Search This Blog

Thursday, July 21, 2022

MVUA YA HUBA - 5

 







    Simulizi : Mvua Ya Huba

    Sehemu Ya Tano (5)



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakamtaka afike kituoni kwa ajili ya mahojiano Zaidi pia wakawachukua raia wengine walioshuhudia lile tukio kwa ajili ya kutoa maelezo yao. Baada ya maelezo kukamilika wakamuachia Lucy na wengine warejee katika kaya zao. Lucy alielekea moja kwa moja hospitalini na kukuta bado hawajapatiwa matibabu, Lucy alishangazwa sana na uzembe ule uliokuwa ukiendelea. Akamchukua baba yake Luis na kumpeleka kwenye vipimo vya X-ray, baada ya muda mfupi majibu yakatoka na hakuitaji daktari kwani aliona mlolongo ni mrefu akaamua ayasome mwenyewe.



    Hali ya mzee yule haikuwa ya kuridhisha kwani kansa ilimtafuna na akawa yupo katika hatua za mwisho za uhai wake, hakuweza kupumua vizuri hivyo ikamlazimu apumue kwa msaada wa mashine ya oksijeni. Kwa upande wa Luis kipigo kilimfanya avunjike mkono wake wa kulia na mguu wake wa kushoto kuteuka huku mwili wake ukiwa na michubuko mingi.



    ******************



    “Inashangaza sana watu waliofanya huu uhalifu si majambazi kama tulivyozani kwani silaha walizotumia zinapatikana katika kitengo cha jeshi la polisi, sasa ni nani atakayekuwa nyuma ya huu mchezo mchafu!” alisema askari aliyepewa jukumu la kuifatilia kesi ile baada ya kukusanya maelezo ya mashuhuda nay eye mwenyewe kufika eneo la tukio.



    “kuna ulazima wa kumuhoji muhusika uhenda akawa na lolote la kuniambia litakalonisaidia kujua naanzia wapi” aliendelea kuongea mwenyewe askari huyo.

    Baada ya kufikiri kwa kina Zaidi akaamua kufunga safari hadi hospitali kuu ya Morogoro kwa dhumuni la kuhojiana na Luis pia na baba yake.



    ******************



    Lucy hakutaka kuondoka kando ya Luis, kijana aliyefanyiwa ukatili mbele ya macho yake, alijua fika kuwa yale yote yalitokea kwa sababu yake na alijua Izack ndiye muhusika wa yote ila hakuweza kumtaja kwa sababu hakuwa na ushahidi wa kutosha ukizingatia alishuhudia uovu kama ule ukitendeka miaka 1000 nyuma swala ambalo sio rahisi kwa vyombo vya dola kusadiki.



    Mama na baba yake Lucy wakapata taharifa juu ya tukio hilo nao kwa haraka wakelekea hospitali na kumkuta binti yao akiwa na huzuni mno. Mama alipomuona binti yake akiwa salama akamkumbatia kwa furaha sana,

    “Nafurahi kukuona ukiwa salama mwanangu”

    “Mama kwa haya yanayotokea siwezi kukaa kimya tena”

    “Mhmh! Unataka kusema nini wewe?” aliuliza baba yake Lucy.

    “Baba na mama naomba mnisikilize vizuri, polisi wakija kunihoji tena sitowaficha nitasema kuwa Izack ndiye muhusika wa yote”

    “Mhmh! Wewe mtoto umelukwa na akili? Izack ni mwanaume uliyempenda na anayekupenda, kijana wa watu mpole mstaharabu hawezi kufanya unyama huu” alisema mama yake Lucy.

    “Mama haya yanayotokea leo yalishanitokea miaka 1000 iliyopita na nimeelewa kwa nini Mungu alinipa nafasi ile, nitautafuta ushahidi na nitahakikisha Izack analipa uovu wote alioufanya juu ya maisha yangu” alisema Lucy.



    Mama yake Lucy hakusema kitu Zaidi ya kuhitaji kwenda kumuona Luis, machozi yakamtoka alipoona majeraha ya kijana yule. Alihisi maumivu makali sana moyoni mwake, tumbo likamkata mno,

    “Hisia hizi zina maana gani, Luis kwanini niwe hivi ninapoona majeraha yako?” alijiuliza mama yake Lucy hasipate jibu.



    Baada ya muda mfupi akaomba nafasi ya kwenda kumuona baba yake Luis, madaktari wakamruhusu na akaangia. Moyo ulilipuka kwa mshtuko baada ya macho yake kutua kwa mzee yule, akajikuta akiita jina lake.



    “John….! John.. Hapana huwezi kuwa ni wewe”



    Alisema mama yake Lucy huku akisogea karibu kilipokitanda cha baba yake Luis, alijikuta mwili ukiishiwa na nguvu, akamkumbatia na machozi yakamtiririka,

    “Siamini kama kukutana kwetu kumekuwa katika dakika hizi za mwisho za uhai wako, John amka basi uzungumze nami walau kidogo” alisema mama yake Lucy.



    Muda wote huo Lucy alikuwa nje akimtazama mama yake hasielewe amekutwa na nini hasa, akatamani kuingia lakini hakuweza maana ni mtu mmoja pekee aliyeruhusiwa kuingia ndani. Baba yake Lucy alikuwa karibu naye akiyashuhudia hayo,

    “Bahati haikuwa upande wao hata hivyo ni afadhali wao kukutana kipindi hiki kuliko wangeonana kabla” alisema baba yake Lucy huku akirudi kwenye benchi na kukaa.

    Kauli hiyo ikamzidishia udadisi Lucy, akatamani kujua kuna lipi ambalo yeye alifahamu kuhusu baba yake Luis na mama yake. Na kwanini baba yake aseme kauli ile na kutoka nje bila kufanya lolote. Lucy akatamani kuyajua hayo yote,

    “Nitamuuliza mama akitoka” alisema nafsini mwake.

    “John ulikua wapi kipindi chote hiko, kwanini hukunitafuta, bora ufe tu umenitenda vibaya sana” alisema mama yake Lucy na kutoka nje ya chumba hiko huku bado akilia.



    Lucy alipomtazama mama yake akashindwa kumuuliza lolote Zaidi ya kumkumbatia na kumtaka atulie, mama alilia kwa uchungu mno. Baba yake Lucy alionekana mwenye kuhuzunika pia na wala hakutaka kuliingilia swala lile.



    **************

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya saa kadhaa kupita Luis akarejesha fahamu na kukuta amefungwa hogo kwenye mkono wake uliovunjika, akajaribu kuinuka kitandani lakini akashindwa kutokana na maumivu aliyoyasikia. Akaomba msaada kwa mmoja kati ya wauguzi walio katika wodi hiyo naye akaridhia kumsaidia. Akamwina na kumwekea mto mgongoni uliomsaidia kukaa vyema,

    “Natamani kujua hali ya baba yangu” alisema Luis.

    “Aah! Hali ya baba inaendelea vizuri tuu na nimeona kuna watu wakimtazama” alisema muuguzi yule wakike ambaye aliwafahamu vizuri Luis na baba yake.

    “Naweza kwenda kumuona”

    “Pumzika kidogo! Baadae nitakupeleka” alijibu muuguzi.

    Luis akaridhia na kuendelea kukaa kitandani pale, mawazo mengi yakamsonga hasa juu ya tukio lile la kutaka kukatishwa uhai wake.

    “Naitwa Inspekta Mtambalike, nimepewa jukumu la kuifatilia kesi hii na kuwatia hatiani wahusika, hivyo nategemea ushirikiano mkubwa toka kwako” alisema askari huyo baada ya kufika alipo na Luis.

    “Nashukuru sana Inspekta”

    “Nimefatilia vitu vingi kukuhusu lakini sijaona kama unamali nyingi kiasi cha kuvamiwa na majambazi au una uadui na mtu yeyote?” aliuliza Inspekta Mtambalike.

    “Hata mimi najiuliza sana kuhusu jambo hilo, ila kiukweli nimekuwa nikipokea sana simu ya vitisho inayonitaka nikae mbali na Lucy” alisema Luis.



    Kufikia hapo Inspekta Mtambalike akamzuia Luis kuendelea kuongea kisha akatazama sana ile wodi na kuhisi kama kuna watu wanaofatilia maongezi yale. Akasimama kisha akaenda ilipo ofisi ndogo ya waaguzi.

    “Naomba kuonana na daktari wa zamu” alisema Inspekta.



    Wahuguzi wakampa maelekezo naye akaenda na baada ya dakika takribani ishirini akarejea pale ilipo ofisi ya wauguzi,

    “Mimi ni Inspekta nina jukumu zito linalohusu usalama wa huyu kijana na familia hivyo nimepewa kibali cha kumuhamisha huyu na kumuweka katika chumba cha peke yake” alisema Mtambalike huku akiwaonesha karatasi iliyothibitisha maelezo yake.



    Wahuguzi wakaridhia na kucukua kiti cha magurudumu kisha wakamuamisha Luis kama maelekezo yalivyosema. Njiani wakakutana na Lucy ambaye alishtuka kidogo kuona hali ile, Inspekta akawa wakwanza kumsemesha Lucy



    “Upepo sio mzuri imenilazimu kumuamisha hili kuhakikisha usalama wake Zaidi”

    Lucy akamuelewa Inspekta na kuungana naye katika safari hiyo hadi alipohakikisha kuwa Luis amepatiwa chumba kingine na mazingira yako salama. Inspekta akamuangalia Lucy na kumuomba ampishe maana ana maongezi nyeti sana na Luis.



    ***********************



    Lucy akaamua kurejea alipo mama yake ila hakumkuta pale alipomuacha akatazama ndani ya chumba alicholazwa baba yake Luis akamkuta akiwa amekumbatia mzee yule huku akilia mno. Akatazama alipokaa baba yake lakini hakumuona. Hakuelewa uhusiano ulipo kati ya watatu wale yaani baba yake, mama yake na baba yake Luis.



    “Nahisi kuna kitu kinaendelea kati yao, lazima nimuulize mama” alisema Luis.



    Muda huohuo daktari akampita na kuingia chumba kile alicholazwa baba yake Luis kisha akamtaka mama yake Lucy atoke nje ili ampe nafasi yakumtabibu Zaidi. Mama yake Lucy alipotoka nje akatazama na bintiye nakugundua kuwa binti yake ana maswali mengi ya kumuuliza. Akamsogelea na kumshika mkono kisha akatoka naye nje na kukaa kwenye moja kati ya bustani zilizoizunguka hospitali hiyo,



    “Najua mwanangu unamaswali mengi yakujiuliza juu ya hili, ila naweza kukuelezea kwa ufupi tuu na naamini utanielewa kwa kuwa wewe pia ni mtoto wa kike. Miaka mingi iliyopita John ambaye ni baba yake Luis kwa sasa ndiye mwanaume niliyempenda na niliyetamani kuolewa naye. Mapenzi yetu yalichanua na kupendeza sana kama ua la uwaridi, yaling’aa kama mwezi mpevu na kupendeza mithiri ya upinde wa mvua. Hakuna aliyeamini kama itafika siku wawili sisi tukatengana, baba yangu ambaye ndiye marehemu babu yako hakutaka kumuona wala kumsikia Luis aliandaa ndoa kati yangu na baba yako kwa kuwa familia zetu zilikua na ukaribu mno. Nilijaribu kwa kila namna kuipinga ndoa ile lakini sikuwa na mtutu yeyote aliyeniunga mkono na hii ni kwa sababu baba John hakuwa na uwezo mkubwa wa kifedha kama ilivyokuwa kwa baba yako.



    John hakuwahi kunijua kimwili tulihaidiana hadi siku tutakapofunga ndoa ndiyo itakuwa nafasi yetu ya kufanya kila kitu ambacho miili yetu ilihitaji. John alinieshimu na kutunza makubaliano yale japo kuna wakati nilishindwa kujizuia lakini yeye alikuwa wa kwanza kunirudisha katika njia iliyo sahihi.



    Nilipata wakati mgumu mno kumueleza John kuwa nimepangiwa kuolewa na mwanaume mwingine, nilikosa ujasiri lakini john aliyajua yote japo hakusadiki, kipindi kile hakukuwa na simu Zaidi ya kuandikiana barua, john alisubiri kusikia kutoka katika kinywa change. Juma moja kabla ya ndoa yangu niliamua kutoroka nyumbani na kwenda kwa kina John, nilimkuta akiwa mwenye kuhuzunika mno nikamkumbatia na kutotamani kutoka mikononi mwake. Usiku huo sikujali tena kuhusu makubaliano tuliyoyaweka nilitamani yeye pekee awe mwanaume wa kwanza kuujua mwili wangu…..



    Hadi kufikia hapo mama yake Lucy akashindwa kuendelea kuongea machozi yakamtiririka mithili ya maji yatokayo mlimani. Lucy akamkumbatia mama yake huku akiwa na shauku kubwa la kujua nini kiliendelea usiku ule,



    “Basi mama usilie ni jambo la kumshukuru Mungu kuwa walau umepata nafasi ya kumuona katika siku zake hizi za mwisho”

    “Mwanangu hivi ni kweli hamna nama yeyote ya kufanya ili yeye apone”

    “Tumuombe Mungu tuu mama naamini ataonesha ukuu wake” alisema Lucy.



    ************

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya matukio ya siku hiyo baba yake Lucy hakuweza kurejea nyumbani kama ilivyokawaida yake siku hiyo aliamua kupitia bar ili kutuliza mawazo.

    “Miongo miwili imepita sasa nilijua haupo katika hii dunia lakini katika hali ya kutoitarajia umetokea na kuchukua kile ulichostahili, sikutarajia kama moyo wa mwanamke huu utakuwa bado ukidunda juu yako nifanye nini sasa! Mimi ni mume halali kisheria lakini bado sijawa na umiliki timilifu wa moyo wake” alisema baba yake Lucy huku akizidi kufakamia bilauri iliyojaa pombe kali.



    Japo baba yake Lucy alimpenda sana mkewe lakini alikiri kuingilia kati mapenzi yale. Alijitahidi kuwazuia wawili wale wasionane lakini ya Mungu mengi wameonana katika kipindi ambacho mmoja anapambania uhai wake.

    “Nimefanya makosa mengi sana katika maisha yangu, najua John unasiku nyingi katika dunia hii, sitowazuia tena namuacha awe karibu yako. Pia ni njia ya kukuomba radhi na usije ukaondoka ukiwa bado hujanisamehe”

    Aliendelea kuongea pasi na kuwa na mtu yeyote aliyemsikiliza, Muda ulizidi kuyoyoma mwishoe akaamua arejee nyumbani akapumzishe mwili na akili yake.



    *************



    Inspekta Mtambalike akafanya mahojiano ya kina na Luis na alipojiridhisha akafunga mjadala na kumuahidi Luis kuwa atafatilia na kuhakikisha mtuhumiwa amafikishwa panapostahili bila kuzingatia wazfa au uwezo aliokuwa nao, pia akamtaadharisha juu ya watu watakaokuja kumtazama na hata watoa huduma wa apo akimaanisha wahuguzi na madaktari. Luis akaupokea ushauri wa Inspekta na kuahidi kuufanyia kazi.



    *************



    “Mama muda umeenda mno twende nyumbani ukapumzike kesho asubuhi tutakuja kuangalia hali zao” alisema Lucy.

    “Nenda tuu Lucy siwezi kumuacha baba yako katika hali ile”

    “Mhmh! Mama baba mbona alishaenda nyumbani muda mrefu na hatojisikia vyema kama hautorejea”

    “Lucy mwanangu nisamehe sana!”

    “kwa kosa lipi mama?”

    “Baba yako mzazi ni huyo anayepigania uhai wake uko ndani, yule aliyekulea siye”



    Kauli hiyo ikamvunja nguvu Zaidi lucy hakuamini kama alifichwa siri nzito ile kwa Zaidi ya miaka ishirini na mitano. Toka alipozaliwa hadi alipoolewa aliamini kuwa Thomas ndiye baba yake mzazi, hakujua acheke au alie, hakujua afurahi au akasirike. Akahisi labda mama yake hataki kuondoka hospital ndiyo maana akaamua amwambie maneno yale,

    “Mama huu si wakati wa kutaniana”

    “Sikutanii Lucy, ukweli usiku ule mmoja tuu niliweza kushika ujauzito”

    “Je! Baba anajua kuwa mimi si damu yake”

    “Baba yako anajua kila kitu, akakubali kuilea Mimba ile kuificha aibu ya familia yangu. Nikajifungua mapacha watatu wawili wakafariki pindi tu nilipojifungua na mmoja uliyesalia ndiye wewe Lucy wangu” alisema mama yake Lucy huku machozi yakimtiririka.



    Lucy naye akashindwa kuzuia hisia zake machozi yakamtiririka kwanza kwa kupoteza ndugu zake hasiowajua pili kwa mama yake aliyepitia changamoto nyingi hadi wakati huo.



    “Nilijua mvua ya huba uwanyeshea vijana mamboleo tuu kumbe hata vijana wa kale wameloeshwa na kushindwa kukaushwa hata kwa joto la jua. Sijui baba yangu anajisikiaje huko nyumbani na huyu anayeumwa sasa sijui aliishi vipi bila ya kuwa na mtu anayempenda. Ila Luis yupo naamini aliweza kumsahau mama yangu na kuzaa na mwanamke mwingine, kwa nini mama naye hawezi kumsahau mhmhm! Huba”

    Alisema Lucy kimoyomoyo huku akiwa amemkumbatia mama yake ambaye macho yake yalivimba na uso kuloana kwa machozi.



    “Pamoja na hayo yote bado Thomas atabaki kuwa baba yako, amejitoa kwa vingi mno na mimi nitaendelea kuwa mkewe, twende nyumbani mwanangu”



    Alisema mama yake Lucy na kuinuka mahala pale, Lucy akamuacha mama yake na kwenda hadi kilipo chumba alicholazwa baba yake, hakuweza kuingia ndani maana muda wa kuona wagonjwa ulishapita akamtazama kwa dirishani.

    “Mungu akupe nguvu baba yangu walau nipate nafasi ya kufurahi nawewe kunitambua mimi kama binti yako” alisema Lucy huku machozi yakimtoka.



    *************



    Lucy na mama yake wakarejea nyumbani na kumkuta baba yake akiwa amelewa mno, haikuwa hali ya kawaida katika nyumba hiyo. Mzee Thomas hakuipenda pombe na aliwasisitizia watoto zake kuwa wasishawishike kutumia kinywaji hiko kwani ni kichocheo hasi kwa maendeleo. Lucy hakuwai kuipinga au kwenda kinyume na kauli hiyo ya baba yake maana yeye ni daktari na anajua vizuri matokeo ya matumizi mabaya ya kinywaji hiko.



    “Yamekusibu yapi baba Lucy, hadi kuwa katika hali hiyo?” aliuliza mama Lucy kwa mshangao sana.



    Baba yake Lucy hakusema lolote Zaidi ya kucheka na kumwangalia bintiye ambaye alikuwa akilia muda wote,

    “Bila shaka umeshajua kuwa mimi siye baba yako, je utanitelekeza?” alisema baba Lucy.



    Lucy kusikia vile akakimbia na kumkumbatia baba yake huku akilia mno, mzee Thomas naye akashindwa kujizua akajikuta akilia, mama yake Lucy pia akaungana nao.



    “Msije mkaniacha upweke maana sijui kama nitaweza kuishi, Lucy tusamehe sana kwa kukuficha hili jambo, siwezi kukunyang’anya haki ya kumtambua au kuwa karibu na baba yako. Mama Lucy mke wangu wewe pia siwezi tena kuzuia nafasi aliyonayo John moyoni mwako, kwa kipindi hiki ambacho yeye yu hoi kitandani ninyi wawili muwe faraja kwake” alisema baba yake Lucy.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Tulimpokea Luis na kumfanya kama mwanetu bila kujua yeye ndiye daraja la kukumbuka ya kale tukamfukuza kama paka aliyekula mboga, nitamuomba radhi naamini atatuelewa japo siye mama yake wa kumzaa nitayafanya yote kama mzazi. Thomas hatutoweza kukutenga kwangu utabaki kuwa kama mume na baba wa Lucy” alisema mama Lucy.



    Baada ya hayo kila mtu akaelekea chumbani kwake kwa ajili ya kupumzika japo mawazo hayakuisha vichwani mwao.





    “Mkuu swala la kesi ya marehemu meja jenerali limekuwa gumu, nafikiri hatuwezi kumlinda muhusika maana juzi tuu hapa amefanya tukio la ajabu tena kwa kutumia silaha za jeshi” alisema Chodo.

    Izack alikuwa na mahusiano mazuri na makubwa na maafisa mbalimbali wa jeshi. Akatumia mahusiano yale vibaya kwa kuvunja sheria za nchi huku akiamini kulindwa na wenzake.

    “Kesi hii imefikia hatua gani?”

    “Mara kwanza ulinipa jukumu la kuinyakua kesi hii toka kwa yule askari wa usalama barabarani ambaye alikuwa na ushahidi wa kutosha, kwa sasa kesi hii ipo mikononi mwa Inspekta kijana na makini Zaidi anayeitwa Mtambalike. Nahofu huyu anaweza akaanika ukweli wazi na ikawa shida Zaidi upande wetu” alisema Chodo.

    “Izack anawezaje kufanya mambo ya kitoto hivi! Lazima tumuwajibishe”

    “Mkuu kumbuka baba yake ni Captain mstaafu, mtu aliyepigania uhuru hata vita dhidi ya Idi Amin dada, sitaki kuishuhudia aibu itakayomkumba akijua uovu wa kijana wake, nashauri ukamshirikishe juu ya hili tuone anasemaje kabla hatujafanya lolote” alisema chodo.

    “Sawa kwa sasa endelea kuwa kimya na makini nitalifanyia kazi hili na kesho jioni kabla sijaondoka uje ofisini kwangu”

    “Sawa mkuu” alisema Chodo kasha akapiga saluti na kuondoka eneo hilo.

    *********

    Izack alitamani sana kuonana na Lucy hakujua kuwa malipo ya uovu wake yamekaribia, akaamua kwenda nyumbani kwa kina Lucy lakini alipofika aliambiwa kuwa Lucy na mama yake wameenda kutazama mgonjwa hospital. Akafunga safari hadi hospital kuu ya mji wa Morogoro ambapo ndipo alipoelekezwa kuwa Lucy ameenda. Alipofika kwa bahati akamuona Lucy akiwa anaendesha kiti cha magurudumu, alipotazama vizuri akagundua kuwa alikuwa Luis, moyo ulimuuma mno akajikuta akijawa na ghazabu sana.

    “Inamaana huyu mwanaharamu hajakoma tuu, sasa nitahakikisha anatoweka kabisa katika dunia hii” alisema Izack kwa hasira.

    Akaamua aondoke bila kutimiza Lengo Lake, wakati anaondoka Lucy akatazama upande ule aliokuwa izack akabahatika kumuona. Moyo ulilipuka kwa hofu akahisi usalama ni mdogo sana kwa Luis kuwa eneo hilo, kwa haraka akageuza kiti kile cha magurudumu hadi kilipo chumba chake.

    “Hali ni njema kwa sasa na leo hii nitaruhusiwa” alisema Luis baada ya kufika katika chumba alichopangiwa.

    “Nahofia sana kuhusu usalama wako hata kama utaruhusiwa sitotaka urejee kwenu” alisema Lucy.

    “Sina pa kwenda Lucy mtu pekee ninayemfahamu ni baba yangu hadi kufika umri huu sikubahatika kuonana na ndugu yeyote, yeye ni kila kitu kwangu” alijibu Luis.

    “Nitaongea na mama ukaishi kwetu”

    “Hapana usifanye hivyo sitaki kuwa mzigo kwenu” alijibu Luis huku hakujua kilichokuwa kikiendelea nyuma ya pazia.

    Lucy akatamani kumwambia Luis kuwa wao ni ndugu wa damu ambao wamechangia baba lakini alikosa ujasiri wa kusema jambo hilo.

    ****************

    Katika chumba cha wagonjwa mahututi ambapo baba yake Luis amelazwa huku mama yake Lucy akiwa pembeni. Baba huyo akafumbua macho yake na kumuona mama yake Lucy, hakuamini hata kidogo na hakuelewa alikua mahala gani,

    “Rozina siamini kama ningekuona ahera” alisema baba yake Luis kwa sauti ya kukwamakwama.

    “John hujafa! Bado unaishi na hapa upo hospitali”

    Kauli ile ikafnya mzee yule kutazama vizuri eneo lile ili kuthibitisha kile alichokisia masikioni kwake, akatulia kwa dakika kadhaa kuupa nafasi ubongo wake kukusanya kumbukumbu vizuri. Baada ya muda mfupi akainuka huku mama yake Lucy akimsaidia kumuwekea mto mgongoni,

    “Luis yuko wapi?” akauliza mzee huyo.

    “Usijali kuhusu yeye, anaendelea vizuri tuu”

    “Mwanangu kweli hawajamuumiza naomba uniitie nimuone” alisema baba yake Luis.

    Mama yake lucy akatuma ujumbe wa wito ule kupitia mmoja wa wahuguzi wa zamu. Taharifa ikafika na Luis akiwa katika kiti cha magurudumu kilichoendeshwa na lucy wakaanza safari ya kuelekea chumba alichopo baba yake.

    “Rozina japo umri umeenda lakini uzuri wako bado upo palepale, naamini umeishi vyema na kuifurahia ndoa yako” alisema baba yake Luis.

    Mama yake Luis akasogea na kumkumbatia huku machozi yakimbubujika,

    “Kwanini uliamua kukaa kimya bila kunitafuta, kila siku nilitamani nikuone na kukwambia ni kiasi gani nakupenda”

    “Naelewa hisia zako ila bado wewe ni mke wa Thomas na utaendelea kuwa hivyo, nashukuru Mungu kwa kunipa nafasi wala ya dakika chache kuonana nawewe, Ukweli ulikuwa ukiishi nami siku zote za maisha yangu. Nilikuja kushuhudia ndoa yako na pale ulipokubali kumpokea Thomas kama mume wako katika kila hali ndipo nilipoamini mwisho wa mapenzi yetu umefika. Baadae nikasikia umeshika ujauzito sikuacha kukufatilia nilihakikisha nakuona japo kwa mbali na hata siku unajifungua watoto watatu kwa pamoja nilikwepo pale……

    Hadi kufika hapo akashindwa kuendelea kuongea wote wakajikuta wakilia kwa uchungu mno, baba yake Luis akatumia kiganja chake cha mkono kumfuta mama yake Lucy machozi. Kisha akaendelea kuzungumza,

    “Rozina nilishuhudia mtoto wako mmoja akipata shida madaktari waliangaika lakini hawakuweza kunusuru uhai wake, wakabaki watoto wawili ambapo mmoja alikuwa ni wakiume na mwingine ni wakike, nikamuhonga muhuguzi na akanipatia mtoto yule wa kiume nikajipiza kumlea na kumfanya awe mtu mkubwa katika nchi hii lakini nafikiri Mungu amenihukumu kwa kunipa ugonjwa huu”

    Kauli hii ikamfanya Luis ainuke katika kiti kile cha magurudumu, hakusikia tena maumivu ya mguu akajikuta akilia huku akisogea alipo baba yake, huku akilia.

    “Hivyo Luis siyo mwanangu wa damu ila nilimnyang’anya toka mikononi mwako na kumfanya awe mwanangu nikiwa na nia ya kutolisahau penzi lako daima”

    Mama Lucy hakuelewa aseme nini Zaidi ya kulia, Luis ambaye alishindwa kutembea kwa sababu ya maumivu ya mguu alijawa na nguvu na kumtazama baba yake. Baba alipomuona mwanaye akatabasamu kisha akamwambia,

    “Mwanangu ulikuwa ukinisumbua kuhusu mama yako na familia yako kwa ujumla, huyu mwanamke hapa ndiye mama yako mzazi na mume wake ndiye baba yako mzazi” Alisema baba yake Luis huku akiwa hajui kama wote wale ni watoto wake wa damu.

    Mama yake Lucy akainuka na kumkumbatia Luis kasha akamuita na Lucy na kuwakumbatia kwa pamoja. Akamtazama John ambaye alikuwa pale kitandani akitabasamu kuhufurahia muungano ule.

    “Sasa ninaweza kupumzika kwa Amani” alisema baba yake Luis.



    “Hapana John! Huwezi kwenda na kuwaacha wanao! Unaukumbuka usiku ule niliotoroka kwetu na kuja kwako, usiku ule ndio uliowaleta hawa wawili hivyo Lucy na Luis ni wanao wadamu”

    Mzee john aliposikia ilo akacheka sana, furaha yake haikuwa na kipimo akanyoosha mikono yake kutaka wanae wamsogelee na kumkumbatia pasi na kuchelewa wote wawili wakafanya hivyo. Akamtazama mama yake Lucy na kumwambia,

    “Watunze wanangu na Luis huyu ni dada yako mlinde kwa nguvu zako zote”

    Kisha papo hapo mwili wake ukaishiwa nguvu, macho yakazingira na giza kuu, mapigo ya moyo yakapungua na taratibu pumzi zikakata.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Baba mbona umelala bila kuuliza mwanao nimepitia mangapi katika maisha yangu, amka basi baba” alisema Lucy huku machozi yakimtoka.



    Mama Lucy alivyoona hivyo nguvu zikamuisha naye akajikuta akianguka chini na kupoteza fahamu. Kwa kweli siku hii ilikuwa ya furaha nay a kuhuzunisha sana kwa wanafamilia wale, Luis hakuamini kama baba yake angemuacha katika wakati ule. Alitambua kuwa yeye ndiye mtoto wa kiume pekee, ikamlazimu kujikaza na kutoa taharifa kwa daktari. Akamchukua Lucy ambaye ni dada yake kwa sasa na mama yake akawekewa dripu ya maji maana presha ilipanda mno.



    “Mungu hunitendei haki mimi! Kila siku unanipa matatizo mazito nisiyoweza kuyastahimili sikuweza kufurahi na mume wangu katika dunia hii na hata ile ya miaka 1000 nyuma, leo umeninyima hata dakika 1 ya kufurahi na baba yangu. Siwezi kustahimili nichukue na mimi nije huko huko” alisema Lucy kwa uchungu mkubwa mno.



    Japo Luis alikuwa katika uchungu mzito wa kumpoteza baba yake ambaye kwake mbali na kuwa baba alikuwa kama rafiki na mshauri. Alijikaza kiume na kumbembeleza dada yake, dakika chache baadae mama yao akarejewa fahamu. Luis akaona hamna sababu za wao kubaki hospitali hapo, akahakikisha mwili wa baba yake umehifadhiwa vizuri kasha akarejea nyumbani na kutoa taharifa kwa majirani. Watu waliguswa sana na kifo cha baba yake Luis wakubwa kwa wadogo wakashirikiana katika shughuli zote za maandalizi ya mazishi.



    **************



    “Mnawezaje kuvumilia upuuzi huu, tumekula kiapo cha kulinda usalama wa taifa letu wananchi wakiwemo na si kuwa sababu ya mateso juu yao, sijali uhusiano ulipo kati yangu na Izack fanyeni kama sharia inavyosema mtatunukiwa tuzo ya heshima kuliko kumlinda mwishoe mkaridharaulisha jeshi letu” alisema baba yake izack baada kupokea maelezo ya uchunguzi juu ya uhalifu wa Izack.



    “Sawa mkuu tutafanya hivyo”



    Izack aliweka mashushu kila kona hivyo kila kilichoendelea akawa anakijua isipokuwa tuu uamuzi uliofikiwa na wakuu wa jeshi hakuwa bado anaufahamu. Roho ya mauaji ikazidi kumuandama akaita kikosi chake na kwenda nacho sehemu ambayo yeye aliona ina usalama.

    “Hali si shwari kabisa sasa nawaagiza mkakate mzizi wa tatizo hili, nahitaji Inspekta mtambalike auawe pia Luis naye afate nyayo za baba yake”

    “Mkuu tunahitaji kujipanga kwa siku chache hatuwezi kulitimiza hilo kwa kukurupuka” alisema mmoja kati ya majambazi anaowatumia Izack.



    Izack akachukia mno akachomoa bastola yake na kumpiga risasi ya mguu kijana yule, wote wakajawa na hofu na kurudi hatua moja nyuma.



    “Sitaki kauli za uoga nilichoagiza lazima kifanyike leo hii”



    Alipokwisha maliza kuzungumza hilo akashtushwa na sauti ya mkuu wa kitengo chao, alipotazama akakuta wamezungukwa pande zote kisha mmoja kati yao akatoa kifaa kidogo kilichotumika kunasa sauti hivyo maongezi yote yalisikika vilivyo. Mkuu akaamuru Izack akamatwe na kupelekwa katika jera ya kijeshi huku akitumikia adhabu kali hadi pale kesi yake itakapo fikishwa mahakamani.



    *********



    “Akhsante sana kwa ushirikiano wako Inspekta tutahakikisha mtuhumiwa anafikisha katika sehemu husika” alisema Chodo huku akimkabidhi ushahidi uliokuwa mikononi mwake.

    “Hatuna haja ya kukawia lazima afikishwe mahakamani na kusomewa mashtaka yake na nafikiri mngeliachia jeshi la polisi kumalizia sehemu iliyobaki” alisema Inspekta Mtambalike.



    Wazazi wa Lucas wakapokea taharifa juu ya kupatikana muhalifu aliyesababisha kifo cha mtoto wao, walipotajiwa jina hawakuamini kama ni Izack aliyefanya hayo yote,

    “Maskini Lucy sijui atafanyaje endapo atagundua mwanaume anayetaka kuolewa naye ndiye muuaji na chanzo cha mateso yote aliyopitia” alisema mama yake Lucas.

    “Kiukweli ni jambo zito sana ila naamini atalimudu” alijibu baba yake Lucas.



    **********



    Taratibu za mazishi zikakamilika hatimaye Luis akiwa na dada yake Lucy pamoja na mama yao wakafanikisha kumsindikiza mzee huyo katika safari yake ya mwisho. Baba yake Luis hakuwa mbali aliungana nao katika swala hilo zito.



    Baada ya Juma moja kupita Inspekta Mtambalike akafika nyumbani kwa kina Lucy na kuweka wazi kila kitu, baba na mama yake Lucy wakashangaa sana kusikia Izack anahusika katika mchezo huo mchafu. Wakayakumbuka maneno ya Luis na wakaona hawakufanya jambo jema, wakamuita na kumuelezea kila kitu kisha wakamuomba radhi. Luis hakuwa na kinyongo aliwasemehe.

    “Luis mwanzo nilikuita mwanangu japo sikujua kama itafika siku na wewe kuwa mwanangu wa kuzaa, nimefurahi sana najua baba yako ndiyo kila kitu kwako ila kwa sasa nayabeba majukumu yote kama mama na huyu mchukulie kama ulivyokuwa unamuona baba yako mzazi” alisema mama yake Lucy.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Luis alifurahi mno kuungana na familia hiyo, Maisha mapya yakaanza huku Lucy akirejea katika kazi yake ya utabibu na Luis akifanya mziki. Hakika kila jambo linalotokea mungu anamakusudi nalo japo binadamu tumekuwa tukijisahau na kutoa lawama kwa Mungu kwa nini ametufanyia hivi au vile. Nguvu ya mapenzi ni kubwa kuliko tuifikiliavyo mapenzi yanaweza mbadilisha jambazi akawa mlokole na hata mlokole akawa Jambazi.



    *MWISHO*

0 comments:

Post a Comment

Blog