Search This Blog

Thursday, July 21, 2022

HUWEZI KUUA MAITI - 5







      Simulizi : Huwezi Kuua Maiti

      Sehemu Ya Tano (5)



      “Hapa nilipo si rahisi kuniona ila nahitaji kuwa na mahali pa kuishi na safari hii nitaishi ardhini ambako hakuna mtu awaye yote ataniona hata wakija kunitafuta hawatanipata ninachohitaji ni maji na chakula, nitakaa ardhini kwa siku nne bila kutoka nje siku ya tano nitatoka nafikiri hali itakuwa shwari, kazi yangu sasa itakuwa ni kuunda jeshi tu!” Aliwaza bibi Nyanjige kisha kuanza kutafakari ni kwa njia gani angeweza kupata mahali pa kuishi.



      “Kwanini nisichimbe ardhini?”Aliwaza bibi Nyanjige na kukubaliana na wazo hilo na bila kuchelewa alipiga mluzi wa ajabu kwa muda wa kama dakika tano hivi, walitokeza wanyama wawili wadogo na wafupi kimo cha Paka , walikuwana mikia mikubwa ya rangi nyeupe! Walikimbia mbio hadi miguuni kwa bibi Nyanjige na mmoja alimrukia mikononi akambeba kama mtoto!

      CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

      Bibi Nyanjige alipiga tena mluzi wa aina nyingine na wadudu wale kama mshale walirukia ardhini na kuanza kuchimba ardhini! Udongo uliruka kama uliotupwa na mashine ya kuchimba kisima, katika muda wa kama dakika ishirini hivi hawakuonekana ardhini na shimo refu kupita kiasi lilishachimbwa ardhini!



      Kazi hiyo iliendelea kwa muda kama masaa mawili ndipo bibi Nyanjige aliposikia mlio fulani wa wanyama hao kutoka shimoni aliielewa maana yake na kuanza kuteremka shimoni taratibu akikanyaga pembezoni mwa shimo hilo na kuzidi kushuka chini, ilimchukua muda wa masaa mawili kufika chini ambako aliwakuta wanyama hao wamelala kifundifundi ardhini! Walionyesha kuchoka.



      Kulikuwa na kiza kila mahali ndani ya shimo hilo lakini kwa msaada wa macho ya wanyama hao ambao macho yao yalimulika kama tochi yenye mwanga mkali bibi Nyanjige aliweza kuona, hakuwa na tatizo la hewa kwani wanyama walitoa aina fulani ya hewa kutoka katika mapafu yao iliyoondoa gesi na hewa nzito shimoni.



      Ni wanyama hao ndio waliomtunza bibi Nyanjige shimoni kwa siku zote tatu alizokaa shimoni alikula matunda na ni wanyama hao waliokwenda mtoni kunywa maji na kwenda kumtemea mdomoni aliposikia kiu..



      Wanajeshi kumi na mbili waliongizwa shimoni kuchunguza wote hawakurudi juu wala kutingisha kamba ili watolewe, hali hiyo ilizidi kuwatia wasiwasi wanajeshi wote.

      “Hebu ngojeni niende mwenyewe inawezekana hawa vijana wanafanya mchezo humo ndani!”Alisema mkuu wa majeshi akafungwa kamba kiunoni na kuanza kushushwa taratibu kuelekea shimoni, mwili wake ulitetemeka kwa hofu.



      Sababu ya mafunzo ya judo aliyoyapata huko China alikuwa tayari kwa lolote ambalo angekutana nalo ardhini, alipotua tu chini naye mzizi ulimzunguka shingoni kwa sababu hakuwa legelege alifanikiwa kuuondoa mzizi na kumtupa mtu aliyeweka mzizi huo shingoni pembeni, mara alisikia kitu kama mluzi na ghafla ukipigwa viumbe kama Paka vilimrukia usoni na kuanza kumng’ata na kumrarua vibaya usoni, lakini tayari alishaitingisha kamba na wanajeshi waliokuwa nje walianza kumvuta kwa nguvu.



      “Jamani ni hatari!” Alisema baada ya kufika juu.

      “Kuna nini?”

      “Bibi……!” Kabla hajamaliza sentensi yake Kamanda alikata roho.

      “Yaani bibi Nyanjige ndiye amemfanya hivi kamanda wetu kama yumo humu ndani basi hakuna la kufanya zaidi ya kutumbukiza bomu na huu ndio uwe mwisho wake!”

      CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

      ‘Lete bomu?”

      “Hili hapa!”

      “Na wenzetu waliomo ndani je?”

      “Nina uhakika hao hawawezi kuwa hai, weka bomu shimoni tu!”Alisema msaidizi wa kamanda na bomu lilitupwa ndani ya shimo, kilichofuata hapo ni mlipuko mkubwa sana.

      Risasi za Msaidizi wa Mkuu wa 
Majeshi zilichimba sentimita 
chache kutoka kwenye kichwa cha bibi Nyanjige. bila shaka alidhamiria kumuua kutokana na maneno machafu aliyopewa.



      Msaidizi yule wa Mkuu alikerwa na bibi Nyanjige kupita kiasi kutokana na maneno yake ya dharau. Pamoja na kuelewa ukweli kuwa bibi Nyanjige ana uwezo mkubwa na ameshalisumbua sana jeshi mpaka hapo walipompata, kitendo cha kuwatambia kwamba atawamaliza kilimchefua zaidi.



      Dereva wake alisimama katika namna ya kumchunga bosi wake asichukue hatua mbaya ya mauaji. Hakuona sababu ya kumuua wakati kulikuwa na kila uwezekano wa kumchukua na kumpeleka jeshini.



      Bibi Nyanjige kama ambaye alikuwa amesoma mawazo ya Msaidizi wa Mkuu yule wa majeshi. Alimtazama kwa sura ya dharau ya hali ya juu. Nia yake ikiwa ni kumjaza hasira zaidi Mkuu huyu ili ampige risasi.



      Alikuwa radhi kufa kwa risasi, kuliko kufikishwa mbele ya wakuu wa majeshi ambao kutokana na jinsi alivyowaudhi na kuwachanganya, alijua lazima atapata mateso makubwa na mabaya sana. Njia bora aliyoiona ilikuwa ni kuendeleza bidii ya kuwaudhi wawili hawa, pengine lengo la kupigwa risasi na kufa pale pale lingekamilika na hivyo kumuepushia na sokomoko ambalo angelipata huko jeshini atakapopelekwa.



      “Nyie Manguruwe pori!.. Nasema kama wanaume kweli vifyatueni hivyo vibunduki vyenu viniue niende zangu peponi. Mbwa wakubwa nyie. Kwanza vijanaume gani vinakuwa vipumbavu-pumbavu kama hivyo.



      Mnamshikia bunduki bibi kizee kama mimi huku mnatetemeka! Niueni sasa mkione cha moto!-Washenzi wakubwa!!” Maneno haya yalimfanya Mkuu wa majeshi kukurupuka na kumnyang’anya bunduki dereva wake na kumwekea bibi Nyanjige kichwani, akataka kufyatua, dereva wake akamsukuma kidogo na kumnyang’anya bunduki.



      Risasi iliyofyatuliwa kwa mara nyingine ikachimba ardhi badala ya kichwa.

      “Kwa nini unanizuia?” Mkuu alimjia juu dereva wake ambaye aligwaya ghafla.

      “Nasema kwa nini unanizuia? Huoni maneno anayoyasema mshenzi huyu yanavyochefua? Unafikiri huyu anafaa kufikishwa jeshini-keshatia hasara ngapi? Nani ana haja ya kumuona akiwa hai?”



      Bibi Nyanjige akaingilia kati akimwita Mkuu yule ambaye alielekea kuingia kwenye mtego wa bibi Nyanjige kwa kupandwa na jazba.

      “We mwanamke!! Unamfokea mwenzako wakati nimeshakupa ruhusa ya kuniua na ...” Kabla hajaongeza neno zaidi, Msaidizi wa Mkuu wa Majeshi akatupa teke zito, likampata chini ya kidevu.

      CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

      Bibi Nyanjige akatoa mguno mkubwa wa maumivu. Akajinyonganyoga pale sakafuni huku akihisi ladha yenye chumvi ya damu kutoka kinywani mwake. Akalia kwa uchungu wa maumivu yale.

      Mkuu wa majeshi alimgeukia dereva. “Unaona.. Unaona?”



      “Sikiliza Mkuu, huyu usimuue, hebu punguza hasira na ukumbuke maagizo tuliyopewa, kwamba tumfikishe huyu akiwa hai mbele ya Wakuu.”

      “Amenitia hasira sana, hawezi kunidharau namna hii”.



      Dereva aliinama kumwangalia bibi Nyanjige kama yu hai, maana teke alilopigwa na Mkuu wake lilikuwa ni zito kiasi kwamba bibi yule alijinyonga kidogo kisha akalala kimya.



      Akagundua kwamba ameumia mno. Kwa kuchanganya na majeraha mengine aliyokuwa ameyapata kutokana na kipigo cha wamasai, Bibi Nyanjige sasa alikuwa hajiwezi. Alikuwa akivuja damu na kuvimba karibu mwili mzima, hii ilimfanya aanze kufikiria upya kuhusu namna ya kumpeleka kwa Wakuu wa Majeshi.

      “Mkuu, huyu ameumia sana, tufanyeje?”

      “Hawezi kutembea?” Mkuu ambaye alikuwa ameegemea gari na kuangalia upande mwingine, alionekana kupunguza makali ya hasira zake.



      “Nadhani, buti ulilompiga ni kubwa sana kwa mtu kama huyu, anaweza kufa kabla ya kufikishwa Makao Makuu”.

      “Unafikiria nini sasa?” Sauti ya Mkuu ilishapoa.

      “Huyu anahitaji matibabu, Mkuu”

      “Na akifia hospitali?”



      “Tusifikiri hivyo mapema, maana kama suala ni kifo anaweza kufa hata wakati tuko njiani kumpeleka Makao Makuu.”

      Mkuu aliendelea kubaki nyuma ya gari huku akili yake ikifanya kazi haraka haraka juu ya nini cha kufanya.



      Alikumbuka kwamba ni kweli walitakiwa kumfikisha mtu yule mbele ya Wakuu wa Majeshi akiwa hai na sio vinginevyo. Japokuwa bibi yule anatisha kutokana na historia za mauaji makubwa na mazito ambayo ameyafanya, lakini kumfikisha kwa wakuu akiwa amekufa, ni matusi kwa mwanajeshi mwenye cheo kama yeye. Kumpeleka mtuhumiwa tena mwanamke kizee akiwa amekufa mbele ya wakuu? Atajielezaje? Kwamba ametusumbua sana? Msumbufu mwenyewe mwanamke!!? Tena kizee? Haikumuingia akilini.



      Mwili wa bibi Nyanjige ulikuwa kama umekufa ganzi. Maumivu yalikuwa makubwa na akajikuta akianza kukata tamaa kutoka mikononi mwa watu wale. Hakujua wakati kama ule anahitaji kutumia mbinu ya namna gani kumuokoa. Suala la kufa, halikuwa na mjadala, alitambua kwamba ni lazima ndani ya siku chache zijazo atakuwa amekufa, lakini mateso atakayoyapata yatakuwa mabaya zaidi ya kifo!



      Msaidizi wa Mkuu wa Majeshi akarudi kutoka nyuma ya gari alikokuwa ameegemea akiwa tayari na suluhisho. “Hebu muingize kwenye gari”. Dereva akamtazama katika hali ya kutoelewa, lakini Mkuu alishaingia kwenye gari na kufunga mlango wake. Dereva akatekeleza hilo, alimbeba na kumwingiza kwenye kiti cha nyuma, akazunguka na kuingia kwenye kiti cha mbele, akawasha gari.

      CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

      “Wapi Mkuu?”

      “Twende Hospitali.”

      * * * * * * *

      Umati wa watu ulikuwa umejazana nje ya Hospitali ya mkoa kutaka kumwona Bibi Nyanjige, mwanamke aliyevuma nchi nzima kutokana na vitendo vya mauaji ya kushangaza. Watu walitaka kuhakikisha kwamba ni kweli mwanamke anayelisumbua jeshi la nchi ni mtu mzima kwa kiasi kinachozungumzwa?



      Wengi walihisi kwamba huenda mwanamke huyo akawa ni mtu wa makamo au kijana na sio mtu mzima sana kama inavyotangazwa kwa sababu kutokana na kiwango cha matatizo anayoyasababisha, inakuwa vigumu kuamini kwamba kikongwe kama hicho kinaweza kufanya yote hayo.



      Polisi walikuwa na kazi ya ziada kujaribu kusuma sukuma wananchi waliokuwa wakilisogelea lango la hospitali ambako Bibi Nyanjige alikuwa ameingizwa.



      Baada ya kufanikiwa kumfikisha hospitali, Msaidizi wa Mkuu wa Majeshi alijihisi kupumzika. Aliacha wamuingize kwenye chumba ambacho yeye hakufahamu ni cha nini, kisha akamgeukia daktari wa zamu.

      “Ameshazinduka?”

      “Hapana, inaelekea amepata kipigo kikubwa sana na itamchukua muda kuzinduka na.....”



      “Hebu nambie, muda gani unafikiri atakuwa ameshazinduka?”

      “Sina hakika Mheshimiwa, lakini nitajitahidi iwe haraka kama mnavyohitaji”

      Msaidizi wa Mkuu wa Majeshi akavuta pumzi za matumaini, kisha akamgeukia tena. “Nambie, atapona huyu?”

      “Siwezi kusema mapema hivyo, lakini sijaona kama ana majeraha makubwa sana, labda iwe ni ya ndani kwa ndani, hata hivyo tutafanya uchunguzi”.



      “Sikiliza, mimi nataka apone,” baada ya maagizo hayo, mkuu aligeuka akatoka nje ya jengo. Wapiga picha za magazeti na televisheni pamoja na waandishi wa habari wakamfuata kwa kasi kutaka kumhoji, lakini hakuwa tayari kuongea kwa muda ule. Akapiga simu ya upepo ofisini kuwafahamisha mambo yalivyo. Muda mfupi baadaye, kundi la wanajeshi lilifika hospitalini kuweka ulinzi mkali ili bibi Nyanjige asitoroke.

      * * * * * * * *



      Bibi Nyanjige hakuwa amezimia kweli kama ilivyoeleweka. Alikuwa na fahamu zake kamili, lakini alifanya hivyo akiamini kwamba mbinu hiyo itamsaidia katika kumfanya apate mapumziko wakati akitafakari la kufanya.

      Ukweli aliuona ni kwamba uhai wake uko hatarini kufuatia kuwekewa ulinzi mkali na wanajeshi. Aliwahi kufikiria kujiokoa kwa kuita wanyama waje pale pale hospitali na kusambaratisha madaktari na wanajeshi na yeye akapata nafasi ya kutoroka, lakini ilikuwa vigumu kwa vile kinywa chake kilitawaliwa na maumivu makubwa kufuatia buti alilopigwa na yule msaidizi wa Mkuu wa Majeshi.



      Kufikishwa mbele ya Wakuu wa Majeshi kama alivyosikia wale wanajeshi wawili wakizungumza ni kitu kilichomuumiza kichwa sana. Juu ya kukata tamaa, lakini bado alijipa moyo kwamba atapata jibu la tatizo lake kadiri maumivu yatakavyopungua.

      CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

      Siku tano baadaye.

      Ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Majenzi ya Ulinzi ulikuwa kimya kana kwamba hakukuwa na watu. Soli za viatu vya Mkuu wa Majeshi pekee ndizo zilizosikika zikigongagonga sakafu, akiizunguka meza ile kubwa ya duara katika hali ya kuonyesha kuchanganyikiwa.



      Ni kikao ambacho kilianza muda mrefu uliopita, wastani wa saa nzima, huku Mkuu wa Majeshi akifoka ukumbi mzima kutokana na operesheni ya kumshughulikia Bibi Nyanjige ilivyokwenda kizembe mpaka kumkamata tena kwa taabu kubwa.

      Ni katika kikao hicho ambapo Makamanda wote waliokuwa wakishughulikia suala la bibi Nyanjige mpaka kufikia kuuawa kwa wapiganaji walifukuzwa katika jeshi na pia kutakiwa kuchukuliwa hatua maalum za kijeshi ili iwe funzo kwa wakuu wengine ambao ni wazembe kama hao.



      Kwa muda wa dakika kumi zilizopita, Mkuu wa Majeshi alikuwa akizungumza kwa hasira mbele ya makamanda wake kutokana na uzembe uliokuwa umefanyika hata kumfanya Bibi Nyanjige kulinyanyasa jeshi na kuua wanajeshi pamoja na kufanya mambo mengine ya kishenzi huku jeshi likionekana dhahiri kushindwa kumkamata.



      “Hamko ‘serious!’ Inakuaje jeshi zima linyanyaswe na mwanamke kikongwe? Ni ujinga gani unafanyika hapa. Tumetuma wanajeshi sitini na magari kwenda Kiambali kufuatilia taarifa za kuonekana kwa bibi huyu, wanarudi watu wawili! wengine wote wameuawa na ng’ombe?



      Aibu gani hii? Ng’ombe wanafanya wapiganaji washindwe kufanya kazi yao? Ng’ombe?” Alipomaliza maneno hayo, akarudi kuketi. Kiha akaendelea kusema, “Ok, sasa tumeshamkamata Bibi Nyanjige na tunatakiwa kumuadhibu kwa adhabu ambayo itakuwa ni halali yake kwa jinsi alivyotusumbua kwa kipindi chote hiki na kutufedhehesha.” Alisema Mkuu wa Majeshi



      “Hata hivyo, kwa kuwa hali yake inaridhisha, nataka aletwe hapa sasa hivi ili tuamue la kufanya mbele yake na utekelezaji ufanyike dakika hiyo hiyo ya makubaliano”.

      Hakukuwa na wa kubisha wala kujadili chochote. Wanajeshi kadhaa waliitwa, wakapewa maagizo hayo kwamba wayatekeleze kwa muda mfupi ujao.



      Kama umeme, wanajeshi wale walivaa bunduki zao, wakachukua gari na kwenda hospitali ya mkoa kumchukua bibi Nyanjige.



      Bibi Nyanjige aliletwa pale haraka kama ilivyotakiwa. Safari hii hakuwa uchi kama alivyokutwa wakati anakamatwa. Alikuwa amevaa gauni lililoraruka-raruka ambalo alipewa bila kujua lilikotoka.

      Mkuu wa majeshi akaendelea na mazungumzo ambayo alikuwa akiyaongea kabla bibi Nyanjige hajafika pale. “Kwa hiyo kumchoma katika tanuru siamini kama kutatusaidia sisi na vizazi vyetu. Ni kweli ametuudhi zaidi, lakini tuangalieni adhabu nyingine ambazo tumezijadili hapa wakati huyu bibi hajafika.



      “ Au kumkatakata na kumwagia acid kwenye sehemu za majeraha na mateso mengine makali tuliyokuwa tumeyajadili, pia sijaafiki kwamba ni adhabu anayostahili.”

      Kutokea hapo, zilijadiliwa adhabu nyingine mbaya na za kutisha zaidi, lakini jibu halikupatikana mpaka ilipotangazwa adhabu ya kumkausha na kumweka katika jumba la makumbusho.

      CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

      “Adhabu hii ninakubaliana nayo na anastahili kabisa.” Mkuu wa Majeshi alizungumza akitabasamu baada ya kazi nzito ya kutafuta jawabu linalostahili.

      Bibi Nyanjige alishtuka! Hiyo ilikuwa ni adhabu kubwa na mbaya zaidi kutekelezwa kwake. Ingawa alijua kwamba wanajeshi wana tabia ya ukatili, lakini hakudhani kwamba adhabu ya kifo kwa kukaushwa ingepitishwa kwake.



      Alijikuta akitetemeka kwa hofu, hasa baada ya kugundua kwamba kwa mazingira yaliyomzunguka, kujiokoa kilikuwa ni kitu kisichowezekana kabisa.

      Eneo lote lilikuwa limezungukwa na wanajeshi wenye silaha nzito nzito.



      Wakati akifikiria hivyo, alishtukia ameshikwa mikono na kuvutwa kinyumenyume mpaka kwenye chumba kipana ambacho hakikuwa na dirisha zaidi ya hewa ya mtambo wa kiyoyozi.

      Moyo ulimdunda bibi Nyanjige. Alifahamu kwamba mbele ya wanajeshi, mwisho wa maisha yake umefika.



      Alifikiri kuita wanyama waje kumsaidia, lakini kutokana na ukali wa silaha zilizoko pale jeshini, alihisi kwamba hilo halitawezekana, na zaidi kuingia ndani ya chumba alichowekwa, itakuwa vigumu kwa mnyama yeyote kuingia.



      Alifungwa kitaalamu kwenye kiti maalum cha umeme ambacho kwa jinsi kilivyo madhubuti, hakuweza hata kujitikisa.Donge la hasira lilimkaba kooni.





      Chumba alichokuwamo kilifungwa na akabaki peke yake ndani. Baada ya dakika chache, wanajeshi zaidi ya 20 na wakuu wao wawili waliingia ndani ya chumba hicho, na kubamiza mlango kwa nyuma. Mlango huo ulikuwa na tundu ndogo kwa juu yenye nyavu zilizochakaa, tundu ambalo lingemwezesha mtuhumiwa anayewekwa mahabusu ndani ya chumba hiki, kuwasiliana na mlinzi yeyote endapo anapata tatizo.



      Mwanajeshi mmoja alikuwa amekamata sindano na boksi lenye chupa yenye sumu. Akaelekea upande mmoja na kuminya sindano akivuta sumu ijae ndani yake.

      Baada ya kumaliza kufanya hivyo, akamrudia bibi Nyanjige na kuinama mbele yake huku akitabasamu kuonyesha kwamba mwisho wake umefika. Akamshika mkono na kusogeza ncha ya sindano.



      Bibi Nyanjige alipagawa, ghafla akapiga mluzi mkali sana katika namna ya ufundi iliyowashtua hata wale wanajeshi. Yule aliyeshika sindano alisita. Wale wengine wakatazamana kuonyesha kutoelewa kinachoendelea. Kusita huko kulimpa mwanya bibi Nyangije kuendelea kupiga uruzi wake wa ajabu.



      Ghafla, kundi la kutisha la nyuki lilipenya kwenye kidirisha kidogo cha mlangoni, likaingia ndani ya chumba na kuwavamia wale wanajeshi. Bibi Nyanjige aliendelea kupiga uruzi na wale nyuki hawakumgusa. Wanajeshi walijaribu kufungua mlango na kukimbia nje, ikashindikana kwani nyuki walitawala chumba kizima. Pamoja na ujasiri wa kijeshi, lakini walijikuta wakilia na kupiga mayowe. Haikusaidia, nyuki walizidi kujaa ndani na kuwashambulia. Vishindo vya kuwakwepa nyuki na kuchanganyikiwa, vilikuwa vikubwa kupita kiasi.



      Dakika tano baadaye, wanajeshi wote 20 walikuwa wameshakufa

      CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



      Baada ya lile kundi la nyuki kutoka humo chumbani, ndipo Bibi Nyanjige alipogundua kwamba nyuma ya kiti alichofungwa, kuna swichi ya kuwasha au kuzima kiti kile. Kwa kutumia mguu wake mmoja, aliigusa swichi ile, na hapo, kamba maalum zilizofungwa sambamba na kiti cha umeme zikaachia.



      Hakuchelewa, akajitoa kwenye kamba na kumvua nguo mmoja wa wale wakuu wawili waliokuwa wameingia mle ndani, akavaa yeye pamoja na miwani! Akaufungua mlango kisha akatoka nje.



      Wanajeshi wote walipomwona wakampigia saluti. Akaenda mpaka yalipoegeshwa magari, akachagua mojawapo, akachomeka funguo na kuliwasha. Akaliondoa taratibu huku wanajeshi wakiendelea kumpigia saluti kwenye kila kizuizi alikopita!!



      Bibi Nyanjige akarudi kuelekea Morogoro. Akapita Chalinze na masaa kadhaa baadaye, akawa ameshaingia kwenye mbuga za wanyama za Mikumi.

      Hapo akaliacha gari na kuingia kwenye msitu mzito.



      Ni huko alikoamua kuwa ndiko kutakuwa kambi yake wakati akiunda jeshi la aina yake litakaloshirikisha wanyama wote kwa mpango kwamba baada ya miaka mitano arejee kufanya shambulio zito la kuivamia nchi.



      NI kama machale yalimcheza bibi Nyanjige kwani wakati bomu likilipuka hakuwa eneo hilo wanyama wake wawili walikuwa wakichimba chini kwa kasi kuelekea upande wa pili moshi wa bomu ulimfikia hadi mahali alipokuwa lakini alizidi kutambaa akiwafuata chimbachimba wake kwa nyuma , kasi yao ya kuchimba ardhini hata yeye mwenyewe ilimshangaza .



      Walipokuwa wamekwenda kama umbali wa mita ishirini chimbachimba walianza kuchimba kuelekea juu kwa amri ya bibi Nyanjige , udongo ukawa ukiporomoka kumfunika lakini bado alipenyenya katikati ya udongo huo na kulipanda … taratibu kuelekea juu ya ardhi.



      Alikuwa amechoka taabani na hakujua nini cha kufanya ghafla alishtukia minong’ono ya watu ikija nyuma yake ! Alipogeuza kichwa kuangalia nyuma aliwaona maaskari wasiopungua ishirini wakiwa na bunduki aina ya SMG mikononi mwao na wote walipiga kelele wakimuamuru atulie vinginevyo wangemuua kwa risasi .



      Tulia hapo hapo ulipo vinginevyo tutakumaliza umetusumbua kwa muda mrefu sana leo mwisho wako umefika !’’

      Hilo hata mimi nalifahamu na ninaomba mniue haraka iwezekanavyo nimechoka kukimbia , lakini hata hivyo niliyowafanyia yanatosha kuwa kisasi kwa waliomuua mama yangu !’’



      Wanajeshi wote walibaki … kwa mshangao kusikia baba Nyangije aliua watu wengi kiasi hicho kwa kisasi cha mtu mmoja ilikuwa siyo rahisi kwao kuamini kuwa hatimaye bibi Nyanjige walikuwa wamemtia mikononi mwao .

      Leo hakuna ujanja ni lazima ufe tu!’’ Hilo ninalolitaka mimi !’

      CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

      Hebu lifanyeni haraka basi!” Hasira ilizidi kuwapanda wanajeshi na wote kwa walijikuta wakiziandaa bunduki zao tayari kwa mashambulizi , hawakutaka kupoteza muda zaidi walichotaka ni kung’oa roho ya bibi Nyanjige mtu aliyewahangaisha kwa muda mrefu .

      Jamani hebu sikilizeni !”



      mmoja wa wanajeshi alisema Tusikilize nini ?” wote waligeuka na kumuuliza

      Ni vema tukafuata maagizo ya mkuu majeshi kuwa tukimkamata hai tumpeleke kwake akiwa hai “

      Haiwezekani kwani huko nyuma tulikwishafanya hivyo akatoroka ! Leo kosa hilo halifanyiki ni lazima tuulie mbali”



      Yalitokea mabishano kidogo baadhi ya wanajeshi wakisema haikuwa sahihi kumuua bibi Nyanjige , wengi walikubali kumbeba na kumpeleka moja kwa moja hadi makao makuu ya jeshi jijini Dar es salaam ambako mkuu wa majeshi angeamua kitu cha kumfanyia bibi huyo hatari na machachari aliyetingisha jeshi .



      Kwa kauli moja wanajeshi wote walikubaliana juu ya kumsafirisha bibi Nyanjige akafungwa kwa kamba mikono na miguu yake pamoja , kipande cha mti kilipitishwa katikati ya mikono na miguu yake na wanajeshi walimbeba kwa kutumia mti huo kama mzega wa maji au mnyamapori na kutembea naye moja kwa moja hadi barabarani walikoacha magari yao.



      “ Jamani hivi kweli mmeshindwa kuniua mpaka mnipeleke kwa huyo mkuu wenu ?” “ Wee kitimoto kaa kimya na ufunge kabisa hilo domo lako !” “Yaani unaniita mimi kitimoto ? Kijana umechoka kuishi siyo ? Nguruwe mkubwa wee! Bibi Nyanjige alifoka aliwatukana sana wanajeshi lengo lake likiwa ni kuwatia hasira ili wamshambulie kwa risasi afe kifo cha mara moja ! Alijua wazi mateso yaliyokuwa mbele yake talikuwa makubwa na hakutaka kukutana nayo .



      Wewe hata utukane matusi gani Dar es salaam lazima ufike tu na kwa taarifa yako unakwenda kukaushwa na kutunzwa katika makumbusho ya taifa ili hata wajukuu zetu waje kuelewa ulikuwa mtu hatari kiasi gani !”

      Aisee kwa hiyo nitakuwa mtu maarufu kama V.L Lenin au Mao siyo ? Hicho ndito nilichotaka , siku zote niliota kuwa maarufu na kweli nimekuwa Hureeeeeeee!”



      Bibi Nyanjige alicheka na kushangilia kw dharau .

      Aliyoyafanya yote yalizidi kuwachefua wanajeshi lakini kwa sababu walishagundua nia yake walizidi kumvumilia na kumpakia ndani ya gari , mawasiliano kati ya vikosi vyote yalifanyika magari yalikusanywa na msafara wa kurudi Dar es salaam ulianza mara moja . Ilikuwa furaha kubwa mno kwa wanajeshi kumpata mtu aliyehangaisha nchi



      Msafara uliingia jijini Dar es salaam masaa sita baadaye na kwenda moja moja hadi makao makuu ambako mbiu ilipigwa wanajeshi wote wakakusanyika na bibi Nyanjige kukabidhiwa kwa mkuu wa majeshi .



      Nawapongezeni sana kwa kumkamata bibi huyu lakini napenda kuwaeleza kuwa suala hili hivi sasa halikuwa mikononi mwetu tena inabidi tulipeleke mikononi mwa sheria , pigeni simu polisi waje wamchukue ni lazima ashtakiwe kwa mauaji mshenzi mkubwa huyu” Alifoka mkuu wa majeshi .

      CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

      Simu ilipigwa na dakika ishirini baadaye polisi walifika na kumchukua bibi Nyanjige moja kwa moja hadi kituo cha polisi ambako alitoa maelezo kisha kutupwa mahabusu !” muda wote alichekelea wala hakuonyesha kuwa na wasiwsi wowote . jambo hilo liliwashangaza watu wengi sana ukilinganisha na kosa la mauaji ya halaiki alilokuwa akishtakiwa nalo .



      Siku mbili baadae alichukuliwa na kupelekwa gerezani keko ambako aliendelea kusota wakati polisi wakiendelea kukamilisha upelelezi wao , kila mwezi alipelekwa mahakamani mara moja ambako alisomewa shitaka la mauaji na kurudishwa tena mahabusu ! kila siku ya kesi yake idadi kubwa ya watu walijaa mahakamani lengo lao ikiwa ni kumuona bibi Nyanjigebibi aliyeushangaza ulimwengu kesi yake iliwavutia watu wengi sana jijini Dar es salaam.



      Polisi walijitahidi kukusanya kila aina ya ushahidi ili kumtia hatiani bibi Nyanjige lakini walishindwa kuupata ushahidi kwa sababu ilikuwa si rahisi kuthibitisha mbele ya mahakama kuwa ni yeye aliyewaamuru wanyama na wadudu kuwashambulia wanajeshi na kuwaua . kesi pekee iliyoonekena kuwa na nguvu ni ya mauaji ya watu karibu mia na hamsini waliokunywa maji kisima ambamo bibi Nyanjige angeweza kushinda katika kesi zote ingawa ni kweli alifanya mauaji kwa kuwaamrisha wanyama .



      Ni kutokuwepo kwa ushahidi wa kutosha ndiko kulifanya bibi Nyanjige asote mahabusu kwa karibu miezi therasini na sita ! Mwezi therasini na saba ulipoingia ghafla alianza kuugua ugonjwa wa ngozi , kikohozi na homa kali ! Walijaribu kumtibu katika hospitali iliyokuwepo gerezani bila mafanikio yoyote hali yake ilizidi kuwa mbaya hata mahakamani wakawa hawampeleki .



      Miezi miwili baada ya kuugua hali yake ilikuwa mbaya zaidi homa ilizidi kupanda madaktari walifikiri homa ya matumbo lakini hata walipompa dawa za ugonjwa huo bado hazikumsaidia ! Alizidi kuzidiwa ndipo walipoamua kumpeleka hospitali ya Tifa ya Muhimbili ambako alipikelewa na kulazwa .



      Alipofanyiwa vipimo aligundulika kuwa na kimeta alioupata sababu ya kuishi na wanyama porini kwa muda mrefu , alipewa dawa za ugonjwa huo ambazo alizitumia kwa muda wa mwezi mzima lakini bado hali yake haikutengemaa , homa ilizidi kuendelea kuwepo ! Madaktari walizidi kuchanganyikiwa na kushindwa juelewa ni nini kingefenyika kumsaidia .



      Kikohozi kilizidi kupamba moto , alikohoa usaha nyakati za usiku pia alitoka jasho jingi mwilini . Alipoteza sehemu kubwa ya uzito wa mwili wake hilo lilifanya madaktari wafikirie kifua kikuu na kuamua kumpima makohozi ! .



      Majibu yalipotoka yalionyesha kweli alikuwa na ugonjwa wa kifua kikuu na kulazimu aanzishwe matibabu ! lakini hata baada ya matibabu ! ya kifua kikuu kumalizika bado hali yake ilikuwa mbaya mno! Hakuwa hata na uwezo wa kunyanyuka kitandani ambako halilala akiwa amepigwa pingu yake mikono .



      ‘Jamani tu mtibu vipi huyu bibi? ”

      “Hata mim nashindwa kuelewa kila dawa tumeshampa lakini bado haisaidii !” “Sasa tufanye nini?

      “Hivi ESR yake ilikuwa ngapi ?” “Mara ya mwisho ilikuwa sitini !”

      "sitini?" "Ndiyo!"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

      Hiyo iko juu sana na inaonyesha wazi kuna tatizo ! unaonaje tungempima Elisa test uone kama ana ukimwi maana dalili zote ni za ukimwi !” Nakuunga mkono daktari yalikuwa ni maongezi kati ya madaktari wawili waliomshughulikia bibi Nyanjige kwa karibu zaidi walifikia uamuzi huo na siku iliyofuata alicchukuliwa damu kwa ajiri ya kipimo cha ukimwi !



      Hakuna aliyekuwa tayari kuamini majibu yalipotoka kuwa bibi Nyanjige alikuwa na virusi vya ukimwi vilivyokuwa vikitishia uhai wake .

      Niliupata wapi jamani ugonjwa huu ? Bibi Nyanjige alijiuliza baada ya daktari aliyekuwa akimpa ushauri nasaha kumueleza wazi juu ya afya yake alishindwa kuelewa lakini alipotuliza akili vizuri aligundua ni wapi aliupata ugonjwa huo.



      Ni siku ile ya ajali ya basi nakumbuka kuna damu ya majeruhi niliyekuwa nikimvuta magwanda ya jeshi na kumvalisha nguo zangu iligusa kwenye kidonda changu nafikiri ni siku hiyo nilipoambukizwa ! Aliwaza bibi Nyanjige .

      Mwisho wa maisha yake aliuona u karibu kupita kiasi alijua wakati wowote ule angeweza kuaga dunia ! Kila alipofikiria roho za watu waliokufa kwa sababu yake aliogopa sababu yake alijua wazi hukumu kubwa ilikuwa ikimsubiri .



      Eee Mungu nisamehe shetani alinidanganya nikaua watu wasio na hatia ! alilia bibi Nyanjige kwa uchungu.

      Septemba 23 1998 ushahidi wote ulikamilika , ilidhibitika wazi mbele ya mahakama kuwa bibi Nyanjige alitia sumu kisimani na kuwaua wananchi 150 wa kijiji cha Usagara mkoani Mwanza !



      Ingawa hapakuwa na ushahidi wa kutosha juu ya wanajeshi zaidi ya 7000 waliokufa nchini Congo na katika mbuga ya wanyama Mikumi baada ya kushambuliwa na wanyama jaji alimtia bibi Nyanjige hatiani .



      Kitanda chake kilizungukwa na watu wapatao kumi , kati yao alikuwepo jaji maarufu jijini Dar es salaam kwa kutoa hukumu za vifo , alikuwa jaji mwanamke asiye na huruma hata kidogo naalikuwa miongoni mwa watu waliochukizwa sana na kitendo alichofanya bibi Nyanjige .



      Huyu alikuwa jaji Angela Ngaiza ilikuwa ni siku ya hukumu ya bibi Nyanjige ingawa alionekana kuwa katiak hatua za mwisho kabisa za uhai wake , alikuwa amekonda mno na aliangalia macho yake huku na kule bila matumaini .



      Nyanjiige !” jaji aliita “Na..am mhe .shi..miwa jaji ” aliitika bibi Nyanjige kwa taabu.

      Mahakama inakutia hatiani kwa kosa la mauaji ya watu 150 waliokufa baada ya wewe kuweka sumu kwenye kisima cha maji huko Usagara ushahidi uliopatikana kutoka kwa wwatu mbalimbali akiwemo mtu aliyenunua sumu hiyo kutoka dukani kwake na majibu ya vipimo vya maji ya kisima uliofanywa na madaktari uonanyesha wazi ulifanya mauaji hayo na kwa sababu hiyo basi kabla ya kukuhukumu naomba ujitete !



      Hakimu alisema akimwangalia kitandani .

      Sina la kujitetea !” Kwa sababu hiyo ninakuhukumu kifo cha kunyongwa !” Jaji alisema bila ya huruma

      Jaji naomba nikukumbushe kitu kimoja kuwa huwezi kuhukumu maiti !

      Huwezi kuhukumu mtu aliyekufa tayari !

      CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

      Mimi ni kama mait….! Bibi Nyanjige hajamalizia sentesi yake , shingo yake ikaanguka pembeni na hasema kitu tena ! Daktari alipompima aliguandua tayari alishaaga dunia .

      Afadhali !” Jaji alisema kwa sauti ya chini



      Mwisho.... Asanteni kwa kufatilia simulizi hii ya kusisimua



0 comments:

Post a Comment

Blog