Search This Blog

Thursday, July 21, 2022

DEAD LOVE ( PENZI LILILOKUFA ) - 5

 





    Simulizi : Dead Love ( Penzi Lililokufa )

    Sehemu Ya Tano (5)



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Winfrida, mhudumu wa kike wa hoteli iliyokuwa ufukweni mwa bahari ya Msasani Peninsula, Kawe jijini Dar es Salaam alikuwa akikimbia huku na kule kukusanya chupa ambazo wateja wake walikuwa wameziacha ufukweni baada ya hali ya hewa kubadilika ghafla.

    Akjiwa anaendelea kukusanya chupa, huku manyunyu ya mvua yakiwa yameanza kuongezeka, anga likiwa limegubikwa na wingu zito la mvua, ghafla alionakitu kilichomshtua.

    Alikuwa ni kijana mtanashati aliyekaa juu ya mchanga, akiwa amejiinamia, akiwa hana habari kabisa na mabadiliko makubwa ya hali ya hewa yaliyotokea. Japokuwa manyunyu ya mvua yalikuwa yakiuloiwanisha mwili wake, badio alikuwa amejiinamia vilevile.

    Winfrida alijaribu kumuita lakini hakuonesha kushtuka wala kutringishika. Wingula mvua lilizidi kutanda na sasa ngurumo za radi zilikuwa zikisikika na kufanya hali iwe ya kutisha mno. Hakukuwa na mtu yeyote aliyekuwa amesalia ufukweni mpaka muda huo zaidi ya watu hao wawili.

    Tayari mvua kubwa ilikuwa imeshaanza kumwagika, ikabidi Winfrida amkimbilie yule kijana pale alipokuwa amekaa na kumshika mkono. Ni hapo ndipo alipozinduka kutoka kwenye dimbwi la mawazo machungu alilokuwa amezama ndani yake kwa muda mrefu.

    Harakaharaka akainuka na kuanza kukimbia kumfuata Winfrida aliyekuwa anaendelea kumsemesha lakini wakawa wanashindwa kuelewana kutokana na mvua kubwa iliyokuwa inamwagika.

    Kijana huyo hakuwa mwingine bali Abdallah ambaye alikuwa kwenye kipindi kigumu sana ndani ya moyo wake kutokana na vituko alivyokuwa akifanyiwa na msichana aliyetokea kumpenda kwa moyo wake wote, Karen ambaye sasa aligeuka na kuwa mwiba mkali ndani ya moyo wake.

    Japokuwa alikuwa amechukua uamuzi mgumu wa kuamua kuyakatisha mahusiano yao kutokana na kugundua kuwa msichana huyo alikuwa amerudia tena kwa mara nyingine tabia yake hatari ya kutumia madawa ya kulevya, moyo wake ulikuwa ukizungumza lugha nyingine tofauti kabisa.

    Bado alikuwa akimpenda sana Karen na alitamani abadilike na kuwa vile alivyokuwa anataka ili waishi pamoja na baadaye kufunga ndoa na kuwa mume na mke halali, lakini hilo lilionekana kuwa gumu sana, hali iliyosababisha apitia kipindi kigumu sana maishani mwake.

    Hata hivyo, aliamua kushikilia msimamo wake wa kutengana na Karen kwani aliamini kama kweli msichana huyo alikuwa na mapenzi ya dhati kwake, anaweza kubadilika na kuacha kabisa matumizi ya madawa ya kulevya ili waendelee kuishi pamoja.

    “Umepatwa na nini?” kauli ya Winfrida ndiyo iliyomzindua kutoka kwenye lindi zito la mawazo, akiwa tayari wameshafika kwenye sehemu ya pili ya hoteli hiyo ambayo haikuwa ikifikiwa na mvua kubwa iliyokuwa ikiendelea kumwagika. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kila mtu alikuwa akimshangaa Abdallah kwani alionesha dhahiri kutokuwa kwenye hali yake ya kawaida na muda mfupi baadaye, radi kubwa ilipiga na kusababisha umeme ukatike, eneolote likamezwa na giza nene huku mvua kubwa ikiendelea kunyesha. Muda mfupi baadaye, mishumaa iliwashwa.

    Winfrida akamfuata tena Abdallah na kuendelea kumuuliza kilichomtokea. Licha ya Winfrida kurudia kumuuliza mara kadhaa, bado hakujibu chochote huku maji ya mvua yaliyomlowanisha Abdallah yakimsaidia kuficha ukweli kwamba alikuwa analia.

    Winfrida hakukata tamaa, aliendelea kumsubiri Abdallah atulie ili amwambie kilichokuwa kinamsumbua, muda mfupi baadaye, Abdallah aliingiza mkono mfukoni na kutoa fedha, akamuagiza mhudumu huyo amletee maji ya kunywa. Muda mfupi baadaye, Winfrida alikuwa tayari amesharejea na safari hii, naye aliamua kuvuta kiti kabisa, huku akionesha kuwa na shauku ya kutaka kujua kilichokuwa kimemtokea Abdallah mpaka akawa kwenye hali ile.

    Abdallah alipoona msichana huo amekaa kwenye kiti kilichokuwa kinatazamana naye, huku akiwa anamtazama usoni kwa huruma, alishusha pumzi ndefu na kumuangalia Winfrida ambaye bado alikuwa ametulia, akisubiri kusikia chochote kutoka kwa Abdallah.

    Kabla hajazungumza chochote, simu ya mkononi ya Abdallah ilianza kuita mfululizo, akaiangalia namba ya mpigaji lakini badala ya kupokea, alijiinamia tena na kuanza kulia, safari hii kwa uchungu zaidi kuliko mwanzo, jambo lililomfanya Winfrida abaki njia panda.

    “Jamani kwani kuna nini? Mbona sikuelewi? Huyo Karen ndiyo nani?”

    “Niache tu dadaangu, acha dunia iniadhibu kwa sababu nilishindwa kusikia la mkuu, acha leo nivunjike guu,” alisema Abdallah huku akijifuta machozi na kamasi zilizokuwa zinamtoka kwa wingi.

    Winfrida aliendelea kumsisitiza amwambie lakini hakuwa tayari, akaendelea kuumia ndani ya moyo wake mithili ya mtu aliyepokea taarifa za msiba. Mvua iliendelea kunyesha kwa muda mrefu, ilipokuja kukatika, tayari ilikuwa ni usiku, watu wakaanza kutoka, kila mmoja akitafuta njia ya kuelekea kwake.

    Abdallah naye aliinuka na kuagana na Winfrida, akamshukuru kwa wema wake na kumwambia kwamba wakijaaliwa, ipo siku watakutana tena. Japokuwa bado Winfrida alikuwa na shauku kubwa ya kutaka kujua kilichomtokea kijana huyo mtanashati, alishindwa kumzuia kuondoka.

    Abdallah alipofika kwenye lango la kutokea, Winfrida alikumbuka kitu, akasimama na kumuita Abdallah kisha akaanza kumkimbilia.

    “Samahani kama nakusumbua, hii hapa ni namba yangu ya simu, unaweza kunipigia muda wowote utakaokuwa na mudi ya kuzungumza na mimi,” alisema Winfrida huku akimkabidhi Abdallah namba iliyokuwa imeandikwa kwenye tishu. Akaachia tabasamu hafifu na kuipokea kisha akaendelea na safari yake, huku akikwepa madimbwi ya maji yaliyosababishwa na mvua hiyo.

    Hatimaye alipata usafiri uliomfikisha mpaka Makumbusho alikokuwa amehamia kutoka Mikocheni alikokuwa anaishi awali. Akateremka kwenye daladala na kuvuka barabara, akaanza kutembea taratibu kuelekea nyumbani kwake ambako aliamini atakuta Karen ameshaondoka kama alivyomwambia asubuhi ya siku hiyo baada ya kugundua kuwa alikuwa amerudia matumizi ya madawa ya kulevya.

    Hatimaye aliwasili kwenye nyumba aliyokuwa anaishi lakini akiwa getini tu, alipatwa na mshtuko baada ya kukutana na mazingira yasiyo ya kawaida. Akasimama kwa sekunde chache na kuanza kuangalia huku na kule. Kitu cha kwanza kilichomshtua ilikuwa ni kuona soksi yake moja ikiwa getini.

    Alipotazama vizuri chini kwa msaada wa taa za nje, aliona pia nguo zake nyingine zikiwa zimedondoka, akapiga moyo konde na kuamua kusonga mbele ili akajionee kilichotokea.

    Alipofika kwenye mlango wa kuingilia ndani kwake, alipigwa na butwaa zaidi baada ya kugundua kuwa mlango ulikuwa wazi kabisa wakati yeye aliufunga kabla ya kuondoka. Huku akitetemeka, aliingia ndani na hali aliyokutana nayo, ilimchanganya kuliko kawaida.



    Chumba kilikuwa kitupu kabisa huku vitu vyake vyote vikiwa havipo. Awali alihisi yupo ndotoni, akafikicha macho na kutazama tena, hakuna kilichobadilika. Ni hapo ndipo alipogundua kuwa kumbe hakuwa ndotoni, nguvu zikamuishia akiwa haamini alichokuwa anakiona.

    Harakaharaka alitoka mpaka kwa mama mwenye nyumba wake ambapo alipomuuliza, alimweleza kwamba Karen ndiye aliyehamisha vitu hivyo kwa maelezo kwamba wanahamia Bagamoyo.

    Abdallah alishindwa kuyazuia machozi yasiulowanishe uso wake, akarudi chumbani kwake na kukaa sakafuni ambapo aliendelea kulia kwa muda mrefu, akijilaumu sana kwa kuangukia kwenye penzi la Karen.

    “Lazima nimtafute mpaka nimpate,” alisema Abdallah huku akiendelea kutokwa na machozi mengi. Alitoa simu yake na kujaribu kumpigia Karen lakini majibu aliyoyapata ni kwamba namba hiyo haikuwa ikipatikana hewani.

    Kwa kuwa muda ulikuwa umeenda sana, aliamua kulala mpaka kesho yake ndiyo aanze kazi ya kumtafuta. Alilazimika kulala sakafuni, akachukua nguo zake zilizokuwa zimezagaa ndani ya chumba hicho na kuzitumia kama godoro.

    Usingizi haukuja kirahisi, muda wote alikuwa akiviwazia vitu vyake vya thamani, chuki kali ikamuingia dhidi ya Karen ambapo alikuwa akijiapiza kuwa atakapomkamata lazima amfunze adabu kwa alichomfanyia.

    Kesho yake asubuhi, Abdallah aliwahi kwenda kazini kuomba ruhusa kisha akapitia Mikocheni alikokuwa akiishi awali. Lengo lake lilikuwa ni kumtafuta yule dereva Bajaj aliyesema anamfahamu vizuri kwani aliamini anaweza kumsaidia kumuelekeza sehemu za kumpata.

    Muda mfupi baadaye tayari alikuwa ameshawasili Mikocheni, akaenda mpaka kwenye kituo cha Bajaj kijana huyo alipokuwa akishinda. Kwa bahati nzuri alimkuta, akamuelezea kwa kifupi kilichotokea kisha akamuomba amsaidie kumpata.

    “Mimi si nilikwambia? Yule demu hafai, nadhani sasa unanielewa nilikuwa namaanisha nini,” alisema dereva huyo wakati akizungumza na Abdallah, akakubali kumsaidia ambapo waliingia ndani ya Bajaj na kuondoka eneo hilo.

    “Tunaanzia wapi?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Juzi kuna sehemu nilimpeleka Kinondoni, tuanzie hapo tukimkosa twende Manzese Uwanja wa Fisi,” alisema dereva huyo wa Bajaj, Abdallah akakubaliana na wazo hilo. Safari iliendelea na dakika kadhaa baadaye, tayari walikuwa wamefika Kinondoni.

    Wakaingia mitaa ya ndanindani na muda mfupi baadaye, walitokezea eneo kijana huyo alipomleta Karen siku kadhaa zilizopita.

    “Sema nini, hapa inabidi tuwe makini kwa sababu panauzwa madawa ya kulevya na wote waliokaa hapa ni wahuni waliopitiliza,” alisema dereva huyo wa Bajaj, wakateremka na kuanza kutembea kwa tahadhari kuelekea upande lilipokuwa limekaa kundi la vijana wahuni.

    Waliwasalimia kisha Abdallah akaeleza shida yao.

    “Huyo demu mwenyewe yukoje?” aliuliza kijana mmoja kwa sauti ya kilevi, Abdallah akatoa simu na kuwaonesha picha ya Karen aliyokuwa nayo.

    “Ahaaa, kumbe ndiyo huyu? Mi najua alipo,” alisema kijana mwingine, akawaelekeza kwamba mtaa wa pili kutoka eneo hilo, kuna gesti bubu moja ndipo mahali msichana huyo alipoelekea jana yake usiku, baada ya kuwa ameshajidunga madawa ya kulevya.

    “Halafu demu mwenyewe ana mihela kinoma,” alisema kijana huyo, harakaharaka wakaongozana kuelekea kwenye gesti hiyo.

    “Samahani namuulizia dada mmoja anaitwa Karen amenielekeza kuwa yupo kwenye gesti hii,” Abdallah alimwambia mhudumu wa gesti hiyo, akamuuliza jinsi msichana huyo alivyo ambapo alimtolea simu na kumuonesha picha.

    Muda huo wale watu wengine aliokuwa ameongozana nao, walikuwa wamesimama nje kwani hawakutaka kuingia wote kwenye gesti hiyo wakihofia mhudumu anaweza kukataa kutoa ushirikiano.

    “Yupo chumba namba saba, nyoosha na hii korido mpaka kule mwisho, upande wa kushoto,” alisema mhudumu huyo, Abdallah akamshukuru na kuanza kutembea kwa tahadhari kuelekea kwenye chumba hicho. Kadiri alivyokuwa anazidi kukisogelea chumba hicho ndivyo mapigo yake ya moyo yalivyokuwa yakimuenda mbio, hakuwa anajua atamfanya nini msichana huyo baada ya kumkamata.

    Hatimaye alikifikia chumba namba saba, akagonga mlango huku mapigo ya moyo wake yakizidi kumuenda mbio. Licha ya kugonga zaidi ya mara tatu, hakukuwa na mwitikio wowote kutokea ndani.

    Akatoa simu yake na kujaribu kupiga namba ya Karen, mara akasikia simu hiyo ikiita ndani ya chumba hichohicho, jambo lililozidi kumpa uhakika kwamba lazima Karen alikuwa ndani. Hata hivyo, aliendelea kugonga kwa muda mrefu bila kuitikiwa, ikabidi arudi kwa yule dada wa mapokezi na kumueleza kilichotokea.

    Wakaja kusaidiana kujaribu kugonga mlango lakini bado hakukuwa na majibu yoyote.

    “Au yupo na mwanaume mwingine anaogopa kufungua?”

    “Hapana, alikuja peke yake na sijamuona mwanaume yeyote kuingia.”

    “Kwani alikuja lini hapa?”

    “Jana mchana ila jioni alitoka na aliporudi alikuwa amelewa sana, sijamuona tena akitoka mpaka muda huu,” alisema yule mhudumu, Abdallah akashusha pumzi ndefu.

    “Hakuna funguo za akiba?”

    “Zipo, ngoja nikachukue,” alisema mhudumu huyo huku na yeye akiwa ameanza kuingiwa na wasiwasi.

    Muda mfupi baadaye, alirejea akiwa na funguo za akiba. Wakasaidiana kufungua mlango.

    “He! Mungu wangu, nini tena?” mhudumu huyo aliyekuwa wa kwanza kuingia ndani ya chumba hicho, alisema kwa sauti ya juu baada ya kuingia ndani, ikabidi Abdallah naye asogee haraka kutaka kuona kilichomfanya mhudumu huyo kushtuka kiasi hicho.

    “Mungu wangu,” Abdallah alisema kwa sauti ya juu zaidi, akionesha kutoyaamini macho yake kwa alichokuwa anakiona mbele yake.



    Harakaharaka wote wawili waliingia mpaka ndani ya chumba hicho na kusogea kwenye kitanda. Karen alikuwa amelala kichwa na mkono mmoja vikiwa vinaning’inia kitandani huku mkono mmoja ukiwa juu ya kitanda, bomba la sindano likiwa limenasa kwenye mshipa wa damu.

    “Kwani nini kimetokea?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Huwa anatumia madawa ya kulevya, si ajabu amejiovadozi,” alisema Abdallah huku akihaha huku na kule kama kuku anayetaka kutaga. Damu nyingi ambazo tayari zilishakauka, zilikuwa zimemtoka msichana huyo na kutiririka kutoka pale kwenye mshipa wa mkono alipojidunga sindano, zikavujia kwenye shuka na kumwagika sakafuni.

    Ungeweza kudhani kuna mtu amechinjwa au kuchomwa kisu kwa jinsi damu hizo zilivyokuwa nyingi. Abdallah alijaribu kumgusa msichana huyo kifuani lakini hakuonesha dalili zozote za kutia matumaini.

    “Tuwape taarifa polisi,” alisema mhudumu huyo wa gesti, harakaharaka akakimbilia mapokezi na kuinua mkonga wa simu, muda mfupi baadaye akawa anazungumza na upande wa pili.

    “Jamani hali ni mbaya huko ndani, tumewapigia simu polisi wanakuja sasa hivi, Karen kajiovadozi,” alisema Abdallah akiwaambia wale ‘mateja’ waliomuelekeza gesti hiyo. Kusikia kwamba kuna polisi wanakuja, mateja hao walianza kutawanyika mmojammoja huku wakipeana pia taarifa na wenzao ambao bado walikuwa wakiendelea kujidunga pale kijiweni.

    Huku uso wake ukiwa umeshaanza kubadilika, macho yake yakiwa yameanza kuwa mekundu akiwa haamini kama kweli Karen atanusurika, Abdallah alijiinamia chini. Japokuwa alikuwa amemkosea sana, mazingira aliyomkuta nayo yalisababisha ile chuki kali aliyokuwa nayo ndani ya moyo wake iyeyuke mithili ya barafu iyeyukavyo juani.

    Muda mfupi baadaye, difenda ya polisi iliwasili kwenye nyumba hiyo, ikiwa na askari kadhaa wenye silaha ambao waliteremka na kuwakuta Abdallah, yule dereva Bajaj aliyempeleka na mhudumu wa gesti wakiwa bado hawaelewi nini cha kufanya.

    Baada ya mahojiano mafupi, askari hao waliongozana nao mpaka kwenye chumba alichokuwemo Karen ambapo wote walipigwa na butwaa kwa walichokiona. Askari mmoja aliyekuwa na kamera, alianza kupiga picha za ushahidi kisha mwingine aliyekuwa amevalia ‘gloves’ mikononi alimchomoa Karen bomba la sindano lililokuwa limenasa mkononi, akakusanya na vithibitisho vingine.

    “Nani ndugu yake hapa kati yenu,” askari mwingine aliyeonesha kuwa na mamlaka kuliko wenzake aliuliza.

    “Mimi hapa,” Abdallah alisema.

    “Una uhusiano gani naye?”

    “Ni mchumba wangu,” alijibu Abdallah, yule askari akaandika maelezo hayo kwenye faili alilokuwa amelishika, akamuuliza jina kamili la Karen ambapo alimjibu kila kitu, akahamia kwa mhudumu wa gesti hiyo ambapo naye alimuuliza maswali machache kisha akawaamuru wenzake kumbeba mpaka nje kwenye gari.

    “Atapona?” Abdallah aliuliza swali hilo huku akilengwalengwana machozi.

    “Mimi siyo daktari kijana ila tunaombea iwe hivyo, tukiwaambia msitumie madawa ya kulevya huwa tunawaepusha na kama haya yaliyomtokea mchumba wako,” alisema askari huyo akitembea kikakamavu kuwafuata askari wengine waliokuwa wamembeba Karen kwenye machela mwenyewe akiwa hajielewi kabisa.

    Walipotoka nje, Abdallah aliomba kuongozana nao kwenda hospitalini lakini wakamwambia kuwa hawezi kupanda kwenye difenda, labda akodi usafiri wake. Dereva wa Bajaj aliyekuja naye akamwambia waelekee kule walikokuwa wameacha Bajaj yao, difenda ilipoondoka tu, na wao walianza kukimbia kuifuata Bajaj yao na muda mfupi baadaye, waliianza safari.

    Njia nzima Abdallah alikuwa amejiinamia, machozi yakimtoka kama maji, hakutaka kuamini kwamba yule alikuwa ni Karen, mwanamke aliyetokea kumpenda kwa moyo wake wote.

    Hakuna aliyemsemesha mwenzake kwenye Bajaj, safari iliendelea huku dereva akijitahidi kuifukuza ile difenda ili isije ikawapotea, dakika kadhaa baadaye wakawasili kwenye Hospitali ya Mwananyamala.

    Gari likaenda moja kwa moja mpaka sehemu ya mapokezi ambapo wale askari waliteremka na kusaidiana kumshusha Karen aliyekuwa amelazwa kwenye machela, manesi kadhaa wakaja kuwapokea na kumkimbiza wodini ambako madaktari walianza kumfanyia uchunguzi kubaini kama bado alikuwa hai.

    Wale askari waliendelea kusubiri palepale mapokezi, huku yule mwingine akionekana kuendelea kuandika vitu kwenye faili jeusi. Muda mfupi baadaye, mlango wa wodi aliyokuwa ameingizwa Karen ulifunguliwa.

    Abdallah aliyekuwa amekaa pembeni ya mlango huo na yule dereva Bajaj, alikurupuka na kusimama, akamfuata daktari huku akiwa na shauku kubwa ya kutaka kusikia hali ya Karen.

    “Dokta mgonjwa wangu anaendeleaje?”

    “Kwani wewe ni nani yake?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mimi ni mchumba wake.”

    “Lakini mimi nimekabidhiwa na polisi hii kazi kwa hiyo ni lazima niwape wao majibu, samahani,” alisema daktari huyo hukuakiwapita akina Abdallah na kwenda mpaka pale wale askari walipokuwa wamesimama.

    Abdallah hakukubali kirahisi, naye alienda mpaka pale huku akiwa ametega masikio kutaka kusikia kilichotokea.

    “Ameshakata roho, tumemfanyia vipimo vyote lakini inavyoonesha, moyo wake ulisimama ghafla kufanya kazi baada ya kujiovadozi madawa ya kulevya.”

    “Whaaaat?” (Niniiii?) Abdallah alipiga kelele kwa sauti kubwa kiasi cha kufanya watu wote waliokuwa hospitalini hapo kugeuka kutaka kujua nini kimetokea. Kutokana na mshtuko alioupata, alidondoka chini kama mzigo, puuh! Akapoteza fahamu.

    Muda mfupi baadaye, mlango wa ile wodi aliyokuwa ameingizwa Karen ulifunguliwa, kitanda cha magurudumu kilichoonesha kuwa na mwili wa mtu juu yake, akiwa amefunikwa na shuka la rangi ya kijani, kilianza kusukumwa na manesi wawili.

    Manesi hao waliokuwa wamejifunga vitambaa usoni, waliendelea kukisukuma kufuata korido na mwisho wakaishia kwenye jengo kubwa lililokuwa na maandishi yaliyosomeka ‘Mochwari’, milango ikafunguliwa na manesi hao wakaingia kisha milango ikafungwa



    Baada ya kupoteza fahamu muda mfupi baada ya kushuhudia maiti ya Karen ikitolewa wodini na kupelekwa mochwari, Abdallah alikuja kuzinduka dakika kadhaa baadaye na kujikuta amelazwa kitandani huku dripu ikitiririka kwa kasi kuingia kwenye mishipa yake.

    “Nini kimetokea?” Abdallah alihoji huku akijaribu kuinuka lakini maumivu makali ya kichwa yakamrudisha chini, alipogeuza kichwa chake pembeni, alimuona yule dereva wa Bajaj akiwa amekaa na kujishika tama.

    “Pole broo,” alisema huku akiinuka pale alipokuwa amekaa.

    “Kwani nimepatwa na nini?”

    “Ulianguka na kupoteza fahamu pale nje.”

    “Karen yuko wapi? Anaendeleaje? Amepona?” Abdallah aliuliza maswali mfululizo yaliyokosa majibu, dereva yule wa Bajaj aliyeonekana kuwa muhimu sana kwake katika kipindi hicho cha matatizo, alishindwa cha kumjibu zaidi ya kuinamisha kichwa chake chini.

    Ni hapo ndipo alipokumbuka kilichokuwa kimetokea muda mfupi uliopita. Alikumbuka jinsi mlango wa wodi aliyokuwa amelazwa Karen ulivyofunguliwa, akawaona manesi waliokuwa wakiusukuma mwili wa Karen uliokuwa umefunikwa mashuka ya rangi ya kijani na kulazwa kwenye kitanda cha magurudumu.

    Kumbukumbu zake ziliishia hapo, akajikakamua na kukaa kitandani, akarudia tena kumuuliza yule dereva wa Bajaj kama alichokuwa amekiona muda mfupi kabla ya kupoteza fahamu kilikuwa ni kweli au alikuwa ndotoni.

    “Ni kweli Abdallah, ila piga moyo konde wewe ni mwanaume, isitoshe kila jambo huja kwa sababu maalum,” alisema dereva huyo wa Bajaj kwa sauti ya chini, Abdallah akashindwa kuzizuia hisia zake, akaanza kulia kwa uchungu huku akitaka kujichomoa ile dripu na kutoka nje kwenda kuhakikisha mwenyewe kama kweli Karen amekufa.

    Sauti ya kilio chake ndiyo iliyowashtua manesi waliokuwa chumba cha pili, harakaharaka wakakimbilia wodini na kumtuliza Abdallah, wakamwambia ni lazima alale kitandani mpaka ile dripu aliyokuwa ametundikiwa iishe.

    Alijilaza huku akiendelea kulia kwa uchungu, licha ya vituko vya kila aina alivyokuwa navyo Karen, moyo wake ulitokea kumpenda mno na kamwe hakutaka atokewe na jambo lolote baya.

    Alijilaumu sana kwa kitendo chake cha kumfukuza Karen nyumbani kwake kwani aliamini kama angeendelea kuwa chini ya usimamizi wake, asingeenda kujiovadozi madawa ya kulevya na kujikuta akifia gesti.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Dereva wa Bajaj ambaye alijitambulishakwake kwa jina la Jonas, aliendelea kumbembeleza huku akimtaka kujikaza katika kipindi hicho kigumu. Kumbukumbu juu ya msichana huyo mrembo, ziliendelea kupita ndani ya kichwa chake kama mkanda wa video.

    “Naomba umwambie nesi aje anitoe hii dripu,” alisema Abdallah huku akiendelea kulia, Jonas akawa hana namna zaidi ya kuwafuata manesi na kuwaeleza alichokuwa anakitaka Abdallah. Ilibidi manesi wakubaliane na wazo la Jonas hasa alipowaeleza kwamba yeye ndiye ndugu pekee wa marehemu hivyo alikuwa anahitaji kuanza maandalizi ya mazishi.

    Muda mfupi baadaye, manesi walifika kwenye wodi aliyokuwa amelazwa Abdallah na kumchomoa dripu, wakampa dawa za kunywa na kumruhusu kuendelea na shughuli zake huku wakimpa angalizo kwamba ajitahidi kushindana na msongo wa mawazo kwani unaweza kumsababishia matatizo makubwa zaidi.

    Baada ya kuruhusiwa kutoka wodini tu, breki ya kwanza ilikuwa mochwari akiwa ameongozana na Jonas. Akawaomba wahudumu wa chumba cha kuhifadhia maiti aende kuuona mwili wa mchumba wake. Kwa bahati nzuri aliruhusiwa kuingia na kupelekwa moja kwa moja kwenye jokofu alilokuwa amelazwa Karen.

    Alipofunguliwa jokofu na kuutazama mwili wa Karen uliokuwa umeshaanza kupoa kutokana na baridi iliyokuwemo ndani ya jokofu hilo, Abdallah alishindwa kuyazuia machozi yasiulowanishe uso wake.

    Akainama na kuubusu mwili wa Karen huku akiendelea kulia kwa uchungu. Kila kitu kilikuwa kimetokea kwa kasi kubwa kiasi kwamba kuna wakati alikuwa anahisi kama yupo ndotoni. Ilibidi wahudumu wa chumba cha kuhifadhia maiti wamtoe nje kwani alikuwa analia sana huku akionesha kutokuwa tayari kutoka na kuiacha maiti ya Karen mle mochwari.

    “Broo kulia hakukusaidii chochote, hapa cha msingi ni kuwataarifu ndugu zake ili maandalizi ya mazishi yaanze kufanywa,” alisema Jonas huku akimpigapiga Abdallah mgongoni.

    Mtihani mwingine aliokuwa nao, ni kwamba hakuwa akimjua ndugu yeyote wa Karen kwani walikutana ‘kimjinimjini’ na kuanza kuishi pamoja. Kwa bahati nzuri, alikumbuka kwamba walipoingia kwenye chumba cha gesti na kumkuta Karen katika mazingira ya kukaribia kukata roho, alichukua simu yake.

    Harakaharaka akaanza kujipekua mwilini na kufanikiwa kuikuta simu hiyo, akajaribu kuiwasha lakini haikuwaka, akajua lazima itakuwa ni kwa sababu imeisha chaji. Akatafuta sehemu ya kuichaji hapohapo hospitalini ambapo aliisubiria mpaka iingie chaji. Aliamini kwa kupitia simu hiyo,anaweza kupata mawasiliano ya ndugu wa msichana huyo.

    “Wewe ndiyo Abdallah?” askari mmoja aliyekuwa amevalia nguo za kiraia, aliyekuwa miongoni mwa wale walioenda kumchukua Karen gesti, alimuuliza.

    “Ndiyo!”

    “Marehemu ni nani yako?”

    “Alikuwa ni mchumba wangu, tulikuwa kwenye taratibu za kufunga ndoa.”

    “Sasa kwa sababu kifo chake kina utata mkubwa, wewe ndiyo mtuhumiwa namba moja na utakuwa chini ya ulinzi ukiisaidia polisi mpaka ripoti ya daktari itakapotoka na kuonesha chanzo cha kifo chake,” alisema askari huyo huku akitoa pingu kiunoni.

    Abdallah alibaki amepigwa na butwaa, akiwa haamini alichokuwa anakisia kutoka kwa askari huyo. Machungu ya kumpoteza kipenzi chake bado yalikuwa hayajaisha, muda ambao alikuwa akijaribu kutafuta mawasiliano ya ndugu zake ili wakausitiri mwili wa msichana huyo, alijikuta akikumbana na kikwazo kingine.

    “Sasa afande, mimi ndiye niliyesaidia kutoa taarifa mpaka mkaja pale gesti, isitoshe usiku kucha hakuwa amelala nyumbani kwangu, unawezaje kuniambia mimi ndiyo mtuhumiwa namba moja na inabidi niwekwe chini ya ulinzi na kuisaidia polisi?”

    “Hayo mambo mengine utaenda kuyaeleza kituoni, ni lazima tufanye kazi yetu, twende,” alisema yule askari huku akimkokota Abdallah kuelekea kwenye difenda ya polisi akiwa amemfunga pingu, bila kujali kwamba muda mfupi uliopita alikuwa hoi wodini baada ya kuanguka na kupoteza fahamu.

    Ilibidi Jonas achukue ile simu na vitu vyake vingine, akawa anawafuata kwa lengo la kutaka kujua nini kitaendelea. Naye alijisikia vibaya sana ndani ya moyo wake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Muda mfupi baadaye, difenda aliyokuwa amepakizwa Abdallah iliwasili kwenye Kituo cha Polisi Kijitonyama, maarufu kama Mabatini ambapo aliteremshwa na pingu zake, akapelekwa mpaka kaunta na kufunguliwa pingu, akaamriwa kuvua viatu, mkanda na kukabidhi vitu vyote alivyokuwa navyo.

    “Naomba nipige simu kazini nimtaarifu bosi wangu kilichotokea,” alisema Abdallah, yule askari aliyekuwa amemsimamia akamruhusu ambapo alichukua simu yake na kupiga simu ofisini kwao na kumueleza bosi wake kwa kifupi kwamba yupo kituoni.

    Alipomaliza, alikabidhi vitu vyote, akaingizwa selo alikokutana na watu wengine wengi wakiwa wamejazana kwenye kichumba kidogo kilichokuwa na dirisha dogo upande wa juu. Akatafuta sehemu ya kukaa na kuegamia ukuta, mawazo mengi yakawa yanaendelea kupita ndani ya kichwa chake huku machozi yakiendelea kumtiririka.

    Muda ulikuwa ukienda taratibu sana kwa Abdallah, akawa hajui hatima yake itakuwa nini zaidi ya kusubiri miujiza. Kutoka ndani ya moyo wake alikuwa anajua hajashiriki kwa namna yoyote kusababisha kifo cha Karen, msichana aliyetokea kumpenda kwa moyo wake wote licha ya kasoro alizokuwa nazo.

    “Nilijitahidi kadiri ya uwezo wangu kumfanya aache kutumia madawa, Mungu shahidi yangu,” aliwaza Abdallah huku akiendelea kutokwa na machozi. Kila kitu kilikuwa kimetokea kwa kasi kubwa kiasi cha kumfanya muda mwingine ahisi kama yupo kwenye ndoto ya kutisha na muda si mrefu atazinduka lakini haikuwa hivyo.

    Hakuwahi kudhani ipo siku ataingizwa selo, tena akikabiliwa na mashtaka makubwa kama yaliyokuwa yanamkabili. Japokuwa alikuwa amemuasi Mungu wake kwa kipindi kirefu, siku hiyo alijikuta akimkumbuka na kuanza kumuomba kimoyomoyo amuoneshe muujiza.

    Kila alipokuwa akimkumbuka Karen, na yote waliyoyafanya pamoja kuanzia siku ya kwanza wanakutana, alikuwa akijisikia uchungu mkali sana ndani ya moyo wake. Alitamani siku zirudi nyuma ili aongeze juhudi za kumsaidia msichana huyo aondokane na tatizo la matumizi ya madawa ya kulevya ambalo ndilo lililoyagharimumaisha yake.

    Huku nyuma, baada ya Abdallah kuwekwa chini ya ulinzi, askari walizungumza na madaktari wa Hospitali ya Mwananyamala na kukubaliana kuufanyia uchunguzi wa kina mwili wa marehemu Karen (Post- Mortem) ili kuwa na uhakika juu ya kilichosababisha kifo hicho.

    Huo ulikuwa ndiyo utaratibu wa kawaida wa jeshi la polisi pamoja na madaktari wanapokuwa na shaka juu ya sababu za kifo cha mtu yeyote, ni lazima uchunguzi wa kina ufanyike.

    Muda mfupi baadaye, bosi wake pamoja na wafanyakazi kadhaa walifika kituoni hapo kwa lengo la kutaka kumuwekea dhamana lakini polisi wakakataa mpaka uchunguzi wa mwili wa marehemu ukamilike. Wakashindwa cha kufanya, ikabidi waondoke kusubiri huo uchunguzi ukamilike.

    Kila mtu akawa anamuonea huruma Abdallah kwa mkasa uliomkumba, huku wengine wakimlaumu kwa kitendo chake cha kuishi na mtu aliyekuwa akitumia madawa ya kulevya kwani yule dereva wa Bajaj aliwasimulia kila kitu kilichotokea.

    Hata hivyo, baada ya uchunguzi huo uliochukua saa kadhaa kukamilika, ilibainika kuwa ni kweli kilichoyakatisha maisha ya msichana huyo ilikuwa ni kujiovadozi madawa ya kulevya. Hatimaye Abdallah akaenda kutolewa selo akiwa ameshasota kwa zaidi ya saa saba.

    Alipotoka, tayari giza lilikuwa limeshaanza kuingia, akavaa viatu vyake na kuchukua vitu vyote muhimu alivyokuwa ameviacha pale kaunta, akatoka nje na kutafuta usafiri wa kumrudisha Hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya kwenda kufanya taratibu za kuuhifadhi mwili wa Karen katika hali nzuri wakati akianza kuwatafuta ndugu zake.

    Akatajiwa gharama za kuulaza mwili wa marehemu mochwari kwa siku moja ambapo aliandikishana na wahudumu wa nyumba hiyo ya kuhifadhia maiti. Baada ya hapo, alimpigia simu dereva wake wa Bajaj, Jonas na kumueleza kuwa tayari ameshaachiliwa huru.

    Alipiga pia simu kwa bosi wake na kumpa taarifa kwamba ameshatoka. Kutokana na uzito wa suala hilo, aliona hakuna ujanja zaidi ya kuwashirikisha wazazi wake waliokuwa wakifanya kazi mkoani, nao wakapigwa na butwaa kwa kilichotokea. Ikabidi baba yake afunge safari ya dharura usiku huohuo kwani alijua mwanaye hawezi kuwa na uwezo wa kushughulikia suala zito kama hilo.

    Abdallah naye baada ya kurejea nyumbani kwake na kuoga kuondoa nuksi za mahabusu na kubadilisha nguo, aliichukua ile simu ya Karen aliyoichukua kwenye chumba alichofia msichana huyo na kuichomeka tena kwenye chaji kisha akaiwasha.

    Akaanza kupekua namba zilizokuwa kwenye simu hiyo na kufanikiwa kupata namba ya bosiwa kwanza wa msichana huyo ambaye kwa mujibu wa maelezoaliyowahi kumpa siku za nyuma, ndiye aliyemchukua kutoka kijijini kwao miaka kadhaa iliyopita kwa makubaliano ya kuja kumsaidia kazi.

    “Samahani, najua mimi hunifahamu, naomba kukuuliza unamfahamu msichana mmoja anaitwa Karen, anasema amewahi kufanya kazi nyumbani kwako.”

    “Bila samahani, ndiyo namfahamu, vipi kwani.”

    “Unajua aliko kwa sasa?”

    “Hapana, mtoto ana mambo mengi sana huyo, kuna rafiki zangu wamewahi kuniambia kwamba siku hizi amekuwa changudoa.”

    “Basi kuna matatizo yametokea, nahitaji msaada wako, naomba nielekeze mahali popote ulipo mi nakuja sasa hivi.”

    “Vipi kwani? Mbona unanitisha?”

    “Nitakwambia tukionana, sasa hivi nakuja,” alisema Abdallah, yule mwanamke akamueleza sehemu ya kukutana naye huku naye akiingiwa na hofu kubwa ndani ya moyo wake.Baada ya dakika chache abdallah akawa amewasiri tayali eneo husika akamweleza A_Z ya kila jambo lililotokea hadi alipokwenda sero kwaajiri ya karen.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakafanya mawasiliano na ndugu zake karen japokuwa uliibuka mtafaruko mkubwa sana baina ya ndugu zake na karen,mwisho wa siku walikubaliana na matokea huku abdallah wakimuona kama mwanaume shujaa na mwenye mapenzi ya dhati kwa mtoto wao.taratibu za kusafirisha maiti zikafanyika huku abdallah akiwa haamini hata kidogo juu ya kile kilichotokea kwa mpenzi aliempenda kwa dhati,aliyasahau yote aliyofanyia na binti huyo huku akijihisi kama yupo kwenye ndoto tu akitengemea ya kuwa ataamka na kusahau yotee yaliyotokea kumbe haikuwa ndoto kila kitu kilikuwa LIVE.

    Baada ya kila kitu kumalizika abdallah aliomba ruksa kazini na boss wake bila hiyani alimpatia likizo ya mwenzi mmja ili akapumzishe hakili yake kwani yaliyomtokea kijana yule yalikuwa ni zaidi ya maumivu.

    Baada ya likizo kuisha abdallah mpya kabisaa akarejea upya kabisaa na kazi zikaendelea hukuakiwa hamwamini hata mwanamke katika ulimwengu huu aliona kila mwanamke ni karen na aliapa ya kuwa hata kuja tena kumwamini mwanamke yoyote duniani .



    MWISHO



    ...

0 comments:

Post a Comment

Blog