na mume wangu , hawezi kufany ahivyo abadani, atakuwa ni mwehu basi, na mimi sitakubaliana na hilo…?’ nikamuuliza kwa hamaki.‘Ndio hapo…nawajibika kuingilia kati, ili kuwasaidia wewe na mume wako…najua kwa vyovyote vile mimi ndiye nitakuwa mtu kati…na nakuelewa sana wewe ulivyo….kuliko unavyojielewa wewe mwenyewe….ndio maana nataka kukusaidia hili. Inawezekana ulim-mshauri mwenzako kitu na yeye akakichukulia juu kwa juu, bila kuelewa lengo lako, …na akijua wewe ni rafiki unaweza kumtunzia siri kuliko mtu yoyote yule, kwahiyo …’mimi hapo nikamkatisha na kusema;‘Mhh, sikiliza, unajua najiuliza kama alikuwa ni mume wangu kama unavyodai wewe, kuwa huenda alikuwa ni mume wangu basi kwanini,  aogope kiasi hicho,mimi namfahamu sana mume wangu..hanificho kitu akikosea, atanipigia magoti kutubu,.., na rafiki yangu alisema huyo ndiye baba wa mtoto wake, …sasa atakuwaje ni mume wangu, hebu na wewe lifikirie hilo, mume wangu ndio aje kutembea na mdogo wangu haiji akilini,…’nikasema.‘Nimekuuliza tu, …kama ikitokea ndio hivyo, ndio yeye, bado utakubali kuwa ndiye baba wa huyo mtoto, …’akasema‘Haiwezekani, akawa ndio yeye bwana, sitakubali kabisa,, ...mume wangu hawezi kutembea na rafiki yangu,  na rafiki yangu ambaye nimemchukulia sawa na ndugu yangu, rafiki yangu hawezi kunisaliti, hilo halina maana, na wala tusiliongelee zaidi maana linaweza kujenga dhana mbaya,,...kabisa haiwezekani...kwanini,,,.’ nakasema nikionyesha kukereka.‘Je ikiwa na kweli, utafanya nini..?’ akaniuliza‘Haaah, weee, tuliache hilo, sitaki hata kufikiri, ndio maana nasema sio yeye, rafiki yangu pamoja na yote ananifaham nilivyo…labda ahame nchi, ..mungu wangu, sio yeye, sio mume wangu…’nikasema nikiwa na kitu moyoni kinaniwasha.‘Unajua nilipomuona mtoto,…na yote yanayoendelea hivi sasa nimekuwa nikiliwazia hilo, nakuelewa wewe sana,…je wewe au mume wako, itakuwaje,… na sijui, kwanini nilimshauri rafiki yako ajitahidi kuzaa kwani umri umepitiliza, nahisi alilichukulia ushauri wangu huo kwa pupa …kiukweli mimi nilimshauri hivyo na sitaki kujilaumu maana sikumshauri akatembee na waume za watu…’akasema‘Mbona hata mimi nilimshauri hivyo…’ nikasema‘Ndio kama ulishauri hivyo kuwa aolewe, ili azae, ulikuwa ushauri mnzuri, kiukweli, kiumri na …rika lake, alitakiwa aolewe, na mimi nilimshauri mengi tu, na hakutaka kuwa muwazi kwangu, kuwa ana mipango gani,…na labda alishanichukulia vibaya, kwasababu tulishakorofishana…kwahiyo nikajua ni lazima atakuwa kaja kwako,….’akasema‘Ndio alikuja kwangu, nikamshauri hivyo,… mengine ni siri yangu mimi na yeye…’nikasema‘Umeona eeh , hapo unanificha, na hapo nahisi kuna siri kubwa, ambayo inaweza kutengua hiki kitendawili…kwahiyo wewe ulimshauri hivyo kuwa ni bora azae kwanza, kwa vipi sasa, maana hilo hakutaka mimi nimuingilie, alisema atalifanyia kazi…’akasema‘Kwahiyo kumbe wewe unanitega ili ujue niliongea nini na rafiki yangu, kuwa labda nimemshauri akatembee na mume wangu, hivi ukiwazia hivyo, unanifanya mimi ni juha au…’nikasema kwa hamaki‘Nakuuliza hivi nikiwa na maana,  unielewe sana hapo,…mpaka nakuuliza haya nimeyatafakari sana, nakupenda, na kukujali, nawapenda wewe na mume wako, sitafurahi ndoa yenu ikija kuvunjika, ubaya unaweza kutendwa, kwa bahati mbaya, na hatujui hadi sasa ni kipi kilitendeka,..mimi kuna muda nilikuambia urafiki wako na mwenzako, ni sawa..siukatai…, lakini usifikikie kumuamini sana kihivyo.., ukasema ni kwa vile mimi eti nilimtongaza huiyo rafiki yako akanikataa…’akasema‘Ndio hivyo..nawafahamu sana nyie wanaume mlivyo…’nikasema‘Sasa nikuulize tena  ulimshauri vipi maana nijuavyo, yeye hakutaka kuolewa kwa sababu zake za kumtafuta mume ambaye hajazaliwa, kawakataa wanaume wengi tu, mimi mwenyewe niliwahi kumwambia kuna rafiki yangu anataka kumuoa, akamkataa, anasema haendani na yeye, na hilo ndilo lilifanya mim na yeye tukosane dio hivyo mnavyofiria nyie, kuwa nilimtongaza akanikataa,….’akasema‘Ndio tatizo lake yeye, kuwakataa wanaume,..ndio nikamshauri hivyo, kuwa bora atafute mume azae naye....lakini hayo yameshapita , kazaa basi, haina haja ya kulijadili hilo saana…, nahisi tukilijadili hilo, tutafikia sehemu sisi wenyewe hatutaelewana, na sitaki tufikie huko…’nikasema‘Una uhakika na hilo kweli, halikuumizi akilini kweli, na baada ya kuyaongea haya nahisi litazidi kukuumiza kichwa, je ..ni kweli kuwa  hutaki kumtambua baba wa huyo mtoto wa rafiki yako,…?’ docta akauliza‘Nitamfahamu tu,….mimi mwenyewe, au yeye mama wa mtoto ataniambia, maana tulishakubaliana hilo, hawezi kunificha mimi rafiki yake,…’nikasema‘Hataweza kukuambia, hilo nakumbia ukweli, kwa jinsi ninavyokufahamu wewe ulivyo, lazima atakuwa kaagopa, huenda alivyofikiria yeye awali, sivyo ulivyokuja kukusikia ukilipokea, na kiukweli,…, sasa naomba tusaidiane kwa hili, ili wewe uwe na amani, leo na baadae …’akasema‘Kwanini unasema hivyo…?’ nikamuuliza‘Nina uhakika kwa hali hii ilivyo, kama rafiki yako atakuja kukuambia ukweli, kitu ambacho sizani kama atakifanya …kwani nina uhakika kuwa mtakuja  kukosana na yeye kabisa…’akasema docta‘Docta, docta….docta, najua wewe umeshajenga dhana fulani, na wewe kila mara umekuwa ukinikanya kuhusu hilo, kwanini sasa wataka kuliendekeza hilo, na kumbuka kama ndivyo hivyo, unavyodhania wewe utakuja kukosana na rafiki yako…je kama akisikia hivyo, na nina uhakika sio kweli…itakuwaje…’nikasema‘Wewe ni rafiki yangu  hatufichani, au sio, na tumekuwa hivyo, nikiwa na tatizo nakuambia wewe hata likimuhusu mke wangu, unanishauri, na mambo yanakuwa sawa…nashukuru sana kwa hilo,…na halikadhalika mimi umekuwa  ukiniuliza maswala mengi haya yanayomuhusu mume wako…nakushauri unayamaliza…’akasema‘Ndio hivyo nikikwama huwa nakuuliza lakini ukiona sijakuuliza ujue sijakwama, na kwa hili sijakwama..ndio maana ….’nikakatisha‘Hapana, sema kwa vile ..unahisi wewe ulifanya makosa …sawa, ila nakuuliza tena, je una uhakika hutaki kumfahamu huyo mwanaume aliyezaa na rafiki yako…?’ akaniuliza‘Nimeshakuambia nitamfahamu mimi mwenyewe…’nikasema‘Sawa kama hutaki, siwezi kukulazimisha, lakini kama unataka nikusaidie hilo, nipo tayari, ila uniahidi kuwa hutalichukulia vibaya, ...nia ni muhimu umfahamu na ujue ni nini utafanya kwa masilahi ya ndoa yako na maisha yako, basi tulimalize hivyo, mana muda umekwenda…’akasema‘Nikuulize kitu, wewe una uhakika na unachokidhania…?’ nikamuulizaNa yeye akaangalia saa halafu akatabasamu, …simu yake ikaita, akaniangalia usoni, halafu akasema‘Ngoja nipokee hii simu…ni rafiki yako, kanipigia…’akasema‘Rafiki yangu…!!!’ nikajikuta nasema hivyo kwa hamaki, sijui kwanini naanza kuhamaki, labda ni kwa vile docta kajenga hizo dhana mbaya, au labda..hata sijui, nikasubiria kusikia docta anaongea nini na rafiki yangu..WAZO LA LEO: Je ukiwa unaufahamu ukweli kuhusu rafiki yako, na unaogopa ukimwambia ukweli huyo rafiki yako inaweza kuleta mtafaruku na mkewe, utafanya nini…?’ ni swali niliulizwa, na jibu langu likawa hivi… ‘ukwel wakati wote ni silaha ya ushindi, lakini hekima yake ni ngao, inatakiwa  tuwe makini sana kwenye baadhi ya mambo, maana ukweli unaweza ukaumiza, japokuwa ni kwa muda mfupi…na uwongo, ni hatari, unaweza ukasaidia kwa muda mfupi lakini ukaja kuumiza kwa kipindi kirefu, na kuharibu kabisa…sasa ni wewe mtoaji ushauri upime mwenyewe.‘Kakupigia nani,…rafiki yangu…?’ nikamuuliza Na docta akaikata ile simu, …haikuipokea ikanifanya niwe na mashaka, ni kwanini docta hakutaka kuipokea nikiwemo.‘Ni kwanini unaikata hiyo simu…ni kwanini hutaki kuongea na yeye,labda anahitajia huduma yako ya kidakitari..?’nikauliza.‘Hapana , tokea jana anataka kuongea na mimi, ..siwezi kuongea na yeye mpaka nimalizane na wewe…’akasema.‘Sijakuelewa hapo,…kuna nini kinachoendelea kati yako na rafiki yangu, ..?’ nikamuuliza.‘Kiukweli,…sijui…alinipigia simu, akasema nikipata muda, anataka tuongee mimi na yeye, nikamuuliza kuhusu nini, akasema ni maswali ambayo hataki kuyaongelea kwenye simu,…nikamuuliza je yanahusu mtoto, au yeye, akasema mtoto….nikamwambia mimi nipo likizo, akasema hahitaji kuongea kiofisi…’akasema‘Unahisi anakuhitajia nini…?’nikamuuliza.‘Yeye anafahamu wewe ni rafiki yangu, nahisi ..yale yale ninayotakakujua kutoka kwako, huenda anataka kuyafunika, kinamna.. au…..’akasema‘Mimi siwezi kukuelewa kabisa,  wewe una hisia zako mbaya dhidi ya rafiki yangu au hebu nikuulize kwanini unawazia hivyo…?’ akaniuliza‘Kuwazia hivyo kuhusu nini…?’ akaniuliza‘Kuwa huenda huyo mtu aliyekuja wakati nipo kwa rafiki yangu anaweza akawa ni mume wangu, kwanini, rafiki yako unamuhisi vibaya, kwanini lakini..?’ nikamuuliza‘Kwanza tukubaliane, upo tayari tusaidiane kwa hili, la kumtafuta huyo mtu ni nani, au kumtafuta mwanaume aliyezaa na rafiki yako ni nani, na tuyafanye hayo kwa nia njema kabisa, sio kwa ubaya…?’ akaniuliza‘Halafu ukishamfahamu,…?’ nikamuuliza‘Tutakuwa tumemaliza tatizo, sasa itabakia kuona jinsi gani ya maisha yaendelee..nina imani wewe utakuwa huru,..hutahangaika tena, na mume wako atapona haraka….’akasema*****************‘Kwahiyo unatakaje hivi…?’ nikamuuliza‘Ninachotaka mimi, ni wewe kuwa muwazi, uwe mkweli, ….’akasema‘Kama hayo yatamsaidia mume wangu sawa, nitafurahi sana, lakini kunisaidia mimi, sijui unataka kunisaidia nini hapo, sijakuambia kuwa nina tatizo…?’ nikauliza‘Nina imani yote yanaendana…kwanza tuanze hivi,..kwanini mume wako akawa mlevi hivyo wakati awali hakuwa hivyo, naomba unijibu kwa uwazi, ili tufike kunakotakiwa…?’ akaniuliza‘Kiukweli, labda nijenge hisia tu…mume wangu kuna kipindi tulijadili kuwa tuzae, tupate watoto, na wazo lake kubwa ni kupata mtoto wa kiume, sijui kwanini analihitajia hilo sana…’nikasema‘Ikawaje…mjadala huo uliishia wapi…au wewe ulisemaje..?’ akaniuliza‘Nilimshauri kuwa hilo lisiwe kipaumbele chetu kwanza, kwasababu tupo kwenye harakati za kujiimarisha kiuchumi, lisubirie, akadai kuwa yeye anahitajia watoto mapema iwezekanavyo, ..hataki kuja kuzaa uzeeni…’nikasema‘Huoni kuwa ana ukweli fulani  hapo, kama wewe ulivyomshauri rafiki yako kuwa azae mapema, mbona wewe hukujiangalia au kuna tofauti kati yako na rafiki yako, unajiamini vipi hapo ..?’ akuliza‘Tofauti yangu na rafiki yangu ni kuwa mimi nina mume na muda wowote nikihitajia kuzaa, kabla sijafikia ukomo,  nitazaa kwa majaliwa ya mungu offcourse , lakini yeye mpaka ahangaike kumpata mwanaume na zaidi anayemtaka yeye, pili awe na uhakika wa ..…na huenda katika kulifanya hilo ikachukua muda, na jinsi gani ya maelewano a huyo mwanaume…’akasema‘Kwahiyo ukamshauri akazae vipi hapo…?’ akauliza docta‘Hilo la kuzaa vipi au na nani, nilimuachia yeye mwenyewe, sikutaka kumuingilia hayo…., si unajua alivyo, kwahiyo kama alizaa na nani, sio muhimu sana kwangu, kama hakuna tatizo…’nikasema.‘Kama hakuna tatizo, nahisi sasa kuna tatizo….ok, ..Je hukuwahi kuongea kuwa azae na kundi gani, walio-oa, au wasio, oa…au azae baada ya kufunga ndoa..najua hilo la kufunga ndoa lilikuwa ni gumu kwake, au sio, kwa jinsi alivyojiwekea misimamo yake,…ya kuchagua chagua sana..sasa ulimshaurije hapo?’ akaniuliza, kiukweli sikutaka kumwambia ukweli wa hicho tulichokubaliana na rafiki yangu.‘Nimeshakuambia hilo la kuzaa na nani, nilimuachia yeye mwenyewe, …’nikasema na kukaa kimia.‘Una uhakika?…anyway, sasa hebu nikuulize, baada ya wazo hilo, ni kwanini asitafute wanaume ambao hawajaoa…?’ akaniuliza‘Aaah, mbona maswali yako ya kujirudia rudia, jibu nimeshakupatia, na sijui alitafuta nani, sijui…’nikasema‘Nasema hivyo nikiwa na maana.  kiukweli mara nyingi huko nyumba alikuwa mbali sana na wanaume za watu, lakini ghafla nikaja kumuona akiwa karibu na wanaume wali-oa….au…mmm mlipanga iwe hivyo…?’akasema‘Docta, mimi sina tabia ya kufuatilia maisha yake, kama wewe una muda huo, mimi sina muda huo kabisa, ..kwahiyo sikujua ni nani na nani alikuwa karibu naye…kama ni wewe au mwanaume mwingine yoyote…’nikasema‘Au shemeji yake…’akasema docta na kunifanya nimtupie jicho‘Shemeji yake..!!? Nani, mume wangu au…na wanini unamtaja yeye, nilishakuambia yeye ni shemeji yake, na hata wakiwa naye, hakuna shida, ..na na…au  wewe unamshuku kuwa huenda ana mahusianio ya siri na mume wangu…mbona unantia mashaka ambayo sikuwa nayo kabisa..?’ nikamuuliza, nikimuangalia moja kwa moja usoni, na yeye akatabasamu na kusema;‘Sijamshuku,… ila nataka kuwa na uhakika, ili tuweze kumsaidia mume wako…, nahisi mume wako ana tatizo kubwa, sasa ni tatizo gani, hilo mimi kama rafiki yake linanisumbua kichwa sana, ....’akasema.Na hapo tukakaa kimiya kwa muda, mimi akilini nikawa nawazia hiyo kauli ya docta, kwanini ni kama anamshuku mume wangu, na nafahamu kuna muda mwingi baada ya kazi wanakuwa naye..japokuwa sio sanaNilimuangalia docta, …huku nikiendelea kuwaza,..labda,  inawezekana kukawa na lolote kati ya rafiki yangu na mume wangu, ..hapana hilo siwezi kabisa kuliamini, ...yule ni rafiki yangu mpenzi nimemuweka kwenye kundi la ndugu, siwezi hata siku moja kumfikiria vibaya, lakini huyu ni docta, na hana tabia mbaya, ni kwanini aliwazie hili, hapa nikaingiwa na mashaka....‘Shemeji huenda utaniona, kuwa naingilia ndoa yenu, huenda ukahisi kwa vile nilikukosa wewe ndio maana najaribu kuona kila mlitendalo sio jema,..au kama unavyodai wewe…, kuwa wazazi wako wamenituma, kufanya lolote ili kuiharibu ndoa yenu, ..lakini kwanini tufanye hivyo..‘Nikuulize wewe…’nikasema‘Sio kweli, mimi nina nia njema kabisa na ndoa yenu, ndio maana nilikuomba sana mapema tu, nilipoona rafiki yangu anabadilika, anakunwya kupitiliza, nikakuomba sana ukae  uongee naye, wewe ukapuuzia, mimi nahisi mume wako ana kitu kinamsumbua...’akasema ‘Mimi bado hapo sijakuelewa, tuongee nini hasa kuhusu starehe yake ya kulewa,..., mimi huko sina muda huo, kama kaona ni starehe yake muache endelee..au wewe unahisi kuna tatizo gani jingine...,mimi ninaanza kuingiwa na wasiwasi,  kuna nini kutoka kwa rafiki yako ulichokiona kingine…, niambie, mimi si rafiki yako unaogopa nini sasa…’nikasema‘Hapana, mimi sijui kitu,..ningekuwa na uhakika ningelikuambia mapema kabisa, ila ninachotaka mimi ni kujua ukweli…, nataka kuwa na uhakika, na uhakika huo nitaupata zaidi kutokwa kwako, na akili yangu inanituma, kuwa kuna kitu ambacho huenda kimesababishwa na mahusiano yenu wawili, wewe na mume wako, na kikaenda hadi kwa rafiki yako, sasa ni kitu gani hicho…’akasema‘Una maana mimi nimemfanya mume wangu atembee nje ya ndoa, …labda kwa vile..si ndio hivyo…na aliyekwenda kutembea naye, au anayetembea naye ni rafiki yangu, kisa kwa vile umewaona wakiwa naye karibu, au sio, na matokeo yake ni huyo mtoto, au sio..niambie ukweli….’nikasema‘Unaweza ukawa , haupo mbali na hisia zangu,…unanifahamu nilivyo, mimi ni docta, au sio, siwezi kutibu ugonjwa bila kujua vipimo, ndio maana natadadavua kuupta huo ukweli, na wewe hutaki kutoa ushirikiano…’akasema‘Kwahiyo…unataka kunipima nini…niambie…’nikasema‘Ukweli…nataka ukweli kutoka kwako…’akasema‘Hebu niambie kuna nini kinachoendelea kati yako wewe na rafiki yako, naanza kuhisi vibaya, kuwa huenda kuna jambo kalifanya, au kuna jambo unalifahamu dhidi ya rafiki yako, labda mlishirikiana wewe na yeye, sasa wewe unatafuta namna ya kujikosha kwangu, ili usionekane kuwa na wewe unahusika, sasa ...niambie rafiki yako kafanya nini?’ nikamuuliza kwa ukali.‘Shemeji siwezi kujua zaidi , ...yule ni rafiki yangu, lakini tuna mipaka yetu, sio rafiki wa kujua kila kitu, kuna yake anayafanya mimi siwezi kuyafahamu,..lakini naomba unielewe , mimi nilichokiona ni hiyo tabia yake ya kunywa kupita kiasi, ilianza tu…nikamuuliza akasema kaamua tu, na unielewe  sio kila siku ni kitoka jioni ninakuwa naye, hapana. Hebu nikuulize je hajawahi kulala nje...?’‘Kulala nje!!!..., hapana, hawezi kulala nje, kwanini alale nje, wakati ana nyumbani yake, labda kuwe na sherehe ya kukesha huko kazini kwao, hilo linatokea…, na hilo kwa siku hizi halijawahi kutokea, ...kuchelewa hilo nalikubaliana au kurudi akiwa kalewa sana huwa inatokea, na yah, …kuna siku alichelewa sana mpaka nikawa na mashaka, kama mara mbili tatu hivi…karudi alifajiri....lakini yeye ni mtu mzima, ulitaka hapo nifanye nini mimi, nijiumize kichwa na starehe za mtu, kaamua, tumuache, dunia itamfunza...’nikasema.‘Na akiwa kalewa sana ni nani anamleta nyumbani kama mimi sipo naye…, maana akilewa sana nikiwa naye, huwa mimi namleta mwenyewe, je kama sipo, ni nani mwingine  anapenda kumleta nyumbani, maana hapo huwezi kunificha kuwa halewi kiasi cha kutokujitambua?’ akaniuliza.‘Wewe unafahamu bwana, kuwa mara nyingi ni mdogo wake anayemleta, huwa akiona kalewa kupitiliza kiasi  cha kutokujitambua, sijui kwanini mtu mzina kama huyo anafanya hivyo…mimi nijuavyo kama haupo, anamuita mdogo wake, na mdogo wake, anafika hapo alipo anamchukua...’nikasema.‘Kwahiyo …eeh, mdogo wake atakuwa anafahamu mengi kuhusu kaka yake ambayo mimi siyafahamu, …sawa hapo eeh,.. umenipa wazo, jinsi  ya kulifuatilia hili jambo, huyo ni mtu mwingine anaweza kutusaidia, umeliona hilo hata wewe.....?’ akawa kama ananiuliza‘Mmhh,…kuliona …!!Lakini nikuulize kwanza, ni kwanini unamshuku rafiki yako, kaua, kafanya jambo gani baya sana,  maana unavyouliza ni kama vile kuna kesi ya mauaji,..., au hahaha, kufamaniwa, …hapana huyo sio mume wangu, …ka-kafanya nini kikubwa hivyo, mbona hutaki kuniweka wazi?’ nikamuuliza.‘Sijasema kuwa kafanya lolote baya, hilo uliweke akilini, ninachotaka kukifanya hapa ni kutafuta kama kuna tatizo, ta-ti-zo ...je  huko kuendesha gari kwake kwa kasi huoni kuwa kuna kitu kilitokea akawa anakimbia, au kuna jambo alikuwa akilifuatilia nyumbani kwa haraka, huenda alikuwa anakuja kuku....’akakatisha‘Unataka kusema alikuwa anakuja kutaka kunifumania au....acha hayo mawazo hayo docta, wewe ni msomi bwana…na familia yangu ni ya watu wastaarabu, hakuna mwenye tabia chafu kama hiyo...kama unayo wewe usifikirie kila mtu ana tabia kama hiyo.’nikasema kwa hasira.‘Hahaha…lakini, unanifahamu sana, nilivyo, lakini vyovyote iwavyo, sote sisi ni wanadamu inaweza kutokea  mtu akateleza, jua ibilisi mkubwa wa mwanadamu ni mwanadamu .., huwezi jua,...hata wewe unaweza kughilibiwa ukajikuta umefanya jambo ambalo baadaye linakuja kukuleta matatizo, ukawa unatafuta njia ya kujisafisha, lakini wenzako wameshaliona na huenda wamekuweka kati, dunia hii ina watu wabaya.....’akasema‘Mpaka sasa sijakuelewa msingi wa maswali yako...unachokitafuta hasa ni nini, kuwa mimi nina matatizo au mwenzangu ana matatizo?’ nikamuuliza.‘Sijawa na uhakika na hilo ndio maana nakuuliza ...maana kama wewe ungeliweka wazi, kuwa kuna tatizo, kwako au kwa mwenzako, ningejua jinsi gani ya kufanya, na nini  nifanye ili niweze kusaidia, lakini naona nyote mnanificha, ndio maana najaribu kuwa mpelelezi, kwa nia njema kabisa ....’akasema.‘Yatakushinda....siku hizi umeacha kazi yako ya udakitari unaanza kufuatilia ndoa za watu, haya na ili upate faida gani...’nikasema na yeye akaangalia saa yake, halafu akasema;‘Kuna watu wawili wanaweza kutusaidia kwa hil tatizo , ...ili kugundua kuwa huenda mwenzetu ana tatizo gani, hadi sasa kwa uoni wangu nimeona kuwa kuna tatizo, sasa ni tatizo gani, ni muhimu sana tusaidiane kulitafuta haraka iwezekanavyo kabla hali haijawa mbaya zaidi, ...’akasema.‘Umeona kuwa kuna tatizo, umeona kuna tatizo gani,..kuwa huenda ajali hiyo ilikuwa na msukumo fulani, si ndio maana yake hiyo, au..?’nikasema kwa upole, kwani hapo niliona kuna hoja ya msingi.‘Ndio ...hebu angalai hili bila kujali kuwa mimi ndiye nalifuatilia, angalia kwa nia ya kumsaidia mwenzako, na hatimaye kuisaidia ndoa yako, na urafiki wenu na huyo rafiki yako, huenda tatizo limeanzia kwako bila kufahamu ...’akasema.‘Nani na nani wanaweza kutusaidia sasa, maana hili naona umelivalia njuga, na ukianzisha jambo lako mpaka upate majibu, haya ili tuyamalize haya, ni nani anaweza kutusaidia, nataka uwe huru, kuwa unavyohisi sio kweli, ni nani atatusaidia....?’ nikauliza na yeye akasogea karibu yangu, na kusema kwa upole.‘Wa kwanza ni mdogo wa mume wako, ....japokuwa kwenye ajali hiyo hakuwepo , lakini nahisi anafahamu mengi kuhusu mienendo ya kaka yake....huyo naweza kuongea naye mimi, naona uniachie mimi huyo mtu,..nitambana mpaka atanieleza...’akasema‘Sawa nakuachia wewe hilo…na mwingine au huyo anatosha…?’ nikamuuliza, hapo nilianza kuingiwa na mawazo , nikijiulia kweli ni kwanini mume wangu aliendesha gari kwa mwendo huo, na ni kinyume na tabia yake, ...basi kulikuwa na jambo, lakini mbona hata mimi niliendesha kwa mwendo kasi,nilipopewa ujumbe huo kuja nyumbani haraka,kumbe  inawezekana ikatokea hivyo ..‘Kama ni kujua kwanini alikuwa akiendesha kwa mwendo kasi, mimi naona hakuna cha muhimu hapo, mbona hata mimi , leo nilijikuta nikiendesha kwa mwendo kasi  uliponipigia simu kuwa nije nyumbani kwa haraka, kwasababu kuna tatizo huku nyumbani...na sikujua kabisa kuwa nilikuwa naendesha kwa mwendo kasi.....’nikasema.‘Unaonaeeh,wewe ulifanya hivyo kuja nyumbani kwasababu hiyo ya msingi, je mume alifanya hivyo kwasababu gani ya msingi.., nikuulize swali ili uone kuwa kuna tatizo, je mume wako ana tabia ya kuendesha gari kwa fujo, hapana au sio namafahamu sana?’ akaniuliza.‘Hana kabisa tabia hiyo, ndio maana nashindwa kuelewa,.....’nikasema.‘Unaonaeeh, sasa tunaanza kuwa pamoja..?’ akawa kama ananiuliza.‘Ninaona nini hapo, kuwa pamoja kwa vipi, mimi nataka nifane unavyotaka wewe, sawa, hisia zipo, na kiukweli sio kwamba sina hisia kama zako, lakini nazipotezea, maana hao ni watu nawaamini, sasa kama kuna walakini, haya ngoja tuutafute, sawa?’ nikamuuliza.‘Ndio maana yake mimi nina imani kuwa  mume wako alikuwa akikimbia tatizo,....maana kama wewe huna tabia anayoihisi mume wako,...na alifahamu kuwa haupo nyumbani, basi huenda alikuwa akikimbia jambo, sasa alikuwa akikimbia jambo gani, au alikuwa akifuatilia jambo gani, ataulizwa hilo na watu wengi wakiwemo watu wa usalama, bima nk......’akasema, na mimi hapo nikatulia kidogo nikiwaza.‘Yawezekana ndio,…ndio maana hata hakutaka kwenda hospitalini...’nikasema.‘Kwahiyo huyo mmoja, anatosha kutusaidia….?’ nikauliza‘Mtu wa pili ambaye anaweza kutusaidia ni rafiki yako, ....’akasema.‘Kwani vipi shemeji ....rafiki yangu anahusikanaje na mambo yangu ya kifamilia..au ajali ya mume wangu, hapo ….ok, ok, ….lakini kama na yeye ni muhusika, atanisaidiaje,, hebu niambie hapo,?’ nikamuuliza .‘Akusaidie kujua kama anafahamu lolote, kuhusiana na mume wako, kama kuna tatizo linalomsumbua, maana inawezekana mume wako yupo kwenye mtego wa watu wanaomtishia amani, labda kama asipofanya hivi au vile anaweza akaingizwa kwenye matatizo, ....nasema tu, kama mfano, ....'akasema'Mhh, huko umekwenda mbali, rafiki yangu amrubuni mume wangu, na amwambie kuwa asipofanya hivyo, atafanya vile..kwanini..hapana, kwa maana hilo alilofanya rafiki yangu, tulishauriana mimi na yeye, sasa kwanini ...'nikasema'Mlishauriana, ndio, lakini umesema, hkumshauri amtafute mume gani, au sio..je kama alimtafuta mume wako,...?' akaniuliza na kunifanya nishtuke'Acha hayo maneno kabisa, usinichafue...hivi nikuulize kuna mtu anaweza kutembea na shemeji yake mwenye akili timamu, unazungumzia hapo rafiki yangu, unamfahamu kabisa alivyo, hapendii kabisa kutembea na wanaume  za watu, ...usimzushie rafiki yangu uwongo....'nikasema'Kuna kitu nataka tukihakiki...je wewe unaweza kufanya hivyo, kuongea na rafiki yako, au, nina wazo, hebu fanya hivi, unaweza ukamuita rafiki yako , akaja hapa hospitalini, na ikiwezekana aje na mtoto wake, anaweza kuja, au sio..?’ akaniuliza.‘Aje na mtoto, ...mhh, kwanini lakini, yupe bado ni mzazi, kwanini tumsumbue, atoke ahuko na mtoto kwanini lakini...na huyo mtoto wake unamuhitajia nini...hahaha nimeshakuelewa, unataka kufanya nini...hapana siwezo...’ akasema.'Sikiliza...ni muhimu sana...fanya hivyo, kuna kitu nimekiona , fanya hivyo, muite rafiki yako aje hapa hospitalini,..na mtoto, ....unaweza kufanya hivyo...?' akasema'Mhh.....' nikaishia kuguna, na sikuelewa kabisa docta anataka nini, lakini, ....NB: Docta anataka nini hapa, …mtoto…mtoto wa nini…?WAZO LA LEO: Urafiki wa kweli ni wa kujaliana, mwenzako akipatwa na tatizo, iwe ni kama wewe umepetwa na tatizo hilo. Ni faraja sana ukiwa na tatizo rafiki yako akawa anatafuta njia ya kukusaidia.‘Ningefurahi nimuone, tukiwa pamoja sote.....kuna mambo nashindwa kukuambia, maana nikikuambia kwa hivi sasa utaona kama nakudanganya, najaribu kuwaza kuhusu baba wa huyo mtoto, kabla ukweli haujabainika...’akasema.‘Mimi sijakuelewa hapo, lengo lako hapo ni nini, ni kutaka kujua baba wa huyo mtoto au unahisi labda huyo mtoto ni wa kwako kwa vile uliwahi kutembea naye nini..nikuambie ukweli, sio wa kwako, kwasababu hafanani na wewe kabisa, umenielewa…?’ nikamwambia‘Anafanana na nani…?’ akauliza akiniangalia kwa uso wa udadisi‘Anafanana na mama yake....’nikamdanganya, na yeye akacheka kicheko cha dharau‘Kweli..umemuangalia vyema..una uhakika kuwa anafanana na mama yake..?’ akaniuliza akitikisa kichwa kwa mashaka‘Nina uhakika kwa vile mimi nimemuona, …kwahiyo kama nia yako ni hiyo basi zoezi lako liishie hapa, na kwanini unatia shaka na jibu langu?’ nikamuuliza.‘Ok….mimi huko sipo kabisa, hayo unabuni wewe, siwazii lolote kuwa huyo mtoto ni wangu maana sio kweli kuwa niliwahi kutembea naye,.na kufanana na mtu fulani wakati huu, sio tija, maana watoto wachanga wengi hufanana, subiria akue kue, utajua anafanana na nani...’akasema na mimi nikatabasamu‘Kwanini umetabasamu,.....?’ akaniuliza.‘Kwa vile jibu lako limenipa faraja, na kuniondoa wasiwasi niliokuwa nao...nahisi itakuwa hivyo...’nikasema bila kusema zaidi‘Sasa fanya hivyo basi usipoteze muda, mpigia rafiki yako uone utakavyofanya ili aje hapa..nina imani akifika hapa, tutagundua meng nyuma ya pazia, niamini mimi‘Ok, hilo hakuna shida maana rafiki yangu ninamuamini sana, kama nilivyokuambia kuwa ni zaidi ya rafiki, ni ndugu yangu..., kama ni kulifanyia kazi hilo, kwa kupitia kwake, basi hakuna shaka, nitamuita aje na mtotoni sitaki kashifa kwenye familia yangu,...’nikasema.‘Sijasema hilo...na sioni kwamba kuna kashifa hapo, usijali, na wala usiwe na wasiwasi....’akasema.Nilitulia kidogo nikiwazia hilo wazo la huyo docta, kwa namna moja nilikuwa nimeliunga mkono, huenda kweli mume wangu yupo kwenye matatizo, makubwa, lakini hataki kunihusisha, ila siungu mkono ya kuwa mume wangu huenda ana mahusiano na wanawake wa nje, hususani kutembea na rafiki yangu‘Kweli atakayeweza kunisaidia kwa hili na kuondoa hii taswira iliyoanza kujengwa nafsini mwangu ni rafiki yangu, na docta atabakia mdomo wazi, ngoja nimuite.Nikampigia simu rafiki yangu huyo, kwa muda huo alikuwa kakaa nyumbani kwake anaangalia runinga, na aliposikua kuwa ni mimi akawa na hamasa sana ya kuongea na mimi…‘Nakuomba uje hapa hospitalini, alipolazwa shemeji yako, mara moja…’nikasema‘Kuna nini..!!! Ina maana..she-she-, shemeji anaendeleaje kwani..?’ akuliza akionekana kuchanganyikiwa kwenye simu‘Tafadhali nakuomba uje tu,…’nikasema‘Sasa na…oh, na mtoto itakuwaje…?’ akauliza‘Njoo naye, usimuache, tafadhali…’nikasema na kukata simu.Nilijua atafika tu, maana mimi nimekuwa nikimtumia sana kwenye shughuli zangu nje ya kazi yake, ili kumsaidia kuongeza kipato, na anafahamu nikimpigia simu ya namna hiyo, basi ni jambo la haraka, na anaitikia alifanyie kazi mara moja.‘Una uhakika atakuja…?’ akaniuliza docta‘Atakuja…ila naona kama nimempa hali ngumu,…asije akapatwa na mengine…’nikasema‘Hamna shida, rafiki yako huyo ni shupavu, namuaminia sana, mtu anaweza kupigana ngumi na wanaume, sio mchezo…’akasema na kucheka kwa mdhaha…‘Lakini sio kwa mambo kama haya, yanashtua sana, sio vitu vya kuchezea, au kumjaribu mtu..hapana, utani mwingine uufanye lakini sio kwa afya, kifo, na…hapana, hayo, hayana uvumilivu…’nikasema‘Ni kweli, hata sisi madocta tunalifahamu hilo, ndio maana hata mimi najaribu kuliweka hili jambo, liwe rahisi kwenu..najua tutalimaliza salama, na rafiki yangu atapona kwa haraka, tushirikiane tu…’akasema na mimi nikamtupia jicho la kujiuliza‘Unajua kiukweli, umenifanya nafsi yangu ianze kufikiria mambo ambayo sikutaka kabisa kuyafikiria,..nimekuwa nikiyapiga vita sana…lakini kila hatua unanifanya nianze kuwaza mengine..mungu anisamehe tu…’nikasema‘Usijali, kama yametokea yametokea, kama hayapo basi, tutayamaliza kwa amani, ila mimi ninachotaka ni kuhakikisha, kuwa hakuna cha kulaumiana..hakuna cha kumuongezea mgonjwa mawazo, na yote ni sisi watu wake wa karibu..tufanye jambo, nakuomba ten asana ulifahamu hilo…’akasema‘Mbona wanachelewa hivyo…?’ nikauliza, nikikwepa maongezi yake, maana muda huo akili yangu ilikuwa kwingine kabisa, namuwazia mume wangu, nahisi kama kuna kitu hakipo sawa, miguu inaanza kuniisha nguvu..‘Ngoja nikaangalie nahisi watakuwa tayari, labda kuna kitu wanakisubiria…’akasema docta na kuondoka kuelekea huko. Na mimi pale nilitaka nimfuate nyuma,lakini sheria ikanikwaza.*************Baadae docta akarudi…hakuonyesha furaha usoni, japokuwa alikuwa akijaribu kujificha kinamna kwa tabasamu la uwongo na kweli, na hali hiyo ikanizidisha mashaka, nikamuuliza kwa haraka haraka…‘Vipi huko ulipokwenda wanasemaje, mume wangu anaendeleaje, maana ungechelewa kidogo tu na mimi ningelikuja huko huko..?’ nikamuuliza‘Hali yake inendelea vyema usiwe na shaka, …wamemchunguza na kuona kila kitu kipo sawa…’akasema‘Sikuamini docta, kwanini…na mimi niende nikamuona tu jamani…’nikasema huku nikishika kichwa.‘Shemuuuh, …huaniamini…anaendelea vizuri, hali ya jana sio ya leo, leo anatizamika, ika kwa vile alikuwa kwenye uchunguzi, lazima hali kama hiyo itakuwepo, kuinuliwa, hivi na vile…wamechunguza wamesema hakuna sehemu iliyovunjika…’akatulia kidogo.‘Na mashaka yao walioyokuwa nayo awali yameondoka, kwani walihisi huenda kuna athari za ndani kwa ndani..kiukweli hakuna athari yoyote iliyojificha ya ndani kwa ndani, ila bado wanaendelea kumfanyia uchunguzi zaidi , kwani bado alikuwa analalamika maumivu, lakini ni kwasababu ya kashikashi hizo, yatakwisha, ndio maana nataka wewe na rafiki yako, tuje tuongee vyema, kwa hili mtaniona mbaya….’akasema‘Kwahiyo uliweza kuongea naye…?’ nikamuuliza bila kujali kauli yake hiyo.‘Bado hawajaruhusu kuongea na mtu, niliongea na docta wake tu, wakati wanamrejesha wodini, na kweli nilimsikia akilalamika maumivu, hasa ya mgongo na kiuno,...inawezekana ni kutokana na hali halisi, kama nilivyosema… na kule kulala muda..unajua mwili ulivyo…, lakini yupo vizuri, yupo… yupo vizuri...’akasema‘Unasema kutokana na hali halisi kwa vipi….?’ Nikamuuliza nikimkazia macho.‘Kwa vile ajali hiyo imegusa uti wa mgongo, kwahiyo kuna maumivi sehemu kubwa ya mwili, kwa hivi sasa bado wanaendelea naye , tuwape muda wafanye kazi yao, ili kuhakikisha kila kitu kipo sawa, usijali mambo yatakuwa sawa...’akasema huyo rafiki wa mume wangu.‘Lakini, niambie ukweli, wewe kama docta unahisi vipi, huko kulalamika mgongo na kiuono, inawezekana ni jambo la muda, litakiwisha ni kweli hakutakuwa na athari zingine zinaweza kujitokeza huko baadae?’ nikamuuliza.‘Mhh, hakuna,..maana vipimo vinasema, ila ngoja tusubirie wamalize kazi yao, nitaongea nao, nitakagua ripoti zao, lakini yale muhimu yanayotuhitajia sisi, tuyafanye, tuhakikishe tunakwepa yale yote yanayoweza kumkwaza, maana kama kuna athari zitakuja kujitokeza zitakuwa ni za kibinadamuu, mimi sina wasiwasi na hilo....’akasema.‘Kwahiyo sasa hivi yupo macho , nikienda naweza kuongea naye…?’ nikauliza‘Ndio yupo macho, kazindukana, lakini bado madocta wanamfanyia uchunguzi wa hapa na pale, naona wamekutana wote, kuhakikisha kuwa hawafanyi makosa, na hilo la kulalamika, nina uhakika na kutokana na hiyo mitikisiko ya kumuinua, inua, itakwisha tu, ....’akasema.‘Mhh, hapo mimi bado nina mashaka, mpaka nionane naye…na kama wameshindwa wasema tumpeleke juu zaidi, au...?’nikasema.‘Hawajashindwa bwana, …nakuhakikishia hilo, huniamini mimi shemeji,…ila mimi nilikuwa nakushauri kitu,naona wewe una shughuli nyingi umeziacha bila ya maagizo,kwa vile mimi nipo likizo, ninaweza kubakia hapa, ili niendelee kuona hali ya mgonjwa kwa ukaribu zaidi na kama kuna lolote la kusaidia, nisaidie, unaonaje,…’akasema‘Kuondoka…haaah weeeh!!! Hapana, kwanza umesahau ulichoniagiza au…?’ nikauliza‘Oooh…hilo achana nalo,muhimu ni wewe na shughuli zako, najua hilo tutalifanyia kazi, maana lina umuhimu wake, hasa kwa mgonjwa, …. Mgonjwa pamoja na matibabu, lakini kuna mazingira akiyaona, akisikia kauli zenu, anaweza akatatizika, hili muwe makini sana …’akasema‘Sasa ndio unanishauri niende nyumbani, akiona sipo, huoni atajisikia vibaya…?’nikauliza‘Hapana, kwa vile mimi nipo najua jinsi gani ya kuongea naye…hilo lisikutie shaka, maana tunaweza kuacha mgonjwa, kwa ajili ya mgonjwa mwingine…’akasemaMimi sikukualiana na wazo lake hilo, la mimi kwenda nyumbani bila kumuona mume wangu, nikawa nimekaa kimia, akilini nikimuwazia mume wangu, ina maana kitu kidogo tu kinaweza kumfikisha mwanadamu hapo, ooh, sijui ni kosa langu au kuna tatizo, jingine kama ni kosa langu sijui nitajijutiaje, ......hapo nikahisi machozi yakinilenga lenga.Nikainua kichwa kumuangalia docta, nikamuona akinichunguza kwa macho, na muda huo machozi yanakuja kwa kasi,… kabla sijaathirika na hiyo hali, nikageuka upande mwingine, docta akaitambua hiyo hali na kusema;‘Usiwe na shaka, ...nakuhakikishia kuwa mume wako hana matatizo, ...ni swala la muda tu, utakuwa naye, ajali ni ajali, na hiyo ajali yake ilikuwa ni kubwa sana, hutegemei mtu aliyetoka pale awe hai, uhai wake bado mkubwa sana, hata yeye sizani kama ataamini kuwa aliweza kutoka hapo salama....’akasema na mimi sikusema.Na ni wakati nainua kichwa kuangalia sehemu ya nje, kwenye mlango mkubwa ndio nikamuona rafiki yangu akija kwa mbali, na wakati huo huo docta akawa anaongea na simu yake. Na alipomaliza kuongea na simu, akanigeukia na kusema;‘Ni vyema kwa leo, hata kama tutaruhusiwa kumuona mgonjwa, wewe hakikisha huruhusu watu wengi kuonana na mume wako, hata kama ni rafiki yako, mimi mwenyewe nitalisimamia hilo ...’akasema‘Kwanini,…si umesema yupo sawa, ..ok, tutawasikiliza madocta watakavyosema au sio,. Kuonana na watu kwa wengine ni faraja au…’nikasema‘Hata mimi ni docta, au huniamini, kwa vile kuna mambo nimeshayaona, nisingelipenda akaja mtu akamzidishia mawazo, hasa nyie wawili,…’akasema‘Ndio maana maana ya kumuita rafiki yangu au..sasa na mtoto ni wa nini,…?’ nikamuuliza, na je rafiki yangu akija hapa, hatamuona mgonjwa,…?’ nikamuuliza‘Yeye kumuita hapa, awali nilitaka iwe hivyo, tumuone mgonjwa pamoja, nyie ni marafiki au sio, lakini kuna kitu nilitaka kiwe wazi,…lakini baada ya kumuona tena mgonjwa alivyo, naona hata akija rafiki yako, tutaongea naye tu,.’akasema‘Haitakuwa vyema, tutamuambia asifanye lolote …amuone tu…’nikasema‘Mhh….kiukweli hivi sasa mume wako hahitaji mshutuko wowote, hahitaji, kitu cha kumpa mawazo, ni bora akutane na wewe tu na mdocta mpaka hapo hali itakapo kuwa sawa…’akasema‘Sawa , hilo halina shida, kama umesema hivyo, hakuna shida,..nitafanya hivyo hivyo, ila tutakuwa tumemsumbua rafiki yangu aje tu, bila kumuona mgonjwa, sio vizuri, lakini sawa, nimekuelewa…’nikasema‘Ok, sasa unaonaje wazo langu, la wewe kurudi nyumbani kidogo, umalizane na mambo ya kazi, halafu utarudi, ikibidi,..nahisi huyo rafiki yako hatafika....na kwa vile ni mzazi, tumuache tu, tutakuja kuongea naye hata nyumbani.....’akasema , alikuwa hajamuona huyo rafiki yangu maana sasa alikuwa anakuja muelekeo wetu lakini docta alikuwa kampa mgongo.‘Anakuja..nashukuru kaja,…hata hivyo, mimi ninachotaka nikaonane na mume wangu kwanza,…au…hapa sina amani kabisa, …’nikasema.‘Mumeo anaendelea vyema, usiwe na wasiwasi, tutakwenda kumuona lakini tukishamalizana huku, najua mengine, au mpigie rafiki yako asije tutaongea naye huko huko…’akasema hivyo.‘Kaja…ili tuweze kuyamaliza haya mambo, ili na wewe uweze kuondoa hofu yako dhidi yake ..’ nikasema na huyo rafiki yangu akawa sasa keshafika, kasimama nyuma ya docta.‘Sawa kama una uhakika …kuwa atafika, sawa, nina mambo yatakuwa sawa, mimi nilikuwa nimekitaka ni kumbana rafiki yako, aseme ukweli, …lakini kwa vile kuna hii hali ya sasa, …haina haja ya kulazimishana…ila nyie kama binadamu ningeliwaomba muwe wawazi, ili na mimi niweze kutoa ushauri unaofaa, kama mtakwua mnanificha ficha mambo, inaniwia vigumu, haya ngoja aje tuone atatusaidiaje, nina uhakika….’kabla hajamaliza rafiki yangu akakohoa na kusema;‘Sam-samahanini kuwakatili kwenye mazungumzo yenu, maana mtoto nimemuacha nje, Haya nipeni habari za mgonjwa, .maana umenifanya nitoke wangu wangu hata bila ya kubadili nguo, niambie kuna usalama huku...’akasema kweli akionyesha mashaka.‘Oh….’docta akashtuka, akisikia rafiki yangu akiongea nyuma yake, akaguna hivyo, halafu kwa haraka akasema;‘Wewe umemuacha mtoto nje ndani ya gari, na nani?’ akauliza docta kwa mshangao.‘Kuna mtu yupo naye, usitie shaka, hahaha, naona ulivyoniangalia, ulifikiri nimemuacha ndani ya gari peke yake, hapana,…weeh, hapa kwenye natamani nirudi, siamini mtu kabisa...’akasema huku akiniangalia mimi machoni.‘Karibu…’nikasema‘Haya niambieni hali ya shemeji ipoje..nakuona kama unalia...kuna usalama kweli…?’akasema rafiki yangu huyo akiniangalia usoni kwa mashaka, na mimi nikapitisha leso machoni.****************‘Kuhusu mume wangu,...mhh, bado,...sijaonana naye tangu wamchue , wanasema wanataka kumchunguza zaidi leo, uchunguzi wa kawaida, …. lakini kwa taarifa za kupitia huyu rafiki yake,…docta…. wanasema hajavunjika mahali,....ila analalamika maumivu kwenye kiuno...na mgongo, na hilo kwangu mimi naona ni hatari au...’nikamwambia huyo rafiki yangu.‘Kwenye kiuno..na mgongo mhh, au huko kulala lala namna moja bila kujigeuza kwa muda, lakini vipimo vitasema au sio docta,.. mimi sioni kwanini uwe na wasiwasi....kwani majeraha ya hiyo ajali yamegusa mgongo, kichwa, au…?’ akasema huyo rafiki yanguDocta aliposkia hivyo alimuangalia huyo rafiki yangu kwa makini…na baadae akasema;‘Hajapata athari kubwa sehemu hizo, kiukweli hali yako haipo mbaya kihivyo, uchunguzi wa leo ni wa kujirizisha tu,.... tumpe muda, tuwape muda madocta wafanye kazi zao au sio.....’akasema huyo docta akimwangali huyo rafiki yangu, na huyo rafiki yangu akawa kama hataki kuongaliana na docta, akawa ananiangalia mimi na kusema;‘Kwahiyo eeh,…. Ulivyoniita kwa haraka hivyo…nahisi kuna jambo la dharura,…unajua mimi nilipanga kuja kumuona lakini ulivyoniita nikajua kuna tatizo jingine kubwa, ooh, umenishtua kweli, ..sasa eeh, hiyo ajali ilitokeaje?’ akaniuliza‘Hata mimi sijajua vyema , mambo yamekuwa ya harakaharaka sana, ila watu nilio-onana nao wanadai kuwa eti mume wangu alikuwa kwenye mwendo kasi, ...ndio ikatokea hiyo ajali, gari likawaka moto...’ nikasema.‘My, my ….mbona mkosi huu…mhh, unajua najiuliza mbona shemeji hana tabia hiyo ya kuendeshe gari kwa mwendo kasi, ilikuwaje lakini, nahisi …oh,…au.., alikuwa anakimbia nini, kuwahi kitu gani, ....aliogopa nini…mmh hapo kuna tatizo....’akasita kidogo na kugeuka kumwangalia huyo docta, na haraka akaniangalia mimi na kusema;‘Na hiyo ajali ilitokea wakati anatokea aah....wapi?.’akasita kidogo na kumalizia hiyo `wapi’ kwa kusita, na kugeuka kumwangalia docta inaonekana hakuwa na amani kuwepo huyo docta. Na huyo docta akawa anajifanya hatuangalii sisi‘Sina uhakika sana....maana kama ninavyokuambia mambo yametokea kwa haraka sana,..sijapata muda wa kulifuatilia hilo,...sina uhakika sana alikuwa katokea wapi...’nikasema na doca akasema.‘Atakuwa alitokea maeneo ya huko kwenu, na sio kazini, kama angelitokea kazini angekuwa upande mwingine wa barabara...ukiangalia lile gari lilivyokuwa ...’akasema docta, na huyo rafiki yangu akasema.‘Yaah, itakuwa hivyo.........’akasema na huyo docta akamkatiza.‘Kwani uliwahi kuonana naye kabla ya hiyo ajali...?’ akauliza na mimi nikainua kichwa kumwangalai rafiki yangu ambaye alikuwa katulia na nilipoona hajibu kitu, mimi nikasema;‘Kama alitokea huko kwako, mimi …si tungeliliona hilo gari likipita maana pale ndani tukiwa tumekaa tunaona bara barani, eti, wewe uliliona gari la mume wangu likipita , yawezekana labda, alitaka kuja kumuona mzazi, sasa kwanini akapita..na kuna muda nilimpigia simu akasema yupo kazini, sasa hapo mimi naona ..lakini tuyaache tu, nitakuja kuyafahamu yote hayo..’nikasema.‘Alikuambia anakuja kumuona mzazi sio ...?’ akauliza docta‘Ndio anakwenda, kumuona mzazi ….’nikasema‘Mzazi gani huyo…?’ akauliza‘Nakumbuka …unajua hata wakati mzazi huyo yupo hospitali alikwenda kumuona na nahisi ndio huyo alikuwa anakwenda kumuona nyumbani kwake…’nikasema‘Ni nani huyo…sizani kama kuna mzazi mwingine zaidi ya huyu rafiki yako, ,…na nakumbuka mimi niliwahi kuongea naye, akaniambia rafiki wa mke wake kajifungua, sasa sizani kama kuna mzazi mwingine, hajaniambia …au …?’ akauliza akimuangalia rafiki yangu.‘Yupo mwingine bwana….nahisi anaweza akawa mke wa mfanyakazi mwenzao, au ..mfanyakazi mwenzao, …sina uhakika, maana sikupata muda wa kumuulizia zaidi….’nikasema‘Mhh…labda….’rafiki yangu akaguna na kusema hivyo..‘Sio labda, ni kweli…’nikasema‘Sizani…ehe, hebu rafiki yako atusaidie hapo…’akasema docta na kabla hajamaliza rafiki yangu akadakia kwa kusema;‘Unajua nimekumbuka, kuna watu walikuwa wakiongea, kuhusu ajali iliyotokea kwenye kona ya barabara ya kuingia barabara inayotokea bara bara kuu, wanasema ni ajali mbaya, na hakuna mtu aliyepona, ina maana ndio hiyo…?’akasema rafiki yangu na kuuliza.‘Itakuwa ndio hiyo…’akasema docta‘Kwakweli hapa nilipo nashindwa hata cha kuongea, maana sielewi, ni kitu gani kilimfanya aendeshe gari kwa mwendo kasi, ...sijui alikuwa kalewa, au alikutwa na janga gani, maana siku hizi kama unavyojua, mume wangu kabadilika, amekuwa mlevi...’nikasema.‘Nahisi ana tatizo, nilikuulizia hilo ..lakini sasa,…tuseme ajali haina kinga…sasa eeh.. hebu niambieni kinachoendelea maana kama nilivyowaambia mtoto yupo kwenye gari, sitaki kukaa sana, ninaweza kwenda kumuona mgonjwa mara moja, ....?’ akauliza rafiki yangu.‘Mhh,…hapana… kwa hivi sasa haitawezekana, tulitaka iwe hivyo, kabla hujapigiwa simu, lakini nilivyokwenda kumuona kwa hivi sasa hitawezekana, rafiki yako alitaka uwe karibu naye karibu …kwa muda huo.., unajua tena mlivyoshibana namuona , ..ana wasiwasi sana, nimemuambia hakuna cha kuhofi…’akasema‘Mhh…ni kweli hata ingelikuwa ni mimi….’akasema rafiki yangu.‘Ila hata hivyo nina mazungumzo mimi na wewe na…shemeji hapa, muhimu sana tukaongea, sasa sijui, na kama huna haraka, basi tusubirie ndani ya gari, maana mgonjwa hatakiwi kwasasa kuongea na watu wengi, mkewe sawa, anaweza kwenda kumuona mara moja, haijuzu…’akasema‘Maongezi kuhusu nini hasa …?’ akauliza kwa mashaka, nakuniangalia mimi‘Kuhusu mgonjwa, …na mengineo yake, wewe utanisaidia sana kwa hili, kama utakuwa mkweli, na halikadhalika rafiki yako, ni muhimu sana hili jambo, mkawa wawazi ili tuone jinsi gani ya kuliweka sawa,..ok, sasa sikilizeni,..eeh,…umesema mtoto yupo kwenye gari, nilikuwa nataka nimuone, unamficha sana, kwanini, unaogopa nini…, hahaha,, ...’akasema huyo docta akimwangalia huyo rafiki yangu, na huyo rafiki yangu akawa anamkwepa wasiangaliane, na kugeuka kuniangalia mimi, na mimi nikadakia na kuuliza‘Mtoto wa nini bwana, wewe kwa sasa hutakiwi kuondoka hapa, mimi naona ..eeh ...’nikasema kabla sijamalizia simu ya docta ikaitaDocta akasema samahani aipokee hiyo simu, ni mteja wake muhimu…na kuchepuka pembeni, na mimi nikabakia na rafiki yangu, na hapo nikaona ni nafasi nzuri ya kuongea nilichotaka kukiongea, na sikutaka maongezi yangu hayo yasikiwe na huyo docta, nikamgeukia rafiki yangu na kusema;.‘Nilikuwa nataka unifanyia kazi maalumu, ni kazi ambayo sikuwa nataka ifanywe na mtu mwingine...,lakini kwa sasa sina jinsi, na kutokana na maongezi yangu na huyu docta, nimeingiwa na mashaka …kuna kitu mume wangu ananificha…, nataka wewe unisaidie kwa hili, uchunguze ni kwanini mume wangu alikuwa na haraka hivyo, nina imani hiyo ajali sio ya bure bure, kuna jambo,…’akasema‘Hata mimi naona hivyo, sio kawaida yake, kuna jambo..sizani kama …’akasita.‘Sasa tuache dhana,..nataka uutafute ukweli, fuatilia nyendo zake, alikuwa anatokea wapi…maana alikuwa kwenye kikao, kwanini akatoka kwenye kikao kwa haraka, kuna nini alikuwa akifuatilia, na ni kwanini akaendesha kwa mwendo wa kasi hivyo, kuna kitu hapo…umenielewa hapo...’nikasema‘Mhh…kwani docta kasemaje..?’ akaniuliza.‘Docta ana mambo yake, ana shuku shuku zake..mimi sijamuelewa, …muhimu kwangu, ifanye hiyo kazi, wewe ondoka ukaifanye mengine niache mimi na docta tutayamaliza…’nikasema‘Hujamuambia docta kuhusu mambo yetu, ..?’ akauliza‘Yapi…?’ nikamuuliza‘Si haya ya mtoto, tulivyokuwa tumepanga, mpaka ikatokea hivi, unakumbuka tulipanga nini, tukasema iwe siri yetu hata iweje tusije kuitia au sio, kumbuka,….ahadi ni deni….’akasema‘Ni siri ...hilo siwezi kusahau, jamaa kanidadisi wee kafika sehemu kasalimu amri sasa anataka kupata taarifa kupitia kwako, mimi nakuahidi kuwa itaendelea kuwa siri, niamini hilo, unasikia, na wewe usije kunisaliti, ufunge huo mdomo wako, maana huyu docta ni mjanja sana, umenielewa…’nikasema‘Sawa nimekuelewa,...kama ni hivyo nimekuelewa sana aheri umenishtua maana sikujua umeniitia nini..., lakini sasa kuhusu hiyo kazi mbona ni inakuja kuturudia, eeh, hebu elewa hapo…’akasema kwa kusita‘Sikiliza mimi, kuturudia kwa vipi, na wewe bwana, haya yetu hayaguswi, unaonaeeh,..ninachotaka ni hivi, nijue kila kitu, kuhusu mume wangu... , sio kawaida yangu kufanya hayo lakini sina jinsi...'nikasema'Nahisi kuna kitu, naanza kuingiwa na mashaka, sasa nataka kujiaminisha mwenyewe, je ni kweli wanayosema watu kuwa mume wangu ana tabia chafu, kuacha hizo za ulevi,...je kuna jambo la kunitia aibu, unajua kazi zetu zilivyo, kashfa zinaua soko, na wazazi wangu wakijua, nitaumbuka...'nikasema'Mhh..lakini....'akataka kujitetea'Mapema nikijua ni bora zaidi, tutajua jinsi gani ya kuyafukia mashimo, unanielewa hapo, hakuna jinsi, kama kafanya kafanya, lakini...kafanya nini...kama ni kazi za hivi hivi kupata soko, sawa, lakini kama ni mambo ya kibinadamu, labda...nasema mfano...tuone jinsi gani tutamsaidia...'nikasema'Kama inatuhusu sisi wenyewe je...?' akauliza'Kwa vipi...?' nikauliza'mfano hii soo yetu...naona kama inakuzwa, na sijui docta kazungumzia nini, ndio nilitaka niongee na yeye nijue anajua nini, labda kasikia kitu...'akasema'Hajasikia lolote, ndio ananichota chota mimi, nimuelezee, na mimi siwezi kuyaongea mambo yetu, kwa vile ni sirii yetu, sasa wewe tafuta bwana mtafute huyo mume muongee naye mliweke sawa, unanielewa...nilitaka nionane naye, lakini naona ..hata sijui kwanini umeninfanyia hivyo...'nikasema'Kwahiyo....?' akauliza'Mii ninachotaka ni kufahamu nyendo za mume wangu, ilikuwaje mpaka ikatokea hivyo, nikijua nitajua jinsi gani ya kumsaidia..nataka hilo ulifanye haraka iwezekanavyo, namuombea apone tu….nampenda sana mume wangu,sitaki aje kukutana na kashfa mbaya, sijui kwanini,...ila nahisi kuna kimwanamke kinamsumbua, kama kipo nataka nikifahamu haraka iwezekanavyo, na nitajua jinsi gani ya kumfanya, atahama jiji...atajiua kabla hayajamkuta mauti…’nikasema‘Mungu wangu, ina maana utamfanya kitu kibaya...?' akauliza'Hutaamini kama nini, mimi na wewe ni rafiki, lakini hujawahi kuifahamu sehemu ya pili ya nilivyo..hutaamini...'nikasema nikionyesha uso ambao hajawahi kuuona kabla, nilimuona akitikisika.'Kama ni hivyo, hapana......siwezi...'akasema'Eti nini huwezi...acha tabia hiyo,…umeshanifanyia kazi zangu nyingi zaidi ya hii, hii ni muhimu kwangu kuliko, nataka nifahamu hili kabla mume wangu hajakaa sawa…unanielewa, na mengine uniachie mimi mwenyewe, nitajua ni nini la kufanya, 'nikasema'Mungu wangu kwanini ....mbona imekuwa hivyo tena...'akasema'Ogopa kuchezewa ndoa yako...unakuja kulifahamu hilo ukiolewa...'nikasema'Kwahiyo, hata kama aliyefanya hivyo ni mtu wako wa karibu...?' akauliza'Mtu wangu wa karibu hawezi kunifanyia hivyo, hilo halipo, ...sizani, ni nani huyo, hapana, sizani, eti docta anakushuku wewe...'nikasema'Docta, kasemaje....?' akauliza kwa mashaka.'Achana naye, ...sasa sikiliza fanya hivi, sehmu ya kuanzia, hebu jaribu kugundua huyo mzazi ni nani, huyo mzazi aliyekwenda kumuona hospitalini, na baadaye akaenda, au akataka kwenda kumuona nyumbani, ni nani,…nahisi ukianzia hapo unaweza kufika mahali, nahisi kuna kitu hapo, sitaki kumshuku mume wangu vibaya, lakini huyo mzazi ana lake jambo, nahis ndiye kidudud mtu….’akasema‘Mzazi…!! Mzazi gani huyo…na kama ni kweli..?’ akauliza‘Sipendi…unasikia, sipendi... nimekutuma kazi, fanya kazi…au…mbona una mashaka mashaka…sio kawaida yako, …utaifanya hi kazi au hutaifanya…?’ nikamuuliza na mara docta huyo akaja..WAZO LA LEO: Ni vyema tukajenga tabia ya kuhakiki mambo, tusikimbilie shuku, au dhana mbaya. Ukiangalia kwa makini, dhana mbaya zinachukuliwa kwa uharaka zaidi kuliko dhana nzuri, watu wanafikia kuchukiana kisa , kasikia, kisa, kaambiwa....!Waliokuwa marafiki wanakuja kuwa maadui, na hata vita vingi duniani vimeanzia huko..watu wanafikia kuuana, kisa ni dhana, kisa alisema fulani, na maadui wanatumia mwanya huo, kuongeza fitina na propoganda potofu. Tujaribuni kuwa na uhakika na mambo ya kusikia, tusikimbilie hatua, kabla ya kujirizisha,.‘Docta ana mambo yake, ana shuku shuku zake..mimi sijamuelewa, najua ni kwanini,…muhimu kwangu, wewe uifanye hiyo kazi niliyokupa…sasa.., wewe ondoka ukaianze hiyo kazi mara moja, mengine niache mimi na docta tutayamaliza…’Tuendelee na kisa chetu….***************Docta alikuwa anakuja, akiwa kashikilia simu yake mkononi, kama anaandika kitu kwenye simu yake, nahisi alikuwa akiongea na mtu fulani muhimu kwake…kuna muda alikuwa akiongea huku anageuka kidogo kutuangalia, ikanipa mashaka kuwa huyo anayeongea naye, anaweza akawa na jambo na sisi..lakini sikuwa na shaka na hilo.Niliona kamaliza kuongea na sasa alikuwa akija pale tulipokaa mimi na rafiki yangu, lakini  alikuwa hatuangalii, anaangalia simu yake,.. na alipotukaribia tu ,simu yake ikaita tena, ikabidi ageuka na kurudi pale  alipokuwa awali, akaendelea kuongea na simu yake, na kwa muda huo rafiki yangu alikuwa kasimama hajui afanye nini,…‘Sasa wewe unasubiria nini, nenda kaifanye hiyo kazi, ukimsubiria docta…akija hapa, ataanza kukudodosa, kwa maswali mengi ya ujanja ujanja…na lengo lake jingine anataka kumuona mtoto, nahisi kuna jambo analifahamu, anataka kulithibitisha,..au kuna jambo analifuatilia….’ nikasema hivyo.‘Mhh,…ni kweli naondoka…ila mimi sijakuelewa hapo.., maana unachotaka ni kama mtu kuchunguza kivuli chako, ni mambo ambayo hata wewe mwenyewe unayafahamu,..’akasema‘Nayafahamu kwa vipi, sijakuambia uchunguze mambo yetu, mimi ninachotaka ni wewe kuchunguza hili tukio la mume wangu, chanzo chake, na ni nini kipo nyuma ya haya yote, unajua…mimi sitaki mambo ya kusikia,..nataka ukweli, nataka uhakika,..sawa hisia hizo zipo, watu wanasema hili na lile, lakini mimi sio mtu wa kihivyo….nataka tuupate ukweli…’nikasema‘Kwahiyo eeh, hili….’akasema na kabla hajamaliza, nikamkatiza kwa kusema;‘Sitaki nikufundishe kazi…. siku zote nikikuelekeza kazi unasema nisikufundishe nimeshakupa kazi basi nikuachie wewe mwenyewe utajua jinsi gani ya kuifanya,…iweje leo,  kulikoni, unajua naanza kukutilia mashaka,…’nikasema na yeye hapo akabakia kimia.‘Katika jambo silitaki, ni kuwatilia mashaka watu wangu ninaowaamini…wewe nakuamini sana, nilikupeleka shule usomee ujasiri, ujua jinsi gani ya kujilinda, na uje kunisaidia na mimi, …unilinde kwa kila hali, unakumbuka, uliapa mbele yangu, ndio, urafiki upo pale pale, lakini mengine ni dhima, unanielewa hapo….’nikasema‘Aaah,..ndio..naelewa…lakini kabla sijaifanya hii kazi, ni lazima tukubaliane…eeh, kuna utata hapa…’akasema‘Kukubaliana husu malipo au, kama ni malipo hakuna shida, toka lini nikakupa kazi bila kukulipa, wewe angalia gharama zako nipatie ankara ya deni,…au unataka kusema nini…?’‘Kwahiyo, mmh, unataka nimchunguze shemeji….mmmh….’akasema‘Ndio…umchunguze, …kwa masilahi yake, na masilahi ya familia,….fanya ufanyalo, ila cha muhimu, nakuomba, na nasisitiza, mimi sitaki kashifa kwenye familia yangu, ..na hili tumeshaonywa na wazazi wangu mara nyingi, hata wewe uliwahi kusikia wakati baba akiongea, ..sasa kama kuna tatizo nataka tuliwahi mapema kabla halijafika kwa wazazi wangu,...’nikasema‘Nikuulize tu, samahani bosi… kabla sijaondoka, sasa kama ni kweli  mume wako kahusika na hicho unachokiita kashfa,..itakuwaje…?’ akauliza na mimi nikamuangalia kwa macho makali, nikasema‘Ninacho-kiita mimi kashfa..una maana gani, lugha gani hiyo…..ok, sikiliza…mimi sitalivumilia kashfa yoyote kwenye familia yangu, hasa zile zenye kuharibu biashara, zenye kuharibu ndoa, zenye kuleta jina baya kwenye familia yangu, zote unazielewa..sitake nianza kuzitaja…’nikasema‘Mhh…’akaguna hivyo.‘Wazazi wangu unawafahamu walivyo, walinikataza nisioane na huyo mume wangu kisa ni kuhusu familia yao, kuwa eti imegubikwa na mambo hayo…mimi sikuamini hayo, najau tabia mtu anaijenga mwenyewe..mimi niliwahakikishia wazazi wangu kuwa kashfa mbaya hataiweza kutokea kwenye familia yangu…’nikasema‘Lakini kashfa yaweza kutafsiriwa vingine,..kama jambo limefanyika kwa makubaliano linawezaje kuwa ni kashfa…muhimu tuliweke sawa,..kuna mambo labda yalifanyika hivyo, sasa labda imekuwa kinyume kutokana na kutokuelewana…sasa sizani ni kama ni kashfa, labda iwe ni kashafa kwa mtizamo wa watu wengine……’akasema‘Kwa makubaliani!!! Weeeeh, makubaliano na nani..kuwa mimi nitendewe ubaya, kwa vipi sasa, kuwa mume wangu, mbona haiji akilini… kuwa yeye akazini nje ya ndoa au, tuchukulie kashfa hiyo ni ya ndoa, mimi sijui..yaani mimi, nikae na mume wangu kuwa akafanye hivyo,…au nimwambie mume wangu akaibe au..najua mume wangu hawezi kufanya hivyo, hata siku moja,..na mimi sio kichaa wa kukubaliana na ujinga kama huo, hata dunia itanicheka au unataka kusema nini…’nikasema.‘Sawa…lakini nikuulize kitu kingine kutokana na hali ya shemeji, ukagundua kuwa kafanya hivyo, na hali kama hiyo, .. utachukua hatua gani, huoni unaweza kumuua mume wako bure....?’ akaniuliza na mimi nikageuka kumuangalia docta, alikuwa bado anaongea na simu, nikasema.‘Kwanza tujue ukweli, unanielewa,, ....cha kufanya baada ya ukweli.. , nitajua mimi  mwenyewe, hiyo sio kazi yako… ila kiukweli, kama ni kweli wanavyosema watu mimi bado siamini,…huyo aliyemghilibu mume wangu, huyo shetani mtu…kama kweli kaghilibiwa, maana mume wangu hakuwa na tabia hiyo,..huyo mtu, huyo shetani,,… nitahakikisha kuwa  hanisahau maishani , na atajuta kuingilia ndoa za watu kupoje…’nikasema kwa ukali, na uso wangu ukiwa sasa umebadilika kabisa,….Mdada aliniangalia usoni, akionyesha wasiwasi mkubwa, mpaka, akawa anarudi kinyume nyume..halafu akasimama ..rafiki yangu  ni jasiri..alipitia mafunzo ya ujasiri, kwahiyo anajua aweje kwa wakati gani…, lakini kwa hali aliyoniona nayo usoni nahisi hakutarajia,…kabisa….‘Ina maana utamuua au,…ha-ha- hata kama…?’ akaniuliza akionyesha wasiwasi, akasita kumalizia.‘Wewe subiria tu…utaona nitakachokifanya, unajua nimevumilia sana, nimekuwa mtu wa watu, nawapenda sana watu wangu wa karibu, nawabeba kwa mbereko....sasa ina maana kwa hali hiyo watu wanipande hadi kichwani, hapana,..hata awe ni nani …’nikasema‘Mhh, rafiki yangu siamini hili kabisa, lakini mume wako ni mtu mwema sana, na kama kafikia kulifanya lolote baya, atakuwa na sababu…sizani kama anaweza kufanya jambo ambalo analifahamu ni kinyume ..msamehe tu…’akasema‘Nimsamehe nini sasa…kwanza, eeh, nisikilize, sio tukurupuke, kwanza, tujue kosa lake ni lipi,…ili tujue jinsii ya kumsaidia,…unajua  yapo makosa ya kusamehe, mimi ni binadamu, nitayapima, …lakini sio kosa la kuingilia ndoa za watu…watu hao wanatakiwa kuuwawa…unasikia, ku-uwawa, sasa mimi niwachekee, ndoa sio kitu cha mchezo bibie…, ..’nikasema‘Sikiliza…mimi naomba urejee yale mazungumzo yetu, mbona….’akasema‘Mbona mbona nini…ile ni kitu kingine…najua unachotaka kukisema…ndio maana nilikusihi iwe siri…sasa kama na wewe umelikoroga huko, acha mwenye mali afanye kazi, yake utajua mwenyewe, na mimi natetea ndoa yangu…sasa nikuulize uUtaifanya hiyo kazi au huwezi nimpatie mtu mwingine..’nikasema kikazi zaidi.‘Mimi naona sitaiweza hiyo kazi, ..na ukizingatia nina mtoto, si unajua tena….’akasema‘Sikiliza, sitaki kusikia kauli hiyo…na nataka uifanye wewe….na nataka iwe siri kubwa, unanielewa, siri kubwa,  sitaki watu wengine waje kuligundua hilo kabla yako, kuna watu wameshaanza kutaka kulifuatilia hilo tatizo la mume wangu,  wanataka kujua kwanini mume wangu akawa hivyo,…hiyo ajali sio ya kawaida,…wameshaanza kutunga hadithi…najua wakitaka jambo watalipata tu…’nikasema‘Akina nani hao…?’ akaniuliza akionyesha mashaka‘Docta anataka na yeye kulichunguza kwa nia ya kumsaidia rafiki yake, najua sio hivyo tu,…najua kabisa… wazazi wangu watakuwa wamemtuma kufanya hivyo,…sasa sitaki aje kugundua kitu kabla ya yako, nataka wewe ukishagundua tunahakikisha hakijulikani kitu tena…unanisikia, umeona jinsi gani jambo hilo lilivyo nyeti,…umenielewa hapo…’nikasema‘Mhh, mbona imekuwa ni tatizo, sikujua kuwa haya yote yanaweza kutokea,…sasa huyu docta anataka kutafuta nini,…ina maana ndio maana umeniita hapa, ili…na wazazi wako wanalifuatilia hili, mungu wangu …mimi sasa naanza kuogopa, naona nijiondokee tu kwenda kusoma haraka iwezekanavyo, ….’akasema sasa akirudi kinyume nyume‘Sikiliza wewe ni rafiki yangu ninayekuamini, ndio maana kila kitu tunaambizana, na huwa tunashauriana kwa kila jambo, sawa si sawa....wewe ndio mimi, na wewe huwezi kufanya jambo la siri kinyume na makubaliano yetu, sizani kama wewe unaweza kunigeuka mimi…nimekuwa nikikulinda kwa kila hali, mpaka sasa.…’nikatulia‘Ni kweli….’akasema sasa akiwa kainama chini kama mtoto mbele ya wazazi wake akiwa kakosa au kuona aibu. Ni lazima awe hivyo kwangu mimi licha ya urafiki lakini mimi nimekuwa kama mlezi, nilitumia gharama nyingi kumjenga huyu binti kutoka kwenye hali ya kukata tamaa hadi akafikia sehemu ya kujiamini..***********Rafiki yangu huyu, niliamua kumsaidia  kutoka kwa wazazi wake, hii ni kutokana na ule ukaribu wetu, sikutaka nimsaidie kipesa tu, lakini pia kumjenga katika hali ambayo anaweza kufanya jambo lake kwa kujiamini.Sisi kwenye familia yetu japokuwa tuna uwezo, lakini wazazi wetu walifanya juhudi kubwa ya kutujenga kihali ambayo mtu anaweza kufanya jambo bila kutegemea wazazi, walitujenga kujiajiri zaidi, pamoja na elimu yetu, na mimi nikaona nimsaidie rafiki yangu awe hivyo hivyo...Wazazi wake kuna kipindi walitaka binti yao aolewe na mtu waliyeona kuwa atamfaa, na binti yao hakuwa tayari naye, kama alivyokuwa hayupo tayari kwa wanaume wengi waliomtaka kumuoa kabla ya huyo ambaye wazazi wake, waliamua kumshurutisha aolewe naye...ndio maana tatizo lake nikalichukulia sawa na la kwangu..kuwa hata mimi nilikataa kuolewa na chagua la wazazi wangu‘Hawa wazazi wangu siwaelewi, kama wamenichoka, na huenda wanaona mimi ni mzigo kwao, waniambie, lakini sio kunitafutia mwanaume,....hivi wananionaje mimi, eti niolewe na yule mzee, ..eti kwa vile ni tajiri, ....hapana, siwezi kuishi na yule mzee, hata siku moja....’akaniambia.‘Lakini yule sio mzee,ukiangalai umri wako na yeye, huwezi kumuita yule mzee, yule ni saizi yako kabisa, au unataka kuolewa na dogodogo, usidanganyike, huko umeshakupita, sio kwako tena, huyo unayemuona ni mzee, ndiye saizi yako...’nikamshauri.‘Simpendi, na simtaki....’akasema na mimi nikamuelewa, nikaona nimsaidie na nione vipi nitaweza kumfanya aishi maisha bila ya kutegemea wazazi wake, , kwani kwa muda huo alikuwa ameshakosana na wazazi wake  kabisa..na wazazi wake, walisema kuwa binti yao huyo kazidi kwani kila mchumba anayemfuata yeye anamkataa,‘Basi rafiki yangu mimi naona nikusaidie kwa hilo, unaonaje tukiwa washirika, ....?’ nikamuuliza.‘Washirika kwa vipi, sisi ni marafiki tangia zamani, hilo la ushirika la kitu gani tena,…?’ akauliza.Mimi namfahamu sana rafiki yangu huyo , hawezi kupata kazi ya kuajiriwa akatulia, sizani kama anaweza kuhimili sheria na taratibu za kazi, mara ngapi anaajiriwa na baada ya hata mwezi kuisha keshakosana na muajiri wake,...nikataka nimbadili kabisa aondokane na hulika hiyo, japokuwa hiyo ya kuchagua wanaume nilishindwa.Nakumbuka wakati tunasoma rafiki yangu huyu alikuwa akipenda sana kazi za upelelezi, kutokana na kusoma vitabu mbali mbali vya hadithi za kipelelezi, na kuangalia sinema za namna hiyo,na hiyo ilikuwa ni ndoto yake kuwa akimaliza shule atajiunga na kazi za upelelezi.Kwa bahati mbaya, ndoto yake hiyo haikuweza kufanikiwa, tulipomaliza shule, akajikuta akifanya kazi nyingine kutokana na matakwa ya wazazi wake, ambazo hakuweza kuzifanya itakiwavyo, akaanza kutafuta sehemu nyingine, na hata huko hakuweza kukaa muda mrefu,ikawa mtu wa kubadili kazi, mara leo yupo hapa , kesho yupo kule.Basi siku hiyo alipokuja kwangu na malalamiko hayo juu ya wazazi wake, kutaka aolewe, mimi nikakumbuka ile ndoto yake hiyo, nikaona kwa vile tumekuwa watu wakusaidiana, kupendana, toka utotoni, ngoja na mimi nijaribu kumsaidia nionavyo mimi, na ndipo nikamapa wazo langu hilo nikamwambia;‘Rafiki yangu mimi nataka kuifufua ile ndoyo yako ya shuleni, upo tayari....?’nikamwambia na yeye akawa kama hakunisikia,kwani wakati huo alikuwa anacheza na simu yake, nafikiri alikuwa akiandika ujumbe kwa watu wake, na baadaye akasema;‘Ndoto ipi...?’ akaniuliza kwa dharau, na huku akiendelea kuangalia simu yake.‘Kwanza rafiki yangu nakutaka unielewe, nikiongea na wewe uhakikishe kweli unaongea na mimi, ....kama bado una tabia za utoto, hutafika mbali, weka hiyo simu pembeni, nataka tuongee kikubwa....’nikasema kwa sauti ya ukali, na yeye aliponiangalia usoni akakutana na uso wa kazi, uso unaoashiria amri, akashangaa, kwanza, halafu akabetua mdomo, na kusema.‘Ok. Bosi, maana kwa vile wewe ni bosi kwenye kampuni zako unafikiria kila mtu utamsimamia hivyo hivyo..lakini kwa vile nimekwama, nitakusikiliza bosi....’akasema huku akiiweka simu yake pembeni.‘Nakumbuka wewe ulikuwa na ndoto ya kuwa askari mpelelezi...lakini haikuwezekana, sasa nataka hilo liwezekane, hujachelewa, utakwenda kusomea hilo, lakini sio askari mpelelezi wa kipolisi, nataka uwe mpelelezi wa watu binafsi,...mpelelezi muhutasi,  hiyo si inawezekana...?’ nikamuuliza. Na yeye kwanza akawa kama haamini hilo kwani muda umeshapita, na huenda hakuwa na wazo hilo tena.‘Mhh, hilo nilishalitoa akilini, hayo yalikuwa ya kishule, ...sijui kama inawezekana, sina uhakika na hilo.na hiyo kazi inapatika kweli, maana nahisi nitahitajika kwenda jeshini, na huu mwili sizani kama utakubali shuruba, na amri.....’akasema.‘Inawekana,....kwanini isiwezekane, kila kitu ni nia, kila kitu ni utashi, na dhamira ya kweli, sasa hivi vipo vyuo vingi tu vya kutoa hayo mafunzo, na hata kwenye mitandao kuna elimu kama hiyo, tuifanyie kazi, ...na na kwa vile mimi nakuhitajia kwenye mambo yangu,...tushirikiane, tutaweza...upo tayari....?’nikamuuliza.‘Sijui...tuone ,..’akasema na mimi nikafahamu kuwa yupo tayari, nikamwambia ili aonyeshe dhamira ya kweli, basi ahangaike mwenyewe kuvitafuta hivyo vyuo, na mimi nitamsaidia kwa hali na mali. Na kweli baada ya siku kadhaa akasema keshapata chuo cha namna hiyo, na yupo tayari kwa masomo, na mimi nikamwambia nitawasiliana na wahusika wa hicho chuo.‘Kwani ni mpaka wewe uwasiliane nao, cha muhimu ni maombi, na maombi nimeshatuma na wao wameshanikubali, kilichobakia na malipo..hakuna zaidi....’akasema.‘Usijali..malipo nitalipa, lakini kama nilivyokuambia, mafunzo hayo ni kwa ajili ya kazi zangu, kwahiyo nataka niongee nao, nione jinsi gani wanaweza kukupika nitakavyo mimi....’nikasema na kweli nikaenda kuonana na wahusika wa hicho chuo, na tutakakubaliana, kwani nilitaka kwanza wamjenge huyo binti kikakamavu, na kuondoa ulegelege wa kutegemea wazazi,..na wao wakasema hiyo kwao ni kazi ndogo tu.Sikuamini, huenda ni kwa vile, alikuwa na ndoto hiyo, au ni dhamira tu, ilimtuma ajitume hivyo, kwani, aliweza, na akafuzu vizuri sana, na kuna muda aliombwa ajiunge na askari polisi, lakini yeye mwenyewe alikataa, na akaja kwangu na kusema yupo tayari kwa kazi zangu, na tukaingia naye mkataba, akawa ni mtu wangu nikimuhitajia, lakini hapo hapo akawa kaajiriwa kwenye kazi fulani.Nikawa kila nikipata kazi inayohitajia mambo hayo, nimampa ananifanyia, namlipa vizuri tu, au wakati mwingine anapata kazi zake nyingine binafsi akikutana na mawakili binafsi kuchunguza kesi fulani, basi ikawa ndio kazi yake nje ya ajira yake.Kwa hali kama hiyo tukawa ni kitu kimoja, na kikazi mimi ni bosi wake, na  haikutokea siku nikampa kazi, akaikataa,...Kwahiyo ni mtu nilishibana naye, na ananiheshimu mimi na familia yangu, na alishaapa kuwa hataweza kunifanyia jambo baya,…je kwa hali kama hiyo ninaweza kuamini mambo ya kusikia tu…hapana, ilihitajia mud asana kuyaamini maneno ya watu****************‘Kwahiyo umenielewa, nikamuuliza , wakato docta naye anaongea na simu‘Nitafanyaje sasa..inabidi…’akasema‘Unajua ni kwanini nataka hili, ni ili  jamii isije kuniona mimi mjinga, kuwa nafuga nyoka,…hilo linawezekana kweli, kuwa nilifanya yote hayo kwa mtu ambaye atakuja kunizunguka, …’nikasema‘Lakini…..’akataka kujitetea‘Sikiliza…mimi sitakubaliana na mawazo yao hata mara moja kuwa wewe rafiki yangu unaweza kunisaliti mimi, nitauweka wapi uso wangu…sasa ni wewe kuilinda hiyo hali, sizani kama unaweza kufanya jambo kama hilo…sizani, …au ..niambie ukweli hapa hapa, je ni kweli…?’ nikamuuliza ‘Mim naondoka….’akasema sasa akitikisa kichwa cha kuchanganyikiwa.‘Sawa, mimi nakuamini, na..unasikia,  …mimi nimeosha mikono yangu, nimechukua dhamana yako mikononi mwangu.., na wewe usije kuniangusha kwa hilo,…umenielewa lakini, na nataka hata wazazi wangu ikiwezekana wasijue kuwa mume wangu kapatwa na ajali, nataka tufanye namna ambayo, sawa ni ajali, lakini kwa mazingira yasiyo kuwa na kashfa, sawa..umenielewa hapo..?’ nikamuulizaNilimuona kama anataka kutoa machozi, lakini mimi sikujali,..najua sio mtu wa kutoa machozi, labda kitu kimemuingia machoni,…na muda huo nilikuwa kikazi zaidi,  sikutaka kupoteza muda, nilitaka yeye aifanye hiyo kazi, na nione ukweli wake kupitia kwake yeye mwenyewe…., nilikuwa na maana yangu kubwa tu.‘Ninataka wewe….uifanye hiyo kazi, sitaki utani, nataka tumfahamu huyo mtu, ni nani anaweza kuingilia ndoa yangu, au kama kuna jingine, tulijue mapema…, kwanini mume wangu awe hivyo…hapo kuna mawili, kashfa ya ndoa, au…kuna tatizo kazini, mimi sijui, wewe ni mtaalamu wa mambo hayo, sasa mimi  nahitaji msaada wako, hii ni kazi nimekupa…’nikasema kwa hasira‘Mimi naondoka….’akasema sasa akitaka kuondoka‘Ondoka bwana,… mimi naondoka, mimi naondoka…ila kumbuka mimi…sitaki utani, …unanielewa, sitaki utani kwenye ndoa yangu kwenye kazi yangu, kwenye maisha yangu…ole wake huyo mtu, sitajali ni nani…hili nakuambia wewe kama rafiki yangu, ukisikia mimi nimefanya jambo, hutaamini….’nikasema kwa jaziba.‘Sawa bosi....naondoka…’akageuka na nikahisi kuna mtu nyuma yangu nikageuka kwa haraka, nikiwa sasa naangalina uso kwa uso na baba yangu mzazi.‘Baba…….’nikasema kwa mshangao mkubwa, wenye wasiwasi,‘Kuna nini kimetokea…?’ ilikuwa sauti ya baba ya kiaskariWAO LA LEO: Mara nyingi tunapokuwa na shida, tunasahau kuwa wenzetu pia na wao wana shida kama hizo za kwetu au huenda shida zao ni zaidi ya shida zetu, wakati huo wa shida, hatujali shida za wenzetuo,cha muhimu kwa wakati huo ni shida zetu, tunachotamani  ni jinsi gani ya kusaidiwa, ni jinsi gani, shida zetu zitachukuliwa kipaumbele, na hapo utaanza kuwachuja marafiki zako, na rafiki utakayemuona ni wa kweli kwako ni yule atakayesimama kwenye shida zako, na kutetea hoja zako. Tukumbuke kuwa,sisi sote ni wanadamu, na shida zimeumbiwa kwetu, na kwahiyo sote ni wahitajia,kama ni hivyo basi,  ili tuwe sawa, tujaribu kuona shida za wenzetu zina umhimu sawa sawa na shida zetu.‘Baba umerudi lini…?’ nikasema, nikiwa nimenywea, maana ili sura ya kutisha ilipotea ghafla, na uso ukawa wa aibu,…uso wa kujipendekeza. Kwa muda huo, baba alikuwa kanikazia macho tu, akimaanisha anasubiria jibu la swali aliloniuliza. Nilipoligundua hilo, nikasema ;‘Ni ajali tu baba,….mume wangu kapatwa na ajali….’nikasema‘Nimeshaonana naye na nimeshapata taarifa zote kutoka kwa dakitari, na bado nasubiria taarifa nyingine, maana ajali hiyo sio ya kawaida,…kuna kitu ndani yake. Ni lazima kujiuliza ni kwanini, akaendesha gari kwa mwendo kasi kiasi hicho, alikuwa kalewa..’ akawa kama ananiuliza‘Hapana….’nikasema‘Una uhakika….?’ Sasa akaniuliza‘Mhh…ndio baba, maana hata Docta wamesema hakuwa kalewa, na hakuwa amekunywa kabisa siku hiyo….’nikamtetea mume wangu.‘Lakini kulewa sasa imekuwa kawaida yake au sio…? Ni kwanini anafanya hivyo…?’ akaniuliza‘Ni starehe zake tu baba, lakini litamalizika hilo…’nikasema‘Una uhakika…?’ akauliza akiniangalia kwa makini‘Baba….’nikasema hivyo na kutulia.‘Nauliza swali langu tena….kuna nini kati yako wewe na mume wako, nilishakuuliza hilo swali awali ukasema ni mambo ya kawaida tu…, nilikuambia, nikusaidie ukasema hapana,..mtayamaliza wenyewe,  sasa kwa hili, sitaweza kusubiria , nataka kujua kila kitu, au uniambie mwenyewe kuna nini…?’ akauliza‘Baba …ni mambo ya kawaida tu ya ndoa, sizani kama wewe na mama mpo na furaha wakati wote, ..kuna muda kunatokea hili na lile, na sizani yote ya ndani ya ndoa nahitajika kuyasema kwako, tutayamaliza tu kwa amani baba, hii ni ajali tu…’nikasema‘Bint, mimi sio mtoto mdogo wa kukuuliza haya, nimesoma, nina uzoefu wa maisha zaidi yako,…unanielewa,..sitaki nikukumbushe kila kitu…kuwa tulikuambia, tulikuambia,.. hukutusikia…, na asiyesikia la mkuu hufanya nini…’akasema‘Lakini baba, nilishawaambia, mimi nitaweza, na ninaweza…, haya ni maisha yangu na mume wangu, tuachieni wenyewe…, maana tumeshaoana sasa…, sizani kama ni busara tukarudia yale yale malumbano ya zamani, sasa hivi tuna watoto, tuna familia..baba maji nimeshayafulia nguo nitafanyaje sasa, hebu niambie baba…’nikasema‘Nafahamu hilo..utasema hivyo, utajitetea tena na tena…., si umekuwa bwana, unajiweza au sio…..haina shida,… ila lile linalogusa familia yangu…, lile linakuja kunigusa na mimi mwenyewe.., sitaliacha lipite hivi hivi, hebu nikuulize ikitokea tatizo, la kikashifa kwako, utaambiwa wewe ni binti wa nani..?’ akaniuliza‘Kuna kashfa gani baba imetokea, mbona baba mnataka kuyakuza mambo, a kuna nini umesikia kibaya,…baba hakuna kashafa yoyote,…kama umesikia hivyo, ni ….watu tu, kama ujuavyo wanadamu hatuna wema, …mimi nakuhakikishia baba haya mambo nitayamaliza mwenyewe,…niamini baba…’nikasema‘Una uhakika …..?’ akaniuliza, baba akikuuliza hivyo ujue hilo jambo analifahamu , anakupima tu.‘Baba…’nikasema na yeye akageuka kuangalia nyuma, ..nahisi alikuwa akimuangalia docta, nikaangalia kule anapoangalia, lakini docta hakuwepo..sijui alikuwa kaenda wapi…lakini badala yake nilimuona  jamaa mmoja kasimama, akiwa anatuangalia..alipoona baba anamuangalia, kwa haraka akaja alikuwa kashikilia  bahasha kubwa mkononi‘Binti yangu..nilikuwa safarini, lakini hata nikiwa huko nimekuwa nikiiwazia familia yangu, na familia yangu ni pamoja na wewe…mimi nina hisa kwenye kampuni zenu, nilifanya hivyo makusudi,  maana siwezi kutoa pesa zangu ziwekezwe tu, bila ya mimi kujua kinachoendelea,....hii hapa ni taarifa ya kibishara ya kampuni yako na mumeo ..umeshawahi kuipitia vyema…?’ akauliza‘Ndi-ndio baba lakini….eeh, kuna matukio mengi yamepita hapa karibu, sijapata muda wa kuipitia vyema, ila naifanyia kazi, kwangu, kwa mume wangu sijawahi kukaa naye, sijui kinachoendelea, nitakaa naye nione tatizo lipo wapi…’nikasema‘Kwanini biashara imeshuka kiasi hiki, hasa ya mumeo…?’ akauliza‘Baba ni hali halisi, sio sisi tu,…na ngoja nitakuja kuipitia, mimi nina nakala zangu, au hii ni nyingine zaidi..?’nikasema‘Na hizo pesa nyingi alizochukua mumeo, ni za nini, ni kwa ajili ya nini, umeshawahi kumuulizia mumeo pesa hizo kazifanyia nini…?’ akauliza‘Pesa gani baba…?’ nikauliza maana sijui kama mume wangu alichukua pesa nyingi kwenye kampuni yake, mimi siingilii kampuni ya mume wangu.‘Anyway..hilo sio tatizo kwa sasa…, lakini ndani ya bahasha hiyo kuna kitu kingine, kuna taarifa ya biashata ya mumeo pia, na mengine utakuja kuyaangalia humo ndani, halafu tutaongea…utaniambia hayo yote yana maana gani..’akasema‘Sawa baba, nita-ipitia..’nikasema‘Na kingine je wewe unakubaliana na hali hiyo ya mumeo …au ni maisha gani mnaishi hivyo…, nataka majibu kutoka kwako, sio leo, tukikutana unanielewa, maana hujalelewa hivyo, sitaki aibu kabisa....’akasemaAlinikabidhi ile bahasha, na kwa mashaka nikaipokea, na kabla sijataka kufanya chochote, akasema;‘Ile hali ya mumeo itachukua muda kupona….na ina maana shughuli nyingi alizokuwa akizisimamia yeye, zitasimama, na..zaidi hatujui mapesa yote aliyochota aliyachukua kufanyia nini…sasa, kazi ni kwako, kabla mumeo hajazindukana, ulifanyie hilo kazi, fuatilia kinachoendelea , baada ya hapo, mimi mwenyewe, nitajua la kufanya, sikutoa mataji wangu upotee bure, umenielewa…’akaangalia saa yake.‘Baba hapa sio mahali pa kuulizana maswala ya biashara baba…mume wangu yupo hali mbaya, nina mawazo kuhusu afya yake, nipe muda kidogo kwa haya…, naomba hayo tuyaache kwanza…’nikasema‘Haya, ninayokuuliza....ni moja ya sababu ya kuchanganyikiwa kwa mumeo, kuna mengine kati yako na yeye, usipoziba ufa utajenga ukuta, akipona akirudia tena, itakuwaje,..ni bora ujua cha kufanya kuanzia sasa..’akasema‘Sawa baba nimekuelewa…’nikasema‘Kuna maelezo muhimu humo, ila mengine..eeh yanafanyiwa kazi, ikithibitishwa kuwa ni kweli…unajua ni nini kitafuta,…maana tulishakubaliana hilo, na sitarudi nyuma tena, unanielewa…?’ akauliza nakabla sijamjibu akasema‘Nilikuambia na narudia tena,…kunguru hafugiki, sasa yanaanza kujitokeza, usizarau maneno ya wazee wako, ukataka kushindana nao, sasa ni lako hili, ila lisiharibu familia yangu kwa ujumla, sitarudia tena hili…’akasemaHapo nikabakia kimia tu…nikiwa nimeishikilia ile bahasha kubwa mkononi.‘Mume wako, ….kabla niliwahi kuongea naye, nikamwambia nikirudi nahitajia majibu na maelezo…. sasa sijui ni sababu hiyo au kuna jambo jingine, nahisi pia kuna jambo jingine limejitokeza…ila ninachotaka isije ikawa ni kashfa kwenye familia…sitavumilia hilo kabisa…’akasema.‘Sawa baba, nina imani hiyo, kuwa hakuna kashfa mbaya….’nikasema‘Na iwe hivyo, na iwe-hivyo,….’akasema akiangalia saa‘Sawa baba, niamini mimi…hakuna jambo baya …’nikasema‘Na huyo rafiki yako, unamuamini sana eeh…’akaniuliza‘Yupi baba…?’ nikauliza‘Huyo mzazi….’akasema na mimi hapo moyo ukalipuka paah.‘Baba huyo ana nini tena…’nikasema‘Najua unamtetea sana,…, niliwahi kukuambia, unachokifanya wewe, ni kama kufuga nyoka mwenye sumu chumbani kwako, ipo siku atakuuma wewe mwenyewe, sikiliza binti,  huwezi kumbadili mtu aliyeshindikana na wazazi wake, hu-we-zi, umepanda mbegu juu ya jiwe…’akasemaHapo nikakaa kimia,… nilikawa nawaza mbali kuwa huenda  docta ndiye anafanya kazi na baba, anachukua kwangu anayapeleka kwa baba, na hili la rafiki yangu inaokena limekwenda mbali, litanisumbua sana, sasa nitafanya nini…lakini moyoni, nikajipa imani kuwa nitalimaliza mimi na huyo rafiki yangu..sizani kama kuna jambo kubwa kiasi hicho.‘Huyo rafiki yako, ndiye atakayekuangamiza,..unajua kuwa yeye anashirikiana na mume wako…?’akasema kama ananiuliza, na mimi hapo nikamwangalia baba yangu kwa macho ya mshangao, ila sikuwa nimemuelewa ana maana gani hapo…‘Anashirikiana na mume wangu, kwenye nini baba, hapana, ni kawaida tu….!!’nikasema kwa mshangao.‘Una uhakika…’akauliza na mimi nikakaa kimia‘Ndio maana nakuambia…kuna tatizo, na tatizo hilo linaweza kuleta taswira mbaya kwenye familia, na …narudia tena sitaki kashfa mbaya kwenye familia yangu, muuguze mume wako apone,…na apone kweli, maana sitarudia tena. ….’akasema na kuondoka.************‘Huyo-huyo rafiki yako, ndiye atakayekuangamiza, akishirikiana na mume wako…’ ilikuwa sauti iliyokuwa imebakia akilini mwangu, na kunifanya niduwae kwa muda, hadi pale nilipohisi mtu kunikaribia.Nikainua kichwa kuangalia ni nani huyo, …alikuwa ni docta.‘Vipi, mwenzako ndio keshaondoka….?’ Akaniuliza docta‘Wewe ulikuwa wapi..?’ nikamuuliza swali kabla sijajibu swali‘Unajua nilimuona docta kwa mbali, akitoka, nikaamua kumkimbilia kumuwahi kabla hajaondoka, kwahiyo sikuweza kuwaambia,…na kweli alikuwa akitoka, ,…na  nimeweza kuongea naye na kwenda kumuangalia mume wako, bado amelala, ila yupo sawa, hana tatizo….’akasema‘Kwahiyo mimi siwezi kwenda kumuona…?’ nikauliza‘Kwa mujibu wa dakitari, ndio huwezi kwenda kumuona, kwa vile anatakiwa kulala ili dawa zifanye kazi....ila unaweza kwenda kumuona tu, kwa mbali, kama unataka, muhimu usije kumghasi, mpaka hapo atakapozindukana kutoka usingizini yeye mwenyewe, …’akasema‘Oh….hata hivyo, ni bora nikamuone tu…’nikasema‘Sawa twende….’akaanza kutembea kuelekea huko alipolazwa mume wangu, na mimi nikawa namfuatilia kwa nyuma hadi chumba alicholazwa mume wangu, alikuwa kweli kalala, ..nilimuangalia kwa muda, na kuhis machozi yakinilenga lenga, akilini sikuwa na wazo jingine zaidi ya kumuombea apone haraka iwezekanavyo.‘Haya umemuona, …twende maana tumejiiba tu, haitakiwi mtu kuja kumghasi, mpaka wakija kuhakikisha kuwa sasa hana maumivu tena….’akasema, lakini nilikuwa kama simsikii, hadi pale aliponishika mkono na kunivuta tuondoke humo ndani.‘Mume wangu jamani…’nikasema‘Atapona ….’akasema docta********* Tulipokuwa nje, docta akaniuliza;‘Kwanini rafiki yako kaondoka kwa haraka hivyo, tuiliongea nini na wewe umafanya nini, ..kuna kitu gani mnataka kukificha, mimi, eeh...nilikuwa nataka kuongea naye maswala mengine….’akasema.‘Ulitaka kumuona mtoto ili utake kuthibitisha uvumi na hisia zako, au…ndio keshaondoka hivyo, ..’nikasema.‘Haya sawa, hamna shida, unaonaje sasa twende nyumbani,…maana kwa hivi sasa utakaa tu, na kwa mahesabu yao, mgonjwa ataamuka baada ya kama masaa manne hivi,…chini au juu ya hapo… na akiamuka watamchunguza kwanza..ili kuhakikisha kama yupo sawa kabla hawajawaruhusu watu kuongea naye, ….’akasema‘Sawa…’nikasema hivyo tu, na tukatoka hadi tulipoweka magari yetu, kila mmoja akaingia kwenye gari lake na ikawa ni safari ya kurudi nyumbani. Na sikutaka kabisa kusimama kwa docta, moja kwa moja nikaelekea nyumbani kwangu. Nilipofika kwangu,  kwa haraka nikampigia simu rafiki yangu.Kwanza simu iliita kwa muda bila kupokelewa, …nikatulia dakika moja hivi nikapiga tena, ikawa hivyo hivyo,…lakini wakati inataka kukatika, ndio ikapokelewa, na mimi nikamuuliza mdada, kwa haraka ni kwanini hapokei simu anajua namuitia nini.., yeye akajibu kwa haraka tu;‘Nilikuwa naanika nguo za mtoto nje, sikuweza kusikia simu ikiita, na wakati naingia ndio nikasikia ikiita, nikaiwahi, habari za mgonjwa, kuna lolote jipya tangia tuachane….?’akasema na kuniuliza.‘Vipi umefikia wapi, au umeamuaje..?’ nikamuuliza , bila kujibu swali lake‘Mhh…nimeongea na watu wa usalama barabarani kujua kinachoendelea kwanza, wamenipa picha halisi ya ajali yenyewe,…nilikuwa sijaipata hiyo, zaidi ya kusikia kwa watu, sasa nimeweza kujua ajali ilivyotokea…zaidi ni mwendo kasi na wakati anakata kona kuingie ile bara bara nyingine ndio wakakutana na lori, …kiukweli ni ajali mbaya…’akasema‘Ndio hivyo, …kwahiyo umeshaianza hiyo kazi…au..?’nikamuuliza‘Ndio nimeianza hivyo…bo-si’akasema na kumalizia neno la mwisho kwa kukata‘Najua umetoka kujifungua na ulihitajia muda wa kupumzika, hilo nalifahamu sana, na sikuona kama kazi hii ina uzito wa kukufanya ushindwe kuifanya kutokana na hiyo hali,…’nikasema, na nilisikia mlio wa simu kuingia, sijui ni ya kwake au ni yangu‘Nitaangalia….’akasema, nahisi alitaka kukata simu.‘Mimi nionavyo, ni kazi unayoweza kuifanya hata bila ya kutumia nguvu, kwani wewe una vyanzo vyako vingi vya kukusaidia bila ya hata ya wewe kutoka hapo nyumbani kwako..'nikasema'Sawa...'akasema'Cha..., muhimu ni kuhakikisha kabla hawajafanikiwa watu wengine kujenga hoja za fitina, uwe umeshajua ni nini kinachoendelea, na je umeshaweka mikakati yako tayari...?’ nikamuuliza, nikasikia mlio wa kuingia ujumbe nahisi ni simu yake. ‘Sawa nimekuelewa …’akatulia kwa muda, halafu akasema‘Bosi…, nafahamu nipo kwenye mkataba na wewe, na niwajibu wangu kutimiza kila utakachoniambia, lakini nilitaka nikuweke wazi, kabla ya kazi yenyewe ndio maana uliniona nasita sita...’akasema sasa kwa sauti ya kujiamini kidogo.‘Kwahiyo umeshaelewa, au bado unasita sita, …’nikasema‘Nitafanya kama utakavyo, hamna shida…na nilimuona baba yako, hapo hospitalini,....mliongea nini na yeye au…?’ akaniuliza.‘Ni mambo ya baba na binti yake, ..ni yale yale…yeye hawezi kunizuia mimi nisifanye kazi yangu, ila kuna jambo..ndio maana nataka ulifanyie kazi, kabla mambo hayajawa mabaya ....’nikasema‘Sawa..nitaifanya tu, hamna shida… ila nami unielewe, ndio nimetoka kujifungua, kitoto changu bado kichanga, hali yangu bado haijawa safi, nahitajia muda wa kutulia kwanza, nahitaji muda wa kukaa na mwanangu na pia nipo kwenye maandalizi ya ile safari ya kwenda nje kusoma, kwahiyo huenda nisiifanye hiyo kazi kwa muda unaotaka wewe,.....’akasema rafiki yangu huyo.‘Hamna shida, mimi naelewa hilo….ila fanya uwezevyo, kabla wengine hawajagundua lolote, kama kuna kashfa ya mume wangu nataka niifahamu mapema ni kashafa gani, na …mengine nitayafanyia kazi mimi mwenyewe …’nikasema‘Hamna shida, nitafanya hivyo…bosi…’akasema kwa kujiamini.Ndio hapo nikakumbuka ile bahasha,..‘Haya badae nitakupigia…’nikasema na kukata simu. Nikakumbuka kuwa sikuichukua ile bahasha kwenye gari, haraka haraka hizi bwana, na mawazo mengi kichwani,….nikatoka hadi kwenye gari, ..nakumbuka niliiweka kwenye kiti cha mbele, kwanza nikawasha kiwambo cha gari ile niweze kufungua mlango,..kwa haraka nikafungua mlango,Hakuna kitu…! Bahasha haipo….!‘Haiwezekani…’nikasema nikikagua kila mahali, na kujaribu kuvuta hisia za kumbukumbu yangu kuwa labda niliondoka nayo, …hakuna kitu….‘Nina uhakika sikuondoka nayo!..ilikuwa hapa..’nikasema mwenyewe.Mara simu yangu ikaita,…nikaangalia, alikuwa ni docta‘Unasemaje , una mzigo wangu…?’ nikajikuta namuuliza hivyo kwa haraka.‘Mzigo gani…?! ‘akauliza kwa mshangao, halafu akaendelea kusema‘Nataka kukuambia hivi, wakati tunakuja,…nikiwa nyumba yako, ..niliona kama kuna mtu alikuwa akikufuatilia kwa pikipiki,…hukumuona…?’ akauliza‘Hapana…sikuwa makini kukagua nje. Mbona zilikuwa pikipiki nyingi tu, una uhakika ….ni nani…?’ nikasema na kuuliza‘Lakini sizani kama alikuwa na nia mbaya, mimi nilipoona kapitiliza ulipokuwa unaingia kwako, nikajua labda ni hisia zangu tu, kuna lolote limetokea…?’ akaniuliza‘Huyo mtu aliishia wapi, hakuingia kwangu…?’ nikamuuliza‘Alipitiliza, hakusimama, sikumuona akisimama,..kwani kuna tatizo…?’ akauliza‘Hakuna tatizo,..ila…lakini sina uhakika, kuna kitu wamechukua kwenye gari langu…’nikasema‘Haiwezekani, muda gani sasa huo..! Ina maana labda,… alirudi akaingia kwako, maana mimi nilipoona kapitiliza, niliingia kwangu, siwezi kujua kama alirudi au laa..hakuna mtu hapo nje kwako unaweza kumuulizia…?’ akasema‘Hamna shida, sio kitu muhimu sana…’nikasema‘Kama wamehangaika kukichukua, kitakuwa muhimu kwao..jaribu kufanya uchunguzi…na kama unahitajia msaada wangu niambi..’akasema, na mimi nikakata simu,Nilipokata simu kuongea na docta,nikatoka nje na kukagua..sikuona dalili ya mtu, hata gari,…sikuona dalili kuwa mtu alilifungua, kwa vipi lakini…nikataka kumpigia rafiki yangu simu, yeye ndiye msaada wangu wa vitu kama hivi, lakini kabla sijaanza kupiga simu, simu ikaanza kuita, ….alikuwa ni baba!NB: mambo ni mengi lakini tutafika tuWAZO LA LEO:  Wahenga walisema hata mbuyu ilianza kama mchicha au mche wa harage ukichipua..Na hata matatizo, yana chanzo chake, kidogo kidogo huja kuwa tatizo kubwa, …nibora kuchukua tahadhari kabla tatizo halijawa kubwa, tusizarau matatizo, na kuyasubirisha , kama lawezekana kushughulikiwa lifanyie kazi haraka iwezekanavyo, ya leo yaweza yasiwe ya kesho. Nilipomaliza kuongea na baba, nilihisi mwili mnzima ukinicheza cheza kwa hasira, lakini sikujua namkasirikia nani, au naogopa nini, lakini anayoongea ni kama ana uhakika nayo,..awali nilijua ni ile chuki kuwa nimeolewa na mtu wasiyemtaka, lakini haya anayoongea sasa yananifanya nianza kuingiwa na mashakaWakati anaongea akili yangu ilikuwa mbali, ikijaribu kuunganisha matukio yaliyofuatana, kujifungua kwa rafiki yangu mtoto anayefanana na watoto wangu, ajali ya mume wangu, ambayo ina utata, na inaonekana alitokea upande anapoishi rafiki yangu.Sasa kuna mtu kaiba bahasha , bahasha ambayo nahisi ilikuwa na ushahidi,…sikupata hata nafasi ya kuifungua,..kwa hali hiyo akili ikaanza kunionya kuwa kuna kitu...kuna mtu, ananichezea, ..ni nani huyoMume wangu, ...hapana, mume wangu anaumwa, hajiwezi,Rafiki yangu....…‘Unasikiliza wewe bint...'baba akaongea kwa ukali kwenye simu'Nakusikiliza baba...'nikasema'Nimekupigia simu, kuwa kampuni ya mume wako, ipo karibu kufilisika, na kuna madeni mengi sana…una hiyo taarifa…?’ baba akauliza‘Baba ndio nimerudi nyumbani, sijapata hata muda wa kuipitia ile taarifa uliyonipa, mimi sijui lolote kuhusu kampuni yake, alikuwa akiendesha mambo yake na mimi yangu…’nikasema‘Unaona sasa, hiyo ndio ndoa mnayoitaka nyie uhuru wa kufanya mtu apendavyo, hata kwa mke na mume, aah…kila mtu kivyake, ..nikuulize hivyo ndivyo tulivyokufunza…’akasema baba na mimi nikabakia kimia.‘Sasa sikiliza mimi sitaweza kutoa chochote tena kwenye kampuni ya mume wako, au hata yako, maana nyie sasa mnajiweza, au sio…na hayo madeni ya mume wako mtajua jinsi gani ya kuyalipa, kama ni kufilisi mali za kampuni mtajua wenyewe, ila mjua kuwa mnahitajika kurejesha mtaji wangu…’akasema‘Baba, hatuwezi kufanya hivyo wakati mtu yupo mahututi hospitalini…’nikasema‘Na huyo rafiki yako alizaa na nani…?’ akanishtukiza na swali ambalo lilikuwa kama mtu kazabwa kibao usoni.‘Mi-mi…baba, sijui…’nikaweza kusema hivyo‘Una uhakika…?’ akauliza‘Mi-mi..sijui baba, kama mwenyewe hajawaweza kunieleza, nitajuaje, nahisi hataki watu walifahamu hilo…’nikasema‘Mtoto wake anafanana na watoto wako au sio…’akasema kama kuuliza‘Mhh, baba umeyajuaje hayo ina maana  umeweza kumuona huyo mtoto…?’ nikauliza na mara kwenye simu yangu kukaingia ujumbe , sikutaka kukatiza simu ya baba, ila yeye akasema.‘Tazama hiyo picha niliyokutumia kwenye simu yako…’akasema ikabidi niache kuongea naye nitazame hiyo picha.‘Huyo ni nani…?’ akuliza‘Hawa ni mapacha wangu, watoto wangu wakiwa wadogo…’nikasemaBaadae ukaingia ujumbe mwingine akionekana mtoto mchanga, .alikuwa mtoto wa rafiki yangu, na pembeni wamewekwa watoto wangu kama kuwafananisha na huyo mtoto, kiukweli wanafanana sana, hana tofauti na watoto wangu kwa sura, isipokuwa yeye hana nyusi nyingi…sura ya kiume ilionekana usoni mwake.‘Hata usemeje,….mtoto wa rafiki yako anafanana sana na watoto wako…sasa niambie ukweli kuna nini hapo, je sio kweli  kuwa mume wako anashirikiana na rafiki yako au kuna nini kinachoendelea kati yenu, mimi nisichokifahamu…’akasema baba‘Una maana gani baba…!!, kuwa rafiki yangu anaweza kutembea na mume wangu…?’ nikauliza‘Nikuulize wewe sasa…’akasema‘Haiwezekani baba, unataka kusema nini kuwa mimi nimeshirikiana na rafiki yangu kulifanikisha hilo, au…’nikasema‘Sasa hilo utajua wewe mwenyewe na mume wako na huyo unayemuita rafiki yako kipenzi…ndugu yako…, lakini kama ikatokea kuwa ni hivyo, sitaweza kuvumilia upuuzi huo, kwanini ukaruhusu hilo, au ulitaka rafiki yako awe mke mwenza wako…au?’akasema baba kwa ukali‘Baba unanijua nilivyo, mimi siwezi kuruhusu kitu kama hicho, na sio kweli baba, kufanana kwa watoto sio ushahidi wa kulithibitisha hilo, ndio hata mimi niliingiwa na mashaka hayo, lakini rafiki yangu hawezi kunifanyia hivyo baba, sio kweli…’nikasema‘Sasa ilikuwaje…jiulize hilo kwa makini,…je ni mume wako kakuzunguka au unataka kusema nini, jitetee sasa….?’ Akauliza‘Baba huyo anaweza akawa mdogo wake mume wangu, anaweza akawa ndiye baba wa huyo mtoto, niliongea na huyo rafiki yangu, na kasema hivyo, hanificho kitu, kiukweli siwezi kuamini hayo, baba haiwezekani, …’nikasema hivyo japokuwa sina uhakika‘Na iwe hivyo…..vinginevyo, utaniambia,  mimi kama mzazi nimeshajua ukweli, lakini siwezi kwanza kuliingilia hilo, …isome hiyo taarifa niliyokupa, halafu na hayo yaliyogundulikana , kila kitu kipo wazi, ukiunganisha hiyo taarifa, matukio na picha, utakuja kuniambia….umesikia, …’akasema na kukata simu‘Bahasha haipo, sasa itakuwaje..siwezi kumuambia baba ukweli kuwa imeibiwa, ataniona mimi ni mzembe..sasa nifanyeje…’nikawa naongea peke yangu  Akilini nikajua kuwa baba atakuwa aliandaa taarifa inayohusiana na mume wangu, huenda na ….ingenisaidia sana, sasa nifanyeje, na ni nani kaiba hiyo bahasha?‘Sasa hiki ni kitendawili kwangu….’ Nikasema nikikaa kwenye sofa, nikashika kichwa nikiwaza…nifanyejeKwa haraka nikachukua simu yangu.***********‘Umefikia wapi…?’ nikamuuliza‘Kuhusu hiyo kazi eeh… bado sijapata lolote la muhimu, ila kuna jambo nalifuatilia bado halijawa sawa, nikiwa na uhakika nalo nitakuambia…’akasema‘Wewe na mume wangu mumeanza lini mashirikiano ..?’ nikamuuliza na nilihsi hali ya kupumua kwa nguvu kutoka kwa rafiki yangu huyo‘Una maana gani sijakuelewa hapo…?’ akauliza‘Yoyote yale…najua unaelewa ninachokuuliza..?’ nikaulizaKukapita ukimia fulani, halafu nikauliza tena`Umenisikaa nilichokuuliza....?’ nikauliza .‘Nimekusikia lakini sijakuelewa bosi, una maana ganu kuuliza hivyo, sijui unachokiongea bosi...’akasema‘Kwanini unakuwa tofauti hivyo, sio kawaida yako unanipa mashaka , mara nyingi nikikuuliza swali unakuwa mwepesi kulitafsiri na majibu yako yanakuwa ya haraka…na mara nyingi yanakuwa ya ukweli, tunageukana siku hizi…’nikasema kwa ukali‘Rafiki yangu,  mimi sijakuelewa,o-bosi, sina mashirikiano yoyote zaidi ya yale tuliyokubaliana, ukiniagiza nifenye ndivyo nafanya, na zaidi subiria taarifa ya kazi uliyonipatia, kwani kuna nini bosi…’akauliza, kiukweli tukiwa kwenye maswala ya kikazi hupenda kutumia neno hilo bosi.‘Ukweli utadhiri,…endelea na kazi niliyokupatia, ila ujue mimi sio mjinga, kukuamini kiasi hicho sio kwamba nimefumba macho na kuziba masikio, akili yangu inafanya kazi vizuri tu, …unanielewa…’nikasema‘Nakuelewa bosi….’akasema‘Watu wanasema , na sio mmoja sasa, na hili kama limefika kwa baba ni hatari sana, kama kaamua mwenyewe kulifuatilia, sijui itakuwaje, mimi nilipomuona mtoto wako kufanana na watoto wangu niliingiwa na mashaka, hayo kama binadamu, lakini najua wewe kama rafiki yangu huwezi kunisaliti…’nikasema‘Ni kweli…siwezi kufanya hivyo….’akasema‘Je kuna kitu unanificha…?’ nikauliza ‘Bosi  unakumbuka ni wewe uliyenishauri kuwa nikatembee nje ili nipate mimba, na ukanishauri nitafute hata mume wa mtu…’akasema‘Ndio ukaamua kutembea na mume wangu…?’ nikamuuliza‘Hapana bosi, mimi najiuliza ni kwanini wewe unapaniki kiasi hicho…’akasema‘Kwasababu lisemwalo lipo…na wewe hutaki kuniambia ukweli, haya basi niambie baba wa huyo mtoto ni nani…kama hayo yanayosemwa sio ukweli…?’ nikauliza‘Yanasemwa mengi bosi na sio yote yana ukweli, …niamini bosi mimi sifanyi kitu kinyume na ulivyoniagiza….na..hebu kwanza subiria nimalize kazi uliyonipa ili tukiongea tuwe na ushahidi….wewe si ndio unataka huo, sasa subiria….’akasema ‘Mume wangu ana kitu kinamsumbua, mdocta wananiuliza kuna jambo gani kalifanya ambalo halimpi amani, nataka kulifahamu, sasa kama ni hilo, ..na wee unamjali shemeji yako, niambie, sema ukweli tuone jinsi gani ya kumsaidia…’nikasema‘Sizani kama …’akatulia‘Huzani nini, ..?’ nikauliza‘Kuwa yeye kuna jambo linalohusiana na mimi au mtoto linamsumbua, sizani, nahisi ni mambo yenu wewe na yeye, au mambo ya kazini kwake…’akasema‘Aliwahi kukuambia hivyo…?’ nikauliza‘Nasema tu..na yote utakuja kuyaona, si umenipa kazi, sasa subiria…’akasema‘Kwahiyo katika ugunduzi wako, umeliona hilo..sawa…?’ nikauliza‘Ndio nahakiki ukweli, siwezi kukujibu kwa sasa unajua nifanyavyo kazi yangu, niamini bosi…’akasema‘Lakini baba anahitajia majibu nitamjibuje mfano akinipigi asimu sasa hivi…?’ nikauliza‘Mwambia tunalifanyia kazi bosi…’akasema‘Sasa nisikilize sana, acha maneno hayo, ya kunizunguka, naona unapima hasira zangu, acha kauli za kufanya niondoe uaminifu wangu kwako, nimeongea na baba, na nimemthibitishia kuwa huenda mtoto wako anafanana na watoto wangu kwa vile ulitembea labda na ndugu za mume wangu, sasa tafuta ushahidi wa kulithibitisha hilo, kama ni kweli, vinginevyo, hutaamini nitakachokifanya…’nikasema‘Kwani kamuonea wapi mtoto wangu, mbona hajawahi kuonana na mimi…?’ akauliza‘Mimi sijui yeye kanitumia picha ya mtoto wako, na mimi nilipoichunguza kiukweli mtoto wako anafanana sana na watoto wangu, kwa mtu yoyote atafikiria hivyo, kuwa wewe umetembea na mume wangu…’nikasema‘Rafiki yangu, ...najua itafika muda ukweli utadhihiri, wa-ache watu wasema, lakini ukweli utabakia pale pale, na ukweli mwingine kama sitaki ujulikane hakuna wa kunilizimisha, hata awe nani…’akasema‘Kwahiyo unataka kusema nini…?’ nikauliza‘Kuwa subiria taarifa ya kazi yako, halafu utakuja kuamua mwenyewe…’akasema‘Kwahiyo ni kweli…?’ nikauliza‘Kuhusu nini sasa…?’ akauliza‘Usitake kunifanya mimi kama mtoto mdogo, unajua nimekuuliza nini…’nikasema kwa ukali‘Hapana, sio kweli, kama ni hivyo unavyofikiria wewe, japokuwa sijui ina maana gani hapo, ukweli wote nitakuambia mimi ambao ni lazima uujue,  ngoja nimalize hii kazi uliyonipatia kwanza…’akasema‘Narudie tena, mimi nimeongea na baba yangu nikamthibitishia hilo, kuwa mume wangu hawezi kufanya upuuzi huo, kwani kama ni kweli, itakuwa kashfa kubwa sana kwenye familia yangu, unalifahamu hilo…’nikasema‘Mhh…nakuomba kitu kimoja,kwanini usisubirie kwanza nimalize hii kazii uliyonipatia, kila kitu kitakuwa wazi, na hata baba yako, ataamini tu, usiwe na wasiwasi kabisa, …’akasema‘Nakuuliza tena, je kuna ukweli wowote wa hizi shutuma kuwa huenda wewe na mume wangu mna mashirikiano fulani, ambayo yamekwenda zaidi hadi kuingilia ndoa yangu…?’ nikamuuliza‘Sio kweli….’akasema‘Nataka ushahidi…wa kumthibitishia baba yangu,,unanielewa, kesho niupate, nakupa muda huo hadi kesho, unanielewa…’nikasema na kumuuliza‘Sawa bosi….’akasema.‘Kama ni kweli, umenithibitishia hilo, basi mimi nataka ukweli wote kuhusu mume wangu, nataka kujua ni kwanini hayo yakatokea, nataka kufahamu  huyo mwanamke mwingine aliye na mashirikiano naye, nilikuambia utafute huyo mzazi ni nani, nimeambiwa, hakuna mzazi mwingine sasa ni nani zaidi yako…’nikasema‘Utamfahamu bosi, kila kitu nimekifuatilia …’akasema.‘Sawa, kwa ajili ya urafiki wetu, kwa ajili ya kupona kwa mume wangu nakusubiria wewe, natumai haitafikia muda tukawa maadui,...’nikasema‘Ni kweli, haitatokea hivyo, niamini, …’akasema‘Una uhakika..?’ nikauliza kama anavyopenda kuuliza baba yangu.‘Siwezi kukuangusha bosi, ndio maana nataka kila kitu kiwe wazi, ili nikikuletea hiyo taarifa, kusiwe na kigugumizi tena, unanielewa nifanyavyo kazi zangu, najua baada ya taarifa hiyo hata baba yako, hatakuwa na tatizo tena, itabakia wewe kuchukua hatua zako...’akasema.‘Sawa ……na nitaichukua hatua ambayo hutaweza kuamini…’nikasema‘Oh,  hatua gani…?’ akauliza‘Nimeliwazia sana hilo,…limeniumiza sana kichwa changu, huyo shetani nikimpata, kuna watu nimewapanga, kuna wale mabaunza, niliwahi kukuambia walishaifanya hiyo kazi kwa rafiki yangu mmoja, unakumbuka yule binti aliyejiua, nataka iwe hivyo kwa huyo shetani, harabiwe kiasi kwamba hatatamani kuishi tena....’nikasema.‘Mungu wangu....’akasema.‘Lakini kwanini kufanya unyama wa aina hiyo …?’ akauliza.‘Wewe  kafanye hiyo kazi…kuna jambo jingine nilitaka wewe ulifanyie kazi, lakini naona nitalifanya peke yangu,  kuna watu wanataka kunichezea…wameingia hadi kwenye anga zangu…sitaki baba anione mimi sijui kazi,…baadae nakwenda hospitalini kwanza...’nikasema na kukata simu.                                         **********Nilifika hospitalini, na kabla sijaenda wodini, akaja docta rafiki yangu, kumbe yeye alihawahi hapo hospitalini, …nilipotoka kwenye gari langu tu, akajitokeza na kuniwahi, akanisalimia kwa haraka halafu akasema;‘Niliongea na docta anayemshughulikia mume wako, hali yake ipo salama kuna mambo kidogo yapo kwenye uchunguzi,  na docta wamesema unaweza kwenda kuongea na yeye, japokuwa anaongea kwa shida, kumbukumbu zake bado hazijawa sawa, ni kawaida tu…zitakuwa sawa taratibu, nab ado hajaweza kujiinua mwenyewe kitandani…’akasema‘Mhh..kwahiyo unataka kusema nini… kuwa hakumbuki kilichotokea au hakumbuki watu….?’ akauliza.‘Yah, kwa hivi sasa hata ukimuuliza atakuwa kama anatafakari, kujiuliza, sasa kwa hivi sasa haitakiwi kumuuliza uliza maswali kama hayo, ..ndio maana walizuia watu kuonana naye, kwa hivi sasa wanaruhsu watu wachache wanaomfahamu..lakini kwa tahadhari hizo…’akasema. ‘Sawa nimekuelewa, ..lakini huenda kukatokea athari gani nyingine, hata kama ni huenda, nataka kujua tu..’nikasema.‘Mhh…athari nyingi ni za muda tu, Inawezekana ikatokea , asiwezi kuzaa tena, inawezekana sio lazima,  athari nyingine ndio hizo kama hiyo kushindwa kutembea kwa muda, kukosa kumbukumbu nk, lakini mengi ni ya muda tu,...’akasema.‘Unaposema kuwa anaweza kushindwa kuzaa, ina maana gani, kuwa hataweza kabisa ku-ku....’nikasema kwa kigugumizi.‘Kufanya kazi ya uanaume..sio hivyo…atafanyakazi kama kawaida, ila..kuzaa, hata hivyo, sio lazima kuwa hivyo…’akasemaMara akaja, docta aliyekuwa akimshughulikia mume wangu, alikuwa anataka kuongea jambo, na huyo rafiki wa mume wangu akamuwahi kabla hajasema lolote, na kitendo hiki sikukipenda, niliona kama anazuia nisisikie jambo fulani, nikawasogelea na yule docta akasema kwa haraka;.‘Mnaweza kwenda kumuona mgonjwa, yupo katika hali nzuri tu, ila kwa tahadhari, msimuongeleshe sana, au kumuuliza maswali ya kumfanya afikirie sana, na mengine bado tunayafanyia kazi, bado yupo kwenye uchunguzi, ....kwa ujumla hali yake inaendelea vyema...’akasema, na mimi nikataka kumuuliza swali, docta  rafiki wa mume wangu akadakia na kusema,..‘Hakuna shida docta, mimi nitahakikisha mgonjwa hapati shida, ...na tunashukuru sana, nitakuja tuongee vizuri....’akasema na yule docta akaondoka, na mimi nikageuka kumwangalia docta na kumuuliza.‘Hivi kwanini unakuwa hivyo, inakuwa kama kuna jambo hutaki mimi nilisikie kutoka kwa huyo docta, mimi ni mke wake, nina haki ya kufahamu kila kitu...kwanini mnataka kuniweka roho juu...?’ nikauliza.‘Sikiliza mimi ni docta, na pili mimi niliwahi kuwa mpenzi wako, nakufahamu ulivyo, ndio maana nataka habari zote kwako ziwe kwa maslahi yako, zisije zikakufanya ukawa na mshituko, na pia usije ukafanya kitu kikaja kumuathiri mgonjwa..’akasema‘Kwahiyo kuna kitu unanificha…?’ nikauliza‘Hakuna…ni tahadhari tu,…niamini mimi, nayafanya haya kwa nia jema kabisa..nilikupenda na nitaendelea kukupenda…na namjali rafiki yangu…sitaki aje kudhurika wakati nafahamu …’akasema na mimi nikamtupia jicho na kuangalia pembeni.‘Wasiwasi wangu ni kuwa inavyoonekana kuna tatizo la kiafya kwa mume wangu, na nyie hamtaki kuniambia, ndio wasiwasi wangu huo...’nikasema.‘Ninachotaka hapa ni hekima, mara nyingi docta akisema mgonjwa wako anahisiwa kuwa tatizo, watu hulichukulia kama ndio tatizo, uvumi husambaa, na hata kumfikia mgonjwa, kwa hivi sasa hatutaki mgonjwa apate kitu cha kumuumiza kichwa, ....inaonekena ana mfadhaiko fulani unaomkera,, unampa shida sana, sasa hilo ndilo ninalotaka baadae tuongee....’akasema.‘Mfadhaiko....?’ nikauiliza kwa mshangao.‘Ndio kunaonekana kuna  jambo lina mkera, linampa shida,na kwa minajili hiyo, anajikuta hana amani...au nafsini mwake, anaogopa kuwa kuna kitu kitatokea kibaya, lakini yupo kwenye hali ambayo hawezi kufanya kitu..naweza kusema hivyo...’akasema.‘Mhh, hapo mimi sijuii....’nikasema.‘Ndio maana nataka utumie hekima kubwa katika kuliongelea hili , tumia hekima sana kuongea na mum e wako, na kwepa sana kumshinikiza kwa maswali magumu na shutuma, ndio maana nilitaka wakati unaongea na yeye na mimi niwepo, kipindi kama hiki kwake ni kigumu sana, ... na hebu nikuulize, je mwenzako hana tatizo jingine kubwa unalohisi kuwa kalifanya....’akaniuliza.‘Kiukweli sijui, labda mambo ya kazini kwake, lakini nitajitahidi kutafuta kama kula lolote zaidi…kuna watu wanalifanyia kazi………’nikasema‘Rafiki yako..au sio?’ akaniuliza‘Yawezekana…’nikasema‘Una uhakika hakuna kitu kingine kinamsumbua mume wako ambacho wewe unakifahamu na unaweza kukifanya kumsaidia ….ili awe na amani…?’ akauliza na mimi sikutaka kumuambia hayo aliyoniambia baba, kuwa huenda ni madeni, …‘Sina uhakika, ndio maana nasema , labda maswala ya kikazi, huko ofisini kwake, na mimi sina ushirika na yeye huko….’nikasema‘Ya kikazi hayo mhh, ni ya kawaida, watu wanadaiwa wengi tu…nahisi kuna jingine kubwa ya hilo,…wewe ndiye mtu wake wa karibu wa kulisaidia hili’akasema. Na kabla sijasema kitu simu ya docta ikawa inaita na yeye akaangalia mpigaji na kusema;‘Tutaongea baadaye hii simu ni muhimu sana...wewe tangulia huko kwa mgonjwa, nakuja, ila kumbuka,....usimuulize maswali mengi ya kumuumiza kichwa’akasema docta  huku akianza kuongea na hiyo simu yake.Nikawa natembea kuelekea huko kwa mgonjwa, nafsini nina wasiwasi, …nitaongea nini na yeye, na nashindwa kuvumilie mengina yanayotokea, nimesikia mengi, nay eye ndio mwenye kauli ya kukubali au kukataaa..je nitaweza kujizuia..Nikashika kichwa nikiwaza,;‘Lakini kwanini niteseke kwa mawazo wakati muhusika yupo...kwanini nisimuulize tu, hapana nitasubiria, lakini nikisubiria baba anahitajia majibu, je kama ni kweli, kuwa mtoto wa rafiki yangu ni wake, nitajuaje, hapana sio wa kwake..mmh, sijui nifanyaje....’nikajisemea mwenyewe kwa sauti ya chini chini. ‘Nitamuuliza tu, kinamna ambayo sitamuumiza…’nikasema, na nikageuka nyumba, kumuangalia docta, alikuwa bado anaongea na simu, sasa akawa ananionyeshea ishara kuwa nisubirie kwanza...mimi sikumsubiri nikaingia ndani kukabiliana na mume wangu...‘Nitamuuliza tu….’nikasema na nilipoingia nilishangaa, mume wangu alikuwa kakaa kwenye kitanda, miguu chini, nikashikwa na butwaa, walisema hawezi kujiinua mwenyewe, mbona…na kwa mdua huo alikuwa …anaangalia mlangoni kama anasubiria mtu, akiwa na tabasamu mdomoni,  na aliponiona mimi, tabasamu lililokuwa mdomoni likatoweka, akakunja sura…                                                             **********WAZO LA LEO: Mwili wa binadamu ni mdhaifu sana, na kosa dogo linaweza likaharibu utaratibu mzima wa mwili wa binadamu, mfano angalia wengi waliofikiwa na matatizo ya kupatwa na kiharusi, kupooza kwa viungo, ...ukichunguza sana utaona kuwa tatizo hilo lilitokea baada ya jambo dogo tu, kwako wewe mzima, uliona ni jambo dogo tu, lakini kwa mwenzako mwenye tatizo, alishindwa kuhimili, hasira kidogo, au  mshituko kidogo tu, na vitu kama hivyo, vimeharibu utaratibu mzima wa mwili wake, na kupelekea kupooza sehemu za viungo vyake.Ni muhimu, tunapokabiliana na watu wenye matatizo kama hayo iwe ni matatizo ya moyo, shinikizo la damu, sukari, au vidonda vya tumbo, tuwe na hekima ya kuongea nao,  tujaribu kufuata masharti ya dakitari, na tusipuuze, maana tunaweza kuja kujuta wakati tumeshaharibu. ‘Mnaweza kwenda kumuona mgonjwa, yupo katika hali nzuri tu, ila kwa tahadhari, msimuongeleshe sana, au kumuuliza maswali ya kumfanya afikirie sana, na mengine bado tunayafanyia kazi, bado yupo kwenye uchunguzi, ....kwa ujumla hali yake inaendelea vyema...’Tuendelee na kisa chetu…..**************Nilisimama nikiwa siamini,…au docta alikuwa ananidanganya,….nikatulia, nikawa namuangalia mume wangu, ambaye kwasasa uso niliouona awali ukitabasamu sasa umekuwa hauna nuru tena, uso ukawa kwenye kukunjamana kwa maumivu au hasira.Unajua wakati nafungua mlango nilikuwa nimepanga kumuuliza maswali yaliyokuwa yakiniumiza akilini, na nilipomkuta kakaa kitandani, nikafurahia kuwa sasa nitaweza kupata majibu ya hayo maswali, ...‘Swali la kwanza nilitaka nimuulize, je ni kweli kuwa ana mahusiano yoyote na mwanamke mwingine zaidi yangu mimi mke wake, jibu liwe  ndio au hapana, hakuna maelezo, sitaki nimchoshe..‘Swali la pili je ana mtoto nje ya ndoa ...jibu ni ndio au hapana.....’ na kama majibu ya maswali hayo mawili yatakuwa ni ndio....basi hakuna jinsi, akipona tu, ndoa imekwisha, kila mtu ashike mipango yake, mkataba wangu na yeye basi, ...niliwazia hilo nikiwa na dhamira ya dhati.Lakini nilijipa moyo kuwa majibu yake yatakuwa hapana, kwani mume wangu hana tabia mbaya, hawezi kunisaliti,….Lakini kabla ya maamuzi ya kuvunja ndoa,  kwanza awe amepona kabisa, pili, ni lazima nimfahamu huyo mwanamke shetai ni nani,…ni lazima nimfahamu huyo mwanamke ili abebe dhamana yake, ni lazima nimfunze adabu, mbele ya.....’Na nilipofika hapo nikawa nimeshafungua mlango, na ndio hapo nikajijuta namuangalia mume wangu akiwa kakaa kitandani.******************‘Mume wangu umepona…’nikasema nikiwa bado nimesimama siamini. Mume wangu alikuwa kakaa, lakini mikono miwili huku na huku imeshikilia kitanda, alikuwa kama anajilazimisha kukaa sawa…nilihisi mikono yake ikitetemeka.Ghafla , nilipotoa kauli hiyo mume wangu akadondokea kitandani, na kilichofuata hapo ikawa heka heka, maana yule mtu aliyekuwa kakaa, kwa shida, maana ilijionyesha kuwa alikaa vile kwa kujilazimisha, kwa jinsi nilivyomuona,.. sasa anatikiswa na bora alidondokea kitandani miguu imening’inia , akawa sasa anatikisika, anatikiswa mwili mnzima.Hapo sasa nikachanganyikiwa kwa haraka nikaanza kuita madocta, kuomba msaada, na haikupita muda, madocta wakaja, na nikaambiwa nitoke humo ndani haraka…nikawa siwezi hata kuinua mguu, na kwa muda huo docta rafiki alishakuja, akanishika mkono, akawa sasa ananikokota, kunitoa nje ya kile chumba.‘Umefanya nini sasa…?’ akaniuliza docta kwa ukali‘Mimi sijui, sijafanya kitu…’nikasema‘Uliongea nini na yeye, si nilikuambia…usimsemeshe kitu cha kumpa mawazo..’akasema‘Sikuwahi kuongea naye, nimeingia, akiwa kakaa kitandani, miguu chini..anatizama mlangoni akiwa na tabasamu, cha ajabu aliponiona tu, akakunja uso…’nikasema‘Unasema ulimkuta kakaa kitandan, haiwezeani,…?’ akaniuliza sasa akishangaa‘Ndivyo nilivyomkuta hivyo…’nikasema‘Mhh…matokeo mazuri hayo,…kama ulimkuta kakaa kitandani, basi tuna matumaini sasa….una uhakika…alikuwa kakaa kukaa..?’ akauliza‘Ndio docta…..kwani wewe ulimuachaje..?’ nikauliza‘Nilimuacha kalala, baada ya kumpatia mazoezi, kiukweli  mwili wake ulikuwa bado haujawa tayari kukaa wenyewe bila msaada, basi nilipomaliza kumfanyia usafi, nikamuacha akiwa amelala..’akasema‘Sasaa, mhh…najiuliza ni kwanini …’nikasema‘Unajiuliza nini…hiyo ni iashara nzuri, kama hukuongea naye, na ulimkuta amekaa peke yake bila ya msaada wa mtu, ujue ni kumbukumbu zinarejea na pia mwili umeshaanza kukubaliana, …’akasema‘Ninachojiuliza mimi ni kwanini alikuwa na furaha kama alitarajia kitu na nilipotokea mimi furaha hiyo ikatoweka…..na hali hiyo ikaja ?’ nikauliza.‘Hapo ina maana kuwa kumbukumbu zinaanza kurejea, huenda katika kumbukumbu zake, alitarajia kuona kitu alichokuwa akikiwazia…lakini ikatokea tofauti na matarajio yake…, inaweza ikawa hivyo, au alipokuona alikumbuka jambo, ..linalomsumbua, akashtuka…vyote au jingine yaweza kuwa hivyo…’akasema‘Sasa mbona naanza kuogopa….’nikasema‘Usiogope, hiyo kwetu ni ishara nzuri..kama kaweza kuinua ule mgongo, na miguu peke yake, basi matajio ni mazuri sasa, ni swala la muda tu…’akasema.‘Sasa alitarajia nini, au kuna kitu gani ananiogopea mimi, au ndio keshajenga chuki na mimi kabisa, au nikuulize wewe ulisema uliwahi kuongea na yeye,, si ulisema mliwahi kuongea naye..?’nikauliza.‘Sikiliza, …usipende kujitwika mzigo kabla haujatua kichwani mwako, utachoka kabla huo mzigo haujatua kichwani, umenielewa, …mume wako hapo alipo anapambana na mitihani mingi, hatujui kilichosababisha hayo yote ni nini..’akasema‘Sasa tutamsaidiaje..?’ nikauliza‘Cha kumsaidia ni kuhakikisha ukija una hali ya kumpa moyo,..usiongee lolote la kumuumiza kichwa, na nahisi kuna kitu anakitegemea au mtu anapenda aje aonane naye, nahisi ndio maana ulipotokea wewe tabasamu likapotea…’akasema‘Ni nani sasa huyo anayetaka kuonana naye…?’ nikauliza‘Hapo mimi na wewe hatujui..tunawazia hivyo tu, lakin wewe ni mke wake, unahitajika kufika, kwasababu kutokufika kwako, kunaweza kumfanya afikirie vibaya zaidi, cha muhimu nikugundua ni kitu gani anakihitajia kwa sasa…’akasema‘Nani ataligundua hilo…?’ nikauliza‘Mimi nitagundua anahitajia nini, usijali…’akasema********** Basi siku ile ilipita, nikawa nafika, namkuta kalala, haongei,..nikimsemesha ahasemi neno, ikawa sasa mimi sina raha…hata rafiki yake, yaani docta akaniambia hali ya mume wangu imekuwa tofauti na matarajiao yao.Siku moja, nikafika hospitalini, nilimkuta mume wangu kalala tu, kaangalia juu, kama kawaida yake, nikamsaidia kumgeuza geuza japokuwa alishafanyiwa mazoeziSasa nikamgeuza aniangalia, nilitaka kujua kama ananifahamu mimi, akawa ananiangalia tu, kama mtu mgeni kwake kabisa, moyoni nikaanza kuingiwa na wasiwasi, nikihisi vibaya, mbona huyu mtu kawa hivi, ni kama mwili mtu.... Ghafla sasa nikaona hisia za uhai kwenye macho yake,  nilimuona akigeuza mboni za macho yake,  na mara machoni niliona machozi yakimtoka...nikasogeza mono na kuyafuta machozi yake..nikawa najiuliza ni kwanini machozi hayo yanamtoka, anahisi maumivu au kuna nini, .nikatulia, na hapo huruma, woga, wasiwasi na kukata tamaa, vikanitawala, ...‘Mume wangu mbona upo hivyo, niambie kinakusumbua nini jamani..?’ nikaulizaNilichoona ni machozi yakiendelea kumtoka kwenye macho yote mawili na mimi nikawa nakazana kumfuta hayo machozi;‘Mume wangu unalia nini, niambie anagalau na mimi nijue, ..mimi ni mke wako, unavyokuwa hivyo mimi naumia sana, niambie kitu ili niwe na amani moyoni, unalia nini, nimekukosea nini…?’ nikaulizaMara mume wangu akawa anahangaika kupanua mdomo, unakuwa kama unatetemeka, kuashiria anataka kuongea jambo;‘Kama huwezi basi usijilazimishe, ila ujue mimi mke wako nakupenda sana…’nikasema na hapo macho yakameta meta, kuashiria uhai, na hali ya kutikisika tikisika kichwa, nikaogopa kuwa huenda ile hali iliyowahi kutokea inaweza kutokea tena, lakini haikuwa hivyo, mara akasema;‘Mke -wangu,…m-ke..w-w-wwngu..’akasema‘Mimi hapa mume wangu, ..’nikasema‘Ni-ni-samehe…na-na- na-kuomba ni-ni-s-s-samehe…’akasema‘Mume wangu hujanitendea ubaya, hata hivyo usiwe na wasiwasi, sina tatizo na wewe…’nikasema‘Ni-ni-ni…..me-me-ku-ku-kosea….’akasema‘Nimekusamahe mume wangu japokuwa sijui …’nikasema‘Yah---ohhhhh……’hapo akavuta pumzi halafu akatulia kwa muda, macho yapo wazi nayaona, na…machozi hayatoki tena…’halafu nikaona kichwa inatikisika, ilichukua dakika chache kikatulia, ikaanza kwikwi….hapo ikabidi niwaite madocta…Nikaambiwa nitoke, nikatoke pale na mimi machozi yakaanza kunitoka, nahisi huzuni, namuonea huruma mume wangu anavyopambana na hiyo hali na siwezi kumsaidia ..Nilikaa nje kwa muda, mara docta akaniita,…nikaingia, na docta akasema‘Haya mwambie mke wako unachotaka kumuambia…’akasema docta‘Mke wangu, so-so-sogea….’akasema na mimi nikasogea na kukaa kitandani karibu yake.‘Ni-ni-sa-mehe..m-m-mke wangu…ha-ha-ya yo-yo-te ya-ya-na-na-natokea ku-ku-ku-toka-ka-kana na dh-dh-dhambi zangu, ni-n-nisamehe sa-ss-sana...’akasema‘Dhambi gani mume wangu...’nikasema na safari hii nikawa nimeshusha sauti na kuongea kiupole‘Wewe kubali kuwa umeshamsamehe, na itoke moyoni…’akasema docta‘Nimekusamehe mume wangu uwe na amani, upone, nakuhitajia sana nyumbani..’nikasema, na nilijikuta pale siwezi kujizuia, machozi yakaanza kunitoka, na nilibakia vile mpaka nikahisi mtu akinishika begani sikutaka kugeuka kumwangala ni nani nikasema;‘Mume wangu ana tatizo gani..mbona kawa hivi tena jamani...?’nikauliza huku nimeshika kichwa.‘Ni tatizo la muda mfupi, litakwisha na ataweza kutembea cha muhimu ni kufuata masharti ya dakitari, dakitari bingwa wa mambo hayo keshamwangalia , kasema hilo litakwisha, hali iankwenda vyema kabisa, kuna kitu anakihitajia, labda ilikuwa ni hiyo kukuomba msamaha,lakini bado, kuna kitu anakihitajia....’akasema.Niligeuka kumwangalia huyo aliyeongea haya, alikuwa docta  rafiki wa mume wangu, na kwa muda huo nilitamani nimkumbatie, ili nisianguke, maana miguu ilikuwa haina nguvu, nilihitajia mtu wa kunifariji na kusema mume wangu atapona tu, hakuna tatizo.....Nikageuka kumwangalia mume wangu, na nilimuona akiwa sasa akiwa kaangalia juu, hatikisiki , alikuwa kama gogo tu, alikuwa kama mwili wa marehemu, lakini unachojua kuwa yupo hai ni machoni, akiyapepesa na kuyageza huku na kule, na sasa machozi yanamtiririka.Pale...moyoni nikaingiwa na huruma, woga ukachukua nafasi nikiwazia mbali zaidi, kuwa sasa mume sina tena, kauli hizi ni za kuniaga, ....na ile hali ya hasira chuki ..vikayeyuka...sasa namkabili mungu anisamehe, kama nina kinyongo na mume wangu mimi sina tena amponye mume wangu tu.‘Ndio maana nilikuwa nakuzuia sana, usiingie bila ya mimi….’akasema docta.‘Hali kama hii hata ingelikuwa ni wewe…’nikasema na mara sauti ya mume wangu ikasema‘Mke wa-wa-ngu, ...usiondoke kabla hujanisamehe, na-na-na taka nikifa niwe huru, na-jua ni-meku-kosea sana, nisa-mehe mke wangu...na baba-ya-ko, ani-sa-sa-mehe..na-na deni…na..na..mto-ooooh..’hapo hakuweza kumalizia, akawa kimiaMilio ya mashine ya hatari ikaanza kulia, hapo ikawa heka heka kwa madocta na mimi nikatolewa nje kwa haraka…hapo ndio nikajua sina mume tena,…..nililia, na kulia….Sitaweza kuisahau siku hiyo…NB: naishia hapa kwa leoWAZO LA LEO: Katika maisha yetu, katika kuhangaika kwetu, maana yabidi tuhangaike, tutafute riziki za halali,..yabidi tupambane na mitihani ya maisha magumu, kuna wenye maradhi ,madeni nk..yote ndiyo maisha yetu, vyovyote iwavyo, hata kama tupo kwenye raha, hatuna shida, tunakula na kusaza…bado sisi ni waja wa mola, hatuna jinsi, tupo kwa rehema zake,…tuyakumbuke mauti, kuwa ipo siku yatatukuta, hata tukiwa nani,…muhimu kwetu, ni kujiuliza je tumejiandaaje na siku hiyo, siku ambayo roho itauwacha mwili,…Sikutaka kuondoka kabisa siku hiyo hapo hospitalini, lakini baada ya ushawishi mkubwa wa madocta ilibidi niondoke, maana walisema hata nikikaa hawataniruhusu nionane naye kwani hawajui ni kwanini ilitokea hivyo baada ya kuniona mimi.Basi baada ya kurejea nyumbani, nikapiga simu kwa rafiki yangu, kabla hata sijamuuliza yeye akatangulia kusema kuwa ile kazi hajaikamilika, kuna vitu bado hajaweza kuvipata kwahiyo nimpe muda zaidi, na mimi sikuwa na cha kumwambia maana mawazo yangu kwa wakati huo yalikuwa mume wangu.‘Mume wangu hali yake sio nzuri…kwahiyo sawa,…kama wahitaji muda, ..sijui wataka mpaka lini,… ila jitahidi, nakupa siku moja ya ziada,  ufanye haraka iwezekanavyo, maana huo uchunguzi ni moja ya mambo ya kumsaidia yeye mgonjwa..’nikasema‘Kwani kazidiwa tena zaidi, si ndio hiyo hali ya kutafuta kumbukumbu au…?’ akauliza‘Hivyo hivyo tu, unasema kumbukumbu, ulipata wapi taarifa hizo…?’nikasema na kuuliza‘Atapona tu…ilimradi yupo na madakitari…’akasema bila kujibu swali langu, na sikutaka kumuuliza tena.‘Ndio hivyo, ila kuna kitu kinamsumbua, mimi sijajua anasumbuliwa na nini hasa, hata madocta hawajui tatizo ni nini hasa…walitarajia mimi nitaweza kusaidia..hata sijui nifanye nini,…, ndio maana nilitaka hiyo kazi uimalize kwa haraka iwezekanavyo, unielewe hapo rafiki yangu ni muhimu sana kwangu na kwa mume wangu, nashindwa mimi nifanye nini sasa…’nikasema‘Sawa nimekuelewa,…ila kiushauri wangu, hata ikikamilika hii taarifa ni bora ukasubiria apone kabisa, kuna mambo mengi, yatamsumbua kichwa ukianza kumhoji ni kwanini, ni kwanini..unanielewa hapo lakini.., hasa ya kazini kwake, na mengine ni wewe na yeye, hakuna zaidi ya hapo, mengine ndio haya sijapata uhakika nayo…’akasema‘Mimi nikiipata hiyo taarifa nitajua kipi ni kipi cha kuongea naye..je huyo mzazi aliyekuwa akimfuatilia umeweza kumtambua ni nani, maana siku hiyo ya ajali nasikia aliondoka kwenye kikao, akiaga kwenda kumuona mzazi, …sasa ni nani..?’ nikamuuliza‘Mhh, nani kuambia hayo..ok,…hapo kuna utata, ndio kuna mzazi alijifungua siku hiyo, siku ambayo na mimi nilijifungua, lakini sio mfanyakazi mwenzao, sasa hakuna uhakika wa moja kwa moja kuwa ndio yeye,..unaona hapo, na ni kweli, kuna kipindi cha nyumba mume wako alikuwa karbu na huyo mama,…sasa huwezi kuchukulia hilo kama kigezo, ndio maaana nasema kuna mambo kidogo hayajakamilika hapo‘ Ni nani huyo…Je huyo mzazi anaweza kuwa mpenzi wa mume wangu , ndio huyo shetani ninayemtafuta mimi au, nataka majibu hayo haraka iwezekanavyo, umenisikia, ..?’ nikauliza kwa ukali kidogo‘Bado sijaweza kupata uhakika, maana kama nilivyosema sio mfanyakazi mwenzao…lakini sasa, huyo mwanamke ana mchumba wake,…nilitaka...niende kwake,..lakini nimesikia kasafiri jana….ooh, hebu subiria kidogo,..’akasema na kutuli baadae akasema‘Kuna kitu nafuatilia, ….ujumbe uliingia, lakini sio muhimu,…sasa ni hivi subiria kidogo,leo nahis nitafikia sehemu, nitakuambia …mambo mengine naogopa kutumia watu, kwasababu za kiusalma na siri zetu, unanielewa hapo…’akasema‘Ok….sawa, nimekuelewa,…mimi  nakusubiria wewe…maana leo nilitakiwa kuonana na baba, kuna mambo ya kuongea naye, muhimu sana..na nilipomueleza hayo mabadiliko ya afya ya mume wangu, akaona tuahirishe hicho kikao, ..na kasema kuna mambo zaidi kayagundua, sasa sijui ni mambo gani…’akasema‘Kagundua nini, hakusema ni mambo gani hayo, mmh…?’ akauliza‘Mimi kwa hivi sasa akili haipo sawa, siwezi kujua, hakusema….labda yanaweza kuwa ya kazini kwa mume wangu au hata sijui, nahisi anaona namficha jambo, kawa mkali sana..’nikasema.‘Unajua baba yako nilionana naye, bahati nzuri sikuwa na mtoto, na kukutana kwetu ilikuwa ni bahati mbaya tu, sio kwa kupanga ilitokea tu, nikiwa nafuatilia jambo fulani nikiwa na haraka kurudi nyumbani, na hakutaka hata kunisalimia, akakimbilia kuniuliza maswali ….’akasema‘Maswali gani…?’ nikauliza‘Kwanza alisema kwanini nimeamua kuzaa bila kuolewa,…nikamwambia ni bahati mbaya tu,…akaniuliza haya baba wa mtoto ni nani, ..nikamwambia hilo ni siri yangu,..akaniuliza mambo mengi-mengu tu mfululizo…, nahisi anajua kitu….sijui kajulia wapi mambo mengi ambayo hata sikutagemea kuwa atayafahamu,…rafiki yangu…, tusipokuwa makini, baba yako anaweza kuchukua hatua ambayo hukutarajia, maana keshafahamu kila kitu…’akasema‘Ndio maana nilikuambia ufanye juhudu za haraka, ili uwahi kuziba sehemu zote nyeti, lakini wewe ukalichukulia taratibu, sijui ulijiamini nini, ujue mimi nina mipaka yangu, na kama kuwajibika kama  baya likitokea, sawa, nitawajibika kama mtendaji, lakini huyo ni baba yangu hawezi kunitupa moja kwa moja lakini nyie je nitawasaidiaje, na ina maana juhudi yangu yote ndio ifike hivyo, inaniumiza sana, kama watu niliowategemea, na lakini sawa....’nikasema‘Nimejitahidi nilivyoweza, nikaziba sehemu nyingi tu…lakini baba yako kama umjuavyo anaweza kufika kokote bila vikwazo, hata hivyo,..hawajafanikiwa kuupata uhakika wa baadhi ya mambo, ndio maana aliniuliza maswali mengi, kuashiria kuwa hana uhakika,…unajua …mimi nimeshaamua, liwalo na liwe, sasa nitafanyaje .…’akasema‘Una maana kusema hivyo, liwalo na liwe…?’ nikauliza‘Sasa rafiki yangu yaliyotendeka, yameshatendeka, utafanyaje sasa hapo…eeh, hebu niambie, wakati mwingine tuangalie mbele, tukirudi kinyume nyume kwa kujiuliza, tutajikuta tupo kwenye lawama sote …na lawama hizo zinaweza kutufikisha kubaya, kama tutajiangalai nafsi zetu tu…na kumbe ilikuwa ni dhamira nzuri tu..lakini sawa, mimi nitakukamilishai huo uchunguzi na uamuzi utakuwa mikononi mwako…’akasema‘Nataka kufahamu tu, je wao wameshagundua lolote kuhusu baba wa mtoto, maana hilo linaweza kuleta picha mbaya kwangu,..kama..lisemwalo lipo sijui nitauweka wapi uso wangu, lakini kama sio kweli..nataka kumkosha mume wangu..awe huru na shutuma hizi..’nikasema‘Kwani …mmh, mume wako si yupo, waache apone atasema mwenyewe, kwanini ulaumiwe wewe…’akasema‘Baba anasema kagundua mambo mengi ambayo kama angelifuatlia awali yasingelitokea na hili limempa fundisho…sasa mimi sipendi hiyo hali ya kuingilia mambo ya mume wangu, …ndio maana nilitaka ukweli kutoka kwako…na hilo la baba wa mtoto wako, lisiwe kama wasemavyo, itakuwa heri sana kwangu, na kwa mume wangu, vinginevyo, sijui baba atachukua hatua gani…’nikasema‘Unajua hizo shuku shuku zao kuhusu mtoto kama nimezaa na nani…nimemwambia baba yako wazi wazi hayo ni maisha yangu, hayawezi kuingiliana na biashara zake, akifanya hivyo anakosea sana..kwani vyovyote iwavyo hakuna nitakayemwambia baba wa mtoto wangu, na sina lawama na mtu, kuwa labda nitambebesha yoyote majukumu ya ulezi, kwahiyo sipendi watu kuniuliza-uliza hayo maswali …’akasema‘Sawa , kwa baba unaweza kuongea hivyo, lakini kila kauli yako anaichukulia kwa uzito wake, maana naye sasa hivi keshasikia mengi, …mimi nakupa angalizo tu, uwe makini sana ukiongea na baba, usimchukulie juu-juu, ana lengo lake, unaweza ukajikuta kubaya sana, na anajua ni nini anachokifanya, hawezi kuingilia mambo ya watu bila sababu maalumu…’nikasema‘Namafahamu sana…najua ni vipi niongee naye, na wapi ikibidi na mimi niwe mkali, maana na mimi nina haki zangu,kiukweli ndio baba yako ni mkali, lakini mimi siwezi kumuogopa tu, ..ninachoogopa ni hatua zake, kuwa labda anaweza kuchukua hatua mbaya zikaumiza wengine bila kujali, na visingizio vije kwangu, hapana kama ni langu aniumize mimi mwenyewe….’akasema‘Baba anachoangalia ni heshima yake, pili bishara zake, maana heshima ndio inamletea wateja na biashara, na mambo ya kisiasa, hataki kashfa mbaya …Na hilo litakuwa ndio ajenda kubwa kwenye hicho kikao, watakuwepo wakurugenzi wote wa vitega uchumi ambavyo ana hisa navyo,…kwahiyo sio kikao kidogo, ni kikao cha maamuzi,..sasa haya mambo ni mengi na yanatokea kipindi hiki, na wewe ulikuwa msaada wangu mkubwa, sijui, umekuwaje sasa…’nikasema‘Niliponana na baba yako, alikuwa na mdogo wa mume wako…’akasema‘Oh yupo yule aliyesafiri au huyu mwingine….kwahiyo wameshaongea, huenda kabanwa na kusema ukweli wote au…?’ nikauliza‘Ndio, lakini huyo mtu nilishaongea naye kabla na kumuweka sawa, sizani kama anaweza kufungua bakuli lake, nina mambo mengi yake mabaya ninayoyafahamu, anajua kabisa akinisaliti nitamuumbua kwa mkewe.., kaahidi hatasema loloye baya dhidi yangu, usiwe na wasiwasi na huyo mtu….’akasema‘Una uhakika hataweza kusema ukweli, maana nilipanga kuonana na mke wake…?’ nikauliza‘Hawezi kusema chochote, …mambo yangu yatabakia kuwa yangu, nina uhakika, hilo litabakia sirini kwangu, hakuna nitayakemuambia nimeshaamua hivyo, mpaka hapo muda muafaka ukifika, , kama ikibid kusema, nitasema…, lakini sizani kama kuna mtu atafahamu siri hiyo,..na unasema unataka kuongea na mke wake unataka kuongea naye nini, …usije ukaharibu…’akasema‘Hapana…kuna mambo yangu mengine na huyo mwanamke..mambo ya akina mama, unajua nimewekeza huko pia, kwa akina mama, sasa yeye ni mmoja wa wahusika wakuu, na nilitaka nijue yeye anasemaje kuhusu haya yanayoendelea hasa kuhusu huyo mtoto wako,je hamshuku mumewe …’nikasema‘Hata sijui….lakini kwangu nimehakikisha kila kitu kipo sawa, …mimi nakushauri wewe hangaika na mume wako, haya mengine yaache kama yalivyo,..hiyo taarifa itakusaidia kidogo tu…sizani kama ina lolote jipya…’akasema‘Unajua nilipokuwa naongea na docta, docta alisema mume wangu anaonekana kama  anataka kuonana na wewe…?’ nikasema, nikahis kama kashtuka na akahema kidogo na kusema‘Kuonan na mimi, aliongea hivyo au…?’ akauliza‘Docta, rafiki wa mume wangu ndiye anahisi hivyo…’nikasema‘Mhh, kuna nini kilitokea mpaka ahisi hivyo, lakini eeh, hata hivyo ni wajibu wangu kumuona au sio , nyie ni kama ndugu zangu, tumeishi nanyi, tumeleleana, shemeji namuona kama ndugu yangu pia, japo,…haya yanayotokea sasa yanaleta kigugumizi, ila …sijui nitafikaje na mtoto,. Si unajua tena, …’akasema‘Wewe fanya mpango uje uonane na yeye, kama itasaidia,..huyo mtoto isiwe kisingizio, huyo unaweza kuja naye…maana kutokana na docta kuna muda akiwa anaweweseka, alitaja mtoto, kama ingelikuwa ni watoto wake, angelisema watoto, lakini katamka ‘mtoto’…hizi ni hisia zinajengeka, na kumfanya docta ahisi kitu…’nikasema‘Mtoto, katamka hivyo mtoto, mtoto wa nini, hapana, labda kamsikia vibaya, na hiyo sio sababu ya kuhisi mtoto wangu…sema kwa vile kuna kitu kinatakiwa hapo, lakini hilo lisikusumbue kichwa, ni langu, najua jinsi gani ya kupambana nalo…’akasema‘Docta analifuatilia hilo kwa karibu na anajaribu kuwa karibu na mume wangu, kusikia kama atapata chochote kutoka kwake…je hamjawahi kuonana na docta ukiwa na mtoto wako…?’ nikamuuliza‘Hajawahi, labda, ..sina uhakia maana huyu ndugu yangu anayekaa na mtoto angeliniambia…kama aliwahi kuja nikiwa sipo, na mimi sijamuacha mtoto wangu kwa muda mrefu na huyo msaidizi wangu…’akasema.‘Unajua kila hatua, naanza kuingiwa na mashaka..anyway, mimi nina imani hujanificha kitu,..sijui, maana, umeshasema huwezi kumuambia mtu kuhusu baba wa huyo mtoto wako.., ikiwemo mimi, na kauli hiyo inanifanya nianza kuwaza mengi, ni kwanini hadi mimi unifiche, najiuliza sana…’nikasema‘Ndio maana naona bora iwe hivyo,…kama mwenyewe umeshaanza kubadili imani yako kwangu, unaanza kupinga hata kauli zako, basi hata mimi naingiwa na mashaka, je mimi rafiki yako naweza kufanya jambo kinyume na kauli zako, aah, kwa hali hiyo, hata safari, sijui itakuwaje….na huenda nikaondoka haraka iwezekanavyo…’akasema‘Huwezi kuondoka kabla sijaufahamu ukweli. Ujue hiyo safari nimeidhamini mimi mwenyewe, sasa usije kuharibu kila kitu…Hilo la kuujua ukweli, nitalijua tu, nimeahidi hivyo…, umesikia, kupitia kwako au kwa njia nyingine, nitamfahamu baba wa huyo mtoto, umesikia, na nina maana yangu kufanya hivyo…’nikasema.‘Haah , sawa…lakini ….hebu kidogo…’ na simu ikakatika, nilishtuka kwa kitendo hicho cha kukata simu kabla sijamalizana naye…, sio kawaida yake kukata simu, kihivyoKwa vile nilikuwa na haraka, sikutaka kumpigia tena simu, …lakini kitendo icho kilinikwanza kweli kweli….*********** Nilifika hospitalini, na nilihitajika kuonana na docta kwanza kama naruhusiwa kuonana na mume wangu.‘Sawa unaweza kuonana naye, ila docta, jirani yako, yupo huko anaongea naye… NA kumpatia mazoezi kuna huduma nyingine tunataka kumfanyia kidogo huenda ikasaidia..’akasema‘Kwahiyo sasa anaongea vizuri…?’ nikauliza‘Ndio ila, kumbukumbu hazijakaa vyema kabisa…kuna muda anajichanganya, na siku ya leo amekuwa akikuulizia wewe, ni mnyonge sana, nahisi wewe utaweza kumsaidia, jaribu sana kuwa naye karibu…’akasema‘Haya ngoja nikaonane naye, kwahiyo unahisi ana tatizo jingine kubwa…’nikauliza nikiwa na hamasa ya kwenda kuonana na mume wangu.‘Hakuna zaidi ni hilo, …mengine hatuwezi kuyafahamu kwa sasa, maana hatua kwa hatua anaanza kuimarika, usiwe na wasiwasi kabisa…’akasema Basi nikaondoka na kuelelea huko alipolazwa mgonjwa, nilipoingia nilimkuta docta akimfanyia mume wangu mazoezi, nilishangaa kuona hata ile kukaa kama kwanza hawezi, …sikutaka kuwashtua kwanza nikatulia kuwaangalia.‘Sasa naona upo tayari,…unajua ni muhimu ukajitahidi mwenyewe ungelifanya kama ulivyojitahid kipindi kile ungelipona haraka tu…’akasema docta‘Hata sijui ilikuwaje, kwani nilijitahidi vipi…?’ akaliza suti yake ilikuwa ya kinyonge ya mgonjwa aliyekata tamaa.‘Uliweza kukaa mwenyewe kitandani…’akasema‘Mimi, nilikaa mwenyewe, ….sikumbuki. maana hata mwili siuhisi ni kama vile sina mwili kabisa….’akasema‘Utakumbuka tu kidogo kidogo,…’akasema docta‘Hivi unasema kweli ..kuwa Mke wangu aliwahi kuja kuniona, mbona mimi sikumbuki kumuona…’akasema‘Mbona kila siku anakuja kukuona…’akasema docta‘Mmhh, kweli nahisi hataki kuja kuniona kwa hayo niliyomtendea, nimemkosea sana, sijui kwanini, nahisi mimi ni mtu mbaya sana, na huyo rafiki yake mhh…’akasema hapo akatulia hakuendeleza neno‘Usijali,..kosa ni kosa, na ukikosa, ukatubu basi kosa linafutika, ila ukirudia kosa, ujue wewe ni mkosaji…’docta akasema‘Nimerudia kosa mara nyingi sana..ndio maana nipo hivi…sijui atanisamehe kabla hajchelewa… unahisi atanisamehe, nataka nafsi yangu iwe huru, nina imani akinisamehe, basi, nitapumzika kwa amani, atakuja leo…?’ akauliza‘Atakusamehe, kwani hujafanya kosa kubwa la yeye kushindwa kukusamehe, makosa ni kawaida ya mwanadamu au sio…’akasema docta‘Wewe hujui tu…nahisi moyo mwake ananichukia sana, tena sana, sijui kwanini ilitokea hivyo, lakini, hata sijui, nilifanya nini…’akasema‘Kwani anafahamu kosa ulilomtendea, ni kosa gani kubwa hivyo..?’ akaulizwa‘Ndio maana hataki kuja kuniona, nahisi keshafahamu, ni kosa kubwa sana, tena sana, lakini sikumbuki, tatizo, nahisi nimekosa, lakini haaa, mbona sikumbuki kitu…’akasema‘Kosa gani…lakini utakumbuka tu usijali…si hukumbuki, basi ni kosa dogo tu, au sio..au unalikumbuka, ni kosa gani…?’ akauliza na hapo akageuka, wakaniona, na kimia kikatawala. Mume wangu aliponiona akaonekana kutokuwa na raha, akawa katulia, nikamsalimia, akaitikia kwa unyonge sana, nikamuuliza anaendeleaje akasema sasa hajambo.‘Sasa ni kujitahidi kula na mazoezi, na nitajitahid kuja kukufanyisha mazoezi mwenyewe, maana walinikataza awali, sasa najua upo tayari, au sio..?’ nikamuuliza‘Sawa, lakini ..ulishanisamehe…’akasema hivyo‘Kukusamehe, mume wangu usiwe na wasiwasi mimi ni mke wako, tunakoseana sana, au sio, kwani wewe si ulishasamehe au sio..’nikasema‘Lakini wewe hujanikosea kitu mke wangu, wewe ni mke mwema, nimeliona hilo, wewe ni mwema,…’akasema‘Mh, mume wangu nimeshakusamehe kabisa…’nikasema, nikimtupia jicho docta na docta akaashiria kukubaliana na kauli yangu japokuwa sikufahamu ni kosa gani analolisemea mume wangu.‘Najua hujanisamehe, niona nafsi yako…unanichukia sana, nakuomba uondoke tu, kama hutaki kunisamehe…’akasema na kunifanya nishtuke na kugeuka kumuangalia rafiki yake.Docta..alipoona vile..kwanza alitulia, kama ananisubiria mimi niseme neno la kumsihi au kitu kama hicho, na aliponiona nipo kimiya yeye  akamsogelea mume wangu pale alipolala, akamwiinamia na akawa anamsemesha sauti ya chini-chini‘Rafiki yangu nimeshakuambia, ukitaka usipone haraka, uendelee kujitesa na hayo mawazo yako, mke wako hana kinyongo na wewe kabisa,…. anafahamu kuwa kila binadamu anakosea, na kutenda kosa sio kosa, bali kurejea kosa, wewe kama uliteleza, uliteleza tu kama binadamu wengine,..na umeshafahamu kosa lako, umetubu, au sio ...hiyo inatosha kabisa..mimi nimeshaongea na mke wako, yeye kasema ameshakusamehe.....’akasema.‘Wewe huelewi tu, .....ninachotaka ni kauli ya mke wangu kuwa amekubali kunisamehe, kutoka moyoni mwake, nafsi yake bado haijanisamehe, naiona kabisa, usimsemee…’akasema‘Nafsi yake umeuonaje wewe…’akasema docta‘Naiona,…naiona, naiona. Naiona…’akawa anaongea hivyo mfulululiza mpaka docta akamgusa begani ndio akanyamyaza‘Mimi najua tu, mimi ni mtu wa kuangamia tu, maana hajanisamehe, ninajua mimi sio mtu kuishi tena, nimepewa muda wa toba, kabla sijafa, niwe nimesamahewa, na mke wangu, lakini mke wangu, hajanisamehe, anaongea tu mdomoni, yeye na baba yake ni kitu kimoja, wanataka niangamie tu,, ....’akasema na kauli hiyo ikanishitua, nikajikuta nikisema.‘Wewe mume wangu unakazania nikusamehe, nikusamehe,  kwa kosa gani,mume wangu mbona hujanikosea kitu, kama ni yale ya nyumba nimeshakusamehe, lakini sijui kama una makosa mengine,labda uniambia makosa gani hayo,na hilo la baba yangu linatoka wapi,,,.?’ nikauliza na rafiki yake akasema.‘Tulishaongea hilo na mke wako, kwake sio kosa kubwa sana, ni mambo yanatokea, hasa kwa wanadamu, baba yake alikuja hapa akasema yeye yupo tayari kuangalia unapona haraka, na kama kuna lolote limekwama aambiwe, sasa unataka nini tena..’akasema docta‘Baba yake au mwingine….hahaha, na akisikia hayo madhambi, si ndio, atanifukuza kabisa,…najua keshayafahamu ila anasubiria kuwa nitapona ili aje kuniumbua, hatawahi kabisa, ila mke wangu, nisamahe jamani, naangamia mwenzako…’akasema kwa sauti ya uchungu kama anataka kulia.‘Kiukweli pale nilitaka kuongea kwa ghadhabu, maana sijui ni kosa gani, na nimetamka kuwa nimeshamsamehe bado ananisihi, …docta akaingilia kati na kusema‘Mkeo anakupenda sana, muda wote yupo na wewe, kaacha kila kitu kwa ajili yako, sasa unataka nini tena hapo, keshakuelewa, muhimi ni wewe kupona hayo ya kufikiria kufa , kila mtu atakufa hata akiwa mnzima au sio....’akasema docta na kunigeuka akaniambia kwa sauti chini chini‘Toa kauli yenye udhabito kuwa umemsamehe, umeshafahamu kila kitu,..tusipoteze muda, kwani hali yake, itaboreka haraka akiwa na moyo wa matumaini,..vinginevyo,…huyu mtu atachanganyikiwa… ‘akatulia kwani dakitari wawili na nesi waliingia wakiwa na vifaa, vikiwemo vyuma, nikashangaa hivyo vyuma vya nini tena .NB: Mambo ndio hayo, msichoke, maana hapo hospitali ndio tutagundua mengi.WAZO LA LEO:Fadhila , baraka na rhema kutoka kwa mola wetu ni nyingi sana, je tunazikumbuka, je tunamshukuru, au tunasubiria mpaka tuanza kuwa na hali mbaya ndio tuanze kusema ‘ooh mungu wangu…. tumkumbuke mola wetu tukiwa wazima, tukiwa na uwezo wetu, tukiwa vijana, ..naye atatukumbuka tukiwa na shida.Tumuombe mola wetu tuwe na imani hiyo, Aamin.‘Jamani tunaomba nafasi...tunataka kumweka mgonjwa vizuri,…kuna jambo tunatakiwa kumfanyia sasa hivi, na muda umekwisha,…na hata hivyo mgonjwa hakutakiwa kuongea na watu kwa muda mrefu hivyo, docta natumai unakumbuka masharti tuliyokupatia, naona hii inatosha, samahani docta,...’akasema huyo docta, akimgeukia docta mwenzake.‘Tunataka tufanye kazi yetu samahani…’akasema docta bingwa wa mifupa, akianz kuweka vitu vyake sawa.‘Hamna shida, tumeshamalizana, .....’akasema docta rafiki, sasa akiniangalia mimi machoni, na kunigusa begani akasema;‘Toa kauli yako haraka, tuondoke....’akasema na mimi nikageuka kumuangalia mume wangu, na nilivyoona vile vyuma, wanavyotaka kumuwekea mume wangu, huruma, machungu yakanishika,…nilijiuliza moyoni, ni kosa gani alilolifanya mume wangu linalostahiki hayo yote, hapana mungu anisaidie, tu, mungu amsaidie tu mume wanguKiukweli pale moyo wangu ukawa mweupe, nikawa sina kinyongo na lolote kwa mume wangu, haraka nikamuinamia mume wangu,  na yeye alikuwa akiniangalia kwa macho yaliyojaa huruma, ….kuonyesha kuwa anateseka moyoni na kiwili wili…tukawa tunaangaliana, niliona machoni kwake akianza kutoa machozi,…na mimi nikahisi machozi yangu yakinijia kwa kasi, kabla hayajaanza kutoka nikasema;‘Mume wangu nimekusamehe, natamka haya kutoka moyoni mwangu, namomba mola mwenyezi akujalia upone, ili tuwe pamoja, sioni dhambi gani kubwa inayostahiki mateso hayo yote, nakupenda sana mume wangu,  pambana na haya, uyashinde, ukijua mimi mke wako nipo kwa ajili yako,..na kama kuna mengine tutayamaliza nyumbani, sawa mpenzi mume wangu....nimeshakusamehe...’nikasema na nilipomaliza kusema maneno hayo;Nikaona tabasamu likijitokeza usoni mwake, ..uso ukapambwa na nuru ya furaha,…akawa kama anataka kuongea kitu lakini hakuweza,mdomo ukawa unatikisika tikisika,,.. na mara akaanza kutikisika hivi,…madocta hawakuwa awali wameliona hilo.Nikawa najaribu kuwaonyeseha ishara madocta, lakini walikuwa wakiongea na yule mwingine alikuwa akiweka vitu vyake sawa..ile hali ya kutikisika haikuchukua mdua mrefu, mara akafumba macho, ...na muda ule ule,  nikasikia milio ile ya hatari ikilia chumba kizima, na wale madakitari wakamsogelea mgonjwa na kutuambia tutoke humo ndani haraka.....‘Nini tena…’akasema docta wake, na haraka wakaanza kazi ya kumuhudumia, hata vile vyuma viliwekwa pembeni, wakawa sasa wanahangaika kumrejesha , azindukane, maana alishapoteza fahamu.Mimi kuiona ile hali, kwanza nilibakia mdomo wazi, siamini,..nishikiwa na bumbuwazi, macho yamenitoka , nikawa sina nguvu kabisa miguu haiwezei hata kuinuka,…nikahisi maumivu makali kichwani ….maumiu makali kweli.., na pale pale nikahisi kizungu zungu, na kabla sijadondoka, giza likitanda usoni, na sikukumbuka kitu mpaka pale  nilipozindukana nikajikuta nipo kitandani.*********Siku mbili nilikuwa kitandani sijiwezi, japokuwa siku nile kama walivyinielezea, nililazwa na kuwekewa maji, yalipoisha, nikawa nimshazindukana, nikauliza kuhusu mume wangu, wakaniambia anahudumiwa, siwezi kumuona.Niligoma kuondoka nikitaka nimuone mume wangu kama yupo hai au la..sijui walifanya nini, usingizi ukanijia, na nilipoamuka tena nilijikuta nipo nyumbani kwangu, kitandani nimelala mwili ulikuwa hauna nguvu kabisa,Ilikuwa sasa ni siku ya tatu ndio  akaja docta rafiki wa mume wangu kuniangalia ninaendeleaje, nikajitutumua na kutoka, nje, kuonana naye, akasema;‘Sasa unatia matumaini,  naona leo upo safi, siku zote nakuja hata hunitambui vyema, sasa jitahidi hivyo hivyo, ujiimarishe mazoezi, na hali hiyo itakwisha,…’akasema‘Sawa umekuja nataka kwenda kumuona mume wangu…kama….angalau niuone mwili wake..’nikasema‘Unasema nini wewe…uuone mwili wake, kwani mume wako amefariki, nan kakudanganya…’akasema‘Usitake kunificha…’nikasema‘Unajua kwa hali kama hiyo, nahisi ni vyema tukaongozana ukaenda kumuona wewe mwenyewe....’akasema‘Docta, usitake kunifanya mimi mtoto mdogo, niliona kwa macho yangu…’nikasema, nikijua wananificha tu.‘Usijali, tutakwenda kumuona mgonjwa, hajambo mwenzako, leo ni muhimu twenxe ukamuone ili uwe na amani ....’akasema.‘Ina maana kweli mume wangu yupo hai,..docta, usinifichei…oh, jamani, nimekua mgonjwa zaidi ya mgonjwa, vipi anaendeleaje lakini…, mimi nilijua siku ile ndio naagana naye…’nikasema sasa nikiwa na imani, na nguvu zikaongezeka mwilini kiaina yake‘Unajua siku ile ilikuwa kizaa zaai, maana ulipotewa na fahamu, ikabidi uhudumiwe wewe kwanza..lakini  baada ya kutolewa mle ndani maana kipindi kile ndicho mume wako naye alikuwa kapoteza fahamu, madota wake walikuwa na yeye , iakbdi mimi nipambane na wewe…’akasema.‘Ahsante mungu wangu, kwahiyo mhh…, mungu mkubwa, mume wangu bado yupo hai…jamani hadi kwenye ndoto nikawa namuota tunaagana, hizi ndoto jamani…’nikasema‘Hajambo kabisa, anaendelea na matibabu ya kuweka viungo vyake sawa, ile kauli yako ilitokea moyoni kuwa umemsamehe, aliihisi,…kwahiyo ila hali ya kuchanganyikiwa ikaondoka baada ya kuzindukana, akaja mtu mpya, mwenye afya yake, akawaanaongea vizuri tu…’akasema‘Hapo sasa umenipa nguvu …sasa naweza kwenda kumuona ila bado mimi naogopa…kwenda kuangaliana naye, unajua tangia mume wangu alazwe, anakuwa kama mgeni kwangu kabisa, sijui kwanini…’nikasema.‘Usiogope ni lazima upambane na hiyo hali, na yeye pia, …hata hivyo baada ya kuzindukana, hali yake imeimarika sana, ..tuna imani mkikutana naye hakutakuwa na tatizo tena, na huenda akaanza kuongea tena, maana ghafla juzi alikataa kuongea kabisa na watu, hatutajua tatizo ni nini…lakini haya yatakwisha tu tu...’akasema.‘Alikataa kuongea au ndio kule kuongea kwakwe kwa shida…?’ nikauliza‘Ile hali ya kuongea kwa shida, ilishamalizika…na akawa anaongea vyema tu…hebu jiandae basi tuondoke, au unakwenda hivyo hivyo ulivyo…?’ akaniulizaBaada ya kujiandaa, nikaingia kwenye gari la huyo rafiki wa mume wangu, na tukaanza kuongea maswala mengine, kwa muda ule nilitaka ninyamze tu, sikuataka kuongea kabisa,  na mara nyingi nilikuwa mtu wa kuitikia tu, lakini aliponiuliza swali hili ikabidi nishtuke na kumjibu;.‘Rafiki yako alikuaga?’ akaniuliza.‘Rafiki yangu gani...?’ nikauliza huku nikionyesha mshangao.‘Usipende kuuliza swali, wakati unafahamu nakuuliza nini, una marafiki wangapi, ..na unafahamu kabisa nikisema rafiki yako nina maana gani’akasema.‘Kwani kaenda wapi?’ nikamuuliza kwa mshangao.‘Haah, ina maana, hujui, si kaenda kusoma ulaya, nakumbuka kuna siku uliniambia kitu kama hicho, sasa kaondoka jana usiku ...’akasema.‘Haiwezekani, hawezi kuondoka bila ya kuniaga, ina maana kaamua kuondoka bila ya kumuona  mgonjwa, angalau angesubiria kuona mgonjwa anaendelea vipi, haiwezekani, ..hapana huyo sio rafiki yangu ninayemfahamu mimi ndio kafanya hivyo ili iweje, au unanitania..?’ nikauliza nikiwa siamini kabisa.‘Ndiye huyo huyo rafiki yako, na kama ni swala la kumuona mgonjwa, mbona karibu siku mbili hizo, ulipokuwa unaumwa nyumbani yeye alikuwa akienda kumuona mgonjwa, alisema kwa vile unaumwa, ni wajibu wake kuchukua nafasi yako...’akasema.‘Mimi sikuelewi, mliniambia nini mimi, kuwa mgonjwa haruhusiwi kuongea na mtu mwingine zaidi ya mimi na wewe, na hao madakitari wanaomshughulikia, ikawaje sasa mkamruhsu huyo mtu…?’ nikauliza kwa mshangao.‘Hakuruhisiwa kumuona mgonjwa, yeye alikuwa akifika na kusimama kwenye kile kiyoo, unachoona ndani, basi, alikuwa akifanyaa hivyo kila siku ila jana, ndio akapata nafasi ya kuingia ndani, ...’akasema.Nilitulia kwa muda, sikuweza kuongea, kwani moyo ulikuwa ukiniuma, nilihisi kuna jambo linaloendelea, na hawa watu, na wanachofanya wao ni kunichezea akili yangu,‘Aliruhusiwa kumuona, sijui ilitokeaje, mume  wako akaulizia kuhusu huyo rafiki yako, kuwa je aliwahi kuja kumuona, tukamwambia kwa vile analea  mtoto mchanga inakuwa vigumu kwake, yeye akaomba aletwe , anataka kuonana nay eye, kama hajaondoka kwenye kusoma...’akasema na hapo nikageuka kumwangalia huyo rafiki yangu.‘Ina maana …mbona sielewi hapo....!?’ nikauliza kwa mshangao,‘Yaonekana mume wako akilini alikuwa anamkumbuka rafiki yako, na anafahamu kuwa atakwenda kusoma, ndio maana akaomba aje waongee naye kabla hajaondoka, na siku hiyo alikuwepo nje, sijui alijuaje kuwa yupo hapo nje, ikabidi aambiwe aingie…’ akasema.‘Siwaelewi hapo kabisa, unazidi kunichanganya, halafu alipoingia alikuwepo nani mwingine aliyesikia wakiongea naye…’nikasema.‘Mimi sikuwepo, nilifika wakati wameshamaliza kuongea nikaambiwa ilivyokuwa, sasa sijui waliongea nini, ..hata hivyo, kipindi wanaongea hakutaka mtu mwingine awepo , kwahiyo waliongea wao wawili tu…’akasema‘Mhh…mimi sipendi hisia mbaya, nimejitahidi sana kulikwepa hilo, lakini kila hatua najikutwa nalazimishwa kuhisi vibaya, naanza kumshuku rafiki yangu mwenyewe ubaya, ni kwanini lakini, ni kwanini ….mimi nilimuamini sana, ..oh, hata sijui, …mungu anisamehe tu…’nikasema‘Sio swala muhimu sana, kwa hivi sasa,…muhimu na la kuzingatia, ni ahadi kwa mume wako, kuwa umeshamsamehe au umesahau hilo?’ akaniuliza .‘Mimi sijasahau, ila sikujua anataka nimsamehe nini, sasa , kosa gani nililomtendea, ndio maana nhitajia kumuuliza, sijui nifanyeje….’nikasema‘Kwa hivi sasa hapana, inatakiwa wewe kuwa hivyo hivyo, kuwa umeshamsamehe, na sitaki kabisa kukulazimisha kuamini ubaya wowote dhdi ya rafiki yako na mumeo, kuwa labda kuna mahusiano ..labda…ila dalili zinajionyesha hivyo, ..’akasema‘Hata mimi sasa naanza kuziona, lakini nafsini mwangu nashindwa kuliamini hilo, na kwanini iwe hivyo, rafiki yangu mwenyewe anifanyie hivyo, ..mume wangu mwenyewe anifanyie hivyo, hivi kweli wewe unaweza kulisamehe hilo…’nikawa nauliza‘Kwa hivi sasa inabidi iwe hivyo, mpaka mumeo apone, mpaka, mumeo awe an nguvu za kukabiliana na wewe….naomba uwe hivyo, ujue lolote utakalolifanya kinyume na ulivyokiri kuwa umeshamsamehe, unaweza kuhatarisha maisha ya mumeo…’akasema‘Ni vigumu sana, kama ni kweli hilo limefanyika, sizani kama msamaha huo utakuwepo, sizani,…hata kama kakimbia , nitafanya nifanyalo, akipate kile nilichoa hidi …sitamsamehe….siwezi kabisa…’nikasema ‘Kumbuka uliyatamka hayo mbele ya mume wako, akaamini kweli umeshamsamehe,..sasa usiwe kigeu geu wa kubadili kauli zako, unaongea vingine unakuja kutenda mengine, sio vizuri, nina imani kuwa siku ile uliyatamka hayo maneno ya kumsamehe kutoka moyoni mwako, au sio….’akasema docta‘Ndio ilitoka moyoni, lakini sikujua kosa , sikujua nasamehe nini sasa, mlinitega tu, najua hata wewe unalifahamu hilo, na kama upo nyuma ya hili jambo sizani kama nitaweza kuwasamehe….’nikasema.‘Mimi sijui lolote zaidi ya kufanya juhudu kuutafuta ukweli, mimi niliona hizo dalili, sikutaka kuamini hivyo, na ilichukua mud asana kuanza kuhis hivyo, japokuwa rafiki yangu alijitahidi kunificha..mimi sikupenda kabisa wewe wakufanyie hivyo, na rafiki yangu alilifahamu hilo, ndio maana hakuwahi kuniambia…’akasema‘Rafiki yangu…siamini, bado sijaamin…’nikasema‘Huenda ikawa sio kweli, kwasababu hata mimi pamoja na juhudi zote sijapata ushahidi wa moja kwa moja…nap engine huyo rafiki yako aliitwa  kwa jambo hilo hilo....’akasema‘Jambo gani…?’ nikauliza‘Kuwa labda kamkosea,..kwahiyo alitaka asamehewe, au labda,…mimi naona labda zipo nyingi sana, na sio vyme kabisa kuwa na shaka shaka hizo tena, muhimu kwa sasa tuangalia afya ya mume wako,..hilo ndilo la muhimu mengine yasubiria kwanza…’akasema‘Ni ngumu sana…’nikasema‘Sasa tunakaribia kufika, leo foleni imezidi sana,…tukifika ukumbuke,  ni vyema ukiingia pale uwe na uso wenye furaha, usionyeshe chuki yoyote, kuwa labda kuna jambo,  maana toka jana alipofika huyo rafiki yako wakaongea naye, alipoondoka tu tulishangaa,…’akasema‘Alikuwaje..?’ nikauliza‘Amekataa kuongea tena na watu, tunahisi huko kukataa kuongea kwake, kuna mahusiano na huyo rafiki yako, hatujui waliongea nini, na mgonjwa mwenyewe akiulizwa kwanini anafanya hivyo hataki kusema, basi tukasema labda ni kwa vile na wewe hujafika, lakini hilo tulimuelezea awali kuwa unajisikia vibaya, akalipokea sasa jana ndio hali hiyo ikajitokeza...’akasema.‘Kwahiyo …sasa kwanini hakuulizwa huyo mtu kabla hajaondoka, ni kwanini anamtesa mume wangu hivyo, kuna nini kati yao wawili, …hapana mimi sizani kama nitaweza kuvumilia tena, niambie nifanye nini sasa?’ nikauliza kwa hamaki.‘Kama nilivyokuambia mengine yasubirie, labda kama hutaki mume wako apone, na hakuna aliyefahamu kuwa kutokuzungumza kwake huko kunaweza kuwa na mahusiano na huyo rafiki yako, tumekuja kulifikiria hilo baadae, asubuhi, wakati mtu aliondoka usiku…’akasema‘Na kuondoka kwake, ni wachache walifahamu, mimi  nimekuja kugundua nilipofika kwake asubuhi, na kuambiwa na jirani yake kuwa keshaondoka, nikauliza wapi, akasema amesafiri kwenda ulaya kusoma,....nikashangaa, mbona sikuwa makini na tarehe yake ya kuondoka, ina maana ulikuwa hujui anaondoka lini?’ akaniuliza.‘Hapana kawahisha kuondoka, ilitakiwa akawie kidogo kwa ajili ya mtoto, sasa yeye akaamua kufuata tarehe ile ile ya awali,..tulikubaliana asubirie kidogo, na mimi nimekuwa kwenye wakati mgumu sikuwa makini kulifuatilia hilo…’nikasema‘Basi yote hutokea ili iwe sababu, nahisi sasa utaweza kumuelewa rafiki yako ni mtu wa namna gani, kama aliyoyafanya kayafanya kwa makusudio yake mwenyewe…’akasema hivyo na kauli hiyo ikanifanya nisinyae kidogo.‘Ok, labda,…ana sababu za kuwahi, basi angeliniambia.. ‘nikasema‘Hapo moja kwa moja kila mtu atafahamu kuwa kuna sababu, na kuna jambo kati yake na mume wako, ..na sijui baba yako atasemaje kuhusu hilo…sasa ni wewe kupambana na hili jambo ili mumeo aweza kupona, huu ni mtihani kwako…akasema‘Na wewe hujaongea naye, hata wewe hataki kuongea nawe…?’ nikamuuliza‘Hata mimi ….hataki hata kuniangalia machoni…’akasema‘Mimi siamini hilo, hata wewe rafiki yake, asiongee na wewe, akufiche mambo yake, usinitanie, nyie wawili, na sio wawili, nyie watatu, na huenda wa nne akawa mdogo wa mume wangu, nahisi nyie kuna jambo mumelifanya pamoja, na mnachokifanya ni kunizuga tu...mnanifanya mimi mtoto mdogo...’nikasema‘Sijui kitu kwakweli, niamini hilo nakuambia zaidi ya shuku shuku tu ….’akasema‘Mimi nawahakikishia kuwa nitaligundua hilo jambo mwenyewe, na ole wenu,...kama kuna jambo ambalo sio jema, sijui kama tutakuja kuongea, sitajali tena urafiki wetu, na huyo mume sijui,…’nikasema na kutulia.‘Tatizo lako wewe unapenda kuchukulia mambo kihasira...na hilo ndilo litakufanya usijue mengi, na hata ukijua utakuwa hufaidiki nalo,utakuwa umeshachelewa....’akasema‘Nimeshakuambia hivyo…’nikasema‘Nikuambie ukweli, mimi nimejitahidi kadri ya uwezo wangu, nifahamu ni nini kinachoendelea kati ya mume wako na rafiki yako, sijaweza kukifahamu....nimejaribu kumhoji mdogo wa mume wako, .....lakini na yeye anaonekana hafahamu lolote...’akasema.‘Mdogo wa mume wangu kasema hivyo, hafahamu kitu..?’ nikauliza kwa mshangao.‘Ndio kama tulivyopanga, kuwa nitaongea naye, nimeongea naye, nimetumia kila mbinu, lakini inaonekana hilo jambo, ni kama tulivyo sisi anahisi hisi tu, hana uhakika, na yupo kama wewe, anamtetea sana kaka yake kuwa hawezi kufany ajambo kama hilo, …’akasema‘Na hakukuambia kuwa zipo siku mume wangu  alilewa sana wakampeleka kwa rafiki yangu wakalala huko…?’ nikajikuta nimeongea kitu ambacho sikutakiwa kukiongea.‘Kwahiyo kumbe unafahamu ….’akasema‘Ilitokea, …akalewa, lakini nafahamu bado wangelilinda ndoa..’nikasema‘Watu wamelewa chakari, wakumbuke kulinda ndoa…hapo unanificha jambo….’akasema‘Kuondoka kwa rafiki yangu huyo bila kuniaga, kunanitia wasiwasi,..tangu siku ile nilipoongea naye, mara ya mwisho, kauli yake imekuwa kama ya kunidharau,kuna kauli zenye kujiamini zaidi, ....sasa sielewi, kuna nini kimemfanya awe hivyo....’nikasema.‘Je kwa mtizamo wako hadi hivi sasa huwezi kuhisi kuwa huenda rafiki yako alikuwa na mahusiano ya siri na mume wako?’ akaniuliza na mimi nikamjibu kw haraka.‘Kwa mantiki hiyo naona kuna dalili hizo, lakini nafsi na akili yangu bado ipo gizani, sawa nahisi hivyo..lakini ushahidi upo wapi, maana sitaki kuja kukosana na mume wangu wakati kweli hana kosa,..nielewe hapo, maana kama ni kweli …’hapo nikatulia.‘Ndio sasa uanze kufunguka masikio, nimekuwa nikijaribu kukueleza uelewe, ila sikutaka kukushinikiza kwa hilo..nimefanya hivyo , isije ikawa sio kweli ukanichukia kabisa, ukafikiria labda nina nia mbaya na ndoa yako au na urafiki wenu, natumai sasa upo na mimi,unaanza kuamini hilo, japokuwa hakuna uhakika wa moja kwa moja au sio, na usikimbilie kwenye kuvunja ndoa yako, hilo usiafanye kabisa, unasikia…?’ akaniuliza.‘Mimi nilikuwa nasubiria hiyio taarifa ya rafiki yangu, ndio niweze kuwa na maamuzi yangu, maamuzi yangu yapo moyoni, hata rafiki yangu halifahamu hilo, lakini yeye akaondoka kabla hajanikabidhi hiyo taarifa, maana yake ni nini…kanidharau, kwa vile kafahamu kuwa kanikosea, si ndio maana yake hiyo…sasa hiyo kazi  nitaifanya mimi mwenyewe ili nipate uhakika….’nikasema‘Oh, nimekumbuka, kuna taarifa , alisema itakuwa ofisini kwako, mezani kwako, ukifika utaikuta, ila alimuambia katibu muhutasi wako asikusumbue, maana unaumwa, na ukijua kuwa taarifa hiyo ipo tayari haraka utakimbilia  ofisini badala ya kusubiria upone vyema…’akasema‘Unasema…!!! Ina maana hiyo taarifa ipo tayari, hiyo kwangu ina muhimu sana inabidi ugeuze gari nifike ofisini kwanza, tafadhali geuza gari…’nikasema‘Tushakaribia hospitalini hatuwezi kugeuza gari tena hapa…na hata hivyo tukifanya hivyo, tutakuwa tumechelewa , tutakuta muda wa kuona wagonjwa umekwisha,..labda kama hutaki kumuona mume wako leo, …’akasema‘Oh….’nikaguna nikiangalia saa kumbe muda ulikuwa umekwenda sana‘Unasemaje maana tumeshafika, je unaiona hiyo taarifa ni muhimu kuliko mume wako….’akasema sasa akiingia eneo la hospitalini...************* Tulifika hospitalini, akili ikiwa imeshavurugwa,…hapa kwa upande mmoja natakiwa kuhakikisha mume wangu anapona, na ili hilo lifanikiwe, natakiwa nimeza machungu..nijifanye nipo sawa, lakini kwa upande mwingine baba ananishinikiza ili mume wangu aonekane mbaya, hafai hata kuongoza kampuni…na mpaka sasa nipo peke yangu, kwani mtu niliyekuwa nikimtegemea kwa kazi zangu nyingine ndio huyo kaondoka.Nilitulia kimiya bila kusema neno, hadi tunakaribia kuingia chumba alicholazwa mume wangu, na hadi muda huo nilikuwa namuwazia huyo rafiki yangu, sikuwa bado nimemuwaza kwa mabaya, kwa chuki, badi nilikuwa nimempa nafasi..hapo nilikuwa nawazia tu huenda nimemtendea vibaya rafiki yangu huyo.., huenda nimemkosea ndio maana kafanya hivyo.Hamuwezi kuamini jinsi gani nilikuwa nampenda huyo rafiki yangu, alikuwa ni kama ndugu yangu…na nilipofika hapo, nafsi ikaniuliza je ikiwa ni kweli katenda hayo yanayosemwa itakuwaje…oooh…kama ni kweli sijui kama nitaweza kuvumilia, sizani, na hata akimbie wapi…nitampata tu......atarudi, tutakutana au huko huko naweza kumtuma mtu..‘Nilijitahidi sana nimuone mtoto wa rafiki yako, lakini mpaka anaondoka, sikubahatika kumuona sura yake....’akasema docta na kunisthua kutoka kwenye dimbwi la mawazo...‘Sura ya mtoto wake ina umuhimu gani kwako…achana naye huyo bwana.., hana maana kabisa kwangu kaniuzi sana…’ nikasema.‘Ingenisaidia kuwa na uhakika kuhusu baba wa huyo mtoto...yeye alijitahidi sana kufanya siri hiyo iwe siri…, dunia hii haina siri, wengi wameshaanza kuongea …sasa jiulize watu wamejuaje kuwa mtoto wake anafanana sana na watoto wako...’akasema.‘Mhh, hata sijui …lakini hata hivyo hayo hayakuhusu au sio..labda uwe umetumwa na mtu fulani, na nafahamu kwanini unasema hivyo kuwa kama anafanana na watoto wangu basi mume wangu anahusika au sio..?’ nikamuuliza kimzaha.‘Kwahiyo kumbe ni kweli, kuwa mtoto wake anafanana na watoto wako, nataka uhakika tu…?!’ akauliza kwaa mshangao.‘Sijui mimi bwana, ....hata kama mtoto wake anafanana na watoto wangu, mbona watoto wakiwa wachanga wengi wanafafa tu, mimi hilo halinisumbui kichwa, na hata kama kanificha kumfahamu huyo bwana wake , mimi nitamfahamu kwa njia zangu nyingine...’nikasema‘Ina maana wewe hujaamini hilo…’akasema‘Nitaaminije hebu kaa kwenye nafasi yangu, jiulize ndugu yako anaweza kufanyakitu kama hicho, eeeh, sawa shuku kwenye nafsi zipo lakini nazishinda kwa kuweka hoja ya msingi, kuwa haiwezekani, yeye ni rafiki yangu, nimijitolea sana kwa ajili yake mpaka nimekosana na wazazi wake, hata huko kusoma ni juhudi zangu, je mtu kama huyo anaweza kunisaliti mimi…siamini..’nikasema‘Mhh, hatujui lakini, hatujui, maana hata mume wako hajaliweka wazi hilo…’akasema‘Mume wangu,…unajua mume wangu anamuheshimu sana huyo rafiki yangu, kuna kipindi aliniambia anavyomuheshimu anamuona kama mama mkwe…ndio uniambie mume wangu kafanya hivyo na rafiki yangu, hivi kweli inaingia akilini hapo, yaani siamini, siamini kabisa, hahaha, lakini lisemwalo lipo, na kama lipo, kutawaka moto, wewe subiria tu…..’nikasema.‘Unajua ..kwanini nawashuku, sio tabia yangu kushuku watu ovyo vila vidhibiti…kama mtoto wake anafanana na watoto wako, ina maana mtoto wake anafanana na mume wako au sio, tunaangalia nadharia…’akasema‘Mimi najua ipo siku tutathibitisha hili kivipimo, ila mimi nmefanya hivyo ili  lituame kwenye nafsi yako mapema, ili usije kulipokea kwa mshtuko baadae…, na nasema hivyo sio kwamba nafahamu kitu, unielewe hapo, hata mimi bado sijawa na uhakika ila nilidhania kuwa labda ni mipango yenu wawili, upendo wenu umefikia hapo..’ akasema na kauli hiyo ilinichefua, nikamwangalia bila kusema kitu, nikajitahdi kulimeza tu…nikajikuta nimesema hivi;‘Pia anafanana na mdogo wa mume wangu, mbona hilo hulisemi....’nikasema.‘Yawezekana pia… lakini  eeh, mdogo wa mume wako, angelianiambia, maana mengi yake ananiambia pia…alishaniambia jinsi gani alivyokuwa akimtaka huyo rafiki yako, na wakaishia kugombana, na tokea hapo wamekuwa hawaelewani , ni kusalimiana tu, sasa iweje leo,..lakini labda, kama alitaka mtoto na akaona haija jinsi amtumie yeey je..yawezekana pia…’ akasema.‘Kama sio yeye, basi huyo ndugu yake mwingine…’nikasema‘Kipindi kingi huyo ndugu yake mwingine amekuwa  hakai sana hapa Dar, ni mtu wa kutoka toka…na hana ukaribu sana na rafiki yako,…sizani kama anahusika hapo…, mtu wa kumshuku alikuwa huyu ambaye mara kwa mara wamekuwa yupo hapa ambaye hata mumeo akizidiwa ndiye humchukua kwenye gari kumrejesha nyumbani….’akasema.‘Mhh..labda hiyo ripoti ya rafiki yangu itasema kila kitu….natamani nipae ili nifike ofisini nione alichoandika,…niliitarajia sana, hata hivyo kwanini, asingeliniletea nyumbani, sawa hamna shida kama hiyo ipo tayari, hamna shida, kazi yangu kaimaliza kwahiyo namuombea kila la heri…’nikasema‘Kwahiyo upo radhi naye, umemsamehe….’akasema‘Nani …? Huyo rafiki yangu…? Kumsamehe kwa lipi, maana ni sawa na hilo la mume wangu kuwa nimsamehe tu, hata kosa hulijui…’nikasema‘Kama ni kweli,..’akasema docta‘Ohh..,  kama ni kweli mnavyosema nyie, kama kweli anahusikana na ….na…ushetani huo, siwezi kumsamehe…katu…na..na.., hata mume wangu kwa hilo,…kama ni kweli, wote wawili kwangu watakuwa maadui… naomba, naombea sana isiwe ni kweli, maana, ohh…. nita-nita-ua mtu, wewe utaona tu…kwanini lakini, this is too much….’nikasemaHapo docta akatulia, ..ukapita muda kidogo, halafu akasema;‘Sasa tunaenda kukutana na mume wako, jaribu kukunjua sura yako, usije ukamuonyesha mumeo hiyo sura ya hasira, ukikunja uso wako hivyo, unakuwa kama unataka kuua mtu kweli.., mume wako akikuona hivyo anaweza kuhisi umefahamu ukweli wote...’akasema‘Ukweli wote gani sasa, mpaka sasa sijafahamu kitu mimi, na nikifahamu,a kuthibitisha kuwa ni kweli,..hii sura itakuwa mara mbili, ok..ok..nahisi sipo vizuri....’ nikasema nikishika kichwa‘Hebu tulia kidogo, vuta pumzi, eeeh, yes, fanya tena, haya tulia, unajisikiaje sasa…’akawa anafanyisha mazoezi ya kuvuta pumzi, nikajisikia sawa. Alipoona nipo tayari,  yeye akatoka kwa haraka kwenye gari na kuja kunifungulia mlango, nilisita kutoka , nikijipima kama kweli nipo tayari kukutana na mume wangu, na nikikutana naye, kweli nitaweza kujizuia.‘Twende bwana, tumechelewa, hakikisha unaonyesha tabasamu,....usije ukamuonyesha mume wako  chuki yoyote na uwe makini kumjibu maswali kwa yake akikuuliza eeh…’akasema‘Maswali!!…hamna shida…’nikasema‘Kumbuka kupona kwake haraka inategemeana na wewe utakavyomtendea....kama hutaki mume wako apone haraka endelea kujenga sura ya chuki......utakuja kujilaumu mwenyewe, usije ukasema sikukukanya ...ni muhimu sana hili, mengine yapumzishe kwanza....’akasema .‘Sawa docta…’nikasema na mara simu yangu ikaita,..nilipoangalia nikaona ni baba ananipigia….NB: Niendelee....WAZO LA LEO: Wengi wetu tunafurahi kutendewa mema, kujali nafsi zetu kwanza na hasa tukiwa na shida, mara nyingi tunamuona mtenda wema huo ni mwema sana, hata kama kutenda kwake huko kunamgharimu.  Lakini pindi ikatokea kuwa wema huo, au kutendewa huo hakupo tena, ni aghalabu kukubali ukweli kuwa na mwenzako anastahiki kutendewa hivyo-hivyo, huenda naye kakwama na yeye  anastahiki kutendewa.  Tujitahidi sana kulipa wema kwa jema, ili baraka ziongezeke, na maisha ya kupendana yazidi kuwepo.Alikuwa ni baba….baba ananipigia simu…nikawa najiuliza kuna nini tena...kwa pale ilikuwa sio vizuri kupokea simu, labda nitoke nje, nikamuangalia docta, docta akawa haniangalii,...na simu ikaita mpaka ikaacha yenyewe... Haikuita tena...tulishaingia chumba alicholazwa mgonjwa na...nikawa nasita kidogo, na docta, akanigusa begani, nikageuka kumuangalia.. akaniashiria nisogee, nitembee kuelekea kule kwenye kitanda….alipolala mgonjwa.Mapigo ya damu yalikuwa yanakwenda kwa kasi, ni kama nina wasiwasi, au kuna kitu kinakuja kutokea, ...sijui kwanini niliwaza hivyo...Mume wangu alikuwa kalala kwenye kitanda huku akiwa kanyooka kabisa, na ilionekana kama kawekewa vyumba pembeni ili asitingishike,..lakini tofauti na ilivyokuwa mwanzo, safari hii kitanda kilikuwa kimeinuliwa kidogo, ili yeye kuweza kulala kama vile ameinuka sehemu ya begani na kichwani…Nikasogea,…nilimchunguza, nikagundua kuwa, shingoni alikuwa kavalishwa, plastiki la kuzuia shingo isicheze cheze, na jinsi alivyowekwa ni kama mtu kakaa mwenyewe kimtindo. Na pale alipokuwa kalazwa, aliweza kuangalia mlangoni, kwahiyo tulipoingia tu, alituona.Rafiki wa mume wangu yeye akawa kasimama, nilijua alifanya hivyo, ili kunifanya mimi nitangulie mbele yake, yeye akawa anakuja taratibu nyuma yangu, huku akinigusa kwenye mkono, kuniashiria kuwa nisogee pale alipokuwa mume wangu , na hata ilifikia hatua ya kuninong’oneza akisema;‘Nenda pale kitandani kamsalimie mume wako,....mpaka nikifundishe,..., na kumbuka niliyokushauri .....’ nikaelewa ana maana gani, nilisogea huku macho yangu yakiwa yanamwangalia mume wangu.Kwa pembeni karibu na ofisi ya docta, walisimama madakitari wawili wakihakikisha kila kitu kinakwenda salama, na mmoja wapo alikuwa dakitari wake bingwa wa maswala ya mifupa, alikuwa kashika makabrasha yake akimuelekeza msaidizi wake ni nini cha kufanya baada ya hapo....Mimi sikuwa na haja na watu hawo kwa muda huo, mawazo na akili  yangu ilikuwa kwa mume wangu, na macho yangu yalikuwa yamelekea pale alipo mume wangu, na nikawa namsogelea huku tumetizamana machoni.Macho yangu na ya mume wangu yakawa yanaangaliana, kwanza niliona usoni kama anashituka,au kama ananishangaa kuniona, na baadaye mdomoni akaonekana kutabasamu, lakini niliona kama tabasamu la kulazimisha,..lakini kadri tulivyokuwa tukimsogelea ndivyo lile tabasamu lilivyozidi kuongezeka, na sasa likawa tabasamu halisi, na alikuwa wa kwanza kutamka neno.‘Hatimaye mke wangu umefika...’akasema. Na kauli hii ilinifanye nigeuke kumwangalia rafiki wa mume wangu , ambaye alikuwa nyumba yangu kama vile wafanyavyo walinzi, nahisi aliogopa nisije nikaongea jambo lisilotakiwa kwa wakati huo.Kiukweli sikuwa nimependa jinsi anavyonifanya, nakuwa sina uhuru wa kuongea, lakini kwa namna nyingine niliona ni bora iwe hivyo, maana ananifahamu vyema, sina uvumilivu wa kumezea jambo, kama ni jambo la kuongewa, ni lazima litaongewa tu, sipendi kunyamaza nyamaza.Nilimwangalia mume wangu huku nikitabasamu , lile tabasamu la kimodo, ili tu mume wangu aone kuwa nampenda, namjali, na sina kinyongi naye, kwakweli kwa hali ilivyo, tabasamu hilo lilikuwa kama la kubandikwa mdomoni, lakini nilijitahidi kuliigiza ipasavyo…Nilipogeuka kumwangalia rafiki wa mume wangu, nilimuona naye akitabsamu, kama vile ananionyeshea kuwa na mimi nitabasamu hivyo hivyo,na akawa ananionyeshea ishara kuwa nisogee mbele karibu sana na mume wangu. Nami nikasogelea kile kitanda alicholala mume wangu , na kumuinamia..Kwa ujumla mume wangu alikuwa amepungua sana, na hali hii ya kupungua, kukonda ilianza kujitokeza hata kabla ya hili tatizo, na baada ya hili tukio, nimeona kapungua kwa haraka sana, hali hii imezidi kumfanya akonde zaidi, hata mashavu, yalishaonyesha kubonyea, moyoni nikasema akipona tu nitahakikisha mashavu yanakuwa dodo...ni lazima nimrejeshe kwenye hali yake ya kawaida....‘Nimefika mume wangu unaendeleaje?’ nikamuuliza nikiwa nimemkaribia, na kumuinamia nikambusu kwenye paji la uso, yeye akaguna kidogo na kusema;‘Mhh, hata sijui niseme nini, kuwa sijambo au naumwa, mwenyewe unaiona hi hali niliyo nayo, maana hapa nilipo ni kama nusu mfu, mwili wote sio wangu tena, kama unavyoona, mwili wote chini hauna kazi,ni kama sio mwili wangu,....’akasema akionyeshea kwa ishara.‘Utapona usijali..’nikaema‘Unajua, eti wanasema ni swala la muda, lakini kwa hali kama hiii ....dakika,saa , siku ni kama mwaka, nateseka sana mke wangu,sijui hii ndio adhabu yenyewe, mungu wangu nisamehe sana.., nimekosa, sitarudia tena.....’akawa anaongea na mimi nikawa namwangalia tu.Kiukweli macho yake yalionyesha huruma, na alivyokuwa akiongea, hata ingelikuwa nani angelimuonea  huruma, …pale nilipo huruma ilinishika, na  nilihis machozi yakianza kunijia, nikakumbuka maneno ya docta...‘Hakikisha humuonyeshi mume wako kuwa anaumwa sana, zuia kulia, jenga tabasamu la kumuonyesha kuwa hajambo...muonyeshe kuwa hali aliyo nayo ni ya kawaida tu...’‘Mume wangu mbona umeshapona tu, ..hatua uliyofikia ni kubwa sana, maana ukiona hilo gari lako lilivyoharibika, huwezi kuamini kuwa kuna mtu katoka hai, lakini mungu wako bado anakuhitajia uwepo dunia, sisi tunaokupenda tunakuhitajia sana..namshukuru mungu kuwa upo salama, na hali uliyo nayo ni ya kutia matumaini, cha muhimu ni kufuata masharti ya madakitari...’nikasema.‘Eti masharti ya dakitari,..masharti gani hayo, hapa nilipo nitafanya nini cha kuvunja hayo masharti, maana kama unavyoona mwili wenyewe hausogei, nitavunja msharti gani, kinachofanya kazi hapa ni akili tu...kuwaza tu, ..haya na huko kuwaza nitawezaje kujizuia, wakati nafahamu fika , kuwa haya yote yametokana na dhambi ....nimewakosea watu.’akasema na hapo nikageuka kumwangalia rafiki wa mume wangu, akanionyesha ishara ya kuwa makini.‘Mume wangu hakuna dhambi hapa duniani isiyoweza kusameheka,kama umetubu ..mimi nina imani kuwa kila binadamu anakosea, na wewe kama binadamu huwezi kujiaminisha moja kwa moja kuwa utaweza kutenda kila jambo sawasawa, ....kama ulitetereka, basi ..imetokea na huna jinsi nyingine, cha muhimu ni kujitahidi kutuliza kichwa chako na mawazo yako ukayaelekeza kwenye kupona, na wamesema kupona kwako itategemeana na wewe mwenyewe...’nikasema.‘Mmh, kupona kwangu itategemea na mimi mwenyewe, sijui kwa vipi,...na wakati nimeshakuambia nimewakosea nyie watu wangu, ..nimewakosea watu muhimu sana, katika maisha yangu..nimekukosea wewe mke wangu …nisamahe sana...’hapo akatulia kidogo, na nilipomwangalia machoni, niliona kama analengwa legwa na machozi, akasema;‘Mimi nimeshakusamahe  mume wangu…’nikasema‘Mke wangu umesema umenisamehe, kwanini ulikuwa huji kuniona mara kwa mara, maana hata kama nilikuwa sina kauli, siwezi kuongea, lakini nilikuwa naona kila kitu kinachotendeka…?’ akauliza na hapo ikabidi nigeuke kumuangalia docta.Docta aliniashiria niwe makini hapo, na kabla sijasema kitu, akaendelea kusema‘Unajua.., wote waliokuwa wakija nawaona, lakini wewe sikuweza kukuona, , nilikuona mara moja tu, siku ile...hali hii inanipa shida na kunifanya nisiamini kuwa kweli umenisamehe....hivi kweli umenisamehe mke wangu..?’akasema na alikuwa kama analalamika, na hali hiyo ikanifanya nigeuka kumwangalia tena rafiki wa mume wangu ambaye alijifanya kama haniangalii mimi, alikuwa akisoma kadi iliyokuwa imewekwa mezani.‘Mume wangu, mimi nilikuwa nafuata masharti ya madakitari, kwani wao waliniambia kuwa huhitajiki kusumbuliwa, na ilitakiwa usikutane na watu wengine zaidi ya madakitari wako, hadi zipite siku saba, ili uweze kutuliza kichwa chako... ni masharti niliyopewa mimi, na ndivyo nilivyofanya, sikutaka litokee jambo la kukufanya usipone haraka...’nikasema.‘Sio kweli, kama ni hivyo mbona rafiki yako wa karibu mara nyingi nilikuwa nikimuona akifika hapa...na aliniambia kuwa anaondoka na mtoto, kwenda kusoma, kwanini aondoke na mtoto bado mchanga, hivi nyie mna akili kweli...’akasema.‘Alifika akakuambia hivyo..?’ nikauliza nikionyesha mshangao.‘Ina maana wewe hujui kuwa keshaondoka, ...usinidanganye wakati wewe ndiye mfadhili wake, mimi sikuona umuhimu wa yeye kwenda kusoma kwa sasa, wakati ana mtoto mchanga,nilimshauri asubiria kwanza, lakini hakunisikiliza, nikajua mumepanga wote...’akasema.‘Haina shida, huko Ulaya unaweza kusoma na mtoto, unaweza kusomea nyumbani,...hilo lisikutie mashaka, anajua ni nini anachokifanya yeye sio mtoto mdogo....’nikasema.‘Kweli Ulaya ni ulaya, lakini mimi namuwazia sana mtoto, yule mtoto bado mchanga bwana, wewe hulioni hilo..yeye angelisubiria angalau miezi mitatu hivi, lakini haelezeki, htaaki kusikia, kaamua kaamua basi, rafiki yako mnajuana wenyewe,....’akasema.‘Yule niachie mimi, namfahamu sana, ni rafiki yangu, usiwe na shaka na yeye, alishaambiwa huko mtoto hatakuwa na shida, kila kitu wamemuandalia....’nikasema.‘Mimi sina shaka na yeye nina shaka na mtoto, mtoto yule bado mchanga, safari na hali ya hewa ya huko, mmh, mimi sijui....’akasema na kutulia, na baadaye akasema;‘Yeye alikuwa anakuja, anasimama pale mbele kwenye kiyoo, ananiangalia kwa muda halafu anaondoka, mimi nilikuwa namuona…’akasema na mimi nikageuka kuangalia kwenye hilo dirisha.‘Nikawa najiuliza kwanini haingii ndani  na mara ya mwisho nikaona niongee na dakitari ili aruhusiwe aingie, inaonyesha alikuwa ana hamu sana ya kuniona, ..rafiki yako ni mtu mnzuri, ila akiamua jambo, hapo humuelezi kitu, hajali tena hisia za wengine..’akasema‘Mhh, ndivyo alivyo…’nikasema maana naona imekuwa maongezi ni kuhusu huyo rafiki tu, sikutaka kumkatili.‘Ila kiukweli kauvunja moyo wangu…kuondoka na mtoto, unajua yule tumeishi naye, tunamjali sana, kwanini hukumshauri wewe…lakini sawa mwache aondoke, si atarudi,....’akasema Hapo nikawa nataka kuongea jambo,  kuuliza maswali, lakini nikaogopa, nikaona nikae kimiya,maana nilipomwangalia rafiki wa mume wangu ambaye alikuwa kwa mbele, eneo la kichwani kwa mgonjwa, na alikuwa akiniangalai moja kwa moja ninavyoongea, akaniashiria nisiseme neno.‘Mke wangu, mimi inanipa shida sana naona kama wewe hujanisamehe kiukweli, na nilikuambia ukinisamehe nahis hivyo,..siku ile kweli ulitamka na ilionekana hivyo, ila kila hatua nahisi kama hujanisamehe..’akasema‘Kwanini unasema hivyo mume wangu..?’ nikauliza‘Kama hujanisamehe sizani kama mimi nitakuwa na amani, na huenda nikarudi kuzimu , unajua nilikufa…ni maombezi tu, kuwa nirudi ili nimalizie toba, nihakikishe kuwa kila kitu kipo sawa…sasa kwa hali kama hiyo, sioni umuhimu wa haya yote...’akasema na mimi hapo nikashindwa kuvumilia nikajikuta nimetamka neno ambalo lilimfanya rafiki wa mume wangu kuniangalia kwa sura ya kunisuta;‘Mume wangu mbona hujafanya kosa, kwani kuna kosa gani kubwa la kukufanya usononeke kiasi hicho...nimeshakuambia kuwa nimekusamehe, japokuwa sijui kosa gani ulilolifanya...’nikasema na nikaona akishtuka, na kunikazia macho, nikaona kama anabadilika.Docta rafiki , akahisi kwa haraka akatoka kule alipokuwa kasimama na kunisogelea, sikuwa nimemuona, hadi pale aliponishika mkono, nilipogeuka nikamuona yeye akinionyesha ishara ya kuwa makini.‘Mhh, mke wangu…unasema nini, ..ndio maana nilikuwa na wasiwasi sana, mungu wangu, ina maana kweli hujui kosa lako ni nini…mmmh,… hapana usinichekeshe,..ina maana kweli kosa lenyewe hulijui, halafu umekubali kunisamehe ..haah , kwahiyo ulikuwa wanichezea shere, unaigiza tu, nilijua tu…’akasema‘Mume wangu mimi najua , kuwa umenikosea kwa yale mambo yetu ya nyumbani, unakwenda unakunywa, unakutana na wanawake huko..sasa sijui huko mnamalizana vipi, hiyo ni siri yako,..kama ni hivyo, basi  mimi nimekusamehe ilimradi umefahamu kosa lako ni nini, ila sipendi kujua zaidi kama, ulipitiliza utajua wewe na mungu wako, ila mimi nimekusamahe, ni wapiti njia au sio..…’nikasema‘Oh…kumbe hata kosa lenyewe unasema hulijui, hapana sio wapiti njia, mimi sikuwa na tabia hiyo…mimi nazungumzia kosa hilo jingine…kwahiyo sio kweli, niambie ukweli..., au unajifanya tu kuwa hulijui kosa langu, kwa vile kuna watu hapa, huyu ni rafiki yangu tu…’akasema akimuonyeshea docta.‘Mume wangu haina haja, yamepita basi…’nikasema‘Hayajapita, ni lazima unisamehe kiukweli,  je hujaongea na mwenzako, mkakubaliana jambo..au kwa vile hayupo leo hapa,…najua angelikuwepo hapa ingelikuwa ni bora zaidi, ili alithibitishe hilo…lakini si atakuja tu, nitahakikisha anaongea kila kitu, hata hivyo mimi sina muda, sijui muda wangu..maisha haya hayana muamala..nataka niutue huu mzigo...’akasema na kutulia.‘Mume wangu mimi nimekusamehe, na kwangu afya yako ni bora kuliko, hayo ya kupita tu, amini kuwa nimekusamehe, nisingelipenda kujua mengine zaidi, inatosha, unanisikia, wewe tuliza moyo wako ili upone haraka…’nikasema‘Hapana mimi nataka kauli yako, nijue ukweli wako, je ni kweli kuwa hulifahamu hilo kosa,… aah..pumzi inakata kwanini docta…ni lazima niliongee hili  leo hii,…niambie ni kwanini usilifahamu wakati wewe ndiye uliyemtuma kwangu ..?’ akauliza‘Kumtuma nani…?’ nikauliza na docta akaniashiria nikubali tu.‘Rafiki yako…’akasema‘Rafiki yangu …ok, ndio, mara nyingi namtuma…alikuambiaje…’nikasema Hapo mgonjwa, akatulia akionyesha kama anawaza jambo halafu nikaona kama anabadilika, anapata taabu ya hewa kitu kama hicho, mimi niligeuka kumuangalia docta, na docta wakati huo alikuwa anashughulika na kitu kingine.Nikageuka tena kumuangalia mume wangu, akawa yupo sawa, …ila ni kama anajilazimisha,…akasema‘Siamini kama hujui kosa langu,..nilijua tu , hukupenda, lakini unajua tena ulevi..na hapo imekuwa sababu ya madhambi mengi tu….ooh, kwanini hii hali haitulii, niongee na mke wangu…’akasema akijaribu kuinua kichwa kumuangalia docta, na docta akamsogelea na kusema;‘Kama hujisikii vizuri usijilazimishe…’akasema docta‘Usiniingilie haya docta,..hata kwangu ni mhimu kwangu kuliko chochote,..huenda nisipate muda tena…’akasema akimuangalia docta. Na docta akawa kama anataka kumzuia asiendeleee kuongea lakini hakuweza, akaniangalia mimi huku akionyesha wasiwasi, na kwa muda ule, mume wangu alikuwa akihangaika kama hewa inamuwia ndogo, lakini aliendelea kuongea.‘Mke wangu, unafikiri mimi nilipenda kufanya hivyo, ilikuwa kazi kubwa sana kukubali hayo…, na nilikubali tu kilevi levi, lakini moyo haukutaka, na ni kwa vile ni rafiki yako, na ni kwa vile kasema mliongea naye ukakubaliana ila iwe siri,..hapo ukichanganya na ulevi, nikajikuta nimeingia kwenye mtego, ningelifanyaje hapo mke wangu nakiri kuwa ni kosa maana sikutaka kuhakiki kutoka kwako…’akatulia huku anaonekana anapata shida‘Docta….’nikasema‘Achana na …na huyo do-docta nisikilize mimi..unasikia , nisikilize mimi mumeo…’akasema, na mimi nikamuangalia, ndio akaendelea kuongea. ‘Ulevi, mawazo..na kauli yake, ikanihadaa…unasikia, nasema haya kiukweli…nisamahe tu, najua nimekosea sana, kwani sheria ya ndoa inanibana,…’akasema na nikaona akizidi kuhangaika.‘Mhh…sikupenda mke wangu…ndio maana najuta sana, inaniuma sana, sijawahi na sikutarajia kufanya hilo, nimekuwa mwaminifu kwako mke wangu, wengi wakiniona nipo na mwanamke wanafikiri vibaya, lakini napoteza nao mawazo tu…’akasema na kukokhoa, halafu akatulia na nilitaka niongee lakini akaanza kuongea yeye.‘Rafiki yako, ananiliwaza, tunaongea ananipa faraja, nikamzoea hivyo, lakini sikuwa na nia mbaya kwake…ila siku , oooh,…ikatokea , hata sijui ilikuwaje, nashindwa kuelezea, kauli yake ikaniponza,, yaani inaniuma sana, nilishindwa mke wangu, nikiri kuwa , ooh, nilitaka m-tttt.ooh wa-waaah, aaah..’akashindwa kuendelea na hapo rafiki wa mume wangu alifika na kumuinamia akamwambia;‘Rafiki yangu acha kuongeza zaidi, mke wako ameshakuelewa, hukukusudia kabisa kujiingiza kwenye dhambi hizo, ulishawishika vibaya, kama ulivyosema, unakumbuka nilivyokuambia, acha kabisa kuongea hayo mambo....ni kosa na kama ni kosa limeshafanyika, ...basi’akasema…kukawa kimia, mimi nilikuwa mwili umekufa ganziMuda kidogo,akafunua mdomo na kusema;‘Mke wangu hana kosa,…wewe huna kosa nisitoe kisingizio kuwa kwa vile..hapana, maana muda wote najizuia,…lakini  rafiki yaka…alichosema, kilikuja kipindi kibaya nikiwa sijitambui…kwahiyo kwa hali kama ile, basi ikawa hivyo, kwahiyo, nisamehe tu mke wangu….’akasemaDocta akamwambia;-‘Basi keshaelewa, tulia, sasa lala..au unataka ulazimishwe kulala kwa madawa…’akaambiwa, mimi kiukweli akili ilikuwa sio yangu, nilikuwa kama naota ..‘Sogea pe-pembeni bwana,.. mimi nataka kuongea na mke wangu…nisipoongea leo, sitaongea tena, unanielewa, nilifunga kuongea, nikiwaza mengi, nikutubu, nikiwazia ya huyo rafiki yake, hataki kunisikiliza…sasa nipo peke yangu ni bora kufa tu, maana sitaeleweka, nakutegemea wewe mke wangu, basi…baba yako, hatanisikia, kampuni,…hata sielewi, ..’akasema. Na hapo docta akageuka kule walipo madocta, nahisi alitaka kuwaashiria kitu , lakini wale madocta walikuwa wameinama wakiangalia kitu mezani.‘Mke wangu unanifahamu sana, wakati wote nimekuwa nawajibika, nimekuwa mwaminifu kwa kazi, tukirudi nyumba wewe na laptop na mimi na laptop, hao ndio wapenzi wetu, haahaa…ni hivyo, basi mimi nikaongeza pombe, kumbe …ndio imenifikisha hapa…’akatuliaPale nilipo najaribu kufunua mdomo lakini siwezi, nimebakia kimwili tu…na yeye akaendelea kuongea;‘Mhh..sa-sa.., japokuwa wakati mwingine nateseka kama binadamu wa kawaida, unatamani kitu, unataka mtoto…..unajua tena…inabidi uvumilie, ndoa ni ndoa..mke yupo, lakini utafanyaje, nisingeliweza kumlazimisha mke wangu…’akasema na hap akawa kama anaongeza kitu kichwani mwangu, natamani nianza kuonega kwa jaziba, lakini siwezi.‘Mke wangu ….kiukweli sikupenda, maana nakupenda sana mke wangu, na sikutaka kukuumiza mke wangu, japkuwa nilikuwa naumia, natamani, ndio nikaanza kulewa, kulewa ikawa ni shida, maana ndio imefanya akili ikaharibika…ila simlaumu mtu, aah, najilaumu mwenyewe dhambi ni zangu, usiponisamehe, basi acha nikaangamie, unasikia, nisimlaumu mtu, kabisa....’akasema‘Mume wangu inatosha, sawa nimekuelewa, inatosha, mimi nimekosa, samahani kwa hilo sitarudia tena sikujua kuwa nakuumiza hivyo, nisamehe mume wangu, oh…ina maana haah, basi, ..hata, basi, hata..sielewi, inatosha mume wangu, basi …’hapo sikuweza kujizuia, nikaanza kulia.‘M-mke -wangu, usilie….najua hujakosea, sikiliza…’akawa anahangaika kutaka kama kuinuka hawezi..‘Ohoo, unafanya nini sasa wewe, utamuua mume wako, nilikuambia nini..’akasema docta akijaribu sasa kufanya lolote kuidhibiti ile hali‘Mke wangu…mke wangu nisamahe tu…nimeongea hayo kukuonyesha kuwa sikutaka..ila nili..zidiwa, na kwa vile alisema mlikubaliana, upo radhi..basi, …’akatulia‘Tulikubaliana nini..…’ hapo nikasema kwa ukali, mpaka docta akashtuka na kuniangalia kwa macho yasiyoaamini,..haraka akanishika mdomoni nisiendelee kuongea.‘Ndio..alisema hivyo..ndio maana nikashindwa,...nikashindwa,....najuta sana kukubali kufanya hivyo , kwanini nilishindwa kujizuia,mbona wakati wote niliweza , kwanini safari ile nikashidwa ...nimeumia sana,…nisamehe sana mke …mke…tamka neno kuwa umenisamehe, niwe huru na mateso haya, aah, aah, aah,….. ’ madocta wakawa wameshafika;‘Nini tena, hebu,..hebu….’nikasukumwa pembeni, maana pale nilipo sikuweza hata kuinua mguu.‘Sogea, sogea, basi hatuwezi kumruhusu kuongea tena, ni vyema ukatoka nje, ...ngoja tumpe dawa,  anahitajia kupumzika....’akasemaHapo ndio nikagundua kuwa nimeharibu, nimeshindwa kuvumilia, kama alivyonitaka docta, badala ya kujenga nimebomoa, nikajua sasa nimeua…mume wangu akawa bado anajitahidi kuongea, nikasikia akilalamika,‘Mbona sijamalizana na  mke wangu, sijamwambia, nilichotaka kumwambia...nipeni dakika mbili niongee na mke wanguuu-uh...’akasema mume wangu, lakini maneno yake hayo ya mwisho yalikuwa kama ya mtu aliyelewa, na akatulia, kumbe kuna dawa waliipitishia kwenye mpira, ilikuwa dawa ya usingizi....‘Mbona inachelewa….’akasema docta akiwa na maana ile dawa ya kumfanya alale imechelewa kufanya kazi‘Mungu wangu nimefanya nini....’nikajikuta nimesema  hivyo, nikijua kuwa nilishindwa aliyoniambia rafiki wa mume wangu  nikageuka kumwangalia rafiki wa mume wangu, ambaye alikuwa akibenua mdomo, kuashiria kuwa hakuna tatizo.Nikageuka kumwangalia mume wangu ambaye alikuwa keshafumba macho, na madaktari walikuwa wakiendelea kumkagua, na hapo kichwani nikaanza kukumbuka maneno yake, maana muda ule wakati anaongea kuna muda akili ilikuwa kama imeganda, sasa maneno yanaanza kujirejea kichwani;‘Mke wangu, unafikiri mimi nilipenda kufanya hivyo, ilikuwa kazi kubwa sana kukubali,...kwa vile ni rafiki yako, na kwa vile kasema wewe ndiye uliyemtuma,‘Oh, mungu wangu…’nikajikuta nimesema hivyoMimi ndiye niliyemtuma, ..aka-aka…sio hivyo, hatukukubaliana hivyo, kwa mume wangu hapana, hili halipo, kwa shameji yake, nimtume mimi, haiwezekani, sio kweli , sio kweli, labda kama …rafiki yangu aliamua kutumia kauli hiyo kutimiza malengo yake…lakini haiwezekani sio rafiki yangu…‘Au mume wangu hana maana hiyo, labda ana maana ya jambo jingine labda sio hivyo, mungu wangu, mungu wangu sio kweli jamani…’maneno hayo nikayasema kwa sauti , na docta akayasikia, lakini wenzake walikuwa wakihangaika na mgonjwa..Docta akaniashiria nitulie…hutaamini bado nilikuwa sijaweza kuinua mguu, nipo pale niliposukumiwa na wale madocta, …miguu haiana nguvuNa muda huo nahisi kama kuna vitu vimeingia kichwani, maneno ya mume wangu yanajirudia rudia kichwani;‘Mke wangu unanifahamu sana, wakati wote nimekuwa nawajibika, nimekuwa mwaminifu kwako na kazi yangu,nimekuwa nikijizuia kutenda dhambi yoyote, japokuwa wakati mwingine nateseka kama binadamu wa kawaida...‘Oh…mbona sielewi, kuna nini hapa, ina maana ni kweli,…’nikasema kwa suti ndogo, kama namnong’oneza mtu..‘Sio kweli, kachanganyikiwa tu mgonjwa sio kweli…’nikasema sasa kwa sauti, mpaka wote pale ndani  wakageuka kuniangalia mimi.Docta akanisogelea na aliponiangalia tu, akagundua kuwa nimeshabadilika na muda wowote naweza kudondoka, ..akanishikilia nikaona anamuashiria docta mwingine aje kusaidia..akawa anamuagiza kitu, sikuelewa ni kitu gani.‘Ina maana ni kweli, aaah, hapana sio kweli jamani …docta niambie kuwa sio kweli..hana maana hiyo kabisa, eti docta ni kweli jamani...?’nikasema huku nashikilia kifuani, kiukweli pale nilihisi maumivu makali yalikuwa upande wa kushoto…nipo kama nimechanganyikiwa.‘Mke -wangu,wakati mwingine kama binadamu wa kawaida natamani nitende dhambi, lakini najizuia, naogopa, ...lakini safari ile nikashindwa,...nikashindwa,....najuta sana kukubali kufanya hivyo , kwanini nilishindwa kujizuia,mbona wakati wote niliweza , kwanini safari ile nikashindwa....’Maneno hayo yalijirudia rudia kichwani...yakanifanya niishiwe nguvu kabisa, kama isingelikuwa ni docta ningedondokea sakafuni, ..‘Inatosha...haina haja, kumpiga sindano.’akasema docta akimwambia mwenzake sikujua ana maana gani, na mimi nikawa naongea tu..‘Umefanya nini na mume wangu, ...mumefanya dhambi gani wewe na rafiki yangu, ina maana ni kweli ..ina maana ni kweli…hapana sio kweli jamani haiwezekani kabisa,…Nikamwamgalia mume wangu ambaye wakati huo alikuwa katulia, kalala, na akili yangu pale ikanituma kuwa keshafariki…sijui kwanini niliwaza vile…;‘Ina maana nimeongea vibaya, nimemuua mume wangu. Mume wangu usife nataka niusikie ukweli wote, jamani…sio kweli jamani, sio kweli, kwanini hivi jamani..mume wangu usife uje uniambie ni kwanini..’ sasa nikawa naongea kama mtu aliyechanganyikiwa..‘Hajafa, tulia, …ukiendelea kuongea hivyo ndio utamuua…’akasema docta...na muda ule akawaashiria kitu, na mara nikahis sindani ikipigwa..haikuchukua muda,  giza litanda usoni…lakini kabla sijafunga macho mlangoni nilimuona baba akiwa kasimama, kama anasubiria kuambiwa aiingie, sijui alifika muda gani ….WAZO LA LEO: Mambo yakijirudia sana mwishowe  watu huja huamini, hata kama ilikuwa sio kweli. Ndivyo akili zetu zilivyo., ni wachache sana wanaoweza kusubiria hadi ukweli uwe bayana hasa kwa mambo yanayokwanza mioyo yetu. Tunaweza kujiaminisha kuwa ni kweli, kwa vile tu linaongelewa sana, kwa vile tu mtu mashuhuri kalisema, nk..lakini hatujiuliza kwanza, je ni kweli, je kama sio kweli itakuwaje, na tujiulize hivyo huku tukifanya tafiti yakinifu…bora ya kuwa na subira kuamini jambo huku ukitafuta ukweli kuliko kukimbilia kuamini halafu ije kuwa sio kweli..Siku kadhaa zikapita na mume wangu akatakiwa kurejeshwa nyumbani, na kabla ya kurejeshwa nyumbani, docta aliyekuwa akimuhudumia, akaniita ofisini kwake, na kunishauri mambo mengi ili kuhakikisha mume wangu anaondoka kwenye hatari na kupona mapema.'Unasikia wewe ni mke wake, na mtu muhimu kwake, wewe ndiye utamfanya apone haraka au....unasikia, muhimu tena sana,jitahidi kuwa karibu sana na mume wangu, na kukwepa kauli yoyote ya kumkwaza...unasikia...'akasema docta akinisisitiza hilo sana'Nakusikia docta...'nikasema'Mume wako, yupo kwenye hali ambayo akipata mshtuko tu inaweza kuzua tatizo kubwa ambalo litamfanya ashindwe kutembea kabisa....na ukijitahidi akawa hana mawazo, mazoezi...na kufuta masharti nilikuambia awali, ...atapona haraka tu...'akasema docta‘Sawa docta mimi nitajitahidi kadri ya uwezo wangu, maana huyo ni mume wangu, sina jinsi…ila nimegundua kitu, hivi sasa ni mbishi sana, na  ubishi huu hakuwa nao , nahisi  umeanza baada ya hili tatizo, kila kitu anataka nimsikilize yeye tu, sasa sijui nikiwa naye huko nyumbani itakuwaje...’nikasema.‘Ndio hivyo, jitahidi uwezevyo, kama kweli unamjali mume wako na unataka apone haraka, basi acha kila kitu kwa ajili ya mume wako …’akasema docta'Sawa docta...'nikasemaKabla ya kuondoka hapo hospitalini baba akanipigia simu, baba siku hizi amekuwa kila mara akinipigia simu , hasa baada ya kushuhudia  nikipoteza fahamu hapo hospitalini, tukio hilo limemfanya awe karibu na mimi, kuliko alivyokuwa baada ya mimi kuolewa..;‘Vipi hali yako na ya mume wako…?’ akaniuliza‘Hajambo jambo, kama walivyokuwa wamesema leo tunaweza kuondoka naye…hapa tu, tupo nje tunataka kuondoka kurudi nyumbani..’nikasema‘Ok, vizuri…sasa ok, naaah, umefikiriaje wazo langu..?’ akaniuliza kwa lugha ya upole, sio tabia ya baba akiongea na mimi, hasa nilipolazimisha kuolewa na mume ambaye hawamtaki.‘Baba mengine yasubirie kwanza, ngoja nibebe hili jukumu la mume wangu maana nimejitakia  mwenyewe, na sihitajii msaada kwenu baba, nitajimudu mwenyewe…’nikasema‘Usiwe mkaidi kwa hilo, hilo ni tatizo kubwa sana, kama unafikia kupoteza fahamu, sio kitu kidogo hicho, sisi wazazi wako hatuwezi kukaa kimia, na mama yako atakuja akae nawewe, tuone jinsi gani ya kukusaidia, unasikia…’akasema‘Baba hapana, mama mwenyewe mbovu, tutazidi kumchosha tu bure, nakuomba hilo liacheni kama lilivyo, ikibidi nitawaambia…’nikasemaKila nikiombea na baba ni lazima akimbilie kwenye lawama, akasema;‘Nilishakuambia huyo mwanaume hakufai, atakuhangaisha mwishowe atakuepeleka  kubaya, utaumwa, unaweza hata kupooza mwili, mwishowe  utaingia kaburini, wenzako wanastarehe..kitu ambacho kinatuuma sana sisi wazazi wako...'akasema'Baba...'nikataka kujitetea lakini hakunipa nafasi akaendelea kuongea'Nikuambie ukweli mume wako halijali hilo, la afya yako,... yeye anachojali ni masilahi yake tu, na anataka akukamue mpaka basi,..na sasa hivi utayaona  hayo, hatukuombei mabaya, lakini yale tuliyowahi kuyasema sasa utaanza kuyaona kwa macho yako,..huyo mume wako atakusumbua sana...'akasema'Baba lakini ni mume wangu...'nikasema'Sawa..ni mume wako,....ngoja tuone itakavyokuwa,….ila ukikwama usiache kutuambia, mimi nitajitahidi kufika kwako mara kwa mara, kulifuatilia hili mimi mwenyewe…’akasema‘Baba nashukuruni kwa kunijali, lakini nakuomba usisumbuke sana kwa ajili ya hili, sasa hivi mume wangu anaumwa, na naona akikuona wewe anakuwa hana amani, kwa hivi sasa, anahitajia, huruma, na baba sio kwamba sitaki ufike, ila ukifika naomba sana baba usije kuzungumza maneno ya kumweka kwenye wakati mgumu, ongea naye maneno ya kumfariji, asiogope, kama alivyotushauri docta...’nikajaribu kumtetea.'Hilo sio la kunifundisha, nafahamu sana,...muda utafika nitapambana naye, sio sasa..usiwe na wasiwasi kwa hilo...'akasema'Nashukuru sana baba...'nikasema‘Ila kuna kitu nataka uniambie, siku ile nilipofika hospitalini nilisikia akiongea maneno, kama anakuomba msamaha, na akasema kitu kama  wewe ulikuwa humjali kitu kama hicho, sikusikia vyema, alikuwa akiongea nini..?’ baba akauliza‘Baba , ....mgonjwa alikuwa anaongea hivyo ni katika hali ya kuchanganyikiwa tu, kwasababu ya huko kuumwa, yeye alijiona kama ni mtu wa kufa tu, kwahiyo ndio akawa anajaribu kujitakasa, akihisi hili kakosea, basi anaomba msamaha, hata wewe ungelikuwepo angalikuomba msamaha ni katika kuhangaika tu baba…’ nilisema sikuelewa baba alisikia kiasi gani, na docta akawa anaongea baadae akasema‘Vyovyote iwavyo mimi  nataka maelezo,..najua kakuoa akiwa na malengo yake binafsi,..yeye kama hawezi kuishi na binti yangu labda ana mipango yake mingine au alikuwa na ndoto zake nyingine , basi awe muwazi tu, nimegundua mambo mengi ambayo hayafai kwa familia yangu…’akasema‘Baba mengine ni ya kuharibu bora tuyapuuze tu..’nikasema‘Sikiliza…anyway,a sitaki nikuumize kwa mawazo, hayo ni yake anatakiwa kuwajibika nayo, sasa.. ngoja apone, sawa poleni sana binti yangu, usijali mimi nitapambana na hili jambo mpaka nione mwisho wake, unasikia, usijali, nipo pamoja na wewe,  …’akawa anaongea hivyona kipindi hicho ndio nimepata fahamu.‘Baba, usiwazie hivyo…mengine yametokea tu, ile iwe sababu ,  mimi nina imani yatakwisha tu, ni sehemu ya changamoto za maisha, sasa nyie kama wazazi wangu sitaki mnitenge mimi tofauti na mume wangu, ….sipendi hivyo baba…’nikasema‘Binti yangu usione nasema hivyo, sisi wazazi wako tunakupenda sana, lakini tunaumia, tunajitahidi kadri tuwezavyo ili uondokane na shida hizi, lakini wewe unakuwa mkaidi, sisi tunafahamu tatizo lipo wapi, hich ni kizalia , asili ya hulka ya mtu, hutaweza kumbadili mume wako, abadani…’akasema na mimi nikataka kuongea lakini hakunipa nafasi, akasema‘Mengi tunayaona lakini hatusemi, lakini kwa hili, hapa lilipofikia, sisi kama wazazi tutalifuatilia mpaka tuone mwisho wake ni nini, ina maana gani ya ndoa eeh, niambie…, na kama nilivyosema awali, sitaki kashfa katika familia yangu…, na  anyway, wewe angalia afya yako, unasikia, kama kuna lolote linahitajika niambie….’alisema . Na leo ndio akanipigia simu akitaka kujua mimi nimefikia wapi, kwani anahitajika kutoa maamuzi kwenye kikao cha wakurugenzi, ..anasema hicho kikao ni muhimu  , hata kama mimi sitakuwepo au mume wangu, maamuzi ya wengi yataheshimiwa.‘Baba mimi naomba usifanye lolote kwenye kampuni ya mume wangu, utoe hija kuwa kwa upande wa hiyo kampuni tusubirie kwanza, …itakuwa sio vyema, hata kama inafirisika, …na madeni yabakie tu, kama wadaiwa wanataka kushitaki waache tu wafanye hivyo, tutapambana huko mahakamani…’nikasema‘Sio rahis hivyo binti yangu…mimi kama mwenyekiti wa makampuni yote, siwezi kukubali hali hiyo ifikie huko, kuna wakurugenzi wa hisa kwenye hiyo kampuni, wananihoji,…wamewekeza pia huko, unataka niwaambieje…wewe sikiliza, wewe endelea na mume wako, mengine niachie mimi, ninajua ni nini cha kufanya, unasikia eeh,…tuliza kichwa chako, ila mume wako akipona nataka nipambane naye mimi mwenyewe, …hilo sitaki majadala…’akasema‘Baba…’nikalalamika‘Kwahiyo leo mimi sitakuja huko , nitakuwa na kikao, na nitakuwa napitia taarifa za uchunguzi, kuhusu mume wako, kuna mengi yamegundulikana, lakini mengine sitaki yawepo kwenye hiyo taarifa, ni aibu, uliweza kuisoma ile taarifa niliyowahi kukupatia ile kila kitu kipo, na mengi ambayo siamini...hebu nikuulize kwanza huyo rafiki yako kwanini kasafiri na mtoto mchanga..?’ akaniuliza‘Ilibidi afanye hivyo kwa vile muhula wa masomo umeanzia hapo, na hakutaka kusubiria, tukaona ni bora tu aende….na huko kuna watu watamsaidia hatapata shida…’nikaongea kujifanya na mimi nimehusika kwenye maamuzi ya rafiki yangu kuondoka.‘Una uhakika,…??... sio kuwa kakimbia,…?? anaogopa ukweli ukija kugundulikana awe keshajipanga vyema kimaisha, binti yangu hao watu wanakutumia vibaya, huyo rafiki yako, anataka ahakikishe hata likitokea jambo awe anajiweza mwenyewe..sawa sio mbaya, lakini kwanini aharibu nyumba iliyombeba..’akasema‘Baba hayo mengine hata sitaki kuyafikiria kwanza,…’nikasema‘Sawa sawa, usijali…nitapambana na hao watu mimi mwenyewe, ilimradi…’akasema na kukata simu.**********Mume wangu akawa hataki mimi niondoke karibu yake , ikawa ni kero, ina maana nisitoke au kwenda mbali na yeye, hata akija mgeni, anataka atoke awe pembeni nikiongea na mgeni,..kwa maagizo ya docta nikawa nafanya kila atakavyo, ila moyoni, pamoja na huruma kila nikiwazia hayo yanayosemwa nilimuona mume wangu kama sio yule ninayemfahamu. Nilitaka niwe na nafasi ya kuipata ile taarifa aliyotayarisha rafiki yangu, lakini sikutakiwa nisome mbele ya mume wangu,..ikafika muda nikaagiza niletewe  hiyo taarifa nyumbani,…lakini muda gani wa kuisoma nikawa sina,Ikatokea siku moja mume wangu amelala kutokana na madawa nilikuja kugundua akinywa hizo dawa anaweza kulala hata saa nzima au zaidi..na siku hiyo ilipoletwa hiyoo taarifa ya rafiki yangu, nikaona nitumie huo mwanya..., ndio nikaanza  kuipitia hiyo taarifa ni ndefu kidogo...;Taarifa ya uchunguzi wa ajali ya mume wangu, aliandika jina la mume wangu, na akaelezea ilivyotokea, kuwa ni sababu ya mwendo kasi, katika kukata kona akakutana uso kwa uso na lori,..akajaribu kulikwepa, na gari likapinduka na kugeuka mara mbili…Dereva aliwahi kutoka, hapo haijulikani aliwezaje kutoka katika hali hiyo, ni kwa uwezo wa mungu tu.Je kipindi ajali hiyo inatokea mlengwa alikuwa katokea wapi, taarifa inasema alitokea kazini, akapitia sehemu za wateja wake, ndivyo alivyoaga kazini, lakini akiwa kwa wateja wake, akaamua kwenda sehemu nyingine …(yawezekana,) akaandika hivyo na kuzungushia hayo maneno,...Kuna kauli za watu kuwa kwa muda huo ndio alimua kwenda kumuona mzazi,  huyo mzazi ni nani, (bado sijamtambua)!. Hili la mzazi halina uzito, ila limetokana na maelezo ya siku kadhaa nyuma kuwa aliondoka kazini akisema anakwenda kumuona mzazi, hospitalini, huyo mzazi hospitalini hakuweza kugundulikana ni nani..(kwahiyo ili kupata jibu kamili, aulizwe yeye mwenyewe)!'Ssshti...'nikajikuta nikisema hivyo.Kabla hajapatwa na ajali, gari lilisimamishwa kwenye geraji, sehemu ambayo pia panaoshwa magari kwa pembeni yake..., na wakati gari lake linafanyiwa usafi, yeye alikwenda mgahawani, kupata chochote,..lakini hakunywa kilevi…akiwa hapo, inaonekana alipokea simu , ya haraka, na kutoka hapo akaenda kulichukua gari kuwa muosha magari,Muosha magari anasema ni kweli, aliwahi kuosha gari la mtu huyo, na ...hata la mdogo wake, na anachokumbuka, yeye, mlengwa,  aliondoka hapo  kwa mwendo wa kasi, lakini sio kasi kubwa, kama ilivyokuwa huko alipopatia ajali... ila alionekana ana haraka, hata chenji ya pesa yake hakuichukua.Kwahiyo hapo akahitimisha kuwa,.simu aliyopigiwa inaonyesha ilikuwa na jambo, la kumfanya aharakishe kufika nyumbani na sivyo kama watu wanavyosema kuwa huenda alikuwa akikimbia jambo la hatari, hata hivyo bado haijafahamika simu hiyo ilitoka kwa nani, na kwanini aliharakisha hivyo (haijafahamika bado). Na huyo aliyefika kwake ni siri yake...akaandika hivyo!‘Hii taarifa haina maana kabisa..’nikasema ni kuiweka pembeni.Na wakati nawazia hiyo taarifa : huyo mzazi  ni nani huyo au ni nani huyo alimpigia simu mume wangu na kumfanya awe na haraka kihivyo, ndio akaja docta rafiki, akanikuta nipo kwenye mawazo, akaniuliza kuna nini kimtokea…‘Mambo ya kazi tu…na nilikuwa naipitia ile taarifa aliyoacha rafiki yangu, lakini hakuna alichokifanya, sio kawaida yake, ni taarifa ya mtu ambaye hajui kazi kabisa, sio yeye aliyeitayarisha…’nikasema‘Hiyo taarifa ina muhimu gani kwako kwa hivi sasa…?’ akaniuliza‘Bado nawajibika kuufahamu  ukweli, najua baada ya hili, mume wangu akipata nafuu, nitahitajika kukaa kikao na baba, na wawekezaji wengine, kuna maswali mengi nitaulizwa, nitayajibu vipi kama siufahamu ukweli..’nikasema‘Ukweli kuhusu mumeo au ukweli kuhusu maswala ya kikazi…ama kuhusu mume wako yeye alishakuambia kila kitu, sasa kama hayo yanaweza kuingiliana na kazi yake, ni jambo jingine linaelezeka... kwa hivi sasa mimi siioni kwanini unabeba mzigo kabla haujatua kichwani mwako…utachoka hata kabla hujahisi uzito wake, tulia kwanza..’akasema‘Unajua siwezi nikaamini yale aliyoongea mume wangu moja kwa moja, na hakuwahi kusema ni kitu gani alikifanya, mpaka afikie kuniomba msamaha..tunahis tu..pale aliongea akiwa kachanganyikiwa, sawa yawezekana ni hilo kuwa kafanya madhambi…lakini mbona taarifa ya rafiki yangu haijabainisha hilo. Sawa naweza kuhitimisha hivyo kuwa ni kweli, labda ni kweli, je hilo latosha tu, hapana ni lazima niwe na ushahidi....’nikasema‘Nikuambie kitu hiyo taarifa ya rafiki yale lengo lake ni kuvuta muda, kuhakikisha kuwa anakuchanganya ili yeye aweze kutimiza haja zake,..na huyo mzazi mume wako aliyewahi kuaga kuwa anakwenda kumuona, sio mwingine ni huyo huyo rafiki yako, amini usiamini huo ndio ukweli….’akasema docta‘Sawa, tunaweza kusema ndivyo hivyo, haya nipeni ushahidi, hapa anasema mdogo wake siku hiyo alifika pia kuosha gari,...swali gari lipi, na muda gani, hajaelezea hapa…kama kweli ni yeye, maana kama ni kweli, basi, huyo sio rafiki yangu ninayemfahamu mimi...'nikatulia kidogo.'Mimi sio mjinga wa kukataa kauli za watu...najua nahisi hata mimi hivyo hivyo, ….lakini siwezi kukubali hivi hivi tu, na kuchukua hatua hiyo kubwa niliyodhamiria moyoni, maana ni kweli nitafanya hivyo,...je nichukue haua hiyo bila ya kujirizisha, ushahidi, upo wapi, unanielewa hapo,…au wewe unao huo ushahidi.?’ nikauliza‘Kwasababu rafiki yako anajua kafanya makosa, anajua yeye alishirikiana na mume wako kulifanikisha hilo, ...'akasema'Ushahidi...'nikasema'Ndio tunaweka nadharia hii sawa,...kuna kitu nataka unielewe, kuwa huenda rafiki yako, alipanga hivyo, au kuna kitu kilimsukuma kufanya hivyo, na kitu hicho akakitumia kama ngao yake, lakini yanayokuja kutokea sasa imekuwa kinyume na alivyotarajia, ndio maana kaamua kukimbia ili kuepusha shari, naanzia hapo…’akasema docta.‘Mimi nataka ushahidi maana baada ya huo ushahidi, mimi nitachukua hatua kali, hutaamini, na sitaweza kurudi nyuma kwa hilo..bila kujali ni nani, sitak nadharia za kuhisi hisi, wewe ni docta, au... …’nikasema‘Sasa hebu nikuulize utachukua hatua kwa nani,  kwa mumeo au kwa huyo rafiki yako...maana kam ni kutenda kosa wametenda wote, ?’ akaniuliza‘Ndio maana nataka ushahidi..na nikiupata huo ushahidi…, sitaojali kuwa ni mume au rafiki yangu, yoyote ataumia,…na kila mtu ataumia kutegemeana na kosa lake yeye mwenyewe, wewe ngoja utaona nitakachokifanya…’nikasema‘Kwa maelezo ya mume wako, wewe ulishirikiana na rafiki yako kulifanikisha hilo, sasa sijui kwa vipi, yeye kadai kuwa wewe ulimtuma, afanye hivyo ni kweli si kweli, ulisikia mwenyewe akiongea pale hospitalini, …’akasema docta, kama ananiuliza‘Mimi nina kichaa!!!…hahaha, hivi kweli inaingia akilini hiyo, mimi nimtume rafiki yangu akazini na mume wangu, hata wewe unaweza kuliamini hilo…?’ nikauliza‘Ili kuweza kulijibu hilo, labda nikuulize wewe, je hamkuwahi kukaa na rafiki yako mkapanga kuwa labda rafiki yake ajitahidi kupata mimba, kwa...sio lazima useme kwa mume wako, kwa yoyote, labda yeye akaona kwa mume wako, au...hatuna uhakika bado hapo, nasema hivyo kukuuliza wewe...?’ akauliza‘Wewe uliwahi kuongea na rafiki yangu akakuambia hivyo...?' nikauliza'Hapana, baada ya kujifungue amekuwa makini sana, hata nikiongea naye ahataki nimuulize chochote,...'akasema'Sasa umelitolea wapi hilo, kuwa mimi nimtume rafiki yangu akazini na mume wangu, au sio…ndio una maana hiyo, kuwa mimi nilimshauri hivyo, na ...yeye akaona kwa mume wangu ndio kwenye usiri ..huo ni ujinga haliji akilini kabisa, rafiki yangu mwenyewe, sawa na ndugu yangu aje kufanya hivyo...ingelikuwa wewe ungelifanya hivyo kweli hebnu jiulize kwanza kabla ya kutoa nadharia yako?’ nikauliza‘Yawezekana mlikaa mkaongea kwa namna ambayo aliona akifanya hivyo haitaleta walakini, lakini sio kwa moja kwa moja kuwa akafanya hivyo kwa mume wako, yawezekana ushauri wako,..ndio uliomsukuma kufanya hivyo labda…’akasema‘Hakuna kitu kama hicho,..kama kweli yeye ni rafiki yangu ananijali na kujali masilahi ya familia yangu, asingeliweza kufanya kitu kama hicho, yeye anafahamu mambo mengi ambayo kama mimi, au mume wangu akiyafanya hakutakuwa na huruma kwa baba, hilo analifahamu, na anamfahamu sana baba yangu, ..ndio maana mimi siamini kuwa kafanya hivyo, ndio maana nataka ushahidi, baba anauhitajia pia huo ushahidi.., …’nikasema‘Baba yako keshajua hilo, kuwa huenda huyo mtoto wa rafiki yako kazaa na mumeo,a u mdogo wa mume wako, keshaniulizia hilo, akataka ushauri wangu kama docta , mdogo wa mume wako, hataki kusema ukweli, ukiongea naye, unaweza ukahisi ndio yeye, kwa jinsi anavyojiuma uma, lakini lengwa mkubwa ni mume wako, unahisi ni kwanini...?’ akauliza‘Baba taarifa alizo nazo ni kama nijuavyo mimi..bado anafuatilia, kasema kama ni kweli, basi, na yeye atakuwa na maamuzii yake, mimi sitaki kusimamia mambo ya wazazi wangu maana nafahamu hukumu yao ni nini…mimi nina namna yangu ya kuhakikisha hao watu, kama ni kweli, wanapata kitu ambacho hawataweza kukisahau maishani mwao…’nikasema‘Hebu niambiea ukweli wako..utachukuaje hukumu, wakati labda na wewe unahusika, ni kwanini hutaki kusema ukweli kuwa wewe na rafiki yako mlikaa mkakubaliana jambo fulani..?’ akauliza‘Hata kama tulikaa tukaongea tukajadili mambo, lakini tunakaa sana, tunaongea sana, lakini sio kwa ….hapana, siwezi mimi na akili zangu nimwambie akatembee na mume wangu, na yeye...'mara kukawa kama kuna sauti, nikahisi huenda ni mume wangu, lakini kwa hizo dawa, bado atakuwa kwenye usingizi.'Anaweza kufanya hayo kwa malengo fulani, au ...kutokana na jinsi mlivyoongea, mimi sijui....na kama anafahamu kuwa kitu kama hicho kikitendeka, yaweza kuharibu kabisa ndoa yako, au..mimi sijui, ...ni kwanini afanye...huoni kuwa kuna kitu ndani yake, na baba yako ndio anakitafuta...'akasema‘Mimi sijui, ila nijuavyo, baba hataki kashfa, hatua ya kwanza ambayo nahisi ataanza nayo, akiugundua ukweli, ni yeye  kutoa hisa zake, na kujitoa kwa baba kwenye kampuni ya mume wangu, ndio kuiua , maana baba ndiye mdau mkubwa wa hiyo kampuni...'nikasema'Na kuna madeni,...'akasema'Ni kweli hata ukiangalia hii taarifa kampuni hiyo ina madeni, ya nje, baba mwenye anamdai pesa nyingi…je hao wanaodai wengine watalipwa na nani…kiufupi kampuni ya mume wangu haipo…na hili ni moja ya mambo yanayomuumiza mume wangu..nimemuambia baba, na sio hayo anayofikiria yeye,…’nikasema‘Je baba yako alisemaje, hawezi kusaidia vyovyote..?’ akauliza‘Kasema anaweza kusaidia iwapo, hakuna kashfa, kama kuna baya, kuna kshfa mbaya, kaifanya mume wangu yenye  kutia dosari, familia yake hataweza kusaidia kwa lolote lile, na atajitoa, na kudai pesa zake zote, na atachukua hatua nyingine kubwa zaidi…’nikasema‘Na wewe huwezi kusaidia chochote..?’ akauliza docta‘Mimi, hahaha...siwezi, maana hata mimi kampuni yangu haifanyi vizuri..na tatizo ni kuwa kampuni ya mume wangu, inataswira fulani  kwa wateja wangu pia, sijui kwanini, kuna wateja wangu wameanza kukimbia kisa ni kutokana na mwenendo wa kampuni ya mume wangu,.. unajua siasa za biashara zilivyo, kuna vita ya chni kwa chini, katika ushindani wa biashara, wateja wengine, hutafuta visa tu,…’nikasema‘Je unahisi kilichotokea kwa  mume wako ni sababu hizo za kibiashara, au kuna jingine limajificha…?’ akaulizaNikaichukua ile taarifa, nikamuonyesha naye akaipitia halafu akasema;‘Unaona sehemu zote alizoweka mabano kuwa haijakamilika ni zile ambazo zinamgusa yeye…na simu ya mume wako  mmh, haiwezi kusaidia kitu, ...lakini itasaidia nini hapa, kuna mambo kayafunika kiaina, ila haya kuwa mumeo anadaiwa, kampuni haiwendi vizuri, kaongea ukweli, na kayachukua kama sababu kubwa, huoni ni kitu kama kimelengwa kinamna fulani..?’ akaniuliza‘Simu ya mume wangu haijulikani wapi ilipo hata yeye anasema hakumbuki, huenda iliungua kwenye gari, au iliibiwa..na nimejaribu kuulizia watu wa mitandao kama wanaweza kunisaidia wamesema hilo ni vigumu kwao…’nikasema‘Ulishaongea na huyu muosha magari, kuhakikisha kuwa huyo aliyeondoka hapo kweli alikuwa mume wako au ni mdogo wa mume wako, maana hapa kwenye taarifa ni kama kulikuwa na watu wawili, huyo hapa alikwenda kupata kitu mgahawani, na huyo aliyekuja kwa rafiki yako ni nani.?’ akaniuliza‘Huyo muosha magari, hayupo…kasafiri, na hata simu yake haipatikani…’nikasema‘Je sio mbinu za kumuondoa hapo Dar….hana jamaa yoyote anayemfahamu, tukajaribu kumfuatilia, nahisi hapa tunaweza kugundua kitu..?’ akauliza‘Sijaweza kufuatilia kiasi hicho, nitategemea hili angalifanya huyo rafiki yangu, lakini ndio hivyo…kama unavyoona, hii sio taarifa ya mtu aliyesomea kazi hiyo, ni kama kaandikiwa na mwanafunzi wake..’nikasema‘Huku kwenye maelezo, ya uoni wake, katupia lawama ndoa yenu kuwa inaweza ikawa sababu nyingine, unahisi kuna ukweli wowote hapa…?’ akauliza‘Sizani, kama kuna ukweli, kwanini hilo lisitokee nyuma, lije litokee siku hiyo..nakiri kuwa mimi nina madhaifu yangu, lakini haijafikia hadi yatendeke hayo,…na ndio maana bado sijaamini..’nikasema‘Hujaamini nini sasa hapo..?’ akauliza‘Kuwa kwanza ajali hiyo inatokana na matendo ya nyuma, pili, hapa kuna matatizo ya mume wangu na kampuni yake kwa upande mmoja, na huku kuna huyo mtoto wa rafiki yangu, lipi lenye uzito, tatu.... rafiki yangu anahusikanaje na mume wangu kwenye kusababisha kampuni ya mume wangu kufikia hapo ilipo, maana baba kalisema hilo. ukiangalia kuna mkanganyiko, na kwanini mdogo wa mume wangu ananipiga chenga, unajua ananikwepa sana, huoni anaweza kuhusika kama sio yeye…’nikasema‘Baba yako anasemaje kwa ujumla wake..?’ akauliza‘Baba yeye hataki kusema lolote mpaka sasa, anasema kuna taarifa anaisubiria, akiipata ndio itampa mwanya wa kusema jambo, ila kaahidi kulifuatilia hili tatizo la familia yangu na kampuni zote, hadi mwisho wake, na kasema sasa hatarudi nyuma, …’nikasema‘Atasamehe tu, nyie ni watoto wake,…maana vyovyote iwavyo, itasaidia nini sasa eeh, atamfukuza, atavunja ndoa yenu, unaonaeeh, hawezi, na ukiangalia kwa makini,.. kampuni ya mumeo ikifa, mumeo atakuwa anategemea ajira yake tu…ambayo haiwezi kumkidhi haja zake,..na nimesikia huko kazini kwake kuna matatizo pia ni kweli…?’ akauliza‘Nimesikia sasa hivi na kusoma kwenye taarifa ya huyo mdada, nilikuwa sijui, kiukweli kuna matatizo,…sijui alifanya nini huko…’nikasema‘Mdada hakuelezea hilo…mmh, hapa…ngoja nisome, anasema, alikopa pesa, na kujikopesha bila idhini,…mmh, kwanini alifanya hivyo, …hapa anasema bado uchunguzi unaendelea…sasa mume akifukuzwa itakuwaje na kampuni ndio hiyonayo inayumba…huo sasa ni mzigo wako ambao sizani kama utaweza kuubeba…’ akasema‘Hilo sio tatizo kwangu, yeye ni mume, na mengi kajitakia yeye mwenyewe, lakini je hayo ndio yamesababisha hayo yote, hiyo ajali sabau ni hayo, au ...na mmh, bado kichwa changu kina giza, ?’ nikauliza‘Jibu hasa la haya yote tutalipata kutoka kwa mume wako,... je atakubali kusema ukweli…?’ akauliza‘Akipona, ni lazima asema ukweli, nitahakikisha hilo analifanya na nitajua la kufanya, wewe subiria tu…’nikasema‘Lakini usije kuongea chochote kwa hivi sasa, wala kumuuliza..’akasema docta‘Nafahamu hilo sana, hapa nipo kama mtumwa, kila analotaka nalifanya, kila kitu kimesimama, nitafanyaje, lakini kuna ukweli huo nautaka, ..hata kabla hajapona, nautaka niufahamu, je ni kweli kuwa mume wangu kazaa na rafiki yangu, nikiwa na uhakika na hilo, basi mengine yote hayana maana kwangu, ….mimi na baba tutakiwa hivi, …’nikasema nikishikisha vidole viwili kwa pamoja.Nikashtuka kusikia mtu anakohoa nyuma yangu,, …nikageuka na kumkuta mume wangu akiwa kwenye kigari chake anatuangalia …akiwa anatokea huko alipokuwa amelala…nikamuangalia mume wangu, alionekana kakasirika kakunja uso..‘Kwanini umefanya hivyo mume wangu…unatakiwa ulale, hizo dawa zinahitajia wewe ulale, unakwenda wapi sasa…?’ nikamuuliza lakini hakunijibu, akawa anakiendesha kigari chake na kuelekea nje‘Kasikia nini…?’ akauliza rafiki yangu‘Sizani….’nikasema, nikiwa sina uhakika.‘Basi ngoja nikaongee naye,..na wewe hakikisha hiyo taarifa unaificha asije kuiona, pili, nataka tuje tuongee mimi na wewe baadae…nataka.., nikusaidia kulimaliza hili jambo, nitahakikisha unaufahamu ukweli wote, na ushahidi unaoutaka, ila uniahidi jambo…’akasema‘Jambo gani…?’ nikauliza na mara mume wangu akawa ananiita huko nje..WAZO LA SIKU: Maisha yalivyo, inafikia muda inabidi ukope, ili kukidhi haja fulani, ni muhimu tukikopa tujue jinsi gani ya kuja kulipa deni la watu, wengine hukopa tu, akisema tutajua huko mbele kwa mbele, na ukianza kudaiwa, unakimbia, unajificha au unajibu jeuri. Tukumbuke kuwa deni ni deni, na deni haliishi mpaka ulipe au mwenyewe kwa ridhaa yake akusamehe. Tusipende kudhulumu tukidaiwa, deni halitaondoka hata ukiondoka hapa duniani,..utaenda kulikuta huko kwa hakimu wa mahakimu.Docta aliposikia mimi naitwa, akasema‘Ngoja mimi nikaongee naye kwanza…’akasema na nilitaka kumpinga maana mume wangu kaniita mimi, ni wajibu wangu kuitika wito wake kwanza, lakini docta akaniwahi na kukimbilia huko nje alipo mume wangu, ikabidi nisubirie tu.Nikiwa nimebakia pale peke yangu, niliweza kuipitia ile taarifa ya rafiki yangu kwa makini,  na mpaka nafika mwisho nilianza kubadilika, kuwa huenda wanayoongea wenzangu yana ukweli fulani. Kwenye hii taarifa rafiki yangu alijaribu kama kuficha jambo, na kujihami kwa namna fulani, japokuwa haionyeshi wazi wazi kuwa kweli anahusika ..Kwa maelezo ya taarifa hiyo, Muosha magari anasema aliosha gari la mume wangu, na pia la mdogo wa mume wangu kuonyesha kuwa wote wawili walifika hapo siku  hiyo, lakini docta anasema mdogo wa mume wangu alikuwa kwake wakiangalia mpira,..je muda gani alitoka hapo na kwenda huko…. nikjiuliza.Hapo nikaona kuna muhimu wa kuonana na mdogo wa mume wangu kwa haraka iwezekekanavyo, lakini nisingeliweza kuondoka hapo, nikachukua simu na kumpigia huyo shemeji yangu, lakini simu haikupokelewa.‘Nitampata tu….’nikasema na muda huo docta akaingia akisukuma kile kigari cha mume wangu, na mume wangu alikuwa kakaa kinyonge, akitikisa kichwa kama kukubali jambo fulani kwenye maongezi yao..na walipofika ndani docta akasema;‘Tumemalizana na rafiki yangu, …mimi nataka kuondoka…’akasema‘Sawa mimi nipo na mume wangu, sikusindikizi…’nikasema‘Ni wajibu wako, lazima mleane kwa shida na raha…’akasemaMume wangu akawa anakiendesha kigari chake peke yake na kuelekea chumbani, nikamuangalia docta, na docta akaniashiria nimfuate mume wangu, basi ikabidi niagane na docta, yeye akaondoka, na mimi nikamfuata mume wangu ndani.‘Mbona unakuja huku, mgeni anabakia na nani, msindikize mgeni au..?’ akaniuliza‘Anaondoka, nimeshaagana naye, kaondoka…’nikasema‘Mimi nipo safi mbona, sasa hivi nataka nilale tu, nasikia kulala tu, nahisi macho mazito…’akasema‘Uliamuka kabla dawa haijaisha nguvu yake…’nikasema‘Niliota ndoto mbaya…’akasema‘Ndoto gani…?’ nikamuuliza‘Docta, ananiibia mke wangu…’akasema sasa akiniangalia huku anatabasamu kama utani vile‘Hahaha, kama nikukuibia basi angelikuibia zamani, sio sasa, keshachelewa, na uzee huu anatakia nini tena kwangu, hizo ni ndoto za shetani usiziamini…kwanza yeye ana mke wake mnzuri..’nikasema‘Mhh,..ni kweli lakini wewe ni mnzuri zaidi yake…, na .. na una mengi ambayo mke wake hana…’akasema‘Kama yapi, …?’ nilimuuliza lakini nikiwa na tahadhari.‘Mali, familia yako ina julikana…na mengine mengi..’akasema‘Na wewe umenioa kwa hayo pia, au sio…?’ nikauliza‘Ofcourse yes, uzuri wako, na hayo mengine vilinifanya nijisikie nina mke wa maana sana,..ndio hivyo, mitihani hii inanifanya nijutie kwa niliyoyafanya, …lakini nakuahidi mke wangu hayo yaliyopita sitarudia tena…’Nilitaka kumuuliza yapi kayafanya, lakini nikaogopa, haitakiwi, nikabakia kimia.‘Sikiliza mke wangu, ngoja nipone, nina uhakika nikipona, na nguvu zangu zikirejea vyema, kila kitu kitakuwa sawa, niamini, kila kitu kitarejea kama kilivyokuwa awali…,nimeligundua kosa langu....’akasema‘Hilo neno mume wangu…, utapona tu, usijali…’nikasema‘Niahidi mke wangu, kuwa hutaniacha…’akasema hivyo na kunifanya nishtuke kidogo, ni kauli yenye utata, sikufahamu ni kwa muda huo au ana lengo gani, lakini sikuruhusiwa kuanzisha mijadala, na pia, sikupenda kusema uwongo‘Mume wangu dawa itakuwa haifanyi kazi, tukiendelea kuongea, wewe lala kwanza, umeshaharibu kwa kuamuka mapema, sasa inabidi ulale tu…ukiamuka tutaongea, unasikia, usipuuze maagizo ya docta, ukifanya makosa hutapona na ndoto yako haitatimia..’nikasema‘Ndoto…!’akasema  kwa mshangao‘Ndio za kuendeleza miradi yako, au sio…’nikasema‘Haya bosi, ngoja nilale..kweli nasikia kulala, lakini sitaki niote hiyo ndoto tena, lakini naomba usiondoke hapa kitandani kabisa, nataka ukae hapa karibu yangu, nikiamuka tuongee, nataka niongee na wewe mambo mengi mazuri, ma-zzzrrr..’akasema‘Haya lala…’nikasema nikiwa nimekaa karibu yake, na baada ya muda nikasikia akitoa ile sauti ya kuonyesha kuwa kweli kalala.***************Siku nyingine, nilikuwa nimekaa nyumbani, sebuleni, na mume wangu alikuwa amelala chumbani baada ya kupata dawa.  Na nilipohakikisha amelala, nikaona nitoke kidogo nje, kitahadhari, maana akiamuka akaona sipo karibu yake,  ni mtihani,..nikasema leo nataka nifanye jambo, angalau nitoke hata kufika madukani,.‘Nani huyo tena…nikasema, niliposikia mtu anagonga geti la nje Muda huo nilikuwa varandani nakagua kuwa kila kitu kipo sawa, kwa vile najua kuwa mfanyakazi wetu wa ndani yupo, atafungua geti sikuhangaika kutok nje, lakini haikuwa hivyo, mfanyakazi alikuwa hayupo karibu na huyo mtu akawa anaendelea kugonga,..‘Kaenda wapi huyu binti…’nikawa naongea peke yangu, nikachungulia kupitia dirishani, na muda huo, huyo mtu akawa anafungua geti mwenyewe, kabla sijajiuliza ni nani, mara akatokea mfanyakazi wetu, kumbe alikuwa anafanya usafi sehemu za ndani.‘Nani kagonga geti na sasa anafungua geti mwenyewe…?’ nikamuuliza‘Hata sijui ni nani ..ngoja nikaangalie…’akasema na kukimbilia nje.Haikupita muda, nikasikia watu wanaongea huko nje na vicheko…nikaingiwa na hamasa ya kumtambua huyo mtu ni nani, maana ni sauti ya kime, nikachungulia dirishani, alikuwa ni mdogo wa mume wangu.Mdogo wa mume wangu mhh, kajileta…!! Kwa haraka nikatoka nje, nilitaka nimuwahi,  kwani sikutaka mtu yoyote kumsumbua mume wangu, japokuwa nafahamu kuwa mdogo wake huyo, akijua kaka yake kalala hawezi kumsumbua, kwani anafahamu utaratibu ulivyo,japokuwa sijaonana naye muda sasa, lakini moyoni nilikuwa na hamu sana ya kuongea na huyu mtu!‘Hii ndio nafasi pekee…’nikajisemea kimoyo moyo nikitokeza kwenye mlango. Sasa hivi nakuwa na tahadhari, sio kama zamani, mume wangu anaweza kunywa hizo dawa ghafla akaamuka, na akiamuka huwa hapendi kukaa ndani, anapenda kuzungushwa nje na kigari chake cha kukokotwa. Ndio maana nikaona nimuwahi mapema huyu mtu kwa tahadhari.Nilihakikisha nimeusindika mlango nyuma yangu, na sasa nikawa naangaliana uso kwa uso na shemeji yangu huyu, alikuwa mlangoni alitaka kufungua,.. inaonekana ni kama vile hakutarajia kuniona hapo nyumbani, akabakia mdomo wazi akishindwa hata kuongea, nikatabasamu ili kumuondoa wasiwasi, na yeye kwa aibu akatizama chini..‘Habari yako shemeji, mbona unaonekana kama umeona kitu cha kukuogofya, hukutarajia kuniona mimi hapa nyumbani nini, au una wasiwasi gani, naona unajaribu kunikwepa kinamna?’ nikamuuliza‘Ni kweli, nilijua labda haupo, labda umetoka kwenda kazini kidogo, sasa kazi inakuwaje shemeji, …mmh, huu ni mtihani, lakini yana mwisho au sio, si kukwepi shemeji ni shughuli tu....’akasema.‘Kuna nini kinaendelea kati yako wewe na mfanyakazi wangu?’ nikamuuliza, nilimuuliza hivyo nikiwa na maana yangu, japokuwa ulikuwa ni utani.‘Hakuna kitu shemeji, hahaha, shemeji naye bwana, na mfanyakazi wako hakuna kitu kama hicho kabisa ...mimi nimekuja kwa ajili ya kumwangalia kaka, na kwa muda sasa sijafika, nilikuwa nimesafiri kidogo, na unajua nikiwepo basi inabidi nije, na ikibidi nikae hapa, ili nisaidie saidie,..na kiukweli mnisamehe sana, sijafika muda kumuona mgonjwa,....’akasema,Nilimwangalia alivyokuwa akipata taabu ya kutaka kujieleza , na baadaye nikasema‘Usijali shemeji nakutania tu, karibu, lakini kaka yako kalala na dawa anazotumia hatakiwi kusumbuliwa, unasikia sana…’nikasema.‘Kama kalala basi …niwasalimie kidogo niondoke zangu, …nilijua nitakuta keshaamuka,..jana alinipigia simu kuwa nijitahidi tuonane…’akasema‘Alitaka muonane mbona hajaniambia..?’ nikauliza kwa mshangao, hata yeye akaonekana kushangaa, na akasema‘Kwakweli mimi sijui, ila alinipigia, simu, tukawa hatuelewani, mawasiliano, maana nilikuwa kwenye gari, akasema nijitahidi nionane naye…’akasema‘Ok, labda kapitiwa kuniambia, hamna shida, ngoja tuongee kwanza‘Ndio shemeji niambie…’ akasema‘Unajua shemeji, wewe ni sawa na mdogo wangu, ....nakuona hivyo licha ya kuwa wewe ni shemeji yangu, ndio maana wakati wote nimekuwa nikihakikisha kuwa maisha yako yanakuwa bora, ili uweze kusimama kwa miguu yako mwenyewe, na natumai hayo yameshakamilika...na hapa ni nyumbani kwako, wakati wowote unaruhusiwa kufika, nilishangaa tu, kukuona kama unani kwepa, hasa pale hospitalini, nikajiuliza kuna nini...’nikasema.‘Hapana sijakukwepa shemeji hizi hisia zako tu, kwanini nikukwepe..’akasema.‘Hakuna tatizo kaka yako ana maendeleo mazuri tu, ila kuna mambo muhimu sana tunahitajika kumsaidia, …ndio najua mengi ni majukumu yangu, maana huyo ni mume wangu, au sio, ....’nikasema.‘Ni kweli shemeji, ila kama kuna lolote la kusaidia wewe niambie tu …’akasema.‘Usiwe na wasiwasi, sio jambo kubwa sana,..’nikasema, nikimuelekeza huyo shemeji yangu twende bustanini, kuna sehemu maalumu tumetengeneza ya kuongelea, upepo wake ni mwanana, kama upo ufukweni mwa bahari, na mume wangu hupendelea kuja kukaa hapo.‘Tuletee vinywaji, na hakikisha kuwa mume wangu akiamuka unaniita mara moja...unasikia.’nikasema.‘Nitafanya hivyo dada.....’akasema.*********‘Shemeji, nataka tuyafupishe  mazungumzo yetu iwezekanavyo, kwani kaka yako akiamuka natakiwa niwe naye karibu, kwahiyo nakuomba nikikuuliza mambo fulani fulani ujitahidi kunijibu kwa ufasaha, bila ya kuogopa....’nikamwambia.‘Uliza tu shemeji.’akasema.‘Ninachotaka kukuuliza ni mambo ya kawaida tu usiwe na shaka...’nikasema.‘Sawa nakusikiliza,...lakini kama ni kuhusu kaka, mimi sijui lolote...’akaanza kwa kujitetea.‘Usijali,....wewe utaongea tu kile unachokifahamu, sio swala la kesi au swala la kulazimishana, kitu ambacho hukijui hukijui,…ila haya yote nayafanya kwa manufaa ya kaka yako…’nikasema‘Ni kweli….’akasema‘Mimi,sizani kama wewe unafurahia hiyo hali aliyokuwa nayo kaka yako,  na sizani utataka hilo litokee tena, ina maana ni lazima na sisi kama tunamjali tuone tunamsaidiaje, na kabla ya hilo tujaribu kuona kama kuna sababu iliyosababisha hilo kutokea, ili lisije kutokea tena, umenielewa hapo....’nikasema.‘Kwakweli shemeji mimi sifurahi kabisa hiyo hali, kaka na wewe ni watu muhimu sana kwangu,  wazazi wetu kama unavyowafahamu, hawana mbele wala nyuma, wewe ndiye umeisaidia familia yetu kupitia kwa kaka,sasa naogopa sana kaka asije akaondoka..sijui itakuwaje, japokuwa nimeanza maisha lakini bila ya nyie bado najiona sina uhakika wa maisha,...’akasema.‘Basi kama unafahamu hivyo ni vyema, tukamsaidia kaka yako, kwani japokuwa kiafya anaendelea vyema, lakini mpaka sasa sijajua ni nini kilichomfanya hadi afikie hapo, je ni jambo la dharura tu, au kuna jambo jingine ambalo huenda bado lipo, na kama lipo ni nini, ,..’nikasema na hapo akakaa kimia tu.‘Unaposema hivyo shemeji unahisi kaka kapatwa na hiyo ajali kutokana na jambo fulani au, mimi nilijua kuwa ni ajali ya kawaida tu, ambayo anaweza kupatwa mtu yoyote’ akasema.‘Ajali ni ajali ndio, lakini kuna ajali inakupa maulizo mengi kutegemea ilivyotokea, ndio maana nataka nikuulize wewe ambaye muda mwingi akirudi kazini, au…ikitokea dharura mnakuwa naye,…’nikasema.‘Shemeji mimi sio kwamba mchana kutwa nakuwa naye, unafahamu hilo, kwani hata mimi ninakuwa kwenye mishe mishe zangu,... na mimi najaribu kutafuta jinsi ya kusimama mwenyewe... wakati mwingine huwa nafanya kazi za kaka, lakini sipendi mimi nifanye kazi  kwenye ofisi yake, kama tulivyowahi kuongea..’akasema.‘Ni kweli, sasa turejee kwa kaka yako, tumsaidie, kuna onekana kuna tatizo, na hueda tatizo hilo lipo nje…kuna kitu kinamsumbua, na huenda kakuitia kwa hilo, kaka yako hatakiwi awaze sana, ndio maana najitahidi kuchuja kila jambo, unanielewa, sasa hebu uwe muwazi kwangu, hajakuambia anakuitia nini, au huna fununu ya jambo fulani…’nikasema‘Nijuavyo mimi , biashara za kaka, huko kazini zilifikia kubaya, hakuna wateja, ..na ikawa watu hawalipo madeni, kwahiyo na yeye akawa hawezi kulipa madeni, hilo likawa linamsumbua sana, na mara nyingi ananituma kwa wateja wake kufuatilia madeni, labda ndio hivyo…’akasema‘Unaona vitu kama hivyo mimi nilikuwa sijui, haniambii,..’nikasema‘Kaka huwa ni msiri sana, hata akiwa na shida hapendi kusema huwa anapambana kivyake, hata mimi nilimshauri akuambie akasema hawezi, atapambana kivyake, kwahiyo sijui, zaidi…ila nilisikia siku moja akilalamika kuwa watu wanaomdai, wanataka kufungua mashitaka…’akasema‘Unawafahamu kwa orodha…?’ nikauliza‘Kwa kichwa hapana, ila ukitaka ninaweza kukutafutia huko ofisini…’akasema‘Hilo liache kwanza, je hakuna kitu kingine umesikia, akilalamika au…ni kwanini akatokea kunywa pombe sana…?’ nikamuliza‘Shemeji mimi nijuavyo, na aliwahi kuniambia ni sababu ya mawazo, amekuwa kwenye wakati mgumu na nahisi anaona kama hana mtu wa kumliwaza vile, ni yeye na kazi yake, na anaogopa kusema kashindwa, ,….nahisi ni hivyo shemeji..madeni, na…sijui, kama kuna tatizo jingine mimi siwezi kufahamu…’akasema ‘Unavyosema hivyo..kumliwaza.., ni kama vile aliwahi kulalamika, kama unavyosema anahisi hana mtu wa kumsaidia, mimi si nipo mkewe jamani,je hujawahi kusikia akilalamika mbele yako, kuwa kuna tatizo analipata dhidi yangu?’ nikamuuliza.‘Shemeji hapana, lakini mimi nimeishi na nyie, kwahiyo mengine nayafahamu, wakati mwingine nilikuwa natamani kuwa kama nyie wachapakazi, mkirudi nyumbani hamna muda wa kuongea ni kazi tu….’akasema‘Naomba uniambie waziwazi, nitafurahi sana ukianiambia ukweli, kuwa labda katika maisha yetu uligundua kasoro fulani, maana wewe tumeishi nawe, ukisoma mpaka ukapata kazi, niambie ukweli shemeji,kuna jambo gani tunakosea, au mimi nimekosea mpaka namkwaza kaka yako?’ nikamuuliza.‘Mhh, shemeji mimi sioni walakini ndio maana nasema natamani niwe kama nyie, lakini kwangu ukifanya hivyo mke ataanza kulalamika, unanielewa hapo, wake zetu sisi, kisomo kidogo, ukiwa nyumbani wanataka usifanye kitu, uwe unawasikiliza wao, ukishika simu ugomvi, uki..ndio hivyo,…mimi hata laptop naogopa kwenda nayo nyumbani….’akasema‘Ina maana kumbe labda hata kaka yako yupo hivyo, kuwa labda alikuwa hapendi hali hiyo ya mimi kuwa na kazi hata nyumbani, lakini hata yeye alikuwa akifanya hivyo au sio…’nikasema‘Kiukweli, nyie mnaishi kama wazungu, ..sizani kama kaka anaweza kulilalamikia hilo, mimi sijui kabisa…’akasema‘Kwahiyo kwa uoni wako, kaka yako …hiyo ajali haijasababishwa na jambo fulani,, unavyohisi wewe…?’ nikamuuliza‘Yaweza ikawa na sababu kwa jinsi nilivyosikia kuwa aliendesha kwa mwendo kasi, na kaka hana tabia hiyo ya kuendesha gari kwa mwendo kasi, ndio maana wengi wanahisi kulikuwa na jambo zito.., hata mimi mwenyewe nimejiuliza sana hilo swali, lakini ajali ni ajali tu shemeji…’akasema.‘Kwahiyo wewe unahisi tatizo la kaka yako ni madeni na sio labda kuna mataizo ya kifamilia, labda, kitu kama hicho...?’ nikamuuliza.‘Inawezekana kuna tatizo nje, mimi na wewe hatulijui, lakini kwa uoni wangu mdogo, nahisi kama alikuwa na msongo wa mawazo, kwanza madeni, pili nahisi alihitajia mtu wa karibu sana wa kuyaondoa hayo mawazo ya kazini, lakini wewe upo, sijui kwanini hakutaka kukushirikisha, na sijui zaidi shemeji…’akasema‘Hapo sasa unaanza kusema ukweli…kuwa pamoja na yote hayo, nahisi ananiona kama sipo karibu naye sana, anaogopa kuniambia, ataonekana mdhaifu…’nikasema‘Sawa sawa shemeji…’akasema‘Kwahiyo akaanza kunywa, kuondoa mawazo…’nikasema‘Sawa sawa shemeji…’akasema‘Na ulevi, nisikiavyo, raha yake uwe na wenza, marafiki, wa kike na wa kiume mnakunywa mnacheka, au sio…’nikasema‘Ndio hivyo hivyo…’akasema‘Na kaka yako ni binadamu au sio, na ni mwanaume au sio, ni lazima akiwa anakunywa alikuwa na marafiki, anakunywa nao ..au sio…?’ nikauliza hapo akasita halafu akasema‘Yawezekana…ndio anakuwa nao, ni kawaida hiyo…’akasema‘Na marafiki wanaweza kuwa wa kike na kiume na wewe unawaona , sema ukweli wako, kumbuka, tunaongea ili kupata namna ya kumsaida kaka yako…’nikasema‘Ni sawa shemeji, kwnye kunywa hivyo vipo, na nijuavyo kaka pia alikuwa na marafiki zake, na wakati mwingine ndio, wanakuwepo wanawake…’akasema‘Na wengi ni wale wa mara kwa mara ..au sio, maana ni lazima mzoeane, huwezi ukawa na marafiki wa siku moja moja, au sio,…?’ nikauliza‘Ni kweli shemeji, ni wale wale marafiki zake….’akasema‘Sasa nataka tu kuliweka sawa, hao marafiki zake, nimeshawafahamu, yupo docta,..yupo wale wafanyakazi wenzake, wapo wale majirani wake wa kazini, na wanawake ni nani na nani…?’ nikauliza‘Mhh…mara nyingi,..wapo, lakini anayekuwa karibu naye ni…unamfahamu shemeji, ni yule…yule mdada rafiki yako, na wanawake wengine ni wapenzi wa marafiki zake,…’akasema‘Kuna kipindi analewa kupitiliza…au sio…?’ nikauliza‘Ndio, hilo siwezi kukukatalia, hata yeye hawezi kulipinga…’akasema‘Na kuna muda aliwahi kulala nje, kwasababu ya kulewa sana…’nikasema‘Mhh..shemeji…lakini mimi namchukua na kumleta nyumbani…’akasema‘Haijatokea nyie mkalala nje na mkaja karibu na asubuhi..au yeye akaja karibu na asubuhi..?’ nikamuuliza‘Mmmh labda kukiwa na sherehe…’akasema‘Lakini ilishatokea au sio..?; nikauliza‘Kiukweli….eeh, ndio ilishatokea…’akasema‘Na muda mwingine huyo mdada rafiki yangu alikuwepo…?’ nikauliza‘Sio muda wote..inatokea tu, na mara nyingi huyo mdada anaondoka mapema..’akasema‘Na ile siku mlichelewa, mkawa mumelewa mkaenda kulala kwa huyo rafiki yangu je,ilikuwaje..?’ nikamuuliza hapo akashtuka na kusema;‘Shemeji, …siku zile, hahaha, nani alikuambia,..ndio..lakini sio kulala, kaka yeye aliondoka, unajua ilikuwaje, tulipotoka kule tukampitisha shemeji kwake, mara kukazuka maongezi, akatukaribisha kwake,..ujuavyo pombe hatukuangalia muda, wengine wakajikuta wamelala kwenye sofa…’akasema‘Yeye ndiye aliwakaribisha, au sio…?’ nikauliza‘Ndio, …na muda huo kaka kalewa, akawa naye anakubali haraka, …basi tukaingia kwake, tukaendelea kunywa, kuongea, wengine usingizi tena,…lakini kaka aliondoka…’akasema‘Kaka yako aliondoka, wew ukabakia na rafiki yangu, mkalala naye hadi asubuhi si ndio hivyo…?’ nikauliza‘Ilibidi mimi nibakie, kwa maaagizo ya kaka, kuhakikisha, kuna usalama, ndio sababu hiyo, sio vinginevyo shemeji, na asubuhi aliponiona huyo mdada akanifukuza…’akasema‘Huyo mdada alilewa hajitambui, na wewe ukachukua nafasi hiyo kufanya ulichodhamiria siku nyingi ni kweli si kweli, usinidanganye nimeshafahamu kila kitu..’nikasema‘Hahaha, shemeji bwana, hakuna kitu kama hicho, kaka angeniua, hapana..’nikasema‘Kwanini kaka yako akuue…?’ nikauliza‘Unajua tena shemeji, yule ni sawa na wewe, hatafurahia kama nitafanya jambo baya dhidi yake…’akasema‘Na hiyo hali ya kwenda kulala kwake, sio mara moja ni zaidi ya mara moja au sio..?’ nikauliza‘Mhh, kama mara mbili, au tatu, sikumbuki vyema…’akasema‘Kaka yako hakuwahi kuingia kulala na rafiki yangu..?’ nikauliza hapo akashtuka na kusema‘Ha-hapana shemeji…mimi sijui , sikuwahi kuona, ..unajua anamuheshimu sana yule mdada, sizani, mimi hapo siwezi kuwa na uhakika…’akasema‘Mdada ana mtoto, na nikuulize tangia ajifungue uliwahi kwenda kumtembelea huyo mdada..?’ nikamuliza‘Hapana shemeji, mimi na yule mdada hatuivani sana, inatokea siku na siku akiwa na shida zake ndio ananiona wa maana, vinginevyo, sina habari na yeye kabisa…’akasema , mara nikahisi sauti kama ya watu wanaongea, nikatega sikio, kukawa kimia, nikaanza kuingiwa na wasiwasi, mume wangu asije akawa kaamuka‘Hebu kidogo…’nikasema na kusimama kusikiliza, nilikuwa sijamalizana na huyo mtu, nikasema‘Sasa sikiliza shemeji…, mimi ninakupa wewe muda wa kuyatafakari haya kwa makini, nataka uniambie ukweli, kuhusu mahusiano ya mume wako na rafiki yangu, je kaka yako hana mwanamke mwingine yupo naye karibu..?’ nikamuliza‘Mhh..mimi simfahamu…’akasema‘Sasa  nitaongea na wewe tena kesho, lakini sio hapa nyumbani, nataka tuyaongelee haya na mengine tukiwa wawili, nataka uniambie ukweli, unasikia, kwa manufaa ya kaka yako, unanisikia,....’nikasema.‘Shemeji hamna tatizo kabisa , lakini yote nimeshakuambia, ..sizani kama kuna jambo ninalolifahamu …’akasema‘Nimefurahia sana maongezi yako ya leo, hatujawahi kukaa na kuongea hivi, ukaniambia ukweli kutoka moyoni mwako,,..nimefurahi sana, na wakati wote ninakuona kuwa ni mtu mwema, unayejali, wale wanaokujali, nimefurahi sana...sasa ili kulihakiki hilo, nataka tena tuongee, kuhusu rafiki yangu, unajua mtoto wake anafanana sana na wewe…’nikasema.‘Eti nini, anafanana na mimi, hapana shemeji, sio kweli, haiwezekani sio kweli….’ Akasema na kushtuka, na muda huo simu yake ikawa inaita lakini hapokei ni kama kachanganyikiwa fulani.Na muda huo nikasikia sauti ya wazi, kuwa mfanyakazi wangu anaongea na mtu ndani, nikajua mume wangu ameshaamuka kwahiyo mimi kwa haraka nikawa nakimbilia huko ndani, na nilimuona shemeji akisikiliza simu na huku anatoka nje....**************Nilifika ndani na kukuta kupo kimia, na wakati nataka kwenda chumbani ndio nikasikia watu wakiongea nje, nilipochungulia nje kwa kupitia dirishani nilimuona yule msaidizi wangu akiwa anasukuma kile kigari cha mume wangu, na mume wangu akiwa kakaa na alikuwa kaegemeza kichwa huku kashika shavu, a macho kayafumba kama lasinzia,  hiyo ilikuwa ni dalili, kuwa alikuwa na mawazo.Kumbe mfanyakazi alimchukua mume wangu na kutoka naye nje wakati tunaongea na shemeji yangu,inaonekana mume wangu aliamuka akanikuta sipo na wakati huo mfanyakazi wangu alikuwa anafanya usafi, au….mume wangu alisikia yupo akamuita, na akamuambia amtoe njeNiliwaangalia, na mfanyakazi alikuwa akikisukuma kigari huku na kule ndivyo anavyopenda mume wangu, kufanyiwa hivyo, hataki kukaa sehemu moja kwa muda mrefu.Kwanza nikaingiwa na wasiwasi, nikijiuliza huyu mtu alitoka muda gani, isije ikawa,walifika hadi kule bustanini, wakasikia maongezi yetu na shemeji yangu,kitu ambacho muda wote nilikuwa nikikikwepa, nikaona nithibitishe hilo, nikafungua mlango na kutoka nje,....Mume wangu alipoisi kuna mtu anakuja akafungua macho na aliponiona akajitahidi kutabasamu, lakini lilikuwa tabasamu la kujilazimisha,  kwanza aliniangalia machioni, mimi nikatabasamu, yeye akabenua mdomo, ila ya dharau au kujifanya anajua jambo‘Mume wangu samahani, nilikuwa na mgeni nikakuacha chumbani peke yako..’nikasem‘Mdogo wangu kashaondoka, mbona hajanisalimia, nilitaka kuongea naye.....’ akasema‘Ndio kapigiwa simu ya haraka, labda atarudi baadae lakini kwanini hukusema , kuwa umeamuka, nije, huyu mfanyakazi sio kazi yake hii, hii ni kazi yangu,..’ nikasema‘Unajua upepo, na hali ya bustanini ni kama dawa kwangu nilipoamuka tu, nikaona haupo nikajua umetingwa na jambo, nikamuambia mfanyakaz anisaidie nitoke nje,..na wakati natoka ndio nikawaona mnaongea, nikaona nisiwasumbue, ….’akasema‘Hutusumbui bwana…yule ni ndugu yako na mimi ni mke wako, wote tunawajibika kwako...’nikasema‘Aaah, ni kweli, lakini na mimi ni binadamu, nakuonea huruma, na…..yawezekana na wewe ulikuwa unatafuta njia za kunisaidia nipone haraka, na mimi nataka kupona haraka, au sio…’akasema na kunifanya nihisi kuwa huenda alisikia jambo.‘Mume wangu na wewe siku hizi una maneno, …’nikasema‘Mke wangu hata mimi sijui yametoka wapi,..ila mengine uwe unaniuliza mimi mwenyewe nitakuambia kila kitu, usiogope kuniuliza mke wangu…nakupenda sana mke  wangu usije kuniacha, ukiniacha na mimi nitaicha hii dunia ya mateso,..naumia mke wangu, kweli hujafa hujaumbika…’akasema kwa unyonge‘Mume wangu kwanini unaongea hivyo…?’ nikauliza‘Najua na wewe unajua, kuwa nimekosea sana, na kiukweli mke wangu, mengine tuyasahu tu, tusonge mbele, ukiwasikiliza sana wazazi wako tutaharibu kila kitu, kiukweli mimi najua nimekosea wapi, na mimi kwa hali kama hii, nimepata fundishi kuba sana, na kwahiyo naahidi sitarudia tena, najua kazini kupoje lakini najua jinsi gani ya kupainua tena, hata bila ya msaada wa baba yako…’akasema‘Hayo usiyawazie sana mume wangu…muhimu ni wewe kupona, muhimu ni afya yako, ukiyawazia hayo hutapona, na kazi zipo tu, muhimu ni afya yako…’nikasema‘Kupona kwangu ni pamoja na kufahamu kuwa wewe upo na mimi na kamwe hutaweza kuniacha…hata iweje ..lakini najua nipo kwenye kuti kavu, kwa hali kama hiyo nitawezaje kupona…, mawazo yataishaje, wakati najua kupona kwangu ni kuingia kwenye jela nyingine ya sintofahamu, najua yote hayo, baba yako, anasubiria tu, nipone, au sio…’akasema.‘Sikiliza mume wangu…’nikasema‘Nisikilize nini bwana,..hata ujifanye vipi najua, wewe na baba yako mpo kitu kimoja, najua..rafiki yako kaharibu kila kitu najua…lakini itasaidia nini kwa sasa, ila nikuambie ukweli, mimi nikiwa hivi miaka nenda rudi, na kama nitaendelea kuteseka hivi, aah, kwanini bwana niwasumbue watu…’akasema‘Mume wangu hayo yametokea wapi, tulishaongea ukasema utajitahidi ili upone haraka…’’nikasema‘Yaaah…nitapona haraka, …ili niingie kwenye kizima cha kesi, …unajua baba yako anatamani sana, ukaishi na watu kama docta, sio watu kama mimi, kwahiyo anatafuta kila namna, ndio maana alinitega, nimeliona hilo kwenye ndoto, na..mke wangu nasema hili kwako, kama ni hivyo, sawa, lakini utanikumbuka, labda, nikiwa huko kuzimu…’akasema na kuanza kusukuma kigari kuondoka.‘Mume wangu…unaongea nini sasa..’nikasema lakini huyoo akasukuma kigari kuelekea ndani. Na muda huo nikahisi kichwa kinaniuma ni hiyo ni dalili mbaya kwangu…NB: Kwa leo inatosha ....WAZO LA LEO:Katika maisha yetu ya ndoa, na katika maisha yetu ya kila siku, tujifunze kuwa wakweli, kila mmoja amwamini mwenzake , awe mkweli kwa mwenzake....kwani, ukweli wakati wote, ni kinga ya uhasama,...japokuwa kuna wakati mwingine inatulazima kukwepa kusema ukweli kwa maana fulani, ili kukwepa madhara..tukihisi tunafanya hivyo kwa nia njema….lakini kama tukianza hivyo kusema uwongo, kidogo kidogo hujenga mazoea, na tutajikuta tunahasimiania, unafiki unatawala nafsi zetu..kwa vyovyote iwavyo, tujifunze kuwa wakweli kwa wenza wetu, ili kujenga uaminifu, upendo na furaha na kujenga familia zilizo boraNilipomaliza kuongea na mdogo wa mume wangu, akili yangu ilikuwa kama imefunguka, japokuwa kwa jinsi nilivyomuona huyu shemeji yangu, nahisi kama anahusika kwa amna moja au fulani, anaweza akawa ndiye baba wa mtoto wa rafiki yangu au anajua lolote kuhusu hilo..na kwa hali hiyo, nikajikuta naanza kutawaliwa na hasira, hasira kwa watu wangu niliowapenda sana…Kuna muda nikawa natamani niongee kwa hasira… , nifoke, kama vile nipo ofisini na wafanyakazi wangu, lakini haikuwa rahisi , kwani nilikuwa kwenye kifungo maalumu,..kifungo cha kuwajibika kwa mume. Tuendelee na kisa chetu…*****************Mume wangu siku hiyo hakutaka kuongea kabisa, na nikaona nisimsumbue zaidi, nikajitahidi kutimiza kila kinachostahki, na akaja kulala… Yakapita masiku kadhaa, na siku hiyo nilikuwa nimetoka nje kidogo, nikiangalia taratibu za usafi, ni baada ya kuhakikisha kuwa mume wangu bado amelala, Nilikaa nje kama nusu saa au karibu saa nzima, baadae nikarudi ndani kuona kama mume wangu amesha-amuka ili nimpatie kifungua kinywa...Wakati naingia ndani nikamkuta kashikilia simu,...simu kuashiria kuwa anaongea na mtu, na aliponiona naingia  kwa haraka  akakata hiyo simu , na kujifanya kama ndio anataka kupiga...‘Ulikuwa unaongea na nani, …mume wangu, kwanini unaharibu,  ulishaambiwa usijisumbue na simu, au huyo mtu kakupigia wewe ndio maana sitaki ubakai na simu…?’ nikauliza, na alitulia kidogo , baadae akaniangalia na kusema‘Mdogo wangu kakukosea nini..?’ aliuliza hivyo na kunifanya nishtuke, swala la mdogo wake nilishamalizana naye, iweje tena aulizie hivyo.‘Mdogo wako…!?’ nikauliza kwa mshangao‘Ndio…’akasema hivyo na kutulia ‘Kama ni ile siku tuliongea naye mambo ya kawaida tu, kwani ndiye umempigia simu au yeye ndio kakupigia simu kwani.. kasema nini…?’ nikauliza.‘Nimekuuliza swali na unakwepa kunijibu, hufahamu jinsi gani ninavyojisikia vibaya familia yangu kuonekana tegemezi, kuwa kama omba mba, au huko kumsaidia imekuwa ni tatizo...’akasema‘Mume wangu kwani shemeji kasemaje, niambie ukweli, ..unajua mume wangu hutakiwi kuwa na mawazo mengine ya kifamilia, utashindwa kupona haraka…’nikasema.‘Inaonekana unamshuku vibaya, na kama ni mambo yangu mimi, kwanini umuulize yeyem niulize mimi mwenyewe…’akasema‘Nilimuuliza kwa nia ya kutaka kukusaidia wewe, sikuwa na nia mbaya mume wangu…’nikasema‘Ok…sasa unahitajia nini, nikuambie mimi mwenyewe..?’ akauliza‘Hakuna kitu nahitajia kutoka kwako…’nikasema‘Kama ni kuhusu kazini, ndio nina madeni mengi tu..na inatokana na biashara kuwa mbaya…ilibidi nikope nikitafuta masoko, ilibid nikope kuweka vifaa vya kisasa, lakini bishara haikutikia, ni hali ilivyo, nikajikuta naongeza madeni juu ya madeni, na hilo litakuja kulimaliza mimi mwenyewe…’akasema‘Nimekuelewa mume wangu, lakini hukuwahi kuniambia hayo au sio, lakini sio shida, na wala lisikuumize kichwa… nashukuru sasa nimekuelewa, tutaangalia jinsi gani ya kufanya, kama itabidi tutakopa pesa kwa baba ili tulipe hayo madeni..’nikasema‘Hahaha, ukope pesa kwa baba yako…labda awes io yeye,…kwa kauli yako hiyo naona wewe na baba yako kitu kimoja, ndio maana aliniwekea mitego, hataki mimi niwe mume wako, hili lipo wazi, lakini mimi sitakubali, hataweza nakuhakikishia,…’akasema‘Mume wangu haya yote hayana maana kwa sasa, hebu achana nayo uangalie kwanza afya yako, kwanini unanipa wakati mgumu, ...?’ nikamuuliza na kabla hajajibu nikasema;‘Jitahidi kusahau kila kitu ili upone haraka , tuendelee na maisha mengine..’nikasema‘Pole sana mke wangu, najua nakupa wakati mgumu, lakini mimi sijapenda hilo, hivi kuna mtu anajitakia ajali…?’ akauliza‘Ni ajali haina kinga nafahamu..’nikasema‘Muhimu kwangu,..ni msamaha wako…na kiukweli sasa naanza kufahamu kuwa nakuumiza, nakuweka kwenye wakati mgumu sana, utanisamehe tu mke wangu, lakini haya yanahusuje  mdogo wangu,…’akasema‘Mdogo wako hana tatizo, nilikuwa naongea naye tu….mambo ya kawaida, kumuulizia maendeleo yake , kama kuna sehemu kakwama niweze kuona kama tutaweza kumsaidia…’nikasema‘Mhh…ndio hapo sitaki,…yeye anajiweza, kwanini asaidiwe, kwanini azidi kuongeza mzigo kwako, baba yako akisikia hivyo atakuja juu, na kutusimanga, mimi sipendi hilo kabisa,  na kama kuna adhabu ya madhambi yangu, basi nipeni mimi....’akasema.‘Mume wangu, ukumbuke shemeji kwangu namuona kama mdogo wangu, kama ulivyooona tumekuwa tukijitahidi kwa pamoja kumjenga katika njia njema,ya kumbadili kutoka kwenye tabia ya utegemezi kwenda kwenye tabia ya kuweza kuishi mwenyewe, na hilo tumefanikiwa, kwahiyo kila hatua pia tunahitajika kumuuliza, wewe sasa unaumwa, ni lazima mimi niwajibike naye...’nikasema.‘Ni kweli mke wangu, na inabidi nikushukuru sana kwa wema wako huo, kama ingelikuwa ni mimi mwenyewe ningelishakata tamaa, maana bwana mdogo alikuwa keshadekezwa na mama,maana yeye ni kipenzi cha mama, na wao walifikiria kwa kmfanyia hivyo ndio wanampenda,wakawa wanamdekeza, kumbe wanamharibu tusingelimwahi mapema, angeshajiunga na hayo makundi ya kuuza madawa ya kulevya....’akasema.‘Ni kweli mume wangu, hilo ni kosa wanalofanya wazazi wengi, ambao kwa kuwadekeza watoto wao ndio wanafikiria kuwa ndio mapenzi kwa mtoto, kumbe ni kinyume chake…’nikasema nikibadili mada. ‘Nashukuru sana mke wangu najua sasa naingiwa na moyo kuwa umenisamehe kabisa, kama una lolote unataa kufahamu niulize mimi mwenyewe, najuta sana kwa hayo yaliyotokea...na kama hutanisamehe, ukaamua kumsikiliza baba yako hewala, lakini mimi sizani kama nitaishi ikitokea hivyo,ni..heri ya kufa tu...’akasema‘Mume wangu usijali,..nimeshakusamehe, cha muhimu ni wewe kupona, hilo ndilo unatakiwa uliwazie jinsi gani unatakiwa kufanya mazoezi na kuondoa mawazo....’nikamwambia‘Nikipona mke wangu, nitakuwa mimi na wewe bega kwa bega, ...unajua mke wangu, wakati mwingine kama binadamu, tunajisahau…mimi nimeliona hilo kivitendo..na eeh,..na wakati mwingine inatokea kwa vile tunakuwa mbali mbali kimawazo, nawaza hivi mwenzangu vile, lakini hayo yamepita au sio mke wangu…?’ akauliza‘Ni kweli…hayo yasahau…’nikasema  


    ITAENDELEA 

0 comments:

Post a Comment

Blog