Simulizi : Msichana Wangu Wa Kwanza
Sehemu Ya Pili (2)
"Mapenzi ni kutendwa" Ni jibu kutoka kwa Mvulana yule aliechaguliwa na mwalimu. Kisha mwalimu aliwapongeza kwa kujaribu, halikadhalika wanafunzi wote wakapiga makofi ikiwa ni ishara za pongezi kwa wanafunzi wale. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hapo ndipo Mwalimu yule wa Sayansi alipoomba usikivu iliawafunze maana ya mapenzi. Kabla hata hajaendelea, aliingia mwalimu wa darasa na kuomba aite majina. Alimruhusu na mwalimu yule akaanza zoezi la uitaji wa majina. Haikupita hata muda mrefu. Tayari mwalimu yule akawa ameondoka.
"ok, wanafunzi. Kabla hatujajua tafsiri halisi ya Mapenzi. Hebu kwanza tujongee kwenye mitazamo mbalimbali ya watu kuhusu neno mapenzi....."
"Watu wengi hulitazama hili neno kwa mitazamo yao tofauti tofauti, labda tuwa weke kwenye makundi mawili watu hao ilitupate mitazamo yao kwa usahihi.
Kuna waleambao wamesha umizwa na mapenzi, na kunawale ambao wanayafurahia mapenzi.
Mtu alie umizwa na mapenzi huyo anayatafsiri mapenzi kwa maana mbaya na hata kuifananisha na vitu vibaya majibu yake huwa ni kama haya; mapenzi ni gereza la mateso, mapenzi ni uchungu wa shubiri, mapenzi ni jahanamu ya moyo.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Lakini pia wale wanaohsi mapenzi ni mazuri, wao pia huwa na tafsiri zao kama; Mapenzi ni utamu wenye asali, mapenzi ni furaha ambyo haina kifani, na mengineyo.
Nadhani tumejifunza mitazamo ya aina mbili kwa kutofautisha makundi mawili. Lakini makundi hayo yana mapungufu, na haya jitoshelezi ki maana. Kuna watu ambao wana umia kwenye mapenzi lakini pia baada ya muda huhisi raha. Je, watu hao wanaingia kwenye kundi gani?.
Labda ni seme jambo kidogo. Wewe kama mwanafunzi ni kazi yako kupembua pumba na mchele maana mapenzi hayana maana moja ila hupambanuliwa kulingana na hisia binafsi za mtu.
Kuna Mtunzi mmoja kwa jina la ZUBERY MAVUGO alitunga riwaya ya HEART ATTACK, na humo ndani alimtumia muhusika wake ilikuwakilisha nadharia ya mapenzi. Alisema., Mapenzi ni muunganyiko wa Furaha na Maumivu.
Labda nichukue nafasi hii kumpöngeza. Nami kama mwalimu wenu huwa na penda sana kuitumia nadharia hiyo, ukitaka ufafanuzi zaidi basi huna mudi kutafuta riwaya hiyo kwa ajili ya kupata elimu.
Hebu sasa tuzame kwa wataalamu wa hisia. Wao walisema kuwa, mapenzi ni hisia za dhati kutoka moyoni, hisia hizo huangukia kwa mtu, kitu, au jambo fulani. Na muangukiaji huitwa mpenda, kisha muangukiwa huitwa mpendwa. Na hii nio maana sahihi ya neno mapenzi." Aliongea mwalimu yule wa sayansi kwa udadavuzi wa hali ya juu, huku akitamba mbele ya wanafunzi mara kushoto mara kulia, ilimradi tu. Kuweka usikivu.
Hakika kila mwanafunzi alilifurahia somo lile na wote kwa pamoja walikuwa wameazima maskio yao mkabala na mdomo wa mwalimu wao.
'nge,nge,nge,nge,nge,nge' ni sauti ya kengere ya mapumziko. Baada ya sauti ile mwalimu aliwaomb wanafunzi wakanywe chai kutokana na kuwa kipindi kimeisha. Kisha aliwaahidi kurejea siku ya jumatano, ambyo ndio ilikuwa kipindi chake na aliahidi kudadavua kiundani mapenzi.
* * * *
Ulifika muda wa kutawanyishwa, wanafunzi wote walirejea makwao. Samir akiwa njiani alikutana na Zulfa ambae alikuwa akimtegea shuleni angalau aione tu sura ya Samir.
Siku hyo ilikuwa tofauti kati ya Zulfa na Samir. Waliongea vizur sana na kuahidiana wakutane usiku huo wa j'nne mida ya saa mbili. Waliagana na samir akaenda kwao, kama kawaida alimkuta Nurdin akijisomea kitabu kimoja.
"ah, nambie L,Y."
"shwari, mishe zinaenda"
"yea, zipo kul, ile mbaya"
Walisalimiana, huku kila mmoja akiwa na furaha na asijue jinsi ya kumueleza mwenzake.
Samir alikuwa na zaidi ya furaha kwa kuweza kukutana na Zulfa, kwani alipoktana nae kuna kitu ni kama kilimuingia ndani ya moyo wake, pia alikuwa akiyakumbuka maneno ya mwalimu wake wa mapenzi. Lakini pia Nurdin hakuwa mbali kuielezea furaha yake juu ya Sumayah, alimueleza kila kitu bila hata kutia chuku.
Pia maelezo yake yalimaliziwa na kisa cha Nurdin kuchelewa shule kutokana na mawazo ya penzi lake ambalo alikuwa ameliwazia na kulipangia majukumu utadhani baba wa familia.
Waliongea mengi huku wakipongezana kwa kupiga tano, kama ishara ya mshahara wa kazi yao. Hakika siku hiyo walikuwa na zaidi ya furaha.
Upande wa sumayah, sina uhakika kama alikuwa akimuwaza Nurdin kutokana na kazi alizokabiliana nazo nyumbani kwao. Ila kwa upande wa Zulfa, yeye alijifungia chumbani mwake na kuweka kufuri kisha akaanza kuwaza maelewano ya siku ile.
"Ameniambia leo tukutane?, siamini!. Nadhani kuna kitu kizuri anataka kuniambia. Au labda nimeongezeka uzuri?, mmmh,, sidhani. Hebu ngoja ni hakiki kwa msema kweli kiøo huenda akanambia kilichomvutia Samir, pengne labda ni mavazi yangu?" Aliongea Zulfa na kujiuliza maswali ambayo hata majibu yake hakufanikiwa kuyapata. Alikiendea kioo, na kugundua kuwa siku hyo alikuwa amevaa nguo zake zile asizozipenda, na kujikuta ni mwingi wa mijasho kutokana na kuendsha baskeli. Bado kioo kile kikawa mtihani na kushndwa kumsaidia jibu la swali aliloulza.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Inamaana Samir ameniona na hili linguo libaya, mijasho yote hii, pamoja na uchafu wa miguu yangu. Mmmh, we kioo acha uongo. Namjua Samir, huwa ananichukia lakini leo kaonesha kunijali zaidi hata ya malikia. Ila... Mbna hivi!!. Mmmh, ama kweli duniani kuna mengi kumbe hata yule chizi wa kwenye kitabu cha MAGIC WOMAN alikuwa sahihi pale alipomfuata Hussen. Dah!" Mpenzi msomaji ama kwa hakika yaacheni mapenzi ya itwe mapenzi, tu. Huwezi amini msichana yule alijikuta akiumia kichwa kutokana na mawazo na asipate jibu sahihi. Usingzi ulimpata na hakusita kulala.
Mida ya saa mbili usiku kila mmoja alikuwa kwenye windo lake, si Nurdin wala Samir...
. Nurdin alikaa kule karibu na kwa Sumayah, tena akiwa peke yake. Huku Samir akimsubir Zulfa pahala walipoambiana kukutana.
Kwa Samir, hazikupita hata dakiki kumi, ikawa tayari Zulfa ameshafika.
"Natumai, umenisubiri kwa muda mrefu. Naomba msamaha kwa kukuweka muda mwingi. Hii imetokana tu na kazi za nyumbani kuwa nyingi" Aliongea Zulfa. Katika maongezi yake hakusita kuviringa macho yake, kutamba na mdomo wake, huku mikono yake ikiadhibu ushungi wake aliokuwa ameuvaa. Mara au kunje mara au kunjue, ilimradi tu awe mwenye kuuadhibu.
"Usijali. Hata hujanikalisha, hayo ni mawazo yako."
"Nashukuru kwa hilo."
"ok, usijali."
"Z, samahani kwa wito huu wa bila kutarajia, lakini ni wazi kuwa. Samir ameona hakuna kioo, kama wewe. Najua nimekutesa sana ikiwemo kuchana barua zako, ila naomba nipe nafasi sasa kwani ni muda wako mzuri kuwa nami unipendae." Aliongea Samir kwa hali ya upole uloambatana na sauti ya kubembeleza.
"Samir, nadhani unatambua kuwa, wewe ni zaidi ya mtu nae kupenda katika maisha yangu, lakini na sikitika toka nilipokupenda wewe mwenzangu huwa unaniumiza tu. Hata kabla hujawa namimi. Je, vipi ukinimiliki si utaniua kabisa kwa mateso na mawazo?"
"Z, unazaidi ya moyo wa chuma. Moyo uliojengeka kikamilifu kwa ajili ya kukabili matatizo ya Samir. Moyo ambao japo niliusukuma na kuutupia mawe kwa ajili ya kuuharibu, uliishia kwenda kwa fundi Mwashi. Sikufichi dhamira ya mapenzi kwako haijafika leo leo, eti kisa nimekuita. Dhamira hii ipo toka muda. Lakini skutaka kuidhihrisha mapema kutokana na kutohtaji kukuumiza. Skutaka kukurupuka, nimefikiri na nimepata uamuzi. Tafadhali, naomba uniruhusu niwekeze katika moyo wako."
"Samir, una maneno matam sana. Na ninatamani kuendlea iskia ladha ya maneno yako, lakini nashndwa. We ni muongo, unataka useme maumivu yote hayo ulonipa lilikuwa ni funzo la uimara?, kwahyo ulinitoa sadaka ya maumivu, iliwewe upevuke kifikra!!, hapana,,, hapana Samir,,, Nahsi moyo wangu unavuja damu.. Niache tafadhali, sihtaji ku..ku....ona, kumbe uliniumiza huku ukijua ipo siku utanifata nami nitakubali kiurahisi." Aliongea Zulfa, huku machozi yakiwa yanamtoka, alishndwa kustahmili uvumilivu wa kutokwa na machozi mbele ya Samir. Bila hata kuaga akaamua kuondoka.
Huku nyuma, Samir alibaki kuita jina la binti huyo. Lakini alikuwa ni kama mwenye kumwaga maji kwenye kinu kisha kuyatwanga iliapate unga. Ndio nidhahri kwamba sauti ya Nurdin, ilipitiwa na upepo. Hakuwa na jinsi, kwa aibu ya hali ya juu aliamua kujikokota hadi nyumbani kwao, na alipofika huko. Hakuna kingne alichofanya, japo alikuwa na ratib ya kujisomea, lakini alionesha ukipofu kwenye ratiba hiyo.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Laiti ungepata muda wa kuufungua ubongo wa Samir bila shaka ungemkuta Zulfa, akitalii na kutamba kwenye ubongo wake. Hakika samir alijiona ni mkosaji na alionesha wazi kulidhia adhabu yoyote ile atakayo hukumiwa. Ili aachiwe, Zulfa wake.
Wakati yote hayo yakiendlea upande wa kwa Samir.
Upande wa Nurdin, yeye alikutana na Sumayah, waliöngea mengi sana. Sumayah hakujihsi mwenye makosa kuukubali moyo wa Nurdin. Bali alijiona ni mwenye makosa kwa kuchelewa kuukubali moyo wa Nurdin, maana raha alizopata alikili wazi kuwa, hakupata kabla.
Utashi wa Nurdin katika uandaaji wa mada, na upangliaji wa matukio, ndivyo vilivyomfanya Sumayah, asijute kuupoteza muda wake kukaa na Nurdin maeneo yale ya msingi uliokaribu na nyumba yao. Achilia mbali utundu wa mdomoni aliokuwa nao Nurdin, vile vile alikuwa ni zaidi ya mcheshi katika uteuaji wa maneno ya kuongea na Sumayah.
Hakika, ilikuwa ni raha mustarehe. Hakuna hata mmoja kati yao aliekuwa na muda wa kutupa macho na kuangalia saa, bali muda walokuwa nao ni wakulikomaza pendo lao.
Ulifika muda wakaagana, kutokana na shule tu, ila sikwasababu walikuwa wameishiwa maneno mdomoni.
Upande wa Zulfa, ni kama alikuwa akifanya kazi ya kujaza ndoo kwa machozi aliyokuwa akiyatoa. Aliwaza mengi juu ya Samir. Na hakuna baya hata moja kati ya mawazo yake. Usiku mzma yeye hakulala, aliendlea kujitesa kwa mawazo tu.
Yalikuwa ni majira ya saa saba usiku, mji wote ukiwa kimya kutokana na watu kujipumzisha, lakini zulfa alikuwa macho huku akijifuta machozi kwa leso yake ambyo nayo ilionesha kulowana kwa kufta machozi yasiyoisha, Samir pia aliendlea kujilaumu kwa kosa alilotenda, huku Sumayah akiwa amelala kwao usingzi murua, halikadhalika Nurdin alionekana kulala vilivyo, kwa furaha.
Ama kwa hakika mapenzi yana leta raha kwa watu flani, na watu wengne yanawaletea shida.
Mpenzi msomaji, narudia tena. Tuyaacheni mapenzi yaitwe mapenzi.
Mapenzi yamemlaza Sumayah kwa furaha, lakini yamemkalisha macho Zulfa tena kwa kilio. Yamemlaza Nurdin, lakini yamemuacha macho Samir muda huo wa usiku.
Hatimae ilifika asubuhi tulivu, asubuhi ambyo ilimfanya Nurdin aamke mapema na kujiandaa, lakin Samir alichelewa shule kutokana na mawazo pamja na kuukosa usingizi.
.. Samir hakua na jinsi ilimbidi ajiandae na kwenda shule. Hata alipofika shuleni, alipatiwa adhabu kwa kosa la kuchelewa. Hakuwa mwenye furaha siku hyo, bahati nzuri yule mwalimu wa sayansi hakuja kutokana na vikao vya walimu.
Samir alikuwa ni mtu mwenye kushangaza sana siku hiyo, hata wanafunzi wenzake wa karibu walishindwa kumuelewa.
"Umepatwa nanini Samir, mbna leo toka uizame class, unaonekana kujilalia tu kweny dawati" Aliongea Rafiki yake kwa jina la Said.
"Mzee side, wewe acha tu. Najua hatakama nikikutonya huwezi kunisaidia" Aliongea Samir huku akiinuka kutoka kwenye dawati.
"We niambie tu. Unajua mkali sisi ni wana. Kwa hyo mishe inapotokea, ni mzuka kushtuana. Kukaa,kaa tu. Hakusaidi, mwisho ujipige kitanzi" Aliongea Said.
"Unajua nini mzee side, wewe ni mwanangu au sio, na siwezi kukuficha mishe kubwa kama hii. Nadhani unamfahamu Zulfa, si ndio" Aliongea samir.
"Ndio, huyo na mpata. Si yule dem ambae huwa anakufil ile mbya."
"yea, huyohuyo"
"dah, mwanangu. Yule dem ni kisu sema we jamaa angu huwa nakushangaa eti unamzingua. Unazingua malaika wewe, hee..."
"Hebu acha mishe zako. Yule pale dem, mimi nimejikuta nampenda ile mbaya, huwezi amini."
"Acha miyeyusho jembe, we sihuwa unamsanifu kila siku akipita. Iweje leo umpende"
"Hata mimi sijielewi. Yaani toka ticha agusie maana ya mapenzi, mi nimejikuta tu. Namuelewa sana yule dogo."CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mmmh, kwani umesha chonga nae"
"yea. Nimechonga nae. Lakini nilivyoingza maswala ya mapenzi mara nikashangaa mtoto anabadilika, mara mchozi ukaanza kumtoka na akaongea maneno ambyo hata mimi binafsi yaka nidhoofisha. Sijakaa vizuri, mara nikashangaa mtoto anaondoka hata bila kuniaga. Nimeita, mpaka kolomeo likauma, hadi wale wazee walokuwa maeneo yale wakaniskia kipindi na muita. Skufichi nimepatwa aibu, pamja na maumivu. Yaani hata akili yangu siielewi."
"dah, pole mwanangu. Ila sema nini, we unatakiwa uelewe lilesomo la jana. Unajua Zulfa kama angekuwa anakuchukia kwa uboya wako. Basi asingekubali wito wako, na kama amekununia basi asingedondosha chozi kwa ajili yako. Hata hvyo nimeamini kuwa yule dem anakupenda tena zaidi ya sana. Unajua yeye kuondoka huku akilia basi ni wazi inaonesha jinsi ulivyo mkaa moyoni. Na nina imani sidhani kama huyo dem amelala jana.
Kumbuka maneno ya mwalimu wa sayansi. Alisema kuwa, Mapenzi ni hisia za dhati.
Basi kama mapenzi ni hisia huna budi kupatapata mawazo hovyo. Yule pale mtoto natumai hisia zake ndizo zilimpelekea aongee maneno yale, ilinawe ya kuchome. Je, unakubali kuzidiwa na hisia?. Kama jibu ni hapana, basi usiwe na mawazo. Zulfa ni wa kwako, we unadhani utakuwa hvyo hadi lini.
Ila ninachokusihi, mpende kama akupendavyo. Chamsingi mtafte na umuombe msamaha maana wewe umemkosea yule dogo.
Kama kumuaibisha umesha muaibisha sana, kama kumliza umesha mliza sana. Sasa nadhani huu ndo muda wa wewe kulidaka chozi lake, chozi ambalo humtoka kwa ajili yako, mpende kwa dhati. Usiruhusu tena chozi limtoke. Tatizo we ni boya. Usicheke.. Unacheka nini sasa.
Kama wewe sio boya mbna unaruhusu mtoto alie mbele yako bila hata kumfuta machozi, huo si uboya. We unadhani mapenzi ninini?, mapenzi si kula ugali, au kujua kuongea. Mapenzi ni matendo wewe. Unatakiwa umfute chozi pale adondokwapo na machozi, umbembeleze pale adekapo. Hayo ndo mapenzi boya wewe."
"dah, mwanangu nashkuru sana. Kunakitu nimejifunza. Kumbe mapenzi ndo yapo hivyo?, dah.. Poa minitaongea nae. Kumbe najipa mawazo bule tu."
Waliongea mengi na kubadilishana mawazo. Samir alipata mtazamo mpya kutoka kwa rafiki yake.
Muda wa shule ulipita na samir akarudi nyumbani.
****
Upande wa zulfa, nae alikuwa amejawa mawazo juu ya Samir, hata alipokuwa anapika alijikuta akiuunguza chakula yote ni kwa sababu ya mawazo.
Upande wa Nurdin, yeye alikuwa amejifungia geto kwake huku akiendlea kuikumbusha akili yake juu ya Sumayah. Hakika alikuwa na zaidi ya furaha kila alipokuwa akikumbuka maneno mazuri aliyokuwa akipewa na mtoto Sumayah.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa upande wa Sumayah, nae mawazo yalikuwa kwa nurdin, kila alipokumbuka ngonjera za Nurdin. Basi alijikuta ni mwenye kujicheka mwenyewe
Kila mmoja alikuwa na mawazo na mwenzake ki vyake, si Nurdin, sumayah, Samir, wala Zulfa.
"Lazma niongee nae, lazma. Tena leo leo" Alijisemea Samir huku akinyanyuka kwenye kitanda alichokuwa amekitumia kujilazia.
Aliangalia saa yake na kugundua kuwa, kumbe Mawazo yaliweza kumpeleka hadi mishale ya usiku.
"Namfata huko,huko kwao. Kama vp nikampigie mingo." Alijisemea nafsini huku tayari miguu yake ikiwa imeshaanza kumchukua na kumpeleka njia ielekeayo kwa kina Zulfa.
Alijizuia sana kiakili, lakini miguu yake iliendlea kumtembeza na kumpeleka mkabla kabisa na geti moja ambalo limezungushwa fensi ya nyavu iliyokaza kwa chuma chuma zilizochomekwa kila pahala ikiwa kama nguzo ya nyavu zile.
Kwa sababu macho hayana bazia, basi yeye alisimama na kupenyeza jicho lake kutoka kwenye nyavu zile hadi kwenye nyumba iliyojengeka kimjengo wa pesa.
Mkazo wa macho yake, pamoja na hamisho la fikra zake. Bila shaka ungegundua kuwa ile ndio nyumba ya kina Zulfa.
Kuachilia mbali kijiupepo cha kiaina yake kilichokuwa kikipiga maeneo yale, vilevile hakuwa na shati ya mikono mirefu, hivyo aliwakabidhi mbu, mwili wake iliwaendlee kutalii nao. Pindi alipoona Mbu wamezidi, aliamua kuichota mikono yake ndani ya shati na kuikumbata kwa ajili ya kuepusha manyanyaso yale.
Alikaa zaidi ya saa moja. Lakini hakufanikisha kuona hata dalili za kumuona Zulfa. Ingawa alikuwa amejianika kwenye moja kati ya saluni ya maeneo yale ambyo kwa nje ina umeme ulioleta mwanga na kummulika samir, kiasi cha kuonwa na yeyote aliekuwa kwenye giza. Aliamua kufanya hivyo, ikiwa kama kumfanya Zulfa aweze kumuona endapo atatupa jicho lake.
Sasa Samir akawa hana jinsi, akaongea na miguu yake na kama sekunde kadhaa hivi. Miguu yake ilianza kumtoa maeneo yale.
Wakati Samir akiwa anaondoka, ndani ya jumba lile kuliskika sauti ya msichana aliekuwa ameangaza macho yake dilishani, huku akiendlea kulia. Hakuwa mwingne bali ni Zulfa. Alitamani sana amfuate Samir, lakini alishndana na hisia zake jambo lililompelekea kumwaga machozi kwa sababu ya Samir.
Lengo la Zulfa halikuwa baya. Yeye alitohtaji kufanya ni kutokujishusha mbele ya Samir. Lakini Je, kufanya vile, alijiongezea mawazo. Au alijipunguzia mawazo. Natumai jibu unalo wewe mpenzi msomaji, kumbe si busara kujiumiza kwa kutumia furaha zetu.
Siku ile.. Samir alifika geto akiwa amechoka, lakini cha kushangaza alichukua daftari na kuanza kujisomea. Alisoma kama nusu saa hvi, kishaakakiendea kitanda chake kwa mapenzi ya dhati, huku akiendlea kujipa maana ya maneno ya wahenga ya semayo 'Majuto ni mjukuu'.
" Nilikuwa nikidhani kwamba, Majuto huwa ni mjukuu piodi utapokuwa babu. Kumbe sivyo. Maskini Samir leo naumia kisa visa vyangu vya mwanzo.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Zulfa, natamani kukusahau, lakini umenikaa kama kiungo cha mwili wangu, natamani kujizuia niskuwaze, lakini unaniumbua kama kikohozi kwangu. Najua mimi ni zaidi ya mkosaji, lakini mbna sipati angalau hizo dakika chache za kupiga goti langu chini ya ardhi, mkabala na nyayo za miguu yako. Huku mikono yangu nikiwa nimeiambata na kuuruhusu mdomo ukuombe msamaha. Kwanini? Kwanini mimi nakosa hata muda huo?, au pengine sikuhzi mimi ninagundu?," Alijiuliza maswali na asipate jibu. Alitulia kidogo na kuyafuta machozi ambayo tayari yalisha jinjenga kwenye kuta za mashavu yake.
"good idea(wazo zuri), lazma ni mshrikishe na Nurdin coz wao wanapatana na Zulfa" Aliongea Samir.
Upande wa Nurdin yeye alikuwa akijisomea masomo waliyokuwa wamefunzwa shule. Kwenye upigaji wa msuli, huyu jamaa usinge msema vibaya, hachezei hovyo nafasi yake kama ambavyo achezei hovyo nafasi ya Sumayah, pindi awapo nae.
Tukienda upande wa Sumayah, yeye alikuwa akimuwaza Nurdin tu.
"Hahahaha, una sura nzuri. Hebu tazama macho yako kwenye kioo, kisha yazungushe vile uyazungushavyo uwapo namimi, natumai utakili uzuri wa asili ulobahatika kuwa nao. Mpenzi kwenye mapenzi yetu. Mimi ni daftari, halafu Elimu ni kalamu. Basi nakuomba unaponiwaza mimi iwazie na kalamu, maana bila kalamu hata mimi sitofaa kuitwa daftari.
Namaanisha soma sana, ili upevuke kifikra na uje kunipa vitu kupitia elimu yako. Nathamini sana mambo yako muhmu, ikiwemo Masomo, Nurdin, nakadhalika. Niombi tu, ukifika nyumbani naomba uniwaze kwa machache nilokupatia. Usiku mwema mpenzi." Ni mawazo ya Sumayah, pale alipokuwa akikumbuka jinsi walivyoagana na Nurdin.
Sumayah, alijikuta anakili wazi kuwa, kweli Nurdini anampenda.
Hatimae safari ya kujisomea iliwawanie mitihani ya kumaliza darasa la saba ilifika. Walipga msuli sana huku, Samir akiwa anajitahdi kuyatoa mawazo ya Zulfa ilikusudi yasimuathiri kwenye masomo yake. Kwa kipindi hicho nae Zulfa alikuwa yupo shule, hvyo hakukuwepo na mikangano ya kifikra.
Masomo haya kuwa kikwazo katika penzi kati ya Nurdin na Sumayah kwasababu, kila mmoja alijitambua na waliiheshimu elimu na kuiona ni sehemu ya maisha yao.
Upande wa Samir, yeye alikuwa bize zaidi na masomo, jambo hilo lilianza kumpelekea kutokumuwaza Zulfa.
Nae Zulfa huko katika shule ya kulipia. Alisoma huku mawazo yote akiwa ana muwaza Samir. Aliishi akiulaumu uamuzi wake wa kwenda shule bila kumuaga Samir, na alikuwa akijuta juu ya yeye kumkwepa kwepa Samir kipindi kile alipoamua kuteseka juu yake.
Kama utani. Zulfa alianza kukonda kwa mawazo, hakuingia darasani kisa maumivu ya kichwa yaliyo sababishwa na kumfikiria sana Samir.
Ilifikia kipindi hadi akadhoofika hali yake na kumpelekea kutokuweza kutembea kabisa, kutokana na mawazo ya Samir. Masomo kwake yakawa hayampati kutokana na ugonjwa ulioletwa kisa haya haya mapenzi. Alipelekwa hospital na kupewa kitanda kisha akapimwa, alikutwa na maradhi mengi sana.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hiyo ilitokana na msongo wa mawazo ya mtu fulani jambo lililompelekea ashndwe jinsi ya kufanya iliaepukane na maradhi.
Kutokana na maradhi yale, walimu waliamua kumrudisha nyumbani kwao iliangalau akapate tiba kwa usalama zaidi kutokana na hali aliyokuwa nayo. Alirudishwa bila yeye kujitambua alikuwa yupo katika mshtuko.
Ndugu msomaji naomba ujifunze kitu hapo, na sikusoma tu. Naam, mapenzi yanaweza kukufanya ukaugua kama yanavyomfanya Zulfa kwa muda huu. Pia unapaswa uelewe Zulfa ameshndwa kukabiliana na masomo pamoja na mapenzi. Anampenda Samir kuliko masomo, na anamuwazia sana Samir kuliko masomo.
* * * *
Samir kwa wakati huo yeye aliamua kuwa bize na masomo, na alijiandaa vilivyo kwa ajili ya mtihani wa taifa wa darasa la saba.
Hatimae muda waliokuwa wa kiusubiri ulifika na wakafanya mtihani. Baada ya kumaliza, wanafunzi wale wakawa huru kwa ajili ya kusubiri majibu ya mtihani wao kutoka balaza la mitihani.
Hawakuwa na laziada tena shuleni kutokana na wao kuwa wamemaliza elimu yao ya shule ya msingi.
Samir alifurahi sana kwani katika mawazo yake hakuwahi kuwaza kama ingekuja siku moja yeye akamaliza elimu ya msingi. Elimu iliyompeleka shule saa kumi na mbili asubuhi ilhali sekondary huenda saa moja. Elimu iliyo mtoa shule saa kumi na moja kasoro ilhali sekondari wanatoka saa nane na nusu mchana. Elimu iliyomuaibisha kwa kumvisha kaptula ambayo kwake ilikuwa ni kama pensi, hakika alikuwa amechoshwa sana na elimu hiyo. Na alikuwa na furaha sana baada ya kutambua kwamba yeye na shule ya msingi basi.
Alijitamba na kujiona kuwa ni mwenye bahati, alilaani sana kutokuwa na mdogo wake kwani alitamani sana kama ingewezekana angekuwa akimsumbua mdogo wake awahi shule ilhali yeye yuko nyumbani ilimradi tu, aoneshe ufalme.
Wazo la kusafiri kwa ajili ya mapumziko lilimuingia akilini na kumfanya atamani kusafiri ili akajiliwaze huko atakapoenda.
* *
Zulfa anafanyiwa ma tibabu ya hali ya juu kutokana na ugonjwa ulompata. Hatimae alipöna na kupewa wiki moja kwa ajili ya mapumziko.
Ilikuwa ni siku ya alhamisi, saa sita kamili mchana Zulfa akiwa katika matembezi yake, huku Samir akiwa kijiweni akipiga stori na marafiki zake.
Mara ghafla Samir alimuona Zulfa. Na papo hapo Zulfa alimuona Samir.
Mpenzi msomaji kumbe macho nayo huwa yanaongea?, huwezi amini, wawili wale walipoangaliana. Ni kama kuna waliitana kupitia macho, Samir alijikuta akinyanyuka na kumfuata Zulfa, huku Zulfa nae akijikuta anajiandaa kumpokea Samir.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Walifikiana, na kupitia macho hayo hayo waliongea kwa huzuni pasina kutumia mdomoni. Kwa kuwa furaha ya macho ni machozi, basi wote kwa pamoja yaliwatoka mchana huo, walishndwa kujizuia na kukumbatiana, ama kwa hakika akili za kujua kuwa muda ule ulikuwa ni mchana ziliwatoka na walikuwa na akili ambazo hawa kuwahi hata siku moja kuwa nazo. Machozi ya Zulfa yalianza kukosa heshma na kuliloanisha shati la Samir upande wa begani. Walikumbatiana kama dakika tano huku kila mmoja akimlaumu mwenzie.
Hakika Zulfa alikuwa amekonda sana. Wakiwa katika hali ile. Mara ghafla walijikuta wakirudiwa na akili zao na baada ya kuhamaki ndipo walipogundua kumbe walikuwa katikati ya barabara kuu, walishangaa baada ya kuona magari yakiwa yamesimama na kuwaangalia wao, huku watu wote waliokuwa maeneo yale wakishangaa tukio lile la kihisia.
Baada ya wao kugundua kumbe wameonwa na umati wa watu, walijihisi aibu sana. Lakini ni kinyume na mawazo yao kwani watu wale waliwapöngeza kwa kuwapigia makofi na wengne waliwatunza pesa kutokana na kufanya jambo la tofauti sana.
Zulfa alitoka hapo akiwa analia huku akikimbia. Samir pia aliondoka huku akiwa ameinama chini na kuelekea geto kwake.
Alijishangaa sana, na alishangaa kitendo kile kilichofanyika japo yeye ndie aliekifanya.
Alianza kupatwa na mawazo. Kichwa kilianza kumgonga ikiwa ni taarifa ya kumuonesha kuwa amewaza sana. Alipitiwa na usingizi uliomlaza hadi usiku kabisa.
Kwa upande wa Nurdin na Samir huko sasa ndiko usiseme.
Penzi lao lilizidi kunoga, walisukumiana maneno magumu na yenye ahadi nyingi sana.
" Mpenzi Natambua wazi kuwa, umemaliza shule. Na endapo matokeo yatakuwa mazuri, bila shaka wewe utaingia sekondari iliuanze kidato cha kwanza. Si ndiyo." Aliongea Nurdin, huku jicho lake akiwa ameliangalizisha chini kama ishara ya jambo aongealo.
"Ndio, mpenzi." Aliitikia Sumayah, huku akimuangalia Nurdin ambae alikua ndani ya hisia kali.
"Mpenzi, unapaswa ujue wazi kuwa. Waschana wengi huwa wana huruma. Huruma yao ni pale wafuatwapo na wavulana huku wakiloa machozi na kuwahtaji. Waschana hujikuta wa kitamani kuwafuta machozi kulingana na huruma walio nayo. Wana sahau kuwa, machozi hutengenezwa. Na kuomba mpenzi wangu usiwe Dada huruma pindi utapofatwa na wanaume wa aina hiyo."
"Ondoa shaka mpenzi. Mimi ni wako, na nitabaki kuwa wako. Uliponifuata nilipembua mchele na pumba, sikukurupuka kukushika mkono na kukukubalia uingie nami ndani ya sayari hii. Nauhakika na maneno yangu, hata kama mvulana akija na huruma gani, hapa ataishia kutwanga maji kwenye kinu. Najielewa mpenzi wangu, ondoa shaka."
"Labda ni kwambie kitu Sumayah, ninapo sema waschana wana huruma, na kuwa na maanisha niongeacho.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
MUNGU, kajaalia wavulana kuwa na matabaka tofauti tofauti. Na amewapa ujuzi wa kucheza na akili za waschana kuliko unavyofikiria wewe. Labda nikupe siri, sekondari si kama huko msingi ulipotoka. Sekondari kuna watu wanajua kurubuni mpaka unajihsi nimerubuniwa na hautamani uache kurubuniwa. Hivyo kuwa makini sana mpenzi wangu. Weka vazi la huruma ndani ya begi na usilivae uwapo kwa wavlana wengine bali ulivae pindi uwapo na mimi." Aliongea Nurdin, na kumpelekea Sumayah, kushndwa vumilia maneno yale makali. Moja kwa moja, machozi yakaanza kumtiririka.
"Nurdin. Unanionea.. Unahisi mimi malaya, mimi kicheche. Uko wapi umalaya na ukicheche wangu Nurdin?. Uko wapi?, natambua wazi kuwa wewe upo na unanipenda iweje niende kwa mwingine, iweje nurdin.
Hebu fikria ni wanaume wangapi hadi sasa wamenifuata ila mimi bado nipo na wewe tu. Huoni kama na kupenda?, siwezi kuwa mama huruma kwenye mechi za ugenini."
" Natambua wazi kuwa unanipenda. Na pia naomba unielewe, hakuna pahala nilipokuita malaya. Wala hakuna dhana ya ukicheche hapo. Lakini natambua Tahadhali ni bora ilikusipatikane ajali.
Pia naomba utambue mpenzi wangu, haya maneno yananitoka kwa upendo tu. Nakupenda sana mpenzi." Aliongea Nurdin. Kisha Sumayah, akaushika mkono wa nurdin na kuuapisha kiapo cha kutobadilika pindi atakapoenda Sekondari.
Ilikuwa ni kawaida yao kuapishana kwa kushkana mikono, ikiwa kama kuonesha ahadi thabiti.
Sumayah. Ali apa huku akiangua machozi, Nurdin alifanya kazi ya kuyafuta machozi yale lakini hiyo haikuya sababisha yaache kutoka.
Upande wa Zulfa, yeye huko alikuwa akilia kilio chenye furaha. Na hata alipoingia rafki yake kwa jina la Hawa. Hakusita kumueleza ukweli wa kila kitu.
Hawa, hakuamini kama kitendo kile kilitokea, aliuliza maswali mara mbili,mbili ikiwa ni kujiridhisha nafsi lakini aliambulia jibu lile lile. Ndipo alipoamini kuwa Mapenzi yana nguvu.
Zulfa na shoga yake Hawa. Walipanga muda wa kuonana na Samir. Na wakakubaliana, halikuwa jambo gumu sana. Maana Zulfa alikuwa na ukaribu na rafiki kipenzi wa Samir ambae ni Nurdin. Hivyo alimtaarifu Nurdin na Nurdin akamwambia kuwa atamtaarifu Samir.
Baada ya muda kupita, Samir na rafiki yake Nurdin walikutana na Samir akamuelezea Nurdin jambo lile la kushangaza.
Hata Nurdin hakutaka kuamini ghafla. Lakini alikuja kuamini tu.
"Kilichopo hapa ni mimi kumvizia Sumayah, iliniongee nae" Aliongea Samir.
"Ndio ni wazo zuri, lakini unapaswa ujue kuwa. Tayari Zulfa amesha kuja hapa na kuniambia mkutane sehemu." Aliongea Nurdin, na Samir alijikuta akipatwa na kijitabasamu mwanana.
"dah, kweli mwana huyo dem, amekufa na kuoza. Au vipi jembe."
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"yeah. Ni kweli."
waliongea mengi na ulipofika muda wa ahadi kati ya Samir na Zulfa. Samir alikuwa wa kwanza na kwenda hadi maeneo walipo ahidiana, haikupita hata Muda. Zulfa nae alifika. Na wote kwa pamoja wakakaa kwenye mti uliokatika Muda mrefu maeneo yale.
Zulfa alifungua Semi kwa salamu, kisha Samir akampokea kwa kuitikia Salamu tena kwa bashasha.
Wote kwa pamoja walitulia huku macho yao yakiongea zaidi kuliko viungo vyote katika mwili.
Samir aliuvunja ukimya ule kwa kuanzisha maongezi...
"Samir, samahani. Nilikuwa nimekuita ilinikuambie kiasi gani nikuchukiavyo.
Samir, sitamani kukuona, sihtaji uniangalie, na ninakuomba usijekunitafuta tena sawa?" Aliongea Zulfa na Samir akatabasamu kidogo kisha akajiinamia chini.
"Zulfa, nashkuru sana kwa kunichukia na nina zaidi ya furaha kwa kubaini kuwa unanichukia. Lakini tafadhali chunga kauli zako," Aliongea kisha akawa ni kama mwenye kushusha pumzi na kuendlea.
"Zulfa, unajua mateso maana yake sikubebesha miba kichwani au kuchomwa na ukuni. Unachofanya ni kuutesa moyo wangu. Wewe ndo sababu ya mimi kukupenda, sasa mbna unanichukia kiasi hcho?"
"Samir, naufurahia uwepo wako pindi niwapo mbali na wewe, ila nikikuona tu. Nakufananisha na mnyama simba anaewinda nyama ya moyo wangu. Ndio maana nakuchukia pindi nikuonapo." Aliongea Zulfa huku kope za macho yake akiwa amezifumba.
"Skia Zulfa. Naomba nikabidhi mkono wako tafadhali." Aliongea Samir, na Zulfa akiwa amefumba macho akajikuta akiponyokwa na mkono wake moja kwa moja hadi mikononi mwa Samir.
"Zulfa, mkono wako unaashiria hamu ya kugusa mkono wangu, ila wewe mbna unauzuia?, kwanini unafanya hivyo Zulfa. Hebu jitazame ndani ya moyo wako, unatamani zaidi uwepo wangu ila wewe unaamrisha mdomo wako utamke bila fikra.
Wewe ni bingwa wa kujitengenezea maumivu ya moyo. Tafadhali fanya kitu ambacho moyo unataka, unajua kuleta mitafaruku kati mdomo na moyo kunaweza kuleta madhara ambayo hata hujawahi yategemea. Tafadhali niruhusu nikushike mkono na nikuvushe kwenye mto huu wa mapenzi, mto ambao umejaza mamba wa aina mbalimbali. Naomba shinda kinywa chako na utumie maamuzi sahihi kutoka Moyoni." Aliongea Samir maneno yale.
Nikama vile aliuchukua moyo wa zulfa na kuufinyanga finyanga, maana Zulfa alishndwa kujizuia na hapohapo chozi likajiunda na kuanza kumtoka bila hata aibu.
"Samir, unanikosea sana. Huoni uzito wa maneno yako mbele ya mschana mimi dhalili monye moyo wenye damu, hunihurumii kabisa, kila napo jaribu kukuchukia. Najikuta nikijichukia mwenyewe. Tafadhali naomba uniite kwa jina la kiwakilishi cha hisia zetu. Staki uniite jina langu." Aliongea maneno yale makali tena yenye kuumiza sana endapo yanapatiwa ufikiri.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" Jina lako ni Mpenzi wangu. Tafadhali naomba ni kuite kwa mara ya kwanza toka dunia hii iumbwe.
Mpenzi wangu..." Aliongea Samir na hapohapo Zulfa alikuwa nikama asiejielewa.
"Ndio. Barafu wa moyo wangu." Alijibu Zulfa na kumpelekea samir kujawa na furaha.
"Jina la mapenzi ni ishara bora ya upendo kwenye mioyo ya wapenda nao. Hizo unazoziona zinakupeleka kisa mimi, basi hizo ndo hisia na kaa ukijua hisia zina uwezo wa kukuua na zinauwezo wa kukupatia furaha pia. Staki utumie hisia zako kunichukia, yaani na maanisha usiwaze mabaya juu yangu."
"Mpenzi wangu, hebu tazama saa yako. Kisha upime mapigo ya moyo wangu. Nadhani itakuwa niishara tosha ya kujua kiasi gani nakupenda. Tafadhali usijekunitenda, mwenzio bila wewe hata chakula hakipandi, bila kunijali hata masomo si chochote kwangu." Aliongea Zulfa na Samir alimpa maneno ambyo laiti ungeyasikia basi ungehamaki sana.
Waliendelea kuongea mpaka hapo walipogundua kuwa muda umeenda tayari ndipo walipoamua kuagana. Samir alipita njia yake na Zulfa alipita njia yake. Zulfa akiwa njiani kuelekea nyumbani kwao, mara ghafla njiani akakutana na Nurdin, ambae kwa muda huo alikuwa akitoka kwa Sumayah.
Walisalimiana na Zulfa alimjuza kuwa tayari ameshaongea na Samir, na ilikuwa ni furaha isiyo kifani baada ya wawili wale kupatana. Kwakuwa muda ulikuwa umekwenda sana, waliagana na kupeana ahadi ya kuongea siku ijayo.
Hata Zulfa alipofika kwao. Alikaribishwa na matusi kutoka kwa mama yake. Alikanywa pia kwa kuchapwa viboko maana haikuwa kawaida msichana kuchelewa nyumbani kiasi kile.
Ingawa Zulfa, aliadhibiwa. Lakini hakujutia kabisa uamuzi wake wa kuonana na Samir. Kisura cha ukiburi kilimvagaa na kumfanya kama mwenye hasira. Kisha akakimbilia ndani mwake na kujitupa kitandani. Mawazo ya matusi ya mama haku yawazia ni kama yaliingilia skio la kulia na kutokea la kushoto. Alilala na kuziagiza hisia zake na kujikta ameanza kukumbuka yale walyo kuwa wakijadili na Samir.
Upande wa pili. Nurdin ilimpasa aende moja kwa moja. Hata alipofika alimkuta Samir. Akamuita na wakajuliana hali kisha Nurdin. Akakata ukimya kwa kumuuliza Nurdin swali la amsha washa.
"Vipi, nimekutana na mtoto. Amesema mmeonana. Je, ni kweli?" Aliongea Nurdin na kumfanya rafik yake Samir kuchanua tabasamu.
"Yea, nimeonana nae mtoto. Kumbe na wewe kakwambia? Dah, mzee Nurdin, yule Zulfa kwa sasa ni shem wako tena wa halali, amesaini mwenyewe." Aliongea Samir na kumfanya Nurdin awe kama mtu asieamini aambiwacho.
"Kweli?" Aliuliza Nurdin ilikupata uhakika zaid.
"kwani hunijui nurdin. Mi huwa scheleweshi. Yaani nimempaswaga hadi mtoto mwenyewe akamwaga machozi." Aliongea Samir na Nurdin akashndwa kujizuia. Alikushanya vidole vyake na kubumba ngumi iliyoungwa na vidole vitano kisha akamrushia Samir. Ikiwa ni ishara ya kumsifu kwa jambo lile.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Dah, mwanangu. Yule mtoto mkali. Ungemuacha ningekuona boya sana. Lakini vipi umempiga kiss?" Aliongea Nurdin na kumfanya Samir kunyong'onyea kidogo.
"Ayaa!, hiyo mishe niliisahau. Lakini minilihofia huenda kange kasirika na kubadili uamuzi." Aliongea Samir huku akiwa amejishka kichwa utadhani ni mwenye kufikiria jambo la muhimu.
"We nani alikwambia kuwa busu inakasirisha. Labda nikwambie kitu Samir, busu ni ishara ya upendo.
Unajua nivigumu binadamu kuchukua mdomo wake na kuuleta mpaka shavuni kwa ajili ya kuliwaza ubaridi wa shavu lake, kitendo hcho cha kushndwa binadamu kuweka mdomo shavuni kwake, huwa kina mnyima amani na kujihisi ni mpweke na amekosa upendo kati ya mdomo na shavu. Sasa wewe unapompiga kiss umpendae hujihisi amani na kurejesha furaha yake japo kwa uchache, kitendo hcho humpelekea kuhisi kuwa wewe unampenda. Hivyo busu sio baya kwa wapenda nao." Aliongea Nurdin.
"Wewe!, nilikuwa sijui. Kumbe busu ni muhimu kiasi hicho. Dah! Nitahakikisha nampga kiss nikikutana nae tena." Aliongea Samir.
"Unajua Busu inaumuhimu mkubwa pia, huleta msisimko wa kimapenzi. Hivyo ni jambo la muhimu kwako kumpiga busu umpendae kama ni kweli unampenda."
waliendlea kuongea, na baadae Samir alimuomba Nurdin amfundisha masomo ya sekondari.
Walipoanza masomo, kila mmoja alikuwa makini. Nurdin alikuwa makini kwenye ufundishaji halikadhalika Samir alikuwa makini kuhakikisha akinasa kila alichoelekezwa.
Ingawa walikuwa makini lakini utani haukuepukika. Mara mwalimu amtishie mwanafunzi, mara mwanafunzi aulize maswali ya kejeli ilimradi tu kuweka utani.
Hata walipomaliza kufundishana. Nurdin alienda kwao kwa ajili ya kufanya kazi aliyokuwa amepewa na mama yake, lakini samir alibaki kwa ajili ya kujisomea. Aliendelea kudurusu na hata alipomaliza aliamua kujichukua na kuenda moja kwa moja hadi kwenye ukumbi wa kuoneshea sinema.
Ndugu msomaji, labda kabla sijaendelea ni kwambie tu, kitu kimoja.
Huyu samir, hakuna starehe aliyoipenda kama kwenye ukumbi wa kuoneshea sinema. Kipindi yupo mdogo sana, alikuwa akichapwa sana kutokana na kwenda sana kwenye sinema. Kwa wakati ule, hakuna muvi ambayo ilioneshwa nae asiijue. Mara nyingi alipokuwa darasani, alipenda kuanzisha makundi na kuanza kuwa simulia wenzake muvi mbalimbali ambazo ameshaziona. Hakuna aliemfikia kwenye masuala ya muvi. Ziwe za action, au romantic. Yeye aliangalia tu. Na ndio maana hata alipomaliza kusoma aliamua kwenda moja kwa moja hadi kwenye ukumbi wa sinema.
Pindi alipokuwa na mawazo, hakuwa na pakwenda zaidi ya sinema. Huko ndiko alikoenda kwa ajili ya kutoa matatizo na kujijengea furaha. Hakika alikuwa ni zaidi ya mlevi kwa mapenzi ya video. Alikuwa yupo ladhi akose hata chakula lakini apate kuangalia sinema.
Siku hiyo ukumbi ulikuwa umefunika sana, kiingilio cha kila siku huwa ni shilingi mia, lakini siku hiyo kiinglio kilikuwa kimepanda hadi shilingi mia mbili kutokana na onesho maalumu la muvi ambayo ndio ilikuwa ikitamba kwa miaka hiyo.
Ilikuwa ni muvi ya kihindi ambayo ilioneshwa sinema siku iliyopita naizungumzia muvi yenye mastaa kumi na mbili ambao wote walikufa na wakabaki mastaa wawili. Nadhani wewe kama ni mpenzi wa muvi za kihindi utakuwa unaijua. Inaitwa 'JAAN DUSHMAN'.
Hata baada ya muvi ilekuisha. Ndipo Samir alipoamua kwenda kujipitisha kwa kina Zulfa huenda akamuona, alipita lakini asimuone.
Ndipo alipoamua kumtafuta rafiki yake Nurdin. Aliamua kwenda maeneo ya kina Sumayah, maana alijua wazi kuwa Samir hatokuwa pengine zaidi ya pale.
Ni kweli mawazo yake yalienda sahihi, kwani alipofika tu. Alimkuta Nurdin akiwa na Sumayah, ndipo alipoamua kuwa fuata angalau nae akapige soga mbili tatu maana hakuwa na pa kwenda kwa muda ule.
Alipofikia aliwasalimu nao wakamuitikia kisha walimkaribisha.
Kama kawaida ya Samir alianzisha soga zake za vichekesho na kejeli...
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
. "Unajua wapendanao kama nyie, lazma muwe mnakaa karibu na maua yanukiayo vizuri, na si kukaa maeneo haya ambayo hata hayana maua." Alikejeli Samir na wote kwa pamoja wakacheka.
"Unajua nini Samir. Shemeji yako ana aleji na maua ndomaana huwa simpeleki huko. Nahofia tunda langu lisije umia." Aliongea Nurdin na Samir akatabasamu kidogo, huku Sumayah akashndwa kujizuia na kuangua kicheko.
"Wewe Nurdin, unamnyima raha shem angu. Mpeleke kwenye maua,maua. Hebu ona sasa hivi unampigsha stori mpaka anaanza kukunja kanga. Vipi angekuwa kwenye maua si angekunja maua na kupata raha." Kwa mara nyingne tena Sumayah, alishindwa kuzuia kicheko chake kwa maneno yale yaliyosheheni utani wenye maana.
"Shem nawe!, unavituko. Sasa Nurdin anipeleke kwenye maua. Kwani kunatofauti gani kati ya manen ya hapa na ya kwenye maua?" Aliongea Sumayah.
"Ndo, ushangae nawewe baby." Alidakia Nurdin.
"Skia shem ni kwambie, staki nijifanye najua lakini nataka nikuombe jambo kama utaweza, jaribu kumuomba Nurdin akupeleke kwenye Maua iliuione ladha ya huko. Nadhani hautokubali kuacha nihadithia." Aliongea Samir.
"Mmmh, haya bwana. Minitaongea nae ilianipeleke hukoo.. Kwenye ladha ya maua." Aliongea Sumayah.
Waliendelea kupiga stori za hapa na pale, wakajikuta wakipanuana ubongo na kujazana mawazo.
Ucheshi wa samir ndio uliokuwa ukiwafanya wastamani kuagana, Sumayah, alijivunia kupata faraja ya vijana wale. Pale Nurdin alipopata upenyo wa kuongea. Hakusita kugusia swala la sekondari na kumuomba mpenzi wake asijekubadilika hata kidogo.
Samir, alipopata mwanya mkubwa wa kuskilizwa alianza kuhadithia muvi ile aliyokuwa ameiona.
Hatimae ulifika muda na wao wakaachana, Sumayah alienda kwao huku Nurdin na rafiki yake Samir wakienda kwenye kijiwe cha uji kwa ajili ya kupata joto tumboni. Hata baada ya wao kuwa wamemaliza shughuli hiyo waliamua kuagana.
Hatimae siku hiyo ilipita na kufuatiwa na siku nyingine.
Kwakuwa Samir alikuwa amehitimu darasa la saba, hakuwa na budi kwenda likizo kwa mjomba wake iliakakae huko na kusaidia kazi mpaka hapo matokeo yatakapotoka ya kujiunga na elimu ya sekondari. Ni siku mbili pekee alikuwanazo kwa ajili ya kujiandaa kabla hajaondoka maana hata nauli tayari alikuwa ameshapewa.
Upande wa Zulfa nae alikuwa amebakiza siku tatu arudi shule kutokana na kurejea kwa afya yake.
Zulfa aliona ni vyema amtafute samir kwa udi na uvumba ilimradi awezekuongea nae maana alikuwa amemkosa kwa siku moja nzima.
Moyo wa zulfa ulikuwa ukitapatapa, kwa kumkosa umpendae, halikadhalika Moyo wa Samir ulikuwa ni kama umeongezewa spidi ya mapigo kwa kumkosa Zulfa wake.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kila sehemu alipoenda Zulfa kwa ajili ya kumtafuta Samir, aliishia kumkosa. Alishindwa kujizuia na kuamua liwalo na liwe lakini lazma amuone ampendae. Ndipo alipoichukua miguu yake kwa hiyari na kwenda hadi nyumbani kwa kina Samir. Alipofika, hakumkuta mtu yoyote ndani ya ngome ile zaidi ya Samir pekee ambae alikuwa kwenye maandalizi ya safari.
"Haa!, Z, umenifata mimiii, au umeijia shida nyingine."
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment