Search This Blog

Thursday, July 21, 2022

MY REPENTANCE (KUTUBU KWANGU) - 2

 







    Simulizi : My Repentance (Kutubu Kwangu)

    Sehemu Ya Pili (2)



    Baadaye nilimuona akitoka akiwa kifua wazi huku akiwa amejifunga taulo tu, akaja mpaka pale nilipokuwa nimekaa, akanishika mkono na kuniinua, taratibu tukawa tunaelekea chumbani huku nikiendelea kushangaashangaa mandhari nzuri ya mle ndani.

    SASA ENDELEA...CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tuliingia kwenye chumba kizuri mno cha Ibra, kilichopambwa utafikiri ndani yake alikuwa anaishi mtoto wa mfalme. Kulikuwa na kitanda kikubwa mno, nadhani hata sita kwa sita ni kidogo, juu yake kulikuwa na mashuka mazuri na mapambo ya kila aina.

    Upande wa kulia, kulikuwa na bafu la kisasa ambalo ndani yake kulikuwa na jakuzi, sijui kama wengi tunalifahamu jakuzi likoje kwani hata mimi ukiachilia mbali kusikia kwa watu na kuona kwenye runinga, siku hiyo ndiyo ilikuwa ya kwanza kuliona na kulitumia.

    Upande wa kushoto kulikuwa na seti ya muziki (music system), zile zinazouzwa zikiwa zimekamilika kila kitu. Ukutani kulikuwa na runinga kubwa kama ile tuliyoiacha pale sebuleni.

    Hapo sijaelezea kuhusu mapambo mbalimbali ya kisasa na vifaa vingine vidogo kama meza ya kujipambia (dressing table) ambayo sikuwahi kuiona sehemu nyingine yoyote.

    “Jaribu mama, jisikie upo nyumbani,” alisema Ibra huku akinioneshea kwa ishara kwamba nikae kwenye sofa za kisasa zilizokuwa ndani ya chumba hicho. Mtoto wa kike kwa mashauzi wala sikutaka kukaa kwenye sofa, nikajitupa kitandani na kujiachia kwa raha zangu.

    “Ngoja nikaoge nakuja sasa hivi,” alisema Ibra huku akielekea kule kwenye jakuzi, aliponiacha nikawa na kazi ya kuchunguza vizuri mandhari ya mle ndani. Ama kwa hakika hapa duniani kuna watu wanaishi maisha utafikiri wapo peponi.

    Muda mfupi baadaye, Ibra alirudi na kuja pembeni yangu pale kitandani, tukawa tunapiga stori za hapa na pale huku muziki laini ukiendelea kutuburudisha. Yaani sikutamani kutoka mle ndani, nilitamani kama Ibra ndiyo awe ameshanioa nijilie raha mtoto wa kike miye.

    Basi kama ilivyokuwa kawaida yangu ninapokuwa na Ibra, nilianza kumchokoza kwani bila hivyo, nilijua tunaweza kukaa mpaka muda wa kuondoka bila Ibra kunigusia chochote kuhusu mambo ya kikubwa, basi nikaanza uchokozi.

    Muda mfupi baadaye, sote tulikuwa kama tulivyokuja duniani, mtoto wa kike nikawa najitahidi kuonesha mbwembwe ili gari la Ibra lipige ‘starter’ haraka tuianze safari ya huba. Kama ilivyokuwa jana yake, licha ya mimi kujitahidi kadiri ya uwezo wangu kumpasha moto, mwenzangu bado alikuwa wa baridi.

    Nikaongeza utundu lakini wapi, Ibra alikuwa amelala doro, jambo lililoanza kunipandisha hasira taratibu kwani mateso niliyokuwa nayapata yalikuwa hayaelezeki.

    “Kwani una tatizo gani Ibra wangu?” nilisema huku nikimkumbatia kwenye kifua changu kilichosheheni vilivyo, akawa anapumua kwa nguvu kama dume la mbuzi akikosa cha kunijibu.

    “Hebu jitahidi kupunguza hofu ndani ya moyo wako, mimi ni wako kwa hali yoyote, nakuomba utulie mpenzi wangu ili unipe raha,” nilisema huku nikisikiliza mapigo yake ya moyo ambayo ama kwa hakika yalikuwa yakimuenda mbio mno.

    Kidogo kauli yangu hiyo ilimsaidia, akashusha pumzi ndefu na kwa mbali nikaanza kuhisi anakaribia kua vile nilivyokuwa nataka awe. Niliendelea kujituma mtoto wa kike, pale nilipotakiwa kughani nilifanya hivyo kisawasawa, tenzi zote za mahaba nikamaliza.

    Taratibu nikaanza kusikia gari la Ibra linataka kupiga starter, nikaongeza kasi na muda mfupi baadaye, kweli liliwaka. Nikafurahi mno kumuona akiwa katika hali ile, sikutaka kupoteza muda, nikamsaidia kuingiza gia kwa haraka na safari ya huba ikaanza, huku nikiwa na papara kuliko kawaida.

    Maskini Ibra, kabla hata sijaanza kuhisi chochote, alitangaza kufika mwisho wa safari yake, akaniacha nikiwa na hali mbaya kuliko hata jana yake kwani sikufaidi chochote kama nilivyotegemea. Kweli waliosema mkamia maji hayanywi hawakukosea, nilishindwa kuyanywa, nikabaki na kiu yangu.

    Hata hivyo, sikutaka kumlalamikia kama jana yake kuogopa kumuumiza kisaikolojia, nikajilaza pembeni huku nikiendelea kuugulia ndani kwa ndani. Harakaharaka Ibra aliamka na kwenda tena bafuni, na mimi nikainuka na kuanza kumfuata.

    “Rudi kwanza mpaka mimi nimalize,” alisema Ibra huku akionesha aibu zilizopitiliza. Ninavyojua mimi wanawake ndiyo huwa na aibu hasa wanapokuwa mbele za wanaume lakini kwa Ibra ilikuwa tofauti, eti yeye ndiyo alikuwa ananionea aibu mimi.

    Kwa kuwa nilishajiapiza kumsaidia, sikutaka kufanya alivyotaka, nikaingia naye bafuni na kumsihi anizoee kwani mimi ndiyo mke wake mtarajiwa na hakuwa na sababu yoyote ya kuniogopa. Akaniongoza mpaka kwenye jakuzi, akaseti maji ya uvuguvugu kisha tukaingia na kujilaza kwenye maji ya uvuguvugu.

    Raha niliyojisikia kuoga kwenye jakuzi ilinisahaulisha kwa muda machungu yangu niliyokuwa nayo. Nikawa nafurahia harufu nzuri ya sabuni maalum iliyokuwa imewekwa kwenye maji hayo na kutoa povu linalonukia mno.

    Tukawa tunacheza na Ibra huku akiendelea kunisihi kuwa nisimkimbie kutokana na udhaifu aliokuwa nao bali nimsaidie kama nilivyomuahidi. Nilimwambia wala asiwe na wasiwasi, tukaendelea kuzungumza mambo mengi kuhusu maisha yetu ya baadaye.

    Baada ya takribani nusu saa ya kula raha kwenye jakuzi, tulitoka na kurudi kitandani. Kwa kuwa sasa Ibra alikuwa ametulia kabisa kimawazo na hakuwa tena na hofu na mimi, nilijaribu tena bahati yangu.

    Angalau safari hii alijitahidi kidogo kwani hakuchelewa kupiga ‘starter’ lakini kama ilivyokuwa mara zote, ndani ya sekunde chache tu tayari alikuwa amemaliza kila kitu. Sikumbuki kama hata dakika moja ilipita, ni hapo ndipo nilipogundua kuwa ukiachilia mbali hofu, Ibra alikuwa na tatizo kubwa.

    Sikutaka kuonesha dalili yoyote ya kukasirishwa, nikajilaza pembeni na kuendelea kutafakari namna ya kumsaidia kuondokana na tatizo hilo. Wakati mimi nikiendelea kuwaza hayo, mwenzangu alikuwa akikoroma.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alikuja kuzinduka baadaye sana na kunikuta nikiwa nasikiliza muziki laini. Japokuwa alikuwa na upungufu huo, mwenzenu nilijiapiza kuwa vyovyote itakavyokuwa lazima niolewe naye ili niendelee kuyafaidi maisha.

    ****

    Wakati mimi nikiendelea kuwaza hayo, mwenzangu alikuwa akikoroma. Alikuja kuzinduka baadaye sana na kunikuta nikiwa nasikiliza muziki laini. Japokuwa alikuwa na upungufu huo, mwenzenu nilijiapiza kuwa vyovyote itakavyokuwa lazima niolewe naye ili niendelee kuyafaidi maisha.

    ****

    “Vipi mpenzi wangu,” alisema Ibra baada ya kuzinduka usingizini, nikamjibu huku nikimkumbatia na kumbusu kwa mahaba, tukawa tunapiga stori za hapa na pale huku Ibra akionesha kuwa na furaha sana.

    Japokuwa moyoni nilikuwa najisikia vibaya sana kutokana na yale mateso niliyokuwa nayapata, nilijitahidi kuvaa uso wa tabasamu ili nisimkwaze Ibra, tukaendelea kupiga stori na baadaye nikamwambia tuamke ili tuandae chakula cha mchana.

    “Wala usipate shida, huwa nakwenda kula pale nje kuna mgahawa mzuri sana, usijali,” alisema Ibra, tukaamka na kwenda tena kuoga kisha tukajiandaa na kutoka hadi nje, tukaingia kwenye gari la Ibra ambapo mlinzi alitufungulia geti, tukatoka na kuelekea kwenye mgawaha mmoja wa kisasa uliokuwa mtaa wa tatu kutoka pale nyumbani kwa Ibra.

    Tukashuka na kuingia ndani, nilibaki nashangaashangaa kwani wateja wengi kwenye mgahawa huo walikuwa ni Wazungu, Wachina, Wahindi na watu wa mataifa mbalimbali, tukatafuta sehemu tulivu na kukaa. Mhudumu akaja na kutuuliza tulichokuwa tunahitaji.

    Nilipewa menu na kuisoma lakini sikuelewa chochote, nikamgeukia Ibra ambaye ni kama aligundua kilichokuwa kinanitaza, akaagiza ‘Chicken Massala’ na muda mfupi baadaye, sahani mbili za chipsi kuku zililetwa zikiwa na vikorombwezo kibao.

    Akaagiza na juisi ambapo yule mhudumu alituletea, tukaanza kula huku tukipiga stori za hapa na pale. Taratibu nilianza kumzoea Ibra, mapenzi yangu kwake yakazidi kuongezeka huku moyoni nikijiapiza kuwa nilikuwa na jukumu kubwa la kuhakikisha namsaidia Ibra ili awe mwanaume aliyekamilika kama walivyo wengine.

    Baada ya kumaliza kula, tuliondoka na kurudi kwenye gari, Ibra akawasha na safari ya kurudi nyumbani kwake ikaanza. Ama kwa hakika siku hiyo nili-enjoy vya kutosha kwani kiukweli kila kitu kilikuwa kigeni kwangu.

    Kutoka kula kwa mama ntilie nikiwa chuoni au kula chakula cha kawaida nyumbani kwetu hadi kuja kula kwenye mgahawa mmoja na Wazungu na watu wa mataifa mbalimbali! Ama kwa hakika nilijiona mwenye bahati ya kipekee.

    Tulirudi mpaka nyumbani kwa Ibra, tukateremka kwenye gari na kuingia ndani lakini safari hii tulikaa sebuleni. Tukaendelea kupiga stori za hapa na pale huku tukisikiliza muziki na kuangalia muvi mpaka ilipotimu saa kumi za jioni.

    “Naomba nisindikize nirudi nyumbani kwani muda wa kutoka chuo umefika,” nilimwambia Ibra ambaye wala hakuwa na hiyana, aliingia chumbani kwake na baada ya muda alirudi akiwa na noti kadhaa za shilingi elfu kumikumi mkononi, mpya kabisa, akanipa na kuniambia kuwa eti zitanisaidia matumizi yangu madogomadogo.

    Nilimshukuru sana, nikamkumbatia mwilini na kumbusu kwa mahaba huku nikiwa siamini macho yangu. Tulitoka mpaka nje na kuingia kwenye gari, kabla hatujatoka alinitambulisha kwa mlinzi na kumwambia kuwa anitazame vizuri siku nyingine hata kama yeye hayupo aniruhusu kuingia ndani.

    Mlinzi aliitikia kwa heshima huku akinipa mkono na kuachia tabasamu pana, tukatoka na safari ya kurudi nyumbani ikaanza. Tofauti na siku zote, siku hiyo Ibra alinipeleka mpaka karibu kabisa na nyumbani kwetu, akaniambia anataka apafahamu nyumbani kwetu hata kwa mbali ili siku nyingine akitaka kuja asiishie kituoni Morocco kama anavyofanya siku zote.

    Kweli nilimuonesha nyumba yetu kwa mbali, akafurahi sana na kunikumbatia tukiwa ndani ya gari, akanibusu na mimi nikafanya hivyohivyo, tukaagana kisha nikashuka kwenye gari na kuanza kutembea kwa maringo kuelekea nyumbani.

    Ibra aligeuza gari lake na safari ya kurudi nyumbani kwake ilianza. Na mimi nilienda mpaka nyumbani huku kila mtu akijua kwamba nimetoka chuoni kumbe mwenzao nilikuwa na mambo tofauti kabisa.

    Japokuwa Ibra hakuweza kukidhi haja zangu, kiukweli siku hiyo alinifurahisha sana kwa mambo yote aliyonifanyia tangu asubuhi na kunifanya nijihisi kuwa mtu spesho sana kwake.

    Nilipoingia ndani nilienda moja kwa moja chumbani kwangu na kujifungia huku nikitoa visingizio kwamba kazi za chuoni zilikuwa zimenichosha sana siku hiyo. Hakuna aliyenitilia wasiwasi, si mama wala wadogo zangu.

    Nikiwa chumbani kwangu, niliendelea kuvuta kumbukumbu ya mambo yote yaliyotokea siku hiyo, muda wote tabasamu pana likawa limetawala kwenye uso wangu. Hata hivyo, furaha yangu ilitibuka nilipoanza kufikiria tatizo kubwa alilokuwa nalo Ibra la upungufu wa nguvu.

    “Nimewahi kusikia kuwa waganga wa kienyeji huwa wanatibu tatizo hili, isitoshe kule mjini nikiendaga chuo huwa naona mabango mengi ya waganga wanaosema wanaweza kutibu tatizo la nguvu za kiume, ngoja kesho nikienda chuo nitalifanyia kazi,” niliwaza kisha nikashusha pumzi ndefu.

    Mara mlango wa chumbani kwangu uligongwa, alikuwa ni mdogo wangu aliyekuja kuniita kwa ajili ya kwenda kujumuika na familia yangu kupata chakula cha jioni. Nilijiandaa na kutoka mpaka sebuleni ambapo nilimsalimia baba ambaye muda huo ndiyo alikuwa akirejea kutoka kwenye shughuli zake.

    “Nasikia leo mmegoma pale chuoni kwenu, kwani tatizo ni nini?” baba aliniuliza swali lililofanya moyo wangu ulipuke kwa kishindo kwani sikuwa najua chochote kilichotokea kwa sababu sikwenda chuoni kama nilivyoaga bali kutwa nzima nilishinda nyumbani kwa mpenzi wangu, Ibra.

    Nilibabaika kidogo lakini baadaye nikajikaza kisabuni na kutoa jibu ambalo hata sikuwa na uhakika nalo.

    “Matatizo ni mengi lakini kubwa ni uongozi.”

    “Kweli kabisa, unajua mahali kama uongozi ni mbovu, kila kitu kitaenda ovyo, pia nimesikia kuwa bodi ya mikopo nayo imejaa urasimu sana, hii serikali yetu sijui inaelekea wapi,” baba alisema huku tukiendelea kupata chakula taratibu.

    Sikutaka kuongeza neno kwa kuogopa kutibua mambo mwisho ibainike kwamba sikwenda chuoni. Kwa bahati nzuri, muda huohuo taarifa ya habari ilikuwa ikiendelea kwenye runinga. Kweli wanachuo wenzangu wakawa wanaoneshwa wakiwa wanaandamana huku wakiwa na mabango yanayolaani bodi ya mikopo kwa kuchelewesha mikopo yao. Moyo ulinilipuka mno na mapigo yangu yakawa yanaenda kwa kasi kubwa nikijua nimeumbuka.



    Kwa bahati nzuri, baba hakutaka tena kuendelea kunihoji kuhusu mambo ya chuoni mpaka taarifa ile ya habari ilipoisha, tukaendelea kula huku tukizungumza mambo mbalimbali ya kifamilia kama ilivyokuwa kawaida yetu.

    Tulipomaliza kula, kama kawaida yangu, sikutaka kuendelea kukaa pale sebuleni, nilielekea chumbani kwangu ambako nilijifungia mlango na kuendelea kutafakari mambo mbalimbali, hisia juu ya Ibra zikiendelea kuniteka akili zangu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Matatizo aliyokuwa nayo ya upungufu wa nguvu, niliona kama ni jambo ambalo lipo ndani ya uwezo wangu na nikajiapiza kuwa kesho yake nitakapoenda chuoni, nitakuwa makini kuchukua namba za simu kwenye mabango mengi ya waganga wa kienyeji yaliyotapakaa karibu kila kona.

    “Haiwezekani wote hao washindwe kumtibu mpenzi wangu Ibra, nilishakula kiapo cha kumsaidia na nitahakikisha nafanikisha hilo,” niliwaza huku nikiukumbatia mto wangu na kujigeuzageuza huku na kule, nikiwa nimevaa nguo nyepesi ya kulalia.

    Narudia tena, sijui niite ni tamaa, ushamba au mapenzi, mwenzenu nilijiona kuwa na bahati ya mtende kuota jangwani kukutana na Ibra na hatimaye kumteka mpaka akakubali kuwa mpenzi wangu. Nilipofikiria utajiri mkubwa aliokuwa nao na maisha ya hadhi ya juu aliyokuwa anaishi, nilijikuta nikizidi kupagawa.

    “Lazima niwe mke wake wa ndoa, lazimaaa,” nilisema huku nikiendelea kujigeuzageuza pale kitandani. Uzalendo ulinishinda, nikachukua simu yangu na kumpigia simu Ibra nikitaka kusikia japo sauti yake. Simu iliita mara ya kwanza mpaka ikakatika bila kupokelewa, sikukata tamaa, nikapiga tena.

    Kwa bahati nzuri Ibra alipokea lakini sauti yake ilikuwa ya kichovu mno. Nikamuuliza kulikoni?

    “Nilikuwa nimelala mpenzi wangu, unajua tangu muda ule niliporudi nimelala tu, najihisi uchovu sana,” alisema Ibra, nikamuonea huruma kwa sababu nilijua kwa nini amechoka vile. Ule mchezo wa kikubwa ulikuwa umemmaliza kabisa, japokuwa hakuwa amefanya chochote cha maana, lakini alionekana kuchoka mno.

    “Basi pumzika mpenzi wangu, utakapoamka hata kama ni saa sita za usiku nipigie kwa sababu sitapata usingizi bila kusikia sauti yako,” nilimwambia kwa sauti iliyokuwa inatokea puani, akacheka sana na kuniambia kuwa hakuwa amechoka kiasi cha kushindwa kuzungumza na mimi kwenye simu.

    Tukaanza kupiga stori za hapa na pale, safari hii Ibra akionekana kuanza kujiamini mbele yangu tofauti na ilivyokuwa mwanzo. Tulizungumza mambo mengi sana kuhusu familia yake na maisha yetu ya baadaye.

    “Kweli unanipenda Ibra?”

    “Nakupenda sana Flaviana wangu, nimeshakwambia wewe ndiye mwanamke wa kwanza kwenye maisha yangu na sijawahi kupenda kama ninavyokupenda, niamini.”

    “Utanioa au unataka kunichezea tu?”

    “Lazima nikuone Flaviana, wewe ndiyo kila kitu kwenye maisha yangu,” Ibra alisema kwa hisia sana, nikajikuta nikisisimka mwili mzima na kutamani kurukaruka kwa furaha niliyokuwa nayo.

    Basi tuliendelea kuzungumza mpaka usiku sana. Naomba nieleweke jambo moja kwamba japokuwa sikuwa na mazoea ya kuzungumza na simu kwa muda mrefu, hasa nyakati za usiku, kwa Ibra nilikuwa kama mjinga kwani wakati mwingine tulikuwa tukizungumza hata saa mbili mfululizo na sikuwahi kuchoka kusikia sauti yake.

    Baadaye tuliagana, tukatakiana usiku mwema kisha tukalala. Nilipokuja kuzinduka, tayari ilikuwa ni asubuhi. Jambo la kwanza kabla sijatoka kitandani ilikuwa ni kumpigia simu Ibra na kumjulia hali. Akafurahi sana kusikia sauti yangu kisha akaniambia nikimaliza kujiandaa nimsubiri anakuja kunichukua kama kawaida.

    Mtoto wa kike nikaelekea bafuni ambako nilijipiga ‘sopsop’ kisha nikarudi chumbani kwangu ambako nilitumia muda mrefu nyuma ya kioo kujipamba ili nizidi kumchanganya Ibra. Nikachagua nguo zangu nzuri ambazo huwa sizivai mara kwa mara. Nilipohakikisha nimependeza kiuhakika, nilimalizia kwa kujipulizia manukato mazuri kisha nikachukua simu yangu na kumpigia Ibra, nikamwamba nipo tayari.

    Aliniambia kuwa yupo njiani nimsubiri hapohapo nyumbani, atakuja mpaka pale aliponishusha jana yake jioni. Kweli dakika kadhaa baadaye, alinipigia simu na kuniambia kuwa ameshafika, nikatoka na kumuaga mama kwani tayari baba alishaondoka kwenda kazini, nikatoka na kutembea harakaharaka.

    “Whaooo, umependezaaa,” Ibra alisema huku tabasamu pana likiwa limechanua kwenye uso wake, mtoto wa kike nikavimba kichwa, akanikumbatia kwa mahaba, bila hiyana nikambusu kisha tukaingia ndani ya gari na muda mfupi baadaye, tuliondoka kuelekea Posta.

    Njiani tulikuwa tukipiga stori za hapa na pale mpaka tulipofika Posta. Kama kawaida, Ibra akanipeleka mpaka chuoni kisha tukaagana huku akiniachia noti mbili nyekundu eti za lanchi! Nilimshukuru na kushuka kwenye gari, nikawa natembea kwa kujitingisha kuelekea chuoni huku nikijua lazima Ibra ananitazama.

    Sikukosea, nilipogeuka kweli nilimuona Ibra akiwa ameganda palepale, macho yake akiwa ameyakodoa kunitazama sehemu zangu za nyumba ambazo zilikuwa si haba! Macho yetu yalipogongana, kila mmoja alitabasamu, nikampungia mkono kwa mbali, akawasha gari na kuondoka.

    Kwa kuwa nilikuwa nimewahi sana chuoni, niliingia na kuweka daftari zangu kisha nikatoka na kuingia mitaani kuanza kuifanya kazi niliyoipanga tangu jana yake; kuzunguka kutafuta mabango ya waganga wa kienyeji na kuchukua namba zao za simu kwa lengo la kutaka kumsaidia Ibra wangu ili na yeye awe mwanaume aliyekamilika.

    Kutokana na utitiri wa mabango ya aina hiyo, wala sikupata shida, dakika kumi tu baadaye tayari nilikuwa na namba zisizopungua sita, kila mganga akijitapa kuwa na uwezo mkubwa wa kumrudishia heshima mwanaume yeyote.

    “Haloo, samahani wewe ni Dokta Agugu kutoka Sumbawanga?”

    “Ndiyo binti, ulikuwa unasemaje?”

    “Nina mume wangu ambaye ana matatizo ya nguvu, nimeona bango lako ndiyo nimekupigia, nataka unisaidie,” nilizungumza na mganga wa kwanza ambaye alinihakikishia kwamba hilo ni jambo dogo sana kwake.

    “Njoo naye hata leo nimshughulikie, hilo ni tatizo dogo sana,” alisema mganga huyo kwa uchangamfu, nikashusha pumzi ndefu na kumshukuru huku nikiahidi kumpeleka Ibra jioni ya siku hiyo. Akanielekeza kwamba ofisi zake zipo mtaa wa Jangwani, Kariakoo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya kumaliza kuongea na mganga huyo wa kienyeji, nilishusha pumzi ndefu na kuanza kufikiria namna nitakavyomshawishi Ibra akubaliane na wazo langu. Nilitafakari kwa muda kisha nikapiga moyo konde na kumpigia simu Ibra.

    Simu iliita kidogo kisha akapokea, nikamwambia kwamba jioni akitoka kazini kuna sehemu nataka anisindikize. Wala sikumwambia tunaenda wapi na kufanya nini, akakubali bila kipingamizi.

    Kwa kuwa jana yake wanachuo wenzangu walikuwa wamegoma, siku hiyo hakuna mwalimu aliyeingia darasani, hata wanachuo wengi walikuwa wamezagaa nje kwenye bustani za maua. Kwa kuwa mimi nilikuwa na kazi nyingi nilizolimbikiza, nilitulia darasani mpaka jioni.

    Ilipofika saa kumi, nilikusanya vitu vyangu na kumpigia simu Ibra ambaye aliniambia kuwa na yeye anajiandaa kutoka. Nikamwambia afanye haraka ili tuende kwenye safari yetu.

    Kweli muda mfupi baadaye, Ibra aliwasili akiwa ndani ya gari lake, akateremka na kuja mpaka pale nilipokuwa nimesimama nikimsubiri, tukakumbatiana kwa furaha kisha akanishika mkono, tukarudi mpaka kwenye gari, akanifungulia mlango na kunisaidia kufunga mkanda.

    “Tunaelekea wapi?” Ibra aliniuliza akiwa ameshakaa nyuma ya usukani, nikamwambia tunaelekea Mtaa wa Jangwani kwa mganga wa kienyeji aitwaye Agugu kutoka Sumbawanga.

    “Kwani unaumwa?” Ibra aliniuliza huku akiwasha gari, nikababaika kidogo lakini nikamwambia asiwe na wasiwasi atajua tukifika. Nilitamani kumwambia ukweli juu ya nilichokuwa nataka kwenda kukifanya kwa mganga huyo lakini kila nilipomtazama, moyo wangu ulisita.

    “Vipi mbona unaonekana huna raha?” Ibra aliniuliza wakati tukiendelea kukata mitaa ya Posta kuelekea Kariakoo. Nikababaika kidogo na kumwambia kuwa uchovu wa siku hiyo ulisababisha niwe katika hali hiyo.

    “Pole, siku hazifanani,” aliniambia, nikatabasamu kwa mbali kisha safari ikaendelea huku sote tukiwa kimya kabisa. Tulifika Kariakoo na kwenda moja kwa moja mpaka Mtaa wa Jangwani, nikamwambia asimamishe gari kwa muda ili tuzungumze.

    Kweli alikubali nilichomwambia, akasimamisha gari na kulizima, akanigeukia akiwa na shauku kubwa ya kutaka kusikia nitamwambia nini. Nilibabaika kidogo, nikiwa sijui nianzie wapi kumfikishia ujumbe lakini baadaye nilijikaza na kumweleza lengo la safari ile.

    “Lakini mimi nimekulia kwenye familia ya kidini, sijawahi kutibiwa kwa mganga wa kienyeji hata siku moja, isitoshe ni dhambi,” Ibra alisema kwa sauti ya chini. Nikashusha pumzi ndefu na kuanza kumbembeleza akubali ili tatizo lake la upungufu wa nguvu likashughulikiwe na mganga huyo.

    Haikuwa kazi nyepesi kumshawishi, baadaye akakubali kwa shingo upande. Nikamkumbatia huku nikimshukuru kwa kukubaliana na wazo langu. Nikatoa simu yangu na kumpigia yule mganga ambaye harakaharaka alipokea.

    “Naomba utuelekeze nyumba, tumeshafika Jangwani, tupo hapa jirani na jengo la Klabu ya Yanga,” nilimwambia mganga huyo ambaye alituambia tumsubiri palepale anakuja kutuchukua.

    Muda mfupi baadaye, mwanaume mmoja mfupi, mweusi mwenye sharafa nyingi alikuja mpaka pale karibu na gari letu, akapiga simu yangu na kuuliza kama tulikuwa tunamuona. Tulishuka kwenye gari, tukasalimiana naye na kujitambulisha.

    “Karibuni sana, gari liacheni hapohapo kwa sababu huku kwangu magari hayaingii,” alisema mganga huyo na kutangulia mbele, akawa anatuongoza kuelekea nyumbani kwake. Tulipofika, tuliwakuta wagonjwa wengine kadhaa wakiwa sebuleni kwake, nao wakisubiri huduma.

    Akatuelekeza sehemu ya kukaa kusubiria mpaka zamu yetu itakapofika. Kweli tulikaa huku tukishangaashangaa mandhari ya sebule yake iliyokuwa imejaa vitu vingi vya asili, ikiwemo mitishamba na tunguli za kila aina.

    Muda mfupi baadaye, zamu yetu iliwadia, tukaingia mpaka kwenye chumba chake anachokitumia kutibia. Nikarudia kueleza matatizo ya Ibra wangu kisha baada ya hapo akaniambia mimi nitoke na kuwaacha wenyewe ili aweze kumtibu. Kweli nilitoka na kurudi sebuleni.

    Wakakaa humo ndani kwa zaidi ya dakika kumi na tano, baadaye nilimuona Ibra akitoka, nyuma yake akifuatiwa na yule mganga, akatutoa mpaka nje kisha tukaagana na kutukaribisha tena.

    Tuliondoka mpaka kwenye gari, Ibra akiwa kimya kabisa. Tuliingia, akawasha gari na taratibu tukaianza safari ya kurudi nyumbani kwani muda ulikuwa umeenda sana. Nilikuwa na shauku kubwa ya kutaka kujua kama Ibra wangu ametibiwa, akanitoa wasiwasi na kuniambia kuwa ametibiwa vizuri na mganga huyo amemuahidi kuwa kila kitu kitakuwa safi.

    “Amenichanja chale na kunipa dawa za kunywa na kufukiza, amesema baada ya siku tatu mambo yatakuwa mazuri,” Ibra alisema huku tukikatiza mitaa ya Kariakoo kurudi nyumbani. Nilifurahi sana kusikia hivyo, nikawa na matumaini kwamba Ibra wangu naye atakuwa imara kama wanaume wengine.

    Ibra alinirudisha mpaka jirani kabisa na nyumbani, tukaagana kisha nikashuka na kuanza kutembea taratibu kuelekea nyumbani tukiwa tumekubaliana kwamba usiku tutazungumza zaidi kwenye simu.

    Aligeuza gari lake na kuondoka kuelekea nyumbani kwake, Mikocheni na mimi nilielekea nyumbani kwetu. Baada ya kupumzika kidogo, baadaye tulikula chakula cha jioni kisha nikaenda kujifungia chumbani kwangu kama kawaida yangu kisha nikachukua simu na kumpigia Ibra.

    Tulizungumza mambo mengi usiku huo mpaka ilipofika saa sita za usiku. Tukaagana kisha nikalala mpaka kesho yake. Asubuhi Ibra alinipitia tena, akanipeleka mpaka chuoni kisha na yeye akaendelea na shughuli zake. Siku hiyo ilipita, ikaja siku nyingine, nayo ikapita. Ibra akawa ameshamaliza dozi aliyopewa na yule mganga wa kienyeji.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kama tulivyokuwa tumekubaliana kwamba akimaliza dozi niende nyumbani kwake tukajaribu tena kwa mara nyingine, siku hiyo nilidanganya tena nyumbani kwamba naenda chuoni wakati ukweli ni kwamba nilikuwa naenda kwa Ibra. Akaja kunichukua na safari ya kuelekea nyumbani kwake ikaanza huku nikiwa na shauku kubwa ya kukatwa kiu yangu na Ibra.

    Kwa kuwa naye alidanganya kazini kwao kwamba anaumwa, tulikubaliana kushinda pamoja siku hiyo kutwa nzima. Tulipofika nyumbani kwake, tulishuka kwenye gari kisha tukaingia ndani. Kwa jinsi nilivyokuwa na shauku, sikutaka kupoteza muda, nikamshika mkono na kumvutia chumbani.



    Nikaanza mwenyewe kusaula viwalo vyangu, kimoja baada ya kingine, mpaka nikabakia na nguo ya mwisho.

    Nilimgeukia na yeye na kuanza kumfanya kama nilivyojifanya, nikaanza na shati lake ambalo nililifungua vifungo kwa pupa, nikalitupa kwenye zulia la manyoya, nikahamia kwenye suruali na muda mfupi baadaye, na yeye alibakia na nguo moja tu.

    Tukakokotana hadi kitandani huku kiu ikizidi kunibana, nikamalizia ile moja iliyobaki na yeye nikamfanya hivyohivyo, tukawa saresare maua.

    Mtoto wa kike nikaanza mbwembwe za kumpasha moto huku na yeye akinionesha ushirikiano tofauti na awali, tukaendelea kupasha misuli moto kwa dakika kadhaa huku hali yangu ikizidi kuwa mbaya.

    Ilifika hatua nikawa nimelegea kama nimekunywa mlenda, hakuna nilichokuwa nakitaka kwa wakati huo isipokuwa kitu kimoja tu, ‘muhogo wa Jang’ombe’. Nikajiweka mkao wa shughuli na kumvutia kwangu lakini cha ajabu, ‘Ibra’ wake alikuwa amenywea kama piriton, akionesha kutokuwa tayari kwa kile nilichokuwa nakisubiria.

    “Ibra jamani, vipi tena? Ina maana dawa za mganga hazijasaidia?” nilihoji huku nikionesha kukasirika kwa sababu kama ni mateso, haya niliyokuwa nayapata mimi yalikuwa yamepitiliza.

    Maskini Ibra, hakuwa na cha kujibu zaidi ya kuendelea kujikakamua ili angalau gari lake lipige starter na kuwaka lakini wapi! Mtalimbo wake ulikuwa umelala doro. Niliendelea kumchokoza kwa kila mbinu kwani mwenzake nilikuw ana hali mbaya lakini bado ilikuwa ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa.

    Kwa hasira nilimsukuma kutoka mwilini mwangu na kuinuka kitandani, nikatembea nikiwa vilevile mpaka bafuni ambako nilijifungia na kuegamia ukutani, machozi yakaanza kunitoka kutokana na maumivu niliyokuwa nayasikia.

    Ibra naye aliinuka na kujaribu kunifuata lakini kwa sababu nilikuwa nimeufunga mlango kwa ndani, alishindwa kuingia zaidi ya kuendelea kuniita huku akilitaja jina langu na kunisihi nipunguze hasira lakini haikusaidia kitu.

    Niliendelea kulia kwa uchungu mpaka hasira zangu zilipoisha, nikaingia kwenye jakuzi nakukaa kwenye maji ya uvuguvugu ambayo kwa kiasi kikubwa yalinisaidia kuwatuliza wadudu waliokuwa wananinyevuanyevua kisawasawa.

    Unajua kitu ambacho wanaume wengi hawakijui ni kwamba, sisi wanawake ni wagumu sana kupandwa na hisia za kimapenzi lakini zinapopanda, huwa tunahitaji kitu kimoja tu, kukidhi haja zetu kikamilifu.

    Inapotokea kinyume na hapo, mumeo au mtu wako akashinda kukidhi haja, iwe kwa kushindwa kabisa kama ilivyokuwa inatokea kwa Ibra au kwa kufanya chini ya kiwango, huwa tunawachukia sana wanaume husika.

    Usishangae kusikia mwanamke ameolewa lakini anapoteza kabisa hamu ya kukutanana mumewe, muda mwingine wanakaa hadi wiki au wiki mbili bila kukutana, visingizio vikiwa lukuki! Hiyo yote ni sababu ya wanaume kushindwa kukidhi haja zao kikamilifu.

    Ushauri wa bure, kama wewe ni mwanaume na unataka kudumu kwenye ndoa au uhusiano na mwanamke umpendaye, hata kama wewe ni maskini wa kutupwa, jitahidi sana kuwa imara kwenye idara hii.

    Nayasema haya kwa sababu kuanzia mwanzo niliwaambia kwamba nataka yaliyonitokea mimi yawe funzo kwa watu aote waliopo kwenye uhusiano. Najihisi aibu kubwa kuyasimulia haya lakini kwa sababu nataka kuwasaidia wengine, ndiyo maana nimejitoa fahamu na kumwaga mchele.

    Basi niliendelea kukaa kwenye jakuzi mpaka akili yangu ilipotulia kabisa, nikatoka na kurudi hadi kitandani ambapo nilimkuta Ibra amejiinamia, macho yake yakiwa yamebadilika kabisa rangi na kuwa mekundu! Maskini, kumbe naye alikuwa akilia kwa muda wote ule niliokuwa nimejifungia bafuni.

    Nilimsogelea kwa upole na kumkumbatia, nikaliachia taulo nililokuwa nimejifunga na kuanza kumbembeleza Ibra kwani ama kwa hakika alitia huruma.

    Nilimwambia kama dawa za yulemganga wa kwanza zimeshindwa kabisa kumsaidia, nitajitahidi kumtafuta mganga mwingine, ikibidi hata kwa Wamasai nitampeleka ilimradi kumaliza tatizo hilo lililokuwa linamsumbua.

    Niiliona nuru mpya ikianza kuchomoza kwenye sura yake, akanikumbatia na kunishukuru kwa jinsi nilivyokuw anamfariji. Tuliendelea kukaa pamoja lakini kila nilipojaribu mambo, hakukuwa na dalili zozote, mpaka nikahisi dawa za yule mganga zimemmaliza kabisa nguvu zake, hata zile kidogo alizokuwa nazo.

    Nikiwa nawaza hayo, kwa mbali nilianza kuhisi Ibra anakujakuja, nikaendelea kumfanyia vituko na hatimaye, jogoo wake akawika kuashiria mapambazuko. Nikafurahi mno na bila kupoteza muda, nikamvutia kwangu.Nikaendelea kumpasha joto huku nikiwa na hamu kubwa ya kuingia mchezoni, sijui kulitokea nini tena kwenye kichwa cha Ibra kwani wakati nikijiandaa kuingiza kisu kwenye ala yake, alinywea na kuwa kama alivyokuwa mwanzo. Niliendelea kujaribu kila mbinu lakini wapi!

    Sikutaka kusema chochote, nikajilaza pembeni na kuendelea kuwaza mambo mbalimbali kwenye kichwa changu kuhusu hatma yangu na Ibra. Na yeye aliendelea kuhangaika akijaribu kila mbinu lakini haikusaidia kitu, baadaye na yeye akatulia.

    “Flaviana.”

    “Abee!”

    “Niahidi kama hutanikimbia kutokana na haya matatizo yanayonitokea.”

    “Usijali Ibra wangu, mimi ndiyo mkeo, nitakuwa na wewe siku zote za maisha yangu,” nilimwambia kwa sauti iliyokuwa inatokea puani, nikambusu kwa mahaba naye akafanya hivyohivyo. Tuliendelea kuzungumza mambo mbalimbali huku akinieleza kwamba tayari alishawaambia wazazi wake kwamba amepata mchumba.

    “Hivi sasa wanashughulikia mambo ya washenga kwa ajili ya kuja kuleta barua nyumbani kwenu.”

    “Kweliii! Ooh! Jamani Ibra wangu, kumbe unanipenda kiasi hicho,” niliinuka kwa furaha na kumkumbatia tena Ibra, nikamwagia mvua ya mabusu huku machozi ya furaha yakinitoka.

    Ukweli ni kwamba mwenzenu nilikuwa nampenda sana Ibra licha ya matatizo aliyokuwa nayo na nilishajiapiza kuwa hata iweje, lazima anioe niwe mke wake halali. Kwangu hiyo ilikuwa ni habari njema mno, nikamkumbatia tena na tena na kuendelea kumwagia mabusu motomoto.

    Baada ya kukaa sana kwake, hatimaye muda wa kuondoka uliwadia, akiwa hajanigusa kabisa. Afadhali hata siku nyingine alikuwa anajitahidi kwa sekunde chache lakini siku hiyo alishindwa kabisa. Hata hivyo sikujali sana, akili zangu zote nikawa nimezielekeza siku washenga wake watakapokuja nyumbani kuleta barua ya posa.

    Kama kawaida, Ibra alinisindikiza mpaka nyumbani huku akiendelea kusisitiza kuwa nisimuache kutokana na matatizo aliyokuwa nayo. Nikamhakikishia kwamba asiwe na wasiwasi mimi ni wake. Alinipeleka mpaka nyumbani, tukaagana kisha nikashuka na kuanza kutembea kwa maringo kuelekea nyumbani huku na yeye akigeuza gari lake na kuondoka.

    “Mh! Mbona una furaha sana mwenzetu,” mama aliniuliza nilipomsalimia kwani kiukweli nilikuwa na furaha mno kiasi kwamba sikuweza kuificha.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nina habari njema nitakwambia baadaye,” nilimwambia mama na kupitiliza moja kwa moja mpaka chumbani kwangu. Nikajitupa kitandani na kuanza kufikiria siku Ibra atakaponioa. Nilijiona mwenye bahati kubwa sana kwani ukiachilia mbali kazi nzuri aliyokuwa anaifanya, Ibra alikuwa amejikamilisha sana kimaisha.

    Nilikaa chumbani kwangu kwa muda mrefu mpaka baadaye niliposhtuka baada ya kusikia mlango ukigongwa. Alikuwa ni mama ambaye shauku ya kutaka kujua kilichokuwa kinanifurahisha siku hiyo ilikuwa imemzidi kiasi cha kushindwa kusubiri, akanifuata na kuniuliza tena.

    “Nimepata mchumba mama na siku chache baadaye atakuja kuleta barua ya posa,” nilimwambia mama, taarifa ambayo hata yeye ilimfurahisha sana, tukakumbatiana kwa furaha kisha akaanza kunipa mawaidha mawili matatu jinsi ya kujitunza na kujiheshimu katika kipindi hicho cha uchumba nilichokuwa nataka kuingia.

    “Mmewahi kukutana kimwili?” mama aliniuliza swali ambalo sikulitegemea, nikawa nababaika nikishindwa nimjibu nini.



    Baadaye nilipiga moyo konde na kuamua kumdanganya, nikamwambia kwamba sijawahi kukutana naye kimwili kwa sababu tumekubaliana kwamba tusifanye chochote mpaka siku tutakayofunga ndoa.

    “Kumbe una akili mwanangu, wanaume wengi siku hizi huwa wanatumia kigezo cha kutangaza ndoa kama njia ya kuwarubuni mabinti wadogo kama wewe, wakishawatumia kimwili mipango ya ndoa inayeyuka na huo ndiyo unakuwa mwisho wa kila kitu,” mama alisema huku akinipigapiga begani kama ishara ya kunipongeza.

    Hakuwa akijua kwamba mila za zamani walizokulia wao zilikuwa tofauti sana na maisha ya sasa kwamba mwanaume na mwanamke hamuwezi kukutana, kuchumbiana na hatimaye kuoana bila kuwa mmekutana kimwili kwanza.

    Najua wazazi wengi watashangaa kusikia kauli hii lakini wasichana wenzangu au wanawake wa rika la kati watakuwa wananielewa vizuri sana. Siyo wote lakini asilimia kubwa ya wanandoa wanaooana siku hizi, wanakuwa tayari wameshavunja sana amri ya sita.

    Kama hiyo haitoshi, wengine wanafikia hatua ya kuoana wakiwa wameshapeana ujauzito, mimi na wewe tunaweza kuwa mashahidi wa hilo kwani maisha yamebadilika mno. Mazingira waliyokulia wazazi wetu ni tofauti kabisa na haya ya sasa.

    Tuliendelea kuzungumza mambo mbalimbali na mama, akawa ananiasa namna ya kuishi nikiwa mchumba wa mtu, akaniasa kumheshimu, kumsikiliza na kumpenda mume wangu pindi nitakapokuwa nimeshaolewa. Pia akanisisitiza kwamba uvumilivu ni silaha kubwa sana ndani ya ndoa ambayo inaweza kufanya watu wakadumu kwenye ndoa kwa maisha yao yote.

    “Usifikiri labda mimi baba yako huwa haniudhi, ananiudhi sana kiasi cha wakati mwingine kutamani anipe talaka lakini kwa sababu nilifundishwa uvumilivu, ndiyo maana mpaka leo hii unaona bado nipo naye mpaka nyie mmekuwa wakubwa na sasa wewe unakwenda kuanzisha familia yako.”

    “Kuna usemi kwamba mwanamke mpumbavu huivunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe, mimi sikukulea wewe kuwa mpumbavu wala mjinga, naamini utakuwa mwanamke bora, mwenye busara, mvumilivu na mwenye mapenzi ya dhati kwa mumeo,” mama aliniambia kwa msisitizo, nikawa natingisha kichwa kuonesha kwamba aliyokuwa anayasema yalikuwa yakiniingia ndani ya kichwa changu.

    Japokuwa kwa wakati huo sikuwa natilia sana maanani yale aliyokuwa ananiambia, lakini kiukweli najuta sana kwa nini sikumuelewa na kuyafanyia kazi aliyokuwa akiniusia kwani huenda yangekuwa msaada mkubwa wa kuinusuru ndoa yangu. Sitaki kuelezea sana hayo ya mbele kwani muda wake bado haujafika.

    Basi mama aliendelea kuniusia pale kwa muda mrefu, akaniambia hata baba akisikia habari hizo njema atafurahi sana. Baadaye mama alitoka na kuniacha nipumzike. Raha iliyokuwa ndani ya moyo wangu ilikuwa kubwa sana kwani nilijiona ni mwenye bahati ya kipekee kuolewa na mtu mwenye uwezo mkubwa kipesa kama Ibra.

    Siku hiyo ilipita, kesho yake Ibra akanipitia kama kawaida na kunipeleka mpaka chuoni, tukaachana ambapo mimi niliingia chuoni na yeye akaelekea kazini kwake kama kawaida.

    Maisha yalizidi kusonga mbele, baba yangu akapewa taarifa juu ya mimi kupata mchumba na taratibu za kuja kutoa posa zikaendelea kama kawaida. Bado tatizo la Ibra lilikuwa palepale kwani niliendelea kuenda nyumbani kwake mara kadhaa lakini bado alikuwa akishindwa kabisa ‘kunishughulikia’.

    Uamuzi ambao tuliufikia kwa pamoja ni kwamba tushughulikie kwanza mambo ya kuvalishana pete ya uchumba kisha baada ya hapo ndiyo tutaendelea kulishughulikia tatizo lake la upungufu wa nguvu za kiume.

    Siku zilizidi kuyoyoma, kweli kama alivyokuwa ameahidi Ibra wangu, wiki tatu baadaye, washenga walikuja kuleta barua ya posa nyumbani kwetu. Naikumbuka vizuri siku hiyo na kamwe sitakuja kuisahau maishani.

    Baada ya kuleta posa, waliambiwa wafuate majibu baada ya wiki moja. Walipoondoka, niliitwa na wazazi wangu, wakaniuliza kama nimekubali kuolewa na Ibra, nikawajibu kuwa nampenda sana na nimekubali mwenyewe kwa hiyari yangu, kauli ambayo iliwafurahisha sana.

    Siku chache baadaye, ndugu zetu kutoka upande wa mama na baba waliitwa pale nyumbani, kikao cha ukoo kikafanyika ambapo kama zilivyo mila za kwetu, barua ilifunguliwa mbele ya ndugu wote, ikasomwa kisha nikaitwa kwa mara nyingine na kuulizwa mbele yao kama nimekubali kuolewa na Ibra, nikawajibu vilevile.

    Kweli siku kadhaa baadaye, wale washenga walifuata majibu ya barua yao ambapo walijibiwa kwamba nimekubali kuolewa na Ibra, wakaondoka wakiwa na furaha kubwa. Wiki mbili baadaye, Ibra aliandaa sherehe ndogo lakini ya kifahari mno ya kuvalishana pete.

    Nikavalishwa pete ya dhahabu ya uchumba na mipango ya ndoa ikaanza kupangwa harakaharaka. Mapenzi yangu kwa Ibra yalizidi maradufu kutokana na jinsi alivyokuwa mkweli kwangu lakini bado tatizo moja kubwa lilibaki palepale, Ibra hakuwa na uwezo wa kunifurahisha na kukidhi haja zangu za kimapenzi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya kuvishana pete ya uchumba, kama tulivyokuwa tumekubaliana na Ibra, kweli tulianza kuhangaika tena kushughulikia tatizo lake. Kwa kuwa awamu ile ya kwanza tulienda kwa mganga wa kienyeji na ikashindikana, safari hii tulikubaliana kwenda kujaribu hospitalini.

    Kitu ambacho nilikigundua ni kwamba Ibra alikuwa anaona aibu sana kujieleza kuhusu tatizo lake. Kwa jinsi nilivyomuona, kama isingekuwa mipango ya ndoa au kukutana na mimi na kuanzisha uhusiano wa kimapenzi, huenda suala hilo lingebaki kuwa siri ya ndani ya moyo wake.

    Tulipanga appointment na daktari kwenye Hospitali ya Aga Khan ambako familia yao ilikuwa ikitibiwa, siku ilipowadia tukaenda kuonana na daktari mmoja mwenye asili ya Kihindi. Ibra akajieleza tatizo lake japo kwa aibuaibu, daktari huyo akampima kisha tukatoka nje kusubiri majibu.

    Baadaye alituita kuchukua majibu, akatueleza kuwa katika uchunguzi aliomfanyia Ibra, hakugundua kama ana tatizo lolote kwa ndani kwani kila kitu kilikuwa safi, mbegu zake za kiume zilikuwa na uwezo wa kutungisha mimba vizuri lakini tatizo lilikuwa kwenye nguvu.

    Daktari alituelekeza kuwa huenda tatizo la mume wangu mtarajiwa linasababishwa na msongo wa mawazo, hofu au kushindwa kujiamini kwani kama kungekuwa na tatizo lingine, vipimo vingeonesha. Akatushauri tukakutane na daktari mwingine hapohapo hospitali ambaye alikuwa na uwezo mkubwa wa kuwashauri watu wenye matatizo ya kisaikolojia.

    Pia alimpa mume wangu vidonge fulani ambavyo alimwambia avitumie kwa muda wa wiki moja, sambamba na ushauri wa kisaikolojia. Kweli baada ya hapo tulienda kukutana na huyo mshauri wa watu wenye matatizo ya kisaikolojia. Awali tuliingia wote mimi na Ibra lakini nikaambiwe mimi nikamsubiri nje ili daktari apate muda wa kuzungumza naye kwa kina. Sijui walizungumza nini kwani Ibra alipotoka hakunisimulia yote zaidi ya kunieleza kuwa amempa mbinu nyingi za kupambana na tatizo lililokuwa linamsumbua.

    Tulirudi mpaka nyumbani kwa Ibra, tukakaa pamoja mpaka baadaye ambapo mimi nilitoka na kurudi zangu nyumbani. Mama alikasirika sana siku hiyo kwa sababu wakati naondoka, kwanza sikumuaga na pia nilikuwa nimevunja makubaliano yetu ya kutotoka nje mpaka nitakapoolewa.

    Nilimuomba mama radhi kwani hata mimi nililiona kosa langu lakini kwa sababu nilichokuwa nakihangaikia kilikuwa muhimu zaidi kuliko hata hiyo ndoa yenyewe, sikuwa na jinsi. Kuanzia hapo ikawa hata chuoni siendi tena, nikaombewa ruhusa kwa ajili ya maandalizi ya ndoa yangu.

    Kama ilivyo kawaida yetu, niliwekwa ndani mtoto wa kike na kuanza kufundishwa mbinu mbalimbali za kuishi na mume, huku mwili wangu ukikandwa na kupakwa vipodozi mbalimbali vya kulainisha ngozi na kunifanya nibadilike sana.

    Hata hivyo, mawasiliano na Ibra yalizidi kunoga, ikawa mara kwa mara tunapigiana simu na kuzungumza mambo mbalimbali. Akaniambia kuwa zile dawa alizopewa hospitali pamoja na ule ushauri wa kisaikolojia vimemsaidia sana kumaliza tatizo lake.

    Akanihakikishia kwamba mambo yameanza kuwa mazuri kwani kila akikaa na kunifikiria, hutokewa na hali ambayo mwanzo haikuwepo. Akaniambia kuwa hata asubuhi akitoka kuamka, mambo huwa mazuri pia. Akanihakikishia kuwa siku tutakayooana, nitafaidi sana. Kauli hiyo ilinifurahisha sana, mipango ya ndoa ikazidi kupamba moto.

    Ndugu kutoka sehemu mbalimbali wakaanza kuwasili nyumbani kwa ajili ya kushuhudia jinsi nitakavyoolewa. Kamati ya harusi ambayo kwa upande mkubwa ilikuwa ikisimamiwa na upande wa mchumba wangu, nayo ilizidi kufanikisha mambo yake, vitu vingi vikakamilika na kilichokuwa kinasubiriwa kikawa ni jambo moja tu, siku ya ndoa.

    Hatimaye siku hiyo iliwadia, tukafungishwa ndoa ya kidini na Ibra, tukaapa madhabahuni kwamba tutakuwa pamoja kwenye shida na raha mpaka kifo kitakapotutenganisha. Kusema ukweli, mwenzenu niliolewa kwa ndoa ya kifahari sana, kuanzia gauni nililokuwa nimevaa, mapambo yangu, gari lililonipeleka saluni na kunirudisha, vyote vilikuwa vya kifahari sana.

    Yote tisa, kumi ni huo ukumbi uliotumika siku hiyo. Ni pale Mlimani City kwenye ukumbi wa sherehe. Ndani kulipambwa kisawasawa, mimi na mume wangu Ibra tulipendeza mno, ungeweza kusema ni watoto wa mfalme. Wazazi wake walihakikisha mtoto wao anafunga ndoa ya kifahari sana ukichanganya na wafanyakazi wenzake ambao nao walijitoa kwelikweli.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Yaani kama ingekuwa ufahari wa ndoa unayofunga ndiyo raha ambazo utakuwa unazipata ndani ya ndoa hiyo, mwenzenu ningekuwa wa kwanza kwa kupata raha. Baada ya taratibu zote za kanisani na ukumbini kumalizika, saa sita za usiku tulitoka ukumbini na safari ya kuelekea Zanzibar kula fungate letu ilianza usiku huohuo.

    Kwa kuwa tayari kulikuwa na boti iliyokodiwa kwa ajili ya kazi hiyo ikitusubiri, tulipofika tu bandarini usiku huohuo tulipasua maji mpaka Zanzibar kwenye hoteli ya kitalii ya Spice Garden and Beach Resort.

    Furaha niliyokuwa nayo siku hiyo haielezeki, yaani nafikiri miongoni mwa matukio ambayo yamewahi kuufurahisha sana moyo wangu, hilo la ndoa yangu ni kubwa zaidi. Tuliingia mpaka kwenye vyumba maalum tulivyokuwa tumeandaliwa, wapambe wetu nao wakaenda kwenye chumba chao na hatimaye tukabaki wawili tu, mimi na Ibra wangu.

    “Siamini Ibra wangu, siamini kama leo nimekuwa mkeo wa ndoa,” nilisema huku nikiwa nimejilaza kwenye kifua chake, machozi ya furaha yakinitoka. Tukavua nguo zetu za harusi na kwenda kuogeshana bafuni, hatimaye tukarudi chumbani na ule muda niliokuwa nausubiria kwa hamu wa kumpa Ibra haki yake aliyostahili kama mume wangu halali uliwadia.



    Kama kawaida yangu, nikaanza utundu wa kumuandaa Ibra wangu kwa ajili ya kumpa haki yake aliyoilipia mahari na kuigharamia kwa kiwango kikubwa. Siku hiyo angalau Ibra wangu naye alionesha ushirikiano ambao kwa kipindi kirefu nilikuwa nimeukosa.

    Kadiri nilivyokuwa namuandaa, ndivyo naye alivyokuwa anaonesha ushirikiano kwa kuniandaa pia, mtoto wa kike nikapagawa kwelikweli, maji yakawa yanachemka vya kutosha na kilichokuwa kimebakia ilikuwa ni kutia mchele tu ili mapishi yaendelee.

    Kweli Ibra alifanya kama vile nilivyomtegemea kufanya, jambo ambalo lilinifanya nijisikie raha ya ajabu ndani ya moyo wangu, nikamganda kama ruba huku nikimuonesha ufundi wangu ambao sikuwahi kupata nafasi ya kumuonesha.

    Tofauti na siku zote, siku hiyo Ibra wangu aliweza kupiga kasia kwa dakika nne bila kuchoka, tena ‘Ibra’ wake akiwa ngangari kuliko kawaida, nikajisikia raha ya ajabu ambayo sikuwahi kuihisi hata mara moja tangu nikutane na Ibra.

    Muda mfupi baadaye, Ibra akanitangazia kufika mwisho wa safari yake, nikampokea vizuri na kumtuliza, mkaka wa watu akapiga ukelele wa ajabu kama anayetaka kukata roho kisha akatulia tuli.

    “Ahsante mpenzi wangu, ahsante sana Ibra wangu,” nilimwambia kwa sauti iliyokuwa ikitokea puani huku nikimwagia mvua ya mabusu. Japokuwa sikuwa nimefika hata robo ya safari yangu, nilifurahi sana kwani angalau siku hiyo Ibra alinionjesha ladha ya ulimwengu wa ndoa.

    Kutokana na jinsi alivyokuwa amechoka, ilibidi nimuinue pale kitandani na kumkokota mpaka bafuni, nikafungulia maji na kwa pamoja tukaanza kuoga. Angalau baada ya kulowanishwa na maji, Ibra alipata nguvu kidogo. Tulipomaliza tulirudi kitandani, nikawa na matumaini makubwa kwamba baada ya kupumzika kidogo, Ibra atajikakamua tena kwa mara nyingine.

    Hata hivyo mawazo yangu hayakuwa sahihi kwani muda mfupi baadaye, Ibra alipitiwa na usingizi mzito na kuanza kukoroma, akaniacha nahangaika mwenyewe. Niliamua kumsamehe kwani angalau siku hiyo alifanya kazi ambayo kidogo niliielewa. Kutokana na uchovu wa pilikapilika za ndoa yetu, muda mfupi baadaye na mimi nilipitiwa na usingizi.

    Tulikuja kuzinduka kesho yake asubuhi, tukakumbatiana na Ibra ambaye naye alionekana kushangaa iweje apitiwe na usingizi mzito namna ile na kuniacha mimi mkewe nikiwa bado nipo macho.

    Kwa kuwa daktari alisema kwamba huenda matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume ya Ibra ambaye sasa alikuwa ni mume wangu wa ndoa yalikuwa yakisababishwa na kuathirika kisaikolojia, niliamua kumpa moyo mume wangu ili na yeye ajisikie kuwa mwanaume aliyekamilika.

    “Ahsante sana mume wangu, jana ulinikata kiu yangu kabisa. Yaani tangu nianze kupata akili za kikubwa, hakuna siku niliyofurahishwa kimapenzi kama jana,” nilimdanganya Ibra na kumbusu sehemu mbalimbali za mwili wake, nikamuona akifurahi kuliko kawaida.

    Muda mfupi baadaye, tulianza tena kujiandaa kwa ajili ya penzi la kifungua kinywa, kama ilivyokuwa usiku, Ibra alinionesha ushirikiano wa kutosha kwani gari lake lilipiga starter kwa urahisi na hata muda wa kuanza safari ulipowadia, sikupata shida.

    Tukaelea kwenye ulimwengu wa mahaba huku Ibra akipiga kasia kwa nguvu kama usiku, dakika tatu baadaye chombo kikawa kimefika pwani. Kwa mara nyingine Ibra alinifurahisha sana kwani angalau alikuwa anaonesha uhai.

    Unajua jambo ambalo wanawake wenzangu wanapaswa kulifahamu ni kwamba, kama mumeo au mwenzi wako anakumbwa na matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume, hakuna sumu mbaya kama kumlaumu au kunung’unika.

    Ukishaanza kumlaumu tu kwamba hajakufikisha popote, uwezekano mkubwa ni kwamba mara ya pili atashindwa kabisa. Ni bora hata kama amechemka kabisa, umpe moyo na kumsifia kwamba ameweza kukidhi haja zako. Ukifanya hivyo, utamjengea uwezo wa kujiamini na mkirudia tena, atajitahidi zaidi na zaidi. Wanaume watakuwa mashahidi wa jambo hili kwamba wakisemwa vibaya au kuoneshwa dharau ya aina yoyote kunako uwanja wa kikubwa, hukosa kabisa kujiamini na matokeo yake, hata zile nguvu kidogo walizokuwa nazo, hupotea kabisa.

    Basi siku ya kwanza ilipita vizuri, mimi na mume wangu Ibra tukiendelea kufurahia fungate, ikaja siku ya pili, ya tatu na hatimaye wiki nzima ikaisha. Kwa kuwa tulikuwa tumepanga kukaa wiki moja tu, tulijiandaa tayari kwa kurudi jijini Dar es Salaam kuendelea na maisha ya mume na mke.

    Ndani ya wiki hiyo moja tuliyokaa fungate, angalau Ibra alikuwa akiendelea kujitahidi kuonesha uanaume wake japokuwa ilikuwa ni kwa kiwango cha chini mno kwani hakuna hata mara moja aliyoweza kulisakata kabumbu kwa zaidi ya dakika tano. Alipojitahidi sana alikuwa akiishia dakika nne au tatu na hakuwa na uwezo wa kurudia tena mpaka baada ya saa nyingi kupita.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hatimaye tulikabidhi chumba katika hoteli ya kitalii ya Spice Garden and Beach Resort tuliyokuwa tukilia fungate letu kisha tukaianza safari ya kutoka Zanzibar kurejea Dar es Salaam.

    Safari hii tulikuwa peke yetu kwani wapambe wetu waliondoka siku ya pili wakiwa na baadhi ya mizigo yetu. Tulikubaliana kupanda boti ya kawaida tu pamoja na abiria wengine.

    Tukasafiri mpaka jijini Dar es Salaam ambapo tulipokewa bandarini na ndugu na marafiki wa Ibra waliotupeleka moja kwa moja mpaka nyumbani kwa Ibra, Mikocheni jijini Dar es Salaam ambako ndiko tulikotakiwa kuyaanza maisha mapya. Hatimaye tukawa tumeyaanza maisha mapya tukiwa mume na mke huku Ibra wangu akiwa bado anasuasua katika suala zima la kunitimizia haki yangu ya ndoa.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog