Search This Blog

Saturday, July 16, 2022

MSICHANA WANGU WA KWANZA - 4







    Simulizi : Msichana Wangu Wa Kwanza

    Sehemu Ya Nne (4)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Nashukuru, mfalme wangu kwa kugundua hilo. Labda ngoja nikufafanulie kidogo. Embe liwapo changa, huwa na ukakasi uliojaa utomvu, lakini huendelea kukuwa na kufikia kuwa katika hali ya ukakasi, hapo sasa huweza kuleta hitilafu kwa watumiaji au lisilete hitilafu kwao kutokana na hali waliyonayo muda huo muafaka. Kuna wapendao maembe mabichi na kuna wasiopenda, lakini embe huvumilia vikwazo vyote hivyo na hadi kufikia hatua ya kuiva. Sasa hapo liivapo, hakuna anaelichukia kila mtu hulipenda na kutamani apate angalau ladha ya'lo."



    "Una maana gani kusema hivyo mpenzi?"



    "anhaa, namaanisha kwamba. Kipindi tunaanza mahusiano hakuna kati yetu aliemjua mwenzie lakini tuling'ang'aniana hivyohvyo kama utomvu na embe changa. Lakini kadri siku zilivyoenda ulifika muda ambao, wewe ulinikwaza na nikakusamehe na hata mimi nilikukwaza nawe ukanisamehe. Kipindi hicho ndicho kilikuwa kikikuza chachu ya embe. Kila mtu huchukulia tofauti. Na hata sasa, mimi na wewe twaweza sema tumefikia kwenye embe lililokwiva. Hivyo nakuomba litumie vizuri nami nitafanya hivyo ilikuepusha Inzi wasilifatilie na kuliharibu." Aliongea Zulfa.





    Baada ya Sumaya kufafanua maneno yake kwa ustadi wa hali ya juu. Hapo Nurdin akabaki ameduwaa kusikia maneno yenye radha tamu kama ile, dalili za machozi zikaanza kuonekana. Naye kwa hiyari akazipeleka hisia zake ilizisindikizane na machozi yake.



    "Mpenzi mbona unaanza kulia?" Aliuliza Sumaya huku akiichukuwa mikono yake na kuifutisha machozi yaliyoendelea kumtoka mpenzi wake. Alipoona Nurdin hamjibu. Hapo akaita kisha nurdin akaitika, "Nurdin au nimekuudhi. Tafadhali sema, nimekukwaza? Eh, mbona hivyo lakini Nurdin wangu! Achakulia." Maneno ya Sumaya nikama yaliendelea kuzidisha machozi kwa Nurdin.



    "Hapana Sumaya. Hujaniudhi wala hujanikera na hata hujafanya chochote kinachofanana na hayo. Haya machozi yanayonitoka. Hayanitoki kwa huzuni bali kwa raha niipatayo ndani ya penzi lako. Raha ambayo inanifanya nishindwe kuyakabili machozi yangu. Hakika unamaneno mazuri sana. Tafadhali kupitia heshma ya machozi hebu naomba ni ahidi kuwa hutoniacha hata siku moja, utanibeba nitakaposhindwa kutembea, utaniokota nitakapoanguka, utakuwa na'mi kwa hali yoyote ile." Aliongea Nurdin. Hapo sasa akawa kama ametekenya machozi ya Sumaya. Taratibu nayoyakaanza kummiminika. Wote kwa pamoja wakaanza kufutana machozi na kila walivyofutana ndivyo walivyoendelea kumwaga machozi.



    "Nurdin wangu.. Na kuahidi mbele ya machozi yetu. Machozi yenye furaha ndani yake... Sitokuacha abadani, hata litokee jambo gani mimi nitakuwa nawe.. Nitasimama upande wako kwenye anguko na ushindi wako. Nitalihifadhi pendo lako kwenye chumba cha furaha kilichomo ndani ya Moyo wangu, sitokuumiza nakuomba nawe usijeniumiza maana nakupenda sana." Aliongea Sumaya huku macho yake akiwa ameyaangalizisha chini. Hali yakuwa Nurdin kwa muda huo akiwa ameyakaza macho yake na kuyaangalizisha usoni mwa Sumayah pasina kuyapepesa.



    Haya ahadi yao ikawa imewekwa toka hapo. Siku zikaenda, zikapita hatimae Nurdin aliamishiwa Dar-es-salaam kimasomo. Alimuaga mpenzi wake huku huzuni ikiwatawala wote wawili. Pia hawakusita kukumbushana juu ya kulinda ahadi. Nurdin alimuacha Sumaya na rafiki yake mpendwa Samir kisha akampa mamlaka Samir yakunasibu furaha ya Sumaya.



    Ndani ya jiji la Dar-es-salaam magari mengi yalionekana kujazana maeneo ya stand ya Ubungo. Yalikuwa majira ya jioni ndipo Nurdin alipotuwa Maeneo ya ubungo na kwa mara ya kwanza akakanyaga ardhi ya jiji hilo. Jiji alilokuwa akilisikia tu nakutamani siku moja aje kuangalau kutua ndani ya jiji hilo iliaweze kuona kile kilichowafanya watu wafurahi na kutamani kufika huko. Alifurahi sana baada ya kukanyaga ardhi hiyo kisha akawajuza wakumpokea kupitia kisimu chake cha nokia ya tochi. Alipokelewa na safari ikaanza kutoka ubungo hadi Tabata ambako ndipo alipotakiwa afikie. Alifikishwa na wakamkirimu vizuri kwakuwa usiku ulikuwa umeingia walimuacha akapumzika kutokana na uchovu wa safari. Kesho yake asubuhi waliamka nakusubiria muda wa chai. Ulipofika alikunywa chai na moja kwa moja alimuomba kijana mmoja wa rika lake ilikumtembeza angalau nae aoshe macho hata kidogo ndani ya mji huo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa muda huohuo ndani ya mkoa wa Shinyanga ambao ndio mkoa aliyotoka Nurdin. Katika shule ya sekondari. Shule ambayo Nurdin alikuwa akisomea.



    "Shem.. Vipi!! Wewe huendi leo kwenye spot and games" Ni swali kutoka kwa Sumaya alilomuuliza shemeji yake Samir na huo ulikuwa ni muda wa darasani. Muda ambao hakuwemo mwalimu. Waliongea pamoja kwasababu walikuwa kidato kimoja tena kidato cha kwanza tu.



    "Hapana.. Mie Ijumaa huwa naiheshimu sana. Kwenye debate nitakuwepo lalini muda wa michezo nitakuwa msikitini. Napenda michezo ila siwezi acha kwenda msikitini kisa Debate."



    "Ni kweli upo sawa kabisa. Lakini hapa shuleni siunajua ratiba wamezibana sana. Mimi itabidi leo nisiende msikitini maana na husika kwenye michezo. Mungu anisamehe kwa leo." Aliongea Sumaya. Hapo Samir akaonesha kutokupendezwa na kauli ya Sumaya.



    "We.. Yaani uache kumuomba Mungu kisa michozo? Aaaah! Kwani kati ya michezo na Mungu bora nini?" Ni mdaharo mpya ambao ulianzishwa. Mdahalo ambao mwisho wa masaa ulileta ugomvi wa darasa zima maana ulipembuliwa na mwisho wa siku ukaishia kwenye maswala ya kiitikadi.



    Kelele za darasa hilo ziliweza kupenya bila vizuizi hadi kwenye ngoma za masikio ya waalimu ambao walikuwa bize na mambo yao. Zilipozidi walimu walikuja na kuwaadhibu wanafunzi wale.



    Haya hatimae ulifika muda wa kuswali Samir yeye alienda msikitini huku Zulfa akibakia kwa ajili ya mchezo wa pete na kwa siku hiyo kulikuwa na mechi kati ya kidato cha kwanza na kidato channe.



    Kama ilivyoada wanafunzi wote hukutana kwenye ukumbi wa shule na kuangalia michezo mbalimbali. Kulikuwa na maigizo, michezo ya karate, na michezo mingine mingi iliyotangulia. Ulipofika muda ha wasanii wa nyimbo za hisia.. Hapo ndipo alipopanda kijana mmoja mgeni ambae kwa siku hiyo ndiyo aliyo ripoti shule na kuomba nae atumbuize japo kidogo.



    Anaitwa Erick.. Kijana mtaalamu wa kuchezea gita pamoja na kuimba nyimbo za kuulalamikia moyo. Siku hiyo aliomba nafasi ya kutoaonyesho japo kidogo. Alipewa nafasi kisha akapanda jukwaani huku mgongoni akiwa amebeba gitaa lililoshikiliwa na mkanda maalumu uliomkaa vilivyo na kumfanya aonekane kapendeza zaidi. Kuachilia mbali nguo za kisasa alizokuwa amezivaa vilevile mwili wake ulionekana kujengeka kimazoezi kwa haraka haraka ungesema kuwa ni mcheza basketball au mpira wa kikapu kwa lugha ya nyumbani.



    Alichukuwa maiki na kuikaribisha mkabala kabisa na mdomo wake. Kisha akafumba macho huku akivuta pumzi. Alipokuja uitoa sauti ilitoka sauti nzuri ingawa alikuwa anaimba kwa kulalamika lakini hiyo haikumfanya ashindwe kuyapangilia maneno ya nyimbo hiyo. Dah! Kila mtu alipatwa na hisia kali. Kuna waliyofakamia huzuni, kuna waliyobaki wamenuna kutokana na ukali wa maneno ya kwenye nyimbo hiyo lakini pia kuna waliyoangusha machozi yao bila kujijua. Hakika ilikuwa ni fulu majonzi.



    Wimbo ule ulionesha kumchoma zaidi Sumaya. Yeye alishindwa kujizuia ndipo alipoona nivyema aondoke ukumbini mule. Alinyanyuka na kukimbia moja kwa moja hadi darasani mwao. Hata alipofika alilifakamia dawati lake na kuliinamia kishaakaanza kutoa kilio cha kwikwi.



    Alivuta hisia kisha akamkumbuka kijana yule mtanashati. Kisha akavuta hisia na kukumbuka jinsi kijana yule alivyokuwa akiimba kwa hisia. Aliukumbuka wimbo ule uliyoitwa 'Who loves me' aaah.. Hapo sasa akawa kama mtu aliyeingiwa na kitu fulani chenye utamu kama asali kisha kikaupiga moyo wake na kumfanya ashtuke wala asijue kama amepatwa na raha ya asali au maumivu ya kupigwa. Kwakuwa alikuwa mzoefu hapo moja kwa moja alitambua kuwa tayari amependa.



    Alitamani angalau apeane hata salamu na kijana yule mpya pale shuleni.



    "Lazma nionane nae. Haijalishi... Kwanza nimeahirisha kwenda mazoezini lazma nimtafute." Alinyanyuka kwenye dawati na kutoka nje ya darasa. Alikuta wanafunzi wakijiandaa kwenda uwanjani. Yeye hakujali zaidi alianza kumuulizia kijana yule. Hakupata usumbufu sana kwakuwa kijana yule alikuwa mgeni istoshe kwa muda huo alipata umaarufu ghafla. Alimuona kwambali akamfuata.



    "Mambo kaka." Alijulia hali Sumaya.



    "powa tu." Alijibu Erick kwa mkato.



    "Samahani kaka. Wewe ni mgeni hapa shuleni?" Aliuliza Sumaya utadhani hajui.



    "Ndio. Mie ni mgeni hapa." Alijibu Erick.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "ok. Karibu."Alimkaribisha erick. Na erick akaitikia kisha akamuaga ilikuondoka maeneo yale na kwenda uwanjani.



    "Ok, kwa heri." Alijibu Sumayah. Erick alipoanza kupiga hatua Sumaya alimuita tena. "mmh! Samahani kaka. Nilitaka kukupa hongera. Unajua kuimba sana" Ni kama alijipendekeza tu. Maana erick maswala ya kusifiwa yeye alikuwa kisha yazoea. Mwanzoni kipindi anaanza kuimba alikuwa akijiona mwenye ufahali na kupenda kusifiwa. Lakini kwa wakati huo. Sifa zilikuwa zimesha mchosha. Alishazizoea kwani alizipokea sana.



    "ok. Nashukuru kwa kunisifia. Labda unajingine dada yangu?" Alijibu kisha akauliza swali la nyodo. Sumaya. Hakukata tamaa..



    "jingine... Labda kiufupi naitwa Sumaya. Nami ningependa kufahamu jina lako. Unaitwa nani?" Aliuliza sumaya baada ya kujitambulisha.



    "Naitwa Erick wengi huniita Eric mavoko." alijibu erick.



    "Waaaohh! Jina zuri kama sura na sauti yako." Akachanua tabasamu eric. Tabasamu ambalo liliishia mdomoni tu. Lakini moyoni alikuwa akiona kero kusimamishwa na Sumaya.



    "ok. Unaonekana unaharaka sana. Lakini erick. Mimi nilikuwa nina ombi moja tu." Hapo erick akamwagia macho Sumaya ambae kwa wakati huo alianza kujing'atang'ata. Ni kama Erick alijua kinachoendelea kwa Sumaya. Kutokana na utaalamu wa mambo yale.



    "ok, usijali. Wewe sema ombi lako nami nitakusaidia kama kunauwezekano huo." Alijibu erick. Hapo sasa sumaya. Akazielezea hisia zake kwa Erick. Nakumuomba amkubali. Kwakuwa Erick anajijua nyota yake. Hapo akaamua kumkubali Sumaya. Na ukurasa mpya wa mapenzi ukafunguka kati ya Erick na Sumaya.



    Kwakuwa Sumaya alikuwa amenunua simu siku iliyopita. Hivyo akaomba namba za erick. Walibadilishana namba siku hiyohiyo.



    Sumaya. Alipofika nyumbani alimuwazia sana kijana yule erick. Akiwa kwenye fikra zake mara simu iliita. Kuangalia kwenye kioo. Jina lilisomeka, 'MY NURDIN'. Alipolisoma jina lile nikama alitoka kwenye mudi. Hapohapo akatengeneza hasira. Kisha akaipokea kwa ghadhabu na kuiweka sikioni.



    "Hello baby!" Ni sauti kutoka upande wa pili. Sauti ya Nurdin iliyoashiria furaha.



    "e.eee. Ukomee hapohapo. Nani unamuita baby?" ni sauti ya Sumaya. Ingawa ilimuingia nurdini ndani ya sikio. Lakini alionesha kutokuliamini sikio lake aliitoa simu yake sikioni na kutumia macho kuangalia kama amekosea namba. Lakini alishangaa kuona kuwa namba iliyosomeka ni ileile ya sumaya. Hakutaka hapo akajifanya hajaisikia sauti ile ya onyo. Akairejesha simu sikioni kisha akasema.



    "Baby... Mbona hivyo. Kuna tatizo gani? Au labda kuna mtu kakuudhi?" alijenga maswali kisha akayatupa sikioni mwa Sumaya.





    Sumaya aliona kama upuuzi kuendelea kuongea na Nurdin akaikata simu. Baada tu ya kukata simu kumbe nae mpenzi wake mpya alikuwa akihangaika kupiga lakini bize. Alipopiga tena simu ilipokelewa na Sumaya.



    "Hello mpenzi. Vipi mbona unautesa moyo wangu. Nimekupigia mara kadhaa nimekuta simu yako ipoinaongea na mtu mwingine. Kwanini lakini unafanya hivyo?" Ni sauti ya Erick iliyotoka upande wa pili wa simu ya Sumaya. Hapo Sumaya akatulia kidogo huku akili yake ikipekuwa uongo wa kudanganya.



    "Nilikuwa naongea na mjomba. Usiwe na shaka kwa hilo mpenzi. Punguza wivu." Alijifanya anaongea huku anaikata hofu yake ambayo tayari ilisomeka.



    "ok, tuachane na hayo. Vipi lakini unajisikiaje kuongea na mpenzi wako." Alianza uchokonoaji Erick. Kwa muda huo alikuwa akiongea huku akiitoa ile sauti yake ya kuimbia."



    "Najisikia raha sana. Nahisi sipo ulimwengu huu wa binadamu pekee bali nahisi nimeingia ndani ya ulimwengu wa mahaba. Sijui hata niseme nini." Alijieleza Sumaya. Huku amefumba macho ilikutengeneza hisia ya maneno.



    Akiwa kwenye maongezi yale alisikia sauti ya Mama yake ikimuita. Akaitika kishaakamuaga mpenzi wake huyo mpya na kumuomba dakika kadhaa.

    Alipotoka kumsikiliza Mama yake alirejea kwenye simu yake. Alipoangalia kwenye kioo akaona ujumbe wa maandishi akafunua kisha akausoma. Ulikuwa ni wa kuomba msamaha kwa kosa lolote lile. Jina lililosomeka lilikuwa ni lile la Nurdin.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "wanamume wengine sijui wagumu wa kuelewa? Kwani mtu akisema hakutaki sianamaana amekuchoka. Eti nikumbuke ahadi, sijui nipembue. Ha.ha.ha.ha. Huu si upuuzi. Mtu akisema hakutaki hakutaki tu. Tena kwasasa namchukia nalisauti lake libaya. Lisauti lisilojua hata kuimba. Siwezi kukubali kuwa na mtu asiyekuwa na kipaji, mwenye kipaji atanitatu lia mengi ataniimbia pale nitakapo boeka, atanipa maneno mazuri endapo nitayahitaji. Aaah! Mungu ameniletea Erick na kumtoa Nurdin. Mvulana asiye na mbele wala nyuma. Hajui afanyenini. Kwanza hana maneno matamu yenye radha ya asali. Istoshe kwasasa yupo mbali na sijui lini atarudi." Alijiambia Sumaya. Kishaakaanza kuandika ujumbe mfupi wa majibu kwa Nurdin.



    "Nurdin.. Sikutaki, kwa sababu sikuhitaji. Sikuhitaji kwa sababu mimi na mapenzi basi. Nimeamua kusoma. Kwa sasa sihitaji mwanamume. Nakuomba usinipotezee muda wangu" Ujumbe huo ulisomeka hivyo kwenye inbox ya Nurdin. Aliuangalia mara mbilimbili huku akikosa uamuzi sahihi ndani ya kichwa chake. Palepale mapigo ya moyo wake yaka zidisha mwendo kasi, hisia zikamrudisha mbali akaanza kukumbuka jinsi penzi lao lilivyokuwa limenoga, akaanza kukumbuka ahadi mbalimbali walizo ahidiana, akakumbuka jinsi alivyo ambawa kuwa hatoumizwa. Masikini Nurdini pasina hiyari akajikuta akitokwa na machozi. Aliirejea ile sms naakaisoma huku ikimshinda kutokana na maneno magumu yaliyo ujeruhi moyo wake.



    "Haiwezekani.. Sumaya... Umenifanyia hivi... Aaah, kosa langu nini mimi. Au kukupenda? Lakini mbona makubaliano yetu hayakuwa hivi? Hapana.. Sikubali." Alijiongelea Nurdin huku akifuta kamasi jembamba lililoendelea kuisaliti pua yake. Hakukubali kabisa maneno yale kumuaminisha kuwa amempoteza mpenzi wake. Hapo akaandika namba za Sumaya ambazo tayari amekwisha zikariri kisha akapiga. Simu iliita.. Ikaitaa.. Mpaka ikafikia hatua ya mwisho ndipo ikapokelewa.



    "Enhee..! Sema." Ni sauti kavu iliyotoka kwa Sumaya. Sauti ambayo hajawahi kuiongea mbele ya mpenzi wake huyo. Nurdin akajifanya haisikii japokuwa tayari alarm ya hatari ilikuwa imeshagönga kichwani mwake.



    "Sam.. Samahani. Mpenzi w..." hata kabla hajamalizia alidakwa na kauli ya Sumaya. "Ishia hapohapo. Nani mpenzi wako? Tena tafadhali ulikome hilo jina kama ambavyo ulilikoma titi la mama yako. Kama unalakuongea ongea. Lakini kama huo upuuzi wako. Nimeshakwambia sihitaji kwasasa. Niache nisome sina shida na mwanamume. Hata kama nikipata shida siwezi kuwa na mtu kama wewe tena." Hapo Nurdin, alishindwa aitoe simu yake sikioni au aiache. Alitaka kuongea lakini mdomo ulishindwa kutoa hata silabi. Alibaki akilia kilio cha maumivu. Hakuwahi kuyapata maumivu hata siku moja. Aliishia kusimuliwa na rafiki yake Samir kuwa mapenzi yanaumiza.



    Ilikuwa jioni, hatimae hadi usiku Nurdin analiatu. Alipokaribishwa chakula hakwenda kula, si kwasababu ya kukasirika mpaka kukinunia chakula. Bali ni kwasababu hakuwa na hamu ya chakula wala hakuitaji kukigusa kabisa. Mawazo yaliendelea kumsumbua usiku huo.



    "Nampenda na yeye hilo analijua, lakini ameamua kuniumiza. Tazama nafsi yangu inasononeka, moyo wangu unaniuma, ona macho yamelia hadi machozi kukauka kisa yeye. Nikama ameingia kichwani mwangu na kuivuruga akili yangu. Sijala toka jana hata nikijing'ang'aniza. Hamu ya kula inatoweka. Samir.. Mapenzi yanauma, we acha tu. Laiti ningejua kuwa mapenzi yanatesa kiasi hiki. Basi nisinge thubutu kupenda." Aliendelea kumuhadithia rafiki yake samir.



    Mpenzi msomaji. Asikudanganye mtu hakika mapenzi yanauma vibaya.



    Mapenzi yanaweza kukufanya ukaamua jambo ambalo hukuwahi kutarajia maishani mwako. Ona leo Nurdin anashindwa hadi kula kisa mapenzi. Analia kilio cha aibu, hata anafikia kuogopa kutoka nje kisa mapenzi.



    "Sikia rafiki yangu Nurdin. Nayajua mapenzi, natambua maumivu ya mapenzi. Ni kweli kwa jinsi ulivyonisimulia hilo ni jambo la kushangaza sana. Sikutaraji kama Sumaya, anaweza kukufanyia hivyo. Lakini amini. Ndivyo ilivyotokea na hakuna njia nyingine hapo. Nadhani kipindi mnakubaliana alikukubali ilhali anasoma, sasa vipi leo akwambie umuache asome. Kwani kipindi uponae alikuwa hasomi? Au una muathiri kitu gani hadi ashindwe kusoma awapo na wewe?. Ukifikiria kwa umakini utapata jibu kuwa huo ni ujanja tu anaoutumia kukuacha. Mimi siwezi kukubali rafiki yangu uanze kumnyenyekea mwanamke. Unajua mwanamke akinyenyekewa hujiona kwamba yeye ndie kila kitu na hapo utaingia kwenye kundi la wale wanaolazimisha mapenzi na kama ujuavyo mapenzi haya lazimishwi hata siku moja. Wanasema jifanye mjinga siku ipite.. Lakini siyo kwa mwanamke. Ukijifanya mjinga kwa mwanamke siku haiwezi kupita bali atakuchafua tu na kukuumiza. Ninajua jinsi gani mapenzi yanauma kwasababu nishaumia hivyo sihtaji wewe rafki yangu uumie kama nilivyoumia. Ona sasa huwezi kula, unakesha ukilia tu. Jiulize Je, utaendelea kumlilia hadi lini mtu asiye na mawazo hata na kukufuta machozi? Je, utaacha kula hadi lini kisa mtu ambae kila muda anajaza tumbo lake na hata hana mawazo na wewe. Sasa hapo jitahidi mfute. Kachukue chakula weka hamu ya kula na uhakika kitalika. Huyo siyo wako tena, wewe muache aende huenda Mungu amemtoa mapema iliasikuletee madhara huko baadae. Tafadhali usiache kula kisa mwanamke." Ni ushauri wa Samir uliyomuendea vilivyo rafiki yake Nurdin. Lakini Nurdin ni kama alikuwa akihitaji maelewano na siyokuachana kama alivyoshauriwa na rafiki yake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Samir... Hivi unadhani nitaweza vipi kula wakati nikila mawazo ya ajabu yananiandama na kuchafua roho kisha hamu ya chakula inatoweka. Na je, unadhani mimi nitaweza vipi kuishi bila yeye? Minilikuwa naomba unipe ushauri jinsi ya kumfanya arudi nasiyo kunishauri ni mtoe." Aliongea Nurdin. Masikini mapenzi yanamfanya Nurdin awe mtumwa. Ati anampenda na anakili kuwa kumuacha hawezi. Japo anatendwa na kudhalilishwa kimapenzi lakini anaishia kushuka chini tu.



    "Sikia ni kwambie rafiki yangu. Hapa nimejiunga cheka time ya elfu moja na ninahisi dakika zimekaribia kuisha. Ila hicho unachotaka kufanya ni kulazimsha mapenzi. Na ukweli ni kuwa, mapenzi haya lazimishwi.. Yanini kujipa makosa wakati unajijua kabisa haujakosea. Ok.. Tuachane na hayo. We jitahidi ule mimi kesho kutwa jumatatu nitaongea nae kwamapana na marefu." Waliongea na kukubaliana kusaidiana kisha mpaka salio lika kata.



    Weekend ilipita hatimae jumatatu. Samir alikuwa ameweka nadhir ya kuongea na Sumaya. Alimuona na kumuita kisha akamwambia kuwa anashida na yeye hivyo muda wa mapumziko amtafute.



    Walikubaliana kutafutana muda ule, lakini ulipofika muda wa mapumziko. Sumaya nikama alipuuza na kwenda kwa Erick yule mpenzi wake mpya. Samir alidhani huenda Sumaya amejisahau ikabidi amtafute yeye mwenyewe. Aliulizia na kuambiwa kuwa Sumaya yupo nyuma ya madarasa ya kidato cha kwanza. Aliamua kwenda huko na ndiko alikomkuta Sumaya na Erick wakiwa wamekaa kimapozi ya walaakini. Kwa harakaharaka Samir aliuelewa mchezo maana alipofika tu. Hofu ya Sumaya ilishindwa kujificha na kubakia usoni mwake. Hapo Samir akaamua kujifanya kama mpitaji tu na kuwapa salamu kisha akaondoka pale. Na hapo ndipo akagundua kwanini rafiki yake ametemwa.



    "Kumbe. Haka kamchizi kasanii ndiko kamempiku jamaa. Ayaaa.. Wanawake bhana. Haya achanijifanye sijui. Nitamvizia muda kukiwa hamna vipindi darasani ilinimfuate tuöngee ilianipe sababu ya yeye kumtosa mshikaji." Alijisemea Samir, na hata ilipogongwa kengele ya darasani. Wanafunzi wote walirejea na kwa bahati nzuri kulikuwa na free double piriod. Samir alipoangalia ratiba alifurahi sana na moja kwa moja akamfuata Sumaya na wakaanza kuongea.



    Alimuhoji maswali kadhaa kama, kisa cha yeye kumuacha Nurdini. Kwanini alikuwa akitoa ahadi za uongo. Maswali hayo yalikuwa ni magumu sana kwa upande wa sumaya hata majibu yake hayakuwa yakuridhisha. Ati nilimuacha tu, mara hakuna sababu yoyote ila ni maamuzi tu. Mara namchukia huyo Nurdin wako hata sitaki kumuona. Kwakuwa Samir ni mzoefu, tayari aligundua kilichokuwa kikimsumbua Sumaya kwa muda huo. Na hakusita kumwambia kuhusu Erick. Lakini Sumaya alikataa katakata na kusema ati. Erick ni rafiki yake tu. Kama walivyo marafiki wengine.



    Haya.. Jioni ilipofika kama kawaida ya wapenzi hao wapya. Erick alimpigia simu Sumaya na kumuita maeneo fulani kisha wakavinjari huko huku Sumaya akizidi kukolea zaidi kwa kuimbiwa nyimbo.



    Samir nae hakuwa nyuma katika upelelezi wake na haikumchukuwa muda tayari aligundua kuwa Sumaya anamahusiano ya kimapenzi na Erick. Alipogundua hivyo aliamua kumwambia Nurdin.





    Nurdini aliumia sana baada ya kupata taarifa zile alijikuta akiwachukia wasichana na kuyachukia mapenzi kwa ujumla. Lakini kuchukia kwake mapenzi hakukuweza kubadilisha chochote. Tayari Sumaya siwake tena. Bali ni wa Erick ambae ni msanii.



    Kidonda cha mapenzi ni zaidi ya kidonda ndugu. Chenyewe huwa hakiponi na hutoneshwa kwa hisia tu, Nurdin alijitahidi kusahau lakini mara kwa mara alijikuta akikitonesha kidonda chake kwa kujikutaamekumbuka mambo kadhaa waliyokuwa wanafanya na mpenzi wake huyo ambae kwasasa hayupo tena nae. Aliumia sana na ndipo alipoamua apoze maumivu kwakutafuta msichana mwingine hukohuko Dar-es-salaam. Naam, alibahatika kupata msichana mrembo na mzuri, mwenye kila sifa za kugombea uongozi wa moyo wake. Msichana huyo aliitwa Hadiya mtoto wa shekh mmoja hukohuko dar-es-salaam. Mapenzi kati ya Hadiya na Nurdin yalipamba sana. Japo kuwa Nurdin aliingia kwa tahadhari kubwa, lakini miaka mitatu tu ilimfanyaaamini kuwa yapo mapenzi ya kweli. Alikaa na msichana yule aliyempoza maumivu mpaka hapo msichana yule alipohama shule na kupelekwa uarabuni kwa ajili ya kwenda kusoma huko.



    Hapo Nurdin akajua tayari kabisa ameshampoteza mpenzi wake huyo. Kwakuwa tayari alikwisha kolea kimapenzi. Alishindwa kumsubiri Hadiya ambae hata kurudi hakujulikana atarudi lini. Siku moja Nurdin alipigiwa simu na alipokea alisikia sauti ya kike ikilalamika.



    "Samahani kaka angu. Nimehangaika sana kupata namba zako hadi leo nimezipata nashukuru sana. Naitwa Milfaty... Nasomea shule moja Ilala.. Mimi ni rafiki yake na Zuwena dada yako wewe. Nadhani umeshanipata." Ni sauti ya upande wa pili wa simu iliyokuwa ikijaribu kumuelewesha Nurdin. Hapo Nurdin akawa amemjua binti yule pale aliposema kuwa yeye ni rafiki yake na Zuwena ambae ni dada yake na Nurdin. Anatambua wazi kuwa Milfaty huja marakwamara nyumbani kwao na anaurafiki wa karibu na Zuwena. Lakini hakutambua kuwa Milfaty tayari alikuwa ameshavutiwa na Nurdin.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Aaaaa.. Nimeshakupata. Wewe siyule ambae hata jana ulikuja nyumbani kumuulizia sista Zuwena?"



    "Enhee.. Ndio mimi," akavuta pumzi kisha akaendelea. "Kaka samahani.. Nilikuwa naomba kuonana na wewe kuna jambo muhimu sana nahitaji tuongee.. Sijui nitakupata vipi?" Alihoji Milfaty.



    "amhh.. Mimi mbona kunipata sio shida.. Wewe njøo tu nyumbani utanikuta."



    "Hapana kaka yangu. Kama ningelihitajikuongea nawewe nyumbani mbona ningeweza. Lakini maongezi ninayohtaji kuongea nawe.. Si yanyumbani."



    "Ok, basi chagua wewe. Wapi tukutane ilituweze kuongea zaidi."



    "...mi ningependa tukutane Cocobeach siku ya leo. Tafadhali naomba tuonane."



    "Dah! Dada yangu mwenzio nipo doro hapa. Sina chochote.. Hata hiyo pesa ya nauli yakuja huko sina."



    "Wewe.. Usijali kuhusu pesa. Nitakutumia ya nauli.. Pamoja na maji ya kunywa kidogo. Fanya njoo sasa hivi." Nurdin kusikia hivyo alishukuru sana na ukizingatia alitamani sana kutoka siku hiyo lakini alishindwa kutokana na kukosa pesa. Alitulia kidogo mara ghafla simu yake ikaleta ujumbe mfupi. Baada ya kutazama kwenye screen aligundua kuwa ni ujumbe kutoka M-pesa. Alipoufungua akakuta amerushiwa shilingi elfu ishirini na tano. Alifurahi sana. Harakaharaka akajiandaa na kutoa pesa ile kisha akachukuwa daladala moja kwa moja hadi cocobeach. Alipofika alimpigia simu na kupewa maelekezo ya mahali pakukutania. Alimkuta binti yule kwenye moja kati ya grosari zilizopo maeneo yale. Aliketi kitini na kupeana salamu.



    Macho ya Nurdin, yalikuwa yameshauzoea uzuri wa milfaty hivyo haikumsumbua sana. Ni kweli milfaty ni mzuri.



    "Pole na uchovu wa safari. Pia samahani kwa wito huu wa ghafla." Alianzisha maongezi Milfaty ambae kwa kumkadiria alisomeka kuwa na umri wa miaka kumi na nane kama alivyo Nurdin ambae kwa sasa yeye alikuwa akisoma kidato cha nne. Na nimiaka minne ilikuwa imepita toka nurdin aachwe na mpenzi wake Sumaya, pia ni mwaka mmoja ulikuwa umepita toka Hadiya alipoenda uarabuni na asijulikane atarejea au hatorejea.



    "Usijali.. Hakuna tatizo dada yangu. Ni kawaida yangu kuitikia wito wa anaenihitaji." Aliongea Nurdin na kumtoa hofu Milfaty.



    Ukimya ulifuatia huku kila mmoja akiwa bize na kinywaji chake. Nurdin alipoona ukimya umezidi aliamua kuchokoza.



    "Vipi dada.. Mbona kimya?" Alihoji kichokozi.



    "Kweli, ni kimya kwasababu najiuliza sijui hata nianzie wapi kuöngea nawe shida yangu." Aliongea Milfaty huku akizidi kulegeza sauti yake na macho yake yakaanza kuona aibu.



    "Kuwa huru dada yangu. Anzia popote pale wala usijali" Ni kama Nurdin alilitambua dhumuni la Milfaty lakini alijifanya hajui chochote kile. Zaidi alimtoa hofu milfaty na kumwambia kuwa awe huru.



    " ok, kwanza nianze kwa kutanguliza samahani kwa hili ninalohitaji kukwambia," Akatulia kidogo kisha akaendelea. " Kaka Nurdin.. Kwa mara ya kwanza kabisa nilipofika nyumbani kwenu nakukukuta wewe.. Nilijikuta nimeingiwa na kitu moyoni mwangu. Nilihisi raha,raha." Akatulia kwa nukta, kisha akapiga funda moja la mate na kuendelea.



     Ni kama aliongeza ujasiri kidogo. Kisha hapohapo akachukuliwa na mkono wake wa kulia ukaenda hadi kwenye mkono wa Nurdin kisha ukaanza kutalii kwenye kucha za Nurdin. "Nurdin.. Nakupenda. Tafadhali naomba nikubali, usiniache nikaendelea kulia nyuma ya mgongo wako. Please accept my request." Aliongea pasina kuziachia kucha za Nurdin. Hapo Nurdin hakusema wala kunong'ona alikuwa kimya tu ni kama hakuwaza jambo kama lile kutokea japo alihisi tu. Milfaty hakuishia hapo akaongeza kwa kusema," Nurdin.. I wish you hear my little voice right now. Please dont afraid it becouse am already know how you real feel about me, and i want you to love me the same way i do for you. Nahtaji uniite darling, queen of your heart na majina mengine ya mapenzi. Tafadhali shika moyo wangu na usiuache uduende mbio kwa kupata hofu ya jibu lako, utetee moyo wangu, ziokoe hisia zangu. Hisia ambazo ni kama zimeshindwa kuvumilia kila nizikanyapo. Hazifurukuti wala hazionyeki juu yako. Naomba nishike mkono wangu ikiwa ni ishara ya kuridhia nikuombacho kisha uniite kwa jina la mahaba ilinijihisi furaha mbele ya upepo mwanana kama huu wa cockbeach." Hayo ni maneno machache kati ya mengi aliyoyatumia Milfaty mbele ya Nurdin. Kiufupi haikuwa rahisi kuubadili moyo wa Nurdin kama alivyodhani. Moyo ambao umesha muweka Hadiya mtoto wa shekh ambae kwa muda huo yuko uarabuni anasoma.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Sikia Milfaty.. Ikiwa kila atakae hukubaliwa na kila apendezae hufuatwa. Basi hakuna mapenzi ya kweli. Milfaty.. Wewe ni dada yangu, basi endelea kuwa dada yangu. Matatizo yako ya kimapenzi, mimi si mtu wa kukutatulia. Labda kiufupi naweza sema, Shamba tayari lina mlimaji."



    "Nurdin.. Usinifanyie hivyo. Hebu sikia mapigo ya moyo wangu jinsi yanavyopiga yote hiyo inatokana na athari ya maneno yako ya siyo na hata chembe ya huruma. Tafadhali usiniadhibu kiasi hiki. Hata kama shamba limepata mlimaji, kuna uwezekano mkubwa wa kubadilisha mlimaji. Tafadhali fanya uniokoe Nurdin." Aliongea Milfaty huku akianza kuyafuta machozi yake ambayo kwa muda sasa yalimtoka pasina kuyafuta.



    "Milfaty kivipi naweza badilisha mlimaji?" Alihoji Nurdin.



    "Mbona rahisi sana Nurdin. Tengeneza ardhi ngumu isiyopitisha jembe hata liwe na makali kiasi gani, toa rutuba uliyoiweka na wala usikubaliana mbolea utayowekewa na hiyo ndio njia rahisi ya kumtoa kisha utaweka mlimaji mwingine."



    " Nauona ukatili unajongea na kukaribia kivuli cha roho yangu. Siwezi kumtupa alienifuta machozi pindi alipoyakuta yananitiririka kwa udhalili wa yule aliyekuwa wa ubani wangu. Ungekuja kabla hajaja, hapo usingekosa nafasi, lakini kwa bahati umechelewa. Nishamwambia nampenda nae akanambia hivyo tunapendana sana. Siwezi kumuacha kisa mwingine." Aliongea Nurdin.



    Milfaty alipoona ni vigumu sana kumfanya Nurdin amuache aliyenae. Hapo akaanza kuomba angalau hata spea taili lakini napopia alikataliwa katakata. Mwisho wa siku maneno yalimuisha, machozi yakamkauka pia. Hakuwa na sentensi mpya tena ya kumshawishi Nurdin mwenye Moyo mgumu. Hakuwahi kutarajia kama Nurdin angekuwa mgumu kiasi kile kwani jinsi alivyomuona nitofauti kabisa. Mwisho wa siku waliagana na kila mmoja akarudi kwao. Milfaty aliomba afikiriwe angalau hata kidogo ilimradi apewe nafasi.



    ..... .. ..... .. .....



    Mapenzi kati ya Sumaya na Erick yalizidi kunoga. Shule nzima ilijua, na Sumaya hakujutia hilo kwani aliona ufahari kujulikana kuwa mpenzi wake ni msanii. Naam, alichokipata alikipata, kila alipohtaji kuimbiwa aliimbiwa. Alipohtaji kupigiwa gita, alipigiwa. Muda wote aliifurahia sauti ya Erick na hakutamani aikose. Ingawa Erick alikuwa na kipaji lakini hakuwa na mpenzi mmoja. Shuleni hapo alikuwa na wasichana kama saba, huko mtaani ndio usiseme kwani alipata wasichana kadri alivyowarubuni kwa sauti yake na umbo lake lililozoea mazoezi ya basketball. Kuachilia mbali uimbaji, vilevile alikuwa na utaalamu wa kuuchezea mpira wa kikapu na hapo ndipo alipowaua kabisa wasichana.



    Sumaya alitambua wazi kuwa Erick nimpenda wasichana, lakini hakukubali kuiacha sauti nzuri ambayo humuimbia pindi atakapo. Aliendelea kujiaminisha kuwa, huenda kama akijitahidi kumshawishi Erick kimahaba atawaacha wasichana wote na kuwanae pekee. Jambo ambalo halikuwahi kuwazwa na Erick ambae aliamini wasichana kwake ni starehe tu. Tena ukizingatia Sumaya hakuwa katika orodha ya wasichana ambao wanamkosha Erick.



    Sumaya alikuwa ni mtumwa wa mapenzi, alitukanwa na Erick mbele ya watu lakini hakuwa na jinsi, pindi alipokosea alishushiwa ngumi na mateke lakini hakuwa na lakufanya zaidi ya kunyenyekea tu. Kila alipokutana na shemeji yake wa zamani Samir aliona aibu sana. Mpaka ilifikia hatua Sumaya akaacha kuongea na Samir kutokana na maneno makali kutoka kwa Samir yaliyotoa ukweli uliyomchoma sana Sumaya. Aliendelea kuwa mtumwa wa mapenzi mpaka ikafika hatua. Ule uzuri wake ukaanza kupungua kutokana na maumivu aliyoishi kuyapoza.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Wanasema penzi ni kitu cha ajabu sana. Huweza kukupa furaha maishani mwako mpaka ukashindwa kukabiliana na furaha hiyo mwisho wa siku ukajikuta unaamua mambo ambayo mtu wa kawaida hayawezi.



    Kumbukumbu pamoja na mazoea ya penzi la mvulana wake wa kwanza wa maisha yake ziliendelea kumtesa na kumuadhibu sana Sumaya. Kila alipokumbuka zaidi ndivyo alivyokonda zaidi, ukichanganya na maumivu aliyokuwa akipatiwa kila dakika na Erick ndio kabisa. Penzi likawa chungu zaidi ya shubiri Erick akawa bize na mabinti wengine huku tena Sumaya akisahaulika. Zile shida za kimapenzi alizozitatua Sumaya sasa zilitatuliwa na kina Suzi, Ana, Rose, Malia na wengine wengi aliowajua yeye. Ubize wa erick pindi atafutwapo na Sumaya ulizidi sana. Bora zamani Sumaya alikuwa na uhuru wa kufoka lakini ilifikia kipindi kila alipofoka aliambiwa anajipendekeza. Shuleni Erick akawa anaona kinyaa kutembea na Sumaya msichana aliyemchezea hadi akamchoka, acha hayo. Pia aliona kinyaa kuisikia sauti ya Sumaya hata kwenye simu yake. Ndipo alipochukua jukumu la kuiweka namba ya Sumaya kwenye orodha nyeusi ya simu yake. Hapo Sumaya hakumpata tena Erick kila alipompigia aling'amua kuwa amewekwa kwenye orodha nyeusi lakini hakukata tamaa alianza kutuma ujumbe mifupi ya kuomba misamaha pasina kujua kosa. Hakuna majibu aliyoletewa hakuchoka japo hakupata ushirikiano aliendelea kutuma zaidi na zaidi huku akibembeleza penzi hakuna pia alichoambulia zaidi ya Erick kuzitangaza zile Sms kwa marafiki zake na kukuza jina zaidi huku Sumaya akiaibika kwani nizaidi ya dhambi kulazimisha mapenzi.



    "Hivi we Sumaya! Nimara ngapi nimekwambia kuwa huyo Erick hakufai. We ulidhani unaweza kukaa na masupasta? Mwenzio akiiamba anasifiwa na waschana sasa we unadhani wanamsifia burebure. Shauri yako. Mie nilikushauri toka mwanzo usimuache Nurdin lakini hukusikia. Hebu ona ulivyokondeana, ulikuwa mtoto unalipa ona sasa umebaki mifupa. Tatizo lako ulimchukulia Nurdin kama chuo cha kujifunzia mapenzi lakini hukutaka awe mpenzi wako. Umeyaona sasa shost? Nadhani haya ndio mapenzi uliyoyataka."



    "Yaani Hawa! Huwezi amini mimi ni mjinga wawajinga. In short am so confused. Tena usiniletee habari za Nurdin hapa sitaki kumsikia. Kwanza simpendi yule boy, kama angejua. Kwanza sjui hata kwanini nilikubali awe mvulana wangu wa kwanza. Haijalishi ananipenda kiasi gani. Then uniache na Erick wangu shost. Najua hanipendi lakini mimi sijali kwani sina shida nakupendwa bali kupenda. Najua haitaji kuniona lakini sinashida hiyo bali shida yangu mimi nimuone. Hata akiendelea kunitangaza sawa tu acha atangaze kwani nafarijika kusikia anajinadi kuwa alishawahi kufanya mapenzi namimi. Achaniteseke tu lakini sio unishauri nimuache kwani nikimuacha yule naweza kufa hapahapa. Maumivu nishayazoea so mind your own business" Hakika Sumaya alikuwa amekufa na kuoza kwa Erick. Ukisema mabaya ya Erick mbele ya Sumaya basi yeye atayasifia tu. Ni wazi kuwa hakujali ni maumivu kiasi gani anayoyapata. Aliona bora aendelee kuumia ndani ya penzi kuliko kuumia nje ya penzi.



    Hawa alishauri mpaka akachoka lakini hakuweza kuuathiri upendo wa Sumaya. Ni kweli msichana huyo mwenye umri wa miaka kumi na saba kuelekea kumi na nane alikuwa amejitolea kufa hata kama ni kwa magonjwa lakini sikumuacha Erick Mavoko mwenye sauti tamu.



    Hawa aliamua kumfuata Samir na kumuelezea juu ya jambo la Sumaya.



    "Yaani Samir. Kile kisharobaro sjui kisanii kitakuwa kimemloga kile. Huwezi amini yote kinachomfanyia lakini yeye anaendelea kukinyenyekea tu. Kuna siku nilikuwa na Sumaya kikapita mara kikaanza kumdunda makofi huku kikifoka. Eti mara ngapi kimeshamwambia aache urafiki namimi lakini hasikii.. Kika mwambia kama anakipenda kweli, hakitaki kimuone akitembea na mimi. Samir, huwezi amini sikuhizi Sumaya analazimishwa kufanya mapenzi hata akiwa kwenye siku zake..."



    "Weweee! Usinitanie. Nayeye anakubali!?" Alidakia Samir.



    "Ha! Akatae nini sasa wakati amependa. Mwanzoni alikuwa anakataa lakini aliambiwa kama hataki basi waachane. Kusikia hivyo tu. Hapohapo akaachia."



    "Mtumeee simama! Kumbe kuna watu wajinga namnahii kwenye hii dunia."



    "Ndohvyo Samir. Tena sihayo tu. Huwezi amini Erick anampiga hadi picha Sumaya za aibu halafu anazituma sijui online yafasibuku sijui ya gugo hata sielewi ila hukohuko kwenye mitandao ya utandawazi."



    "Usiniambie Hawa. Unataka kusema Sumaya ni mjinga kiasi cha kukubali aaibishwe namna hiyo!?" Alihoji Samir kwa mshangao wa hali yajuu.



    ..... ... ....



    Upande wa Nurdin huko dar-es-salam. Yeye aliendelea na masomo huku akiamini kuwa mpenzi wake hadiya anampenda sana. Aliendelea kuwakataa kina Milfaty wengi waliyojileta na alizidi kuonesha urijali wake kwenye kitabu huku akiwaaminisha wavulana wa rika lake kuwa. Kuitwa rijali sio kufanikisha kuivua nguo ya ndani ya msichana bali ni kuwa makini na masomo.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Kuna wale waliyomcheka na wengine kumuona ni aliyepitwa na wakati huku rafiki zake wengine wakimuitia wasichana mbalimbali kwa ajili ya kumjaribu Nurdin.



    Nurdin alikubali afeli mtihani wa mapenzi kwa ajili ya kufaulu mtihani wa kidato cha nne. Aliendelea kusoma kwa bidii zaidi. Matokeo yake yalikuwa mazuri sana tu toka alivyoenda huko miaka minne iliyopita. Anakumbuka kuwa alipoenda huko aliamua kuanza kidato cha kwanza iliawe sawa na rafiki yake Samir aliyekuwa akimzidi kidato kimoja. Siku zilienda na miezi ikasonga hatimae wanafunzi wote wa Tanzania wa kidato channe walifanya mtihani wao wa kuhitimisha kidato hicho. Mtihani ulichukuwa wiki mbili kwa masomo ya Nurdin. Baada ya wiki hizo mbili. Hakuwa na ziada shuleni kwao zaidi ya kuaga tu.



    "Oy.. Mwanangu, acha yale mambo yako yakiboya. Kwa time hii tumeua channe kwahiyo usilete huo uostadhi wako hapa. Kama ulikuwa unaogopa kuchanganya mapenzi na kitabu. Sasa nadhani huu ndio muda wa kuonesha urijali wako kwa mademu au sio." Aliongea Malundi mmoja kati ya marafiki wa Nurdin.



    "Upo sawa Malundi, Nurdin lazma achanwe makavu. Eti unaleta uostadhi hapa halafu ukiwa mwenyewe unaiendea sabuni. We tafuta dem wa zugiazugia. Angalau hata uwe unashiriki valentine day. Sio wewe eti mgumu. Umekuwa jiwe wewe...?" Aliunga mkono rafiki yao Mmbaga waliyekuwa nae kwenye msafara huo wa kutoka shuleni na wasirudi labda kuijia vyeti vyao tu pindi vitapo hitajika.



    Marafiki wengine wao waliendelea kukenua meno yao kwa kufurahia mtazamo aliokuwa akipatiwa Nurdin. Huku nao wakichangia. Kuna muda Nurdin alielemewa na maneno katika moyo wake hadi hasira zikampanda lakini hakuwa na jinsi maana angezionesha hasira zake mbele za rafiki zake ungekuwa udhaifu mkubwa sana.



    "Tena sikia mkali. Maswala ya kujifanya unawakataa madem hayo ni ya kiboya. We unadhani unapata sifa ila hakuna zaidi ya kuonekana fala tu. Hizo pigo za kukataa ni zakike hizo mshkaji wangu. Milazma nikuchane live hata kama unamaindi ohooo! Eti vulana zima unaambiwa unapendwa wewe unazingua. Kwanza lione eti, lilinyoa kipara kwenye graduation ililionekane liboya na lisifatwe na waschana. Na kwataarifa yako utakumbuka ulivyojiharibia mahafali boya wewe." Marafiki zake waliendelea kumsakama tena wengine kama kina Malitine wao walimpiga piga na ngumi za utani huku wakimtemea na mate.



    "Poa wana... Yaishe nimewaelewa. Kama vipi pigeni chini hiyo mada au siyo? Au muipotezee kabisa." Aliongea Samir huku akirusha rusha mikono hewani ilikuwakilisha alichosema. Marafiki zake wote wakamkebehi wengine wakamcheka vicheko vya kutafuta.



    "Unajua we Nurdin usijifanye ostadhi kumbe mbwiga tu. We unawaogopa madem na ndio maana hutaki kuwanao. Sisi tunakwambia hivi si kwamba hatukupendi bali tunakuchana iliujue inshu zako ni zakike na sio zakiume." Aliongea mmoja kati yao.



    "Poa wana, mi... Nimewapata. Hata mimi nilifanya hivyo kwa ajili ya masomo tu ila kwasasa siwaangushi." akawaomba tano kisha wakampa.



    Haikupeta hata dakika moja akajipitisha mrembo mmoja mkabala na wao. Mrembo yule alionekana kuchezea simu yake ya kufagia na kuvalia mavazi ya kileo yaliyomfanyaaonekane kama ametoka mbiguni na kuletwa moja kwa moja bila kuzaliwa.



    Hapo rafiki zake na Nurdin wakampa Nurdin mtihani wa kuhakikisha anapata namba kwa mdada yule iliaöneshe urijali wake na kuwaaminisha kuwa ameshabadilika. Alifanikiwa kumfuata binti yule na dakika tatu tu zilimtosha kuchukuwa namba za binti yule. Hapo wenzake wakamuamini na wengine pia walimshangaa sana kwani sirahisi kuchukuwa namba kwa muda mfupi kiasi hicho. Hapo na mada ikabadilishwa.



    ... .. ...CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Upande wa Samir, siku hiyo kwake aliitumia kuzunguka ndani ya msitu wa shule yao huku wakitafuta matunda na kupigana picha, utadhani wanafanya utalii wa ndani kumbe walikuwa wakiiaga tu shule yao. Waliongea mengi wakacheka sana huku wengiwao wakijua kuwa hawataonana tena katika maisha yao hivyo wenye simu walibadilishana namba huku ambao hawana wakiishia kuchukuwa namba za wenzao. Walipiga picha nyingi sana.



    "Oyaa. Wanangu eee. Wangapi tunaenda pre-form five??" Aliuliza Alex. Mmoja kati ya wanafunzi wenye vituko sana.



    Wenzake wote wakacheka huku wakitaniana kwa kutajana majina na waliotajwa majina wao pia waliigiza hasira ilimradi tu kudhihirisha ya moyoni mwao.



    Ulipofika muda wa kuagana, wote kwa pamoja walishikana mikono na kutakiana maisha mema huku wengine wakipatwa na machozi kwani waliamini kuna baadhi yao hawatoonana tena.



    "Najua mtasema Sipo.. Sijui mtanimis. Eti Samir alikuwepo.. Mademu mtanikiss. Mengi mtayamiss ikiwa wangu usumbufu na hamtaniona tena ka muda wanipige tafu.



    Oyaa.. One love wanangu ausio. Ipo siku, kwani wazee walisema binadamu sio milima." Ni baadhi ya maneno aliyoyatamka Samir ikiwa ni kumbukumbu ya wimbo wake aliyouimba siku ya mahafali yao. Waliagana na kila mmoja akaenda kivyake



    Samir alipofika kwao yeye alibadili nguo kisha akaenda kuoga ilikuondoa jasho lililogandamana mwilini mwake. Baada ya zoezi hilo alipata chakula huku akifurahia zaidi kumaliza kidato hicho cha nne. Alipomaliza kula alirudi kulala kwa ajili ya kuipumzisha akili yake kwani aliamini ile hekaheka ya siku hiyo ilitosha kabisa kumfanya awe hoi. Akiwa kitandani kabla usingizi haujamuijia mawazo yalimrudisha mbali na kukumbuka tukio lililotokea wiki moja kabla ya wao kuanza mitihani ya kidato channe



    * * * *



    "Sikuhitaji wala siku taki mjinga wewe.. Halafu mbona unaning'ang'ania wakati sikupendi. Tafadhali achana namimi we huoni mpenzi wangu Suzi ananisubiri? Ebo! Shtuka wewe kumekucha. Nilikukubali ilinikutumie kwakuwa sikuwa na msichana kipindi hicho na kwanza ndio nilikuwa nimeingia shule. Acha ushamba.. Mie sikupendi kwahiyo jikatae." Ni maneno yaliyomtoka Erick Mavoko usiku wa siku ile ya mahafali. Siku hiyo ilimuharibikia sana Sumaya. Japo ilikuwa ni siku ya furaha mchana lakini usiku wa siku ile ulibadilika na kuwa aibu isiyo na mfano. Hiyo ni baada ya Sumaya kuhtaji kucheza na mpenzi wake Erick Mavoko usiku wa kwani baada ya mahafali kulikuwa na disko. Alipomfuata mpenzi wake na kumkuta anacheza na msichana mwingine kwa jina la Suzi. Njisi walivyokuwa wameng'ang'aniana huku wakifatiza wimbo wa Mallow uitwao daima na milele ilimpelekea Sumaya kupandwa na hasira maradufu akasahau kuwa yeye kwa Erick ni mtumwa wa mapenzi na wala simpenzi wa haki. Akavuta mkono wake kwa hasira na kuachia kofi lenye hasira lililoenea vyema kwenye shavu la Suzi. Suzi palepale aliyumba na kupoteza muelekeo kama sekunde thelathini hivi. Huku Erick akiduwaa kuona kitendo kile pamoja na wanafunzi wengine waliyofanikisha kuisikia kelele ya Suzi pindi alipopigwa kofi. Ilikuwa ni vigumu zaidi kusikika kelele za Suzi kwani spika zilikuwa zimeachiwa na kusababisha wimbo umezee sauti zote ndogo ndogo.



    Hapo baada ya Suzi kumgundua aliyemchapa kofi, hakutaka kuvumilia wala kuuliza. Akamvagaa moja kwa moja Sumaya. Wote wawili wakashikamana na kuanza kupiganda, Sumaya aling'atwa mkononi huku Suzi akijeruhiwa kwa meno maeneo ya tumbo lake. Wanafunzi walijaa na kuacha kucheza tena kwa ajili ya kushangaa mabondia wale waliyougeuza ukumbi wa disko kuwa ukumbi wa masumbwi.



    "Achaneni. Nasema achaneni!" Aliendelea kufoka Erick mavoko. Hakuna aliyemsikia lefa huyo zaidi ugomvi uliendelea kati yao. Ndipo Erick alipochukua hatua ya kumwasha makofi matatu ya nguvu Sumaya. Makofi yaliyomfanya aumie sana, hakuishia hapo tu. Alimdhalilisha kwakumtukana matusi ya kwenye nguo. Kisha kwakumdhalilisha zaidi alimshika mpenzi wake Suzi na kumkumbata kisha yeye na Suzi wakabadilishana mate yao mbele ya macho ya Sumaya na umati wa wanafunzi.



    Erick aliona haitoshi akamfuata Sumaya ambae kwa muda huo alikuwa chini na kuanza kumdhihaki huku akitoa tablet yake na kuanza kuuonesha umati ya wanafunzi picha za uchi alizompiga Sumaya.



    Samir hakuwa karibu. Alikuwa nyuma ya madarasa na marafiki zake wa kidato cha tatu na pili . Alikuwa akiomba flash iliyokuwa na bit alilokuwa anahtaji kulitumia usiku ule jukwaani. Akiwa na wenzake mara ghafla akaja Hawa.



    "Samir, njoo." akaenda Samir.



    "Hebu twende ukaone jinsi Sumaya rafiki yangu anavyoaibishwa. Maskini hadi namuhurumia. Hana la kufanya." Samir alivyosikia jina la Sumaya na neno kuaibishwa hapohapo uvumilivu ulimshinda na moja kwa moja akaenda hadi pale kwenye tukio. Samir aliumia sana baada ya kumuona Erick akionesha picha za utupu za Sumaya, hapohapo akamfuata Erick mavoko na kumpiga ngwala. Erick alianguka kama mzigo akaangusha na tablet yake kwa pembeni kisha Samir kwa hasira akaiendea ile tablet na kuikanyaga kwa makusudi kisha akamfuata Erick na kumpa onyo.



    " Acha dharau mpuuzi wewe. Unajua huyu dem anathamani gani kwenye maisha yangu hadi unafikia kumdhalilisha namna hiyo? Sasa rudia tena kufanya upuuzi wako ndipo utajua kwanini nimeitwa Samir. Boya wewe.." Kwa muda wote huo Erick mavoko alikuwa ametulia huku akitathmini pesa aliyonunulia tablet. Hakuwa na lakufanya kwani anamjua vizuri Samir na anazijua akili za Samir kuwa huwa ni mkorofi endapo utamuudhi. Yupo ladhi aende kunyea ndoo kwa kukujeruhi bila uoga. Alipomaliza kuongea alichukua kadi ya kumbukumbu iliyokuwa ndani ya tablet na kumchukua Sumaya kishaakaondokanae.



    * * * *



    Kumbukumbu za tukio lile zilitoka kichwani mwa Samir baada ya kusikia mlio wa Simu yake. Akaitazama kwenye kioo na kumgundua mpigaji kisha akaipokea na kuiweka sikioni.



    "Hello, nambie Nurdin" Aliongea Samir kuiambia sauti ya upande wa pili wa simu.



    "Fresh tu kijana. Vipi mzima wewe?" Alijibu na kuuliza Nurdin.



    "Yap. Nikopoa tu. Hofu kwenu."



    "Sie tuna mshukuru Mungu. Tupo wazima. Mie nilikuwa nakutaarifu tu kwamba kesho kutwa mie naanza safari ya kuja huko mkali wangu kwahiyo jiandae kunipokea." Aliongea Nurdin kwa sauti ya bashasha.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/





    "Acha utani wewee.. Kisho kutwa!! Mmmmh! Usiniyeyushe." Aliongea Samir kwa mshangao kidogo kwani hakutarajia kusikia kile kilichoingia kwenye ngoma za masikio yake.



    "Ndo hivyo mkali wangu. Nimekumiss ile mbaya. Yaani hata hizi siku ninazoendelea kukaa huku naziona nyingi kichizi." Aliongea Nurdin.



    "Bora wewe unaeziona nyingi angalau ipo siku zitapungua na kufika. Ila mimi naziona zimeganda tu."



    "Usijali Samir, muda simrèfu tutakuwa wote ilituendeleze shoo za kibabe." Aliongea Nurdin.



    "dah! Nimekukosa sana jembe langu. Mihuku nilikuwa niko peke yangu tu. Siunajua tena washkaji wengine wazinguaji tu. Mara wakusnichi mara wakupe kampani. Sasa mie huwa nawazingua tu." Aliongea Samir huku akilalamika.



    "Ok... Vipi lakini zile itikadi zako za kutokuongea na Zulfa. Ziliishia wapi mkali wangu. Maana nanyie mlikaushiana hadi salamu." Aliongea Nurdin huku akijenga utani.



    "Aaaa! Huyo dem sialijifanya anazingua. Kipindi yupo kidato chapili sisi tulishangaa amerudi hom wakati skul kwao ni bodi.. Basi sinikajua labda mtoto, anau... Anaumwaa. Kuja kushangaa mwanangu. Kumbe kesha pigwa bendi na kamsela ka hukohuko skul kwao. Aisee mkali sikufichi nilipopata hiyo inshu nilitamani kulia ghafla. Lakini poa wajanja washafanya yao na sasa hivi anamtoto. Ila hai kama kawaida, siku hizi ni mshkaji wangu tu na zinapanda kiaina." Aliongea Samir kwakulalamika ilikuonesha jinsi swala lile lilivyomchoma.



    "wewee!! Usiniambie mwanangu... Unajua kuna inshu za kutaniana ila sio hizo. Kwahiyo unataka kusema Zulfa mpaka sasa hasomi tena.?" Alishangaa sana Nurdin na kuhoji.



    "Ndohivyo kesha haribu.. Sasa hivi anaitwa Mama Hadija. We unadhani mchezo ee." Alijibu Samir.



    "Kwa hiyo mwanangu, wewe na Zulfa ule mchezo wenu wa mapenzi ndo umeishia hapo. Dah! Pole sana mkali wangu."



    "Kawaida tu siunajua dunia inajua kulipa. Yeye alinizingua kwakudhani huenda mimi ni simpendi eti kisa nilienda kwa anco. Amewapata wanaempenda, wamemgeia mimba halafu wamesepa. Tena bahati yake ni kwakuwa kwao ni wapole tu ila wangekuwa magadafi sjui hata angeishi wapi."



    "Ok, na vipi kuhusu yule mtoto yule."



    "Yupi huyo. Funguka sio ulete habari za viwakilishi hapa."



    "Aaaaahh! Inamaana unajifanya humjui? Si yule mtoto wa nani? Yule aliyenitosaga?"



    "Unamuongelea nani? Sumaya?" Alihoji Samir.



    "Yea. Huyohuyo... Vipi kitambo sana. Huwa haniulizii kweli au ndo tuseme kale kasharobaro ulikonambia kameshamteka kabisa." Aliongea Nurdin.



    "Aisee mwanangu nawewe... Kwani we hukupata dem huko jijini hadi unaulizia hawa wasiojua hata kuoga?" Alikebehi samir.



    "Aaah! Mwanangu acha hizo. Misijauliza kwa ubaya."

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "ok, kama hujauliza kwa ubaya. Basi tuachane na hadithi za huyo aliyekufanya moyo wako ukaumia poa?"



    "Lakini kwani kuna ubaya kumuulizia my ex-girlfriend wangu."



    "Ndio upo. Tena upo ubaya mkubwa sana. Ila huu si muda wake weendelea na mishe zako."



    Waliendelea kupiga soga mpaka hapo maneno yalipo waisha ndipo wakaagana na Nurdin akakata simu.



    ..... ..... ..... ......



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog