Search This Blog

Friday, November 18, 2022

SITOWEZA KUKUSAHAU - 1

 






IMEANDIKWA NA : SWEDI SHAURY



*********************************************************************************



Simulizi : Sitoweza Kukusahau
Sehemu Ya Kwanza (1)


 Gari aina ya mercedes Benzi nyeusi ilikimbia kwa kasi na kuacha barabara ya lami na kuifuata barabara ya vumbi huku ikikata kona bila kupunguza spidi kama zile za magari ya mashindano na kufanya msitu huu mnene kujawa na kelele za mlio wa gari hiyo.Ving’ora vya gari ya polisi vilikuwa vinatoa sauti ya juu huhku wakijaribu kuifukuza gari ile kwa nyuma.Ndege waliokuwepo kwenye miti na vichaka vilivyopo katika msitu ule walianza kuruka kwa makundi na kutokomea kusikojulikana huku wakisaliti makazi yao ambayo yalionesha kuingilia na binadamu hawa.

Benzi hiyo iliyokuwa na namba za usajiri T 346 DFP ilisimama katikati ya barabara hii ambayo haikuwa inatumiwa sana na watu zaidi ya gari za wapasua mbao.Ilikuwa inajaribiwa kuwashwa bila matumaini,mlango wa upande wa dereva ulifunguliwa na kutoka mtu mwembamba aliyeshika bunduki aina ya AK 47.Usoni kwa mtu huyu mwembamba kulijawa na hasira zilimwonesha kuwa ni wa roho mbaya.Mlango ungine ulifunguliwa na msichana mrembo alitoka huku na yeye ameshika bastola ndogo mkononi,vazi jeusi alilovaa na buti kubwa jeusi lilimpisha juu na kumfanya aonekane mrefu zaidi.

“Let’s go(Tuondoke)” jamaa huyu mwembamba aliyekuwa na rangi ya maji ya kunde alimwambia msichana yule ambaye alikuwa anachukua baadhi ya mizigo muhimu uliyokuwa ndani ya gari lile na kutokomea porini.Gari za polisi zipatazo tano zilifika eneo lile na kulizunguka gari huku kila mmoja wao ameshika bunduki aina za SMG na kuanza kulisogelea gari lile kwa umakini mkumbwa.

“One…two…three....shut(moja…mbili….tatu….piga)” Inspekta Makurumla alihesabu moja mpaka tatu na kuwaamulisha polisi wake waanze kuishambulia ile gari,wakiamini kuwa kuna watu ndani yake.Zaidi ya risasi 40 ziliishambulia gari lile la kifahari na kuliacha limechaa kama la miaka sabini iliyopita.Mmoja wa polisi alifungua mlango wa gari hilo na kukuta hakuna mtu zaidi ya picha ya msichana mrembo iliyoachwa kwenye gari hiyo.

“Mkuu,kuna picha ya msichana hapa tumeifuma ndani ya gari”Alisema yule polisi aliyekuwa anahusika na ukaguzi wa gari hiyo.

“My God sogea sogea wote pembeni” Inspekta Makurumla alipaza sauti na kuwaambia wenzake wasogee pembeni na gari lile.Haikuchukua sekunde hata tano tayari mafuta yalidaka moto uliokuwa unawaka katika gari lile na kusababisha mlipuko wa hatari.Moshi ulitanda sehemu ile,hakukuwa na polisi yeyote aliyekuwa anaongea zaidi ya dakika 1.Ndipo sauti za kukohoa zilisikika na mmoja mmoja walianza kuinuka huku wakijifuta vumbi kutokana na mlipuko ule.

“Wote salama?” Inspekta Makurumla alihoji na wote wakaitikia.

“Ndio mkuu”

Wakati wanaendelea kupanga mipango yao ghafla mmoja wa polisi hao alidondoka puuu! Mpaka chini.Wote walijikuta wanashambulia ovyo bila kuona kitu chochote wanachokishambulia.

“Tulia,acheni woga wa kishamba,mnapigapiga nini mlichokiona?” Inspekta Makurumla alifoka kwa jazba na hasira.

“Afande Ngudu na Afande Kipinda,chukua huyu waisha hospitali”

“Ndio mkuu” wawili hawa walichukua mwili wa mwenzao na kupandisha kwenye gari kuchomoka kwa kasi ya ajabu.



“Harakisha tunafuatwa unajua?”

“Ramso mimi nimechoka” msichana huyu alilalamika kuchoka hutokana na kukimbia kwa muda mrefu katika msitu ule mnene ulijaa kiza kilichosababishwa na mshonano wa miti na nyasi ndefu .

“Hapana Zulfa usichoke,ndo kwanza hata nusu ya msitu huu hatujamaliza” Ramso alisema huku anamwinua Zulfa alikuwa amechoka na kuwa hoi bin taabani.Safari ilianza upya huku Ramso kavaa begi la mzigo lililojaa pesa za kutosha.

Walifika mahali penye utulivu na kukaa kisha wakaanza kunywa maji na kula baadhi ya biskuti walizopata kununua super market kabla ya kupatwa na msala huo wa kufukuzwa na polisi.

“Sasa Ramso tunatokaje ndani ya msitu huu?” Zulfa alimuuliza Ramso.

“Tufanyaje inabidi tuvumilie na kumuomba Mungu wetu atuokoe ndani ya msitu huu”

Usiku uliingia katika msitu huu huku Ramso na Zulfa wakiendelea na safari yao isiyofahamika inaenda kuishia wapi.Walifika sehemu na kujikuta wanaketi chini na kuutafuta usingizi,kila mtu alikuwa anaangalia upande wake kwani hawakuwa wapenzi zaidi ya kazi tu.

Asubuhi mapema jua lilichomoza na kuwamuliza Ramso pamoja Zulfa.Walijificha macho na kufumbua macho ghafla waligongana macho kwa macho na Simba aliyekuwa kalala pembeni yao.wakati wanaendelea kutaka kujinasua kutoka katika lile janga la Simba mara walisikia mlio wa Helkopta juu yao.

***

Mzee Kibangara aliyezungukwa na vijana ambao walikuwa na vifua vinene,walikuwa wameinamisha sura zao chini.Mzee kibangara alionekana kuchukizwa sana jambo lililofanywa na vijana wake hao.

Alivuta fundo moja la sigara na kuitupa chini na kuikanyaga kwa hasira za hali ya juu.

“Ni uzembe gani mmeufanya,nimekwisha waambia kuwa sitaki hata mmoja wenu hapotee katika misheni yangu si ndiyo?”

“Ndiyo Bosi” wote waliitikia

“Sio kwiyoo,pumbavu zenu toeni mbaliga zenu hapa na msirudi mpaka Ramso na Zulfa niwaone la sivyo naua wote” Mzee kibangara aliwafokea wafuasi wake huku amewaelekezea bastola na kuwafanya waanze kutawanyika.

“Na ninawapa masaa kumi na nane muwe mmewaleta hapa”

“Ndio bosi” wafuasi hawa walitoka mpaka nje na kujadiliana waanze wapi kuwatafuta watu hawa.Lakini kabla hawajamaliza kuongea mara simu ya Peter ambaye ni mfuasi mkuu wa Mzee Kibaranga iliita.

“Hallo” Peter aliitikia

“Ramso hapa tumezungukwa na polisi na tupo ndani kabisa ya msitu,fanyeni mje kutuongezea nguvu”

Ramso aliongea kupitia simu ile na kuwafanya wafuasi hawa warukie ndani ya gari zao na kutia gia kuelekea msituni.

“Wekeni sawa mashine zetu ndo tunakaribia ndani ya huo msitu,hakikisha kila mmoja anachukua risasi za kutosha” Peter aliendelea kuongozi kikosi chake.Walipofika msituni hapa walificha gari zao na kuanza safari kuelekea ndani ya msitu huo mnene.

“Godwin the sniper” Peter alimwita mfuasi anayeitwa Godwin

“Ndiyo mkuu”

“Tafuta target kisha fanya yako,mliobaki tano upande wa kulia,tano upande wa kushoto,wewe na wewe nifuateni” kamanda Peter aliendelea kutoa maelekezo na baada ya sekunde tano wote walifanya hivyo.

Kasi ya wafuasi hawa iliongezeka huku wakipiga mguu kuelea ndani kabisa ya msitu huo na kila mmoja bunduki yake ameiweka tayari kwa mashambulizi.

“Lala chini wote,Afande mgimwa funga pingu hawa tuondoke” Inspekta Makurumla alitoa amri kwa mwenzake na kutekeleza ya kuwafunga Ramso na Zulfa ambao walikuwa chini wamelala huku bunduki zao zimekamatwa na polisi.Helkopta ilikuwa imetuwa katika sehemu yenye uwazi ili kuwasubiri polsisi wa kikosi cha chini.

Walianza kutembea kwa mwendo wa haraka kuelekea ilipo helkopta hiyo.Lakini kabla hawajafika mbali walianza kushambuliwa wafuasi wa mzee Kibangara kutoka vichakani,na wao bila kusubiri walianza kupeleka majibu na kuanza kujibizana.

Msitu ulianza kuchafuka kwa shaba ambazo zilikuwa zinachafuliwa na vikosi hivi viwili na hapo Ramso pamoja na Zulfa walipata mpenyo na kuanza kukimbia huku wakiwa na pingu walizofungwa kwa nyuma.

***

“Bosi bosi Ramso,zulfa na Peter wamekamtwa” mfuasi huyu alisema huku pumzi zinamtoka kama mbwa aliyekimbizwa na mnyama mkali na kumfanya atoe ulimi huku pumzi nyingi zinamtoka.Mzee kibangara kwa hasira zaidi alichomoa bastola yake na kumpiga mfuasi yule risasi za kifuani bila kuangalia idadi mpaka risasi zote zikaisha.

“Pumbavu sana,unaniambia upuuzi wako,kaseme huko kuzimu” Mzee kibangara ambaye alikuwa katili na mwenye hasira za muda mfupi.

“Sasa basi natoa order(amri) tena nataka kuziona sura hizo hapa,na sihitaji upuuzi kama wa hii maiti hapa chini”

“Sawa mkuu”

“Sio sawa kuku nyie,mimi na nyinyi tuko sawa?”

“Hapana mkuu”

“Sema ndiyo mkuu”

“NDIO MKUU” wafuasi hawa wote waliitikia na kutoka zao nje.

Walipanga mikakati jinsi gani wataweza kuwatia mikononi wenzao .Ndio walifikia muafaka wa kutaka kuvamia kituo cha polisi ili wawatoe wakubwa wao ikiwa kama ni moja ya kuokoa maisha yao.



Inspekta Makurumla pamoja na msaidizi wake walikuwa mezani huku mbele yao kuna sura tatu ambazo ni Ramso,Zulfa pamoja na Peter.

“Mnaweza kutuambia kwa nini mlithubutu kupora super market na kuua watu?” Inspekta huyu ambaye alikuwa amezikabiri sura zote tatu,aliwapiga swali na hakuna hata mmoja aliyejibu.

“Nauliza tena kwanini mmeiba na kuua?” safari hii Inspekta aliuliza kwa ukali huku anainuka juu.Kimya tena kiliingia bila jibu kutolewa.Ramso ambaye alikuwa kainamisha sura yake chini kama kuna kitu anakiwaza.Mawazo yalimpeleka mbali na kuyakumbuka vizuri maneno ya Mzee Kibangara.

‘NAWAPA OVYO NA ANGALIZO SITAKI NITAJWE NA MTU YOYOTE KATIKA KAZI HII,IWE NJE AU NDANI YA NCHI HII SAWA?’

Mara Ramso alishtuliwa na konde la kichwani na kumtoa katika mawazo yake ya muda mfupi.

“Mimi nauliza halafu nyie mnakaa kimya sasa subirini.Inspekta Makurumla alifungua mlango na baada ya dakika chache waliingia polisi watatu walikuwa na vifaa kadhaa ikiwemo mikasi,visu na vifaa vingine vya kuwatesa wale watu wanaojifanya wagumu kutoa ushirikiano.

Usiku huo Inspekta Makurumla alipanda gari yake na kuwasha moto kuelekea barabara kuu iendayo Morogoro.Masaa yaliendelea kuongezeka wakati Inspekta huyu yupo njiani kutokana na foleni aliyoikuta katika mtaa wa Suka maeneo ya Mbezi.Alijikuta anafika maeneo ya nyumbani kwake Kimara mwisho huku akiwa amechoka sana.

Ghafla mapigo ya moyo yalianza kumuenda mbia baada ya kuona tone la damu getini kwake na hakumuona kabisa mlinzi wake.

“Muck! Muck” Inspekta Makurumla alijaribu kumuita mlinzi huyu bila mafanikio.Wakati anaendelea kuchunguza ndani ya nyumba yake hii ndipo alimwona mlinzi wake Muck akiwa amejifunika kofia yake na kujieegemea kwenye mti huku rungu lake likiwa pembeni yake.

“Muck,mimi nakuita kumbe umelala hapa,mlinzi gani wewe” Inspekta Makurumla aliongea kwa jazba huku anamfunua kofia yake.

“My God! (Mungu wangu)” Inspekta alishikwa na mshangao baada ya kumuona mlinzi wake amelowa damu kichwa kizima.Alitoa bastola yake na kuanza kunyata kuelekea mlango wa nyumba yake,alijikuta anaangusha machozi kwani alijua kama mlinzi wake amekufa basi iko wazi kuwa mke wake pamoja na watoto wake wawili watakuwa wameuawa pia na watu wasiojulikana.

Alifungua taratibu huku amehakikisha kuwa yuko tayari kwa jambo lolote lililopo mbele yake.Baada ya kufika sebleni alikuta vitu vimekaa ovyo ovyo bila mpangilio.Aliendelea kuangalia mazingira ya ndani kwa uangalifu mkubwa,alipofika chumba cha kwanza alijikuta anatupa bastola chini na kukimbilia ndani ya chumba hicho.

Alijawa na hasira baada ya kuwaona watoto wake karim na Pili wamefungwa kamba miguuni na kwenye mikono yao huku wameshindiliwa rundo la vitambaa kinywani.Kitu cha kwanza alichokifanya Inspekta Makurumla kuwatoa yale matambala ya kinywani yaliyoonesha kuwanyima pumzi watoto hao.

Jasho la gadhabu lilimtoka Inspekta huyu ambaye alijikuta anahema kama mbogo aliyejeruhiwa.Macho yake yaliiva na kuwa mekundu mithili ya nyanya,laiti kama angelimwona aliyefanya kitendo kile basi angeliagizwa kuwasalimia kuzimu.Baada ya kuwafungua watoto wake wapendwa tena mapacha,aliwapenda sana tena sana,hakuna kitu alichokipenda zaidi kama familia yake,kitendo cha kutoonekana kwa mke wake katika mazingira yale kilimfanya achukie zaidi kwani hakuwa na penzi la dhati duniani kama kwa mke wake,baada ya kufariki kwa Mama yake mpendwa kwa kupingwa risasi na baba yake mzazi.

“Mama yenu yuko wapi?” Inspekta Makurumla aliwaliza watoto wake

“Hatujui,wamekuja watu wamejiziba uso wao…wakamchukua mama na kutufungia sisi kwenye chumba hiki” alieleza yule wa kiume anayeitwa Karimu.

Watoto hao waliokuwa na umri mdogo iliyopungua miaka saba walikuwa wamefungiwa ndani ya chumba kile na watu hao waliokuwa wameziba nyuso zao kwa mizura,walionekana wamechoka kwa kukosa pumzi kutokana na kushindiliwa vitambaa kinywani na kuachwa wakipumlia pua huku wakiwa ndani ya chumba kidogo kabisa kilichojaa giza na kukosa hewa kutokana na madirisha ya chumba hicho kuwa madogo sana.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Inspekta aliwatoa watoto wake mpaka sebleni na kuwapatia maji waweze kulainisha koo lao.Mikono ya Makulumla ilikuwa kwenye kiuno chake huku akitafakari kitu cha kufanya kwa harakaharaka.Lakini alipojaribu kuaangalia chini ya meza alikutana na karatasi iliyokunjwa mara moja huku imekandamiziwa kwa rimoti ya Tv.Aliinama na kuichukua kisha kuifunua ili akione kilichoandikwa katika karatasi hiyo.Ulikuwa ujumbe ulioandikwa kwa herufi kubwa ukieleza kuwa;

‘HEY INSPEKTA CHIFU KAMANDA MWENYEWE,NAJUA UTAJIULIZA KWA NINI UMEKUTA HALI YA NYUMBA YAKO IPO MBAYA,USIUMIZE SANA KICHWA SISI NI WATU WEMA KABISA NA MKE WAKO YUPO KATIKA MIKONO SALAMA.KAMA KWELI UNAMPENDA MKE WAKO NA KUMTHAMINI TUNAKUOMBA UFANYA KITU KIMOJA.TUNATAKA UWATOE WATU WETU NDANI YA SIKU HIZI MBILI LA SIVYO MKE WAKO ATAKUWA MALI YETU.PIGA HII NAMBA 0687533735 KWA MSAADA ZAIDI.

CHIFU MAKU…………’

Inspekta Makurumla alijikuta anakooa macho asijue nini cha kufanya na alishindwa kumalizia kuisoma ile barua ilioandikwa na watekaji hao ambao hakuwajua,kutokana na kuhisi macho yake yanataka kutoka.Mke wake ndio kila kitu kwake,hakupenda hata siku moja ampoteze katika mikono ya watu isipokuwa ni kifo tu kitakachosababishwa na Mwenyezi.

Hapohapo alijikuta anatoa simu yake ya mkononi na kuingiza zile namba zilizoandikwa ndani ya ujumbe na kubofya sehemu ya kupiga kisha kuiweka sikioni.

‘SAHAMANI NAMBA YA MTEJA UNAYOPIGA INATUMIKA KWA…….’ Sauti kutoka kwenye simu ilisema.

Hakuishia hapo alichukua radio call yake na kazini na kupiga.

“Nataka msaada wa haraka mkuu nimengiliwa katika nyumba yangu” Inspekta Makurumla aliongea.

“Over over” Alikata simu na kuiweka pembeni ya mkanda wake wa suruali.Jasho liliendelea kumvuja kwa wingi na hasira zilimzidi mara dufu.Alijaribu tena kupiga ile namba ya kwenye barua na kuiweka sikioni kisha ikaanza kuita………………………..



Mazungumzo baina ya Inspekta Makurumla na wafuasi ya mzee Kibangara waliendelea kuzungumza ili kuweka mambo sawa na Inspekta Mkurumla amkomboe mke wake.Baada ya dakika chache kupita gari ilikuwa na polisi wapatao sita ilifunga breki nje ya nyumba ya Inspekta Makurumla na kushuka,baadhi yao waliingia ndani na wengine walibaki nje kulinda usalama wa nyumba hiyo huku wakiwa wameshikilia mitutu ya bunduki zao.

Inspekta huyu hakuwa na jinsi zaidi ya kuangalia upande mwingine ili mradi mke wake awe salama na arejee katika mikono yake.Basi asubuhi yake baada ya kumaliza kuweka mambo sawa katika nyumba yake huku akiacha askari kadhaa walioweka dolia katika nyumba yake.Alikuwa na kazi moja ya kuwatoa watuhumiwa wa uporaji na uuwaji katika supamaketi,hakujua aanzie wapi ili aweze kufanikisha suala hilo.Aliingia mpaka ofisini kwake na kufungua faili ambalo lilikuwa limehifadhiwa taarifa za wavamizi wa supamaketi.Akaanza kufunua karatasi moja baada ya nyingine,ndipo akainuka na lile faili na kuingia chumba walichokuwa wale wafuasi wa mzee Kibangara.Akawatazama wote kwa umakini na kumuinua Ramso juu kisha akamsogeza pembeni.

“Sikia,inatakiwa niwatoroshe humu baadaye ila kuweni makini,mimi nitakuwa nawasaidia sawa?” Makurumla alisema kwa kunong’ona.

“Sawa” Ramso alijibu na kurudi sehemu aliyokaa mwanzo.Ramso akawaeleza wenzake taarifa aliyopewa na wote wakakubaliana kuwa baadaye watatoroka.Inspekta Makurumla aliendelea kuwaza na kuwazua juu ya jambo lililomkabili mbele yake bila kupata jibu.Hakuwa na jinsi tena zaidi ya kwenda kinyume na wenzako ili anusuru roho ya mke wake kipenzi.Mara simu yake ikaita.

“Yamebaki masaa saba tu,watu wetu wawe wametoka ama sivyo your wife going tu die” sauti mzito ya mpigaji huyo ilichoma ngoma za sikio la Makurumla na kumpandisha hofu.

“Haaa…kuna shi..ida kila kitu kiko ….safi wajomba” alisema kwa kigugumizi na kwa uchungu mkubwa,alijua kama atashindwa kuwatowa watu hao basi mke wake atampoteza.

“Naa…omba ..niongee na mke wangu tafadhali” Makurumla alisema huku jasho linamtoka japokuwa ofisini mwake kulikuwa kuna A/c alikini haikusaidia.

“Haalo mke wangu unaendeleaje?” aliuliza baada ya mke wake kupewa simu na watekaji hao.

“Mume wangu nitoe nateseka mimi” mke wa Makurumla alisema huku analia.Kitendo cha Makurumla kusikia sauti ya mke wake analia ndicho kilimpelekea na yeye aanze kuangusha chozi la kumuonea huruma.Akawa na kazi ya kumpa moyo kuwa atatoka muda sio mrefu.

“Mke wangu nakutoa leo hii hii ondoa shaka kila kitu kitakuwa sawa” alisema huku anabubujikwa na machozi.

“Sawa mume wangu nakupenda sana”

“Nakupenda pia mke wangu” alisema Makurumla na simu ikakatwa.Akachomoka mpaka nje ya ofisi yake na kutazama mazingira yote.Alianza kuzunguka eneo lote huku akitafuta njia mzuri ya kuwatoa wafuasi hao ili arudishiwe mke wake.Baada ya kusoma mazingira na kubaini kuwa kuna sehemu ambayo haina askari wanaolinda ndipo akarudi ofisini na kuendelea na kazi.Kila muda alitazama saa yake ya mkononi na kuona muda unachelewa ili atimize mipango yake ya kuwatorosha watuhumiwa hao.

Hatimaye ikahitimu saa mbili za usiku,mkuu wake alikwisha ondoka zamani na kuachiwa majukumu yote Inspekta Makurumla.Akaingia hadi kwenye chumba walichopo watuhumiwa hao na kuwafungua pingu kisha akawaambia wamfuate nyuma.Taratibu wakaanza kunyata kwa uangalifu wakiongozwa na Makurumla.Ulikuwa mchezo rahisi kutokana na Inspekta Makurumla kuchunguza mazingira yote ya kituo hicho.Kwa bahati mbaya Zulfa alijikwaa na kuangukia juu ya bati lililotoa sauti na kuwashtua askari waliokuwa wanalinda usiku huo.Kwa kasi ya umeme Inspekta Makurumla alimwinua Zulfa na wote wakajibanza pembeni na kukaa kimya kumshuhudia asakri aliyekuwa anakuja na tochi kubwa iliyotoa mwanga mkali.Askari huyo alitazama huku na huko na kutoona kitu chochote.Akarudi na kuendelea na lindo lake.Inspekta Makurumla akafanikiwa kuwatoa nje na kukuta gari iliyokuwa inawasubiri imesimama mita chache kutoka kituoni hapo.Baada ya kukabidhiana watu wao gari iligeuza kwa kasi na kupotea machoni mwa Inspekta Makurumla.

“Pole sana mke wangu” Makurumla alisema huku amesimama sehemu ile na mke wake.

“Asante kwa kunitoa mume wangu” alisema huku anatokwa na machozi.Makurumla alimvuta machozi mke wake na kumbusu kwenye utosi kisha wote wakaondoka kuelekea nyumbani kwao mara baada ya kuwaaga askari wa zamu.

“Hakikisheni kuwa mnakuwa makini sana,kumbukeni kuwa kuna watuhumiwa hatari humu ndani sawa?” alisema Makurumla kwa mkazo,lakini siri alikuwa nayo moyoni kuwa alikwisha watorosha.

“Ndiyo mkuu” askari huoo alibana miguu na kukubali amri.Inspekta alipofika nyumbani aliwakuta askari wanaendelea na ulinzi katika nyumba ya mkubwa wao.Ndipo baada ya kurudi aliwaamulu waondoke na kuwasisitizia kuwa mambo yamekaa sawa.Mke wa Makurumla alipoingia tu ndani alirukiwa na watoto wake kwa furaha,kitu kilichomfanya atokwe na chozi la uchungu.Hapo Makurumla na yeye alikuja ilipo familia yake na kuwakumbatia wote huku akitokwa na machozi.



***

“You’re welcome back guys(karibuni tena)” Mzee Kibaranga alisema huku ameshika sigara kubwa ambazo mara nyingi hutumiwa na matajiri nchini Marekani,sura zilizopo mbele yake ni Ramso,Zulfa na Peter.Vijana wake ambao anawaamini sana katika kazi zake.

“Tunajitaji kuongea na wewe mkuu” Ramso alisema kwa sauti mzito iliyomshangaza kidogo mzee kibangara.

“Right now?(sasa hivi)”

“Of course(bila shaka)” Ramso akamjibu.Wakasogea pembeni kabisa na kuketi kwenye viti.Wa kwanza kuongea alikuwa Ramso huku amekabiliana na sura ya mzee huyo ambaye ni bosi wao.

“Mzee nataka kurudi nyumbani Durban” alisema Ramso kwa sauti mzito.Mzee Kibangara alimtazama Ramso na kisha akainuka.

“There is another mission,so unataka kuondoka wakati hatuja maliza mkataba wetu?” Mzee Kibangara alisema huku amesimama mbele ya Ramso.

“Noo! I’cant(hapana siwezi)” Ramso alisema kwa sauti ya juu.Mawazo ya Ramso yalikuwa tayari yamekumbuka maisha yake yote nchini Afrika Kusini.Kutokana na Mzee Kibangara kutafuta vijana ambao angeliweza kuwatumia katika kazi yake ya kiugaidi,utekaji pamoja na matukio mbalimbali ya kiujambazi,basi akajikuta anampata Ramso huko nchini Afrika kusini,huko Ramso ndiko aliweka makazi yake kwa miaka mingi iliyopita.Mzee Kibangara akapumua kwa nguvu na kumtazama Ramso.

“Ok worry out(sawa ondoa shaka)” alisema Mzee Kibangara kisha akamgeukia Zulfa.

“Ehee na wewe ombi lako” Mzee huyu aliyeanza kujawa na hasira alisema.

“Mimi nahitaji pesa zangu tu,kwa sababu kazi yangu nimemaliza” alisema Zulfa kwa kujiamini.Mzee Kibangara akacheka kidogo na kumtazama tena Zulfa kisha Peter na kumalizia na Ramso.

“Ina maana mnataka kuniambia kuwa wote mnataka kuvunja mikataba yetu?” aliuliza mzee huyo huku mate yanamtoka kwa hasira.



“Mzee mimi siwezi kuendelea na kazi yako,kazi gani haina usalama” alisema Ramso kwa kujiamini,akaendelea kusema “Kule madiba mambo ya kukamatwa na hawa maaskari wenu hakuna” alimaliza Ramso na kukaa kimya.

“Konzo” Mzee kibangara aliita na baada ya sekunde chake aliingia kijana mnene aliyepanda juu huku amevalia nguo zilizombana na kuonesha kifua chake jinsi kilivyoshibiana kwa mazoezi anayoyafanya.

“Niletee brifikesi” Kijana yule akatoka na kurudi na brifikesi mkononi.Akaiweka mezani na kusimama pembeni.

“Fungua” alisema Mzee kibangara.Baada ya kufungua,ndani ya brifikesi ile mlikuwa na pesa nyivgi zilizopangwa vizuri.Ramso na wenzake wakatazamana kisha wakarudisha macho kwenye brifikesi.

“Mko huru kuchukua hizo pesa na kuondoka” alisema Mzee Kibangara huku amekunja sura kwa hasira.Ramso aliinuka kwenye kiti na kuchukua lile brifikesi kisha akawakonyeza wenzake waondoke.Kama walivyopanga wakatoka nje ya jumba hilo na kutoka zao nje.



“Nataka nione vichwa vyao wale wote” Mzee kibangara aliamrisha watu wake waliobaki mle ndani,kwa kasi vijana hao wakaingia kwenye gari huku kila mmoja akiwa na silaha inayomfaa………………………..



Baada ya Ramso,Zulfa na Peter kutoka nje,wakapanda taksi mpaka kwenye hoteli ambapo waligawana pesa pasu kwa pasu kisha kila mmoja akaficha mahali anapopajua kabla hawajaondoka.Wa kwanza kutoka nje ya chumba hicho alikuwa Peter ambaye pesa zake aliziweka kwenye mfuko wa ndani wa bukta yake.Wakati anatoka nje ghafla alikutana na tundu la bastola kwenye kichwa chake.

“Shiiiiiiii” alizimishwa na jamaa hao wapatao watatu na kila mmoja alikuwa na bastola yake.Wawili kati yao wakazama ndani ambamo kulikuwa na Ramso pamoja na Zulfa.Mlio wa risasi ukasikika kutoka nje ya chumba hicho na kuwafanya wawili hao kurudi nje kwa kasi na kumkuta mwenzao anavuja damu kichwani mara baada ya kufumuliwa risasi na Peter.Kwa mbali walimuona Peter anakimbia kwa kasi ya ajabu.Hakufika mbali Peter akadondoka na kutulia tuli huku damu zinamvuja mithili ya juisi.Wafuasi hawa wa Mzee kibangara hawakuwa peke yao bali kulikuwa na wafuasi wengine ambao walikuwa nje ya gari katika hoteli hiyo,ndipo mmoja wapo ambaye anaaminika sana katika utaalamu wa kudungua akamfyatulia risasi Peter na kumpoteza maisha yake.Ramso na Zulfa walijibanza sehemu waliojificha bila kutingishika.Ramso aliyekuwa ameishika bastola yake kwa umakini alijitoa ile sehemu aliyokuwa amejificha na kumuacha Zulfa.Alianza kunyata kuelekea mlango wa chumba ila kabla hajaufikia aliingia mfuasi mmoja akiwa na bastola huku akiwa ameielekeza mbele.Kitendo cha haraka kama umeme Ramso aliruka tiktaka na kuupiga mkono ulishikilia bastola ya jamaa huyo na kuiputa pembeni.Hapo ndipo alipata nafasi ya kumuwasha risasi mbili za kichwani kisha mfuasi huyo alipoaga dunia.Ile anatoka nje ya mlango tu akiwa na bastola yake ameielekeza mbele kwa mikono miwili akakutana uso kwa uso na polisi walioshika SMG mashine,ndipo akawekwa chini ya ulinzi,pingu zikafuatia na kupelekwa kwenye gari.Zulfa alibaki sehemu ileile aliyokuwa kajificha na Ramso huku akisikiliza kila kitu kinachoendelea nje ya chumba hicho.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

***

Mzee kibangara akiwa na hasira kali huku akijipoza na pombe kali aina ya wiski,alifungulia TV yake huku pembeni yake kukiwa na wasichana wawili waliokuwa wamevalia bikini na sidilia waliendelea kumshikashika mzee huyo mafia ambaye ana mtandano mrefu wa kigaidi.Wakati anaendelea kutazama taarifa mbalimbali kupitia ITV mara wakasitsha na kuweka habari za punde(Breaking News).Aliwashuhudia wafuasi wake wawili wamepigwa risasi na wawili wamejeruhiwa na wapo chini ya mikono ya polisi.Hapo hapo wakamuonesha Ramso ambaye nae alihusika katika tukio hilo.

“Fu*k” Mzee Kibangara alijikuta anatukana na kuitupa glasi aliyokuwa anaitumia kunywea wiski kisha ikavunjika kaa!,kitendo kile kiliwashtua baadhi ya walinzi waliokuwa karibu na yeye,hapohapo wakajiweka vizuri kukabiliana na kitu chochote mabcho kilikuwa kimemshtua bosi wako.

“Vipi dear” msichana mmoja alimuuliza Mzee Kibangara huku akiwa amesikamama mbele yake na kumzuia asione kinachoendelea kwenye TV.Alichokifanya Mzee Kibangara ni kuchukua sigara yake ilikuwa imekolea vizuri moto na kumchoma nayo shavuni msichana hyuo mpaka ikazimika.Msichana huyo alitoa kelele kali ya maumivu yaliyopitiliza kutokana na motot wa sigara ile.

“Nitokeeni hapa” Mzee kibangara alifoka na kuwafanya mabinti hao kukimbia kwa mwendo wa haraka mpaka chumbani kwao.Kilichofuata kichwani mwa Mzee huyo ambaye ni katili kupita kiasi,alichukua begi yake na kujaza nguo na bila kusahau bastola yake iliyonakishiwa kwa vipande vya dhahabu.Akaiweka na bastola nyingine kiunoni mwake kisha akatoka nje ya chumba.

“Neshaz” aliita mfuasi wake mmoja.

“Nasafiri leo naenda nchini Somalia,ila hakikisha unasimamia suala zima la ulinzi wa hii himaya yangu”.

“Sawa bosi hakuna kitu kitakachoharibika” alisema Neshaz kwa ukakamavu,mzee kibangara aliogopeka sana hata kwa wafuasi wake kwani haoni hasara yoyote ya kumtoa roho mtu ndani ya sekunde tano tu.Baada ya kuacha maagizo kwa watu wake muhimu aliingia ndani ya gari lenye thamani sana ambalo liliendesha na mfuasi wake kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere.Gari hiyo ambayo ilikuwa ya kisasa iliaanza kupanda juu kwa kutumia lifti maalumu na baada ya kufika kwenye sehemu iliyo wazi ndani ya jengo hilo ikaanza kutembea taratibu hatimaye ikafika kwenye geti kuu lililolindwa na walinzi wenye siraha kali.Geti hilo lilifunguliwa kwa namba za siri kisha gari likaondoka na kuuacha mjengo huo uliokuwa umejengwa chini ya ardhi kitaalamu zaidi.

Hatimaye walifika airport na kukuta ndege moja ambayo ilitakiwa iondoke kuelekea kenya,hakukuwa na ndege ya somalia wakati,Mzee kibangara alifanyiwa utaratibu wa tiketi na kwa bahati mzuri alifanikiwa kuipata,mpaka anakuja kusafiri alipumua kidogo na kutoa sigara yake kisha akaiwasha.

“Heii hauruhusiwi kuvuta ndani ya ndege,tazama hilo tangazo hapo” alikuwa mhudumu aliyekuwa anamkanya Mzee kibangara asivute sigara.Alipotazama pembeni kweli akakutana na kijibango kilichoandikwa ‘NO SMOKING’.Mzee Kibangara akamtazama mhudumu yule kisha akazima sigara ya na kuiweka mfukoni,ndege iliendelea kupasua anga kuelekea nchini Kenya.

****

Mji mzima watu wake walizungumzia juu ya kuuawa kwa majambazi ambao wanasadikika kuwa walivamia hoteli na kuanza kuua watu.Ramso alikuwa mmoja wa majambazi hao ambao walifumwa hotelini hapo,chini ya ulinzi mkali huku utaratibu wa uchunguzi unaendelea.Baada ya dakika chache aliingia askari mmoja aliyevalia sare zake huku akiwa na asakri mwenzake wa kike.Ramso ambaye alipigwa pingu kwa nyuma na mfuasi mmoja wa kibangara,waliinua vichwa vyao na kuwatazama wale askari.Polisi huyo wa kike akamchukua kiti na kumkarisha Ramso ambaye bado yupo katika pingu.

“Unaweza kuniambia unaitwa nani?” aliuliza Polisi huyo huku ameshika kalama na karatasi.Ramso alibaki kimya bila kuongea chochote,mara akashtukizwa na ngumi ya shavu iliyorushwa na askari yule wa kiume.

“Taja jinaaa” alifoka askari huyo.Haikuwa rahisi kwa Ramso kutaja taarifa zake zaidi ya kukaa kimya huku akiwatazama polisi kama wamejinyea.Hapohapo wakaanza kumshushia kipigo kwa mfulilizo na baada ya kuhakikisha kapata kipigo cha kutosha wakamtoa na kumuweka mwingine.Huyu naye pia alikuwa kama Ramso,alikataa kutaja kabisa kumtajia taarifa zake.Kama kawaida ya polisi hawa,wakaanza kutoa kipigo cha paka mwizi,damu nyingi toka kwenye milango ya fahamu zilimwagika na kumfanya jamaa huyo kuzimia.Wakatoka nje huku wakiwaacha wawili hao wakika katika hali mbaya hasa yule mfuasi wa Mzee kibangara.Kutokana na kipigo kikali walichotembezewa,hatimaye Ramso akajikuta amelala kwenye chumba hicho kidogo kilichojaa giza totoro.Wakiwa katika hali ya usingizi wote wawili Ramso na mwenzake walishtuka mara baada ya kusikia mlango wa geti wa chumba hicho unafunguliwa.Askari mmoja aliingia na tochi huyu mkononi akiwa na bunduki.Ramso alipong’amua macho vizuri akafyatuka kwa kasi na kumpiga mtama polisi yule uliomfikisha mpaka chini.Hajatulia vizuri akapiga kichwa cha puani huku Ramso akiwa na pingu vilevile.Ni mavunzo yaliyopea kabisa ambayo aliyapata.

“Fungua pingu boya weweeee” alifoka kwa sauti ya chini na kumfanya polisi huyo kuzama mfukoni na kuchomoa kijifunguo cha pingu.Baada ya kufunguliwa Ramso alichukua pingu hizo na kumfunga polisi huyo kwenye geti.Akaichukua bunduki ya askari yule na kutoka nje haraka.Akaanza kunyata kutafuta sehemu ya kutokea huku kaishika bunduki ile kwa umakini.Ghafla akasikia sauti ya polisi yule aliyemfungia getini anapiga yowe.Akaanza kukimbia kuelekea getini,ila kabla hajafika akajikuta anaanguka chini baada ya kupigwa risasi ya bega na polisi mwingine aliyekuwa lindo usiku huo.

“Ayaaaaaa!” Ramso alitoa sauti ya maumivu huku akiitupa bunduki na mwenyewe kudondokea pembeni.Damu zilianza kuvuja na kulowanisha mwili wake.Kilichofuata hapo ni kurudishwa rumande na kufunguliwa kesi ya pili ambayo ni ya kutaka kupora bunduki ya polisi.Ramso alijisogeza pembeni kwenye kijichaka cha maua na kuketi kimya.Maumivu ya bega yalianza kumsumbua Ramso,akachana kipande cha nguo yake na kujishindia mdomoni huku akiking’ata kwa nguvu ili mradi azuie maumivu kwa kiasi fulani.Polisi huyo ambaye alikuwa kashikilia shortGun alifika kwenye eneo lile na kushangaa kutomkuta Ramso.Akachukua tochi na kuanza kumulika vichakani kama atabahatika kumuona.Wakati huo wote polisi aliyekuwa anapiga yowee alikuwa anapewa kisago na mfuasi huyo wa Kibangara.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Leta funguo ya pingu” alifoka mfuasi huyo.

“Sinaaa” aliongea huku akilia kama mtoto mdogo.Bunduki yake alidhani ndio basi imechukuliwa kwani ni kosa kubwa sana kwa polisi kupoteza bunduki.Alilia kwa mengi sana,maumivu ya kipigo alichokipata,kuporwa kwa bunduki yake na kumtorosha mtuhumiwa na mengine.Askari ambaye alimtandika Ramso risasi,baada ya kumulikamulika tochi huku na kule mara akamwona Ramso akiwa amejibanza kwenye kichaka cha pembeni huku akitweta kwa maumivu makali ya jeraha la risasi.Hapohapo polisi huyu aliikoki bunduki yake na kumuamrisha Ramso atoke mwenyewe pale alipo……….



Ramso alitazama pembeni yake na kuliona jiwe kubwa kiasi na kwa kasi akamrushia polisi yule lililompata kichwani,alianguka chini huku akitoa yowe la maumivu kutokana na kutobolewa na jiwe hilo.Ramso aliinuka haraka na kukimbia huku akimuacha polisi huyo analia.Jopo la maaskari liliongezeka kituoni hapo mara baada ya kupewa taarifa ya kutoroka kwa jambazi mmoja.Kila kona ya sehemu ya kituo hicho kulikuwa na ulinzi mkali huku wakijaribu kutazama kama jambazi huyo atakuwepo.Waliamini kuwa risasi aliyopigwa haitamfisha mbali kabla ya kuaga dunia.

****

Zulfa baada ya kutoka kwenye chumba cha hotelini ambako alijificha na Ramso kabla ya kukamatwa kwake,akatoka na kupanda taksi iliyomfikisha mpaka maeneo ya buguruni kwa rafiki yake Jamila.Alipofika bahati mzuri alimkuta yupo anaandaa chakula cha usiku ule.

“Hee jamani best vipi mbona uko juu juu namna hiyo?” aliuliza Jamila

“Mmmmh best niache kwanza nipumzike nitakuadithia vizuri baadae”

“Mmmh sawa mwaya ila kitambo sijakuona?”

“Nitakuambia bana Jamila mbona unakuwa na haraka namna hiyo” alisema Zulfa huku akizotoa nguo zake na kujifunga tenge kifuani.Akachukua ndoo na kutoka nayo uani ambapo akajimwagia maji kisha akarudi zake chumbani humo.Mara siku yake ikaanza kuita alipotazama aliona namba ngeni lakini kabla hajaipokea simu ikazima chaji.

“Mwaya simu yako iko wapi?” aliuliza Zulfa

“Hiyo hapo juu ya kabati”

Zulfa akaichukua simu na kuitoa laini kisha akaweka laini yake.Akabofya ile namba ambayo ilikuwa imepiga muda mfupi kabla simu yake haijazima chaji.Baada ya kuita kwa sekunde tano ikapokelewa na sauti ya kike toka upande wa pili ikasikika.

“Wewe ni Zulfa sio?” aliuliza mwanamke huyo kwa sauti ya chini.

“Ndio nani mwenzangu?”

“Naitwa Layla,kuna mtu hapa anakuulizia amepigwa risasi begani,kasema nikupigie hali yake mbaya sana”

“Kakuambia anaitwa nani?”

“Hawezi kabisa kuongea yaani,fanya uje nipo mtaa wa Tazara” mwanamke huyo alitoa maelekezo kwa Zulfa.Harakaharaka Zulfa akavaa nguo zake na kumuaga Jamila kisha akatoka mpaka kwenye kituo cha taksi.Ndani ya dakika kumi na tano Zulfa alikuwa amefika tayari kwenye nyumba hiyo ambayo ilikuwa na vyumba viwili.Zulfa akajikuta anaishiwa nguvu mara baada ya kumuona Ramso amelala kitandani akiwa anahema kwa shida sana,bega lake lilikuwa limefungwa bandeji baada ya kupigwa risasi na polisi.

****

Ramso alimrudhia jiwe na kumpiga nalo polisi ambaye alimpiga risasi ya bega.Akakimbia kwa kasi huku mkono wake mmoja ameshikilia bega ambalo lilikuwa linavuja damu nyingi.Kwa bahati mzuri akakutana na taksi bubu.Ramso akalipungia mkono na gari hiyo ikasimama na Ramso akajitupa ndani ya gari hilo.

“Vipi ndugu yangu mbona umeumia namna hiyo?” dereva huyo aliuliza

“Braza nipeleke Tazara haraka” Ramso alisema kwa shida huku akihema kama mtu anayetaka kukata roho.Gari hiyo ikatia moto na kupasua ardhi kuelekea Tazara ambako alisema Ramso.

“Nishushe hapo hapo” Ramso alisema huku machozi yanamtoka.Baada ya gari kusimama Ramso akashuka na kukimbia huku anapepesuka.

“Sasa broo pesa iko wapi?” aliuliza dereva lakini Ramso hakujibu kitu chochote.Dereva huyu alijua kuwa Ramso amezidiwa na hakutaka kabisa kumsumbua.Akasukuma mlango na kuingia ndani ambapo akamkuta mwanamke anapika.Hakuwa anajua yupo wapi kwani alijikuta anasukuma mlango huo huku akilia kwa maumivu makali.

“Dada nisaidie tafadhali nakufa” alilia Ramso kwa uchungu.

“Wee nani?” aliuliza

“Ra…m..so” alisema kwa shida

“Unatoka wapi?” mwanamke huyo ambaye alianza kuingiwa na wasiwasi alianza kumuuliza maswali mfululizo.

“Dada nitakuambia naomba unisaidie” Ramso aliomba msaada wa hali na mali.Kweli bahati ya Ramso iko njema mara baada ya kuomba msaada kwa mwanamke huyo alifanikiwa kuupata,na kumbe alikuwa nesi.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Eeeh umepigwa risasi?” aliuliza kwa mshtuko mara baada ya kukifunua kidonda cha Ramso.

“Nd…io da…ada nakufa mimi ooh” Ramso alilalamika mno.Akachukua mto na kuubana mdomoni kwa nguvu huku akisikilizia maumivu ya kidonda.Mwanamke huyo alichukua sindano na kufyoza dawa iliyokuwa kwenye kichupa kidogo na kumchoma nayo Ramso.Baada ya dakika tano Ramso alitulia tulii huku jasho jingi linamvuja mwilini.Nesi huyo aliendelea na huduma na sasa alichukua mkasi na kisu kidogo cha oparesheni.Akachukua sindano ingine na kumchoma nayo tena kisha Ramso akalala usingizi mzito.Akaanza kumtengeneza kidonda huku Ramso akiwa hajitambui kabisa.Akafanikiwa kukitoa kipande cha risasi na kumfungia bandeji begani.Ndipo baada ya masaa mawili mbili Ramso alishtuka na kitu cha kwanza ni kupapasa bega lake.Akashangaa kuoga bega lake gumu.Alipogeuka akakutana na sura ya mwanamke aliyemsaidia.Alipotaka kujaribu kuinuka mwanamke akamtuliza.

“Usijitingishe utauumiza mkono wako,endelea kulala tu”

“Nani kanifunga hii bandeji?” aliuliza

“Ni mimi”

“Sawa umetoa risasi?”

“Ndio nimeitoa kwani ilikuwaje?”

“Nilivamiwa na majambazi” Ramso alidanganya alijua kuwa akisema ukweli anaweza kusababisha matatizo mengine.

“Naomba umpigie simu rafiki yangu” alisema Ramso na kumfanya mwanamke huyo kuchomoa simu na kumpatia.Alibonyeza namba anazozijua na kumpa mwanamke huyo aongee nae kwani yeye alihisi kichwa kinamuuma.Hapo ndipo Zulfa alipigiwa simu na kujua mpaka kwenye nyumba hiyo ambapo alimkuta Ramso amelala kitandani huku bega lake likiwa na bandeji.



“Ra..mso nini tena?” aliuliza Zulfa kwa hofu huku akimshika kichwa Ramso na machozi yakaanza kumlengalenga.

“Kichwa Zu..lfa” alilalamika Ramso huku akijishika kichwa kwa nguvu.

”Pole basi,da..da nisaidie panado kama zipo” aliomba zulfa na kumfanya mwanamke huyo kufungua kabati na kutoa kijifuko kidogo.Ramso akameza dawa na kutulia.Haikuingia muda mrefu mara wakasikia mlango unagongwa nje.Aliyekwenda kufungua ni mama mwenyewe wa nyumba ile na kukutana macho kwa macho na tundu la bunduki.Waliokuwa mbele ya mwanamke huyu msamalia mwema kwa Ramso ni polisi waliovalia ngwanda zao.

“Shiiiiii” polisi mmoja alimnyamazisha mama huyo na kumuweka chini ya ulinzi.Polisi hao wakafungua chumba cha kwanza na kukuta pa tupu na wakaendelea na cha pili,hapo wakakutana na msichana Zulfa ambaye alikuwa amejilaza kitandani akiwa hana habari nao.Alifanya hivyo ili kuficha uwepo wa Ramso mle ndani kwani kuwa na wasiwasi kwake kunaweza kuwafanya polisi hao kugundua kitu fulani.

****

Dereva ambaye alikuwa amembeba Ramso ambaye alikuwa kajeruhiwa vibaya kwa risasi.Baada ya kumshusha njiani Ramso kabla ya kumfikisha Tazara,alichomoka na gari yake mpaka kwenye baa ambapo hapo aliagiza bia zake kadhaa na kuanza kuzinywa.wakati anaendelea kunywa,mara akaingia msichana aliyevalia kigauni kifupi na kumuacha mapaja yake meupe kuonekana kwa uwazi kabisa.

“Habari kaka,samahani naweza kukaa?” aliuliza msichana huyo.

“Aaah hehe bila samahani kabisa” alijikanyaga kanyaga kujibu huku akitazama mapaja ya msichana huyo aliyekuwa ameumbika vya kutosha.Kabla hawajavunja ukimya wao mara TV iliyokuwepo kwenye baa ile ikatoa tangazo lililoambatanishwa na picha ya Ramso.

‘JAMBAZI SUGU ASIYEFAHAMIKA KWA JINA ANATAFUTWA BAADA YA KUTOROKA NA KUJERUHI POLISI,KWA YOYOTE ATAKAYEPATA KUMKAMATA AU KUTOA SEHEMU ALIPO ZAWADI NONO ITATOLEWA KWAKE’.Dereva huyo baada ya kuiona sura hiyo,kumbukumbu zikamjia na kugundukua kuwa alikuwa amembeba jambazi huyo muda mfupi uliopita.

“Eeeeh” alistuka dereva huko na kushtua kidogo msichana yule ambaye alikuwa ameleta bia na kuanza kunywa.

“Vipi kaka?” aliuliza msichana huyo.

“Yule unaemuona kwenye TV nimetoka kumuacha hapo njiani kumbe ni jambazi?” alishangaa sana.Lakini kwa upande mwingine alihisi kama zari kwake kwani anakujua fika sehemu ambayo alimuacha jambazi huyo.Haraka sana akachukua simu yake na kuziandika namba za polisi kisha akawarukia hewani.

“Haloo,,eeeh ndio mimi ni raia mwema,nasema kuwa jambazi ambae amejerui polisi ninapajua sehemu ambayo anapatika”

“Ndio nina uhakika sana” aliendelea kutoa ufafanuzi kwa polisi hao “nipo hapa buguruni”.

“Sawa ila zawadi yangu msiisahau wazee” alikazia na zawadi bila ya kazi kuanza.Kitendo cha dakika kumi gari ya polisi(Defender) ilifunga breki nje ya baa hiyo na kufanya baadhi ya wateja kuanza kukimbiakimbia.Hawakujua kuwa dhamira yao haikuwa hiyo bali ni kuja kumchukua mtu ambaye anadai kuwa anapajua mahali alipo jambazi anayetafutwa.Baada ya kumpata raia huyo alipanda kwenye gari yake na kuelekea njia ya Tazara huku gari ya polisi ikifata nyuma.Kikosi hicho cha polisi kilitua sehemu ya tukio na baada ya kuoneshwa nyumba husika,wakaanza kuinyatia kwa umakini huku kila mmoja akiwa ameshika silaha yake.Walipofika mlangoni waligonga na mwanamke alifungua mlango huku kisha wakamuweka chini ya ulinzi huku wengine wakizama ndani kutazama kama kuna mtuhumiwa huyo ambaye anadadikika kuwa ni jambazi sugu aliyetoroka kituoni.Walipohakikisha kuwa hakuna mtu yeyote ambaye walikuwa wanamtafuta wakarudi na kumtazama yule dereva kwa macho ya hasira.

“Umeamua kuunguzia mafuta yetu sio?”

“Aaaah sasa kwa sababu gani ndugu Afande?”.

“Afande huyo itakuwa anahusika nae,tumkamate akatoe maelezo kituoni” Askari mmoja alishauri.Haikuwa na mjadala walimkamata na kumtia ndani ya difenda huku akilalamika njia mzima.Kilichomponza ni tamaa ya pesa bila kufanya utafiti wa kina kuwa kile anachokifanya kiko sahihi kwa kiasi gani.

“Maafande unavyotumia sio kabisa eeh,mimi niliwaonesha sehemu tena kiroho safi tu lakini bado mnanikamata mimi………….” Alilalamika mno lakini hakun hata polisi aliyekuwa na muda wa kumsikiliza jamaa huyo,kwani ameonesha usumbufu wa hali ya juu kwa jeshi la polisi na ni lazima wamtoze faini na kutoa maelezo juu ya tukio hilo.

****



****

Ramso alitoka sehemu aliyokuwa amejificha na kuketi juu ya kitanda huku mwili wake unatokwa jasho kwa wingi.Hakuwa na raha tena ya kukaa katika kile chumba,kitu alichokiona sahihi ni kuaga mwenyewe wake na kumpatia pesa kwa shukruani kisha akapanda gari akiwa Zulfa mpaka kwa rafiki yake Zulfa Jamila.Walipofika walikaribishwa vizuri na kupewa chakula.Walipomaliza kula wakatulia kidogo huku wakipanga mambo kadhaa juu ya mustakhabari wa hatima ya maisha yao.

“Nafikiri mji umechafuka Zulfa,mimi nitakuwa natafutwa kila kona,ila nakuomba ufanye kitu kimoja” Ramso alisema

“Kitu gani hicho?”

“Kesho utaenda kuninunulia wigi la nywele bandia na ndevu,ninunulie na pama la kofia” Ramso alimpatia maelekezo Zulfa ya kununua vifaa vyote vitamuwezesha asifahamike endapo pale atakaposafiri kuelekea nchini Afrika Kusini.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Lakini na mimi natafutwa unatambua hilo?” aliuliza

“Hawawezi kukusumbua,basi utavaa baibua litakalokufunika uso mzima” alisema Ramso na Zulfa akakubali.Kesho yake mapema sana Zulfa alidamka mpaka MLIMANI CITY ambapo alinunua vifaa vyote kama alivyoagizwa.Mwili wake ulikuwa umefunikwa na baibui jeusi,ikawa sio rahisi hata kidogo kwa mtu yoyote kumgundua.Mipango ya safari ya Ramso iliendelea kuimalika mara baada ya kupasa visa na tiketi ya ndege iendayo nchini Afrika Kusini.Pesa ambazo walizipata kwa Mzee Kibangara na Ramso kumpatia Zulfa kule hotelini kabla ya kukamatwa kwake,waligawana kisha kila mmoja akatumbukiza sehemu anayaofahamu.Ramso pamoja na Zulfa walipanda gari mpaka uwanja wa ndege ambapo ndege inayotarajiwa kuondoka usiku huo.Mwonekano wa Ramso haukuwa tofauti na babu wenye miaka themanini kwani alikuwa na ndevu bandia zilizochafua kidevu chake,nywele zilijaa mvi ndio zilimuonesha dhahiri kuwa ni babu aliyepea.Ukaguaji ulipokamilika Ramso alimuaga Zulfa kwa kukumbatiana kwa sekunde zaidi ya kumi,Zulfa alilia sana kuagana na Ramso kwani alikwisha mzoea sana.Ramso alimshika Zulfa mashavuni na kumfuta machozi huku akimbembeleza asilie.

“Zulfa usilie nitarudi mwaka wowote,milima haikutani binadamu ukutana Zulfa” baada ya kumliwaza kwa maneno mazuri na yenye matumaini Ramso aliingia kwenye ndege na kuketi kwenye siti yake.Muda wote kabla ya ndege kupaa angani alikuwa anamtazama Zulfa kupitia dirishani huku kwa mbali machozi yakimlenga.Alikuja kushtushwa na sauti ya mhuduma ya kufunga mkanda,ndipo akajizungushia mkanda huo na kutulia tulii.Ndege ikaanza kutembea kwa kasi na kuanza kupaa angani hatimaye ikaacha ardhi ya Tanzania.

Anga mzima ilikuwa imetulia usiku ule na kuifanya ndege hiyo ya kisasa ivume vizuri na kukata mawingi bila wasiwasi.

“Wote vichwa chini,vichwa chiiiniiii” ilikuwa sauti ya mtu mmoja ambaye alikuwa ameshika bastola na bomu la mkono.Usoni alikuwa amezuiwa na maski nyeusi kitu ambacho kilimfanya asifahamike kwa haraka.Watu wote waliokuwa wametulia wakaanza kupiga kelele na kuinamisha vichwa vyao chini kwa woga.Ramso ambaye bado bega lake halijatengamaa aliinamisha kichwa chini huku anamtazama kwa kuibia jamaa huyo ambaye alikuwa anataka kuiteka ndege.Mara wakaiuka wengine kutoka nyuma kabisa ya ndege huku na wao wakiwa na bunduki aina ya SMG na usoni wakiwa na maski nyeusi.Ramso alijaribu kutazama kwa umakini akaona chapa moja kwenye tisheti ya watekaji hao,ndipo alipobaini kuwa chapa hiyo ilikuwa ni ya kampuni ya kijasusi ya Mzee Kibangara na wale watekaji ni wafuasi wakubwa wa Mzee huyo ambaye ana mipango mikumbwa ya kuiangamiza serikali teule ya Tanzania kiuchumi na kusababisha machafuko ya kisiasa.Ramso alipiga mahesabu ya haraka haraka na kugundua kuwa alikuwa na bastola ambayo aliiweka kwnenye kiuno chake.Akaichomoa na kuiseti bila watekaji hao kujua.Mmoja wao akapitiliza mpaka kwenye chumba cha marubani.Wale waliobakia wakaanza kuwasachi watu na kila aliyekuwa na silaha alitolewa nayo.Ni zaidi ya watu kumi ambao walikuwa na silaha walitolewa na kubaki hawana jinsi,msako huo uliendelea na hatimaye wakafika kwa Ramso.

“Weee mzee,hetu inuka” alisema mtekaji mmoja na kumfanya Ramso ajiseti vizuri kwa mashambulizi.Ghalfa kama umeme Ramso alijipingua na kulala cha kwenye sakafu na kuanza kuwamiminia risasi watekaji hao ambao walikuwa na nia mbaya na ndege hiyo.Mchezo ulifanyika ndani ya sekunde kadhaa na kuwafanya watu waliokuwa mle ndani kushikwa na mshangao kumuona mzee kama yule ambaye alikuwa na ndevu nyingi na nywele za mvi anawezaje kuwateketeza watekaji ambao walishika silaha mzito.

Pulukushani kati ya marubani na mteka nyala mmoja ambaye aliingia kwenye chuma hicho iliendelea huku jamaa huyo ambaye alikutaka kuwacontro marubani hao.Mara jamaa huyu alifyatua risasi na kumpita rubani msaidizi shingoni na hapo ndipo ndege hiyo ikaanza kuyumba na kukosa muelekea kutokana na kukosa wa kuiongoza kwani yule aliyetakiwa kuiongoza alipigwa risasi na kubakia rubani mkuu naye ambaye aliendeleza kurukashani hizo kwa hiyo hakuwa na muda wa kutazama muelekeo wa ndege.Abiria wakaanza kukimbizana huku na huko mara baada ya Ramso kuwapiga risasi kwa kasi ya umeme,mmoja wao ambaye alishika mabomu ya mkono alianguka chini na kuyafanya maboya hayo kusambaa uvunguni kwa siti za abiria,punde si punde bomu moja likategeka pini na kulibuka.Kitendo ambacho kilisababisha upande mmoja wa dirisha la ndege hizo kupasuka na kuwa na uwazi tupu .Mpepo mkali ulikuwa unavuma ulianza kupeperusha mizigo na abiria ambao walikuwa karibu na dirisha hilo walipeperushwa nje kwa upepo ule.Hapo ndipo ndege ilipoanza kupoteza muelekeo sahihi.Ramso ambaye alikuwa anasukumwa na upepo kuelekea kwenye dirisha lililopasuka,alijifunga mkonda wake vizuri na kuking’ang’ania kiti alichokalia kwa nguvu zake zote.Ndege ikaanza kuvilingika na kuwafanya watu wagongane na wengine kujikuta wapo angani baada ya kupita kwenye lile dirisha.Kutokana na kuvunguka kwa ndege hiyo ikasababisha bomu lingine kuteguka pini na kulipuka tena nyuma ya ndege,hapo ndipo watu wengi walipoteza maisha yao baada ya kutupwa nje.Ndege ilishuka chini kwa kasi na kujikuta inadondokea baharini na kuzama yote.Mlipuko mkubwa ukatokea katika sehemu hiyo ya bahari na kusababisha moshi kutanda angani.

****

Mzee Kibangara alitua nchini Kenya na kufikia katika hekalu ambayo aliandaliwa na wafuasi wake.Hapo aliingia kwenye chumba maalumu chenye mawasiliano ya moja kwa moja kupitia intaneti yenye mtandao wa kigaidi.Akawasha kompyuta kubwa na kuiseti vizuri,mara akatokea mtu mwenye asili ya kiarabu akiwa amevaa kilemba cheupe huku kidevu chake kimechafuka ndevu za kutosha.Gwanda la kijeshi ambalo alikuwa amelivaa lilimuonesha dhahiri kuwa alikuwa mpiganaji mwenye ukatiri sana.Baada ya Mzee Kibangara kumaliza kuwasiliana na mzee huyo wa kiarabu,akafungua programu nyingine ambayo sasa ikawa inaonesha mjengo wake uliopo chini ya ardhi nchini Tanzania.Mara akatokea mtu mkoja na kuanza kuongea naye kupitia kompyuta hiyo.

“Mmekwishawakamata?” aliuliza Mzee Kibangara

“Hapana Bosi hatujawatia nguvuni” alijitetea mfuasi huyo ambaye alikuwa na wasiwasi mkubwa.

“Kwa nini?” Mzee kibangara aliuliza kwa ukali na kumfanya jamaa huyo kushindwa kujibu swali hilo zaidi ya sekunde tano mzima.

“Sasa nataka uwapeleke vijana kwenye uwanja wa ndege wa mwalimu Nyerere wakiwa na silaha” alieleza Mzee kibangara

“Ndio bosi”

“Kisha waingie kwenye ndege hiyo kinyemela na wakae kabisa kwenye buti la mizigo kabla haijaondoka,pia lazima wawe na parachuti pindi watakapolipua bomu katika ndege hiyo waruke na kuwaacha wafu waliomo ndani.Cha kuzingatia kuweni waangalifu na hakikisheni mna mabomu ya kutosha sawa?” Mzee Kibangara alieleza na kukata mawasiliano kutoka nchini Tanzania.

Baada ya kumaliza mawasiliano,alitoka kwenye hekalu hilo na kuingia kwenye ndege ndogo ilikuwa inamsubiri nje.Akapanda zake na safari ya kwenda somalia ikaanza.Majira ya kumi na mbili jioni,ndege hiyo ndogo iliyombeba tajiri wa magaidi ikatua kwenye sehemu ambayo inapori sana yaani katikati ya msitu uliopo nchini Somalia.Ikatua juu ya chuma lililozagaa kwenye ardhi hiyo na baada ya dakika mbili ndege hiyo ikatitia chini kupitia kwenye chuma hilo kisha likajifunga tena.

“Naam Asalam Aleykum” alitoa salama mwarabu ambaye aliongea nae muda mfupi uliopita kwenye intanent.

“Waleyko slamu,lete habari chifu”

“Alhamdulliah”

“Basi jambo la kheri Shekh” Wawili hawa walisalimia kwa lungha ya kiarabu kilichochanganywa na kiswahili.Wakaletewa mzinga mmoja wa pombe kali.Wakaanza kunywa huku wakipiga stori mbili tatu kwa furaha.Walipoona inawatosha wakainuka na kuingia kwenye chumba kikubwa ambacho kilikuwa na wataalamu wengine wa kompyta wakiendelea na kazi zao.Kila mmoja alikuwa bize kutekeleza majukumu aliyoachiwa.Mara kompyta moja ya mmoja wa wafuasi hao iliyopo upande wa kulia ikaanza kupiga king’ora na kuonesha taa nyekundu.Kilichokuwa kinaonekana ndani yake ni video iliyoonesha moshi mkubwa kwenye ukanda wa bahari wa Maputo nchini Mozambique.Ndege hiyo ambayo ilitoka Tanzania kuelekea Afrika Kusini,iliwabeba wafuasi wa mzee Kibangara waliotumwa kwenda kuiangamiza ndege hiyo.Mzee Kibangara alipoona tukio lile alikenua kinywa yake na kutabasamu.Akachukua kifaa kimoja kitumikacho kwa mawasiliano ya masafa ya mbali na kupiga simu.Ikapokelewa simu hiyo kutoka Tanzania.

“Yes bosi” simu iliitikia kutoka nchini humo.

“Tafuta rada ya watu uliowatuma kuilibua ndege,kuna ndege hapa nimeiona imedondoka kwenye mkondo wa bahari Maputo” Mzee alieleza.Kweli baada ya sekunde tano sita rada hiyo ikasoma na kuonesha kuwa kuna ndege imeanguka na imelipuka.Alipojaribu kupiga simu ya mfuasi aliyekuwa anasimamia mishine hiyo haikuweza kupatikana.Akajaribu na mfuasi mwingine,ila nae hakupatikana.Ikamlazima amuambie bosi wake kuwa watu hao hawapatikani,lakini kabla hajafanya hivyo kifaa chake kiliwaka taa nyekundu na maandishi mekundu yaliyosomeka kwa maandishi makubwa ‘MAPUTO ATTACKED’,akaipokea na kusikiliza.

“F 26 naongea ku…toka maputo nde….ge ime….angu…ka wote wamepoteza maisha nime…baki mimi mwenyewe naomba msa…da wako mkuu” sauti hiyo iliyokuwa inaongea kwa shida ikakata.Hapo jamaa huyo akampigia simu mkuu wake Mzee Kibangara na kumtaarifu juu ya taarifa hiyo.

“Shiiit” mzee Kibangara alifoka kwa jazba.

“Hebu shughulikia mwenyewe ”Mzee Kibangara alifoka na kukata simu.

Alichokifanya mfuasi huyu kwa kuwa alipotewa mamlaka ya kuongoza kundi la Tanzania ,akawaita watu wapatao sita na kuwapa kazi ya kumchukua mfuasi huyo aliye Maputo kwa maafa ya ndege.

“Ile rada ni ya muhimu sana hakikisha mnarudi nae au kama sio kurudi naye basi rada irudi hapa,kwani ndio siri zetu zinapatikana mule”

“Chukueni helkopta mbili muwahi haraka sana kabla eneo hilo hawajavamia polisi” Mfuasi huyo alisema na kuwafanya watu hao kuepa haraka na kuingia kwenye helkopta zao kisha wakapaa angapi kwa kasi ya ajabu kuelekea Maputo.

****

****

Wanajeshi wa maji wa nchini msumbiji walikwishapata kuona ajari ile na waliwasili huku wakiwa na maboti yao.Usiku huo bahari ilifuka moshi kutokana na ndege hiyo kulipuka.Wakakaa kando kabisa na sehemu ilipo ndege kwani kitendo cha wao kukaribia eneo hilo wanaweza kupoteza maisha yao.Upande wa kulia umbali kama mita kumi na tano kutoka kwenye ndege alikuwepo Ramso akiwa anajitoa parachuti yake mgongoni.Wigi lake lilikuwa limemtoka zilizobakia ni ndefu peke yake.Akatoka ndani ya maji huku amejishika bega lake alilopigwa risasi na kukaa ufukweni.Ghafla akashuhudia helkopta mbili zinampita kwa kasi na kuelekea sehemu ilipo ndege,mara zikawa zinasikika risasi kutoka kwenye ndege kwenda chini na chini kwenda juu,yalikuwa ni majibizano kati ya wanajeshi wa maji na wafuasi wa Mzee Kibangara ambao walitumwa kuja kuifuata rada ambayo ilishikiliwa na mfuasi mmoja aliyekuwa anaendesha misheni ya kuilipua ndege hiyo.

Kadri muda unavyozidi kwenda bahari ilizidi kuchafuka na hapo ndio helkopta moja ikadunguliwa na kombola lililorusha na wanajeshi hao.Helkopta moja iliyobaki iliendelea kujibu mashambulizi dhidi ya adui zao walio chini.Wakati wanajeshi wa maji wanaendelea kujibizana mara wakashtukia kombolo kutoka kwenye helkopta hiyo ambayo iliepa kiufungi na kuachia kombolo,likawasambalatisha moja kwa moja,hakukuwa na hata mwanamaji wowote yaliyebakia.Taratibu helkopta hiyo ikatua chini na wafuasi hao ambao walivalia nguo nyeusi zilizo na maski wakashuka na kuanza kumtafuta mwenzao ambaye alipewa rada muhimu katika kundi lao.Kutokana na kifaa walichokuwa nacho waliweza kumuona jamaa huyo yupo upande gani katika eneo lile.Sehemu alipo si mbali bali alikuwa ndani ya msitu mara baada ya kuona jeshi la majini linakaribia eneo ilipokuwa ndege.Wakaanza kumfuata huku wakiwa katika uangarifu wa hali ya juu.

Ramso baada ya kuona mashambulizi hayo akajikongoja na kukimbilia katikati ya msitu na asijue anaweza kutokea wapi.Hakika maisha ya Ramso yalikuwa kama ni kitendawili,alijuta sana kuja kufanya kazi ile Tanzania.Akaikubuka sana familia yake iliyopo nchi Afrika Kusini,alimkumbuka sana mke wake na mtoto wake Gadna.Alikuwa katikati ya msitu hakujua aende wapi usiku ule,akaamua kukaa chini ya mti mkubwa,maumivu ya bega yaanza kumsumbua,baridi iliyokuwa inatoka usawa wa bahari ikawa inamtesa mno.Mwili wote ukaanza kutetemea.Hakuwa na kiberiti,hakuna na hata chanzo chochote cha moto.Meno yake yakaendelea kuumana kutokana na kutetemeka kwake.Mara kwa mbali akaona mwanga wa taa nyekundu unawaka huku ukimfuata mahali alipo.

***

Bomu ambalo lilitengenezwa kwa ghalama kubwa,lilikuwa linasetiwa ndani ya hekalu iliyopo nchini Somalia katikati ya msitu ambako jumba hilo liko chini kabisa ya ardhi na sio rahisi kwa watu kuliona.Mzee kibangara wakishiriana na Mzee wa kiarabu ambaye ni mkuu wa waasi nchini Somalia walipanga bomu hilo kuteketeza mji wa Nairobi kenya.Utekaji wao na kulipua ni ndia ya kujipatia pesa zao na malengo makubwa ya kutawala Afrika mzima,ndio ndoto zao.Mipango ya kulipia karibia kila nchi wakianza na Tanzania baada ya kulipua ndege ya abiria sasa mpango unahamia kwenye mji huo wa Nairobi

“Hii inatembea kwa masafa marefu na kulipua zaidi ya kilometa saba mpaka nane” mfuasi mmoja alitoa maelekezo kwa Mzee kibangara na yule mwarabu mwenye sharafu.

“Hili linaruka zaidi ya kilometa kumi na tano,lilitaka kufanana na lile la wamarekani lililolipua mji wa Nagasaki na Heroshima” alieleza mfuasi huyu ambaye alikuwa ni mtaalamu wa mabomu mazito.

“Okay sasa hili tunahitaki likatengwe kwenye jengo la katikati ya Nairobi” alisema mwarabu mwenye sharafu.

“Remote control iko wapi?”

“Hii hapa” akatoa rimoti ndogo ya kuruhusu bomu hilo.Mzee Kibangara akachukua rimoti hiyo na kuiweka mfukoni.

Kama ilivyopangwa wafuasi wapatao tano walipakia bomu hilo kwenye sanduku lake na kulitumbukiza kwenye Helkopta yao.Wakapewa ramani na mtaalamu wao kishwa wakaingia ndani ya helkopta na kutoka nayo nje kutoka chini ya ardhi.Walipokaribia kufika nchini Kenya wakatelemsha helkopta mpakani na kuingia kwenye gari ambayo ilikuwa inawasubiri.Sasa wafuasi hao waliongezeka na kuwa saba.Wakawa wanapita barabarani ili kuingia nchini humo.Hawajafika mbali sana wakasimamishwa na trafiki.

“where your Visa?”(Visa zenu zenu ziko wapi?)

“Here(hizi)” kila mmoja akatoa Visa yake na kumuonesha trafiki huyo.Ila alipoonesha mmoja aliyebakia,trafiki huyo akajikuta anapiga saluti na kubana miguu kwa ukakamavu.Mfuasi huyo ambaye alikuwa ana kadi ya uafisa upelelezi alikuwa amevalia suti zilizomkaa vyema.Nae alikuwa kwenye kikosi hicho kinachokwenda kuangamiza mji wa Nairobi.Walifika nje kidogo ya jiji hilo kisha wakaingia ndani.Humo wakaitoa ramani ya jengo husika na kuanza kupeana majukumu mbalimbali.Walipohakikisha kuwa wamekamilisha kila kitu,kila mmoja akashika njia yake na kuondoka katika jumba lile.

Habari yako?” mfuasi ambaye alikuwa na kazi ya kulichunguza jengo hilo ambalo ni hoteli inayokaliwa na watu wenye pesa zao wakiwepo mawaziri pamoja na wageni toka nje.

“Salama kaka karibu”

“Nyumba vipo?” aliuliza jamaa huyo

“Yaah vipo karibu sana”.Alipomaliza kufanya muhamala wa kulipia chumba akapewa funguo na kuoneshwa chumba husika ambacho kinapatikana ghorofa namba kumi na tano.Aliingia chumbani na kitendo cha haraka akatoa kijifoni kidogo na kukiweka sikioni.Moja kwa moja akaweza kuwasiliana na wenzake kupitia kifaa hicho.

****

Inspekta Makurumla aliichukua familia yake na kusafiri nchini kenya,huko ndiko alikoweza kumpata mke wake huyo wakati anasoma chuo kilichopo mjini Nairobi.Kipindi hicho alikuwa anasomeshwa na mjomba wake mara baada ya Mama yake kuuawa kikatiri na Baba yake.Leo hii walikuwa wapo kwenye moja ya hoteli ambayo ilikuwa inatembelewa na mawaziri wakubwa pamoja na watu wenye hadhi ya juu.Baada ya kutoka kwa wazazi wa mke wake,wakaamua kuja kupata chakula cha mchana na jioni ili kesho yake warudi Dar es Salaam kwa ajiri ya kazi.Basi walipofika mapokezi wakamkuta binti ambaye alikuwa anaandikaandika vitu fulani.Alipomaliza akawahudumia Inspekta Makurumla na kuwapatia vyumba viwili.Watoto wao wawili wakapewa chumba chao huku Insepkta Makurumla akiwa na mke wake.Kutokana na uchovu mwingi akaingia moja kwa moja mpaka bafuni na kuanza kujimwagia maji.Akiwa katika hekaheka hizo akastaajabu kusikia sauti ya mtu kutoka upande wa pili wa chumba hicho ikitoa maelekezo juu ya sehemu ya kuliweka bomu hilo ndani yake.Haraka haraka akatoka akiwa na povu mwilini,kitendo kilichomfanya mke wake aliyekuwa amelala kitandani huku akibonyeza simu yake amshangae mme wake.

“Eeeh jamani vipi?” aliuliza mke wake.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Aaah hamna kitu mke wangu” Inspekta Makurumla aliamua kumficha mke wake ili kuondoa wasiwasi juu yake.

“Mmmmh makubwa haya” alistaajabu mke wake.Makurumla akarudi bafuni haraka na kuendelea kuoga.Baada ya kumaliza akavaa nguo zake kisha wote wakatoka na kwenda chini kupata chakula.Akiwa njiani mara akapigana kikumbo na watu wawili ambao walishikizana begi kubwa huku wanaongoza juu ghorofani.Inspekta makurumla alipata sana wasiwasi juu ya ujio wa wale watu wawili wenye asili ya kiarabu.Alichokifanya na kuwaacha watoto na mke wake kwenye meza ya chakula kisha akadai kuna kitu kasahau.Alipofika tu kwenye ngazi za kupandisha juu,akachomoa bastola yake ndogo na kuanza kwanyatia jamaa hao waliobeba bomu.Wakafika kwenye lifti,ndipo Makurumla akasita kwanza ili awape nafasi watu hao ya kupanda juu kisha na yeye akafuata.Ilikuwa jino kwa jino kati ya Inspekta Makurumla na kikundi kile cha waasi waliotumwa kutega bomu katika jengo hilo lililopo katikati kabisa ya jiji la Nairobi.Hakika bomu hilo lilikuwa na uwezo mkubwa sana,lina uwezo wa kusambalatisha jiji zima kwa dakika chache tu.Ndio ulikuwa mpango wa Mzee Kibangara na mzee wa kiarabu mwenye sharafu.Walipofika chumbani humo ambapo ndio walitaka kulitega wakafunga mlango na kuanza kushuguli za kulitega kwa umakini mno.

“Elekeza huku,kisha funga hiyo nati taratibu” alitoa maelekezo jamaa mmoja ambaye ni mtaalamu sana wa kutega mabomu ya aina hiyo.

“Nimekuambia funga taratibu boya wewee” alifoka mtalaamu huyu.

“Oya mimi sio boya sawa!”

“Wewe boya utakuniambia nini?” wakaanza kuzozana huku wakitambia vifua vyao vilivyojazia kutokana na mazoezi makali wanayoyafanya.

“Acheni ufala nyie,tufanye kazi iliyotuleta” alisema mkuu wa misheni hiyo ambaye alikuwa hana maneno mengi.Wakaachana na mzozo huo na kuendelea na kazi.

Inspekta Makurumla akasogea kwa uangalifu mpaka akaufikia mlango huo wa wafuasi waliobeba bomu hilo.Bahati mzuri waliufunga mlango kwa ndani lakini tundu la kupitishia funguo lilikuwa wazi kabisa.Mpenyo huo ulimuwezesha Inspekta Makurumla aone kila kitu kilichokuwa ndani.Mapigo ya moyo yakaanza kumuenda mbio mara baada ya kuliona bomu hilo lenye mfumo wa nyuklia likiwa kimewekwa chini sakafuni na watu hao wakiliseti kwa umakini.Jasho lililokuwa lina mtoka hakulihisi kabisa kwani hatari iliyokuwa mbele yake na wana wa Nairobi kwa ujumla sio hatari ndogo,ni kubwa mno tena ni kubwa kupita kiasi.

“Kumbe Kenya kumechafuka namna hii” alijisemea mwenyewe kimoyomoyo wakati anaendelea kulitazama tukio hilo.Wafuasi hawa wakamaliza kulitega vizuri na baada ya hapo wakatoa godoro na kuzichukua chaga zilisukwa kwa nongo nene.Wakalifunga bomu hilo kwa kutumia tengo kisha wakawasha kijiswichi kidogo ambacho kiliwasha kitaa chekundu mbele kabisa ya bomu hilo.Wakarudishia godoro hilo na kuanza kutoka nje ya chumba hicho.Inspekta alikimbia kwa kasi na kufyatua lifti iliyomfikisha mpaka chini.Mapigo ya moyo yalizidi kumuenda mbio,hata pale alipofika kwenye meza ya familia yake walimshangaa kwa nini anahema namna hiyo na kutokwa na jasho.

“Vipi kwani Baba Karimu?” aliuliza mke wake kwa shauku.

“Mke wangu we acha tu,fanya maliza tuondoke” alisema Inspekta Makurumla huku akiwa na hofu kubwa.Walipomaliza wakachukua mizigo iliyopo chumbani.Moja kwa moja Inspekta Makurumla alienda kulipoti kituo kikuu cha polisi jijini hapo huku akisisitiza kabisa kuwa ni hatari sana.

“Naitwa Inspekta Makurumla natokea Tanzania,nimefika nchini Kenya kwa mapumziko mafupi na kufikia kwenye hoteli ya TOWER ROYAL HOTEL,lakini nimekuta hali si shwari kabisa” alipumua kidogo.

“Hali si shwari unamaanisha nini mkuu?” alihoji Askari huyo mkuu aliyekuwa ameketi kwenye kiti cha kuzunguka.

“Nimeshuhudia kwa macho yangu,raia wenye asili ya kiarabu wanatega bomu kwenye hotel hiyo na ninavyosema sasa,wamekwisha maliza kazi yao” alisema,ndipo hapo askari yule aliposhtuka na kutoa macho kwa mshangao.

“Eeeh acha utani,kweeli?”

“Naongea namaanisha siwezi kusema uongo kwenye mambo kama haya”

“Hebu naomba naomba uje huku mkuu” alisema Askari huyo huku anatembea kuelekea chumba kingine,nyuma yake akiwa Inspekta Makurumla.Chumba walichoingia Inspekta Makurumla alikutana na mitambo mingi mno iliyokuwa inaendeshwa na watu mbalimbali ndani yake.Kompyta zipatazo ishirini na kila moja ilikuwa ina mtu zilikuwa zinafanya kazi yake ya kuratibu kazi za jeshi la polisi.

“Mkuu unamwingizaje mtu asiyehusika huku ndani?” alisema mmoja wa maaskari waliokuwepo ndani humo.

“Tulia kidogo.Heee naomba msikilize kutoka kwangu” aliwaamuru Askari wote na kuwafanya waache kazi zao.Walimshangaa sana Inspekta Makurumla ambaye alikuwepo katika chumba kile asichohusika.Baada ya wote kutulia akaanza kueleza kitu alichoambiwa na Inspekta Makurumla kutoka Tanzania.Wote wakajikuta wanaziba midomo yao na wengine kushika vichwa vyao.Hawajamaliza kuelezea mara TV iliyokuwa ndani humo ikazima ghafla na wote wakajikuta wanaitazama,baada ya sekunde tano ikawaka na sasa ikawa inamuonesha mtu mmoja ambaye alikuwa na gwanda za kijeshi akiwa ameziba uso wake mzima kwa kiremba na kitambaa chekundu,pembeni yake kukiwa na wafuasi wawili walioshika bunduki aina ya AK 47…………………..



“Ni lazima mtambue wakazi wote wa Nairobi kuwa,kuanzia sasa ninavyoongea mpo katika mikono yangu na nina uwezo wa kuteketeza jiji kwa sekunde mbili tu.Mnachotakiwa kufanya ni kitu rahisi tu,salini sala ya mwisho kabla hatujafytua kombolo hilo ambalo lipo katikati ya mji wenu.La sivyo tunamtaka raisi wenu aje kuwepa masharti ili kuepukana na hatari hiyo.Ndani ya dakika kumi na tano kama hajatokea nawafykelea mbali na hiki kidude” alionesha rimoti kontro mtu huyo ambaye alikuwa anatoa taarifa kutoka kwenye televisheni.Ghafla Tv ikazima na kuwaka tena kisha ikaendelea na vipindi vyake.Wakabaki wanatazamana tu hakuna mtu aliyeongeza zaidi ya dakika tatu.

****

Watu waliotazama habari hiyo na kuwaacha midomo wazi,mmoja wapo ni mheshimiwa raisi wa Kenya Noran Mkwakwacha ambaye alikuwa ofisini kwake anaendelea na kazi zake.Jasho jembamba likamtoka huku mwili mzima ukawa unamtetemeka kama aliyepilizwa na baridi kali.Akachukua simu ya mezani haraka na kumpigia simu mtu wake wa karibu.

“Hebu nipeleke makao makuu ya mawasiliano” alisema raisi Noran Mkwakwacha.Mpaka kwenye dakika tano alikuwa tayari amewasili kwenye kituo hicho.Hata wao walikuwa wameshikwa na butwaa kutokana na taarifa ile.Walipojaribu kulitafuta bomu hilo wakabaini kuwa lipo katika hotel ya TOWER ROYEL chini ya kitanda katika chumba namba 507,likiwa limesetiwa moja kwa moja.

“Niwashie niongee nao haraka sana” Mheshimiwa raisi alisema kwa hofu kbwa mno.Mtaalamu wa mawasiliano nchini humo alitafuta code za kituo hicho cha magaidi na kufanikiwa kuipata.Akawasha na kujiunganisha kabisa hewani.

“Njoo ukae hapa” alimwambia raisi na kitendo cha haraka,raisi akafanya hivyo kama alivyoambiwa.Baada ya sekunde akatokea mtu kwenye kioo cha komputa hiyo aliyekuwa kaziba sura yake kama awali.

“Ndi…o mimi ni rais wa Kenya tafa….dhalin jama…ni msi..lipue,nawasikiliza ninyi” alisema raisi kwa kigugumizi.

“Ni jambo dogo tu mheshimiwa,unachotakiwa kufanya ni kutuma dolla milioni ishirini tu bomu linatoka” aliongea jamaa huyo ambaye alikuwa ameziba sura yake.Raisi Noran alikaa kimya kwa sekunde kadhaa huku akifikilia kitu fulani.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Sawa nitajitahidi”

“Sio kujitahidi zimebakia dakika kumi tu,kama hujatuma naruhusu kombola lifyatuke” alifoka jamaa huyo.

“Sawa dakika mbili mkuu” alisema raisi huku akiwa anatokwa na jasho kwa wingi.

“Namba ya kutumia 565878479373,tunaendelea kuhesabu dakika na sasa bado nane” alisema jamaa huyo,mara baada ya kusema hayo akazima mawasiliano yale.

“Fanya haraka kachukue hizo pesa kwenye akiba ya taifa” raisi aliagiza haraka huku akiwa anahema kama mbwa aliyekuwa anakimbizwa.



****


ITAENDELEA 

0 comments:

Post a Comment

Blog