Simulizi : Laiti Ningejua
Sehemu Ya Tatu (3)
ILIPOISHIA...
Baada ya kufika kileleni kichwa changu nilikiegesha katika kifua kizuri cha Fadhili mlinzi wangu huku tukizungumza mawili matatu kwa furaha kupongezana kwa kupeana mambo hadimuhadimu lakini ghafla nilihisi haja ndogo kwa mshtuko nilioupata baada ya kusikia mlango wa sebuleni ukigongwa.
“Ngo! Ngo! Ngo!”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com
ENDELEA...
Ngo! Ngo! Ngo! Mlango ulizidi kugongwa.
“Uuwiii” furaha niliyokuwa nayo ilitoweka ghafla mithili ya maji yaliyomwagika mchangani baada ya kuhisi kuwa mume wangu karejea nyumbani kutokea safarini wakati kitandani nilikuwa nakula raha na mchepuko. Jasho lilianza kumtoka Fadhili na alianza kunilaumu kwasababu mwanzoni aliniuliza kuhusu mume wangu nikamtoa wasiwasi kuwa kasafiri.
“Umeniingiza matatizoni.” Sauti ya lawama ilimtoka fadhili huku akiwa ananitazama kwa hasira baada ya kusikia mlango ukizidi kugongwa.
“Ingia uvunguni?” nilimwambia Fadhili aingie uvunguni mwa kitanda ili kama ni mume wangu asiweze kugundua kilichokuwa kikiendelea alitii kile nilichomwambia kwasababu hapakuwa na namna isipokuwa kujificha asiweze kunasa kwenye mikono ya Enrique kwasababu anamfahamu vizuri kuwa ni mtu mbaya sana pindi anapokuwa amekasirika kwani aliwai kushuhudia mwanzo mwisho kipigo ambacho Enriqque aliwai kunishushia nje ya geti baada ya kusikia kuwa nimemdharau mama yake mzazi.
Pamoja na kwamba nilikuwa nimeingiwa na wasiwasi mwingi lakini Fadhili alinizidi kwasababu alivaa suruali yake kaigeuza nje ndani kwa haraka na hofu aliyoipata ghafla baada ya kusikia mlango wa nyumba yangu ukigongwa na kuhisi moja kwa moja atakuwa ni baba Sweetness ndio karejea.
Baada ya Fadhili kuingia chini ya uvungu mwa kitanda changu kwaajili ya kukwepa asikutane na hasira za mume wangu nilikitandika kitanda changu harakaharaka ili Enrique atakapoingia asipatwe na wasiwasi baada ya hapo nilijifunga kanga nakwenda kwa haraka haraka kwenye dirisha la sebuleni kuchungulia yule mtu aliekuwa akigonga mlango wangu ni nani.
Kidogo moyo wangu ulipata amani baada ya kumwona dereva wa gari la shule la mwanangu ndie alikuwa akigonga mlango japokuwa nilijiuliza kulikuwa na tatizo gani kwasababu sio kawaida yake kuingia ndani ya geti langu kwahiyo bado nilibakiwa na chembechembe za uwoga ndani ya moyo wangu kwa kuwaza ujio wa mtu yule ulikuwa ni wa amani ama sio.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com
“Mbona hajaongozana na mwanangu wakati huu ni muda wa kutoka shule?” niliwaza wakati nausogelea mlango ili niweze kumsikiliza ananieleza nini.
Nilifungua mlango ili niweze kufahamu sababu ya msingi iliyompelekea yule kaka kuja kunigongea mlango wangu.
“Habari za kwako Anti.”
“Nzuri tu za kwako.”
“Njema.”
“Karibu.”
“Samahani Anti kunatatizo limejitokeza nimekuja kukutaarifu kwamba mwanano alipokuwa akishuka kwenye gari kwa bahati mbaya mwenzie alimsukuma na kuanguka chini na kuumia.” Nilihisi kuzirai niliposikia maneno ya kaka yule akinieleza kuwa mwanangu ameumia.
“Kwani gari halina matroni?” nilimuuliza kwa hasira kwasababu niliona ni uzembe umefanyika hadi mwanangu akaumia.
“Yupo.”
“Kwahiyo mwanangu yupo wapi?” nilizidi kumuhoji kwa hasira huku nikimtazama kwa jicho baya.
“Yupo nje ya geti.”
Niliongozana na dereva yule kuelekea nje ya geti kwenda kuangalia hali ya mwanangu kipenzi huku kichwani mwangu nikiwa na hamu ya kumwona matroni wa gari lile la shule niweze kumuogesha kwa mvua ya matusi kwasababu uzembe wake ndio umepelekea mwanangu kuumia.
***
Nilihisi uchungu sana ndani ya moyo wangu nilipomwona mwanangu akiwa analia kwa maumivu makali aliyokuwa akiyahisi kwa wakati ule kwani alikuwa na jeraha kubwa la mchubuko kwenye paji la uso wake damu zilikuwa zinamtiririka sana na kusababisha sare zake za shule kutapakaa damu.
“Masikini mwanangu.” Nilijikuta nazunguza peke yangu huku machozi yakinitoka baada ya kumuonea mwanangu huruma kutokana na tatizo lililokuwa limempata.
Wewe kazi yako nini mpaka watoto wanaumizana kiasi hiki.” Kwa hasira na sauti ya juu nilizungumza na matroni ambae huwa ndie anahakikisha kuwa watoto wanapanda salama kwenye gari na kushuka salama.
“Samahani dada kweli nakiri nimekosa naomba unisamehe.” Yule dada alizungumza kwa sauti ya upole huku machozi yakimlengalenga baada ya kuniona nimekasirika na kuvimba kama chatu.
“Wewe ni mzembe.”
“Hawa watoto ni watundu sana naomba unisamehe.”
Inajulikana kuwa watoto ni watundu ndio maana ukawekwa ufanye kazi hii kwahiyo nashangaa sana kazi yako ni ipi au ndio mnakaa na kuchekacheka na huyu dereva mnajiona wajanja haiwezekani hizi taharifa ni lazima nizifikishe kwa mkuu wako wa kazi.
“Tafadhali nakuomba dada yangu usifikishe habari hizi kwa bosi wangu kwasababu utahatarisha kibarua changu isitoshe nahudumia familia yangu mwenyewe kwani mume wangu kanitelekeza na familia.” Yule dada aliniomba msamaha huku akiwa amepiga magoti machozi yakiwa yanamtoka sana na kunisababishia kuingiwa na huruma kwasababu nilikuwa nafahamu ugumu wa maisha ulivyo.
“Basi nyanyuka nimekusamehe ila uwe makini na kazi yako kwasabaabu ingemtokea mtu mwingine pengine asingeweza kuvumilia huu ushenzi.”
“Asante sana dada Mwenyezi Mungu akubariki sana.”
“Tunashukuru sana dada.” Sauti ya dereva ilisikika ikinishukuru kwa kuweza kumaliza jambo lile palepale kwa njia ya amani.
Nilikwenda ndani kwangu na kumweleza Fadhili kilichokuwa kimetokea kwahiyo alirudi kazini kwake na mimi nilivaa nguo kwa haraka sana ili nikamuwaishe mwanangu hospitali akapate matibabu. Niliwasha gari langu na kwenda nje ya geti na kumpakia mwanangu sweetness na kumuwaisha hospitali na kwa bahati nzuri alitibiwa na aliruhusiwa siku ileile.
Wiki iliyofuata miezi miwili ilikamilika na mume wangu alirejea kutokea kwenye safari ya kikazi nchini Afrika ya kusini kwenye ukumbi mkubwa wa kimataifa ujulikanao kwa jina la Cape town international convention centre uliopo katika jiji la Cape town nilifurahia sana ujio wa mume wangu kwasababu alifungasha zawadi nyingi nzuri kwaajili yangu mimi na Sweetness japo kuwa alisikitika sana baada ya kumkuta mtoto anaumwa kutokana na ajali aliyokuwa ameipata siku chache zilizopita.
***
Ufanisi mzuri wa kazi wa mume wangu ulijidhihirisha kwenye macho ya watu wengi kwani baada ya kurejea nyumbani kampuni yake ilimpa zawadi ya gari jipya kabisa aina ya Toyota hilux kwa kuiwakilisha vema kampuni katika semina iliyokuwa imejumuisha mataifa mbalimbali. Tulifurahia sana zawaidi ile kwasababu tulifahamu kuwa itatusaidia katika kazi zetu za kiujasiria mali.
Enrique alikuza zaidi biashara yangu kwasababu ya faida kubwa tuliyokuwa tukiipata kwa kupitia kazi ile hivyo niliongeza juhudi mara dufu kwenye gazi yangu ilikuweza kupata faida zaidi na zaidi na hatimae siku za mbeleni tuweze kumiliki mradi mkubwa zaidi.
Siku zilivyozidi kusonga ndivyo ambavyo mwanangu alizidi kupata afueni na mwishoe alipona kabisa na kurejea katika hali ya uchangamfu kama awali.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com
Maisha yalizidi kuwa ya furaha sana kwani mume wangu aliniridhisha kwa mambo mengi sana isipokuwa katika suala moja pekee ambalo ni la haki yangu ya ndoa ambayo sikuweza kuipata kwa kiasi cha kunirisha hivyo kunisababishia nitafute msaada nje ya ndoa yangu. Ingawa mara kwa mara nilinusurika kukamatwa lakini nilishindwa kuvumilia ile hali kwasababu hapakuwa na mabadiliko yeyote kwa mume wangu na nilipojaribu kukaa nae kuzungumza kwa upole huwa anakasirika na kunifokea kana kwamba jambo ambalo huwa namshirikisha ni la kipuuzi.
Kunasiku alirudi nyumbani akitokea kazini nilimweleza kwamba ile siku nilikuwa namwitaji lakini alinijibu kuwa amechoka sana kwahiyo hawezi kushiriki tendo la ndoa kwa wakaati ule nilikasirika sana na moyo uliniuma kwasababu huwa ananichukulia poapoa sana pale ninapomshirikisha mambo ya msingi.
Enrique huwa anafanya kazi sana kiasi kwamba anaporudi nyumbani anapojilaza kitandani huwa analala fofofo kutokana na uchovu ambao anakuwa ameupata kwa siku nzima. Hivyo basi baada ya kusikia anakoroma nilijua tayari ameshalala niliamua kutumia nafasi ile harakaharaka kwenda getini kwa mlinzi akanipatie nilichokikosa kwa mume wangu kwa wakati ule. Kwa hali ya utaratibu sana nilijiondoa katika lile blanketi tulilokuwa tumejifunika pamoja na kushuka kitandani taratibu huku chumbani kukiwa na giza nene. Polepole nilianza kuelekea kwenye kitasa cha mlango wa chumbani ili kufungua niweze kutoka kwenda nje kwa bahati nzuri nilifanikiwa kufungua mlango bila mume wangu kuzinduka usingizini.
Nilizidi kunyata hadi mlango wa sebuleni na kufungua mlango kwa taratibu sana ili kisisikike kishindo chochote ambacho kitamsababishia kushtuka katika usingizi mzito aliokuwa amelala. Nilipotoka nje nlitembea kwa mwendo wa taratibu na umakini wa hali ya juu hadi getini kwa mlinzi.
Mlinzi alishtuka sana baada ya kuniona nikiwa nimemwendea usiku ule nikiwa nimevaa pajama.
“Aah bosi unazinguza sasa” sauti ya kunong’oneza ilisikika ikitokea kwa mlinzi ambae alionekana kushangaa sana.
“Usiogope Fadhili mume wangu kalala fofofo.” Nilizungumza huku nikifungua mkanda wa lile pajama ili niweze kupata nilichokuwa nimekiendea.
“Hivi hujui kuwa mume wako akigundua huu mchezo anaweza kuniua?”
***
“Acha kupoteza muda bwana we ni mwanaume unaogopa kitu gani.”
“Hakuna cha uwanaume mbele ya mali ya mtu.”
Niliona yule mlinzi ananipotezea muda kwa maneno mengi aliyokuwa nayo kwahiyo nilianza kufungua mkanda wa suruali yake na kuishusha chini kwa haraka uzuri mmoja ni kwamba jogoo wake alikuwa tayari ameshawika kwahiyo nilijishika ukutani harakaharaka nikaanza kufurahia utamu niliokuwa nikiupata kutokana na kasi ya mlinzi yule kunitimizia haja yangu ili nirudi chumbani kwa mume wangu kulala. Baada ya kupokea kichapo cha mabao mawili ya fasta fasta nilijiona hata nikirudi ndani nitaweza kupata usingizi kwahiyo nilifunga mkanda wa pajama langu na kurudi ndani kwa umakini sana ili nisiweze kusikika nilifanikiwa kufungua mlango wa chumbani na kukuta mume wangu bado kalala usingizi wa pono kwahiyo nilichukua uwamuzi wa kwenda bafuni kujitawaza na kurudi kitandani kulala.
Nilifurahi sana baada ya kumaliza jambo lile salama ingawa sikutosheka ila angalau nilipunguza kiu yangu kwa kiasi fulani. Palipokucha asubuhi wakati nilipokuwa natoka kuelekea kazini kwangu nilimpatia mlinzi elfu 50 kama zawadi ya kumpongeza kwa jinsi ambavyo alikuwa ananitimizia haja zangu kwasababu sikujua ningekuwa napata msaada wapi kama Fadhili asingekuwa amekaba nafasi.
Pamoja na kwamba domo la mlinzi wangu lilikuwa linatoa harufu mbaya ya sigara na ugoro aliokuwa akibwia lakini sikujali kabisa kwasababu alikuwa ananipatia kwa ufanisi wa hali ya juu kile nilichokuwa nakihitaji.
Baada ya kugundua kuwa naweza kuutumia ule muda wa usiku vizuri wakati mume wangu akiwa amelala niliutumia vizuri muda ule kwasababu mara kwa mara nilikuwa nikimwendea mlinzi wangu getini usiku ili aweze kuniburudisha. Nilifanikiwa kumpumbaza Fadhili kwa vijisenti nilivyokuwa nikimpatia kwahiyo tulizidi kupeana mapenzi mazito na kusababisha nimwone mlinzi yule kama ndie mume wangu na mume wangu kama ndie mlinzi. Kwa jinsi ambavyo mlinzi yule alikuwa akinibamba nilipokuwa nikipata nafasi wakati mwingine nilikuwa nikimuandalia chakula kizuri kwaajili ya kumpa nguvu.
Kwa siri nilimuwekea bili ya maziwa freshi na mayai mawili kila siku kwa mama ntilie aliekuwa jirani na pale nyumbani kwangu kwaajili ya kuujenga mwili wa kijana yule aweze kunipa burudani ya aina yake pale ninaponasa kwenye mikono yake. Nafurahi pia kwasababu Enrique alinielewa nilipomshawishi amuongezee mshahara kwasababu ya ufanisi wake wa kazi kuwa mzuri.
Mapenzi ya mlinzi yalininogea na nilidhamiria kumzalia mtoto ingawa sikumweleza kusudi langu kwasababu nilihofia akifahamu kuwa nimebeba ujauzito wake anaweza kukosa ujasiri na kuamua kutoroka pale nyumbani kwangu hivyo basi nilitegea siku za hatari katika mzunguko wangu wa hedhi halafu nikashiriki tendo la ndoa na Fadhili kwa lengo la kupata mimba.
Mlinzi alitingisha nyavu zikatingishika kwasababu baada ya muda nilikwenda hospitali baada ya kuona mwili wangu haupo sawa na kwa bahati njema vipimo vilionyesha ninaujauzito. Japokuwa nilikuwa na wasiwasi kutokana na ile mimba niliyokuwa nimeitoa kwamba inaweza kusababisha nisishike ujauzito mwingine lakini kwa neema za Mungu nilibeba ujauzito wa kamanda wetu wa getini.
***
Nilimweleza mume wangu kuwa nimeshika ujauzito mwingine na alifurahi na kunitakia kila la heri.
Fadhili alishtuka sana baada ya kuona tumbo linajitokeza ingawa nilimwondolea mashaka kwa kumdanganya kuwa mume wangu ndie alikuwa amefanya mambo kumbe sivyo. Kadiri miezi ilivyozidi kusonga ndivyo ambavyo nilikuwa nachoka sana kutokana na mimba niliyokuwa nimepatiwa na kamanda bila mume wagu kuwa na habari.
Miezi tisa haikuwa mingi na hatimae nilifanikiwa kujifungua watoto mapacha wawili wa kiume ambao kwa kiasi fulani pia walifanana na mimi mama yao ila walichukua rangi ya chokoleti ya baba yao kwahiyo hakuna alieweza kugundua ule mchezo niliokuwa nimeucheza kwa mara nyingine katika familia ya Enrique.
Mpenzi mume wangu alifurahi sana baada ya kumzalia watoto wawili tena wote wanaume.
“Kiukweli mke wangu sijui nikupatie zawadi gani kwa hii furaha uliyoniletea katika maisha yangu sielewi nikutendee nini ama nikupeleke wapi ambapo utaweza kupata furaha kama ambayo naihisi ndani ya moyo wangu kwa wakati huu.” Baba Sweetness alizungumza kwa furaha sana.
“Asante sana dia ila usijali kwasababu mimi pia nimefurahi kupata watoto mapacha.”
“Naomba nikubadilishie gari lako la kutembelea.”
“Woow asante baba watoto wangu.” Nilifurahi sana baada ya mume wangu kuniambia kuwa anataka anibadilishie gari la kutembea ila nilitamani nifahamu kuwa anataka aninunulie la aina gani.
“Unataka uninunulie la aina gani kipindi hiki.”
“Ntakufanyia surprise.”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com
“Mmh! Sawa bwana yangu macho.” Nilibaki roho juu nikisubiri nione ataninunulia gari la aina gani japo kuwa sikuwa na wasiwasi kwasababu mume wangu alikuwa anajua kuchagua vitu vizuri.
“Nakuahidi utakapomaliza uzazi utarudi kazini kwako kwa gari jipya ambalo litasababisha mashoga zako wakuogope kwasababu utakuwa matawi ya juu mno.” Enrique alizidi kunitamanisha zawadi ile ambayo alikuwa ameniahidi.
Upendo wa mume wangu ulizidi kupanda daraja kila kukicha kwani alinipa matunzo mazuri sana kipindi cha uzazi kiasi kwamba nilizidi kuonekana mbichi kama mwanamke ambae hajazaa kabisa kiukweli kama ni mume ambae anafahamu namna ya kumtunza mke wake nilikuwa nimempata kwasababu kila siku alijaribu kuwa mbunifu kupalilia penzi letu ili lizidi kuhimarika.
Miezi mitatu baadae baada ya kujifungua mume wangu aliniletea zawadi ya gari aina ya Nissan Murano. Nilimsifia mume wangu kwa kujua kuchagua kwasababu alininunulia gari ambalo mara nyingi nilikuwa namuonea gere dada mmoja mfanyabiashara jirani na pale kazini kwangu ambae alikuwa analimiliki. Nilifurahi sana kwa mapenzi ya dhati aliyokuwa akinionyesha mume wangu kwasababu alinifanya nionekane mwanamke miongoni mwa wanawake.
Enrique alipendekeza pacha wa kwanza (kurwa) aitwe Dylan na pacha wa pili (doto) aitwe Logan nilifurahia majina yale kwasababu ni majina ambayo yalikuwa na mvuto sana. Walipofikisha miezi sita walibatizwa na tuliwafanyia sherehe kubwa sana kuliko hata ile ya mtoto wa kwanza. Kusema kweli maisha yangu na mume wangu yalizidi kuwa ya furaha sana japokuwa moyo wangu ulikuwa umeficha siri nyingi nzito ambazo mume wangu hakuzifahamu.
Tulizidi kufanya kazi kwa bidii sana kuhakikisha kwamba watoto wetu wanafurahia uwepo wetu kama wazazi. Mwenyezi Mungu alizidi kutubariki kwani mapambano yetu dhidi ya umasikini yalizidi kufanikiwa kwa kuweza kufungua biashara nyingingine kubwa sana ya uuzaji wa mavazi ya kike na ya kiume ambapo tulimuajiri mtu wa kuweza kutusaidia kwasababu sisi tulikuwa na shughuli zetu zingine ambazo zilikuwa zikituweka bize.
Familia yangu tayari ilikuwa imeshakuwa kubwa kwahiyo mume wangu aliaamua kuniletea mfanyakazi wa ndani mwenye asili ya singida ambae alijulikana kwa jina la Katarina kwa lengo la kunisaidia katika kazi ndogondogo za pale nyumbani ili niweze kuendelea kuwa na ufanisi mzuri katika biashara yangu.
Nilijisikia vizuri sana baada ya kumpata dada wa kazi ambae alikuwa anafahamu majukumu yake ipasavyo kwani mwanzoni nilikuwa nikichoka sana kwasababu nilipaswa kuamka alfajiri sana ili niweze kufua nguo za watoto wangu pamoja na kuwaandalia chakula cha siku nzima halafu naondoka kwenda nao kazini kwasababu sikuwa na wakumwachia jambo ambalo lilikuwa linadumaza utendaji kazi wangu kwasababu mara nyingine nilishindwa kuwahudumia wateja kwa kuwa bize kuwaudumia watoto.
Mwanangu Sweetness baada ya kumaliza elimu ya awali aliendelea na elimu ya msingi katika shule ileile ya St Thomas kutokana na kuridhishwa na maendeleo yake darasani.
Dylan na Logan walipofikisha umri wa shule nilishikwa na taharuki baada ya kushauriana na baba yao kuhusu shule ya kuwapeleka na kuniambia kwamba hafikirii watoto wake kusoma Tanzania bali anataka awapeleke nchi ya jirani Kenya.
“Unathubutu vipi kuwapeleka watoto wadogo hivi nje ya nchi wakasome wakati bado wanahitaji ukaribu wa wazazi wao kutokana na umri wao kuwa mdogo.” nilimuuliza huku nikimuona waajabu sana kutokana na ushauri wake ambao haukunifurahisha kabisa.
“Usijali mke wangu watoto watakuwa salama kabisa na watapata kila kitu ambacho walipaswa kukipata kwetu sisi wazazi pia hivi ninavyozungumza na wewe nina rafiki yangu mmoja ambae anafanya kazi katika kampuni ya Tigo Tanzania, anawasomesha watoto wake katika shule ambayo ndiyo nataka kuwapeleka hawa wanajeshi wetu lakini kubwa zaidi ni kwamba watapata msaada wa karibu kutoka kwa bibi yao mdogo mama Levis ambae ni mwenyeji wa jiji la Nairobi ambapo ndipo shule ilipo. Nadiriki kufanya haya yote kwaajili ya kuwatengenezea msingi wa elimu ambao utakuwa mzuri na pia wakue kwa kuona jamii za nchi zingine wanaishi vipi na wajifunze yale yaliyo mema na kuja kuyapandikiza katika nchi yetu nzuri ya Tanzania. Naomba utambue pia kwamba huu ni mwanzo tu nitafanya kazi kwa bidii sana na nitajibana kwa kula chakula cha chumvi ilimradi wanangu waweze kusoma katika shule za mataifa ninayoyatamani kama vile Afrika ya kusini pia.” Mume wangu alizungumza maneno ambayo yalinishawishi na hatiame nilikubali watoto wakapate elimu yao ya awali na ya msingi katika nchi ya jirani.
***
Watoto walijiunga na shule ya Aga khan academy iliyopo umbali wa kilometa 19.2 kutokea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta. Ingawa roho ilikuwa ikiniuma kukaa mbali na wanangu ambao bado nilikuwa natamani kuwa nao karibu lakini ilibidi waende shule kwanza wakaandae maisha yao ya baadae. Mara nyingi nilikuwa nakwenda kuwatembelea shuleni kuwaangalia wanaendelea vipi na masomo yao lakini uzuri mmoja ni kwamba walikuwa wakikua kwa afya njema kimwili na kiakili nilihisi furaha sana pale ambapo nilikuwa nikifanya mazungumzo mara kwa mara na mwalimu wao wa taaluma na kunieleza kuwa wanangu wanafanya vizuri sana darasani na kwenye michezo pia.
Baada ya mwaka moja siku moja jioni wakati tupo mezani na mume wangu tukipata chakula niliingiwa na wasiwasi baada ya kumwona dada wa kazi akinyanyuka kwa kasi kutoka pale alipokuwa amekaa na kukimbia kwenye sinki kwenda kutapika. Nilijiuliza chakula kilikiwa kibaya au kunatatizo gani sikuweza kumuhisi vibaya kutokana na umri wake kuwa mdogo kwahiyo nilinyanyuka na kumwendea akanieleze tatizo lake ni lipi.
“Katarina.”
“Abee dada.”
“Unaumwa?”
“Hapana.”
“Sasa mbona unatapika?”
“Hata sielewi dada.”
“Usikute ushaanza kujihusisha kimapenzi na wanaume.”
“Hapana dada sijawai kufanya hivyo.”
Tulirudi mezani lakini alipojaribu kupeleka kijiko cha chakula mdomoni alitoka mbio kwa mara nyingine kwenda kutapika ndipo nikahisi lazima kutakuwa kunakitu haiwezekani awe katika hali ile wakati sisi tulikuwa tunakula chakula bila tatizo lolote.
“Hapa tatizo litakuwa kwake na sio chakula.” Niliwaza wakati nilipokuwa nikimsindikiza kwa macho wakati alipokuwa akitoka nduki kwenda kutapika.
“Anashida gani huyu mtoto.” Mume wangu aliuliza baaada ya kushuhudia kilichokuwa kikiendelea.
“Mimi mwenyewe nashangaa kwasababu nimemuuliza anaumwa akaniambia haumwi.”
“Sasa hali hii inasababishwa na nini?” mume wangu aliniuliza swali ambalo kiukweli lilikuwa gumu kulijibu.
***
“Kiukweli sifahamu kwasababu angekuwa ni mtu mzima pengine ningesema labda anamimba lakini napata kigugumizi kutokana na umri wake kuwa mdogo sidhani kama anaweza akawa ameshaanza kujihusisha na suala la mapenzi katika umri alionao.”
“Kesho kabla hujaenda kazini mpeleke hospitali ili tuweze kufahamu kuwa anashida gani.”
“Sawa.”
Ilibidi aende kitandani kulala kwasababu chakula kilimshinda kabisa kwani alipojaribu kukitia mdomoni kilikuwa kinarudi. Ile siku sikulala kwa amani kabisa nilitamani pakuche mapema ili niweze kumpeleka hospitali nikafahamu anasumbuliwa na kitu gani kwasababu nilikuwa njia panda sielewi kilichokuwa kikimsibu.
Palipokucha asubuhi mume wangu alinikumbusha kwa mara nyingine nimpeleke yule binti hospitali kabla ya kwenda kazini na mimi nilifanya hivyo. Nilimpeleka katika hospitali inayomilikiwa na wahindi ijulikanayo kwa jina la Total care iliyopo njiro. Nilishindwa kuamini baada ya vipimo vya daktari kuonyesha kuwa Katarina alikuwa ni mjamzito. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com
“Ama kweli maji yaliyotulia ndio yenye kina kirefu.”niliwaza kwa masikitiko makubwa sana kwasababu siukuwai kufikiri kama yule mtoto mdogo vile tayari alikuwa ameshawajua wanaume.
Nilimpakia kwenye gari la abiria na kumwambia kondakta amshushe njiro kwa msola kwasababu binti yule alikuwa ni mgeni maeneo ya njiro na mimi nilikwenda kazi kwangu bila kuzungumza vibaya na binti yule asioge akakimbia tukashindwa kufahamu ujauzito kapewa na nani. Nilijiuliza maswali mengi sana wakati nilipokuwa kwenye gari nikielekea kwenye shughuli zangu.
“Hii mimba huyu mtoto kapatia wapi wakati muda wote anakuwa ndani ya geti? au mida ya mchana huwa anatoka kutokana na upenyo anaoupata kwasababu huwa nakuwa sipo nyumbani? hapa kwa namna moja au nyingine lazima mlinzi atakuwa anafahamu kinachoendelea kwasababu kama ni kutoka ni lazima atakuwa anatokea getini.” Niliwaza sana hadi nikahisi kichwa kinaniuma.
Nilipofika maeneo ya Haile selasie simu yangu ya mkononi ilisikika ikitoa mlio wa kupigiwa ikiwa ndani ya mkoba ambao niliuweka kwenye siti ya pembeni yangu, nilipunguza mwendo kidogo wakati nilipokuwa naitoa simu kwenye mkoba ili niweze kufahamu ni nani aliekuwa akinipigia kwa wakati ule baada ya kuitoa simu yangu juu ya kioo palisomeka “My honey.” Ambae ni mume wangu ndie alikuwa akinitafuta, nilihisi moja kwa moja ananiuliza habari za Katarina kwahiyo nilipokea na kumweleza kuwa nipo barabarani nitamtafuta nitakapofika kazini.
“Nipo kwa gari Enrique wangu nitakupigia nikifika.”
“Ok.” sauti ya mume wangu ilisikika upande wa pili na simu ilikatika.
Baada ya kufika kazini nilimpigia simu kumweleza vipimo vya daktari vinasemaje kuhusu dada wetu wa kazi.
“Vipi mmepata huduma?” mume wangu alianza kuzungumza mara baada ya kupokea simu.
***
“Ndio.”
“Anatatizo gani?”
“Ni mjamzito.”
“What?” (nini?) Mume wangu alionekana kushtuka sana baada ya kusikia vema kile nilichokuwa nikimweleza.
“Ndio hivyo yani hata mimi mwenyewe nimeshangaa.”
“Sasa itakuwaje?”
“Itabidi tutakaporudi jioni tumuulize aliempa ujauzito ni nani?”
“Ok fine have a nice day.” (poa uwe na siku njema.) Enrique alizungumza kwa kifupi na kukata simu.
“Duuh ama kweli wanaume ni watu wabaya sana.” niliwaza huku nikihisi kuchoka wakati nilipokuwa nikijaribu kufikiri umri wa Katarina na ujauzito alionao. Siku yangu iliharibika kabisa kwasababu sikuweza kupata amani tena kwani nilikuwa nikiwaza sana imewezekana vipi akapata ujauzito katika mazingira ya pale nyumbani kwangu wakati vitu vya ndani huwa nanunu kwa bei ya jumla?
Tuliporejea nyumbani wakati wa jioni tulipata wakati mgumu kwa kukosa ushirikiano kutoka kwa Katarina wakati tulipokuwa tukimuhoji kwani alikuwa hazungumzi chochote zaidi ya kulia. Tulimbembeleza sana ili aweze kutuonyesha ushirikiano lakini hakusikia bali aliendelea kulia wakati hakuwa amehadhibiwa jambo ambalo liliibua hasira za mume wangu na kuanza kumuwasha makofi ili aweze kuzungumza.
“Nisamehe.” Katarina aliomba msamaha baada ya kuona mvua ya makofi inamnyeshea.
“Nieleze aliekupa hii mimba ni nani shwaini wewe.” Mume wangu alizungumza kwa hasira sana huku akizidi kumpa kichapo cha maana dada wa kazi.
“Nakueleza.”
“Ok sema ni nani?”
“Niii... niii...” katerina alishikwa na kigugumizi cha kumtaja aliempa mimba kana kwamba alikuwa anaogopa.
“Nakwambia nieleze haraka kabla sijakuvunja shingo.”
“Ni naniii…”
Enrique aliona kama yule binti anacheza na akili yake hivyo alimkamata kwa mara nyingine kumpa kipigo nusura nipige ukunga nikifikiri anamuuwa mtoto wa watu kwa jinsi ambavyo alikuwa akimshushia kipigo cha mbwa mwizi.
***
“Sasa wewe siuseme ni nani!” nilitamka kwa nguvu kumsihi amtaje kusudi aweze kuchomoka kwenye mikono ya mume wangu kwasababu alikuwa kama amepandwa na mashetani kwa namna ambavyo alikuwa akimuangushia mkong’oto mithili ya kibaka aliebambwa na wananchi wenye hasira kali.
“Dada niombe msamaha nakufa.”
“Mume wangu subiri kwanza amekubali ku….” Kabla sijamaliza kuzungumza Enrique alinisukuma nikaanguka pembeni wakati nilipojaribu kumshika amwachie tumsikilize anasemaje.
“Enrique utamuua mtoto wa watu.” Nilizungumza huku mapigo ya moyo yakinienda mbio mithili ya saa mbovu.
“Acha afe kabisa, pimbi kama huyu hawezi kunisumbua akili yangu.” Enrique alizungumza kwa hasira huku akihema juujuu wakati akiendelea kumuadhibu vibaya yule dada wa kazi. Nilipata wazo nitoke niende nikamwite mlinzi aje kumuokoa Katerina kwasababu mimi nilishindwa.
Nilikwenda nje harakaharaka kwenda kumwita mlinzi lakini nilipofika getini sikumkuta mlinzi nilikwenda moja kwa moja hadi kwenye nyumba yake kumwangalia lakini napo sikumkuta nilijiuliza atakuwa amekwenda wapi kwa wakati ule wakati sio kawaida yake kutoka bila kuaga.
“Fadhili.”
“Fadhili.”
Baada ya kuita bila mafanikio nilichukua simu yangu ili niweze kuwasiliana nae nifahamu alipokuwa lakini hakupatikana hewani hivyo niliingiwa na wasiwasi kwa kuwaza alikuwa wapi kwa ule muda ambao alipaswa kuwa kazini.
Niliporudi ndani nilihisi kupoteza nguvu kwa mshtuko nilioupata baada ya kumkuta Katarina amelala chali sebuleni kama marehemu nikahisi mume wangu amemuuwa mtoto wa watu kwa kipigo ambacho alikuwa anamuangushia. Huku nikihema juujuu kutokana na hofu niliyokuwa nimeipata nilimsogelea pale chini ili niweze kufahamu kama alikuwa amekufa au amepoteza fahamu lakini kwa bahati nzuri nilibaini kuwa alikuwa amezirai.
“Ehuuu!” nilishusha pumzi kwasababu nilichoka ghafla, nguo nilizokuwa nimevaa zililowa jasho ndani ya muda mfupi japo kuwa kulikuwa na baridi kali jioni ya siku ile.
Nilianza kulia kwa kuwaza kwanini mume wangu aliweza kumfanyia yule binti unyama mkubwa namna ile. Ghafla Enrique alimnyanyua yule binti pale chini alipokuwa amelala na kumpeleka nje akapigwe na upepo ili fahamu ziweze kumrejea. Nilishangazwa sana ujasiri ambao mume wangu alikuwa nao kwasababu haukuwa wa kawaida.
***CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com
“Fadhili.” Sauti ya mume wangu ilisikika ikimuita mlinzi wakati alipokuwa nje bila kufahamu kuwa alikuwa anashida gani nae nilizidi kupoteza matumaini ya uwepo wa mlinzi kazini kwa wakati ule baada ya kuitwa kwa mara kadhaa bila kuitikia.
Nilibaki pale ndani nikiwa nimeshika tama kwa mawazo ambayo yalikuwa yakiumiza kichwa changu.
Baada ya dakika kumi na tano nikiwa bado nimekaa pale sebuleni sijielewi mume wangu aliingia ndani akiwa amemshika mkono yule binti wetu wa kazi na kumkalisha kwenye kiti na kuanza kuzungumza nae kwa mara nyingine.
“Naomba kwa ustaarabu bila shari tena bila kuvunjianaa heshima unieleze umepataje huu ujauzito ulionao.”
“Ujauzito ni wa Fa…dhili.”
“Unamaanisha mlinzi wa getini?”
“Ndio.”
“Sasa kwanini ulikuwa husemi muda wote huo?”
“Nilikuwa naogopa kwasababu alinitishia kuwa ataniua endapo nitamtaja kuwa yeye ndio muhusika.”
“Ahaa!” Nimeelewa sasa ndio maana hayupo kazini kumbe amenikimbia ila kwa kadiri ya uwezo wangu nitahakikisha nakula nae sahani moja ninauhakika hana nguvu na akili za kunishinda ni lazima nitamuonyesha mimi ni nani shenzi kabisa.”
Nilihisi kama nimepigwa sindano ya gazi kwasababu nilikuwa nimeganda kama barafu pale kwenye kiti nilichokuwa nimekalia kwa kuwaza sababu ya iliyompelekea Fadhili na kile kifua chake kama meza ya kamari kumrubuni binti mdongo mwenye umri wa miaka kumi na tano na hatimae kumpa mimba.
“Kapaki nguo zako kesho unaenda nyumbani.” mume wangu alizungumza kwa hasira kumweleza Katarina huku akinyanyuka alipokuwa amekaa na kutoka nje bila kujua alikuwa amekwenda kufanya nini. Baada ya muda alirudi na kuurusha ufunguo wa getini kwenye meza iliyokuwepo chumbani halafu akapanda kitandani akalala bila kuzungumza na mimi kitu chochote jambo ambalo lilidhihirisha kuwa alikuwa kachukia kupita maelezo.
Palipokucha alfajiri alikwenda kumgongea Katarina aamke ajiandae ili aweze kumpeleka alipokuwa amemtoa kwasababu tabia yake ilikuwa imetushinda. Baada ya maandalizi aliniaga anampeleka kwa mama yake mdogo anaeishi maeneo ya Ngaramtoni nje kidogo ya jiji la Arusha ambapo ndipo alimpatia.
Kwa jinsi ambavyo nilikuwa nimechukizwa na kile kitendo cha Fadhili kumpa mimba mfanya kazi wangu wa ndani nilitamani laiti ningeletewa nimkamate nimng’ateng’ate kwa ujinga alioufanya, roho iliniuma pale ambapo nilikumbuka muda wangu nilioupoteza na pesa pia nilizokuwa nikimuhonga ili asitamani kwingine kumbe hana maana kabisa.
“Atajua mwenyewe acha apambane na Enrique kwasababu tamaa zake ndio zimemponza.” Nilijisemea kimya kimya baada ya kuhisi kukasirishwa na tabia ya Fadhili.
Nilipokuwa kazini mume wangu alinipigia simu na kunieleza kuwa ameshamfikisha kwa mama yake mdogo kwahiyo ndio alikuwa njiani anaelekea kazini kwake. Niliendelea na shughuli zangu lakini moyo wangu ulikosa amani kabisa pale niliokuwa nikikumbuka tukio la Fadhili kumpa ujauzito yule dada wa kazi ila nilijitahidi kukubaliana na matokeo ili nisiweze kuendelea kuumiza moyo wangu.
Baada ya miezi miwili mume wangu alimleta mlinzi mwingine pale nyumbani ila kwa wakati huu niliona kama alikuwa ameshtukia mchezo mbaya niliokuwa namfanyia kwa Fadhili kwani alinikomesha ubishi kwasababu alimleta mmasai ambae Kiswahili chenyewe kilikuwa bado kinampa shida kukizungumza. Kiukweli sikuvutiwa kabisa na ujio wa yule masai pale nyumbani kwangu kwasababu alikuwa hana swaga kabisa na pia nilikuwa natumia muda mwingi kumuelewesha jambo pale nilipokuwa nampa maagizo kutokana na tatizo lake katika lugha ya Kiswahili. Japokuwa nilimshawishi mume wangu amuondoe masai yule amlete mwingine ambae angalau amechangamka kidogo lakini aligoma na kuniambia kwamba yule ndie mzuri kwahiyo hatuna budi kumuonyesha ushirikiano.
Baada ya ujio wa Olesaibulu mlinzi mpya wa pale nyumbani kwangu alifuata mfanyakazi mwingine wa ndani aliejulikana kwa jina la Fatuma kutoka Tanga ambae nilitafutiwa na rafiki yangu Doroth baada ya kumweleza kuwa nilikuwa ninashida ya mfanyakazi wa kunisaidia kazi za ndani. Nilifurahishwa nae kwasababu alikuwa anajituma katika majukumu yake kama ilivyopokuwa kwa Katarina pia alikuwa na heshima sana halafu isitoshe alikuwa anajua sana kupika chakula kitamu. Kila mara mume wangu alikuwa akimsifia pindi alipokuwa akikaa mezani kula chakula kwasababu ya ufundi wa mapishi aliokuwa nao binti yule ambae kwa mwonekano alikuwa ni mtu mzima.
Mume wangu hakupata fununu za alipokuwa amekwenda kujificha Fadhili kwahiyo alizidi kumtafuta katika kona mbalimbali za jiji kwa hudi na uvumba bila mafanikio ingawa alihapa kutotulia hadi ahakikishe anamtia mikononi mwake. Nilizidi kumwomba Mungu asifanikiwe kumpata kwasababu kwa hasira zake angeweza kumdhuru kijana wa watu ambae bado nilikuwa nampenda kwa kiasi fulani japo kuwa alikuwa amenikosea lakini moyo wangu ulishindwa kuendelea kumbebea kinyongo kwasababu alikuwa ni mtu muhimu sana katika maisha yangu kutokana na kwamba alikuwa ni baba wa watoto wangu mapacha Dylan na Logan ingawa ni kwa siri.
Siku za jumapili mara nyingi baada ya kutoka kanisani mimi na mume wangu na binti yetu huwa tunarudi nyumbani kwaajili ya kupumzika lakini jumapili moja nililazimika kwenda kuwasalimia wazazi wangu baada ya mwanangu Sweetness kunisumbua zaidi ya mwezi mzima akinitaka nimpeleke kwa bibi yake akamsalimie kwasababu kiukweli ulipita muda mrefu bila kwenda kusalimia nyumbani kwetu na kibaya zaidi wazazi wangu hawakuwa hata na simu ya mkononi ambayo ingekuwa inaniunganisha nao mara kwa mara. Enrique alinikubalia nilipomweleza kuwa nahitaji kwenda nyumbani kwa wazazi wangu kusalimia, alinipatia shilingi laki mbili kwaajili ya kuwanunulia vitu vidogovidogo na itakayobaki niwaachie kwaajili ya kuwasidia. Hivyo nilianza safari ya kuelekea kwa babu naa bibi yake Sweetness maeneo ya moshono arusha kutokea njiro nyumbani kwangu. Njiani niliwanunulia wazazi wangu zawadi mbalimbali kama vile sukari, mchele, sababuni ni vitu vingine kadha wa kadha.
***
Tulifika mida ya saa sita mchana na kuwakuta baba na mama wapo mezani ndio wanaanza kula chakula cha mchana ambacho kilikuwa ni ugali kwa dagaa. Nilifurahi sana kuwaona wazazi kwasababu ilikuwa imepita muda mrefu bila kuonana nao ingawa mama alinieleza kuwa alikuwa akisumbuliwa na mgongo lakini alikuwa akiendelea vizuri bila shida. Maisha ya pale nyumbani kwetu yalikuwa ni yaleyale ya taabu na shida nyingi kwani wazazi walikuwa wakilia shida maisha yanazidi kuwa magumu kila kukicha na hilo lilijidhihirisha wakati tulipokuwa tunakula chakula kwani chakula hakikuwa kizuri kwasababu mboga haikuwa na mafuta ya kutosha. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com
Wazazi walinituma nimsalimie mume wangu na pia nimfikishie shukrani za dhati kwa kile alichonipatia niwapelekee baada ya hapo tulipanda kwenye gari na kuanza safari ya kurudi nyumbani kwangu ambapo tulifika salama mida ya saa kumi na mbili kasoro na kumkuta mume wangu akiwa amepumzika chumbani akiangalia picha zetu za harusi. Uso wa mume wangu ulionyesha furaha sana wakati alipokuwa akifunua kile kitabu kilichokuwa kimejaa picha ya siku yetu ya muhimu sana. Nilivua nguo nilizokuwa nimevaa na kuingia bafuni kuoga kwasababu nilikuwa nahisi kuchoka baada ya hapo nilirudi kitandani nikakaa pembeni ya mume wangu ambae alikuwa anaendelea kuzingalia zile picha.
“Unajua mke wangu lile gauni la harusi lilikupendeza sana.”
“Asante! Japokuwa hata na wewe ulipendezwa na suti yako vilevile.”
“Hata hivyo ulikuwa na kila sababu ya kupendeza kwasababu gauni lenyewe nililinunua kwa gaharama kubwa sana.”
“Ni kweli kabisa mume wangu.”
Tulitosheka kuangalia zile picha na tulikwenda sebuleni kupata chakula cha jioni ili tuweze kupumzisha miili yetu mapema kusudi kesho yake tuweze kuamka na nguvu za kutosha tukafanye kazi. Ile siku dada wa kazi alikuwa ametuandia wali nazi kwa samaki, alikuwa amepika kwa umakini na ufundi wa hali ya juu kwasababu chakula kilikuwa ni kitamu hadi nikawa namuonea wivu kwajinsi ambavyo alikuwa anafahamu mambo ya kurosti. Mume wangu alikuwa ananisifia kuwa nafahamu kupika lakini baada ya dada yule kuja hata wakati nilipokuwa nikiingia jikoni sikuweza kupika hadi kufikia kumkonga mume wangu moyo kama ilivyokuwa kwa yule dada wa kitanga. Uzalendo ulimshinda mume wangu ikambidi azungumze.
“Hivi wewe dada umesomea mapishi?”
“Hapana kaka.”
“Sasa umejulia wapi kupika namna hii.”
“Nimefahamia tu nyumbani kwetu.”
“Ama kweli wewe kiboko kama ni kuugeuza mwiko nakuvulia kofia upo vizuri sana.” mume wangu alimsifia yule dada hadi nikamwonea gere.
“Au unaseamje wife?”
***
“Ni kweli kabisa anafahamu sana kupika chakula kikawa kitamu.”
Utamu wa chakula ulisababisha tule kupita kiasi na baada ya hapo tulikwenda kitandani tukiwa tumeshiba sana. Kalipokucha asubuhi dada alikuwa ameshatuandalia chai kwa vitafunwa mbalimbali hivyo tulifungua vinywa harakaharaka nakuondoka kuelekea kwenye majukumu yetu ya siku zote.
Wakati nilipokuwa nafungua mlango wa duka langu ili niweze kuingia ndani mlio wa meseji ulisikika kwenye simu yangu kuashiria kuwa kunaujumbe mfupi wa maandishi ulikuwa umetumwa kwangu. Nilitoa simu yangu kwenye mkoba mdogo nilikuwa nimeuning’iniza begani ili niweze kuangalia ile meseji iliyokuwa imeingia muda mfupi uliopita.
“Habari yako bosi.” Ujumbe mfupi wa maandishi ulisomeka katika simu yangu ukionekana kutumwa na namba ambayo ilikuwa ni ngeni na kunifanya nijiulize ni nani ambae ndie alikuwa ametuma meseji ile.
“Nzuri nani mwenzangu.”
“Fadhili.” Baada ya kugundua kuwa ni yeye niliamua nimpigie simu ili tuweze kuzungumza kwa kirefu zaidi kwasababu nilikuwa na mengi ya kuweza kuongea nae kwahiyo nilimpigia simu baada ya kuusoma ujumbe ule.
“Hallo.”
“Bosi naomba samahani kwa kile kitendo nilichokifanya pale nyumbani kwako kwasababu ni shetani tu ndie alinipitia.”
“Yani umeniudhi sana, na nilikuwa natamani nipate nafasi nikuulize ulichokitamani zaidi kwa mtoto yule ni nini wakati nilikuwa nakupa kila kitu.”
“Ndio hivyo bosi naomba unisamehe kwasababu hakuna binadamu aliemkamilifu kila mmoja anamapungufu yake.” Fadhili alizidi kuniomba msamaaha ingawa moyo wangu haukuwa na kinyongo nae tena.
“Kwahiyo kwa sasa upo wapi.”
“Nipo tu hapa mjini nimejichimbia chimbo kwasababu nasikia mume wako ananiwinda kama swala anitie mikononi mwake.”
“Ni kweli kabisa tena anahasira na wewe sana kwahiyo ni vema ukaendelea kujificha asiweze kukuona kabisa kwasababu anaweza kukuumiza.”
“Basi hakuna tatizo hapa nilipo hawezi kunipata kabisa kwasababu nimepata kazi ya ndani kwa ndani kwahiyo atanisikilizia kwenye redio tu.” Fadhili alizungumza kwa kujigamba kuwa hawezi kukamatwa na Enrique.
“Kwahiyo sasa tutakuwa tunaonanaje kwasababu ninakiu nimemiss sana mambo yako mazuri.”
***
“Ni wewe tu bosi kama upo tayari nawezaa nikakuelekeza nilipo ukaja nikakupa dozi ukaondoka kwasabaabu hapa nilipo nipo kwenye nyumba ambayo naishi peke yangu mwenye nyumba anaishi Australia kwahiyo hapa nipo kwaajili ya kuweka mazingira yawe safi nyumba isionekane kama gofu.”
“Poa nitakuja kesho tukae kuanzia asubuhi hadi jioni kwasabaabu huu ugwadu nilionao hata nikija sasahivi sitatosheka.”
“Karibu sana.”
‘Ahsante.”
Nilimaliza kuwasiliana na Fadhili huku nikiwa na furaha sana ndani ya moyo wangu kwasababu sikutegemea tena kumpata mwanaume yule maishani mwangu. Nilifanya kazi kwa furaha sana ile siku kwasababu fadhili aliifanya siku yangu kuwa nzuri kwani nilikuwa nimemmiss kupita kiasi dume lile la mbegu. Kesho yake nilimuaga mume wangu kuwa nakwenda kazini lakini badala yake sikwenda kazini niliwasiliana na hawara wangu na kunipa ramani ya kunifikisha alipokuwa akiishi na nilifika bila hata kupotea.
Saa mbili kamili niliegesha gari langu ndani ya geti alipokuwa akiishi mwanaume Fadhili. Nilifurahi sana kumuona fadhili kwa mara nyingine na yeye alifurahi vilevile. Tulipofika ndani tulianza kupigana mabusu ya nguvu yaliyoashiria kwamba kila mmoja alikuwa amemmiss mwenzie kwa kiasi kikubwa. Hisia za kufanya mapenzi ilizidi kumpanda kila mmoja wetu kwanamna ambavyo tulizidi kujazana mabusu huku tukitomasana taratibu bila papara. Taratibu alianza kuzisasambua nguo zangu moja baada ya nyingine na hatimae nilibaki mtupu. Nje mvua ilianza kunyesha na kusababisha ule mchezo wetu unoge kwa kiasi kikubwa kutokana na hali ya ubaridibaridi uliokuwepo. Tangu saa mbili asubuhi hadi saa saba mchana bado tulikuwa tukipagawishana kitandani. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com
Mchezo ulishindwa kuendelea kunoga kwasababu sote tulihisi njaa kwahiyo niliandaa chakula harakaharaka halafu tukala tukashiba tukarudi uwanjani kuendelea na pambano la kupeana utamu. Mahaba ya siku zile yalikuwa ni ya nguvu kuliko ya siku zote kwasababu kwanza tulipata muda wa kutosha na hakuna aliekuwaa na wasiwasi, akili zetu zote tulielekeza katika ule mtanange wa kukata na shoka. Mchezo ulimalizika jioni kabisa ya saa kumi na mbili tukiwa tumechoka sana kwa namna ambavyo kila mmoja wetu alikuwa na jukumu la kuhakikisha mwenzie anatosheka. Tulikwenda bafuni pamoja kuoga huku kila mmoja akimshukuru mwenzie kwa namna ambavyo alionyeshaa ushirikiano wa kutosha katika kulisakata lile rumba pale kitandani. Japo kuwa mvua ilinyesha siku nzima na kusababisha hali ya hewa kuwa na ubaridi lakini kitanda cha Fadhili kilikuwa kimelowa jasho ambalo lilikuwa likitutiririka pindi tulipokuwa tukipeana mahaba niue.
Wakati nilipokuwa namuaga nilimpatia shilingi laki moja kama kumpongeza kwa jinsi ambavyo alikuwa mstari wa mbele kunipa penzi la dhati ambalo nilikuwa silipati kwa mume wangu wa ndoa. Alifurahi sana na alinitakia kila la heri katika safari yangu ya kurejea nyumbani. Nilifika kwangu nikiwa nimechelewa kuliko siku za kawaida lakini kwa bahati nzuri mume wangu nae hakuwa amerejea nyumbani kwasababu angeweza kuniuliza kwanini ile siku nimechelewa wakati mara nyingi alikuwa ananisisitiza niwe nawahi nyumbani mapema kabla giza halijaingia.
***
Mume wangu aliporejea nyumbani alinikuta nipo chumbani nimejilaza kitandani nimechoshwa na mwanaume ambae kila siku anaumiza kichwa chake namna ya kuweza kumpata lakini niliona itakuwa ni vigumu sana kwa yeye kuweza kumshika kwasababu Fadhili alikuwa katika maficho ya aina yake.
“Pole mpenzi kwa majukumu.” Nilimpa pole Enrique baada ya kufungua mlango wa chumbani na kuingia.
“Asante pole na wewe pia kwasababu unaonekana umechoka pia.”
“Kweli kabisa yani leo wateja walikuwa wananisumbua sana.”
“Usijali komaa mke wangu hakuna kinachopatikana kwa urahisi isipokuwa kupambana.” Enrique aliongea na mimi huku akibadilisha ngua aelekee bafuni kwenda kujimwagia maji kupunguza uchovu. Baada ya kutoka bafuni tuliongozana kwenda sebuleni kupata chakula cha usiku. Japokuwa Fatuma alikuwa ameandaa chakula kizuri ambacho ni chapati kwa mchuzi wa nyama na saladi lakini sikukifurahia kwasababu sikuwa na hamu ya kula kabisa kutokana na uchovu nilikuwa nao, baada ya baba Sweetness kumaliza kula tulikwenda kulala.
Kwanzia siku hiyo penzi letu na Fadhili lilifufuka kwa makeke ya hali ya juu kwani tulizidi kupeana mapenzi kwa siri bila kushtukiwaa na mtu yeyote. Mara kwa mara nilikuwa nikienda kwenye ile nyumba aliyokuwa akiishi kwaajili ya kupata penzi ambalo nilikuwa silipati kwa mume wangu. Baada ya muda biashara ilianza kufifia kwasababu muda mwingi nilikuwa nafunga duka nakwenda kujivinjari na mwanaume yule ambae alikuwa ameiteka akili yangu kwa penzi la nguvu alilokuwa ananipatia. Nilijikuta nimenasa matatizoni baada ya kumkopea milioni 4 ambazo aliniahidi atanirudishia kabla haijafika mwisho wa mwezi lakini ilishindikana na kunisababishia mzozo mkubwa kwa mume wangu pindi alipohoji mapato ya mwisho wa mwezi na kushindwa kumpa maelezo yakuridhisha. Enrique aliguka mbogo kwasababu kulikuwa na shoti ya shilingi milioni 7 ambazo zote nilizichezea pindi nilipokuwa nikijilamba na penzi la hawara wangu.
“Naomba unieleze pesa zimekwenda wapi.” Baba sweetness alipamba moto alipokuwa akihitaji kufahamu pesa za kazi zilipo huku akinikata jicho baya kuashiria kwamba hakupendezwa kabisa na kitendo kile. Nilizidi kumumunya maneno kwasababu sikuwa na namna isipokuwa kumchengachenga kwa kauli zangu ambazo zilikuwa zikigonga mwamba kila wakati kutokana na maswali magumu niliyokuwa nikipokea kutoka kwake.
Amani ilipotea kabisa ndani ya nyumba yangu kwasababu aliniambia kwamba hatutaweza kwenda sawa mpaka nitakapomweleza nilipozipeleka pesa. Nilijuta sana kumuamini na kumkopesha yule hawara pesa nyingi kiasi kile bila kufahamu namna ambavyo atanirejeshea. Nilibanwa zaidi nieleze ukweli nilipozipeleka pesa za biashara lakini sikuthubutu kufungua kinywa changu kumweleza kwamba kuna mtu nilikuwa nimemkopesha kwasababu angekasirika zaidi kwasababu sikumshirikisha halafu pia angehitaji kumfahamu mdaiwa jambo ambalo lingezidi kuniingiza matatizoni.
Kitendo cha kushindwa kumpa mume wangu majibu ya kuridhisha kilisababisha asiishiwe na kisirani cha mara kwa mara ikiwamo kunisusia chakula, kuongea na mimi kwa kifupi, kwa lugha ya ukali na mwishowe hata haki yangu ya ndoa niliikosa kabisa japokuwa haikuwa adhabu kwangu kama alivyokuwa anadhani kwasababu nilikuwa nazidi kupata penzi la maana kutoka kwa mchepuko wangu. Nilimweleza Fadhili hali halisi ya ndoa yangu na kuniahidi kwamba atapambana zaidi ili aweze kuzirejesha zile pesa na hatimae amani irejee katika ndoa yangu. Siku zilizidi kusonga nikiendelea na kazi yangu ingawa nilipunguza matumizi mabaya ya fedha ili niweze kujaribu kuziba lile pengo la milioni 7 zilizokuwa zimepotea katika starehe lakini bado sikufanikiwa vizuri kwasababu pesa zile zilikuwa ni nyingi mno.
Jitihada za baba sweetness kunibana nimweleze ukweli wa pesa zilipo ziligonga mwamba na hatimae alinichukulia poa na maisha yakaendelea ingawa alinisisitiza niwe makini na kazi yangu kwasababu hategemei kilichokuwa kimefanyika kifanyike na siku zijazo na pia alisisitiza kama kuna jambo nahitaji kulifanya nisiogope kumshirikisha kwasababu hawezi kuwa kikwazo kwangu kwasababu mafanikio yangu ni sawa na yake. Nilifurahi sana baada ya mume wangu kunisamehe kutokana na ule upuuzi niliokuwa nimeufanya na nilihapa kutorudia tena.
Nilijituma sana katika kazi yangu ili niweze kupata mafanikio ambayo yatarudisha imani ya mume wangu na kusahau kabisa makosa niliyokuwa nimeyatenda awali. Mara kwa mara nilikuwa nikimkumbusha Fadhili anirejeshee zile pesa lakini ilishindikana baada ya kufilisika kwa biashara ambayo alikuwa ameifungua. Sikuwa na la kufanya niliamua kumsamehe kwasababu pia mume wangu alikuwa ameacha kunisumbua. Penzi letu lilizidi kuota mizizi kwasababu licha ya changamoto nilizokuwa nikikumbana nazo lakini sikuweza kukaa mbali na mchepuko ule kutokana na raha nilizokuwa nikizipata.
Kiukweli Fadhili alikuwa ananifurahisha sana katika mapenzi hadi nikatamani kuhamia kwake kabisa ili nimfahidi vizuri. Moyo wangu ulimpenda sana yule kaka kiasi kwamba ingetokea akatangulia mbele za haki ningeumia zaidi kuliko hata ambavyo ingekuwa kwa mume wangu. Alikuwa masikini wa mali lakini alikuwa ni tajiri mkubwa wa mapenzi, kila siku sikuchoka kumuombea kwa Mungu ampe maisha marefu hapa duniani tuzidi kupeperusha bendera yetu ya mapenzi.
Mume wangu nilikuwa namuona kama kinyago cha kuchoga kwasababu hakuwa na thamani kabisa katika moyo wangu, kama angekuwa ni karata basi angekuwa ni garasha isiyo na thamani katika mchezo. Laiti mtu angekuwa anafahamu kilichopo ndani ya moyo wa mwingine basi mapenzi yangu na Enrique yangefutika kama maandishi ya penseli kwenye karatasi kwasababu moyo wangu ulikuwa unalelewa pengine. Kilichokuwa kinasababisha niendelee kuishi kwa Enrique ni heshima kwa wazazi wangu la sivyo ningetengana nae na kwenda kwa mwanaume aliekuwa anafahamu namna ya kunikuna.
Wakati mwingine nilikuwa najiuliza hivi Fadhili kaniloga au inakuwaje kwasababu baba Sweetness alijitahidi kunifanyia mambo mbalimbali kunifurahisha lakini nilikuwa naona kama anajisumbua kwasababu nilikuwa sifurahii kabisa mapenzi yake kwangu kwasababu hayakuwa na mvuto hata kidogo. Mapenzi ya kweli niliyokuwa nikiyapata kwa hawara wangu yalisababisha moyo wangu ujenge chuki na dharau kwa mume wangu na kumfananisha na mende aliengia ndani ambae anapaswa kukanyagwa afe.
Niliamua kujitoa sadaka liwalo na liwe lakini nipo tayari kufa kwaajili ya Fadhili. Kwahiyo nilizidi kumpenda na kumuheshimu halikadhalika na yeye pia alinipenda na kunijali kuliko kitu chochote.
***CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com
Watoto wangu walikuwa wakiendelea na shule vizuri kabisa bila tatizo lolote na kizuri zaidi ni kwamba kila mmoja baba yake alikuwa amemfungulia akaunti ya milioni 20 kwaajili ya kuwaendeleza kimasomo na hapo haikuwa mwisho kwani Enrique alisema kwamba anahitaji kumtengea kila mtoto bajeti ya milioni 50 ya kumsomesha. Kwahiyo maisha yangu yalikuwa yakienda poa kabisa kwasababu pia tulifungua duka lingine la vipodozi katikati ya jiji na lilikuwa likifanya vizuri zaidi ya lile la kwangu kwasababu ya uwekezaji ukubwa uliofanywa kwa kusudi la kutufikisha pale ambapo tulikuwa tunahitaji kufika katika malengo ya familia yetu.
Siku moja ilikuwa ni siku ya maadhimisho ya kifo cha baba wa taifa kwahiyo siku hiyo mume wangu hakuingia kazini kwake kwasababu ilikuwa ni siku ya mapumziko kwahiyo aliamua kuongozana na mimi hadi ofisini kwangu kwenda kunisaidia katika majukumu yangu. Tulipokuwa kazini kwangu kwenye mida ya saa tisa alasiri maduka matatu yaliyokuwa jirani na kwangu kwa mpigo tulivamiwa na majambazi na kutuweka chini ya ulinzi na kutupora pesa taslimu pamoja na simu. Katika duka langu walinipora milioni 3 naa laki 7 pamoja na simu zetu za gharama.
Sote kwa pamoja tulisikitika na kulaani sana kile kitendo cha kuvamiwa mchana kabisa kibaya zaidi hatukuweza kujihami kwasababu hatukuwa na silaha yeyote, ilibidi tuwe wapole kama maji ya kwenye mtungi wanaume wafanye yao wasepe. Pesa zilizokuwa zimechukuliwa kwa namna moja au nyingine ingesababisha biashara iyumbe kwasababu pesa zenyewe zilikuwa kwenye mzunguko. Kilichotuumiza zaidi ni kwamba ile ilikuwa ni mara ya pili tunavamiwa maeneo yale na kuibiwa, siku ya kwanza walinipora milioni moja na laki moja baada ya kuniweka chini ya ulinzi kimya kimya bila watu kujua kilichokuwa kikiendelea.
Tukio hilo lilisababisha mume wangu apate wazo la kununua silaha kwaajili ya ulinzi wa mali zetu kwasababu biashara zetu zilikuwa zinapanuka kila kukicha.
“Haraka iwezekanavyo naanza utaratibu wa kupata bastola kwaajili ya ulinzi wa mali zangu haiwezekani wapuuzi wakachukua jasho langu kirahisirahisi.” Enrique alizungumza kauli ambayo ilidhihirisha kwamba alichukizwa sana na kitendo kile cha uporwaji wa hadharani.
“Ni wazo zuri mume wangu kwasababu biashara zetu zinakuwa kwa kasi kwahiyo tunahitaji kuwa na ulinzi wa uwakika.”
“Nalifanyia kazi ndani ya wiki hiihii.”
“Sawa.”
Kweli ndani ya muda mfupi alianza kufuatilia utaratibu wa kupata silaha ili aweze kupambana na waalifu wanaomrudisha nyuma katika malengo yake. Haikuwa zoezi gumu kwake kama ambavyo inakuwaga kwa watu wengine kupata silaha ya moto kwasababu aliwai kupita jeshi la kujenga taifa wakati alipokuwa amemaliza kidato cha sita kwahiyo alikuwa anafahamu namna ya kutumia silaha mbalimbali za moto hivyo basi alipata silaha aina ya bastola kwaajili ya ulinzi wa mali zetu jambo ambalo alilifurahia sana na kuniahidi kwamba wezi wazembe wazembe atawatwanga risasi bila huruma. Maisha yalizidi kusonga bila shida yeyote na mambo yalizidi kukaa juu ya mstari kwasababu juhudi zetu zilizidi kutengeneza pesa. Penzi la Fadhili lilizidi kuwa asali na niliona nimpe heshima nyingine ya kumbebea ujauzito mwingine ingawa sikupanga na mume wangu nibebe ujauzito ila niliamua mwenyewe kutoka na mapenzi yangu kwa hawara wangu. Baada ya kujihisi nimeshika ujauzito nilimweleza mume wangu kuwa nina mimba ingawa alishtuka sana kwasababu hakutegemea kuwa nitabeba ujauzito mwingine kwa wakati ule kwasababu hatukuwa tumepanga kama ilivyo kawaida.
***
“Mke wangu watoto wanne wanatutosha kabisa kwahiyo ukishajifungua itabidi tufanye mpango ufunge kizazi usizae tena, ibaki kazi ya kuwalea hawa watoto ambao Mungu katujalia.”
“Hata mimi naona wanne watakuwa wanatutosha.”
“Kwasababu tukiendelea kuzaa hatutaweza kuwatimizia ndoto zao hususani za kielimu.”
“Nimekwelewa kabisa baba Sweetness.”
“Nafurahi kusikia hivyo.”
Tuliendelea kuwa sambamba na mume wangu katika kuilea mimba ambayo tuliona ndio iwe ya mwisho kwangu kwasababu tulikuwa tumejaliwa uzao wa kutosha. Mimba ilizidi kukuwa huku nikiwa na maudhurio mazuri kliniki kuhakikisha kwamba afya yangu na ya kiumbe kilichopo tumboni tunakuwa salama kabisa. Mungu sio Athumani miezi tisa ilijiri na nilijifungua mtoto wa kiume mwenye afya njema kabisa ingawa mume wangu alikuwa safarini kipindi najifungua ila alifurahi sana aliposikia nimejifungua salama tena mtoto wa kiume. Mtoto alifanana na baba yake kwa asilimia kadhaa ingawa sio kwa kiasi cha kuweza kushtukiwa na mtu yeyote kwasababu hakuna aliekuwa anafahamu kilichokuwa kikiendelea kati yangu na yule mchepuko kwani ilikuwa ni siri yangu binafsi kwasababu Fadhili mwenyewe sikumweleza kuwa nimembebea ujauzito. Siku ilifika na Enrique alirejea nyumbani akitokea Zanzibar kikazi na kumkuta mtoto anawiki mbili.
“Hongera sana mke wangu.” Enrique alizungumza huku akimbusu mtoto kwenye paji lake la uso.
“Asante dia.”
“Katoto kazuri sana.”
“Mtanashati kama baba yake.”
“Kweli kabisa jicho hili ni langu kabisa.”
“Umeonae!.”
“Nimeona kabisa asante sana kwa kuniletea simba.”
“Hahah! Acha kumuita mtoto simba.” Tulizungumza na Enrique katika hali ya kutaniana huku nyuso zetu zikiwa zimetawaliwa na furaha ya kumpata mtoto mwingine katika familia yetu. Kama tulivyokuwa tumekubaliana awali kwamba baada ya kujifungua mtoto wa mwisho nifunge uzazi nilifanya hivyo kwa moyo mweupe kabisa kwasababu hata mimi mwenyewe nilikuwa nimeridhika na watoto ambao nilikuwa nao. Enrique aliniletea zawadi nzuri ya simu mpya kabisa ambayo aliinunua Zanzibar.
***CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com
Timu ya watoto ilikamilika, kitinda mimba tulimwita Jordan jina ambalo sote tuliona litamfaa mwanetu. Nilifurahi sana na kumshukuru Mungu kunijalia watoto wazima kabisa wasio na tatizo lolote la kiafya. Baada ya kumaliza uzazi nilirejea katika kazi yangu ya dukani na mambo yaalizidi kwenda muruwa. Wahusianao yangu na Fadhili yaliendelea kama kawaida kwasababu sikuwa tayari kuwa mbali nae kwasababu huwa naumwa pale ambapo anakuwa mbali na mboni za macho yangu kwa muda mrefu.
Bila hiyana nilizidi kumfaidisha vilivyokuwa vikigharamiwa na bosi wake wa zamani kwasababu moyo wangu ulikuwa umemzimikia balaa. Siku moja baada ya mwaka mmoja na nusu niliaga nakwenda kazini kumbe haikuwa kweli nilikwenda kwa mchepuko wangu kujizolea raha kama kawaida yangu. Ilikuwa imepita muda kidogo bila kupata nafasi ya kukutana nae kutokana na ubize wa kazi kwahiyo iyo siku nilikuwa ninahamu nae kupita maelezo.
Penzi lilininogea nakujikuta nang’atuka saa moja na nusu jioni bado nipo kitandani kwa Fadhili nilianza kuhaha nitakwenda kumdanganya vipi Enrique aweze kunielewa kwasababu huwa hapendi kabisa mambo ya usiku. Niliteremka kitandani haraka haraka mithili ya mtu aliechanganyikiwa na kwenda bafuni kuoga fastafasta na kurudi chumbani kuvaa nguo na kuondoka huku nikiomba Mungu atende muujiza nikute Enrique hajarudi nyumbani hadi muda ule. Simu yangu nilikuwa nimeizima na sikuthubutu kuiwasha kwasababu zingemiminika meseji za mume wangu ambazo zingenichanganya zaidi.
Hakuna siku niliyoendesha gari langu kwa mwendo kasi kama ile siku tangu niliponunuliwa, nilikanyaga mafuta sawasawa ili niweze kuwai nyumbani kwangu. Saa mbili na dakika kumi na tano nilipiga honi getini kwangu ili niweze kufunguliwa niweze kuingia ndani.
“Pipiiiii.”
“Pipiii.”
Nilipiga honi kwa fujo baada ya kuona mlinzi anachelewa kunifungulia geti niingie ndani. Mapigo yangu ya moyo yalizidi kunienda mbio huku nikisali kimoyomoyo nisikute mume wangu kafika nyumbani lakini maombi yangu yalikuwa ni kama sehemu ya kujipa moyo kwasababu kwa kawaida mume wangu huwa anarejea nyumbani mapema.
“Pipiiiii.” Nilizidi kupiga honi bila kufunguliwa geti.
“Huyu mpumbavu yupo wapi.” Nilijikuta nazungumza peke yangu kwa hasira baada ya mlinzi kuchelewa kunifungulia.
Ghafla mwili wangu ukaanza kutetemeka huku joto langu la mwili likipanda kwa kasi sana mithili ya mtu alieshikwa na malaria kali baada ya kushuhudia mume wangu ndie ananifungulia geti ili niweze kuingia ndani kwa muda ule jambo ambalo si la kawaida.
“Uuwii nimekwisha.” Nilijisemea kimyakimya huku nikizidi kuvuja jasho kwa hofu iliyokuwa imeniingia ndani ya muda mfupi. Nililiingiza gari taratibu na kwenda kuliegesha katika sehemu maalumu ya kuegesha magari pale nyumbani kwangu halafu nikateremka na kukutana na sura ya mume wangu ikiwa imekunjamana kupita kiasi ikionyesha kwamba alikuwa amechukizwa sana na kitendo cha kurudi nyumbani usiku hivyo nilizidi kutetemeka kwa kukosa kujihamini kwasababu nilikuwa nimeshamkosea mume wangu.
“Pole sana mama Sweetness.” Sauti ya mume wangu iliyokuwa imeambatana na macho ya ukali ilisikika ikinipa pole japo kuwa hakuwa akimaanisha kweli kunipa pole kwa majukumu yangu ya siku nzima bali alikuwa ananikejeli.
“Samahani mume wangu gari liliniaribikia njiani ndio maana nimechelewa kurudi.” Nilianza kujitetea kwasababu sura ya mume wangu ilikuwa inaonyesha kuwa tayari nimeshachafua hali ya hewa.
“Kwanini simu yako haipatikani?”
“Imezima chaji.”
“Kwahiyo umekosa kabisa namna ya kuweza kuwasiliana na mimi kunijulisha kuwa umepata matatizo.”
“Ndio.”
“Kazini uliondoka saa ngapi?”
“Saa kumi na moja.”
“Unauwakika?”
“Ndio ninauwakika mume wangu mbona maswali hayo jamani.”
“Leo duka ulifungua saa ngapi?”
“Saa mbili asubuhi.”
“Pole sana kwa majukumu ya kutwa nzima.”
“Ahsante.”
“Naomba twende ndani tukazungumze vizuri kwasababu nahisi maelezo yako hayajanitosheleza hata kidogo.” Niliongozana na Enrique huku nikiwa nimeshachoka kwa maswali aliyokuwa akiniuliza wakati nilipoteremka kwenye gari. Nilipoingia ndani nilimsalimia dada wa kazi ambae alikuwa jikoni anapika, pamoja na mwanangu Sweetness ambae alikuwa sebuleni anajisomea baada ya hapo nikapitiliza moja kwa moja hadi chumbani ambapo niliingia na mlango ulifungwa kwa ufunguo jambo ambalo lilinipa hofu kidogo nikawaza lazima nichezee kichapo cha kuchelewa nyumbani kwasababu nimeonywa mara nyingi bila kusikia.
“Sasa nilisikilize vizuri kwa hali ya amani kabisa, tena bila kukwaruzana wala kuumizana naomba unipe maelezo yaliyojitosheleza kuhusu uliposhinda siku ya leo kwanzia asubuhi ulipoaga unakwenda kazini hadi muda huu unarejea nyumbani kwangu usiku.”
***
“Haah! Nilikuwa kazini jamani.”
“Usinifanye mtoto mdogo nahitaji unieleze ukweli halisi kabla sijageuka chui nikurarue hiyo sura yako sasa hivi.” Enrique alizungumza kwa sauti ya chini huku akionekana kuwa na hasira sana.
“Asubuhi nilikuaga nakwenda kazini na ndio huko nilipotoka mda huu.”
“Usijifanye unakichwa kigumu kuelewa nakuuliza kwa upole sana naomba usiniudhi kwasababu naweza nikakuumiza.” Maneno ya baba sweetness yalinitia wasiwasi kwa kuhisi pengine labda alikuwa tayari ameshafahamu kuwa sikushinda dukani kwangu.
“Sasa nimdanganyaje.” Ubongo wangu ulishindwa kutunga uongo wa kumdanganya baba watoto wangu aweze kunielewa kwahiyo nilikaa kimya kwa unyonge kana kwamba alikuwa ananisingizia jambo ambalo sikulitenda.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com
“Kukaa kwako kimya sio sababu ya kunizua kushindwa kuendelea kutaka kufahamu ukweli kutoka kwako.”
“Kweli nimeshinda kazini kwangu.” Ilinibidi niendelee kushikilia msimamo wangu bila kutetereka kwasababu sikuwa na namna nyingine ya kuweza kumuongopea ili aweze kunielewa.
“Nakuuliza kwa mara ya mwisho ulikuwa wapi kutwa nzima ya leo?” Alizidi kunikomalia nimweleze jambo linaloeleweka kwasababu nilikuwa nababaika babaika kujieleza, baada ya kuona nimeshindwa kumshawishi anielewe ilinibidi nianze kudondosha machozi ili aweze kunionea huruma kwasababu ni kweli ndege mjanja nilikuwa nimenasa kwenye tundu bovu.
Machozi yangu ndio yaliharibu kabisa kwasababu yalipelekea nikapokea kofi moja iliyoshiba kutoka kwa mume wangu ambayo ilinifanya nipepesuke kama kuku anaekatwa shingo na kuanguka chini huku nikiona nyotanyota nyingi mbele yangu.
“Kwa hasira nilizonazo nikisema nakupiga naweza nikakuua kabisa kwahiyo naomba usiendelee kunishawishi niendelee kuunyanyua mkono wangu kukupiga.”
“Kweli nakuapia kwa jina la Mungu nilikuwa dukani.”Nilijitahidi kuhapa ili aweze kunielewa kwasababu niliona akinipiga kofi lingine anaweza kunizimisha kabisa kwasababu kofi moja tu liliniachia maumivu makali pamoja na michirizi ya vidole vyake shavuni mwangu na pia nilihisi dunia inazunguka na masikio yaliziba ghafla.
Ubishi wangu ulisababisha mume wangu aendelee kunishushia makofi mazito katika mashavu yangu na kusababisha damu kuanza kunivuja puani lakini haikuwa sababu ya yeye kuacha kuendelea kuniadhibu badala yake alibadili mfumo nakuanza kunishushia mangumi na mateke kimya kimya tukiwa chumbani, kilio changu hakikuweza kufika popote kwasababu nilikuwa nikilia kwa kwikwi kwani aliniambia nikijaribu kufungua mdomo wangu kupiga mayowe ataniua kwahiyo nililia kwa sauti ya chini kutokana na maumivu makali niliyokuwa nikihisi.
***
Ama kweli ile siku ndio niliamini kuwa njia ya mwongo ni fupi na pia lakuvunda halina ubani kwasababu njia zote nilizojaribu kujitetea nazo ziligonga mwamba kwani nilizidi kukumbana na maswali mengine mazito kutoka kwake na kushindwa kutoa majibu ya kueleweka kibaya zaidi ni kwamba mkong’oto ulivyozidi kupamba moto ndivyo nilivyozidi kutoa sababu tofautitofauti ambazo ndio zilisababisha anione namdanganya.
“Leo nakuuwa.” Alizidi kunipiga vibaya mno huku akinitolea maneno ya vitisho. Baada ya kuona alikuwa anamaanisha kweli kwamba anataka kuniua niliona nibora nipige kelele kuomba msaada kwasababu alikuwa ameshanipiga kwa muda mrefu na kuniumiza vibaya sana.
“Yeleuwiiii.”
“Uwiiiiiii.” Nilifanikiwa kuangua ukunga mara mbili kwa sauti ya juu sana lakini nilishindwa kuendelea kwasababu alinipiga teke la kwenye mbavu nikaanguka chini nikashindwa kulia wala kufanya chochote kwasababu nilikuwa napumua kwa shinda sana.
Niliona ule ndio mwisho wa maisha yangu kwasababu alinipiga vibaya sana, kwa bahati nzuri sauti ya kuomba msaada iliwafikia Fatuma na mwanangu ambao walikuja kwa kasi katika uelekeo wa chumba changu lakini kwa bahati mbaya waliishia mlangoni kwasababu mlango ulikuwa umefungwa kwa ufunguo.
“Dada.” Fatuma aliniita wakati alipokuwa akigonga mlango wangu wa chumbani huku nikimsikia mwanangu akilia kwa uchungu baada ya kuhisi kwamba mama yake sikuwa salama kwasababu ya kelele nilizokuwa nimepiga ndani ya muda mfupi uliopita na kunyamaza kimya.
Sikuweza kuzungumza chochote kwasababu nilikuwa nikipumua kwa taabu sana huku macho yakinitoka mithili ya panya alienaswa na mtego kutokana na teke alilokuwa amenipiga na kunisababishia maumivu yasiokuwa na mfano. Baada ya mume wangu kuona wale watoto wanasumbua pale mlangoni aliamua kufungua redio kwasauti ya juu kabisa kusudi wasiweze kufahamu kabisa kilichokuwa kikiendelea mule chumbani kwangu.
***
Enrique alinipiga hadi akachoka ikabidi aniache kwasababu niligoma katakata kumweleza nilipokuwa nimeshinda kwa siku nzima kwasababu ningejaribu kufanya hivyo ndoa yangu ingevunjika na pengine angeweza kuniumiza zaidi kwasababu huwa ananipa kila kitu ninachotaka ili penzi letu liimarike lakini ilinibidi niwe sambamba na Fadhili ambae ndie alikuwa ananiridhisha kitandani kuliko yeye. Aliniumiza sana ile siku kwasababu nilipoteza fahamu mara mbili na kila nilipokuwa nikizinduka alizidi kunishushia kipigo kikali sana ambacho kilinisababishia majeraha yaliyoambatana na maumivu makali mno mwilini mwangu.
Mara ya pili nilipopoteza fahamu nilikuja kuzinduka saa kumi alfajiri nimelalaa sakafuni sijiwezi damu zimenitapakaa kwenye nguo zangu kutokana na majeraha makubwa yaliyokuwa yakivuja damu kutokana na ubabe wa mume wangu. Nilijionea huruma sana kwasababu nilikuwa nimeumia sana halafu mwili wangu haukuwa na nguvu kabisa. Kwa wakati huo Enrique alikuwa amelala kitandani anakoroma, niliamua kutumia nafasi hiyo kwenda bafuni kuoga kwasababu nilikuwa nanuka damu sana. Baada ya kutoka kuoga nilirudi chumbani kwangu na kuwasha simu yangu kwasababu nilikuwa nimeizima kwa takribani siku nzima wakati nilipokuwa nikijivinjari na penzi la hawara wangu. Jumbe fupi za maandishi zilianza kumiminika katika simu yangu kutoka kwa watu mbalimbali lakini nilishtuka kidogo baada ya kukutana na meseji kibao za wafanyabiashara mbalimbali ambao walikuwa wananitaharifu kuwa moto ulikuwa unateketeza fremu za biashara katika ile nyumba yangu ya biashara kwahiyo walikuwa wananitaka nikafungue ili wajaribu kunisaidia kuokoa baadhi ya mali kwasababu moto ulikuwa umeanzia chumba cha jirani. Mwili ulipoteza nguvu kabisa baada ya kusoma zile jumbe fupi za maandishi ambazo zilikuwa zinamiminika kwa fujo kuingia kwenye simu yangu na kibaya zaidi meseji hizo zilikuwa zimetumwa mida ya saa nne asubuhi siku ya tukio wakati simu yangu ilipokuwa imezimwa nikiwa kwa mchepuko nachepuka.
“Ahaa kwahiyo itakuwa baada ya kunikosa hewani ndio wakaamua kumpigia mume wangu kumtaarifu kilichokuwa kikiendelea kule dukani.” Niliwaza huku nikijiona mjinga kwa jinsi nilivyokuwa nikidanganya nilikuwa dukani kumbe sio.
“Sasa duka litakuwa salama au ndio litakuwa limeteketea kwa moto.” Nilizidi kujiuliza maswali mengi akilini mwangu ambayo yalizidi kuniumiza akili yangu kwasababu sikuweza kupata majibu sahihi.
Palipokucha asubuhi Enrique alijiandaa na kwenda kazini bila kuzungumza na mimi kitu chochote. Kutokana na maumivu niliyokuwa nikihisi mwilini mwangu niliamua kwenda kwenye duka la dawa la rafiki yangu Doroth nikapate matibabu. Baada ya kutibiwa nilirudi nyumbani kwangu kupumzika kwasababu sikuwa nikijihisi vizuri kabisa kiafya. Jioni ilipofika mume wangu alirejea nyumbani lakini hakuzungumza na mimi kitu chochote zaidi sana alikuwa akiongea na kucheka na mwanae pamoja na dada wa kazi. Nilijitahidi kumuomba radhi mume wangu ili aweze kunisamehe lakini aliniambia hawezi kunisamehe wakati hafahamu kosa langu ni lipi kwahiyo alinitaka nimjuze kwanza kosa langu ndio anisamehe la sivyo alihapa kutokuwepo kwa amani ndani ya ndoa yangu. Nilizidi kuwa katika wakati mgumu kwani maelewano kati yangu mimi na mume wangu yalizidi kwenda mrama.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com
Nilikosa amani kabisa na nilifahamu kuwa nilikuwa nimemkosea sana mume wangu baada ya kugundua kuwa duka lote lilikuwa limeteteketea kwa moto na kilichoniuma zaidi ni kwamba ndani ya duka kulikuwa na pesa taslimu milioni 9 ambazo sikuzipeleka benki kwa uzembe wangu mwenyewe kwasababu mume wangu alikuwa ananiambia mara kwa mara nisikae na pesa zaidi ya milioni mbili dukani ila nilikuwa sisikii. Kwajinsi mume wangu alivyokuwa ameamua kunichunia nilikonda na kunyong’onyea kabisa kwasababu sikujua alikuwa ananiwazia nini kichwani mwake kwasababu huwa ananiangalia kwa jicho baya kila mara. Baada ya kutimu mwezi wa tatu pasipo maelewano mazuri baina yangu na mwenzi wangu niliona niwashirikishe marafiki zangu wa karibu ili waweze kunisaidia namna ya kuweza kupata suluhisho. Wengi waliniambia nirudi nyumbani kwa wazazi wangu kwasababu huyo mwanaume anaweza kuniua ila nilipata wazo la tofauti kabisa kutoka kwa rafiki yangu Glory kwani aliniambia nimuendee kwa mganga nikamtengeneze. Nililifurahia wazo lake kwasababu lilikuwa ni wazo la kunifanya niendelee kuwepo nyumbani kwa mume wangu tofauti na lile la kurejea nyumbani kwa wazazi.
Rafiki yangu aliniahidi kunisindikiza kwa mganga nikapate dawa ya kumtengeneza mume wangu ili tuweze kwenda sawa kwasababu kwa muda mrefu hapakuwa na maelewano baina yangu na yeye jambo ambalo lilinifanya nikonde kwa kukosa amani ndani ya moyo wangu ingawa mimi ndie nilikuwa nimemkosea lakini nilitamani tumalize ule mzozo kimyakimya bila kufika kwa wazazi au watumishi wa Mungu. Nilifurahi sana baada ya Glory kuniahidi kunisindikiza kwasababu sikuwahi kwenda kwa mganga tangu nizaliwe na wala sikuwahi kufikiri kwamba ipo siku nitakwenda kutafuta msaada kwa mganga wa kienyeji.
Nilipanga siku ya kwenda iwe ni siku ambayo mume wangu atakuwa kazini kusudi asiweze kugundua kuwa nilitoka. Ingawa nafsi yangu ilikosa amani kabisa mara baada ya kupata wazo la kwenda kwa mganga kutafuta suluhisho la matatizo yangu ila nilijipa moyo kwamba nitakapopata suluhisho la lile tatizo sintakaa nitie mguu wangu kwa mganga kwa mara nyingine tena.
Siku moja ya jumatatu mida ya saa tano asubuhi baada ya mume wangu kwenda kazini nilimuaga dada wa kazi kwamba ninakwenda nyumbani kwetu kuwasalimia wazazi wangu. Nilifanya hivyo ili hata ikitokea mume wangu akawahi kurudi na kunikosa nyumbani asiweze kunihisi vibaya. Niliwasha gari langu kwenda kukutana na Glory maeneo ya Impala Kijenge ambapo ndio alikuwa ananisubiri baada ya kuteremka kwenye daladala kutokea nyumbani kwao moshono.
Nilipofika nilimchukua na kwenda kwa mganga ambae alinieleza kuwa anaitwa Mbengwa, kiukweli nilishawishika sana kwasabaabu tulipokuwa kwenye gari kuelekea huko alikuwa akimmwagia sifa kedekede kwamba ni kiboko hajawai kushindwa na kitu chochote. Nilitamani sana nifike nishuhudie ufundi wa huyo mtu ambae nilizipata sifa zake tangu siku ya kwanza tulipopata wazo la kwenda kwake.
Gari lilizidi kusonga kuingia mtaa ya ndani ndani Ungalimitedi uswahilini moyo wangu ulikuwa na hofu sana ingawa nilijitahidi kujikaza kwa kujichekesha chekesha kwa rafiki yangu ili asiweze kunishtukia kwasababu angekasirika na kuniona kigeugeu na pengine kwa wakati mwingine asingekubali kunisaidia kama ningekuwa wa kubadilika badilika kama kinyonga.
“Mh hivi kweli ndio nakwenda kwa mganga?” niliwaza huku nafsi yangu ikihisi kukosa amani kwa kiasi kikubwa mno.
Saa sita kasoro niliegesha gari katika mtaa mmoja wa uswahilini ambao ulikuwa na nyumba nyingi sana. Tuliteremka kwenye gari na kuanza kutembea harakaharaka kupita kwenye uchochoro mmoja ambao ulikuwa na harufu kali ya mkojo na kutokea upande wa pili wa mtaa.
“Gari langu litakuwa salama kweli?” nilimuuliza rafiki yangu baada ya kuona tumeliacha mbali kidogo kwasababu hapakuwa na barabara ya kupita gari.
“Usijali lipo salama kabisa wala usijali kwasababu pamoja na kwamba huu mtaa ni wa uswahilini lakini hakuna wezi kutokana na uwepo wa waganga mbalimbali kila kona.”
“Unauwakika lakini shosti yangu?”
“Ondoa shaka.”
***
“Basi sawa kwasababu lisije likatokea la kutokea nikakuta gari langu limechokonolewa na vibaka wa mtaani kwasababu nitakuwa nimeongeza tatizo juu ya tatizo.”
“Poa.”
Baada ya mwendo wa kama dakika kumi tulifika kwa mganga ila kwa bahati mbaya hatumkuta nyumbani ila tulichukua namba za simu zilizokuwa zimebandikwa mlangoni na kuwasiliana nae na kutujuza kwamba yupo njiani anakuja kutokea kutafuta dawa. Tulikaa kwenye benchi lililokuwepo pale nje kwake kumsubiri arudi ili aweze kunisikiliza na kunisaidia katika matatizo niliyokuwa nayo.
“Shoga angu basi hapa ndio kwa yule mtaalamu niliekuwa nikikusimulia.”
“Nimefurahi kupafahamu.”
“Ngoja aje uone mambo yake yalivyo supa.”
“Sawa mwaya.”
Lisaa limoja baadae mganga alifika na kutukuta tumekaa kwenye benchi tunamsubiri kwa hamu ili aweze kutusaidia na hatimae turejee majumbani kwetu mapema. Nilishangaa kumwona mganga kwasababu kwa muonekano wa nje huwezi kujua kama anajishuhulisha na kazi ile kwani uvaaji wake ni wa kawaida sana. Tuliingia ndani baada ya kuruhusiwa ambapo napo palionekana pa kawaida sana na hapakuwa na vitambaa vya rangi yeyote kama nilivyozoea kuona kwenye filamu na wala mganga hakujipaka kitu chochote usoni cha kumfanya awe na muonekano wa kutisha. Ila mule ndani kulikuwa na mishumaa miwili inayowaka pamoja na kifuu kilichokuwa kikifuka moshi uliokuwa ukitoa harufu kali ya dawa zake. Alitukaribisha tukae kwenye mkeka uliokuwa umetatikwa chini wakati yeye akiwa amekaa kwenye kigoda kilichokuwa mbele yetu akiwa kifua wazi.
Nilitaharuki na kumuona mganga sio mtu wa kawaida kama nilivyokuwa nadhani baada ya kunieleza tatizo lililokuwa limenipeleka pale nyumbani kwake bila ya mimi kufungua mdomo wangu kumweleza sababu ya kumwendea.
“Duuh! Kafahamu vipi jamani wakati mambo mengine sikuwahi kumshirikisha mtu yeyote.” Niliwaza huku nikianza kuogopa kutokana na jinsi ambavyo mganga alikuwa akinieleza mambo yangu kwa ufasaha wa hali ya juu kana kwamba niliwahi kumshirikisha.
“Usiogope binti tatizo lako naweza kulimudu.” Alizungumza mganga huku akikizungusha kibuyu kilichokuwa na shanga nyingi kuzunguka kichwa changu huku akiimba wimbo ambao maneno yake nilishindwa kuyaelewa.
“Tawire.” Niliitikia kwa moyo mmoja baada ya kusikia kwamba tatizo langu linawezekana kutafutiwa ufumbuzi.
“Nahitaji shilingi laki 2 pamoja na jogoo wa pinki.” Nilishtuka sana baada ya kusikia anahitaji nimpe jogoo wa rangi ile wakati siwahi kumwona tangu nizaliwe.
***CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com
“Naomba nikulipe pesa unisaidie kumtafuta jogoo wa rangi hiyo.”
“Elfu thelasini.” Alinitajia bei huku akicheka kicheko ambacho kilinitia woga na kunifanya nitetemeke kwasababu mambo yale yalikuwa mageni kwangu.
“Hakuna tatizo mtaalamu.” Nilizungumza wakati nafungua mkoba wangu kutoa pesa zilizokuwa zinahitajika kwaajili ya kutengezeza dawa ya mume wangu. Sikujali kuhusu pesa kwasababu nilikwenda na pesa za kutosha ambazo nilizidroo kutoka kwenye akaunti yangu ya M-pawa ambayo ilikuwa na shilingi laki nane.
“Safi sana binti, sema haraka unataka mume wako aweje.”
“Nataka anipende na kunijali sana na pia nikimwambia jambo lolote anisikilize na kunielewa.”
“Hadi hapo nimeshakuelewa.”
“Tawire.”
Mganga aliniambia nikinge mikono yangu mithili ya mtu ambae anasubiri kupokea kitu huku akifungua mifuko yake na kutoa dawa na kukitia katika kifuu kilichokuwa kikiendelea kuwaka baada ya hapo alizidi kuimba nyimbo ambazo hazieleweki huku akiita jina la mume wangu mara tatu. Ghafla nilitamani kukimbia mara baada ya taswira ya mume wangu kutokea katika viganja vyangu vya mikono nilivyokuwa nimevikinga. Nilianza kutetemkeka kwa hofu kwasababu nilikuwa namwona mume wangu mubaashara (live) bila chenga akiwa ananitazama.
“Sasa binti mnenee mume wako mambo ambayo unataka akutendee katika maisha yako ili kukufurahisha.”
“Tawire.”
“Enrique kwanzia leo nataka unipende mara dufu, unijali na kuniheshimu kama mkeo, chochote nitakachotaka basi unitimizie bila kigugumizi wala kuangalia ndugu jamaa na majirani wanasemaje.”
“Rudia mara tatu.”
“Tawire.” Nilifanya kama mganga alivyonielekeza na baada ya hapo taswira ya mume wangu ilifutika ghafla viganjani mwangu.
“Umefanya vizuri sana.”
“Tawire mtaalamu.”
“Shika dawa hii ambayo utapaswa umchanganyie mumeo kwenye chakula cha jioni ila uwe makini kwasababu chakula hicho kitakachokuwa kimetiwa hii dawa hatakiwi mtu yeyote aweze kukila tofauti na mlengwa. Lakini pia nakupa hirizi hii ambayo utapaswa kuificha katika chumba mnacholala wote na haitakiwi kuonekana na mtu mwingine yeyote isipokuwa wewe pekee. Sina la ziada isipokuwa nawatakia kila la heri katika mahusiano yenu.” Mganga alizungumza baada ya kunikabidhi dawa na hirizi ambazo zilikuwa na masharti makali ya matumizi.
***
“Ahsante sana.” nilizungumza wakati nilipokuwa nanyanyuka ili niweze kuondoka kurejea nyumbani kwangu. Saa nane na robo kila kitu kilikuwa kimekwisha hivyo tuliongozana na rafiki yangu hadi kwenye gari langu ambalo tulilikuta salama kama ambavyo niliahidiwa na Glory. Nililiwasha na tulianza safari ya kurejea nyumbani.
“Shoga angu uwezi amini nilishtuka sana sazile baada ya kuona taswira ya Enrique pale kwa mganga.”
“Nilikuona ulivyokuwa umeshtuka.”
“Kwahiyo unataka uniambie kwamba mume wangu atakaporudi jioni nitaona mabadiliko?”
“Nakwambia huyu mganga ni moto wa kuotea mbali we mwenyewe utakubali.” Glory alizidi kumwagia sifa yule mganga utafikiri ni Mungu.
“Mh! sawa bwana tusiandikie mate angali wino upo jioni haipo mbali.”
“Tuliza presha mtoto wa kike mwanaume yupo kiganjani mwako sasa hivi chochote utakachomweleza nilazima akusikilize, hata ukimwambia akununulie meli atajitutumua hadi atimize lengo.”
“Nitafurahi sana kwasababu sitaki tena kuendeshwa na mwanaume.”
“Mambo ya kizamani kupelekeshwa na mwanaume sasa hivi hata sisi tunaweza kuwa vichwa vya familia bwana wanawake tuheshimiwe jamani.” Glory alizidi kufunguka kuhusu hisia zake juu ya wanaume ambao wamezoea kunyanyasa wanawake kwa madai kwamba wao ndio vichwa cha familia. Tulizungumza kwa kucheka kwa furaha sana wakati tulipokuwa kwenye gari kuelekea nyumbani tukitokea kwa mganga. Hatukuweza kupitia sehemu nyingine yeyote kwasababu muda ulikuwa umekwenda sana kwahiyo nilimfikisha mwenzangu sehemu ambayo ataweza kupata usafiri wa kumpeleka moja kwa moja hadi nyumbani kwao na kumpatia shilingi elfu ishirini kama shukrani na mimi nilielekea nyumbani kwangu.
Saa tisa kamili nilifika nyumbani kwangu na kukuta kila kitu kinakwenda shwari nilitumia ule muda ambao mume wangu hakuwepo kwenda chumbani kutafuta sehemu nzuri ya kuficha ile hirizi ambayo nilikuwa nimepatiwa kwa sharti la kutoonekana na mtu yeyote. Nilikwenda kuificha katika begi langu la nguo nikiamini kwamba sio rahisi mume wangu kupekua katika begi langu. Baada ya kuhakikisha nimeiweka katika sehemu ambayo ni salama kabisa nilikwenda kumweleza Fatuma kwamba asiandae chakula cha jioni kwasababu ile siku nilikuwa nataka nimsaidie. Ufundi wa yule mganga ulianza kujidhihirisha jioni mida ya saa kumi na mbili nikiwa jikoni naandaa chakula nilishangaa kumuona mume wangu karejea nyumbani huku akiwa ameninunulia mkufu wa dhahabu ambao ulikuwa mzuri sana. Enrique alionesha kuwa na furaha sana na mimi kana kwamba sio yeye ambae asubuhi alipoamka kitandani hakunisemesha. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com
“Mh! kweli yule mganga sio mtu wa mchezo mchezo.” Niliwaza baada ya kushuhudia upendo wa mume wangu ukiwa umefufuka kwa kasi ambayo sikutegemea kabisa.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment