Search This Blog

Friday, November 18, 2022

YAMENIKUTA SALMA MIE - 3

 






Simulizi : Yamenikuta Salma Mie
Sehemu Ya Tatu (3)


“Tumefika na kaka amepimwa presha”

“Ikoje?’ nikamuulizza haraka.

“Iko juu kidogo lakini daktari ametuambia macho yake hayakutokana na presha”

“Ni nini?”

“Ametuambia ni suala linalohitaji uchunguzi. Ametushauri kesho twende kwa mtaalamu wa macho”

“Sasa mko wapi?”

“Ndio tunarudi”

“Sawa”

Nikakata simu.

Jibu la zacharia lilizidi kunitia wasiwasi na nikahisi kwamba hakukuwa na kingine kilichompofua macho mume wangu isipokuwa ni ile dawa niliyomtilia kwenye maji yake ya kuoga.

Wakati wanafika nyumbani nilijisikia kupata uoga kutokana na ile hisi ya hatia kwamba mimi ndiye niliyempofua

macho mume wangu.

Ibrahim na Zacharia walipoingia ndani Zacharia alikuwa amemshika mkono kaka yake. Akaenda naye hadi lilipokuwa kochi akamkalisha.

“Kaa hapa” akamwambia.

Ibrahim akakaa.

“Mke wangu, daktari tuliyemuendea hakugundua tatizo” Ibrahim akanimbia kabla ya kumuuliza chochote.

Alinyamaza kwa sekunde chache kama mtu aliyekuwa akiwaza jambo kisha akaongeza.

“Ameniambia nisubiri kesho niende nikaonane na mtaalamu wa macho anifanyie uchunguzi”

Nilikuwa nimesimama nikimtazama Ibrahim wakati akizungumza. Kusema kweli nilimuhurumia sana. Nikakaa kwenye kochi lililokuwa karibu naye.

“Salma umenisikia nilivyokwambia?” Ibrahim akaniuliza alipoona nipo kimya.

“Nimekusikia. Tutasubiri hadi hapo kesho kama alivyokwambia huyo daktari mkaonane na huyo mtaalamu wa macho”

“Sijui hili tatizo limetokana na nini?” Ibrahim akauliza kama aliyekuwa akijiuliza mwenyewe kisha akatikisa kichwa kusikitika.

“Kwani kichwa bado kinauma” nikajidai kumuuliza.

“Kwa sasa kichwa kimeacha. Tatizo liko kwenye macho”

“Tusubiri hiyo kesho, sasa mwende mkale chakula”

“Mimi sitakula tena. Nimeshapatwa na wasiwasi”

“Nenda ukale japokuwa kidogo”

“Sisikii tena njaa”

“Unataka ulale hivyo hivyo”?

“Nitalaa tu”

Aliposema hivyo Ibrahim akauelekeza uso wake upande aliosimama Zacharia.

“Zacharia nenda ukale chakula” akamwambia mdogo wake.

“Sasa kaka kwanini wewe hutaki kula?” Zacharia akamuuliza.

“Siwezi. Ile njaa pia sina tena”

“Twende ukale japokuwa kidogo kaka”

“Wewe nenda tu, mimi niache”

Zacharia akamtazama kaka yake kisha akaondoka kwenda mezani.

“Hapa ninawaza mengi, kama macho yangu hayataona tena, kazi zangu nyingi zitaharibika” Ibrahim akaniambia.

Nilikubaliana naye kimoyo moyo.

“Mimi nina imani kuwa ukishughulikiwa na hao wataalamu wa macho utaweza kuona” nikamwambia kumpa moyo lakini moyoni mwangu nilikuwa nimeshapanga kurudi kwa yule mganga kutakapokucha.

Niliamini kuwa kama tatizo hilo limetokana na dawa zake, anaweza kujua jinsi ya kumtibu.

Usiku ule si Ibrahim wala mimi aliyepata usingizi. Nililala nikiwa macho kwa muda mrefu kitandani. Baadaye niliinuka nikaketi kitandani na kuanza kuwaza huku nikimtazama Ibrahim alivyokuwa akijigeuza geuza pale kitandani. Ilikuwa ni dalili kuwa hata naye hakuwa amelala usingizi.

Nikiwa nimeshika tama nilikuwa nikimfikiria mume wangu huku nikijiuliza endapo hatatibika na atabaki kuwa kipofu, nini kitatokea katika maisha yetu?

Kweli tutaweza kupata maendeleo na kuishi maisha ya furaha endapo mume mwenywe atakuwa hawezi kufanya kazi kwa sababu haoni?”

Kwa upande mwingine nilijuta kukubali ushawishi wa Rita wa kwenda kwa mganga kumroga mume wangu. Nilikuwa nikijiambia kama nisingekwenda kwa mganga, macho ya mume wangu yasingepofuka.

Asubuhi kulipokucha nilikwenda kuyafungua yale maji kwenye mita, nikamsindikiza mume wangu bafuni kwenda kuoga. Alipomaliza kuoga nilimuandalia chai. Akanywa pamoja na mdogo wake.

Muda wa kwenda hospitali ulipowadia nilimwambia kuwa baadaye nitatoka kwenda sokoni. Nilimwambia hivyo kwa makusudi ili kama watawahi kurudi na kunikosa wajue kuwa nimekwenda sokoni. lakini lengo langu lilikuwa ni kwenda kwa yule mganga.

Ibrahim na Zacharia walipoondoka, na mimi nikatoka. Sikutaka kwenda kwa Rita. Nilikwenda kwenye kituo cha bodaboda nikapakiwa kwenye pikipiki na kuelekea Kisosora.

Nilipofika niliitafuta nyumba ya yule mganga hadi nikaigundua. Nilimwambia mwenye bodaboda anisubiri. Nilipokwenda kwenye kile kibanda cha mganga sikukuta mtu yeyote nikapiga hodi.

“Pita ndani” sauti ya mganga ikasikika kutoka ndani.

Nikaingia. Nilimkuta mganga ameketi akikatakata vipande vya mizizi.

“Shikamoo” nikamwamkia.

“Marahaba. Habari ya tangu juzi?”

“Ni nzuri kama si nzuri”

“Kwanini?”

“Nimefanya makosa. Ile dawa ambayo uliniambia nimtilie mume wangu kwenye chakula niliikosea nikamtilia kwenye maji ya kuoga”

“Eh! Ile dawa haitaki povu la aina yoyote. Kama alioga na sabuni inaweza kumletea matatizo”

“Ndiyo hivyo, alipomaliza kuoga akanimabia haoni…”

“Haoni mpaka hivi sasa?”

“Haoni. Dawa yenyewe nilimtilia jana, siku ile uliponipa alikuja mgeni nyumbani nikashindwa kumuwekea”

Mganga akanyamaza kimya. Uso wake ulionesha kuwa ile habari ilikuwa imemshitua.

“Sasa sikiliza, njoo kesho. Kuna dawa nitakwenda kukuchumia umfikichie kwenye macho yake”

“Nije kesho saa ngapi?”

“Njoo asubuhi. Nitakwenda kuichuma leo jioni”

“Sawa, basi nitakuja kesho asubuhi”

Nilipomaliza kuzungumza na mganga huyo nikamuaga na kuondoka. Nilipofika kwenye mlango niligeuza uso wangu nikamtazama. Nilimfuma alikuwa akinitazama kwa nyuma kwa jicho ambalo halikuwa la kawaida. Sikuweza kujua alikuwa ananifikiria nini.

Mwendesha bodaboda alikuwa akinisubiri. Nikajipakia tukaondoka. Nilipitia sokoni nikanunua nilivyonunua na kurudi nyumbani. Ibrahim na mdogo wake walikuwa hawajarudi. Nikaanza kupika.

Kidogo yale maelezo ya yule mganga kwamba atanipa majani ambayo nitamfikichia mume wangu machoni mwake, yalinipa matumaini.

Nikawaza sasa jinsi ya kumfikichia hayo majani machoni mwake. Nikajiambia itabidi nimueleze kwamba nimepewa majani hayo na mtaalamu wa kienyeji na ameniambia kuwa yanaweza kukusaidia.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Ibrahim na Zacharia walirudi majira ya saa sita mchana. Ibrahim akanieleza kuwa amefanyiwa uchunguzi na macho yake yamegundulika kuwa hayakuwa na tatizo.

“Nimepewa dawa hizi nitumie kwa siku tatu” akaniambia.



Nilipoingia ndani nilimkuta mume wangu amekaa sebuleni peke yake. Zacharia hakuwepo.



“Habari ya hapa?’ nikamsalimia.



“Nzuri, mbona umechelewa sana?”



“Nilikwenda huko kwa mama yangu. Kuna mtabibu pale mtaani kwetu amenipa dawa nije nikufanyie”



“Dawa gani?”



“Dawa ya majani. Ameniambia nikufikichie kwenye macho kwa siku tatu”



“Haya tujaribu”



“Ameniambia nikufanyie asubuhi na jioni. Asubuhi imeshapita tusubiri jioni tuanze”



“Unanifikichia vipi?”



Nikamueleza vile nilivyoagizwa na yule mganga.





“Haya utanifikichia tujaribu”



“Amenihakikishia kuwa itakusaidia”



“Lakini haiwashi machoni?”



“Hakuniambia lakini nafikiri haiwashi kama inawasha angeniambia”



Baada ya hapo niliingia jikoni na kuanza kupika. Ile dawa niliitunza mahali pazuri ambapo ingeweza kukaa bila kukauka.



Ilipofika jioni nilichomoa majani matatu ya dawa hiyo nikaenda sebuleni ambako mume wangu alikuwa amekaa nikamwambia alale chini kichalichali ili nimfikichie machoni.



Mume wangu aliondoka kwenye kochi alipokuwa ameketi akasogea mbele kidogo na kukaa chini kisha akajilaza kichalichali.



Nilichutama  na majani yangu nikayashika na kuyafikicha kabla ya kumkamulia machoni mwake.



Maji maji yaliyotoka kwenye  majani hayo yalipomuingia machoni alifumba macho.



“Usifumbe macho, yafumbue” nikamwambia. “Yafumbue dawa ikuingie vizuri”



Akayafumbua kiuoga.



“Fumbua bwana!”



“Nimeshayafubua”



“Bado, fumbua zaidi”



Macho yake yalikwishakuwa maoga. Alishindwa kuyamfumbua sawa sawa.



Nikamkamulia majani majani hayo hivyo hivyo. Maji maji machache yalimuingia machoni, mengine yalichirizika kingoni mwa macho na kumwagika chini.

 http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Nilirudia kumkamulia mara tatu.



“Umeshamaliza?” akaniuliza.



“Nadhani imetosha”



Alikuwa anataka kuinuka nikamzuia.



“Ngoja kwanza dawa ikuingie vizuri, una haraka ya nini?”



Akatulia.



Baada ya dakika tatu hivi nikamwambia ainuke. Akainuka na kukaa kwenye kochi.



“Yanawasha?” nikamuuliza.



“Yanawasha kwa mbali”



Nilichukua kitambaa nikamfuta futa yale maji maji yaliyokuwa yamemchirizikia pembeni mwa macho kisha nikaondoka.



Asubuhi nilimfanyia tena,  nikarudia tena jioni.



“Vipi, hujaanza kuona ona” nikamuuliza.



“Bado. Naona kiza tu”



“Mganga mwenyewe ameniambia nikufanyie kwa siku tatu”



“Labda mpaka kesho kutwa”



Niliendelea kumfanyia Ibrahim dawa hiyo kwa siku tatu lakini macho ya Ibrahim hayakuona chochote. Siku ya nne yake nikarudi tena kwa yule mganga.



Nilipomueleza nilimuona akikunja uso.



“Bado hajaweza kuona?” akaniuliza.



“Hajaona bado”



Mganga akafikiri kisha akaniambia.



“Njoo kesho nitakupa dawa nyingine”



Nikaondoka. Kwa vile hata zile dawa alizopewa  hospitalini hazikuweza kumsaidia, kesho yake nilirudi tena kwa yule mganga. Kwa kweli aliniweka sana. Alipomaliza kuhudumia wateja wake akaniita na kuniambia niende tena kesho kwani hakupata nafasi ya kwenda kunichumia dawa nyingine.



Nikaondoka. Siku iliyofuata Ibrahim alipelekwa hospitali na mdogo wake na mimi nikatoka kwenda kwa mganga.



Nilipofika alinipa dawa ya ungaunga mweusi, akanimbia nichote kidogo niroweke kwenye maji ya vugu vugu kwa dakika moja kisha nimpe mume wangu anawe uso.



“Niroweke kwenye maji ya kiasi gani?” nikamuuliza kwa matumaini.



“Kama nusu lita hivi”



“Anawe uso yote?”



“Ndiyo anawe yote. Unamtilia asubuhi na jioni kidogo kidogo”



“Kwa siku ngapi?”



“Kwa siku tatu”



Baada ya mazungumzo hayo nikaondoka. Nilikuta mume wangu alikuwa amesharudi kutoka hospitali. Alikuwa amepewa dawa nyingine za kutumia kwa siku tatu.



“Na mimi nimekwenda kwa mtaalamu mwingine” nikamwambia.



“Amekwambiaje?”



“Baada ya kumueleza matatizo yako amenipa hii dawa”

 http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Ni dawa ya aina gani?”



“Ni ya unga unga. Ameniambia nitie kwenye maji ya vugu vugu kisha uoshe uso asubuhi na  jioni”



“Kwa sababu tuna shida tutafanya” Mume wangu aliponiambia hivyo niliona huzuni sana.



Tulifanya ile dawa kwa siku tatu bila mafanikio. Zile dawa za hospitali nazo hazikuleta matumaini yoyote.



Kwa vile niliona lile tatizo lilitokea kwa yule mganga nikarudi tena bila kuchoka. Mganga akanibadilishia dawa nyingine. Nazo pia hazikufaa.



Kwa upande wa hospitalini tulimaliza hospitali kadhaa za macho. Mume wangu aliambiwa hawezi kuona tena!



Sasa maisha yetu yalianza kuwa magumu. Mume wangu alikuwa hawezi tena kufanya kazi. Tulikuwa tunakula mtaji. Kusema kweli pesa nyingi zilimalizika kwa uchunguzi na matibabu yake.



Mwisho wake akanimabia anafikiria kuuza ile gari yake ili apate pesa za kuendelea kujitibu. Kulikuwa na watu ambao walikuwa wakimpa moyo kwamba asikate tamaa.



Akauza lile gari. Pesa hizo nazo zikaisha kwa chakula na kuwalipa madaktari. Siku za mwanzo mwanzo marafiki zake waliokuwa wanakuja nyumbani kumjulia hali walikuwa wakimpa pesa kumsaidia. Lakini mwisho marafiki hao walichoka. Nikawa sioni mtu.



Tulifikia mahali umeme ulikatwa nyumbani kwa sababu tulikuwa na deni kubwa. Tukawa tunatumia taa za mafuta



Kwa vile niliona lile tatizo lilianzia kwa yule mganga wa kienyeji nikarudi tena kule kule kumueleza hali halisi.



“Mpaka dakika hii ni kwamba mume wangu bado haoni” nikamwambia.



“Bado haoni hadi sasa?” Mganga akajidai kuniuliza kwa mshangao.



“Bado”



“Nilipoona hutokei nilijua mume wako amepona”



“Tulikuwa tunashughulikia matibabu ya hospitali. Kwa kweli tumetumia pesa nyingi sana bila mafanikio. Mume wangu kwa sasa haweza kufanya kazi, pesa hatuna. Juzi juzi ameuza gari lake na pesa tulizopata pia zimekwisha. Imefikia hadi nyumbani tumekatiwa umeme!”









Nilipomwambia hivyo mganga huyo aligwaya. Uso wake ukaonesha wazi kufedheheka.



“Sasa nyinyi mmeharibu” akaniambia.



“Tumeharibu nini?”



“Wakati ule nilipokupa zile dawa zangu, kama uliona hazikumsaidia ungerudi kunieleza. Badala yake mmekwenda kuchanganya na matibabu ya kizungu. Hizi dawa zangu zina miko”



“Sasa ningefanyaje wakati mume wangu alipoona dawa hazikumsaidia ametaka apelekwe hospitali na huko ameambiwa hawezi kuona tena”



Mganga akanyamaza kimya. Baada ya kupita sekunde chache aliniambia.



“Kama ungerudi tena nina hakika hivi sasa mume wako angekuwa anaona”



“Sasa ndio nimerudi hivi”



“Umechelewa!”



“Nimechelewa kivipi?” nikamuuliza.



Mganga akanyamaza kimya. Alionesha alikuwa na jibu lakini hakutaka kulitoa, labda aliona halikuwa jibu la kufurahisha.



Na mimi sikutaka kumuuliza tena, nikabaki kimya nikiwaza.



Baada ya ukimya wa sekunde kadhaa mganga akanimabia.



“Basi njoo kesho nahitaji kupata muda wa kulichunguza hilo tatizo la mume wako”



“Utalichunguzaje tatizo la mume wangu bila mwenyewe kuwepo hapa?” nikamuuliza.



“Ninajua mwenyewe, wewe nenda zako kesho njoo”



“Nimekuelewa lakini naomba unifanyie bidii kwani hali ya maisha yetu imekuwa ngumu kwa sasa. Mume wangu hawezi kwenda kufanya kazi kutokana na hali aliyonayo”



“Umeshanieleza na nimeshakuelewa”



“Sawa”



Nikanyanyuka na kumuaga yule mganga kisha nikatoka. Nilitoka nikiwa na matumaini madogo sana ya mume wangu kupona lakini kama wasemavyo waswahili uongo wa mganga, nafuu ya mgonjwa.



Hata kama yule mganga atakuwa ananidanganya, bado nitaendelea kufuatilia maelezo yake kwa sababu sikuwa na jinsi. Niliyataka mwenyewe na nimeshayapata.



Siku iliyofuatia nikarudi tena kwa mganga huyo. Sikukuta watu pale nje lakini nilikuta gari jipya aina ya Rav 4 limeegeshwa.



Kwa vile sikukuta watu nilikwenda kubisha mlango moja kwa moja.



“Pita ndani” nikaisikia sauti ya mganga ikiniambia kutoka ndani. Nikaingia.



Nilimkuta mganga huyo akizungumza na kijana mmoja aliyekuwa amekaa kwenye kiti.



Kwa kudhani alikuwa mteja nilisita kwenye mlango.



“Karibu ukae” mganga akanisisitiza.



Nikawaamkia kabla ya kukaa kwenye jamvi.



“Huyu hapa ni mwanangu tu, si mteja kama ulivyodhani” mganga akaniambia nilipoketi.



Nikamtazamam vizuri kijana huyo. Alikuwa amevaa vizuri na alionekana kama alikuwa mgeni.



“Anaishi Dar, amekuja jana usiku, ndiye mwenye gari yake hapo nje”



“Nimefurahi kumuona…kaka habari za Dar?” nikamsalimia.



“Nzuri, sijui nyinyi hapa Tanga? Mnatunyima nini?” kijana huyo akaniuliza huku akitabasamu.



“Jua kali tu na shida za kilimwengu zimetuandama, ndiyo maana tunahangaika”



Kijana huyo akacheka kidogo.



“Ndio maisha. Maisha ni kuhangaika”



“Mambo yake huyu mama ni makubwa” Mganga akadakia kisha akaniambia.



“Nimelichunguza tatizo la mume wako, nimeona ni kubwa. Siyo kama tulivyodhani hapo mwanzo. Mume wako amerogwa, kwa hiyo tatizo limekwenda kwenye macho”



Hapo nikashituka.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Unataka uniambie sio zile dawa nilizozibadili zilizompofua macho?”



“Zile dawa zilikuwa ni kisibabu tu lakini kuna tatizo kubwa nyuma yake. Kama zingekuwa ni zile dawa, mume wako angekuwa ameshapona”



Nikashusha pumzi ndefu kisha nikamuuliza.



“Sasa tutafanyaje na sisi ni weupe, pesa zote zimeisha”



“Nitawasaidia hivyo hivyo kidogo kidogo. Nitakupa dawa zangu aanze kwenda kutumia”



“Sawa”



Wakati mganga huyo ananiandalia hizo dawa, yule kijana akainuka kwenye kiti.



“Baba, sasa mimi natoka kidogo” akamwambia baba yake.



“Unakwenda mijini?”



“Ndiyo nataka nifike mjini mara moja”



“Subiri umsaidie huyu mama, anaenda huko huko”



“Nimsaidie lifti?”



“Ndiyo. Subiri kidogo”



“Basi namsubiri kwenye gari”



“Sawa”



Yule kijana akatoka.



Mganga huyo alinipatia dawa za mizizi. Akaniambia nianze kumchemshia na kumywesha mume wangu kikombe kimoja asubuhi na kikombe kimoja jioni.



“Atatumia kwa siku saba. Baada ya siku saba utafute laki mbili ili nimfanyie kafara la kuondoa ule uchawi”



Mganga aliponiambia hivyo niliguna.



“Nitazipata wapi hizo laki mbili?” nikamuuliza.



“Fanya mipango katika hizi siku sita. Ni lazima hizo pesa zipatikane kama unataka mume wako apone kabisa”



Baada ya kuwaza kidogo nilichukua ile mizizi niliyopewa ambayo mganga huyo alikuwa ameitia kwenye mfuko wa nailoni, nikainuka.



“Haya nitakwenda kufanya mipango, kama nikishindwa nitakuja kukwambia” nikamwambia.



Nilipotoka nje nilimkuta yule kijana akinisubiri kwenye gari. Aliponiona alinifungulia mlango wa upande wa pili wa dereva akaniambia.



“Ingia twende”



Nikaingia kwenye gari na kufunga mlango.



Kijana huyo akaliwasha gari tukaondoka. Kupata hiyo lifti nilishukuru sana kwani ningeweza hata kurudi nyumbani kwangu kwa miguu.



“Mimi naitwa Chinga, sijui mwenzangu unaitwa nani?” Kijana huyo akaanza kuniuliza.



“Miye naitwa Salama” nikamjibu.



“Huyo mwenye matatizo ni mume wako?” akaniuliza.



“Ndiyo ni mume wangu”



“Ana matatizo gani?”



“Amepofuka macho. Na sababu ya kupofuka ni dawa nilizopewa na mzee. Dawa ambayo niliambiwa nimtilie kwenye chakula nilimtilia kwenye maji ya kuoga. Baada ya kuoga yale maji, macho yalipofuka hapo hapo”



Kijana huyo nilipomwambia hivyo alitikisa kichwa kusikitika.



“Ulipomueleza mzee alikwambiaje?”





Alinipa dawa nimfanyie lakini hazikusaidia. Hivi sasa maisha

yamekuwa magumu kwa sababu mume wangu hawezi kufanya

kazi. Tumehangaika mahospitalini bila mafanikio. Pesa zote

zimetuishia. Hivi tunavyozungumza umeme pia umekatwa

nyumbani kwa sababu tumeshindwa kulipia bili”

Chinga alikuwa akinisikiliza huku akitikisa kichwa kusikitika

“Sasa leo umepewa dawa gani?”

“Leo ameniambia kuwa mume wangu amerogwa na wenzake,

ndio amenipa hii mzizi nikamchemshie kwa siku saba. Sasa hilo si

tatizo, tatizo ni kuwa baada ya hizo siku saba mganga ametaka

niende na shilingi laki mbili. Nitazitoa wapi?”

“Kweli ni tatizo” Chinga akanikubalia.

“Kama nitashindwa basi, nitashukuru tu”

Chinga alinyamza kimya. Bila shaka alikuwa akinionea huruma.

“Unaishi maeneo gani?” akaniuliza baada ya ukimya mfupi.

“Tunaishi Usagara”

"Ngoja nikupeleke"

"Usinifikishe nyumbani kabisa. Nitakuonesha mahali pa

kunishusha" nikamwaambia. Akanielewa.

Wakati tunaelekea Usagara aliniambia.

"Mimi ninaishi Dar, nimekuja mara moja tu kumsalimia baba. Pengine keshokutwa nitaondoka"

"Kumbe yule ni baba yako mzazi?" nikamuuliza.

"Ni baba yangu mzazi isipokuwa mama yangu alikufa"

"Kwa hiyo yule aliyenaye pale ni mama yako wa kambo?"

"Yule ni mama wa kambo"

"Vizuri sana"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Pakapita kimya kifupi kabla ya Chinga kuniuliza tena

"Utarudi lini tena kuchukua dawa?"

"Nimeambiwa nirudi baada ya siku saba"

"Huenda nikawa nimeshaondoka" akaniambia na mimi sikumjibu kitu.

Tulipofika Usagara nilimwambia anishushe kwenye kituo cha daladala. Tukaagana hapo hapo. Akaenda zake na mimi nikaenda nyumbani kwangu.

Nilipofika nyumbani nilimdanganya mume wangu kuwa dawa hizo nilipewa na bibi yangu ambaye alikuwa ni mtabibu. Akaamini.

Kama nilivyoagizwa na mganga nilimchemshia mume wangu dawa hizo kwa siku saba. lakini kama zilivyokuwa dawa za mwanzo hazikuleta mafanikio yoyote. Niliona uvivu kurudi tena kwa yule mganga, nikawa sijui la kufanya.

Siku zikapita. Maisha ya nyumbani yakawa ya tabu zaidi na ya kukata tamaa. Siku moja walikuja maofisa wa benki nyumbani kumtafuta mume wangu. Kumbe Ibrahim alikuwa akidaiwa mkopo wa benki ambao ulikuwa umepita nuda wake wa kulipa. Ile nyumba yetu ndiyo alikuwa ameiwekea dhamana ya mkopo. Masafisa hao wakamwaambia kwamba walikuwa wanahitaji pesa zao.

Mume wangu akaomba kusubirishiwa kidogo kutokana na hali yale lakini maofisa hao wa benki walikataa kumuongezea muda kwa madai kuwa riba itazidi kuongezeka na kutokana na hali yake hatoweza kulipa. Walimpa wiki moja za kulipa pesa alizokuwa anadaiwa, vinginevyo walimwaambia nyumba yetu ingenadiwa kufidia deni hilo.

"Macho yangu yangekuwa mazima yasingenikuta hayo, ningeweza kulipa deni hilo na hata kama ningeomba muda zaidi wangenikubalia" mume wangu akaniambia kwa masikitiko.

"Sasa tufanyeje mume wangu, nyumba hii ikinadiwa tutaenda kuishi wapi?" nikamuuliza.

Mume wangu hakuwa na la kujibu. Kumbe Ibrahim alikuwa akimiliki kiwanja pale pale Usagara lakini kilikuwa ni siri yake. Ikabidi anieleze. Ili kuokoa nyumba yetu isiuzwe ilimbidi auze kiwanja hicho. Pesa iliyopatikana akalipia deni alilokuwa anadaiwa. Nyumba yetu ikasalimika.

Kutokana na maisha kuendelea kuwa ya dhiki nikarudi tena kwa yule mganga. Nikamueleza matatizo yaliyokuwa yanatukabili kutokana na mume wangu kutoona.

"Kama angekuwa anaona angeendelea na kazi zake na pesa ingepatikana lakini sasa hawezi kufanya kazi" nilimwaambia. mganga huyo kwa kusikitika.

Mganga huyo hakuchoka kunipa dawa. Kama kawaida yake akanipa dawa nyingine ya utomvu utomvu, akaniambia nichanganye na rangi ya chai kisha nimpake kwenye macho yake asubuhi na jioni kwa siku tatu.

Nikarudi nyumbani. Nikamfanyia mume wangu dawa hiyo kwa siku tatu kama nilivyoagizwa na mganga huyo, lakini pia haikuleta mafanikio yoyote.

Nikataka kurudi nikamueleze mganga huyo lakini nikawa sina nauli.

Siku moja nilikuwa nimekwenda sokoni. Wakati ninarudi nyumbani nikaona gari inanifungia breki miguuni, nikashituka. Nilipotupa macho nikaona ni ile Rav 4 ya yule kijana niliyekutana naye siku ile kwa yule mganga.

Akatoa kichwa kwenye dirisha la gari na kunisalimia.

“Asalaam alaykum”

"Alaykum salaam" nikamjibu huku nikitabasamu.

"Habari za huko?" nikamuuliza

"Nzuri. Ingia nikusindikize" akaniambia.

Nikazunguuka upande wa pili wa gari nikajipakia.

"Umekuja lini?" nikamuuliza.

"Nimekuja juzi"

"Mzee hajambo?"

"Hajambo"

"Nilikuwa nataka kwenda kumuona nimjulishe hali ya mgomjwa lakini sijapata nafasi" Nilisingizia nafasi lakini ukweli ni kuwa sikuwa na pesa ya nauli.

"Kwani yule bwana mpaka sasa hajapona?"

"Bado hajapona. Tuna hali mbaya kweli hivi sasa!"

"Ninakuona, sivyo ulivyokuwa"





"Mume hawezi kufanyakazi, hatuna pesa. Yaani sijui nikwaambie nini!"

"Pole sana"

Tulikuwa tumeshafika kwenye kile kituo cha daladala alichonishusha siku ile. Akasimamisha gari na kutoa pochi mfukoni. Akaifungua na kuchomoa kitita cha noti, akanipa.

"Chukua hii laki moja itawasaidia kwa siku mbili tatu" akaniambia.

Kwa wakati ule niliona ni hela kubwa sana.

"Ahsante, nakushukuru sana" nikamwaambia.

"Sasa ungependa kwenda lini kwa mzee?" akaniuliza.

"Siku yoyote tu"

"Basi kesho nikienda huko nikupitie twende pamoja"

"Kwani wewe unalala wapi?" nikamuuliza.

SASA ENDELEA

"Mimi ninalala huku mjini"

"Mna nyumba yenu huku mjini?"

"Hapana. Nyumba yangu ipo Dar. Nikija huku ninalala hoteli"

"Hoteli gani?"

"Mtendele Hotel. Ipo pale Chuda. Ni Hoteli ninayoitumia kila ninapokuja Tanga kwa sababu huduma zake ni bora sana"

Nikafikiri kidogo kisha nikamuuliza

"Utanipitia saa ngapi twende huko Kisosora?"

"Saa nne asubuhi"

"Basi nitakusubiri hapa kwenye kituo cha daladala"

"Sawa" akaniambia.Tukaagana.

Kutokana na shida tuliyokuwa nayo pale nyumbani, pesa

nilizopewa na yule kijana nilizificha ziwe akiba yangu. Sikutaka mume wangu ajue kuwa nilikuwa na kiasi hicho cha pesa.

Baada ya kumaliza kupika nilimtengea chakula mume wangu nikamuacha aendelee kula, mimi nilikwenda kukaa uani na sahani yangu. Sikutaka kula naye. Kusema kweli japokuwa ni mimi niliyemsababishia upofu, sikuwa nikimuona raha tena. Hata tulipokuwa tunalala usiku tulilala tukiwa mzungu wa nne. Nilikuwa nikielekea upande wangu.

Sasa niliamini kuwa mapenzi ya kweli yapo kwenye pesa. Kama pesa hakuna na matumaini ya kuzipata hayapo tena, hakuna mapenzi. Wakati mwingine hali inapokuwa ngumu sana nyumbani mimi ndiye niliyelazimika kutoka kwenda kwa ndugu zangu kuwaomba pesa za matumizi.

Mume wangu mwenyewe alikuwa ameshagundua kuwa nilikuwa nimebadilika. Sikuwa yule Salma wa mwanzo. Hata ile lugha ya kistaarabu kwake nilikuwa sinayo tena. Wakati mwingine nilikuwa nikimjibu mbovu na yeye kwa kujua hakuwa na uwezo na alikuwa akinitegemea mimi, alikuwa akinyamaza.

Wakati ninakula pale uani nilisikia akiniita. Kwa kweli sauti yake ilikuwa ikinikera sana kwa sababu ya kuniita kila wakati.

Nikajifanya kama sikumsikia, nikanyamaza kimya. Akaniita mara ya pili na ya tatu.Kelele zake zikanifanya nihamaki.

“Wataka nini babu wewe!?” nikamuuliza kwa sauti ya juu na kuongeza.

“Huchoki kuniita?”

“Njoo mke wangu” akaniambia kwa sauti ya upole.

“Mimi ninakula, unataka nini?”

“Kumbe umekwenda kula huko?”

“Kula ni kula tu, popote unaweza kula. Sema unataka nini?”

Akanyamaza. Nikanyanyuka pale nilipokuwa nimeketi nikaingia ndani. Nilimkuta ameshamaliza kula.

“Unataka nini?” nikamuuliza kwa sauti ambayo haikuwa tulivu

“Nipeleke sebuleni. Nitakaa hapa mpaka saa ngapi?”

“Kwani wewe utajizoesha lini kutembea mwenyewe? Mbona kuna wenzako wasioona wanapapasa kuta wenyewe mpaka wanafika wanakotaka. Utanitegemea mimi mpaka lini? Je kama sipo?”

“Zacharia hayupo, ningemuita yeye lakini ametoka mara moja”

Nikamshika mkono, akainuka. Nikaenda naye sebuleni.

“Sasa kaa hapa kama unataka kukaa, siyo tena uanze kuniitaita!” nikamwambia.

“Nivumilie mke wangu usikasirike” akaniambia.

“Ningekuwa mimi si ungekwisha nitimua!”

Nilipomuambia hivyo akanyamaza kimya.

Nikaondoka. Sikurudi tena kule uani, nikaenda kukaa kwenye meza ya chakula kwa vile yeye alikuwa ameondoka. Nikala chakula mpaka nikamaliza. Nikaingia jikoni kuosha vyombo.

Wakati ninaosha vyombo mume wangu akaniita tena. Nikaguna. Kama kawaida yangu sikumjibu. Nilimaliza kuosha vyombo kisha nikamfuata.

“Si nilikuambia sitaki kuitwaitwa, mimi nina kazi zangu!” nikamwaambia kwa ukali.

“Nimekuwa sina raha, kila saa Salma! Salma!Salma! nikufanye nini?”

“Sikuiti mimi. Kuna mtu anabisha mlango”

Aliponiambia hivyo nikanyea.

“Ni nani?” nikamuuliza.

“Nitajuaje!”

Nikaenda kwenye mlango na kuufungua. Kumbe alikuwa mmoja wa rafiki zake aliokuwa akifanya kazi nao TRA. Nikatahayari kwani nilijua kuwa alikuwa ameyasikia yale maneno niliyomuambia mume wangu.

“Karibu shemeji” nikamkaribisha huku nimeinamisha uso wangu kwa aibu.

“Ahsante”

Jamaa huyo akaingia ndani. Jinsi uso wake ulivyofadhaika, nilihisi aliyasikia yale maneno niliyomuambia Ibrahim.

“Habari za nyumbani” nikajidai kumsalimia huku nikitabasamu

“Nyumbani ni kwema. Sijui nyinyi hapa?”

“Sisi ndiyo kama unavyotuona, kwacha hakuchi lakini siku zinapita”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Ibrahim akaisikia sauti ya rafiki yake.

“Msangi umenitupa ndugu yangu” akaanza kumshutumu.

“Sijakutupa kaka, mihangaiko imekuwa mingi. Unajionaje hali yako kwa sasa?”

“Sijambo lakini hali yangu ni ile ile kama unavyoniona. Karibu ukae”

Msangi akakaa karibu na Ibrahim. Wakaanza kuzungumza. Na mimi nilikuwa pale pale.

Baada ya mazungumzo marefu Msangi akatia mkono kwenye mfuko wa suruali yake, akatoa noti mbili za elfu kumi kumi.

“Nimekuletea hizi senti kidogo zikusaidie kaka”

Ibrahim akanyoosha mkono. Msangi akamuwekea kwenye kiganja.

“Ahsante ndugu yangu” Ibrahim akamshukuru na kumwambia.

“Usiache kunikumbuka. Ukikaa siku mbili tatu uwe unakuja kutujulia hali. Siku nyingine tunashinda bila kuijua riziki”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Sawa kaka. Kuja kuwajulia hali ni lazima nije. Wewe ni kaka yangu, siku ambazo hunioni ni kwamba na mimi pia hali siyo nzuri”

“Ninajua. Nakushukuru sana ”

Baada ya hapo Msangi akatuaga na kuondoka.

Kwa vile nilishaziona zile pesa zilizotolewa na Msangi nikaenda kuketi na Ibrahim ili nimsomeshe ziingie mikononi mwangu.

“Mume wangu unajua kuwa nilimkopa jirani pesa tuliyotumia juzi. Sasa kama umepata nipe nimrudishie” nikamwaambia

“Mbona hukuniambia tangu hiyo juzi?” akaniuliza.

“Ningekuambia ungekuwa nazo hizo pesa za kumlipa?” nikamng’akia.







ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog