Search This Blog

Thursday, July 21, 2022

LAITI NINGEJUA - 5

 







    Simulizi : Laiti Ningejua

    Sehemu Ya Tano (5)



    ILIPOISHIA...

    Nilikosa amani kabisa nikawaza labda ni mambo ya kwa sangoma ndio yalikuwa yamemchachia na kuwa chanzo cha yeye kuangua kilio kikubwa namna ile. Zilikuwa ni hisia zangu ambazo hazikuweza kuthibitika kwasababu mlengwa alishindwa kunieleza kwa kinywa chake na kunifanya nibaki njia panda bila kujua cha kufanya.



    ENDELEA...

    Baada ya dakika tano mlio wa ujumbe mfupi wa maandishi ulisikika katika simu yangu na kunifanya nichukue simu yangu ili niweze kuusoma. Ghafla joto la mwili lilianza kupanda kwa kasi mfano wa mtu mwenye homa kali kutokana na mshtuko mkubwa nilioupata baada ya kusoma meseji iliyokuwa imetumwa na rafiki yangu kunijulisha kwamba mume wake amemrudisha yumbani kwa wazazi wake baada ya kufanikiwa kuiona hirizi aliyokuwa ameificha chumbani mwake. Nilitaka kufahamu vizuri jinsi tukio lilivyotokea kwahiyo nilimpigia simu ili nijaribu kuzungumza nae kwa utaratibu sana ili aweze kunifafanulia tukio zima na kwa bahati nzuri aliweza kuzungumza na mimi japo kwa taabu sana kwasababu bado alikuwa akilia.

    “Pole mwaya.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    “Asante.”

    “Ila unaonaje kesho tukirudi kwa mganga Mbengwa kwenda kumweleza kuhusu tatizo lako pengine anaweza akapata njia ya kukusaidia.”

    “Kiukweli Teddy mimi naona bora nife tu kwasababu sioni maana ya kuendelea kuishi katika dunia hii ambayo kila mtu atakuwa akininyooshea kidole. Nimefedheheka sana pale niliposhuhudia ndugu jamaa na marafiki wakifika pale nyumbani kwangu kushuhudia ile hirizi niliyokuwa nimeitoa kwa sangoma. Watu walishikwa na butwaa kwasababu hawakuamini kwamba binti mdogo kama mimi naweza kujihusisha na masuala ya kishirikina.

    “Achana na fikira potofu za kutaka kujiua kwasababu matatizo tumeumbiwa binadamu kwahiyo hatuna budi kukabiliana nayo.”

    “Huo ndio msimamo wangu.” Simu ilikatika na nilipojaribu kumtafuta kwa mara nyingine hakupatikana. Nilibaki nikiwa sielewi cha kufanya huku moyo ukinienda kasi mfano wa kibaka alienusurika kutiwa kiberiti na wananchi wenye hasira kali.

    Japokuwa nilikuwa nahisi njaa lakini chakula kilipoiva nilishindwa kabisa kula. Mume wangu alinisisitiza sana nile japo kidogo lakini nilimuongopea kwamba najihisi kuchoka sana kwahiyo nitakua kesho yake asubuhi. Hivyo basi nilikwenda chumbani kwangu kulala lakini niliishia kujigeuzageuza kitandani mithili ya nyoka anaeshambuliwa na siafu kwasababu usingizi uligoma kabisa kunijia kutokana na wimbi la mawazo lililokuwa likigubika kichwa changu.

    “Sasa Glory akijiua itakuaje?” hilo ni swali ambalo lilizunguka sana akilini mwangu usiku kucha bila kufahamu matokeo yatakuwaje. Palipokucha asubuhi baada ya mume wangu kuelekea kazini nilifunga safari kuelekea nyumbani kwa kina Glory kwenda kuzungumza nae kwasababu jana yake hakuwa vizuri kutokana na tukio lililokuwa limemtokea. Baada ya dakika 25 niliegesha gari langu nje ya nyumba yao ingawa palionekana kama hapakuwa na mtu yeyote kwa wakati ule kwani mlango ulikuwa umefungwa. Nilipiga honi mara kadhaa lakini hakutokea mtu yeyote na kibaya zaidi simu yake haikuwa hewani kwahiyo akili yangu ilikuwa inachacharika kuwaza cha kufanya ili niweze kufahamu pa kumpata shosti yangu. Mara baada ya kushuka kwenye gari ili niweze kwenda kwa jirani kutafuta msaada ghafla nilipata faraja baada ya kumuona mama yake akiwa amejitanda kanga huku mkononi mwake akiwa ameshika kikapu kidogo cha plastiki ndani yake kukiwa na chupa ya chai pamoja na hotpot yaa chakula. Nilishtuka kwa kuwaza alikuwa ametokea wapi kwasababu ule muonekano ni wa kama mtu alietoka hospitali kumjulia mgonjwa hali.

    ***

    “Shkamoo mama.”

    “Marahaba Teddy hujambo.”

    “Sijambo.”

    “Vipi habari za hapa.”

    “Za hapa sio njema hata kidogo, rafiki yako yupo hoi mahututi hospitali anapumulia mashine.”

    “Yalaah! Kakumbwa na nini?”

    “Kanywa sumu jana usiku.”

    “Masikini rafiki yangu mie.” Nilizungumza huku machozi yakinilengalenga kwasababu alishanieleza dhamira yake ya kutaka kujitoa uhai kisa fedhea aliyokuwa ameipata.

    “Ndio hivyo yani tumuombe tu Mungu kwasababu kama sio wa leo basi ni wa kesho.” Roho iliniuma sana baada ya kusikia maneno ya mama yake alieonekana kukata tamaa kutokana na hali ya binti yake hospitali.

    “Lakini Teddy wewe ni miongoni mwa marafiki wakubwa wa mwanangu hivi ni kweli shutuma za mume wake zinauhalisia ndani yake? Kwasababu hadi sasa nahisi kama naota kwasababu siamini kabisa kilichotokea.”

    “Sidhani kama ni kweli kwavile hajawahi kunishirikisha katika suala nyeti kama hili.” Ilinibidi nizungumze kauli ya kumsaliti rafiki yangu ingawa nilikuwa nafahamu kila kitu kuhusiana na hirizi iliyozua kizaazaa.

    Nilimuaga mama Glory na kwenda hospitali alipokuwa amelazwa rafiki yangu angalau nikashuhudie hali yake ambayo niliambiwa kuwa ilikuwa ni ya kutisha. Nilifika katika hospitali ya Mount Meru jiji arusha ambapo ndipo alikuwa amelazwa mgonjwa wangu. Nilikutana ndugu zake Glory wamekaa kwenye benchi nje ya wodi wakisubiri kupewa taharifa ya hali ya mgonjwa wao ambae alikuwa akihudumiwa na jopo la madaktari. Niliungana nao kwa kukaa kwenye lile benchi lililokuwa kwenye korido kusubiri taarifa kutoka kwa daktari kutujuza kuhusu maendeleo ya mgonjwa.

    Nusu saa baadae daktari mmoja aliekuwa akipigania uhai wa Glory alitoka nje ya wodi na kutukuta tumekaa tunasubiri taharifa ya hali ya mgonjwa wetu. Alimshika mkono baba mkubwa wa Glory na kusogea nae pembeni jambo ambalo lilitutia woga na wasiwasi mkubwa mno. Daktari alizungumza na mzee yule kwa sauti ya chini, macho yetu yote yalikuwa yakiwatazama kwa makini sana ili tuweze kufahamu walichokuwa wakikizungumza lakini hatukufanikiwa kubaini. Baada ya maongezi yao baba yule alirudi pale tulipokuwepo na kutujuza kwamba mgonjwa wetu kafariki dunia kwahiyo turudi nyumbani tukapange mipango ya mazishi. Watu wote tuliokuwepo pale tulianza kudondokwa na machozi kutokana na hisia kali za kupotelewa na ndugu yetu kipenzi. Nililia sana kwa kumpoteza rafiki yangu kipenzi ambae ndie aliekuwa mshauri wangu wa karibu na pia ndie rafiki yangu ambae tulikuwa tunatunziana siri zetu nyeti.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Mwili uliishiwa nguvu kutokana na mshtuko nilioupata baada ya kupewa taharifa ya kifo cha rafiki yangu wa karibu, nilitamani niwe usingizini naota lakini haikuwezekana kwasababu ilikuwa ni mubaashara kabisa bila chenga. Nililia sana huku moyoni nikijilaumu sana kwanini nilikubali kujifunga katika jela ya mambo ya kishirikina ambayo ni rahisi kuingia ila ni mtiti kutoka.

    Nilirudi nyumbani kwangu nikiwa nimenyong’onyea, macho yakiwa yamenivimba kutokana na kulia sana. Njiani niliwaza mambo mengi mno lakini sikupata jibu kuhusiana na ile hirizi niliyoificha chumbani kwangu kwamba nikaichome au nikaitupe. Nilipofika nyumbani nilimweleza mume wangu taharifa ya msiba na alisikitika sana kwasababu alikuwa anamfahamu vizuri Glory kwasababu alikuwa anakuja mara kwa mara pale nyumbani.

    Alipohoji chanzo cha kifo chake nilimdanganya kwamba amejiua kutokana na fedhea aliyoipata ya mume wake kumshutumu kuwa ni mshirikina. Moyo wangu ulizidi kujiganda kwa Fadhili kwasababu alikuwa karibu sana na mimi kunifariji kipindi nilipokuwa katika wakati mgumu wa kupotelewa na rafiki ambae alikuwa ni kama ndugu yangu.

    Siku ya nne baada ya roho ya Glory kutoweka katika uso wa dunia nilijumuika na halaiki ya watu waliojitokeza kutoka katika kona mbalimbali kuhudhuria kwenye mazishi. Taratibu za kuaga mwili uliendelea na hatimae tulikwenda makaburini kuupumzisha mwili wa marehemu katika nyumba yake ya milele. Katika hali ya kutokutegemea wala kutarajia nilishikwa na butwaa baada ya macho yangu kutua katika uso wa Derick mtu ambae nilikuwa nimepotezana nae kwa muda mrefu angali moyo wangu ulikuwa bado unamuhitaji kutokana na umuhimu wake maishani mwangu kwani yeye ndio chanzo cha kurejea kwa amani katika ndoa yangu kipindi nilipopitia katika misukosuko ya kutokushika ujauzito. Japokuwa moyoni mwangu kulikuwa na giza totoro la huzuni palianza kupambazuka mara baada ya kumuona baba halali wa mwanangu Sweetness.

    Shughuli ya maziko iliendelea huku macho yangu pamoja na akili yangu nikiwa nimeelekeza kwa mwanaume yule kusudi asiweze kuondoka bila kuonana nae kwavile yeye hakuwa ameniona. Nilitamani ningekuwa na namba zake niweze kumtumia meseji kumtaharifu asiondoke bila kuonana na mimi lakini kwa bahati mbaya namba zake nilifutaga kipindi fulani niliokuwa nikipiga halafu inapokelewa na mwanamke ambae alijitambulisha kwangu kama mke wake. Mara baada ya mazishi nilimfuata kwenda kusalimiana nae kwasababu moyo wangu ulikuwa na shauku sana ya kutaka kuzungumza nae kwavile nilikuwa nimemmisi kwa kitambo kirefu sana. Nilifika hadi sehemu aliyokuwa amesimama bila kuniona kwasababu macho yake alikuwa ameyaelekeza upande mwingine akipiga stori na watu wengine waliokuwa wamehudhuria msibani. Nilimgusa begani mara mbili ndipo aligeuka na kukutana uso kwa uso na mimi jambo ambalo lilifanya tukumbatiane kwa furaha sana hadi machozi yakaanza kunidondoka.

    ***

    “Habari za siku nyingi Teddy.” Derick alizungumza huku akinifuta machozi yaliyokuwa yakitiririka mashavuni mwangu kutokana na hisia kali zilizokuwa zimenipanda baada ya kukumbuka mambo kadha wa kadha niliyokuwa nimepitia nae maishani.

    “Safi tu vipi za kupotea.”

    “Salama kabisa.”

    “Yani nimekumiss balaa.”

    “Halikadhalika kwangu mimi nimekumisi vilevile.”

    Tulisogea kando kidogo ambapo tuliridhika kwamba tutakachokuwa tunakizungumza hakitaweza kuwafikia watu wengine. Tulianza kuzungumza mawili matatu wakati shughuli ya kuvunja matanga ikiendelea. Hakika sikuamini kabisa kama nilikuwa nazungumza na mwanaume yule kwa wakati ule kwasababu alikuwa tayari ameshapotea katika akili yangu baada ya kukata tamaa kwamba sintampata tena maishani mwangu.

    “Aisee pole sana kwa msiba kwasababu najua wewe ni miongoni mwa watu walioguswa sana na msiba huu kwavile alikuwa ni rafiki yako mkubwa kipindi ulipokuwa shule. Nakumbuka pia wakati mwingine nilikuwa namtuma akuletee barua za mapenzi nilizokuwa nakuandikia.”

    “Nashukuru sana, pole na kwako pia.”

    “Asante.”

    “Mbele yake nyuma yetu jina la Bwana lihimidiwe.”

    “Amen.”

    “Vipi umekuja lini Arusha?”

    “Leo nina siku ya tatu tangu nije.”

    “Karibu sana.”

    “Nimeshakaribia.”

    “Utakuwepo kwa muda gani?”

    “Nipo likizo kwahiyo nitaendelea kuwepo kwa takribani mwezi mmoja kwasababu ninamuda mrefu sana sijaja kuwasalimu wazee wangu.” Nilifurahi sana baada ya kusikia kwamba Derick ataendelea kuwepo Arusha kwa huo muda kwasababu na mimi pia nilikuwa nahitaji kuendelea kumtia machoni kwavile ni kitambo kirefu sana nimepotezana nae bila hata mawasiliano ya kwa mwaka mara moja.

    ***

    “Vipi hajambo Sweetness?”

    “Hajambo kabisa ingawa ameshapata wenzie ambao ni Dylan, Logan na Jordan.”

    “Hongera sana.”

    “Asante.”

    Nami pia nilijaribu kumuuliza habari za familia yake lakini aligoma na kunitaka tutafute siku nyingine na pahala pengine ili tuweze kuzungumza juu ya jambo lile. Tuliendelea kuzungumza mambo mbalimbali ya kimaisha pamoja na changamoto kadha wa kadha tunazokumbana nazo katika utafutaji wa mkate wa kila siku. Kwa muda mfupi niliokaa nae niliinjoi sana kutokana na ucheshi wake kwani kwa kiasi kikubwa alifanikiwa kunipunguzia upweke mkubwa ulikuwa umenijaa ndani ya mtima wangu. Tuliongea mengi sana pia tulikubaliana kukutana siku za usoni kwaajili ya maongezi zaidi na zaidi kwavile pale hatukuwa katika mazingira mazuri ya kuzungumza mambo mengi hivyo basi tulibadilishana namba za simu na hatimae tuliagana kila moja akaelekea nyumbani.

    Furaha niliyoipata baada ya kukutana na mwanaume yule ilidhihirisha kwamba mbado alikuwa ni mtu mwenye umuhimu mkubwa sana maishani mwangu. Fikra zangu zilinasa kwake na kuthubutu kukiri kwamba kumbe nilikuwa najidanganya kwamba nafasi yake ilikuwa imezibwa na Fadhili na kumbe sio kweli kutokana na kwamba nafasi ya mlinzi moyoni mwangu aliporomoka kama chati za nyimbo redioni. Nilitamani kwa ule muda ambao yupo likizo angenionjesha yale mambo yake mazuri ya kitandani kwasababu alikuwa na upekee fulani pindi tuwapo faragha.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Siku iliyofuata tulianza kuwasiliana kwa njia ya simu ambapo tulipanga kukutana baada ya siku moja kutokana na kwamba kila mmoja alionyesha kuhitaji wa kuwa karibu na mwenzie. Siku ya miadi ilifika ambapo tulikutana katika loji inayojulikana kwa jina la Moivaro Lodge iliyopo jirani na nyumbani kwao. Nyuso zetu zilitawaliwa na furaha sana baada ya kukutana katika loji ile ambayo ina mazingira mazuri iliyotawaliwa na utajiri mkubwa wa miti inayotoa hewa safi pamoja na sauti za ndege mbalimbali ambao nao pia walijitokeza kufurahia uzuri wa mazingira ya loji ile yenye mvuto wa kipekee.

    Derick aliniomba achukue chumba ili tukakumbushiane kidogo mapenzi motomoto tuliyokuwa tukipeanaga zamani. Nilimruhusu achukue kwasababu nilijua tayari alikuwa ameshanitamani kwajinsi alivyokuwa ananitazama utafikiri ngedere alievimbiwa na ndizi kwani ni dhahiri kwamba nilikuwa na mvuto wa hali ya juu kutokana na matunzo ya gharama niliyokuwa nikipewa na mume wangu lakini yote tisa kumi hiyo siku nilivaa kimini ambacho kilikuwa ni kifupi mno na kusababisha mapaja yangu yote yawe wazi yakicheza na akili za wanaume.

    Nilivaa hivyo makusudi ili niweze kufanikiwa kumshawishi Derick aweze kunitamani na hatimae tufanye mapenzi kwasababu bado nilikuwa nampenda na pia huwa nahisi msisimko mkali pale ninapokumbuka ile mikunjo aliyokuwa akinikuja kitandani kipindi nilipokuwa nimefukuzwa kwa mume wangu kwasababu nilichelewa kushika ujauzito. Nilitamani nionje tena ile raha kwasababu nilikuwa nimeipoteza kwa muda mrefu sana. Tuliingia chumbani na baada ya muda mfupi tulizama katika mahaba ya kukata na shoka. Mitindo mbalimbali aliyokuwa akiniweka ilinifanya nisisimke mwili mzima kwa utamu niliokuwa nikiupata na kufanya nione yale mapenzi niliyokuwa nikipewa na Fadhili ni cha mtoto.

    ***

    Mapenzi niliyokuwa nayapata kwake yalikuwa ni ya daraja la kwanza kwani kwa raha niliyokuwa naipata nilikuwa najihisi kama nina paa angani kwavile alinikuna nikakunika hadi kiherehere chote kiliniisha. Jasho lilitutoka huku tukihema juu juu utafikiri tulikuwa tumekabwa na jinamizi. Mchezo ulimalizika nimechoka nyang’anyang’a sijiwezi kutokana na mikunjo niliyokuwa nakunjwa ili kitumbuwa kiweze kuliwa kisawasawa. Pamoja na kwamba hatukuonana kwa miaka mingi lakini hakuna hata mmoja aliekumbuka kondomu kutokana na midadi tuliyokuwa nayo.

    “Derick asante sana kwa mapenzi yako matamu, yani umenipa hadi nimetosheka kabisa.” nilizungumza wakati kichwa changu nimekilaza juu ya kifua chake huku nikisikilizia mapigo ya moyo wake yaliyokuwa yakimwenda kasi kutokana na shughuli nzito aliyokuwa amemaliza kuifanya.

    “Asante pia.”

    “Hivi ile video ulioyoirekodi kipindi kile bado ipo?” nilikumbuka kumuuliza baada ya kuona anapiga selfi kwa kutumia simu yake wakati tulipokuwa uchi pale kitandani.

    “Yeah ipo kwenye laptop yangu tena uwezi amini huwa naiangalia mara kwa mara na kunifanya nikukumbuke haswa mpenzi wangu.

    “Poa ila naomba uwe makini isivuje kwasababu tutazua kali ya mwaka.”

    “Usijali baby nipo makini sana.”

    “Mpenzi naomba nikuulize jambo?”

    “Uliza tu dia.”

    “Mkeo yupo wapi na pia unawatoto wangapi hadi hivi sasa.”

    “Mke wangu yupo Dare s salaam ambapo ndipo makazi yangu yalipo, kuhusu suala la watoto bado Mwenyezi Mungu hajanibariki.”

    “Unamaana gani kusema hujabarikiwa.”

    “Tumehangaika kila mahali hospitali na kwa waganga, tukadiriki kwenda mpaka nchini South Africa pamoja na India kwaajili ya kutafuta tiba ya mke wangu ili aweze kushika ujauzito lakini imeshindikana. Hali hii imenitesa na kuniumiza kwa muda mrefu na ndio chanzo cha mimi kuwa mbali na wazazi wangu kwa miaka mingi kukwepa kero zao za kuhitaji mjukuu. Ndugu jamaa na marafiki wote nimeamua kupotezana nao kwa makusudi ili wasiweze kunishawishi nimwacha mke wangu kutokana na tatizo alilonalo kwasababu nampenda kupita kawaida.” Derick alizungumza kwa masikitiko makubwa sana hadi nikamuonea huruma.

    “Pole sana Derick, Endelea kumuomba Mungu kwani ipo siku atatenda muujiza ndani ya maisha yako.” Nilizungumza kwa kauli ya kumtia moyo ili asikate tamaa katika harakati zake za kumtafutia mpenzi wake tiba.



    “Ahsante sana mpenzi kwa kunitia moyo kwasababu watu wengine niliojaribu kuwashirikisha juu ya suala hili walionyesha kulipokea kwa namna tofauti kwa kudiriki kunikatisha tamaa na kuniona mjinga kuendelea kuishi na mwanamke asiezaa. Ila kama nilivyoapa kanisani mbele ya Mungu na washarika kwamba nitampenda na kumjali kwenye shida na raha basi ndivyo ambavyo najitahidi kuilinda ahadi ile ambayo niliitamka mwenyewe kwa ridhaa yangu huku watu wakipiga makofi na vigelegele.” Derick alizidi kuzungumza maneno ambayo yalinisisimua sana na kunifanya nishangazwe kwa upendo ambao alikuwa nao kwa mke wake.

    “Usichoke kumtumainia Mungu kwani yeye ndie muweza wa yote, naamini ipo siku atafanya njia pasipo na njia.” Ilinibidi niendelee kutamka maneno ambayo yataendelea kumfariji kwani kiuhalisia alikuwa anapitia wakati mgumu sana katika ndoa yake, kwavile yalishawahi kunikuta kwahiyo nilikuwa nafahamu hali halisi wanayokuwanayo wanandoa pindi wanapokuwa wanatafuta mtoto kwa muda mrefu bila mafanikio.

    “Endelea kutuombea Mungu na sisi tujaliwe utajiri wa watoto.”

    “Tupo pamoja dia.”

    Kiukweli nilisikitika sana baada ya Derick kunieleza kwamba hajajaliwa kupata mtoto mpaka wakati ule ingawa nilipendezwa sana na ujasiri wake wa kujitenga na nduguze kusudi kulinda penzi lake lisitetereke kwani ni dhahiri kwamba alionyesha moyo wa kishujaa na wa kipekee sana ambao hauwezi kudhihirika kwa mwanaume asie na msimamo. Tulizungumza mengi na jioni ilipofika nilirudi nyumbani kwangu nikiwa najihisi kuchoka sana kutokana na mikikimikiki niliyokumbana nayo kitandani nilipokuwa nafahidi penzi lake. Kesho yake sikuweza kwenda kokote wala kufanya chochote kwasababu bado nilikuwa najihisi uchovu wa hali ya juu, siku nzima nilishinda kitandani kwangu nikichati na Derick na kumweleza vile nilikuwa nahisi japokuwa na yeye pia aliniambia kuwa alikuwa anajihisi hali ya uchovu sana.

    Kiukweli ule muda wa likizo wa hawara wangu Derick niliutumia vizuri sana kufurahia utamu wa penzi lake kwasababu tulikuwa tukikutana mara kwa mara na kupeana uhondo usiokuwa na mfano. Penzi lake lilininogea na kusababisha kumdanganya mume wangu kwamba nahitaji kwenda kuwasalimu wanangu shuleni Mombasa nchini Kenya halafu nikatumia nafasi hiyo kwenda kujichimbia hotelini kula bata na mchepuko wangu ambae alikuwa kwenye himaya yangu kwa muda wa mwezi mmoja. Tulitumia muda wa siku tatu hotelini ambapo nilifanikiwa kuziteka vilivyo hisia za Derick kwa manjonjo niliyokuwa namuonyesha kitandani hadi mwenyewe akakiri kwamba mapenzi niliyomuonyesha hakuwai kukutana nayo kwa mwanamke yeyote tangu alipoanza mahusiano ya kimapenzi.

    Niliamua kujituma sana ili niweze kumridhisha kama ambavyo alivyokuwa akionyesha ubunifu wake ili kuweza kuhakikisha kwamba ananifikisha kileleni. Baada ya muda kuisha nilirudi kwangu huku mume wangu akijua kwamba nimetoka nje ya nchi kuangalia maendeleo ya watoto kumbe sivyo. Nilimdanganya kwamba watoto wanaendelea vizuri kabisa na wanazidi kufanya vema katika masomo yao kwahiyo alifurahi sana. Muda wa Derick kuwepo Arusha ulikwisha hivyo basi aliondoka na kurudi Dar es salaam ila aliniahidi kwamba atakuwa ananitafuta mara kwa mara ili tuweze kujuliana hali. Ingawa moyo uliniuma sana kipindi nilipokuwa naagana nae ila sikuwa na namna isipokuwa kumtakia kila la heri huko aendapo.

    ***

    Kitendo cha Derick kuondoka kilisababisha niendeleze mapenzi yangu na Fadhili kwasababu sikuwa na namna nyingine ya kuweza kuendelea kupata burudani ya mapenzi isipokuwa kwake. Japokuwa hakufahamu kuwa nilikuwa nimemuweka pembeni kwa muda kwasababu ya mwanaume ambae nafikiri sintakuja kumsahau maishani mwangu hadi siku naingia kaburini kwasababu ndie alienitoa usichana wangu na pia ndie alienizalisha mtoto wangu wa kwanza kwahiyo kwa namna moja au nyingine ndio maana moyo wangu umeshindwa kabisa kuacha kumuhusudu. Laiti kama angekuwa fukara basi ningefanya kila namna ili niweze kumuwezesha kiuchumi kusudi aweze kuwa na maisha mazuri kuliko hata ya Fadhili kwasababu ni mtu wa muhimu sana maishani mwangu lakini jambo la heri ni kwamba Mungu kamjalia ni msomi ambae anakazi yake nzuri inayomuingizia kipato kizuri cha kumtosha. Hata gharama zote zilizokuwa zikitumika faragha alikuwa akilipa yeye mwenyewe. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Nafasi ya mume wangu ndani ya moyo wangu ilizidi kwenda mrama kwani nilikuwa namchukulia kama kinyago cha mpapure. Pamoja na kwamba nilikuwa nashiriki nae tendo la ndoa lakini nilikuwa sifurahii kama ambavyo nilikuwa nafurahishwa na mahawara zangu ambao nilikuwa nawaona kama vile walikuwa wamesomea shahada ya kumpagawisha mtoto wa kike. Nilitamani ule utundu wa mapenzi niliokuwa naonyeshwa nje ya ndoa niupate ndani ya ndoa yangu lakini mume wangu alikuwa sikio la kufa lisilo sikia dawa kwani nilishawahi kumweleza kwamba huwa hanifikishi kileleni lakini alionyesha kutokujali. Kwahiyo ndio sababu ya kuwapa wanaume wengine wanaouweza mchezo ili waweze kumsaidia kulimega tunda kwavile alionekana hawezi kulifaidi kama inavyotakiwa. Tena ana bahati sana akanishinikiza kufunga kizazi baada ya kumzaa Jordan kwasababu ningeendelea kumzalia watoto wa wanaume wengine hadi timu ya mpira ingekamilika ndio akili za ubunifu kitandani zingemfunguka.

    Miezi minne baadae kwa bahati mbaya mume wangu alikumbwa na kesi ya ubadhirifu wa pesa za kampuni zaidi ya milioni 400 alizozichukuwa kwa wakati tofautitofauti ili aweze kunitimizia mahitaji niliyokuwa namweleza kama vile magari ya kifahari pamoja na vito vya thamani nilivyokuwa nabadilisha kila mara .Alikosa raha baada ya wakaguzi kupitia akaunti ya kampuni na kugundua huo ufisadi uliokuwa umefanyika kwahiyo alisimamishwa kazi na kufunguliwa kesi mahakamani ili aweze kujibu shtaka lililokuwa linamkabili. Jambo hilo liliniumiza na mimi vilevile kwasababu nilijua kuwa zile starehe nilizokuwa naziponda bila kujali ni januari ama disemba ndio zilikuwa zimefika ukingoni. Enrique aliingia katika msongo mkali wa mawazo hadi nikawa namuonea huruma kwajinsi ambavyo alidhohofika na kukonda ghafla. Nilijaribu kumtia moyo kwa kumweleza kwamba hiyo ndio mitihani ya maisha kwahiyo hana budi kupambana nayo kwa hali na mali ili aweze kuishinda.

    Pamoja na hayo yote lakini haikuweza kuleta mabadiliko yeyote kwake zaidi sana alizidi kupoteza matumaini kutokana na kesi iliyokuwa imefunguliwa mahakamani dhidi yake. Niliwaza sana ni jinsi gani naweza kumsaidia katika ule wakati mgumu uliokuwa ukimkabili lakini sikuweza kupata suluhisho kwasababu ushahidi ulikuwepo kabisa unaoonyesha kwamba kwa asilimia mia moja yeye ndio muhusika wa ubadhirifu wa fedha uliofanyika. Kiukweli kusimamishwa kazi kwa Enrique kuliathiri hadi ile ahadi yake ya kutaka kuwajengea wazazi wangu nyumba nzuri ya kuishi yote hayo ni kwasabau kazi aliyokuwa anaifanya ndio ilikuwa muhimili mkuu wa uchumi wake ingawa alikuwa na biashara zingine kadhaa lakini zilikuwa na uwezo wa kusomesha watoto pamoja na kufanya mambo mengine madogo madogo ya pale nyumbani.

    Usiku na mchana mume wangu hakuwa na lakufanya isipokuwa kushinda tu ndani akiwaza namna atakavyoweza kuishi bila kazi wakati majukumu ndio yanaongezeka kila kukicha. Ule mchezo niliokuwa nimezoea kuucheza na Fadhili pale nyumbani kwangu pindi mume wangu anapokuwa kazini ulikwama kwa muda kwasababu ya uwepo wake wa kila wakati. Kesi ilizidi kurindima mahakani baina ya kampuni aliyokuwa anafanya kazi mume wangu dhidi ya mawakili waliokuwa wamewekwa na mume wangu uli waweze kumtetea ingawa kulikuwa kunaonekana kuna kila dalili ya upande wa mume wangu kushindwa katika kesi ile kutokana na kwamba hawakuwa na hoja zenye mashiko katika kumtetea mume wangu ili asiweze kuhukumiwa kifungo jela na mahakama tukufu. Tulianza kupitia mambo magumu mno kwasababu kesi ile ilikuwa inatugharimu pesa nyingi sana katika mapambano dhidi yake kibaya zaidi ni kwamba hatukupata msaada wowote kutoka kwa ndugu yeyote kwasababu hatukuwa na maelewano mazuri na ndugu wa karibu ambao wangeweza kutusaidia hata kutufariji katika yale magumu tuliyokuwa tukipitia.



    Hakika furaha ilitoweka kabisa ndani ya moyo wangu kwasababu nilikosa kabisa pesa a matumizi. Nilichoka na kuchakaa, hata watu waliokuwa wamezoea kuniona nikipendeza kila siku walikuwa wakinishangaa na wengine walionyesha dharau kwa kunicheka hadharani. Sikubadili magari kama ilivyokuwa mwanzo, mbwembwe za saluni kila baada ya siku chache ziligonga mwamba kwasababu baba watoto wangu hakuwa na chochote cha kuweza kunipa ingawa alikuwa anatamani sana mke wake niwe katika muonekano mzuri. Niliteseka sana kwasababu nilikuwa nimezoea kuishi maisha ya starehe mithili ya malikia. Pamoja na hayo yote namshukuru Mungu Fadhili alizidi kunipenda na kunijali kwani hakuonyesha dalili yeyote ya kunichukia kwasababu nilikuwa nimeyumba kiuchumi. Tulizidi kuhudhuria mahakamani kufuatilia kesi iliyokuwa inamkabili Enrique, lakini kadiri siku zilivyokuwa zinazidi kwenda ndivyo tulivyokuwa tunapoteza matumaini kwa mume wangu kuweza kushinda kesi.

    Mawakili waliokuwa wakipambana na kesi ile walizidi kuzichuma pesa kwa mume wangu ili waweze kupambana na kesi jambo ambalo lilisababisha baadhi ya magari yaliyokuwepo pale nyumbani yauzwe ili pesa iweze kupatikana. Enrique aliuza magari 9 na kulibakiza limoja kwaajili yangu. Familia ilizidi kuwa katika wakati mgumu wakati mwingine niliwasiliana na Derick na kumweleza magumu niliyokuwa napitia na kunitia moyo kwa kunieleza kwamba tusikate tamaa bali tuzidi kumuomba Mungu nae atatusikia katika vita tunavyopigana. Ilifikia pabaya kwasababu Enrique alinieleza kwamba inabidi tumsimamishe kazi Fadhili kwasababu hapakuwa na pesa za uwakika kwaajili ya kumlipa.

    Sikuwa na pingamizi kwasababu hali ya mume wangu nilikuwa naiyona mwenyewe ingawa roho iliniuma sana kwasababu ndio ulikuwa mwanzo wa kutengana na mchepuko wangu ambao nilikuwa naupenda sana kwani ulikuwa ukinitimizia haja zangu kwa wakati. Baada ya makubalianao hayo na mume wangu kuhusu kusitishwa kwa kibarua cha Fadhili ilibidi aondoke lakini alielekea katika ile nyumba niliyokuwa nimemjenge maeneo ya Sorenyi jijini Arusha. Siku aliyokuwa anaondoka nilimsihi sana asinisaliti huko aendapo kwasababu nampenda sana na pia nilimtia moyo kwamba familia yangu ilikuwa katika kipindi kifupi cha mpito kwahiyo baada ya muda mfupi mambo yatakaa vizuri tutamrudisha kazini ili aweze kuendelea na kazi yake. Tuliendelea kupambana na kesi na maisha yalizidi kuwa magumu kila kukicha. Siku moja ya jumanne majira ya saa tatu asubuhi mume wangu alikuja kuchukuliwa nyumbani asubuhi na mawakili waliokuwa wakiendesha kesi yake na kwenda mahakamani na kuniacha mimi nikijiandaa ili niweze kuwafuata.

    Mara baada ya maandalizi yangu niliwasha gari yangu nakuanza safari ya kuelea kituo kikuu cha polisi jijini Arusha ili kwenda kusikiliza kesi. Nilipofika kijenge impala ili nishike njia ya kupandisha mjini gari langu lilizima ghafla jambo ambalo lilinitia hasira sana kwasababu lilizima katikati ya barabara na kusababisha foleni kubwa. Madereva wengi walinitukana na kunisema kwa dharau hayo yote ni kutokana na kwamba nilijitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu ili niweze kuliwasha lakini ilishindikana kabisa.

    “Mpigie aliekuhonga aje akusaidie kulitoa.” Dereva mmoja wa gari la mizigo alisikika akiropoka sauti ya juu.

    “Pipiiii.” Dereva mwingine wa daladala asikikika akipiga honi mfululizo huku kinywa chake kikitoa maneno makali ambayo yalinitia hasira sana.

    “Panda kitandani tena ili upatiwe lingine kwasababu hilo limeshakuwa kimeo.”

    “Hivi hawa wajinga wanafikiri wanawake wote wanaoendesha magari barabarani basi wamehongwa?” niliwaza kwa hasira. Baada ya dakika chache alishuka mzee mmoja katika gari moja la kifahari aina ya Toyota landcruiser VX na kunifuata kwenye gari langu.

    “Hujambo binti.”

    “Sijambo shkamoo.”

    “Gari lako linamatatizo gani?”

    “Hata sijui mzee yani limezima tu ghafla jambo ambalo si la kawaida kabisa.”

    “Umeweka mafuta ya kutosha?” CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    “Ndio mafuta yapo ya kutosha.” Punde wakati nilipokuwa nikizungumza na yule mzee niliona vijana wawili waliokuwa wamevaa maovaroli ya gereji wakikatiza huku wakiwa wameshika spana zao mikononi.

    “Psiiii, psiiii.” Niliamua kuwashtua ili waweze kuniona na kwa bahati nzuri waliniona na kuanza kuja katika uelekeo wangu harakaharaka.

    “Sema sista!” Mmoja wa wale vijana alinitaka nizungumze fasta kwasababu walionekana kuwa na haraka sana.

    “Gari langu limezima ghafla.”

    “Yani hapa tulipo tumepigiwa simu kunamtu amepata matatizo kama yako kwahiyo kama utalipa ghali tutakufanyia fasta.”

    “Ghali shilingi ngapi.”

    “40.” Yule kijana alisema kwa kifupi kumaanisha 40,000.

    “Mungu wangu sasa itakuwaje wakati hapa kwenye waleti ninawanja na pafyumu tu.” Niliwaza kimya kimya huku nikitunga cha kuwaeleza wale vijana ili waweze kunisaidia.

    “Jamani mbona pesa nyingi hivyo kaka zangu.”

    “Sio kesi sista! kwani wewe unabongaje?” Wale vijana wote kwa pamoja walijikuta wakitoa kauli inayoendana kimaana kwani wote walinitaka niwaeleze kwamba mimi ninashilingi ngapi ili waweze kunisaidia.

    “Kiukweli hapa nilipo sina pesa kabisa labda mpaka tuende nyumbani kwangu.”

    We sista unazingua.” Mmoja wa wale vijana alitamka huku akimvuta mwenzie mkono ili waweze kuondoka. Ndipo yule mzee aliekuwa amekuja kunisaidia, aliwazuia na kuwataka wafanye kazi halafu atawalipa pesa yao. Nilifurahi sana kwasababu sikutegemea kabisa kuweza kupata msaada kama ule kwani niliona kama madereva wote pale barabarani walikuwa kama maadui zangu kutokana na lugha zao mbaya.

    “Kwani unakwenda wapi binti.” Yule msamaria mwema aliniuliza wakati mafundi wakiliangaikia kuliwasha gari.

    “Nakwenda central police.”

    “Kuna nini.”

    “Ni matatizo tu ya hii dunia mzee wangu.”

    “Pole sana.”

    Baada ya dakika kumi gari langu liliwaka. Yele mzee alitoa pesa ya wale vijana na kuwapa kisha akatoa shilingi elfu 20,000 pamoja na business card yake kisha na kunikabidhi halafu akawasha gari lake akaondoka. Nilimshukuru sana kwa msaada aliokuwa amenipatia kwasababu sikuwa na hili wala lile. Nilijiuliza maswali mengi sana ni kwanini baba yule aliamua kunisaidia kiasi kile ili hali hakuwa akinifahamu kabisa na wala nilikuwa simfahamu vilevile. Bussness card yake alionipa niliitupia kwenye dashboard ya gari langu na kuendelea na safari. Sikuwa na muda wa kuiangalia vizuri kwasababu nilikuwa barabarani halafu isitoshe ilinibidi niendeshe kwa kasi kwavile nilikuwa nimechelewa kufika mahakamani. Baada ya dakika nane nilipaki gari langu mahakamani kwaajili ya kusikiliza kesi ya mume wangu kwa bahati nzuri kesi ya mume wangu ilikuwa ni ya tatu kati ya kesi tatu zilizokuwepo mahakamani kwa siku hiyo kwahiyo muda wake ulikuwa bado haujafika. Zamu ya mume wangu ilifika ambapo alipanda kizimbani lakini kesi ilipigwa tarehe baada ya walalamikaji kushindwa kufika mahakamani kwa siku ile. Tulirudi nyumbani kwa pamoja huku kichwa changu kikiwaza kuhusu msaada wa yule mzee ambae alijitolea kunisaidia pale ambapo wengi walikuwa wakinitusi na kunidhihaki. Nilipofika nyumbani nilichukua ile bussness card niliyokuwa nimepewa na yule mzee na kuingia nayo ndani bila mume wangu kufahamu chochote. Wakati nilipokuwa jikoni nikiandaa chakula cha jioni niliona ndio muda wa kuichukua ile namba ya yule mzee na kumpa shukrani zangu za dhati kwa msaada wake. Mara baada ya kuishika ile bussness card ili niweze kuchukua namba za simu nilitabasamu kwa kushangaa baada ya kuona kwamba yule mzee alikuwa ni mkurugenzi wa makampuni matatu ya uuzaji wa magari jijini arusha.

    “Wow! Kumbe nimekutana na mtu mkubwa.” Niliwaza huku nikiwa na furaha ndani ya mtima wangu kwa kuwa sikutegemea kuwa yule alikuwa ni mtu mkubwa kiasi kile. Niliona nisipoteze muda nimpigie simu nimshukuru.

    “Krii krii.” Simu iliita.

    “Haloo.” Sauti ilisikika upande wa pili.

    “Habari za sahizi mzee wangu.”

    “Njema vipi hali.”

    “Salama tu! Unazungumza na yule binti uliempa msaada sazile barabarani.”

    “Ooh! Sawasawa.”

    “Ninashukuru sana kwa Masaada wako, ubarikiwe sana.”

    “Amen! Asante sana.”

    “Usiku mwema.”

    “Nashukuru! na kwako pia binti.” Nilimaliza kuwasiliana na mzee yule huku moyo wangu ukiwa na furaha kubwa baada ya kuisikia sauti ya yule msamaria mwema. Chakula kiliiva na ndipo nilikitenga mezani ili tuweze kula. Kesi iliyokuwa mahakamani pamoja na kitendo cha Enrique kufukuzwa kazi kilisababisha ashindwe kula chakula kwa kiwango kinachotakiwa. Pamoja na hayo yote lakini pia alishindwa kupata usingizi wakati wa usiku mara nyingi huwa anakesha usiku kucha kwa kupiga mihayo mfululizo. Mwili wake ulizidi kudhoofu kila kukicha kutokana na mawazo mengi yaliyokuwa kichwani mwake. Nilimtia moyo angalau aweze kula lakini alishindwa kabisa ingawa alijitahidi sana. Siku moja usiku wakati tulipokuwa tumelala nilizinduka usingizini baada ya kusikia mume wangu akiniita kwa sauti ambayo iliashiria kwamba hapakuwa na usalama.

    “Mke wangu.” Enrique aliita huku akinipigapiga mgongoni ili niweze kuamka.

    “Abee!” nilizinduka huku moyo wangu ukienda mbio nikijiuliza sababu iliyopelekea aniamshe kwa mtindo ule ni upi wakati sio kawaida?”

    “Tumboo...” Niliruka nikakaa kitandani baada ya kusikia kauli ya mume wangu ambayo ilinishtua kupita maelezo.

    “Kwani kunatatizo gani?” nilizungumza huku nikifikicha fikicha macho yangu ili niweze kumtazama barabara.

    “Tumbo.” mume wangu alizidi kuzungumza huku akiwa amejikuja sana jambo ambalo liliashiria ni kweli alikuwa akihisi maumivu makali sana ya tumbo.

    “Basi ngoja nikusaidie twende hospitali.” Nilizungumza huku nikishuka kitandani fastafasta na kuvua pajama niliyokuwa nimeivaa na kuvaa gauni. Nilimshika begani tukaenda hadi kwenye gari ambapo nilimpakia na kwenda moja kwa moja hadi hospitali ya AICC ambapo alipatiwa masaada wa haraka wa matibabu. Baada ya daktari kuchukua maelezo pamoja na kumfanyia vipimo mbalimbali alisema kwamba mume wangu anavidonda vya tumbo. Alilazwa hadi kesho yake mida ya saa nne asubuhi ambapo aliruhusiwa kurudi nyumbani. Daktari alitupa orodha ya baadhi ya vyakula ambavyo anaruhusiwa kuvila pamoja na ambavyo haruhusiwi kuvila. Pia alishauriwa kuzingatia muda wa kula pamoja na kupunguza mawazo kwasababu ndio kichocheo kikubwa cha ugonjwa huo. Tulirudi nyumbani tukiwa na mawazo mengi sana kwasabaabu hatukujua ni kwanamna gani tutaweza kulishinda jaribu lingine lililokuwa limejitokeza ndani ya maisha yetu kwasababu uchumi wa familia ulizidi kwenda mrama.

    Hali ya mume wangu ilizidi kuwa mbaya kwasababu masharti aliyopewa na daktari yalionekana kuwa magumu kwani alishindwa kabisa kujizuia kuwaza, na pia wakati mwingine vyakula alivyokuwa ameshauriwa na daktari vilikuwa vinakosekana kutokana hali ya maisha pale nyumbani kwangu ilizidi kuwa mbaya. Tarehe ya kurudi mahakamani ilikaribia jambo ambalo lilifanya mume wangu aendelee kuwaza namna ambavyo itakuwa endapo atahukumiwa kifungo gerezani. Siku moja nikiwa njiani nikielekea mjini simu yangu ya mkononi iliita na nilipoitazama ilikuwa ni namba ya yule mzee ambae aliwahi kunipa msaada wakati nilipokuwa nimeharibikiwa na gari barabarani. Kwa furaha niliyoipata nilipunguza mwendo gari langu kisha nikaliegesha pembeni ya barabara ili niweze kuzungumza na mtu yule.

    “Haloo!” sauti ilisikika upande wa pili.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    “Hivi binti ulisema unaishi wapi?” sauti ya yule mzee ilisikika ikiniuliza swali mara baada tu ya salamu.

    “Naishi njiro kwa msola.” Nilimjibu kwa kifupi.

    “Samahani! unaweza ukatafuta muda tukakutana tukazungumza zaidi.” Nilishtuka kidogo baada ya kusikia yule fogo anahitaji kukutana na mimi kwajili ya mazungumzo.

    “Mh! kwani hilo jambo halifai kuzungumza kwenye simu?” niliamua kumzungusha kidogo ili asinione kibonde.

    “Inawezekana ila nafikiri ingependeza zaidi kama tungekutana ana kwa ana.”

    “Nimekwelewa.”

    “Sawa basi tukutane kesho katika hoteli ya mount meru mida ya saa saba mchana.”

    “Ok!.” Nilimwitikia, ingawa aliniacha na maswali mengi akilini mwangu kwasababu sikujua hasa yule mzee alikuwa na lipi hasa alilokuwa anahitaji kuzungumza na mimi tena hotelini na sio pahala pengine. Kwahiyo nilitamani iyo kesho ifike kusudi niweze kukutana nae ili niweze kujua alikuwa na lipi la kunieleza babu yule ambae pesa zilimfanya aonekane bado kijana. Niliendelea na safari yangu hadi mjini na baada ya muda nilirejea nyumbani kwangu.



    Mara baada ya kuingia chumbani kwangu nilishtuka sana baada ya kukuta vitu vimerushwa huku na kule. Mume wangu alikuwa bize akipekuwa kila sehemu. Ilinibidi nimuulize kwa harakaharaka alichokuwa anakitafuta ili niweze kumsaidia kutafuta kusudi asije akaitia machoni ile hirizi niliyokuwa nimechimbia ndani ya begi langu la nguo.

    “Kuna document mmoja ya kazini mawakili wangu wanahitaji ndio maana napekua kila mahali kwasababu ni juzi kati tu niliitia machoni sasa sijui nimeiweka kwenye kona gani.”

    “Basi ngoja nikusaidie kuitafuta mpenzi!”

    “Sawa! Embu nisaidie kwasababu nimetafuta hadi najihisi kuchoka.” Moyo wangu ulilia paa! Mara baada ya kusikia sauti ya mume wangu ikinieleza kuwa amepekuwa kila mahali.

    “Inamana amepekua hadi huku kwenye nguo zangu.” niliwaza huku moyo ukinienda mbio sana.

    Nilianza kumsaidia kutafuta huku na kule lakini kwa bahati mbaya hadi inatimu usiku bado tulikuwa hatujafanikiwa kuipata. Nilikosa kabisa raha, mwili wangu ulikuwa unatetemeka kwa kukosa kujiamini ingawa sikukata tamaa. Muda ulisonga sana bila kupata tulichokuwa tunakitafuta. Kwahiyo ilibidi tuhairishe hadi kesho yake kwasababu muda ulikuwa umesonga sana. Nilikwenda jikoni kuandaa chakula na kumuacha mume wangu chumbani akiwa amejilaza kitandani kwavile alinieleza amechoka kutafuta kwahiyo ataendelea kesho yake. Siku iliyofuta tuliendelea kuitafuta document ile ambayo ilikuwa inahitajika kesho yake mahakamani kwahiyo tulizidi kuisaka kila kona ya nyumba yangu. Nilipekuwa kijanja mpaka kwenye begi lililokuwa limeficha hirizi bila yeye kugundua chochote. Nilifanya hivyo ili aridhike kwamba napo pamekaguliwa kwahiyo hapatahitaji tena ukaguzi mwingine. Hadi ina timu saa tano na nusu bado tulikuwa hatujafanikiwa kuiona.

    “Sasa itakuwa imekwenda wapi?” Enrique aliuliza huku akionekana kukasirika.

    “Kiukweli hata na mimi nashangaa kwavile ulisema uliiona juzikati, ila kwa maoni yangu nafikiri itakuwa humuhumu ndani. Cha msingi ni kutuliza akili ili uweze kujua uliiweka wapi.”

    “Tatizo ni kwamba hiki kichwa kina mambo mengi sana ndio maana.”

    “Kweli kabisa dia ila ninaimani itapatikana tu.” Niliendelea kumtia moyo ili asikate tamaa. Muda wa miadi yangu na yule mzee ulikaribia kwahiyo ilinibidi nimdanganye mume wangu kwamba nahitaji kwenda kwa rafiki yangu Doroth kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa ya mwanae. Kwahiyo aliniruhusu nikaanza kujiandaa ili niweze kumuwahi yule mzee kule hotelini. Nilivaa nikapendeza hadi nikawa najionea wivu mwenyewe kwajinsi ambavyo nilikuwa namwonekano wa kuvutia, kwani mapaja yangu meupe yalikuwa wazi. Nilitamani muda wote niwepo mbele ya kioo ili niweze kujiona jinsi ambavyo nilikuwa nimetoka bomba. Nilijipulizia marashi yangu ya bei rahisi aina ya Chastity kwa vile sikuwa na pesa ya kununua marashi ya gharama kubwa kama ilivyokuwa awali. Niliondoka na kumuacha mume wangu bado anaendelea kupekua ndani ya nyumba ili aweze kuipata document aliyokuwa anaitafuta. Wasiwasi ulinipungua kidogo kwasababu mume wangu alitoka chumbani na kwenda sebuleni kuendelea kuisaka, jambo hilo lilinipa faraja kwavile nilijua kwamba uwezekano wa yeye kuendelea kupekua ndani ya begi langu la nguo ni mdogo.

    7.02 mchana niliegesha gari langu katika eneo la kuegesha magari katika hoteli ya mount Meru. Kabla sijashuka kwenye gari nilimtext yule mzee kumjulisha kwamba nimeshafika. Ndani ya muda huohuo alijibu meseji yangu na kunieleza kwamba gari lake ndio linaingia getini. Nilipohamaki nililiona gari moja la kifahari likiingia nikajua atakuwa ni yeye. Macho yangu yalizidi kutembea na gari lile lililokuwa likiingia hotelini pale hadi lilipofika katika eneo la maegesho ya magari ambapo ni jirani kabisa na nilipokuwa nimeegesha la kwangu. Muda huohuo nilimuona akishuka kwenye gari huku akiwa amevaa suti nyeupe ambayo ilikuwa imempendeza sana. Niliteremka na kusimama pembeni ya gari langu.

    “Ooh binti! You look so beautfull.” (umependeza sana binti) Mzee yule alianza kuniporomoshea sifa kabla hata ya salamu wakati alipokuwa akitembea kunifuta nilipokuwa nimesimama nje ya gari langu.

    “Thank you. Of course you look good too.” (asante sana! umependeza pia.) nilimjibu wakati alipokuwa amenikaribia kabisa wakati nilipokuwa nimefungua mikono yangu ili niweze kumkumbatia.

    “How are you! by the way.” (Vipi hali yako lakini) alizungumza yule mzee wakati alipokuwa amenikumbatia kwa furaha.

    “Am fine.” (sijambo)

    “Ok! you are welcome.” (karibu sana.)

    “Asante!” Tulianza kutembea taratibu hadi tulipofika katika meza iliyokuwa maalumu kwaajili ya watu wawili tu. Muda huohuo alifika muudumu ambae tulimwagiza chakula pamoja na vinywaji. Tulianza kupiga stori za hapa na pale wakati tunasubiri chakula lakini kabla ya yote nilibaini kuwa yule mzee alikuwa ananitaka kimapenzi kutokana na jinsi ambavyo alikuwa ananimwagia sifa za ulimbwende kila mara. Baada ya dakika 15 tulichokuwa tumeagiza kilikuja tukaanza kula na kunywa huku tukiendelea na maongezi yetu.

    “Kiukweli wewe ni binti mrembo sana.” nilizidi kupokea sifa kedekede kutoka kwa babu Benjamini.

    “Ahsante sana.”

    Nafsi yangu liligundua hilo tangu siku ya kwanza nilipokuona kwasababu umeshindwa kabisa kutoka katika akili yangu. Binti mimi sina longolongo kama vijana wa siku hizi, ombi langu kwako ni moja tu, naomba tuwe wapenzi.” Nilishtuka sana baada ya kusikia mzee yule anahitaji kuwa na mimi kimapenzi japokuwa tayari nilikuwa nimeshajua tangu mwanzo kwamba mwisho wa siku atazungumza jambo kama hilo.

    “Kiukweli haitawezekana kwasababu mimi ni mke wa mtu tena mwenye watoto kadhaa, naomba samahani sana.” ilinibidi nimweleze yule mzee ukweli wangu kusudi aweze kufahamu kuwa yupo na mke wa mtu.

    “Kwani ndoa inazuia nini mrembo? Mimi sijasema kwamba nahitaji kukuoa bali nahitaji tuwe na mahusiano ya siri kwasababu hata mimi pia nina ndoa yangu na nina watoto kama wewe.” Mzee Ben alizidi kunibana ili niweze kumkubalia.

    “Sasa huyu mzee hata nikimpa ataweza kunitimizia?” niliwaza wakati nilipokuwa namtazama machoni babu yule ambae alikuwa ananicheki kwa jicho la uchu.

    “No! no! no! it is imposible Mr Ben.” (Hapana! Hapana! Hapana! Haiwezekani bwana Ben.” Ilinibidi nimweleze kwamba sipo tayari baada ya kukumbuka kuwa mume wangu yupo kwenye matatizo makubwa ambayo nimeyasababisha mimi mwenyewe. Halafu badala ya kumpa faraja nitumie muda ule kuchepuka. Niliona ni dhambi kubwa sana kwahiyo nilimweleza kwamba haiwezekani.

    “Why not?” (kwanini haiwezekani.)

    “Kwanza itakuwa ni dhambi kubwa sana endapo nitakuwa na wewe kwa kipindi hiki wakati mume wangu yupo katika wakati mgumu kutokana na kesi inayomkabili mahakamani.”

    “Mumeo anashida gani?” aliuza.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Kwa masikitiko makubwa nilimsimulia mzee yule kila kitu kilichokuwa kikiendelea katika familia yangu pamoja na ugumu wa maisha unaotukabili ila sikuthubutu kumweleza kwamba mume wangu alikuwa akiiba ili aniridhishe kwavile angeniona kiumbe wa ajabu sana. Alinionea huruma sana kwa yote niliyomweleza na aliahidi kunisaidia ili mume wangu asiweze kufungwa gerezani. Nilimkumbatia kwa furaha huku machozi yakinitoka baada ya kusikia kwamba atanipa msaada ambao utamnusuru mume wangu kukaa ndani ya nondo za gereza.

    “Ila nitafanya hayo yote endapo utakubali kuwa na mimi.”

    “Sawa nimekubali ila naomba iwe siri sana kwavile sihitaji kabisa kuvunja ndoa yangu.” nilimkubalia kwa masharti hayo.

    “Usiwe na wasiwasi kwavile hata mimi nina ndoa ambayo sipotayari kuivunja kwasasa.” Yule mzee aliniomba akachukue chumba ili aweze kuanza kujilia tunda lake aliloliokota barabarani. Nilimdanganya nipo kwenye siku zangu lakini akili ya mzee yule ilikuwa ni pana sana kwani aliniomba twende japo tukaendelee na mazungumzo yetu chumbani bila kufanya chochote. Nilimkubalia tukazama chumbani huku moyo wangu ukinidunda dunda mithili ya tenesi. Sikuwa nikiamini macho yangu kwamba leo hii nimenasa katika mikono ya babu ambae nikimtazama kwa harakaharaka naona kabisa hataweza kuzituliza hisia zangu endapo ataziamsha. Chumbani sikuweza kuendelea kuwa na ujanja kwasababu mzee alihitaji kuhakikisha kwamba ni kweli nipo mwezini au ninamuongopea na ndipo nilipojikuta naanza kujiumauma kwa maneno lakini sikufanikiwa kumshawishi na ndipo nilipozama kwenye kumi na nane za mzee Ben. Bila kutegemea mzee yule alikuwa akinihemesha kwa mapigo yake hadimu hadimu. Kama waswahili wasemavyo usimdharau usiyemfahamu ndicho kilichonikuta kitandani kwasababu mzee Ben alinikuna barabara hadi nikajikuta nalia kwa kilugha cha kwetu. Nilikolea sana ikanibidi nimpe ushirikiano wa kutosha kwa vile sikujua kuwa mambo yangekuwa vile. Baada ya mchezo kila mmoja alionyesha kuridhika kabisa. Ilinibidi nimuangalie mzee yule kwa mara mbili mbili kwasababu sikuhamini kabisa kwamba angeweza kuniridhisha kama ambavyo alikuwa amefanya.

    “Asante sana Mr Ben. Nimeinjoi sana penzi lako.”

    “Asante pia mrembo! Hakika wewe ni mzuri kila idara.” Alizungumza mzee yule wakati anajifunga taulo ili tuelekee bafuni kwavile muda ulikuwa umekwenda sana.

    “Nashukuru!” tulikwenda kuoga katika bafu iliyokuwepo hapohapo chumbani na baada ya muda mfupi tulimaliza kuoga na kurejea chumbani ambapo nilikuta simu yangu ikiita. Niliisogelea ili niweze kuona aliekuwa akipiga alikuwa ni nani niliona kwenye kioo panasomeka ‘Darling…incoming call.’ Niliinyanyua simu ili niweze kuipokea ila simu ilikatika kwavile ilikuwa imeita kwa muda mrefu. Baada ya simu hiyo kukatika niliona kuwa kulikuwa kuna missed call 4 ambazo zote zilikuwa zinatoka kwa mume wangu. Nilianza kuingiwa na wasiwasi kwa kuwaza kulikuwa na tatizo gani hadi ananipigia simu mara nyingi kiasi kile wakati nilimuaga kuwa nakwenda kwenye sherehe?” sikupata jibu. Muda huohuo simu iliita tena kwa mara nyingine kutoka kwake ikanibidi nipokee harakaharaka ili niweze kumsikiliza anasemaje.

    “We mbwa hirizi imetoka wapi ndani ya nyumba yangu, shetani mkubwa wewe.” Enrique alizungumza kwa hasira sana kiasi kwamba nilihisi endapo ningekuwa karibu angeshanitoa macho au angesha nivunja taya kama sio kuning’oa meno.

    “Mbona sikuelewi dia.” Nilijifanya sijui chochote kinachoendelea. Mwili wangu ulihisi kupoteza nguvu ikanibidi nikae kitandani kwasababu niliona nikiendelea kusimama ningeweza kudondoka chini. Joto la mwili lilipanda kwa kasi ya ajabu kama mtu alieshikwa na homa kali. Tumbo nalo lilianza kunguruma mithili ya mtu mwenye maradhi makubwa ya tumbo. Hayo yote yalisababisha jasho lianze kunivuja ingawa nilikuwa nimetoka kuoga muda sio mwingi.

    “Huku kwenye begi lako umetia nini? Wewe mwanamke ni mchawi? Wewe mwanamke unaniloga? Nikipi ambacho nilikuwa sikufanyii hadi udiriki kuniendea kwa mganga? Unataka kuniua sio? My dia kabla hujaniua nitakuua mimi mwenyewe kwa mikono yangu, mwanaharamu mkubwa wewe.” Enrique alizidi kubwata kwa maneno makali, ilinibidi nimkatie simu kwasababu niliona ataweza kuniharibia kwa yule mzee.

    “What is going on?” (nini kinaendelea.)Mzee Ben aliuliza baada ya kuniona kama nimechanganyikiwa ghafla baada ya kuipokea simu ile.

    “No! I want to leave.” (hapana! Nahitaji kuondoka.) nilimjibu kwa kifupi kwasababu sikuhitaji kumweleza kabisa kilichokuwa kimetokea kwasababu roho ilikuwa ikiniuma sana.

    “Take this.” (chukua hii.) Mzee Ben alitoa kitita cha pesa na kunikabidhi japokuwa sikujua kwa harakaharaka ilikuwa ni shilingi ngapi. Bila kuzungumza chochote nilipokea na kutoka mbiombio mithili ya mtu alierukwa na akili hadi kwenye gari langu. Niliwasha na kuondoka kwa kasi ya ajabu huku akili yangu ikiwaza nitatumia njia gani ili kuweze kutatua lile tatizo lililokuwa limejitokeza.

    “Nikienda kwake anaweza kuniua.” Niliwaza huku nikiwa barabarani naendesha gari kwa kasi kuelekea kwa mganga ambapo niliwaza ndipo sehemu pekee ambapo naweza kupata msada wa haraka. Mume wangu alizidi kunipigia simu lakini niliogopa kabisa kuipokea kwasababu angezidi kunipanikisha kwa maneno yake makali. Saa 1.53 usiku niliegesha gari sehemu ambayo tulizoea kuegesha gari kila mara tulipokuwa tunakwenda kwa mganga. Kwake palikuwa hapafikiki moja kwa moja kwa gari kwa sababu kuna vichochoro vingi ambavyo ni vya kukatiza ili uweze kufika kwa mtaalamu. Nilishuka kwenye gari langu na kuanza kutembea kwa mwendo wa haraka haraka. Viatu nilivyokuwa nimevivaa vilikuwa ni virefu sana kwahiyo vilinifanya nijikwae mara kwa mara.

    Ilinibidi nivue ili nivishikilie mkononi kusudi niweze kutembea kwa haraka zaidi. Nilipomaliza uchochoro wa kwanza ambao ulikuwa na harufu kali ya vinyesi vya binadamu pamoja na giza kali nilimshukuru Mungu. Ulibaki mtihani mwingine ambao ulikuwa ni uchochoro wa pili ambao ndio ulikuwa unatisha zaidi kutokana na giza kali lililokuwepo. Nilipoanza uchochoro wa pili ambao ulikuwa ni mrefu zaidi ilinibidi niongeze mwendo zaidi ili niweze kuumaliza kwa haraka. Kwa bahati mbaya nilipofika katikati ya uchochoro niliona watu wawili wakiwa wamesimama mbele yangu jambo ambalo lilinitia hofu sana na kunifanya nihairishe safari baada ya kuhisi hali ya hatari. Nilipogeuka ili niweze kurudi nilipotoka macho yangu yalikutana na sura za watu wengine wawili wakiwa wamesimama, kwahiyo nilikuwa nimewekwa kati sina ujanja. Nilianza kutetemeka kwa hofu kubwa iliyokuwa imenitanda.

    “Naombeni msiniue jamani.” Ilinibidi niwaombe wasiniue baada ya kuona wanazidi kunisogelea.

    “Kaa chini.” Sauti moja nzito ilisikika kutoka kwa mwanaume mmoja ambae nilimpomtazama kwa makini niligundua kuwa alikuwa ameshika panga lililokuwa lina wakawaka kwa makali. Nilikaa chini huku moyo wangu ukizidi kunienda mbio.

    “Leta simu, pamoja na pesa kwa usalama wako.”

    Kwa jinsi sauti ilivyokuwa ya kutisha sikuwa na la kujitetea kwahiyo ilinibidi niwapatie simu yangu pamoja na kile kitita cha pesa nilichokuwa nimepewa na mzee Ben. Huku nikitetemeka kwa hofu nilizidi kumwomba Mungu wale wezi wasiweze kunidhuru kwasababu sikuwa na namna yeyote ya kuweza kujitetea.

    “Ok simama juu.” Jizi moja liliamuru nilisimame, nikafikiri kuwa ndio wananipa ruhusa ya kuondoka. Kwahiyo nilisimama kama mshale ili niweze kusikiliza amri nyingine itakayofuata.

    “Vua hilo gauni lako fasta.” Nilishtuka sana baada ya kusikia amri ile, nikawaza pengine labda walikuwa wanalitaka lile gauni kwa kuwa lilikuwa la kuvutia mno na la thamani kubwa vilevile. Nilionyesha kuwa mbishi kidogo kulivua jambo ambalo lilisabisha nikapata bapa mbili za panga mgongoni na kunisababishia maumivu makali mno mwilini mwangu. Nilivua chapuchapu na kumkabidhi mmoja wanaume wale ambapo alilipokea na kulitupa chini.

    “Vua na hizo zilizobakia, fanya haraka kabla hatujakufanya kitu mbaya sasahivi.” Kauli hiyo ilisikika ikinitaka nivue sidiria pamoja na chupi. Nilizidi kutokwa na jasho kutokana na hofu niliyokuwa nayo kwasababu nilihisi pengine labda walikuwa wanahitaji kuniingilia kimwili. Huku nikilia sana nilizidi kuwaomba wasinibake lakini walionekana kutojali kwani mara baada ya kumaliza kuvua nguo zote na kubaki uchi wa mnyama walianza kunibaka kwa zamu tena kibaya zaidi bila hata kinga yeyote. Walinishambulia mithili ya tembo waliofuma shamba la miwa. Waliniumiza sana kwasababu waliniingilia kwa muda mrefu bila kujali kwamba nilikuwa peke yangu. Nilipojaribu kujitetea pale ambapo maumivu yalizidi niliambulia mangumi pamoja na makofi ili niweze kutulia. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Licha ya maumivu makali niliyokuwa nikihisi mwilini mwangu lakini moyo wangu uliniuma sana kutokana na kitendo kile cha kinyama walichokuwa wakinitendea mtoto wa mwanaume mwenzao. Maumivu makali niliyokuwa nikihisi yalipelekea damu kuanza kunivuja sehemu zangu za siri. Pamoja na damu nyingi zilizokuwa zikinivuja lakini bado hawakuona kwamba inatosha zaidi sana walizidi kunibaka bila huruma.

    “Tuamsheni P1 kasema kunadili mtaa wa pili wa mkwanja mrefu.” Sauti ya mmoja kati ya wanaume wale ilisikika ikiwapa wengine taharifa baada ya kuongea kwa simu iliyoita muda mfupi wakati walipokuwa wakiendelea kunibaka. Walianza kufunga mikanda ya suruali zao wakati nikiwa chini sijiwezi. Muda huo huo simu yangu iliita katika mfuko ambao walikuwa wameweka vitu ambavyo walikuwa wamevichukua kutoka kwangu. Walisahau kuizima mara baada ya kunipokonya.

    “Mtolee laini ya simu yake ili hao washenzi wake wasiendelee kutusumbua.” Nilipata faraja kidogo baada ya mmoja wa wezi wale kutoa wazo hilo ambalo lilikuwa ni msaada kidogo kwangu. Nilipewa laini yangu ya simu nikavaa gauni langu huku nikilia sana kutokana na kitendo nilichokuwa nimefanyiwa bila ridhaa yangu. Nguo ya ndani niliishikilia mkononi sikuweza kuivaa kutokana na maumivu makali niliyokuwa nahisi. Nilijihisi kama mtu ambae ameunguzwa na maji ya moto kumbe sio. Wezi wale walitokomea kusikojulikana na kuniacha nikiwa katika hali mbaya. Sikuthubutu kupiga kelele kuomba msaada kwasababu nilihofia kwamba taharifa zangu zinaweza kufika kwenye vyombo vya habari jambo ambalo lingenitia majaribuni zaidi na zaidi kwasababu watu wanaonifahamu wangeshangaa nilikuwa nimetoka wapi katika maeneo yanayosifika kwa kuwa na waganga chungu mzima, tena majira kama yale.

    Nilichechemea kwa shida hadi kwenye gari langu ambalo nilikuwa nimeliegesha mbali kidogo naa eneo la tukio. Wazo la kwa mganga lilipotea kwasababu nilikuwa nimeumia sana na pia sikuwa na pesa yeyote niliyokuwa nimebakiwa nayo kwahiyo sikuwa na uwezo wa kuendelea na safari ya kwa sangoma. Kwa bahati mbaya zaidi nilikuta gari langu halina saidi mira hata moja, tayari vibaka wengine walikuwa wameshafanya mambo yao. Saa ya kwenye gari langu ilionyesha ni saa 4.02 usiku. Maumivu ya moyo yalisababisha macho yaendelee kudondosha machozi.

    “Piga ua garagaza ila kwa Enrique siwezi kurudi. Atakwenda kuniua.” Niliwaza wakati naligeuza gari langu kwa hasira sana. Baada ya hapo nililiondoa kwa kasi ya ajabu sana mithili ya gari la majambazi linapokuwa linaondoka eneo la tukio. Nafsi yangu ilinituma niende nyumbani kwetu japo kuwa sikupata jibu nitakwenda kujieleza vipi endapo nitafika salama. Hasira zote nilizokuwa nazo niliangushia kwenye gari nililokuwa naliendesha kwani sikujali bamsi wala korongo. Nilikuwa naendesha kama gari lililoibwa. Kwa mwendo niliokuwa nakwenda nao watu waliziba vinywa vyao kwa mikono kwasababu haikuwa kasi ya kawaida. Nilipofika maeneo ya ‘Massai camp’ nilipigwa mkono na maaskari waliokuwa doria usiku huo.



    Nilikasirika sana mara baada ya kuona askari moja akinionyesha ishara ya kusimama huku wengine wanne wakionekana kusimama makini kuonesha utayari wa kukabiliana na mimi endapo ningegairi amri ya polisi. Nilishusha pumzi kubwa wakati huo akili yangu ilikuwa ikifanya kazi kama kompyuta kutafuta namna ya kujitetea ili wasiweze kunipeleka kituoni. Nilipunguza mwendo na kulisimamisha gari langu kando ya barabara na kukilaza kichwa changu juu ya uskani kuwasubiri maaskari ambao nilikuwa nimewapita kidogo kutokana na kasi ya gari yangu.

    “Naomba kadi ya gari pamoja na leseni ya udereva.” Askari mmoja aliagiza huku wenzie wakilizunguka kulikagua gari langu. Sikupoteza muda kwasababu nilikuwa sijisikii vizuri kabisa kwahiyo niliona kama wananipotezea muda wangu. Nilitoa vitu alivyokuwa anahitaji na kumkabidhi.

    “Kwanini unaendesha gari kwa mwendo mkali.” Askari aliuliza huku macho yake yakiwa kwenye kadi ya gari pamoja na leseni.

    “Samahani afande nimepata taharifa kwamba mwanangu ni mgonjwa, kwahiyo ndio nawahi ili nikamuwaishe hospitali. Kwahiyo naomba mniruhusu niwahi kwenda kuokoa maisha ya mwanangu kwasababu hali yake ni mbaya sana.” niliamua kutoa kauli ya uwogo ili niweze kuwashawishi wasinifikishe mbele ya sheria kwasababu tayari nilikuwa ni mkosaji.

    Hiyo sio sababu ya wewe kuvunja sheria. Mwendo unaokwenda nao ni hatari kwa maisha yako na hata kwa watumiaji wengine wa barabara.

    “Naomba mnisamehe afande. Uchungu wa mwana anaujua mzazi ndio maana nimejikuta navunja sheria kwa lengo la kunusuru maisha ya mwanangu lakini nakuhaidi kuwa sintarudia tena.” Nilijitahidi kujitetea huku machozi yakiniririka mashavuni mwangu ili aweze kunionea huruma.

    “Halafu mbona gari lako halina saidi mira hata moja?” askari alizidi kuniandama na maswali ambayo yalikuwa yananikera kupita kawaida.

    “Nimetoka kwenye sherehe, kwahiyo nilikuwa nimeliegesha katika eneo ambalo halikuwa na usalama wa kutosha ila kesho nitaamkia gereji.” Nilizidi kumchega yule afande kwa majibu ya haraka haraka ya kufikirika.

    “Inabidi ugeuze gari tuelekee kituoni haiwezekani ukavunja sheria kwa sababu zisizokuwa na msingi.”

    “No! afande nakuomba unisaidie, hakuna binadamu asie kosea hata siku moja. Imetokea kwa bahati mbaya tu. Tafadhali nakuomba unisamehe.” Nilizungumza huku machozi yakizidi kunidondoka hadi wakawa wananishangaa kwasababu haikuwa hali ya kawaida. Mbinu zangu zilionyesha kugusa hisia zao kwani waliamini ni kweli mwananngu alikuwa mgonjwa ndio maana nilikuwa naangua kilio namna ile.

    “Nimekusamehe ila jitahidi kuzingatia sheria za usalama barabarani kwasababu ni kwamanufaa ya kwako na watu wengine wanaotumia barabara.” Askari yule alitamka huku akinikabidhi leseni yangu pamoja na kadi yangu ya gari. Niliwasha gari langu na kuondoka. Muda ulikuwa umekwenda sana kwasababu ilikuwa tayari ni saa 4.49 usiku. Nilipofika moshono stendi tayari nilikuwa nimeshabadili maamuzi yangu ya kwenda nyumbani kwetu usiku ule kwahiyo nilishika barabara inayoelekea baraa sekondari nikaendesha gari langu kwa kasi hadi nilipofika Sorenyi ambapo nililiegesha gari langu nje ya nyumba ya Fadhili. Nilishuka kwa kuchechemea kwasababu bado nilikuwa nikijihisi maumivu makali mno mwilini mwangu. Niligonga mlango kwa mara kadhaa bila kufunguliwa. Nilipata wazo la kwenda kwenye dirisha la chumbani kwa Fadhili ili niweze kugonga pengine inaweza ikawa njia rahisi kwake kuweze kunisikia kama kweli alikuwa amelala fofofo. Niligonga dirisha la Fadhili huku nikiita jina lake kwa nguvu, kwa bahati nzuri alizinduka katika usingizi mzito aliokuwa amelala.

    “Nani?” Fadhili aliuliza ili kufahamu aliekuwa akimgongea mlango usiku ule.

    “Teddy.”

    “Duh! Kulikoni tena muda huu. Kwema?”

    “Kwema kabisa! fungua mlango.” Nilimtoa wasiwasi ndani ya muda huohuo alikuja kunifungulia mlango, nikajikongoja hadi ndani.

    “Kuna tatizo gani, mbona unaonekana kuwa na damu nyingi miguuni mwako?” Fadhili aliuliza swali ambalo lilinikumbusha machungu yaliyokuwa moyoni mwangu na kunifanya niangue kilio.

    “Acha kulia. Jitahidi kujieleza ili nifahamu namna gani nitaweza kukusaidia.” Fadhili alizungumza huku akinifuta machozi yaliyokuwa yanachuruzika mashavuni mwangu.

    “Kiukweli nimegombana na Enrique hata sielewi itakuwaje halafu kesho ndio siku ya hukumu ya kesi yake.”

    “Pole sana. Kwahiyo yeye ndio kakuumiza namna hii.”

    “Hapana! Hii nimeumizwa na vibaka walionipora pesa na simu yangu wakati nilipokuwa nimeshuka kwenye gari kwenda kununua vocha.” Nililazimika kumficha Fadhili kwamba nilikuwa nimebakwa, nikihofia kwamba angeweza kunitenga.

    “Pole mpenzi. Vipi sasa utaweza kulala hadi kesho ndio uende hospitali?”

    “Hakuna tatizo nitajitahidi kuvumilia hadi kesho.”

    “Sawa.”

    Baada ya hapo nilibandika maji jikoni ili niweze kujikanda kupunguza maumivu makali niliyokuwa nahisi. Maji yalipopata uvuguuvugu nilikwenda bafuni kujikanda pamoja na kuoga kupunguza uchovu uliokuwa umeambatana na maumivu yasiokuwa na mfano. Baada ya hapo nilikwenda kujitupa kitandani. Moyo wangu ulifuka hasira kutokana na kitendo cha kinyama nilichokuwa nimefanyiwa na binadamu wenzangu. Sikujua itakuwaje endapo mume wangu atawaeleza ndugu zake kuhusu ile hirizi aliyoifuma kwenye begi langu la nguo. Niliwaza kuwa wazazi wangu watakuwa katika hali gani endapo watasikia kuwa binti yao nina mambo ya kishirikina. Kiukweli kichwa changu kilikuwa kinamaumivu makili ambayo yalisababishwa na mawazo mengi niliyokuwa nayo. Haikuishia hapo nilitaamani kufa nilipokuwa nikikumbuka kuwa wale vibaka waliniingilia bila kinga. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Nilikosa kabisa raha, usiku ulikuwa mrefu kwangu sikuweza kufumba macho yangu hadi palipokucha asubuhi. Mara baada ya mwanga wa jua kuanza kupenyeza dirishani nilishuka kitandani na kwenda bafuni kuoga. Fadhili alinipa simu yake moja ili iweze kunisaidia katika mawasiliano ndipo nilipoweka laini yangu ya simu na kukutana na meseji kibao kutoka kwa Enrique zikionyesha kwamba alikuwa ananisaka kwa hudi na uvumba ili aweze kunitia katika mikono yake. Nilimpigia mzee Ben nakumweleza kwamba ninamatatizo kidogo ya kifamilia kwahiyo nilimuomba anipatie fedha kidogo.

    Nilifurahi baadaa ya babu yule kunielewa na kunitumia shilingi laki mbili kwa njia ya m-pesa. Nilimuaga Fadhili na kuingia kwenye gari langu na kwenda moja kwa moja hadi sheli ambapo niliweka mafuta ya shilingi 40,000. Pamoja na kwamba bado nilikuwa najihisi kuumwa sana lakini sikupata muda wa kupumzika wala wa kwenda hospitali kwani nilichoamua kufanya ni kwamba nilifunga safari ya kwenda kwa sangoma kwa mara nyingine ili nikatafute namna ya kuweza kunusuru familia yangu. Palepale nilipokuwa nimeegesha gari langu usiku wa jana yake na kujikuta nimeingia kwenye matatizo makubwa ndipo nilipoliegesha gari langu kwa mara nyingine wakati nilipokuwa nimejitosa kwenda kumuonda mganga.

    Nilishuka na kupita kwenye vile vichochoro vyote salama bila shida na hatimae nilifika katika nyumba ya mganga. Nilishtuka sana baada ya kukuta mlango wa mganga umefunga. Nilijifariji huenda alikuwa amekwenda kutafuta dawa zake kwahiyo nilikaa katika benchi lililokuwepo pale nje kwa muda mrefu bila matumaini ya aina yeyote. Ilipotimu lisaa la nne bado nipo pale nje namsubiri mtaalamu, nilikata tamaa huenda labda hakuwa karibu. Nilitazama kwenye mlango wake kama ningeona namba zingine za simu kwasababu nilizokuwa nazo zilikuwa hazipatikani. Baada ya kuona muda unazidi kusonga nilikwenda katika nyumba ambayo ilikuwa ni jirani na nyumba ya yule mganga ili niweze kuuliza kama wanafahamu lolote kuhusiana na mzee Mbengwa.

    Mara baada ya kujitambulisha na kueleza shida yangu kwa jirani yake na yule mganga nilisikitika sana kutokana na jibu nililolipata.

    “Dah! Kiukweli unaonekana hujaja eneo hili siku nyingi sana. Pole sana kwasababu mganga tulisha mzika siku nyingi sana. Alikufa ghafla bila hata kuumwa kwahiyo alisafirishwa kwenda kwao sumbawanga.” Taarifa ile ilikuwa ni mbaya sana kwangu kwasababu ilipelekea nikajikuta nakaa chini kwenye vumbi baada ya kuhisi miguu imeishiwa nguvu ghafla.

    “What? Is it possible?” (nini? Inawezekana?) nilishindwa kuamini kabisa kama mtu ambae nilikuwa nafikiri ndie kimbilio langu na leo hayupo tena duniani. Kwa dhambi nilizokuwa nazo niliona mimi ndie nafuata kuionja adhabu ya kaburi. Niliaga na kuondoka huku nikitembea mithili ya mtu aliebeba mzigo mzito kichwani. Nilishindwa kulia kwasababu machozi yalikuwa yamenikauka kwahiyo macho yalibadilika na kuwa mekundu kama mvuta bangi. Nilifika nilipokuwa nimeliacha gari langu ili niweze kuwasha na kuondoka. Nilizidi kukosa amani pale ambapo nilikumbuka kuwa siku hiyo ndio siku ya hukumu ya mume wangu dhidi ya kesi iliyokuwa inamkabili kuhusu ubadhirifu wa fedha za kampuni. Sikuthubutu kujitokeza mbele ya macho ya mume wangu kwavie nilihisi ningemuumiza sana kutokana na kosa nililokuwa nimelitenda dhidi yake.

    Niliwasha gari langu ili niweze kurejea kwa Fadhili kwenda kuendelea kuwaza ninamna gani naweze kutafuta amani ya moyo wangu. Nilipokuwa njiani kumbukumbu ya wanangu Sweetness na Jordan ilinijia akilini mwangu na kuhisi kwamba ni lazima watakuwa wameumia sana kutoniona mama yao tangu siku iliyopita. Nilipofika maeneo ya ‘Kona ya banana’ simu yangu ya mkononi iliita na kunishtua sana kwasababu nilikuwa kwenye mawazo makali halafu isitoshe mlio wa simu ile sikuwa nimeuzoea. Niliichukua simu yangu ambayo ilikuwa kwenye siti ya pili na kuitazama ili niweze kufahamu aliekuwa akipiga alikuwa ni nani. Kwa bahati nzuri niliona jina la rafiki yangu Doroth ndie alikuwa akinipigia simu kwa wakati ule.

    “Halo.” Sauti ya rafiki yangu ilisikika upande wa pili.

    “Mambo vipi.”

    “Safi tu mwaya! nimesikia hukumu ya mumeo nikaona nikupigie nikupe pole shoga yangu.” nilishtuka nusura niingize gari mtaroni pindi nilipokuwa naliegesha kando ya barabara ili niweze kumsikiliza kwa umakini.

    “Jana usiku nimegombana na Enrique, nimeamua kuondoka nyumbani kwake kwahiyo sifahamu kabisa hukumu aliyoipata.”

    “Duuh! makubwa kwahiyo hukuwepo mahakamani?”

    “Sikuwepo.”

    “Basi mumeo kahukumiwa miaka saba gerezani kwa kosa alilolitenda.” Taharifa niliyoipata ilikuwa ni mbaya kama vile ya msiba. Moyo uliniuma sana kwasababu mimi ndie nilikuwa sababu ya mume wangu kuingia katika matatizo ambayo leo hii yamemuingiza gerezani. Niliumia sana kwa kitendo cha mume wangu kwenda gerezani bila kuwa na maelewano mazuri na mimi. Niliwaza nitakuwa mgeni wa nani. Nililia sana lakini haikusaidia na wala hakuna msaada wowote nilioupata pindi nilipokuwa nilikilia ndani ya gari langu. Baada ya nusu saa niliendelea na safari yangu hadi nyumbani kwa wazazi wangu na kuwaeleza kwamba mume wangu amehukumiwa kifungo cha miaka kadhaa gerezani. Wote kwa pamoja walisikitika sana. Mama yangu mzazi alidondokwa na chozi baada ya kusikia habari ile ya kufungwa kwa Enrique. Sikuthubutu kuwaeleza kwamba nilikuwa ninaugomvi na mume wangu. Wanangu nyumbani walikuwa wamebaki peke yao hawakuwa na msaada wowote. Sikuwa tayari kushuhudia wanangu wakiteseka angali nipo hai kwahiyo niliamua kurudi nyumbani kwangu kuwalea wanangu.

    “Mama mbona jana hukurudi nyumbani?” mwanangu Sweetness aliniuliza swali ambalo lilikuwa ni gumu sana kwangu.

    “Nilikuwa kwa bibi yenu moshono, anaumwa.”

    Niliendelea kuishi nyumbani kwangu lakini nilikuwa sina amani kabisa kwasababu ya ugomvi wangu na mume wangu. Nilikuwa nawaza siku Enrique akimaliza kutumikia kifungo anaweza kuja kuniua kwasababu alikuwa na hasira sana na mimi. Wakati mwingine nilikuwa natamani nijiue asinione tena machoni mwake lakini niliona sio suluhisho la matatizo niliyokuwa nayo. Kitendo cha mume wangu kutupwa sero kilinisitiri sana kwasababu hakuna mtu ambae alifanikiwa kufahamu mambo ya hirizi. Uzuri mmoja ni kwamba wazazi wake walikuwa wamekata mahusiaano kabisa na sisi kwahiyo hata kitendo cha Enrique kufungwa gerezani walisikia kwa majirani. Mwishowe niliona nibora nijishushe, nikiri kosa halafu niombe msamaha itasaidia,kuliko kuendelea kujifanya kwamba sifahamu mambo ya hirizi.

    Baada ya miezi mitatu niliamua kwenda kumtembelea gerezani kumjulia hali pamoja na kumuomba msamaha kwa yote yaliyotokea. Mara baada ya kunitia machoni alianza kulia hadi akashindwa kabisa kuzungumza chochote. Niliondoka bila kuzungumza naye jambo lolote kutokana na hisia kali ambazo zilimpelekea kutokwa na machozi kwa uchungu sana. Baada ya muda nilijaribu kwenda kwa mara nyingine nikiwaza pengine hasira yake inaweza ikawa imetulia kidogo. Bado ilishindikana kwasababu alishindwa kuzungumza kabisa na kuishia kulia kwa hasira sana. Jambo hilo lilininyima raha kwasababu licha yaa juhudi nyingi za kumbembeleza na kumuomba msamaha kwa yote yaliyotokea lakini bado hakuweza kudhibiti hisia zake za uchungu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Ugumu wa maisha nyumbani kwangu uliashiria kwamba hata watoto waliokuwa nje ya nchi kimasomo watarudi nyumbani kwasababu pesa zakuendelea kuwasomesha nje ya nchi hazikuwepo kabisa. Babu Ben alininunulia simu nyingine pamoja na kunipatia pesa kwaajili ya manunuzi ya mambo mengi madogomadogo ya pale nyumbani kwangu. Nilikwenda gerezani kwa mara ya tatu ili niweze kutimiza adhma yangu ya kuomba radhi. Enrique alifanikiwa kuzungumza na mimi mambo kadhaa kwa uchungu mkubwa.

    Uhuru uliokuwa unautafuta najua umeupata, ahsante kwa yote ulionitendea, nafikiri umetimiza dhamira yako ya kunisweka rumande ili uweze kufanya mambo yako kwa uhuru zaidi, nakutakia kila la heri ila hakikisha kwamba watoto wangu hawateseki.” Kwa masikitiko makubwa sana Enrique alizungumza huku akilia sana. Hakika maneno aliyokuwa anazungumza mume wangu huku akilia kwa uchungu yalinifanya nijisikie vibaya kupita maelezo, Nilijutia kosa langu. Nilimuonea huruma sana kwasababu afya yake ilionyesha kudhoofu zaidi ya kipindi alipokuwa akihudhurua mahakani. Majukumu ya familia yalinielemea nikashindwa kujua cha kufanya hata muda wa kukutana na Fadhili niliukosa kabisa. Nilikuwa nahangaika huku na kule kufuatilia miradi ya mume wangu ili niweze kuhakikisha kwamba watoto wanaendelea na shule bila shida yeyote. Pamoja na jitihada zote nilizojaribu kuzionyesha ili miradi yake iweze kuendelea kukua lakini haikuwezekana kabisa kwani yote kwa pamoja zilidorora na kuniacha njia panda. Kila nilichokipanga kiligoma nikahisi pengine huwenda ndugu wa mume wakawa labda waliniendea kwa mganga ili kunikomoa lakini sikuweza kupata jibu. Ilipotimu mwaka wa pili mume wangu akiwa gerezani nilishindwa kabisa kuwalipia wanangu karo za shule kwasababu miradi yote ilikuwa imeporomoka. Nilipata wazo la kuwapelekeka katika shule za kata. Hivyo basi nilikwenda Kenya na kuwachukua Dylan na Logan na kuwaamishia katika shule iliyokuwa jirani na nyumbani kwangu. Nilifanya hivyo pia Sweetness na Jordan. Maisha yalizidi kuwa magumu kwasababu sikuwa na msaada wowote. Nilikonda sana hadi nikawa naogopa kujitazama kwenye kioo. Siku zilizidi kusonga japo kwa shida sana, mara kwa mara nilikuwa nakwenda gerezani kumsalimia mume wangu na kumweleza maendeleo ya familia. Enrique alikuwa na moyo wa ajabu sana, pamoja na mambo yote niliyokuwa nimemtendea alitangaza kunisamehe kabisa. Nilifarijika sana baada ya mume wangu kunieleza kwamba amenisamehe na kunionya nisirudie kufanya jambo kama lile.

    Alinisisitiza nimtegemee Mungu kwasababu yeye ndie muweza wa kila jambo kwani hajawai kushindwa na lolote na wala hatakaa ashindwe na jambo lolote. Kiukweli gereza lilimbadilisha sana mume wangu kwani imani yake ilikuwa zaidi na zaidi. Nililigundua hilo kwa kipindi chote nilichokuwa nakwenda kumtembelea gerezani. Mwaka wa tatu ulikatika mume wangu akiwa bado yupo gerezani, nilianza kuandamwa na homa za kila mara. Wasiwasi ulinizidi ndani ya nafsi yangu kwasababu nilikuwa siishi kuumwa kila mara. Maradhi ya mara kwa mara yalisababisha nipate ujasiri wa kwenda kituo cha ushauri na saha ili kupima afya yangu



    Niliamka asubuhi na mapema na kuwaandaa watoto na kwenda shule baada ya hapo nilikwenda moja kwa moja kucheki afya yangu. Njiani nilikuwa nawaza sana namna ambavyo nitaishi endapo nitajikuta nimeathirika. Niliwakumbuka wanaume wote ambao niliwahi kulala nao tena bila kinga. Jasho lilinitoka mwili mzima kutokana na kasi ya mapigo ya moyo. Nilimwomba Mungu sana aweze kuninusuru nisiwe nimeathirika. Nilinyong’onyea zaidi nilipokumbuka tukio la kubakwa miaka mitatu iliyopita. Niliona endapo nitaelezwa nimeathirika ningeweza kupoteza maisha kwa mshtuko. Nilifika salama angaza nikiwa tayari najihisi kuchoka sana. Nilipokelewa vizuri na mtaalamu mmoja ambae alijitambulisha kwa kwa jina la Mollel. Baada ya kueleza nia yangu ya kutaka kupima alianza kuzungumza na mimi mambo kadhaa ambayo ilipunguza hofu niliyokuwa nayo moyoni mwangu kwa asilimia zaidi ya 80.

    Baada ya kufanyiwa vipimo nilisubiri majibu kwa muda kidogo. Woga ulikuwa umenipungua kwa kiasi kikubwa nikawa natamani nipate majibu yangu kusudi niweze kujua nimeathirika ama la. Muda wa kupokea majibu ulifika ambapo nilirudi tena kwenye chumba cha mshauri kwenda kupokea majibu ya afya yangu. Mshauri alinieleza kwamba nimeathirika. Nilishtuka ingawa haikuwa sana kwasababu nilikuwa nimeshajiandaa kupokea majibu yale kutokana na ushauri niliokuwa nimepatiwa mara ya kwanza.

    CD4 zangu zilikuwa zimeshuka sana kwahiyo nililazimika kuanza kutumia ARV’s haraka iwezekanavyo ili kuweza kupandisha kinga ya mwili wangu. Mshauri alinisisitiza nizingatie yale aliyonieleza, ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi mara kwa mara, kula matunda na mboga za majani kwa wingi. Nilirudi nyumbani kwangu nimenyong’onyea huku nikiwaza ugonjwa ule nilikuwa nimeambukizwa na nani? Akili yangu ilinituma kwamba ugonjwa huo itakuwa niliambukizwa na wale wabakaji au babu Ben kwasababu ndio watu ambao sikuwa na imani nao. Nilijisikia kuumia zaidi kwani niliwaza itakuwa nimemuambukiza Fadhili kwasababu ndie mtu ambae nilikuwa nae kwenye mahusiano hata baada ya kubakwa. Kichwa kiliniuma zaidi baada ya kumkumbuka mume wangu na kuwaza je itakuwaje endapo atagundua kuwa nimeathirika?

    “Je nimpelekee taharifa gerezani? Hapana! Siku akitoka atakuja kuniua.” Niliwaza mambo mengi sana hadi nilipofika nyumbani kwangu nikiwa nimechoka sina hamu na kitu chochote. Niliona kama dunia imenielemea. Wakati mwingine kutokana na kuwaza sana hatma ya maisha yangu nilikuwa nikiona kama picha ya majeneza mbele ya macho yangu. Niliona ndio kifo kinanijia kwasababu hali ya uchumi nayo ilizidi kuwa mbaya sana pale nyumbani kwangu. Nilikata tamaa ya maisha. Kwa asilimia mia moja nilizidi kuamini kuwa wabakaji ndio walioniambukiza VVU kwahiyo moyo wangu ulijenga chuki na wanaume wote. Nilianza kuwachukia sana wanaume. Sikutamani kuwaona wakiendelea kuishi kwasababu niliona roho zao ni za kikatili sana. Nilianza kuwanza namna ya kuweza kulipa kisasi kwa wanaume. Lakini nilikosa kabisa namna ya kuweza kumwaga damu zao bila kutiwa kwenye mkono wa sheria.

    Nilianza kutumia madawa ya kupunguza makali kwa siri, baada ya muda mfupi hali yangu ilibadilika na kurudi kuwa kama zamani. Sura yangu ya mvuto ilirudi kama awali jambo ambalo lilifanya wanaume waanze kunishobokea upya. Sikupoteza muda niliona hiyo ndio njia pekee ya kuweza kulipiza kisasi kwa kuwaambukiza kwa makusudi. Nilifanya hivyo kwa kuanza na babu Ben, pamoja na wanaume wengine kadha wa kadha.

    Kiukweli niliingiwa na roho ya kinyama sana kwasababu sikuwa na huruma hata kidogo. Niliona wanaume wote walikuwa wamenikosea kwahiyo sikujali mkubwa wala mdogo. Nilizidi kuwa na moyo wa chuki kwa wanaume baada ya kugundua kuwa Fadhili alikuwa akiishi na mwanamke ndani ya nyumba niliyokuwa nimemjengea kwa mikono yangu. Kwa jinsi alivyokuwa ameniudhi nilitamani kama ningekuwa na uwezo niweze kumnyang’anya lakini ilishindikana kwasababu hatimiliki ilikuwa na jina la Fadhili kwahiyo niliamua kumuacha na maisha yake na mwanamke wake, Katarina.

    “Afadhali sikumueleza huyu pimbi kuwa nilikuwa nimezaa nae kwasababu nahisi angeshaniletea matatizo kwa jinsi kichwa chake kinavyoonekana kuwa na akili kama ya kuku.” Nilizungumza kwa hasira baada ya kusalitiwa na Fadhili.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Baada ya miaka mingine mitatu nilikuwa nimeshalala na wanaume wengi sana hata idadi yao sikumbuki. Ilibaki mwaka mmoja ili mume wangu aweze kumaliza kifungo na kurudi uraiani, ingawa nae nilipanga kumuambukiza kwa makusudi kwasababu yeye ndie kasababisha yote kwa kushindwa kunitimizia haja zangu za ndoa. Hasira ilinizidi baada ya kukumbuka majibu ya dharau aliyokuwa ananijibu kipindi nilipojaribu kumweleza kuwa haniridhishi kimapenzi. Nilifikia tamati kwa kuona kwamba hana sababu yeyote ya kuepuka mkono wangu wa kisasi dhidi ya wanaume.

    Miaka saba ilikatika na mume wangu alitoka gerezani na kuja nyumbani. Alifurahi sana alipokutana na watoto wake. Hakujua pa kuanzia kwasababu miradi yote ilikuwa imeporomoka. Mambo yalizidi kuwa mabaya sana. Alipata wazo la kwenda nyumbani kwa wazazi wake kwenda kuwaomba radhi kwa yote yaliyowahi kutokea kipindi cha nyuma. Wazazi wake walitangaza kutusamehe sote na kututakia baraka tele. Siku chache baada ya msamaha wa wazazi, mume wangu alipata kazi katika kampuni nyingine ya simu na maisha yalianza kuwa mazuri kwani pesa za kula zilikuwa hazipigi chenga. Nilizidi kutumia madawa yangu ya kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI bila mume wangu kugundua chochote. Kwa wakati huo niliendelea kushiriki nae tendo la ndoa bila kujua nimeathirika. Hasira dhidi ya wanaume ilizidi kuniandama kwasababu nilizidi kuendelea kuwaambukiza bila huruma.

    Siku moja wakati nipo nyumbani nafanya shughuli zangu ndogondogo nilishtuka sana mara baada ya kudowload video niliyokuwa nimetumiwa na rafiki yangu Doroth kwenye simu yangu kwa njia ya whatsapp. Ilikuwa ni video iliyokuwa inaonyesha nikifanya mapenzi mubashara na Derick. Moyo ulianza kunienda mbio ikanibidi nimpigie simu Doroth ili niweze kumuuliza ameipata wapi video ile.

    “Nimeikuta mtandaoni, hadi mwenyewe nimeshangaa kwanini umeamua kujidhalilisha kiasi hiki.” Mara baada ya kusika maneno ya Doroth nilikata simu na kuamua kumpigia Derick ili niweze kumuuliza kwanini ameamua kufanya vile.

    “Krii! Krii!” simu iliita upande wa pili na kupokelewa muda huohuo.

    Huku nikilia mithili ya mtu aliyechanganyikiwa nilimuuliza kwanini ameamua kuweka ile video ya kutudhalilisha mtandaoni.

    “What? Video? Mtandaoni? Oooh nimekwisha!” Yalikuwa ni maneno aliyoyatamka Derick baada ya kumpa taharifa ile.

    “Hacha unafiki wewe, inamana hiyo video imejipost mtandaoni au umeamua kufanya makusudi ili uweze kumpata mwanao Sweetness.” Nilizungumza kwa hasira sana kwasababu video ile ilikuwa inaonyesha tayari imeshaangaliwa na watu zaidi ya 20,000 ndani ya masaa mawili.

    “Naomba uelewe siwezi kufanya huo upuuzi kwasababu hata mimi nadhalilika pia. Video haionyeshi sura yako mwenyewe bali hata yangu inaonekana pia. Kompyuta yangu sipo nayo kwa sasa niliipeleka kwa fundi siku tatu zilizopita akanibadilishie screen (kioo) kwasababu ilikuwa imevunjika. Kwahiyo nahisi labda huyo fundi ndie kavujisha hiyo video mitandaoni. Ila nitahakikisha namburuza mahakamani kwa kosa alilolitenda kwasababu kompyuta yangu sijawai kumpa mtu yeyote tofauti na yeye. Hawezi kunidhalilisha kizembezembe namna hii naomba niwai nikatoe taharifa polisi muda huu.” Derick alizungumza maneno ambayo yalionesha wazi hausiki katika suala la kuvuja kwa video ile. Watumiaji wa facebook, whatsapp walizidi kuifurahia video ile na kusababisha kusambaa kwa kasi ya ajabu. Nilitamani ardhi ipasuke inimeze nipotee kabisa katika uso wa dunia, kwasababu nilijiona sina thamani tena mbele ya kiumbe chochote.

    “Kwa hili Enrique hataweza kunisamehe kabisa. Ni lazima ataniua.” Niliwaza huku nikitetemeka kwa hofu sana kwasababu nilijua ni lazima itakuwa tayari ameshaaipata kwasababu kunaakundi moja la whatsapp ambalo huwa tupo mimi na mume wangu na tayari video ilikuwa imesharushwa humo. Meseji za malalamiko kutoka kwa watu mbalimbali zilianza kumiminika katika simu yangu.

    “Kwa nini unadiriki kujidhalilisha kiasi hicho.” Huo ni mfano wa jumbe fupi za maandishi zilizoonyesha kuingia kwa kasi katika simu yangu ya mkononi. Nilitamani kuipasua simu yangu ili nisiweze kupokea zile meseji zilizokuwa zinazidi kunipanikisha. Sura yangu ilionekana vizuri sana katika video ile kuliko hata ya mwanaume. Sikuwa na namna yeyote ya kuweza kujitetea kuwa sio mimi ndie niliekuwa kwenye video ile. Jioni ilipofika mume wangu alirudi nyumbani akitokea kazini kwake. Hakuonyesha tofauti yeyote ile nikahisi pengine labda hajakutana na video ile. Siku iliyofuata aliamka na kuniaga na kwenda kazini kama kawaida.

    ******************

    Enrique alikuwa na maumivu makali sana moyoni mwake. Aliumia sana kutokana na kitendo alichokuwa amekifanya mke wake wa ndoa. Video ya ngono inayomwonyesha mke wake akiliwa uroda na jamaa mwingine aliiona mtandaoni. Alikasirika kuliko siku zote alizowahi kukasirika. Alitamani amuuwe mke wake kwa kosa alilokuwa amelitenda, hakuona sababu ya mke wake kuendelea kuishi hapa duniani angali ni wa kumuumiza mara kwa mara.

    “Yeye ndie sababu ya mimi kufungwa, yeye ndie sababu ya mimi kugombana na ndugu zangu, yeye ndie sababu ya mimi kutokufikia malengo yangu kwa wakati. Kama anaweza kufanya hayo yote, inawezekana pia hata watoto ninaohangaika nao kila siku kuhakikisha wanapata elimu bora wakawa sio wa kwangu, kwahiyo ninakila sababu ya kwenda kuwapima DNA ili niweze kujua kama ni wangu ama la! ila endapo nitakuta ambae sio wangu nitampiga risasi yeye pamoja na mama yake na mimi nitajimaliza.” Hayo ndio mawazo ya Enrique mara baada ya kukutana na video ya ngono iliyokuwa ikimwonyesha mke wake aliefunga nae pingu kanisani tena kwa harusi ya kifahari.

    “Ila nitakaporudi nyumbani sitamwonyesha kuwa nimefahamu jambo hili kwasababu ataweza kutoroka na kunipa kazi ya kuanza kumtafuta.” Yalikuwa ni maneno yaa Derick alipokuwa kwenye gari yake akirudi nyumbani siku hiyo. Siku iliyofuta alikwenda kuwachukua watoto wote shuleni na kwenda nao hadi hospitali moja mashuhuri iliyopo jijini arusha kufanya vipimo vya DNA, bila mke wake kufahamu kilichokuwa kikiendelea. Walifanya pia na vipimo ya VVU. Daktari alitoa majibu kwamba watoto wote wanne hawakuwa wa Enrique jambo ambalo lilimfanya ahisi kurukwa na akili. Kibaya zaidi alielezwa kuwa ni muathirika wa virusi vya UKIMWI ingawa hakuna mtoto ambae alikuwa ameathirika na VVU. Aliumia sana, alijua moja kwa moja aliekuwa amemuambukiza ugonjwa ule ni mke wake na wala sio mtu mwingine kwasababu hakuwahi kufanya tendo la ndoa nje ya ndoa yake. Aliwatazama wale watoto kwa hasira sana.

    Aliwaza pesa zake alizotumia kwenda kuwasomesha nje ya nchi. Aliwaza namna ambavyo alikuwa akipigana usiku na mchana ili watoto wapate chakula, kumbe hawakuwa wanae. Alijiuliza ni kwanini mke wake aliamua kumfanyia ushetani mkubwa namna ile ili hali alifanya kila kitu ambacho mwanaume anapaswa kufanya. Mawazo mengi aliyowaza yalimpelekea kupandwa na hasira ambayo ilimfanya adondoshe machozi kama mtoto mdogo. Enrique pamoja na watoto wote walianza safari ya kurudi nyumbani. Alijikatia tamaa kabisa, hakuona sababu ya kuendelea kuishi, aliona ni bora afe kuliko kuendelea kuishi katika dunia hii ambayo inampa maumivu kila mara. Aliendesha gari kwa spidi ambayo hakuwai kuendesha tangu alipojua kuendesha gari.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    “Daddy! It seems like your not fine, why?” (baba! unaonekana haupo sawa, kwanini?) Sweetness alijitosa kumuuliza baba yake swali baada ya kuona muonekano wa baba yake sio wa kawaida. Hawakujua kilichokuwa kikiendelea kwasababu majibu ya vipimo vya DNA alipewa baba wakati akiwa peke yake.

    Iam not your dady. (mimi sio baba yenu.) Enrique alimjibu mwanae kwa hasira jambo ambalo lilifanya watoto waingiwe na hofu na kuanza kuogopa. Mwendo kasi wa gari uliishia kandokando ya duka moja lililopo maeneo ya pepsi ambapo alisimamisha gari na kuingia dukani na kununua pakiti moja ya sigara. Japo kuwa haikuwa kawaida yake kuvuta sigara lakini siku hiyo alikwenda dukani kununua. Baada ya hapo alirudi kwenye gari kuendelea na safari ya kuwahi nyumbani kwenda kuitoa roho ya mke wake.

    “Daddy! Why are you smoking cigarette while its dangerous for your health?” (baba! Kwanini unavuta sigara wakati ni hatari kwa afya yako?) Daylan alizungumza na baba yake kwa upole na kujikuta akiambulia kofi la nguvu lililopelekea mashavu ya mtoto kuvimba. Kitendo kile kilisababisha watoto wote waanze kulia baada ya kuona kuwa baba yao amepoteza kabisa ubinadamu. Enrique hakujali alizidi kuvuta sigara yake huku akiendesha gari kwa mwendo mkali. Akili yake ilikuwa inawaza bastola aliyokuwa ameihifadhi chumbani kwake ndio ilikuwa suluhisho la matatizo yaliyokuwa yamejitokeza kwa wakati ule.

    ************

    Ukimya aliouonyesha Enrique siku iliyopita ilimfanya Teddy ashinde siku nzima bila kula wala kunywa na kubaki na mawazo mengi akilini mwake. Aliendelea kuwaza inawezekana vipi ikawa mume wake hajaona video ile mpaka muda ule wakati kuna baadhi ya ndugu wa mume wake walishampigia simu na kumlaani kwa kitendo alichokifanya. Aliona kuendelea kuishi kwa Enrique ni kujihatarishia maisha ni bora atoroke na kwenda kusikojulikana kwasababu mume wake anaweza kumtoa roho. Aliingia chumbani kwa mume wake kuangalia kama atapata pesa kidogo za kumsaidia mbele ya safari kwasababu hakuwa na chochote mfukoni mwake.

    Alibahatika kukuta shilingi elfu sabini kwenye mfuko wa suruali aliyokuwa ameivaa mume wake siku iliyopita. Alichukua na begi dogo la nguo na kuanza kutoka chumbani lakini muda huohuo alisikia mlio wa gari ya mume wake jambo ambalo lilimtia wasiwasi sana juu ya ujio wa mume wake kwa wakati ule. Aliamua kuhairisha safari kwasababu hakuwa na pakutokea kwahiyo alirudisha lile begi dogo alilokuwa amechukua kwaajili ya kumtoroka mumewe. Alikwenda kumfungulia mume wake geti kwasababu alikuwa ameshapiga honi kwa mara kadhaa. Baada ya kufungua geti gari liliingizwa na kuegeshwa katika sehemu ya kawaida ya kuegeshea magari.

    Teddy alishtuka sana baada ya kusikia sauti ya wanae wakiwa wanalia ndani ya gari. Moyo ulianza kumwenda mbio. Baada ya Enrique kushuka kwenye gari ndipo ambapo Teddy aligundua kuwa ujio wa mume wake haukuwa wa amani, alikuwa akimtazama kwa hasira hadi machozi yanamtoka. Teddy alianza kulia kujitetea ili mume wake apunguze hasira aliyokuwa nayo.

    “Hile video sio yakwangu mume wangu, yule mwanamke kafanana tu na mimi. Naomba unisamehe.” Teddy alizungumza huku akilia kwa uchungu baada ya kuhisi kuwa pengine labda ndio ilikuwa imemkasirisha mume wake. Teddy alitembea kwa magoti hadi ndani akimuomba mume wake msamaha huku akilia sana. Baada ya kufika ndani Enrique aliwaacha watoto sebuleni wakiwa na sare zao za shule huku wakiendelea kulia. Teddy alitumia ile nafasi kupiga simu kituo cha polisi kuomba msaada baadaa ya kuhisi hali ya hatari kutoka kwa mume wake. Enrique alikwenda chumbani na kuangalia alipokuwa ameificha bastola yake na kuikuta ipo salama kabisa. Akili yake ilikuwa inawaza mauti na sio kitu kingine. Alirudi sebuleni akiwa ameishika bastola yake mkononi na kumkuta mke wake pamoja na watoto wamekaa kwenye sofa huku wakiendelea kulia.

    “Naomba uniambie hawa watoto ni wa nani.” Enrique alizungumza kwa hasira akimtaka mke wake aseme wale watoto walikuwa ni wa nani kwasababu tayari alikuwa ameshafahamu kuwa hakuwa na mtoto hata mmoja kati ya wale watoto wanne.

    “Wote ni wa kwako mume wangu.” Baada ya Teddy kuzungumza kauli hiyo alijikuta anaambulia risasi ya paja kutoka kwa mumewe jambo ambalo lilimfanya ajihisi maumivu ambayo hakuwai kuhisi hata siku moja maishani mwake.

    “Risasi ya pili nakupiga kichwani. Nieleze hawa watoto ni wa nani.” kutokana na usiriazi aliokuwa nao Enrique ilibidi Teddy azungumze kila kitu ili asiweze kupigwa risasi ya kichwa kama ambavyo alipewa taharifa. Enrique alizidi kuumia sana baada ya kusika kuwa yule mwanaume aliyopo kwenye video ndie aliekuwa baba yake na Sweetness. Hasira ilizidi kumpanda kwa kasi ya mwanga baada ya kufahamu kuwa watoto wengine waliobakia walikuwa ni wa mlinzi wake wa getini ambae aliwahi kumpa mimba mfanya kazi wake a ndani. Maneno ambayo Enrique alikuwa akiyasikia kutoka kwa mke wake yalisababisha apandwe na hasira kali ambayo ilimfanya atetemeke kama mgonjwa wa homa.

    Umeenda kwa mganga kunifanya ndondocha ukaona haitoshi, ukaona bora unizalie nje ya ndoa, ukaona nayo haitoshi ukaona uniletee na UKIMWI, no! no! I have to kill you (hapana! Hapana! Napaswa kukua.)

    “Hapana baba usimuue mama.” Sweetness alizungumza maneno machache kumtetea mama yake lakini maneno yake yalisababisha awe wa kwanza kupigwa risasi ya kichwa na kudondoka chini. Mwili wa Dylan ndio ulikuwa wa pili kudondoka chini baada ya risasi kupenyeza kwenye ubongo wake. Miili ya watoto iliyokuwa ikianguka chini kama magunia ilisababisha Teddy kudondoka chini na kupoteza fahamu kwasababu hakuaamini kabisa kilichokuwa kikitokea mbele ya macho yake. Logan na Jordan walikimbilia chumbani baada ya kuona wenzao wamepigwa risasi na kupoteza maisha lakini huko napo hapakuwa mbali kwani Enrique aliwafata na kuwatwanga risasi wote.

    Mara baada ya kuhakikisha amemaliza kuwaua watoto wote alikwenda sebuleni alipokuwa mkewe amezimia. Kabla hajampiga risasi alisikia king’ora ya gari la polisi lililokuwa limekuja na kuchuna breki nje ya geti lake. Bila kupoteza muda alitizama chini alipokuwa amelala mkewe na kumpiga risasi harakaharaka kisha na yeye kujipiga risasi ya kichwa. Polisi walifanikiwa kuingia ndani na kukutana na maiti zikiwa zimelala chini. Hali ilikuwa ni ya kutisha sana kwani nyumba ilikuwa inanuka damu kwa jinsi damu ilivyokuwa imesambaa nyumba nzima. Polisi waligundua kuwa Teddy alikuwa bado hajapoteza maisha kwahiyo walimuwaisha hospitali harakaharaka ili kuweza kuokoa maisha yake. Enrique pamoja na watoto wote walipakiwa katika gari la polisi na kupelekwa mochwari.

    *************

    Mama yake Teddy baada ya kusikia kilichokuwa kimetokea nyumbani kwa mwanae alishikwa na kiharusi na kupoteza maisha. Kila mtu aliesikia habari ya mauwaji yaliyokuwa yametokea alisikitika sana. Miili ya marehemu ilionyeshwa katika taharifa mbalimbali za habari nchini. Hakuna alieweza kubahatika kufahamu sababu halisi ya kutokea kwa mauwaji yaliyokuwa yametokea. Kila mtu alikuwa anasema lake. Polisi waliendelea na uchunguzi ili kuweza kubaini sababu ya Enrique kuwauwa watoto wake na yeye kujitoa uhai huku mke wake akiwa hospitali anapumulia mashine. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha alitoa ufafanuzi kwamba mwanamke ambae anadhaniwa kuwa ndie mke wa marehemu alipiga simu kituo cha polisi cha jirani na kuomba msaada. Polisi walikwenda kwa haraka lakini kwa bahati mbaya walikuta mauwaji yameshafanyika. Kamanda huyo aliwataka wananchi kutokuchukua sheria mkononi kwasababu vyombo vya dola vipo kwa ajili yao. Wazazi wa Enrique waliumia sana baada ya mwanao kupoteza maisha. Flora na Zubeda walipoteza fahamu kwa siku tatu baada ya kusikia taharifa ya kifo cha kaka yao mpendwa. Hakuna aliekuwa anaamini kilichokuwa kimetokea ilikuwa ni kama filamu ya kimarekani. Kilichowashangaza watu wengi ni kwamba Enrique alikuwa ni mpole sana asie penda fujo ya aina yeyote. Walishindwa kuhusianisha mwonekano wake wa awali pamoja na kilichokuwa kimetokea.

    **********

    Derick alisikitika mno baada ya kusikia taharifa ile kwenye vyombo vya habari. Alilia kama mtoto mdogo, kibaya zaidi aliekuwa amevujisha video ile mtandaoni hakufanikiwa kuonana nae kama ambavyo alikuwa anatamani kumkamata na kumpeleka mbele ya sheria. Fundi yule aligongwa na gari wakati akivuka barabara wakati alipokuwa ametoka kula chakula cha mchana katika mgahawa uliokuwa jirani na eneo lake la kazi. Wakati Derick alipokuwa amefika ofisini kwa yule fundi ndio alipata taharifa hizo ambazo zilimsikitisha sana.

    Pamoja na kwamba video ile ya ngono ilimfikia hadi mke wake lakini alimuomba radhi na kumsamehe. Mke wa Derick alifanikiwa kushika ujauzito na hatimae siku moja baada ya kujifungua ndio siku ambayo video ya ngono ya mume wake akijivinjari na mwanamke mwingine ilivuja. Aliumia sana lakini Derick alipokiri kosa na kuomba radhi kwa yaliyokuwa yametokea alisamehewa na maisha yaliendelea. Derick aliamua kumuita mwanae Sweetness kwasababu ya historia ya jina hilo katika akili yake.

    Baada ya Fadhili kumsaliti Teddy aliamua kutafuta kazi ya kufanya ili aweze kuhudumia familia yake ya mtoto mmoja japokuwa mke wake alikuwa tayari ni mjamzito wa mtoto mwingine. Alipata kazi maeneo ambayo ni jirani na nyumbani kwake. Kwahiyo alikuwa anaingia kazini wakati wa usiku na mchana anakuwa nyumbani kwake. Maudhurio ya kliniki yalisababisha Fadhili afahamu kuwa ni muathirika wa VVU. Aliumia sana baada ya mke wake kupimwa na kubainika kuwa ni muathirika. Lakini na yeye alipopimwa aligundulika kuwa ni muathirika wa virusi vya UKIMWI kwahiyo walipewa ushauri na saha namna yaa kuweza kuishi kwa matumaini. Mwezi mmoja baadae Fadhili alipoteza maisha baada ya kupigwa risasi na wezi waliokuwa wamevamia eneo lake la kazi. Taharifa ya mshtuko aliyoipata Katarina baada ya kusikia kifo cha mume wake kilipelekea mimba yake kuharibika.

    ***********

    Ilipita mwezi mmoja na nusu hali ya Teddy ikiwa bado ni tete katika chumba cha uangalizi maalumu (ICU) Fahamu zilikuwa bado hazijamrejea, alikula na kunywa kwa kutumia mirija maalumu, kibaya zaidi alipumua kwa msaada wa mashine. Baba yake ndie mtu pekee aliekuwa anapigana kuhakikisha kuwa mwanae anarudi katika hali yake ya kawaida kwani mamae tayari alikuwa ameshatangulia mbele za haki. Kwa jinsi hali yake ilivyokuwa mbaya hakuna mtu aliyeweza kuamini kuwa ipo siku ataweza kupona.

    Daktari alithibitisha kwamba pamoja na kwamba Teddy alipigwa risasi ya kichwa lakini ilimparaza tu, haikusababisha madhara yeyote katika ubongo wake kwahiyo kuna uwezekano mkubwa wa kupona ingawa itamchukua mda kidogo. Mwezi wa pili Teddy akiwa hospitali fahamu zilimrejea. Lakini alipokumbuka kuwa wanae ni marehemu alizimia tena ambapo alizinduka baada ya masaa matatu. Hakujua kuwa mama yake tayari nae alikuwa amepoteza maisha baada ya kusikia kilichokuwa kimefanywa na mumewe.

    Teddy aliumia sana baada ya kufahamu kuwa watoto wake wote walipoteza maisha pamoja na mama yake. Alijutia sana makosa yake, aliona alikuwa anakila sababu ya kumuomba Mungu msamaha kwa yote aliyokuwa amemfanyia mume wake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com

    “Laiti ningejua haya yote yangekuja kutokea nisingefanya ushetani niliomfanyia mume wangu kipenzi” alijuta sana huku akilia kama mtoto mdogo lakini hakuwa na la kufanya isipokuwa kukubaliana na hali.

    Mke wa Fadhili aliuza nyumba na kutokomea kusikojulikana. Wakati taratibu za msiba zilipokuwa zikifanyika ile nyumba aliyokuwa akiishi Enrique na familia yake iliuzwa na ndugu zake. Enrique na watoto walizikwa katika makaburi ya njiro. Kwahiyo Teddy hakuwa na pa kwenda hali ya nyumbani kwao ilizidi kuwa ngumu. Mawazo yalimzidi Teddy hatimae alichanganyikiwa na kuwa chizi.



    “MWISHO.”

0 comments:

Post a Comment

Blog