Search This Blog

Friday, November 18, 2022

PAIN OF LOVE - 4

 






Simulizi : Pain Of Love

Sehemu Ya Nne (4)





“Anayebisha hodi, ni nani?,” Benson aliuliza kwa hofu mara baada ya kusikia mgongaji mlango akiwa anaendelea kugonga kwa nguvu.



“Sijajua...ngoja nikamwangalie,” Yulietha alisema huku akielekea mlangoni kufungua mlango.



Alifungua mlango kwa kusita mwisho akafungua mlango mwaaa, wa nje akawa anaona ndani vyema na wa ndani akawa anaona wa nje bila chenga. Mgongaji hakuwa mwingine bali alikuwa ni Msomali alisimama pale mlangoni kwa kufura kama Fisi aliyeliwa mzoga wake, Yulietha akiwa ameduwaa pale mlangoni kwa kumshangaa Msomali kuwa amefuata nini akashtuka kupigwa makofi matatu na Msomali moja kwa moja Yulietha akachutama kwa kuugulia makofi yale. Yulietha akiwa anaugulia Msomali akapeleka mkono wake wa kuume shingoni mwa Yulietha akamkaba huku akimwinua na kumtupa kule ndani kisha akasema kwa sauti ya jazba.



“Hili zezeta lako, ndiyo linalokufanya unikatae mimi,” Msomali alisema huku akimnyoshea kidole cha husda Benson.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Ai..hu.!!,” Yulietha aliongea kwa nyodo kisha akarudi tena mlangoni kumzuia Msomali asiingie.



Lakini mwanaume ni mwanaume tu Msomali alimsukuma Yulietha kwa nguvu hadi Yulietha akaenda kudondokea kando ya kitanda na kumpatia nafasi Msomali ya kuingia ndani, Msomali aliingia ndani akamwangalia Benson kwa hasira kisha akauliza kwa sauti ya juu.



“Wewe, hanithi umefuata nini hapa?.”



“Sikutaka kuja.... Yulietha ndiye aliyenileta,” Benson alijibu kwa kujijitetea huku akionyesha kuwa na hofu kubwa.



“Benson, usijishushe hivyo wewe ndiye mwenye penzi la kweli huyo ni kidudu penzi anayetaka penzi kibabe,” Yulietha alijaribu kumtia moyo Benson asiweze kumuogopa mtu anayetaka kumpokonya tonge mdomoni kibabe.



“Unasemaje, wewe mwanamke?,” Msomali aliuliza kwa jazba huku akimkata jicho kwa hasira Yulietha. Kisha akazamisha mkono wake kwenye soksi kwa ghadhabu akaibuka na mguu wa kuku Puret 7.



Akamlenga Benson na kumshuti kwenye kifua kisha akatoweka eneo lile na kumwachia Yulietha msala. Benson hakuchukua dakika alienda chini na alipodondokea pakatapakaa damu, Yulietha alichanganyikiwa hakujua hata cha kufanya akili zilimruka na mwili wake ukawa wa baridi ghafla kwaajili ya uwoga. Muda kidogo ulipita ndipo akili yake ikatulia na akakumbuka kumpigia Peter rafiki wa Benson alichukua simu akatafuta namba ya Peter akampigia, simu iliita kwa muda bila majibu hatimaye ndani ya dakika chache ikapokelewa.



“Peter, njoo hosteli yetu kuna tatizo” alizungumza Yulietha huku akionekana kuwa na wasiwasi.



“Kuna, nini?” aliuliza Peter lakini swali lake halikujibiwa kutokana na Yulietha kukata simu kabla ya kumaliza mazungumzo.



*********

Mzee Deus Swai alizidi kumkokota mwanae kinguvu waelekee nyumbani, wakiwa wanavutana pale nje ghafla baba Coletha presha ikapanda na kudondoka tiii kama zigo. Coletha kwa kuwa anajua magonjwa ya baba yake kwa kipindi kirefu anasumbuliwa na presha na moyo basi haraka akapiga simu kwa dereva taxi aliyempeleka mama yake hospitali simu iliita na kupokelewa. Alimuelekeza kwa kufika kisha akakata simu dakika kadhaa mbele dereva taxi aliwasili wakampakiza mgonjwa ili kumuwahisha hospitali kabla awajafika hospitali wakiwa njiani Coletha akamtafuta rafiki yake kupitia simu ambaye ni shoga yake walioshibana tangu udogo wao akamuomba aende Ilala kwa mama yake akamtizamie, walikubaliana na shoga yake safari hii hawakwenda hospitali ya MUHIMBILI bali walimpeleka Mzee Swai hospitali ya ILALA walifika hospitali dereva taxi akalipwa na kuondoka. Coletha aliita wauguzi wamsaidie kumchukua baba yake na kumpeleka wodini akafanyiwe vipimo, Mzee Swai alifanyiwa vipimo kisha akaitwa Coletha ofisini na muuguzi akapewe majibu ya baba yake aliketi kitini mara baada ya kufika ofisini Coletha akamsikiliza muuguzi kwa makini.



“Baba yako, tumempima tumegundua ana presha na moyo wake una tundu...amezimia bado hajazinduka hivyo akizinduka nitawaruhusu,” Muuguzi aliongea kumhabarisha Coletha.



“Sawa.”

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Sasa nitakuandikia dawa, ukamnunulie.”



“Dawa zake anazo, akifika nitampa dozi yake.”



“Okay...lakini nakusihi epuka kumpa stress mzee huyu stress zinaweza kummaliza mapema.”



“Nimekuelewa, nitazingatia hilo.”



Baada ya mazungumzo muuguzi na Coletha wakaenda wodini kuangalia hali ya mzee Swai, walipofika wakamkuta tayari kashazinduka huku akiwa anashangaa shangaa asijue kilichomkuta hapo awali. Coletha alimpa muhtasari baba yake kisha wakaondoka mara baada ya kuruhusiwa na muuguzi walitoka nje wakakodi bajaji iwapeleke Kigogo, mara baada ya kupanda kwenye bajaji dereva bajaji akaondoa bajaji maeneo yale aliendesha bajaji hadi Karume njia panda ya magari ya kuelekea K/koo, Buguruni, Tandika na Kigogo Mungu wangu! ghafla likatokea gari la wanajeshi na kugonga bajaji waliyopanda Coletha na baba yake mara baada ya dereva bajaji kuendesha bajaji bila ruhusa ya trafiki. Bajaji ilipinduka na Mzee Swai akapata mshtuko pale pale akaaga dunia yeye na dereva bajaji, Coletha alichubuka mwili na kuzimia wote wakapelekwa hospitali upesi.



**********

Dosagon alirudi alipoagizwa akapaki gari kisha akaingia ndani, hakukaa sana Norman nae akatia timu wote walimkuta bosi sebuleni akipitia gazeti la THE GUARDIAN kutoka huko Uingereza waliungana kumpa kampani Mzee Panta Guno. Mzee Panta Guno baada ya kuwa makini kwa kupitia gazeti kwa muda akachoka kisha akalifunika gazeti na akawatazama vijana wake kisha akauliza.



“Vijana, nahisi mmechoka leo Bata wapi?” alifurahi Norman kisha akajibu swali la bosi.



“Kiongozi, leo nasikia MALAIKA MUSIC BAND wanapiga muziki kwenye Club ya 5N unaonaje tukale Bata huko.”



“Oooh, basi ni vizuri jiandaeni twende” alisema Mzee Panta Guno.



Baada ya dakika kadhaa Norman na Dosagon walitoka chumbani wakiwa wamejiandaa mara baada ya kuambiwa na bosi wao wakajiandae. Mzee Panta Guno aliwachukua vijana wake kisha akaondoka nao kwa njia ya gari yake aina ya LANDCRUISER PRADO huku nyuma wakimwacha Anitha akiwa kwenye kile chumba alichofungiwa, Anitha akiwa kwenye kifungo akawaza na kuwazua lini na saa ngapi atatoka kwenye kifungo akiwa anawaza na kuwazua jirani na dirisha alilokuwepo akasikia mruzi wa mlinzi akipita.



“Mponda” aliita Anitha.



“Naam” aliitika mlinzi.



“Sogea, nikuulize,” Mponda akasogea amsikilize Anitha atasema nini.



“Nasikia kuko kimya...baba kaondoka?” aliuliza Anitha mara baada ya Mponda kusogea.



“Eeenh, tena muda sana.”



“Sasa sikia baba kanifungia mlango kwa nywila, nakuomba njoo unifungulie.”



“Mmmh, utaniponza nifukuzwe kazi sitoweza.”



“Hapana, njoo nifungulie nitakulinda.”



“Lakini mimi sijui, nywila ya chumba chako.”



“Njoo, nitakutajia.”



Mponda akaingia ndani kisha Anitha akaanza kumtajia nywila ya chumba chake, alimtajia mlango ukafunguka Anitha akatoka alimshukuru Mponda kisha wakatoka nje.



“Anitha, mzee kakufungia Kwanini?” aliuliza Mponda kwa kutaka kujua.



“Baba kanifungia kwasababu anajua mimi natembea na Gerald Eduardo, mzungu wa Uholanzi aliyeloea Tanzania na ambaye ni kijana tunayefanya naye kazi” alijibu Anitha.



“Mzee anamjua, huyo mzungu?.”



“Hamjui...yeye anamtuhumu kijana mmoja hivi anaitwa Mathias anadhani huyo ndiye Gerald Eduardo kumbe lahasha amewrong number.”



“Una hatari, wewe.”



“Kwanini?.”



“Huoni unamweka, kijana wa watu matatani.”



“Kijana, yupi?.”



“Si, Mathias.”



“Aaah, nitajitahidi kumtoa matatani na naahidi hatopatwa na tatizo lolote.”



Wakiwa wanazungumza Coletha na Mponda ghafla wakasikia Kengele ya getini ikilia haijulikani ni nani anawasili, haraka Anitha akaingia ndani na kumwacha Mponda akienda kufungua geti hakuwa mwingine aliyewasili bali alikuwa ni Mzee Panta Guno na vijana wake.



**********

Kijana yule anataka kupeleka njiti ya Kiberiti kwa Mathias mara ghafla akatokea dada yule aliyeibiwa na kusimamisha zoezi lile.



“Dada, unafanya ujinga gani?,” Kijana yule aliyetaka kumchoma Mathias aliuliza kwa kumfokea yule dada.



“Mwizi sio huyu mwizi kakimbia...kaka huyu namjua hawezi fanya wizi ni jirani yangu,” Dada yule alimkomboa Mathias kwenye mdomo wa Mamba hadi Mathias mwenyewe hakuamini kama atakuja kutetewa.



“Hebu...siku nyingine usifanye hivi namna hii tunaweza kuua mtu asiye na hatia,” Kijana yule alizidi kulaumu kisha akawazuia raia wenye hasira kali wasimdhuru Mathias mara baada ya kujua ukweli.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Raia wote walitawanyika wakamwacha Mathias na yule dada wakiongozana kuelekea kila mtu nyumbani. Mathias akiwa njiani na yule dada alimshukuru kwa kumuokoa katika janga lile maana asingekuwa yeye sasa hivi sijui angekuwa wapi, baada ya kushukuru Mathias mbele kidogo wakaachana na yule dada. Dada yule alielekea kwake na Mathias akaendelea mbele kidogo akafika kwake alipofika akafikia moja kwa moja bafuni kujikosha harufu ya petroli aliyomwagiwa pindi alishuiwa kama mwizi na baada ya hapo akaamua kujitupa kitandani kulala, usingizi ulimchukua akaja kushtuka saa moja kasoro asubuhi alijiandaa na kwenda ofisini alifungua ofisi mara baada ya kufika kisha akatulia kidogo akamgusa Coletha kwenye simu. Simu iliita kwa muda mrefu kisha ikakata yenyewe aliendelea kupiga kama mara tatu lakini mambo yalikuwa ni yale yale akaacha kupiga akaendelea na kazi yake alihudumia wateja wake hadi muda wa saa nane kamili akafunga akaenda kupata chakula cha mchana. Mama Bonge alishangaa mno na akacheka sana mara baada ya kumtia machoni tena Mathias maana tokea walivyoachana siku ile hakubahatika kumuona tena Mathias.”





“Wee, mtu upo?” aliuliza Mama Bonge.



“Nipo” alijibu Mathias mara baada ya kuketi kwenye benchi akisubiri kuhudumiwa.



“Mbona, tokea siku ile sijakuona tena?.”



“Nilipatwa na majanga, kidogo.”



“Majanga gani, tena?.”



“Nilidondoka njiani kisha nikaenda kulazwa, mara baada ya kuachana siku ile.”



“Aisee, pole sana.”



“Nishapoa.”



“Kwa kuwa, hukuingia kazini jana leo nitakupa ofa ya chakula kijana wangu” alisema Mama Bonge kisha akamuita mfanyakazi wake wanayesaidiana ili amhudumie Mathias chakula ambacho amekiagiza.



Mathias akiwa anaendelea kupata ulaji kwa mama Bonge akaamua tena amjaribu kumpigia Coletha simu, safari hii bahati ikamdondokea simu iliita kisha ikapokelewa haraka sana kabla ya mpigaji kughairi kupiga na kuamua kukata.



“Coletha” aliita Mathias mara baada ya Coletha kupokea simu yake.



“Niambie Mathias, mzima wewe?” alitoa ushirikiano Coletha kwa Mathias mara baada ya kuzinduka na japo anaugulia maumivu aliyoyapata kwenye ajali.



“Coletha, mimi mzima...CD ushamaliza?.”



“Sijamaliza.”



“Basi, maliza tu.”



“Mmmh, ila muda wenyewe sina kabisa.”



“Basi kesho, nakuomba ilete CD.”



“Sawa, Mungu akipenda nitakuletea” aliongea Coletha kisha upesi akataka kukata simu ila Mathias akawahi kumwambia kwa sauti ya juu.



“Coletha, usikate simu kuna mazungumzo ya faragha ya kuongea na wewe.”



“Now no, panga muda siku nyingine” alimalizia kusema Coletha kisha akachezea kitufe chekundu cha simu.



**********

Peter haraka alijiandaa na kuelekea hosteli ya wanawake kwenye chumba cha Yulietha kusikiliza wito, alipofika hakuamini alichokiona alimkuta rafiki yake yupo chini akiwa bado anatokwa na damu kwa wingi, upesi akamkaribia rafiki yake kisha akasema kwa hasira huku akimtazama Yulietha.



“Umeua, sasa umefurahi.”



“Sijaua.”



“Kumbe, nani aliyeua?.”



“Msomali.”



“Umeona, nilijua tu...sasa roho kwatu kumuua rafiki yangu.”



“Kwasasa sio jambo la kuongelea, nimekuita ili unipe kampani ya kumkimbiza hospitali.”



Peter ikabidi awe mnyonge ili wawahi kumpeleka Benson hospitali waliita usafiri wa taxi kisha wakampeleka Benson hospitali, walipofika hospitali mgonjwa akachukuliwa na madaktari kisha akapelekwa kwenye chumba cha uchunguzi kwanza mara baada ya kugundua hajafa wakamhamishia kwenye chumba cha upasuaji huku nyuma wakaachwa Yulietha na Peter wakiwa mapokezi wakisubiri majibu ya mgonjwa wao kutoka kwa daktari. Yulietha na Peter wakiwa mapokezi mara ghafla wakaja vijana wawili hadi walipo wao kisha wakajitambulisha.



“Naitwa Inspekta, Majaliwa,” Kijana wa kwanza alijitambulisha.



“Naitwa Inspekta, Bajanda tunatokea kituo cha polisi cha TUSIIME kilichopo maeneo ya Kolokoroni,” Kijana wa pili naye alijitambulisha kwa weredi ulio stahiki.



“Dhumuni letu la kuja hapa, ni kumkamata huyu binti,” Inspekta Bajanda aliendelea kuongea.



“Kwa kosa, lipi?” aliuliza Peter.



“La kumuua, mpenzi wake” alijibu Inspekta Bajanda.



“Nini?” aliuliza kwa mshangao Yulietha baada ya kupokea taarifa zile.



“Hatuna muda wa kuulizana maswali...Inspekta Majaliwa kamata huyo kama kujieleza ataenda kujieleza mbele,” Inspekta Bajanda alitoa amri akamatwe Yulietha.



Bila kuchelewa Inspekta Majaliwa alimkamata mkono Yulietha na kutoka naye nje kinguvu, walimpakiza Yulietha kwenye kalandinga kisha wakatimka naye kuelekea kituoni huku wakimwacha Peter pale mapokezi asijue kinachoendelea nyuma ya pazia. Peter aliendelea kukaa mapokezi akisubiri daktari aje ampe dondoo za Benson kama, nusu saa mbele daktari alikuja mapokezi na kumkuta Peter amekaa kwenye benchi peke yake naye akakaa kisha akamueleza Peter yaliyojiri kwa rafiki yake.



(Hey! Brother who is that guy to you?)

“Kijana, yule ni nani yako?,” Daktari alianza kwa kuuliza.



(He is my friend)

“Rafiki, yangu” alijibu Peter.



(Is he having any relative here?)

“Ana ndugu, hapa nchini?.”



(No! his relatives are in Tanzania)

“Hapana, nduguze wapo Tanzania.”



(Oooh! Your friend has been shooted on his the chest, but he hasnt died because bullet passed aside of his heart. Weve done an operation and now weve let him rest awhile.)

“Oooh...rafiki yako amepigwa risasi ya kifua ila hajafa bahati nzuri hakupigwa eneo la moyo hivyo tumemfanyia upasuaji na kumwacha apumzike” alisema daktari kisha akaendelea tena kusema.



(But your friend has lost most of his blood that may cause a several troubles later, if there is a possibility you have to buy a blood or getting a volunteer to giveout a blood to this patient)

“Lakini rafiki yako amepoteza damu nyingi mwilini hivyo mbeleni itakuja kumletea matatizo, kama kuna uwezekano inunuliwe damu au mtu ajitolee kutoa damu tumuongezee mgonjwa,” Peter alifikiri haraka kisha akaendelea kuongea mara baada ya daktari kumueleza.



(Okay let me contact his relatives and then Ill getback)

“Basi ngoja nifanye mawasiliano na ndugu zake, kisha nitarudi” alisema Peter huku akitoka nje ya geti kuu na kumuacha daktari mapokezi.



Bahati nzuri namba za ndugu wa Benson alikuwa nazo hivyo hakupata tabu sana alichukua simu yake mfukoni kisha akaanza kuipekua majina katika kupekua akapata namba ya Mzee Swai. Namba ya Mzee Swai haikuita bali ilisikika sauti ya kike anayefanyia kazi katika mtandao wa Airtel ikisema;



“Namba unayopiga kwasasa imefungwa, hakikisha namba unayopiga na upige tena...karibu sana katika mtandao wetu wa Airtel” kisha ikakata.



Peter akaendelea kutafuta namba nyingine akaona namba ya Bi Consolatha ambaye ni mama yake Coletha akaipiga namba hile ikaita kwa muda mrefu na haikupokelewa akapiga tena safari hii simu ikapokelewa na rafiki yake Coletha ambaye anaitwa Doreen.



“Hallow, mama” aliongea Peter mara baada ya simu kupokelewa.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Mimi sio mwenye simu, mwenye simu anaumwa” aliongea Doreen kwa kujieleza.



“Oooh, wewe ni Coletha?.”



“Hapana, ni rafiki yake.”



“Aaaah, Coletha upo naye hapo?.”



“Hapana, Coletha kampeleka baba yake hospitali anaumwa.”



“Basi.”



“Ulikuwa una, shida naye?.”



“Yaah.”



“Mpigie kwenye namba, yake.”



“Sawa, ngoja nijaribu” alimaliza kuzungumza Peter kisha akakata simu na muda huo huo akamtafuta Coletha. Simu ya Coletha iliita mno mara baada ya kupiga Peter alitaka kukata tu punde ikasikika sauti ya Coletha ikizungumza mara baada ya kupokea simu.



“Oooh!!!, Peter mambo vipi?” kumbe wanajuana na Peter basi aliongea kwa kuuliza Coletha kwa uchangamfu.



“Sio, safi sana” alijibu Peter kinyonge kama mtoto yatima aliyekutana na mama katili.



Coletha alitaka kuuliza tu daktari akaja kumkatisha maongezi, Coletha akakata simu kisha akamsikiliza daktari kaja na sera gani.



**********

“Coletha, nakuomba ofisini” aliongea Daktari mara baada ya kuingia kwenye wodi aliyolazwa Coletha kisha akaelekea ofisini.



Coletha baada ya muda akamfuata daktari yule ofisini kumsikiliza kuwa anataka kusema nini, kufika alikaribishwa kitini na daktari kisha daktari akaanza mazungumzo.



“Natumai, wewe ni mtoto wa mzee Swai.”



“Hujakosea, mimi ndiye.”



“Nahuzunika kukuambia kuwa, baba yako amefariki dunia.”



“Eeeh, haiwezekani baba yangu aniache kwenye kipindi kigumu” alisema Coletha huku machozi yakimlenga lakini baada ya muda alilia kweli hadi wauguzi wakaitwa wamtoe nje wakambembeleze na kumfariji.



Wauguzi wawili walimrudisha Coletha mapokezi kwaajili ya kumbembeleza, walimbembeleza Coletha kuanzia mchana hadi jioni ndipo akaja kunyamaza aliponyamaza akaitwa tena na daktari ofisini. Coletha alienda alifika akaketi kitini na kumpa nafasi daktari ya kuzungumza.



“Najua unaumia, ila nakusihi jikaze ili urudi nyumbani ukaendelee na mazishi” alizungumza daktari kwa kumfariji Coletha, akatulia kidogo daktari kwa kumwangalia Coletha kwa muda kisha akaendelea kuzungumza.



“Kwasasa mwili wa baba yako upo Mochwari...kesho ukishaandaa mazishi njoo uufuate.”



“Sawa, nimekuelewa” alisema Coletha kisha akaruhusiwa aende nyumbani na daktari kwaajili ya kwenda kuandaa mazishi.



Coletha kabla hajaenda akatafuta usafiri wa bajaji umpeleke Ilala Boma kwa mama yake, aliupata kisha akapelekwa alifika usiku wa saa moja Ilala Boma akamkuta Doreen na mama yake wamelala akachukua simu kwenye pochi akampigia rafiki yake simu ikapokelewa.



“Doreen, nifungulie mlango nipo nje” aliongea Coletha kwenye simu.



“Nakuja, subiri kidogo” aliongea Doreen huku akijifunga khanga kifuani na kwenda kufungua mlango.



Coletha aliingia ndani kwa kuchechemea kutokana na ajali waliokumbana nayo, mwendo ule ulimuogopesha Doreen shauku ya kuuliza ikamjia na akauliza.



“Coletha, mbona unachechemea?.”



“Ni majanga makubwa, tuingie chumbani nitakusimulia” alijibu Coletha kwa mkato kisha wakaingia na Doreen chumbani.



“Mama, ameshindaje?” aliuliza Coletha mara baada ya kuingia chumbani na kuketi kitandani na Doreen.



“Kashinda salama...wewe umepatwa na nini?” alijibu na kuuliza Doreen.



“Nimepata, ajali na baba” alijibu Coletha huku akilia kwa sauti ya chini kwa kumuogopa mama yake asisikie.



“Poleni sana...sasa baba yeye yupo wapi?” swali lile lilizidi kumpa machungu Coletha na kumfanya azidi kulia kila akikumbuka kilichotokea kwa baba yake.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Mbona unalia, halafu hunijibu swali langu?,” Doreen alizidi kuuliza mara baada ya kuona Coletha analia wala hamjibu swali lake.



“Baba amefariki, na sasa yupo Mochwari” alijibu Coletha safari hii huku akijifuta machozi kwa leso yake aliyoishika mkononi.



“Unasema, kweli?” aliuliza Doreen kwa kutoamini kabisa kama Mzee Deus Swai ameaga dunia.



“Ni kweli, kwasasa mzee wetu hatunaye tena” alisisitiza Coletha kwa uchungu kwa kuondokewa na mzazi wake mmoja.



“Pole sana...kwa hiyo mazishi yatafanyika kesho?” aliuliza Doreen huku akionyesha kuumizwa na msiba wa Mzee Swai.



**********

Mzee Panta Guno na vijana wake waliingia ndani na gari mara baada ya kufunguliwa geti na mlinzi, walishuka ndani ya gari na kuelekea ndani kwa kupepesuka kuashilia wamelewa sana wakafika ndani mzee Panta Guno akapitiliza chumbani kulala na kuwaacha vijana wake sebuleni wamelala. Asubuhi na mapema simu ya mkononi ya Anitha inaita, Anitha akiwa chumbani kitandani akaamka akaipokea simu kisha akaongea kwa kuuliza kwa sauti ya chini.



“Nani, mwenzangu?.”



“Dada, ni mimi mdogo wako” sauti ya upande wa pili ilijieleza.



“Oooh, Yulietha mzima?.”



“Mzima...Dada nina shida na baba halafu baba mwenyewe hapokei simu” aliongea Yulietha.



“Ulimpigia, saa ngapi?.”



“Jana, usiku.”



“Alilewa sana jana, hivyo nakushauri mpigie kwenye simu ya mezani labda atapatikana maana si unamjua baba yako akilewa tu simu anazima.”



“Sawa dada, ngoja nijaribu kumpigia” alizungumza Yulietha kisha akakata simu.



Baada ya masaa mbele simu ya mezani iliita ndani mwa mzee Panta Guno bahati nzuri mwenyewe alishaamka yupo sebuleni basi upesi ile simu ikapokelewa.



“Baba, Shikamoo” sauti ya upande wa pili ilitoa salamu.



“Nani?...Yulietha mziwanda” aliuliza Mzee Panta Guno kabla ya kuitika salamu.



“Eeenh, baba” alijibu Yulietha.



“Marahaba mwanangu, hujambo?” aliitika salamu na kuuliza Mzee Panta Guno mara baada ya kufahamu kuwa anaongea na mwanae kipenzi.



“Baba, huku si kwema.”



“Kwanini, mwanangu?.”



“Nimekamatwa, nipo kituo cha polisi.”



“Kisa, nini?.”



“Nimesingiziwa, nimeuwa.”



“Looh, umekamatwa kituo gani?.”



“Cha, TUSIIME.”



“Mkuu wa kituo, yupo hapo?.”



“Yupo, na ninavyoongea anakusikia.”



“Mpe simu niongee, naye” aliongea Mzee Panta Guno kisha Yulietha akamkabidhi simu mkuu wa kituo aongee na baba yake.



“Hallow, bwana Panta Guno” aliongea mkuu wa kituo mara baada ya kukabidhiwa simu na Yulietha kisha akaonyesha kujuana na Mzee Panta Guno kwa kuwa Mzee Panta Guno ni mfanyabiashara mashuhuri katika nyanja mbalimbali.



“Eeenh, niambie nasikia mtoto wangu mmempa kesi ya mauaji...ni kweli?” aliuliza Mzee Panta Guno.



“Sijajua, kumbe huyu ni mwanao?.”



“Yaah, ni mtoto wangu wa mwisho.”



“Aisee, tusamehane sana lakini tupo kwenye uchunguzi maana sisi wenyewe tulipata taarifa kwa raia mwema...ikibainika hana kosa tutamwacha huru.”



“Sawa, naombeni mfanye uchunguzi upesi mtoto wangu atoke huko sio kuzuri” alisema Mzee Panta Guno kisha akakata simu na kumwachia fursa mkuu wa kituo.



Baada ya lisaa Anitha akatoka chumbani akaenda jikoni kupika kifungua kinywa akiwa anapita pale sebuleni baba yake alimuona akamuita, akatii wito akaenda kumsikiliza baba yake.



“Wewe, nani kakutoa chumbani?” aliuliza Mzee Panta Guno mara baada ya mtoto wake kukaa sofani.



“Hata hamkupiga lock vizuri mlango, ndiyo nami nikachukua chance hiyo kutoka” alijibu Anitha.



“Dosagon huyu msheeenzi sana...mimi sikutaka utoke mapema namna hiyo” aliongea Mzee Panta Guno kwa kufoka.



“Mimi ndiyo nishatoka hivyo...na tangu lini ukaona mtoto wa kike anachungwa hivyo hiyo ilikuwa kitambo hicho.”



“Naona ushatoka...sasa nasema hivi ukiendelea kutembea na Gerald Eduardo utamuweka kijana wa watu kwenye matatizo” alimaliza kusema Mzee Panta Guno kisha akatoka nje kutulia kwenye bustani ya nyumbani.



**********

Mathias aliachwa njia panda hakuwa na jinsi tena akaweka simu yake mfukoni kisha akaendelea kula, muda kidogo akawa kamaliza kula akamuaga mama Bonge kisha akarudi ofisini kuendelea na majukumu. Alirudi na akaendelea kuhudumia wateja hadi mishale ya kufunga ofisi yapata kama saa mbili na nusu alifunga ofisi na kurudi nyumbani, kufika chumbani alifikia kujilaza na usingizi ukamkumba alikuja kushtuka ngoma inaenda saa nne kasoro akaenda kuoga kisha akaingia ndani kubadili nguo kisha akatoka tena nje kwenda kula chakula cha usiku mgahawani. Mathias aliagiza msosi na akala mara baada ya kuletewa msosi na maman'tilie alimalizia kula akalipa pesa kisha akarudi nyumbani kabla hajafika nyumbani akiwa njiani mbele yake akaona jopo kubwa la vijana likija upande wake, vijana hao walikuwa si wengine walikuwa ni PANYA ROAD ambalo ni kundi la kihuni liloleta tishio viunga mbalimbali vya jiji la Dar es salaam hususani maeneo ya Kigogo, Mabibo, Manzese, Tabata na Tandale.



“Yalaaa” ilisikika sauti ya Mathias ikigugumia kwa maumivu aliyoyapata kwa kupigwa na ubapa wa Panga mara baada ya kundi la PANYA ROAD kumuweka mtu kati.



“Nimesema, kaa chini” ilisikika sauti ya kiongozi wa PANYA ROAD ambaye ni kijana aliyechafuka uso kwa mangeu ya kila aina ikisema kwa ukali na kumuamuru Mathias akae chini.



Mathias alitii alikaa chini kwa hofu akiogopa kudhurika na kundi hilo matata lenye kila sifa mbaya kwenye mitaa ya uswazi.



“Una nini, humo mfukoni?,” Kijana mwingine mdogo mdogo tu alisikika akimuuliza Mathias huku akimsachi mifukoni.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Mathias alinyamaza kimya kwa hofu pana moyoni mwake maana ukisema fyoko wanakumaliza na silaha zao za ncha kali yaani wana Mashoka, Mapanga, Bisi bisi, Mikuki na Mikasi pamoja na Marungu.



“Kiongozi, ana pochi yenye pesa ya kiasi cha shilingi thelathini elfu tu,” Kijana yule aliendelea kuongea mara baada ya kumsachi Mathias na kumkuta na pochi yenye pesa huku akimuonyesha kiongozi wake. Ashukuru Mungu Mathias hakuwa na simu angekuwa nayo tu simu ingeenda na maji.”



“Zinatosha hizo...twendeni” alisema kiongozi wa PANYA ROAD huku akitaka kuondoka.



“Kiongozi kwanini tusimdhuru, ili iwe fundisho kwa wale wote watembea usiku?” aliuliza kijana yule aliyemsachi Mathias kwa kumhamasisha kiongozi wake.



“Hapana, tusimdhuru kwa kuwa ameonyesha upole mbele yetu” alikemea kiongozi yule wa PANYA ROAD huku akiondoka na baadhi ya vijana wake.



“Unabahati sana wewe bwege, kosa kiongozi kukutetea ningekumaliza shingo hiyo,” Kijana yule alimwambia Mathias huku akimpiga Mathias makofi mawili ya shavu kisha akawakimbilia wenzake na kutokomea eneo lile.



Mathias alinyanyuka toka chini kinyonge kisha akaendelea na matembezi ya kurudi nyumbani, alifika nyumbani akaingia ndani akaenda hadi kwenye swichi alipochomeka simu yake chaji akabonyeza kitufe chekundu mara moja simu ikawaka kuangalia akaona missed call ya Coletha. Mathias alijaribu kumpigia Coletha lakini kwa muda ule nahisi Coletha alilala hivyo simu haikupokelewa. Akaacha simu yake chaji hatimaye akarukia kitandani kisha akapitiwa na usingizi kabambe asubuhi ya saa moja na nusu simu yake ikamuamsha kwa kuita akakurupuka kitandani akaifuata simu kisha akapokea alikuwa ni Coletha.



“Hallow” sauti ya Coletha ilisikika ikiongea.



“Niambie...Coletha” alisema Mathias huku kwenye uso akiachia tabasamu mwanana.



“Safi...kuna dharura imetokea kwa hiyo leo sitoleta CD.”



“Usijali...utaniletea hata kesho.”



“Sawa, nitakuletea kesho.”



“Lakini Coletha... kwanini leo usinisikilize maongezi yangu.”



“Nimekuambia tafuta muda wako mzuri na sehemu nzuri, unialike nije kuzungumza nawe kwa kina” alimalizia kusema Coletha kisha kitufe chekundu cha simu kilimhusu na kumwacha Mathias akiwa ameduwaa na kujihisi ana mikosi kwa Coletha.



**********

Peter hakukata tamaa ya kumpigia Coletha simu alipiga tena simu na simu punde tu ikapokelewa na Coletha.



“Eeenh, Peter samahani kwa kukatisha mazungumzo mwanzo,” Coletha aliongea kwa kujihami mara baada ya kupokea simu.



“Usijali...nakusumbua sana kwa kuwa huku kuna matatizo kidogo” alisema Peter.



“Matatizo gani, tena?.”



“Benson, amepatwa na ajali na sasa yupo hospitali amepungukiwa na damu,” Peter alidanganya.



“Sasa, kashawekewa damu?.”



“Bado...daktari kaniambia kuwa inahitajika damu kununuliwa au mtu ajitolee kumchangia.”



“Ngoja nitume pesa, sasa hivi kupitia kwako ikanunuliwe damu.”



“Sawa, tuma ili muda huu awekewe dripu la damu.”



“Usihofu” alisema Coletha kisha akakata simu na muda huo huo akaangalia muamala wa Airtel kama una salio, alikuta una salio la kutosha.



Haraka akaingia airtelmoney kwa kupiga nyota moja tano sifuri nyota sita sifuri reli kisha sawia akachagua namba moja tuma pesa kisha akachagua namba moja tena weka namba akaweka namba kisha akaweka kiasi cha pesa na nywila hatimaye akatuma pesa kwa Peter ili ahudumiwe Benson kipenzi chake wa maisha. Peter mara baada ya kutumiwa pesa kwenye simu yake akaelekea kwa wakala kutoa ile pesa alitoa kisha akarudi kwa daktari kumkabidhi pesa ya kununulia dripu za damu kadhaa, daktari alipokea pesa kisha akaenda maabara ya hospitali kuchukua dripu za damu alichukua dripu tano za damu na kwenda nazo kwenye wodi aliyokuwepo Benson kumuwekea.



**********

Coletha kama alivyomjibu shoga yake kuwa mazishi kesho hivyo ilivyofika siku akafuata mwili wa baba yake hospitali na kujumuika na majirani kuzika mwili wa mzee Swai. Mazishi yalivyoisha alimchukua mama yake na kuhama naye Kigogo katika nyumba ya baba yake kisha nyumba ya Ilala ya mama yake akaiuza, walianza maisha mapya na mama yake katika nyumba ya Kigogo zilipita kama siku kadhaa za kupumzisha akili yake na kumhudumia mama yake na mara baada ya kumrudishia Mathias CD yake. Siku moja ya weekend akiwa anamwandalia mama yake uji rafiki yake Doreen alikwenda kuwatembelea alimkaribisha rafiki yake ndani kisha akaenda kumalizia kupika uji jikoni aliivisha kisha akamnywesha mama yake, baada ya kumnywesha uji mama yake akampeleka chumbani kujipumzisha kisha yeye akarudi sebuleni kupiga soga na rafiki yake.



“Mama, hajambo lakini?” aliuliza Doreen mara baada ya Coletha kuketi sofani na kumuazima sikio kwa umakini.



“Hajambo” alijibu Coletha huku akibonyeza vitufe vya simu yake aliyoishika mkononi.



“Nashukuru...Coletha, hivi unamjua Mathias?” aliuliza Doreen.



“Yule wa, CD?” aliuliza naye Coletha.



“Yes.”



“Eeenh, namjua...wewe umemjuaje?.”



“Ofisi yake si ipo karibu na nyumbani, hivyo ni wepesi kumjua” alijibu Doreen kisha akatulia kidogo na kuongezea mazungumzo.



“Basi leo, nimekutana naye njiani.”



“Kasemaje?.”



“Kaniambia nije kukuuliza kuwa maongezi yake, kwanini unayapuuza?.”



“Doreen, sijapuuza bali sitaki aje kuumia maana lengo lake nishalijua...wewe mwenyewe shahidi kuwa ni jinsi gani ninavyompenda Benson hii leo nije kumkabidhi moyo mtu nisiyemfahamu.”



“Coletha, si lazima umpende kimahusiano mpende kama rafiki tu, ili mradi kijana wa watu asuuzike moyo.”



“Nitafikiria ushauri wako, kwasasa niache kidogo nipumzishe akili yangu.”



“Sawa...lakini wewe mwanamke mchoyo yaani tokea nimekuja hujanikaribisha hata soda wala maji” alibadili mada Doreen kwa kuchombezea utani.



“Nisamehe rafiki yangu, siunajua nimepitiwa na ubuyu.”



“Nishasamehe.”



“Unakunywa, kinywaji gani?.”



“Acha tu shoga yangu, nilikuwa nakutania” alisema Doreen huku akivika miwani yake kwa usahihi.



Baada ya maongezi ya muda mrefu Doreen aliaga kwa shoga yake Coletha kuwa anaondoka, kwa kuwa Coletha mama yake amelala bado akachukua uamuzi wa kumsindikiza rafiki yake alimsindikiza rafiki yake hadi jirani na kwao kisha akarudi nyumbani akiwa anarudi njiani alikutana na Mathias akiwa anaenda kufungua ofisi.



**********http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Anitha alipika kifungua kinywa akamuita baba yake aje kula kisha yeye akaingia chumbani akakaa kidogo simu yake ikaita kuangalia anayepiga ni Gerald Eduardo, akakata simu lakini mpigaji hakuchoka alipiga tena hata hivyo Anitha akakata tena ikapigwa tena safari hii Anitha akapokea simu yake kwa ghadhabu.



“Hallow.”



“Anitha, mbona unanikatia simu?” lilikuwa swali la Gerald Eduardo mara baada ya Anitha kupokea simu.



“Tatizo wewe huelewi, sijui kiziwi mtu akikuambia hakutaki kwanini unamlazimisha” alijibu Anitha huku akionekana na kuchukizwa na simu ile aliyopiga Gerald Eduardo.



“Leo sikutaka nikuudhi na sikutaka nikuambie neno langu ninalokuambiaga, bali leo nimekupigia simu ili uje tufurahi na tuanze ukurasa mpya wa urafiki wa kawaida.”



“Sina, muda.”



“Anitha, kunikataa umenikataa hata ofa yangu leo nayo unaikataa...hebu usinifanyie hivyo.”



“Sawa, nitakuja ili nikufurahishe lakini sitokaa sana.”



“Ondoa shaka, kwa hilo.”



“Upo wapi, sasa?.”



“Nipo, SERENA HOTEL.”



“Sawa, nitakuja” alisema Anitha hatimaye akakata simu na kuanza kujiandaa.



Mzee Panta Guno akiwa peke yake sebuleni akipata kifungua kinywa ghafla akapigiwa simu na mwanae Yulietha aliye South Africa kimasomo, haraka mzee Panta Guno alipokea simu.

Baba nafurahi kukutaarifu kwamba, kwasasa nipo huru alieleza Yulietha mara baada ya baba yake kupokea simu.



“Maafisa, walifanya uchunguzi?” aliuliza Mzee Panta Guno kwa kutaka kujua.



“Walichunguza, na wakakuta sina hatia.”



“Mwenye hatia, ni nani.?”



“Msomali mmoja hivi, na kwasasa yupo rumande kesho anataka kupelekwa mahakamani kusomewa hukumu.”



“Safi sana...sasa soma kwa uangalifu si unajua kuwa huu ni mwaka wako wa mwisho wa kupata masters ya uhandisi.”



“Najua, nitakuwa mwangalifu.”



“Sawa, nakutegemea” aliongea Mzee Panta Guno kisha Yulietha akakata simu. Dosagon na Norman walitoka chumbani wakamuaga bosi wao mara baada ya mzee Panta Guno kumaliza kuongea na mwanae.



“Mzee, sisi tunatoka mara moja” aliaga Dosagon.



“Mnaelekea, wapi?” aliuliza Mzee Guno.



“Tunaenda, SERENA HOTEL” alijibu Norman.



“Kuna ishu gani, huko?” aliuliza tena Mzee Guno.



“Hakuna ishu, tunaenda matembezi tu” alijibu tena Norman.



“Okay.”



Norman na Dosagon mara baada ya kuaga wakatoka nje wakapanda gari la bosi wao na kutoka nalo. Lisaa limoja likapita naye Anitha akatoka chumbani akaja sebuleni kumuaga baba yake safari hii mzee Panta Guno alipitiwa na usingizi pale sebuleni mara baada ya kumaliza kunywa kifungua kinywa, Anitha alitoa vyombo alivyolia baba yake kisha akamwamsha baba yake na kumuaga.



“Baba, natoka baadae” aliaga Anitha huku akimwangalia usoni baba yake aone atasema nini mara baada ya kumwamsha.



“Unaenda, wapi?” aliuliza Mzee Panta Guno huku akimkazia mwanae macho.



“Naenda Mbezi Beach, kwa rafiki yangu” alijibu Anitha kwa kuongopa.



“Sio unanidanganya, unasema unaenda kwa rafiki yako kumbe unaenda kwa mshenzi mwenzako Gerald Eduardo” machale yalimcheza Mzee Panta Guno.



“Hamna baba, siwezi kwenda huko,” Anitha alimpeti peti baba yake kisha akakubaliwa kwenda huko Mbezi Beach kama alivyodai mwenyewe.



Dosagon na Norman walifika Serena hotel na punde meza yao ikachafuka kwa vinywaji vikali vya baridi. Zilipita kama nusu saa Anitha alionekana naye kuingia kwenye ile hoteli ya Serena akashangaa baadhi ya watu kwa dakika kisha akamuona mhusika wake aliyemuita taratibu Anitha akamfuata mlengwa wake bwana Gerald Eduardo halisi.



“Anitha, karibu,” Gerald Eduardo alimkaribisha Anitha kitini kwa tabasamu bashasha.



“Asante” alisema Anitha kisha kuketi kitini.



Upesi Gerald akamwagizia kinywaji Anitha vinywaji vikaletwa wakawa wanapata vinywaji huku wakiendelea kupiga soga mbili tatu.



**********

Benson aliwekewa dripu ndani ya masaa mawili madripu yalikwisha akapumzishwa kidogo kisha akaruhusiwa kurudi nyumbani, walirudi hosteli na Peter kufika tu wakamkuta Yulietha yupo nje akiwasubiri. Peter alichukia mno kiasi cha kutamani amnase hata makofi Yulietha akijua yeye ndiye chanzo cha Benson kuwa katika hali ile alitaka kumnasa tu Benson akamzuia.



“Peter, muache” aliongea Benson huku akishika mkono ambao Peter aliotaka kumpiga nao Yulietha.



“Kwanini?...hujui kama huyu ndiye aliyekusababishia matatizo” aliuliza na kusema Peter mara baada ya kuona kuwa rafiki yake anatetea maovu.



“Hapana, huyu hajanisababishia matatizo aliyenisababishia matatizo ni Msomali” alizidi kutetea Benson.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Bila yeye Msomali angekushuti na Bastola?...si yeye ndiye aliyesababisha” alizidi kupinga Peter na kuonyesha sura ya kumchukia Yulietha.



“Peter, unalaumu kwa kuwa hujaona na hujajua ni jinsi gani Yulietha anavyonipenda.”



“Anakupendea, nini haswa?.”



“Nimeshuhudia kwa macho yangu anavyomkana Msomali kisa mimi, hivyo basi sina budi kumpenda” alisema Benson huku akionyesha ishara ya hisia ya upendo kwa Yulietha.



“Basi nami sina budi tena ya kuingilia mapenzi yenu, ili hali mwenyewe umekufa umeoza kwa mtoto wa kitanga” alisema Peter kwa utani huku akimwangalia shemeji yake Yulietha na kuliachia tabasamu bashasha.





ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog