Search This Blog

Thursday, July 21, 2022

SONONEKO - 5

 







    Simulizi : Sononeko

    Sehemu Ya Tano (5)



    ILIPOISHIA



    Umbile la Maimartha ndani ya khnga ile lilinipandisha midadi kwa kiasi kikubwa kwani lilikuwa ni umbile lilikaa kihubahuba.



    Maimartha alijinyanyua na kuja kunikali amapajani mwangu huku akinifungua vifungo vya shati langu. Nami bila ya ajizi nilimpokea kwa mikono yote na kumkumbatia kiuno chake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    SASA ENDELEA



    Maimartha alianza kunipapasa kifua changu kwa mikono yake laini sana. Mpapaso huu uliibua hisi za kimahaba ndani ya mwili wangu na kuufanya mwili wangu uwe kama unatembewa na wadudu wadogowadogo ambao walikuwa wakinyevuanyevua.

    .

    Nami kwa wakati ule niliifungua khanga ya Maimartha na kuyashuhudia matiti yake mazuri, meupe na yaliyosimama tisti mithili ya embe bolibo.



    Nilianza kuyachezea taratibu kwa kuyasukasuka kitendo ambacho kilisababisha pumzi za Maimartha zianze kubadilika na kuwa mithili ya mtu anayeanza kupagawa na mapepo.



    “Twende chumbani Maimartha”. Nilimwambia Maimartha ambaye nilimwona anaanza kubadilika na kuwa mlaini mithili ya mlenda kutoka Tabora nchini Tanzania.



    Maimartha alinielekeza mahali ambako chumba kiliko. Tulikokotana mithili ya walevi wa gongo huku tukisindikizana kwa mabusu tele.



    Tulipofika chumbani wala hata sikumkawiza. Nilimnyanyua na kumbwagwa juu ya kitanda kizuri cha thamani. Wakati huohuo nami nikaja juu yake.



    Khanga ya Maimartha ilikuwa imekwishatoka sasa na kuliacha umbile lake motomoto kuwa wazi kabisa.



    Nilianza kuutembeza ulimi wangu taratibu kuanzia masikioni mpaka unyayoni. Kitendo hiki kilimfanya Maimartha ajisikie raha sana isiyo kifani ambapo alikuwa akitoa miguno mbalimbali ya kujisikia raha.



    Wakati huohuo nami mjomba alikuwa amechachamaa. Maimartha alikuwa amemthibiti akimchezeachezea jambo lililomfanya achachamae zaidi.



    Tuliendelea kuchezeana kwa mahaba motomoto kwa muda mrefu sana kwa lengo la kupandishana midadi. Na kwa muda wote huo nilimwonyesha Maimartha kwamba mimi nilikuwa fundi niliyekubuhu katika sekta hii ya mahaba.



    “Ooopps! Aaaiiissssh! Ooooooh! Stanley give me please”. Maimartha aliomba kupewa dozi yake ya ugonjwa wa mahaba mara baada ya kuwa amelainika vya kutosha.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sikutaka kumchelewa. Nilizivua nguo zangu na kumwendea Maimartha. Wakati wote huo mjomba alikuwa amechachamaa yuko mstari wa mbele vitani tayari kuzifyatua risasi kwa adui atakayekuja mbele yake.



    Nilimwendea Maimartha juu yake naye akanipokea kwa huba na bashasha tele. Tulianza kupeana haja za miili yetu kila mtu kwa ufundi na utaalamu wake. Mchezo ulikuwa ni mzito sana na miili yetu ilitoa jasho vilivyo.



    Hakika siku ile tulilicheza singeli kwa staili za aina zote. Tulicheza sindimba, muda mwingine mdundiko na baadaye na mdumange.



    “Ahsante sana Stanley mpenzi wangu. Hakika wewe ni mwanaume wa shoka”. Maimartha alishukuru mara baada ya kuumaliza ufisadi wetu.



    “Nashukuru sana kama umefurahia. Hakika nawe u mwanamke wa pekee na mtamu sana”. Nilimwambia Maimartha.



    Baada ya dakika kadhaa tukaamka na kuelekea bafuni kwa ajili ya kuisafi miili yetu ambayo ilikuwa hoi.

    *****************

    “Karibu mume wangu”. Rose alinikaribisha majira ya saa moja jioni nilipokuwa nikirejea nyumbani.



    “Ahsante”. Nilijibu kwa kifupi huku nikiyakwepesha macho yangu kukutana nay a mke wangu.



    “Pole kwa uchovu wa mizunguko”. Rose aliniambia na nikaona kama akinisanifu hivi.



    “Ahsante”. Niliendelea kujibu kwa kifupi huku sasa nikitaka kuelekea chumbani.



    Mbona umechelewa kurudi mume wangu”. Rose aliniuliza swali ambalo nililihisi lilikuwa ni mtego.



    Niliamini kwamba huyu mwanamke alikuwa amehisi kitu juu yangu. Niliamini hivyo kwani Rose alikuwa ni mwanamke makini sana na mwenye akili nyingi pia. Nilitakiwa nifanye jambo la haraka kuinusuru hali hii.



    “Kwani asubuhi nilikuaga kwamba naelekea wapi? Mbona umeanza maneno wewe mwanamke!”. Niliamua kumjibu kwa ukali ili kuyakatisha maswali yake ambayo yangenifanya niteleze na kubainika uhalifu nilioufanya.



    “Nisamehe mume wangu. Nilihoji tu kwani si kawaida yako kuchelewa kurudi. Naomba niwie radhI”. Rose aliongea huku machozi yakimlenga machoni.



    Sikumjibu chochote. Nilichofanya ni kuelekea chumbani kwa ajili ya kujipumzisha. Sikupenda kugombana na mke wangu. Sikujua kwa kufanya vile nilikuwa napalia makaa.



    Nilipofika chumbani nilizivua nguo zangu na kujitupa kitandani kwa ajili ya kulala. Mwili wangu ulikuwa umechoka sana kwa shughuli pevu ambayo Maimartha alikuwa amenionesha.



    “Mume wangu, basi uende ukaoge kisha uende kula”. Rose aliongea jambo ambalo niliona kwamba alikuwa kizidi kunivuruga.

    “Hivi jamani si nimekwambia kwamba sihitaji usumbufu?”. Nilimfokea Rose.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kwani una nini mume wangu leo hii”. Rose alihoji huku akinitazama kwa macho ya huzuni.



    “Sihitaji usumbufu. Niache nilale mimi”. Niliongea huku nikivuta shuka na kujifunika gubigubi.



    Rose aliumia sana moyoni. Nilisikia mihemo ya kilio huku akitoka nje ya chumba huku akiwa amechanganyikiwa asijue nilikuwa nimepatwa na nini. Ilikuwa ni mara ya kwanza kabisa katika ndoa yetu kutokea hali hii ya kutokuelewana na kufokeana.



    Ki ukweli Rose aliumia sana moyoni kwani siku zote alikuwa akiombea amani ya ndoa yake kwa mwenyezi Mungu.

    ***************

    Kesho yake baada ya kutoka kazini nilipitia tena kwa Maimartha kwa ajili ya kujipatia burudani ya moyo wangu. Hakika mrembo huyu sasa alikuwa ameniteka moyoni. Nilionja asali na sasa nilitaka kujenga mzinga kabisa. Na pia wahenga walisema mchovyaji huwa hachovi mara moja.



    “Karibu Stanley mpenzi wangu”. Maimartha alinikaribisha ndani huku akinikaribisha kinywaji cha pombe aina ya Kilimanjaro.



    NIliipokea glasi yenye ile pombe na kuanza kuifakamia kwa hamu kubwa sana. Ilikuwa ni Kilimanjaro baridi ambayo ilinikata kiu yangu hasa. Na miaka ya nyuma katika sekta hii ya kutafuna pombe mimi nilikuwa ni mahiri hasa.



    Ni kwa miaka mingi sana nilikuwa sijanywa pombe kwani Rose alikuwa amefanikiwa kunishawishi niache kunywa pombe kabisa.



    Rose alikuwa ni mwanamke mwokovu ambaye alikuwa amemkabidhi Mungu maisha yake. Hivyo pindi siku ile ya kwanza aliponiokoa kutoka katika mikono ya mauti alinishawishi kuachana na mambo mengi ambayo yalikuwa ni chukizo mbele za uso wa Mungu likiwemo suala la ulevi wa pombe.



    Leo hii nikajiona kama ni mfungwa ambaye nilikuwa nimeachiwa huru. Nilizitandika chupa za Kilimanjaro ipasavyo nikisaidiana na Maimartha ambaye naye alikuwa ni fundi mkubwa katika kuvipiga vyombo.



    Baada ya kulewa sana tukaenda chumbani ambako tulipeana mahaba ya kutosha yaliyokata kiu yetu ya huba. Yalikuwa ni mahaba moto ambayo yalikuwa yanazidi kunipeleka katika ulimwengu wa kumsahau kabisa mke wangu na kuzama kwa Maimartha.



    Kwa kifupi mwanamke huyu alijua kuukonga moyo wangu kwa kunipa mahaba moto. Alikuwa ni mwanamke wa pekee sana ambaye nilifurahia sana kuwa naye.

    ****************

    “Mume wangu umekunywa pombe?”. Yalikuwa ni maneno ya upole na mshangao ya Rose pindi nilipowasili nyumbani majira ya saa tano usiku.



    “Achana na mimi wewe kunguru. Pombe zangu zinakuhusu nini wewe?”. Nilimjibu Rose kwa sauti ya kilevi iliyojaa dharau na ukali huku nikielekea ndani.



    “Mume wangu unamkosea Mungu. Umeanza lini kulewa jamani?”. Rose aliongea huku machozi ya huzuni na uchungu yakimtoka.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Wewe mwanamke nadhani huelewi ninapokwambia uachane na mimi! Sasa ngoja nikufunze adabu kuku wewe”. Nilimjibu Rose na kumfuata.



    Nilimshika na kuanza kumpa kipigo kikali sana. Kipigo kile kiliendelea kwa muda mrefu huku Rose akilia kwa uchungu na kuomba msamaha. Mimi sikujali nikaendelea kumshushia kipigo kitakatifu ambacho kilimsababishia maumivu makali.

    *************

    Kesho yake niliamka kwa kuchelewa sana kutokana na uchovu mkubwa uliokuwa umesababishwa na pombe ambazo nilikunywa siku ya jana. Yaani hata muda wa kwenda kazini ulikuwa umepita.

    Niliyafikicha macho yangu na kutazama huku na kule katika kile chumba cha kulala. Akili yangu ilikuwa haifanyi kazi vizuri.



    Nilimwona Rose akiwa amekaa juu ya zulia akiwa amejikunyata huku uso wake ukiwa umevimba sana.



    Jambo lile lilinishtua sana. Nikajiuliza ni nini ambacho kilikuwa kimempata Rose mpaka akawa yuko katika hali ile.



    “Nini kimekupata mke wangu?”. Nilimuhoji Rose.



    “Mume wangu hivi ni kwa nini umeanza kunywa pombe?”. Rose aliniuliza swali ambalo liliirejesha kumbukumbu yangu.



    “Nisamehe mke wangu. Ni shetani tu”. Niliamua kujibu kinafiki kwa lengo la kumtuliza mke wangu.



    “Kwa nini wataka kurudi kule ulikotokea Stanley mume wangu?”. Lilikuwa ni swali jingine nililopigwa ambalo lilikosa jibu.



    Sikumjibu Rose bali nilichofanya ni kuamka na kuelekea bafuni. Nikaoga kwa lengo la kuondoa uchovu. Nikavaa nguo na kuondoka kuelekea kazini huku nikimwacha Rose akiwa na huzuni sana.





    Huo ukawa ndio mwanzo wa tabia yangu ya ufuska na ulevi wa kupindukia. Kila mwanamke ambaye alikatiza mbele yangu basi ni lazima nilihakikisha kwamba ninatembea naye kimapenzi.



    Mke wangu nilimsahau kabisa na nikawa simtimizii kabisa haki yake ya ndoa. Hali hii ilimfanya akonde na kunyong’onyea. Yeye alizidi kufunga na kumwomba Mungu ili aweze kuiponya ndoa yake ambayo kwa sasa ilikuwa inakwenda mrama.



    Wakati Rose akikazana kwa maombi, shetani naye alikuwa akizidi kukaza uzi kwangu na kunizamisha kabisa katika dimbwi kubwa la dhambi.



    Jina langu likakua sana na kwa kasi kubwa jijini Kano. Nikajulikana kwa ulevi wangu na ufuska wangu. Hakuna kona ya jiji hili ambayo ilikuwa hainifahamu. Nilipewa jina la utani kiwembe.



    Mara kadhaa nilijikuta niko polisi kutokana na kufumaniwa na wake za watu. Mke wangu ndiye ambaye alichukua jukumu kubwa la kuhahikikisha kwamba ninatoka lakini sikumthamini hata kidogo.

    ***************

    Nakumbuka siku moja nilikuwa nakunywa pombe na msichana mmoja aitwaye Irene. Huyu alikuwa ni mmojawapo wa wapenzi wangu lukuki ambao nilikuwa nao.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Leo tulikuwa tukiifurahia sana siku yetu hii kwa kunywa pombe kali. Halafu tulikuwa tumekubaliana ya kwamba tukitoka hapa basi tungekwenda nyumbani kwangu ambako tungeifurahia siku yetu vilivyo.



    Ama kweli pombe zilitufahamu kweli siku ile. Irene naye alikuwa ni mnywaji stadi kabisa wa pombe na hasa pombe kali.

    Usiku wa kama saa sita tulikuwa njiani tukirejea nyumbani huku tukiwa tumelewa chakari.



    “Mume wangu, mbona unanikosea heshima kiasi hiki. Yaani unaniletea mwanamke mpaka ndani ya nyumba yangu?”. Rose aliongea kwa uchungu.



    “Una nyumba wewe hapa? Tena jiandae muondoke wewe pamoja na huyu kunguni wako Petro”. Niliongea kilevi nikiingia na Irene ndani huku nikiwa nimemshika kiuno.



    Rose alilia kwa uchungu sana. Aliwaza mengi sana toka siku ambayo aliniona kwa mara ya kwanza na kunisaidia kutoka katika hali ya ufukara wa kutupwa niliyokuwa nayo mpaka kuwa mume wake wa ndoa leo hii.



    Hakuamini kwamba Mungu alikuwa amepanga kumwadhibu kiasi kile bali alimshukuru Mungu kwa yote. Aliamini pia Mungu alikuwa na makusudi yake kwa kuliacha lile litokee.



    Rose alikuwa ni mtu wa Mungu. Aliniheshimu na daima hakupenda kubishana nami kwani aliamini Mungu ndiye mtetezi wake na daima atampigania.



    Alichokifanya ni kuingia ndani na kukusanya nguo zake na za mwanetu kisha usiku huohuo wakachukua gari na kuelekea Gasi kijijini nyumbani kwa wazazi wake ambako alienda kuishi maisha mapya ya huzuni.



    Mimi huku mjini sasa nikaona kwamba nilikuwa nimepata nafasi kubwa ya kuweza kutanua vizuri. Kazini nikawa siendi muda wote nikiwa nakunywa pombe na kukesha na wanawake ambao walikuwa wakiiuza miili yao kwa ajili ya pesa niliyokuwa nayo.

    **************

    Ilikuwa ni ajali mbaya sana ambayo ilikuwa imetokea katika barabara hii ya Seaway. Gari langu lilikuwa limeacha njia na kwenda kuivaa nguzo ya umeme. Ajali hii ilisababishwa na mimi kuendesha gari huku nikiwa nimelewa chakari.



    Nilipata majeraha makubwa sana ambayo yalinipelekea kupoteza damu nyingi sana. Wasamaria wema walinichukua na kuniwahisha hospitali nikiwa sijitambui.



    “Niko wapi hapa?”. Yalikuwa ni maneno ambayo niliyaongea mara baada tu ya kuzinduka.



    “Uko hospitali mume wangu”. Ilikuwa ni sauti ambayo nilikuwa nimeizoea ya Rose mke wangu.



    “Wewe umefikaje hapa?”. Nilimwuliza.



    “Shemeji Morris alinipigia simu akinieleza kwamba umepata ajali na kunielekeza hospitali ambayo umelazwa nami nikafanya haraka sana kuja hapa”. Rose aliongea.



    “Pole baba”. Ilikuwa ni sauti ya Petro mwanangu ambayo ilinitia huzuni sana.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilishindwa kumjibu mke wangu na mwanangu na badala yake nilitiririkwa na machozi ya huzuni sana.

    ************

    “Ulikuwa umepungukiwa na damu kwa kiasi kikubwa sana. Hivyo madaktari wametoa damu yangu na kukuongeza”. Maneno haya yaliniumiza sana hasa nilipoona mwanamke huyu mara zote amekuwa ndiye mwokozi wa maisha yangu lakini mimi nimekuwa nikimtendea mambo mabaya sana.



    Alikuwa ni mwanamke ambaye alihitaji heshima kubwa sana kutoka kwangu. Pia nilipaswa kumlinda na kumthamini kwani yeye alikuwa ndiye sehemu ya maisha yangu. Nilifungwa na ukungu na sikuliona hilo.

    *************

    Baada ya kutibiwa kwa muda mrefu hatimaye niliruhusiwa kurejea nyumbani mara baada ya kupata ahueni.



    Mke wangu alinichukua katika gari letu na kunipeleka nyumbani huku tukiwa sambamba na mwanetu Petro. Petro alihuzunika sana kutokana na hali ambayo nilikuwa nayo.



    Mke wangu aliendelea kunihudumia kwa upendo wa hali ya juu sana. Hakika huyu alikuwa ni mwanamke wa tofauti sana. Yaani ninaumia sana moyoni kwa madhambi makubwa niliyomfanyia ambayo leo yananiangamiza.

    *************

    “Mume wangu, kuna maneno ninataka kukwambia”. Rose aliongea siku moja tukiwa tumekaa nje ya nyumba yetu tukipunga upepo.



    “Niambie tu mke wangu”. Niliongea huku nikimtazama machoni.



    “Ni jambo kubwa sana na unapaswa ulibebe kiume mume wangu”. Rose aliongea.



    “Usijali mke wangu, niko radhi kulibeba”.



    “Kipindi ambapo ulipata ajali, ulipungukiwa damu kwa asilimia kubwa sana. Ulipopelekwa hospitali ilionekana unatakiwa kuongezewa na benki ya damu pale hospitali walikuwa wameishiwa damu. Hivyo mimi nikaamua kujitolea kukuongezea damu yangu”.



    Alipofika hapo Rose alivuta pumzi na kuzishusha kwa nguvu. Sikufahamu ni nini ambacho alikuwa akitaka kuniambia lakini nikaamua kuendelea kumsikiliza.



    “Damu yangu ikapimwa na ikaonekana inafanana na kundi la damu yako. Pia madaktari walichukua kipimo cha VVU”. Rose alikomea hapo na kupumua kidogo.



    Hapo nikawa nimeelewa ni nini ambacho Rose alitaka kuniambia. Machozi yalianza kunitoka taratibu.



    “Aaaaahaaa! Nimewaua mke wangu!”. Nililia kwa uchungu nikifahamu kile alichotaka kuniambia mke wangu.



    “Jikaze mume wangu. Vipimo vikaonesha kwamba una maambukizi ya VVU”. Rose aliongea.



    “Nisamehe mke wangu. Uzembe na tamaa zangu sasa vinaleta madhara kwa familia”. Niliendelea kulia kwa uchungu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Pia niliamua kumpima mwanetu Petro pia. Lakini sisi tulionekana tuko salama”. Rose alihitimisha huku machozi yakimtoka.



    “Nisamehe mke wangu. Laiti ningekusikiliza haya yote yasingenipata. Tamaa zangu zimeniponnza. Ona sasa hatima ya maisha yangu ilivyo mbaya”. Nililia kwa uchungu sana.



    “Usijali mume wangu. Mimi niko pamoja nawe kwa kila hali. Sitakuacha na daima nitakuwa nawe”. Rose aliongea huku akinikumbatia kwa upendo wa dhati.



    Nilijiuliza hivi Rose alikuwa ni mwanamke wa aina gani? Nilimtenda mabaya sana katika maisha yake. Nilimwumiza vya kutosha lakini yote haya ameamua kusamehe na kuwa nami katika nyakati hzi ambazo naugulia maradhi ya UKIMWI.



    Hakuna chema chochote ambacho nimemzawadia mwanamke huyu zaidi ya kuuleta UKIMWI nyumbani. Jambo ambalo nilimshukuru Mungu ni kwamba walikuwa wameepushiwa na maambukizi haya ya VVU.



    Hili liliwezekana kwani nilikataa kukutana kimwili na Rose muda mrefu kipindi nilipoanza mahusiano na wanawake wa nje.



    Pia Petro hakuwa na maambukizi kwani naye alizaliwa katika kipindi ambacho ndoa yetu ikiwa katika usalama.



    Kwa muda mrefu sasa nimekuwa naugua maradhi haya ya UKIMWI huku mke wangu Rose akiwa ndiye msaada wangu wa pekee.



    Rafiki zangu wote wamenikimbia na kunitenga. Wale wanawake ambao nilikuwa nikitembea nao sasa sijui hata habari zao kwani wote walikata mawasiliano pindi walipogundua kwamba nimeukwaa UKIMWI.



    Moyoni nimekuwa na SONONEKO kubwa sana ambalo sasa limekuwa kama donda ndugu. Natamani hata mwenyezi Mungu auchukue uhai wangu sasa kwani ninaona aibu pindi ninapomtazama mke wangu kutokana na mambo mabaya ambayo nimemtendea.



    Pia sifahamu mwanangu atapata picha gani pindi atakapokuja kupata historia ya chanzo cha kifo changu. Sijui ataniona mimi ni baba wa namna gani?.



    Nawaomba ndugu, jamaa na marafiki zangu ambao mna tabia kama hizi ambazo nilikuwa nazo mimi, tabia za uzinzi na ulevi mziache kabisa. UKIMWI upon a unazidi kututeketeza kila siku.

    Najuta kwa kutokuwa baba mwema kwa familia yangu.



    Naumia sana moyoni. Hakika maisha yangu yamebaki kuwa SONONEKO kuu la moyo wangu.



    *********** MWISHO ***********



    MUHIMU

    Hadithi hii ni simulizi ya kweli ambayo nilisimuliwa na rafiki yangu hapa mjini Njombe ambaye kwa sasa ni marehemu. Rafiki yangu huyu alikufa kutokana na maradhi ya UKIMWI.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Maradhi haya kwa sasa yameshika kasi hapa nchini Tanzania na mkoa wangu wa NJOMBE ukiwa ndio kinara kwa maambukizi ya gonjwa hili la UKIMWI.



    Hadithi hii naitoa kama zawadi kwa watu wangu wa NJOMBE iwe kama tahadhari juu ya maradhi haya ya UKIMWI.

    Pia simulizi hii na iwe FUNZO kwa watanzania wote katika kuchukua tahadhari juu ya janga hili ambalo linatukabili.

0 comments:

Post a Comment

Blog