IMEANDIKWA NA : MKAPA JR
*********************************************************************************
Simulizi : Usilie (Don't Cry)
Sehemu Ya Kwanza (1)
"Kuanzia leo sikutaki nyumbani kwangu,nasema toka,toka nenda kwa aliyekubebesha hiyo mimba ukaishi kwake,nasema ondoka au nikuvunje vunje sasa hivi," ilikuwa ni sauti ya mwanaume mmoja aliyeitwa Gozbert,alikuwa akimfukuza mwanaye aliyekuwa anaitwa Glory.Glory alikuwa msichana mkimya sana,vijana wengi walimfuata kwa lengo lakutaka kuwa naye kimapenzi,lakini alikataa vijana walimchukia kwa tabia yake hiyo.
"Siwezi kutembea na kijana yeyote ndani ya hiki kijiji"yalikuwa maneno ya Glory akijisemea moyoni hasa vijana wengi walipokuwa wanamsumbua.Bahati mbaya kwake alikutana na mwanaume mmoja aliyekuwa amehamia kwenye kile kijiji,yule mwanaume aliitwa Peter,Peter baada ya kujua kuwa amembebesha mimba Glory aliamua kutoroka na kwenda kusikojulikana,hivyo msala mzima alimuachia Glory.
"Siamini huyu Glory niliyekuwa namfuatilia kila siku leo ana mimba?siwezi kuamini maneno yako"alikuwa kijana mmoja akimwambia mwenzake baada ya kusikia taarifa ile iliyosambaa kwa kasi sana.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Kweli mwanamke mkimya muogope sana,sikutegemea kabisa kama Glory angeliweza kukitia hiki kijiji aibu"yalikuwa maneno ya mama mmoja wa makamo.
"Acha kabisa,hawa mabinti zetu wanapotea kabisa,harafu mwanaume mwenyewe aliyembebesha hiyo mimba hana mbele wala nyuma,nasikia ni mkimbizi kaja hapa kijijini kufanya kazi ya vibarua"mama mwingine alisema huku akiwa ameshikilia shavu lake kumaanisha alikuwa na majonzi.
Safari ya Glory ilianza japo kuwa hakujua aelekee upande gani,alikusanya baadhi ya nguo zake,akiziweka kwenye mfuko wa rambo na kuondoka huku akidondosha machozi,mama yake hakuweza hata kumuonea huruma,hata yeye alikubali kuwa Glory aondoke ili wadogo zake waweze kujifunza kupitia yeye.
"Ondoka kabisa,yaani mwanamke tuliyekutegemea kuwa utakuwa maarufu hapa kijijini leo hii umetutia aibu?uko wapi ukimya wako?iko wapi nidhamu yako uliyokuwa nayo hapa?aibu hii tutaiweka wapi sisi wazazi wako?nenda ukateseke huko"yakikuwa maneno ya mama yake.
Safari ya Glory ilianza usiku huo huo,hakujua ni wapi atakwenda.
"Hakika wanaume mungu atawalaani,yaani wewe Peter si uliniambia utakuwa na mimi kila sehemu?leo hii uko wapi?nakumbuka mara yakwanza kabla ya mapenzi,ulikuwa ukipiga magoti mbele yangu nakutoa machozi kabisa,kosa langu kukubali kushiliki tendo la ndoa na wewe.najuta mimi Glory"yalikuwa maneno ya Glory akijisemea moyoni huku akifuta machozi yaliyokuwa yanamtoka.
"Let's listen to this girl his parent drove home,so we have to force to do sex with her,remember that we were dating he refused,so we use our strength to know that we are the children's of the city,cannot use we follow the an innocent man in front or behind"(sasa sikilizeni huyu msichana wazazi wake wamemfukuza nyumbani,hivyo tunatakiwa kumlazimisha kufanya naye mapenzi.kumbuka tulimfuata akakataa hivyo na sisi tuoneshe kuwa tuliumia,hawezi kutuacha sisi watoto wa mjini eti akatembee na yule mwanaume asiyekuwa na mbele wala nyuma)yalikuwa maneno ya kijana mmoja aliyeitwa Frank wakiwa na vijana wenzake wsliokuwa wametoka mjini.walionekana ni vijana watanashati sana,kila mda walibadili nguo tofauti na vijana wengine wa pale kijijini.mda mwingi walionekana kuongea kingereza jambo liliwapa umaarufu,kila msichana walimfuata na kumchezea.pamoja na unadhifu wao wote,kijana Frank alimfuata mara kwa mara Glory lakini juhudi zake ziligonga mwamba.
"Hivi wewe pamoja na kuvaa nusu uchi,unafikiri kuwa mimi naweza kukubali kutembea na wewe?hilo kwangu haliwezekani,tafuta mabinti wengine wasiojielewa ila sio mimi Glory"yalikuwa maneno ya Glory akimwambia Frank.yote hayo aliyakumbuka Frank akiwa na vijana wenzake wawili.walipopata taarifa kuwa Glory kafukuzwa nyumbani kwao walipanga mbinu za kumkomoa Glory.
"He was planning a period of the past,but currently has no cunning,already has a pregnancy,work remains on our side"(Alikuwa analinga kipindi cha nyuma,lakini kwa sasa hana ujanja,tayari ni mjamzito,kazi imebaki kwa upande wetu)Frank aliendelea kuwaambia wenzake wote walikubaliana na moja kwa moja wakaongozana kupitia ile njia aliyokuwa amepitia Glory,Glory aliendelea kutoa machozi,hakujua ataenda wapi kwa usiku ule,akiwa anazidi kusonga mbele ghafla walitokea vijana watatu,Frank ndo alikuwa mstari wa mbele,bila kuongea lolote walimshika na kumziba mdomo kisha wakafanya kile walichokuwa wamekusudia,wote waliporidhika walimuachia Glory aliyekuwa hajitambui,alitoa machozi ya maumivu,yote kwa yote alimlaumu Peter,mwanaume aliyevuruga ndoto za maisha yake.
Frank na kundi na vijana wenzake walipongezana kwa kazi waliyoifanya,Frank aliongea kwa sauti ya furaha.
"We the childrens of the town do not fail anything"(Sisi ni watoto wa mjini hatushindwi na kitu chochote)walipeana mikono ya pongezi,ni vijana waliomiwa wanasoma shule za mijini,badae walifukuzwa kutokana na vitendo vyao viovu.
Glory aliinuka huku akihisi maumivu,hakujua waliomfanyia kitendo kile ni watu gani alizidi kusonga mbele huku akichechemea,baada ya kutembea sana,usiku huo alichoka,hivyo alipumzika kando kidogo na barabara,usingizi ulimpitia,alikuja kustuka kushapambazuka tayari,alitafuta maji yaliyokuwa yametuama pembeni kidogo,alisaficha uso wake kisha akaendelea na safari.
"Hapa ni kwenda mjini hakuna namna nyingine"alijisemea Glory huku akiufungua mfuko uliokuwa na nguo zake,aliangalia pesa na kuona kiasi cha shilingi elfu therathini na saba.
"Nakumbuka hii pesa nilipewa na Peter kabla hajanikimbia"alijisemea Glory huku akifuta machozi.kila alipokuwa unaukumbuka upendo wa Peter alijikuta akitoa machozi.safari yake iliishia stendi ya mabasi yaliyokuwa yanatoka Arusha kwenda Jiji mbeya.kabla hajapanda basi alifikiria.
"Kwanini nisikae hapa hapa mjini Arusha?alijiuliza moyoni,bila kupata majibu alianza kulizunguka jiji la Arusha.
"Dada naomba kazi"aliongea Glory baada ya kumuona mwanamke mmoja akiwa dukani.
"Hapa hamna kazi"yule dada alimjibu.bado hakukata tamaa aliendelea kuzunguka.hadi inafika jioni hakufanikiwa kupata sehemu ya kulala.
"Hapa hapa pananitosha"alijisemea moyoni huku akivuta maboksi aliyoyakuta eneo lile.
"Ninani huyu kavamia nyumba yangu"alijisemea kijana mmoja alipokuwa anakuja kulala kwenye eneo lake.
"Loo!binti mdogo kama huyu kafuata nini huku"slijisemea yule kijana huku akiangalia mfuko uliokuwa na nguo za Glory. Baada ya kuukagua alikutana na pesa.
"Hili Bahati tayari,endelea kulala binti"alisema yule kijana huku akigeuka na kumuacha Glory akiwa usingizini.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Glory alikuja kustuka kesho yake asubuhi,alichukua mizigo yake nakuondoka eneo lile.
"Ngoja nichukue hera nikanunue vitumbua"alijisemea moyoni huku akiangalia kwenye mfuko wake,lakini hakukuta kitu chochote.
"Mungu wangu nimedondosha wapi?,alijiuliza huku zile nguo zile akizimwaga chini zote lakini hakuona kitu chochote.
"Sasa nitaishi vipi hapa mjini?na je Peter anajua kweli haya mateso ninayo yapata?alijiuliza Glory huku akizidi kutembea sehemu ambayo alikuwa haijui.
"Mungu ndo atajua hatima ya maisha yangu"alijisemea moyoni baada ya kuona bango lililokuwa limeandikwa kwa kingereza.
"No one in this entry unless employees only"(hakuna mtu yeyote kuingia humu ndani isipokuwa wafanyakazi pekee"bango liliandikwa hivyo lakini Glory hayo maneno hakuyaelewa.
"Ngoja nikajaribu kuomba kazi pale"alijisemea huku akisogea mlangoni,baada ya kuchungulia nani aliwaona watu wenye ngozi nyeupe.
"Habari zenu"alisalimia Glory.
"Here we do not allow anyone to enter,your problem?(Hapa huwa haturuhusu mtu yeyote kuingia,shida yako nini?)Glory alijibiwa kwa kingereza.alikaa kimya kwa mda akijalibu kuunganisha yale maneno lakini alishindwa.
"Why are you surprised you have followed here?(Mbona unashangaa umefuata nini hapa?)Glory alikosa jibu aligeuka na kuondoka.
"Watu wengine bwana,sasa mimi na kingereza wapi na wapi"alijisemea Glory huku akizidi kwenda mbele.
"Mama naomba kazi angalau nipate chakula"aliongea Glory baada ya kupita kwenye mgahawa mmoja.
"Karibu binti,hapa kazi ipo utapata kikubwa kufanya kazi kwa bidii,karibu ukae"aliongea mama mmoja aliyeitwa mama Suzi.Glory alifurahi sana kupata kazi.
"Hapa nitafanya kazi kwa bidii ili badae nimtunze mwanangu"alijisemea moyoni Glory.mama Suzi alionekana kuwa na upole sana,kila mda alimuelekeza Suzi namna ya kupika.
Baada ya miezi mitatu Suzi alikuwa ashazoea mazingira yale,tatizo lilikuja kwenye kwenye ujauzito wake ulioanza kukua,mda mwingi alikuwa mchovu na kushindwa kufanya kazi.
"Kumbe huyu kaja na mimba hapa?alijiuliza mama Suzi baada ya kumuona Glory akitapika.
"Karibu sana sijui mnataka huduma gani"
"Dada kuna nini na nini?
"Kuna supu chapati na vitumbua"
"Mimi naomba supu na chapati"
"Samahani supu inaanzia elfu moja mia tano"
"Kalete hiyo hiyo"yalikuwa maongezi ya Glory na vijana wawili.
"Haka kabinti kazuri nikikapata wallah ntakaoa"alisema kijana mmoja aliyeitwa Issa.
"Harafu mbona kanaonekana kama vile kana mimba?kijana mwingine aliongea.
"Hapana hakuna cha mimba hapo"Issa alijibu huku akimuangalia Glory.
"Mungu anajua kuumba asikwambie mtu"alisema Issa.
Maongezi ya wale vijana yaliishia pale Glory alipoleta chakula.
"Nitakuendea kwa waganga mpaka nikupate"alijisemea moyoni Issa.kijana mwingine aliyekuwa anaitwa Fikiri naye alikuwa akiwaza yake moyoni.
"Naam huyu ananifaa ila nina hofu akiwa na mimba"alijisemea Fikiri.Issa na Fikiri walikuwa marafiki walioshibana sana,kila sehemu walihakikisha hawaachani,mara nyingi walikuwa wakifanya kazi kwenye mgodi wa merelani jijin Arusha.waliishi pamoja baada ya kumaliza kula Issa alitoa noti ya elfu kumi na kumpatia Glory.
"Dada hiyo chenji utakunywa soda"aliongea Issa huku akitabasamu.
"Asante sana kaka yangu"alijibu Glory.
"Hata uhonge million ila piga uwa huyu ni wangu"alijisemea Fikiri.
Maongezi yale hayakudumu baada ya kuingia watu wengine.
"Ujue Fikiri huyu binti nimetokea kumpenda"
"Muoe basi nipate shemeji"
"Ngoja kesho tukirudi ntajalibu kumwambia ukweli"
"Wewe toa hera kwanza harafu utampata kwa urahisi"
Yalikuwa maongezi ya Issa na Fikiri wakati wanatoka kupata chai ya asubuhi.
"Huyu mkaka naona ashaanza mambo yake,naona kaniachia pesa ili iwe rahisi kunipata,lakini siwezi wanaume waongo sana hawaaminiki,sikutegemea mwanaume kama Peter angaliweza kunikimbia"yalikuwa mawazo ya Glory akikumbuka pesa alizoachiwa na Issa.
"Mimba nayo inazidi kukua sina hata mia"aliwaza Glory huku machozi yakimtoka.
"We Glory huoni hao wateja?
"Samahani mama"
"Haya wahudumie"
Yalikuwa maongezi ya mama Suzi na Glory aliyekuwa kwenye dimbwi la mawazo.kwa siku alizokaa hapo Glory mama Suzi alijikuta akipata wateja wengi ambao hakuwa nao hapo awali.
"Kweli vijana wa sasahivi wamehalibika na mapenzi,sasa hawa wote wanamtaka Glory hawajui kuwa tayari ana mimba"yalikuwa maneno ya mama Suzi baada ya kuona vijana watano wanakuja.
Maisha yaliendelea huku taratibu tumbo la Glory likianza kukua na kuonekana.Glory alijitahidi kuvaa nguo pana ili asionekane.
Issa alizidi kuwaza jinsi gani atampata Glory.
"Mshahala wangu nitaupeka wote kwake,najua siwezi kumkosa"baada ya kuwaza sana kijana Issa alishusha pumzi na kujisemea hayo.
"Wacha ampe hera nyingi ila mimi nitampata kwa urahisi"alijisemea Fikiri.
"Mama Suzi njoo nikwambie"ilikuwa sauti ya mwanaume mmoja aliyeshuka na gari aina ya Toyota Hilux.mama Suzi alitii wito.
"Habari yako"
"Salama karibu"
"Aya asante kuna kitu nataka kukwambia"
"Kitu gani"
Ni kizuri kama utafanya mpango ukakamirika"
"Ndo niambie sasa"
"Namhitaji huyu binti"
"Mmh ni vigumu kidogo ila ngoja nitaongea naye harafu nitakupa jibu"yalikuwa maongezi ya mama Suzi na yule mwanaume aliyeonekana mtu mwenye pesa.
"Hawezi kuruka hapo kesho nakuja na gari nyingine"aliongea yule mwanaume aliyeitwa Daudi.Daudi alikuwa mwanaume mwenye pesa sana,aliishi na virusi vya UKIMWI,kila binti aliyemuona alihakikisha anamuambukiza.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Siwezi kufa peke yangu"alijisemea Daudi huku akipaki gari yake na kuingia kwenye baa moja.
Watoto wa shule mbali mbali waliokuwa wanapagawa na magari,aliendelea kuwatumia atakavyo,alikuwa anatumia dawa iliyokuwa inamfanya asiwahi kumaliza,kila aliyekutana nae alihakikisha anamchubua na kuhakikisha amepata hivyo virusi.mawazo yake yalimpeleka kwa Glory.
"Lazima nimpate"alijisemea hayo Daudi huku akiendelea kunywa pombe.
"Mwanangu Glory leo nina jipya kweli"
"Jipya gani hilo mama"
"Tulia basi kwanza mambo mazuri hayataki haraka"
"Nambie mama nina shauku ya kujua"
"Leo kaja mwanaume yule uliyeona naongea naye"
"Eeh ndio mama nilimuona"
"Basi kasema kwamba uchague chochote unachokitaka,bahati hizo mwanangu"
"Kivipi mama?
"Namanisha kakupenda yule ana magari na kila kitu"
"Sasa magari yake mimi yananihusu nini?
"Sikiliza mwanangu pesa sahivi ndo kila kitu"
"Hata kama mama mimi siko tayari"alijibu Glory na kuondoka akaendelea na kazi.
"Wanaume wenye pesa hawajahi kuwa na upendo wa dhati"alijisemea Glory.
"Lakini namimi nina mwanangu Suzi huyu Glory akikataa yule baba nitampa Suzi"alijisemea mama Suzi.
Issa baada ya kupokea mshahara wa laki tatu alikuja mpaka pale kwa mama Suzi,alimkuta Glory akiwa anaosha vyombo lakini hakuonekana kuwa na raha.
"Dada mambo"alisalimia Issa.
"Poa kaka karibu"
"Asante dada,ahaa nina maongezi nawewe"
"Samahani kaka huu mda wa kazi"
"Kama hutojali chukua hii hapa itakusaidia,pia ukiwa na shida utanitafuta kwa hizo hapo namba"aliongea Issa huku akimkabidhi Glory zile pesa.lakini Glory alikataa kabisa,baada ya kumbembereza mda mrefu Glory alikubali.
"Kweli nina shida ya pesa hapa naenda kupanga chumba ili kuja kujifungua niwe kwangu tayari"alijisemea Glory huku akizipokea zile pesa,
"Kama unafanya haya kwa ajili ya mapenzi kwangu utakwama,mimi tayari nina mimba"alijisimea hayo Glory wakati akiagana na Issa.
"Hakuna mkate mgumu mbele ya chai"alijisemea Issa huku akiondoka.
Glory baada ya kupokea ile pesa,aliiweka mfukoni kisha akaendea na kazi.jioni ya siku ile alimtafuta darali wa nyumba,alipata chumba kimoja,maisha aliyaanza taratibu.
"Yaani nimempa mshahara wangu wote kumbe ana mimba?asee sikubali"alijisemea Issa hasa baada ya kuona tumbo la Glory likizidi kukua.
Ilikuwa siku ya juma tano,siku ambayo Daudi alikuja akiwa na gari nyingine,moja kwa moja alipaki kando kidogo na mgahawa wa mama Suzi.
"Eee mama Suzi nimekuja sasa"
"Karibu baba"
"Asante vipi kakubari"
"Hapana kwanza mtu mwenyewe ana mimba"
"Oooh shit!!mimba??
"Ndio alikuja nayo hapa"
"Oooh,tunafanyaje mama Suzi"
"Ila usijari kuna mzigo mwingine"
"Mzigo upi?
"Kuna binti mwingine hapa atakufaa"
"Mlete nimuone"moja kwa moja Suzi aliitwa.
Maongezi yale aliyasikia Glory.
"Mungu wangu kumbe anamuuza mwanaye?hii dunia inaenda wapi?alijiuliza Glory.
"Siwezi kuendelea kukaa hapa huyu mama hafai"alijisemea Glory huku akipanga njama za kuacha kazi.
"Hujambo binti"
"Sijambo shikamoo"
"Marahaba,ingia kwenye lile gari"yalikuwa maongezi ya Daudi na binti Suzi.
"Kanaonekana hakajatumika haka"alijisemea moyoni Daudi huku akigeuka kumuangalia nyuma.
"Kweli watu mungu kawajaria sana"alijisemea Suzi baada ya kuingia kwenye gari,alikutana na upepo wa kiyoyozi.
"Huyu huyu simwachii"alijisemea Suzi baada ya kuona Daudi akitoa pochi yake iliyotuna na kutoa pesa kisha kumkabithi mama yake.
"Mabinti wenye tamaa lazima niwamalize"alijisemea Daudi huku akipanda ndani ya gari.
Safari yao iliishia kwenye Gest iliyokuwa karibu na maeneo yale,walilipa na kuingia ndani.
"Baby humalizi tu jaman"alikuwa sauti ya Suzi baada ya kuona zimepita dakika arobaini Daudi akiwa hajamaliza.saa moja na dakika arobaini ndo Daudi alikuwa anamaliza,Suzi alishindwa hata kusimama.
"Tamaa zenu zitawaponza"alijisemea Daudi baada ya kuona damu iliyokuwa inamtoka Suzi.
"Pole sana mpenzi shika hii hapa"aliongea Daudi huku akitoa laki moja na kumkabidhi Suzi.
"Yaani mama niko hoi kabisa"
"Pole mwanangu utazoea"
"Sawa mama nipumzike kidogo badaa nitaenda mjini kununua simu nzuri"
"Sawa mwanangu pumzika"
"Haya mama chukua hii kidogo"yalikuwa maongezi ya Suzi na mama yake.
"Yes(ndio)hayo ndo maneno sasa"alijisemea mama Suzi baada ya kupokea elfu ishilini kutoka kwa mwanae.yote hayo aliyaona Glory.
"Kesho sirudi tena hapa"alijisemea Glory.chumba alichokuwa amepanga hakuna aliyekuwa anakijua hakumwambia mtu yeyote.
"Mbona nilimpa namba yangu na hajawahi kunitafuta?alijiuliza Issa.
"Huyu Dada atakuwa tapeli ndo maana ana mimba"alisema Issa akiwa na rafiki yake Fikiri.
Kesho yake Glory hakuonekana alipokuwa,aliondoka kimya kimya bila kumuaga mama Suzi.
"Sasa atakuwa wapi?
"Au kashikwa uchungu wa kujifungua"
Mama Suzi alikuwa akimuuliza mwanaye.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Hii sasa kesi ndo hasara ya kupokea mtu usiyemjua,kama akipatwa tatizo basi kesi itakuwa kwa upande wangu"alisema mama Suzi.
Glory alianza kufanya maandalizi madogo kwa ajili ya kumpokea mtoto,pesa aliyokuwa amepewa na Issa bado alikuwa nayo ukijumlisha na mshahara wake.
"Bado miezi minne ili nijifungue lazima hii pesa nifanye biashara ndogo ndogo ili mwanangu asije akateseka"alijisemea Glory.
Siku ya ijimaa Issa alikwenda mgahawani kwa mama Suzi alistuka kutomkuta Glory.
"Mama Suzi huyu mhudumu mwingine yuko wapi?
"Tangu jana haonekani na sijui aliko"
"Unataka kuniambia kuwa hata wewe hajakuaga?
"Ndio katoroka,binadamu bwana bora mfadhili mbuzi"
Yalikuwa maongezi ya Issa na mama Suzi.
"Nilisema huyu binti ni tapeli"alijisemea Issa huku akiondoka.
Glory alifungua genge katika maeneo aliyokuwa anaishi,kila siku alikuwa akiingiza hera ndogo ndogo.
"Haijawahi kutokea mimi nikatapeliwa na binti mdogo kama yule"alijisemea Issa huku akipanga kumtafuta Glory.
"Najua bado atakuwa maeneo haya haya,sasa Fikiri tumtafute"aliongea Issa huku akimshika bega rafiki yake.
"Lakini si ulimpa mwenyewe sasa kakutapeli vipi hapo?aliuliza Fikiri.
"Hata kama"alijibu kwa mkato Issa.
Glory aliendelea kulikuza genge lake alijitahidi kubana matumizi.kila siku zilivyokuwa zinasogea ndivyo genge lake lilivyozidi kukua.
"Issa hakuchoka,kila mtaa aliuzunguka kumtafuta Glory.
"Siku nikimpa huyu binti lazima atanitambua"alijisemea Issa huku akizidi kukatika kwenye mitaa tofauti tofauti.
Daudi aliendelea kuwa na Suzi walizunguka sehemu nyingi sana ndani ya jiji la Arusha,Suzi kila dakika alilala kifuani mwa Daudi.
"Baby nataka unioe nikuzalie watoto"aliongea Suzi.
"Kwahilo tu usjal nataka wiki ijayo twende Zanzibar"aliongea Daudi.
"Ntafurahi baby"aliongea Suzi huku akizishika ndevu za Daudi.
"Pole sana,bahati nzuri sinaga tabia ya kukaa na msichana miezi miwili kwa sababu wanaonitaka ni wengi"alijisemea moyoni Daudi.
"Baby naomba maji nimeze panadol kichwa kinaniuma"aliongea Daudi huku akiwa na vidonge vitano mkononi,hazikuwa panadol ukweli ni kwamba zilikuwa dawa za kumfanya asimalize haraka kwa kuwa tukio lililokuwa linaenda kutokea alilijua vyema.
"Mpaka nihakikishe amepata huu ugojwa ndo nitaachana naye"alijisemea Daudi huku akimeza zile dawa.
Safari yao iliishia kwenye fukwe za bahari,zile dawa zilikuwa zinafanya kazi baada ya dakika arobaini,hivyo kabla ya dakika hizo walikuwa tayari chumbani.
"Huyu mwanaume kweli ataniua hadi kanichukua kanichubua hivi lakini bado anaendelea"alijisemea Suzi.
"Hapa huponi tayari nawewe ni mwathirika"alijisemea Daudi huku moyoni akifurahi.
Issa hakuwa na raha kabisa,mda wote alikuwa mtu wa mawazo,rafiki yake aliyeitwa Fikiri alikuwa akimcheka moyoni.
Zikiwa zimesalia miezi miwili ili Glory ajifungue,Issa aliweza kuambiwa mtaa aliokuwa anaishi Glory,bila kupoteza mda alienda moja kwa moja mpaka kwenye pale kwenye genge la Glory,alishangaa kumkuta Glory akiwa amebadilika kabisa,tumbo lake lilikuwa kubwa,mpaka Issa alimuonea huruma.
"Miezi kama hii,wanawake wengine wanakuwa wametulia kabisa wakisubiri kujifungua"alijisemea Issa.
"Ama kweli shida zinazidiana"Issa bado alizidi kushangaa Glory alivyokuwa anapanga vitu pale gengeni alimsogerea karibu yake.
"Kaka karibu"alisema Glory akimkaribisha Issa.
"Asante ila umenifahamu"alingea Issa,Glory alimgeukia tena na kumuangalia.
"Ooooh!ni wewe?
"Ndio mimi,kwanini ulinikimbia?
"Hapana kaka sijakukimbia niliamua kutoka pale baada ya kugundua kuwa mama Suzi hakuwa mtu mwema"
"Sasa unaishi nanani?
"Naishi mwenyewe huku nikiendeleza biashara yangu hii kama unavyo niona"aliongea Glory.Issa alijikuta akiinamisha kichwa chini kana kwamba anatafakari kitu.
"Pole sana dada mungu atakusaidia sana,hii mitihani ya dunia amini utaishinda"Issa alimtia moyo,hasira zake alijikuta zikiisha kabisa.
"Lazima nimsaidie huyu mwanamke ikiwezekana nimuoe kabisa,anaonekana mwanamke mpambanaji kweli"aliwaza Issa,huku akitafari msaada gani atoe ili aweze kuishi na huyu mwanamke.
"Nyumba gani unayoishi?aliuliza Issa.
"Ile pale kwenye lile dirisha lililowekewa mabox ndo naishi humo"alijibu Glory huku akimuelekeza kwa mkono.
"Sawa nimepaona ntakuja kukutembelea siku za hivi karibuni"alisema Issa na kutoa noti ya elfu kumi kisha akampa Glory.
"Lazima nimuoe,mama yangu kabla hajafa kuna maneno aliniambia"alijisemea Issa huku akiondoka.
"Mwanangu msaidie mwanamke yeye anayehitaji msaada kama akiwa mjamzito,huwezi kujua atajifungua mtoto awe nani hapa duniani,mimi siwezi kupona kwa sababu nimekosa huduma mapema,baba yako alinikimbia wewe hapo ukiwa mdogo,nimejitahidi kuwa tunza sasa huu ndo mwisho wangu"alisema mama Issa,aliyekuwa anajitahidi kujifungua lakini mtoto alifia tumboni,hakuwa na pesa ya kwenda hospital kufanyiwa upasuaji hivyo alisubiri umauti umkute,hayo yalikuwa maneno yake mafupi kabla hajaaga dunia"Issa aliyakumbuka hayo maneno akiwa njiani anaondoka.
"Lazima nimsaidie pia nimuoe"alijisemea Issa.
"Oyaa yule deme nimemuona"alisema Issa akiwa na rafiki yake Fikiri.
"Sasa mzee baba nilitegemea kuwa utakuja na kichwa chake ulivyokuwa na hasira"
"Hapana man moyo wangu umempenda"
"Hahahahaha,unanichekesha mzee baba demu mwenyewe kapigwa mimba harafu kakimbiwa eti wewe unataka kumuoa?hahaha"
"Hiyo sio sababu mimi nimempenda hivyo hiyo haijalishi"
"Tatizo hufuatilii mitandao ya kijamii hasa Facebook"
"Kwanini unasema hivyo"
"Kwasababu vijana wamesema wanaweka mgomo kuoa binti aliyezaa kabla ya ndoa,huoni utajiabisha?
"Mzee bado unanichekesha,eti hamuoi mabinti waliozaliaa nyumbani,sasa hao mabinti nani kawabebesha hizo mimba?
"Sisi wenyewe lakini mabinti wengi sahivi tamaa zinawaponza yaani unakuta chips kuku ndo zinasababisha wao kubeba mimba hivi wanakwama wapi hawa dada zetu?http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Nadhani sio wote wako hivyo,hivyo kuliko kuwadhihaki ni bora ungeandika hata kitabu kisambae nchi nzima ili dada zetu waelewe"
"Binafsi nasema kwa msisitizo SIWEZI KUOA MWANAMKE ALIYE ZAA KABLA YA NDOA"
"Hayo yako mimi siangalii binadamu anasema nini,mimi naangalia maisha yangu hivyo FIKIRI kama jina lako.
"Sawa lakini usikute huyo sijui unayemuita demu wako ukakuta kabebeshwa mimba hata kwa chips kavu"
"Huko sasa umefika mbali,hebu tuyaache hayo twende tukapige chandimu"yalikuwa maneno ya ya Issa pamoja na rafiki yake Fikiri.Fikiri alionekana kumpinga vikari rafiki yake, lakini moyoni alikuwa anampenda sana Glory.
Suzi kila alipokuwa anarudi nyumbani alikuwa akimletea mama yake zawadi mbali mbali.
"Mama hapa tumeramba dume"alisema Suzi huku akizitoa pesa alizokuwa amepewa na Daudi.
"Kwanini unasema hivyo mwanangu"
"Mama angalia zote hizi,sijui tuachane na kazi ya umama ntilie tuwe tunatumia hizi pesa?aliongea Suzi akitaka eneo walilokuwa wanauzia chakula kupauza kabisa,mama yake hakupingana naye moja kwa moja alitafutwa mteja kisha eneo hilo likauzwa kabisa.basi wakifurahi wote,pesa waliyokuwa wakiipata walikuwa wakienda kwenye vilabu vya pombe na kuzichezea walivyokuwa wanataka.
"Mama tumia pesa,hapo kwa Daudi ni kuchota pesa,hivyo tumia mama yangu usiwe na kigugumizi"aliongea Suzi huku akimwaga bia chini,kila pia aliyokuwa anaifungua aliishia kunywa mara moja na kumwaga kabisa.
"Hawa machangudoa sijui nani kawahonga pesa ya kuchezea kiasi hiki"alijiuliza mwanaume mmoja alipoona Suzi na mama yake wakimwaga bia.
Hadi inafika asubuhi Suzi na mama yake walikuwa bado wanakunywa pombe.siku zilisogea huku maisha yao yakiwa ni yale yale,Daudi hakuwa na tatizo la pesa kabisa,kila pesa alizokuwa anahitaji Suzi alikuwa anapewa.
"Sasa hapa kwa mtoto nimemaliza bado kwa mama yake,lazima niwe kuku na mayai yake"alijisemea Daudi huku akimpigia mama Suzi simu.mama Suzi hakuchelewa ndani ya dakika kumi na tano alikuwa tayari yuko na Daudi.
"Hapa lazima nimeze vidonge saba"alijisemea Daudi huku akitoa vile vidonge na kuvimeza vyote.
"Vipi mbona dawa zote hizo?aliuliza mama Suzi.
"Huwa nina mambo mengi kichwani,nawaza biashara zangu ndo maana kichwa kinaniuma kwa sana,hivyo hizi dawa zinatuliza kichwa"alisema Daudi akimdanganya mama Suzi.
"Ooh,pole sanaa nipo ntakupa burudani za kukuondoa mawazo"alisema mama Suzi.
"Sawa tukanunue chips huko mbele"alisema Daudi lengo apoteze mda ili zile dawa zifanye kazi.kabla ya dakika arobaini tayari Daudi alikuwa na mama Suzi.
"Hili dume kweli linaweza kukua"alijisemea mama Suzi baada ya kupita masa matatu.
"Naam hii famiria tayari nimeimaliza"alijisemea Daudi huku akitoa pesa na kumpa mama Suzi.
"Mama ulikuwa wapi mda wote huo"alisema Suzi huku akimpokea mama yake mkoba ambaye alikuwa hawezi hata kutembea.
"Nilitoka kidogo,tukafika njiani gari ikahalibika nimechoka sana"
"Pole sana mama pumzika kidogo ili badae tukachangamshe akili"yalikuwa maongezi ya Suzi na mama yake.
"Khaaa,mwanangu ana nguvu kuhimiri mshindo ule"alijisemea mama Suzi alipojiangalia na kukuta anatokwa damu zilizosababishwa na mchubuano.
Ilikuwa siku ya juma tatu,siku hiyo Suzi na mama yake hawakuwa na pesa hasa baada ya kumpigia Daudi simu na kuwaambia kuwa yupo jiji mwanza kibiashara.hivyo wote walishinda ndani.
"Sasa mama hapa tutaishi vipi"Suzi alimuuliza mama yake.
"Usiwaze pesa tutapata ondoa hofu,alisema mama Suzi na kutoa simu yake akamtumia ujumbe Daudi.
"Nakuja subiri"alisema mama Suzi na kunyanyuka kisha akaondoka,ukweli alikuwa anachati na Daudi na Daudi aliamua kumdanganya Suzi kuwa kaenda jijini Mwanza lengo akutane na mama yake.
"Leo ndo siku ya mwisho kwa nyinyi kuchukuwa hera zangu"alijisemea Daudi akiwa na mama Suzi.
"Hakuna wa kupona hapa lazima tufe wote,mnatoka hapa naenda kuwaambukiza wengine wenye tamaa kama zenu,mwisho wa siku utasikia dunia nzima imeathirika"yalikuwa mawazo ya Daudi.
"Twende tukalewe mwanangu pesa tayari"alisema mama Suzi baada ya kufika nyumbani.
"Mbona ghafla mama hiyo pesa umepata wapi"aliuliza Suzi kwa mshangao.
"Mjini hapa mwanangu,na siku zote mtoto wa mjini hawezi kulala njaa labda atachelewa kula,twende tukatumie pesa"aliongea mama Suzi.
Kadri siku zilivyokuwa zinasogea ndivyo Daudi alizidi kubadilika,hakupokea simu ya Suzi wala ya mama yake,mwisho kabisa alifunga namba zao kila walipokuwa wanapiga walikuta inatumika.maisha yao yalianza kuwa ya shida sana,ule mgahawa uliokuwa unawaingizia pesa walikuwa tayari walishaiuza.kila mtu alianza mbinu yake ya kutafuta pesa.
"Niko tayari kukuoa,lakini kwanza tukapime tujue afya zetu ndipo tutaishi wote"yalikuwa maneno ya mwanaume akimwambia Suzi.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Hicho tu niko tayari twende hata sasa"alijibu Suzi kwa kujiamini sana.baada ya kufika kwenye hospital ya Maunt meru walifanya vipimo.
"We kijana huyu binti umeishi naye kwa mda gani?aliuliza dakitari.
"Sijaishi naye bado nimeamua kwanza tufanye vipimo ndo niishi naye"alijibu yule mwanaume.
"Vizuri sana,wewe binti kabla ya hujaonana na huyu kuna mtu uliwahi kuishi naye?aliuliza yule daktari huku akimgeukia Suzi.
"Ndio ila tuliachana"alijibu Suzi.
"Ok,pole sana lakini kupata huu ugojwa sio mwisho wa maisha hivyo nafasi ya kuishi bado unayo"aliongea yule daktari,bado Suzi alibaki ameduwaa.
"Ngoja nikwambie kijana,vijana wa sahivi wanashindwa kufanya maamuzi kama haya,kabla hujaoana na mtu ama kushiriki tendo nae lazima kwanza mfanye vipimo kujua afya zenu,hii itasaidia kutopoteza nguvu kazi ya taifa,hongera kwa hilo"aliongea yule daktari,kisha akamgeukia Suzi.
"Pole sana,tayari wewe ni muathirika pia una mimba ya mwezi mmoja,zingatia haya niliyokuandikia kwenye karatasi naamini utaishi kwa furaha na amani,pia kila mwisho wa mwezi jitahidi kuja kupata dawa"aliongea yule daktari kisha akampa karatasi Suzi ambaye alishindwa hata kuipokea alianguka chini,machozi yalimtoka mda kidogo alipata nguvu za kwenda nyumbani.
"Sahivi hakuna mtu wa kumuamini,inamaana leo ningelikwisha kabisa,asante mungu kwa kunipa hii akili"alijisemea yule mwanaume huku akijaribu kumpa moyo Suzi.
"Daudi huyu ndo kayakatisha maisha"alijisemea Suzi huku akikumbuka vidonge alivyokuwa anavimeza Daudi kabla ya tendo.
"Yote haya kanisababishia mama"alijisemea Suzi huku akifuta machozi yaliyokuwa yanamtoka.
"Usilie jaribu kujipa moyo,wengi hapa duniani wanaishi nao lakini maisha yao yanaendelea kama kawaida"yule mwanaume alijaribu kumbembereza Suzi ambaye alikuwa hawezi hata kutembea.
"Mama umeniua,umeniua mama kwanini ulinifanyia vile?aliongea Suzi baada ya kufika nyumbani.
"Nimekuua vipi mwanangu mbona nashindwa kukuelewa"
"Mama mimi siwezi kuishi miaka mingi"
"Ujue sikuelewi Suzi unamanisha nini?
"Hunielewi kivipi mama?wewe sindouliniuza kwa yule Daudi?sindo wewe hapo eti kisa anapesa,siwezi kukuita mama tena wewe nimuuaji"aliongea Suzi huku akitoa machozi mengi.
"Sema basi nini tatizo"
"Tayari mimi nimuathirika pia nina mimba asante kwa kuniua mama,bila wewe nisingelimjua Daudi muuaji kama wewe"mama Suzi baada ya kusikia mwanaye ameathirika moyo wake ulimuenda mbio sana,naye alijua bila shaka atakuwa tayari.
"Ndo maana alikuwa anameza vile vidonge"alikumbuka mama Suzi wakati huo mwanaye akiwa anagaragara chini.
"Lakini lazima nikapime"alijisemea mama Suzi huku akitoka mbio mbio kuelekea hospitalini,huku nyuma alimuacha Suzi akitoa machozi.
"Mama yangu ndo kanisababishia haya,siwezi kuendelea kuishi,hata huyu mtoto aliyeko tumboni najua ni wa Daudi hivyo naye atakuwa mwathirika"alijisemea Suzi na kuingia ndani kisha akafunga kitenge chake juu ya mbao kisha akapanda juu ya kiti kwa lengo la kujinyonga.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment