Search This Blog

Friday, November 18, 2022

PENZI LA MFUNGWA - 2

 






Simulizi : Penzi La Mfungwa 
Sehemu Ya Pili (2)




Zabroni alirudi nyumbani baada kutoka kumsindikiza mzee Maboso,akiwa njiani aliwaza kipi afanye nini sasa baada kumtambua mbaya wake. Je, aendelea kuchoma nyumba ama adili na mbaya wake? Akili ya fasta ikamjia kwamba bora aendelea kuchoma nyumba ikiamini kuwa maumivu aliyonayo moyoni mwake huwenda yakatulia kama sio kupotea kabisa. Yote hayo kijana Zabroni alikuwa akiyawaza huku akirejea nyumbani mikono nyuma kichwa chini,alipo fika nyumbani alikuta karatasi ndogo kwenye meza iliyokuwepo sebuleni. Zabroni alionekana kustuka huku moyo wake ukihitaji kufahamu kilicho andikwa kwenye karatasi hiyo,hatimaye aliichukuwa akakuta maneno yaliyoandikwa "Kijana Zabroni, mjukuu wangu mwanangu pia. Nimekupa dawa hii ili uweze kulipa kisasi juu ya kile ulicho fanyiwa,hakuna ubishi mzee Fungafunga ndio muhusika mkuu wa vifo vya wazazi wako. Alifanya kitendo kile baada kuona baba yako anamzungusha kumlipa deni lake alilokuwa akimdai. Zabroni Zabroni lipa kisasi kijana unyama huo kamwe huwezi kuupuzia abdani,mwanaume haogopi. Yote kwa yote nikutakie maisha marefu kijana wangu,mimi narudi nyumbani ila najua ipo siku tutakuja aonana tena", yalieleza maandishi hayo yaliyokuwa kwenye karatasi, Zabroni aliyasoma kwa umakini na uchungu mkubwa, aliyafuta machozi, punde akaendelea kusoma "Kwisha kusema haya napenda kukwambia kuwa dawa hiyo unaweza kujigeuza kiumbe chochote chini ya jua,sharti moja tu ambalo inakubidi utekeleze, usithubutu kufanya mapenzi", ilieleza hiyo barua, Zabroni alishusha pumzi ndefu,mwili wake ukasisimka hasira zisizo na mfano zikatawala ndani ya moyo wake akatamani kumfuata mzee Fungafunga muda huo huo lakini akajitahidi kuzizuia hasira zake ambapo aliamua kulala mpaka jioni saa kumi na moja hata hivyo aliamka baada kusikia Tina akigonga hodi. Siku hiyo Tina alikuja na chakula kwa niaba ya mpenzi wake. Zabroni alionyesha kufurahia kitendo kile cha Tina ila moyo wake ulikuwa na kiza kinene,alipiga moyo konde akamkaribisha Tina ndani wakapiga story mbali mbali ilihali muda huo anakula chakula hicho alicholetewa na mpenzi wake.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Kulikoni mpenzi,mbona babu simuoni?.", aliuliza Tina huku akionekana kumfuta futa vumbi uzushi kijana Zabroni kunako shati yake,Zabroni akameza tonge lililokuwa mdomoni mwake kisha akamjibu "Babu kasafari,karudi kwao"

"Kwao? Kivipi yani"

"Ndio, hakuwa mtanzania kwahiyo jana alikuja ndugu yake kumchukuwa kwa hiyo amerudi nchini kwao" alijibu Zabroni.

"Anha kwahiyo karudi Nigeria ? Jamani babu alikuwa mkarimu yule! "

"Ndio hivyo" alihitimisha Zabroni wakati huo sasa ameshamaliza kula chakula alicholetewa na mpenzi wake,baada kumaliza Tina alihitaji kutulia faragha na Zabroni siku hiyo na ndio maana alimjia saa ya jioni. Tina kwa sauti ya upole na yamahaba alimwambia Zabroni asimame ,Kweli Zabroni akasimama bila kupoteza muda Tina alimshika mkono moja kwa moja mpaka chumbani. Walipofika chumbani Tina akamsukuma Zabroni kwenye kitanda cha telemka nikaze,Zabroni alianguka chali, muda huo huo Tina nae alimpanda na kuanza kumpapasa kifuani huku pole pole akitaka kupitisha ndimi yake kwenye kinywa cha Zabro. Zabroni naye baada kufanyiwa hicho kitendo,mwili wake ulianza kupata hisia mawazo yake yote yakazamilia kuvunja sharti. Lakini kabla kitendo hicho hakijatokea akakumbuka maneno ya ile barua,haraka sana akang'atuka akamsukuma Tina kisha akatoka ndani. Tina alishangazwa na kitendo hicho alichokifanya Zabroni kafanye akajiuliza "Kwanini lakini", wakati anajiuliza swali hilo akazipiga hatua kumfuata Zabroni nje. Zabroni muda ulionekana akiwaza na kuwaza jambo akilini mwake. Punde tu Tina akamfikia, kwa sauti ya upole Tina akasema "Zabroni una nini mpenzi wangu? " , kabla Zabroni hajamjibu Tina alishusha pumzi ndefu kisha akajibu "Hakuna tatizo Tina, ila siku ya leo siko poa kabisa"

"Unatatizo gani?..", aliongeza kuhoji Tina huku akionekana kuwa na shauku ya kutaka kujua kinacho msibu Zabroni. Lakini bado Zabroni hakuwa tayari kumwambia Tina ukweli alionao moyoni mwake. Tina alikasirika sana, akamua kurudi nyumbani ingawaje moyo wake bado ulikuwa na mashaka juu ya kitendo kile alichokifanya Zabroni kwani haikuwa kawaida yake.



Baada Tina kuondoka, Zabroni alirudi ndani moja kwa moja akazama mpaka chumbani kwake. Alisimama wima huku akitazama ile karatasi iliyosoma muda mchache ulio pita, kwa mara nyingine tena akaishusha pumzi ndefu kisha akajiuliza "Hivi ni kweli naweza kujigeuza kuwa kiumbe chochote?.."

"Hebu ngoja nijaribuy, nijigeuze kuwa mzee nione kama kweli itawezekana", aliongea baada kujiuliza, kwisha kuongea maneno hayo akanunia na punde si punde akaonekana katika hali ya uzee. Alistaajabu sana, akanyoosha mikono yake kuitazama ngozi ya mwili wake, bado hakuyaamini macho yake, upesi akatoka ndani akaelekea nje kwenye mwanga. Napo bado alishuhudia kitendo kile kile, "Ahahahaha hahahahah", aliangua kicheko Zabroni ndani ya moyo wake akajisemea "Kweli huu ni moto wa Nigeria. Sasa kwa hali hii nipo salama kila idara. Hawa watu wamekwishaaaaaaa". Alifurahi sana Zabroni, asilimia za kujiamini zikaongezeka zaidi.



Lakini wakati yupo kwenye hali hiyo ya furaha, upande wa pili kijijini anaingia mzee mmoja wa makamo. Mzee huyo alionekana kubeba begi kukuu, pasipo na hofu alijikongoja huku akionekana ni mgeni kijijini hapo. Hakuwa peke yake mzee huyo, kando alikuwa sambamba na mwenyekiti wa kijiji. Taharuki baadhi ya wanakijiji inazuka, wale waliomfahamu mzee huyo walionyesha nyuso za furaha, na wale ambao hawakumfahamu waliishia kuzama kwenye taharuki.

"Huyu mzee Baluguza amefuata nini huku?..", moja ya vijana waliopata wasaa wa kumuona mgeni huyo aliuliza.

"Mmmh kiukweli haujui lakini nahisi amekuja kumsaka huyu kirusi wa matukio haya", alijibu kijana wa pili, mtu wa tatu akaongeza kusema "Ya ngoswe tumuachie ngoswe na kwa jinsi ninavyo mfahamu huyu mzee ukweli lazima atajulikana tu huyu mtu aliyeanziasha zahma la kuchoma nyumba hovyo hovyo", yote hayo yalikuwa ni mazungumzo kilingini. Upande wa pili napo zogo baina ya mwenyekiti na mgeni wake liliendelea. Mwenyekiti alikuwa akimpa habari namna kijiji kinavyo karibia kuwa jangwa na hata mfanyaji wa matukio hayo asijulikane. Mzee Baluguza alihuzunika sana hasa familia ile ya watu saba iliyokufa kwa pamoja, kwa kinywa chake akamthibitishia Mwenyekiti kuwa mtu huyo atajulikana, na atathubutu kumpoteza sehemu isiyojulikana. Mwenyekiti alifurahi sana kusikia maneno hayo, na punde mbele yao alionekana Zabroni. Mzee Baluguza alisita kidogo baada kumuona, alistuka wakati huo mwili wake ukimsisimka. Mwishowe alitikisa kichwa ishara ya kukubali jambo fulani, akaishusha pumzi ndefu kisha ndani ya moyo wake akajisemea "Naam! Kazi imekwisha"



http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Kwisha kujisemea maneno hayo aliachia tabasamu bashasha huku akimsindikiza kwa macho Zabroni kitendo ambacho kilipelekea mwenyekiti kuingiwa na hofu akajiuliza maswali mengi ambayo aliyakosa majibu yake,ilihali upande wa pili Zabroni o naye aligeuka kumtazama mzee Baluguza ambaye kwa macho yake ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kumuona. Alistuka baada macho yake kugongana na macho ya mzee Baluguza ila hakujali zaidi aliendelea na safari yake kama alivyofanya mzee Baluguza.

"Huyu ni nani?..", ndani ya kichwa chake Zabroni alijiuliza. Upande wa pili mwenyekiti alimkalibisha nyumbani mzee Baluguza kwa furaha huku akimpa tumaini kwamba ajisikie yupo nyumbanin,Baluguza akakaribia kwa bashasha ya hali ya juu. Baada ya maongezi mawili matatu,mwenyekiti akazipiga hatua kuelekea nyumbani kwa mzee Ngurumo ambaye ndio balozi wa nyumba kumi. Alimkuta. Akamwambia nia na dhumuni ya ujio huo,mzee Ngurumo alimuelewa vema tena akampongeza kwa hatua aliyochukuwa ya kumleta mzee Baluguza mganga mashuhuli aliyefamika kwa huduma yake maridadi isiyokuwa na utapeli.

"Ama kweli wananchi waliokuchagua hakika hawakukosea,kiukwe hili ni tatizo tena sugu. Tusipo chukuwa hatua mapema tutajikuta tukipoteza mpaka familia zetu", aliongea mzee Ngurumo huku akifunga mlango wa nyumba yake. Mwenyekiti alikaa kimya kidogo kisha akajibu "Ni kweli ,si unajua tusipo ziba ufa tutajenga ukuta? .."

"Kabisa ndugu mwenyekiti"

"Basi hima twende tukazungumze naye tujue hili tatizo atalikomesha vipi" aliongeza kusema mwenyekiti wakati huo tayari wameshatoka nyumbani hapo kwa mzee Ngurumo na sasa walionekana kuanza safari kurudi nyumbani kwa mwenyekiti. Ila kabla hawajafika,Ngurumo akatoa wazo akasema "Unaonaje tukamuone na mzee Fungafunga? Maana hili suala kama linamuhusu na yeye?.."

"Sawa hakuna shida twende ingawa sidhani kama atakuwa karudi kutoka shamba,nasikia ngedere wanasumbua sana shambani. Wami unamsumbua sana"alijibu mwenyekiti.

"Loh. Nikweli lakini tukajaribu"

"Sawa twende"

Mwenyekiti na mzee Ngurumo walielekea kwa mzee Fungafunga, bahati nzuri walimkuta akiwa tayari ametoka shamba alionekana kuchoka sana.

"Hodi! Hodi! Bwana Fungafunga " Ngurumo alisema.

"Anhaa KARIBU bwana,karibu sana. Mama Tina leta vigoda haraka", alijibu mzee Fungafunga kwa tabasamu bashasha ,na punde si punde Mama Tina alileta vigoda. Mzee Ngurumo na mwenyekiti wakapata kuketi kisha soga zikaendelea.

"Naam! mzee mwenzangu,pole sana nasikia ngedere wanamsumbua sana huko", aliongea mzee Ngurumo. Wakati mzee Fungafunga akajitayarisha kumjibu Ngurumo. Upande wa pili kijana Zabroni alionekana kasimama kando kando ya nyumba,alitazama kulia na kushoto hakuona mtu. Giza tayari lilikuwa limeanza kutanda kwa maana hiyo kijiji kilianza kupoa zaidi zilisikika kelele za vijana wa kijiji kijiweni wakibishana mambo mbali mbali,gumzo ilikuwa ni ujio wa mzee Baluguza kijijini hapo. Wapo waliombenza kwamba mzee huyo si chochote si lolote,lakini pia wapo walimnadi ya kwamba huyo mzee ni moto wa kuotea mbali. Hivyo hali hiyo ndiyo iliyoweza kuleta ubishi katika kijiji hicho eneo la kijiweni. Kelele zilipasa kila kona hakuna aliyegusia masuala ya siasa abadani bali wote waliongelea ujio wa Baluguza. Lakini pindi mada hiyo ikiwa imepamba moto, mara ghafla ulionekana mwanga mkali angani ulio ambatana na moshi. Kwa maana hiyo tayari nyumba ya mtu ilikuwa inateketea kwa moto mapema tu saa moja usiku. Taharuki ilizuka, soga la kumnadi mzee Baluguza upesi zilikatishwa ,hima wakakimbia kuelekea kule kunako fuka moshi na moto. Pindi vijana hao walipokuwa wakielekea huko,upande wa pili nyumbani kwa mwenyekiti walionekana mzee Ngurumo,mzee Fungafunga pamoja na mwenyekiti wa kijiji bila kusahau mzee Baluguza. Nao walikuwa wakijadili namna gani ya malipo yatakavyo fanyika pindi mzee Baluguza atakapo kamilisha kazi iliyo mleta, ila makubaliano hayo yaliingia dosari baada mama Tina kupasa sauti ya mayowe alipoona moshi mkali ulioambatana na kipupwe cha moto. "Unaona sasa?..mapema tu leo" alisema mzee Ngurumo huku akinyoosha kidole kule ilipokuwa nyumba inateketea.

"Nadhani hapo mzee mwenzangu utakuwa umeamini kuwa hata zile nyumba za awali sio mimi niliyezichoma moto", alidakia mzee Fungafunga akijitetea mbele ya mwenyekiti ambaye hapo awali baada kuchomwa nyumba tano,Mwenyekiti alimuhisi yeye kwamba ndiyo muhusika kwani aliwahi kung'atwa sikio na mzee huyo kuwa yeye ndiyo aliyechoma nyumba ya mzee Ndalo baba yake Zabroni kwahiyo Mwenyekiti akawa hana imani na mzee Fungafunga lakini siku hiyo alimuamini baada kuona nyumba ikiteketea kwa moto. Wazee hao waliazipiga hatua kuelekea kwenye ajali hiyo,walipo fika waliwakuta vijana wakishughulika kuuzima moto lakini hawakuweza kufanikiwa. Nyumba iliungua yote huku ndani akiwemo mzee Kadili mchongaji nguli wa mipini kijijini hapo,mzee ambaye aliishi yeye peke yake, hakuwa na familiahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Kwa mara nyingine tena yanatokea majonzi kijiji hapo,kila mwanakijiji roho juu ilihali huzuni nayo ikitawala mioyoni mwao. Walihofia usalama katika kijiji chao, lakini wakati wanakijiji hao wakiwa katika hali hiyo,mara ghafla mzee Baluguza akamuita kando mwenyekiti kisha akasema "Hivi yule kijana tuliyepishana mude ule yupo hapa? ", Mwenyekiti hakujibu upesi, alikaa kimya huku akijaribu kumkumbuka. Akamkumbuka na ndipo alipo tazama upande ule waliosimama vijana wengi akamuita mmoja wao, naye alitii wito wa mwenyekiti "Zabroni yupo hapa? ..", kijana huyo aliyetii wito wa mwenyekiti aliulizwa.

"Hapana ", alijibu kijana huyo,jibu hilo alilisikia na Mzee Baluguza.Akalizika nalo akatikisa kichwa halafu akamuuliza tena Mwenyekiti "Unapajua anapoishi?..", lakini kabla Mwenyekiti hajamjibu Baluguza, ghafla ilionekana mwanga mkali angani na moshi mwingi. Kiashiria hicho kilimanisha kuwa tayari kuna nyumba nyingine inateketea,Mwenyekiti aligeuka akatazama kule akaona mwanga ule unatokea mahali ilipo nyumba yake. "Lahaulla nyumba yangu", alitaharuki mwenyekiti huku akiweka mikono kichwani alijua fika nyumba yake inateketea. Haraka sana vijana wa kijiji wakajigawa magundi mawili, kundi moja liliendelea kuuzima moto kwenye nyumba hiyo inayoteketea, na kundi lingine lilielekea kule inapoungua nyumba nyingine ambayo mwenyekiti aliamini kuwa ni nyumba yake. Mzee Baluguza aliposikia maneno ya mwenyeji wake ambaye ni Mwenyekiti, haraka sana akapotea eneo hilo akaibukia nyumbani kwa Mwenyekiti. Alikuta nyumba ya mwenyekiti ipo salama, ila nyumba nyumba ya jirani yake ndiyo iliyoonekana ikiteketea. Mzee Baluguza akastaajabu kumuona mchomaji akiendelea kufyatua njiti. Mtu huyo hakuwa mwingine ni Zabroni ambaye baada kuchoma nyumba hiyo aliamua kujibadilisha umbile lake akachukuwa umbile la mzee Ngurumo. Hivyo alipokuwa katika umbile hilo la mzee aliendelea kufyatua njiti kuchochea moto wakati mzee Baluguza akimtazama mara mbili mbili mwishowe akakumbuka mtu huyo kamuacha kule alipotoka, aliingiwa na hofu akaona ni mchezo mchafu anachezewa. Aliguna kisha akajisemea "Nimekupata ila siku zako zinahesabika nitakukomsha"., maneno hayo mzee Baluguza alijisemea ndani ya moyo wake huku Zabroni naye akiwa na umbile la mzee Ngurumo alionekana kuishia zake kwenye giza totoro akiacha nyumba ikiteketea vile vile akimuacha mzee Baluguza akiishia kumsindikiza kwa macho tu wakati huo akifahamu fika kijana huyo anauwezo wa ajabu sana. Na pindi Zabroni alipokuwa njiani akitembea kwa kujiamini katika umbile la mzee Ngurumo, mbele yake walionekana wazee wa wawili wakitembea kuelekea kule anakotokea yeye wazee hao ni mwenyekiti wa kijiji sambamba na mzee Ngurumo mwenyewe!





Lakini kabla kijana Zabroni hajawafikia wazee hao,machale yalimcheza. Bila kuchelewa alijibadilisha akawa katika sura yake ya kawaida kisha akapotea maeneo hayo ambapo mzee Ngurumo na mwenyekiti walipo fika eneo lile alilopotelea Zabroni kamwe hawakuweza kumuona,zaidi walijikuta wakihisi joto ambalo nalo hawakuweza kulitilia maanani kwani walikuwa na haraka za kwenda kutazama nyumba ya nani inaungua. Mwenyekiti alipo kuta nyumba yake ipo salama alifurahi sana lakini pia hakusita kutoa pole kwa jirani yake aliyechomewa nyumba,wakati huo huo mzee Baluguza naye alionekana kuinamisha uso wake chini akitafakari jambo fulani. Lakini punde si punde mzee huyo alitoka kwenye dimbwi la tafakari baada kuguswa bega na mwenyekiti,Baluguza aligeuka akakutana na uso wa Mwenyekiti. "Kulikoni mwenzetu naona umetukimbia kimaajabu" Alisema Mwenyekiti akimwambia mzee Baluguza, kwa sauti ya unyonge huku akiutazama ule moto unaolanda kwenye nyumba alisema "Hii ni kawaida yangu mzee mwenzangu,naona hakuna muda wa kupoteza. Kesho naomba uitishe mkutano wa kijiji ili nimuumbue mbaya wenu " alisema mzee Baluguza.

Kesho yake palipo pambazuka mbiyu ya kijiji ililia, taarifa zikagonga masikioni mwa wanakijiji kwamba kutakuwa na mkutano wa wakijiji siku hiyo. Hivyo haitakiwa mwanakijiji yeyote akose kuhudhulia. Mbiyu hiyo aliisikia na kijana Zabroni ,akiwa kitandani kwake. Akajiuliza "Wanamikakati gani mbweha hawa?..ni lazima na mimi nihudhulie ili nijue wanamikakati gani ",alisema Zabroni huku akisimama kutoka kwenye kitanda chake,alichukuwa bukta yake iliyokuwa imekatwa miguu kwa kuzidiana kisha akaelekea mahili yalipo makaburi ya wazazi wake. Hapo Zabroni alienda kwa niaba ya kuyasafisha kabla muda wa mkutano haujawadia, na pindi kijana huyo akifanya hicho kitendo upande wa pili kijiji kilionekana kuzizima majonzi. Wanakijiji walikuwa wakisikitika kuwapoteza wanakijiji wenzao waliokufa usiku wa jana kwa ajari ya moto,hali hiyo ikawafanya kuwa na shauku kila mmoja kufika mkutano ni. Hali hiyo ilimpelekea mazishi kufanyika mapema sana ili watu wawahi,haikuwepo haja tena ya kukaa msibani mpaka jioni kwani hali iliyokuwepo sasa ilitisha kila familia haikuwa na amani nyumbani kwake,wazee kwa vijana wote walianza kuogopa. Hivyo siku hiyo waliposikia mbiyu wakaamini kuwa huwenda mbiyu hiyo ikawa na jambo la heri katika kijiji chao.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Na hatimae Muda uliwadia sasa,watu walianza kukusanyika mkutanoni. Kwa muda wa nusu saa wanakijiji wote walikuwa wamefika ingawa si wote kwani kuna baadhi walikuwa bado wanajiandaa kuanza safari,ilihari wengine tayari walikuwa wameanza. Vile vile Upande mwingine Zabron naye alianza safari ya kujongea kwenye mkutano huo,nia na madhumuni kutaka kusikiliza mikakati gani inayo endelea kijiji hapo. Na wakati Zabroni alipokuwa akitembea njiani,Ghafla mbele yake akaona kamba. Alipoiona kamba hiyo akajipapasa kwenye mfuko wa bukta yake akakuta kibiriti. Aliachia tabasamu baada kujihakikishia kwamba kibiriti anacho upesi akaichukuwa kamba hiyo akaenda nayo mpaka kwenye nyumba moja ambayo ya mzee Ngurumo. Alipo fika hapo alitazana kulia na kushoto kuangalia usalama wake akagundua hakuna mtu yoyote mahali hapo. Pasipo kupoteza muda aliifunga kamba kwenye fito ya nyumba kisha akailaza hatua mbili za mtu mzima kutoka mahali ilipo nyumba. Kwa mara nyingine tena akarudia kutazama kila pande, alitazama kulia na kushoto pia nyuma yake hakuona mtu,haraka sana akachukuwa nyasi kavu akizisambaza kidogo juu ya kamba ile kisha akafyatua njiti, nayo ikaripua moto akaishusha kwenye zile nyasi nazo zikanasa moto ambao pole pole ulitembea kwenye ile kamba ya kitambaa. Kamba ambayo pia ilikuwa pana na ndefu kwa kiasi chake. "Mchezo umekwisha", alijisemea ndani ya nafsi kisha akaondoka kuelekea kwenye mkutano wakati huo huo huo mzee Baluguza alionekana kutoka ndani ya nyumba ya Mwenyekiti huku mkononi akiwa na jungu ambalo lilikuwa na makorokoro mengi ndani yake, wanakijiji walitulia kimya mpaka mzee huyo anafika kwenye umati wa wanakijiji. Alipo fika alisimama akitaka kusema jambo,lakini kabla hajasema akamuona Zabroni naye akijisogeza kwenye mkutano. Mzee Baluguza alimkazia macho ila mwishowe akajifanya kupotezea ili mtukutu Zabroni asijishuku. Zabroni alifika mkutanoni akaungana na wenzake alitulia chini akisubiri kujua kipi kinacho taraji kutokea. Muda huo huo Baluguza akamnong'oneza Mwenyekiti, akamwambia "Nenda kanichukulie nyayo za yule kijana"

"Kijana yupi? .."alihoji Mwenyekiti huku akiwa makini kumsikiliza mtalamu Baluguza.

"Kijana yule tuliyepisha naye juzi jioni wakati ulipokuja kunipokea", mwemyekiti alivuta kumbukumbu kwa muda wa sekunde kadhaa mwishowe akakumbuka kuwa mtu mwenyewe ni Zabroni mtoto wa mzee Ndalo. "Sawa nitazijuaje hizo nyayo?..", kwa mara nyingine tena aliuliza Mwenyekiti. Mzee Baluguza alikaa kimya kidogo huku akichukuwa kipande cha kitambaa ambacho kilionekana cheusi kisha akamkabidhi Mwenyekiti halafu akamwambia "Kavaa saganyoka,hivyo ni rahisi sana kuzigundua. Nenda haraka chukua mchanga kudogo hapo alipo kanyaga kisha niletee hapa nimalize kazi", alijibu mzee Baluguza. Mwenyekiti akiwa na wasiwasi kwa kijana Zabroni alifanya kama alivyo ambiwa kisha haraka sana akarudi wakati huo mzee Fungafunga akiwa kama mmoja ya baraza la wazee kwenye mkutano huo yeye alikuwa akiwaongelesha huku mzee Baluguza akifanya yake. Mara baada kumaliza ndipo huyo mzee alipo simama na kisha kusema "Habari zenu wanakijiji, jina langu naitwa Baluguza nadhani wapo wanaonifahamu na wasio nifahamu. Nimekuja hapa kutokomeza hili janga linalo endelea hapa katika kijiji chenu. Haya mauwaji yakinyama, yanatisha lakini leo ndio siku kuu ambayo mtu huyu mshenzi na mjinga atagundurika. ", aliongea kwa kujiamini kabisa Baluguza punde akaendelea kusema." Rafiki yako ndio huyo huyo adui yako, kwa maana hiyo basi kikulacho kinguoni mwako. Mtu anayefanya vitendo hivi wala hatoki nje ya kijiji hiki ila mpo naye humu humu" alisema Baluguza, akameza mate halafu akaendelea kusema. "Kwa maana hiyo basi leo lazima agundulike huyu mtu anaye uwa watu wasiokuwa na hatia, na akishagundulika ndipo kijiji kitaamua mtu huyu afanywe kitu gani. Je, mpo tayari?.." Sauti za wanakijiji zilipasa zikisema "Tupo tayariiiiii!" Lakini wakati wanakijiji hao wanapasa sauti zao kutaka kumfahamu kirusi wa kijiji mara ghafla ule moto uliokuwa ukitambaa kwenye kamba hatimae ilifika kwenye nyumba,nyumba ya mzee Ngurumo ikaanza kuteketea ikiwa mchomaji yupo hapo hapo kwenye mkutano wakati huo mzee Baluguza akitaraji kumuumbua mchomaji huyo mbele ya wanakijiji.







Moto ule uliokuwa unawaka kwenye nyumba ya mzee Ngurumo uliwastua sana wanakijiji,pia hata mzee Baluguza naye alionyesha kustuka ingawa sio rahisi kutumbua endapo kama ukimtazama usoni kwa pupa. Ngurumo alitaharuki baada kuona nyumba inaungua, alipasa mayowe huku akijing'atua eneo alilokuwa amekaa akitaka kwenda walau kuokoa baadhi ya vitu vilivyokuwemo ndani,lakini kabla hajaondoka,Mwenyekiti alimshika mkono akamvuta karibu yake kisha akasema "Hata ukiondoka hutaweza kuokoa kitu chochote mzee mwenzangu, kwahiyo nakusihi hebu punguza jazba ili leo tumtambue kirusi wa kijiji hiki" alisema Mwenyekiti akimwambia mzee Ngurumo ambaye muda huo alikuwa akilia kilio cha mtu mzima. Mke wake alisimama akilia machozi mithili ya mke aliyefiwa na mumewe,mwanamke huyo akamkumbatia mumewe huku akiangua kilio. Kitendo hicho kilitia simanzi mkutanoni hapo,baadhi ya wakina mama na wakina baba wenye hekima walijaribu kuwatuliza wazee hao,nao kila mmoja alitulia kwa muda wake ingawa mioyoni mwao wakiwa wamefura hasira zisizo na mfano.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Utulivu ulipo tawala,mzee Baluguza akaanza kufanya mambo yake akiwa na nia ya kumuweka hadharani kirusi huyo wa kijiji,kwenye mti mnene kiasi alibandika kitambaa cheupe huku akiimba nyimbo zake za asiri. Alipo maliza aliwaambia wanakijiji wawe makini kukitazama hicho kitambaa umakini na utulivu ukaongezeka kwa wanakijiji hao ilihali kijana Zabroni naye akiwa hajui chochote ila aliamini kuwa huyo mzee hawezi kitu chochote juu yake. Na wakati akijiaminisha hayo ndani ya nafsi yake,Ghafla kwenye kile kitambaa cheupe alionekana Zabroni akiwa anafanya kile kitendo kwenye Nyumba ya mzee Ngurumo. Wanakijiji walitaharuki kila mmoja alionekana kushungaa, ilihari Zabroni naye alijikuta akijishangaa na kujiuliza maswali mengi kichwani mwake juu ya kile kilicho kuwa kikiendelea kwenye kitambaa kile cheupe. Aliingiwa na hofu pasipo kuchelewa alisimama akaanza kunuia maneno yake ili apate kupotea maeneo hayo lakini kabla hajatamka chochote,kundi la wanakijij likaanza kumvagaa na kisha kumpiga. Zabroni alichezea kipigo cha mbwa mwizi ila baadaye kidogo alifanikiwa kupotea katikati ya umati wa watu,ajabu aliwaachia nguo zake tu. Kitendo hicho kiliwastua wanakijiji,hapo sasa kila mmoja akajawa na hofu huku maswali yaliyokosa majibu yakitawala akili mwao. Ni kitendo ambacho kilimshangaza sana mzee Baluguza, alijiuliza uwezo gani alio nao kijana huyo, Na baada kumaliza shughuli hiyo aliona hakuna haja ya kuendelea kukaa kijijini hapo kwani kwa maono yake aliona kamwe hatoweza kufua DAFU kumkabili Zabroni, ili kulinda uhai wake aliamua kufunga safari usiku wa manane kurudi kijijini kwao. "Nayapenda maisha yangu", alijisemea mzee Baluguza ndani ya nafsi yake huku akiandaa vilago vyake. Hatimaye kila kitu kilikaa sawa, na sasa alianza safari wakati anatoka nyumbani hapo kwa Mwenyekiti alipokuwa amefikia,punde si punde Zabroni alitua maeneo hayo. Akiwa na lengo moja tu ambalo ni kutekeleza ahadi yake aliyojiwekea. Pasipo kupoteza muda Zabroni alichukuwa kamba yake akaitambalika kisha akachoma moto. Moto ambao ulianza kutembea pole pole kuelekea kwenye nyumba wakati huo yeye tayari ameshapotea eneo hilo,nia kuu ya kijana Zabroni kuwahi kuchoma moto nyumba ya Mwenyekiti ni kumuuwa mzee Baluguza ili apate kufanya kazi yake kwa uhuru zaidi bila kubuguziwa na mtu yoyote, aliona kama mzee huyo anataka kuharibu mkakati wake.

"Kufa tu hakuna namna mwanaharamu mkubwa wewe", aliongea Zabroni na hata asijue kuwa tayari amechelewa kwani mzee Baluguza alishafungasha vilango vyake na kuondoka zake. Ule moto uliendelea kutembea kwenye kamba ile kwa kasi ya ajabu ila kabla haujanasa kwenye nyasi za nyumba,zilisikika kelele za mbwa wakibweka kwa nguvu kiasi kwamba mkewe Mwenyekikiti ilimfanya aamke na kisha kumwamsha mumewe ili atoke nje akatazame ni nini kinacho endelea huko. Kumbe wakati Zabroni anaondoka nyumbani hapo kwa Mwenyekiti alijibadilisha akawa katika umbo la kutisha liliacha harufu mbaya ambayo iliwafanya mbwa kubweka kuashiria nje kuna kitu cha hatari, Mwenyekiti akamsikiliza mkewe haraka sana akatoka nje ambapo alizunguka nyuma ya nyumba akakuta moto tayari umeshika nyumba. "MOto moto motoooo" alilalama Mwenyekiti usiku ule wa manane, mkewe akiwa ndani akastuka alipotaka kukimbia akajikuta anazima kibatali kilichokuwa kinawaka. Hapo sasa aliukosa mlango wa kutokea kwamaana ndani palikuwa na giza nene,upande wa pili napo Mwenyekiti alikuwa akihaha japo kuuzima kwa mchanga lakini alipoona moto unazidi kukolea alirudi hima upande ulipo mlango ili amuamshe mzee Baluguza pia amtoe ndani mke wake,lakini kabla hajafanya jambo lolote,moto ulifunika nyumba nzima kwani muda ule kulikuwa na upepo mkali uliofanya moto kutambaa kwa kasi zaidi. Mwenyekiti akajikuta anashindwa afanye nini, alibaki amesimama huku mikono akiwa ameweka kichwani pia akilia kilio cha mtu mzima akilitaja jina la mkewe aliyepoteza maisha kwa ajari hiyo ya moto. Baada ya lisaalimoja mwanakijiji mmoja mmoja alijitokeza kwa Mwenyekiti kuja kushuhudia kitu gani kimetokea,walimkuta Mwenyekiti wao akiwa mnyonge asijue cha kuwaambia. Hakika walichoka sana kila moja aliona hakuna haja ya kuendelea kuishi katika hicho kijiji cha mauaji ya kinyama,na hivyo baadhi za familia zilianza kufanya mikakati ya kukikimbia kijiji hicho. Alfajiri mapema mbiyu ililia kwa mara nyingine,mbiyu hiyo ilitangaza maafa yalitokea kwa Mwenyekiti huku mtoa taarifa aliwajuza wanakijiji kuwa Mwenyekiti kafiwa na mke wake usiku wa jana,alienda mbali zaidi na kusema si mke wake bali na mzee Baluguza. Hapo wanakijiji walizidi kuchanganyikiwa kwa taarifa ile "Mmh sio bure huyu mtu atakuwa anakisasi na kijiji hiki ", alisema mzee mmoja mlemavu akiwa ndani ya nyumba yake ya matete asubuhi hiyo baada kusikia hiyo taarifa. Na wakati mpiga mbiyu anaendelea kutangaza taarifa hapo kijiji,mara ghafla akafika eneo lile walilo fanyia mkutano siku iliyopita. Punde alistua mpiga mbiyu huyo baada kuona damu chini ya mti huo ambao waliutumia kumwona mtukutu Zabroni akichoma nyumba ya mzee Ngurumo. Mpiga mbiyu akajiuliza "Damu hii kakamatwa nguruwe pori ama?..", akiwa na wasi wasi alijiuliza hilo swali,tonya la damu likamdondokea kutoka juu ya mti huo. Aliinua uso wake kutazama juu akauona mwili wa mzee Baluguza ukiwa unaning'inia huku damu zikivujia kwenye shingo. Alichinjwa kikatiri mtaalamu Baluguza. Mpiga mbiyu alistuka,mwili ulimsisimka huku akitetemeka kwa hofu, muda huo huo ilisikika sauti ikijirudia mara mbili mbili, ilikuwa sauti ya Zabroni Sauti ya ilisema "Zabroni! Zabroni " sauti hiyo ilimaliza kwa kicheko kizito.



Mpiga mbiyu alipo sikia sauti hiyo alitimua mbio huku akipiga kelele,watu waliokuwa wanaishi jirani na eneo hilo walikurupuka na kutoka nje ili kuja kushuhudia nini hasa kilicho mkuta mpiga mbiyu huyo. Walipigwa na butwaa baada kuuona mwili ukining'inia juu kwenye mti huku damu zikivujia kwenye shingo, walipo mtazama vizuri waligundua kuwa mtu yule ni mzee Baluguza. Walichoka sana,pumzi walishusha,hofu nayo ikiendelea kutanda mioyoni mwao ilihali upande wa pili mpiga mbiyu wa kijiji alikuwa akiendelea kukimbia kuelekea kwa Mwenyekiti,alipo fika akasema "Mwenyekiti,kama kijiji kuchafuka basi hiki kijiji tayari kimechafuka haswaa. Unahabari kama mzee Baluguza kanyongwa kwenye mti ule tunapo fanyia mkutano?.." alisema mpiga mbiyu huku akihema mithiri ya faru aliyekuwa akiukimbia mtutu wa bunduki ili usimzuru. Mwenyekiti pamoja na watu wengine ambao tayari walikuwa wamefika nyumbani hapo kwake kila mmoja alipigwa na butwaa kiaina yake,bila kupoteza muda walinyanyuka wakaenda kushuhudia.

Upande mwingine,asubuhi hiyo na mapema mama Tina ambaye ndio mke wa mzee Fungafunga alimuita binti yake ili aseme naye jambo kabla hajaelekea msibani. "Tina mwanangu"

"Abee mama" Tina aliitikia huku akijikusanya vizuri kutoka kitandani ili aweze kumsikiliza mama yake. Mama Tina aliongeza kusema "Umeamkaje?.."

"Nimeamka salama,shikamoo"

"Malakhabaaa,Tina leo mimi nataka kusema na wewe. Nakumbuka uliwahi kuniambia kuwa unamchumba hapa kijijini, na mchumba mwenyewe ni yule kijana mtukutuku. Si ndio? Hivi Tina,uzuri wako huo unaweza kuolewa na yule kijana ambaye hana hata chembe ya huruma? Tazama mauaji anayo yafanya kwa kuchoma nyumba za watu,wakubwa kwa wadogo wanakufa. Kiukweli mimi kama mama yako sitaki yule kijana awe mkwe wangu ", aliongea mama Tina wakati huo Tina alikuwa amejiinamia. Tina alikaa kimya ila mwishowe akajibu "Sawa mama nimekuelewa lakini tatizo sio mimi bali ni moyo,moyo wangu umempenda Zabroni mama nitafanyaje mimi", jibu la Tina, halikumfurahisha mama yake, ghafla akakunja uso na kisha akamuuliza kwa sauti kali "Kati ya mimi na Zabloni ni nani bora?..", kabla Tina hajamjibu mama yake,Ghafla mlango uligongwa kisha ikasikika sauti ya mzee Fungafunga ikisema "Mama Tina na mwanao hebu njooni hapa mara moja" Tina akavaa nguo haraka haraka akatii wito. "Jamani mnahabari lakini? Mzee Baluguza kauwawa", "We unasema kweli?..", mama Tina pamoja na binti walistuka kusikia taarifa hiyo,punde si punde akamtazama mwanaye kisha akamwambia "Unaona? Haya sasa nambie sisi wazazi wako tunaweza kuwa na mkwe muuwaji kama yule? Loh! Yule sio ameingiliwa na shetani, Zabroni ni shetani"

"Tina..Tina...Tina. yani nikikufuma upo na yule mtu? Hiyo pua kama kinu nitaing'oa pumbafu toka mbele yangu mwanahidhaya mkubwa wewe", alidakia mzee mzee Fungafunga, aliongea kwa sauti kali juu ya suala la binti yake kuwa na mahusiano na kijana Zabroni. Haraka sana Tina akarudi chumbani kwake huku akilia,aliona wazazi wake wanamkosesha amani ya moyo maana kupenda sio mchezo.

Wakati hayo yanajili nyumbani kwa mzee Fungafunga, kwingineko vijana wa kijiji wenye hasira kali walishika siraha mbali mbali kisha wakaelekea nyumbani anapoishi Zabroni,kwa dhumuni la kumuuwa kabisa. Ukweli vijana hao walijitoa muhanga kwani ni rahisi sana mwanamke kuruka tikitaka kuliko kumuuwa mtukutu Zabroni, ila walipofika hawakumkuta zaidi walichoma nyumba huku wakijizatiti kwamba lazima na wao walipe kisasi kwani wamechoka kuwa wanyonge. Jioni Zabroni aliporudi kutoka shamba alistaajabu kuona nyumba yake ikiwa imeteketezwa na moto. Hapo sasa hasira zikampanda zaidi ya! Ilihari baadhi ya wanakijiji walipo gundua kwamba Zabroni kachomewa nyumba haraka sana walihama kijiji kwani waliamini kijana huyo hatomuacha mtu salama abadani. Na wale wasio kuwa na pa kwenda waliomba Mungu tu ili kijana huyo asifanye kitu chochote kibaya,ukweli kijiweni sasa pakawa hapakaliki. Watu waliogopa kulala majumbani mwao,walilala nje kama mateja wa Kariakoo. Yote hayo kuogopa kufia ndani na familia zao,ukweli Zabroni alitishia maisha ya watu yote hayo akifanya ikiwa kama kulipa kisasi juu ya kifo cha wazazi wake waliokufa kwa pamoja wakiuliwa na mzee Fungafunga aliyechoma nyumba huku msibani napo wakijitokeza wanakijiji wachache,wengi hawakujitokeza kwa madai kwamba wazazi wake hawana utu wala ushirikiano na wanakijiji wenzake. Uzushi huo ulitokea baada mmoja wa mwanakijiji kunyimwa kibarua cha kulima na mzee Ndalo. Baba yake Zabroni. Kwani marehemu mzee Ndalo alikuwa na mashamba mengi ila ilikuwa nadra kutoa vibarua kwa walima kwa mikono,aliingiza Trekta lakini baada mkewe kuugua ugonjwa wa kupooza alijikuta akifirisika kila leo,akihangaika huku na kule kutafuta tiba. Mwishowe aliishiwa kabisa,na ndipo ilimbidi akope fedha ambayo mwishowe ilimghalimu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Mmmh", siku moja aliguna Zabroni, ilikuwa yapata usiku wa saa mbili muda huo alikuwa katika matembezi yake huku akitafuta nyumba ya kuchoma usiku huo,ghafla alisikia bwana mmoja akijinasibu kwa mkewe kwamba yeye ndio shujaa aliyefyatua njiti ya kibiriti kuunguza nyumba ya Zabroni.

"Huwezi amini mke wangu, karibia wote waliogopa ila mimi nikasema hebu nipeni kibiriti hapa. Wakanikabidhi, nami upesi sikutaka kupepesa macho. Nikakiwasha", aliongeza kujisemea maneno hayo tena kwa mbwembwe zote mbele ya mkewe.

"Mmh lakini wewe jiangalie isije kuwa balaa bwana", alijibu mke wa huyo jamaa. Jamaa akajitutumua halafu akaongeza kusema "Hakuna balaa hapa mke wangu,ila naomba kesho uende kwa shangazi nilisha andaa kila kitu,tutaishi huko utajifungua salama kabisa bila hofu yoyote"

"Anhaa sawa! Na namuomba Mungu nizae mtoto wa kike sitaki wa kiume asije akawa kama hili jitu linalo uwa watu hovyo hivyo", alisema mke wa jamaa huy. Jamaa alicheka kidogo kisha akajibu "Haya bwana,kwahiyo kesho asubuhi mapema anza safari. Mimi nitakuja jioni kwa sababu kuna shamba nitaenda kuliuza ili tupate Fedha za kutumia siku mbili tatu hizi"

"Sawa mume wangu nimekuelewa", walipo kwisha kusema hayo mke na mume walirudi ndani kulala,wasijue kuwa ni kosa kubwa walilofanya hawakujua kwamba Zabroni yote waliyoongea alikuwa akiyasikia. Na punde si punde alikatiza eneo hilo huku Moyoni akijisemea "Naam! ukila tambua ipo siku zote na wewe utaliwa.. Ngoja nitakukomesha", kwisha kusema hayo ajabu macho yake yaliwaka kama macho ya simba kisha akapotea ikasalia sauti ya mtoto mchanga akilia ambayo nayo haikudumu ikatoweka. Usiku huo hakuchoma nyumba hata moja,waliolala ndani walifurahi sana kusikia jogoo anawika kwani waliamini tayari pamekucha salama. Alfajiri hiyo mapema mke wa yule jamaa aliyekuwa anajinadi kwa mkewe juu ya kuchoma nyumba ya Zabroni, alianza safari pole pole kwenda kijiji jirani kama walivyopanga yeye na mumewe usiku wa jana ikiwa njia ya kuyakimbia maafa yanayo endelea. Akiwa njiani kwenye giza totoro lililo jichanganya na ukungu kwa mbaali, mwanamke huyo mwenye ujauzito alizipiga hatua pole pole huku akihofia kukutana njiani na mtukutu Zabroni. Katika ya kijiji hicho ambacho Zabroni anafanya mabalaa na kijiji jirani palikuwa na msitu mkubwa ila sio sana,huo msitu kwa mwendo wa miguu inakubidi utatembea saa moja na dakika kumi na tano kuumaliza msitu huo wenye miti mirefu na mifupi, uoto wa asiri nao ukiunakshi vema. Mwanamke huyo alijawa na hofu,alikazana huku kimoyomoyo akimuomba Mungu afike salama. Lakini wakati anatembea,ghafla mbele yake alimuona mtu ni baada kuondoka ungungu ule uliokuwa umetanda,mwanamke huyo alifurahi akakazana zaidi ili kumfikia yule mtu aliyeonekana amebeba kifurushi kidogo mgongoni. Mtu huyo alionekana mzee wa makamo, ndani ya nafsi yake akaamini kuwa ndio wale wale wanao kikimbia kijiji. Upesi akaongeza mwendo ili wawe sambamba katika safari hiyo isiyokuwa na matumaini. Alipo mfikia alimsalimia kisha akasema "Afadhali hapa naweza kuwa na amani"

"Amani gani tena mwanangu?.. ", alihoji mzee huyo huku wakiendelea kutembea.

"Mmh hujui kama kuna muuwaji anakitikisa kijiji?.." Mzee huyo alikaa kimya kidogo kisha akaongeza kusema "Nasikia hivyo ila sijawahi kumuona katika uso macho yangu, we vipi ukimuona utajua kweli? .."

"Ndio kwanini nisimjue? Yani ni kijana mdogo sana huwezi amini lakini mambo yake ni makubwa mno" alijibu.

"Doh! Ila nasikia analipa kisasi, sasa sijui ni kweli? Na hata hivyo jana nimepata habari kwamba amechomewa nyumba.."

"Ni kweli"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Mmh waliochoma kweli ningewajua basi ningewapa mzizi wa kumtia hatiani yule kijana maana nasikia anatumia dawa na ndio maana hakamati", alisema mzee huyo,yule mwanamke aliposikia maneno hayo alihamaki kisha akasema "Kweli? Basi nadhani ningekuwa nipo na mume wangu ungempatia ili amkomeshe. Naye jana alishiriki,tena yeye ndio aliyefyatua njiti kuichoma nyumba yake. Lakini bahati mbaya nimemuacha kijijini kuna mambo anayeweka sawa" Mzee huyo aliposikia maneno hayo alisimama kisha akasema "Basi mimi ndio mhangwa. Naitwa Zabroni Zabroni ", sauti ilijirudia mara mbili mbili,Ghafla alibadilika akageuka Zabroni mwenyewe mtukutu kutoka kwenye hali ya uzee. Yule mwanamke alistuka akaanza kupiga mayowe akiomba masaada,lakini Zabroni hakujali kelele hizo. Macho yake yakabadirika, yakawa kama macho ya nyoka upesi alichomoa kisu kisha akampiga ngumi nzito mwanamke yule, naye hakuteteleka zaidi aliangua chini, akashuka naye akamtumbua tumbo mwanamke huyo mjamzito, akavitoa vijusi mapacha viwili ndani ya tumbo la huyo mwanamke kisha akavitumbua style ya mshikaki,akavining'iniza juu kwenye mti ambao kila mpita njia akipita lazima avione vijusi hivyo,ambavyo ndio kwanza vilikuwa vikikaribia kuwa katika hali ya kuitwa mtoto.. Zabroni baada kufanya kitendo hicho cha kutisha akapotea kwa kishindo kikubwa ambacho kilimpelekea nyasi mbichi kukauka!





ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog