Simulizi : Pain Of Love
Sehemu Ya Tatu (3)
Yulietha kutokana na kuzuiwa na Peter kuingia chumbani kwao ikabidi atumie nguvu kuingia akaone ni nani yupo ndani mule, wakasukumizana na Peter pale mlangoni huku akilalama kwa sauti ya juu.
“Peter, hebu acha ujinga niache niingie nimuone uliyenaye ndani humo,” Yulietha alisema huku akihema kutokana na purukushani za kutaka kuingia kwenye chumba kile.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nipo, na rafiki yangu” alidanganya tena Peter.
“Yupi?.”
“Huwezi, kumjua.”
“Siwezi kumjua, kwani jini?.”
“Hapana ni mwanamke fulani hivi, amazing,” Peter alizidi kudanganya huku wakiwa bado wanapurukushana na Anitha mlangoni pale.
“Mwanamke!!!, wakati nimesikia sauti ya mwanaume humo.”
“Ni masikio yako tu, ndiyo yamekufanya usikie vibaya.”
“Haiwezekani, kuna kamchezo mnanichezea” aliongea Yulietha kwa kuashilia amehisi jambo.
Purukushani za wawili hao zikiwa bado zinaendelea mara ghafla Peter akazidiwa nguvu na Yulietha. Yulietha akapata nafasi yakuingia ndani huku akimwacha Peter amedondoka chini na kushikwa na aibu kwa kudondoshwa na mwanamke.
“Peter, hebu mwogope Mungu wako si ulisema Benson hayupo. Huyu nani?” aliuliza Anitha mara baada ya kuingia ndani na kukutana na Benson.
“Usimlaumu rafiki yangu, kwa maana mimi ndiye niliyemtuma aseme hivyo,” Benson akaingilia mazungumzo yale. Ndipo akaendelea kuongea kwa hasira.
“Wewe, mwanamke kwanini ni muuaji?.”
“Kivipi?.”
“Unatuchanganya katika mapenzi wanaume wawili...je, msomali wako angeniua kwako ingekuwa furaha, sio?.”
“Benson, msomali yule aliniapproch na nikamkataa.”
“Si kweli, ingekuwa umemkataa asingekuganda kama ruba.”
“Ni kweli, Benson.”
“Na mimi, kanijuaje kama nina mahusiano nawe?.”
“Itakuwa kapeleleza kwa watu, si unajua kuwa mtu akipania lazima ataulizia hadi afanikiwe.”
“Aliniambia niachane nawe, mimi naona bora tuachane.”
“Benson, siwezi kuachana nawe na kwanini nikuache kisa kidudu mtu aliyeingia kwenye penzi letu au umepata mwanamke mwingine?.”
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nishasema tuachane kwa kifupi, sikuhitaji nenda kwa huyo msomali wako.”
“Kwanini unaniumiza na kunitoa machozi?, angalia unavyonitoa machozi Benson huoni ni kiasi gani ninavyokupenda?.”
“Naona unajisumbua tu, ningependa utoke kwenye chumba chetu unapachulia tu,” Benson aliongea huku akimtoa Yulietha kwenye chumba chao kinguvu.
Benson roho ya huruma hakuwa nayo akamtoa Yulietha mkuku mkuku kama Mbwa koko aliyemlia mnofu na huku akimvuta kwa nguvu aweze kumtoa nje, kwa bahati mbaya akiwa anamvuta mkono Yulietha ukamponyoka. Yulietha moja kwa moja akaanguka na kujigonga sakafuni papo hapo akakata moto, hali ile ikamjengea Peter na Benson hofu wakijua Yulietha ameshakufa.
“Umeuaaa!!!” alisema Peter kwa mshangao.
“Nini?,” Benson aliuliza huku akionyesha kutoelewa na kuchanganyikiwa.
“Umeua, yaani bonge la msala lazima jela ikuite.”
“Nyamaza, yaani wewe bila tukae tushauriane jinsi gani utanisaidia ndio kwanza unanitisha.”
“Nisamehe rafiki yangu, akili yangu iliruka kidogo.”
“Sasa cha kufanya, tumchukue tumhifadhi usiku tukamtupe barabarani ijulikane alipata ajali maiti hii isije ikanikatisha ndoto zangu.”
“Nitaungana nawe, lakini yatupasa tuwe makini tusije onekana maiti ikatusababishia mengine” aliongea Peter kwa uwoga.
**********
Coletha akiwa bado yupo mapokezi akipunga upepo. Daktari mkuu alikuja kumfuata mpaka pale alipo kwaajili ya kumuona ajue anaendeaje.
“Naimani, kwasasa upo vizuri,” Daktari mkuu aliongea vile mara baada ya kufika mapokezi na kukaa jirani na Coletha.
“Nipo, vizuri,” Coletha aliongea kwa unyonge.
“Si vizuri kuendelea kukaa hapa, ngoja nikakuandikie dawa ukachukue duka la dawa uende nyumbani ukapumzike na mama” aliongea Daktari mkuu kisha wakaongozana na Coletha hadi ofisini kwake.
Coletha akaandikiwa dawa akaenda duka la dawa kununua dawa hizo hatimaye akarudi kumchukua mama yake, na kutoka naye nje kutafuta bajaji iwapeleke nyumbani.
“Bajaji,” Coletha aliita bajaji mara baada ya kutoka nje na kumuona dereva bajaji akiwa ndani ya bajaji yake. Dereva bajaji akafika aliposimama Coletha kisha akauuliza.
“Dada, una shida na usafiri?.”
“Eeeh...lakini ngoja niongee na simu ndiyo twende” alisema Coletha kisha akatoa simu yake kwenye handbag na kumtafuta baba yake akampigia.
“Daddy,” Coletha aliongea na kunyamaza kumsikiliza baba yake ajibu kwenye simu mara baada ya Mzee Swai kupatikana.
“My daughter, kwema?” aliuliza Mzee Swai kwa kujibu simu ile ya mwanae.
“Si, kwema.”
“Kwanini?.”
“Mama, amepalalaizi.”
“Mmmm, sasa,” Mzee Swai alionyesha kupuuzia ugonjwa aliopata mkewe kutokana na magomvi yao.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Naona nije naye, nyumbani.”
“Nini?, uje naye nyumbani wapi?.”
“Kigogo.”
“Ebu, nitokee huko...hana kwake?.”
“Kwake naona mbali kumhudumia, bora tuwe naye jirani kidogo ni wepesi kumhudumia.”
“Sitaki, aje kwangu.”
“Lakini, baba....”
“Hakuna cha lakini, wewe kama unataka kurudi nyumbani rudi mwenyewe lakini siyo na mama yako,” Mzee Swai aliongea kwa kufoka kisha akakata simu. Coletha hakuwa na jinsi akaweka simu yake kwenye handbag na mwisho akapanda na mama yake kwenye bajaji huku akiwa mwenye mawazo.
“Niwapeleke, wapi?” lile swali lililoulizwa na dereva bajaji likamwondoa kwenye lindi la mawazo Coletha.
“Tupeleke, Ilala Boma,” Coletha alijibu huku akiwa hana hata furaha moyoni mwake. Dereva bajaji mara baada ya kupata muelekeo akatembeza bajaji hadi eneo la Ilala Boma stendi akasimamisha bajaji kisha akauliza tena.
“Mnaishi, nyumba namba ngapi?.”
“Namba, 95,” Coletha akajibu.
“Okay,” Dereva bajaji aliitika huku akikamata chochoro za mtaa ule. Akakanyaga mafuta hadi kwenye nyumba iliyozungushiwa fensi ya bati ndipo hapo akasimamisha bajaji na kusema kwa sauti ya utiifu.
“Dada, nyumba namba 95 ni hii mbele yetu.”
“Yaah, ndiyo yenyewe,” Coletha aliitika huku akitoa pesa kwenye handbag ya kumlipa dereva bajaji. Akatoa elfu kumi na tano kisha akauliza.
“Itakuwa, bei gani?.”
“Ni, elfu kumi tu,” Coletha alipopata jibu toka kwa dereva yule akamkabidhi dereva bajaji elfu kumi kisha elfu tano yake akarudisha kwenye handbag.
Dereva bajaji alivyolipwa akawashusha abiria zake kisha akatoweka zake eneo lile, Coletha alivyoshushwa na mama yake akamkokota mama yake pole pole hadi ndani kufika ndani Coletha alipotaka kumkalisha mama yake kwenye kiti mama yake akaanguka sakafuni kutokana na kutoshikwa nga nga nga.
**********
“Maongezi, yenyewe ni...,” Anitha kabla hajamaliza kusema alishtuka kuwekewa pistol mbavuni. Kisha akasikia wakiambiwa yeye na Mathias maneno ya vitisho.
“Msilete usumbufu, mkileta fyoko tu tunawalipua.”
Mathias mwili wote ukafa ganzi kwa uwoga mara baada ya kuona njemba mbili zilizoonekana kuvalia suti nyeusi na miwani myeusi ya tinted, akaogopa zaidi alipoona Anitha ameshikiwa pistol na njemba moja lililonyoa kipara mwenye sura ngumu nyeusi. Bila kipingamizi zile njemba zikamnyanyua Anitha kinguvu huku wakiwa bado wamelengesha pistol yao mbavuni mwa Anitha, wakatoka naye hadi parking wakampandisha Anitha kinguvu kwenye gari na kuondoka naye kusipotambulika huku nyuma wakimwacha Mathias kwenye hali tata asijue alipopelekwa mlengwa wake. Kinyonge akanyanyuka kitini na kukamata lango kuu la hotelini pale alipotoka nje ya hoteli ile akaongoza stendi na kupanda gari, akapanda gari la Buguruni akashukia Tabata relini akashuka kituo kile kisha akakamata reli aelekee nyumbani Mabibo Loyola. Akapiga chochoro moja mbili tatu ghafla akasikia nyuma akiitwa na mtu asiyemtambua.
“Psiiiiiiii,” Mathias aligeuka kumwangalia mtu huyo amwitaye.
“Nisubiri,” Mtu yule alisema huku akimfuata Mathias. Mathias akasubiri hadi mtu yule alipomkaribia amsikilize.
“Ahaaa, ha haaaaah,” Mtu yule alifika huku akicheka baada ya kufika karibu na Mathias.
“Mbona sikuelewi...umefika na kucheka?” aliuliza Mathias baada ya kuona ile ni kama moja ya kejeli ya yule bwana.
“Yaani, kijana mwenyewe ndiyo wewe unayemsumbua bosi wangu,” Mtu yule aliongea maneno yake kwa dharau huku akikunja uso kwa hasira na kumkazia Mathias macho bila kupepesa.
**********http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Benson na Peter wakiwa wanashauriana. Peter akashangaa na kuduwaa kuona mwili wa Yulietha ukitingishika wenyewe akaongea kwa kupayuka kwa furaha.
“Benson, kumbe Yulietha bado hajaaga dunia.”
“Umejuaje?.”
“Nimeona, ametingishika.”
“Una macho ya kengeza, uoni mtu wa baridi huyu halafu unaniambia hajaaga dunia.”
“Acha ubishi, wewe msikilize mapigo ya moyo,” Benson akamsikiliza mapigo ya moyo Yulietha mara baada ya kupokea ushauri kwa rafiki yake. Alisikiliza mapigo ya moyo na kuguna.
“Mh, mbona mapigo ya moyo hayadundi huyu ame...,” Benson kabla hajamaliza kuongea akamsikia Yulietha akikohoa hapo ndipo akaamini kuwa Yulietha bado yu hai.
Yulietha baada ya muda akazinduka toka kwenye manusura ya kifo, na kuwaona Benson na Peter wamemsimamia mbele yake huku wakiwa wameduwaa kwa kumshangaa. Akajifikicha macho aone vyema kisha akawatundika swali Benson na Peter.
“Kuna nini?, mbona mnanitumbulia macho?” lile swali liliwafanya kila mmoja wao arudi kwenye ufahamu wake na haraka Benson akaropoka.
“Ulizimia.”
“Nilizimia!!!?,” Yulietha aliuliza na kuonyesha hatambui chochote kilichotokea.
“Eeenh,” Benson akajibu.
“Nini sababu, ya kuzimia?,” Swali lile lilimjengea hofu ya kuendelea kujibu Benson kwa kuwa yeye ndiye chanzo cha kupelekea kuzimia kwa Yulietha hakujibu.
“Nini sababu, ya kuzimia?” liliulizwa tena lile swali na Yulietha mara baada ya kuona hajajibiwa swali lake. Peter akakohoa mfululizo kisha akamtazama Yulietha kwa haya na kumwambia kilichojili hapo awali.
“Uliponyoka kwa bahati mbaya, kwenye mikono ya Benson.”
“Wakati, nafanya nini?,” Maswali hayakumuisha Yulietha. Akazidi kuuliza kama afisa upelelezi.
“Wakati mkiwa, kwenye purukushani na Benson.”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Purukushani, ya nini?.”
“Ya kutolewa nje kinguvu, baada ya kugoma kutoka nje kwa hiari yako,” Yulietha alimgeukia Benson ambaye kwa muda wote alikuwa akiangalia chini kwa haya kama mtu aliyeshikwa ugoni. Kisha akampachika swali huku akimuinua uso waweze kuonana ana kwa ana bila kuoneana aibu.
“Eti, ni kweli anachozungumza Peter?.”
“Ni ni, kweli” alijibu Benson swali lile kwa kigugumizi. Tendo lile lilifanya Yulietha aangue kicheko na kumfanya apate ujasiri wa kummudu Benson kwa kumpelekesha atakavyo mara tu alipogundua Benson ametawaliwa na woga.
“Kumbe ni jasiri wa sura tu, ndani ya roho kumbe ni mwoga wa kutupwa,” Yulietha aliongea huku akizidi kucheka hadi kupelekea gego lake kuonekana hadharani.
“Acha niwe mwoga...unadhani kuozea segerea kuna mtu anapenda” aliongea Benson kisha akashusha pumzi ndefu.
“Nitaanzaje kwa mfano, kumpeleka mtu nimpendae segerea” aliongea Yulietha kwa utani uliojaa ucheshi ndani yake.
“Unanipenda, au unaniigizia tu?.”
“Kweli nakupenda...ninavyokupenda sidhani kama kuna mwingine nitampenda kama wewe.”
“Haya, kama kweli unamaanisha.”
“Umenisamehe?.”
“Nishakusamehe.”
“Nisindikize basi, kwenye hosteli yangu.”
“Siwezi, toka leo.”
“Kwanini?.”
“Tunajisomea.”
“Nisindikize, hutokawia kurudi.”
“Nitakusindikiza...lakini timiza kauli yako,” Benson alisema kisha akamwangalia rafiki yake na kumuaga.
“Peter akaachwa peke yake ndani. Benson na Yulietha waliondoka huku wakiwa wameshikana mikono na kukaribiana kwa ukaribu mkubwa miili yao, mapenzi yao yalikuwa ni moto moto kwa muda ule kama nyuki achavuapo ua. Walishikana namna ile hadi katika hosteli ya wanawake bila kumuonea haya kiumbe hai chochote, Yulietha alipofika kwenye chumba chake akafungua mlango. Benson alitaka kumtoa Yulietha mkono kwenye mkono wake aondoke lakini Yulietha hakukubali akawahi kumdaka mkono na kumvuta chumbani kilazima na kufunga mlango, Benson akakalishwa kitandani kisha Yulietha akaelekea kwenye jokofu kuchukua mzinga wa Konyagi na glasi mbili hatimaye akarudi alipomwacha Benson na akataka kumkabidhi glasi moja Benson. Benson alitahamaki kisha haraka akauliza kabla hajapokea glasi ile.
“Yulietha, haya ndiyo makubaliano yetu?.”
“Hapana...ila nisamehe” alijibu Yulietha huku akionyesha sura ya kutabasamu kama aliyoyafanya ni mazuri.
“Kwa hiyo, uliyoyafanya ni makusudi” alisema Benson kwa kukunja ndita.
“Sijafanya makusudi...ila nimefanya hivi ili nikudhihirishie kuwa nakupenda.”
“Unidhihirishie nini, wakati nishakuambia kuw...,” Benson ajamaliza kuongea akasikia mlango ukibishwa hodi kwa nguvu kwa kuashilia kuwa mtu anayegonga amejawa na ghadhabu.
**********
Coletha alimuinua mama yake sakafuni japo kidogo mama Coletha alitoka uvimbe kwenye paji la uso kutokana na kuanguka. Akamketisha mama yake kitini kwa umakini, kisha akaenda kumchukulia maji ili ameze dawa alimnywesha dawa kisha akamwacha apumzike kwa muda. Mama yake alipolala naye Coletha akachukua nafasi ile kujipumzisha kwa muda palepale sebuleni, masaa kadhaa mbele kwa mbali Coletha akiwa usingizini alisikia hodi ikibishwa kwenye mlango wao. Mdogo mdogo akaelekea mlangoni kufungua mlango ili ajue ni nani anayebisha hodi, alipofungua akakutana na uso wa baba yake. Uso ulioonesha kubeba kitu cha siri ndani. Mzee Deus Swai alipomwona mwanae amesimama mbele yake akamvuta mkono watoke nje kuzungumza.
“Wewe mtoto, tahira?,” Mzee Swai aliongea kwa kufoka na kuonyesha kana kwamba tendo alilofanya mwanae hajalipenda.
“Kivipi?,” Coletha aliuliza ili ajue baba yake anamaanisha nini pindi alivyosema vile.
“Umesahau kuwa, huyu mama alikutelekeza.”
“Sijasahau.”
“Kama hujasahau, mbona umejitolea kumhudumia kama mtu usiye na kinyongo kabisa rohoni.”
“Baba hukumbuki ule msemo usemao kuwa, adui yako akikutendea baya mlipe kwa jema.”
“Lakini, siyo kwa huyu mwanamke...mwanamke baladhuri sana huyu.”
“Acha kuhukumu baba, maana kila mmoja hapa duniani hajakamilika.”
“Nitaacha kuhukumu kwa watu wengine, lakini si kwa mama yako...nashangaa wewe mtu kakufanyia unyama lakini bado unamganda una nini wewe?.”
“Bado, nampenda mama yangu.”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Unampenda, mama yako!!!?...mimi napinga na leo ulali hapa niking'oa mguu wangu nawe nyuma unanifuata” alifoka Mzee Swai kwa sauti kali na kuonyesha wazi wazi kuwa anamchukia mkewe kutokana na kutalakiana kipindi cha nyuma kwa sababu ya malumbano yao.
**********
“Mlimpata, wapi?” aliuliza Mzee wa makamo aliyetambulika eneo lile la Masaki kwa majina ya Panta Guno mara baada ya Anitha kufikishwa kwenye mjengo wake na kijana wake wa kazi.
“Tumempata, kwenye hoteli ya LANDMARK akiwa na kijana mmoja hivi,” Njemba lililonyoa para na kujulikana kwa jina la Dosagon lilijibu swali aliloulizwa na bosi wake.
“Kijana huyo ndiye anayetembea na binti yangu...Norman yupo wapi?.”
“Norman, amemfuatilia kijana huyo.”
“Huyu, hakwenda na gari?.”
“Anitha?.”
“Eenh.”
“Ameenda, nalo.”
“Sasa fanya hivi, mwanangu mfungie chumbani kwake kisha nenda kamfuatie gari lake,” Mzee Panta Guno alitoa maagizo kisha akachukua simu ya mkononi iliyokuwa mezani akatafuta namba ya Norman na kupiga mara baada ya Dosagon kumpeleka Anitha chumbani kwake kinguvu na kuondoka kufuata gari.
“Hallow, bosi” ilisikika sauti ya Norman upande wa pili ikizungumza kwa sauti ya wastani.
“Mpuuzi huyo, umemfuatilia hadi wapi?” aliuliza Mzee Panta Guno huku akichukua Kiko yake iliyo mezani avute.
“Nimemfuatilia hadi Mabibo, na sasa nipo naye hapa.”
“Hebu...mpatie simu niongee naye,” Norman akampelekea simu Mathias sikioni mara baada ya kupokea agizo kwa mzee Panta Guno. Kisha akamwamuru Mathias aongee haraka na bosi wake.
“Kijana Gerald Eduardo, wewe ndiye galacha wa kutembea na watoto wa watu...acha mara moja kabla sijakuharibu na kukuangamiza,” Mzee Panta Guno aliongea kwa vitisho na kumuonya Gerald kama anavyodhani asiendelee kumfuatilia mwanae kipenzi.
“Mimi si Gerald Eduardo, mimi ni...,” Mathias kabla hajamalizia kusema Norman akatoa simu sikioni mwa Mathias na kuendelea yeye kuongea na bosi wake.
“Bosi, nadhani ushamsikia.”
“Nimemsikia na nishampa onyo, hivyo basi achana naye ila akirudia nitajua nini cha kufanya,” Mzee Panta Guno alitoa oda kwa kijana wake kuwa Mathias aachwe kisha akakata simu.
Norman akamuacha kweli Mathias kisha yeye akaenda kudandia daladala na kurudi Masaki kwa bosi wake. Mathias alivyoachwa akaendelea na kuzimalizia chocho na hatimaye akatokea kwenye nyumba aliyopanga na kuingia ndani, alijilaza kitandani kwa muda mara baada ya kuingia ndani jioni aliamka akaingia mtaani kutafuta chakula migahawani kwenye mgahawa mmoja wapo ndipo alipopata chakula alinunua kisha akakamata njia ya kurejea nyumbani. Baada ya kukatiza chochoro zipatazo mbili, hamadi! akavamiana na kibaka aliyekuwa anakimbizwa na raia kwasababu ya kukwapua handbag ya mdada mmoja humo mtaani, kibaka aliacha handbag pale chini alipodondoka Mathias kisha akaendelea na mbio huku nyuma akamwachia balaa lile Mathias. Mathias aliinuka na kujikung'uta mara punde raia hawa hapa wameshamweka mtu kati na kila raia alionekana kushika silaha kali za kumsurubu kibaka yule, raia wote walionekana na hasira kila mmoja wao aliweka sura ya mbuzi kwa Mathias wakijua ndiye mwizi wao kumbe la hasha! mwizi wao alishakimbia na kuamua kumuuzia kesi Mathias bila kujua.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mwizi wetu, ndiyo huyu?” alisikika mzee mmoja akiuliza raia wenzake kwa sauti ya juu.
“Mzee huoni handbag hapo chini...huyu ndiye mwizi wetu,” Kijana mmoja alimjibu mzee yule huku akifungua dumu la petroli na kummwagia Mathias mwilini.
Akatokea kijana mwingine asiye na huruma aliyejawa na roho ya ukatili akapeleka mkono wake wa kushoto kwenye mfuko wa shati yake, kisha akaonekana kutoka na kiberiti cha njiti alitoa njiti moja ya kiberiti na akahangaika kuwasha. Njiti ya kwanza ikagoma kuwaka akachukua ya pili akawasha ikawaka.
**********
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment