Search This Blog

Friday, November 18, 2022

FUNDO LA UMIVU - 2

 






Simulizi : Fundo La Umivu
Sehemu Ya Pili (2)




Wiki mbili baadaye, matangazo ya kujiunga na mafunzo ya kujitolea ya Jeshi la kujenga Taifa (JKT) yalitoka. Kwa bashasha ya hali ya juu, shauku na msukumo, hawakusita, mapema tu, walivyoyaona, kuandika barua za maombi na kupeleka ofisi husika inayohitajika. Habari za wizi walishazisahau kabisa, na kumbukumbu ya haraka kama walikwishaiba, ilitoweka akilini mwao. Kuanzia hapo, waliwaza maombi tu. Ya wao kujiunga na mafunzo ya kijeshi. Hivyo muda mwingi, wakawa wanatafuta habari, namna gani mambo yanakuwa katika kambi za mafunzo kwa watu waliomaliza mikataba, kutoroka ama waliokwisha ajiriwa katika taasisi mbalimbali pamoja na majeshini. Huku wakisubiria tarehe ya kwenda kusailiwa. Vilevile ni ufahamu wa kupata dondoo, maswali yapi hupendelewa kuulizwa kwenye usaili. Kila walipopita, walijinasibu kwa subira wanayoendelea nayo, kuhakikisha hawafanyi kosa la aina yoyote, wapate kuwa vizuri na ikibidi wote katika kampani yao, wafanikiwe kufaulu kwenye usaili huo.



Sekunde, dakika, saa na hatimaye siku zilizidi katika. Siku tano zikasalia, kuufikia usaili, utaowaondoa na mihemko waliyonayo na iongezekayo kila kukicha, na kutwaa sehemu kubwa akilini. Wakiwa na hamu ya kuifikia siku hiyo, walipata kumbaini mtu aliyeiba simu, ile waliyoambiwa kuwa wao wameiba. Ambaye ni mmoja miongoni mwa wale wauzaji wa maduka jirani, aitwaye Abillah. Namna walivyodhalilishwa, ndiyo fikra za kwanza zilizoteka akili. Kumbukumbu ilijirudia, hasira ikawaiva, walipwe kile walichotoa. Kingine kilichoongeza hasira, kitendo cha wao pekee, kuorodheshwa katika uhusika wa uibaji, na kuwaacha wauzaji maduka, kisa tu wanasehemu za kufanyia kazi wao hawana. Hiki kiliwaumiza. Hivyo iliwabidi kuondoa kadhia hiyo waliyoipata mwanzo. Na namna pekee, ni kumpeleka mwizi wao kwa mhusika wa simu.



Walimsomba juujuu, hadi bandani kwa Makashata. Na ilivyo bahati walifanikiwa kumkuta. Kwa mwendo walioenda nao, shari iliwatambulisha. Ujio wao haukuwa na wema, hata majirani walioona walitambua hilo, hali iliyowasukuma kusogea karibu washuhudie kiendeleacho.

“Makashata! Awali ulitufungulia kesi kwa kosa la wizi, wa kuiba simu yako, ilhali hatukuwa wahusika. Tulijaribu kujitetea, lakini mwenzetu hukutuelewa. Kuwa sio wahusika. Leo tumekuletea mtu aliyeiba simu yako, hivyo turudishie pesa yetu.”

“Siwezi rudisha hela?”

“Kwanini?”

“Ninyi malizaneni na huyo, mliyomkamata.”

“Kwanini unakuwa mgumu kurudisha?”

“Nishasema sirudishi. Mimi wezi wangu walikuwa ninyi. Kama hamkuiba basi. Si mshapata aliyeiba? Basi awarudishie hela mliyonilipa. Abii eh! Warudishie pesa waliyonipatia ubaki na simu. Mimi hiyo simu siitaki tena.”

“Sina hela.” Alisema Abii na kutulia. Sura ikiwa ngumu.



Mzozano ulikuwa mrefu. Hadi ilifikia hatua ya kupelekana kituo cha polisi, wapate muafaka utaokuwa sahihi kwa kila mmoja. Haikuwa safari ya muda mrefu, muda mfupi tu, japo kituoni palikuwa na umbali mrefu toka bandani kwa Makashata. Walivyofika, hawakuchelea kuanza mazungumzo. Kwa Makashata, kuhadithia namna ilivyokuwa kuanzia mwanzo hadi mwisho.

“Kwa hiyo huyu ndiyo mwizi wa simu?” aliuliza Askari waliyemkuta, ambaye walikuwa wanampatia maongezi. Anayetambulika kwa jina la Afande Ally.

“Ndiyo afande.”

“Ninyi bado ni vijana wadogo. Haya mambo hayapaswi fikishwa sehemu kama hii, maana ni hatari. Hivyo wewe walipe pesa yao mambo yamalizike. Ni kiasi gani kwanza?”

“Elfu thelathini!”

“Jitahidi.”

“Sawa afande. Nitawalipa, ila hapa sina hela. Naomba wanipe muda, kufikia jumatatu nitawakamilishia,” alijibu Abii.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Ombi lilijadiliwa, walivyoafiki, walianza safari ya kuondoka kituoni hapo. Huku wakipiga yowe, kulaumiana kwanini wamefanyiana kitendo hicho, chenye picha mbaya kwa jamii. Umbali, mita mia moja na hamsini toka kituoni, kwa mbali, kuna sauti waliisikia ikiwaita. Ila kutokana na raha ya maongezi, wakafahamu wao sio wahusika wa wito huo, hivyo hawakugeuka kule sauti inakosikika kuangalia nani anaita. Waliendelea na safari.

“Wee! Makashata........!” ilisikika sauti hiyo. Kwa ukaribu kabisa, baada ya aliyekuwa anawaita, kufanya jitihada za kuwakaribia.



Kwa pamoja walishtuka. Wakasimama, kisha kuangaza macho yao, kule sauti ilikosikika. Sura iliyoonekana ilikuwa ngeni, kwa baadhi ya mboni za watu wengine tofauti na Makashata aliyeitwa, ila kwa muonekano tu, alitambulika kuwa ni askari. Wa kituo walichotoka. Baada ya sekunde kadhaa yule aliyeita, aliyetambulika kwa jina la Aziz aliwafikia, akiwa anahema ishara kuwa alitumia mbio kuwafuata. Pasi na salamu, akaanzisha maongezi.

“Makashata, hawa ndiyo wale waliokuibia simu?” aliuliza askari huyo, sura ikiwa imejaa mikunjo ya ndita, akitumia kama silaha kuwatisha.

“Ndiyo wenyewe. Lakini tushayamaliza.”

“Turudi kituoni,” aliamuru kwa kukaripa askari huyo. Aziz.



Sauti iliyotoka, iliwaogopesha. Kurudi hawakuwa na budi. Waligeuka nyuma kisha kinyonge kabisa wakaanza piga hatua kufuata kituo kilipo. Walivyokifikia, waliingizwa kaunta. Afande Aziz akatoa jalada la watuhumiwa na kuwasoma. Katika orodha ya kina Vumilia alisalia mmoja tu. Kila aliyesomwa alisogezwa pembeni, idadi husika ilipokamilika, waliamriwa kuvua mikanda na vitu vingine ambavyo ni hatarishi kwa mtuhumiwa kuwanavyo ndani ya mahabusu. Pindi hayo yote yanaendelea, na kipigo kiliendelea, kwa kutumia rungu na mikanda ya haohao watuhumiwa sehemu ya maungo yao hatarishi. Huku wakiambatanishiwa kauli kali na za vitisho.

“Wajinga nyie ndiyo mnajifanya kujua kuiba sio? Watu wanakesha kununua mahitaji yao yatayowasaidia baadaye ninyi mnawarudisha nyuma, sasa leo mtatutambua.”

“Wafundishe hao afande,” alishadadia askari aliyoko pembeni.



Walitembezewa rungu takribani dakika tano. Maumivu makali yakaanza chanua sehemu walizokuwa wanapigwa, magotini na kwenye kifundo cha mguu. Yaliyotengeneza machozi yaanze kuwatoka kwenye mboni zao. Baadaye walipelekwa mahabusu, kila mmoja akiwa anafikiria lake, lakini kikubwa usaili wa JKT uliopo siku za karibuni, pamoja na watachukuliwa vipi na wazazi wao. Ukizingatia mambo yalishaisha. Yule mmoja aliyesalia, alitumika kutoa taarifa kwa wazazi na ndugu, wa wale waliowekwa ndani. Ambao waliwasili kituoni hapo haraka sana punde taarifa zilivyowafikia. Baba yake Vumilia, Mzee Matatizo na rafiki yake, aitwaye Jogoo. Pasi na kawia, taratibu za dhamana zilianza. Huku umaarufu wa wazee hao wawili katika harakati za kisiasa, kijijini hapo na wilaya kwa ujumla, ukiwa msaada tosha, wa kuwawezesha kufanikisha haraka sana. Kwani walitambulika na wengi, watumishi wa kila idara na wananchi wengine pia wasiokuwa waajiriwa.



Na ndivyo ilivyo! Hadi kufikia saa 12 jioni walifanikiwa kupata dhamana. Iliyowataka kurejea tena kituoni jumatatu ya wiki inayofuata. Jumatatu ilivyowadia, mapema sana waliripoti. Watuhumiwa wakawekwa chumba maalumu kuchukuliwa maelezo, tayari kwa taratibu za mahakamani, wakati huo Mzee Matatizo na rafikiye, Jogoo wakiwa nje kutazamia nini kifuatacho. Mle chumbani, Vumilia na wenziye walifanyiwa vingi vya ajabu, katika kuwatisha, wajewe na hofu angali hawakuhusika.



Kule nje, Mzee Matatizo, alionekana kuteta jambo na wenziye. Wakati huo wakifanya subra, kumsubiri kamanda wa polisi wilaya, OCD. Ambaye walikuwa na miadi naye. Pindi afande Aziz anakamilisha kuandika maelezo na kufunika jalada, nje OCD aliwasili. Aliteremka garini na kuonana na Mzee Matatizo na rafiki yake. Walivutana pembeni, kisha kuzungumza jambo. Ambalo halikuchukua muda mwingi kuhitimishwa. Baada ya hapo OCD akatoka na kauli.

“Aziz!” OCD aliita, sauti iliyosikika vyema kabisa chumbani alipo afande Aziz.

“Afandeeee...!”

“Futa jalada la hawa.”

Kimya kidogo kilipita, kisha akajibu.

“Sawa afande,” aliitikia. Kwa sauti iliyojaa manung’uniko, ishara ya kutokubaliana na maamuzi ya mkuu wake wa kazi.



Hakuwa na budi. Alilazimika kutii maamuzi tajwa. Jalada lilifungwa, na watuhumiwa kuachiwa huru. Kitendo hiki kiliibua matumaini mapya kwao. Kwamba uwezekano wa kufanya usaili umebakia palepale tofauti na walivyoanza hisi, wenda wakahukumiwa kwenye kesi hiyo. Na kuzima ndoto walizoanza zitengeneza. Siku ya usaili ilivyowadia, waombaji waliwasili sehemu husika ya kusailiwa. Ofisi ya mkuu wa wilaya ya Nanyumbu, iliyopo kijiji cha Ngalinje. Kilomita chache toka Mangaka. Zoezi la usaili lilianza rasmi saa 2 asubuhi, baada ya bodi kuwa timilifu, huku ikiongozwa na Kaimu Mkuu wa wilaya. Wasailiwa waliwekwa katika makundi, ya watu kumikumi, iwape urahisi wa kufanya kwa haraka na kuwazuia vijana wasailiwa wabaki sehemu moja, wasijenge mazoea ya kutoka toka.



Juu ya kuwa katika makundi, ni kijana mmojammoja tu, ndiyo alipaswa kuingia. Akishasailiwa hutoka na kuingia mwingine. Yalitumika zaidi ya masaa kumi na mbili zoezi hilo kufikia tamati, huku wale wa mwisho, wakisailiwa kwa harakaharaka, kuufukuzia muda usiwatupe mkono sana. Kwani kuna vijana wengine walitoka vijiji vya mbali na Mangaka, na usafiri wa kuwafikisha watokako kwa jioni hiyo ulikuwa ni shida. Haupatikani!

Ilivyofikia saa 1 usiku, matokeo yalitangazwa. Vumilia akiwa mmoja wa wafanikiwa. Alifurahi, tena alifurahi sana. Furaha iliyodhihirishwa kwa tabasamu lililoenea usoni wakati wote ilhali awali alitawaliwa na unyonge. Matokeo yalivyotangazwa, hakuna kilichoendelea. Watu walirudi makwao, ila wale waliopita waliombwa kurejea kesho yake wapatiwe maelezo ya kina kuhusu usaili mwingine ulioko mbeleni, wa mkoa. Na mambo mengine pia, ya kufanya baada ya kufanikiwa ngazi ya wilaya.



Vumilia alitii agizo hilo mapema sana kabla muda pangwa kuwadia. Kwa sababu ya shauku iliyoenea moyoni mwake, ya kuhitaji kufahamu kipi wataenda ambiwa, pamoja na umbali mrefu ulioko toka nyumbani kwao hadi ofisi iliko. Takribani kilomita tatu. Maana alikuwa anatembea kwa mguu. Safari yake ilisindikizwa na nyimbo chache alizokuwa anasikiliza, kwa kutumia ‘earphone’ kupitia simu aliyokuwa anamiliki, aina ya Alcatel, aliyokabidhiwa na wazazi wake. Ladha zilizosikikana ndani ya ngoma za sikio, zilimfanya awe tulivu na kile anachosikiliza. Mambo yaliyoendelea pembeni hakuwa na habari nayo, ili yasimuondoe katika mstari wa burudani.



Taratibu, alikanyaga na kuacha ardhi, kusongesha hatua mbele, awahi aendako, ndani ya muda uliopangwa. Kuna muda alitumia simu yake kuangalia namna muda unavyoenda, kisha kufanya tathmini ya umbali na muda uliosalia kama utamwezesha kuwasili ofisini ndani ya muda husika. Pale alipofanya tathmini, na kuhusi atachelewa, aliongeza hatua za utembeaji. Akijihisi kuchoka hupunguza. Alifanya hivyo karibia mara tatu. Alipohitaji kufanya mara ya nne, honi ya pikipiki ilimshtua, na kumfanya asitishe alichokuwa anahitaji kufanya kisha akageuka nyuma, kuangalia kulikoni. Sura aliyokutana nayo, ya mwendeshaji ilikuwa ngeni machoni mwake. Ila hakuwa dereva pekee, kuna mtu alimpakiza. Msichana! Alitambua kwa haraka jinsia yake, kutokana na nguo aliyovaa huyo aliyopakizwa. Gauni! Hata alivyoangaza sura, aliweza kumfahamu. Alikuwa mmoja miongoni mwa watu waliopita kwenye usaili. Sabina ndiyo jina lake.

“Njoo pande tuondoke,” alisema msichana huyo, Sabina. Kwa sauti nyororo iliyosheheni mvuto ukongayo moyo wa mwanamume yeyote amsikiaye.



Hakusita! Haraka sana aliivamia pikipiki na baada ya sekunde kadhaa tayari alishadandia. Safari ikaendelea. Usafiri uliwasaidia. Dakika chache tu, walilifikia jengo la ofisi. Kusubiri muda husika wa wito. Waliteremka! Wakati huo tayari washaanza kutengeneza mazoea ya kuwafanya wafahamiane zaidi. Na kilichochangia haswa ni simu walizokuwa wanatumia. Zilikuwa aina moja. Alcatel! Halafu Sabina hakuwa na uzoefu nao sana wa matumizi. Mnamo saa 3:45 asubuhi, ndipo mtu aliyetakiwa kutoa maelezo ya wito walioitiwa alijitokeza mbele yao. Baada ya vijana wote kukamilika. Maelezo hayakuchukua muda mrefu, muda mchache tu, baada ya hapo walirudi makwao kuendelea na shughuli zingine.



Msaada wa lifti aliopatiwa Vumilia toka kwa Sabina, ulijenga mazoea. Japo sio kwa sana. Pale waonanapo, ila ilitosha kuwafanya watu waliofahamiana na kuzoeana pia. Kwani tabasamu walilokuwa wanapatiana pindi wakutanapo mtaani ilikuwa ishara tosha ya kutoa imani hii. Ijapokuwa Sabina alikuwa mwenyeji wa jijini Dar es salaam, hivyo alifika Mangaka kwa nduguze na maalumu kwa zoezi la usaili. Mwezi juni, walifanikiwa kujumuika kwenye zoezi la usaili wa mkoa. Ambalo Vumilia, lilimsongesha hatua nyingine, ila isivyo bahati, msichana aliyeanza jenga mazoea ya urafiki naye hakufanikiwa. Sababu ikitajwa, uzito wake kuwa pungufu dhidi ya ule unaotakiwa. Matokeo hayo, yaliwafanya wawili hawa, kusitisha kila walichokuwa wanaendelea nacho. Kwani Sabina alirejea kwao Dar es salaam na Vumilia Mangaka, kusubiri muda wa kwenda kambini atakochaguliwa tayari kwa mafunzo. Hakuna aliyekumbuka mawasiliano. Kwamba waendelee kuwasiliana baada ya hapo. Kila mmoja alijawa na fikra zingine, kukosa umuhimu wa kila mmoja kwa upande wa mwenziye ikiwa ni fikra moja wapo.

“Wapi nitaonana naye nikishatoka hapa? Wakati anarudi zake mjini, na lini na kwa dhumuni lipi? Hawezi rudi kijijini huyu mrembo wakati alichofuata kakosa,” aliwaza Vumilia, akiwa anamsindikiza Sabina kwa macho yaliyoongezeka ukubwa sababu ya kushangaa.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Hiyo ilikuwa hatua moja wapo ya mafanikio, kwa upande wake. Ile shughuli ya kuzurura zurura, sasa alienda kuachana nayo. Muda wote akili ikajenga dhana ya ajira, akiwa kama Mwanajeshi wa jeshi la wananchi. Ambayo ilimpa matumaini ya kuheshimiwa na kukubalika mtaani, na kwa jamii kwa ujumla. Wale waliokuwa wanamdhihaki sasa, aliamini ndiyo wakati wa wao kutambua thamani yake. Kuwa naye ni binadamu, na anahitajika kuthaminika kama wanavyothaminika watu wengine. Furaha imtawalayo, haipimiki. Wala kuhisiwa, kuwa ni kiasi fulani. Ilikuwa furaha isiyoelezeka. Wala dhaniwa. Aliyojihakikishia kuwanayo, mpaka pale afanikiwapo kuwa ajirani. Au asipofanikiwa kuwa, ndani ya ajira, ajenge heshima ya kupitia mafunzo ya kijeshi, ambayo ni mwiba mkali kwa wengi. Huogopa!



Hakuna siku ilihisiwa. Kuwa furaha aliyonayo inaweza kata. Hadi pale atapofanikiwa kuondoka kijijini kwao. Lakini ilikuwa sivyo. Kwani, jioni moja pindi akipata chakula, alipatiwa taarifa iliyosononesha sana moyo wake. Amani ya moyo ilitoweka. Hasira, ndizo zilitawala. Taarifa aliyopatiwa haikuwa ya kweli. Lakini, alikadhaniwa kuhusishwa moja kwa moja na juhudi zote alizotumia, kuikana.



.

“Kweli! Hatujaiba nguo. Na hiyo sehemu, hakukuwa na suruali, iliyodondoka.”

“Usikatae. Yule hawezi kurupuka na kunipatia hizi taarifa. Alishwandwaje kuwaambia watu wengine kuwa wamehusika? Hadi awaambie ninyi?”

“Sijajua. Ila pindi anapeleka mzigo wake stoo, alitukuta barabarani ielekeayo kwenye stoo yake.”

“Mwanangu, ushakuwa mwizi. Fanyeni mlipe hiyo nguo mliyomuibia.”



Haikuwa taarifa njema. Ilijaa umizo kwa upande wake. Japo hakufanya, ila alishindwa namna ya kujisafisha mbele ya mzee wake. Sababu tu, alishindwa kuzungumza. Na kauli ya moja kwa moja, ya kuambiwa mwizi. Ilimtatiza. Ilimuuma na kufikiria namna ya kuepukana nayo. Ila kwa wakati huo alishindwa afanyaje, ili asiendelee kupata umizo moyoni mwake. Tafakuri yake iliambatana na kilio cha kimyakimya. Kilichochukua muda mwingi, lengo kuondoa uchungu uliokithiri. Uliozalishwa kwa kisingizio.



Mjumuisho wa matukio hayo, yalimpunguzia kasi ya utembeaji. Tembea tembea ovyo pasi na mpangilio. Sasa alishinda sehemu moja. Hasa nyumbani. Kuuficha utu wake, uliokuwa unaharibiwa kila uchao kwa visingizio visivyo na uhakika. Mtaani, akawa anaonekana kwa nadra. Asiaibike, kwani wengi wao walishamtambua kwa sifa njema, na sio hizo zilizoanza ibuliwa. Aliijenga hali hiyo, hadi siku aliyoondoka kuelekea kambi ya mafunzo ya JKT. Ambapo safari ilianzia mjini Mtwara, baadaye jijini Dar es salaam kisha kambi husika. Ambayo alichaguliwa. Mafinga. Mkoani Iringa. Safari kutoka Dar es salaam kuelekea Mafinga, ilitawaliwa na shangwe sana. Alifurahia, ndoto zake za ajira, alizokuwa anaziota kila siku kwenda kutimia. Sio yeye pekee. Hata wenziye aliombatana nao pia, walionekana wenye furaha. Kwani gari zima ilikuwa na watu wanaoelekea mafunzoni. Basi la Upendo. Haikuwa safari fupi. Ni ndefu. Na ilichukua zaidi ya masaa kumi, kuwasili kambini.



Baridi iliwakaribisha. Kama ilivyo ada ya mazingira ya ukanda yalivyo. Ila walijitahidi kujikinga nayo, kwa nyanja mbalimbali kuhakikisha hawahudhuriki. Kukaa sehemu moja, huleta shida. Na ukomavu wa fikra. Mtu hukosa maarifa, na utambuzi wa tamaduni zingine zilivyo. Hii hujenga imani, isiyo thibitika kwa kutotambua mageuzi ya ulimwengu yanavyoendelea. Ndicho kilichojiri kwa Vumilia. Kubadili mazingira. Ilimpatia wakati mgumu. Aliteseka. Kwa kila muda kukumbuka nyumbani, kiasi kwamba alitamani kutoroka arudi. Kingine, ni taarifa za vitisho. Alivyokuwa anasikia toka kwa watangulizi wao, waliokwisha fanya mafunzo miaka ya nyuma.

“Nitapona kweli?” aliwaza. Siku moja akiwa tuli, kaketi kitandani kwake baada ya kumaliza fatiki.



Hapa uoga na hofu vilirudi upya. Pasi na sahau aibu. Ilimchukua siku nyingi, kujenga mazoea na watu wengine. Kumbukumbu ya mazingira ya nyumbani ilimuumiza. Na kumfanya muda mrefu kuwa mpweke. Hali ambayo ni mbaya sana kwa mtu yeyote. Kwani, hupelekea kukumbwa na fikra nyingi zisizo sahihi. Ama matamanio yenye majuto mbeleni. Hofu iliyochimbuliwa mapema tu, moyoni mwake ilianza mwendesha. Kwa kuviondosha vitu vyenye msaada kwake, kutii sheria ya matakwa ya mafunzo, kabla muda wa mafunzo haujawadia. Kama vile simu. Aliyokuwa anatumia kuwasiliana na wazazi wake. Aliiuza!



Mafunzo yalianza rasmi Agosti 2012. Taratibu zote zilipokamilika. Huku mamia ya vijana walijitolea, achilia mbali walioletwa kwa msaada wa ndugu. Kufukuzia ndoto zao za kimaisha. Zitazokuwa msaada tosha siku za baadaye. Hayakuwa mafunzo ya lelemama. Yalikuwa magumu na yaliyohitaji nguvu kwa kiasi kikubwa ili kufanikisha. Waliokosa uvumilivu, siku ya kwanza tu, hawakusita, kutoroka. Baada ya kuamini hawatoyaweza. Juu ya hofu na uoga alionao, Vumilia alibarikiwa uvumilivu. Hivyo tabu zote zipatikanazo alithubutu kuzivumilia, ilimradi ahakikishe hitajio la moyo wake linatimia.

****



Upendo Mgumu. Ni msichana toka mkoani Katavi. Mrefu kiasi, aliyobarikiwa rangi angavu nyeusi, na umbo nene wastani liachalo mvuto apitapo. Chunusi na makovu meusi ya chunusi zilizokauka ni sehemu iliyopamba sura yake. Alikuwa ni msichana mrembo miongoni mwa warembo, ambaye hakustahili kukosa katika orodha ya warembo mtu aorodheshapo. Naye alikuwa mmoja miongoni mwa kuruta. Wafanyao mafunzo ya kujiunga na jeshi la kujenga Taifa, kambi ya Mafinga. Kwa mwaka huo wa 2012.



Alijaliwa ukarimu. Ufahamu wa dini katika dhehebu alilopo, la Sabato, na mambo kadha wa kadha. Kama vile urafiki, kwa kila mtu aliyopo mbele yake na viumbe vingine vilivyopo ulimwenguni. Hali hii alijengewa angali yupo mdogo na wazazi wake. Kwani nao walikuwa ni watu waliojawa na sifa hizi. Jamii iliwatambua. Kama Upendo alivyotambuliwa. Ila yote ni kutokana na misingi ya dini alikuwanayo toka utotoni. Kila jumamosi hakukosa kanisani. Kumuabudu Mungu wake, na kila awapo na mwenziye ama katikati ya kundi kujadiliana jambo fulani, aliuonesha uumini wake uliokithiri kwenye dini. Kwa kuchangia hoja zilizobeba matamko takatifu ya kidini, toka kwenye kitabu cha Biblia.



Hakika alistahili, utaalamu katika nafasi hiyo, japo sio kwa ujuvi. Ila uwezo alionao, ulidhihirisha ni namna gani yupo hodari. Wapo waliombeza. Kwa tabia yake hiyo. Kisa tu wao ni maadui wakubwa wa maandiko. Lakini hakujali, alikesha kufanya kile alichodhamiria. Alitii matakwa ya Mungu wake kwa kiasi fulani juu ya vile alivyoagizwa katika maandishi yaliyopo kwenye vitabu takatifu vya Biblia na Quran. Upendo, alijitengenezea sifa kuu. Ya kunyooshewa kidole kwa sababu ya kuipenda dini. Ilhali wengi wao, walikesha kuzungumziwa namna wateswavyo na mafunzo wanayoendelea nayo. Huu ulikuwa utambulisho wa kipekee, mtu yeyote, akimhitaji, akiulizia kwa watu, mwisho wa maongezi ayatoayo lazima amalizie na neno mwanadini. Ili iwe rahisi kujibiwa.



Huyo ndiyo Upendo. Kwa tabia hizi tu, alianza kukosha mioyo ya wengi. Wake kwa waume. Huku wanaume waliojawa na uchu, hulka na papara walitengeneza mazingira ya kuwa karibu naye, kila wakati, si kwa lengo la urafiki wa kawaida, hapana! Bali kwa dhumuni la kuanzisha mahusiano ya kimapenzi.

“Huyu msichana anafaa kabisa kuwa ndani ya nyumba kama mke. Maana hizi tabia zake ni za kipekee,” alisema kijana mmoja, mara baada ya kumuona Upendo akikatiza karibu yao.

“Sahihi kabisa. Mwenyewe huwaga namtamani mbaya,” kijana mwingine alichangia hoja.



Wanaume wengi walivutika na tabia zake. Waliothubutu kumtamkia, hawakusita kuketishwa kwenye orodha ya wasubiri. Kama wana imani sahihi, wasubiri hadi siku ya kufunga ndoa ndipo wadiriki kufanya watakacho. Mtihani uliokuwa mgumu, na kuwashinda vijana wengi waliojitokeza. Hivyo kumfanya Upendo abaki na sehemu ya usichana wake. Alishinda vingi vishawishi. Tamaa ya maono ya uharaka hakuwanayo, alijidhatiti kujibidiisha, kuifikia yake ndoto. Na si kuishia njiani, kwa sababu zinazoweza zuilika. Baada ya mlolongo mrefu wa vidume kukataliwa, waliishia kugeuka marafiki. Hali iliyomzidishia idadi ya marafiki wa kiume kila uchao kulinganisha na wa kike.



Vumilia alibahatika kuwa mmoja miongoni mwa marafiki wa msichana huyo. Upendo. Lakini hakuwa katika orodha ya wanaume waliomtongoza. Anaanzaje? Wakati hata hisia hakuwanazo? Mafunzo yalichukua matamanio yake. Na kumwachia mawazo tele ya mwenendo wa mafunzo. Urafiki wao ulizalishwa, kwa sababu ya watu walio kombania moja. Hivyo kufahamiana ikawa lazima, kwa kuwa fatiki nyingi, walijumuika. Urafiki wao ulikuwa wa kusalimiana tu, na sio kuketi sehemu kujadili jambo. Tena salamu yenyewe, ni pale wakutanapo. Na sio kwamba, wakosanapo onana, mmoja huagiza mtu kumsalimia. Hawakuwa na mazoea ya aina hiyo.



Mafunzo yao yalikuwa ya miezi sita tu. Baada ya hapo walipelekwa kikosi cha malezi. Kutumikia shughuli za kitaifa. Hususani kilimo cha mazao ya kahawa na maharage. Ambapo wote kwa pamoja walipelekwa kikosi cha Itende, kilichopo jijini Mbeya. Hata huku mazoea yao, hayakuwa na tofauti, na jinsi yalivyokuwa Mafinga. Hayakubadilika! Yalikuwa vilevile na kwa namna fulani, kwa kiasi kidogo yalipungua, kwa sababu ya kazi nyingi zilizopo ndani ya kikosi hiki. Katika kuelekea ndoto za kila mmoja. Wakiwa hapa, walifanya usaili wa ajira mbalimbali, uliomtanguliza Upendo mafunzoni. Ya jeshi la wananchi.



Kuondoka kwa Upendo, halikuwa pigo kwa Vumilia. Kwa sababu hakuwa na mazoea naye. Wala haikuleta hata chembe ya athari, bali alizidisha tu jitihada zake, ili asitoke nje ya ndoto. Dhahiri! Alikuwa msitari wa mbele. Kutii maagizo yatolewayo siku zote, na kufanya utekelezaji wa maagizo hayo kwa asilimia mia moja, japo utendaji huo ulichangiwa na mienendo ya tabia za kijeshi. Aliogopa adhabu zitolewazo. Wakati huo, alishafikisha umri wa miaka ishirini. Lakini bado, aliendelea kuwa mwenye hofu, uoga na aibu kwa kiasi fulani.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Umri huo ulikuwa sahihi, kuanzisha, ama kuwa na msichana wa kuelekea katika hatua ya familia. Ila kwa Vumilia haikuwa hivyo. Hadi rafikiye wa wakati huo waliopo pamoja ndani ya kambi ya Itende, ajulikanaye Samson Alimwene alimshangaa, tatizo gani alilonalo. Muda mwingine alihisiwa kutokuwa rijali, ama anajihusisha na mchezo mchafu. Wa yeye kushughulikiwa, badala ya kushughulika.

“Dogo vipi? Shemeji yangu yuko wapi?” aliuliza Alimwene. Jioni moja wakitoka kufanya usafi eneo la kombania yao.

“Dah! Hawa wasichana wa humu utawaweza basi. Humu wamejaa gharama tu. Pesa yenyewe tulipwayo mwenyewe hainikidhi, vipi nikiwa na huyo mtu unayemsema?”

“Kweli! Lakini hata wa siku mojamoja?”

“Wa aina hiyo nitaenda tafuta huko mtaani.”

“Lakini mwenge unamulika vizuri?”

“Tena sanaaa!” alisema Vumilia. Kauli iliyofuatia kicheko kwa wote.



Mshangao huu haukuwa kwa rafikiye pekee. Hata vijana wengine, wakike kwa wakiume walimshangaa. Kwa kutosikia, habari yake yoyote ihusianayo na mahusiano ya kimapenzi. Mshangao huo ulitengeneza, hisia tofautitofauti kwa kila mmoja, lakini walishindwa mfuata mwenyewe kumuuliza, mwishowe walibaki na hisia zao zikiwaumiza. Kwa Vumilia hakujalisha, aliendelea na msimamo wake. Na dhana halisi aliyonayo, ambayo alijihakikishia kutoyumbishwa na mtu. Ili asiitengue. Japo matamanio yalikuwepo, kuyatoa ikawa shida. Unufaika wa pekee aliobarikiwa kujitwalia katika hali hiyo ni kuzoeleka. Alifahamika na wengi. Hivyo asilimia kubwa mtu akimuulizia hakupata shida kufahamishwa. Kama ilivyokuwa kambi iliyopita pia. Mafinga JKT.



Siku za wikendi, ilivyotolewa ruksa ya mapumziko na utawala wa kikosi, Vumilia na Samson ni miongoni mwa vijana waliokuwa wanatoka, kwenda kusafisha macho. Kupooza miili yao na akili baada ya kazi ngumu wafanyazo kwa muda mrefu siku za kazi. Safari zao mara nyingi, zilikuwa zinaishia Baa, iliyoambatana na nyumba ya kulala wageni ndani. Ama siku yenye shida na baadhi ya mahitaji, huenda kwanza sokoni baada ya hapo huelekea baa. Huo ndiyo ulikuwa mfumo wao, kila siku watokapo. Ndani ya baa hawakuketi kushangaa. Walikuwa wanaitisha vinywaji kukonga nyoyo na kulainisha koo, akili ipate tulia. Samson alikuwa mkata kilevi, kwa uzuri kabisa. Tena mjuvi wa mambo hayo, huku Vumilia akipata mafunzo kupitia kwake. Kwa kuanza na vinywaji laini. Soda! Ni siku chache, ambazo alishawishiwa aonje ladha ya kilevi, naye akakubali. Ambapo kilevi husika kilichanganywa kwenye kinywaji atumiacho, siku nyingine kunywa kinywaji chenye kilevi pekee.



Baadaye aligeuka kuwa mjuvi wa baa nyingi ndani ya jiji la Mbeya. Hasa maeneo ya Mwanjelwa. Kutokana na kila wikendi kuhudhuria sehemu hizo. Sanjari kabisa na Samson. Walikuwa hawabanduki kufuatana kila watokapo. Hali iyoendeleza ushawishi. Toka kwa Samson, na Vumilia kuutekeleza ushawishi huo, kila aambiwapo.

“Vumi eeh!” Samson aliita kwa kifupi. Akimaanisha Vumilia.

“Niambie jembe langu.”

“Vipi warembo hao? Fanya mambo leo, nafsi ifurahi,” alisema Samson, wakiwa wameketi kwenye baa moja ifahamikayo kwa jina la Furaha.

“Wako wapi?”

“Si hao tuliowaona hapo nje, pindi tunaingia. Sema nao, ama nikuitie mmoja nikuunganishe nao?”

Vumilia alivuta hisia kufikiri. Tafakuri ya kina, kama dakika nne hivi, mkono wa kushoto tamani, macho kayafumba, kuonesha namna alivyokuwa hisiani,sekunde chache baadaye ndipo akatoka na jibu la swali la Samson.

“Yeah! Nirekebishie.”



Haikuchukua muda mrefu, mmoja wa wahudumu aliitwa. Msichana mdogomdogo, akadiriwaye kuwa na umri wa miaka kumi na tisa. Umbo jembamba, macho madogo, meupe yalembuayo kila sekunde. Vilima vilivyopo kifuani kwake, ndiyo shida zaidi. Ni vilima vilivyosimama, vioneshavyo kilele nyakati zote hata kama vikiwa vimefunikwa na ukungu. Hivyo vilijipenyeza, kuonesha namna ving’aavyo. Rangi adhimu, nyeusi! Ilisheheni mwilini mwake, na kumfanya awe mwenye mng’aro zaidi ya wahudumu wengine wapatikanao ndani ya baa hiyo. Vidume vyenye uchu, kila waingiapo huyu ndiyo alikuwa wa kwanza kutolewa macho, kwani urembo wake ulimbeba, na kutangazika.



Hivyo, punde alitii wito. Alivyoketi aliagiziwa kinywaji baada ya hapo maongezi yakaanza. Kama ilivyozoeleka. Wanawake wa baa sio wa kutumiwa maneno mengi. Maneno machache tu, ndivyo alivyofanya Samson, akisaidizana na mhusika mwenyewe. Vumilia. Maneno yaliyojaa hisia na mvuto wa kubadili akili ya msichana huyo yalisheheni sawia kabisa, ndani ya midomo ya vidume hivyo. Yaliyofanya ushawishi, mapema tu aridhie ujumbe aliopatiwa. Pasi na kawia chumba kililipwa, kisha wakaingia mtanangeni. Kazi ilianza mapema, hadi kuja kuhitimisha, yalishakata zaidi ya masaa sita. Huku kila mmoja wao akionekana kuwa legevu. Dhihirisho walichokuwa wanafanya haukuwa mchezo wa kitoto. Kitendo hicho kikageuka kuwa tabia kwa Vumilia. Kila atokapo pasipo kuonana na msichana kisha kupeana utamu uliofichwa, hakuridhika kabisa. Ilikuwa ni lazima, aupate utamu huo, tena kwa udi na uvumba. Moyo wake uridhike.



Hadi anakuja kufanikiwa kumaliza mkataba wa kujitolea, wa miaka miwili ndani ya jeshi hilo, Vumilia alikuwa na muendelezo wa tabia hiyo. Kutoka na wadada wa baa, na wale wajiuzao. Mkataba ulimalizika akiwa na waraka wa ajira mkononi. Ajira ya jeshi la polisi. Hivyo alisubiri muda wa mafunzo tu, uwadie ili akajumuike na wengine waliokwishachaguliwa kwa ajili ya mafunzo kabla ajira rasmi hawajaianza. Habari ya kuendelea na wadada wa baa na wajiuzao, hapa ikawa mwisho. Kwani alivyorejea nyumbani hivi vitu havikuwepo. Hakukuwa na sehemu wajiuzao wanawake, ama baa zenye nyumba ya kulala wageni ndani, na isitoshe wahudumu wengi walikuwa ni wamama na vijana wa kiume.



Kusitisha, ama kuacha ikamlazimu. Akili ikajipambanua, kutafuta mbadala utaomridhisha hisia zake zinakuwa ngangali, na zinatimiziwa haja zake. Kama tamanio lake limsukumavyo. Kupata msichana, atayemuita mpenzi ama mchumba siku moja. Akili akaipa utambuzi, kuwa hiyo ndiyo shughuli kuu, iliyoko mbele yake. Hivyo haitajiki kuchelea, kwa kuwa siku si nyingi ataondoka kijijini hapo kuelekea mafunzoni. Ya ajira!

“Sijawahi kutoka kimapenzi na msichana wa hapa kijijini kwetu, lakini awamu hii nitajitahidi, kadri niwezavyo nifanikiwe kutokanaye,” aliwaza Vumilia akiwa kaketi gogoni nyumbani kwao akisubiri chakula cha mchana.







Baada ya kupata chakula hakuwa na uhitaji wa kuendelea kukaa. Aliondoka. Kuelekea kwa shemeji yake, aitwaye Zamda. Aliyeolewa na kaka yake, yule aliyempatia mitandio akauze mnadani siku za nyuma. Maeneo ya Sauti moja, mtaa maarufu uliopo karibu na sokoni. Sehemu hiyo ilikuwa genge la kudumu, toka alivyorudi baada ya kumaliza mkataba. Kikubwa kilichomvutia ni stori walizokuwa wanapeana na uonaji wa watu mbalimbali. Pasi na sahau lilikuwa eneo mahususi alilolichagua kufanya tathmini ya kufanikisha azimio alilojipangia.



Si muda wote alikuwa anadumu hapa. Kuna muda alikuwa anaondoka na kwenda sehemu nyingine, ambazo nazo, alikesha kuweka genge kwa muda kisha kuendelea na ratiba zingine alizojipangia. Ni septemba 19, 2014. Majira ya saa 9 alasiri, jua likiakisi vyema ulimwenguni, kwa miali ya wastani iliyokuwa inapiga ardhini. Na kuwafanya watu wengi kuwapa nafasi kwa uhuru wa kushughulika na majukumu waliyokuwa wanaendelea nayo pasi na wasi wa kusitisha kwa muda, wasubiri jua lipoe ndipo waendelee. Hata walio matembezini, walitembea kwa uzuri kabisa. Kwa kutohofia nguo na mwili kwa ujumla kulowana na jasho. Muda huo Vumilia alikuwa katikati ya barabara, akipishanisha miguu kusonga mbele, kuutafuta uelekeo wa mahali alikothubutu kuelekea. Macho yake yaliyoiva rangi nyekundu, aliyapepesa huku na kule, mithili ya mtu anayedaiwa apitapo karibu na nyumbani kwa mdai, hukesha kuiba jicho kumuangalia kama yupo. Angalia yake ilikuwa ya tathmini. Kuwatathmini wasichana akutana nao ama wale walioketi sehemu wakifanya jambo.



Tathmini iliishia alipofika sehemu husika. Kazini kwa shemeji yake, alipopokelewa na lundo la kina mama na wadada waliokuwa wanajadili jambo. Miongoni mwao aliwafahamu, achilia mbali Zamda, shemeji yake. Mwingine ni Aminata, aliyehitimu naye pamoja elimu ya sekondari mwaka 2010, aliyekuwa anapata mafunzo ya ushonaji kwa fundi mwingine, jirani na kwa Zamda. Alitafuta eneo akaketi. Maongezi ya wenyeji wake yalivyohitimishwa, alijumuika na shemeji yake kuanza soga. Maongezi yao yalikuwa mazuri. Yalitawala furaha, na msisimko kana kwamba hamna shida zinazowakabili. Furaha yao ilifunika huzuni, ikawasahaulisha, chanuo likachimbua faraja iliyokidhi na kuenea sehemu yote. Hakukuwa hata na chembe ya hisia, katika maongezi kukumbuka jambo fulani lenye udhia.



Aminata, ndiye alikatisha maongezi yao. Baada ya kumuita Vumilia aende sehemu anayofanyia kazi, na Vumilia kufanya hivyo. Alienda pale alipo, ambapo alikuwa pekee, japo kulikuwa na mashine za cherehani kama sehemu tatu. Walisabahiana. Baada ya hapo walianza maongezi, kwa kukumbushiana habari za shule na nyinginezo. Kwa Vumilia ilikuwa kama ndoto, kuketi mbele ya msichana huyo na kuanza kuongea naye. Kwani kipindi wako shule, hakupata nafasi hiyo, na sababu moja wapo ni tofauti ya umri. Aminata alikuwa na umri mkubwa zidi ya Vumilia. Pia hakuwa na mazoea naye, zaidi ya kujuana tu majina. Aminata alikuwa anga zingine. Kubwa!



Hivyo kitendo cha leo hii kuitwa, na kumuomba waongee, ilikuwa bahati tosha. Tena kilichomshangaza zaidi, mada za maongezi, zilikuwa tofauti na alivyohisi. Hakufikiri, kama wanaweza zungumzia hicho kitu. Mapenzi!

“Mimi baada ya kumaliza shule, niliolewa. Na mwanajeshi mmoja hivi, jijini Dar es salaam. Ila hatukudumu sana kwenye ndoa yetu. Maana mume wangu alikuwa mtu wa wanawake vibaya mno. Nikashindwa, na nikaamua kuondoka zangu. Pasipo hata kunipatia talaka,” alisema Aminata.

“Kwanini sasa uliondoka pasipo kukupatia talaka? Pia huwa hakusumbui kuwa urudi muendelee na maisha?” aliuliza Vumilia. Jicho pima usoni kwa Aminata kumuangalia namna aongeavyo. Na mabadiliko aliyonayo.

“Tabia zake zilinishinda. Na mara kibao huniomba nirejee, lakini sihitaji.”

“Mmmmh! Una lako jambo. Ama kuna mwingine anayekuzuzua ndiyo maana unamkataa?”

“Hapana! Nimeamua tu. Kwani wewe unahitaji mkewe aweje?” lilikuwa swali lililomfanya Vumilia atulie kwa muda atafakari. Kwanini kaulizwa hivyo na jibu lipi ampatie. Wakati hajawahi kupanga mazingatio yake anayoyahitaji mkewe awenayo.

“Mbona hunijibu?” aliuliza Aminata baada ya kuona kimya muda mrefu.

“Aaah! Mke wangu atakuwa wa kawaida tu. Wewe ulikuwa vipi ndani ya ndoa yako?”

“Naamini, nilitekeleza majukumu yote kama mke kwa mume wangu. Ila sijajua kama mume hakuridhika na kile nimfanyiacho ama ndiyo tabia yake. Maana ninyi watu wa majeshini sijui mkoje? Si unawaona hata hawa askari wa hapa kwetu? Ni malaya vibaya mno.”

“Hiyo ni tabia ya mtu. Usiwajumuishe watu wengine kwenye mkumbo usiowahusu.”



Maongezi yao yalikuwa marefu, na yaliyochukua muda mwingi kufikia tamati. Huku wakihitimisha kwa kupeana namba za simu, ili iwarahisishie mawasiliano, pale mmoja atapohitaji kuwasiliana. baydala ya kumfuata atapopatikana kwa muda huo, atatumia tu simu kuzungumza naye. Tukio hilo lilijenga historia nyingine kwa Vumilia. Kwani, kila muda hakuisha kukumbuka. Na kikubwa alichokumbuka ni maswali ya msichana huyo Aminata kwake, kuhusu habari za mke. Kumbukizi alilonalo ni kubwa. Lote kumfikiria Aminata. Amfanye vipi. Hisia za kupendwa zikachipuka, tena kwa kiasi kikubwa akilini mwake, ila alikosa uthibitisho wa kuhakikisha.

“Yule atakuwa ananipenda,” aliwaza Vumilia, akiwa kitandani amelala akipepesa macho huku na kule kulitanabaisha paa, pindi akisubiri apitiwe na usingizi.



Siku iliyofuata, hisia za wazo alilokuwanalo usiku wa jana yake halikubanduka. Alilitafakari zaidi ya mara mbilimbili kutafuta upi uhalisia sahihi bila mafanikio. Muito wa simu, ulioashiria ujumbe kuingia ndiyo ulikatisha tafakuri yake. Taratibu, aliivuta na kusogeza jirani naye. Jina la mtu lililoonekana kwenye skrini lilimshtua, na kumpa shauku ya utambuzi ujumbe gani kautuma. Ulikuwa ni ujumbe toka kwa Aminata. Aliufungua chap, na kukutana na maandishi machache yaliyosomeka ‘Vumi! Mambo?’ moyo ulilipuka shangwe. Mwili ukasisimka, mithili ya maji ya baridi yatuavyo mwilini, kwani, halikuwa tarajio lake, msichana huyo kuanza kumchatisha. Pasi na ajizi, alijibu.

“Niko poa. Niambie?”

“Uko wapi?”

“Nyumbani!”

“Unafanya nini nyumbani mchana wote huu? Badala ya kutoka Mungu akuone?”

“Nimelala.”

“Utalalaje mchana wote huu? Njoo huku nikuone. Maana mwenzio siishiwi hamu ya kukuona.”



Ujumbe huu ulimfanya atulie. Kisha kutafakari, na kuunganisha hisia za wazo alilonalo. Jibu sahihi akafanikiwa kulipata.

“Huyu ananipenda,” alijisemeza kimoyomoyo. Baada ya hapo akajibu jumbe hiyo.

“Poa! Nakuja.”



Punde alivyojibu, alivaa viwalo vyake na kuondoka. Mwendo ulikuwa wa haraka, awahi kufika. Na kufanya maongezi naye kabla hakujajaa watu. Mafundi wengine washonao. Baada ya muda wa robo saa aliwasili eneo husika. Ila alianza kwenda kwa shemeji yake kumsalimia, ndipo akaenda kwa Aminata kutii wito wake. Walisabahiana, maongezi ya mada zingine yakafuatia, huku Vumilia akitawaliwa na wazo moja pekee, msichana aliyoko mbele yake anampenda, ndiyo maana anadiriki kufanya yote hayo. Japo anatumia mzunguko mkubwa kumfikishia ujumbe. Maongezi yalijaa mambo ya mahusiano, yaliyomfanya kumpa imani zaidi Vumilia, juu ya kile akihisicho muda wote toka walivyokutana na Aminata.

“Huyu ananipenda. Ila nitaanzaje kumuambia kwa namna alivyokuwa mkubwa hivi?” aliwaza, kwa kuhofia umbo nene na umri mkubwa alionao Aminata. Kwani, alizidiwa miaka miwili.



Jioni, ya saa 11 ndiyo walimaliza maongezi yao. Baada ya hapo Vumilia alirejea nyumbani, akitawaliwa na mawazo tele yamhusuyo Aminata. Anaanzaje kumuambia? Ndilo jambo kubwa lililomsumbua. Ukizingatia hisia zilishaanza msukuma uhitaji wa kutoa haja zake. Kabla hajawasili nyumbani, alipitia nyumbani kwa kina Ngungu. Na kumhabarisha matukio yote yaliyojiri.

“Wewe tongoza tu, unaogopa nini?”

“Namna alivyokuwa na umbo kumbwa vile na umri wote alionao atanielewa kweli? Maana nahisi ataniona kama mtoto kwake ambaye sitoweza kumridhisha.”

“Kwa hiyo stori uliyonihadithia, kaonesha dalili zote za kukupenda. Hapo ni wewe tu, umalizie.......Malizia dogo asije kukuona boya,” alisema Ngungu kwa msisitizo.

“Sawa. Acha nifanyie kazi kauli yako.”

Aliaga na kuondoka!



Alivyorudi nyumbani fikra hazikubanduka. Neno tongoza, na hapana usitongoze, yalikinzana vikali. Na kushindwa kuyapatia maamuzi. Neno lipi sahihi kwake. Yote aliyaona yana manufaa, lakini alilazimika kuchagua moja kati ya hayo. Chaguzi rasmi aliifanya usiku. Alipokuwa banda moja la biashara ya CD na kava za simu akisikiliza muziki. Ambapo alinunua vocha na kumpigia Aminata. Usiku wa saa tatu. Ndipo alifanya tukio hilo, moyo ukienda mbio, mapigo yakimtawala, atamuambiaje alipokea, ilhali alishakata shauri, lazima aporomoshe maneno yenye ushawishi yatayomsukuma Aminata aondoe nguo zake abaki kama alivyozaliwa na kuruhusu kuingiliwa himayani. Wakati huo kichwani alijawa na fikra, mpangilio wa maneno ya kumuambia, yatayoweza kumshawishi. Baada ya sekunde kadhaa simu ilipokelewa. Sauti ya usingizini ilisikika. Iliyomtambulisha Vumilia huyo mtu alikuwa amelala. Alijikohoza kidogo, kisha akaanza maongezi.

“Mbona unalala mapema hivyo?” aliuliza baada ya kutakiana hali.

“Sina cha kufanya. Isitoshe niko peke yangu.”

“Fundi wako kaenda wapi?”

“Kwa mumewe Masasi.”

“Harudi leo?”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Ndiyo harudi.”

“Vipi naweza kukutembelea?”

“Heee! Wewe usiku wote huu uje kufanya nini? Na ukiangalia wewe ni mwanaume nami ni mwanamke?” aliuliza Aminata, kwa mshangao mkubwa uliochanua aibu kwa Vumilia, na kupoteza nguvu ya uongeaji.

Alitetemeshwa. Ajibu vipi alihangaika kutafuta, takribani sekunde sita pasi na mafanikio.

“Kwanza, ninunulie vocha tuchati, hivi unaniumiza sikio,” aliendelea kusema Aminata. Kauli iliyomsaidia asijibu swali la awali aliloulizwa.

“Poa!” alisema Vumilia na kukata siku.



Pasi na kuchelea, alinunua vocha kisha kumtumia. Alivyoipata walianza kuchati. Wakati huo taratibu alianza safari ya kurejea nyumbani kwao, kwenda kulala baada ya kuona ndoano aliyoitupa haijatoa manufaa. Haijang’ata! Alirejea kiunyonge sana. Huku akiwazua itakuwa vipi siku zijazo, akionana naye? Na endapo kama atawahadithia wenziye anaofanya nao kazi. Alianza hisi, kuwa huo ndiyo mwisho wa safari alizokuwa anafanya, kumtembelea shemeji yake. Alihisi kuhaibika. Baada ya mwendo wa dakika kadhaa aliwasili nyumbani kwao. Na kumkuta baba yake Mzee Matatizo, akiingia ndani kwenda kulala. Aliongoza chumbani kwake, aliitoa funguo alipoihifadhi na kufungua tayari kwa kuingia ndani, ila ghafla, alisikia muito wa simu. Uliomfanya aachane na shughuli aliyokuwa anaendelea nayo, kisha kuhiamishia akili yake kwenye simu. Haraka sana, aliitoa alikoiweka, akakumbana na jina la Aminata kwenye skrini. Alivyofungua, alikutana na maandishi yaliyoondoa unyonge wote alionao. Upya, furaha ilianza rejea. Tabasamu likachanua, aibu, fukutoni likafundwa.





“Njoo!” ulisomeka ujumbe huo.



Alishindwa kupiga yowe kushangilia. Ila kiasi cha furaha kilichosheheni hakikupimika. Kilifurahisha kila kiungo cha mwili wake. Na kumfanya awe mwenye nuru ing’aayo sehemu yoyote, hata kama iliyotawaliwa na kiza kingi. Hakuona haja ya kuingia ndani. Alifunga mlango na kuondoka, kitendo kilichomshangaza baba yake. Alipewa jina la eneo alilopaswa kufika, ambalo ni mtaa wa Mchangani. Kisha akakaza mwendo himahima kuelekea, kwani ulishakuwa usiku mwingi. Ambao barabara nzima hakukutana na mtu yeyote. Mwendo aliotembea nao ulikuwa zaidi ya wa kawaida. Alikuwa anatembea kwa haraka mno, na muda mwingine alifikia hatua ya kukimbia, ili awahi kufanya afuatacho na awahi kurudi.



Wakati huo wote alikuwa anaendelea kuchati na Aminata, kufahamishwa sehemu anayoishi, naye kumfahamisha kila alipofikia. Walifanya utaratibu huo hadi alipofanikiwa kuwasili na kumkuta mwenyeji wake akiwa ameketi mlangoni akimsubiri. Huku akiwa amevaa kitenge, alichofungia kifuani, ndani patupu. Akiruhusu ubaridi wa usiku upooze sehemu adhimu ya kujivunia baada ya purkushani nyingi za mchana. Zichangiazo viungo vingi, karibia vyote kushughulika. Walilakiana, kisha wakaingia ndani na kujitupia kitandani. Hadithi za hapa na pale zilianza. Zilizojenga hisia taratibu, na kuupa ubongo ufahamu, kitu waendacho kufanya. Dakika tano zilikuwa nyingi! Kila mmoja akaanza tembeza kiungo kimoja wapo cha mwili wake, mkono! Katika mwili wa mwenziye. Hali ilianza kubadilika. Ni mihemo tu ndiyo ilisikika kwa nguvu. Maneno yalijificha. Kusikika kwake, ni wenyewe tu ndiyo walielewa nini waongeacho.



Safari ya kuelekea ulimwengu wa huba ilianza. Safari yenye kusahaulisha kwa muda mambo ya kidunia, na yale yaliyoko kwenye maandiko takatifu. Vumilia alianza neemeka. Katika mwili wa Aminata, msichana aliyeanza kuwa na hofu naye hapo awali ya kutokubaliwa hitajio lake. Sasa akawa haamini. Kama ameweza kutusua ngome na kushuhudia usichana wake. Hakuweka masihara, alifanya. Tena alifanya haswa, ili akishatoka kama ndiyo utakuwa mwisho kwa wawili hao kukutana, basi kile afanyacho kibaki kwenye kumbukumbu ya Aminata maishani mwake. Kama ilivyo ada. Matumizi ya kinga kwake yalikaa kushoto. Hakubahatika kukumbuka, kila aingiavyo mchezoni, yote ni kutokana na hulka na shauku, ikabayo koo kwa matamanio. Hata Aminata naye hakudiriki kukumbushia hilo. Alihitaji ladha kamili, na sio ya kusindikwa. Naam! Aliuchezea mwili atakavyo. Alisawajika nao, aliuviringisha huku na kule, ili aweze kumridhisha, na kulilegeza umbo nene alilokuwanalo zaidi yake. Hadi wanafikia tamati, alishafika kileleni mara mbili. Na kumfanya Aminata kutoa muangalio wa aina nyingine, tofauti na ule wa awali kabla hawajaanza pambano, huku akigubikwa na aibu na kicheko kidogo cha furaha, kilichoashiria kutoamini alichofanya. Kutoa usichana wake kwa Vumilia.



Kifuatacho kilikuwa habari nyingine. Walisinzia, walivyokuja shtuka, Vumilia alivaa nguo zake na kuondoka kurudi nyumbani kwao. Historia binafsi aliitengeneza. Kuingia kwenye ngome ambayo hakuiamini kama inaweza ingilika. Hata alivyokuja muambia Ngungu siku iliyofuata hakuamini. Ikabidi Vumilia amhadithie mkasa mzima namna ilivyokuwa hadi kafanikiwa, kumvulisha nguo msichana huyo. Kwa uthibitisho zaidi, alimuonesha jumbe walizokuwa wametumiana.

“Dogo, sasa nimekukubali. Nahisi ushakuwa hodari kwenye hayo mambo,” alisema Ngungu, baada ya kuhakikisha na kumrejeshea Vumilia simu yake.

“Hamna, kawaida. Mimi mwenyewe siamini. Hivi enzi za shule angekubali kweli ningethubutu kumtongoza?”

“Aaaaah!........Asingekubali. Kwanza ungeanza vipi?”

“Najiuliza hilo swali, sipati jibu.”

“Jaribu kumuuliza mwenyewe, tuone atakujibu vipi.”



Vumilia alifanya hivyo. Alituma jumbe mbili za kupotezea kisha ikafuatia husika, ya kumtaka Aminata amueleze endapo kipindi wapo shule angemtongoza jibu gani angelitoa. Jumbe hiyo ilijibiwa dakika moja baadaye. Ilijibiwa ikiwa na lundo la maandishi, yaashiriayo maelezo ya jibu. Nao walianza yasoma, hadi wanafanikiwa kuhitimisha, ni cheko tu ndilo liliwatoka, tabasamu nalo likifuatia. Ishara tosha jibu halikuwa baya.

“Huyu mwanamke anaonekana kukuelewa,” alisema Ngungu.

“Yumkini! Sahihi ungeacho.”



Hatimaye yalianza mahusiano, baina ya wawili hao. Huku wakiyafanya siri, pale eneo la kazi afanyalo Aminata wasifahamu, na Zamda pia. Shemeji yake na Vumilia. Kila mmoja alionesha kiasi cha upendo alichonacho kwa mwenziye. Ulioonekana kuwa kiasi kikubwa ukijumuishwa pamoja. Ila Aminata alizidi. Alionekana kuwa na upendo mkubwa kwa Vumilia. Hilo lilidhihirishwa kwa matendo yake. Yaliyomsukuma muda mwingi awe jirani naye. Hakuweza pitisha siku pasipo onana. Kwa namna yoyote, hata awe na shughuli nyingi kiasi gani, zilizomhitaji atumie muda mwingi. Alilazimika, katika muda huohuo aweze kuonana na Vumilia. Siku nyingine alimtoroka fundi wake, kumfuata, awapo eneo la karibu. Hasa kwa shemeji yake Zamda. Kwenye simu, ndiyo zaidi. Jumbe walizokesha kutumiana, zilionesha uhalisia wa upendo walionao.



Mwisho wa upendo wao ulijitokeza mara baada ya kila mmoja kuondoka ndani ya Mangaka. Walivyoondoka, kwenda maeneo tofauti tofauti. Vumilia Nyangamara, kijiji kilichopo wilaya ya Lindi vijijini, mkoani Lindi. Na Aminata Tunduru, mkoani Ruvuma. Kila mmoja akamsahau mwenziye. Ule ukaribu waliokuwanao ukapungua. Hivyo wakawa wanawasiliana kwa siku mojamoja. Ila hisia za kuwaongoza kuwa ni wapenzi hazikupotea. Huo ulishakuwa mwezi oktoba. Mwezi uliokaribu kwa Vumilia kuhitajika mafunzoni ya jeshi la polisi, ndani ya chuo cha polisi Moshi, mkoani Kilimanjaro. Na alienda huko kufuata mahitaji kwa baadhi ya ndugu yatayomwezesha kujikimu awapo mafunzoni. Ujio wake ndani ya kijiji hiki ulikuwa mara ya kwanza tangu awe na akili za kiutu uzima. Kujitambua! Ukiachana na awamu hiyo, mara ya kwanza ilikuwa pindi angali mdogo. Pindi hana ufahamu tosha wa utambuzi. Mwaka 2000. Ndugu, jamaa na majirani walikesha kumshangaa, jambo lililomkosesha amani ya moyo wake, ila alivyokuja zoeleka, hilo nalo alilizoea. Kwani kikubwa kilichomfanya wamshangae, ni historia aliyonayo. Kupitia mafunzo ya kijeshi, ya jeshi la kujenga Taifa. Huku wakimtathmini na mwili alionao, wengi walijiuliza aliweza vipi? Ukilinganisha na imani walizonazo kuhusiana na mafunzo yalivyo. Kuwa magumu!



Ugeni ulivyomtoka aligeuka kuwa mwenyeji. Alizoeana na kila mtu. Wake kwa waume. Wazee kwa vijana pasi na sahau watoto. Miongoni mwa watu hao, achilia mbali jamaa zake, ni mwanamke mmoja afahamikaye kwa jina la Mama Moza. Aliyekadiriwa kuwa na umri wa miaka ishirini na nane kwa mwaka huo 2014. Ikiwa na maana alizaliwa mwaka 1986. Mazoea aliyojenga Vumilia kwake, yalikuwa ya salamu. Na kupiga stori za hapa na pale kwa uchache. Kwani, alimuogopa. Na kilichomfanya amuogope ni umbo, na umri kuwa mkubwa zidi yake. Tofauti ya miaka Saba. Vumilia alikuwa na umri wa miaka ishirini na moja kwa wakati huo. Ukiachana na salamu, na hizo habari zingine zihusuzo mafunzo atokako, hakukuwa na kitu kingine walichozungumza. Tena maongezi hayo yalikuwa katikati ya watu wengine, na si wao kuketi sehemu wakawa wanazungumza.



Alivyofahamika haswa. Matamanio yakaanza. Kuwa na msichana ndani ya kijiji hicho. Ukijumlisha na stori alizozisikia toka sehemu tofauti tofauti juu ya habari za wanawake wa kimakonde, kuwa na ufundi wa kutosha kwenye mambo hayo, ambao wapatikanao kijijini hapo, alizidi kuhamasika kutekeleza tamanio lake. Kwa gharama yoyote alijiapiza. Huku akiweka angalizo, asipofanikiwa kwa wakati huo, akirudi hilo litakuwa jambo la kwanza. Habari kuhusu Aminata hapa alishazisahau. Sasa akili ilikuwa inawaza wanawake wa umakondeni pekee. Atawapata vipi? Naye aingie kwenye historia aisikiayo na kuithibitisha.



Alianza taratibu zake. Baadhi ya rafiki aliowapata wakimsaidia. Haikuwa shughuli ya siku moja, alihangaika nao, pasi na mafanikio, ila hakukata tamaa, aliamini ipo siku, yake nia itatimia. Rika pekee aliyoihitaji ni rika yake, hata wale aliowazidi kidogo, ila wengi wao walikuwa wasumbufu, walikuwa na baadaye baadaye nyingi zilizomchosha. Tamanio siku zote halichagui. Huushawishi moyo kujawa na hisia za kuvutiwa na rika yoyote, mtu aionayo mbele yake. Pale unono unapotawala sehemu kubwa ya umbo la yule atamaniwaye. Ni jambo la kawaida mzee apataye kuwa na umri wa miaka sitini, kumtamani mtoto apataye umri wa miaka kumi. Hii kwa pande zote. Wake kwa waume. Hivyo tamanio la Vumilia, kwa Mama Moza, halikukwepeka. Umbo la mama huyo alihamasika nalo. Na kweli! Alikuwa mwanamke mzuri sana pale kijijini. Mtu yeyote apewapo kazi ya kuwaorodhesha warembo watatu wa kijiji, jina la mwanamama huyu halikosekani. Kabarikiwa sura, umbo lenye mvuto na rangi adhimu duniani, nyeusi. Yampendezesha. Si mtu wa mkorogo, vipodozi vyake ni vya kiasili, vyenye kutoa mng’aro wa hali ya juu.



Uzungu hakuutaka. Kufanya hivyo aliamini kwenda kinyume na maadili ya taifa lake. Vivyo hivyo alivyoumbwa, alidhamiria kuendelea navyo, na si kuongeza kitu kingine cha ziada kilichobuniwa na binadamu. Chenye kumbadilisha muonekano. Kama kalio, kabarikiwa la kiasili. Ya nini kuongeza? Hakuhitaji. Mabishano ya vilima vilivyoko nyuma vilisukuma wachuro wengi, hata wale walioukimbia, apitapo wasitishe shughuli kumtathmini. Na kuvitathmini vilima hivyo vinavyobishana kwa kila kimoja kuonesha ufundi wa kucheza. Umbo bambataa, guu la bia, jicho lembelembe, kifua noti, ushawishi alistahili kutoa. Japo Vumilia alikuwa na umri mdogo kwa mama huyu, lakini aliingia katika orodha ya watamanio.

“Dah! Ukimpata mwanamke kama huyu, unafanya naye mambo usiku kucha,” aliwaza Vumilia, baada ya kumuona Mama Moza anakatiza mbele yake.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Hakika! Alimtamani. Na alitamani kumtongoza. Ila anaanzaje? Kama ilivyo ada, akumbukapo hapo huishiwa nguvu. Amtamaniye ni mkubwa kwake. Atumie maneno yapi kumfikishia hisia zake? Kila awazavyo hukosa jibu. Kila siku aliwaza juu ya jambo hilo. Tatizo likabaki sehemu moja tu. Ileile anayokuwa nayo siku zote. Hujawa na woga. Ila kwa hapa woga alistahili, kwa kuwa mtu anayemtamani kamzidi sana umri. Maneno yote atumiayo kutongoza, aliona yanafaa kutongozewa wasichana wa rika yake, sio wenye umri mkubwa kama Mama Moza. Tamanio lilimtesa. Kumshirikisha mtu, hakuafiki. Akabaki nalo moyoni liendelee kumuumiza, huku akiwa na fikra yumkini ipo siku atafanikiwa. Usiku alalapo akawa na tabia ya kujenga taswira, kama yupo na Mama huyo kitanda kimoja, wakiburudisha mioyo yao, katika ulimwengu wa huba. Hali iliyopelekea kujichafua, na kuchafua nguo zake avaazo pindi awapo taswirani.



Ilikuwa ni oktoba 21. Kijiji cha Nyangamara kiligubikwa na sherehe ya utoaji watoto jando. Sherehe ilifana, kwa mtumbuizo wa ngoma iitwayo Singenge. Ngoma maarufu ukanda huo. Wananchi walijumuika, wenye mwali na wasio na mwali kukonga mioyo yao, waondokane na mawazo yasiyo na msingi. Burudani ilikuwa ya uhakika. Walizunguka kijiji kizima, na kusomba watu wengi mno. Wa rika zote. Shughuli hiyo ilianza mapema tu. Mnamo saa 12 asubuhi. Ilivyowadia saa 9 alasiri ilisitishwa, kisha karibia watu wote, walielekea uwanja wa mpira. Ambako kulikuwa na mtanange mkali baina ya Nyangamara na kijiji jirani. Nyangamara B. Al-maarufu Kilimani. Huko nako kulijumuisha watu wengi. Wananchi wa vijiji vyote viwili. Uwanja ulifurika, kilichosaidia hukujengewa. Hivyo iliwapa fursa watu wajitawale. Laiti ungelikuwa umejengewa, wangelikesha kusukumizana na kukanyagana. Mtanange ulianza rasmi saa 10:00 adhuhuri. Ushangaliaji nao ukafuatia toka pande zote. Mashabiki wa Nyangamara na wale wa Kilimani. Yote ni furaha waliyonayo, kabla hawajaelekea kuhitimisha usiku, kwa kupata burudani ya muziki.



Vumilia alikuwa mmoja miongoni mwa mashuhuda wa matukio yote mawili. Kuanzia lile la ngoma na la mpira pia. Kazi yake kubwa ikiwa ni kuwaangalia watu wanavyoburudika, huku yeye akipata ladha ya burudiko hilo kimya kimya. Moyo ujinafasi. Kwenye ngoma kazi kubwa, ilikuwa kuwaangalia wachezaji wanyongavyo. Hasa wa kike. Mama Moza akiwa mmoja wapo. Na ndiye aliyemtazama sana. Na kumfanya ahamasike zaidi, kuongeza tamanio lake. Muda fulani hisia zilimshawishi, kwa adha hiyo ya tamanio alipatalo arudie mchezo aliokuwa autekeleza awali. Wa upigaji punyeto! Ila halmashauri ya kichwa ikajenga ukinzani wa kupambunua hisia hiyo.

“Sina namna. Ikishindikana, huo ndiyo mbadala. Hakuna njia nyingine.” Alijisemeza kimoyomoyo, huku akizidi kukodoa macho, pima kwa wasichana na kina mama kuangalia wanavyojitahidi kuoneshana ufundi wa kukata nyonga.



.



Hata uwanjani nako. Kazi yake ilikuwa ni kutazama mpira unavyochezwa na washangiliaji, walivyokazana kuzunguka uwanja, kushangilia. Aliondoka mahala hapo dakika za mwisho karibu na mchezo kumalizika. Moja kwa moja akafikia kwenye banda moja lililoko maeneo ya soko la kijiji, akaketi hapo kupumzika baada ya kusimama kwa muda mrefu. Punde! Alishuhudia, watu wengine wakimiminika kwa wingi kuelekea kule aliko, walioompa ufahamu mechi ishamalizika.

“Aaaah! Mama Moza,” aliita Vumilia. Alivyomuona Mama Moza akipita jirani yake, akiwa kaambatana na baadhi ya watoto, usoni akitawaliwa na michirizi ya jasho iliyokauka. Iliyochangiwa na ushangiliaji.

“Niambie!”

“Nimekuona ulivyokuwa unaburudika leo. Kumbe unaweza kucheza vile?”

“Kawaida. Siku mojamoja si mbaya. Maana mambo yenyewe hutokea kwa nadra sana ndani ya mwaka,” alijibu. Huku akipunguza mwendo na kusimama.



Kuona hivyo! Vumilia akajiongeza. Aliinuka pale alipoketi akamfuata. Alivyomfikia walianza maongezi. Huku taratibu wakiianza safari kuelekea kule Mama Moza alikokuwa anaelekea.

“Baadaye si kuna burudani nyingine?” aliuliza Vumilia.

“Ndiyo. Ni hapo kwa Mzee Jalasi.”

“Vipi tunaweza burudika pamoja hiyo baadaye?” aliendelea kuuliza wakati hajawahi kwenda klabu, ama kumbi wapigazo disko usiku au mchana hata siku moja.

“Ondoa shaka.”

“Nipatie basi namba zako, ili iwe rahisi kutafutana baadaye.”



Hakubisha! Mama Moza alitaja namba kisha Vumilia kuzihifadhi katika orodha ya kitabu cha simu kwenye simu yake. Baada ya hapo kila mmoja alielekea uelekeo wake. Furaha ikajivika. Mwanya wa kukamilisha tamanio lake kuwa halisi alianza uona. Kwa kuamini tayari mama huyo anaenda kuruhusu ngome yake iingiliwe naye. Kwa jinsi alivyomtamani, muda aliona unakawia. Ule waliyoahidiana wakutane. Alitamani awe muongoza muda japo kwa wakati huo hadi alifikie lile saa la tukio. Kwani alifahamu, wakishaenda disko, itakuwa nafasi pekee ya kutimiza hitajio lake, mara baada ya disko kumalizika. Kuingia ngomeni mwa mama huyo. Kiza kilianza ingia. Mwanga ukafukuzwa. Harufu ya tamanio ikatamalaki. Kila kitu akawa anafanya kwa uharaka, ili awe ndani ya muda, apepee ndege, asitoweke kudandia mti mwingine. Kiza kilivyoimarika, usiku ukawa rasmi. Ukamuongezea mshawasha wa kuondoka. Alitamani asipate chakula, lakini kelele nyingi za kulalamikiwa kutopenda kula, ikamlazimu asubiri kwanza ndipo aondoke. Kilivyotayarika, alikula chapchap na kuondoka huku akiaga kwa kuongopa kuwa ataenda kulala kwa kaka yake disko litavyomalizika. Kwa sababu ya kuepeka umbali wa kurudi.



Aliondoka moja kwa moja hadi maeneo ya sokoni. Ambako ndipo disko lilitakiwa lipigwe. Na ni maeneo waishiyo wazazi wa Mama Moza. Alijipamba kwa koti kubwa jeusi, boshori juu, na raba chini kujikinga na baridi. Alitafuta eneo akaketi, kisha kuanza kuchati naye kumtaarifu kuwa ashawasili. Walitumia muda mwingi kuchati. Lakini isivyo bahati, pindi wako katikati ya mawasiliano, walifikiwa na ujumbe uliowataarifu, disko limeghairishwa. Vumilia alihamaki, ile furaha iliyoanza jipambanua kuonesha mafanikio ya kuingia ngomeni kwa Mama Moza ikaanza toweka. Alijihisi mwenye gundu, na kupoteza nafasi ya wazi, kwani kumpata tena zaidi ya siku hiyo, hakuamini kama inaweza patikana.



Juu ya hilo, maongezi yalizidi kuiva. Kwa Vumilia kuweka wazi kila kitu, kuhusu hisia alizonazo kwa mwanamama huyo. Alizidadavua, hadi zikatoa mshawasha kwa Mama Moza ashawishike nazo.

“Uko wapi sasa hivi?” Mama Moza aliuliza, baada ya maneno yaelezeayo hisia kutoka kwa Vumilia kumtekenya.

“Niko mbele ya genge lenu hili la mkahawa.”

“Njoo basi nyumbani. Nimekaa huku nyuma.”

“Poa!” alijibu Vumilia, kisha kuinuka pale alipoketi na kwenda alikoelekezwa.



Alipiga hatua kadhaa akafanikiwa kufika sehemu husika. Na ilivyobahati, alimkuta Mama Moza akiwa kitini ameketi tuli peke yake. Walisabahiana, baada ya hapo Vumilia alikaribishwa kwenye kiti kilekile kilichokaliwa na Mama Moza aketi. Alistaajabu, kwa woga. Ila baadaye alipiga moyo konde, akapiga kilio kitini. Pasipo tegemezi! Ulimwengu wa huba ulianza. Kwa Mama Moza kuonesha hisia za waziwazi za uhitaji wa kushikwashikwa sehemu ya maungo ya mwili wake. Vumilia hakuvunga! Barabara, akatii hitajio. Mitomasano ya hapa na pale ilifuatia, ndimi walibadilishana, hadi sehemu husika zilifikiwa. Vidole vya mikono yote kwa kila mmoja ilifanya kazi hiyo. Kushtuka mzuka ulipanda, tendo likahitajika, lakini walikuwa nje, japo ni usiku, hivyo iliwabidi watafute eneo mahususi waianze safari ya kina ya kubarizi ulimwengu wa huba.

“Kanisubiri maeneo ya kwa Baba yake Ahmad Mmalala, ili tuende tukafanye yetu kule nakoishi,” alisema Mama Moza kwa sauti legevu.



Hakupingana naye. Japo mwenge ulishakuwa kidete, kuhitaji kupoozwa. Ilimlazimu afanye uvumilivu, hadi waende huko alikoambiwa ili wakafanye yao kwa uhuru. Akili ilitawala hisia za kwenda kufaidi, unono wa mama huyo. Na aliamini hayo yote ayafanyayo hakuna anayeshuhudia. Ila jicho la mwanadamu ni kali. Linapenyeza sehemu yoyote hata kama kuna kiza kiasi gani. Wachache walishuhudia liendealo. Nao kugawanyika katika mitazamo tofauti tofauti kama mwenyewe alivyokuwa na mtazamo wa kwenda kufaidi. Baadhi yao walienda sambamba na mtazamo wake, wengineo walienda tofauti, kwa kuamini, amejipeleka kwenye dimbwi la moto lifukalo muda wote. Hivyo kuangamia kulikuwa mbele yake. Alielekea sehemu aliyoambiwa. Na baada ya dakika chache Mama Moza aliwasili kisha wakaongozana hadi nyumbani kwake. Walivyofika hawakuremba. Uchu uliwajaa kooni, mambo yakaenda chapchap, ulimwengu husika wakaufikia. Ulimwengu wa huba.



Raha ilijivika ndani ya mioyo. Iliyosisimua miili yao wakati wote na kutoa hamu ya kuendelea kufanya kila wapumzikapo. Ufundi wa nguvu ulioneshwa. Mabadiliko ya mitindo kila baada ya sekunde kadhaa ili kila mmoja aridhike, na kukamilisha safari ya kuumaliza mlima. Kileleni. Hadi wanakuja kuhitimisha, walishapanda mlima, kwenda na kurudi mara tatu. Hali iliyowapa uchovu. Kwa kuwa muda ulishaenda, Vumilia aliamua kulala hapohapo. Huku akijawa na tafakuri namna alivyotusua ngome kwa urahisi.

“Ama kweli uoga ni dalili za umasikini. Watu wengi hushindwa kutimiza malengo yao sababu ya hofu. Nilikuwa namhofia nini awali?” aliwaza Vumilia pindi akivuta shuka kulikaribisha lepe la usingizi.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Alijiona hodari. Kuishinda hofu. Na kumpeleka mama huyo atakavyo. Asubuhi kulivyopambuzaka aliamka mapema mno. Hakuwa na haja ya kufanya usafi wa mwili wake, kuosha uso na kuswaki. Aliogopa kuonekana na watu wengine waishio jirani. Alilazimika kuondoka mapema ili asionekane. Na alifanikiwa. Kwani, mara baada tu ya kumuaga, alipiga hatua za kasi kuwahi nyumbani kwao. Huko ndipo alifanya usafi wa mwili na mambo mengine, baada ya hapo aliingia mtaani. Kila amuonapo Mama Moza, akili ilikumbuka mchezo walioufanya jana yake, kumbukizi iliyomfanya achanue tabasamu amalizapo kukumbuka. Hakuisha kuwa mwenye furaha. Utamu wa mapenzi alianza uonja, shubiri ikawa kando kusubiria. Ila tatizo hakuwa na msichana mwenye malengo naye. Kwani kila aliyebahatika kutokanaye, alitokanaye kwa ajili ya kutimiza haja zake.



ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog