IMEANDIKWA NA : ZULFA HUSSEIN
*********************************************************************************
Simulizi : Kazi Za Ndani Nchini Oman Zilivyonikutanisha Na Kifo

Sehemu Ya Kwanza (1)
ILIKUWA ni mara ya kwanza katika maisha yangu kupanda ndege. Licha ya kuwa na wasiwasi juu ya maisha ninayokwenda kuishi katika nchi ngeni ya Kiarabu, nchi yenye utamaduni na sheria tofuati na nchi yangu, hilo halikunifanya kutoona fahari kuwa ndani ya Fly Emirates Airlines iliyokuwa ikikata mawingu kwa kasi ya ajabu.
Nikiwa nimeketi katika siti ya dirishani ndani ya ndege hiyo kubwa. Niliyatupa macho nje, kupitia dirisha dogo ndani ya dege hilo. Niliona tupo katikati ya mawingu meupe yaliyozagaa katika anga na kuleta taswira kama shamba la pamba lililomea.
Nilijisikia raha isiyoelezeka.
Masikioni mwangu nilikuwa nimevaa visikilizio, nikisikiliza muziki mzuri wa Craig David uitwao ‘Walking Away’ uliokuwa unatokea kwenye ipod yangu kupitia kwenye visikilizo hivyo vya masikioni.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sikumbuki tulitumia muda gani kusafiri angani, ninachokumbuka baada ya muda mrefu kupita sauti ya mhudumu wa ndege kupitia spika zilizokuwa ndani ya ndege ilisema:
“We are about to land, all passangers of fly Emirates Airlines, wake up and make sure your belt is close”
Sauti laini ya kike ilisikika, aliongea kwa kimombo akimaanisha abiria tunatakiwa kufunga mikanda kwani ndege inakaribia kutua.
Ni sauti hiyo ndiyo iliyonistua, nikaangalia saa yangu ya mkononi ikanionyesha ilikuwa ni saa mbili usiku, nilifunga mkanda kama tulivyotakiwa, kisha nikatulia kwenye kiti, mapigo ya moyo yalianza kwenda kasi, hofu ikanijaa moyoni mwangu.
Maneno niliyoambiwa na mama kabla ya kupanda ndege hiyo yakijirudia akilini mwangu.
“Wasichana wanaokwenda kufanya kazi Oman, mara nyingi baadhi yao wanabakwa, wanamwagiwa maji ya moto, na hata kuuawa, kubwa kuliko vyote nchi ile inasheria kali dhidi ya makosa mbalimbali. ”
Sauti ya mama yangu ilikuwa ikijirudia akilini mwangu mara kadhaa tangu mwanzo wa safari hiyo.
Taswira ya mandhali ya kijiji cha Makose huko mkoani Tanga ilinijia kichwani, na wakati taswira ya kijiji inapita ubongoni mwangu ilikwenda sanjari na picha halisi ya maisha yangu nikiwa miongoni mwa wenyeji wa kijiji hicho kinachokaliwa zaidi na wakazi wa makabila ya Wasambaa na wapare waliojipenyeza wakitokea mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.
Baada ya kumaliza kidato cha nne nilikuwa miongoni mwa wanafunzi wachache waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano kwenye Shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa iliyoko jijini Dar.
Zilikuwa ni nyakati za furaha maishani mwangu pengine kuliko nyakati nyingine zozote, lakini ni nyakati hizohizo furaha yangu iligeuka na kuwa majonzi yasiyoweza kusahaulika kichwani mwangu.
Ilikuwa ni pale wazazi wangu niliponieleza hawawezi kunisomesha kwa kuwa hawakuwa na uwezo huo, tena mbaya zaidii nikiwa mbali na nyumbani.
“Hutuwezi kumudu gharama za kukusomesha mwanangu. Shule uliyofaulia ni shule ya kutwa. Hii inamaana kwamba, upangishiwe chumba, na upate huduma kama mwanamfunzi. Hiyo ni mbali na ada, sizungumzii nauli na mambo mengine ya shule...
Jambo baya zaidi, jiji la Dar lina sifa kuwa na gharama kubwa ya maisha.”
Sikubishana na ukweli wa maneno yale. Alichokisema mama kilikuwa sahihi kabisa, familia yangu ilinuka ufukara, mara kadhaa nilikuwa nikishuhudia tukishinda na kulalia uji usiyokuwa na sukari.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siyo mara moja kuchekwa nikiwa shuleni, lilikuwa ni jambo la kawaida kudharauliwa, hata kutengwa kwa kuvaa nguo za kuchanikachanika kiasi cha kutoa picha kamili ya kiwango cha ufukara ulionizingira.
Wala halikuwa jambo la kushangaza kuacha kwenda shule na kufanya vibarua kwenye mashamba ya wanakijiji, pesa kidogo iliyoipatikana ndiyo ilitumika kwa kula, kununulia madaftari na sare za shule.
Niliishi maisha ya kifukara tangu nazaliwa hadi nilipokuwa binti. Nikiwa msichana mrembo wa miaka 21 nilikuwa ni mtu mwenye ndoto na matarajio makubwa sana kama vijana wengine.
Nilisumbuliwa na wanaume wakware pale kijijini na baadhi yao, walitumia umasikini wangu kama njia rahisi ya kunipata. Ajabu nilikuwa na misimamo isiyoyumba. Niliamini mwanaume pekee atakayeujua mwili wangu ni yule atakayekuwa mume wangu. Kwa kweli nilikuwa ni mwanamke mwenye matarajio makubwa sana, lakini ndoto zote zilizimishwa na ufukara ulionizingira.
*
Niliyakumbuka hayo nikiwa nimetulia ndani ya ndege iliyotarajiwa kutua dakika chache katika nchi ya Oman. Nilitokwa na jasho lililotokana na hofu huku nikihisi tumbo likichemka kadiri tulivyokuwa tukiusogelea uwanja wa ndege wa Jijini Muscut nchini Oman.
Dakika chache badaye, ndege ilikuwa ikiserereka kwa kasi kwenye ardhi ya nchi ya hiyo. Baada ya kusimama, tulianza kuteremka abiria mmoja mmoja.
Nilipoikanyaga aridhini, nilijiona nikiwa kiumbe mdogo mithili ya sisimizi, utitiri wa magorofa yaliyojichomoza kama uyoga sambamba na barabara za flyover zilinifanya nijione kama ndiyo nakwenda kupotelea katikati ya Jiji hilo.
“Are you Agripina?” nilisikia sauti moja akinisemesha, nilipogeuka nilimwona mama mmoja mnene wa umbo, aliyevaa baibui sehemu yote ya mwili wake isipokuwa machoni pekee, mkononi akiwa na bango lililoandikwa jina langu.
“Yes. I’m Agripina, who are you?” nilimjibu nikimuuliza, mimi ndiye Agripina na yeye alikuwa ni nani.
“Naitwa Mariamu Rashidi, ninataarifa za ujio wako, mimi ndiye nitakuwa mwenyeji wako hapa Oman.”
Yule mama alisema kwa Kiswahili huku akipokea begi langu la nguo.
“Kumbe unazungumza Kiswahili?” Niliuliza kwa wahaka
“Ndiyo, mimi ni Mbongo kama wewe, tena ni Msambaa wa Milimani, natokea maeneno ya huko Lushoto kijiji cha Mlalo,”alisema.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa kweli nilifurahi kukutana na mwanamke yule anayezungumza Kiswahili kwenye taifa lile la Kiarabu tena akiwa anatokea kijiji jirani na chetu.
Hata hivyo, kwa muda mchache sana niliotumia kutambuna na yule mwanamke aliyejitambulisha kwa jina la Mariamu Rashidi, kuna mambo niliyoyagundua kutoka kwakwe, mambo ambayo yalinitisha vibaya mno.
Pamoja na kuwa na wasiwasi dhidi ya yule mtu, sikutaka kabisa kuonesha hali ya hofu waziwazi, wakati wote nilitengeneza uso wenye tabasamu bandia mbele ya macho ya mwanamke huyo.
Tulitoka nje ya uwanja ule na kuchukua tax kisha tukaanza safari ya kuelekea mahali nisikokujua.
Tulitumia nusu saa kufika sehemu iliyokuwa na nyumba nyingi, ambazo siyo tu hazikujengwa kiramani lakini pia zilikuwa ni nyumba zilizochoka. Nachelea kusema, ilikuwa ni ‘Uswahilini’ ya Oman.
“Hapa panaitwa Deira,” Mariamu alisema, tukiwa mbele ya nyumba moja iliyoonekana kuchakaa kwa kukosa ukarabati wa muda mrefu.
“Ndipo ninapoishi, lakini kwa sasa tutaishi wote kwa siku mbili. Nitatumia muda huo kukueleza sheria na taratibu za nchii hii kabla ya kwenda kuanza kufanya kazi za ndani.”
“Watu wanasema sheria za Uarabuni ni ngumu na kali sana?” nilimuliza.
“Hapana. Siyo ngumu. Inategemeana na wewe utakavyozipokea. Ukizipoea sheria za hapa katika mtazamo wa ugumu, kwa kweli utashindwa, lakini ukizichukulia kwa wepesi na ukazitekeleza, huwezi kupata tabu.”
Pamoja na maelezo ya Mariamu, bado hayakunifanya kutoogopa, matukio ya mabinti wa kitanzania kubakwa, kuunguzwa kwa maji ya moto wakati mwingine hata kusukumwa juu ya majengo marefu.
Sambamba na hayo yote, kila nilivyofikiria familia yangu. Familia iliyozingirwa na umasikini wa kupindukia. Nilijikuta napata nguvu hata kutoogopa lolote.
Taratibu za kisheria juu ya wasichana wa Kitanzania wanaokwenda kufanya kazi za ndani nchini Oman, tasisi ya ubalozi ilikuwa haiusishwi kabisa. Mambo mengi yalifanyika kinyamela.
Masaa arobaini na nane badaye, mimi na Marimu tulikuwa kwenye tax tukielekea sehemu moja iitwayo Suwaiq kilometa 50 kutoka mjini Muscut. Huko ndipo mahali nilipotakiwa kwenda kufanya kazi ni huko ambapo kulikuwa na familia ya tajiri aliyeitwa Abdallah Mustapha ambaye ndiye niliyetakiwa kwenda kuanza kazi nyumbani kwakwe.
“Karatasi za majibu yako ya vipimo vya hosptali unazo?” Mariamu aliniuliza wakati gari likikunja kushoto na kuiacha barabara kubwa ya lami na kuingia kwenye barabara iliyokuwa na changarawe nyingi.
“Karatasi zipo kwenye begi, kwani majibu ya vipimo, bado yanahitajika hadi huku?”
“Ndiyo” alinijibu kwa ufupi. Nilijiuliza moyoni inaamna huko niendako, wao waajiri hawajui kuwa siwezi kuwa kwenye nchi hiyo pasina kupima, vipi tena wahitaji majibu ya vipimo.
Wakati nikiwa bado najiuliza, gari lilikata kona na kuiacha ile njia yenye changarawe na kuingia kwenye njia nyembamba iliyokuwa na marumaru, pembeni ya njia hiyo kukiwa na miti mingi iliyopandwa kwa mpangilio mzuri.
Gari lilikwenda kwa mwendo wa taratibu. Mita kama ishirini tukawa mbele ya nyumba kubwa iliyokuwa na sifa zote za kuitwa nyumba ya kifahari.
Baada ya dereva tax kulipwa ujira wake na kuondoka , tukasogea kwenye geti la jumba lile. Mariamu alibonyeza Swich ya kengele iliyokuwa pale getini na muda mfupi badaye, alikuja mvulana wa Kisomali kufungua.
Nilipogonganisha macho na yule mvulana kitu fulani kisichoelezeka lilipita kichwani mwangu. Macho yangu yalinata kwa yule mvulana kwa nukta kadhaa.
Alizungumza na Mariamu kama watu wenye kufahamiana kwa muda mrefu kilichonishangaza zaidi aliongea kwa Kiswahili. Alikuwa ni mtu mcheshi na makalimu. Kiswahili chake kilikuwa na lafudhi ya Kimombasa, kwa kweli alionekana ni mtu mwenye kufurahia maisha wakati wote.
Baada ya maongezi ya hapa na pale, alitufungulia geti na kuingia ndani.
Ndani ya lile jumba lile kifahari kulikuwa na eneo kubwa la wazi ambalo lilipandwa bustani ya maua na nyasi fupi za kijani kibichi, upande wa kaskazini kukikuwa na bwawa dogo la kuogelea sanjari na viti vichache vya kukalia vilivyokuwa chini ya miavuli midogo mahususi kwa kimvuli, mbele ya nyumba hiyo kulikuwa na magari ya bei mbaya yaliyopaki kwenye ‘parking’ maalumu iliyojengwa kiustadi.
“Hapa ndipo utakapo fanya kazi” hatimaye Mariamu aliniambia.
“Pazuri sana”
“Ndiyo ni pazuri, hata mshahara utakaolipwa utakuwa mnono, mradi uwe tayari kukabiliana na changamoto zitakazo kukabili” aliposema hayo taswira ya kubakwa ikanijia.
Kabla sijatia neno wakati huohuo, alitokea mwanamke mmoja wa kiarabu aliyekuwa na sifa zote za kuitwa mrembo. Pamoja na uzuri wake lakini midomo na macho yake yalinijulisha kuwa mtu yule alikuwa na majivuno na dharau.
“Asalam aleykum,” alitusalimiahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Waleykum salama.”
“Huyu ndiye yule mtu mweusi kutoka Tanzania?” alisema. kauli ile ilinifanya niendelee kuamini kuhusu fikra zangu juu ya tabia ya yule mwanamke wa Kiarabu.
“Ndiye” Mariamu alimjibu.
“Mmepima na mmeona hana Ukimwi”
“Hana?”
“Ebora na Tb je?”
“Hana pia”
“Piteni ndani” alisema yule mmwanamke.
“Huyu anaitwa Zakia Almajidi mke wa Abadallah Mustapha.” Mariamu alininong’oneza tukiwa tunaingia ndani, nilishusha pumzi ndefu na kwa mara ya kwanza nafsi yangu ikikiri kuwa nipo kwenye uwanja wa vita.

ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment