Simulizi : Nilivunja Ndoa Zangu 3 Kulipiza Kisasi
Sehemu Ya Tatu
(3)
Dah, mume sasa naona kashtuka,
sijui kashtuka nini, naona anatamani kabisa kunifuatilia siku ya leo, sasa
anataka kupata lunch na mimi. Hii sio tatizo.
Muda wa lunch ulifika,
Jones alinifuata ofcn peke yake, siku ya leo kila mtu alinisifia sana kwa namna
nilivyovalia, Anti kudrati aliniita na kuniambia umevalia vyema sana isipokuwa
tu hujapaka marashi yanaoyendana na vazi hilo,, njoo.. Anti kudrati aliniita
kisha akanipatia marashi yanayonukia kama udi Fulani hivi,, huwa sipendi sana
marashi haya, lakini ilibidi nikubali ili kuleta heshima ya vazi
lenyewe.
Nilijipaka manukato yale kisha nikashuka ngazi nikiwa na jones
kuelekea kwenye lunch kama alivyohitaji.
Tuliondoka mimi nay eye wawili
tu. Tulifika sehemu ambayo walikuwa wakipika vyakula vya kitanzania, vyakula
vyenye asili ya kitanzania. Alijua napenda matoke. Hivyo tuliagiza matoke na
tukala.
Tukiwa kwenye hotel hiyo kila mmoja alikuwa akiniangalia sana,
nafikiri walimfahamu zaidi Jones kuliko mimi, kwani kwa jinsi nilivyovalia sio
rahisi ungeweza kugundua mimi ni Charlote. Na ninafikiri walifikiri kwamba
pengine Jones kajipatia jidada la pwani na anatoka nalo.
Tulikula
chakula na tukamaliza. Baada ya kumaliza, Jones aliniambia, Mke wangu Charlote,
tafadhali naomba yaishe , naomba sana tujenge ndoa yetu.
Nilimtazama na
kumwambia nini yaishe? Kitu gani? Alniambia nilivyokukosea sana, nilishindwa
kuwa muaminifu kwako na kuwa na mahusiano na Husna, naomba
unisamehe.
Nilimtazama na nikasema sasa huu ni muda muafaka kumhoji ni
kitu gani alikosa kwangu.
Nilimtazama na kumgeukia, kisha kumkazia macho
na kumuuliza,
Jones mume wangu,, ninaombe tu unieleza ni kitu gani
kilikufanya ukaamua kuwa na mahusiano na Husna.
Jones alinitazama na
kuniambia siwezi kusema kitu gani ila ni tamaa tu.
Nilimwambia hapana ,
haiwezekani, lazima kuna jambo na kitu kilikuvutia kwake. Tafadhali niambie ili
nijirekebishe na isije kupelekea tena ukawa na mahusiano nje ya ndoa
yako.
Jones aliniambia kwa kweli siwezi kusema kwamba wewe ni sababu ya
mimi kuwa na mahusiano na Husna, ila ni mimi peke yangu tu nilishindwa
kukuheshimu. Naomba nisamehe.
Nilimwambia nimekusamehe siku nyingi
sana,
Aliniambia asante sana, na kisha akatoa mfuko ambao ulikuwa na
perfume, viatu na saa.
Akaniambia hizi hapa zawadi zako asante
kunisamehe.
Nilimwambia asante sana kwa zawadi, nilichukua zawadi zangu
na tukaondoka. Alinielekea ofcn kwake na mimi nilelekea ofcn
kwangu.
Aliniandikia msg na kusema,, CHARLOTE MKE WANNGU, MAMA WA WATOTO
WANGU, MKE WA UJANA WANGU, MKE WA AHADI NA KIAPO KITAKATIFU, NAOMBA NISAMEHE,
NAKUPENDA SANA, SITEGEMEI KUKUKOSEA TENA, NAJUA NIMEKUUMIZA SANA, ISIPOKUWA
NISAMEHE, NIPENDE KAMA ZAMANI, NAMISS SANA PENZI LAKO MKE
WANGU.”
Niliitazama ile msg, machozi yalinidondoka, ujumbe huu
ulinionyesha wazi namna ambavyo Jones amekiri kosa lake. Nililia sana, kisha
nikanyamaza, Ujumbe huu niliusave tena, ni ujumbe wa pili kwenye maisha yangu
nauserve. Jones, jones, jones, kwa nini umesababisha nikawa na roho ngumu hivi
wewe mwanaume? Aghhhhh.. niligonga meza kwa nguvu na kuchukia sana, kwani
alipelekea nikawa nimejiingiza kwenye jambo ambalo kuliachia kati
siwezi.
Siwezi kuachia jambo hili kati kati, lazima Husna na mama yake
kiwaume kama kilivyoniuma.
Haraka nilifuta machozi, na baada ya hapo
niliangalia saa yangu ya mkononi ilikuwa ni saa kumi na robo. Tulikubaliana
kukutana na Majidi saa kumi na moja na nusu kwenye hotel
Fulani.
Nilianza kujiandaa kumalizia kazi zangu za siku ile, kisha baada
ya hapo nilienda kwa muajiri wangu ambaye kwa sehemu alijua kuwa siko vizuri
kutokana na matatizo ya kindoa.
Muajiri aliniruhusu na nikaondoka.
Niliwasha gari yangu, kabla sijaanza kuendesha, niliinama kwenye stsaling,
nikitafakari tena maneno ya Jones, ni maneno mazito.
Mungu wangu… si ni
msamehe tu jamani Jones… dah,, amejuta kweli, si kawaida yake, Jones anamaanisha
kukosea, nimsamehe.
Haraka akili yangu iliniambia….. HUMTOSHELEZI… sauti
ya mama Husna ilijirudia kwenye masikio yangu,
Niliwasha gari na moja
kwa moja nilielekea kwenye hoteli hiyo.
Majidi namfahamu, ila mimi
hanifahamu kabisa.
Nilifika , niliona gari yake ikiwa imepaki, kwani
ilkuwa na tyer cover la maandishi ya duka lake la vifaa.
Nilijua
kashafika.
Moja kwa moja nilishuka kisha nikaelekea sehemu ambayo amekaa
kwani nilimfahamu.
Alikuwa akiniangalia sana kabla hajajua ni mimi
ninayemfuata.
Nilifika na kumsalimia. Habari…. Aliitika njema habari
yako.
Niliitika nzuri. ..
Mimi ni Charlote,,, tulikubaliana
kukutana leo kibiashara..
Ahaa.. karibu karibu sana charlotte, tayari
alisimama na kunisogezea kiti. Mezani alikuwa na laptop ya apple, kisha alikuwa
na diary na funguo za gari, na simu kama tatu hivi, zote smart
phone.
Alisogeza vitu vyake vyema kisha nikakaa.
Alinitazama na
kusema dah,,charlotte,,,, why charlotte? Aliniuliza…
Are you musilm or
Christian? Nilitabasamu nikasema am Christian.
Aisee,, umependeza sana
ulivyovyalia, kama muarabu bwana,, manshalah… alimaliza
kusema,
Nilimshukura na kumwambia asante.
Kisha nikamwambia sina
mud asana kukaa naye kwani ninahitaji tu kumueleza ninachohitaji. Nilifungua
pochi yangu na kutoa karatasi ambayo ilikuwa imendikwa baadhi ya bidhaa, na
niliandika mwenyewe as if ni oder kutoka mahali Fulani. Kwa nini
asiamini?
Kisha nikamueleza mahitaji yangu, Aliniambia kweli aina za
flat screen hizo kwa sasa hana, ila anauwezo wa kuwa nazo kwani hata kwenye
mzigo wake hakuna aina hizo. Nilimueleza inachukua muda gani hadi mzigo kufika
tangu kuagiza? Aliniabia ni ndani ya siku 21 mpaka 40.
Dah,, nilimjibu
ni siku nyingi sana, kwani mwenye anahitaji anazihitaji kwa haraka sana kutokana
na kutaka kufungua hotel yake.
ALinihoji kama hotel hiyo iko mjini,
nilimwambia hapana iko nje ya mji tena mkoani.
Alifurahi sana kwa mimi
kumpa biashara.
Asante sana charlotte, asante sana. Nashukuru kunipatia
biashara hii.
Nilimwambia asante sana, huwa watu wengi hukusifia unauza
bidhaa zenye ubora hivyo nikaona sio mbaya nikihitaji vifaa kutoka kwako.
Aliniambai nisiwe na shaka kwani pia bidhaa zake zina guarantee ya mwaka
mzima.
Nilimshukuru, na tukakubaliana kwamba angenipigia simu kunipa
feed back ya kinachoendelea.
Dah… Mimi ni mke wa mtu Majid, singependa
unipigie simu kabisa, kiusalama zaidi, si unajua wanaume mlivyo na wivu? Ha ha
ha, kisha nikacheka.
Na ni kweli, , sasa tutawasilianaje?
Alihoji.
Nilimueleza kila nitakapokuwa nahitaji kuwasiliana naye mimi
ndiye nitampigia simu, na nitatumia simu ya ofcn kama
kawaida.
Alikubali, kisha akaniambia, Ninaharusi mwezi huu hivyo
ningependa kujua kabisa oder yako niifanyie kazi mapema kabla sijatoka kwa
honeymoon.
Ohooo,, unaoa? Nilionyesha kushangaaa…
Ndio,, ninaoa
mwezi huu,, ila dah,, ulivyomrembo natamani kama ungekuwa hujaolewa
ningekuoa.
Tulicheka wote kisha nikamuaga na kumueleza kwamba
tutawasiliana, anipe saa na siku ya kumpigia simu.
Aliniambia atafanyia
kazi hiyo oder na hivyo nimpigie simu baada ya siku mbili tu, kwani anajaribu
kuangalia kwa baadhi ya mawakala kuona kama anaweza kupata hizo pc 10 haraka
iwezekanavyo ili asikose tender hiyo.
Tulimaliza kuzungumza,, kisha
nikamuaga.
Charlote,, wewe ni mrembo sana, umependeza sana, wewe ni
mzuri sana,, manshalah,,, dah….
Majid alisema ,, kisha nilitabasamu na
kuondoka.
Nilienda moja kwa moja nyumbani, Nilimkuta Jones yuko nyumbani
akinisubiri.
Niliingia ndani, nilisalimia na kuangalia watoto wakoje,
kisha nikaingia bafuni mara moja kuoga na baadae nikatoka ili kuandaa chakula
cha jioni, najua Jones anapenda chapatti. Niliandaa chapatti zake chache na beef
stew kwani hupendelea sana. Nilimtengenezea pia na juice ya matunda, kisha
nikaanda chakula mezani ili ajipatie mlo wa usiku.
Alikuwa anaonekana
kuwa na furaha sana. Alifurahia mlo ule, alikuwa akiongea kwa furaha na kucheka
sana huku akinikumbusha baadhi ya mambo mazuri ya zamani.
Tulicheka. …
ni kama alianza kunirudisha kwenye mood. Lakini kila nilipokumbuka mission
yangu, dah mood ilinipotea ghafla.
Asbh niliamka, nilimuandalia vyema
kwa ajili ya kazini, alijiandaa na tukaondoka.
Mzee Zuberi alnipenda
sana, kila siku ashb alipofika ofcn kwake alinipigia simu na kunisalimia.
Nilideka kwa mzee Zuberi sana, nilikuwa nadeka mno. Na yeye alinidekeza haswa,
kila nilichohitaji nilipata kutoka kwake, hakuna nilichokosa.
Asbh
alinipigia simu na kunisalimia, kisha akaniambia Mamii mbona huko na
furaha?
Nilimueleza kuna kitu nimeona mjini nimekipenda na ningetamani
kukipata.
Aliniuliza ni kitu gani, na nilimueleza na viatu ambavyo
vinauzwa pamoja na handbag yake ni lether one hundred paceee, na ni made in
Italy.
Aliniambia Charlote sijui hivyo vitu mama, wewe sema ni shilingi
ngapi nikupatie.
Niliona ni muda wa kumsumbua… nilimueleza
vinapopatikana . sikutaka kumwambia ni shilingi ngapi.
Aliniambie
angepita hapo muda wa lunch time kucheki, kisha atanijulisha nikavichukue
hapo.
Mzee Zuberi ni baba wa miaka kama 58 hivi. Sio mzee sana. Na kwa
vile alikuwa na pesa na kujipenda basi alionekana tu ni kijana mzee, alijipenda
sana.
Saa saba mchana on dot. Simu yangu iliita, nilitazama, ni Mzee
Zuber.
Charlote,, bi mdogo… Abee niliitika.
Haya mama mzigo wako
nimeuona sema unataka rangi gani, ziko rangi mbili tu hapa, black an
red.
Nilitabasamu na kumwambia nahitaji rangi ya red.
Aliniambia
sawa, uje kuchukua basi mzigo wako nimeshalipa sawa mama.
Ndio.. Asante
sana.
Hakuna shaka sema kingine.
Alimaliza na kukata
simu.
Dah… kweli mzee kajitosha. Viatu na pochi hizo huuzwa dola 400.
Ama kweli mzee kapenda.
Nilijichekea mwenye .
Niliendelea na
kazi na baadae nilienda dukani kuchukua mizigo yangu.
Nilifika na
kumkuta muuzaji wa duka, ni dada ambaye mara nyingi nanunua vitu hapo, ananijua
kwa sura tu sio jina.
Na nilipofika niliweka sura ya kazi ili nisimpe
nafasi ya kuhoji.
Habari dada… samahani nimeambiwa nikifika hapa nitaje
namba hizi ili unipatie mzigo wangu.
Alizitama zile namba kisha akasema
ahaa, ni Mr Zuberi sio kakuambia uje uchukue?
Ndio nilijibu kwa mkato.
Kisha nikapatiwa mzigo wangu na kuondoka.
Huyooo mpaka nyumbani, I love
the shoes,, I love tha handbag… ziko kiwango. Nilicheka kisha nikasema ahaaa…
kumbe nimemtosheleza mr Zuberi ee ndo maana ananinunulia vitu vya gharama.
Nilikumbuka jambo,,, nilimkumbuka mke wa mzee zuberi, ni mama mwenye miaka kama
50 ama 52 hivi ama 55, hakuzidi hapo. Ila hajipendi hata kidogo, sijui ni umri
ama ni nini. Nilijichekea nikasema sasa upele umepata
mkunaji.
SEHEMU YA SITA
Majidi hakuweza kuvumilia. Ni
saa mbili na robo niko ofcn kwangu nakunywa kikombe cha maji ya moto. Simu yangu
ya mezani inaita. Nikiwa naendelea kujiuliza ni nani,,
niliipokea.
Habari? Habari,, upande wa pili ulijibu,, ahaaa, niliweza
kuitambua Sauti ni ya Majidi.
Habari Charlote…. Nilijibu ni njema sana
habari za tangu majuzi?
Ni njema pia. .. enhe jipya?
Nilimhoji.
Aliniambia sina jipya, nimekukumbuka tu nikasema nikusalimie,
japo bado nafuatilia kazi yako, uwezekano wa kupata oder yako sio mgumu lakini
sio mrahisi sana, naweza kupata ila bei itakuwa ghali kidogo kutokana na aina ya
mzigo. Aliniambia Majid.
Ohooo, haina shaka,, nilimjibu, kisha
nikamwambia wewe hakikisha unafuatilia kisha unirudie na jibu sahihi ili
nimueleze anayezihitaji, huenda akaamua kuongeza bei.
Okay , haina
shaka…ila pia…. Ila…. Majidi aliongea kwa kuguguma.
Sema. Mboan
kigugumizi? Nilimuuliza…
Majidi alicheka,, kisha akasema dah,,
ukinikatalia nitajisikia vibaya sana.
Nilishajua lengo lake, kisha
nikamwambia wewe bwana kata simu kama huna la kusema.
Sikia, usikate,
usikate… alisema Majidi, kisha nikakata simu.
Baada ya sekunde kama 30
hivi simu iliita tena.
Akaniambia,, Charlote unajua nikuambie tu ukweli
kama utanikubalia sawa kama utakataa sawa.
Ila ukweli ni kwamba tangu
nimekuona nimetokea kuvutiwa sana na wewe na nimekupenda sana, najua wewe ni mke
wa mtu na mimi karibuni nitakuwa mume wa mtu, ila nimetokea kukupenda sana
Charlote, nimevutiwa na wewe sana sijui una kitu gani chenye nguvu kiasi hicho.
Alisema Majidi.
Nilikata simu ,, kana kwamba sitaki kusikia habari
hizo.. kumbe ndizo nilizokuwa nikizisubiri. Kisha nikacheka na kutoka kwenye
washroom.
Nilimaliza na kurudi tena kukalia kiti cha ofcn na kuanza
kupiga kazi. Nilifanya kazi mpaka saa nne na nilikuwa nimeshamaliza kazi
zangu.
Mume wangu aliniandikia msg, Hi mamii, hujambo? Unaendeleaje?
Pole na kazi.
Niliutazama ujumbe ule, kisha nikamjibu, sijambo naendelea
vyema, kazi njema.
Aliniambia Asante sana.
Baada ya kumaliza tu
kujibizana kwa msg na mume wangu, mara simu ya mezani iliita tena.
Haloo
Charlote… nilitikia haloo… ni majidi.
Naomba unisamehe kama nitakuwa
nimekukwaza…. Aliongea Majid kwa mbwembe nilimgndua. Nilimwambia haina shaka,
nafurahi kuona kwamba ni mke wa mtu lakini ninavutia.. ila pia nafurahi kuona
kwamba naweza kumvutia bwana harusi mtarajiwa.
Alisema dah,,, kweli
umenivutia kabisa, najuta kuoa mapema?
Ha ha ha, nilicheka,, akaniambia
kwa nini unacheka? Nikamwambia maneno yako,, kwani ni ujute? Hata usingejuta
mimi ni mke wa mtu, hungeweza kunioa.
Kwa nini nisiweze kukuoa? Sina
utajiri wala chochote ila nina mapenzi?
Nilicheka nikajua hizo ni gear
tu za kiume, ila moyoni tayari nilishakuwa nimenuia kuwa naye, hivyo ni kama
nilikuwa nazuga Fulani hivi.
Sikia Majid, kweli mimi ni mke wa mtu,
isipokuwa naogopa mume wangu akijua ni hatari sana, ama mkeo akijua ni hatari
sana.
Majidi ni kama alishangaa mimi kusema vile, ni kama aliona
nimeshamkubali..
Sikia Charlote, nitaiheshimu ndoa yako sana, nakuapia,
na mimi pia mchumba wangu hatajua.
Sikia Majid,, naelewa, ila wewe oa
kwanza wala usiwe na haraka mimi nipo, wewe oa kwanza.
Majid alniambia,
ninasafiri kwenda Zanzibar kufuatamzigo wangu ijumaa, tafadhali kama unaweza
nisindikize.
Ni haraka sana, ni haraka sana Majidi, ni haraka sana.
Tafadhali wewe nenda tu.
Hapana Charlote kama unaweza nisindikize
tafadhali.
Nilimueleza kwamba siwezi kumsindikiza na nikakata
simu.
Zilikuwa zimebaki kama wiki tatu za harusi. Nilijiuliza je
nilikoroge kabla ya harusi ama?
Niliona intakavyonoga nikisababisha ndoa
kutokufungwa, hasara ya sare , ukumbi, na vyakula kwani najua wameshafanya
maandalizi.
Lakini nikajiuliza kitu kingine, hapana hii haitauma kama
nikilikoroga baada ya kuwa mume, tena sio mume wa siku tatu ama nne, ni masiku
mengi haswa, aone raha ya mume na ndoa, kisha ajue nina mahusiano na mumewe. Hii
ndiyo niliitaka, niliitamani.
Hivyo sikuwa na haraka kabisa, nikawa
nasubiri simu ingine ya Majidi nilijua atapiga tu.
Mara kweli simu
ikaita. Majid alipiga,, nilipokea.
Charlote tafadhali tuonane
tuzungumze.. nilimueleza kwamba asijali, nitampangia siku ya mimi na yey
ekuzungumza, ila ni vizuri kama akisettle kwenye maswala ya harusi yake
kkwanza.
Majid, mimi nipo tu, hembu shughulikia harusi kwanza, mimi
nipo.
Aliniambia mimi ni mwanaume harusi niachie mimi. Nilicheka,,
akaniambiambia mbona unanicheka? Hujui kama uzuri wako
umenichanganya?
Nilimwambai nacheka kwa vile najua ninyi wanaume ni
waongo sana.Aliniambia kweli huwa wanaume ni waongo, ila sio mimi, nakupenda
haswa wewe ni wewe na husna ni husna, huwezi kuwa kama husna na husna hawezi
kuwa kama wewe, ila bahati mbaya umeolewa, kama ungekuwa hujaolewa ningekuoa
hata mke wa pili, na kama huamini niachie hiyo kazi mimi, na ninakuapia
hutateseka, nakupenda charlotte.
Nilimuitikia na kumwambi a basi
usijali, ngoja niangalie ratiba zangu zikoje kisha nitakujuza tutasafiri wote
kwenda Zanzibar.
Kweli? Ndio,, kwelil … ndio, alirudia kama mara tano
hivi na mimi nikamhakikishiani ndio.
Kisa cha Charlote,, bado
anaendelea Malipizi,, na sasa ameafanikiwa kumpata Majidi, mchumba ama mume
mtarajiwa wa Husna, ambaye anategemea kufunga ndoa ndani ya wiki tatu.Hembu soma
uendeleea kupata Mafunzo ndani ya kisa hiki katika sehemu ya
SABA.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment