Simulizi : Penzi La Mfungwa
Sehemu Ya Nne (4)
Ghafla jeshi la polisi lilifika eneo la tukio,polisi hao walikuja na gari lao huku mbavuni mwao wakiwa na bunduki. Polisi mmoja aliyeonekana ndio mkuu wa msafara alitelemka kwenye gari kisha akazipiga hatua kuufuata ule umati,akiwa amekunja uso mithiri ya mtu aliyekula shubili. Polisi huyo alisema "Kuna nini mahali hapa?..", lakini wanakijiji hawakujibu,kila mmoja alionekana kukaa kimya ambapo ndipo yule mkuu wa msafara alipo muita kijana mmoja wa makamo falagha kisha kusema naye. "Kijana habari yako"
"Ni nzuri tu Afande sijui ya kwako",alijibu huyo kijana huku akionekana kujiamini kabisa,kwani hakuonyesha hofu yoyote kusimama na kamanda. Polisi alitazama kwanza upande ule waliosimama watu kabla hajaongeza nanl la pili,baadaye kidogo alirudisha uso wake kwa kijana huyo aliyekuwa naye falagha halafu akaendelea kuasema. "Naomba uniambie kuna kitu gani kimetokea hapa"
"Afande hapa bwana,tumekusanyika kuja kutazama mwili wa mtu aliyefariki usiku wa kuamkia leo. Sisi wanakijiji taarifa hiyo tumeipata asubuhi ya leo kutoka kwa mmoja ya vijana wa hapa kijijini,alitueleza kwamba kuna mtu kauliwa hapa Kwahiyo ndio maana mimi pamoja na wanakijiji wenzangu tumejumuika kuja kushuhudia. Lakini cha kustaajabisha ndugu Afande,maiti hatujaiona", alijibu kijana huyo.
"Unaweza kunitajia jina la huyo mtu aliyefariki?..", alihoji kamanda.
"Ndio, anaitwa Zabroni "
"Zabroni? ..", Afande alistuka kusikia jina hilo ni kama halikuwa jina jipya kuwahi kuisikia masikioni mwake,upesi akamuita kamanda mwenzake.
"Kamanda Pilo hebu njoo mara moja hapa",Afande huyo ambaye alifahamika kwa jina moja tu ambalo ni Pilo, alitii wito haraka sana. Alipomkalibia kiongozi wake alitoa heshima kisha akasema"Naam Afande" aliitikia.
"Pilo,chukua maelezo ya huyu kijana kisha report yake utanikabidhi tukifika ofisini", kwisha kusema hivyo kamanda huyo aliondoka zake akimuacha Pilo akimdadisi mwana kijiji kuhusu tukio nzima,lakini wakati Pilo anamdadisi kijana huyo ghafla alistuka kusikia jina la mtukutu Zabroni. Anamfahamu vizuri Zabroni, hasa hasa kipitia matukio mbali mbali aliyowahi kuyafanya huyo kijana. Wakati Pilo akifikilia matikio hayo,upande wa pili kamanda mkuu akiwa ndani ya gari aliwaza na kuwazua akajikuta kuwa jina hilo sio jipya masikioni mwake,kuthibitisha hilo akaamua kumuita kamanda mwingine aliyekuwa akizungumza na baadhi ya wanakijiji. Nahe alitii wito wa mkuu wake ambapo alipofika,kamanda alimuuliza "Je, unamfaham Zabroni ", kamanda huyo aliyeulizwa alitaharuki sana kisha akasema "Mkuu huyo mtu tema mate chini,nimeshangaa sana kutuamuru kuja kumtafuta huyu kiumbe wakati mwenzetu anatumia uchawi. Eh unona umati huu wa watu uliojikusanya hapa,walikuja kwa niaba ya kuchukua maiti yake waliamini kwamba amekufa lakini cha kushangaza hawajamkuta..", alijibu kwa hofu kamanda,wakati huo Pilo naye alikuwa amefika hapo ambapo naye alimuunga mkono kamanda mwenzake akisema kuwa maelezo aliyoyapata kutoka kwa yule kijana na ambayo amezungumza akamanda mwenzake hayana utofauti kabisa. Hapo mkuu alishusha pumzi ndefu kisha akahoji "Kwahiyo tunacheza na kifo?.."
"Kabisa "
"Ndio kamanda maisha yetu tumeyaweka rehani kabisa",walijibu hivyo hao maafande kitendo ambacho kilimkasilisha mkuu,kwa hasira akasema "Mkumbuke mliweka kiapo,sasa inakuaje mnakuwa waoga? Kwanza serikali yetu haimini masuala ya kishirikina,naomba kila mmoja afanye majukumu yake mpaka huyu mtu atiwe hatiani sawaaa?.."
"Sawa mkuuu ", walijibu wote kwa pamoja afande Pilo na mwenzake. "Haya nendeni mkuwaambie na wenzenu",aliongezea kusema hivyo kamanda kisha akawatawanya wanakijiji warudi majumbani mwao.
Bruno alionekana kuchoka maradufu,asiamini kama kweli Zabroni ni mzima. Alijiuliza ni dawa gani anayotumia kijana huyo kiasi kwamba awe moto wa kuotea mbali?. Kibaya zaidi zaidi kilicho mtia hofu kijana Bruno ni baada kufikiria kisasi gani atakacho kuja nacho huyo Zabroni ikiwa hapo awali alimueleza kuwa hayupo tayari tena kufanya unyama baada kukamilisha azma yake. "Inahitaji moyo pia na nguvu za ziada ",alijisemea Bruno huku akiwa na mwenyeketi wakitembea kurudi kijijini baada kutawanywa na jeshi la polisi. .
Usiku ulipo ingia hali ilikuwa shwari kijijini hapo,siku takribani tatu sasa zilikatika bila balaa lolote kutokea. Siku ya nne usiku,Bruno alimwambia Mwemyekiti wa kijiji ambaye pia ndio alikuwa mwenyeji wake hapo kijijini,alimwambia kuwa muda wa kurudi nyumbani kwao sasa umefika. "Mzee nimekaa sana hapa kijijini mimi pamoja na marehemu kaka yangu enzi ya uhai wake, nimeona changamoto mnazo kutana nazo kiukweli zinatisha. Kaka yangu amejaribu kupambana na huyu mtu lakini hajaweza kufua dafu,mwisho wa siku ameambulia umauti. Mimi pia nimejaribu kupambana na huyu mtu mpaka tonya la mwisho mpaka nikajua nimemmaliza,ila wapi kumbe jamaa bado yupo hai. Kiukweli huyu mtu hafai hata chembe,anatisha sana inatakiwa nguvu ya ziada kumdhibiti. Je, nguvu hii nitaipata wapi? Kwani bado inanibidi nilipe kisasi cha kifo cha kaka yangu. Nisipo fanya hivyo sitokuwa na amani ndani ya moyo wangu mpaka naingia kaburini. Sasa basi ili nilipe kisasi ni lazima nikaongeze nguvu kwenye mizimu ya ukoo wetu ili niweze kumkabili huyu mtu. Kesho narudi nyumbani mzee wangu,lazima nipambane na huyu mtu mpaka mwisho ",alisema Bruno huku akiongea kwa uchungu kutoka moyoni. Mwemyekiti alimtia moyo akimwambia kuwa hakuna mwamba chini ya jua ipo siku yake naye atakwama.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kesho yake asubuhi mapema Bruno alianza safari ya kurudi nyumbani kwa niaba ya kuongeza makali ya kuweza kumkabili mtukutu Zabroni, lakini wakati yupo njiani,alionekana kijana Zabroni akizurula katika kijiji chakina Bruno. Na punde si punde Zabroni alijibadilisha akawa katika umbo la Bruno kisha akajongea mpaka nyumbani huku mkononi akiwa na mifuko iliyojaa vitu mbali mbali,huku mgongoni akiwa amebeba begi. Hakika watu walimshangaa sana Bruno mlowezi aliyerejea,wakati huo wengineo wakitamani kumuona na kaka yake malehemu Madebe kwani waliondoka wote katika shughuli za utafutaji maisha. Ni kiini macho na ujanja aliotumia mtukutu Zabroni ili amalize hasira zake, watu waliamini kuwa ni Bruno karejea wasijue kwamba huyo sio Bruno wanao mjua wao,bali huyo ni mtukutu Zabloni aliyechukuwa taswira ya Bruno ili afanye balaa kwa kutumia kivuli cha Bruno,mwisho wa siku msala uangukie kwa kijana huyo ambaye naye yupo njiani anarudi kuongeza dawa za kufanikisha kumkabili Zabroni. Wazazi wa Bruno walifurahi kumuona mtoto wao,Bruno alijieleza kuhusu kutokuwepo sambamba na kaka yake. Akiwa na furaha alisema "Kaka nimemuacha huko anafuatilia madeni yake,ila nafikiri kesho naye atafika "
"Aaah hakuna tatizo baba yetu, yani kama umerejea salama basi Mungu atamsaidia na yeye kurejea salama pia", akiwa na wingi wa furaha mama Bruno alimwambia kijana wake.
Kesho yake asubuhi Zabroni aliwauwa wazazi wa Bruno kisha akaondoka zake,hiyo ikiwa kama moja ya malipo ya kufatiliwa na mtoto wao aliyejikita kwenye vita isiyo muhusu. Ila atafanya nini sasa ili amuachie msala Bruno?. Hapo sasa ndipo alipomuuwa mmoja ya vijana hapo kijijini hadhalani huku baadhi ya watu wakishuhudi balaa hilo la kinyama kwani tayari ilikuwa ni asubuhi. Hivyo alivyokwisha kufanya hicho kitendo alijigamba "Mimi ndio Bruno,hakuna atakae niweza. Nimeua kwa mikono yangu ",alisema Zabroni akiwa na taswira ya Bruno kisha akatokomea zake huku akiacha maswali mengi kwa wenyeji. Habari zilizagaa upesi kila pande kuhusu hayo mauwaji, walijua dhahiri shahili Bruno ndiye aliyefanya mauwaji ilihali wakati huo huo stendi ya gari alionekana kijana Bruno mwenyewe akishuka kwenye gari baada kufika kijijini kwao alipo zaliwa,macho na hisia akitamani kuonana na wazazi wake ili wamsaidie katika kitu alicho pania kula nacho sahani moja na mtukutuku Zabroni.
Bruno alipigwa na butwaa baada kuona watu wakimnyooshea vidole,alijiuliza kitu gani ambacho kinapelekea mpaka yeye anyooshewe vidole? Je, wameshajua kama kaka yangu kafa? Ama kuna jambo gani linalo endelea. Hatamaye alikaribia kufika nyumbani kwao,alistuka kuona umati wa watu ukiwa umejikusanya nyumbani kwao huku sauti za vilio zikisikika masikioni mwake. Bruno alishitu mara dufu, hapo sasa kijasho kikaanza kumtoka,mwili wake nao ukihisi kukosa nguvu. Upesi aliachia mazaga zaga aliyokuwa ameyabeba,mazaga ambayo yalifanana fika na yale aliyokuwa nayo Zabroni kipindi anaingia hapo kijijini kwa taswira ya Bruno. Macho ya watu walio jikusanya hapo walipomuona Bruno walikunja nyuso zao huku baadhi yao wakizungumza maneno ya kumkashifu,maneno ambayo yalisikika vema ni pale mzee mmoja wa makamo aliposikika akisema "Ama hakika damu ya mtu nzito kuliko maji,ona sasa muuwaji kajileta mwenyewe. Hebu akamatwe haraka sana iwezekavyo"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mmh huyu sio mtu wa kawaida jamani,tukimfuata kizembe tutajikuta tunapoteza maisha ",alidakia mtu wa pili akisema hivyo,huyo alikuwa ni kijana wapata umri miaka ishirini na mitano. Hoja yake hiyo iliungwa mkono na baadhi ya watu wengine waliokuwepo hapo wakati huo tayari Bruno alikuwa ameshafika nyumbani kwao ambapo alistaajabu kuona watu wanamkwepa,hali hiyo iliendelea kumjengea hofu moyoni mwake,na ndipo alipopasa sauti akisema "Jamani kulikoni mbona siwaelewi?.." Alihoji huku akijitazama akigeuza shingo huku na kule kutazama sehemu mbali mbali za mwili wake. Lakini hakujibiwa,hivyo aliamua kuingia ndani ambapo huko walionekana wanawake wakilia kwa uchungu ila walipo muona Bruno haraka sana walikaa kimya kisha mmoja mmoja akatoka ndani. Hakika watu walimuogopa Bruno,walijuwa ndio kafanya mauwaji kwani wakati anatoka ndani baada kuuwa alionekana na mmoja ya jirani yao huku nguo zake zikiwa zimetapakaa damu. Achilia hapo,kitendo kingine ambacho kilipelekea Bruno kuogopwa, ni pale alipomuua hadharani mmoja wa kijana kijijini hapo huku akijigamba kuwa amefanya mauaji kwa kukusudia napia hakuna mtu wa kuweza kumtia hatiani. Lakini yote hayo yaliyofanyika hakuyafanya Bruno kama watu walivyodhani,bali mtendaji alikuwa ni Zabroni ambaye alichukuwa taswira ya Bruno na kisha kuuwa ikiwa kama njia ya kumsababishia msala Buruno. Hayo yote Zabloni aliyafanya baada kuingilia ugomvi usio muhusu huku akijaribu kufanya jaribio la kumuuwa.
Bruno alikabaliana na hiyo hali watu kumuogopa,hakujali bali alijongea mpaka mahala pale ilipo lazwa miili miwili ikiwa imefunikwa vitenge. Alipo ifikia akaifunua, alistuka kuona miili ya wazazi wake ikiwa imeuwawa kikatili. Alilia sana huku akiwataja wazazi wake walio uliwa, na mwishowe alinyanyuka akatoka ndani. Nje alimuita mzee mmoja aliyemuona anabusara,mzee huyo alipoona anaitwa na Buruno aliogopa kwenda lakini wazee wenzake walipo mtaka aende alitii wito. "Habari yako mzee" alisema Bruno huku moyo wake ukiwa umefura hasira kama nyoka aliyemkosa binadam.
"Nzuri..nzuri kijana wangu ", alijibu huyo mzee akiwa na wasiwasi mfano wa mtu aliyefumaniwa ugoni.
"Hivi unawez kunitajia ama unaweza kunieleza ni nani aliyefanya hiki kitendo?.." alihoji, swali hilo lilimshangaza huyo mzee akajikuta akishindwa jibu la kumpatia kwani anafahamu fika kuwa Bruno ndio muuwaji sasa inakuwaje atake kutajiwa muuwaji?..Mzee akajiongeza kwa kukataa kwamba hamjui muuwaji. "Sawa nenda ", mzee alirudi kujichanganya na wenzake. Wakati huo huo jeshi la polisi likiambatana na mbwa watano huku likiwa na siraha mbali mbali lilifika eneo hilo la tukio,kwa niaba ya kumkata muuwaji. Bruno bado alikuwa katika hali ya kupigwa na bumbuwazi asijue kinacho endelea,lakini punde alifahamu kinacho endelea baada mama mmoja ambaye alionekana kulia kwa uchungu huku akimnyoshea kidole . Mama huyo akilia alisema "Yule pale muuwaji,kaniulia mwanangu. Hafai kabisa sitaki hata kumuona machoni mwangu",kamanda mkuu alitoa amri kuwa Bruno akamatwe. Bruno alishangaa,akajiuliza "Mimi nimekuwa muuwaji?mmmh hapana!.." baada kujiuliza hivyo ikabidi ajitetee lakini Bruno hakueleweka,alikamatwa huku wakimtaka akajieleza mbele kwa mbele. Ndani ya gari la polisi Bruno alirushwa kisha gari likatimua mbio ilihali huku nyuma wakisalia baadhi ya polisi kwa niaba ya kuzika hiyo miili iliyo uwawa kikatili. Bruno akiwa ndani ya gari hilo la polidi,alijiinamia huku akijiuliza maswali mengi kichwani mwake. Alijiuliza "Hivi ni nani muuwaji wa wazazi wangu? Na nikipi kinacho pelekea nikamatwe mimi ilihali mimi sio muuwaji?na endapo nitafungwa nitawezaje kulipa kisasi? Na iweje nifungwe kwa kosa ambalo sijafanya?..", alijiuliza Bruno huku akiwa amejiinamia . Hatimaye walifika kituo cha polisi ambapo hapo Bruno alishushwa mfano wa gunia la mkaa kwa niaba ya kuuingiza selo ili uchunguzi ufanyike kabla hajapelekwa kizimbani, lakini wakati anaingia ndani ghafla alisikia sauti ikimuita. Upesi Bruno aligeukia kule ilipo tokea sauti hiyo ajabu sana alimuona mtu aliyefananae kuanzia sura mpaka nguo alizovaa, si mwingine ni Zabroni. Hapo sasa ndipo Bruno alipofahamu fika mtandaji wa lile jambo ni Zabroni ambaye alifanya jambo lile huku akiwa katika hali yake ili kumsababishia msala yeye. Hakika Bruno akiwa na pingu mkononi aliumia sana,machungu yaliongezeka mara mbili kwani tayari Zabroni alikuwa amemuulia wazazi wake. Lakini yote yote Bruno aliingizwa ndani huku nje Zabroni naye akijinasibu kwa kusema "Mimi ndio Zabroni",kwisha kujisemea hivyo alirudi katika umbile lake la kawaida.
Kazi ikawa imemalizika sasa,wabaya wake alikuwa aneshamalizana nao. Hivyo akawa mtu wa amani wakati wote,alijichanganya na wenzake kwani mahali hapo alikuwa mgeni kwahiyo hakuna mtu hata mmoja aliyefahamu historia yake. Lakini wakati kijana Zabroni akiwa mtu wa amani wakati wote huku akiacha utukutu wake, upande wa pili kule kijijini kwao bado jeshi la polisi lilikuwa likiendelea kumuwinda kwa udi na uvumba. Na mara baada kumtafuta kwa muda mrefu bila mafanikio,hatimaye kamanda wao alipata wazo. Wazo ambalo aliwaeleza wenzake kwamba ili wamkamte Zabroni basi itawalazimu wamtumie mwanamke,kwani kufanya hivyo inaweza kupelekea kijana huyo kukamatwa bila kutoa jasho. Kwa sababu siku zote mwanaume kwa mwanamke huwa ni mzaifu sana,hivyo Mwanamke huyo atakaye teuliwa ni lazima aweke ukaribu na Zabroni wakati huo akimuuliza mambo mbali mbali kuhusu uwezo wake wa kupotea katika mazingira yoyote. Na pia asisahau kumuwekea utani kwa kumdadisi kwamba ili ujanja wake ufike tamati njia gani itatakiwa ifanyike. Kufanya hivyo inaweza kuwa rahisi sana kumkataa Zabroni pasipo kutoa jasho lakini pia mwanamke mwenyewe lazima awe mrembo,sio mwanamke awe na uso mkavu kama fenesi, pua kama nyundo. Kichogo kama kinu . Mwanamke awe mzuri kiasi kwamba akijiweka kwa Zabroni,basi mtukutu asisite kujenga naye uhusiano. Walikubaliana hilo suala wakaona linafaa, lakini ugumu kujua mahali alipokimbilia mtukutu huyo vile vile wapi watampata mrembo wa kuvutia. "Kamanda kuhusu hilo halina shaka,yupo huyu binti aliyeanza kazi wiki iliyopita Afande Veronica,huyu anafaa sana siunaona alivyokuwa mrembo? .."
"Ni kweli anafaa itabidi aje ofisini leo ili niweze kuzungumza naye hili suala ili siku yoyote aanze kazi"
"Sawa kamanda"
Siku hiyo hiyo Afande Veronica alitii wito aliambiwa jinsi hali inavyotakiwa kuwa huku akiahidiwa ZAWADI nono pia kupandishwa cheo pindi atakapo funga ukurasa wa mishe hiyo. Wakati wanafikia muafaka Veronica na mkuu wake, mara ghafla kituoni hapo alikuja raia kutoa taarifa kwamba Zabroni yupo mahali fulani anaendelea na maisha yake. Jambo la heri kiukweli kwa upande wa hao Makanda hao kwani waliona tayari mchezo unakwenda kumalizika.
"Vero,"
"Yes kamanda"
"Wewe mrembo bwana,siku mbili hizi anza kazi,hautokuwa peke yako bali na sisi tupo nyuma yako kukupa ushirikiano. Vaa nguo za kiraia anza kazi"
"Usijali kamanda,wanaume nyie wa kwetu kamwe hamruki katika suala zima la mapenzi hasa kwa mwanamke mzuri kama mimi. Nakuhakikishia hapa kanasa ",alijibu kwa masihara na kujiamini pia Afande Veronica,Afande ambaye alionekana kuvutia kila kona ya mwili. Ngozi nyororo uso mzuri mpaka mwili wake ulivutia umbo namba nane.
Wahenga waliwahi sema kwamba,ukitaka kuruka?sharti uagane na nyonga. Abadani hawakukosea kusema msemo huo,bila shaka waliona mbali sana na ndio maana wakaamua kusema huo msemo ambao unatumika sana kwa mtu aliyeamua kujitosa kutenda jambo fulani. Ndivyo ilivyokuwa kwa kamanda wa kike Veronica, kamanda ambaye aliamua kujitolea kumtia Zabroni kwenye mkono wa sheria kwa kutumia mbinu ya aina yake. Ikimbukwe Zabroni kipindi cha nyuma aliwahi kufanya mauaji mbali mbali,alitia watu hasara mali zao lakini alifanya kila jambo mbaya ambalo hata mwenyezi mungu hapendi. Vitendo hivyo vilipo shamili,jeshi la polisi ndipo lilipo amua kuingilia kati ingawa bado walichemka kwa sababu Zabroni hakamatiki kwa siraha. Baada kumshindwa kwa siraha ndipo walipoona kwamba watumie njia ya mapenzi,kwani mapenzi siku zote yananguvu kuliko kitu chochote hapa duniani kwani mapenzi hayana komando. Sasa basi njia hiyo itweza kumtia mtukutu Zabroni kwenye mkono wa dola? Je, Veronica ataweza?
****
Baada ya makubaliano kufanyika, siku tatu zilikatika. Siku ya nne kamanda Veronique alianza kazi ambapo aliambiwa mahali ambapo Zabroni hupendelea kukaa katika hicho kijiji,hiyo ikawa rahisi kwake kwani alipotembelea maeneo hayo siku ya kwanza hakumkuta lakini siku ya pili alimkuta akishirikiana na wenzake katika shughuli za jamii. Baada kumuona alichomoa picha ndogo aliyokabidhiwa,aliitazama kisha akamtazama Zabroni kule alipokuwa akichakarika. Alipo jihakikishia kuwa ndiyo huyo,aliirudisha kwenye mkoba wake picha ya Zabroni kisha akarejea mjini nyumba ya wageni alipokuwa amepanga chumba. Akiwa amechoka alijilaza kitandani huku akiwa na nguo ya kulalia,kifua chake kikiwa wazi. Kiukweli kilivutia sana,chuchu zilikuwa zimesimama. Ngozi yake ikiwa nyororo pia kitovu chake kilikuwa kina shimo kidogo,tumbo lake likiwa laini kama nyama ya ulimi. Kamanda Veronique alivutia sana kizuri kisifie. Basi hapo baada kujilaza kitandani,akili yake yote aliifikiria namna ya kumkamata Zabroni. Mawazo ambayo yalimpelekea kupitiwa na usingizi ila aliamshwa na sauti ya simu ikiwa inaita,alikurupa kutoka usingizi alipo tazama jina la mtu aliyempigia akaona jina limeandikwa "Kamanda Molisy" alibonyesha kitufe cha kijani kisha akaweka sikioni alisema kwa sauti ya upole "Afande"
"Mmmh Veronique habari yako?..",ilisikika sauti ikijibu hivyo kwa mbali.
"Salama tu sijui kwenu huko"
"Kwetu salama,mbona wasikika kwa upole?..", alihoji kamanda Molisy ambaye ndio mkuu wa kikosi hicho cha kina Veronica.
"Aahmm.. nilikuwa nimelala siunajua kazi ilivyo? Lakini ondoa shaka leo nimebahatika kumuona,nina uhakika kazi itakuwa nyepesi sana", aliongea Veronica huku ikijonyoosha akizipiga hatua kwenye begi lake ili achukue taulo aingie bafuni kuoga.
"SAWA kazi njema,tutakuwa tunawasiliana. Ikitokea tatizo usisite kutupa taarifa mapema ili tuweze kulitatua", alisema Molisy.
"Sawa Afande" Veronica akakata simu kisha akaitupia kitandani,akajongea mpaka kwenye mlango wa bafuni akafungua akaenda kuoga.
Kesho yake asubuhi kabla Veronica hajaanza safari ya kwenda kijijini kuendelea na majukumu yake,alikatiza mitaa ya mji huo mdogo alikuwa amepanga chumba akatokea sokoni kufanya manunuzi mbali mbali matunda na vitu vinginevyo. Lakini wakati yupo ndani ya hilo soko, mara ghafla alimuona Zabroni akiwa na jamaa mmoja ambaye bila shaka alikuwa ni rafiki yake. Veronica alistuka, haraka sana akazipiga hatua mpaka pale alipo simama Zabroni. Alipo mkalibia alimkanyaga makusudi huku akijifanya kumpisha mtu aliyekuwa akipishana naye,kwani eneo hilo palikuwa na msongamano wa watu. Veronica alipo mkanyaga Zabroni alinyanyua mguu haraka sana kisha akasema "Jamaani pole mkaka", Zabroni aliposikia hiyo sauti nyororo alitabasamu kisha akajibu "Usijali najua ni bahati mbaya", alijibu kwa upole huku macho yake akitupia kwenye uso wa Veronica kitendo ambacho kilimfanya Veronica kuachia tabasamu pana huku aking'ata mdomo. Ghafla Zabroni alipagawa ilihali muda huo huo Veronica aliondoka zake,nyuma mkungu wake wa ndizi ukitikisika kiaina yake. Vijana walio mtazama Veronica hawakusubitu kupepesa macho,mirunzi ilisikika kutoka kwa madereva piki piki na wasukuma mikokoteni. Yote hiyo ikiwa ni shamra shamra ya kumuona Veronica akitembea huku makilio yake yakicheza,kiukweli alijaliwa ingawa sio sana.
"Daah ama kweli mjini kuna mambo Zabroni" ,alisema huyo jamaa aliyekuwa na Zabroni.
"We acha tu,tuachane na hayo. Vipi mzigo huu tutauza ama? Kwa sababu bei tuliyoikuta tofauti na tuliyo tegemea"
"Ni kweli,lakini ujue hata tusipouza ni sawa na bure tu. Hizi ni nyanya Zabroni hazichelewi kuoza, Kwahiyo kuliko tupate hasara ni bora tuuze tukagange yajayo", alisema jamaa huyo. Zabroni alijikita katika mambo ya kilimo baada kuona kumaliza kisasi chake. Hivyo siku hiyo yeye na rafiki walikuwa mji mdogo kwa niaba ya kuuza mazao yao.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Walikubalina wakawa wameuza mazao ya kwa hiyo hiyo bei waliyoikuta gulioni,na mara baada kupokea ujira wao walianza safari ya kurejea kijijini ambapo huko hukukuwa na mtu hata mmoja aliyemfahamu Zabroni. Aliishi kwa amani pasipo kuwa na shaka. Lakini kipindi wanatoka gulioni mara ghafla Zabroni akakutana tena Veronica, wote kwa pamoja waliachia tabasamu hasa Zabroni baada kukumbuka kwamba kuna muda aliyekanyagwa na huyo binti akawa amemuomba radhi. Safari hiyo Veronica alikuwa anafungua mlango wa gari teksi,kabla hajaingia ndani alimuuliza Zabroni wapi wanapo elekea,Zabroni akataja na hapo ndipo Veronica alipowataka wapande kwa madai kwamba naye anaelekea huko. Zabroni na rafiki yake walifurahi sana kupata lifti,Veronica akamwambia dereva wake afungue buti nyuma ili waweke tenga ambalo walibebea nyanya. Safari ikaanza kuelekea kijijini,wakiwa ndani ya gari walipiga zogo mpaka mwisho wa safari ya safari ya Zabroni na rafiki yake ambapo walishuka kisha wakatoa shukrani zao. Kabla hawajaondoka Veronica alimuita Zabroni ndani ya gari huku nje akibakia rafiki yake akiwa amesimama...Ndani ya gari Veronica alimwambia Zabroni "Smahani kama hutojali nilikuwa naomba kesho uje mjini tukale pamoja chakula cha mchana,usistuke nimevutiwa sana na ukarimu wako unaonekana kijana mpole,kiukweli kaa ukijua tu kwamba umenivutia sana na pia nitafurahi endapo kama utanikubalia", alisema Veronica kwa sauti nyororo huku uso wake ukionyesha haibu. Zabroni aliposikia maneno ya huyo dada,moyo wake ulistuka. Ndani ya nafsi yake akajiuliza "Bahati gani hii inanitokea? Hili ni zali la mintali siwezi kulipuuzia " kwisha kuwaza hayo alijibu "sawa nipo tayari usijali. Je, tukutane wapi?",Veronica alimuelekeza mahali pakukutana,Zabroni akawa amemuelewa ambapo alisisitiza kutokukosa.
Baada ya hapo waliagana,Veronica akaondoka zake lakini pia Zabroni naye akajua hamsini zake huku kila mmoja akijanasibu kiana yake. Mtukutu Zabroni akijigamba kwamba huwenda akawa amepata zali la mentali kwa Veronica, ilihali Veronica naye akiamini kuwa yule ndege mtutundu anakaribia kunasa kwenye tundu bovu!
Zabroni na rafiki yake wakuitwa Bukulu walipokuwa njiani wakirudi nyumbani,alimuuliza kipi hasa kilichomfanya yule dada ambaye ni Veronica kumuita ndani ya gari huku akionekana kumwambia jambo fulani. Zabroni alicheka kidogo baada kusikia swali la swahiba wake,na kabla hajamwambia, alisema "Ujue tumesahau kununua mafuta ya kupikia, pia chumvi nayo tumeishiwa ndani". Bukulu alishusha pumzi kwa kasi huku akiwa ameshika kiuno chake kisha akajibu "Basi ningojee hapa hapa nikimbie dukani mara moja nikanunue,hatuwezi kula CHUKU CHUKU ilihali hela tunayo bwana",alijibu huku akifatisha na tabasamu pana lililomfanya Zabroni naye kuachia lake. Baada ya hapo alitumua mbio kufuata hayo mahitaji yao,nyuma nako Zabroni akiwa amejiinamia akifimfikiria yule mwadada Veronica.
"Daah hivi ni kweli mimi Zabroni leo hii napendwa na mrembo kama yule? Kwa kipi hasa,maana sina SWAGA sio mtanashati. Yani nipo nipo tu. Ama kweli nimeamini kupendwa ni nyota tu nasio uvaaji ama muonekano. Hapa ni sawa nimeokota chungwa chini ya mnazi ",kwisha kuwaza hayo alichia tabasamu kwa mara nyingine tena wakati huo huo Bukulu naye tayari alikuwa amerudi ambapo alishangaa sana kumkuta rafiki yake akiachia tabasamu. Kimoyo moyo akajisemea "Sio bure huyu jamaa atakuwa kapewa zawadi na yule binti "
"Zabroni vipi naona utabasamu mwenyewe unatabasamu tu", aliongea Bukulu kwa sauti akimwambia Zabroni, Zabroni aliposikia maneno ya Bukulu alicheka kidogo kisha akajibu "Daah! We acha tu,kiukweli yule msichana nilipo muona mara ya kwanza pale sokoni aliponikanyaga. Moyo wangu ulilia paa,hata maumivu siku yasikia"
"Unamaana gani Zabroni? " Bukulu alihoji.
"Maana yangu ni kwamba,Mungu anajua kuumba kaka. Kusema kweli wakati mungu anamuumba yule msichana alitulia, sio wale ambao aliwaumba akiwa na haraka. Ndio maana utakuta mwanamke anakichogo kama mkono wa bunduki,ukimtazama macho mithili ya nyanya chungu..." , alijibu hivyo Zabroni maneno ambayo yalimfanya Bukulu kuangua kicheko kisha naye akaongezea kusema "Kweli kabisa uyasemayo Zabro,utakuta mwanamke kwanza hajui kutembea. Anatembea upande kama ngadu,sura mbovu mbovu tu halafu maajabu ya watu kama hao mtaani wanalinga. Utasikia mimi nataka mwanaume mwenye gari wakati nyumbani kwao hata baiskeli hawana", alitania Bukulu,hapo sasa ndipo vicheko vilipo sikika huku wakigongeana mikono.
Baaada ya kusema hayo kimya kidogo kilitawala huku wakizipiga hatua kurudi nyumbani kwao,lakini muda mchache baadaye Bukulu alifungua kinywa chake na kisha kusema "Haya sasa niambie yule dada alikuitia nini ndani ya gari"
"Sawa ngoja nikwambie rafiki yangu. Ujue yule dada ni kama anashindwa kuniambia ukweli ila mimi kwa kuwa ni mtalamu wa hayo mambo, nimecheza na hisia zake nimegundua kuwa amenipenda. Na kaniambia kesho niende mjini nikaonane naye", alisema Zabroni, Bukulu alikaa kimya kwa muda wa dakika kadhaa kisha akaongeza kusema.
"Enhee umemjibu nini?.."
"Doh Bukulu,ningemjibu nini sasa zaidi ya nipo tayari? Nimemjibu nipo tayari", alijibu Zabroni huku akionekana kulishangaa swali la Bukulu.
"Sawa lakini sio wewe uliyeniambia unatafuta nauli ya kwenda Dar es salaam kumfuata mpenzi wako Tina?..", alirudia kuhoji Bukulu swali ambalo lilimfanya Zabroni kushusha pumzi kwa kasi na kisha kujibu "Ni kweli lakini Bukulu tambua Dar ni kubwa sana halafu istoshe inawatu wengi. Sawa Tina yupo Dar lakini sijui yupo Dar maeneo gani"
"Kwa maana hiyo Zabroni unataka kumsaliti Tina?.."
"Hapana ila kaa ukijua siku zote mwanaume lijali hakai na mwanamke mmoja",alijibu Zabroni kwa kujiamini kabisa. Bukulu alistaajabu kusikia jibu la rafiki yake. Akataharuki "Nini Zabloni? .."
"Mimi naona tufanye mikakati ya kuandaa chakula tu hayo mengine hata baadaye tutazungumza",alijibu kwa mkato Zabroni.
"Sawa pika mboga mimi nitapika ugali"
Zabroni huku akicheka akajibu "Aaawapi huwezi kunilisha ugali mbichi tena leo"
"Alaah! Umeshau wewe ulipo pika wali bila kuuosha mchele? .."
"Afadhali mimi. Je, wewe uliyetia chimvi nyingi kwenye mboga istoshe mboga yenyewe maharage. Osha ujuavyo lakini chumvi ipo pale pale. Kukosea kupo ila kwa leo sitaki turudie makosa"
Vijana hao wawili walitaniana , hayo yalikuwa ndio maisha yao utani ukichukuwa nafasi kubwa huku Zabroni akiwa ameshatundika daluga la kisasi cha damu alichokuwa akikifanya.
Usiku ulipo ingia,usingizi kwa kijana Zabroni ulionekana kikwazo sana kuja siku hiyo hisia zake zote alizipeleka kwa Veronica. Alijipindua huku na kule kitandani huku akitamani pawahi kukucha ili akaonane naye,lakini mwishowe usingizi ulimpitia. Hiyo tayari ilikuwa saa sita usiku. Kesho yake asubuhi alikuwa wa kwanza kuamka akajianda kwa niaba ya kwenda kuonana na Veronica kama walivyo kubaliana. Alimuaga swahiba wake,lakini kabla hajaondoka Bukulu akamwambia "Mbona mapema hivi Zabloni? Subiri basi hata saa nne ama tano ndio uende",Zabloni akatoka nje akaenda kutazama jua kisha akarudi ndani kumjibu Bukulu "Bukulu saa hizi mpaka kufika mjini muda utakuwa umesonga,Kwahiyo acha niwahi"
"Sawa lakini kuwa makini usione vyaelea!"
"Usijali swahiba"
Zabroni akaondoka zake huku nyuma akimuacha Bukulu akitamani ile bahati ingeangukia mikononi mwake.
********
Hatimae Zabroni anaingia mjini,hiyo tayari ilikuwa yapata saa nne kasoro robo asubuhi. Kijijini na mahali ulipokuwa huo mji mdogo palikuwa na umbali kadhaa hivyo licha ya Zabroni kutoka nyumbani mapema lakini alijikuta akifika muda huo,alitumia masaa takribani matatu kwa mwendo wa kawaida.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mahala pale pale walipokubaliana kukutana ndipo Zabroni alipokwenda kutulia, ambapo muda sio mrefu Veronica naye alifika. Veronica alifurahi sana kumuona Zabroni, huku Zabroni naye pia akifurahi kumuona Veronica. Baada ya maongezi mawili matatu walikwemda moja kumbi maarufu hapo mjini,wakala chakula cha bei. Na mwisho wa yote Veronica akamwambia Zabroni kwamba ametokea kumpenda tangu mara ya kwanza alipomuona,hivyo angefurahi zaidi endapo kama Zabroni atamkubalia ombi lake. Zabroni aliposikia habari hiyo kutoka kwa Veronica alijifanya kuringa ingawa mwishowe alikubali,kitendo ambacho kiliwafanya wote kutabasamu.
Mahusiano kati ya Veronica na Zabroni yakawa yameanzia hapo,huku kila hatua anayo fikia Veronica aliwataarifu makanda wanzake kwani ikumbukwe Veronica alipewa kazi ya kumkata Zabroni mtukutu aliyefanya mauwaji ya kutisha kipindi cha nyuma. Kwahiyo baada jeshi la polisi kumuwinda bila mafanikio ya kumpata,ndipo wakaamua kutumia nguvu ya mapenzi ambapo walimteua Veronica Afande mrembo aweze kuimaliza hiyo kazi wakiamini kwamba mapenzi yananguvu sana kwenye huu ulimwengu. Kweli hatimaye Veronica anafanikiwa kumtwaa kimapenzi Zabroni,shughuli ikiwa imebakia kumpeleleza kijana huyo ili kujua ni nini hasa kinamfanya apotee katika mazingira yoyote? Pia ili ujanja wake huo utoweke njia gani itumike? Na je, hatomstukia pindi atakapo muuliza hayo maswali?
Maswali hayo yalimuumiza sana kichwa Veronica ila swali ambalo aliliona ni pasua kichwa ni kuhusu pindi pale Zabroni atakapo mstukia na kumuona kuwa hayupo naye kimapenzi zaidi ya kumpeleleza. Siku moja asubuhi mapema Veronica alimpigia simu kamanda mkuu ili amsaidie japo ushauri kuhusiana na hilo swali. Kamamda akamjibu "Mpe mapenzi ya dhati,mfamye awe na furaha wakati wote. Naamini atanogewa na kukuona mtu wa muhimu kwake. Wanaume tukipenda tunakuwa kama mazezeta Kwahiyo nafasi hiyo itumie kumuuliza historia ya maisha yake japo kwa ufupi akisita kukwambia basi mtoe muende kupata kinywaji sehemu nzuri ya utulivu,hapo mmbembeleza kumnywesha pombe. Akilewa yote atasema ", aliongea kamanda mkuu. Veronica aliposikia maelezo ya kamanda wake alishusha pumzi ndefu kisha akajibu "Ahsante sana tutaendelea kuwasiliana"
"Sawa kuwa makini"
Baada ya maongezi aliirudisha simu juu meza halafu akajitupa kitandani. Siku hiyo hakwenda kokote, aliamua kupumzika.
Siku zilisonga..Mapenzi ya Vero na Zabroni nayo yakiendelea kushika kasi. Wiki mbili baadaye zilikatika bila ya wapenzi hao kuonana,hakika kila mmoja alimkumbuka mwenzie hasa hasa Zabroni aliyezama kwenye penzi la Veronica,alitamani sana amtie machoni kwani siku nyingi hawajaonana. Hivyo wakati analitamani hilo suala litokee,mara ghafla Veronica alifika kwenye ghetto lao ambalo aliwakuta vijana Zabroni na Bukulu wakicheza drafti. Walimkaribisha lakini Veronica hakuweza kukaa bali baada ya salamu alimuita faragha Zabroni kisha akamwambia "Mpenzi unajua siku nyingi hatuja onana? Yote ni kwa sababu ya haraka za masomo chuo ndiyo ilinifanya nikawa kimya. Kwahiyo rasmi nimekuja nina hamu na wewe sana sijui hata nisemeje. Chazaidi naomba ujiandae twende mjini ukakae japo siku sita tu tufurahi pamoja istoshe sijawahi kulala na wewe au hujui kama mimi na wewe ni wapenzi?.." alisema Veronica kwa sauti nyororo huku akimfuta futa Zabroni nyuzi za buibui kichwani,kwani alikuwa ameegemea ukuta. Kuta nyingi za nyumba za vijijini zinakuwa na utandu wa buibui.
"Najua kama unanipenda, basi kaa kidogo nijiandae ili twende lakini siku sita tu sizidishi sawa?.."
"Sawa mpenzi wangu",alijibu Veronica huku moyoni akiamini kuwa hizo ndio siku pekee za maangamizi. Siku ambayo Zabroni atakamatwa baada kusumbua sana. Siku za hatari.
Zabroni alijiandaa haraka haraka,alipokuwa tayari kwa safari alimuaga rafiki yake ambaye ni Bukulu. Bukulu alimtakia kila raheri huku akimtania kwamba ahakikishe anamfyonza mpaka yaliyofichwa. Zabroni alicheka sana akifurahishwa na maneno ya Bukulu, lakini yote kwa yote Zabroni aliondoka zake sambamba na Veronica.
Zabroni alijikuta akisahau masharti ya yule babu kutoka Nigeria, ikumbukwe kipindi Zabroni anajiwekea nia ya kulipa kisasi cha wazazi wake tayari alikuwa nyumbani kwa huyo babu. Kwani hakuwa na sehemu nyingine ya kuishi,nyumba yao iliteketea kwa moto huku wazazi wake wakifia ndani ingawa baba yake alikuwa ameshajinyonga. Hivyo mzee yule kutoka Nigeria alimkabidhi dawa Zabroni ya kumfanya apotee mazingira yoyote,kitu kilicho mplekea Zabroni kulipa kisasi kwa uhuru huku akijivunia hiyo dawa. Na kila aliyejaribu kumfuatilia alipotezwa kama mzee Baluguza mganga nguli,lakini pia Madebe bila kumsahau Bruno. Wote hao walipotezwa kiani yake. Lakini sharti moja ya hiyo dawa aliyopewa Zabroni ni kufanya mapenzi,endapo kama atafanya mapenzi basi dawa hiyo itapotea.
Walifika mjini,hapo sasa ndipo mkakati wa Veronica ulipoanza. Siku ya kwanza Veronica aliitumia kuzurula mjini hapo na Zabroni huku akimpitisha kwenye kumbi mbali mbali za starehe, kumbi za hadhi huku wakila na kunywa kwani bajeti aliyopewa Veronica ilidhihirisha kabisa. Hapo Zabroni akaamini kwamba mke kapata, kiasi kwamba ilimpelekea pole pole kumsahau Tina.
Siku ya pili,siku hiyo Veronica aliitumia kuzungumza na Zabroni kuhusu mahusiano yao ambayo yalionekana kunawili kila kukicha. Kiukweli mtukutu Zabroni alionekana kumpenda sana Veronica ikiwa upande wa Veronica,yeye hakumpenda abadani ingawa usoni alionyesha hisia kwa kwake ila ukweli ukiwa ni kwamba alikuwa kikazi. Ukitaka cha uvunguni sharti uiname ndio msemo aliodumu nao moyoni Veronica, afande aliyekabidhiwa jukumu la kumkamata Zabroni.
Katika ya mgawahawa mmoja ndani ya huo mji mdogo. Mgahawa ulionekana kuwa wa kifahari ,walionekana Veronica na Zabroni wakiwa wameketi huku wakinywa vinywaji. Tabasamu lao lilionyesha kuwa bashasha,vile vile kila muda walikuwa wakigongeana mikono kudhihilisha kwamba zogo walililokuwa wakipiga lilikuwa limenoga.
"Zabroni unajua kwamba wewe ni mwanaume mzuri sana?..na pia namuomba Mungu atujalie tuje tuzae watoto!", alisema Veronica akimwambia Zabfoni. Zabro aliachia tabasamu pana kisha akanywa kinywaji chake kilichokuwa ndani ya grasi halafu akamjibu "Asante sana,vile vile hata mimi naona ni bahati kuwa na mrembo kama wewe. Veronica we mzuri bwana"
"Kweli?.." alihoji Veronica.
"Ndio kwani huamini? "
"Sawa naomba tupendane mpenzi wangu",aliongeza Veronica ambapo waligongeana grasi ishara ya furaha halafu wakanyeshwana. Zabroni akimnywesha Veronica kinywaji chake,ilhali Veronica nae akijibu mapigo. Hakika furaha ilionyesha kutawala eneo hilo,na mwisho wa yote walishikana mikono wakarejea nyumbani kupumzika.
Usiku wa siku hiyo wala wa jana Veronica hakutaka kufanya naue mapenzi Zabtoni ingawa alimuweka katika matamanio,kitendo hicho kilimuumiza sana Zabroni kwani usiku wa jana aliamini kwamba huwenda akapewa kitumbua siku ya kesho ambayo ndio siku hiyo ambayo nayo ilionekana hakuna dalili yoyote ya kupewa ili ajilie vyake.
Sio kwamba Veronica alikuwa hajui jinsi Zabroni anavyoumia,lahasha alifahamu fika ila alifanya hivyo makusudi ili kesho yake amuulize mambo kadhaa wa kadha huku akimuahidi kumpa $$## chake endapo kama atamjibu inavyotakiwa.
Kesho yake asubuhi, siku ya tatu hiyo. Veronica aliamka akaelekea bafuni kuoga huku akimwacha Zabroni kitandani akiwa bado amelala,haikuchukuwa muda mrefu alitoka bafuni akajiandaa haraka haraka kisha akamuaga Zabroni kuwa anaenda chuo. Utaratibu mzima wa chai pia na chakula cha mchana alimuelekeza muhudumu wa hotel hiyo aliyochukuwa chumba Veronica,akimwambia kwamba ampelekee huduma hizo mtu wake ambaye ni Zabtoni. Zabtoni aliamini moyoni mwake kuwa mpenzi wake Veronica ni mwanafunzi wa chuo,lakini upande wa pili Veronica hakwenda Chuo kama alivyomuaga Zabroni kwani hakuwa mwanafunzi ila plan yake ni kumuacha Zabroni kwa muda ili akirudi ajionyeshe kukasirika,kitu ambacho aliamini lazima Zabroni amuulize nini tatizo pindi atakapo onekana kukasirika. Kupitia nafasi hiyo sasa ndipo aanze kufanya upelelezi.
Wakati Veronica akiamini hayo,upande wa pili Zabroni alikuwa na shauku ya kutaka kuonja penzi la Veronica. Hasa hasa kila alipofikilia umbile la huyo mrembo,mwili wake ulijihisi kusisimka huku moyoni akipania siku hiyo avunje ukimya azungumze kuhusu hisia zake. "Nitamwambiaje?.." alijiuliza Zabroni,akifikiria namna gani atamueleza Veronica juu ya yeye kutaka penzi lake. Kwani siku zote alikaa kimya akidhania kuwa huwenda Veronica akajiongeza akawa amembalikia siku yoyote,lakini sivyo kama alivyo dhania. Kila siku walikula na kutembea baadhi ya kumbi ya starehe kuponda raha,kasoro starehe moja tu ambayo ndiyo hiyo Zabroni alikuwa akiitamani siku yoyote itokee. "Nitajikaza lazima nimwambie,haiwezekani kila siku tunalala kama kaka na dada leo lazima niseleleke naye" alisema Zabroni,akisahau kabisa masharti ya dawa aliyopewa.
Muda ulitaladadi,hatimaye jioni iliwadia. Veronica alipofika chumbani hakusema na Zabroni, alijitupa kitandani huku akiwa amelala kifudi fudi. Zabroni alitaharuki kuona kitendo hicho alichokifanya Veronica, alijiuliza "Nani kamkera? Na mbona sio kawaida yake?..", kabla Zabroni hajapata jibu la hilo swali alilo jiuliza, Veronica akamuuliza "Zabroni unanipenda kweli ama unanizuga?.." Zabroni alistuka kusikia swali hilo la Veronica, akamgeukia kisha akamjibu "Swezi kuchezea hisia zako,nakupenda sana. Kwanini upo hivyo leo,istoshe kitu gani kilicho kufanya unilize hilo swali?..", alijibu Zabroni kwa sauti ya upole huku akimkodolea macho Veronica ambaye muda huo alikuwa amejilaza kitandani akijifanya kukasirika.
"Mimi nahisi hunipendi,laiti kama ungekuwa unanipenda basi ungenipeleka kwa wazazi wako",aliongeza kusema hivyo Veronica,maneno ya mtego kwani alifahamu fika Zabroni hana wazazi. Na chanzo cha mauwaji yaliyokuwa akiyafanya chanzo ni wazazi weke, Kwahiyo alisema hivyo ili kumtega Zabroni. Zabroni kabla hajamjibu Veronica, alishusha pumzi kwa nguvu kisha akasema "Veronica mpenzi, mimi sina wazazi"
"Huna wazazi?..",aling'aka Veronica akijifanya kusituka.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ndio walifariki kwa ajari ya moto ",aliongeza kusema Zabroni,hapo Veronica aliamka akamsogelea karibu kisha akasema "Pole sana mpenzi wangu,lakini unaweza kuniambia hiyo ajari ilikuwaje kuwaje? Samahani mimi mkeo naomba uniambie nikae nikijua",alisema Veronica kwa sauti nyororo iliyomfanya Zabroni kushusha pumzi kwa mara nyingine kabla hajaanza kumsimulia.
Upande wa pili, ndani ya mji huo huo mdogo. Alionekana Bruno akikatiza moja ya mitaa ya sokoni,lakini punde si punde alipotea kimazingara wakati huo huo jeshi la polisi likiambatana na mbwa wao wakionekana kulisambalatisha soko hilo baada kugundua kwamba Bruno yupo mahali hapo. Bruno alikuwa ametoroka kabla siku ya kupandishwa mahakamani kusomewa hukumu haijawadia, nia ya kutoroka ni kutaka kulipa kisasi kwa Zabroni. Ikumbukwe Zabroni alimuuwa kaka yake Bruno ambaye ni Madebe,lakini pia aliwauwa wazazi wake huku akiwa na sura ya Bruno ili Bruno agundulike ndio muuwaji mwishowe ahukumiwe jela,nage Zabro aishi maisha bila kusumbuliwa. Ndivyo alivyo amini Zabroni kwamba Bruno kamwe hatorudia kumsumbua kwani atakuwa jela kwa kesi ya mauwaji aliyomsababishia, na ndio maana hakujali sharti la dawa aliyokuwa nayo, sababu alijuwa kazi kuu alishaikamilisha. Asijue kwamba Bruno karudi uraiani huku anasakwa na jeshi la polisi, naye anamsaka mbaya wake popote pale alipo ili akamilishe lengo lake la kulipa kisasi.
"Nimekukubali wewe ni mwanaume wa shoka, kama kweli ulilipa kisasi hakika ulistahili kufanya hivyo. Lakini uliwezaje kutembeza hiyo dozi katika hicho kijiji? ",alisema Veronica akisindikiza na swali,kwani alisema hivyo baada Zabroni kumsimulia kisa na mkasa kuhusu kifo cha wazazi wake. Zabroni hakuishia hapo,alienda mbali zaidi kwa kusema kwamba alilipa kisasi. Jambo ambalo lilimfanya Veronica kumsifia kijana huyo,ambapo hakuishia hapo alimuuliza pia ni namna gani aliweza kutembeza dozi katika hicho kijiji.
Zabroni alikaa kimya kidogo huku akionekana kutafakari jambo fulani,Veronica alipoona hiyo hali akamsogolea karibu zaidi kisha akasema "Niambie shujaa wangu,kidume kati ya vidume. Uliwezaje kutembeza kichapo kijijini. Ikumbukwe wewe ni mtu mmoja,sasa iweje upigane na uma? Ama ndio hivyo unanidanganya?..", aliongea Veronica wakati huo sasa mikono yake ikishughulika kuvua nguo ya juu huku akibaki na sindilia. Kifua chake kikawa wazi, ngozi nyororo isiyo na mikwaruzo ilionekana kwenye mwili wake,kiasi kwamba ilimfanya Zabroni kusisimkwa mwili wake baada kutupia jicho upande aliokaa Veronica.
"Niambie basi" ,aliongeza kusema Veronica. Zabroni alishusha pumzi ndefu kisha akasema "Kiukweli sikuogopa kitu,kile kifo cha wazazi wangu kilinipa shinikizo. Mmoja baada ya mwingine niliuwa. Hasa hasa yule aliyejaribu kunifuatilia kwa niaba ya kunikatisha kile nilicho kipanga. Nilichoma nyumba hovyo pale kijijini wakati huo tayari ninacho cha kujivunia."
"Mmh kitu gani hicho? Alihoji Veronica. Zabroni akajibu huku akianza kwa kicheko "Hirizi,Nilipewa dawa na mzee yule ambaye nilikwambia kwamba baada wazee wangu kufa nikawa naishi kwake. Huyo mzee ni mtu kutoka Nigeria, alinisaidia kunipa hiyo dawa ili niweze kulipa kisasi kwa uhuru zaidi" . Kimya kilitawala kidogo,kimya ambacho kilimstua Zabroni ambapo alimuuliza nini hasa kilicho mfanya akaye kimya,aidha maneno aliyomuambia? "Vero mbona upokimya ama umeogopa maneno yangu? Usiogope bwana hiyo ilikuwa zamani. Kwanza kwa sasa nipo kawaida sana,istoshe wabaya wangu nilishawapiteza Kwahiyo wala usiwaze. Nakupenda sana tena sana Veronica wangu",alisema Zabroni akimwambia Veronica, ndani ya moyo wake Vero aliamini tayari Zabroni hana ujanja kwake. Hivyo kupitia nafasi hiyo alimuuliza "Mmh nitakuaminije? Usije ukaniuwa na mimi humu ndani"
"Kukuuwa? Hapana siwezi bwana hebu acha utani",alijibu Zabroni huku akiyastaajabu maneno aliyoyasema Veronica.
"Kwahiyo unataka kusema kwamba dawa imeshaisha mwilini? ", akijifanya mtu mwenye hofu alimuuliza swali hilo Zabroni.
"Kabisa,hata hivyo yule babu alinambia kwamba ili dawa aliyonipa ili ipoteze nguvu ni pale nitakapo fanya mapenzi, na tangu niachane na yale matukio sijawahi kufanya mapenzi ingawa naaamini kwamba dawa imeshapoteza ubora kwani kitambo sana sijaitumia"
"Mmmh",aliguna Veronica wakati huo moyo wake ukiwa umefura furaha isiyo kifani.
"Ndio hivyo"
"Kwahiyo unataka kusema hujalala na mwanamke?.."
"Niamini Veronica kama mimi nilivyokuamini mpaka nikaweza kukwambia hii siri nzito. Sijawahi kumwambia mtu yoyote ila wewe,ingawa nakusihi usimwambie mtu yoyote. Ingawa wanasema hakuna siri ya watu wawili lakini naomba hii iwe siri ya watu wawili tu. ", Zabroni alisisitiza.
"Zabroni mpenzi ", kwa sauti ya upole Veronica akamuita Zabroni.
"Naam! Mpenzi Veronica "
"Unanipenda kweli?.."
"Ndio nakupenda sana"
"Sawa nikuulize swali?.."
"Uliza tu upo huru"
"Hivi ikitokea labda nimevujisha hii siri utanifanya nini?..", akastuka Zabroni baada kuulizwa swali hilo,alikaa kimya kidogo kisha akajibu "Sitikufanya chochote ila nitafurahi kama utaniomba msamaha". Veronica alicheka kidogo halafu akasema "Hapana siwezi kufanya hivyo kwani hata mimi nakupenda sana"
Siku ya tatu ikawa imeishia hivyo,hapo Veronica alibaki kumaliza kazi aliyopewa kwani tayari kile alichokuwa alikitaka amekipata. Ndani ya nafsi yake akajikuta akijisemea "Ama kweli dunia ina mambo. Kwa mwendo huu kamwe wasingemuweza huyu mtu". Upesi akatoa taarifa kwa uongozi "Safi sana Veronica, wewe ni jembe unafaa sana. Sasa nafikiri ng'ombe mzima umeshamaliza bado mkia tu", alijibu kamanda wake mkuu akifurahishwa na hatua nzuri aliyofikia kamanda Veronica ambaye ametwishwa jukumu nzito la kumpeleleza mtukutu Zabroni ili mwisho wa siku atiwe katika mkono wa sheria baada kusumbua kwa kipindi kirefu sana.
Siku ya pili yake ilipo fika,siku ya nne sasa. Asubuhi mapema Zabroni alimuamsha Veronica ili ampe madini ajilie,lakini Veronica muda huo akajifanya kuamka kwa haraka haraka akidai kwamba kachelewa shule. "Baby unajua mimi nikadhani lao mapumziko. Afadhali ulivyoniamsha acha niwahi ingawa leo nitatoka mapema ili nije nicheze na wewe mpaka pale hamu yako utakapo kata. Alisikika akisema hivyo Veronica akimwambia Zabroni ambaye yeye muda huo alimuamsha kwa niaba ya kutaka $$## lakini Vero akawa ameingizia mambo mengine tofauti na aliyo yatarajia Zabroni.
"Subiri atakuja kunielewa atakavyo nipa nafasi lazima aombe mchuzi wa supu",alijisemea Zabroni ndani ya nafsi yake akionekana kumkamia Veronica pindi atakapo mpa penzi lake. Na wakati Zabroni anajisemea hayo,Veronica alikuwa bafuni kuoga. Punde si punde alirejea akajiandaa haraka haraka kisha akamuaga mpenzi wake akawa ameondoka zake akiwa katika hali ya kujifanya mwanafunzi.
Huko alikokwenda,aliwataarifu police wenzake ili wajisogeze karibu na tukio. Kamanda mkuu Molisy alionekana kutoyaamini maneno ya Veronica,lakini alipowahakikishia mara mbili mbili hatimaye walikubali.
Jioni aliporejea nyumbani alimchukua Zabroni akampeleka moja ya kumbi ya starehe,ambako huko walikula na kunywa. Waliporejea nyumbani kila mmoja alionekana kuwa tayari kwa niaba ya kucheza mechi,mechi ambayo ilikuwa ya malengo kwa Veronica. Walifanya mapenzi,baada ya tendo Zabroni alilala moja kwa moja mpaka asubuhi ambapo alipo amka hakumkuta Veronica. Alistuka sana kwani haikuwa kawaida ya Veronica kuondoka pasipo kumuaga,wakati akiwa ameshikwa na bumbuwazi..mara ghafla kichwa kikaanza kumgonga kwa kasi mfano wa nyundo inayotua kwenye chuma. Hali hiyo ilimtia wasi wasi Zabroni, akatoka ndani huku akiwa ameshika kichwa chake. Nje alikutana na muhudumu wa mle ndani ya hoteli waliyokuwa wakiishi na Zabroni na Veronica. "Umenionea mdada kapita hapa asubuhi hii?..", akiwa na hofu dhufo lihali Zabroni akamuuliza muhudumu wa mapokezi kuhusu Veronica.
"Ndio ila..",kabla muhudumu huyo hajaendelea kusema,mara ghafla alidakia braza mmoja aliyekuwa amesimama kando. Braza huyo alisema " Si yule dada mzuri? Anaishi humu ndani? Mweupe kidogo!.."
"Ndio huyo huyo",alijibu Zabloni huku akiwa amekunja uso kwa sababu ya maumivu ya kichwa.
"Doh nimemuona kule maeneo ya gulioni ameambatana na jeshi la polisi lakini baadaye wakawa wameachana sasa sijui kaenda wapi?.." alieleza Braza huyo. Ghafla Zabroni akastuka kusikia habari hiyo, woga ulimjaa kwa mshangao akahoji "Polisi?.."
"Mmh sawa nisubirini nakuja hivi punde ",Kwisha kusema hivyo alitimua mbio kurudi kijijini kwa swahiba wake huku akiamini kwamba tayari maji yamezidi unga, Veronica amemuingiza mkenge. Hivyo aliamua kurudi kijijini kwa niaba ya kuchukua hirizi yake aliyopewa na yule mzee Maboso, hirizi ambayo Bruno aliwahi kuitwaa mikononi mwake baada kumchezeshea kichapo Zabroni cha mbwa mwizi lakini mwishowe akaidondosha pasipo kujua ikawa imerudi mikononi mwa Zabroni kwa mara nyingine tena. Kwahiyo dhumuni kuu ni kuchukuwa hirizi hiyo ambayo alikuwa hatembei nayo,ajifunge ili ajitetee kwa jambo lolote litakalo mkabili ingawa uwezo wa kupotea kama awali hakuwa nao tena. Alipofanya mapenzi,nayo ikawa imepotea. Hivyo hirizi hiyo ni kwa niaba ya kuwa na nguvu za ziada za kuweza kupambana hata na watu mia kasoro lisasi aidha panga.
Alipofika nyumbani alizama moja kwa moja chumbani, alikuta mlango upo wazi,huko alimkuta Bukulu akitupa miguu huku na kule wakati huo damu zikivuja tumboni. Akastuka Zabroni, upesii akamvagaa kumuuliza swahiba wake kipi kimemsibu "BUKULU Bukulu nini kimekupata?.." alihoji Zabroni huku akiwa amechuchumaa kumtazama.
"Bru bru...nooo ", alijibu Bukulu kisha akakata roho. Zabroni alizidi kuchanganyikiwa kusikia jina hilo,akajiuliza "Bruno? Inaamana Karudi?..", kabla hajapata jibu alisikia amri ikitoka nje. "Zabroni toka humo ndani kabla hatujafyatua risasi ", akastuka zaidi Zabroni huku kijasho kikimtoka, alitoka ndani. Nje alikuta jeshi la polisi likiwa na siraha zao mbali mbali huku pembeni akionekana Veronica akiwa amevaa kwanda la kipolisi. "Vero? Ni wewe?", kwa TAHARUKI alihoji Zabroni.
"Ndio mimi nilikuwa kikazi Zabroni,hakuna mwamba chini ya jua. Hatimaye umekamatika mshenzi mkubwa wewe",alijibu kwa dharau na kebehi Veronica. Mkuu wa msafara huo uliofika kumkata Zabroni akatoa amri Zabroni akamatwe. Hukumu ikatolewa kuhukumiwa kifungo cha maisha huku akizushishwa kumuua Buruno kwa mikono yake.
*****
Ndio hivyo ilivyokuwa washkaji, ila siwezi kuendelea kuishi jela. Adui yangu kajitokeza mwingine, lazima nikale nae sahani moja vile vile nikammalize na yule dogo aliyemuuwa Swahiba wangu. Alisema Zabroni huku akiwa amezungukwa na kundi la wafungwa,katika gereza la Ukonga jijijini Dar es salaam. Wafungwa hao walikuwa wakisikiliza mkasa wake huo ambao uliwaacha vinywa wazi.
"Kwahiyo utafanye sasa mwamba?.?", alihoji mmoja wa mfungwa aliyekuwepo hapo. Zabroni alikaa kimya kidogo kisha akajibu "Nitatoroka siku yoyote"
Gumzo gerezani,kila sehemu wafungwa walikuwa wakimtazama Zabroni kwa jicho la tatu,yote ikitokana na simulizi fupi aliyowasimulia wafungwa wenzake kisa na mkasa kilicho muingiza jela. Na kitu pekee kilicho mpelelea Zabroni kuogopwa zaidi na wafungwa baadhi,ni kauli aliyoitoa kwamba atatoroka gerezani hapo muda wowote.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mkasa huo wa kutisha aliosimulia Zabroni, hatimaye ulimfikia kijana mmoja aliyefamika kwa jina Bluyner. Kijana aliyetunikiwa cheo cha nyampala gerezani. Ni kijana ambaye alionekana kujazia mbavu na misuli ya mikono yake,uso wake nao ukiwa mkavu zaidi ya kiatu cha mtemebeza nyegere. Sio kwamba Bluyne hakumfahamu Zabroni,la hasha alimfahamu fika ila Hadithi ya maisha yake hakuifahamu. Hivyo siku hiyo akawa ameambiwa, alistuka sana lakini hakutaka kuamini kama kweli Zabroni anaweza kufanya hayo yote sababu matendo hayo hayaendani na muonekano wake. Kupitia hilo Bluyner akihisi huwenda ufalme wake ndani ya gereza hilo ukifikia tamati kwani kupitia simulizi ile ya Zabroni itawafanya wafungwa kumuogopa na kisha kumzarau yeye,kitu hicho Bluyner hakuta kitokee hata mara moja. "Ipo siku nitamfumua mbele yao ili heshima izidi kubaki kwangu",alijisemea Bluyner baada ya kumtafakari Zabroni kwa muda mrefu.
Siku iliyofuata asubuhi ya mapema,kengere iligongwa. Wafungwa wote walikurupuka kutoka vyumbani mwao haraka sana wakawahi mstarini kuhesabu namba ilihari huku upande wa pili kijana Bluyner alionekana akitembea chumba baada ya chumba akimsaka Zabroni. Hatimaye alimuona,muda huo Zabroni alikuwa akielekea mstarini. Lakini kabla hajafika,mara ghafla aliguswa bega. Zabro alistuka akasimama akageuka kumtazama mtu aliyemgusa bega akamuona Bluyner kiongozi wao. Kwa sauti ya ngumu iliyojaa utashi wa kibabe Bluyner akamwambia Zabroni "Kijana wewe mzuri sana",aliongea hivyo Bluyner huku akimgusa kidevu Zabroni. Zabri alibaki kumshangaa Bluyner, lakini mwishowe alimshika mkono kisha akamng'atua Kwenye mwili wake halafu akasema "Kwahiyo kama mimi mzuri,inakuhusu nini wewe?..",Bluyner akacheka kwa madaha kisha akajibu "Leo kikombe chako cha uji nakunywa mimi",Hapo Zabroni hakujibu chochote,zaidi aliishia kumsonya kisha akazipiga hatua kuelekea mstarini kuhesabu namba kabla hawajanywa uji na kisha kwenda kulitumikia taifa kwa nguvu. Wakati Zabroni anaondoka zake,huku Bluyner aliishia kucheka ingawa naye alijisogeza mahali hapo japo hakujipanga mstari kama ilivyokuwa kwa wafungwa wenzake.
Sauti za kuhesabu namba zilisikika zikipasa,punde si punde zoezi hilo likawa limemalizika ambapo amri ya kupanga mstari kwa niaba ya kupokea uji ilitoka kwa mkuu wa magereza. Wafungwa wote walipanga mstari kisha mmoja baada ya mwingine alipokea kikombe cha uji pamoja na viazi viwili. Hatimaye zamu ya Zabroni ilifika ambapo naye alipewa kikombe cha uji na viazi viwili kama ilivyokuwa kwa wafungwa wenzake. Alienda kujiweka kando kabisa na eneo lile la kupokelea uji ili apate kujinafasi ingawa walitangaziwa muda maalumu wa kuhitimisha hilo zoezi la kunywa uji,hivyo Zabroni aliketi chini akaanza na kiazi kabla hajabugia funda la uji. Na baada ya hapo alihitaji kisukumizio ambacho ni uji,kabla hajachukua hicho kikombe ili anywe,mara ghafla akatokea Bluyner akachukuwa uji huo na kisha akaunywa. Alikunywa funda la kwanza akanywa la pili akanywa la tatu,uji wote wa Zabroni akawa ameumaliza hakujali ni wamoto kiasi gani. Zabroni alibaki kumshangaa Bluyner, akajiuliza "Ananitafutia nini mimi? Au anataka ugomvi?", wakati Zabro anajiuliza maswali hayo kichwani mwake,Bluyner akacheka nakisha kusema "Usikasirike kijana mzuri. Ukikasirike utaonekana mbaya na mwishowe utazikosa sifa zako",akamaliza na kicheko Bluyner,papo hapo akachukuwa na kiazi cha pili cha Zabroni halafu akaondoka zake akimuacha Zabroni na kipande kidogo cha kiazi mkononi. Kwahiyo asubuhi hiyo Zabroni akawa ameambulia kiazi kimoja tu. Aliumia sana.
Punde si punde amri ilitoka kuwa umefika muda wa kwenda shambani kulima, gari mbili za wazi zilikuja. Kwa puta ya hali ya juu,wafungwa walipandishwa ndani ya hizo gari. Baada wote kupanda,dereva alilisongesha mpaka kwenye shamba la magereza ambapo napo wakati wa kushuka walikurupushwa huku wakipigwa mateke,kitendo kilicho pelekea kutokea purukushani za hapa na pale.
***********
Kipindi hayo yanatokea gerezani,upande wa pili Bruno baada kumtafuta Zabroni kwa udi na uvumba bila mafanikio ya kumpata hatimaye aliamuwa kutimkia ndani ya jiji la Dar es salaam. Huko alienda kwa niaba ya kujificha kwa sababu kipindi chote hicho alichokuwa akimtafuta Zabroni, naye vile vile alikuwa akitafutwa na serikali kwa kosa la kutoroka rumande kabla hajapandishwa kizimbani. Kwahiyo Bruno alipofika Dar es salaam alibadilisha jina na muonekano wake,ambapo alijiita Mr Rasi. Hakuwa na rasta lakini alijitahidi kuzifuga nywere,zilipokuwa ndefu ndipo akasokota rasta. Na hapo ndipo rasmi kijana Bruno akawa Rasta man,jina ambalo liliendana na muonekano wake. Nitaishije ndani hili jiji? Ndilo swali alilojiuliza kijana Bruno ama Mr Rasi. Kwani baada kujificha kwa kipindi kirefu nje ya kidogo ya Dar akingojea nywere zake zikue zimuweke katika muonekano mwingine ambao utamfanya mtu asimtambue,hatimaye akawa ameingia mjini sasa ambapo hilo ndilo swali alilojiuliza huku akiwa amesimama moja ya eneo ya kinondoni saa za usiku. Muda ambao jiji la Dar es salaam linaonekana kuwa na mishe mishe nyingi utaweza sema mchana ndio usiku na usiku ndio mchana,watu hawalali wanatafuta salali.
Mr Rasi akiwa haelewi jinsi atakavyoishi ndani ya hilo jiji,mara ghafla kando yake alipo simama alionekana binti mmoja wa makamo akingojea daladala. Lakini punde si punde yule binti akasikika akipiga mayowe "Mwizi mwizi mwizii jamani kanikwapulia mkoba wangu",Mr Rasi aliposikia sauti hiyo akatoka kwenye dimbwi la mawazo,akatazama upande ule alio simama huyo binti kisha akautazama ule uma wa watu uliokuwa bize kugombania daladala huku wengine wakiendelea na mambo yao bila kumsaidia dada huyo aliyekuwa akilalama kuibiwa. "Kwanini hawajishughilishi na hili lililotokea?..",alijiuliza Mr Rasi. Papo hapo akapotea kama upepo kumfukuzia yule mwizi, punde si punde akasimama mbele yake. Kibaka alistuka wakati huo huo Bruno ambaye ndio Mr Rasi akamwambia "Dondosha mkoba chini kisha utimue mbio",kauli hiyo ukilinganisha na namna alivyomtokea,ilimuogopesha yule kibaka ambapo alifanya kama alivyo amrishwa kisha akatimua mbio. Mr Rasi akuchukuwa mkoba huo upesi akamkabidhi yule binti huku akimsihi awe makini. Binti alishukuru sana lakini pia alihitaji kumjua jina sababu amemsaudia kwa kiasi kikubwa mno. Ni mgoba ambao ulikuwa na vitu kadhaa vya thamani "Naitwa Mr Rasi",alisema Bruno huku uso wake akiwa ameinamisha chini, kofia aina ya kepu aliyovaa ukiuficha vema uso wake.
"Naitwa Tina, ahsante sana Rasi kwa msaada", alijibu binti huyo. Ni yule Tina mpenzi wa Zabroni,siku hiyo anakutana na mbaya wa mpenzi wake pasipo kujua.
Naam! Siku zilisonga,jina Mr Rasi likiendelea kujizatiti kwa kijana Bruno. Ilihari upande wa pili napo gerezani baada Zabroni kuchoshwa na mnyanyaso kila uchwao kutoka kwa Bluyner,hatimaye siku moja akaamuwa kutangaza pambano. Taarifa hiyo ilipomfikia muhusika mwenyewe kiongozi Bluyner alifurahi sana,kwa maana ndicho alichokuwa akikitafuta kwa muda mrefu. Na wakati Bluyner akifurahia taarifa hiyo, upande wa Zabroni yeye alipania siku hiyo ya pambano ndiyo siku ambayo atakayotumia kutoroka gerezani huku akijanasibu kuwa endapo kama atafanikiwa kurudi uraiani atabadilisha jina hali ya kuwa kimya kimya akiwasaka wabaya wake.
"Haya manyanyaso siwezi kuyavumilia,mimi ni mwanaume na yeye pia ni mwanaume. Sasa kwanini niogope? Iweje niitwe mzuri na mwanaume mwenzangu,ama kwanini ajione yeye ni mwamba humu ndani eti kisa amepewa cheo cha kutuongoza? Hapana. Mimi ni Zabroni, hivyo kile nilicho kisimulia itabidi nikiweke hadharani ili heshima itawale",alisema Zabroni ndani ya nafsi yake,muda huo akiwa amelala na wafungwa wenzake. Baada kusema hayo alijishika kwenye msuri wa mkono akakumbuka hana hirizi ambayo ingempa walau nguvu. Hapo sasa ndipo kumbukumbu ilipomjia zaidi,akakumbuka namna gani Veronica alivyomteka kimapenzi mpaka kupelekea kupoteza dawa yake ambayo ingemfanya asikamatike kirahisi. Zabroni hakuishia hapo,alikumbuka pia kifo cha Bukulu ambaye alikuwa ni rafiki yake kipenzi. Neno la mwisho ambalo Bukulu alimwambia Zabroni kabla hajakata roho ni kwamba Bruno ndio aliyemfanyia hicho kitendo,kwa maana hiyo Zabroni alijua fika kuwa Bruno karudi uraiani kwani alidhani kwamba baada kumsababishia msala basi atakuwa anehukumiwa jela kitu ambacho kilienda kinyume na jinsi alivyodhania. Bruno yupo,na ndio huyo aliyeamua kujibadisha jina na kujiita Mr Rasi.
Pumzi alishusha Zabroni mara baada kutoka kwenye dimbwi la mawazo,kisha akaanza safari ya kulitafuta lebe la usingizi ambalo kiukweli lilimuwea ngumu kumjia ingawa mwishowe alifanikiwa japo alichelewa sana.
Kesho yake aljajiri kama ilivyo ada,kengere ya kuwamsha wafungwa iligongwa. Wafungwa wote walikurupuka haraka sana kukimbilia mstarini kasoro Zabroni ambaye yeye alikuwa bado amelala kwa sababu usiku wa jana alichelewa kulala kwahiyo alikuwa akimalizia usingizi aliokuwa nao,asijue tayari kumekucha. Wafungwa walihebu namba,na hapo ndipo namba ya Zabroni ilipo kosekana. Amri ikatoka kwa mkuu wa gereza,amri ambayo ilimtaka nyampala Bluyner akakague kila chumba wanacholala wafungwa. Bluyner kwa madaha huku akitunisha mbavu zake,alizipiga hatua kwenda kukagua chumba kimoja baada ya kingine ili kujihakikishia kama kuna mfungwa kasilia ama katoroka. Hatimaye akiwa nje alimuona mfungwa mmoja akiwa amelala,aliingia ndani akamkuta ni Zabroni.
Alichuchumaa kisha akamtingisha kitendo ambacho kilimkurupusha Zabro kutoka usingizi akakutana na uso wa adui yake ambaye ni Bluyner. Bluyner akacheka kidogo kisha akasema "Naona unalala tu kama upo kwa mama yako" alisema Bluyner, maneno ambayo yalimfanya Zabroni kumkumbuka marehemu mama yake. Alijitahidi kufanya juu chini ili akamtibie mama yake ugonjwa aliokuwa akiumwa ugonjwa wa kupooza,lakini bahati mbaya juhudi hizo zikawa zimeota mbawa baada mama yake kufia ndani kwa kuteketezwa nyumba yao. Hivyo nikama Bluyner aliweza kumkumbusha Zabroni machungu aliyokuwa ameanza kuyasahau kichwani mwake,hasira za ghafla zilimjia ambapo alikunja ngumi nzito kisha akamtupia Bluyner. Bluyner aliiona,akaikwepa kisha akasimama ili amuadabishe vizuri. Zabroni naye akawa si haba, alisimama kidete ili akabiliane naye.
Wakati hayo yanaendelea kati ya Zabroni na Bluyner,upande wa pili alionekana Tina akiwa sebuleni na shangazi yake wakipiga zogo. Tina alisema "Yani Ant nikwambie kitu?.."
"Niambie wala usijali "
"Kweli nimeamini siku zote usimdhanie mtu kutoka na matendo yake"
"Ni kweli ulicho kisema Tina,haya nieleze unamaana gani kusema hivyo?.."
"Maana yangu ni kwamba. Kuna siku fulani nilikuwa kwenye kituo cha daladala nasubiri gari ili nirudi nyumbani,sasa bwana akatokea kibaka akanipokonya mkoba wangu akakimbia nao. Nilipiga kelele kuomba msaada lakini hakuna mtu hata mmoja aliyenisaidia ila mkaka mmoja hivi ambaye yani kimuonekano alionekana yupo yupo tu..alimkimbiza yule kibaka akamkamta akanirudishia mkoba wangu. Kiukweli nlishukuru sana sijui hata nisemeje dah"
"Daah hapo sasa nimekuelewa "
"Ndio hivyo we unadhani yule kibaka angekimbia na hela zote zile ingekuaje?.."
"Mmh ndio siku ile nilipokutuma ukanitolee pesa Bank?.."
"Ndio siku hiyo hiyo"
"Laah! Mungu wangu, enhe huyo mtu aliyekusaidia ulimpa hata ya maji?."
"Hapana sijampa lakini usijali ant. Siku zote milima haikutani ila binadam hukutana. Nina uhakika ipo siku nitakutana naye nitampa japo kidogo ili akafanyie mambo yake.."
"Huo ndio uugwana mwanangu sawa?.."
"Sawa ant"
"Ulimuuliza jina lake?.."
"Ndio kaniambia anaitwa Mr Rasi"
"Anhaa sawa hapo nadhani itakuwa rahisi sana kumfahamu pindi mtako kutana. Haya chai tayari sijui utakunywa ama utawangojea Wenzako"
"Ngoja niwasubiri tu,kwani wameenda wapi? "
"Angel kaenda kwa rafiki yake mara moja, Gift naye sijui kaenda wapi. Maana anatembea sana siku hizi"
"Doh basi ngoja ninywe, sijui watarudi muda gani"
Baada ya maongezi hayo,shangazi yake Tina alifurahi sana kumuona Tina akiwa katika hali ya furaha. Kwani Tina alipofikishiwa taarifa ya kuhusu kifo cha wazazi wake alijikuta muda wote akiwa mnyonge hana furaha,kiasi kwamba hatakama umchekeshe namna gani abadani hacheki zaidi ya kuachia tabasamu kidogo na kisha kurudi katika hali yake ya ukiwa. Lakini siku hiyo Tina alionekana kuwa katika hali tofauti kabisa kitu ambacho kilimfanya shangazi yake kufurahi akiamini kwamba tayari binti huyo anaanza kusahau yaliyopita.
Kwingineko ule ugomvi wa Zabroni na Bluyner uliingiliwa kati na askari ambao waliwaamulia,haikuwa kazi nyepesi ila walifanikiwa. Bluyner alionekana kumkunjia uso Zabroni ilihari Zabro naye akionekana kumkunjia uso Bluyner ingawa tayari muda huo Zabrini alikuwa akivuja damu puani na mdomoni,alizidiwa nguvu na ujanja katika hilo pambano. Na endapo kama askari wasinge ingiliaa kati basi Zabroni angekiona cha mtema kuni.
Siku hiyo Zabroni hata uji hakunywa,moyo wake ulikuwa umefura hasira. Mawazo mfurulizo yalilindima kichwani mwake huku damu kama maji ikimtoka puani,hivyo punde si punde alizidiwa akaanguka chini akapoteza fahamu. Alizinduka akiwa Hospital akiwa ametundikiwa dripu ya damu na maji,mkononi akiwa amevishwa pingu huku kando kando yake amesimamiwa na askari mkononi akiwa na bunduki. Askari huyo alikuwa mzee wa makamo. Zabroni akastuka kujikuta katika mazingira hayo kwa sauti ya chini akamuuliza Askari huyo aliyepewa jukumu la kumlinda"Nimefikaje mahali hapa?.."
Askari huyo aiimtazama Zabroni,hakika alitia huruma. Akajibu "Baada ya ule ugomvi ulitokwa damu nyingi iliyokupelea kupoteza fahamu ndio maana upo mahali hapa unapatiwa huduma",Mara baada kujibiwa hivyo alinyamanza kidogo kisha akarudia kusema "Sawa asante kwa jibu lako lakini naomba kufahamu kwanini huyu mtu anafanya matendo kama haya halafu mnachukulia kawaida? Je, ikowapi haki ya mfungwa kama kunamanyanyaso kama haya",Hapo huyo Askari hakumjibu Zabroni bali alikumbuka siku kadhaa zilizopita jinsi Bluyner alivyomtishia kumpiga. Ukweli Bluyner alionekana kuwa tishio kwa wafungwa wenzake hata na Askari baadhi pia.
"Loh huyu binadam sijui anaroho gani, kiukweli hata mimi tabia yake nimeichoka. Nafikiri siku nikihamishwa hapa nitafurahi sana ",alijibiwa Zabroni na askari baada kukumbuka jinsi alivyonusurika kupigwa na Bluyner.
"Upo tayari kuona mtu huyu anaibishwa?..",alihoji Zabroni.
"Unamaana gani?.
"Maana yangu ni kwamba huyu mtu nimuadabishe"
"Acha utani,umenusirika kifo halafu leo hii umuadabishe?..", alijibu Askari huyo huku akimtazama kwa jicho la huba mtukutu Zabroni. Zabroni akakaa kimya kidogo kisha akasema.
"Ndio kila kitu kinawezakana ila kama utanisaidia jambo moja"
"Jambo gani?..", aliuliza Askari huku akimkodolea macho Zabroni. Zabroni akajibu "Wakati rasmi nakabidhiwa jezi za gerezani nilivuliwa hirizi yangu,ambayo ndio kila kitu kwangu kujihami na maadau. Sidhani kama itakuwa imetupwa,naimani itakuwa imehifadhiwa tu"
"Enhe kwahiyo? .."http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Naomba ufanye juu chini ukanichukulie kisha unikabidhi tafadhali sana",alijibu Zabroni safari hiyo akiongea huku machozi yakimtoka. Askari huyo aliyemsimama kiukweli alimuonea huruma. Akamwambia "Je, unauhakika utaweza? Nipotayari kukuletea hicho kitu chako"
"Nitaweza asilimia mia moja"
"Sawa ",alijibu Askari huyo aliyepewa jukumu la kumrinda mfungwa Zabroni wakati huo anafanyiwa matibabu.
Baada ya siku nne Zabloni tayari alionekana kuwa sawa kiafya kimwili na akili pia,siku hiyo anarudi jela ilikuwa shagwe na vifijo kutoka kwa wafungwa wenzake. Pole kwa wingi zilimfikia Zabroni kwa yaliyomkumba huku wengine wakimsifu kwa kuamua kujitosa kupigana na nyampala Bluyner kijana ambaye ni tishio kwa kila mfungwa. Kitendo alichokifanya Zabroni kilikuwa cha kishujaa sababu tangu jamaa huyo ahukumiwe jela hakuna mfungwa hata mmoja aliyejaribu kukabiliana naye lakini Zabro alithubutu japo alichezea kichapo. "Zabro...Zabro..Zablo..Zabrooooni",Ni shangwe zilizokuwa zikitoka kwa wafungwa ambao walionyesha kufurahishwa na ujio wa Zabroni. Zabroni alibaki kusimama huku akiachia tabasamu pana,alipogusa upande bega lake alipofunga hirizi yake mkono wa kulia akagundua hirizi ipo. Haraka sana akatazama upande wa kushoto umbao walionekana Askari magereza wanne akiwemo na yule aliyemsaidia kumpatia hirizi,Askari huyo akamnyooshea Zabroni dole gumba akimanisha ishara kuwa mambo ni safi. Naye Zabroni akajibu kwa kuitikia kwa kichwa kisha akajiunga na wafungwa wenzake,wakati huo moyoni akijisemea "Veronica Veronica Zabroni nakuja kuifanyia upasuaji sehemu hiyo iliyopoteza nguvu zangu sababu hicho ndio chanzo cha haya yote "
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment