Search This Blog

Thursday, July 21, 2022

SONONEKO - 4

 







    Simulizi : Sononeko

    Sehemu Ya Nne (4)



    ILIPOISHIA

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nami sikutaka kumwangusha mfadhili wangu huyu hata kidogo. Niliamua kuchapa kazi vilivyo mpaka yeye mwenyewe alifurahi sana.



    Sikuyapenda kabisa maisha ya kifukara ambayo nilikuwa nikiishi hapo awali. Maisha yale yalikuwa si mazuri. Ni maisha ambayo sidhani kama kuna mtu yeyote pia ambaye anapenda kuyaishi. Sikupenda kurudi huko kamwe.



    SASA ENDELEA



    Sina kumbukumbu mapenzi kati yangu na msichana mrembo na muhimu kwangu Rose yalianzaje lakini tulijikuta tukiwa tumezoeana na kuaminiana sana jambo lililozaa mapenzi kati yetu.



    Mapenzi kati yangu na Rose yalidumu kwa muda mrefu huku tukiwa tunayafurahia maisha yetu ya mahusiano.



    Jambo ambalo ninampongeza na kulifurahia kutoka kwa mwanamke huyu lilikuwa ni UMAKINI. Rose alikuwa ni mwanamke makini sana katika maisha.



    Alikuwa makini katika kila jambo alifanyalo na hii ndiyo maana nadhani amekuwa ni mwanamke mwenye mafanikio katika umri mdogo aliokuwa nao.



    “Stanley naomba twende tukapime afya zetu”. Rose aliniambia maneno hayo siku moja tukiwa tumepumzika nyumbani katika bustani nzuri ya maua.



    “Rose, kwani wewe una hofu gani nami. Mimi ninajiamini kwamba sina UKIMWI”. Nilimwambia Rose maneno hayo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hapana Stanley. Kukuomba twende tukapime sina maana kwamba nakutuhumu kwamba wewe una UKIMWI. La hasha! Bali kumbuka kuna njia nyingi ambazo mtu anaweza kupata maambukkizi ya VVU kama vile sindano zisizochemshwa, kushiriki kutumia vifaa vyenye ncha kali pamoja na mwathirika”.



    “Halafu pia, ni katika kujihakikishia usalama wa afya zetu kwani mahusiano yetu yaweza zaa ndoa hivyo ni lazima tuchukue tahadhari”.



    Mimi nilipumua kidogo kwani somo hili sasa lilianza kuniingia akilini mwangu. Mambo haya yote mimi nilikuwa siyajui. Mimi nilidhani kuwa mtu anapata UKIMWI kwa kukutana kimwili na mtu ambaye ni mwathirika.



    “Pia kuna ajali. Siku hizi ajali zimekuwa nyingi Stanley mpenzi wangu. Waweza pata ajali na ukapata maeraha na kisha damu yako ikachanganyika nay a mwenye maambukizi ya VVU huoni kwamba waweza pata maambukizi pia?”.



    “Mh! Ni kweli kabisa Rose”.



    “Pia kitu kingine Stanley mpenzi wangu, hupaswi kumwamini mtu asilimia mia moja. Je, wewe una uhakika gani kwamba mimi sina maambukizi ya VVU?”. Rose aliniuliza.



    “Lakini nikikutazama jinsi ulivyotulia na mwenye heshima nadhani huwezi kuwa na UKIMWI”.



    “Basi usimwamini mtu kwa kumtazama mwonekano wake kwani UKIMWI haupimwi kwa macho”.



    “Basi nimekuelewa Rose mpenzi wangu”.



    “Ahsante kwa kunielewa mpenzi”.



    “Lakini katika maelezo yako kuna kitu uliniacha gizani. Sikuweza kukuelewa”. Nilimwambia Rose.



    “Kitu gani?”. Rose aliuliza.



    “Katika maelezo yako ulikuwa ukitamka neno VVU, sijui ulikuwa unamaanisha nini?”. Nilimwuliza Rose.



    “VVU maana yake ni VIRUSI VYA UKIMWI. Hivyo kwa kifupi inaitwa VVU”. Rose alifafanua.



    “Anhaaa! Sasa nimekupata”.



    “Okay, sasa tunakwenda kupima lini?”. Rose alihoji.



    “Mh! Hata kesho mimi nipo tayari”. Nilimjibu Rose kwani mimi nilikuwa nikijiamini kwamba niko salama salimini.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ok, basi kesho tutakwenda kupima”. Rose aliongea.

    “Bila shaka mke wangu”.



    Tuliendelea kubadilishana mawazo pale kwa furaha, amani na upendo

    ****************

    Maisha yalienda kwa kasi huku tukiyafurahia maisha yetu ya mahusiano. Hakuna nyakati ambazo niliweza kuyafurahia maisha kama nyakati hizi.



    Mimi na Rose hakika tulipendana. Pia nahisi Rose ndiye aliyenipenda zaidi kuliko hata mimi ambavyo nilimpenda.



    Mahusiano yetu hatimaye yakapelekea kuzaliwa kwa ndoa. Mimi na Rose Tulifunga ndoa na hatimaye kuwa mume na mke. Hapa ndipo upendo wa Rose juu yangu uliongezeka maradufu.



    Nami pia nilikuwa bado siyaamini macho yangu. Yaani kutoka Stanley yule fukara kibaka mpaka kuwa Stanley milionea ambaye ana mke mzuri na mwenye pesa nyingi! Ama kweli Mungu hamtupi mja wake.



    Maisha yetu ya ndoa yaliendelea kwa furaha ileile. Mwenyezi Mungu akatubariki tukapata mtoto mmoja wa kiume ambaye tulimwita Petro.



    Mtoto huyu alizidisha upendo katika familia yetu na kutengeneza mahusiano imara kabisa.

    **************

    BAADA YA MIAKA MIWILI



    Sasa nilikuwa nimemzoea mke wangu pamoja na mwanangu. Rose nilianza kumwona ni mwanamke wa kawaida kabisa.

    Nilipokuwa nikiwatazama wasichana wabichiwabichi mtaani nikaanza kupatwa na tamaa ya kuwa nao.



    “Mimi ni mwanamume mwenye pesa sana na pia ni mwanaume wa kisasa. Ninatakiwa kuwa na wasichana wazuriwazuri wa kisasa”.



    Mawazo machafu yalianza kukipitia kichwa changu. Nayaita mawazo machafu kwani yalikuwa ni mawazo ya kisaliti ambayo yangenipelekea mimi kuanza kutoka nje ya ndoa.



    ‘Sidhani kama ni kosa kwangu kuwa na mwanamke zaidi ya Rose. All ina all itakuwa ni siri yangu ambaye katu mke wangu hawezi kuigundua. Yanipasa niyafaidi maisha bwana”.

    ****************

    “Stanley umependeza sana leo”. Maimartha katibu muhtasi wa kampuni ile niliyokuwa nafanyia kazi alinilaki siku ya leo.

    “Ahsante Maimartha. Nawe umependeza pia”. Nilimjibu huku nikichekacheka.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mh! Acha uongo wako Stanley. Mbona mimi niko hovyohovyo tu”. Maimartha alijibu huku akijinga’atang’ata vidole vyake na akinirembulia macho.



    “Mimi ninayekuona ndiye ninayekuambia. Hebu niamini. Umependeza sana”. Nilimwambia Maimartha.



    “Ahsante sana Stanley. Vipi leo twaweza kwenda pata lanchi wote au una ratiba nyingine?”. Maimartha aliongea.



    “Usijali tutakwenda pamoja. Sina ratiba ya kunifunga mchana huu”. Nilimjibu Maimartha huku nikielekea ofisini kwangu.



    Maimartha alikuwa ni msichana mrembo sana. Alikuwa na urembo ambao ulikuwa ukikodolewa macho na wanaume wengi marijali.



    Alikuwa ni mweupe kiasi mwenye sura ya mviringo na macho makubwa ambayo yalikuwa kama yanasinzia hivi muda wote akutazamapo.



    Midomo yake ilikuwa minene kiasi na pua yake ilikuwa si nene sana. Mashavu yalikuwa ya kawaida na alikuwa na vijishimo vyenye kumpendeza mashavuni ambavyo wataalamu wa mambo haya ya mahaba huviita dimples.



    Alikuwa na kiuno chembamba lakini alikuwa na milima miwili nyuma ambayo ilikuwa ikivibrate kwa mvuto kila atembeapo. Miguu yake ilikuwa ni ile waiitayo ya bia.



    Hizi ni sifa za mrembo Maimartha kwa ufupi japo alikuwa na sifa kadha wa kadha za kuvutia.



    Moyoni nilikuwa namtamani sana huyu mwanamke ila sasa nilikuwa na domo gundi. Sikuwa na ujasiri wa kuweza kumtamkia Maimartha ni kiasi gani nilikuwa nampenda.



    Niliamini tu kwamba ipo siku ningejipa ujasiri na kumtapikia yangu ya rohoni huyu mwanamke. Nilizidi kujipa moyo.



    Niliamua kuachana na mawazo juu ya Maimartha na nikaamua nichape kazi. Niliona nikiendelea kumuwaza huyu mwanamke basi ninaweza kuiharibu kazi kwa wehu wa huba.

    ***************



    “Stanley hebu agiza chochote ukipendacho na bili yote ni juu yangu”. Maimartha aliongea pindi tulipokuwa katika mgahawa fulani maarufu ambao ulikuwa jirani na ofisi yetu.



    “Hapana Maimartha. Nitakuharibia bajeti zako. Acha mimi nilipie bili yote kwani pesa ninayo”. Niliongea.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Usijali Stanley, mimi ndiye ambaye nimeamua kukupa ofa. Naomba ufanye hivyo”. Maimartha alisisitiza.



    Niliamua kuacha kubishana na Maimartha kwani hatungeweza kufika muafaka. Niliamua kukubaliana na matakwa yake.



    “Unakionaje chakula hiki Stanley?”. Maimartha alinihoji mara tu vyakula tulivyoagiza vilipoletwa na sisi kuanza kuvila.



    “Chakula ni kizuri sana na nimekipenda”. Nilimjibu Maimartha.



    “Stanley, kuna jambo moja nyeti sana napenda nikwambie”. Maimartha aliongea huku akinitazama machoni kijiko kikiwa mkononi.



    “Ongea tu Maimartha wala usijali”.



    “Lakini naomba usikasirike”.



    “Hapana. Mimi siwezi kasirika hata kidogo kwani si mtu wa hasira”. Niliongea.



    “Stanley, mimi nakupenda sana. Yaani moyo wangu haujiwezi juu yako. Nakuhitaji uwe mpenzi wangu”. Maimartha aliongea maneno ambayo yalinishtua sana kwani sikuyataraji hata kidogo.



    Sikujua nimjibu nini Maimartha kwani moyo wangu ulipatwa na mshtuko mkubwa sana wa furaha. Ni lazima moyo wangu uwe na furaha kwani ni kwa muda mrefu nilikuwa nikihitaji kuwa na Maimartha kimapenzi lakini sikuwa na ujasiri wa kumweleza.



    Sasa leo kama bahati vile yeye mwenyewe kafunguka na kunirahisishia kazi kubwa ambayo ningekuwa nayo ya kumweleza ukweli wa upendo wangu mrembo huyu wa kimataifa.



    “Lakini Maimartha, wewe si unafahamu mimi ni mume wa mtu? Mume wa bosi wako?”. Nilijibaraguza



    “Hilo nalifahamu Stanley, lakini penzi halibagui wala halichagui. Mapenzi ni upofu Stanley. Mimi sijiwezi juu yako”. Maimartha aliongea.



    “Sasa wewe unafikiri Rose akigundua kwamba mimi natoka na wewe itakuwaje? Si atakuua yule mwanamke?”. Nilimwambia Maimartha.



    “Mahusiano yangu na wewe yatakuwa ni siri yetu mimi na wewe katu mtu mwingine hatoweza fahamu. Hivyo ondoa shaka juu ya hilo. Hatokuja fahamu asilani”. Maimartha aliongea kwa sauti tamu yenye mvuto.



    Niliona huyu ndiye mwanamke wa mimi kuwa naye. Mwanamke mwenye fikra pevu za kiutu uzima.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Poa Maimartha. Nimekubali kuwa nawe. Lakini mahusiano yetu yawe siri”. Niliamua kumkubalia Maimartha.



    Lakini kuna kitu kimoja ambacho nilikisahau kwamba mapenzi daima hayana siri. Mwanzoni yaweza kuwa siri lakini yanapokuja kukolea basi huwa si siri tena.

    *************

    “Vipi mume wangu? Kazi unaionaje?”. Rose aliniuliza jioni ya leo tukiwa mezani tukipata chakula cha usiku.



    “Kazi inaenda vyema kabisa mke wangu. Namshukuru Mungu mipango yote inazidi kunyooka”. Nilimjibu Rose.



    “Ok, basi panapo tatizo usisite kunishirikisha”.



    “Bila hofu mke wangu”.



    Usiku wa leo nikiwa kitandani mawazo yangu yote yalikuwa kwa Maimartha. Mke wangu nilimwona si lolote si chochote. Huyu mwanamke kwa kweli alikuwa amekichanganya kichwa changu.



    Nilikuwa nikiyatafakari kwa kina maneno yake matamu aliyonipa mchana wa leo. Nilijiona ni mwanaume mwenye bahati kuliko wanaume wote duniani. Kupendwa na mrembo Maimartha halikuwa jambo dogo.



    “Huyu ndiye mwanamke wa kisasa ambaye ana vigezo vyote vya kuwa nami. Si huyu Rose kwani sasa yeye amekwishaeksipai”. Niliendelea kutiririkwa na mawazo lukuki.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mawazo yaliendelea kwa kasi yake ileile na hatimaye bila ya kujitambua nikapatwa na usingizi mzito. Usingizi huu uliambatana na ndoto tamutamu zilizohusisha mapenzi kati yangu na Maimartha.

    ****************

    “Mke wangu, mimi ninatoka. Nataka nikaoshe macho kidogo”. Nilimuaga Rose asubuhi ya Jumamosi hii ya leo.



    “Usijali mume wangu. Mimi nipo hapahapa nyumbani leo hii. Sitakwenda kokote”. Rose aliongea.



    “Alright basi nitaitumia hii VX ya bluu”.



    “Ok, kama mafuta hayatoshi utajaza. Nakutakia matembezi mema Stanley mume wangu”.



    “Ahsante”. Nilijibu huku nikielekea mahali lilikokuwa limepaki gari.

    Jumamosi ya leo nilikuwa na miadi na mrembo Maimartha. Miadi yetu ilikuwa ni kukutana nyumbani kwake na kuipitisha siku nzima huko tukifurahi kwa pamoja.



    Maimartha alikuwa akiishi katika mtaa wa Dolphine ambako alikuwa amepanga nyumba nzima yenye vyumba vinane.



    Alikuwa ni mwanamke wa kisasa ambaye alikuwa bado hajaolewa na alikuwa hana mchumba pia. Hii ni kwa mujibu wa maelezo yake mchana ule alipoyaleta maombi ya mimi kuwa naye.



    Nilipiga honi mara tu nilipofika mbele ya geti la jumba ambalo Maimartha alikuwa akiishi. Mlinzi alilifungua geti nami nikaliingiza gari na kwenda kulipaki katika uga wa kuegeshea magari katika jumba hili.



    Wakati huohuo Maimartha alitoka ndani akiwa katika vazi la khanga moja tu na kuja kunilaki kwa bashasha tele zilizoambatana na mabusu motomoto.



    Mwonekano wa Maimartha kwa wakati ule ulinipandisha mzuka wa mapenzi. Yaani nilitamani nimrukie na kumtafuna mzimamzima.



    “Umetoka bomb asana Maimartha”. Nilimpa sifa zake.



    “Ahsante sana Mpenzi”. Maimartha alijibu kwa sauti tamu huku akinizawadia zawadi ya busu moja matata sana.



    “Karibu sana Stanley mpenzi wangu”. Maimartha aliongea huku akiniongoza kuelekea ndani ya jumba lile.



    “Hapa ndipo ambapo ninaishi Stanley mpenzi. Karibu sana”. Maimartha alinikaribisha ndani na kunielekeza kuketi juu ya sofa moja la thamani sana.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ahsante sana”.



    Wakati huohuo Maimartha alikuja na kuketi pembeni yangu.

    Umbile la Maimartha ndani ya khanga ile lilinipandisha midadi kwa kiasi kikubwa kwani lilikuwa ni umbile lililokaa kihubahuba.



    Maimartha alijinyanyua na kuja kunikalia mapajani mwangu huku akinifungua vifungo vya shati langu. Nami bila ya ajizi nilimpokea kwa mikono yote na kumkumbatia kiuno chake.

    ******************



    ITAENDELEA



0 comments:

Post a Comment

Blog