Search This Blog

Thursday, July 21, 2022

LAITI NINGEJUA - 2

 







    Simulizi : Laiti Ningejua

    Sehemu Ya Pili (2)



    ILIPOISHIA...

    “Ninyi wanawake mimi nawafahamu vizuri sana nitabia yenu mkishaolewa mnakuja kuharibu uhusiano wa mume na ndugu zake jambo ambalo sintaweza kulivumilia hata japo kwa sekunde moja, kama huwezi kuelewana na ndugu zangu hata mimi utakuwa unanidanganya vilevile kwahiyo mimi nakushauri ufungashe virago vyako uondoke nyumbani kwangu siwezi kuendelea kuishi na wewe kwa mtindo huu.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    ENDELEA

    Mume wangu alizungumza na mimi kwa kunikazia macho baada ya kushuka kwenye gari wakati tulipokuwa tumetoka hospitali.

    Sikuweza kuzungumza chochote kwasababu nilikuwa nahisi uchungu mkubwa ndani ya moyo wangu kutokana na uwamuzi aliokuwa ameamua Enrique mwanaume ambae nilimwamini sana kipindi tulipokuwa kwenye uchumba kumbe alikuwa amejivika ngozi ya kondoo kumbe ndani mbwa mwitu.

    Tulifika ndani na muda huohuo alianza kunisaidia kupaki nguo kwenye begi ili niweze kuondoka ingawa nilikuwa njia panda kwamba naondoka kwasababu nimemdharau mama yake au naondoka kwasababu nimeshindwa kumzalia mtoto? Niliwaza bila kupata jibu.

    “Ni bora urudi kwa baba yako ndie ataweza kuvumilia huo upumbavu wako, nikiendelea kukaa na wewe unaweza kufia kwenye mikono yangu. Na ukifika kwenu uwe huru kabisa akijitokeza mwanaume mwingine atakaekosea njia kama mimi wewe mkubalie muoane kwasababu mimi sina habari tena na wewe nitamwoa mtoto mbichi zaidi yako wala hainipi shida.” Mume wangu alizidi kuzungumza na mimi maneno ambayo yalinipa maumivu makali zaidi ya tindikali.

    Hivi kwanini huyu mwanaume amebadilika kiasi hiki, inamana watu wote walioko kwenye ndoa ndio wanaakumbana na magumu ninayopitia mimi? Au tuseme basi ananinyanyasa kwasababu anafahamu kuwa kwetu masikini ndio maana. Siwezi kuendelea kuvumilia kwasababu hata kama kwetu kuna dhiki alinikuta naishi.” Niliwaza.

    “Hakikisha unachukua kila kilicho chako usije ukafika huko ukarudisha makanyagio hapa ukasema kunakitu umesahau nitakuvunja shingo.”

    Baada ya kumaliza kufungasha nilichukua begi langu na kutoka nje ili niweze kuondoka.

    “Wasalimie nyumbani waambie maisha ya kwa mume yamenishinda.” Hayo ndio maneno aliyonipa mume wangu kuniaga wakati nilipokuwa nafungua mlango niweze kuondoka nyumbani kwake.

    Kilichoniumiza zaidi ni kwamba nauli ya kwenda hadi nyumbani kwetu kutokea pale kwa Enrique ni shilingi 800 lakini mwanaume yule bila hata chembe ya huruma hakunipatia hata shilingi 50 aliniambia nitembee kwa miguu ndio nitapata akili. Nilisikitika sana kwasabaabu sikuwa hata na shilingi mfukoni mwangu kwahiyo ilinibidi nitoke niende hadi kwa Doroth nikamuombe nauli ya kunifikisha nyumbani kwetu.

    Kwa bahati mbaya sana nilipofika dukani kwa Doroth sikumkuta na nilipojaribu kupiga namba yake ya simu haikupatikana hewani kwahiyo sikuwa na jinsi isipokuwa nilichukua begi langu na kuliweka kichwani na kuanza kutembea uelekeo wa nyumbani huku machozi yakinitoka kama mtu aliefiwa kutokana na uchungu uliokuwa umetanda moyo wangu.

    Nilianza kutembea kuanzia nyumbani kwangu njiro kwa msola hadi nikafika chuo cha uhasibu Arusha mkabala na kampuni ya Tanzania wildlife research institute (TAWIRI) nikapumzika kwasababu nilikuwa nimechoka sana na pia mwili wangu wote ulikuwa na maumivu kutokana na kipigo nilichokuwa nimekipata.

    Wakati nilipokuwa nimekaa kwenye kalvati moja kandokando ya barabara nikisubiri nipate nguvu kwa mara nyingine ili niweze kuendelea na safari ilikuja gari moja nzuri sana yenye vioo vyeusi na kusimama kando yangu na nilishuhudia kioo cha upande wa dereva kikishuka taratibu macho yangu yakamuona mama mmoja wa makamo alionekana kujiremba kama binti.

    “Pi piiii.” Alinipigia honi ili niweze kusogea pale katika dirisha la gari yake na mimi bila hiyana nikaona ngoja nikamsikilize yule mama alikuwa anataka nini kwangu.

    “Shkamoo.”

    “Marahaba binti hujambo?”

    “Sijambo.”

    “Mbona umekaa barabarani peke yako.?

    “Napumzika tu mama.”

    “Halafu mbona unaonekana kama unamajeraha mwilini mwako kwani unamatatizo gani.”

    “Hamna nipo vizuri kabisa nilipata ajali ya bodaboda.”

    “Umetokea wapi unakwenda wapi?”

    “Nimetokea kwa msola naelekea moshono.”

    “Kwa miguu?”

    ***

    “Ndio.”

    “Mh we binti kuna usalama kweli uko ulipotoka?”

    “Ndio.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    “Lengo la mimi kukufuata hapa ni kwamba nahitaji nifahamu unashida gani ili nikusaidie, kwasababu unaonekana kabisa kuwa unamatatizo, au kama ulikuwa unafanya kazi nyumbani kwa mtu akakufukuza wewe nieleze kwasababu tunaweza kwenda hata nyumbani kwangu kutokana na kwamba ninashida ya mfanyakazi wa ndani.”

    “Hapana mimi sio mfanyakazi wa ndani bali ni kwamba nimegombana na mume wangu ndio maana nimeamua kurudi nyumbani kwetu.” Nilizungumza kwa hisia sana.

    “Masikini pole sana, inamana huyo mwanaume ndie kakupiga namna hiyo?”

    “Ndio.”

    “Kwani umemfanyaje?”

    “Kwasababu tumeishi kwenye ndoa kwa muda bila kupata mtoto.”

    “Pole sana ngoja nikusaidie japo nauli ikufikishe nyumbani kwa sababu giza likikukuta njiani unaweza kupata matatizo mengine.” Alizungumza yule mama huku akichomoa noti ya shilingi elfu kumi kwenye wallet yake iliyokuwa kwenye dashboard.

    Nilimshukuru sana yule mama kwasababu alikuwa amenipa msaada mkubwa sana ambao sikuutarajia kabisa kuupata katika mazingira yale. Nilisimamisha gari la abiria ambalo nilipanda likanipeleka hadi kijenge impala ambapo nilipanda daladala ya moshono ambayo ilinifikisha stendi ya kona ya kiseriani ambapo nilichukua pikipiki ambayo ilinipeleka nyumbani kwetu ambapo palikuwa ni jirani na St jude boading and campus.

    Nilifika nyumbani mida ya saa moja na nusu usiku nikiwa nimechoka sana na kumkuta mama akiwa mezani na baba wanakula kiporo cha makukuru kwa chai, wote kwa pamoja walishangaa kuniona nikiingia nyumbani kwa wakati ule huku nikionekana kuchoka sana na pia kuwa na majeraha sehemu mbalimbali za mwili wangu.

    “Kulikoni mwanangu.” Alizungumza mama huku akionekana kushikwa na butwaa.

    “Acha tu mama Enrique anataka kuniua yeye na familia yake.”

    “Kisa nini.?” Baba alidakia akionekana kutaka kufahamu kisa na mkasa cha Enrique kunisababishia majeraha makubwa ndani ya mwili wangu.

    “Yani katika hali ya kushangazaa Enrique kabadilika ananipiga kama ngoma kiasi kwamba hadi nakwenda hospitali kutibiwa kwasababu ya kipigo ambacho huwa ananiangushia kila siku huku akinitishia kuniua eti kwasababu sizai, kibaya zaidi leo dada zake wameniamkia kunichangia kunipiga vibaya mno na nilipojaribu kumpigia mama yake Enrique kumueleza kuwa wanae walikuwa wananitesa alinipa onyo kwamba nisimshirikishe kwenye mambo ya kipuuzi kwasababu kama ni kupigana hata na mimi nina mikono ya kupigana.”

    ***

    “Pole sana mama.” Kwa masikitiko makubwa baba alinipa pole.

    “Mbona yule kijana nilimwona ni mtu mpole na mstaarabu sana iwaje leo afanye upuuzi mkubwa namna hii.” Sauti ya baba ilizidi kusikika ikilalama huku mama akiwa amenyanyuka akinitazama kwa umakini katika yale majereha yaliyokuwa yamesababishwa na mume wangu.

    “Kiukweli baba yule mwanaume ana roho ya kikatili mno kwasababu huwa ananipiga kama vile anapigana na mwanaume mwenzie.” Nilizidi kuwaeleza wazazi wangu hali halisi ya maisha yangu baada ya kuingia kwenye ndoa.

    “Haukuwashirikisha watumishi wa Mungu katika huo mzozo wenu?” aliuliza mama.

    “Kwa zaidi ya mara 3 nimeshamwita mchungaji pale nyumbani kuja kuzungumza na mume wangu lakini imeshindikana.”

    “Pumbavu sana kwanini asiende kupigana na wanaume wenzie walionyonya maziwa ya mama zao wamuonyeshe kazi, hawa vijana wa sasahivi bure kabisa.” Alizungumza baba akionyesha kukasirika.

    “Haya peleka begi lako uje ule chakula.” Mama alizungumza.

    “Wala hata sijisikii kula kabisa nitakula kesho ngoja kwanza nikaoge nilale kwasababu nahisi kuchoka sana.”

    “Bandika basi maji ya kuoga jikoni kwasababu kunabaridi mno.”

    “Nitakwenda kuoga hivyohivyo.”

    “Sawa shauri yako.” Mama alinijibu.

    “Ila fanya haraka kwasababu kibatari hakina mafuta ya taa ndio tulikuwa tunakula na baba yako harakaharaka hapa kabla hakijazimika kwahiyo jitahidi kuharakisha.” Mama alizidi kuzungumza.

    Nilichukua ndoo nikaweka maji ya kuoga na kwenda bafuni kuoga ili niweze kurudi kulala kwasababu usiku uliopita sikulala usingizi kutokana na kwamba nilimsubiri mume wangu hadi saa saba usiku ambapo alirudi na kuanza kuniangushia kipigo.

    Baada ya kumaliza kuoga niliporudi ndani nilikuta kweli kile kibatari kimezima kama mama alivyokuwa amenitaadharisha mwanzoni. Ilinibidi nitumie tochi ya simu yangu kunimulikia ili niweze kuingia chumbani kulala.

    Nililala usingizi mzito sana ule usiku kana kwamba nilikuwa nafidia zile siku ambazo nilikuwa nikikesha kumsubiri mume wangu ambae wakati mwingine alikuwa harudi kabisa nyumbani bila kufahamu ambapo amelala.

    ***

    Baada ya kurudi nyumbani kwa wazazi wangu niligeuka gumzo pale mtaani kwetu kwasababu kila mtu alikuwa na lake la kuzungumza juu yangu.

    “Na mbwembwe zote za harusi kubwa namna ile mara hii karudi nyumbani.”

    “Anaringa sana huyu binti hawezi kuishi kwa mume.”

    “Alikuwa anajaza choo cha watu bure mwanamke gani hazai.”

    Maneno yote hayo yalisemwa juu yangu lakini sikuthubutu kugombana na mtu isipokuwa nilinyamaza kama mjinga huku nikizidi kumuomba Mungu anirudishie furaha ya moyo wangu. Kama kawaida yangu kuchacharika kupambana na hali ya uchumi wa nyumbani kwetu, nilianza kufanya vibarua vya mashambani na wakati mwingine nilikuwa saidia fundi ilimradi sikai bila kujishuhulisha.

    Baada ya muda mfupi afya yangu ilirudi katika ubora wake kutokana na maisha ya uhuru na amani niliyokuwa nayo pindi nilipokuwa nyumbani kwa wazazi wangu. Nilirudi katika hali yaa mvuto kiasi kwamba nilikuwa nakumbana na usumbufu mkubwa kutoka kwa wanaume ambao walikuwa wakinipaparikia lakini sikuthubutu kumkubalia hata mmoja kwasababu nilikuwa nimepoteza imani kabisa na wanaume na pia bado Enrique alikuwa hajanitoka moyoni licha ya kunifanyia mambo mengi ya kuniumiza moyo.

    Ugomvi wangu mimi na Enrique niliuchukulia kama moja ya changamoto za maisha kwasababu hata watoto mapacha kunawakati wanagombana sembuse mimi na Enrique tuliekutana ukubwani sio kitu cha kushangaza kabisa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Siku zilizidi kusonga na sikuweza kupata taarifa za mume wangu kwasababu hatukuwa tukiwasiliana kwenye simu kila mtu alikuwa anapambana na maisha yake kivyake kwahiyo sikujua kama alioa kama alivyokuwa akinieleza ama la!.

    Ilipotimu mwezi wa tisa nikiwa nyumbani kwa wazazi wangu nikiwa bado sijawai kuingia kwenye mahusiano na mwanaume mwingine siku moja nilikwenda mjini kununua sare ya nguo ya harusi ya rafiki yangu ambae anaitwa Rebeka. Nilikuwa nimeogozana na huyo rafiki yangu tukipita katika maduka mbalimbali mjini tukitafuta urahisi wa bei kwasababu pesa niliyokuwa nayo ilikuwa ni pungufu kutokana na bei nilizokuwa nikitajiwa katika maduka niliyokuwa nimekwenda kuulizia gharama ya kitambaa hicho.

    Tulifanikiwa kupata kitambaa cha sare ya nguo ambao tulikuwa tumepanga kuvaa siku ya harusi katika duka la muhindi lililopo maeneo ya soko kuu jijini Arusha. Baada ya kupata tulichokwenda kutafuta hatukuwa na kitu kingine tulichokuwa tunaakihitaji kwahiyo ilitubidi tuanze kutembea kuelekea kilombero kituo cha daladala ili tuweze kurejea nyumbani.

    Tulipofika kilombero stendi tulikutana na daladala ambayo ilikuwa ndio inaondoka tuliwai na kuingia ndani ya gari na kwabahati nzuri zilikuwa zimebaki siti mbili tu ambazo tulizijazia na kuanza safari ya kuelekea moshono Arusha. Niligeuka nyuma baada ya kusikia mtu akinigusagusa begani na nilijisikia furaha baada ya macho yangu kukutana na Derick mwanaume ambae ndie alinikaribisha kwenye ulimwengu wa mapenzi.

    ***

    “Jamani Derick mambo.” Nilimsalimia kwa furaha sana kwasababu nilikuwa nimepotezanana nae kwa muda kwani alikuwa masomoni chuo kikuu cha Dare es salaam.

    “Poa tu vipi za kwako.”

    “Njema tu nimekumiss balaa.”

    “Naona mmekuja mjini kufanya shoping.”

    “Shoping wapi ndugu yangu kwa usawa huu wa magufuli mambo sio mambo kabisa pesa hakuna.”

    “Kweli kabisa kila mtu analia kwa sasa.”

    “Ila ninyi wanafunzi si ndio mna hela.” Nilizungumza kwa kumtania Derick.

    “Uwezi amini hata sisi hili joto la jiwe linatuwakia vilivyo.”

    “Umekuja lini Arusha?

    “Nina mwezi mmoja sasa.”

    “Jamani hata kutafutana.?”

    “Nilipata taarifa kuwa umeolewa sasa ningeanzia wapi kumtafuta mke wa mtu.?” Alizungumza kauli ambayo ilinikata maini ikanibidi nipotezee yale maongezi kwasababu niliona kama alikuwa anaelekea kukitonesha kidonda kilichokuwa kimekaribia kupona. Tulifika katika kituo cha kuteremka kwenye gari ambapo tulianza kutembea kuelekea usawa wa nyumbani ingawa kwao kulikuwa ni mbali zaidi kama mtaa wa tatu kutokea pale mtaani kwetu.

    Tulizungumza mambo mengi sana na Derick na hatimae tulibadilishana namba za simu na kila mtu alienda nyumbani kwao. Kitendo cha mimi kukutana na Drerick kilinipa furaha moyoni na nilitamani tena tungeweza kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na kaka yule ambae kwa hakika alinipa furaha sana kipindi nilipokuwa nae kwenye uhusiano wa kimapenzi ingawa tulitenganaga lakini sio kwamba alinitamkia kuwa hanitaki bali niliona kama alikuwa ananipotezea kwasababu alikuwa bize sana na wakati mwingine nilikuwa nampigia simu hapokei nikituma meseji hajibu nikaona lazima atakuwa ameshapata mtu mwingine jambo ambalo liliua hisia za mapenzi ndani yangu hadi zilipokuja kufufuliwa na Enrique ambae nae bila huruma aliziua kwa mara nyingine.

    Baada ya siku tatu nikiwa kitandani kwangu mida ya saa nne usiku nikiubembeleza usingizi uweze kunichukua simu yangu ya mkononi iliita na aliekuwa akipiga si mwingine bali ni Derick.

    “Mambo Teddy.”

    “Poa tu.”

    “Samahani kwa usumbufu.”

    ***

    “Bila samahani.”

    “Teddy nafahamu kabisa kuwa umeolewa ila naomba unisamehe kwa kitendo ambacho niliwai kukifanya kwako ambacho moja kwa moja kilikuumiza moyo wako nakiri kuwa ulikuwa ni akili ya kitoto ndio ilikuwa inanisumbua kwahiyo naomba tufufue uhusiano wetu tuweze kujikumbushia japo kwa muda mfupi kwa hiki kipindi ambacho upo nyumbani kwenu kabla hujarudi kwa mume wako.” Sauti ya Derick ilizungumza kwa unyenyekevu wa hali ya juu na kusababisha ule usingizi niliokuwa nikiuhisi kwa mbali upotee kabisa.

    “Am I dreaming?” (hivi nipo ndotoni ama la!) niliwaza huku nikijaribu kukaa kujidhihirishia kuwa sikuwa ndotoni.

    Sikuwa na namna ya kumkatalia Derick ingawa bado nilikuwa nampenda sana mume wangu lakini niliona ni bora nimtumie yule kijana ambae alikuwa na sifa kubwa kuliko hata ya mume wangu yaani sifa ya mwanaume ambae ndie alienitoa usichana wangu lakini pia kwa muda mrefu nilikuwa nimeishi bila kufanya tendo la ndoa kwahiyo nilikuwa na hamu kwelikweli.

    “Poa Derick nimekwelewa.”

    “Asante sana basi naomba kama vipi tukutane kesho.”

    “Mh kwa kesho hapana kwasababu nanyesha.”

    “Basi siku utakapokuwa vizuri utanijulisha.”

    “Sawa.”

    “Kweli Mungu utanisamehe kwasababu sikuwa tayari kumsaliti mume wangu licha ya madhaifu makubwa niliyomkuta nayo nilikuwa tayari kuishi nae kwenye shida na raha kama nilivyokuwa nimeapa kanisani lakini kutokana na kwamba yeye ndie aliesababisha nifanye hivi sina budi kushea tunda lake na mtu mwingine ambae nilikuwa nimeshamfuta kabisa katika akili yangu.” Niliwaza baada ya kumaliza kuwasiliana na Derick.

    Siku ya 5 baada ya kumaliza siku zangu nilikutana faragha na Derick na tulianza kupeana raha za kimahaba. Derick alikuwa ni mwanaume wa kweli kwasababu aliweza kunikuna ipasavyo kwani moto wake haukuwa wa kuungaunga kama wa mume wangu na kama kawaida yake alinipa raha hadi mwenyewe nikatosheka nikamwambia sihitaji tena kwasababu mchezo ulikuwa na ushindani mkubwa mno, nilikuwa nikinywa maji kila saa kwa jasho ambalo lilikuwa likinitoka kwa namna ambavyo Derick alikuwa akinibinuabinua kama mdoli.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    “Kweli huyu mwanaume sio wa mchezomchezo.” Niliwaza wakati nilipokuwa nikihisi mwili mzima ukiniuma kutokana na mikao ambayo Derick alikuwa akiniweka ili aweze kulifaidi tunda vizuri, baada ya kumaliza tuliongozana hadi bafuni kuoga ili tuweze kuondoka lakini nilipokuwa bafuni aliniongezea goli lingine la kuniaga.



    Tulimaliza mchezo wetu ambao ulikuwa na ushindani wa hali ya juu kutokana na kwamba kila mtu alikuwa na usongo wa hali ya juu na mwenzie nilirejerea nyumbani ugwadu wote niliokuwa nao ukiwa umeisha kabisa kutokana na ufundi wa Derick.

    Nilipofika nyumbani jioni nilikuta mama ameandaa ugali kwa maziwa ya mtindi lakini sikuweza kula kutokana na uchovu niliokuwa nao alafu isitoshe pia nilikuwa nimeshiba kuku na Grand malt ambavyo nilinunuliwa na Derick kule kwenye nyumba ya wageni kwahiyo nilikwenda moja kwa moja kitandani kulala. Nililala usingizi mzito sana ile siku kwasababu nilikuwa nimechoka sana kwahiyo nilishtuka asubuhi na mapema baada ya kusikia sauti ya mama ikiniita huku akigonga mlango

    “Ngo! Ngo! Ngo!”

    “Teddy.”

    “Abee mama.”

    “Umeamkaje.”

    “Sijambo mama shkamoo.”

    “Tunatoka tunakwenda kibaruani kwa mzee Ndemo kwahiyo teremka huko kitandani ubandike kande jikoni alafu utuletee shambani wakati wa mchana.” mama alinipa maagizo baada ya kuitikia salamu.

    “Sawa mama.”

    Ilipofika mida ya saa nane na nusu mchana chakula kilikuwa kimeiva kwahiyo nilipakua nikaweka kwenye hotpot ili kisiweze kupoa kwasababu kulikuwa kuna umbali kidogo kutokea pale nyumbani hadi walipokuwa wazazi wanafanya kibarua cha kupalilia mahindi. Nilianza safari ya kutembea kwa haraka ili kuwaisha chakula shambani kwasababu muda ulikuwa umesonga sana. Hotpot niliyokuwa nimeweka chakula niliidumbukiza kwenye ndoo ambayo niliiweka kichwani na mkononi nilishika jagi kubwa la maji ya kunywa.

    Nilifika shambani salama na niliwakuta wazazi wakiwa chini ya mti wanasubiri chakula ambacho kilichelewa kuiva kutokana na uhaba wa kuni wakati nilipokuwa nikiandaa chakula

    “Umechelewa mno Teddy yani tumehisi njaa na kiu hadi nikataka nikufuate huko nyumbani nije kufahamu kulikoni.” Mama alizungumza akionekana kuwa na uchovu sana.

    “Yani mama zile kuni za kupikia haziwaki kabisa sijui ni kwasababu zilinyeshewa na mvua juzi ndio maana?” nilizungumza huku nikipakulia chakula kwenye sahani ili tuweze kula wote kwa pamoja kwasababu hata mimi nilikuwa sijala kwahivyo nilikuwa nikihisi njaa pia.

    Baada ya kumaliza kula baba na mama waliendelea na kazi hadi jua lilipozama ndipo tulirejea nyumbani nikiwa nimewasaidia kubeba majembe pamoja na mihogo ambayo baba alipewa na mama mmoja wa shamba la jirani na pale walipokuwa wakilima.

    ***

    Nilifika nyumbani ikanibidi nichemshe ile mihogo kwasababu baba alisema ajisikii tena kula kande kwa usiku ule. Wakati nilipokuwa jikoni peke yangu wakati mama alipokuwa bafuni anakoga nilishikwa na taharuki baada ya kuona Enrique ananipigia simu jioni ile.

    “Mthyuuuu..” nilisonya kwa dharau bila kupokea simu yake kwahiyo iliita hadi ikakatika lakini muda huo huo alipiga tena kwa mara nyingine lakini sikuipokea.

    “Huyu ananisumbua nini.?” Nilijiuliza baada ya simu yake kuita kwa mara ya tatu nikaona nipokee ili niweze kumsikiliza anajipya gani la kunieleza.

    “We mat*ko kwanini hupokei simu yangu.” Sauti ya mume wangu ilisikika ikianza kuzungumza kwa kuniporomoshea tusi huku akionekana kulewa sana.

    “Au hao mahawara zako ndio wanakupa kiburi.” Niliona bora nikwepe ile kero kwa kumkatia simu na kuizima.

    “Hivi huyu mwanaume anamatatizo gani jamani kwanini yeye ni wa kuninyima amani kila siku.” Nilijikuta nazungumza peke yangu hadi nikajishtukia baada ya kusikia sauti ya mama ikitokea bafuni ikiniuliza nazungumza na nani ikanibidi nimdanganye nazungumza na simu.

    Nilimaliza kuandaa miogo ya baba na kwenda ndani ambapo nilitenga mezani na mimi kwenda kitandani kulala japo kuwa nilikuwa natamani nile hata vipande viwili vya mihogo na kikombe cha maji nilale lakini hamu ilipotea ghafla baada ya kuwasiliana na mume wangu ambae sauti yake kwenye masikio yangu ilikuwa ya kutisha kama ya simba.

    Niliwaza mambo mengi sana usiku ule wakati nilipokuwa kitandani kwangu kuhusu namna ya kuweza kunusuru ndoa yangu ambayo ilikuwa hatihati kubaki historia lakini bado sikupa jibu la kuweza kunusuru uhusiano wangu na mume wangu.

    Kwa jinsi utamu ulivyoninogea mara ya mwisho nilipokutana na Derick faragha baada ya wiki moja tulipanga pambano lingine kwaajili ya kupeana mahaba motomoto, tulikutana katika gesti moja inayoitwa Tarakea bar and guest house iliyopo maeneo ya levolosi jijini Arusha kiukweli Derick alikuwa akinipooza majeraha ya mapenzi yaliyokuwa yamesababishwa na mume wangu kutokana na mapenzi matamu aliyokuwa akinipatia. Nilisahau kabisa kero zilizokuwa nikizipata kwa mume wangu kutokana na utundu wa kijana yule.

    “Hivi huko chuo huwa mnafundishwa somo la mahaba?” nilijikuta nikimuuliza baada ya kushangazwa na ufanisi wake wa kunipagawisha huku nikihema juujuu hadi machozi yakawa yananitoka kwa utamu niliokuwa nikiuhisi. Niliyaona maisha ni matamu sana kwa mapenzi matamu ambayo kila wakati yalinifanya niwe na tabasamu la nguvu usoni mwangu. Kusema kweli sikutamani dakika zisogee pindi nilipokuwa mikononi mwa Derick kwa namna ambavyo alikuwa akinipa raha.

    Ni kwamba sikuwa na namna ya kuweza kudanganya nyumbani lakini ile siku nilitamani sana ningelala na Derick katika ile nyumba ya wageni ili azidi kunikonga moyo kwa penzi lake motomoto, kwahiyo muda ulifika na nilirudi nyumbani.

    ***

    Kama ilivyo kawaida siku hazigandi zilibaki siku chache sana ili Derick aweze kurudi chuoni kwake kumalizia elimu yake ya chuo kikuu kwahiyo Derick alinipigia simu siku moja mida ya usiku na kuniambia kuwa baada ya siku mbili atasafiri kurudi chuo kwahiyo alinihitaji kesho yake ili tuweze kukutana tupeane mahaba ya kuagana. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    “Sasa itakuwaje wakati kesho ni siku ya hatari sana katika mzunguko wangu wa hedhi kwasababu zimebaki saa 48 ili niweze kuingia kwenye siku zangu? niliwaza sana lakini nilifikia muwafaka kwamba kwasababu mume wangu amenitelekeza sina budi kumzalia Derick mtoto kudhihirisha upendo wangu kwake achilia mbali kwamba hata nioa kwasababu tayari alikuwa amempata mchumba ambae ni msomi mwenzie lakini kwasababu nampenda sana nitafarijika kipindi nitakapokuwa namtazama mtoto wake na nitakapobeba mimba yake nitawaziba midomo wanafamilia wa Enrique na jamii kwa ujumla ambao wamenibatizia jina jipya la mgumba.

    Nilipokutana na Derick ilinibidi nimweleze hali halisi ya ndoa yangu na sababu ya mimi kuwepo nyumbani kwetu kwa wakati ule hivyo basi wakati tulipokuwa tukila na kunywa kabla ya kuanza kupagawishana niliona nitumie ule mda kumshirikisha Derick katika suala ambalo nilikuwa nimekusudia ile siku.

    “Derick samahani kuna jambo nahitaji kukueleza mpenzi wangu.”

    “Nieleze tu sweet manka wangu.”

    “Nafikiri hufahamu lolote linaloendelea kati yangu mimi na mume wangu.”

    “Ni kweli kabisa kwasababu niliwai kukuuliza ukapotezea.”

    “Basi ngoja leo nikueleze ila naomba iwe siri yako usijaribu kumweleza mtu yeyote.”

    “Usijali.” Derick alionyesha kutega masikio kwa umakini kunisikiliza.

    “Yani hata sijui nianzie wapi.”

    “Come on baby am listening.” (nieleze bwana nakusikiliza.)

    “Iko hivi ni kwamba mimi na mume wangu tumetengana baada ya mimi kuonekana kuwa sizai lakini nahisi kuwa mume wangu ndie anamatatizo kwasababu kwanza anaupungufu mkubwa wa nguvu za kiume kwa maana kwamba huwa hawezi kuendelea na tendo baada ya goli la kwanza, lakini pia nilithibitisha kuwa tatizo ni lake baada ya kwenda hospitali kupima ili nifahamu kama ninauwezo wa kubeba ujauzito na vipimo vikaonyesha kuwa nipo vizuri kabisa hivyo nilimshauri mume wangu akapime ili na yeye aweze kufahamu kuwa ni mzima ama la! Lakini aligoma kwenda hospitali akinitupia lawama mimi kuwa ndie mgumba hadi ikazua ugomvi nikaamua kurudi nyumbani kwetu.”

    “Pole sana Teddy.”

    “Asante sana ila nakuomba unisaidie kitu kimoja.”

    ***

    “Sema tu nakusikiliza kama lipo ndani ya uwezo wangu nitakusaidia kwa moyo wangu wote.”

    “Derick naomba nikuzalie mtoto.”

    “Vipi kuhusu ndoa yako?” yani hapa nacheza kamari ambayo kwa kawaida huwa na matokeo ya kushinda au kushindwa, namaanisha kwamba nikifanikiwa kurudi nyumbani kwa mume wangu kabla ujauzito haujajionyesha itakuwa jambo la heri lakini akizidi kuchelewa ndio itakuwa imekula kwake kwasababu atafahamu kuwa mimba nimepewa na mtu mwingine kwahiyo ndoa itakuwa imeishia hapo. Ila nina imani kuwa nitarudi nyumbani kwa mume wangu kwasababu leo asubuhi kanipigia simu na kuniomba msamaha sana.”

    “Huo ndio msaada pekee ambao nauhitaji kwako ili kuweza kunusuru ndoa yangu ambayo iko mbioni kusarambatika kwa tatizo ambalo unawezaa kulimudu kulitatua.” Nilizungumza kwa sauti ya upole sana na kunyenyekea.

    Derick aliinamisha kichwa chake chini huku akionekana kuwaza sana juu ya kile nilichokuwa nimemweleza.

    “Tafadhali naomba unielewe mpenzi.”

    “Duuh! Na vipi je hii siri itakapokuja kuvuja?”

    “Nakuahidi itakuwa siri yangu na wewe labda wewe ndio uamue kuivujisha.”

    “Hapana mimi siwezi kufanya upuuzi huo, ila pia vipi mtoto akitoka kopiraiti na mimi itakuwaje?”

    “Hilo wewe niachie mimi.” Nilizungumza kwa hali ya kumuondoa wasiwasi kwasababu Derick alikuwa anafanana vitu vingi na Enrique tofauti yao kubwa ni kwamba masikio ya Derick kidogo yalikuwa yamesimama kitu ambacho hakikuniumiza kichwa sana kwasababu hata baba yangu alikuwa na masikio ya namna ile.

    “Basi poa usijali ngoja nakutemea sumu kali kama koboko muda sio mrefu.” Derick alinikubalia ombi langu huku akinitania. Baada ya kumaliza kula nilishikwa na bumbuwazi kwasababu Derick alionekana kutegesha kamera ya laptop yake ili iturekodi wakati tukifanya tendo la ndoa lakini nilimkatalia katakata kwasababu haikuwa kawaida na sikujua anamaanisha nini.

    “Uwezi kufanya huo upuuzi na mimi kama haupo tayari niambie lakini sio kuleta mzaha sehemu ambayo sio mahala pake.”

    “Please Teddy usinielewe vibaya narekodi kwasababu nitakumiss sana kipindi nitakapokuwa chuo kwahiyo itakuwa inanifariji nitakapokuwa naiangalia.”

    “Hapana bwana mi staki.”

    “Nakuahidi itakuwa siri yangu mimi na wewe.”

    “We Derick unataka unitie matatizoni ujui mi mke wa mtu?”

    ***

    “Nafahamu sana ila nakuahidi sintamwonyesha mtu yeyote tafadhali nielewe.”

    “Embu jaribu kufikiri mwenyewe kwa jinsi ninavyokupenda nitaanzia wapi kukudhalilisha halafu isitoshe na mimi pia nitakuwa naonekana kwenye video uwezi kuona kwamba zikivuja tutadhalilika wote? Ndio maana nakwambia itakuwa siri yetu wawili.” Derick alizidi kunishawishi kwa maneno yake ambayo yaliniridhisha kwa kiasi fulani kwahiyo nilimkubalia aweze kurekodi mtanange mzima pale kitandani sikuwa na jinsi kwasababu pia alikuwa ameshanichojoa nguo zote na mzuka ulikuwa umeshanipanda.

    Ndani ya dakika chache tuliingia katika ulimwengu mwingine wa mahaba mazito haijawai kutokea kwa namna ambavyo kila mmoja alionyesha kutamani kumfaidi mwenzie katika mchezo ule wa aina yake, kama kawaida ya Derick hajawai kuniangusha kila aliponikamata nilazima niombe poo kwajinsi alivyobarikiwa kuwa na nguvu za kutosha. Derick alinipa mambo hadimu ambayo hakuwai kunipa hata siku moja hadi mwenyewe nikashangaa ule ufundi alikuwa ameujulia wapi kwasababu kila wakati nilipolala nae nilikuwa nikimuona mpya katika namna ya kulimega tunda.

    Mchezo ulimalizika kila mmoja akiwa ameridhika kabisa.

    Wanaume wote wangekuwa kama wewe michepuko isingekuwepo kwa kasi kama ilivyo sasa.” nilimweleza Derick ambae alikuwa ndio ameshuka juu ya kifua changu baada ya kutosheka.

    “Kwanini sweety.” Alizungumza huku akihema juujuu.

    “Sasa huyo mwanamke ataenda nje kutafuta nini ambacho atakuwa amekosa kwa mume wake? Labda ashawishike na mambo mengine lakini sio penzi.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    “Asante sana kwa penzi lako hakika nimefaidi mno.” Nilizungumza huku kichwa changu nikiwa nimekilaza juu yaa kifua cha Derick ambacho kilikuwa na nywele zilizokuwa zikinitekenyatekenya.

    “Asante mpenzi wangu nashukuru kwasababu nimetosheka pia.”

    “Ama kweli wewe ni moto wa kuotea mbali yani nimechoka utadhani nilikuwa napasua mawe.” Ilinibidi nimweleze kuwa nilikuwa najihisi uchovu wa hali ya juu.

    “Hahaha! Pole sana mpenzi nitakumiss sana Teddy.” Alizungumza Derick huku akishuka kitandani na kusogea kwenye laptop yake iliyokuwa juu ya meza iliyokuwa pembeni kidogo mwa kitanda na kustopisha ile muvi aliyokuwa anarekodi.

    “Nitakumiss pia ila nitafarijika sana nitakapokuwa namwona mwenetu.” Nilizungumza kauli ile kwasababu nilijua moja kwa moja ni lazima nitakuwa nimebeba ujauzito wake kwasababu ile siku ilikuwa ni ya hatari sana katika mzunguko wangu wa hedhi halafu isitoshe nililala nae bila kinga yeyote.

    Ghafla simu ya Derick iliita kabla hajaipokea alinihitaji niwe mtulivu kwasababu aliekuwa akipiga ni mchumba wake ambae alikuwa akisoma katika chuo kikuu kishiriki cha elimu Dar es salaam (DUCE) na alikuwa amepanga kwenda kumtambulisha nyumbani kwao baada ya kumaliza chuo miezi kadhaa ijayo.

    “My sweety how was your day.” (vipi mpenzi siku yako imekwenda vipi) Derick alimsalimia mpenzi wake.

    ***

    “Extremely fantastic honey.” (ilikuwa nzuri sana.) Sauti nyororo ilisikika kwenye simu ya Derick ambayo alikuwa ameiweka sauti ya juu.

    “When will you come my dear because I real need you.” (utakuja lini mpenzi kwasababu naakuhitaji)

    “The day after tomorrow I will be there my lovely queen.” (Siku baada ya kesho nitakuwa huko malikia wangu.) Derick alizidi kubonga ung’eng’e na mpenzi wake huku mkono wake mmoja ukichezea nywele zangu wakati kichwa changu nilipokuwa nimekilaza juu ya kifua chake.

    “Naomba nikitafute baadae kidogo kwasababu kunakazi baba alinipa kwahiyo ndio nataka niifanye mara moja halafu nikimaliza nitakupigia.” Derick alimdanganya mpenzi wake ili wasitishe yale maongezi yao.

    “Poa.”

    “Kumbe ndio mnavyotundanganyaga hivyo?”

    “Hapana ila imenibidi.”

    “Laiti angejua unachokifanya sasahivi angekumeza mzimamzima.”

    “Kweli kabisa lakini ntaanzia wapi kulikosa penzi la binti mzuri kama wewe.”

    “Ila anafaidi sana huyo huyo mwenzangu.”

    “Uwezi amini tumekubaliana tusifanye chochote hadi tuoane.” Nilishtuka sana baada ya kusikia Derick akitamka sentensi ile kwasababu ile ndio iliniponza mimi kwasababu laiti ningejua mapema kuwa moto wa Enrique ni wa mabua nisingekubali kuingia nae katika mahusiano.

    Ile siku nilichelewa sana kurudi nyumbani hadi mama alinigombeza ila nilimuongopea kuwa nilikuwa kwa rafiki yangu mkubwa wa pale kijijini ambae alikuwa ni Glory ambae nae alifeli baada ya kumaliza kidato cha nne na tayari alikuwa na mtoto mmoja ambae alizalishwa na mwanaume ambae alimtelekeza baada ya kubeba ujauzito.

    Wiki moja baadae siku moja nilipokwa njiani nikitokea kanisani ilikuja gari ya mpenzi wangu Enrique na kusimama kando yangu na alizidi kuniomba sana kwa kuninyenyekea ili niweze kumsikiliza kwasababu nilionyesha kutohitaji mazungumzo na yeye. Baadae niliamua kumsikiliza ambapo aliniomba msamaha kwa yale yote yaliyotokea na kunieleza kuwa ni shetani tu ndie alikuwa amempitia yeye na familia yake kwahiyo alikuja kuniomba radhi ili niweze kumsamehe yeye na familia yake na turudi nyumbani tukajenge maisha yetu.

    Kutokana na kwamba bado nilikuwa nampenda licha ya mapungufu makubwa aliyokuwa nayo alafu isitoshe nilikuwa najua nilichokifanya kwahiyo niliona nisipoteze muda nilimwelewa na kwamwambia kuwa akajipange ili aweze kuja nyumbani kwetu kuzungumza na wazazi wangu kwasababu siwezi kuondoka nyumbani bila wazazi wangu kuridhika na maelezo yake kwasababu niliwaeleza mambo yote aliyonitendea kipindi nilipokuwa kwake.

    ***

    “Kiukweli mke wangu naomba unisamehe sana na pia nakuahidi kuwa nimebadilika na nimetambua kuwa mtoto ni zawadi kutoka kwa mwenyezi Mungu kwahiyo hatuna budi kuendelea kumuomba yeye ili aweze kutujalia watoto katika ndoa yetu.”

    Baada ya siku tatu Enrique alikuja nyumbani kwetu akiwa ameongozana na watumishi wa Mungu ambao walikuja kuzungumza na wazazi wangu ilikumuombea Derick msamaha kwasababu alitambua kuwa yeye ndie alikuwa amenikosea. Kama ilivyo kawaida wanapokusanyika watumishi wa Mungu ni lazima lifikiwe suluhisho jema nilifanikiwa kurudi nyumbani kwa mume wangu wakati tayari nikiwa najihisi hali ya tofaauti katika mwili wangu kwasababu nilianza kuchoka sana, kichefuchefu cha mara kwa mara, kulala sana kuliko kawaida jambo ambalo lilinifanya siku moja ya jumamosi kumuomba mume wangu anisindikize hospitali kwasababu nilikuwa sijihisi vizuru kiafya kwahiyo tulifika hospitalina na kujieleza na daktari akanipima na vipimo vikaonyesha kuwa ninaujauzito wa miezi miwili.

    “Hongera sana bwana Enrique mkeo ni mjamzito wa miezi miwili.” Kwa uso uliojaa tabasamu daktari alizungumza huku akimpa mkono mume wangu.

    “Woow! Thank you God.” Enrique alionyesha furaha ambayo sikuwai kuishuhudia kwake tangu nilipomfahamu kwasababu alifurahi hadi akawa ana rukaruka huku kijasho chembamba kikimtoka kwajinsi ambavyo ali suprise.

    Enrique alizidi kuonyesha furaha yake kwasababu alinikumbatia kwa furaha sana huku akinishukuru kwa kuweza kumbebea ujauzito.

    “Asante sana mke wangu kweli nimeamini hakuna linaloshindikana kwa Mungu.”

    “Hongera pia mume wangu.”

    Enrique alifurahi sana baada ya kusikia majibu ya vipimo vile akijua kuwa yeye ndie aliesababisha mimba ile lakini haikuwa hivyo kwani aliefanya shughuli ile nilikuwa namfahamu mwenyewe.



    Tulirudi nyumbani nyuso zetu zikiwa zimetawaliwa na furaha isiyokuwa na kifani. Enrique aliwajulisha ndugu zake wote kuhusu ile habari njema ya mimi kuwa mjamzito ambapo wengi wao walidhihirisha hisia zao za upendo kwa kutupongeza.

    Hisia za furaha zilizokuwa zimekita kambi katika nafsi ya mume wangu ilimpelekea aninunulie gari jipya aina ya Brevix. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    “Mke wangu nataka kwanzia leo uwe unatembea kwa motokaa ili usiwe unachoka sana.” Enrique alizungumza wakati tulipokuwa mezani tunakula matunda huku akishikashika tumbo langu ambalo bado lilikuwa halijaanza kujionyesha barabara.

    “Asante sana mume wangu.” Kwa tabasamu bashasha nilimshukuru sana huku nikichezea kidevu chake kilichokuwa na ndevu ndefu kiasi ambazo zilikuwa zinanichomachoma vidole vyangu na kunifanya nihisi raha.

    Kutokana na kwamba alikuwa tayari ameshanifundisha gari kipindi tulipokuwa kwenye uchumba alinipeleka kozi fupi ya udereva ili kujifunza alama za barabarani pamoja na kupata leseni ya udereva. Maisha yangu ya kwenye ndoa yalibadilika ghafla na kuwa ya furaha sana kwani Enrique alinipenda, alinijali, alinithamini kama mboni ya jicho, na alinipa kila kitu nilichokuwa nakitaka kuhakikisha kuwa kila siku nakuwa na furaha ndani ya moyo wangu.

    Nilishuhudia mabadiliko makubwa sana kwake kwasababu hata ile pombe aliyokuwa akinywa mwanzoni hakunywa tena alibadilika na kuwa mstaarabu, mpole na mnyenyekevu kama kile kipindi ambacho tulikuwa kwenye uchumba.

    Siku zilizidi kusonga huku nikiwasiliana na Derick mara moja moja kwa njia ya simu kusema kweli mwili wangu ulikuwa ukiishi kwa Enrique lakini nafsi yangu ilikuwa ikiishi kwa Derick hususani pale nilipokuwa nikikumbuka zile raha alizokuwa akinipa. Nilimuwaza sana hasa pale nilipommiss kwasababu mume wangu hakuwa na mabadiliko yeyote kitandani zaidi sana tabia yake ndio ilibadilika na kuwa ya kuridhisha.

    Wakati mwingine nilikuwa naingia kwenye msongo mkubwa wa mawazo kwa kumuwaza Derick hadi kichwa kinaniuma kutokana na kulia sana nilipokuwa nikikumbuka mambo mazuri ambayo alinitendea kwenye maisha yangu.

    Nilianza kumchukia sana mume wangu kiasi kwamba nilikuwa sihitaji kabisa kumwona mbele ya macho yangu nilijitahidi nisimwonyeshe ile tabia ya kumchukia lakini nilishindwa kabisa ingawa sikumtamkia kuwa namchukia ila nilikuwa nikimpinga kwa mambo mengi hata ambayo yalikuwa na manufaa kwangu ilimradi tu akasirike na kukaa mbali na mimi, lakini kutokana na kwamba Enrique alikuwa ni mtu mzima alifahamu kuwa ile hali ilisababishwa na kile kiumbe kilichokuwepo tumboni mwangu. Hivyo baada ya muda mfupi ile hali ilipita nikaendelea vizuri na Enrique wangu.

    Siku moja mida ya saa saba usiku nilianza kuhisi uchungu wa kujifungua hivyo mume wangu alinichukua kwa gari lake hadi hospitali ya AICC iliyopo jijini Arusha ambapo ilipofika mida ya saa mbili asubuhi nilijifungua mtoto wa kike ambae kwa zaidi ya asilimia 80 alikuwa amefanana sana na mimi mama yake jambo ambalo lilinipa raha mno ndani ya nafsi yangu kwasababu nilijua sio rahisi kwa Enrique wala ndugu yake yeyote kuweza kuwa na mashaka na mtoto aliezaliwa.

    Enrique alifurahi sana baada ya kuona kuwa nimejifungua mtoto wa kike ambae alikuwa mzuri mweupe kama mama yake. Ingawa kipindi cha ujauzito alikuwa ananitania sana kwa kudai kuwa mtoto atakae zaliwa atakuwa ni mtoto wa kiume lakini mimi nilikuwa nambishia kuwa sio wa kiume kwasababu nilikuwa natamani zaidi mtoto wa kike kwahiyo baada ya mtoto kuzaliwa nilikuwa kama mimi ndie mshindi wa yale mabishano ya kipindi kile nilipokuwa mjamzito juu ya mtoto atakaezaliwa.

    “Mungu ninakushukuru kwa kuniwezesha kujifungua salama.” Nilinena na Mungu kimyakimya kudhihirisha hisia zangu za shukrani kwake yeye mwenye nguvu na mamlaka.

    “Hongera sana mama mtoto wangu.” Enrique alinipa hongera huku uso wake ukidhihirisha furaha iliyokuwa ndani ya moyo wake.

    ***

    “Asante sana.”

    “Naona umeniletea mama yangu.”

    “Ndio nimeona aje kwanza mama mkwe wangu kwasababu nampenda sana.”

    “Nashukuru sana laazizi wangu ngoja nimpigie mama nimweleze habari hii natumaini atafurahi sana.” Enrique alizungumza kwa furaha huku akiweka simu yake sikioni kuzungumza na mama yake.

    “Shkamoo mama, tupo hospitali ya AICC mke wangu amejifungua salama mtoto wa kike.”

    Baada ya kumaliza kuzungumza na mama yake aliniambia kuwa mama yake amefurahi sana na amesema tukiruhusiwa tumpigie simu ili tukutane nyumbani kwasababu kwa sasa yupo kwenye kikundi chao cha kikoba. Ilipofika mida yaa saa nane mchana niliruhusiwa kurudi nyumbani kwasababu afya yangu na ya mtoto ilikuwa ni yakuridhisha kabisa.

    Tulipofika nyumbani baada ya nusu saa gari la mama mkwe wangu ilipaki nje ya nyumba yangu na aliteremka na kuja moja kwa moja hadi chumbani kwangu kunipa hongera zangu na alifurahi sana kumwona mtoto ambae kwa kiasi kikubwa alikiri kuwa amefanana mimi. Alikwenda jikoni kuniandalia uji wa ulezi kwasababu alikuwa amekuja na maziwa ya mtindi kutoka nyumbani kwake.

    “Hongera sana mwali wangu.”

    “Asante sana mama.”

    “Mtoto mzuri sana.”

    “Ukue kwa afya njema mjukuu wangu Mwenyezi Mungu akukinge na mabaya ya mwovu ibilisi sheteni.” Sauti ya mama mkwe wangu ilisikika ikimnenea maneno ya baraka mwanangu wakati alipokuwa amempakata.

    Baada ya muda mfupi wifi zangu nao walifika nyumbani kwangu kunipongeza kwa kujifungua salama. Ingawa nyuso zao zilijawa na aibu mno kwasababu yule mtu waliokuwa wakimtangaza kila kona ya mtaa kuwa ni mgumba muda ule alikuwa amempakata mtoto mwenye afya njema mikononi mwake.

    “Jamani wifi naomba nikashike hako kamalaika.” Sauti ya Zubeda ilisikika ikionyesha hamu ya kutamani kumshika mwanangu nami bila chuki wala kinyongo nilimpa mwanangu ili nafsi yake izidi kumsuta kwa kile kitendo cha kinyama walichokuwa wamenitendea.

    “Jamani kana uso mwembamba kama mama yake.” Alizidi kuzungumza baada ya kumpokea mtoto.

    “Ila pua ni kama ya baba yake kabisa.” Flora nae alidakia na kutoa yake ya moyoni kuhusu muonekano wa mtoto wangu.

    Kila mmoja alikuwa akimwelezea mwanangu kwa namna yake japokuwa walikosa kujiamini kabisa kwasababu sikuonyesha dharau wala kinyongo chochote bali nilikenua meno yangu yote 32 ingawa moyoni nilikuwa sitamani hata kuwaona pale nyumbani kwangu kutokana na tabia yao kuwa mbaya kupita maelezo.

    ***

    “Wifi umepanga kumwita jina gani?” Flora aliuliza.

    “Bado sijapanga ila kufikia wiki ijayo atakuwa ameshapata jina.”

    “Mimi naona umwite Vannesa.” Zubeda alitoa pendekezo lake kuhusu jina analopenda apewe mtoto.

    “Hapana mwite Viola.” Flora alipinga pendekezo la mwenzie.

    Wifi zangu walizidi kubishana wenyewe kuhusu jina ambalo walitamani mtoto wa kaka yao apewe lakini hakuna hata jina moja la kwao ambao nililipenda na pia kwa jinsi ambavyo nilikuwa siwapendi wale wifi zangu hata wangetamka jina zuru namna gani nisingekubali kumpa mtoto wangu.

    “Hawa wapuuzi si ndio walidiriki kunipiga kwasababu sizai leo wanabishana kuhusu jina la kumpa mwanangu ama kweli unaemdharau siku moja utamsalimia kwa heshima.” Niliwaza wakati nilipokuwa nikiwatazama na kuwasikiliza kwa jinsi walivyokuwa wakijishebedua kuumiza vichwa kuhusu jina la kumpa mwanangu.

    “Wanafiki wakubwa.” Nilizidi kuwajibu kimoyomoyo kwa sababu ni dhahiri wale wifi zangu walikuwa ni wazandiki wasiokuwa na hata chembe soni.

    Jioni ilipofika mama mkwe wangu aliondoka na Flora na kumwacha Zubeda anisaidie katika kile kipindi cha uzazi. Niliona ni jambo jema sana kwasababu nilikuwa sina uweze wa kujihudumia kwa kile kipindi cha uzazi kwasababu pia sikuwa na mfanya kazi wa ndani.

    Siku ya tano baada ya kujifungua niliona nitumie ile siku kuumiza kichwa kuhusu jina la kumpa mwanangu kwasababu nilikataa jina la mama mkwe wangu ambalo mume wangu alilipendekeza awali tumpe mwenetu. Baada ya upembuzi wa majina mengi sana akilini mwangu nilifikia hitimisho kuwa mwanangu nimwite SWEETNESS kwasababu nilikumbuka siku moja Derick aliwai kuniambia kuwa analipenda sana jina hilo kupita maelezo. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    “Mume wangu unaonaje tukimwita mwanetu Sweetness.” Nilimuuliza mume wangu ili aweze kunipa mtazamo wake juu ya jina lile.

    “Sweetness jina zuri sana kwasababu hapa mtaani hakuna mtoto mwenye jina hilo kwahiyo sina budi kulikubali kutokana na kwamba pia linamvuto.”

    Kwahiyo tulikubaliana kwamba tumbatizie mtoto jina hilo.

    Nilipokuwa mzazi wa miezi miwili siku moja nilipokea simu kutoka kwa Derick wakati nilipokuwa peke yangu nyumbani nimekaa kitandani kwangu.

    “Habari yako Teddy.”

    ***

    “Nzuri ila kwasasa naitwa mama Sweetness na sio Teddy tena.” Ilinibidi nimweleze kuwa tayari nilikuwa nimeshajifungua kwasababu nilimtafuta hewani mara kadhaa bila mafanikio.

    “Hahaha I real love that name, hongera sana (kiukweli napenda sana jina ilo.)

    “Ila kwanini umeamua kumwita hivyo.”

    “Kwasababu ni jina ambalo uliwai kunieleza kuwa unalipenda sana.”

    “Ni kweli kabisa asante sana kwa kuzidi kunionyesha upendo wako.”

    “Upendo wangu kwako hautafikia kikomo kwasababu nipo tayari kwa chochote na kwa lolote juu yako Derick.”

    “Asante sana mpenzi na vipi mtoto anamwonekano gani?”

    “Hahaha! damu yangu kali sana kwasababu katoka kopirati na mimi mama yake.” Nilimjibu baada ya kucheka kwasababu tangu ile mara ya kwanza wasiwasi mwingi wa Derick alihofia mtoto kufanana na yeye.

    “Afadhali kwasababu sijui ingekuwaje endapo angefanana na mimi kila kitu. Hongera sana mama Sweety.

    “Thank you my love.” Nilizungumza kwa kutabasamu baada ya Derick kulitamka jina lile kwa swaga.

    “Nimekutafuta nikutaarifu kuwa wiki mbili zijazo nitafanya mahafali ya kuhitimu elimu yangu ya chuo kikuu hapa chuoni halafu baada ya hapo nitaongozana na wageni wangu hadi kwenye ukumbi wa mlimany city ambapo nitafanya bonge la tafrija itakayo ambatana na tukio la kihistoria la kumtambulisha mchumba wangu kwa wazazi wangu pamoja na ndugu jamaa na marafiki wote. Hivyo basi wewe kama mtu wa muhimu sana katika maisha yangu nimeona nikushirikishe ili uweze kujumuika nami katika siku hiyo ya aina yake.

    “Jamani asante sana sweety wangu kiukweli natamani sana ningekuwepo niweze kushuhudia tukio ilo la kihistoria ila naomba nishiriki kwa kutoa zawadi kwasababu kuudhuria haitawezekana kwasababu siunajua nipo kwa mume wangu alafu isitoshe nipo kwenye uzazi.”

    Baada ya kukata simu nilimtumia shilingi laki tano zilizokuwepo kwenye m-pesa hela ambayo mume wangu alinipatia inisaidie katika mahitaji madogo madogo kama mafuta ya gari na ununuzi wa mahitaji yangu mengine lakini kwa upendo niliokuwa nao kwa kijana Derick nilimpa zote nikifahamu kuwa mume wangu atanipa zingine.

    “Thanks a lot baby.” Sauti ya Derick iliyokuwa ikinishukuru iliambatana na furuha ndani yake.

    “Poa dia nakupenda sana baba mtoto wangu.”

    “I love you too sweety.” (nakupenda pia mpenzi.)

    ***

    “Yani ningekuwa na uwezo ningemzawadia nyumba au gari ili aweze kufahamu kuwa nimempa thamani kubwa ndani ya moyo wangu.” Niliwaza baada ya kumaliza kuwasiliana na Derick mwanaume ambae alifanya mapinduzi makubwa sana ya kimapenzi ndani ya moyo wangu.

    Mwezi wa tatu mama alikuja nyumbani kwangu akiwa ameongozana na wanawake wengine kutokea kule nyumbani kwetu kuja kunipa hongera. Nilifurahi sana kwasababu waliniletea zawadi kedekede. Nilifarijika sana kwasababu licha ya kwamba nimetoka katika familia ya chini lakini wazazi wangu wanamahusianao mazuri na majirani na ndio maana mama yangu aliweza kuongozana na wanawake wengine kuja nyumbani kwangu kunipa hongera. Ndugu jamaa na marafiki kwa upande wa mume wangu nao walifika kwa wingi pale nyumbani kunipa hongera.

    Mume wangu aliniudumua vizuri sana kipindi cha uzazi kwasababu nilikuwa napata lishe bora kabisa kusudi mtoto aweze kupata maziwa ya kutosha. Matunzo mazuri niliyokuwa nikipatiwa na mume wangu yalinipelekea ngozi yangu kuwa nyororo kama ya mtoto mchanga na pia nilinawiri sana yani mpaka wanawake wenzangu wakawa wananitamani kwa jinsi nilivyokuwa namwonekano wa kuvutia kama madini ya tanzanite.

    Baada ya miezi sita mume wangu aliandaa sherehe kubwa sana ya ubatizo wa mtoto wetu. Ilikuwa kama harusi kwa namna ambavyo ilikuwa kubwa na ya kupendeza. Ilizua gumzo pale mtaani kutokana na gharama kubwa zilizotumika kwa tukio lile la kwanza kwa mwanetu Sweetness. Ndugu jamaa na marafiki walijawa na furaha sana ile siku ya ubatizo na walijitokeza watu wengi sana kujumuika na sisi katika ghafla fupi tuliyokuwa tumeanda katika ukumbi wa Diamond Star Hall iliyopo mbauda nje kidogo ya jiji la Arusha.

    Baada ya sherehe ya ubatizo maisha yalizidi kusonga na amani ilizidi kutawala katika maisha yangu ya ndoa, sikuwai kumweleza mtu yeyote kuhusu siri yangu na Derick na wala sikuwa na mpango wa kumweleza mtu yeyote kwasababu nilihofia pengine inaweza ikaja kunivunjia ndoa yangu nilizidi kumwomba Mungu siri ile ibaki kuwa yangu na mwanaume yule kwasababu nilikuwa nampenda sana na ile ndio njia pekee niliyokuwa nimeamua kudhihirisha upendo wangu kwake.

    Mtoto alitimiza mwaka mmoja wa kuzaliwa na tulimfanyia sherehe ndogo ambapo tuliwaalika watoto wote wa pale mtaani kuja pale nyumbani kwangu kushiriki katika sherehe ya mtoto mwenzao. Nilifuraahi sana baada ya kusikia watoto wale wakimwimbia mwenzao wimbo wa kumtakia heri ya kuzaliwa.

    “Happy birthday sweetness,

    Happybirthdaya sweety,

    Happy birthday dear friend,

    Happy birthday to you...”

    ***

    Siku ile ilikuwa ni ya kipekee sana kwangu kwasababu tangu nizaliwe sikuwai kusheherekea siku yangu ya kuzaliwa wala ya mtu mwingine na ile siku ndio nilikuwa na sheherekea ya mwanangu kwa kutimiza mwaka mmoja. Wale watoto ambao wengi wao walikuwa wanasoma katika shule za internantional walikuwa wakizungumza lugha ya kiingereza mwanzo mwisho. Jambo ambalo lilinivutia sana nikaona itabidi nimweleze mume wangu tumpeleke na mwanetu katika shule za International kwaajili ya kumtengenezea msingi mzuri wa kielimu kama ilivyo kwa watoto wa majirani. Wale watoto walicheza, walikula na kunywa na hatimae walirudi majumbani mwao wakiwa na furaha tele.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Sweetness alipofikisha miaka minne alianza elimu ya awali katika shule inayojulikana kwa jina la St Thomas nursery school iliyopo moshono jijini Arusha, nilimshawishi mume wangu tumpeleke Sweetness katika shule ile kwasababu ni shule ambayo nilikuwa nikiifahamu kwa muda mrefu kwasababu ipo mitaa ya nyumbani na inasifika sana kwa kutoa elimu ambayo ina ubora wa hali ya juu. Hivyo basi mwanangu alikuwa anachukuliwa na kurudishwa kila siku na gari la shule, jambo la kufurahisha ni kwamba ndani ya muda mfupi Sweetness alifahamu kusoma na kuandika kwa ufasaha wa hali ya juu jambo ambalo liliniongezea imani ya ufundishaji juu ya ile shule aliyokuwa akisoma mtoto wangu, nilipata moyo wa kumkazania zaidi ili aweze kuwa na mafanikio zaidi kitaaluma na hatimae aje kuwa miongozi mwa mabinti wasomi kwasababu mimi mama yake sikwenda shule.

    Nilipotezana na Derick kwa muda mrefu sana kwasababu tangu awasiliane na mimi kipindi alipokuwa akifanya mahafali ya elimu yake ya juu sikuwai kumpata tena hewani sikujua kuwa alikuwa akifanya kazi wapi na sikufahamu aliishia wapi na mchumba wake, nilikuwa njia panda kwasababu bado mume wangu alikuwa haniridhishi kimapenzi kwahiyo nilikuwa namwitaji kiboko wangu Derick ili aweze kunitibu ule ugonjwa niliokuwa nao kwasababu yeye ndie alikuwa tabibu wangu wa ukweli na sikuwa tayari kuingia kwenye mahusiano na mwanaume mwingine nikihofia pia magonjwa ingawa kutokana na matunzo mazuri niliyokuwa nikiyapata kutoka kwa mume wangu yalisababisha wanaume wengi wanisumbue sana bila kujali kuwa nilikuwa ni mke wa mtu.



    Siku moja majira ya mchana nilikuwa jikoni naandaa chakula cha mchana kwa haraka zaidi kwasababu nilichelewa kutoka shoping Nakumat supermakert Ngarenaro kwahiyo nililazimika kuwa na maandalizi ya chapuchapu kusudi mwanangu atakaporejea nyumbani akute chakula kipo tayari. Ghafla nilipokea simu kutoka kwa mume wangu kipindi chakula kinaendelea kuiva jikoni.

    “Habari za wakati huu mke wangu.”

    “Salama tu vipi hali yako mpenzi.”

    “Njema, naomba ujiandae jioni ya leo nitakaporejea nyumbani nataka tutoke out mke wangu.”

    “Waoo thanks dear, ungependa nivaaje mume wangu?”

    “Sina shaka na uvaaji wako kwasababu hata ukivaa gunia mke wangu utapendeza tu.”

    “Hahaha!” maneno ya Enrique yalinifanya niangue kicheko ambacho sikukitegemea kwa wakati ule.

    Licha ya kucheka na kufurahi lakini baada ya kuzungumza na mume wangu kwa njia ya simu nilijiuliza maswali kadhaa.

    “Kwanini leo mume wangu ananitoa out wakati baada ya kunioa hatukuwai kutoka hata siku moja? Sasa leo kulikoni! Au ndio utaratibu mpya?”

    Ilipofika jioni alikuja nyumbani akanichukua tukaongozana hadi hoteli inayojulikana kwa jina la New Arusha Hotel, kiukweli hoteli ile nilikuwa naiona ya kawaida sana wakati nilipokuwa nikipita mara kwa mara maeneo yale nikielekea katikati ya jiji, lakini ile siku baada ya kuingia ndani ya hoteli ile ya kitalii nilifurahishwa sana na mazingira yake yaliyo ya kipekee na ya kuvutia. Furaha yangu iliongezeka wakati nilipokuwa nikimtazama mume wangu ambae matendo yake yaalidhihirisha upendo wake kwangu.

    “Utapendelea chakula gani mpenzi wangu.” Mume wangu aliniuliza wakati alipokuwa anatazama menu ya chakula wakati muudumu alipokuwa amesimama pembeni yetu.

    “Nimemiss Tilapia.”

    “Isindikizwe na nini Anti?” Sauti nzuri ya upole na kuvutia kutoka kwa kijana mtanashati Wilhelmin muudumu ambae alijitambulisha kwetu kwa jina ilo ilisikika ikinitaka nitoe maelezo ya kutosha.

    “Chipsi pamoja na Ariel Cabernet Sauvignon Non Alcoholic Red Wine.” Nilihitaji chakula na kinywaji hicho ambavyo nilivutiwa navyo sana kipindi kile nilipokuwa fungate na mume wangu katika hoteli ya Ngurdoto Mountain Lodge.

    “Na wewe brother unapendelea nini?”

    “Aisee niletee kama mke wangu.”

    “Karibuni sana.”

    Baada ya muda mfupi meza yetu ilipambwa na vyakula, matunda na vinywaji.

    Mke wangu nimekuleta hapa hotelini kwenye mazingira tulivu ili tuweze kuzungumza mambo kadhaa kwaajili ya familia yetu.” Enrique alizungumza na mimi mara baada tu ya kuanza kula chakula.

    “Chakula kitamu.” Nilikisifia chakula baada ya kuninogea.

    “Ni kweli kabisa ila hakifikii ambacho huwa unanipikia mke wangu.” Mume wangu alininidhihirishia kuwa huwa anafurahia mapishi yangu.

    “Asante mpenzi wangu, kiukweli huduma za hapa nimezipenda pia.”

    “Usijali mke wangu nafanya haya yote kwasababu nakupenda sana.”

    “Nakupenda pia mume wangu kipenzi.”

    “Mke wangu kuna yule mpangaji aliehamia miezi kadhaa iliyopita katika ile fremu yetu ya biashara ambapo alifungua biashara ya vipodozi, yule jamaa alikopa mkopo benki sasa ameshindwa kurejesha mkopo na benki wanakaribia kupiga mnada mali zake kwahiyo amezungumza na mimi kama nitaweza kumpa shilingi milioni 30 aweze kuniachia duka lile ambalo gharama yake ni milioni 50. Embu nieleze wewe mke wangu unamaoni gani juu ya suala hili kwasababu anauza kwa gharama nzuri sana kiasi kwamba tukilichukua na kuliendesha vizuri inaweza kutuletea mafanikio makubwa sana kwenye maisha yetu.”

    ***

    “Ni wazo zuri sana mume wangu mimi sina pingamizi juu ya suala hilo kwasababu linamanufaa juu ya familia yetu.”

    “Asante sana mama mtoto wangu itabidi haraka iwezekanavyo niweze kufanya malipo ili tuweze kulichukua lakini ningependa ufahamu kuwa endapo tutafanikiwa kulichukua duka hilo ni wewe ndie ambae utaliendesha.” Nilihisi furaha kubwa ndani ya moyo wangu kwa kitendo cha mume wangu kutaka na mimi niwe najishuhulisha na utafutaji wenye tija ya kukuza uchumi wa familia yetu.

    “Jamani asante sana mpenzi wangu.” Kwa furaha kubwa nilimshukuru mume wangu kwasababu kiukweli kushinda nyumbani kulikuwa kunanichosha sana isitoshe nimezaliwa katika familia iliyozoea kuchacharika ndio mkono uende kinywani kwahiyo kile kitendo cha mimi kuwa na kaa tu pale nyumbani halafu mume wangu ananiletea kila kitu kilikuwa kinanichosha mno.

    “Lakini pia ukiachilia mbali suala hilo ninajambo jingine ambalo nahitaji kukushirikisha.”

    “Nilitega masikio yangu ili nizidi kumsikiliza Enrique ambae alikuwa anazungumza na mimi kwa sauti ya chini huku akitabasamu kila wakati.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    “Mke wangu nahitaji tupate mtoto mwingine kwasababu Sweetness ameshakuwa alafu pia inapendeza tukizaa watoto wetu harakaharaka ilituweze kuwasaidia kufikia malengo yao angali bado vijana tunanguvu ya utafutaji.” Maneno ya mume wangu yalifanya moyo wangu uanze kwenda kasi mithili ya ndege ya kivita.

    Ile furaha niliyokuwa nayo ilipotea ghafla kwakuwaza nitampata wapi Derick ili aweze kunipa ujauzito mwingine.

    “Au unasemaje mke wangu?” Enrique aliniuliza baada ya kuniona nipo kimya.

    “Sawa mume wangu usiwe na wasiwasi.” Niliitikia tu ingawa nilifahamu kuwa haitakuwa kazi rahisi kwasababu sikuwa na mawasiliano na Derick.

    Moyo wangu ulikosa amani kabisa hata kile chakula nilishindwa kuendelea kula baada ya mume wangu kugusia lile suala la kupata mtoto. Kitendo cha amani kutoweka ndani ya moyo wangu kilisababisha uso wangu kupoteza tabasamu zuri lilokuwa limejidhihirisha kwa muda mrefu na kusababisha mume wangu kutaka kufahamu nini chanzo cha tabasamu langu kupotea ghafla.

    “Vipi mbona umechange ghafla au kuna tatizo?”

    “Nahisi kichwa kinagonga mno.” Nilimdanganya mume wangu ili tuweze kuondoka pale hotelini turudi nyumbani kwasababu hata kile chakula nisingeweza kuendelea kula kwahiyo sikuwa na sababu ya kuendelea kukaa pale hotelini.

    ***

    “Pole sana twende nikupeke hospitali.”

    “Hamna shida mume wangu nitakwenda kumeza panado nyumbani.”

    Wakati nikiwa bado nimekaa kwenye kiti Enrique alitoa koti lake la suti na kunivisha baada ya hapo alininyanyua tukaelekea kwenye gari ili tuweze kurudi nyumbani Njiro kwa Msola.

    Wakati nilipokuwa kwenye gari mume wangu alikuwa ananiongelesha mara kwa mara lakini nilishindwa kumuonyesha ushirikiano kwasababu akili yangu ilikuwa inawaza namna ya kumpata Derick.

    “Hivi itakuwaje endapo nitamkosa Derick aweze kunitatulia huu msala.” Akili yangu ilizidi kupasua mawimbi kufikiri namna ya kumpata Derick.

    Kutokana na mawazo mengi juu ya Derick nilijikuta najisahamu kumwita mume wangu jina lake na kumwita kwa jina la Derick na kusababisha mzozo mkubwa kati yangu na mume wangu usiku ule kabla hatujafika nyumbani.

    “Derick ukifika maeneo ya nanenane usimame tununue mkate wa kunywea chai kesho asubuhi kwasababu hakuna kitafunwa chochote nyumbani.”

    “Derick ndio nani?” mume wangu aliniuliza swali ambalo lilinifanya nihisi kuchanganyikiwa kwasabaabu mimi mwenyewe nilijishtukia kuwa nimechanganya majina.

    “Unamaanisha nini?” nilijifanya sijui chochote kinachoendelea.

    “Nimesikia umeniita Derick sasa napenda kufahamu huyo ndie nani ambae amekukaa kwenye akili yako hadi ufikie hatua ya kuchanganya majina au ndio utajifanya bado hujakariri jina langu?” mume wangu alizungumza huku akiwa makini na uskani wa gari.

    “Mh samahani mume wangu itakuwa nimekosea tu kutamka si unajua utamkaji wa Enrique na Derick unafanana kwa kiasi fulani?”

    “Ahaa kumbe ndio hivyo basi sawa ila naomba utambue njia ya mwongo siku zote huwa ni fupi. Kama kuna kitu kimejificha nakuhakikishia ipo siku nitaujua ukweli ila naomba uwe makini kwasababu hasira zangu ni mbaya kupita kiasi.” Maneno ya mume wangu Enrique yaliniogopesha kwasababu alikuwa akizungumza akionyesha kuwa serious kupita kiasi.

    “Jamani mume wangu mbona unanitisha kwa maneno mabaya hivyo wakati sijafanya chochote kwani wewe huwezi kukosea?”

    “Hapana kukosea kila mtu anakosea ila nakutaadharisha tu usikute una mpango wa kando (mchepuko) ambae anakuzuzua hadi kufikia hatua unanifananisha nae nikigundua kiukweli hata mimi mwenyewe kwa sasa siwezi kukueleza kitatokea nini ila nafikiri kwa namna moja au nyingine inaweza ikawa simanzi kwa ndugu jamaa na marafiki.”

    ***

    “Ondoa shaka mume wangu kwasababu hakuna mwingine zaidi yako na hata tokea hadi siku naingia kaburini.” Ilinibidi nizungumze maneno ambayo yataondoa wasiwasi aliokuwa ameupata juu yangu.

    “Mimi nafurahi kusikia hivyo ila michepuko sio dili kama kunatatizo lolote linakukabili usisite kunishirikisha ili tuweze kulitafutia ufumbuzi kwasababu dunia ya leo imejaa magonjwa kwahiyo mtu usipotulia unaweza ukapata magonjwa katika mambo yasiokuwa na msingi wakati kinachotafutwa nje ya ndoa kipo ndani ya ndoa.” Maneno ya mume wangu yalinidhihirishia kuwa tayari alikuwa ameshaingiwa na wasiwasi mwingi juu yangu.

    “Usijali mume wangu kwasababu ni jukumu letu sote kulindana.”

    Mzozo ule wa maneno baina yangu mimi na mume wangu ulisababisha apitilize lile eneo ambalo nilimwagiza asimame tununue mkate. Aliendesha gari moja kwa moja hadi kwenye supermarket moja inayojulikana kwa jina la Home mini supermakert iliyopo stendi kwa msola na kuteremka na kuchukua mkate na kurudi kwenye gari na kuwasha gari na kuelekea umbali wa mita 150 kutokea pale stendi kwa msola.

    Majira ya saa tatu usiku ndio tulikuwa tumerejea nyumbani nakumkuta mwanetu ameshalala kwasababu tumemzoesha kulala mapema kwasababu huwa namuamsha mapema kila siku kumuandaa ili aweze kuwai shule kwasababu utaratibu wa shule ni kwamba dereva akipita akamkuta mtoto bado hajajiandaa huwa wanamuacha kwasababu gari la shule huwa linazunguka maeneo mengi kuchukua watoto na kuwawaisha shuleni.

    Kutokana na kwamba nilikuwa najihisi kuchoka nilipanda kitandani ili kupumzisha mwili wangu na kumwacha mume wangu sebuleni akiangalia movie ya Titanic ambayo aliinunua siku mbili zilizopita ila kutokana na ubize wa kazi akakosa muda kwa kuiangalia kwahiyo akaona bora atumie ule muda kuingalia kwasababu alikuwa mpenzi mkubwa wa picha za matukio ya historia za kweli.

    Kabla sijalala nilijaribu kwanza kuitafuta namba ya Derick hewani lakini bado haikupatikana hivyo nilikosa usingizi kwa kuwaza cha kufanya ili kuweza kubeba ujauzito wa mtoto wa pili kama ambavyo mume wangu alikuwa anataka.

    “Tena inanibidi niwe makini sana kwasababu mwanaume mwenyewe kashaonesha hali ya kutokuwa na imani na mimi.” Nilizidi kukodoa macho yangu bila kupata usingizi kutokana na wimbi la mawazo lililokuwa limeghubika kichwa changu. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Mume wangu alikuja kitandani na baada ya muda mfupi alipitiwa na usingizi wakati mimi usingizi ulikuwa umenigomea kabisa. Nilijigeuza geuza kitandani hadi jogoo alipowika.

    Siku zilizidi kusonga ikiwa bado sijafanikiwa kumpata Derick hewani, nilinyong’onyea na kukosa raha kwasababu sikujua cha kufanya, kibaya zaidi hakuna hata mwanaume mwingine ambae nilimwona anakili iliyotulia kama ya Derick kwahiyo nilibaki njia panda bila kujua nichukue uwamuzi gani ili kuweza kumridhisha mume wangu mpenzi.

    ***

    Majukumu yangu yaliongezeka kwasababu mume wangu alifanikiwa kununua lile duka la vipodozi kwahiyo kila siku kwa kutumia usafiri wa gari nililokuwa nimenunuliwa na mume wangu nilikuwa natoka nyumbani kwangu njiro hadi katikati ya jiji la Arusha kwenye biashara mabayo mume wangu aliinunua kutoka kwa mpangaji wetu ambae alikuwa amepanga kwenye nyumba ambayo tulizawadiwa na wazazi wa mume wangu siku ya harusi yetu.

    Ufanisi wangu ulikuwa ni mzuri sana kutokana na kwamba nilitokea kuipenda sana kazi ile ambayo ilinikutanisha na watu wengi wanaume kwa wanawake. Wateja wengi walinipenda kutokana na kwamba nilikuwa na lugha nzuri iliyokuwa inamdhihirisha mteja kuwa namjali na kumthamini. Wingi wa wawateja katika duka langu ulisababisha mauzo yaende kwa kasi sana kwani ndani ya mwezi mmoja mume wangu aliagiza mzigo mwingine.

    “Sikujua kuwa wewe ni mwanamke mchapa kazi namna hii hongera sana mke wangu kiukweli nimependa sana utendaji kazi wako, ukiendelea hivi baada ya mwaka tutajenga kiwanda.” Mume wangu alinimwagia sifa ambazo zilinifanya nivimbe kichwa na kujiona kuwa mimi ni mwanamke wa nguvu.

    “Asante sana mume wangu nakuahidi mengi mazuri katika jukumu hili ulilonipatia hakika sintakuangusha.”

    “Nafurahi kusikia hivyo.” Hayo yalikuwa ni mazungumzo yetu siku moja ambapo Enrique alikuja kushinda dukani kwangu kuangalia utendaji wangu wa kazi kutokana na kwamba yeye alikuwa off chakufurahisha ni kwamba alivutiwa na bidii yangu asilimia mia moja.

    Siku moja nilipokuwa dukani kwangu nilijaribu kuitafuta ile namba ya Derick kama nitaipata hewani lakini pasipo kutarajia simu yake ilisikika ikiita na kufanya uso wangu uchanue kwa tabasamu mwanana.

    “Haloo.” sauti ya mwanamke ilisikika upande wa pili.

    “Mh atakuwa mke wake au?” niliwaza kwa haraka.

    “Habari yako.”

    “Nzuri tu nani mwenzangu.” Aliuliza swali ambalo lilikuwa ni gumu sana kwangu, hivyo basi nililipotezea kwa kumtwanga na mimi swali juu ya swali.

    “Mwenye simu yupo wapi?”

    “Mwenye simu ndio mimi kwani wewe unamtafuta nani?”

    “Namtafuta Derick?”

    “Unashida nae gani?” sauti ya yule binti upande wa pili ilizidi kuniangushia maswali ambayo sikuweza kuyapatia majibu ya haraka.

    ***

    Swali lilinishinda ikanibidi nikate simu ili niweze kujipanga zaidi halafu ndio niweze kumtafuta kwa mara nyingine. Lakini kabla hata sijawaza uongo wa kumdanyanya ili aweze kunieleza alipo Derick simu yangu ilianza kuita na nilipoitazama nilikumbana na namba ya Derick ikinipigia.

    “Mbona umekata simu dada?” nilikumbana na swali lingine.

    “Salio ndio limeisha kwenye simu yangu.” Nilimdanganya kwasababu haikuwa kweli kwani simu yangu ilikuwa na vocha ya kutosha.

    “Ok kwani wewe ni nani na unashida gani na Derick?”

    “Mimi naitwa Teddy namtafuta Derick ambae ni fundi wa magari.” Nilizidi kumdanganya yule binti ili kama ndie mke wa Derick asiweze kunihisi vibaya kwasababu sikuwa tayari kuiweka ndoa yake matatizoni.

    “Samahani dada utakuwa umekosea namba kwasababu hii namba ni ya mume wangu ambae nae anaitwa Derick ila sio fundi wa magari.

    “Kwani wewe upo wapi.” Nilimuuliza.

    “Mimi nipo Dar es salaam na hivi ninavyozungumza na wewe ndio kwanza tumefika nyumbani tukitokea safari nje ya nchi.

    “Sawa dada asante ngoja nitafute msaada kwingine kwasababu gari lenyewe ninalo moja tu.” Niliamua kuridhika na majibu niliyopewa kwasababu ningeendelea kuhoji pengine angeweza kuhisi pengine labda kuna kitu kinaendelea kati yangu mimi na mume wake.

    Nilipomaliza maongezi na mke wa Derick nilijaribu kuumiza kichwa kufikiri sababu ambayo ilipelekea Derick kwenda nje ya nchi lakini nilikosa kabisa.

    “Je atanitafuta kweli? ila kwa kuwa leo ndio karejea kutoka nje ya nchi basi ngoja niendelee kusubiri labda anaweza kunitafuta.” Nilizidi kuwaza nakuishia kujipa moyo mwenyewe.

    Ilitimu siku ya tatu ikiwa bado sijafanikiwa kuwasiliana na Derick jambo ambalo liliniumiza na kuninyima raha kwa kuwaza mambo mengi juu yake kwanini asinitafute hadi muda ule, kilichoniumiza zaidi ni kwamba kwenye mitandao ya kijamii napo hakupatikana kabisa account zake zote nilizokuwa nazifahamu facebook, instagram, whatsapp zilikuwa zimedorora kwa kutokutumika. Nilichukua uwamuzi wa kutuma ujumbe mfupi wa maandishi ili niweze kufahamu kulikoni awe kimya kiasi kile.

    “Habari yako Derick mbona upo kimya sana kwani kunatatizo gani mpenzi?” baada ya kumaliza kuandika ujumbe huo nilituma lakini ghafla nilitamani ardhi ipasuke nidumbukie nipotee kabisa baada ya kugundua kuwa ujumbe sikuutuma kwa Derick bali nilikosea nikautuma kwa mume wangu.



    Nilishindwa kuendelea kumudu kushika simu yangu baada ya kuhisi imekuwa nzito ghafla kutokana na mwili wangu kupoteza nguvu kabisa kwahiyo ilidondoka chini paaa! nilikosa raha nafsi ilikata tamaa, jasho lilikuwa linatiririka mithili ya mtu alienyeshewa na mvua, nguo zote nilizokuwa nimevaa zililowa jasho kutokana na hofu niliyokuwa nimeipata baada ya kukosea kutuma ujumbe mfupi wa maandishi niliokuwa nimekusudia uende kwa mchepuko na kwenda kwa mume wangu. Tumbo lilianza kunisumbua kwa kunguruma na baada ya muda mfupi nilitoka mbio kuwai chooni kwasababu nilihisi kuharisha.

    “Ee Mungu naomba unisaidie.” Nilijikuta nazungumza peke yangu wakati nilipokuwa chooni namwaga uharo sawasawa.

    Kwa jinsi nilivyokuwa nimepaniki ilipelekea wateja waliofika pale dukani kwangu kwa wakati ule wanishtukie kuwa sipo sawa.

    “Vipi dada unaumwa?” Mteja mmoja ambae alikuwa mtani wangu aliniuliza swali baada ya kuona kuwa sipo sawa na siku zingine alizozoea kunikuta pale dukani.

    “Sipo vizuri kiukweli.” Nilimjibu kwa kifupi huku tumboni nikisikilizia mingurumo ambayo ilikuwa ikiambatana na maumivu ya tumbo ambayo ilinianza ghafla baada ya wasiwasi kunizidi.

    “Pole sana ila fanya mpango ufunge uwai hospitali kwasababu unaweza kukuta ni malaria.”

    “Sawa asante.” Pamoja na kwamba nilikuwa nazungumza na huyo mteja lakini akili yangu ilikuwa mbali sana ikiwaza ni namna gani nitaweza kumdanganya mume wangu ili aweze kunielewa. Nilikuwa nikitoa macho kama mjusi aliebanwa na mlango kuitazama ile meseji kama nikweli imeenda au la! Lakini ujumbe ulionyesha umepokelewa upande wa pili jambo ambalo lilizidi kunivuruga akili yangu.

    “Ukisikia kifo ndio hiki ambacho nimekitafuta mwenyewe.” Niliwaza huku nikizidi kusumbua kichwa kutafuta namna ya kuweza kumdanganya mume wangu.

    Nilipata wazo nimpigie nimuombe msamaha kwa kile kilichotokea kwasababu lazima kitakuwa kimemuumiza sana kwani nikiendelea kumdanganya kwa hasira zake anaweza kunifanya kitu kibaya sana kwasababu huwa anapenda mtu amweleze ukweli kuliko kumdanganya.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    “Halafu pia nikizungumza nae nitafahamu kuwa amepaniki kwa kiasi gani ili kama ataonekana amechukia sana na hanielewi kabisa nisirudi nyumbani kwasababu anaweza kwenda kuniua.”

    Nilihisi kuzirai baada ya kumpigia simu mara ya kwanza, ya pili ya tatu ya nne bila kupokelewa.

    “Mmh hapa lazima nitakuwa nimelikoroga sasa sijui ni nani atanisaidia kulinywa kwasababu ni ngumu kumeza.” Niliwaza huku mapigo yangu ya moyo yakizidi kunienda kasi mithili ya mbwa mwenye kichaa.

    Sikukata tamaa niliendelea kumtafuta Enrique hewani kwa mara ya tano lakini bado simu yake haikupokelewa.

    Nilimtafuta kwa mara nyingine huku nikizidi kumwomba Mungu kimyakimya aweze kunisaidia ndoa yangu isiweze kuvunjika lakini kwa bahati njema simu ya mume wangu ilipokelewa na nilikumbana na sauti ambayo haikuwa ya mume wangu na kupata wasiwasi zaidi kwa kuwaza ni nini kilichokuwa kinaendelea.

    ***

    “Samahani dada simu hii imesahauliwa na mteja hapa hotelini kwetu kama nusu saa iliyopita lakini tayari ameshapiga simu kuwa atakuja kuichukukua muda sio mrefu kwahiyo nakwomba umtafute baadae kidogo.” Maneno ya kaka yule yalikuwa ni kama maji kwa mtu aliekuwa akihisi kiu jangwani. Matumaini yalirejea ndani ya nafsi yangu kwa kuwa na uhakika kuwa ndoa yangu bado ipo salama kwasababu tukio la mimi kukosea kutuma meseji ile halikuwa limejiri nje ya huo muda alionitajia kuwa mume wangu alisahau simu yake.

    “Asante Mungu.” Nilijisemea kimyakimya kwa kuona kama ule ulikuwa ni muujiza mkubwa ambao Mungu alinitendea katika maisha yangu kwasababu sikuwa na maelezo ya ushawishi wa kutosha kupunguza hasira ambayo ingekuwa imempanda mume wangu. Sikuogopa sana baada ya kusikia kuwa amesema kwamba ataifuata simu ile kwasababu niliona ndani ya ule muda mfupi nilipata matumaini yakuweza kulitatua lile tatizo.

    “Sawa kaka nimekwelewa lakini kunajambo moja nakuomba unisaidie.” Nilizungumza wakati bado nikiwa na chembechembe za hofu ndani yangu kwasababu bado sikuwa na uhakika kama yule kaka anaweza kuwa msaada kwangu.

    “Unatatizo gani?”

    “Mimi ni mke wa mwenye simu ila kuna meseji nilikuwa naituma kwa mchepuko wangu nikakosea nikaituma kwa mume wangu kwahiyo naomba msaada wako hiyo meseji niweze kuifuta kabla mume wangu hajafika hapo hotelini kwenu kuchukua simu yake.”

    “Duuh! mbona unanipa mtihani mkubwa mno?”

    “Naomba unisaidie tafadhali nitakupa zawadi yeyote utakayohitaji endapo utanisaidia kutatua tatizo hili linalonikabili kwasababu sina msaada wowote isipokuwa wewe kaka, usinitose jamani hakuna binadamu aliyemkamilifu nihurumie binadamu mwenzio nimenasa kwenye mtego ambao unanisababishia maumivu makali ya mwili na roho.” Nilizungumza kwa sauti ya huruma ili yule kaka aweze kunihurumia.

    “Usijali Anti ingawa nakwenda kinyume na maadili ya kazi yangu ila sina budi kukusaidia.” Kaka yule alionyesha huruma ya kunisaidia baada ya kunisikiliza nikizungumza kwa hisia zilizodhihirisha nilikuwa nahitaji msaada wake.

    “Nashukuru sana Anko.”

    “Nipe password ya simu ya mume wako.”

    “41144114.”

    “Meseji uliyokosea kuituma inasomekaje?”

    “Nilimweleza harakaharaka.” Baada ya hapo alikata simu ili aweze kuifuta meseji ile niliyokuwa nimekosea kuituma.

    ***

    Baada ya dakika mbili kupita simu yangu ya mkononi iliita nilipoitazama niliona ni namba ya mume wangu inanipigia moja kwa moja nikafahamu kuwa atakuwa ni yule kaka ndie ananijulisha kuhusu lile zoezi nililokuwa nimempatia.

    “Tayari nimeshafuta.” Nilikumbana na sauti ya kaka yule baada ya kupokea simu kunijulisha kuwa amefanikisha kazi niliyokuwa nimempatia. Nilijisikia furaha sana kwasababu sikutegemea kabisa kama zoezi lile lingefanikiwa.

    “Asante sana Anko Mungu akubariki sana kiukweli umenipa msaada ambao sintakaa niusahau mpaka siku naingia kaburini.”

    “Usiwe na wasiwasi Anti maisha ni kusaidiana.”

    Asante sana. Ila samahani kaka sijui unaitwa nani?”

    “Naitwa Mohamed Ally, ni meneja wa Z.P hotel.

    “Jamani nimefurahi sana kukufahamu, isitoshe nimeshakuja hapo hotelini kwenu kama mara mbili kupata chakula nikiwa na mume wangu.”

    “Karibu tena.”

    “Asante sana nitakutafuta nikupatie zawadi yako.”

    “Poa usijali Anti.”

    Nilimaliza kuwasiliana na na meneja wa ile hoteli huku moyo wangu ukimshukuru sana Mungu kwa ule muujiza ambao aliutenda kwangu ile siku.

    “Kweli Mungu ni waajabu sana.” niliwaza kwasababu bado nilikuwa siaminiamini kile kilichokuwa kimetokea.

    “Hivi mume wangu kwa jinsi anavyonihudumia kwa kunipa kila kitu ninachotaka angejua namsaliti si angeweza kuniua?” nilijikuta nazungumza peke yangu pale dukani kama mtu aliyechanganyikiwa.

    Niliwai kutoka kazini ile siku na kupita soko kuu kwenda kununua ndizi nikampikie mume wangu kwasababu huwa anapenda sana ndizi. Nilipofika nyumbani kwangu mida ya jioni nilianza kuandaa chakula ambacho huwa mume wangu anakipenda sana. Mume wangu aliporejea nyumbani alikuta ndio namalizia kuandaa chakula.

    “Pole sana dia.” Nilimpa pole mpenzi wangu huku nikipokea koti lake la suti pamoja na mfuko aliokuwa ameubeba ukionekana kujaa mapochopocho.

    “Asante mke wangu.”

    “Mume wangu alipotoka kuoga na mimi nilikuwa nimeshamaliza kuandaa chakula kwahiyo tulijumuika pamoja mezani kupata chakula cha jioni.”

    ***

    “Mke wangu chakula kitamu sana.”

    “Asante mume wangu.”

    “Kula mwanangu ukalale mapema kesho uwai shule.” Mume wangu alizungumza na Sweetness ambae alikuwa anatazama televisheni badala ya kula chakula.

    “Halafu sijakweleza mke wangu yani leo mchana baada ya kumaliza kula katika ile hoteli ya Z.P nikasahau simu yangu kutokana na haraka zangu.”

    “Mmh! kwahiyo ikawaje sasa.” nilijifanya sifahamu kabisa kinachoendelea ili hali nilikuwa nafahamu kila kitu.

    “Ile hoteli ina wahudumu waaminifu sana kwasababu sio mara ya kwanza nasahau simu pale ila nikirudi huwa wananipatia simu yangu.”

    “Pole.”

    “Ahsante sana.”

    “Punguza mawazo mume wangu.” Nilijifanya namshauri apunguze mawazo wakati mawazo aliyokuwa nayo yakamsahaulisha simu ndio yaliyoniokoa ile siku la sivyo ndoa yangu ingesarambatika kama glasi iliyodondoka sakafuni.

    Siku iliyofuata asubuhi wakati nilipokuwa nakwenda kazini kwangu nilipitia katika ile hoteli ambayo mume wangu jana yake alisahau simu ili nikamwone yule meneja niweze kumpatia zawadi ambayo nilikuwa nimemuandalia kwa msaada ambao alinipatia.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Nilipofika nilifanikiwa kukutanana nae nilivutiwa sana na muonekano wake wa utanashati, mpole na mnyenyekevu. Pamoja na kwamba nilipokuwa kwenye gari nilikuwa nimepanga nimpatie shilingi laki moja kama zawadi ya shukrani kwa msaada wake ila nilibadili mawazo ghafla baada ya kupiga nae stori kwa dakika kadhaa na kushuhudia uzuri wa kaka yule na kusababisha nimpatie zawadi ya shilingi laki mbili lakini nilishangaa sana baada ya kaka yule kukataa kupokea zile pesa kwa kunieleza kuwa aliamua kunisaidia tu kwahiyo nisiwe na wasiwasi kabisa.

    Niliumia sana roho kwasababu nafsi yangu ilikuwa inatamani kulipa fadhila kwa wema ambao alinitendea. Japo kuwa nilimlazimisha sana lakini alizidi kuonyesha msimamo wake wa awali wa kukataa ile zawadi niliyompatia na kuzidi kunisisitiza kuwa amenisaidia kwa moyo mmoja kwahiyo nisiogope.

    Basi kaka naomba namba zako ili siku tukutane hata sehemu tuweze kupata chakula pamoja.” Nilijaribu kutafuta namna nyingine ya kuweza kumwonyesha yule kaka kuwa nilikuwa na kila sababu ya kumshukuru.

    “Ok.” aliitikia huku akichomoa business card yake.

    “Napatikanaa kwa namba hizo hapo kwenye kadi.”

    ***

    “Sawa kaka nashukuru sana.”

    “Usijali Anti.”

    “Asante sana kaka tutawasiliana.” Nilizungumza wakati nashikana mkono na Mohamedi kumuaga ili niweze kuwai kazini kwangu.

    “Nashukuru.” Sauti ya upole ya yule kaka ilisikika ikinishukuru.

    Nilirudi kwenye gari langu nikitokea kwenye hoteli hiyo ambayo inapatikana maeneo ya Metropol kuelekea ofisini kwangu maeneo ya shekhe amri abeid stedium. Niliumiza kichwa changu kuhusu zawadi ambayo nitaweza kumpatia yule kaka. Nilifika kazini kwangu na kufungua ofisi yangu lakini nilikuwa kama sijielewielewi kabisa kwasababu akili yangu ilikataa kuacha kumuwaza Mohamedi ambae nimemwona kwa mara ya kwanza na kumpenda. Taswira ya mwonekano mzuri wa kaka yule ilinifanya nishindwe kabisa kuzuia hisia zangu juu yake kwani alikuwa ni mrefu kiasi halafu shombeshombe akicheka anamwanya mzuri wa kuvutia.

    Nilishindwa kuzuia hisia zangu ikanibidi nimpigie simu asubuhi ileile.

    “Samahani Mohamedi.”

    “Bila samahani Anti.”

    “Samahani nimevutiwa na harufu ya marashi yako naomba unielekeze inaitwaje kusudi niweze kuitafuta.” Nilimuuliza ili hali nilikuwa nafahamu alikuwa amejipulizia pafyumu ambayo nilikuwa naifahamu kwasababu ilikuwa dukani kwangu na niliifahamu kwasababu ndio pafyumu ambayo naiuza bei ghali kuliko zote pale dukani kwangu.

    “Ooh! Thank you inaitwa AnnickGoutal Eaud’Hadrien.”

    “Nzuri sana jamani nitaipataje?” nilizidi kuuliza ili nizidi kusikia sauti yake ambayo ilikuwa na mvuto masikioni mwangu.

    “Inapatikana kwenye maduka mengi sana hapa mjini.”

    “Sawa asante samahani kwa usumbufu.”

    “Bila samahani Anti karibu sana.”

    “Asante sana bye.”

    Nilikata simu nafsi yangu ikiwa imeridhika kwa kiasi fulani baada ya kuzungumza na Mohamedi. Nilianza kuwasiliana rasmi na meneja yule ambae alionekana bado alikuwa na umri mdogo. Nilikuwa nikijisikia vizuri sana wakati nilipokuwa nikifanya mazungumzo na yeye kwasababu moyo wangu ulikuwa umeshampenda, hata Derick sikumkumbuka tena kwasababu nilihisi kaama amenichunia kwahiyo sikuwa na sababbu ya kuendelea kumsumbua wakati moyo wangu ulikuwa umempenda mwanaume mwingine.

    ***

    Ilikuwa wiki ya pili baada ya kujuana na Mohamedi, siku moja baada ya kufika kazini nilimuandikia ujumbe mfupi wa maandishi kumtakia kazi njema lakini muda huohuo alinijibu meseji yangu.

    “Asante sana japo kuwa leo siingiii kazini nipo off.” Nilifurahi sana baada ya kusikia kuwa ile siku ilikuwa siku yake ya mapumziko.

    “Kwahiyo leo utakuwa wapi?”

    “Leo napumzika tu nyumbani kwangu wala sina mpango wa kutoka.”

    Jamani njoo bwana mjini?”

    “Hapana kiukweli siji kabisa huko labda kama unaweza wewe ndie uje kwangu.”

    “Nitajieleza vipi kwa mke wako?”

    “Sina mke naishi peke yangu.”

    “Unaishi maeneo gani?”

    “Naishi sakina kibanda cha maziwa.”

    “Poa nakuja sasa hivi.”

    Kwa namna ambavyo nilikuwa nimempenda Mohamed wala sikuwaza endapo mume wangu angekuja dukani na kunikosa ningemdanganyaje ingawa nilifahamu sio rahisi kuweza kufika pale dukani kwasababu huwa anakuwa bize sana pindi anapokuwa kazini kwake kwahiyo sikuwa na wasiwasi kabisa.

    Mohamedi alinielekeza kwa simu hadi nikafika nyumbani kwake. Nilishangaa sana nilipofika nyumbani kwa kaka yule kwasababu kiumri alikuwa bado ni mdogo lakini alikuwa na mafanikio makubwa sana kiasi cha kuchanganya akili yangu.

    “Hongera sana Anko unamafanikio makubwa mno.”

    “Asante.”

    “Unatumia kinywaji gani.”

    Juisi yeyote natumia.”

    “Alisogea kwenye friji kubwa iliyokuwepo pale sebuleni kwake na kunimiminia juisi ya parachichi kwenye glasi na kuniletea. Nilikunywa huku nikiinjoi stori mbalimbali alizokuwa akinisimulia kaka yule ambazo zilikuwa zimesheheni vichekesho vya kuvunja mbavu.

    ***CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Hivi kumbe wewe ni mwongeaji kiasi hiki.” Nilishangazwa na uchangamfu aliokuwa ananionyesha yule kaka kwasababu sikuwai fikiri kuwa ni mcheshi kiasi kile. Tulikuwa tunazungumza kana kwamba tulikuwa tumefahamiana kwa muda mrefu. Stori zilizidi na hatimae zilianza kuambatana na michezo ya kimahaba ambapo baada ya muda uzalendo ulimshinda kila mmoja wetu na kupelekea kuhamia chumbani kwa Mohamedi ambapo tulijitosa katika bwawa kubwa la mahaba. Baada ya tendo nilishtuka sana baada ya kukumbuka kuwa sikuwa nimetumia kinga na nilikuwa katika siku za hatari. Nilianza kujilaumu kwa kile kitendo nilichokuwa nimekifanya kwasababu sikujua uzima wa afya ya mtu niliekuwa nimeshiriki nae tendo la ndoa.

    “Yani tumelala bila kinga?”

    “Sijawai kula tunda na ganda na wala haita kaa itokee.”

    “Inamana wewe kila mwanamke unamwamini?”

    “Yani hata kama simwamini lakini siwezi kabisa kutumia kinga kwasababu sifurahii kabisa tendo.”

    “Vipi kama nitakuwa nimeshika ujauzito.”

    “Kwani wewe ni mtoto hadi ushindwe kujua namna ya kujikinga na mimba.”

    “Uuwii nimekwisha ” Niliwaza kwa kujuta baada ya kusikia majibu yale.

    Baada ya kuondoka nyumbani kwa Mohamedi nilifika nyumbani nikiwa nimechoka sana, sikuweza kula chakula nilichokuwa nimekiandaa kutokana na hali ya uchovu niliyokuwa nayo, nilimdanganya mume wangu kuwa nilikuwa najihisi maumivu makali ya kichwa ingawa alinishauri anipeleke hospitali lakini nilimgomea kwa kumweleza kuwa nilikuwa nimeshameza dawa aina ya parasetamo kwaajili ya kutuliza maumivu ya kichwa.

    Baada ya kushiriki tendo la ndoa na Mohamedi wiki mbili baadae nilihisi ninaujauzito baada ya mwili wangu kuonyeshaa kila dalili ambayo humkuta mwanamke mwenye mimba.



    Nilihisi kuchanganyikiwa kwasababu nilijiua endapo nitakubali kubeba ujauzito ule mwisho wa siku nitaumbuka na itasababisha kuibuka kwa kizaazaa na kimbembe kikali baina yangu mimi na mume wangu kwasababu mtoto atakaezaliwa lazima atakuwa na ufanano na mwanaume alienipa ujauzito.

    “Ukisikia kuumbuka ndio huku.” Niliwaza baada ya kuhisi mate kujaa mdomoni kwa sababu ya kichefuchefu kilichonijia pindi nilipokuwa nakunywa chai.

    Sikuwai kumshirikisha rafiki yangu yeyote kuhusu siri zangu lakini kwa mara ya kwanza ilinibidi niwasiliane na rafiki yangu Glory ili niweze kumshirikisha juu ya tatizo lile kusudi aweze kunisaidia kwasababu nilikuwa nahitaji msaada wa haraka kabla mambo hayajaaribika. Nilimpigia simu na kumweleza kuwa anifuate dukani kwangu kwasababu kuna jambo nilikuwa nahitaji kuzungumza nae. Hivyo basi kwasababu alikuwa ni rafiki yangu damudamu alivunja ratiba zake kwa kuitikia wito wa kufika pale dukani kwangu muda ule. Alitia timu pale dukani na kukuta fikra zangu zimetekwa na wimbi la mawazo juu ya ujauzito niliokuwa nimeupata pasipo kudhamiria.

    “Karibu shoga angu” moyo wangu ulipata faraja kidogo baada ya kumwona rafiki yangu nikiamini hakuna kitakachoshindikana.

    “Asante, vipi kwema hapa.”

    “Huku kwema kabisa sijui huko utokapo shosti yangu.”

    “Alhamdulillah tunamshukuru Mungu.”

    “Utatumia chakula gani na kinywaji gani?”

    “Chipsi kuku na fanta pineapple ya moto.”

    Nilimpigia simu dada ambae mara nyingi huwa ananiletea chakula pale dukani kwangu ili aweze kuleta chakula ambacho rafiki yangu alikihitaji na baadaa ya dakika 25 chakula kililetwa. Sikuweza kuagiza chakula kwaajili yangu kwasababu nilikuwa nahofia kutapika kwasababu chochote kilichokuwa kikifika tumboni mwangu ni lazima kirudi isipokuwa maji ya kunywa.

    “Ehee niambie mama Sweetness.” Alizungumza rafiki yangu wakati alipokuwa anaendelea kula chakula.

    “Mwenzio ninamajanga.”

    “Vipi umekosana na Enrique?”

    “Hapana ila ndiko nakoelekea kama sitojiadhari.”

    “Unamaanisha nini?”

    Shoga angu kunajambo moja la siri sana nahitaji nikushirikishe kwasababu wewe ni rafiki yangu mkubwa halafu isitoshe tumetoka mbali sana kiukweli sina msaada mwingine isipokuwa nategemea ushauri wako ndio uweze kuniokoa kwa haya maji yaliyonifika shingoni. Yani hapa nilipo ninaujauzito ambao nimeubeba nje ya ndoa yangu sipati picha kabisa mume wangu atakapogundua kuwa nimezaa na mwanaume mwingine kwasababu anaweza kunipa kilema au kuniua kabisa kwasababu anasimamia majukumu yake ipasavyo kama mwanaume.

    “Pole sana, lakini sasa kwanini usiuchune tu umshikishe?”

    “Weweee! Siwezi kujaribu kufanya hivyo kwasababu alienipa ujauzito huu ni shombeshombe.”

    “Duuh! Kweli majanga sasa na wewe shoga yangu umetoka wapi na huyo mwanaume na ikawaje ukalala nae bila kinga wakati unajua upo kwenye siku za hatari na isitoshe wewe ni mke wa mtu?”

    “Acha tu Glory ni stori ndefu nikisema nikusimulie hii siku haitatosha.”

    “Huyo mwanaume yeye anasemaje?”

    “Wala hata sijathubutu kumshirikisha na wala sipo tayari.”

    “Kwanini?”

    ***

    “Hata na yeye atanishangaa na kuniona mtu wa ajabu kwasababu uzembe ni wangu na sina mtu wa kumlaumu.”

    “Ama kweli kazi ipo.”

    “Sio mchezo nahitaji kutuliza akili sawasawa ili niweze kukabiliana na jambo hili.”

    “Hapo hakuna njia ya kutatua tatizo hilo isipokuwa kuchomoa huo ujauzito kabla mume wako hajafahamu kinachoendelea.” Maneno ya Glory yalinitia hofu sana kwasababu sijawai kutoa mimba kwasababu madhara ya kutoa mimba nilikuwa nayafahamu vizuri.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    “Mmh! Nitaanzia wapi wakati sijawai kufanya kitendo hicho hata siku moja na itakuwaje endapo mume wangu atahitaji haki yake ya ndoa.”

    “Itabidi umdanganye unaumwa kwani atakubaka ukimweleza unaumwa.”

    “Hapana.”

    “Ok kazi kwako.”

    “Wewe ushawai kutoa mimba?” ilinibidi nimuulize kwasababu alionyesha ujasiri wa hali ya juu wakati alipokuwa akishauriana na mimi.

    “Ndio, tena tatu.”

    “Mmh! Hukuogopa pengine unaweza ukapata athari ambayo itapelekea kushindwa kuendelea kushika ujauzito.”

    “Ukimchunguza bata huwezi kula nyama yake kwahiyo mambo mengine unapotezea tu.”

    “Ni wapi huko ambapo ndio nitaweza kupata huo msaada?”

    “Kwa mama mmoja mtaalamu wa tiba za asili anakuchomolea fasta unarudi katika hali yako ya kawaida.”

    “Mmh! Huko mimi siendi.”

    “Yupo vizuri kupita maelezo.”

    “Hapana aisee bora nizae tu.” Nilimkatalia katakata kwasababu nilikumbuka kwamba kipindi nikiwa kidato cha pili kuna msichana alifia kwa mama mmoja mtaalamu wa tiba za asili wakati alipokuwa akitoa mimba kwahiyo ilinipa hofu sana nikaona kuliko iwe hivyo ni bora nizae chotara wangu.

    Tulipiga stori sana na yule rafiki yangu kwa muda mrefu na ilipotimu saa kumi naa moja jioni nilifunga duka na nilimpa lifti hadi kijenge ambapo alipanda gari linaloekea moshono nyumbani kwao na mimi niliekea njiro nyumbani kwangu.

    ***

    Baada ya siku tatu nilimshirikisha rafiki yangu Doroth kuhusiana na lile tatizo lililokuwa linanikabili baada ya kukataa kulifanyia kazi wazo la Glory la kunitaka niende kwa tatibu wa tiba za asili ili aweze kunipa dawa ya kutoa ule ujauzito nikihofia usalama wa maisha yangu.

    Doroth alinishauri kwamba niende hospitali nimuhonge daktari pesa halafu tufanye njama ya kumdanganya mume wangu kuwa ujauzito umetoka.

    Niliona ni wazo zuri sana kwasababu pia nitaepuka usumbufu kutoka kwa mume wangu pindi atakapokuwa anahitaji haki yake ya ndoa. Kwasababu nilikuwa sijamweleza kuwa ninaujauzito ilinibidi nijipange nimweleze kuwa tayari nilikuwa na ujauzito.

    Mida ya usiku nilipokuwa chumbani mume wangu alionesha kufurahi sana mara baada ya kumweleza kuwa nina ujauzito wa mtoto wa pili.

    “Hongera sana mke wangu kipindi hiki nafikiri utaniletea dume la mbegu.”

    “Hahaha! hakuna cha dume ni mwendo wa majike mwanzo mwisho.” Nilizungumza kwa kumtania Enrique kwasababu alikuwa anapenda sana watoto wa jinsia ya kiume.

    Taarifa ya kuwa na ujauzito niliyokuwa nimempa mume wangu ilimfanya ajione rijali na muda huohuo akatamani alimege tunda lake ambalo alikuwa hajaligusa kwa muda wa siku tatu. Kusema kweli nilikuwa sioni raha yeyote ya kushiriki tendo la ndoa na mume wangu kwasababu nilikuwa naona kama ananichafua tu kwani mchezo wake ni wa muda mfupi sana hadi nakereka ndio maana huwa nawapa watu wengine wenye ufundi mzuri wa kulitafuna tunda wamsaidie kulimega tunda.

    Kwasababu ni haki yake sikuwa na namna ya kumwambia sipo tayari kwasababu isiyokuwa ya msingi kwahiyo nilimtengea tunda lake vizuri ndipo alianza kulimega taratibu na baada ya muda mfupi kama ilivyo kawaida kijasho chembamba kilianza kumtoka huku akihema mithili ya punda kuashiria kuwa alikuwa ameshachoka tayari. Ilinibidi nmng’ang’anie abaki juu ya kifua changu kwasababu sikuwa nimetosheka lakini aliniambia kuwa amechoka anahitaji kupumzika ili kesho awai kazini. Nilikasirika sana na kujikuta nimeropoka.

    “Sasa inamana mume wangu usiponiridhisha unataka nani aniridhishe?”

    “Embu tulale bwana kesho tuwai kwenye majukumu yetu.” Jibu la mume wangu lilinifanya nizidi kujihisi vibaya kwa kuwaza pengine anamwanamke mwingine ambae huwa anamaliziaga nguvu huko ndipo anakuja kwangu. Lakini moyo wangu ulikataa kutoa ushirikiano kwa fikra zangu baada ya kukumbuka kile kipindi cha fungate wiki nzima hotelini na hali ilikuwa vilevile.

    “Mume wangu haya maisha hadi lini lakini?” nilizidi kumsakama kwa maneno kusudi aweze kufahamu kuwa nilikuwa namaanisha kwa kile nilichokuwa nakizungumza.

    “Hivi we mwanamke unamatatizo gani? Nimekwambia sihitaji kelele nimechoka.” Ilinibidi nifunge mdomo wangu kwasababu Enrique alianza kukasirika.

    ***

    “Its ok Enrique I have understood.” (sawa Enrique nimekwelewa.) nilikubali mzozo uishe lakini moyo wangu ukiwa unaniuma sana kwasababu yeye ndie chanzo cha mimi kuangaika nje ya ndoa kutafuta mwanaume wa kuniridhisha kimapenzi.

    Wiki moja baada ya kumweleza kuwa ninaujauzito ilinibidi niende hospitali ambayo nilielekezwa na Doroth kwamba naweza kupata huduma nzuri itakayonifaa nilifanya harakaharaka kwasababu Doroth alinieleza kwamba kwa kadiri mimba inazidi kukuwa ndivyo ambavyo itasumbua wakati wa kuitoa na mbaya zaidi inaweza kunigharimu maisha endapo nitazidi kuchelewa kwahiyo sikuwa na jinsi isipokuwa kuitoa kwa wakati ule kabla haijawa kubwa sana.

    Siku hiyo mara baada ya kupata kifungua kinywa nikaagana na mume wangu kuwa nakwenda kazini na yeye akaelekea kwenye shughuli zake nilipofika kazini nilikaa kwa muda kidogo halafu nikafunga duka nikaenda hospitali ambapo nilifika na kumkuta Dokta Nkya ambae Doroth aliniunganisha nae. Alikuwa ni mzee wa makamo na mstaarabu sana kwa namna ambavyo alikuwa akizungumza kwa busara ya hali ya juu.

    “Karibu sana binti nimepata habari zako kutoka kwa Doroth.”

    “Ndio dokta huu ujauzito nimeubeba nje ya ndoa yangu kwahiyo nahitaji baada ya kufanikisha kuutoa nifanye mawasiliano na mume wangu nimweleze kuwa nimelazwa hapa na akija umweleze kitaalamu sababu ambayo utaiona inafaa kumdanaganya kuwa ndio imepelekea ujauzito kutoka.” Nilijieleza kwa daktari kwa sauti ya chini.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    “Usijali hilo ni tatizo dogo sana wenye matatizo kama yako huwa wanakuja wengi sana na hivi ninavyozunguza na wewe nimetoka kumsaidia mtu mwenye tatizo kama lako.” Nilipata moyo baada ya daktari kuzungumza na mimi vile kwa hali ya kunitia moyo.

    “Sawa dokta.”

    “Gharama yake ni shilingi laki nne.”

    “Sawa hakuna tatizo.”

    “Basi tumalizane muda huu ili tufanye kazi mara moja.” Sauti ya dokta ilinifanya nikurupuke nipeleke mkono kwenye mkoba wangu ili niweze kutoa pesa kwasababu mawazo yangu yalikuwa mbali nikiwaza itakuwaje muda mfupi ujao ambao nitakuwa nafanya dhambi ambayo sikuwai kuifanya hata siku moja katika maisha yangu. Nilitoa bunda la pesa zaidi ya milioni moja nilizokuwa nimefunga kwa rababendi na kumuhesabia dokta kiasi ambacho amenitajia na kumpatia.

    “Panda hapo kitandani.” Nilitii amri ya daktari ingawa moyoni nilikuwa na hofu kubwa juu ya tendo lile linalokwenda kutendeka.

    “Vipi dokta nitakuwa salama?” nilimuuliza huku moyo wangu ukiwa umejaa wasiwasi mwingi kwasababu watu wengi sana nimeshasikia kuwa wameshapoteza maisha wakati wakitoa mimba.

    ***

    “Usijali binti utakuwa salama kabisa kwasababu mimba yako bado ni ndogo.” Dokta alizungumza kwa lafudhi ya kichagga kunihakikishia kuwa sintapatwa na tatizo lolote.

    Lisaa limoja baadae kwa jitihada za dokta kiumbe kile kilichokuwa ndani ya tumbo langu kilifanikiwa kutoka kikiwa kimeharibiwa mno kwa namna ambayo dokta alifanya kuhakikisha anakichomo ndani ya tumbo langu. Tukio lile liliambatana na maumivu makali sana na damu zilinitoka nyingi kupita kiasi hadi nikaingiwa na wasiwasi lakini dokta Nkya alinitowa woga kwa kunileza kuwa ile ni hali ya kawaida moyo wangu uliniuma sana na kujutia ile dhambi ambayo nilikuwa nimeitenda kwasababu sikuwai kufikiria kama ipo siku nitaweza kufanya tukio la kinyama kama lile.

    Baada ya tukio kumalizika daktari alinieleza kuwa napaswa kupumzika hospitalini pale hadi jioni ili aweze kuona maendeleo yangu kiafya hivyo basi nilimpigia mume wangu simu kumweleza kuwa nimelazwa katika kituo cha afya kijulikanacho kwa jina la Menon health care.

    Kiukweli mume wangu alishtuka sana aliposikia nimelazwa kwa vile wakati naondoka kazini kwangu nilimtumia ujumbe mfupi wa maandishi kumjulisha kuwa nilikuwa nikihisi maumivu ya tumbo hivyo nilimweleza nakwenda hospitali kupata uchunguzi wa daktari kwahiyo hakupata wasiwasi sana kwani alijua ni tatizo dogo.

    Usingizi ulinipitia pale kitandani nilipokuwa nimelazwa na nilipokuja kuzinduka macho yangu yalikutana na sura ya mume wangu akiwa anafanya mazungumzo na daktari alienifanyia tukio lile.

    “Pole sana mke wangu.” Mume wangu alinipa pole huku akinibusu katika paji langu la uso.

    “Asante.” Nilimshukuru mume wangu huku machozi yakinitiririka usoni mwangu kumdhihirishia kuwa niliumizwa sana na tukio lile la ujauzito wangu kutoka lakini haikuwa kweli kabisa kwasababu nilikuwa namng’ong’a kwa kumuona kama nyuki wa mashineni asiekuwa na madhara.

    “Usijali dia Mungu atatujalia mtoto mwingine.” Sauti ya upole na masikitiko ya hali ya juu ilisikika ikitoka kinywani mwa Enrique.

    Jioni ilipofikia nilirejea nyumbani nikiwa na mume wangu japokuwa hali yangu bado haikuwa ya kuridhisha kwasababu mwili ulikosa kabisa nguvu. Ndugu jamaa na marafiki walifika nyumbani kwangu kunijulia hali kutokana na tatizo lililokuwa limenipata. Hakuna mtu aliekuwa anafahamu ile mbinu niliyokuwa nimeitumia kuitoa mimba ile isipokuwa rafiki yangu Doroth pamoja na Glory ingawa niliwasihi sana wanitunzie siri yangu isiweze kuvuja kwasababu inaweza kuhatarisha maisha ya ndoa yangu.

    Enrique alizidi kunionyesha upendo wa hali ya juu kwasababu alifanya kila mbinu kusudi niweze kurejea katika afya njema alinisisitiza sana niwe nakula matunda na mboga za majani ambavyo alikuwa akileta mara kwa mara pale nyumbani, kwa bahati njema baada wiki mbili afya yangu ilianza kwenda sawa ingawa sikuweza kushiriki tendo la ndoa kwasababu bado nilikuwa nikihisi maumivu.

    Nilimshukuru sana Doroth kwa kuweza kunipa msaada wa mawazo ambayo yaliweza kunisaidia kumaliza tatizo lililokuwa likinikabili kwa amani kabisa bila mume wangu kushtukia mchezo mchafu niliokuwa nimemchezea. Siku zilizidi kusonga huku afya yangu ikihimarika vema kwani maumivu yalikwisha kabisa na nilirudi katika hali yangu ya kawaida. Nilirejea katika kazi yangu ya uuzaji wa vipodozi katika duka ambalo mume wangu alikuwa amenikabidhi niliendeshe.

    ***CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Nilifanya kazi kwa bidii sana kufidia zile siku ambazo nilikuwa nimefunga duka langu kutokana na matatizo niliyokuwa nayo. Sikuhitaji kuwasiliana tena na Muhamedi kwasababu ile siku baada ya tendo sikufurahishwa kwa jinsi ambavyo alikuwa akizunungumza na mimi uzuri mmoja hata na yeye hakunitafuta kabisa kwahiyo ndio tulikuwa tumemalizana kwa mtindo huo.

    Jioni moja siku ya ijumaa baada ya kuandaa chakula nilikuwa sebuleni na mwanangu tunaangalia CD ya mchezo wa makatuni ambayo nilimnunulia binti yangu kipindi nilipokuwa natoka kazini kwaajili ya kumburudisha kwasababu huwa anapenda sana picha za namna ile. Baba yake alikuwa bado hajarejea hadi ule mda ingawa ndio ilikuwa mida yake kwasababu ile siku niliandaa chakula mapema sana ili niwai kupumzika.

    “Pi piii” honi ilisikika getini.

    “Mom dady…dady” Sweetness alizungumza kwa furaha huku akiwai kunyanyuka kwenye kiti mbiombio kwenda kumlaki baba yake baada ya kusikia mlio wa honi getini muda huohuo na mimi nilinyanyuka kwenda kumpokea mume wangu kipenzi. Nilipofika nje nilikuta Enrique ndio anafunga buti la gari baada ya kutoa mfuko ambao alikuwa amemkabidhi Sweetness.

    “Pole mume wangu.” Nilimpa pole kipenzi changu huku nikipokea koti la suti ambalo alikuwa amelining’iniza begani mwake.

    “Asante baby.”

    Alipomaliza kuoga tulijumuika pamoja mezani ili kuweza kupata chakula cha usiku. Uso wa mume wangu ulidhihirisha furaha iliyokuwa ndani ya moyo wake japokuwa sikujua alichokuwa akikiwaza na kumpa furaha. Ila kabla sijamuuliza chochote alianza kuzungumza.

    “Mke wangu kazini yamependekezwa majina ya watu wawili mimi na mfanyakazi mwenzangu tupigiwe kura kesho kwaajili ya kumpata mtu mmoja ambae atakwenda kuiwakilisha kampuni yetu katika semina ya kikazi itakayofanyika Afrika ya kusini mapema wiki ijayo kwahiyo sijajua kama nitapata hiyo nafasi ama laah!” taarifa ya Enrique haikuwa nzuri sana kwangu kwa sababu niliona nitakuwa mbali nae kwa muda mrefu kwani miezi miwili sio haba kwa wapenzi.

    “Mmh sasa mume wangu ukipata hiyo nafasi mimi nitabaki na nani kwa muda wote huo?”

    “Usijali mke wangu itabidi ujitahidi kukabiliana na hali kwasababu endapo nitapata nafasi hii nitaweza kupata maslahi makubwa kutokana na bajeti ambayo imepangwa kwani mwakilishi wa kampuni atakabidhiwa hundi ya milioni 40 kwaajili ya matumizi yake kwa muda wote ambao atakuwepo huko ughaibuni, pesa hizo ni nyingi sana kwasababu sitaweza kuzitumia zote kwasababu nitajibana ili niweze kubakiza fungu kwaajili ya kuiendeleza familia yangu.”

    ***

    “Sawa nimekwelewa ingawa ukifanikiwa kupata nafasi hiyo nitakumiss kwelikweli.”

    “I know that. (nafahamu ilo.) ila jitahidi kunilindia penzi langu tafadhali.” Enrique alizungumza kunipa tahadhari ingawa nilikuwa nafahamu kuwa anawivu wa hali ya juu.

    Kesho yake wakati nilipokuwa kazini mume wangu alinipigia simu kunieleza kwamba muda huo ndio wametoka kwenye kikao na kwa bahati nzuri alifanikiwa kupitishwa aende akawakilishe kampuni yake nje ya nchi. Kiukweli mara baada tu ya kupokea simu ya Enrique kabla hata ajanieleza kuwa alikuwa ameshinda nafasi ile niliweza kufahamu ameshinda kwasababu ya furaha ambayo ilikuwa ikienda sambamba na sauti yake.

    “Hongera sana laazizi wangu.”

    “Ahsante sana dia.”

    “Pia wamenipa mapumziko ya siku kadhaa kwaajili ya maandalizi ya safari yangu kwahiyo ngoja nije hapo dukani tufanye tathmini ya manunuzi ili tuweze kuagiza mzigo mwingine kabla sijaondoka.”

    “Sawa karibu mume wangu.”

    Muda mfupi baadae alifika na kuniuliza nilikuwa nimeuza bidhaa kiasi gani na imepatikana kiasi gani na mzigo gani ndio unapaswa kuongezwa zaidi kulingana na uhitaji wa wateja na mambo mengine kadha wa kadha. Nilimweleza kuwa pesa zilizokuwa zimepatikana ni milioni 9 ndani ya mwezi mmoja haikuwa taarifa nzuri kwasababu mapato yalidorora kwasababu ya kile kipindi nilichokuwa naumwa kwani kwa kawaida huwa mara kwa mara baada ya mwezi mmoja huwa tunauza milioni 17 hadi milioni 20. Kwahiyo aliagiza mzigo wa pesa zilizopatikana kwasababu duka lilionekana kusheheni mzigo wa kutosha.

    Muda ulipofika mume wangu alisafiri kuelekea Afrika ya kusini kwenye semina ya kikazi. Nilibaki mpweke sana nyumba niliiona kama imekuwa kubwa zaidi kutokana na ukimya uliokuwa umetawala pale nyumbani kwangu.

    Ni takribani mwezi mmoja na wiki tatu tangu mume wangu aliposafiri siku moja mida ya saa tano asubuhi nikiwa kazini nilihisi maumivu makali ya kichwa nilimeza vidonge aina ya panado kwaajili ya kutuliza maumivu lakini sikupata nafuu ndipo nikaamua kuchukua uwamuzi wa kufunga duka kurudi nyumbani kupumzika. Nilipofika nyumbani kwangu wakati mlinzi alipokuwa akinifungulia geti ghafla joto langu la mwili lilinipanda ghafla baada ya kushuhudia kifua cha mlinzi wangu kikiwa kimetuna mithili ya mtunisha misuli nilipagawa kwasababu sikuwai kudhani kwamba alikuwa na kifua kizuri namna ile kwasababu mara nyingi huwa anavaa sare zake za kiaskari lakini ile siku asubuhi nilimwomba anisaidie kurekebisha banda la mbwa kwahiyo alivua shati lake kutokana na kazi aliyokuwa anaifanya.

    “Ooh my Gosh” nilipandwa na midadi wakati nilipokuwa nikiliingiza gari ndani ya geti. Maumivu ya kichwa yalikwisha ghafla baada ya ujanja wangu kunaswa na mwonekano wa yule korokoroni.

    Nilipoteremka kwenye gari nilikwenda kuangalia amefikia wapi katika ile kazi niliyokuwa nimempatia nilifurahi sana kwasababu alikuwa amefanya kama nilivyokuwa nimemuelekeza.

    ***

    “Asante sana Fadhili kwa kazi nzuri.”

    “Usijali bosi.”

    “Basi twende ndani ukapate chochote kitu.”

    “Bosi na hivi nilivyolowa jasho mwili mzima?”

    “Usijali bwana utaenda kuogea bafu za ndani.”

    Niliondoka na mlizi akiwa haamini amini kilichokuwa kikiendele baada ya kuingia ndani nilifunga mlango kwa funguo ili niweze kutumia ule muda kujivinjari na mlinzi wangu. Nilimpeleka moja kwa moja hadi chumbani kwangu ambapo ndipo kulikuwa na mlango wa kuingia bafuni japokuwa alikuwa akiogopa sana ila nilijaribu kumweleza asiogope.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    “Vipi mume wako akitukuta?” sauti yake ilidhihirisha hofu ambayo alikuwa nayo ndani ya nafsi yake.

    “Usiogope kwasababu mume wangu kasafiri kwahiyo nahitaji burudani ya penzi lako.” Nilizungumza kwa sauti ya mahaba huku nikitoma tomasa mwili wake ambao bado ulikuwa ukichuruzika jasho. Fadhili alikuwa mpole kama maji ya kwenye mtungi kwani hakuwa na ujanja kwasababu alikuwa amenasa kwangu mke wa bosi wake ambae nilikuwa mrembo mithili ya malaika. Nilijifunga kanga na kwenda nae bafuni kuoga na baada ya dakika kadhaa tulirejea chumbani ambapo tulianza kupeana mambo motomoto asikwambie mtu mchezo ulikuwa ni wa kukata na shoka. Fadhili alikuwa ni mzuri sana kitandani kwasababu alinikosha balaa nilijilaumu mda wote nilikuwa nasubiri nini wakati utamu nilikuwa nauvuka getini kwangu na kwenda kuhangaika na wanaume wengine ambao hawana maana. Baada ya kufika kileleni kichwa changu nilikiegesha katika kifua kizuri cha Fadhili mlinzi wangu huku tukizungumza mawili matatu kwa furaha kupongezana kwa kupeana mambo hadimuhadimu lakini ghafla nilihisi haja ndogo kwa mshtuko nilioupata baada ya kusikia mlango wa sebuleni ukigongwa.

    “Ngo! Ngo! Ngo!”



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog