Search This Blog

Friday, November 18, 2022

PAIN OF LOVE - 5

 





    Simulizi : Pain Of Love

    Sehemu Ya Tano (5)





    Waliingia naye Yulietha ndani mara baada ya kusuluhisha tofauti zao na kuanza ukurasa mpya. Baada ya mwaka mmoja Benson na Yulietha walihitimu na kwa kuwa ni raia wa Tanzania walifungasha kila kilichokuwa chao kwa kujiandaa kesho yake kurudi nchini Tanzania. Yulietha alimtaarifu baba yake kupitia simu ya kuwa aje kumpokea kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE, pia hivyo hivyo naye Benson kwa kuwa hana ndugu na alikuwa ni mtoto yatima aliyeokotwa na marehemu mzee Deus Swai na akasomeshwa naye ikabidi apige simu kwa mzee Deus Swai kumtaarifu kuwa anarudi huku asijue kama mlezi amtegemeae hayupo duniani, alipiga lakini hakumpata alizidi kujaribu kupiga simu zaidi ya mara tatu lakini hola!! akaamua kubadilisha maamuzi badala ya kumpigia mlezi wake akaamua kumpigia Coletha. Simu ya Coletha iliita ikapokelewa na Benson akazungumza naye.



    “Coletha,” Benson aliongea kwa kuita mlengwa wake ili athibitishe ni kweli kana kwamba anaongea na Coletha.



    “Niambie, laazizi,” Coletha aliitika kwa huba pana kumthibitishia Benson kuwa yeye ndiye.



    “Leo, narudi unaweza kuja kunipokea?...maana nimempigia baba hapatikani.”



    “Oooh!!!, shit” alijibu Coletha kisha akanyamaza kwa muda akiwa analia.



    “Mbona, unalia?” aliuliza Benson mara baada ya kugundua kuwa Coletha alikuwa analia.



    “Njoo, tutakuja zungumza” alijibu Coletha kwa kifupi kisha akakata simu.



    **********

    “Mambo,” Mathias alimjulia hali Coletha mara baada ya kubumiana njiani.



    “Poa,” Coletha aliitika huku akimalizia kujifuta machozi kwa leso.



    “Nimekuona muda kidogo ukilia tangu ukiwa unaongea na simu...nini shida?.”



    “Hamna shida sana, bali kuna mtu ameitibua tu nafsi yangu” alidanganya Coletha ili hali Mathias asijue kilichokuwa kinamliza.



    “Aaaah, basi sawa...ila una nafasi leo?.”



    “Sina” alijibu Coletha kisha akataka kuondoka ghafla Mathias akashindwa kujizuia akamdaka Coletha mkono wa kuume kisha akaongea kwa uchungu na huzuni.



    “Sawa Coletha najua huna muda wa kunisikiliza wala kuongea nami, lakini leo kwanini usinisikilize maongezi yangu hata kwa sekunde...Coletha nakuomba unielewe kwanini hutaki kunielewa au unaona mimi ni kijana hoehae kijana sina mbele wala nyuma wala sina hadhi ya kuongea nawe, niambie Coletha kama sina hadhi maana kila siku nikufuatapo mwenzangu unanikwepa mimi kwani nanuka harufu ya taka au harufu ya kinyesi” alinung'unika Mathias mbele ya Coletha kwa kutoa shutuma zinazomlenga Coletha.



    Coletha manung'uniko yale yaliyotolewa na Mathias nafsi ikamsuta na huruma ikamtawala ikabidi amkubalie tu siku hiyo Mathias kwenda kuzungumza naye sehemu tulivu kabla hawajaanza safari, Coletha akampigia simu shoga yake Doreen ili amtaarifu kuwa anatoka na Mathias hivyo anaomba arudi nyumbani kumshikia kukaa na mama. Doreen hakuwa na kipingamizi alikubali akaenda kumhudumia mama wa rafiki yake huku Coletha na Mathias walipanga sehemu tulivu ambayo wanaweza kutulia kwaajili ya mazungumzo. Katika kupanga ndipo Coletha akapanga kuwa mazungumzio yao wakazungumzie SERENA HOTEL walikubaliana na wakaongozana hadi kwenye hiyo hoteli.



    **********

    Anitha na Gerald Eduardo waliendelea kupiga soga huku wasijue kama pale hotelini kuna wafuasi wa mzee Panta Guno, walizidi kupiga soga huku wakiwa kwenye hali ya furaha wakiwa kwenye furaha punde wakaingia Coletha na Mathias katika hoteli ile wakatafuta viti vya kukaa wakakaa kisha wakaagiza vinywaji katika meza yao. Coletha alikaa ndani ya masaa kadhaa simu yake ikaita akaangalia anayepiga alipomjua akapokea simu upesi.



    “Laazizi, ushawasili Tanzania?” lilikuwa swali la Coletha akimuuliza Benson huku asijue kama kuwa lile swali kuna neno moja lililomuumiza Mathias.



    “Nishawasili, na sasa nipo airport nakungoja” alijibu Benson.



    “Ningoje, nakuja sasa hivi” alisema Coletha kisha akapiga fundo moja la kinywaji na kukata simu akamuaga Mathias hatimaye akaondoka.



    Alimuacha Mathias peke yake pale hotelini akiwa katika njia panda huku akijifariji moyoni asikiamini kilichotokea. Mathias siku ile alijikatia tamaa aliona siku kama ya mkosi kwake yaani alifikiria kuwa mlimbwende alikubali ofa yake lakini simu tu imemfanya amuache kwenye mataa bila kujali, akiwa ndani ya lindi la mawazo kuhusu Coletha mara ghafla akasikia mzozo kwenye viti vya jirani kuja kupinduka akamuona Anitha akiwa anaongea huku akiwa analia kwa hisia na pembeni ya Anitha akaziona njemba mbili zikitoka nje ya hoteli huku wakiwa wamemshika kijana wa kizungu. Njemba zile Mathias alizikumbuka sana upesi akasogea alipo Anitha ili apate kujua kinachoendelea kufika jirani na Anitha akasalimu kisha akauliza.





    “Anitha, unalia nini?” alishtuka Anitha kumuona Mathias eneo lile kisha akajibu.



    “Sijisikii, vizuri” alidanganya Anitha ili asijue Mathias kilichotokea.



    “Anitha, unanidanganya...wale vijana wametoka hapa sasa hivi na si mara ya kwanza kukufuata mara ya pili hii mara ya kwanza walikufuata LAND MARK HOTEL ukiwa na mimi, unakumbuka?.”



    “Nakumbuka” alijibu Anitha huku akijifuta machozi.



    “Wale vijana nimeona wamemshika mzungu mmoja wakitoka naye nje, yule mzungu nani yako na wale vijana nani zako?” alipeleleza Mathias kwa lengo la kutaka kufahamu.



    “Yule mzungu ni mfanyakazi mwenzetu kazini, na wale vijana ni vijana wa baba.”

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mbona wametoka mkukumkuku na yule kijana, wanampeleka wapi?.”



    “Nahisi wanampeleka, kwa mzee Panta Guno.”



    “Ndiyo, nani?.”



    “Baba, yangu.”



    “Oooh!!!...na yule kijana wa kizungu anaitwa nani?.”



    “Anaitwa, Gerald Eduardo” alishangaa sana Mathias kulisikia lile jina maana si geni kwake alishawahi kutajiwa siku moja akiwa anaongea kwenye simu na Mzee Panta Guno.



    “Sasa yule kijana, anakosa gani maana nimeona akipelekwa msobemsobe kama ugomvi.”



    “Baba anamhisi kuwa, anatoka na mimi kimapenzi.”



    “Kwani, kuna ubaya akiwa boyfriend wako?.”



    “Sioni ubaya, lakini kwa baba ubaya upo.”



    “Kwanini?.”



    “Kwasababu, hataki mtoto wake yoyote kuolewa ughaibuni na wala kuolewa na watu wa ughaibuni.”



    “Kwanini, sasa?.”



    “Aliwahi kunieleza kuwa, nchi za ughaibuni watu wake wana tabia ya ubaguzi wa rangi...hivyo anapiga vita sana mtoto wake akimuona na mtu wa kighaibuni” alieleza Anitha kisha akaomba namba ya simu ya Mathias na mwisho akaondoka mara baada ya mazungumzo mafupi baina yake na Mathias.



    **********

    Mzee Panta Guno alienda kumpokea mwanae na kurudi naye nyumbani kabla hajapumzika hata kidogo akiwa sebuleni na mwanae Yulietha alisikia simu yake mfukoni ikiita akaitoa akaangalia anayepiga kisha akapokea.



    “Eeenh, Dosagon nieleze” alisema Mzee Panta Guno mara tu alipopokea simu ya kijana wake.



    “Mzee, tupo na Gerald Eduardo hapa ndani ya gari tumemfumania akiwa na mwanao katika hoteli ya Serena” aliongea Dosagon huku akisikika kuendesha gari kwa kasi.



    “Mnasemaje?” aliuliza Mzee Panta Guno kana kwamba hajaelewa kinachoongelewa kisha akanyanyuka sebuleni akaelekea kuongelea na simu chumbani ili kumkwepa mwanae asisikie maongezi. Kufika chumbani akaendelea na mazungumzo.



    “Msimpotezee muda, ueni tu” alikazia maneno ya kikatili Mzee Panta Guno.



    “Sio tumlete kwako, kwanza?” aliuliza Dosagon.



    “Sina muda wa kumuona, kwa kuwa ni mkaidi kifo kinamhusu.”



    “Sawa, bosi” wanamaliza mazungumzo tu Mzee Panta Guno na vijana wake.



    Mzee Panta Guno alisikia sauti ya mtoto wake mkubwa Anitha akiongea na mdogo wake sebuleni kwa furaha akajua mwanae tayari kashawasili toka kwenye matembezi yake hivyo akatoka chumbani akarudi sebuleni. Akakuta watoto wake bado wapo kwenye nyuso za furaha mara baada ya kupotezana kwa muda kidogo, sura ya Anitha ikabadilika alikunja ndita na kukasirika mara baada ya kumuona baba yake akitoka chumbani na kuja sebuleni walipo yeye na mdogo wake. Akamtundika swali baba yake kwa ghadhabu.



    “Gerald Eduardo, mmempeleka wapi?” hakujibu swali lile Mzee Panta Guno bali alimshika Anitha mkono na kumuinua watoke nje wakaongee asije akamwaga mchele kwenye kuku wengi na kufanya mdogo wake Yulietha akajua madhambi yake.



    “Unajifanya kuzuga...wewe uliniaga Unaenda wapi?” aliuliza Mzee Panta Guno mara baada ya kutoka na mwanae nje.



    “Nilisema, naenda kwa rafiki yangu” alijibu Anitha huku akimtupia jicho kali baba yake.



    “Wapi?.”



    “Mbezi Beach.”



    “Sasa huko Serena hotel, ndiyo Mbezi Beach?.”



    “Nilienda Mbezi Beach, ndiyo tukachukuana na rafiki yangu na kwenda Serena hotel.”



    “Rafiki mwenyewe, ndiye Gerald Eduardo.”



    “Ndiyo...kwani kuna ubaya?.”



    “Ubaya upo tena mkubwa sana...uoni kama unadharirisha rangi yetu na tamaduni zetu.”



    “Kivipi?.”



    “Nishakueleza kuwa watu wa ughaibuni ni wabinafsi wanadharau rangi yetu na tamaduni zetu pia...nasema hivyo kwa kuwa yalinikuta na nikayaona kwa mama yenu, mama yenu alikuwa ni mtu wa Mexico alikuja Tanzania kikazi hatimaye akakutana nami tukapendana lakini pingamizi lilikuja kwa ndugu zake hawakutaka kabisa ndugu yao aolewe na muafrika wa aina yoyote hiyo ndiyo sababu ya kuachana na mama yako na hiyo mimi ndiyo sababu ya kuwakataza wanangu kuolewa na watu hao” alieleza Mzee Panta Guno.



    **********

    Coletha alienda uwanja wa ndege kumpokea Benson na kurudi naye nyumbani. Nyumbani walimkuta Doreen akiwa muangalizi kwa mgonjwa hali ile ilimshtusha Benson kwa kumkuta Bi Consolatha amepooza alimgeukia Coletha na kumkandamiza swali la papo kwa hapo.



    “Coletha, hali ya mama imeanza lini?.”



    “Yapata, mwaka sasa” alijibu Coletha.



    “Upo, serious?.”



    “Yeah.”



    “Kumbe wee mwanamke hufai, yaani mama yupo hali hii wala hujanijulisha.”



    “Benson, nimeogopa.”



    “Umeogopa, nini?.”



    “Ningekuambia, ningekufanya uchanganyikiwe na masomo ndiyo maana nilinyamaza.”



    “Sasa nimekuelewa...baba naye sijamuona tokea nifike hajarudi kazini?” swali lile lilikuwa gumu kwa Coletha likafanya amwangalie Benson kwa jicho la huzuni na kuangua kilio.



    “Unalia nini sasa, Coletha?” aliuliza Benson mara baada tu ya kuona Coletha analia. Coletha kwikwi ilimshika hakuweza tena kumjibu Benson kutokana na donge la uchungu likipwita kooni.



    “Sasa Coletha nitakuelewa vipi, nijibu basi...baba hajarudi kazini?” alizidi kuuliza Benson apate kujua Mzee Swai alipo.



    Doreen alivunja ukimya mara baada ya kuona shoga yake hatoweza kujibu wala kuongea tena hivyo basi akachukua jukumu la kumsaidia shoga yake kulijibu lile swali alilouliza Benson ili amuondoe Benson kwenye fumbo tata.



    “Benson, mzee Deus Swai amefariki dunia hivyo kwasasa hatunaye tena kashatutangulia kwenye makazi ya milele” jibu lile lilimuumiza sana na lilimnyong'onyesha sana Benson kwa maana Mzee Swai alimchukulia kama baba yake na kama mlezi wake aliyemlea kipindi chote tangu alipomuokota mitaani akiwa kwenye umri mdogo.



    Basi Benson baada ya kujua hayo akagundua kuwa kamtonesha Coletha kidonda kilichopona basi ikamlazimu kumsogelea amfariji, alimfariji mpaka pindi Coletha aliponyamaza alipothibitisha Coletha kanyamaza akaingia chumbani na mabegi yake kisha akajipumzisha kitandani kwa muda. Doreen baada ya kuona mlengwa wake kasharudi aliaga na kuondoka nyuma akimwacha Coletha akiendeleza kumhudumia Bi Consolatha kama kumhudumia kufua nguo zake na kumtayarishia mlo wa usiku, mara baada ya kuondoka shoga yake Coletha akaendelea na majukumu yake akiwa anaendelea na majukumu yake mara paap!! simu yake ikaita kuangalia jina juu ya kioo kidogo akabaki na kizungumkuti kuwa mtu yule anapiga simu ana lengo gani kipindi kile.



    **********

    Mathias aliondoka hotelini na kurudi nyumbani alifungua mlango wake akaingia ndani na akaelekea moja kwa moja kitandani kujibwaga kama furushi la viazi, akiwa bado anautafuta usingizi muda si muda akaingia kwenye lindi la fikra alimfikiria sana Coletha jinsi anavyoumiza hisia zake na kuzitesa.



    “Coletha, nitampata kweli?...lazima nitampata tu iwe isiwe Coletha lazima awe wangu” alijisemea Mathias kwa kujipa moyo na kucheka kwa kujifariji pale kitandani, aliendelea kumkumbuka hadi Anitha kwa maongezi waliyokuwa wanayaongea kwa kipindi kifupi tu kabla hajafika nyumbani na kujilaza kitandani.



    “Sasa yule kijana, anakosa gani maana nimeona akipelekwa msobemsobe kama ugomvi.”



    “Baba anamhisi kuwa, anatoka na mimi kimapenzi.”



    “Kwani, kuna ubaya akiwa boyfriend wako?.”



    “Sioni ubaya, lakini kwa baba ubaya upo.”



    “Kwanini?.”



    “Kwasababu, hataki mtoto wake yoyote kuolewa ughaibuni na wala kuolewa na watu wa ughaibuni.”

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kwanini, sasa?.”



    “Aliwahi kunieleza kuwa, nchi za ughaibuni watu wake wana tabia ya ubaguzi wa rangi...hivyo anapiga vita sana mtoto wake akimuona na mtu wa kighaibuni” alicheka sana Mathias baada ya kukumbuka vyema maongezi ya awali aliyokuwa akiongea naye Anitha.



    Mathias hakuchoka kufikiri kwenye ubongo wake alizidi kuendelea kufikiri taratibu huku akipepewa na kafeni kake ka uzushi kalikotundikwa na msumari juu ya kuta, akaanza na kugugumia kwa kucheka kisha akaingia moja kwa moja fikrani na papo hapo akaanza kunena moyoni.



    “Wazazi wengine bwana, sasa ya nini kumpa mtoto changamoto.”



    “Yaani mtoto uhuru hata hana wa kumchagua ampendaye, akihofia akimchagua ampendaye baba yake anaweka kikwazo.”



    “Eti, mtoto akiolewa ughaibuni kosa, kisa ughaibuni kuna ubaguzi...nani kasema ubaguzi ulikuwa zama hizo za ukoloni sasa hivi ni zama za mamboleo yaani full upendo hakuna kuchaguliwa wala hakuna ubinafsi wa kunyanyapaliwa, eti sijui huyu hana pesa siolewi naye sasa hivi pesa ni gonjwa ukizifuata tu unakalishwa chini unauguza donda” alimaliza kujiwazia Mathias kisha mwishowe kabisa akaongezea mbolea ya tabasamu ili mawazo yake yavunwe bila manung'uniko.



    Punde tu usingizi nao ukachukua chaguo, Mathias alikuja kulala usingizi mzuri usio na dhoruba wala kimbunga na patashika ya misukosuko ya hapa na pale ndani ya ndoto aliuchalaza kweli usingizi hadi usingizi ukachalazika kisawia. Lakini kwa mbali sikio moja likasikia kuitwa akiwa bado yupo usingizini upesi akakurupuka kitandani akanyanyuka akajinyosha viungo na hatua zikaanza kwenda kufungua mlango yamkini apate kumjua anayemuita, alifungua mlango hatimaye mlangoni akamkuta mama mwenye nyumba akiwa kamshikia kiuno na kumchezeshea mguu kwa kuinua kisigino na kuvitingisha vidole kama msutaji wa mtaa.



    **********

    Dosagon na Norman kama walivyopewa oda na bosi wao ya kumuua Gerald Eduardo, basi walimpeleka Gerald Eduardo kwenye pori la Kisukuru lililopo mbali na lililovuma kwa matukio ya kiharifu walimchapa risasi za kichwa nne na punde Gerald Eduardo akatangulia mbele za haki, kisha wao wakatimka kurudi Masaki kutoa ripoti kwa bosi wao kama kazi yake imeenda kama alivyotaka walimkuta bosi wao nje akiwa bado anaongea na mwanae mkubwa faragha. Walimvutia pembeni mzee Panta Guno wapate kuongea naye na kisha mzee Panta Guno akamuamuru Anitha arudi ndani akamchangamshe ndugu yake, Anitha alirudi ndani kiustaarabu huku nje akamwacha baba yake akiongea na vijana wake wa nguvu.



    “Kazi yangu imetendeka, kama nilivyotaraji?” lilikuwa ni swali la Mzee Panta Guno mara baada ya kukaa faragha na vijana wake anaowategemea na anaowaamini kikazi.



    “Kiongozi, kazi yako imetendeka tena bila makosa wala hitilafu zozote,” Norman alijibu kwa kujiamini huku akionyesha tabasamu kwenye kinywa chake.



    “Vizuri sana...kwa kuwa mmetenda kazi hadi roho imependa sasa basi leo jiandaeni twendeni mkoani tukale bata” alisema Mzee Panta Guno.



    “Mkoa gani, kiongozi?,” Dosagon alidakia kwa kuuliza apate kufahamu mkoa watakaoenda.



    “Tunakwenda, Arusha,” Mzee Panta Guno alijibu kisha akaingia ndani na vijana wake.



    Dosagon na mwenzie walimsalimu Yulietha mara baada ya kufika sebuleni kisha wakaingia chumbani nyuma wakimuacha mzee Panta Guno akiongea na wanae kwa kuwaonyesha uso wa upendo na furaha kubwa. Maongezi ya mzee Panta Guno na wanae yalifika tamati saa moja kamili Dosagon na Norman wakatoka chumbani wakiwa wamejiandaa kwa safari wakamhimiza bosi wao akajiandae ili waweze kuanza safari ya kwenda Arusha, mzee Panta Guno alijiandaa kisha akawaaga wanae kuwa anasafiri kidogo ila hatokaa sana atawahi kurudi ili aje kuongea na mwanae Yulietha zaidi, wanae walitoa ruhusa kisha akaanza safari na vijana wake wa ubavu. Usiku ule Anitha na Yulietha baada ya kuachwa na mzee wao na kwa kuwa kila mmoja alikuwa hajisikii kula chakula cha usiku basi kila mmoja akaingia chumbani kwake kwaajili ya kujipumzisha, kabla ya kulala Yulietha akamtafuta mpenzi wake Benson kwa njia ya simu apate kumjulia hali na kumsikia sauti yake tu ndipo alale alipiga simu.



    “Hallow” ilisikika upande wa pili sauti ya Benson ikizungumza kwa sauti ya chini mara baada ya kupokea simu.



    “Hallow...umefika salama?,” Yulietha aliuliza kwa kutaka kujua kwa shauku.



    “Nimefika salama, sijui wewe.”



    “Nami, nimefika salama.”



    “Safi sana, tumshukuru Mungu.”



    “Sanaaa...kesho tunaweza kuonana?.”



    “Hapana...fanya kesho kutwa, kesho nahitaji kupumzika vya kutosha.”



    “Hamna shida, basi usiku mwema,” Yulietha alimtakia Benson usiku mwema kisha akakata simu kwaajili ya kulala sasa mara baada ya kusikia tu sauti ya Benson kwa siku ile.



    **********

    Coletha alipigiwa simu na daktari mkuu wa Muhimbili, bila kuchelewesha muda akapokea ile simu na moja kwa moja akaanza mazungumzo.



    “Daktari, habari yako” alianza kwa salamu Coletha.



    “Salama...mama anaendeleaje?” salamu ilijibiwa na Daktari mkuu kisha akauliza.



    “Hali yake mama, bado haijawa nzuri kabisa yaani.”



    “Sasa imetimia mwaka...unaonaje nikakuacha umpe huduma mama hadi hapo hali yake inaporejea ndiyo urudi kazini.”



    “Yote ni nzuri...lakini si inabidi tutoe taarifa ngazi ya juu ili wajue tujue jinsi gani watanisaidia.”



    “Ni sawa...sasa ngoja kesho niwasiliane nao ili nije kukupa majibu waliyoyapanga.”



    “Sawa...usiku mwema” alimalizia Coletha maongezi ya mwisho kisha akabonyenza kitufe chekundu tayari kwa kukata simu. Na kwa vile alimaliza majukumu yote na usiku uliingia ikabidi akajilaze chumbani kabla hajalala akakamata simu akatuma ujumbe kwa Benson ampendae.



    “Laazizi, umelala?” ujumbe wa Coletha uliingia kwenye simu ya Benson na Benson akauona na kuujibu.



    “Ndiyo, usingizi unaninyemelea mpenzi...vipi wewe bado hujalala tu?.”



    “Nitawezaje kulala, wakati nimpendae naye hajalala.”



    “Nami nilitaka nishangae, yaani mume asilale wewe mke ulale...inapendeza kweli hiyo?.”



    “Haipendezi hata kidogo...vipi kesho una nafasi tutoke?.”



    “Kwako tena laazizi, nafasi ikosekane kwa kipi kwako nafasi zimejaa bwelele ushindwe wewe tu yaani.”



    “Basi kesho nakuomba tutoke mara moja, maana sijatoka nawe muda kipenzi.”



    “Ondoa shaka, nipo kwaajili yako kipenzi” ujumbe ule Coletha hakuujibu kutokana na kupitiwa na usingizi hivyo hata ujumbe unavyoingia hakuwa hata na habari.



    Benson alivyoona ujumbe wake haujajibiwa akajua wazi Coletha amepitiwa na usingizi hivyo naye hakujichosha kutuma ujumbe mwingine bali alianza upya kutafuta usingizi ule aliopata mwanzo baada ya kuongea na Yulietha kwenye simu akaupata.

    Asubuhi na mapema Jimbi la tatu kuwika Coletha akawa kashaamka akamwandalia maji ya kuoga mama yake, alimwandalia na hatimaye akaenda kumuamsha aende kumuogesha alimuogesha maji moto kutokana na mama yake maji ya baridi mwili wake hauruhusu kuoga. Alimwandalia kifungua kinywa mara baada ya kumuogesha na kumvesha vazi baada ya hayo yote akamtafuta Doreen kwa njia ya simu ili aje kukaa na mama yake pindi yeye anapotoka na Benson matembezi, alipewa taarifa Doreen bila kuchelewa aliwasili nyumbani kwa rafiki yake baada ya kuwasili kwa Doreen tu Benson na Coletha walijiandaa na mwishowe wakaanza safari.



    **********

    “Za wewe,” Mathias alitoa salamu mara baada ya kufungua mlango na kukutana na mama mwenye nyumba wake.



    “Salama...mwaka sasa umeingia kodi yangu ya pango unaitoa lini?” swali la mama mwenye nyumba lilifuata mara baada ya kuitika salamu.



    “Nitakulipa mwezi huu wa sita...nivumilie kidogo,” Mathias alisema kinyonge na unyenyekevu wa hali ya juu.



    “Mwezi wa sita utanilipa...lakini bado sijakuelewa utanilipa mwezi wa sita mwanzoni, katikati au mwishoni?,” Mama mwenye nyumba aliuliza ili apate kufahamu siku ya kukabidhiwa pesa yake ya pango.



    “Mwishoni,” Mathias alijikuta akijibu kwa kuropoka bila kufikiria kuwa amemkera mama mwenye nyumba.



    “Unasemaje?...sitaki kusikia eti mwishoni pesa yangu naitaka iwahi kidogo nipate kujikimu mahitaji yangu,” Mama mwenye nyumba alisema kwa ukali mara baada ya kusikia majibu ya ushupavu yaliyotolewa na Mathias.



    “Basi nitajitahidi kukulipa, katikati ya mwezi pesa zako.”



    “Hayo ndiyo maneno, nilipe changu kila mtu afe na chake.”



    “Kuwa na subira mama yangu, naimani mambo yatakaa sawa tu.”



    “Haya...lakini timiza ahadi yako usije ukaniingiza mkenge na kuniacha solemba hiyo siku ikifika.”



    “Usijali,” Mathias alizungumza mara baada ya kumaliza kuongea na mama mwenye nyumba.”





    Alifunga mlango wake na akarudi ndani kujiandaa mara baada ya kupambazuka na kuhakikisha kuwa mama mwenye nyumba kaondoka. Baada ya kujiandaa akafunga mlango akaelekea kuchakalika kazini alichakalika kweli sio utani hadi mishale ya mchana, uvivu ulimkata akashindwa kabisa kunyanyuka kwenda kula aliona ni busara kunyanyua simu yake na kupiga sehemu husika alipiga kwa mama Bonge.



    “Mama, unaweza niagizia chakula?” alizungumza Mathias mara baada ya Mama Bonge kupokea simu na kumsikiliza kwa umakini zaidi.



    “Naweza...unataka chakula gani?” aliuliza mama Bonge mara baada ya kusikiliza haja ya Mathias.



    “Kuna chakula, kipi na kipi?.”



    “Kuna Ugali dona, Wali samaki na Wali nyama.”



    “Leo, si Jumapili hujapika Pilau?.”



    “Nimepika, na limeisha lote.”



    “Aaaah, basi niagizie Wali samaki nile maana nisijivunge.”



    “Sawa...muda si mrefu utaletewa chakula chako subiri kidogo tu” alimalizia kuongea Mama Bonge kisha akacheza na kitufe chekundu kakata simu.



    Mathias anatoka kuongea na mama Bonge kabla hajaweka simu yake chini anaona namba ngeni inapiga akafikiria kwa haraka haraka na hakupata jawabu ndipo akili ikaambatana na mkono ikamtuma kupokea simu ile alipopokea akasikia sauti ya kike ikimuongelesha kwa huba loh! alikuwa ni Anitha toto la Tanga waja leo waondoka leo.



    “Nafikiri, naongea na Mathias.”



    “Hujakosea, ndiyo mwenyewe.”



    “Sasa, kwa kesho tunaweza kuonana?.”



    “Maeneo, gani?.”



    “Africa sana Hotel.”

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Tutaonana.”



    “Nitashukuru...naomba usiniangushe.”



    “Usikonde” alikata simu Mathias kisha akaendelea kuhudumia wateja na huku akisubiri chakula mara baada ya kumalizana maongezi na Anitha.



    **********

    Coletha na Benson walitembelea WATER WORLD kupunga upepo wa bahari na kuzungumza hatma ya pendo lao, waliendelea kula raha za dunia kuanzia alasiri hadi jioni ya saa kumi na mbili kijua taratibu kilikuwa kinaambaa ambaa kinakaribisha usiku wa saa moja kutimia. Kila raha walizimaliza siku hiyo ndipo wakajikongoja kurudi nyumbani wakiwa njiani kwenye taxi simu ya Benson haikuchoka kuita iliita bila Benson kuipokea mpigaji hakuchoka akahamia kwenye ujumbe alituma ujumbe wee karibia kumi lakini Benson akakaza roho hakuzijibu zote, hali ile ilimshangaza Coletha na ilimchukiza sana akabwata kwa sauti ya tetele.



    “Mbona unaipotezea hiyo simu...kulikoni mwenzetu?.”



    “Ukiona hivyo, haina umuhimu” alijibu Benson huku akiangalia pembeni kumkwepa Coletha ili asimgundue uzinzi wake anaofanya na Yulietha.



    “Nani, huyo?” alizidi kuuliza Coletha huku akijitahidi kumkazia macho Benson.



    “Ni mtu, amekosea namba tu ananisumbua kweli.”



    “Akipiga tena, unaweza nipatia simu niongee naye” alishtuka kidogo Benson alihisi Yulietha akipiga tena atamuharibia kila kitu kwa Coletha, aliomba sana Mungu Yulietha asipige tena na kweli maombi yake yalisikilizwa Yulietha hakupiga tena na wala hakutuma ujumbe wa aina yoyote ile hadi walipofika nyumbani salama bila ya mzozo wowote.



    Walimlipa dereva taxi pesa yake akaondoka kisha na wao wakaingia ndani, walimkuta Doreen kapitiwa na usingizi sebuleni kwenye sofa mara baada ya kumhudumia Bi Consolatha na hatimaye kulala, walimuamsha kisha Benson akamsindikiza kwao wakiwa njiani Doreen alishtuka na alishangazwa kuona mkono wa kushoto wa Benson ukishika kiuno chake alisisimka akamtazama kwa dharau kisha akaongea kwa hasira.



    “Unamaanisha, nini?.”



    “Kwani, wee mtoto?...huelewi ninachotaka kutoka kwako.”



    “Nakuheshimu, siwezi fanya ujinga kama huu...na wewe naomba jiheshimu.”



    “Unaniheshimu tuna undugu, mimi na wewe hebu...usiwe mgumu kiasi hicho utajutia baadae kunikosa kijana kama mie.”



    “Acha nijutie..kwanza ushaniboa rudi tu usinisindikize nakwenda mwenyewe.”



    “Shauri yako bahati haiji mara mbili...wenzako wengi wananililia.”



    “Wanaokulilia ni hao hao mazumbu kuku wenye ulimbukeni wa mapenzi...lakini kwangu ushafua dafu hunipati ng'o, mfyooooo” aliongea Doreen kwa kejeli na kumalizia na sonyo kali la kuogopesha kisha akaondoka kwa ghadhabu huku akimwacha Benson akimwangalia hammalizi kwa jinsi mwanamke alivyo na msimamo kama mjasiriamali alivyo na msimamo na biashara yake.



    Benson alichukua maamuzi ya kurudi nyumbani alirudi nyumbani mpole kama Ngamia kwa kumkosa mtoto mlimbwende Doreen mwenye shepu lake na jicho lake, nyumbani alimkuta mpenzi wake Coletha yupo sebuleni akimsubiri siku hiyo walale wote chumba kimoja kwa mawazo ya kumfikiria Doreen alitaka kupita aelekee chumbani kwake akajiegeshe mwili, lakini Coletha alivunja ukimya wa muda mrefu aliokaa peke yake akamuita mwanaume ampendaye Benson aje aketi naye kwenye sofa wazungumze.



    “Muda sana sijalala nawe, unaonaje leo tukalala wote” alisema Coletha mara baada ya Benson kuketi sofani.



    **********

    Ndani ya dakika mfanyakazi wa mama Bonge alileta chakula bandani kwa Mathias, Mathias alikipokea vyema akakilipia pesa chakula kile hatimaye mfanyakazi wa mama Bonge akaondoka mara baada ya Mathias kumaliza kula. Mathias akaendelea kuhudumia wateja hadi muda wa kufunga ofisi alifunga ofisi akarudi nyumbani, Moyo! moyo wa Mathias umependa pasipopendeka alimpemda Coletha hadi homa mawazo chungu mzima yalilandalanda kwenye ubongo yote kwaajili ya msichana mmoja Coletha. Akiwa anarudi nyumbani Mathias mawazo yalihama yalikwenda moja kwa moja kwa Coletha msichana anayeamsha hisia zake kila wakati, mawazo yalimpeleka mbali mno hadi anapigiwa honi na gari lililo nyuma yake na hasikii. Alikuja kushtuka mpaka pale mwenye gari aliposhindwa na uvumilivu na kuamua kumpitia pembeni kwa kasi na kummwagia tope lililomo pembezoni ya barabara ile ya vumbi. Alishtuka Mathias kisha akasema kwa hasira huku sura akifura kumfuria mwenye gari lile aina ya FUSO.



    “Mijitu mingine bwana, barabara lote hili hadi anipitie jirani yangu” alijisemeza.



    “Yaani yote hii kuzaliwa Afrika, ningezaliwa mbele huko kwa Trump huyu mtu nishamchapa risasi” alizidi kujisemeza Mathias huku akijikagua kuona ni jinsi gani alivyochafuliwa na tope na yule dereva Fuso.



    Akiwa bado anatembea kurudi nyumbani na huku akiendelea kunung'unika mara simu ikaiita. Anitha! ndiyo Anitha alipiga na ndiye binti aliyetokea kumpenda Mathias naweza sema hivyo, Mathias kwa vile alichafukwa na yule dereva Fuso alishindwa kupokea simu ile. Ukipenda nako tabu! Anitha hakuchoka kupiga simu aliendelea kupiga huku akijipa matumaini kuwa Mathias labda alilala ndiyo maana anachelewa kupokea simu, angejua kama Mathias hajalala bali alichafukwa kwa muda huo asingezungumza. Mathias alifika nyumbani lakini muda wote simu ya Anitha alikuwa anaikaushia hakupokea hadi alipoingia ndani akajibwaga kitini kisha akabonyeza kitufe cha kijani akapokea simu iliyokuwa muda mrefu ikiita bila mpigaji kukata tamaa, alisikia sauti ya upande wa pili ya Anitha ikinung'unika mara baada ya kupokea simu ile.



    “Mathias, ndiyo nini kutopokea simu.”



    “Samahani, nilikuwa mbali na simu” alitaka radhi na kuongopa Mathias kwaajili ya kumridhisha Anitha asiendelee kunung'unika na kufikiria fikra potofu.



    “Nimekuelewa, ila siku nyingine nakuomba usifanye hivyo tena.”



    “Sawa my...eeenh kuna kitu gani unataka kunieleza.”



    “Nilitaka kukumbusha tu, kuwa kesho usivunje miadi yetu naomba uje.”



    “Usijali, nitafika.”



    “Nitafurahi...nakutakia usiku mwema.”



    “Na wewe, pia” alikata simu Anitha mara baada ya kufika muafaka na Mathias.



    Mathias akanyanyuka kitini akaenda kusafisha mwili alisafisha kisha akarudi ndani kubadili nguo akabadili akajipikia chakula akala alitulia tuli kitini akiwaza na kuwazua mara baada ya kumaliza kula na kutoa vyombo kwenda kuviosha, alipowaza na kuwazua na kuligundua deni analodaiwa na mama mwenye nyumba akaenda kwenye akiba yake ya pesa anayohifadhi kwenye droo yake ya kitanda akazihesabu akakuta hazitoshi, akaziongezea kidogo na zile pesa alizopata leo ofisini kwake zikatimia akaenda kumgongea mama mwenye nyumba amkabidhi pesa zake alimkabidhi mama mwenye nyumba pesa mara baada ya mama mwenye nyumba kufungua mlango na kutoka nje. Mama mwenye nyumba alifurahi na kumshukuru Mathias kwa kumlipa pesa zake kisha akaingia ndani wakati akimuacha Mathias akielekea kwenye chumba chake kwenda kulala alilala na hatimaye kesho yake asubuhi akaikaribisha kwa shamrashamra na pilikapilika za kufagia ndani, kufua nguo na kukunja nguo na kuziweka sandukuni.



    **********

    Benson kabla hajaongea simu ya Coletha ikawa inaita, Coletha alipokea simu yake na kumsikiliza mpigaji yule kwa makini.



    “Rafiki, yangu kuna ubuyu nataka nikupe” sauti ya Doreen ilisikika kwenye simu ikiongea mara baada ya kupokelewa na Coletha.



    “Ubuyu gani, huo?” aliuliza Coletha kwa shauku ya kutaka kumung'unya huo ubuyu.



    “Mbona unaonekana una papara, relax shosti.”



    “Nishatulia, haya nieleze maana mwenzio mdomo unaniwasha nasikia hamu ya kumung'unya huo ubuyu wa shilawadu.”



    “Sasa, ndiyo utulie tuli nikupe vitamini...kwanza hapo hupo na nani?.”



    “Peke yangu.”



    “Unanidanganya, eeenh?...hapo haupo na hawala yako.”



    “Nani?.”



    “Benson,” Coletha anataka kukataa tu kuwa hayupo na Benson, Benson akamuumbua kwa kubanja. Ikabidi isiwe siri alimueleza ukweli shoga yake.



    “Kama upo na Benson, nakuomba nyanyuka uende sehemu ya faragha nikusambazie ubuyu” alisema Doreen mara baada ya kuambiwa na Coletha kuwa yupo na Benson. Coletha alitii agizo alinyanyuka sofani akaelekea msalani kuendelea kuongea na shoga yake.



    “Eeenh, niambie sasa,” Coletha alipenda kuambiwa mara baada ya kufika msalani.



    “Sasa, nisikilize kwa makini.”



    “Mmmh.”



    “Benson hakufai.”



    “Kwanini?.”



    “Ni malaya, Mbwa...yaani ninavyoongea leo hii katoka kunitongoza bila haya,” Coletha alicheka sana mara baada ya kusikia shutuma zinazotolewa kuhusu kipenzi chake. Ghafla alifura akakasirika na kuongea kwa ukali.



    “Yaani, najua kuwa muda wote umeleta ubuyu wenye vitamini kumbe umeniletea ubuyu wenye changa...sasa naona ushanichoka, yaani wewe kweli wa kutaka kunitenganisha na Benson ijapokuwa unafahamu ninavyompenda. Wewe si rafiki mzuri kwangu kuanzia leo naomba tusijuane kamata hamsini zako nami nitakamata zangu,” Coletha mapovu yalimtoka alinung'unika kwa hasira mno.



    “Yamekuwa hayo, best.”



    “Best yako nani...tusizoeane nadhani umenielewa usiponielewa ni kiburi” akakata simu kwa hasira Coletha kisha akatoka msalani akarudi sebuleni kuungana tena na mwanaume ampendaye ambaye ndiye Benson.



    Benson aliporudi Coletha hakuwa na usemi zaidi ya kukubali ombi aliloomba Coletha kabla hajaanza kuongea na simu. Waliongoza chumbani kwa Coletha kwenda kulala pamoja walilala pamoja hadi majogoo, simu ya Benson asubuhi ile ikalia kwa mfululizo tena kwa sauti ya nyikani. Benson akiwa bado ana usingizi akachukua simu iliyokuwa ikiita mfululizo iliyoko pembeni ya mto akanyamazisha akaendelea kulala kivivu, punde tu simu ikalia tena akaachia bonge la sonyo mbele ya Coletha ambaye kwa muda huo alionekana bado kulala.



    **********

    Muda wa mchana Mathias alijiandaa kabla hajaondoka kwenda kuonana na Anitha akakamata simu yake akatafuta namba ya Coletha akamtwangia, simu ya Coletha haikuita sana Coletha akawa kashapokea kwa sauti ya maringo kiasi.



    “Hello” sauti ya Coletha ilisikika ikisema mara baada ya kupokea simu ya Mathias.



    “Samahani...Coletha, unaweza nipa nafasi kidogo ya kunisikiliza?” alitanguliza samahani Mathias ili apate kuongea na mwanamke asiyetambua hisia zake.



    “Bila shaka...zungumza lakini, kuwa shapu kuongea maana sina muda wa kuongea sana.”



    “Nashukuru Coletha...acha nianze na kusema kuwa Coletha wewe ndiye mwanamke uliyeteka hisia zangu na ndiye mwanamke unayeumiza mtima wangu.”



    “Una maanisha nini?...mbona sikuelewi?” alisema Coletha kwa kubeza na kujifanya kutofahamu anachozungumza Mathias.



    “Unaweza usinielewe Coletha kwa kuwa nimeanza mbali sana kuzungumza, ila ngoja nije moja kwa moja kwenye point na lengo langu...Coletha nakupenda sana nahitaji uwe mama wa watoto wangu na...” kabla hajamaliza kuzungumza Mathias akakatishwa kuzungumza na Coletha.



    “Wee, kaka koma tena uishie hapo hapo...yaani kujuana isiwe sababu ya kuongea huo utumbo wako, umenielewa?.”



    “Lakini....”



    “Sio cha lakini, nakuambia hivi sasa kuwa mimi sikupendi na nahitaji kuanzia hivi sasa futa namba zangu...nadhani tumeelewana” alimaliza kusema Coletha kisha akabonya kitufe chekundu huku akimuacha Mathias njia panda asijielewe kwenye pango alilopanga kwa bei chee.



    Mathias siku hiyo aliiona mbaya hata safari aliiona imeingia mdudu akahairisha safari alishinda nyumbani akilala kama mtu aliyebanwa na gonjwa la Ngiri. Hata Anitha alipomtafuta kupitia simu aliona mikono ikitetemeka kupokea simu hakupokea simu ya Anitha hadi ilipowasili saa kumi na moja jioni ndipo akapokea simu ya Anitha mara baada ya Anitha kupiga kwa muda mrefu, alipokea Mathias simu kinyonge na aliongea sauti ya chini kama mwanamke au mwanaume msaliti anayeongea na hawala.



    “Mathias, mbona unaniweka mwenzako nishafika kwenye hoteli ya Africa Sana muda sana nikikungojea wewe tu ufike” alilalama Anitha mara baada ya kupokelewa simu na Mathias.



    “Nisamehe sana Anitha, leo sitoweza kuja” alizungumza Mathias huku akionyesha sura ya huzuni.



    “Kwanini?.”



    “Nahisi, kuumwa sana.”



    “Umeenda hospitali?.”



    “Sijaenda.”



    “Basi nielekeze nyumbani, nije nikupeleke hospitali.”



    “Acha tu, naamini hadi baadae nitakuwa poa tu.”



    “Usijivunge Mathias, nielekeze nije hata kama hutaki kwenda hospitali mimi nitamuita daktari aje hapo nyumbani akutibu na nikusaidie kazi za hapo nyumbani kidogo,” Mathias alijifikiria akaona bora amuelekeze Anitha aje nyumbani kuliko kuendelea kumuweka pale Africa Sana Hotel.



    Anitha aliondoka pale hotelini mara baada ya kuelekezwa na Mathias anapoishi, alifika Mabibo Loyola kwenye shule ya Loyola akasimama kwa muda akampigia Mathias tena amuelekeze vema. Mathias alimuelekeza Anitha kisha Anitha akavuka ng'ambo ya pili na kuingia mitaa ya ndani ndani ilipokuwa shule ya Mabibo Secondary mara baada ya kukata simu. Alifika nyumbani kwa Mathias jioni akamkuta Mathias akiwa chumbani kalala aliingia ndani mara baada ya kufunguliwa mlango alimsabahi Mathias kisha akatoa simu kwenye handbag na kutaka kumpigia daktari simu, akazuiliwa kupiga simu kwa daktari na Mathias akaelezwa asipige kwa kuwa tayari kashapata ahueni Mathias. Basi alitii akupiga simu aliendelea tu kusaidia kazi mbili tatu kisha akaaga anaondoka mara baada ya kumaliza kusaidia kazi na mara baada ya kuona usiku ushaingia, alipanda karandinga lake alilopaki nje kwenye uwanja wa nyumba aliyopanga Mathias kisha akaondoka kurudi mjengoni kwao Masaki.”





    **********

    Siku ya ahadi ya Yulietha na Benson ikatimia, Yulietha akajiandaa kwa kuvaa umini mwekundu na blauzi ya damu ya mzee kisha akajipulizia manukato kadhaa akatoka nje kuanza safari ya kwenda kuonana na Benson katika vyumba vya wageni (Guest) iliyopo Mbezi Beach. Akafika na Benson akafuatia, baada ya kufika wakakodi chumba no.15 kwa muda kwaajili ya faragha, siku hiyo Yulietha akatulia na kujiachia sana akijua Benson ni wake pekee kweli asiyelijua ni sawa na usiku wa giza. Yulietha akaagiza pombe kali aina ya K VANT wapate kunywa na mpenzi wake wakiwamo kwenye maongezi walikunywa kisawa sawa kila mmoja pombe ikamvaa wakalewa chakali hadi Yulietha akashindwa kustili sehemu zake nyeti. Maskini Benson siku hiyo akamtoa usichana wake Yulietha bila kujua wala kutegemea. Asubuhi kulivyopambazuka Yulietha alipogundua kama katolewa usichana akasikitika na kulia sana maana halikuwa lengo lake la kumpa utamu Benson wakati bado hawajaoana akalia mno kwa sauti hadi ikapelekea kumuamsha Benson aliyelala kwa wakati huo.



    “Kuna nini?” aliuliza Benson kwa kujifanya hajui kilichojiri.



    “Usiku, ulinifanya nini?,” Yulietha nae akauliza apate kuthibitisha kama kweli alichokihisi.



    “Unahisi nimekufanya, nini?.”



    “Umenitoa usichana wangu...si ndiyo?.”



    “Ndiyo.”



    “Kwanini sasa, umefanya hivi?.”



    “Nimesubiri sana, bila kupata kila siku nikikuambia unaniambia subiri...sasa uvumilivu ushanishinda nimeona bora nifanye tendo la ndoa bila ridhaa yako.”



    “Wakati, unafanya umetumia kinga?.”



    “Sijatumia...halafu wewe ni mtu wangu sasa nitumie kinga ili iweje, ina maana hatuaminiani?.”



    “Si hivyo Benson, wewe unafikiri nikipata ujauzito mapema hivi nitamueleza nini Mzee Panta Guno?.”



    “Huwezi pata mrembo, nilikuwa muangalifu...acha basi kulia tukaoge tuondoke,” Benson alibembeleza hatimaye Yulietha akanyamaza wakaongozana kwenda kuoga walipomaliza wakajiandaa na kuondoka pale kwenye chumba cha wageni na kurudi nyumbani.



    Yulietha akarudi Masaki akiwa anachechemea na kuugua maumivu akamkuta dada yake akiwa yupo sebuleni akiangalia televisheni. Akajikongoja kwa kuchechemea hadi kwenye sofa akaketi pembezoni na dada yake hakupumzika sana akaitwa na Anitha kwa sauti kidogo mara baada ya kuonekana na Anitha akiwa mbali kifikra.



    “Yulietha mdogo wangu, uko poa?.”



    “Nipo poa.”



    “Sidhani, nahisi unanidanganya mimi nakujua wewe...nakujua ukiwa na furaha hata ukiwa na huzuni.”



    “Kweli dada, nipo poa mbona.”



    “Acha kuongopa Yulietha, mimi nakujua wewe kuliko unavyodhani...hivyo basi naomba uniambie kinachokusumbua na kama hakuna kinachokusumbua, mbona nimekuona unachechemea?.”



    “Kuhusu kuchechemea, nilianguka tu na mguu ukashtuka lakini sikuumia sana” aliongopa Yulietha ili dada yake asigundue kilichomkuta katika nyumba ya wageni. Lakini uongo wake ni bure akashtukiwa na dada yake mara baada Anitha kuona damu ikichuruzika mapajani mwa mdogo wake.



    “Yulietha, umebakwa!!!?” aliuliza Anitha kwa mshangao.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “Kwanini, umeniuliza hivyo?.”



    “Naona damu zinakuchirizika mapajani...au nakosea?,” Mara baada ya kuona kashtukiwa Yulietha ikabidi asimfiche tena dada yake akamueleza Anitha mambo yote aliyofanyiwa na Benson. Hakumficha hata kitu dada yake.



    Benson akafika nyumbani akamkuta Coletha asubuhi ile akiwa nje anafua nguo za mama yake akasalimu kisha akataka kuingia ndani kabla ya kuingia Coletha akamuita kwa sauti ya ukali na jazba.



    **********

    Ndani ya masiku Mzee Panta Guno akawa kasharejea na vijana wake toka safari, wakapokelewa vyema nyumbani na watoto zake na mwisho mishale ya usiku wakajumuika kwa pamoja kupata ulaji. Wakati wakiwa wanakula Yulietha akaonekana kupatwa na hamu ya kichefu chefu akakimbilia msalani kucheua matapishi, akacheua hatimaye akarudi dinning kuendelea na kula lakini safari hii hakuachwa salama na baba yake akatwangwa swali moja liloleta taharuki kwake.



    “Nimesikia unatapika...unaumwa?.”



    “Kwa mbali, nasikia wadudu wananinyevua.”



    “Isiwe ujauzito ukanificha, maana nyie watoto wa kike wa siku hizi mnakuwa wasiri,” Mzee Panta Guno akajisemea.



    “Hakuna baba...,” Kabla hajamaliza kuzungumza Yulietha pale pale akashikwa na kigugumizi akawa anaona maluwe luwe si maluwe luwe kizungu zungu si kizungu zungu na punde akazimia.



    Anitha na baba yake wakamuwahisha hospitali kupata matibabu, japo Anitha anajua kinachomsumbua mdogo wake lakini hakutaka kumueleza baba yake akaacha aje kusikia mwenyewe kwa masikio yake vipimo atakavyotoa daktari kuhusu mziwanda wake, kufika hospitali Anitha akaachwa mapokezi Yulietha, Mzee Panta Guno pamoja na daktari wakaingia wodini kwaajili ya kuanza kuchukua vipimo vya Yulietha. Daktari akachukua vipimo kisha wakaongozana na Mzee Panta Guno ofisini akampatie majibu ya vipimo vya mwanae. Mzee Panta Guno mwili ukapoa hasira zikampamba na zikampanda mara baada ya kusikia mtoto wake ni mjamzito akatoka kwenye ofisi ya daktari kwa jazba bila kupewa ushauri na mtaalamu. Akafika mapokezi akamuamuru mwanae mkubwa aende wodini kumchukua mdogo wake waondoke, muonekano aliokuwa nao Mzee Panta Guno Anitha akaugundua akajua kuwa tayari baba yake kashapata ukweli kuhusu mdogo wake hivyo ikamlazimu aende wodini upesi bahati nzuri anafika wodini anamkuta Yulietha kashazinduka akamchukua na kuondoka naye hadi walipopaki gari lao huko wakamkuta baba yao wakaingia ndani ya gari na kurudi nyumbani. Mzee Panta Guno akafika nyumbani na wanawe akamweka kitako mwanae apate kudadisi ujauzito kapewa na nani katika kubanwa sana Yulietha akamtaja mhusika wa ule ujauzito, Mzee Panta Guno akakasirika sana kusikia jina alilotajiwa na mwanae akataharuki na hakuweza kuamini.



    “Ujauzito, umepewa na Benson Chilangwa?” aliuliza Mzee Panta Guno kwa kutaka kupata uthibitisho.



    “Eeenh...kwani huyu mtu unamfahamu?,” Yulietha akauliza.



    “Namjua fika, kuanzia yeye hadi wazazi wake.”



    “Umemjuaje?.”



    “Baba yake huyu kijana, alikuwa rafiki yangu mkubwa sana...lakini....”



    “Lakini nini, baba?.”



    “Baba yake, tulikorofishana.”



    “Kisa nini?.”



    “Alinidhulumu pesa, wakati tukiwa tunafanya biashara pamoja.”



    “Sasa baba, unataka kusema nini?.”



    “Nataka kusema hivi, huyo kijana achana nae mara moja na huo ujauzito wake katoe upesi.”



    “Haiwezekani baba.”



    “Kivipi?.”



    “Bado nampenda Benson baba, hivyo mimi ni ngumu kumuacha.”



    “Sasa kama unampenda, mimi ndiyo nishaweka kikwazo sitaki nikuone nae huyo kijana...full stop,” Mzee Panta Guno alifoka kwa kufura kisha akaingia chumbani kwake kwa kuvimba kama mnyama Fungo huku nyuma akiwaacha wanae wakijadili kiundani suala lile la ujauzito.



    **********

    Benson akiwa amesimama akatundikwa swali na Coletha lenye utata na kitete kwake akaulizwa aliposogea jirani kuwa siku ya jana alikuwa wapi...Maana siku ya jana hakurudi nyumbani ni nini kilimkuta kikamfanya asirudi nyumbani hakuwa na jibu la swali lile kwani lilikuwa gumu sana kwake kujibika kwa haraka, akajikuna kidogo kichwa na kufikiria jambo la uongo. Kabla hajatamka chochote simu yake ikaita akasogea pembeni apate kupokea simu akapokea akasikia sauti ya Mzee wa makamo ikimpa vitisho.



    “Kijana, achana na binti yangu mapema kabla sijakufanyia kitu mbaya.”



    “Sasa hii ni tamaduni ya wapi...hiyo ndiyo salamu?.”



    “Salamu kwangu, haina nafasi...leo nakupa onyo achana na mwanangu...umeelewa?.”



    “Sijaelewa.... Wazee wengine bwana kama wanga yaani mapema yote mnaleta mikosi tu” aliongea Benson kwa kupuuza kisha akakata simu kwa hasira na kurudi kumsikiliza Coletha.



    Akamsikiliza akamdanganya kuwa alilala kwa rafiki yake mara baada ya kumaliza kusheherekea siku ya kuzaliwa ya rafiki yake na kuchelewa kurudi nyumbani, Coletha akaelewa na akakisikiliza alichoelekezwa hivyo akamuamuru Benson aingie ndani akapate kifungua kinywa alichokiandaa. Kweli bwana Benson akaingia ndani kupata kifungua kinywa alipomaliza akatulia kidogo chakula kishuke, ghafla Benson akiwa ameketi dinning simu yake inaita akapokea baada ya kugundua anayepiga ni Yulietha.



    “Benson, kuna kitu nahitaji nikuambie,” Yulietha aliongea huku akionyesha sura ya kujenga hofu mara baada ya kupokelewa simu.



    “Kitu gani?,” Benson akauliza.



    “Naamini nikikuambia, utafurahi.”



    “Usipindishe maneno, sema nikuelewe.”



    “Benson, kwasasa nina ujauzito wako...punde tu nawe utaitwa baba.”



    “Eti, nini?.”



    “Nina ujauzito, wako.”



    “Malaya wee, nani kakuambia kuwa mimi nataka mtoto umeniona nina dhiki ya watoto mie” aliongea Benson kwa kejeli.



    “Mbona sikuelewi Benson...are you serious?.”



    “Ndiyo nishakuambia, sina shida na mtoto kama una shida na mtoto ni wewe mie sina haja na huyo kibwengo utakayejifungua.”



    “Benson, najua huo ni utani wako hebu...acha huo utani.”



    “Utani kivipi?...mimi sina utani na wewe na kwanza nahisi unataka kunibambika tu tafuta baba wa huyo mtoto mimi sihusiki kabisa na huyo mtoto.”



    “Benson, unazungumza nini wewe?...kule kwenye vyumba vya wageni ulivyofanya tendo la ndoa bila idhini yangu umesahau eenh?.”



    “Itakuwa umenilanda, sio mimi niliofanya upuuzi na mwanamke asiyejitambua kama wewe...sorry,” Benson akakata simu mara baada ya kukatisha mazungumzo yake na Ex wake.



    Alipokata simu akaiweka simu mfukoni kisha akatoa vyombo na kuingia chumbani kulala. Coletha akamaliza kufua nguo akataka kuingia ndani tu akasikia anaitwa akageuka kuangalia anayemuita akakunja ndita alipokutana na sura ya Doreen akimuita akiwa na Mathias, akahairisha kuingia ndani akarudi kwa jazba kwenda kuwasikiliza kuwa walikuwa wanashida gani.



    “Mmefuata nini?” lilikuwa swali lenye ukali lililotoka kwenye kinywa cha Coletha.



    “Nisamehe kama nimekosea...lakini nimekuja hapa kumleta Mathias aliniomba nimlete ila kwa kuwa hutaki kutuona ningeomba mimi niondoke ila nimuache Mathias umsikilize,” Doreen alijibu kwa mapana hatimaye akaondoka akamuacha Mathias akiwa na Coletha pale nje. Coletha walipoachwa wenyewe akamsogelea Mathias karibu halafu akauliza kwa kebehi iliyoshiba na inayoleta chukizo.



    “Inaelekea wewe, si muelewa...nilikuambiaje kwenye simu?.”



    “Lakini...mie siwezi kuishi bila wewe Coletha ndiyo maana nazidi kukusumbua nitakomaje sasa.”



    “Sasa naona wewe mwanaume, kwa mdomo hatuelewani ngoja nifanye vitendo nahisi utanielewa,” Coletha alizungumza na kupaza sauti kumuita Benson ambaye muda wote hakulala alikuwa ndani akisikiliza malumbano tu yanayoendelea nje.



    “Mpenzi, kuna shida gani?,” Benson aliuliza kwa kujifanya kuonyesha kutotambua chochote mara baada ya kufika alipoitwa.



    “Si, huyu chizi yaani msumbufu kama nini sijui yupoje,” Coletha alijibu kwa kumdharau Mathias kwa kumuita jina kituko na kujaribu kumuelewesha kipenzi chake.



    “Msumbufu kivipi?.”



    “Yaani mtu, unamwambia sikupendi lakini bado anakung'ang'ania kama ruba...sijui yupoje huyu mtu?.”



    “Eti!!!, kijana ni kweli yasemwayo?,” Baada ya kusikia hayo Benson akamkazia macho Mathias kisha akauliza kwa makini apate kujua na kutambua.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mathias akajibu kuwa ni kweli asemayo huyo binti hakuna alichokosea ni ukweli mtupu, kweli kabisa nampenda Coletha niko radhi nife kwaajili yake. Akafurahi mno kwa dharau Benson mara baada ya kumsikia Mathias akijinadi kuwa Coletha ni mwanamke ampendaye, ghafla sura ya Benson ikabadilika macho akayatoa kwa hasira akamkaribia Mathias akakunja shati lake la mikono mirefu akampa konde zito Mathias mara baada tu ya kusikia kuwa anataka kupokonywa tonge mdomoni. Mathias alikwenda chini kabla ya kuinuka Benson akaangalia huku na huku akaona chini kuna fimbo nene yenye miiba akaokota kwaajili ya kumchalaza na kumfundisha heshima Mathias, akamchalaza kila maeneo tani yake bila ya kuwa na roho ya huruma wakati akiwa bado yupo chini Mathias akiugulia. Kwa makusudi Benson akanyanyua fimbo yake na kuitua kichwani mwa Mathias papo hapo kutokana na kupigwa kwa nguvu kichwani Mathias akazimia na ndani ya lisaa akazinduka lakini baada ya kuzinduka akawa mwendawazimu kutokana na matatizo ya kwenye mfumo wa fahamu aliyoyapata pindi aliposhambuliwa vibaya alipokuwa akiadhibiwa na Benson.



    “Utanisamehe sana Mathias, mimi sikupendi, sikuhitaji, nakuchukia sana na mimi ndiye mwanamke mwenye msimamo...ama kweli wewe kijana mpumbavu katika mapenzi,” Coletha alijisemeza moyoni mara baada ya kumuona Mathias amepata uchizi kwasababu yake.



    **********

    Maneno ya shombo ya Benson yakamfanya Yulietha achukue maamuzi magumu sana ambayo yaliyomsababishia matatizo makubwa katika maisha, akachukua maamuzi ya kutoa ujauzito na kwa bahati mbaya tunaweza sema kuwa Mungu hakupenda tendo la kutoa ujauzito kwa Yulietha hivyo alivyofanya vile Yulietha akajipa passport atangulie. Mungu alimpenda sana Yulietha kuliko familia yake basi kutoa ujauzito ndiyo kukamsababishia akapumzike kwenye makazi ya milele ambako huko hakuna shuruba kama za duniani. Yulietha akahifadhiwa kwenye jokofu mochwari mara baada ya kuaga dunia ndani ya masaa kadhaa wanandugu walikwenda kuchukua maiti ya ndugu yao mochwari waende kuzika, wakazika na hatimaye wakatawanyika kurudi nyumbani. Mzee Panta Guno akakijua chanzo cha mwanae kutoa ujauzito na kupelekea kufariki mara baada ya kuambiwa na mwanae pindi ya uhai wake, akajenga chuki kwa Benson akiamini ndiye chanzo cha mwanae kufariki roho yake ikajaa kisasi cha kumuondoa duniani Benson kama mwanae alivyoondoka. Dosagon na Norman wakaagizwa mara moja kufanya tukio la mauaji na bosi wao wakaelekezwa na Mzee Panta Guno Benson anapopatikana, wakafika katika hilo eneo wakaongoza kukaribia nyumbani mwa kina Coletha mara baada ya gari yao kuliacha kilometa kadhaa kutoka ilipo nyumba. Wakafika eneo husika na kuingia mpaka ndani bila kubisha hodi wakawakuta wenyeji wakidalizi na kusafisha macho sebuleni kwa kutazama runinga.



    “Naamini, wewe ndiye Benson...si ndiyo?,” Dosagon aliuliza huku akimkazia macho Benson kwa hasira mara baada ya kuingia ndani.



    “Ndiyo, mwenyewe,” Benson alijibu kwa kujiamini akijua vijana wamekuja kwa lengo zuri.



    “Okay, sasa unamjua mwanamke mmoja anaitwa Yulietha?.”



    “Simfahamu,” Benson akaongopa.



    “Kweli?.”



    “Yaah,” Ghafla Norman akavikwa na roho ya ukatili mara baada ya kugundua kuwa wanaongopewa.



    Sura yote ikabadilika ikawa na makunyanzi kutokana na kukunja ndita pia kutokana na hasira, akazidi kumsogelea Benson akamuangalia kwa jicho la kumkazia kisha akamtundika swali kuwa kwanini anajifanya kuwadanganya lakini Benson hakuelewa akazidi kung'ang'ania kuwa Yulietha hamfahamu. Norman akachoka tena kumbembeleza akaona ambembeleze na vitendo akamuuliza tena lakini Benson kabla hajadanganya tena akatundikwa gumi la shavu, Benson kwa kuona kadhalilishwa mbele ya mwanamke Coletha hakukubali akaelekea kabatini akachukua kisu aje kumchoma Norman ile anataka kumchoma kisu Norman kile kisu akawahi kukiona Dosagon haraka akachomoa bunduki kiunoni na akamshuti risasi mbili za dabodabo Benson, palepale Benson akaaga dunia baada ya kufanya mauaji Dosagon na mwenzake wakataka kuondoka lakini kabla hawajafika nje tu wakasikia Coletha akipiga simu kituo cha polisi. Kwa kupoteza ushahidi ikabidi warudi waje kumuondoa uhai Coletha, Norman akaingiza mkono wake kwenye mfuko wa koti jekundu akatoa grops nyekundu akavaa mikononi akakifuata kisu kilichopo chini kilichotolewa kabatini akaenda kumchoma nacho Coletha shingoni na Coletha kufariki palepale kisha wakaondoka huku nyuma wakimuacha Bi. Consolatha aliye sofani muda wote ajiwezi akiwa ameshuhudia mauaji yote yaliyotendeka, Bi. Consolatha mapigo ya moyo yakamuenda mbio asijue cha kufanya, presha ikatawala mwilini mwake kwaajili ya kuhofia kifo. Taharuki ikamjaa kinywani mwake pamoja na kigugumizi mara baada ya kuona mauaji ya kutisha, mshtuko ukatokea kwa Bi. Consolatha na kwa kuwa hakuzoea kushuhudia mauaji kama yale mshtuko huo ukampelekea na yeye kupoteza maisha.



    **********

    Mauaji ya Gerald Eduardo, Benson na Coletha yakasikika katika kituo cha polisi cha Kigogo. Polisi wakapeleleza wakagundua kuwa anayehusika na mauaji hayo ni mfanyabiashara mkubwa Mzee Panta Guno na vijana wake, hivyo wakaenda moja kwa moja kumkamata kingunge mwenye wadhifa mkubwa katika nchi huko nyumbani kwake Masaki. Maafisa wakafika pahala husika na wakamkuta Mzee Panta Guno na vijana wake pamoja na bintiye Anitha wakitazama runinga, wakajitambulisha kama kuwa wao ni maafisa wa polisi kisha wakawatia pingu Mzee Panta Guno pamoja na vijana wake Dosagon na Norman hatimaye wakaondoka nao wakatumikie kifungo chao. Huku nyuma wakamuacha Anitha akihuzunika na kulia akimlilia baba yake ambaye aliyemlea tangu udogo wake na tangu alipofariki mama yake hii leo anamuacha kwenye upweke ulioshiba na kunona.



    **********

    Mathias mapenzi ndiyo yaliyosababisha kuwa chizi na mapenzi ndiyo yanayomfanya hivi sasa atangetange mitaani mchana na usiku, kiangazi na masika akapoteza dira katika maisha kwaajili ya marehemu Coletha. Maana alipenda pasipo pendeka alimpenda mtu ambaye hana hisia nae wala hana ndoto nae akazidi kutaabika Mathias kona zote za mtaa kama Kunguru wa Zanzibar wenye baka jeupe shingoni, akatangatanga na kuzurura mitaani Mathias akapotezana na Anitha takribani miezi mitano. Mwezi wa sita ndiyo wakaja kuonana katika kituo cha Kimara mwisho Anitha yeye akiwa anatokea Mbezi Makabe kwenye harusi ya rafiki yake ndipo alipofika Kimara mwisho akamuona Mathias kituoni ameketi akiwa anakula mkate ulioharibika pembeni mwa Mathias likiwepo ndoo kubwa lililochakaa na lililojaa vikorokoro vya kila aina bila shaka lilikuwa la Mathias maana kwa muonekano wa ile ndoo haifai hata kidogo kutumia mtu mwenye akili timamu. Anitha huruma ikamjia akashindwa hadi kuzuia machozi yasitiririke yakatiririka machozi kwa wingi na kusababisha leso aliyojifutia itapakae machozi, alipomaliza kulia akazidi kushangaa na hakuamini kama ataweza mkuta mwanaume ampendaye katika hali kama ile. Akashuka ndani ya gari aina ya TOYOTA PASSO ya bluu bahari akajongea hadi alipo Mathias akamtazama kwa muda kisha akaomba vijana wawili waliokuwa pale kituoni wamsaidie kumkamata Mathias wamuingize ndani ya gari, vijana wale wakamkubalia Anitha wakamkamata Mathias wakamuingiza ndani ya gari kisha wakalipwa na kuendelea na pilikapilika zao. Anitha akaondoa gari eneo lile akaenda moja kwa moja hospitali ya KAIRUKI kumpeleka Mathias akafanyiwe vipimo na mwisho afanyiwe matibabu apate kurudi katika hali yake ya awali.



    “Dada yangu, mgonjwa wako tumempima vipimo vyote tukakuta sehemu ya kichwani ameumizwa sana...pembeni ya pituitari damu imevilia kuvilia kwa damu ndiyo imemfanya kuwa chizi,” Daktari alitoa maelezo kwa Anitha mara baada ya kufika mgonjwa hospitali na kumfanyia vipimo.



    “Ina maana, hatoweza kupona?,” Anitha aliuliza kwa kutaka kujua kuwa kama mgonjwa wake hatapona.



    “Kupona atapona...nitakuandikia dawa kisha ukamnunulie kwenye maduka ya dawa akaanze dozi ndani ya mwezi mmoja au miezi miwili atakuwa kasharudi kwenye hali yake ya kawaida.”



    Anitha akaandikiwa dawa na daktari akaruhusiwa na mgonjwa wake mara baada ya maelezo ya daktari kuisha, akaelekea duka la dawa akanunua dawa aliyoagizwa kununua, akanunua kisha akapanda ndani ya PASSO yake na kutimka eneo lile na Mathias wakielekea nyumbani Masaki upepo unapovuma. Akaishi na kumuuguza Mathias kwa upendo wote hadi Mathias alipopona, yapata mwezi mmoja baada ya Mathias kupona kwa kuwa Anitha alitokea kumpenda Mathias hivyo basi alivyopona akaeleza hisia zake kwa Mathias na Mathias akamkubali baada ya kutambua hisia za mwenzake. Wakaishi kwa upendo na amani katika uchumba wao baada ya kukatika mwaka wakafunga ndoa wakawa mume na mke pia wakala kiapo kanisani kuwa watapendana hadi kifo kitakapo watenganisha katika maisha.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Eti, ya nini ujitese kwa mtu asiyekupenda wahenga wanasema; Mpende akupendaye asiyekupenda achana nae, kwanini wakasema msemo huo? walisema msemo huo kutokana na mwanadamu kutojali hisia za mwenzake. Basi hebu...jaribu kupenda panapopendeka uone mavuno ya matunda yaliyo mema, wengi wanakuwa wana papara katika kuingia kwenye mapenzi hawajui kama kuna mafungu mawili ya kuchagua katika mapenzi. Fungu la kwanza katika mapenzi ni usaliti, fungu hili wengi linawatesa na wengi wanalitumikia kwa wingi bila kujua madhara wanayokumbana nayo, wanasema majuto huwaga baadae hivyo wakishakumbana na huu usaliti baadae wengi ndiyo hujuta. Fungu la pili ni upendo, fungu hili wachache sana wanalitumikia wanaolitumikia ndiyo wale wenye uelewa na wenye upendo wa dhati kwa wenzao. Kumradhi kwa kusema wenye uelewa wengi tunauelewa lakini sio kwenye mapenzi, kwenye mapenzi wenye uelewa ni wachache sana katika asilimia 100% wenye uelewa ni asilimia 50% tu katika mapenzi.”



    **********MWISHO**********


0 comments:

Post a Comment

Blog