Search This Blog

Friday, November 18, 2022

MASKINI MAYASA - 1

 






IMEANDIKWA NA : DAMIANI CHIKAWE



*********************************************************************************



Simulizi : Maskini Mayasa

Sehemu Ya Kwanza (1)



 Mvumilivu hula mbivu!! , ni methali ambayo imezoeleka na inatumiwa sana na wanajamii walio wengi katika kuhamasisha watu ili waweze kuvumilia shida na hatimaye nyakati za raha ziwafikie au kufikia malengo yao.

Kwake Mayasa, yeye anaona ni kama methali inayowafaa baadhi ya watu,ila si yeye!.Nazani itakuwa vizuri kama ikiwa mvumilivu hula mbichi,ila hiyo ni kwake yeye Mayasa tu,na wala awashauri watu wengine waamini kama aaminivyo yeye Mayasa.

Mwaka 1988 ndio mwaka ambao Mayasa aliingia katika ulimwengu huu wenye kila aina uovu na ubaya.Hiyo haimaanishi kwamba wema haupo ila Mayasa anasema dunia yenye kila aina ya uovu ni kwasababu wa yale ambayo anayaona katika maisha yake ya kila siku na jamii ambayo inamzunguka yeye.

Katika familia ya Mzee Diko yenye watoto wanne Mayasa alikuwa ni mtoto wa tatu kuzaliwa akitanguliwa na dada pamoja na kaka na wa mwisho ni ndugu yake wa kiume anayeitwa Apolo.Alipokuwa na umri wa miaka kumi kipindi hicho yupo darasa la pili,mara kwa mara alikuwa anapenda kufuatana sana na baba na mama kwenda shambani kujifunza kulima pamoja nao.Na alitamani sana kuwa mkulima bora hapo baadae.Aliwaza kuwa na mashamba makubwa sana amabayo atayalima na kuyatunza yeye na familia yake hapo baadae.

Maisha ambayo walikuwa wanayaishi wazazi wa Mayasa pamoja na watoto wao, Mayasa aliyapenda sana na yalimvutia sana kiasi cha kutamani naye kuwa na familia bora kama familia ya Mzee Diko, ni familia yenye upendo na raha .Ingawa alikuwa na umri mdogo kipindi hicho lakini akili za kujua jema na baya alikuwa nazo na ndio maana kichwani mwake aliwaza ni jinsi gani atakuwa na familia bora kama yao.Mama yake alimfundisha mambo mengi sana kuhusu maisha.Alimsihi sana kuhusu kuwaheshimu watu wote hata kama hawajui watokako kwani hiyo itamfanya kuongeza upendo wake kwa jamii inayomzunguka na hivyo kuishi maisha ya ushirikiano na upendo katika jamii itakayomzunguka,kwani ukiishi na watu vizuri basi hata ukiwa na shida watakusaidia.

Shuleni alikokuwa anasoma walimpenda sana waalimu kutokana na nizamu ambayo alikuwa anaionesha kwa waalimu wake na hata kwa wanafunzi wenzake lakini si hivyo tu hata aliporudi nyumbani wanakijiji wengi wa kijijini kwao kinachoitwa Ruponda kilichopo katika wilaya ya Nachingwea mkoa wa Lindi walikuwa wanamsifu sana kwa bidii ya kazi na nidhamu na sifa zilizagaa na hadi shuleni kwao na hata miti ikimuona ilikuwa inafurahi uwepo wake chini ya kivuli cha mti huo ambao alisimama.Alipofika darasa la tano alichaguliwa kuwa dada mkuu wa shule kutokana na nidhamu kubwa ambayo alikuwa anaionesha kila siku akiwa shule na hata nyumbani kwani sifa zake za nyumbani zilitoka kwa wanakijiji wenzake zilifika hadi kwa waalimu.

Kwenye mitihani ya shule alikuwa anafanya vibaya sana ingawa kila siku alikuwa anahudhuria darasani.Jambo hili lilimnyima raha sana Mayasa na hakujua sababu ni nini hasa.Waalimu pia walijaribu kumhoji lakini hawakugundua sababu hasa ni nini.

Mayasa alipojaribu kumuuliza baba yake mzee Diko juu ya hali hiyo,jibu alilopewa na baba yake ni kuwa katika ukoo wao wote hakuna aliyesoma hivyo ata yeye amerithi akili zao za kutosoma.

Mzee Diko alimweleza Mayasa kuwa maji yanafuata mkondo kwa hiyo hata yeye hafanyi vizuri darasani ni kwa sababu ya kurithi kutoka kwa wazee wake waliotangulia.

Maneno ya Mzee Diko, baba yake yalimuumiza sana Mayasa kwani yeye alipanga kusoma sana mpaka afike chuo kikuu lakini kila akijaribu kusoma ikija mitihani ya shule bado aliendelea kufanaya vibaya.Ila maneno ya baba yake wala hakuyaamini sana na alisema alijisemea moyoni kuwa hakuna uhusiano uliopo kati ya kufaulu au kufeli na sababu za kurithi,hivyo alijiapiza kupamabana mpaka naye siku moja afaulu na afanane na wenzake.

Waalimu wake walimwambia asikate tamaa aendelee kukazana tu na atafaulu vizuri lakini pia maneno ya waalimu hayo hayakufanikiwa katika kulitatua tatizo la Mayasa,bado aliendelea kufanya vibaya kila ilipokuja mitihani.

Baada ya kufanya mtihani wa taifa wa darasa la saba,Mayasa alikuwa na matumaini ya kufaulu na kwenda sekondari.Kipindi anasubiri majibu Mayasa alikuwa anawasaidia wazazi wake kazi za nyumbani na shambani.

Vijana wengi walimiminika kama mvua za masika kwenda kwa Mzee Diko kuulizia posa kwa Mayasa.Hii ilitokana na tabia njema ambayo alikuwa nayo Mayasa hivyo kila mwanaume alipenda kumuoa binti huyo ili apate mke aliye bora.

Mzee Diko alikuwa teyari kumwozesha binti yake hata kabla matokeo hayajarudi lakini pingamizi lilikuwa kwa Mayasa mwenyewe ambaye yeye alikuwa ana matumaini ya kwenda sekondari.Mzee Diko hakupenda kabisa kusikia habari za kusoma kwani yeye aliamini kuwa ukoo wao umerithi tangu vizazi vilivyopita vya kutosoma,hivyo hata kumsomesha Mayasa aliona ni kupoteza pesa tu kwani ni lazima atafeli tu katika masomo yake.



Matokeo yalitoka na kwa bahati mzuri Mayasa alipata nafasi ya kwenda sekondari kati ya wanafunzi kumi waliofaulu kutoka shule hiyo aliyokuwa anasoma.

Mzee Diko pamoja na wazee wenzake yaani kaka zake na dada zake walikaa kikao kujadili ufaulu wa Mayasa kwenda sekondari kama wanaweza kumpeleka shule au la! .Wazee hao walimjadili sana Mayasa na hatimaye wakaja na msimamo wao wa kutompeleka shule kama ilivyokuwa desturi yao.

Katika kikao hicho mzee mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mzee Mchopa ambaye ndiye alikuwa Mzee sana kati yao alisimama kwa kutumia mkongojo wake na kusema,



"Jamani ndugu sangu,kila mtu nazani anatambua ukoo wetu ulikotokea na hata ulipo,hajawahi kutokea mtu kufaulu na huyu ndiyo mtu wa kwanza,lakini kumpeleka shule huyu ni kupoteza maana ya ukoo wetu na hata hivyo akienda shule akirudi hapa hataweza tena kukumbuka mila zetu maana nasikia huko mashuleni wanafundishana mambo ya kizungu na kuyaacha mambo ya waswahili ,,hivyo akitokea bwana sasa ni wakati wa kumwozesha hizo habari za shule ni kupoteza muda na pesa tu kwa hiyo msimamo wetu huu wa kutompeleka shule ni maridhawa haswaaa"

Maamuzi yalipita lakini kabla hawajatawanyika katika kikao hicho mama mmoja(dada wa mzee Diko ambaye ni shangazi wa Mayasa) akanyanyuka akasema,



"Ndugu zangu kama mlivyosema kuwa katika ukoo wetu hakuna hakuna aliyewahi kusoma na kufaulu lakini kwake Mayasa ametuondolea huu mkosi hivyo ni jukumu letu tumpeleke shule na lama tatizo ni pesa mimi nipo teyari niwauze wale mbuzi wangu ili mtoto aende shule"



Mzee Diko alimwambia yule mama kuwa mjadala wa Mayasa ulishafungwa teyari hivyo hakuna haja ya kuendelea kujadili tena hilo suala.

Watu walianza kuondoka kwenye kikao cha ukoo cha kumjadili Mayasa binti wa Mzee Diko wakiwa na furaha sana ya kuona sasa Mayasa atapata mume naye ataheshimika kama baba yake Mzee Diko.Ni mama mmoja tu na Mayasa ambao walikuwa hawana furaha na maamuzi ya ukoo wao ila kwa kuwa ni mambo ya mila na utamaduni hawakuweza kupinga zaidi ya kuungana nao tu kama wasemavyo wanaukoo ili kuzienzi tamaduni zao.

Mayasa aliona safari yake ya kusoma ndo imeishia njiani teyari.Changamoto ambayo alibaki nayo ni nani anayefaa kumuoa!??.

Alijaribu kuwaangalia vijana wa pale kijijini wengi walikuwa bado hawajamvutia Mayasa.Alifikiri sana nani atajitokeza kumuoa na akamfaa lakini mwishoni aliamua kumwachia Mungu mwenyewe.

Siku zilizidi sogea mbele Mayasa akiwa bado yupo nyumbani asijue ni nani atamuoa.Baadhi ya vijana waliojitokeza kwa ajili kumuoa walipewa masharti makubwa sana na Mzee Diko ikiwemo suala la mahari ndilo wengi walishindwa kufikiana muafaka na Mzee Diko ili waweze kumuoa Mayasa.

Hali hiyo iliwafanya vijana wengi wa pale kijijini kuacha kabisa hata kwenda kuulizia kuhusu posa, kwani wengi walipatwa na hofu kuhusu mahari ambayo baba yake Mzee Diko alikuwa anaitaja.

Ulikatika mwaka akiwa nyumbani pasi na kuolewa.Mayasa alikuwa anawaona wenzake ambao baadhi ya wale waliofaulu pamoja naye wakiwa wamependeza wakirudi kutoka shule na sare za shule.Kila alipowaona aliwaonea wivu sana na kutamani kuwa kama wao lakini mwaka ulikuwa teyari umepita nazani hata shule ya sekondari ambayo alipangiwa aende jina lake lilikuwa teyari limeshafutwa.

Siku moja Mayasa alimuuliza baba yake,



"Hivi baba kwa nini unanifanyia hivi?,,umesema nisiende shule ili niolewe,nilisema sawa siendi lakini cha ajabu kila anayetaka kunioa wewe unaweka masharti makubwa sana mpaka watu wananiogopa siku hizi....Yaani hata nikienda kisimani kuchota maji vijana wote ninaokutana nao hata habari hawanipashi,ni mwaka sasa nipo nyumbani tu.Baba haya ndo maisha yangu ulioniandalia kama mwanao?"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Mzee Diko alikuwa anampenda sana mwanaye ingawa alikuwa na mambo ya kienyeji sana,Mzee Diko alimjibu Mayasa "Mwanangu ni kweli nilijichanganya sana kuhusu mahari amabayo nilikuwa naitaka na ndio maana vijana wengi wameshindwa,sasa nilipanga akitokea bwana mwingine nitampa masharti madogo tu ambaye angeyaweza siku hiyohiyo au unasemaje mwanangu?"

"Baba mimi naomba unipeleke nikajifundishe kushona nguo tu ,maana hizo habari za mume mimi nishazichoka sasa"

"Ni wapi huko sasa unataka uende?"

"Ni mjini"

"Mmmh ! Mbona mbali!? ila ngoja nikae na mama yako tuongee tuone tunafanyaje hilo swala"

"Yaani baba naomba ufanye hivyo yaani kukaa nyumbani mimi nimeshachoka sasa"

"Aya mwanangu,namsubili mama yako arudi huko shambani niongee naye,nazani majibu yatakuwa mazuri sana wala usiwaze sana Mayasa mwanangu "



Mzee Diko alimsubiri mkewe mpaka aliporudi waliamua kuzungumza suala la Mayasa waone jinsi gani watalitatua.Mzee Diko alimwambia mama Mayasa yale yote aliyasema Mayasa kuhusu kupelekwa kwenye ufundi wa kushona nguo huko mjini.Wote walikubaliana na wazo hilo.Lakini kikwazo kiliibuka kwani kutoka hapo kijijini kwao hadi mjini ni mbali sana yaani unaweza tumia hata masaa matatu hadi manne kwa mwendo wa gari hivyo Kwenda na kurudi kwa usafiri wa baiskeli lilikuwa ni jambo gumu sana hivyo waliona ni bora waongee na dada yake anayeishi hukohuko mjini ili kipindi chote cha mafunzo hayo aishi kwa dada yake huyo.

Mzee Diko alienda hadi mjini kutafuta sehemu ili ampeleke mwanaye na pia kumtaarifu mtoto wake (dada yake Mayasa) kuwa Mayasa ataishi kwake kipindi ambacho atakuwa anajifunza ufundi wa kushona nguo.

Safari ya Mzee Diko ilikuwa ya mafanikio kwani kila kitu kilitimia kama alivyopanga,aliweza kupata sehemu ya kujifunzia na pia ameshampa taarifa dada yake aishiye huko mjini.

Mayasa alizipokea taarifa hizo kutoka kwa baba kwa furaha kubwa sana kwani alikuwa teyari amechoshwa na maisha ya kukaa katika hali ya upweke akiwa nyumbani tu.Mayasa aliona siku ya kwenda huko mjini ilikuwa inachelewa sana na kama ingekuwa ndo kwa amri yake basi angeamuru siku hiyo hiyo aondoke.

Mama na baba yake walimsisitizia kuwa na tabia njema huko aendako na wala asibadrike,aendelee na tabia aliyoionesha tangu mwanzo ambayo ilimpa umaarufu pale kijijini kwao na kupelekea kila kijana kutaka kumuoa binti huyo.

Muda ulipofika Mayasa alisafirishwa na baba yake kwenda mjini kwa ajili ya mafunzo ya ushonaji nguo.Mayasa alipofika mjini alipokelewa na dada yake anayeishi na bwana wake huko mjini ambaye yeye aliolewa miaka mitatu mbele mara baada ya kuacha shule akiwa darasa la sita.

Mayasa alianza maisha mapya kwa dada yake huku mipango ya kuanza kujifunza ushonaji nguo ilikuwa ikikamilishwa na dada yake huyo ambaye alipewa jukumu na Mzee Diko baba yake la kuhakikisha Mayasa anaishi vizuri pasi na kuharibikiwa na chochote.



Dada yake Mayasa almaarufu kama mama Vumi kwani alikuwa na mtoto anayeitwa Vumilia,hivyo pale mtaani kwao walizoea kumuita mama vumi, Alikamilisha mipango yote ya Mayasa na baada ya hapo Mayasa alianza kujifunza ushonaji wa nguo kwa fundi maarufu sana ambaye ukifika Nachingwea mjini ukiuliza kwa "Makalanga Tailoring" kila mtu anapajua kwa fundi huyo.

Mayasa alianza kwa tabu sana kujifunza nyakati za mwanzo kwani kabla ya kufika hapo alikuwa hajawahi kushika hata sindano hivyo ilimwia vigumu sana kujifunza kwa hatua za mwanzo.

Sehemu ambayo Mayasa alikuwa anajifunza ufundi huo ilikua ni mbali na nyumbani kwa dada yake ingawa si saana.Nyakati zingine alichelewa kurudi nyumbani kutokana na umbali ambao uliokuwepo ila Mayasa aliendelea kuvumilia kwani alijua kuna siku atakula mbivu.Dada yake hakupata hofu sana juu ya kurudi akiwa amechelewa kwa sababu hata yeye alitambua umbali ambao ulikuwepo na mara nyingi sana Mayasa alikuwa anatembea kwa miguu,ni mara chache tu ambapo alitumia usafiri wa pikipiki ama wapendavyo watu kuita bodaboda.



Baada ya kupita mwezi mmoja,Mayasa alianza kuzoea mazingira ya kazi na hata ule umbali wala hakuufikilia tena.Alianza kujua aina za vitambaa na baadhi ya mitindo maarufu wapendao 'watoto wa mjini'.Mayasa alijisifu sana na kuanza kuona tumaini jipya la maisha yake ya baadae hata kama akiolewa basi atakuwa na kazi yake ya ushonaji nguo.



Fundi mkuu Mr Makalanga alimsifia sana Mayasa kwa kuwa na kichwa cheepesi yaani alikuwa anaelewa kwa haraka sana yale ambayo alikuwa akimwelekeza kwani ni mwezi tu teyari Mayasa alianza kujua mambo mengi sana yanayohusiana na ushonaji.



Siku moja Mayasa alikutana na kijana mmoja ambaye alijitambushilisha kwa jina la Damaso.Damaso ni kijana ambaye alikuwa anafanya kazi ya ufundi wa kutengeneza samani yaani fundi selemala.Mayasa alikutana na Damaso siku ambayo Damaso alienda katika ofisi ya Mr Makalanga kwa ajili ya kutengeneza kitasa cha mlango wa ofisi hiyo na hapo ndipo walipokutana.

Siku hiyo Damaso alimkuta Mayasa akiwa peke yake kwani ilikuwa asubuhi sana.

Damaso alipofika alimsalimu Mayasa.

"Mambo dada?"

"Safi,habari yako?"

"Habari yangu mzuri tu dada yangu"

"Mnhh! Karibu ,sijui nikusaidie nini!!"

"Oooh! Wewe ni mgeni kwenye ofisi hii?"

"Nimekuuliza nikusaidie nini,,sasa hizo habari za mimi mgeni sijui mwenyeji hazina faida kwangu wala kwako"

Mayasa alijihami kwa kujibu jibu ambalo kama Damaso alikuwa na nia ya kumwitaji Mayasa basi ingeyeyuka mara moja.Mayasa alifanya hivyo ni kwa sababu aliambiwa na dada yake kuhusu tabia za wanaume wa mjini hivyo Mayasa alikuwa ni mtu wa kuchukua tahadhari mapema sana. Damaso alitabasamu kisha akasema,

"samahani dada yangu,nimekuuliza wewe ni mgeni nikiwa na maana ya kuwa mimi huwa nakuja kuja sana hii sehemu kwa ajili ya kutengeneza hii milango,sasa kila nikija hapa nilikuwa nawakuta akina dada fulani hivi ila kwa bahati mbaya nilikuwa huwa siwaangalii usoni sasa uliponiuliza unisaidie nini ndo maana nimeshangaa sana kana kwamba hunijui vile"

"Haya nimekuelewa;kwa hiyo shida yako ni nini maana naona una maelezo mengi sana alafu hoja yako kuu husemi"

"Haah haa !! Mmh ! Dada inaonesha hupendi wenzako,ila sio vibaya kama tukitambuana kwa majina basi,mimi naitwa Damaso, enheee mwenzangu waitwa nani?"

"Jina langu ni Mayasa,tafadhali kama huna la kusema naomba uniache niendelee na kazi"

"Oooh! Mayasa! !!! Jina lako nimewahi kulisikia mahari fulani ila sikumbuki ni wapi,,ila yote kwa yote jina lako ni zuri sana,,Samahani dada kwa usumbufu inaonekana ni mkali sana wala hupendi mtu akutanie....Anyway nilipigiwa simu na Mr Makalanga kuwa kitasa kimoja cha mlango huu kimeharibika hivyo nimekuja kutengeneza"

"Anhaaa kumbe wewe ni fundi!!! Mbwembwe nyingiii si ungesema tu nikuoneshe kitasa kibovu ukitengeneze,lakini wewe fundi mbona umewahi sana kuja hapa,yaani asubuhi asubuhi hata watu hawajaamka?"

"Haa haa nimewahi kwa sababu nilijua nawe utawahi kuja"

"Mmmh wewe mimi kuja mapema katika ofisi hii ni leo tu na hii ni kwa sababu kuna kazi fundi alinipa niifanye jana ila kwa bahati mbaya jana sikuweza kuimaliza ndo maana nimeamua kuwahi mapema leo hata kabla fundi hajafika na wanafunzi wenzangu ili niimalize mapema ,,sasa wewe kilichokufanya uwahi mapema hapa ni nini?"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Nimeshakujibu binti kuwa mawazo yangu yalinituma kuwa nikiwahi tu ni lazima nitamkuta mtu na ninashukuru nimekukuta,,hivi umesema waitwa Mayaka?"

"Hapana siitwi hivyo,naitwa Mayasa,kitasa kibovu ni hicho hapo,unaweza kitengeneza mana nimeshakungundua huishiwi maneno"

"Haa haaa Mayasa,,.....binadamu aliye hai huwa haishiwi maneno,anayeishiwa maneno ni yule aliyekufa tu" Mayasa hakujibu tena neno lolote.



Damaso alianza kukikagua kitasa na alianza kukitengeneza lakini akiwa anatengeneza alianza kumuuliza maswali madogo madogo Mayasa. Lengo lake ni kufanya kazi yake iende haraka pasi na upweke hivyo alikuwa anamuongelesha Mayasa mara kwa mara.

"Mayasa ni kwa nini umeamua kuchagua kuwa fundi wa kushona nguo?"

"Nimependa tu kushona nguo"

"Oooh! Sawa ! Kwani unaishi wapi?"

"Naishi kule karibu na kanisa la walokole la kule juu kama unaenda mahakamani hivi"

"Aaah! Sawa napajua vizuri sehemu ile niliwahi fika kupaua bati nyumba ya askari polisi fulani hivi,ndo unaishi na mume wako huko?"

"Ngoja nikufundishe jinsi ya kuuliza swali,,ulitakiwa uniulize 'unanishi na nani?' lakini sio kama ulivyoniuliza,,au hukwenda shule nini?"

"Enhee ! Umekuja sehemu niliyohitaji kukuuliza kwani wewe hukufauru hadi uje hapa kufanya ufundi huu?"

"Kwa hiyo mtu akifeli ndo huwa anashona nguo eti wewe kijana!!?"

"Hapana sina maana hiyo ila lengo langu kutaka kujua ulisoma wapi na kama ulifaulu au ulifeli"

"Kufaulu au kufeli kwangu ,wewe wala hautaongeza wala kupunguza kitu hivyo siwezi kukuambia kuhusu kusoma kwangu,kwanza endelea na kazi maana naona unanichelewesha tu"



Damaso aliendelea na kazi yake mpaka alipomaliza,akaamua kumpigia simu Mr Makalanga kuhusu malipo yake kwani mpaka anamaliza kutengeneza pale ofisini kwao alikuwa bado yupo Mayasa pekee.

Mr Makalanga alimwambia kuwa yeye yupo mbali na ofisi na hata hivyo atachelewa kuja ofisini, kwakuwa walikubaliana shilingi 5000, Mr Makalanga

Alimwambia fundi Damaso kama kuna mtu yeyote hapo ofisini ampe simu aongee naye. Damaso alimpa simu Mayasa ili aongee na Mr Makalanga.

"Haloo fundi mkuu,shikamoo"

"Marahaba,ooooh bila shaka ni Mayasa maana nimeitambua sauti yako,sasa kama utakuwa na shilingi elfu tano hapo naomba mkabidhi huyo aliyekupa simu alafu mimi nitakuja kukupa nikija maana leo nitachelewa sana"

"Sawa fundi nitampa"

Mayasa alitoa noti ya shilingi elfu kumi akampa Damaso, Damaso baada ya kuipokea alimwambia kuwa hana chenji' ya kumrudishia kwani kwa wakati huo ilikuwa ni asubuhi sana hivyo alimuomba amwachie alafu jioni atampitishia elfu tano yake kipindi anatoka kazini kwake.

Mayasa alikubali kwakuwa alijua kuwa fundi Damaso anajuana na bosi wake hivyo ni lazima atarudisha tu elfu tano yake.

Damaso aliaga na kuondoka zake kwenda anakoelekea kila siku yaani kazini kwake.



Jioni ilipofika, Mr Makalanga pamoja na wanafunzi wake akina Mayasa walifunga ofisi yao lakini Damaso alikuwa bado hajatokea.Mayasa alimwelezea mwalimu wake Mr Makalanga na hapo ndipo Mr Makalanga aliamua kumpigia simu Damaso,Damaso alijibu kuwa yupo njiani anakuja pale muda si mrefu.

Mr makalanga alimwambia Mayasa kuwa aendelee kumsubiri kwani amesema anakuja .

Mayasa ilibidi aendelee kumsubiri peke yake kwani wanafunzi walishaondoka na fundi mkuu Mr Makalanga naye aliondoka.

Baada ya dakika kama kumi na tano hivi, Damaso alifika pale alipokuwepo Mayasa.Alimkuta Mayasa akiwa amenuna sana na pia alikuwa amechoka sana.

"Mayasa jamani pole sana,nimekuchelewesha ila sijafanya makusudi ni majukumu ya kazi tu ndio yamenifanya hivi"

Mayasa alionekana kuchukia kuchelewa kwa Damaso,alimjibu kwa mkato tu na wala hakutaka kuongea maneno mengimengi,

"Haya nipe ela yangu niondoke"

"Mayasa tafazali rafiki yangu usinichukie,sijafanya makusudi ni mihangaiko tu imenifanya hivi,ela yako ni hii hapa"

Mayasa aliiopokea ile pesa na kuondoka bila hata kumuaga Damaso.Damaso alijaribu kumuita Mayasa ila Mayasa wala hakugeuka nyuma aliendelea kwenda mbele.

Damaso alisimama kama dakika tano kumwangalia Mayasa kama atageuka nyuma ili ampungie hata mkono ila Mayasa alizidi kupotea machoni pake.



Damaso alijikuta akiingia katika mawazo juu ya Mayasa. Mawazo hayo yalimjia tu na hakujua kwa nini aliyawaza. Damaso alianza kuona kama ndo yupo na Mayasa wanaelekea nyumbani kwake anakoishi na aliwaza wapo na mtoto wao mdogo ambaye anasoma chekechea hivyo muda huo walikuwa wamempitia shuleni.Damaso aliwaza sana lakini mawazo yake yote yalikuwa yanawaza juu ya ukaribu wake na Mayasa.Alijiona kama yeye ndio bwana wa Mayasa na teyari wamepata mtoto wa kiume.Damaso alishtushwa na oni ya pikipiki ambayo ilikuwa inapita karibu yake.Damaso ndipo akazinduka kutoka kwenye mawazo ambayo hayakuwa hata na uhalisia.Damaso akaamua kuondoka nyumbani kwake anakoishi ambako amepanga chumba kimoja.

Damaso kipindi yupo kijijini kwao mara kwa mara alikuwa anawaza kuwa na mke na mtoto na hii ilitokana na familia yake hasa bibi yake mzaa mama kumtaka kuwa na mtoto pamoja na mke,hivyo basi kipindi yupo kijijini kwao Damaso aliiingiwa katika wimbi la mawazo mazito juu ya kauli za familia yake.

Maneno haya ya familia yake ndio yaliyomfanya Damaso atoke kijijini kwao na kuja mjini kujifunza ufundi wa kutengeneza samani ili akae mbali na maneno yao.Na alipofanikiwa kuujua huo ufundi aliamua kuanzisha sehemu yake kwa ajili ya kazi hizo za uselemala. Damaso tangu aende mjini hakuwahi hata siku moja kuwaza kuishi na mke na kuwa na mtoto,alishangaa sana kwa nini alipomuona Mayasa alianza kuwaza kuhusu familia. Ila hilo alilipotezea wala hakuliruhusu liendelee kutawala kichwa chake.



Mayasa alichelewa sana kufika nyumbani siku hiyo na alipofika aliwakuta dada na shemeji pamoja mtoto wao aitwaye Vumilia wakiwa nje na mlango umefungwa.Alipouliza kwa dada yake kuhusu wao kuwa nje mpaka wakati huo maana giza lilianza kuingia teyari, dada yeke alimjibu kuwa funguo imepotea.

"Kwa hiyo hamjafanya utaratibu wowote kumtafuta angalau hata fundi auvunje huu mlango?"

Shemeji yake alimjibu kuwa wamefanya mpango lakini kwa bahati mbaya mafundi wote anaowafahamu kwa sasa wako mbali,na mpaka kufikia hatua hiyo walishindwa kabisa wasijue wanafanya nini.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Mayasa alimkumbuka fundi Damaso lakini kibaya hakuwa na namba yake na hata kama angekuwa nayo nazani asingempigia kwani mara ya mwisho wanaachana na Damaso,hawakuachana kwa amani na ni yeye Mayasa mwenyewe ndiye aliyeondoka kwa shari.Ama kweli usiache mbachao kwa msala upitao. Mayasa hapa ndipo alipoyakumbuka maneno ya mama yake ambapo aliwahi kumwambia kuwa asimzarau mtu yeyote hata kama hajui atokako. Siku hiyo Mayasa alijilaumu sana kwa nini hakumjibu vizuri Damaso kwani kwa wakati huo angekuwa na uwezo wa kuja kuwasaidia na kwa jinsi ya kitasa cha mlango wao ulivyo wasingeweza kuuvunja bila kuwa na zana za fundi selemala. Walijaribu kila namna ila walishindwa.Mayasa akawaambia kuwa anakojifunzia ushonaji aliwahi muona fundi selemala hivyo ni bora amtafute yeye ingawa anakaa tofauti na mitaa yao. Mayasa aliaumua tu kumtafuta Damaso kwa sababu hakuwa na namna kwa wakati huo ingawa alimfanyia ujeuri walipokutana.

Mayasa alimpigia fundi wake mkuu Mr Makalanga na akamuomba namba ya fundi Damaso baada ya kumweleza tatizo lililokawa nyumbani kwao.Baada ya kuipata namba ya Damaso alimpigia na kumwelekeza tatizo la kwao.Damaso alimkubalia Mayasa ingawa alikuwa amechoka ila aliona bora akawasaidie tu. Damaso alikuwa ni mtu anayeamini kuhusu kutoa kuliko kupokea.

Baada ya dakika kama ishirini hivi aliweza kufika mitaa ambayo alielekezwa na Mayasa kwa kutumia usafiri wa bodaboda.Alipokelewa na mwenyeji wake Mayasa na akampeleka hadi nyumbani kwao.

Damaso kwa kuwa ni mzoefu na kazi hizo aliweza kuufungua mlango ndani ya dakika tano tu.

Baada ya kuufungua mlango, Damaso aliwaambia kama wanaweza watafute kitasa kingine ili awatengenezee moja kwa moja kabla hajaondoka. Kwa bahati mzuri nyumba yao ilikuwa jirani na duka la vifaa vya ujenzi, hivyo shemeji yake Mayasa alienda kununua kitasa kipya na kumkabidhi Damaso kisha baada ya muda mfupi tu aliweza kukifunga na mlango ukawa unafunga na kufunguka kama kawaida.

Shemeji wa Mayasa alimuuliza gharama yake fundi Damaso.Damaso aliwajibu kwa kuwa ameitwa kama dharura tu basi anawaomba walimpe ela aliyoitumia kwenye bodaboda tu yaani elfu mbili tu kwenda na kurudi. Watu wote walimshangaa sana kile alichokisema kwani walihisi kuwa ela itakuwa kubwa sana ikizingatiwa kuwa aliitwa muda wa dharura na tena kazi ilikuwa kubwa. Shemeji wa Mayasa alimwambia Damaso kuwa yeye atampa shilingi elfu kumi.Damaso akasema "Jamani hii ilikuwa ni dharura na mimi nimefanya kama msaada tu kwani hii taaluma yangu na pia kusaidia watu wakiwa na shida ambazo mimi ninao uwezo wa kuzitatua ndio ninachokifanya siku zote katika maisha yangu,ndo maana nikasema nipeni hiyo elfu mbili ya bodaboda tu" Mama vumi dada wa Mayasa akasema "pamoja na msaada lakini na sisi pia tunashukuru kwa msaada wako,chukua tu hiyo pesa kaka!"

Damaso aliamua kuichukua tu ile pesa kisha akawaaga na kuondoka. Mayasa muda wote huo alikuwa kimya na aliwaza sana juu ya wema aliouonesha kwao ingawa si ndugu. Mayasa alijilaumu sana kwa mawazo ambayo alikuwa anamwazia Damaso kwa mara ya kwanza wanakutana kule ofisini kwao kwani alizani Damaso anataka kumtongoza kwa jinsi ambavyo alikuwa anamwongelesha mara kwa mara,, mzaniaye kumbe ndiye siye! na Mayasa aliamini usimhukumu mtu yeyote kwa mwonekano wake. Mayasa alijiapiza kutozani tena kwa kitu chochote bila hata kukijua vizuri.



Kipindi Mayasa anaenda kulala aliamua kutumia ujumbe Damaso ili kama ikiwezekana amwombe msamaha.

Mayasa alimtumia meseji Damaso "Habari za mda huu, vipi ulifika salama?"

"Kufika salama? Wap? Na wewe ni nani?" Kwa jibu la Damaso alionekana dhahiri hakuhifadhi namba ya Mayasa mara baada ya kumaliza kuongea naye. Mayasa alijiuliza sana kwa nini hakuhifadhi namba yangu wakati alimpigia simu siku ileile tena jioni sana.Mayasa aliwaza labda Damaso atakuwa amechukia kwa alichomfanyia Damaso wakiwa kule sehemu anayofanyia kazi.

Ila akaamua kumtumia tena sms ili aone kama aliyokuwa anayawaza ndiyo yenyewe.

Mayasa aliandika "Samahani kwa usumbufu ,mimi ni Mayasa yule ambaye nilikupigia simu kuja kutengeneza kitasa kule nyumbani jioni ya leo "

"Oooh ni wewe kumbe!!!, nilifika salama na sasa najiandaa kupika"

"Mmmh kwani unakaa peke yako?"

"Ndilo jibu hilo, wala usiulize"

"Mmmh ! Jamani pole sana, nimeamua nikutafute ili nijue kama ulifika salama nyumbani kwako na pia kukuomba msamaha kwa nilichokufanyia"

"Heeeh! Msamaha?"



Damaso alishangaa sana aliposikia habari za kuombwa msamaha na Mayasa hali ya kuwa hajamkosea kitu. Mayasa akarudisha sms " Ndio msamaha,naomba unisamehe kwa nilichokufanyia leo"

Damaso alizidi kushangaa na akili yake ikamtuma kuwa Mayasa atakuwa amekosea kutumia ujumbe kama ule ,akaamua kutuma sms,

" mmmh! Kwani wewe ni Mayasa gani maana labda umechanganya namba,sikumbuki kama kuna mtu anayeitwa Mayasa kama amenikosea"

"Hapana sijakosea namba,ni wewe Damaso tulikutana asubuhi kwa Mr Makalanga na yule ambaye alilikupa elfu kumi na hapo bado unazani nimechanganya namba?"

"Sasa unanichanganya unaposema unataka kuomba msamaha,umenikosea nini?

"Damaso, naomba unisamehe kwa kukujibu vibaya pia tena wala sikuonesha nia ya kukujali tukiwa kule ofisini, nimegundua kuwa wewe ni mtu unayejali sana na ndio maana nimekutumia sms hii ya kukuomba unisamehe"

"Mmmmmh!! Mayasa mbona mbona mimi sikuona kosa lolote? Tena mimi ndio nazani napaswa kukuomba msamaha wewe kwani nilikuchelewesha sana hadi nikakukuta umechoka sana"

"Hapana mimi ndiye niliyekukosea nakumbuka ulikuwa unaniita jina langu ila mimi sikuitika wala kugeuka nyuma,naomba unisamehe kwa dharau niliyoionesha kwako sikukusudia hata sijui ilikuwaje"

"Aaah !! Usijali Mayasa, kawaida tu hiyo kwa watoto wa kike,kwanza najua ulichukia kwa sababu ulikuwa umechoka alafu na mimi nikazidi kuchelewa kuja pale kwa hiyo usiwaze sana tuko pamoja"

"Aya poa basi ,mimi nilikuwa na hilo tu, usiku mwema!!"

"Sawa, ukiwa na shida siku nyingine inayohusu kazi yangu usisite kunipigia maana ndo majukumu yangu hayo ya kila siku, usiku mwema nawe pia!"



Baada ya kuagana,Mayasa aliamua kulala akiwa na amani kwa kuona amemuomba msamaha mtu ambaye alimdharau bila sababu maalumu.



Siku iliyofuta ilikuwa ni jumapili,ni siku ambayo ofisi ya kina Mayasa huwa haifunguliwi yaani huwa wanapumzika.

Mayasa aliamka mapema sana na kufanya usafi nyumba mzima na baada ya hapo akachukua nguo zake na kuanza kuzifua. Baada ya kumaliza aliandaa kifungua kinywa kwa ajili yake na wengine wanaoishi katika nyumba hiyo.



Baada ya kunywa chai,Mayasa aliagizwa na dada yake kwenda sokoni kununua samaki na viungo vingine.

Kwa kuwa ilikuwa bado mapema yaani hata muda wa chakula cha mchana ulikuwa bado sana, Aliamua kutembea kwa miguu kwa kupita njia za mkato za vichochoroni.Lengo Mayasa lilikuwa ni kuijua mitaaa ya mjini kwa sababu tangu ameenda mjini hakuwahi kuzunguka sana zaidi ya sehemu amabayo alikuwa anajifunza kushona.



Akiwa anatembea katika moja ya uchochoro alishangaa kuona kijana anamfuata kwa nyuma tena katika hali ya kumkimbiza. Mayasa alianza kuhisi kuwa atakuwa kibaka anataka kupora mkoba wake hivyo aliamua kujihami kwa kuanza kukimbia. Yule kijana naye akaongeza mwendo baada ya kumuona Mayasa anakimbia. Hapo ndipo Mayasa alipoamini kuwa yule kijana alikuwa na lengo baya kwake. Mayasa alijitahidi kuongeza mwendo na mbaya zaidi sehemu ambayo alikuwepo ilikuwa imebana sana upande wa kushoto kulikuwa na Ukuta ukubwa sana hali kazalika na upande wa kulia hivyohivyo. Mayasa hakuwa na msaada wowote kwa wakati huo zaidi ya kuongeza mwendo na kukimbia zaidi.Mayasa alianza kumuomba Mungu wake aliye sirini ili amwokoe na janga hilo. Baada ya kukimbia sana alifika kwenye kona na hapo ghafla alijikuta yupo kifuani kwa mtu. Yule kijana ambaye alizaniwa ni kibaka baada ya kuona kuna mtu mwingine yupo na Mayasa, akasimama na kugeuka nyuma kisha kukimbia alikokuwa anatoka.

Mayasa alikuwa anahema sana,kipindi hicho bado alikuwa yupo kifuani mwa mtu huyo, aliinua kichwa chake kumwangalia usoni yule mtu ili amjue ni mtu gani. Alipomuangalia alikutana na sura ya Damaso.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Damaso naye akashangaa sana kumuona Mayasa.

"Heeeh Mayasa!!"

"Damaso"

"Vipi mbona hivi?"

"Kuna kijana alikuwa ananikimbiza"

"Oooh! Pole sana,vipi hujaumia sehemu yeyote?"

"Hapana, niko salama?"

"Na vitu vyako vyote salama?"

"Ndio vyote vipo sawa"

"Aaah! Pole sana,kwanini ulipita njia hii tena ya uchochoro hivi?"

"Niliamua kupita njia ya mkato,ndo mara ya kwanza napita leo hii njia"

"Mmmh asee hii njia ina vibaka wengi sana,mara nyingi akipita mwanamke ndio huwa wanamuonea sana,wanawake wengi sana wamenyang'anywa pesa zao walipopita njia hii.Na siku hizi wanawake hawapiti kabisa njia hii kama wakiwa peke yao kwa kuwahofia vibaka hawa ila jambo zuri upo salama. Enhe vipi ulikuwa unaelekea wapi?"

" Naelekea sokoni"

"Ooh sasa mbona umejizungusha sana si ungepita njia ya kule mwanzo hata kabla hujaanza kuingia ndani ya uchochoro huu?"

"Unajua leo ndo mara yangu ya kwanza kupita huku,ndo maana hizi njia sizijui vizuri, siku zote nilikuwa natumia usafiri wa bodaboda kwenda sokoni"

"Basi sawa kwa kuwa nami naelekea hukohuko sokoni hebu twende tufuatane wote ,imekuwa kama bahati tu maana hata mimi huwa sipiti njia hii huwa nazunguka njia yailiyoko nyuma ya kuta hizi."



Mayasa alimshukuru Mungu kwa kuweza kukutana na Damaso siku hiyo kwani bila yeye angenyang'wanywa kila kitu.

Walifika mjini wote na kila mtu akanunua alichoenda kununua, na baada ya hapo wote kwa pamoja walirudi huku njia nzima walikuwa wanapiga story mdogomdogo. Wakafika sehemu fulani ambapo wote wakaagana na kila mtu kuelekea nyumbani kwake.



Usiku wa siku hiyo, Damaso aliota ndoto ya ajabu kidogo. Aliota yupo na Mayasa pamoja na teyari mayasa ana mimba yake lakini ilipofikia miezi mitatu, mimba ya Mayasa iliharibika.Siku hiyo alianza kumuona Mayasa akitokwa na damu nyingi sana na walipofika hospitali baada ya vipimo daktari alisema kuwa teyari mimba imeshaharibika. Ila kipindi wanarudi nyumbani kwa kutumia 'bajaji' wakiwa wapo njiani kwa mbele alimuona bibi kizee kimoja aliyefanana sana na bibi yake mzaa mama akimnyooshea kidole na kumtumbulia sana macho maangavu, cha ajabu zaidi kila bajaji ikienda mbele bado alimuona yule bibi kizee akifanya vilevile .Damaso alimwambia dereva bajaji asimame kwanza kuna mtu alikuwa anamwona. Baada ya bajaji kusimama, Damaso alishuka na kusogelea yule bibi kizee. Alipofika karibu naye yule bibi kizee alitoweka.

Damaso akashtuka kutoka ndotoni akawasha taa akaangalia saa ilikuwa mida ya saa nane usiku. Akajiuliza hii ndoto ina maana gani kwake ,ila hakupata majibu. Usiku huohuo aliamua kwenda kwa jirani ambaye ni mpangaji mwenzake katika nyumba hiyo.Huyo jirani wa Damaso alikuwa na umri mkubwa kuliko hata wa Damaso mwenyewe , kumwelezea juu ya ndoto yake kwa sababu baada ya ndoto hiyo usingizi wa Damaso wote uliisha. Alipomwelezea yule mwenzake alishangaa kidogo kisha akamuuliza "huyo Mayasa unamfahamu?"

"Ndio"

"Vipi mmewahi kukaa pamoja kwa muda mrefu siku yeyote? "

"Ndio tumewahi"

"Aaaah bwana Damaso,mimi nilijua haumjui kabisa huyo Mayasa kumbe ulishawahi kumuona bwana!!! Hayo yalikuwa mawazo tu, na mara nyingi watu huwa wanaota ndoto ambazo zinahusu mambo mengi ambayo teyari umeshawahi kuyaona na ndio maana hata siku moja mtu hawezi kuota ndoto kuhusu Mungu jinsi alivyo hii ni kwa sababu hajawahi kumuona hata siku moja,,ila vile tulivyoviona mara nyingi ndio hutokea kwenye ndoto kwa hiyo mimi naamini huyo binti itakuwa teyari umeshaanza kumpenda ndio sababu amekutokea kwenye ndoto, tena kama hajachukuliwa fanya mpango tuletee shemeji Mayasa hapa"

Maneno ya mpangaji mwenzake yalimjenga Damaso na kuamini kweli ile ilikuwa ni ndoto na wala haikuwa na uhalisia wowote. Damaso alipanga siku moja akutane na Mayasa amuulize kama ana mchumba,kama hatakuwa hana basi Damaso atatumia nafasi hiyo kumwambia kuwa anamwitaji awe naye.

Damaso alienda tena kulala mpaka asubuhi hakuota tena ndoto ya aina hiyo.

Baada ya kujiandaa kwa ajili ya kwenda kazini kwake aliamua kumwandikia sms Mayasa " habari za asubuhi Mayasa? Natumaini u mzima, leo jioni kipindi unaenda kwako tafazali naomba unisubiri"

Mayasa baada ya kuiona sms ya Mayasa alishtuka sana,hakujua Damaso kwa nini amemwambia hivo naye akajibu,

"Niko poa Damaso, nitajitahidi kukusubiri ila nawe naomba usichelewe"

"Mimi leo nitafunga mapema sana kwa ajili yako, ni muhimu sana leo mimi kuonana na wewe"

"Aya poa badae!"



Ilipofika jioni kwenye majira ya saa kumi hivi,Damaso alisitisha kila kitu kazini kwake na akaamua kuaga na kumwacha mfanyakazi mwenzake maana walikuwa wawili sehemu hiyo alipokuwa anafanya kazi zake.

Damaso alipofika maeneo ya ofisini kwa Mr Makalanga wala hakutaka kujionesha,alipita akaenda hadi mbele kidogo hivi kuna sehemu fulani hivi huwa wanauza vinywaji baridi.Akakaa hapo kisha akaagiza soda.Akamtumia sms Mayasa kuwa ameshafika na yupo maeneo hayohayo ila ni kwa mbele kidogo wanakouza vinywaji. Mayasa naye alijibu kuwa amsubiri kama dakika kumi na tano hivi atakuwa teyari naye 'ameshatia timu uwanjani'.

Mayasa kama alivyoahidi, baada ya dakika hizo kupita aliweza fika ile sehemu na kumkuta Damaso.Damaso alimwambia naye aagize kinywaji. Mayasa akaagiza naye soda.



Damaso alianza kumwambia Mayasa ,

"Samahani sana Mayasa kwa kuupoteza muda wako,pengine muda huu ungekuwa unafanya mambo yako mengine lakini mimi ndio nitakuwa nimevuruga mipango yako,kwa hiyo samahani sana sana"

"Usijali Damaso, haina shida kuwa na amani tu wala hujapoteza muda wangu"

"Oooh sawa! Nashukuru kusikia hivyo, Mayasa naomba usichukie kwa yale nitakayokuuliza au niseme tu maongezi yote kwa ujumla wake wala usiyachukie "

Mayasa akatumbua macho kisha akamuuliza Damaso " kwa nini umesema hivyo?"

"Nimesema hivyo kwa sababu labda maneno yangu yanaweza yakakukwaza kwa namna moja au nyingine,,ndio maana nimekuomba wala usichukie ikitokea nimekukwaza"

"Anhaa!! Haya nakusikiliza"

Damaso kwa utulivu mkubwa na umakini wa hali ya juu akaanza kumweleza alilomwitia Mayasa siku hiyo " Mayasa ni kipindi kifupi tu tangu nimejuana na wewe,na unaweza ukashangaa kwa nini nitakuuliza swali lifuatalo; Hivi Mayasa una mume?"

"Mmmmh! Kwa nini unaniuliza habari za mume?"

"Utajua tu sababu Mayasa,ila tafazali kwa sasa naomba unijibu tu"

"Hapana sina mume"

"Kwa nini?"

"Kwa nini? Heeeh Damaso unataka nikupe jibu gani?"

"Yaani lengo nijue kwa nini huna mume,yaani hutaki au bado hujampata au nini sababu?"

"Ni kwa sababu sijamuona wa kunioa"

"Oooh kwa hiyo ukimuona?"

"Nitafikilia kama ni wakati sahihi au la!"

" kwa hiyo hujawahi kuwa na hata mchumba?"

"Sijawahi kuwa naye"

"Nashukuru sana kwa majibu yako na lengo langu la kukuita hapa ni kutaka kujua hayo tu"

"Mmnnh!! Kwa hiyo baada ya kujua?"

"Basi tu hivyo yaani nijue tu"

"Mmmh !! Aya sawa kama ndo ivyo sijui naweza kuondoka, si umemaliza?"

Damaso alihitaji kumwambia Mayasa kuwa anamwitaji ila alihisi Mayasa atamuona yeye ni mtu wa ajabu sana kwani ni muda mfupi tu tangu wamekutana, Damaso alisahau kuwa mapenzi hayana dakika wala saa ni muda wowote ule yanatokea na yakitokea huwezi kuyazuia, jambo hili Damaso alilisahau kabisa.

Damaso naye akamjibu Mayasa ,

"mimi nimeishiwa cha kukuliza tena ni hayo tu labda kama wewe una chochote unaweza niambia"

"Mimi sina chochote ila umenishangaza sana kwa ulichokifanya leo"

"Mmmh kivipi Mayasa? "

"Sasa wewe maswali yote hayo kumbe huna sababu ya kutaka kuyajua?"

"Mayasa kuna jambo lingine la msingi nilitaka kukuambia ila tatizo muda naona muda ushaenda sana alafu kwako mbali nahisi utachelewa"

"Aya poa mimi naenda basi"

Damaso akaagana na Mayasa kisha kila mmoja akaelekea na njia yake.

Damaso akiwa kwake nyakati za usiku taswira ya Mayasa ilikuwa inamjia na alijiona mwanaume muoga kuliko wote duniani kwa kushindwa kumwambia ukweli Mayasa wakati ule.

Akachukua simu akamtumia ujumbe Mayasa ,

"Leo nimefurahi sana kuongea na wewe ingawa nilikuwa na jingine kubwa zaidi amabalo sikuliongea"

Mayasa alikaa kimya bila kujibu.Damaso aliingiwa na wasiwasi kuwa labda Mayasa amekasirika kwa yale ambayo amemuuliza.

Damaso akatuma tena sms nyingine,

" samahani sana kwa usumbufu inawezekana umenichukia sana leo kwa yale niliyokuuliza"

Mayasa pia hakurudisha ujumbe wowote. Damaso alianza kuhangaika na kuingia katika vita ya mawazo mazito juu ya ukimya wa Mayasa. Lakini kubwa alilowaza ni kuzani kuwa Mayasa alichukia sana yale aliyomuuliza. Mawazo ya Damaso ya kumtaka Mayasa yaliyeyuka ghafla na akawa anawaza jinsi ya kumuomba msamaha Mayasa kwa alichokisema kwake.Ukimya wa Mayasa ulizidi kumchanganya sana maana Damaso alianza kuweka uhakika kuwa atakuwa mume wa Mayasa lakini kwa kutojibu sms zake alijua ni kwa jinsi gani Mayasa amechukia.Alijilaumu sana juu ya haraka haraka zake kwa Mayasa.Lakini pia Damaso alisahau ile methali ya ngoja ngoja.........

Akiwa anaendelea kuwaza na kuwazua simu yake iliingia ujumbe. Akaichukua ili ausome ujumbe huo..http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Unazani nani katuma ujumbe? Na kwa nini Mayasa hakujibu?



Baada ya kuangalia aliona jina la Mayasa.Alikaa vizuri ili ausome vizuri ujumbe huo, ujumbe ulikuwa unasomeka hivi ,

" samahani sana Damaso kwa kuchelewa kukujibu ujumbe wako, nilikuwa napika"

Kipindi anamaliza kusoma na huku akishusha pumzi ndefu sana,baada ya dakika moja ikaingia sms nyingine ya Mayasa,



"Hivi ni kwa nini kila mda unapenda kuniomba msamaha hali ya kuwa hujanikosea?"



"Huwa nafanya hivyo ni kwa sababu moyo wangu unaogopa sana kukukosea na kukuchukiza pia"

"Mmmmh, Damaso wewe yaani una maneno mengiiii!!"

"Aaaah! Kawaida tu Mayasa, wala sina maneno mengi....mbona wapangaji wenzangu wote wananiambia mimi ni mpole tu!!"

"Aya bana kuwa na amani,mimi hata hujanikwaza kwa chochote niko poa tu"

Damaso alikaa kama dakika tatu hivi bila kurudisha ujumbe kwa Mayasa ila baadae akatuma ujumbe,

"Mayasa hivi unajua kama wewe ni mzuri sana?"

"Yaweza kuwa ni kweli ulisemalo na pia isiwe kweli, kwa kawaida kila mtu huwa anajiona mzuri yeye kama yeye,ingawa watazamaji nao huwa na mitazamo waangaliapo....”



"Oooh sawa vip lakini umewahi kuambiwa na mtu yeyote kuwa wewe ni mzuri sana?"

"Hapana sijawahi,kwani wewe unanionaje?"

"Ndo maana nilianza kukuambia kuwa wewe ni mzuri,,kama hujawahi kuambiwa wewe ni mzuri basi watu walikuwa wanakuonea wivu tu,,wewe ni mzuri sana"

"Oooh! Kumbe!"

"Tena wewe sio mzuri tu pia hata tabia zako ni mzuri pia,nimegundua wewe ni mkarimu sana na una upendo wa hali ya juu"

"Mmmh Damaso! Yaani wewe leo umeamua kunichambua ..enhee endelea"

"Sio hivyo tu,ata unavyoongea unatia hamu ya kukusikiliza,ukicheka ndo kama usiache vile, kiufupi wewe una sifa nyingi za kuwa mama bora wa familia"

"Mmmmh labda! ,ila mimi najiona nipo kawaida tu"

"Mayasa, nikuambie kitu?"

"Kipi?”

"Naomba jumapili hii uje upaone nyumbani kwangu ninapoishi"

" ooh, nitaangalia kama nitakuwa na muda,ukipatikana nitakuambia"

"Kwa nini unasema kama ukipata muda?"

"Mimi nipo chini ya uangalizi wa dada yangu,,hivyo ratiba nyingi nimekuwa nikipangiwa tu na wale ninaokaa nao"

"Anhaa! Poa nimekuelewa ila jitahidi upate huo muda ili hiyo siku upajue kwa Damaso"

"Aya poa usiku mwema Damaso"

"Poa poa nimefurahi sana leo, nawe pia usiku mwema"



Baada ya hapo, Mawazo ya Damaso yakarudi kama mwanzo kabisa akaanza kuwaza tena kuhusu Mayasa kuwa naye kama mke wake. Kwa jinsi Mayasa alivyokuwa anajibu sms za Damaso, Damaso alijihakikishia kuwa bila shaka Mayasa atakuwa wake muda si mrefu.Damaso hakutaka kumwambia mapema Mayasa juu kile anachowaza katika kichwa chake. Damaso alijua kula na vipofu,siku zote ukila na kipofu wala usimshike mkono usije ukamuuzi,mwache kipofu afanye atakalo lakini akijizuika unachukua kipande cha nyama kisha unakula bila ya yeye kujua.

Damaso alikuwa na moyo wa subra,juu ya Mayasa wala hakuwa na pupa sana.

Siku hiyo Damaso alilala usingizi mzuri sana.

Kwa upande wa Mayasa naye kwa kiasi fulani siku hiyo alilala usingizi mnono na wenye tabasamu bashasha.



Ilipofika siku ya jumamosi usiku, Damaso alimkumbusha Mayasa juu kukutana kwao siku ya jumapili. Mayasa alijibu kama alimvyomjibu mwanzo kuwa muda ukipatikana atamuona.Kilichokuwa kinampa ugumu Mayasa ni kwa namna gani ataaga kwake kuwa anaenda wapi,hilo ndilo lilokuwa linamsumbua Mayasa.

Siku ya jumapili ilipofika majira ya saa tano hivi alimwambia dada yake kuwa anataka aende kumtembelea rafiki yake ambaye wanajifunza wote kushona kwa MR Makalanga. dada yake alimruhusu na pia alimwambia awe makini kila anapoenda na kutenda chochote alimkumbusha maneno ya walioshi kabla yao kuwa ukitaka kuruka agana na nyonga.

Mayasa alifurahi ndani ya nafsi yake kuwa sasa ataenda kuonana na Damaso bila tatizo.Furaha ya Mayasa haikujulikana ilitokana na nini kwani hata alichoitiwa alikuwa hakijui, lakini yeye alikuwa na furaha bila kujua ni kitu gani kinamsukuma mpaka awe na furaha kiasi hicho.

Mayasa alimtumia ujumbe Damaso kuwa yupo teyari kwenda kwake siku hiyo. Damaso alifurahi sana na akamwambia anamtumia bodaboda itamchukua na kumfikisha hadi kwake.

Damaso alifanya usafi chumbani kwake na kutandika kitanda vizuri sana. Vitu vyake alipanga vizuri na kupulizia marashi.

Baada ya dakika thelethini mlango wa Damaso uligongwa na alipotoka nje alikutana na dereva bodaboda pamoja na Mayasa. Damaso alichukua 'buku mbili' akampa dereva bodaboda kisha akamkaribisha Mayasa ndani.

"Karibu sana Mayasa hapa ndipo ninapoishi"

"Asante ni pazuri"

"Aaah! Pazuri wapi nyumba za kupanga hizi!!"

"Hata kama nyumba ya kupanga mimi nimesifia uzuri wa chumba chako"

Chumbani humo, Damaso alitandika vizuri kitanda chake kwa shuka rangi ya 'pink' kukiwa sambamba na mito yake rangi hiyo hiyo. Kwa kuwa Damaso ni fundi selemala alitengeneza sofa zuri la watu wawili na kuliweka ndani mwake. Chini ya chumba hicho kulikuwa na kapeti zuri la drafti lenye rangi nyeusi na nyeupe. Pia Damaso aliweka televisheni 'TV' ndogo ya chogo na redio kubwa 'subwoofer'. Kwa ufupi chumba cha Damaso kilikuwa kinavutia ukikitazama.

Mayasa alishangaa sana uzuri wa chumba hicho na hii ni kwa sababu hakuwahi kukiona chumba kama hicho kabla ya siku hiyo.

Damaso alimuuliza Mayasa kama atatumia kinywaji amfuatie maana nyumba aliyokuwa anaishi Damaso ilikuwa na duka kwa mbele hivi. Mayasa alisema amletee soda.

Dakika chache tu Damaso alileta soda na kuifungua kisha akampatia Mayasa.

"Mayasa karibu sana"

" Asante"

"Alafu mbona unaonekana kama mnyonge hivi,nini tatizo?"

"Mmmh! Hujanizoea tu,mimi ndio nilivyo hivihivi"

"Mmh kweli au una wasiwasi?"

"Walaaa! Hata sina wasiwasi"

Mayasa alikuwa amekaa katika sofa na wakati huo Damaso naye akakaa kwenye kitanda chake alichokitandika vizuri ambacho kilikuwa kinavutia wakati wote kukiangalia na hata kukilalia. Kwa jinsi kilivyokapendeza kitanda hicho bila shaka hata wale wasiopata usingizi mapema endapo wangekilalia kitanda hicho basi ndani ya dakika chache tu usingizi ungewachukua na wangelala fofofo.

Damaso akajichekesha na kumwambia Mayasa kuwa amependeza sana na hii ndio kawaida ya wanaume wengi kusifia sana hata pasipohitajika kusifia ili mradi tu wanawake wajisikie wenye furaha. Mayasa akasema,

" Damaso acha uongo bana,nimependeza wapi ? Mbona nipo kawaida tu!"

"Labda kama unajiona! ,ila mimi si ndio ambaye nakuona hapa,hongera sana, vipi lakini uko poa?"

"Ndio niko poa, sijui wewe"

"Mimi niko vizuri, vipi na huko utokako?"

"Hawajambo tu"

"Vipi hawajanisalimia?"

"Wakusalimie kwani wanakujua?"

"Mmmh Mayasa!!! Kwani ulivyotoka kwako umeaga unaenda wapi?"

"Kwa rafiki yangu tena wakike,mimi si nilishakuambia kuwa nipo chini ya dada yangu hivyo nisingeweza kumwambia nakuja kwako,kwanza angenishangaa sana na maswali yangekuwa mengi,bila shaka usingeniona leo huku”

"Mmmmh! Kwanini lakini unamuogopa hivyo dada yako,ila tuachane na hayo, hivi Mayasa hapa mjini ndio ulipozaliwa?"

"Hapana"

"Wapi sasa?"

"Kuna kijiji kinaitwa Luponda"

"Mmmh, mbona mimi pia nimezaliwa jirani tu na kijijini chenu kinaitwa Mnero"

"Ooh kumbe wewe Damaso ni mmwera wa kulekule kwetu?"

"Hapana mimi ni Mmakua wazazi wangu waliamia Mnero zamani kidogo wakitokea Masasi."

"Na huku mjini ulifikaje?"

"Mayasa , iko ivi baada ya kumaliza darasa la saba nilifaulu kwenda sekondari ila kwa bahati mbaya wazazi wangu hawakuwa na uwezo wa kunipeleka shule ,sikuwa na namna nyingine ya kufanya zaidi ya kujishughulisha na ufundi,nilianza ufundi kulekule mnero ila niliamia mjini Nachingwea baada ya kuona wazazi wangu wananilazimisha sana kuoa"

"Kumbe historia yako kidogo inataka ifanane na yangu mimi asee!!"

"Mmmmh kivipi Mayasa? "

"Mimi nilifaulu kwenda sekondari ila wazazi wangu walikataa kunipeleka shule hivyo basi walitaka niolewe ila bahati mzuri haikutokea hivyo"

"Ooh pole sana, ila mimi nilikuwa ninaishi na babu na bibi wazaa mama nikiwa kule mnero, mama yangu aliondoka kwenda Mwanza baada ya kutengana na baba na baba naye yupo Mtwara mjini sasa, ila kabla hawajatengana wakiwa pamoja walikuwa wakinilazimisha sana kuwa na mke, na mke mwenyewe eti ni mtoto mmoja hivi wa jirani yetu,mimi nikaona ni ujinga, nilikuwa na kuku wangu wengi kiasi hivi nikawapiga bei wote na nikatimka kuja huku ila siku hizi king'ang'anizi mkubwa ni huyo bibi yangu, yaani kila nikimtembelea hakosi kuniambia habari za mke na mjukuu"

"Damaso jamani kwa nini unamtesa bibi yako si uoe tu!"

"Haaa haaa Mayasa nitamuoa nani sasa?"

"Si utaoa mwanamke?"

"Yuko wapi sasa?"

"Si wamejaa tu mitaani huko?Kwani Wewe huwaoni?"

"Haa haaa kwani kila mwanamke aliye mtaani anafaa kuolewa?"

"Ndio wanafaa..”

“Hapana,sio kweli ,wenye sifa ni wachache”

"Lakini si unajua hakuna binadamu yeyote aliye mkamilifu?

"Ni kweli Mayasa ulisemalo lakini wanawake bora wanaostahili kuolewa kama wewe wapo ila ni wachache sana"

Mayasa alicheka sana kisha akasema,

"kwani mimi ni bora kuolewa?"

Kwa tabasamu lenye hamasa, Damaso alimwambia Mayasa "haswaa wewe bora kati walio bora"

Ukatokea ukimya kidogo humo chumbani mwa Damaso , huku kila mmoja asijue aanzie wapi kumsemesha mwenzake. Damaso kama kawaida kichwa chake wakati huo kilikuwa kinawaza jinsi ya kumwambia Mayasa kile anachowaza juu yake.

Ila kilichomtia hofu Damaso kumwambia mapema ni sura ya Mayasa ilivyokuwa inaonekana kwa wakati huo, yaani Mayasa alionekana ni mtu ambaye alikuwa anamchukulia Damaso kama kaka tu wala hakuonesha hisia zozote za kimapenzi kwa Damaso , na labda hili lilisababishwa na kutokuwa na uzoefu na mambo hayo ya mapenzi kwa upande wa Mayasa na ndio maana alikubali kwenda na kuingia chumbani kwa Damaso bila hofu ya kutokea chochote. Kwa upande wa Damaso naye hakuwa hodari kwenye mambo hayo, alikuwa sawa na simba mzee huwa analetewa nyama na simba vijana lakini yeye mwenyewe akiwa mawindoni wala hana mshikemshike.

Waliendelea kukaa kimya huku kila mmoja akiwa anachezea simu yake. Baada ya ukimya mrefu kutawala ndani ya chumba hicho Mayasa akasema,

" Vipi Damaso mbona upo kimya sana?"

"Hamna sema nilikuwa nachati na jamaa mmoja hivi alikuwa ananiulizia kazi yake fulani hivi alinipa niifanye"

Damaso alijikakamua na kumwongopea Mayasa ili asionekane kama aliishiwa maneno 'swaga'.

"Anhaa!! Maana niliona upo kimya sana hadi nikapata hofu,hivi umesema unakaa na wifi yangu humu?"

Mayasa alimuuliza Damaso swali la kichokozi hali ya kuwa Damaso alishawahi kumwambia Mayasa kuwa anaishi pekee yake. Damaso alimwangalia Mayasa kwa muda kisha akacheka tu ila kichecko cha tabasamu pana.

Mayasa akasema,http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

" mbona unaniangalia na kunicheka?"

"Sasa Mayasa kweli humu kama mungekuwa na mke si ungeona hata kanga?

"Kwa hiyo lini utaoa unipe kadi ili nikuchangie?"

"Mmmh! Mayasa Mayasa mbona una haraka ya mambo kiasi hicho?"

"Hapana sina haraka si nakuhimiza tu jamani kama unavyohimizwa na bibi yako!"

Damaso aliishia kutabasamu tu bila kusema kitu lakini wakati huo akiwa na wazo la kumwambia mke mwenyewe ndiye yeye Mayasa ila jinsi ya kuanza ndio alikuwa anashindwa, Damaso hapo alikuwa sawa na golikipa kuanzisha mpira katikati ya uwanja wakati kipindi cha kwanza kinaanza, ni vigumu sana, zaidi zaidi wataanzisha washambuliaji.

Damaso alikuwa na kauoga fulani kumwambia ukweli wa moyo wake unataka nini, labda Damaso angekuwa mzee wa viwanja basi angeujua huu msemo wa watoto wa mjini ambao wao wanasema 'uoga wako ndio umaskini wako'.







ITAENDELEA 

0 comments:

Post a Comment

Blog