Simulizi : Niliishi Dunia Ya Peke Yangu
Sehemu Ya Nne (4)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com
Miezi sita toka tununue gari jingine ujenzi wa nyumba ya vyumba vya kulala sita, viwili vya watoto masta bed, jiko mabafu mawili ya ndani sehemu ya kulia pamoja na sebule kubwa ilikuwa imefikia kwenye madirisha na kujipanga kwa ajili ya lenta ambayo ilihitaji fedha nyingi kidogo. Niliamini kutokana na biashara ya gari kwenda vizuri na kuengeza akiba yangu iliyokuwa kama milioni na nusu iliyobaki baada ya kununua vitu vyote muhimu vya dukani vilivyogharimu milioni zaidi ya tano. Mwanangu Fatuma naye aliendelea vizuri katika afya njema. Siku moja nikiwa dukani nilipigiwa simu na dereva wetu aliyekuwa akiendesha teksi ya pili, baada ya kupokea simu upande wa pili ulisema katika hali ya wasiwasi.
“Haloo shem.” “Vipi Jimmy?” “Umepata taarifa zozote za Tony?” “Taarifa za nini?” Nilishtuka. “Nimepigiwa simu kuwa Tony amechanganyikiwa.” “Eti, amefanya nini?” Nilishtuka kusikia vile.
“Nasikia Tony amechanganyikiwa, kaliacha gari kwenye mataa na kusimama pembeni akihubiri dini.” “Mbona sikuelewi, Tony anafanya nini?” habari zile zilinichanganya sana. “Amekutwa anahubiri dini.” “Jimmy acha utani,” nilijua Jimmy ananitania.” “Kweli shem.” “Wewe uko wapi?” “Ndiyo nakaribia eneo la tukio.” “Hebu kwanza muone, ameanza lini tena kuwa mlokole wa kutangaza dini!” “Sawa shem, nitakujulisha.” Kutokana na kuchanganyikiwa nilitoka dukani na kumsahau mwanangu, nilikodi teksi kwenda Ubungo ili nikamuone mume wangu ambaye nilielezwa kuwa amechanganyikiwa. Nikiwa njiani nilimpigia simu Jimmy, baada ya kupokea nilimuuliza. “Vipi Jimmy, Tony yupo kwenye hali gani?” “Shem inaonekana kama malaria imempanda kichwani, sasa hivi tunamkimbiza Hospitali ya Amana.” “Nami nipo njiani basi nakuja hukohuko,” nilimueleza dereva ageuze gari kuelekea Amana, bahati nzuri nilikuwa nimefika Buguruni Kwa Ali Hamza, tuligeuza gari. Ilikuwa kama bahati baada ya teksi niliyoikodi kufika tu na gari alilokuwemo mume wangu nalo liliwasili hospitalini hapo. Ajabu Tony hakuonesha kuchanganyikiwa, alikuwa katika hali ya kawaida lakini mkononi alikuwa na Biblia ambayo ilionekana kuwa mpya. Aliponiona alipaza sauti.” “Ester mke wangu.” “Abee, mume wangu.” “Mke wangu dunia inaangamia, hasira za Mungu ni kubwa.” “Kwa nini tena Mume wangu?” “Mke wangu roho mtakatifu aliniagiza ninunue Biblia ili nihubiri Injili, baada ya kununua niliiweka ndani ya gari na kutembea nayo. Kumbe Mungu hakufurahishwa mimi kutembelea gari. Wakati naendesha kila kitu kilikuwa cha moto kasoro hii Biblia. “Kama nisingetoka haraka ndani ya gari lingewaka moto.” Maneno ya mume wangu yalinichanganya, kwani hata siku moja sikuwahi kumuona akijikita katika dini kiasi cha kusahau hata kanisa. Siku ile nilimshangaa kusema maneno yale ambayo hata mlokole asingeyasema vile. “Mume wangu upo sawa?” nilimuuliza nikiwa nimemkazia macho. “Nipo sawa mke wangu, japokuwa wananilazimisha kwa kusema eti nimechanganyikiwa, mke wangu wote mnatakiwa kumrudia Mungu. Muda wowote anaweza kuiangamiza dunia.” “Mume wangu mbona sikuelewi?? “Huwezi...huwezi kunielewa mke wangu, shetani kakuzunguka mke wangu, hutaona milele bila ya kupokea wokovu,” mume wangu alisema huku akitiririkwa machozi.
Nilizidi kuchanganyikiwa, kwa kila aliyekuwa akimfahamu mume wangu aliamini kuwa amechanganyikiwa. “Sasa shemeji mna mpango gani?” nilimuuliza Jimmy. “Haya shemeji ni malaria tu, atatulia muda si mrefu akipata tiba,” Jimmy alimwambia shemeji yake. “Jamani siumwi, nimewaeleza muda mrefu natakiwa kueneza Injili kwa mataifa.” Wakati huo rafiki yake mmoja alikuwa ameshaandikisha cheti na tukaongozana naye hadi kwa daktari baada ya kupewa upendeleo maalum. Baada ya kuingia kwa daktari tukiwa watu zaidi ya watano, daktari alituomba tubakie wachache. Kwa vile Jimmy ndiye aliyenipa taarifa nilibaki naye. “Ndiyo jamani, mheshimiwa ana matatizo gani?” Daktari alituuliza. “Sina tatizo lolote, Injili itamfikia kila mwenye sikio, hata wewe unatakiwa kuokoka, acheni kutoa mimba za wanawake, kumbukeni adhabu ya Mungu ni kali kwenu.” “Mume wangu hebu nyamaza basi.” “Ninyamaze kwani mimi ni mfu?” “Hapana, msikilize daktari.” “Haya namsikiliza,” mume wangu alisema huku akifumbata mikono juu ya mapaja yake. “Mmh! Ipo shughuli,” daktari alisema huku akitikisa kichwa kisha aliuliza swali la awali. “Nilipigiwa simu kuwa ndugu yangu amechanganyikiwa na ameliacha gari kwenye taa za kuongozea magari pale Ubungo. Nilipomkuta kwa kweli nilishtuka, amekuwa mlokole na Biblia mkononi.” “Mnataka kuniambia hali hii ndiyo leo imemtokea?” “Ndiyo,” nilijibu. Nini kiliendelea? Je, Tony atakuwa chizi? Usikose kusoma katika Gazeti la Risasi Jumamosi. Antony Joseph,” alijibu vizuri. “Ushawahi kuumwa hivi karibuni?” “Dokta nikueleze mara ngapi siumwi na sitaumwa milele, roho mtakatifu yumo ndani yangu.” “Mpelekeni akapime maralia na majibu mniletee.” Tuliondoka na mume wangu hadi maabara na kupima, baadaye tulirudisha majibu kwa daktari. Majibu yalinichanganya baada ya kuonekana kwamba mume wangu hana maralia. Nilijiuliza itakuwa nini, kwa vile alikuwa akiongea sana mambo ya kilokole doktari alimchoma sindano ya usingizi na kumpa mapumziko ya muda.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com
“Dokta itakuwa malaria imempanda kichwani tu,” Jimmy alichangia. “Samahani ndugu yangu unaitwa nani?” daktari alimuuliza mume wangu. “Victor Joseph,” alijibu vizuri. “Ulishawahi kuumwa hivi karibuni?” “Dokta nikueleze mara ngapi siumwi na sitaumwa milele, roho mtakatifu yumo ndani yangu.”
“Mpelekeni akapime malaria na majibu mniletee.” Tuliondoka na mume wangu hadi maabara na kupima, baada ya kupima tulirudisha majibu. Majibu yalinichanganya baada ya mume wangu kukutwa hana malaria. Nilijiuliza ile itakuwa nini, kwa vile alikuwa akiongea sana mambo ya kilokole, dokta alimchoma sindano ya usingizi na kupewa mapumziko ya muda. Saa moja usiku, mume wangu alipewa ruhusa, aliponiona alionesha kushtuka: “Mke wangu!” “Mume wangu.” “Mbona hivi?” “Kwani hujui kilichokuleta hapa?” “Hata sijui.” “Kweli?” nilimuuliza kwa kumshangaa. “Kweli, kwani nilipatwa na nini?” “Ulikutwa ukihubiri Injili maeneo ya Ubungo.” “Mimi?” mume wangu alishtuka. Kauli yake ilinishtua na kujiuliza kitu gani kilichomtokea mume wangu, kama angekutwa na malaria ningejua labda ilimpanda kichwani. “Tena ulikuwa umejaza watu wakikushangaa ukitangaza Injili kwa uwezo mkubwa,” Jimmy alisema. Tuliingia ndani ya gari ili turudi nyumbani ikionesha kabisa yaliyomtokea asubuhi ameyasahau. Mume wangu alikuwa tofauti na mchana, hata yale maneno yake ya kutangaza Injili hakuyasema. Kingine kilichonishangaza ni kusahau hata Biblia aliyokuja nayo. Tuliibeba na kurudi nayo nyumbani, tukiwa tunarudi mume wangu aliniuliza: “Unasema nilikuwa nafanya nini Ubungo?” alionesha kushangaa. “Unatangaza Injili, nashangaa hujauliza hata Biblia yako,” nilimjibu. “Mmh!” Mume wangu aliguna na kutulia akivuta kumbukumbu kisha alisema: “Kweli nimekumbuka.” “Umekumbuka nini?” nilimuuliza. “Tangu juzi kuna kitu sikielewi.” “Kitu gani?” “Kama kuna nguvu fulani ambazo sizielewi zinanituma nitangaze Injili, jana nilinunua Biblia na kuiweka kwenye gari. Leo nilipokaribia mataa ya Ubungo kuna sauti ilikuwa ikinifukuza kwenye gari eti niteremke nikatangaze Injili. Ndipo nilipoliona gari kama likitaka kuwaka moto, nilitoka na kuliacha, baada ya hapo sielewi mpaka nilipojikuta hapa.” “Huna malaria?” Jimmy alimuuliza. “Si umesikia sina ugonjwa wowote.” “Sasa ni nini?” niliuliza. “Hata sijui, yaani nashangaa.” Victor alijibu. “Au watu wameanza?” Jimmy alisema.
“Waanze nini?” Victor aliuliza. “Kutia mkono, si unajua kwenye neema hapakosi fitina?” “Mmh! Jamani mawazo gani hayo, mimi nafikiri ni tatizo dogo, la muhimu tumrudie Mungu. Inaonesha jinsi gani tulivyomhasi Mungu, Victor una muda gani hujaingia kanisani au kushika Biblia?” nilimuuliza mume wangu. “Mmh! Mwaka wa pili sasa.” “Basi leo ulikuwa mchungaji ukihubiri neno la Mungu tena kwa ufasaha mkubwa,” Jimmy alisema. “Sasa hiyo imaanisha nini?” Victor aliuliza. “Haimaanishi kitu zaidi ya kumrejea Mungu na Jumapili lazima uende kanisani,” nilitoa mawazo, pamoja na kuwa na wasiwasi wa labda mume wangu alikuwa amechanganyikiwa, lakini maneno aliyosema kuhusu wanadamu kumrudia Mungu, niliamini kabisa ile haikuwa kuchanganyikiwa bali kukumbushwa kutokana na kumsahau. Hata mimi uvivu wa Victor ulinifanya nilione kanisa kama kituo cha polisi na kibaka. “Sawa nitaenda lakini mimi Roma na ulokole wapi na wapi?” Victor alihoji. “Itabidi uokoke,” nilimwambia. “Hata siku moja,” Victor alikataa, katika vitu ambavyo alikuwa hakubaliani navyo ni kusikia walokole wanaponya, siku zote aliwaona waongo na wazushi. Lakini jirani yangu mwanaye aliyekuwa na matatizo ya majini tangu alipokwenda kwenye moja ya makanisa ya maombi, hali yake ilitulia. Lakini wengine walikwenda miaka nenda rudi na hawakupata nafuu yoyote na kuishia kubadili makanisa. Niliamini huenda ni imani yao kuwa ndogo iliyowafanya wasipokee uponyaji ambao uliegemea sana kwenye imani. Mazungumzo yalitufanya tufike nyumbani bila kujua, tuliingia ndani, Victor alisema amechoka sana hivyo alikuwa akiomba kupumzika. Siku ya pili mume wangu aliamka katika hali ya kawaida, hakuonesha kitu chochote zaidi ya uchovu wa mwili kama alikuwa na malaria. Kwa vile gari lilikuwa limechukuliwa na polisi wa usalama barabarani, tulimtuma Jimmy kulifuata polisi pamoja na faini ya kuliacha gari barabarani. Alipofika alilikuta lipo kwenye hali nzuri hata simu na vitu vyake vilikuwa katika hali nzuri. Alilirudisha gari nyumbani na yeye kuendelea na kazi yake, siku ile nilishinda na mume wangu sikwenda kwenye biashara zangu mpaka usiku.
Hali ya mume haikubadilika, ilikuwa ya kawaida alishinda vizuri na kunihakikishia kuwa siku ya pili atarudi katika kazi zake za kawaida. Kweli siku ya pili aliondoka nyumbani asubuhi akiwa na gari lake kama kawaida yake na kuniacha nikimuandaa mtoto kabla ya kuelekea kwenye biashara zangu. Majira ya saa moja na nusu, nilikuwa dukani nikiendelea na kazi zangu, muda ambao wateja
hawakuwepo dukani nilijikuta nikikumbuka maneno ya mume wangu ya kuitangaza Injili. Kwangu bado sikuamini kabisa kama mume wangu kachanganyikiwa japokuwa maneno yake ya gari kutaka kuwaka moto yalinichanganya. Niliamini ule ulikuwa ujumbe tosha wa kutukumbusha kumrudia Mungu kutokana na mimi na mwenzangu kusahau kama kuna siku muumba naye alikuwa akihitaji kuabudiwa. Sikutaka mawazo yale yachukue muda wangu mwingi. Niliachana nayo na kujipanga kwa ajili ya kuanza kwenda kanisani kila Jumapili. Majira ya saa tano nikiwa nahudumia wateja, nilipigiwa simu na Jimmy. “Haloo shem, za asubuhi?” “Nzuri tu,” nilijibu huku nikisikia sauti za zogo hali iliyoonesha alikuwa sehemu ya watu wengi. “Upo wapi?” “Dukani.” “Mambo yameibuka upya.” “Mambo! Mambo gani tena?” Sikumwelewa. “Ile hali imemrudia tena safari hii inatisha.” “Mungu wangu hali gani tena hiyo?” Nilishtuka bila kujua ni hali gani. “Ya Victor?” “Ya Toooni?” nilishtuka. “Ndiyo.” “Jesus, Victor kafanya nini tena Yailah?” “Naomba uje haraka.” “Jamani Jimmy nije wapi na Victor kafanya nini tena?” “Victor kakamatwa na watu baada ya kulisimamisha gari ghafla na kutoka mbio huku akipiga kelele kuwa kuna watu wanataka kumuua.” “Mama yangu mzazi aliyetangulia mbele ya haki, Victor kafikia hivyo?” Sikuamini nilichokisikia. “Huwezi kuamini hata mimi nimechanganyikiwa maneno anayozungumza si ya kawaida.” “Nakuja Jimmy, Mungu wangu Victor wangu kapatwa na nini?” “Fanya haraka shem.” “Mko wapi?” Nilimuuliza Jimmy. “Soko la Temeke Stereo.” “Nakuja,” nilikata simu na kumfuata msichana wangu wa dukani aliyekuwa akihudumia wateja. “Suzy nakuja,” nilimuaga huku nikitaka kutoka. “Dada kuna nini mbona hivyo?” ”Wee acha tu, hata sijui hii ni nini?” “Kuna nini tena dada?” “Suzy niache kwanza.”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com
Nilichukua fedha kama laki moja na kuiweka kwenye matiti na kutoka dukani. Nilikwenda barabarani kutafuta gari, kabla sijapata gari simu toka kwa Jimmy iliita. “Vipi Jimmy?” “Umefika wapi?” ”Ndiyo natafuta gari nije.” “Usije huku tukukute nyumbani.” “Vipi hali yake?” “Bado.” ”Sasa kwa nini msimpeleke moja kwa moja hospitali?” “Ugonjwa huu si wa hospitali.” “Ni wa wapi?” “Waliomuona wanasema wa Kiswahili.” “Una maana gani kusema wa Kiswahili?” nilikuwa sijamuelewa. “Wa kishirikina.” “Unataka kuniambia Victor amerogwa?” “Kwa hali hii lazima atakuwa amerogwa tu hii si hali ya kawaida.” “Mungu wangu nakuja.” Kwa vile kutoka dukani kwangu hadi nyumbani hapakuwa mbali sikuwa na haja ya kukodi gari. Nilitembea kwa mwendo wa kurukaruka na ndani ya dakika saba nilikuwa nimefika. Kutokana na umbile langu kubwa nilipofika nilikuwa nikihema huku jasho likinitoka. Nilikuwa nimewahi sana, wakati nikikaribia nyumbani, nikaiona teksi ya Jimmy ikiwa inafika. Nilisogea kwenye gari na kumuona mume wangu. Walimtoa kwenye gari huku akiwa kafungwa kamba kifua wazi, aliponiona alianza kulia, kitu kilichonifanya na mimi niangue kilio cha kwikwi. “Mke wangu nimewakosea nini wanataka kuniua?” Mume wangu alisema kwa sauti yenye majonzi, nilipomwangalia vizuri hata miguuni hakuwa na viatu. Sikuweza kuzungumza zaidi ya kulia kwa sauti na kuwafanya rafiki wa mume wangu waliomleta kuanza kazi ya kunibembeleza. “Shemeji tunakutegemea ukilia itakuwaje?” “Inauma kwa nini kila siku iwe mimi tu?” “Hakuna tatizo shem mkiwahi tatizo hili linatatulika.” “Basi mwingizeni ndani.” Mume wangu aliingizwa ndani na kuketishwa kwenye kochi, aliendelea kulalamika: “Jamani kosa langu nini la kutaka kuniua, kama gari chukueni mniachie roho yangu,” mume wangu aliendelea kulalamika huku akitokwa machozi. “Kina nani mume wangu?” Nilimuuliza huku nikimsogelea. “Wanadamu mke wangu, wameficha sura zao ili kunidhuru.”
“Jamani basi mfungueni kamba,” nilimuonea huruma mume wangu aliyekuwa katika hali ya kuumia.
(Intro ya next part; ILIPOISHIA: “Ina maana ilikuwa ajali mbaya sana?” “Sana...kwa yeyote atakayeliona lile gari lilivyokunjwa, ukimwambia kuna mtu ametoka salama hawezi kukubali.” “Mmh! Mbona unanitisha kusema hivyo, kwani ikoje?” “Si ya kuhadithiwa shemeji kama haendi kanisani huu ni wakati wake wa kumshukuru sana Mungu kwani bado ana mapenzi mazito naye.” SASA ENDELEA...)
Nilibaki na maswali mengi kichwani mwangu kuhusiana na ajali hiyo ambayo mume wangu alikuwa amepona kimuujiza. Marafiki zake walizidi kujazana kuja kumpa pole, kila mmoja akilishangaa gari na yeye kuwa hai. “Kaka kama hukufa leo, hufi tena,” mmoja wa rafiki zake alimtania. “Kifo ni ahadi nimeamini kwa ajali ya leo, mtu hawezi kufa bila siku yake kutimia,” mwingine alichangia na kuzidi kunichanganya mtoto wa kike. Kwa vile hali yangu na mume wangu zilikuwa za kuridhisha na muda ulikuwa umekwenda sana, niliwaruhusu shoga yangu Salome na wasichana wangu wa dukani wakapumzike kwani siku nzima waliipotezea kwangu. Baada ya kuondoka shoga na wasichana wangu wa dukani, nikabakia na kazi ya kupokea majirani na marafiki kuja kutupa pole kutokana na ajali mbaya iliyompata mume wangu. Siku ile tulipata muda wa kupumzika saa 4:00 usiku baada ya watu kukubali kutuacha tupumzike. Pamoja na mwili kuwa na uchovu, bado sikutaka kulala mpaka nijue nini kilichomsibu mume wangu kukutwa na masahibu kama yake, hasa mshangao wa dunia kupona kwake kulikokuwa kama ngamia aliyepenya kwenye tundu la sindano. Tukiwa kitandani kabla ya kulala, nilimuuliza mume wangu: “Mume wangu hebu nieleze ilikuwaje? Maana kupona kwako kila mtu anayekuja anakuona kama ngamia aliyepenya kwenye tundu la sindano!” “Mpaka sasa sielewi na siamini kama nipo hai,” mume wangu alisema kwa sauti ya chini yenye kusikika ikifuatia michirizi ya machozi. “Ilikuwaje mume wangu?” nimuuliza nikimkazia macho. “Katika siku niliyokuwa na kismati cha biashara ni leo, tangu asubuhi gari langu limekuwa likikimbiliwa na wateja kila liliposimama kituoni hata kama nitakataa abiria walikataa kupanda teksi nyingine. Nilikuwa nimerudi kutoka Pugu kupeka abiria. Hata kabla sijapumzika, walikuja abiria wawili, mtu na mkewe na kuniomba niwapeleke Kigamboni. Nilitaka kuwakatalia lakini bahati nzuri teksi iliyokuwa kijiweni ilipata abiria hivyo sikuwa na budi kukubali kuwapeleka.
“Baada ya kupanda na kukubaliana bei, niliondoa teksi kijiweni kuelekea Kigamboni kupitia Barabara ya Sokota nipitie Mbozi hadi Keko inayoungana na Barabara ya Mandela. Nilipofika kwenye makutano ya Barabara ya Sokota na Mandela, kabla ya kuvuka niliangalia kulia na kushoto na kuona barabara nyeupe ila lori la mafuta lilikuwa mbali sana karibia na Vetenari. “Nilikanyaga mafuta kuwahi kuvuka, hamadi! Sikuamini gari lile kuliona limefika karibu yetu. Nilikanyaga mafuta ili niwahi kuvuka japo sikuwa na uhakika kama nitafanikiwa, kwa ajabu ya Mungu gari lilizimika. Kilifuatia kishindo kizito cha gari letu kugongwa na kushtukia nimerushwa juu na kutua chini nikiwa nimepoteza fahamu. “Niliposhtuka nilijikuta hospitali, baada ya uchunguzi nilionekana sina jeraha lolote mwilini zaidi ya maumivu kidogo ya mkono wa kulia ambayo baada ya kuchomwa sindano ya maulivu yalitulia mpaka muda huu,” mume wangu alimaliza kusema huku machozi yakiendelea kumtoka na kuufanya moyo wangu uzidi kuniuma. “Mmh! Pole sana mpenzi wangu. Mungu akulinde na balaa lingine.” “Amina.” “Na gari?” “Mke wangu gari halifai, nilipotoka hospitali nilipitia polisi pale Chang’ombe. Wee acha tu, kwa ajali ile, siamini na sitaamini kama nilitoka salama, kile kilikuwa kifo,” mume wangu alisema kwa sauti ya majonzi. “Jamani, sasa hii itakuwa amri ya Mungu au bado watu wako wanakufuata?” nilimuuliza mume wangu kutokana na wasiwasi wa matukio. “Watakuwa haohao.” “Mbona yule mzee alisema hawawezi tena?” “Wanadamu tuache tu, tuna kila hila kuhakikisha tunatimiza ubaya wewe, kwa jinsi lile gari lililosogea kama mshale wakati navuka, nasema si bure ni mkono wa mtu. Tena mtu huyo anataka roho yangu.” “Basi turudi kwa yule babu?” “Kuna umuhimu huo.” “Vipi gari linaweza kupona?” “Haliwezi, limeharibika vibaya, injini haifai imepasuka vibaya, lile gari mke wangu sasa ni skrepa.” Japo roho iliniuma kupoteza gari, lakini kupona kwa mume wangu lilikuwa jambo muhimu kwa kuamini gari linapatikana si roho ya kiumbe ikitoka imetoka.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com
BAADA ya mazungumzo marefu nilimruhusu mume wangu aende kulala mara aliposema anajisikia maumivu ya mbali sehemu ya bega lililoshtuka. Nami kwa vile nilikuwa nimechoka kiasi cha kumruhusu mtoto wangu kwenda kulala na msichana wa kazi, sikuchelewa kupitiwa na usingizi mzito. Katikati ya usiku nilisikia sauti kwa mbali kama mtu ananiita. Niliposhtuka nilimsikia mume wangu akilalamika kwa sauti ya maumivu makali. “Mungu wangu nakufa miye...ooh mke wangu nakufa.” Niliwasha taa na kumkuta akitokwa na machozi kama mtoto mdogo huku mkono mmoja kashikilia bega
linalomuuma. “Vipi mume wangu?” nilimuuliza macho yakiwa yamenitoka pima. “Nakufa mke wangu...nakufa...nakufa,” mume wangu alilalamika alikuwa na maumivu makali. “Mungu wangu! Nini tena mume wangu?” “Mamaa...nakufa kaniitie kaka...nakufa mke wangu...mama...mama...uko wapi nakufa kifo kibaya mwanao.” “Mume wangu unaumwa nini?”nilimuuliza huku nikitetemeka. “M...mm...kono...mkono...na...na...kufa...kichwa kinapasuka nakufa mke wangu huku najiona,” mume wangu alilalamika kama mtoto huku makamasi yakimtiririka kama maji. Mume wangu alijitupa chini kutoka juu ya kitanda mzima mzima kama mtu aliyerushwa na kuanza kugaagaa akipiga kelele za maumivu makali ya mkono na kichwa, kila muda ulivyokwenda ndivyo sauti yake nayo ilivyopungua, mwishowe kabisa alinyamaza na kutulia tuli. Wakati huo nilikuwa nahangaika na kushindwa sehemu ya kumshika, nilijiuliza nifanye nini mtoto kike kila dakika duniani nilikuwa mgeni kwani kucheka kwangu kulikuwa kidogo lakini kulia kila kukicha. Baada ya kutulia nilimfuata na kumshika, cha ajabu nilipomgeuza alilegea kitu kilichonishtua na kuanza kupiga kelele kuomba msaada kwa majirani. Wazo lililonijia haraka ni kumpigia simu rafiki yake Jimmy. Nilimpigia Jimmy huku nikiangua kilio. “Nini tena shem?” Jimmy alishtuka. “Njoo.” “Kuna nini tena shem?” “Victor.” “Victor! Kafanya nini tena?” “Jimmy njoo haraka.” “Nakuja.” Kwa vile alikuwa hakai mbali alifika haraka sana, akaanza kushangaa kutokana na hali aliyomkutana nayo mume wangu, baada ya kumuona aliniuliza huku macho yake yakiwa yamemtoka pima. “Shem vipi tena! Mbona hivi?” Nilimueleza hali iliyomtokea na kushangaa sana, tulimchukua haraka na kumuwahisha Hospitali ya Amana. Muda wote mume wangu alikuwa kama mtu aliyelala usingizi mzito lakini pumzi zake zilikuwa zikisikika kwa mbali sana. Tulipofika tulipokelewa na mgonjwa kubebwa kwa kitanda cha magurudumu hadi wodini. Kabla ya kuhudumiwa tuliulizwa matizo yake, ajabu kabla sijajibu Victor alishtuka alipokuwa amelala na kufumbua macho kisha akajinyoosha na kujishangaa kuwa pale. “Vipi mke wangu?” aliniuliza. “Si unaumwa wewe?” nilimjibu huku nami nikimshangaa.
“Mimi?” Mume wangu alizidi kushangaa huku akikunja uso baada ya kutaka kauegemea mkono unaomuuma. “Jamani haya makubwa, si ulikuwa ukiumwa mkono na kichwa kiasi cha kulia kama mtoto mdogo mpaka akapoteza fahamu.” “Sina kumbukumbu hizo, mbona nilikuwa nimelala baada ya kuhisi kama mkono unataka kuniuma, zaidi ya hapo sikumbuki kitu.” “Kweli mume wangu?” nilizidi kumshangaa mume wangu. “Kweli kabisa.” “Kwani kuna tatizo gani?” daktari aliuliza. Nilimueleza yote ambapo mume wangu alishangaa sana, alichukuliwa vipimo vingine japokuwa vya awali vilionesha hana tatizo lolote. Jibu lilikuwa lilelile hana tatizo lolote, baada ya kudungwa sindano ya maumivu tuliruhusiwa kurudi nyumbani usiku uleule. Njia nzima nilikuwa naona kama maajabu, mume wangu kusema hajui lolote lililotokea. Tulipofika nyumba wakati nikimsindikiza shemeji Jimmy alinieleza kitu: “Shemeji, kwa ajali ya leo kuna kitu kizito naomba kesho asubuhi muwahi kwa yule mganga, nikimuangalia Victor namuona hayupo sawa kabisa, kuna jambo linaendelea ambalo hatulijui, tukifanya mzaha tutajuta baadaye.” “Nitafanya hivyo, namuomba Mungu muda uliobaki tuvuke salama.” “Basi nikutakie usiku mwema.” “Na wewe pia, nashukuru kwa msaada wako.”
Nilirudi ndani na kumkuta mume wangu akikoroma katika usingizi mzito, nilimuomba Mungu alale vilevile hadi asubuhi. Lakini kwangu sikupata tena usingizi hadi kunapambazuka. Alfajiri nilishukuru wazazi wa mume wangu walikuja baada ya kuchelewa kupata taarifa ya ajali ya Victor. Nilipowaona nilijikuta nikibubujikwa machozi kuwaona wazazi wa mume wangu. “Vipi kuna usalama?” “Upo, lakini mdogo sana wazazi wangu,” niliwajibu kwa sauti ya kilio. “Yupo wapi mumeo?” “Amelala, lakini simuelewi tangu apatwe na ajali.” “Kamuamshe.” Nilikwenda ndani kumuamsha mume aliyekuwa bado amelala, baada ya kumuamsha aliamka. “Vipi mke wangu? Niache nilale bado nina usingizi.” “Wazazi wamekuja.” “Wanasemaje?” aliniuliza bila kunitazama. “Mume wangu hujui yaliyokutokea?” “Ooh! Nilisahau, acha niamke nikawaone.” Alinyanyuka kitandani na kuvaa nguo kisha tulitoka pamoja sebuleni walipokuwa wamekaa wazazi.
“Shikamooni,” aliwasalimia huku akikaa kwenye kochi karibu na walipokuwa amekaa. “Marahaba baba, pole sana.” “Asante.” “Unavyoiona ile ajali ni ya kawaida au mauzauza?” baba mkwe alimuuliza mume CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.comwangu. “Wazazi wangu nina imani maisha yangu hayana muda mrefu hapa duniani,” mume wangu alisema kwa sauti ya chini huku akitazama chini. “Kwa nini?” mama mkwe aliuliza. “Mambo ninayokutana nayo hata kuyazungumza siwezi.” “Mambo gani mume wangu?” nilimuuliza baada ya kushtushwa na kauli ya mume wangu na kujiuliza kwa nini aseme maneno kama yale kwa wazazi wake wakati mimi mkewe sijui lolote zaidi ya ajali mbaya na matukio yaliyomkuta. “Mke wangu mengine nikikuelezea unaweza kufa kwa presha, lakini siri nzito ninayo mwenyewe.” “Siri gani tena mume wangu?” nilimuuliza huku nikimkazia macho. “Nashindwa nianzie wapi kuielezea, usiku kwangu ulikuwa mgumu sana tena sana maishani mwangu na sikuamini kama nitaliona jua la leo.” “Kivipi?” nilimuuliza mume wangu ambaye alionesha ana siri nzito moyoni mwake lakini hakutaka kuisema. “Unajua sisi wanadamu ni viumbe wabaya sana, sisi tuna utajiri gani? Gari mbili, kiwanja hata nyumba hatujamaliza wananitoa roho?” mume wangu kufikia hapo aliinama na kutulia huku akilia kilio cha kwikwi. “Sasa mama sikiliza,” baba mkwe alisema na kunifanya nimwangalie yeye. “Hapa hakuna muda wa kupoteza, twende moja kwa moja kwa mganga tuangalie tulikosea wapi.” Kwa vile lilikuwa limebakia gari moja, nilimpigia simu Jimmy aje atuchukue, atupeleke kwa mganga. Lakini ilikuwa bahati nzuri alikuwa na yeye yupo jirani kuja kujua hali ya mume wangu kabla ya kwenda kazini. Alipofika alituchukua na kutupeleka kwa mganga Mtoni Mtongani. Baada ya kufika tulipokelewa na mganga na kuingizwa kwenye chumba cha huduma. Sote tulikaa kwenye mkeka, baada ya mganga kumaliza shughuli zake, aliingia chumbani na kukaa mbele yetu. Kama kawaida alichukua kitabu chake na kukisoma kwa muda kisha alinyanyua macho na kutikisa kichwa akisema: “Mmh! Jana kijana alikuwa anakufa kifo kibaya, yaani hata asingeomba maji. Ile iliyotokea si ajali ya kawaida, wale waliokuja kukukodi ni majini wa kutumwa. Si walikuwa mwanamke na mwanaume waliovaa kiheshima kama Wapemba?” “Ndiyo,” mume wangu alijibu. “Basi wale hawakuwa watu kama ulivyofikiria, walikuwa majini ambayo ndiyo waliolizima lile gari ili ugongwe na kufa ili kionekane ni kifo cha kawaida. Dawa niliyokupatia ndiyo iliyokusaidia bila hivyo ungebakia jina na watu kuona wewe ni mzembe kuingiza gari barabarani bila kuangalia.” “Ina maana waliokufa si watu wa kweli?” mume wangu aliuliza, muda huo alikuwa kwenye hali ya kawaida kabisa. “Wale hawakuwa watu, kile ni kiini macho kuona watu wamekufa ili hata wewe ukifa, ijulikane umekufa na abiria wako wawili.” “Mbona inasemekana zile maiti zilichukuliwa na kupelekewa hospitali?”
“Niamini mimi kuwa pale hakukuwa na watu, kama mnabisha, nendeni mkaangalie zile maiti kama zitakuwepo. Pia kaliangalieni gari kama utakuta kuna damu.”
“Ni nani aliyefanya hivyo?” “Kwa kweli kila nikimtafuta naona kiza, inaonekana amejizatiti baada ya kutegua mtego wa awali. Lakini bado nitapambana naye mpaka pumzi za mwisho.” “Na huu mkono?” “Pigo ulilopigwa limepitia hapo, lakini hakuna tatizo nitalitatua,” kauli ya mganga ilinipa moyo na kunifanya nipunguze mawazo kidogo.
“Kuna kitu gani kinachomtisha kiasi cha kusema ana imani maisha yake yamebaki kuwa mafupi sana?” Baba mkwe aliuliza. “Ni wasiwasi wake tu kutokana na vitu vinavyomtokea ndotoni.” “Vitu gani?” “Usiku alipolala ile safari ilijirudia upya, alichokiota ndicho ambacho kingetokea.” “Kipi hicho?” Niliuliza.
“Ameota baada ya gari kuzimika na kugongwa hakutoka na kugongwa kichwa chake kikapasuka na mkono huu ulinyofoka na kuangukia upande wa pili. Maumivu ya kunyofoka mkono na kupasuka kichwa aliyasikia kiasi cha kushtuka usingizini na kuendelea na maumivu yale. “Acha alie kama mtoto mdogo, jana usiku kateseka sana na angeweza kufa kwa maumivu yale, baada ya kunyamaza vile ndiyo ilikuwa mwisho wa safari yake. Lakini kinga niliyompa bado ilimsaidia sana badala ya kufa alipoteza fahamu. Maumivu yale yangemuandama kila usiku na mwisho asingevumilia angeamua kujiua kwa kunywa sumu au kujinyonga kutokana na maumivu makali sana ambayo yangekimbilia moyoni mwake. Na ugonjwa ule siku zote hospitali huwa hauonekani zaidi ya kwa wataalam kama sisi.”
Nilikubaliana na mganga kwani mume wangu kila alipokwenda hospitali na kupimwa ugonjwa haukuonekana. “Kwa hiyo utatusaidia vipi?” Mama mkwe aliuliza. “Dawa nitakayompatia leo itamaliza kila kitu wala msihofu.” Baada ya kusema vile alianza kumshughulikia mume wangu kwa sisi kutolewa chumbani. Baada ya nusu saa alitoka akiwa amechanjwa sehemu iliyomletea maumivu na kupakwa dawa. Baada ya matibabu tulipewa tena dawa za kuoga na kufusha kisha tulirudi nyumbani.
Tulipofika mume wangu alionekana amechoka sana, baada ya chai aliingia chumbani kulala. Alipovua nguo na kulala ndipo nilipomuona vizuri alivyochanjwa kuanzia juu ya bega hadi chini ya mkono, mbavuni mpaka kiunoni na kupakwa dawa nyeusi iliyochanganywa na mafuta mazito. Wakwe zangu siku ile hawakuondoka walilala palepale kusikilizia hali ya mume wangu ambayo iliendelea vizuri. Usiku alilala vizuri kitu kilichotufanya tuamini mganga ameweza kutatua tatizo, hata yale matatizo ya maumivu ya mkono hayakuwepo, alilala vizuri.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com
Siku ya pili tuliamka salama, pamoja na mkono kuisha maumivu tatizo lingine lilikuwa kukosa nguvu kitu kilichofanya atumie mkono wa kushoto katika kazi zake zote. Niliamini baada ya muda kutokana na matibabu na kauli ya mganga atarudi katika hali yake ya kawaida. Baada ya kufungua kinywa na kuhakikisha hali ya mume wangu imetulia nilikwenda Polisi Chang?ombe kuangalia gari alilopata nalo ajali mume wangu ili nilinganishe na mastaajabu ya watu.
Kwa vile baadhi ya maaskari walikuwa wakinifahamu waliponiona walinitania. “Shemeji umekuja kuona maajabu ya Musa?” Swali lile lilizidi kuniweka njia panda na kujawa na mawazo mengi juu ya ajali ilivyokuwa. “Ndiyo shem, la kusikia si sawa na la kuona.” Walinipeleka kwenye magari yaliyokuwa yamewekwa sehemu moja, mengi yalionekana kupata ajali za kugongwa lakini mengine yalikuwa mazima, sikujua na yale yapo pale kwa ajili gani.
Nilipofika nilijikuta nikilitafuta gari letu na kushindwa kuelewa lipo upande gani hadi askari niliyeongozana naye aliponiambia: “Hili hapa shemu.” “Hili?” nilishtuka. “Ndiyo.” “Hapana...hapana, siyo hili,” nilijikuta nakataa baada ya kuliona gari lililokuwa kama chapati. “Ndilo hili shemu si unazijua namba zake, angalia.” Nilichungunza gari, lilikuwa limekunjika vibaya, baada ya kulichunguza, niligundua ndilo lenyewe. Nilijikuta nikitokwa na machozi nisiamini kama kweli mume wangu alitoka salama kwenye ajali ile. “Sasa shemu unalia nini?” aliniuliza askari aliyenipeleka kuliona gari. “Siamini...siamini...kama mume wangu alitoka salama kwenye ajali hii!” nilisema huku nimeshikilia kifua na machozi yakiendelea kunitoka. “Mumeo lazima atakuwa ameaga kwao, ajali hii hakuna anayeweza kukubali kama dereva alitoka salama labda useme gari liligogwa bila dereva ndani.” “Mmh! Mungu mkubwa sifa ni haki yake, asante Mungu.” Nilimshukuru Mungu kwa kupiga ishara ya msalaba kwa kuyaokoa maisha ya mume wangu kwenye ajali ile. Nilizidi kuamini kila kitu kwa Mungu kinawezekana kama alivyoweza kumuokoa Musa kwa Firauni. Pia kumponya Yona katika tumbo la samaki na mitume wengine wote aliowaponya pale uwezo wa kibinadamu ulipofika kikomo. Kutokana na kuamini kila tuliloahidiwa na Mungu kuwa hakuna zito mbele yake. Niliamini hata mume wangu naye alimnusuru kwa njia hiyohiyo japo sikujua kipi kikubwa alichokifanya kwa Mungu kupewa kinga kama ile. Nilirudi nyumbani bado nikiwa na picha ya gari letu lilivyokuwa na kupona kwa mume wangu. Nilijiuliza nini hatima yetu kama watu kila kukicha wanatafuta mbinu za kutupoteza. Niliamini ule ni muda muafaka wa kumshukuru Mungu kwa kumtumikia yeye mimi na mume wangu, japo bado nilikuwa na wasiwasi wa kuchanganya nguvu za giza na Mungu aliye hai aliyetukataza kumshirikisha kwa miungu mingine kwa vile yeye ni mwenye wivu.
Lakini niliamini bado tuna nafasi ya kutubu na kukubaliwa, kwa vile Mungu wetu ni mpole msikivu na mwenye huruma. Nilipanga baada ya kumaliza tiba ya mume wangu tuanze kazi ya kumtumikia Mungu kwani niliamini kupona kwa mume wangu haikuwa nguvu ya mganga bali uwezo wa Mungu kutuonesha kuwa hakuna mwenye uwezo zaidi yake. Pia ni ili tuamini kuwa yupo na mwenye kutenda kile kisichotarajiwa na mwanadamu. *** Mwezi ulikatika bila mabadiliko makubwa ya hali ya mkono wa mume wangu. Kila tuliporudi kwa mganga alitubadilishia dawa huku tukizidi kupoteza fedha bila mafanikio. Kilichonishtua sana kilikuwa kuuona mkono wa mume wangu ukipungua na kuanza kusinyaa. Kwa kweli kitu kile kilinishtua sana na kutaka ufumbuzi kwani hali ilishakuwa mbaya. Hata biashara zangu nazo zilianza kuyumba kwani sikuwa na uwezo tena wa kuongeza vitu dukani kutokana na fedha nyingi kuipeleka katika matibabu ya mume wangu. Mume wangu naye kutokana na mawazo ya ugonjwa, alianza kupungua siku hadi siku kila nilipomwangalia roho iliniuma sana na kufikia hatua ya kuwachukia wanadamu. Sikuamini kitu chetu wenyewe kifikie hatua ya kututesa vile, moyoni nilifikia hatua ya kujilaumu kununua gari. Niliona heri ningeongeza maduka kuliko gari lililotuletea dhahama nzito kama ile. Kuchanganyikiwa kubaya, kila mganga niliyeelekezwa nilikwenda. Nilielekezwa sehemu moja huko Muheza, Tanga, kwa vile muda huo fedha ilikuwa imeniishia, ilibidi niuze kiwanja na nyumba iliyokuwa imefikia dirishani kwa bei ya kutupa ili tu niokoe uhai wa mume wangu. Nilikwenda Muheza vijiji vya ndanindani, nilipofika nilikutana na mapya kuwa mkono wa mume wangu kuna vitu vimewekwa vinavyomnyonya kila siku. Sikuamini vitu vilivyotolewa kwenye mkono wa mume wangu, kulitolewa sindano ndogo za kushonea zaidi ya kumi, viwembe sita na pini ndogo tano. “Basi hivi mwanangu ndivyo vilivyokuwa vikimtesa mumeo,” mganga alinionesha na kunifanya nipigwe na butwaa. Nilichanganyikiwa na kujiuliza vitu vile viliingiaje mwilini kwa mume wangu.
“Kama ni hivyo heri nirudi nyumbani ili hata wewe uweze kuhangaika.”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com
Wazo la mume wangu japokuwa sikuliafiki moja kwa moja lakini kwa upande mwingine niliona linafaa kutokana muda mwingi kuupoteza nikiwa nimekaa tu bila ya kufanya kazi.
Lakini kama ningekuwa nyumbani ningeweza hata kwenda dukani na kuingiza fedha kidogo ya matumizi.
Nilimueleza mganga ambaye alikubali turudi nyumbani huku akitupa dawa za kutumia tukiwa nyumbani.
Tulirudi nyumbani kama tulivyoondoka hakukuwa na mabadiliko yoyote zaidi ya mgonjwa na muuguzaji kupungua kutokana na mawazo na mkono kuzidi kusinyaa kiasi cha bega nalo kuanza kukonda.
Kila nilipomuangalia mume wangu roho iliniuma sana, kuna kipindi nilikuwa nikijifungia ndani na kulia mpaka macho yakanivimba huku nikimuuliza Mungu kosa langu ni nini, kwani kila matatizo ni yangu. Nilimuomba Mwenyezi Mungu basi anitazame na mimi kwa jicho la huruma kwani hali kwa upande wangu ilikuwa mbaya sana iliyopoteza matumaini na kuhofia kufikia hatua ya kumkufuru.
Katika kuhangaika kuna dada mmoja alinieleza jambo, kuwa pengine kutopona kwa mume wangu huenda ni chukizo la Mungu kwa kuwa tumekuwa tukutumia nguvu za giza na kumsahau yeye aliyemuokoa mume wangu kwenye kinywa cha mauti.
Alinieleza miujiza ya maombi jinsi yanavyowaponya watu wengi, hivyo nilitakiwa kutubu na kumrudia Mungu.
Nilikubaliana moja kwa moja na wazo lake, kwanza alisema jioni ya siku ile angeniletea mchungaji wa kanisa analosali.
Japokuwa nilikuwa ni muumini wa dhehebu la Romani Katoliki, sikuweza kubisha kwani niliamini kinachoponya ni imani na kuyaamini maneno ya Mungu aliye hai wala si dhehebu.
Jioni alikuja mchungaji ambaye aliendesha ibada ya maombi.Kila alipokuwa akioomba mume wangu aligaagaa chini kama kuna kitu kinataka kutoka mwilini. Mchungaji kila alivyofanya ilikuwa kazi bure pamoja na kukemea pepo litoke mpaka shati lake likalowana na jasho kama mtu aliyenyeshewa na mvua, mume wangu aliendelea kugaagaa lakini pepo lilionekana kuwa na nguvu sana kiasi cha kugoma kutoka.
Mchungaji aliamini kila siku akilikemea pepo mwishowe lingetoka, baada ya jitihada zake kugonga ukuta, nilielekezwa niende katika moja ya makanisa makubwa ya maombezi yenye sifa ndani na nje ya nchi na lazima pepo lile kaidi lingetoka.
Nami nilifanya kama nilivyoshauriwa kwa kuzunguka na mume wangu kwenye makanisa nikiamini kuwa Mungu atatuona nasi kama alivyowaona wengine waliokuwa wakitoa ushuhuda wa kupona kwenye runinga.
Kwangu ilikuwa tofauti na wengine, wengi waliopanda mbele baada ya maombezi walitoa ushuhuda kwa midomo yao kuwa wamepona lakini kwangu ilikuwa tofauti mume wangu alikuwa vilevile.
Hata hivyo, sikuchoka kila kanisa kubwa unalolijua nilifika na mume wangu, lakini sikuona miujiza yoyote, nilijiuliza sisi na wengine tuna tofauti gani ya imani.
Iweje kila aliyepanda alitoa ushuhuda kuwa amepona lakini sisi hata robo ya mabadiliko hayakuwepo.
Nilipouliza mbona kwangu hakuna tofauti kila siku nilielezwa huenda mume wangu imani yake ilikuwa ni ndogo.
Niliamini matatizo humfanya mtu kumjua Mungu, mume wangu naye aliokoka akawa anatumia muda mwingi kusoma Biblia na kuhudhuria misa zote, ilibidi tuhame kutoka ukatoriki na kuhamia ulokole ili kuitafuta huruma ya Mungu.
“Usiseme hivyo mume wangu, nitazungumza nao.” “Sidhani kama watakuelewa.” “Hebu subiri,” nilinyanyuka na kumfuata mama mkwe aliyekuwa akisuka ukili. “Mama.” “Abee mama mkwe,” mama mkwe aliitikia. “Mna mpango gani na baba Fatu?” “Mpango gani tena?” “Hamjui kama anaumwa?” “Tunajua.” “Sasa mbona hakuna juhudi yoyote?” ”Juhudi gani?” “Si mnajua tumbo limeanza tena? Kwa nini tusimpeleke hospitali?” “Hili litakuwa tatizo lingine si la hospitali,” alinijibu mama mkwe bila kuonesha kushtushwa na nilichokizungumza. “Mamaaa, jamani mbona mnamtesa mume wangu?” “Wee mtoto kuwa na heshima, wewe na sisi nani mwenye uchungu kati yako muolewaji aliyemjua Tony akiwa mtu mzima na sisi wazazi wako tuliyemzaa na kumlea.” “Mama tusifike huko, tunatakiwa kurudi tena hospitali, Tony ana hali mbaya sana.” “Mimi si msemaji msubirii baba yenu.” Siku ile sikuweza kuondoka kwa ajili ya kumsubiri baba mkwe ili nizungumze naye juu ya kumpeleka mgonjwa hospitali. Baba alirudi usiku sana hivyo ilinilazimu kulala ukweni. Aliporudi alielezwa na mama mkwe na kutoa jibu la kuwa wao ndiyo wanaojua hivyo nisiwaingilie kwani wamepoteza fedha nyingi kwa ajili ya matibabu ya mume wangu. Majibu yale yalikuwa kama kuupasua moyo wangu kwa kisu butu bila ganzi. Usiku ulikuwa mrefu kwangu kwani kilio cha maumivu ya tumbo cha mume wangu kilinifanya nishindwe kulala. Tulikesha wote huku nikimgeza kwa kumlaza miguuni kwangu kutokana na kusema anasikia maumivu kila kona ya mwili. “Mke wangu nimemkosea nini Mungu? Kwa nini asinichukue nikajua moja,” mume wangu alisema kwa sauti ya kukata tamaa yenye maumivu makali. “Usiseme hivyo mume wangu.” “Hujui ninavyoumwa. Siamini kama hawa ni wazazi wangu.” “Kwa nini tena jamani?” “Wanataka nife? Nikifa watapata faida gani?” “Hata nashindwa kuelewa wamekuwa wabishi, hili tatizo tungerudi hospitali lingeisha.” Kilio cha maumivu kilikuwa mateso mazito moyoni mwangu. Nilimwonea huruma kwani kuna kipindi alikuwa akitweta kwa maumivu kama anataka kukata roho. Alipotulia nilikuwa na wasiwasi labdaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com
amekufa. Nilipomshtua alikuwa amelala hivyo nilimwacha huku nikiendelea kumsikilizia hadi kunapambazuka. Asubuhi nilirudi kwangu nikiwa nimechoka sana kutokana na kukesha. Asubuhi nilizidi kuwambembeleza tumpeleke hospitali lakini waligoma na kuniona kama mwanga ninayetaka kumuua mtoto wao. Kauli ile iliniliza sana lakini sikuwa na jinsi kwa vile nilelewa katika malezi mazuri, sikuwajibu kitu nikaondoka. Nilijikuta nikiwaona wakwe zangu kama wanga wanaochangia kutaka kumuua mume wangu, lakini sikuwa na jinsi kwa vile wao ndiyo wazazi wake kama walivyosema na mimi nilikuwa muolewaji hivyo nilionekana nina uchungu wa kuigiza ila wao ndiyo walioumia zaidi yangu. Kwa hali aliyokuwa nayo mume wangu nilianza kukata tamaa ya kumpoteza hasa baada ya wazazi wake kukataa kumpeleka hospitali kwa ajili ya imani ya kishirikina. Nilimweleza Salome ambaye alinishauri niachane nao nifanye mambo mengine kuliko kuendelea kuteseka wakati kuna watu wanajiona wao wapo sawa kumbe wanaharibu. Nilizidi kuamini dunia ninayoishi si yangu. Wiki mbili baada ya sakata langu na wakwe zangu, mwanangu Fatuma alianza kuumwa ugonjwa wa kuchemka sana usiku ukimshika mwili anaunguza kama amechemshwa. Siku ya pili nilimpeleka hospitali ya Temeke. Baada ya vipimo vyote tulipatiwa kitanda. Niliendelea kumshukuru Salome kwa msaada wa hali na mali huku majirani nao wakinisaidia kwa kipindi chote hata kuchanga fedha iliyonisaidia kununua baadhi ya dawa zilizotakiwa kwa ajili ya mgonjwa. Baada ya matibabu yaliyochukua wiki moja na nusu, tatizo la kuchemka mwili lilisha, lakini likazuka lingine la miguu kuwa ya baridi na kukosa nguvu. Ilibidi tuendelee kuwepo hospitali kwa ajili ya matibabu zaidi, vipimo zaidi vilichukuliwa na kusubiri majibu ambayo yalichukua wiki nzima. Mwanangu naye alianza kupungua mwili na tumbo kuanza kuvimba, chakula akawa hataki kula kitu kilichozidi kummaliza. Wakwe zangu nao walikuja kunijulia hali na kunieleza hali ya mume wangu. Walinieleza anaendelea vizuri lakini sikuwaamini. Nilijikuta nikiwa na hamu ya kumwona mume wangu nijue hali yake lakini sikuwa na mtu wa kumwachia mwanangu aniangalizie pale hospitali. Wakati nasubiri vipimo, dawa alizopewa kwa wakati ule zilimuwezesha kula kidogo japo choo kilipatikana kwa shida lakini kulikuwa na mabadiliko madogo yenye kutia matumaini.
“Nimekuelewa shoga yangu, nitafanya hivyo, mpaka sasa sijui nifanye nini nimechanganyikiwa hata sijui nishike mti gani,” maneno ya shoga yangu yaliniingia na kunichanganya sana. “Usichanganyikiwe, imani yako katika maombi ilikuwa kubwa ukasahau kwamba uweza wa Mungu ni mkubwa si katika maombi tu hata katika miti aliyotuletea kwa ajili ya chakula na dawa, hivi nikikuuliza wakati wa Yesu hapakuwepo maskini?” “Nina imani hawakuwepo,” nilijibu kwa vile niliamini kama wachungaji wana uwezo kama ule Yesu alikuwa yupo vipi, na wote waliponya kwa jina lake. “Nataka nikueleze mpaka Yesu anasalitiwa na Yuda pia kukanwa na Petro inaonesha bado walikuwepo wenye mioyo dhaifu pia maskini vipofu hata wagumba walikuwepo. Na kama maombi ni kila kitu hospitali zisingekuwepo kila atakayeombewa angepona bila kwenda hospitali. Lakini haohao
wanaoombea watu wanatibiwa na dawa hizihizi kwa vile kumeza au kunywa dawa si dhambi.” “Inaonekana unaijua dini vizuri?” Nilishangazwa na uwezo wa yule dada katika kuichambua dini. “Si kwamba naijua dini sana, kuna mambo mengine wanadamu tunayakuza kwa faida zetu wenyewe.” “Kwa hiyo maombi ni uongo?” “La hasha maombi si uongo kila mwenye imani maombi yake hupokewa na vilevile hata yakichelewa huwa mvumilivu.” “Kwa hiyo hata mimi sikutakiwa kukata tamaa.” “Kama ingekuwa hakuna njia mbadala ulitakiwa uendelee na hayo maombi japokuwa si kwenda kwa mtu bali kujazwa imani na wewe kusimama popote kumlilia Mungu kilio cha kweli chenye kumtegemea yeye hakika Muumba wetu ni msikivu.” “Kwa nini waumini tunadharauliana?” “Wapo wanaodharau watu kwa kuamini wao ndiyo wapo sahihi, lakini Mungu ni mmoja na katufundisha tufanyeje tunapokuwa kwenye matatizo.” “Unaweza kuchanganya maombi na dawa za hospitali?” “Unaweza kwa vile yote ni kutafuta ufumbuzi, maombi si wakati wa kuumwa tu muda wote unatakiwa kuzungumza na Muumba wako. Ukimkumbuka Mungu kila wakati hata yeye atakukumbuka.” “Nimekuelewa shoga yangu, leo umeniondoa ukungu kwenye akili yangu.” “Si ukungu aliyekushawishi kuokoka alikushawishi vibaya na kujikuta kila kitu amehamishia huko na matokeo yake amekuacha ukipata maswali yasiyo na majibu kila siku.” Baada ya kuachana na shoga yangu ambaye alikuwa Mkristo kama mimi, angekuwa Muislamu ningekuwa na uwalakini. Maneno yake CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.comniliyafanyia kazi na kufikiria jinsi nilivyohangaika na mume wangu bila mabadiliko yoyote japokuwa tulionekana hatuna imani. Nilijiuliza imani hiyo ni kwetu tu wakati kuna watu wengi walikuwa na mapungufu ya kibinadamu yaliyokuwa yakijulikana na wengine kukiri kuwa walikuwa wachawi na wazinzi waliokubuhu. Kwa upande wangu niliingiwa na wasiwasi na uponyaji wa kwenye makanisa yote niliyokwenda kwa kuwa ulikuwa ukichagua baadhi ya watu. Niliamua kuachana na makanisa ya uponyaji na kurudi katika dhehebu langu la Kikatoliki na kumuachia Mungu aamue chochote juu ya hatima yetu. Niliamua kumpeleka hospitali mume wangu ingawaje familia yake bado ilikuwa ikitaka twende kwa waganga wa kienyeji. “Wazazi wangu kwa nini turudi sehemu iliyoshindikana?” “Kila mganga ana uwezo wake tujaribu na kwingine,” alisema mama mkwe. “Jamani wazazi wangu kuna waganga kama tulipokwenda huko Tanga mlipokuwa mnapasifia, nimekaa zaidi ya miezi mitatu bila mafanikio mnfikiri kuna mganga gani zaidi?” “Tumekueleza unaweza kutumia nguvu nyingi asifanikiwe, lakini ukatumia kidogo tu akafanikiwa.” “Wazazi wangu nilikuwa naomba tumpeleke baba Fatu hospitali,” nilizidi kuwabembeleza. “Kwa waganga kumeshindikana, kwenye maombi pamoja na kuokoka kwenu lakini imeshindikana. Mi nilijua huko ni utapeli mtupu ningewakatalia mngeniona mbaya nafikiri mmejionea wenyewe.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment