Simulizi : Umutwali
Sehemu Ya Pili (2)
“Habari.... Karibuni sana.”
“Ahsantee,” Familia ya Mzee Zungu wote wakaitika.
“Niwasaidie nini, tafadhali?,” Mhudumu akauliza.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Tuletee, chipsi kuku,” Baba Donald alijibu kwa niaba ya familia.
“Sawa nitaomba mtuvumilie dakika chache tu, chakula chenu kitakuwa tayari.”
“Sawa hakuna shida, ila isichukue muda,” Mama Donald akasema.
Mhudumu baada ya kuchukua maelezo akaelekea jikoni akatoa agizo kwa mwenzake kuwa vyakula viandaliwe, baada ya muda mhudumu akarejea tena kwetu na vyakula alipofika akagawa sahani za chipsi kwa kila mmoja. Alipogawa vyakula akataka kuondoka lakini akasitishwa na wito wa Mzee Zungu.
“Mhudumu, naomba tuletee na vinywaji. Tafadhali” lilikuwa ni agizo kutoka kwa Baba Donald.
“Sawa.... Naleta...lakini ningependa kujua mnatumia vinywaji gani?,” Kabla ya kwenda kufuata vinywaji mhudumu akauliza.
“Mimi na mke wangu tuletee HEINKEN za baridi mbili...na wananguuu?. Hebu wasikilize wenyewe,” Mzee Zungu akazungumza.
“Tuletee KINGSLEY mbili za bariidi za pineapple,” Donald alidakia mara baada ya kumuona Dada Angel akimtupia jicho aseme.
Mhudumu akaondoka mbiombio na kwenda kuvifuata vinywaji huku nyuma Donald na familia wakiendelea kula na kunywa tena wakipiga soga na mzaha wa hapa na pale.
“Huyu naye kila siku Kingsley Kingsley, si ungesema hata Azam Tropical.!!,” Dada Angel akanitania.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ha! ha! ha!. Ndio ulevi wenu huo wala msishushuane,” Mama Donald alidakia huku akicheka.
Baada ya dakika chache tu mhudumu akaleta vinywaji nasi tukashushia kusindikiza shibe. Siku ile SUN CIRRO HOTEL ilichangamka kwani kulikuwa na burudani kabambe kutoka bendi ya FM ACADEMIA iliyokuwa ikitumbuiza. Walipomaliza kunywa wakati wa kuzipumzisha nafsi na kuingoja shibe ishuke taratibu wakahamua kugeuka kutazama FM ACADEMIA wanavyotupa burudani. Wakatazama na kuburudika hadi majira ya usiku wa saa mbili, ndipo Mzee Zungu akahimiza familia iondoke kwani muda haukuwa rafiki kuendelea kusalia eneo lile.
“Muda umekwenda sasa, tuondokeni,” Mzee Zungu alisema huku akiinuka kitini.
Wote wakakubaliana wakaanza kuelekea ilipo parking nje ya jengo la SUN CIRRO HOTEL, wakaingia ndani ya gari kisha Mzee Zungu akachukua jukumu la udereva tayari akaanza safari ya kurudi nyumbani. Safari hii Ubungo hakukuwa na foleni kama mwanzo hivyo ikapelekea wao kuwahi kufika nyumbani, na kwa kuwa hawakuwa na njaa hivyo kila mmoja alipofika nyumbani akaelekea chumbani kupumzika. Donald alichoka akalala fo fo fo akaja kushtuka asubuhi ya siku ya Jumapili kukiwa tayari kushapambazuka, akaingia bafuni kuoga na alipotoka akaelekea kwenye kabati la nguo akachagua shati la mikono mirefu lenye rangi ya bluu na suruali ya kitambaa cha mtelezo yenye rangi nyeusi. Akatoka chumbani baada ya kuvaa nguo akaelekea sebuleni, wakati huo Dada Angel hakuamka bado. Basi akachukua jukumu la kujiandalia na kujitengea chai alipomaliza kunywa akatoka ndani akaanza safari ya kwenda kanisani. Kiujumla familia yakina Donald ilikuwa ni dhehebu la Roman Catholic hivyo Donald akakamata njia ya kwenda kanisa la katoliki la MAVURUNZA lililopo Kimara Suca jirani na barabara kuu, akiwa njiani hajafika kanisani akakutana na wazazi wakiwa kwenye usafiri nao wakitoka kanisani. Wazazi wakasimamisha gari pembezoni mwa barabara ya vumbi, wakamuita Donald.
“Donald!!,” Wazazi wote kwa pamoja wakamuita Donald.
“Naam,” Donald akaitika.
“Unaenda kanisani?,” Baba Donald alihoji huku akijifuta jasho kwa leso mara baada ya Donald kufika walipopaki gari.
“Yes, daddy,” Donald alijibu huku akionyesha kama kutabasamu.
“Ni vizuri...lakini sadaka unayo?,” Mama Donald nae akahoji. Swali lile likamfanya Donald ajipapase mifukoni athibitishe kama pale pesa anayo au lah, kujipapasa akagundua kwamba sadaka alisahau.
“Hapa, hapana...sina,” Donald alijibu kwa kigugumizi kama mtu mwenye kigugumizi alichozaliwa nacho.
Mama Donald baada ya kusikia jibu la Donald akachukua pochi yake ndogo “Handbag” akaifungua akatoa noti mbili za elfu tano akamkabidhi Donald. Donald alipopatiwa zile noti wazazi wakamuaga kisha wakaondoa gari wakaelekea nyumbani, nyuma wakamuacha Donald akiendelea na safari ya kwenda kanisani. Baada ya muda mfupi akawasili kanisani akiwa kwenye hali ya unyenyekevu na utulivu wa tayari kusikiliza neno la Mungu mpaka pale ibada itakapokwisha. Alipomaliza ibada akaongoza moja kwa moja kurudi nyumbani, kufika akawakuta wazazi wakitazama runinga.
“Shikamo’ni,” Donald akaamkia.
“Marahaba...ibada imeendaje?,” Mama Donald aliuliza mara baada ya kupokea salamu ya Donald.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Imekwenda, vizuri tu.”
“Sawa...nenda kale sasa,” Mama Donald alimaliza kwa kusema.
Donald akaenda moja kwa moja dinning kupata chakula, na baada ya kula akaenda chumbani. Akaingia chumbani kubadili nguo na alipobadili akahamua kuchukua nguo za shule “Uniform” kwa ajili ya kufua. Akafua akaanika hatimaye akarejea tena chumbani kupumzika, akalala hadi muda wa jioni hapo akahisi mlango wa chumbani ukibishwa hodi. Akaamka haraka akaelekea kufungua mlango, alipofungua tu akakutana na Dada Angel amesimama mlangoni huku akiwa ameshikilia nguo za shule mkononi.
“Donald, nguo zako tayari zishakauka...chukua,” Dada Angel aliongea huku akimkabidhi sare za shule Donald.
“Asante sana...maana nilipitiwa na usingizi na mimi mwenyewe nilishasahau,” Donald alizipokea nguo kisha akarudi chumbani kwa ajili ya kupasi. Akamuacha Dada Angel nae akienda chumbani kujipumzisha.
Yote yalikuwa ni maandalizi kwaajili ya kujiandaa kwenda shule, akanyoosha sare za shule hadi usiku wa saa mbili. Baada ya zoezi hilo akatoka chumbani akaelekea sebuleni kutazama tamthilia ya MERLIN iliyokuwa ikirushwa kwa wakati huo katika chaneli ya ST KUNGFU, Dada Angel yeye alikuwa jikoni kwa wakati huo akirekebisha chakula cha usiku. Na kwa wakati huo pia wazazi wa Donald walikuwa wamechoka hivyo wakahamua kuingia chumbani kupumzika. Ilipotimu saa tatu ya usiku chakula kikawa tayari kishaiva na Dada Angel akakitenga dinning kisha akamuita Donald akale.
“Namaliza kipande hiki, nakuja!!,” Donald alisema mara baada ya Dada Angel kumkaribisha chakula. Itiko na tamko la Donald likafanya Dada Angel hasishughulike nae tena, akaenda moja kwa moja kwenye chumba cha wazazi kuwaamsha kwa ajili ya kula nao.
“Ngo, ngo, ngo,” Dada Angel alibisha hodi mara baada ya kufika katika mlango wa chumba cha wazazi.
“Nani wewe...Angel?,” Mama Donald aliuliza apate kumjua mtu aliyebisha hodi.
“Ndiyo mimi, Angel...nimekuja kuwaambia chakula tayari,” Dada Angel alijibu kwa utiifu.
“Asante kwa kutuhabarisha...kaanzeni kula sisi tutakuja,” Baba Donald akaongea.
Dada Angel baada ya kujibiwa akarudi dinning akamkuta Donald ameshamaliza kuangalia kipande chake cha tamthilia amehamia dinning kula chakula, Dada Angel akajumuika mezani na Donald punde wazazi wakaja nao kuungana na kina Donald. Wakajipakulia chakula kisha wakaanza kula.
“Wanangu, kama hamjatosheka chakula ongezeni,” Mzee Zungu alisema mara baada ya kuona kina Donald wanakaribia kumaliza chakula, Donald akatazamana na Dada Angel kidogo kisha wote kwa pamoja wakamwambia Mzee Zungu huku wakikombeleza kichele kilichosalia.
“Tushatosheka.”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Donald na Dada Angel wakanawa mikono baada ya kumaliza kula, Dada Angel akaenda kuketi sebuleni huku akiwasubiri wazazi wamalize kula ili atoe vyombo akavioshe. Na kwa kuwa Donald hakufunzwa kukaa na kuwatazama wazazi wakiwa wanakula ikamlazimu awaage wazazi akaenda chumbani. Wazazi walipomaliza kula Dada Angel akatoa vyombo akaelekea kuosha, baada ya kumaliza kuosha nae akawaaga wazazi akaingia chumbani kulala nyuma akiwaacha wazazi wakiendelea kupiga soga pale dinning. Baada ya muda nao wakachoka kupiga soga wakanyanyuka vitini wakaingia chumbani kupumzika. Donald akiwa chumbani akachomeka simu chaji kwa muda akachomoa akaingia katika mtandao wa FACEBOOK, Fatuma kwa kuwa alikuwa rafiki wa Donald hadi Facebook hivyo Donald alivyoingia tu online akamuona Fatuma akamchokoza kwa jumbe fupi.
“Ulali?.”
“Wewe umelala?,” Fatuma nae akarejesha ujumbe akiuliza swali. Wakaendelea kuchati.
“Mimi, ndiyo nataka kulala hivyo.”
“Sawa, ukilala nami nitalala.”
“Duh...halafu Fatuma, urafiki wetu wa muda kidogo cha kushangaza hatujapeana hata mawasiliano wala nini. Naomba nipatie basi mawasiliano yako.”
“Wewe tu hukuzitaka namba zangu ungezitaka tokea muda ningekutumia, ila usijali kwa kuwa leo umezitaka basi chukua hizi 0685276697,” Fatuma alituma jumbe ya mwisho kisha akaonekana kutoka online. Donald kuona vile hakuchelewa nae akatoka Facebook akahifadhi namba ya Fatuma kwenye simu baada ya zoezi hilo akahamua kupiga, mara moja simu ikapokelewa kisha sauti nzuri ya kike ikasika.
“Nilijua utalala,” Fatuma akaongea.
“Siwezi kulala...na hata nikilala huo usingizi utakuja vipi wakati sijatimiza dhamira yangu,” Donald akazungumza.
“Dhamira gani tena hiyoo, Donald?.”
“Fatuma,” Donald aliita kwanza ili kuteka umakini wa Fatuma.
“Abee..!!.”
“Ujue ni muda sasa nina dhamira juu yako lakini nimeitunza tu moyoni, nikiamini kuna siku nitakueleza...na leo ndio siku muafaka.”
“Mh!. Dhamira ipi hiyo Donald?. Nieleze basi.”
“Dhamira yenyeewe...daah sijui utanielewa.”
“Kwanini nisikuelewe, wewe nieleze tu.”
“Fatuma mie nakupenda, neno nakupenda ndiyo lilikuwa kusudio langu kuu nililokaa nalo moyoni na ndiyo nililotaka nikueleze siku zote hizo...naomba nikubalie Fatuma,” Ukimya ukatawala kwa Fatuma mara baada ya kuelezwa na Donald dhamira kuu, ukimya ule ukasadifu dhahiri ya kwamba Fatuma alikuwa anajifikiria baada ya muda kidogo Fatuma akasikika akicheka kicheko kilichoambatana na kikohozi cha kinafki. Hatimaye akaongea.
“Sasa Donald, kusudio lako mbona hujalieleza mapema?.”
“Unamaanisha....?.”
“Mie, ninaye nimpendaye mwaya,” Ghafla moyo wa Donald ukalipuka mara baada kusikia maneno yale kutoka kwenye kinywa cha Fatuma. Akahamua kuuliza.
“Ni nani?.”
“Niii...,” Fatuma kabla hajamtaja Donald akahisi kizunguzungu sasa akimtaja si atazirai kabisa akamkatisha asimtaje.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Basi, si lazima umtaje utaniumiza mwenzio.”
“Lakini Donald ni vizuri tu ukajua jina la shemeji yako, pengine unaweza pata mtoto ukamuita jina hilo” aliongea Fatuma kwa utani.
“Hapana usinitajie...nitakufa,” Lakini Fatuma akajifanya kama hajasikia akataja jina hilo la mtu ampendae.
“Nimpendae jina lake ni, Donald,” Donald alishtuka kidogo mara baada ya kutajiwa lile jina. Akauliza.
“Donald!!!.... Donald gani?.”
“Donald Mtalanze,” Donald alifurahi sana kusikia jina la ampendae Fatuma. Akaongea kwa furaha.
“Fatuma, unamaanisha nawe unanipenda mimi...siamini.”
“Yakupasa sasa uamini, Donald nakupenda tena sana.”
“Nashukuru sana, Fatuma.”
“Haina haja ya kushukuru kwa maana wote tumependana...lakini kabla ya yote naomba nisamehe sana Donald kwa kukurusha moyo maana ulikuwa si ukweli bali ulikuwa uongo tu,” Fatuma alitaka radhi mara baada ya kugundua kosa.
“Usijali,” Donald aliongea huku akiwa moyoni ana furaha tele mara baada ya kusikia Fatuma nae anampenda.
“Asante sana...lakini huu ni usiku heri tuongee zaidi kesho, usiku mwema Donald,” Fatuma alimtakia usiku mwema Donald kabla hajakata simu.
“Nawe pia...ukilala niweke karibu yako nilale nawe.”
“Ondoa shaka tutalala pamoja ili usiku wetu uwe mzuri...lala sasa ili kesho tuwahi shule, si unakumbuka kuwa kesho ni zamu ya Sir Daniel tusipowahi tutaadhibiwa,” Fatuma akahabarisha.
Baada ya maongezi Fatuma akakata simu. Donald akachomeka tena simu chaji iendelee kuchaji, akazima taa akarejea kitandani kwa kujitupa. Haikuchukua muda usingizi ukamchukua akaja kushtuka pindi baba yake alipobisha hodi mlangoni mwake. Donald akajinyoosha viungo huku jicho akilitupa dirishani akijaribu kuangaza aone kulivyopambazuka, akaona kumepambazuka akaelekea kufungua mlango.
“Shikamoo,” Donald aliamkia mara baada ya kufungua mlango na kumkuta Mzee Zungu mlangoni.
“Marahaba...kumekucha salama?,” Mzee Zungu aliuliza huku akifunga taulo kiunoni vyema.
“Nashukuru Mungu, kumekucha salama,” Donald alijibu huku akijaribu kufikicha macho yaliyojaa ukungu.
“Hakika tunapaswa, kumshukuru Mungu kwa kutuamsha salama na kwa kila kitu.”
“Haswaaa.”
“Achana na hayo...jiandae tuongozane ninapotoka na mama yako kuelekea kazini nawe uende shuleni,” Mzee Zungu alimhabarisha Donald na mwisho akaingia chumbani kujiandaa. Akamuacha Donald akiingia chumbani nae akajiandae. Donald akajiandaa akachomoa simu chaji akaizima akaiweka kwenye droo ya kitanda kisha akatoka chumbani akaelekea kwenye mlango wa chumba cha wazazi kugonga hodi.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nani?,” Sauti ya Mama Donald ikasikika ikiuliza mara baada ya kusikia mtu akigonga mlango wao.
“Ni mimi, Donald,” Donald alijibu huku akisimama pale mlangoni akisubiri mlango wa wazazi ufunguliwe. Mlango ukafunguliwa.
“Shikamoo,” Donald alitoa salamu kwa mama yake mara baada ya Mama Donald kufungua mlango.
“Marahaba...umeamshwaje?,” Mama Donald aliuliza huku akijikuna nywele mara baada ya kuhisi muwasho kichwani.
“Nimeamka salama,” Donald akajibu.
“Ushajiandaa?.”
“Ndiyo.”
“Kama umejiandaa tusubiri kidogo, maana mimi na baba yako ndiyo tunamalizia kujiandaa.”
Donald moja kwa moja akaelekea sebuleni kuwasubiri wazazi, wakati huo Dada Angel bado hajaamka. Donald basi kwa kupoteza muda akaelekea hadi sebuleni sehemu iliyohifadhi vitabu vya mama yake akachagua kitabu kimoja kinachoitwa MAKILANABE kilichoandikwa na kutungwa na SADARI KISESA, akakisoma huku akivuta subira kwaajili ya kuwangojea wazazi.
“Tunakwenda kazini, ila tutachelewa kurudi leo,” Donald akiwa bado sebuleni akiendelea kusoma kitabu. Akasikia sauti ya mama yake ikimueleza Dada Angel mara baada ya Mama Donald kugonga mlango wa Dada Angel na kufunguliwa na Dada Angel.
“Sasa, kuhusu chakula je niwawekee?,” Dada Angel akauliza.
Usituwekee, lakini kama kawaida muwekee Donald,” Safari hii Donald akamsikia baba yake nae akijibu swali la Dada Angel. Na mara akasikia vishindo vya kutembea vya wazazi vikija sebuleni.
“Umesubiri sana?” lilikuwa swali la Baba Donald alilomuliza Donald huku akichukua Briefcase aliyohifadhi juu ya kabati ya sebuleni.
“Yah..nimewasubiri sana hadi nimeanza kujisikia uvivu,” Donald alijibu huku akifunika kitabu kisha kukihifadhi kwenye droo la vitabu lililopo pembezoni mwa kabati la vyombo pale sebuleni.
Baada ya kukiweka kitabu akaongozana na wazazi hadi kwenye parking ya nyumbani, wakapanda ndani ya gari na mwisho Baba Donald akaliondoa gari. Wakiwa njiani kwenye barabara ya vumbi wakikamata kituo cha daladala cha Suca, Mama Donald akauvunja ukimya.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Donald, ukitoka shule pitia kwa Fundi Castle umchukue uje naye nyumbani anitengenezee gari langu...maana ina siku kama ya tatu imeharibika,” Mama Donald akaelekeza.
“Sawa mama, nitafanya ulichoniagiza,” Donald akakubali.
Wakati mazungumzo yakiendelea wakawa washaingia barabara kuu. Baba Donald akazidi kukanyaga mafuta hadi walipokamata kituo cha daladala cha External, Baba Donald akasimamisha gari akamshusha Donald ndani ya gari kisha akatoa pochi “Wallet” mfukoni na kumpatia noti moja ya elfu tano Donald. Donald baada ya kukabidhiwa pesa Mzee Zungu akaliondoa gari akamuacha Donald akitafuta bodaboda ya kumpeleka shule, bahati nzuri Donald akaipata bodaboda ikampeleka hadi katika geti kuu la shule. Bodaboda ikaondoka mara baada ya dereva bodaboda kulipwa pesa, ikamuacha Donald akiingia eneo la shule. Akajongea kuelekea eneo la mstarini kabla hajafika ghafla akasikia kengele ya namba ikipigwa, haraka akakimbia kupanga mstari nae apate namba. Jumatatu ilikuwa ni zamu ya Sir Daniel basi Sir Daniel akawahi mno kuja shule siku hiyo kwaajili ya kusimamia zamu. Akawahesabu namba wanafunzi waliowahi alipomaliza akawaruhusu wanafunzi waende maeneo ya usafi, Fatuma yeye Jumatatu hiyo akachelewa maana Donald hakumtia machoni tangu afike shuleni. Hivyo Donald akawa mnyonge akimuwazia kipenzi lakini hata hivyo baada ya muda akajichangamsha akaendelea na usafi pamoja na rafiki yake anayefahamika kwa majina ya David Chipili. Wakiwa wanafanya usafi ghafla akashangaa kuona David akimshtua kwa kumgusa bega na kumfanyia ishara ya kumbinyia jicho kuwa ageuke nyuma aone.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment