Simulizi : Nilivunja Ndoa Zangu 3 Kulipiza Kisasi
Sehemu Ya Tano
(5)
Nimeamua kukupatia kiwanja hichi , Na
ninakuahidi mambo yangu yakiwa mazuri nitakujengea nyumba mpenzi, sawa
mama?
Alinibusu tena. Wakati huo huo alipomaliza kunibusu,, mlango wa
ofcn kwake ulisukumwa.
Hamadi… nilitamani ardhi ipasuke, niliogopa
sitakaa nisahau katika maisha yangu yooote, mapozi yaliniisha,, uwiiii,,,
niliogopa.. Nilikuwa natetemeka vibaya mno.
Aliyefungua mlango naye
alishangaa kwani alitukuta tumekumbatiana na mzee Zuberi, Mkumbato wa nguvu na
kumaanisha kwa kila mmoja. Mzee zuberi akushukuru mimi kumpatia penzi tamu, na
mimi nikimshukuru kunipatia kiwacha cha nusu heka. Nilikuwa namaanisha
kumkumbatia kwa dhati, nay eye alikuwa anamaanisha kunikumbatia kwa dhati. Wote
tukiwa tumekumbatiana haswaaaaa. Hivyo hata aliyeingia alishuhudia tukio hilo na
lilimshangaza kama tulivyoshangaa na sisi.
Baada ya sekunde kadhaa baada
ya kugundua kuna mtu kaingia ofcn tuliachiana, huku mzee Zuberi akiniambia sogea
pale. Na aliyeingia akionekana kushikwa na jazba huku akihema kwanguvu sana,na
akitetemeka asijue la kufanya.
Mungu wangu, shit, Mungu wangu, shit, ni
maneno ambayo alikuwa akiyatoa mama yake Husna baada ya kuniona ni mimi Charlote
nimemkumbatia mumewe,,, shit,, huku akinisogelea, shit…. Mzee Zuberi aliniambia
Charlote tupishe,, huku nikiwa najificha mgongoni mwa mzee Zuberi. Niliondoka
lakini sikusahau Bahasha ile, niliikwapua na kuondoka nayo. Nilishakuwa
mang’aaa, yani ndani ya zali kama hilo lakini sikusahau Bahasha ile. Niliondoka
kwa speed ya ajabu na kuelekea Ofcn.
Nilifika ofcn na kumuomba rafiki
yangu anihifadhie bahasha ile. Alinihifadhia kisha nikaingia ofcn na kumpigia
mume wangu simu kumuomba aje kunipitia akitoka kazini ili tuelekee nyumbani
wote. Jones alifurahia sana, alifurahia mno.
Jioni kweli alikuja
kunichukua na nilijichangamsha sana kwake ili asijue kama kuna jambo limetokea,
na hangeweza kujua kwa namna nilivyokuwa mchangamfu.
Na niliamini hata
kama Yule mama angekuja kunishtakia ningemruka futi mia na kumrudishia kesi yeye
kwamba bado ananifuata fuata.
Baada ya kama lisaa limoja baada ya kula
mimi na mume wangu, simu yangu ya mkononi iliita.. niliitazama sikujua ni nani.
Niliamua kuipokea baada ya kuita mda mrefu.
Nilipokea… … Asante sana
mwanangu asante sana.. ni sauti ya mwanamke ilikuwa ikiongea,,, niligundua ni
sauti ya mama Husna. Nilisjisahau kama mume wangu yuko karibu,, nilishikwa na
hasira na kujikuta nimemjibu na kumwambia,, MTOSHELEZE MUMEO…. Na nikakata
simu.
Neno hili mume wangu alilifahamu kwani nilipomuelezea kuwa
nilizungumza na mama yake husna na akanijibu hivi aliona nilivyokuwa
nimelishikilia na lilivyokuwa linaniummiza. Hivyo aliniambia tu Charlote mke
wangu , charlotte mke wangu,,, hembu achilia basi mama.
Nilimwambia kuna
mtu kanikera, akaniambia sitaki kuongelea issue yako mamiii, tulia mke wangu.
Nilijjidekeza na kuamua kutulia kama alivyosema. Ila usiku kucha ile hali ya
kufumaniwa nilikuwa naikumbuka, nikasema natamani kuzungumza na mzee Zuberi
nisikie ataniambia nini. Nilitamani pakuche haraka sana ili nimpigie simu
nimuulize kulikoni.
Ni siku kadhaa tu baada ya harusi ni kama siku tano
ama nne sasa harusi ifungwe, na shamra shamra zimepamba moto, kwa vyovyote vile
hawezi kususa na kuondoka, kwanza mtu mzima ataenda wapi? Atachekwa,, niliwazz
peke yangu kisha
nikatabasamu.
***************************************************************************************************
Nilichokuwa
natamani ni kuongea tu na Mzee Zuberi, sikuwa natamani kuongea na mtu mwingine
yeyote.
Nilifika ofcn mapema sna, nafikiri ni saa kumi na mbili na robo.
Nilikuwa sina la kufanya, ila tu ni kutamani kuongea na mzee Zuberi anieleze
kulikoni? Sikuwa najali kabisa mkewe kuniona, ila nilikuwa natamani kujua ili
nijue je nitafanyeje kuhusu Husna na Majid, kwani bado natamani Husna naye
kimuume bara bara,,, na sasa nilikuwa najipongeza kwa nilichokifanya kwa mke wa
Mzee Zuberi, japo ilikuwa mapema sana, lakini bado nilijipongeza yeye kuniona,
kwani lengo langu ilikuwa ni siku moja nimshawishi mzee Zuberi tukutane hoteli
moja mjini na nitafuta mtu atakayemueleza mkewe yaaani mama Husna kwamba niko na
mumewe na aje kushuhudia, ni kama nilikuwa nimepanga kutafuta mmbea
atakayemueleza Mama huyo taarifa zamahusiano yangu na mumewe. Lakini kama
nilivyopanga ilitokea hivyo hivyo, isipokuwa kuja kwa mama Husna ofcn kwa mumewe
haikuwa kuja kufumania ila kuja kuongea na mumewe kwa habari ya harusi ya mwanao
na kupeana taarifa kama sio kuja kuchukua michango aliyoitiwa .
Saa
mbili kamili, nilichukua simu yangu ya ofcn na kumpigia mzee Zuberi…. Iliita kwa
dakika kadhaaa.
Kisha ikapokelewa… alipokea mzee Zuberi, mara zote
nilimsalimia.
Shikamoo … marahana bi mdogo,, hujambo?
Aliiitikia
kwa furaha sana,, nikajua hakukuwa na tatizo kubwa, wala hakuonekana
kujali.
Pole sana dadiii.. pole sana. Nilimwambia hivyo… aliniambia
mamii pole wewew tena pole sana, ni mimi nilifanya makosa, nilisahau kwamba mama
Husna tuliongea aje kuchukua pesa za sherehe ofcn, nilisahau mamii,,, lakini
hakuna lililoharibika. Mimi mwanaume,,, kwani wewe vipi?
Hapana
nilikuhurumia tu dadii… aaa haina shaka…
Mimi naogopa sana dadii, hembu
niambie imekuwaje? Nilimhoji…
Aaaa, mimi nwanaume bwana,, usiogope.
Alilalamika sana, alilia sana, na kunishtakia kwa dada zake wawili………… ambao ni
wakubwa, na wakamuonya asiharibu sherehe ya mtoto, wala wasimshirikishe mtoto
jambo lolote kuhusiana na matatizo yetu kwani hayamhusu. lakini pia mimi
sikushirikishwa kwa kikao hicho, ila watakusumbua kidogo hao wanawake . lakini
usijali, wewe usijibizane nao, sawa mama.
Mzee Zuberi alinipa mkanda
mzima, na kunionya na kunitaarifu kwamba ni wanawake wa Kiswahili ambao wana
maneno sana hivyo nisijaribu kushindana nao. Nilimhakikishia nitatulia, na
kumuomba kwa sasa tujaribu kutuliza kwanza mahusiano mpaka tuone mambo
yametulia.
Aliniambia una akili sana shalote mpenzi wangu,, ndio maana
nakupenda na kufurahia mapenzi yako.
Nilimueleza pia namshukuru kwa
kiwanja. Aliniambia usijali, usijali kabisa, nitakusaidia kujenga usijali
.
Nilijiuliza ni kitu gani cha mno ambacho nimemfanyia mzee huyu wala
sikupata jibu. Tulimaliza kuzungumza kisha nikakata simu na kuendelea na siku
yangu kama kawaida.
Nilikuwa nimejipanga vyema, sikuwa najali hata
kidogo, nilisema endapo hao wanawake watanijia na maneno basi ningeajibu na mimi
bara bara wala singejali na ningewaeleza mkuki kwa nguruwe mtamu kwa binadamu
mchungu. Nilikuwa na wasubiri kwa hamu wanijie.
Na kwa bahati nzuri
sana, hakuna aliyenifuata, nafikiri ni wanawake ambao wana hekima Fulani, kwani
hata kumshauri mke wa mzee zuberi kutogombana ni moja ya hekima tu ilitumika. Na
pia nafikiri mama Husna alikuwa akirewind mkanda na kuona ni kama nilikuwa
najaribu kulipiza kisasi, japo najua hakuamini lakini baada ya kunipigia simu
ndo nilijua kimemuuma.
Haikuishi hapo tu, baada ya dakika chache kabla
sijatoka kwenda nyumbani, mke wa mzee Zuberi alinipigia tena simu,, lakini
sikutaka kuipokea wala kujibizana naye, kwani nilihisi yuko na jopo la wanawake
wale na sikutaka kuharibu jioni yangu.
Aliniandikia msg na kuniambia,
Nitakuliza…. Sikujibu msg ile. Nilikaa na kutafakari sana
nifanyeje.
Kisha nikampigia simu, na alivyo wa ajabu akapokea, nikwambia
mama sikiliza, mkuki kwa nguruwe mtamu kwa binadam mchungu,,, mimi nilishalia,
ila najua sasa hivi ndo zamu yako kulia na unalilia machozi yanadondokea tumboni
, nab ado utalia sana. Nilimaliza kumueleza hivyo huku akitukana lakini sikujali
nilikata simu na kuizima kabisa . kisha niliiwasha na nikamblock. Sikutana
usumbufu naye.
Kilipita kiya cha siku kadhaa, na Harusi ikafanyika,
kweli ilikuwa harusi nzuri sana na iliyopendeza mno, kwani mzee Zuberi alikuwa
na pesa za kutosha, lakini pia Majdi na familia yao nao walikuwa na pesa ya
kutosha, na baada ya harusi Majid na Husna walisafiri kwenda Dubei kwa ajili ya
honeymoon. Majid ni mfanya biashara anayechipukia, hivyo alisafiri na kuelekea
Dubei na mkewe kwa ajili ya fungate.
Na mimi nilikuwa nawasubiri kwa
hamu.
Baada ya wao kusafiri, mimi akili yangu ikiwa imetulia kiasi huku
nasubiri warudi na waendelea na maisha yao ya wana ndoa.
Niliamua
kubadilika kabisa, mawasiliano yangu na mzee Zuberi yalikuwa ya nadra sana na
kwa siri sana, hatukutaka kufumaniwa tena na tulionana mara chache chache sana
na kwa vile nilikuwa nataka tu pesa ya kujenga nyumba nilikuwa nikiwasiliana
naye ili asisahau ahadi yangu, na siku zote aliniambia anakumbuka, na saa
nilimpatia bank accaount number yangu na ilikuwa ni rahisi yeye kuniwekea pesa
mara anapoenda bank, na aliniambia kwamba niwe naangalia salio kujua kwamba
ananipenda na hatonisahau.
Lakini kwangu na mume wangu, nilirudisha
mapenzi, na tukawa tunaishia kwa upendo wa hali ya juu kama hakuna kitu
kilichowahi kutokea. Jones alifurahia sana namna nilivyokuwa namjali na kumpenda
na kumtunza, alijifunia mimi.
Niliendelea kunawiri na kupendeza sana. Na
siku moja nilipoelekea bank nilishangaa sana kukuta account yangu imeingiziwa
milioni 11, hii ilikuwa ni maajabu kwangu, Haraka sana nilijua tu ni Mzee
Zuberi, nilifurahi sana na kweli alikuwa ni yeye, nilifurahi sana na nisingeweza
kuacha kumshukuru, niliamua kumpigia simu. Nilimpigia simu na iliiita sana
haikupokelewa, iliiita mda mrefu sana, na haikupokelewa kabisa. Badae niliacha.
Kwani sikupenda kuandika msg.
Na sikuandika kabisa msg. Badae sana mzee
Zuberi alinipigia simu kwa namba ingine na kuniambia mkewe ameshkilia simu,
hivyo nisipige wal akuandika msg, nilimwambia samahani nilitaka kukushukuru tu
kuhusu pesa niliyokuta kwenye account yangu,, aliniambia haina neno mwanangu
usijali.. mhh, nilishangaa kaniita mwanawe… nilishangaa sana.
Nilimuaga
na kkubaliana sasa tuwe tunawasiliana kwa simu za ofcn tu na sio za mikononi.
Nilimuelewa, na alinipenda kwani kila alichoniagiza nilikifanya sawa sawa na
alivyosema.
Shaloo naomba uwe makini ili niweze kukusaidia, sitaki
kukutafutia matatizo, ndoa yako bado changa. sawa mama,,, ndio nilijibu.. na
alinipenda sana kwa utii wangu.
Nilirudi nyumbani nikiwa na furaha ya
milioni kumi na moja. Na kiwanja hiki sikutaka k umshirikia mume wangu hata
kidogo, sikutaka kabisa.
Ni kiwanja kizuri, kikubwa na kilichopo maeneo
ambayo ni hot cake, ni kiwanja ambacho nikikigawa mara mbili na kuamua kuuza pc
moja ni zaidi ya mamilioni ya pesa, pc moja tu ya mita 35 x 20 ni kama milioni
40 hivyo ni pesa nzuri sana. Na nilishaanza kuwazakuuza pc moja ili moja
nijenge.
Na wateja walikuwa kila mara wakiulizia hicho kiwanja ni cha
nani na je anauza? Hizi ni taarifa nilizokwua nazipata kutoka kwa majirani ambao
wanaishi kwenye eneo hilo, na majirani wote wamejenga mijumba ya haja, ni mtaa
ambao husifika kwamba ni mtaa wa wenye nazo. Kwani majuumbo yote ya mtaani hapo
ni ya kifahari. Na mimi nilikuwa nataka niweke kitu chenye adabu
pia.
********************************************************************************************
Maisha
yalisonga sana, Majid na Husna walirudi kutoka Dubei, waliishi maisha yao mazuri
sana, walikuwa wamepangisha nyumba nzuri tu ya kifahari, Husna alikuwa na gari
yake nzuri ya kutembelea, na mara nyingi alikuwa akipendelea kukaa tu nyumbani,
hakuwa ni msichana wa kupenda kujishughulisha, zaidi ya kukaa nyumbani. Na
alikuwa ni mke wa kwanza kwa Majidi, na majidi naye alikuwa ni mume mkewe wa
kwanza.
Walikuwa na ndoa nzuri. Miezi sita ilikuwa imeshapita, Husna
alipendeza sana, alikuwa ni mke ambaye bila shaka aliipenda na kuimudu ndoa
yake, alikuwa ni mke wa kujitanda sana na kuvalia vyema, hakuwa mke mang’aa,
alimpenda sana mumewe.
Muda wote Majid aliponitafuta nilimueleza
tafadhali naomba kaa na mkeo kwanza, afurahie ndoa yako. Mimi nipo tu wala
kisikusumbue. Mimi wakati huo nilikuwa ni mtu wa kupanga taratibu zangu, sikutak
Husna asiumie, nilitaka aumie kama nilivyoumia, Na nilipogundua Husna ana mimba
nilifurahia sana, nilifurahia sana, nikasema sasa huyu ndiye mke haswa, na kama
nikilipiza kisasi kipindi hiki ndipo kitanoga.
Bado sikuwa na haraka.
Deal la flat screen nilishalikancell kwa Majid na nilimueleza tumepata ambaye
atatupatia flat screen hizo. Hivyo bado aliamini ninaweza kumpatia
biashara.
Na nilimueleza tu kwamba na mimi nahitaji kufanya biashara za
kutoka na kwenda china, na je ni shilingi ngapi kama nikitaka kufanya biashara?
Aliniuliza ni biashara gani nataka kufanya? Nilimueleza yoyote ambayo ingelipa,
na aliniambia atanisaidia ila niandae kama milioni 50 hivi atanisaidia na
kuniambia nifanye biashara gani.
Haraka nilikumbuka kiwanja, na
nilikiweka sokoni. Na baada ya hapo nilikumbuka nina cach yangu kama milioni 15
hivi.
Kiwanja niliuza pc moja tu na nikapata milini 48, nilifurahia
sana, na kisha nilimueleza Majid nina pesa ya kutosha
kabisa.
Alinishangaa nawezaje kuwa na pesa nyingi hivyo? Nilimueleza
huwa napokea tenda za watu wengi na wakinituma vitu huwa Napata na faida. Hivyo
hizo pia ni kazi zangu.
Aliamini, kwani aliijua tabia yangu vyema, na
sikuwa mwanamke was kendo mtaani, ila asijue ndo natengeneza skendo nay
eye.
Aliniambia akitaka kusafiri atanijulisha, na atashughulikia kila
kitu change, kuanzia ticket na visa na kil a kitu, na safari ya kwanza ilikuwa
ni tunaenda Hongkong. Nilikuwa nimeshajipanga.
Niliongea na mume wangu
na kumueleza nataka kufanya biashara hivyo anitafutie mtaji. Jones alinipenda
sana, na hakuwa akiniwazia mabaya, aliniambia ni biashara gani nataka kufanya?
Nilimwambia nataka kufanya biashara ya nguo na chochote ambacho nitaona kinafaa,
ila taget yangu ni nguo.
Alifurahi kwa namna ambavyo nachanganya akili,
na aliniambia yeye hana pesa ila kuna mikopo hutokea kazini, anaweza kunikopea
kama milioni 20 ila nijue kwamba atakuwa hana pesa kwa yeye kukatwa marejesho ya
kila mwezi.
Nilimhakikishia kwamba mimi ninapokea mshahara mzuri tu, na
nitampatia card yangu ya bank ili awe nayo yeye kila mshahara ukiingia basi
tusaidiane kubajet, tulimaliza makubaliano yetu vyema.
Sasa ikawa
imebaki muda ufike ili nisafiri.
Ni kama miezi mitatu mpaka kusafiri, Na
tayari nikawa natafuta frem.
Na jones naye akinisaidia kutafuta
frem.
Husna ujauzito uliendelea kukua, nafikiri sasa ni mimba ya miezi 7
ama 8.
Safari ya China iliwadia. Nilikuwa nimekamilisha kila kitu
change, kuanzia pesa, passport na visa. Hakuna ambacho sikuwa
nacho.
Kazini niliomba ruhusa yangu ya mwaka mzma. Siku 28. Na pia
sikujali sana kazi wkani sasa nilikuwa nataka kuwa mfanya biashara na kujikita
kwenye biashara, niliona inavyolipa na mtu pia kupata muda wa kupumzika na
kujipangia mambo mwenyewe. Niliamini ili uwe tajiri ama matajiri wengi ni wale
ambao wametoka kwenye kuajiriwa, kujiajiri kisha Kuajiri, hawa ndio niliamini ni
matajiri. Nilitamani kujiajiri kisha niajiri na mimi watu siku
moja.
Nilishaanza kuona ukubwa wa duka langu la nguo, pochi na viatu,
nilitaka kuwa famours in town ndizo ndoto zangu.
Saa kumi na mbili jioni
tayari safari ya kuelekea airport ilianza. Mume wangu alinisindikiza mpaka
airport.
Nilifika na tukawa tumekaa kwenye restaurant huku tukiwa
tunapata kahawa tukisubiri muda usogee kidogo kwani tuliwahi sana kuogopa jam za
mji.
Baada ya nusu saa nilimuona Husna na mumewe, niliweza kumgundua
Husna baada ya kumuona Majdi, Nilitaka Husna anione na ajue ninasafiri. Hivyo
nilimwambia mume wangu kwamba sasa nataka kucheck in kabla foleni haijawa
kubwa.
Mume wangu alinikumbatia na tukaagana na akaondoka.
Kisha
nilienda kukaa kwenye vitu nikisubiri kucheki in.
Baada ya kuhakiki
Jones kashaondoka, nikiwa nimevalia Skin tight nyeuzi ambayo imeshika umbo langu
sawia nd dress top nzuri ambayo ilinikaa vyema,, nilichukua cheni zangu mbili za
miguuni kwenye pochi na nikazivaa, zilikaa vyema mguuni kwani Mungu kanijali
mguu wa chupa ya bia,, na sendoz nilizovaa zilikamilisha umaridadi wa muonekano
wangu wa miguuni. Kila mwanaume alinitazama kwa kunitamani.
Baada ya
sekunde kadhaa nilitazama huku na huku, kisha nikaona Majdi na Husna wakiwa
wanaagana… Nilipata kicheko moyoni,, huku nikishangilia sana .
Majid
alikuwa na uhakika kabisa kwamba mke wake hanifahamu, hivyo hakuwa na wasi
wasi.
Nilipita mbele yao,, Husna nilimuona kama ameshangaa Fulani hivi…
Kisha nikapiga simu kumuaga rafiki yangu na kumueleza naenda china na nitarudi
baada ya siku kadhaa.
Nilimuaga na Husna akasikia, lengo langu ilikuwa
ni Husna atambue kwamba ninasafiri na mumewe.
Kisha nilisogea na kurudi
kukaa kwenye kiti nikisubiri muda wa kucheki in ufike.
Muda ulifika na
nailicheki in. Nilijua tu Husna ana mawazo, kwani kila nilipogeuka nilikuta
akinitizama. Asiweze kuniambia lolote, na mumewe alipocheki in nilimsogelea na
kumsalimia kwa mmkono, huku tukiwa tunaongea mawili matatu, Na husna alituona
tukiongea,, maskini tayari nilishamuwekea alama ya ulizo. Na ndilo lilikuwa
lengo langu, ajue maumivu ya mume na utamu wa mume. Hili ndilo nilikusudia miaka
miwili iliyopita ya seke seke zima, na kuhakikisha KISASI CHANGU
KINAFANIKIWA.
Tulisafiri, na Majid alizima simu
yake.
Nilishangaa kupigiwa simu na mtu ambaye nina takribani miezi kama
tisa hatuwasiliani,, akili ikaniambia huyu lazima ametumwa na Husna, kwani ni
mtu ambaye pia alimfahamu husana na kisanga kizima.
Nilisema sasa ni
muda wa kumueleza kila kitu kuhusu safari yangu. Nilimueleza nasafiri kwenda
china, hongkong nitakaa huko siku kama 14 hivi, nimeenda kuvuta raha tu na
kutuliza akili.
Aliniambie niko na nani? Nilimjibu si juu yako kufahamu,
ila take care, nikirudi nitakuletea zawadi. Akaniambia basi usiache kunitumia
mapicha yaw hats app, nikamwambia poa hizo umezipata,, na kwa kuanza tu
nilimtumia picha kama mbili hivi ambazo mimi niko mbele form y amble na Majdi
yuko form ya nyuma yangu tukisubiri ku board, nilifanya makusudi nikijua na
kuhisi katumwa.
Husna roho yake ilikuwa ikidunda sana, bila shaka. Kwani
huyu aliyekuwa akiwasiliana na mimi ni kama aliyekuwa akisukumwa kufanya hivyo
na nilijua tu ametumwa. Baada ya dakika chache nilimuaga na kumueleza ninazima
simu tutaongea nikifika, nikakata simu, na hao tulikuwa tunaelekea kwenye
ndege.
Safari yetu ilikuwa nzuri sana nay a utulivu wa hali ya
juu.
Tulifika na kupokelewa na mwenyeji wa Majid, Majid aliniambia huwa
hapendelei kufikia hotelini na huwa anafikia kwa mwenyeji wake huyo, na tulienda
pamoja .
Kweli nilikuwa nashangaa sana kwani ilikuwa ndiyo mara yangu ya
kwanza kutoka nje ya nchi na kwenda kwenye nchi kama hiyo, nilikuwa nashangaa
kila kitu, majengo bara bara na kila kitu.
Wiki ya kwanza ilikuwa ni
wiki ya kutembea na kuujua mji, kisha nikaingiwa uchizi, nikaona kuliko kufanya
biashara ya nguo ni bora nifanye biashara ya stationery,, niliona inavyolipa,
basi nilkaa na kupiga mahesabu na kuona endapo nitamua kufanya biashara ya
stationery nitapata pesa nyingi sana na kufanikiwa sana kuliko biashara ya nguo,
na tayari niliamua kuwasilian na Jones na kumueleza. Hivyo akaniambia ni sawa
tu, kikubwa nihakikishe kwamba nakwua makini kweye biashara na sio mchezo
mchezo.
Mara zote Husna alipokuwa akizungumza na Majid ni kama walikuwa
wangombana, Nilimuuliza Majid ni nini tatizo?
Aliniambia yani mke wangu
sijui kaambiwa umbea gani, kaambiwa nimesafiri na mwanamke ila hataki kumtaja,,
na ninajua hakuna mtu anajua issue yangu mimi na wewe. Nilimwambia ni kweli, ila
wanawake tuna wivu tu, wewe ongea naye vizuri na muulize anataka ufanye nini ili
asikie raha?
Majid alicheka na kusema dah kuoa kazi kweli kweli.
Tulicheka wote, kisha tukaenda kupumzika na kukubaliana siku inayofuata ni
kukusana mizigo baada ya kutembea maduka mengi kujua tunataka vitu
gani.
Kweli siku iliyofuata ilikuwa ni siku ambayo tuko busy sana,
tulitiembea sana na kuchoka sana, kisha tukapata mizigo yote na kuikusanya, Na
majidi akaniambia kwamba ataaweka mzigo wangu kwenye contena lake hivyo nisijali
kwani haoni sababu ya kuniombea mizigo yangu kwa baadhi ya watu anaowafahamu,
hii ni ili kulinda usalama wa mahusiano yetu.
Nilifurahia sana na kweli
siku mbili zilizofuata ikawa ni kufunga mizigo kwenye contena kisha kuanza hatua
za kukabidhi mzigo ili usafirishwe. TUlimaliza process zote hizo salama na sasa
kujipongeza, na siku sita zilizobaki kabla ya kurudi Tanzania, tuliazimia
kujirusha na kutembea baadhi ya miji ya jirani kuvuta raha tu.
Tulivuta
raka kama tulivyokubaliana. Na baada ya kupongezana tulijiandaa kurudi Tanzania.
Kiusalama zaidi, Nilitangulia mimi na siku iliyofuata Alikuja
Majid.
Jones alifurahia kuwa na mwanamke kichwa ambaye anawezakubuni
biashara nzuri kwa haraka. Nilifika na kumueleza kila kitu kuhusu safari yangu,
na miji ya china ilivyo, alitamani sana kusafiri nay eye. Nilimwambia tuombe
Mungu biashara iwe nzuri kisha tutasafiri tu.
Aliniambia ameshapata
frem, na tulianza kuifuatilia na kuiandaa kwa ajili ya kuweka biashara
yetu.
Baada ya muda kidogo tu, mizigo iliwasili na kufngua stationery.
Ilikuwa kubwa, nzuri ,nilikwua na mashine za photocoyy. Scarner na kila kitu,
kila mteja aliyekuja pale alipata huduma zote alizohitji pamoja na kuuza bidhaa
zote za muhimu ambazo zinahitajika kwenye stationery. Nilianza kuktafuta wateja
kila mahali, Na mzee Zuberi alinisifia sana kwa kazi nzuri niifanyayo na
alinitafutia wateja kwa hali na mali. Sasa nilikuwa naingiza pesa bara
bara.
Maisha yalianza kuwa matamu, na niliandika barua ya kuacha kazi.
Na niliacha kazi. Wala sikujuta, stationery yetu tuliiweka karibu na maeneo
ambayo watu walihitji huduma hiyo.
Siku moja nikiwa ofcn, Majid aliamua
kunitembelea, Alikuja na hakuamini kunikuta kwenye stationery ambayo imejaa,
imependeza sana, na kwa vile kazi hiyo niliisomea nilitafuta pia wasichana
wawili wambao ni liwakagua vyema na kujua wanaijua kazi hiyo vyema na kuwaajiri.
Biashara ilikuwa nzuri sana, Majid alinisifia sana na alinipenda
sana.
Sasa kupatikana kwangu kukawa shida, kwanza kumbuka Sikumpenda
Majidi kimapenzi ila kulipiza kisasi.
Kisha sasa nina biashara yangu
naifanya na sitaki kuharibu biashara yangu, hivyo kunipata kwangu ikawa taabu
sana, na hakuweza kuvumilia, ikawa anapiga simu kila mara hajali tena, na mkewe
akawa yuko kwa mama yake akila uzazi, alijaliwa mtoto wa kike.
Maisha
yangu yalikuwa mazuri mno, ni kama nilikuwa natamani sasa nisilipize kisasi,
lakini hapana nitaachejee kulipiza kisasi ili hali Husna hajaonja joto ya
jiwe?
Hili ndilo lilikuwa likinikera, ni lazima kimuume kama
kilivyoniuma
mimi.
*************************************************************************
Sehemu
ya Mwisho ya kisa cha Charlote. Alivyoamua kulipiza kisasi baada ya kugundua
mahusiano yamapenzi ya mumewe, na kuvunja ndoa Tatu
SEHEMU YA
KUMI
Majid alinisumbua sana. Hakunipa kabisa nafasi ya
kupumzika. Muda mwingi alinitaka. Na mimi nilikuwa busy. Lakink pia sikutaka
jones ajue lolote. Majidi alinisumbua kila mara kwa simu. Alishindwa kabisa
kujizuia. Nilijaribu kuongea naye kwamba ajaribu walau kuwa na kiasi asijisahah
sana. Aliniambia wazi kwamba hawezi. Penzi langu limekuwa zito sana moyoni
mwake.
Alinieleza namna ambavyo kinamuuma kunikosa.
Sasa alipiga
simu mpaka usiku. Na aliniambia mamii ni bora upokee simu kwani ukiacha
nashindwa kukuelewa. Nilijaribu kupokea kwa kificho hivyo hivyo. Sasa alianza
kunikera. Na nikaona ni bora walau nimridhishe kidogo.
Niliendelea
kupanga miadi na yeyw ya kukutana. Ili mradi tu mume wangu
asijue.
Mimi na Jones tukishakubaliana kwamba kila mtu simu
yake iwe huru. Na hivyo hatupaswi kuweka pw. Hivyo niliacha simu yangu wazi. Na
kila mmoja alikiwa huru na simu ya mwenzake.
Sasa majid kawa kichomi. Ni
lazima niweke simu yangu pw. No mata what.
Niliweka. Jones alikasirika
sana. Lakini sikujali. Bora akasirike kwa asilolijua kuliko ajue.
Ugomvi
ulikuwa mkubwa sana. Ila nilimwambia sina tatizo isipokuwa nimeweka kwa ajili ya
mambo yangu biñfsi. Na baafae nilimwambia nimesahau pw. Ilikuwa ugomvi. Simu ya
kwanza tuligombana sana. Alitaka kujua nani kapiga simu saa nne usiku tukiwa
tunawatch movie. Na kwa nini nimepimelea jikoni. Nilimueleza nilienda kufuata
maji. Akasea kwa nini niliongea pole pole?
Sikuwa na jibu.
Tukikurupushana. Akaichukua simu na kuibamiza
ukutani.
Jones
alichukia sana. Bado niliona bora kaona hiyo ya kuvunja simu kuliko kujua niko
na majid.
Maisha yakaanza kuwa mabaya. Sasa jones alinifuatilia
sana.
Nikiwa na majid nilimueleza ajaribu kuwa makini.
Sikia
shaloo… nakupenda sana. Siwezi kujikaza. Siwezi. Kumbuka na mimi nina mke. Na
mke wangu karudi. Ila kuna saa natoka nje kuongea na wewe. Hembu ona hili
mamiii. Nakupenda. Sana mnoo. Jaribu kulitambua hili mama. Nakupenda
sana.
Alinieleza hivyo nguvu zikaniishia.
Majid alishindwa kweli
kujizuia.
Husna alishaaanza kuwa na mashaka na mumewe. Tena mashaka yake
aliyaweka wazj juu yangu. Japo hakutaka kuliweka wazi kwa mumewe aliogopa
kuhisi.
Na ninafikiri alitaka kuwa na uhakika.
Ni miezi imepita
sasa. Husna mwanaye ana miezi sita. Ni siku ya birtday ya mwanae.
Jambo
hili nililifahamu mapema. Na siku hii nilimueleza majid ni birrhday yangu pia.
Ila nilimanganya.
Nilitaka kumsumbua tu katika kuhakiki nakamilisha
kisasi changu.
Akili hizi za kishetani na kifirauni sijui nilizitoa
wapi. Sikuwa na woga hata kidogo.
Nilimuomba Majid niwe naye usiku
huo.
Sikujali sana kwangu. Ila nilitaka kuwa na majid.
Majid
alihangaika huku na huko kutafuta zawafi zangu. Na
alishakamilisha.
Kisha akanipigia simu kuniambia tukutane
wapi.
Niliendelea kumsumbua sana siku huo kwa ajili ya birthday yangu
feki.
Mkewe alihisi jambo. Na akamuuliza mumewe hiyo ni namba ya
shalote?mum alikana. Hivyo kukawa na ugomvi fulani hivi nyumbani.
Majid
akaamua kuondoka. Na birthday ikaanza kuharibika. Maana husna aliijua namba
yangu. Hakuwa anabahatisha.
Baada ya kukutana na majid
alinieleza kama mkewe ananifahamu. Nilimueleza sijui labda ila sina mazoea
naye.
Aliniambia kaona simu inaita akaweza kugundua namba yako. Mh…
nilishangaaa ila moyoni nilikuwa na raha sana.
Nilifurahia kuona sasa
Husna anaanza kukosa usingizi kama mama yake.
Nikifurahi
mno.
Usiku wote huo nilikuwa na Majid. Sijui aliahaje kwake. Na mimi
niliaga nilivyojua. Wote tukawa hotelini.
Jones alishanichoka sasa.
Alishajua nimekuwa mke sugu nisiyesikia. Na alishajipanga kwa lolote. Alichoka
kunibembeleza.
Haikuwa kawaida kwa Majid kulala nje.
Majid
aliingia kuoga na kuacha simu yake. Niliichukua na kutoka nayo nje. Kwani
ilikuwa inaita sana.
Nilipoangalia niliona jina la my wife
ikiita.
Nilipokea na kucheka kwanza
Ha ha ha.. Husna.. usijali.
Anakuja muda si mrefu. Tulikuwa wote na yeye hotelini. Pole mamiii. Jifunze
kumtosheleza mumeo. Bye.
Na nilizima simu. Sikumpa nafasi ya kujibu wala
kupiga. Ni kama aliyekosa nguvu. Akilalamika sana na kukosa muelekeo nilimgundua
kwenye simu.
Majid alitoka kuoga. Kisha tukanywa chai na
kuondoka.
Nilipitia stationary kwangu. Nilikaa kwa muda kisha nikaenda
nyumbani. Sikumkuta mr. Hakuwepo.
Nilijibwaga kitandani nikishangilia
seke seke la majid na mkewe .
Baada ya kama nusu saa simu ya majid
iliita. Nikiwa kitandani nimekaa niliongea na majid kwa uhuru sana. Huku
akinielezea kuhusu mkewe kulalamika mimi kumpigia simu.
Nilimueleza
kwamba ni kweli. Akaniambia kwa nini umefanya hivyo shalote?alionekana kugomba
ssna. Mimi nikiwa nacheka tu.
Huku akiniambia mkewe anahasira na anaweza
kuvunja ndoa.
Nilimwambia tafadhali naomba tukutane mahali tuongee
nimueleweshe jambo.
Alikubali. Asijue kama mkewe anamsikiliza kwa
maongezi hayo.
Na kujua tunapoenda kukutana.
Haraka aliwasha
gari. Na mimi nilikurupuka nilipokuwa. Kisha nikamfuata majid. Tulikutana kwenye
hotel yetu kama kawaida.
Sikutaka tuzungumze nje. Nilimwambia tuzungumze
ndani. Alikubali.
Tuliingia ndani.
Nilimueleza majid kila kitu
kuhusu mkewe na jones. Nilimueleza mwanzo mwisho.
Alisikitika sana na
kuniambia Shaloo kwa nini umenipa penzi feki? Na kuniharibia ndoa yangu na
kutembea na baba mkwe wangu?kwa nini?
Majid alilia sana na kujilaumu
mno.
Nilimueleza hii ndiyo njia pekee ya kuganga moyo wangu na ninaomba
tu unisamehe.
Tukiwa tunaendelea kulumbana na Majid. Mara tukishangaa
mlango unagongwa. Na niliona askari wawili. Wa kike na wa kiume.
Kisha
wakatuambia mko chini ya ulinzi.
Dakika chache tukisikia kishindo cha
watu wakitembea.
Alikuwa ni husna.jones. wadhamini wangu wa ndoa na mama
yake husna.
Walikuja pamoja wote. Na husna akidai
talaka.
Ilikuwa aibu fulani ila mimi nilikuwa nashangilia fulani kujiona
mshindi.
Tulifikishwa polisi. Na kuandika maelezo. Jones alikuwa akilia
ssna. Na husna pia.
Baada ya maelezo tuliachiwa kwq dhamana. Na kutoka.
Majid alielekea kwake na akatoa talaka.
Na mimi nikagoma kwenda
nyumbani. Nikaenda kwa mdhamini. NikamueleA kwamba sasa naweza samehe jones kama
atanisamehe. Jones alikuwa akilia tu. Na akisema hawezi kunisamehe
kamwe.
Niliwaambia wadhamini hili ndilo nililitaka. Waone je msamaha ni
jambo jepesi tu?
Jones alijilaumu sana kunikosea.
Nilikaa kwa
wadhamini wiki nzima na ndipo nikawaeleza kwamba sasa nahitji kuwa na maisha
yangu.
Wakasema hapana mpaka wazazi
wajulishwe.
Sikutaka kukaa kikao cha aibu na wazazi wangu.
Singekuwa na la kuongea. Kila walipouliza kuna shida gani niliwaambia jones
anajua. Na walipomuuliza jones aliwajibu shaloo anajua.
Maisha
yakabadilika. Nikaanza kuishi mwenyewe. Ila mwenye furaha sana. Husna alirudi
kwao kwa talaka kabisa na kuiacha ndoa. Majid alisikitika sana.
Mzee
zuberi nilimheshimu. Hakutaka kuongea na mimi mapema.
Na alitambua jambo
hilo. Alisikitika sana. Maana sasa alijua yeye na mkwe wake wameshea msichana
mmoja.
Na bahati mbaya sana mama husna alimueleza Husna juu yangu na
dadiye. Kiliwauma sana. Waliumia sana.
Husna alikonda na kuanza
kuparama. Hii ni kwa sababu ya maumivu ya ndoa yake. Lakino shaloo kuwa na baba
yake pia kikimuuma.
Jones aliendelea kuwa na hasira. Sasa alilewa.
Hakupenda kula. Maisha yakamuwia magumu hasa.
Story zilianza
kichini chini. Watu wasiamini kwa kilichotokea. Maana walijua shaloo mimi mpole
sana. Nikapiga mahesabu nitafanyaje.
Nikaanza kuhangaikia sasa future
yangu. Sina jipya kwenye mapenzi na mahusiano. Nimeshachefukwa. Nimelipiza
kisasi nafsi yangu kwatuuu. Nilichofanya ni kuuza ile stationary. Nikapata
chance ya kwenda Denmark. Nikakaa huko miaka miwili kwa rafiki yangu huku
natafuta kazi. Kisha nikamaliza miaka miwili. Nikapata rafiki wa kizungu m
denmark ambaye alitaka nichukue wanangu. Nikarudi tz nikakuta Jones amechoka na
pombe nikamaa naye miezi miwili huku namuomba watoto ambao walikuwa kwa mama
yake. Mama yake akakubali na nikachukua wanangu
Husna mpaka leo
hajaolewa.
Jones ameshajaribu mahusiano zaidi ya mara tatu. Na msichana
mmoja alishi naye na kuzaa naye ila wakashindwana. Ndiye ambaye alinipokea
nilipotoka denmark.
Sasa Naishi na wanangu Denmark. Jones yupo
tu. Husna yupo tu.
Maisha yamekuwa Mazuri kwangu. Nimeathirika sana
saikolojikali. Maana najiuliza mwanaume mzuri ni yupi?jones hakufaa. Majid
hakufaa. Mzee zuberi hakufaa. Wote sio waaminifu.
Hili limenifanya
nachukia sana mahusiano na kuchukia mwanaume.
0 comments:
Post a Comment