Simulizi : Kilio Changu
Sehemu Ya Tano (5)
Sherehe ilizidi kunoga nyumbani kwa Miriam, magari yakifahari yaliegeshwa ndani na nje ya ukuta mkubwa, kwa ujumla ilikua sherehe iliyowakutanisha karibu matajiri wote wa jiji la Arusha.
Genes na Angel walikua hawajui lolote linaloendelea hapo nyumbani,
"we mwanamke ndio tunaondoka KIA" ilikua sauti ya Genes akimtaarifu Miriam kwa njia ya simu baada ya kushuka kwenye ndege,alifuata gari yake ilipoegeshwa na kuliondoa kwa kasi ya ajabu.
Miriam alilia kwa furaha kwani aliona siku hiyo ndio ataweza kupata furaha zaidi ya siku zote za maisha yake,kitendo cha kuja kuishi na watoto wa mumewe kilimfanya ajione mshindi,
"wageni waalikwa mabibi na mabwana wageni rasmi ndio wanakaribia kuingia ukumbuni hivyo basi naomba wakiingia mpige makofi na vigelegele kwao" sauti ya Miriam ilisikika kupitia kipasa sauti akimaanisha wageni rasmi ni watoto wa mumewe pamoja na mama yao yaani Eledy na Eledius na Angel,
"sawaaa mamaaaa" watu wote waliitikia huku wakigonganisha glass.
Genes aliendesha gari kwa kasi katika barabara ya Moshi na Arusha kulikua hakuna foleni hivyo ndani ya dakika 45 tayari alikua Mianzin akishika barabara inayoelekea Ngaramtoni,
"Angel hii njia nimeipita sana inanikumbusha mbali" Genes aliongea huku akinyooshea kidole barabara ya kuelekea kituo kikuu cha mabasi yaendayo mkoani,
"hata mimi naikumbuka sana jamani watu wanatokea mbali lakini acha tu" Angel alijibu huku akitikisa kichwa kuweka nywele zake za bandia vizuri.
Eledy na Eledius walikaa viti vya nyuma wakiwa wamefungwa mkanda vizuri.
****
"Mbona kama sielewi magari yote yale ya nini pale" Genes aliongea kwa mshangao baada ya kuona magari mengi yameegeshwa nje ya geti lao,
"kwani pale ndio kwenu" Angel aliuliza,
"usiseme kwenu sema kwetu, ndio ila sio kawaida magari mengi hivi kuegeshwa hapo hapa itakua kuna kitu Miriam kaandaa na kama kuna sherehe basi leo Miriam ataonja pombe sasa cha kufanya tutumie upenyo huu huu kumuua" Genes aliongea sauti ya chini ili watoto wasisikie,
"sasa tutamuuwaje ili wasije nihisi mimi mgeni ndio nimemuua ?" Angel aliuliza,
"hapa kwanza tugeuke haraka tukanunue bunduki alafu usiku wa leo nitatafuta vijana niwape kazi ya kutuvamia,na kwa sababu najua Miriam atakua amekunywa pombe basi nadhani ataongea hapo wammiminie risasi hadi afe" Genes aliongea huku machozi yakimlenga kwani alijua kitendo anachokifanya sio kizuri ila alilazimika ili asimkwaze mama watoto wake,
"basi sawa mpenzi" Angel alijibu huku akimshika Genes begani.
Gari iligeuzwa kwa haraka walianza safari ya kurudi katikati ya mji,
"kuna duka moja pale karibu na soko kuu panauzwa bunduki,sijui kama hadi sasa wanauza maana napajua tokea nikiwa shule" Genes aliongea huku akiongeza mwendo wa gari.
"Tuegeshe gari mbali na hilo duka" Angel aliongea walipoanza kuingia katikati ya mji,
"sawa mke wangu" Genes alijibu kuashiria ametii amri ya mkewe, wote walionekana kuwa na nyuso za huzuni na msongo wa mawazo huku Eledy na Eledius wakiwa tayari wamepitiwa na usingizi.
Gari iliegeshwa nje jengo la Jogoo maarufu kama Jogoo House, Genes na Angel wakashuka na kuwaacha watoto ndani,http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"waheshimiwa vipi" Genes alisalimia vijana waliokua wamekaa karibu na mahali alipoegesha gari lake. Hapo kijana mmoja aliinuka kwa haraka na kumfuata,
"vipi boss na shem mambo" kijana huyo aliongea huku akijaribu kuvuta kumbukumbu kana kwamba kama aliwahi kuona sura hizo mahali,
"sijui kama nakufananisha au lah" kijana huyo aliongea huku wakiendelea kuzoena,
"au basi sio wewe" kijana huyo aliongea hayo lakini lengo lake lilikua ni kumchanganya Genes asahau kubana milango, hivyo kutokana na mawazo aliyokua nayo alijisahau na kuacha funguo zikining'inia mlangoni.
Kijana mwingine aliinuka na kuchukua funguo kisha kurudi kuketi huku mwingine akiwafuata akina Genes nyuma.
Udogo wa Eledy na Eledius ulifanya kuonekane kama kwenye gari hakuna mtu mwingine,
"OYA FASTA WAKO HUKU OFISI ZA DHL" ni ujumbe mfupi uliongia kwenye simu ya kijana aliyechukua funguo ya gari ya Genes,
bila kusita kijana huyo aliingia ndani ya gari na kuiondoa kwa kasi eneo hilo.
****
Genes na Angel walifika katika duka la kuuza silaha,wakachagua bunduki,baada ya kukamilisha usajili wa haraka ukichangia na pesa ilitumika kurahisisha mambo kukwepa mlolongo.
"nani ataishika sasa" Angel aliuliza,
"wewe shika" Genes alijibu,
"ahka" naogopa Angel alijibu, baada ya mabishano na wote kukataa kuiweka mkononi basi walikubaliana waiache pale waende kutafuta mtu wakuichukua.
walitoka eneo hilo kwa haraka,
"twende haraka watoto kule kwenye gari wakiamka watalia" Angel alisema huku akimshika Genes mkono wakiongeza mwendo wa Kutembea.
Bila kuzingatia sheria za barabara kwa kuangalia pande zote kabla ya kuvuka kulikua na lori lililobeba sabuni lilikua mwendo kasi,
"mamaa nakufaaaaa" ilikua sauti kutoka kwa Angel aliyotoa huku akimkumbatia Genes kutaka msaada àmbao Genes pia asingeweza kuutoa kwani mbele yao lori hilo lisingeweza kuwakwepa,waligongwa vibaya na kukanyangwa, kundi la watu lilikusanyika kushuhudia ajali hiyo mbaya,
"hawawezi kupona hawa" yalikua maneno ya watu wakisubiri askari wa usalama barabarani kuja kupima ajali,
Genes na Angel walikua wakigara gara chini,damu ziliwatoka kwa kasi,sura zao hazikutambulika vizuri na hiyo ilitokana na majeraha waliyopata zaidi sehemu za kichwani,waandishi wa habari walifika kwa haraka na kuanza kuripoti mitandaoni,
MTU NA MPENZI WAKE WAPATA AJALI MBAYA WAPO HALI MAHUTIHUTI ulikua ujumbe ulioambatana na picha ya Genes pamoja na Genes wakiwa bado ardhini uliotumwa katika Facebook.
***
Nyumbani kwa Miriam bado shamrashamra ziliendelea kupamba moto,nyama choma zilizidi kupaliwa mkaa taratibu, kundi la muziki la Arusha maarufu kama WEUSI liliitwa kutumbuiza na kulingana na mda Genes aliotoa taarifa ya kutoka KIA basi Miriam aliamini mda sio mrefu ataonana na Genes,watoto na mama watoto na hadi wakati huo pia hakujua kama mama watoto ni Angel aliyewahi kupigana nae kipindi cha nyuma...
Mwendo wa saa kumi na moja jioni habari kubwa katika jiji la Arusha ni kuhusu ajali mbaya kwa mtu na mkewe kugongwa na gari. Habari hiyo ilisambaa kwa kasi ya ajabu huku walioshuhudia wakiamini hakuna atakayepona.
Genes na Angel walianza kuongezewa damu pamoja na kushonwa vidonda,huku utaratibu wa kutafuta ndugu zao kupitia mawasiliano ukiendelea,simu ya Genes ilipekuliwa na namba ya Miriam ilionekana ndio namba inayowasiliana sana,
"Sasa huyu jina kaandika MKE WANGU atakua katoka wapi na huyu mwanamke mwingine" alisema daktari mmoja huku matibabu yakiendelea
"hawa vijana utawaweza sasa ndio maana Ukimwi hautaisha milele sasa ona huu utakua nchepuko wake" daktari mwingine alijibu na hapo Miriam alipigiwa simu ili apewe taarifa,
"habari yako" ilikua sauti ya upole iliyosikika katika simu ya Miriam aliyekua na hamu kubwa ya kumuona Genes akirejea nyumbani,
"salama tu nani mwenzangu?"Miriam alijibu na kuuliza swali,
"mimi naitwa doctor Emanuel napiga simu kutoka hospital ya Mount M.....)
"kwani vipi kuna nini tena" Miriam alimkata daktari maneno,
"aha hapa kuna tatizo kidogo, kuna mwanaume mmoja aidha ni mume wako au mchumba wako yupo na mwanamke mmoja hivi sasa wamepata ajali na kuletwa hapa hospital, tunaomba ufike kuthibitisha wodi ya kwanza chumba namba 7" daktari alimueleza kifupi,
"vipi watoto wako hapo au wapi?" Miriam aliuliza kwa haraka kwani slishajua ni Genes na mwanamke mwenye watoto wake.
Ilikua taarifa mbaya iliyofanya kila mtu pale ukumbini alie,
"yaani Mungu kwa nini umeruhusu haya yatokee,baba wa mbinguni nakuomba ona machozi yangu nayomwaga kila kukicha kila napokaribia kupata faraja Mungu hunipa kilio naomba nisamehe kama kuna kosa nimewahi kufanya lenye kuelekea adhabu hizi" yalikua maneno ya Miriam kupitia kipasa sauti kisha kufuatiwa na kilio kikubwa.
Haraka alimuita mmojawapo wa madereva wake,
"tuwahi hospital haraka" Miriam alitamka akiandamana na marafiki zake watatu ambao pia ni matajiri wa jiji la Arusha.
Walifika hospital mwendo wa saa moja kamili Miriam hakuweza kumtambua mumewe kwa haraka kwa jinsi alivyoumia sehemu za usoni na kufungwa kwa vitambaa pia hata sura ya Angel haikuweza kuonekana pia,
"kwanza wanaendeleaje?" lilikua swali la kwanza kutoka kwa Miriam mara baads ya kuingia wodini,
"kweli hali zao sio nzuri sana saivi tunawahamishia katika chumba ya uangalizi maalumu ICU (intensive Care Unit) kwa sababu wote pia wamepata majereha hadi kwenye ubongo,hapa hawawezi kuongea wala hawasikii kitu kwa kifupi hawa tuombe tu Mungu "daktait aliongea huku akimbembeleza Miriam aache kulia,
"ila kuna watoto pia wako wapi au wamekufa mnaogopa kusema" Miriam aliuliza swali ambalo madaktari na maaskari walioitwa kuja kupima ajali hawalumuelewa,
"watoto gani hawa waligongwa na gari hapo karibu na bank ha NMB kama daktari alivyokwisha kueleza,
"no! no! no! ( hapana!, hapana! hapana!) mimi huyu ni mume wangu na huyu ni mke mwenzangu wametoka Dar es salam pamoja na watoto wawili mapacha sasa watoto watakua wapi na gari lipo wapi au itakua watoto wapo kwenye gari ??" Miriam aliuliza kwa wasiwasi mkubwa huenda watoto hawapo salama
***
Gari yenye watoto ilipelekwa moja kwa moja hadi kwa mafundi stadi maeneo ya Ungalimited haikuisha lisaa tayari gari lilibadilishwa namba na pia walizuia rangi halisi ya gari kwa sura ya kuvisha zilizoundwa maalumu kwa ajili ya wezi wa magari.
Gari hiyo ilitakiwa ipelekwe nchini Kenya usiku huo huo kupitia Namanga, kila kitu kilikamilika askari wa barabarani waliokua wanashirikiana na majambazi hao walitoa ruhusa kua gari isafirishwe.
"Hawa watoto tutawatupa njiani huko wafe wenyewe maana tukiwaacha mahali ovyo wanaweza kusababishwa tukamatwe
"alisema jambazi mmoja,watoto walipuliziwa sumu ya kuwafanya walale usingizi mzito na safari ikaanza,gari lilitembea mwendo kasi ili liweze kufika eneo husika kabla ya mapambazuko.
***
Nyumbani kwa Miriam sherehe iligeuka kilio,kila mtu alimuonea huruma Miriam japo hakueleza chochote anachofanyiwa na Genes,
"sasa kama anajirusha na vimada wake kwa nini Mungu asimuadhibu ?" alitamka dada mmoja,
"sahivi tusiseme hivyo inabidi tuangalie ni kwa jinsi gani watapona" Miriam aliongea huku akilia.
Taarifa ya kupotea kwa watoto pamoja na gari ilifika kituo cha polisi na haraka askari wa barabarani wote walipewa taarifa ya kukaa makini,hasa askari wa mipaka ya Arusha,walitaka kuhakikisha gari hiyo haitatoka nje ya Arusha.
***
"vipi kuna mbaya?"
"haina mbaya kabisa ila jaribuni kuwahi maana tayari taarifa ziko polisi"
"basi sawa chukua hii kidogo nyingine tutakamilisha mzigo ukitoka".
Yalikua mazungumzo kati ya jambazi aliyekua anaendesha gari iliyoibwa akimpa askari wa barabarani rushwa ili asiweze kumzuia,safari ikaendelea
***http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Miriam akiondoka hospital nakuwaachia madaktari kazi ya kuwapa matibabu ya uhakika ili waweze kurudia hali zao za kawaida.
***
Katika pori moja lililopo Longido barabara ya kuelekea Namanga hadi Nairobi kulikua na Nyani mmoja aliyeishi kwa kujitenga alikua nyani jike, aliishi peke yake porini hapo na hiyo ilitokana na kuua binadamu kitu kilichomuumiza na kuamua kuishi mbali na wenzake kama ishara ya kutubu.
Mida ya usiku alizunguka zunguka kujitafutia chakula porini hapo na bila kutegemea alijikuta anaelekea karibu na barabara, lakini kuona gari alikimbia kwa kujificha alikua hataki kabisa kuonekana aligeuka na kushuhudia gari likiingia porini, watoto walishushwa kwenye gari kisha kufukiwa na majani makavu na ghafla nyani huyo alishuhudia moshi ukivuka kana kwamba moto utawaka mda huo,gari liliondoka kwa kasi na kuacha moshi ukivuka,huyo nyani haraka alielekea mahali hapo na kuzima moto huo kwa kutumia majani mabichi kwani ulikua bado haujakolea,kwa haraka nyani huyo aliwabeba na kuingia nao katikati ya pori.
"itakua wamekufa maana hawahemi" nyani huyo aliewaza baada ya kuona hawahemi lakini ukweli ni kwamba walipuliziwa sumu ambayo ingewafanya walale ndani ya saa 24.
Basi nyani kuona wamekufa usiku huo huo alichimba shimo ili aweze kuwazika watoto hao,tena aliamini kwa kufanya hivyo ndipo atasamehewa kosa lake la kuua binadamu kipindi akifanya mazoezi ya kulenga shabaha kwa manati aliyofanya porini huko kwani siku moja alimuua muwindaji mmoja kitendo hicho ndicho kilimfanya ajitenge.
Alichimba shimo kwa haraka kutumia mti uliochongoka akisadiana na kucha zake ndefu,hadi wakati huo Eledy na Eledius walikua katika usingizi mzito.
Shimo lilifika futi tatu kuenda chini, hapo aliwachukua na kuwalaza hapo ila kabla hajaanza kuwafukia wazo lilimjia,
"ngoja niwaache hadi waanze kunuka ili niwafukie kwani huenda wamezia" nyani huyo alijawa na wazo hilo na haraka alichukua majani na kuwafunika kisha akalala pembeni.
***
Alfajiri Miriam aliamka na haraka alianza safari ya Mount Meru kujua hali za akina Genes,
"bado hawajazinduka?"
"bado hata dalili kwa kweli hatujaona" yalikua majibizano kati ya Miriam na daktari aliyekua wodini.
Bila kuchelewa Miriam alifanya utaratibu wa kuwasafirisha Genes na Angel hadi hospital kuu ya nchini Kenya ijulikanayo kama Kenyatta national hospital iliyopo jijini Nairobi. Ndege ilikodishwa maalumu kwa ajili ya kuwabeba wagonjwa hao,
"huku hakuna wagonjwa wengine wanaotakiwa kuenda kutibiwa huko Nairobi?" Miriam alimuuliza mganga mkuu wa pale,
"wapo wengi wameshindwa gharama" mganga mkuu alijibu,
"Basi najitolea kuwasapa usafiri na matibabu ya wote" Miriam alijitolea kuwalipia wagonjwa wote waliokosa uwezo wakuenda kupata huduma nje ya nchi. Hivyo ndege yenye uwezo wa kubeba wagonjwa 90 waliotakiwa kusaidiwa na Miriam walipakizwa kwenye ndege maalumu na kusafirishwa hadi Nairobi Kenya.
***
Hadi mwendo wa saa saba mchana bado Eledy na Eledius walikua hawajazinduka, lakini nyani hakuenda mbali na eneo alilowahifadhi kwani alihofia wanaweza kudhuriwa na wanyama wengine wakali, alikaa na manati yake kuhakikisha usalama eneo lile.
Polisi nao waliendelea kufanya uchunguzi wa gari ya Miriam, walifanya msako katika maficho yote bila mafanikio,
"achaneni na gari sahivi tafuteni tu watoto wa mume wangu gharama zote nitalipa au kwa yoyote atakayekua na taarifa basi zawadi aitakayo itatolewa" yalikua maneno ya Miriam kutoka Nairobi,Kenya kupitia njia ya simu.
Je nini kitatokea baada ya hapo,Eledy na Eledius watapatikana au nyani atawafukia na je wasipofukiwa wataweza kuishi na nyani porini ? Je Angel na Genes watapona na itakuaje Miriam atafanyaje mara atakapogundua mke mwenzake ni Angel ?? Haya na mengine tukutane jumatano mahali hapa.....
Hapa naunganisha sehemu ya kwanza ya ile chombezo sasa anza nayo??
SAFARI YA MAREKANI-01
Deo Massawe 0653195298.
"Mambo mrembo"
"Poa kaka za sahizi"
"Nzur tu dada nimekuona tokea nkiwa mbali umesimama hapa juani vipi dada kunani ?"
"Acha tu kaka nina mawazo yangu binafsi kuna ofisi nilipeleka vyeti vyangu vya kuombea kazi wala sijafanikiwa me nimechoka kabisa saiv heri tu nirudi nyumbani nikakae na mama yangu nimsaidie angalau kazi,"
"Kwa nini dada unasema hivo ?/kwani huna ajira?"
"Kaka angu huu ni mwaka wa sita natafuta ajira sijapata na ndo hivo sina mtaji wa kufanya hata biashara yoyote sijui hata nifanye nini",
"ooh sawa dada mimi naitwa Anekke naishi Tanga ila hapa Dar es salam nipo kwa ajili ya kutafuta watu wanne yaani wavulana wawili na wasichana wawili,wote wawe na mvuto maana wanahitajika kufanya kazi katika mgahawa mmoja huko Marekani,sijui kama nawe utakuabali hiyo tenda dada uangu",?
" ooh my God (ooh mungu wangu) umejibu maombi yangu, naomba kaka yangu nisaidie tu maana nimeteseka sana kupata ajira sasa kama ipo ya kutoka tena nje ya nchi ndo nzur nkakae na wazungu",
"Sawa dada nitakusaidia, tena wewe itabidi ukakae reception (mapokezi) maana una mvuto wa kutosha,sasa chukua namba zangu za simu ili tuwasiliane ila cha kufanya we tafuta msichana mmoja mwenye mvuto kama wewe na wanaume wawili wenye mvuto maana mgahawa wenyewe lazima wakae watu wakuvutia wateja".
Hayo yalikua maongezi kati ya Anekke na mwanadada alieitwa Sikujua, waliokutana katika kituo cha daladala huko Posta,Dar es salaam, Sikujua alikua kashika bahasha yenye vyeti na bahasha ilionekana kuchakaa kana kwamba hubebwa Mara kwa Mara akizunguka katika maofisi mbalimbali kuomba kazi bila mafanikio kwani alikua mtu wa kujiheshimu hivyo alijikuta kila ofisi anayoingia anakutana na viongozi wa kiume hivyo kwa uzuri aliokua nao basi aliombwa rushwa ya ngono kwenye kila ofisi aliyopeleka vyeti,na yeye alishaapa hatokaa atoe mwili wake kupata kazi na ndo kitu kilimfanya kutopata kazi kwani kila alipoombwa mapenzi alijibu kwa zarau na kuondoka.
*********
Anekke ambae aliejitambulisha kwa Sikujua kwa uhalisia wake alikua mzaliwa wa Lagos Nigeria, ila alikaa sana nchini Tanzania ambapo pia alijitahidi kujifunza lugha ya kiswahili na kwa hiyo kwa alivyokua kila mtu aliamini ni mtanzani.
Anekke alijihusisha na biashara ya kuuza binadamu kutoka nchi mbali mbali za Africa na kuwasafirisha nchi za ulaya na uarabuni ambapo alijipatia utajiri mkubwa sana,kwani biashara hiyo alifanya kwa siri sana na alitumia pesa nyingi kuhonga ili kupata visa na kuhonga balozi husika kutia sahihi ya safari za halali. Kazi hiyo aliifanya kwa kuagizwa na matajiri wakubwa zaidi yake na kwa wakati huo ilikua ni kazi ya kumtafutia tajiri mmoja alieitwa Michael Reuben, aliishi jimbo la Los Angeles,Marekan ila alikua mtu wa kuzunguka sana katika majiji makubwa duniani ili kujiingizia kipato kwa kazi aliyokua anafanya.
**********
"Shoga hebu njoo hapa home chapu nikupe mchapo na wewe acha kujifungia tu ndani wanakwambia mtembea bure sio sawa na mkaa bure"
"Hee! nawe Sikujua ukishapata mwanaume akikununulia kichupi tu lazima uniite ili nikuone ukikijaribisha, kwa nini huyo mwanaume asikuvalishe huko huko ?"
"Shoga njoo mwenzio tunakwea pipa huyoo Marekani,"
"Mm Kweli leo umelewa marekani tena? ila ngoja nifike hapo kwako maana nilitoka kwa Jumannne saiv kuzungumza nae kuhusu lile suala la kikundi chetu kuanza kilimo cha matikiti huko Hedaru",
" weeeee! shogaa mambo ya matikiti tuwaachie waliokataa shule sie tunaenda Marekani ".
Yalikua maongezi kati ya Sikujua na rafiki yake aitwae Gema, kwa pamoja walihangaika kwa siku nyingi kutafuta ajira baada ya kumalizia masomo ya chuo kikuu,na hadi wakati huo walishakata tamaa ya kutafuta ajira kwani walishaunda kikundi chao cha watu sita kwa ajili ya kuenda kulima matikiti maji Baada ya dakika 20 Gema alikua kashafika kwa Sikujua,
" sasa shoga angu leo nikiwa nasubiria daladala pale posta akatokea kaka mmoja sio mkaka sana yaani ni mwenye umri kama miaka 40 hivi tena handsome sana, tukaongea then (alafu) akanipa namba ya simu ili nimpigie kwani kanambia tunaenda kupewa kazi huko marekani ya kuendesha mgahawa wa kitalii sasa kanambia mimi nitafute msichana mmoja tuwe wawili na wanaume wawili,maana mgahawa unahitaji wahudumu wanne ndo maana nkakuita wewe hapa",
"Heeee! nikweli au unatania ?",
" nikweli kabisa we lazima tufanye haraka maana tiketi zishaandaliwa kila kitu yani sisi hatutoi hata mia yeye anatugaramia kila kitu",
"Sasa wewe Sikujua kama umeambiwa wanne na sisi unajua tuko kikundi cha watu watano marafiki tusiotengana itakuaje na ndo hivi tunataka tukalime kwa pamoja ??
" haaa ! Gema nishakuambia jembe tuachie waliokimbia umande na pia nimesisitizwa kua nitafute wenye mvuto hivyo basi sisi wawili tushakamilika wasichana wanaume wenye mvuto wenye mvuto katika kikundi chetu ni Hilary na Jumanne, ila huyu furaha na Benjamini mungu kawanyima mvuto hivyo watabaki huku wakalime pamoja,tena ikiwezekana waoane ili wazidi kuendeleza kizazi cha watu wenye sura mbaya",
Sikujua na Gema waliongea mengi na hapo wakaamua kuwaita akina Hilary na Jumanne ili kuwajulisha huo mpango wakupata kazi nchini Marekani.
********
"Ongea dada nakusikia"
"Nilikua nakwambia tayar nishapata wenzangu"
"Wana mvuto lakini ?"
"Kama ulivonambia yaani kama huyu mwenzangu ana viziwa viko kama vya mtoto wa miaka sita kwa kweli tuko vizuri kaka na pia tushajipanga tayar kwa safari.
" sasa Fanya hivi wapige picha pamoja na wewe unitumie kwenye WhatsApp ".
Yalikua mazungumzo kati ya Anekke na Sikujua.
Hapo hapo Anekke aliwasiliana na Michael Reuben kwenye barua pepe (E-mail) ambapo kwa wakati huo alikua Ontario nchini Canada kwa shughuli zake, alimfahamisha kurudi Los Angeles Marekani,kwani atamletea watu wake alioagizwa ili aweze kulipwa pesa yake,kwani Anekke ndo ilikua kazi yake akishakukabidhi watu wako basi yeye huchukua hela yake na kuondoka.
**********
Jumanne na Hilary waliandamana pamoja na marafiki zao yaani Furaha na Benjamini,
"sasa jamani Sikujua shoga angu unaniacha huku mwenyewe ?" Furaha alimuuliza Sikujua,
" utabaki na Benjamin usiogope sisi tutawatumia pesa kidogo kwa Western Union,nyie mtakua mnalima matikiti kwa wingi huku" Sikujua aliongea kwa kejeli na hapo Benjamin na Furaha wakaondoka kwa hasira kwani waliona wivu wenzao kuondoka na kuwaacha,ila Benjamin alikua na upeo wa akili sana na ghafla alimuamuru Furaha warudi kuna kitu alisahau kuwaeleza hao wanaosafiri na bila ubishi Furaha akakubali warudi.
"Ila Sikujua angalieni huko mnakoeda maana kuna mtoto wa shangazi yangu alichukuliwa hivyo hivyo kupelekwa kwa wazungu ila mateso aliyoenda kupata mungu ndo anayajua maana alie___"
Kabla hajamalizia Sikujua alimtemea mate ya usoni na Benjamin aliondoka kwa aibu pamoja na Furaha.
"Nendeni huko na lifuraha lako tena mkalime pamoja yaani mungu angewapa mvuto nanyi tungeenda na nyie ila rafiki yenu jembe wivu tu mnao hapa nyooooo!" Sikujua aliwasindikiza kwa maneno ya kejeli.
Tayari kikosi cha watu wanne kilikua tayari kwa safari na hapo wote walipanga waage nyumbani kua wamepata kazi huko Bujumbura,Burundi, kwani Sikujua alipewa mashariti ya kutosema ukweli kwa wazazi wao na wote wakawa wasiri kwa wazazi wao.
Baada ya kujipanga kwa kila kitu basi safari ilipangwa ifanyike jumamosi. Na hapo waliwasiliana na Anekke kwamba wapo tayari ndipo wakapanga wakutane uwanja wa Julius Nyerere.
**********
Mida ya saa tatu kasoro robo usiku siku ya jumamosi tayari Sikujua,Gema, Jumanne na Hilary walikua uwanja wa Julius Nyerere wakimsubiri Anekke huku wakipiga story mbali mbali
"Yaani mwaka huu ni wangu nikifika kitu cha kwanza namtafuta Rihhana nipige nae selfie nipost kwenye Facebook" Sikujua alisema,
"Mimi nataka Beyonce awe mwenyeji wangu" Gema alisema,
"Mimi namuonaga tu Anord Schezniger kwenye runinga sasa nitamuona uso kwa uso" Hilary alisema
"Mimi kuanzia saiv nataka mniite J'Four" nae Jumanne alisema wote wakacheka na hapo Anekke akatokea akiwa na visa zenye hadi passport size.Hapo hakuna alieuliza wa kujiuliza visa imeandaliwaje maana walikua na hamu tu ya kusafiri.
Walipanda ndege ya shirika la ndege la Ethiopia ambapo safari ilitakiwa waende watue Addis Abab nchini Ethiopia kisha waruke tena hadi Qatar na hapo wapande ingne kutoka Qatar hadi Los Angeles Marekani hivyo basi kutoka Qatar hadi Los Angeles walitakiwa wakapande ndege yenye kutembea masafa marefu angani nayo ilikua ndege kutoka kampuni ya Emirates.
Anekke alikaa siti ya nyuma huku Sikujua na wenzake wakikaa siti za mbele.wote wakiwa na hamu ya kufika mapema.
Huko Los Angeles nako Michael Reuben alikua akisubiria Anekke alete watu wake.
Fursa ya kuwatafuta watoto wa Genes iliyotokewa na Miriam ilipokelewa vizuri, kila mtu alikua akijaribu bahati yake.
Hatimaye taarifa zilifika jijini Nairobi,
"mpenzi msikilizaji twende nchini Tanzania ambapo dau la milioni 30 lililovunja rekodi limetangazwa kwa mtu yeyote atakayefanikisha kupatikana kwa watoto wawili mapacha waliopotea jana,watoto hao walikua ndani ya gari hivyo muhimu watoto wapatikane gari haina haja" ilikua sauti ya mtangazaji Denis Mwambi wa kituo cha Kenya Barbocost cooperation kwenye taarifa ya habari.
***
Hali ya Angel na Genes ilizidi kua mbaya hata ile kujaribu kufungua macho kwa mbali ilitoweka kabisa,
"tufanyeje kuokoa maisha yao" Miriam alimuuliza muuguzi mkuu,
"hapa kweli tuzidi kuomba Mungu atende miujiza tu maana hali zao ni mbaya sana"muuguzi huyo alijibu huku akitikisa kichwa kutoka kushoto kwenda kulia kuashiria kukata tamaa.
Miriam aliamini Genes na Angel wakifa basi kuna asilimia kubwa ya watoto wao kupotea kabisa,
"haiwezekani lazima wapone nipo tayari mali zangu ziyumbe ila wapone" Miriam alisema kisha aliomba kujua hospital yoyote duniani ambayo wangeweza kurudisha afya ya mumewe na mke mwenza wake.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"hospital kuu ya Japan ina wataalamu wa mambo ya ubongo na mifupa sana sema gharama zake ni kubwa sana" muuguzi huyo alimjibu Miriam,
"kuhusu gharama ondoa shaka we niandikie niruhusiwe kuwasafirisha hata leo sitaki kuwapoteza watu wangu na kikubwa kuna watoto wanaoteseka kama hawa wangekua wazima nahisi wangepatikana kirahisi" Miriam alijibu na haraka taratibu za safari zilipangwa.
***
Wale majabazi walioiba lile gari kisha kuwatupa watoto porini walipagawa kusikia dau lililotangazwa kuhusu kwa mtu atakayewezesha kupatikana kwa watoto hao,
"turudi kama tutawakuta maana huenda malaika walishuka wakawaokoa kwenye ule moto maana hatujapata hata taarifa za lile pori kuungua" jambazi mmoja alimueleza mwenzake kisha kikundi kizima kilijipanga kuvamia pori hilo kutafuta hata mifupa yao.
***
Mwendo wa saa kumi na moja jioni katika hali ya kushangaza nyani aliyekaa pembeni mwa shimo alomowahifadhi Eledy na Eledius alishtuka kusikia mmojawapo ya watoto akilia,
"mama! mama! mama!, Eledy alizinduka wa kwanza,alikua na njaa hadi tumbo kurudi ndani,
nyani alichangangikiwa kusikia sauti hiyo hakujua cha kufanya kwani aliamini kama angeenda na kuondoa majani aliyoweka juu ya shimo basi watoto wangeogopa sana kutokana sura yake,
" nyani akapata akili ya kusubiri hadi giza liingie ili awatoe shimoni kwani usiku huo wasingeweza kumuona,hapo alitafuta matunda pori yaliyokua karibu na eneo lile kwani aliamini watoto watakua na njaa kali.
Eledius nae alizinduka kisha wote wakawa wanalia kwa unyonge kutokana na ukosefu wa nguvu mwilini lakini nyani alizidi kuwa na subira akisubiri giza liingie.
***
Kikundi cha majambazi watano kiliondoka nchini Kenya ili kuvamia katika pori la Namanga lengo likiwa ni kuwatafuta watoto waliowatupa.
"tukiwapata tutaacha hata ujambazi kwani million 30 tutagawana kila mmoja" mojawapo ya majambazi alisema
***
Giza lilipoingia kitu cha kwanza nyani aliondoa majani yaliyofunika shimo,kisha kuwatoa wale watoto waliokua hawajitambui kwa njaa kali waliyokua nayo,alichukua zabibu akawalisha kwa shida kwani hakutaka wajue ni nini kinachowalisha na mazingira gani wapo,
"mechiba mama" Eledius alitamka baada ya kujihisi kushiba, nyani aliacha kumlisha kwa kuona mtoto akizuia mdomo kuashiria kutotaka tena, hapo alianza kumlisha Eledius kwa haraka wote waliposhiba walianza kuchangamka kwa,
"mama juice" Eledius alisema kwani alizoea kila amalizapo kula alikua akipewa juice lakini alishangazwa kitendo cha mama yake kutojibu kitu, zaidi ya kulazwa vizuri kwenye majani malaini,
Baada ya mda usingizi uliwapitia na kulala,
nyani alikaa macho akiwalinda na hakujua pakikucha nini kitafuata baada ya watoto kuona mazingira waliyopo na mtu anayewalea.
***
hatua ya kwanza waliyofanya majambazi baada ya kuingia porini, ni kuenda moja kwa moja hadi mahali walipowatupa wale watoto na kuwasha moto,
"basi wapo hai" jambazi mmoja alitamka baada ya kuona moto ulizimwa hata kabla haujawaka vizuri,
"sasa itakua wapo hai ndio je wako wapi?" jambazi mwingine alitamka kisha wote wakawasha kurunzi (torch) zao kutafuta angalau nyayo za watu,
"hizi hapa nyayo zilizotokea hapa" mmojawapo alisema na safari ikaanza kuzifuata na hakika zilikua nyayo za yule nyani.
***
usiku huo nyani alikaa akitafakari jinsi binadamu walivyo na roho ngumu ya kutupa watoto walio hai, bila sababu na hakika aliapa kutoona binadamu yoyote akiwachukua akins Eledy,
"hawa nitawatunza mimi kama mimi na watanizoea tu sitaki hawa binadamu wenye roho ngumu wawachukue" nyani huyo aliwaza huku akiishika manati yake na kutikisa kichwa kuashiria ndio ulinzi wa watoto hao.
Majambazi nao walipiga hatua kubwa ,lakini kichwani kila mmoja alijiwa na wazo la kuwasaliti wenzake mara watoto wakipatikana.
***
hali ya Angel ilizidi kuwa mbaya tena ndege ikiwa angani damu zilimtoka puani na mdomoni,
Miriam alipiga magoti na kumuomba Mungu afanye miujiza wapate kufika Japan ili matibabu yapatikane..
Hali ya hewa ilibadilika ghafla,mvua ilianza kunyesha katika pori la Namanga, nyani alipata kazi ya kuwabembeleza watoto huku akijaribu kuwakinga kusudi wasidondokewe na hata tone la maji, aliwaviringishia majani malaini ili kuwazuia baridi.
Majambazi walizidi kufuata nyayo zilizotoka sehemu watoto walipotupwa lakini walianza kuzipoteza kwa sababu ya mvua iliyoendelea kunyesha,
"itakua wapo maeneo haya haya tu, kama bado wapo hai hii million 30 lazima tugawane wote kesho jioni" mojawapo wa majambazi aliyeitwa Miraj aliongea,
"hapa lazima tuwapate" wote walijibu" lakini kila mmoja kichwani akipanga kuwauwa wenzake ili abaki na watoto.
Mvua iliongezeka zaidi hadi kuyashibda nguvu majani waliyovishwa akina Eledy, hapo walianza kulia kwa sauti kubwa huku wakipiga kelele kumuita mama,
" mamaa baridi mama baridi"Eledius alilia kwa sauti,Nyani aliendelea kuwabembeleza bila mafanikio, na ghafla kwa mbali aliona miangaza ya kurunzi (torch) zilizoshikiwa na watu kama watano, nyani huyo moja kwa moja alijua ni wawindaji haramu wa swala na digidigi, haraka alipata wazo juu ya watoto wanaolia,
"hapa nitawaziba midomo kwa mda hadi hawa wapite maana wakiendelea kulia lazima watawachukua kwani watashangaa mimi kulea binadamu" nyani huyo aliwaza kisha kwa haraka aliwashika akina Eledy na kuwaziba midomo yao, aliziba na kuachia kila baada ya dakika moja na nusu, bado mwanga ulizidi kusogea walipokua wameweka kambi
Na mvua iliongezeka zaidi.
"we tulia" Miraj alliongea kwa furaha baada ya kusikia sauti ya watoto wakilia kwa mbali,sauti iliwachanganya inakotokea kwa sababu ya mvua na upepo mkali,
"twendeni na huku" Miraj aliongea huku akielekeza wenzie,wote walitembea kasi kuhakikisha hawapotezi sauti zile kwani walishajua upande gani zinatokea.
Nyani kwa mbali aliona kabisa watu ni watano na wameshika silaha mkononi,
"itakua wana nia mbaya,mbona wako makini kufuatilia hizi sauti za vilio vya watoto?" Nyani huyo aliwaza,kukaribu kuwaziba mdomo ndio kabisa walirusha mateke,hapo nyani kwa haraka alichukua kamba akawafunganisha sehemu moja ili hata kama ni kuwaokoa basi iwe rahisi.
Alipomaliza kuwafunganisha aliwaacha chini kwenye shimo aliloweka majani juu yake na kupanda juu ya mti uliokua jirani,ili aangalie nini kinachoendelea,manati yake yakiwa mkononi aliamini kama akikulenga moja lazima uzimie,
"wale Mungu kweli anatupenda" jambazi mmoja alitamka huku akilengesha mwanga chini ya mti walimoachwa Eledy na Eledius. Eledy na Eledius waliona mwanga mkali ukimulika walishtuka sana na kujikuta wanakaa kimya
Nyani alitulia juu ya mtu akiwaza ni mwa jinsi gani angeweza kupambana na kundi la watu wenye silaha,
"Mungu aliye mbinguni atasaidia niokoe hawa watoto wasio na hatia" nyani aliwaza na kuinua kichwa juu kama ishara ya kumuomba Mungu.
Kundi la majambazi lilifika eneo sauti zilipokua zinatokea ila kwa mda huo kukawa kimya,
walimulika huku na huko bila mafanikio yoyote wakaaza kukata tamaa lakini mmojawapo akahisi harufu ya manukato ambayo baada ya kurudisha kumbukumbu nyuma aliikumbuka harufu hiyo aliiskia kwa watoto aliowatupa ,hivyo kwa uhakika wote wakajua wapo maeneo yale waliendelea kutafuta,
Nyani alizidi kuchanganyikiwa hasa alipoangalia akiba ya mawe akakuta ana jiwe moja na maadui wako watano,
"nitawaokoa kweli? Ila Mungu atanipigania" Nyani aliwaza.
Shimo walimohifadhiwa akina Eledy na Eledius lilichimbwa hapo hapo chini ya mtu mkubwa sehemu yenye kilima ili kuzuia maji kuingia ndani,jambazi mmoja alipanda hapo kilimani,ghafla kwa kishindo alidumbukia kwenye shimo, kwa haraka alihisi lilikua shimo la kutegea wanyama kama swala na ngurue mwitu, ila katika hali ya kushangaza ndani ya shimo hilo waliwakuta Eledy na Eledius wakitetemeka kwa woga,
Jambazi huyo alitaka kukaa kimya ili awaondoe wenzake eneo lile kisha aje awachukue mwenyewe,
Wakati huo nyani alikaa juu ya mti akiendelea kuomba Mungu awalinde watoto,
"itakua hawapo maeneo haya bhana" jambazi huyo aliwaambia wenzake huku akitaka waondoke maeneo yale, kabla hawajapiga hatua nyingi Eledius alilia wa sauti baada ya kuumwa na siafu na majambazi waligeuka haraka,walishika bastola mkononi zenye uwezo wa kuua bila kutoa sauti (silence) kurudi mahali sauti ilipotokea Miraj alishuhudia watoto wakiwa shimoni na bila kusita alimfyatulia risasi yule jambazi aliyedumbukia kule shimoni,
"Shiiiit, kumbe ndio maana ulituambia tuondoke maeneo haya ulitaka kutugeuka pumbavu zako" Miraj kama kiongozi wa kundi hilo alimfyatulia risasi na kumuua mwenzao,lakini kwa hasira jambazi mwingine aliamua kumfyatulia Miraj risasi,http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"hata kama wewe ni kiongozi hustahili kuwa mkali na kuua watu ovyo" jambazi huyo alisema huku akimuongezea risasi nyingine ya kifuani,
"nani alikuambia kua kiongozi akiamua kitu anapingwa?" jambazi mwingine alisema huku akifyatulia risasi yule aliyemuua kiongozi Miraj, hivyo wakabaki majambazi wawili pale.
Nyani aliendelea kushuhudia kitendo kile kilichoendelea pale, alifurahi sana kuona wameanza kuuwana wenyewe kwa wenyewe,
"sasa hapa million 30 ni yetu wawili" majambazi wale walijadili na haraka waliwachukua watoto wakaanza safari ila kabla hawajaenda mbali walisimama na katika wale wawili kuna mmoja ambaye hakufanya mauaji yoyote,
"mimi ndio inatakiwa nichukue nyingi zaidi yako" jambazi aliyeuwa alianza kuongea,
"acha mambo yako pasu kwa pasu hapa" alijibiwa.
"na wewe nakuua" wote walinyoosheana bastola, aliyebeba watoto alidai yeye ndio katoa watoto shimoni hivyo achukue nyingi kidogo,
Nyani aliwafuata kimya kimya bila kuonekana na alipoona wamesimama na kuanza kubishana hapo ndipo aliamua kutumia manati yake,aliivuta sawa sawa huku akielekeza shabaha kwa yule asiyebeba watoto, alipoachia jiwe lilitua katika kisogo, damu iliruka juu na kuanguka chini kama kiroba,huyo mwenzake hakujua nani aliyefyatua risasi kwani hukuamini kama ni jiwe, itakua kuna mwenzetu amefufuka, alijisemea huku akikimbia kuelekea alikopaki gari, huku nae nyani akimfukuzia kwa pembeni, Nyani aliapa kuliko wale watoto waende heri afe yeye.
***
Ndege kutoka Nairobi Kenya, ilitua katika kiwanja kikuu cha Japan kilichopo jijini Tokyo,Miriam wakati wote wa safari alikua akisali na kulia,aliomba Mungu afanye miujiza kuwaokoa watoto pamoja na wazazi wao,
Haraka gari maalumu iliyoandaliwa kuwabebea wagonjwa iliwasili uwanjani hapo na kuwapakia Angel na Genes kwa safari ya hospitalini.
"watapona" lilikua neno la kwanza kutoka kwa daktari wa hospital juu ya Japan, kwani kwa kuwaona waliamini utalaamu wao utawaponesha, neno hilo lilimpa Miriam nguvu,machozi yalipungua swali lake likabaki je watoto wapo wapi ??..
Mita kama ishirini kutoka sehemu majambazi walipoegesha gari basi jambazi aliyewabeba watoto aliwatua chini na kuwapulizia hewa ya kuwafanya walale usingizi,
"hapa ndio ile unalala maskini na kuamka tariji,million 30 zote lazima nioe mke wa pili" jambazi huyo alijisemea kisha akawabeba watoto na kuendelea na safari,hakika zilibaki kama hatua kumi ili alifikie gari.
Nyani alizidi kuchanganyikiwa kwani aliamini watoto ndio wanamtoka na wakati ameapa kuwasaidia tena ikiwa ni kama sehemu yake ya kufanya toba"
"Lazima niwaokoe" Nyani huyo aliwaza huku akitikisa kichwa chake kutoka kushoto kwenda kulia kuashiria kutokata tamaa,licha ya kuapa kuwasaidia basi hakujua namna ambavyo angepambana na mtu mwenye bunduki,
"ahaaa anenda kupanda nao lile gari pale" Nyani aliwaza baada ha kuona gari lililoegeshwa pembeni mwa barabara,hakutaka kupoteza mda,alikimbia haraka na kuwahi mahali gari ilipoegeshwa akajaribu kufungua mlango na kwa bahati nzuri mlango ukafunguka,haraka akachukua kisu alichokikuta ndani na kushuka kisha kukitega chini ya gurudumu kana kwa gari ikisogea tu lazima gurudumu lipasuke,alifanya kwa haraka kisha kusogea pembeni na kujificha,huku akiendelea kumuomba Mungu afanye miujiza.
***
Kati ya majambazi walipigana risasi mmoja alijitahidi kuchukua simu yake na kuwasiliana na mwenzake ambae alimuandaa barabarani ili wakachukue pesa baada ya kuwasaliti wenzake,
"sasa mimi hapa nipo mahutihuti,sasa cha kufanya hakikisha hiyo gari ikifika hapo unailipua,mimi nakufa ila sitaki hiyo pesa ikaliwe na mtu heri tukose wote hivyo li..li..pua" kisha akakata roho,
Jambazi mmoja kwa jina Jonas alikaa tayari barabarani akisubiri maelekezo ya gari ambayo ingekua imewabeba Eledy na Eledius,alishika bomu la kurusha kwa mkono ambalo lina uwezo wa kulipua mita 20 za maraba hivyo alisubiri tu gari lifike ili alirushie bomu.
***
Eledy na Eledius walirushwa ndani ya gari wakiwa hawajitambui kwa usingizi,
"Hapa nimemaliza kazi" alijisemea jambazi huyo na kufungua mlango wa mbele na kuondoa kuwasha gari tayari kuanza safari bila kujua anasubiriwa kuuawa njiani.
Kabla ya kuondoka aligeuza shingo na kuangalia nafasi ya nyuma aliyowalaza akina Eledy,
"Asante Mungu" jambazi huyo alijisemea kisha kuondoa gari kwa kasi,
"Paaaaaaaa" ilikua sauti ya gurudumu kupasuka,
"shiiiiit mchawi gani tena anaingilia kazi yangu na wakati sina historia ya kushindwa kitu?" jambazi huyo alijisemea huku akishuka kwenye gari kwa hasira alipigiza kurunzi yake kwa nguvu zote chini na kuipasua ,aliangalia gurudumu lililopasuka kwa hasira kisha kulipiga teke,haraka alifungua mlango wa gari na kutoa gurudumu la akiba,
"sasa hapa sioni vizuri na torch yangu nimepasua" jambazi huyo alijisemea.
Kwa mbali aliangalia akaona mwanga wa torch ya mwenzake aliyeuawa ila torch bado iliendelea kuwaka,
"Heri nikaichuke haraka na kurudi ili nije kufunga hili gurudumu vizuri" alisema kisha kuwafunika akina Eledy na Eledius vizuri kwa kutumia mfuko wa sulphate.
Aliondoka kwa haraka na wakati huo huo nyani hakuona sababu ya kuzubaa kwa haraka alipijichomeka haraka ndani ya gari na kuwatoa akina Eledy ,kisha kuingia nao porini. Nyani alifurahi kupita maelezo kuona ameokoa watoto tena kwa akili ndogo sana,aliinamisha kichwa chini kumshukuru Mungu, licha ya utelezi wa mvua alijitahidi kuwabeba na kutokomea nao porini.
Jambazi alifika mahali mwenzake wa mwisho alipofia na kuokota torch kisha kuondoka nayo akisindikiza kwa maneno
"Shiiit salimia shetani huko uendako."
Alianza kazi ya kubadilisha gurudumu na baada ya dakika 20 alimaliza kila kitu na kuukamata usukani,kila baada ya mda alikua akigeuka nyuma kuhakikisha watoto aliowafunika wapo,
"nashukuru sana watoto kwa kuwa mnaenda kunipa utajiri" alijisemea kimoyomoyo lakini ukweli ni kwamba kwa wakati huo tayari watoto walishachukuliwa na kilichobaki pale ni mfuko wa sulphate ambao kwa jinsi Nyani alivyouweka basi utadhani bado watoto wako pale pale.
Gari liliongeza mwendo na jambazi aliyekua akisubiri kichakani ili aweze kulilipua basi nae aliandaa bomu alilolishika kisawasawa baada ha kusikia mlio wa gari jinsi alivgoagiziwa,
"Moja,mbili, tatu" jambazi alihesabu kisha kurusha bomu lililotua moja kwa moja kwenye kioo cha mbele cha gari ,
Gari iligawanyika vipande vipande,hata haikujulikana kama imebeba mtu au la,
"wape salamu zetu huko uendako na uache tamaa" alisema mlipuaji kisha kutokomea.
***
katika hospital kuu ya Japan huko jijini Tokyo Genes na Angel walipewa huduma za haraka na za hali ya juu, walitudukiwa chupa za maji na damu,macho ya Miriam yaligeuka rangi na kuwa mekundu alilia mfululizo hasa alilia kwa sababu ya watoto ambao hajui wako wapi, simu kutoka kwa matajiri wenzake wa Arusha na Tanzania nzima zikimpigia kwa kumtaka kama anahitaji msaada wowote,
"mama ukihitaji msaada wowote utujulishe tupo kwa ajili yako" yalikua maneno ya baadhi ya wafanyakazi wa hotel Aquiline waliofanikiwa kwa wazo la Miriam la kuunda vikundi kwa ajili ya kuwezeshana kimawazo hadi kimtaji.
Anitha nae kwa mda huo alikua tajiri na kila alipowaza juu ya utajiri wake basi jina Miriam lilimjia kichwani kwani ndie chanzo cha utajiri wake,hivyo wote waliofanikiwa kupitia Miriam waliishi kumuombea aweze kutoka Japan salama na wagonjwa wake wapone pia watoto waliopotea wapatikane na yeye mwenyewe aweze kubeba mimba na kujifungua.
***
mwendo wa saa kumi na moja asubuhi katika pori la Namanga jua lilianza kuchomoza kwa mbali, mawazo yote ya nyani yakiwa ni juu ya akina Eledy na Eledius watakaposhtuka kutoka usingizini na washuhudie mazingira waliyopo na kiumbe walicho nacho hapo nyani alipata wazo la kuchana nguo ya Eledius na kuwafiringishia machoni ili wasiweze kuona kitu.
Waliposhtuka walilia sana wakitaka kufunguliwa lakini nyani hakuwaonea huruma kwani aliamini kwa kuwafungua na kuona mazingira waliyopo basi wangeweza kufa kwa woga.
Aliwatafutia matunda na asali akawalisha na hata walipotaka kujisaidia nyani aligakikisha kila kitu kinaenda vizuri,
"Siku moja watanizoea" Nyani alijiwazia zikiwa zimepita siku kumi.
***
"Genes mpenzi wangu usife tafadhali nakuomba usiniache mwenyewe" Miriam alijikuta akilia mbele ya umati wawatu hasa pale alipoambiwa kua hali ya Genes inazidi kuwa mbaya,
"huyu mwanamke anaendela vizuri na ataweza kupona ila kumbukumbu zitarudi taratibu lakini huyu mwanaume Mungu amsaidie" yalikua maneno yadaktari kwa Miriam,
"Sasa utanisaidiaje ninataka mume wangu apone"
"Hapa labda kuna madaktari bingwa kutoka katika hospital moja inayoitwa Apolo Iliyopo New Delh,India kule ndipo unaweza kutana na madaktari bingws kuliko sisi sasa gharama ya huko ni kubwa sana,hapa yenyewe tuna wagonjwa wengi wakupelekwa huko sema serikali yetu haina gharama hizo sasa huwa tunawaacha wanakufa tu huku"
"Kuhusu gharama ondoa shaka daktari,mimi gharama zote natoa na kama kuna wagonjwa walio tayari kusafirishwa huko basi waandikieni utaratibu wakupata matibabu kwa gharama zangu" Miriam aliongea hayo kisha kupiga simu kwa matajiri wenzake wa Tanzania kuwapa taarifa juu ya safari ya kuelekea India,matajiri wenzake walimuahidi kumpa ushirikiano wakila namna lakini baada ya kujadili na madaktari wa hospital kuu ya Japan basi waliamua kufanya utaratibu wa kuwatoa madaktari India waje Japan kufanya matibabu ili kuokoa gharama ya wagonjwa wengi kusafiri.
***
Katika hospital kuu ya Japan pia kulisifika kwa kuwa na wanasayansi mashuhuri sana duniani walitengeneza kemikali za aina mbali mbali
hadi nyingine zikawa ni aina ya mabomu,hivyo kutokana sababu hiyo kikosi cha kijeshi kutoka Korea kaskazini kilitamani sana kuingia katika maabara ya hospital kuu ya Japan, ili kiweze kuiba hizo kemikali na kuenda kupigana na mataifa makubwa kama Marekani, China na Russia, kikosi cha kijeshi cha Korea kikasikia taarifa hiyo ya Madaktari kutoka India watasafiri kuenda Japan,kwa ajili ya kutoa elimu na matibabu kwa wagonjwa sugu,
Walipanga namna ya kuteka ndege ya madaktari ikiwa angani ili wao waweze kusafiri na kupokelewa nchini Japan kama madaktari na haraka walianza mazoezi makali usiku na mchana,
"kwanza tukitua Japan tutaanza kufungulia wale wagonjwa wa akili waanze kupiga watu ili sisi tuweze kuiba hizo kemikali vizuri" yalikua majadiliano ya wakorea wakiendelea na mazoezi,
***
Nyani aliendelea kukaa na watoto na haraka akaanza kuwafundisha kitu kinachoitwa self difence (namna ya kujihami/kujilinda) aliwapa mafunzo bila kujali udogo wao aliwafundisha kukwepa mshale huku wakiwa wamezibwa macho,kurusha jiwe na kulenga shabaha bila kuona,yalikua mafunzo ya hali ya juu sana,watoto walizoea maisha hayo na hadi wakati huo hawakujua lolote linaloendelea,Police waliendelea kuwatafuta usiku na mchana ,na baada ha wiki sita wakahesabu watoto hao itakua wamekufa,
"ngoja tusubiri tu Miriam atoke Japan aje tufanye maziko kimawazo maana hawapo hawa watoto" yalikua maneno ya Mzee Massawe mmiliki wa Aquiline hotel Kwa wakati huo tayari umri wake ulishaenda lakini alibaki kuwa mshauri wawatu na hotel yake ilisimamiwa na Miriam.
***
Walikua madaktari kumi bingwa,kila mmoja alibeba begi kubwa lililojaa vifaa vya kazi,pamoja na nguo za kubadilisha walianza walikua tayari katika kiwanja cha ndege jijini New Delhi,walipanda ndege binafsi ambayo ingewaafirisha moja kwa moja hadi Japan.
Nchini Korea kikosi cha kijeshi kilijipanga tayari kazi iliyokua mbele yao,walivaa sura za bandia ili wafanane na hao madaktari
***
Ndege ilipaa angani marubani walikaa makini kuongoza ndege kwani hao madaktari walikua watu wamuhimu sana nchini India.
Kikosi cha Korea kilika Tayari na waliweka kambi kisirisiri kwa majirani zao Korea kusini, kwani ili ndege ifike Japan kutoka India basi lazima itumie anga ya Korea kusini, hivyo lengo lao la kuweka kambi Korea kusini ilikua ni kupaa angani na kuwachanganya marubani wa nje.
Wataalamu wa kucheza na tarakilishi (computer) kutoka Israel walikua makini kuifuafilia ndege hiyo,
Ilipofika anga ya Korea kusini basi kikosi cha Korea kaskazini kilipaa angani na ndege iliyondwa maalumu kwa mfano wahiyo ya madaktari bingwa,nao wataalamu wa computer walikata mawasiliano ya ndege iliyobeba madaktari na marubani wa nje kisha wakaunganisha mawasiliano yao hivyo wakawa wanaongozwa na kusubiriwa Japan kwa furaha.
Ndege iliyobeba madaktari ililipukiwa ikiwa katika anga Taiwan na moja kwa moja ikadumbukia katika bahari ya pasikifi.
***
Hospital ya Japan kulikua kunafanyika maandalizi makubwa kila kitu kilipangwa kuwekwa mahali pake lakini katika hali ya kustajabisha alitokea mtoto mmoja na kupiga maabara bila kuonekana na mtu, alikua mtoto mdogo ambaye ndio alikua anaanza kutembea,ghafla akaparamia meza iliyokua imesheheni kemikali ambazo zilikua zikifuatwa na kikosi cha Korea kaskazini,lilikua tukio la kushangaza kuwahi kutokea mtoto kupenya ulinzi wa maabara hadi kufikia kufanya uharibifu wa bidhaa iliyogharimu mamilioni ya pesa.
***
Miriam akiendelea kusubiri madaktari bingwa kutoka India aliamua kuingia katika chumba cha matibabu ya magonjwa ya kina mama na kueleza tatizo lake la kutoweza kutunza mimba, alishangazwa majibu,
"mbona mimi sijawahi kupigwa" Miriam alijiiuliza kwa sauti baada ya kuambiwa tatizo lake limetokana na mfumo wake wa uzazi kuna namna amewahi kupigwa aidha kwa rungu au ngumi kubwa,baada ya kufikiria sana akaweza kukumbuka siku ile aliyopigana na Angel,
"Ahaaa nimemkumbuka sema ni miaka nyingi imekatika tokea nipigane nakumbuka alinibahatisha teke la chini ya kitovu yule aliyekua mwanamke wa mume wangu Genes,
Miriam aliumia sana moyoni kugundua aliyekua mwanamke wa mumewe zamani ndiye aliyemsababishia matatizo yote hayo lakini bado hakujua kama ni huyo anayemuuguza ..
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Katika uwanja mkuu wa ndege jijini Tokyo Japan macho ya watu wote yalielekezawa kwa madaktari bingwa kutoka India, walivaa mavazi ya kidaktari na miwani iliyoambatana na kofia kubwa,wagonjwa waliokata tamaa walipata matumaini upya huku wakimshukuru Miriam kwani ndie aliyesababisha yote hayo yafanyike,wagonjwa waliokua na uwezo wa kuongea basi walisali wakiamini watapona kabisa.
Bila kupoteza mda walipanda gari maalumu lililoandaliwa kutoka uwanaja wa ndege,
"Hawa madaktari wastaarabu na hawana maringo yaani hawaataki hata kusaidiwa na mtu mizigo yao"alisema mmojawapo wa madaktari kutoka Japan alioenda kuwapokea kwani hadi wakati huo hakuna hata mmoja aliyehisiswa kua ni wanajeshi wa korea na lengo lao ni kuenda kuiba kemikali yenye uwezo wa kuunda mabomu makali.
***
Hospitalini nako furaha ilizidi kutawala Miriram alikaa pembeni ya kitanda alicholazwa Genes na Angel mda mwingi aliutumia kusali na kumshukuru Mungu kwa yote anayopitia,
"Hivi kama huna pesa dunia ya sahivi unakufa kama kuku maana hapa kama nisingekua na uwezo basi hawa ungekuta wamekufa na kuzikwa ama kweli watu wafanye kazi kwa bidii ili tufanikiwe kuyaokoa maisha yetu maana serikali saivi haimwangalii mtu tena" Miriam alikua anajisemea maneno ambayo yalikatishwa na vigelegele vya wauguzi wakiwapokea waliodhaniwa ni madaktari kutoka India,
"Asante Mungu Genes wangu na huyu mke mwenzangu wamepona'Miriama alisema bada ya kuona madaktari wakiingia ndani ya chumba cha mapokezi.
Lakini yule mwanamke aliyesababisha nisipate mtoto ndie mtu ninayemchukia tu maana amenifanya nidharaulike sana huku duniani nina pesa ila hazina thamani tu kwa kua sina mtoto" Miriam alijisemea kimoyomoyo huku akiikumbuka ile siku aliyopigana na Angel,
"Sijui kanaitwa nani tena kale kadada nikirudi Tanzania nikatafute"Miriam alijaribu kukumbuka jina lake lakini hakulipata kabisa ila sura yake ilimjia,
"Nitamjua tu"alijisemea Miriam.
***
Kwakua ilikua jioni basi madaktari waliomba kutembelea wodi zote hospitalini hapo na kuahidi kuanza kazi siku inayofuata, bila pingamizi walitembelea kila wodi huku wakitega camera ndogo ndogo kila chumba huku picha zikienda moja kwa moja hadi Korea.
***
"Jamani amezinduka njooni muone Genes anaongea"ilikua sauti ya Miriam akiita wauguzi kuja kuwaonesha kilichotoeka kwani Genes aliyekua anapumua kwa mashine alifumbua macho na kutaka kutamka neno na baada ya kujaribu kuongea bila mafanikio kwani alikua kama kakabwa na kitu shingoni,
"Miriam mke wa...ngu ni...sasame..he mimi na huyu Angel kwani tu..lipa..nga kuja kukuuwa huyu ndio yu..le mliyepigana sisi..siku ile pale Sakina hata nikifa leo nisamehe sana mke wangu na utunze watoto wangu"Genes alitamka maneno hayo na kukaa kimya kama alivyokuwa mwanzo,furaha ya Miriam kuona Genes ameongea ilikua kilio baada ya kusikia maneno yaliyotamkwa aliona kama ndoto ambayo angeziduka mda mfupi ujao,aligeuka na kumwangalia Agel kwa makini na hapo ndipo alipokumbuka sura yake vizuri ingawa kwa wakati huo ilikua imeharibiwa vibaya lakini alipata jibu kamili baada ya kukumbuka jeraha alilomtia shingoni,
"Ngoja niangalie pale nilipomng'ata siku ile kama mdio yeye nitapata uhakika"Miriam alisema hayo huku akifunu shingo ya Angel kuhakikisha jeraha.
***
Usiku huo magaidi waliojifanya ni wauguzi waliapanga kufanya kilichowaleta kwakuwa waliaminiwa na kuruhusiwa kutemebea popote basi wote waliamua kuweka kambi katika maabara ya hospital hiyo,wakiwa na mabegi yao mkononi ambayo tokea wafike hospitslini hapo hawakutaka kuyaweka chini basi walianza kufanya kitu kilichomshangaza mwenweji wao kwanza walianza kumuua mlinzi wa maabara,tayari mwenyeji akiwa ametekwa akipewa machaguo mawili achague moja aidha ikiwa ni kuonesha mahali kemikali waliyoitaka ilipo au kuuawa kwa kukatwa kiungo kimoja kimoja.Daktari huyo hakuamini kilichokua kikiendeklea na ndipo alipojua watu hao hawakuwa watu wazuri,walianza kufanya upekuzi ndani ya maabara na kila alipoigia daktari wa Japan aliwekwa chini ya ulizi na mateso makali na hakuna aliyeweza kumtaarifu aliye nje.
***
Kitendo cha Genes kuongea kilimfanya Miriam achanganyikiwe hasa baada ya kusikia walitaka kumuua haraka alianza kumuita daktari aliyekua anamhudumua kwa mda mrefu ili amtaarifu juu ya Genes kuongea kisha kunyamaza,
"Itakua yupo maabara" Miriam alisema huku akishika njia kuelekea maabara lakini kwa mbali akaona damu ikitiririka kutoaka maabara,
"Itakua kuna majaribio wanafanya na hawa madaktari wageni"alijisemea huku akiongeza mwendo lengo lake likiwa kumtaarifu daktari aliyewekwa maalumu kuwaangalia wagonjwa wake,Damu ilizidi kutiririka kutoa maabara nae Miriam alipokaribia mlangoni alisikia sauti kali ilimuita kwa nyuma,
"You lady just come; jus come" (wewe dada hebu njoo; hebu njoo) Miriam aligeuka nyuma na macho yake yakaeleka katika chumba alichotoka na haraka aliamini itakua kuna kitu kimetokea,
"Itakua kafariki ama kaongea tena"Miram alijisemea moyoni na kugeka kuenda kukaangalia alichoitiwa na aliyemwita alikua bado amesimama mlangoni.
"pa; pa; pa; pa;pa;pa;pa;pa; ilikua ni milio ya risasi ikimlenga Miriam sehemu mbali mbali za mwili kumbe wakati Miriam alipoitwa na kurudi wale waliojifanya madaktari walihisi wameoneka kwani hadi wakati huo walikua washakata baadhi ya madaktari vichwa kwa kudai wapewe kemikeli waliyoifuata.
kitendo cha kumfyatulia Miriam risasi kiliashiria hali ya hatari hoispitalini hapo kila mtu alianza kukimbia ovyo ili kujiokoa wagonjwa waliokua na uwezo wa kutembea basi waliamka vitandani na kukimbia ovyo huku wengine wakiuawa kutokana na majibizano ya mashambulizi kati ya magaidi hao na walinzi wa hospitali hiyo.
Miriam alikua chini hapakua na wakumsaidia kwani kila mmoja alijaribu kujiokoa hivyo Miriam alizidi kukanyagwa na watu kila mahali katika mwili wake,alivuja damu nyingi,vikosi vya ulinzi vya Japan vilipata tarifa juu ya magaidi hao na haraka waliagizwa wanajeshi wa umoja wa mataifa UN kupambana nao.
Mapigano makali yaliendelea kati ya kikosi cha madaktari bandia kutoka Korea na kikosi cha kijeshi cha umoja wa mataifa UN wakishirikiana na wanajeshi wa Japan. Ndege za kijeshi kutoka Korea zilitua katika ardhi ya Japan ili kusaidia wanajeshi wao watu wengi hasa wagonjwa waliokua wakiuguzwa katika hospitalini hapo waliaga dunia kwa kupigwa risasi wengine kwa mshtuko hasa waliokuwa na matatizo ya moyo waliaga dunia kwa wingi. Baada ya siku mbili mapigano yaliisha
baada ya jeshi la Korea kufanikiwa kuwakomboa wanajeshi wake hivyo hospitali kuu ya Japan ikabaki na uharibifu mkubwa kwani dawa zote zilisambaratishwa pamoja na wauguzi wengi kupoteza maisha.
Miriam alikutwa katika hali mbaya sana mwili wake ulitapakaa majeraha ya risasi hakika kila aliyemuona hakuweza kuamini kama angeweza kupona.
Ili kupisha ukarabati wa hospital hiyo wagonjwa waliosalia hai waligawanywa katika hospital mbalimbali za nchini Japan na kwa pamoja Genes,Miriam pamoja na Angel wakipelekwa katika hospital iliyopo mji wa Hiroshima ili kupatiwa matibabu.
***
AFTER SIX MONTH (baada ya miezi sita).
Dar es salaam, Tanzania.
baada hali ya Miriam kuzidi kua mbaya katika hospital kuu ya mji wa Hiroshima huko Japan basi marafiki zake Miriam waliamua kumsogeza nyumbani kuokoa gharama za kusafirisha maiti na hapo ndipo alipoletwa katika hospital kuu ya Muhimbili hali ya Genes na Angel ilikua nzuri lakini bado hawakuweza na uwezo wa kutunza kumbukumbu wala hawakukumbuka kitu chochote kilichowahi tokea nyuma hivyo walikaa chini ya uangalizi wa Anitha aliyekua rafiki mkubwa wa Miriam,
"We Anitha nakuamini sana hivyo huyu binti naomba umuangalie na kama atakufa afie mkononi mwako maana kuna watu wengi wenye wivu katika biashara na kama ujuavyo Miriam ni mfanyabiashara mkubwa hivyo chunga asije kuuawa naomba ukae nae"
hayo yalikua maneno ya mzee Massawe tena kwa msisistizo kwani aliuamini sana urafiki baina ya Anitha na Miriam na ndipo alipoamua kumpa kazi ya kumuangalia.
***
Hapo Anitha mda wote alikua akikaa pembeni ya kitanda cha Miriam akingoja angalau azinduke kwani kila kitu alifanya kwa usaidizi wa mashine.
"Hali yake inazidi kuwa mbaya hivyo nawashuri msogezeni nyumbani" yaliku maneno ya mganga mkuu wa hospital ya taifa Muhimbili,yalikua maneno yakukatisha tamaa kana kwamba Miriam asingeweza kupona tena na kweli vidonda vyake vilizidi kuoza pamoja na kupewa dawa za kila aina kutoka kwa madaktari bingwa kote Afrika Mashariki.
Miriam alisafirishwa hadi nyumbani kwake Arusha huku mtu wake wa karibu akiwa Anitha kwa kusaidiwa na muuguzi mmoja aliyepewa kazi ya kuhakikisha mashine zake za kupumulia zinakua sawa mda wote,Genes na Angel mara nyingi walicheza michezo ya kitoto kana kwamba ndio wanazaliwa.
Afya ya mzee Massawe ilianza kudorora,uzee ulimzidi naye akawa ni mtu wa kukaa chini na kufanyiwa kila kitu lakini pamoja na hayo hakuacha kumtembelea Miriam na kuzidi kumsisistiza Anitha kutobanduka pembeni yake,
"Mwanangu ukiwa tajiri unakua na maadui wengi hivyo huwezi jua maadui wa Miriam watatumia njia gani kumuangamiza hivyo nakusisitiza hata usikie nimekufa leo usije msibani badli mlinde Miriam nampenda sana huyu binti"alisema mzee Massawe huku akipakizwa kwenye gari lake na kurudishwa nyumbani.
***http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Eledy,Eledius pamoja na Nyani walizidi kupiga mazoezi hasa ya kujilinda, Nyani aliwafundisha watoto hao kukwepa mishale,kulenga shabaha pamoja na dawa zote za miti shamba,hivyo watoto hao walizidi kuwa wataalamu siku baada ya siku hadi wakati huo walishazoe maisha ya porini na washamzoea nyani huyo hata kwa kidogo walivyokua wakijua kuongea na binadamu walisahau na kujikuta wanajua kuongea na nyani na kuelewana.Nyani hakutaka kuona watoto hao wakichafuka,alihakikisha anawajali kama binadamu hivyo kila mchana wenye jua aliwaogoesha katika chemchemi huko porini kisha kuwasogeza karibu na mahali panapochomwa mkaa ili wapate joto.
Muuguzi aliyeajiriwa kwa ajili ya Miriam na kukaa nae nyumbani alipata mchumba lakini kutokana na kubanwa mda wote basi waliishia kuwasiliana tu kwenye simu bila kuonana,
"usijali mpenzi siku nikipata upenyo nitajiiiiba haraka nije kwako"yalikua Maneno ya muuguzi huyo kwa mpenzi wake kila siku.
***
Baada ya miezi miwili tangu akina Miriam kuletwa Arusha Genes alipatwa na tatizo la kupoteza fahamu na kuanguka chini na kuzimia hata kwa siku mbili mfululizo, lilikua tatizo lililokua linatokea hata mara kumu kwa mwezi mmoja,madaktari walimpima na kudai hiyoi ni hali itakayofika mwisho hivyo wasiwe na wasiwasi.
***
"Genes; Genes; Genes; gari hilo Genes tunakufa"ilikua sauti ya Angel iliyomshtua Anitha pamoja na muuguzi pale ndani,Angel alionekana kama mtu aliyezinduka usingizini huku akitaka kukimbia kwani aliona kila kitu ni kigeni kwake,
"Dada hapa ni wapi?" Angel alimuuliza Anitha,
"Hapa ni Arusha,huyu hapa anaitwa Genes na huyu anaitwa Miriam, hawa ni mtu na mke wake na wewe ulipata ajali ukiwa na huyu Genes mkapelekwa Japan kwa ajili ya matibabu lakini mkiwa kule vita vikatokea ndipo huyu Miriam akapigwa risasi nyingi na amepewa matibabu karibu hospital zote hata Tanzania ila zimeshindikana kumtibu hivyo hapa kila kitu anafaya kwa msaada wa nashine,wewe pia kwa zaidi ya mwaka mmoja umekua huna kumbukumbu yoyote sahivi ndipo zinakurudi"Anitha alimweleza Angel kwa kifupi juu ya mambo yaliyotokea.
Angel aliinamisha kichwa chini na kukumbuka kila kitu kilichotokea katika maisha yake na kukumbuka mpango waliokua wameupanga na Genes kuhusu kumuua Miriam.
Anitha alifurahi kwa Angel kurudia kumbukumbu zake kwani waliangalizi waliongezeka na kupeana zamu ya kuwahudumia Miriam na Genes, biashara za Miriam ziliendelea vizuri mtaji uliendelea kupanuka,Anitha alianza kumfundisha pamoja na kuitambulisha miradi ya Miriam kwa Angel ili iwe rahisi kusaidiana, alimwonesha nyaraka zote,
"Jamani watoto wangu wangekuepo ndio wangerithi hizi mali zote"Angel alijisemea moyoni huku akitokwa na machozi kwani alikua akiumia baada ya kuambiwa watoto wake walipotea na kwakua walitafutwa kwa mda wa miezi sita bila mafanikio basi ilichukuliwa kua wamekufa.
"Ila haina shida hata hapa nitawamaliza maana nishakabidhiwa nyaraka zote na hatimiliki nishazijua basi nitawaondoa duniani wote nibaki na hii mali alafu nitafute kijana mdogo nimuoe ili nipate raha kwa sababu Genes mwenyewe ndio huyu hajitambui sasa haki yangu kama mwanamke nitaipata wapi?" Angel alijisemea moyoni hakukumbuka wema hata mmoja Miriam alioufanya kwake hadi kumpeleka Japan kwa ajili ya matibabu hayo yote yalimtoka na kuwaza kuwauwa pamoja na Genes.
***
Hali ya mzee Massawe ilizidi kuwa mbaya hadi yeye alikata tamaa ya kuishi akaamua kuja kuwajulia akina Miriam hali akiamini itakua ni mara ya mwisho kwani kwa afya yake basi atakufa siku za karibu.
"ANITHA NAOMBA UKAE MAKINI SANA NA HAWA WAGONJWA NI SAWA MMOJA AMEPATA FAHAMU VIZURI NA MNASAIDIANA VIZURI ILA NAKUOMBA USIMAME WEWE UKAE PEMBENI YA MIRIIAM HADI DAKIKA YA MWISHO USIMUAMINI MTU YEYOTE HUYO SIJUI ANGEL UNAESEMA HANA SHIDA MIMI SIMJUI NAKUTAMBUA WEWE NA HII KAZI NIMEKUPA WEWE HAKIKISHA SIKU MIRIAM ATAKAYOZINDUKA ANAIKUTA MALI YAKE KAMA ALIVYOIACHA TENA AENDELEE KUENDESHA HOTEL YANGU MIMI SIJUI KAMA SIKU YA LEO ITAISHA" yalikua meneno machache yaliyotamkwa na Mzee Massawe kwa Anitha kisha kugeuza macho na kuaga dunia hapo hapo nyumbani kwa Miriam.
***
Ilikua taarifa iliyofanya jiji la Arusha kusimama kwa mda,vituo vya habari vilitawaliwa na habari ya kufariki kwa tajiri huyo wa jiji la Arusha ,
"Ama kweli wema hawadumu"yalikua maneno ya watu mtaani kwa kumuenzi tajiri huyo aliyekua na moyo wa kipekee kwenye utoaji wa misaada bila majivuno.
Mwili wake ulihifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Mount Meru huku taratibu za mazishi zikiendelea kupangwa katika hotel ya Stanley iliyopo katikati ya jiji la Arusha.
***
" Vipi mtaenda msibani ?" Angel alimuuliza Anitha,
"Yaani huyo marehemu akiniona huko msibani nahisi atafufuka kwa jinsi alivyokua akinisisitiza juu ya kukaa na Miriam hapa yaani aliwahi niambia hata akifa nisiende msibani" Anitha aliongea kwa huzuni,
"Mzee wa masharti yule"Angel alisema,
"Ila Angel sikia sasa tupange kitu hapa mimi nitaenda msibani bhana ubaki na huyu muuguzi hapa nina hamu ya kuandamana na msiba kupeleka Rombo siunajua tena mbege na ndizi nitaleta"yalikua maneno ya Anitha kwa Angel,
"Jamani usijali nitawaangalia' Angel alijibu kwa huzuni huku moyoni akiwa na furaha kwani alijua atatumia upenyo huo kufanya mauaji ya Miriam na Genes,
"Huyu muuguzi sasa nitamtoaje hapa siku hiyo ya msiba ili asiwe kikwazo kwangu ?" Angel alijiuliza swali ambalo lilimsumbua kichwani kwani kizuizinpekee ni yule muuguzi.
Amgel alifanya mawasiliano na kundi fulani la majambazi na kupanga nao mpango wote,
"nataka hii kazi muifanye kimataifa yaani isije kugundulika' Angel alikua akitoa msisitizo kwa vijana ambao wangefanya kazi ya kuwauwa Miriam,Genes pamoja na muuguzi.
siku ya jumamosi ilikua ndio siku ya mazishi ya mzee Massawe msafara wa magari ulijipanga kutika barahara ya Moshi Arusha gari ya kwanza ilifika himo na nyingine bado hazijaondoka Arusha ulikua msiba uliovunja historia kuwahi kutokea kua na wahudhuriaji wengi kiasi hicho, magari jijini Arusha yalipungua sana kwa siku hiyo Anitha akiwa ni mmojawapo ya wahudhuriaji wa msiba huo ingawa kwa shingo upande kwani maneno ya marehemu yalimyima raha na amani moyoni mwake.
***
Muuguzi alimuona Angel akiwa na furaha sana siku hiyo hadi akaona amchokoze,
"Yaani shoga acha tu nina mpenzi wangu nilompata huku Arusha na hatujawahi hata kulala pamoja jamani kwa nini leo usiniachie tu nikaenda kupashwa kidogo siuajua mwanamke akishapandwa na hamu jamani" muuguzi aliomba apewe japo dakika 30 atoke, Angel alipata furaha ya ajabu bila pingamizi alimruhusu na kuamini kazi itakua rahisi zaidi.
"Ngoja nikuitie gari na dereva uende chapu na urudi" Angel alisema huku moja kwa moja akipiga simu kwa vijana wake na kuwaatarifu,
"Mmoja aje na gari haraka huyu muuguzi kuna mahali anahitaji kuenda hivyo hapo hapo nataka apelekwe kisha akitoka muwe mumemteka mmuhifadhi mahali kisha Anitha akitoka msibani pia atekwe kabla hajaingia ndani kisha mje kuchukua hizi maiti ambazo hazitaki kufa huku ndani mkaziteketezee sehemu moja pamoja na hao wauguzi wao wafe pamoja sitaki wafie hapa wataacha mkosi hapa nataka mkishawaondoa hapa nilipue hii nyumba ili ifahamike wamefia ndani kwa ajali ya moto" Angel alimaliza mipango ukawa umebaki utekelezaji...
Baada ya dakika ishirini tangu Angel aongee na vijana wake watakaofanya kazi ya kuua basi gari aina ya Toyota prado new model ilifunga breki mbele ya lango lao tayari kumpeleka muuguzi kukutana na mpenzi wake hakika kwa muuguzi ilikua ni furaha kubwa sana kukutana na mwanamke mwenye moyo mzuri kama Angel,
“Yaani mwanamke ananiruhusu kuenda kwa mpenzi wangu tena namuachia wagonjwa wanaotoa harufu ya muozo”yalikua maneno ya muuguzi huku akijiremba chumbani kwani alihakikisha kuenda kumteka mwanaume huyo mpya,
“Mwanaume mgeni lazima uhakikishe mara ya kwanza hufanyi kosa” huyo muuguzi aliendelea kujisemea moyoni.
“Harakisha jamani au unabeba na nguo kwani unaenda kubaki ?” ilikua sauti ya Angel huku akigonga mlango alimokuwepo muuguzi huyo.
Baada ya dakika ishirirni na tano tayari gari ilifunga breki mbele ya mlango alimokua akiishi huyo mwanaume, muuguzi alishuka na kuingia ndani kisha dereva akaegesha na kubaki ndani ya gari kama alivyoelekezwa na Angel.
“Tayari nishamfikisha kwa huyu mtu wake ndio wako chumbani sahivi”
“Hapo hapo hakikisha hata mifupa haitaonekana kamwe ila msimuue sahivi subirini hadi usiku mje mchukue na hii mizoga huku nyumbani mkaizike pamoja sawa ?”
“Sawa boss” hayo yalikua mazungumzo baina ya Angel na dereva aliyetumwa kumpeleka muuguzi kwa mchumba wake wakijadili ni namna gani watawateketeza Genes,Miriam,Anitha pamoja na huyo muuguzi.
Takribani nusu saa nzima muuguzi alikua bado katika uwanja wa mahaba na mpenziwe,walipeana kila aina ya burudani kwa wapendanao huku wakiahidiana mambo mengi ya maisha ikiwemo ni pamoja na kutoachana siku zote za maisha yao.
***
Hakika msiba wa mzee Massawe ulisimamisha wilaya yote ya Rombo huko mkoani Kilimanjaro ambako ndipo nyumbani kwake,watu walikula na kunywa pombe zote zilikuepo bila idadi watoto walikusanyika hapo wakila kila walichotaka hakika kwa harakaharaka yalikua mazishi ya kifahari.
Anitha alikumbuka maneno yake kwa msisitizo juu ya kutomuacha Miriam mwenyewe hata siku moja,alilia na kuwaza,
“Hivi Miriam anajua ni kwa jinsi gani anapendwa na huyu babu yetu anayezikwa leo naomba babu yetu nenda kamuombee tu Mungu amrehemu Miriam apone ili aendeshe miradi yako” yalikua maombi ya Anitha wakati anaaga mwili kwa mara ya mwisho
****
"Dada vipi umefurahia uliochoenda kufanya eh,?" dereva aliongea huku akimwangalia muuguzi aliyekaa pembeni yake kwa safari ya kurudi nyumbani,
"Nimefurahi sana tu natamani hata kesho nirudi tena" muuguzi huyo alijibu kwa utani kwani tayari walishazoeana na huyo kaka,
"Kwa mfano ungejiskiaje kama mtu angekuambia kua leo ndio mwisho wa maisha yako" kaka huyo aliuliza huku akiingiza mkono katika droo ya gari na kutoka na chupa iliyo mfano wa manukato,
"Wewe nife leo na utamu wangu nitataka nibaki kwanza waendelee kuufaidi faidi" muuguzi alijibu kwa utani bila kuelewa kama dereva alikua akimaanisha ukweli na haraka alipuliziwa dawa ya kumpa usingizi na hapo akajilaza huku safari ikiendelea.
Moja kwa moja alipekekwa hadi Moshono ndani jumba kubwa ambapo ndipo kuliishi kikosi cha watu watano waliotisha kwa ujambazi katika jiji lote la Arusha.
Hapo walianza kumbaka bila huruma,walifanya kwa zamu bila yeye kujitambua.
Mwendo wa saa kumi na moja jioni alizinduka na ndipo alipojikuta mazingira yale na kuwa katika hali ya kushangaa,
"Kweli huyu kaka niliyemuona mstaraabu hivi ndio kanifanyia ukatili huu" wakati huo bado hata hajafumbua macho alihisi sauti za watu watu wako pembeni yake lakini hakuthubutu kusema kitu,
"Zamu yako Fredy" ilikua sauti ya mmojawapo ikimuamrisha huyo Fredy kua ni mda wake wa kumbaka muuguzi huyo,na kwa hapo muuguzi alisikia neno hilo na sekunde kama tano alipata maumivu baada ya kulaliwa kifuani bila huruma na kuanza kufanyiwa ukatili,alijitahidi kukaa kimya kwani alijua kama ataongea basi atauawa,
"Mgeuze sahivi tumechoka huko" ilikua sauti ya mmojawapo ikiamrisha muuguzi ageuzwe kwa aliji ya kufanyiwa mapenzi kinyume na maumbile tena bila ridhaa, na hapo pia sauti hiyo ilipenya masikioni mwa muuguzi ila hakuweza kuvumilia aje kufanyiwa kitendo hicho,
"Ngoja kwanza msimgeuze nataka nimfanye mdomoni" alisema jambazi mwingine na muuguzi aliyaskia pia na kwa haraka jambazi alipanua mdomo.
Muuguzi alihisi kitu kinene kikipenya katika mdomo wake, naye bila kuchelewa alimuuma uume wake na kuukata, jambazi alilia kwa maumivu na kuwapa wenzake kazi ya kumtesa kwa kulipiza kisasi, hapo walianza kumvunja meno ya mbele juu na chini.
Muuguzi alilia kwa uchungu lakini hapakua na msaada wowote kwani sauti iliishia pale pale ndani kisha zoezi la kumbaka liliendelea huku wakisubiri simu kutoka kwa Angel ili wakawachukue waliosalia na kuwateketeza.
***
"Haraka ndio anakaribia kuingia"ilikua sauti ya Angel ikiamrisha mmojawapo wa majambazi kuenda kumteka Anitha.
***
Anitha alifika nyumbani majira ya saa moja na nusu baada ya kuagana na marafiki waliomsindikiza basi walirudi.
Anitha akiwa katika hali ya majonzi alishtukia kukamatwa na watu waliokua ndani ya geti wakitoa amri za kijambazi,hapo alifungwa mikono na miguu kisha kushindiliwa matambara mdomoni ili asiweze kusema lolote, Kisha majambazi hao walingia chumba walimokua Genes na Miriam, hapo Genes akiwa tayari kashapuliziwa dawa ya kumfanya apate usingizi walipakiwa wote kwenye gari wakati huo Anitha aliyaona yote yaliyoendelea lakini hakuwa na la kufanya zaidi ya kusubiri kuona matokeo ila aliamini yote hayo yalipangwa na Angel,http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Huku mwili wa Miriam ukiwa unatokwa na damu kwa jinsi alivyobebwa na kuchomolewa mirija aliyokua akitumia kulia na kupumulia ulilazwa juu ya Anitha huku mwili wa Genes ukilazwa juu ya muuguzi kwani walitoka naye ili wakawauwe na kuwatupa sehemu moja.
***
Pori la Namanga kulikua na eneo ambalo serikali ilitoa ruhusa ya kuchoma mkaa , watu walichimba mashimo na na kuyaacha wazi ili waje na magogo na kufukia yaweze kuungua na kua mkaa.
Nyani akiwa na Eledy pamoja na Eledius walikua wakifanya mazoezi ya kukimbia porini huko, lakini kwa bahati mbaya Eledy akachomwa na mwiba mguuni,
Kitendo cha Eledy kuchomwa na mwiba kilimuudhi sana nyani kwani alishawapa mafunzo ya kukimbia gizani tena wkiwa wamefumba macho, hapo nyani akawapa adhabu ya kulala pale pale ili wajifunze siku nyingine.
Walitafuta sehemu nzuri yenye joto la mkaa unaochomwa na kujilaza.
Usiku wa saa tano Nyani alishtuka kuona mwanga mkali wa gari kwa haraka akajua ni askari wa misitu kwani hata wabeba mkaa huwa hawaruhusiwi kubeba usiku.
Namna ya kuwaamsha watoto ilikua ni kufinywa, Eledius aliamshwa kwa haraka na kumwamsha Eledy aliyekua na jeraha mguuni,Eledy alimwonesha nyani ishara ya kuwa waondoke pale lakini nyani aligoma kwani alijenga tabia ya kuangalia kitu ambacho hakielewi.
Waliendelea kujificha kwa majani ili wasionekane kwa mwanga mkali wa kurunzi walizokua wamebeba watu hao.
"Nyani kwa mbali alishangaa kuona vitu mithili ya watu vikishushwa na kutupwa katika shimo moja lenye urefu wa mita mbili.
Haraka aliamini ni miili ya binadamu,
Eledy alishtuka na kutaka kupiga kelele lakini nyani alimziba mdomo kuashiria akae kimya aangalie nini kinataka kufanyika.
Baada ya kuitupa miili ile kuna vitu walikua wanatupa tupa huko shimoni kisha kiroba cha mkaa uliokua tayari ulishuswa kutoka kwenye hiyo gari,kiroba kilichanwa na kumwagwa shimoni,huku yakifuata majani makavu kisha wakafukia kidogo na wote walipanda gari na kuondoka.
Miili hiyo ni Miriam,Anitha, Genes na muuguzi wa Miriam, walitupwa shimoni hapo wafe kwa kukaangwa taratibu kwa mkaa,ndio maana wakafungwa na kuwekewa matambara mdomoni,yalikua mateso makali kwa Anitha na muuguzi kwani ndio walikua na fahamu kwa mda huo,walikosa hewa ndani ya shimo muuguzi akaanza kupoteza fahamu.
***
Kwa mbali Anitha alisikia vindindo vya mtu akifukua shimo hapo ndipo aliamini mda wowote angeuwawa.
Ndani ya shimo kuliwekwa kemikali ambayo hubadilika na kulipuka baada ya mda,na kabla haijalipuka huanza kwa kuvuka moshi mkali.
Bila kutarajia Anitha alisikia vishindo vidogo akaamini vishindo vya watoto, walizidi kuondoa mkaa na hatimaye walifanikiwa kuwafikia na kukuta kitu chenye sura ya bomu kikivuka moshi, kana kwamba kinataka kuwaka,nyani aliyekua juu alirusha kibuyu chenye maji na Eledius alikipokea na kuzima kitu hicho, Macho ya Anitha hayakuamini kitu kilichokua kikiendelea mahali hapo aliona ni kama miujiza inafanyika.
Lilifuata zoezi la kuwatoa ndani ya shimo, kwa woga mkubwa Anitha alikubalia kufunguliwa mkono na nyani,
"Asante mungu kwa kumtuma mnyama huyu atuokoe" Anitha alijisemea moyoni huku bado akiwa na wasiwasi juu hao watoto walioshirikiana na nyani,
"Sasa hawa watoto mbona sio wanyani lakini wako pamoja huku porini" Anitha alijiuliza huku akitoa ushirikiano wa kumtoa Miriam ndani ya shimo.
***
"Mama kazi yako imekwenda vizuri sana tunakuja kuchukua mpunga wetu" jambazi alifanya mawasiliano na Angel kumpa taarifa ya kumaliza kazi yao,
"Njooni hapa nyumbani usiku huu huu basi ili tulipue na hii nyumba kama tulivyopanga" Angel aliongea kwa furaha kwani aliona ameshakua tajiri mkubwa wa Arusha.
***
Mwendo wa saa saba usiku tayari gari ya majambazi wanne na akiwemo dereva iliegesha mbele ya lango la Miriam,majambazi waliingia ndani na kumkuta Angel akiwa mezani akijipongeza kwa wyne iitwayo Sant Anne, siku hiyo ilikua siku ya furaha sana kwake aliingia chumbani akatoa furushi lenye hela zote,
"Hapa kuna dola elfu tano " Angel aliongea kwa kujigamba na hapo majambazi hawakuona sababu ya kulipwa milioni tano na wakati kuna zaidi ya Million mia nane zilizo kwa mfumo wa dollar,
Kilichofuata jambazi mmoja alitoa kamba na haraka akamfunga Angel mikono,
"Kwa uzuri wako lazima tukubake kwanza" aliongea jambazi huyo huku akimvua Angel gauni,
"Nyie jamani mbona tunageukana tena?" Angel aliongea huku akirusha miguu bila mafanikio kwani asingeweza kujitoa mikononi mwa wanaume wanne,
"Tumepanga nini ? hapa tunakuua na utakapoenda siku zote " make sure you don't make any dill with a terrorist" (popote utakapoenda hakikisha hufanyi mpango wowote na gaidi) kwa kua gaidi ni mtu mwenye roho ya usaliti hivyo atakusaliti mara moja na kukuua hivyo basi kaa makini, na hapo utaenda motoni utaenda kuungua kama hao wenzako wanaoungua huko porini "Jambazi huyo aliongea huku akiendelea kumbaka.
Baada ya wote kumbaka walichukua mafuta ya petrol wakamwaga huko ndani kisha wakatega bomu,ambalo lingelipuka baada ya dakika moja, walichukua pesa zote kwenye kiroba ila kufika mlangoni walinza kulalama kwani mlango ulifungwa kwa namba (password) Angel alikua anasali alioona bomu linawaka alama nyekundu.
Majambazi wakiwa wanakazana kuvunja mlango bomu lililipuka na moto mkubwa uliwaka kila upande wa nyumba hiyo,gari ya kuzima moto ilifika kwa kuchelewa baada ya majirani kupiga simu.
Lilikua tukio la kuhuzunisha sana hakuna mtu aliyeamini kama Miriam kipenzi cha watu ameaga dunia kwani uhakika ulipatikana kesho yake baada ya kukuta mavuvu ya watu watano na bila mtu yoyote kupinga basi walijua ni jumla yao wanaoishi ndani ya nyumba hiyo yaani Genes, Miriam, Angel,Anitha na yule muuguzi kwani alishazoeleka nyumbani hapo.
Baada ya siku tano mavuvu yale pamoja na majivu yale yalizikwa kwa heshima zote, kila mtu alilia na kumsikitikia hasa Miriam kijana aliyepata mafanikio makubwa hata bila kuyafaidi.
Mali za Miriam zilibaki chini ya uongozi wa kikundi chake na miradi ilizidi kuongezeka siku baada ya siku.
***
Kwa utaalamu nyani aliokua nao wa dawa za miti shamba basi akishirikiana na Eledy na Eledius walikua wakipambana usiku na mchana kumuokoa Miriam, aliyekua na hali mbaya zaidi huku wakiishi katika pango kubwa.
Anitha na muuguzi walijitambua ila walihisi kama bado ni ndoto inayoendelea na watazinduka tu mda wowote,waliongea pamoja ila nyani hakuwapa ruhusa ya kutoka mahali hapo.Anitha hakubisha kwani aliamini ni malaika aliyetumwa pamoja na wale watoto.
Miezi mitatu tayari Miriam alishapona kabisa, ila wakaendea kuishi msituni kwani hakuna aliyetaka kumuacha yule nyani.
Nyani ndiye aliyewatunza kwa kila kitu kuanzia kupata matunda,asali,dawa,na hata ulinzi walijijuta wakiishi maisha ya furaha lakini bado Genes akiwa hana kumbukumbu yoyote.
***
Siku moja nyuki walivamia pango walilokua wakiishi na kulazimika kulala nje ya pango,baridi kali iliwapiga na hapo ndipo Genes aliporudiwa na fahamu alianza kupiga kelele huku akitaka kukimbia, hakuamini kama angeweza kuwa maeneo yale,
"Miriam nisamehe" lilikua neno la kwanza kutoka kwa Genes lakini hadi wakati huo Miriam alishamsamehe kwani yote aliyashayajua kutoka kwa Angel kwani aliwaambia wale majambazi na majambazi wakawa wanayazungumza ndipo Anitha alipoyasikia na kuja kumwambia Miriam alipozinduka.
Maisha yalianza mapya na mapenzi yakaanza upya kwani kila mtu ameshapona,
"Mbona hawa watoto ni kama mapacha kwani ni wanani" Genes aliuliza swali lakini hakuna aliyemjibu kwani wote walimtolea jicho nyani waliyemkuta na watoto hao.
Kwa mbali watoto wale walifanana na Genes kitu kilichowatamanisha kuja mjini na kukaa na binadamu wengine ili waweze kupima damu kama wanaweza kua Eledy na Eledius.
"Yawezekana ni Eledius huyu" Genes alitamka jina na ghafla aliona mtoto akishtuka kama kasikia kitu anachojua.
Hapo ilikua ni furaha kubwa sana wao kukutana tena wakiwa hai, Miriam alifurahi zaidi kujua wale watoto ndio waliokua wakitafutwa bila kupatikana na hatimaye wamekuja kuwaokoa.
Waliamua kukaza roho na kurudi mjini kila mmoja akitokea kuwachukia binadamu waliokua wametawaliwa na roho ya kinyama zaidi ya simba.
Jiji lote la Arusha lilitawaliwa na habari za watu walioungua moto kuonekana tena mjini.
Ilikua ni furaha na kilio kwa wote waliopata taarifa hiyo,
"Huyu nyani ndio Mungu alimtuma kutuokoa" Miriam aliongea mbele ya umati mkubwa wa watu waliokusanyika kusikia ushuhuda uliotolewa, mtaalamu wa kuzungumza na wanyama aliitwa na kuongea na nyani ndipo nyani nae alieleza jinsi alivyowaokoa wakiwa wametupwa katikati ya pori usiku na ndipo aliposema na gari iliyokua imewabeba, baada ya kufutilia wezi walioiba gari walienda kukamatwa Nairobi Kenya kikiwa ni kikundi kikubwa kiliwekwa gerezani.
Nyani alijumuika na kuwa sehemu ya familia ya Miriam na kila kitu kikaendelea.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Miriam alijitibu tatizo lake la kutobeba ujauzito na kupona hatimaye akabeba mimba yake akajifungua mtoto wa kike akiwa na miaka 31, akambatiza Zawadi.
Wakawa jumla ni familia ya watu saba pia watoto wa Genes aliozaa na Angel pamoja na Zawadi mtoto wa Miriam wakaandikishwa mali zote kama wamiliki,
Muuguzi nae akabaki kua sehemu ya familia pamoja na Anitha. Maisha yalizidi kunoga wakaamua kubadili makazi wakaamua kuhamia nchini Ufaransa, na kuishi jijini Paris, Miradi yao iliendelea vizuri nyani alianzisha kilimo cha ndizi huko Paris, kwa kushirikiana na binadamu basi wakajulikana duniani kote.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment