Search This Blog

Friday, November 18, 2022

KILIO CHANGU - 3

 






Simulizi : Kilio Changu

Sehemu Ya Tatu (3)





Mwendo wa saa kumi na moja kamili Miriam aliamka akiwa na hamu kubwa ya kuwahi kazini ili ujumbe wa Genes uweze kufika mapema.

Baada ya kusali sala ya asubuhi, alichukua vile vipande viwili vya barua akavisoma kama desturi yake, alivisoma kila asubuhi na jioni na kila alipomaliza kusoma alijikuta akitokwa na machozi ila kwa siku hiyo machozi hayakumtoka kwani baada ya kusoma hiyo akichukua ile iliyokua inatumwa kwa Genes na kuibusu na kuiombea,

"baba naomba unisaidie huyu mwanaume nilieamua kumpenda kwa dhati aweze kunielewa, kwani sina nia mbaya nayeye naomba umfumbue macho aweze kuona upendo wangu kwake" Miriam aliomba akiwa kapiga magoti.

*******

"Saivi nishachelewa alafu nikienda na huku Aquiline nitachelewa zaidi" Josephat alijisemea kabla ya kutoka nyumbani,

"ila pale naweza pewa zawadi nzuri,sasa mwanamke akikwambia nakupa zawadi basi inawezekana ni penzi, ila sasa mwanamke mwenyewe ananituma kwa mwanaume wake sasa nitapewa nini?,ila ngoja nimpitie chapu nikimkosa sitamsubiri" Josephat baada ya kujishauri aliamua kupitia njia ambayo angemkuta Miriam.

********

"Waooh Genes leo umependeza sana" Angel alimtamkia Genes ambae walipanga wawahi shule ili wawe wanaongea pamoja kabla ya shughuli za usafi kuanza,

"hivi Angel mbona wewe umewazidi wanawake wote hapa shule ulimpa mungu zawadi gani,?au mungu alikuumba asubuhi na mapema maana hakukosea kitu" Genes alimpamba kwa maneno ya kumsifu hadi Angel akashindwa kusimama mwenyewe na hapo akamsogelea Genes na kumwegemea mabegani huku akilegeza macho,http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Angel angalia bhana tukionekana itakua magazeti shule nzima au ukute kuna mtu mwenye simu ya kisasa nakwambia badae tutakua Facebook" Genes alimnong'oneza Angel,

"sasa Genes nimeshindwa kuvumilia yani hapa nimepandwa na hisia za ajabu jaman nisaidie" Angel alimnong'oneza huku akipenyeza ulimi katikati ya sikio la kushoto la Genes,

"Angeeeeel acha jaman huoni huku ni shuleni" Genes alisema huku akijaribu kujitoa mikononi mwa Angel,

"sasa hata wanafunzi hakuna situfanye tu" Angel alimnong'oneza tena huku ulimi ukizidi kumtekenya masikioni.Genes alijisikia hali ambayo hajawahi kuisikia tangu azaliwe, alijihisi kama yupo katika sayari ya Mars ambayo anaisoma katika somo la Geography.

"Angel tuache alafu jumapili tukutane tufanye yetu basi" Genes alimbembeleza Angel kisha Angel akakubali kumwachilia.

Angel aliposikia kua jumapili atafanya mapenzi na Genes basi alimshukuru kwa kumsogolea kisha kumshika katika eneo la zipu ya suruali kama vile anataka kumfungua zipu,

"nini tena sasa Angel sinshakupa ahadi kua ni jumapili?" Genes alimsihi Angel atoe mkono wake sehemu hiyo,

"nataman niguse hii fimbo yangu ndo nisubirie kunichapa jumapili" Angel alimnong'oneza tena Genes huku akipitisha mkono ndani ya suruali ya Genes,

"weee acha" Genes aliruka nusura avunje kioo kwani alihisi msisimko wa ajabu ingawa alitamani aendelee kushikwa hapo pia aliogopa kwani tayari wanafunzi wengi washaanza kuingia shule.

Genes na Angel walitawanyika kila mtu kuendelea na shughuli zake huku wote wakiwa wanaisubiria jumapili kwa hamu hasa Genes ndio alikua kachanganyikiwa zaidi.

********

"Jaman huyu alinidanganya au vipi" Miriam alikua anaongea mwenyewe kama kichaa kwani alikua kasimama kwa mda mrefu bila kumuona Jesophat,

"au ndio yule" Miriam alisema baada ya kuona mwanafunzi aliekuja kwa mbali, na alivyoangalia kwa makini na kumtambua kua ni Jesophat,

"waooooh jaman nikasema umenidanganya kumbe unakuja jaman pole sana" Miriam alianza kuongea kwa sauti huku akiruka ruka kwa furaha hata kabla Jesophat hajamfikia,

"mmmh Genes na akili zake zote kumbe ndo maana kamkataa huyu kumbe ni kichaa kabisa, sijui namimi nimtoke maana anaweza niparamia hata aninyang'anye haka kamkoba kangu, ila kwa kua nishamfikia ngoja nimsikilize tu" Josephat aliwaza baada ya kuona Miriam anarukaruka bila kujielewa kabisa.

"Dada mbona kama una furaha sana" Josephat alianza maongezi kwa haraka,

"nimekusubiria sana hivyo kukuona lazima nifurahi" Miriam alijibu huku akitoa bahasha na kuibusu kisha kumkabidhi.

"hii hapa nisaidie kumpa alafu badae nitakusubiria hapa unipe majibu basi,nikusubirie saa ngapi ?" Miriam aliuliza,

"saa tisa kamili nisubiri ila vipi sasa kama akikataa kupokea," Josephat aliuliza,

"jaman asipopokea naomba nirudishie pia" Miriam alijibu ila ghafla alianza kutokwa na machoz kusikia mambo ya kurudishiwa,

"sawa basi nitafanya hivo" Jesophat alimjibu kwa huruma,

"chukua hii basi unywe chai,ila zawadi yako ni kubwa zaidi ya hii wewe nisaidie tu kwanza" Miriam aliongea huku akimkabidhi Josephat noti ya elfu tano.

Josephat hakuamini macho yake pale alipoona noti ya elfu tano,

"asante sana dada niatakufanyia kazi yako vizuri" Josephat alijibu kwa furaha na hali ya kutoamini,

"alafu usiiite tena dada, niite shemeji" Miriam alimtania Jesophat huku wakiagana.

"Sasa huyu mwanamke ana hela hivi alafu Genes anamkataa anamng'ang'ania yule mwanamke mweupe anaejipodoa anakua kama mdoli" Josephat aliwaza.

"uko wapi huo ujumbe uliosema unaagiziwa?" Genes alimuuliza Jesophat mara tu ya kuingia getini na kukutana,

"cheki sasa na wewe mikwara mingi eti jana unaongea kwa ubabe kua hutaki mazoea nae" Josephat aliongea kwa kicheko,

"we ungempitia uone namna ningeuchana chana na kuutupa" Genes nae alijibu kwa hasira,

"ninao bhna ngoja upo kwenye begi,nitakupa saa nne" Josephat alijisemea baada ya kuwaza kitu,kwani aliona uso wa Genes ni wakuonesha dhdhiri kua angechana au kuutupa ujumbe ambao angepokea.

Kengele ya saa nne ambayo iliashiria watu kupata pumziko kwa mda mfupi basi waliobanwa na haja mbalimbali ndio waliutumia kuenda sehemu husika pia waliokua na hela kidogo basi katika duka la shule walizidi kuongea jeuri, ambao walikua na baridi walilazimika kuota jua huku wakiwaangalia waliopanga foleni dukani sasa mda huo Angel aliutumia kumtembela Genes darasani kwake kwani tayari washaanza mahusiano.

"wee jihesabuni wote mpate kitu cha mia mia" Jesophat aliongea kwa sauti kubwa eneo la dukani kwani siku hiyo alikua na hela ambayo tokea aanze shule hajawahi miliki.

Baada ya kuitumia yote yeye na marafiki zake basi alielekea darasani na kuchukua bahasha ingine na kuweka huko karatasi isiyo na maandishi yoyote,

"hebu ngoja nimpime kwanza na hii nione" Jesophat alijisemea akielekea darasani kwa Genes huku bahasha kutoka kwa Miriam ikibaki ndani ya begi.

*******

"Angel vile vitu vya asubuhi ulijulia wapi maana hadi saivi nahisi furaha tu" Genes alikua katika mazungumzo na Angel kama kawaida yao kila ifikapo saa nne,

"naona kwenye movie za kizungu pamoja na kufundishwa kama hivi kwenye biology na hivo ni kidogo tu jumapili yani ndo hadi mtu azimie" Angel alimjibu,

"vipi mwanangu Genes naona uko na shem langu ila nakuomba kidogo tubonge" Josephat aliingilia na kuwakatiza maongezi,

"aah wivu tu sasa anamwitia nini" Angel alijisemea huku akivuta mdomo,

Genes na Josephat walisogea pembeni huku Genes akiingiza mikono mfukoni kuzuia kitu fulani ambacho aliona aibu wanawake kumuona katika hali ile.

"Nambie man" Genes alianza maongezi,

"hii apa barua yako" Josephat alimjibu huku akiingiza mkono mfukoni na kutoa bahasha, Genes aliipokea haraka na kuichana chana mbele yake,

"nilikuambia sitaki mazoea na huyo kenge aise chali angu mbona hatuelewani,au unataka urafiki wetu ufe nini man" Genes aliongea huku akimwangalia Angel ambae kwa wakati huo alilaza kichwa kwenye meza,

"haya basi poa tuachane na hayo mambo nilijua unatania kumbe ni hutaki kupokea ujumbe wake kweli" Josephat alimjibu huku akishangaa kwa kitendo cha Genes kuichana ile bahasha,

"nilihisi tu ndo maana nikamjaribu kwanza" Josephat alijisemea huku akitoka nje kwani kengele ya kuashiria mda wa kupumzika umeisha.

"sasa huyu shemeji angu itabidi nimrudishie tu hii bahasha yake nimweleze kilichotokea ili ajue hapendwi kabisa" Josephat alijisemea.

*********

"Dada Anitha leo saa nane kamili wote lazima tuwe wagonjwa na tuende hospitali" Miriam alimfuata Anitha na kumweleza hayo,

"sasa kama unaletewa majibu saa tisa kwa nini saa nane tuwe wagonjwa na tuende hospitali? hapo sijaelewa" Anitha alimuuliza Miriam,

"yaani namaanisha ikifika saa nane hapa kazini tudanganye tunaunwa ili tupewe ruhusa ya kuenda kupata dawa na hapo tusubirie majibu basi ili unisomee basi" Miriam alimuelewesha,

"sasa jaman tutaugua wote?wewe sema unaumwa ili Mimi nikusindikize hospitali maana watashangaa kuugua siku moja wote" Anitha alimpa wazo ambalo wote walikubaliana.

"Ndio yule nini?" Miriam alikua anafananisha kila mwanafunzi aliyemuona baada ya kudanganya anaumwa,

"Miriam hakika huyo mwanaume amekuchanganya sana akili" Anitha alikua anacheka tu maana Miriam alifanya kila aina ya kituko kila alipoona mwanafunzi yeyote alihisi ni Jesophat analeta majibu.

"Haya sasa ndo yuleeee" Miriam alisema baada ya kumuona Jesophat kwa mbali,

"tukatafute miwani au" Miriam aliongea utani huku akishusha sketi yake ili shem ake asije sema anavaa kimini.

Josephat nae alianza kuonesha uso wa furaha ili Miriam aondoe wasiwasi na wote walijikuta wakitabasamu kabla hata hawajaanza maongezi Miriam alianza kunyoosha mikono kwa mbali.

"Miriam acha basi nawe ukichaa wako siatafika hapa tu" Anitha alimsihi Miriam ambae alikua anaanza kutoka nduki kumfuata Josephat kwani aliona kama anachelewa kufika waliposimama.





"We Miriam nilikuambia huyu mwanaume atakuua" Anitha aliongea huku akiwa na kazi ngumu ya kumbembeleza Miriam ambae kwa wakati huo alikua akilia machozi kwa kurudishiwa bahasha hata bila kufunguliwa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Josephat Kwa wakati huo alikua anashangaa jinsi Miriam anavolia,

"kweli kuna wasichana wanaolia uongo ila huyu hatanii ila kapenda kweli" Josephat alisema kwa sauti,

"jaman huyu Genes nimemkosea nini ananifanyia hiviiiii mungu siumfumbue macho jaman huyu wamoyo wangu?" Miriam aligaragara ardhini akilia kwa uchungu,

"haya best acha kulia basi watu wanatushangaa ujue" Anitha alizidi kumsihi Miriam atulie.

"kakaka we ne_ne_nda jumapili tuonane hapa" Miriam alimwambia Josephat na hapo Jesophat aliondoka kuelekea nyumbani kusubiria jumapili ifike.

Baada ya dakika ishirini tayari Miriam alikua nyumbani kwake ambako alienda baada ya kushindwa kuendelea na kazi.

"best unaendealeje?" Anitha jioni alipotoka kazini alimpitia Miriam nyumbani,

"best sina hamu yani heri nife" Miriam alimjibu huku akijizungusha kitandani,

"usiseme hivo mdogo angu mapenzi yanauma sana pale unapompenda mtu ambae hakupendi" Anitha alimjibu huku akimfunika mapaja yaliyokua wazi,

"alafu huyu mwanaume hakuoni ulivyo mzuri nini,cheki mtoto ulivyo laini" Anitha alijaribu kumtania Miriam ili afurahi kama kawaida walivyozoea kutaniana ila Miriam alizidi kuloanisha shuka kwa machozi,

"au hukuandika vizur nini?" Miriam alimuuliza Anitha huku akishikilia ile bahasha,

"hapana mdogo angu niliandika kila ulichokua unanambia" Miriam alijibu,

"sasa dada Anitha nifanyeje maana me nishapenda tayari na sitoweza kumuacha huyu mwanaume aende anaweza kukutana na mwanamke asie na mapenzi ya dhati kwake"Miriam aliongea kwa machungu makubwa.

Anitha alimpikia rafiki yake na kuhakikisha anakula,

" jaman mdogo angu kula tu hata hiki kijiko kimoja tu"Anitha alikua anambembeleza Miriam huku akimlisha kama mtoto.

Hakika lilikua pigio kubwa ambalo Miriam hakuamini kama angerudishiwa barua,

"kweli huyu mwanaume hanipendi ila sikati tamaa nitahakikisha atafaidi penzi langu LA dhati nishaapa kua na msimamo kwake" Miriam alijisemea siku ya ijumaa asubuhi akielekea kazini kwani alipanga jumapili atoke na Josephat ili waende kununua kitabu,

"nikimtumi kitabu atapokea naamini" Miriam aliendelea kujipa moyo.

*********

"We Angel mbona hatukuelewi" kijana aitwae Chris aliekua anasoma kidato kimoja na Genes alikua alifanya mazungumzo na Angel katika njia ya simu ila kila mmoja akiwa chooni, yaani Angel akiwa katika choo cha wanawake na huyo Chris akiwa choo cha wanaume na vyoo hivyo vilitenganishwa na madarasa yenye umbali wa mita hamsini,

"apaan sio kwamba hamnielewi bali jumapili hii namaliza kazi yake" Angel alijibu kwa sauti ya kujiiba uskute kuna mtu anamsikiliza,

"hakikisha unamaliza hiyo kazi basi la sivyo siri zote zitawekwa wazi" Chris aliongea na simu ikakatwa.

**********

"Genes weekend ndio hiyooo" lilikua neno la kwanza siku ya ijumaa pale Angel alivyoingia darasani kwa Genes,

"hata mimi naiona inakuja" Genes alijibu kwa sauti ya chini kwani tayari washakaa na kuegemea meza ambapo waliendelea kupanga mipango yao ya kukutana jumapili iliyokua mbele yao.

"we unapendekeza twende wapi tukapate tunda letu" Angel aliauliza,

"wewe chagua tu popote mimi nipo tayari" Genes alijibu huku akicheka kwa furaha,baada ya kurushiana mpira kwa mda,basi wote waliamua waende mitaa ya Sakina,jirani kabisa na Ngaramtoni ambako ndiko walipoona kunafaa kutokana na kuwa na hali ya utulivu hivyo waliamini hakutakua na magazeti.

*********

"Mdogo angu nakushauri tulia kwanza utapata mwanaume mwingine" Anitha aliendelea kumwimbia Miriam wimbo wa kila siku ambao haukumwingia akilini hata kidogo,

"dada Anitha kupenda ni haki ya kila mtu,mimi siwezi kumsubiri mwanaume anipende wakati kuna niliempenda tayari,mbona mwanaume anakutongoza kwani mimi sina moyo wa kupenda?" Miriam alijibu kwa hasira,

"kwa hiyo kesho ndo unaenda kumnunulia kitabu sio" Anitha aliuliza,

"ndio, kesho yule Jesophat atakuja niende nae kwenye duka la vitabu nikamtafutie kitabu chake kizuri akisome" Miriam alijibu kwa uso wa tabasamu.Anitha na Miriam waliagana.

Siku ya jumapili asubuhi Josephat aliwahi kuamka na kujiandaa tayari kuelekea kumchukua Miriam ili wakatafute kitabu dukani,

"kila siku nasema nataka niende Sakina alafu nakosa nauli, sasa leo nitamwambia huyu demu kua vitabu vizuri vinapatikana Sakina ili niende nae" Josephat alijisema moyoni.

"Sasa dada vitabu vizur kuna duka moja lipo huko Sakina maeneo ya Kwa Iddi pale ndo vinauzwa tena bei rahisi" Josephat alianza kumwambia Miriam alipomfuata Aquline hotel,

"mimi nakusikiliza wewe popote tutaenda" Miriam aliongea huku akijiamini kua yupo vizuri kifedha,

"sawa twende tukatize hapa stand ndogo tupige zoezi hadi Kilombero tupande hice"Josephat aliongea huku wakianza kutembea kwa miguu mwendo wa haraka haraka.

"Hebu nambie ukweli basi Jesophat, vipi huko shuleni Genes ana mademu au mbona ananifanyia mimi hivi" Miriam alimuuliza Jesophat swali wakiwa ndani ya hice,

"wala hana mademu" Jesophat alimtetea Genes ingawa alimjua Angel kua ni demu wake,

"sasa mbona hataki kua na mimi" Miriam aliongea huku machozi yakianza kumshuka kwa mbali,

"atakupenda tu usiogope" Jesophat alimjibu huku akimpa moyo,aliamini kufanya hivo kutamtuliza machozi aliyoona yanaanza kumshuka,

"we mamdogo hapo hebu nigaie hizo silva fasta,mbona unalia au shemela anazingua nini, ?njoo kwangu nitakupa gari hili" kondakta aliongea huku akimnyooshea Miriam mkono kuashiria kutaka nauli,

"hiyo hapo kata wawili tuache Kwa Iddi" Miriam aliongea huku akimkabidhi kondakta noti ya elfu kumi.

"chenchi hiyo mama" kondakta alimshtua Miriam aliejilaza kwenye kiti ila hakushtuka alikua kama kajisahau vile na hapo Jesophat aliipokea chenchi.

"oyo suka dondosha Kwa Iddi" kondakta alitoa sauti kwa dereva kuashiria kuna watu wanashuka.

"sasa duka lenyewe lile pale" Jesophat aliongea huku akinyoosha duka moja la vitabu lililokua pembeni ya barabara, walielekea hapo ila hawakumkuta muuzaji kwa mda huo,

"kaeni hapo kidogo anakuja saivi" walipewa viti vya kukaa na dada mmoja waliyemkuta hapo,walikubali kukaa kumsubiri kwani hawakua na haraka.

********

"sasa bby unajua hiyo lodge iko sehemu gani kabisa?" Angel alimuuliza Genes tayari wakiwa kwenye hice ya kuelekea Sakina,

"nakumbuka ukifika Sakina kituo wanaita Kwa Iddi kuna njia ipo upande wa kulia mwa barabara ndio tunaenda nayo kama mita mia mbili tunakuta kibao kimeandikwa KIMYA KIMYA LODGE,hapo tutafuata huo mshale" Genes alijibu,

"sawa mpenzi leo utanifaidi hadi ufurahi" Angel alimnong'oneza ili abiria wapembeni asisikie,

"we acha tu usiseme saivi zipu isije katika bhana ngoja tufike tu" Genes nae alimnong'oneza.

"Kwa Iddi njooni mlangoni" kondakta alitamka na hapo Angel na Genes walisogea mlangoni.



Itaendelea alhamisi....

Basi wadau kama Jana nilivyotoa pendekezo la kuhusu kujadili mada fulani siku moja katika wiki basi nimeona kesho niwawekee mada mezani katika ukurasa huu,, cha kufanya ni kutoa wazo lako na maoni,lengo letu sio kubishana wala kugombana Bali ni kueleweshana na kupeana mbinu mbalimbali kuhusiana na mada husika..Hivyo basi kesho saa mbili asubuhi nitapost mada hapa na utachangia unachoweza ,utapitia coment ya mwenzako utaisoma ili kujifunza zaidi.. Hiki kitendo nimekipa jina MJADALA KUTOKA KWA DEO MASSAWE.



"Yule sio Genes Kweli" Miriam alisema huku akisimama ili aweze kuona vizur mtu aliyemfananisha na Genes akivuka barabara kuelekea upande waliopo,

"naona ni yeye" Jesophat alijibu,

"na huyo msichana ni wawapi?"Miriam alisema huku akivua mkoba (kipima joto) aliokua ameubeba na kumkabidhi Jesophat,

"leo ni leo" alisema Miriam.

*********

"Vipi aise Chris"

"powa mkuu wangu Brown"

"huyu Angel ndo yupo na Genes leo"

"ndio jana sinimempa tahadhari?"

"nimemwambia asiopomuua leo tutaweka mambo yote hadharani"

"powa powa man wangu".

Yalikua mazungumzo ya kwenye simu kati ya vijana wawili akiwa ni Chris na Brown.Hawa vijana walikua ni watu wenye wivu na maendeleo ya mtu na walikua wanafunzi wenzake na Genes maendeleo ya Genes shuleni yaliwafanya wakose raha na kuamua kumtafutia mtu wa kumuua ndo hapo walimtumia Angel kufanikisha kazi yao.

Angel alikua ashawaua zaidi ya wanafunzi wawili ambao mmoja alimuua kwa kumpa sumu na mwingine alimnyonga alipokua akiwa nae chumbani kwa lengo la kufanya mapenzi,ingawa Angel alikua bado bikra.

Hivyo Chris na Brown walipojua kuhusu Angel kuua watu walimfuata siku moja na kumwambia,

"Angel hivi mbona unaua watu"

"jaman naombeni iwe siri yenu kua naua watu nawaomba msimwambie mtu,lolote mnalotaka nitawafanyia",

"ahaa sasa hatumtaki Genes huku duniani"

"sawa nitamuua ila iwe siri kubwa sana".

Baada ya hapo ndipo Angel alipoanzisha mahusiano na Genes ili iwe rahisi kumuua.

"Kweli huyu mwanaume nishampenda ghafla ila nitamuua tu ili nitimize lengo langu" ndiyo maneno Angel aliyosema asubuhi ya jumapili alipokua anaweka sindano ya sumu pamoja na wembe katika mkoba wake tayari kwa kuenda kukutana na Genes.

********

"Weweeeee! waacheee watoane nyongo,vita vya panzi ni furaha kwa kunguru,hahahaha lazima watoane chupi hapa".

Zilikua kelele za watu waliokua wakishuhudia pambano la Miriam na Angel,

"leo tutajua kati ya jogoo mweupe na mweusi nani kiboko ya mwingine" alisema dereva bodaboda mmoja.

Miriam na Angel walikua chini kila mmoja akijaribu kumvua mwenzake nguo,

"ananipiga maziwa!ananipiga maziwa" yalikua maneno ya Angel alipokua ameshikwa na kikunjwa,Miriam hakutaka mchezo alipiga mfano wa John Cena. Kwa wakati huo Jesophat alikua amemvuta Genes pembeni,

"mwanangu huu msala sasa" Jesophat alisema,

"aise huyu Miriam kumbe unatembea nae aise alafu unanipiga upepo tu pale shule,saivi umetoka nae wapi man wangu?" Genes aliongea huku akiwa na hasira za ndani,

"kweli huwezi amini tumekuja pale duka la vitabu nimemsindikiza hapo huyu Miriam"Jesophat alimjibu Genes,http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

" umekuja kununua kitabu?huyu kahaba anasoma wapi?"Genes alizidisha hasira,

"nitakuja kukuelezea vizuri" Jesophat alisema huku akiinama chini kuokota mkoba wa Angel uliokua umedondoka chini,

"oya utajuana nao" Genes alisema kisha kuondoka eneo lile huku akiacha pambano likiendelea,

"we utanambia leo umetoka wapi na bwana angu" Miriam aliuliza huku akimshushia Angel ngumi za macho,

"ni bwana angu we kahaba mweusi kama mkaa" Angel alijibu huku akijitahid kujifunika sehemu za siri ambazo zilikua nje kutokana na kuvaa sketi,yeye Miriam alihimili pambano kwa kuwa alivaa suruali.

"Hii sindano ni ya kazi gani pamoja na huu wembe?" Jesophat alijiuliza baada ya kutupa macho ndani ya mkoba wa Angel,

"hapana! hapa kuna kitu sio bure" Jesophat alizidi kujisemea, alitoa ile sindano na zile wembe akazificha katika mkoba wa Miriam aliokua ameushikilia.

"Nyie basi inatosha acheni vita" Jesophat alianza zoezi la kuwaachanisha ila hakuna alietemani kumwachia mwenzake.

"weee mkoba wangu" Angel alisema kwa sauti baada ya kuona Jesophat ndie kashikilia mkoba wake,alitumia nguvu zote kujitoa mikononi mwa Miriam na kuvaa Jesophat kisha kuchukua mkoba wake,

"jogoo mweupe ni mwoga" watu walipiga makelele,

"mimi siwezi pigania mabwana na sokwe" Angel alisema huku akifuta machozi,

*********

Genes baada ya kuondoka pale aliwaza mengi huku akimtupia lawana zote Miriam,

"yaani huyu Miriam sijui alinitokea wapi,kaniharibia kuenda kujua penzi la mke wangu Angel" aliwaza mengi na kuzidi kumchukia Miriam.

*********

"mama yangu hii sindano iko wapi?" Angel alijisemea Baada kuchungulia ndani ya mkoba wake,

'Itakua Jesophat kaichukua,na atakua amejitafutia matatizo mwenyewe" Angel alijisemea huku akimwangalia Jesophat machoni na hapo Jesophat akawaza kitu,

"Miriam tuondoke hapa" Josephat alimshika Miriam mkono na kutaka waondoke pale,

"ngoja kwanza tununue hicho kitabu cha mume wangu" Miriam alijibu huku bado akihema kwa hasira,

"apana tuachane na hayo, tutakuja siku nyingine saivi mambo yashaharibika" Josephat na Miriam waliondoka pale kuelekea kituoni ili waweze kurudi.

Katika kituo walichoenda kusubiri gari walimkuta pia Angel nae akisubiri gari ila alionekana kuwa na wasiwasi sana na kwakua alikua anasoma shule moja na Josephat basi alimwita na kumuomba nauli,

"mimi mwenyewe sina hata shilingi moja hapa" Josephat alimjibu kwa sauti ambayo Miriam alisikia.

"mpe mia tano kwenye ile chenchi" Miriam aliongea kwa sauti kuamuru Angel apewe nauli,

"asante sana" Angel alimjibu Miriam, gari ilikuja na wote wakapanda bila ugomvi wowote.

"Yaani huyu mwanamke amemponesha Genes sijui nitawaeleza nini akina Chris" Angel alikua akiwaza sana akiwa kwenye gari,

"ila huyu Josephat lazima afe maana kama kafanikiwa kuchukua hii sindano iliyokua ndani ya mkoba basi nitaweza gundulika" Angel aliumia sana kichwa na haraka alianza kupanga mbinu za kumuua Josephat ili asije kutoa siri ya yeye kutembea na sindano.





"Huyu mwanamke sio mtu mzuri" Jesophat alijisemea huku bado akiwaza ile sindano na wembe ni vya kazi gani?

"au huyu mtoto ni mshirikina nini?" alijiuliza maswali mengi sana bila kupata jibu,

"ila itajulikana tu nitaanza uchunguzi kesho" alijisemea gari tayaribikiingia kituoni ambapo wangeshuka.

"We mwanamke njoo hapa nikupe somo" Miriam alimuita Angel alieshuka kwenye gari wakwanza, na bila ubishi Angel alitii amri,

"siku nyingine ukiwa unaenda mahali kama upo na mtu usikubali akae na pesa yote,je mkipotezana utabaki bila nauli ya kurudi alafu ukikosa mtu wa kukufadhili itakuaje? kuanzia leo uwe unatembea na pesa kidogo mfukoni,sasa kama saivi huna hata senti mfukoni,chukua hii ikusaidie njiani" Miriam aliongea kwa huruna bila kujali ugomvi walioufanya hapo nyuma,

"Asante sana ubarikiwe" Angel alijibu huku akipokea noti ya elfu tank kutoka kwa Miriam,

"we hiyo pesa unampa ya nini siunipe mimi?" Jesophat alijisemea moyoni.

Miriam alikua mtu mwenye uruma na mtoaji kutoka moyoni hakutaka mtu ateseke mbele ya macho yake kama akiwa na msaada aliutoa kwa moyo.

"haya nenda basi ila yule ni bwana angu hivyo naomba umuache la sivyo tutatoana nyongo" Miriam alimnong"oneza Angel

"sawa nashukuru nitaachana nae sikua najua kama ni wako" Angel alijibu kwa mdomo ila moyoni akiwaza,

"wewe una bahati sana maana kesho ungezika huyu mumeo ila hakuna tatizo utazika huyu rafiki yako kwanza" Angel aliwaza kumuua jesophat, sababu alihofia siri ya yeye kutembea na wembe na sindano.

Waliagana na Angel kuondoka zake,akiwaacha Miriam na jesophat kituoni,

"nishikie niende chooni nikakojoe tu" Miriam aliongea huku akimkabidhi jesophat kimkoba chake,

"haina shida" Jesophat alijibu huku akipokea kwa furaha kwani aliwaza ni kwa jinsi gani angeweza kutoa ule wembe na sindano ila akajua ndio mda sahihi wa kuvitoa,na haraka aliingiza mkono wake mfukoni na kutoa kitambaa chake ili kushikia,aliogopa kushika kwa mkono kabisa.

"sasa Miriam kuna kitu kingine cha kukusaidia?"Jesophat alimuuliza Miriam,

"sahivi sina" ila basi ukitoka shule uwe unapita hapa kunipa maendelo ya huyu bwana angu kipenzi"Miriam aliongea huku akiagana na Jesophat,

"sawa nitakua nakupitia" Josephat alijibu na kila mmoja kutawanyika.

********http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Hapa lazima itakua kuna kitu,mimi najua mwanamke huwa anatembea na kanga ya dharura katika mkoba wake ila sio,sindano na wembe" Josephat alijisemea huku akiingiza mkono mfukoni na kuvitoa,

"tena vina kama rangi rangi nyeusi,kwanin? kumbe ndo naskia watu wanachanwa na wembe kwenye gesti na huyu ndo mambo yake nini ngoja kesho jumatatu maana huyu jamaa angu Genes angekufa kizembe aise au sasa walikua na nia gani ? au ni wanga nini" Josephat alijiuliza maswali na kujijibu mwenyewe.

"Ngoja kwanza niende maabara nikavipime maana huyu msichana hata kwenye gari niliona anavokaa na wasiwasi nikahisi tu kuna kitu"Josephat alijisemea huku akieleka hospitali moja iliyokua karibu na makao makuu ya PPF tawi la kaloleni.

Josephat aliingia moja kwa moja hadi kwa daktari tena ambae alikua jirani yake na kwakua ilikua siku ya jumapili maabara hiyo haikua na foleni kubwa hivyo aliweza kuonana na huyo daktari mapema.

"aah Mr Jose! naona leo umetoka mchicha unaenda kwa demu ako nini" moja kwa moja doctor aliyeitwa August aliongea baada ya kumuona Josephat,

"awapi doctor niko mzunguko tu ila nkaona nkupitie hapa nikupe hata salamu tu,sema kuna kitu nilitaka kukijua kutoka kwako maana wewe ni mtalaamu wa mambo haya" Josephat aliongea huku akiingiza mkono mfukoni na kutoa kitambaa chake huku akikikunjua kwa umakini,

"umevitoa wapi kwani" daktari August aliuliza,

"nimeviokota juzi darasani sasa nikashindwa kuvielewa" Josephat alijibu kwa kutumia uongo huo kwani yeye alichokua anatafuta ni ukweli kuhusu hivyo vitu.

"hebu ngoja nivipeleke kwenye vipimo" daktari August aliongea huku akielekea kwenye vipimo kwani hakua mtu wa kupuuzia kitu chochote.

"leo nitajua tu maana mimi nilihisi tu huyu Angel sio mtu mzuri" Josephat alijisemea huku akipanguza kiti ili akae.

*******

"Yaani dada Anitha leo ndo kitu cha kihistoria kabisa" Miriam alianza kuongea kwa hasira baada ya kukutana na Anitha,

"kunani kwanza mbona kama umeparuliwa uso? au umefumaniwa?" Anitha aliongea huku akimkagua Miriam jinsi alivyochafuka,

"heri ingekua fumanizi! hii ni zaidi ya fumanizi" Miriam alijibu na kumwelezea Anitha kila kitu kilichotokea.

"Jaman Miriam utakufa ujue kua mapenzi sio mazuri,mwenyewe unaona mwanaume mwenyewe hakupendi ila unajilazimisha kwake tu huoni ni ujinga huo mdogo angu,achana na hayo mambo kaa mwenyewe tu" Anitha aliongea mengi ila msimamo wa Miriam ulikua ule ule,

"mimi nikishapenda nimependa sitaki mchezo kwenye mapenz yaani hako kamwanamke nimekafinyanga kama tonge la ugali na weupe wake kama mdoli kamekua kekundu kama nyanya" Miriam aliongea kwa dharau.

"Sawa mimi sina usemi kaa makini lakini na biashara zako na hawa kuku wako maana yule mtetea na jogoo ulonipa napambana nazo tu.Waliongea mengi na waliagana huku Miriam akikaa na mawazo mengi kichwani kumhusu Genes,

" sasa huyu mwanaume atafanyaje ili ajue nampenda,au kwa sababu mimi ni mweusi nini, ila mbona wanasema cheusi dawa, na wengine husema weusi asili weupe hutafutwa, mimi ni mzuri bhana" Miriam alijipa moyo huku akijiangalia kwenye kioo.

*******

"Aise sikaniponyoka alafu Jose ndio kavuruga mpango mzima aise"

"hatujakuelewa unamaanisha nini maana saivi haistahili awe duniani"

"ndo hivo aise yenyewe nimedundwa na mwanamke mwenye nguvu utazania anakula ugali wa zege yaani ila naona Josephat ashaharibu mpango wote"

"kwa hiyo sasa kama Jesophat kashtuka lazima aje kuropoka na akiropoka lazima wakubane na ukibanwa utatutaja sasa inabidi huyo Jesophat aanze kufa".

Yalikua mazungumzo katika njia ya simu katibya Angel na Chris.

********

" Huyu Josephat sio mtu mzuri hata kidogo ingawa ni jamaa yangu ila leo nimemshutuka sio rafiki wa kweli,yaani ametoka wapi na Miriam mazingira yale isipokua ni mtu anaeng'ata na kupuliza?" Genes alijisemea huku akiapa kuuvunja urafiki wake na Jesophat kwani alimatisha kuenda kufanya mapenzi na mtoto mzuri Angel,

"sasa kama sio Jesophat kuja na huyo kima wake wake Miriam siungekuta saivi nishajua ladha ya mapenzi tena kwa mwanamke mzuri vile ungekuta leo nimepata joto la kutosha" Genes alimlaumu sana Josephat pamoja na kumchukia zaidi Miriam.

*********

"We Jose umesema umetoa wapi?" daktari August aliuliza kwa mshangao na wasiwasi mkubwa,

"Nimeokota" Josephat alijibu kwa hofu,

"hebu njoo hapa" daktari August alimuita pembeni, na Josephat alimfuata haraka na kuingia nae chumbani,

"Hebu angalia huyu panya" daktari August aliongea huku akimchukua panya alieko hai na kumtoboa na ile sindano,

"hebu hesabu sekunde katika hii saa yangu"daktari August aliongea huku akimsogezea Josephat mkono wenye saa ili ahesabu sekunde bila kujua huyo daktari anamaanisha nini.

"Mama yangu inaua ndani ya sekunde 30 ?" Josephat aliongea huku akitaka kukimbilia nje kwa woga kwani hakuamini kuona panya anakauka kwa kuchomwa sindano aliyoitoa ndani ya mkoba wa Angel,

"aise nilihisi hiki sio kitu kizuri" Josephat aliongea kwa sauti kubwa mbele ya daktari August,

"kwanini ulihisi?" Daktari August alimuuliza kwani aliona jinsi Josephat alivyobadilika na kua katika hali ya wasiwasi,

"yaani nilivyoikota darasani nilijua sio kitu kizuri" nae Josephat aliongea kumuondoa wasiwasi daktari.

"ngoja mimi niende kesho nikienda niangalie vizuri kama kuna zingine" Josephat alimuaga daktari kwa haraka.

"ngoja nifike nyumbani haraka nikaende kwa Genes nikampe taarifa ya hiki kitu maana nahisi kuna kitu Angel anataka kumfanyia huyu rafiki angu" Josephat alitembea kwa haraka sana huku akiwa na mawazo mengi kichwani.

Doctor August alibaki akiwaza kwa jinsi ile sumu iliyopakwa kwenye sindano na wembe ilivyo na nguvu kubwa ya kuua,

"kama imeua panya kwa sekunde 30 sasa ukimchoma binadamu hata atafika hospital kweli ?" August aliedelea kuishangaa sumu ile.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

********

"hapa naenda kwa Genes namtaarifu hiki kitu kisha nitarudi kwa Miriam nimpe taarifa kua huyu mtu sio wakuchezea" Jesophat alizidi kusema huku akipiga hatua kubwa kubwa.

Alipofika katika njia panda ya Sanawari basi kwa mawazo aliyokua nayo alijisahau kuzingatia taa za barabarani,

"we kijana rudi" sauti ya mbaba mmoja ilitoka kwa ukali ikimwamuru Josephat arudi,

"pita haraka" mama mmoja nae alisema kwa sauti kwani mbele ya Josephat kulikua na lori linakuja kwa kasi na hapo Josephat alipoliona limemkaribia basi alinyoosha mikono juu kama mtu anaetii amri ya polisi kwani hakuweza kuendelea mbele wala kurudi alikotoka.





"Hivi mbona Jackie Chan alilala chini siku ile anakimbika na kushtukizia gari?"ni wazo lililomjia Josephat kwa haraka aliweza kulala kifudifudi na gari kumpita ila kwa bahati mbaya kulikua na chuma iliyokwaruza kichwani,

"nakufaaaaaaa" Josephat alitoa sauti kubwa chini ya gari na kukaa kimya akivuja damu kichwani.

Kelele za watu zilifanya magari kusimama na hapo Josephat alizingirwa na kwa sababu ya maaskari wa barabarani kua karibu basi walifika na kupima ajali ambapo kila mtu alishuhudia kua dereva hakua na makosa,

"kaumia tena mgongoni" askari mmoja alisema baada ya kumgeuza Josephat aliekua kakwaruzwa tena mgongoni na damu ikiendelea kumtoka.

"sogea! sogea! sogea!" ilikua sauti ya mmoja wa wahudumu katika gari la kubebea wagonjwa (ambulance).

"ni wale wale wa toyo kila siku tunawaambia wapeleke taratibu au" lilikua swali alilouliza daktari katika chumba cha wagonjwa wa ajali katika hospitali ya Mount Meru, ambacho kilijaa vijana wengi, tena wengine wakiwa wamekatwa miguu wengine mikono na wengine wakipasuka vichwa kwa makosa ya kutozingatia sheria za barabarani kitu kilichowapelekea kupata ajali ovyo,

"hapana huyu kagongwa,alikua anatambea kwa miguu" mhudumu wa gari alijibu huku akitoka maelezo ya askari mfukoni na kumkabidhi.

Josephat alikua kimya, na hata hakua anajitambua kwa wakati huo na haraka baada ya kuanziwa matibabu alilazimika kuongezewa damu.

"msiogope huyu mgonjwa wenu atapona kwani hakuumia sana" yalikua maneno ya daktari baada ya wazazi wa Josephat kufika pale hospitalini,

"kwanza huyu mtoto wako alitoka wapi we mama" baba Josephat amuuliza mkewe kwa ukali,

"jaman baba Josephat usiseme hivo,maana tayari yashatokea sasa cha kufanya ni kumpambania apone" mama Josephat alijibu huku akiendelea kufuta machozi,

"mimi nakwambia kila siku mtoto akae nyumbani asome huniskii sasa angalia matokeo ya kulea ujinga sasa leo tunaingia gharama" baba Josephat alizidi kumlalamika mkewe yaani mama Josephat.

Josephat alilazimika kulazwa na mama yake akabaki nae kumuuguza.

*********

"Aise Genes jana best ako kapata ajali mbona hujaenda kumsalimia hapo Mount Meru" yalikua maneno ya Florah ambae alikua jirani yake Josephat,

"ajali gani tena mbona unanitania ? au ndo maana hajaja shuleni leo?" Genes alijibu kwa mashaka,

"jana alipata ajali ya kugongwa na gari ila hakuumia sana na hospitali wanasema anaendelea vizuri" Florah alijibu kwa masikitiko,

"embu ngoja badae utanambia vizuri" Genes alikatiza mazungumzo kwa kusema kua badae ataongea nae vizuri ili ajue jinsi ajali ilivyotokea.

"alipatia ajali wapi akati asubuhi ndo nimemkuta akiwa na Miriam kule Sakina? au walipigana sana wakaumia alafu anasema ni ajali nini" Genes alijiuliza na kuhisi jana yake alivyowakimbia kule Sakina yalikuja kutokea makubwa zaidi,

"hebu ngoja mke wangu Angel aje shule kwanza nimuulize nitajua nini shida,kama jana wamepigana nitajua" Genes alikaa na wasiwasi sana akimsubiri Angel aje shule,

"yaani huyu Miriam sijui kanitokea wapi maana kila siku nikimuona napata mkosi,ama kweli wasichana weusi wanakuaga na mkosi nimeamini" Genes aliwaza.

"Yaani we Genes kumbe upo hivo, yaani jana uniache nipigane na hawara wako tu hata kumsaidia jaman,je ningemuua" yalikua maneno ya Angel alipofika mbele ya geti la shule na kumkuta Genes akimsubiri,

"we tulia Angel naskia kuna majanga" Genes aliongea huku akimhamasisha Angel atulie,

"majanga gani ? mimi ningemuua huyu hawara wako na nilijua tu unao wanawake wengi" Angel aliendelea kuongea kwa hasira,

"apana sio kuua kwani mlimfanyaje Josephat mbona naskia kalazwa?" Genes aliuliza akitarajia jibu kua tulimpiga bali alishangaa kumuona Angel alitabasamu,

"mbona unatabasamu Angel au hujaelewa nilichokuambia" Genes aliongea kwa ukali,

"nimekuelewa sana ndo maana nimefurahi" Angel alijibu huku akizidisha tabasamu,

"mbona sikuelewi Angel" Genes alionesha hali ya kutoelewa kwa kugeuzageuza kichwa,

"yeye sialijidai kutuharibia mpango wetu wa kuenda kukutana jamani my love" Angel alibadilika na kuonesha uso wa huzuni,

"nikweli ila naskia kapata ajali eti kugongwa na gari nimeambiwa ila sina uhakika kama kagongwa kweli au ni nyie mlimpiga jana baada kuwaacha pale" Genes alipunguza hasira na kuongea kwa upole tena kwa hali ya mahaba,

"kwa hiyo amekufa?" Angel aliuliza,http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"hajafa na anaendela vizuri" Genes alijibu,

"yaani yule hata sitaki kumuona kabisa jana katukatisha utamu jamani" Angel aliongea akionesha uso wa huzuni sana,

"sasa itakua kapata ajali wapi,je jana wewe ulimuacha wapi maana yule mwanamke alietokea pale ananitaka ila mimi simtaki kweli hivyo nisamehe tutafanya hata wiki ijayo tu mpemzi usijali, sawa eh"Genes aliongea kwa sauti ya kubembeleza,

"kwani kile kidada kinakaa wapi" Angel aliuliza,

"Kipo hapo Aquiline hotel kinafua mashuka ya quest" Genes alijibu kwa kuonesha uso wa madharau makubwa,

"yaani Genes sasa wewe utampendaje yule mwanamke mweusi kama kima?" Angel aliongea,

"wala hata simpendi ila yeye tu ananishobokea na sina mda nae" Genes alijibu,

Baada ya kuongea mengi kila mmoja alitawanyika kuelekea darasani na hapo ndipo Angel alipopata upenyo wa kuenda chooni na kutoa simu aliyokua anaificha katikati ya maziwa yake yaliyofichwa ndani ya sidiria ya kubana,

"we Chris yule Josephat naskia yupo hospital jana kapata ajali, sasa sijui itakuaje maana ndie pekee aliyeona ile sindano niliyoipaka sumu ya kumuua Genes na sasa sijui kama ni kweli kapata ajali au ukute ni ile sindano imemtoboa"

"ngoja nipo darasani,ngoja nitoke niende chooni nikupigie" Chris alimjibu na kuinuka pamoja Brown kutoka kiti cha nyuma kabisa ambapo walikaa.

Angel, Chris na Brown walifanya mazungumzo ambayo mwisho waliamua kufanya mpango wa kuenda kumtembelea Josephat hospital,

"tena hapo hospital ndo vizur akifa maana hawatagundua kirahisi" Angel alisema,

"sasa sisi tukienda kutembelea mgonjwa si shule nzima itashangaa" Brown aliuliza kwani wao machoni walionekana watu wasiokua na huruma na pia hawakua tayari kumjali mtu mwenye kasoro,

"hiyo niachie mimi, yaani hiki kipindi tutazika wengi, kwanza huyu Josephat afuate Genes mwenyewe kisha tumalizie hiki kimwanamke chake kiitwacho Miriam sijui Miraa" Angel aliongea,

"sasa wewe inabidi leo uongee na Genes kwanza mpange kesho mchukue ruhusa kwa mwalimu kisha mumtafute huyo Miriam ili achukue kesi" Chris alimpa Angel akili ya kutumia ili asihisiwe kufanya kitendo hicho.

********

"Sasa Genes huyu rafiki yako huendi kumsalimia?" Angel alimuuliza Genes wakiwa wamekaa pamoja katika break ya saa nne,

"ndo nawaza hapa ila sinimekuambia sina uhakika sana hadi leo itabidi leo nimpitie Miriam tu nimuulize huenda anajua zaidi ingawa sitaki kuongea nae ila itabidi tu," Genes alijibu,

"powa muone basi alafu kesho tuende nae ikiwezekana ili tukapatane hapo,sio vizuri tugombane" Angel aliongea huku akionesha uso wa huruma sana.

********

"Dada Anitha yaani naskia kamgongo kanauma" Miriam alikua na Anitha wakitoka kazini,

"si kile kichapo cha jana kweli?" Anitha alimjibu,

"apana sio kichapo! mimi ndio nilimchapa" Miriam alijibu,

"pole" Anitha alimwambia Miriam,

"sasa dada we nenda mimi ngoja nimsubirie yule rafiki wa mume wangu hapa"

"haa Miriam umeanza sasa unamsubiri tena shemeji au ndo yale ya hainaga ushemela,?"

"apana dada ndo ananiletea habari za mume wangu na jana nimeachana mchana sasa sijajua kama alifika nyumbani salama" Miriam alijibu na wakaagana Miriam akabaki njiani kumsubiria Jesophat ambae kwa wakati huko hakujua kama yupo hospital.

Baada ya kusubiri kwa nusu saa alikata tamaa na kuanza kuondoka, ila akageuka mara ya mwisho nakuona mwanafunzi,

"waaooooh, Genes yuleeee" Miriam alianza kurukaruka kwa furaha,na kwa wakati huo Genes bado alikua hajamwona Miriam,

"acha hizo bhna" ilikua sauti ya Genes ikimkataza Miriam kuendelea kupata denda kwani tayari Miriam bila hata kusalimiana alimrukia na kuanza kumpiga mabusu mbele za watu bila woga.

"Mimi nimeleta habari mbaya"

"zipi hizo?"

"Jesophat naskia alipata ajali na sijaamini",

" dah! sangapi alipata maana nilikua nae jana mchana?"

"hapo hata mimi sijajua ila kesho tunaeda kumwangalia hapo Mount Meru kwani naskia kalazwa hapo"

"utanipitia basi na mimi niende, ila saivi Genes nataka tuende kwangu ukapaone tu tuongee kidogo" Miriam alimuomba Genes kuenda nyumbani pamoja ila Genes aligoma na mwisho walikubaliana kuenda wote hospital kwa ajili ya kuenda kumjulia Jesophat hali.

********

Usiku huo bado Jesophat alikua hajitambui,na alikua bado akiedelea kupata matibabu,

"mama acha kuchati kaa makini na huyo mtoto wako naona anajaribu kunyoosha mkono" yalikua maneno ya daktari kwa mama Jesophat aliekua anachat na kujisahau kama anamuuguza mgonjwa,kwani mda huo Jesophat alinyoosha mkono kama mtu aliehitaji msaada,ila alirudisha mkono na kutulia.

Asubuhi na mapema, Angel alichukua sindano yake na kuichovywa kwenye unga wa sumu na kuiweka katikati ya daftari"

"mungu nisaidie" Angel alisema na kutoka nje kuanza safari ya kuenda shule.

Mchana wa siku hiyo walikusanyika wanafunzi watano akiwemo Angel na Genes kuelekea hospital.

"tununue matunda kidogo" Angel alisema na wote waliingia sokoni na kununua matunda.



"Samahani mama! mwanano naona kidogo kapata tatizo katika ubongo hivyo usishangae anaweza kuongea kitu usichokielewa" yalikua maneno ya daktari kwa mama Josephat akimtoa hofu juu ya Jesophat aliyekua anatamka vitu bila mpangilio.

******

"Kalazwa wodi ile pale" Genes alitamka huku akinyooshea mkono wodi aliyolazwa Josephat lakini kabla hawajaingia mmojawapo ya mwanafunzi aliyeandamana na Genes basi alitaka kwanza wasimame,

"asa Genes hapa tumekusanya pesa zaidi ya laki mbili ina maana tutazipeleka zote?"

"ndio itabid tuzipekeke zote" Genes alimjibu huyo rafiki ake alietaka wagawe pesa waliyokusanya kama mchango wa kuenda kumuona mgonjwa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Miriam hakuwa anasikia chochote kwa sababu waliitana pembeni na kumuacha Miriam mlangoni.

Baada ya mabishano ya mda basi Genes hakutaka kuwakwaza wenzake na hapo waliamua kurudi nyuma kidogo ili wapunje kiasi cha pesa ili wagawane japo Genes hakufurahishwa na kitendo hicho.

"Hawa mbona hawaji" Miriam alijiuliza baada ya kusimama zaidi ya dakika mbili pasipo akina Genes kurejea,

"we anti ingia kama unaenda mwona mgonjwa maana zoezi la kuona wagonjwa litasimama mda sio mrefu" ilikua sauti ya mlinzi ikitoa maelezo juu ya utaratibu wa kuwaona wagonjwa,

"ngoja kuna wengine nawasubiri" Miriam alijibu huku akipapasa macho walikoelekea akina Genes,

"we ingia kumuone mgonjwa,wao wakija watasubiri mda mwingine" mlinzi alijibu na Miriam kutowaona akina Genes wakitokea basi aliingia wodini.

"shikamoo mama na pole kwa kumuuguza mwanao"Miriam alikua anamsalimia mama Jesophat aliemtambua kwa sura kwani alifanana sana na Jesophat,

"marahaba mwanangu nishapoa karibu" mama Josephat alijibu huku akimwelekeza Miriam sehemu ya kukaa,

"asante mama, mimi naitwa Miriam nipo na wanafunzi wanaosoma na mwanao Josephat, mimi pia huyu ni rafiki yangu nimesikitika sana siku anapata ajali nilionana nae" Miriam aliongea huku akitokwa na machozi.

Jesophat alikua kajilaza tu na kufunikwa lakini ghafla alianza kuonge bila kupangilia maneno,

"mama Angel anaua, mwanake ni sumu sitaki aje karibu mama mwanao watamuua nawaona hao na sumu zao hawana nia nzuri mama" Josephat aliongea kwa kukatakata maneno na hatimaye alikaa kimya,

"mama mbona sasa anatamka maneno hayo"Miriam alishtuka sana kusikia maneno ya Jesophat hasa alipotaja jina la Angel,

"huyu tokea jana anaongea utumbo sana ila daktari amenambia ni kawaida kwa mtu kupata ajali na kuongea hivi" mama Josephat alijibu huku akiwa makini kuangalia picha za umbea katika mtandao wa Instagram,

"ila umemsikia maneno anayosema?" Miriam alizid kuuliza,

"wala sijamsikia mimi,maana anavyoongea kila kitu nitasikiliza kipi na kipi niache?" mama Josephat alijibu.

Miriam alikaa na kuwaza mengi kuhusu jina la Angel kutamkwa kama muuaji,

"au kwa sababu nilipigana na huyo Angel juzi" Miriam alijiuliza maswali mengi ila hakupata jibu zaidi ya kuona sababu ya Josephat kusema hayo ni kwa kupigana kwao.

"Atakua alichukia sana kile kitendo cha mimi kupigana na Angel ndo maana anasema Angel ni muuaji" Miriam alijisemea.

Ukweli wa Jesophat kusema vile ni pale aliposkia sauti ya Miriam na hapo akakumbuka alichotaka kuwahi ndo akapata ajali hivyo Miriam pia hakuelewa ukweli wa mambo Ukweli wa Jesophat kusema vile ni pale aliposkia sauti ya Miriam na hapo akakumbuka alichotaka kuwahi ndo akapata ajali hivyo Miriam pia hakuelewa ukweli wa mambo hayo.

********

"Subirini baada ya lisaa limoja ndio mda wa kuwaona wagonjwa" sauti ya mlinzi ikiwaamrisha akina Genes kusubiri na hiyo ilitokana na wao kuchelewa walipoenda kugawana kiasi cha pesa walizopunja kutoka kwenye fungu alilotumiwa Josephat"Subirini baada ya lisaa limoja ndio mda wa kuwaona wagonjwa" sauti ya mlinzi ikiwaamrisha akina Genes kusubiri na hiyo ilitokana na wao kuchelewa walipoenda kugawana kiasi cha pesa walizopunja kutoka kwenye fungu alilotumiwa Josephat,

"afadhali huyu Miriam kaanza kuenda kumwona mgonjwa ndo kazi yangu sasa itafanyika bila shida" Angel alijisemea kimoyomoyo.

Walirudi katika viti vya kusubiria wagonjwa ili lisaa litimie. Na hapo Angel alitoka haraka na kuenda chooni kwa lengo la kujisaidia ila haikuwa hivyo kwani alitoa kikaratasi na kalamu na kuandika maneno fulani ambayo alipanga kuyaacha kitandani kwa Josephat bila mtu yeyote kumuona, baada ya kuyaandika vizuri alikunja karatasi na kuiweka mfukoni,kisha kurudi pale walipokua wamekaa kuendelea kupiga hadithi za uongo na kweli kusudi lisaa liishe.

"Baby una furaha leo" Genes alimnong'oneza Angel baada ya Genes kushindwa kuelewa kwanini Angel ana furaha kiasi hicho,

"kweli baby nikiwa nawe najiskia sana furaha,yaani siwezi kununa nikiwa na wewe hata kwenye msiba natabasamu" Angel alijibu kwa furaha na kuzidisha tabasamu,

"sawa mpenzi basi potezea kidogo maana hapa ni kumuona mgonjwa hivyo tabasamu na furaha sio vizuri" Genes alimshauri nae Angel akajitahid kuonesha uso wa huzuni.

********

"mama mda wa kazini kwangu unakaribia maana nimeomba ruhusa tu haraka" Miriam aliongea hayo wakati akimuaga mama Jesophat,

"chukua hii kidogo mama,nitakua nakuja kukusalimia hapa" Miriam aliongea huku akiingiza mkono wake wa kulia kweye sidiria na kutoa noti kadhaa za elfu kumi kumi bila kuzinyoosha akamkabidhi mama Josephat,

"asante mwanangu wewe nenda hawa wanafunzi nahisi wamezuiwa kidogo kwani huu mda sio wa kuona wagonjwa ila wataruhusiwa mda sio mrefu" mama Jesophat aliongea huku akitoa simu yake ambayo aliomba kuchukua picha na Miriam nae Miriam alikubali na wakachukua picha tena sura ya Josephat ikionekana imejilaza kitandani,Miriam kuona jinsi picha ilivyotoka vizuri,

"hebu nipige nikiwa namshika kichwa" Miriam alisema huku akipeleka mkono pale kweye kidonda kilichofungwa kwa kitamba.

Baada ya hapo Miriam alitoka na kukutana na akina Genes mlangoni,

"samahan Genes nakuomba kidogo" Miriam aliongea kwa uso wa huruma akitaka mazungumzo ya pembeni kidogo na bila kubisha Genes alisogea nae pembeni ili kumsikiliza,

"sasa tutaonana lini maana sasa tumepatwa na tatizo kidogo la huyu Jesophat" Miriam alianzisha maongezi,

"ndo ulichoniitia?" Genes alijibu kwa hasira,

"ok babaaa samahani basi,tutaongea siku nyingine" Miriam aliongea kwa huzuni.

"jaman mimi acha nirudi kazini" Miriam aliwaaga akina Angel,

"sawa tutaonana siku nyingine" Angel alijibu kwa mdomo ila moyoni akijisemea,

"nenda kahaba wewe, sikiliza kesa itakatokujia pumbavu wewe".

*********

Genes na kundi lake waliingia wodini kila mmoja akionesha uso wa huzuni,

" mama pole sana"kila mmoja alimtakia mama Josephat neno hilo ila kwa mda huo Josephat alikua katulia tu hakuongea hata yale maneno akiongea bila mpangilio.

Walikaa nae wakimfariji na kumpa matunda na kiasi cha pesa walizokuja nazo kama kuendelea kumuuguza mwanafunzi mwenzao,

"inabidi tuwahi kurudi tuje siku nyingine" Angel alisema,

"sawa wanangu jaman tuombeane uzima" mama Josephat aliongea huku akiwapa mkono wa shukrani, na Genes aliinama na kumshika Josephat sehemu ya kichwani palipofungwa kama ishara ya kumtakia pole na wengine wakafuata kwa kumshika hapo hapo kichwani na hapo Angel aliingiza mkono mfukoni nae pia akamshika hapo tena kwa bahati mbaya au nzuri wakati Angel anamshika kuliingizwa mgonjwa aliekua anapiga makelele sana kiasi kwamba kila mtu aliekua amelala basi aliamka kumtazama na hadi Genes nae alipiga kelele,hivyo hakuna mtu alieshuhudia kitendo Angel alichokifanya pale.

Genes na kundi lake wakatoka nje kila mmoja akiwa na majonzi ya hali ya juu.

Baada ya masaa mawili daktari alikua anapita kugawa dawa kwa wagonjwa,

"sasa huyu daktari atamuamsha tena mwanangu aanze kusumbua tena" mama Josephat alijisemea baada ya kumuona daktari anakaribia kumfikia,kwani tokea akina Genes waondoke yamepita masaa mawili bila Genes kusema wala kujigusa.

"mama muamshe mwanao" muuguzi alisema na haraka mama Josephat alianza kumgusa kwa mbali ili ashtuke.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Itaendelea ijumaa mahali hapa..... NA HUU NI MJADALA KUTOKA KWA Deo Massawe..

Juzi nilipokea ujumbe mfupi kutoka kwa msomaji wangu akitaka tujadili mada fulani inayohusiana na mapenzi nayo iko hivi...



Kwa mfano mwanaume amempenda msichana kweli ila hana ujasiri wa kuongea nae au kwa lugha nyingine hajui kutongoza kabisa yaani hana (swagaa) je atatumia njia gani ili mwanamke amuelewe ?? Na je kwa mwanamke ukimpenda mwanaume alafu ukawa na hofu ya kuwasilisha hisia unafanya nn ili ueleweke..







ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog