Simulizi : Kilio Changu
Sehemu Ya Nne (4)
Katika siku za furaha basi hiyo siku ya jumamne ndio ilikua siku ya iliyozidi kwa Angel kwani alijipongeza kwa kuua mtu bila kutumia nguvu,
"yaani nimemuua kama panya" Angel alijisema moyoni.
"Yaani huyu rafiki angu namuombea mungu apone jaman" Genes alisema kwa sauti hadi Angel akasikia,
"mimi leo usiku kabla ya kulala nitasali kwa ajili yake" Angel nae alidakia huku akionesha uso wa huzuni, lakini moyoni akiwa na furaha tena akitamka,
"tutakutana peponi".
Genes aliripoti ofisini na kueleza walimu hali ya Jesophat,
"hakuumia sana hivyo atapona siku za karibu" Genes alielezea kwa machungu kwani Jesophat alikua rafiki yake siku nyingi.
"We Chris mambo ni kwinei nimeua yani hadi nanuonea huruma maana atafia mbele ya mama yake" Angel alikua chooni akiongea na Chris kwa njia ya simu,
"si nakujua wewe hukosei" Chris alijibu huku akitoa pongezi kwake
"ndio hivo nimemaliza kilaini na kesi itamuangukia Miriam maana nimemuuzia msala kwa maandishi" Angel alimjibu na kukata simu.
********
"Josephat, Josephat,Josephat,Josephat mwanangu,Joseeeeeeeeeeeee, amkaaaaaaa" ilikua sauti ya mama Josephat iliyoshtua watu wote wodini na kila mmoja kuamka na kutaka kujua kimetoea nini.
Mama Jesophat hakuamini kumwona mwanae haongei na tayari ashageuza macho na mwili ushaanza kukauka,
"daktari, mwanangu kafanyaje?" Mama Josephat alimuuliza daktari aliyekua anagawa dawa,na hapo daktari alisogea karibu na kujionea,
"he mama nini tena mbona maajabu kawa mweusi hivo ghafla?" daktari alishtuka sana huku akikimbia na kuita wauguzi wakuu,
"mama usimguse tena sogea pembeni" daktari alimuamrisha mama Jesophat kusogea pembeni ili madaktari wakubwa waje kufanya uchunguzi,
"jaman mwanangu usife,mwanangu usife kwani bado tunakuhitaji,mwanangu naomba usife jaman amka" mama Jesophat aliendelea kulia huku akirukaruka kwa machungu kwani hakuwahi kuona binadamu aliye hai akiwa katika hali ile.
"mama huyu mtoto wako hajafa usiogope" muuguzi mkuu wa wodi hiyo alimuondoa mama Jesophat woga ingawa ukweli ni kua Josephat alikufa lisaa limoja na nusu lililopita,
"kaa hapa tukamfanyie uchunguzi zaidi" muuguzi huyo alisema huku wakimtuliza mama Josephat kwani walipanga kumpeleka Josephat katika chumba cha kumfanyia uchunguzi,kwani hata wao walishangaa,
"tayari ashaanza kukauka", alisema muuguzi mmoja wakiwa katika chumba cha uchunguzi,
"hebu mfungue kwanza hivo vidonda" alisema mkuu wa uchunguzi na haraka muuguizi mmoja alianza kufungua kitambaa kilichofunika kidonda cha kichwani,
"we kiache endelea na kazi" alisema mkuu wa uchunguzi huku akiinama chini na kuokota kikaratasi kilichodondoka baada ya huyo muuguzi kufungua kitambaa cha kichwani, huyo muuguzi mkuu alikificha mfukoni bila hata kukisoma.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya dakika 20 madaktari wote waliofanyia mwili wa Josephat uchunguzi walikua midomo wazi kwani walishindwa nani kampa Josephat sumu kali kiasi hicho,
"ona utasema kakaushwa na umeme" daktari mmoja alisema.
Walijadiliana wao kwa wao na kuamua baba Josephat aitwe,
"tumuite baba ndie anaweza pokea majibu kiume" daktari mmoja alisema kwa kumaanisha kama ukimpa mwanamke majibu kama hayo basi atakumbuka hadi kilio cha wakati anajifungua hivyo atalia sana.
"amepona?" lilikua swali la mama Josephat kwa daktari,
"hajapona ila anaendelea vizuri" daktari alijibu huku akiwa na uso wa furaha uliomuondoa mama Josephat wasiwasi,
"sasa mama cha kufanya tunamtaka baba hapa,kuna mambo tuongee nae" daktari aliongezea, na hapo mama Josephat alinyanyua simu na kumpigia mumewe,
"anaendeaje huyo mwanangu?" baba Josephat alianza kuuliza mara baada ya kupokea simu,
"anaendelea vizuri kabisa ila unahitajika hapa" mama Josephat nae alijibu,
" washaanza sasa, na mimi sina pesa yani hata kidogo,maana wakishaniita ni mambo ya pesa" baba Josephat aliongea kwa kufoka,
"sio unaitiwa pesa babaa wewe njoo hata kama ni pesa ipo" mama Josephat aliongea kwa kujiamini kwani alikua na pesa ya kutosha alizopewa na Miriam pamoja na Genes,
"sawa nakuja saivi mke wangu" alijibu baba Jesophat na simu ikakatwa.
"yaani hawa wanaume kila wakipigiwa simu wanafikiri ni hela tu" mama Josephat alijisemea huku akikaa kitandani.
********
"ngoja ninunue matunda nikamsagie Josephat juyce" Miriam alisema huku akiingia kwenye kibanda cha kuuza matunda na kumuacha Anitha nje,
"haa! matunda yote hayo" Anitha alimuuliza Miriam kwa mshangao kwani alitoka na matunda mengi sana mchanganyiko,
"nataka niwe namtengenezea juyce kila siku asubuhi"
"sawa ila nawe una huruma sana na moyo wa kijitolea lazima ufanikiwe tu na utaolewa na huyo Genes" Anitha alimwambia Miriam huku wote wakitabasamu.
********
Muuguzi mkuu,aliingia katika chumba chake na kutoa karatasi aliyoiokota akiamini itakua na ujumbe wowote,baada ya kuinyoosha vizuri hakuamini baada ya kusoma maandishi haya,
NI MIMI MIRIAM NIMESABABISHA KIFO CHA HUYU JESOPHAT, NAOMBA MNIUE NA MIMI LA SIVYO NITAUA BABA NA MAMA YAKE TENA, NAOMBA MKINIKUTA TU MNIUE MAANA MKINICHELEWESHA MTAJIKUTA PABAYA.
Maneno hayo yalimtoa daktari jasho,
"ni Miriam yupi sasa maana huyu tokea aje hapa yupo na mama yake na leo katembelewa na wanafunzi wenzake" daktari alijiuliza huku akirudisha karatasi mfukoni na kumfuata mama jesophat,
"samahani mama hivi hawa wanafunzi waliomtembelea huyu mtoto wako walijitambulisha?"
"aise kwa kweli hawajajitambulisha ila kuna mmoja aliyeandamana nao ila yeye aliwahi kuingia na pia akawahi kutoka,huyo anaitwa Miriam,tena huyo sio mwanafunzi ila ni rafiki tu na amenambia jumapili kabla ya mwanangu kupata ajali walionana" mama Josephat alitoa maelezo huku akitoa simu yake na kumuonesha picha waliyopiga pamoja,
"kwa hiyo umesema anaitwa Miriam?" daktari aliuliza huku akikaza jicho kwa kutazama picha vizuri.Mama Josephat hakuelewa sababu ya kuulizwa maswali hayo ila alishangaa kumuona daktari akitikisa kichwa kuashiria kukubali jambo fulani,
"basi ni yeye tu, kwanini awahi kuingia na kutoka bila hao wenzake na kwanza sio mwanafunzi mwenzake, jamani huyu binti kwa nini anaua mtu mgonjwa tena hapa wodini,huyu atakuja kuua hata madaktari" alisema moyoni muuguzi huyo huku akiomba kurushiwa hiyo picha ya Miriam kupitia WhatsApp.
"wewe naona mnapeana namba za simu, we mwanamke ushaanza kuleta biashara za umalaya huku" baba Josephat alifoka kwa kuingia wodini na kumkuta mkewe anampa daktari namba za simu ili waweza kurushiana picha,lengo la daktari likiwa ni kupata picha ya Miriam na kuipeleka kituo cha polisi ili aweze kukamatwa,
"sio umalaya jaman,kua mstarabu basi" mama Jeso alimtuliza mumewe, na mumewe akahakikisha kweli haikua lengo baya kupeana,
"sasa mzee hebu njoo na hapa" daktari alimvuta baba Jose katika chumba alicho mwanae ambae kwa wakati huo ni marehemu, huku mama akizuiwa kufuata,
"huyu mwanao ametutoka na hatuna jinsi kwani sisi wenyewe tumeshindwa kuelewa kauwawa kwa sababu gani," daktari alimueleza kila kitu na jinsi sumu aliyopewa inavyofanya kazi haraka, pia mwisho alimuonesha karatasi iliyokutwa katika kitambaa kilichofungia kidonda,
"kweli huyu ndie kamuua mwanangu?"
"baba Jose aliongea huku akibubujikwa na machozi,hadi akataka kuichana karatasi ile ila daktari akamzuia,
"we mwanaume jikaze,cha kufanya amini kwanza mwanao kafa na kwa sababu tayari saivi siku imeenda basi kesho asubuhi lazima tuwakamate wote waliokuja kumuona Jana yaani wale wanafunzi wenzake pamoja na huyu anayejiita Miriam ili tuwachunguze vizuri maana hata wewe na mke wako mmepokea vitisho, na kama huyu mtu anaua kwa sumu hii basi ni mtu hatari sana.
Mama Jose alishindwa kuvumilia na kujikuta nae anasukuma mlango wa chumba alichoingia mumewe pamoja na daktari ili kujionea kinachoendelea kwani alihisi kuna taarifa mbaya.
Usiku wa jumanne Miriam alitembelewa na dada mmoja,
"Miriam mambo"
"safi dada mzima wewe?
" mimi mzima kabisa,nimeagizwa hapa kwako kuna ujumbe nilete,si unamkumbuka yule mama uliyekua unakaa nae kipindi cha nyuma ?"
"ndio yule mama mbaya sana kwangu siwezi kumsahau,namkumbuka vizuri"
"sasa basi tunavyoongea basi anaumwa sana,amenituma nikutafute akuombe msamaha kwa makosa yote aliyowahi kukufanyia,hivyo basi kesho anaomba ukamtembelee hapo St Thomas"
"jaman poleni anaumwa wapi?"
"yule alikua mwathirika na saivi kazidiwa sana sijui kama atapona,hivyo anakuhitaji kesho,tena asubuhi ikibidi"
"sawa basi asubuhi unipitie hapa,tuelekee kazini kwangu niombe ruhusa ndo tuende"
"sawa usiku mwema jaman ulale unono".
Miriam aliskia uchungu kwa taarifa hiyo kua mama mlezi wake anaumwa sana,hapo aliinamisha kichwa na kukumbuka baadhi ya vitu alivyowahi kumfanyia vya kikatili,
" yaani siku ile alingiza kidole kwenye uchi wangu ina maana alijua sitaumia,? na je siku alitaka kuniuza ili nikafanye ngono alifikiri jamani mimi nimeshindwa kujiuza mwenyewe? ona sasa yeye kajiuza lakini hatua ya mwisho ndo hii kaathirika" Miriam aliwaza hayo kisha machozi yakaanza kumtoka.
"Sasa sijui nianzie wapi maana kuna Jesophat na huyu mama tena, ila nitaanza kwa huyu mama alafu nimalizie kwa Jesophat" Miriam alijipanga ratiba ya kesho yake kisha kuanza kuandaa vinywaji vya matunda.
Mwendo wa saa tatu Miriam alikamilisha kazi yake ya kusaga matunda,alihifadhi sehemu nzuri, akala na kusali kisha akalala.
********
Jumatano asubuhi taarifa za kifo cha Josephat zilianza kuenea mtaani kwao,
"hapo itakua kuna mkono wa mtu maana niliskia kapata nafuu sasa itakuaje tena afe" ni maneno ya watu waliosema mtaani kwani hakuna mtu aliyembiwa kafa kwa sumu,hiyo ilikua siri ili uchunguzi ufanyike, hivyo kila mtu alijua ni ile ajali imemuua.
Nae Miriam aliamka asubuhi na mapema ila yeye hakua na taarifa yoyote na alipanga ratiba yake mchana ataenda kumtembelea Josephat hospital,
"ahaa Miriam kumbe ushajiandaa tayari, ama kweli unazingatia mda" yule dada wakuelekezana nae kwenda St Thomas alifika na kumkuta tayari Miriam anamsubiri nje,walianza safari kwanza kuelekea kazini kwa Miriam kuchukua ruhusa.
Miriam kila alipoomba ruhusa alipewa bila pingamizi kwani alikua mfanyakazi mzuri aliyependwa na kila mtu kwa ukarimu wake wa kujitoa kwa watu,yaani hakufurahi kumuona mtu analia njaa ingali yeye ameshiba,lazima angempa chakula,hapo alipata umaarufu kwa moyo wa utoaji.
********
Kabla taarifa za kifo cha Jesophat kufika shuleni tayari askari polisi walikua shuleni hapo,
"samahani mwalimu tunawaomba wanafunzi wa nne waliotoka hapa jana na kuenda kumsalimia mwenzao anaeunwa hapo Mount Meru" alisema askari mmoja alievalia kiraia,
"nini kwani wamefanyaje na wewe ni nani " mwalimu aliuliza kwa mshangao,
"mimi ni askari kuna uchunguzi tunafanya hivyo nawaomba" askari huyo alijibu huku akimuonesha mwalimu kitambulisho cha kazi,
"ahaa sawa,ngoja niwaite" mwalimu alijibu na kunyanyuka kuelekea darasa alilokuepo Genes maana ndie aliefahamika kama kiongozi wa msafara huo,
"we Genes njoo hapa," mwalimu aliita
"naam mwalimu" Genes aliitika huku akinyanyuka haraka na kumfuata mwalimu,
"hebu njoo na kundi lako mlioenda kumtembelea Jesophat jana"
"sawa ngoja niwaite" Genes alijibu na kuelekea madarasa ya kidato cha nne kumchukua Angel,
"naona zile pesa tulizopunja jana ndo kimesanuka leo" Genes aliwaza kabla hawajajua kua wanitwa na maskari.
"Hebu wewe njoo hapa" askari mmoja alisema huku akimnyooshea Genes kidole,Genes aliinuka na kumfuata huyo askari kwani mda huo walishajua wanaongea na maaskari,
"hebu eleza jinsi mlivyotoka hapa jana hadi wakati mnafika hospital na jinsi mlivyomuona mgonjwa na hadi kurudi hapa shuleni" aliuliza askari huyo alieshika karatasi na kalamu, huku akina Angel wakiwa kama umbali wa mita kumi hivyo hawakusikia kinachoongelawa.
Genes alitoa maelezo jinsi walivyoondoka na jinsi walivyonpitia Miriam na walivyopitia kibandani kununua matunda ila hakusema jinsi walivyomuacha Miriam kasimama mlango wa wodini na kuenda kugawana pesa hapo aliongea uongo,
"tulipofika nje ya wodi,huyo mwezetu alitangulia kuingia na sisi tukabaki nje,na kwabahati mbaya mlinzi akatuzuia kuingia,hivyo tulibaki nje na badae tuliporuhusiwa kuingia nae huyo mwezetu alitoka" Genes alieleza hayo yote na mengine yaliyotokea,
"Ahaa sawa" alisema askari na kumuamuru kukaa sehemu tofauti na wenzake,
"Njoo wewe" askari alitamka huku akimnyooshea Angel kidole ishara ya kumuita,
"hebu nielezee jinsi mlivyotoka hapa kwenda kumtembelea huyu mwanafunzi mwenzenu hadi kurudi" askari huyo alimuuliza huku akikaa tayari kuanza kuandika,
Angel aliwaza kwa sekunde kumi, bila kusema kitu,http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"sasa hapa nitasemaje,niseme ukweli alafu ukute Genes kadanganya,au nidanganye ukute Genes kasema ukweli" Angel aliwaza
"eleza basi dada"askari aliongea kwa kuamrisha ,ila angel aliwaza na kuamua kuutumia uzuri wake kumchanganya yule askari hapo akaanza kutabasamu na kulegeza macho na kusimama upande kidogo, askari yule alianza kuvutiwa jinsi Angel alivyojiweka,Angel aliona sehemu ya suruali iliinuka taratibu na akajua askari ashapitiwa na hajielewi tena,
"unajua sisi tulitoka hapa tukaeda tukafika na kulikua na msichana fulani hata cjui kwa nini aliandamana na sisi,ndie alianza kuingia na kuwahi kutoka tena alitoka akiwa na wasiwasi" Angel alipomaliza kuelezea basi askari moja kwa moja aliamini kua muuaji ni Miriam,hivyo hakua na haja ya kuuliza tena wengine,
"hebu naomba namba yako ya simu" huyo askari alimuomba Angel namba na bila ubishi Angel alitoa namba na kuiandika hapo hapo alipokua anaandika maelezo yao,hivyo hakuna aliyejua kitu chochote.
Pamoja na kufuatwa hadi shuleni Genes hakuelewa sababu yao kuja kuchunguzwa,ila Angel alijua kila kitu ila hakusema chochote.
"Tunashukuru mwalimu" askari aliaga na kuondoka.
"Ni yule Miriam bhana,unajua hawa wahudumu wa bar wana roho mbaya sana wanakuua huku wakikuchekea" alisema askari mmoja wakiwa njiani kuelekea hotel Aquline kumkamata Miriam.
Baada ya dakika kumi tayari gari ya polisi ilikua kwenye maegesho na askari tayari wameshuka kwenye gari,
"jaman tukae makini maana akikudunga na kitu chenye hiyo sumu basi hufiki hata pharmacy ( duka la dawa)" askari hao walipeana tahadhari kwani tayari washamchukulia Miriam kama muuaji hatari.
"Yupo wapi huyu" askari mmoja aliulizia mapokezi huku akionesha picha ya Miriam, na mapokezi walikutana na Anitha,
"katoka kidogo" Anitha alijibu,
"kaenda wapi muuaji mkubwa huyu" askari aliuliza kwa hasira,
"muuaji??" Anitha aliuliza kwa mshangao,
"wewe tuambie kaenda wapi,utajua ni muuaji au la" askari alisisitiza,
"kaenda hapo hospital ya St Thomas kumwangalia mgonjwa,ila mimi namjua huyo sio muuaji" Anitha alijibu ila alizid kushangaa kwani askari waliondoka kwa kasi ya ajabu,
"endesha haraka kabla hajamuua mwingine" alisema askari mmoja kwani waliamini basi Miriam huulia watu wodini,gari ilitembea mwendo mkali kuelekea hospital ya St Thomas,kila askari akijihami kudungwa hiyo sumu.
**naumia Miriam alilia sana baada ya kufika St Thomas na kukuta hali ya mama aliyemlea ilivyo mbaya,alikua anaharisha hadi amefungwa nepi kama mtoto,
"mwanangu ulinisaidia sana kwenye kazi zangu,uliniingizia faida kubwa sana ila nina uchungu kwasababu nilikudhulumu mshahara wako,mbaya zaidi natumia sana kwa kuwa nilitaka kukufanyia biashara ambapo kama ningefanikiwa kukufanyia biashara basi ungekuta umethirika kama mimi, mwanangu naomba unisamehe sana,mimi sina cha kukulipa zaidi ya mungu ndie muweza wa yote atakulipa,kingine mwanangu naomba usiwe na tabia ya uasherati naomba ufanye kazi kwa bidii na kama ni hisia za mwili basi utafute mume maana ukahaba sio mzuri,ona navyoteseka yote ni kwa sababu ya ukahaba,fanya kazi kwa bidii mwanangu usimtegemee mwanaume" baada ya kuongea hayo mama huyo aligeuza macho na kukata roho,Miriam hakuamini kilichotoea mbele yake,
"mama usife,mama usife jaman,mama usife" Miriam alilia kwa uchungu huku akiinama na kujaribu kumuamsha lakini hakuamka,madaktari walikuja na kitambaa kwa ajili ya mtu aliyeaga dunia.
"huyo huyo,chini ya ulinzi haraka nyoosha mikono juu" ilikua sauti ya maskari polisi walioingia hospitalin hapo na kinyooka moja kwa moja hadi kitanda alichokuepo Miriam,
"ameshammaliza tena huyu mama wawatu" askari mmoja alisema baada ya kumuona mama aliyekua kitandani hapo amekufa.Kila mtu wodini pale alishangaa kwani Miriam alifungwa pingu na kubururuzwa kutoka nje ya wodi,
"jamani mbona mnanishika na kunifunga kwani nimefanyaje?" Miriam aliuliza huku akirusharusha miguu kwa kujitetea kwa bahati mbaya alimpiga teke la sehemu za siri mmojawapo wa askari,
"Pumbavu zako unampiga nani teke unajua huku kuna nini" askari aliongea na kumshushia Miriam kofi la usoni,
"twende utajua huko mbele kua umefanyaje" askari mmoja alitamka na kumrusha Miriam ndani ya Land Rover ya police.
Miriam alilia kwa uchungu huku damu ikimtoka mdomoni kwa kofi alilopigwa.Gari lilitembea mwendo kasi kuelekea kituo cha kukuu cha police Arusha kupitia njia ya Kaloleni.
Taarifa za kifo cha Josephat zilizidi kuenea mtaani,
"alipata ajali ila naskia kuna msichana mwingine aliekuja kumlisha sumu"
"ha jaman binadamu hatuna huruma tena tumekua wanyama,wamuue na huyo aliyemlisha sumu basi"
yalikua maneno ya watu kila mtaa wakielezea kifo cha Jesophat, waandishi wa habari wa baadhi ya vituo vya radio basi walifika nyumbani kwa Jesophat ili kupata habari,
"hapa unaongeoa na mwandishi wa Arusha one fm,naskia wewe ndo mama mtoto,kwanza pole sana kwa yaliyokukuta,hebu tueleze kidogo ilikuaje na je mhalifu mmeshamkamata?"
"jaman kaka yangu sijui nikuelezeje,mimi niko na mwanangu namuuguza,wanakuja watu kumjulia hali jaman wanampa sumu bila huruma,na huwezi amini huyo alomlisha sumu ndie alionesha sana masikitiko,hadi alinipa elfu hamsini ya pole,kumbe alitoa rambirambi jaman binadamu sio wema,naskia amekamatwa saiv tena amekatwa akiwa na mgonjwa mwingine huko St Thomas, saivi napigiwa simu kua huyo mgonjwa aliyetembelewa nae ndo akakata roho ndo anafanyiwa uchunguzi kama nae kalishwa sumu hii aliyolishwa mwanangu" mama josephat alitoa maelezo huku akibubujikwa na machozi ya uchungu,
"kwa hiyo mhalifu ameshakamatwa?" mwandishi aliuliza kwa mshangao,
"ndio kakamatwa mida hii,tena wanahisi kuna tukio lingine kafanya huko,maana kaenda tembelea mgonjwa mwingine akafa jaman ni shetani kabisa huyo" mama Josephat alishindwa kuongea zaidi ya hapo,
"haya mama pole sana" mwandishi alimaliza na kuanza safari ya kuelekea St Thomas hospital ili kuchukua matukio zaidi.
*******
"Wewe mtoto una baba na mama hapa mjini?"askari mmoja alimuuliza Miriam wakiwa kwenye gari chini ya ulinzi mkali,huku mwili wa mama mlezi wake ukifanyiwa uchunguzi,
"sina hata naishi mwenyewe, najitafutia maisha" Miriam alijibu bila wasiwasi,
"unajitafutia maisha yapi kwa kufanya mauaji ya watu, au ukiua unalipwa ?"
"mimi sio muuaji hata kidogo na kama mnaniona ni muuaji basi nipelekeni na mimi mkaniue basi," Miriam alijibu kwa hasira kwani aliona kama ana mkosi katika maisha yake,
"yaani wewe siku ya ajali ulitoka na huyu mtu wapi,?"askari alimuuliza Miriam,ila Miriam hakujibu kitu kwani aliona akitoa maelezo yoyote basi Genes atahusika hivyo aliamua kubeba msalaba wote mwenyewe,
"yaani kama nikisema ile jumapili kua tulikutana na akina Genes na Angel basi wataitwa na sio vizur niwahusishe kwenye hili sakata,acha wanifanye watakacho wenyewe" Miriam alijisemea moyoni kwa hasira.
*******
Daktari August ambae bado alikua akiishangaa ile sumu Josephat aliyokuja nayo siku ya jumapili kwa kutaka ifanyiwe uchunguzi,
"kalishwa sumu?" daktari August alishangaa sana kupata hiyo habari,
"hapana mimi niliskia kapata ajali bhana na yupo Mount Meru"
"ndio hivo alipata ajali,ila akiwa hospital kalishwa sumu na mtoto fulani wa kike naskia ashakamatwa tayari,tena wanadai ni sumu kali sana"
"basi kuna kitu" daktari August alisema kisha kufunga maabara kwa haraka na kuanza safari ya kuelekea Mount Meru,huku akibeba sindano ambayo Josephat alifika nayo maabara kwake kabla ya kupata ajali,
"mbona alinambia ameviokota shuleni? basi kifo chake ni mwanafunzi wa huko shuleni kwake kasababisha"alijisemea akiwa njiani.
Katika hospital ambazo daktari August alikubalika kwa umahiri wake kazini ni Mount Meru, kwani kabla ya kuamua kufungua maabara yake basi alihudumia pale Mount Meru kwa mda mrefu,alipendwa na wafanyakazi wenzake hata wagonjwa walivutiwa na huduma kutoka kwake,alikua habagui pia alikua daktari asiependa hongo,
"habari ya kazi daktari"
"nzuri daktari mwenzangu"
"sasa hapa nifanye kwanza kilichonileta,naskia kuna kijana mmoja anaitwa Josephat amezusha hali ya kusikitisha hapa hospitalini kwenu"
"ndio mkuu,hapa bwana wamekuja wenzake kumtembelea kumbe wauaji kabisa wamemlisha sumu,ila naskia mhalifu kashakamatwa huko St Thomas yani katupagawisha kweli maana alitaka kutushushia heshima kazini tuonekanae sisi wauaji",
"Ila sasa daktari mimi nimekuja na jipya maana niliposkia hii taarifa nimepatwa na mshtuko maana siku huyo kijana alipata ajali alikua katoka maabara kwangu,na alinishangaza sana kwani alikuja na sindano na wembe, na Mimi nilivyovifanyia majaribio nikakuta vina sumu kali sana pia akanambia ameviokota shuleni,baada ya yeye kuona jinsi nilivyomchoma panya hiyo sindano na panya kufa pale pale basi huyo kijana alitoka kwa haraka huku akiongea maneno ambayo sikuyaelewa, sasa maana huyu mtoto ni jirani yangu nashindwa kujua ni kitu gani kimesababisha kifo chake" daktari August alitoa maelezo hayo,na kuonesha hiyo sindano na wembe kisha waliingia maabara na kuvifanyia uchunguzi,
"kweli ni sumu hiyo hiyo" daktari wa Mount Meru alisema baada ya kufananisha majibu ya uchunguzi wa mwili wa Josephat,uliokua chumba cha kuhifadhia maiti.
*******
Baada ya dakika kumi na tano uchunguzi ulimalizika juu ya mwili wa mama mlezi wa Miriam,
"huyu Israel kachukua roho yake" daktari alitoa majibu baada ya kuthibitisha mwili wa huyo mama hauna tatizo lingine zaidi ya virusi vilivyomuua.
Waandishi wa habari walizidi kuchukua matukio na kumpiga Miriam picha akiwa katika gari ya polisi, hadi taarifa zikafika kazini kwake,Anitha hakuamini kile kilichokua kikiendelea kwani alianza kumlaumu Miriam kwa kupenda,
"namwambia aachane na haya mambo ya mapenzi ila hata haniskii sasa anataka nini huyu mtoto jamani ona sasa jina lake linavyochafuka kuitwa muuaji,na mimi navomjua Miriam sio mtu wa kuua mtu" Anitha alijisemea moyoni.
Kila kona habari zilienea na hatimae zilifika hadi shule ya sekondari ya Arusha (Arusha sec) kwani katika mfululizo wa habari hadi akina Genes walitajwa kama watu waliomtembelea marehemu mara ya mwisho,na walioandamana na mhalifu,
"haa! kumbe huyu mwanamke ni katili hivi, tena muuaji kabisa,auawe na yeye,ndo maana nasema hawa wanawake wote wanaofanya kazi katika mahotel ni wahuni wote" Genes alijisemea moyoni huku akimuita Angel,
"kumbe ndo maana tukaja kuchunguzwa na askari"
"aise yule mwanamke nyoka" Angel alijibu.
********
Daktari August alijua kuna kitu kimefanyika tu kwani kutokana na utaalamu wake katika kazi na umakini wake achilia mbali uelewa wa kufananisha matukio alijua kuna kitu tofauti na hicho kinachoendelea yaani aliamini huyo aliyekamatwa atakua hahusiki.
"sio huyo mwanamke aliyekamatwa twende tukamuokoe kwanza tuchunguze vizuri" daktari August alimsihi mwenzake wachunguze hicho kitu kwani inaelekea kuna siri kubwa ndani ya hayo mauaji,
"angalia na maelezo aliyoacha maana niyapiga picha" daktari wa muhimbili alionesha maelezo hayo yaliyohifadhiwa katika picha kwani karatasi ishakabidhiwa kwa askari,
"mimi sijaamini haya,maana huyu Jesophat ni jirani yangu na jumapili kabla ya kupata ajali alikuja na vifaa vyenye sumu ofisini kwangu nimsaidie kuvipima,hivyo kuna kitu hapa,naomba tukalifuatilie hili jambo kwa umakini zaidi watu wasije kuuawa zaidi.
*****
Mzee Massawe ambae ndio mmiliki wa Aquline hotel,sehemu ya Miriam ya kazi alipata hizo taarifa kua Miriam kwa wakati huo yupo kituo cha polisi Central,
"sio Miriam huyu wakwangu mfanyakazi nayemuamini mpambanaji kuliko wote,itakua wamekosea naona" Mzee Massawe alijisemea baada ya kusikia taarifa hiyo nae alitoka haraka na kuwasha gari yake kumfuata Miriam kwani alimpenda kama mwanae.
Baada ya mda daktari August nae alisikilizwa na wenzake wa Mount Meru wakaamua kuchunguza upya hali iliyotokea,
"sisi tuchunguze kidaktari na polisi wachunguze kipolisi ila huyu mtoto wakike sidhani kama ana kosa,tena inabidi apewe dhamana kwanza.
Baada ya dakika ishirini gari ya madaktari ilifika kituo cha central, ili kuweza kumchunguza Miriam mwenyewe kwa ambao walikua hawamjui,
"haa! hadi mzee Massawe yupo" daktari mmoja aliongea baada ya kumuona mzee Massawe tajiri aliyemiliki mahoteli makubwa na maduka jijini Arusha nae akiulizia kuhusu Miriam.
Taarifa ilizidi kusambaa kuhusu hilo tukio la kusikitisha na kila mtu alilipokea kwa majonzi,katika familia ya Jesophat wanandugu walikua na hasira juu ya Miriam ambaye aliiaminika kua muuaji,ila kwa upande wa watu wanaomjua vizuri Miriam basi walizidi kupata machungu wakiamini Miriam amesingiziwa kwani wanamjua alivyo na ukarimu kutoka moyoni.
"Hapa hadi tuandamane ndo wamuweke huru,sio mtu wa kuua yule ni mtu wakusaidia wasiokua na kitu" ni maneno waliosema wafanyakazi wa hotel Aquiline huku nao wakiwa na majonzi makubwa.
*******
"Katika kituo cha police cha central basi madaktari walikua katika uchunguzi,wakiongozwa na doctor August,
"we dada ni kweli uliuwa au unasingiziwa?"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"ningeanzaje kumuua huyo rafiki yangu?je kanikosea nini hadi nimuue?"
"na mbona ulisema unataka kuua na wazazi wake katika yale maandishi?"
"maandishi yapi tena mimi sijaua mtu wala sijui kitu yule ni rafiki angu mwenyewe nasikitika kwa kifo chake kwani nimepoteza mtu muhimu sana katika maisha yangu?"
"kwani ni mpenzi wako?"
"sio mpenzi ila ni zaidi ya mpenzi kwani mimi nikishakua rafiki na mtu basi tunakua zaidi ya wapenz kabisa?".
Hayo ni baadhi ya mahojiano ya madaktari waliofanya na Miriam akiwa chini ya ulinzi wa polisi kwani madaktari waliomba wafanye uchunguzi kidaktari.
"sidhani kama ni huyu kaua,hapa kuna kitu" daktari August aliwaza kichwani mwake huku akitikisa kichwa kutoka kushoto kwenda kulia.
Mzee Massawe nae alimwita askari mmoja pembeni na akawa anazungumza nae,
"hivi afande hapa mbona sielewi hili tatizo?"
"hilo mzee ndo hivo lishatokea huyu mtoto wa kike kaua yani bila huruma yani sidhani kama atakua uraiani tena" huyo askari alijibu kwa heshima kwani alijua anaongea na mtu mwenye pesa,
"ila si kuna dhamana?" mzee Massawe aliuliza kwa kumchokoza askari,
"hapatawezekana kua na dhamana kwanza kwa usalama wake.
"sasa hii kesi itakuaje,maana siamini kama huyu mtoto anaweza fanya hichi kitendo nimekaa nae mda mrefu sana hajawahi kunionesha jambo baya,nimekua nikimuamini sana ofisini kwangu" mzee Massawe aliongea mengi na huyo askari ila mwisho huyo askari alimpa moyo kwa kumwambia uchunguzi utafanyika kwa makini na kisha itagundulika.
Jioni ilifika Miriam aliwekwa rumande,
"naomba nimtumie rafiki yangu ujumbe aniangalizie nyumba yangu" Miriam aliongea huku akitokwa na machozi,
"ujumbe gani?" Askari mmoja aliuliza kwa hasira,
"si aniangalizie nyumba yangu na kuku wangu naofuga" Miriam alijibu kwa hasira kwani alikua na machungu sana.
"haya karatasi hiyo hapo andika tumpe huyo boss wenu" aliongea askari mmoja huku akimkabidhi Miriam karatasi na kalamu, ila walishangazwa na Miriam kuomba msaada wa kuandikiwa,
"hujui hata kuandika wewe mwanamke utaolewa na nani" aliuliza kwa madharau askari mmoja mwanamke,
"nitaolewa na Genes" Miriam alijibu kwa tabasamu kwani aliona kama kaulizwa swali zuri sana,
"sema tuandike nini" huyo askari mwanamke aliuliza huku akishika kalamu tayari kuanza kuandika,
"MAMBO ANITHA,MIMI NI MIRIAM NAOMBA UNIANGALIZIE NYUMBA YANGU NA MIFUGO WANGU WOTE UHAKIKISHE WAPO SALAMA,ALAFU NASKIA KESHO NDO MAZISHI YA JESOPATH HIVYO NAOMBA UNIWAKILISHE HUKO,USIACHE KUHUDHURIA MAZISHI NA UTOE PIA RAMBIRAMBI YANGU,ZINGATIA UMAKINI HAPO NYUMBANI KILA KITU NIMEKUKABIDHI WEWE UFUNGUO CHUKUA PALE OFISINI KWANGU" Miriam alitamka hayo na kisha alimaliza kwa kilio kikubwa.
Karatasi alipewa mzee Massawe aipeleke kwa Anitha,
Pia madaktari waliokua pale walishangaa kumuona Miriam hajui kuandika,
"hii karatasi aliandikiwa na nani?" Dr August aliuliza wenzake,
"kweli hapa kuna utata" Dr mwingine alijibu,
"huyu kijana itakua alijiua mwenyewe,au alikua anatembea na hizi sumu,aidha ikamwingia bahati mbaya" Dr August alikua anasisitiza sana kwani kilichompa uhakika wa kumtetea Miriam ni ile jumapili Josephat alivyoenda na sumu iliyomuua ofisini kwake.
"Hii hapa karatasi mwenzako kanipa" mzee Massawe aliongea huku akimkabidhi Anitha karatasi, Anitha aliipokea na kuisoma kisha alizidi kumwaga machozi,wafanyakazi wote walimwaga machozi kuskia mwenzao tena kipenzi cha watu kinalazwa rumande,
"kama hadi boss kashindwa kuhonga atoke basi ni kesi kubwa sana" alisema mfannyakazi mmoja kwani waliamini boss wao ataenda kuhonga pesa na Miriam atolewe.
Mda huo huo Anitha aliondoka na kuenda kwa Miriam kuanza shughuli ya kulisha kuku na badae kuenda kwake kufanya usafi kisha arudi kulala kwa Miriam kwani ndiko kulikua na miradi mingi.
*******
"Jaman poleni sana jirani zangu,ni kazi ya mungu" ni maneno ya Dr August alipofika kwa marehemu Jesophat usiku wa mwisho kabla ya mazishi,
"kazi ya mungu yaani mtu amuue alafu iwe kazi ya mungu?" baadhi ya waombolezaji walijibu kwa hasira.
Dr August alimuita baba wa marehenu na kukaa nae pembeni ambapo alimueleweshe kila kitu kuhusu sumu aliyokua nayo marehemu Josephat kabla ya ajali kumkuta,hadi mama wa marehemu alitwa na kusimuliwa,
"hivyo itakua kajidunga mwenyewe au vipi?" mama marehemu aliuliza kwa machungu,
"kweli hapo sijui ila kwa kweli yule mwanamke kule mahakamani hana hatia yoyote" Dr August aliongea kwa uhakika,wazazi wote wa marehemu walishangaa sana na kuulizana wenyewe kwa mwenyewe kwamba kwa nini yote hayo yatokee,
"sasa yale maandishi yanamaanisha nini,na kwa nn ayaandike?"mama Jesophat aliuliza,
"ndo nashangaa alafu yule mwanamke hajui kuandika hata kidogo" Dr August alijibu.
Wazazi wa marehemu walikua watu wenye huruma nahapo wakajikuta wakimhurumia Miriam zaidi hata ya mwanaye aliyekufa,
"ngoja kesho asubuhi kabla mazishi tutamtoa na ikiwezekana kesi itafutwa,Mungu ndo ataona hili na ndo atatoa hukumu kwa muuaji, sisi binadamu wote tunapita" baba wa marehenu alijikuta akitoa machozi kwa ajili ya Miriam anaeteseka rumande.
Waliendelea kuomboleza, huku vijana wakicheza karata,wazee walicheza bao na wengine wakicheza drafti ilimradi tu mtu asilale,wote walisubiria kesho ifike kwa ajili ya mazishi,na wanafunzi waliokua wanasoma na marehenu Josephat walisubiria kwa hamu siku ya mazishi kila mmoja akiwa na sababu yake,
wengine wakitaka kuandamana na marafiki zao wa jinsia tofauti, pia waliokua hawapendi masomo basi walifurahia sana siku kama hizo.
Kwa Miriam ilikua ni kilio kisichoisha,
"itakua Genes au yule mwanamke wake ananisingizia mimi nifungwe ile nisije kuolewa nae" Miriam alijisemea ila bado aliamini mapenzi yake kwa Genes hayatapungua kamwe,
"natamani hata nihudhirie mazishi" Miriam alijisemea kisha alizidi kuangua kilio huku akiomba na kumwamini Mungu kua ndie muweza wa yote.
Ilikua asubuhi yenye hali ya hewa iliyotulia vizuri, nyumbaji kwa marehemu Josephat siku hiyo kulitawaliwa na vilio na machungu yasiyopungua,vijana wenye nguvu walianza zoezi la kuchimba kaburi kwani ilikua siku ya kumzika Josephat,wazazi wake walilia kwa uchungu mama yake alipoteza fahamu mara kadhaa huku bado akiwa haamini kama mwanae kipenzi ndio kashakufa na atakiwa afukiwe ardhini mda mfupi ujao,
"jamani mwanangu siuamke kwenye huo usingizi unaolala tangia jamani" mama marehemu aliongea kumuomba mwanae aamke kitu ambacho hakingewezekana kutokea milele. Wanafunzi waliokua wakisoma na marehemu walikua wakijiandaa kwa kuchangisha rambirambi, "jamani ndio hivo kashakufa,usilie sana mwaya Happy"ni maneno Angel aliyotamka kumpa moyo rafiki yake aitwae Happy,ambae alikua girlfriend (rafiki wa kike) wa marehemu, lakini Happy alizidi kulia kwa uchungu huku akiamini hakuna siku atakayomsahau rafiki yake kipenzi, "juzi tu jamani tumeonana alafu leo unakufa mungu wangu nionee huruma nisaidie kumuamsha hata aniage basi nimpige busu la mwisho" Happy alizidi kulia kwa machungu, nguvu ya mapenzi kwa upande wa Happy ilikua kubwa hadi akajikuta akiishiwa nguvu na kugaragara chini, "huyo analia nini au marehemu kafa na deni lake" Chris alitamka kwa madharau, "hata sielewi ila nimchumba wake bhana" Angel alijibu, "hata kama ni mchumba basi avunge maana atafanya wengine walie bure,kama vipi hata mimi mbona handsome tu" Chris aliongea kama utani lakini aliwakera sana wanafunzi wenzake kwa kauli zake chafu alizokua anatamka. *** "Huyu mtoto uchunguzi wake umefikia wapi?" baba wa marehemu alimuuliza askari mmoja aliyefika nyumbani kwake, "hii kesi kweli ni ngumu maana hata ushahidi mwenyewe tunashindwa kuupata maana binafsi tunaona kama yale mauaji hayamhusishi huyu tunayesema mhalifu" askari alijibu akiwa katazama chini, "basi hii kesi mimi namwachia mungu ndio muweza wa yote,ila nyie chunguzeni mjue hili tatizo linatoka wapi, mimi naamini mungu ndiye msemaji wa mwisho" baba wa marehemu alitamka kisha kuinama chini na kumwaga chozi kwa uchungu. *** Ilifika saa nne kamili ya asubuhi Anitha aliomba ruhusa ya kuenda kuangalia nyumba ya rafiki yake kwani alikabidhiwa kuangalia kila kitu, "dada samahani" ilikua sauti ya kijana mmoja aliyekua amesimama kama mita mia hivi kutoka kilipo chumba cha Miriam, "Bila samahani kaka" Anitha alijibu huku akihisi labda kijana yule alikua anaulizia njia au kuna kitu anataka kuulizia,hivyo alisimama na kuanza kumsikiliza, "kwanza pole na kazi dada" kijana yule alivaa suruli ya kitambaa na shati alilochomekea vizuri kitu kilichomfanya Anitha aone mwanaume wa heshima ambae hatamwambia mambo ya kihuni, "asante kaka nawe pia pole na kazi" Anitha alijibu huku akipokea salamu ya mkono aliyopewa, "nimeagizwa kwako dada" yule kijana aliongea huku akitoa karatasi mfukoni na kumkabidhi,Anitha alianza kuisoma,haikua na maandishi mengi sana, "MIMI MIRIAM,NIMEMTUMA HUYU KAKA AJE KUCHUKUA KILA KITU CHANGU HAPO NDANI,NIMEHAMA SITAKAA TENA HAPO KUNA MKOSI HIVYO MPE KILA KITU NA HAKIKISHA HAKIHARIBIKI KITU HAPO,BAADAE NITAKUJA KUKUJULISHA NILIKOHAMIA AU KAMA UNA MDA BASI ANDAMANA NAO HADI WANAKOPELEKA HIVYO VITU ILI UPAJUE."baada ya Anitha kusoma aliinua macho na kumtizama yule kijana kwa huzuni, "yaani huyu mtoto amenisumbua acha tu nimemwambia asubirie baadae aje ila kalazimisha kua nije nitakukuta,sasa cha kufanya inabidi kwanza nikaone mizigo yenyewe ili nikalete gari
inayotoshea" kijana yule alinza kuongea tu mara baada ya Anitha kumwangalia. Ndani ya dakika tano Anitha na huyo kijana ambae hata jina hakujitambulisha basi walikua ndani ya chumba cha Miriam, na baadae waliingia katika banda la kuku, "ngoja nikalete gari", alisema kijana huyo na kuondoka.
"uyu mtu itakua kaenda wapi?” Anitha alizidi kuchanganyikiwa baada ya kusubiri kwa mda, lakini ghafla alijiwa na wazo la huenda katapeliwa kwani alianza kujiuliza kuhusu ujumbe toka kwa Miriam,kwani alikumbuka Miriam hajui kuandika wala kusoma, “itakua nimefanyiwa kama yule dada wa siku ile pale kituo cha mabasi” Miriam alijisemea huku akirudisha kumbukumbu nyuma kwa kukumbuka jinsi siku ,moja dada mmoja aliibiwa kwa kutoa kila kitu kisha kuja kukumbuka badae hivyo nae kumbukumbu zilianza kurudi taratibu alianza kulia kwa uchungu kwani kumbukumbu zilishamjia na ashaamini kua kaibiwa, “kulilkoni binti mbona unalia?” aliuliza baba mwenye nyumba ya Miriam, “kuna watu wameniibia baba” Anitha alijibu huku ameinamisha kichwa chini, “wamekuibia nini na mbona umetoa godoro nje,kwani huyu ndugu yako anaendeleaje huko?” huyo baba aliuliza akiwa anashangaa godoro lililokua nje wakati siokawaida, “ndio hivo baba kuna kaka kaja kasema ametumwa na Miriam kua niwape vitu eti anahama sasa ameniambia nimsubiri aje kuchukua hili godoro lakini cha ajabu masaa mawili yameshaisha nabado hajaja na kwanza walipoondoka nimegundua hawajatumwa na Miriam,maana Miriam namjua anajua sana kuzingatia suala la umakini hivyo kuna kitu hapa”Anitha alijibu huku akirudisha godoro ndani tayari kupanga safari yakuelekea kituo cha polisi kuripoti pia kumtaarifu Miriam, “hutampa presha kweli ukienda kumtaarifu huko aliko maana ni kwenye matatizo mengine ?”huyo baba alimuuliza, “sasa baba nisipoenda sahivi sijui atanielewaje maana alinikabidhi kila kitu chake hapa sasa sijui kama atanielewa jamani” Anitha alijibu kisha kutimua mbio ili aweze kupitia kazini kwake na kumpa tajiri yake taarifa. *** “Mumpe ulinzi wa kutosha”ilikua sauti ya askari akithibitisha Miriam akitoka kuenda kuhudhuria msiba waJosephat “sawa mkuu” alijibu mwenzake. Miriam alipakizwa kwenye gari ya polisi chini ya ulinzi wa askari wawili, “tena una bahati wewe mtoto kwani washtaki wako wamekuombea tu ukazike nahii kesi yako inaweza kuisha maana umeua mtoto wa wazazi wenye utu sana,sijui
wewe mchawi gani maana unaonewa huruma kabisa na wazazi wa marehemu”yalikua maneno ya askari mmoja akiyaelekeza kwa Miriam wakati wakiwa njiani. Miriam alilia sana kuitwa muuaji ingali anajua kabisa hajaua na hana roho ya kuua “mimi sijaua” Miriam alijibu kwa hasira ingawa moyoni alifarijika sana kusikia anaonewa huruma na wazazi wa Josephat kwani alifikiri labda itakua imejulikana kua yeye sio muuaji *** “Parapanda inalia parapanda,parapanda inalia parapanda,ndugu yetu amekwisha nyakula kumlaki bwana yesu mawinguni” zilisikika sauti za wakina mamawakiimba kwa uchungu katika msafara uliotokea Mount Meru hospital ambapo ndiko mwili wa Josephat ulihifadhiwa. Wanafuzi wa shule ya sekondari Arusha waliandamana na mwili wa marehemu kutoka chumba cha kuhifadhia maiti,wanafunzi wa kike walionekana kulia zaidi njiani huku wakiume wakitembea kwa ukakamavu huku wakiacha vifua wazi kuashiria hasira ya kuondokewa na mwenzao. “Am crying because he is my husband”(nalia kwa sababu huyu ni mume wangu) Happy aliongea kwa uchungu huku akizidi kulia njai nzima kwani aliyekufa alikua rafiki wake wa kiume,alikua akikumbuka mipango yao ya kuoana badae na jinsi walivyozoea kuongea pamoja, “siamimi kama ndio tunaenda kukuhifadhi katika nyumba yako ya milele,wakati tulipanga kuja kujenga nyumba yetu sote” hakika ilikua siku ya huzuni kubwa kwa Happy,alibebwa na wenzake hadi msibani. “Hadi huku msibani kumekuja maaskari?”Angel alijiuliza baada ya kuona gari lenye nendo ya PT (POLICE TANZANIA) likiwa limepaki nje.Msiba ulikua na watu wengi lakini sare za shule ziliwatambulisha vyema wanafuzi waliosoma na marehemu.Katika taratibu za mazishi baada ya mwili kufika nyumbani uliingizwa ndani kwa ajili ya kuagwa kwa mara ya kwnza ndipo ifanyike ibada fupi ya kikristo kasha mwili ukazikwe, “ndugu waombolezaji basi tayari mwili ushaingizwa ndani na tutaanza kwa utaratibu wa kuingia ndani kuuga mwili kwa mara ya kwanza kabla ya ibada,hivyo basi tupange mstari mmoja kwa haraka kuokoa mda, tuanze na wanafunzi waliosoma nae enzi za uhai wake tukatoe heshima za mwisho” yalikua maneno ya MC John Shirima akitoa utaratibu wa kutoa heshima za mwisho. *** “Jamani kuna wezi wameiba vitu vya Miriam vyote” yalikua maneno ya Anitha mara baada ya kufika kazini kwake huku akionekana kuhema sana, “mbona hatukuelewi au umechanganyikiwa “aliuliza mmoja wa wafanyakazi “sio kuchanganyikiwa,boss yuko wapi nimpe hii taarifa aipeleke kituo cha polisi ili ampe na Miriam taarifa?”Anitha alizidi kuongea kama mtu aliyechanganyikiwa hadi wenzake wakawa wanamcheka “boss kaenda kwenye huo msiba wanaodai Miriam ndiye kauwa,maana piahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/
am kaitwa kwenye msiba pia na siunajua Miriam na boss wanaenda sana hivyo boss kasema anaenda hakikisha usalama wa Miriam” alijibu msichana mmoja. Anitha alizidi kuchanganyikiwa kwani hakujua afanye nini kwa mda huo “nakuishi kwangu mjini mda mrefu hivi leo natapeliwa, tena mali za mtu”Anitha alijisemea moyoni huku akiona kilichotokea kama ndoto ambapo atazinduka mda wowote na kukuta vitu vya Miriam vikiwepo tena, “hata ningejua nikakariri namba za lile gari afadhali,sijui kama Miriam atanielewa mimi”ni maneno ya Anitha ambayo yalimaanisha ningejua inavyokuja baada ya tendo. *** Watu walizidi kulia kwa uchungu kwa kifo cha Josephat,nae Miriam alizidi kuomboleza akiwa ndani ya gari kwani watuwakiwa wanatoa heshima za mwisho kwa mara ya kwanza bado Miriam alikua ndani ya gari ya polisi yeye aliona kila kitu kupitia kioo cha gari ambacho hakikuruhusu mtu aliyeko nje kuona ndani. “Sasa simnitoe namimi nikatoe heshima za mwisho jamani?” Miriam aliomba kushushwa kwenye gari, “wewe subiri utashuka tu”alijibiwa na mmojawapo ya askari, “jamani naomba” Miriam alizidi kuomba msaada wa kuruhusiwa kuenda kutoa heshima za mwisho lakini alinyimwa ruhusa kutokana na sababu za kiusalama ,wao walisubiri hadi mda wakuuaga mwili kwa mara mwisho ndipo atapewa ruhusa. “aise umecheki alivyokauka?”Brown alimuuliza Chris walipotoka kungalia mwili maana walifuatana, “kawa kama kama mamba”Chris alijibu huku wakijisifu kwa kazi waliyompa Angel kua aliifanya kwa ustadi wa hali ya juu na akafanikiwa kwa asilimia mia. Baada ya dakika arobaini na tano zoezi la kutoa heshima za mwanzo lilikamilika na mwili ulitolewa nje tayari kuanza ibada. *** “Mamasamahani ni kwenye huu msiba wa kijana aliyeuawa kwa sumu mnaenda?”Anitha aliuliza kinamama aliowakuta njiani wakiwa wamejifunga doti za kanga, “ndio mwanangu ni huko tunaenda kama na wewe unaenda basi tunaweza kuandamana” huyo mama alijibu na wakaanza kutembea kwa kasi. Sehemu ya (iii) Hakika siku ilikua mbaya kwa Miriam kwani alijiona mkosefu mbele za mungu na jamii yote hasa pale alipotolewa kwenye gari ili aangalia na kuaga mwili wa Josephat ambae kila mtu aliamini kua ndiye aliyetekeleza mauaji hayo. "Kwani nimekufanyaje mungu wangu mbona mwanao nataseka au wazazi wangu walinilaani kwa kutoroka kifo ambacho kingetokana na mimi kukeketwa ?" Miriam alisema kwa sauti akirudishwa ndani ya gari la polisi kwani tayari alikua kashaaga mwili wa marehemu na alishuhudia jeneza likibebwa na vijana ili kuenda kaburini tayari kufukiwa. Wakati huo Chris na Brown walikua wakipongezana kwa kilichokua kikiendelea, "Hata Angel hafai aise" Chris alimnong'oneza Brown, "aise hata mimi nimemwaminia kabisa amemuua kama mtu anayeua kuku" Brown alijibu.
Baada ya mda waliamua kuondoka na kuenda kujipongeza kwa kunywa pombe, "twende zetu tukapige mvinyo bwana, hicho chakula cha marehemu sisi hatuli" Chris aliongea huku wakiondoka eneo la msiba na kuacha waombolezaji wakipata chakula. Walienda kwenye duka moja wakaagiza pombe za karatasi (viroba) wakanywa kwa hasira, "hawa wanafunzi wanakunywa pombe hivi watafaulu kweli?" muuzaji alijiuliza kimya kimya kwani walikua wakinywa kupita kiasi. Baada ya masaa mawili walikua wamelewa sana, "twende zetu mwana" Chris alimtaka Brown waondoke kuelekea nyumbani, "dah mwana naona nishazimika kabisa hebu nishike mkono" Brown alijibu huku akinyoosha mkono wake aweze kusaidiwa, "watafika kweli hawa?" muuza duka alisema baada ya kuona jinsi Brown na Chris walivyoondoka kwa kukokotana huku wakipepesuka huku na huko, "wanajifariji mwanafunzi mwenzao kafariki" mama mmoja alisema baada ya kuona wamevaa sare za Arusha sekondari.
***
Anitha alizidi kuchanganyikiwa kwani hakuamini kama ametapeliwa kila kitu cha Miriam tena ambaye yupo chini ya ulinzi wa polisi, "sasa haya mawazo aliyonayo juu ya hii kesi anayopewa je nikimuongezea haya ya kupoteza kila kitu siatachanganyakiwa kabisa" Anitha alijisema baada ya kuona msiba ukiisha na Miriam kupakiwa kwenye gari. Anitha alimfuata mwajiri wake na kumueleza kila kitu kilivyotokea, "huyu mtoto ni mchapakazi sana lakini mbona wanamtesa hivi"Mzee Massawe aliongea huku akilengwa machozi, "acha tu boss mimi sijui nitamlipa nini maana yeye ndie amenisaidia hadi hapa nilipo" Anitha alimuelezea mzee Massawe kila kitu na jinsi Miriam anavyopambana na maisha. Hadi kufika kazini tayari mzee Massawe ashazidi kumuamini Miriam na kumuona ni mmoja kati ya wanawake wapambanaji sana wanaopenda mabadiliko, "usijali nitamsaidia kila kitu kitakua sawa" mzee Massawe alimuondoa Anitha wasiwasi na Anitha alishukuru mungu kimoyomoyo kwani aliamini boss wake atamuanzishia Miriam maisha mengine. Waliokua wanafanya kazi na Miriam akiwemo Anitha,walikua na majonzi makubwa hadi kukafanania kana kwamba ni mfanyakazi mwenzao kafariki, "boss nenda kituoni jamani kamtoe Miriam tunampenda akiwa kazini" wafanyakazi walilalamika kwa majonzi, "nenda hata utumie mishahara yetu kumtoa" alisema mmoja wa wafanyakazi ambae alilia machozi kabisa, "msiogope atatoka kesho kutwa maana imechunguzwa na imegundulika yeye sio aliyesababisha mauaji ya huyo kijana" mzee Massawe aliwaondoa wasiwasi juu ya Miriam kufungwa gerezani.Wote walifurahi kusikia hivyo walilia machozi ya furaha na mzee Massawe akazidi kujionea ni jinsi gani Miriam alipendwa na kila mtu.
***
Usiku wa mazishi ya Josephat ulikua wa majonzi kwa wanafunzi na waalimu wote wa shule ya sekondari Arusha. Aliyekua rafiki yake wa kike alilia sana lakini alijipa moyo kua ipo siku atakutana nae mbinguni na wataendeleza mapenzi yao ili waweze kufikia malengo ya kuishi pamoja waliyopanga. Wanafamilia na majirani wa marehemu Josephat walikusanyika nyumbani usiku moto
uliwashwa nje watu wakakesha kuomboleza, "yule mtoto hajaua naona kuna kitu kilifanyika hapa" mwanafamilia mmoja alisema kwa kuelezea hisia zake juu ya Miriam alivyoonekana mwenye majonzi makubwa, "mimi nimeamua kumsamehe namuachia mungu ndio muweza wa yote na ndio anajua sababu ya haya" baba marehemu alijibu. Majira ya saa mbili usiku watu waombolezaji wakiendelea na maomboleza,kijana mmoja alifika ghafla na kutoa habari iliyoshtua watu wote na kuwafanya waanze kilio upya.
***
"Ina maana kweli mimi ndiye niliefanya watu wote pale watokwe machozi pia mimi ndiye niliempotezea mama Josephat mtoto wake aliyeteseka naye miezi tisa tumboni ? ama kweli nina makosa makubwa sana ila yote haya ni kwa sababu akina Chris wanalijua lile tukio langu kumuua yule mwanaume mwingine sasa watanitesa hadi lini?" Angel aliwaza hayo kwa machungu kwani alilazimishwa kuuwa ili atunziwe siri yake ya mauaji, "hiki kifo cha Josephat kimenitoa machozi kwa kweli na sitaua tena, na hata mbele za mungu naapa kuacha mauaji" Angel alilia sana huku akijutia kitendo alichofanya cha kutia watu machungu mbaya zaidi alimfikiria Miriam anayeteseka mahakamani. "Sasa mungu atanisamehe vipi?" Angel alizidi kulalamika na baada ya mda usingizi ukamchukua.
*****
"Kuna vijana wawili wamekufa alafu ni wanafunzi wa hii shule aliyosoma marehemu Josephat" ilikua taarifa ya ghafla sana kila mtu alionesha hali ya kutoamini, "wamekufaje?" aliuliza dada mmoja aliyejifunga doti, "wamegongwa na gari ila kwa uzembe wao maana walikua walevi wakasimama katikati ya barabara" kijana huyo alijibu kwa sauti ya chini.Hali hiyo ilipelekea kila mtu pale kuangua kilio kwani walihisi kama kuna pepo la kuua wanafunzi kwa kipindi hicho,
"mh! kuna kitu,,haiwezekani hata wiki haijaisha wafe wanafunzi watatu kwenye shule moja" kijana aliongea kwa hasira. "hao vijana majina yametambulika kweli?" mama mmoja mwenye mtoto wake anayesoma Arusha Secondary,aliuliza kwani mama huyo alipatwa na na wasiwasi maana mtoto wake ni mnywaji wa pombe sana,
"kwa nilivyosikia majina waliyokua wakiitana kabla ya kugongwa na gari ni Brown na Chris ila siwezi kuwajua nani Brown na nani Chris, "ahaa pole zao jamani kwa hiyo miili imepelekwa Mount Meru au wapi?" mama mwingine aliuliza, "ndio hapo imepelekwa" alijibu kijana huyo na maombolezo yakaendelea kama kawaida,hali ya huzuni ikiongezeka mara mbili zaidi ya ilivyokua mwanzoni.
*****
Mwendo wa saa kumi na mbili asubuhi Angel alishtuka usingizini, haraka aliingia bafuni na kujiandaa na shule,kichwani mwake alijaa mawazo kuhusu kifo cha Jesophat,
"mungu nisamehe kwa kosa hili" Angel alianza kuumia na kulia kwa kitendo alichokifanya.
Genes naye alikua akisikitika kumpoteza rafiki yake kipenzi,
"dah chali wangu aise kafa kiutani aise ama kweli dunia mapito leo unakua naye kesho hayupo jamani inauma sana" yalikua maneno ya Genes akikaribia lango la shule, "leo vipi mbona makundi sana huku shule" Genes alishangaa kwani aliona wanafunzi wakiwa katika makundi pia aliona kila kundi likiwa katika mfumo wa kupashana habari mpya,
"vipi mpenzi umesikia tena habari mpya?" Angel alimfuata Genes na kumuuliza, "ipi tena zaidi ya kuzikwa kwa Josephat jana?" Genes alijibu huku akitaka kujua ni habari gani mpya, "nasikia jana usiku Brown na Chris wamepeta ajali na kufa" Angel alijibu,
"sangapi wamepata hiyo ajali?" Genes aliuliza kwa mshangao,
"usiku"Angel naye alijibu,
" itakua walikua walevi kama kawaida yao,wakishalewa huwa wabishi na mara nyingine hujifanya traffic (askari wa barabarani )"Genes alieleza kwa machungu huku akikilaani kitendo chao cha kulewa sana.
Majonzi yalizidi kutanda kila kona ya shule kwani ndani ya wiki moja walikufa wanafunzi watatu kwa ajali, bendera ilipepea nusu mlingoti kwa tukio hilo,kila mtu aliamini kitu kinachoendelea ni mambo ya kishirikina, lakini haikua hivyo kwani kila kitu kilichotokea kilikua na sababu ya kutokea. Kwa Angel ilikua furaha kubwa kutokea kwa kifo cha Chris na Brown kwani ndio walikua maadui zake waliomshurutisha kuua,
"Mungu anisamehe sana sitakaa nifanye mauaji yoyote maishani mwangu" Angel aliapa kimoyo moyo.
***
Shughuli za mazishi ya Chris na Brown zilifanyika na baada ya siku tatu walizikwa ,yalikua majonzi makubwa sana kwa familia zao kupoteza vijana wao, wazazi walisikika wakisema
"jamani vijana wa kiume wanakufa wakiwa bado wadogo na hata watoto hawana,mimi mtoto wangu wakiume akizalisha akiwa na miaka kumi na nane ni halali jamani waache kizazi chao kikiendelea".
***
Baada ya wiki mbili Miriam aliachiwa huru na kurudi uraiani kama kawaida,
"Miriam ni wewe?" Anitha alimkimbilia Miriam aliyeshushwa kwenye gari la polisi,
"ndio ni mimi"Miriam alijibu huku akimfuta Anitha machozi. Kila mtu pale alilia sana kiasi hadi Miriam akachukua jukumu la kuwabembeleza,
"jamani msilie nishaachiwa huru" Miriam alisema kuwaihi wenzake wasilie,
"yanini sasa walienda kukukondesha huko gerezani tu huna hata kosa jamani" mfanyakazi mmoja alisema kwani Miriam alikua kama vile kapungua sana,
"acha tu ndugu yangu,usiombe uingie kwenye mkono wa serikali nakwambia utakonda tu tena ukute umeingia hujui hata kosa lako lazima uwe hivi" alijibu Miriam huku akionesha jinsi alivyokonda mikono na shingo.
Siku hiyo katika hotel Miriam aliyofanya kazi basi kulifanyika tafrija ndogo,iliyoongozwa na mzee Massawe ambaye alikua mmiliki,http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"jamani basi wapendwa leo hii tafrija ni ya kusherekea kitendo cha mfanyakazi mwenzetu kuachiwa huru kwani alikua jela bila hatia,licha ya kusherekea basi kutakua na mchango wa
kumpa pole kwani alipokua gerezani,aliibiwa vitu vyake vya nyumbani kwa utapeli aliofanyiwa rafiki yake Anitha bila kujua" mzee Massawe aliongea mengi na baadaye shughuli ya kuanza kumchangia ilianza, wafanyakazi wenzake walimchangia kwa moyo mmoja,
"ama kweli ukikaa vizuri na watu unavuna matunda mazuri" dada mmoja alisema kwa sauti ya chini baada ya kuona hadi wafanyakazi wengine wakiahidi kumpa Miriam mshahara wao wa mwezi mzima, hakika Miriam alipata furaha kuona anapendwa na wengi.
"Unaona kama nilivyokuambia Miriam utakuja kua mtu mkubwa na tajiri sana" mzee Massawe alimnong'oneza Miriam kwani walikaa wote kwenye jukwaa. Tafrija iliisha na mchango ulihesabiwa pale pale,
"jamani sisi kama wanafamilia,tunaopendana kwa shida na raha tumemaliza zoezi letu kwa uzuri,nimefurahi kwa mchango wenu mkubwa mlioonyesha kwa huyu ndugu yetu,ni vizuri mkawa mnafanya kazi mkiwa na upendo kama huu,msibaguane kama baba wa taifa hili Nyerere alivyotusihi tuishi kwa upendo na umoja,kweli kwa tafrija hii basi tumepata kiasi cha shillingi Milioni tatu pesa taslimu na ahadi ni milioni moja na nu,,,,,,". Hata kabla ya kumaliza kuongea shangwe na vigelegele vilisikika kwa kishindo.
" Haya tumpe Miriam nafasi kidogo atoe shukrani zake pia" mzee Massawe aliongea na kumkabidhi Miriam kipasa sauti naye aseme neno,
"jamani kwanza niwashukuru kwa upendo wenu kwani sisi ni kama wanafamilia na tunatakiwa kukaa kwa upendo huu hadi mwisho kwani umoja ni nguvu, kwa sababu jumla ya pesa zote ni milioni nne na nusu basi mimi nitachukua milioni mbili tu nikanunue vitu vyangu vilivyoibwa lakini hii milioni mbili na nusu sisi kama wanafamilia basi tutaanzisha mradi wetu ambao kila mfanyakazi akipatwa na tatizo basi unamsaidia, au tuwe tunakopesha watu pesa na kutulipa kwa riba ndio tutafika mbali zaidi kwani tukifanya kazi kama familia basi tutafanikiwa kwa kiasi kikubwa au mnasemaje ndugu zangu?"
"ndioooooo tufanye hivo" Kila mtu pale alifurahia wazo la Miriam kwani hakuna mtu aliyewahi kuwaza hivo pale kazini na kila mtu alishangaa jinsi Miriam alivyokataa kuchukua pesa zote,
"hakika hapa huwezi amini kama huyu mtoto hajaenda shule wala hajui hata kusoma wala kuandika kitu" Anitha alijisema moyoni kwa kuona jinsi Miriam anavyowaza mbali.
***
Kwakua basi Miriam hakua na mahali pa kulala kwa siku hiyo alienda kulala na Anitha,
"Vipi Genes hajawahi hata kuniulizia hapa?" Lilikua swali la kwanza Miriam alilomuuliza Anitha walipoingia ndani,
"ha wewe acha ujinga yani mimi najua hutamuwaza tena huyu mbwa aliyekufanya uteseke hivi kama sio huyu mbwa Genes unafikiri ungeenda polisi kwa mambo haya?" Anitha alimjibi kwa hasira,
"usimuite mume wangu mbwa hata siku moja" Miriam alijibu kwa hasira za utani,
"haya ila unapoelekea mapenzi yatakupeleka pabaya" Anitha alijibu,
"kwa hiyo nisipende ? kama nimeumbwa na hisia ni haki yangu kupenda" Miriam alijibu kwa kujiamni, "subiri upendwe basi mdogo wangu" Anitha alizidi kumsisitiza Miriam ila Miriam katu hakusikia kitu,
"sasa kama nimemuona mwanaume nikampeda kuna haja gani ya kusubiri kupendwa, cha kufanya ni kumwelezea hisia zangu,allah?" huo ndio ulikua wimbo wa Miriam kila kukicha.
Mirim alipekua katika pochi yakeakatoa kitambulisho cha Genes chenye picha yake ndogo (passport) na kuibusu,
"haaa! kile kitambulisho unacho tu" Anitha aliuliza kwa mshangao kwani aliamini kitakua kishapotea,
"sasa nitapotezaje,,," Miriam alijibu kwa tabasamu zito.Waliongea mengi hadi usingizi ukawachukua.Asubuhi waliamka na kujiandaa tayari kwenda kazini.
***
Penzi la Angel na Genes lilizidi kukua,"hivi mpenzi una mpango gani na mimi" Angel alimuuliza Genes,
"mpango gani kivipi mamii?" Genes alijibu huku akijidai hajaelewa swali kwani wanaume wengi huwa hawapendi kuulizwa juu ya mpango wa baadae,
"liniutajenga kwako unioe"Angel alimuuliza Genes ambaye kwa wakati huo aliinamisha kichwa kwenye dawati,
"usijali mke wangu nitajenga tu na nitakuoa cha muhimu tusome kwa bidii ili tuje kushirikiana kujenga" Genes alijibu huku kichwani akiwaza jinsi akili ya wasichana ilivyo ndogo kwani mara nyingi mwanamke huwaza kumsubiri mwanaume ajenge ili aolewe naye wakati huo huo mwanaume anamsubiri aoe mwanamke ili wajenge wote.Angel alifurahi kusikia hivyo.Siku zilizidi kusonga huku Angel akijikuta akizidisha upendo kwa Genes kwani waliokua wanamshurutisha kuua wao walishakufa,"huyu atakua mume wangu"Angel alijisema kimoyomoyo.
***
Miriam alishaanza kufuga na tayari ashaanza kukuza mtaji aliopewa na wafanyakazi wenzake na sifa zake zilizidi kuenea mtaani,watu wote walimpenda,
" jamani kwa nini asiwe dada yangu"watoto waliomjua walimpigania kwani alipenda sana watoto pia alikua na roho ya utoaji sana.
"sasa Miriam nataka ufungue biashara yako uiendeshe mwenyewe" muajiri wake alimshauri Miriam licha ya Miriam kusikia ushauri ule bado aliaahidi kuendelea na kazi pale lakini kwenye biashara zake ataajiri watu,
"lakini yakupasa uende shule kwanza ujifunze kusoma.
Miriam baada ya kuulizia mahali ambapo angeweza kupata elimu ya watu wazima ili aweze kujua kusoma na kuandika ambayo ilijulikana kama kufukuza ujinga,
"hapoArusha Secondary inaanza kesho kutwa jumatatu nenda hapo tena ni bure kabisa" alipewa taarifa na mfanyakazi mmoja,bila kupoteza mda Miriam alianza masomo,japo ilikua vigumu alijitahidi na kwakua alienda kwa moyo basi alielwa mapema,
"hapa nisipompata Genes basi sitompata tena"Miriam alijisemea baada ya kumuona Genes amesimama mwenyewe katika lango la shule,
"mambo" Miriam alianzisha maongezi,
"powavipi" Genes alijibu huku akiwa kainamisha kichwa chini akijifanya kama hamjui,
"mbona uko hapa mwenyewe na wenzio washaishia nyumbani?" Miriam aliuliza,
"nina matatizo kidogo nilikua natafuta pesa yangu nimepoteza yaani sijui hata nifanyeje hapa" Genes alijibu huku machozi yakimtoka,
"shilingi ngapi"Miriam alimuuliza kwa huruma,
"elfu hamsini (50,000)" Genes alijibu,
"basichukua hii" Miriam aliongea huku akiingiza mkono katika sidiria yake na kutoa noti kadhaa za elfu kumi na kumpa Genes bila hata kuhesabu.Genes alipokea na kuzificha mfukoni.
"vipi naomba namba yako ya simu basi leo nataka niongee nawewe kidogo" Miriam aliongea kwa sauti ya chini.Genes alimpa Miriam namba ya simu kisha wakaachana.
"Huyu msichana itakua ananipenda ila sasa nishampenda Angel"Genes aliwaza jinsi Miriam anavyojitoa kwa ajili yake na bila kutarajia akajikuta akisahau mambo yaliyowahi kutokea kipindi cha nyuma,
"akinitafuta kwenye simu namkubalia sasa, na nitamuacha Angel" Genes aliwaza.Tayari Genes alishaanza kumuwaza Miriam, ashasahau kila kitu kibaya ambacho kilitokea kwa kasababishwa na Miriam..
Miriam alimshukuru mungu kwa mema anayomjalia kikubwa alishukuru sana kwa kuona kipenzi cha moyo wake Genes anaanza kuelekea kumkubalia.Alizichukua namba zake na kumpigia,waliongea sana na Genes alimpa ahadi ya mapenzi ya dhati,licha ya kumaliza maongezi waliendelea kutumiana ujumbe mfupi,kwani tayari Miriam alishaanza kujua kusoma na kuandika.Maisha yalizidi kusonga mbele huku Angel akiona dalili za Genes kutovutiwa naye kama alivyozoea,
"mbona hata hanipigii tena simu usiku kama ilivyo kawaida yake?" Angel alijiuliza,ila hali hiyo ilitokanana Miriam kukaa kichwani kwa Genes mda mrefu.
"Au kwa sababu sijawahi kumpa penzi langu" Angel alijiuliza labda kutompa Genes penzi ndio kunamfanya akae kimya mara kwa mara,
"jumapili ijayo nitampa mapenzi kisha nimuangalie kama atanipenda kama zamani" Angel alijisemea na ilikua siku ya ijumaa.Miriam naye alizidi kupambana na mifugo yake aliyonunua kwa pesa ya mchango,na kikundi kilianza kwa mfumo wa kila mfanyakazi kukatwa mshahara kidogo kidogo na kuuwekeza katika pesa walizokua wanakopesha watu pamoja na kununua mifugo. Wazo hilo la Miriam liliwafanya wafanyakazi wenzake wazidi kumpenda,kwani walianza kuona matunda yake.Furaha ya Miriam ilizidi kuongezeka siku baada ya sikukwa kuona Genes amekubali kua wake.Genes alianza kufanya vibaya darasani,aliporomoka kutoka nafasi ya kwanza hadi ya thelathini.
Siku ya jumapili asubuhi Angel alipiga simu ya Genes ila haikupokelewa kwa marambili lakini hakukata tamaa hapo alipiga tena mara ya tatu,
"huyu anatakaje?" Genes alisema baada ya kuona Angel anamsumbua,lakini aliinua simu na kuipokea,
"mbona hupokei simu yangu jamani?"
"nilikua bafuni,unasemaje?"
"jamani ungeniambia ningekuja kukuogesha"
"usijali"
"sawa nambie unaoga,unataka kutoka asubuhi hii?"
"ndio natoka kidogo"
"unaenda wapi maana nataka nikuone leo, au uje kwetu mama na baba hawapo nipo mwenyewe nyumbani"
"sawa nitakuja basi mida ya saanne".Yalikua mazungumzo ya Angel na Genes kwa njia ya simu.Angel hakumuambia Genes kitu kinachotakiwa kuja kufanyika maana alitaka kumshutukiza.Genes alitoka na kuanza safari ya kuelekea kwa Angel, kutokana na ujirani waliokua nao basi haikuchukua mda mrefu kufika nyumbani kwa Angel,
"alafu usikute mama yupo atukute huku chumbani" Genes alimnong'oneza Angel huku wakiwa wamekaa kitandani.Angel aliongeza sauti ya radio iliyoimba nyimbo ya Z Anthon ,kisiwa cha malavidavi, Genes alijikuta akitikisa kichwa chake kwa kusikia wimbo huo,alipaona pale chumbani padogo baada ya Angel kumshika mkono na kumuinua alipoketi na kuanza kumsogelea taratibu,alikutanisha midomo,huku wakishikana nyonga.
"jamani mpenzi nimechoka naanguka" ilikua sauti nyembamba iliyopenya masikioni mwa Genes huku akipulizwa nakuingiziwa ulimi masikioni,Genes alimshikilia Angel vizuri kwani Angel alishaanza kuishiwa nguvu.
"tukae basi" Genes alimkaliasha Angel kitandani.Genes tayari alielewa lengo aliloitiwa pale na hakutakiwa kuzubaa,
"tena kanga moja?" Genes alijisemea huku akimvua Angel kanga aliyovaa na kuanza kumpapasa sehemu mbali mbali zinazoamsha hisia,Angel alimvuta Genes kuashiria anataka kumnong'oneza kitu,bila kukawia Genes alisogeza sikio,
"lakini mpenzi usiniache kwa sababu leo utapata penzi langu" Angel aliongea kwa hisia kali,kwani mara nyingi alishasikia wasichana wengi wakilalamika juu ya mwanaume anapopata penzi la mwanamke basi huwa ndio mwisho wa mahusiano hayo.
"siwezi kukuacha hata kidogo usijali" Genes alimjibu kwa sauti ya chini,Angel alifurahi kusikia jibu hilo,alijiona wamaana kuliko wasichana wote duniani,alihisi kitu kitamu kama asali kikipenya moyoni mwake.Genes alimsisimua Angel hadi akajikuta akilia,
"unajualia wapi jamani hivi vitamu hivi" Angel aliuliza baada ya kumuona Genes jinsi anavyochezana mwili wake,
"kwani mchina alileta hizi simu za kisasa kwa sababu ya nini?" Genes alijibu kwa utani huku wote wakiendelea kupeana raha.Angel alikua hajawahi kukutana na mwanaume kimwili, hivyo kitendo kile kilimfanya ajihisi yupo dunia nyingine,lakini kwa bahati mbaya wakati Genes alianza kumuingizia uume na kumtoa usichana wake basi Angel alizimia,na kwakua Genes ilikua mara ya kwanza kufanya mapenzi basi alifikiri ni hali ya kawaida kwa mwanamke kutulia hivo wakati akifanya mapenzi,
"mbona hapumui tena" Genes alijiuliza huku akitoka kifuani kwa hofu,
"Mungu wangu na hii damu tena" Genes alizidi kuchanganyikiwa kwa damu iliyomtoka Angel. "atajua ngoja mimi niondoke zangu afe mwenyewe" Genes alisema huku akifungua mlango wa chumbani na kutoka,lakini mlango mkubwa wa subuleni ulikua umefungwa na ufunguo haukuonekana pale,
"Mungu wangu hapa nitatokaje na huyu mwanamke kashakufa,heri hata ingekua vichakani" Genes alijisemea huku akihema kwa kasi kwani hakuona msaada wowote ambao
ungemuwezesha kutoka pale.
Genes alirudi katika chumba alichomwacha Angel,alipata furaha ya ajabu kumwona Angel ameamka kitandani akijifuta,
"ulifanyaje?" Genes aliuliza huku akimshika mkono,
"mbona sijafanya kitu?" Angel alijibu,
"mbona mlango umefungwa na ufunguo haupo hapo?" Genes aliuliza huku akiwa na haraka ya kuondoka maeneo yale.Angel alitoa ufunguo na kumkabidhi,Genes alimuaga kwa kumbusu shavuni kwa kumshukuru kwa penzi tamu alilopata.
***
Baada ya wiki mbili Angel alianza kujihisi hali ya tofauti tumboni,tabia ya kutema mate,kutapika na tumbo kuvuruga ilianza,
"usikute nina mimba" Angel alijiuliza,lakini kwakua alikua kidato cha nne alijikaza na kusema hata kama ni mimba basi yupo karibu kuhitimu hivyo isingemwachisha shule,
"ngoja ikifika siku ya kawaida ya kuingia mwezini nitapata jibu kamili" alijisemea Angel.
Genes alijihisi mshindi kwa kukuta msichana mrembo kama Angel kua bikra,mara nyingi alisikia mwanaume wenzake wakisema ni vigumu sana kumkuta msichana mrembo kua na bikra.Licha na hayo mapenzi yake na Miriam yalizidi kukua kadri siku zilivyozidi kusonga,Miriam alijiona mwenye bahati kila siku alisali sana na kumshukuru Mungu kwa zawadi hiyo, alifanya kazi kwa bidii na umakini ili kuhakikisha anapata mafanikio makubwa ili aweze kuanza maisha na Genes.Jina la Miriam lilizidi kukua alifungua duka la vifaa vya ujenzi (hardware) katikati ya jiji la Arusha, alitoa ajira kwa vijana wengi na wafanyakazi wake walimpenda kwani alihakikisha kila mfanyakazi wake anafanikiwa.
***
Baada ya miaka mitatu tayari Miriam alishakua katika orodha ya matajiri wakike tena kwa umri mdogo katika jiji la Arusha, alijenga nyumba za kifahari,alifungua hotel za kitalii na kuanzisha miradi katika mikoa mbalimbali,alifungua super market kubwa mtaa wa Kariakoo jijini Dar es salam,hivyo alifanya safari nyingi mikoani,alimiliki mashamba ya mpunga huko kahama.Genes alizidi kufurahia maisha kwani alipomaliza kidato cha nne alishindwa mtihani hivyo hakuendelea tena na masomo na kwa bahati nzuri Miriam alikua ashakua tajiri mkubwa,
"sasa tuoane tuanze kuishi pamoja" Miriam aliongea kwa utani kutaka waanze maisha na Genes,na bila ubishi kwa kua naye Genes alishaanza maisha yake mwenyewe basi walianza maisha rasmi wakiishi pamoja katika nyumba yao waliyoijenga maeneo ya Sakina.Waliishi maisha ya furaha wakifanya kazi kwa bidii,
"nataka siku moja tuwe matajiri wa kwanza Tanzania" Miriam alimwambia Genes huku
akicheka,
"yote yanawezekana tukifanya kazi kwa bidii" Genes alijibu.
Huko Manyara nyumbani kwa Miriam walipata taarifa kuhusu mwanamke tajiri anayeitwa Miriam,mwenye asili ya kimasai,
"usikute ni yule mtoto wetu aliyetoroka nyumbani?" Mzee Lizery alimwambia mke wake,
"haiwezekani akawa huyo kwani yule itakua alifia msituni akitoroka mila zilizoletwa na mababu zetu" mama yake Miriam alijibu.Wote waliamini huyo mtoto wao alishaaga dunia kwani ni zaidi ya miaka kumi na tisa tokea aondoke nyumbani.
Maisha yalizidi kuwa mazuri na Genes alishaanza kuzunguka mikoani kuangalia biashara zake na mkewe.Asubuhi moja siku ya Jumamosi,Genes aliagana na mkewe Miriam kwa safari ya kuenda Dar es salam,
"uwe makini njiani mme wangu" Miriam alimuaga mumewe kwa kumrukia na kupata denda kisha Genes akapanda ndani ya Toyota Prado nyekundu.
"byee mwaaaah!" Miriam alimuaga tena kwa kumpungia kupitia (side mirror) kioo cha pembeni.
Ili kukwepa foleni Genes alikatiza Chalinze na kupitia barabara ya Bagamoyo na ndani ya masaa nane tayari alikua ameshaingia jijini Dar es salam.
"Ngoja nielekee Kawe nikatafute hotel ya kulala ili nipunge upepo wa bahari taratibu" Genes alijisemea,kwani alihitajika kupumzika ili kesho aamkie kukagua biashara zake.
Jumapili mwendo wa saatatu asubuhi Genes alikua katikati ya foleni maeneo ya Morocco akisubiri taa zimruhusu,
"mbona kama hii sura naijua?" Genes alijiuliza huku akishusha kioo cha gari na kumtazama mwanadada aliyekua akiomba msaada eneo lile,
"eti dada samahani" Genes alijikuta akimuita dada huyo, na kwa haraka dada huyo alitii wito kwa furaha kwani ilikua nadra sana ombaomba kuitwa,
"samahani nikuulize swali" Genes alianza maongezi huku akiwa bado kwenye gari akizidi kuvuta kumbukumbu juu ya msichana huyo,
"ndio niulize" msichana huyo alijibu huku akitetemeka,
"wewe unaitwa nani?" Genes aliuliza ila kabla hajajibiwa alishtushwa na mlio mkali wa honi,gari iliyokua nyuma ilimtaarifu kwani taa ya kijani ilishawaka kuashiria kupita.Genes aliondoa gari kuendelea na safari,yule dada alishuhudia tena gari ikienda na kuegesha pembeni ya barabara mara baada ya kuvuka mataa,hapo akaamini mazungumzo yataendelea. Hakuona sababu ya kukaa pale,alitoka haraka kulifuata gari liliposimama,
"huyu kaka ana heshima sana kumbe angekuja hapa aliponiacha" huyo dada alisema,na akiendelea kupiga hatua kubwa kumfuata.
"mbona kama nimekufananisha" Genes alianzisha tena mazungumzo,
"na nani" dada alijibu,
"kwanza nambie unaitwa nani" Genes alirudia swali,
"mimi naitwa Lissa" huyo dada alijibu baada ya kufikiria kwa sekunde tano, Genes alizidi kupata wasiwasi juu ya sura ile,
"sasa samahani basi sio wewe" Genes alitamka hayo huku akitoa noti yaelfu kumi na kumkabidhi,
"asante sana,lakini mbona umeniuliza swali hilo la jina?" huyo dada alipokea pesa kisha
kuuliza,
"apana dada nilikufananisha namsichana mmoja anayeitwa Angel, niliyesoma naye shule moja lakini yeye akitangulia kwa kidato kimoja" Genes aliongea maneno hayo na ghafla alishuhudia dada huyo akitoa machozi na kilio kikubwa,
"ndio mimi hata wewe nimekufananisha na Genes,sijui kama ndio wewe" huyo dada alijibu huku akijifuta machozi,
"ndio mimi" Genes alijibu,
"unaona navyoteseka kwa ajili yako"huyo dada ambaye kwa wakati huo ashaweka wazi jina lake kua ni Angel.Hakika Genes hakuamini macho yake kukutanana Angel mazingira yale wala haikumuingia akilini msichana aliyekua akitikisa shule nzima kwa uzuri alafu awe jinsi alivyokua,Genes aliona kama ndoto kwani kwa miaka mitatu Angel amebadilika sura,amekonda,na kuwa ombaomba barabarani.Genes hakutaka kuendelea kukaa naye maeneo yale,
"twende tuondoke hapa" Genes alitamka kichwa kikiwa kimeinamishwa chini,
"ngoja nipo na watoto wangu" Angel alisema na mara moja aliwaitwa watoto wake waliokua wamekaa pembeni ya barabara.Walikua watoto wawili mapacha,walivaa matambara yaliyoacha sehemu kubwa ya mwili wazi.Genes aliwachukua na kurudi kwanza kufanya mazungumzo na Angel.
"ehe nambie Angel imekuaje hadi upo katika mazingira haya ambayo sijatarajia kama nitakukuta,Genes alianzisha maongezi wakiwa katika chumba kimoja pamoja na watoto wa Angel,
"yani ni hadithi ndefu,ila kwa kifupi maisha haya yalianza siku ile tuliyofanya mapenzi pale chumbani kwangu,kwani baada ya siku ile wazazi wangu walikuja kugundua kwa kutumia camera za CCTV zilizofungwa ndani namimi nilikua sijui,na pia nilipata ujauzito wa hawa watoto hapa,lakini siunakumbuka tulifanya mapenzi nikiwa karibu nahitimu pale shuleni,hivyo basi maana na wewe ulinikataa baada ya kulala na mimi,nilikuja kufukuzwa nyumbani nikiwa na ujauzito wa miezi sita nikaja huku Dar es salaam nikajifungua nikiwa ombaomba hadi leo,hivyo hawa watoto hapa ni wako" Angel hakuweza kuendelea zaidi ya hapo kwani machozi yalishamjaa.Genes aliinua kichwa na kuwatazama watoto wake, kisha kuinama na kuanza kutoa machozi upya,
"yaani mimi nakula na kusaza alafu kuna watoto wangu wanateseka njaa ?" Genes alijiuliza kimoyo moyo.Angel na watoto wake waliondoka na kuingia katika duka la nguo kila mmoja akavalishwa aliyoipenda,wakapata chakula Genes hakuamini macho yake kile kitendo kilichokua kikiendelea pale,bado aliamini ni ndoto.Baada ya kupata chakula na nguo Genes aliwachukua na kuwapeleka katika nyumba moja iloyopo Sinza.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"kaeni hapa nitakuja kuwatembelea mara kwa mara" Genes aliwapa makazi mapya na pesa za matumizi.Hapo alirudisha kumbukumbu nyuma na kukumbuka siku ya kwanza alivyokutana na Angel jinsi alivyozimia katikati ya tendo,yote hayo yalimfanya kumuona Angel hana makosa wala hastahili kuteseka hata kidogo.Baada ya siku tatu Genes alirejea Arusha,
"mbona una mawazo sana mpenzi kuna nini huko" Miriam alimuuliza mumewe,
"acha tu mama watoto huko yani wale mafundi wanaojenga nyumba yetu wanapeleka kazi taratibu sana itabidi niwe naenda mara kwa maraili wamalize mapema" Genes alimdanganya mkewe kwani uhalisia wa mawazo yake yalitokana na Angel.Genes aliwaza ni kwa jinsi gani angemweleza mkewe juu ya mambo yanayoendelea, hakutaka kupoteza uaminifu kwa mkewe na hakutaka kuona Angel akiteseka na watoto wake. Hivyo safari za kuenda Dar es Salam ziliongezeka kadri siku zilivyoenda,Angel alianza kurudia uzuri wake, maziwa yalianza kusimama na weupe wake ulianza kuonekana,mapaja yalianza kutengeneza hips.Siku moja Genes alimuuliza Angel,
"vipi una mpango gani?"
"mimi nikipata mume naolewa ila hawa watoto wako sasa"
"wewe usiolewe kaa hapa hapa nitakua nakutunza na tutaendelea kufanya yetu".Baada ya hayo penzi lilianza upya kati ya Genes ana Angel kikubwa kilichozingatiwa ni mahusiano ya Miriam na Genes kwani Genes ashamueleza Angel kila kitu.Penzi lilizidi kukua,wale watoto mapacha waliitwa Eledy na Eledius,wote walifurahi sana kumjua baba yao.Miaka miwili badae Genes alikua akisafiri hukaa hata wiki moja bila kurudi nyumbani,
"sasa Angel yule mke wangu sijui hazai au vipi"
"kwani vipi"
"tokea nimeoana naye hajapata mtoto kabisa"
"atakua ni tasa huyo"
"hata sijui ila wewe ni mzuri sana na umenizalia watoto mapacha hivyo Miriam kama hazai nitamuacha kabisa tuedelee pamoja,Yalikua mazungumzo kati ya Angel na Genes kumhusu Miriam ambaye kila alipobeba mimba ilitoka.
"Mpenzi nataka Valentine day (siku ya wapendanao) hii tusafiri kidogo hata tukafurahishe macho nchi yoyote au sehemu yoyote nzuri ya kutembea"Miriam alimuambia mumewe ikiwa ni siku tano kabla ya tarehe 14 mwezi wa pili,
"apana mke wangu tusitumie pesa ovyo hiyo siku nitakua Dar es salam kufuatilia biashara zetu" Genes alijibu lakini machoni alionesha hali ya kutofurahia kauli hiyo ya mkewe,
"najua mume wangu pesa tunatafuta kila siku sasa yatupasa siku moja moja tufurahie tunachotafuta" Miriam aliongea taratibu akimbembeleza mumewe waweze kusafiri pamoja lakini hadi mwisho Genes aligoma.
"Haya basi wewe ndie baba wa familia ukiamua kitu umeamua njoo basi tulale" Miriam aliongea huku akipanda kitandani.
Hadi kufikia siku hiyo Genes alikua ashaishiwa hata hamu ya tendo la ndoa kutoka kwa Miriam,
"hivi Miriam wewe huzai kila siku nachezea mbegu zangu tu bila faida yoyote, kwa nini tusigawane mali wewe ukabaki na nusu na mimi nusu alafu mimi nioe mwanamke mzima mwenye kupokea mbegu za mumewe na kumzalia mtoto" Genes aliongea huku akimsukuma Miriam aliyevua nguo zote ili kumvutia mumewe angalau aweze kumpa haki yake ya ndoa,
"sikia mume wangu mimi sijapenda haya yatokee na pia Mungu ana makusudi yake kufanya hivi,wewe labda utasema nilitoa mimba nyingi katika usichana wangu,kumbuka wewe ndie ulienifanya nikajua mapenzi,sijawahi kupenda mwanaume mwingine, kumbuka siku ya kwanza wewe unanivunja bikra yangu,mume wangu sisi tuna mali,tuna pesa,tuna kila kitu lakini vyote hivi havitakua na maana kwangu bila penzi lako,nipo tayari kutoa kila kitu ili niwe na wewe mali si kitu maana vinatafutwa lakini kumbuka wewe ni mtu ukiondoka kwangu sitapata kama wewe niliyekupenda naomba nivumilie mume wangu nakupenda sogea karibu basi weka simu chini tuongee" Miriam aliendelea kumbembeleza Genes bila mafanikio kwani Genes alikua ameshikilia simu yake kana kwamba kuna mtu anayewasiliana nae kwa njia ya ujumbe mfupi,
"wewe lala bhana" Genes aliongea huku akimtoa Miriam mgongoni alipokua amemkumbatia na Miriam alifanya yote haya kumhamasisha mumewe afanye naye tendo la ndoa.
"Mume wangu kumbuka tumetoka wapi kumbuka siku ya kwanza ulivyonihurumia nikiwa kwa yule mama kule mgahawani naomba na leo nihurumie tena,naomba basi univumilie mwaka huu na huo ujao nisipozaa nitakuruhusu kwa moyo mmoja uzae nje ya ndoa yetu lakini tumlee mtoto sisi,yaani mimi na huyo mama wa mtoto tukae pamoja siunajua ni vibaya mtoto kukosa malezi ya baba na mama ? hivyo basi mimi nipo tayari kukaa na mke mwenzangu kwa ajili ya hili tatizo langu" Miriam aliongea huku akilia machozi,
"kwani unafikiri sina watoto?" Genes aliongea kwa sauti huku akisogeza simu yake kumuonesha Miriam ujumbe uliongia katika simu,Miriam alisoma na kujikuta anatokwa na machozi mfululizo kwani alikutana na maandishi haya,
FANYA HIMA UJE MAANA HAWA WATOTO WAKO WATAFURAHI SANA KUANDAMANA NA WEWE SIKU HIYO YA WAPENDANAO, MSALIMIE HUYO PAKA WAKO ASIYEZAA.
Yalikua maneno machache yaliyomuumiza sana Miriam,Genes alicheka kisha na kumwambia
"mimi ni dume wewe ungekua na uwezo wa kuzaa nakwambia mimi nikikukamata lazima uzae mapacha ila wewe dah nitakua nachezea mbegu bureeeee" alimaliza na kulala.
*****
Asubuhi na mapema Miriam aliamka na kumuandalia mume wake chai,kisha kumfuta chumbani na kuenda kumwamsha,
"waooh mume wangu kipenzi umeamkaje"Miriam alimuamkia mume wake kama ilivyo kawaida lakini mume hakuitikia,
"yaani jana usiku namuonesha kua nina watoto alafu leo hii ananipapatikia hivi hapa hiyo chai kashaitia limbwata na atainywa mwenyewe" Genes alijisemea moyoni na kuamka kisha kuingia bafuni, bila kunywa chai alitoka na kuchukua gari kuenda mjini.
Miriam aliumia sana kutokana maisha anayopitia kujitunza kwake kwa ajili ya Genes kumemfanya awe ni mtu wa huzuni kuliko furaha.
Jioni ilifika Genes alirejea nyumbani moja kwa moja aliingia bafuni kisha kuelekea chumbani na kulala,hakutaka kula chakula kilichopikwa na Miriam.
"Mume wangu niambie ukweli kuhusu ujumbe wa kwenye simu, kwanza kama una watoto tena mapacha nikupongeze kwa hilo kwani hata mimi nilikua natamani sana nipate watoto mapacha ila kwa kua wewe umebahatika kupata basi nafurahi sana naona kama ni mimi nimepata sasa cha kufanya ni vizur ukawaleta huku basi tukae nao hata kama itawezekana mama yao pia aje nitamuheshimu kama ninavyokuheshimu wewe mume wangu nakupenda sana tena ikiwezekana hata sasa tuwaite waje na siku hii ya wapendanao tusafiri nao au kama hatutasafiri basi tufanye sherehe kubwa basi, na bila kupoteza muda tuanze kuwaandalia watoto wako miradi yao kwa maisha ya badae maana wao ndio wataangalia mali zetu, tena wakiume jamani hadi raha alafu watakua wazuri kama wewe ? yaani nitawapenda sana wanangu bila kumsahau mama yao pia" Miriam aliongea kwa furaha lakini Genes alitulia tu,
"unafurahia sana kulea eh, zaa wako uwapende" Genes alijibu kwa dharau
"jamani mpenzi watoto wako ni wangu pia"Miriam alizidi kumbembeleza Genes bila mafanikio
Siku zilizidi kusonga hadi ikawa imebaki siku moja kabla ya siku ya wapendao kuwadia,
Genes aliongea na Angel juu ya maneno Miriam aliyosema kuhusu kuja kuishi pamoja,
"we mpenzi nikija kuishi naye atanidharau au ataweza kunionea wivu maana yeye hazai na mimi nimekuzalia hivyo njoo tupange ni kwa jinsi gani tutafanya ili tuishi pamoja bila kipingamizi cha Miriam" Angel alisema na haraka Genes alipanga safari ya ghafla ili aweze kukutana na Angel kwa mipango ya kuishi pamoja.
Alikata tiketi ya ndege na haraka alisafiri hadi kiwanja cha KIA ( Kilimanjaro International Airport) na kupanda ndege, alisafiri bila hata kumuaga Miriam, baada ya masaa mawili tayari Genes na Angel walikua chumbani "alafu mpenzi nina moto sana leo ukinigusa tu hapa wataibuka tena mapacha na safari hii wataibuka wakike" Angel aliongea huku wakinyonyana ndimi na Genes, Angel alifanya utundu wote wa chumbani kumteka Genes,
"ehe mpenzi nipe sasa ripoti" Genes alisema baada ya salamu za kukaribishana ikiwa ni pamoja na kufanya mapenzi kwa raundi moja,
"ndio kama hivo huyu mwanamke wangu anataka eti wewe uandamane na watoto tukaishi pamoja,
"ana kichaa huyo" Angel alisema "
"sio kidogo" Genes alijibu
Walijadili mengi kuhusu maisha yao lakini Angel hakuonesha utayari wa kuenda kuishi na Miriam sehemu moja zaidi alitaka yeye waanze maisha na Genes.
"Sasa twende tukaoge ndio tuje kufurahia penzi letu tena" Angel alisema na wote waliingia bafuni kuogeshana,kisha kurudi chumbani ambapo walianza kupeana raha,Angel alitumia maziwa yake yaliyosimama kumchoma Genes kifuani huku wakitomasana sehemu mbalimbali za miili yao,
"kwani mpenzi unaonaje tukimdhulumu Miriam mali zote au ikishindikana tumuue kabisa ili tuishi wote kwa amani ??" Angel alimuuliza Genes wakiwa katikati ya mchezo,
"niwewe tu mke wangu amua lolote nitakusapoti
"Genes alijibu huku akijikaza kwani alikua karibu kufika mwisho (kukojoa)
"sawa kama utakua na ushirikiano basi kazi itakua rahisi" Angel alisema huku akimuachia ili aendelee kumpa utamu wa nje ndani nje ndani kwani alikua amembana kwa miguu kabla ya kumuuliza.
"Kesho Genes namfanyia suprice kubwa" Miriam alijisemea moyoni akiwa ndani ya duka moja la kuuza suti katikati ya jiji la Arusha barabara ya Uhuru, alichagua suti nyekundu ambayo alipanga kumpa Genes kama zawadi ya wapendao,kisha alienda katika duka maarufu la kuuza vitu vya nyumbani na ofisini maarufu kama Benson Company limited hapo alinunua saa iliyopambwa kwa dhahabu rangi nyekundu,baada ya hapo alishika njia ya nyumbani kwa furaha,licha ya manyanyaso aliyopata kutoka kwa Genes hakutaka mtu amjue kua ana huzuni moyoni, alijirahidi kutabasamu kile aongeapo na mtu.
***
Baada ya Genes na Angel kufurahi miili yao walirudi sebuleni na kuketi,
"kwa hiyo mpenzi kesho tutaanzia wapi safari" Angel alimuuliza Genes,
"nataka tukatembee Bagamoyo,alafu sijamuga hata huyu paka wangu Miriam " Genes alijibu,
"ah kwani kuna haja gani ya kumuaga nishakwambia mimi nipo tayari kuolewa na wewe hivyo ondoa shaka" Angel alijibu huku akimpapasa Genes kifua chake kilichojaa nywele.
Cha kwanza Miriam alipofika nyumbani alinyanyua simu na kumpigia Genes,
"Unasemaje?" Genes aliuliza hata kabla ya salamu,
"mume wangu kipenzi uko wapi kwa sasa,umeshakula kama hujala nakusihi uje nyumbani basi ndio mimi nafika nataka nikupikie kile chakula ukipendacho sana" Miriam aliongea kwa sauti ya kumbembeleza,na hadi wakati huo bado hakujua kama mumewe yupo Dar es salam,
"mimi sipo nyumbani wala sitakuja leo wala kesho labda tuangalie tarehe 17 (kumi na saba) huku nafuatilia ile nyumba kubwa tunayojenga Genes alijibu huku akiongeza sauti ili Angel aliyekua kamlalia kifuani kwa mda huo asikie vizuri
"uko wapi mbona hujaniaga mume wangu au hutaki mkeo nijue uko wapi?" Miriam alimuuliza kwa huzuni,
"nipo na watoto wangu hapa nimekuja kuwasalimia kesho nataka nitoke nao kuenda kuwatembeza ili wafurahie uwepo wa baba yao" Genes alijibu kwa sauti ya dharau huku Angel akimpongeza kwa kwa kutikisa kichwa chake,
"ahaaa vizuri mume wangu ni vizuri ukizunguka na watoto wetu nao wafurahi ila kwa nini usinijulishe na mimi nije kuwaona wanangu" Miriam aliongea kwa sauti ya upole hadi Angel alishanga kwani alitegemea matusi kutoka kwa Miriam,
"watoto wako wapo wapi tofauti na chooni?" Genes alimuuliza Miriam kwa maana ya mimba zinazotoka na kutupwa ndio watoto wake,kauli hiyo ilimkosesha Miriam amani na furaha,alijiona mkosefu mbele za Mungu na dunia nzima,
"sawa basi watoto wangu wako chooni ila sijapenda mimi hata yatoke lakini sasa hata kama wewe umebahatika kupata kwa nini na mimi nisiwafurahie hao watoto wako hata unipe niongee nao kuwasalimia?" Miriam aliomba kuwasalimia bila pingamizi Eledy na Eledius waliitwa,
"msalimieni bibi yenu" Angel aliongea kuwaamrisha watoto wake wamuite Miriam bibi,
"shkamoo bibi"
"mimi sio bibi niite mama mdogo"
"sawa mama mdogo" "WE NANI KAKWAMBIA HUYO NI MAMA MDOGO WAKO" Angel aliingilia maongezi kwa kumkaripia mwanawe kwa kumpiga kofi,
"mama anapigaa" Eledy alitamka hayo kwa sauti,
"kwa nini anakupiga" Miriam aliuliza,
"naita mama mdogo" Eledy alijibu,
"basi poleee sana usiite tena hivyo ,unaitwa nani mtoto mzuri?" Miriam alimuuliza Eledy kutaka kujua jina,
"Eledy"
"na mama anaitwa nani?"
"mama Eledy"
"mwenzako yupo wapi"
"huyu hapa,chukua mchalimie bibi" Eledy aliongea huku akimkabidhi Eledius simu.
Maongezi ya Eladius hayakutofautina na ya Eledy.Baadae Miriam aliomba kuongea na Angel lakini hadi wakati huo Miriam hajamjua mke mwenzie kua Angel,
"habari mama Eledy"Miriam aliongea kwa upole,
"nzuri tu nikuite mama nani vile?"Angel alijibu
"bado cjabahatika kuitwa mama kwa sasa niite mama
Eledius tu au sio shosti wangu nimewapenda sana wanao" Miriam aliongea kwa furaha,
"hahaha eti umependa wanangu sawa bhana wapende tu ni ruksa" Angel alimjibu Miriam kisha simu ikakatwa.
Miriam aliketi kitandani huku akitokwa na machozi aliamini mume wake tayari ameshachukuluwa, alipiga magoti chini na kumuomba Mungu afanye miujiza ili mumewe apate kurudi nyumbani ili waweze kubadili hati za mali ziwe za akina Eledy kwani tayari Miriam ashawapenda na kwa kua ni watoto wake Genes basi amewachukulia kama wanae.
Giza liliingia,kwa Angel ilikua furaha ila kwa Miriam bado kilio kilitawala.
"Sasa mpenzi tutammalizaje huyu mwanamke ??
"Angel aliamzisha maongezi,
"nakusikiliza wewe utakachoamua tutakifanya lakini ukumbuke hii miradi tuliyonayo ndio yeye alianzisha na pia ndio anaiongoza vizuri,hivyo basi sijui itakuaje kama tukimuua na kushindwa kushindwa kuendeleza hizi mali itakuaje" Genes aliongea kwa wasiwasi wa labda atamkwaza Angel na kweli Angel alionesha uso wa kutofurahishwa na jibu la Genes,
"we mpenzi unanisaliti tena mbona saile mchana uliahidi kunipa ushirikiano wa kumpoteza kabisa sahivi unakataa au hunipendi jamani huoni nimekuzalia watoto mapacha?" Angel aliongea huku aliingiza mkono ndani ya suruali na kumpapasa sehemu za siri,
"aaaaash mke wangu unanitia wazimu basi niko na wewe kwa lolote hivyo nakubali kukupa ushirikiano ili tuishi wote, sasa tusafiri tarehe 17 ili tukammalizie mbali ila inabidi tufanye kwa akili kubwa sana hapa inabidi kwanza ukubali kuishi nae pamoja na watoto alafu ndio tupange namna ya kumuua" Genes alitamka ingawa kwa shingo upande huku akiendelea huhema kwani alipata msisimko mkubwa kwa jinsi Angel alivyompapasa sehemu za siri kwa ustadi wa kucheza na korodani.
***
Miriam alipitiwa na usingizi baada ya kuwaza sana,asubuhi aliamka na kuendelea na shughuli zake, zawadi alizomnunulia mumewe alizihifadhi vizuri na kutoka kuenda kwenye mizunguko yake,siku hiyo aliona wivu watu wakiwa na wapenzi wao wakiambatana njiani,
Nako jijini Dar es salam Genes, Angel pamoja na watoto walizunguka katika mahotel ya kifahari wakiambatanisha nguo nyekundu.
Hakika ilikua siku yenye furaha sana.
***
Tarehe kumi na saba basi ikawa ndio siku ya Genes kurudi Arusha, aliambatana na Angel pamoja na watoto.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Miriam aliandaa sherehe kubwa sana,matajiri karibu wote walikusanyika nyumbani kwa Miriam.
"Tayari wamepanda ndege" Miriam aliongea kwa sauti mbele ya umati wa watu, alikua na furaha sana kuonana na watoto wa mumewe na alifurahi sana pale alipovuta picha na kwa kufukiria siku akiwa ndani ya gari alafu mtoto akae pembeni yani ni furaha sana na siku nyingine uje nyumbani ukute kila kitu kimeharibiwa, hayo yote yalimpa furaha sana kuja kuanza maisha ya kuishi na watoto.
Lakini kwa upande wa Angel na Genes mpango wao ukiwa ni kumuua na walipanga wafanye mauaji kwa haraka iwezekanavyo pindi watakapotua Arusha.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment