Search This Blog

Friday, November 18, 2022

MUHANGA WA MAPENZI - 4

 






Simulizi : Muhanga Wa Mapenzi 
Sehemu Ya Nne (4)






Alipofika alimkuta ametulia sebuleni akiangalia tivii. Hata bila ya salamu alimvamia kwenye kochi huku akisema:

“Darling, mambo safi sasa hivi ushindwe mwanyewe.”

Alimkumbatia kwa furaha baada ya kuamini kamba iliyokuwa imemfunga imefunguka. Siku hiyo walifanya sherehe ambayo walipanga kuifanya atakapomaliza mtihani wa mwisho.

Walijikuta wakifanya sherehe ya wawili na kujikuta wakitumia hata vinywaji ambavyo hawajavizoea kwa kunywa pombe ambayo Rachel alijifanya mzoefu kumbe wapi. Alikunywa pombe zilizomzidi na kulala fofofo. Muda ulizidi kukatika bila Rachel kuonesha dalili zozote za kupata unafuu wa pombe. Athuman alijikuta akichanganyikiwa na kujiuliza atamwambia nini baba yake kama akitokea kama sio kuozea gerezani au kufa kwa kipigo au kuhukumiwa bila kupelekwa Mahakamani.

****http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Mzee Mulisa alipotoka katika shughuli zake majira ya saa tatu na nusu usiku, alipoingia ndani kitu cha kwanza alitaka kuonana na mwanaye na ili ampe tathimini nzima ya mtihani na kujua nini matumaini katika mtihani ule.

“Mama Rachel hebu niitie huyo mwanao ili atupe picha ya mtihani kaonaje ili tumuandalie zawadi mapema,” Mzee Mulisa alisema huku akimpatia koti mkewe.

“Mbona mwanao toka alipotoka hajarudi.”

“Yaani mpaka saa hizi?”

“Si alishamaliza mtihani sijui kama atashikika.”

“Hayo siyo majibu mke wangu …hebu nipe hiyo simu yangu nimuulizie shoga yake.”

Mama Rachel alimpa mumewe simu baada ya kubonyeza za nyumbani kwao Joyce haikuchukua muda mrefu iliita na kupokelewa.

“Haloo nani ninayeongea naye?” Mzee Mulisa aliuliza.

“Mimi mama Joy,” sauti upande wa pili ilijibu.

“Ni Mzee Mulisa hapa.”

“Aah, shemeji, vipi leo maajabu kupiga simu.”

“Shemeji mbona Rachel amechelewa kurudi nyumbani mwambie awahi kurudi.”

“Shemeji mbona leo sijamwona Rachel?”

“Hujamwona vipi naye ameaga majira ya alasiri anakuja kwa Joyce.”

“Kwa kweli sijamwona labda nimuulize shoga yake.” Mama joyce alimwita joyce, baada ya kufika alipewa simu aongee na mzee Mulisa.

“Shikamoo baba,” Joy alimuamkia Mzee Mulisa.

“Aah! Joyce, marahaba mama hujambo?”

“Sijambo baba.”

“Eti shoga yako yupo wapi?”

“Toka tuachane shuleni sijaonana naye tena.”

“Etiii! Unasema hujamwona mbona sikuelewi atakuwa amekwenda wapi?” Mzee Mulisa nusra azirai kwa mshtuko.

*****

Wakati huo Rachel akiwa kwa Athuman hakuonesha

dalili zozote za kurudiwa na nguvu, Athuman alizidi kuchanganyikiwa kila alipouangalia muda ulizidi kukimbia saa ilionesha saa mbili usiku.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Alijikuta akichanganyikiwa asijue afanye nini, mapigo ya moyo yalimwenda kwa kasi woga ulitanda na kushindwa kujua afanye nini. Aliamua kumbeba Rachel hadi bafuni huku akionesha hajiwezi, alimvua nguo na kumwagia maji ya baridi ambayo kidogo yalimsaidia kupata nguvu kidogo.

“Rachel mpenzi wangu jikaze uende nyumbani,” Athuman alimbembeleza Rachel.

“Athuman usiniudhi hapa nimefika siondoki,” Rachel alisema kwa sauti ya kilevi.

“Hapa Rachel utaniingiza matatizoni baba yako atanila nyama.”

“Hawezi kwani kupenda mtu ni utashi wa mtu na si wazazi kama mtihani nimemaliza.”

Athuman alijitahidi kumbembeleza kumpeleka kwao alikubali japo kwa shingo upande. Alimkodia gari mpaka karibia na kwao, alipokaribia alishangaa kuona nje ya nyumba ya Mzee Mulisa kuna gari la polisi.

Baada ya muda gari la Mzee Mulisa ilitoka na kufuatiwa na magari mawili ya polisi. Athuman alimuomba dereva asimamishe gari mbali kidogo na nyumba ya mzee Mulisa.

Gari la mzee Mulisa liliwapita likiongoza msafara wa magari mawili ya polisi. Baada ya kuhakikisha yamepita alimwomba Rachel aende kwao mwenyewe . Aliteremka na kwenda kwao huku akipepesuka kidogo, alipohakikisha ameisha vuka geti lao aliondoka.

***

Baada ya majibu ya Joy, Mzee Mulisa alijikuta amesimama kama amepigwa na shoti ya umeme kitu kilichomshtua mkewe na kumuuliza.

“Vipi wanasemaje?” Mama Rachel alimuuliza mumewe aliyekuwa ameganda kama kapigwa na shoti ya umeme.

“Inasemekana hajafika nyumbani kwa kina Joyce.”

“Hajafika? Mbona sikuelewi, kama hajafika kaelekea wapi sasa, au kapata ajali. Baba Rachel tupeleke taarifa polisi ili tujue kama kuna ajali iliyotokea leo jijini,” mama Rachel alichanganyikiwa.

“Mama Rachel isiwe amekwenda kwa yule mwanaharamu wake?”

“Kweli mume wangu inawezekana, kabla ya kwenda huko lazima tuitaalifu polisi ili tukafanye msako kwa yule kijana,” mama Rache alitoa wazo.

“Nikimkuta nitaua mtu leo.”

Mzee Mulisa alipiga simu polisi kwa mkuu wa kituo wa polisi wa mkoa, mkuu alimuahidi kumpa ushirikiano. Alileta gari mbili lililojaa polisi, gari lilisimamishwa mbele ya nyumba ya mzee Mulisa.

Mzee Mulisa aliongozana na polisi hadi sehemu anayoishi Athuman nyumba ilizingilwa kama kuna gaidi aliyejificha ndani ya nyumba akiwa na bomu. Polisi waligonga mlango kwa nguvu bila kupata jibu. Wakati huo Athuman alikuwa amekwisha rudi na kuelekea nyumbani kwake.

Alipokaribia kwake alishangaa kuwaona askari wakigonga mlango wake, walipoanza kugonga kwa nguvu alijitokeza.

“Jamani mna shida gani mbona mnataka kunivunjia mlango?” wote waligeuka.

“Si huyu hapa,” Mzee Mulisa alisema kwea sauti ya mshtuko baada ya kumuona Athuman.

“Vipi wazee mbona mnavamia nyumba kama kuna jambazi lililokimbilia ndani?”

Mzee Mulisa alizidi kuchanganyanyikiwa baada ya kuufungulia mlango, waliingia ndani na kufanya upekezi wa nguvu. Baada ya pekua bila kuona mtu chochote, nilimshuru Mungu kimoyomoyo. Nilijiona nimecheza kama pele la sivyo ningesahaulika gerezani

****

Baada ya kumkosa ndani walimuuliza kwa vitisho lakini Athuman alionesha msimamo wa kutomtatambua Rachel. Baada ya kukosa ushahidi mzee Mulisa aliaga na kuondoka na kikosi cha polisi waliokuja na kazi moja. Athuman alimshukuru Mungu jinsi alivyokuta na jinsi walivyovamia na kumkosa Rechel.





Aliamini kabisa kama wangemkuta na hali aliyokuwa nayo lazima polisi wangemuulia ndani au mzee Mulisa angemuua kwa risasi. Baada ya kuondoka Athuman alipigwa na butwaa baada ya kugundua juu ya kitanda kulikuwa na nguo ya ndani ya Rachel, aliamini kama mzee Mulisa angeiona lazima angeitambua kutokana na yeye kumnunulia kila kitu binti yake. Aliitoa pale na kuificha kisha alizima taa na kujilaza.

Usiku mzima alijiuliza Rachel akiulizwa na wazazi wake alikuwa wapi atawajibu nini. Lakini alimuamini Rachel alikuwa msichana msiri tena mwenye msimamo. Usingizi ulimpitia bila kujijua na kujikuta ameamka siku ya pili.

******

Majira ya saa nne asubuhi mlango uligongwa Athuman alikwenda kufungua, alipofungua alivamiwa na Rachel kwa furaha.

“Wawooo my husband to be.”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Rachel vipi! Za toka jana?”

“Zipo bomba ile mbaya.”

“Mmh! Vipi jana ilikuwaje?”

“Hakuna kitu chochote.”

“Rachel, hukuulizwa ulikuwa wapi na wazazi wako?”

“Aah, mama aliniuliza.”

“Ulimjibu nini?”

“Nilimjibu nimeisha maliza mtihani.”

“Yeye akasemaje?”

“Anijibu nini kwani mi mtoto mdogo?”

“Basi jana baada ya kukufikisha tu na kurudi nyumbani nimemkuta baba yako.”

”Mzee Mulisa?” Rachel alishtuka.

“Ndiyo.”

“Wapi?”

“Kwangu.”

“Kwako anafanya nini?”

“Alikuwa amekuja kufumania?”

“Serious?”

“Kweli kabisa, tena alikuja na jeshi utafikiri wamegundua Osama kajificha hapa.”

“My Jesus.”

“Kweli kabisa elewa kabisa siku ambayo baba yako atanifumania nipo na wewe uhai wangu utakuwa mikononi mwake.”

”Akikuua wewe aniue na mimi.”

“Rachel unajua kuwepo kwako hapa nikunitia matatani?”

“Matatani kivipi, hivi Athuman mimi siyapendi maisha yako?”

“Rachel, kuja na gari la kwenu ni kidhibiti tosha hata mtu akipita na kuliona lazima atajua wewe upo hapa.”

“Kumbe wasiwasi wako ni huo, kwa taarifa yako baba ameondoka amekwenda Marekani na kurudi hadi mwezi mmoja ukatike.”

“Usiniambie! Na mama je?”

“Mama hana noma mnoko huwa baba siku zote.”

“Ooh! Kidogo moyo umetulia hukujua hali yangu ya mapigo ya moyo yalivyokuwa ikikimbia.”

Athuman alisema huku akishusha pumzi ndefu na kujasho chembamba kikimtoka.

“Pole sana mpenzi wangu kwani mimi siwaogopi wazazi wangu, nawaogopa lakini wewe nakupenda zaidi sipendi uumie kwa ajili yangu,” Rachel alimtoa hofu Athuman.

“ Asante kwa hilo. ”

Athuman alimbeba juu juu Rachel hadi juu ya kochi, kweli paka akitoka panya alikuwa na uhuru mkubwa wa kufanya atakalo bila woga wowote.

“Mmhu, ulikuwa unasemaje?”

“Leo nataka twende Bagamoyo tukapumzike ikiwezekana turudi baada ya siku tatu.”

“Na mama yako je?”

“Mama anajua mimi mtu mzima hawezi kufanya lolote.”

“Hapana Rachel japokuwa mama si mkali, lazima naye tumuheshimu ili siku likitokea upate wa kukutetea.”

“Basi tutarudi kesho.”

“Hapo kidogo sio mbaya sana.”

Athuman alijiandaa baada ya muda walielekea Bagamoyo kwenye hoteli ya kitalii kujirusha na mpenziwe.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

********

Mzee Mulisa kabla ya kuondoka aliwaita vijana wake na kuwaeleza wamlinde Rachel na kumfuatilia kila kona atakayo kwenda kwa kupigwa picha za video na za kawaida ili akirudi awe na ushahidi kamili.

Vijana wa mzee Mulisa waliifanya kazi ile kwa kufuatilia kila kona ya Rachel atakapo kwenda. Rachel alipotoka asubuhi walimfuatilia bila yeye kujijua huku wakimpiga picha za kawaida na video.

Rachel mpaka anaingia kwa Athumani na kutoka kuelekea Bagamoyo, hakujua kama kuna watu wanamfuatilia yeye. Hotel aliyopanga vilevile nao walipanga na kuendelea kumpiga picha za ushahidi kwa siri. Kila kona aliyokwenda Rachel na Athuman walikuwa ubavuni kwao bila kujua na kuzidi kuwapiga picha za ushahidi.

****

Ilikuwa ni siku ya furaha kwa wapenzi wawili ambao siku hiyo walijirusha kila kona katika mapenzi mazito nao watu waliotumwa walifuatilia kila kona na kupiga picha za ushahidi walizotumwa na mzee Mulisa.

Baada ya kujirusha majini walipumzika mchangani kisha waliingia chumbani kwao, ile kidogo iliwapa ugumu watu waliokuwa wakiwafuatilia kwa kuzikosa picha za ndani kutokana na mazingira.

Ilibidi wawasiliane na Mzee Mulisa aliyekuwa Marekani jinsi mchakato ulivyokuwa ukiendelea.

“Mzee hapa tupo Bagamoyo Rachel yupo na yule kijana uliyemweka ndani kipindi kile wapo katika starehe za hali ya juu.”

“Aisee, basi mfuatilieni kila kona ili nikirudi nipate ushahidi wa kumshikisha adabu huyo mshenzi.”

“Lakini kwa nini mzee tusimshikisha adabu?”

“Hapana najua kunaweza kutokea makosa ya kusababisha mwanangu apate matatizo kitu ambacho sitaki kitokee. Endeleeni tu kumfatilia kazi zingine nisubirini nikirudi.”

“Sawa mzee.”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Muda huo wakiwasiliana na mzee Mulisa, Athuman na Rachel walikuwa wamejipumzisha ufukweni baada ya kuingia ndani na kujikuta wakikosa picha zingine za ushahidi. Ilibidi waende hadi mapokezi ili kujua kama wamechukua chumba muda au wanalala palepale.







Walipofika mapokezi walimuulizia muhudumu aliyekuwa mwanamke.

“Samahani dada eti Athuman na Rachel wanalala au wanaondoka?”

“Ndio kina nani hao?”

“Wale vijana wawili wa kike na kiume.”

“Ooh! Wale ngoja niangalie,” baada ya muda alisema.

“Wamechukua chumba kwa siku mbili.”

“Wapo chumba namba ngapi?”

“111”

“Tunaomba chumba cha jirani na wao.”

“Chukueni 112.”

“Tupe hicho.”

Walichukua chumba namba 112 jirani na chumba walichopanga Rachel na Athuman ili waweze kuwa karibu nao. Walikwenda katika chumba walicho panga na kutumia muda mwingi kuwavizia huenda watatoka, lakini baada ya kuingia hawakutoka tena zaidi ya kupata kila kitu wakiwa ndani.

Kila mmoja alikuwa na hamu na mwenzake hakuna aliyekubali kuwa mbali na mwenzake hasa siku adimu kama ile. Baada ya kusubiri kwa muda ili wapate picha zingine kwa kuwa karibu ya mlango wa chumba cha Rachel bila mafanikio na muda nao ulikuwa ukiwatupa mkono walimpigia simu tena mzee Mulisa kumweleza mambo yaliyokuwa yakiendelea.

“Mzee hapa wamepanga chumba na kupanga kutoka baada ya siku pili.”

“Ina maana mama yake anafanya nini, okay kazi hiyo niachie mimi.”

Mzee Mulisa alimpigia simu mkewe ambaye aliipokea.

“Mhu! Mume wangu za huko?”

“Mbaya.”

“Kivipi tena mume wangu?”

“Rachel yupo wapi?”

“Ametoka.”

“Amekwenda wapi?”

“Mmh, sijajua huenda yupo kwa kina Joy”

“Una uhakika?”

“Mimi nitajuaje mume wangu sitembei nae.”

“Kwa taarifa yako Rachel yupo Bagamoyo na yule kijana.”

“Muongo! Umejuaje nawe haupo nchini?”

“Kuna watu niliwapa kazi ya kumfuatilia Bagamoyo nasikia amepanga chumba kwa siku mbili.”

“Mungu wangu Rachel huyu ana nini mwanangu? Huyu kijana kamlambisha kitu gani kinachomfanya asione wala kusikia. Sasa itakuwaje mume wangu?”

“Fanya hivi nitamtuma mkuu wa polisi aende kumchukua Rachel na kumuweka ndani kisha yule kijana wampe kipigo kitakatifu nikimkuta nimkute amevunjika kila kona ya mwili hata wakumuua sio tatizo.”

“Mmh! Mume wangu sasa hivi hunipeleki Bagamoyo kilichopo mtume huyo mkuu wa polisi akamkamate na kumuweka ndani mimi nitakwenda kesho.”

“Okay wacha niwaliane naye, lazima nimtie adabu yule kijana hawezi kunichezea kiasi hicho,” Mzee Mulisa alisema kwa hasira.

Mzee Mulisa akiwa amefura kama amekula amira alimpigia simu mkuu wa polisi aliyekuwa ameishalala.

“Sawa mzee nimekusikia niwatuma vijana wangu.”

“Siyo vijana wako nataka uende wewe,” alisema kwa kufoka kama anasema na mtoto wake.

“Sawa mzee.”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Ilibidi mkuu wa polisi aamke usiku ule aongozane na vijana wake mpaka Bagamoyo hoteli waliyoelekezwa. Askari walivamia hoteli kama kuna gaidi na kwenda hadi kwenye chumba alichopanga Rachel na Athuman na kugonga kwa nguvu.

Baada ya kugonga kwa nguvu Rachel alikwenda kufungua akiwa amejifunga shuka, alikutana uso na mkuu wa polisi. Lakini hakuonesha kushtuka cha kwanza alikunja uso na kumfokea.

“Ni ustaarabu gani kuja kuwaamsha watu usiku ndiyo mafunzo uliyojifunza katika chuo chenu cha polisi? Hivi mzee huna kazi za kufanya? Huwezi kupumzika na mkeo unafuatilia upumbavu huu? Hivi kwa nini lakini kila ninachokifanya mnanifuatilia. Nanyonya? Bado nasoma? Lakini kwa nini lakini?”

Rachel alimfokea mkuu wa polisi kama mtoto mdogo, mkuu wa polisi alipigwa na butwaa asijue afanye nini nguvu zilimuishia. Rachel aliwageukia polisi waliongozana na mkuu wa polisi waliokuwa na bunduki mkononi.

“Hivi nanyi hamna kazi za kufanya, ni matukio mangapi yametokea ya ujambazi hamjaenda mnakuja kwa watu wanaostarehe. Bila aibu watu mnakuja na bunduki kuna jambazi mbona kwenye majambazi mnakwenda baada ya masaa sita baada ya tukio?

“Sasa nasema hivi kama kuna mwanaume wa kweli aingine ndani amkamate mpenzi wangu nasema hivi, japokuwa mnaniona mdogo lakini chochote mtakacho kifanya tutafikishana mbali.

“ Ninyi si mnamuona baba ndiye kila kitu sasa mguseni mpenzi wangu nitakufa na mtu, nimechoka kufuatwa kama mkia na kiuno” Rachel alifoka huku machozi yakimtoka alijua ni baba yake tu ndiye aliye watuma mama yake asingefanya mjinga kama ule.

Wote waliokuja kumkatata hata wapelelezi wa mzee Mulisa waliosogea eneo la tukio kuchukua picha walibakia vinywa wazi. Rachel hakutaka kuendelea kuzungumza alirudi ndani na kufunga mlango kwa komeo huku akisema

“Mwenye nguvu avunje.”

Mkuu wa polisi alisimama kama dakika tano akitafakari maneno ya Rachel kisha aliwaeleza vijana wake.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Twendeni zetu.”

Vijana wake waligeuka na kuondoka njiani kila mmoja alisema lake.

“Mzee mimi nilifikiri tunakuja kuvamia jambazi kumbe ni starehe za watu, ona tulivyo dhalilishwa, mzee vitu vingine fikiria kabla ya kufanya.”

Mkuu hakujibu kitu alijikuta akipandwa na hasira na kumpigia simu mzee Mulisa.

“Baada ya kumpigia simu mzee Mulisa alipokea na kuuliza.

“Halo mmefikia wapi?”

“Nasema hivi kuanzia leo usinitume upumbavu wako na mwanao.”

“Mkuu unadiriki kunitamkia hivyo?”

”Nimesema hivyo siwezi kudhalilishwa na mtoto yule mdogo wa kumzaa.”

“Ooh! Basi thamahani, lakini yule kijana mmemkamata?”

“Nasema hivi sitaki tena kusiki issue yeyote ya mwanao.”

Baada ya kusema vile alikata simu.









ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog