Search This Blog

Friday, November 18, 2022

FUNDO LA UMIVU - 1

 






IMEANDIKWA NA : HASSAN MBONECHE



*********************************************************************************



Simulizi : Fundo La Umivu
Sehemu Ya Kwanza (1)


 “Hitajio nililopata kuwanalo, ipate tokea siku, sauti yangu iwe na nguvu yenye kusikika. Na yule aisikiaye aielewe na kufanyia kazi asikiacho. Niliyomchagua kuwa msikilizaji, niliomba awe msikivu zaidi, ya wote wanisikiao japo nina matatizo ya matamshi. Ila niliamini na kuwa na uhakika, juu ya kasoro zote nilizonazo atanisikia vyema. Kila herufi niliyothubutu kuitamka toka ndani ya mdomo wangu, niliitamka kwa nguvu, kumfanya yule mteule afarijike, na si kuhuzunika, asikiapo harufu ya tamshi nilitamkalo.”



Usiku wa Oktoba 22, 1993 mnamo majira ya saa 7 ilisikika sauti ya mtoto mdogo, yenye uashirio wa kuingia duniani, akipokelewa na wamama wachache waliozingira na kukizunguka kitanda alicholazwa mama wa mtoto. Alipokelewa kwa shangwe na shamra shamra nyingi, kufurahia ujio wake, sababu tu, mama wa mtoto kaingia kwenye ulimwengu mwingine. Ulimwengu wa wana, alioulilia muda mrefu na mumewe. Alivyopatiwa taarifa, hakusita kuonesha furaha yake, baada ya kuyatua matatizo ya muda mrefu aliyoyavumilia, pindi alivyombeba mwanae tumboni. Kingine kilichoongeza furaha yao, ni jinsia, ombi waliloliomba mara baada ya ujauzito kupatikana, wapate mtoto wa jinsia ya kiume. Kwa kuamini atakuwa na msaada mkubwa siku za usoni.



Mtoto ni baraka! Familia, waliuhusudu huu msemo. Kwa kumtunza vyema asihudhurike na matatizo yasiyo na msingi, yenye kuwagharimu. Walihitaji mtoto wao awe miongoni mwa watoto bora mtaani, hata kama uwezo kiuchumi uliwapiga chenga. Ilikuwa familia maskini, iishio nyumba ndogo yenye chumba kimoja na sebule ikiwa imeezekwa kwa nyasi. Sakafu, waliisikia! Ndani ya nyumba yao ilitawaliwa na udongo chini, tena ambao kwa muda fulani hukuisha kujitengeneza kichuguu, kutoa makazi kwa mchwa. Wadudu watambaao na warukao hawakukosa, yote ni kutokana na mazingira jirani yalivyo. Yalikuwa machafu, japo walijitahidi kuyasafisha kila baada ya siku fulani.



Hali ya uchumi kuwa chini, hakikuwa kigezo kwao kupunguza upendo kwa mwanaye. Walimpenda, tena walimpenda sana. Upendo ulioigwa na majirani, ndugu, rafiki na jamaa wengine pia kumpenda mtoto huyu. Ambaye tayari alishakuwa gumzo. Kwa sababu ya maumbile aliyonayo. Alikuwa mwembamba, mwenye sura ya mvuto, huku akibashiriwa kuwa mrefu. Ucheshi wa kila muda kwa kila aliyediriki kumbeba, uliwavuta wengi wawe na mapendo naye na kutamani kila baada ya muda awe jirani naye, ili aondoe fukuto la huzuni awanapo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Hakika! Alikuwa sehemu ya kumbukumbu kwao. Kwani, ndiyo kwanza, aliwafungulia ulimwengu wa watoto, pia alisahaulisha sehemu ya maumivu kwa wazazi. Siku aliyozaliwa, ni siku ambayo, baba wa baba wa mtoto alipoteza uhai na kuelekea ulimwengu mwingine wa raha na tulivu tele utaopitiwa na kila binadamu. Hivyo kuendeleza kumbukumbu yao, mwanaye walimpatia jina la babu yake, ili naye atavyokuwa, awe na ufahamu rahisi wapi jina lake litokeapo.



Vumilia! Ndiyo jina pendwa alipatiwa. Jina la marehemu babu yake, huku baba akiitwa, Matatizo, na kufanya mtoto kuitwa Vumilia Matatizo. Waliyejiuliza, na kuuliza wanafamilia kulikoni, katika wakati huo wa kisasa mtoto wao kumpatia jina hilo, walipatiwa historia fupi tu, namna mama wa babu, alivyopatwa na matatizo akavumilia, hivyo uvumilivu alioufanya akaamua kumpatia mwanaye jina la vumilia. Wakati huo Matatizo, lilimaanisha matatizo yaliyowapata Mzee Vumilia na mkewe. Pindi mkewe akibeba ujauzito.



Baadhi yao walikuwa hawajibiwi, baada ya kubaini wanasumbuliwa na kutumia muda mwingi kuhadithia. Uvutio toka kwa Vumilia, ulikuwa mwingi tu, sio umbo pekee, bali hata jina, lilikuwa sehemu ya kivutio. Watu walisisimka wamuitapo, japo walijawa na dhihaka kwa kiasi kikubwa kulidhihaki jina hilo. Hawakujali maneno ya watu! Kadri siku zilivyozidi kusonga mbele, ndivyo Vumilia alivyozidi kukua, kuimarika kiafya na kuendelea kupendwa pia na watu wa rika na jinsia zote. Kila mtaa aonekapo, hakuisha kunyooshewa vidole, mtoto wa Matatizo anapita. Mzee aliyozoeleka kwa harakati za kisiasa za chama tawala kijijini kwao, ngazi ya kata. Liberation Party (LP). Akiwa kama Katibu Kata, na ndiyo kazi pekee aliyokuwa anajihusisha nayo, achilia mbali kilimo, shughuli kuu.



Alivyofikisha umri wa miaka minne, aliandikishwa kuanza masomo ya chekechea katika shule ya msingi Kilimanihewa, iliyopo wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara. Kuungana na wanafunzi wenziye, wenye umri unaolingana naye, japo kuna baadhi walimzidi na wengine kuwa chini yake. Kupitia malezi aliyolelewa, alikuwa rafiki wa kila wanafunzi katika darasa lao na wanafunzi wote wasomao chekechea kwa ujumla. Na hiyo yote ilitokana na umbo lake, wembamba alionao, uliomfanya kila amuonaye kumtania naye kujibu mapigo kwa kurudisha matani. Hiyo ilimjengea kujiongezea umaarufu, sio kwa wanafunzi, bali hata kwa waalimu, kwani yeye ndiyo alikuwa mwanafunzi pekee mwenye umbo dogo darasa na shule nzima. Achilia mbali hayo, uwezo wa kielimu pia alikuwa nao. Uwezo wake ulikuwa mkubwa, uliomjumuisha kuingia katika orodha ya wanafunzi kumi bora wafanyao vizuri kidarasa.



Jitihada zake zilionekana wazi, kupitia muonekano wake. Muda mwingi alionekana mkimya, hali iliyochangiwa na namna alivyokuwa analelewa. Kwani wazazi wake walikuwa wakali mno, hali iliyomjengea woga kwa kiasi fulani, ili atii matakwa yao. Ukimya wake ulimfanya kupatiwa majina ya ajabu, angali yuko mdogo, kama vile lofa, mshamba, na mengine mengi yaliyomfanya naye azidi kujisikia vibaya. Huku wazazi wake nao kwa wakati fulani, kupitia hali hiyo pale akoseapo hawakusita kumuita mtu wa hasira na lofa. Neno lofa, halikuwa jema kwake, na lilichangia kuanza kujiweka nyuma, katika shughuli mbalimbali za michezo na wenziye, sio nyumbani, hata shule pia. Muda mwingi akawa mtu wa kujitenga, hali iliyochangia kwa kiasi kikubwa, uthamani aliokuwa anajiona anao kuanza kupotea.



Hata uwezo wa kuzungumza mbele ya watu, iwe kwa watoto wenziye ama waliomzidi umri ulikuwa mgumu kwake. Hakuwanao! Uoga na aibu vilimtawala. Hali hiyo ilimpa na kumuondolea unguvu wa uanaume, mbele ya watoto wa kike. Kujieleza lilikuwa jambo gumu sana, akibananishwa ajitetee. Juu ya kasoro hizo, juhudi za kimasomo darasani hazikupungua, aliendelea nazo, na kuwa miongoni mwa wanafunzi tishio darasani. Alipofika darasa la nne, alibahatika kuingia kwenye mahusiano ya urafiki, na mmoja wa wasichana wa darasa moja anayesomanae, ajulikanaye Shakila. Ambaye alikuwa mtoto wa mwalimu wa shule wasomaye. Urafiki wao, haukuchangiwa na uwezo wa darasani, ni maelewano tu, ya namna kila mmoja anavyomkubali mwenziye moyoni mwake. Kila kukicha, mara baada ya masomo kumalizika hawakuisha kukutana, ama hata kipindi cha masomo pia, kucheza michezo ya hapa na pale, au kufanya maongezi kadha wa kadha, juu ya matamanio waliyonayo.



Haukuwa urafiki wa kishule shule pekee, hata nyumbani pia. Kwani, mara nyingi, Vumilia hakuisha kudhuru nyumbani kwa kina Shakila, kiasi kwamba, mfanyakazi wa ndani na mzazi wake, mama aliyekuwa anaishi naye walipata kufahamu urafiki wao. Watu wa pembeni, wakawa na macho mengine, juu ya mahusiano waliyonayo, ilhali wahusika walikuwa nje na mtazamo wa watu hao, japo kuna wakati walikuwa wanasikia kitu kipi wanazungumziwa.

“Ninyi munafaa kuoana,” alisikika mama mmoja aishiye karibu nyumbani kwa kina Shakila, alipowaona wakikatiza nyumbani kwake.



Siku zilizidi kusonga mbele, hadi wanafikia darasa la saba, urafiki wao uliendelea kuwa imara. Walivyohitimu elimu yao ya msingi, ndiyo uliimarika zaidi, muda mwingi walionekana kuwa pamoja, hadi ikawa kero kwa baadhi ya watu wawaonao. Hamna sehemu walikosa kushirikiana hasa mchana, katika shughuli mbalimbali waagizwazo, kama vile kuteka maji, kwenda sokoni kununua mahitaji na nyinginezo. Dhamira ya kuwa, wako katika mahusiano ya kimapenzi nayo ilipanda ndani ya mioyo ya watu waliokuwa wanawaangalia kila uchao na wale wanaofahamu mahusiano yalipoanzia. Hususani marafiki wa kiume wa Vumilia, hadi ilifikia kumuita baba shakila na kumshinikiza amtongeze, ili wadumishe mahusiano yao zaidi. Hapa! Ulikuwa mwiba mkali kwa Vumilia. Kwani, neno kutongoza, aliliona kama sumu kwake, anaanzaje kumtamkia msichana anampenda, maneno yapi yanatumika, ni mtihani! Alikuwa domo zege.

“Tongoza yule mtoto wewe, sio unamlea mlea kila siku,” alisema rafiki yake mmoja wakiwa wanabangua karanga, chini ya mti wa muembe, nyumbani kwao rafiki yake.

“Aaaah! Naanzaje kumtongoza? Yule ni rafiki yangu tu.”

“Sema domo zege, mtoto anakuonesha anakukubali kabisa, halafu unasema rafiki. Kama huwezi kutongoza, omba mtu akutongozee. Ama la sivyo subiri uone vijana wengine wakijichukulia. Wewe zubaa tu.”

“Kama hauna lingine la kuongea, achana na hizo habari.”



Sio kama hakuhitaji kutoa neno, litalofanya awe na mahusiano ya kimapenzi na Shakila, kwani matamanio alikuwanayo, tatizo lilikuwa mdomo wake kufunguka kulitoa hilo neno. Hakuwa na uwezo wa kusimama mbele ya msichana kumtamkia maneno yahusuyo mapenzi, aliishia kuwaza na kujawa na matamanio kila kukicha, nitamwambia na fikra namna itavyokuwa mara baada ya kuwa wapenzi. Lakini matokeo yake yalikuwa hivyo.



Alikuwa na matamanio, naye kuingia katika mahusiano ya kimapenzi siku moja, ila kubwa, ndiyo hivyo, hawezi kuzungumza. Ataimudu vipi hii hali? Hakujua.

“Nikiwa mkubwa, nitapata tu mpenzi,” alisema kimoyomoyo, usiku mmoja akiwa katika kitanda cha kambaa amelala.



Japo umri wake haukuruhusu kuanza, ama kuingia kwenye mahusiano ya mapenzi, ila alishawishika kuingia humo, baada ya vishawishi vingi toka kwa marafiki zake wa kiume alionao, ambao walishajihusisha na hayo mambo tangiapo. Kitendo cha wenziye kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi, halafu yeye kushindwa, kiliendelea kumsononesha, na kumuongezea utengano na wenziye. Kwani mara nyingi alikuwa anataniwa, hivyo kuepukana na hilo, ilimlazimu muda mwingi kutulia nyumbani, hata kwenda na kuonana na Shakila, ikawa kwa nadra sana.



Hali ilibadilika! Usiku mmoja wa siku ya jumapili, alipopatiwa taarifa na mmoja miongoni mwa marafiki zake kwamba, ameshaingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na Shakila, huku akiwa mwanaume wa kwanza kumtoa bikra. Aliumia, mfadhaiko hakukosa, kwani zake hisia nazo zilionesha mapendo kwa msichana huyo, japo kutamka ilikuwa ngumu. Taarifa hii ilivunja mahusiano ya urafiki, baina yake na Shakila, hata yule rafiki aliyempatia taarifa. Waligeuka maadui, tena hakutamani hata kuwaona mbele ya mboni zake, hali iliyochangia kuendeleza kujiona mtu asiye sikilizwa mbele ya watu. Na yule asiyethaminika pia! Akijumlisha kauli aambiwazo, na zile za utani.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Mdomo, ulikuwa mzito, hakuweza kuzungumza, kiasi kwamba fursa mbalimbali aliishia kuziangalia, kutokana alijawa na uoga wa kuzungumza. Akihofia kuchekwa na kudharauliwa zaidi kila muda. Naam! Vumilia alikuwa mwingi wa mambo, hasa ya huzuni, ya furaha kwake, aliyasikia ndotoni, kutokana na hisia zilizomtawala.



Mnamo mwaka 2007 alibahatika kujiunga na elimu ya sekondari, katika shule ya kutwa ya sekondari Mangaka. Huku nako mambo hayakubadilika, alikuwa kama vile alivyokuwa shule ya msingi. Uoga uliendelea kumsumbua, japo hakubanduka katika orodha ya wanafunzi wafanyao vizuri darasani. Jina lake lilizidi kukua, siku hadi siku, jitihada alizozionesha zilimbeba, na kupelekea kumuweka karibu na watu wengi. Wasichana baina yao. Ukaribu huo uliendeleza hitajio, la muda mrefu, lililopo moyoni mwake, kuhakikisha kuwa, anapata msichana, atayekuwa kwenye mahusiano naye. Ukizingatia na uwezo wa darasani alionao, aliamini, haitomsumbua katika ufanikishaji. Kwa kujua siku zote watu wenye akili hupendwa. Ilhali kutamka, liliendelea kuwa suala ngumu. Hitajio halikuwa kwa wasichana wa sekondari pekee, hata shule ya msingi, msichana yeyote atayetokeza kuvutiwa naye atupe karata. Hatimaye alianza tafiti, sehemu ya kwanza, ni sekondari alikokuwa anasoma kwa wakati huo. Aliwatathmini wasichana wote, alionao kidato kimoja, wengi wao, alivutiwa nao, na kujiapiza, ahakikishe anakuwa na mmoja wapo.

“Tuna wasichana warembo sana humu darasani, kama yule, msichana mweupe aitwaye Mwajuma, ni mzuri sana. Nifanye jitihada nimfukuzie. Ila nitaweza kweli kumgharamia? Maana hawa wanahitaji pesa, nami sina hata uwezo wa kumiliki shilingi elfu moja kwa mwezi, labda mpaka niombe kwa wazazi,” aliwaza Vumilia, siku moja akiwa dawatini kwake tuli ameketi.



Wazo, alilifanyia kazi. Siku zilizofuata alianza kuwa karibu na msichana huyo, afahamikaye kwa jina la Mwajuma Stambuli. Muda mwingi akawa karibu naye, katika maongezi ya hapa na pale kuhusu masomo na mambo mengine ya ziada. Hakikuwa kitendo cha siku moja, hapana! Ilikuwa ni muendelezo, lakini kila kukicha maongezi yalikuwa yaleyale, yakiongezeka ni machache, kwani uoga na aibu, viliendelea kumsumbua, pia kikubwa kilichomtesa ni kujilinganisha na watu. Kwamba yeye hana uwezo, hivyo hawezi pendwa. Kutoa hisia zake ikawa ngumu, tena baada ya kuona wanaume wengi walio nadhifu zaidi yake walivyokuwa wanamfuatilia msichana huyo, akaamua kukata shauri la kutoendelea naye.

“Acha niangalie upande wa pili, wasichana wa kule ndiyo nilio na uwezo nao,” alisema Vumilia kimoyomoyo. Akiwa na maana, amtafute msichana wa shule ya msingi awe kwenye mahusiano naye.



Kauli hii aliitekeleza siku iliyofuata, mara baada ya kukutana na rafiki yake, asomaye shule ya msingi, aitwaye Rajab na kumueleza shida aliyonayo.

“Sasa unahisi ni msichana gani atakufaa?” Aliuliza Rajab baada ya kuambiwa.

“Nawe yafaa kunishauri. Maana ndiyo unawafahamu wasichana wazuri waliopo shuleni kwenu kwa sasa.”

“Wazuri ni wengi. Niambie yupi unavutiwa naye, mimi nikikutajia, naweza taja msichana ambaye hatokuvutia.”



Vumilia alifikiria kwa muda, takribani dakika mbili, kuzitathmini sura za wasichana, yupi amchague. Alivyokuja zinduka, alitoka na jibu sahihi.

“Somoe Omar!”

“Basi haina shida. Njia ipi utaitumia kumfikishia ujumbe?”

“Mmmmmh!............ Barua.”

“Sio ukutane na mwenyewe umuambie, maana ndiyo njia nzuri zaidi ya barua.”

“Hapana! Kwangu, barua ndiyo sahihi.”



Karatasi, ilitafutwa. Plane paper kisha akaanza kutiririka muandiko mzuri uvutiao. Haikumchukua muda mrefu, ni muda mchache tu, alihitimisha, baada ya hapo, alifuatia kuchora marembo rembo mengi yanayoashiria upendo. Kopa! Hakuhitaji kupeleka ikiwa wazi, hivyo alitafuta bahasha, kwa kuwa hakuwa na uwezo wa kununua, alimuomba mmoja miongoni mwa marafiki zake, aitwaye Emmanuel, baba yake aliyekuwa hakimu wa kijiji chao, amtafutie. Emmanuel alitii ombi lake, mapema siku iliyofuata alimpatia Vumilia bahasha naye kuihifadhi vizuri barua yake isionwe onwe ama kuchafuliwa na yule atayemkabidhi. Muda wa kuelekea shule ulipowadia, tayari barua ilishamfikia Rajab, apeleke kwa mhusika.



Wakati huo Vumilia alikosa uvumilivu, muda mwingi akili yake iliwaza mrejesho wa barua aliyotuma utakuwa vipi. Pili alikuwa anakesha kuomba isionwe na mtu mwingine, zaidi ya mpelekaji na mhusika pekee ili ibaki kuwa siri. Lundo la mawazo, lilikuwa la kutosha, mambo yatakuwa vipi yakiharibika? Aliumiza kichwa pasi na muafaka. Hali iliyochangia kwa kiasi kikubwa siku hiyo akose amani moyoni mwake. Mnamo saa 9 alasiri, walivyoondoka shule, hawakuhitajika kurudi, uamuzi ambao kidogo ulimpatia furaha, kwa kuamini muda uliosalia, atautumia kusubiri majibu yake na si vinginevyo.



Ilikuwa ni mara ya kwanza kutupa karata kwa mtoto wa kike, japo haikuwa njia ya ana kwa ana, ila ilimuaminisha hata hiyo inasaidia kwa hali aliyonayo. Hakuwa na hisia, kwamba mwenziye anaweza mgeuka, kwa kuivujisha ile barua ama kwenda mwenyewe kumtongoza msichana huyo. Alimuamini! Saa 10:30 jioni wanafunzi wa shule ya msingi walianza rejea mtaani toka shule. Wakati huo Vumilia alikuwa nyumbani kwao anahitimisha kuosha vyombo walivyotumia kulia chakula. Mara baada ya kuviweka sehemu husika, alitoka mbio kuelekea nyumbani kwa kina Rajab. Aonane naye ili ampatie taarifa ya nini kilichoendelea, kama kafanikisha kumpatia mhusika barua, ama bado. Akiwa njiani, alipishana na wanafunzi wengi, waliokuwa wanacheza na kufanya vitu vingine pindi wanaelekea makwao.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Kwa haraka aliyonayo, hakuwatilia sana maanani, alizidi kupiga hatua kusonga mbele, hulka ya kutaarifiwa kitu kisumbuacho moyo wake kilitamalaki sehemu kubwa ya akili na moyo pia. Lakini ghafla, hulka hiyo ilisitishwa na kicheko kilichoambatana na kauli mbele yake iliyoonekana moja kwa moja kumhusu, na kumsitisha ghafla, kisha kuangalia sauti hiyo itokako. Umbali wa mita mia mbili, upande wa mkono wake wa kuume.

“Eheheheeeeee!...... Barua yako tumeiona,” ilisikika sauti hiyo toka kwenye kundi la wasichana wapatao tano, barabara kabisa, pasi na kizuizi cha kuifanya ipindishe maneno ndani ya ngoma za Vumilia.



Alisita, hulka iliisha, uoga na aibu, vitu vya asili yake, viligubika na kumkosesha amani ya moyo. Taratibu, aligeuza macho yake, kuwaangalia wasichana waliotoa kauli hiyo, kama kuna anayemfahamu miongoni mwao, baada ya tathmini kwa kina, na kwa sababu walishasogea, baadhi yao aliwang’amua. Ni wasichana walioko darasa moja na yule aliyemuandikia barua. Aliduwaa, kuficha aibu kabisa mbele yao, alianza upya mwendo wa kukimbia, tena kwa kasi zaidi ya mwanzo. Kitendo kilichowapa nafasi, wale wasichana kwa mara nyingine kutoa kauli kumfikia.

“Lako hilooooo! Mwenzangu na mimi, ulivyokuwa hujiwezi hadi bahasha umeazima.”

“Eheheheeeeee! Unalooooo,” waliendelea kusema wasichana hao. Kauli zilizokuwa umivu kwa kiasi kikubwa moyoni mwa Vumilia. Ila hakuweza kuzijibu, sababu hakuwa muongeaji. Pia aibu na uoga alionao, ulichangia, kwani ungemfanya ashindwe kukamilisha neno, ama asisikike aongeacho. Hivyo ilimlazimu kukaa kimya, ili asionekane kuwa hawezi kuzungumza.





Baada ya mwendo wa dakika sita alifanikiwa kuwasili nyumbani kwa kina Rajab. Ilivyo bahati, alifanikiwa kumkuta. Walivyoonana, waliitana chemba na kuanza kuzungumza.

“Nini kimetokea?” lilikuwa swali la kwanza toka kwa Vumilia.

“Nini tena? Mbona uko na haraka hivyo?”

“Kuna watu nimekutana, wameniambia wameona barua yangu. Ilikuwaje hadi waione?”

“Duh! Kuhusu hilo sijajua. Maana nilimkabidhi kisha nikaondoka zangu.”

“Lini kaahidi kutoa jibu?”

“Yeah! Atatoa jibu lako kesho!”

“Shukrani sana rafiki. Nakutegemea.”

“Hamna shida.”



Ujumbe tu, wa kuambiwa kesho atapatiwa jibu ulikuwa sehemu ya ushindi kwake. Alifurahi, japo hakufahamu jibu la aina gani atapatiwa. Alirejea nyumbani kwao, akitawaliwa na morali ya hali ya juu, ya shauku kuisubiria kesho afahamu hatma ya maombi. Lepe la usingizi alilipata kwa tabu sana usiku wa siku hii, kutokana na lindi la mawazo, yaliyochanganyikana, furaha na huzuni, huku akiona kuchelewa kupambazuka. Usingizi ulimjia usiku wa kiza kinene, karibu kabisa na mapambazuko. Hakutumia muda mwingi kulala, kwani asubuhi, kama ilivyo ada, aliamka na kuendelea na ratiba zake.



Jioni ilivyowadia hakusita, kuelekea nyumbani kwa kina Rajab, kupokea mrejesho wake kama alivyoahidiwa. Alibahatika kumkuta, wakasogezana pembeni kisha kuanza kumwagiana umbeya. Habari iliyotoka kwa Rajab kumfikia Vumilia, ilikuwa habari njema, iliyokonga moyo na kujaza tabasamu tele usoni, aliruka na kushangilia, kwani alikuwa haamini kama itapata tokea siku, kilio chake kikajibiwa.

“Dogo kakubali, ila kasema msubiri hadi amalize shule, ndiyo muanze vizuri hayo mambo. Si unajua kuwa mwaka huu ni darasa la saba?”

“Yeah! Nafahamu.”

“Kwa hiyo ni hivyo tu, hamna kitu kingine kazungumza zaidi.”

“Hamna shida nitamsubiria tu,” alisema Vumilia, kwa sauti iliyojaa furaha, kufurahia jibu alilopatiwa.



Walivyomaliza maongezi, Vumilia alirejea nyumbani kwao, na Rajab pia.



Mahusiano yalianza, lakini cha ajabu hakuna hata siku moja wawili hao walibahatika kuonana, japo kutakiana hali. Vumilia alimuogopa Somoe, kwa namna moja ama nyingine, kwa sababu ya uoga wake uliokithiri. Hadi ilipofikia mwezi oktoba, Somoe alivyohitimu elimu yake ya msingi, hakuna siku yoyote wawili hao walikutana. Huku akili ya Vumilia ikimuaminisha kuwa ana mpenzi. Aliyeshindwa kujuliana hali tangu atoe ujumbe wa hisia alizonazo. Mpenzi gani wa kushindwa kuonana? hata kusalimiana? Lilikuwa tatizo. Kikubwa aliogopa macho ya watu. Wiki kadhaa baadaye, punde Somoe alivyohitimu masomo yake, alitaarifiwa kuwa Somoe kasafiri kuelekea wilaya jirani, Masasi, mjini Ndanda. Ilikuwa taarifa mbaya, iliyomfanya ajifikirie mara mbilimbili na afikirie nini kitatokea baada ya hapo. Kubwa aliloliamini kuwa huo ndiyo mwisho wa mahusiano, kwani kule alikoenda aliamini atapata mwanaume mwingine atayekuwa kwenye mahusiano naye, ukizingatia ni mjini.

“Dah! Yangu yashaisha,” aliwaza Vumilia.

Tamaa ya kushindwa mbele yake ilimjaa, mwisho wa mahusiano huo ulianza nyemelea teka sehemu kubwa ya akili na moyo wake.

“Mjini alikoenda atakutana na wanaume wazuri zaidi yangu,” alijisemea kimoyomoyo, kauli iliyodondosha chozi toka kwenye mboni zake.



Muda mwingi Vumilia alikuwa mwingi wa hisia, tena hisia ambazo anaziamini pasipo kuzihakikisha. Na ndizo humuongezea aibu na uoga alionao. Afanye vipi kuziondoa? Akili iwe na hisia za maana, ulikuwa mtihani kwake.

Mwezi mmoja baadaye, Somoe alirejea kijijini kwao toka safari. Mara baada ya matokeo ya mtihani wa taifa wa darasa la saba kutoka. Ila hakubahatika kuwa mmoja wa wanafunzi waliofanya vizuri. Alifeli, hivyo hakuweza kuendelea na elimu ya sekondari. Kurudi kwake, Vumilia ilimuaminisha kuwa ndiyo muda sahihi wa kuanza vizuri mahusiano yao. Ukizingatia Somoe hawezi kuendelea na masomo, lakini ilikuwa tofauti. Kwani, Somoe, hakuonesha ushirikiano wa aina yoyote, wala chembe ya dalili kwamba aliahidi kuingia kwenye mahusiano ilikosekana. Hata kukumbushia, Vumilia alishindwa kufanya hivyo, alikesha kusubiri, Somoe akumbushie, ila mwisho wa siku hakuna aliyemkumbusha mwenziye. Wote walikufa na tai shingoni, japo hawakuisha kuwa na matamanio.



Hakuwa na budi, Vumilia alikubaliana na matokeo. Yaliyomfanya ajione mtu mwenye mkosi muda wote. Kwanini hapendwi? Ilimuumiza. Mwishowe alijikuta anaaingia kwenye orodha ya makuwadi wazuri shuleni kwao. Alianza kutumika na baadhi ya marafiki zake anaosoma nao na vijana wengine wa mtaani. Aligeuka kuwa mtaalamu, bingwa na hodari kwa kupeleka ujumbe wa wanaume wenzake kwa wasichana wao, lakini ujumbe wa kwake kupeleka kwa msichana ampendaye ilikuwa tatizo. Haikuwa kazi ya siku moja, kila siku, tena alivyoonekana mahiri katika nafasi hiyo, asilimia kubwa wakawa wanamtumia. Mwenyewe hakuona tatizo, aliipenda, sababu hakukuwa na namna nyingine ya kuwa karibu na wasichana zaidi ya hiyo.



Waliokesha kumsema hawakukosa, ila mwenyewe hakuona tatizo, aliziba masikio na kuongeza kasi, japo kwa baadhi ya siku alikuwa anawakwepa kukutana nao wale waliokuwa wanambeza kuhusu kazi hiyo aifanyayo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Dogo hata ukimbie, acha uboya, utatumwa mpaka lini? Acha hiyo kazi tafuta manzi ya kwako, utulie. Si unatumwa tumwa kama mtoto mdogo mwenye umri wa miaka mitano,” alisema mwanafunzi mmoja aitwaye Abdallah, mara baada ya kumuona kwa mbali Vumilia akibadili njia ya kupita alipowaona wanaenda kukutana njia moja.

“Yaani ni boya balaa. Anatumwa hadi na watu waliotoka pori huko. Mtoto wa mjini utatumwa vipi? Badala ya wewe kutuma?” Alichangia mwanafunzi mwingine.

“Huyu tufanye tumkomeshe, aachane na hii tabia. Hamna namna nyingine, anatudhalilisha sana,” alisema mwingine pia.



Pindi wao wanapanga namna ya kumdhibiti aachane na hiyo kazi, naye akawa anajipanga na kuongeza mbinu mbadala za kuwakwepa. Hadi anafikia kuhitimu elimu ya sekondari, hakuacha. Alishaathirika nayo. Hivyo kumfanya neno mpenzi, kuishia kulisikia wengine wanavyoitana. Kwake ilikuwa ndoto, japokuwa hakuisha kutamani itokee siku apate kutamkiwa.



Mara baada ya kurudi mtaani, shughuli yake kuu ilikuwa kuwasaidia wazazi. Shughuli za shamba, nyumbani na vibarua kadha wa kadha maeneo mengine, vilivyomuwezesha kupata kiasi kidogo cha pesa. Kilichomuwezesha kununua baadhi ya nguo, na matumizi mengine ambayo hayakupaswa, kuomba pesa kwa wazazi, ama jamaa wengine. Alihangaika huku na kule, kujitafutia, aondokane na nafasi ya utegemezi kwa wazazi kwa kiasi fulani ukizingatia alikuwa na ndugu wanaomfuatia. Kwa wanaomfahamu, waliamini hatua hiyo itamsaidia kuondoa aibu na woga, kulingana na namna alivyokuwa anajichanganya na watu wa aina tofauti tofauti, ila ilikuwa sivyo. Hakubadilika!



Na vilikuja ongezeka maradufu, jioni moja alivyoitwa na kaka yake, katikati ya kundi la vijana wa kiume waliokuwa wanabadilisha mawazo juu ya mada mbalimbali zihusuzo mpira.

“Ndugu vipi?” Aliuliza kaka yake.

“Poa! Niambie.”

“Uko kimya sana dogo sikusikii kulikoni?”

“Kivipi labda kaka yangu? Mbona nipo muda wote?”

“Sijawahi kukusikia kwenye purkushani yoyote dogo. Hata ya kusingiziwa kuwa ushawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msichana fulani. Hivi ushawahi kuwa na mpenzi kweli?” Aliuliza kaka yake, halaiki ya watu waliokusanyika macho pima kumuangalia Vumilia namna anavyojibu maswali aulizwayo.



Hali fulani ilimshika! Ghafla pasi na kutaraji, swali aliloulizwa hakuhisi kuulizwa. Taratibu aliyageuza macho yake, kwa kila mmoja kumuangalia namna anavyomtathmini, alivyowamaliza wote, chini aliyatupia. Kuinuka! Uso ulijaa unyonge, machozi, mbonini yakaanza mlenga, dalili tosha za aibu zilizomaanisha kadhalilishwa. Hata kaka yake akajiona kuwa kakosea. Na alijutia kwanini kafanya hivyo, hali iliyomsukuma kuchakalisha akili kutafuta mbinu ya kumuondoa nduguye. Alitumia takribani dakika mbili kuifikiri, alivyojiwa na ya usahihi, hakuijadili.

“Dogo nitakutafuta baadaye tuongee vizuri, sasa hivi naenda kwanza mchangani kuchukua mafuta, nikisema nikusikilize, sitokuwa makini katika usikilizaji,” alisema kaka yake, kumuondolea aibu zaidi mbele ya watu waliomzunguka. Japo kinyonge, Vumilia aliinuka mahali alipoketi na kuianza safari, mdogomdogo kutafuta uelekeo wa nyumbani kwao.



Wakati huo tayari, alishafikisha umri wa miaka kumi na nane, lakini bado aibu, uoga na hisia nyingi zisizo na mantiki zilikithiri moyoni mwake. Alijihisi muda wote kuongelewa, tena kuongelewa kwa mabaya na sio mema. Alivyofika nyumbani, alianza kujifikiria, kuhusu maswali aliyoulizwa na uamuzi gani utamfaa kuuchukua. Alitumia takribani nusu saa, kutafuta muafaka wa tafakuri zake, lakini hakubahatika kupata suluhu zaidi ya mkanganyiko wa mawazo, toka hili ingia lile. Mwishowe akapitiwa na usingizi.



likuwa ni Mei 2011, mara baada ya shule za msingi na sekondari kufungwa. Serikali ya kijiji cha Mangaka, kiliendesha zoezi la unyago kwa watoto wa kike na kiume, kuanzia umri wa miaka mitatu na kuendelea. Wazazi baadhi walijitokeza kuunga mkono jambo hili, kwa kuwaorodhesha watoto wao waliowaona wanastahili kwenye zoezi kulingana na sheria tajwa. Baada ya kujitokeza kwa wingi, tarehe husika ya kuingiza jando ilipangwa. Ambapo siku hiyo, hufanyika mkesha maalamu wa ngoma, kuwabariki watoto hao wakaishi vyema jando. Usiku wa ngoma, ni siku pendwa ambayo watu wengi hufurahia. Hufurahia sio kwa sababu kapeleka mtoto jando, hapana! Hufurahia burudani aipatayo. Kwani sio jamaa pekee wa watoto hufurahia, hata wengine pia, ambao watoto wao ama wasio na watoto wa kupeleka jando huudhuria.



Furaha ipatikanayo hapa si ya kifani, watu huburudika haswa, hukonga mioyo yao vilivyo, kwa kuwa ni burudani adimu, ambayo hufanyika mara chache sana ndani ya mwaka mmoja. Kile kifanywacho kwenye mkesha wa siku ya kuingia jando, ndiyo vivyo hivyo hufanywa mkesha wa siku ya kutoa. Japo siku hii huwa maradufu zaidi ya kuingiza. Siku hii huzoa watu wengi, ngoma nazo huwa nyingi, ya kila aina, kiasi kwamba mtu anapata fursa ya kucheza ngoma iliyo chaguo lake. Watu wakusanyikao viwanja vya mkesha, si wa kuhesabika kwa urahisi, na namna gani utaanza kuhesabu? Inakuwa ngumu kupata idadi sababu huchangamana mno.



Wenye biashara, za matunda, sharabu na nyinginezo siku hizi huwa sehemu ya kumbukumbu zao. Kwa namna wafanyavyo mauzo ya kutosha, hasa sharabu na sigara, kwani asilimia kubwa hufurahia watoto kurudi salama toka jando. Siku ya mkesha wa kutoa, Vumilia alikuwa miongoni mwa mamia ya watu waliohudhuria, akiambatana na rafiki yake aitwaye Ngungu, taratibu wakikatiza ngoma hii kwenda ngoma nyingine, wapandwapo na mzuka huingia ndani kusakata. Walikuwa na morali ya hali ya juu, iliyochangiwa kwa kiasi kikubwa namna ngoma za sikio zilivyoruhusu kusikika kwa ladha tofauti ya midundo.

“Dogo, hapa lazima leo upate mwanamke,” alisema Ngungu, pindi wakitoka kwenye foleni ya watu waliokuwa wanacheza ngoma ya Liwayawaya.

“Kweli?”

“Yeah! Leo hii nawe utoe ugwadu uliokukithiri kwa muda mrefu. Lazima ule kisusio dogoooo,” Ngungu aliendelea kuongea, wakati huo Vumilia akiwa makini kumsikiliza na kutafakari namna itavyokuwa hadi afanikiwe kupata mwanamke.

“Kama nitakataliwa itakuaje?”

“Tutaenda kupiga hata mande, kwa msichana nitayempata.”



Kweli! Walianza zunguka, kundi moja baada ya lingine, takribani muda wa nusu saa, huku wakiwaita wasichana mbalimbali, ila isivyo bahati, wasichana waliokuwa wanawaita, hawakutii wito. Walikuwa wanakataa na pale walipojaribu kuwafukuzia, hawakuacha kutoka mbio.

“Mmmmh! Hili mbona gundu?” Aliuliza Ngungu, baada ya kuzunguka kwa muda mrefu pasi na mafanikio.

“Hapa bilabila, hamna mwanamke tutayefanikiwa kumpata,” Vumilia alichangia hoja, wakati huo wakiwa wameketi sehemu kupumzika, baada ya mizunguko waliyoifanya kuwapatia uchovu.



Dakika nane baadaye, jirani na mahali walipoketi kuna mwanamke alienda kujipumzisha. Umbali wa mita kumi toka wao walipo. Hamu! Paaa! Ilitawala ndani ya mioyo, kumsogelea walitamani, kwani shauku, ilishinda nguvu ya uvumilivu.

“Dogo niachie nikamalize,” alisema Ngungu, kumtuliza Vumilia ambaye naye alionekana kuwa na tamanio la kumfuata mwanamke huyo, ilhali hawezi kufanya ushawishi wa kumrubuni msichana aingie naye kwenye mahusiano ya kimapenzi.

“Hamna shida nenda, ukifanikiwa, fanya kama ulivyoniahidi.”

“Ondoa shaka.”



Ngungu alinyanyuka na kumsogelea msichana huyo. Pasi na haraka, wala jazba neno likaanza teremshwa, lililojaa uongo na ukweli kwa kiasi kidogo. Kushtuka! Msichana, alianza legea kwa matamshi aliyokuwa anaambiwa. Moyo, ulianza ruhusu neno kukubalika, hisia za kile alichokuwa anaambiwa akilini kilijijenga, kuhamaki! Ulegevu wa kutosha ulikithiri sehemu kubwa za maungo ya mwili wake.

“Unaishi maeneo gani?” Aliuliza msichana huyo, wakati huo tayari alishausogelea mwili wa Ngungu na kulaza kichwa chake kifuani.



Kwa bashasha, Ngungu akaanza chezea nywele za binti huyo, zilizosukwa mtindo wa “twende kilioni” na kushusha mkono wake hadi sehemu ya uti wa mgongo.

“Si mbali toka hapa uwanjani. Twende ili tuwahi kurudi kuburudika na magoma kabla wapigaji hawajaanza kuchoka.”

“Sawa! Tuondoke,” alisema binti huyo, aliyefahamika kwa jina la Zaitun baadaye. Huku akijinasua kifuani kwa Ngungu tayari kuianza safari.

“Basi nisubiri hapo nimuage rafiki yangu,” aliongea Ngungu, akiwa tayari ashaianza safari ya kumfuata Vumilia pale alipoketi. Alipomfikia, hakuchelea kumueleza kilichojiri.

“Mambo yako poa. Dogo kakubali, kama nilivyokuambia awali, endapo mmoja wetu atapata mwanamke, mwingine akikosa, aliyepatikana ataenda kupigwa mande, hivyo fuata nyumanyuma asibaini,” Ngungu alimnong’oneza Vumilia.

“Ndiyo maana nakuaminia,” alisema Vumilia. Moyo ukichanua furaha, kufurahia anaenda kutoa kufuli kwa mara ya kwanza baada ya mihangaiko ya muda mrefu.



Safari ilianza. Ngungu akiwa katangulia na Zaitun, Vumilia akiwafuata kwa nyuma, umbali mita mia moja nyuma, msichana asishtuke kama kuna njama kaundiwa. Baada ya mwendo wa takribani dakika ishirini na moja, walifanikiwa kufika nyumbani kwa kina Ngungu. Ambako alikuwa anaishi pekee, mzazi wake akiwa anaishi shamba. Wakati huo Vumilia alikuwa amebana nje ya ua wa nyumba hiyo, akisubiri waingie ndani. Alipojihakikishia washaingia, alisogea hadi chumba husika, na kubana pembezoni kidogo na mlango wa chumba hicho ambacho mtanange wa kufikisha mwenge kileleni hufanyika.



Muda wote mapigo ya moyo, hayakumuisha kwenda kasi. Kutokana na fikra nyingi zilizomjaa kichwani. Itakuaje? Ndicho kitu kikubwa alichowaza. Akigundulika, na namna ya kufanya. Aliumiza akili, namna ya kuushika mwenge na kuweka katika stuli yake tulivu itumikayo kupoozea, baada ya kushikwa na kukimbizwa kwa muda mrefu. Fikra hizo ziliambatana na fikra za kufanikisha, kile walichopanga, msichana asiwe kigeugeu, kwa mkimbizo wa kijiji kimoja tu, abloo mapigo. Aliomba, aendelee kuwa na hamu, ya kuhitaji kufika kijiji cha pili, ashuhudie miradi mbalimbali iliyoandaliwa kwa ajili yake. Katikati ya fikra hizo, alishuhudia mlango ukifungliwa. Ngungu alitokeza kisha wakavutana pembeni kupeana neno.

“Haupaswi kuwasha kibatari, fanya kilichokupeleka, ukishamaliza tu, haina haja ya kuendelea kukaa, tokeza nje haraka ili asibaini kama tumemchangia,” alisema Ngungu, kwa sauti ya kunong’oneza.

“Poa! Nimekuelewa,” Vumilia aliitikia.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Baada ya dakika mbili, toka Ngungu alivyotoka, Vumilia akaingia. Huku mapigo ya moyo, bado yakimsumbua, kwa kukosa uzoefu wa shughuli, kwani ndiyo siku yake ya kwanza, na hajawahi kaa hata kijiwe akapatiwa maarifa namna inavyokuwa.

“Nikiiendeleza hii hofu nitashtukiwa,” aliwaza Vumilia, akiwa ananyemelea kitandani aweze kuketi.



Baadaye alipiga moyo konde, na kujitupia juu ya mwili wa Zaitun, alivyosaula nguo alizovaa, ambayo ni bukta tu, kwani nguo zingine alikwishavua pindi yuko nje anasubiri. Ukosefu wa mwanga chumbani humo ulimsaidia. Chumba kilitawaliwa na kiza, tena kiza kinene kilichonyima nafasi ya kutambua kitu hata kiwe kikubwa kiasi gani. Hivyo ujio wake ulimfahamisha Zaitun kuwa ndiyo mtu aliyokuwa nayo awali, hata hakutaka kuhoji sana, alichohitaji ni kufanya mapokezi tu ya mwenge aukimbize kijiji cha pili. Vumilia alijivika ushujaa, rasmi alianza zoezi, na kupewa ushirikiano wa nguvu na Zaitun, ambaye sasa alihitaji kuonesha vyema ufundi wake.



Kutokana na hofu, alifanya mambo kwa uharaka asibainike. Haina uhakika, kama mwenziye alifikia sehemu husika, kileleni, kwa namna ambavyo sakata liliendeshwa. Dakika mbili tu, ndizo alizitumia, kwa upande wake, majeshi ya nguvu yalimtoka na kuvamia kwa kasi ngome pinzani. Naam! Raha ya mwanzo ya mapenzi hakuipata, aliyofaidika nayo ni ile ya mwisho. Kufika kileleni. Na punde baada ya kumaliza, kwa kasi alichoropoka na kutoka nje, hali iliyomfanya Zaitun kumuweka njia panda. Na kujiuliza maswali mengi aliyokosa majibu. Nje hakukaa, alivaa mavazi yake kisha kurudi ngomani.



Kuanzia hapo alijiona shujaa, mbele ya simba, waliokuwa wanakesha kumdhihaki. Kuwa hajawahi fanya mapenzi. Sasa hakukosa la kuwajibu, tena kwa mbwembwe nyingi zenye kuthibitisha na kuwa na uhakika nacho kile anachozungumza.

“Wewe, watu tushafanya hayo mambo ila hatutaki tu kujitangaza. Mimi sio limbukeni kama ninyi,” alisema Vumilia, akishusha dongo katika halaiki ya vijana aliokuwa anacheza nao mpira wa miguu.



Raha aliyoipata ilikuwa sehemu ya kumbukumbu. Kwani, ndiyo mara ya kwanza kudiriki kufanya kitu hicho. Kila akaapo peke yake hisia hazikuisha kumjia, kukumbuka namna alivyokata utepe kuzindua ulimwengu wa mapenzi maishani mwake. Tena akikutana na msichana aliyefanya naye jambo hilo pasi na kufahamu, hisia humjia maradufu, za pande mbili, kukumbuka tukio na kuhisi msichana huyo ashafahamu kuwa alichangiwa siku hiyo. Lakini ilikuwa tofauti. Hivyo ilibaki kuwa mapisi. Toka siku aliyofanya, kufanya tena ilibaki kuwa sehemu ya matamanio. Alihitaji kufanya, lakini, hakuweza kumpata msichana wa kufanya naye.



Hamu ya uhitaji wa kufanya ikaanza msumbua. Kama wasemavyo waswahili, mchovya asali hachovi mara moja. Wapi ataenda kukumbushia? Ilikuwa tatizo. Ugwadu ukaanza rundikana kwa mara nyingine, wakati huo akijaribu kubahatisha kama ataweza fanikiwa kumpata msichana wa kumtwika, ila hakufanikiwa. Mwishowe, alikutana na kijana aitwaye David, aliyeamua kumfundisha tabia ya upigaji wa punyeto. Baada ya kumgundua ana matamanio makubwa ya kuwa na msichana lakini anashindwa kuwaweka himayani.

“Hii ndiyo njia mbadala ya kumaliza haja zako, pale ushindwapo kuwa na msichana,” alisema David akiwa anajichua kumuonesha Vumilia. Huku akiwa makini kufuatilia kila hatua inayohitajika.

“Ili usiumie, unaweza tumia sabuni ama mafuta ya mgando. Na kikubwa kinachohitajika, pindi unafanya, unapaswa kuvuta hisia kama uko na mwanamke unafanya naye mapenzi,” aliendelea kusema David.



Rasmi! Alianza ingia ulimwengu huo. Ulimwengu wa kitumwa, wa kusumbua akili kumfikiria mwanamke alivyo, maungo yake ya ndani na nje pia. Pia zoezi hilo lilimfanya, muda mwingi awapo karibu na wanawake, kupepesa macho yake, ili aweze kushuhudia baadhi ya sehemu za maungo yao, kama vile matiti na nyama za paja. Afanikiwapo kuzishuhudia, usiku wa siku hiyohiyo, muda mahususi aliokuwa anatumia kufanya shughuli hiyo, huvuta hisia kuhusu mwanamke huyo kama wapo kitanda kimoja wakihitimisha haja zao. Ilikuwa shughuli ya kila siku, siku ikipita pasipo kushuhudia maungo ya mwanamke yaletayo msisimko, haachi kufanya, anafanya, kwa kumvutia hisia yule aliyemvutia jana. Iligeuka desturi, habari za mwanamke hakuhitaji tena kuzisikia, aliamini akifanyacho ni sahihi kwake, sababu anaondokana na usumbufu. Hakufikiri kuhusu madhara, aliangalia haja zake zinavyomtuma, akikamilisha ndipo taarifa kuhusu hicho kitu huzitafakari.



Unguli ulimtwaa, japo hakutaka jiweka bayana, alihofia kuchekwa na kudharauliwa kama kawaida ahisivyo. Ilikuwa ni kimyakimya, hata yule aliyemfundisha hakudiriki mtaarifu, kama anajihusisha na hayo mambo. Aliifanya kuwa siri, kwani hata muda mwingine awapo na wenziye, endapo wakihadithiana juu ya tabia hiyo hutulia tuli, kama hafahamu na wala hajihusishi na hilo jambo. Kadri siku zilivyozidi kusonga mbele ndivyo alivyozidi imarika na kuwa kinara wa jambo hilo, pamoja na kuchunguza maungo ya wanawake. Wakati huo pia alizidi sikia taarifa nyingi juu ya madhara na faida ya kile afanyacho. Hivyo kumfanya aanze kuzipambanua, moja baada ya nyingine aweze baini ukweli ni upi. Taarifa za madhara zilizizidi nguvu taarifa za kutokuwa na madhara, kutambua hilo, ikamfanya apunguze kwa kiasi fulani, huku akiapa kuacha kabisa pamoja na kuanza upya harakati za kutafuta msichana.



Katikati ya harakati hizo, alipata safari ya ghafla, ya kwenda kumfanyia biashara kaka yake mdanani, ya uuzaji wa mitandio na suruali za kiume. Safari hiyo ilimpa imani, kuwa huo ndiyo wasaa wa kumiliki msichana, kwa ufahamu alionao, wa wafanyabiashara wengi, ama wafanyao kazi kwenye maduka ya matajiri, kupata mwanamke ni jambo rahisi. Safari hiyo ilikuwa ya vijiji vitatu, vilivyoko nje kidogo na kijiji chao kilipo. Na ilimpasa pekee aelekee kufanya biashara hiyo, baada ya kuaminiwa vyema kwenye mambo ya mahesabu na kaka yake.



Hakika! Siku ya safari, Vumilia alikuwa mmoja miongoni mwa wafanyabiashara walioenda mnadani, akimuwakilisha kaka yake. Safari ilianza jioni, saa 12:45 baada ya wahusika wote waliotakiwa kwenda kukamilika. Ni pekee, katika orodha ya wafanyabiashara hao, ambaye alikuwa na umri na umbo dogo, wengine walikuwa wababa wenye familia zao. Waliwasili kijiji cha kwanza, saa 4 usiku, wakafanya mapumziko tokana na uchovu wa safari, na tayari kwa kuanza biashara siku inayofuata. Kulivyokucha pilikapilika zilianza, wenye kujenga banda za miti kwa ajili ya kuwekea bidhaa zao walifanya hivyo, na wenye kutandika kapeti chini kumwaga bidhaa nao hawakusita kufanya. Vumilia alikuwa miongoni mwa wale walitandika kapeti chini na kumwaga bidhaa alizonazo, baada ya hapo shughuli ya kuwavutia wateja ilianza, kwa mfululizo, kuwatajia bei.

“Buku jeroooo!... Buku jerooo!...buku jerooo!... Ayaaaa weee buku jerooo mitandio hapa,” alisikika Vumilia muda wote, koo likiwa kavu, mkononi kakamatia maji yafahamikayo maji ya kandoro. Ambayo alikuwa anayatumia pale alipoona pana uhitaji wa kutumia.



Shughuli hiyo iliambatana na ya uombaji wa namba za simu kwa wanawake mbalimbali, waliokuwa wamejitokeza kununua na wengine kuangalia wakipendezwa wanunue. Alihaha, kunadi na kuomba, lakini hadi anahitimisha jioni hakuambulia namba ya msichana yoyote, zaidi ya kuambiwa neno sina simu na sizifahamu namba zangu kwa kichwa. Hata kijiji cha pili, ambacho ni Nandembo, hakufanikiwa pia. Ile imani iliyomuaminisha ukiwa kwenye biashara unafanikiwa kupata msichana kwa uharaka ikaanza toweka na kutoiamini tena. Jioni ya siku ya pili baada ya kumaliza na kufunga biashara zao kijiji cha pili walielekea kijiji cha tatu, kifahamikacho Likokona. Hapo alijiona asiye na bahati, na kumfanya ajitafakari wapi anakosea, lakini tafakuri yake haikumpatia matunda.



Kumaliza mnada pasi kupata mwanamke, ni kitu ambacho hakuhitaji. Dhana ilimtuma, huo ndiyo wakati wa kukata mzizi wa fitina, kwani siku zote wafanyabiashara wa shughuli kama hizo hawakosi, iweje yeye asifanikiwe? Hivyo punde baada ya kuteremka garini alienda kutega barabarani, mfukoni akiwa na lundo la pesa za mauzo aliyofanya. Alijihaidi, ikibidi kutumia kiasi kadhaa cha pesa hiyo, yake nia itimie. Pitapita za watu wa kila rika na jinsia tofauti alizishuhudia, wale aliowahitaji kuwaeleza hitajio lake walimkosesha ushirikiano, wengi wao kila alivyowaita hawakutii. Waliendelea na safari zao.

“Huu ndiyo wasaa wa kupata. Nikishindwa, sitopata nafasi nyingine, sijui nina gundu gani?” aliwaza Vumilia.



Baada ya kuita wasichana wengi, kwa muda mrefu, alibahatika mmoja miongoni mwa waitwa kutii wito wake. Alifurahi, na kuupa moyo nguvu ya kuongea maneno yenye ushawishi utaomuwezesha msichana aliyesimama mbele yake akubaliane na kile aambiwacho. Alianza kwa kujikohoza, kisha sauti yake iliyoko nzito akailainisha maneno yamtoke pasi na kizuizi.

“Wewe unatokea wapi?” aliuliza msichana huyo baada ya Vumilia kuhitimisha maelezo ya hitajio lake.

“Nimekuja mnadani.”

“Mmmmh! Sasa nisubiri niende nyumbani baadaye nitarudi ndipo tuelewane zaidi.”

“Hapana, wakati ni sasa. Huu ndiyo muda mzuri.”



Vumilia alivaa ujasiri, wa ghalfa, kilichomsaidia kiza kilichoingia baaada ya kufukuza mwanga, uliomwezesha kutoonana vyema. Hivyo alipania iwe isiwe msichana huyo havuki ndoano yake baada ya kuonesha kila dalili ya kukubaliana.

“Twende basi,” alisema msichana huyo, baada ya kufikiria kwa kina.



Hakuuliza! Sababu ni bahati ya mtende, hakuhitaji ipotee, pasi na kuchelea wala kujitafakari wapi msichana kasema waelekee, alithubutu kuongozana naye. Huku njiani wakisindikizwa na maongezi machache ya utambulisho wa kila mmoja. Walipiga hatua, sio kwa muda mfupi, ni mrefu, na sehemu waliyotoka waliicha mbali. Walikatiza kona za hapa na pale, wakati huo Vumilia alikuwa anawaza namna atavyoenda faidika na penzi la msichana huyo, aliyompata kwa jitihada zake binafsi. Kufanya ndicho kitu pekee alichokuwa anafikiri, hakufikiri kuhusu usalama wake, na madhara yapi yanaweza tokeza ukizingatia hawafahamiani na msichana huyo wala mazingira hayafahamu. Hakujalisha! Baada ya matembezi ya muda mrefu, hatimaye waliifikia sehemu husika, ambayo msichana huyo aliipendekeza kuwa inafaa kwa wao kutekeleza hitajio la haja zao. Ambalo ni makaburini.



Kutokana na uwingi wa hamu aliyonayo, pupa ilimjaa Vumilia, na kumshinikiza msichana huyo avue nguo zake wafanye yao kwa uharaka. Msichana hakupinga, aliiondoa chupi tu, kisha akalivuta gauni lake kwa juu, na kuacha sehemu kubwa ya maungo yake kuwa wazi. Uwanja akaachiwa Vumilia, auchezee atakavyo na kutumia mitindo yote aipendayo ila si kulalishwa chini. Kwa madai kuwa chini kuna upupu.

“Hamna shida, hiihii ya juu inatosha,” alisema Vumilia, pindi akimuinamisha msichana huyo, aushuhudie uwanja vizuri. Alivyoelezwa jambo.



Japo kulikuwa na kiza, achilia mbali ulikuwa ni usiku, kiza kingine kilichangiwa na miti ya mikorosho iliyofungamana mahali hapo, lakini Vumilia aliyafanya macho yake kuwa makali asikosee, kuutumia uwanja ili asionekane kama hajui maufundi mbele ya msichana huyo wa pori. Baada ya mbwembwe za muda mfupi, kabumbu lilianza, kwa nyakati tofauti kumtafuta mshindi atayetangulia kuongoza pambano kabla ya mwenziye.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Vumilia aliingia kwenye pambano hilo pasi na zana sahihi za kujikinga na madhara yanayoweza kuepukana. Alienda peku, na yule msichana hakutaka kukumbusha hilo. Kila mmoja aliwazia utamu tu waupatao, na sio hali ya kiafya ya mwenziye iko vipi. Baada ya dakika chache, lilifikia tamati, kwa kwenda sare, ya bao moja moja, huku yule msichana ndiyo aliyetangulia kuongoza, akifuata Vumilia kusawazisha dakika za mwishoni kabisa. Walivyohitimisha na kila mmoja alivyoridhia kuridhika, Vumilia alitoa kiasi kadhaa cha pesa katika mfuko wake wa suruali aliyovaa akamkabidhi yule msichana kama shukrani.



Hatimaye waliondoka, Vumilia alirejea kule iliko gari yao na msichana alielekea nyumbani kwao. Furaha iliyotawala akilini mwa Vumilia haikuwa ya kawaida. Hakuamini, kukata mzizi uliokuwa unamshinda siku zote. Alijiona zaidi ya shujaa na kuamini sasa anaenda kuwa bingwa katika ulimwengu huo. Wale watu waliokuwa wanazodoa sasa alipata cha kuwaongezea kuwajibu, na kuendelea kujivunia taratibu.



Siku iliyofuata alifanya biashara, akili ikiwa na kumbukizi la tukio alilofanya jana. Hali iliyompelekea kuonekana mwenye tabasamu tele muda wote. Ile dhana aliyoianza kuipotezea ilichanua upya na kukubalika tena akilini, kuwa ni sahihi. Ukiwa kwenye kitu kama hicho ni lazima, usivyobahatika ni uzito wa mtu binafsi kama iliyokuwa kwake awali. Hata alivyorudi nyumbani baada ya kuhitimisha zoezi la mnada katika vijiji husika, hakuondokewa na furaha iliyotawala sehemu kubwa moyoni mwake. Kisa tu kakata utepe wa ulingo wa mapenzi, sasa yuko ulingoni tayari kwa mapambano. Mwanamke yeyote mwenye rika lake, ama ambaye hata kamzidi aliye na hisia za matamanio au upendo juu yake, alikuwa radhi kumueleza. Hakutaka kurudi nyuma, kwani kufanya hivyo ingemrudishia maumivu aliyokuwa anayapata awali. Sasa ulikuwa muda wa kwenda mbele, kuwa na mahusiano sahihi ya kimapenzi.



Hatimaye siku zilizidi kusonga mbele, Vumilia akiwa mtaani pasi na ajira ya aina yoyote, ama kupata kibarua cha kueleweka sehemu fulani. Kazi yake kubwa ikawa kutembelea rafiki zake, waliopata vibarua na kusaidia wazazi shughuli za shamba kwa baadhi ya siku. Sio kama hakuwa na matamanio ya kujishughulisha, hapana! Alikuwanayo, ila wapi anaanzia, wazo hilo halikuwepo akilini mwake. Baadaye sana, tena kwa ushawishi wa rafiki yake, yule aitwaye Ngungu, ndiyo alishawishika kufanya vibarua, baada ya kumuona anazunguka sana mtaani, ila sio vya kudumu, ni vya muda, siku mojamoja. Kupanda miti ya mbao katika mashamba ya watu, kusomba mawe ya kujengea mifereji kando ya barabara, pamoja na usombaji wa mbao. Shughuli aliyoenda kuifanya kijiji jirani, kiitwacho Mtambaswala, kilichopo mpakani kati ya taifa la Msumbiji na Tanzania. Vibarua hivyo vilimwezesha kupata kiasi cha pesa, alichoweza kutumia kujikimu kwa baadhi ya mahitaji yake binafsi kama vile mavazi, sabuni na kuwasaidia ndugu zake pale aombwapo.



Shughuli ya usombaji wa mbao, aliifanya kwa muda wa miezi miwili, ikimuwezesha kuingia na kumpatia ufahamu wa vijiji jirani vya nchini Msumbiji ambako mbao hizo zilikuwa zinapasuliwa. Sio vijiji tu, na baadhi ya watu na tabia zao, ambazo alikuwa hajawahi ziona. Shughuli ya upasuaji wa mbao ulivyosimama, alirejea Mangaka. Akaungana na marafiki zake waliohitimu pamoja elimu ya sekondari ya kidato cha nne, kufanya maombi ya ajira mbalimbali yaliyokwishatolewa. Ualimu na uuguzi. Hivyo wakawa wanakesha kuzunguka ofisi nyingi na tofautitofauti wakiwa na bahasha zao zilizo na vyeti, kopi za vyeti pasi na sahau barua za maombi zilizokosewa pindi wanaandika.



Ilikuwa kazi nzito. Kutembea sio mchezo, tena kwa mguu, huku wakivuka mabonde na vilima, wakibuka vumbi na kuoga jasho lililozalishwa na jua kali lililokesha kuwaka muda wote. Yote kutafuta hatma ya maisha yao ya siku za baadaye. Hapa Vumilia aliondoa uoga na nishai aliyonayo, alijivika roho ya ujasiri, kama aliyonayo mfalme wa nyika, simba! Ili kile akitafutacho kisipotee pasi na kukifanyia jitihada. Ila isivyo bahati, hadi mwaka unakata maombi yao hayakukubaliwa, jambo linalomrudisha Vumilia kwenye shughuli zake za awali.



Si kila mtu umuonaye anaweza kuwa mwema kwako, hata kama muda wote haachi kukuchanulia tabasamu. Ndivyo ilivyokuwa kwa Vumilia na wenziye. Walianza chukiwa na baadhi ya watu, tena waliokuwa wanafanya nao maongezi kwa baadhi ya siku. Jina la utani wakabandikwa “wazururaji” sababu tu hawana kazi maalumu ya kufanya. Mwaka uliofuata, 2012. Vumilia aliendelea na jitihada zake zilezile. Hakuwa na mipango, wala malengo thabiti, zaidi ya matamanio kuwa anahitaji kuwa ndani ya ajira. Ila mikakati ya kumfikisha ilikuwa shida. Hakuwanao, ukizingatia bado anaishi kwa wazazi na vitu vingi alikuwa anategemea wao ilhali alishafikisha umri wa miaka kumi na tisa.



Dhihirisho la kuchukiwa kwao lilijiweka wazi jioni moja, walivyomtembelea rafiki yao aitwaye Sadiki aliyekuwa anauza mchele. Maeneo ya barabara kuu ielekeayo Masasi. Walikuwa ni Vumilia, Hussein, Kanje na Maundu. Kwa kuwa sehemu afanyayo biashara Sadiki haikuwa rafiki kwa kuweka genge la kufanya maongezi, walisogea pembeni, karibu na banda lingine la kijana aitwaye Makashata. Ambaye walihitimu naye kidato kimoja pia. Alikuwa anauza vyombo vya ndani. Taratibu walianza kupiga soga za hapa na pale. Zilivyonoga, ziliwavuta hata wauzaji wa maduka jirani, wakajumuika nao. Wale wauzaji wakawa wanapiga soga, mteja akifika dukani kwake huondoka kwenda kumhudumia, akishamaliza hurejea kuendelea na stori. Hakika! Zilinoga, kwani asilimia kubwa walikesha kufurahi, juu ya kile walichokuwa wanazungumzia, hadi inafikia jioni muda wa maduka mengi kufunga, bado genge liliendelea na soga. Kiza kilivyoanza kuchukua nafasi, ndipo wale wauzaji mmoja mmoja alinyanyuka kwenda kufungasha biashara yake.



Vumilia na wenziye ndiyo walikuwa wa mwisho kuondoka, pindi Sadiki na Makashata wanafunga biashara zao. Waliaga na kuondoka.

“Wewe usiyumbe, peleka kituoni hao, wamezidi kuwa wazururaji wakubwa,” ilisikika sauti, toka katika ya halaiki ya kundi walioonekana kujadili jambo.

“Eeeh! Ndiyo. Ni walewale, hamna mtu mwingine mwenye uwezo huo zaidi yao.”

“Mzururaji akizidi, lazima ageuke mwizi.”



Yalikuwa ni maongezi, yaliyoongozwa na Makashata, akilalamika kuibiwa simu, pale alipokuwa anapiga soga na kina Vumilia na wauzaji wengine. Aligundua hilo baada ya kumaliza kufungasha vyombo vyake na kwenda kuvihifadhi sehemu anayohifadhigi. Moja kwa moja alikuwa anawatuhumu, Vumilia na wenziye ndiyo wahusika wa wizi huo. Hakupeleka hata chembe ya hisia kwa wauzaji wenziye ambao nao walijumuika kupiga soga. Shinikizo la watu waliomzunguka, ukichanganya na lake, lililosukumwa na fuadi alilokosa kuliamulia, sasa alipata muafaka. Kipi aamue. Alikwenda kituoni!





Usiku wa saa mbili, ripoti ilimfikia Vumilia. Akiwa ndani ya banda umiza, akiangalia kionjo cha filamu. Kupitia kwa marafiki, aliokuwa nao mchana wakipiga soga. Mkononi wakiwa wamekamatia RB. Alichanganyikiwa! Akili haikutulia, hofu tele, ilimjaa. Kutuhumiwa wizi, ndiyo tatizo. Ataonekana vipi? Ilhali alizoeleka kuwa mwema? Mafundisho ya wazazi kwake, alianza yahisi kutokuwa na manufaa. Kwa kipindi chote alichofundishwa, kwa kutojihusisha na vitendo visivyofaa, kama hivyo alivyoanza tuhumiwa. Na wazazi ndiyo watu wa kwanza aliowaogopa, punde wakifikiwa na taarifa hizo. Adha atayokumbana nayo, haitokuwa ya kawaida.

“Kuna yeyote aliyechukua baina yetu? Katika orodha ya watu tuliotajwa kwenye hii tuhuma?” aliuliza Vumilia.

“Hapana.”

“Na imekuaje tuambiwe sisi pekee wakati tulikuwa wengi pale?”

“Sijajua katumia kigezo gani kututuhumu.”

“Mmmmmh! Ndugu zanguni, hili soo. Hata kama hatujachukua, si mnafahamu polisi kulivyo? Na mkizingatia kuna zoezi la usaili wa JKT usoni.”

“Kwa hiyo unashaurije?”

“Tumlipe kuondoa shari.”

“Tutamlipaje wakati hatujaiba?”

“Kaka! Polisi si unakufahamu? Tukiingia pale hatutatoka salama.”



Iliwabidi washauriane. Maamuzi kuyatafuta. Yatayokuwa msaada kwao, utaowaepusha na balaa. Wapate kuwa salama. Usaili wa JKT, ndicho kitu kingine kilichowasukuma, wafanye jambo hilo wamalize pasi na fikishwa kituoni, ama sehemu ya juu zaidi ya hiyo. Mahakamani! Kulingana na sheria za matakwa ya maombi ya muombaji kutoshitakiwa au kufungwa. Baada ya mashauriano ya muda mrefu waliridhia kulipa. Kwa kila mmoja kuchanga kiasi kadhaa cha pesa. Shilingi elfu saba! Baadhi yao, uhakika wa pesa ulikuwepo. Shida ilikuwa kwa Vumilia. Anaitolea wapi? Kama sio kwenda kuomba kwa wazazi. Aliitafakarisha akili, afanye vipi wazazi, taarifa isiwafikie. Ndugu ndiyo suluhisho. Hitimisho alilifikia.



Pasi na kawia. Kwa usaidizi wa marafiki alioambatana nao, alipiga simu kwa kaka yake, shida alianza ilia, kwa kuelezea mkasa mzima, wa kile kilichomtokea. Maongezi yalijaa sauti yenye huruma. Kumuaminisha yule anayewasiliana yupo matatizoni, ambayo yanapaswa tatuliwa haraka iwezekanavyo. Alishindwa kutoa machozi. Ila namna alivyokuwa anatoa matamshi, dhahiri! Alionekana kutingwa. Alijipambanua vya kutosha. Maneno yakaleta ushawishi, kwa yule aliyekuwa anawasiliana naye, mwishowe akapatiwa ahadi ya kukamilishiwa ombi alilotoa.

“Subiri baada ya dakika kumi, nitakuwa nishakutumia,” ilisikika sauti ya upande wa pili wa simu.

“Sawa, nashukuru sana,” alisema Vumilia na kukata simu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Kweli! Baada ya muda alioahidiwa, kiasi cha shilingi elfu nane kiliingia kwenye simu, kwa njia ya ujumbe mfupi. Kisha wakafanya mjumuisho kwa watu wote wanaohusika, kilipokamilika, waliwateua wawili miongoni mwao, kuwasilisha kiasi hicho kwa mhusika. Makashata! Juu ya kufanya hivyo, walitengeneza aibu. Na moyo wa kutoaminika kwa watu waliokuwa na ufahamu wa tukio lililojiri. Walijisikia vibaya. Tena zaidi walipopata taarifa, kuwa wanaitwa wezi eneo lile ambalo tukio lilifanyika, japo hawakuhusika.



Morali ya kutembelea ile sehemu ikapotea. Sio hapo tu, hata sehemu nyingine walizojizoesha kutembelea kwa sana. Yote, kuuficha utu wao, usiharibiwe. Ilichukua muda kidogo, kuanza onekana mitaa hiyo, tena kwa nadra, na kwa sababu maalumu. Zaidi ya hapo hawakutembelea. Wakati huo walishaanza sahau habari za wao kuitwa wezi. Japo kuna muda iliwaumiza wakumbukapo, kwa kuwa hawakuwa wahusika waliofanya.



ITAENDELEA 

0 comments:

Post a Comment

Blog