Search This Blog

Saturday, July 16, 2022

MSICHANA WANGU WA KWANZA - 3

 







    Simulizi : Msichana Wangu Wa Kwanza

    Sehemu Ya Tatu (3)



    " Ujio huu ni kwa ajili yako tunda na asali wa moyo wangu." Aliongea Zulfa na wote wakakaribiana kisha wakapeana salamu na Samir akaingia ndani, alipotoka akatoka na stuli. Kisha akampa Zulfa kwa ajili ya kukalia.



    "Nimekaa nyumbni toka jana naangalia filamu lakini hazinisaidi, na skiliza redio lakini nayopia hairejeshi furaha yangu. Nimekuwa mpweke utadhani mgonjwa. Nimeshindwa kuvumilia kuteseka kwa ajili yako mpenzi ilhali nawe upo. Ndomaana nimeamua kuja moja kwa moja hadi kwenu. Samahani kwa kuingia ukweni bila ridhaa yako, lakini mwenzio nimeshindwa kuvumilia my love." Aliongea Zulfa na kumfanya Samir, amuhurumie sana.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Pole sana mpenzi, najua kiasi gani hupendi niwe mbali nawe. Mioyo yetu ni kama sumaku, tukiwa mbali inavuta na kuhitaji tuwe karibu. Ujiskiavyo mpenzi wangu juu yangu. Ndivyo hata mie ninavyojiskia kwa ajili yako.



    Nakupenda sana mpenzi wangu. Hata hapa ninafua nguo lakini akili haipo kwenye sabuni bali akili yangu yote ipo kwako." Aliongea Samir.



    "Baby.. Mbna unafua nguo zote hizo?"



    "Mpenzi, mwenzio nasafari kesho kutwa na haya ni maandalizi ya safari hiyo. Mjomba ameniita niende nikamsaidie kazi mpaka hapo matokeo yatakapo toka." Aliongea Samir.



    "ha!, kumbe unaondoka?, unaniacha sio?, why?. Nimekukosea nini Samir. Kwanini unataka kuondoka kipindi ambacho ndokwanza nahitaji uwepo wako mpenzi wangu. Natambua umuhimu wa mjomba, lakini! Mbna mapema sana. Sihtaji kuwa mbali nawe kwa muda huo, tafadhali usiniumize mpenzi wangu." Aliongea Zulfa na majimaji yakaanza kumtoka ndani ya macho yake, alishndwa kuvumilia. Ndipo alipochukua leso yake na kutaka kujifuta machozi, ile anataka kujifuta Samir alikiwahi kitamba kile na kumnyanganya kisha akaamua kumfuta machozi yake kwa kutumia mkono wake wa kuume.



    Hakika yalikuwa ni majonzi kwa wote wawili. Zulfa alilia na Samir aliangua machozi pia..



    "Mpenzi wangu, nikweli inauma lakini sina jinsi, inabidi nikubaliane na kauli ya mjomba maana tayari amesha nipa hadi nauli." Aliongea Samir.



    "Samir, we unadhani nini maana ya uwepo wangu kama wewe haupo mpenzi. Niliugua kwa ajili yako na kuletwa nyumbani, eti leo ndo kwanza penzi linaanza halafu unataka uniache. Fikiria, mimi sjaenda shule mpaka sasa kwa ajili yako, nakuomba usiue furaha yangu na kuzaa maumivu mpenzi.



    Mjomba ni muhimu kwenda kumsaidia kazi lakini mimi mpenzi wako sihtaji uöndoke kwa muda huu mpenzi." Aliongea Zulfa huku kwa muda huo akiwa amejiinamia ilikuficha macho yake ambayo tayari yalikwisha kuwa mekundu kwa sababu ya kulia.



    Aliendelea kumwaga machozi bila hata kuongea. Walikuwa kimya kwa muda wa dakika kama tano hivi pasina kusemeshana.



    "Zuuu,," Aliita samir kwa kifupi.



    "Usiniite. We si hutaki kuniskia mimi mpenzi wako! Niache niendlee kuumia." Aliongea Zulfa kwa sauti ya hasira.



    Samir alionesha sura ya unyonge. Alibaki shindwa amukhalifu mjomba wake au mpenzi wake, alikunja ngumi na kuanza kuigongesha mara kadhaa kwenye paji la uso wake, alipochoka aliuruhusu mkono wake kuanza kutalii katika kichwa chake huku akiziadhibu nywele zake kwa kuzihamisha makao, mara azilaze mara aziinue. Alikuna kichwa mpaka akajikuta akianza kupata michubuko kichwani kutokana na kucha ndefu alizokuwa nazo, pamoja na kufanya yote hayo lakini hakuweza kupata jibu la kumjibu mpenzi wake Zulfa.



    "Zulfa mbona unanipa mtihani mpenzi wangu. Tafadhali usiende mbali. Haya nimaneno tu yakuongea na yaishe mpenzi.



    Hapa chamsingi tujadili niende lakini niwahi kurudi na si unikatalie kabisa." zulfa, hakuwa mwenye kuskiliza maneno ya Samir, zaidi hakutaka tena kukaa maeneo yale. Taratibu bila hata kuaga alianza kuondoka. Huku nyuma Samir alibaki kuita na asipate jibu, hakuwa na jinsi zaidi ya kuinua mikono yake yote kwapamoja na kuikutanisha kichwani.



    Mawazo yakamjaa kwa muda mfupi, ghafla akawa kama mtu alieshindwa kuzitumia akili zake. Alichukua ndoo yenye povu na kujimwagia mwilini mwake bila hata kufikiria.



    Hakuishia hapo, aliingia ndani na bila hiyari yake alijikuta akichukua kiberiti na mafuta ya taa, moja kwa moja hadi kwenye nguo zake zote alizotaka kuzifua, akazitia moto bila hata kuwazia gharama alizotumia kununulia nguo zile.



    Wakati anafanya yote hayo, hakuwa katika akili yake ya kawaida kwani angekuwa katika hali yake ya kawaida ni wazi kuwa asingefanya hvyo.



    "Zulfa wewe ndo sababu ya mimi kufanya hivi. Njoo uchukue majivu ya nguo zangu iliuridhike. Nakupenda Zulfa. Sihitaji kukufanya ukasirike.



    Huwezi kuteseka mbele ya macho yangu, yeyote atakae diriki kukufanya ulie machozi ya maji basi mie nitamfanya atoe machozi ya damu.



    Zulfa umekasirika kisa mimi kufua nguo za safari, nimeamua kuzichoma moto ikiwa ni adhabu ninayotakiwa ni ipate kwa kukufanya ulie. Popote ulipo naomba usichukie uwepo wako kwangu, endelea kuchunga pendo langu, staki unidadisi. Nahtajiwa na mjomba hivyo lazma niende.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Najua nitakuacha na majonzi lakini sinabudi na endapo utadondosha chozi kwa ajili yangu basi majivu ya nguo hizi yatakufuta na kukufanya ujue jinsi gani ninatumikia adhabu ya kukuliza. Nakupenda sana Zulfa." Yalimtoka maneno yale Samir huku akiwa ameinama na kushka jivu la nguo alizozichoma.



    Ndugu msomaji, upande mwingne waweza muona samir ni mwenye makosa, lakini unapaswa utambue kuwa Moyo ukipenda, huweza kula hata nyama mbichi. Maskini Samir hana nguo za kuvaa, kila akiangalia jivu la nguo zake anakosa la kufanya. Hakuwa na jinsi zaidi ya kuchukua mfuko na kuweka jivu lile ndani yake kisha akaandika barua na kuiambatanisha ndani ya mfuko ule.



    Ilipofika jioni, alikutana na rafiki yake Nurdin kisha wakaongea mengi sana yaliyowaumiza mioyo yao.



    Kwakuwa urafiki wao ni wa damu, Nurdin hakuweza kukubali rafiki yake akose nguo, ndipo alipoamua kumpatia viji nguo vichache kwa ajili ya kujistiri lakini pia hakusita kumpatia ilani rafiki yake kuhusiana na jambo lile.



    Samir alimpatia rafiki yake mfuko ule wenye majivu pamoja na barua kisha wakaagana na rafiki yake. Lakini alimsihi ahakikishe anafikisha mzigo ule kwa Zulfa.



    Siku ile ilipita na hatimae siku ya kuondoka Samir iliwadia. Samir hakutaka kwenda kumuaga wala kuonana na Zulfa kwani alijua angeishia kujiumiza tu.



    Hatimae Samir aliondoka na kwenda kwa mjomba wake kwa ajili ya kumsaidia kazi. Hata alipofika kule alipokelewa kwa furaha. Alipewa fursa ya kwenda kuoga ilikuondoa uchovu wa safari, sasa ulikuwa ni wasaa wa yeye kukiendea chakula kilichokuwa kimeandaliwa kwa ajili yake akiwa kama mgeni.



    Wali na samaki alieungwa kwa nyanya kitunguu pamoja na chumvi kiasi iliyowekwa kwa ajili ya kusapoti ladha kati ya chakula. Ni chakula alichokipenda sana hvyo alikula kwa furaha sana.



    "Karibu sana mjomba, naona umekuwa bwana. Eeeh! Skuhizi hadi kakifua kameanza kukufukuzia. Umekua mpwa wangu" Ni maneno ya Mjomba wake na Samir. Maneno ya ukaribisho.



    . "Anco na wewe kwa kejeli, unaongoza. Yaani nimekonda hivi, kakifua kenyewe kametumbukia ndani utadhani baba ubaya halafu wewe unasema nimetanuka kifua. Ah, anco acha utani wako." Alilalamika Samir, kwa kufuatia kauli ya mjomba wake. Alikula hatimae sasa akamaliza.



    Mjomba wake alirejea kazini baada ya kumaliza kula, mke wa mjomba wake alitoka nje na kuanza kazi yake ya kutupia chanuo kwenye vichwa vya wadada wenzie kisha kuzifunga nywele kwa staili ya kamba kamba, kazi hiyo huitwa Ususi.



    Naam, Mke wa mjomba wake Samir, almaarufu kwa jina la Mama ...sudi, alikuwa ni fundi maridadi kwenye suala la ususi. Wanawake wa mitaa mbalimbali hawakuwa na kimbilio zaidi ya pale kwake kama wangetaka kupendeza. Mkono wake haukuwa mgumu hivyo hakuwa mwenye kutumia muda mwingi kwenye Usukaji wa vichwa na hiyo pia ni sababu nyingne iliyopelekea Mama ...sudi apendwe sana.

    Upande wa Samir, yeye aliachwa ndani peke yake akiangalia televisheni. Kwa kuwa ugonjwa wake mkubwa ni muvi, basi niwazi kuwa pele walikuwa wamemfikisha. Alitazama cd baada ya cd. Mpaka kichwa sasa kilichoka na kujikuta akifuatwa na usingizi, hakuwa na chakufanya zaidi ya kupozi muvi iliyokuwa ikiendelea na moja kwa moja akasinzia kwenye makochi.



    Baada ya muda kama wa saa moja hivi kupita toka Samir apitiwe na usingizi. Aliingia kijana mmoja mwenye umri kama wake, kijana huyo alionekana kuvaa suruali iliyombana mpaka kumpelekea sasa kucholeka maungo yake, shati iliyonakshiwa kwa manukato huku ikiwa nayo pia imembana vilivyo na kumchora maungo yake kitendo kipelekeacho aonekane na kifuachake chenye afya ya panzi. Kijana huyo kwa kumuangalia tu basi ungebaini ucheshi alionao, alikuwa na muondoko wa aina yake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "haa! Samir!?. Umekuja!" Aliropoka kijana yule baada ya kumuona Samir kajilaza kwenye kochi. Usingizi mzito ulioambtana na mchoko wa safari, ndivyo haswa vilivyopelekea Samir asiisikie sauti ya kijana yule.



    Nae kijana hakuishia hapo alianza kumuamsha Samir kwa kumuita jina lake na asipate majibu ya kuamka kwake. Hakuishia hapo tu, sasa aliitupa mikono yake mwilini mwa samir na hapo sasa alianza kuutikisa mwili wa Samir mara kadhaa kwa kuuachia huku mtikiso ule akiuambatanisha na jina la samir.

    Juhudi zake zilizaa matunda na kumpelekea Samir kuamka, walipeana salamu kwa pamoja, na hiyo ni baada ya samir kumtambua kijana huyo kuwa aliitwa Masudi na ni mtoto wa mjomba wake.



    Masudi alienda kuchukua chakula huku Samir akichukua maji kwa ajili ya kunawa uso iliwaende kutalii.



    "hey, cousin. Just wait me over there. Am eating right nw." Aliöngea Sudi kwa lugha ya kighaibuni, ikiwa ni kumtaka binamu yake amsubiri mpaka atakapomaliza kula.



    "Ok, dont mind." Alikubali Sudi kwa lugha na kumtoa wasiwasi binamu yake kwa lugha ile ile.

    Alisubiri kama dakika saba hivi. Hatimae sasa Sudi alimaliza kula na kisha kutoa vyombo. Baada ya hapo wote kwa pamoja walitoka ndani na kwenda kumuaga Mama masudi, kisha wakaelekea matembezini.



    Wakiwa njiani walipiga stori mbili tatu ikiwa ni pamoja na kukumbushana mambo yao ya nyuma ambayo waliyoyafanya kwa pamoja.



    "Bina.. Samahani kidogo. Hivi una demu kweli?" Ni swali lililotoka kwa Sudi na kumpelekea Samir achanue tabasamu la mshangao, kisha alipotezea.



    "Hapana, sina dem. Kwanini umeniuliza hivyo?" Jibu lile liliamsha kicheko cha dharau kutoka kwa Sudi.



    "Sasa unaishije bila demu. Hata mimi nilijuatu, maana kwa maneno yako sikudhani kama unauwezo wa kumtokea du yoyote na akakukubali. Kiufupi huna swaga." Aliongea Sudi maneno yale yenye wingi wa dharau yaliyomchoma vilivyo Samir na kujutia jibu lake. Alishindwa kuongea na kubakia kutikisa mikono tu. Sudi aliendelea kuongea.



    "Skia, unajua hapa ulipo unaongea na Sudi a.k.a Sukari ya warembo kama wanijuavyo wanangu wa kitaa. Usijali, mbna utapata swaga. Huwezi kutembea na mimi bila kuwa na dem, afu mi siwezi kukuacha hivi hivi lazma nikutafutie demu.

    Waliongea mengi sana kwenye utalii wao na hatimae waliamua kurudi nyumbani kupumzika.

    * * * *



    Nurdin alimtafuta Zulfa siku hiyohiyo na kumpatia mfuko ule wenye majivu na barua. Hakumwambia lolote maana Samir alimdokeza kuhusu maudhui ya barua ile.

    Hata Zulfa alipomuuliza Nurdin kuhusu Samir, hakuna alichoambulia zaidi ya kuambiwa kuwa majibu yamo humo. Hatimae waliachana. Nurdin alienda kumtafuta kipenzi chake cha moyo, msichana ambae laiti kama ungemuongea vibaya mbele ya nurdin basi asingejutia kukutwanga ngumi. Alifika kwa kina sumayah, na kuanza kupiga mingo.



    Upande wa Zulfa yeye alikuwa na shauku ya kutaka kujua Zawadi gani aliyopewa na mpenzi wake Samir.

    Alienda ndani na kujifungia kwa furaha, huku shauku la kutaka kufungua mfuko ule, alitumia miköno yake kufungua.

    Tabasamu alilokuwa nalo lilimyeyuka ghafla na kumpelekea mshangao baada ya kugundua kuwa ndani ya fuko lile kulikuwa na kopo lenye majivu. Hasira zilimpanda ghafla baada ya kutoipenda zawadi ile. Alikutana na barua ambyo iliuumiza sana moyo wake.



    Vazi la hasira lilimvuka ghafla baada ya kuisoma barua ile, hakuwa na ghadhabu tena bali alidumbukia kwenye dimbwi la upweke na kujihisi ni kama alieachwa nyikani peke yake. Huzuni ilimjaa na hata kuulaumu uamuzi wake.



    "Kwanini?, hivi! Nimeshakosea kitu gani mi... Jamani. Mbna kila siku kilio na mimi. Hakuna siku hata moja ambyo nimeshawahi kufurahia penzini. Tafadhali samir, usiwe na roho ya aina hiyo." Nimaneno ya Zulfa aliyokuwa akiyatamka peke yake chumbani pindi tu alipomaliza kusoma barua ile ya Samir.

    Hakuishia kulalamika tu, sasa alijizoa kwenye kiti alichokuwa amekalia na moja kwa moja akajitupa kitandani na kuanza kujitandaza kila upande wa kitanda huku akijikunyata kila sekunde na asiweke makao maalumu kwenye kitanda hicho. Shuka lilishindwa kukabiliana na mwili ule wa Zulfa ambao ulikuwa ukilitambia vilivyo, na palepale likaanza kujitandua taratibu.

    Zulfa, aliangua kilio cha nguvu ilikudhihirisha maumivu aliyonayo, lakini hakuna aliemsikia maana chumba chake kilipambwa na silingibodi zilizozuia sauti kutoka nje, huku.

    Machozi, yalimtoka mpaka yakamkauka lakini aliendelea kulia na kujibaragua kitandani pale.

    Hata barua aliyokuwa ameishikiria mkono wake wa kushoto, sasa ilimponyoka na kuanguka chini.



    Baada ya muda kidogo, aliamua kushuka chini na kuiokota barua ile, ili arudie tena kuisoma. Alishindwa kuikamata mara kadhaa kutokana na kitete alichokuwa nacho kwenye mikono yake. Hatimae alifanikisha kuiokota barua ile kisha kuisoma tena kwa mara nyingine iliajiridhishe na asijutie machozi yake.

    Barua yenyewe ilisomeka hivi:

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mpendwa, Zulfa.



    Salamu za haki ya Samir zipokelewe kwenye himaya ya Zulfa. Ama baada ya kupokea Salamu zangu, ningependa kujua kuwa bado umenihifadhi moyoni? Au najidanganya tu.



    Mpenzi, mtu asie na ulimi siku zote huwa hapatii lugha. Na mchungaji anaechinja mbuzi wa bwana yake machungani huyo hawezi kazi.



    Mpenzi, najua ghadhabu lilikutawala na ukasahau kuvumilia. Ukatumbua jipu la kauli kutoka kinywani mwako na kunipakaa majimaji yenye chembe chembe za damu chafu yenye harufu za hasira moyoni mwangu. Najua ulishindwa kukumbuka kuwa jipu huambukizwa ndio maana uliponichafua ukaniongezea na makohozi ya maumivu kisha ukaniacha ni ngali mchafu, nilibaki nikiita angalau urudi nikupe mfumo wa kunisafisha, lakini huku taka hata kusikiliza shida yangu, hatimae uliniacha nami nikadhulika na ule uambukizi wa jibu lenye hasira.



    Sikuthamini nguo tena, hapo nilijua nikuchoma tu, na wala nisijutie kuzichoma na mpaka hivi sasa sina nguo.



    Mpenzi, ule msemo usemao kwamba, ukipenda boga penda na maua yake. Wewe huku wahi kuusikia? Sasa mbona unamshusha kaka wa mama yangu ambae ni shemeji wa baba yangu tena mbele ya upeo wa wacho yangu na ngoma za masikio yangu.



    Najua utanichukia kwa kukhalifu amri yako na kwenda kwa mjomba. Lakini tambua huko ndiko chimbuko la penzi letu lilipo.



    Mpenzi, sababu kubwa ilonifanya nizichome nguo zangu ni furaha yako mpenzi.



    Niliwaza ni vipi nitafuta chozi lako ndipo nilipogundua kuwa nguo zangu ni sababu kubwa ya wewe kutoa chozi. Kwa kuwa sipendi uumie mbele yangu na nilisha apa, atakaekuumiza basi atagharamikia adhabu nitayomteulia hata kama haipendi. Basi mimi nami skuwa na budi kujipa adhabu hiyo ya kuchoma nguo.



    Tafadhali, pokea jivu la nguo zangu na unapaswa ujue hadi dakika hii mimi sipo mahali hapo, nipo kwa mjomba nimeenda kumsaidia kazi.



    Wako akupendae kwa dhati. SAMIR.



    Baada ya kuirudia mara ya pili, sasa tena hasira zilimrejea.



    "Samir, kweli umeniacha tena bila kuniaga. Nimekukosea nini mimi. Kama ulikuwa hunipendi ni bora ungenambia Samir, kuliko kunibebesha mzigo ambao siwezi hata kuutua.

    Samir, umeshusha heshma ya mapenzi mbele yangu, naskitika kung'ang'aniza mapenzi.

    Nakuapia mbele ya majivu yako kuwa, sito kaa na kuwaza kuwa na wewe tena. Hakika umenifanyia udhalilishaji wa hali ya juu. Hhm.. Hmmh.. Zile ahadi za kutokuumizana, na yale maneno yako matamu ndivyo vinavyoshawishi machozi yangu.

    Najuta kukufahamu, Samir, nakupenda sana lakini. Siwezi kustahmili msongo wa maumivu. Nitajaribu kukufuta japo ni ngumu sana...."



    Maskini Zulfa, alilalamika mpaka sauti ikagoma. Kila alipotoa neno kinywani, lilitoka kama hewa bila hata kusikika, palepale kichwa kilianza kumgonga utadhani kuna nyundo na msumari ndani yake, kifua nacho hakikukaa hivi hivi, nacho kilimbana mpaka akawa anataja jina la mama yake, lakini hakusikika kutokana na kukata kwa sauti. Mwili mzima ulipoteza nguvu na akabaki ameyatumbua macho yake na asiyafumbe.

    Hatimae sasa nuru ya macho ilianza kumuisha taratibu kope za macho yake zilianza kujifumba na asijitambue kabisa.



    Alibaki kwenye hali ile kwa muda wa kama nusu saa hivi. Mpaka hapo mama yake aliporudi na kukosa chakula kisha akaenda kumfokea mwanae Zulfa. Hapo ndipo Mama yake alipomkuta mwanae kajilaza. Alimuita mara kadhaa bila mafanikio, ndipo akaamua kumtikisa kwa kutumia mikono yake lakini Zulfa hakuamka.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Ni kwamba, baada ya Zulfa kusoma barua ya mpenzi wake Samir. Hapohapo alianguka chini na kuzimia, alipelekwa hosipitali na kuanza kutibiwa. Upande wa Nurdini nae, mambo yalienda kombo kwani huko nako alikosana na mpenzi wake mpendwa, jambo lililompelekea ashindwe kula na kukondeana tu. Samir, anaendelea kukumbana na vishawishi vya binamu wake anaejiita sukari ya warembo.



     Akiwa njiani, nafsi ilikuwa ikimsuta huku ikibainisha msimamo wake wa wazi kuwa haitaji kuongea na kuonana na Nurdin. Lakini ilishindikana maana Nurdin sasa nikama aliingia mawazoni mwake. Kila akifikiria jambo lazma ligote kwa Nurdin.



    Wanaseama, Moyo ukiamua jambo huwa haujali vikwazo wala matatizo unayokumbana nayo, bali hupenda utakalo liwe. Kwa ubinafsi wa Moyo ni vigumu sana kusimamia maamuzi yake mbele ya nafsi. Huyu nafsi, huwa ni mwenye kupeleka tamaa, mwenye kukinai, na mengineyo. Hivyo moyo hurubuniwa na kujikuta unafanya majukumu ya nafsi.



    Kitu pekee kilichobaki kwa ajili ya kumuongoza mtu ni hisia pekee. Moyo unaopenda bila hisia huo ni vyepesi sana kushambuliwa na matamanio ya nafsi, endapo mtu atazitumia hisia zake basi anauwezo wa kupambana na maelfu ya watu kisa mapenzi na asijutie kwa hilo. Wazee wazamani walishindwa kuelewa muongozo wa moyo kupitia usukani wa hisia, ndipo waliposema kuwa. Kipendacho Moyo, hula nyama mbichi.



    Naam, nadhani wote tunasadiki jambo hilo. Sasa Sumayah, amejivuta hadi kwenye ngome ya kina Nurdin. Anafika, anasalimia, kisha anaulizia, sasa anaoneshwa. Nae, moja kwa moja anaingia kwa mara ya kwanza kwenye chumba cha Nurdin. Anapiga hodi, ilikumfanya alie ndani ajiandae kumpokea na sio kumshtukiza. Ingawa pia anaweza.



    Anakaribishwa hadi ndani, anatazama chumba cha Nurdini na kumuona kijana aliekonda utadhani ni muathirika wa ugonjwa wa ukimwi. Hali ile inamuogopesha sana. Hakuishia hapo ndipo alipotupa jicho lake upande wa pembeni mwa kitanda hicho na kuiona meza iliyojaa kila aina ya dawa. Mwili ulimsisimka na asijue kijana yule aliekuwa amejilaza pale ninani.



    "Samahani kaka. Namuulizia mkaka mmoja hivi anaitwa Nurdin. Nimeambiwa yupo ndani ya chumba hiki. Je, nimemkuta? Au ametoka." Sauti ya Swali lile kutoka kwa Sumayah, liliweza kumuingia vilivyo Nurdin ambae hakuwa na Uwezo hata wa kuinua sauti yake na kujibu. Alijigeuza kutoka ubavu wa kushoto na kuulalia wa kulia iliaweze kuonekana mbele ya Sumayah.



    Sura yake ilikuwa imesinyaa, huku macho yake yakiwa kama yameingia ndani. Alama za michirizi ya machozi ndizo zilizo pelekea atambulike kuwa alilia sana.



    Kwa haraka haraka, Sumayah, hakuweza kumtambua Nurdin vizur. Alihisi huenda ni ndugu yake na si.. Yeye. Ila nikama sumaku iliyovuta moyo wake na kumpelekea aumie na kuhisi kabisa huyo ndie Nurdin wake.



    Sasa alimvagaa, na kumkumbatia huku akiwa amemuinua.



    "Upepatwa nanini. Jamani Nurdin wangu. Ona ulivyokonda, tazama mabega yalivyopanda juu utadhani yanang'ooka. Pole sana. Mbona hujapelekwa hospitali? Au pesa hakuna." Aliongea Sumayah, huku machozi ya kiendelea kuonesha ufahari wake kwa kumwagika.



    Hakuna jibu alilolipata kutoka kwa Nurdin, japo aliuliza swali. Si, kwa sababu Nurdin hataki kumjibu. Bali ni kwa sababu hawezi hata huko kuongea.



    Sumayah, alitoka nje na kwenda kuulizia kwanini mgonjwa haongei, na anaumwanini, toka lini. Ndipo alipoambiwa chanzo cha hali ile na sikwamba Nurdin hakupelekwa hospitali. Alipelekwa bali hakupata matibabu kutokana na kukosekana kwa ugonjwa, lakini daktari aliwaambia kuwa. Kuna jambo la siri, linalomtatiza huyu bwana na hilo jambo ndilo litalosaidia. Walisema pia. Mgonjwa kabla ya kukaa kimya alikuwa akitajataja jina la Sumayah. Wao, walijitahdi kumtafuta huyo Sumayah, lakini wasimpate. Na hiyo ikawa historia fupi ya mgonjwa.



    Sumayah, aliangua kilio baada ya kugundua kuwa yeye ndo chanzo cha Samir kuugua. Hakuwa na jinsi zaidi ya kuaga na kuondoka kisha akarudi nyumbani kwao. Alipofika tu. Alijitupia kitandani na kuanza kuyawazia yale aliyokumbana nayo huko kwa kina Nurdin.



    - - - - -



    Upande wa Zulfa yeye hali yake ilikuwa bado haijakaa sawa kivile. Lakini alikuwa tayari amekwisha zinduka. Pamoja na kuzinduka hali yake ilikuwa hairidhishi hata kidogo. Swala la yeye kurudi shule likawa limeshindikana na kuendelea kukaa hospitali pale.



    Alitamani sana angalau amuone Samir na kila alipomkumbuka aliishia kuzidiwa tu.



    Alijitahidi kumchukia Samir lakini aliishia kujiumbua kwa mapenzi aliyokuwa nayo kwa mpenzi wake.



    Mama yake muda wote alibakia akilia na kudhani huenda mwanae akawa analogwa, aliwaza kama itashindikana kwa hospitali basi atampeleka kwa mganga.



    - - - - -

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Nurdini, mpenzi wangu. Nakuomba unisamehe sana kwani sikujua kama yote haya yangetokea. Nia yangu ilikuwa nikuupima upendo ulonao kwangu na si, kukuumiza kama ulivyoumia leo. Nakuomba usiache kula mimi nipo kwa ajili yako, wala usiwe na mawazo kwani mimi nipo muondoa mawazo yako. Nakupenda sana na nimeamini kuwa unanipenda sana. Tafadhali nipo chini ya miguu yako mpenzi wangu." Ni kilio cha Sumayah alichokuwa akikitoa mbele ya mpenzi wake Nurdin, ambae kwa muda huo alikuwa amejilaza kwenye kitanda chake.



    Labda nikufahamishe kitu ndugu msomaji. Sumayah, alipofika kwao aliamua kurudi tena kwa kina Nurudin baada ya kushindwa na uvumilivu, hata baada ya kufika ndipo alipoamua kuomba msamaha.

    .. "Mpenzi naomba tanua mdomo wako iliniweze kukunywesha uji huu mpenzi wangu, tafadhali." Aliongea Sumayah, na Nurdin hakusita kutanua mdomo wake na kuruhusu kijiko kilicho jazwa uji kuingia kinywani.



    Nurdin alikuwa na siku tatu bila kula lakini siku hiyo alikunywa uji. Alipiga kijiko cha pili, cha tatu, cha nne, mdogo mdogo hadi ukaisha uji uliokuwemo kwenye kikombe kile. Kisha Sumayah akatoka nje na kwenda kuomba uji mwingine kwa Mama yake na Nurdin.



    "Haa!, unataka kunambia amekunywa huo uji wote yeye mwenyewe na ameumaliza!. Mtumee!!. Usinitanie. Kweli?" Ni maneno aliyotoa Mama Nurdin baada ya kupatiwa hali ya mgonjwa. Alipatwa na furaha kisha kwa bashasha akamuwekea uji mwingine Sumayah, na kumuomba akamnyweshe tena.



    "Usijali Mama. Hapa Nurdin lazma apone na kurejesha afya yake Mama angu."



    "Nashukuru sana mwanangu kwa msaada unipao. Hakika wewe ni mtoto mwema. Endelea kuwa na moyo huo huo Mungu ataendelea kukusaidia."



    "Kawaida mama. Nijukumu langu kumfanya yeye apone."



    waliongea mawili matatu kabla ya Sumayah, kwenda kumywesha uji Nurdin.



    Siku zilienda, siku zikapita. Hatimae sasa Nurdin hali yake ikaanza kurejea. Muda wote huo, alipata msaada mkubwa kutoka kwa Sumayah. Hatimae alipona kabisa na mapenzi yao yakaendelea.



    Upande wa Zulfa nae hali iliendelea kuwa vizuri, hatimae sauti ilirejea, na baada ya siku kupita sasa aliweza kutembea, na kufanya mambo mengine.



    Siku moja Zulfa alimfuata Nurdin dukani kwao na ilikuwa mshangao sana kwa Nurdin maana ni muda mrefu walikuwa hawajaonana.



    "Naona leo umeamua uje kututembelea. Karibu, jiskie upo kwenu." Aliongea Nurdin na kumkaribisha Zulfa, na hiyo ni baada ya kusalimiana na kujuliana hali.



    "Ahsante, Nurdin." Aliitikia Zulfa kwa sauti ya unyonge isiyo hata na chembe ya furaha.



    "Vipi, mbona leo upo mnyonge hivyo? Au umemkumbuka sana Samir" Alitania Nurdin kwa kutegemea Zulfa atatabasamu na kutengeneza furaha, lakini ndio kwanza zulfa alisonya na kutema mate chini.



    "Bora hata ningemkumbuka marehemu Babu kizaa babu yangu kwa wema alioutendea ukoo mpaka nikapatikana mimi. Kuliko kumkumbuka huyo, ambae hana heshima wala adabu, ana umiza watoto wa watu na kuwaachia tabu makwao.

    Labda ni kwambie kitu Nurdin, huyo rafiki yako simuhitaji na wala sihitaji kuiona sura yake machoni mwangu, sitaki wala kusikia sauti yake, hata harufu yake pia.



    Namchukia sana. Baada yakujua kuwa nampenda akaamua kunitesa. Ona nilivyokonda. Je, yeye amekonda kama mimi?



    Nimetundikwa madripu hosipitali kisa yeye, nimechelewa muhula wa masomo kisa yeye, tazama mwaka unakata hivi hivi. We unadhani mwakani nitapanda darasa wakati hata darasa nilopita sijalisoma.



    Kwenye pendo lake, mimi amenifanya mtumwa wa kumfanyia kazi ya kumpenda na yeye kunilipa furaha kisha ananitunukia tunzo za dhihaka.



    Najuta kumpenda, nazilaumu hisia zangu zilizong'ang'aniza pendo lililokuwa limefichwa na moyo wangu, na kulitoa nje.



    Nenda kamwambie rafiki yako kwamba simuhitaji tena." Ni maneno yenye ghadhabu na hasira za wazi. Yaliyomtoka Zulfa huku Nurdin akibaki kuyasikiliza na asijue atafanya nini. Hakuwa na kauli mdomoni, kila neno la utetezi alilotaka kulitoa ni kama lilienda na upepo na kushindwa kuyaruhusu mawimbi ya sauti kutoka kinywani.



    "Nurdin, hebu fikiria hata wewe, mtu unampenda, umemuomba asikuache kwa sababu za msingi, unajizuia mpaka kwenda shule kwa sababu yake harafu yeye anakuona wewe hauna maana. Eti, kisa ulishamwambia unampenda, eti kisa ulishalia kwa ajili yake, eti kisa, ulishashndwa kula kwa ajili yake. Dah!!CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Mama anajua nimerogwa na anahitaji kunipeleka kwa wataalamu kisa huyu Samir. Simuhitaji, mvulana gani asiependeka. Hebu fikiria toka aondoke mpaka leo ni muda gani? Sijapata salamu zake kutoka kwenye simu, wala kwenye barua.

    Hajui kama mimi ni mzima au mgönjwa, amekaa tu huko. Shem Nurdin inauma shemeji yangu." Aliendelea kulalamika kwa hisia kali mbele ya shemeji yake Nurdin. Hapo sasa akafungua kijibegi alichokuja nacho maeneo yale na kutoa yale majivu pamoja na ile barua kisha akamkabidhi Samir na kuaga iliaondoke.



    "Hapana shem Zulfa, usifanye hivyo. Ndio, nakubali Samir hajakutendea haki lakini nakataa uamuzi wako wa kuitafuta haki kwa kusababisha machafuko ya moyo.



    Anakupenda, anakujali, anakulinda, anakufikiria, na wewe ndio kila kitu kwake. Kwanza kabisa naomba nimuombee samahani kwa kosa alilokufanyia, pili naomba nimsaidie kukupa pole huku nikiambatanisha na pole yangu kwa maumivu uliyoyapata. Naomba kapumzike kwanza kisha unitafute baadae nami nitakuelewesha mambo yaliyotokea, usijali shem wangu. Samir anakupenda sana pengine kuliko wewe unavyofikiria." Aliongea Maneno yale Nurdin na kumuaga bila ya kumuongezea kitu chochote kile.



    Labda pengine Samir, hakuwa anajua athari ya maneno yale aliyoyatamka. Lakini ndugu msomaji, maneno kama hayo yanapotumika mahali kapa hapo, basi hujenga na siokubomoa..



    .. Zulfa, alijiondoa taratibu. Hapo sasa hasira zilianza kumshuka kutokana na maneno yenye busara kutoka kwa Nurdin. Alienda hadi kwao lakini tayari maneno ya nurdin yaliendelea kujirudia kichwani mwake.

    Aliyapa muda na kuanza kuyatafakari, ndipo alipoanza kujihukumu bila yeye kutaka. Moyo ulifikia maamuzi ya kutoa msamaha, lakini nafsi yake ilibaki na kinyongo huku roho ya kisasi cha maumivu ikiendelea kumjaa. Kila alipokumbuka matendo ya Samir mbele yake, aliishia kuchukia tu na kukubaliana na nafsi yake. Lakini pia kila alipokuwa akikumbuka maneno ya hekima kutoka kwa shemeji yake Nurdin, Moyo wake ulikuwa mkunjufu na kuhitaji kutoa msamaha. Ila tatizo lilibaki kwenye roho;roho ambayo muda wote ilikuwa inauchungu kwa yaliyotokea na wazo kuu ilikuwa ni kulipiza kisasi cha maumivu.



    "Nurdin, amesema kweli, maana hata Samir alishanitamkia wazi kuwa ananipenda na kunijali. Lakini!! Mbona maneno yake hayaendani na vitendo vyake?, ahnh, hapa nitakuwa nachezewa mchezo wa kuigiza.



    Inabidi niwe mjanja na nisijitie kimbelembele kumuamini mmoja kati yao. Najua samir hataaniumize vipi, lazma tu, atanambia kuwa ananipenda, na hata huyu Nurdin, yeye hata anihurumie vipi. Lazma tu, atamtetea rafiki yake. Hawezi taka niachane nae japo nimekuwa tajiri wa maumivu na hilo analijua.



    Sikubali. Lazma nicheze mchezo wa mapenzi. Ndio, huu ninaoenda kuucheza, ni mchezo wamapenzi. Endapo nitaumia Mungu ndie anajua na endapo nitaumiza Mungu ndie anajua pia. Lakini siri itabaki palegale. Na endapo nitashindwa kwenye mchezo huu. Basi sitojitia ukiherehere na kuhitaji tena kuucheza bali nitatulia na kumkatisha tamaa mpinzani wangu.



    Ee, Mwenyezi-Mungu. Naomba unipatie Moyo wa kishujaa, na uniondolee Moyo wenye unyonge. Nipe uwezo wa kustahimili maumivu ya aina yeyote ile, hakika wewe ndio muweza wa yote... AAMIN." Ni maneno aliyoyaongea Zulfa, huku akiwa peke yake chumbani mwake, juu ya kitanda ambacho kimetandikwa na shuka lililotengenezwa kwa maua, huku upande wa kichwa chake kukiwa na mto, kwa ajili ya kumuondolea kero za hapa na pale.



    Hakuishia hapo tu, sasa alitangaza chanzo cha mchezo huo, peke yake chumbani mwake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    " Siku zimezoeleka na hutumiwa kila juma, mara nyingi siku huwa zimegawanyika katika makundi mawili au zaidi.



    Siku hii ninayoipanga ndio siku ya mchezo wenyewe. Na ndio siku ambayo itatengeneza vidonda ndani ya mioyo yetu. Vidonda ambavyo, havitofutika mpaka mwisho wa pumzi zetu.



    Mimi ninachofanya, ni kumuhitaji arudi siku hiyo. Akifanikisha kurudi na nikamuona machoni mwangu, basi nitampenda na hata kwenda kujiroga kwa ajili yake. Lakini ikifika siku hiyo bila yeye kuja, basi ninamuacha papo hapo na wala sitojutia uamuzi wangu hata kidogo. Sihitaji kuwa msafiri ndani ya basi bovu hata siku moja. Na siku yenyewe ni tarehe ya kwanza baada ya kubandikwa matokeo yao.



    Mungu niongoze." Hakika Zulfa, ni msichana mwenye maamuzi magumu sana. Mchezo anaoucheza ni wa hatari na hana uhakika kama ambae anacheza nae amejiandaa au atauafiki mchezo ule. Yeye anachojua ni kuucheza hivyohivyo.

    * * *



    Taarifa za malalamiko ya Zulfa ziliweza kumfikia Samir, kupitia rafiki yake Nurdin.



    " Yaani tena, Zulfa amekasirika ile mbaya. Mwanzoni alikuwa hahitaji hata kukuona, lakini kwa sasa afadhali kidogo na hiyo ni baada ya mimi kuwa nimemshawishi kwa maneno kuntu." Ni sauti ya Nurdin ambayo ilisikika upande wa pili ambapo ndipo alipo Samir, kutoka kwenye simu ya Samir.



    "Dah! Nashukuru sana mkali wangu kwa kunilindia penzi langu. Afu kumbe dogo hana masihara!! Umesema alikuwa amelazwa kisa mimi. Dah! Hapa unaweza kukutana na kesi hivi hivi kumbe." Ni sauti ya Samir ambyo ilitoka kwenye simu yake hadi kwenye simu ya Nurdin, kisha ikapokelewa na Nurdin.



    "eeh, mi... Si,nakuchana. Angalia usije ukaua mtoto wa watu hivi hivi." Aliongea Nurdin.



    "Lakini mwanangu, baada ya mishe hiyo kuwaimeisha. Si akanifata tena Zulfa!"



    "enhee, baada ya kukufata?"



    "hee, ametoa kauli nzito mpaka nashindwa kukuambia mkali wangu."



    "acha mambo yako, wewe nipe mchongo."



    "Aliponifata akasema: anakupa taarifa, siku ya kwanza baada ya matokeo yenu kutoka, inabidi uwepo hapa. Ukijifanya kubaki yeye atajua umempuuza na haumpendi, hivyo hatoendelea kujipendekeza kwa ajili yako. Atakuacha hapohapo, ule taimu na yeye achukue taimu. Kwahiyo, mwanangu jitahidi ufanye michakato ya kurudi. Usije ukamuua bure mtoto wa watu."



    "Dah! Mimi kuja huko mbona inakuwa ngumu sana. Mjomba amesema nisubirie matokeo yatoke yakitoka freshi basi anifanyie maandalizi yote ya skuli huku huku. Na baada ya maandalizi kuisha ndio nigeuze na sio nigeuze tu, bila hata mishe....."



    "hallo.., hallo..., hallo... Mbona huongei. Oh, shit, kumbe simuimekata?" Aliongea Nurdin baada ya kuona ukimya kwenye simu yake.



    Alijaribu tena kupiga kwa mara ya pili. Lakini aliambiwa kuwa mteja anaempigia hapatikane, na akaombwa ajaribu tena badae.



    Moja kwa moja alijua hilo litakuwa ni tatizo la betri..



     Ni kweli, simu ya Samir ilikata kutokana na ubovu wa betri;betri ambalo halikuweza kukabili utunzaji wa moto kwa muda wa dakika hata kumi na tano.



    Upande wa Samir, baada ya simu yake kukata hakuwa na jinsi zaidi ya kumuomba binamu yake simu na kumpigia Nurdin kwa mara nyingine. Jambo hilo halikuwa tatizo maana Samir alikuwa na namba za rafiki yake kichwani.



    Alipiga na simu ikapokelewa kisha wakaendelea na maongezi yao waliyokuwa nayo.



    Samir alidai kwamba hawezi kuja kutokana na mambo ya kimsingi na mwisho wa siku rafiki yake Nurdin alichanganua sababu na kuona nijambo la kweli.



    Tatizo lilibaki kwa Zulfa ambae kwa muda huo, alikuwa tayari ameshatoa maamuzi yake na wala hakuhtaji ushauri.



    "Nimeshaongea nimemaliza. Yeye kama haji, ndohvyo asihesabu kama anampenzi wake anaitwa Zulfa. Staki mjadala zaidi."



    "Tafadhali Zulfa, usiwe na maamuzi magum kiasi hicho. Fikiria kwanza jambo linalomsubirisha huko kisha umjaji na sio kumjaji bila kosa."

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Hapana, siwezi hata kidogo. Mimi najua Samir hanipendi na haya yote anafanya kama vijisababu tu. Sasa namimi sihitaji kung'ang'aniza mtu, siwezi. Yeye kama hatokuja basi aelewe kabisa hana mpenzi kama mimi."



    Ni maongezi kati ya Nurdin na Zulfa. Maongezi ambayo yalimalizika bila muafaka wowote. Mpaka wanaachana. Zulfa alibaki kuushikiria msimamo wake huku Nurdin akikosa la kuongea.



    Ulipofika usiku mida ya kulala, Simu ya Nurdin iliita na alipoitazama kwenye kioo alikutana na jina lililosomeka 'SAMIR', aliipokea na kuiweka sikioni.



    "Hello!" Ni sauti iliyotoka kwenye simu iliyopigwa na Samir. Kisha naye akaiitikia.



    Maongezi kati yao yalikuwa ni juu ya Zulfa. Walijadili jinsi ya kumfanya awaamini lakini kila njia waliyoitumia waliona kama haina msaada.



    Msimamo wa Samir ulibaki palepale huku pia msimamo wa Zulfa ukiwa pale pale. Kila Zulfa alipofatwa na kupewa ushauri, hakuwa mwenye kushaurika, hatimae waliamua wa muache tu.



    Siku zikaenda na hatakujirudia tena. Ulifika muda wa kutazama matokeo.



    Siku hiyo nyoyo za wanafunzi waliomaliza darasa la saba zilikuwa katika hali tofauti sana kwenye kituo cha kuangalizia matokeo. Kuna wanafunzi ambao nyuso zao zilipambwa kwa furaha, hawa ni wale ambao walichaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari, vile vile kuna wanafunzi ambao nyuso zao zilipambwa na huzuni huku wengine matumbo yakisokota kwa uoga wa hali ya juu, huku kwa kuwaona wenzao ambao wameyapokea matokeo yao vibaya.



    Si, wanafunzi pekee, waliokuwapo katika kituo hicho. Bali hata wazazi, walezi, ndugu, jamaa na hata marafiki walikuwapo maeneo yale ilikuhakikisha hawasimuliwi matokeo ya fulani.

    Zulfa nae hakuwa mbali, na yeye ndie wa kwanza kuliona jina la Samir. Alifurahi sana baada ya kugundua kuwa mpenzi wake amefaulu, si.. Yeye tu, hata Nurdin alikuwa ni mwingi wa furaha baada ya kung'amua hilo.

    Samir, alipewa taarifa na mjomba wake kuwa, matokeo yametoka na yeye amechaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari. Samir, alifurahi pia, na hata kumshukuru Mungu kwakuwa aliamini kuwa ni yeye pekee aliemfanya afaulu.



    Siku hiyo Samir, alishinda bila furaha na hiyo ni baada ya kukumbuka matakwa ya Zulfa. Japo alikuwa na furaha ya kufaulu, lakini sasa alianza kuchukia hata ujio wa matokeo menyewe.



    Hatimae siku ya kwanza ikapita baada ya matokeo. Ndipo Zulfa alipojifungia chumbani na kujiapisha kwamba hatokuwa tena na Samir ndani ya maisha yake. Kisha akajipa masharti magumu sana.



    Mchana wa siku hiyo ulikata hatimae giza liliivaa dunia kwa muda wa masaa kadha mpaka hapo palipo pambazuka. Kijua cha alfajiri kilikuwa kikiendelea kujichomoa. Samir, akiwa anatoka mazoezini, alikumbana na muito wa simu. Hata baada ya kuiangalia Simu ile alikutana na ujumbe mfupi wa kwenye simu. Aliamua kuufungua kwa ajili ya kuusoma. Ulikuwa ni ujumbe uliohusu mtengano wa kimapenzi kati yake yeye na mpenzi wake Zulfa, tena kwa maneno yaliyo jaa hisia kali.



    Maskini Samir, anampoteza ampendae kisa kusubiria mahtaji ya shule. Ilimuuma sana kwa kuwa hakuwa na haki ya kupinga matakwa ya mtu tena aliyoyaamua kwa moyo mmoja, ndipo alipoamua kupiga simu na kuhakiki, majibu aliyokutana nayo. Aliona ni bora hata barua ile.



    Hata alipojaribu kuomba msamaha kwa sababu madhubuti. Zulfa hakumuelewa hata kidogo. Mpenzi msomaji, laiti kama ungebahatika kumuona Zulfa kwa muda ule, basi ni dhahiri ungeshangaa sana.



    Samir, hakuwa na jinsi zaidi ya kuangusha machozi na kisha kujifuta kwa kutumia nguo yake aliyokuwa ameivaa kwa muda ule.



    Hatimae sasa, alianza kukonda, hamu yakula alikosa. Alishindwa hata afanye nini kwani kila alipotazama huku na huko, hakuna msaada zaidi ya kuhisi dunia imemuelemea.



    Haya mapenzi bwana, dah!! Ama kwa hakika mapenzi yana uchawi. Yanaweza kukuloga na ukaumia, pia yanaweza kukufurahisha. Ndicho kilichomtokea Samir, ambae Sasa hapo alikuwa ni mwingi wa maumivu. Kwa muda huo, aliyachukia mapenzi na kuamini kuwa mapenzi ndio yaliyo msababishia kuwa katika hali ile.



    Upande wa Zulfa, yeye aliacha kumuwaza Samir, na kujikita kwenye masomo zaidi. Kila alipomkumbuka alitoka na kuliendea daftari au kwenda kufungulia muziki na kuanza kusikiliza. Alijiweka bize sana na kwa muda wa mwezi mmoja alifanikiwa kumfuta kabisa.



    Hatimae Samir, alikamilisha vifaa vya shule na moja kwa moja alirudi maeneo ya kwao ambapo alitoka kwa ajili ya kwenda kwa mjomba wake. Alipofika alienda kuripoti shulen4 na kuanza kusoma masomo yake ya sekondari, huku mawazo ya msichana Zulfa yakiwa yamemjaa. Zulfa kwa muda huo nae alikuwa shuleni kwa hiyo hawakuweza kuonana. Masomo kwa samir yalikuwa hali tete kutokana na mawazo aliyokuwa nayo. Alikuwa akiyachukia mapenzi na kuyahitaji muda huohuo, jambo lililopelekea ufaulu wake kuwa chini sana.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kama kawaida ya shule zote hapa Tanzania, huwa zinakuwa na likizo. Ulifika muda wa likizo na wanafunzi wote walifunga shule. Wenye kusomea shule za mbali walirudi makwao na wenye kusomea karibu nao tayari walikuwa makwao.



    Zulfa nae alirejea kutoka shuleni. Alikaa siku kama tatu hatimae waliweza kukutana yeye pamoja na Samir. Walisalimiana lakini Zulfa hakuonesha kabisa kumjali Samir.



    "Samahani, unanipotezea muda. Nikobize sawa?" Aliongea Zulfa baada ya kuona Samir anaendelea kujing'atang'ta mbele yake.



    Samir nae ni kama hakuwa anasikia alichoambiwa, badala amuache, yeye ndio kwanza aliongeza maneno yake.



    "Zulfa, yaani kiukweli mie siwezi kuishi bila wewe. Ni kama umeshika maisha yangu na wewe pekee ndio kiongozi wayo. Tafadhali Z.. Usinipatie hukumu kama hiyo, hukumu ambayo siwezi hata kuifanya. Nakuomba niko chini ya miguu yako, si, kwa ajili ya kukulowanisha miguu kwa machozi yangu. Bali ni kukuomba unisamehe. Najua kwa sasa moyo wako umejenga kisasi. Lakini fikiria mara mbilimbili, nitaishi vipi bila uwepo wako. Nakupenda, nakuthamini, na sihitaji hata kukukosa mpenzi wangu. Hebu kumbuka mangapi tul'o panga mimi na wewe. Sasa iweje leo uniache kisa kosa dogo kama hili ambalo hata halifikii robo ya ahadi yako. Naomba nipe adhabu nyingine lakini si.. Adhabu hii. Tazama mwenzio naporomoka kimasomo darasani, kisa wewe. Niangalie mwili ulivyodhoofika kwa mawazo ya kukuwazia. Nakuomba mpenzi wangu nihurumie, bila wewe siwezi kuishi. Kama kukuchukia nimeshajitahidi sana. Lakini naishia kukupenda tu, sijui hata nifanye nini. Kila nifanyalo haliwezekani, naomba basi niwe hata mtumwa wa penzi lako iliunisaidie mwenzio nateseka." Ni kauli zilizojaa uchungu na kiukweli hizo ndizo hisia za Samir. Hakuna aliloongeza wala kupunguza.



    Nikama alikuwa ameongeza ghadhabu la Zulfa, maana alifonzwa kwa dharau na kutolewa pembeni mwa miguu ya Zulfa ambyo alikuwa akiilowanisha kwa machozi yake, na kutupwa pembeni.



    " Muone kwanza na machozi yake ya kinafki. Sasa unamlilia nani hapa. Hivi umesahau kipindi ulichokuwa ukiniumiza na kunimwagisha machozi kama yako, kipindi ulichonifanya nisisome na hata kuugua kwa ajili yako. Unatambua ni majiraha kiasi gani uliyoniwekea moyoni. Eti, leo unakuja na kutaka kuyatonesha. Acha unafiki wewe. Ulinikimbia ukaenda sjui kwa mjomba wako na ukaniacha mie niendelee kutapatapa nikiwa peke yangu. We unadhani mimi niliwezaje kuishi bila wewe. Ishi kama nilivyoishi. Kumbuka Mtenda akitendewa hujiona kaonewa. Wewe ulitaka kunifanya mimi zezeta wa mapenzi, ukawa unanipandisha na kunishusha kisa nipo kimya. Nasikitia ukimya wangu wewe uliuchukulia vibaya. Ulihisi kila usemalo mbele yangu nami nikakaa kimya basi jibu lake ni ndio. Kumbe uliwaza kinyume.



    Nimesha sema, sikuhitaji, na wala sihitaji kuwa na mvulana wa aina yeyote ile kwa muda huu. Bora nitulie kuliko kujiingiza tena kwenye ulimwengu wa maumivu. Kama utaendelea kupenda, wewe penda. Lakini mie Zulfa, siwezi tena. Yaliyonisibu yanatosha sihitaji tena kupenda." Zulfa aliyatoa maneno yale kwa uchungu wa hali ya juu. Na aliendelea kulalamika sana jambo lililomfanya Samir awe mpole na akose cha kuongea. Kwa maneno aliyotamkiwa Samir, yalimpelekea akate tamaa na kujiona yeye ni mkosaji. Alikosa njia ya kuyapoza mawazo yake na yeye pia akatoa kiapo cha kutopenda tena kama alivyosema Zulfa. Lakini pia hakusita kutoa onyo kwa Zulfa kwamba, endapo atasikia Zulfa ana mvulana mwingine basi yupo radhi apelekwe jela kwa ajili ya mapenzi kwani huo utakuwa ni usaliti.



    Haya, siku zikaenda siku zikapita bila Samir, kumsahau Zulfa. Ndipo alipoamua kuenda nje ya mji kwa bibi yake na huko ndipo alipopata mtazamo mpya juu ya wasichana. Bila hata bughudha Zulfa alitoka kichwani mwa Samir, na hakuhtaji kumuweka msichana yeyote kwa muda ule.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya likizo kuisha. Wanafunzi wote walirejea mashuleni kwao. Samir, alijitahidi kwenye masomo na uwezo wake ulianza kuonekana darasani kwani kila mtihani alionesha kujitahidi kutokana na kutokuwa na mawazo.



    Hatimae Zulfa na Samir, wakasahauliana na ikabaki kumbukumbu juu yao. Samir, alimchukia Zulfa na hakuhitaji hata kumuona lakini Zulfa hakumchukia Samir.



    Siku zilienda siku zikapita huku upande wa Samir akiwa bize na masomo.



    Upande wa Nurdin nao, penzi lake na Sumaya. Kama kawaida liliendelea na kwa muda huo lilikuwa tamu sana zaidi hata ya Asali. Kama ungetaka ukosane na Sumayah, basi mseme Nurdin kwa ubaya na kama ungetaka kukosana na Nurdin, basi mseme Sumaya kwa ubaya.



    "Mpenzi, natambua kuwa unanipenda na kunijali. Lakini naendelea kukusisitiza uwe na msimamo iliusije tema bigi ji kwa karanga za kuonjeshwa." Aliongea Nurdin, siku ambayo wawili hao waliamua kutoka na kwenda mahali tulivu kwa ajili ya kujadili penzi lao.



    "Usiwe na shaka nami.., nathamini sana upendo wako na sihitaji kukukwaza japo kwa funda hata moja la maumivu. Mapenzi, ni maisha na maisha ni mimi na wewe, haitotokea siku hata moja ukajutia kuwa nami.. Mpenzi wangu. Nimezaliwa na kupewa upendo, sikuoneshwa mtu mwingine wa kumpa upendo, zaidi yako. Niamini maana imani ndio kila kitu mpenzi wangu.



    Najua, jinsi gani maumivu yanauma. Mimi sihitaji niwe kero kwako na ndio maana najiheshimu na kuhakikisha na kuwa muadilifu mbele yako na hata niwapo mbali na upeo wa macho yako.



    Hakuna niombacho na kikawa ndani ya uwezo wako nawe ukaninyima. Hujawahi kuniudhi hata kwa uchache wa kokwa la embe. Acha nikusifu Nurdin, maneno yako ni matamu hakuna mfano, sijawahi kusikia wala kutaraji kusikia maneno matamu kutoka kwa mvulana yeyote zaidi yako. Unajua kulinda pendo lako kwani kila ninapokuhitaji huwa karibu zaidi hata ya nikuhitajivyo. Nathubutu kusema wewe ndio mimi na mimi nimo ndani yako. Ilove you(nakupenda)" Aliongea Sumaya, huku akiendelea kudeka kwenye mwili wa Nurdin. Ambae aliamua kumvuta kipindi wametulia na kusababisha mkumbato wa hali ya juu baina yao. Nurdin alikuwa akiendelea kutomasa tomasa maeneo ya mgongo wa Sumaya. Huku Sumaya, nae akiwa amemkaza Nurdin vilivyo tena ukizingatia na kaubaridi kalikopamba maeneo yale ndio basi kabisa.



    " Sijui nikupe nini ilinikufanye uthibitishe upendo wangu kwako. Sijui ni kuite jina gani ililikupendeze kuliko yote. Hebu fumba macho mpenzi," Akajitoa kwenye kumbato kisha Zulfa akayafumba macho kama alivyoambiwa na Nurdin.



    "Mmmhhh!, vizuri sana mpenzi wangu. Sasa unaweza niambia unaona nini ndani ya macho yako?" Ni swali alilotupiwa Sumaya, swali hilo lilimfanya Sumaya atabasamu na kuuongeza uzuri wake maradufu, jambo lililompelekea Nurdin ajisifu kupata mrembo kama yule.



    " Ndio, nimefumba macho yangu. Na sioni chochote kile lakini, hisia zinamuona Nurdin, akili ina muwaza Nurdin, na hata moyo bado umemuhifadhi Nurdin, kuachilia mbali yote hayo, bado naendelea kuskia sauti nzuri, yenye matamshi yaliyojipangilia kwa ustadi kutoka kwa Nurdin. Nakupenda sana Nurdin, umenikaa kila pahali, hata mikono yangu inawaza kukukumbatia tu." Zulfa, aliongea maneno makali sana. Maneno ambayo hata Nurdin mwenyewe hakuyategemea.



    Fumbua macho yako mpenzi. Alisema Nurdin kisha Sumaya akafanya kama alivyoambiwa na mpenzi wake, kisha akaulizwa tena anaona nini kwenye upeo wa macho yake. Nae akajibu anamuona mwanaume wa ndoto zake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Nurdin, natamani kukutekea maji ya kuoga pindi utokapo kazini, kukukaribisha chakula na kukukaribisha kitandani ufikapo muda wa kulala. Lakini pia natamani sana kukusindikiza kazini muda ambao nitakuwa nikimpeleka mwanetu shuleni kwa ajili ya kupata elimu kama tuipatayo sie wazazi wake wa baadae." Aliongea Sumaya, kisha akamshika mkono mpenzi wake kwa mapozi na kumkimbiza mpaka kwenye mti wa embe mbichi.



    "Mfalme wangu, unajua matunda haya yanaitwaje?" Aliuliza Sumaya kwa jina la heshma, jina ambalo laiti kama ukiitwa kwa kuthaminiwa na mpenzi wako basi utajihisi umepaa.



    "hahahahahaha. Malikia wangu, huu, si. Mti wa muembe na hayo matunda simaembe." Alicheka Nurdin kisha kicheko chake akakiambatanisha na majibu.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog