Search This Blog

Friday, November 18, 2022

PENZI LA MFUNGWA - 3

 






Simulizi : Penzi La Mfungwa 
Sehemu Ya Tatu (3)




Zabroni alipotea baada kufanya unyama ule,alimuacha mama mjamzito tumbo lake likibubujika damu baada kutolewa vijusi vilivyokuwemo kwenye tumbo hilo,ulikuwa ni unyama ulio pitiliza kipimo kiasi kwamba binadamu mwenye roho nyepesi hawezi kufanya hicho kitendo.

Upande wa pili yule jamaa alipo maliza mikakati yake alianza safari kumfuata mkewe huku moyoni akiwa na hofu kwani mapigo ya moyo wake kuna muda yalikuwa yakimuenda mbio pia wasiwasi nao ukimtawala kila mara,alijiuliza maswali kuhusu hali hiyo ambayo ningeni kabisa kuwahi kumtokea. Lakini jamaa huyo alipiga moyo konde kisha akaanza safari,kabla hajakimaliza kijiji ghafla akasikia mzee mmoja akimshuhudia mzee mwenzake kitu alichokiona huko porini. Mzee huyo alisema "Ama hakika tunako elekea sasa hii dunia imefika mwisho"

"Kwanini tena mzee mwenzangu? .."http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Dah huwezi amini nimekuta mama mmoja pori lile la miti mingi kapasuliwa tumbo,vile vitoto sasa vimetundikwa juu kama mishikaki " alijibu huyo mzee huku akifatia na sikitiko.

"Lahaulla..Mungu tutazame waja wako sisi mmmmh ", alisikika mzee msimuliwa akisema maneno hayo kwa sikitiko, na wakati wanasemazana hayo, kijana yule mwenye mke aliyetumbuliwa tumbo alistuka bila kupoteza muda alitimua mbio kuelekea huko ili akatazame kama ni mkewe ndio kafanyiwa hicho kitendo. Alipofika alimkuta ni mkewe kauliwa kikatili, hakika alilia sana hasa hasa alipovitazama vijusi vile vilivyo ning'inizwa juu kwenye mti kama mshikaki. Hali hiyo ilimpelekea kudata, uchungu wa kufiwa na mkewe aliyempenda kwa dhati ulimfanya kuwa kichaa. Dhambi na dumu nzito ikazidi kutanda juu ya kijana Zabroni,alifanya hayo akiamini kwamba analipa kisasi juu ya kifo cha wazazi wake. Habari ya hayo mauaji ilisambaa kila kona,na kila aliyeipata alihuzunika huku baadhi yao wakijiuliza ni roho gani aliyonayo muuwaji huyo?. Majibu alikosa,na baadhi ya watu kutoka vijiji vya jirani walitamani japo kwa dakika sifuri wamtie machoni mtukutu huyo. Na mara baada ya kufanya mauaji hayo,alitulia kwa takribani wiki mbili. Wanakijiji walipata ahueni wakiamini kuwa huwenda Zabro kauliwa kutoka na dhambi zake,lakini imani hiyo punde ilitoweka baada kuchomwa nyumba nyingine usiku wa manane. Na hapo ndipo hofu ilipo rudia kutanda kunako mioyo yao. Kwa kuamini hilo,mzee Fungafunga ambaye ndio chanzo hasa ya matatizo hayo aliingiwa na hofu aliamini kuwa muda wowote naye zamu yake itafika. Na wakati huyo mzee akiamini hilo jambo kutendeka muda wowote, upande wa pili kijiji jirani. Kijiji ambacho kilionekana kuchangamka kulingana na mishe mishe zake,lilionekna kundi la vijana wakicheza kamali. Kamali hiyo kimuonekano ilikuwa ya mazingaombwe. Unapewa lingi ndogo unailipia pesa kisha unaambiwa uchague mahala pakuirusha kwenye mazaga zaga waliyosambaza. Palikuwa na pesa zaidi ya ile unayoliyolipia lingi, vile vile palikuwa na juisi soda na mazaga zaga mengine ambayo ukiirushe ile lingi iwezekanike kuvivaa. Mchezo huo uliandelea kwa vijana wa pale,wengi walikosa kiasi kwamba baadhi yao iliwapelekea kununua lingi nyingi wakiamini kuwa huwenda wakafanikiwa. Lakini mambo bado yaliendelea kuwa vile vile bado waliangukia pua,wenye moyo mwepesi waliondoka zao huku wenye roho ngumu wakizidi kukomaa. Na wakati kamali hiyo inaendelea,ghafla walionekana vijana wawili wakiwa na mabegi yao mgongoni. Vijana hao wa makamo walionekana ni wageni katika hicho kijiji,kwani nyuso zao zahili shahili zilionyesha. Walipokuwa katika pitapita yao waliuona mchezo ule wa kamali uliokuwa unaendelea. Kijana mmoja ambaye aliitwa Madebe alimshika bega mwenzake kisha akasema "Bruno,pesa imetuishia. Kiukweli iliyobaki haitoshi halafu istoshe bado tunasafari ndefu. Vipi tufanyeje?..",alisema Madebe huku akikodolea macho upande ule uliojaa watu wacheza kamali pamoja na watazamaji.

"Doh ni kweli kaka,lakini unadhani tutafanyaje sasa"

"Hivi ile hirizi ipo humo kwenye begi?.." alihoji Madebe.

"Ndio ipo" alijibu Bruno.

"Sawa hebu nipe tusogee pale Kwenye kamali,unajua huu mchezo wanatia kiini macho,kwahiyo kwa kuwa wao wanafanya ujinga acha na sisi tufanye upumbavu", alisema Madebe. Bruno akaangua kicheko huku akifungua zipu ili ampe kaka yake hirizi. Alipo mkabidhi, Madebe aliivaa kisha akasogea eneo lile, alilipia lingi. Safari ya kwanza aliirusha kwenye pesa,akawfanikiwa. Akarudia kurusha kwenye pesa lingi ya pili,nayo vile vile akifanikiwa. Hapo sasa taita akaona Madebe anawaumbua,upesi alimuita kando kisha akasema "Ndugu naomba tusihalibiane kazi,nina familia inanitegemea sawa. Kwahiyo naomba upotee hapa mara moja kabla hatujahalibiana siku" Taita kiongozi wa kamali ile aliongea kwa sauti ya kunong'ona huku uso wake akiwa ameukunja. Madebe alipo ambiwa maneno hayo hakutaka kubishana naye,alimuita mdogo wake kisha wakaondoka zao wakati huo nyuma yao wakimuacha Taita anawasindikiza kwa macho.

Madebe na Brruno tayari walikuwa na pesa ya kuanzia huko wanako elekea, walikwenda kwenye mgahawa kula chakula kabla hawajaendelea na safari ya kuelekea kijiji kilw kinacho endelea maafa kwa niaba ya kutafuta vibarua ikiwa kama njia ya utafutaji wa pesa. Walanguzi. Wawili hao walipokuwa mgahawani, ghafla akaingia Zabroni . Hakutaka kuongea na mtu zaidi aliketi kisha akaagiza chakula akala, alipomaliza akaondoka zake bila kulipa. Hiyo ndio ilikuwa tabia yake sasa baada kujiona ni tishio kila pande. Ni tabia ambayo iliwakera mama ntilie wa kijiji kile lakini kutokana sifa mbaya na yakutisha aliyokuwa nayo Zabroni,mama ntilie hao walimuogopa sana kwa maana hiyo hata pesa ya chakula walikuwa hawamdai. Ila siku hiyo ilikuwa siku tofauti kidogo kwa mama ntilie huyo,alisikika akisema kwa jazba "Mijitu mingine bwana. Akha yanakera sio siri "

"Kwanini mama?..",alihoji Madebe baada kusikia mama huyo akilalama.

"Yani we acha tu,huyu jamaa hafai hata kidogo. Anachoma nyumba za watu anauwa bila hatia yani sijui anaroho gani huyu mtu. Ubabe na yeye na na ubabe sijui kwanini serikali inaendelea kumuangalia. ", Madebe na Bruno walistuka kusikia habari hiyo, ni habari ambayo iliwacha midomo wazi Kiukweli.

"Kwahiyo unataka kusema kashindikanika?..", kwa taharuki Bruno aliuliza.

"Kabisa hawezekaniki,anatumia dawa"

"Daah poleni sana", alimaliza kwa kusema hivyo Madebe kisha wakalipia chakula walicho kula wakaendelea na safari yao. Walitumia saa moja na nusu kufika,walipofika walipigwa na butwaa baada kukuta nyumba zikiwa majivu huku nyinginezo zikisalia kuta. Vilio kila kona kijijini hapo,Madebe akamgeukia Bruno kisha akasema "Hii hali inatisha sana, na bila shaka huyu ndio yule mshenzi tuliye ambiwa na mama ntilie..."

"Kweli kabisa kaka, je tuchukue hatua gani sasa maana hii hali yatisha ujue" alijibu Bruno huku akiangaza kila kona ya kijiji.

"Daah! Nafikiri ni kupambana naye tu hakuna namna"

"Je, tutampataje?.." ,Madebe aliingiza mkono mfukoni akatoa kitambaa cheusi chenye fundo akafungua fundo ambalo lilikuwa na unga mweusi. Unga huo aliupakaza kwenye kiganja kisha akasema "Tazama kiganjani kwangu ", Bruno akatazama alimuona Zabroni akiwa kwenye makaburi mawili,makaburi ya mama na baba yake. "Umeona? Huyu jamaa hapa ndio makazi yake. Sasa mdogo wangu lazima tule nage sahani moja..tuombe kwanza kibali cha kuishi kijijini hapa kisha tufanye kazi yetu kwa utulivu", aliongea Madebe,kijana aliyetunikiwa miradhi ya ndagu kutoka kwa marehemu babu yake.





Madebe pamoja na Bruno walizipiga hatua kuelekea kwenye nyumba moja kijijini hapo wakiwa na lengo la kumuulizia Mwenyekiti wa kijiji,kwenye mji huo waliwakuta watoto. Watoto hao walionekana wanyonge sana hasa kutokana na mambo maovu yaliyokuwa yanaendelea hapo kijijini huku wao wakishuhudi kwa macho yao,hali hiyo ya unyonge kwa watoto iliwauma sana Madebe na Bruno lakini iliwapasa kupiga moyo konde wakawauliza watoto hao wapi walipo wazazi wao. Mtoto mmoja mkubwa kuliko wote alijibu "Mama na baba hawapo wameenda shamba", alijibu mtoto huyo huku akionekana kuwa na hofu,nao hao vijana baada kupata jibu hilo kutoka kwa mtoto huyo waliendelea na safari yao,ilihali macho yao yakionekana kutazama kila pande ya kijiji kutazama jinsi kijiji kilivyo chakaa majivu yaliyotokana na nyumbaa kuungua.

Hatimaye walifika kwenye nyumba ya pili,hapo waliwakuta wenye nyumba. Madebe alijitambulisha pia alimtambulisha na mdogo wake kisha wakasema nia na dhumuni ya kufika kijijini hapo,nia yao ni kusaka maisha kwa njia ya kilimo. Vile vile walisema kuwa ni vema kabla ya kuanza kazi waonane kwanza na Mwenyekiti wa kijiji ili pindi yatakapo tokea matatizo basi wajue ni jinsi gani ya kuweza kusaidiana. Baba mwenye nyumba hiyo aliwaelekeza mahali ilipo nyumba ya Mwenyekiti wa kijiji,Madebe na Bruno wakaelekea huko ambapo walimkuta Mwenyekiti akijenga nyumba yake ndogo baada kubwa aliyokuwa akiishi hapo wali kuungua na moto.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Hodi hapa ", alisema Madebe,mwenyekiti alipo sikia sauti hiyo alisitisha zoezi lake la kuparata udongo pembeni kisha akageukia kule ilipotokea sauti. Aliwaona vijana wawili. Vijana hao walikuwa wageni kabisa machoni mwake. Hivyo kimoyo moyo alijisemea "Ugeni huu", wakati anasema hayo tayari hao vijana walikuwa wameshajongea Karibu yake kabisa.

"Shikamoo mzee"

"Shikamoo babu" Madebe na Bruno walimsalimia Mwenyekiti. "Malahabaa hamjambo? Karibuni sana", alijibu Mwenyekiti huku akiwasogezea benchi ili wapate kukaa. Walikaa kisha utambulisho ukafuatia,Madebe alijitambulisha pia akamtambulisha na Bruno. Na mwisho wa yote Madebe alieleza lengo kuu lililowafanya waje hapo kijijini,na katika malengo hayo hawakuweza kusema kama wanamikakati ya kulikomesha tatizo sugu linalo kikumba kijiji hicho.

"Karibuni sana vijana,kweli siku zote ujana ndio nafasi pekee ya kujijenga kiuchumi ili uzeeni usipate shida. Hakika nyinyi ni mfano wa kuigwa, lakini je mtapaweza hapa?..", alihoji Mwenyekiti, Madebe na Bruno walitazamana kisha Bruno akajibu "Siku zote mtaka cha uvunguni sharti ainame. Kwahiyo sisi tuatapewaza tu kama nyinyi wazee mnapaweza sembuse sisi? Tena vijana wanye nguvu zetu?.." Madebe naye alidakia akasema "Kwani ni sababu ipi ambayo inakutia hofu kuwa sisi hatukiwezi kijiji hiki? .." Mwemyekiti hakujibu zaidi alishusha pumzi kwanza kisha akajibu "Zabroni! Zabroni, kijana mtukutu ambaye tangu nizaliwe sijawahi kumuona kijana kama huyu. Hana hata chembe ya huruma,tangu wazee wake wauliwe kwa kuchomwa moto wakiwa ndani ya nyumba basi amekuwa muuaji,katili yani doh",alidondosha machozi Mwemyekiti huku akisimulia jinsi mtukutu Zabroni anavyofanya mambo ambayo binadamu wa kawaida hawezi kufanya,jambo kuu ambalo lilimuuma Mwenyekiti wakati anasimulia hayo ni kuhusu kifo cha mkewe pia na kifo cha mzee Baluguza.

"Pole sana mzee wetu lakini kuhusu hilo wewe usijali sisi tutavumilia istoshe tuna malengo na maisha yetu,mpambanaji hachoki mzee wetu" alisema Buruno.

Walipata nafasi ya kulaza mbavu zao,kesho yake asubuhi Mwenyekiti aliambatana na vijana hao mpaka nyumbani kwa muhindi,ambaye ndio tajiri wa kijiji. Hapo mwenyekiti aliamini lazima jamaa huyo atakuwa na shida na vibarua kwani ni mara chache sana shambani kwake kukaukiwa vibarua lakini kutokana na mambo yaliyokuwa yanajili kijijini hapo ikafikia hatua vibarua wakaadimika. Vibarua walipata, hekari mbili walikabidhiwa za kupalilia zao la muhogo huku hifadhi yani mahali pa kulala ikiwa ni kwa Mwenyekiti.

Kesho yake asubuhi walianza kazi,walifanya kazi huku mioyoni mwao wakiwa na lengo lao lile lile ambalo ni kumshikisha adabu mtukutu Zabroni, na lengo lao hilo waliliweka siri yao wawil pasipo kumwambia mtu yoyote.

Siku zilisonga wakiendelea kufanya vibarua, walisaidiana na Mwenyekiti kujenga nyumba kwa mapema zaid wakawa sasa wanalala ndani kwa amani kwani kipindi hicho Zabroni alikuwa ametuliza makeke yake. Miezi takribani miwili sasa ilikatika,hali ikiwa shwari kijijini hapo. Hakika ilikuwa ni jambo la furaha sana kwa wanakijiji, na hapo ndipo uvumi ulipoa anza kuzagaa kila kona ya kijiji pamoja na vijiji jirani wakivumisha kwamba Zabroni kauliwa,wengine wakisema katiwa uchizi huku wengine wakidiriki kuvumisha ya kwamba kijana huyo mtukutu kafungwa jela. Ila baadae uvumi huo ulikuja kuonekana si chochote si lolote baada usiku mmoja kuungua nyumba. Lakini pia usiku huo huo jeshi la polisi lilivamia kijiji hicho wakimtafuta Zabroni pasipo kujua kuwa kijana huyo anatumia dawa hakamatiki kirahisi. Jeshi hilo lilikesha likifanya dolia, kesho yake asubuhi ndipo lilipogundua kwamba kijana huyo wanayemtafuta ni mtu hatari sana. Polisi hao waliamini hilo jambo baada kuona nyumba nyingi zimeunguzwa kuachilia mbali hiyo iliyounguzwa usiku wa jana huku wao wakiwa humo humo kijijini. Hivyo waliendelea na kazi yao wakizunguka huku na kule huku wakishirikiana na mwanakijiji mmoja ambaye alijitolea kuwatembeza polisi hao akiwapeleka maeneo ambayo Zabroni hupenda kukaa. Walitembea kila sehemu lakini hadi jua linazama kamwe hawakuweza kumuona,ila kesho yake asubuhi hivyo hivyo harakati ziliendelea. Kama ilivyo ada walizulura kila kona kuanzia asubuhi mpaka jua la saa saba mchana,bado hawakuweza kumuona. Jioni ilipofika,polisi hao wakiwa tayari wamekata tamaa walirudi sasa kwenye gari yao ili wakapumzike. Ghafla mwanakijiji walio kuwa nae alimuona Zabroni akiwa juu ya tanuru akipangua matofali,mwanakijiji huyo alistuka akasimama kisha akasema kwa sauti ya chini. "Haya sasa mtu mwenye yuleee", alisema huku akinyoosha kidole chake kuelekea kule alipo Zabroni ambaye alionekana kuwa bize kupangua matofali kwenye tanuru la mzee Maguso,mzee ambaye anamkubali sana katika maisha yake. Kwa maana hiyo baadhi ya shughuli mbali mbali alikuwa akimsaidia,lakini pia kilichokuwa kikimfanya Zabroni ampende huyo mzee ni pale alipokuwa akimtia moyo na ujasiri katika mambo yake ya kulipa kisasi.

Jeshi hilo baada kumuona mtuhumiwa,hawakutaka kuamini mapema. Hivyo walichukuwa picha waliyokuwa nayo wakaitazama kisha wakamtazama na Zabroni kule alipo,ingawa alikuwa ameinamisha uso wake lakini kuna baadhi ya vitu walivitazama wakaamini kuwa ni yeye. Hapo ndipo waliposogea mpaka kwenye tanuru,kwa amri wakamtaka Zabroni ashuke kutoka juu ya tanuru. Zabroni aligoma alisema "Sishuki,kwani nyinyi akina nani? Na mnataka nini?.." majibu ya Zabroni yaliwastua polisi hao,mmoja akasema kwa sauti kali "Alo kwahiyo unapingana na serikali? Shuka haraka sana ..", alisema polisi huyo huku akimnyooshea bastora Zabroni. Lakini bado Zabro alionyesha kutostuka,kwa ujasiri alijibu "Sishuki mkitaka fanyeni jambo lolote,siogopi. Kwani serikali ndio nini? Achanani na mimi bwana", Zabroni alipokwisha kujibu hivyo aliendelea na kazi yake ya kupangua matofali wakati huo polisi nao wakizikoki bastora zao ili wamshuti kwa kigezo cha kukaidi matakwa yake,punde si punde polisi hao walifyatua risasi kama njugu lakini cha ajabu zilipomkuta Zabroni alicheka huku damu zikibubujika mwilini mwake kisha akapotea pale kwenye tanuru zikabaki nguo na vumbi huku mwenye mtukutu akiwa ameshayeyuka. Polisi hoi kila mmoja alikimbia anapo pajua yeye,ilimradi wafike kwenye gari lao. Lakini pia cha ajabu walipofika kwenye gari lao walimkuta mzee wa makamo akiwa na mkongojo wake kando kando ya gari hilo .





Jeshi lile la polisi walitaharuki kumuona yule mzee,ghafla waliingiwa na hofu huku kila mmoja akisita kulisogelea gari. Wakati huo upande wa pili alionekana polisi mwingine akija hea hea kwa kasi ya ajabu,alipolifikia gari alifungua mlango kisha akaliwasha. Kabla hajaondoka aliwatazama wenzake kisha akasema kwa sauti kuu "Mnashangaa nini? Hebu pandeni juu tuondoke ebo ", alisema hivyo huyo kamanda huku akivutia resi kiasi kwamba ilifanya gari hilo ya polisi kutoa mlio mkali. Makamanda nao baada kuambiwa kuwa wapande gari waondoke,walimtazama kwanza yule mzee waliomkuta pembeni ya gari lao kisha haraka sana walidandia ambapo kamanda yule aliyeshikiria usukani akaliendesha gari kulikimbia balaa la Zabroni. Baaada kutoweka, ghafla yule mzee aligeuka kutoka katika hali hiyo akawa mwenye Zabroni.

"Ahahahah", Zabroni aliangua kicheko kisha akasema "Mimi ni Zabroni", sauti hiyo ilijirudia mara mbili mbili.

Upesi akanuia maneno yake ili apate kupopetea maeneo hayo. Lakini kabla hajapotea, mara ghafla kijana Madebe alitokea akamshika bega kisha akamuuliza "Kwanini unauwa raia hovyo? Wanamakosa gani?.." Zabroni aliposikia sauti hiyo iliyoambatana na kuguswa kwake bega,aligeuka akamtazama mtu aliyemshika kisha akahoji "Hii ngoma ya kikabila hupaswi mrusi ama mzungu kutii maguu, kwani wewe unaniuliza kama nani labda" alihoji Zabroni huku akiwa amekunja uso wake. "Mimi Madebe, mtetezi wa wanyonge" alijibu Madebe.

"Ala! Kwahiyo umeamua kujitolea kwa ajili ya watu wa kijiji hiki?.." Zabroni alirudia kumuuliza Madebe,lakini Madebe hakujibu. Zaidi alinyoosha mkono wa kulia juu,punde si punde kwenye kiganja cha mkono ulitokea upanga. Panga ambalo lilimelemeta sana huku likionyesha makali yasiyo na mfano. Zabroni alistuka haraka sana alipotea akaibukia sehemu nyingine tofauti na ile ya awali,hapo sasa naye aliinyoosha mkono juu ila abadani hakikutokea kitu chochote. Hofu ilimjaa akajiuliza "Nifanye nini sasa ili nimkabili huyu mtu anaye taka kuharibu mipango yangu? ", wakati anajiuliza swali hilo,Madebe alitokea mbele yake akiwa na panga lake. alimtazama Zabroni kisha akasema"Wewe si mwanaume? Mbona sasa unanikimbia?", aliongea kwa kujiamini kijana Madebe huku akimsogelea Zabroni ilihari Zabroni naye akirudi nyuma. Mwishowe Zabroni aliamua kujibadilisha akawa katika umbile la nyoka aina ya cobra,hapo sasa ndipo ugomvi ulipo anza. Madebe alijitahidi kurusha panga lake kwa umahiri ili akate kichwa cha huyo nyoka, pia Zabroni naye ambaye yupo katika umbile la nyoka alifanya juu chini ili amgonge Madebe amtie sumu kali aliyokuwa nayo. Na alipoona hilo zoezi linakuwa ngumu,ndipo aliporusha mate lakini nayo hayakuthubutu kufua dafu kwa Madebe. Hakika ilikuwa vurugu maeneo hayo,ndege na wadudu mwitu walitulia kuona ugomvi huo wa aina yake.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Na wakati hayo yanajili kati ya Zabroni na Madebe,upande wa pili mzee Fungafunga alipata taarifa kuwa dada yake anamtaka Tina aende Dar es salam kuishi naye kwa maana kamkumbuka sana. Hivyo nafasi hiyo mzee Fungafunga aliitumia kama moja ya kuyatenganisha mahusiano ya mwanaye na kijana Zabroni. Alisubiri baadaye muda wa chakula cha usiku aseme na binti yake kuhusu taarifa hiyo ilihari moyoni akijisemea kwamba "Iwe isiwe lazima ataenda tu,sitaki mimi nipate mkwe katili kama huyu" alijisemea mzee Fungafunga huku kwingineko ugomvi ulikuwa bado unaendelea ila mwishowe Zabroni alipotea akaibukia juu kabisa ya kile cha mlima. Alisimama huko wakati huo akihema kwa nguvu ya ajabu akionekana kuchoshwa na balaa la mtukutuku mwenzie ambaye si mwingine ni Madebe. Hofu sasa ilianza kumtanda Zabroni, alijiuliza "Ni dawa gani anatumia huyu mtu?..", kabla hajapata jibu ,Madebe akatokea kwa mara nyingine tena. Safari hiyo alikuwa na sime mkononi yenye chata ya fuvu. Madebe akasema "Zabroni ulipo lala wewe ndipo tulipo amkia,nafikiri umefika wakati wako wa mwisho. Damu nyingi umemwaga lakini leo hii zitamwagika zako" alisema Madebe huku macho yake yakionekana kutisha yalifanana na macho ya nyoka,hali ambayo ilizidi kumtisha Zabroni. Aliogopa sana ila hakuwa na budi kupiga moyo konde ili amalizane na Madebe. Mvua ikaanza kunyesha,radi pamoja na ngurumo mbali mbali zililindima angani. Wakati huo huo Madebe akarusha sime yake,kabla haijamkuta mlengwa ambaye ni Zabroni. Zabro alilala,sime ikapita juu kisha papo hapo akajiugeuza akawa katika hali yake ile ile ya nyoka. Hakuwa na njia nyingine kwani kwa kasi aliyokuwa anatumia Madebe, ilimbidi Zabroni kutumia njia hiyo. Kweli juhudi yake hiyo iliweza kuzaa matunda,kwani alifanikiwa kumgonga Madebe mguuni baada Madebe kuzubaa kwa sekunde kadhaa. Madebe alianguka chini lakini pia kabla Zabroni hajafanya jambo lingine lolote juu yake,ghafla ile sime aliyoirusha ilirejea mkononi mwake ambapo bila kuchelewa aliitupa kwa Zabroni ambaye yupo katika umbile la nyoka,nayo ilimpata ubavuni hali ambayo ilimfanya arudi kwenye hali ya kawaida ambapo napo hakupoteza muda alipotea kisha Madebe naye akatoweka.

Kijijini alionekana Madebe akichechea huku mguu ukiwa umevimba,nyoka aliyemgonga alikuwa na sumu kali mno. Na kipindi Madebe akiwa na hali hiyo,ndani Mwenyekiti alimuuliza Bruno "Wapi alipo elekea kaka yako?.." Bruno hakujibu chochote,zaidi aliishia kujisonya kwani hakufahamu ndugu yake alipo elekea..aliondoka bila hata kumuaga. Ila wakati Mwenyekiti na Bruno wakiwa na sintofahamu,ghafla nje walimuona Madebe akija huku akkchechema mara ananguka na kuinuka. Bruno alistuka hima akamkimbilia,alipo mfikia alimnyanyua huku akimuuliza kilicho msibu. Lakini Madebe hakuweza kujibu chochote,hali yake tayari ilikuwa mbaya sana,sumu imeshapanda kwenye moyo. Bruno alizidi kuchanganyikiwa alirudia kumuuliza kaka yake "Kaka nini kimekusibu?..", lakini Madebe hakujibu,zaidi alijifungua hirizi yake akamkabidhi mdogo wake kisha akasema kwa taabu sana "Zabroni.. Za..broni. mdogo wangu lipa kisasi li..pa ki sa..sasiiii", kwisha kusema hivyo Madebe akaaga dunia. Kiukweli Bruno alilia sana kwa uchungu wa kumpoteza kaka yake. Aliamini aliyefanya kitendo hicho ni Zabroni. Wakati huo upande wa pili,Zabroni alikuwa kwenye Makaburi ya wazazi wake huku akijitazama kidonda chake alicho jeruhiwa na sime. Zabroni aliwaza na kuwazua akaona kabisa siku zake za kuishi zina hesabika hivyo hana budi kumaliza mchezo kwa kumuadabisha mlengwa mkuu ambaye ni mzee Fungafunga ili kisasi chake kiweze kutimia. Wakati anawaza hayo Zabroni, kwingineko Tina alipoambiwa kuwa anatikiwa kwenda Dar es salam kwa shangazi yake,aliona hawezi kwenda bila kukwichi na mpenzi wake wakuitwa Zabroni ilihari Zabroni naye dawa alizo nazo hatakiwi kufanya mapenzi. Na endapo atafanya basi zitapotea mwili mwake.





Siku tatu sasa zilikatika tangu Madebe afariki dunia,siku iliyofuata ambayo ni siku ya nne ndio siku ambayo Tina alipanga akutane na Zabroni ili wafanye mapenzi. Hivyo siku hiyo asubuhi Tina alidamka akaelekea mahali anapoishi Zabroni, alikuta majivu tu huku nyumba ikiwa imeteketezwa na moto. Tina alistuka sana baada kukuta hali ile,alitazama kulia na kushoto wakati huo akijiuliza ni wapi anapoishi Zabroni? Na kabla hajapata jibu mara ghafla alisikia sauti ikimuita,alistuka kisha akatazama kule ilipo tokea sauti akamuona kijana Zabroni akiwa chini ya mti mdogo huku pembeni yakionekana makaburi. Tina alizidi kushangaa kiasi kwamba alionyesha uso wa hofu ila Zabroni akawa amemuondoa hofu yake kwa kumwambia "Njoo mpenzi wangu usiniogope,haya ndiyo maisha yangu kwa sasa"

"Kwanini lakini umeamua kuishi huku?ujue tabia yako mimi sijaipenda" alisema Tina huku akizipiga hatua kumsogelea mpenzi wake. Alipo mfikia alikaa kando kando yake halafu akaongeza kusema "Hivi Zabro unajisikiaje kukaa kwenye mazingira haya? Sehemu nyingine zooote hujaziona mpaka uje kukaa eneo hili?.." Zabroni akajibu "Tina,kama nilivyokwisha kusema hapo awali kwamba haya ndio maisha yangu. Nimeamua kuja kukaa huku na wazee wangu ili nipate amani ya moyo wangu kwahiyo naomba usiwaze wala kuumiza kichwa kwa suala hili" alisema Zabroni tena kwa msisitizo.

"Zabro,.."

"Naam "http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Unanipenda kweli?.."

"Ndio tena nakupenda"

"Sawa asante,ila leo kuna jambo naomba nikuulize"

"Jambo gani?.."

"Naomba uniambie kwanini unauwa hovyo, unawarudisha wanakijiji nyuma kwa kuchoma nyumba na malighafi zao kwanini lakini.. tazama mpaka baba kaniambia niachane na wewe kutokana na tabia zako eti hawezi kuwa na mkwe mwenye roho mbaya. Kwahiyo Zabro mpenzi hatakama hutaweza kuniambia sababu ila basi achana na unyama huu tafadhali.." yote hayo alikuwa akiyasema Tina akijaribu kumshawishi Zabroni aachane na matendo anayo yafanya,lakini mara baada Zabroni kusikia maneno hayo ya Tina. Ghafla alipandwa na hasira,alimtazama Tina mara mbili mbili kisha akayatazama makaburi ya wazazi wake. Akasema tena huku akiwa na hasira kiasi kwamba mdomo wake ulionekana kutetemeka "Abadani Tina huwezi kunibadilisha tabia mimi,lengo nililo liweka moyoni mwangu huwezi kulipangua. Tena kawaambie washauri wako waniache ,pia vile vile waambie dawa ya moto ni moto" kwisha kusema hayo Zabroni alisimama kisha akaondoka zake,Tina naye alisimama akaanza kumfuata huku akiomba msamaha pia akiomba japo dakika moja ili aseme nae jambo. Zabroni alizidi kutembea huku akikazana lakini aliposikia msamaha wa Tina,hatimaye alisimama kisha akamgeuki halafu akahoji kwa hasira "Unasemaje?.." Tina alijishusha akawa mnyonge kisha akasema huku akilia "Zabroni, samahani kama nimekukera. Pia nashukuru kwa kunipa nafasi ya kunisikiliza. Mpenzi mimi naenda Dar es salam siku yoyote. Hivyo naumia sana kukuacha mwenyewe mpenzi wangu,lakini pia nilikuwa nina ombi moja" hapo Tina alisita kidogo ambapo ndipo Zabroni naye alipo pata nafasi ya kumuuliza huku akimtazama usoni "Kitu gani?.."

"Unajua siku..siku siku nyingi mimi na wewe hatujafanya mapenzi,kwahiyo naomba tukumbushie basi hata kwa nusu saa. Ikiwa kama njia pia ya kukuaga, hakika nitafurahi sana nikiondoka huku nikiwa nimefanya mapenzi na wewe kwani nitajiona mwepesi sana" Tina aliongea huku akichezea chezea vidole vyake, uso wake nao ukiona haya. Zabroni kijana mtutuku anayelipa kisasi huku tegemezi lake kuu ikiwa ni dawa,dawa ambayo sharti yake kuu hutakiwi kufanya mapenzi. Aliwaza sana,ukweli anampenda sana Tina istoshe anauchupa usio wa kawaida ila tatizo ni hapo tu. Je, atafanya mapenzi? Ilihali tayari anaadui nyuma anamnyemelea. Lakini pia kabla Zabroni hajatoa jibu juu ya ombi la mpenzi wake,alikumbuka kuwa mlengwa mkuu bado hajamalizana naye ambaye ni mzee Fungafunga baba yake Tina. Mtihani kwa Zabroni ila mwishowe alimpa jibu moja tu Tina "Nenda tutakatana jioni kwa sasa sina hamu yoyote,siunajua mapenzi hisia?.."Tina alitabasamu baada kusikia maneno ya Zabroni kisha akamwambia "Sawa lakini umenisamehe?.." Zabloni akajibu "Ndio "http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Mmh basi cheka kama kweli umenisamehe", Tina alitania Zabroni akacheka kama Tina alivyotaka huku ikiwa moyoni analake jambo,muda huo huo waliagana Tina alienda nyumbani kwao huku akiamini kuwa jioni atakuwa na mchezo dhidi ya Zabroni. Hakika furaha isiyo kifani ilimjaa moyoni ilihari upande wa pili Zabroni alijisemea kwamba hatoweza kufanya mapenzi mpaka pale atakapo kamilisha zaezi lake la kulipa kisasi. Tina alipo fika nyumbani,baba yake alianza kumfokea. Alimuuliza wapi alipokwenda,lakini binti huyo alikosa majibu ya kumpa baba yake ambaye ni mzee Fungafunga. Hivyo kitendo hicho kilimfanya mzee huyo kuhisi kuwa huwenda mwanaye katoka kwa Zabroni jambo ambalo halipendi katika maisha yake. Kwa hasira alimuamuru mkewe amuhimze binti yake wajiandae ili waanze safari ya kwenda mjini ili kesho yake iwe safari ya moja kwa moja Dar es salam. Upesi maandalizi yalifanyika,maandalizi ambayo waliyafanya huku Tina akilia kwani aliona anondoka bila kurudia kuhonja penzi la mtukutuku Zabroni. Alijiuliza ni lini tena itatokea hiyo nafasi? Kwa maana hakuwa na imani kama Zabroni ataishi miaka mingi kutokana na mambo anayo yafanya. Safari ilianza kati ya Tina na mama yake huku mzee Fungafunga akimsisitiza mkewe awahi mapema kwani hali sio shwari kwenye kijiji. Wakati mama Tina na mwanaye wakiwa njiani,Zabroni aliwaona. Alijua dhahiri Tina atakuwa anasafiri kama alivyomwambia hapo awali, Zabroni alifurahi sana kwani alijua tayaru kapata nafasi ya kukamilisha malengo yake. "Bado muhusika" alijisemea Zabroni kisha akatoweka eneo lile alilokuwa amekaa muda wote.

Usiku ulipoingia, aliamka tayari kwa niaba ya kwenda kukamilisha jambo lake. Siku hiyo mzee Fungafunga na mkewe walilala ndani wakiamini kwamba huwenda siku hiyo mtukutuku Zabroni asitembeze moto. Mke na mume walilala tena kwa furaha huku mzee Fungafunga akijisemea moyoni "Hapa moyo wangu umetulia sasa, kumtoa mwanangu kijijini hapa ni jambo la heri. Sasa ngoja nione huyu mwana haramu atachukuwa hatua gani,siwezi kuwa na mkwe mwenye roho mbaya kama huyu",kwisha kujisemea hayo Fungafunga alijivutia shuka tayaru kwa kuanza kuutafuta usingizi. Na punde si punde usingizi ulimpitia yeye pamoja na mkewe,walilala fo fo fo ilihari muda huo wazee hao wakiwa kwenye dimbwi la ndoto,Zabroni naye alitua nje ya nyumba. Alifyatu njiti akawasha sigara yake aina ya ngaja kisha moto uliosalia kwenye njiti akatupia juu kwenye nyumba. Sekunde dakika moto ulisikika huku mzee Fungafunga na mke wakiwa ndani,walistuka kutoka usingizini huku tayari moto ukiwa mkali kiasi kwamba walishindwa kujiokoa. "Ahahahaha hahahahah", Zabloni alicheka sana baada kufanya kitendo kile,katika akili yake aliamini kuwa tayari shughuli imekamilika. Lakini wakati akiwa katika imani hiyo mara ghafla aliguswa bega!







Baada kuguswa bega alistuka upesi akamgeukia mtu huyo aliyemgusa usiku huo wa manane. Ni Bruno. Mdogo wake marehemu Madebe,sura ya huyo kijana ilikuwa mpya kwa kwa Zabroni japo alimtazama kwa mwanga wa moto ulio tokana nyumba inayoteketea hivyo hakuweza kumtambua,zaidi alijiuliza "Huyu ni nani? Na anawezaje kunigusa bega?..", kabla hajapata jibu la hilo swali,Bruno alisema" Hujui sikujui ila kwa kumbukumbu naweza sema utanikumbuka endapo kama nitakukumbusha"

"We ni nani?..", alihoji Zabroni kwa kujiamini kabisa. Bruno alicheka sana kisha akafumbua kiganja chake,ulitokea mwanga mfano wa video. Katika mwanga huo kiganjani hapo lilionekana tukio lile la Zabroni na Madebe walipokuwa wanapigana,na mwisho wa tukio lile ilionekana ile sehemu ambayo Madebe alikuwa akimkabudhi hirizi mdogo wake huku akimtaka alipe kisasi. "Ndio mimi hapa natakiwa nifanye kile kitu kaka alicho nituma,hakika damu yake inanidai", alisema Bruno baada kumaliza kumuonyesha Zabroni ile video fupi kwenye kiganja chake. Lakini kijana Zabroni licha ya kuambiwa hayo maneno,kamwe hakuonyesha kustuka. Alicheka kisha akajibu "Nirahisi sana kunitamkia hayo maneno lakini ni vigumu kuyafanyia kazi kwa vitendo. Dogo, mimi leo ndio rasmi nimekamilisha kazi niliyofanya miezi kadhaa iliyopita. Hivyo sistahiri kuendelea kutenda dhambi zaidi,niliyo yafanya yanatosha", Kwisha kusema hayo Zabroni aliondoka zake. Bruno akamfuata,na ndipo Zabroni alipo amua kupotea kimazingara. Akaibukia kando kando ya mto,ilihali muda huo huo Buruno naye akatokea. Alistuka Zabroni baada kumuona kijana huyo anazidi kumganda wakati yeye hayupo tayari tena kufanya mauaji. "Bwana mdogo unataka nini tena kutoka kwangu?.." Zabroni alimuuliza Bruno tena kwa hasira. Bruno akajibu "Nataka kichwa chako Zabroni, sifa zako mbaya zimezagaa kila pande kwa sababu ya mauwaji yako,inakuwaje unauwa watu bila hatia? Hivyo basi kama utaweza niuwe na mimi basi lakini tofauti na hivyo utakufaa wewe ", alijibu Bruno huku akijiandaa kumrushia kombola Zabroni, ila kabla hajarusha. Zabroni akamwambia "Sawa, siunataka kuniuwa? Tazama juu kuna nini"

"Hapana huo ni ujanja wako Zabroni, sitegeki kishamba mimi", Bruno alijibu kisha akamtupia Zabroni moto wa kichawi. Moto huo ambao ulikuwa na nguvu ya ajabu ndani yake ulimpata Zablrni ukamtupa katikati ya mto ambapo muda huo huo Bruno alipaa juu huku akiwa amekunja ngumi nzito,ambayo alishuka nayo mpaka kwenye tumbo la Zabroni. Kitendo ambacho kilimzamisha chini zaidi kijana huyo mtukutu. Mamba samaki pia na wadudu wengineo waishio majini kwenye mto huo walitulia kupisha mpambano huo uliojumuisha nguvu za giza, Bruno alifanikiwa kumuadabisha Zabroni kwani kila Zabroni alipotaka kujitetea alijikuta akizidiwa ujanja na Bruno kwa kupigwa ngumi za haraka haraka zilizo changanywa na nguvu ya giza. Dakika kumi tu Zabroni hoi alisahau hata yale maneno ya kunuia ili abadilike kuwa kiumbe chochote kwa maana ngumi nzito iliyotua kichwani kwake iliweza kuyumbisha ubongo,hali iliyopelekea Zabroni huo muda kupoteza fahamu. Alipigwa sana kila mahala,Bruno alionyesha kujawa na hasira moyoni mwake. Hasira hiyo ndiyo iliyompelekea kumpiga Zabroni bila huruma kwani kila alipomkumbuka kaka yake ndivyo nguvu za kuchezea na mashavu ya Zabroni zilivyozidi kuongezeka. Mwishowe Zabroni alionekana kulegea kabisa mithiri ya kambale,hapo Bruno akajua tayari kazi imekwisha lakini ataamini vipi kama kweli kafa? Ndipo alipoamua kumvuta nchi kavu ili amuhakikishe. "Naam! Kazi imekwisha,hakuna mwamba chini ya jua zaidi ya muumba aliyekuumba. Zabroni Zabroni sasa ni wakati wako wa kwenda kulipwa yale uliyo yafanya hapa duniani", alisema Bruno baada kumkagua Zabroni kila sehemu ya mwili wake na kukuta tayari mtukutu kaaga dunia. Mara baada kusema hayo alimalizia kusema tena " Mimi ni Bruno shujaa... kwani siku zote shujaa hafi vitani bali shujaa ni yule anaye pambana na kurudi nyumbani na ushindi", Hapo alikata hirizi iliyokuwa kwenye mkono wa Zabroni kisha akawaza aondoke zake amuache Zabroni pale nchi kavu aidhaa amtupie mtoni apelekwe na maji sehemu isiyo julikana ikiwezekana awe chakula cha mamba? Kwani kwa hali ile kamwe mamba wasingemuacha salama,hirizi ambayo ingemlinda tayari ilikuwa mikononi mwake. Hivyo Zabroni atakuwa chakula cha mamba na samaki. Lakini kabla Bruno hajafanya huo uamuzi akajiuliza kwa mara nyingine tena "Tayari huyu mtu alikuwa ni tishio hapa kijijini je, hata nikipeleka habari ya kifo chake kwa wanakijiji wataniamini kweli?", alijiuliza Bruno mwishowe akaona ambebe begani moja kwa moja akaenda kumtunduki juu ya mti mkubwa kando ya barabara nyembamba ipitikayo kwa wingi na watu waendao na kurudi gulioni. Hapo ndipo Zabroni alipo tundikwa juu juu kwenye huo mti ule ambao kipindi cha nyuma aliwatundika vijusi alivyo vitoa tumboni kwa mama mjamzito. Kwisha kufanya hayo Bruno aliondoka zake na hirizi ya Zabroni. Akiwa amelowa jasho na damu aliitia hirizi ile kwenye mfuko wa koti alilokuwa amelivaa,kabla hajapotea kimazingara alizipiga hatua kadhaa kutoka pale alipo Zabroni hatua zipatazo kumi na tano kisha akasimama, akageuka kuutazama mti ule aliomtundika Zabroni akatikisa kichwa na akasema "Kufa tu hukuna namna mwanaharamu mkubwa wewe", kwisha kusema maneno hayo akachukuwa kitambaa akajifuta damu kwenye mikono yake halafu akapotea. Alipo fika kijijini alikuta nyumba tatu zimeteketea kwa moto usiku huo huo. Ndipo hapo Buruno alipokumbuka maneno ya Zabloni alipo mwambia

"Sawa, siunataka kuniuwa? Tazama juu kuna nini" Buruno alipokumbuka hayo maneno akajiongeza kwa kusema "Alaah! kumbe huyu mshenzi alimanisha nitazame juu kuangalia mwanga wa nyumba zinazo ungua? Ooh Mungu wangu" Bruno aliumia moyoni kisha akajipa moyo akisema "Sawa natumaini pindi wahanga hawa watakapo kuona ukiwa maiti basi mioyo yao itajaa tabasamu bashasha",alisema Bruno huku akiingiza mkono mfukoni aitoe hirizi ile aliyoichukua kwa Zabroni ili aitupie kwenye moto,lakini ajabu hakuikuta. Alistuka sana huku asijuwe kwamba muda ule alipotoa kitambaa kujifuta damu kiganjani aliidondosha chini. Pumzi ndefu alishusha na pindi alipotaka kurudu kuichukuwa, Mwemyekiti aliifka eneo la tukio kisha akamwambia "Hii ndio taabu ya hapa kijijini kijana wangu,hakika sitoamini siku nikimuona huyu mwanaharamu kauwawa". Hapo sasa Bruno alishindwa kumtoka Mwenyekiti ili aifuate hirizi ile kwani angeonekana hajaguswa na kitendo hicho cha nyumba kuungua. Muda huo sasa alfajiri tayari ilikuwa imeingia,umande na baridi ulimfanya Zabroni kutikisa kiuongo kimoja cha mwili wake,kumbe mtukutu alikuwa bado hajafa! U hai.





Zabroni alitikisa mkono wake ambao ulikuwa unabembea,wakati huo chini ya ule mti aliotundikwa alikatiza kijana mmoja hivi wa makamo. Kijana huyo alikuwa katika harakati za kuwinda alfajiri hiyo mapema, hivyo akiwa chini ya mti aliotundikwa Zabroni ghafla tonya la damu lilimdondokea kichwani. Lakini alipuuzia akidhania kuwa huwenda tonya la umande ndilo lililomdondokea,ila mwishowe alistuka baada mchirizi wa damu kumdondokea kama maji. Hapo ndipo kijana huyo muwendaji alipoinua uso wake kutazama juu akamuona Zabroni akining'ia,alitaharuki. Haraka sana alitimua mbio huku akianguka mielekea mara mbili mbili wakati huo akipiga kelele akimuogopa Zabroni. Ila alipo fika mbele kidogo alisimama kisha akageuka kutazama nyuma alipotokea, mapigo ya moyo yalimuenda mbio akijiangalia yupo mikono mitupu. Sime mkuki pamoja na upanga vyote akiwa amevitupa pasipo yeye mwenywe kujielewa, yote hiyo ikiwa ni hofu ya kumuogopa Zabroni.

Kwa kutumia mkono wake wa kushoto,kijana huyo muwindaji alijigusa kichwani kisha akajitazama vidole vyake akaona damu. Akajisemea moyoni "Hii si damu? Mmh huyu jamaa atakuwa amekumbwa na nini sasa,na mbona asubuhi yote hii kanasa juu ya mti wakati sio kawaida yake?..Loh! Sio bure hapa kutakuwa kuna kitu kimetokea, Zabroni huyu ni naye mjua mimi hawezi kufa kizembe kizembe wala sio wa kujeruhiwa tu hovyo hovyo ", alijisemea muwendaji huyo huku akionekana kutaka kurudi kuchukuwa zana zake za mawindo. Lakini dhumuni hilo lilitoweka baada kukumbuka kasheshe kadhaa alizofanya Zabroni, aliamuwa kitimua mbio kuelekea kijijini kwa niaba ya kueleza kile alicho kiona. Na wakati huyo muwendaji alipokuwa akitimua mbio kwenda kutoa taarifa, upande wa pili kijijini. Alionekana Bruno akikuwa na Mwenyekiti wa kijiji pia na wazee wengineo wa kijijini hicho,walikuwa wamekaa wakiomboleza msiba mzito wa mzee Fungafunga na mkewe waliofia ndani pia na vifo vya wahanga wengine. Kiukweli yalikuwa ni majonzi ya aina yake,kila mmoja alisikitika kwa staili yake ilihari mioyoni mwao wakitamani Zabroni auwawe kwa njia yoyote kwani unyama aliokuwa akiufanya ulipitiliza kipimo hata Mungu hapendi. "Bruno,Huu ni wakati wa wewe kurudi nyumbani kwenu. Umempoteza kaka yako,chunga na wewe usije kupotea. Wazazi wenu mkawacha na viulizo,chukua mizigo yako uanze safari,haya mambo tuachie sisi",ilikuwa ni sauti ya Mwenyekiti akimwambia Bruno kwa masikitiko kabisa. Bruno naye aliposikia maneno hayo,alishusha pumzi kwanza kwa nguvu kisha akajibu. "Najua pia natambua ni namna gani mnavyopata shida,lakini mzee wangu labda nikwambie kitu. Siku zote Mungu akitaka kukupa mafanikio haji yeye kama yeye ila atapitia kwa binadamu mwenzako, lakini pia ukae ukijua hapa duniani hakuna mwamba. Bali mwamba ni Mungu pekee aliyejuu na sio sisi binadamu tulio umbwa kwa udongo na mwisho wa siku tunarudi kwenye udongo", alijibu Bruno,Mwenyekiti na wazee wengineo waliokuwepo mahala pale kila mmoja alitaharuki kusikia maneno ya kijana mdogo. Mzee mmoja alimgeukia kisha akamuuliza "Unamaana gani?.." Lakini kabla Bruno hajamjibu huyo mzee,mara ghafla yule kijana muwindaji alifika mahali hapo kwa kasi huku akihema juu juu. "We nawe vipi unawazimu?.." alihoji mzee wa pili huku akiwa amemkodolea macho. Mwenyekiti akaongezea kusema "Huyu kijana huwa namuangalia sana,kiukweli yani akili zake hazina tofauti na akili ya ndezi ama kobe. Chizi sio chizi,mwehu sio mwehu. Sijui ana akili gani huyu konono", alisema Mwenyekiti kwa hasira kali kwani huyo kijana aliwastua sana kwa kasi aliyokuja nayo,baadhi ya walitaka kukimbia wakidhania kuwa tayari mtukutu katia maguu. "Haya zungumza kilicho kufanya utoke huko mbio mbio mpaka hapa", muwendaji huyo ambae ni shuhuda,alituliza nafsi yake kwanza kabla hajaanza kuongea kile alicho kiona kule mstuni. Watu wote waliokuwepo pale kwenye maombolezo walimtazama yeye,naye alipo jihakikishia kuwa tayari yupo sawa alisema "Zabroni....",watu wote kasoro Bruno walistuka kulisikia hilo jina,Ghafla mmoja mmoja aliinuka na kisha kuondoka zake wakiogopa kwamba huwenda Zabroni yupo nyuma,ndio aliyekuwa anamkimbiza kijana huyo muwendaji aliyekuja mbio mbio. Upande wa Bruno yeye hakuwa na hofu kwa sababu aliamini kuwa tayari huyo kijana atakuwa ameona maiti ya Zabroni na hivyo atakuwa amekuja kutoa taarifa rasmi hapo kijijini kuhusu kifo cha huyo mtukutu,kitu ambacho ndicho alikuwa akikitamani na ndio maana alimtundika eneo lile la wazi ili mpita njia ama muwindaji yoyote atakae katiza eneo lile aweze kuishuhudia. Hivyo hofu ilitanda hapo,mama mmoja alisikika akiitikia kwa kusema "Heeh Zabroni? Aawapi jamani nilikuwepo nitarudi baadae", aliongea huku akiambaa na njia kutafuta mahali pa kujibanza ili kama Zabroni atafika pale yeye asiwepo. Lakini kabla hajafika mbali alisikia sauti zikisema "Mmmh jamani kweli ? "

"Aah sidhani,mzee Baluguza mtalamu. Mganga kati ya waganga kamshindwa eti leo hii ndio afe. Tena kirahisi rahisi tu? Teh teh teh..hiyo ndoto ya mchana "

"Sio bure huyu jamaa anakuwa kajambiwa na ndezi wake huko polini,anakuja kutueleza ujinga wake"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Teh teh teh teh..Ni rahisi sana panya kubeba mimba ya paka kuliko mtu wa kawaida kumuua Zabroni, acheni kudanganyana bwana", zote hizo zilikuwa ni sauti moja ya maongezi yaliyosikika kwa fujo maeneo hayo,yote kutoka na kijana yule muwindaji kusimulia kile alicho kiona huku akisisitiza kuwa Zabroni kafa. Fujo ilisikika huku baadhi ya watu wakidiriki kumtukana,lakini baada Bruno kuona utata unazidi ndipo alipotaka kukata mzizi wa futina ili kuwaweka wanakijiji katika hali ya amani. Alifikinya kiganja chake kwa kutumia mkono wa kulia alifikanya kiganja cha mkono wa kushoto,kisha akafumbua kiganja hicho ambapo ulionekana ule mpambano aliopigana naye mpaka tamati. Hakika wanakijiji walishusha pumzi kila mmoja akimtazama Bruno kwa jicho la tatu na kumuona ni shujaa wa kukumbukwa katika hicho kijiji,yule mzee aliyemuuliza swali hapo awali alipata jibu la swali lake . Ambapo Bruno alipo mtazama,naye akamuonyeshea dole gumba kuonyesha kuwa tayari jibu analo. Furaha ilitawala sasa,hata wale walio kimbia mwanzo walirudi kuungana na wenzao kufurahia kifo cha Zabroni.

Baada ya hapo msafara wa wanakijiji ukiambatana na shujaa wao Bruno huku kiongozi akiwa Mwenyekiti,ulijikusanya ukaenda kuufuata mwili wa Zabroni ili wauchome moto. Lakini walipo fika eneo hilo hawakuuta mwili huo,walitaharuki wakamtazama Bruno ilihali Bruno naye akionekana kushindwa kujua kilicho tokea. Hofu kwa mara nyingine tena ilitanda mioyoni mwao,kila mmoja akionekana kuwa na sintofahamu kuhusu mtukutu. Na wakati wote wakiwa katika hali hiyo mara ghafla ilisikika sauti ikisema huku ikijirudia mara mbili mbili. Sauti hiyo ilisema "Mimi ndio Zabroni. Nimerudi ",sauti hiyo ikamaliza kwa kicheko kikali. Punde baada kusema hivyo ghafla....!



ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog