Simulizi : Nilivunja Ndoa Zangu 3 Kulipiza Kisasi
Sehemu Ya Nne
(4)
SEHEMU YA SABA.
Ilikuwa siku ya
ijumaa, nilikuwa nimejikali nyumbani tu, siku hiyo nilikuwa nimeomba ruhusa ya
kumpeleka mtoto shule kwa ajili ya sports day, na ilikuwa ni lazima kuhuwepo,
hivyo niliongea na muajiri wangu na akanipatia likizo ya siku sita kama
nilivyoomba. Kwani nisingeweza kupewa ruhusa ya siku moja kutokana na taratibu
za kazi, akanishauri ni bora nichukue likizo ya siku saba kama kuna ambalo
nataka kulifanya nilifanye kabisa.
Zaidi ya kuwepo shuleni kwa siku moja
hiyo kwa sports day sikuwa na jambo lingine la kufanya. Sijui ni furaha ya
kulipiza kisasi ama ni nini, Nilipendeza sana na kunawiri mno, uzito
uliongezeka, lakini kutokana na umbo langu bado nilionekana nimependeza sana na
kunawiri, kila aliyeniona alinisifia sana na kuniambia nimependeza mno. Hii
ilinifanya niendeleee kupata moyo, wasijue yanayonisibu.
Ninazo siku 6
za kukaa tu nyumbani, hapana haiwezekani, nitasafari na Majid, kwani si
kanihitaji mwenyewe, nitasafiri.
Je nitaombaje ruhusa? Lazima nitafute
ugomvi, Jones nikimuomba ruhusa hivi hivi hataniruhusu, hawezi, hawezi,
ananilinda sana sasa hivi, lazima nitafute ugomvi.
Ahaa, naweza kutafuta
ugomvi, naweza hili halinishindi, naweza.
Niliporudi kutoka shuleni,
Jones alikuja na kunikuta nimekaa chumbani, alikuwa na furaha sana. Ama Kweli
ashukuriwe Mungu ambaye mwanadamu huwezi kuona moyo wa mtu anavyokuwazia,
tungechinjana sana.
Aliingia ndani na kunikuta nimejibwaga kitandani,
alikuwa na furaha sana,
Aliniuliza habari za mtoto shule, na nilimueleza
ni njema sana,
Akaingia bafuni kuoga na akatoka, bado nilikuwa
nimejilaza kitandani, kila nilipokuwa kimya nilikuwa nikitunga sheria, Kimya
change siku zote kilikuwa sio cha kutulia tu hivi hivi la hasha, ni kimya cha
kutunga shiria nitalipizaje kisasi ili wahusika waumie haswa.
Jones
alitoka na alipotoka ikawa kama alijua namtaka uchokozi. Cha kwanza aliniuliza
mbona kama umechoka? Ama umekunywa pombe zako tena Charlote?
Heeeee,
alijuta,, nasema ungekuta nalumbana naye ungemhurumia.
Nilikaa, nilikuwa
nimefunga khanga ya kifuani tu na kwani nilihitaji kupigwa na upepo. Kwa umbo
langu lilivyo kubwa nilisimama na kila kiungo cha mwili wangu kilitetemeka kwa
namna nilivyokuwa naongea, sio makali, mapaja , wala mikono na matiti,,
nilisimama na kushika kiuno.
Nilimtazama na kumwambia,,, Jones, naona
umenichoka,,hivi kwa nini huniamini? Nakuuliza hivi kwa nini huniamini? Kwa nini
unapenda kuniambia sana kuhusu pombe? Si tumekubaliana ni ache na leo ni karibu
wiki ya pili sinywi? Hivi mbona unapenda maneno wewe mwanaume? Khaaaa,,,
nilikuwa nimeshika chupa ya perfume nikaipigiza chini, tena ile perfume
aliyoninunulia.
Jones alishikwa na butwaaaa. Akanishika mikono na
kusema, Charlote,, sipaswi kukuliza mama? Sipaswi mke wangu kukuuliza lolote? Ni
makosa? Aliongea kwa upole sana,, niliitoa mikono yake kwangu kwa kuirusha ili
iiachane,,
Kisha nikamtazama na kumuuliza,, hivi nikikuuliza Bado tu
hujaachana na Husna utajiskiaje?
Jones, alisema basi mama, basi mke
wangu yaishe,, yaishe…
Nilianza kulia na kulalamika ndoa gani hii ambayo
haina furaha wala amani, ndoa gani hii jamani? Nililia sana na huwa nina machozi
ya karibu sana.
Lakini nilikumbuka kwamba kinachoniliza ni uchungu wa
Jones kuwa na mahusiano na Husna, yani jambo hili liliumiza sana moyo wangu na
kuwa na Donda kuu lisilopona. Ndicho kiliniliza, nilimpenda sana jones, sikutaka
kusikia habari hizi kabisa, na kusamehe nilishindwa, isipokuwa ahueni nilikuwa
naipata kwa mimi kulipiza kisasi, na ni ahueni ya kuniliwaza kwa muda tu, lakini
sio ya kuniliwaza kwa moja kwa moja.
Jones alinifuata na kuniambia mke
wangu samahani, samahani Charlote mke wangu am sorry mami,, sikujua nimekuumiza
samahani, yaishe.
Nilikuwa nalia sana, kweli hakukuwa na pombe kabisa
ndani kwani nilishaacha kabisa kunywa, kwa sababu niliona najiumiza maini yangu.
Kwa namna nilivyokuwa nakunywa nyingi bila kipimo. Nikaogopa kuwa abused na
alcohol.
Ilifika saa mbili usiku bado tunalumbana, Jones aliniomba sana
msamaha, nikawa siongei tena ila nalia tu.
Jamani,, ni kukuuliza tu ama
kuna jengine charlotte? Mbona un hasira hivi? Huwezi kusamehe na kuachilia mke
wangu?
Nilimtazama na kumwambia sio kirahisi hivi, Je wewe ukigundua
nina mahusiano nje ya ndoa utajisikiaje? Nijibu nakuuliza
utanisamehe?
Jones alisema ndio nitakusamehe. , nitakusamehe
charlotte.
Nikamwambia, basi subiri siku niwe naye alafu nikuombe
msamaha unisamehe.. mfyuuuu nikafyonza na kuondoka kuelekea chumba cha watoto
ambacho hakitumini ila hutumika kwa waageni tu na kujifungia
humo.
Nilifyonza kwani ninajua waname wengi ambao hawawezi na
hawakuwasamehe wake zao mara baada ya kusikia, kuhisi ama kuiona wana mahusiano
na wanaume wengine, hivyo nilijua kusamehe kwa mwanaume ni ngumu
sana.
Nilikaa chumbani huko mpaka nikalala, nikiwa nimejifungia mlango.
Jones alikuwa anajuta kwa nini alifanya mahusiano na Husna, ndoa yake sasa
alianza kuiona achungu. Asijue mkewe nina agenda ya kulipiza kisasi na karibu
sana mission yangu itatimia.
Aligonga sana, badae mida ya saa saba usiku
nilifungua na kuelekea chumbani, nilimkuta amekaa anasoma kitabu, ni mpenzi wa
kusoma, hakuwa na usingizi.
Aliniambia Charlote unanitesa sana, naumia
sana juu yako.
Nilimwambia … Jones, maumivu unayoyapata ni moja ya nane
na yamumivu niliyo nayo mimi kuhusu wewe na Husna, na sijui hili donda
litaponaje, kila nikijaribu kuliponya inakataa.
Jones alinitazama na
kuniambia,, kwa hivyo unataka kuniambia hukunisamehe?
Kwa sauti kabisa
nilijibu, NDIO NIMESHINDWA KUKUSAMEHE, NIMESHINDWA.
Jones alifunga
kitabu chake na kunitazama tena, Aliniambia Charlote niambie nifanye nini ili
unisamehe juu yangu na kosa nililokukosea naomba uniambie nifanye
nini/
Nilimtazama na kumwambia,,, Iko siku na mimi nitakukosea pengine
unaweza kushindwa kunisamehe, na itakuwa ni sehemu yaw ewe kupima na kujua je
msamaha ni kitu RAHISI AMA KIGUMU???
Unasemahe Charlote? Umepanga
kunilipizia kisasi? Unataka kunilipizia kisasi?
Nilimtazana na kumwambia
umesema wewe ila ni lazima ukosewe ili ujue msamaha ni jambo rahisi ama
gumu.
Sina ninaloweza kukueleza zaidi, nilimaliza na kupanda kitandani
na kulala.
Jones hakuwa kashiba alikuwa na njaa. Alienda jikoni na
nilimskia akiwasha microwave na kama anayepasha kitu.
Alikuja chumbani
na sahani na kuniambia, Charlote, hujala na mimi sijala usiku huu, tafadhali
amka tule.
Nilimhurumia sana Jones, ni mwanaume ninayempenda sana,
lakini kwa nini KISASI kimenikali kooni? Kwa nini?
Niliamka huku machozi
yakinichuruzika. Nilimambai Jones kula, kula sitakula. Nilitoka chumbani na
kwenda kukaa sebuleni.
Nilitafakari mambo mengi sana muda ule, najiuliza
hivi mwisho wa familia yangu ni nini?
Mwisho wa ndoa yangu ni nini?
Mbona nimejirahisi sana? Kwa nini lakini nimekuwa na mahusiano na Mzee Zuberi
kwa nini? Na sasa nataka kuwa na Majidi kwa nini? MOyo wangu uliniuma
sana,
Nililia sana, wanangu je,, mume wangu je? Wazazi wangu
je?
Aghraaaaaa… niliendelea kuulia sana, Jones alikuja na kukaa kochi la
pembeni, kisha wote tulipitiwa na usingizi mpaka ashb.
Asbh huwa Jones
huenda kazini na kufanya kazi nusu siku.
Alipokuwa anaondoka
nilimwambia, Jones nina likizo ya siku 6. Nahitaji kupumzika, nahitaji kwenda
mahali kupumzika,
Jones alinitazama na kuniambia ni haraka sana, unaenda
wapi? Nilimwambia najua mwenyewe nitakapoenda mahali ambapo nitatuliza kichwa na
akili yangu, najua itanisaidia.
Jones aliniambia hapana
hutaenda,
Niliwambia je wewe nilikukataza kuwa na Husna?
Nilikukataza?
Jones alitingisha kichwa na kusema , Charlote naomba kosa
nililofanya isiwe sababu ya kunikosesha amani na furaha kwenye maisha yangu,
nimeshakuomba msamaha sana, nimejuta sana lakini huoni.
Fanya utakavyo,
na kama unataka ndoa hii ife na ife, nimechoka… siwezi kuwa mtumwa wa ndoa kisa
kosa.
Aliongea kwa hasira na kufoka sana.
Nilimwambia ahaaa. Kwa
hivyo unaona ni sawa u livyofanya mpaka unasema kama ndoa kufa na ife eee,
okay.
Niliingia ndani, Alipark gari na kuja ndani,
Alinishika
kwa nguvu mkono kwa nyuma na kuniambia unataka nini wewe mwanamke? Unataka
nini?
Nilianza kulia tena. Kisha alipigiwa simu ya ofcn akiambiwa
anahitajika haraka sana.
Aliondoka na kuniacha peke
yangu.
Nilianza kufungasha kibegi change cha safari. Na kisha baadae
nilitoka na kumuaga dada kwamba nitarudi baada ya sikuu tano.
Dada
aliniaga na nikawabusu wanangu na kutoka.
Nilichukua taxi mpaka hotel
Fulani ambayondiyotulikutana na Majid mara ya kwanza.
Nilipofika pale
nilimpigia simu majidi na kumueleza kwamba ninahitaji kuonana
naye.
Kwanza alipenda kuniutii kwani alijua ni biashara, lakini pia
alinitii kwa vile alinihitaji kimapenzi. Hangekuwa na ujanja wa kukataa kuja,
hili nililitambua.
Nilikua nimevalia blauzi nzuri na jeans ambayo
ilishika mwili wangu vyema na kuonyesha umbo langu lilivyokaa.
Nikiwa
pale hoteli kabla majid hajafika tayari nilishasalimiwa na wanaume zaidi ya
watatu wakitaka kuiongea na mimi kuhusu mapenzi. Niliwaona na kujua lengo
lao.
Lakini sikuwa kwa ajili ya hayo, ila kulipiza kisasi.
Baada
ya dakika 45, Majid alikuwa ameshawasili, Aliniona nikiwa nimevimba macho yakiwa
mekundu. Na akaniulizakulikoni? Alipomaliza tu kuniuliza machozi yalinidondoka
tena, nikamwambia tumepishana kauli na mume wangu, akaniambia pole.
Huyu
mwanaume ambaye haoni na kujua thamani yako anawezaje kukuudhi kiasi hiki?
Niliendelea kulia, kisha nikamueleza nimeamua kutoka kwa siku 6 kwenda kutulia
mahali. Ndo maana nimekuja kukuuliza kama una nafasi kutokana na ombi lako ili
tuwe pamoja.
Majid hakuamini, aliniambia sawa kabisa, sawa, Sasa naomba
siku moja ya leo tu, na kesho jioni tusafiri na ndege ya saa tisa kuelekea
Zanzibar ama unaonajee?
Nilimueleza ni sawa.
Hivyo akanilipia
hotel night moja na kuniambia kesho saa tisa tutasafiri pamoja.
Tulikaa
pamoja muda wote huo, kuanzia saa sita mchana mpaka saa kumi na mbili jioni,
huku tukizungumza, kula na kunywa, na akinisifia sana.
Kilichonishangaza
simu zake ziliuwa on lakini husna hakuwa akiongea naye wala kuwasiliana naye,
hali kazalika na mimi pia sikuwa nawasiliana na Jones, japo mimi nilizima simu
zangu.
Niligundua wanawake tuna madhaifu katika mawasiliano, unawezaje
kutowasiliana na mchumba wako ama mume mtarajiwa muda wote huo?
Baadaye
mida ya saa kumi na mbihli na robo aliniaga na kunieleza tukutane airport saa
saba kwa ajili ya ndege ya saa tisa kwa safari ya
Zanzibar.
***********************************************************************************************
SEHEMU
YA NANE:
Simu zangu nilikuwa nimezima zote, hakuna ambayo
ilikuwa iko available. Nilizima makusudi, sikutaka kusumbuliwa, nilijua tu Jones
atakaponitafuta akinikosa ataongea na wadhamini wetu wa ndoa, kwani ndivyo
tulikubaliana kwamba endapo kutakuwa na tatizo kabla ya kushrikisha wazazi ni
lazima tuongee na wadhamini kwanza endapo tatizo litakuwa kubwa
sana.
Hivyo haraka nilitoka na kwenda kibanda cha simu, ambapo
nilimpigia mdhamini wa kike kumueleza situation nzima. Nilimueleza kwamba
nimtoka nyumbani kutokana na matatizo, hivyo nimeamua kupumzika na niko salama,
na nitarudi nyumbani baada ya wiki.
Mdhamini alipoendelea kuhoji na
kunishauri kwa nini nimefanya hivyo nilimueleza kwamba nitakaporudi nitaeleza
tatizo.
Hata hivyo alinieleza kwamba Jones alishazungumza na mumewe na
kumueleza kwamba tumekorofishana na kumueleza kisa kizima , sikutaka kuongea
sana na mdhamini wa kike kwani sikutaka kupoteza mood yangu, lakini nilijua
kumpa nafasi ya kuongea zaidi anaweza kunishauri jambo na nikajikuta nimeghairi
ninachotaka kukifanya. Hiyo nilimkwepa.
Sikia,,, niko salama, nitarudi
nyumbani in 6 days, angalia watoto. Kwaheri.
Nilimkatia simu na
niliondoka, na hata angepiga tena ni lazima angeambiwa mteja ameshaondokana
hatujui alipoeleokea kwani hapa ni kibanda cha simu tu.
Nilifika
hotelini, sikutaka kujishughulisha na lolote, zaidi ya kula, na kulala tu
basi.
Nilikula nikalala, na wala sikutumia pombe kwani nilijua Majidi
sio mtumiaji wa pombe na ningemkwaza endapo asbh ningeamka na
hangover.
Usiku haukuwa mzuri sana, kwani nilifikiria familia yangu
sana.
Lakini mara nilipowaza niko kwenye kisasi usingizi ulikuwa mzuri
na kujikuta Napata mbinu mpya kila mara ninapotafakari.
Nilishangaa ni
saa tatu na roho asbh. Dah,, nimechelewa sana kuamka. Nilianza kujiandaa,
nilishuka chini kwa kifungua kinywa, nilikunywa na kushiba. Kisha nilipigiwa
simu nikiwa chumbani na kuambiwa kuna mtu anataka kuzungumza na wewe. Nilijua
fika ni Majidi na si mtu mwinigne yeyote Yule.
Ni kweli ni
Majid.
Charlote,,, aliita… yes.. niliitika.
Ninatuma mtu aje
akupeleke airport… mh.. niliguna.
Mbona unaguna? Nilishangaa kwa nini
anatuma mtu.. nilimuuliza huyo unayemtuma ni salama?
Aliniambai ni
swaiba wangu hana shaka. Anakuja hapo Omary kukupeleka airport.
Usijali.
Niliitika sawa. Kisha baada ya muda mchache sana alikuja kijana
na kuuliza.. aliniulizia, kisha nikaitwa kwani nilikuwa room.
Nilishuka
na begi langu, na kumkuta kijana reception akinisubiri.
Habari dada,,
bila shaka wewe ni Charlote… ndio niliitika.
Basi nimeambiwa nikupeleke
airport… asante nilijibu.
Safari ya airport iliianza. Nilifika na
kumsubiri Majidi afike.
Baada ya muda mchache sana, majidi aliwasili.
Nilimuona nikaburudika, nilisika faraja.
Moyoni niliwaza kumkomesha, na
kupanga kufanya kila kituto cha kimapenzi ili kumlobesha,,, nilitaka kumfanya
achachawe haswa, na niache chapa ya penzi langu kwake.
Ki umri tulikuwa
tunalingana, lakini bado alionekana mdogo kwangu kutokana na nilivyojazia
.
Alionekana kuridhika na mimi.
Nilijua tunaenda Zanzibar, hivyo
nguo zote nilizobeba zilikuwa ni nguo zinazofaa kutumika sehemu za pwani,
niliamua kumkomesha Majidi, asijue lengo langu ni nini.
Muda wa kusafiri
uliwadia. Tulisafiri salama, rubani wa ndege aliendesha ndege salama kabisa, na
ndani ya dakika 30 tayari ndege ilikuwa imeshatua na tulikwua
tukishuka.
Mh,, Majid alikuwa akinibana sana, alinisogelea karibu sana,
na kuniambai usiogope Charlote,, mh.. kuna wakati nilikuwa naogopa. Lakini
nikasema nani ananiona huku Zanzibar, nani ananiona?
Hakuna ambaye
ananifahamu, na hata angenifahamu maisha yangu yanamhusu nini?
Mimi peke
yangu ndiye nilikuwa najipa moyo kwani sikuwa na wa kuweza kumshirikisha jambo
na azma yangu.
Tunaenda stone town,,,, Mkwezi hotel…. Majid alimpa
maelezo dereva taxi.
Haoo, ndani ya dak 10 tulikuwa ndani ya hotel ya
mkwezi, hotel ya kifahari, nzuri, na ilikuwa na wazungu tu. Tuliingia kwenye
room yetu, na moja kwa moja Majid alinikumbatia na kuniambia, Charlote nashukuru
sana, kwa muda na nafasi hii ambayo umenipatia, umeniheshimu sana na
sitakuangusha.
Nilimwambia wala usijali, nashukuru pia kwa nafasi hii
ambayo umejitolea kwangu, ni nafasi yap ekeee kwa bwana harusi mtarajiwa kuamua
kutoka na mimi. Hii kwangu na hesabu ni heshima ya pekeee.
Majid
alitabasamu kisha akasema ama kwa hakika Charlote umeniteka moyo wangu na fahamu
zangu. Mpaka sioni thamani ya ndoa dah?natamani ungekuwa hujaolewa
ungenisababishia nifanye kituko cha duniani.
Wote tulicheka, lakini
alionekana mwenye furaha sana, sasa sijui ni kwa ajli yangu tu ama kwa ajili ya
jambo gani.
Baada ya kama muda wa nusu saa aliniambia Husna anapiga
simu… nilinyamaza kimya,, na kumuacha azungumze na Husna.
Alitumia tu
dakika chache sana ambazo hazikuzidi 3. Na alikata simu na kumtakia usiku
mwema.
Dah.. nilishangaa inakuwaje…. Mume mmtarajiwa yuko safarini alafu
ulale salama saa mbili na robo???
Nilijua ndiyo maisha
yao.
Tulioga na akaniambia kwamba anataka kunitoa niutazama mji wa stone
town usiku nione unavyofanania.
Tulijiandaa na kwenda kutembea mjini
usiku huo. Mji wa Zanzibar ulikuwa unavutia sana, mzuri sana, na wenye
kupendeza. Tulitembea mpaka saa sita, tulipitia soko la zanzibari ambalo ni
maarufu sana Forodhani, na nilikula chakula ambacho sikuwahi kukila hapo mwanzo.
Mbatata za urojo,, ama kweli kilikuwa kitamu.
Baada ya hapo tulirudi
hotelini. Nilijua nitakuwa na kazi nzito usiku huo, hivyo nilikuwa nimejiandaa
bara bara.
Asbh tuliamka, na aliniaga na kuniambia anaelekea bandarini
kwa ajili ya kucheki mizigo yake. Aliniacha hotelini nikiwa nimekaa tu chumbani.
Baada ya muda mchache alikuja na kuniambia.. dah mwanamke una kismart sana wewe.
Contena zangu zimefika salama salmin, na sio kawaida kuja siku moja na kukuta
mambo sawia mara zote ninakaa zaidi ya siku tatu nakuendelea ila leo dah, niko
na mwanamke mwenye ngekewa.. mambo swari.
Jiandae tukapate chakula cha
mchana mamiii.
Nilijiandaa na kutoka kwa ajili ya chakula cha
mchana.
Tulipata lunch nzuri sana, kisha baada ya hapo tulitoka na
kuelekea sehemu za kuutazama mji wa Zanzibar ambazo ni za makumbusho.
Tulizunguka mji huo haswa , na baada ya hapo tulienda bandarini kuangalia
contena zake ambazo zilikuwa zimewasili, kisha kukagua baadhi ya mizigo yake
kuona kama imefika yote salama.
Ilikuwa ni zoezi zito kidogo, lakini
tulimaliza na aliita vijana ambao walimsaidia pia kuhesabu baadhi ya mizigo
ambayo alikuwa akiiacha Zanzibar na mingine ya kuelekea dar.
Tulitoka
hapo tukiwa tumechoka wote, kwani hata na mimi nilimsaidia kuhesabu baadhi ya
bidhaa.
Siku zote tulizokaa Zanzibar zilikuwa nzuri sana, tulifurahiana
wote wawili, ungetuona wala usingefikiri ni mtu na kimada, ila moja kwa moja
ungejua ni mtu na mke wake tena wanaopendana sana. Majid alinipenda
sana.
Safari ya kurudi dar iliwadia, dah, moyo wangu ulianza kuniuma
naenda kukutana na kero zngine, sikupenda kabisa mimi kuondoka Zanzibar mji wa
maraha.
Saa nne na nusu nilikuwa nimeshafika dar, moja kwa moja
nilielekea nyumbani, nilfika nyumbani na kumkuta dada na watoto hawapo. Na
funguo huwa kama nyumba imefungwa tunazichukua kwa jirani, nilienda kwa jirani
na kuchukua funguo. Nilifungua nyumba, na mlangoni nilikuta ujumbe kwenye
karatasi.
NAOMBA USIINGIE NDANI KWANGU, RUDI ULIPOTOKA…. Nilicheka
sana.
Kisha na mimi nikachukua kalamu na karatasi na kuandika… UJUMBE
NIMEUKUTA, SAWA NARUDI NILIKOTOKA TAKE CARE.
Sijui ni kiburi gani
nilikuwa nacho, sijui ni roho gani iliniingia. Niliingia na kuchukua nguo za
kunitosha kama begi mbili hivi kwani niliweka na pochi na viatu kwa ajili ya
kazini.
Kisha nikafungu nyumba na kuondoka. Na hapo niliwasha simu
zangu.
Nilijiuliza ni hoteli gani ya bei rahisi? Nilipata na kulekea
hotelini hapo ambapo chumba ni shilingi 35000 kwa siku. Nilimpigia mzee Zuberi
simu kumsalimia na kumueleza nimerudi salama safari yangu, kwani nilimuaga na
kumueleza niko nje kikazi. Na alinitumia pesa za safari. Kisha nikamueleza pia
kwamba nimerudi salama isipokuwa mume wangu kanifukuza kwa vile ya wivu.
Alinihurumia sana na kuniambia nisijali, kama nina tatizo nimueleze. Nilimueleza
niko hotelini kwa sasa mpaka hapo nitakapomjulisha
kitakachoendelea.
Alinihurumia sana na kuniambia ninyi bado ni watoto
hivyo kuonena wivu ni lazima.
Nilijilaza hotelini wala nikiwa sijali, na
niliamua kumpigia simu Majid kwa simu ya hotelini kumueleza
kilichojiri.
Haloo…. Aliitika,, niliongea kwa upole,,, uko mahali salama
tunaweza kuongea ni mimi shalooo… mwenyewe aliniita baby
shalo.
Aliniambia ndio kuna tatizo? Kama aliyeshtuka. Ndio kuna
tatizo,,,, ila sio kubwa,,
Enhe… niambie nini shida? Dah.. kama aliogopa
kidogo.. nilimueleza kwamba nimefika nyumbani na kukuta ujumbe kwamba nirudi
nilikotoka,, hivyo nimeamua kuchukua hotel.
Majid alisema sikia shalo,
usiogope tuko pamoja, usiogope kabisa,,, wewe tulia hapo, kisha utanijulisha
kitakachoendelea, kama ni pesa ya hotel nitalipa,, ila usipanick wala kusema
lolote, sawa???
Nilimwambia sawa kisha nikashanga imekuwaje hajali? Ni
anavunga ama?
Baada ya lisaa limoja niona Jones akipiga simu,, kwanza
niliitazama sana simu, kisha ikakata,, nikasubiri ipigwe tena.
Akapiga
tena ikakata, nikasubiri apige tena.
Akapiga tena nikapokea.. haloo…..
Akapokea haloo…
Hivi charlotte ni maisha gani haya? Nikamuuliza yapi?
Wewe si umesema nirudi nilikotoka nimerudi.
Mh.. akaguna akaniambia uko
wapi? Nikamwambia nilikotoka. Kisha nikakata simu na kuzima
kabisa.
Ninafikiri alihangaika sana kunitafuta, nilikuwa sina la
kumueleza kwani nilijua ana hasira sana, hivyo sikutaka hata tukutane tuongee
maana tungepigana mpaka basi.
Asbh nilijiandaa na kuelekea kazini.
Nilipofika tu kazini huyu hapa, namuona Jones na wadhamini wa ndoa wako
pamoja.
Niliwasalimia,kisha wakataka kuzungumza na mimi, niliwaeleza
naingia kazini kwanza, pengine wapange tuongee saa ngapi. Wadhamini hawakuamini,
licha ya Jones.
NIliwapiga nikaingia kazini na kufanya kazi zangu. Lunch
time jones alipiga sikupokea, Jioni saa kumi na moja wakati natoka , nilitoka na
hakukuwa na mtu, nilichukua taxi na kuelekea hotelini kwangu. Nilipofika tu, ni
kama walikwua wananifuatilia, waliiingia na kunikuta niko
reception.
Charlote aliita Jones, niligeuka na kuitka, yes… ni wewe
ama?
Nikajiangalia na kumwambia yes ni mimi. Hata na mimi nakushangaa ni
wewe ama?
Wadhamini waliona kwamba wote tuna hasira hivyo walisogea na
kusema yapaswa tuongee. Inatakiwa tuongee, tafadhali charlotte tunaomba
utukaribishe chumbani kwako tukazungumze.
Nilipaacha rafu naomba
nikaparekebishe kwanza. Niliondoka na kuwaacha wamekaa,, kisha mdhamini wa kike
akanifuata na tukaingia chumbani.
Akaniambia Charlote wewe ni kiboko,,
unawezaje kufanya haya lakini?
Nilimwambia yakikufika utaweza,
yakikufuka utaweza mama,, niache tu maana ni issue nzito.
Akaguna.. mh…
lakini mbona wala sio nzito mama yangu? Mbona mpaka na msamaha kakuuomba jamani?
Si umsamehe kiishe? Angalia usije kujuta mama yangu, najua unapendwa na
utapendwa na wengi ila utaishia pabaya.
Mdhamini wa kike alikwua
anaongea kama kameza kanda.
Sikuwa namsikiliza hata kidogo maana sikuona
sababu ya kuweka hayo maneno moyoni, na hayakuwa na
nafasi.
SEHEMU YA TISA:
Baada ya dakika chake aliingia
Jones na mdhamini wa kiume.
Jones alionekana kuchoka sana, na hakuongea
lolote zaidi ya mdhamini wa kiume na wa kike.
Lengo lao ilikuwa ni
kutupatanisha, walitueleza kwamba mtu unapokosewa na mwenzako anapoomba msamaha
basi ni lazima umsamehe. Na akasema kukosa mara ya kwanza sio kosa bali kurudia
ndio kosa.
Mdhamini wa kiume alieleza kwa namna ya kueleweka kabisa, na
akijaribu kumueleza Jones namna ambavyo wanawake wakikosewa na wakichefukwa
wasivyoweza kurudi kwenye nafasi zao za kwanza zaidi ya kuumia sana, isipokuwa
yeye kuonyesha kubadilika ndiko ambako kutamfanya mke aweze kuamini ameombwa
msmaha na kuamua kusamehe. Hivyo alimtaka Jones kukirii kosa lake mbele yangu
kwa mara ingine tena.
Jones hakuonekana kuwa mgumu. Aliniomba msamaha na
kusema anatamani tuendelee na maisha yale ya mwanzao.
Mdhamini wa kiume
alinigeukia na kuniambia Charlote ni lazima umsamehe mumeo. Nilimwambia ni ngumu
kumsamehe kirahisi, ila nitajitahidi kumsamehe moja kwa moja na ninakiri
kumsamehe ila asipobadilika basi msamaha unaweza usitoke
kabisa.
Mdhamini aliniomba sana nimsamehe, na nilikubali.
Na
alimwambia Jones, nivyema sasa ukawa karibu sana na mkeo ili aaminmi umemuombe
msamaha kwa kumaanisha, vinginevyo ukikosea tena unazidi kumfanya awe na moyo
mgumu na wakutosamehe na kusababisha madhara zaidi.
Jones alikubali na
kusema amebadilika kabisa na hana mahusiano na mtu yeyote Yule.
Mdhamini
wa kike alinitazama na kuniambia, Charlote unaivunja nyumba yako mwenyewe, huyo
shetani aliyewaingilia ashindwe kwa jina la Yesu.
Tulimaliza kuzungumza
an kukubaliana kurudi nyumbani na kuendelea na maisha. Lakini kabla ya kuondoka
tulikunywa na kula chakula hotelini kisha mdhamini wa kiume akaenda kuchukua
watoto na msichana wa kazi na kuwaleta nyumbani.
Nilikuwa niko tu okay,
sikuwa natatizo lolote lile. Jones alikuwa karibu sana na mimi, akijiongelesha
sana, lakini sikuwa namjibu kwa wakati, sio kama nilikuwa nampuuza la hasha, ila
kuna hali Fulani iliniingia ya kumchukia tu na si vinginevyo, nikimuona na
kumhesabu ni Msaliti mkubwa sana kwenye ndoa yangu.
Maisha yaliendelea,
Mtaani shamra shamra za Harusi ya Husna na Majid zilishamiri na kupamba
moto.
Kila kona ilikuwa ni story ya harusi yao.
Kila mmoja
alikuwa amejiandaa vyema kwa ajili ya harusi hiyo.
Kwa vile sikutaka
jambo lolote lijulikane la mahusiano kati yangu na Mzee Zuberi wala Majdi,
nilijitahidi kufanya siri sana, tena siri kubwa sana.
Mzee Zuberi
tuliendelea kuwasiliana. Na siku moja aliniita ofcn kwake akinitaka niende
kuchukua mzigo, ambao sikujua ni mzigo gani.
Ilikuwa ni majira ya
mchana. Niliondoka ofcn mara moja na kuelekea kwa mzee Zuberi.
Nilifika
ofcn kwake na alinikaribisha vyema kama kawaida, alizoea kuniita Bi mdogo.
Nilifurahia sana jina hilo. Alinipenda sana.
Nilifika na alinitazama na
kuniambia,, wewe mtoto nakupenda sana na leo nina zawadi yako ambayo nataka
usinisahau hata nikifa unikumbuke. Nilijiuliza ni zawadi gani? Sikuwa na idea
hata kidogo. Kwani amekuwa akinipa pesa na viatu na nguo ila leo ananipa
nini?
Alivuta droo yake na kutoa bahasha kubwa ya A4 ya rangi ya khaki.
Na kuniambia chukua fungua.Bado sikuwa nawaza ni nini.
Niliichukua
bahasha ile na kuifungua, Dah… waoo, nilijikuta nikitamka kwanguvu baada ya
kufungua habasha ile.
Uwiii, sikuamini nilichoona ndani
yake.
Nikiwa nimekaa kitini huku nikiwa ninashangaa karatasi ile iliyo
mezani kwake, alisimama na kunisogelea karibu kabisa, na kuzunguka nyuma ya
mgongo wangu na kunishika mabega, huku nikiwa nimegeuza uso wangu kwa nyuma
nikimtazama.
Alinibusu na kuniambia,Charlote wewe ni msichana mzuri
sana, unayenipenda, unayeniheshimu na kunijali sana, na kukifanya kichwa change
kitulie kwa penzi lako, unastahili zawadi nzuri kama hizi za
maisha.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment