Search This Blog

Thursday, July 21, 2022

PENZI LA FUKARA MATESO - 2

 










    Simulizi : Penzi La Fukara Mateso

    Sehmu Ya Pili (2)





    fahamu zikamrejea akamsimulia kila kitu yule mtu naye yule mtu akaanza kumsimulia historia ya maisha yake mpaka akaweka kambi msituni.alianza kwa kujitambulisha.....

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "jina langu naitwa JAFETH KIKO,ni mzaliwa wa mkoa wa ARUSHA,mimi na wenzangu watano ambao kwa sasa ni marehemu tulijiunga na jeshi la jwtz tulivumilia mateso,fedheha manyanyaso katika mafunzo yetu mpaka tukamaliza! tatizo ilikuwa ile siku ya kupokea vyeti! tukaitwa mbele na kuambiwa kwa ukiukwaji wa mafunzo atutopatiwa vyeti na ndo tumefukuzwa rasmi,tulishindwa kuyazuia machozi kutudondoka! je tungeweka wapi macho yetu.wenzetu wanaanza ajira siye tunarudi nyumbani! kwa kosa lipi tulilofanya? atukuwa na budi kutihi sheria bila shurti...



    tukaingizwa kwenye gari la jeshi tukaja kubwagwa mjini ARUSHA.sote watano atukukubali kurudi nyumbani kwa kuwa kila mtu alikuwa na fungu la maana kwenye akaunti yake tukatafuta silaha,tukapata kambi.tukafanya kazi ya ujambazi,tulionesha uwezo mkubwa mpaka pale tulipobainika na serikali basi tukaanza kuwindwa mmoja mmoja na kuuwawa.mpaka nilipobakia mwenyewe ndo nkatorokea huku....huu ni mwaka wa saba naishi humu.najuana na maaskari wa porini "tanapa" hivyo kuniwezesha kuishi kwa amani.

    Baada ya mzee yule kumaliza stori yake ilomsisimua ZUBER akanyanyuka na kutoka na shoka.





    ZUBERI akamwangalia mzee yule kwa tabasamu akaubetua mdomo wake!



    "we mzee mtata! na hilo shoka umelipata wapi porini huku?"



    "mjeda ashindwi kitu wacha nikapasue kuni! malizia hapo uje unsaidie kubeba kuni ntakuwa hapo minyarani!"



    akajitapa kidogo mzee yule na kuendelea na safari,



    akimwacha ZUBER akiendelea kula nyama ile ya kuchoma...



    katu akujua hatari ilokuwa mbele yake na laiti kama angejua asingeenda...



    Kundi lile la watu sita liliiendelea na safari katika msitu ule kwa msako wao!,



    kikundi cha watu wale kilizidi kusonga mbele wakiwa sasa wamemaliza wiki tatu bila mafanikio yeyote,



    katu hawakutakiwa kukata tamaa



    wakasonga!



    kitu pesa ndicho kilichotawala katika fikra zao yakinifu, wakati wakiwa wanaendelea na mwendo ghafla wakasikia sauti kama ya kukatwa kuni.



    -umakini baina yao ukaongezeka

    wakaanza kunyata kwa umakini kuelekea kule sauti ilipotokea,



    mori,hari na muamko wa kumtia zuber mkononi ukiwa umeongezeka mara dufu.



    mzee JAPHET aliendelea kukata kuni,bila ya wasiwasi wowote,katu hakuijua hatari kubwa ilokuwa mbele yake.



    bastola yake GOBOLE lilikuwa begani.lau angetambua ujio wa majambazi wale angesitisha zoezi lile lakini akujua chochote tayari alishazingirwa.



    akastushwa na sauti kali,sauti ilotawaliwa na amri!



    "kwa mwendelezo hai wa maisha yako weka silaha chini,tofauti na ivyo,twautawanisha ubongo wako kwa risasi uwe chakula cha wanyama."



    mzee akaganda kwa haraka akatembeza macho kwa watu wale.



    wote walikamata bastola kubwa za kivita.



    ashhh!!! bila shaka ni wanausalama nimeingia mtegoni maskini mie ila lazima nifanye kitu!



    wazo hilo likapita katika kichwa chake akifikiria kwa haraka cha kufanya ghafla risasi zikachimbika pembeni ya miguu yake,



    akatii sheria na kuweka silaha chini,usoni mwa viumbe wale akukuwa na mzaha ata chembe.



    wakatoa picha ya ZUBER na kumuonesha mzee yule.



    mzee akashtuka,mshtuko ulosomwa na majambaz wale wakautafsiri ilivyotakiwa kutafsiriwa.



    kabla mzee japhet ajajibu kitu risasi zikatua katika mguu wake!.....



    Risasi ile alopigwa mguuni ilimfanya mzee JAPHET aachiye yowe,lakini majambazi wale awakuacha wakaendelea kumtembezea kipigo,wakimshurutisha awapeleke nyumbani kwake.



    Walijua kwa vyovyote atakuwa kamuifadhi ZUBERI



    Awakukosea



    mwishowe kabisa mzee JAPHET akakubali akipanga kuwapeleka eneo lingine tofauti na lile

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *******



    ZUBERI baada ya kumaliza kula,akajinyanyua tayari kwenda maeneo ya minyarani.



    kwa lengo la kumsaidia mzee yule kuni,



    mdomoni alipiga mluzi mdogo ambao aukuweza kujulikana ni mluzi wa wimbo gani!,



    ghafla akashtushwa na mlio wa risasi kwa mbali akatabasamu

    sijui huyo atakuwa digidigi,swala,puma au sungura?



    mzee kamdedisha wazo lile likapita kichwani kwake likiongezwa na kuongezeka kwa mwendo wake.



    ghafla akashtushwa na kilio kwa mbali.



    Kwa haraka ZUBER bila kujielewa akaunyanyua mguu wake na kuutupa mbele kwa haraka akaunyanyua tena na kuutupa mbele huku akihema.



    alikuwa akikimbia...



    akiikimbilia hatari! tena kwa spidi kali!



    baada ya kukimbia kidogo akashtuka baada ya kuiona damu chini!,shoka aliloondoka nalo babu yake alopenda kumwita kamanda likiwa chini alipoigusa damu ile aikumpa tabu kugundua kuwa ni damu ya mtu!...



    mbaya zaidi akaanza kuifata ile damu taratibu,umakini na woga ukiutawala moyo wake



    lakini umakini huo ulifunikwa na umakini wa kutaka kujua kulikoni,umakini wa kuchunguza kilichotokea ukiongezeka maradufu

    mzee atakuwa kapatwa na nini?!



    ni mnyama mkali kamkamata,ni watu wa PATRICK,au ni wanausalama wamskao kila siku?



    swali ilo likapita katika kichwa chake lakini akuacha kujipa tahadhari ya uko aendapo



    paaaaaa!!!



    ghafla akagutushwa na mlio wa risasi hatua chache toka alipokwepo,sononeko,majonzi,vi

    kamvaa,moyo wake,bila shaka watu wale watakuwa wameshamwangamiza babu yake.



    wazo ilo likazidi kumsononesha akazidi kusonga mbele kujipeleka kwenye kitanzi!,akujua hatari alokuwa akiifata laiti kama angeijua hapo hapo angegeuka ila alishachelewa kufanya maamuzi...



    akasonga,woga ukimzidi,nywele zikimsisimka.



    Watu wale KATILI walizidi kusonga mbele ghafla JAPHET akaachia tabasamu hafifu!,



    tabasamu la dhihaka,lililobeba dharau na kejeli ndani yake ambalo lilipelekea kuonwa na kijana mmoja wapo kati ya majambazi wale.



    SORONKO ndo jina lake,pacha wa x,y bila kuwaza SORO akamshushia kitako cha bunduki katika kisogo chake,



    mzee yule akaachia yowe la maumivu,na papo hapo akamtemea mate soro,mate mekundu yalochanganyikana na damu,



    kilichofatia hapo ni kipigo kikali bila huruma,damu nyingi zikamtoka na kulowanisha eneo lile,



    wakaanza kumburuza wakimsisitizia aeleze wapi anapoishi mzee yule akawa kiburi,jeuri akawa akitoa cheko la dharau.



    chelo lililozidi kuwakera maharamia wale,



    wakamfunga katika mti na kuanza kumpiga,mzee alilia kwa maumivu lakini katu akufungua domo lake,alikuwa tayari kufa,ndipo majambazi walipomtwanga risasi mzee yule,



    na kumuulia palepale huo ndo ukawa mwisho wa maisha ya mzee JAPHET komandoo.



    alosalitiwa na jeshi ,wale majambazi wakaanza kurudi kule walipotokea wakijua kwa vyovyote nyumba ya yule mzee aikuwa mbali na maeneo yale,



    lakin bado katika vichwa vyao walikuwa na maswali lukuki ya kujiuliza,kuwa yule mzee ni nan? na kwanini anaishi katika pori lile?,



    Waliacha maswali yao yakielea katika vichwa vyao,wao wakazidi kusonga,kukata mbuga katikati ya pori lile wakipishana na wanyama wa kila aina aliyetishia maisha yao walimuwai kwa risasi.



    Inawezekana ikawa ni bahati nzuri kwao,au pengine ni bahati mbaya kwa kijana ZUBER,kwani ueleleo walioelekea ndio huo huo yeye alielekea japo waliachana kwa umbali mrefu kidogo.

    lakini umbali ule ulizidi kupungua pale ZUBERI alipopumzika chini ya mti mkubwa pasina kuelea akapitiwa na usingizi

    kutokana na uchovu na miguu kumuwaka moto akulijua hatari ilokuwa mbele yake na laiti angelijua?!!



    *******



    PATRICK alizidi kuchanganyikiwa pale alipowasiliana na vijana wake na kumwambia kuwa bado awajamtia zuber mkononi,kijana huyo alikuwa ni hatari katika maisha yake.alizi kufoka.akiitaji wafanye kazi!....



    PATRICK alijaliwa roho mbaya,furaha yake ni kupata taharifa ya kupatikana kwa zuber na kuuwawa



    tena wamuuwe hukohuko huku kiletwe kichwa kwa mahana nkimuuwa kwa mkono wangu nita "deal" na kiungo kimoja kimoja.



    Bado mawazo hasi yalikitesa kichwa chake.Alikuwa ndani ya ndege kwa safari ya kurudi MOSHI.



    kichwani mwake aliwaza vitu viwili tu,SHONAIZAR wake na ZUBER,kitendo cha mpenzi wake yule kupoteza kumbukumbu kilimfuraisha sana,aliitaji kumjenga kiakili upya.



    alipofikiria hivyo akatabasamu.



    Tabasamu ambalo lilijumuishwa na kujua kuwa shone kwa sasa amtambui tena ZUBER kazi ilobakia kwake ni kumtongoza upya.



    kitendo cha kuakikishiwa na daktari kuwa kumbukumbu zisingekaa zirudi tena kilimfuraisha,tabasamu lake likageuka kuwa cheko,cheko hafifu...



    naam akaishika simu yake na kumpigia SHONE



    "simu ile ikapokelewa na sauti nyembamba ilojaa mahaba ni wazi shone alikuwa usingizini muda huo."



    "nambie mpz!"



    "mh! mpz? nan mwenzangu?"



    "mimi ni PATRICK mumeo!"



    "mume? yupi?"



    "usijali mke wangu pumzika nipo njiani nakuja."



    upande wa pili ukanyamaza kwa sekunde kadhaa kisha binti yule kwa unyonge akajibu



    "sawa"



    simu ikakatwa.



    **********



    MVURUMO wa simu ndio uliomzindua toka katika usingizi,tangu atoke hospitalini alikuwa akipewa madozi ya usingiz ili akili yake ikawe sawa.



    sasa nguvu ya dawa ile ilimuisha na akili ilikaa sawa.



    alikuwa kama kashtuka usingizini.



    akapokea simu ile alopigiwa na huyo alojiita mume wake,



    Baada ya kukata simu macho yake yakatambaa katika chumba kile,kilikuwa ni kipya kwake,tangu amezinduka amekuwa akifikiria vitu ambavyo akuvielewa,



    macho yake yakatua ukutani kulipokuwa na picha kubwa sura yake na ya PATRICK zilionekana.



    akajinyanyua na kwenda kuitazama vizuri picha ile.akiilinganisha na ya kwake aliyoiangalia katika dressing table chumbani mule.



    "ina mahana yule ndo mimi? na huyu mwanaume ndo mume wangu?"



    akuwa na jibu!,akaunyanyua mguu wake na kutoka nje alipolakiwa na kordo kubwa.akanyoosha mpaka sebuleni aliposhtuka kumuona msichana!.....



    Kwa sekunde kadhaa SHONE na dada yule wakatazamana,katu SHONE akujua kuwa yule dada alikuwa kapachikwa ghafla yule dada akashtuka kwa kumuamkia



    "shikamoo mama!"



    "marhaba"



    aliitikia SHONE akienda kuketi katika kochi



    "MERY! umesema unaitwa MERY eeh!?"



    "naam mama"



    msichana yule akakubali



    "samahani kwa maswali ntakayokuuliza!"

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "sawa mama amna shida!"



    "ok! mimi ni nan?"



    "wewe ni mama!"



    "sawa najua mimi ni mama ila jina langu kabisa na kilichontokea mbona sijielew elewi?"



    "ok mama wewe unaitwa SHONAIZAR ulipata ajali na kupoteza kumbukumbu ukiwa pamoja na baba miezi sita nyuma"



    mfanyakazi yule alieleza jinsi alivyoambiwa na bosi wake PATRICK



    "eti? miezi 6 sina kumbukumbu?"



    "ndiyo mama"



    "ok kuna picha zozote za huyu mume wangu PATRICK?"



    Mfanyakazi yule akusema kitu kwani kila kitu alisha mbiwa na patrick ikiwa SHONE atajiwa na fahamu akiitaji hiki mpe hichi ivyo alienda kuchukua albamu ilojaza picha za kimapenzi za kutengeneza SHONE akaanza kuchambua picha moja moja tabasamu likiumba mdomo wake,kufurahia pozi walolipiga katika picha zile.



    hisia za mapenzi juu ya PATRICK zikijaa ndani ya moyo wake,katu akutakidi kwamba zile ni picha feki ghafla AKASHTUKA!! moyo wake ukampasuka paaaaa....



    ni baada ya kuiona picha moja,picha ilowekwa kimtego,patrick aliyoiacha maksudi,dada yule alokuwa makini kumsoma SAIKOLOJIA SHONE kwa makini katika tukio lile



    "Uyu ni nani?" shone akauliz huku mdomo ukimtetemeka



    "nakuuliza huyu ni nani mbona unijibu?"



    SHONE alizidi kuoji huku akiwa kabadilika alijihisi moyo kumuuma akujua kwa nini alijijuka ameikumbatia picha ile ghafla akamgeukia dada yule alokuwa kachanganyikiwa na akibabaika kulijibu swali hilo



    "ni...ni...ni rafiki yake na baba"



    hatimaye alijibu japo kwa kigugumizi SHONE akabaki kuiangalia picha ile ya ZUBERI ilowekwa kosa ikimaanisha kwa sasa ni marehemu na kwa uchungu akasema



    " NAITAJI KUKUMBUKA..."



    mfanyakazi yule akatoka sebuleni pale na kuingia chumbani kwake ambapo kwa umakini akampigia bosi wake na kumueleza



    Baada ya PATRICK kuambiwa juu ya SHONE kushtuka baada ya kuiona picha ya ZUBER jambo hilo lilimshtua sana kijana yule lakini mshtuko ule aukudumu baada ya kukumbuka kuwa kilichoathirika kwa shone ni ubongo na si moyo hivyo soln ni kupatikana kwa kijana yule na kuuwawa haraka sana.

    Kwa upande wa SHONE



    "huyu ni nani mbona moyo unaniuma hivi?"



    binti yule alijiuliza huku akijitaidi kuvuta kumbukumbu ambazo katu akuweza kurejea kwa urahisi huo alioutaka yeye,akakunja sura yake kwa hasira.Katu akujua kile afanyacho kilichunguzwa na yule aliyemjua kama mfanyakazi na pia kilionekana katika camera na kitendo cha yeye kushtuka,mfanyakazi kufikisha taharifa mahali usika,kilimuweka kijana wa watu pabaya zaidi.



    ******



    Wasichana 3 wale waliingia katika msitu ule wakibishana,mmoja wapo kiumbo alikuwa ni mrembo zaidi...na hata kimavazi alionekana ni wa mjini,alilalamika kuchoka wenzake wakawa wakimcheka na kumsihi waingie "wakasanye" kuni,katika hali isiyo ya kawaida ghafla wakashtuka kumkuta mtu kalala akikoroma,



    haikuwa kitu cha kawaida katika msitu ule.



    Wasichana wale wakaangaliana kwa mshangao wakiongea lugha wanaoifahamu wao,wawili wale wakashauri wakimbie kwa uoga,akabaki yule mmoja wa mjini na kumsogelea taratibu na kuanza kumuamsha

    ZUBER akagutuka kwa mshangao,woga na kutaka kukimbia ila mdada yule akamzuia zuber akatii akiomba msahada kwa lugha sanifu ya Kiswaili,wawili wale ambao awakukimbia mbali wakazidi kushangaa na kumkodolea macho mwenzao wa mjini ambaye alielewa lugha ile wamjini akawatoa khofu wenzake kwa kuwa mkalimani kwa akisemacho zuber.



    ZUBER akaanza kuwasimulia story ya maisha yake,wote walishangaa machoz yakawatoka! hakuna alokuwa na hamu tena ya kukata kuni ikabidi warudi kijijini ambapo apakuwa mbali na eneo lile.



    awakujua kitendo kile kingesababisha machafuko



    katu awakujua nyuma yao vijana wa PATRICK wenye uchu na uhai wa mtu walikuwa wakija kwa kasi na wangechelewa kidogo pale wangekutwa



    Kijiji kile kilichojulikana kama MZAGHE,kilivami

    wa na wanaume wale wa shoka sita!,



    wasiyo hata na chembe ya huruma,walipita nyumba baada ya nyumba wakitoa kipigo kikali na kuuwa watu wasio na hatia wakilazimishwa waeleze mahali ZUBER alipofichwa

    wakijidahi ni wanausalama kutoka DAR.



    mwenye kiti wa kijiji aliitisha kikao migambo wakaingia uraiani kwa msako mkali,sasa msakwa alisakwa na watu wengi!,hata vijana wa kijiji waliacha kulima mashamba wakazagaa mitaani kwa msako baada ya kusikia zawadi nono iliyokwisha tangazwa kwa vyovyote vile ilikuwa ni lazima ZUBER apatikane tu! vizuizi vyote vilizuiliwa,magari yote yalikaguliwa.



    hapakuwa na namna ya kutoroka nje ya kijiji hiko bila kuuingia mikononi mwa watu hao.katu akukuwa na mtu aliyedhani kuwa wale hawakuwa na roho ya binadamu na laiti wangejua?,kila aliyetembea mkononi alishika picha ya ZUBER alisakwa kama madini mgodini.



    ********



    Wasichana wale wa tatu mioyoni mwao hawakuwa na amani kabisa.Waliingia kijijini kabla hata wale wasaka roho awajaingia JANETH yule mwanamke aliyeonekana ni wa mjini akili ilifanya kazi zaidi ya kompyuta ilibaki kuwa ni siri zao hata familia zao hawakujua JANETH aliitaji kwa vyovyote vile amtoroshe ZUBER,alihisi KUMPENDA,



    hakuwa tayari kumwona akiingia mikononi mwa mabedui wale wakiwa na wenzake wakamuifadhi kijana yule katika chumba alicholala janeth wakaapishana kiapo kutotoa siri.



    ila hilo alikufanikiwa baada ya wanaume wale kuingia,zawadi nono kutangazwa tamaha ikawapanda wawili wakamsaliti mwenzao.wakatoa taharifa kwa mwenyekiti.migambo na mabedui wakaongozana kwenda kwa kina JANETH,binti yule akuwa akijua hili wala lile...wazee wa kazi wakaingia wakiwa na migambo na marafiki zake.JANETH hakika aliamini kikulacho kinguoni mwako alitetemeka kwa hasira na kicheko wenzake walitabasamu kwa kejeli na dharau.



    "tunamuitaji mtu wetu kabla atujamtoa wenyewe"



    xy alitamka bastola ikiwa mkononi mwake tayari kwa kuifetua kama binti yule angekuwa mbishi



    JANETH akaiangalia ile bastola iloelekezewa kwake kwa sekunde kadhaa,lakini mawazo yake hayakuwa katika silaha ile..



    alifikiria cha kufanya



    "haya migambo ingieni chumba hadi chumba mtoke na huyo kiumbe! akiwa katapakaa damu"



    "xy alomuelekezea silaha JANETH akatamka!"



    "PASKALINA...SELINA nashkuruni sana! kitendo cha kukataa kwenda nanyi mjini ndo mnanipakazia nashkuruni!"



    alitamka JANETH machoz yakiushambulia uso wake.



    "eti nini?" wote walishangaa



    "ndiyo kaka hawa wenzangu waliniomba niwatoroshe niende nao mjini mi nkakataa kwa kuwa najua maisha ya mjini yalivyo magumu wakasema watanionesha! ndo ivi selina asanten sana."



    sasa macho yote ya watu waloko maeneo yale yakaamia kwa wasichana wale waliokataa kuwa si kweli!,mwisho ikasubiriwa wapekuzi warudi.



    "amna kitu mh!"

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "mmepekua kila chumba mpaka chooni?"



    "ndiyo mh!"



    "ok haya hawa wawekeni chini ya ulinzi wote wa tatu wafungeni kamba...tukawauwe haiwezekani watusumbue..."



    "lakini bosi huyu janeth anamakosa tungemuacha tuondoke na hawa wawili wanaoleta mzaha katika kazi za watu!"



    mgambo mmoja aliongea akimtetea JANETH kwa kasi ya ajab x,y Alimgeukia mgambo yule na kummiminia risasi

    kabla ajashtukia akipigwa teke kali katika mkono wake bastola ikaruka juu.



    akamwangalia alomshambulia ni mwenzake.



    "bashaat! mwanaharamu wewe! kwa nini unaua viumbe visivyo na hatia?



    sasa huyo mlinzi sijui mgambo kakukosea nini?"



    x,y akanywea



    BASHAAT alikuwa ni kijana katili kwa kiumbe kilicho ndani ya kazi ila mwenye huruma kwa kiumbe kisicho ndani ya kazi,bashaat alipewa ilo jina kutokana na kupendelea kutamka neno ilo kabla ya kuongea ndo alikuwa kiongozi wa msafara ule wa majambazi!



    "nsamehe bosi" xy akatamka kwa unyonge



    "bashaat! nikikwambia ulipie uhai wa huyo mtu utaweza? au unataka mpaka serikali ituingilie kwa mauaji yako ya ovyoovyo"



    BASHAAT aliongea kwa lugha ya kingereza.watu wote awakuisikia zaidi ya JANETH!



    "Yameisha mkuu"



    "Bashaat! nnachoamua huyu binti JANETH aachwe na hawa wapuuzi wanaochanganya kazi na bifu lao twendeni nao porin! bashaat wakatukidh haja zetu,watajua kilichomtoa kanga manyoya"



    Huyo ndo alikuwa BASHAAT! kijana katili asiye na huruma hata chembe kwa mwenye mzaa ndan ya kazi.



    wakawabeba wasichana wale wazaz wao wakilia na kwenda nao porini kule walipomuokotea ZUBERI.



    awakurudi!!!



    ************



    JANETH akiwa nyumbani pale wazazi wake wakiwa shambani mwili wote ulimsisimka!.

    zawadi nono ilotajwa hakuwa na khofu juu ya usaliti wa marafiki zake..



    milioni 70 hata kama ni yeye kwa maisha ya kijijini pale angemtoa kijana yule.



    ila yeyealishaapa kumsaidia, akatafakari kwa sekunde kadhaa akapata jibu! akaenda kumtoa ZUBER katika chumba kile na kumuifadhi stoo kwenye kiroba ambacho juu yake kiliongezewa maindi ilikuwa ni vigumu kugundua kama kuna mtu ndani yake,



    baada ya migambo kuridhika walitoka kumwambia bosi wao amna mtu.baada ya mafedhuli wale kuondoka JANETH kwa siri sana alirudi stoo na kumfungulia ZUBER akampa chakula.



    ZUBER alimshukuru sana,naye pia kwa upande wake moyo wake ukaanza kufunguka juu ya mwanamke yule aliyezionesha hisia zake kwake wazi.

    JANETH alikuwa ni msichana mdogo mwenye maendeleo jijin DAR,ki tahaluma alikuwa ni wakili wa kujitegemea,wakili mdogo aliyewajengea nyumba ya kifahari walezi wake kijijini pale,



    ni msichana aliyeishi ktk maisha kutokana na eneo usika,akiwa kijijini akusita kuwasaidia wazazi wake kazi,kama kuteka maji,mbali na kijiji kukata kuni na wenzake porini na hata kazi ndogondogo za nyumbani.hakuwa mwanamke mwenye dharau hata kwa marafiki zake alikuwa ni binti aliyeumizwa sana katika mapenzi na wanaume wote aliowah kuwa nao mjini na hata wa huko kijijini,akuitaji kupenda tena,ila kwa ZUBER moyo uliitaji kufunguka alipojaribu kuupotezea alijizalishia maumivu yalopenya moyoni na kumwacha katika majonzi makuu.sasa ALIMPENDA na ilikuwa lazima afanye chochote kumuokoa kipenzi chake kile.

    "ZUBER utavumilia tu itabidi ulale kwenye buti wakati wa safr"



    ZUBERI akuwa na sababu ya kukataa kwani msako bado ulikuwa mkali kijijini pale.



    **********



    Wakati SHONAIZAR na MERY wakiwa sebuleni wanaangalia tv mara kengele ya hodi ikasikika MERY akanyanyuka kwa lengo la kwenda kufungua mlango ule.

    SHONE tayari mawazo yake akutaka kuyarudisha nyuma tena aliona kitendo cha kujilazimisha KUKUMBUKA asichokumbuka ni kujiumiza alikuwa na hamu ya kumjua aingiaye hakuwa na shaka kuwa alikuwa ni mumewe ambaye sura yake aliikumbuka kwa kuiona katika picha alizoziona.

    alijiinua na kupanua mikono yake kumkumbatia PATRICK akimsindikiza kwa mvua ya mabusu hakuwa na shaka kuwa yule ndo mumewe.

    PATRICK moyo ulimpasuka kwa tumaini jipya,walikaribia mezani,waliongea mengi,patrick akionesha kufurah sana kwa shone kupata nafuu.

    wakaufungua ukurasa mpya wa kuyaanza maisha.

    SHONE akamsahau ZUBER kwa kutokuwa na kumbukumbu dhahiri juu yake.ZUBER akukumkumbuka SHONE akijua tayari yu maiti! kwa ile ajali aloipata,PATRICK hakuwa na shaka tena na zuber kwan alikuwa na uhakika alifia porini kama alivyoambiwa na vijana wake wale.na hata kama angekuwa hai shone asingemkumbuka kwa juhudi zake binafsi alifanikiwa kuziteka hisia za mtoto yule wa kike..na kumuweka kwenye himaya yake.

    alimtafutia mwalimu alomfundisha english corze,shone alikuwa na kichwa chepesi miezi michache baadaye akampeleka chuo kusoma maswala ya biashara ambapo alimfungulia kampuni kubwa ya kuuza magari,maisha yao yakabadilika visasi miongoni mwao vikatoweka wakawa miongoni mwa matajir wakubwa jijini MOSHI.hayo ndo mafanikio PATRICK aloyaitaji.



    ************



    UPANDE WA PILI



    Gari ilombeba ZUBERI ndani ya buti ilizidi kukata mbuga,ndani ya gari alikwepo msichana JANETH

    mara nyingi sana alipishana na migambo ambao baada ya kumuona yeye pekee ndani ya gari ile walimwacha bila kuikagua.baada ya kupita vijiji kwa vijiji,pori kwa mapori,hatimaye walianza kuingia mjini ambapo kama walivyoongea ZUBER alitolewa ndani ya buti ile na safari kuendelea wakipiga stori za hapa na pale.



    Maongezi yakaendelea kama kawaida na JANETH akajitambulisha wadhifa wake



    "Mimi ni wakili lazima tumfunge huyu mwaharamu!..."



    Janeth aliongea kwa hasira,moyoni mwake alimchukia PATRICK



    "hapana jane namjua vizur PATRICK anamtandao mkubwa atakuuwa beby wangu nami pia please nakuomba tuangalie maisha yetu.hata ikiwezekana tukaishi nje ya nchi tukae nae mbali."



    JANETH akacheka,katu hakujua kama kuna viumbe vilivyokuwa vikiogopwa moyoni mwake aliapa kumfatilia na kumchunguza PATRICK kwa ukaribu bila kujua hatari ilokuwa juu yake na laiti angeitambua angefanya kama vile ZUBER alivyopendekeza lakini katu usilolijua ni sawa na USIKU WA GIZA.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ******



    DAR ES SALLAM



    MASAKI



    ZUBERI mwenyewe alipagawa kwa bonge la nyumba alokuwa akiishi mwanamke yule.kama ni pesa alikiri JANETH alikuwa nazo zaidi ya alivyofikiria alikuwa ni tofauti na JANETH wa kijijini ila alichoshangb mwanamke huyu aliishi peke yake na msichana wa kazi na walinzi pekee ili lilimshangaza sana ZUBER.ndipo JANETH ilipomlazimu amsimulie storia ya maisha yake stori iliyomsisimua



    ******



    SURA YA TATU



    MIAKA 15 NYUMA



    DAR ES SALLAAM



    Ilikuwa ni asubuhi yenye manyunyu madogo madogo,baadhi ya watu katikati ya jiji walionekana ni wenye haraka ama kwa kuwahi makazini au kukwepa manyunyu hayo yenye kutia kiubaridi mwilini.



    Ilikuwa yapata saa mbili asubuhi,



    nilikuwa miongoni mwa watu hao lakini tofauti yangu mi nilikuwa nimejibanza kando ya duka moja la mhindi ambalo lilikuwa bado alijafunguliwa labda kutokana na kamvua hako ndicho kilichosababisha mhindi huyo kuchelewa kufika kibaruani kwake,



    nilijiinamia chini huku kwikwi zikiskika kwa mbali,kwiwi zilikatika pale nilipohisi kuna mtu ananigusa begani,



    niliponyanyua macho yangu nikastaajabu na kupigwa na butwaa baada ya kumuona yule mhindi akiwa amesimama mbele yangu akinitazama kwa jicho la tamanio...



    yule mhindi akanisabahi kwa kiswaili chake kisichoeleweka



    "jambo binti?"



    aliniuliza yule mhindi huku sasa akiniangalia kwa macho ya kuniuliza umekaa hapa? lakini akudhubutu kuitoa sauti yake.jicho la tamaa alilificha



    "sijambo!"



    niliitikia huku nikinyanyuka taratibu kumpisha yule mhindi afungue duka lake.



    "wewe hapana ondoka mvua bado iko nyesha."



    aliniongelesha yule binti ili kunionesha utu kwangu kwa mwenye majonzi,kwel muda huo mvua ilizidi na ilikuja na upepo mkali uloipeperusha mvua kuja maeneo yale na kunifanya nianze kuloana,iliambatana na radi niliogopa..nilichuchumaa nikieka kichwa changu katika magoti yangu.



    "wewe toto iko ingia huku

    dukani,utonyesh

    ewa.."



    mhindi yule alizidi nikirimu huku akifagia,sikuji

    uliza mara mbili "nikajitoma" ndani cha ajabu kitendo tu cha mimi kuingia ndani aliacha kufagia na kubana mlango.



    akanifata pale nilipo uchu ukionekana waziwazi nilitetemeka nikilia nikimwomba asinifanyie alichotaka kunifanyia.



    nilichelewa

    akalirarua gauni langu kwa kulichana,akani

    bana madhubuti na kuanza kuniingilia kwa nguvu bila ridhaa yangu.



    mhindi yule alikuwa na maumbo makubwa yalonichana,sijui hakuwa na mke alikuwa katawaliwa na "ugwadu" bila kujali kilio changu,bila kujali maumivu nloyapata aliendelea na ukatili wake mpaka aliporidhika.



    akaniacha tena kwa kejeli nyingi,ilikuwa ndo mara yangu ya kwanza kufanya mapenzi.



    akanfukuza tena bila huruma bila kujali mvua inyeshayo.



    bila kunistiri nikaenda nyumba ya jirani kukaa.mpaka mvua ilipokata nkaendelea na safari.



    nikichechemea maumivu makali yakinicheka,sikuwa na kimbilio mimi JANETH ningekimbilia wapi?



    ila hasira ilinikaa kooni juu ya mhindi yule niliapa kumuua kwa mkono wangu...



    kwa kuwa ndo adhabu niliyoiona inamstaili

    nilifata barabara ndogo ya vumbi ambayo ilikuwa imejaa maji na baadhi ya sehemu ambazo zilikuwa zimetifuliwa na magari zilijaa maji na kufanya barabara nzima ijae maji,nilitembea kandokando ya barabara kwa uangalifu ili kuepuka kutumbukia kwenye vidimbwi vidogo vidogo nilitembea huku kichwa nikiwa nimekiinamisha chini si kwamba nilikuwa nikiangalia maji la hasha! bali nilikuwa nikiifikiria ninini hatma ya maisha yangu?

    nilikuwa mgeni kwenye hili jiji lenye kila aina ya purukushani sikuwa na pakukaa,kula na hata pa kutegemea!



    Mimi JANETH sikuwa na ndugu wala mwenyeji ambaye ningeweza kufikia kwake,nilifikiria jinsi siku yangu itakavyoisha..



    nikakumbuka siku chache nilivyotua dar nikakaribishwa mjini na kuchukuliwa kila kitu hata nguo zangu zote zilichukuliwa nikibakizwa na nguo nilizokuwa nimevaa,



    viumbe vyenye jinsia ya kiume ndivyo vilivyonifanyia hivi....



    nikazidi kulia kimyakimya pasina wa kunionea huruma... niliendelea kutembea na hatimaye safari yangu iliishia kwenye nyumba moja ambayo ilionekana kama gofu kwani ilikuwa imeezekwa mabati yalochakaa tena ikiwa aina milango wala madirisha.



    ilionesha wakaaji walishaondoka siku nyingi na kuiacha nyumba ile.



    ambacho ndicho chanzo cha kuzeeka kwa nyumba hiyo



    niliingia taratibu kwenye nyumba hiyo ambapo pamoja na kuchakaa ilikuwa imejaa maji yalotokana na kuvuja kwa mapaa yake.



    nilisogea mpaka kwenye kona moja ambayo ilionekana na afadhali nikaketi chini huku nikiiangalia nyumba hiyo ambayo haikuwa na hadhi ya kukaliwa na binadamu mwenye uhai.



    nilijiegemeza ukutani na ghafla usingizi ulianza kunipigia honi kutokana na uchovu nlokuwa nao niliamua kujilaza pale nilipitiwa na usingizi...



    kwa mbali nikiwa katikati ya usingizi nilisikia watu wakiongea,kwa sauti za kiteja...



    nilijua pengine ni ndoto, sauti zao zikimezwa na usingizi ule mzito.



    vijana wale 6 ambapo pale ndipo makazi yao walifurah sana kuniona pale kwa haraka wakanivamia na kuanza kunitolea nguo tena kwa kuzirarua.



    nilishtuka toka usingizini ila nilishachelewa.



    walikuwa wamenibana hata kupiga kelele sikuweza.



    JANETH akashindwa kuongea huku kilio kikimkaba,akaanza kulia,ikabidi sasa nianze kumbembeleza.akatulia.



    "ZUBER leo naitaji unipikie..."



    akatamka huku akiwa anafuta machozi



    "wewewewe tena unyamaze kapike mumeo nile naisi njaa"



    nami nilimjibu kwa utani wote tukacheka.



    "mume wangu wataka ule nini?"



    "kile ukipendacho mpz!"



    JANETH akanyanyuka pale na kuelekea jikoni kupika.akiniacha pale sebuleni na mawazo tele.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    baada ya kumaliza kula nilimuomba aendelee kunsimulia historia yake ile...



    JANETH akuwa na pingamizi,taratibu akaufungua mdomo wake na kuendelea kunsimulia!



    "nilitembea kwenye kibarabara kidogo uku nikichechemea,niliazimia kupata chochote kwa ajili ya kuweka tumboni kwan nilikuwa nikisikia njaa sana."



    nilitembea umbali mrefu na hatimaye nilifanikiwa kukiona kibanda kimoja cha mama ntilie.



    nliingia taratibu na kukutana na mama mmoja wa makamo na kuamua kumueleza shida zangu sikuwa na hela ya kula hivyo nilimuomba anipe japo ukoko niweze kupoza njaa yule mama kabla ajanipa chakula kile akanipa ndoo kubwa akanielekeza mahali wanapochotea maji nkaenda kuchota maji ndoo tatu



    baada ya kumaliza akanambia nioshe vyombo vingi sana achilia mbali masufuria! nilichoka, ila baada ya kumaliza mama yule alienda kwenye moja ya masufuria yake na kunchotea ukoko,



    ambao aliumiminia na supu kidogo ya nyama,nilikifakamia kama mtu mwenye njaa ya siku 40,



    baada ya dakika zisizozidi tano nilimaliza kula na kumshukuru mama yule na kuondoka kuelekea nisipopajua huku nyuma yule mama akanambia kesho tena muda kama ule nirudi pale,



    nilitembea mita chache ghafla wazo flan likanijia kichwani nikageuka nyuma na kuangalia kile kibanda,



    niliona kuliko kwenda nisipopajua wakati nilimuacha yule mama akijiandaa kufunga ni bora nisubiri aondoke nikajibanze katika kakibanda kale,kusudi nipitishe usiku ule wenye kila aina ya kuogofya niliamua kusogea pembeni ya barabara ambapo kulikuwa na mti mdogo na kuamua kukaa chini ya mti huo,



    ilikuwa yapata saa nne na nusu pale nilipomuona yule mama akipita upande wa pili wa barabara akiwa amebeba baadhi ya vifurushi alipopita niliamka taratibu na kuanza kuelekea kwenye kile kibanda nilitembea kama dakika tano hatimaye nilifika kwenye kibanda hicho kilichokuwa na mabati tu bila mlango kikiwa kimetengenezwa kwa mbao



    niliingia ndani na kujilaza kulikuwa na mende wengi ila ilo sikulijali nilijifunika kwa kutumia mikono yangu,nilijaribu kuutafuta



    usingizi usingizi ukagoma.



    Nilijaribu kuyafumba macho kwa kujilazimisha lakini aikusaidia...



     Janeth bado anaendelea kumsimulia Zuberi historia ya maisha yake mpaka akafanikiwa na kuwa wakili wa kujitegemea!



    Songa nayo sasa....



    Nilikuwa nikimkumbuka sana marehemu mama yangu Bibi MAGRATH ALPHONCE sikuelewa ni vipi ningeweza kuyamudu maisha bila kuwa na mama yangu kipenzi tena katikati ya jiji ambalo sikuwa hata na mwenyeji ambaye angeweza kunisitiri pindi ntakapokuwa jijini hapa



    "ZUBERI mpz wangu!,"



    JANETH aliniita,kwa sauti ya majonzi! nami nkamwangalia nikitabasamu , kumfariji!



    "naam!"



    nikaitika ili kusudi aendelee.



    "nahitaji ukalale uniache nipitie pitie vifungu vya sheria kabla sijamwadabisha huyu mwanaharamu PATRICK!"



    Nikashtuka!!...



    sikutegemea kusikia maneno kama yale hasa kwa mwanamke nlompenda,mwanamke aloyaokoa maisha yangu! nikavimba kwa hasira.ishara ya kutokubaliana na jambo lile



    "JANETH nimekwambiaje lakini juu ya huyo kiumbe? upendi unione mimi naishi kwa raha?,"



    "uc ogope mtu zuber! utake usitake PATRICK ntamfunga,ntamchunguza nyendo za maisha yake na ntamweka hatiani tu"



    maskin! JANETH akumjua PATRICK ni mtu wa namna gani? kiualifu,



    nikanyanyuka kwa ghadhabu ila binti yule akan' daka mkono na kunrudisha chini...



    "usiwe na roho ya uwoga ZUBERI bado tupo katika vita amini tutashinda sote tumepitia wakati mgumu katika maisha yetu mpaka unaniona naishi katika nyumba hii ya kifahari yenye ulinzi mkali"



    Akashusha pumzi na kuendelea



    "wakati nakuelezea story ya maisha yangu pengine nimepita maisha ya hatari zaidi yako wewe ujui zuber! usimwogope mtu! akuulie mpz wako SHONE,akuweke maisha yako rehani alafu umuache huru tu no so mimi JANETH"



    "PATRICK namjua vizur JANET"



    "kama unavyonijua mimi?"



    ni kabaki na mshangao



    "ujanijua mimi ni mwanamke wa namna gani ZUBER?!"



    Kwa mara ya kwanza sikusema kitu nikajinyanyua na kuelekea chumbani kulala.



    kila nilipojaribu kuvuta usingizi ulikataa,



    nilipocheki saa ilisomeka saa nane kasoro JANETH hakuwa kitandani,



    nikajinyanyua na kumfata sebuleni pia sikumkuta, taharuki likauvaa uso wangu.



    "usiku huu mwanamke huyu atakuwa kaenda wapi?"



    nkamfata chooni pia akwepo,ikabidi ntoke nje kuwauliza walinzi kama ametoka jibu walonipa likazidi kunchanganya...



    Awakumwona Janeth wangu!



    Nikajirudisha mpaka sebuleni



    Sikuweza kuyazuia mawazo kukiandama kichwa changu!



    nikajibwaga katika kochi!,macho yangu yakatua tena ukutani palipokuwa na saa,tayari ilikuwa saa tisa kasoro...



    "zuber my darlng"



    ghafla nkagutushwa na sauti tamu,kutupa macho mbele nkamwona JANETH wangu akiwa na nguo yake ile ya kulalia...



    "ulikuwa wapi wewe?"



    nikauliza kwa jazba,hasira zikisomeka usoni mwangu



    "nilikuwa maktaba nikisoma soma!"



    "maktaba usiku?!"



    niliuliza kwa mshangao nikikumbuka kweli sikwenda huko kukagua kwa kuwa sikuwa na wazo la kuwa mpz wangu atakuwa huko



    "ndiyo mpz!"



    "mh! aya twende tukalale..."



    tukajikokota mpaka chumbani,hakuna alokuwa hata na tone la usingizi kila mtu akiwaza yake.



    mim niliwaza iweje bint yule ansimulie kuwa amepitia maisha ya shida sana vipi na hizi mali?!



    Ghafla nkashtushwa na mikono laini ikinipapasa taratibu



    "zuber mpz wang!"

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    akaniita taratibu!



    "nambie mpz!"



    "nadhan unatambua mimi ni wakili mzur sana! hivyo muda wangu wa kusoma na vitu kuniingia vizur ni usiku....



    ivyo usijal ucponiona kitandani!"



    "lakin janeth?! embu niendeleze...maana bado na hali ya sintofahamu!"



    "mh na usiku huu?"



    "kesho asubuh si unaenda kazini?"



    "ila si nnarudi!"



    "mh! niendelezee kidogo tu my!"



    JANETH akakubali kuniendelezea akaanza kwa kusema



    "michirizi ya machozi ilianza kuonekana mashavuni mwangu nililia taratibu kwa kwikwi na sikujua ni muda gani usingizi ulinipitia nilikuja kushtuka saa kumi na moja alfajiri nikajinyanyua pale kwenye mti nikajiondoa taratibu nikijifuta matongotongo huku nikitembea mwendo wa uchovu



    nilianza kufata barabara ndogo ilokuwa upande wa kulia sikujua niendapo ila nlitaka niondoke maeneo yale nilipita nyumba moja moja nikiomba kazi bila mafanikio.



    mchana ilipofika nilirejea kwa mama ntilie yule alonipokea kwa bashasha na rundo la vyombo tena akanambia kuna mtu anatafuta mfanyakazi nilifurah sana baada ya kumaliza kuosha vyombo vile akanipa ukoko alouchanganya na maharage kidogo nikaula kwa kuufakamia kwa kuwa toka jana yake nilipokula ukoko ule sikuweka kitu kingine tumboni



    Wakati nikiendelea kuwaza hili na lile pale kibandani!,



    ghafla akaja kijana mmoja nikamwona yule mama akiongea naye huku wakintazama mimi! yule kaka akaondoka...



    yule mama lishe akanfata na kuniambia huyu kaka ndo yule anayetafuta msichana wa kazi hivyo nimsaidie saidie kazi usiku angekuja kunchukua akitoka kazini



    nilifanya hivyo!



    kweli usiku yule kaka akaja na pikipiki yake nikapanda tukaelekea katika nyumba moja ya uswahilini



    akanikaribisha ndani! hapo ndipo machale yaliponicheza baada ya kugundua kijana yule anaishi peke yake katika chumba kimoja tena cha kupanga!



    baada ya kumaliza kuoga akatoka...



    akaufunga mlango kwa nje aliporejea alikuwa na kamfuko ka chipsi sikuweza kula chipsi zile.



    wasiwasi ulinijaa!,



    Nilitetemeka ndipo alipoanza kunsifia huku akinishika hapa na pale nkamzuia.



    akanawa mikono yake na kunifata pale nilipo.akanambia nipande kitandani nikakataa nkamwambia ningelala palepale kwenye kochi akanambia



    "usinchekeshe we binti ujue we nimekulipia kwa mama makombo!"



    nikashangaa!!!...



    Ila ghafla alinifata pale akannyanyua na kunibwaga kitandani akaniwekea nguo mdomoni akanibana mikono kwa nguvu na kunipanua miguu yangu na kuanza kuniingilia bila ridhaa yangu."



    Alipofika hapo JANETH akaweka tuo!,



    machozi yalikuwa yakimtiririka...



    akaendelea huku akiwa analia



    "ZUBER mpz wangu kuna viumbe vikatili sana kwani baada ya jamaa yule kutosheka akanifukuza usiku ule ule moyo uliniuma baridi nje ilinipiga,



    nikazidi kuwachukia wanaume nikiapa kuwalipizia visasi nilienda kwenye nyumba moja nikajikunyata nje katika baraza mpaka asubuh kichwani niliwaza mengi sana hatimaye michirizi ya machozi ilianza kuonekana mashavuni...



    sikujua kwa namna gani ningeweza kuyamudu maisha nikiwa peke yangu katikati ya jiji ambalo nishaumizwa na aina tofauti tofauti ya wanaume wenye uchu wa ngono!,



    wanaume wasiyo hata na chembe ya huruma akukuwa na mwenyeji ambaye angeweza kunisitiri,



    nilitembea mwendo wa uchovu huku tani ya maswali yakikiandama kichwa changu



    nilitembea mpaka katika mti mmoja wa mwembe ambao niliona bora nipumzike kidogo chini ya mwembe huo nikisubiria NUSRA YA ALLAH

    kama angekuwa upande wangu,



    sikuwa na pakuelekea nilijiegemeza chini ya ule mti,huku nikiwaza hili na lile,lile na hili kisha hili na lile.



    niliwaza niwapi ningepata pesa walau zinikimu kimaisha!....



    ni wapi ningeweza kupata malazi ya kudumu!....



    ,maswali ambayo hayakuwa na majibu kwa wakati huo.



    ikiwa yapata saa moja kamili asubuh niliwashughudia baadhi ya wafanyabiashara wadogo wadogo wakipita kwenye kinjia kilichokuwa karibu na mwembe huo



    Hakuna alojishughulisha nami kila mmoja alikuwa na hamsini zake



    ghafla nkasikia kishindo karibu yangu niliruka na kutaka kukimbia lakin nilishika kiuno na kuanza kutabasamu.



    nilijua ni mdudu alodondoka toka katika mti ule,kumbe lilikuwa embe lililodondoshwa na upepo baada ya kuiva,



    nilirudi na kukaa chini kisha nikaliokota lile embe na kuanza kulifakamia kwa vujo bila kujali kama lilikuwa na wadudu au lah!...



    nilikula embe lile huku nikibakisha kokwa likiwa leupe,niliamin hicho ndicho kilichokuwa kifungua kinywa changu kwa siku hiyo. niliendelea kuegemea mti ule huku nikiendelea kuwaza hili na lile...



    katu sikuwa na uhakika kama ningeweza kuishi maisha hayo ,maisha yasiyo na matumaini,maisha yasiyo na mwelekeo,nilish

    aanza kuona ugumu kuendelea kuishi maisha yale...



    niliwaza sana cha kufanya lakini sikupata jibu.



    ********



    MIEZI MIWILI MBELE



    ilikuwa imepita miezi miwili tangu niingie jijini DAR nilishayazoea maisha ya mtahani,



    maisha ya kubahatisha,



    nile,nisile ilo kwangu ilikuwa sawa nilikuwa binti wa miaka ishirini lakini nilikuwa nikipitia maisha ambayo sikuwah kuyafikiria hata siku moja....



    nilishazoea kuomba omba,na sasa nilikuwa nikiitwa chokoraa au mtoto wa mtahani kama ilivyozoeleka jioni hii ilinikuta katika dampo moja nikijaribu kupata japo kitu cha kutia kinywani kwani njaa ilikuwa ikiniuma sanaa



    Njaa ilikuwa ikinisimanga,niliokota baadhi ya vipande vya mikate vilivyooza na vyakula vya makopo vilivyopitwa na wakati wake,



    niliporidhika na muozo huo nilikaa chini ya mti na kuanza kula, sikuitaji kwenda tena kwa mama ntilie ambao waliutumia udhaifu wangu kujipatia kipato!,...

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    wakati nikiendelea kula ghafla gari moja la kifahari likapiga breki na mama mmoja wa makamo na mume wake ambaye alikuwa ni kigogo wa chama tawala wakashuka,



    kundi lote la watoto wa mtaani likakimbilia gari lile...



    na kupanda ndani mule!



    mimi nilibaki nimezubaa pasina kujua ili wala lile! mama yule alinifata na kwa sauti ya upole akaniuliza!



    "je we uitaji kwenda?"



    "kwenda? wapi huko!"



    "wenzako wanapoenda!"



    sikutamka kitu,nikapanda ndani ya gari na dereva akaliwasha gari....



    tukaondoka maeneo yale.



    moyon sasa amani ilintawala.



    MKOMBOZI AMANI CENTERE



    nilisoma geti kubwa lililofunguliwa na gari lile likaingia kichwani nikangamua kumbe pale ni kituo cha kulelea watoto yatima.



    kwa mawazo yangu nilijua vituo ni kwa ajili ya watoto wadogo tu ila kituo kile kilikuwa na watoto wakubwa!



    tena wasichana tu walokuwa katika umri wangu na chini ya hapo..



    tulikabidhishwa kwa mkuu wa kituo...



    mama yule na mke wake wakaondoka.



    "warembo karibuni MKOMBOZI hapa kuna masharti wenzenu watawaambia, kutoka nje airuhusiwi bila idhini ya uongozi! kiendeleacho ndani ni siri na atakayejaribu vunja au kutaka kufanya lolote hukumu yake wenzenu watawaambia!,...

    karibuni sana."



    akili ikacheza baada ya maneno yale kutoka kwa mwangalizi wa chuo kile niliyemtambua kama MADAM ANNA,



    sura za upole,masikitiko nazo nilizingamua baada ya kuondoka kigogo...



    KUNA KITU NYUMA YA PAZIA. nkawaza.



    sikukosea nilikuwa nimeingia katika vita!



    vita ambayo mara kadhaa iliyaponesha maisha yangu, laiti ningejua nisingekubali kwenda katika kituo kile...



    hayo niliyagundua baada ya kupewa chumba changu na wenzangu wakaanza kunipa siri ya mule,...



    maskini kumbe nilikifata kifo changu mwenyewe! ni siri ilojificha



    Niistoria ambayo katu sikuikubali katika kichwa changu!



    "dada janeth! ni bora na maisha ya mtaani!,kuliko maisha ya hapa kituoni,



    kituo hiki ni kama danguro la waheshimiwa ambao uja hapa kukuchukua kwa kuwatumia walinzi wao wanaenda kututumia na kuturudisha,



    wakituletea misaada uja na waandishi ili waonekane watu wema kumbe ni wanafki walovaa ngozi ya chui katika miili yao....



    kuna kipindi wenzetu uja kuchukuliwa na huwa atujui upelekwa wapi shuleni atupelekwi,manyanyaso mengi utajionea tu dada..."



    alinieleza msichana rika langu ambalo alikuwa na asili ya alibino VERO! moyo uliniuma kwa kugundua kuwa bado nilikuwa mtumwa..



    mtumwa katika nchi yangu



    Tulilala



    lakini usiku huo wa kwanza katu sikupata usingizi nikifikiria jinsi ya kukichunguza kituo kile.



    sikujua madhara ambayo yangenikuta pindi nikiwa katika kuyachunguza mazingira yale.



    asubuhi tuliamshwa na kengele tukaanza kufanya kazi ya kusafisha mazingira ya ndani ya kituo kile.



    baada ya kumaliza usafi tukaoga...



    hakika kimuonekano nilibadilika nilikuwa mrembo maradufu ya nilivyokuwa mtaani,



    ilipofika mchana rafiki yangu VERO aliitwa kwa madam aliporudi uso wake ulijaa simanzi.



    ilikuwa ni siku yake naye kutumia akanambia ameambiwa ajiandae usiku angechukuliwa na gari la kituoni kuna mahali angepelekwa.



    moyo wangu ukapiga paaa!



    chachu ya kutaka kujua kulikoni ikanivaa



    "lazima niende"



    nikawaza,



    nikipanga kitu nimepanga japo sikumwambia vero dhumuni langu usiku kwa kunyata na kujificha nilienda nikaingia katika buti ya gari ya kituo kile...



    baada ya masaa kadhaa gari ikaondoka pasina kuelewa ni wapi inapoelekea safari ilikuwa ndefu na ghafla ikasimama nikamsikia vero akilia



    huku hatua za watu vishindo vikisikika,nilikaa dakika chache pakiwa kimya nami nikaamua kujishusha toka ndani ya ile buti kumbe tulikuwa porini nilistaajabu lipi lengo la kumleta binti huyu huku.



    nikawaza kwa mwendo wa taratibu nikachungulia ndani ya gari ile ambapo nilikuta simu moja ipo katika kiti kilichokuwepo karibu na mlango nlokuwepo!.....





    mara mbili sikuwaza kuikwapua ile simu!,nikaanza kunyata kuelekea kule nliposikia sauti ya VERO akilia huku akiomba msaada!



    nilinyata kwa uangalifu mwili wote ukintetema mpaka karibu na eneo la tukio...



    mbele nilimshuhudia "kigogo" mmiliki wa kituo kile akiwa nadhifu ndani ya suti maridadi ya ghali mno,kushoto kwake alikuwa kijana mmoja aliyechakaa usoni kwa manundu,mkononi alishika kamba,



    pembeni ya manundu alikwepo kijana mwingine dizaini yake alishika kisu chenye muwako,wenye makali ya kutosha wa mwisho alikwepo ni dereva ambaye akushika kitu chini kulikuwa na mifuko maalumu shoka,panga vyote vikionekana kunolewa.



    "wanamchinja!"



    nikawaza....



    VERO walimfunga kwa kamba madhubuti katika mti ule.



    manundu aloshika fimbo akiiteremsha katika mwili wake pasina huruma.



    bila shaka acount zao zilituna.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "wamemkosea nini huyu binti!"



    nikanong'ona,kabla sijakumbuka uwepo wa simu katika mkono wangu! nilijua cha kufanya kwanza nikaweka "silence" ikiwa mtu atapiga istoe kelele



    pili nikaweka pin cord zangu kwa kuwa aikuwekwa nkaenda upande wa camera nikampiga mmoja mmoja kwa siri kubwa sana huku nikiadhibika kwa kilio cha rafiki yangu



    "don G yatosha sasa maliza kazi!"



    nikatoka upande wa camera nkawa narecord kabisa,kijana aloshika kamba nlomtambua kama DON G kutoka kusikia kwa kigogo alimvamia VERO na kuanza kumnyonga kwa kamba ile nilishindwa kuvumilia uovu ule,aja ndogo bila ridhaa yangu ikantoka.vero akatulia tuli,wakamfungua katika mti ule kama kifurushi akadondoka...



    wakaanza kumkata kiungo kimoja kimoja na kumuweka katika mifuko ile laini.



    kwa haraka baada ya kuchukua tukio zima na kuridhika ni karudi kuelekea katika buti,..



    mwili ukintetemeka.katu sikujua kama vifurushi vile vya viungo vya rafiki yangu VERO vingekuja kuifadhiwa katika buti lile



    USILOLIJUA NI KAMA USIKU WA KIZA.



    nikajikunyata ndani ya buti lile kabla ya kusikia hatua za watu zikija kuelekea upande wa nyuma na ghafla buti likafunguliwa.....



    moyo ukanipasuka paaaa



    "nimekwisha JANETH miye..."





    Saa moja usiku tuliishia pale ambapo vijana wamelisogelea buti tayari kwa kulifunguwa waweke furushi la viungo vya albino



    'Nimekwisha Janeth mimi'



    Nikawaza kabla ya kugutushwa na sauti kali,kutoka kwa kigogo yule wa chama tawala....



    "DON G hiyo malighafi si yakuweka kwenye buti inatakiwa niishikilie ndani ya gari...si unajua tena masharti? kuwa waziri si kazi nyepesi!"



    mwenye sura mbovu ilotawaliwa na ngeu DON G akaachia boneti la buti pasina kuangalia kilichomo ndani ya buti lile, macho yake yalikuwa kwa bosi wake aloniingiza katika kituo kile.



    giza lililotawala na kunakshiwa na mwangaza angaavu wa nyota chache zilizokwepo muda ule wa usiku ulikuwa msaada kwangu wa kutoonekana kirahisi na binadamu yule mwenye roho mbaya.



    na pia masharti ya mganga alompa kigogo yule juu ya kuleta viungo vya mwili wa albino akiwa kavishika pasina kuviweka chini ilikuwa chachu ya mimi kuendelea kuiona dunia...



    baada ya dakika chache gari ikaondoka! ilifika mahali ikasimama nikafungua boneti kidogo kuchungulia akashuka mheshimiwa yule na mfuko wake aloifadhi viungo vile akaingia navyo katika nyumba ilokuwa maeneo yale,



    nyumba ya mganga



    nilitamani kushuka ila uwepo wa viumbe katili ndani ya gari ilinisitisha wazo langu ilo.,.nikabaki nimetulia mule mule!



    dakika chache mheshimiwa akarudi koti lake la suti likiwa limechafuka damu.



    niliizima ile simu nikikwepa kupigwa pindi mwenyewe akigundua!



    kutokuwepo kwa simu yake japo nilijua alishagundua.sikujua kilichoendelea juu yao...



    gari ikaondolewa.



    tukafika mpaka nyumbani kwa muheshimiwa naye akashuka na vibaraka wake. tukarudi kituoni...



    baada ya kuwasili kituoni dereva akaipaki gari na kuondoka.



    nilikaa kidogo nami nikatoka kule kwenye buti.na kuelekea chumbani kwangu.



    akukuwa na mtu nilipocheki saa ilikuwa saa 4 kasoro usiku muda huo walikuwa kwenye sala.



    nikaingia bafuni kuoga baada ya kutoka bafuni nikafunga mlango nikatoa ile simu na kuanza kuangalia matukio yote niliyorekodi! mwili wote ukisisimka.....



    "ongera!,ongera!,ongera!...."



    niligutushwa na sauti kali huku mtu akitoka chini ya mvungu wa kitanda.



    "nilijua utarudi,nilikuona ukiingia kwenye buti..."



    Mshtuko nilioupata,sitoweza kuuwasilisha kwa maneno ZUBERI!



    niliiachia ile simu kwa uoga lakini mtu yule aliwahi kuidaka...

    na kuntumbulia macho ya mshangao!



    JANETH aliendelea kunsimulia!



    "nsamehe madaam!"



    kwa uoga nikapiga magoti kumuomba msamaha dada yule ambaye alikuwa upande wa afya kituoni pale.,



    akusema kitu akaangalia ile simu tukio zima uso wake ukipambwa na tabasamu.



    "ni mwanamke wa kwanza kugundua ulichokugundua!...



    ni mwanamke wa kwanza jasiri machoni mwangu! karibu mchezoni JANETH!"



    yah! sikumuelewa,pasina kusema kitu kwa mwendo wa madoido MADAM yule akatoka! simu yangu akunikabidhi.



    kichwa changu kilitawala mawazo sana!



    'huyu madam vipi? ana mahana gani? ndo nini sasa?! niondoke ntaondoka vipi? nilichanganyikiwa!



    KARIBU MCHEZONI,...'



    Mchezo gani alomaanisha madamu yule! kwa nini akunichukulia hatua?!



    nikawaza bila kuwazua!

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    sifa moja ya madam ni upole,usiri uliongezeka...



    nilishtuka mlango ukifunguliwa wasichana wenzangu wakaingia walitoka kwenye sala.



    "JANETH mbona ujaja kwenye sala?"



    binti mmoja akanioji!, sikujibu, nikajibwaga katika kitanda nikishika kichwa kwa mawazo.



    MADAM SALOME alinchanganya!, sikuitaji kuongea na mtu,kaondoka na ushaidi ntafanya nini miye nkazidi kuwaza.



    japokuwa usingizi ulintenga muda ulienda haraka haraka! sikuitamani kesho ifike kwa kujua ndo hatma yangu!...



    VERO hakuwepo duniani tena naimani kesho ndo siku yangu ya mwisho.



    nikajiwazia kabla usingizi wa mangamungamu ujachukua hatamu na kunlaza...



    ilikuwa saa NANE na ushee usiku.



    ************



    Kengele ilinishtua ya saa kumi na moja alfajiri macho yalikataa kufumbuka,



    kutokana na uchovu,kichwa kiliniuma kutokana na mawazo pengine na rundo la usingizi nikajiamsha wakati natoka nikakutana na MADAM S mlangoni



    "ndo nilikuwa nakufata wewe! nakuitaji ofisini kwangu baada ya kupata kifungua kinywaa"



    aliongea pasina mzahaa,akusubiri nijibu akageuza na kuondoka...



    kimbelembele kimeniponza mimi sasa naenda kufa kikatili eeeh MUNGU WANGU NILINDE mimi...





    Mawazo yalitiririka kichwani mwangu!...



    wito wa madam S! ulinifanya mwili ufe ganzi! ila sikuwa na budi kwenda!



    kama ni maji yameshamwagika,..



    nimeshayavulia nguo sina budi kuyaoga...



    baada ya kazi ndogondogo...



    nikiacha baadhi ya wasichana wakijipara kuwavutia vigogo kwa walopenda kazi ile,na wengine wakiwa kiunyonge kwa kukosa tumaini la uponyaji wa maisha yao...



    nikapiga hatua fupifupi kuelekea kwa madamu...



    nilifika nikabisha hodi mara moja kabla ya kukaribishwa nikaingia...



    madam akanipa ishara niketi nikaketi...



    akauendea mlango na kuufunga

    moyo ukapiga paaaaa!



    "sasa ndo namalizwaa!"



    nikawaza huku nikianza kurudi nyuma.



    kabla sijazuiwa na kiti kile.



    madam aliniangalia huku akitabasamu akatoa karatasi moja na kunipa nisome....



    "ongera JANETH,wewe ni mwanamke jasiri mwenye kiu ya ukombozi wa wanawake wenzako...



    usiniogope mimi ni mpelelezi kutoka katika nchi ya Kinte nimekuja kwa lengo moja tu,lengo kama la kwako...



    Ila sasa kazi yangu imekuwa ngumu kwa kuwa wahusika ni vigogo wa nchi hii,wakiwemo mawaziri,wabunge...



    ivyo kutokea kwa msaada ni faraja kwangu! nyumba hii inaulinzi wa camera katika kila kona hata hapo usomapo unaonekana...



    na wataitaji kujua unasoma nini?!...



    katika chumba cha camera tunakaa kwa zamu...ile siku wakati ukiingia katika gari ile ilikuwa ni zamu yangu nilikuona...



    sikutaka kukufatilia kwa kuwa nilijua dhumuni lako nikaharibu ile camera nkaja kujificha huku kukusubiri mpaka leo hii camera ijajengwa



    najua ninalakujibu tuachane na hayo simu yako ipo posta katika box langu lenye namba 101 ufunguo wake upo nyumbani kwa madam mery katika mto wake sijui utaingiaje huko utoe kwa kuwa nyumba inaulinzi imara.



    lazima uingie,nimeuweka ivyo kwa maana mchawi mpe mtoto wako akulelee...



    najua sina muda mwingi sana, ukishindwa nenda mtaa wazambi mwone bi mtama mwambie akupe namba za mkuu.



    uzipige atajua jinsi ya kukusaidia ikiwa utatoka humu salama mwisho umalizapo kusoma karatasi ili litafune na utoke kimyakimya ntakutengenezea mazingira utoke ukafanye kama Nilivyokwambia...



    baada ya MADAM S kunambia vile nikalitupa lile karatasi mdomoni..na kuufata mlango nkaufungua na kutoka katu atukuongea kitu.



    kweli nilijiona nimeshakuwa mpelelez tena si wa nchi hii teh teh teh..."



    wote mimi na JANETH tukacheka.



    "zuberi mpz wangu!"



    akaniita.



    "endelea beby"



    nikamwambia



    "sa kumi sasa waitajika ulale.,"



    "amna kulala endelea kidogo"



    "ok mpz nikatoka katika ofisi ile mbele kidogo moyo ukapiga paaa baada ya kuwaona watu wawili,



    "ndo wenyewe"



    nikajisemea macho yangu yakiwa katika sura zao mbovu.



    yah ni MANUNDU na mwenzake DON G wakanipita bila kunsemesha.hari ya upelelezi ikanivaa.



    "wanaenda kwa madam kufanyeje?!"

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    nikawaza,ghafla nkasikia yowe...



    sikusubiri kurudi kule mbio.



    nkaingia



    mandhari nlokutana nayo mule ndani ilinisababisha niachie yowe yowe lilitotawaliwa na wahka!...



    khofu miguu ikintetema...





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog