Search This Blog

Friday, November 18, 2022

MASKINI MAYASA - 3

 






Simulizi : Maskini Mayasa

Sehemu Ya Tatu (3)





Baada ya siku moja Damaso alirejea mjini kwa ajili ya kuendelea na shughuli zake lakini hakutoka kwa amani sana nyumbani kwake kwani bibi yake hakuwa na furaha naye huyo binti ambaye Damaso alikuwa anamtaka.

Baada ya kupita mwezi mmoja,mara baada ya kukamilika kwa taratibu zao za mahali, Mayasa aliamia kwa Damaso, Maisha ya kuishi kama mume na mke yalianza. Kula pamoja na kulala pamoja,kila kitu walifanya kwa pamoja.

Walianza kuishi kwa furaha sana, hakuna aliyekumbuka shida ,hakika kila mmoja alifarijika sana. Ilipita miezi sita wakiwa pamoja. Mayasa alinawiri sana na kupendeza mno. Siku moja walienda kumtembelea babu na bibi wa Damaso. Bibi Damaso hakuonesha kumjali hata kidogo Mayasa. Wakati huo wanaenda huko ,teyari Mayasa alikuwa mjamzito ,alikuwa mjamzito wa miezi miwili.

Walikaa siku moja kisha wakarejea tena mjini kwa ajili ya kuendelea na mambo mengine.

Mayasa alipata hofu juu ukaribisho wa bibi wa Damaso, hakufurahi hata kidogo, walipofika mjini ,Mayasa aliamua kumuuliza Damaso kuhusu bibi yake.

"Hivi Damaso mbona bibi alikuwa kama hajapenda vile uwepo wetu ?"

"Kwanini unasema hivyo?"

"Aaah! Nilikuwa namuona tu,maana kila nililoongea naye hakuonesha kunijali,yaani ilikuwa kama kuna kitu nimemchukiza vile"

"Aaah hamna kitu ,yule bibi ndivyo alivyo,mara nyingi unaweza ukadhani kama ana ugomvi vile na mtu, na kama hauko makini unaweza ukakosana naye,mvumilie tu ndio bibi yetu huyo....."

Damaso aliamua kuua jambo hilo kwa kumtetea bibi yake ili asionekane kama ana chuki na Mayasa lakini Damaso alikuwa anajua kila kitu kuwa bibi yake hakupendezwa na yeye kuamua kumuoa Mayasa kwani yeye alitaka amuoe Neema ,mwanamke ambaye ni mtoto wa jirani yao. Damaso hakutaka kumwambia jambo hilo Mayasa kwani alikuwa anajua itasababisha chuki kati ya Mayasa na bibi yake hivyo aliamua kuacha ili chuki ibakie kwa upande wa bibi yake tu.

Siku moja nyakati za usiku, Damaso na Mayasa wakiwa wamelala,ghafla walianza kusikia kelele kama paka katika chumba chao. Waliamka na kuwasha taa. Hawakumuona ,wakaambiana pengine walisikia vibaya itakuwa alikuwa analia nje ya chumba chao. Wakaingia kitandani na kuendelea kulala. Sauti ya paka ikajirudia tena.

Damaso akaamka na kumwambia Mayasa kuwa alisahau kufunga mlango,bila shaka paka atakuwa ameingia mara baada ya kuna mlango upo wazi.Mayasa akamwabia kuwa mlango aliufunga vizuri na hakumbuki kama aliuacha wazi.

Damaso na Mayasa wakaamka ili wawashe taa na wamfukuze paka huyo katika chumba chao maana alikuwa kero sana hata usingizi ulikuwa shida sana kuupata ,safari hiyo walipowasha taa walimuona paka mwenye rangi nyekundu akiwa amkeaa juu ya sofa,ilikuwa ajabu sana,hawakuwahi kupata kumuona paka mwenye rangi kama hiyo hata siku moja. Kila mmoja alipigwa na butwaa,Mayasa aliingiwa na hofu zaidi ,Damaso alikomaa akajikaza kinaume,akawa anamtuliza Mayasa ambaye teyari alianza kuchanganyikiwa.

Wakajiuliza ameingiaje paka huyo wakati mlango ulifungwa. Walifungua mlango wao na kumfukuza lakini hakutoka,alibaki akiwakodelea macho kodo.

Kila walivyojaribu kumfukuza ,paka hata hakutikisika, alitulia tuli.

Damaso aliamua kwenda kwa jirani yake, ili aje kumuona paka huyo wa ajabu ambaye hakuwahi kumuona hata siku moja katika maisha yake. Wakati anatoka Mayasa alimuacha katika chumba chake.



Ghafla yule paka aligeuka na kuwa binadamu,lakini sura haikuonekana ,Mayasa alianza kupiga kelele za woga. Damaso na jirani yake walifika kwa haraka sana baada ya kuzisikia kelele za Mayasa. Hawakukuta chochote zaidi ya Mayasa tu. Hata yule paka hakuwepo tena. Jirani wa Damaso kama kawaida yake ,alimwambia Damaso kuwa walikuwa wanaota tu maana paka hawezi kuingia ndani na mara akatoweka kama mzimu bila wao kujua.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Mayasa naye akasema alichokiona, lakini hilo hata Damaso hakulielewa,alilipinga.

"Mmmmh Mayasa inawezekana kweli ilikuwa ndoto,sasa paka anawezekanaje akajibadili na kuwa binadamu?,jirani usiku mwema ndugu yangu,nenda kapumzike nami nasi tupumzike samahani kwa usumbufu uliojitokeza"

Baada ya kuondoka jirani huyo, Damaso na Mayasa wakapanda tena kitandani. Mayasa akamwelezea kwa utulivu kile alichokiona.

Damaso hakumwelewa kwa haraka,aliona kama anamzingua tu hivyo akamtaka Mayasa wajifunike shuka na walale.

Baada ya kupita nusu saa, Damaso alilala fofofo tena alikuwa anakoroma sana. Mayasa hakulala hata kidogo kila alipokumbuka alichokiona ,usingizi haukumfika hata kidogo.

Akiwa anaendelea kuwaza na kuwazua,ghafla mlango wa chumba chao ambao ulikuwa umefungwa kwa ndani alisikia kama kuna mtu anagonga vile. Alitaka kwenda kuufungua lakini alisita. Akasikiliza tena ,akasikia tena mlango unagongwa tena kwa nguvu sana.

Akaamua kuuliza,

"nani?"

Hakuna aliyejibu, mlango uliendelea kugongwa tu,

"Ngo...ngo...ngongooo...ngo"

"Wewe nani?"

Mayasa aliuliza tena,lakini hakujibiwa,

"Kama hutaki kusema wewe nani sifungui mlango...."

Mayasa akatulia na kujifunika shuka, lakini haikupita hata dakika moja, mlango ulianza kufunguka. Yaani ilikuwa kama kuna mtu yupo kwa nje anataka kuingia ndani. Mayasa alisikia na kujifunua shuka,aliona kweli mlango upo wazi.

Mayasa alijipikicha macho yake ili ajiridhishe kama kweli au ni hisia tu,aliona vizuri hazikuwa hisia ni kweli kabisa mlango ulikuwa umefunguliwa.

Mayasa fikra zake zikamtuma pengine ni jirani yao ambaye ni rafiki wa Damaso,akaita tena ili kujiridhisha.

"Shem.....!shemejiiii..."

Hakusikia sauti yeyote iliyemjibu kwa kuita kwake.

Mayasa alijaribu kumwamsha Damaso lakini hakufanikiwa hata kidogo, Damaso alikuwa anakoroma kama gari vile. Mayasa alijaribu tena na tena lakini hakuweza,Damaso alikuwa kama pono,amelala fofofo,ukimgeuza hivi ,anageukia huku. Mayasa aliingiwa na hofu sana. Alianza kutetemeka .

Baada ya dakika moja kupita,vilianza kusikika vilio vya mtu anayetembea ambaye amevaa viatu virefu. Sauti ilisikika ko...ko...ko.

Baadae akahisi harufu ya ajabu sana kama ya kitu kilichooza na kuanza kutoa funza. Mayasa alipiga alitaka kujaribu kupiga kelele lakini sauti haikutoka.Alikuwa kama amewekewa pamba mdomoni.

"Ni balaa gani tena hili? nani sasa huyu? Mungu wangu! Naomba unisaidie...."

Mayasa aliwaza moyoni mwake baada ya kuona kila jitihada za kujiweka magala salama zimegonga mwamba.

Baadae akaamua kusubili aone kitakachoingia ni kitu gani.









Aliingia mtu ambaye alikuwa amevalia mavazi meupe,kunzia kwenye kichwa hadi miguuni,mavazi hayo yalifunika hadi sura yake. Lakini kwa mwonekano wake alikuwa alikuwa ni mwanamke kwani sehemu ya kifuani alikuwa anaonekana pamepanuka. Na hiyo ilimfanya Mayasa kujua mtu huyo alikuwa mwanamke.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Mayasa hofu yake iliongezeka, akajifunika shuka hadi usoni ili kujizuia asiweze kumuona mtu huyo. Lakini baadae yule mtu alikuja karibu na alipolala Mayasa akamfunua shuka Mayasa.Wakati huo bado Mayasa alikuwa ameyafumba macho hata baada ya shuka yake kufunuliwa.



Mtu aliyefunua shuka bado alikuwa haonekani usoni.Sauti ya kike ikasikika ikisema,



"Fungua macho yako"



Mayasa akazidi kuogopa sana. Sauti ikarudia tena,



"Fungua macho yako unione"



Mayasa akajikakamua akafumbua macho yake na kutazama.



Hakuiona sura yake,bado alionekana kama mwanzo. Mayasa akiwa na hofu ,akauliza,



"Kwani wewe ni nani na unataka nini hasa katika chumba hiki?"



"Mimi ni mwenye Damaso, nimekuja kuchukua kilichopo tumboni mwako"



"Heee tumboni mwangu? Kitu gani?"



"Hujui eeeh? Hujui tumboni kwako kuna nini? Basi subiri kesho na kuendelea utajua zaidi una nini humo tumboni mwako"



Baada ya kuyasema hayo, yule mtu akamuonesha kidole Mayasa maeneo ya tumboni mwake. Mayasa alianza kuhisi maumivu makali sana katika tumbo lake, baada ya muda mfupi fu damu zikaanza kuchurizika katika mapaja yake. Yule mtu akatoweka katika mazingira ya ajabu,yaani alitoweka kwa ghafla sana kama upepo vile.



Mayasa aliendelea kuugulia maumivu makali sana,Damaso alikuwa bado amelala. Mpaka inafika asubuhi,Damaso alikuwa bado amelala. Mayasa hakuweza kupata usingizi tena hadi asubuhi. Kitu kilichomshangaza Mayasa mara baada ya kuamka asubuhi hakuona tena dalili ya damu katika shuka wala sehemu yeyote. Damaso alipoamka alimkuta Mayasa akiwa amejiinamia katika sofa.



"Heee! Vipi umeamka saa ngapi? Mbona upo hivyo?"



Damaso baada ya kuamka alimsemesha mke wake Mayasa baada ya kumkuta yupo katika hali ya tofauti.



Mayasa akamsimulia Damaso yote yaliyotokea usiku. Damaso kwa mshangao akasema,



"Mayasa huo ni uongo sana,haiwezekani uniamshe alafu nisiamke wakati mimi sina kawaida hiyo, mimi nikiwa nimelala hata akipita mjusi lazima nishtuke na niamke, sasa wewe tumelala kitanda kimoja,uniamshe alafu nisiamke kweli? Aaah Mayasa unaniongopea jamani"



"Hivi Damaso ni lini nimekuongopea?"



"Si ndio leo umeanza?"



"Mmmmh! Damaso,hivi nikudanganye wewe ili nipate kitu gani? Hili jambo lina faida gani kama nikiwa nasema uongo?"



"Aaah! Basi tuachane na hayo,niandalie chai niwahi kule kwa jana nikamalizie kazi yangu...."



Mayasa alifanya hivyo, Damaso aliondoka kazini kwake na kumwacha Mayasa naye akijiandaa kwenda kazini kwake. Mayasa kabla hajatoka alianza kuhisi maumivu makali sana katika tumbo lake. Aliamua kulala kidogo ili yatulie kisha aondoke vizuri. Lakini hayakukoma ,maumivu yaliendelea kuwa makali sana.



Wakati huo huo ,wakati Damaso anakaribia kufika kazini kwake, simu yake iliita ,alipoipokea ,akasikia sauti ya bibi yake,



"Mjukuu wangu hujambo?"



"Sijambo ,shikamoo bibi yangu"



"Marahaba, mnaendeleaje huko na mke wako?"



"Vizuri tu bibi wala hamna tatizo"



"Kweli?"



"Ni kweli,kwani kuna lipi umesikia?"

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Kuna mtu ametupigia simu jana, kuwa mke wako ameonekana maeneo ya siri akiwa anatoa mimba, jambo hili kuna mtu katuambia wa huko huko mjini,tena yeye alisema anakaa katika nyumba hiyo hiyo mnayoishi nyinyi,je hizi habari ni za kweli?"



"Mmmh! Mbona hili jambo mpya,maeneo ya siri! Ndio maeneo gani hayo?"



"Mimi hakuniambia kwa undani sana, yeye alisema ameshindwa kukuambia mambo hayo kwa kuhofia kuharibu mahusiano yenu ndipo aliamua kunitafuta mimi ili nikuambie wewe, cha msingi hizi taarifa hebu zifanyie uchunguzi uone kama kweli au la"



"Mmmh...haya bibi ngoja nitafanya hivyo,kwakuwa sasa hivi nipo kazini basi nikirudi nitashugulika na jambo hilo"



Damaso alipoagana na bibi yake, akashusha pumzi,alafu akashika kiuno kwa mshangao wa taarifa hizo.



Kabla hata hajarudisha simu mfukoni, simu yake iliita tena na safari hiyo alikuwa ni Mayasa. Baada ya kupokea tu hata kabla hajasema halo, Mayasa alishaanza kusema kwa tabu sana, sauti yake ilionesha wazi kuwa alizidiwa sana.



"Damaso Damaso....nakufa...nakufa...njoo nyumbani haraka"



"Kuna nini Mayasa?"



Mayasa hakujibu na hata simu alishindwa kukata, akabaki analia tu. Damaso akachukua usafiri wa bodaboda na kuwahi haraka sana nyumbani kwake. Baada ya kuingia chumbani,alimkuta Mayasa akiwa ameshika tumbo huku akilalamika sana kwa maumivu.



"Vipi tena,kimekupata nini?"



Damaso aliuliza swali kwa haraka sana, hakujibu ,Mayasa alishindwa hata kufunua mdomo. Yule bodaboda alikuwa bado hajaondoka, akashirikiana na Damaso kumnyanyua Mayasa na kumweka katika pikipiki kisha safari ya hospitali ikaanza.



Walipofika hospitali ya wilaya ya Nachingwea, walipokelewa na kupatiwa kitanda. Mayasa aliwekewa dripu ya maji.Damaso ndiye aliyekuwa anatoa Maelezo ya mgonjwa, baada ya kusema kuwa Mayasa ni mjamzito. Daktari alienda kufanya vipimo vya mimba.



Majibu yalivyorudi, ilionekana mimba imeharibika. Damaso alipojaribu kumhoji daktari mimba imeharibika kwa njia gani,daktari alieleza,



"Mimba huwa zinaharibika kwa sababu nyingi sana, kuna sababu za hiyari,yaani unaamua wewe mwenyewe kuiharibu na kuna sababu zisizo za hiyari yaani hukupanga mimba itoke, ila kutokana na mazingira mimba inaharibika yenyewe,sababu hivi huwa zipo nje ya uwezo wetu , sasa basi ,kwa mujibu wa vipimo vyetu tumegundua kuwa mimba hii imeharibika kwa sababu za makusudi, inawezekana mkeo alikunywa dawa ambazo zimekatazwa kwa wajawazito, au anafanya mambo ambayo hayaruhusiwi kwa wajawazito, hebu nikuulize bwana Damaso....hakuna siku yeyote ambayo muliwahi kugombana kuhusu ujauzito?"



"Hakuna dokta"



"Nimeuliza hivyo kwa sababu ,pengine mkeo alikasirika hadi akaamua kufanya hili lililotokea, kakini hilo limeshapita ngoja tunaangalie jinsi ya kuokoa maisha yake tu"



Damaso alichanganyikiwa sana, hakujua amfanye nini Mayasa. Alishikwa na hasira hadi meno yake yakawa yanaumana yenyewe kwa wenyewe. Alianza kuyaamini maneno ya Bibi yake kuwa Mayasa ametoa mimba.



"Nilijitahidi kutimiza kwa kila alichohitaji, niliahangaika huku na kule ili kuhakikisha anaishi maisha mazuri lakini yeye kwa makusudi anathubutu kuutoa ujauzito, nilijisifu kwa marafiki zangu kuwa sasa nakaribia kuitwa baba,hivi Leo hii wakisikia nitaificha wapi aibu hii? Lazima anieleze kwa nn amefanya upuuzi kama huu"



Damaso alijisema moyoni mwake huku akianza kuyaamini maneno ya bibi yake kuwa mke bora kwake angekuwa Neema yule jirani yake na sio Mayasa ambaye leo ameshaanza kuyaonja machungu yake.



Siku hiyo ilipita Mayasa bado akiwa hospitali, asubuhi yake Mayasa alipata nafuu, baada ya kupata nafuu ,Mayasa alishtuhswa na taarifa ambazo alikutana nazo kuwa mimba yake imeharibika na inaonesha imeharibiwa na yeye mwenyewe.



Damaso alikuwa na hasira hadi alishindwa kuongea chochote hospitali hapo. Damaso alikaa kimya ili hasira zake akazimalizie nyumbani watakapofika.



Walikodi bajaji hadi kwao, Damaso alikuwa kimya tu njia nzima, hata Mayasa naye alibaini Damaso hakuwa katika hali ya kawaida ambayo amezoea kumuona akiwa nayo.



Baada ya kufika ,waliingia chumbani kwao, kabla hata hawajafanya chochote ,Damaso akaufunga mlango kwa funguo alafu akasimama wima na kumwangalia Mayasa kwa dakika kama mbili hivi huku sura ikiwa imekunjana kwa hasira kali sana.



Mayasa akamuuliza Damaso,



"Kwani kuna nini Damaso mbona sikuelewi?"



Damaso alimjibu Mayasa kwa kibao kizito kilichotua katika shavu la Mayasa na kumdondosha kitandani.



"Nataka uniambie mimba yangu imeenda wapi?"



"Mimi sielewi Damaso hata kilichonipata"



Damaso akamwongezea kofi lingine Mayasa,



"Kama Leo hutasema ukweli hakika nipo teyari kwenda jera lakini wewe utaenda kaburini"



"Ni maneno gani hayo unaongea Damaso? Mimba ilivyotoka hata mimi hapa nilipo wala sielewi imetokaje, tena mimi mshangao wangu ni mkubwa sana na haufanani na wako"



"Wewe mwanamke usijifanye hujui kinachoendelea ,mimba umeitoa kwa makusudi kabisa, nataka uniambie kwanini umeitoa mimba yangu?"



"Damaso , hivi mimi nina kichaa kiasi gani hadi nifikie hatua ya kutoa mimba? Nitoe mimba ili nipate nini kwa mfano? Furaha ambayo niliipata siku ninaambiwa ni mjamzito ilikuwa haina kifani hata wewe unakumbuka vizuri alafu nitoke hapa niende sehemu nikaitoe mimba ili iweje? Yaani hata sikuelewi kabisa Damaso hayo mambo ambayo unanieleza"



Damaso akakaa kimya kama dakika mbili hivi, alikumbuka siku walivyoambiwa na daktari kuwa Mayasa ni mjamzito,Mayasa alikuwa na furaha sana. Damaso alijiuliza mwenyewe inawezekana vipi mtu mwenye furaha kiasi kile alafu aje kuitoa mimba kirahirahisi. Damaso aliona pengine anachosema Mayasa kina ukweli.



Damaso akiwa anaendelea kuwaza hayo, alimkumbuka bibi yake jinsi alivyomwabia. Hapohapo akageuka tena kama mbogo,

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Mayasa kama unasema hujui mimba imetokaje kwa hiyo unataka kuniambia hiyo mimba imejitoa yenyewe?"



"Damaso hata sijui mimi nikuambie kitu gani maana swali lako hata mimi najiuliza Lakini sipati majibu"



"Sasa ni hivi, mimi ninaenda kazini nikirudi hapa baadae nataka nikute jibu sahihi, kama hautakuwa na jibu basi nisikukute humu ndani"



Damaso baada ya kusema hayo, akatoka nje na kuondoka kazini kwake.



Mayasa alibaki akiwa na mshangao mkubwa sana. Alijaribu kufikiria kwa namna gani mimba yake ilitoka na wala hakupata jibu. Mayasa alitamani kumpigia simu dada yake ili amweleze jambo hilo lakini akaona ataharibu mambo ,na kufanya mambo hayo kujulikana kwa watu wengi zaidi. Maana aliona akimwambia dada yake na dada yake naye atawaambia watu wengine na mwishowe mambo yakazagaa kila mahali.



Mayasa aliwaza sana yaliyotokea usiku wa siku moja kabla mimba haijaaribika. Alianza kuona kuna imani za kishirikina zimeanza kujionesha kwake. Alijaribu kuwaza kama kuna mtu yeyote ambaye amemkosea lakini hakuona. Aliwaza sana ni nani sasa ambaye anamfanyia vitendo vibaya kama hivyo. Kila alilowaza jibu liliegemea kwenye imani za kishirikina.



Suala la imani za kishirikina aliona akimwambia Damaso hataweza kumwelewa kabisa.Mayasa aliamua kutafuta uongo ambao alidhani akimwambia Damaso basi ataelewa. Mayasa aliwaza sana hadi akajikuta amelala usingizi.



Damaso naye siku hiyo hakufanya kazi kwa amani, kila alipokumbuka tukio la mke wake kutoa mimba hakuweza kupata raha hata kidogo.



"Vipi Damaso, mbona leo upo katika hali ambayo si ya kawaida hata kidogo?una matatizo gani?"



Mmoja wa mafundi wenzake ambaye ni rafiki yake wa karibu sana, aliyeitwa Karim alimuuliza Damaso. Damaso hakutaka kumwambia mapema rafiki yake huyo, alimuongopea,



"Aaah leo kichwa kinaniuma sana, nahisi maralia hii inaninyemelea"



"Daah pole sana, kama nenda tu nyumbani kampumzike alafu uone utakavyoamka kesho, mambo yakizidi wahi hospitali haraka"



"Aah! Karim ,ngoja nitajikaza hadi jioni wala usihofu sana,tuko pamoja tu"



Damaso alijikaza kisabuni hadi jioni,alafu akarudi kwake. Kabla hata hajafungua mlango wa chumbani kwake,simu yake iliita ,alikuwa bibi yake,



"Wewe Damaso mbona upo kimya tu? Vipi yale niliyokuambia yalikuwa yakweli?"



"Aaah ! Bibi ni kweli kabisa yule mwanamke ni mjinga sana"



"Damaso ,mimi nilishakuambia kuwa hao watu usiowajua ni tatizo wewe hukutaka kunisikia, huyo mfukuze kwako kabisa ,sio mwanamke huyo"



Baada ya kuyasema hayo akakata simu, Damaso aliingia chumbani kwake ambapo alimkuta Mayasa akiwa amelala. Akamwamsha na kumuulizia jibu lake.



Mayasa akamwambia Damaso kuwa alitereza kwenye sakafu na kuanguka chini.Sasa alivyofika chini alifikia tumbo,kwahiyo anahisi mimba ilitoka katika mazingira hayo. Mayasa aliamua kumwongopea Damaso huku akidhani hiyo ndiyo utakuwa salama yake. Baada ya jibu hilo, Damaso akahamaki,



"Wewe mwanamke hakika leo kuna kitu unakitafuta na ninavyoona utakipata muda sio mrefu, yaani wewe ulianguka ,sasa kwanini usiseme mapema? Unanifanya mimi mtoto mdogo sana"



"Jamani Damaso kila ninalosema hunielewi sasa unataka jibu gani?"



Damaso akashikwa na hasira sana baada ya kuulizwa swali hilo na Mayasa. Pembeni kulikuwa kuna kisu. Kwa haraka sana ,Damaso alikinyanyua kisu hicho na kutanua mkono wake ili amchome Mayasa tumboni. Mayasa alipiga kelele lakini Damaso alianza kuupeleka mkono ulioshika kisu kwa kasi sana katika tumbo la Mayasa.







Kabla hata kisu hakijagusa katika tumbo la Mayasa,mlango wa chumba chao uligongwa. Harakaharaka Damaso akarudisha kisu mahala alipokitoa alafu akaenda kufungua mlango na kumsikiliza aliyekuwa anagonga mlango. Alikuwa ni mama wa jirani ambaye alienda kuangalia ela ya umeme kwani siku hiyo ilikuwa zamu yake kulipa. Damaso aliingia ndani na kutoka na kiasi cha pesa kisha akampatia mama huyo.

Baada ya hapo, Damaso aliufunga mlango kwa funguo alafu akachukua kisu na kumwambia Mayasa aseme ukweli wake.

"wewe si unataka kuniua? Niue tu, maana hunielewi kila ninalosema"

"Mayasa mimi sitanii nipo serious ,tafadhali sema ukweli kabla mengine hayajatokea"

Mayasa akajieleza tena mbele ya Damaso.



Maelezo ya Mayasa hayakuwa tofauti na yale ya mwanzo, ila sasa alikazia katika upande wa ushirikina. Baada ya maelezo hayo, Damaso akasema,

“Mayasa naona unataka kucheza na hisia zangu,hivi unadhani utaeleweka kirahisi rahisi tu....kwanza nahisi nikiendelea kukaa na wewe humu ndani ,basi bila shaka kesho nitaamka jera,sasa jiandae kwa haraka sana nikupeleke kwa dada yako, siwezi kukakaa na muuaji”

"Mmmh Damaso! Mimi muuaji kweli....!!!"

"Haswaaa wewe ni muuaji"

"Damaso yaani umefikia hatua hiyo ya kuniita muuaji....."

"wewe muuaji ,narudia tena wewe ni muuaji..."

"Heee! Jamani mbona umebadirika ghafla kiasi hicho, yaani Damaso niliyemjua mimi wala sio huyu ninayemuona sasa"

"Utanitia hasira zaidi, naomba ujiandae nikupeleke kwa dada yako,ninavyozidi kukuona ndio nazidi kupandwa na hasira"

Damaso baada ya kusema hayo,akachukua simu yake na akampigia dereva wake wa bodaboda. Mayasa alidhani Damaso anatania ,lakini baada ya simu kupigwa hapo ndipo alianza kuamini kuwa hakuwa na hata chembe ya masihara. Baada ya dakika tano tu, pikipiki ilinguruma nje ya nyumba yao.

Damaso akamwamuru Mayasa atoke nje waanze safari ya kwenda kwa dada yake. Mayasa hakupinga ,alijua Damaso yupo katika hasira hivyo chochote anaweza kufanya,alikubali kutoka nje na wote wakapanda bodaboda hadi kwa mama vumi.

Walipofika waliwakuta wote ,wakati huo jua lilikuwa limeanza kuzama. Baba na mama vumi walijua wametembelewa kama kawaida tu, yaani hakuna shari yeyote.

Waliposalimiana ndipo walipogundua kuwa Damaso na Mayasa hawakuwa na amani.

"Jamani mbon sura zenu na jinsi mnavyoitikia inaonesha kuna tatizo kati yenu,kulikoni?"

Mama vumi aliwauliza, Mayasa akadakia harakaharaka ili kumfanya Damaso agairi lengo lake,

"Wala hamna tatizo dada, tumetoka mjini huko, tukaona tupitie hapa ili tuwasalimie"

Wakati Mayasa anajibu hivyo, Damaso alimkata jicho la hasira na alipomaliza kusema tu, Damaso naye akatia neno lake,

"Unaacha kusema ukweli wako alafu unaendelea kumumunya maneno,jamani eeeh huyu ndiye Mayasa ndugu yenu,mambo aliyoyafanya mimi siwezi kuyavumilia hata kidogo na sio mimi pekee bali ni kila mtu hata nyinyi mkisikia hamuwezi kumvumilia hata kidogo"

Baada ya kusema hayo, Damaso alinyanyuka na kuanza kuondoka . Baba Vumi alijaribu kumwita Damaso lakini Damaso hakuangalia nyuma,alizidi kusonga mbele na akatoweka kabisa machoni pao.

"Kwani kuna tatizo gani? Mbona hivi shemeji?"

Baba Vumi alimuuliza shemeji yake Mayasa ambaye wakati huo alikuwa analia tu. Mayasa akajibu,

"Tatizo mimba imetoka"

"Imetoka?"

Baba Vumi na mama Vumi wote walishangaa. Alafu mama Vumi akahoji kuhusu hiyo mimba imetoka kwa namna gani. Mayasa akawaelezea kila kitu, Ilikuwa ngumu kueleweka.

Dada yake akahoji,

"Mayasa sema ukweli kama umetoa mimba,tuambie hapa ili tujue jinsi ya kukusaidia ndugu yangu"

"Dada hayo ndiyo maelezo na ndio ukweli wangu, siwezi kutoa mimba kwa makusudi hata siku moja...."

Baada ya mabishano sana, baadae baba Vumi alifananisha na tukio la rafiki yake mmoja hivi ambapo mazingira ya kuharibika mimba yalikuwa yanafanana kabisa, baadae wakaja kugundua kuwa ilikuwa ni mshtuko wa ndoto mbaya ambazo alikuwa anaziota, hivyo hata Mayasa naye atakuwa amepatwa na mshtuko ndipo ukasababisha mimba yake kuharibika.

Moyoni mwa Mayasa hakutaka kuamini lingine zaidi ya mtu wa ajabu aliyewahi kumuona usiku siku moja kabla ya mimba kuharibika.

Baba Vumi alisema yeye ataenda kwa Damaso kumwelekeza jambo hilo kuwa mimba imetoka kwa sababu ya mshtuko.

Asubuhi na mapema kabisa hata jua halijachomoza, Baba Vumi alienda kwa Damaso.

Baada ya kufika huko alijaribu kumwelezea kwa utulivu sana. Ila Damaso akasema,

"Yaani mmekaa huko ,mkapangana alafu wewe ndio umetumwa kuja kunilaghai mimi....haha hamuniwezi,nenda kawaambie waliokutuma kuwa Damaso sio chizi ana akili zake timamu"

Baba Vumi akatabasamu kisha akamwambia,

"Ndugu yangu Damaso, mimi si mtu wa aina hiyo ambayo unanifikiria, mimi sina tofauti na wewe, wale sio ndugu zangu mimi nilienda pale kuoa tu, kwa hiyo siwezi kuja hapa eti kumpendelea Mayasa, wewe ndiye mtu ninayepaswa nikupendelee sio wale, Damaso mimi namfahamu vizuri Mayasa kwani kabla hajafika hapa alikuwa anaishi nyumbani kwangu,kwa jinsi ninavyomfahamu Mayasa kiukweli yule mwanamke hawezi kufanya ujinga wa kutoa mimba kwa makusudi kwani hata wakati anakaa nyumbani alikuwa anatamani sana kuitwa mama, hivyo ndugu yangu Damaso twende nyumbani ukamchukue mkeo, punguza jazba na hasira"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Maelezo ya baba Vumi yalimwingia sana Damaso. Damaso alitulia kimyaa na hapo baba Vumi alizidi kupigilia maneno ya ushawishi, Baadae Damaso alilainika na kukubali Mayasa arudi kwake.

"Bro kwa heshima yako, Mayasa atarudi hapa na maisha yataendelea kama kawaida."

Damaso na baba Vumi wote walitoka na kwenda nyumbani kwa baba Vumi. Damaso alirudi na Mayasa nyumbani kwao.



Waliyaanza tena maisha yao na kwa furaha kama zamani. Siku zilisogea mbele ,miezi miwili ilikatika ,hatimaye Mayasa akashika ujauzito tena. Alianza kuhudhuria kliniki kwa lengo la kuangalia maendeleo ya mimba yake na kila alivyoenda aliambiwa kuwa mimba inaendelea vizuri sana.







ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog