Search This Blog

Friday, November 18, 2022

UMUTWALI - 5

 





    Simulizi : Umutwali

    Sehemu Ya Tano (5)







    “Nimewaweka eheeh?,” Fatuma akauliza mara ya kuwasili katika wodi walimo kina Donald.



    “Hapa pana, hujatuweka wala nini,” Donald akajibu kwa shida kutokana na kuugulia maumivu ya mshono alioshonwa.



    “Bora, kama sijawaweka. Basi malizia kunywa uji tuanze safari ya kurudi nyumbani,” Fatuma akasema. Kimya kikachukua nafasi, nusu saa ikakamilika Donald akamaliza kunywa uji. Akalazwa kitandani kisha Dada Angel akatoka nje kutafuta usafiri.



    “Kaka, nahitaji usafiri wa kwenda Kimara suca. Sijui utafanya kwa shilingi ngapi hadi hapo?” aliuliza Dada Angel mara baada ya kuonana na Dereva taxi.



    “Ni wewe tu?,” Dereva taxi akauliza.



    “Hapana, tupo watatu.”



    “Oooh, basi kwa kuwa mpo watatu, nitawafanyia kwa kila mmoja shilingi elfu saba. Jumla itakuwa shilingi elfu ishirini na moja tu,” Dereva taxi akapigia debe kazi yake.



    “Kaka, mbona unakandamiza sana. Hebu...fanya punguzo kidogo tu.”



    “Dada yangu, hiyo ndiyo bei yetu. Isitoshe bei imepanda kutokana na hizi mvua kipindi cha mvua barabara ni mbovu kweli.”



    “Hilo nalijua, lakini naomba unipunguzie japo kidogo tu. Kaka.”



    “Basi sawa nitapunguza, utanilipa elfu kumi na nane badala ya elfu ishirini na moja,” Dereva taxi aliongea kwa makubaliano kati yake na Dada Angel.



    Dereva taxi wakakubaliana na Dada Angel, Dada Angel akawafuata kina Donald kule wodini akatoka nao kisha wakapanda taxi kwa pamoja. Dereva taxi akaondoa taxi eneo lile la hospitalini hatimaye akawapeleka mpaka nyumbani kabisa, walipofika tu nyumbani dereva taxi akasimamisha taxi nje ya nyumba ya kina Donald akalipwa pesa na Fatuma. Wakashuka wakaondoka wakamuacha dereva taxi nae akiondoka zake, Dada Angel akapitiliza moja kwa moja chumbani kwake kwa ajili ya kwenda kubadili vazi. Akawaacha sebuleni Donald na Fatuma kipenzi chake wakiongea maongezi ya faragha.



    “Ulikuwa na wasiwasi, nilivyokuwa hospitalini eh?,” Donald akauliza. Kwa kuchombeza ucheshi na furaha kufurahia uwepo wa Fatuma machoni mwake kwa mara nyengine tena.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sanaaa,” Fatuma akajibu. Kisha akafuta machozi ya furaha yaliyokuwa yakimtiririka mashavuni mara baada ya kutokwa machozi pindi alipoulizwa swali na Donald.



    “Wasiwasi wa nini?.”



    “Nilijua nitakupoteza...si unajua ninavyokupenda sasa nikikupoteza katika dunia hii unafikiri nitakuwaje.”



    “Najua unanipenda nashukuru sana kwa hilo...nami nitakupenda milele yangu yote.”



    “Utanipenda milele yote!!!. Je, baba yangu alivyo mkali kama hatotaka unipende mie mwanae, itakuwaje?.”



    “Nitamuhandle tu ataelewa.... Siwezi tumia ubabe sababu ni wajibu wa kila mzazi kumlinda mtoto wake asipite kwenye njia si salama. Maana wanajua wanaume wengi wa sasa ni walaghai wanakupenda ukiwa mbichi lakini wakishakula tunda wakakuzeesha watakukimbia tu,” Donald akaeleza vema sana. Kisha akatulia tuli pale sofani, akamuangalia kipenzi mwishowe akatabasamu mara baada ya kuangaliana ana kwa ana na Fatuma.



    Dakika kadhaa kupita Dada Angel akawa kasharudi sebuleni akiwa na glasi mbili za juisi ya Embe. Akawakabidhi glasi za juisi Donald na Fatuma kisha akaungana nao kwa kuketi nae sofani, Fatuma alipomaliza kunywa kinywaji akatulia kidogo masaa mawili kupita akaaga kisha akaomba asindikizwe. Donald akajikongoja taratibu akamsindikiza hadi kwenye geti kuu, hakumsindikiza mbali sababu hakupona kabisa.



    “Kipenzi changu, ngoja leo niishie hapa maana mwili wangu bado haujawa na afya nzuri,” Donald akasema.



    “Najua, naomba rudi sasa ndani mimi nitafika tu nyumbani,” Fatuma akaamuru. Donald kweli akasikia akarudi ndani.



    Fatuma sasa akaelekea katika kituo cha daladala kwa ajili ya kupanda daladala ili ajirudishe nyumbani akapumzike. Fatuma akapanda daladala baada ya kufika katika kituo cha Suca akaja kuwasili nyumbani yapata usiku wa saa mbili, akamkuta mama yake amekaa sebuleni akisoma gazeti la UWAZI.



    “Shikamoo mama'angu,” Fatuma akasalimu.



    “Marahaba.... Habari,” Mama Fatuma akachangamkia salamu ya mtoto wake.



    “Salama tu.”



    “Vipi huko utokapo?” aliuliza Mama Fatuma mara baada ya kusalimiana na mwanae.



    “Safi tu, na sasa rafiki yangu yupo poa ameruhusiwa nyumbani. Anakusalimia.”



    “Nashukuru sana...lini atakuja kwetu?.”



    “Ipo siku nitamleta usiwe na wasiwasi.”



    “Basi vizuri.... Hivi na yule baba'ake kesi yake inasomwa lini?, maana kimya kingi.”



    “Unamzungumzia Mr. Msungu, si ndiyo?.”



    “Hata jina lenyewe nimelishika vizuri basi. Nahisi ndiye huyo huyo.”



    “Mr. Msunga kesi yake. Mungu akipenda inasomwa 8/06 mwaka huu.”



    “Kumbe!!!, kesi yake mwaka huu...na kumbukizi ya mama'ake. Je, lini?.”



    “Ni 17/05 Ijumaa ya mwaka huu, halafu mama ngoja nikapumzike maana nimechoka.”



    “Lakini ulipotoka ushakula?...kama bado chakula kipo mezani pale dinning.”



    “Kuhusu kula, usijali nitakula hata kesho. Ngoja nikapumzike tu,” Fatuma akaongea. Hatimaye akamuaga mama yake kisha akaongoza chumbani.







    Wakati fulani Donald akiwa amelala akashtuka kitandani akateremka kitandani taratibu akarudi tena sebuleni alipomuacha wakati ule Dada Angel, akafika lakini safari hii hakumkuta Dada Angel sebuleni bali akakuta runinga haijazimwa. Akaizima mwisho akaenda kwenye sanduku la marehemu mama yake lenye vitabu akachukua kitabu kisha akaketi sofani, baada ya kuchukua kitabu cha Mwandishi Irene Mwamfupe kilichotambulika PADRI MLA NYAMA ZA WATU ambacho kimejaa uchawi wa kutisha. Akiwa ametulia sofani akijisomea kitabu mara simu ikaita haraka akapokea baada tu ya kugundua aliyepiga ni Amina.



    “Niambie shem,” Amina akamchangamkia Donald.



    ”Sina cha kusema,” Donald akaongea kimkato.



    “Umenisusa.”



    “Sijakususa shem, ni matatizo tu ndiyo yanayotuweka mbali.”



    “Matatizo yapi?.”



    “Nimerudi kutoka chuo, nikakuta mama amefariki katika mazingira ya kutatanisha. Basi nikawa bize kushughulikia baadhi za taratibu.”



    “Mh. Aisee, pole sana.”



    “Asante shem.”



    “Lakini shem. Pamoja na yote kuna kitu nahitaji kukuambia.”



    “Kitu gani?.”



    “Kitu chenyewe nahisi si kikubwa sana.”



    “Sawa niambie sasa.”

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Utanielewa?.”



    “Mbona unaniacha njia panda, si useme.”



    “Nitasema...ujue Donald kipindi kirefu tu nami nilikuwa nakupenda sana hadi sasa nakupenda. Nahitaji kuwa nawe Donald.”



    “Eti nini!!!?.”



    “Nakupenda Donald.”



    “Sasa Amina, leo ndiyo umeona siku sahihi ya kuniambia maneno yako?.”



    “Ndiyo Donald, naomba nikubalie na wala usinifikirie vibaya kuhusu hili. Nimeshindwa kujizuia.”



    “Lakini Amina, itawezekana vipi wakati wewe mwenyewe unajua kama mimi na rafiki yako tunapendana kiasi gani. Sasa kwanini unataka kuniweka majaribuni?.”



    “Sikuweki majaribuni Donald...lakini mimi nami ni mwanamke kama wanawake wengine nahitaji kupendwa kama wanawake wengine. Hivyo siwezi kuzuia kirahisi hisia zangu kwa mtu nimpendae.”



    “Sikatai unapaswa upendwe, ila kwangu mimi nishampenda mwingine, ukweli umechelewa jaribu kwingine.”



    “Ina maana unanikataa Donald?, kwaajili ya Fatuma tu...si ndiyo?.”



    “Ndiyo, nampenda sana Fatuma.”



    “Sawa tu.”



    “Ni sawa.... Pia mimi kama shem wako yakupasa uniheshimu nami nikuheshimu,” Donald akakata simu. Akakatisha mazungumzo kabla hayajaisha, baada ya kukata simu ghafla akaonekana kama kuchanganyikiwa na kuelemewa na msongo wa mawazo.



    “Amina ananitakia nini?,” Akajifikiria.



    “Lengo lake ni nini hasa?...ananipenda kweli?. La hasha!, naona hanipendi bali ananitamani tu.”



    “Hata hivyo wanaume si wengi. Si ampende mwanaume mwingine hadi anipende mimi tena.”



    “Itawezekana vipi?.”



    “Kwangu haitowezekana nitakuwa na msimamo huu, sitobadili maamuzi ng'o. Nitampenda mwanamke mmoja tu ambaye ni Fatuma tu na si mwingine,” Donald akatoka kwenye kufikiri kwa kukatisha baada ya kusikia sauti ya Dada Angel ikimuita huku akimtikisa mabega mara baada ya Dada Angel kurudi tena sebuleni.



    “Donald, Donald,” Dada Angel akaita kwa ustaarabu.



    “Eenhe!!!,” Donald akaitika kwa mshtuko. Akashusha pumzi kwa nguvu akaendelea na maongezi.



    “Umenishtua sana.”



    “Samahani.”



    “Usijali.”



    “Donald, sasa mbona unaonekana kama haupo sawa?.”



    “Kweli sipo sawa.”



    “Ni nini shida?.”



    “Kuna kitu cha binafsi kinanitatiza.”



    “Pole sana...najua unapitia katika wakati mgumu sana pindi mama yako alipofariki.”



    “Saaana.”



    “Basi jizuie hiyo hali isitokee. Inakupasa uwe mkakamavu kwa hili usiwe mpweke sana ukaona dunia inakuendea mrama.”



    “Sasa itanibidi niwe hivyo, bila hivyo tatizo kubwa litatokea kwangu.”



    “Kweli kabisa...sasa ngoja nikuache naenda chumbani kwangu kukunja nguo.”



    “Sawa...acha nami niendelea kusoma kitabu changu,” Wakaagana kisha Donald akaendelee kusoma kitabu mara tu Dada Angel alipokwenda chumbani kukunja nguo.



    **********

    Masaa kadhaa usiku Fatuma akaamka kutoka kitandani kiu ikamshika akatoka chumbani akaelekea sebuleni kunywa maji. Baada ya kunywa akarudi tena chumbani kujilaza, akajilaza hatimaye akazama ndotoni na moyoni akajisemea bila kukiwekea maanani anachosema.



    “Nakupenda Donald, naomba usijiue bado nakuhitaji katika mtima wangu,” Fatuma akaongea.



    “Acha nijiue tu. Yaani unanipenda lakini mimi leo hii nakusaliti, aibu yangu nitaficha wapi?.... Acha nife tu,” Donald akazungumza. Mwishowe akajiachia katika ghorofa la tano. Akadondoka puuuuu!!! papo hapo akaaga dunia.



    “Mamaaaaaaa!!!,” Fatuma alipiga ukunga mfululizo bila kujali mara baada ya kushtuka katika ndoto ile. Ule ukunga ukasikika katika ngoma za masikio ya Mama Fatuma akashtuka usingizini haraka akakimbilia chumbani kwa Fatuma.



    “Fatuma,” Mama Fatuma akaita mara baada ya kufika chumbani kwa Fatuma.



    “Abeeeh!!!,” Fatuma akaitika kinyonge.



    “Mbona umepiga kelele usiku huu. Kuna nini?.”



    “Ni ndoto nimeota ni mbaya. Kweli.”

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Inamhusu nani?.”



    “Inamhusu Donald.”



    “Kafanyaje?.”



    “Nimeota Donald anajiua kwaajili yangu.”



    “Kisa?.”



    “Kisa kanisaliti. Nimeshindwa kumsamehe”



    “Kwani una malengo nae. Kweli?.”



    “Ndiyo, tena nampenda sana.”



    “Basi kama unampenda naamini nae anakupenda. Hawezi fanya hivyo, hiyo ni ndoto tu si kweli. Isikuumize kichwa.”



    “Sawa mama, nimekuelewa. Nalala sasa.”



    “Lala.... Usiku mwema.”



    “Na wewe pia, mama,” Fatuma aliaga akalala. Mama Fatuma akamfunika mwanae shuka na kumtegea chandarua vizuri mwishowe akarudi chumbani nae kuendelea na kulala.



    **********

    Hakujapambazuka vizuri Donald akaamshwa na mlio wa simu, akajivuta vuta kivivu pale kitandani akaamka akajaribu kuangalia kioo cha simu kwa muda tena kwa shida kutokana na mawenge ya kuamka. Akaona namba inayopiga ngeni akafikiri kwa sekunde itakuwa ya nani lakini hakuweza kutambua, hivyo akajipa ujasiri apokee ile kupokea tu mshtukizo akasikia sauti ya mwanamke yenye mkwaruzo kiasi na besi ajabu ikiwa kwenye muonekano wa jazba.



    “Naongea na Donald?,” Sauti ile ya mwanamke ikauliza mara baada ya Donald kupokea simu na kusikiliza kwa heshima.



    “Hujakosea, ndiye mwenyewe,” Donald akajibu.



    “Sasa wewe kijana, unaona raha sana ukiona mwenzako akilia na kuteseka kwa ajili yako?,” Ile sauti ya yule mwanamke ikazidi kuuliza maswali na kuacha sintofahamu kwa Donald.



    “Siwezi kumliza mtu wala kumtesa kwa ajili yangu. Wewe ni nani?,” Donald akajibu. Hatimaye nae akauliza huku akionyesha ishara ya uwoga kidogo.



    “Mimi ni Bibi Amina. Upo hapo?,” Bibi Amina akajitambulisha.



    “Oooh!!! shikamoo, bibi.”



    “Sina haja na salamu yako kwa sasa, sina.”



    “Mbona sielewi, bibi.”



    “Huelewi nini mfano. Amina wewe ulimjibuje hadi anafikia hatua hii ya kutaka kujiua.”



    “Kujiuaaa!!!, yaani anataka kujiua kisa mapenzi. Mbona sasa yeye analeta mapya tena.”



    “Unashangaa eenh, unadhani ni mazuri?.”



    “Sio.”



    “Sasa?.”



    “Lakini bibi.... Amina mie nishamueleza ukweli kuwa mimi ninaye nimpendae. Mbali ya hivyo Amina mwenyewe anajua fika kama nina mpenzi ambaye tunapendana kupita maelezo, sasa yeye kwanini ananing'ang'ania?.”



    “Lakini nawe si unajua kuwa mapenzi yanaua kama unajua hilo, naomba fikiria ni jinsi gani ya kumsaidia mjukuu wangu.”



    “Sasa bibi mie nitamsaidia vipi Amina...nishasema kuwa mie siwezi kuwa nae. Yeye ni rafiki wa mchumba wangu, sasa hapo bibi huoni kama nitakuja vunja urafiki wao.”



    “Kwani wewe ni mtoto. Si itakuwa siri ili Fatuma asijue kinachoendelea na Amina nae hasiweze kujiua.”



    “Kwa hilo sitoweza. Mimi nampenda sana Fatuma na hivi karibuni, mimi na yeye tunataka tufunge ndoa. Hivyo Amina kwangu hana nafasi...kwa heri bibi. Utanisamehe na nakutakia siku njema,” Donald akakata simu. Akajilaumu kidogo kwa kuona kama mikosi inamwandama kisha akarejea kujipumzisha.



    **********

    Bibi Amina hakuwa na chaguo akakubaliana na matokeo na msimamo wa Donald, katu hakujaribu tena kushawishi na kuchochea ili Donald ampende Amina. Siku ifuatayo asubuhi akatoka chumbani kinyonge akajikongoja mpaka sebuleni akaketi kitini kitabu tabu kisha akamuita mjukuu wake aje amsikilize asemacho.



    “Amina, huyu kijana hakupendi kwanini usiachane nae tu, ukamtafuta yule mtu akupendaye. Wanaume wapo wengi tena ni wazuri kushinda yeye.... Fanya hivyo mjukuu wangu, nawe utakuwa na furaha baadae. Usijiue,” Bibi Amina akashawishi, na Amina akashawishika na maneno ya bibi'ake.



    “Nimekusikia bibi, acha nifanya hivyo.... Nitatafuta upendo kwengine. Wao nitaacha waendelee na maisha yao. Na kuthibitisha hili dhahiri siku ya harusi yao nitajumuika nao,” Amina akakubali.



    “Safi kabisa.... Sasa hiyo ndiyo moja ya tabia njema tunayojivunia sisi waislamu. Upendo kwetu ndiyo nguzo yetu. Asante sana mjukuu wangu ama kweli umekua sasa,” Bibi Amina akapongeza, kisha akarudi chumbani kwa ajili ya kwenda kuanza shughuli za ndani.



    **********

    Ikapita miezi kila kitu Donald akasahau akaanza kurasa mpya yeye na Fatuma. Juma moja vichwa viwili vikashirikiana mawazo, yeye na Fatuma wakashauriana kuwa wakati wa Donald kwenda kujitambulisha ushawadia, hivyo Donald aende kwa wakwe akajitambulishe taratibu zingine zifuate. Kweli Donald akapokea ushauri akaambatana na mshenga wakaenda kwa wakwe, walipofika wakapokelewa na wakwe lakini si kwa mapokezi ya uchangamfu labda kwa kuwa Donald alivaa rafu au kwa kuwa alikuwa anabwabwaja sana kwa wakwe maana walikaribishwa kibandidu. Baba mkwe akawa kauzu na Mama mkwe akawa nununu awakuonyesha hata tone la furaha kwa wageni.





    Ndani ya dakika kumi wenyeji wakawa bado wamenuna wamebaki wakiwakata jicho tu kina Donald hata kusema karibu kwa ucheshi hamna. Dakika zikayoyoma hapo ndipo sura ya Mama Fatuma ikaangaza tabasamu kwa mbali na akashindwa kujizuia kufurahi, akafurahi mbele ya ugeni papo hapo akawachangamkia wageni.



    “Karibuni sana,” Mama Fatuma akakaribisha kwa furaha kubwa. Donald na mshenga awakujizuia kupandisha na kushusha pumzi polepole maana walikuwa na wasiwasi pamoja na hofu wakijua jiko washalikosa, hapo sasa wakaketi kwenye kiti kwa furaha na starehe huku katika vinywa vyao wakionekana kuchanua kwa ajili ya tabasamu bashasha.



    “Asante, mama.... Habari,” Wote wakaitika. Kisha Donald akasalimu huku akiambatanisha na furaha moyoni mwake.



    “Eehe, tuwasaidie nini?,” Mama Fatuma akauliza.



    “Mwenzangu hapa ni Mzee Tanza, yeye ni mshenga. Nami naitwa Donald,” Donald kwanza akajitambulisha kwa wakwe wamjue.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Oooh, kumbe ni wewe Donald, nasikiaga tu mwanangu akikuzungumzia,” Mama Fatuma akaongea huku akiwaangalia Donald na mshenga kana kwamba anawatathimini na kuchunguza chochote kitu.



    “Aaah, basi ndiye mie Donald Mtalanze.”



    “Ooh, stori zako nyingi nazipata kwa mwanangu Fatuma.”



    “Shukrani sana mama.... Mama, hivi Fatuma mwenyewe yupo?.”



    “Yupo, ngoja nimuite aje,” Mama Fatuma akasema punde akamuita mwanae.



    “Abeeh,” Chumbani sauti ya Fatuma ikasikika ikiitika wito, haikupita dakika sekunde tu Fatuma akawa kashawasili sebuleni kwa ajili ya kusikiliza wito wa mama yake.



    “Mwanangu, ugeni huu umekuja kwa ajili yako nahisi. Kaa chini tuwasikilize wageni,” Mama Fatuma alimwambia mwanae mara baada ya kuona Fatuma ameshaketi kitako anasikiliza ujio wa Donald.



    “Jamani, wazee. Nimekuja kwenu leo na mshenga ili nijitambulishe mnifahamu na taratibu zengine ikiwezekana zifuate. Kwa majina mimi ni Donald Mtalanze kama nilivyojitambulisha hapo awali, nami ndiye mchumba wa mwanenu. Na ukweli ni kwamba nampenda mwanenu sana hivyo ningeomba ruhusa yenu kama wazazi, niweze kuoana nae mwanenu,” Donald akajieleza kwa ufasaha na akaonyesha furaha akimaanisha anapenda anachotaka kufanya kwa huu wakati. Lakini baada ya kujieleza na wakwe kusikia ghafla Baba Fatuma akavunja ukimya aliohifadhi kwa muda kidogo akakunja ndita akaongea kwa ukali kana kwamba kiziwi anatoa taarifa hatarishi kwa mlengwa.



    “Hili suala ni la muda gani?. Mbona mimi kama baba nilikuwa sijui.... Najnat, unalifahamu hili?,” Mzee Kandir akafoka hatimaye akageuka upande alipo mkewe akamuuliza vile vile kwa kufoka.



    “Nalifahamu, ila sikutaka kukueleza mapema nilitaka hadi hapo mwenyewe uje kutambua. Na sasa ushatambua, fanya maamuzi,” Bi. Najnat akajibu kwa heshima. Hakumvunjia heshima mumewe.



    “Maamuzi yapi?.”



    “Si ya kuwakubalia watoto, hitaji lao.”



    “Kuwakubalia!!!, wewe mwanamke vipi?. Unachukulia suala hili ni la kubwabwaja bwabwaja tu au ni la kumpeleka peleka mtoto tu popote.... Mimi kama Baba Fatuma siwezi kumuozesha binti yangu kiholela holela, kwanza leo mmenishtukiza. Aisee, kijana pamoja na mzee mwenzangu naomba mje siku nyengine,” Mzee Kandir alimaliza kufoka. Akapinduka alipo Donald na Mzee Tanza akawaamuru waondoke kisha yeye akaingia chumbani akanyuka mavazi akatoka kwa jazba akaondoka anapotambua mwenyewe.



    **********

    Mzee Kandir akafika anapopatambua mwenyewe, akabisha hodi geti mara punde tu anafunguliwa geti na mlinzi wa nyumba ile wanaonyesha kufahamiana wanasalimiana hatimaye. Mzee Kandir anaruhusiwa kuingia mpaka ndani kufika ndani sebuleni anaonekana kusalimiana na kijana mmoja hivi ambaye si mchezo anaonekana mwenye mawe ya kutosha, kwanini nasema hivyo kwa kuwa kijana yule mwili mzima alivaa pesa tu. Shingoni alivaa cheni ya dhahabu, mkononi alivaa saa ya dhahabu, vidoleni alivaa pete za dhahabu, alijipulizia marashi ghali, kwenye meno alijiweka meno ya dhahabu na kwenye nguo sasa alivaa nguo kama si za laki mbili basi ni za laki tatu. Mzee Kandir akakaribishwa kwa furaha na yule kijana akaletewa mpaka kinywaji anywe, Mzee Kandir akapiga fundo moja ya glasi ya juisi aliyoletewa kisha akaweka glasi mezani akakohoa mfululizo hatimaye akaanzisha mazungumzo na yule kijana.



    “Kijana.”



    “Eehe, niambie. Mkwe.”



    “Unataka kuoa, kweli?.”



    “Mzee, sasa swali gani hilo?. Ningekuwa sitaki kuoa hata posa ningetoa.”



    “Posa kutoa si tatizo unaweza kutoa posa, lakini ukatelekeza mzigo wako.... Hivyo basi mguu huu nimekuja kukukumbusha tu haraka uje uoe, chelewa chelewa utakuta mwana si wako.”



    “Mzee, nimekusikia. Nipe two weeks nitakuwa nishakuja kuoa.”



    “Two weeks iwe kweli.... Mie naenda tutaona tena,” Mzee Kandir akaaga. Yule kijana akamsindikiza mzee wake mpaka getini wakaachana pale, Mzee Kandir akarudi nyumbani na Kijana Sefu bin Zerunga kama atambulikanavyo na majirani kutokana na mali alizoachiwa na marehemu babu yake nae akarudi ndani kuendelea kutazama runinga.



    **********

    Baada ya kutimuliwa Donald na mshenga wake, wakaondoka kinyonge wakajikatia hadi tamaa. Huku wakamuacha Fatuma nae akiwa na majonzi na haraka akakimbilia ndani kujifungia mlango, akajifungia mlango mpaka majira ya jioni aliporudi baba yake ndipo akatoka aliposikia sauti ya baba yake sebuleni akiongea na mama yake. Akamfuata baba yake akakaa kando yake kwa upendo akaeleza hisia zake juu ya Donald.



    “Baba, kwanini umefanya vile?. Unajua jinsi gani nampenda Donald na unajua tumepanga mambo mangapi na Donald, Baba hebu.... Kuwa na utu kidogo. Mimi yule ndiye nimpendae na sio huyo uliyemchagua wewe, nampenda Donald mimi. Niache niwe nae” alisema Fatuma huku machozi yakimtiririka mashavuni, lakini yeye hasijali hata kuyafuta.



    “Kelele, mimi ndiye kichwa cha familia nikipanga jambo lazima lisikilizwe. Nishasema Sefu ndiye atakayekuoa imeisha.... Sio hapa unaniletea sijui Donald. Donald na sisi wapi na wapi, yeye ni mkristo na sisi waislamu. Sasa wewe nikuozeshe kwa mkristo nani anataka biashara hiyo. Wewe utaolewa na bin Zerunga basi,” Mzee Kandir akang'aka hatimaye akanyanyuka kitini pale sebuleni akaelekea chumbani, kufika katika mlango wa chumbani akalaumu akasonya sonyo takatifu. akafungua mlango akaingia chumbani akabamiza mlango wa chumbani kwa jazba mwishowe akaenda kujitupa kitandani mwenyewe, akajitenga ili atulize akili kwa kutosikiliza ngenga ya familia yake.



    **********

    Wiki mbili ikafika na ikapita. Mzee Kandir akiwa sebuleni pamoja na familia yake wakitazama runinga mara Bi. Najnat akaomba kwa mumewe amuweke kipindi cha ITV SUPER BRAND ili atazame taarifa ya habari ya saa mbili usiku, kweli bwana Mzee Kandir akamtii mkewe akaweka kipindi cha ITV kuweka tu wakakuta habari za kimataifa zinaanza. Na habari ya kwanza yenyewe ikawa ni gumzo kwa Mzee Kandir pindi alipomsikiliza na kumuona mtangazaji habari akitangaza ile habari ya wakati ule ya kusikitisha akiwa kwenye masikitiko na majonzi.



    “Dar es salaam, mjini Dar es salaam. Eneo la Osterbay B, natangaza kuwa majambazi sugu watatu wamevamia nyumba ya wadhifa. Ya kibopa mmoja hivi ambaye aliyekuwa bado kijana mdogo, umri wake unaosadikika kwa makadirio kuwa atakuwa na miaka 25 au 28. Kijana huyo aliyetambulika kwa majina ya Sefu bin Zerunga alivamiwa na majambazi hao usiku wa kuamkia jana, kijana Sefu na mlinzi wake wakauwawa na majambazi hao kwa kupigwa risasi kichwani zinazotoka kwenye bastola aina ya Durgun 412 na kupoteza maisha papo hapo mara baada ya kuibiwa vitu vya thamani na majambazi hao. Mkuu wa polisi wa kituo cha polisi cha Osterbay, anasema kuwa kwa sasa bado wapo kwenye uchunguzi. Kuchunguza waharifu wapi wanapoishi na wapi wanapopatikana kwa urahisi, Mkuu wa kituo huyo akamaliza na kusema kuwa endapo wakafanikiwa kuwapata majambazi hao mara moja watakamatwa na moja kwa moja watafikishwa mahakamani,” Taharuki ikajengeka katika kinywa cha Mzee Kandir, mdomo akaacha wazi mithili ya Mamba anapovizia Nyumbu mara tu baada ya kumaliza kusikiliza na kuona habari ile kwa kina. Mzee Kandir punde akajilaza kichwa kitini akafikiri akawaza akawazua mara akainuka na wazo jipya kwanza akakohoa kikohozi cha kubanja mfululizo kinafiki.





    “Fatuma, bado unampenda Donald?,” Mzee Kandir akauliza.



    “Baba, mie nampenda Donald. Leo kesho nahitaji tuwe mume na mke,” Fatuma akajibu huku akionekana maneno yake yale akiyapendezesha na tabasamu la mbali.



    “Basi naomba kesho, mwambie mwenzako aanze taratibu za kukuchumbia. Umenielewa?.”



    “Nimekuelewa baba. Asante sana,” Fatuma akajibu kisha kwa upendo akamkumbatia baba yake mwishowe upesi akakimbilia chumbani. Akachomoa simu chaji akamtwangia Donald akamueleza yote yaliyojiri nyumbani kwao, Donald hilo akaliweka akilini kesho yake bila kuchelewa yeye na mshenga wakaingiza maguu kwa Mzee Kandir huku nyuso zao zikiwa zimenawili kwa furaha zama hii. Walipofika wakawakuta wakwe wapo sebuleni pamoja na mlengwa, safari hii hakukuwa na longo longo walipokelewa kwa ucheshi na heshima zote kama wageni wengine.



    “Habari,” Mzee Tanza alisalimu wazee wenzake mara baada ya kuwasili na kukaribishwa kitini yeye na Donald.



    “Salama tu, kwanza naomba tusamehane sana yaliyotokea awali,” Mzee Kandir akaomba radhi.



    “Mzee mwenzangu, usijali kuhusu lile wote ni binadamu na siku zote hakuna mwanadamu mkamilifu wote tuna mapungufu. Basi naomba ondoa shaka kabisa,” Mzee Tanza akaongea.



    “Shukrani, sasa mie leo sina mengi bali nimewaita ili kueleza kuwa nimeridhia Donald na mwanangu wawe pamoja.... Ila kuna kitu kimoja lazima mfuate,” Mzee Kandir akasema.



    “Kitu gani, mzee?,” Donald akadakia kwa kuuliza.



    “Yakupasa sasa, mshenga aje kukamilisha taratibu” aliongea Mzee Kandir huku akimuangalia mkewe jicho la kichokozi.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hilo halina shida mzee mwenzangu.... Utaratibu wenu kwani upoje?. Maana nyie ni wapemba mwajuana kwa viremba,” Mzee Tanza akachomekea kautani tu kidogo. Utani ule ukabaki kumuacha hoi Mzee Kandir kwa kuangua kicheko kisha akajibu.



    “Mzee mwenzangu, ina maana hujui kifuatacho. Kifuatacho ni kijana wako alete mahari ili mambo mengine yakamilike,” Mzee Kandir akadadavua.



    “Naomba niambie mzee. Mahari yenu ni nini?” aliuliza Donald huku akijaribu kukunja leso na kuweka katika mfuko wa shati.



    “Mwambie mama yako, akutajie,” Mzee Kandir akatoa ruhusa. Donald kwa shauku akamgeukia mama mkwe kisha akalirudia swali alilouliza baba mkwe hapo kabla.



    “Mama. Eti, mahari yenu nini?.”



    “Nitakujibu,” Mama Fatuma alisema kisha macho yake yakaganda kwa Donald kwa muda akimtazama, kisha hatimaye akajibu swali.



    “Mwanangu, mahari zetu ni kama zifuatazo inahitajika; Kanzu, Baibui, Msuli, Ijabu na Milioni tisa tasrimu.”



    “Shukrani, sasa nishajua. Ngoja tuwaache leo ili nikalishughulikie hili suala,” Donald aliongea kisha akaaga wakaondoka.



    Donald akarudi nyumbani akajichanga changa baada ya wiki tu akajikamilisha. Akamtuma tena mshenga apeleke mahari kwa kina Fatuma, mshenga akachukua jukumu lake akapeleka mahari kwa wahusika. Donald ashukuru Mungu mahari imefika na imekubalika na taratibu upesi zikapangwa, siku ya ndoa ikawadia ikafungwa ndoa ya kiislamu mara baada ya Donald kubadili jina pamoja na dini.



    “Mustapha bin Mtalanze, umekubali kufunga ndoa ya kiislamu na Bi. Fatuma binti Kandir?,” Huyo alikuwa ni Sheikh akimuuliza Donald ili apate uthibitisho.



    “Nimekubali,” Donald akajibu.



    “Nawe Bi. Fatuma binti Kandir umekubali kuolewa na Mustapha bin Mtalanze, awe mume wako wa ndoa,” Safari hii swali la Sheikh alilomuuliza Donald likampindukia Fatuma.



    “Nimekubali,” Fatuma akajibu.



    Sheikh akamaliza kufungisha ndoa majirani na ndugu wakatawanyika kurudi majumbani. Mustapha na mkewe wakaianza kurasa mpya ya maisha yao, baada ya mwezi mmoja Mustapha na mkewe wakabahatika kupata kazi japo ni za tofauti. Mustapha akabahatika kupata kazi katika kampuni ya FOUNDATION MASON, kampuni ambayo inahusika na utengenezaji wa majengo katika kampuni hiyo Mustapha wakamuajiri kama Mhandisi Engineer wa majengo. Fatuma nae akabahatika kupata kazi ya ukalani katika kampuni ya GLOBAL PUBLISHERS ambayo inajumuisha Global TV, Global Radio na uchapishaji wa magazeti ya Ijumaa, Uwazi na Champion. Kweli Mungu ni mkuu na ni mwema sababu amejalia Mustapha na Fatuma wapate watoto wawili katika ndoa, akawajalia wapate watoto Husna na Hussein. Mustapha na Fatuma wakawapenda watoto wao kama Almasi kama sio Rubi alizowapatia Mwenyezi Mungu. Usiku tulivu wa siku nyengine Mustapha akiwa amejipumzisha chumbani na mkewe huku wakiwa kwenye maongezi ya faragha na furaha wakakumbuka.



    “Mke wangu, sasa tumetimiza ndoto tulizotaka zitimie,” Donald akaongea.



    “Mume wangu, tumetimiza ndoto nyingi. Sasa wewe sijui unasemea ndoto gani?,” Fatuma akauliza.



    “Si ile tuliyopanga tukiwa shule.”



    “Mh, ndoto gani hiyo. Hebu...nikumbushe.”



    “Si ndoto tuliyopanga ya kuwa wazazi bora...sasa wewe huoni kama tayari tushatimiza.”



    “Nimekumbuka. Naamini kweli tumetimiza ndoto yetu...ila si kwa uwezo wetu yote haya ni kwa uwezo wa Allah, bila yeye sisi tusingekuwa hapa hii leo.”



    “Ni kweli, hivyo basi mke wangu hatuna budi kumshukuru Mungu sisi sote kwa kila jambo. Tulale sasa,” Donald akaongea kisha wakalala.



    **********

    Mwaka mmoja sasa ukatimia Mr. Msunga akaja kusomewa hukumu na jaji mahakamani, akaja kuhukumiwa kifungo cha maisha jela. Mr. Msunga hukumu ile ikamfanya ajilaumu sana.



    “Mimi ni Ibilisi gani?.... Mimi ni Ibilisi yule anayezungumziwa kila kukicha kwa kufanya matendo yasiyompendeza Mungu.”



    “Mali zile sasa zingenipeleka wapi?...si ndiyo hizi zinanipeleka pabaya. Ama kweli mkataa pema pabaya panamuita.”



    “Lakini haya yote yanatokana na tamaa. Bila kuwa na tamaa haya yote yasingenikuta...ama kweli tamaa mbele mauti nyuma.”



    “Ewe, Mwenyezi Mungu naomba toba kwako katika dunia hii kweli nimekosa. Sistahili kabisa hata kusema neno msamaha kwako naona aibu.... Ama kweli asiyesikia la mkuu huvunjika guu,” Mr. Msunga aliendelea kujilaumu sana na kujitupia kila majuto mule gerezani alimokuwepo.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    **********

    Napenda kuwasihi wasomaji na watanzania kuwa tamaa mbaya, tamaa ukiiendekeza inakuweka pabaya. Tamaa ukiiendekeza unakosa mambo yote. Pia nazidi kuwasihi haswa vijana wa kimamboleo kuwa ukimpata akupendae mshike usimwache, ukimwacha wenzako wanachukua. Mkipendana msisalitiane usaliti ni mbaya nao kama gonjwa la ukoma, pendaneni haswaa kama watoto mapacha vile ili wenye roho ya korosho mdomo wabaki kuachama.... Nashukuru sana.



    MWISHO.


0 comments:

Post a Comment

Blog