Simulizi : Usaliti Wa Kiapo
Sehemu Ya Tano (5)
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Uwezo wake darasani ulimfanya azidi kuwa maarufu chuoni hapo, kila mmoja alikubali kuwa yeye ni msichana mwenye kipawa cha pekee, hakupewa uzuri tuu hata akili zilikuwemo, pamoja na hayo yote hakuweza kumsahau barafu wa moyo wake ambaye kwa wakati huo alijua kua amemuacha katika wakati mgumu, akawa anajitahidi kuwasiliana nae karibu mara mbili au tatu kwa siku.
Ucheshi na ukarimu wake ulimfanya awe na marafiki wa kila haina, hakubagua aliongea na kucheka na kila mmoja. Kadri siku zilivyozidi kwenda ndivyo thamani ya mrembo huyo ilivyozidi kupanda katika kipindi iko cha masomo, akajikuta akipewa mkataba mnono na wa malipo mengi katika kampuni moja inayojihusisha na maswala ya mitindo na matangazo (Tae Xhian Sung Group).
Ndani ya kipindi kifupi akawa ni mwafrika wa kwanza kutikisa korea pamoja na ukanda wote wa Asia. Siku moja Tae Xhian Sung Group ikaandaa sherehe ambayo ikapangwa kufanyika katika visiwa vya Jeju.Hivyo wahusika wote wakaambiwa wawe tayari, wakati safari ya kutoka Selou hadi Jeju inaanza Martha yeye alikuwa kwenye mitihani, hakuweza kuungana na wenzie kwa wakati, lakini kampuni haikutaka kumkosa katika sherehe iyo hivyo ikamuacha nyuma kijana mmoja mtanashati hasa na mwenye muonekano maridhawa aliyetambulika kwa jina la Kim Chang Lee. Kijana huyu yeye anaasili ya Kikorea na anafanya kazi katika kampuni hiyo kama mwanamitindo pia. Kim Chang Lee alipewa jukumu la kuhakikisha Martha anafika Jeju bila shida yeyote.
“Daah! They did well to left me behind, (wamefanya vizuri kuniacha mimi)”.
Kim Chang Lee akajikuta akitamka punde tuu alipomuona Martha, kwa hakika hakujutia kuachwa nyuma na mrembo yule. Martha akamtazama Kim na akatabasamu,
“I like the way you smile, (napenda jinsi unavyotabasamu)”
“I think it’s my first to see you, my name is Martha, (nadhani ni mara ya kwanza kukuona, mimi naitwa Martha)”
“No need for introduction, I know almost each and everything about you! My name is Kim Chang Lee, am working at Tae Xhiang Sung Group as the Fashionist, so am your work mate, let’s keep intouch, (haina haja ya kujitambulisha najua kila kitu kuhusu wewe, mimi naitwa Kim Chang Lee ni mwanamitindo, tutakuwa pamoja katika kazi, ivyoo tuanze kuzoeana”.
Martha akacheka na tayari safari ya kwenda visiwa vya Jeju ikaanza, Kim akawa muongeaji sana karibu njia nzima yeye tuu akawa anaongea huku akijaribu kuiteka akili ya mrembo yule, kwa kiasi flani alifanikiwa maana wakajikuta wakiwa marafiki ndani ya kipindi kifupi.
Safari ilitia nanga hatimae wakajikuta wametua katika uwanja wa kimataifa wa ndege katika visiwa maarufu kwa utalii nchini korea (Jeju). Moja kwa moja walienda kwenye hotel ambako huko ndiko sherehe nzima iliandaliwa.
“Ladies and gentlemen, I would like to take this opportunity to welcome our honorable Model from Selou University, Miss Martha, applause for her please, (Mabibi na Mabwana, napenda kuchukua nafasi hii kumkaribisha mwanamitindo wetu toka Chuo Kikuu cha Selou, Martha makofi kwake tafadhali”
Yalikuwa maneno ya mshehereshaji wa siku iyo akimkaribisha Martha kwa ajili ya kusema chochote.
“Good evening everyone! (habari ya jioni!)”
Salamu ile ya Martha iliwapa nafasi watu wengi kumtazama mrembo yule kwa umakini, mwanga hafifu uliokuwapo sehemu ile ulifanya ngozi ya mwanadada huyo kung’aa mithili ya mshumaa. Kim akabaki kuduwazwa na uzuri wa msichana yule, hakuwa anasikiliza nini kinachoongelewa hadi pale aliposhituka kuona watu wakipiga makofi nae akaungana nao. Kim akajiapiza kuwa ni lazima ampate mrembo yule kwa gharama yeyote. Akamgeukia rafiki yake aliye kaa karibu na kumuuliza,
“Did you know anything about that girl? (Unajua lolote kuhusu msichana yule?)”
“I don’t get you! (Sijaelewa swali lako)”
“I want to know the man whom in love with, (naitaji kumfahamu mwanaume anayempenda)”
Swali lile lilimfanya jamaa acheke sana nusu ya kuanguka, Kim akamtazama jamaa kwa mshangao kisha akaendelea kusema;CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Why are you laughing? That girl capture my heart within this short period of time, (mboni unacheka msichana huyu ameuteka moyo wangu kwa kipindi hiki kifupi)”.
“That girl is not cheap as you think, She reject all my friends, (Msichana sio mrahisi kama ufikiliavyo, rafiki zangu wote wamekataliwa)”.
“So none succesed to have her? (Kwa hiyo hamna aliyefanikiwa kumpata?)”.
“Exactly! But they said she has a man of of her destiny, (Ndiyo! Ila inasemekana ana mwanaume wa maisha yake)”.
“Where is he? (Yuko wapi?)”
“He is from her mother Country Tanzania, (yupo nchini kwao Tanzania)”
“It’s too far from here! And I assure you, that woman will be mine within two weeks, (ni mbali sana toka hapa na nakuhakikishia ndani ya wiki mbili atakuwa wangu)”.
“All the best broo! (Kila la kheri kaka)”
“Thanks! The game started now, (Akhsante! Mchezo ndio unaanza sasa)” alisema Kim Chang Lee.
Sherehe iliendelea kila mmoja aliburudika na kufurahi sana, wakati wa kucheza muziki Kim akaona Martha akiwa sehemu ya peke yake, akajisogeza. Martha bila kinyongo akamkalibisha na wakaanza kuzungumza. Wakati wakiendelea kuzungumza wakawa wanapata burudani toka kwa mwanamuziki maarufu nchini Korea ambaye alialikwa kutumbuiza siku hiyo. Mwanamuziki huyo aliimba nyimbo za taratibu zilizowafanya watu wacheze bila kutoa jasho. Kim akaamua kutumia huo kumchombeza Martha,
“Mwanaume yeyote atakayekukalibia wewe atajihesabia kuwa ni mwenye bahati katika siku zote za maisha yake,” alisema Kim Chang Lee.
“Oooh! I thought you do not know how to speak Swahili, (Ooh! Nilidhani kuwa hujui kuzungumza Kiswahili),” alisema Martha.
“am fluently on it, (nakijua vizuri tu)”.
“Congrats! (Hongera)”.
“Thanks! (Akhsante)”
“Your welcome”.
“Ukweli wewe ni msichana mrembo sana, katika maisha yangu yote ya korea sijapata kuona wa kufanana nawe”
“Mhmh! Asante kwa hilo”
“Martha, can we be friends? (Martha, Je twaweza kuwa marafiki?)”.
“Ofcourse Kim, why not? (Bila shaka Kim)”.
Huo ndio ukawa mwanzo wa ukaribu kati ya Kim na Martha, Kim alijitahidi kufanya vitu vingi kwa mrembo yule kuhakikisha anateka akili yake. Kwa kiasi kikubwa alifanikiwa, Martha akapunguza mawasiliano na Tony. Kim alichipusha hisia za penzi jipya kwa Martha, wengi waliwapongeza wawili hao kuwa pamoja. Umaarufu wao uliongezeka maradufu, kiasi cha kuweka maisha yao ya kila siku mitandaoni, hii ikawaongezea watu wengi waliofata. Martha alijua wazi kuwa Tony asingeweza kuvumilia hali ile, hakutamani aone kinachoendelea ikabidi azuie kuonekana kwenye akaunti za Tony.
Mambo yakazidi kwenda kombo kwa Tony, ambaye alijikuta akishindwa kumakinika katika shughuli zake, alimpenda sana Martha lakini hayo yanayotokea sasa alishindwa kuelewa nini hatima yake. Hakutaka kusadiki yale aliyoyasikia kwa rafiki wa Martha kuwa yupo kwenye penzi jipya, aliamini kuwa hayo ni maneno yanayolenga kuvunja Imani yake kwa Martha. Jioni moja Yassir na Darmy wakamzuru Tony kwa minajili ya kumjulia hali, walimuhurumia sana swahiba wao huyo ambaye muda mwingi tabasamu lilikuwa likichanua usoni mwake,
“Kuwa mvumilivu kaka, sisi tunaamini Martha anakupenda labda anabanwa sana na masomo,” alisema Yassir.
“Kubanwa huko na masomo ndio hadi kuzuia nisimuone katika mitandao ya kijamii,” alisema Tony.
Hapo wazo jipya likaja vichwani mwao, Darmy na Yassir wakatoa simu zao na kuingia facebook, kisha wakatafuta jina la Martha cha ajabu Zaidi nao wakakuta wamezuiwa wasiweze kuona chochote katika akaunti ya Martha.
“Daah! Ebhana eenh! Hadi sisi ametuzuia,” alisema Darmy.
“Ngoja tujiridhishe, nafungua akaunti mpya ya muda hili tuweze kuona,” alisema Yassir.
Akatumia kama dakika 10 kufungua akaunti mpya ya facebook na bila kupoteza muda wakatafuta jina la Martha, kwa bahati nzuri wakaliona. Wakaanza kuangalia picha moja baada ya nyingine. Tony akajikuta akishindwa kuvumilia yale aliyokuwa akiyashuhudia, mapigo ya moyo yakaenda kwa kasi mno, machozi yakatengeneza mifereji kwenye mashavu yake.
“Daah! Kweli hapa kuna ulazima wa kumtafuta Martha na kumuuliza kulikoni,” alisema Darmy.
“Yeah ni kweli bora tufanye hivyo mapema!” Yassir akaitika.
Muda wote huo Tony hakujiweza kwa lolote, Machozi ndiyo yakawa rafiki yake, Maumivu aliyoyasikia alishindwa kuyafananisha na maumivu yeyote katika dunia hii. Akaanza kujenga urafiki mpya na pombe, rafiki zake walifanya juhudi kubwa kumzuia lakini haikufaa kitu.
Jumapili moja baada ya Tony kutoka kanisani rafiki zake wakaamua wampeleke katika moja kati ya fukwe maarufu jijini Dar es Salaam, walau akatulize akili yake. Mambo hayakuwa hivyo kama wao walivyodhani kwani ni katika siku hiyo Martha aliamua kumuandikia ujumbe mzito Tony,
“Naomba unisamehe kwa haya nitakayokwambia, ukweli nimeshindwa kuitunza ahadi tuliyopeana, kwa sasa nina mpenzi mpya na nafikiri kuwa naye katika siku zote za maisha yangu. Sina hisia zozote zilizobaki juu yako, naomba unisahau ikiwezekana utafute mwanamke atayekufaa kwenye maisha yako. Najua nimekosa ila ndiyo hivyo imeshatokea”
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Tony alihisi kuzirai alipousoma ujumbe ule, haikuwa rahisi kwake yeye kusadiki maneno yale, akarudia tena na tena lakini maneno yakabaki vile vile. Tony akajikuta akicheka mno, alicheka mpaka akagalagala huku machozi yakimtoka. Hali iyo ikawaogofya sana maswahiba zake wakahisi labda Tony anaweza kuwa amepata tatizo la akili, Tony akaanza kukimbia kwa kasi huku akicheka. Darmy na Yassir wakapata kazi mpya ya kumfukuzia hili wamkamate, Tony akawa na nguvu ya ajabu siku hiyo, rafiki zake wakajitahidi kumshika na kumtuliza,
“Mwanamke ninayempenda anampenda mwanaume mwingine, niambieni je kuna umuhimu wowote wa mimi kubaki katika dunia hii?” aliuliza Tony huku akilia.
“Tony wewe ni mtoto wa kiume tulia kwanza!” alisema Darmy.
“Niliposoma riwaya ya UKO WAPI, nilicheka sana kuona Nelly anamlilia Patricia, sikuwa najua maumivu yake lakini leo nimejua na sidhani naweza kuwa kama yeye,” alisema Tony.
“Kwa sasa kila utakalolifanya ni sawa na bure, turudi kwanza nyumbani utulize akili,” alisema Yassir.
Tony akawa kama nusu chizi, kuna wakati Alilia na kucheka kwa pamoja, hali ile ilimuumiza sana dada yake, ambaye hata yeye hakuamini kama Martha angebadirika kiasi kile. Dada aliamua kujiridhisha kwa kutaka kuongea naye yeye mwenyewe, akatafuta mawasiliano ya Martha na kupiga simu. Simu iliita kwa muda na baada ya muda ikapokelewa,
“Hallo! Are you Martha? (Hallo! Je wewe ni Martha?)”
“Yes! Who are you? (Ndio nani mwenzangu?)”
“Mimi ni dada yake na Tony”.
Martha aliposikia hivyo akakata simu, hakutaka kuongea lolote na dada huyo. Rozina akafikiri juu ya hatua ile aliyoichukua Martha, akapata majibu kuwa uhenda ni kweli mapenzi kwa mdogo wake yameisha. Wakati akiendelea kufikiri hayo ujumbe mfupi ukaingia katika simu yake,
“Samahani sana sina ujasiri wa kuongea nawe na hata hivyo siwezi kubadili msimamo wangu, kila kitu nimeshamuambia Tony, hivyo tafadhali naomba mniache”.
Dada alizidi kuchanganyikiwa aliposoma ujumbe ule hakuwa na haja ya kumficha mdogo wake, akamuonesha ingawa alijua ni wazi utamzidishia maumivu. Tony hakuongea lolote Zaidi ya kuendelea kufakamia pombe iliyopo kwenye bilauri.
“Mdogo haukuzaliwa kuwa dhaifu, inuka sasa haya ni majaribu na hutokea katika maisha ivyo pambana mdogo wangu,”
“Kwanini aliuteka moyo ilihali alijua kuwa atakuja kuumiza, kwanini alinitega nikategeka wakati hakupanga kudumu name, aliufunza moyo wangu kudunda nami nikajifunza kuvumilia kila gumu, dada najihisi siwezi tena bila ya yeye,” alisema Tony.
*******************************
Maisha ya Tony yakabadirika sana toka kipindi hiko, akawa ni mtu wa kunywa pombe tuu kila kukicha, akaachana na maswala ya muziki kwani aliamini kufanya vile kungemsaidia kutoka kwenye kizungumkuti cha huba alichonacho kwa Martha.
Miaka miwili baadae, Tony akafungua kampuni ndogo iliyojihusisha na maswala ya video production, kampuni hiyo ilizidi kukua siku baada ya siku na kupata umaarufu mkubwa nchini. Kidogo alichokipata kutokana na kazi yake hiyo alikiongezea katika ununuzi wa vifaa vya kisasa. Falsafa yake mpya ikamfanya awe na staha kwenye matumizi ya mapesa. Toka aliposalitiwa na Martha hakuweka Imani yeyote juu ya mwanamke, hapo ndipo alipoanza uchakaramu, Tony hakuweza kuwa na penzi la dhati. Aliwatumia wasichana kukidhi haja zake na katu katika maisha yake hakuwahi kutamka neno nakupenda kwa kumaanisha. Kwa waliofahamu shida na dhahama alizopitia Tony hakuna aliyethubutu kunyanyua kinywa chake kusema kwa anakosea kuwa na uhusiano Zaidi ya msichana mmoja, japo ni kweli haikuwa sawa.
Mshauri wa kampuni alimaliza simulizi yake kwa kusema,
“Hayo ndiyo Tony aliyoyapitia na Martha anajua wazi alichofanya kuwa si sahihi na ndiyo maana anajaribu kutetea walau kulipa uovu alioufanya. Ninyi leo hii mnamuita Tony Malaya sijui hajatulia ila hamkujua nini amepitia, haya semeni sasa wangapi manta kuacha kazi eti kisa mkataba wa Tony”.
Wote wakakaa kimya na kujikuta wakimuangalia Martha kwa jicho baya, hawakuamini kama mrembo huyo angeweza kuwa mkatili. Wengi wakaelewa kwanini Martha alimtetea Tony mara zote alizojaribu kuzembea katika kazi. Jose akapata kufahamu kilichojificha nyuma ya pazia akakumbuka jinsi Martha alivyojipa shida ya kufanya kazi Zaidi na hata kufanya kazi za Tony. Alimuhurumia Martha kwani alijua ni wazi msichana yule bado anaumia kwa kile alichokifanya.
Swali likabaki kwa Martha kuwa huyo Kim Chang Lee bado wako katika mahusiano au la! Kama wameachana nini kilitokea na kama hawakuachana kwanini Martha aliamua kurudi Tanzania kufanya kazi. Hiyo ikabaki siri ya Martha mwenyewe ingawa wote walitamani kujua.
Ni mwezi wa 4 sasa toka Tony apate tatizo lile, Hali yake iliwakatisha tamaa sana, Mjomba alihangaika kadri alivyoweza lakini hakuweza kufanikiwa, alitumia pesa nyingi katika matibabu ya Tony. Mara ya mwisho kwenda hospitali wakaambiwa kuwa mguu ulishaaribika wote na sumu ilisambaa hadi usawa wa kiuno, hivyo ata kama watamkata mguu bado hawataweza kuzuia sumu kuendelea kushambulia sehemu nyingine za mwili.
Daktari akawaambia kuwa Tony anaweza kuishi walau kwa miezi mitano Zaidi ya hapo sumu itakuwa ishafika kwenye moyo na ndio utakuwa mwisho wa maisha yake.
Taarifa hiyo ikawafikia wafanyakazi wote, wengi walihuzunika kwa hilo Martha, akajihisi ni mkosaji Zaidi. Hakuelewa nini atakifanya endapo Tony atafariki, akaitisha kikao cha dharula kwa wafanyakazi wote.
“Nina wakati mgumu kwa sasa, nashindwa kumakinika katika kazi, hivyo naomba niache kampuni mikononi mwenu. Jose utakaimu nafasi yangu hadi pale mambo yatakapokaa sawa, naomba sana mzingatie kazi,” alisema Martha huku machozi yakimbubujika.
Wafanyakazi wote wakaa na kumsikiliza mkurugenzi wao huyo, simanzi ilikuwa kubwa mioyoni mwao. Kabla Martha hajaongea Zaidi akahisi kizunguzungu, kiza kikatawala macho yake na taratibu akaanguka chini. Jitihada za haraka zikafanyika kumuwahisha hospitali, baada ya dakika kadhaa daktari akatoka na kuwatazama Jose na Darmy,
“Nani ni mume wa binti huyu?”
Jose na Darmy wakatazamana wasijue nini la kujibu,
“Mbona mnashangaa au hamkuelewa nini nilichowauliza?”
“Daktari tuambie hali ya mgonjwa wetu,” akasema Jose.
“Ooh! Kumbe ni wewe! Hongera mkeo anaujauzito wa mapacha ambao huu ni mwezi wa 4 sasa!” alisema daktari huku akimpa mkono wa pongezi Jose.
Jose na Darmy wakaendelea kuduwazwa na habari ile, wakaingia chumba cha mapumziko ambacho Martha amelazwa.
“Atleast now I have a reason to live, (walau sasa nina sababu ya kuishi),” alisema Martha.
“Hongera! Tumesikia kila kitu toka kwa Daktari, sasa baba wa watoto hao yuko wapi?” akauliza Darmy.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Swali lile likamfanya Martha ashindwe kuzuia machozi yake kwa mara nyingine akajikuta akilia kama mtoto mdogo, Jose na Darmy wakafanya kazi kubwa kumbembeleza.
“Ni sawa tuu kama inakuwia ugumu kutuambia! Unauhuru huo pia,” alisema Darmy.
“Tony is the father of this kids, (Tony ndiye baba wa watoto hawa),” akasema Martha.
Darmy akahisi kama anaangalia tamthilia ya kifilipino, hakutaka kusadiki wala hakutaka kukataa kauli ya Martha. Jose alionekana kukubaliana na kile alichokisikia kwani alijua kila kitu kilichotokea kipindi walichokuwepo Tanga, hakuwa na shaka kwani ni kweli miezi 4 imepita toka watoke huko na ujauzito una umri huo.
“So it’s true that Tony is a biological father of those kids you conceive? (Kwa iyo ni kweli kuwa Tony ndiye baba halali wa watoto hao uliowabeba kwenye tumbo lako),” Darmy akauliza.
“Yeah! Its true, (ni kweli)”
Mbali na yote yaliyotokea Darmy alijawa na furaha sana kuona walau rafiki yake atapata warithi, japo mwenyewe hakuwa analifahamu hilo. Maandalizi ya kuelekea Mbeya yakakamilika Martha akaongoza na Darmy na Yassir, njia nzima Martha alijawa na hofu juu ya kipi atakachozungumza pindi akifika huko. Akakumbuka jinsi alivyoongea na dada yake Tony akajikuta nguvu zikimuisha,
“Usijali! Habari hizi zinaweza zikamfanya Tony atamani kuendelea kuishi, sizani kama atakufa na kuwaacha watoto wake nyuma bila malezi ya baba,” alisema Darmy.
“japo tunajua ni kiasi gani umemkosea rafiki yetu, ila sisi kinyongo hatuna kwa sasa tunataza hatima ya hao watoto walio tumboni mwako,” Yassir naye aliongea.
Kwa kiasi kikubwa Martha alianza kupata Amani ya moyo kwa kuona walau kuna watu walioweza kusamehe uovu wake na kuamua kuanza upya.
“Nitafurahi sana kama Tony atanisamehe, na wala sitohuzunika kama hatonisamehe sababu nastahili yote hayo,” aliongea Martha.
Maongezi yaliendelea huku wakiwa kwenye ndege inayoelekea jijini mbeya na saa chache baadaye wakafika na kuchukua usafiri mwingine wa kuelekea Tukuyu.
******************
“Dada niahidi kuwa kuanzia leo hutolia tena,” alisema Tony.
“Hapana mdogo wangu siwezi, naumia sana ujue,” alijibu Rozina.
“Sasa dada kilio hiki hadi lini, mimi nimeshakubali kila kitu hata hivyo bado kitambo kidogo utasahau kila kitu kuhusu mimi, usilie dada,” alisema Tony kwa huzuni.
Rozina alishindwa kabisa kujizuia kila alipomtazama mdogo wake ambaye miezi michache iliyopita alikuwa ni mwanaume mwenye muonekano mzuri na mvuto wa aina yake, leo amelala, ngozi iliyong’aa imekuwa nyeusi kama kama mkaa. Mwili uliojaa leo umeisha mithiri ya muathirika wa ukimwi, hakika ilikuwa huzuni na pigo mno.
“Mdogo wangu hata wale wasichana zako wote hawaonekani!”
Tony alijikuta akicheka sana, hadi dada akamshangaa kwanini iwe vile, Tony akamtazama dada yake na kumwambia,
“wanahaki ya kufanya hivyo na walau wamepata mtu wa kuniadhibu kwa niaba yao, kwa niliyowafanyia kwa kweli acha waendelee na maisha yao,” alisema Tony.
Wakati wakiwa chini ya muembe na kuendelea na mazungumzo jioni hiyo ya saa 10, Rozina akawa wa kwanza kuwaona Darmy na Yassir alifurahi mno, hakuweza kumgundua Martha kwa haraka hadi pale walipofika karibu kabisa. Rozina akasimama tena kwa hasira sana,
“Umefata nini Martha! Au ndiyo umekuja kummalizia mdogo wangu?”
Martha hakuwa na la kujibu Zaidi ya kutoa tu machozi, Darmy na Yassir wakajalibu kumtuliza dada atulie hili wazungumze lakini dada hakukubali aliendelea kufoka na kumtaka Martha aondoke eneo hilo. Rozina hakutaka kuelewa wala kumsikia yeyote alimshushia lawama zote Martha, akadai kuwa hayo yote yaliyotokea kwa mdogo wake sababu ni yeye na wala hakuwa na umuhimu wa yeye kuja pale. Muda wote huo Tony hakusema lolote kwani naye alijua wazi kisa cha yeye kuwa vile ni Martha kama msichana huyo angetunza kiapo chake basi hakukuwa na namna yeyote ya Tony kukengeuka.
Baada ya mzozo wa muda mrefu mjomba akafika naye alishangaa sana kumuona Martha pale, wahenga wansema Jungu kuu siku zote alikosi ukoko. Mjomba akatumia ukubwa wake kumtuliza Rozina na kuwakaribisha wageni. Martha akasogea hadi alipo Tony na kuomba radhi huku akisindikizwa na machozi.
“Niko radhi kwa adhabu yeyote utakayonipa, sitojali ila kikubwa nahitaji msamaha toka kwako,” alisema Martha.
Rozina akamuangalia Martha kwa jicho la chuki mno hakutamani kumuona eneo lile.
“Sasa Martha kwanini ulimtenda mwenzako kiasi kile!, hadi kufika hatua ya kuharibu maisha yake kabisa,” Mjomba akauliza.
“Uncle! Nitawaambia kila kitu ila naomba nipumzike kidogo,” alisema Martha.
Mjomba akaridhia ombi lile, Rozina ikabidi aingie jikoni kuandaa chakula kwa ajili ya wageni. Darmy, Yassir na Martha wakabaki pale alipo Tony,
“Tumekumisi sana wa obey, inuka jamaa tukapige misele,” alisema Darmy.
“Ndiyo kama hivi nipo! Vipi Yassir mkeo hajambo,” alisema Tony.
“Yeah yuko poa sana! Salamu na pole nyingi toka kwake,” alijibu Yassir.
“Vipi Darmy na wewe jambo zako hazielewekagi au ndio mzee wa ngumu hiphop moja!” alisema Tony.
Kwa mara ya kwanza baada ya kipindi kirefu kupita wakajikuta wakicheka kwa pamoja. Muda wote huo Martha alikuwa ni mtu mwenye mawazo na huzuni nyingi,
“Martha binafsi nilishakusamehe siku nyingi, huna haja ya kuishi kwa majuto, kuwa huru na ufurahi na mwanume umpendaye, mimi mwisho wangu umekaribia. Bado miezi 5 tuu,” alisema Tony.
Martha akamsogelea Zaidi na kumkumbatia Tony huku akilia,
“Ni makosa yangu Tony samahani sana, ila sikuwa na jinsi kwa wakati ule.
“Basi usiseme kitu Martha usije pata homa bure,” alisema Yassir.
Hadi kufika hapo hakuna mtu aliyekuwa tayari kufichua siri ya ujauzito wa Martha, kwa kuwa hawakujua taarifa ile itapokelewa vipi kutokana na tofauti kubwa iliyotokea katika maisha ya wawili hao.
Muda ukasogea hatimaye giza likaingia, hakuna aliyeweza kukaa nje kutokana na baridi kuwa kali mno, wote wakaa sebuleni na kuendelea na mazungumzo.
“Nadhani ni wakati sahihi wa mimi kusema kile kilichonifanya hadi kuja hapa,” alisema Martha.
“Huna haja ya kusema, tushaelewa na tushakusamehe hivyo fanya tu uondoke,” alisema Rozina kwa hasira kidogo.
“Najua ni kiasi gani nimesababisha matatizo katika familia hii, nimemkosea Tony mwanaume aliyenipenda name ninampenda kuliko maelezo..”
“Wee! Koma! Ungekuwa unampenda ungemuacha,” Rozina akasema kabla ya Martha kumalizia sentensi yake.
“Rozina tulia basi tumsikilize,” alisema Mjomba.
Martha akakohoa kidogo kuweka koo lake sawa, kisha akamtazama kila mmoja usoni kwa zamu, alafu akaanza kusimulia..
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
**************
Chuo kikuu cha Selou kinashikilia rekodi ya kuwa na mrembo wa vyuo vikuu nchini Korea aidha chuo kile ni moja kati ya vyuo vichache vinavyojali vipaji vya wanafunzi wake. Mimi nilienda kwa lengo la masomo tuu sikupanga kufanya lolote nje ya kusoma, lakini nilijikuta kuvutiwa kuwa mwanamitindo hasa baada ya marafiki zangu kufanya mambo hayo. Mashindano yaliandaliwa na nikaibuka mshindi mbele ya wenyeji, ushindi ule ukanipa mkataba mnono wa kufanya mambo ya mitindo katika kampuni moja maarufu nchini humo inayotambulika kwa jina la Tae Xhiang Sung Group.
Mambo yakabadirika baada ya mimi kuwa mshindi na pia kuanza kufanya kazi katika kampuni hiyo, mkataba ukanizuia mimi kuonekana na watu hovyo. Nikalazimika kufanya kila kitu change kwa usiri mkubwa mno. Ikatokea nikafahamiana na kijana mmoja aitwaye Kim Chang Lee, yeye huyu ni mwanamitindo wa kimataifa kwani kazi zake zilivuka mipaka ya asia na kusogea kabisa katika bara la ulaya na amerika. Akaniomba urafiki nami sikuona sababu ya kumkatalia sababu wote tulikuwa tunafanya kazi sehemu moja. Kijana yule alizidisha ukaribu sana upande wangu ikafika hatua ikabidi aeleze hisia zake waziwazi,
“Martha! I love you and I want you to be mine, (Martha nakupenda na nahitaji uwe wangu)” alisema Kim Chang Lee.
Kauli ile ilizua mshtuko sana kwangu, ukweli hata mimi nilimpenda lakini kama rafiki wa kawaida sikuwa na hisia zozote za kimapenzi juu yake. Mara zote alizoniambia hivyo nilimkataa na kumwambia kuwa nina mwanaume ambaye sifikirii kumpoteza.
Kim ikabidi aanze kufanya uchunguzi kupitia mtandao wake, na akamgundua Tony. Ukweli alinidhiaki sana na mwisho akaniambia,
“Usijali najua kuna mtu unampenda, hivyo sioni sababu ya mimi kuingilia kati mapenzi yenu, tuendelee kuwa marafiki wa kawaida”
Baada ya kuniambia hayo tukawa tunatembea sehemu nyingi na watu wengi wakajua kuwa wawili sisi ni wapenzi, tulipiga picha nyingi katika sehemu tofauti tofauti. Kuna siku ambayo siwezi nikaisahau katika maisha yangu, Kim alinialika sehemu Fulani akiwa na rafiki zake, nikaitikia wito na ndiyo siku hiyo iliyobadili kabisa muelekeo wa maisha yangu. Kim akishirikiana na rafiki zake waliniwekea madawa kwenye kinywaji nikawa sielewi wala kutambua lolote lilioendelea.
Nikaamka siku iliyofata na kujikuta nikiwa nyumbani kwangu, sababu sikuwa nahisi hosteli kampuni ilinipa nyumba ya kukaa. Sikuwaza chochote wala sikuona badiliko lolote katika mwili wangu Zaidi ya kichwa kuniuma mno. Niliendelea kulala kwa kuwa sikua na vipindi siku hiyo, nilishtushwa na ujumbe mfupi ulioingia kwenye simu yangu,
“Vipi mpenzi! Bila shaka uko poa, nataka nije niwe nawe siku ya leo”
Ulikuwa ujumbe kutoka kwa Kim, nilipousoma nikafikiri labda amekosea namba lakini nilivyomuuliza alisistiza kuwa aliukusudia kwangu. Nikashangaa sana, nikamkumbusha mipaka tuliyojiwekea kuwa sisi ni marafiki tuu na hamna cha ziada. Kim alicheka mno kisha akanambia,
“sizani kama utaweza kunikataa baada ya dakika 3 zijazo”
“hata Kama itakuwa mwezi ukweli siwezi kuwa nawe,” nilimjibu.
Baada ya dakika 2 nikapokea picha kwenye simu yangu, picha hizo zilionesha nikiwa kitandani na wanaume watatu, nguvu ziliniisha sana sikuelewa nini cha kufanya. Kim akatuma ujumbe mwingine,
“Muda mfupi dunia itatikisika kama utaendelea kunikataa, na huyo mpenzi wako unayelinga naye sizani kama atakuwa na mapenzi nawe tena,” alisema Kim.
Niliogopa sana, sikuwa na ujanja Zaidi ya kufata masharti yake, akanilazimisha niweke picha kwenye mitandao ya kijamii zilizoashiria kuwa mimi naye tupo kwenye mahusiano, kwa kuwa sikutaka kumuumiza Tony ikanilazimu nimzuie asione kinachoendelea. Haikuishia hapo nikalazimika kufanya mahojiano na vituo mbalimbali vya habari nchini Korea na kuelezea uhusiano wetu, ndani ya muda mfupi tukaongeza watu ambao wanatufata na kuziangalia kazi zetu. Nilijiona mkosaji sana sikuwa na ujasili wa kuwasiliana na Tony nikiwa katika hali ile, hapo nikalazimika nimtumie ujumbe wa kumtaka anisahau na awe katika mahusiano mapya.
Kadri siku zilivyozidi kwenda ndivyo nilivyozidi kuwa mtumwa kwa Kim, nililazimika kufanya vitu ambavyo sikuvipenda ila kutokana na yeye kushikiria mpini nami makali sikuwa na budi. Nikatafuta mtu ambaye alinishauri vizuri na kunitafutia mwanasheria, ambaye kwa pamoja tukatafuta ushahidi wa kumuweka Kim hatiani. Tulibahatika kupata vipande vya video vilivyorekodiwa na CCTV kamera zilizokuwa eneo la hotel na ilionesha kila kitu toka wakiniraghai na kuniwekea madawa, jinsi walivyonibeba na kunipeleka chumbani japo hatukuweza kupata picha juu ya kilichofanyika ndani ila walionekana wakitoka huku wakiwa na kamera. Hii ikaturahisishia kufungua mashtaka na Kim akapewa adhabu ya kulipa faini na kuhukumiwa miaka 10 jela kwa kosa la udhalilishaji. Hapo ndipo uhuru wangu ukarudi na kwa kipindi hiko nikawa nimeshahitimu masomo yangu. Nikashawishi kampuni kufungua tawi nchini Tanzania sababu sikupenda kabisa kubaki Korea, kampuni ikakubali ombi langu na kunipa mimi jukumu la kusimamia kila kitu. Hapo ndipo tukatoa nafasi kwa makampuni zawa kutuma maombi ya kuingia na kampuni yetu. Nilifurahi sana nilipoona Tony akiwa mmoja kati ya kampuni 50 zilizoomba, sikuwa na haja ya kuziangalia kampuni hizo nikaipitisha kampuni ya Tony huku nikiamini ni sehemu tuu ya kulipa uovu mabao naweza kusema niliufanya juu yake.
Hadi kufikia hapo kila mmoja alijikuta akilia na kumuhurumia Martha kwa yale aliyoyapitia, Rozina hakujizuia akamsogelea Martha na kumkumbatia,
“Nisamehe sana Martha, sikujua kama ulipitia magumu hayo,” alisema Rozina.
“Nisamehe pia,” Martha akasema.
Tony akamuangalia Martha na kuangusha tena machozi, Martha akamsogelea na kumkumbatia kisha wote wakaungana kulia.
“Haya yote ni majaribu ambayo wawili ninyi mmepitia, hivyo yazikeni yaliyopita na kufikilia mapya,” alisema Mjomb.
“Tony, nilikupenda, nakupenda na nitaendelea kukupenda siku zote za maisha yangu,” alisema Martha.
“Martha nataka uishi maisha yako kwa furaha na Amani tele, mimi siwezi tena hapa unionavyo nimebakiza miezi 5 tuu,” alisema Tony.
“Hata kama ungebakiza siku 5 bado Tony siwezi kukuacha, nataka nifurahi nawe”
“Hapana siwezi kuruhusu hilo, Martha wewe ni msichana mrembo na unahitaji mwanaume mwenye nguvu na uwezo, katika hali yangu hii hapana sitoweza”
“Tony nami sitoweza kuwa na mwanaume mwingine tofauti nawewe”.
“Kwanini?”
Martha akafikiri kidogo kabla hajasema kile ambacho moyo wake umekusudia, kisha akawatazama Darmy na Yassir ambao walikaa kimya kwa muda mrefu kuacha wawili hao wazungumze. Darmy na Yassir wakatikisa kichwa kuashiria kuridhia lile ambalo Martha anahitaji kulisema.
“Tony! Tumboni kwangu kuna watoto wawili mmoja wakike na mwingine wakiume nawewe ndiye baba yao”CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Taarifa hiyo ilimfanya Tony ainuke na kukaa kitako kama vile hakuwa anaugua na kwa muda mrefu hakuweza kunyanyuka mwenyewe Zaidi ya kubebwa kutokana na upande wake mmoja kupooza. Jambo ambalo lilimshangaza hata mjomba,
“Martha unasema kweli?”
“Ndiyo Tony! Usiku ule mmoja tuu ulitosha kufanya haya yote”
Tony akamkumbatia Martha, furaha ikalejea upya katika familia ile, Rozina alifurahi mno, mjomba, shangazi, Darmy na Yassir pia wote wakaungana kufurahia lile jambo.
“Eeh! Mungu naomba uniongezee muda kidogo niweze kuwaona watoto wangu,” alisema Tony.
“Hakuna lishindikanalo kwa Mungu naamini atatupa hitaji la nyoyo zetu”
******************
Baada ya Siku kadhaa Darmy na Yassir wakarudi jijini Dar es salaam kuendelea na shughuli za kampuni. Martha hakutaka kwenda popote akatamani kuendelea kubaki na Tony wake,
“Tony nimeongea na mama amekubali mimi niendelee kukaa huku nawe, sababu nilishamueleza kila kitu,” alisema Martha.
Ilikuwa habari njema kwa Tony, wawili hao wakarudisha upendo upya, ingawa Tony alikuwa mgonjwa lakini alijitahidi kufanya kila aliloliweza kwa mpenzi wake. Siku moja Martha aliamua kwenda shambani na akiongozana na Rozina dada yake Tony,
“Wifi ungepumzika tuu,” alisema Rozina.
“Mhmh! Ni sehemu tu ya mazoezi wifi yangu, natamani sana watoto wazaliwe wakiwa na afya ndio maana najitahidi kufanya kila niliwezalo kuhakikisha naepuka magonjwa yasababishwao na uzembe au uvivu wa kutofanya mazoezi”.
Wakaendelea kutembea taratibu huku wakiongea hili na lile, wakafika sehemu yam to ambayo Martha aliikumbuka vizuri kuwa ndiyo sehemu ambayo kimbunga kikali kilitokea ile siku aliyokuja na Tony kwa mara ya kwanza. Martha akasogea karibu kabisa na mto ule, hapo hapo hali ya hewa ikabadirika ghafla, wingu zito likatanda na upepo mkali ukawa unapiga. Rozina akaogopa sana ile hali ikabidi arudi nyuma kwa haraka hadi alipo Martha,
“Hatuwezi kwenda shamba kwa hali kama hii, turudi usije nyeshewa na mvua,” alisema Rozina.
Martha hakupinga akainuka lakini wakajikuta wanashindwa kurudi walipotoka kutokana na upepo mkali kupiga na kusababisha baadhi ya matawi ya miti kuanguka,
“Sehemu iliyosalama kwa sasa ni hapa mtoni, tusubili kwa muda hadi upepo utakapo kata,” alisema Martha.
Rozina akakubali na wakaa eneo hilo, wingu likazidi kuwa jeusi na kuruhusu giza kutawala, tofauti na mafikirio yao mvua nyepesi ilinyesha badala ya mvua kubwa walioyotarajia. Wakati wakiendelea kufikiri pa kujifa akatokea yule mzee ambaye Tony na Martha walimsaidia miaka kadhaa iliyopita, akawapa ishara ya kuwataka wamfate nao wakatii,
“Wewe wifi! Unamjua yule mzee au ndio tunaenda tuu?” aliuliza Rozina.
“Anaonekana ni mtu mwema hawezi kutudhuru twende tukamsikilize,” Martha akajibu.
Wakatembea kwa hatua za haraka na kumfikia mzee yule ambaye alikaa chini ya mti mmoja,
“Simameni hapa, mtakuwa salama na mvua haitowalowesha,” akasema mzee yule.
“Akhsante babu”
Mzee yule akamtazama Martha kuanzia chini hadi juu kisha akamtazama Rozina na kutabasamu, akanyanyua kinywa chake na kusema,
“Nafikiri unaikumbuka vizuri kauli yangu kwamba wawili ninyi mtakuwa na furaha kama mtakuwa pamoja, na niliamini mtakiishi kiapo chenu. Hayo yaliyotokea ni malipo ya usaliti uliofanyika hata hivyo Mungu amewapa nafasi ya kufurahia matunda ya mbegu iliyopo tumboni mwako”
Martha akainua uso wake uliolowana kwa machozi na kumtazama mzee yule,
“Je! Vipi kuhusu Tony amebakiza miezi 3 sasa ya kuishi, kuna namna yeyote ya kufanya hili yeye awe mzima na kuwaona watoto zake?” aliuliza Martha.
“hilo siwezi kulizungumzia,” akajibu mzee.
Martha akainama chini na kuendelea kuangusha chozi, mzee akawaambia kuwa wanaweza kwenda maana upepo ulishatulia na mvua imekata. Safari ya shamba ikafa na wakaamua kurudi moja kwa moja nyumbani.
*****************************
Katika mwezi wa 9 wa ujauzito wa Martha na mwezi wa tano toka Tony alivyoanza kuhesabu siku za kuishi. Ulikuwaa ni usiku mtulivu sana, baridi halikuwa kali kama ilivyozoeleka kwa siku zote, Martha alianza kusikia uchungu usiku huo. Juhudi za kumuwahisha hospitali zikafanyika kadri Martha alivyozidi kulalamika kwa uchungu ndivyo na hali ya Tony ilivyozidi kuwa mbaya. Mjomba akawaambia Rozina na Shangazi watangulie hospitali yeye amuangalie Tony.
Manesi wakampokea Martha na moja kwa moja wampeleka chumba maalumu kwa ajili ya wamama wajawazito walio tayari kwa kujifungua. Huku nyuma mjomba naye akashindwa kuvumilia kumuona Tony akiwa katika hali ngumu vile, ikabidi akodi gari na kumpeleka hospitali ambayo Martha alipelekwa. Tony hakujali hali yake alichokifikiri ni watoto wake na Martha,
“Hatuna namna ya kufanya kwake, sumu imeshafika eneo la Moyo hapa tusubili kudra za mwenyezi Mungu,” alisema daktari.
Kauli hile ilimsikitisha sana mjomba na Tony hakutaka kukubaliana na hilo,
“Uncle nizuieni nisife kwanza hadi niwaone watoto zangu,” aliongea Tony kwa shida mno.
“Hutokufa utawaona tuu”
“Daktari mbona naishiwa nguvu hivi, nisaidie daktari niwaone watoto zangu,” aliendelea kusema Tony.
“Tunaweza kumpeleka chumba alichopo mkewe lakini ni hatari mno, kama ikitokea amefariki mbele ya mkewe ni wazi tutawapoteza wote,” alisema daktari.
“Tumsogeze basi hata chumba cha karibu,” alisema mjomba.
“Hospital yetu ni ndogo mno hivyo, tuombe ajifungue salama na awaone watoto zake,” daktari aliongea.
Mjomba akamsogelea Tony na kumwambia,
“kwa wakati huu unapaswa kumuombea Martha awe na nguvu hili aweze kuwaleta watoto wako salama, omba Mungu atakusaidia,” alisema Mjomba.
Tony alifumba macho yake na kuomba Mungu ampe nguvu Martha katika jambo lile.
Martha akafanikiwa kujifungua mtoto wa kwanza ambaye alikuwa wa kiume, na muda mfupi baadaye akajifungua mtoto aliyesalia ambaye ni wakike. Rozina, shangazi na Martha mwenyewe walifurahi mno. Daktari akawahakikishia kuwa watoto wapo katika hali ya usalama. Wazo la Tony likamjia Martha na kumuomba daktari kuwa watoto hao lazima waonane na baba yao, mjomba wakiongozana na wauguzi waliowabeba watoto wakaingia chumba alichopo Tony na kukuta amefumba macho na mikono kama mtu anayefanya maombi. Shangazi na Rozina wakawachukuwa watoto na kusogea karibu na kitanda,
“Tony fumbua macho uwatazame watoto zako, hakika ni wazuri mno, wakike kafanana na mama yake na kidogo shangazi yake na huyu wakiume ni sura yako kabisaa!” alisema mjomba.
Tony hakutikisika wala kusema lolote, mjomba ikabidi asogee na kumtingisha lakini tayari Tony pumzi zilishakata, wauguzi walivyoona hiyo hali ikabidi wamuite daktari kwa haraka na kuwataka shangazi na Rozina watoke nje,CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kuna nini daktari mbona mdogo wangu asemi kitu?” aliuliza Rozina huku machozi yakimbubujika.
“Wee Tony inuka bwana! Utani sio mzuri ujue utaniua dada yako!” alizidi kuongea Rozina.
“Naomba msubili hapo nje kidogo tumfanyie uchunguzi,” akasema Daktari.
Wauguzi wakawachukua watoto na kuwarudisha kwa mama yao, Martha alifurahi kuwaona watoto zake wakia na afya nzuri,
“Vipi wamefanikiwa kuonana na baba yao! Bila shaka watakuwa wamefurahi!” Martha akaongea.
Lakini wauguzi wale hawakujibu lolote swala ambalo likampa mashaka kidogo Martha,
“Naomba mnitie Rozina!”
Wauguzi wakatoka bila kumjibu wala kumwambia lolote juu ya kilichotokea kwa Tony. Rozina ni kama alielewa kilichotokea kwa kaka yake, hakuwa na uwezo wa kusimama Zaidi ya kulia na kuongea hovyo,
“Shangazi mdogo wangu amelala eenh! Ataamka muda si mrefu, nitamuonesha watoto wake eenh!”
Maongezi hayo yalimfanya hata shangazi mwenyewe kushindwa kuvumilia na kuanza kulia, huku akimkumbatia Rozina.
“Jikaze mwanangu! Tony atakuwa sawa tuu,” aliongea shangazi.
***********************
Daktari akakuta mapigo ya moyo ya Tony yakiwa chini sana ikabidi kwa haraka wawashe mashine ya kushtua mapigo yake ya moyo, lakini hawakuweza kufanikiwa kingine kilichowachanganya Zaidi ni ile ngozi iliyokuwa nyeusi ikawa inabanduka mithiri ya nyoka ajivuavyo gamba, mashine ikasimama na mapigo ya moyo yakakata. Daktari akatoka nje japo ni taaluma yake kuonesha ujasiri ila naye akajikuta anatoa chozi, Rozina alivyoona kuwa daktari naye ametoa chozi akapoteza fahamu.
Jitihada za kumpa huduma ya kwanza Rozina zikafanyika na baada ya muda mfupi akazinduka lakini alipokumbuka tuu kuwa mdogo wake amefariki akapoteza fahamu tena.
“Wewe ndiye mwanaume hapa, najua hawa watoto wakike hawawezi kufanya lolote katika hali hii, jikaze uwataarifu wengine huku nafanya utaratibu wa kupeleka mwili wa marehemu monchwari,” alisema daktari.
“Naomba umruhusu mkewe na watoto wamtazame kwa mara ya mwisho,” alisema Mjomba.
Kauli ile ilipenya moja kwa moja kwenye masikio ya Martha, hakutaka kusubili akaingia moja kwa moja na kushuhudia Tony akiwa amefunikwa shukwa mwili mzima, akajipiga vibao usoni hili aone kama ilikuwa ni ndoto au ni kweli. Akasogea na kumtingisha Tony,
“Wewe baba wawili amka huko! Wanao wanataka wakusalimie! Sasa utalalaje bila kuwaona,” alisema Martha.
“Daktari njoo umuamshe ngoja nikawalete watoto wake awaona”
Mjomba alitaka kumzuia lakini daktari akamwambia amuache afanye kile ambacho moyo wake unamtuma, Martha akawachukua watoto zake na kuwalaza mmoja kulia mmoja kushoto, watoto wale wakaanza kulia,
“Unaona wanao wanalia, amka basi uwabembeleze, muone huyu wa kiume kama wewe vile yaani, amka Tony!”
Juhudi zote zikawa ni bure, wauguzi wakawachukua watoto sababu walishaona Martha ni kama amechanganyikiwa vile.
“embu waacheni watoto kwa baba yao, Tony ona wanao walee wanachukuliwa amka basi!”
Ilikuwa ni simanzi kubwa sana, wauguzi na madaktari walijikuta wakiguswa mno na msiba huo, haikuwa kutokea katika kipindi chote walichofanya kazi hapo. Sanduku maalumu kwa ajili ya kuweka mwili wa marehemu likaletwa tayari kwa kumuingiza Tony humo, Martha alilia kama mtoto mdogo akasogea hadi alipolala Tony kwa mara nyigine,
“Tony sitokusamehe kwa hili, wewe nenda tuu, nakupenda sana,” alisema Martha.
Bila kutarajia Martha akikumbatia maiti ile na kuanza kuibusu, akaendelea kufanya hivyo kwa muda mrefu kidogo kisha akainuka, kabla hawajamweka kwenye sanduku akarudi tena na kuzibusu lips za Tony. Papo hapo Tony akapiga chafya na kuzinduka mithili ya mtu aliyekuwa na safari asubuhi sasa kutokana na usingizi akajikuta amechelea hivyo alihitaji kuwahi usafiri. Chafya ile ikamlazimu daktari kurudi na kumfanyia upya vipimo. Maajabu ya Mungu akakuta mapigo ya moyo yamerudi katika hali ya kawaida. Wakatoa lile sanduku na kumuamishia katika chumba cha wagonjwa mahututi, furaha ililejea katikati ya wanandugu hao hata daktari pia alifurahi.
Baada ya siku chache Tony akapata ahueni na kuruhusiwa kurudi nyumbani japo miguu haikuwa na nguvu ya kutembea vizuri. Nyumbani ilikuwa furaha tupu taarifa zikawafikia wafanyakazi nao walifurahia mno, wakasubili siku na saa ambayo wawili hao watarudi jijini.
Jioni moja watu karibia wote walitoka, akabaki Martha na Tony na watoto zao, Martha akawa jikoni anapika wakati alikaa pembeni kidogo, siku hiyo walisahau kufunga mlango ivyo nyoka mkubwa akaingia na kusogea hadi walipolala watoto, Tony hakujua chochote hadi pale aliposikia watoto wanalia, alipotazama. Laa hulah! Nyoka akawa ameinua kichwa chake kuashiria kutaka kumuua yule mtoto wa kiume ambaye walimpa jina la Irenius na wakike akaitwa Irene. Tony aliinuka kwa haraka mno, hakuelewa nguvu amepata wapi ila alijikuta akimshika yule nyoka na kumtupa chini kwa nguvu, hakumchelewa akachukua nondo iliyopo upenuni mwa kabati, na kumpiga kichwani. Nyoka yule akafa pale pale. Martha aliposikia kishindo ikabidi naye aje kwa haraka ila akakuta kila kitu amekimaliza Tony, hiyo ndiyo siku ambayo Tony aliweza kupona na kurudi katika hali ya kawaida.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
BAADA YA MIEZI 6
Tony na Martha wakaamua kuhalalisha mahusiano yao kanisani kwa ndoa takatifu. Martha akamilikishwa kampuni ya Tae Xhiang Sung Group kama zawadi ya harusi yako toka kwa mabosi zake, na kuambiwa sasa ana uhuru wa kuifanyia lolote. Kampuni mbili zikaungana na kuwa kampuni moja waliyoiita ITIM MEDIA LTD. Huku maana halisi ikiwa ni majina ya watoto zao na ya kwao.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment