Search This Blog

Thursday, July 21, 2022

NILIISHI DUNIA YA PEKE YANGU - 1

 





    IMEANDIKWA NA : ALLY MBETU



    *********************************************************************************



    Simulizi : Niliishi Dunia Ya Peke Yangu

    Sehemu Ya Kwanza (1)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    NILIISHI DUNIA YA PEKE YANGUNILIISHI DUNIA YA PEKE YANGUNILIISHI DUNIA YA PEKE YANGUNILIISHI DUNIA YA PEKE YANGUNILIISHI DUNIA YA PEKE YANGUNILIISHI DUNIA YA PEKE YANGU NILIISHI DUNIA YA PEKE YANGUNILIISHI DUNIA YA PEKE YANGU NILIISHI DUNIA YA PEKE YANGUNILIISHI DUNIA YA PEKE YANGUNILIISHI DUNIA YA PEKE YANGUNILIISHI DUNIA YA PEKE YANGU NILIISHI DUNIA YA PEKE YANGUNILIISHI DUNIA YA PEKE YANGU NILIISHI DUNIA YA PEKE YANGUNILIISHI DUNIA YA PEKE YANGUNILIISHI DUNIA YA PEKE YANGU NILIISHI DUNIA YA PEKE YANGUNILIISHI DUNIA YA PEKE YANGUNILIISHI DUNIA YA PEKE YANGUNILIISHI DUNIA YA PEKE YANGU

    MATESO na shida ni sehemu ya maisha ya mwanadamu lakini kwa upande wangu yalikuwa tofauti na kujiona naishi dunia nyingine tofauti na wanayoishi wanadamu wenzangu. Kwa hili Mungu atanisamehe kwa kuamini Mungu aliyekuwa nikielezwa kuwa mwingi wa rehema na huruma kutokana na mafundisho ya dini yangu hayupo na kuniacha peke yangu. Niliamini kama angekuwepo niliyokutana nayo yalikuwa na tofauti kubwa na wanadamu wenzangu. Kucheka kwangu kulikuwa kwa bahati mbaya zaidi ya muda mwingi kuwa nalia huku nikiamini huenda mimi si kiumbe wa dunia hii kwani hata nyumba za ibada na mafundisho ya dini havikuweza kuninyamazisha kilio changu hata kunifuta machozi yaliyokosa kizuizi kila kukicha. Kifo nacho kilinikimbia kila nilivyokikimbilia kama sehemu ya kuepuka tabu za dunia hakikutaka kuonesha ushirikiano kwangu. Niliwaonea wivu wote niliosikia wamejiua kwa kujinyonga au kunywa sumu, lakini si kwangu kila hila nilizofanya ili nami nife lakini kifo kilinikataa na kusema hakina urafiki na mimi. Nilijiuliza sina raha mateso kila kukicha toka nilipokuwa tumboni kwa mama yangu, suluhu nyepesi ilikuwa ni kifo nacho kilinikana katukatu hakinihitaji. Hebu niambie ni kiumbe gani kilichokosa yote hayo. Ni kweli maandiko ya vitabu vitakatifu yalitueleza mwenye dhambi ndiye anayestahiri adhabu, lakini kwa upande wangu dhambi hiyo niliifanya lini ikiwa mitihani ilianzia toka kutunga kwa mimba yangu. Vitabu vya dini vinatueleza kuwa mtoto hatahukumiwa kwa dhambi ya mzazi wake, vile vile mzazi hatahukumiwa kwa makosa ya mwanaye. Kama nivyo basi naamini kabisa japo nipo katika dunia ya kawaida lakini niliishi dunia ya peke yangu isiyo na Mungu wenye upendo na huruma. Najua maneno yangu yameutikisa moyo wako na kujiuliza kwa nini niseme maneno yanayoonesha kabisa namkufuru Mungu na kuamini naishi dunia ya peke yangu. Wakati hakuna dunia nyingine zaidi ya hii kwani baada ya maisha ya duniani kuna maisha mengine kutokana na imani za dini zetu baada ya kifo kuna maisha mengine ya milele peponi kama umetenda mema au motoni (jehanamu) kama umetenda mabaya. Nakuomba unipe muda wako ili ujue nimekutana na mambo gani yaliyonifanya nikufuru Mungu na kuamini hayupo. Naitwa Mwanani jina maarufu ambalo nimekuwa nalo japo jina la kusomea shule niliandikishwa jina la Salha. Elimu yangu kidato cha pili, si kwamba sikuwa napenda kuendelea na masomo, yote haya yalianza miaka miwili baada ya kifo cha mama yangu mpenzi. Kwa kweli kila ninapohadithia mkasa huu moyo wangu huwa unakufa ganzi kwani maisha yangu yalianza misukosuko toka nikiwa tumboni baada ya ujauzito wangu kutaka kutoka baada ya kipigo cha mbwa mwizi alichokipata mama toka kwa baba baada ya kumshtumu alikuwa akitembea na mfanyakazi wa ndani na ujauzito wangu si wake. Unaweza kujiuliza yote haya nimeyajua wapi wakati mama yangu kufariki nikiwa na miaka kumi sita na wakati huo nilikuwa nimeanza darasa kidato cha kwanza. Mengi nilielezwa na bibi baada ya kuona nategwa na mtu niliyefahamu kuwa ni baba yangu mzazi. Pia kunieleza maneno mazito ambayo nilipata

    ufafanuzi mpana toka kwa bibi kizaa mama kijijini. Malalamiko yangu niliyapeleka kwa bibi kutengwa na baba pia kuelezwa kuwa mimi si mtoto wake eti nina baba yangu wakati mama yangu alipokuwa hai hakuwahi kutamka. Wakati huo kidogo akili ilianza kufanya kazi wakati huo nilikuwa na umri wa miaka kumi na sita. Baada ya kumueleza bibi manyanyaso niliyokuwa nayapata kutoka kwa baba yangu. Bibi alinieleza kisa kimoja ambacho kwa kweli kilinitisha na kunifanya nianze kupoteza mwelekeo wa maisha kwa kuamini sikuwa na haki toka kwa baba niliyemtegemea. “Mjukuu wangu napenda kukueleza jambo moja ambalo halikuwa siri tulilijua hata sisi wa pembeni lilikuwa wazi kwa kila mtu alilijua. Mama yako kweli alikuwa mwingi wa habari nilimuonya mara nyingi ikawa nafanya kazi bure sawa na kutwanga maji kwenye kinu hakuwa muaminifu katika ndoa yake. “Baba yako alikuja kunishtakia mara nyingi kuwa mama yako si muaminifu, nilimwita na kumueleza malalamiko ya mumewe, lakini yaliingilia kushoto na kutokea kulia. Mara ya mwisho aliwafumania wakifanya mapenzi na huyo mfanyakazi wa ndani.

    “Mjukuu wangu napenda kukueleza jambo moja ambalo halikuwa siri tulilijua hata sisi wa pembeni lilikuwa wazi kwa kila mtu. “Mama yako kweli alikuwa mwingi wa habari, nilimuonya mara nyingi ikawa kazi bure sawa na kutwanga maji kwenye kinu, hakuwa muaminifu katika ndoa yake. “Baba yako alikuja kunishtakia mara nyingi kuwa mama yako si muaminifu, nilimwita na kumueleza malalamiko ya mumewe, lakini yaliingilia kushoto na kutokea kulia. “Mara ya mwisho aliwafumania wakifanya mapenzi na huyo mfanyakazi wao wa ndani. “Kutokana na baba yako kumpenda sana mkewe, alimfukuza mfanyakazi lakini aliendelea na mama yako, kwa bahati mbaya mwaka huo huo ndiyo mimba yako ilipoingia. “Japo kitanda hakizai haramu lakini baba yako aliikataa mimba yako kwa kuamini mwenye ujauzito huo ni yule kijana. “Kutokana na maelezo ya baba yako kabla ya ujauzito wako, miezi karibia miwili mama yako alikuwa akimnyima unyumba baba yako kwa kisingizio cha kuumwa. “Kumbe usiku alikuwa akimtoroka mumewe kitandani na kwenda kufanya mapenzi na mfanyakazi, kijana dhalili ambaye hakuwa na mbele wala nyuma. “Mjukuu wangu nilisema mpaka mdomo wangu ukataka kupasuka lakini sikio la kufa siku zote halisikii dawa. “Basi tangu ujauzito wako ulipotungwa palizuka mifarakano mikubwa huku baba yako akilazimisha mimba yako itolewe. Lakini mama yako aligoma na kumueleza hata kama hatamhudumia basi angekuhudumia yeye.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    “iku moja waligombana sana huku baba yako akimpiga mama yako tumboni ili kuhakikisha kwamba mimba yako inatoka. “akini Mungu mkubwa pamoja na kuumizwa sana, bado ujauzito wako haukutoka. Muda ulipofika, mama yako alijifungua salama mtoto wa kike ambaye ni wewe. “Hata hilo jina la Mwanani maana yake ni mtoto wa nani kwa vile ulikataliwa na baba yako. Baada ya kuzaliwa sura yako ilifanana sana na yule mfanyakazi hapo ndipo palipozuka chuki huku ukitafutiwa kila njia ya kukuliwa bila mafanikio. “Mara ya kwanza mama yako alikuja huku alikaa mpaka baba yako alipokubali kukutambua kama mwanaye na kukubali kukupa huduma zote kama mtoto wake hata kadi yako ya kliniki alikubali liandikwe jina la kaka wa baba yako mzazi. “Kwa vile mama yako alijua baba yako hana mapenzi na wewe ya kweli alikununulia kiwanja ili akujengee nyumba kama urithi wako akiwa hai kwa kuamini akifa mapema hutapata kitu kwa baba yako. “Lakini kwa bahati mbaya mama yako alifariki kabla hajatimiza dhamira yake, kwa kweli mpaka leo sijui mwanangu aliugua ugonjwa gani. Toka niishi katika dunia hii na umri wangu sijawahi kuuona ugonjwa huo. “ Mama yako alipoingia katika siku zake za mzunguko wa hedhi alitokwa na damu mfululizo ambazo hazikukoma mpaka alipokata kauli. “Kwa kweli baba yako alikuwa akimpenda sana mama yako, alipoteza fedha nyingi kuokoa maisha yake lakini hakufanikiwa. Hata kifo cha mama yako kilimliza sana. Kama utakumbuka alikonda sana baada ya kifo mama yako. “Baada ya kifo chake kulizuka tetesi kuwa ule ulikuwa uchawi aliofanyiwa na mwanamke mmoja aliyekuwa akitembea na mume wake. Kwa hilo siwezi kumkingia kifua kwani mama yako kwa kweli alikuwa mwingi wa habari. Nina imani ulimuona, Mungu alimjalia sura na umbile zuri basi, alifanya chochote alichokitaka bila kuogopa aibu.” Maelezo ya bibi yalinipa picha kamili kwa kuamini kuwa baba yangu hakuwa na mapenzi na mimi, kwani kuna siku moja alituita watoto wake wote na kunieleza mbele yao kuwa mimi si mtoto wake na kunitaka nimtafute baba yangu ambaye ni mkata majani ya ng’ombe. Alisema: “Sikiliza we mwana wa haramu mimi si baba yako, kamuulize mama yako huko kaburini alipolala kuwa baba yako yuko wapi. Kuhusu huduma kama mtoto wangu kuanzia sasa sahau, sitaendelea kukuhudumia hata ukiendelea kukaa hapa utakuwa kama mfanyakazi lakini suala la kukusomesha sahau. “Fedha zangu zina kazi nyingi, wanangu wote hawa wanazitegemea, siwezi kuhudumia mtu asiye na faida kwangu nakuona kama nguruwe.”

    “Na baba yangu yupo wapi?” “Mmh! Kuna habari zisizo rasmi kuwa baada ya kufukuzwa kazi aliokotwa akiwa amekufa na tuhuma zilikwenda kwa baba yako kuwa ndiye aliyefanya kitendo hicho cha kikatili baada ya kujua aliihujumu ndoa yake.” “Kama kamuua baba yangu wa kweli sasa alitaka niende kwa baba yupi?” niliuliza kwa uchungu na kujikuta nikianza kujenga chuki ya kweli kwa baba. “Hizo zilikuwa habari za juu juu japo hazikuwa na uhakika mkubwa. Naamini marehemu mama yako alikuwa akijua mambo mengi, kama angekuwepo angekueleza kila kitu.” “Sasa nitajuaje baba yangu yupo hai au amekufa, kama yupo hai nitampenda na kumheshimu hata kama hana kitu kwa vile ndiye mzazi wangu, hakuna mwingine.” “Hilo ndilo lililobakia, achana na mawazo mabaya ya kujiua.” “Sasa nitamuona wapi?” “Kwa vile unamhitaji baba yako tutafanya utaratibu wa kumtafuta.” “Kwani mara mwisho kumuona ilikuwa lini?” “Toka alipofukuzwa kazi baada ya kufumaniwa na mama yako sijamuona tena.” “Kuhusu habari zake?” “Kwa kweli baada ya kifo cha mama yako ndipo niliposikia taarifa za kifo chake, sasa sijui habari zile zina ukweli gani juu ya kifo chake.” “Sasa bibi mbona sikuelewi baba yangu yupo hai au amekufa?” “Mmh! Hapo kidogo pananichanganya.” “Au nikamuulize baba?” “Amekukataza usifike kwake hebu achana naye kama yupo siku moja Mungu atamleta na utamuona.” Niliyaanza maisha mapya ya kijijini ya kwenda shamba na kuchota maji kisimani pia kupikia kuni, maisha ambayo mwanzo niliyafanya kwa hamu ya kumsaidia bibi. Lakini yalibadilika na kuwa maisha yangu ya kudumu, nilizoea kulala kwenye nyumba ya umeme, maji ya bomba, kupikia mkaa na jiko la gesi, tena kazi hiyo niliianza baada ya kugeuzwa mfanyakazi wa ndani na si mtoto wa pale. Lakini kwa bibi tulitumia kibatari na siku nyingine tulilala giza kutokana na kukosa fedha ya kununua mafuta ya taa. Tulilala sehemu nzuri kwani marehemu mama alijitahidi kumkumbuka mama yake. Maneno ya bibi yalinipa moyo na kuamini ule ulikuwa muda wangu wa kumsaidia bibi ambaye umri ulikuwa umemchukua sana. Hali ya bibi ilifuta wazo langu la kutaka kujiua kwa mara ya pili. Nilimlea bibi kwa kufanya kazi zote ngumu huku tukisaidiana kazi za shamba. Nilijikuta nikikomaa kiakili japo umri wangu ulikuwa mdogo, uliotakiwa niwe chini ya uangalizi wa wazazi wangu. Maisha yalikuwa magumu sana kwani tulitegemea shamba na kuuza kuni ambazo tulikuwa tukizifuata porini na kuziuza. Wakati wa mvua hali ilikuwa mbaya kwani tulikosa biashara na kujikuta tukiishi maisha ya kubahatisha, siku nyingine tukilala bila kula. Kwa kweli mateso yale yalinirudisha katika dhamira yangu mbaya ya

    kutaka kujiua. Lakini hali ya bibi ilinizuia kwa kuamini kufanya vile nitakuwa nimefanya ukatili wa hali ya juu. Nilijiuliza mimi mwenye nguvu nipo lakini tunalala njaa, kama bibi akibakia peke yake, tena katika kipindi ambacho afya yake ilikuwa mgogoro itakuwaje? Nilikubali kuendelea kupambana na matatizo kwani hali ile ilikuwa fasheni pale kijijini. Wasichana kama mimi walipunguza ukali wa maisha kwa kutembea na wanaume wenye unafuu wa maisha. Lakini siku zote nilikumbuka wosia wa marehemu mama ambaye pamoja na sifa mbaya ya kukosa uaminifu katika ndoa yake pamoja na bibi waliniusia nisijiingize kwenye ngono katika umri mdogo kwani kama nitaukwaa naweza kupoteza malengo yangu. Kauli zile zilikuwa zikijirudia kichwani kila nilipotongozwa na kunifanya niwe mgumu tofauti na wasichana wa rika langu ambao kila mmoja alikuwa na bwana zaidi ya mmoja. Kingine kilichonitisha, msichana mmoja alibebeshwa mimba na bwana kumkimbia, matokeo yake aligeuka kuwa ombaomba. Siku zilivyozidi kukatika hali ya bibi nayo ilizidi kuzorota, akawa wa kusaidiwa kila kitu. Kutokana na ugumu wa maisha huku nikihitaji matumizi muhimu mimi na bibi, nilijikuta nikiangukia kwa kijana mmoja muuza chipsi ambaye kwa kweli alinisaidia mambo mengi sana ikiwemo fedha ya kumnunulia bibi dawa. Siku zilikatika huku nami nikiingia katika dunia ya wakubwa, bila kutarajia nikajikuta nimepachikwa ujauzito. Kutokana na malezi mazuri ya mwanaume wangu niliamini atailea hiyo mimba.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Tokea hapo niligeuka kuwa mfanyakazi wa ndani na si mtoto wa nyumba ile tena, kwa vile niling?ang?ania mwenyewe kukaa, wafanyakazi wote walifukuzwa na kubaki peke yangu kama mfanyakazi wa ndani, kazi ya watu watatu nilizifanya peke yangu. Kwa kweli roho iliniuma sana, baada ya kukatishwa kwa ndoto zangu, nilipokosa uvumilivu muda mwingi nilikuwa nikilia na kumkumbuka mama, kitu kilichonituma kunywa sumu ili nife kwani sikuuona mwelekeo wa maisha. Siku zote nilimlilia mama yangu mzazi kwani pamoja na makosa yake, bado alionesha mapenzi ya dhati kwangu na kama Mungu asingemchukua, basi nami ningetimiza malengo yangu kama bibi alivyonieleza kwamba mama yangu alikuwa akinijali. Kila nilipomkumbuka mama nililia sana, baada ya uvumilivu kunishinda siku moja niliamua kunywa sumu ya panya ili nimfuate mama yangu. Baada ya kuikoroga niliinywa na kwenda kujilaza chumbani kwangu. Maumivu makali ya tumbo yalinifanya nipoteze fahamu, niliposhtuka nilijikuta hospitali huku wadogo zangu wakiwa pembeni ya kitanda wakilia.

    Nilipata huduma nzuri na kuruhusiwa kutoka hospitali baada ya siku tatu, niliporudi nyumbani sikuruhusiwa kuingia ndani. Nilikuta vitu vyangu vyote vikiwa nje na kuelezwa kuanzia siku niliyotaka kuwaingiza kwenye matatizo sikutakiwa tena pale. Nilipewa nauli ya kwenda kuishi kwa bibi kijijini. Pamoja na kumuomba msamaha baba lakini ilikuwa ni kazi bure, kwani alikataa katakata. “Pamoja na upumbavu alionifanyia marehemu mama yako wa kuniletea mtoto wa haramu, bado umeona haitoshi unadiriki kunywa sumu ijulikane nimekuua ili nikafie jela wanangu wateseke?. “Naomba kuanzia leo nyumba hii uione kituo cha polisi na muuza bangi.” “Nisamehe ba...ba...nimechanganyikiwa mzazi wangu,” nilipiga magoti kuomba radhi. “Nani baba yako? Sitakusamehe milele tena umetonesha donda la miaka kumi na saba aliloniumiza mama yako. Naomba uondoke mimi siyo baba yako nenda ukamfuate baba yako siyo mimi,” baba alisema maneno yaliyonikata maini. “Lakini si ulimueleza mama utanilea?” nilimuuliza kutokana na kauli yake muda mfupi kabla mama hajafariki. “Siwezi kufuga adui yangu, leo umekunywa sumu kesho utatuua nyumba nzima. Naomba uondoke mbele yangu,” baba bado alikuwa na roho ya kikatili. Pamoja na wadogo zangu kuniombea msamaha, baba hakuwa tayari kunisamehe zaidi ya kunifukuza kama mbwa. Mmh! Mtoto wa kike jaribio langu la kwanza la kujiua lilishindikana na kufukuzwa. Lakini sikukata tamaa kwani niliamini bado nina nafasi ya kutimiza lengo langu la kujiua popote si lazima pale. Nilikwenda kijijini kwa bibi na kupokelewa, nilimueleza nimefukuzwa lakini sikumueleza kama kisa ni baada ya jaribio langu la kutaka kujiua kushindikana. Bibi pamoja na maisha yake kuwa ya kubahatisha alinipokea kwa mikono miwili. Kumbe taarifa za kutaka kujiua kwangu zilishamfikia, siku moja baada ya chakula cha usiku aliniuliza: “Salha mjukuu wangu kwa nini ulitaka kujiua?” “Ha! Nani?” Nilishtuka kwani niliamini ilikuwa siri. “Hapa nazungumza na nani?” “Nani kakwambia?” niliuliza swali badala ya kujibu.

    “Si muhimu kujua nani kaniambia, nataka uniambie kwa nini ulitaka kujiua?” bibi alikuwa mkali na majibu yangu ya kupindisha. “Bibi kwa kweli sina faida ya kuendelea kuishi, hebu angalia uingiaji wa mimba yangu, pia msukukosuko tangu nikiwa tumboni. “Ni wazi hata kuja kwangu duniani nimekuja kimakosa,” nilijibu huku nikilia kwa uchungu, swali lake lilikuwa ni sawa na kutonesha kidonda kilichoanza kupona. “Mjukuu wangu wewe si wa kwanza kutokewa na matatizo kama haya, hebu mtangulize Mungu mbele, yeye ndiye anayejua nini makusudia yake kwa kila kiumbe aliyemleta duniani. “Pia kujiua ni kosa kubwa kwani ni kufuru, ni sawa na kuingilia kazi yake kwa vile hakuna binadamu atakayeishi milele, kila mwanadamu ana siku zake za kuishi duniani na mwisho atakufa. “Vitabu vya dini vinasema unapojiua ukizikwa tu unaanza kupewa mateso mpaka siku ya kiama, hebu achana na mawazo ya kijinga. Wewe umekataliwa na baba yako si walimwengu, hebu angalia hapa kijijini kwetu kuna watoto wangapi wazazi wao walikuwepo lakini kwa bahati mbaya walikufa kwa ukimwi au magonjwa mengine na wapo wanaishi, kwani wamepungukiwa nini?”

    “Lakini hawakutengwa na wazazi wao?” “Nimekueleza mama yako alikupenda kuliko ndugu zako wote, hasa lilipotokea tatizo kama hilo.”

    Sehemu hii haikuweza kupatikana.

    (Intro ya next part; ILIPOISHIA Jumamosi: Siku zilikatika huku nami nikiingia katika dunia ya wakubwa, bila kutarajia nilijikuta nimepachikwa ujauzito bila kutegemea. Kutokana na malezi mazuri ya mwanaume wangu niliamini atailea ile mimba. SASA ENDELEA...)

    BAADA ya kupata uhakika kuwa nimenasa, siku moja nikiwa nyumbani kwake ambako kila siku nilipokuwa nikitoka kazini usiku ilikuwa ni lazima niende na usiku wa manane anirudishe nyumbani kwa kuwa hali ya bibi haikuniruhusu kukaa naye mbali muda mrefu. Tukiwa chumbani na mpenzi wangu ambaye naye alikuwa ndiyo kwanza anaanza maisha, akiwa na kitanda cha mbao cha futi nne kwa sita na godoro chakavu la sponji na sturi moja.

    Kwa kweli ndiyo alikuwa akianza maisha, baada ya mchezo wetu nilimweleza nilivyo: “Samweli mwenzio ni mjamzito.” “Ati?” alishtuka. “Ina maana umenisikia au...?” nami nilimuuliza baada ya kuonesha ameshtuka. “Lazima nishtuke kama hutanii.” “Ninachokisema ni kweli mimi ni mjamzito.” “Mmh!” Samwel aliguna. “Mbona sikuelewi?” ilibidi niwe mkali kidogo. “Si kwamba sikuelewi, bado sijajua nitafanya nini.” “Kufanya nini kivipi?” nilimuuliza nikiwa nimemkazia macho. “Si unaona maisha yangu ndiyo nayaanza na mtoto akija unafikiri itakuwaje?” “Nina imani ulijua utafanya nini, haya nilikueleza toka awali kuwa kufanya mapenzi bila kinga kuna madhara ulichojua kwenda kupima vvu tu ukasahau mimba leo unashangaa nini?” “Ni haraka sana kuwa na mtoto.” ”Sasa tutafanya nini wakati mtoto yuko njiani?” “Lazima tuitoe.” ”Ha! Tuitoe?” Nilishtuka. “Hatuna jinsi, acha hii tuitoe ili tujipange kwa mimba itakayokuja tutakuwa tumepiga hatua.” “Lakini nasikia kutoa mimba mtu anaweza kupoteza maisha.” “Kuna wataalamu wa kutoa mjini, tutakwenda kuitoa na tutarudi bila mtu kujua kama umetoa mimba.” “Samwel katika vitu nilivyokatazwa na bibi ni kutoa mimba,kwani mama yangu mdogo aliyekuwa akimfuata marehemu mama yangu mzazi alikufa kwa kufanya kitu kama hicho.” “Hiyo ilikuwa zamani, siku hizi hakuna vifo vya kutoa mimba, kuna vifaa vya kisasa. Unamuona shoga yako Silivia, unajua kama amekwishatoa mimba mbili?” “Ha! Utani mimba mbili?” nilishtuka kusikia vile. “Eeh! Ukimuangalia utajua? mimba hiyo ya pili ametoa hata wiki mbili hazijapita.” “Mmh! Ngoja nitamuuliza.” “Hawezi kukueleza ukweli ile ni siri kati yake na mpenzi wake na mimi nimejua kutokana na ukaribu wangu na Sosi.” Nilikubaliana na mpenzi wangu kwamba Ijumaa ya siku ile twende mjini alfajiri ili nikatoe mimba na kunifanya niwahi kurudi kumhudumia bibi. Usiku wa kuamkia siku ya kwenda kutoa ujauzito nilipatwa na ndoto nyingi za kutisha ikiwemo ya kujiona nimo ndani ya jeneza, kwa kweli ndoto zile ziliniogopesha sana na kujiuliza zilikuwa na maana gani. Wasiwasi wangu mkubwa huenda ulitokana na kutaka kuitoa mimba kuwa ndiyo ingekuwa sababu ya mauti yangu. Nilipanga asubuhi nimkatalie Samwel kwa kuamini kwamba ndoto zile zilikuwa na ujumbe wa kweli kwa kitendo nilichotaka kukifanya. Kwa hofu ya ndoto kujirudia kila wakati niliamuaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    kumaliza usiku kwa kukaa kitandani mpaka alfajiri na kuwa wa kwanza kuamka kwa ajili ya kufanya usafi. Nikiwa bado naendelea na usafi Samwel alifika kuonesha amejiandaa. “Vipi bado tu,” aliniuliza. “Sam mbona mapema sana?” “Salha tuwahi mapema ili uwahi kurudi si unajua usafiri shida.” “Najua, lakini siwezi kuondoka bila kumuandalia uji bibi.” “Basi fanya haraka.” Kwa vile chungu kilikuwa jikoni nilifanya kazi nyingi kwa wakati mmoja baada ya muda nilimaliza usafi na wakati huo uji ulikuwa umeiva. Nilimpatia bibi aliyekuwa amekwisha amka, nami nilijiandaa kwa kuoga kisha nilimuaga bibi kwa kumdanganya kuwa nilikuwa nakwenda kufuata cheti changu cha shule ambacho kingenisaidia kwa kazi yoyote pale kijijini. Bibi alinieleza niwahi kurudi kwani hali yake niliijua, kwa vile usiku tulipika viazi nilijua atakula mchana kama nitachelewa. Baada ya makubaliano yangu na bibi nilimpitia Samwel aliyekuwa akinisubiri njiani na kuelekea kituo cha basi, tulikuta gari limejaa ilibidi nasi tuingie kutokana na basi la alfajiri kuwa moja, mengine yangefika saa mbili au tano na la mwisho ni saa kumi ambalo huwa halirudi mpaka kesho yake. Tulifika mjini saa mbili na nusu asubuhi, kabla ya kwenda tulipita sehemu kupata kifungua kinywa kisha tulipanda daladala kuelekea huko kwenye hiyo hosptali. Tuliteremka sehemu kisha Samwel alisema nimfuate, tulipita kwenye kichochoro na kutokea kwenye nyumba yenye geti. Alinieleza pale ndipo hospitali iliyoonekana kama nyumba ya mtu, tuliingia ndani ya nyumba hiyo kupitia mlango wa uani, moyoni sikupendezwa na uamuzi aliochukua mpenzi wangu wa kuitoa ile mimba. Ndani tulipokelewa na dada mmoja ambaye alituuliza shida yetu, nilimueleza akaniomba fedha ya kutolea mimba. Samwel alimpa baada ya kumpa nilipelekwa kwenye chumba cha ndani ambacho kilikuwa na vifaa vya matibabu. Baada ya kupokelewa Samwel alitoka na kuniacha ndani ya chumba na kaka mmoja wa umri wa kati ya miaka 28 mpaka 30. Alinielekeza nivue nguo na kupanda kitandani, nilifanya kama alivyonieleza. Alichukua vifaa na kuanza kunitoa mimba.

    Ilikuwa tofauti na nilivyoelezwa kuwa kutoa ujauzito ni muda mfupi, tena rahisi.

    Nilishangaa kuona muda ukikatika huku nikimuona yule kaka akitokwa na jasho na uso wake ukionesha wasiwasi.

    Kwa vile nilikuwa mgeni kwenye mambo yake sikujua nini kinaendelea.

    Nilisikia maumivu makali kupita kiasi, nikauma meno.

    Damu ilinitoka kwa wingi na kumuona akihangaika kuniweka pamba kuzuia wingi wa damu, kila dakika ilivyozidi kwenda ndivyo nilivyoanza kuhisi kizunguzungu.

    Yule kaka alihangaika sana mpaka mwisho jasho likawa linamtoka chapachapa.

    Taratibu nilianza kupoteza uwezo wa kuona, nikawa kama nimo ndani ya maji.

    Baada ya muda nilipoteza fahamu, sikujua kilichoendelea mpaka niliposhtuka na kujikuta nimo kwenye mtaro wa maji huku mvua ikininyeshea.

    Kwa kuwa kulikuwa na giza sana, sikujua pale ni wapi.

    Nilijitahidi kunyanyuka na kutoka kwenye mtaro, muda huo bado mvua ilikuwa ikiendelea kunyesha.

    Nilipojaribu kutembea baada ya kutoka mtaroni nilihisi maumivu makali chini ya kitovu, hivyo kunifanya nitembee taratibu kwa kuinama.

    Niliziona taa za umeme kwa mbali sana. Nilijiuliza pale nipo wapi na nilifikaje lakini sikupata jibu.

    Pia nilijiuliza mpenzi wangu Samweli yupo wapi na mbona nimejikuta sehemu ile peke yangu? Kwa kweli nilikosa jibu.

    Nilitembea taratibu kufuata sehemu zinapoonekana taa. Nilijikuta nimetokea kwenye barabara ya lami, mvua nayo haikuwa na huruma, iliendelea kuninyeshea.

    Magari makubwa yalipita, nikajitahidi kupunga mkono lakini hakuna lililosimama, nikahisi labda nilikuwa nimesimama pembeni, tena gizani.

    Maumivu ya tumbo yalikuwa makali kiasi cha kusababisha nishindwe kuendelea kusimama.

    Nilijiuliza lile ni balaa gani ambalo liliongeza maumivu moyoni mwangu, nikaamini kabisa yaliyonitokea ni laana ya mama na bibi ya kukatazwa kutoa mimba.

    Nilijua kama ni kweli ni laana ya kutoa mimba basi ningekufa, lakini si kwa mateso kama yale.

    Kutokana na maumivu makali ya tumbo huku baridi kali ya mvua ikinichanyata, taratibu niliteremka chini na kukaa huku nikitamani mtoa roho atokee pale ili anipunguzie mateso.

    Lakini haikuwa vile kizunguzungu nacho kilijirudia, nikajitahidi kushindana nacho lakini nilishindwa, nikaamua kulala kwenye maji huku mvua nayo ikiendelea kuninyeshea. *****

    Nilizinduka na kujikuta nimelala kwenye kitanda cha hospitali.

    Nikiwa natafakari pale ni wapi, muuguzi aliingia na kuja moja kwa moja kwenye kitanda nilichokuwa nimelala.

    “Vipi mdogo wangu?” “Sijajua dada yangu.” “Pole sana.” “Asante.” “Vipi unaendeleaje?” “Sijambo kidogo.” “Eti ilikuwaje?” “Kwa kweli sijua kitu dada yangu, naona kama njozi ya giza na nilipoamka asubuhi nikajishangaa kujikuta hapa.” “Unakaa wapi?” “Kijijini.” “Ilikuwaje ukaokotwa sehemu mbaya kama ile.” “Kwa kweli dada sijui, naona kama miujiza.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    “Hebu nilieleze ilikuwaje, maana inaonekana ulikuwa unatoa mimba, kwa nini mdogo wangu?” Kwa kweli sikuwa na jinsi niliamua kumueleza ukweli kwani sikuwa na la kuficha, ilionesha yule dada ambaye alikuwa mtu mzima anajua mengi kwani suala la kutoa mimba alilijua kirahisi.

    Nilimueleza kwa ufupi jinsi nilivyoshawishiwa na mpenzi wangu kutoa mimba na kumweleza mara ya mwisho nilikuwa kwenye kitanda cha hospitali nikitoa mimba na hali iliyonitokea na nilivyojikuta kwenye mtaro wa maji sehemu ambayo nilikuwa siijui. “Mpenzi wako yupo wapi?” “Hata sijui.” “Umesema unakaa na bibi yako, mama na baba yako wapo wapi?” “Mama alifariki miaka minne iliyopita.” “Baba yako?” “Sina baba.” “Alifariki?” “Simjui.” “Ooh! Pole sana.” “Sijapoa kwa vile sijajua hatima ya maisha yangu.” “Unafikiri kwa nini ulitupwa?” “Hata najua! Kwani nani alinileta hapa?” “Polisi wa doria.” “Mungu wangu! Walinikuta wapi?”

    “Kwa maelezo yao wakati wanapita waliona mwili wako umelala pembeni ya barabara huku ukiendelea kunyeshewa na mvua.

    Wao walijua umefariki, walikuchukua mpaka hapa na kutaka upelekwe mochwali lakini mganga mkuu alisema huwezi kupelekwa chumba cha maiti bila kufanyiwa uchunguzi, ndipo ilipogundulika kuwa hujafa bali umepoteza fahamu.” “Mungu wangu!” nilishika mdomo baada ya kusikia habari mbaya kama zile za kutaka kupelekwa chumba cha maiti.

    Ilikuwa tofauti na nilivyoelezwa kuwa kutoa ujauzito ni muda mfupi, tena rahisi.

    Nilishangaa kuona muda ukikatika huku nikimuona yule kaka akitokwa na jasho na uso wake ukionesha wasiwasi.

    Kwa vile nilikuwa mgeni kwenye mambo yake sikujua nini kinaendelea.

    Nilisikia maumivu makali kupita kiasi, nikauma meno.

    Damu ilinitoka kwa wingi na kumuona akihangaika kuniweka pamba kuzuia wingi wa damu, kila dakika ilivyozidi kwenda ndivyo nilivyoanza kuhisi kizunguzungu.

    Yule kaka alihangaika sana mpaka mwisho jasho likawa linamtoka chapachapa.

    Taratibu nilianza kupoteza uwezo wa kuona, nikawa kama nimo ndani ya maji.

    Baada ya muda nilipoteza fahamu, sikujua kilichoendelea mpaka niliposhtuka na kujikuta nimo kwenye mtaro wa maji huku mvua ikininyeshea.

    Kwa kuwa kulikuwa na giza sana, sikujua pale ni wapi.

    Nilijitahidi kunyanyuka na kutoka kwenye mtaro, muda huo bado mvua ilikuwa ikiendelea kunyesha.

    Nilipojaribu kutembea baada ya kutoka mtaroni nilihisi maumivu makali chini ya kitovu, hivyo kunifanya nitembee taratibu kwa kuinama.

    Niliziona taa za umeme kwa mbali sana. Nilijiuliza pale nipo wapi na nilifikaje lakini sikupata jibu.

    Pia nilijiuliza mpenzi wangu Samweli yupo wapi na mbona nimejikuta sehemu ile peke yangu? Kwa kweli nilikosa jibu.

    Nilitembea taratibu kufuata sehemu zinapoonekana taa. Nilijikuta nimetokea kwenye barabara ya lami, mvua nayo haikuwa na huruma, iliendelea kuninyeshea.

    Magari makubwa yalipita, nikajitahidi kupunga mkono lakini hakuna lililosimama, nikahisi labda nilikuwa nimesimama pembeni, tena gizani.

    Maumivu ya tumbo yalikuwa makali kiasi cha kusababisha nishindwe kuendelea kusimama.

    Nilijiuliza lile ni balaa gani ambalo liliongeza maumivu moyoni mwangu, nikaamini kabisa yaliyonitokea ni laana ya mama na bibi ya kukatazwa kutoa mimba.

    Nilijua kama ni kweli ni laana ya kutoa mimba basi ningekufa, lakini si kwa mateso kama yale.

    Kutokana na maumivu makali ya tumbo huku baridi kali ya mvua ikinichanyata, taratibu niliteremka chini na kukaa huku nikitamani mtoa roho atokee pale ili anipunguzie mateso.

    Lakini haikuwa vile kizunguzungu nacho kilijirudia, nikajitahidi kushindana nacho lakini nilishindwa, nikaamua kulala kwenye maji huku mvua nayo ikiendelea kuninyeshea. *****

    Nilizinduka na kujikuta nimelala kwenye kitanda cha hospitali.

    Nikiwa natafakari pale ni wapi, muuguzi aliingia na kuja moja kwa moja kwenye kitanda nilichokuwa nimelala.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    “Vipi mdogo wangu?” “Sijajua dada yangu.” “Pole sana.” “Asante.” “Vipi unaendeleaje?” “Sijambo kidogo.” “Eti ilikuwaje?” “Kwa kweli sijua kitu dada yangu, naona kama njozi ya giza na nilipoamka asubuhi nikajishangaa kujikuta hapa.” “Unakaa wapi?” “Kijijini.” “Ilikuwaje ukaokotwa sehemu mbaya kama ile.” “Kwa kweli dada sijui, naona kama miujiza.”

    “Hebu nilieleze ilikuwaje, maana inaonekana ulikuwa unatoa mimba, kwa nini mdogo wangu?” Kwa kweli sikuwa na jinsi niliamua kumueleza ukweli kwani sikuwa na la kuficha, ilionesha yule dada ambaye alikuwa mtu mzima anajua mengi kwani suala la kutoa mimba alilijua kirahisi.

    Nilimueleza kwa ufupi jinsi nilivyoshawishiwa na mpenzi wangu kutoa mimba na kumweleza mara ya mwisho nilikuwa kwenye kitanda cha hospitali nikitoa mimba na hali iliyonitokea na nilivyojikuta kwenye mtaro wa maji sehemu ambayo nilikuwa siijui. “Mpenzi wako yupo wapi?” “Hata sijui.”

    “Umesema unakaa na bibi yako, mama na baba yako wapo wapi?” “Mama alifariki miaka minne iliyopita.” “Baba yako?” “Sina baba.” “Alifariki?” “Simjui.” “Ooh! Pole sana.” “Sijapoa kwa vile sijajua hatima ya maisha yangu.” “Unafikiri kwa nini ulitupwa?” “Hata najua! Kwani nani alinileta hapa?” “Polisi wa doria.” “Mungu wangu! Walinikuta wapi?” “Kwa maelezo yao wakati wanapita waliona mwili wako umelala pembeni ya barabara huku ukiendelea kunyeshewa na mvua.

    Wao walijua umefariki, walikuchukua mpaka hapa na kutaka upelekwe mochwali lakini mganga mkuu alisema huwezi kupelekwa chumba cha maiti bila kufanyiwa uchunguzi, ndipo ilipogundulika kuwa hujafa bali umepoteza fahamu.” “Mungu wangu!” nilishika mdomo baada ya kusikia habari mbaya kama zile za kutaka kupelekwa chumba cha maiti.

    “Hata najua! Kwani nani alinileta hapa?” “Polisi wa doria.” “Mungu wangu! Walinikuta wapi?” “Kwa maelezo yao wakati wanapita waliuona mwili wako ukiwa umelala pembeni mwa barabara huku ukinyeshewa na mvua. Wao walijua umefariki. Sasa endelea... walikuchukua mpaka hapa na kutaka upelekwe mochwari lakini mganga mkuu alikataa na kusema huwezi kupelekwa chumba cha maiti bila kufanyiwa uchunguzi. Ndipo ilipogundulika kuwa hujafa bali umepoteza fahamu.” “Mungu wangu!” nilishika mdomo baada ya kusikia habari hiyo mbaya. “Mdogo wangu baada ya kufanyiwa uchunguzi wa mwili wako tulikutana na michirizi ya damu sehemu za siri, tulipoichunguza ilionesha umetolewa mimba vibaya.” “Jamani, mbona niliambiwa kutoa ni rahisi?” “Sasa mdogo wangu nina imani baada ya kupata ufahamu unatakiwa kupata kifungua kinywa nimekununulia maziwa na chapati.” “Nashukuru dada.” Nilipatiwa maziwa na chapati, kwa kweli nilimshukuru sana yule dada kwa roho yake ya kibinaadamu. Wakati napata kifungua kinywa aliingia askari mmoja mwenye nyota moja na kukaa pembeni ya kitanda changu. “Hujambo binti?” “Sijambo, shikamoo.”

    “Marahaba na pole sana.” “Asante.” “Maliza kula tuzungumze.” Nilipomaliza, nilisogea karibu yake, ajabu sikuwa na maumivu ya tumbo kama niliyokuwa nayo baada ya kutoka kwenye ule mtaro na kunisababishia kushindwa kusimama. Baada ya kuniacha nitulie kwa muda yule askari alianza kwa kuniuliza jina langu. “Unaitwa nani binti?” “Salha.” “Salha nani?” “Sina baba.” “Mama?” “Pia sina.” “Unaishi na nani?” “Bibi.” “Unaishi sehemu gani?” “Kijijini.” “Umefikaje huku?” Nilimweleza jinsi nilivyopata mimba na kuletwa mjini na mpenzi wangu kwa ajili ya kuitoa. “Mpenzi wako anaitwa nani?” “Samweli.” “Anaishi wapi?” “Kijijini.” “Anajishughulisha na nini?” “Anauza chipsi.” “Hiyo sehemu uliyopelekwa kutoa mimba unaijua?” “Naikumbuka sehemu yenyewe lakini nyumba ipo ndani kidogo sijui kama nitaikumbuka.” “Unaweza kwenda kutuonesha?” “Nitajitahidi.” Baada ya kusema vile yule askari alinyanyuka na kutoka nje, baada ya muda alirudi na daktari. “Hujambo binti?” “Sijambo, shikamoo.” “Marhaba, unaendeleaje?” “Sijambo kiasi.” “Unaweza kutembea?” “Nitajaribu.” Nilinyanyuka kitandani na kujaribu kutembea niliweza, nilipewa nguo za kuvaa, zilikuwa hazitamaniki kwa tope na damu. Tulitoka hadi nje ya hospitali, nikatambua kumbe nilikuwa hospitali ya mkoa, niliingizwa kwenye gari na kuwapeleka sehemu niliyonyofolewa ujauzito wangu. Nilijitahidi kuikumbuka njia tuliyopita ili niweze kufika katika ile nyumba bila kupotea. Tulipofika tulikuta nyumba imefungwa, lakini askari walikwenda kwa mjumbe na kuuliza ni shughuli gani zilifanyika pale. “Kwa kweli mimi najua nyumba ya mtu, sijui kazi nyingine.” “Kama hujui tunaomba kuingia ndani kwa kuvunja mlango na wewe ukiwepo.” Baada ya kuvunja niliwaelekeza hadi katika chumba nilichoingia, tulikuta kuna vifaa vya hospitali vya kutolea mimba na baadhi ya dawa.

    Vitu vyote vilichukuliwa na mimi kurudishwa hospitali kwa ajili ya matibabu zaidi ikiwemo kusafishwa uchafu baada ya kutolewa ujauzito vibaya. Siku ya tatu nilitolewa hospitali na kupelekwa kijijini pamoja na askari ambao walimfuata mpenzi wangu aliyekuwa akikabiliwa na kosa la kinyama la kukusudia kuua akisaidiana na mganga aliyenitoa ujauzito wangu. Tulipofika kijijini niliwapeleka moja kwa moja kwa Samweli lakini hatukumkuta, waliulizia na kuelezwa kuwa alipotea zaidi ya siku nne. Niliposikia vile nilijua kuwa amekimbia baada ya kujua ameua. Baada ya kumkosa nilipelekwa nyumbani kwa bibi. Nilishangaa kukuta nyumba ikiwa katika hali iliyoonesha kuwa haijapitishwa ufagio, hata vyombo vilikuwa vichafu. Nilijiuliza bibi alikwenda wapi! Niliingia ndani na kuwaacha nje wale maaskari ili nimwite bibi, hali ya ndani ilitawaliwa na kimya kitu kilichonishtua na kujiuliza kama bibi alikuwa amekwenda shamba. Lakini mawazo yangu yalipingana, kama angekuwa amekwenda shamba basi hata uani kungekuwa kusafi kwani bibi alikuwa anapenda sana usafi kiasi cha kuniambukiza na mimi. Niliingia ndani huku nikimwita kwa sauti.” “Bibi...bibi...upo wapi?” Sikupata jibu lolote, kwa vile nilikuwa nimetoka kwenye mwanga, giza la ndani lilinifanya nisione vizuri ndani. Nikiwa natembea kuelekea chumbani nilijikwaa na kuangukia, kumbe nilipoangukia ilikuwa juu ya mwili wa bibi. Nilimshika bibi alikuwa amepoa kama vile alikuwa kwenye jokofu.

    Nilimtikisa huku nikimwita lakini hakujibu chochote, pembeni ya bibi kulikuwa na harufu kali ya kinyesi.

    Nilijiuliza iweje bibi afikie hatua ya kujisaidia bila kujisafisha, pamoja na kuumwa lakini hakuwa kwenye hali ya kujisaidia ndani. Nilimtingisa kwa sauti lakini hakushtuka.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    “Bibi, mimi mjukuu wako nimerudi,” nilitamka kwa sauti lakini hakukuwa na jibu, nikatoka nje walipokuwa askari na kuwaomba msaada. Waliingia ndani na kuutazama mwili wa bibi. Mmoja aliniuliza: “Mna ndugu wengine zaidi yako?” “Hapana, tupo wawili.” “Kuna majirani watu wazima mnaofahamiana nao?” “Ndiyo.” “Basi wafuate uje nao.” “Kwani bibi kafanya nini?” “Hebu fanya haraka,” askari alisema kwa sauti kali kidogo. Nilikimbia kwa jirani yetu, mama Solomoni, aliponiona alishtuka na kuniuliza: “Wee Salha ulikuwa wapi?” “Nilienda mjini mara moja.” “Mlikwenda pamoja na bibi yako.” “Nilikwenda peke yangu.” “Sasa na bibi yako kaenda wapi, kila nikipita simuoni, nilijua labda wote hampo.”

    “Mbona bibi yupo.” “Mmh! Kama yupo mbona sijamuona, kwani hata hali ya kwenu ilionesha hakuna mtu.” “Mama Solomoni unatakiwa nyumbani mara moja.” “Kuna nini?” “Twende mara moja.” Niliongozana na mama Solomoni, tulipofika yule askari ambaye alionekana ndiye kiongozi wao alimwita pembeni na kuzungumza naye kwa muda, niliwaona wakiongozana kuingia ndani.

    Mama Solomoni alitoka na nguo alizokuwa amevaa bibi.

    Baada ya usafi niliitwa kuelezwa ukweli kuwa bibi yangu amefariki. Naapa kuwa tangu nizaliwe mpaka nitakapoingia chini ya ardhi sitalia tena kama nilivyolia baada kuelezwa bibi amefariki.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog