Simulizi : Usilie (Don't Cry)
Sehemu Ya Nne (4)
Ndani ya ule mgahawa kulikuwa na kijana mmoja aliyekuwa inaitwa Tino,alikuwa kijana aliyevutiwa na uzuri wa Glory,mara nyingi alitafuta mbinu za kumwambia Glory lakini alishindwa,hii ni kutokana na Glory kuwa bize mda mwingi.Jambo lile aliweza kuligundua Glory lakini mpaka kwa wakati ule hakutaka kumuamini mwanaume yeyote,mwanaume aliyebaki moyoni mwake ni Issa peke yake huyo ndo aliamini kuwa alikuwa mwanaume wa pekee.Jambo lililomtia Glory hofu ni yule kijana Tino kushindwa kula kabisa.
"Dada naomba wali na nyama"aliongea Tino,lakini baada ya kupewa ule wali alishidwa kuula,alijiinamia kisha alilipia hera akaondoka,tabia hiyo iliendelea kila siku kwa Tino alikuwa hivyo hivyo.Mara nyingi alikuwa anaagiza vitu vya bei kubwa lakini alishidwa kuvitumia.Glory alitamani kumuuliza lakini moyo wake ulikuwa mgumu alihisi labda linaweza kutokea jambo baya ambalo hakutaka litokee kwa wakati ule.Kijana Tino tabia yake ilikuwa ile ile moyo wa Glory ulijawa na huruma kila alipokuwa anamwangilia Tino,siku moja alijitahidi akamuuliza.
"Kaka una tatizo gani?unaonekana mda mwingu unamawazo sana nini shida kaka angu?aliuliza Glory.
"Sina tatizo ila waweza nisaidia kuondokana na mawazo haya Kama utakuwa tayari"aliongea Tino na bila kusubiri jibu la Glory alilipa hera kisha akaondoka.
"Huyu mkaka vipi?mbona simuelewi?alijisemea Glory huku akiendelea kazi yake.Zilipita wiki mbili, Tino akiwa hajaja pale Hotelini,huku Glory aliendelea na kazi,hera alipokuwa anaipata alijitahidi kuweka akiba,lakini zikiwa zimepita miezi sita tangu Glory aliingie kwenye ile hotel kulijitokeza wanaume wengi wakimtaka Glory kimapenzi lakini hakuwa tayari kwa hicho kitu.Bado Tino aliendelea kuwaza njia ya kumnasa Glory.Kama kawaida yake aliendelea na kuagiza chakula ila hakutaka kukitumia.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Glory"aliita Tino.
"Abee"aliitika Glory.
"Kuna kitu nataka kukwambia"
"Kitu gani hicho"
"Unaniona hapa nashindwa kul haya yote ni kwa ajili yako,moyo wangu unakupenda Glory tafadhali usikie kilio changu"aliongea Tino kwa hisia Kali,bado hakutaka Glory atoe jibu,alitoa kikaratasi kilichokuwa nanamba akampa Glory kisha yeye akaondoka.
"Kuhusu suala la mapenzi utanisamehe"alijisemea Glory huku kile kikaratasi akikifunga kwenye kanga yake.
Ghafla ulizuka ugojwa wa kipindupindu ndani ya jiji la Arusha,ugojwa huo ulionekana kuja kwa kasi,watoto wengi walipoteza maisha ndani ya mda mchache,watu waliogopa sana ulionekana ni ugojwa uliokuwa hatari sana.Baadhi ya wakazi waliokuwa na uwezo kifedha walilazimika kuhama kwenye jiji hilo,yote hayo kuukimbia huo ugonjwa ulionekana kuenea sana kwa mda mfupi.Wale ambao hawakuwa na uwezo wa kuhama waliendelea kumuomba mungu awaepushe na ule ugojwa hatari.
"Kuanzia kesho hoteli zote zinafungwa,hakuna kufunguliwa mpaka itakapotoka ruhusa,hii ni kutokana na ugojwa unakuja kwa kasi"lilikuwa ni gari la matangazo lililokuwa linazunguka jijini humo.Watu waliokuwa wanategemea kazi za Hotelini kuendesha maisha yao walijikuta wanapoteza matumaini kabisa.Hali ile ilimkumba Glory,bado hakujua maisha atayamudu vipi kulingana na pesa aliyokuwa ameiweka kama akiba kuwa ndogo.Hali ilizidi kuwa mbaya ndani ya jiji la Arusha.Wizi ulizidi kushika kasi vijana walianza ukabaji yote hayo yalisababishwa na hali kuwa ngumu.Pesa aliyokuwa ameiweka Glory kama akiba ilizidi kupungua taratibu.Siku moja akiwa anafua nguo ndipo alipoona kila kikaratasi chenye namba alichokuwa amepewa na Tino.
"Ngoja nijaribu kumtafuta huyu"alijisemea Glory huku akiinuka na kwenda kununua vocha.Baada ya kupata vocha aliziweka zile namba na kujaribu kuzipiga,simu iliita kwa sekunde kadhaaa kisha ikapokelewa.
"Hallow,Glory anaongea hapa"
"Waoooh uko wapi nije"
"Nipo nyumbani bila shaka unapajua"
"Sawa nakuja sasa hivi"aliongea Tino ambaye hakutaka hata salamu.Tino alikuwa akiuza duka la vyakula,hivyo alifunga na kuja mpaka nyumbani kwa Glory,hakutaka kuja mikono mitupu,alikuja na vyakula mbalimbali, Glory alipomuona alimpokea kwa tabasamu.
"Anaonekana atakuwa na upendo kama Issa"alijisemea Glory wakati huo akimpokea Tino,waliongea mambo mengi sana.
"Sawa nipe muda nijifikirie"alijisemea Glory.Tino alifurahi sana alitoa noti nakumkabidhi Glory.
"Mimi naenda ila kukitokea tatizo la pesa usikose kunitaarifu"aliongea Tino kisha akaondoka.
"Elfu sabini?alijiuliza Glory baada ya kuhesabu pesa alizokuwa amepewa na Tino.
"Issa mwingine ndo huyu"alijisemea Glory upendo wa Tino aliulinganisha na wa Issa japo ilikuwa bado mapema.
Ndani ya China kulitoka nafasi za watanzania kurejea nchini kwao kupitia ndege ya Tanzania illiyokuwa chini humo.Issa hakutaka kuja nchini Tanzania akiwa bado hana pesa.
"Nataka mimuonyeshe huyo aliyemchua Glory"aliwaza Issa hivyo aliendelea kupambana usiku na mchana taratibu moyo wake ulianza kumsahau Glory.
"Naimani ipo siku atanikumbuka"alijisemea Issa.hiyo nafasi aliipuzia.
Upendo wa Glory na Tino ulianza kwa kasi sana Glory alikuwa ameepa kutopenda lakini ugumu wa maisha ndo ulimlazimu kujihusisha tena na mapenzi
"Tino naomba usije ukaniumiza"aliongea Glory kwa hisia Kali.
"Usjal kuhusu hilo"aliongea Tino kwa wakati ule walikuwa nyumbani kwa Glory.Siku zilisogea huku upendo wao ukkendelea.
"Sasa hapa sitaki ukae bure,ntakufungulia duka la nguo uwe unauza"aliongea Tino.Wiki moja badae Glory alikuwa na duka tayari,bado alizidi kumpenda Tino.
"Huyu sasa ndo mwanaume,hakika sitakaa nimsaliti nimejifunza mengi"alijisemea Glory.Pamoja kuwa tayari Glory ana mtoto lakini uzuri wake ulianza kuonekana tena,mwili wake ulikuwa mlaini sana,jambo lile lilipelekea wanaume wengi kumsumbua lakini hakutaka kusikia la mtu.Baada ya miezi mitatu tayari Glory biashara ya Glory ilikuwa nzuri sanaa,alipata wateja wengi.
"Kweli ukitaka. Biashara yako iwe nzuri muweke mwanamke mzuri,naamini utawakamata"yalikuwa maneno ya vijana wa bodaboda hasa baada ya kuona wanaume wengi wakiingia dukani kwa Glory.
Miezi mitatu ilipita,hapo Glory aliongeaza vitu,duka lilikuwa kubwa zaidi,hali ile ilizidi kumfurahisha Tino ambaye aliyaona mafanikio siku za mbeleni.
"Mwakani nataka tununue gari la kutembelea"aliongea Tino akiwa na Glory.Mtoto wa Glory naye alizidi kukua,kwa wakati ule afya yake ilikuwa nzuri.Kadri siku zilivyokuwa zinasogea Tino alitamani kupata mtoto,lakini mpaka zinapita miezi tisa Glory hakuonesha dalili yeyote ya kupata mimba.
"Au hana kizazi huyu mwanamke"alijisemea Tino,lakini alivuta subira.
"Ngoja kwanza nikafanye vipimo nione tatizo kama lipo upande wangu basi ntafanya kitu"alijisemea Tino.Moja kwa moja alichukuwa usafiri uliomfikisha mpaka hospital ya Mount Meru.
"Vipi kaka uliwahi kupata ajali yeyote?aliuliza Dakitari mmoja wa kike.Tino alivuta pumzi ndefu na kuishusha kisha akakumbuka mwaka 1999 alivyopata ajali wakati anatoka Morogolo kwenda Arusha.
"Ndio lakini ni mda ni sana yapita miaka kama ishirini"alijibu Tino kwa wasiwasi.
"Ilikuwa ajali ya nini?
"Ajali ya gari"walipoteza maisha watu wengi lakini Mimi niliumia sehemu za magotini"alijibu Tino.
"Pole sana je kwa kipindi hiki uliwahi kuishi na mwanamke?
"Hapana"alijibu Tino.
"Sawa majibu yanaonyesha huna kizazi,bila shaka ulivyopata ajali ndo uliumia,pole sana jipe matumaini"aliongea yule Dakitari.Tino hilo jambo alilijua mapema japo hakutaka kupima lakini alikuwa anajijua hivyo hayo majibu hayakumshutua sana.Alirudi nyumbani huku moyoni akifikiria namna atakavyoishi na Glory.
"Sasa sina kizazi huyu mwanamke wa kazi gani? alijisemea Tino.
Siku zilisogea taratibu moyo wa Glory ulianza kuwa na hofu.
"Inamaana mungu alinipangia mtoto mmoja pekee?aliwaza Glory huku akianza kuwa na hofu juu ya upendo wake na Tino.
"Hakuna Mwanaume wa kumvumilia mwanamke asiyekuwa na kizazi"alijisemea Glory.Baada ya kugundua kuwa upendo wake uko matatani alianza kuweka akiba ya pesa.Maisha yao yalisogea lakini Tino hakuonyesha kupunguza upendo.
"Mke wangu hili tatizo la kutokupata ujauzito huwezi kujua liko upande wa nani,hivyo kuna mganga wa kienyeji naamini tukienda atatusaida"aliongea Tino akijaribu kuuficha ukweli.
"Sawa mme wangu nakubariana na wewe, kwahiyo tutaenda lini sasa na ni wapi? aliuliza Glory.
"Ni Arusha vijijini nadhani twende kesho"aliongea Tino.Kesho yake asubuhi waliamka asubuhi na mapema baada ya kupata chai walikodi tax iliyowafikisha mpaka nyumbani kwa yule mganga.
"Karibuni viatu vyenu viache nje"aliongea yule mganga huku akiimba nyimbo zake za asili.
"Tatizo lenu nimeshalijua,muondoe hofu kabisa litaisha,ila mko tayari kwa masharti?aliuliza yule mganga.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ndio tuko tayari"Glory na Tino waliitikia kwa wakati mmoja.
"Vizuri sana,sasa mizimu yangu inaniambia kuwa inahitaji damu ya huyu mtoto"aliongea yule mganga huku mkono akiuelekeza kwa mtoto wa Glory.
Glory alipigwa na butwaa baada ya kusikia maneno ya yule mganga,alishusha pumzi ndefu huku akimwangalia mwanaye.
"Siko tayari siwezi kumuua mwanangu"alisema Glory kwa sauti ya ujasiri.
"Tambua kabisa kuwa niliwaambia toka mapema kuwa masharti mtayakubali nawewe ndo ulikuwa wa kwanza kukubali sasa masharti yenyewe ndo haya lakini unatakataa,ujue utaikasirisha mizimu"aliongea yule mganga.Tino alikaa kimya kwa mda akionekana kutafakari kitu.Bado Glory alionekana kulipinga suala hilo.
"Mganga tupe mda tukajadiliane"aliongea Tino.Baada ya kufika nje kila mtu alionekana kulifikiria suala hilo.
"Sasa huku tumekuja wapi?hebu tuondoke"aliongea Glory.
"Mke wangu tulia yaani kwenye hii damu ya mwanao tunachukuwa na dawa ya kukuza utajiri wetu"aliongea Tino, Glory alionekana kulipinga suala hilo,lakini Tino aliendelea kumshawishi mpaka Glory akakubali japo kwa shingo upande.
"usiogope kumpoteza mmoja ili upate zaidi ya kumi.Hivyo kama watoto tutapata wengine zaidi ya huyu mwanao"aliongea Tino.Maneno Yale yalimfanya Glory kulikubali suara hilo.
"Ndio mganga tumekubali lakini tulikuwa tunaomba utupatie na dawa ya kuongeza utajiri wetu"aliongea Tino.
"Ondoeni shaka vijana wangu,hebu mshushe huyo mtoto hapa"aliongea mganga lakini Glory alisita kufanya vile, Tino alimlazimisha mpaka Glory akakubali,basi mganga alifanya mambo yake na baada ya mda aliwapa dawa kisha wakaondoka.Njiani Glory alidondosha machozi lakini Tino hakuonyesha kuguswa na tukio lile.Lengo la Tino kumlazimisha Glory amuue mwanaye aliogopa kwamba wakishakuwa matajiri mali zao atazirithi mtoto wa Glory ilhari sio damu ya Tino.Tino hakutaka kumuacha Glory,hivyo alifanya vile ili waishi kwa amani.Baada ya kufika nyumbani mtoto wa Glory hakuonesha dalili yeyote ya kuumwa,wote walishangaa tukio hilo, Glory moyoni alifurahi sana kwa sababu hakutaka mwanaye aliyemzaa kwa mateso apoteze maisha.
"Niliwahi kusikia kwamba ukitoa kafara ikagoma inakurudia wewe"Glory aliwaza hayo maneno aliyowahi kuyasikia kutoka kwa babu yake.Moyo wake ulianza kuingiwa na wasiwasi.
"Lakini Mimi sijatoa kafara"alinisemea Glory.Hadi inapita wiki mtoto wa Glory alikuwa bado na afya tele.
"Mke wangu nadhani wiki ijayo turudi tena kwa yule mganga"aliongea Tino akimwambia Glory.
"Sawa mme wangu au tusubiri tuone"alijibu Glory.Baada ya kupita wiki mbili Tino alimwambia Glory kuwa kesho yake warudi tena kwa yule mganga, Glory hakuw mbishi alikubaliana naye.Usiku huo huo ghafla Tino alianza kutokwa na damu puani na masikioni
"Mkeeeeee waaaang nakuuuuuu....hakumalia sentensi aliaga dunia.Glory alipiga kelele kuwaita majilani walioshangaa tukio lile la ghafla,kila mtu alisema lake.
"Hawa wanawake watatumaliza,yaani akiona una pesa tayari anakuua"yalikuwa maneno ya vijana waliokuwa nje ya nyumba waliyokuwa wanaishi Glory na Tino.
"Ndio umeambiwa hawa viumbe ishi nao kwa akili,na mpaka sasa bado sijajua ni akili gani ya kuitumia ili uishi na hawa wanawake"kijana mwingine alidakia, wote waliamini kuwa Glory ndiye aliyesababisha kifo kile.
"Kama amemuua kwa ajili ya kupata mali zake nasema hapa amekwama,hapati kitu"aliongea bibi mmoja aliyekuwa na undugu na Tino.Mwili wa Tino ulidafirishwa mpaka mkoani mbeya huko ndiko alikokuwa anazaliwa.
"Mwanamke aliyekuwa anaishi naye yuko wapi? aliongea baba yake Tino.
"Hakuna kifo cha ghafla namna hiyo waiitwe police haraka"wajomba zake Tino waliongea,ndani ya dakika kumi tano Askari police walikuja wakiwa na daktari, Glory alishikiliwa na kwa mahojiano
"Daktari hebu fanya vipimo huenda huyu mwanamke kamlisha sumu"aliongea mdogo wake marehemu Tino.Uchunguzi uliofanywa na Daktari ulisema kuwa Tino alikuwa na shinikizo la damu hivyo ndo limesababisha kifo chake,ndugu wa marehemu walifuatiria mali zake zote, Glory alipewa kidogo lakini moyoni alifurahi kubaki na mwanaye.Pesa aliyopewa na Glory alienda mpaka benk na kuiweka kisha akaendelea na duka lake la nguo ambalo ndugu wa marehemu Tino hakuweza kulifahamu.Glory aliendelea kufanya biashara yake iliyompatia pesa za kutosha,bado faida aliyokuwa anaipata aliweka benk.Baada ya miezi kumi Glory alikuwa na maduka mawili ya nguo,alitafuta mtu wa kumsaidia.Utajiri wake ulianza taratibu aliongeza duka lingine la vyakula,baada ya miaka mitano Glory alihesabika kwa matajiri waliokuwa jiji humo.
"Umeona alivyomtoa kafara mme wake utajiri alioupata tena kwa mda mfupi?Mimi nawaambia kuwa kufa maskini ni kupenda kabisa"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Kweli njia zipo nyingi za kutafuta pesa labda vijana mfeli wenyewe"yalikuwa maneno ya vijana waliokuwa kuwa kijiweni.Jina la Glory lilianza kutamba ndani ya jiji la Arusha.Watu walizidi kushangaa utajiri huo uliokuwa unakua kwa kasi,miaka miwili Glory alikuwa tajiri namba moja ndani ya jiji la Arusha.Hakuishi tena kwenye nyumba za kupanga alijenga nyumba yake ya kisasa.Mwanaye alimpeleka Uingereza kwa ajili ya masomo,alinunua magari ya kifahari,ndani ya nyumba yake aliweka watu ambao kazi yao ilikuwa kusafisha nyumba.Vijana aliwapa bodaboda kwa ajili ya kujiajili,watoto yatima aliwasadia sana.
"Mpaka naona aibu kwenda kuomba pikipiki"alisema kijana mmoja.
"Kwani unaogopa. Nini?yule mwanamke hana tabu kabisa ili mradi kila wiki mperekee malipo yake"kijana mwenzake aliongea.
"Hapana sio hivyo mzee baba"
"Ila nini?
"Yaani nakumbuka kipindi mwanaye anaumwa aliniomba nimpereke hospital lakini nikagoma,leo hii najihisi aibu,kweli msaidie kila mtu kwa kadri unavyoweza huwezi kujua kesho yake Kuna nini"yule kijana aliyekuwa anaitwa Yasin aliongea.
"Sahivi hawezi kukumbuka,ana mambo mengi kichwani twende tukapewe pikipiki"basi wale vijana waliongozana mpaka nyumbani kwa Glory,walipokelewa na walinzi waliokuwa nje ya geti,baada ya kueleza shida yao walikaguliwa kisha wakaingia ndani.Licha ya kuwa tajiri aliyeheshimika Glory hakupenda kuwafukuza watu,hakupenda kujiweka juu watu wote aliwaona wako sawa,wale vijana aliwapa pikipiki kwa mikataba kuwa kila mwisho wa wiki walete hera.Mpaka hapo Glory alimiliki kila aina ya duka,alinunua majumba makubwa ndani ya jiji Hilo.Kama ilivyo kwa matajiri wakubwa kufuatwa na makampuni mbali mbali,ndivyo ilivyotokea kwa Glory,Makampuni makubwa yalimfuata kwa ajili ya kufanya nayo biashara,hakutaka kuacha kitu kila fursa iliyokuwa inatokea mbele yake hakutaka kuiacha jambo lile lilimzidishia utajiri,kwa wakati huo alimiriki magari ya kutembelea matano,mengine ya abiria yalikuwa yakimwingizia hera.Mtoto wake aliyekuwa anaitwa Bahati alikuwa nchini Uingereza, Glory alihakikisha mwanaye anapata elimu iliyo bora ili aje asimamie mali zake.
"Mwanangu ukitaka hata ukasomee marekani ni wewe tu chagua"yalikuwa maneno ya Glory akimwambia mwanaye Bahati.Utajiri wa Glory uliwafikia wazazi wake,wote walijikuta wanatamani kumuomba Glory msamaha,lakini yeye hakuwawaza hata kidogo bado alifikiri kuwa watakuwa na hasira naye.
"Ngoja niagize gari la kifahari kutoka Paris Ufaransa ili niwape kama zawadi hapo wanaweza kunisamehe"alijisemea Glory huku akifanya mawasiliano na watu waliokuwa Ufaransa.Matajiri mbali mbali wa kiume hawakusita kumfuata Glory kwa ajili ya kuwa naye lakini Glory hakuhitaji
Mwanaume wa aina yeyote.
"Natamani mafanikio haya ayasikie Peter pamoja na Fikiri wanaume walioniharibia maisha yangu"alijisemea Glory.Baada ya miezi miwili gari iliyoagizwa kutoka Ufaransa ilikuja na ndege mpaka kwenye uwanja wa KIA (Kilimanjaro International Airport)lililetwa gari la kifahari,kila lilipokuwa linapita watu wote waligeuza shingo kuliangalia,minong'ong'ono ya hapa na pale ilisikika.
"Hilo gari nahisi kalinunua milioni mitano,yaani watu wanatumia pesa hivyo wakati huo mimi tangu asubuhi nimeuza maandazi ya elfu moja"yalikuwa mawazo ya kijana aliyekuwa anauza mandazi hasa baada ya kuliona gari hilo.
Licha ya kuwa tajiri Glory bado alihisi kuwa wazazi wake hawawezi kumsamehe.
"Sasa niwanunulie zawadi gani hawa,naona kama gari haitoshi"alijisemea Glory.Nguo kwa ajili ya wazazi wake ziliagizwa kutoka nchini Sweeden na zawadi nyingine alizitafuta kwa ajili ya wazazi wake.
"Hapa lazima wafurahi"alijisemea Glory huku akiangalia suti ya baba yake mzazi.Kila aliyekuwa anamuona Glory alitamani kuwa kama yeye.
"Vijana fanyeni kazi muache kuwaza njia za mkato"alisema mwanaume mmoja akiwa ndani ya gari aliwakuta vijana wakimjadiri Glory.
"Ngoja nisubiri likizo ya mwanangu ili niende naye tukawaone wazazi kisha niwatoe kijijini ili niwalete mjini"aliongea Glory.Walinzi aliokuwa nao Glory alihisi hawatoshi kabisa hivyo aliagiza walinzi wengine kutoka nchini Vietnam.
"Nawahitaji baada ya miezi mitatu wawe wamefika hapa,pia nahitaji wanawake pekee wawe na mafunzo ya kijeshi"yalikuwa maneno ya Glory akiongea na wakala wake.Hatimae likizo ya Bahati iliwadia alifika nchini Tanzania huku taratibu akiwa ameanza kusahau lugha ya kiswahili.
"Kesho ndio Safari ya kwenda kwa wazazi,nikitoka huko namfuata mpenzi wangu Issa huko China"alijisemea Glory.
A SITA-16.
Maandalizi yalikamilika usiku wa siku ile, Glory alihakikisha kuwa wazazi wake lazima wafurahi,madereva wawili waliandaliwa kwa ajili ya kuendesha hilo gari kwa ajili ya zawadi ya wazazi wake.
"Hapa hawawezi kumifukuza tena,lazima wafurahi ntahakikisha wanaishi maisha mazuri"aliongea Glory wakati huo msafara wa magari matatu ukianza.Kila walipokuwa wanapita watu waliishia kugeuza shingo zao kuangalia.
"Utadhani msafara wa rais,kweli ukiwa na pesa unafanya lolote"yalikuwa maneno ya mzee mmoja.Gari ziliendeshwa kwa umahiri mkubwa.
"Sipidi ya gari naomba isizidi ishirini"aliongea Glory,moja kwa moja madereva walifuata amri.
Mkuu wa mkoa Arusha alianza kuwa na hofu na utajiri wa Glory,moja kwa moja vikosi vya upelelezi vilitumwa kuanza kumchunguza.
"Yawezekana anafanaya biashara haramu,huyu mwanamke anakuja juu kweli,hivyo hakikisha mnamchunguza mwanzo mwisho"yalikuwa maagizo kutoka kwa mkuu wa mkoa kwenda kwa Askari upelelezi waliokuwa wamevalia kiraia.Uchunguzi waliufanya kwa umakini sana lakini hawakuona biashara yeyote iliyokuwa kinyume.
"Mheshimiwa hakuna kitu huyu mwanamke anaonekana mpambanaji"Askari mmoja alimwambia Mkuu wa Mkoa.
Msafara wa Glory uliishia nyumbani kwao hakuna aliyeamini kumuona Glory akiwa na utajiri ule,hata wazazi wake walishangaa,japo utajiri wa Glory waliusikia kwa watu lakini mpaka hapo nadhani walikuwa wameamini.
"Baba na mama naombeni mnisamehe mwanenu,yote haya yaliyotokea huenda yalikuwa ni neema kwa upande wetu,hivyo zawadi yenu hiyo hapo,hilo hapo gari na dereva wenu atafuata masharti yote mtakayo mwambia,kingine mwanangu ndo huyu hapa alikuwa nchini Uingereza kimasomo hivyo ndo kapata likizo fupi na ndo amelejea.Najua ni miaka mingi sana tangu niondoke hapa lakini mateso niliyopitia ni mengi sana siwezi kusimulia ila yote tushukuru tuko salama kabisa ni hayo wazazi wangu zawadi nyingine hizo hapo"aliongea Glory wazazi wake walibaki kushangaa kuona gari walilokuwa wameletewa.
"Sisi hatuna neno la kuongeza hongera mwanangu mungu akuongezee zaidi"aliongea mama mtu huku akiwa amemkumbatia mwanaye.
"Safari sio kifo karibu mwanangu"aliongea baba yake Glory.Wazazi walifurahi sana.
"Jiandaeni kesho kutwa tunaenda mjini"aliongea Glory kwa furaha.
"Mjini tena sisi wazazi wako tumezoea kulima sasa mjini huko tutaenda kufanya nini?aliuliza baba yake Glory.
"Hapana baba zamu yenu kula matunda ya mimi mwanenu"aliongea Glory.Wazazi wake hawakuwa na kipingamizi chochote.
"Sawa tumekubali"alijibu mama mtu kwa furaha.
"Sawa mama nataka wadogo zangu hawa wakasome hata Marekani au China"aliongea Glory,kila alichokuwa anakisema wazazi wake walikubaliana naye.Kila mtu ndani ya kile kijiji alijiuliza kuhusu utajiri wake uliokua kwa kasi tena kwa mda mfupi.
"Kweli watu mungu anajua kuwajalia,yaani magari yote haya tena mtoto wa kike??sisi vijana tunakwama wapi?alijiuliza kijana mmoja alipopata taarifa kuwa Glory wazazi wake anawahamisha kuwapeleka mjini.
Ilikuwa siku ya juma nne,siku hiyo alipanga Glory ndo iwe siku ya kuwahamisha wazazi wake.Maandalizi yalifanyika kwa wepesi huku baadhi ya vijana wakisaidia kupakia mzigo,ndani ya hicho kijiji aligawa pesa sana.
"Nadhani mtanikumbuka"alijisemea Glory huku akiwapa akina mama hera waliokuwa eneo hilo.
"Mungu akuongezee zaidi na hapa uweze kufanikiwa huko uendapo"alisema mama mmoja huku akipokea pesa kutoka kwa Glory.
Wazazi wa Glory waliingia kwenye mpya kabisa iliyokuwa imetoka Ufaransa,humo ndani walikutana na upepo wa kiyoyozi ulikuwa unapuliza,kijiji kilisimama kwa mda.Safari yao ilianza mwendo ulikuwa wa tararibu.
"Yaani lazima niongeze ulinzi najua wanaoniona ni wengi sana wanaweza hata kunivamia"alijisemea Glory huku akiwasiliana na mtu aliyekuwa mahususi kuwatafuta hao walinzi.Bado alitaka walinzi watoke Vietnam,nchi hiyo aliiamini kwa kupigana vita.Safari yao iliishia nyumbani kwa Glory, Wazazi wake walishangaa nyumba aliyokuwa ameijenga Glory.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Tayari kashakua tajiri"mzee Gozbert baba yake Glory aliongea.
"Tuombe tu mungu usije ukawa utajiri wa njia za mkato"Mama yake aliongea,bado alionekana kuwa na hofu kabisa.
"Mungu tuongoze zisije kuwa mali ya haramu"Mama yake Glory hakutaka kuamini kuwa utajiri wote aliokuwa Glory alikuwa hana mme.
"Mwanangu sasa hapa ndani unaishi nanani?aliuliza mama mtu.
"Naishi na hawa hapa walinzi basi"alijibu Glory.Lakini mama yake hakutaka kuamini kuwa Glory alikuwa anaishi peke yake.
"Sasa huu utajiri kaupata wapi"alijiuliza mama yake Glory.Wafanya kazi wa ndani walihakikisha kila kitu kilichohitajika kilikuwa kinapatikana kwa mda sahihi.
"Mama nategemea kwenda China mwezi ujao kuna bidhaa naifuata huko"aliongea Glory,hakutaka kumwambia mama yake kuwa anamfuata Issa.
"Sasa huko China ntaenda sehemu gani?alijiuliza Glory huku akishika simu yake ya kisasa na kuliangalia jiji hilo lilivyokuwa kubwa.
"Nakumbuka Issa aliwahi kuniambia kuwa walifikia kwenye mji wa Guangzhou,sasa nikifika ndani ya jiji hilo siwezi kupotea mhimu ni kwenda na pesa ya kutosha"alijisemea Glory wakati akiangalia ile picha ikilionyesha vyema jiji la Guangzhou.Alianza kujiandaa vyema alipanga kuwa baada ya mwezi mmoja mbele ndo asafiri kwenda China.Walinzi kutoka nchini Vietnam walifika nyumbani kwa Glory, Glory aliwapangia majukumu,kwakuwa walikuwa hawawezi kuongea kiswahili moja kwa moja aliletwa mwalimu wa kuanza kumfundisha kingereza Glory.Bahati yule mtoto wa Glory likizo yake ilipata kuisha,hivyo alijiandaa kwa ajili ya Safari ya kuelekea Uingereza.
"Mwanangu sasa huyu mtoto wako huko anaenda nanani?aliuliza mama yake Glory.
"Mama sahivi sio kama zamani mtu anaweza kusafiri kwenda sehemu yeyote hata kama hapajui"aliongea Glory.Mama yake aliishia kutabasamu tu .Pombe mbalimbali za kisasa zilikuwa tayari kwa ajili ya baba yake Glory,mle ndani kulikuwa na kila kitu.Walinzi wanne kutoka Vietnam walikuwa sambamba na Glory.Sasa ilifika hatua ya Glory kusafiri kwenda jiji Dar es salaam,huko alipanga kuwa akaangalie sehemu za kufanyia biashara.Safari yake iliishia Kariakoo,huko aliangalia namna palivyochangamka nakujikuta anatabasamu.
"Nahitaji kununua ghorofa kwa ajili ya kuja kuishi huku"aliongea Glory akimwambia mlinzi wake,Basi baada ya kuzunguka sana alichukuwa usafiri wa ndege huku dareva wake akirudi na gari.
"Asee pesa kweli inaongea"walijisemea walinzi wake pale walipomuona Glory akifanya kile anachokitaka.
"Bwana Gasto alikuwa tajiri mkubwa jijj Dar es salaam,alimiliki kila aina ya biashara ndani ya jiji hilo.Utajiri wa Glory alipata kuusikia hivyo alianza kumfuatiria Glory lengo awe naye,alisafiri mpaka mkoani Arusha alipokutaka na Glory alimwambia kila kilichokuwa moyoni mwake lakini Glory hakutaka kusikia hizo habari.
"Kama una maada za biashara tuongee,lakini kama una mambo mengine waweza kuondoka"aliongea Glory kwa hasira.
"Hapana biashara tutafanya tukiwa wapenzi tayari"aliongea Gasto.
"Nadhani sina la kusema zaidi ya hayo hapo hivyo naomba nielewe"aliongea Glory.
"Mimi nina pesa nina kila kitu hivyo tutaongeza utajiri wetu uwe mkubwa zaidi"aliongea Gasto.
"Kama utajiri ninao tayari na wewe unao hivyo usilazimishe kitu kisichowezekana"aliongea Glory.
"Kwahiyo umekataa siyo?
"Ndio siko tayari kuwa na mwanaume kwa sasa"
"Sawa kwaheri na kazi njema"
"Karibu tena ndani ya himaya ya Glory"yalikuwa maongezi ya Glory na tajiri mkubwa zaidi ndani ya jiji la Dar es salaam aliyekuwa anaitwa Gasto.Glory hakutaka kuwa na mwanaume yeyote hivyo msimamo wake ulikuwa ule ule.Gasto baada ya kufika nje aliingia kwenye gari lake na kutafakari kitu kisha akamruhusu dereva wake Safari ikaanza kutoka Arusha mpaka Dar es salaam.
"Anaonekana kajiimarisha kwa ulinzi ila pamoja na kuwa na ulinzi anaweza kuibiwa kijinga kabisa,sisi ndio watoto waliozaliwa mjini"alijisemea Gasto akiwa ndani ya gari lake,alitoa simu yake nakuiweka sikioni.
Katika Hotel ya Serena iliyoko jiji Dar es salaam,ndani ya ile Hotel wanaonekana wanaume wanne wakiwa wamekaa kwenye meza moja wanajadiliana jambo,mmoja mwenye ngozi nyeupe akiwa kando yao.
"Make sure all plans go right, the other a solemn plan herself another man, she shall always remain low so she won't be rich we men do not have such a thing impossible"(hakikisha mipango yote inaenda sawa,kingine kuwa makini huu mpango asijue mtu mwingine,siku zote mwanamke ataendelea kuwa chini hivyo mwanamke hawezi kuwa tajiri sisi wanaume hatuna hicho kitu hakiwezekani)aliongea yule mwanaume aliyekuwa na ngozi nyeupe.Mwanaume mmoja alitumwa kutoka Dar es salaam kwenda Arusha kwa ajili ya kufanya jambo walilokuwa wamelipanga.
Ilikuwa siku ya jumapili,siku hiyo Glory alipanga kwenda kanisani,kama kawaida yake kila alipokuwa anaenda kanisani hakutaka kwenda na mlinzi yeyote.Akiwa ndani ya gari lake yeye na dereva wake kwa nyuma linaonekana gari likiwafuatiria....
Glory akiwa hana analolijua aliendelea kuchezea simu yake ya kisasa,hata dereva wake aliliona lile gari lakini hakulitilia maanani,lile gari lilihakikisha liko sambamba na gari alilokuwa amelipanda Glory.Ndani ya lile gari alionekana mwanaume mmoja aliyekuwa amevalia mavazi ya kawaida sana,hakuna mtu ambaye angeliweza kumtilia shaka.Kila kona alihakikisha yuko sambamba na Glory,dereva wa Glory lile tukio alipata kuliona lakini hakutaka kumwambia Glory na alijua vyema kuwa kwa siku ile hakuwa na walinzi kama alivyokuwa amezoea.
"Kama kufa wacha tufe lakini siwezi kumwambia Glory hiki kitu atachanganyikiwa"alijisemea yule dereva huku akiwa makini sana kuendesha gari,alipunguza mwendo na lile gari lilipita hapo yule dereva alijipa matumaini kuwa lile gari lilikuwa linapita.Safari yao iliishia kanisani,hata lile gari lilipaki pale pale kanisani,alishuka mwanaume mmoja huku akijifanya kuangalia gari yake.Baada ya kuona Glory ameingia ndani ya lile kanisa naye aliingia,bahati nzuri kwake yule dereva alibaki kwenye gari.
Sehemu aliyokaa Glory na yule mwanaume alikaa kando na hapo,ibada iliendelea.
"Kwaya namba mbili weka wimbo sasa ni mda wa kutoa sadaka"ilikuwa ni sauti ya mhubili aliyekuwa anaiongoza ibada.Mda wa sadaka uliisha yaliendelea matangazo mengine.
"Sasa tufumbe macho tuombe ili kila aliyeko humu apate kuondoka na baraka zake mungu"aliongea yule mchungaji,waumini wote walifumba macho akiwemo na Glory,lakini yule mwanaume hakufumba macho,aliuchukua mkoba wa Glory uliokuwa na vitu vingi vya thamani kulikuwa na simu kali ya kisasa alioiagiza kutoka nchini China ilikuwa na thamani ya billion 1.8 za kitanzania,vile vile kulikuwa na pete za dhahabu pamoja na viza vya kusafiria.Maombi yalipoisha waumini wote waliruhusiwa kuondoka,somo lililokuwa limehubiriwa siku ile lilikuwa somo la ndoa,hali ile ilimfanya Glory kumkumbuka Issa,hivyo hakuweza hata kuukumbuka mkoba wake alitoka mpaka nje,yule mwanaume baada ya kuuchukua mkoba wa Glory alienda mpaka kwenye gari lake akatulia . Glory baada ya kulifikia gari lake ndo aliukumbuka mkoba wake,wakati huo waumini wote walikuwa washatowanyika, Glory alichanganyikiwa sana alirudi mpaka kwa mchungaji na kutoa taarifa kwa baadhi ya waumini waliokuwa bado eneo like lakini bado haukupatikana.Glory alikubali hasara hivyo alizipiga hatua kuelekea kwenye gari lake lakini ghafla aliguswa bega aligeuka kwa haraka sana lengo amuone aliyemgusa bega,alikutana na sura ya kiume,alipoangalia mikononi mwa yule mwanaume hakuona kitu chochote jambo lile lilimzidishia hasira.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Habari yako"yule mwanaume alisalimia.
"Salama shida yako"alijibu Glory kwa sauti ya kukasirika.
"Naitwa De......"hakumalizia sentensi alikatishwa na sauti ya Glory.
"Hatupo shuleni hapa kutambulishana majina,sema shida yako"Glory aliongea kwa hasira.
"Haya mama lakini mimi unayenifokea naweza kuwa msaada mkubwa sana kwako"aliongea yule mwanaume aliyekuwa anaitwa Deus.
"Msaada upi huo unaoweza kunipa mtu kama mimi?aliuliza Glory.
"Kwahiyo mimi siwezi kukusaidia kitu chochote?
"Acha kuniharibia mda wangu hebu kwenda zako"Glory hakuwahi kumjibu mtu hivyo lakini hiyo yote ilikuwa hasira ya kupotelewa na vitu vyake mhimu.Glory alifungua mlango wa gari yake kwa hasira kisha akamwamuru dereva wake kuendesha gari.Deus naye aliwasha gari yake na kuanza kuwafuata kwa nyuma.Bado dereva wa Glory aliendelea kuliangalia lile gari kupitia kwenye kioo chake.Deus aliongeza mwendo kisha akalipita gari la Glory kisha akasimama mbele,kitendo kile kilimkwaza Glory,alitafuta simu yake ili awapigie police lakini alikumbuka kuwa simu yake ilikuwa kwenye ule mkoba uliopotea,Deusi alishuka kwenye gari na kulifuata lile gari la Glory akiwa na ule mkoba mkononi mwake, Glory aliganda kama vile kapigwa na shoti.
"Shika mkoba wako"aliongea Deus baada ya kulifikia gari la Glory.
"Kaka kumbe ni wewe uliyeuokota"aliongea Glory akiwa haamini kabsa.
"Sikiliza nikwambie Dada yangu,hata uwe na pesa ya kuijaza dunia lakini utu utaendelea kusimama kama utu,wengi mnapenda kujiweka juu sana na kuwazalau walioko chini yenu,mnasahau kabisa kuwa huwezi kujua mtu atakayekusaidia hata kama una pesa,hivyo Dada yangu mheshimu kila mtu hivi vitu ni vya kupita"aliongea Deus huku akimkabidhi Glory ule mkoba, Glory alipoukagua aligundua kuwa kila chake kilikuwemo.
Kwa aibu kabisa Glory alishuka kwenye gari na kumfuata yule Deus alitoa pesa nyingi sana na kumkabidhi Deus lakini alizikataa kabsa.
"Pokea hiyo basi Kama zawadi yako"aliongea Glory huku uso wake ukitazama chini.
"Kama pesa ninazo,wahenga walisema kuwa tenda wema nenda zako,hivyo sina haja na shukrani yako,matusi yako ndo naimani yataniongezea baraka"aliongea Deus kwa uchungu.
"Hayo yashapita tayari kaka angu nimeomba msahama naomba unisamehe nakuomba tena sana pokea na hii hera kwa moyo mmoja kabisa"aliongea Glory.
"Pesa siwezi kuipokea ila kuna kitu ukinipa naweza kukipokea"aliongea Deus.
"Kitu gani hicho"
"Naomba namba yako ya simu we pesa zako baki nazo"aliongea Deus.
"Hicho tu haya hii hapa"aliongea Glory huku akiitoa kadi ya mawasiliano na kumpa Deus.
"Sawa naomba nikikupigia pokea simu yangu"alisema Deus huku akiingia ndani ya gari lake na kuondoka akimwacha Glory akitafakari wema wa yule kijana.
"Dunia hii bado kuna watu waaminifu kama huyu kijana,nimempenda bure"alijisemea Glory huku akiingia ndani ya gari lake na kuondoka.Kule kwenye gari Deus alioanekana akitabasamu mda wote alitoa simu yake na kuiweka sikioni.
"Hallow"
"Sema kijana"sauti ya upande wa pili ilisikika.
"Naona hatua ya kwanza tayari kama tulivyo panga"aliongea Deus.
"Safi sana kijana wangu hii kuwa makini tusije kufeli kirahisi hakikisha mipango yote inakwenda sawa"
"Kuhusu hilo usjali hakuna mkate mgumu mbele ya chai"aliongea Deusi,basi baada ya maongezi yao Deus alikata simu.
Glory baada ya kufika nyumbani kwake aliwasalimia wazazi wake kisha akatuma taarifa kwa walinzi wa getini kuwa hakuna mtu yeyote kuingia humo ndani hivyo haitaji usumbufu wa aina yeyote.Moyo wake ulijikuta ukimpenda Deus.
"Mwanaume muaminifu yule"alijisemea Glory huku kila mda akiangalia simu yake kuona kama kuna ujumbe umeingia.
"Mbona sasa hajanitafuta?sijui kwanini sijachukua namba yake"alijisemea Glory huku akijigeuza geuza pale kitandani,akiwa kwenye dimbwi la mawazo mara alisikia kwenye simu yake ujumbe ukiingia.
"Hai mambo Glory"ilikuwa namba ngeni lakini Glory alihisi atakuwa Deus.
"Safi nambie"
"Safi,Deus hapa"
"Oooh nambie"
"Asee poa unafanya nini mda huu"
"Ahaa nimelala tu hapa"
"Nilijua hutojibu message zangu"
"Kwanini?
"Aha si unajua wewe mtu wa mishe mishe,pengine shemeji anaweza kukubana"
"Hapana shemu huyo atoke wapi"
"Kwahiyo wataka kuniambia jinsi ulivyo unaishi peke yako?aliuliza Deus.
"Ndio halafu wengi hawaamini"
"Okay sasa nilikuwa naomba tukutane jioni hii"
"Sawa ondoa shaka"
"Ila usije na walinzi si unajua tena"
"Kwahilo usiwaze"baada ya kumaliza kuwasiliana kwa njia ya ujumbe Glory alijipumzisha huku akiwaza atakavyo kuwa na Deus.
"Hawa wanawake bhana wanadanganyika kwa kitu kidogo sana"alijisemea Deus.Jioni ya siku ile Glory alichukua gari kisha akaenda kule walikokuwa wamepanga kukutana na Deus,mawazo ya Issa yalimtoka kichwani kabsa.
"Potelea mbali fimbo ya mbali haijawahi kuua nyoka"alijisemea Glory pale alipoijiwa na mawazo ya Issa..
Baada ya kukutana na Deus waliongea mambo mengi sana,Deus alipogusia suala la mapenzi Glory alijifanya kukataa lakini moyo wake tayari ulikuwa ushampenda Deus.
"Ni mapema mno nipe mda nifikirie"alijibu Glory.Maongezi yao hayakudumu sana badae waliagana kisha kila mtu akaenda nyumbani kwake.
"Kweli mapenzi upofu,yaani na ubosi wangu huu nimejikuta nakuwa mpole kabisa"alijisemea Glory akiwa ndani ya gari.Alikiri kabisa kumpenda Deus,kila alipokuwa anafikiria vitu vilivyokuwa kwenye mkoba wake lakini Deus kauleta kama ulivyokuwa alizidi kutoa tabasamu akiwa anarudi nyumbani kwake.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Naam mda wako wa kuwa masikini naona umewadia,tangu lini mwanamke akawa tajiri kiasi hiki?alijiuliza Deus.
Mapenzi ya Glory na Deus yalianza kwa kasi sana,kila kona Glory alikuwa na Deus,alianza kumtembeza kwenye miradi yake mingi,Deus mda wote alikuwa mtu wa kutabasamu alijua kitu atakachokifanya kitampa utajiri kwa mda mfupi,bado aliendelea kuwasiliana na wenzake na kuwajuza mambo yote aliyokuwa anayaona kwa Glory.
"Safi sana usionyeshe hofu yeyote kwa sasa mzoeane kwanza"ilikuwa sauti ya upande wa pili ikimwambia Deus.Kila sehemu Glory aliyokuwa anasafiri alikuwa na Deus.Baada ya miezi mitano Glory alimwambia Deus.
"Mme wangu nataka tufunge ndoa mwezi ujao"aliongea Glory akiwa kifuani kwa Deus.
"Sawa hakuna tatizo hata kesho Niko tayari"alijibu Deus.Basi waliendelea kufurahi huku mavazi yao yao wakiyaagiza nchini Uingereza.
"Sasa mambo yanaenda kukamirika, kuniambia tufunge ndoa hapo ndo nitamaliza mchezo"ulikuwa ujumbe aliouandika Deus na kuutuma kwa watu wajo.
"Sawa sawa tunaenda kuwa mabilionea na kuitangaza Arusha"upande wa pili ujumbe ulirudishwa kwa Deus.Glory hakutambua mpango uliokuwa unataka kufanyika,yeye alizidi kumuonyesha mapenzi ya kweli Deus huku mawazo ya Issa yakitoka kichwani mwake kabisa.
"Huyu huyu ntafunga naye ndoa ya kimataifa"alijisemea Glory.
"Mme wangu nataka ndoa yetu ifanyikie nchini Uturuki"aliongea Glory akimwambia Deus.
"Usijali nafikiri siku ile itakuwa ya furaha kwa upande wetu"alijibu Deus huku moyoni alifurahi.
"Sasa hebu nambieni mpango niufanye kabla ya ndoa au baada ya ndoa?Deus aliongea na watu wake.
"Mkishafunga ndoa kila mtu atajua kuwa wewe ni mme wake hivyo hata ukimpindua wote watajua kuwa zile mali zilikuwa zako"sauti ya upande wa pili wa pili ilisikika.
"Mpango mzuri sana huo nimeupenda"alijibu Deus.
"Ok vizuri sana fanya kitu kimoja kuanzia sasa,hakikisha unajua hatimiriki ya nyumba zake zote pia hakikisha kadi ya benk unaifahamu ikiwezekana na pesa yote iliyoko benk"sauti ya upande wa pili ilimwambia Deus.Basi baada ya maongezi yao waliagana huku Deus akiwaza jinsi ya kumwambia Glory ili ajue pesa zilizoko benk na baadhi ya mikataba.
"Lakini anavyonipenda lazima ataniambia kila kitu"alijisemea Deus huku akiingia ndani na kumkuta Glory akiwa anaangalia baadhi ya mikataba.
"Mke wangu kwani hii nyumba ulijenga mwenyewe au vipi?aliulizaza Deus.
"Hapana hii nimeinunua labda wanayoishi wazazi wangu ndo nimeijenga"alijibu Glory,tangu alipokuwa na Deus alikuwa anaishi nyumba tofauti na ile waliyokuwa wanaishi wazazi wake,bado hakuwaambia neno lolote kuhusu huyo mchumba wake.Ila mama yake aliweza kumgundua kutokana na kutokaa nyumbani mda mwingi.Baba yake na Glory alikuwa mtu wa kunya pombe kila mda,kila pombe aliyokuwa anahitaji alikuwa anaipata, Glory hakutaka wazazi wake wateseke.Bado Deus aliendelea kumchunguza Glory mpaka hapo alipata kufahamu kuwa Glory alikuwa na utajiri mkubwa sana.
"Sijui atajisikiaje,kuanza mwanzo ni ngumu sana"alijisemea Deus huku akiwa anamwangalia Glory aliyekuwa anapanga pesa ili azipeleke benk.
"Sasa mke wangu si tunaenda wote huko benk au hutaki kuongozana na mimi?aliuliza Deus kwa uchokozi.
"Jiandae twende mme wangu"alisema Glory.
"Naam miezi miwili ijayo utaanza kuokota makopo"alijisemea Deus.Baada ya kufika benk Glory aliweka pesa lakini Deus alitaka aone pesa iliyokuwa pale ilikuwa kiasi gani.
"Sasa mke wangu humu Kuna shingap"
"Ngoja tuangalie"alisema Glory.Baada ya kuangalia walikuta million Mia tatu zilizokuwa benk.
"Hongera mke wangu,umejitahidi sana"aliongea Deus.
"Ndio lakini bado tupambane tuwe zaidi ya hapa"aliongea Glory.Baada ya kutoka benk Deus zile taarifa alizifikisha kwa watu wake,mipango yao iliendelea kupangwa.
"Baba na Mama leo nina habari njema kwenu"aliongea Glory mbele ya wazazi wake.
"Zipi hizo mwanangu ongea"
"Ongea binti yangu usiwe na hofu kabsa"alijibu baba yake kwa sauti ya kilevi.
"Mwezi ujao natarajia kufunga ndoa hivyo naomba baraka zenu wazazi wangu"aliongea Glory.
"Ondoa hofu kabsa huu ndo wakati wako,miaka yako ndo hii ni jambo jema"alijibu mama yake.Maongezi ya hapa na pale yaliendelea.
Ndoa ya Glory na Deus ilianza kutangazwa ndani ya jiji la Arusha na mikoa jilani,kila mtu alitega kusikia sikio kusikia kuwa huyo mwanamke tajiri ataolewa nanani,magazeti hayakuacha kuandika ile taarifa.
"Hatimaye mwanamke tajiri jiji Arusha anatalajia kufungua ndoa na mwanaume hoe hae"kilikuwa kichwa cha habari kwenye baadhi ya magazeti mkoani humo.Habari zike zilisambaa mpaka jiji Dar es salaam,wale waliokuwa na mpango na Deus walianza kuhesabu siku chache za kuwa matajiri.Matangazo ya ndoa yalianza kuwekwa kwenye materevisheni na kwenye mitandao ya kijamii.
"Yaani hata siku yenyewe ya ndoa bado lakini matangazo yanasambaa kiasi hiki,kweli hakuna linaloshindikana mbele ya pesa"kijana mmoja alijisemea baada ya kuona tangazo hilo.
Ndani ya China,Issa mawazo ya Glory yalimwishia kichwani kabsa.
"Namshukuru mungu kwa hili,sasa nikufanya kazi kwa bidii ili niwe tajiri mkubwa"alijisemea Issa.Alichoamua kukifanya alijiunga na mtandao wa Facebook ili angalau apate kujua kinachoendelea nchini Tanzania.Alitafuta makundi ya Arusha hapo alijiunga nayo lakini moyo wake ulipigwa na butwaa baada ya kuona lile tangazo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Whaaaat!!!?(nini) Glory tajiri?inamaana baada ya kuwa na pesa ndo kanisahau mimi?kumbe mtu mwenyewe yupo halafu katangaza ndoa?ziko wapi ahadi zake?msaada wangu wote Leo kanisaliti? sasa nasema kwa herufi kubwa kuwa SIKUBALI najua huo utajiri kautoa kwenye pesa zangu nilizomwachia hivyo lazima niende nikavuruge ndoa yao"Issa aliongea kwa hasira kali sana.Alivuta subira kusubiri siku yenyewe.
"Yaani upendo wangu wote leo kanisaliti?hapana hili siwezi kurikubali,pia nasikia wakimuita tajiri lakini utajiri wake hauwezi kuniogopesha mimi"aliongea Issa huku akikunja ngumi kwa hasira.Siku hiyo alishinda ndani akiwa anatafakari moyo wake ulimwambia kuwa aende hata siku hiyo lakini alijizuia.
"Nataka niende siku yenyewe"alijisemea Issa.
Mavazi yaliyokuwa yanatoka yanatoka nchini Uingereza yalifika Arusha,yalipokelewa na wapambe wa Glory,kwa wakati huo Glory alikuwa na wazazi wake walipoyaona yale mavazi kila mtu alishangaa sana,yalikuwa mavazi ya bei ya juu mno.
"Lakini mwanangu kwa nini usimlete huyo mkwe wetu tukamjua?aliongea mama yake Glory kwani mpaka mda huo hawakumjua mtu aliyekuwa anataka kumuoa.
"Jamani mtamuona tu msijali"aliongea Glory.
Ndege binafsi ilikodiwa na Glory ilikuwa inapambwa zaidi,kwakuwa zilibaki siku sita basi maandalizi yalikuwa yanaenda kwa kasi sana.
"Yaani mme wangu nataka hii iwe harusi ya kwanza Tanzania hii kuwahi kutokea,nadhani itasimuliwa na kila mtu"aliongea Glory.Deus alizidi kukubali kila alichokuwa anaambiwa na Glory.
"Lakini mke wangu kwanini tusiende tu hata nchini Kenya huoni Uturuki ni mbali sana?ni mawazo tu lakini"aliongea Deus akimwambia Glory.Lengo la Deus kusema hivyo hakutaka kutumia gharama nyingi kwakuwa alijua mda mfupi ujao hizo mali atazimiriki yeye.
"Sawa mme wangu tutaenda kutembelea tu kama kufurahi kisha tunarudi"aliongea Glory.
Siku hazigandi hatimaye zilibaki siku mbili,Issa alijiandaa kwa kila kitu kwakuwa alijua vyema kuwa Pete itavalishwa kesho yake naye alipanga siku hiyo hiyo.
"Glory na Deus waliendelea kujiandaa hata wazazi wake na Glory nao walifurahi kila walipokuwa wanaona maandalizi yalivyokuwa,matajiri mbali mbali walialikwa kutoka sehemu tofauti tofauti,siku yenyewe ilitimia.Watu walikula na kunywa kila kitu kilikuwepo, Glory na Deus pamoja na ndugu wengine walipanda ndege kwenda nchini Kenya,huko walifurahi,walizunguka sehemu mbali ikiwemo Mombasa, Nairobi na sehemu nyingine yote hiyo ilikuwa ni furaha,walipanga Pete wavalishane kesho yake.Baada ya kuzunguka sana walijipanga kwa ajili ya kurejea jijini Arusha.
Matangazo yalikuwa live kabsa kila kona ya ya nchi hivyo ambaye hata hakubahatika kufika aliendelea kuangalia kupitia kwenye runinga.
Kwa wakati huo Issa ndo alikuwa anakwenda Baiyun International Airport uwanja wa ndege ulioko katikati ya jiji la Guangzhou kwa ajili ya kuja nchini Tanzania ili aharibu ndoa ya Glory na Deus.
Ndege iliyokuwa imewabeba akina Glory ilianza Safari kutoka Kenya kuja jiji Arusha,watu waliendelea kufurahi nyumbani kwa Glory.
"Hii harusi haijawahi kutokea"alisema kijana mmoja wakati akila wali.
Matajiri waliendelea kunywa vinywaji vya bei juu wakati huo akina Glory ndo walikuwa wanafika kwenye uwanja wa ndege uliopo.Kilimanjaro,hapo hapo walipokelewa na magari ya kifahari,jiji la Arusha lilisimama kwa mda na yote hayo harusi ya Glory.
"Huyu mwanamke ana hela kweli yaani kakodi ndege kwa ajili ya kuwazungusha tu,halafu cheki msafara wa magari,utafikiri na msamaha wa Rais"mwanaume mmoja alijisemea wakati akiangalia tukio like kupitia kwenye runinga yake.
Msafara wa Glory uliishia nyumbani kwake,shangwe na vigelegele vilisikika,mziki mkubwa uliendelea kusikika,hata waliokuwa mikoa jirani walitamani kufika,ukumbi mkubwa uliopabwa vyema ulikuwa tayari umejaa.Watu waliendelea kujaa ukumbini kadri mda ulivyokuwa unasogea.
Ndani ya China kulizuka wizi wa vitambulisho mbalimbali yaani waliokuwa wanaiba hivyo vitambulisho walikuwa wanasajiri laini na kutapeli mitandaoni,hivyo lilipokuwa linatokea kosa walikuwa wanakamatwa wale walioibiwa,serikali nchini humo ilijitahidi sana sana kufanya uchunguzi lakini ilikuwa ni ngumu kuwabaini hao wezi,ilichukuwa mda sana,hicho kitu ndo kilichotokea kwa Issa,alichomolewa waleti yake,uzuri hakuwa na vitambulisho,bali alikuwa na VIZA vya kusafiria waleti ilichukuliwa akiwa hajui lolote,yeye alizidi kusogea uwanja wa ndege lengo uwahi nchini Tanzania,kila mda alionekana kujiinamia huku akimkumbuka Glory,baada ya kufika uwanja wa ndege kabla hajakata tiketi aliambiwa aonyeshe viza vya kusafiria,baada ya kuangalia mfukoni hakuona kitu chochote,alijaribu pia kuangalia kwenye begi lake lakini bado hakuona kitu,kawaida ya nchi za wenzetu kama huna vizaa huruhusiwi kusafiri,ndicho kilichomkuta Issa,alijikuta akienda chini kama mzigo,aliona mipango yake ya kuharibu ndoa inaenda kombo.
"Lakini siwezi kukubali"alisema Issa na kutoa pesa kuwapa wale waliokuwa wanahusika na mambo ya tiketi lakini waligoma,Issa alichanganyikiwa sana.
"Ipo siku najua nitakwenda tu ila kwa njia zozote lazima Glory arudi mikononi mwangu,mimi ndo nimemsaidia kwa kila kitu,lazima upendo wangu auone tena"alijisemea Issa huku akigeuka na kurudi alipokuwa anakaa.
Kalibia mikoa yote nchini Tanzania ilikuwa inafahamu ile ndoa ya Glory na Deus,wengi walizidi kujiuliza kuwa tajiri kama Glory inawezekana vipi kaolewa na mwanaume ambaye hata hajulikani?,kila mtu alibaki nalo moyoni.Wengi waliamini kuwa upendo hauchagui yeyote unampenda lakini watu wengine walijua kuwa kuna kitu kinaendelea.
Kesho yake asubuhi kulipambazuka na hali ya hewa safi,bado watu waliendelea na kuburudika kabsa,hakuna kilichokuwa kinapungua.Kanisa la Parokia ya Mt.vicent pallot,lilikuwa tayari,msafara wa magari uliongozana mpaka kanisani,saa sita mchana ndo ulikuwa wakati wa kuvalishana Pete,zoezi hilo lilidumu kwa mda wa dakika kumi,baada ya kukamirika magari yalirudi nyumbani kwa Glory.Sherehe iliendelea,baada ya siku nne tayari sherehe iliisha wazazi wake na Glory walifurahi kupata mkwe wao.
Baada ya miezi mitatu tayari Deus alijua kila kitu cha Glory.Maisha yao yalisogea huku Deus akiwa makini sana kuangalia kila kitu.
"Sasa mke wangu kuna hela nataka kuipeleka benk"aliongea Deus.Glory hakuwa na mashaka naye kabisa hivyo alimpa na namba ya siri ya benk.Deus baada ya kufika benk alihamisha pesa yote iliyokuwa kwenye akaunti ya Glory alizihamishia kwake,baada ya kumaliza zoezi hilo alirudi nyumbani,aliiba hatimiriki zote pamoja na mikataba mbali mbali ya Glory,baada ya kuhakikisha kila kitu kiko mikononi mwake aliwapigia wale wenzake waliokuwa jiji Dar es salaam,moja kwa moja walikuja na kupewa ile mikataba pamoja na vitu vingine yote hayo yalipokamirika walihesabu wiki moja mbele ya kuweza kumpindua Glory.
"Mke wangu nataka tusafiri twende huko Nairobi tukaangalie biashara ya kufanya huko,kukaa sehemu moja hakutaweza kutufanya tuwe na mafanikio makubwa,hivyo jiandae kesho twende"aliongea Deus, Glory hakuwa na kipingamizi chochote kwa kuwa alikuwa anamuamini sana huyo mme wake.
"Sasa huko Nairobi tutafanya biashara gani?aliuliza Glory.
"Biashara hazikosi mke wangu kikubwa twende tukaangalie"aliongea Deus.Basi walikubaliana kuwa wiki ijayo ndo wasafiri, Deus hakuacha kufanya mawasiliano na watu wake ambao tayari walikuwa jijini Arusha.
"Wiki ijayo ndo tunamaliza mchezo"ulikuwa ujumbe kutoka kwa Deus kwenda kwa watu wake.
Huko China Issa hakuacha kufuatilia habari za Glory kupitia mtandaoni.
Hatimaye wiki moja ilitimia, Glory na Deus walijaindaa vyema,kwakutumia ndege ya kukodi iliwafikisha mpaka Nairobi Kenya,huko waliishia kuzunguka na kuangalia mazingira, mawasiliano kati ya Deus na watu wake yalifanyika,moja kwa moja wale watu walienda mpaka kwa Glory alipokuwa anaishi na wazazi wake,waliingia mpaka ndani walinzi walipojaribu kuwazuia walionyesha vitambulisho vyao.
"Tumekuja hapa kwa lengo moja tu kuanzia sasa mtafuata amri itakayotolewa na mme wake Glory na sio Glory nadhani mmenisikia"aliongea mwanaume mmoja huku akiiweka sawa suti yake.Walinzi wote walishangaa sana kila walipojaribu kumpigia Glory simu hawakuweza kumpata.Mpango uliokuwa unaendelea Deus aliufahamu vyema,wale walinzi walikuwa wapole kabsa.
"Hizi ni mali za Deus na sio Glory,tangu lini mwanamke akawa na utajiri Kama huu? aliongea mwanaume mmoja akiwaambia walinzi wa Glory.
"Ila hilo kweli,basi tunaomba msitufukuze tukae hapa tuendelee na kazi"aliongea mlinzi mmoja.
"Hata msijali kikubwa kuwa upande wetu"aliongea yule mwanaume,walinzi wote waligeuka na kuwa upande wao.
"Hakuna mwanamke anayeweza kumiriki utajiri kama huu"alijisemea mlinzi mmoja.
Saa kumi jioni Glory na Deus ndo walikuwa wanafika kwenye uwanja wa ndege wa Kilimanjaro, Deus aliichukuwa simu ya Glory lengo Glory asijue kilichokuwa kinaendelea.Gari lao walilokuwa wameliacha uwanja wa ndege iliwapakia mpaka nyumbani kwa Glory.
"Mbona kuna watu tofauti hapa nani kawapa ruhusa ya kuingiza watu msiowafahamu?aliuliza Glory.
"Kwani wewe unaongea kama nani kwenye hii nyumba?aliuliza mwanaume mmoja aliyekuwa anaitwa Inno.
"Unasemaje wewe?aliuliza Glory.
"Mbali hapo hujasikia au?
"Walinzi fanyeni kazi ya kuwatoa hawa watu"aliongea Glory.Lakini walinzi walibaki kimya wakiangaliana.
"Mme wangu kuna nini hapa mbona sielewi?aliuliza Glory.
"Kwani wewe hapa una kipi chako?hapa sio kwako tena labda ntakupa kazi uwe mfanya kazi wa ndani"aliongea Deus kwa kejeli.
"Nini wewe?aliuliza Glory kwa wakati huo wazazi wake walikuwa wakitamtaza Glory.
"Nilisema toka mwanzo kuwa hizi mali sio zake,sasa sijui hii aibu tutaiweka wapi"alijisemea mama Glory.
Glory aliingia mpaka ndani na kuangalia mikataba yake pamoja na hatimiriki mbali mbali lakini hakukuta kitu chochote,alizidi kuchanganyikiwa.
"Yaani mme wangu leo hii umenigeuka? aliongea Glory.
"Umejigeuka mwenyewe sahivi huna chako,ukikataa kazi za ndani rudi kijijini kwenu na hawa wazazi wako"aliongea Deus.Glory alizikumbuka hera zake zilizokuwa benk,alichukuwa simu yake kwakuwa alikuwa na uwezo wa kuangalia salio kupitia kwenye simu yake ya mkononi,baada ya kuangalia hakukuta kitu chochote,alipoteza fahamu pale pale.Deus na watu wake walizidi kufurahi kwa ushindi ambao waliupata.
"Jamani wazazi wangu huyu mwanenu huu utajiri haukuwa wake hivyo ataendelea kubaki kama mke wangu lakini akiwa chini yangu,hawa wanawake ukiwapa nafasi wanakutawala"aliongea Deus akiwaambia wazazi wake na Glory nao walijikuta wakiyaamini yale maneno.Baba yake Glory pombe ziliisha kichwani ghafla.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Sasa kwa nini katuleta huku kutupa aibu sisi wazazi wake?aliongea baba yake Glory kwa hasira.
"Tulivyoondoka kijijini kwa mbwembwe sasa sijui tutarudi vipi huko"aliongea baba yake Glory.
"Katutia aibu kwakweli"alijibu mama yake aliyeshindwa kuyazuia machozi.
"Sasa hapa tunaenda kubadirisha wafanyakazi wote kisha tunawaweka wapya"aliongea Inno,moja kwa moja wenzake walimuunga mkono,walinzi walikuwa wametoka Vietnam walijikuta wanapoa,kwakuwa walimkuta Deus tayari ameshakuwa mme wa Glory hivyo walishindwa kuingilia kati sakata hilo.Bado taarifa zile zilibaki mle ndani zilikuwa bado hazijasambaa kabsa.
"Sasa tukatangaze magazetini kuwa huyu mwanamke kagombana na mme wake hivyo wameachana"aliongea Inno.Pesa iliyokuwa kwenye akaunti ya Deus ilikuwa kubwa sana,Deus aliweza kuwahonga kituo cha police cha Arusha ili hata Glory akianziasha kesi isiwe na nguvu.
"Zamu yetu ya utajiri imefika,hongera sana Deus kwa kufanya mpango huu bila kuwa na tatizo lolote"aliongea mwanaume mwingine aliyekuwa anaitwa Andrea.Bado Glory alikuwa bado hajarejewa na fahamu.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment