Search This Blog

Thursday, July 21, 2022

HUWEZI KUUA MAITI - 3







    Simulizi : Huwezi Kuua Maiti

    Sehemu Ya Tatu (3)



    “Maaskari wengine bwana yaani walitegemea bibi Nyanjige wampate humu? Yule bibi ni hatari bwana, yule ni gaidi si mtu wa kukamatwa ovyoovyo! Badala ya kumtafuta huko huko Kongo eti wanakuja kuweka kizuizi hapa Chalinze! Wamechanganyikiwa nini?” Alifoka dereva wakati akiliondoa basi kwa kasi ili kufidia muda uliopotea wakati wa kukaguliwa!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Dereva alikuwa na sababu ya kuondoka kwa kasi kwa sababu maagizo aliyopewa na tajiri yake yalikuwa ni kuwahi kurudi Dar es Salaam ili kuja kuchukua watalii kuwapeleka Mbuga za Mikumi, aliliendesha basi kwa kasi ambayo mara nyingi huwa haitumiwi na magari yaliyobeba maiti. *****************



    Macho ya binadamu hayana pazia! Ilikuwa si rahisi kwa watu wote waliokuwa msibani Kigamboni kutomgundua bibi Nyanjige. Msichana mmoja alimwona bibi Nyanjige na kumfananisha lakini hakuwa na uhakika sana na macho yake.

    Aliporejea nyumbani baada ya gari kuondoka na maiti kuelekea Kilimanjaro, aliliona tangazo katika luninga likitangaza msako wa bibi Nyanjige, kwa sura aliyoiona hakuwa na sababu ya kutoyaamini macho yake tena! Alikuwa na uhakika asilimia mia kuwa mtu aliyemwona msibani alikuwa bibi Nyanjige.



    Alipiga kelele kwa nguvu na kushangilia alijua zawadi iliyotolewa kwa mtu yeyote ambaye angefanikisha kukamatwa kwa bibi Nyanjige ilikuwa yake.

    “Baba nimemwona huyu bibi anayetangazwa msibani!”

    “Wewe mtoto unaota au unataka kuchanganyikiwa?” Baba yake aliuliza.

    “Sio hivyo baba ni kweli alikuwa msibani na tulitoka nae chumba cha maiti!”

    “NI lazima utakuwa umefananisha!”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hapana baba nina uhakika asilimia mia moja, mimi siyo mtoto!”

    “Alivaa nguo gani?”

    “Alivaa gauni hilihili lenye rangi ya kijivu na nyekundu analoonekana nalo kwenye televisheni ila lilikuwa mchafu kupita kiasi!” Alisema binti huyo akilionyesha gauni pekee la bibi Nyanjige katika Luninga picha yake iligandishwa ili watu wamwone vizuri.



    “Huyu bibi ni mtu hatari popote atakapoonekana basi akamatwe na mtu atakayewezesha kukamatwa kwake atapatiwa zawadi”Ilisema sehemu ya habari hiyo.

    “Baba tupige simu kwa polisi?” Binti alimweleza baba yake.



    “Wewe mtoto una uhakika na unachokisema?”

    “Ndiyo!”

    “Sasa na hao polisi watampataje kama ameondoka na basi kwenda Kilimanjaro?”

    “Wanaweza kulifuatilia basi alilopanda!”

    Dakika mbili baadaye msichana huyo alikuwa kwenye simu akiongea na polisi juu ya mahali alikokuwa bibi Nyanjige, hata polisi wenyewe walionekana kutoyaamini maneno ya binti huyo.

    “Binti una uhakika lakini? Usije kulisumbua jeshi la polisi bure?”

    “Ni uhakika!”



    “Kwa hiyo yupo wapi?”

    “Ameondoka masaa matatu yaliyopita kupelekea maiti huko Marangu Moshi, kama mtaweza kulifuatilia gari lililobeba maiti basi mtakuwa mmempata!”

    “Kweli?”

    “Ndiyo!”

    “Namba za basi walililopanda unaifahamu?”

    “Ni TZO 8507!”



    “Ok! Ahsante!” Alishukuru askari na kumuaga binti huyo akimpa uhakika kuwa kama bibi Nyanjige angekamatwa huko alikosema basi yeye ndiye angepewa pesa yote iliyoahidiwa kama zawadi, bila kupoteza hata sekunde mbili baada ya kuongea na simu maaskari walinyanyua simu ya upepo na kuanza kuwasiliana na maaskari waliokuwa maeneo ya Chalinze.



    “Unanipata afande, ova!”

    “Ndiyo ninakusoma, ova!”

    “Yule bibi! Yule bibi! Yumo ndani ya basi dogo linalosafirisha maiti kwenda Marangu, ova! Basi dogo lililobeba maiti!”

    “Namba zake ni ngapi?”

    “TZO 8507,hakikisheni mnamkamata, ova!”

    “Mungu wang....!”Alisema askari wa upande wa Chalinze.

    “Niniii? Kuna nini kwani?”



    Askari aliyekuwa makao makuu hakupata jibu lolote kutoka upande wa pili, askari aliyekuwa akiongea nae alihisi baridi kali ikipita katikati ya uti wake wa mgongo! Mikono yake ilikufa ganzi na simu ya upepo ilianguka chini!



    “Vipi?” Mwenzake aliyekuwa jirani alimuuliza hata yeye pia hakumpa jibu zaidi ya kumwambia kuna matatizo yametokea.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Gari lenye namba zilizotajwa ndio lililokuwa limepita kama saa nzima kabla ya simu hiyo ya upepo kupigwa!



    Hawakuamini kama bibi Nyanjige alikuwa ndani ya basi hilo kwani waliwakagua karibu watu wote ndani ya basi hilo isipokuwa mtu mmoja tu!

    “Nafikiri aliyekuwa amejifunika khanga kwenye kiti cha mwisho kabisa nyuma ya basi, niliyetaka kumwamsha halafu wewe ukasema tuachane alikuwa bibi Nyanjige sasa tutafanya nini?”



    “Hakuna kingine isipokuwa kufuatilia mpaka tulipate basi hilo tumkamate na kumrejesha Dar es Salaam vinginevyo tutaonekana wazembe na kusababisha matatizo makubwa!”

    Maaskari wote walikubaliana na kuingia ndani ya gari lao lililokuwa limeegeshwa pembeni na kwa kasi ya ajabu walianza kuondoka kuelekea mbele hofu yao kubwa ilikuwa kufukuzwa kazi na hiyo ndiyo iliwafanya wawe na usongo wa kulipata basi hilo na kumkamata bibi nyanjige, walikuwa wamefanya uzembe mkubwa ambao ungefanya wahusishwe na rushwa na kwa kosa hilo wangepoteza kazi zao.



    “Hapana jamani mimi nahisi hiki kibibi ni kichawi, sasa pale kilitokea kitu gani mpaka tusimfunue kilemba chake kichwani?”:

    “Hata mimi sielewi lakini kwa spidi waliyokuwa nayo ni lazima tutawapata tu!” ****************

    Barabara ya Chalinze Segera ni miongoni mwa barabara zilizotengenezwa vizuri kupita zote nchini Tanzania! Ilikuwa ni barabara ya lami na aliyeitengeneza lami hiyo alikuwa ni mtaalam kweli kweli kwani ilikuwa ni mkeka wa nguvu! Magari yote yalipita katika barabara hiyo yalikimbia hadi kilometa mia mbili kwa saa.



    Baada ya basi kuondoka eneo lilipokamatiwa dereva aliliendesha kwa kasi ya ajabu kiasi cha kuwatisha abiria, abiria wote walikuwa kimya roho zao zikiwa mikononi ilikuwa si rahisi kuamini gari hiyo ilikuwa ikisafirisha maiti! Dereva alipoangalia mshale wa kuonyesha kasi aligundua ulikuwa umegota mwisho!

    Alishtuka lakini aliziamini tairi za gari lake zilikuwa na siku tatu tu tangu ziwekwe!



    “Kanyaga moto mwanangu!” Kondakta wake alimchochea!

    “Usiwe na shaka babu hii ni nenda ugaruke mwanangu!” Aliitikia dereva.

    Bibi Nyanjige alikuwa bado amejifunika na khanga yake kichwani, kasi hiyo ilimshtua lakini hakuwa na la kufanya, aliendelea kumshukuru Mungu kwa kumuokoa! Mara kwa mara alijitingisha kama vile alikuwa na kwikwi za kilio, hakuongea kitu na mtu yeyote ndani ya basi, alijifanya mtu mwenye huzuni kupita wengine wote!

    Kilometa kama hamsini na tano mbele yao basi lao lilikuwa likipandisha mlima na mbele yao lilikuwepo lori kubwa na tela lake lililokuwa likienda kwa mwendo wa taratibu sana, dereva wa basi lao alikerwa na kasi hiyo ya lori na kuamua kulipita kwa mwendo wa kasi.

    Aliamua kufanya hivyo bila kujua kuwa mbele kulikuwa na lori jingine likija tayari walikuwa wamefika darajani!



    Akiwa katikati ya lori alilokuwa akilipita alishtukia akikutana uso kwa uso na lori lililokuwa likija mbele yake, alijitahidi kukwepa na kugongwa mbavuni,basi lake lilianza kuyumba kutoka upande mmoja wa barabara hadi mwingine akielekea darajani.

    Abiria ndani ya gari walianza kupiga kelele, ikabidi bibi Nyanjige ajifunue na kukuta watu wote ndani ya basi wakiwa wamesimama wima huku wakilia! Dereva alionekana kuchanganyikiwa.



    Ghafla mlipuko mkubwa ulisikika tairi lilikuwa limepasuka! Basi likatoka barabarani na kuanza kuingia kwenye mtaro, mbele kidogo lilipinduka na kutumbukia katika daraja refu ambalo chini yake ulipita mto mkubwa uliokauka maji.



    “Jamani ajali imetokea anayeweza kujiokoa afanye hivyo!” Ilikuwa ni sauti ya dereva.

    Dirisha la upande wake lilipasuka, pamoja na uzee aliokuwa nao bibi Nyanjige alijivuta akatokeza nje na kusimama wima dirishani akiwa ameshika keria ya basi kwa juu!



    “Stering hauwawi bwana!” Alisema bibi Nyanjige na kabla gari halijfika chini alirukia upande wa pili na kutua kwenye nyasi, alihisi kiuno chake kuteguka.



    Akiwa hapo alishuhudia basi likijibamiza chini na kuzunguka kama mara tatu hivi ardhini, hakusikia tena kelele ndani ya basi ikawa kimya kabisa!



    Hali iliyomfanya aamini kuwa watu wote ndani ya basi walikuwa wamekufa lakini sekunde chache baadaye alishuhudia watu wawili wakitoka ndani ya basi huku damu nyingi zikiwavuja, hawakuishi sana kwani walipotembea hatua chache mbele walianguka chini.



    Bibi Nyanjige alisogea hadi eneo walipoangukia na kugundua wote walikuwa wamekufa! Alitembea kwenda mbele na kuchungulia ndani ya basi lililobondeka aliona watu wengi wakiwa wamelala ndani ya basi damu nyingi zikiwatoka, maiti nyingi hazikuwa na viungo muhimu kama vichwa, mikono na hata miguu!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Jeneza lililobebea maiti wakiondoka Dar es Salaam lilikuwa wazi na maiti haikuwa ndani yake! Ilikuwa ni ajali mbaya kuliko ajali zote ambazo bibi Nyanjige aliwahi kushuhudia maishani mwake!

    Ghafla wazo lilimwijia kichwani mwake lilikuwa wazo la kujiokoa lilikuwa wazo zuri kuliko mawazo yote aliyowahi kuyawaza!



    Alijua ni lazima ingegundulika alisafiri na basi lililosafirisha maiti, hivyo ili kupoteza kabisa habari zake aliamua kuufanya ulimwengu wote uamini kuwa naye alikufa katika ajali hiyo.

    “Hakuna mtu atakayeamini nimeokoka katika ajali hii hivyo ni lazima niyafanye mawazo yao yawe kweli!” Aliwaza bibi Nyanjige.



    Alipita katika dirisha lililovunjika na kuingia ndani ya basi lililobondeka na kuivuta moja ya maiti iliyoharibika vibaya haikuwa na kichwa kabisa, alikiona kichwa cha maiti hiyo pembeni lakini hakukijali, aliubeba mwili na kutoka nao hadi nje kupitia dirishani, alikuwa bibi kizee lakini mwenye nguvu za ajabu.



    Alipoifikisha maiti hiyo nje aliilaza chini na kuruka tena hadi ndani ya basi ambako alikichukua kichwa na kutoka nacho hadi nje! Ilikuwa ni kazi ya kutisha lakini aliifanya bila hofu, mikono yake yote ilitapakaa damu kutoka shingoni mwa kichwa alichokibeba na damu hiyo ilipenya katika vipele alivyokuwa navyo mikononi mwake lakini hakujali.



    Alikiweka kichwa hicho pembeni na bila kuchelewa aliamua kutekeleza mpango aliokuwa nao, aliivua maiti hiyo nguo ilizovaa na kuzitupa pembeni kisha akavua gauni lake na kubaki kama alivyozaliwa, kwa haraka aliivalisha maiti hiyo gauni lake na pia mkufu wake wa shaba ulioandikwa jina lake! Alitaka kuidanganya dunia kuwa hata yeye alikufa katika ajali hiyo ili aweze kuandaa jeshi zuri zaidi porini.



    Alipomaliza tu kazi ya kuivalisha maiti gauni lake alisikia muungurumo wa gari nyuma na alipogeuza macho yake kuangalia barabarani aliliona gari la polisi na maaskari wapatao watatu waliteremka ndani ya gari hilo huku bunduki zikiwa mikononi mwao.



    Alijua wazi watu hao walikuwa wakimtafuta yeye hakuna kilichokuwa mbele yake zaidi ya kujiokoa tena, ili kutimia lengo lake alikichukua kichwa cha marehemu na kuanza kukimbia nacho mbio kuelekea vichakani.

    “Jamani yule anayekimbia ni mtu au nyani?”



    “Mtu yule!”

    “Hapana labda ni nyani sidhani kama kuna binadamu mweusi kiasi kile hapa duniani!” Alijibu mmoja wa maaskari.

    Kabla hata hawajalifikia basi walikutana na maiti moja na mmoja wao maaskari alibaki akiimulika maiti hiyo na tochi, wenzake walinyoosha moja kwa moja hadi mahali lilipokuwa basi hilo, walipomulika ndani walishuhudia maiti nyingi zikiwa zimelaliana, hapakuwa na mtu aliyeonekana kuwa hai, maiti nyingi zilikuwa zimekatikatika vibaya!



    “Masikini hii ina maana hata bibi Nyanjige atakuwa amekufa au?”

    “Ni lazima itakuwa hivyo!” Maaskari waliokuwa wakilikagua gari waliongea na ghafla walisikia mwenzao akipiga kelele.

    “Huyu hapa?”

    “Nani?”

    “Bibi Nyanjige!”



    Waliokuwa ndani ya basi walitoka ndani ya basi mbio na kurudi hadi mahali mwenzao alipokuwa akipiga kelele, hawakuamini macho yao kuukuta mwili uliovaa gauni la bibi Nyanjige ukiwa hauna kichwa!

    “Kichwa chake kiko wapi? Ni lazima tuupeleke pamoja na kichwa vinginevyo hakuna mtu atakayeamini kuwa huyu ni bibi Nyanjige!”



    “Lakini ni afadhali amekufa ametuhangaisha sana!”

    “Huyu bibi alikuwa hatari mno!”

    Walijaribu kukitafuta kichwa cha marehemu bila mafanikio mwisho wakaamua kupiga simu ya upepo Chalinze kuomba msaada na dakika kama ishirini baadaye gari kubwa la polisi liliwasili na kupakia maiti zote zilizokuwa ndani ya basi hilo na kuondoka nazo.

    “Na hiyo?” Aliuliza mmoja wa askari waliokuwa wakipakia maiti.



    “Hii hapana! Tunakwenda nayo Dar es Salaam makao makuu ni lazima tuipelekea hospitali kuu ya Jeshi ili wakubwa waione tena usiku wa leo hii hii! Maana huyu bibi aliisumbua sana dunia!”

    “Sasa wataamimi vipi bila kichwa?”



    “Alama zote zipo, hii cheni yake imeandikwa jina lake si unaona!” Alisema askari mmoja na akamwonyesha askari mkufu ulioandikwa neno Nyanjige walioukuta shingoni mwa maiti!

    “Na hata hizi nguo alizovaa ndio zake kabisa!” Alisema askari huyo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Magari yote yaliondoka moja likiwa kimbeba maiti zote kuelekea hospitali ya Tumbi na gari jingine la polisi likiwa limebeba maiti moja lilielekea Dar es Salaam! Gari hilo la polisi halikusimama Chalinze lilinyoosha moja kwa moja kuelekea jijini Dar es Salaam ambako lilifika baada ya kama dakika arobaini na tano!



    Maiti ilipelekwa moja kwa moja hadi chumba cha maiti cha hospitali ya jeshi ambako usiku huohuo wakuu wa jeshi walifika na kuanza kuikagua maiti hiyo.

    “Jamani mna uhakika huyu mliyemleta ni bibi Nyanjige kweli?”



    “Ni yeye afande si mnaona hata huu mkufu wake afande!!”
“Hebu niuone!” Afande Mwita Mitiro aliuomba mkufu huo, alipokabidhiwa alianza kuukagua, alipoliona jina la Nyanjige kwenye mkufu huo hata yeye aliamini ulikuwa ni mwili wa bibi Nyanjige.



    “Kweli bwana si unaona hata gauni ndilo lilelile lililopo katika hii picha!” Alisema mkuu huyo huku akiimulika picha aliyoshika mkononi mwake kwa tochi.

    “Hebu ivueni hiyo maiti hizo nguo ili tuikague zaidi!”



    Bila kuchelewa vijana waliikamata maiti hiyo na kuivua nguo zote ilizovaa hakuna aliyekuwa tayari kuamini macho yake walipokuta mwili maiti hiyo una sehemu nyeti za kiume! Waligundua bibi Nyanjige aliwachezea tena mchezo.

    “Ni akina nani walioileta maiti hii?”

    “Ni sisi afande!”



    “Yaani mmetuletea maiti ya mwanaume?” Aliuliza afande kwa ukali.

    “Hatukujua afande!”

    “Hebu wawekeni mahabusu hawa haraka na msako ni lazima uendelee!



    Bibi Nyanjige atakuwa hai amefanya tena ujanja wake wa kuvalisha nguo maiti, nataka akamatwe mara moja na kuletwa hapa!” Askari mia mbili waondoke kwa magari na helkopta tano zifuate usiku huu huu kwenda kuuzunguka msitu wote ulio jirani na mahali ajali ilipotokea nina uhakika atakuwa maeneo hayo hayo!



    Mpaka kesho saa sita kamili namtaka awe hapa akiwa hai mmesikia?” Aliuliza mkuu wa majeshi hasira zikiwa zimempanda.

    “Ndiyo afande!”

    Kipenga kilipulizwa wanajeshi wote wakakusanyika na dakika kama ishirini baadaye mkuu wa majeshi alishuhudia helkopta na magari yakiondoka kwa kasi, kila askari alikuwa na bunduki yake mkononi!



    Hofu kubwa ya wanajeshi ilikuwa ni wadudu na nzige ambao bibi Nyanjige aliwatumia, ingawa alikuwa nchini Tanzania ambako hapakuwa na nzige wala mbung’o bado wanajeshi waliogopa vita vya wadudu!



    Saa tisa ya usiku bibi Nyanjige akikimbia uchi wa mnyama katikati ya pori kuelekea asikokujua, alishangaa kuona helkopta tatu zikitokea juu yake “Mungu wangu wamekuja tena?”



    Bibi Nyanjige aliziona helkopta za jeshi zikielekea upande wake bila shaka alijua zilikuwa zikimfuata yeye!

    “Hawaniwezi na nitawamaliza mpaka wajute kwanini walimuua mama yangu!”Aliwaza bibi Nyanjige.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alikitupa kichwa cha mtu alichokuwa nacho na kuinama akaweka mikono yake chini akaanza kutembea kama Sokwe kwa miaka mingi aliyoishi porini na wanyama alijua muondoko wa kila mnyama! Ilikuwa si rahisi kumtofautisha na Sokwe halisi.



    Alizidi kutokomea katikati ya vichaka huku helkopta zikimmulika kwa mwanga mkali wa taa uliofanya usiku porini kuonekana kama mchana, mwanga huo ulimtia hofu na kumfanya aamue kujiangusha ardhini na kunyooka wima kama mti.



    Marubani walipomulika na taa zao walimwona kama kipande cha mti kilichounguzwa na moto! Ilikuwa si rahisi hata kidogo kuamini walichokiona ardhini kilikuwa binadamu! “Najipumzisha ila hali ikitulia nitaendelea!” Aliwaza bibi Nyanjige.



    Alibaki amelala eneo hilo kwa muda wa masaa zaidi ya mawili, hali ilipotulia alinyanyuka na kuanza kutembea taratibu akisonga mbele kwenda mahali kusikojulikana, lengo lake likiwa kufika Serengeti.



    Alitembea kwa usiku mzima bila kufika au kutokezea barabarani,kulipokucha alishindwa kuendelea na safari yake kwa kuhofia kukamatwa na kuamua kujificha chini ya kichaka akisubiri usiku mwingine uingie ndio aendelee.



    “Nitatembea kila siku usiku kama Bundi na asubuhi nitajificha vichakani hadi nifike ninakokwenda, ninajua ninasakwa sana lakini hawatanikamata hata siku moja!” Bibi Nyanjige aliongea peke yake huku akitetemeka kwa baridi ndani ya kichaka alichojificha.



    Alikuwa bado hajakata tamaa na hakutaka kufanya hivyo, alikuwa na matumaini ya kujinasua kutoka mikononi mwa kifo kilichokuwa kimemzunguka! Usiku ulipoingia alitoka kichakani na kuendelea na safari yake, hiyo ndiyo ikawa staili yake ya safari!



    Kwa siku kama tatu alitembea usiku na mchana alijificha kichakani.Njaa haikumsumbua sana kwani alishazoea maisha ya porini, alikula matunda na majani ya miti.



    Ilikuwa ni siku ya nne akiwa amejificha kichakani miguu yake ikiwa imevimba kama matende kwa sababu ya safari, mwili wote ulikuwa umechoka na alikuwa akijaribu kuwaza angefanya nini ili aendelee na safari yake hadi Serengeti ambako alitaka kwenda kuunda jeshi kama alilokuwa nalo Kongo ili kupambana na majeshi ya serikali.



    Akiwa katika mawazo hayo ghafla alisikia sauti za watu nyuma ya kichaka alichojificha! Zilikuwa ni sauti za wanaume wakitembea kuelekea eneo alilokuwa, alipenyeza macho yake katika majani ya kichaka na kuangalia nje! Aliliona kundi kubwa la askari waliovaa magwanda ya kijeshi wote walikuwa na bunduki mikononi mwao alitetemeka akijua tayari alishaingia mikononi mwa wabaya wake.



    “Na hizi alama za miguu ni za nani?” Aliuliza mmoja wa askari huku akiangalia ardhini.

    Swali hilo lilimfanya bibi Nyanjige afe ganzi mwili mzima na kuona mwisho wake ulikuwa umefika, meno yake yaligongana ovyo,alijua ni nyayo zake zilizoongelewa na maaskari walizigundua sababu ya mvua kubwa iliyonyesha siku moja kabla.



    “Bwana achana na nyayo za wachungaji wa kimasai tuendelee na msako na siku nitakayomtia mkononi huyo bibi yenu atanikoma sababu kanisumbua sana!” Alisema mmoja wa maaskari hao na kupiga risasi kama tatu hivi hewani ili kuonyesha hasira aliyokuwa nayo dhidi ya bibi Nyanjige.



    “Wee acha tu watu tumeacha wake zetu kuja kuhangaika hapa porini na baridi sababu ya kibibi kijingajinga!” Mwingine alidakia

    Lilikuwa kundi la maaskari wengi mno na walizidi kupita pembeni ya kichaka taratibu hakuna askari hata mmoja aliyefikiria kuchungulia ndani ya kichaka hicho kuona kilichokuwemo Bibi alizidi kutetemeka kwa hofu.



    “Sitakiwi kulaza damu hata kidogo lazima nijiokoe hata nikifa kazi niliyoifanya ni kubwa!” Aliwaza Bibi Nyanjige na sekunde chache baadaye alipata wazo alitaka kuitumia nafasi hiyo ya kupita maaskari kuokoa maisha yake, alitaka kumwiiga Sylivester Stallone Rambo katika sinema zake.

    “Nafikiri na mimi nikitumia utaalam ule ule nitamnasa mmoja!” Aliwaza bibi Nyanjige na kusimama wima akiupima mwili wake nguvu.

    “Niko bombaaa!” Alijitapa na kuamua kujaribu kutumia nafasi hiyo

    Aliangaza macho yake pembeni na kuona mzizi mkubwa wa mti ukiwa chini, akajinyoosha na kwa kutumia nguvu nyingi aliukata na kuushika mkononi, ulikuwa mgumu na ulifanana kabisa na kamba.



    Alipatwa na ujasiri wa ajabu na kujisogeza hadi pembeni kabisa mwa kichaka alichojificha na kuwashuhudia maaskari wakizidi kupita taratibu bunduki zao zikiwa mkononi, hakuwa na shida nao wote alimtaka mmoja tu! Alitulia akisubiri wa mwisho apite huyo ndiye alikuwa mlengwa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wengi walipita akamuona mmoja wao ambaye aliamini alikuwa wa mwisho akija taratibu, yeye alibeba mtambo mkubwa zaidi ya wenzake uliomuelemea kwa uzito! Alitembea peke yake akionekana kuchoka kupita kiasi na alikuwa legelege na mwenye afya mbovu.



    “Huyu huyu ananitosha!” Aliwaza bibi Nyanjige huku akiweka mzizi wake vizuri, askari alipofika karibu yake bibi Nyanjige aliruka kwa kasi na kuuzungusha mzizi aliokuwa nao shingoni mwa askari kama ambavyo vibaka hufanya wanapomkaba mtu.



    Mwanajeshi hakupiga kelele hata kidogo bali alianguka chini kimyakimya,macho yalimtoka vibaya askari, bibi Nyanjige naye akazidi kubana kwa mzizi kwa dakika kama mbili huku akiwaangalia wanajeshi wenzake waliozidi kutokomea bila kujua yaliyompata mwenzao! Bibi Nyanjige alijipongeza kwa kazi aliyoifanya.



    Kwa haraka alimvutia askari huyo na kumwingiza ndani ya kichaka ambako alimbana zaidi na mzizi hadi akafa!

    “Sasa mambo yameanza upya!” Alisema bibi huku akimvua askari huyo magwanda yake na kuyavaa mwilini mwake! Ingawa yalimbana sana aliyalazimisha. Kofia ya jeshi aliyovaa askari huyo ilikuwa kubwa kiasi kwamba bibi Nyanjige alipoiweka kichwani ilimfunika uso wake wote, haikuwa rahisi hata kidogo kumtambua.



    Baada ya kumaliza kuvaa mabuti ya jeshi aliuchukua mtambo aliokuwa nao askari huyo na kuubeba begani mwake, kwa utaalam wa kijeshi aliojifunza akiwa masomoni huko Uingereza ambako ilikuwa lazima kwa wanafunzi wa chuo kikuu kupata mafunzo ya jeshi aligundua mtambo huo ulikuwa ni wakutungulia ndege.



    “Sasa watanitambua na nina uhakika kwa nilivyovaa hakuna hata askari mmoja atakayegundua kuwa mimi ndiye bibi Nyanjige wanayehangaika kumsaka! Na kwa kutumia mtambo huu leo hii nafanya kazi ambayo dunia haijawahi kushuhudia!” Aliwaza bibi Nyanjige akiwa amebeba mtambo wake begani!



    Ulikuwa mtambo mzito kiasi cha kumyumbisha ukizingatia umri wake kuwa mkubwa, lakini mazoezi ya mwili aliyoyafanya akiwa kijana na aina za vyakula alivyokula vilimfanya awe imara hata kuwa na uwezo wa kubeba mtambo mzito kama ule.



    Ghafla alishuhudia helkopta mbili zikija angani nyuma yake badala ya kusikitika kama ilivyokuwa awali alifurahia! Alilala chini na kuuelekeza mtambo angani akiwa ameilenga vilivyo moja ya helkopta bila kusita aliachia kombora moja zito lililokwenda moja kwa moja na kuilipua ndege,bibi Nyanjige alichekelea.

    Kabla helkopta ya pili haijafika mbali nayo ilipokea kombora jingine na kuanza kuwaka moto ikielekea ardhini!



    “Wamefanya kosa sana kunipa mtambo huu hii ni sawa na kumpa mwehu rungu! Sasa na hakikisha kila ndege inayopita hapa inapokea kipigo na kulipuka leo ni le…….!” Kabla hajamalizia sentensi yake alisikia muungurumo mwingine tena upande wa Mashariki, furaha nyingine tena ilimjaa moyoni na kuunyanyua mtambo wake na kuitungua helkopta hiyo ilidondoka chini mara moja huku ikiwaka moto na alifanya hivyo hivyo kwa ndege ya pili pia!



    Matukio hayo yalimshangaza karibu kila mtu aliyekuwepo porini, walishindwa kuelewa ni nani aliyefanya ukatili huo kwani ni ndiyo waliokuwa na mtambo wa kulipulia ndege katika pori hilo jambo lililoonyesha kuwa mtu aliyekuwa akizilipua ndege hizo alikuwa mwanajeshi mwenzao, lakini nani? Hilo ndilo lilibaki swali la kila mmoja wao ikabidi mkuu wa kikosi apige kipenga ili wanajeshi wote wakusanyike kuhesabiwa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Bibi Nyanjige aliposikia mlio wa kipenga ha jeshi alijua mambo yameharibika! Alichukua mtambo wake na kwenda kuuficha porini mahali alipofahamu yeye mwenyewe alirudi haraka na kujichanganya ndani ya kundi la askari mia mbili bila kugundulika! Mpaka wakati huo hapakuwa na askari mmoja wa jeshi la nchi kavu aliyekuwa ameuawa!

    “Jamani nani amekabidhiwa mtambo wa kutungulia ndege?”



    “Ni afande Laurian!”

    “Yupo wapi sasa?”

    ‘Hatujui afande ila alikuwa anakuja kwa nyuma!”

    “Na mtambo wenyewe upo wapi?”

    “Alikuwa nao, ila sababu ya uzito wake alitembea taratibu nyuma yetu!”

    “Mmekwishajaribu kumtafuta?”

    Hakuna mtu aliyejibu swali hilo askari wote walianza kuzungusha macho yao huku na kule wakimwangalia askari huyo bila mafanikio yoyote.



    “Haya hesabuni nambaaaa!” Kamanda wa kikosi aliamuru na maaskari wote walianza kuhesabu namba zao taratibu wakianzia na moja hadi kufikia mia mbili! Hesabu ilitimia.

    “Jamani mbona hesabu yetu imetimia yupo wapi Laurian?” Aliuliza mkuu wa kikosi na kuamuru askari wahesabu tena namba zao taratibu lakini bado hesabu ilikuja ile ile na kumshangaza Kamanda.



    “Laurian! Laurian!” Kamanda aliita lakini bado hakuitikiwa na mtu yeyote, kila askari alishangaa na walishindwa kuelewa kitu gani kilikuwa kimetokea kwani kama askari huyo asingekuwepo ni lazima idadi ya askari ingepungua mtu mmoja.



    “Haya wote kaeni katika mstari ili nikague lakini kama nikimpata huyo Laurian adhabu yake itakuwa kifo hawezi kunihangaisha kiasi hiki!” Alisema kamanda na wanajeshi wote walijipanga tena mstari na Kamanda alianza kupita taratibu akiwakagua mmoja baada ya mwingine juu hadi chini kama vile ambayo mwalimu mkuu hufanya shuleni anapokagua usafi!



    Bibi Nyanjige alikuwa amesimama katika mstari wa nyuma akitetemeka kwa hofu, alijua tayari alishaingia matatizoni alikuwa na uhakika wa kugundulika kwa sababu angejulikana ni mwanamke na kugundulika kwake kungemaanisha ni yeye aliyekuwa akizilipua helkopta.

    “Afande simama wima mbona umejikunja hapa mgongoni? Na huo mguu sawa ulioweka si wenyewe panga vizuri miguu yako hunioni mimi? Huyu kamanda anaweza kukuletea matatizo makubwa sana sababu amekasirika!”

    Askari mmoja aliyekuwa jirani alimwambia bibi Nyanjige lakini alipojaribu kujinyoosha mgongo ilishindikana kwa sababu mgongo wake ulipindwa na uzee!



    “Nyooooka kidogo afande huu mgongo utakuletea matatizo!” Alisema tena askari huyo lakini Bibi Nyanjige hakujibu kitu alijua kufanya hivyo kungefanya agundulike na kuhatarisha maisha yake alizidi kuinamisha kichwa chake chini.

    “Hebu toeni kofia zenu kichwani upesi ili niwaone vizuri!”Kamanda aliamuru na kwa sababu ilikuwa ni amri hapakuwa na njia yoyote ile ya kubisha, askari wote walianza kutoa kofia zao vichwani na mkuu wa kikosi alipita kwa askari mmoja baada ya mwingine.



    Macho ya askari aliyesimama jirani na bibi Nyanjige yalimfuata kamanda kila alikopita akikagua na kumsahau kabisa bibi Nyanjige, alipogeuza kichwa chake dakika chache baadaye alishangaa kukuta askari mwenzake hayupo! Hakutaka kuuliza sababu Kamanda alikuwa amekaribia sana eneo hilo, alizidi kukauka ili kuonyesha heshima ya jeshi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mbona idadi imebaki ileile 199! Kuna askari amepotea na huyo ndiye anatungua ndege zetu wenyewe, sijui anatumiwa? Ni lazima asakwe” Alisema kamanda. ************

    Bibi Nyanjige alikuwa katikati ya vichaka akitembea kuelekea mahali alipouacha mtambo wake wa kulipulia ndege alipokuta bado upo alifurahi kupita kiasi na nusu saa baadaye akiwa bado katikati ya nyasi alianza kuona maaskari wakipita kuelekea mahali walikotokea.



    Aliiona hiyo kama bahati nyingine kubwa zaidi alinyata taratibu na kujichanganya katikati maaskari bila kugundulika na kuanza kutembea pamoja nao, hakuna aliyeligundua jambo hilo! Umbali wa kilometa kama kumi na tano katikati ya pori walifika kambini na wanajeshi walijipumisha ndani ya mahema waliyojenga.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog