Search This Blog

Thursday, July 21, 2022

NINGE - 3

 







    Simulizi : Ninge

    Sehemu Ya Tatu (3)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    WAKATI naendelea kushangaa pale katika chumba kile nilizisikia hatua kwa mbali na kisha mlango ukafunguliwa. Hatua zikazidi kujongea hadi pale nilipokuwa.

    Alikuwa ni bwana mmoja nadhifu akiwa amevalia suti yake iliyomkaa vyema katika mwili wake. Alipofika pale aliketi tukiwa tunatazamana, alijifunika na gazeti kisha akaanza kulisoma huku akiamini kuwa kila alichokuwa akisema nilikuwa nasikiliza. Na kweli nilikuwa nasikiliza.

    ‘’Tarehee… hii haina maana, ila ilikuwa usiku, kijana tajwa hapo juu alimuua mama yake mzazi na kisha kujaribu kutoroka, lakini kabla hajatoroka polisi walimkimbiza na kumkamata, akiwa katika karandinga ya polisi wale majambazi wenzake walivamia ile karandinga na kumtorosha kijana huyo huku wakiua maaskari wawili na wengine wawili kujeruhiwa vibaya sana. Majambazi hao walilitupa gari la polisi mtoni ili kupoteza ushahidi. Polisi bado inaendelea na upelelezi.’’ Akasita kidogo akalitoa gazeti na kunitazama kwa sekunde kadhaa kisha akaniambia, ‘’ na kijana huyo aliyetajwa hapo juu ni wewe bwana kassim….. aisee siku hizimajambazi wana miili midogo sana…’’ alizungumza yule bwana kana kwamba anao uhakika wa asilimia mia moja na kile alichokuwa akikisema.

    ‘’BWANA Kassim, ukamuua mama ili iweje sasa. Yaani mama, kina nani walikutuma umuue mama yao, usije ukasema eti haukumuua, wakati nimehangaika kuzikata pingu walizokuwa wamekufunga…. Ehe nambie kwanini ulimuua mama yako, tena huyu mwandishi anasema kuwa ulimchomachoma visu hadi akafa…..’’ aliuliza yule bwana kisha akaliweka gazeti kando akasimama akawa anatembea huku na kule.

    ‘’Kassim, nini kilitokea hebu nielezee achana na hawa waandishi wanaoandika kitu ambacho hawajakiona huku wakiaminisha kila mtu kuwa ni kweli walichoandika….. achana na hilo gazeti nambie, nini kilitokea mdogo wangu.’’ Aliniuliza yule bwana kwa utulivu sana akaketi na kunisikiliza bila kuingilia kile nilichokuwa namueleza.

    Alinisikiliza mpaka mwisho kabisa kisha akanitazama machoni na kwa sekunde kadhaa kisha akajitambulisha.

    ‘’Naitwa Ogunde… na kama unahisi hapa bado upo Tanzania unakosea sana, hapa tupo nchini Zambia , tupo hapa kwa shughuli maalumu na zisizokuwa maalumu…. Mtu kama wewe ni wa muhimu sana kwetu. Sisi ni watu tunaousaka ukweli kisha tunauuza huo ukweli, naona kama ukweli wako una gharama kubwa sana… aaah kabla sijasahau hata mimi ni mtanzania pia, ila nipo huku kikazi, nimependa sana maelezo yako naona kama kuna kitu katika taifa letu hakiendi sawa… ikiwa tu haujanidanganya…..’’ akasita kisha akalichukua lile gazeti akafunua kila ukurasa kwa utulivu huku akisoma upesiupesi….

    ‘’mbona hawa jamaa hawajaandika kama Gadna ameuwawa, au ulimfananisha..’’ aliniuliza.

    ‘’hapana mkuu sijamfananisha ni yeye Gadna wamemuua, huku wakisisitiza kuwa awaambie juu ya kitu fulani, kuwa ni wapi kilipo.’’CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Yule bwana ambaye tayari alinieleza kuwa jina lake ni ogunde alinitazama kwa makini, kisha akawa kama anayezungumza mwenyewe.

    ‘’Ogunde ameuwawa, hii inamaanisha kitu gani hapa……’’ alisita, akasimama na kuiendea simu yake na kupiga simu, bila shaka ilikuwa kwa mtu ambaye yupo tanzania ama anayekielewa vyema Kiswahili.

    Walizungumza kwa dakika kadhaa kisha akakata simu.

    Akaiendea kompyuta akabonyeza mara kadhaa kisha akaniita, akanionyesha picha…

    ‘’huyu ni nani..’’ akaniuliza.

    ‘’Gadna…’’ nikamjibu.

    ‘’Una uhakika huyu ni gadna mdogo wangu..’’

    ‘’ndio nina uhakika…’’

    ‘’ona sasa, awali ulisema gadna amekufa, halafu unasema huyu ni gadna.. nikueleweje sasa…’’

    ‘’aah samahani ni picha ya Gadna… marehemu gadna…’’ nilimjibu ila hakutilia maanani.

    ‘’hivi unajua Gadna alikuwa na mpango wa kuwania kiti cha ubunge…. Kwa mara ya kwanza katika maisha yake.’’ Alinieleza yule bwana kisha akaendelea.

    ‘’kwa hiyo kama ameuwawa huu ni ukweli ambao utatuletea pesa nyingi sana, utarejea Tanzania ukiwa huru na mwenye pesa nzuri tu.. au hupendi pesa wewe…’’ alinihoji.

    ‘’napenda sana, na ninapenda kuwa na uhuru wangu kwa sababu mimi sijaua..’’ nilimjibu. Akanikata jicho kali sana.

    ‘’dogo nani kakueleza kuwa hapa ni mahakamani labda….’’ Alinihoji lakini hakusubiri nimpe jibu, akaendelea.

    ‘’uhuru hauji kwa maneno bali kwa harakati mdogo wangu, umekutana nasi mahali ambapo hata haujui sisi tulikuwa tunafanya nini… unachotakiwa sasa ni utayari wako katika harakati hizi za kuuwania uhuru wako, sio wewe wa kwanza kunyimwa uhuru na haki yako, sema wengine basi tu hatupendi kulalamika sana kwa sababu hakuna wa kutusikiliza…’’ alisita kidogo kisha akanitazama tena.

    Hakusema neno lolote akatoweka, akarejea baada ya dakika zisizopungua tano akiwa na jagi lililosheheni chai ya maziwa pamoja na mfuko uliobeba mkate katika mkono wake mwingine.

    Akaandaa chai tukanywa huku akiendelea kunisihi kuwa ninatakiwa kufanya maamuzi na kisha kuingia katika harakati.

    Maneno ya yule bwana yaliniweka katika fumbo kubwa maana aliyarudia rudia sana na kunifanya nianze kupatwa na hofu kubwa.

    Baada ya kupata chai alinichukua katika gari kisha akaondoka nami hadi hospitali huko nilienda kusafishwa lile kovu la kupigwa risasi.

    Akanirudisha nyumbani na mtindo ukawa vilevile hadi siku niliyopona na kuweza kusimama imara kabisa.

    Swali langu lilikuwa bado kuwa hawa watu ni akina nani na kwanini wameamua kuishi Zambia na sio Tanzania, bila shaka kuna jambo zito.

    Walinitunza kama mdogo wao hadi pale nilipopona ndipo kikaitishwa kikao.

    Lilikuwa jopo la watu wapatao kumi na moja waliovaa suti nyeusi, mimi peke yangu sikuwa na suti.

    Walikuwa wameyaziba pia macho yao kwa miwani nyeusi.

    Walinitisha sana…….

    Ilikuwa yapata saa nane usiku wakati nilipoamshwa na kuingizwa katika kikao kile……..

    Nilipoingia na kuketi kila mmoja akavua miwani yake kana kwamba walikuwa wameambiana……

    Mapigo ya moyo yalienda kasi sana……



    Ulikuwa usiku mnene haswa wakati nilipokaribishwa katika mkutano ule na watu wale ambao sikuwa bado natambua kama ni wema ama wabaya.

    Baada ya kimya cha muda kiasi huku wote wakiwa wamevua miwani zao wakiwa wametulia kabisa.

    Mmja alijikohoza kisha akazungumza.

    ‘’Kassim…. ‘’ sauti tulivu kabisa iliniita. Nikaitika na yule bwana akaendelea kuzungumza.

    ‘’hautujui sisi na hata sisi hautujui, lakini kikao hiki cha dharuyla ni kutokana na mwenzetu ambaye umezungumza naye kuna taarifa ametupatia ambayo tumeona si vibaya tukiwa hapa kwa pamoja ukatuhadithia kila kitu kama ulivyokiona.’’CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alisita kisha wote wakanitazama, ni hapo nikajieleza tena upya kabisa hatua kwa hatua juu ya tukio la mama yangu kuuwawa na jinsi nilivyomuona baba yangu akinunua kile kisu kikubwa. Nikawaeleza pia juu ya kumshirikisha taarifa ile mtoto wa mwenyekiti wa mwenyekiti juu ya jambo lile na hatimaye ghafla kujikuta nikitafutwa, katika kukimbia kwangu nikajikuta nashuhudia mauaji ya kutisha ya bwana Gdna.

    Nilipofikia hapo ndipo maswali yalikuwa mengi sana, lakini kama ilivyokawaida ukweli siku zote husimama bila kuyumbishwa, ukisema ukweli hauna haja ya kujikumbusha mara kwa mara.

    Niliusema ukweli wote huku nikijisemea kuwa iwapo ukweli ule utaniingiza matatani basi nitakuwa naonewqa tu kwa sababu sikuwa nimeua na sikuwa nimeshiriki mpango wowote mbaya.

    ‘’unaweza kulikumbuka eneo ambalo tukio hilo lilitokea na unaweza kutupeleka…..’’ alizungumza yule ambaye alionekana kuwa kiongozi wa mkutano ule wa dharau usiku wa manane.

    Nilitikisa kichwa kumaanisha kuwa nilikuwa nakumbuka kila kitu.

    ‘’sisi ni wanaharakati ambao tunaipigania Tanzania kimyakimya, kuna jambo baya sana huenda linaendelea nchini kwetu na tukiwa kama wazalendo ni sharti kuipigania nchi yetu…’’ alizungumza kwa sauti ya chini huku akihamisha macho kutoka kwangu na kwenda kwa wenzake ambao walitikisa vichwa kumaanisha kuwa wamekubaliana na hali.

    ‘’kuanzia sasa na wewe ni mzalendo, kama umeingia humu bahati mbaya basi tambua kuwa kuwa mzalendo si jambo jepesi hata kidogo, kuna watu na pesa zao na nyadhifa zao serikali ama uraiani wapo kwa ajili ya kuziba midomo ya watu wanaosema ukweli./… kama ulikuwa haumfahamu vyema gadna kabla hajaingia katika siasa alikuwa ni mzalendo na alihitaji kuendelea kuipigania nchi akiwa katika siasa lakini kuna mpuuzi mmoja naona amejaribu kumziba mdomo katika namna hiyo ya kumuua… hivyo na wewe usishangae siku ukizibwa mdomo katika namna ya kuuwawa… hi indo maana halisi ya uzalendo…’’

    Alizungumza kwa hisia kali yule bwana huku sasa akiwa ananitazama mimi tu.

    Uzalendo aliouzungumzia pale sikuuelewa kwa maana ya mbali zaidi nilielewa kwa maana fupi ambayo alinielezea.



    Naam, kikao kikafikia ukomo nikarejea katika chumba ambacho nilikuwa nikilala. Lakini sikulala sana nikashtuliwa na kuelezwa kuwa ulikuwa umefika wakati wa kuondoka.

    Nilipewa kotio zito jeusi, nikalivaa kisha nikatoka nje na kuongozana na wale mabwana hadi katika gari.ile ikawa safari ya kurejea nchini Tanzania.

    Maisha yana siri nyingi jamani, na huku nilizitambua siri kadhaa ambazo hadi wakati huu wa kuyaandika na kisha kusimulia haya najiuliza ikiwa utajaliwa kuishi miaka mingi lakini usipate kashkashi kama niliyopitia mimi basi huwezi kujua kama nyuma ya pazia kuna mambo mengi hivi.

    Gari lilitembea kwa mwendo wa kawaida hadi tukafika katika pori kubwa, huko tukashuka kutoka garini kisha wakaniongoza hadi katika kichaka fulani.

    Kabla sijaingia pale waliniita na kuninong’oneza.

    ‘’Unaingia kwa mtaalamu, hakikisha unafuata yote ambayo atahitaji wewe uyafanye…’’ baada ya kuninong’oneza vile alinisukuma ndani nikaingia na kukutana na mzee mweusi sana ambaye nilimtambua kutokana na mshumaa uliokuwa ukiwaka.

    Alizungumza lugha zake za maajabu ajabu huku akiunguruma, akanipaka majivu kichwani na kisha akaniosha uso wangu kwa maji fulani yenye harufu nzuri. Na kisha akaniamuru nitoke nje bila kugeuka.

    Nikatii alichonieleza nikatoka nje katika namna ile. Nikawakuta wale wenzangu wakiwa pale nje. Wakaingia pia zamu kwa zamu hadi wakamalizika kisha tukaondoka safari ikaendelea.

    Nilikuwa mdogo kabisa kati ya kundi lile la wale jamaa wenye miili mikubwa na wakakamavu.

    Safari ilikuwa ndefu sana, hadi waliponieleza kuwa tulikuwa tumeingia tunduma. Bado giza lilikuwa limetawala.

    Wakanieleza kuwa pale ni watu wawili pekee wanaoweza kuvuka wakiwa ndani ya gari hao wenyewe wanazo pasi za kuwaruhusu kuvuka pale, kwa hivyo sisi ambao hatuna pasi tunatakiwa kutembea kwa miguu kupitia njia ya panya.

    Niliwafuata wenzangu walipokuwa wanaelekea nikiwa nyumanyuma.

    Giza lilikuwa nene sana na nilikuwa muoga kwa sababu sikuwa najua nmi harakati zipi zinazoturejesha nchini Tanzania kwa sababu sikuwasikia wakizungumzia uhuru wangu hata kidogo.

    Tulipita katika vichaka kadhaa, tukavuka mto, na kisha kwa mbali tukaiona boda ya tunduma jinsi ambavyo ilikuwa imechangamka sana.

    Tukazidi kukaza mwendo na hapo tukaona kundi la watu kama watatu hivi kwa mbele na wenyewe wakija upande wetu.

    ‘’hao ni waTZ wanaingia Zambia, hi indo mida yao. Na kama sio waTZ hakikisha ukisemeshwqa haujibu chochjote, sisi tunajua maneno kadhaa ya watu wa huku tutajibu..’’ alinieleza yule bwana ambaye siku zote aliishi na mimi katika nyumba ile.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilitikisa kichwa kumaanisha kuwa nimeelewa, sasa hapakuwa na baridi tena kutokana na kutembea upesiupesi tena nikiwa nimetawaliwa na hofu kubwa sana.

    Tulipolifikia lile kundi wakawa kawa wanatupisha hivi tupite, lakini mmoja akapita kati yetu na hapa ndipo nikafahamu amakweli akili kumkichwa.

    Yule aliyepita katikati yetu akanifikia mimi na kujigonga kwangu, na hapo akaanza kunigombeza katika lugha nisiyoielewa, alinigombeza huku akiwa amenikaba.

    Japokuwa sikuwa nimeelewa alichokuwa anasema lakini nilihisi kama anayelalamika kuwa nilikuwa nimemkanyaga.

    Nilishindwa kusema neno lolote kwa sababu nilikuwa nimezuiwa kabisa kusema neno lolote lile kwa sababu hakutakiwa mtu anayezungumza Kiswahili pale.

    Wale wenzangu wakajaribu kunitetea huku wakimsihi yule bwana kikabila. Sikujua kabisa maana halisi ni ipi.

    Na hapo likatokea kundi la watu wengine kama sita hivi.

    Hawa sasa wakatuzunguka na kutoa mapanga na mwingine akatoa bunduki.

    Sasa walizungumza Kiswahili na hapa tukagundua kuwa walikuwa wamoja wale watu.

    ‘’Ukitikisika tu roho yako mali yetu halali kabisa..’’ walitukaripia. Nilihisi jasho kali likivuja katika mgongo wangu.

    Nikapepesa macho kutazama macho ya wenzangu ili nijue kama lile ni tukio la kawaida ama la, nikaiona hofu machoni kwa kila mtu.

    Na hapo sasa nikakiri kuwa hali ilikuwa mbaya sana. Lile halikuwa tukio dogo.

    Kuna mwenzetu mmoja alijaribu kuleta ubishi walipotuamrisha kukaa chini, yeye akagoma na kuwaambia kama wao ni wanaume wasitumie silaha zao.

    Hili likawa kosa kubwa sana mmoja akamsogelea na kumdunga sindano akatokwa na mayowe na kisha akaanza kutetemeka akatua chini kama mzigo.

    Alijaribnu kuzungumza lakini ulimi wake ukawa mzito kuliko maneno aliyotaka kuzungumza hivyo akawqa anaunguruma tu huku akitokwa na povu, na wakati huohuo mwili ukaanza kuumuka.

    Ndani ya dakika kadhaa alikuwa amegeuka kuwa na mwili mnene sana.

    ‘’bandua….’’ Aliamrisha bwanba mmoja.

    Ndugu msikilizaji kilichotokea pale hakikufaa kushuhudia kwa macho lakini tulipewa onyo kali sana kuwa iwapo mtu mmoja atajaribu kuangalia pembeni basi itakuwa zamu yake kufanywa kama yule.

    Nikatazama kwa mara ya kwanza mwanadamu akichunwa ngozi yake.

    Nilikuwa nikisikia tu hizi habari kama tetesi, sasa nilikuwa najionea mwenyewe.

    Mkojo ukanitoka….

    Nikalazimika kukaza macho kutazama kitendo kile cha kikatili kutoka kwa watu wale ilimradi nisijekuwa mtu ambaye atafuata katika dhahama ile.

    Ila hata kama sitafuata niliona kuna kila dalili kuwa hakuna hata mmoja ambaye atapona….



    JIFUNZE.



    Wanasema kuishi kwingi kuona mengi. Lakini piga goti na fanmya dua kwa Mungu ambaye unamuamini akuepushe usije ukaishi miaka mingi kisha ukaona mambo ya kutisha kama haya. Mambo ya kuogofya na kutia hofu hudumu katika kumbukumbu ya akili zetu milele, na hutufanya tuishi maisha ya mashaka na wasiwasi kila siku iitwayo leo.



    Baada ya kumchuna yule bwana ile ngozi ndipo nilipotambua kuwa wanadamu tunapendeza sana ndani ya vazi la ngozi lakini tunatisha sana tukiwa hatuna vazi hilo. Inastaajabisha pale mwanadamu anapoikataa ngozi yake na kuamua kujichubua ili afanane na fulani.

    Tuithamini ngozi tuliyopewa jama.

    Mwenzenu niliona mtu aliyechunwa ngozi, yaani kwa kipindi kifupi ntu nilikuwa nimepata bahati mbaya ya kukutana na wanadamu wenye roho za kinyama kupindukia.

    Niliendelea kutazama mwili ule usiokuwa na ngozi kwa jinsi ulivyokuwa unatisha.

    Ama kwa hakika wanadamu tunatembea na kifo katika visogo vyetu, mbaya zaidi ni kwamba ukigeuka kukitazama kisogo chako na chenyewe kinageuka. Ni hivyohivyo ilivyo ngumu kutambua iwapo kifo chako kinakuja lini.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Yule mtu ambaye alikuwa anatuongoza njia sasa hana ngozi na ni mfu.

    Baada ya bwana yule wale watu walitufunga na pingu, sijui ni wapi walikuwa wamezitoa nyara zile za serikali wale watu, baada ya hapo wakaingia nasi porini zaidi penye kiza kinene.

    Huko tuliingizwa katika kitu mfano wa handaki, wakati huo majuto yakinicheka kwa sababu tayari yalikuwa yamezaana na kufikia mjukuu nisingeweza kuyabadili kuwa kama ninavyotaka.

    Nikabaki kutawaliwa na kauli yangu maarufu ya ninge….. ninge…. Ninge.

    Lakini sikuwa nimejua kama yatakuwa haya makubwa kiasi hiki.

    Baada ya kuingizwa katika handaki lile, taa zikawashwa, zilikuwa ni taa ambazo hujazwa chaji kabla ya kutumika na baada ya kutumika, mwanga ukawa wa kutosha tu.

    ‘’Mwenye dola tunamuacha huru…’’ alizungumza bwana mmoja mweusi aliyekuwa na alama nyingi sana usoni.

    ‘’Mimi…’’ mmoja kati yetu alijibu kwa sauti iliyotawaliwa na uoga.

    ‘’Dola ngapi…’’ aliuliza kwa ukali yule bwana mweusi katili.

    ‘’DOLA kumi…’’ alijibu.

    Yule bwana akacheka kiasi kisha akaendelea kuzungumza huku akienda mahali na kufunua kitu mfano wa jokofu chakavu. Akaingiza mkono mle ndani na kisha akatoka na ngozi ya mwanadamu mbichi kabisa.

    ‘’Hii moja inauzwa dola mia moja na hamsini… wewe unasaema una dola kumi….’’ Alizungumza huku akitabasamu.

    Na bila kusubiri la kujibiwa alimvuta yule bwana mwenye dola kumi na kuondoka naye.

    Sisi tulibaki pale handakini, kule nje tukasikia kelele za maumivu makali.

    Mtu mzima akilia kwa kiasi kile pasi na shaka yoyote anapitia wakati mgumu sana.

    Ilikuwa vile, baada ya muda kimya kikatanda, na punde yule bwana akiwa ametapakaa damu mwili mzima alirejea katika lile handani ambapo tulikuwa tumebaki kila mmoja akimuomba Mungu kumuepusha na baya lolote lililokuwa mbele yetu.

    Akiwa bado na zile damuu. Allifika na kuanza kufanya kama anayekagua hivi, alifika na kuminya upande wa mashavu, kisha anaminya shingo,m na baadaye mapaja, akatufanyia hivyo wote kisha tukaanza kutenganishwa. Mimi nikajikuta nikiamriwa kutoka nje.

    Ndugu msikilizaji, ni kweli nilikuwa nimejikojolea mara kadhaa kwa sababu ya uoga lakini hii ya sasa ilikuwa zaidi ya zote zilizotangulia.

    Kifo ni kitu ambacho hakizoeleki hata kidogo, mbaya zaidi kifo ambacho unakiona kikienda kukutokea.

    Kifo cha kuchunwa ngozi.

    Niligeuka na kuwatazama wenzangu wale wababe wakiwa na nyuso za huzuni sana na wengine walikuwa wanalia.

    Kitendo cha kugeuka nyuma yule bwana akaniona, akanipiga kofi kali usoni, ukiongezea na ule uoga ambao ulikuwa umenitawala tayari nikaanguka chini.

    ‘’simama upesi….’’ Akaniamuru.

    Nikasimama lakini nikaanguka tena, akainama na kunishika mkono na kuanza kuniburuza kuelekea nje.

    Niliumia sana tumbo kwa sababu ya ugumu wa ardhi ile, nililia sana lakini ni kama alikuwa hanisikii yule bwana.

    Aliponifikisha kule nje akanimwagia maji ya baridi sana kwa wingi hadi mwili mzima ukashika ganzi.

    ‘’’’Nisamehe… nisamehe kaka…’’ nilitokwa na maneno yale kwa sauti ya chini, na sidhani hata kama alinisikia.

    ‘’Haya ondoka zako bwana mdogo..’’ alinieleza yule bwana. Kisha akaondoka na kuniacha pale.

    Dah, wale watu walikuwa wanajua ni kitu gani walikuwa wanafanya, nilijaribu kujigeuzageuza labda nitaweza kuzimama lakini sikuweza, nikatumia ujasiri wangu wa mwisho kabisa lakini hali ikaendelea kuwa tete.

    Mwili wote ulikuwa umekufa ganzi.

    Nikiwa bado nipo palepale alipita mtu mmoja ambaye bila shaka ni mwenzao. Akainama pale chini na kunieleza kwa sauti ya chini.

    ‘’jitahidi ukimbie dogo, utauwawa vibaya sana……’’ alisema huku akiwa makini kabisa kana kwamba haongei na mimi.

    ‘’siwezi hata kusimama kaka…’’ nilimjibu kwa tabu.

    ‘’Nitwa hamduni, mkazi wa dar es salaam temeke kwa azizi ali, baba yangu ni maarufu kwa jina la kibesi. Nahitaji kutoka huku pia, nataka utoroke na unisaidie kufikisha ujumbe huu… ukikamatwa tafadhali usije ukataja jina langu…’’ alizungumza kwa sauti ya chini na akionekana wazi kumaanisha kile alichokuwa akikisema, nilikuwa natikisa kichwa kukubaliana na hali kwa sababu8 hakuna kitu kingine nilichokuwa nahitaji kama sio kutoka katika mdomo wa kifo kile cha mateso makali.

    Baada ya kusema vile akatoweka, nikabaki kujiuliza huyu mtu anayo maana ipi hasa. Ameniomba nitoroke na nisimtaje wakati huo hakuna lolote alilokuwa amefanya kwangu ili niweze kutoroka.

    Nilibaki kusikitika mwili nao ukizidi kuumia kwa ganzi ile, punde akarejea akiwa anatembea upesi upesi.

    Alipofika akawa ananitukana kwa sauti ya juu matusi ya nguoni na wakati mwingine akichanganya na kikabila.

    Halafu kwa sauti ya chini alikuwa ananisemesha maneno ambayo niliyasikia vyema.

    ‘’meza hicho kidonge, ni kichungu lakini hakikisha unakimeza…’’ alinieleza na kisha akapandisha sauti na kuendelea kutukana.

    Niliogopa sana klumeza kile kidonge nilihisi kuwa yawezekana ni mpango uleule wa kunivimbisha ngozi na kisha kuichuna kilaini.

    Lakini hata kama nisingemeza kidonge kile kama kuniua wangeniua tu lazima.

    Nilikipokea mdomoni na kukimeza.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kweli kilikuwa kichungu sana, lakini nilikimeza huku nikikumbuka kumsihi Mungu asinipe hukumu ya kufa kwa kuchunwa ngozi.

    Nilipokimeza nikaanza kuhisi muwasho katika mwili wangu. Nikakata tamaa na kutambua kuwa nilikuwa naanza kuwashwa ngozi na kisha itavimba halafu watanichuna.

    ‘’naondoka na wewe ondoka, hii njia mbele wewe nyoosha moja kwa moja….’’ Alinieleza kisha akaondoka, nikajaribu kusimama.

    Naam nguvu zilikuwa zinarejea katika mwili wangu kwa kasi.

    Ile nataka kusimama nikamuona yule mtu ambaye awqali alinimwagia maji akipita.

    ‘’simama uondoke umeachwa huru bado unagalagala..’’ alinidhihaki kisha akaondoka.

    Nilipotazama mbele alikuwepo HAMDUNI yule aliyenipatia kidonge, alikuwa ameweka ishara ya kidole katika mdomo wake akimaanisha kuwa natakiwa kuwa kimya kabisa.

    Nikatii huku nikianza kupata mwanga kuwa yawezekana kweli hamduni alikuwa mtu mwema kwangu.

    Baada ya yule bwana katili kutoweka hamduni akanionyeshga ishara ya kusimama na kukimbia.

    Sikupoteza sekunde, nikasimama wima nikiwa pekupeku miguuni na kuanza kutimua mbio kuelekea katika pori nisilokuwa nalielewa.

    Lakini nilikuwa katika kuiokoa roho yangu.



    Miti ya miba na mingine mikavu iliushambulia na kuupa majeraha mwili wangu lakini sasa ile hofu ya kuchunwa ngozi na watu wale ilikuwa imenifanya kusahau kabisa kama kuna kitu kiitwacho maumivu kwa kuguswa na miba na miti ile.

    Nilikimbia sana huku nikiwa sijui hata nini hatma yangu katika kukimbia kule.

    Nilikimbia hadi jua lilipoanza kuchomoza ndipo nilipoanza kutembea mwendo wa kawaida huku kila mara nikitazama nyuma iwapo kuna mtu ama kiumbe chochote kinafuatilia nyendo zangu niweze kujihadhari.

    Mkononi nilikuwa nimebeba jiwe tu kwa kujihami iwapo itabidi, nilikuwa natetemeka sana matumbo yangu, hii ilikuwa ni njaa jumlisha na uoga wa kifo.

    Ni muda ulikuwa umepita pasi na kutia kitu chochote mdomoni.

    Baada ya jua kuchomoza kwa mbali kabisa niliona umati wa watu, hapakuwa karibu na upeo wangu na nilitambua kuwa natakiwa kutembea sana ili niweze kuufikia umati ule.

    Ilikuwa heri kuufikia umati ule kuliko kuendelea kubaki katika hali ile ya kuwa peke yangu.

    Lakini pia nilikuwa ninayo hofu kubwa sana kuwa itakuwaje ikiwa hata umati ule utakuwa ni wa watu wabaya, mimi sikuwa mtu wa nchi ile na sikuwa hata na kibali cha kuwa pale, walau basi ningekuwa najua kuzungumza lugha yao ningeweza kujibizana nao wakanielewa.

    Nilijiuliza sana na mwisho nikaamua kuwa liwalo na liwe kama ni ninge nyingine inakuja mbele yangu na ije, kwa sababu naweza kuukwepa umati ule na kisha nikajikuta pabaya zaidi kisha nikasema ninge, ama naweza kwenda kwenye umati ule na kukutwa na dhahama na kisha nikasema ninge.

    Nikajikuta natabasamu na kisha nikakiri kuwa katika maisha neno ninge haliwezi kukwepeka kirahisi, wakati unadhani unalikwepa kumbe ndo unalifuata tena kwa miguu miwili huku midomononi tabasamu likichanua.

    Ziliponituma fikra zangu ndipo nilipoelekea, nikaamua kwenda katika umati ule.

    Ilikuwa safari ndefu sana hadi nilipofanikiwa kuukaribia umati ule.

    Na pale ndipo nikatambua kuwa pale palikuwa ni mpakani mwa Tanzania na Zambia, kwa jina pakiitwa Tunduma mkoani Mbeya.

    Nilimshukuru Mungu kimyakimya kwa kunirejesha katika nchi yangu tena, japokuwa sikuwa naelewa ni kwa namna gani nitaupata uhuru wangu tena ama kurejea kijijini kwetu.

    Nilipofika pale haukuwa umati mdogo kama nilivyoona kwa mbali palikuwa na umati mkubwa na palikuwa na hekaheka nyingi sana, kila mmoja akifanya ambalo limemfanya kuwa hapo.

    Labda ni mimi tu na watu wengine wachache waliokuwa pale bila kuwa na kazi maalumu ya kufanya.

    Ila kazi ilikuwa kuwajua ni akina nani waliokuwa na kazi maalumu na akina nani wasiokuwa na kazi ya kufanya eneo lile.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Njaa ilikuwa inaniuma sana na miguu ilikuwa inaishiwa nguvu kabisa, nikatambua kuwa bila kutia chochote mdomoni muda si mrefu hali yangu itakuwa mbaya sana.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog