Search This Blog

Saturday, July 16, 2022

MSICHANA WANGU WA KWANZA - 5

 







    Simulizi : Msichana Wangu Wa Kwanza

    Sehemu Ya Tano (5)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Najua haya ndio malipo ya kazi ya jana. Kazi niliyoifanya kwa majigambo huku nikiupaka moyo wa mtu vidonda kwakudhani kuwa nitalipwa tofali la dhahabu. Dah! Leo naumia, natokwa na machozi, mpaka sauti yangu imebadilika na hata kugoma kisa haya wanayoyaita mapenzi. Hakika ndani ya maisha yangu sikuwahi kutaraji kufungua ukurasa wa maumivu hata kidogo. Kweli nimeamini. Ukiua kwa upanga nawe utakufa kwa sime.



    Erick.. Erick.. I hate you. Ona leo umechafua mboni za jicho langu la upendo. Nasikitika sana kuutoa udhu wangu na kukimbia kwenye penzi lakweli eti kisa tamaa ya Kipaji.



    Nilikuwa nikijidanganya kuwa, mpenzi bora ni yule mwenye kipaji na ndio maana nilikung'ang'ania.. Iko wapi ile maana ya nyimbo nzurinzuri ulizokuwa ukinitungia. Yako wapi yale maneno matamu uliyokuwa ukinitamkia.. Kumbe unajua kuimba mapenzi lakini hujui kupenda. Kumbe unajua kubembeleza lakini hujui kuhurumia. Siwezi kukulaumu wewe kwakunitendea haya kwani niliyataka mwenyewe.



    Kila siku nilishauriwa kuwa hunifai, lakini mimi niliyaamini mashairi yako kuliko maneno ya marafiki zangu wa karibu. Ona.. Umenitolea usichana wangu mbele ya shuka lako jeupe na kubakisha alama ambayo unaishi ukiionesha mbele ya rafiki zako ili kunidhalilisha zaidi.



    Ulinifanya nikamchukia Nurdin wangu kwakuwa hakuwahi kunitaka kimwili, na ukanifanya ni muone kama sio rijali baada ya wewe kunifunza mambo ya baada ya ndoa na kunifanya niwe mtumwa kwayo. Hakika wewe ni firauni. I hate you more than you think.



    Umenidhalilisha sana." Ni sauti iliyosikika ndani ya chumba kimoja. Sauti hiyo ilikuwa ikiongea kwa hasira zenye malalamiko huku mwenye sauti hiyo akiendelea kufanya shughuli ya kuchanachana barua mbalimbali za mapenzi pamoja na picha nyingi za mpenzi wake ambae kwa sasa ni kama hayupo nae. Bila shaka msichana yule alikuwa simwingine bali ni Sumaya.





    . Akiwa kwenye harakati za kuendelea kuchana zile picha pamoja na barua za Erick Mavoko mara akakutana na moja kati ya kadi aliyotumiwa na Nurdin kipindi cha pendo lao. Aliitazama mara mbilimbili kwa nje kisha akaamua kuifunua kwa ndani iliaweze kuona kilichoandikwa kwandani.



    '' Hivi ninini? naomba unijibu Sumaya... ninini hasa? Je ni nywele zako ndizo zinazonifanya niumie zaidi na niteteleke ilhal nahitajika kwenda shule? Au sura yako ndio inanifanyanisitamani kuwa mbali nawewe? sumaya.... naomba unijibu nasio kusoma tu kadi hii.. ndio, naenda lakini naomba chunga ahadi yako. kumbuka maneno uliyo yaandika kupitia wino wako wa mdomo. Yote yalikaa vizuri na yamehifadhiwa katika daftari la mapenzi lililopo ndani ya moyo wangu. Najua unanipenda na hata lakini najaribu tu kukukumbusha kwani ajali huja hata kwenye tahadhari. Tafadhari, zalisha msimamo wako, heshimu ahadi zako, thamini pendo lako na ulitunze kwani hakuna atakae kufuata na kukutunzia. Sumaya, tambua wazi kuwa mapenzi ni kama vita hivyo nakukumbusha tu, usisahau kutumia silaha yako mbele ya maadui watakaohitaji kulivuruga penzi letu. Nakuaga mpenzi wangu huku nikiamini ipo siku nitarejea na kwa uwezo wa Mungu tutatimiza yote tuliyopanga.



    Amini kila kitu kitamu kinaweza kuwa sumu hivyo usipumbazwe na hao wasiyo penda pendo letu. Watakapofika waambie kuwa wewe ni wangu tu. Walimwengu wapo wasiyopenda kuona upo nami hivyo nijuu yako kulihifadhi pendo langu. nina mengi yakusema lakini hatakama nitayasema hayawezi kuenea kwenye kadi hii. Baki salama mpenzi wangu. mwaaaah!!!!'' Ni maneno yaliyosomeka katika kadi ile aliyokuwa akiisoma Sumaya, ni kadi iliyo yarejesha machozi yake. Ukurasa wa pili wa lawama aliufungua na kuanza kujilaumu. Aliendelea kujiona kama ni mkosaji kwa kutoa maahadi kemkem kisha kutoyatimiza.



    ''Nurdin... nahisi nina laana ya penzi lako. Moyo wangu unaniuma, huku nafsi yangu ya tamaa ikijilaumu. Nakumbuka siku uliyo niambia kuwa kitu kitamu chaweza kuwa sumu. Nilipenda utamu wa sauti ya Erick iliyokuwa ikiyanadi mapenzi kwa hisia kali. kwa mawazo yangu nilidhani kwakuwa alijua kupangilia mashairi yamapenzi katika daftari kisha kuyaimba basi nilidhani na moyo wake upo hivyo kumbe niliwaza kinyume kabisa. Sina haki ya kuiona sura yako tena kwani niliibabua kwa maji ya moto bila huruma bora nife kuliko kukubali macho yangu yaangaliane na macho yako tena.'' Aliendelea kulalamika Sumaya. Alilia mpaka kichwa kikamuuma sana kutokana na kuwaza muda mrefu. Alijikuta akianguka chini na kuzimia.



    Alikuja kushtuka yupo katika kitanda ambacho hakukizoea, alipotazama shuka alilojifunika aligundua kuwa yeye ndani mwake hakuwahi kuwa na shuka lenye langi moja tu. Zaidi shuka lile halikuwa na mauamaua. Ndipo alipogundua kuwa kumbe hakuwa chumbani kwake. Aliamuakugeuza macho yake upande wa kushoto akashangaa kumuona dada mmoja aliyekuwa amevaa nguo za kidaktari. Dada yule alipoona kuwa ametazamwa alichaua tabasamu dogo huku nae akifanya kuyatupa macho yake pembezoni mwa miguu ya Sumaya ambapo alikuwa ameketi mama yake na Sumaya ambae kwa mdahuo nikama alikuwa amepoteza matumaini ya mwanae.



    ''Mamaaa!!! naona mwanao amezinduka'' Hapo Mama Sumaya akafurahi na kurejewa na tabasamu ambalo kwa mara ya mwisho lilimpata pindi alipotoka sokoni kuhemea na kukutana na rafiki zake aliyocheka nao lakini lilimuisha pindi tu alipomshuhudia mwanae amejilaza chini na ndio ukawa mwanzo wa kitete na machozi yaliyomtoka bila hata yeye kujijua. Alimuendea mwanae na kumshika kichwa kwa ajili ya kusikiliza joto la mwanae ndipo alipogundua kua kidogo kichwa kilikuwa kimepoa nitofauti na dakika kumi nyuma ambapo Sumaya amechemka sana hadi alikuwa akiogopeesha.



    '' Mama.... Niko wapi hapa? na mbona kuna nesi. kwani hapa kuna mgonjwa?'' Alihoji Sumaya lakini hakuweza kujibiwa zaidi ya kumuona mama yake akiangusha chozi tu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ''Mama, mbona unalia?'' Aliuliza Sumaya lakini hakupata majibu pia. Ndipo alipomgeukia nesi na kumuhoji.



    '' Nesi mbona Mama yangu namuuliza hata anijibu chochote? Anatoa tu machozi'' Hapo ndipo Nesi alipoelezea. Alieleza kuwa pindi mama yake aliporejea kutoka sokoni alipita na kumkuta yeye akiwa chini amezimia huku mkononi akiwa ameshikiria kadi. Nesi aliichukua kadi ile kisha akampatia Sumaya. Ndipo Sumaya akakumbuka kuwa alikuwa nayo ile kadi na alikuwa akiisoma na baada ya kuisoma alijilaumu sana. Anakumbuka kuwa kuna muda alijihisi kama anapoteza nuru ya macho na kuanza kuona kwa mbali kisha hakuona tena na mwisho wa siku ndio akajikuta yupo hospital.



    ''Oooooohh My God.'' Alivuta pumzi na kulitaja jina la Mungu wake kwa lugha ya ughaibuni. Hapo mawazo yakaanza kupita katika kichwa chake.

    Ina maamna Mama ameshajua kwanini nilizimia? mh! tena kisa mwanaume... Sijui nifanyenini. Mbona hapa sioni kamba ya kujinyongea ilangalau ni epuke aibu hii.. Enhee nahisi kutakuwa na visu vya kutolea huduma.. mmhhmhh!!! Kwani mie nimefanyiwa upasuaji. sasa kama sijafanyiwa upasuaji basi visu havimo.Sasa nifanye nini iliniepukane na aibu hii?... Hayo ni baadhi ya mawazo yaliyoendelea kuzurula kichwani mwa Sumaya kwa wakati huo.



    Alikuja kuhamaki baada ya kusikia sauti ya kiume ikiongea wodini mule. Alipotupa jicho aligundua kumbe ni Dokta. Kwamuda wote ule alipokuwa mawazoni hakujua kuwa Nesi alitoka na kumuita Dokta na hapo Dokta alikuwa tayari amesha mpima na hapo alikuwa akiongea na Mama yake baada ya kumuita Ofisini mwake na kumpatia ruhusa ya mgonjwa wake. Lakini pia hakusita kumshauri Mama Sumaya kuwa ajaribu kukaa karibu na Mwanae kisha ampatie na saha kutokana na yaliyotokea pamoja na ushauri ilikumlinda na zaidi ya yaliyo mtokea.



    Hatimae waiondoka Hospital baada ya kupatiwa ruhusa.



    ............................... .................................... .................................. ................................................................



    Siku ile ya Nurdin kutoka Dar-es-laam iliwadia nae alioka nakuja moja kwa moja hadi kwao ambako ni ndani ya mkoa wa Shinyanga. Alipofika tu pale stand mtu wa kwanza kumuona alikuwa ni rafiki yake Samir.



    ''Naona umekonda sana, au tuseme nd'o masomo nini mkali wangu'' Alihoji Samir huku akiushikashika mkono wa rafiki yake Nurdin na kumkagua nyama.



    Nurdin huku akicheka, ''aaaaaah! mwanangu usinitanie... inamaana unataka kuniambia nimekonda kiasi cha wewe kutambua wakati wewe huwa haujui kutoa kasoro za watu.'' Aliongea Nurdin huku akilichukua begi lake na kumpatia Samir ambae aliliomba kwa ishara.



    Waliendelea na maongezi ya hapa na pale huku safari yao ikiwapeleka mpaka kwa kina Nurdin na walipofika Nurdini alipokelewa kwa kukumbatiwa huku busu zikifatiza ilimradi tu kuonyesha jinsi gani ndugu zake walivyokuwa wamemkumbuka. Alipatiwa chakula akala yeye pamoja na rafiki yake huku wakiendelea kupiga soga mbalimbali na kurejelea vituko vyao vya nyuma kisha wote kwa pamoja wanakumbuka jambo na kujikuta wanacheka huku wakijitetea kwa kuyaita yale waliyokuwa wakiyafanya nyuma kwamba ni utoto.



    ''Nurdini kwakuwa umefika sasa inabidi uende ukamuone Babu yako angalau hata akakuone maana amekukumbuka sana, mara kwa mara alikuwa akija hapa na kukuulizia huku akimlaumu Baba yako kwa kukupeleka shule ya mbali.'' Aliongea Mama Nurdin. Nurdin alifurahi sana kusikia Banu yake huwa anamuulizia na hata alitamani aende kwa muda huohuo akamuone lakini aliambiwa apunguze pupa nakuambiwa kuwa ni bora aendelee kukaa hata kwa muda wa siku mbili ndipo atakapoenda kwa babu yake.



    Baada ya maongezi yale Nurdin aliamua kumuomba rafiki yake iliangalau wakanyooshe miguu. Wakiwa katika pitapita ao za hapa na pale mara ghafla walikutana na Hawa, rafiki wa Sumaya. Hawa alishangaa sana kumuona Nurdin kwani hakuwahi kudhani kama ipo siku atakuja kuonana na Nurdin tena katika maisha yake.



    ''Enhee!!! zawadi gani kutoka huko Dar-salama'' Aliongea Hawa huku akiwa kwenye hal ya bashasha. Nurdin alijibu kuwa uwepo wake tu tayari ni zawadi tosha. Basi nikama alitekenya mbavu za Hawa kwa kiceko.



    ''Enhe1!1! nilitaka kusahau. vipi shoga yako Sumaya yupo?'' Aliuliza Nurdin huku akitengeneza sura yake ya kutabasamlia





     Akiwa kwenye harakati za kuendelea kuchana zile picha pamoja na barua za Erick Mavoko mara akakutana na moja kati ya kadi aliyotumiwa na Nurdin kipindi cha pendo lao. Aliitazama mara mbilimbili kwa nje kisha akaamua kuifunua kwa ndani iliaweze kuona kilichoandikwa kwandani.



    '' Hivi ninini? naomba unijibu Sumaya... ninini hasa? Je ni nywele zako ndizo zinazonifanya niumie zaidi na niteteleke ilhal nahitajika kwenda shule? Au sura yako ndio inanifanyanisitamani kuwa mbali nawewe? sumaya.... naomba unijibu nasio kusoma tu kadi hii.. ndio, naenda lakini naomba chunga ahadi yako. kumbuka maneno uliyo yaandika kupitia wino wako wa mdomo. Yote yalikaa vizuri na yamehifadhiwa katika daftari la mapenzi lililopo ndani ya moyo wangu. Najua unanipenda na hata lakini najaribu tu kukukumbusha kwani ajali huja hata kwenye tahadhari. Tafadhari, zalisha msimamo wako, heshimu ahadi zako, thamini pendo lako na ulitunze kwani hakuna atakae kufuata na kukutunzia. Sumaya, tambua wazi kuwa mapenzi ni kama vita hivyo nakukumbusha tu, usisahau kutumia silaha yako mbele ya maadui watakaohitaji kulivuruga penzi letu. Nakuaga mpenzi wangu huku nikiamini ipo siku nitarejea na kwa uwezo wa Mungu tutatimiza yote tuliyopanga.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Amini kila kitu kitamu kinaweza kuwa sumu hivyo usipumbazwe na hao wasiyo penda pendo letu. Watakapofika waambie kuwa wewe ni wangu tu. Walimwengu wapo wasiyopenda kuona upo nami hivyo nijuu yako kulihifadhi pendo langu. nina mengi yakusema lakini hatakama nitayasema hayawezi kuenea kwenye kadi hii. Baki salama mpenzi wangu. mwaaaah!!!!'' Ni maneno yaliyosomeka katika kadi ile aliyokuwa akiisoma Sumaya, ni kadi iliyo yarejesha machozi yake. Ukurasa wa pili wa lawama aliufungua na kuanza kujilaumu. Aliendelea kujiona kama ni mkosaji kwa kutoa maahadi kemkem kisha kutoyatimiza.



    ''Nurdin... nahisi nina laana ya penzi lako. Moyo wangu unaniuma, huku nafsi yangu ya tamaa ikijilaumu. Nakumbuka siku uliyo niambia kuwa kitu kitamu chaweza kuwa sumu. Nilipenda utamu wa sauti ya Erick iliyokuwa ikiyanadi mapenzi kwa hisia kali. kwa mawazo yangu nilidhani kwakuwa alijua kupangilia mashairi yamapenzi katika daftari kisha kuyaimba basi nilidhani na moyo wake upo hivyo kumbe niliwaza kinyume kabisa. Sina haki ya kuiona sura yako tena kwani niliibabua kwa maji ya moto bila huruma bora nife kuliko kukubali macho yangu yaangaliane na macho yako tena.'' Aliendelea kulalamika Sumaya. Alilia mpaka kichwa kikamuuma sana kutokana na kuwaza muda mrefu. Alijikuta akianguka chini na kuzimia.



    Alikuja kushtuka yupo katika kitanda ambacho hakukizoea, alipotazama shuka alilojifunika aligundua kuwa yeye ndani mwake hakuwahi kuwa na shuka lenye langi moja tu. Zaidi shuka lile halikuwa na mauamaua. Ndipo alipogundua kuwa kumbe hakuwa chumbani kwake. Aliamuakugeuza macho yake upande wa kushoto akashangaa kumuona dada mmoja aliyekuwa amevaa nguo za kidaktari. Dada yule alipoona kuwa ametazamwa alichaua tabasamu dogo huku nae akifanya kuyatupa macho yake pembezoni mwa miguu ya Sumaya ambapo alikuwa ameketi mama yake na Sumaya ambae kwa mdahuo nikama alikuwa amepoteza matumaini ya mwanae.



    ''Mamaaa!!! naona mwanao amezinduka'' Hapo Mama Sumaya akafurahi na kurejewa na tabasamu ambalo kwa mara ya mwisho lilimpata pindi alipotoka sokoni kuhemea na kukutana na rafiki zake aliyocheka nao lakini lilimuisha pindi tu alipomshuhudia mwanae amejilaza chini na ndio ukawa mwanzo wa kitete na machozi yaliyomtoka bila hata yeye kujijua. Alimuendea mwanae na kumshika kichwa kwa ajili ya kusikiliza joto la mwanae ndipo alipogundua kua kidogo kichwa kilikuwa kimepoa nitofauti na dakika kumi nyuma ambapo Sumaya amechemka sana hadi alikuwa akiogopeesha.



    '' Mama.... Niko wapi hapa? na mbona kuna nesi. kwani hapa kuna mgonjwa?'' Alihoji Sumaya lakini hakuweza kujibiwa zaidi ya kumuona mama yake akiangusha chozi tu.



    ''Mama, mbona unalia?'' Aliuliza Sumaya lakini hakupata majibu pia. Ndipo alipomgeukia nesi na kumuhoji.



    '' Nesi mbona Mama yangu namuuliza hata anijibu chochote? Anatoa tu machozi'' Hapo ndipo Nesi alipoelezea. Alieleza kuwa pindi mama yake aliporejea kutoka sokoni alipita na kumkuta yeye akiwa chini amezimia huku mkononi akiwa ameshikiria kadi. Nesi aliichukua kadi ile kisha akampatia Sumaya. Ndipo Sumaya akakumbuka kuwa alikuwa nayo ile kadi na alikuwa akiisoma na baada ya kuisoma alijilaumu sana. Anakumbuka kuwa kuna muda alijihisi kama anapoteza nuru ya macho na kuanza kuona kwa mbali kisha hakuona tena na mwisho wa siku ndio akajikuta yupo hospital.



    ''Oooooohh My God.'' Alivuta pumzi na kulitaja jina la Mungu wake kwa lugha ya ughaibuni. Hapo mawazo yakaanza kupita katika kichwa chake.

    Ina maamna Mama ameshajua kwanini nilizimia? mh! tena kisa mwanaume... Sijui nifanyenini. Mbona hapa sioni kamba ya kujinyongea ilangalau ni epuke aibu hii.. Enhee nahisi kutakuwa na visu vya kutolea huduma.. mmhhmhh!!! Kwani mie nimefanyiwa upasuaji. sasa kama sijafanyiwa upasuaji basi visu havimo.Sasa nifanye nini iliniepukane na aibu hii?... Hayo ni baadhi ya mawazo yaliyoendelea kuzurula kichwani mwa Sumaya kwa wakati huo.



    Alikuja kuhamaki baada ya kusikia sauti ya kiume ikiongea wodini mule. Alipotupa jicho aligundua kumbe ni Dokta. Kwamuda wote ule alipokuwa mawazoni hakujua kuwa Nesi alitoka na kumuita Dokta na hapo Dokta alikuwa tayari amesha mpima na hapo alikuwa akiongea na Mama yake baada ya kumuita Ofisini mwake na kumpatia ruhusa ya mgonjwa wake. Lakini pia hakusita kumshauri Mama Sumaya kuwa ajaribu kukaa karibu na Mwanae kisha ampatie na saha kutokana na yaliyotokea pamoja na ushauri ilikumlinda na zaidi ya yaliyo mtokea.



    Hatimae waiondoka Hospital baada ya kupatiwa ruhusa.



    ............................... .................................... .................................. ................................................................



    Siku ile ya Nurdin kutoka Dar-es-laam iliwadia nae alioka nakuja moja kwa moja hadi kwao ambako ni ndani ya mkoa wa Shinyanga. Alipofika tu pale stand mtu wa kwanza kumuona alikuwa ni rafiki yake Samir.



    ''Naona umekonda sana, au tuseme nd'o masomo nini mkali wangu'' Alihoji Samir huku akiushikashika mkono wa rafiki yake Nurdin na kumkagua nyama.



    Nurdin huku akicheka, ''aaaaaah! mwanangu usinitanie... inamaana unataka kuniambia nimekonda kiasi cha wewe kutambua wakati wewe huwa haujui kutoa kasoro za watu.'' Aliongea Nurdin huku akilichukua begi lake na kumpatia Samir ambae aliliomba kwa ishara.



    Waliendelea na maongezi ya hapa na pale huku safari yao ikiwapeleka mpaka kwa kina Nurdin na walipofika Nurdini alipokelewa kwa kukumbatiwa huku busu zikifatiza ilimradi tu kuonyesha jinsi gani ndugu zake walivyokuwa wamemkumbuka. Alipatiwa chakula akala yeye pamoja na rafiki yake huku wakiendelea kupiga soga mbalimbali na kurejelea vituko vyao vya nyuma kisha wote kwa pamoja wanakumbuka jambo na kujikuta wanacheka huku wakijitetea kwa kuyaita yale waliyokuwa wakiyafanya nyuma kwamba ni utoto.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ''Nurdini kwakuwa umefika sasa inabidi uende ukamuone Babu yako angalau hata akakuone maana amekukumbuka sana, mara kwa mara alikuwa akija hapa na kukuulizia huku akimlaumu Baba yako kwa kukupeleka shule ya mbali.'' Aliongea Mama Nurdin. Nurdin alifurahi sana kusikia Banu yake huwa anamuulizia na hata alitamani aende kwa muda huohuo akamuone lakini aliambiwa apunguze pupa nakuambiwa kuwa ni bora aendelee kukaa hata kwa muda wa siku mbili ndipo atakapoenda kwa babu yake.



    Baada ya maongezi yale Nurdin aliamua kumuomba rafiki yake iliangalau wakanyooshe miguu. Wakiwa katika pitapita ao za hapa na pale mara ghafla walikutana na Hawa, rafiki wa Sumaya. Hawa alishangaa sana kumuona Nurdin kwani hakuwahi kudhani kama ipo siku atakuja kuonana na Nurdin tena katika maisha yake.



    ''Enhee!!! zawadi gani kutoka huko Dar-salama'' Aliongea Hawa huku akiwa kwenye hal ya bashasha. Nurdin alijibu kuwa uwepo wake tu tayari ni zawadi tosha. Basi nikama alitekenya mbavu za Hawa kwa kiceko.



    ''Enhe1!1! nilitaka kusahau. vipi shoga yako Sumaya yupo?'' Aliuliza Nurdin huku akitengeneza sura yake ya kutabasamlia





    ''Nilijua tu lazma utauliza. Maana na wewe jinsi alivyokukaa huyo Sumaya...mmmmh!!!!!'' Aliongea Hawa huku akimuangalia Samiri kwa kumkonyeza kana kwamba kuna jambo lililoendelea kati yao. Samiri alitoa ishara ya kumtaka Hawa akae kimya na asiseme chochote kinacho muhusu Sumaya. Nae Hawa aliielewa ishara ile lakini ilikuwa vigumu sana kwa Nurdin kuelewa kilichoendelea kwa wakati ule.



    ''Vipi Hawa? mbona hunijibu. Au unawazia yale ya nyuma?. Usijali sina nia mbaya nayeye bali ninajaribu tu kumuulizia kwa heri. Au labda kuna makosa mimi kumuulizia My ex-girlfriend?'' Aliongea Nurdin huku akimshika bega rafi yake Samir.



    ''Hapana Nurdin. Sina maana hiyo..''



    ''Kumbe maana ipi Hawa??'' Nurdin alimkata kauli hawa kishaakaendelea kwa kusema. '' Inamaana tuseme mimi leo sina haki ya kujua yanayo muhusu Sumaya. Au nd'o alikwambia ukiniona usinisemeshe tena eti.. eeh? poa. Lakini sikuwa na lengo baya miniliuliza tu kwakuwa licha ya kuwa ex kwangu vile vile ni rafiki yangu. Au sio Samir?'' Alijieleza sababu iliyomfanya amuulizie Sumaya na kuwahakikishia kuwa, shida yake ilikuwa si ile waliyoidhania.



    '' Mimi tena? mh! sihitaji kushirikishwa kwenye hizo mada zenu za sjui huyo Su nini? wala sihitaji kujua amefanya nini. Na mara nyingi nimeshakwambia kuwa usilitaje ilo jino mbele yangu maana nikama lina nitia hasira tu, ok.. Kama mnaongea hebu ongeeni vitu vya maana nasio kuanza kumjadili huyo dem. Au kama vipi mie nitangulie ili muendelee kumuongelea poa?'' Aliongea Samir na kuanza kuondoka.



    ''Acha hizo jamaa yangu. Kwani hiyo nd'o inshu ya kumaind namna hiyo?'' Aliongea Nurdin kwa lawama.



    ''mmmh!!! Samir nae? huwa anapenda kukasirika'' Alichombeza Hawa ikiwa ni kama kunogesha kauli ya Nurdini. Lakini kiukweli huo ulikuwa ni mpango tu wakumfanya Nurdin asiendelee kumuongelea Sumaya.



    Samir alipoondoka hapakuwa na soga tena kati ya Nurdini na Hawa. Waliagana na Nurdin akatoka mbio kumkimbilia rafiki yake ambae alikuwa amemuacha kwa hatua kadhaa.



    Waliendelea na safari yao ya mizunguko ya hapa na pale na walipo yaridhisha macho yao waliamua kurejea geto.



    ''Oy, minajikataa zangu.''



    ''Wapi sasa na wewe''



    ''Naelekea mishemishe. Siunajua tena huku kwetu kama ukiwa al-watani kama mimi huwezi kukosa mishemishe?''



    ''Wapi na wewe una umaarufu gani?'' Alakebehi Nurdin.



    Kilichofuata ni utani kama ilivyo kawaida yao na baada ya dakika kadhaa mbele Samir aliondoka na kumuacha rafiki yake akiendelea kujipumzisha.



    ............... ..........................................................



    Mama Sumaya baada ya kuona mwanae anaendelea vizuri aliamua kumuita na kumkalisha kisha akampatia nasaha mbalimbali.



    ''Mwanangu, huko ulipojiingiza, sipo ulipo hitajika uwepo kwa muda huu. Usipende kujikuza mwanangu, ona leo na unauguza majiraha ambayo hukupaswa kuwa nayo kwa muda huu. Hujafikia kiwango cha kulia kisa mwanamume.. Hujafikia kuzimia kisa mwanamume. Wewe bado mdogo sana. Unapaswa kulitoa chozi lako kwenye kitabu au upoteze fahamu kwa kujisomea sana hadi kicha chako kikashindwa kuya himili masomo. Nizaidi ya aibu mbele ya mashoga zangu pindi watakapogundua kuwa wewe mwanagu sikuhizi huwa unayuaruhusu machozi yako ya kumwagike kisa mwanamume.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Usiyawahi mapenzi nakujifanya unapenda kwani utalia kila siku au kuliza kila siku, kumbuka wanaume wote Baba yao ni mmoja tu. Watakuliza kadri utavyo wabadilisha pia jua wao huwachukulia wanawake kama matoleo mapya yanguo pindi wawatakapo na huwa chukulia kama matoleo yaliyo pitwa na wakati pindi wawatumiapo kisha huwa fuata wengine ambao wanahisi ni matoleo mapya kwao. Wanapokuja huyavua yale mavazi yao ya usaliti na unafki kisha huazima vinyago vya huruma na wana maneno matamu ambayo si virahisi kuacha kuyaamini kwani usipowaamini wapo radhi hata kucheza michezo ya jukwaani kwa kuyatafuta machozi ya kinafki na kuyatumia kuyaaminisha macho yako kuwa wanalia kwa ajili yako.Hakika ni vigumu viyachenga maneno magumu ya wanaume na maswali yao ambayo kama wakikuuliza basi huwezi kuyajibu kisha huku tega kwenye kitendawili chao ambacho jibu lake ni kuwa nao tu. Tafadhali mwanangu usiwaamini wanaume wote na wewe huna haki yakuingia kwenye mapenzi kwa sasa hivi kama ulivyojiingiza. Basi nakuomba chukua leso hii na ufute machozi yako yanayokuanguka kisa hao wanaume. Mwanaume atakutoa kwenye malengo yako na kukurubuni uwapo kifuani kwake huku yeye akisimamia malengo yake kila leo. napenda kukupa neno jipya kuwa mtoto wa kiume huwa hapendi kwa kutumia moyo bali hutumia akili.''

    Aliendelea kufyatua maneno yake makali ambayo nikama yalikuwa yakizifungua nguo za ndani za moyo wake na kumuacha uch kabisa kitendo kilichopelekea ajihisi aibu na kuumia kutokana na maneno makali aliyo kuwa akiyatoa mama yake.



    Naam, wanasema maneno ni zaidi ya sumu. Nibora unywe sumu ya panya ambayo unaweza kutmia maziwa na ukupota. Kuliko maneno ambayo kama yakitumiwa huweza kuutoa uhai wamtu kwa nusu sekunde tu.

    Neema aliendelea kuathirika na maneno ya mama yake huku fikra zikimpeleka mbali na kuwaza siku aliyojifanya anaupendo wa dhati hadi akamfuata mtoto a kiue na kujitongozesha, hakuishia hapo tu. pia alikumbuka siku aliyo zichojoa nguo zake mbele ya Erick kufuatia urubuni wa maneno. Akabaki kajiinamia huku soni ikimjaa akawaza vipi zile picha za utupu zisinge chukuliwa na Samir. Je, Mama angeshindwa kuziona? Nakama hivi tu amefikia hadi kushidwa kula. Je, angejua kuwa mwanae nishapigana kisa mwanaume?. Hapo akaupokea ushauri wa mama yake kwa kiwango cha hali ya juu huku akimuahidi Mama yake kutojihusisha tena na Mapenzi. Mama yake alimuelewa lakini zaidi alimsihi kuwa ni bora ajishughulishe na michezo ili angalau amsahau huyo aliyemfanya kuwa katika hali ile.

    Sumaya aliachwa na mama yake huku akitafakari. Alichukua simu yake kisha akabonyeza vitufe kadhaa na kupiga. Simu iliita kisha ikapokelewa aliongea na aliyempigia lakini zaidi alimuomba wakutane mida fulani kisha akakata simu. Kuna namba alianzakuiangalia mara kumi kumi huku akijiuliza. Je aipigie, lakini kila alipojaribu kupiga aliishia kuikata hata kabla haijaita. Nafsi ilikuwa ikimsuta kutokana na maudhi aliyo yafanya kwenye namba ile. Aliamua kuachana nayo na kwenda kuendelea nashughli za hapa na pale.

    ...................... ..............................................................



    Simu ya Nurdin iliita na alipoangalia kwenye kioo ilikuwa ni namba ngeni. Huwa hana tabia ya kuharakisha kupokea namba ngeni hivyo aliiacha ikaita mara kadhaa kisha akaipokea. Wakati huo Samir alikuwa amemuaga Nurdin kuwa anatoka kidogo kuna sehemu anaelekea hivyo Nurdin alikuwa peke yake kwa muda huo.



    ''Hello King of my Heart'' Iisikika sauti iliyotoka upade wa pili wa simu ile. Sauti ilikuwa nyororo yenye kuvutia katika masikio ya rijali wa aina yeyote yule. Nurdin ghafla nywele zika msisimka, mapigo ya moyo akaanza kuyaona yakikimbia, furaha iliyo changanyikana na uoga ikamvagaa pasina kutaraji. Kwaharakaharaka alishindwa ajibu nini kwani namba ile ni ngeni. Akaanza kutafuta katika ramani ya kichwa chake iliaone kama ana msichana yeyote lakini aliishia kutoiona ramani hiyo.

    ''Samahani!! Nani mwenzangu?'' Alihoji Nurdin kwa hofu kwa kudhanikuwa huenda kuna mtu alikuwa akimdhihaki.

    ''Mimi mpenzi wako.''

    ''Yupi'' Alihoji Nurdini huku akiuhamisha umakini wake wote katika simu.

    ''Kwani we unawapenzi wa ngapi?'' Ilihoji sauti ile ya upande wapili.

    Nurdin alihisi kama usumbufu tu. Akaanza kubadili ile sura yake ya furaha la uoga na kuitafuta ile ya kikatili.

    ''Unapopiga simu ina bidi ujitambulishe nasikusumbua watu haba. kingine haya maswala mimi kuwa na wasichana wangapi, hiyo si kazi yako. Ongea shida yako kama huwezi kata simu tusije kuvurugiana siku hapa sawa?' aliongoa Nurdin.

    ''Anhaa!!! kumbe hata na namba yangu ulifuta eti? nashukuru sana!! mie kwa muda wote nakufikiria wewe kumbe wewe hata kuniwazia tu hamna eee.....'' Kabla hata hajamalizia. Nurdini alidakia.

    '' Sikia mwanamke.... Sipendi usumbufu, kama namba yako nimefuta basi inatosha kudhihirisha kuwa sikuwazii wala sikujui ok. Kingine mimi sina muda wa kucheza michezo ya ngonjera na wapuuzi kama nyie. We kama hauna bwana nenda katafute hata Ng'ombe au mbuzi wawe ma king of your heart ok. Then i dont have time to speak with bitch like you. Dont call me again, ukinipigia tenanitakushtaki mtandaoni kwakosa la usumbufu iliufungiwe namba yako I think you catch me '' Nurdin aliongea maneno yale yaliyompelekea yule msichana asiye taja jina kukata simu.

    '' Leo Nurdin ananiita malaya? Leo anafikia kunitukana namna hii na kuniamba niwe na mahusiano na ng'ombe? sikubali, hapa lazma kuna jambo hapa. Dada nahisi kuna mtu anaingilia penzi langu. Siwezi kumuacha Nurdin wangu arubuniwe wakati mimi ni wake na nina mpenda kweli. Siwezi'' Aliongea Hadya baada tu ya kukata simu iliyomfanya apatwe na huzuni ilhali aliipiga kwa furaha.

    ''Ina maana Nurdin haijui hata sauti yako?, Hata namba kasha futa? pole sana mdogo wangu'' Aliongea Dada yake kisha akamkumbata mdogo wake huyo ambae nikama akili ilimuhama ghafla kwa jinsi alivyokuwa akitapatapa.

    Dada mtu anamfahamu mdogo wake na anafahamu jinsi gani alivyomuweka Nurdin moyoni. Anakumbuka kuwa Hidaya alikuwa wazi apigwe na hata alishatiwa majiraha mbalimbali mwilini mwake kisa Nurdin. Pia anatambua wazi kabisa chanzo cha Hidaya kupelekwa uwarabuni kusoma ni kwa ajili ya mikakati ya Baba yake katika kumnusuru mwanae mikononi mwa Nurdin sasa kwa jinsi alivyomuona mdogo wake, bila shaka alijua yupo radhi kufanya chochote kile kwa muda huo. Hakuwa na lakufanya kwani hata kama angesema atoe ushauri ni kama angepoteza muda wake bure tu maana mdogo wake alipenda kupitiliza.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ile simu ya Hadya iliwahi kutumiwa na ndugu yao mmoja ambae alikuwa ni mgeni pale kipindi hadya alipopelekwa uarabuni; ndugu yao huyo alikuwa ni mwngi wa masihara hasa pindi alipokuwa akiongea na marafiki zake. Mara nyingi alipenda kuichukuwa simu na kwenda kwenye magic sound kisha kubadilisha sauti alizotaka yeye na kuwatania marafiki zake. Hata kipindi anaondoka aliacha amesahau kutoa ile seting yake ya magic sound hadya alipofika tu nchini. Namba ya kwanza kuipigia ilikuwa ni ya Nurdin na hata Nurdin alivyopokea simu ile hakujua ninani aliyempigia zaidi alihisi kuna mtu alikuwa akimtania tu. Ndio, Nurdin alikuwa na namba ya hadiya lakini siku moja kipindi anatoka twisheni aliibiwa simu pindi alipotoka shule na alipoibiwa hakununua tena mpaka hapo karibuni walipokuwa wakijiandaa na mitihani ya taifa. Wazo la namba ya mpenzi wake Hadya, halikuwemo kabisa kichwani mwake istoshe hakuwa na uhakika wa kumuona kirahisi namna ile.

    Nurdin akiwa katika hali ya kukereka kwa kusumbuliwa, mara simu yake ikaita lakini hakujishughulisha nayokwani alidhani kuwa huenda atakuwa yule msumbufu wake. Alipoona usumbufu umezidi ikabidi aichukue simu na kuitazama iliaikate na kuizima, ile anaitazama akagundua kuwa haikuwa namba ile ya mwanzo bali ile ilikuwa ni namba ya Hawa rafiki yake Sumaya. Akaipokea kisha wakazungumza nao pia wakapeana ahadi ya kuonana kwa ajili ya maongezi.

    .......................... .............................................

    '' Inshot nd'o hivyo Samir. Yaani hapa unaponiona mimi sijielewi hata ni fanye nini?'' Aliongea Sumaya na hiyo ni baada ya kuwa wamekutana mahali walipo ahidiana wakutane baada ya Sumaya kupimpigia simu Samir.

    ''Nikuulize kitu Sumaya?'' Alihoji Samir.

    ''Uliza tu.'' Aliitikia Sumaya.

    ''Unampenda Nurdin au unaongopa kwakuwa umezinguliwa na huyo boya wako''

    ''Samir nashindwa kurudiarudia neno moja muda wote.''

    '' Hilo nd'o jibu la swali langu''

    ''anhaa....'' Huku akitikisa kichwa.

    '' sasa kumbe jibu ni lipi?'' Akahoji tena Samir.

    ''Nampenda tena sana.'' Akajibu Sumaya.

    Samir huku akicheka'' Unajua we.. Sumaya unafurahisha sana. eti, unampenda!! sasa mbona ulimtosa kisa yule boya''

    ''Samir nd'o hapo nahitaji msaada wako kwani mimi nilifanya hivyo si kwamba nilimpenda sana Erick. Mi, nilipenda tu kuwa na superstar ilinipate nami umaarufu na kuimbiwa nyimbo. Nikweli nilisahau kuwa mtu humpenda mwenzie baada ya ridhaa ya moyo na si kipaji kama nilivyodhani. tafadhali nisaidie mwenzio kwani najua hata Nurdin huko alipo ananichukia. Nakuomba Samir mpigie simu huko Dar kisha niombee msamaha''

    ''Inamaana hujui hata kama Nurdin amesharudi!!!! Mamaaaaaa!! ok, hayo yakujua tuyaache ila tambua kabisa Nurdin yupo geto namimi kipindi nakuja nimemuacha japo sikumwambia kama nilikuwa nakuja kwako'' Aiongea Samir na kupelekea mshangao kwa Sumaya. Kwa mara nyingine tena Sumaya akahisi kuwa huenda Samir ameshamuonesha hata zile picha za utupu.

    ........................... .....................................................

    Nurdini alikutana na Hawa na huko ndipo alipopewa ukweli wote wa Sumaya na yule msanii kwa jina la Erick.

    Kumbe aliniacha mimi iliawe na msanii? kwa hiyo amefikia hadi kujipendekeza hatakwi lakini anang'ang'aniza mapenzi wakati mimi nilikuwepo tu. Dah!!. Hayo ni machache kati ya mengi aliyo yawaza Nurdini baada yakupatiwa habari nzima.





    Mpaka Nurdin na Hawa wanaachana tayari ukweli alikuwa nao Nurdin. Alijua kumbe Samir alipomwambia kuwa Sumaya ni msaliti hakuwa na makosa bali alipatia kabisa, kichwa kilimuuma sana Nurdin kwani niwazi kuwa alikuwa akimpenda sana Sumaya na lengo kubwa la Nurdin kurejea shinyanga ilikuwa ni kuja kukutana na Sumaya iliwayamalize kwani Nurdin alihisi huenda umbali wake ndio ulileteleza yeye aonekane ana makosa. Niwazi kabisa upendo hutoka moyoni nasi kinywani kama wadhaniavyo wengi, kuumiza moyo kwakutumia silaha kama risasi au kisu si kazi rahisi kwasababu risasi haina uwezo wa kupenya kiurahisi ndani ya moyo lakini mapenzi yanauwezo wa kuupatia moyo furaha na hata kuumiza kuliko hata risasi. Sikuzote donda lililoanza kupona huuma zaidi ya jiraha la mwanzo pindi litoneshapo.

    Nurdin alikilalia kitanda chake huku akiyazuia machozi kiume lakini hakuweza hata kidogo kila alipofikiria kumuacha Sumaya mapigo ya moyo ni kama yalizima ghafla alikuwa akijihisi kufakufa.

    ''EEE, Mola wangu... Hakika wewe ndie uliyeweka mapenzi, na uliyaweka kama fumbo kwetu. Tuna penda, tunalia, tunaumizwa na kupakwa mafuta ya usaliti lakini hiyo haina maana ya kwamba hatujui kupenda. Najua unatambua wazi kuwa mimi ninampenda sana Sumaya na kila nikiulazimisha moyo kumta naishia kuumia tu. Nakuomba niainishie pendo langu la dhati, sina uhakika kwamba hukuweka haki mbele yangu. Kama mimi ni mtumwa wa penzi la Sumaya basi nipatie uhuru wangu kutoka kwake. Najua nimengi ameyapitia kama nilivyokwisha kuambiwa na Hawa, lakini nia yangu sikuweka mapinduzi bali ni kumfanya arudi kwangu japo anaendelea kutumikia tamaa za mtu mwingine na kuendeshwa kisa kipaji. Ndio nina uwez wa kuwa na msichana yeyote nimtakae lakini sitakuwa na itendea haki nafsi yangu japo nita yanusuru maungo yangu ya matamanio kwa muda. Najua nko ndani ya mchezo wa mapenzi lakini nashangaa utofauti wa mchezo huu ambao kama nikifanya makosa basi naipoteza roh yangu. Nakuomba nifumbulie hili fumbo la mapenzi ili nami nijitape barabarani kwa uhindi.'' Ni maneno yaliyoendelea kumtoka Nurdin geto kwake pasina kujua kuwa Samir alikuwa tayari ameshafika na maneno yote aliyasikia. Hakika Samir alishangaa sana maajabu ya mapenzi, katika maisha yake hajawahi kumshirikisha mwenyezi Mungu kwenye mapenzi. Samir alijikuta akitokwa na machozi bila kutarajia alimuhurumia sana rafiki yake kwani ingawa anajua wazi kuwa Sumaya alimsaliti lakini alibaki kumuomba Mungu angalau hata Sumaya abadili maamuzi na kurejea tena kwake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Samir alimfuata rafiki yake na kumkumbatia huku machozi ya kiume yakichuruika kutoka machoni mwao na moja kwa moja hadi migongoni mwa kila mmoja.

    ''Huna haja yakulia namna hiyo Nurdin. Utaugua ugonjwa ndugu yangu.'' Aliongea Samir huku akiwa bado kamkumbatia rafiki yake.

    '' Nurdin, nipo radhi kupatwa na ugonjwa wa aina yeyote ile na hata kifo kama kikiwezekana lakini si mimi kumkosa Sumaya. We, hujui tu. kiasi gani nimeumia kisa yeye. Mwenzio nimejikaza sana kumfuta na nilipoonma afutiki niliamua kuwa na msichana mwingine kwakudhani huenda akaniliwaza kama alivyo kuwa akiniliwaza Sumaya lakini chakushangaza yule mschana alivyoondoka tu. Mawzo yote yakahamia kwa Sumaya. Nurdin nampenda sana Sumaya naniporadhi kufanya chochote kile ili arudi kwangu.''

    ''Nurdin, nadhani unatambua kuwa haya mapenzi ni kama mvua hata kama yatanyesha vipi lakini mwisho wa siku yatakatika tu. Kama uliweza kujizuia miaka takribani saba kasoro basi niuzushi pale utaponiambia kuwa huwezi kumuacha aende Sumaya kwani tayari kesha najisika na kudhalilika. Nakupenda sana rafiki yangu .''

    '' Samir, nisawa kabisa mapenzi nikama mvua lakini huo ni upande wako ila si kwangu. Kama mapenzi yangekuwa sawa na mvua hebu tazama ni misimu mingapi ya kiangazi imepita ndani ya kila mwaka lakini mbona mvua za upendo wangu hazijakatika juu yake? Ndio ni haki ya kila mmoja kumchagua anaempenda hata awe na kasoro ya aina yoyote ile, kama Sumaya ni mwenda wazimu basi mimi nampenda hivyohivyo na ninafurahia kuwa nae, na kama Sumaya kasoro yake si uaminifu basi mi niporadhi kwa lolote. Hakuwahi kunisaliti kipini nipo nae karibu, naimani umbali wetu ndio ulipelekea yeye kufanya yote yale.'' Samir alitoa kila aina ya ushauri lakini wahenga waliwahi kusema kuwa moyo ukipenda huweza kula hata nyama mbichi na ubichi wake pasina kujali wala kutetereka. Hapo ikabidi akubaliane na rafiki yake.

    Alimuahidi kumsaidia kwakumkutanisha ana kwa ana na Sumaya iliwaweze kuyaongea na kuyamaliza wapenzi wale ambao kati yao kila mmoja alimuhitaji mwenzie lakini hawakujua kama walikuwa na wazo moja.

    Samir alimpigia simu Sumaya na kumtaarifu kuwa inabidi ajiandae ili kukutana na Nurdin kwa ajili ya kujaribu kusuluhisha matatizo yao. Sumaya alifurahi sana baada ya kusikia jambo kama lile, alimshukuru sana Samir na kupanga muda yeye mwenyewe wa kukutana kama ambavyo alivyopewa nafasi ya upendeleo.

    ........................... ..................................................

    Erick nae kwakuwa alikuwa amemaliza kidato cha nne nae hakuwa na lakungoja huko shinyanga kwani hapakuwa kwao bali alikuwa huko kwa ajili ya masomo tu. Aliondoka na kurejea nyumbani kwao jijini Dar-es-salaam. Alipofika huko siku tatu nyuma aliamua kwenda kanisani kutubu kufuatia madhambi aliyo wafanyia mabinti mbalimbali huko Shinyanga. Alilitambua kosa baada ya kuonywa na Samir. Kumbe siku ile alivyopewa onyo na Samir alienda geto na kujifikiria sana ndipo alipogundua kuwa alikuwa amefanya makosa sana, siku hiyohiyo aliingia kwenye mitandao ya kijamii na kuzifuta picha za Sumaya alizokuwa amezipangia kuzitangaza muda si mrefu ili kila mtu aliyomo mtandaoni aweze kuzipata. Sikuhiyo alikuwa cockbeach akibarizi huku akiendelea kutafakari kila kosa alilofanya na kuendelea kujihisi mkosaji tu.

    Erick akiwa pembezoni kabisa katika kuangaza angaza huku na kule mara ghafla alishangaa kumuona msichana mrembo aliyekuwa ameshikiria kisu kwa mikono yake yote miwili huu akikielekeza kisu kile kwenye tubo lake. Erick hakuweza kuvumilia jambo lile kuliona kwa macho ndipo alipoamua kusogea karibu kabisa na binti yule kwa tahadhari ya hali ya juu mpaka pale alipomfikia karibu kabisa. Binti yule aliamua kukichoma kisu kile katika tumbo lake ile anakipeleka tu, tayari Erick alikuwa ameshafika na kumkwapua binti yule kile kisuu kwa nguvu zake zote. Yule binti hakuweza kukubali kirahisi achukuliwe kisu na kukatishwa hukumu ambayo tayari alikwisha isaini. ''nIache nife!!!! Niache kwani unakufa wewe!!!'' Aliongea binti yule mwenye hasira kwa wakati huo Erick alikuwa amekishikiria kisu upande wa mpini huku yule binti mwenye kutamani kifo akiwa amekishikiria kisu kile upande wa makali. Kilikuwa kikimkata sana kadri alivyo zidi kukivuta kwa lazma ilikitoke mikononi mwa Erick lakini hakuna maumivu aliyo yasikia binti yule mwenye uchu na kaburi. Alipoona Erick ananguvu kuliko yeye hapo yule binti akamg'ata Erick na kukimiliki kisu kile tena kwa mara ya pili huku Erick kwa muda ule akiugulia maumivu chini. Yule binti mwenye uchu na kaburi hapohapo akakilegesha kisu kile tumboni mwake kisha akafumba macho na kujichoma. Ilisikika sauti ya maumivu makali kisha binti yule akaamini kuwa hapo ndipo ameiaga dunia lakini alihamaki baada ya kujaribu kufungua macho ili aione ahera badala yake alimuona Erick akiwa chini amelala huku mkabala na bega lake kukiwa na kisu kilicho zama vilivyo begani. Yule binti mwenye uchu na kaburi palepale hamu ya kufa ikamtoka na kuanza muangalia Erick aliyekuwa amelala chini. Kwa uoga binti yule alikimbia na kwenda kutafuta msaada kisha akapata na alipopata alishirikiana na wale aliyowaomba msaada kumbeba Erick na kumpeleka moja kwa moja hadi Hospitali kwa ajili ya matibabu. Alipofika hospitali nae pia alilazwa na kutbiwa mikono yake ambayo iliumia sana pale kwenye purukushani ya kunyakuwa kisu. Baadae aliruhusiwa lakini Erick yeye hakuruhusiwa muda huo kwahiyo ikabidi amsubiri mpaka pale aliporuhusiwa. Waliondoka wote kwa pamoja siku hiyo hiyo na kwenda kukaa sehemu ambayo kwao ilikuwa nzuri walipofika pale waliketi na kujitmbulisha.

    ''Naitwa Erick'' Alijibu Erick baada ya kuulizwa jina lake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ''mie naitwa Hadya.'' Alijibu Hadya kisha akaulizwa sababu iliyompelekea ahitaji kujiua.

    ''Ni mapenzi tu kaka Erick.'' Alijibu kisha akajielezea kiufupi kuwa Boyfriend wake alimzingua ilhali alisha ahidi kuwa endapo akimkosa basi lazma ajiue. Kabla hajaamua vile ilimbidi aende kwao na Boy wake huyo na alipofika kwao akaambiwa kuwa Boy wake ameshaondoka na kwenda kwao wala haijulikani ni lini atarejea kwani tayari amesha maliza masomo yake, alicho waza Hadya aliwaza kuwa lazma atakuwa kisha achwa kwani hata alipopiga simu yake ilipokelewa na kuishia kutukanwa tu. Ndipo alipopita sehemu wanapochonga visu na kuchukua kimoja kwa ajili ya kujitolea uhai wake na kabla hajatimiza lengo lake ndipo Erick alipo ingilia.

    ''Pole sana Hadya, kingine hukupaswa kuamua maamuzi ya mbali kama huko ulipoamua kwenda wewe kaa chini tulia na umfute uliyempoteza kwani hata kama ukijiua hauwezi kumpata bali utajikosea mwenyewe tu.........'' Akiongea mengi Erick kama ushauri kwa Hadya, mwisho wasiku Hadya akamuelewa.

    Mapenzi ni kama ukurasa wa pepa iliyoandikwa maandishi ya aina yeyote yale. Pindi msomaji anapolizishwa na muandishi katika dibaji ndipo hujikuta akifungua ukurasa wa mapenzi palepale. Hakukuwa na sababu ya Hadya kuanza kumuomba Erick moyo wala Erick kumuomba hadya moyo bali mapenzi yalijitengeneza palepale kufuatia wema waliotendeana hapo punde tu.

    Hadya akamsahau Nurdin na kulivaa penzi la Erick ambae kwasasa alikuwa mwema na asiehitaji makuu. Siku hiyo ya kwanza tu kukutana ndio siku ambayo Erick aliamua kumpeleka moja kwa moja hadya na kumtambulisha kwa mama yake. Hadya alikubaliwa kwa baraka tele kutoka kwa mama wa Erick.

    .................................. .......................................................................



    Macho ya wawili waliyokuwa wakipendana kwa dhati yaliweza kukutana kwa mara ya kwanza toka mmoja kati yao aliposimamisha gurudumu la mapenzi kati yao. Kila moyo wa mmoja ulitegemea wa mwingine ilikuweza kuunganisha mioyo ya wawili hao iliyotengana kwa muda.

    Kila mmojaalikuwa akimtegea mwenzake kwenye kuongea, Sumaya moyo wake ulikuwa ukitililika mchozi muda wote kwakudhani kuwa yeye pale ndie mwenye makosa, hata uande wa Nurdin nae alijua kuwa yeye yupo kwa ajili ya kujipendekeza tu kwani alijua kuwa mpenzi wake atakuwa tayari kisha hamisha pendo lake kwa mtu mwingine.

    ''Sumaya, kwanza nianze kwa kumlaani shetani aliyeingilia pendo letu na kuleta mitafaruku ya hapa na pale. Shetani ambae alikufanya wewe ukimbie mikononi mwangu bila hata kuniambia kwa heri. Sikufichi wewe ndie utembeae na moyo wangu. Miaka yote hiyo nimeishi na kiwiliwili kisichokuwa na moyo huku wewe ukiendelea kulisaliti penzi langu mbele ya umati wa watu tena pasina kujificha. Je, unajua ni mara ngapi nimepoteza hamu ykuwaza chakula na kukuwazia werwe pindi ulipo niacha? Je ulikuwa radhi na uko radhi kuniona nikiumia au hata kwenda kaburini kwa ajili ya kulikosa pendo lako nililolizoea? Nakili kosa mbele yako mpenzi wangu kuwa, uliponiacha nami nilitumia nafasi hiyo kwenda kwa mwingine ilikupoza angalau maumivu kwa kudhani huenda moyo wangu utaridhika. Huko nako sikuambulia chochote kile cha kuuridhisha moyo wangu, ndipo nilipogundua kuwa moyo ushakuweka wewe tu na tamaa zangu zakuiridhisha nafsi yangu kwa kulipa visasi haiwezi kusaidia mchochote kwakuelewa hilo ndipo nikaona ni heri kukaa bila msichana nilikubali kuitwa majina ya kike mbele ya wavulana wenzangu kisa sikuhitaji kuwa na msichana, hadi ilifikia kipindi nikaitwa hanisi kisa sikuhitaji msichana kwa ajili ya kuhifadhi pendo lako huku nikiamini ipo siku nitakutana nawe mpenzi wangu wa kwanza. Sumaya najua kabisa sina tena nafasi kwako kwani umeshaamua kumuweka mwingine kwenye nafasi yangu lakini naomba utambue ninauwezo wa kubadili wasichana zaidi hata ya nguo, ila hawawezi kuziba pengo lako lililomo moyoni mwangu zaidi watafurahisha nafsi yangu kwa muda tu. Nilichokiona kutoka kwako ndicho kinachoitwa uzuri wa kike, Sura yako ndio ya kwanza kupendwa na macho yangu na moyo haupendi mara mbili hivyo hata kama nikisema kuwa nipende tena siwezi fikia hata robo ya upendo wangu kwako. Kama hunitaki tafadhali niambie hapa hapa ilinife mbele ya macho yako nasi kubaki nikisumbuliwa na maumivu ya moyo,'' Alishusha pumzi kidogo kwani toka aanze kuongea hakuweza kuruhusu pumzi yake ishuke kwa hiyari. Muda huo chozi la kiume lilikuwa tayari limeshakauka na kuachia alima yake huku Sumaya yeye akiwa ni kama hajielewi kabisa na aliendelea kuumia kila alipozidi kusikia maneno makavumakavu kutoka kwa Nurdin. Nafsi ilimsuta kutokana na kila neno alilolisikia kutoka kwa Nurdin. Hapo Nurdin akaendelea huku Sumaya akiwa hajiwezi hata kuongea tu.

    ''labda nikwambie kitu Sumaya;

    Nimeshndwa kuvumilia adhabu ambayo haina mwisho, hivi toka useme basi unajua ni muda gani sasa?.



    Najua huwezi nijibu kwakuwa, ulilichoma pendo langu kwa tindikali, na kuliangamiza hivyo sitoshangaa endapo utakosa jibu la swali langu.



    Ndio, mpenzi wa kwanza ni zaidi ya chuo, wote huanza kuyajua mapenzi kupitia kwa mpenzi wa kwanza.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Ni bora ungenichukuwa na kuniangamiza ilinisibaki tena katika dunia hii, kuliko adhabu kama hii uliyonipatia.

    Adhabu ambayo hata ukiipeleka mahakamani, bila shaka, mahakimu na wanasheria watashangaa sana kwani hakuna kifungu kilichoandika adhabu kali kama hii uliyonipa.



    Sidhani hata kama kuna katiba yenye sheria kali kama hii ulioitunga kwa ajili yangu.



    Hebu jiulize mwenyewe, toka unipe adhabu hii ni muda gani sasa?



    Najua huwezi kukumbuka, hata kama memory ya kichwa chako itapelekwa katika komputa na kukumbushwa kwa sababu, huioni thamani yangu mimi ulie ni geuza tambala deki, ilhali ulininunua dukani na kunipenda kila siku kwa kunivaa.



    Ngoja nikukumbushe, toka useme basi mpaka hivi sasa ni sawa na Masaa,SITINI NA MOJA ELFU NA MIA NNE THEMANINI, ambayo ni sawa na siku MBILI ELFU NA MIA TANO ISHIRINI, pia siku hizo ni sawa sawa na miaka SABA timilifu,tangu uniache mpaka leo.



    Hata kama shule mpenzi, je ni kweli hata huko shuleni haukuwa na wavulana?, hakika nimeteseka sana mpenzi wangu juu yako.



    Hivi unadhani kipindi chote hicho nimeweza kuishi na tani ngapi za Maumivu?



    Achilia mbali maumivu, je, vipi kuhusu kuuharibu mfumo wa maisha yangu?.



    Ama kwa hakika nathamini aibu za msichana yeyote katika dunia hii, dunia ambayo imeamua kunipa wewe na kutonionesha mwingine zaidi yako. Na tambua aibu zao pia mbele ya marijali kama mimi, siku shangai kwa wewe kukaa kimya muda wote huo. Huenda ni aibu uliyonayo kama msichana.



    Najua mpaka sasa umejifunza nini maana ya mapenzi, tafadhali. Nikiwa kama mwanaume nilieanza kukupenda kabla ya wengine kukupenda basi nakuomba urudi mpenzi wangu.



    Sitojali ni wanaume wangapi umepitia, tafadhali rudisha upendo wako kwangu kwani wewe ndio chaguo langu la kwanza.

    Natamani na ninahtaji, historia yangu ya mapenzi iishie kwako mpenzi wangu. Kumbuka tumetoka mbali sana mimi na wewe, na mwanamke nilotoka nae mbali ndie anaeweza kuni zalia wanangu na kunifanya niishi kama mwanaume ndani ya familia.



    Please, reconsider and comeback to your firstboyfriend'' Maneno yale yalimpelekea Sumaya aamke kitini kwa furaha yenye kilio na kusogea mkabala kabisa na miguu ya Nurdin kisha akaishikiria huku akiibusu.

    ''Nashukuru sana Samir kwakuweza kunifikiria kwa muda wote huo niliokuwa mbali nawe, hakika una moyo wa dhahabu sana. Nilijua kwamba mimi ndie nitaelia kwa ajili yako kwa kukuomba m,samaha muda ambao wewe utaiona sauti yangu kama ni ya kinafki kila ipitapo kweye masikio yako. Hakika nimejifunza mengi sana kutokana na penzi hili, penzi ambalo toka lianze mpaka leo hii tayari ni miaka saba sasa. Naomba utamke wazi kwamba umenisamehe kwani moyo wangu bado unauma kila nikikumbuka mabaya niliyokutenda uwaridi wa moyo wangu. Nashukuru kwa kutambua kuwa niliteleza tu ila sikumaanisha kuwa sikukupenda bali nilikupenda sana tatizo langu mimi niliingiwa na tamaa na kuacba mbachao kwa msara upitao. Nilisahau kabisa kuwa sipaswi kudharau nazi langu na kufuata embe. Ndio nilidharau nazi pasina kujua kuwa embe ni tunda la msimu akuomba tamka kuwa umemsamehe msichana wako wa kwanza.'' Aliongea Sumaya Nurdin aliinama na kuichukua mikono iliyokuwa miguuni mwake na kumsimamisha Sumaya. Kisha, akamwambia kwa upole kuwa, ''Nimekusamehe mpenzi wangu.''

    Wote kwa pamoja wakakumbatiana kwa muda huku hisia za kila mmoja zikienda mbali sana ndipo Nurdini akayakumbuka yale maneno matamu ya Sumaya siku walipokuwa wote;

    **************************** **********************************************

    " Sijui nikupe nini ilinikufanye uthibitishe upendo wangu kwako. Sijui ni kuite jina gani ililikupendeze kuliko yote. Hebu fumba macho mpenzi," Akajitoa kwenye kumbato kisha Zulfa akayafumba macho kama alivyoambiwa na Nurdin.



    "Mmmhhh!, vizuri sana mpenzi wangu. Sasa unaweza niambia unaona nini ndani ya macho yako?" Ni swali alilotupiwa Sumaya, swali hilo lilimfanya Sumaya atabasamu na kuuongeza uzuri wake maradufu, jambo lililompelekea Nurdin ajisifu kupata mrembo kama yule.



    " Ndio, nimefumba macho yangu. Na sioni chochote kile lakini, hisia zinamuona Nurdin, akili ina muwaza Nurdin, na hata moyo bado umemuhifadhi Nurdin, kuachilia mbali yote hayo, bado naendelea kuskia sauti nzuri, yenye matamshi yaliyojipangilia kwa ustadi kutoka kwa Nurdin. Nakupenda sana Nurdin, umenikaa kila pahali, hata mikono yangu inawaza kukukumbatia tu." Sumaya, aliongea maneno makali sana. Maneno ambayo hata Nurdin mwenyewe hakuyategemea.



    Fumbua macho yako mpenzi. Alisema Nurdin kisha Sumaya akafanya kama alivyoambiwa na mpenzi wake, kisha akaulizwa tena anaona nini kwenye upeo wa macho yake. Nae akajibu anamuona mwanaume wa ndoto zake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Nurdin, natamani kukutekea maji ya kuoga pindi utokapo kazini, kukukaribisha chakula na kukukaribisha kitandani ufikapo muda wa kulala. Lakini pia natamani sana kukusindikiza kazini muda ambao nitakuwa nikimpeleka mwanetu shuleni kwa ajili ya kupata elimu kama tuipatayo sie wazazi wake wa baadae." Aliongea Sumaya, kisha akamshika mkono mpenzi wake kwa mapozi na kumkimbiza mpaka kwenye mti wa embe mbichi.



    "Mfalme wangu, unajua matunda haya yanaitwaje?" Aliuliza Sumaya kwa jina la heshma, jina ambalo laiti kama ukiitwa kwa kuthaminiwa na mpenzi wako basi utajihisi umepaa.



    "hahahahahaha. Malikia wangu, huu, si. Mti wa muembe na hayo matunda simaembe." Alicheka Nurdin kisha kicheko chake akakiambatanisha na majibu.



    "Nashukuru, mfalme wangu kwa kugundua hilo. Labda ngoja nikufafanulie kidogo. Embe liwapo changa, huwa na ukakasi uliojaa utomvu, lakini huendelea kukuwa na kufikia kuwa katika hali ya ukakasi, hapo sasa huweza kuleta hitilafu kwa watumiaji au lisilete hitilafu kwao kutokana na hali waliyonayo muda huo muafaka. Kuna wapendao maembe mabichi na kuna wasiopenda, lakini embe huvumilia vikwazo vyote hivyo na hadi kufikia hatua ya kuiva. Sasa hapo liivapo, hakuna anaelichukia kila mtu hulipenda na kutamani apate angalau ladha ya'lo."



    ************** ************* **************************************************'Kumbukumbu zilimtoka Nurdin na kisha kumkumbusha na Sumaya ambae ndie aliyeiandaa safari ya siku ile. Walicheka na kulia kwa furaha kisha wote kwa pamoja wakaagana na kuteua siku ambayo wangefanya tafrija kwa ajili ya pendo lao kisha wataarika rafiki wa aina mbalimbali ili waweze kushuhudia tafrija hiyo ya wapendanao.

    Kadi za mualiko zilitembea na mchango ukafika, hata Erick nae alipewa mualiko wa kwenye simu tena walimsihi asiache kuhudhuria.

    Erick alimwambia mpenzi wake kuwa alihitajika kwenda shinyanga kwenye tafrija. Mpenzi wake, aliomba waendenae kwani walikuwa wakipendana sana. Erick, kwakuwa alikuwa ameshabadilika alikubali na siku ilipofika walipanda gari yeye pamoja na mpenzi wake Hadya, moja kwa moja hadi Shinyanga. Safari ilikuwa ndefu sana hivyo iliwalazimu kulala njiani na siku iliyofuata ndio ilikuwa siku ya tafrija ille fupi. Walifika siku hiyohiyo na kupitiliza moja kwa moja hadi kwenye sherehe.

    ''Nurdin!!!!???'' Aliita Hadya baada ya kumuona yupo na msichana mwingine.

    Sauti ile ilisikika vizuri masikioni mwa Nurdin pamoa na kwa wageni wote waliyohudhuria. Hadya alitaka kuanzisha tifu ndipo alipogundua kuwa ile sherehe ilikuwa ni ya Nurdin kama angemsumbua basi angeharibu sherehe. Erick alimvuta mpenzi wake pembeni na kumuuliza kama Nurdin alikuwa anafahamiana na Hadya ndipo Hadya alipo muambia kuwa huyo Nurdin ndio mvulana aliyemfanya hadi atamani kujiua. Waliamua kusameheana na kuambiakuwa kujuana katika maisha yao ilikuwa ni sababu ya kutengeneza tu historia za kuhuzunisha na kuwa kiigizo chema kwa vizazi vijavyo.

    Sherehe ilienda vyema na kila mmoja aliifurahia sherehe hiyo. Hadya hakuwa na kinyongo juu ya Nurdin kwani tayari alikuwa ameshampata Erick wake wa maisha, na wala Sumaya hakuwa na kinyogo kwa Erick kwani tayari alikuwa ameshampata Nurdin wake. Wote kwa pamoja walipiga picha huku wa kipongezwa na wageni wengine waalikwa na zaidi kila mmoja aliondoka na funzo kutoka kwenye sherehe ile.

    Erick akarejea Dar-es-salaam yeye pamoja na mpenzi wake Hadya huku Nurdin akibaki na mpenzi wake Sumaya na wote kwa pamoja waliishi maisha ya raha mustarehe.

    Mwisho wa siku ndoto za Sumaya na Nurdin zilitimia. wakawa mke na mume baada ya miaka kupita. Miezi mitatu tu ilisababisha mimba na aliilea Sumaya huku akiamini mwisho wa siku atakuja kumbeba mwanae, Siku ya kujifungua ndio siku ambayo Sumaya aliiaga dunia na kumuacha mtoto wake akilelewa na Nurdin pekee. Hata Nurdin hakumaliza miezi alipata ajali ya gari kutokana na msongo wa mawazo aliokuwa nao kufuatia kifo cha mkewe.'' Na hiyo ndio historia ya Baba yako na Mama yako.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *************************************************

    Samir ambae ni Baba mlezi wa Najma ndivyo alivyoimaliza hadithi ile ambayo aliishi nayo moyo ni mwake kwa muda wa miaka ishirini huko nyuma. Najma alifurahia sana historia ya wazazi wake na ndipo alipo ahidi kwenda kuandaa historia fupi ya wazazi wake ili akaielezee kwenye tamasha la wazazi lililotarajiwa kufanyika baada ya siku hiyo. Kwakiasi kikubwa historia ya maisha ya wazazi wake ilimfunza mambo makubwa na aligundua kumbe Samir alikuwa mtu wa muhimu sana katika maisha ya wazazi wake. na kwanzia hapo Najma akaijua historia ya wazazi wake ambao tayari wamesha tangulia nayo alipewa na baba yake ambae ni Samir. Hapo pia aligundua ni kwanini Baba yake huyo huwa hana shida na kuoa katika maisha yake.



    ****************** MWISHO **************************



0 comments:

Post a Comment

Blog