Simulizi : Penzi Bila Maumivu
Sehemu Ya Tatu (3)
Uwezo wa Dk. Buffet ulikuwa mkubwa mno, alipoliangalia tatizo la Tatiana, alijua kwamba kulikuwa na mishipa kadhaa ambayo ilikuwa imelegea hivyo kuanza kazi ya kuirudisha katika hali yake ya kawaida.
Ilikuwa kazi kubwa lakini hakutaka kulala kwa kipindi kirefu kama zamani, kitu pekee alichokuwa akishughulika nacho kwa kipindi hicho ni mgonjwa huyo aliyekuwa ameletwa hospitalini kwake.
Magazeti na vyombo vingine vya habari viliendelea kuripoti kila hatua aliyokuwa akipitia Tatiana, kila mtu alitamani kuona msichana huyo akipata nguvu ya kuona ili ajue ni kwa jinsi gani ulimwengu ulikuwa ukiendelea.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya matibabu kufanyika kwa mwezi mzima, hatimaye Tatiana akaanza kuona vivulivivuli. Mtu alipokuwa akipita mbele yake, hakuwa akimuona vizuri kitu kilichomfanya kuhisi kwamba alikuwa akienda kupona.
“Vipi?” aliuliza Dk. Buffet.
“Naona vivulivivuli,” alijibu.
“Haya ni maendeleo makubwa sana, amini kwamba utakwenda kupona kabisa,” alisema Dk. Buffet.
Maendeleo yake yalimfurahisha kila mmoja, baada ya wiki mbili kukatika, Tatiana akafanikiwa kuona kabisa, upofu aliokuwa nao tangu alipozaliwa, ukakoma na mishipa yake kukaza na kuwa kama mtu ambaye hakuwahi kuumwa macho maishani mwake.
“Dokta! Naona,” alisema Tatiana huku akionekana kutokuamini.
“Unasemaje?”
“Naona dokta! Naona,” alisema Tatiana.
“Hebu subiri, hivi vidole vingapi?” aliuliza Dr. Buffet.
“Vinne.”
“Na hivi?”
“Viwili, naona dokta,” alisema Tatiana huku akipiga kelele kwa furaha.
Hiyo ilikuwa taarifa njema kwa kila mtu, hakukuwa na aliyekuwa akiamini kile kilichokuwa kimetokea, hapohapo alichokifanya Dk. Buffet ni kuchukua simu yake na kumpigia Smith akimtaka afike hospitalini hapo kwani mpenzi wake alifanikiwa kupona ugonjwa ule.
“Nakuja,” alisikika Smith na kukata simu.
Tatiana hakulala tena, akasimama na kuanza kuzunguka chumbani mule, kila alichokuwa akikifanya, madaktari walikuwa wakimwangalia, huku nyuso zao zikiwa na furaha tele, hawakuamini kama msichana huyo alifanikiwa kuona kama watu wengine.
Kila wakati Tatiana alikuwa akimshukuru Mungu kwa kumpa uwezo wa kuona. Kuna wakati alikuwa akirukaruka kwa furaha, wakati mwingine alikuwa akikimbia humohumo chumbani, yaani vyote hivyo alikuwa akivifanya huku akiwa kwenye furaha tele.
Ndani ya nusu saa tu Smith akafika hospitalini hapo, moyo wake ulikuwa na furaha tele, hakuamini kile alichokuwa amekisikia kwamba mpenzi wake alikuwa amepona na kuona kama kawaida.
“Nimekuja...”
“Kufanya nini?”
“Kumuona mpenzi wangu! Kumbe amepona,” alisema Smith, alikuwa akizungumza na dada wa mapokezi.
“Karibu sana,” alisema dada yule kwani alichokijua ni kwamba mtu pekee aliyeuwa akifanyiwa matibabu ya macho alikuwa Tatiana tu. Hapohapo akaelekezwa chumba alichokuwemo muda huo kwani kile chumba cha siku zote alikuwa amehamishiwa na kupelekwa kwingine.
Smith hakutaka kutembea kwa mwendo wa taratibu, alikuwa akitembea kwa kasi kubwa kuelekea katika chumba hicho, msichana ambaye alikuwa amepewa kwa ajili ya kumpeleka chumbani huko alikuwa amemuacha nyuma kana kwamba yeye ndiye alikuwa akimpeleka msichana huyo.
“Ni huku,” alisema msichana huyo mara baada ya kuona Smith ameelekea njia nyingine.
“Tangulia wewe basi, tena kwa mwendo wa kasi kidogo,” alisema Smith na dada yule kufanya hivyo.
Walipofika ndani ya chumba hicho, Smith hakuamini kumuona mpenzi wake akitembeatembea chumbani mule huku wakati mwingine akiviruka vyombo vya kuweka uchafu (dust bin) ili kuwaonyeshea watu wote kwamba alikuwa amepona.
“Tattie,” alimuita Tatiana huku akionekana kutokuamini.
“Smith...” aliita Tatiana huku akionekana kuanza kunywea, furaha kubwa aliyokuwa nayo ikaanza kupungua. Hivyohivyo, tena kwa kujivuta akaanza kumsogelea Smith na kisha kumkumbatia.
“Hatimaye umepona,” alisema Smith huku akiwa na furaha tele.
“Nashukuru kwa msaada wako Smith, nimepona,” alisema Tatiana.
Smith hakujisikia vizuri, alimfahamu Tatiana, hakuwa mtu wa kupenda kulita jina lake, kila alipokuwa akizungumza naye, alimuita jina la mpenzi, kitendo cha kuitwa Smith na kule kunywea kwa Tatiana kukaonekana kumtia mashaka makubwa.
Hakutaka kujiuliza sana, kwa kuwa lengolake la kila siku lilikuwa ni kumuona mpenzi wake huyo akipona, kwake ilikuwa ni furaha tu.
“Nashukuru sana Buffet, umekuwa msaada mkubwa kwangu,” alisema Smith huku akiachia tabasamu.
“Nashukuru sana. Hii ni kazi yangu, nafurahi sana kumuona Tatiana akiwa amepona,” alisema Buffet.
Tatiana hakutakiwa kuondoka siku hiyo, alihitajika kukaa kwa siku mbili kwani alitakiwa kufanyiwa baadhi ya mambo ili hali itengemae kabisa.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Taarifa zikaanza kusambaa kwamba Tatiana alikuwa amepona macho yake na alikuwa akiona kama kawaida. Hiyo ndiyo ikawa habari kwa kipindi hicho, taarifa hizo zilisambaa kwa kasi kubwa sana kiasi kwamba ndani ya nusu saa, kila mtu aliyekuwa akitumia mitandao ya kijamii alilifahamu hilo.
Nchini Tanzania, watu wengi walimshukuru Mungu kwa kuwapa mtu kama Tatiana ambaye aliipeperusha vilivyo bendera ya Tanzania na kuifanya nchi hiyo ijulikane zaidi.
“Amepona bwana...” alisikika jamaa mmoja.
“Ndiyo hivyo! Daah! Kweli Mungu mkubwa. Ila nao hawa Wazungu nuksi sana,” alisema jama mwingine.
Jina la Dk. Buffet likaanza kujulikana, kazi kubwa aliyokuwa ameifanya ilimfanya kupata sifa kubwa duniani kiasi kwamba kila mtu alisema kwamba hakukuwa na daktari aliyekuwa na uwezo mkubwa kama yeye.
Watu wengi hasa marafiki zake walikuwa wakimpigia simu Dk. Buffet na kumpa pongezi juu ya kile alichokuwa amekifanya. Kwake ilikuwa sifa kubwa, jina lake na hospitali hiyo vikatangazika sana kiasi kwamba wengi wakashauri kwamba apokee tuzo maalumu ya heshima kutokana na kile alichokuwa amekifanya jambo lililoungwa mkono na kila mtu.
*****
Mtu wa kwanza kabisa kumuona mbele yake alikuwa Dk. Buffet. Alivalia koti refu jeupe huku shingoni mwake akiwa ameipitisha mashine ya kusikilizia mapigo ya moyo. Kwa kumwangalia tu, alikuwa mwanaume mzuri wa sura ambaye kila alipokuwa akitabasamu, uzuri wake uliongezeka zaidi.
Tatiana alipomuona Dk. Buffet, akausikia moyo wake ukimripuka kwa furaha, hakuamini kama duniani kulikuwa na watu wenye sura nzuri kama alivyokuwa daktari huyo. Hapohapo, akauhisi moyo wake ukimuingiza daktari huyo na kumpenda kwa mapenzi ya dhati.
Hakujua Smith alionekanaje, hakujua sura yake ilikuwa vipi lakini kitu alichokuwa akikiamini ni kwamba mwanaume huyo hakuwa na sura nzuri kama aliyokuwa nayo Smith. Dk. Buffet alipokuwa akitabasamu, Tatiana alijiona kama anamwangalia malaika.
Kuna wakati alitamani kumvutia kwake, ambusu kwani hakukuwa na kitu alichokuwa na hamu kukifanya kwa daktari huyo kama hicho. Kila wakati alipokuwa akimwangalia, mapigo yake ya moyo yalikuwa yakimdunda tu huku akihisi damu yake ikizunguka kwa kasi kubwa mishipani mwake.
“Vipi?” aliuliza Dk. Buffet kwani hata macho aliyokuwa akimwangalia yalionekana tofauti.
“Poa, nafurahi kuona,” alisema Tatina kwa sauti iliyojaza mahaba tele, sauti ndogo ambayo hakutaka manesi waliokuwa chumbani humo kuisikia.
Huo ndiyo ulikuwa wakati wake wa kuangukia katika penzi la mtu mwingine kabisa ambaye hakuwa amemtegemea kabisa maishani mwake. Hata Smith alipokuja hospitalini hapo na kumwangalia, hakuvutiwa naye kama alivyokuwa Dk. Buffet ambaye kila alipokuwa akitabasamu tu, moyo wake ulikuwa hoi.
Siku hiyo ambayo alitakiwa kubaki hospitalini hapo alitaka kuitumia vilivyo, hakutaka kuona akiendelea kuteseka mapenzini na wakati mtu ambaye alimuweka katika hali hiyo alikuwa na uwezekano mkubwa wa kumpata.
Alichokifanya usiku alipokuwa kitandani akichati na Smith ni kumuomba nesi amuitie Dk. Buffet ambaye pasipo kuhisi chochote kile alifika haraka chumbani hapo.
“Naomba manesi watoke, kuna kitu nataka kukwambia,” alisema Tatiana kwa sauti ndogo, hilo halikuwa tatizo, Dk. Buffet akafanya hivyo na kubaki wawili chumbani.
“Naomba uniguse hapa,” alisema Tatiana, alitaka kuguswa kifuani upande wa moyo.
“Kuna nini?”
“Nahisi kuna kitu, hebu niguse,” alisema Tatiana huku akiushika mkono wa daktari huyo na kuupelaka kifuani mwake.
“Unahisi nini?” aliuliza dokta.
“Hebu shuka chini kdogo.
“Mmmh! Tatiana.”
“Naomba ushuke jamani, shuka kidogo,” alisema Tatiana kwa sauti ndogo, sauti iliyomfanya Dk. Buffet kujua kilichokuwa kikifuatia. Akafanya hivyo.
“Nahisi matiti yangu yanawasha sana,” alisema Tatiana.
“Kivipi?”
“Yaani kama kansa inanianza.”
“Kansa?”
“Ndiyo! Hebu jaribu kuyashikashika,” alisema Tatiana.
Lilikuwa jambo gumu lakini hakuwa na jinsi, kwa maneno ya Tatiana kwamba alihisi kuwa anaanza kuwa na ugonjwa wa kansa yakamtia wasiwasi kwa kuhisi kwamba ni kweli kwani dalili moja ya wanawake waliokuwa wakianza kuumwa kansa ya matiti, yalianza kuwasha.
Alichokifanya Tatiana ni kulala chali kitandani, akaivua blauzi yake na kuyaacha matiti wazi hali iliyomfanya Dk. Buffet apigwe na mshangao.
“Nitakufa dokta, naogopa sana kansa, naomba uyashikeshike,” alisema Tatiana huku akionekana kuzidiwa.
“Ngoja nikamuite dokta wa magonjwa ya wakinamama.”
“Hapana! Nataka uanze kuyashika wewe jamani, au unataka nife?”
“Hapana.”
“Basi yashike.”
Hakuwa na jinsi, kila alipokuwa akikiangalia kifua cha msichana yule, yeye mwenyewe alichanganyikiwa. Mbali na kifua hicho, Tatiana alikuwa na sura nzuri ambayo hata yeye mwenye ilimpagawisha mno.
Kabla ya kuyashikla, alichokifanya ni kuufunga mlango na kushusha pazia la kisasa ili wasiweze kukutwa kisha kumrudia msichna huyo kitandani pale. Alichokuwa akikitaka ni kufanya kile alichokuwa ameambiwa hivyo kuanza kufanya hivyo.
Kila aliposhikwa, Tatiana alikuwa akitoa sauti ya kimahaba tu, alichanganyikiwa mno, alipoona akizidi kuchanganyikiwa, akaanza kuvua sketi yake jambo lililomfanya Dk. Buffet kuacha.
“Unataka kufanya nini?”
“Nimezidiwa doka.”
“Hapana! Siwezi. Namheshimu sana Smith. Siwezi kufanya hivyo,” alisema Dk. Buffet huku akimaanisha kile alichokuwa akikisema.
Hakutaka kuendelea kubaki chumbani mule, aliyaona majaribu yaliyokuwa yakiendelea, alichokifanya ni kuondoka zake huku akimuacha binti huyo akiwa kwenye muhemko mkubwa wa kufanya naye mapenzi.
Huo ukawa mwisho wa Dk.Buffet kuingia ndani ya chumba hicho usiku huo , hata Tatiana alipowaambia manesikwamba alitaka kumuona daktari huyo, alikataa kuonana naye kwa kujipa ubize na kwamba kama kumuona angemuona asubuhi.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Asubuhi ilipofika, Smith alikuwa hospitalini hapo, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kumjulia hali mpenzi wake ambaye bado hakuonekana kuwa na furaha kabisa kwani mapenzi yake hayakuwa kwa mwanaume huyo hata kidogo, alianza kumpenda Dk. Buffet ambaye aliuteka moyo wake kwa kiwango kikubwa mno.
Smith alijaribu kujikesha kwa kumfanya mpenzi wake awe na furaha lakini hilo halikusaidia. Hakuingia hospitalini hapo mikono mitupu, alikuja na zawadi mbalimbali lakini bado Tatiana hakuonekana kuwa na furaha kabisa.
Baadae wakapokea maelekezo kwamba kila kitu kilikuwa tayari na Tatiana aliruhusiwa kuondoka hospitalini hapo. Hiyo haikuwa kawaida, mara zote mgonjwa anapotoka, mtu anayempa ruhusa kwa njia ya mdomo ni daktari mwenyewe ila siku hiyo, mtu aliyekuwa akiwapa taarifa alikuwa nesi ambaye aliagizwa na Dk. Buffet ambaye hakutaka kumuona kabisa Tatiana.
“Sawa, utamwambia kwamba ninashukuru sana,” alisema Simth.
“Hakuna tatizo, akija nitamwambia,” alisema nesi aliyetoa taarifa.
Walipoanza kutoka nje ya jengo la hospitali hiyo, tayari waandishi wa habari walikuwa wamekwishajikusanya na kuanza kuwapiga picha mfululizo. Jina la Tatiana lilikuwa kubwa na hatimaye hata Smith akaanza kujulikana sehemu mbalimbali duniani kupitia msichana huyo mrembo
Waandishi wengine walikuwa na vidaftari vidogo mikononi mwao, walitaka kumsikia Tatiana akizungumza kitu chochote kile kutokana na ule muujiza uliokuwa umetokea katika maisha yake. Hakuzungumza kitu, kwa kumwangalia tu alionekanakuwa na kitu kilichokuwa kikimtatiza moyoni mwake.
“Kuna nini? Mbona unaonekana hauna furaha?” aliuliza Smith.
“Nipo kawaida tu mpenzi,” alijibu Tatiana, hata hilo jina la mpenzi alilitamka tu ili mradi.
“Sawa. Zungumza chochote na waandishi.”
“Hapana! Kwa sasa sijisikii vizuri.”
Kila kitu kilichokuwa kikiendelea kilimshangaza sana Smith, hakutegemea kama angekutana na mabadiliko makubwa namna hiyo kutoka kwa mpenzi wake. Ni kweli alikuwa amepona na kuwa mzima kabisa lakini ni kitu gani kilichomfanya kuwa hivyo? Hakupata jibu lolote lile.
Kila kitu kilibadilika, hakuwa Tatiana yule aliyepita, huyu wa mara hii alikuwa tofauti kabisa. Bado Smith aliendelea kujiuliza labda kulikuwa na kitu kibaya alichokuwa amekifanya kwa mpenzi wake lakini alikosa jibu kabisa, hakuhisi kama kulikuwa na tatizo lolote lile, kila kitu kwake kilikuwa poa kabisa.
“Sasa kwa nini? Mbona amebadilika hivi?” alijiuliza Smith pasipo kupata jibu kwamba kwa kipindi hicho, mapenzi ya Tatina hayakuwa kwake kabisa, alichanganyikiwa na uzuri wa sura aliyokuwa nayo Dk. Buffet.
*****
Umaarufu wa Tatiana ukazidi kuongezeka, duniani akawa gumzo kutokana na urembo aliokuwa nao na sauti nzuri aliyokuwa akiitumia kuimba. Baada ya kukutana na washauri wengi wakamwambia kwamba ingekuwa jambo jema kama angekuwa muimbaji ili aweze kuliteka soko la muziki kama Celine Dion kitu ambacho akakubaliana nacho moja kwa moja.
Alijua kwamba Mungu alimpa sauti nzuri kwa kuwa alitaka awe maarufu na tajiri kupitia sauti hiyo, hivyo akaanza kufanya kama alivyoshauriwa.
Kwa kuwa ndiyo kwanza alikuwa akianza, wimbo wake wa kwanza wenye mahadhi ya R&B haukuwa mzuri lakini sauti aliyokuwa akiitumia ndiyo ilikuwa balaa kabisa. Sauti ile ikawa chachu ya watu waliokuwa wakiusikia na kujikuta wakiupenda ghafla huku kwa wiki ya kwanza, tayari wimbo huo ukaanza kutikisa katika Chati za Billyboard.
Jina lake likaendelea kutikisa, alikuwa akiitwa huku na kule kwa ajili ya kufanya matamasha na wimbo wake huohuo mmoja. Smith alijisikia fahari, alijua kwamba kujulikana kwa mpenzi wake hata naye angejulikana sana tu, na hivyo ndivyo ilivyokuwa.
Kupitia mgongo wa Tatiana, naye akaanza kuitwa sehemu mbalimbali kwa ajili ya kutoa semina za biashara kwa kuwa tu alikuwa na PhD, hivyo watu wengi walimheshimu.
Siku zikaendelea kukatika, bado Tatiana aliendelea kubadilika, hakuwa kama alivyokuwa kipindi cha nyuma, alionekana tofauti sana na katika kipindi hicho alitaka kuonekana kama supastaa hivyo hata mavazi yake yalikuwa hivyohivyo, kama supastaa.
Maisha yake hayakutofautiana na Miley Cyrus, kama msichana huyo alivyokuwa akijiheshimu alivyokuwa akiigiza filamu mbali na kubadilika alipoanza kufanya muziki ndivyo ilivyokuwa kwa Tatiana.
Akasahau alipotoka, umaarufu ukamlevya, fedha alizokuwa akizipata, hakupasahau kule alipotoka, alikisaidia kijiji chake lakini kwenye kila kitu, alisahau kabisa kama aliwahi kukutana na mtu aliyeitwa kwa jina la Peter.
Moyo wa Tatiana haukumsahau Dk. Buffet, mara kwa mara alikuwa akiwasiliana naye simuni na kumwambia hisia kali alizokuwa nazo juu yake. Kwa daktari huyo, hakutaka kukubaliana kuwa na msichana huyo, alikuwa msichana mzuri, alimpenda lakini hakuwa radhi kuwa naye kitu kilichomuuma mno Tatiana.
“What are afraid of?” (Unaogopa nini?) aliuliza Tatiana simuni.
“Smith is my friend, I can’t do such a thing,” (Smith ni rafiki yangu, siwezi kufanya kitu kama hicho) alisema Dk. Buffet.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“C’mon Smith, I will never let him know, please, make me happy papito,” (kamwe sitomjulisha, tafadhali, nipe furaha mpenzi) alisema Tatiana kwa sauti nyororo.
Hilo wala halikuweza kuubadilisha moyo wa Buffet, bado alikuwa akimwambia kwamba alikuwa akimuogopa Smith kwa kuwa alikuwa rafiki wake wa karibu mno hivyo asingeweza kufanya kitu kama hicho.
Ulipita mwaka mzima, Tatiana hakuwa amerudi nchini Tanzania, aliendelea kukaa nchini Marekani huku akiwa mwanamuziki mkubwa mwenye jina kubwa ambaye aliheshima kwa sauti yake nzuri aliyokuwa akiitumia.
Mwaka uliofuata, akaamua kutoa wimbo wa pili aliouita kwa jina la That’s Why Am happy. Mashairi ya wimbo huo yalimlenga zaidi Buffet, alimwambia ukweli kwamba alikuwa akimpenda, hata kama alimkataa lakini kitendo cha kuchati naye simuni, kuzungumza naye kilimpa furaha.
Wimbo ukamuongezea mashabiki wengi zaidi, akazidi kupendwa na kuingiza kiasi kikubwa cha fedha. Tatiana yule aliyekuwa akiishi katika maisha ya kimasikini, leo hii alikuwa bilionea mkubwa, sauti yake ikabadilisha maisha yake kwa ujumla.
Mbali na sauti yake, pia hata uzuri wake ulikuwa gumzo kubwa nchini Marekani. Watu walimpigia sana kura na kuchaguliwa kuwa mwanamke mwenye sura nzuri kuliko wanawake wote duniani ambao walikuwa maarufu.
Kutokana na uzuri wa sura yake, akasainia mikataba mikubwa na majarida mbalimbali likiwemo Forbes kwa ajili ya kupiga picha kwa ajili ya kupamba majarida hayo katika kurasa za mbele. Akaunti ilisoma fedha tu, fedha hazikukauka, kila siku ziliendelea kuingia zaidi na mpaka anatimiza mwaka mmoja na nusu, tayari alikuwa na kiasi cha dola milioni mia tano katika akaunti yake (zaidi ya trilioni moja) kitu kilichomfanya kuona kwamba aliyapatia maisha, kungekuwa na nini tena huko mbele? Alijiona kumaliza kila kitu alichokuwa akikihitaji, sasa akajipanga kummwaga Smith kwani hakuona faida yake kwake zaidi ya kulitumia jina lake kujipatia fedha na umaarufu wa bure pasipo kufanya kazi yoyote ile. Kiburi kikamjaa Tatiana.
*****
“I want you to tell me the truth,” (Ninataka uniambia ukweli) ilisikika sauti ndani ya nyumba ya kifahari alilonunua Tatiana.
“What truth?” (Ukweli gani?)
“Do you love me or not?” (Unanipenda au haunipendi?)
“Why do you ask me such a question?” (Kwa nini unaniuliza swali hilo)
“I only want to know, tell me, do you?” (Ninataka kujua tu, niambie, unanipenda?)
Smith alikuwa amechoka, mambo aliyokuwa akifanyiwa na Tatiana yalimchosha na hakutaka kabisa kuona yakiendelea, dalili zote kwamba penzi lao lilikuwa likienda mlama zilionekana na hivyo alichotaka kujua kwa wakati huo ni kwamba alikuwa akipendwa au la.
Alichoka, hakutaka kuona akiumia zaidi, mambo aliyokuwa akiyafanya msichana huyo yalimuumiza mno. Kuna kipindi, wao kama wapenzi wanapolala kitandani kufanya mapenzi ni jambo la kawaida, lakini kwa kipindi hicho, Tatiana hakutaka kusikia kabisa suala la kufanya mapenzi.
Alipokuwa akishikwa kiuno, aliutoa mkono wa Smith, alipokuwa akishikwa kitovu chake, hakutaka kabisa hicho kitokee, hivyo alisogea pembani na kusema kwamba alichoka na hakuwa akijisikia kabisa.
Smith alimpenda mno msichana huyo kiasi ikawa ngumu kwake kumsaliti, ni kweli kulikuwa na wasichana wengi waliokuwa wakimpenda lakini kwa Tatiana ni kama alikuwa amepigwa upofu, hakusikia lolotelile zaidi ya kila siku kumwambia kwamba alikuwa akimpenda mno.
Tatiana akavimba kichwa, alijua fika kwamba piga ua, Smith angekuwa analalamika sana lakini asingeweza kumuacha kwa kuwa alimpenda sana. Maumivu ya moyo wa Smith yaliendelea kila kila siku, kuna kipindi alikuwa akikaa chini na kujuta kumsaidia msichana huyo kwa kuamini kwamba yale matibabu yaliyoyafanya macho yake kuona ndiyo yaliyopeleka kuwa katika hali hiyo kipindi hicho.
“Kwa nini unanigeuka?” aliuliza Smith, alikuwa na hasira mno, alihisi kama muda wowote ule angeweza kumpiga Tatiana.
“Nimekugeuka, nimefanya nini?”
“Mapenzi yako yapo wapi?”
“Mapenzi gani?”
“Tatiana, hivi haujui tulipotoka kweli? Umeasahau kila kitu mpenzi?” aliuliza Smith, kadiri alivyokuwa akiongea na hasira zake zilizidi kuongezeka.
“Bwana eeee unanipigia kelele,” alisema Tatiana, akavuta blanketi na kujifunika.
Smith aliona Tatiana akimpanda kichwani, huku hasira zikiwa zimemkaba kooni, akamvuta Tatiana upande wake na kuanza kumwangalia usoni. Mishipa ilimsimama, alionekana kuwa na hasira mithili ya simba aliyechukuliwa mtoto wake.
“Unanijibu nini wewe malaya?” aliuliza Smith, alikuwa amekasirika mno.
“Nani malaya, wewe mpumbavu nini.”
Smith akashindwa kuvumilia, pasipo kutegemea akaanza kumpiga Tatiana kipingo kikubwa kilicholifanya blanketi kutapakaa damu kutokana na kupasuliwa mdomo. Tatiana alikuwa akilia tu, akashindwa kuvumilia kwani aliona kwamba endapo angeendelea kubaki mahali hapo basi mwanaume huyo angeweza kumuua, hivyo akakimbia.
Siku iliyofuata, tayari taarifa zikasambaa kwa kasi ajabu kwamba Smith alimpiga Tatiana nusura kumuua. Hiyo ndiyo ilikuwa taarifa iliyozagaa sana kipindi hicho. Wanawake wakaungana na kuanza kuandamana huku wakilalamikia kile kilichokuwa kimetokea kwamba Tatiana hakutakiwa kupigwa na hivyo waliitaka mahakama kuingilia kati na Smith kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.
Smith hakutaka kuzungumza kitu chochote, aliwaacha watu waongee wanavyotaka lakini kamwe hakutaka kuzungumza lolote lile kwa kuona kwamba asingeweza kuaminika hata mara moja.
Si nchini Marekani tu ambapo maandamano yalitokea bali hata katika baadhi ya nchi za Kiafrika ikiwemo Tanzania wanawake walijikusanya mitaani na kuanza kulaani kile kilichokuwa kimetokea.
Wote hao hakukuwa na mtu aliyejua ukweli kwamba msichana Tatiana alikuwa amebadilika na hakuwa na shukrani, kwao, Smith alionekana kuwa mwanaume mbaya kitu ambacho hakikuwa kweli kabisa.
Alichokiamua Tatiana na kumuita mwanasheria wake na kesi kufikishwa mahakamani. Dunia nzima ikatega sikio lake katika kesi hiyo, bado Tatiana alionekana kuwa na sababu kubwa ya kumshitaki Smith kwa kile kilichokuwa kimetokea.
“Nitahakikisha mpaka anafungwa,” alisema Tatiana, alikuwa akiwaambia marafiki zake katika kipindi alichokuwa kwenye Kisiwa cha Hawaii wakila maisha.
“Tena ni bora iwe hivyo, wamezidi kutunyanyasa, haiwezekani akupige bila sababu,” alisema mmoja wa marafiki zake.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kesi haikuchelewa, ikaanza kunguruma mara moja. Bado Smith hakuzungumza kitu chochote kile, alichokifanya ni kuomba msamaha kwa kila kilichokuwa kimetokea. Alijua kwamba Tatiana alikuwa supastaa hivyo kama angeamua kusema kile kilichokuwa kimetokea basi inawezekana angelichafua jina lake, hivyo hakutaka kufanya hivyo.
Katika kipindi cha miezi sita chote watu walikuwa wakifuatilia kile kilichokuwa kikiendelea mahakamani na mwisho wa siku mahakama kuamua kumuadhibu Smith kwa kufanya kazi za jamii kwa masaa elfu mbili, pia akae mbali na Tatiana kwa zaidi ya kilometa kumi, asimpigie simu wala kumtumia ujumbe wowote ule, uwe simuni au kupitia kwa mtu fulani kwa kipindi cha miaka miwili.
Kwa Smith hiyo ilikuwa adhabu kali mno, kuwa mbali na Tatiana kilikuwa kitu ambacho hakuzoea kabisa kukiona hivyo aliamini kwamba maisha yake yangekuwa na matatizo mno, lakini hakukata rufaa, kile kilichoamuliwa na mahakama, akikacha hivyovhiyo na kuanza kufanya adhabu yake.
“Ila kwa nini ulimpiga?” aliuliza bwana Warren.
“Ni matatizo ya kimapenzi.”
“Kivipi?”
“Tatiana amebadilika sana baba.”
“Haiwezekani, amekuwaje?”
“Ni mbaya sana, huwezi amini. Sijutii kumpiga hata mara moja,” alisema Smith na kuanza kuwahadhithia wazazi wake kile kilichokuwa kimetokea.
Kila mmoja alibaki kimya akimsikiliza Smith, maneno aliyokuwa akizungumza yalimsikitisha kila mtu aliyekuwa mahali hapo, hawakuamini kama msichana Tatiana angeweza kufanya vile vyote ambavyo Smith alikuwa akihadithia.
Huo ndiyo ulikuwa ukweli, Smith hakupunguza neno wala kuongeza neno, kila kitu alichokuwa amekihadithi kilikuwa sahihi kabisa kwamba msichana huyo alikuwa amebadilika kwa asilimia mia moja.
Tatiana akawa huru, kitendo cha kuachana na Smith kilimpa nafasi kubwa ya kuishi kama alivyokuwa akitaka,. Alikulia katika maisha ya dini, alikwenda sana kanisani na hata kuimba kwaya lakini mara baada ya kupata fedha na umaarufu, kila kitu kikabadilika, Tatiana yule wa kipindi cha nyuma hakuwa huyu.
Akajifunza kunywa pombe kwani ndiyo aliamini kwamba kilikuwa kitu pekee alichokuwa amekibakiza katika maisha yake. Kadiri maisha yalicyokuwa yakisonga mbele, Tatiana aliendelea kuharibikiwa zaidi kiasi kwamba akasahau alipotoka.
“Tatiana,” aliita rafiki yake, alikuwa amelewa mno.
“Unasemaje?”
“Naomba niendeshe gari.”
“Hapana! Nitaendesha mimi, gari hii ni yangu,” alisema Tatiana.
“Hapana! Haiwezekani kuendesha na wakati umelewa,” alisema rafiki yake huyo.
Hiyo ilikuwa ni usiku wa saa saba, walikuwa wanatoka katika Klabu ya Casanova iliyokuwa katikati ya Jiji la New York. Siku hiyo Tatiana alikuwa amekunywa pombe nyingi, alilewa chakari huku akiwapa nafasi wanaume kushika maungo yake.
Japokuwa alikuwa amekunywa kiasi kikubwa cha pombe, bado alihitaji kuendesha gari kitu kilichokataliwa na rafiki yake huyo. Huku akibisha, Tatiana akaingia garini, rafiki yake hakuwa na jinsi, naye akaingia na kuanza kuondoka mahali hapo huku watu wakiwaangalia kwani hapo nje bado kulikuwa na wengi waliokuwa wakimpiga picha.
“Puuuuuuuu......!!” ulisikika mlipuko mkubwa wa bomu, watu wakshtuka, wengine wakaanza kukimbia huku na kule, gari alilokuwa amepanda Tatiana likalipuka na kuanza kuteketezwa kwa moto.
Sauti za wasichana wawili zikaanza kusikika wakipiga kelele, moto mkubwa ulikuwa ukiliteketeza gari lile jambo lililowafanya watu wengi kushtuka, hawakuelewa kile kilichokuwa kimetokea, badala ya kuanza mishemishe ya kuuzima moto ule, walibaki wakiangalia kwa mshangao mkubwa huku kelele za Tatiana na rafiki yake zikiendelea kusikika ndani ya gari hilo.
Kwa jina aliitwa Kashmovic Petrov, alikuwa Mrusi aliyekuwa akiishi sana barani Afrika. Alikuwa mwanaume mwenye mwili mkubwa uliojengeka kimazoezi, alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa na roho mbaya ambaye baadaye akafukuzwa kwa kuwa alitaka kuipindua serikali tawala.
Kwa kumwangalia Petrov, alionekana kuwa kijana mpole, msikivu lakini alikuwa makini wa kazi zake. Katika kipindi ambacho Urusi ilikuwa ikifanya mapinduzi mwaka 1917, babu yake Petrov ndiye alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba mtawala Nicolus II anaachia ngazi na hivyo nchi kutoka katika utawala wa Kifalme na kuondoa ubepari.
Ilikuwa kazi kubwa lakini mwisho wa siku walifanikiwa. Huku akionekana kuwa mwanaume mwenye nguvu, babu yake Petrov akafanikiwa kumuoa mwanamke aliyeitwa Juliana na hatimaye kupata watoto huku mmojawapo akiwa Udzoniv, baba yake Petrov.
Kiubavu, Petrov alikuwa amerithi kutoka kwa babu yake. Baada ya kukulia katika maisha ya kijeshijeshi na utemi mkubwa mitaani ndipo baba yake alipoamua kumpeleka katika jeshi la Urusi ambapo huko akapambana sana mpaka kupata nyota tatu.
Mwili wake uliendelea kujengeka sana, alijulikana karibu kambi zote za kijeshi nchini Urusi, aliwekwa katika kitengo nyeti cha upelelezi kwa ajili ya kufuatilia mbinu mbalimbali zilizokuwa zikifanywa na Wamarekani, baadae walipomuona kwamba aliifanya kazi kwa utaalamu mkubwa, wakamhamisha na kumuweka katika jeshi la maji.
Mbali na kila kitu alichokuwa nacho, Petrov alikuwa akitisha sana katika kutengeneza mabomu. Alikuwa mtaalamu mkubwa ambaye aliheshimika sana jeshini kiasi kwamba asilimia sabini ya mabomu yaliyokuwa yakitengenezwa nchini Urusi, yeye ndiye aliyekuwa akiagiza yatengenezwe vipi.
Hayo ndiyo yalikuwa maisha yake, hakutoka jeshini lakini baada ya kulitumikia jeshi hilo kwa miaka kumi, akaamua kuigeuka hasa kwa kupanga mikakati ya kuipindua nchi hiyo. Serikali ililigundua hilo na hatimaye kumkamata, hawakutaka kumuua, walichokifanya ni kumfukuza nchini Urusi.
Baada ya kufukuzwa, hakwenda sehemu yoyote ile barani Asia, bali alichokifanya ni kukimbia na kukimbilia barani Afrika na kwenda nchini Liberia ambapo akaungana na rais Charles Taylor na kuendelea na maisha yake kama kawaida pasipo watu kufahamu.
Ingawa baadaye rais huyo alikamatwa kwa makosa tofautitofauti, Petrov akabaki na jeshi kubwa na kuendelea kulipa mafunzo kwani bado walikuwa wakiihitaji nchi hiyo.
“I want to see Petrov,” (Ninataka kumuona Petrov) alisema Nathan, alikuwa amesimama mbele ya wanajeshi wa waasi.
“What is your problem?” (Una tatizo gani?)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nathan hakutaka kusema kile alichokuwa akikihitaji zaidi ya kuomba kuonana na Petrov tu. Ilikuwa ni kazi kubwa, haikuwa kazi nyepesi hata mara moja kuonana na mtu huyo lakini kwa sababu aliomba sana na pia alijulikana kutokana na utajiri mkubwa wa baba yake, akaruhusiwa kuonana naye.
“Kuna nini?”
“Nataka unisaidie,” alisema Nathan huku akionekana kuhitaji msaada wa hali na mali.
“Nikusaidie nini?”
“Kuna mtu nataka afe.”
“Nani?”
“Unamfahamu huyu Tatiana?”
“Yupi huyo?”
“Huyu mwanamuziki anayetamba sasa hivi?”
“Namsikiasikia, amefanya nini?”
“Ninataka umuue, tena kwa kumlipua na bomu,” alisema Nathan.
“Anaishi wapi?”
“Marekani, ila kumpata siyo tatizo. Nitagharamia kila kitu,” alisema Nathan.
Alionekana kuwa na hasira na Tatiana, kwa kile alichokuwa amemfanyia kwa kuamua kuwa na mtu mwingine kilimuumiza mno, hakutaka kuona msichana huyo akiendelea kuishi kwa kuwa aliuumiza mno moyo wake.
Hiyo wala haikuwa kazi kubwa kwa Petrov, alichokifanya ni kuhitaji kiasi cha dola lefu ishirini ambazo ni zaidi ya milioni arobaini kwa ajili ya kufanya kazi hiyo tu. Hilo wala halikuwa tatizo kwa Nathan, alichokuwa akikitaka ni kuona kazi inafanyika, hilo tu.
Baada ya wiki moja, akawasilisha malipo yake na moja kwa moja Petrov kuanza kazi ya kuingia nchini Marekani kwa kutumia meli kubwa ya mizigo iliyokuwa ikimilikiwa na Wagiriki. Hakuhofia maisha yake, kile alichokuwa akikihitaji kwa wakati huo ni kukamilisha kazi aliyokuwa amepewa, hivyo alilazimika kwenda kuifanya kwa mikono yake.
Baada ya kufika jijini New York huku akipewa hifadhi na rafiki yake mmoja, huyo ndiye aliyemfadhili kila kitu kuanzia maladhi, usafiri na mambo mengine. Hata pale ambapo Petrov alipokuwa akihitaji vifaa kwa ajili ya kutengeneza bomu, rafiki yake huyo ndiye alikuwa akihusika.
*****
Petrov alifika mapema sana katika Klabu ya Casanova, akalipaki gari lake pembeni na kuanza kusikilizia muda ambao msichana Tatiana angeingia ndani ya eneo la klabu hiyo. Bomu lake lilikuwa ndani ya gari, aliliweka vizuri na alikuwa amekwishaliseti lilipuke mara baada ya uzito kuwa mkubwa gari wakati gari likianza safari.
Alitulia hapo kwa zaidi ya masaa mawili huku wakati mwingine akihisi kama alidanganywa kwamba Tatiana angekuwepo katika klabu hiyo. Aliendelea kukaa garini, ilipofika majira ya saa tatu usiku, akaliona gari aina ya Hammer likianza kuingia ndani ya eneo hilo, kwa jinsi gari lile lilivyoonekana kuwa la kifahari, akahisi kwamba huyo alikuwa Tatiana.
Hakutaka kuteremka garini, alitaka kuwa na uhakika kwamba mtu huyo alikuwa Tatiana au la. Gari liliposimamishwa, mlango ukafunguliwa na Tatiana kuteremka akiwa na rafiki yake. Petrov akatoa tabasamu pana, hakuamini kama kazi yake ingekuwa rahisi namna ile.
Alichokifanya ni kuwasuburi mpaka waondoke na kuelekea ndani. Kila kitu alichokuwa akikitaka mahali hapo kikafanyika, hivyo akaanza kulisogelea gari lile, akaangalia huku na kule, alipoona hakukuwa na mtu aliyekuwa akimuona, akainama chini, akaingia uvunguni na kulitegesha bomu lile kisha kuondoka zake.
******
Kelele ziliendelea kusikika mahali hapo, gari lilizidi kuteketea huku watu wote wakiwa wamepigwa na butwaa wasijue la kufanya. Baada ya sekunde kadhaa, watu wawili waliokuwa na mashine za extinguisher wakalisogelea gari lile na kuanza kuliupulizia hewa lile na hatimaye moto ule kuzima.
Hiyo ikaonekana kuwa nafuu, moto ukazimika na kuufungua mlango ule. Bahati mbaya, rafiki yake Tatiana alikuwa ameteketezwa na moto na hakuwa akihema, alifariki palepale garini. Hilo likawatia wasiwasi kwamba inawezekana hata Tatiana naye akawa amekufa lakini walipomgusa, alishtuka huku akikohoa mfululizo kutokana na moshi mzito.
“Vipi?” aliuliza jamaa mmoja.
“Hata hajajeruhiwa,” alisema jamaa mwingine.
Hawakutaka kupoteza muda, walichokifanya ni kumchukua na kisha kumpeleka hospitalini huku mwili wa rafiki yake ukitolewa garini na kuwekwa chini, kila mtu aliyeuona, alijikuta akibubujikwa na machozi, picha iliyoonekana ilimuumiza kila mtu.
Kutokana na matatizo makubwa yaliyokuwepo baina ya Smith na Tatiana, kila mmoja akajua kwamba kwa kila kitu kilichokuwa kikiendelea, Smith alikuwa akihusika nacho.
**** Taarifa za habari, mitandao ya kijamii, kote huko wakawa wakitangaza juu ya kile kilichokuwa kimetokea, mwanamuziki aliyelishikilia soko la muziki duniani, Tatiana alilipuliwa na bomu akiwa ndani ya gari lake.
Zilikuwa taarifa zenye kushtua sana, kila aliyezisikia, hakuamini kama kweli kitu kile kiliuwa kimetokea hivyo kuanza kuelekea katika Hospitali ya St. Mariana Medical Center ili kwenda kujionea kwa macho yao.
Taarifa ambazo hazikuthibitika zilisema kwamba Tatiana alikufa kwenye mlipuko huo kitu kilicholeta huzuni kubwa kwa kila mtu aliyezisikia, lawama zote juu ya mlipuko hizo zikaenda kwa Smith kwani ndiye mtu aliyekuwa na uhasama mkubwa na msichana huyo.
Watu wakachukulia kile kama kisasi kwamba Smith alitaka kulipiza kwa kile alichofanyiwa na msichana huyo ambaye alionekana kuwa mtu asiyekuwa na hatia yoyote ile na hivyo watu kuanza kuishinikiza Serikali ya Marekani imkamate Smith na kumfunga jela kwa kile kilichokuwa kimetokea.
Hakukuwa na mtu aliyefahamu mengi kuhusu Tatiana, alionekana msichana mwema asiyekuwa na tatizo lolote lile, alipendwa na kila mtu, sauti yake nzuri ilimpagawisha kila mtu kiasi kwamba kuna wakati watu walifikiri kwamba msichana huyo alishushwa kutoka Mbinguni.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Huyu ni Smith tu, yeye ndiye aliyefanya mpango huu,” alisema mwanaume mmoja, alionekana kuwa na hasira mno, alikuwa amevalia fulana iliyokuwa na picha ya Tatiana.
“Huo ndiyo ukweli! Nahisi alichukia sana alipopelekwa mahakamani, yeye ndiye aliyefanya hivi, lazima serikali iingilie kati,” alisikika mwanamke mmoja.
Watu waliamini kwamba Smith ndiye aliyefanya mpango wa kulilipua gari lile kutokana na kile kilichokuwa kimetokea katika maisha yao ya nyuma. Magazeti, pasipo kupata ufumbuzi wowote ule waliandika kwamba kulikuwa na madai mengi kwamba mwanaume huyo ndiye aliyesababisha mlipuko huo.
Smith hakuzungumza kitu, alisoma kila kitu kilichokuwa kikiandikwa lakini aliamua kubaki kimya kwa sababu alijua fika kwamba si yeye aliyefanya jambo hilo, zaidi sana, akaelekea nchini Hispania kwa ajili ya mapumziko.
Tatiana alifikishwa ndani ya Hospitali ya Mariana akiwa hoi, moshi ulimfanya kuwa kwenye hali mbaya kiasi kwamba hata kupumua kwake kulikuwa kwa shida sana. Mapafu yalijaza moshi mwingi uliomfanya madaktari kumchukua na kumpeleka katika chumba maalumu kwa ajili ya matibabu.
Kila mtu aliyeuona mwili wa rafiki yake Tatiana kwa jinsi ulivyoteketea, alimuona mwanamuziki huyo kuwa na bahati kubwa mno kwani kuungua kwa rafiki yake na kufariki huku yeye akiwa mzima wa afya ilionekana bahati kubwa sana.
Ndani ya saa moja tangu mlipuko huo utokee, tayari watu zaidi ya elfu tano walikuwa wamekwishakusanyika nje ya hospitali hiyo kwa ajili ya kumuona msichana huyo ambaye aliendelea kuwa gumzo kila kona duniani.
Wengi walihuzunika, tetesi zilizokuwa zikisikika mitandaoni kwamba binti huyo alikuwa amefariki dunia zilimhuzunisha kila mtu, wengine wakashindwa kuvumilia hivyo wakajikuta wakibubujikwa na machozi.
“Anaendeleaje?” aliuliza Buffet alipokuwa amekwenda hospitalini hapo.
“Anaendelea vizuri tu, ingawa moshi ulijaa sana kwenye mapafu yake,” alijibu daktari aliyekuwa akimshughulikia Tatiana.
“Kwa hiyo yupo salama sasa hivi?”
“Ndiyo! Tunamshukuru Mungu.”
“Na huyo mwenzake?”
“Aliyekuwa naye alifariki hapohapo, ni Mungu tu mpaka msichana huyo kuwa mzima,” alisema daktari huyo.
Japokuwa hakutaka kuwa mpenzi wake lakini Dk. Buffet alimheshimu sana Tatiana, alimchukulia kama rafiki yake wa karibu na ndiye alikuwa mtu pekee aliyemfanya kujulikana zaidi duniani na kujikuta akiheshimiwa kila alipokuwa.
Hakutaka kumuacha binti huyo, aliendelea kuwa karibu naye huku kwa kila alichokuwa akikifanya, alikifuatilia kwa karibu mno.
Kitendo cha Smith kumpiga msichana huyo kilimkasirisha mno, alitamani akutane na Smith na kumwambia ni kwa kiasi gani alikichukia kitendo hicho lakini pia akahofia kuingilia mapenzi ya wapendanao, hivyo akaachana naye.
Aliposikia kwamba gari alilopanda msichana Tatiana lililipuliwa kwa bomu, akashikwa na presha, alihisi mwili wake ukitetemeka mno. Hata yeye mwenyewe alijua kwamba aliyefanya kila kitu alikuwa Smith, hivyo akaanza kumchukia mno.
“Huyu si rafiki tena,” alisema Buffet huku akikunja uso wake kwa hasira.
Mara baada ya kuona gari likiwa limelipuka, Petrov hakutaka kubaki mahali hapo, moja kwa moja akawasha gari lake na kuondoka mahali hapo. Moyoni alikuwa na furaha mno, hakuamini kama ile kazi aliyokuwa amepewa angeikamilisha kwa haraka na kwa wepesi namna ile, moyoni mwake akawa na furaha tele kwa kuona kwamba rekodi yake ya kukamilisha kazi zake kwa asilimia mia moja ilikuwa ikiendelea kama kawaida.
Hakutaka kukaa sana nchini Marekani kwa kuogopa kukamatwa, alichokifanya, kesho yake akaondoka kurudi nchini Liberia huku moyo wake ukiwa na furaha mno.
“Nimekamilisha kila kitu,” alisema Petrov alipokuwa akizungumza simuni na Nathan mara baada ya kufika Liberia.
“Hapana! Kazi haikukamilika.”
“Haikukamilika, kivipi na wakati gari lililipuka na yeye akiwa ndani?” aliuliza Petrov huku akionekana kushtuka.
“Tatiana hakufa!”
“Hakufa? Kivipi?”
“Upo sehemu yenye televisheni?”
“Ndiyo!”
“Hebu tazama LTV,” alisema Nathan na Petrov kuwasha televisheni yake na kuweka kituo hicho cha habari ambacho kilijiunga na CNN.
Hakuamini macho yake kile alichokuwa akikiona mahali hapo, Tatiana alikuwa akihojiwa huku akiwa hospitalini, alikuwa akizungumzia kile kilichokuwa kimetokea wakati mlipuko mkubwa ulipotokea.
Petrov hakuamini kile alichokuwa amekisikia, hakujua binti yule alinusurikaje na wakati gari lililipuka na kusikia kelele za yeye na rafiki yake wakipiga kelele na yeye kuondoka. Akajikuta akibadilisha muonekano wa sura yake, akayauma meno yake kwa hasira huku akipanga kurudi tena nchini Marekani.
“Ni lazima nirudi kukamilisha kazi,” alisema Petrov, alikuwa akimwambia Nathan.
“Hapana! Unatafutwa huko.”
“Natafutwa?”
“Ndiyo! Kila mtu anajua kwamba wewe ndiye uliyehusika katika mlipuko huo,” alisema Nathan.
“Haiwezekani!”
“Wewe endelea kutazama televisheni utaliona hilo.”
Petrov akatulia na kuendelea kutazama televisheni, baadae akaiona picha yake ikiwekwa hadharani siku ambayo alihusika katika kulitega bomu lle, picha ile ilikuwa imepigwa kwa kamera ndogo za CCTV zilizokuwa zimewekwa nje ya ukumbi ule.
“Siwezi kurudi, ila nitafanya juu chini huyu mpumbavu afe,” alisema Petrov.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Tatiana aliyafumbua macho yake, mtu aliyemuona mahali hapo alikuwa Buffet, tabasamu kubwa likautawala uso wake, hakuamini kama mwanaume huyo angekuwa mtu wa kwanza kuingia chumbani mule kuja kumuona.
Alimpenda sana Nathan, alimchukulia kuwa kila kitu katika maisha yake. Mpaka katika kipindi hicho, mwanaume huyo hakuwa amekubaliana naye kitu kilichompa huzuni kubwa moyoni mwake.
Alichokifanya ni kumuita na kisha kuangaliana kwa karibu. Kila alipokuwa akimwangalia Buffet alishindwa kujizuia na kumwambia tena juu ya hisia kali za kimapenzi alizokuwa nazo kitu kilichomfanya Buffet kuelewa zaidi.
“Tatiana....”
“Abeeee...”
“Pona kwanza, mengine tutayazungumza,” alisema Buffet.
“Najua, lakini ninakuhitaji wewe. Tangu kipindi kile niligundua kwamba Smith hakuwa mwanaume wangu sahihi, ukapingana nami, si umeona mwenyewe.”
“Nimeona Tatiana, lakini bado tunatakiwa kukaa chini na kuzungumza.”
“Sawa. Ila nakupenda sana.”
“Asante.”
Buffet hakuwa na jinsi, Tatiana alipotoka hospitalini, wakakutana katika chakula cha usiku kwenye Mgahawa wa McDonald, wakaanzisha uhusiano mpya wa kimapenzi ambao ulivuma sana katika magazeti na majarida mbalimabali.
Huo ulikuwa mwaka wa tatu tangu amuache Peter, na hakuwa amerudi nchini Tanzania.
**** Kama kuumia Peter aliumia sana lakini hakukuwa na kilichobadilika maishani mwake. Mapenzi yalimtesa mno, yalimkondesha kupita kawaida lakini hakuwa na la kufanya, bado mpenzi wake wa siku nyingi, Tatiana hakurudi maishani mwake.
Mpaka mwaka unamalizika na kuingia kidato cha sita, Tatiana hakuwa amerudi nchini Tanzania, maisha yake yalibadilika na hakuwa msichana yule aliyekuwa masikini bali alikuwa msichana tajiri, mwenye jina kubwa na fedha nyingi.
Peter hakujua kama msichana huyo angeweza kumkumbuka maishani mwake, kila alipokuwa akimwangalia kwenye televisheni, alijikuta akibubujikwa na machozi kwani hakujua ni kitu gani angefanya mpaka msichana huyo kurudi na kuwa kama zamani.
Mwaka huo alijitahidi sana katika masomo yake na alipomaliza, akaanza kukaa nyumbani huku akisubiri matokeo ya mtihani wa kidato cha sita.
Katika kipindi hicho ndicho alichokutana na msichana Lydia Andrew. Alikuwa msichana mrembo, mwenye heshima kubwa huku akiwa Mkristo mwenye kumaanisha. Peter alikutana na msichana huyu katika Kongamano la CASFETA lililofanyika mkoani Dodoma.
Hilo ni kongamano kubwa la Vijana wa Kikristo ambalo hufanyika kila mwaka katika mkoa ambao hupangwa. Katika kongamano hilo, vijana walikuwa wakiweka kambi sehemu ambapo huko humuimbia Mungu na kufanya maombi mbalimbali. Alipokutana na msichana huyo, akahisi moyo wake ukianza kumpenda na kuona kwamba inawezekana msichana huyo akawa mke wake baadae.
“Bwana Yesu Asifiwe,” alisalimia Peter.
“Amen!” aliitikia Lydia.
“Umependeza mno, na umenibariki sana kwa siku ya leo, una sauti nzuri sana,” alisema Peter.
“Utukufu kwa Mungu mpendwa!”
Huo ndiyo ukawa mwanzo wa mazungumzo yao, Peter hakutaka kumuonyeshea Lydia kwamba alikuwa akimpenda, alimheshimu kwani alijua kwamba huo haukuwa muda sahihi wa kumwambia kile alichokuwa amekipanga maishani moyoni mwake.
Aliyahisi mapenzi mazito moyoni mwake, kila walipokuwa kanisani wakiimba, macho yake yalikuwa yakimwangalia Lydia aliyekuwa na sauti nzuri kila alipokuwa akiimba. Hakujua ni kwa namna gani angeweza kuzifikisha hisia zake kwani kila siku moyo wake uligalagazwa vibaya.
Kongamano hilo lililofanyika Dodoma lilichukua wiki mbili na ndipo wakatakiwa kurudi nyumbani kwao. Kwa Peter hakutaka kukubali kirahisi, hakutaka huo uwe mwisho wa kuonana na msichana huyo, alichokifanya ni kumfuata na kuanza kuzungumza naye.
“Lydia...” aliita.
“Abee kaka Peter!”
“Hahaha! Kumbe unanijua!”
“Ndiyo! Wewe si mtoto wa mchungaji Lazaro?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Yeah! Ndiye mimi! Wewe ni mtoto wa mchungaji pia?”
“Ndiyo!”
“Mmmh! Mchungaji gani?”
“Marcus wa Morogoro!”
“Waooo! Kumbe! Nimefurahi kukufahamu kwa undani.”
“Asante sana. Nakutakia mchana mwema,” alisema Lydia na kuanza kuondoka, Peter akamuwahi mkono.
“Subiri kwanza...”
“Kuna nini?”
“Kwani huu ndiyo mwisho wetu?”
“Mwisho wa nini?”
“Kuonana na kuzungumza pamoja?”
“Mmmh! Sijui.”
“Ningependa niwasiliane nawe Lydia, nimefurahia huduma yako, hakika Mungu amekubariki,” alisema Peter
Lydia alionekana msichana mpole, msikivu na aliyekuwa makini kwa kila kitu. Alipoambiwa hivyo, akabaki akimwangalia Peter usoni, alimkazia macho, alitaka kuona kama mwanaume huyo alimaanisha kile alichokuwa akikizungumza au la.
Tabasamu pana likaonekana usoni mwa Lydia na kisha kutoa simu yake na kumpa namba ya simu Peter ambaye alionekana kuwa na furaha tele.
Huo ndiyo ukawa mwanzo wa ukaribu wao. Kila siku usiku ilikuwa ni lazima Peter kuwasiliana na msichana Lydia huku akificha kile kilichomfanya mpaka kusisitiza kuchukua namba yake. Baada ya miezi kadhaa, matokeo ya kidato cha sita yakatoka na hatimaye Peter kuchaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
“Hongera sana,” alisema Lydia walipokuwa wakizungumza simuni.
“Nashukuru. Ila kuna kitu.”
“Kitu gani?”
“Lydia, unajua kwa nini niliamua kuwa na mawasiliano nawe?”
“Hapana.”
“Nilitokea kukupenda sana, nilipokuona kwa mara ya kwanza, moyo wangu ulikufa juu ya penzi lako, nikaona si vib....” Peter alisema kwa hisia kali za mapenzi, hata kabla hajamalizia sentensi yake, Lydia akakata simu.
“Hallow...hallow...” aliita Peter.
Peter hakutaka kukubali, alikataliana na ukweli uliokuwepo kwamba msichana huyo alikata simu bali alijifariji kwamba kulikuwa na tatizo la network na hivyo kuanza kumpigia tena. Simu ikaanza kuita, iliita na kuita lakini haikupokelewa kabisa.
Peter hakukata tamaa, hakutaka kuona akimpoteza Lydia kirahisi namna hiyo, alichokifanya ni kuendelea kumpigia lakini matokeo yalikuwa yaleyale kwamba simu haikupokelewa, na alipoendelea zaidi, ikawa haipatikani.
Moyo wake uliumia, hakukuwa na kitu alichomuomba Mungu kila siku kama kutokumpoteza msichana Lydia, moyo wake uliumia sana, aliyakumbuka maumivu makali aliyokutaka nayo kwa Tatiana ambaye kwa wakati huo alikuwa mwanamuziki mkubwa duniani, hakutaka kujiona akiumia tena kwa msichana ambaye aliamini kwamba angekuwa mke wake hapo baadae.
Hakukata tamaa, aliendelea kumtafuta msichana huyo lakini hakuwa akipatikana kabisa, na kama alipatikana, hakupokea simu. Peter hakutaka kukubali, alijiona kuwa radhi kupoteza kitu chochote lakini si msichana huyo mrembo, alichokifanya ni kuwaambia wazazi wake kwamba anakwenda Morogoro kutembea.
“Una uhakika ni Morogoro?” aliuliza mchungaji Lazaro.
“Ndiyo baba. Nakwenda Morogoro,” alisema Peter.
Kwa kuwa alikuwa kijana mkubwa aliyejitambua, wazazi wake hawakutaka kumzuia, wakampa ruhusa na hatimaye kuelekea mjini Morogoro huku lengo lake kubwa likiwa ni kuonana na msichana huyo mrembo.
Ndani ya basi Peter alikuwa na mawazo tele juu ya Lydia tu, alikuwa akimpenda mno na kwa kipindi chote ambacho alikuwa hajawasiliana naye, aliona pengo kubwa sana moyono mwake.
Basi lilichukua masaa mawili mpaka kufika Morogoro ambapo akateremka na kuelekea hotelini kisha kuwapigia simu wazazi wake na kuwaambia kwamba alifika salama. “Kwanza ngoja nimpigie simu Lydia,” alisema na kisha kuchukua simu yake na kumpigia simu msichana huyo.
Majibu yalikuwa yaleyale, hakikubadilika kitu chochote kile, simu iliita na kuita lakini haikupokelewa kitu kilichomuongezea huzuni moyoni mwake. Alichokifanya ni kukata simu kisha kujipanga kulitafuta kanisa lao.
Kwa kuwa Kanisa la Praise And Worship lilikuwa maarufu hapo Morogoro, wala hakupata shida kulipata, alipoulizia mara moja tu, akaelekezwa na kuanza mahali kanisa hilo lilipo katika Mtaa wa Madaraka na kuelekea huko.
Alipofika kanisani hapo, akakutana na washirika watatu waliokuwa wakifanya usafi kanisa. Akawasalimia na kuanza kuzungumza nao.
“Mchungaji anaishi Mtaa wa Kingo,” alisema mshrika mmoja.
“Upo mbali kutoka hapa?”
“Si mbali. Twende nikupeleke,” alisema mshirika mmoja na kuanza kuelekea huko
Njiani, mapigo ya moyo yalikuwa yakimdunda mno, kiu ya kumuona Lydia ilikuwa imemkamata lakini alikuwa akiogopa mno. Hakuwahi kufika nyumbani kwao na hakujua wazazi wa msichana huyo wangefikiria nini, ila alichokuwa akikihitaji ni kuwa na msichana huyo tu.
“Nyumba ile pale, ile yenye maua nje,” alisema mshirika huyo.
Mapigo ya moyo yakazidi kudunda kwa nguvu, kwa mbali akaanza kuhisi kibaridi kikali kilichomfanya kuanza kutetemeka lakini cha ajabu kijasho chembamba kilikuwa kikimtoka. Wakati mwingine alitamani warudi nyuma ili aweze kujipanga upya lakini akapiga moyo konde, wakafika na kuanza kugonga hodi na mlango kufunguliwa, wakaingia ndani.
“Nimemleta mgeni wenu mama mchungaji,” alisema mshirika yule baada ya salamu.
“Asante. Karibu mgeni.”
“Asante.”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Peter akaanza kujitambulisha alikuwa nani, mama mchungaji akafurahi mno kumuona mtoto wa mchungaji Lazaro ndani ya nyumba yao kwani mara nyingi alimwambia mchungaji huyo aje na familia yake lakini ratiba iligongana sana. Alichokifanya akamuita mume wake na kuanza kuzungumza na Peter.
“Nimekuja kwa lengo moja tu,” alisema Peter.
“Lengo gani?”
“Kuzungumza na binti yenu, Lydia.”
“Lydia?”
“Ndiyo,” alisema Peter.
Mchungaji na mkewe wakashtuka!!
Mara baada ya kukaa nchini Marekani kwa miaka mitatu mfululizo, Tatiana akaamua kupanga safari ya kuelekea nchini Tanzania kwa ajili ya kuwaona wazazi wake na kuwashukuru Watanzania kwa kila kitu walichokuwa wamekifanya kwa ajili yake.
Alijipanga, alichokifanya ni kuchukua ndege yake binafsi, akapanda na mpenzi wake, Buffet na hatimaye safari ya kuelekea nchini Tanzania kuanza.
Ndani ya Jiji la Dar es Salaam mambo yalikuwa balaa. Mara baada ya taarifa kutangazwa kwamba mwanamuziki Tatiana anafika nchini Tanzania, watu wakajiandaa vilivyo kwa ajili ya kumpokea mwanamuziki huyo aliyeiletea Tanzania sifa kubwa na kuifanya ijulikane kimataifa.
Fulana zaidi ya elfu kumi zikachapishwa kwa ajili ya kumkaribisha mwanamuziki huyo, vikundi mbalimbali vya ngoma vikaandaliwa tayari kwa ajili ya kumpokea, watu wengi wakajiandaa vilivyo kumpokea mwanamuziki huyo.
Siku ambayo ndiyo Tatiana alikuwa akifika nchini Tanzania, watu wengi walisimama nje ya uwanja wa ndege kwa ajili ya kumpokea. Kwa sababu kulikuwa na watu zaidi ya milioni moja waliokuwa na hamu ya kumpokea, wakaambiwa wajipange barabarani kwa ajili ya kumpokea mtu huyo.
Hilo halikuwa tatizo, kila mtu alitaka kumuona Tatiana. Kama mwanamuziki huyo aliyekuwa akifanya kazi kubwa nchini Marekani watu walilipia kiasi kikubwa cha fedha kumwangalia, hilo halikuonekana kuwa tatizo kwao kujipanga pembeni mwa barabara kwa ajili ya kumpokea mwanamuziki huyo.
Kama ilivyokuwa katika msiba wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ndivyo ilivyokuwa siku hiyo. Watu walijipanga katika Barabara ya Nyerere, kote huko barabara ilizungukwa na umati wa watu ambapo baada ya kufika Buguruni, wakaunganisha mpaka katika Barabara ya Mandela na walipofika njia panda kwenye maunganiko na Barabara ya Uhuru, wakajipanga pia, katika kila kona, watu walikuwa barabarani kwa ajili ya kumuona mwanamuziki huyo mkubwa.
Saa 8:20 mchana, ndege binafsi ya Tatiana ikaanza kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, watu waliokuwa nje ya eneo la uwanja ule wakaanza kujipanga vilivyo kwani waliisikia sauti iliyokuwa ikitangaza kwamba ndege hiyo ndiyo iliyokuwa imembeba Tatiana aliyekuwa akifika nchini hapo kutokea nchini Marekani.
Waziri wa Wanawake Jinsia na Watoto, bi Paulina Gilbert ndiye aliyeandaliwa kwa ajili ya kumpokea mgeni huyo aliyezua gumzo kubwa duniani kwa kipindi hicho. Mara baada ya ndege kusimama katibu na kapeti jekundu likaandaliwa.
Tatiana aliyekuwa ndani hakuamini kile alichokuwa akikiona, hakuamini kama msichana yeye aliyekulia kijijini Chibe mkoani Shinyanga leo hii alikuwa akipokelewa kama kiongozi mkubwa duniani, alishindwa kuvumilia, akaanza kububujikwa na machozi tu.
“Usilie mpenzi,” alisema Buffet huku akimbeleza Tatiana.
“Sikutarajia jambo kama hili maishani mwangu, hii ni ndoto mpenzi,” alisema Tatiana huku akiendelea kububujikwa na machozi tu.
Mlango wa ndege ukafunguliwa, mtu wa kwanza kabisa kuteremka katika ndege alikuwa Tatiana. Machozi yaliendelea kumbubujika tu. Akaanza kuwapungia watu mikono huku akipiga hatua kuteremka ngazi.
Watu walioandaliwa kwa ajili ya kupiga ngoma za asili, wakaanza kupiga na kucheza kwa furaha huku wakirukaruka. Alipoteremka chini tu, tayari watoto waliokuwa na maua wakamgawia na kisha kusalimia na waziri huyo.
Alishindwa kujizuia, alimwambia waziri yule jinsi alivyokuwa akijisikia kipindi hicho. Bado aliendelea kusisitiza kwamba hakuamini kwani yale maisha aliyokuwa ameyapitia kipindi cha nyuma yalimuumiza mno.
Tatiana, Buffet na waziri wakaanza kupiga hatua kuelekea katika gari la wazi kisha kuingia na safari ya kuelekea katika Hoteli ya Blue Pearl iliyokuwa Ubungo kuanza. Njiani, Tatiana hakuamini, watu walikuwa wamejiopanga barabarani huku wakimpungia mkono, hakuamini kile alichokuwa akikiona, watu wengi walikuwa wamesimama pembezoni mwa barabara wakimpungia mkono kama alivyokuwa akifanya.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Barabara nzima ya Nyerere mpaka makutano ya Barabara ya Mandela, watu walikuwa wamejipanga barabarani tu huku wakiendelea kumpungia mkono kitu kilichoonekana kuwa kama ndoto machoni mwake.
Walikwenda kwa mwendo wa taratibu mpaka walipofika Ilala ambapo wakachukua Barabara ya Kawawa na walipofika Magomeni, wakachukua Barabara ya Morogoro na kuanza kuelekea Ubungo hotelini.
Kote huko, Watanzania walikuwa wamejazana barabarani, walikuwa wakimpungia mkono mwanamuziki aliyekuwa na jina kubwa ambaye alilipa sifa kubwa Taifa la Tanzania.
Walichukua dakika arobaini mpaka kufika Ubungo ambapo wakaingia hotelini na kisha kupumzika na siku iliyofuata, wakaelekea Ikulu kwa ajili ya kuonana na rais ambapo wakala chakula cha mchana na kesho yake kuanza safari ya kuelekea mkoani Shinyanga huku akiwa na furaha tele.
**** Peter hakuonyesha uoga wowote kwa kuamini kwamba ukweli ndiyo ungemfanya kuwa huru kuonana na binti huyo ambaye mpaka katika kipindi hicho hakujua kama alikuwepo au hakuwepo.
Mchungaji na mkewe walionekana kuwa katika hali ya sintofahamu, ilikuwaje mtu atoke Dar es Salaam na kwenda Morogoro kwa ajili ya binti yao? Walibaki wakimwangalia, Peter alizungumza kwa kujiamini sana, hiyo kidogo ikamfanya mchungaji na mkewe kuona kwamba mtu huyo alimaanisha alichokuwa akikisema.
Walichokifanya ni kumuita Lydia, msichana huyo alipofika sebuleni na macho yake kutua kwa Peter, akashtuka mno, hakuamini kumuona Peter nyumbani hapo, akajikuta akianza kutetemeka kwa hofu kwani alijua iwe isiwe aliitwa na wazazi wake kwa ajili ya kijana huyo.
Peter akaonyesha tabasamu pana, hakuamini kumuona msichana huyo mahali hapo, moyo wake ulikuwa majonzi kwa kipindi kirefu, ukafarijika, kumuona msichana huyo kukamtia nguvu.
“Abeee...” aliitikia Lydia mara baada ya kufika sebuleni hapo.
“Unamfahamu huyu kijana?” aliuliza baba yake.
“Ndiyo!”
“Unajua kwa nini yupo hapa?”
“Hapana baba!”
“Peter, hebu sema kwa nini upo hapa manake hata huyu uliyemfuata naye hajui kwa nini upo hapa,” alisema mchungaji Marcus.
Peter hakutaka kuficha lolote lile, alisafiri kwa umbali mrefu kwa ajili ya kumuona msichana huyo, hiyo ilikuwa nafasi pekee aliyokuwa nayo ambayo aliamini kwa vyovyote vile endapo angezungumza ukweli basi angeweza kuelewekana hivyo kuwa huru.
Alichokifanya ni kuanza kuhadithia kila kitu kilichotokea walipokuwa Dodoma, alipoanza kuzoeana na msichana huyo mpaka pale walipoanza kuwasuiliana kwenye simu. Hakutaka kuficha lolote lile, katika kipindi chote alichokuwa akisimulia, Lydia alikuwa akitetemeka tu huku wakati mwingine akitamani kumwambia Peter anyamaze lakini mwanaume huyo hakunyamaza, aliendelea kueleze huku mara kwa mara akimwangalia Lydia.
“Ninampenda Lydia, siwezi kuficha hisia zangu. Lengo langu si kumchezea, ninataka kumuoa, kila ninapomwangalia, naona kabisa yeye ni mwanamke wa maisha yangu. Nadhani Mungu alitukutanisha pale Dodoma kwa dhumuni maalumu la mimi na Lydia kufahamiana na hatimaye baadae kuwa mke na mume,” alisema Peter huku akiwaangalia wazazi hao.
“Ooppss...” mchungaji Marcus alishusha pumzi nzito.
“Mchungaji, huo ndiyo ukweli. Mimi si kijana mhuni, ninajiheshimu lakini nimeamua kuja hapa kwa kuwa sikutaka ukaribu na Lydia ufike mwisho kwa kuwa niliona mambo mengi yakiwa mbele yetu,” alisema Peter.
Kila sentensi aliyokuwa akizungumza mahali hapo ilikuwa kama msumari wa moto moyoni mwa msichana huyo, kila alipokuwa akimwangalia Peter, ujasiri aliokuwa nao, akajikuta akianza kuvutiwa naye kwani alionyesha kwamba yeye ni mwanaume asiyeogopa chochote kile na alijitoa kwa lolote lile.
Mchungaji Marcus na mkewe wakabaki wakiangaliana tu. Kijana aliyekuwa mbele yao hawakumfahamu kwa kumuona japokuwa walimfahamu sana baba yake. Hawakujua ni kitu gani walitakiwa kufanya kama wazazi.
“Subiri nimpigie simu baba yako,” alisema mchungaji Marcus, akachukua simu yake na kuanza kupiga.
Alitaka kuzungumza naye kama mzazi hivyo alichokifanya ni kuelekea chumbani. Mama mchungaji hakutaka kubaki sebuleni hapo, kama mzazi, naye alitaka kusikia kile ambacho wachungaji hao wangezungumza simuni. Sebuleni wakabaki wawili.
“Peter! Ndiyo umefanya nini?” aliuliza Lydia kwa sauti ya chini, alikuwa akilalamika.
“Nimefanya nilichofanya, unafikiri ningefanya nini?”
“Si ungenipigia simu!”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mara ngapi? Nimekupigia simu kila siku tena zaidi ya mara tatu, lakini simu zote haukuzipokea, nilikuandikia meseji lakini haukujibu hata moja, ulitaka nifanye nini?”
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment